MADA YA KWANZA. UTANGULIZI
I.
MAANDALIZI YA KUJIFUNZA NENO LA MUNGU.
Kuna maswali kadhaa ambayo
yanaweza kutusaidia katika kujifunza Neno la Mungu. Maswali haya ni moja
ya mbinu muhimu ya kujifunza Biblia.
Mbinu hii ikifuatwa itakusaidia katika kuielewa Biblia na kuihusisha na
maisha yako ya kila siku. Maswali hayo ni:
1.
Nani ?
Sawli hili
ilnamtaka msomaji kutambua au kujua nani anazungumza katika andiko alisomalo na nani
anaambiwa katika andiko hilo.
Mfano katika
Mwanzo 22:2 Mungu ndiye msemaji
a Ibrwahimnu ndiye anaeambiwa.
2.
Nini ?
Swali hili linahusu msomaji kutambua mada inayoongelewa katika andiko husika analosoma
Ni muhimu sana unaposoma andiko ujue mada
inayoongolewa na andiko hilo. Hivyo kwa kujiuliza swali hili wweza kuja mada
inayoongelewa katika andiko husika. Andiko
hili linasema nini?
Mfano Yohana
3:16, Luka 10:2 Yohana 4:35, Yohana 1:29.
3.
Lini ?
Swali hili linalenga kumfanya msomaji kutambua
wakati andiko lilipoandikwa na wakati wa utekelezaji wa andiko hilo. Kutambua wakati ujmbe huo ulipotolewa.
Kutambua wakati uliohusika ni muhimu sana kwani kuna mambo kadha kaika vipindi
fulani yaliruhusiwa lakani baadae Mungu aliyakataaa.
Kabla ya sheria kutolewa Sinai Haikuwa dhambi kuoa
ndugu wa karibu, lakini sheria ilipotolewa jambo hili lilikatazwa kabisa.
Kutokana na dhana ya wakati ndoa ya Ibrahimu na Sara ilikuwa halali kwani
ilikuwa kabla ya kutolewa sheria. Warumi
4:15. Matendo ya Mitume 17: 37
4.
Wapi ?
Swali hili linalenga kumfanya msomaji atambue
mazingira na utamaduni wa mahali husika
andiko lilipotolewa.Kutambua eneo husika na utamaduni kutamfanya msomji
kutambua namna andiko lilivyohusika na watu wailoandikiwa na namna linavyoweza
kusika na watu wa nyakati hizi zetu.
5.
Kwanini?
Swali
hili linalenga kumfanya msomaji atambue sababu ya andiko hilo kutolewa kwa watu
walioandikiwa kwanza kabla ya kulihusisha na maisha yake binafsi. Kwanini andiko hili linasema hiki linachosema.
Kwa sababu gani andiko hili liasema hivi ?
Mfano tzama bikira atachunua mimba na kuzaa motto mwanamme
nae atamwita jina lake Imanueli . Isaya 7:114
Kwanini ilikuwa ni lazima Yesu
kuzaliwa na bikira ?
Warumi
5 inajibu swali hili.
6.
Kwa namna gani ?
au kwa jinsi gani?
Swali hili linalenga kumfanya msomaji kutambua mbinu
au njia zilizotumika katika kutekeleza kile andiko liachosema
Mfano Yesu
kutembea juu ya maji.
Kivuli cha Petro kuponya wagonjwa na leso za Paulo
kuponya wagonjwa.
7.
Ninajihusishaje
?
Swali hili ni la kimatumizi zaidi. Fundhisho hili
linahusikaje katika maisha yangu. Namna gani naweza kulifanyia kazi mimi
binafsi?.
Kumbuka kwamba Mungu huzungumza na mtu binafsi.
·
Waweza
kulihusisha Neno na Mungu unalosoma kwa kujiuliza maswali yafuatayo.
·
Tukokana na
Andiko hili kuna dhambi ninayotakiwa kutubu na kuiacha ?
·
Je uhusiano
wangu na mungu, wamini wzangu na watu wengine ukoje?
·
Kuna ahadi
ninazoweza kuzidai kwa Mungu?
·
Kuna jamboi
ninalowea kumshukuru Mungu kwalo ?
·
Weka katika
matendo Kile ulichojifunza katika Neno la Mungu.
Kumbuka kujifunza bila kuyaishi yale unayojifuna
haina maana na nikupoteza muda.
Yakobo
1:22 Lakini iweni watendaji wa neno wala
siwasikiaji tu hali kijidanganya nafsi zenu.
MADA
YA PILI. UTAFITI WA VITABU VYA HISTORIA.
Maana ya Historia
Historia
ni taaluma/elimu inayohhusu rekodi ya
matukio yaliyotokea katika vipindi mbalimbali.
Ni
Elimu ya matukio yaliyopita, yaliyopo na yajayo.
