MADA YA KWANZA.
UTANGULIZI JUU YA HISTORIA
YA KANISA.
A.UTANGULIZI
Somo hili linaanza na
kupaa kwa Yesu Mbinguni katika mlima wa mizeituni kama mwaka wa 30 .AD na
linaishia na kurudi kwa Yesu mara ya pili ya pili kupitia kwenye mlima wa
mizeituni katika kipindi cha mwisho {ufu 19-16-26, Zek 14:1-9}
Waandishi wahistoria ya
kanisa hawakubaliani katika namna ya ugawaji wa vipindi vya historia ya kanisa
.Baadhi hugawa vipindi kulingana na matukio muhimu kuhusu watu Fulani maalufu,
mfano kutawazwa kwa papa wa kwanza mnamo mwaka 590 A.D, au wakati wa
matengenezo ya Martini Luther, alipoandika maandiko {Thesis} yake 95 na
kuyabandika katika mlango wa kanisa huko Witenberg Ujerumani mwaka 1517 .
Baadhi pia hupenda
kugawa vipindi katika historia ya kanisa kulingana na matukio mbalimbali yalioleta
athari katika kanisa mfano kuongoka kwa Kiongozi mkuu wa Dora y aRoma Mfalme
Kostantino mwaka 313 AD .Au patano la amani la Westphalia mwaka wa 1646.
Pia wataalamu wengine
hugawa vipindi vya kanisa kwa kufuata mtindo wa kinabii kwa kuzingatia orodha
ya makanisa saba (7) kama yalivyoainishwa katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana
sura ya pili nay a tatu.
Katika somo hili tutagawa vipindi vya historia
ya kanisa kwa kufuata mhutasari wa
makanisa saba yanayopatikana katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana Sura ya pili na
ya tatu ambapo vipindi mbalimbali vya kanisa vimeorodheshwa kwa njia ya
kinabii.
B. DHANA YA HISTORIA.
Historia kama somo inafafanuliwa
kwamba ni somo linalohusu matukio mbalimali katika vipindi mbalimbali vya
maendeleo ya mwanadam.
Baadhi ya wataalamu wanafafanua
kwamba historia ni rekodi za shughuliza binadamu katika vipindi viliyopita.
Kwahiyo historia huhusika na kuainisha matukio mbalimbali muhimu yaliyotokea
katika vipindi mbalimbali katika jamii ya mwanadamu.
C. MAANA YA HISORIA YA KANISA
Ni taaluma inayoelezea vipindi mbalimbali
ambavyo kanisa limepitia tangu kuanzishwa kwake mpaka Yesu kristo atakapokuja
kulichukua kwenda mbinguni .
D. SABABU ZA KUJIFUNZA HISTORIA YA
KANISA
Kuna sababu nyingi ambazo zinatufanya
tujifunze historia ya kanisa na kuifanya kuwa mojawapo ya somo linalotakiwa
kufundishwa katika shule za Biblia na vyuo vya thiolojia .Baadhi ya sababu hizo
ni:-
Historia ya kanisa
inatusaidia kutambua jinsi kanisa lilivyoanza na jinsi lilivyokabiliana na
changamoto mbalimbali.
Inatusaidia kujifunza
misimamo ya kiimani ya mababa wa kwanza wa kanisa na kututia moyo sisi kuitetea
imani kama wao walivyoitetea.
Inatusaidia kujua
changamoto mbalimbali kanisa lilizopitia tangu kuanzishwa kwake mpaka
sasa.mfano changamoto ya mateso wakati wa watawala mbalimbali wa Dola ya Rumi
waliyowapata kanisa la kwanza, kama vile kusulubiwa kwa mtume Petro, kunyongwa
kwa Mtume Paulo, Kuchunwa ngozi na kutumbukizwa kwenye mafuta yanayochemka
motoni Mtume Bathromeyo.
Inatusaidia kujua jinsi
wakristo waliotutangulia walivyoitetea imani kwa kuwa tayari kufa bila
kuisariti imani mfano John Huss Martini Luther, Porykap, Klement Origen, Urlich
Zwingri. N.k
D.MAKANISA
SABA YA ASIA NDOGO
Mfalme Domitiani alimpeleka
mtume Yohana uhamishoni katika kisiwa cha Patmo kwa sababu ya imani. Akiwa
katika kisiwa hiki mtume Yohana alipokea jumbe toka kwa Bwana Yesu Kristo kwa
ajili ya makanisa saba yaliyokuwa katika Asia ndogo. Jumbe hizo baadae
ziliingizwa kwenye orodha ya kanuni ya Maandiko na sasa ni kitabu cha Ufunuo
wa Yohana. Mtume Yohana alipokea jumbe hizi akiwa na umri wa miaka 90.
Jumbe
hizi zilikuwa na matuimizi ya aina nne ambayo ni
1. Zilikuwa ni jumbe
maaalum kwaaiili ya makanisa katika wakati wa mwandishi.
2. Zilidhihirisha na
kufunua hai ya kiroho ya kila kanisa lililoandikiwa jinsi ilivokuwa . 3.
Zilikuwa ni jumbe kwa waamini wote wa zama zote za kanisa.
4. zilikuwa ni muhtasari wa kinabii wa
historia ya kanisa.
F.
MUHTASARI WA MPANGILIO WA MAKANISA SABA
YA ASIA NDOGO.UFUNUO 1
KANISA
|
KIPINDI
|
MUDA
|
EFESO
|
KIPINDI
CHA MITUME (Kanisa la Mitume)
Tangu
kupaa kwa Yesu Kristo Mbinguni mpaka kifo cha Mtume Yohana.
|
30
.BK- 100 B.K
|
SMIRNA
|
KIPINDI
CHA MATESO (Kanisa la mateso).
Tangu
kuchomwa moto mji wa Rumi mpaka kuongoka kwa mfalme kostantino.
|
64.
B.K – 313 B.K
|
PEGAMO
|
KIPINDI
CHA KIHARI (Kanisa la Kifahari)
Tangu
kuongoka kwa mfalme Kostantino mpaka kuanguka kwa dola ya Rumi.
|
313
B.K -476. B.K
|
TIATHIRA
|
KIPINDI
CHA KIPAPA (Kanisa la Kipapa)
Tangu
kuanguka kwa dola ya Rumi mpaka kuanguka kwa Kostantinopali
|
476.
B.K - 1453 .
|
SADI
|
KIPINDI
CHA MATENGENEZO (Kanisa la Matengenezo)
Tangu
kuanguka kwa Kostantinopali mpaka patano
la Westphalia
|
1453.-
1648
|
FILADELFIA
|
Kipindi
cha umisheni au uinjilisti. (KANISA LA UMISHENARI)
Tangu
patano la Westphalia mpaka vita ya kwanza ya Dunia.
|
1648-1914
|
LAODEKIA
|
KIPINDI
CHA UONGO (kanisa la uongo/vuguvugu)
Tangu
vita ya kwanza ya Dunia mpaka kipindi cha Milenia mpya.
|
1914…
|
MADA
YA PILI
KIPINDI
CHA EFESO.
{Kanisa
la Mtume}
A.
UTANGULIZI.
Kanisa la Efeso Ufu 2:1-7.
MUDA; Tangu kupaa kwa
Yesu Kristo kama mwaka 30.AD.Mpaka kifo cha mtume Yohana kama mwaka wa 100. B.K.
Efeso ulikuwa mji
muhimu katika pwani ya Asia ndogo na ulipewa jina la heshima la Nuru
ya Asia. Waefeso waliabudu miungu ya kiasia ambayo ni Artemi, ambae pia aliitwa Diana.
Hekalu la artemi lilihesabiwa kuwa mojawapo ya maajabu ya dunia ya wakati ule.
Mahali pengine walipoabudia paliitwa Augusteum. Mahali hapo walitumia kumwabudu
mfalme . kiwango cha kiburudani za kidunia zilikuwa nyingi na inakadiriwa kuwa
Ukumbi wa Efeso ulikuwa na uwezo wa kuchukua watu 25,000.
Kipindi hiki kinaitwa
kipindi cha mitume kwa sababu mitume wote12 wa mwa nakondoo {Yesu} waliishi
katika kipndi hiki. Na kipndi hiki kiliishia na kifo cha Mtume Yohana ambae
alikufa kifo cha kawaida akiwa mzee mwenye umri wa kama miaka 100.
Tabia za kanisa la
Efeso ni muhimu sana katika kipindi hiki . Kuna walimu wa theologia wanaofundisha
kwamba mitume na manabii waliishia katika kipindi hiki. Jambo ambalo si kweli
kabisa kwani huduma hizi zimekuwepo katika vipindi vyote vya kanisa japokuwa
katika vipindi fulani zilififia. Lakini zimekuwepo katika zama zote za kanisa.
B.ULIMWENGU
WA WAKATI WA MITUME
Mitume walipambana na
upinzani mara tu kanisa lilipoanza. Upinzani huo ulitokana na makundi mbalimbali
. 1.
Wayahudi, Wayahudi walikuwa ni adui namba moja wa kanisa .walilivamia kanisa wakati
lingali changa kwa kushirikiana na mfalme wa kirumi walimsulibisha Yesu Kristo.
a). Masafarisayo. Hawa walianza katika
kipindi cha Ezra na Nehemia . waliporudi toka uhamishoni Babeli. Wakati ukuhani
mpya ulipoanzishwa. Waliamini ufufuo wa
wafu, adhabu ya wenye dhambi , kutokufa kwa nafsi,uwepo wa malaika na huduma
zao na kwamba kila kitu kinamtegemea Mungu. Mtazamo wao wa kisiasa ulikuwa ni
wa kiyahudi. Na
Waliogopa kushirikiana na watu wasiokuwa
mafarisayo. Mfano Wasamaria, na Wamataifa na kwa namna zote walizishika sheria
za Musa na walifanya tohara.
b.Masadukayo,
Hawa jina lao lilitoka kwa Sadoki kuhani mkuu wa wakati wa Daudi toka uzao wa
Haruni Kuhani Mkuu. Hivyo walikuwa ni uzao wa kikuhani.Wao hawakuamini ufufuo wa
wafu wala uwepo wa malaika.
2. Dora
ya Kirumi,. Mwaka 63 mfalme wa Rumi Julius Kaizari aliivamia na kuishinda Parestina
na akaanzisha utawala wa kirumi katika nchi ya parestina . Huu ulikuwa ni
ufalme wanne uliokuwa umeishinda na kuitawala Israeli kulingana na unabii wa Danieli
. Israeli ilikuwa chini ya utawala wa dola ya Rumi Yesu Kristo alipozaliwa na
katika kipindi cha maisha yake hapa duniani.
a. Upagani,
hii ilikuwa ni dini ambayo mianzo yake ni mtawala Nimrodi katika mnara wa Babeli
na dini hii baadae ilisambaa katika maeneo mbalimbali yaliyoizunguka Babeli
mpaka Misri, Ugiriki na Rumi.Waliabudu miungu ya kigeni {Yer 2:25}. Ilikuwa ni
miungu ya zamani sana ya Kibabeli, ilikuwa na majina mbalimbali katika nchi
mbalimbali, mfano artemi ,Diana, Osiris, Jupita Appos Zeus. N.K
b.Ibada ya mfalme. .Hii ilikuwani moja wapo ya tamaduni za dola ya
kirumi. Baadhi ya wafalme wakirumi walijitangaza kwamba wao ni miungu na
wakadai kwamba wananchi wao wanatakiwa kuwaabudu.hivyo Ibada ya kuwaadudu
wafalme {makaisari} ilianzishwa. Kukataa kumwabudu Kaisari kungepelekea mtu kuhukumiwa adhabu ya kifo.
Ibada ya kumwabudi mfalme ilikuwa imerithiwa toka kipindi cha babeli.
C.Wanafasalsafa wa Kigiriki. Kulizuka falsafa za kigiriki ambazo
zilikuwa zinasisitiza kwamba lengo la maisha ni furaha na anasa. Walisisitiza
kwamba maarifa yanaweza kupatikana kwa njia ya kufikiri {Logic}.Waliegemea
katika vitu vinavyoonekana tu. Falsafa hizi ndizo ambazo zilikuwa zimeshikiliwa
na watu mbalimbali katika kipindi hiki.
Falsafa hizi zilisisitiza
kwamba maisha ni kula na kunywa kwa sababu baada ya kufa mwanadamu alikuwa anaoza
na kwamba hakukuwa na maisha baada ya kufa.
C. KUANZA KWA KANISA.
Kanisa lilianza Yerusalemu siku aliposhuka Roho mtakatifu
katika chumba cha juu katika hekalu la Yerusalem. Baada ya Yesu Kristo kupaa
Mbinguni wanafunzi walirudi toka mlima wa Mizeituni mpaka hekaluni na kukaa
katika chumba cha juu. Waliomba na kusubiri kuvikwa nguvu. Baada ya siku kumi
Roho Mtakatifu alishuka na wote waliokuwemo kwenye chumba cha juu walijazwa na
Roho Mtakatifu na kuanza kumwazimisha Mungu kwa Lugha zingine. Kazi ya
uinjilisti ilianza papo hapo mtume Petro alihubiri na watu 3000 wakaokolewa na
kubatizwa. Hii inahesabiwa kwamba ndio mwanzo wa kanisa la agano jipya.
Sifa za kanisa la
kwanza.
1.
Lilikuwa na utii kwa sehemu
2.
Utendaji.
Lilikuwa na hali ya utendaji
3.
Utendaji lilikuwa na utendaji
Matokeo ya kujazwa Roho Mtakaifu
1.
Kutiwa nuru. Waamini kwa
kwanza walitiwa nuru katika akili na
fahamu zao na wakapata kuyaelewa maandiko matakatifu.
2.
Kutiwa
nguvu na ujasiri, wamini hawa walitiwa nguvu na ujasiri
na na kuwezeshwa Kulihubiri Neno la Mungu kwa ujasiri.
3.
Kutenda
ishara na maajabu. Mitume waliwezeshwaq kutenda miujiza sawasawa na ahadi
ya Yesu Kristo Mk 16:15-20.
D. WANACHAMA
KTIK A KANISA.
Wanachama katika kanisa la mwanzo walikuwa ni
wayahudi {proselytes} ambao twaweza kuwagawanya katika makundi manne. ambayo ni
;
1.
Waebrania
. hawa walikuwa ni wayahudi ambao baba zao walikaa Palestina na walikuwa ni uzao
wac Kiebrani.
2.
Hellenists, walikuwa ni
wayahudi waliokuwa wanakaa katika nchi zingine wengi wao walikaa Uyunani.
3.
Proselytes.Walikuwa ni watu
wamataifa waliokuwa wamefanyika kuwa raia wa kiyahudi, walifuata sheria za
kiyahudi na walijiunga na dini ya Kiyahudi. Pia walitahiriwa kama wayahudi.
Mfano Nikolasi {Mdo 6:5}
E.
UONGOZI
NA UTAWALA WA KANISA.
Kanisa la kwanza
halikuwa na Mfumo wa uongozi wa kiutawala kama ilivo sasa. Kila kanisa la mahali pamoja
lilikuwa na uongozi wake uliojitegemea. Hakukuwa uongozi uliokuwa unasimamia
makanisa yote. Mitume walikuwa ni
waangalizi wa kanisa na hawakujiweka kuwa watawala wa kanisa. Bali watumishi wa
kanisa.
F.
MAFUNDISHO YA KANISA LA KWANZA. Mafundisho ya kanisa
la kwanza yalikuwa rahisi, Agano jipya lilikua halijaandikwa. Ujumbe wao
ulikuwa na maeneo machache ambayo ni ; Uungu
wa Yesu Kristo. Yesu kristo wa
nazareti ni mwana wa Mungu na ni nafsi hai. Maelezo haya yalisababisha
mateso katika kanisa .
Ufufuo
wa Yesu Kristo. Ufufuo wa Yesu kristo ulikuwa ni kiini cha mahubiri au
ujumbe wa kanisa la kwanza.
Kurudi
kwa Yesu Kristo mara ya pili. Walihubiri kwamba Yesu
Kristo atarudi tena {Mdo 3:20-21, 1The 4;15-17}Hili lilikuwa ni tumaini la
Baraka kwa waamini wote.
G.
KUSHINDWA KWA KANISA LA
KWANZA.
Kanisa la kwanza
lilishindwa kufikia kusudi kwa sababu zifuatazo.
Kukosa
maono ya umisheni
. Mungu aliliagiza kanisa kwenda kuhubiri Injili ulimwenguni kote MT20:28, Mk
16:16} lakini kanisa la kwanza hawakufanya hivyo bali walijihusisha na umisheni
katika Yerusalemu tu.
Kujihusisha na shughuli za kijamii, Mitume walianza kujihusisha na mambo ya kijamii {kiutawala}
kwani shughuli zote za kanisa za kila siku zilifanywa na wao.Tunaona Petro
aliyekuwa mhubiri anaanza kujihusiha na mambo ya kiutwala.
Mitume walifika mahali
wakagundua tatizo hilo na wakachagua wahudumu saba waliotakiwa kushughulikia mambo
ya kiutawala ili wao wadumu katika
kulihubiri Neno na Kuomba.
Bwana alilionya kanisa lake “Tubu na ukafanye
mambo ya kwanza la sivyo nitakiondoa kinara chako mahli pake. Mungu alitimiza
Neno lake kama Tutakavyo ona hapo baadae.
H.
KUENEA KWA KANISA LA KWANZA.
Kupanuka kwa kanisa tangu mahubiri ya Stefano {mwaka 35. AD} hadi mkutano wa
Yerusalemu {mwka 48. AD}.Mambo ya msingi katika kipindi hiki yalikuwa ni
upandaji wa makanisa. Kipindi hiki kifupi kilikuwa na umuhimu mkubwa kwa kanisa.
Japokuwa kanisa mwanzo lilikuwa Yerusalemu tu sasa lilipandwa katika maeneo mengine kama vile Siria na Asia ndogo
na kuelekea Ulaya.
