Maombi haya ni kwa ajili ya wale ambao wanataka au wanatamani
kujiondoa kwenye maagano ya Uharibifu,au maagano na nguvu za giza.Maagano ya
Uharibifu yapo kwa ajili ya ya kuharibu tu na si vinginevyo,na kadiri
yanavyoendelea kuwepo Uharibifu hauepukiki.Maagano yanayozungumziwa hapa ni
yale ya kurithi au yaliyoingiwa na mhusika aidha kwa kujua au pasipo kujua kama
anaingia kwenye maagano.Kwa sababu ni maagano ya uharibifu ni muhimu kujiondoa
au kuvunja maagano hayo.Ili kuyavunja ni lazima utangaze kuyavunja,na
inawezekana maagano mengine yapo hapo muda mrefu,kwa hiyo ni lazima kuomba kwa
bidii [Yakobo 5:16]
Angalizo:Usiombe Maombi haya bila maelekezo,kama huelewi chochote
Aya za kukiri: Wakolosai 2:14-15, Wagalatia 3:13-14
1. Ninarudisha mamlaka yote aliyopewa shetani na mababu/mababa ,katika
Jina la Yesu.
2. Nina zilaani roho zote zinazoendelea kutilia mkazo hayo maagano
katika maisha yangu na naziamuru kuniachia kwa Jina la Yesu[ Sema mara 3 na
anza kusema hivi,”niachie kwa jina la Yesu
3. Kitu chochote kilichoingizwa kwenye maisha yangu,kwa mkono wa
kipepo,ninakiamuru kiachie kwa JIna la Yesu
4. Kila
aina ya sumu iliyopenyezwa kwenye maisha yangu nina iamuru itoke nje
sasa,katika jina la Yesu,nina sukuma nje kwa damu ya Yesu.
5. Ee Bwana Yesu,shusha moto juu ya kila roho ya mauti na
kuzimu,iliyoandaliwa kwa ajili yangu,katika jina la Yesu
6. Nina ponda kichwa na kukanyaga kila mkia wa
majoka ya kiroho,katika jina la Yesu
7. Upanga wa moto,na uanze kukata kila kifungo walichokifunga
wazazi,katika jina la Yesu
8. Ee Bwana,nifunulie agano lolote la siri ambalo shetani amefunga na
nafsi yangu au anataka kufunga na nafsi yangu,katika jina la Yesu.
9. Kila pando,ambalo baba yangu wa mbinguni hakulipanda katika maisha
yangu,nina kungo”a katika jina la Yesu.
10. Baba
nina pitisha umeme katika ardhi ya mahali hapa sasa na kila agano na miguu
yangu lianze kuvunjika sasa katika jina la Yesu.
11. Agano
lolote la siri ambalo ni la uovu,ninakuvunja katika jina la Yesu
12. Nina
nyunyiza damu ya Yesu kuvunja laana zote
13. [Imba
wimbo huu: Kuna nguvu ya ajabu,damuni mwa Yesu ]
14. Nina
nyunyiza damu ya Yesu kuvunja laana zote za dhambi za wazazi wangu
15. Ee
Bwana,badili laana zote zilizoelekezwa kwangu kuwa Baraka
16. Kila
nguvu ya uovu iliyoelekezwa kwangu,ninakuamuru kurudi moja kwa moja ,kwa
mtumaji katika jina la Yesu.
17. Ee
Bwana Mungu, ninaomba kila alichosema adui kwamba hakitawezekana katika maisha
yangu, kikawezekane sasa kwa jina la Yesu.
18. Nina
jiondoa na kujitenganisha katika kambi yoyote ya mateka inayomilikiwa na
adui,katika jina la Yesu.
19. Nina
jifungua na kujiondoa kutoka kwenye kila kifungo cha kurithi ,katika jina la
Yesu.
20. Ee
Bwana,tuma shoka lako la moto kwenye misingi ya maisha yangu na uharibu/ulikate
kila pando ambalo amelipanda adui katika jina la Yesu.
21. Nina
ipitisha Damu ya Yesu,katika mifumo yote ya mwili wangu[mfumo wa damu,wa
fahamu,wa chakula,wa upumuaji,wa takamwili n.k] na kuisafisha mabaki yote ya
urithi wa vitu viovu katika jina la Yesu.