Maana ya vitabu vya Historia
Ni
vitabu vinavyoeleza histoia ya taifa la Israeli
tangu kuiteka nchi ya kanani chini y uongozi wa Yoshua mnano kama mwaka 1400 KK
mpaka waliporudi toka utumwani Babeli na mwisho wa Agano la Kale kama
mnamo mwaka wa 430 KK.Hivyo kipindi hiki kinachukua muda wa karibu miaka 1000.
Vitabu
hivi viko 12 kuanzia kitabu cha Yoshua hadi kitabu cha Esta.
Usuli wa vitabu vya histoia
Kwa
mujibu wa Mock 1990 vitabu vya vya ushaili isipokuwa cha Ayubu huingiliana sana
na na nyakati za wafalme wakakati wa
utawala ulioungana (1050-931KK) chini ya himaya ya Sauli, Daudi na Sulemani.
Jambo
la kukumbuka unapojifunza vitabu vya historia ni Agano ambalo Mungu aliweka kati yake na wana
wa Israeli ambalo kwalo aliahidi kuwapa Baraka
kwa sababu ya utii na adhabu kwa kutokutii kukaidi Soma Kumbukumbu la Torati 28.
Vitabu
hivi vya historia vinaonesha matkio ya
dhambi katika taifa la Israeli mpaka
kukawa na miaka 70 ya utumwa Babeli (605-535 KK). Hueleza kufnikiwa na
kushindwa kwa taifa hili teule la Mungu
Bwana wa majeshi.
vitabu
hivi vinaonesha na kuelez jinsi Mungu alivyokkuwa mwaminifu katika kutimiza agano lake kwa kutekelezza kila alichoahidi.
Ni ni mwaminifu katika kutimiza ahadi zake japokuwa watu hwake(Israeli)
hawakuwa waaminifu.
Vitabu
hivi vinaonesha jinsi Mungualiuvyothibitisha uaminifu wake kwa kuwakomboa wale
waliosalia kuwarudisha nchini
baada ya kuwahukumu kwa dhambi
zao.
vitabu
hivi kumi na mbili vinaeleza habari ya kutekwa na kutawaliwa kwa nchi ya
Kanani, utawala wa Waamuzi, Wafalme, mgawanyo wa Israeli wa kaskazini na
kusini, kuanguka kwa utawala wa kaskazini mikononi mwa Waasria na uhamisho wa
utawala wa kusini kwenda Babeli na kurudi Yerusalemu chini ya utawala
wa watu kama Nehemia na Ezra.
MUHTASARI WA VITABU VYA HISTORIA
Yoshua
Waamuzi
Ruthi
|
Umiliki
wa nci kwa taifa na ukandaminzwaji wa taifa
|
Utawala
na Mungu:
Vitabu
hivi vinafunika kipindi cha Waisraeli walipokuwa wakitawaliwa na Mungu
(1405-1043 K.K.).
|
1 Samweli
2
Samweli
1
Wafalme 1-10
1
Wafalme 11-22
2 Wafalme 1-17
2 Wafalme 18-25
1
Nyakati
2 Nyakati
|
Uimarisho
wa taifa
Kuongezeka
kwa taifa
Utukufu
wa taifa
Mgawanyo
wa taifa
Kuharibiwa kwa ufalme wa kaskazini
Kuondolewa
kwa ufalme wa Kusini
Maandalizi ya Hekalu
Kuharibiwa
kwa Hekalu
|
Ufalme:
Vitabu
hivi vinaeleza historia ya ufalme wa Israeli tangu kusimamishwa kwake hadi
kuharibiwa kwake 586 K.K.
|
Ezra
Nehemia
Esta
|
Kurejeshwa
kwa Hekalu
Ujenzi
wa Yerusalemu tena
Ulinzi wa watu wa taifa
|
Kurejeshwa:
Vitabu
hivi vinaeleza kurudi kwa wageni katika nchi baada ya miaka 70 kuwa mateka
(605-536 K.K.).
|
Ujumbe
mkuu
wa vitabu vya Historia ni maandalizi ya Kristo.
II.
KITABU CHA YOSHUA. USHINDI KWA NJIA YA IMANI NA UTII
Kitabu
hiki kinasimama kamadaraja kati ya
kitabu cha Pentatki a vitabu vya historia. Jina la kitabu kiki
linatokana na jina la mhusika wake mkuuambaye ni Yoshua. Kitabu hiki cha Yoshua
kinaeleza habari za kuiteka na kuimiliki nchi na mgawanyo wan chi hiyo kwa
makabila 12 ya Israeli.
Katika
kitabu hiki tunamwona Mungu akitimiza ahadi za alizowaahidi mababa(Ibrahimu,
Isaka na Yakobo) na taifa l Israeli kwa ujmla
kama taifa lake takatifu.
Mwandishi
wa kitabu.
Yoshua ndiye
anaedhaniwa kuwa mwandishi wa kitabu hiki
Because Joshua believed God would give Israel
victory, regardless of the
strength of the
nations in the Promised Land, Moses changed his name to
"Joshua"
which means "Jehovah is salvation".