Waamini wa kwanza
walikuwa ni Wayahudi lakini baada ya kipindi hiki kifupi waamini wengi walikuwa
ni wamataifa .
Mwanzoni Injili ilihubiriwa kwa kiebrani na kwa kiaramu lakini baadae iligundulika kwamba ulimwengu mzima
ungefikiwa na Injili kupitia lugha ya Kigiriki
kwa sababu kigiriki wakati huo kilikuwa ni lugha ya mawasiliano ya kimataifa kama ilivyo kiingereza kwa dunia
nzima ya sasa.
I.
KUTESWA KWA KANISA NA
VIONGOZI WA KIYAHUDI.
Yesu aliwaagiza mitume kwenda kuhubiri Injili
duniani kote lakini wao walipenda kukaa Yerusalemu .Mungu alikasirika na akaamua
kuruhusu mateso katika kanisa .{Mdo 9}
1. Mahubiri
ya Stefano{.Mdo 6:1-4, 7} Kwa sababu ya imani yake kwa Neno la Mungu Stefano alihukumiwa
kuuawa na kuwa mfia dini wa kwanza katika imani ya kikristo. Kijana mmoja
mfalisayo wa tarso Sauli alishuhudia mauaji ya Stefano na Baadae kijana huyo
akawa kiongozi mkuu wa mauwaji ya wakristo katika taifa la wayahudi.
Kutokana na tukio hili
waamini wote walikimbia Yerusaelimu
isipokuwa mitume {Mdo 8:1-4}.Waamini hao walisambaa maeneo mbalimbali na
kila mahali walipokwenda walilihubiri Neno . Kwa njia hii kwa muda mfupi Injili
ilipata kuenea kwa haraka katika maeneo yote yaliyoizunguka Yerusalemu.
2. Kanisa Linakwenda Samaria,{
Mdo 8}.Wasamaria walikuwa ni chotara ambao asili yao ilikuwa ni Ashuru ambpo walihamishiwa katika eneo la
Kaskazini mwa Israeli. Pale waisraeli walipochukuliwa
kwenda utumwani Ashuru {Irani}. Mchanganyiko wa wageni hao na mabaki ya waisraeli
ambao hawakwenda utumwani Ashuru yaliunda kabila la Ashuru kutokana na kuoana .Watoto
waliozaliwa walikuwa chotara.
Wasamaria
Walikuwa
na hekalu lao katika mlima Gelzimu na walivitumia vitabu vitano vya Musa pekee
kama Biblia yao. Kwahiyo Wayahudi hawakuchangamana nao.
Roho Mtakatifu alimwambia Shemasi Filipo
kwenda kuhubiri Neno Samaria Mungu alimtumia kufanya ishara na maajabu kwa jina
la Yesu huko Samaria. Uamsho mkuu ulitokea huka Samaria. Watu wa huko Samaria waliokoka
na kubatizwa .Mitume walipopata habari hii walikuja kuwaombea ujazo wa Roho
Mtakatifu. Baada ya maombi hayo Wasamaria
walijazwa Roho mtakatifu.
Angalizo. Wasamaria waliokolewa na
kubatizwa katika maji chini ya huduma ya Filipo, lakini walikuwa bado
hawajabatizwa kwa Roho Mtakatifu . Ubatizo wa Roho mtatifu ni upako maalumu
ambao kupitia huo tunapokea nguvu toka kwa Mungu.
3. Injili inakwenda Afrika
{Mdo 8 }. Roho mtakatifu alimtuma mwinjilisti Filipo kwenda kumhubiri Neno
Towashi wa Kushi {Waziri wa fedha wa Ethiopia}. Filipo alimwongoza towashi huyu
kwa Bwana na kasha akambatiza. Inaaminika kwamba towashi huyu alipeleka injili
Afrika . Kwa sabau alikuwa ni mkza wa Barala Afrika katika nchi ya Ethiopia
J. MTESI WA KANISA ABADILI UPANGA {Mdo 9 }
Sauli wa tarso ambae
ndiye aliekuwa mtesi mkuu wa kanisa kwa kipindi hiki aliokoka baada ya kukutana
na Yesu Kristo alipokuwa safariki kuelekea Dameski kuwakamata na kuwaua waamini
{Mdo 9:20 }. Mara baada ya kuokoka alianza kuihubiri injili {Kumhubiri Kristo
Yesu}. Paulo aliweka chini upanga wake
wa mauaji na kuchukua upanga wa Neno la mungu Ambao hakuuacha mpka kifo chake.{
2Tim 4:7}.
Paulo alikwenda katika jangwa la Arabia kwa
miaka Mitatu ambapo alipata mafuo zaidi toka kwa Mungu. Baada ya hapo alirudi Yerusalemu kuonana na
mitume. Baada ya Sauli kukutana na Ndugu alirudi tena Tarso. Kanisa lilipata
raha baada ya kuokoka kwa Sauri wa Taso.{Gal 1:16-18, Mdo 9:20-31}.
5.Injili
inakwenda kwa watu wa mataifa{Mdo 10 }. Mtume Petro alitumwa kwenda kumhubiri
Kornelio mtu wa Mataifa Injili . Mtume petro ndiye aliyefungu mlango wa Injili
kwa wayahudi na kwa Watu wa mataifa. Petro
alihubiri injili kwenye nyumba wote waliokuwa wamekusanyika wakimsikiliza
walishukiwa na Roho mtakatifu na wakaanza
kunena kwa Lugha Mpya kisha Petro akawabatiza .Huu ulikuwa ni mwanzo wa Injili
au kanisa kuwafikia watu wa mataifa.
6.
Injili inakwenda Asia Ndogo {Mdo 13} Katika sura hii tunaona wito wa
wamishenari wawili kwenda kuhubiri katika nchi ya kigeni. Wito
huu na kutumwa huku kulifanyika Antiokia mahali ambapo wanafunzi walipewa jina na kuitwa wakristo kwa mara ya kwanza {Mdo
11:26}.
Balnaba alikuwa ni
mchungaji wakati Paulo alipokuja kutoka Dameski. Wanafunzi wote walimwogopa, Balnaba alimpokea na
kumtambulisha kwa kanisa {mitume Yerusalemu} Mdo 9;26-29.
Japokuwa mitume
walimtuma Balnaba Antiokia mahali ambapo kanisa lilikuwa na uamsho mkubwa
aliamua kufunga safari kutembea zaidi ya KM 150 kwa meli ili kwenda kumtafuta
Sauli wa Tarso .Alimpata na kisha akamchukua na kuja nae Antiokia bila kujua
kwamba miaka ya mbele sauti ya Bwana ingemwita kupia njia ya unabii
‘Nitengeeni Balnaba na Sauli kwa
kazi niliowaitia.{Mdo 13:1-5 }.
Balnaba na Paulo
waliombewa na kanisa na kisha kwenda kwenye umisheni wao kuelekea Asia ndogo mahali
ambapo walianzisha makanisa mengi. Kama inavyoainishwa katika Matendo ya Mitume
13 na 14. Baadae walirudi Antiokia mahali ambapo palikuwa ni kituo chao cha
umisheni.
K.
KUTENGANA KWA WAMISHENARI . Wakati mitume hao {Paulo na Balnaba}
walipokuwa wanajiandaa kwaajiliya safari yao ya pili ya umisheni walipishana.
Kulitokea kutokuelewana katika jambo moja. Balnaba alitaka kumchua Marko{ ambae
aliwaacha katika safari ya kwanza ya umishenari na kurudi Yerusalemu}waende nae
katika safari ya pili ya umisheni lakini Paulo alikataa kuambatana nae, hivyo
kukatokea mgongano kati yao na kisha wakaamua kutengana. Hapa tunaona moyo wa kichungaji
wa Balnaba japokuwa Marko alishindwa katika safari ya kwanza ya umishenari aliamua
kumpa nafasi nyingine. tuna mwona
Paulo akiwa mtu wa kushikilia kanuni kuliko kumpendeza mtu yeyote. Mtu ambae
yuko tayari kuvunja mahusiano na Balnaba kuliko kukubaliana nae. Miaka ilipita
na Mtume Paulo akakomaa kiimani. Mtume Paulo ambae alisema katika uchanga wake
: mimi
si duni kuliko hao mitume wakubwa {2Kor 11:5}. Baadae alisema ‘Mimi
ni wa kwanza kwa wenye dhambi {1Tim 1:16}. Paulo alfika mahali pakujitambua,
kujisifu kulibadilishwa na kujishusha na upendo ulichukua nafasi mahali pa
chuki na kanuni. Katika waraka wake wa pili kwa Wakorintho alisisitiza sana
upendo na msamaha. Baadae tunamwona Mtume Paulo akiwa katika upweke gerezani akisubiri
kunyongwa. Alimwagiza Timotheo kumleta Marko. Marko huyu
huyu ndiye aliyemkataa wakati wanafanya huduma na Balnaba.
Kutokana na hili tunajifunza
ya kwamba tusimkatae mtu kutokana na makosa aliyoyafanya kwa sababu twaweza kumhitaji
tena baadae.
7. Mkutano wa Yerusalemu. {48.B.K}. Tatizo lilitokana na kuokoka kwa
wamataifa na kujiunga na kanisa. Wakristo wakiyahudi walikuwa na
mitazamo tofauti tofauti juu ya hili .Walikuwa na mitazamo ifuatayo:
1. Kundi lenye msimamo mkali liliamini ya kwamba hakuna
wokovu nje ya Israeli . Kwa hiyo ingawa wamataifa wamempokea Yesu Kristo kama
masihi wao kwahiyo walipaswa kutahiriwa na kushika Torati ya Musa {Sheria za
Kiyahudi}Ili waweze kuokolewa Bila kufanya hivyo wokovu wao ungekuwa ni batili.
Kundi la wenye
mabadiliko.Hawa waliamini kwamba wokovu ni kwa
njia ya imani katika Yesu Kristo.Bila ya kushika sheria za kiyahudi. Wao
waliamini kwamba sheria za kiyahudi haziwahusu watu wa mataifa. Paulo na
balnaba walikuwa mojawapo wa watu wenye mtazamo huu. Mkutano uliitishwa
Yerusalemu ili kushughulikia jambo hili muhimu la mafundisho kutokana na watu
wa mataifa kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wao. Baada ya majadiliano
marefu Mitume na Wazee walifikia hitimisho ambalo lilithibitishwa na Roho
mtakatifu kwamba Wamataifa hawakuwa chini ya Sheria za kiyahudi na kwamba walichotakiwa
kufanya ni kujiepusha na Ibada ya sanamu, kula nyama iliyosongolewa na
damu, kujiepusha na uasherati na uzinzi. Barua iliandikwa na mitume na
ikapelekwa kwa kanisa la mataifa kwa mikono ya Paulo, Balnaba Yuda na Sila.
Walipofika Antikoa walilikusanya kanisa na kuwapa ujumbe wa kikao cha mitume na
wazee kilichofanyika Yerusalemu kuhusu tatizo lao. Waamini hawa walifurahi sana
kupata ujumbe wenye kuwatia moyo {Mdo 15:30-31}
L.
KANISA MIONGONI MWA MATAIFA.
Tangu mauaji ya Stefano
(48 B.K) mpaka mauaji ya Paulo mtume mwaka 68 B.K
Katika kipindi hiki
chote tunategemea kitabu cha Matendo ya Mitume, nyaraka za Paulo na mwanzo wa
waraka wa kwanza wa Petro. Um isheni wa mtume Paulo na Watendakazi wenzake ulifanyika
katika dola yote ya Rumi. Wakati mitume wengine walikwenda nchi za
mbali zaidi. (hii ni kulingana na mapokeo).
Idadi ya waamini wa
kimataifa ilikua kwa kasi sana wakati idadi ya waamini wa kiyahudi iliendelea
kushuka.Wayahudi walianza kukasirika na kufanya fitina
dhidi ya kanisa na walikuwa
tayari kuanzisha mateso dhidi ya wakristo.
Safari
Ya Pili Ya Mtume Paulo
Kwa sababu ya kupisha
kwa Balnaba na Paulo, Balnaba alimchukua mpwa wake Yohana(Marko) na kwenda
katika nchi ya kwao Kipro, Paulo alimchukua nabii Sila katika safari yake ya
pili ya umisheni na kwenda kuyatembelea
makanisa waliyokuwa wameyafungua katika safari ya kwanza walipokuwa na Balnaba.Paulo
likusudi kwenda Bithinia lakini Roho Mtakatifu akamkataza. Kisha walielekea
Troa mji wa Kaskazini Magharibi ya Asia ndogo.
Injili
inakwenda Ulaya. (Wito wa Makedonia)
Usiku mmoja wakati
Paulo na Sila wakiwa Troa mtu wa Makedonia alimtokea kwenye maono akisema “Vuka
uje Makedonia utusaidie” Mara Paulo na Sila walikwenda Makedonia katika
bara la Ulaya na wakaanzisha kanisa katika mji wa Filipi, Thesolanike, Beroya,
Athene na Korintho.
Tunakumbuka kwamba
mwanzoni kila mahali Paulo alipokwenda , aliwaendea Wayahudi kwanza. Wayahudi toka sehemu mbalimbali zadunia ya
wakati ule walikuwepo katika siku ya Pentekoste na walishuhudia kumiminwa kwa
Roho Mtakatifu na ubatizo wa waaini
wapya 3,000. Wengi wao walitoka nchi za mbali kuja kusherehekea sikukuu ya Pasaka
katika mji wa Yesulasalemu na kurudi nchini kwao. Inawezekana baadhi yao mtume
Paulo alikutana nao, kwasababu baadhi yao walionekana kuwa naurafiki zaidi na
Paulo.
Wakati wayahudi wengi
walipoikataa Injili ya Kristo kama mfufuka mwana wa Mungu, Paulo aliwageukia watu
wa mataifa.
Kanisa
katika Filipi, Mwamini wa kwanza katika Ulaya alikuwa
ni mwanamke aliyeitwa Lidia muuzaji wa rangi za zambarau mwenyeji wa Tiathira. yeye na nyumba yake walibatizwa na alifungua
mlango wa nyumba yake kwaajili ya
watumishi wa Mungu.
Kanisa katika
Thesalonike. Pia katika mji huu mtume Paulo alikwenda kwa Wayahudi kwanza kama
ilvyokuwa desturi yake. Baadhi ya Wayahudi na Wayunani waliamini. Wayahudi
wasioamini walianzisha ghasia dhidi ya watumishi wa Mungu, yaani Paulo na watendakazi
wenzake. Kwa hakika washitaki hawa
walijua nini cha kusema. Kama mitume
wangekamatwaq kwa kuanzisha dini nyingine hakuna tatizo ambalo lingetokea kwa watesi kwa
sababu Ugiriki ilikuwa ina dini nyingi na k walizikubali karibu zote.
Wao walikuja na uvumi
mwingine kabisa kwa kusema kwamba “Watu hawa wanadai kwamba kuna mfalme
mwingine”.
Inaonekena Wayahudi hao
Walianzisha uvumi huo ili serikali iweze kushiriki katika zoezi la kuwadhibiti
mitume.
Kanisa
katika Beroya.
Injili ilikubaliwa kwa watu wote Wamataifa na Wayahudi Wakati Wayahudi wa
Thesalonike waliposikia walikuja tena kufanya ghasia dhidi ya mitume hivyo
iliwalazimu Paulo na Sila kuondoka mjini hapo, lakini Neno la Mungu lilikuwa tayari limehubiriwa.
Hakika mitume hawa
waliishi sawasawa na Neno la Kristo “Watakapowafukuza katika mji mmoja
kimbilieni katika mji mwingine. (Mt 10:23)
Kanisa
katika Athene. Hapa pia mitume hawa waliwaendea Wayahudi ,
lakini wayahudi hao hawakulipokea Neno. Baadae mtume Paulo aligundua ya kwamba Mungu
aliwapofusha macho Waisraeli kwa muda kwa sababu walimsulubisa Kristo Yesu.
Wanafalsafa wa Kigiriki
walimpa mtume paaulo changamoto japo kuwa si sana kwa sababu walitaka kulisikia
Neno, hawakutubu bali walivutiwa tu na mdahalo.
Walipokuwa hawajui chakujibu
walidhihaki.
Kanisa
katika Korintho. Pia mahali hapa kama
ilivyokuwa kawaida yake mtume Paulo alikwenda kwa Wayahudi kwanza. Alikaa na Wayahudi watengeneza mahema(Akila na
Prisila). Inadhaniwa kuwa alitengeneza nao mahema ili kujipatia pesa kwaajili
ya kujikimu ili aweze kuhubiri Injili
pasipo kumlemea mtu yeyote.(Mdo 20:34). Japokuwa Paulo alikuwa ni Rabi
aliyeelimika na Mtume hakudharau kazi ndondogo kwaajili ya kueneza Injili.
Maamuzi
Thabiti. Wayahudi waliipinga Injili tena na hii ilileta kwa huduma ya Injili ya Paulo. Mtume Paulo
alisema
Damu yenu na iwe juu ya
vichwa vyenu mimi ni safi tangu sasa nitakwenda kwa watu wa mataifa.s (Mdo
18:6)
Paulo na Sila walikaa
Korintho kwa muda wa miezi kumi na nane (18) wakiwafundisha waamini. Kutoka
Korintho mtume Paulo aliandika nyaraka mbili kwa Wathesalonike
Baada ya shambulio
linguine lililfanywa na Wayahudi dhidi yake (Paulo) aliamua kuondoka Korintho na kurejea Antiokia kwa kupitia Efeso
na Kaisaria.
m.
SAFARI YA TATU YA UMISHENI YA MTUME PAULO (Mdo 18:23-22:17)
Katika awamu hii mtu
aliyeambatana na mtume Paulo ni Timotheo
aliyejiungas katika timu yake katika safari ya pili ya umisheni huko Listra. (Mdo
1-3) na kwa muda mfupi idadi kubwa ya wanatimu walikuwa pamojanae kabla
hajamaliza safari hii. Mmojawapo wa watu hao muhimu alikwa ni Dk. Luka.
n.