22.Damu ya Yesu na moto wa Roho
mtakatifu,unisafishe kila kiungo cha mwili wangu
[Figo,moyo,mapafu,macho,masikio,n.k] katika jina la Yesu
23. Nina
vunja mikataba yote ya kiukoo na kikabila inayonihusisha mimi katika jina la
Yesu.
24. Nina jiondo/ninajivua/vunja laana zote za kikabila na kiukoo katika
jina la Yesu
25. Nina tapika chakula chochote cha uovu nilicholishwa katika maisha
yangu,katika jina la Yesu
26. Mapepo,majini,mizimu
na wachawi manao fuatilia maisha yangu,na mpararaizi[mpooze] sasa katika jina
la Yesu.
27. Shambulio
lolote lilopangwa juu ya familia yangu,ninalibatilisha kwa ajili yangu katika
jina la Yesu
28. Nina
vunja matoke mabaya yote kwa ajili ya jina la kiuovu,lilipachikwa kwenye nafsi
yangu katika jina la Yesu
29.Nina batilisha laana
zote,mikosi,majanga,ajali,maradhi yote yaliyoelekezwa kwenye maisha yangu
katika jina la Yesu.
30. Muombe
Mungu aondoe laana zote alizo ziachilia kwenye maisha yako kwa sababu ya
kutotii neon lake[kumb 28:]
31. Pepo
lolote lililo jipachika kwenye laana yoyote inayonihusu mimi,toka,katika jina
la Yesu
32. Laana
zote katika maisha yangu,badilika na kuwa Baraka,katika jina la Yesu
33.Utakapokuwa unataja laana zilizoorodheshwa
hapo chini,sema kwa kumaanisha “vunjika,vunjika ,vunjika” katika jina la
Yesu.Nina jitenganisha na nyinyi katika jina la Yesu.
· Laana zote za udhaifu wa kiakili na kimwili
· Laana zote za kushidwa katika kila ninalofanya
· Laana zote za umaskini
· Laana zote za kuvunjika kwa familia
· Laana zote za kuonewa na kudharauliwa
· Laana zote za Uharibifu wa mtu binafsi,kama vile
kujinyonga n.k
· Laana zote za magonjwa sugu
· Laana zote za kishirikina
· Laana zote za kuharibikiwa mambo ya uzazi na
viungo vya uzazi
· Laana zote za kufanya kazi kwa bidii pasipo
kuiona faida
· Laana zote za kulowea mambo ya uovu kama vile
zinaa,pombe,sigara n.k
34.Jitamkie maneno ya Baraka wewe mwenyewe,kwa
mfano kwa kusema “hakutakuwa na umaskini tena,magonjwa tena n.k katika maisha
yangu katika jina la Yesu.
35. Nina
jifungua na kujitenganisha na vifungo vya madhabahu zote za giza katika jina la
Yesu.Sema mara kadhaa ukifuatiwa na maneno yafuatayo “nina jitenganisha” katika
jina la Yesu.Tumia muda kidogo kwenye hilo.
36. Nina tapika sumu zote za mashetani nilizozimeza katika jina la
Yesu.
37.[Weka mikono yako juu ya kichwa chako] Nina
vunja kila mamlaka za giza katika maisha yangu,katika jina la Yesu.Rudia “nina
vunja katika jina la Yesu.
38. Taja
mambo yafuatayo kwa mamlaka na sema “vunjika kwa jina la Yesu.
· Mamlaka zote za mizimu na miungu ya
familia,ukoo,na kabila
· Mamlaka zote za roho za kichawi zilzopo ndani ya
familia,ukoo,kabila
· Mamalaka zote zilizoshika rimoti za kudhibiti
familia,ukoo,kabila
· Mamlaka zote ovu ndani ya Familia,ukoo,kabila nk
39. Kila
mmiliki wa mzigo niliobebeshwa beba mzigo wako katika jina la Yesu[Mzigo
unaweza kuwa ugonjwa,mikosi wabebeshe wamilki]
40. Nina
zipoodhesha/nina zipararaizi madhabahu zote za giza katika jina la Yesu
41. Nina
zilaani madhabahu zote za uovu zilizoelekezwa zidi yangu katika jina la Yesu
42. Nina
agiza nyundo ya Mungu aliyeumba mbingu na nchi,iponde kila madhabahu ya
giza zilizoelekezwa kwenye maisha yangu katika jina la Yesu.