Jina
la halisi la Yoshua awali lilikuwa ni
Hoshea (Hesabu 13:80) lenye maana ya Wokovu
Kwa
sababu Yoshua alimwamini Mungu kwamba angewapa Israeli ushindi na kuimiliki nchi ya ahadi bila kujali nguvu
ndogo walizokuwa nazo Israeli Musa alimbadilisha jina na kuwa Yoshua ambalo
maana yake ni YEH OVA ni wokovu.
Tarehe ya kitabu: kitabu hiki kimeandikwa
kama mwaka wa kati ya 1400-1370 K.K
Kusudi/
Lengo la kitabu.
· Kuonesha
kutimizwa kwa ahadi za Mungu kwa watu wake.
· Kuonesha
sababu za Israeli kushindqa kuimiliki nchi yote kikamilifu.
Kutokana
na mapambano makali kati ya Israeli na vikosi vikuu 30 vya maadui zao, Israeli
walijifunza somo kuu ya kwamba ushind
hupatikana kwa njia ya imani na utii kwa Mungu
na sio kwa Nguvu za. Kijeshi
Zeka
Muundo wa kitabu.
Kitabu
hiki kina sura tatu 24
Migawannyiko
mitatu.
v Mgawanyo wa kwanza Kujitayarisha
kwa ushindi.
Sura ya 1-5
Jukumu la Yoshua. Yos 1:1-9
Mungu anampa yoshu maagizo Kushusu kazi
iliyo mbele yake.
Ø Agizo
la kwenda.(Ebr 4:8-11)
Ø Kuwa
shujaa.(Yn 16:33)
Ø Kuwapa
watu urithi. Efe 4.
Ø Kuwa
watendaji wa Neno Yak 1:22.
· Taarifa
ya wapelelezi kule yeriko. Yos 2
· Rahabu
Y os 2
· Kuvuka
mto Yordan Yos 3
· Mawe
ya ukumbusho 4.
· Tohara Yos 5
· Amirijeshi
wa majeshi ya Bwana. Yos 5:
v Mgawanyo wa pili: Kuiteka nchi.
· Sura
ya 6 -12.
· Uvamizi
wa kijeshi Yos 6
· Ushindi
kule yeriko Yos 6
· Dhambi
na kushindwa kule Ai. Yos7
· Uvamizi
wa Kusini. Yo 9-10
· Uvamizi
wa Kasakazini Yos 11
· Ushindi
. Bwana alipigana upande wa watu wake Israeli. Yos 11:23
v Mgawanyo wa tatu: Kugawanya nchi.
Baada ya kuiteka nchi, Yoshua anaigawanya nchi hiyo kwa
makabila 12 ya waisraeli.
Mahali pa katikati pakatengengwa
kwaajili ya kuabudia kule Shilo.
Miji ya Makimbilio.
Miji ya Walawi.
Israeli wanashindwa kuwafukuza baadhi ya
maadui zao.
Hotuba ya Mwisho ya Yoshua
Muhtasari
wa mgao wa nchi.
Kasakazi
: Nchi
ya upande huu ilichukuliwa na makabila ya
Reubeni, Gadi na Nusu ya kabila
ya manase.
Kusini:
Nchi
ya upande huu ilichukuliwa Yuda na ndiko
mji wa Yesrusalemu ulikuapo. Karebu walipewa mji wa Hebroni.Kisha miji a
kikimbiliua ikachaguliwa na walawi wakapewa miji 48 kw a sababu hawakupewa
urithi wowote katika nchi yenyewe.
Mashariki
ya kaanani. Nchi ya upande huu
ilichukuliwa na makabila mengine tisa
yaliyobaki.
Jambo
muhimu.
Ilikuwa ni jukumu la
kila kabila lenyewe kuwaondoa wakaanani waliokuwa wamebaki katika maeneo yao. Lakini cha kusikitisha ni kwamba jambo hili
halikutekelezwa kikamilifu kwani baadhi ya wakaanini waliachwa na hii ikawa ni
mtego na kitanzi kwao kama tutakavyoona katika kitabu cha waamuzi.
Bwana
aliwapa nchi yote Yoshua 21:43. Halikuanguka jambo lolote lilikuwa ni jema ambalo Bwana alikuwa
amelinena kwa habari ya nyumba ya Israeli; yalitima mambo yote. Yoshua 21:45.
Hii inamaana kwamba Mungu alitimiza
Agano lake alilomwahidi Ibrahimu. Ahadi za Mungu ni za kweli akiahidi anatenda.
Watu
muhimu
· Yoshua
· Rahabu
· Akani
· Amirijeshi
wa majeshi ya Bwana.
Matukio
muhimu
· Kuanguka
kwa Yeriko.
· Kushindwa
kwa Israeli mbele ya Ai
· Kusimamishwakwa
dunia (Jua).
Mafundisho
Makuu.
Mungu ni mwaminifu kwa ahadi zake.
Mungu hutuwezesha kutimiza makusudi yake
tukiwa watiifu.