PAULO MTUME KATIKA MINYORORO (Mdo 22:23-28: 31)
Paulo alitumia miaka kadhaa akiwa gerezani lakini kamwe hakuacha kufanya kazi ya
umisheni. Mazingira hayakubadili kusudi lake. Baada ya safari ndefu Paulo
alifika Rumi jiji ambalo alitamini sana kuliona. Alikuwa na uhuru wa kuishi
katika nyumba aliyokuwa ameipanga mwenyewe huku akiwa chini ya uangalizi wa
askari mageza, japokuwa alikuwa mfungwa bado alileta athari kubwa katika kanisa huko Rumi. Moja ya mambo makuu aliyofanya ni kuandika nyaraka kwa Waefeso, Wafilipi, Wakolosai na
Filemoni.
Inaaminika kwamba baada
ya miaka miwili ya kukaa kifungoni mtume
Paulo aliachiwa huru (Mdo 28:30-31) lakini hakuna rekodi kamili katika kipindi
hiki isipokuwa taarifa chache tu.
Mapokeo yanasema kwamba
mtume Paulo alikamatwa Nikroporisi Kaskazini
mwa Ugiriki chini ya mtawala wa Rumi aliyeitwa Nero na akarudishwa Rumi katika kifungo hiki cha pili aliandika
nyaraka zifuatazo:- 1&2Timotheo, na Tito. Barua hizi zikikuwa ni barua zake
za mwisho mnamo mwaka 68. B.K. Mtume Paulo aliuawa kwa amri ya mfalme Nero.
h.
UANDISHI WA MAANDIKO MATAKATIFU.
Inadhaniwa kwamba mpaka kipindi cha Mkutano Yerusalemu mnamo
mwaka 48. B.K hakuna hata kitabu kimoja
cha Agano jipya kilichokuwa kimeandikwa, lakini karibu ya mwaka 68.B.K idadi
kubwa ya Maandiko ya Agano Jipya yalikuwa tayari yameandikwa, hii ikijumlisha
Injili ya Mathayo, marko, Luka, nyaraka za Paulo, Yakobo na 1Petro. Katika
kipindi cha miaka ya 68- 100.B.K
MADA YA TATU.
KANISA
LA SMIRNA(KIPINDI CHA MATESO)
KIPINDI CHA SMIRNA
A. UTANGULIZI.
Simirna ni mji ambo
ulikuwa umbali wa Km 65 Kaskazini mwa
Efeso na ulijulikana kama bandari ya salama kwa wakati ule. Ulikuwa katikati
ya njia kuu kutoka Rumi kwenda India na Persia(Irani)
Katika moja ya mitaa
yake kulikuwa na hekalu la mungu wa kigiriki aliejulikana kwa jina la zeus Mungu
mkuu na katika upande mwingine wa mji kulikuwa na hekalu la Cybele {mama wa
mungu}.
Mji wa Smirna pia
ulikuwa ni kituo cha ibada ya kumwabudu kaisari. Kulikuwa na hekalu la mfalme
wa Rumi Teberio Kaisari
B. VIPINDI VYA MATESO
Historia
ya kipindi cha smirna Inaaminika kwamba siku kumi za mateso
yaliyotakiwa kuja juu ya smirna huhusisha vipindi maalum kumi vya mateso chini
ya watawala mbalimbali wa kirumi pia na
wao watawala wangekuwa kumi.
Majina ya wafia dini
mbalimali katika kipindi hiki cha
Smirna chini ya wafalme mbalimbali wa Rumi yanaorodheshwa hapa.
1. Klaudi Nero
(64-68 B.K). Petro alisulubiwa katika kipindi cha utawala wa Nero. Paulo
alikatwa kichwa katika kipindi hiki.
2. .
Domitiani (90-95 B.K) alijaribu kumuua
mtume Yohana akashindwa na baadae akaamua kumpeleka uhamishoni katika kisiwa
cha Patmo.
3. Trajani (104-117
B.K) Simoni ndugu wa Yesu aliuawa
katika kipindi hiki mwaka wa 107 B.K.
Askofu Ignatious
wa Antiokia aliuawa pia katika
utawala wa mfame huyu mwaka 110.B.K. Watu
wengine waliouawa katika kipindi hiki ni Polikap mwanafunzi wa Mtume Yohana (155 B.K),
4. Marcus Aurelius. (161-180 B.K).
Yustini aliuawa katika utawala huu
katika mwaka 165 B.K. Pia alifanya
mauaji ya wakristo wengine wengi pia.
5. Septimus Severio. (200-211 B.K) alimuua Leonidus
baba wa Origeni mwanatheolojia mkuu., Pia aliwaua na Perpetua na Felistas na
ireneos mwaka 202 B.K
6. Thraker Maximus (235-237 B.K).alifanya mauaji lakini hatuna
majina ya watu aliowaua.
7. Desiusi.
(250-253 B.K. ) katika kipndi cha utawala
wake mateso yaliibuka tena juu ya kanisa na kwa bahati nzuri utawala wake
ulidumu kwa muda mfupi sana na baada ya kuanguka kwa utawala wake kipindi
kifupi cha amani kilikuja juu ya kanisa.
8. Vareliani
(257-260 AD.) Alipanga mauaji lakini
hayakufanyika katika utawala wake.
(270-275 B.K.) Askofu Spriani wa Kathegi na askofu
Sextus wa Rumi waliuawa katika kipindi hiki.
C. Mateso
ya kitaifa. Tabia za msingi katika historia ya
kanisa katika karne zote mbili yaani karne ya
pili na ya tatu ni kanisa au wakristo kuteswa na wafalme wa kirumi.
Mateso haya hayakuwa
endelevu lakini yalitegemea mtazamo aliokuwa
nao mfalme aliyekuwa akitawala katika kipindi hicho. Mateso ambayo yalikuwa yakijirudia katika
kipindi hiki yalidumu kwa karibu miaka 200 mpaka mfalme Kostantino
alipookoka na kutangaza tamko la
amani.(Edict of c Torelance) katika mwaka wa 313 B.K
D. SABABU ZA KANISA KUTESWA.
1.
Imani juu ya Mungu mmoja. Warumi walikuwa na miungu
mbalimbali ambayo walikuwa wakiiabudu pamoja na sanamu zao. Wakristo
walitangaza kwamba kuna Mungu mmoja tu Mfalme wa Rumi alijenga hekalu ambalo
lilipaswa kutumiwa na watu wote kuabudu miungu yao na akawapa wakristo nafasi
na ya kushiriki kumwabudu Mungu wao katika hekalu hilo. Wakristo walikataa fursa hiyo na kusababisha
wao kuonekana kwamba wako tofauti na wananchi wengine. Hivyo mateso yalianza
dhidi yao.
2. Kukataa kumwabudu kaisari. Kama ilivyokwisha elezwa katika sura iliyopita
kwamba makaisari wa kirumin walijitangaza kwamba wao ni miungu na wakadai
waabudiwe na wananchi au raia wao. Hivyo raia wote wa dola ya Rumi walilazimika
kushiriki ibada ya kumwabudu kaisari. Mahekalu ya ibada za kaisari yalijengwa
kila mahali na sanamu za makaisari zikawekwa na watu wakalazimishwa kumwabudu
kaisari na kutoa dhabihu mbele ya sanamu
za kaisari. Hii ilikuwa mojawapo ya
ibada za kitaifa katika dola ya Rumi.
Wakristo walipinga
vikali iabada hizo na hawakuwa tayari
kushiriki ibada hizo wala kutoa dhabihu mbele ya sanamu za kaisari. Kutokana na
asababu hiyo wakristo waihesabiwa kuwa wasaliti wa kaisari na dola kwa ujumla
na hivyo walipaswa kuhukumiwa kifo. Wakristo walianza kuteswa na dola ya Rumi
kwa sababu ya kukataa kumwabudu kaisari na kumwita Yesu Mfalme (Kurious).
3.Kutojihusisha kwenye ibada za sanamu. Ibada hizi za sanamu zilikuwa sehemu ya maisha ya kila siku
katika dola ya Rumi. Sanamu hizo zilisimamishwa katika kila nyumba na
ziliabudiwa katika kila sherehe. Dhabihu za vinywaji zilitolewa kwa
sanamu hizo. Hivyo wakristo walikataa kujihusisha katika shughuli za
kila siku za kijamii zilizohusiusha ibada za sanamu(mfano sherehe mbalimbali).
Wakristo walipokataa kujihusisha na hayo mambo walionekana wako kinyume na
jamii nzima.Kwa sababu hiyo jamii iliwahesabu kama maadui.
4.Kutambuliwa rasmi kwa dini ya kiyahudi: Dini ya kiyahudi
ilitambuliwa rasmi na dola ya Rumi kama dini ya kitaifa. Mwanzoni kanisa wakati
linaanza lilitambuliwa kama kikundi tu ndani ya dini ya kiyahudi chenye msimamo
mkali na hivyo kanisa lilipata upendeleo
wea serikali kwa namna fulani. Lakini mara baada ya kuanguka kwa Yerusalemu na kubomolewa kwa hekalu katika mwaka wa 70 B.K, kanisa au ukristo ulisimama peke yake na
dini ya kiyahudi walikuwa tayari kushirikiana na serikali kulitesa kanisa.
5. Kanisa kufanya mikutano ya
faragha. Kuokana na mateso kanisa lilianza kukutana katika maeneo ya siri
na hasa wakati wa usiku. Hii ilipelekea kanisa kuhisiwa vibaya na selrikali
kwamba lilikuwa linafanya njama ya kupindua serikali au kufanya maasi kwa
sababu serikali ya rumi ilipiga marufuku mikutano yote isiyo harali pia
mikutano ya usiku ilipigwa marufuku. Kwa kuogopa kwamba mikutano yote iliyokuwa
haina kibali cha serikali na iliyofanyika vifichoni haikuwa na nia njema kwa
dola ya Rumi. Kwa sababu hiyo wakristo walitazamwa na dola kama waasi. Watu
wanopanga njama na maadui kuleta vurugu na maasi ndani ya dola na hivyo dola
ilianzisha mateso juu ya kanisa.
6. Usawa katika kanisa.
Kanisa liliwaona watu wote kuwa sawa. Hakukuwa na matabaka katika kanisa.
Waliwaona watu wote kuwa sawa a hawakumwogopa mtu yeote na wala hawakuogopa
cheo cha mtu. Kuokana na sabu hiyo kanisa lilionekana kuwa na dharau, lisilo na
heshima na hivyo kanisalilifanyika adui wa dola.
7. Kuharibu biashara za sanamu.:
Kulikuwa na biashara iliyokuwa inafanywa
ndani ya dola ya Rumi.Biasharahiyo ilikuwa ni ya uuzaji wa sanamu. Watu
wengi walijipatia faida kutokana na
biashara hiyo. Mitume walipohubiri Injili watu waliokoka na kuachana na ibada za
sanamu .
Mitume walifundishwa kwamba sanamu si kitu na
hazipaswi kuabudiwa anaepaswakuabudiwa ni Mungu muumba Mbingu na nchi pekee. Watu wengi waliacha kununua sanamu
hizo . Kitendo hicho kilisababisha biashara hiyo ya uuzaji sanamu
kudolola. Watengenezaji na wauzaji wa
sanmu hizo walipata hasara na wakaamua
kuanzisha kuja juu na kuanzisha ghasia dhidi ya kanisa kwani
walipoteza wateja wao.
E.HATUA ZA MATESO.
Kuna mwingiliano kati
ya kipindi cha efeso na Smirna. Kipindi cha Efeso kiliisha na kifo cha mtume
Yohana mwaka 100 B.K. Wakati kipindi cha
Smirna kilianza wakati wa mateso ya kitaifa.(dola) wakati mfalme nero
alipouchoma mji wa Rumi mwaka 64 B.K.
F.
VIPINDI KUMI VYA MATESO YA KITAIFA.
MATESO
YA KWANZA Chini ya Kaisari Nero.(54-68 B.K)
Klaudi Nero alikuwa na
umri wa miaka 16 alipoingia katika utawala (ufalme) katika mwaka 54 AD. Alikuwa
mjukuu mkubwa wa Agustus aiyetoa amri ya watu wote kuhesabiwa sensa (Lk 2).
Nero alikuwa mfalme wa kwanza katka wafalme kumi kuanzisha mateso dhidi ya kanisa.Alichoma mji wa rumi mwaka
64 B.K .Theruthi mbili ya mji wa Rumi iliteketea. Mfalme Nero aliwasingizia
wakristo kwamba ndiyo waliohusika na uharibifu huo. Hivyo kanisa lililazimika kuingia kwenye mateso makali.
Katika kipindi hiki mtume Petro
alisulibiwa miguu juu kichwa chini mnamo mwaka 67 B.K. Pia mtume Paulo alikamatwa na kufungwa
Rumi ambapo alihukumiwa kifo na kisha
akauawa kwa kukatwa kichwa mwaka 68 B.K . Mjini Rumi.
Mfalme Nero alikuwa
katkili kuliko makaisari wote wa dola ya Rumi waliomtangulia na waliomfuata.
Kwani hajatokea kaisari katika dola ya
Rumi aliyefanya mauaji kama Nero. Mwaka 59 B.K . Mfalme Nero alimuua mama yake . pia alimuua
mke wake wa kwanza (Octavia)na kisha mkewe wa pili(Pompea) na baadae alimuua
kaka yake na rafiki yake mwalimu Seneka.
Mpaka mwaka wa 64 . B.K Rumi ilikuwa katika ghasia kuu. Mfalme Nero
alituhumiwa kwamba yeye ndiye aliyehusika na kuuchoma moto mji wa Rumi. Lakini
yeye alikanusha na kuwashutumu wakristo kuwa ndiyo waliohusika na tukio hilo. Kutokana na hilo kanisa liliingia katika
kipindi cha mateso makali. Maelfu ya wakristo waliuawa baadhi yao walitupiwa
kwenye hifadhi za wanyama ili waliwe na wanyama wakali na baadhi yao walichomwa
moto na mfalme akaendesha gari lake juu yao katika bustani yake. Bustani ya
mfalme ambako tukio hili lilifanyika leo
ni eneo la la jiji la Vatikani makao makuu ya papa na kania la MT. Petro.
Kaisari Nero alijiua mwenyewe mwaka68.
B.K
KIPINDI
CHA PILI CHA MATESO CHINI YA DOMITIAN. (90-96 B.K).
Baada
ya Nero kujiua mwaka wa 68 B.K kanisa
lilipata amani mpaka alipoinuka mtawala mwingine ambaye ni Domitiani. Wakristo
wengi waliuawa . Mtume Yohana alipelekwa uhamishoni kwenye kisiwa cha Patmo
ambapo ndipo mahali alipopokea ufunuo ambao sasa ni kitabu cha Ufunuo wa
Yohana.
KIPINDI
CHA TATU CHA MATESO CHINI YA TRAJANI 104-107 AD.
Trajani husemekana kuwa
mtu muimusana miongoni mwa watawala wa Rumi. Alikuwa mtawala mzuri kwa nchi
yake lakini aaliwaua wakristo. Mmoja wa mahakimu wake aliyeitwa Plin the younger. Gavana wa behtania
alichunguza maisha ya wakristo na mafundisho yao na kugundua kwamba mafundisho
hayo hayakuwa na chochote chenye kuleta uasi kwa serikali ya Rumi. Alileta
ripoti yake mbele ya mfalme Trajani lakini mfalme alijibu “ Kama watu hawa
walioletwa mbele yako wamepatikana na hatia kwa sababu ya kuwa wakristo na
wauawe lakini ikiwa wataikana imani yao ya kikristo na na ikathibitika kwamba
wanaabudu miungu yetu na waachiwe huru. Katika kipindi hiki waliuawa wakristo
mbalimbali kama ifuatavyo.
Simoni mdogo wa Bwana
Yesu. Alisulubiwa katika mwaka wa 107 AD.akiwa na umri wa miaka 110.
Alisulubiwa kwa amri ya mfalme wa Rumi {Trajani}.
Askofu Ignatious wa
Antiokia ambaye aliandika nyaraka mbalimbali kwa makanisa mbalimbali ambazo
baadhi yake zinapatikana katika kitabu kiitwacho “Mababa wa Kitume”{Apostolic
fathers}. Alikuwa tayari kuuawa kwaajili
ya Bwana Yesu. Aliandika barua za kuwafariji wakristo akiwa njiani kuelekea
Rumi ambapo alitumwa katika hifadhi ya
wanyama wakali na akaliwa na wanyama
wakali mnamo mwaka 110.AD
PORIKAP. {69-155 AD}
Alikuwa mwanafunzi wa mwaanfunzi wa mtume Yohana na rafiki wa trajani na
mwalimu wa Irenius. Inadhaniwa kuwa Polikap aliteuliwa na mtume yohana kuwa
askofu wa makanisa saba ya Asia. Alipoamriwa kumkana bwana Yesu Kristo ili
kuepukana na kuuawa yeye alijibu:
“Miaka 86 nimemtumikia
Bwana wangu na hajatenda Jambo lolote baya kwangu, nawezaje kunena vibaya juu
ya Bwana wangu aliyeniokoa? Alichomwa kwenye moto na akafa kifo cha kishujaa
kwaajili ya Imani yake juu ya Yesu Kristo. Aliuawa chini ya utawala wa mfalme
Antonius Pius mwaka 155 A.D.
KIPINDI
CHA NNE CHA MATESO CHINI
MARCUS
AURELIUS 161-180 A.D.
Marcus alikuwa alijulikana kam
mfalme borawa nchi yake na mwandishi mwenye maadili. Japokuwa alikuwa mtumzuri
kwa taifa lake alikuwa mtesi wa kanisa. Alifikiri kurejesha maisha ya zamani ya kirumi na dini za zamani.