43. Ee
Bwana tuma moto wako na uteketeze madhabahu zote za giza zinazoinuka dhidi ya
maisha yangu,
44. Makuhani
wote wa madhabahu zote za giza wanaocheza na maisha yangu,wakutane na
upanga wa roho mtakatifu. Katika jina la Yesu.
45. Mkono
wowote unaotaka kunikamata na kuniteka kwa ajili ya Maombi haya ninayoomba
kauka katika jina la Yesu.
46. Nina
waamuru makuhani wa madhabahu za giza kunyweni damu wenyewe katika jina la Yesu
47. Nina
rudisha urithi wangu ulioibiwa na madhabahu za giza katika jina la Yesu.
48. Ninafuta/ninaliondoa
jina langu kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu
49. [Weka
mkono wako mmoja kifuani] Ninaziondoa Baraka zangu kwenye madhabahu za giza
katika jina la Yesu
50. [Weka
mkono mmoja kifuani na mwingine kichwani] Ninaondoa kitu chochote kile
kinachoniwakilisha mimi [kama vile nguo] kwenye madhabahu za giza katika jina
la Yesu.
51. [Taja
kiungo chochote katika mwili wako ambacho akifanyi kazi ipasavyo au kama ni
mwili wote taja mwili] na useme maneno yafuatayo “nina kuondoa kwenye madhabahu
za giza” katika jina la Yesu.Tamka hivyo mara saba.
52. Nina
jitenganisha kutoka kwenye maagano yote ya damu na nguvu za giza katika jina la
Yesu
53. Damu
ya Yesu na unene kwa ajili yangu dhidi ya maagano yote na nguvu za giza
54. Nina
tamka Uharibifu dhidi ya roho chafu zote katika maisha yangu.Katika Jina la
Yesu.
55. Nina
jitenganisha na laana zote za maagano katika jina la Yesu
56. Nina
jitenganisha mimi na familia yangu kutoka katika kila agano la damu katika jina
la Yesu.
57. Ninajitenganisha
na kila agano la damu la kurithi katika jina la Yesu.
58. Nina
iondoa damu yangu kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu
59. Nina
iondoa damu yangu kutoka kwenye benki za damu kwenye ulimwengu wa giza katika
jina la Yesu
60. Nina
vunja kila agano la damu la kutokukusudia kwa jina la Yesu
61.Ee bwana ,damu ya mnyama yeyote iliyomwagika
kwa niaba yangu,Naipoteze nguvu ya agano sasa,kwa jina la Yesu
62. Kila
tone la damu linalotamka mabaya dhidi yangu,na ikae kimya sasa, kwa damu ya
Yesu
63. Ninajifungua
na kujiondoa kutoka kwenye kila agano la damu la kifamila,kiukoo,kabila katika
jina la Yesu.
64. Nina
jitenganisha na kila agano la damu nililoingia kwa kujua au kutojua kwa jina la
Yesu
65. Ee
Bwana kila agano la damuna nguvu za giza lipoteze nguvu na uhalali wake juu
yangu katika jina la Yesu.
66. Damu
ya agano jipya la Bwana na Mwokozi wangu Yesu Kristo,naiikemee damu ya
agano na nguvu za giza ilijipanga kinyume name.Kwa jina la Yesu
67. Nimepewa
mamlaka ya kubatilisha haki zote zilizopo kwenye maagano yote ya damu na
nguvu za giza .kwa jina la Yesu.
68.Agano lolote la damu na nguvu za giza
lililofungwa kwenye kiungo chochote kwenye mwili wangu,nalivunjike sasa.Kwa
jina la Yesu
69. Ninapokea
vitu vyote vilivyoibiwa au kuchukuliwa na adui kupitia maagano na nguvu
za giza.Kwa jina la Yesu.
70. Nina
vunja agano lolote la damu na nguvu za giza kwenye damu yangu .Kwa jina la Yesu