Neno la mungu lapaswa kuyaongoza maisha
yetu.
Dhambi huondoa uwepo wa Mungu a
kutufanya tushinde mapambano mbele ya
maadui zetu.
Ni lazima kufanya uchaguzi wa kumtii
Mungu au la na si kuwa katikati.
Mitajo
ya Kristo.
Amirijeshi
wa majeshi ya Bwana. Huyu ni yesu mwenyewe aliyemtokea Yoshua na
kumthibitishia kwamba Mbingu ilikuwa inapigana upande wake hivyo hakupaswa
kuogopa aana vita ilikuwa ni ya Bwana.
Yoshua:
Huyu
ni kivuli cha kristo kuanzia jina lake na kazi yake aliyopewa ya kuwarithisha
watu nchi. Yesu nae anakazi ya kutuithisha mbingu.
Kamba
nyekundu ya Rahabu:Kamba hii ilikuwa ni kivuli
ikiwakilisha damu ya
Yesu ambayo ilitakiwa kumwagika kwaajili
ya ukombozi wa ulimwengu.
Kamba hii ilikuwa ni kielelezo kwamba
ukombozi wa kweli ungepatikana kwa kumagwa kwa damu isiyona hatia na watu wote wenywe kufunikwa na damu hiyo
wangekuwa salama salimini.
III.
WAAMUZI. Kushindwa kwa sababu ya kuasi
Jina
la kitabu:
Jina
la kitabu hiki kwa Kiebrania ni Shophetim, ikiwa na maana ya Waamuzi, Watawala
Wakombozi au Mwokozi. Shophet siyo tu kwamba inabeba maana ya kulinda haki na
kutengeneza mashtaka lakini pia ilikuwa na maana ya “mapinduzi na kukomboa”.
Kwanza kabisa Waamuzi waliwaokoa watu halafu walitawala na kulinda haki.
Kitabu
kinapata jina lake kutoka kwa idadi ya viongozi wanaoitwa “Waamuzi” ambao Mungu
aliwainua ili wapate kuwaokoa waisraeli kutoka katika kukandamizwa. Kichwa cha
habari cha kitabu hiki kinaonekana vizuri 2:16, “Kisha Bwana akawainua
waamuzi waliowaokoa na mikono ya watu hao waliowateka nyara.”
Hata
hivyo Mungu alikuwa mwamuzi wa Israeli na mwokozi kwa sababu alikuwa ni Mungu
ambaye aliwaweka kakika Mateso kwa kuwa walikuwa wamekengeuka (waligeukia njia
zao wenyewe na hivyo Mungu akainua Waamuzi ili walete ukombozi baada ya taifa kuwa limetubu na kujuta
likihitaji msaada) (11:27 ;823).
Waamuzi
ni daraja kutoka nyakati za Yoshua hadi nyakati za Samweli na mwanzo wa utawala
wa kifalme chini ya Sauli na Daudi. Kinatoa historia ya kushindwa kwao,
ukandamizwaji, maombi, na hata wokovu pia. Kwa kufanya hivyo kinakuwa ni kitabu
cha maelezo na cha sababu ya mahitaji ya ufalme katika Israeli. Kwa kuwa kila
mtu alikuwa akifanya kitu kinachompendeza machoni pake (21:25) hivyo, hitaji la
taifa lilikuwa ni kupata Mfalme atakayewaongoza katika haki.
Kimafundisho,
Waamuzi kinatupa mambo mazuri
yaliyo katika ukweli. Kama Mungu alivyotahadharisha katika kitabu cha
Kumbukumbu la Torati kutii kunatupa baraka, lakini kutotii ni laana. Waamuzi
wanatukumbusha kuwa ikiwa watu watamrudia Bwana wakamlilia na kutubu, Mungu
ambaye anatuhangaikia sisi, mwingi wa neena atatusikia na kutuokoa. Waamuzii
inatuonesha kusudi lake la jinsi walivyojifungua katika maelezo yao kwa
kuonesha madhaifu na jinsi gani walivyofanya katika kutubu yote na Bwana
akainua na kuokoa taifa lao.
Mwandishi wa kitabu. Mapokeo yanadai kuwa
Samweli ndiy mwandishi wa kitabu hiki cha waamuzi.
Tarehe ya kuandikwa. Kitabu hiki kiliandikwa mnamo kama mwaka wa 1000 K.K.
Kusudi/Lengo
la kitabu :
·
Kuonesha kutangatanga kiroho kwa Wana wa Israeli katika nchi ya ahadi.
Tambua kwamba Wana wa Israeli walitangatanga kiwmili
wakiwa jangwani, sasa wakiwa katika nchi ya ahadi walitangatanga kiroho( yaani
uhusiano wao na Mungu).
·
Kuonesha kwamba kuasi neno la Mungu huleta kushindwa.
Ujumbe wa kitabu.