Kwa wakati huo ukristo ulikuwa na mashiko zaidi.Waamini wengi walikuwa tayari
kufa kwa ajili ya imani yao na wala hawakuogopa kifo. Walikikabili kifo kwa
shangwe na ushindi mkuu. katika kipindi
hiki waaminni wengi waliuawa na wengine walitupwa katika hifadhi za wanyama wakali na wakaliwa na wanyama .
YUSTINI (Justine)Marty
100-165 A.D alizaliwa na alielimishwa vizuri mpaka kuwa mwanafalsafa na
aliendelea kufundisha hata baada ya kuwa mkristo. Alirejerea kwa manabii wa
zamani wa Kiebrania. Aliandika maneno yafuatayo dhidi ya ukatili na mauaji
yaliyokuwa yanaendelea dhidi ya wakristo. “wanatushitaki, wanatusulubisha
kwenye misalaba na kutupa kwenye hifadhi za wanyama wakali na kwenye moto. Lakini wanapofanya
mabaya zaidi juu yetu ndivyo idadi ya wakristo inaongezeka na kuwa kubwa zaidi.
Mnamo mwaka 165 A.D .alikamatwa na mfalme wa Rumi Marcus Aureliusi na kuuawa.
KIPINDI
CHA
TANO CHA MATESO CHINI
YA SEPTIMUS. 202-211. A.D.
Baada ya kifo cha
Marcus Aurelius kanisa lilipata amani mpaka alipoinuka mtawala mwingine
aliyejulikana kwa jina la Septimus Severus. Mtawala huyu alimuua Leonides baba
wa Origeni mwanatheologia mkuu. Katika mji wa kathegi Perpetua na mtumwa wake
Felistas walitumwa katika hifadhi ya wanyama poli wakali na wakauawa.
Mfalme Karakala alitoa uraia uraia kwa kila
mtu katika dola yake. Huu ulikuwaq ni uhuru mkubwa kwa wakristo. Watumwa pekee
ndio ambao wangeweza kusulubiwa au kutupwa kwenye hifadhi za wayama poli wakali.
KIPINDI
CHA SITA CHA MATESO CHINI YA THRAKA MAXIMUS
235-237. A.D.
Baada ya kipindi cha amani Thraka
alikalia kiti cha enzi cha Rumi. Alikua mpiganaji na alikusudia kuonyesha
huruma zake kwa dini za kipagani kwa kuwatesa wakristo. Utawala wake ulikuwa
mfupi kwa sababu ya kutawala kwake kwa njia ya udikteta. Maadui zake
walitengeneza kikundi ambacho kilifanikiwa kumuua.
KIPINDI
CHA SABA CHA MATESO.CHINI YA DECIUS
250-253 A.D.
Katika kipindicha
utawala wake mateso makali yaliibuka tena na kwa bahati nzuri kipindi chake cha
utawala kilikuwa kifupi na kanisa lilipata raha kwa kipinda raha na amani kwa
miaka 40.
KIPINDI
CHA NANE CHA MATESO CHINI YA VARELIANI. 257-260. A.D.
Askofu Sipriani wa
Kathegi aliuawa pia askofu wa Rumi Sextus aliuawa.
KIPINDI
CHA TISA
CHA MATESO. CHINI YA AURELIUS.
270-275. A.D
Mfalme Aurelius alikuwa
mwabudu jua japokuwa hakulitesa kanisa moja kwa moja mwanzoni lakini hakuwapa
uhuru wakristo. Hatimae aliamuru kwamba
wakristo wateswa. Kwa bahati nzuri amri yake haikutekelezwa Kutokana na kifo
chake cha ghafla.
KIPINDI CHA
KUMI CHA MATESO CHINI YA DEOCLETIAN 303
3010. A.D
Mfalme Deocletiani na
wasaidizi wake waliwafunga wakristo gerezani. Baadae sehemu ya jingo hili
lilibadilishwa na kuwa Kathedro ya Mtakatifu Petro. Deocletiani aliagiza
kuchomwa moto kwa kila nakala Biblia, makanisa kubomolewa na wakristo wenye
msimamo mkali kunyang’anywa uraia. Akiwa na umri wamiaka 80 deocletiani
aliondoka kwenye kiti cha utawala, lakini wafuasi wake Galarius na Kostantinusi
waliendeleza mateso mpka mfalme Kostantino mototo wa Kostantinus alipotoa tamko
la amani kwa kanisa mwaka 313 A. Tamko hili la amani lilisitisha mateso kwa
kanisa kwa kipindi cha karne mbili
Siku kumi za kujaribiwa
zilizotajwa katika Ufuno wa yohana 2:10 zilifikia mwisho. Baadae mfalme
Deocletiani alipotambua kwamba yuko karib na kufa alitubu dhambi zake mbele ya
askofu wa mji.. Mwka 337 A.D alibatizwa. Mtu aliyeamini kwamba angeweza kuufuta
ukristo alijikuta yeye mwenyewe anakuwa
mkristo.
G.
UONGOZI KATIKA KANISA KATIKA KIPINDI HIKI.
Wakati mitume wakiwa
hai uongozi ulionekana ni utumishi yaani kutumikia au kuwajibika. Wakati Luka
alipoandika kitabu cha matendo naPaulo alipoandika nyaraka zake tuna kuta
maneno askofu na wazee yakiwa na maana sawa yaani yakimaanisha ofisi moja.
Lakini katika miaka ya 125’s tunakuta maaskofu wamekuwa watawala katika maeneo
yao. Katika baraza la yerusalemu mwaka 48 A,D {Mdo 15} mitume wote na wazee walihusika. Lakini
katika baraza la mwaka 150 A.D waliohusika ni maaskofu pekee. Hii inadhihirisha
kwamba kanisa liliondoka taratibu kwenye mafundisho halisi ya mitume. Huduma ya
mitume ilizimwa na ikachukuliwa na maaskofu . Maaskofu walijifanya watawala wa
kanisa. Hii ndio sababu inayosababisha baadhi ya wataalam kuamini kwamba
kipindi cha mitume kiliishia na kifo cha mtume Yohan, jambo ambalo si kweli.
Huduma za mitume, manabii, waalimu wachungaji na wainjilisti kama zinavyoelezwa
katika waefeso 4:11 ziliendelea kuwapo katika kipindicha mitume na vi[pindi
vingine vyote vya kanisa, japokuwa zimekuwa
zikikataliwa na katika vipindi fulani ilionekana kama zimetoweka
lakini kwa uhakika zimekuwapo na bado zimekuwa zikifanya kazi katika kanisa hata sasa.
H.
SHULE ZA THEOLOGIA.
Shule ya Alexandria. Ilianzishwa mwaka 180. A.D
na Pantaenusi ambaye alikuwani mwanafalsafa wa kigiriki na baadae akwa
mkristo. Kisha alikwenda India, irani na Saudi Arabia katika huduma. Alikufa
mwaka 200.A.D .
Klementi wa Alexandria.
Alikkuwa mwanafunzi wa Pantaenus na
alimsaidia katika uendeshaji wa shule. Alikuwa ni mkuu wa shule hadi
alipoondolewa kwenye wadhifa huo katika kipindi cha mateso cha septimus Severusi
mwaka 2002. A.D. Baadhi ya vitabu vyake
mpka sasa vipo.
Origeni (185-254 A.D).
Alikuwa ni mwanatheologia mkuu. Baba yake Alikuwa ni motto wa Leonidas. Baba
yake aliuawa kutokana na imani yake katika Kristo chini ya utawala wa mfalme
Severus katika mwaka wa 2002 A.D. Wakati huo Origeni alikuwa na umri wa miaka
17. Origeni aliisdaidia familia yake kwa kufundisha falsafa ya kigiriki pamoja
na fasihi. Aliianzisha kwa upya shule ya Biblia iliyokuwa imefungwa kutokana na
kuondoka kwa Klementi. Baadae alikuwa ni mwandishi wa vitabu vya dogma na
thiologia. Baadae alikwenda Kaisaria na alianzisha shule nyingine ya Biblia
ambapo alikuwa ni kiongozi wa shule hiyo kwa karibu zaidi ya miaka 20. Alifungwa jela chini ya mateso Deciani na
alikufa kutokana na kutendewa kinyama akiwa gerezani.alikufa akiwa na umri wa
miaka 69 mnamo mwaka 254. A.D.
Shule ya Asia ndogo.
Shule hii haikuwa katikamji wowote ilikuwa ni shule ya masafa (mobile Bible
School). Ilihusisha waalimu wa thiolojia na waandishi. Baadhi yao ni
Ireneus(130-202A.D) aliyezaliwa Smirna. Alipata elimu yake ya awali ya Biblia chini ya Porkap.
Kansa la Asia ndogo lilimpeleka Ufaransa kama mmisionari. Aliuawa wakati wa
mateso ya Severusi mwaka wa 202 A.D.
Shule
ya kathegi: Shule hii ilikuwa kaskazini mwa Afrika na ilifanya
vizuri kuliko shule zingine kubadili imani ya Kithiologia katika Ulaya. Watu
wakuu katika katika shule hii walikuwa ni Tetullani na Sipriani. Tetullani (160-200 A.D)
Alikuwa ni mteteaji shujaa wa imani ya kikristo dhidi ya dini ya kiyahudi na mafundisho
potofu alijiunga na umontano na alitumia
kalamu na mahubiri kuthibitisha kile alichofikiri ni mambo ya kidunia na mabishano katika kanisisa.
Sipriani
Askofu wa Kathegi (195-258 A.D) Alikuwa ni motto wa afisa
wangazi ya juu wadola ya Kirumi. Alikuwa mkristo wakati wa ujana wake. Mambo
matatu yaliyomtukia mpaka kuwa mkristo ni Maandiko ya tetullani, mafundisho ya
Cellius toka Rumi na Maandiko matakatifu (Biblia).
Mwaka mmoja baada ya
kuwa mkristo alikuwa askofu na kiongozi mkuuwa makanisa ya Afrika Kaskazini
mwaka 248 A. D. Mnamo Mwaka 257 A.D.
Mfalme Valentine alimfungia kufanya huduma mwaka na mwaka 258 aliuawa.
Kanisa la karne ya pili
lilipambana na mambo makuu mawili ambayo ni Mateso na uzushi(Heresy)
yaani mafundisho potofu. Mtume Pulo alitabiri ya kwamba:
“ Najua mimi yakuwa
baada ya kuondoka kwangu mbwa mwitu wakali wataingia kwenu wasilihurumie kundi.
Tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao
wanafunzi wawaandamie wao”
I.
UZUSHI NA MAFUNDISHO YA
UONGO.
Mafundisho yasiyokubaliana na
mafundisho rasmi ya kanisa yaliitwa uzushi na waamini waliamriwa na kanisa
kutokuyapokea mafundisho hayo.
Kanisa katika historia yake lilitangaza mafundisho fulani
kuwa uzushi kutokana na kutokukubaliwa kwa mafundisho hayo na uongozi wa
kanisa.
Si kila mafundisho waliyoyaita uzushi yalikuwa mabaya, kwani
kile kilichoitwa uzushi kilikubaliwa baadae na kanisa na kile ambacho
kilionekana chema kilikataliwa na kuitwa uzushi baadae. Hoja au mawazo
yale waliyoyaita uzushi baadhi yalikuwa na mambo mema ndani yake.
Kanisa halikupambana na mateso tu bali pia na mafundisho ya
uongo, sawsawa na unabii uliotolewa na mtume Paulo katika Matendo ya mitume
20:29-30.
J. MAKUNDI YA UZUSHI.
1.
UYAHUDISHAJI.
Hili lilikuwa ni kundi la wakristo
wa kiyahudi lililojitokeza wakati kanisa linapanuka katika miji ya
wamataifa. Wayahudishaji hawa
walifundisha kwamba wakristo wote walitakiwa kuzifuata sheria za Musa na
mapokeo ya dini ya kiyahudi. Waliyakataa maandiko ya mtume Paulo kwa sababu yalipinga
mafundisho yao. Kundi hili lilitoweka katika karne ya pili BK.
2. UNOSTIKI
Unostiki ilikuwa ni
falsafa iliyojaribu kutumia imani ya ukristo katika kuthibitisha ukweli wake.
Kundi hili waliamini kwamba Baada ya ngazi ya Mungu mkuu kulikuwa na miungu
wengine wengi ambao baadhi wakiwa wema na wengine waovu. Unosti ulikuwa na elementi za falsafa
za kiyunani na dini za kipagani.
. Hivyo kanisa
lilipinga vikali mno unosti likikana kwamba imani yake si falsafa na wokovu
hautegemei falsafa na mafumbo bali
ufunuo wa Yesu kristo.
Wanostiki walipunguza thamani ya
maisha na huduma ya Yesu Kristo. Habari nzima juu ya maisha na huduma ya Yesu
ilielezwa kwa njia ya mafumbo (allegory). Unostiki ulizuka katika karne ya pili
baada ya Kristo na ulishamiri katika karne ya tatu na ya nne.
Unostiki hata sasa unajidhihirisha katika karne hii ya
ishirini na moja katika dini mbalimbali
hapa ulimwenguni. Hususani kupitia
falsafa ya mpango mpya wa dunia (New World order Philosophy)
MAFUNDISHO
YA UNOSTIKI.
1. Maarifa ya pekee hufunuliwa kwa
watu wachache tu.
2. Wokovu si kwa watu wote, ni kwa
watu wachachetu wenye kuyaelewa maarifa
yanayofunuliwa.
3. Ulimwengu huu na vitu vilivyomo
ndani yake umeumbwa kwa nguvu isiyo kamili na hii ndio asili ya maovu yote
katika ulimwengu.
4. Yesu si mwanadamu, alikuwa na
roho tu. Yesu alikuwa ni roho aliyejifanya aonekane katika umbile la binadamu.
5. Waliamini kwamba mmoja wa miungu
wadogo alikuwa ndani ya Yesu na ndio aliyekuwa asili ya uungu wake.
4.
MARSION
Huyu alikuwa ni mtoto wa askofu wa Pontus.
Alikuja Rumi yapata mnamo mwaka
138BK. Alipofika Rumi alijulikana kwa
haraka sana kutokana na jinsi alivyojitolea sana katika kanisa kwa mali zake.
Pia mafundisho yake yalimpa umaarufu na kumfanya ajulikane sana. Kutokana na
umaarufu huo Marsion alipata wafuasi wengi. Mafundisho yake hayakukubaliwa na
kanisa hivyo alitangazwa kuwa mzushi na
alitengwa na kanisa mnamo mwaka 144 BK.
Marsioni aliunda chama chake ambacho
kiliwaunganisha wafuasi wake wote. Chama chake hakikuongezeka kwa njia ya
kuzaliana kwa sababu ya kukataa mambo ya ndoa. Waliongezeka kwa njia ya
wanachama wapya kujiunga. Marsion
alikuwa ni mtu wa kwanza kutunga kanuni
ya maandiko.
v MAFUNDISHO YA MARSION
1. Kwa kiasi kikubwa mafundisho yake
yalifanana na mafundisho ya wanostiki.
2. Aliweka sharti la wafuasi wake
(wanandoa) kutokutana kimwili na kwamba walitakiwa kuachana na kuishi maisha ya
upweke.
3. Alikaza kwamba wokovu ni kwa watu
wote. Wokovu hutegemea Injili ya Yesu na si kwa kufunuliwa mafumbo kifalsafa.
4. Injili ya upendo wa Mungu
inahitaji kusikika zaidi katika kanisa.
5. Kanisa limeichafua Injili kwa
kuichanganya na mambo ya dini ya kiyahudi.
6. Mungu wa Agano la kale ni tofauti na baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Kwa sababu Mungu wa agano la kale alifurahia dhabihu za damu.
7. Mungu aliyeumba ulimwengu na watu
wake ni Mungu mwovu, Mungu mwingine mwema alijificha hadi wakati wa Yesu
Kristo.
4. UMONTANO.
Kilikuwa ni kikundi kilichoanzishwa
na mtu mmoja aliyeitwa Montano mwenyeji wa Frigia. Wafuasi wa kikundi hiki
waliitwa wamontano. Kikundi hiki
kilienea sana kuanzia mwishoni mwa karne
ya pili na kuendelea kwa karne mbili zaidi.
Wakati wa ubatizo wake Montano
alinena kwa lugha nyingine na kutabiri na hivyo akajiita kuwa ni kinywa cha
Roho Mtakatifu aliyetabiriwa na Yohana. Alikuwa na wasaidizi wawaili wanawake
ambao nao pia walijitambulisha kuwa ni vyombo pekee vya Roho Mtakatifu. Karama
za kinabii zilijidhihirisha katika mlengo wa umontano. Kutokana na mikazo
yao, Wamontano walihukumiwa uzushi na
kutengwa na kanisa.
v MAMBO MUHIMU YA
MONTANO.
1. Walikaza kwamba wamefunuliwa juu
ya mwisho wa dunia uliokuwa karibu sana kutokea.
2. Baadhi ya wafuasi wa umontano
walikataa kulima kwa sababu Yesu angekuja kabla ya msimu wa mavuno.
3. Baadhi walikataa ndoa kwa kuwa
mwisho wa dunia ulikuwa karibu.
4. Kiongozi wao mmoja wa huko Pontus
aliwapeleka washirika wake porini kwenda kumlaki Bwana Yesu wakati anarudi
duniani kwa mara ya pili.
5. Kiongozi mwingine wa huko Shamu
aliwakataza washirika wake wasilime kwa sababu Yesu angerudi kabla ya msimu wa
mavuno.
6. Alikataa hali ya kanisa kumezwa
na ulimwengu.
7. Alidai kuwa kanisa lilikuwa
limepoa na hivyo lisitarajie kurudi kwa Yesu.
8. Walipinga suala la uaskofu
kuchukua mamlaka katika kanisa. Waliweka mkazo katika huduma ya unabii na
ukuhani wa waamini wote.
v KUMEGEKA KWA KANISA CHINI YA UONGOZI WA NOVATIANO NA DONATO.
Katika karne ya tatu na ya nne kulitokea na kumegeka kwa kanisa. Mmeguko huo uliongozwa na Novatiano katika karne ya tatu na Donato karne ya nne.
Kugawanyika huko kulitokana na kurejeshwa kwa
viongozi na wamini waliokuwa wameikana imani katika kipindi cha mateso.
Pia makundi haya yalijitenga kutokana na kuona wakristo wengi walikuwa wanaishi
maisha machafu kama wapagani waliokuwa wanawazunguka.
v UASI WA NOVATIANI.
Katika karne y tatu askofu wa Rumi aliyeitwa Kalisto
alitangaza kwamba dhambi yoyote ili
inaweza kusamehewa kiwa mkosaji anaonesha toba ya kweli.Fundisho hili
lilienea sana. Wakristo waliokuwa wameikana imani yao wakati wa mateso walitaka
kurudi kanisani na askofu Kalisto alikubali kuwapokea watu hao.
Kiongozi mmoja wa kanisa aliyeitwa Novatiani, hakukubaliana
na jambo hilo na alilipinga vikali na akaungwa mkono na wachungaji wengine
ambao nao walikuwa kinyume na maamuzi hayo ya askofu. Walijitenga na
kanisa na kuanzisha ushirika wao. Novatiani alichaguliwa kuwa kiongozi wao.
v UASI WA DONATO.
Mmeguko wa kanisa chini ya uongozi wa Donato ulitokea Afrika
ya kaskazini karne ya nne baada ya utawala wa mfalme Deokletiani. Mfalme huyu
katika kipindi cha utawala wake alikuwa na mpango wa kufuta ukristo na kuchoma
moto Biblia zote. Wakati wakipindi cha
mateso makali baadhi ya viongozi wa kanisa waliasi imani wakaamua kutoa
maandiko matakatifu (Biblia) yateketezwe ili kujinusuru na kifo.
Baada ya kipindi cha mateso kumalizika viongozi hao yaani
wachungaji na maaskofu walioasi walitaka kurudi kanisani. Kanisa katoliki lilikuwa limekubali kuwapokea. Kanisa
lilikubali kuwarudishaviongozi hao katika sharika zao. Katika mji wa Karthegi waamini wengi sana walikataa kuongozwa na mtu
aliye mkana Yesu na kutoa Biblia kwa serikali ili ziteketezwe.
Donatusi alikuwa kiongozi wa mgomo huo na alipata wafuasi wengi.
Watu hao walijitenga na kanisa na kuanzisha huduma yao. Kulikuwa na ugomvi kati
ya wakatoliki na wadonato kwa kwa muda mrefu.
K. HALI YA KANISA KATIKA KIPINDI CHA MWISHO
WA KARNE YA PILI:
Kanisa lililotakasika.
Mateso yaliwaondolea mbali wale ambao hawakuwa waaminifu katika imani yao. Wale
ambao hawakuwa na imani kamilifu na waliojiunga na kanisa kwa masilahi yao
binafsi.
Mafundisho yenye mfumo mmoja. Japokuwa kanisa lilihusisha watu
wa tamaduni , rangi na jamii mbalimbali bado lilikuwa na umoja wa imani wa
ajabu katika kanisa lote. Walifuata mafundisho ya mtume Paulo, Petro na
wengine. Mdo 2:42.
Kanisa lenye muundo:
kazi iliyofanya na Paulo ya kuweka viongozi wa Kanisa katika kila mji ilileta
ufanisi. Viongozi hao walikutana katika mikutano na kujadili
mambo mbalimbali muhimu kuhusu kanisa. Hii ilisababisha kutokea kwa
ushirikiano imara wa kimataifa.(International Fellowship) ambao umekuwepo
mpaka sasa.
Kanisa lenye kusitawi {kukua}. Licha ya mateso
yaliyolikumba kanisa, kanisa liliendelea kukyua kwa kasi. Kanisa lilikumbana na
mateso makali chini ya watawala mbalimbali wa Kirumi, lakini kanisaliliendelea
kukabiliana na mateso hayo na likawa tayari kuwapelekea watesi hao Injili ya
uzima.
Hakika
Malango ya kuzimu hayakulishinda kanisa
KUANDIKWA
KWA AGANO JIPYA.
Hatuwezi kueleza kwa udhahiri au kikamilifu
kwamba ni lini hili lilifanyika.
Baadhi ya vitabu kama
vile nyaraka za Paulo zilikubaliwa kila mahali, wakati vingine kama vile
Waebrania, Yakobo na Ufuno wa Yohana vilikubaliwa Mashariki peke yake na
kukataliwa Magharibi.
Kanisa la mashariki
lilikubali baadhi ya vitabu ambavyo
havipo katika Biblia. Baadhi ya vitabu
hivyo ni Waraka wa Balnaba, Mafundisho ya mitume kumi
na wawali na Ufunuo wa mtume Petro. Mabaraza yalikutana mara kwa mara ili
kutambua ni vitabu gani vilivyokuwa vimevuviwa na vipi havikuvuviwa. Inadhaniwa kwambaAgano jipya halikutambuliwa rasmi mpka
baada ya mwaka 300 B.K
MADA YA NNE
KIPINDI CHA PERGAMO
KANISA LA KIFAHARI/KITAIFA.
A.
UTANGULIZI.
KIPINDI:
Toka patano amani la mfalme Kostantino
(313 BK) hadi kuanguka kwa dola ya Rumi
mnamo mwaka 476 BK.
B.
USHINDI
WA WAKRISTO
Baada ya miaka miambili ya mateso
kanisa liliishinda dola ya Rumi na kupata amani. Mfalme Deokletiani katika
utawala wake aliweka watawala wasaidizi
katika majimbo yake kutokana na ukubwa wa dola
ya Rumi. Baba wa Kostantino
alikuwa ni mmoja wa watawala wasaidizi, aliongoza majimbo ya Galia, Uingereza
na Hispania, Baada ya kufa kwa watawala wasaidizi kulitokea na kugombea madaraka baina ya watoto wao.
Baba wa Kostantino alipofariki
Kostantino alitangazwa kuwa mtawala badala ya baba yake, na hivyo watoto wa
watawala wengine waliamua kuanzisha mapigano ili kuuchukua utawala huo.
Miongoni mwa hao waliokuwa na nguvu ni Maksentio, huyu alikuwa ni mtu aliyeshabikia
mauaji ya wakristo. Walianzisha mapigano huko Italia maili kumi kutoka Rumi
mnamo 28.10. 312 BK
Wakiwa katika eneo la mapigano kabla
ya vita kuanza Kostantino aliona alama ya msalaba angani ikiwa imeandikwa
maneno yafuatayo, “Kwa alama hii utashinda”. Kostantino aliitikiakwa sala na
akaifanya alama ya msalaba kuwa nembo ya Jeshi lake na walipokuwa vitani
Kostantino aliwashinda kabisa maadui zake, adui yake mkuu Maksentio alikufa
katika vita hiyo, hivyo Kostantino akawa mshindi.
Kostantino alitambua kwamba msalaba
ilikuwa ni alama ya wakristo na hivyo Mungu wa wakristo ndio aliyekuwa
amemsaidia katika vita hiyo. Mwaka uliofuata Kostantino alitangaza PATANO LA AMANI na Wakristo, (Edict of
Torelant). Patano hili lilikomesha mateso juu ya wakristo katika
dola yote ya Rumi. Patano hili lililowaletea amani wakristo katika dola ya Rumi
lilikuwa na matokeo chanya na hasi katika kanisa.
C.
MATOKEO
YA TAMKO LA AMANI
Matokeo ya patano
la amani yanaweza kuainishwa katika pande mbili ambazo ni matokeo mazuri
na matokeo mabaya;
I.
MATOKEO
MAZURI,
1. Mateso juu ya wakristo yalikomeshwa.
2. Makanisa yaliyokuwa yamebomolewa wakati wa mateso yalijengwa
tena kwa fedha ya serikali.
3. Maaskofu na wachungaji walisamehewa kodi.
4. Watumishi wa kanisa walianza kufadhiliwa na serikali na
hawakutakiwa kuhukumiwa kwa sheria za kawaida.
5. Wakristo waliruhusiwa kujenga makanisa mahali popote katika dola ya Rumi.
6. Dhabihu za kipagani zilikomeshwa.
7. Kostantino alijenga makanisa makubwa katika miji ya Yerusalemu, Bethlehemu na katika mji wa Kostantinapoli ambapo ndio uliokuwa makao makuu yake mapya.
8. Kusulubiwa kwa wahalifu na desturi za kuua watoto wasiotakiwa zilikomeshwa.
9. Watumwa waliachiwa huru.
10. Siku ya
jumapili iliwekwa kuwa siku ya mapumziko kwa watumishi wa serikali.
11. Alisaidia kuunda umoja wa kanisa kupitia mikutano mbalimbali
aliyoiitisha, mfano mkutano wa Naikea mwaka 325 BK.
12. Alikusudia kuufanya ukristo ukubaliwe na serikali kama dini
zingine.
II. MATOKEO MABAYA.
1. Ilikuwa ni fahali kuwa mkristo, hivyo watu wengi walijiunga
na ukristo kwa maslahi binafsi.
2. Watu walijiunga na ukristo ili waweze kupata vyeo katika
kanisa na serikali.
3. Maadili ndani ya kanisa yalianza kumomonyoka.
4. Mambo ya kiroho yaliachwa kupewa kipaumbele na badala yake
programu mbalimbali zikapewa kipaumbele.
5. Sherehe na tamaduni za kipagani polepole zilihamia kanisa,
kwa kubadilishwa jina na malengo na badhi zilibadilishwa kuwa sikukuu za kikanisa, mfano Krismasi.(Kuabudiwa kwa bikira Maria
kuliasiliwa kutoka ibada za kipagani za kuabudu miungu , Zeusi, mungu wa uzuri
wa warumi na Diana mungu mwezi).
6. Katika jimbo la mashariki serikali ililitawala kanisa mpaka
likapoteza nguvu na maisha ya kiroho.
7. Katika jimbo la magharibi kanisa lilipata nguvu dhidi ya
serikali.
WATAWALA
WALIOFUATA BAADA KOSTANTINO
Kostantino hakutaka kutumia nguvu
katika kuwafanya watu kuwa wakristo, alitaka jambo hili lifanyike taratibu na
kwa uchaguzi wa mtu mwenyewe, jambo hili halikufuatwa na watawala waliofuata
baada yake.
Baada ya utawala wa Kostantino
watawala waliofuatia walikuwa wakali mno walipiga marufuku ibada za kipagani na
waabudu dini hizo walihukumiwa kifo na mali zao zilitaifishwa. Walivunja
mahekalu ya kipagani, watawala wakristo
kwa kutumia jina la ukristo sasa walitumia
njia zilezile mbaya zilizokuwa zimetumiwa na serikali kulitesa kanisa
kuwatesa wapagani.
D.
AINA
MBALIMBALI ZA MATESO.
·
Katika kipindi cha Efeso kanisa
liliteswa na wayahudi.
·
Katika kipindi cha Smirna kanisa
liliteswa na dola ya Rumi.
·
Katika kipindi cha Pergamo ugomvi ulizuka miongoni mwao
wenyewe (wakristo).
F.
UMOJA
NA UTAWALA WA KANISA.
Kanisa lililazimka kuwa na umoja kamili ili liweze kuwa na
nguvu ya kukabiliana na mateso yaliyoliandama na uzushi uliokuwa unajitokeza.
Hivyo kanisa lilipambana na maadui wakubwa wawili ambao ni mateso na mafundisho
potofu.
Kutokana na uzushi kutokea,
kanisa ilibidi liwe na utambulisho
au jina litakalowa tofautisha na
makundi ya uzushi, hivyo kanisa lilianza kijiita Katoliki.
Jina katoliki linatokana na neno la kiingereza universal, lenye maana “ya
popote au ya mahali popote” Kanisa
lilianza kutumia jina Katholiki kwa maana mbili, ambazo ni:
1. Kanisa lisilo na mipaka ya majimbo au ya nchi.Kanisa moja
lililo katika nchi zote ulimwenguni.
2. Kanisa leye mafundisho sahihi.
v SABABU ZA KANISA KUHITAJI UTAWALA WENYE NGUVU.
1. Kutokea kwa ukiri wa imani.
2. Kutokea kwa Kanuni Ya Maandiko Matakatifu.
3. Kutokea kwa maaskofu waliopewa mamlaka ya kutunza mafundisho
yaliyotokana na mitume wa kwanza.
v Ukiri Wa
Imani.
Huu ulikuwa ni ushuhuda mfupi
uliotumiwa katika kazi za kawaida sharikani kama vile ubatizo. Ukiri wa imani
ulieleza kwa kifupi kile kanisa linachoamini naa ulitumika kama kiapo kuwa mtu
anakubaliana na taratibu za kanisa hilo hivyo anastaili kubatizwa na kupokelewa
katika kanisa.
v Kanuni Ya Maandiko Matakatifu.
Kanuni ni kawaida inayotumiwa kupima
usawa na usahihi wa kitu. Kanuni
huelezea vitabu vilivyokubaliwa na kupokelewa na kanisa kama maandiko Matakatifu.
Kanisa liliweka kanuni ili kubainisha kati ya vitabu vilivyokuwa ni neno la
Mungu na vile visivyokuwa Neno la Mungu. Mfano wa vitabu visivyokuwa neno la
Mungu ni vile vilivyoandikwa na wanosti.
Makundi ya uzushi kama vile
wanostika na Marsion waliharakisha kutungwa kwa kanuni hii.
Mababa wa kanisa
walitumia kanuni mbalimbali katika kuvibaini vitabu hivyo. Baadhi ya njia hizo
ni kumtambua mwandishi kama alikuwa ni mtume au la, Kupokelewa kwa kitabu
na watu walionadikwa kwa mara ya kwanza
na matumizi ya kitabu hicho katika makanisa mbalimbali na mamlaka ya kitabu
chenyewe N.k
v Haja Ya Kutokea
Kwa Viongozi Wenye Mamlaka.
Maaskofu walitokea kama watu wenye mamlaka ya kutafasili maandiko na
kufundisha wazi mafundisho ya mitume. Neno askofu maana yake ni
mwangalizi/msimamizi. Neno hili hapo awali lilitumiwa na watu wote na kulikuwa
na maaskofu katika idara mbalimbali za serikali, baadae matumizi ya istilahi
hii yalibakia katika Kanisa tu.
Uaskofu ulisaidia kuleta utawala
wenye nguvu na umoja katika kanisa kupitia mambo mawili ambayo ni mafuatano ya mitume na ibada.
·
Mafuatano
Ya Mitume
Ilidaiwa kwamba maaskofu walikuwa badala ya mitume. Kwa namna fulani uaskofu ulitokana na mitume, yaani maaskofu waliwekwa
na mitume kuwa watawala katika kanisa na mamlaka ya utawala wao ilihusisha
kuhubiri na kuitetea Injili.
·
Umoja
Wa Ibada
Ibada mbalimbali zilizokuwa
zikifanywa na kanisa kwa pamoja zilisaidia kukuza umoja wa kanisa na kutokea
kwa viongozi wenye mamlaka. Kulikuwa na ibada mbalimbali ambazo zilifanywa na
kanisa, baadhi ya ibada hizo ni ibada ya
ubatizo na ibada ya meza ya Bwana.
Pia kanisa liliadhimisha sikukuu
mbalimbali ambazo pia kwa namna fulani zilichangia kukuza umoja wa kanisa.
G.
MABISHANO
YA KITHIOLOJIA.
Mabishano ya kithiolojia
yalisababishwa na mitazamo mbalimbali ambayo wakristo walikuwa nayo juu ya Yesu
Kristo. Baadhi ya mitazamo hiyo ni .
v Uungu wa
Yesu Kristo.
Wakristo wa awali walimpa Yesu heshima kwa kumwita majina mbalimbali kama vile
Masihi, Kurios, Kritos na Logos.
Jina la Logosi lilitokana na falsafa
za kigiriki, Kutokana na falsafa hizo Logos ilikuwa ni njia ya Mungu kufanyika
mwili na kukaa na watu hapa duniani. Hivyo wakristo wa awali walimtambua Yeus
kama Mungu.
v Kristo
kama Logosi.
Katika kipindi cha karne ya pili na
ya tatu karibu wanazuoni wote wa kikiristo walifundisha kwamba Kristo alikuwa
ni Logos. Kulikuwa na mwanazuoni moja
aliyeitwa Yustini Shahidi ambae
aliweka mkazo kuwa Logos alikuwa ni
Mungu wa pili.
Wanazuoni wengine waliweka mkazo
katika umoja wa Yesu.Walikubali
kwamba Logos amefanyika kuwa mwili
katika Yesu Kristo lakini alikuwa ni
Mungu halisi, Mungu mwana ndiye aliyefanyika mwili, si Mungu wa pili.
Kulingana na mtazamo waYustini ni
dhahiri kwamba alikana ubinadamu wa
Yesu. Yesu kama Logos alikuwa Kweli
Mungu na mwanadamu kweli.
v Monarchianism.
Dhana ya Mungu mmoja.
Kulikuwa na wanazuoni wengine waliopinga
mafundisho ya kumhusisha Yesu na Logos kwa sababu jambo hili lilielekea kupinga imani yakuwa Mungu ni mmoja. Wanazuoni hao waliona
kwamba dhana ya utatu wa Mungu ilielekea
kuwa ni uzushi wa kuwa na miumngu
mingi.
Wamonarchianism waligawanyika katika
makundi mawili ambayo ni;
1. Wamonarchianism
wa kimabadiliko,
hawa walikuwa na mtazamo wenye kumwona
Yesu kama mwanadamu pekee tu, ambae hakuwa Mungu aliyefanyika mwili. Kundi
hili liliongozwa na Askofu Paulo
Samosota wa Antiokia.