Tunapomwasi
Mumgu na kutenda yale tunayoyaona kuwa sawa machoni petu tunakuwa watumwa wa dhambi na ukomboi waweza
kuonekana tu pindi tunapomgeukia Mungu na kutubu.
Mistari ya misingi
Waamuzi
2:1-3, 2:20-32, 21:25.
Watu Muhimu: Mwamuzi-Othniel, Ehudi, Shamga, Debora na Baraka,
Gideon, Tola na Yairo, Yeftam, Ibzan, Elon, na Abdoni, na Samsoni. Waamuzi
wazuri wanaojulikana ni Debora, Gideoni na Samsoni.
Muundo wa kitabu.
Kitau
hiki kin sura 21
Migawanyo
mikuu 3.
Mgawo wa kwanza.Hali
ya kiroho ( sura za 1& 2). mmomonyoko wa maadili.
Baada
ya kifo cha Yoshua Israeli hawakumtii Mungu kikamilifu katika zoezi la kuwaondoa watu waovu
waliokuwa wakiishi nchini. Makabila ya
kaanani yalikkuwa na tabia ya kuabudu sanamu, tamaa za kimwili, kukosa uadilifu na ukaidi na
Israeli walibadilika na kujihusisha na matendo hayo ya wakaanani.
Watu
hawa wapagani waliweza kuwa na ushawishi kwa waisraeli na kusababisha Israeli
kuanza kuabudu Miungu mingine na
kujiingiza katika dhambi mbalimbali .
Mgawanyo wa pili. (3-16) Mizunguko saba ya
dhambi – ukaidi/ukombozi.
Kwa
kipindi cha muda wa miaka miatatu wana wa Israeli walinaswa katika
mizunguko isiyo na mwisho ya dhambi- kukombolewa-dhambi. Habari inajirudia
mara kwa mara.
Kuna
mizunguko saba ya dhambi inayojitokeza katika kitabu hiki cha Waamuzi. Watu walimuasi Mungu na kujiingiza katika
dhambi kisha Mungu aliwacha waonewe na kuteswa na maadui zao, baada ya
kukandamizwa na maaduikwa muda mrefu waliamua
kumgeukia Mungu kwa kutubu kisha Mungu alituma waamuzi kuwaokoa, baada
ya Ukombozi huo Israeli walipata raha na baada ya muda si mrefu tena walianguka
dhambini tena na kuanza kuteswa na kuonewa na maadaui zao. Mzunuko huo
unajirudia mara saba.
Ungu
aliendelea kuonesha hhuruma, rehema na uvumilivu mkubwa mno kila walipolilia
msaada wake na kutubu. Mungu aliwapa Waamuzi ali wawaokoe katika mateso yao.Pamoja
na kupewa waamuzi bado waliendelea kukengeuka na kurudi dhambini tena na tena
zaidi.
Mgawanyo
wa tatu.(sura ya 17 -21). Kuvunjika kwa
uadilifu na upotovu kukithili.
Sura
tano za mwisho za kitabu cha waamuzi ni nyongeza kadhawakadha za mambo
yaliyochaguliwa ambayo yalitokea wakati
wa waamuzi ambayo yanaonesha udhaifu mkubwa way a hali ya uadilifu ya wana wa
Israeli. Yaani upotovu ulivyokuwa umekithiri.
Soma sua ya 21:25. “Siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israaeli; kila mtu alifanya
yaliyokuwa ni mema machoni pake mwenyewe”
Israeli
walikuwa na mfalme wa wafalme ambaye ni
Mungu mwenyewe. Vivyo waliamua kumuasi
na kila mtu akachagua lilikowa jema machoni pake mwenyewe na kwa sababu ya
kutend dhambi kia mtu aliishi masiha ya pekee bila Mungu. Soma Mwanzo 3: 1-4, Warumi 1:25. Matokeo yake kukawa hakuna
serikali , kuwa na mtapakoa wa dhambi na machafuko. Kitabu hiki cha waamuzi kinaleta utangulizi
wa vitabu vya Samweli, Wafalme na Mambo ya Nyakati.
Mafundisho makuu
· Kutomtii
Mungu huleta matokeo mabaya sana.
· Rehema
na subira za Mungu ni kuu.
· Mungu
huwaadhibu watu wake wanapotenda dhambi.
· Mungu
huwakoa watu wake kutoka katka vifungo vya dhambi wanapogeuka na kutubu.
· Mungu
daima huthibitisha mapenzi yake kwa dalili zionekanazo.
· Iwapo
Mungu si Bwana wa Maisha yetu basi sisi si kitu kabisa.
Muhtasari
wa waamuzi
Mwamuzi
|
Othinieli
3:7-11
|
Ehudi/shamgari
3:12-31
|
Debora/Baraka
4:1-5:31
|
Gideoni
6:1-8”32
|
Tora/Jaili
8:3310:5
|
Jefta/Ibzani
Eloni,
Abdoni
10:6-
12:15
|
Samsoni
13:116:31`
|
Adui
|
Wamesopotamia
|
wamoabu
|
Wakanani
|
Wamidiani
|
Wabimeleki
|
Waamori
|
Wafilisi
|
Miaka
ya utumwa
|
8
|
18
|
20
|
7
|
3
|
18
|
40
|
Miaka
ya amani
|
40
|
80
|
40
|
40
|
45
|
6,7,10,8
|
20
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Mzunguko wa waamuzi
Bwana
alighairi kwaajili ya kuugua kwao Kisha Bwana akawainusa waamuzi
waliowaokoa
2:18 2:16
KITABU CHA
RUTH.
I.
Usuli wa kitabu
Kitabu cha Ruthi
ni mwangaza katika kipindi cha giza
katika wakati wa waamuzi. Ni hadithi
ya mwanamke wa kimoabu (Ruthi) mwenye upondo mkamilifu na mwenye kujitoa
kikamilifu kwamama mke wake
Naomi.Ni hadithi inayoelezea thawabu ya
Mungu kwa watu wanaojiyoka kikamilifu katika kutumikia kusudi lake takatifu.
Ruthu ni historia ya
wanandoa wawili katika Israeli ambao wakati wa njaa walihamia Moabu. Huko mme
wake na watoto walikufa wakamwacha mwanamke (Naomi ) peke yake akiwa na wakweze
wa kike (Orpa na Ruthu). Naomi aliamua kurudi Israeli pamoja na Ruthu alimsihi
arudi pamoja naye. Katika Israeli walirudi kwa ndugu yao Boazi ili awasaidie na
Ruthu aliolewa na Boazi.
Kama dhahabu ing’aayo Ruthu alionekana kung’aa
katika siku za giza nene za kitabu cha Waamuzi. Ruthu ni kitabu cha
uaminifu,utakatifu,na upendo katika siku za vurugu na shida. Ubinafsi na
ukengeufu ndio ulikuwa unatawala siku hizo.
Hivyo katika kitabu hiki Ruthu anatupa picha
ya imani na utii katika matatizo na anaonyesha ni kwa jinsi gani imani yaweza
kuleta baraka .
Ruthu anatumika kama mtumishi mwaminifu kwa
mfalme Daudi na kama ilivyokwisha kusemwa hapo juu kuwa yeye anamwakilisha
Yesu. Kusudi jingine la Ruthu linaonesha ukweli katika ukombozi wa kinsmani,
uwepo wa mabaki ya watakatifu hata katika zile nyakati za shida na uaminifu wa
Mungu kwa wale wanaomtegemea na kutembea naye kwa imani. Kwa kuwa Ruthu alikuwa
mtakatifu, kitabu kinaonesha shauku ya Mungu ya kuuleta ulimwengu katika
familia yake.
Inaweza kushangaza kuwa kwa yeyote yule
anayemtumaini Mungu kwa hakika ni Moabu. Uaminifu wake katika familia ya
Israeli ambako aliolewa (Ruthu) na kuomba kwake huko kwa wakweze
inamthibitishia kuwa mtoto halisi wa Israeli na Mtumishi mwema wa Daudi mfalme.
Anatoa mfano halisi katika ufalme ujao wa Mungu kuwa hii haitafanyika tu kwa
sababu ya kuzaliwa au kwa sababu ya damu, hapana, ila ni kwa sababu ya kukiri
katika mapenzi ya Mungu kwa njia ya kutii kwa imani (Warumi 1:5).Na sehemu yake
katika ukoo wa Daudi inaonyesha kuwa mataifa yote yatamilikishwa katika ukoo wa
Mwana wa Daudi.
Kitabu cha Ruth ni
Miongoni mwa vitabu viwili vyenye majina ya wanawake, kikiwemo na kitabu cha Esta. Kitabu cha Ruthi
kikihusika na mwanamke mmataifa aliyeolewa na mwisraeli na kitabu cha EWsta
kikihusika na mwanamke mwisraeli aliyeolewa na mmataifa.
Uwakilishi wa kitabu cha Ruthu. Kwa kuolewa katka ukoo wa Daudi (4,17,22)
Ruthu kinabii Ruthu anawaleta wamataifa
wote kwa Masihi. Mathayo 1:5
Matukio
ya kitabu hiki ni ya kipingi cha waamuzi
kulingana na ushaihdi wa kitabu chenyewe soma.Ruth 1:1
II.
Tarehe ya kuandikwa. Kitabu
hiki kinadhaniwa kuwa kimeandikwa kama mwaka wa
1050KK
III.
Mwandishi wa
kitabu. Samweli ndiye anae dhaniw kuwa mwandishi wa kitabu cha Ruthu.
IV.
Ujumbe wa kitabu.
Imani na utii huleta thawabu.
Mungu huheshimu wertu nye imani na
watiifu wanaoshi maisha matakatifu wakia
katika huku wakiwa katika wakati uliojaa
na maovu na uchafu wa kila aina.
V.
Kusudi/lengo la kitabu.