2. Wamonarchianism
wa kimfano.
Hawa waliona kuwa hakuna tofauti
kati ya baba na mwana. Baba ndiye aliye vaa mwili. Kwa hiyo majina haya baba, mwana na Roho mtakatifu yalitumika kuonesha
kwetu njia au hali tatu Mungu alizotumia kujidhihirisha. Hivyo hakuna nafsi tatu bali ni nafsi moja.
Kundi hili liliongozwa na Sabelio.
Baada ya mateso kukoma katika kanisa
kulitokea mgogoro mwingine ndani ya kanisa uliohusisha
mgongano wa kimafundisho (doctrinal controversals).
Baadhi ya viongozi wa kanisa
walianza kuibuka na mafundisho yaliyoonekana kuwa mageni katika kanisa na hivyo
walihukumiwa uzushi na kutengwa na kanisa.
Wakristo walitumia muda mwingi kujadiliana wao kwa wao
badala ya kuipeleka Injili mbele. Katika moduli hii tutajadili badhi tu ya
mabishano ya kithiolojia yaliyotokea
ndani ya kanisa.
1.
Mabishano
Baina Ya Mchungaji Ario Na Askofu Alexander.
Ario alimshutumu askofu wake kuwa
alikuwa anaweka mkazo sana juu ya uungu wa Yesu katika mafundisho yake.
Alexander alifundisha kwamba mwana ni wa
milele sawa na baba. Ario alipinga fundisho hilo yeye alidai kwamba baba ni wa milele lakini mwana alikuwa na
mwanzo wake. Kuna kipindi ambapo
mwana hakuwapo. Askofu Alexander aliitisha mkutano wa sinodi huko Iskanderia ili kujadili suala hilo na hatimae Ario alitangazwa kuwa mzushi na alitengwa
na kanisa.
Ario aliungana na Askofu Euzebio wa
Nikomedia na wakaandika nyaraka mbalimbli
ambazo zilitetea fundisho lao na wakazisambaza maeneo mbalimbali ili ziendelee
kusomwa na wakristo mbalimbali.
v Mkutano Wa
Naikea.
Baada ya nyarakahizo kusomwa majadiliano
miongoni wa viongozi wa kanisa yalipamba moto na kuleta mgawanyiko ndani ya kanisa.
Mfalme Kostantino hakupendezwa na mgogoro huo ulioleta mgawanyiko miongoni mwa
wakristo hivyo aliwaomba viongozi hao wapatane na iliposhindikana kupatana kwa viongozi hao,
mfalme akitumia nguvu ya dola aliamua kuitisha mkutano wa viongozi wote wa kanisa
toka seheu mbalimbali ili aweze kuwapatanisha. Mkutano huo ulifanyika mwaka
325BK katika mji wa Naikea na hutambulikana kama mkutano wa kwanza wa kanisa
zima, kwa sababu ulihusisha viongozi mbalimbali toka sehehemu mbalimbali.
Katika mkutano huo Askofu alexender
alishinda kwa hoja na hatimae Ario alitangazwa kuwa mzushi na akatengwa na
kanisa. Katika kipindi hiki kanisa lilitunga ukiri wa imani ambao ulipaswa
kutumiwa na makanisa yote. Ukiri huo ulikweka mkazo katika uungu wa Yesu kuwa Yedu ni sawa na
baba.
Mkutano wa Naikea
haukuweza kumaliza majadiliano na badala yake uliyachochea kwani majadiliano
hayo yaliendelea kwa muda wa miaka therathini
na tano baada ya mkutano wa Naikea. Baadhi ya viongozi wa kanisa walitiria
mashaka ukiri wa Naikea kwasababu hawakuuzoea.
v Mkutano Wa
Kostantipali
Kutokana na majadiliano hayo ya muda mrefu na makali kulikuwepo na haja ya
kuitisha mkutano mwingine wa kanisa zima. Mkutano hu uliitishwa katika mji wa Kostantinopoli mnamo mwaka wa 381 BK.
Katika mkutano huu walifanya marekebisho
kidogo ya ukiri wa imani wa Naikea.
Mkutano Wa Efeso.
Baada ya Apolinari kuhukumiwa
uzushi, kuliendelea mabishano makali
katika kanisa. Baadhi ya mabishano hayo
yalikuwa baina ya askofu Sirilo wa
Iskandelia na askofu Nestori wa Kostantinopoli.
Sirio alipinga fundisho la
Apolinari Aliona kwamba uungu na ubinadamu wa Yesu kuwa ni hali mbili zisizo weza kutenganishwa
. Alipokuwa anataka kueleza uungu wa Yesu alianza kwa kumwita bikira Maria ‘Theotokos’ yaani mama wa Mungu.
Askofu Nestori alibaini uzushi
katika maelezo ya Sirilo, yeye alipendekeza
Mariamu aitwe mama wa Kristo.
Maaskofu hao walishambuliana vikali sana kwa maandishi. Shauli hilo lilipelekwa
kwa askofu wa Rumi ili aweze kutoa uamuzi. Askofu wa Rumi alimpa ushindi Sirilo
na kumtangaza Nestori kuwa mzushi.Hayo
yalifanyika katika mkutano wa tatu wa kanisa uliofanyika katika mji wa Efeso
mnamo mwaka 433 BK.
2.
Majadiliano
Ya Apolinari.
Apolinari alikuwa ni askofu wa
Laodikia. Askofu huyu alijaribu kueleza uhusiano uliopo baina ya hali mbili tofauti alizo nazo Yesu. Yaani hali ya uungu na hali ya ubinadamu.
Yeye alikuwa na mtazamo wa kwamba
mwili wa Yesu ni ubinadamu na akiri
na roho yake ni Logosi aliyefanyika mwili. Katika kueleza fundisho hilo
askofu huyu alikaza uugu wa Yesu uliokana ubinadamu wake. Kutokana na
fundisho hili Apolinari alitangazwa kuwa mzushi
katika mkutano wa Kostantinopali mnamo mwaka 381BK.
3.
Mabishano
Ya Pelegio.
Pelegio alikuwa ni mmonaki,
mwingereza aliekuja Afrika Kaskazini kwajili ya kuhubiri Neno la Mungu katika
kanisa la Afrika ya Kaskazini.
Peregia alifundisha kwamba mtu
harithi dhambi toka kwa Adamu, lakini
kila mtu ni lazima afanye uchaguzi yeye mwenyewe.
Pelegio alipingwa vikali na Agustino mkuu kwa mafundisho yake. Agustino alifundisha
kwamba Adamu alipotenda dhambi alikiwakilisha kizazi chote cha binadamu na
kwamba mtu hawezi kuokolewa kwa uchaguzi wake mwenyewe, bali ni kwa mapenzi ya Mungu na kwamba neema ya Mungu
haiwezi kukataliwa na wanadamu.
Mafundisho ya pelegio yalipingwa
vikali na kanisa na kuonekana ni uzushi. Kanisa lilikubalia na na ya mafundisho ya Agustino mkuu.
H. KUZUKA KWA UMONAKI.
Utawa au umonaki ulianza katika
karne ya tatu BK. Kabla ya kipindi hicho
wakristo waliishi katika jamii na familia. Mara baada ya ukristo kushamiri
mambo ya dunia yalianza kuingia kanisani, baadhi ya wacha Mungu hawakuridhika
na hali hiyo hivyo waliamua kujitenga na kukaa peke yao nje ya mji katika mapango
au katika nyumba walizokuwa wamejijengea. Nyumba hizo zilijulikana kama nyumba
za watawa maarufu kama Monastery.
Baadhi ya mambo yaliyochochea kuanzishwa kwa
utawa ni mvuto wa Injili, maovu kukithirikatika kanisa na falsafa ya uovu wa mwili. Kulikuwa na
watu ambao waliuza kila kitu walichokuwa nacho wakawagawia maskini na kisha
wakajitenga na kuamua kuishi maisha ya kimasikini mbali na jamii yao. Baadhi ya watu hao ni;
v Antoni
Mtawa Wa Kwanza.
Mtu huyu alikuwa ni mwenyeji wa Misri na ndiye
mwanzilishi wa utawa. Antoni aliuza kila kitu alichokuwa nacho na kuwagawia
maskini mali zake na kisha akaishi nje
ya mji akilima na kuwapatia maskini
chakula alicholima.Baada ya muda alijitenga na
kuishi peke yake pangoni mlimani.
Watu mbalimbali walimwendea huko pangoni ili kujifunza na kisha alifanikiwa
kupata wafuasi ambao nao waliamua kuungana nae kuishi maisha ya utawa. Alipat
wafuasi karibuni elfu mbili.
v Pokomeo
Mwanzilishi Wa Nyumba Za Utawa.
Huyu alikuwa mdogo wa Antoni na ndie aliyeanzisha nyumba za utawa.
Yeye alijenga boma kubwa ambalo wafuasi wake waliishi ndani wakijitenga
na mambo ya ulimwengu. Watawa hawa walijishughulisha
na ibada na kazi, utawa huu ulikaza ushirika na ulipendwa na watu wengi.
Jerome (Hironimo)
Utawa ulienea sana sehemu ya
magharibi kwa njia ya Jerome. Mtu huyu alikuwa na uwezo mkubwa kufasiri
Maandiko na alifanywa kuwa katibu wa Papa wa Rumi kwa kipindi kirefu. Aliishi
maisha ya kujikana. Alisema “ Mtu asieoa hujipatia sifa ya pekee mbele a Mungu.
Alikiri kuwa kwa wazi kabisa kwamba “
Maisha ya utawa hayawezi kuondoa majaribu yote”
Alidai kwamba alipokaa katika boma la utawa huko mlimani bado aliwaza juu ya wasichana wa Rumi.
Jerome alikuwa fundi wa Maandiko na
elimu. Alitafsiri Biblia kwa lugha ya Kilatini iliyojulikana kwa jina la
Vulgate. Tafsiri inayopendwa sana na wakatoliki wa Rumi mpaka sasa.
Yeye alishirikiana na wanawake watawa
kutunza yatima Huko Bethrehemu na Palestina. Walikuwa na nyumba mbili za
watawa, moja ikiwa ya watawa wa kiume na nyingina ya watawa wa kike.
Benedikto Mwanzilishi Wa Kanuni Za Utawa.
Benedikto wa Nusia alianzisha
shirika la utawa huko Monte Kasino Italia.
Yeye aliweka mkazo katika umoja. Aliweka uongozi uliosimamia nyumba zote
za utawa. Aliona kuwa kila nyumba ya utawa ni jeshi la Yesu waliotayari
kumtumikia wakati wowote.
Kiongozi wa kila nyumba ya utawa
aliitwa Aboot, na watawa wote walipaswa kumtii. Aliweka mpangilio mzuri wa saa
za ibada, sala na kusoma. Nyumba za kanuni za Benedikto zilikuwa mahali pa kuu
pa elimu na kilimo. katika majimbo mengi Ulaya.
v Faida Za Utawa.
1. Ulifanyika kuwa vituo vya
wakimbizi.
2. Walitoa msaada kwa watu wenye mahitaji , mfano kusaidia maskini
na wasiojiweza.
3. Walileta mchango mkubwa katika kuinua kilimo.
4. Walikuza elimu kwani watawa walitumia muda mwingi katika
kusoma na kuandika maandiko mbalimbali.
5. Walipeleka wamishenari katika mataifa mbalimbali
kueneza Injili.
6. Walitoa viongozi bora katika jamii na katika kanisa.
7. Walitafsiri Mandiko katika lugha mbalimbali.
v Madhaifu
Ya Utawa.
1. Mkazo wa juu ya kuishi maisha ya useja.waliwakataza wafuasi
wao wasioe wala kuolewa.
2. Upendeleo na anasa. Baada ya utawa kupata umaarufu, walianza
kuishi maisha ya anasa na kukwepa kulipa kodi.
I.
KUANGUKA KWA DOLA YA RUMI
Mfalme Kostantino mara baada ya
kuingia katika utawala alihamishia mako makuu ya dola ya Rumi katika mji wa
Kostantinopoli. Tutatazama namna Rumi
ilivyokuwa makao makuu ya kanisa. Wakati kanisa la Orthodox la mashariki
lilikuwa likitawaliwa na serikali, Patriaki wa Rumi alidai kuwa na mamlaka katika kanisa lote la ulimwengu wa
magharibi, ambao ulikuwa kupitia kanisa la Katoliki la Rumi. Hii iliwezekana
kwa sababu kadhaa, badhi zikiwa ni;
Kufanana kiutawala.
Kulikuwa na mazoea kuongoza kanisa kwa
mfumo wa kiserikali ambapo kunakuwa na kiongozi mkuu mmoja anaetakiwa
kusikilizwa . wakati huu kulikuwa na
maaskofu karibu kila mji, ambao katika miji mikubwa waliitwa Patriaki (patriarch) yaani baba mkubwa.
Kulikuwa na mapatriaki katika miji ya Yerusalemu,
Antiokia, Iskanderia, Rumi na Kostantinopali.
Kulikuwa na mashindano ya kugombea ukuu
miongoni mwa mapatriaki. Swali lilikuwa nani angekuwa kiongozi mkuu wa kanisa
lote ulimwenguni. Rumi ikiwa imetengeneza njia ya kuwa makao makuu ya kanisa
ilikuwa na viongozi bora. Kwa muda mrefu
kanisa la Rumi lilikuwa imara. Lilisimama kidete kupinga mafundisho potofu. Kanisa la Rumi liliihudumia Jamii
kiroho na kimwili kwa kuanzisha kazi za kijamii dunia nzima. Nyumba za utawa, shule na hospitali
zilianzishwa katika maeneo mbalimbali, jambo hili lililipa umaarufu kanisa la
Rumi. Wamishenari walitumwa katika ulimwengu mzima wa wakati ule kueneza Neno
la Mungu.
Wakati nguvu ya kanisa ilikuwa inakua, nguvu ya dola
iliendelea kuzorota, nguvu ya kisiasa ya Rumi ilizidi kuporomoka.
Kwa muda mrefu wa utawala wake dola
ya Rumi ilikuwa imetajirika sana.
Maadui zake waliokuwa wanaishi jirani nae waliutamani utajiri wa
wake. Maadui hao waliivamia Rumi ambayo sasa
haikuwa na uzoefu wa kivita. Baadhi ya maadui walioivamia Rumi na
kuishambulia dola ya Rumi ni wavisigothi, wasaksoni, wavandali, , wahuni, wabarigandiana
na wafranka. Uvamizi wa mataifa haya
ulipunguza nguvu ya dola ya Rumi.
Janga lingine lilikuwa ni vita ya wenyewe kwa
wenyewe, baina ya wanachama wa seneti kugombania kiti cha utawala. Kabila la
kijerumanilililojulikana kama Herulisi
liliivamia na kuishinda dola ya Rumi mnamo mwaka 476 BK.
MADA YA TANO
KIPINDI CHA THIATIRA;
KANISA LA NYAKATI ZA GIZA.
KIPINDI. Tangu
kuanguka kwa dola ya Rumi hadi kuanguka kwa Kostantinopoli.
A.
UTANGULIZI
Katika kipindi cha Pergamo tuliona
jinsi Patriaki wa Rumi alivyochukua
mamlaka ya uongozi wa kanisa na kuinuka kwa Rumi kuwa makao makuu ya
kanisa. Tuliona jinsi mafundisho potofu
pamoja mambo ya kipagani yalivyoingia kanisani
Haikutosha kwa Patriaki wa Rumi kuwa
Askofu mkuu wa kanisa lote duniani na kuwa na mji wa Rumi kama makao makuu ya
kanisa lote duniani, baada ya hapo alijitangaza kuwa kiongozi wa mataifa kwa njia ya kukuza upapa katika karne kumi za
kipindi cha giza. Kipindi cha giza kilikuwa na hatua tatu ambazo ni, kukua, kusitawi na
kuanguka.
1.
Kukua.
Gregori I alipokuwa kijana
aliteuliwa kuwa msimamizi wa majengo na vyakula katika Mji wa Rumi. Baada ya kifo cha baba yake aliamua
kutoa kwa kanisa mirathi ya babaye. Mnamo mwaka 578 BK Gregori I aliteuliwa na
papa kuwa balozi wake katika mji wa Kostantinopali. Mwaka 585 hadi 590 BK alikuwa msaidizi wa papa huko Rumi na
kiongozi mkuu wa Monastery(nyumba za utawa). Baada ya papa Pelegio II kufariki
dunia kwa ugonjwa wa tauni mwaka 590 BK, Grogori I aliteuliwa na umati wa watu huko Rumi kuwa Askofu badala
ya Peregio II.
Kukua kwa nguvu ya upapa kulianza baada ya Gregori
I kushika wadhifa wa upapa katika
mwaka wa 590 BK. Mfumo wa kubadilisha majina mtu
alipokuwa anaingia katika nafasi ya upapa ulianza katika kipindi hiki.
Gregori aliitwa mkuu kwa sababu ya mafanikio yake ambayo baadhi ni,
1. Alitumia uwezo wa kikanisa katika kuwasaidia watu, (kuwapa
chakula na nguo).
2. Serikali ilipolega aliimarisha ulinzi katika mji wa Rumi.
3. Alimtambua papa wa Rumi kuwa na mamlaka juu ya viongozi wengine wote wa kanisa.
4. Alilipatia kanisa nguvu ya kisiasa na kidini.
5. Alitengeneza dogma ya kanisa.
Kutokana
na misaada ya kijamii aliyokuwa
anaitoa papa Grogori I, wanachi wa Rumi
walianza kumheshimu na kumhesabu kama
kiongozi wao. Hivyo basi Gregori Mkuu aliimarisha nguvu ya upapa katika mambo
ya kidini na kisiasa pia.
v Sababu za
kukua kwa upapa
Mbali na
mchango wa Gregori Mkuu katika kukuza nguvu ya upapa kulikuwa mambo mengine
kadhaa yaliyopelekea kukua kwa upapa katika kipindi hiki. Baadhi ya sababu hizo
ni:
1.Nguvu ya haki, kanisa
liliwatetea raia dhidi ya watawala dharimu
hivyo likapendwa na watu.
Kuzolota kwa serikali,
Wakati serikali inazolota kanisa lilizidi kujiimarisha, kiuchumi na kijeshi
hivyo viongozi dhaifu walihitaji msaada wa kanisa katika kupambana na adui zao hivyo kanisa likazidi kuwa na
mamlaka na nguvu ya ushawishi.
2. Ulaghai, Kanisa lilitumia kigezo cha ujinga wa watu kujipatia mamlaka. Kanisa lilitengeneza
nyaraka mbalimbali zenye kulipa mamlaka ya kiutawala na kudai kwamba
ziliandikwa na wahusika walioandikwa kumbe sivyo. Zifuatazo ni baadhi ya nyaraka
hiz
v Waraka wa
mfalme Kostantiono kwa askofu Silvesta (314-335 BK).
Huu ulikuwa ni waraka uliogushiwa na kanisa kwamba uliandikwa na Kostantino
kumpa mamlaka ya kiutawala askofu wa
Rumi (Silvesta) juu ya wafalme wote wa Ulaya na Ulaya nzima.
v Tamko la
uongo la Isodore(850 BK). Kulikuwa na maandiko
yaliyokuwa yanadai kwamba askofu wa Rumi alikuwa amepokea waraka toka kwa
mitume uliokuwa unamtangaza asofu wa
rumi kuwa askofu wa kanisa dunia nzima na kwamba kanisa lilitangazwa kuwa huru
(yaani kanisa kutokuwa chini ya serikali).
2
KUSITAWI
KWA UPAPA (1073- 1216 )
Nguvu ya upapa ilifikia kilele chake
katika utawala wa Gegori VII ambaye
pia alijulikana kama Hildebrand.
Katika kipindi hiki upapa ulikuwa na nguvu kamili kikanisa na kiserikali katika mataifa yote ya
kule Ulaya.
1. Papa Gregori VII alifanya matengenezo ya ukreli na kukataza
ndoa kwa wakreli.
2. Aliliondoa kanisa chini ya utawala wa serikali, kanisa
likaanza kujitawala, alifuta suala la maaskofu kuteuliwa na watawala wa
serikali (wafalme).
3. Alilifanya kanisa kuwa juu ya selikali.
v Papa
Innocent III (1198 -1216).
Huyu alikuwa ni papa mwingine mwenye nguvu
kubwa. Katika siku yake ya kutawazwa kuwa papa alitoa usemi wenye maneno yafuatayo.
“ Mahalifa wa mtakatifu Petro wako
katikati ya Mungu na watu; wadogo kuliko Mungu lakini wakubwa kuliko watu, wenye uwezo wa kuwahukumu watu wote lakini
wasioweza kuhukumiwa na yeyote”
Katika barua yake ya kiofisi
aliandika “ papa hajapewa mamlaka kwa
kanisa pekee bali kwa ulimwengu mzima. Akiwa na haki ya kuwaondoa na kuwaweka watawala katika
uongozi. Papa innocent III alijitwalia mamlaka ya serikali ya mji wa Rumi akijifanya yeye mwenyewe kuwa bwana kwa
kuanzisha nchi ndani ya nchi ijulikanayo kama nchi ya Vatikani.hivyopapa
akawa kiongozi wa kidini na kiserikali.
3
KUANGUKA
KWA UPAPA.
Kuanguka kwa upapa kulianza wakati
wa papa Bonifasi VIII katika mwaka
1303. Jambo hili lilisababishwa na
kuanza kuibuka kwa roho ya utaifa miongoni mwa nchi mbalimbali. Jambo hili
lilileta mtikisiko dhidi ya Bonifasi VIII. Watu walianza kuwaheshimu viongozi
wa nchi zao kuliko kumheshimu papa. Amri na maagizo mbalimbali ya papa yalipuuzwa na viongozi wa nchi. Baada ya mfalme wa ufaransa
kukata kutii maagizo ya papa, papa
Alianzsha vita na mfalme wa ufaransa na
hatimae Bonifasi VII akashindwa vita hiyo na kuwekwa kizuizini mpaka mauti
ilipomfika.
B.
KUINUKA
KWA UISLAMU
Kanisa lilipata mashambulizi makuu katika
karne ya saba kutoka kwa waislamu. Dini ya Uislamu ilianzishwa na kijana mmoja
aliyeitwa Mohamed. Kijana huyo alizaliwa
mnamo mwaka 570 BK katika mji wa Maka. Alianza kazi yake kama nabii na mwana
matengenezo kwa kuanzisha dini yake
mnamo mwak 610 BK katika mji aliozaliwa. Kutokana na kutokukubaliwa na watu wa
mji huo aliamua kuhamia katika mji wa Madina katika mwaka wa 622 BK. Kipindi hicho kinaitwa Hajira. Kalenda
ya Waislamu inaanza wakati huo wa kuhama kwa Mohamed toka Maka kwenda Madina.
Ndani ya kipndi cha miaka miambili waislamu
walikuwa wameisha zishinda sehemu mbalimbali za dunia na kuanzisha dini yao ya
uislamu, Uanzishaji wa dini hiyo ulienda sambamba na uanzishaji wa dola ya
Kiislamu katika maeneo yoyote waliyoyashinda. Baadhi ya maeneo waliyokuwa
wameyashinda na kuanzisha utawala wao ni
nchi za Mashariki ya kati, Afrika ya Kaskazini, Asia ndogo. Mouhamedi na
wafuasi wake walieneza dini yao kwa kutumia upanga, mahali popote watu
walipokataa kuipokea dini hiyo walilazimika kutumia vita na nguvu ya kijeshi.
Maeneo yoyote waliyofanikiwa
kuyateka hatua ya kwanza ilikuwa ni kufuta dini zingine zote zilizokuwa maeneo
hayo na kuwalazimisha raia wote kujiunga na dini hiyo.
Kuinuka kwa dini ya Uislamu
kulichangia katika kuanguk kwa upapa na kuzoofisha nguvu ya kanisa kwa ujumla.
Kwa mfano Afrika kaskazini kanisa lilizoofika na hatimae likafifia kabisa.
C.
KUTENGANA
KWA KANISA KATOLIKI.
Kanisa la katoliki la mashariki lile
la magharibi yalitengana rasmi mwaka
1054 BK, japokuwa kihuduma
yalitengana tangu zamani. Daima kulikuwa
na kushindania madaraka ya kwambani nani
aliyekuwa mkuu kati ya papa wa Rumi na Patriaki wa Kostantinopoli.
Hatimae katika mwaka 1054 BK makanisa
haya yalitengana ramsi.
v SABABU ZA
KUTENGANA
Kutofautiana kimafundisho, Kuhusu asili ya Roho mtakatifu. Kanisa la
magharibi lilidai kwamba Roho mtakatifu alitoka kwa baba na kwa mwana wakati
lile la mashariki lilidai kwamba Roho
mtkatifu alitoka kwa baba pekee.
Ndoa kwa makuhani. Kanisa la magharibi lilikataza makuhani kuoa wakati la kanisa la
mashariki liliruhusu makuhani kuoa.
Sababu ya kisiasa, Baada ya kuanguka
kwa dola ya Rumi mataifa ya magharibi
yalitaka kuwa chini ya Kostantinopoli.
Kuabudu sanamu.Kanisa
la magharibi lilianzisha matumizi ya sanamu katika ibada wakati kanisa la
mashariki lilipinga matimizi ya sanamu.
Kugombea ukuu,
Madai ya kanisa la mashariki
ya kuwa ni kanisa la kitawala.
D. KUSITAWI KWA UTAWA.
Mashirika mbalimbali ya kitawa
yalisitawi katika kipindi hiki na yakajitolea kusaidia jamii katika maeneo
mbalimbali. Baadhi ya mashrika hayo ni :
Wabenedectino walianza mwaka 529 BK
Wasisteri mwaka 1098.
Wafransiska mwaka 1209.
Wadomeni mwaka 1215.
Kipindi cha karne za katikati
kulichangia sana katika ustaarabu wa ulimwengu, hasa katika mambo ya elimu,
maandiko, na mambo ya ufundi, katika kipindi hiki zilijengwa kathedro kubwa .
kuna baadhi ya vyuo vikuu vikubwa vilivyojengwa wakati huu, mfano wa vyuo vikuu
hivyo ni Chuo kikuu cha Parisi huko Ufarasnsa, Chuo Kikuu cha Kambridge, Chuo
Kikuu cha Oxford, nacho vyote iwili vikiwa
huko Uingereza. Kuanzishwa kwa vyuo vikuu hivi kulipelekea elimu kukua
na kuleta mtazamo mpya katika jamii kama tutakavyoangalia baadae katika kipindi
kitakachofuata.
E.
WATANGULIZI
WA MATENGENEZO YA KANISA.
Katika mwaka wa 1229 kanisa la
Rumi lilikataza waumini wa kawaida wasisiome Biblia isipokuwa
makuhani tu. Lugha ya kilatini iliteuliwa kuwa lugha takatifu na hivyo mtu
yeyote asiyejua kilatini alizuiliwa kuhubiri.
1. PITA
WALDO.
Katika miaka ya 1970 alitokea
mfanya biashara mmoja aliyeitwa Pita waldo mwenyeji wa Loyona Ufaransa. Mtu huyu
alipenda kujua mambo yaliyo katka Biblia lakini hakuweza kwa sababu hakufahamu
kilatini hivyo aliwaajiri mapadri wawili
wamtafsirie Biblia katika lugha ya
kifaransa. Baada ya kusoma neno la Mungu
alivutiwa nalo sana hivyo akauza kila kitu alichokuwa nacho na akala kiapo cha
umaskini, akajitoa kikamilifu kuhubiri neno la Mungu.
Pita Waldo Alianzisha timu
iliyoitwa watu maskini. walianza
kuhubiri, lakni walipingwa na papa. Mwaka 1184 walijitenga na kanisa kwa sababu hawakukubali kitendo cha wao
kuzuiwa kuhubiri,
Waldo alipinga baadhi ya mafundisho
ya kanisa la Katoliki. Baadhi ya mambo aliyoyapinga ni mafundisho
kuhusu toharani, misa na kwaajili ya wafu na kumwabudu Mariamu mama wa Yesu.
Watu hawa waliamini kwamba kili mtu
alitakiwa kuwa na Biblia katika lugha yake ya asili na ya kwamba
Biblia ilitakiwa kuwa mamlaka ya mwisho na iliyokuu katika mambo ya imnani na
maisha. Kanisa lilianzisha mateso dhidi ya wawadeni yaani wafuasi wa Waldo.
Kadili walivyokuwa wanateswa ndivyo
walivyokuwa wakiongozeka. Mnamo mwaka
1211 wawadeni themanini walichomwa moto
huko Ujerumani. Pita waldo alisaidia
kuleta matengenezo ya kanisa kwani alisaidia kupatikana kwa Biblia katika Lugha
zingine na kuhamasisha kila mtu kusoma Biblia. Waldo anajulikan kama mmoja wa
wanamatengezo ya kanisa watangulizi.
2.
JOHN
WIKRIF.
Huyu alikuwa mwalimu wa Chuo kikuu
cha Oxford. Mnamo mwaka 1378 Wikrif alitaka kuleta matengenezo katika kanisa
kwa kuwaondoa watumishi wa kanisa waliokuwa dharimu,na kuwanyang’anya mali
ambazo aliamini kwamba ndizo zilizokuwa chanzo cha watumishi hao kuwa dharimu. Alichapisha andiko lililoeleza maadili
wanayotakiwa kuwa nayo watumishi wa kanisa.
Alifundisha kwamba wakati viongozi wa kanisa
wanapokuwa mafisadi serikali ilitakiwa kuchukua mali zao na kuwapa watu wengine
wenye nia ya kumtumikia Mungu. Katika mwaka wa 1379 alianza kupinga
dogma ya kanisa kwa kutoa madai
yafuatayo;
Ø
Yesu pekee ndiye aliyekuwa kiongozi
mkuu wa kanisa na si papa.
Ø
Biblia pekee ndio yenye mamlaka kuu
na ya mwisho kwa waamini na si kanisa wala papa.
Ø
Kanisa lilitakiwa kuiga mfano wa
kanisa la agano jipya.
Ø
John Wikrif kwa msaada wa tajiri Lord Cobham alitafsiri Biblia katika lughaya kiingereza na kuisambaza
katika maeneo mbalimbali . Alianzisha
chama cha Wahubiri maskini na wakaanza kuzunguka katika maeneo mbalimbali
ya nchi hiyo wakihubiri watu neno la Mungu.
Mwaka 1382 alipinga fundisho la mageuzo ya maumboya mwili na damu ya Yesu linalojulikana kama transubstan-tiation.
Mawazo yake yalipingwa vikali na
kanisa na serikali na akafukuzwa ukufunzi.
Mwaka 1402 Bunge La
Uingereza lilipitisha sheria ya hukumu
ya kifo kwa watu wanohubiri mafundisho
kinyume na yale yaliyokubaliwa na kanisa. Wahubiri maskini waliteswa vikali
sana, baadhi walifungwa nakuchomwa moto na kufukuzwa nchini. Viongozi wa
kanisa walijaribu kuchoma moto Biblia zote
za Kiingereza. Wikrif alifariki mnamo mwaka 1384.
Shujaa
huyu anakumbukwa sana katika historia ya kanisa kwa mchango wake wa kutafsiri
Biblia katika Lugha ya kiingereza. Wikrif ndiye mtu wa kwanza kutafsiri Biblia
kwa lugha ya kingereza.
3.
JOHN
HUS
Huyu alikuwa ni mkuu wa chuo kikuu
cha Plague huko Bohemia, mtawa na padre
wa kanisa la Rumi la katoliki. Mwaka
1401 John Hus alipata upadrisho. Padri
huyu alipendezwa na maandiko ya John Wikrif na hivyo alianza kuhubiri mafundisho ya mtangulizi wake Wikrif.
Alipinga mafundisho mbalimbali yasiyo ya kiBiblia ya kanisa la Romani
katoliki na akasisitiza watu kuishi maisha matakatifu. Alisisitiza kwamba
Biblia ndiyo mamlaka ya mwisho kwa
mwamini na katika huduma za kanisa.
Katika kitabu chake alichoandika juu
ya kanisa, alifasili kwamba kanisa ni mwili wa Kristo, na Yesu Kristo pekee akiwa kiongozi wake mkuu.
Alitetea nafasi ya ukuhani na kudai kwamba
Mungu pekee ndiye aliyekuwa na uwezo wa kusamehe dhambi.
Alieleza kwamba hakuna mamlaka ya kanisa inayoruhusiwa kuanzisha mafundisho
(doctrine) yaliyo kinyume na Biblia
na kwamba Waamini hawatakiwi kutii
maagizo yasiyo ya kimaandiko.
John Hus Alipinga mambo yafuatayo, udharimu wa
mapadri, kuuzwa kwa vyeti vya
msamaha, kuondolewa kikombe cha divai
kwa walei. Baada ya mashambulizi hao mazito dhidi ya mafundisho ya
kanisa Hus alifukuzwa upadri na akaambiwa abadilishe msimamo wake kwa
kufuta kauli, jambo ambalo Hus hakukubaliana nalo. Hatimae Hus alihukumiwa kifo
na akachomwa moto. Hus akiwa anachomwa
moto alitoa unabii kwa kusema “leo
mnaniua mimi lakini miaka miamoja ijayo Mungu atamwinua mtu mwingine ambaye
matengenezo yake hayaatweza kuzimwa”
Kweli baada ya kipindi hicho Mungu alimwinua Martini Luther mwana matengenezo
mkuu kama tutakavyoona hapo baadae.
4.
JEROME
SAVANAROLA.
Alizaliwa Ferrara Italia mnamo mwaka
1452, alikuwa ni mtawa wa shiriki la
wadominiko.Alijaribu kuleta matengenezo katika kanisa na serikali.
Alipinga uovu uliokuwa unafanywa na mapapa.
Alisomea mambo ya ubinadamu na
utabibu. Kufikia mwaka 1491 alikuwa mhubiri maarufu kule Frolence.
Alitabiri kwamba papa na mfalme wa Naples wangekufa siku moja,
jambo ambalo lilitokea kama
alivyotabiri. Katika mahubiri yake alitabiri hukumu kubwa ambayo ingekuja juu ya mji ikifuatiwa na kipindi chema ambapo Frolence ingewaunganisha watu
wote wa Itali. Utimilizo wa unabii huu ulionekana kuwa ni kuvamiwa kwa Itali na mfalme Charles VIII. Ambaye
mwaka 1494 aliuondoa utawala dhalimu wa
Frolence.
Baada ya kuanzishwa kwa serikali
mpya Saravano alipaata umaarufu sana pale Frolence kupitia mahubiri yake na
alileta mabadiliko mengi katika jamii. Alianzisha matengenezo ya kodi, Kusaidia
maskini na matengenezo katika
mahakama. Aliubadilisha mji kutoka
katika maisha ya kimwili na kuishi
maisha ya kiroho.
Kutokana na mabadiliko hayo kila mtu
katika mji alikwenda kanisani na matajiri waliwapa misaada masikini.Wafanya
biashara walirudisha vitu walivyokuwa wamewatapeli wateja wao. Waimbaji
waliacha kuimba nyimbo za kidunia na kuanza kuimba nyimbo za kumsifu Mungu.
Waliachana na maisha maovu, walichoma
moto mawigi, vinyago, vitabu vya kipagani,
picha za ngono na kila kitu walichodhani kuwa ni kiovu. Hakika uamsho
mkuu ulitokea kama alivyokuwa ametabiri.