Eileen
Crowhurst, (2008,uk 8&9) anaainisha malengo makuu ya kiabu cha Ruth kama
ifuatavyo:
i.
Kuonesha picha ya Neema ya Mungu.
ii.
Kuonesha mwanzo wa ukoo wa Daudi
iii.
Kuthibitisha kwamba wamataifa nao wanahusika katika mpango wa
Wokovu Wa Mungu.
Hivyo tunaweza kusema
kwamba kusudi au lengo la kitabu ni kuonesha kwamba Imani ndiyo njia kuu inayowaingiza
watu katika mpango wa Mungu na si undugu wa kidamu Hili linathibitishwa kwa
kuwaangalia wanawake wawili wa mataifa yaani Rahabu na Ruthu walivyoingizwa
katika mpango wa wokovu wa Mungu kwa njia ya imani na utii. Wanawake hao wote
wawili wapo katika orodha ya ukoo wa daudi ambao ndiko masihi alitakiwa kutoka yaani Yresu Kristo. Yesu anatoka katika nasaba mchanganyiko yaani
myahudi na mmataifa. Hivyo na kazi yake ya ukombozi inahusu nasaba zote.
VI.
Muundo
wa kitabu.
Kiabu hki kina sura 4 na
Migawo iine kulingana na sura za kitabu.
Magawo wa kwanza (sura ya 1) Kurudi kwa Ruthu.
Kiatbu kinaanza na habari ya uhamisho wa Elimeliki
na familia yake kwenda katika nchi ya Moabu kwa sababu ya njaa iliyokuwa
imeanguka katka nchi ya Israeli. Elimeliki alifikiri kwamba mambo yangekuwa
mazuri huko Moabu hivyo akaamua kuhamia huko. Uamuzi huo alioufanya ulitoa
hatima ya maisha yake kwani hakuweza kuiona tana nchi ya ahadi maana alifia
ugenini katika nchi ya kipagani. Yeye na watto wake wawili walifia ugenini.
Jambo hili
linatufundisha kuwa wavumilivu katika kungoja ahadi za Mungu wetu tunapokuwa
katika shida na matatizo. Kutafuta njia mbadala
isiyo ya ki Mungu katika kukabiliana natatizo huwqeza kuharibu hatima ya maisha yetu na familia zetu.
HIi inatufundisha pia kwamba aamuzi tunayoyafanya
hayatuathiri sis tu bali huathili mzunguko mkubwa sana, kuanza wewe mweyewe,
familia yako, kanisa na jamii kwa ujmla. Hivyo tuwe makini n maamuzi
tunayoyafanya. Kutokana na maamuzi ya elimeliki, Naomi alibaki mjane na mpeke
kwani aliondokewa na watu watatuambao ni
mme na wana wawili.
Baada ya mkasa huo Naomi mke wa elimeluki aliamua
kurudi nchini kwao (Israeli) na
akawaomba wake za watoto wake (Olpa na Ruthu) waliouwa wajane kama yeye kila
mtu arudi kwao. Olpa baada ya kulia kwa
muda mrefu aliamua kurudi kwao lakini na kwa Mungu wake.(1:14-15)
Ruthu alikataa kumuacha mama mkwe wake kwani alikuwa
na mtazamo wa mbali hivyo aliamua kujiunganisha na Mungu wa mama mkwe wake.
Ruthu aliwezq kudhihirisha uelewa wake kwa mambo ya kiroho. Aliweza kuuuona
mpango wa Mungu wa wokovu na akaamua kushikamana nao kwa gharama zozote zile.
Mgawo wa pili; (sura ya 2)Kuvuna.
Ili Naoni ajipatie riziki Ruthu akafanya kazi ya kuvuna gano shambani
kwa Boazi aliyekuwa mwisraeli aliyekuwa anahusiana na Elimeliki.Boazi aliiona
bidii na kazi njema ya Ruthu hivyo akwa anamtunza.Naomi akatoa ushari kwamba
Ruthi afanye kazi kwenye shamba la Boazi tu kwaani Boazi alikuwa jamaa yao na
alikuwa ni mkombozi. Ruthu akatii agizo hilo.
Mgawo
wa tatu. (sura ya 3) Kustarehe
kwa Ruthu.
Naomi anatoa ushauri kwamba ruthu
anatakiwa apate pumziko kwa njia ya
kuolewa. Naomi Anatoa ushauri Ruthu
amwombe Boazi avunje undugu ili amuoe Ruthu. Hili linafanyika baabda ya ndugu
wa karibua lityekuwa jamaa ya mjane kukataa kumkomboa Ruthu. Boazi alikubali
kumkomboa na akamwoa.Boazi alipoikomboa ardhi ya jamaa ya Elimeliki alikuwa
akinunua haki za urithi za mwanae aliyefariki
aliyeitwqa Mahloni na kwa kufanya
hivyo alitakiwa kumuoa mjane wa mahloni ambaye ni Ruthu ili kuendelezajina la
ukoo.
Mgawo wa nne(sura ya 4) Kutuzwa kwa
Ruthu.