Jerome alitabiri kwamba angehubiri
kwa miaka nane tu pale Florence na kisha
angeuawa. Katika mwaka 1498 Jerome
alimshutumu papa Alexander VI kwa kutangaza hadharani maovu aliyokuwa
anayafanya yeye na wasaidizi wake. Baada ya mkasa huo Alexander VI aliamua kumwekea vikwazo na kisha baadaye
akamnyonga na kuuchoma moto mwili wake mnamo
mwaka huohuo wa 1498. Maneno yake
ya mwisho akiwa anauawa alisema “ Bwana Aliteseka sana kwaajili yangu”.
Mapambano yake dhidi ya papa yalimfanya kuwa shujaa na kuwa mtangulizi wa matengenezo ya kanisa.
Alikuwa tayari kuitetea imani kwa gharama yoyote.
Wanamatengenzo watangulizi
walionyesha ushujaa katika kuitetea imani. Hawakukubali kusalimu amri kwa
uongozi wa kanisa au serikali na hawakuwa tayari kunyamaza kimya na kuacha hali
mbaya kuendelea kulitafuna kanisa, walikubali kulipa gharama katika kuitetea
imani na kupinga uovu. Walitengeneza njia ambayo ilifuatwa na wanamatengenezo wakuu baadae kidogo katika kipindi cha kanisa la Sardi yaani
kanisa la matengezo.
Kuna mengi ambayo twaweza kujifunza
kwa watu hao kutokana na vile kila
mmoja alivyosimamia kusudi lake kwa ujasiri na imani kuu. Kama tutajifunza na
kutetea imani kama wao tunaweza kuleta matengenezo katika kanisa vuguvugu la
wakati huu wa utandawazi.
F.
KUANGUKA
KWA KOSTANTINOPALI.
Wanahistoria wengi wana tazama kuanguka kwa Kostantinopoli kama mpka wa kipindi cha karne
za katikati na nyakati hizi zetu. Waislamu toka Uturuiki waliivamia
Kostaninopoli na kuishinda mnamo mwaka
1453. Hekalu zuri liliojengwa na mfalme Kostantino lililojulikana kama Saint Sophia liligeuzwa na kuwa
msikiti. Huu ndio uliokuwa mwisho wa kipindi cha giza au mediaval Period.
MADA YA SITA
KIPINDI CHA SARDI KANISA LA MATENGENEZO
KIPINDI : Tangu kuanguka kwa Kostantinopoli hadi Patano la Amani la Westpharia.
A.
SABABU
ZA KUZUKA KWA MATENGENEZO YA KANISA.
Kitendo cha Kanisa la Rumi kutokuwa
tayari kupokea mabadiliko
yaliyokuwa yanapendekezwa na watu wema kama vile, Wikrif na Hus, viongozi wa
baraza la matengenezo na mengine mengi kulipeleka kuanza kwa nguvu wimbi kubwa la matengenezo.
Hadi kufikia miaka 1500 misingi ya
jamii ya kipindi cha giza ilikuwa
inabadilika kutokana na mabadiliko ya
kielimu, kisiasa, kidini na kiuchumi. Kanisa la ulimwengu lilianza kupoteza
nguvu na kanisa la kitaifa
likaanza kuchukua nafasi
Kupanuka kijiografia kulileta mabadiliko mengi katika kufikiri.
Kwa kifupi kulikuwa na sababu mbalimbali zilizopelekea wimbi la matengenezo ya
kanisa kutokea, baadhi ya sababu hizo
ni;
1.
Kukua
kwa utaifa(nationalism).
Kila nchi ilianza kuweka mkazo
kujijenga yenyewe, hivyo nchi mbalimbali zilianza kujitenga na ushirikiano wa
kimataifa, Hii ilipelekea kanisa la
ulimwengu kokosa nguvu kwani utaifa ulisababisha kuanza kwa kanisa la kitaifa
kila mahali.
Mgogoro wa kanisa katika karne ya 14 na 15.(Utumwa wa
Babeli. Kugombania madaraka yaupapa.)(Great Schism)
2.
Kuvumbuliwa
kwa mashine za uchapishaji.
Johann Guthenberg alivumbua mashine
ya uchapaji mwaka 1456. Mpaka wakati huu
vitabu vyote viliandkwa na kunakiliwa kwa mkono. Kuvumbuliwa kwa mashine hii
kulisababisha Biblia na maandiko mengine
kuchapwa na kusambazwa katika maeneo mbalimbali. Kusambazwa kwa maandiko haayo
kulipeleka kuamsha akiri za watu na kutambua hitaji la kuwepo kwa mabadiliko
katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kanisa.
3.
Kuzuka
kwa mwamko wa kujifunza.
(Renaissence)
Hiki kilikuwa ni kipindi
ambacho ulizuka mwamko mkubwa
wa kujifunza . Kipindi hiki kilianza huko
Ulaya Italia karne ya 14 na kuendelea
hadi karne ya 17. Wasomi wengi waliibuka
katika kipindi hiki. Watu walianza kufikiri mambo kwa upya kutokana na
elimu waliyokuwa wamepata. Kutokana na elimu hiyo watu walihitaji mabadiliko
katika maeneo mbalimbali ili kuweza kuleta maendeleo. Hivyo kanisa nalo
likajikuta linahitaji mabadiliko japo kuwa halikuwa tayari kwaajili ya
mabadiliko hayo.
Ø Mgogoro wa kanisa katika karne ya 14 na 15.(Utumwa wa
Babeli. Kugombania madaraka ya upapa.)(Great Schism)
Ø Rushwa.
Ø Kanisa
kutojali maisha ya kiroho ya watu na kujikita katika mambo ya kiuchumi.
Ø Kuuzwa
kwa vyeti vya msamaha
Ø Upendeleo.
(Mtu mmoja kuwa na vyeo vingi kwawakati mmoja)
Ø Mapapa
kukosa maadili.
Ø Mapadri
kuwa na elimu duni.
Ø Kuzuka
kwa falsafa ya Mantiki.
B.
VIONGOZI
WA MATENGENEZO YA KANISA.
Katika kipengere hiki tutawatalii
baadhi ya wana matengenezo ya kanisa, yaani tutawachunguza watu ambao Mungu
aliwasimamisha kuleta kweli ya neno la
Mungu katika kanisa lililokuwa limepotoka na lisilokubali matengenezo kwa
hiali. Tutawatalii wanamatengenezo wafuatao, Martn Luther, John Calvin, Ulrich Zwingli na John Knox.
ULRICH ZWINGLY
Alikuwa ni mwanamatengenezo wa
kanisa wa kiswisi asiyejulikana sana kama Martn Luther na John Calvin lakini
aliye na mchango mkubwa katika mategenezo ya kanisa.
Alizaliwa mwaka 1484, na kuelimishwa katika Chuo kikuu cha Basel na Vienna akisomea fani
ya ubinadamu. Alifanya kazi kama Padre
wa Parish Huko Glarus Uswisi mwaka 1512. Katika mwaka wa 1515 Ulrich alianza
kuyatilia shaka mafundisho ya Kanisa la Katoliki na alianzisha kile kilichoitwa
matengenezo ya Zurich. Alihubiri jumbe za kiBiblia na kufanikiwa kulibadilisha baraza la mji kuwa na mtazamo
kama wa kwake.
Baraza hili liliufanya mji kuwa
ngome ya Uprotestant. Hoja 67 za Zwingli
ziliasiliwa na kufanywa Mafundisho rasmi ya mji na mji uliweza kubadilika kwa
haraka sana. Mahubiri na mafundisho yalifanywa mara kwa mara, sanamu
ziliondolewa , mapadre waliruhusiwa kuoa, Watawa walihamasishwa kutoka katika makao yao yaliyowatenga na
jamii na kuja kuishi na jamii. Nyumba za kitawa zilivunjika na wakatumia mali
zao katika kufadhili elimu na misaada kwa maskini.
Mwaka 1525 Zwingly alijitenga na
kanisa la katoliki, na akaanzisha mlengo wake.
Mnamo mwaka 1450 baada ya kuongoka
Zwingly alianza kuwakusanya wanafunzi waliopenda kujifunza,kigiriki, baadhi ywa
wanafunzi hawa waliongoka na wakavutiwa sana na Biblia.
Katika mdahalo wa mji uliofanyika
katika ukumbi wa mji Zwingly aliwasilisha hoja 67 Mnamo Februari1523 ambamo aliambatisha mamlaka ya Kanisa la Romani Katoliki. Mamlaka ya papa,
kuwabudu watakatifu, wokovu kwa matendo mema, mifungo, sikukuu, hija, oda ya watawa, useja kwa mapadre, Uuuzaji wa
vyeti vya msamaha, adhabu na toharani. Viongozi wa mji walivutiwa sana na hoja
za Zwingli.
Katika mdahalo mwingine wa Oktoba
1523 Zwingli alishambulia matumizi ya sanamu na akataka kuiondoa Krismas.
Viongozi wa mji hawakukubaliana na jambo hili na hivyo zwingly alikaa kimya. Zwingry aliwaogopa watawala.
Kutolizishwa kwa wanafunzi wake.
Baadhi ya wanafunzi wake waliokuwa wamemsaidia
katika kuhitimisha hoja zake zote mbili walijisikia kwamba wamesalitiwa na
Zwingli. Kwa kuacha kushughulikia swala la Sakramentili kuwapendeza watawala.
Walikuwa wamefundishwa na yeye mwenyewe kufuata mafundisho ya Biblia hivyo
wakatambua kwamba Zwingly alianza hakuwa
anawaongoza katika mwelekeo sahihi. Hivyo wakaamua kuanza kujisimamia wenyewe.
Vijana hawa walikuwa ni Conrad Grebel na
Felix Manz. Conrad alikuwa ni mwanazuoni wa kigiriki na Felix alikuwa ni
mwanazuoni wa kiebrania. Kwa pamoja
vijana hawa waliongoza kikundi cha watu katika kujifunza kikailifu mafundisho
ya Biblia juu ya ubatizo.
Mwaka 1524 walihitimisha
kwamba ubatizo usifanywe kwa watoto wadogo.
Walifundishwa kwamba watu waliompokea Yesu kama Bwana na mwokozi wao
ndio wanaostahili kubatizwa. Pia alitengeneza mawazo mapya kuhusu kanisa
wakiamini kwamba kanisa la kweli lilikuwa linahusiha watu wale walibatizwa
baada ya kukiri.
Vijana hawa walijaribu
kumshawishi mlezi wao wa zaani akubaliane na mawazo haya,
kwa kiasi fulani Zwingli
alikubaliana na mawazo haya, japo shauku
yake ya kuwapendeza watawala kulisababisha, kuwakataa na kuwpinga mawazo ya
hawa wanafunzi wake wa zamani.
Katika mdahalo wa Januari 18-19 – 1525 vijana hawa walibishana
Zwingli kuhusu suala la ubatizo wa watoto, Kiongozi wa mji alimtangaza Zwingly
kuwa mshindi wa mdahalo huo na akatangaza ya kwamba yeyote ambaye hangefanya ubatizo wa watoto wadogo au angebatiza
ubatizo wa waamini alitakiwa ama kutubu au kuondoka Zurich ndani ya siku
nane.
Kuanzisha kwa kanisa huru la kwanza.
Katika nyumba ya Colad
Grebel walikusanyika watu wachache ili
kujadili nini walitakiwa kufanya. Baada ya majadiliano hayo walifikia uamuzi wa
kwamba wanatakiwa kubatizwa upya kwa kwa sababu wote walibatizwa wakiwa watoto
katika kanisa la Katoliki. Conlad alimbatiza George Blaurock ksa sababu mtu huyu alikuwani padre. Hivyo baada ya
kubatizwa kwake alipewa jukumu la kuwabatiza wengine. Kwa sababu hii walianza kuitwa wanabatisti, maana yake ikiwa ni wabatizwa upya.
Hii ilikuwa ni moja ya
mapinduzi ya matengenezo. Mapinduzi haya yalianzisha kanisa jipya. Watu
hawa walianza kukutana kwaajili ya ibada na wakaanza kueneza kanisa lao katika
maeneo mbalimbali.Kikundi hiki pia kiliitwa undugu wa uswisi.
Baada ya mlango huu
kukua na kuenea, ulishambuliwa na kupingwa sana karibu katika Ulaya nzima.
Kanisa la Romani Katoliki, pamoja na wanamatengenezo yaani Martin Luther pamoja
na John Calvin walihusika katika kuwaua Wanabatisti. Zaidi ya wanabatisti 4000 walinyongwa.
Mnamo mwaka 1529 wanamatengenezo
walikutana katika mji wa Marbag ili
kuweza kuimalisha umoja wao. Wanamatengezo hao walikubaliana katika mambo
kadhaa, lakini kulitokea kutokukubaliana katika jambo moja ambalo ni meza ya
Bwana. Zwingli alisema kwamba mkate na divai ni kielelezo tu cha ukumbusho wa
mauti ya Yesu, wakati Luther alikaza kwamba kwa namna fulani Yesu alikuwa
katika mkate na divai kwa njia ya fumbo. Jambo hili lilileta utegano mkubwa
baina ya wanamatengenezo hawa.
Kulizuka vita baina ya Kanisa la
Romani katoliki Waprotestant, katika
vita hiyo Zwingly aliuawa, hii ilikuwa mwaka 1531.
MARTNI LUTHER.
Martin
Luther alizaliwa mnamo mwaka 1483. Baba
yake aliitwa Hans na mama yake aliitwa
magareth. Alizaliwa katika familia ya
kimsikini, baba yake alikuwa mfanyakazi
katika mgodi wa madini. kujiunga
Martin alisoma Theolojia katika vyuo vikuu vya Erfurt na Edburg. Mnamo mwaka
1505 alitunukiwa shahada ya kwanza katika falsafa na katika mwaka 15012 alipata shahada ya pili ya udaktari katika
Theolojia. Baada ya masomo yake alianza kufundisha Biblia katika Vyouo Vikuu vya Erfurt na Witternberg
Mnamo mwaka 1507 alipata ubarikio na
kuwa padre. Mnamo mwaka 1510, Martn na
mmonaki mwingine mmoja walisafiri kwenda Rumi kwaajili ya shughuli za Chama
chao cha umonaki. Akiwa Rumi alishangaa kuona udharimu uliokuwa ukifanywa na
mapdre huko Rumi. Martin akiwa mmonaki
alipata mabishano makubwa moyoni mwake, na alijiuliza namna gani ambavyo
angeweza kupata rehema za Mungu. Alijipiga, Alifunga na kujitesa kwa muda mrefu
ili aweze kusamehewa dhambi zake. Alipata majibu ya maswali yake yote baada ya
kusoma Waraka wa Warumi 1:16-17. Ukiwa
na maneno mwenye haki ataishi kwa imani.
Wakati huo huo papa Leo X aliwatuma wawakilishi wake katika
nchi mbalimbali kukusanya fedha kwajili ya ujenzi wa kanisa la Mt Petro. Walikusanya fedha hivyo kwa njia ya kuuza vyeti
vya msamaha. Wakristo waliweza kununua vyeti kwajili yao wenyewe na kwaajili ya
ndugu zao waliokwisha kufariki ili waweze kupata msamaha.
Luther alipinga vikali jambo hili
pamoja na mambo mengine ambayo yalikuwa
kinyume na Maandiko matakatifu kwa kuandika hoja 95 na kuzibandika katika
mlango wa kanisa kule Huko Wittenberg. Marafiki
Luther walipiga kopi hoja hizo na kuzisambaza katika maeneo mbalimbali
ya nchi ya ujerumani ili ziweze kusomwa na watu wote. Kwa muda mfupi nakala hizo
ziliweza kuenea na mafundisho ya Luther yakaenea katika maeneo mbalimbali.
Baada ya hoja hizo kuenea Luther
aliitwa na Kardinali, Cajetan katika mji wa Dusgbarg( 1518). Kardinari huyo
alimtaka Luther kukiri makosa yake lakini Luther alipinga swala hilo.
Papa Leo wa kumi alimwandikia Luther
barua ya kumtishia kumtenga na kanisa iwapo hangekiri makosa yake. Baada ya Luther ya kuipata barua hii aliichoma hadharani
mbele ya watu wengi.
Mnamo mwaka 1521.Luther alitengwa rasmi na
kanisa Katoliki.
Luther aliitwa katika mkutano uliofanyika katika mji wa worms ulioitishwa
na kaisari Charles V, ili aweze kusikilizwa na kumaliza mgogoro. Katika mkutano huo Luther alitakwa kukiri
makosa yake kuhusu vitabu alivyokuwa
ameviandika na kuvisambaza.. Luther alikataa kubadili msimamo wa
kuyakana maandishi yake, na hatimaye kaisari na wafalme wake walitangaza hukumu ya kifo
dhidi ya Luther. Katika mkutano huo kulitokea fujo na hatimae Luther alitoroka
na kuokolewa na mfalme Fredrick wa Saksoni na kupelekwa katika boma lake la Wartburg. Akiwa huko alijificha kama
mfungwa na alibadilishwa jina na kuitwa Jorg
na kupelekewa nguo zingine. Alibadili sura yake
kwa kufuga ndevu.
Akiwa katika boma hilo alianza kazi ya
kutafsiri Biblia katika lugha ya kijerumani.
Katika muda huu wa kukaa
mafichoni Luther alifanya kazi kubwa ya matengenzo kuliko wakati mwingine kwake
wote.
Mnamo mwaka 1529 Wafalme walibadili msimamo
wao wakaamua ya kupigana dhidi ya wanamatengenezo. Wafalme 19
walipinga uamuzi huu, na hivyo wakaitwa waprotestanti. Hivyo neno hilo wakapewa
watu wale waliokubali matengenezo ya
kanisa. Martin Luther alifariki dunia
mnamo m 17, Februari, 1546. Na kuzikwa
katika kanisa alikobandika zile hoja 95 kule wartnbarg.