Mungu alibariki uaminifu wake na
Ruthu akaolewa na Boazi na kwakbarikiwa kumpata motto aliyeitwa Obedi ambaye
ndiye aliye mzaa Yese baba wa Daudi. Hivyo Daudi ni mjukuu wa Naomi Mmoabu.
IV.
Watu Muhimu.
Naomi, Ruthu na Boazi.
V.
Mitajo ya Kristo:
Ruthu na boazi.
VI.
Mafundisho muhimu.
§ Urafiki
uliojengwaq juu ya upendo una nguvu kuliko undugu.
§ Mungu hwabariki watu wake waliowaaminifu na
kuwatukuza.
§ Mpango wa Mungu wa wokovu ni kwa watu wote wayahudi
na wamataifa.
§ Inawezekana kuishi maisha matakatifu katikati ya
uovu mwingi.
§ Subira na uvumilivu kwa ahadi za Mungu ni jambo la
msingi sana.
KITABU
CHA SAMWELI. I
I.
Usuli
wa kitabu
Kitabu hiki
kinajulikana kama kitabu cha mpito toka utawala wa Mungu hadi utawala wa
mwanadamu.
kawaida
kitabu cha Samweli wa 1 na 2 viliwekwa pamoja kama kitabu kimoja katika kitabu
cha Kiyahudi. Vitabu hivi viwili vinatupa historia ya ufalme wa Israeli katika
kipindi cha mwanzo kabisa cha utawala wa kifame. Hata hivyo 1Samweli inaeleza
habari za mfalme Sauli na 2 Samweli inaeleza habari za mfalme Daudi.
Japokuwa
kitabu hiki asili yake kilikuwa ni kitabu kimoja katika kitabu cha kiyahudi,
lakini ilibidi kigawanywe katika vitabu viwili na mkarimani wake wa Septuagint
(hii ni tafasiri ya kiyunani katika Agano la Kale). Mgawanyo huu baadaye
ulifuatiwa na Yerome kwa kilatini ni Vulgate (tafasiri ya Biblia kwa Lilatini)
na hata katika tafasiri zingine.
Kitabu
hiki kinaeleza kipindi cha mpito toka katika utawala wa THEOCRACY kwenda katika
utawala wa ki MONARCHY yaani utawala wa kifalme.
Kunaushusiana
mkubwa katika vitabu vya 1&2 Samweli, 1&2 Wafalme na 1&2 Mambo ya
nyakati. Vitabu vya Samweli na wafame vinaeleza historia ya Samweli, Sauli, Daudi, Sulemani na ufalme uliogawanyika katika
mtazamo wa Kihistoria wakati (Historical point of view). Wakati vitabu vya
Mambo ya Nyakati vinarudia kwa kiasi kikubwa yale yaliyoandikwa katika Samweli
1na II kwa mtazamo wa kiroho(spiritual point of view). 1Samweli 4:18
1&2 Samweli
1&2
Wafalme
1&2 Mambo ya
nyakati Vinaelezea
kuanguka na kuinuka kwa ufalme wa Israeli
wa kimonaki
Kitabu cha Isamweli kinachukua kipindi
cha muda wa miaka 115, kikanza na
kuzaliwa kwa Samweli na kuishia na kifo cha Sauli.
Samweli ndiye aliyetumia na Mungu
kuanzisha utawala wa kimonaki baada ya Israeli kutaka kuwa na mfalme juu yao
kama mataifa mengine. Pia Samweli
alitumia na mungu kuanzisha huduna ya kinabii na kuanzisha shule ya manabii. Historia
inatuambia kwamba Samweli alifungua shule katika mjiwa Rama alifundisha kusoma
na kuandika na Neno la Mungu hivyo Samweli alichagngia sana katika kukua kwa
mfumo wa elimu katika taifa la Israeli. 1 Samuel 10:5).
Wayahudi wanamchukulia Samweli kuwa ni
nabii wa pili baada ya Musa. Zaburi 99:6. Na Nabii wa kwanza katika mpangilio
mpya wa manabii. 1 Samweli 3:20; Matendo ya mitume 3:24; 13:20.
Si kwamba Mungu
alianzisha huduma ya manabii na shule ya
manabii tu kupitia Samweli bali pia
Mungu alianzisha matengenezo ya
kurejesha ibada na maadili mema katika taifa la Israeli kwa kupitia mtumishi
wake Samweli. Jambo hili lilifanyika kupitia mfumo wa elimu ambao aliuanzisha
Samweli.
Mfumo huu wa elimu uliwafunza watu
mafundisho sahihi ya kiungu ambayo waliwarejesha watu kuanza kuwa na ibada na kurudi kwenye maadili ya kiM-ungu. Mfumo huu
wa elimu ulipelekea kukua kwa ustaarabu wa taifa na kupatikana kwa viongozi
waliokuwa wanauwezo wa kuwaongoza watu walioelimika, mfano wa viongozi hao ni Daudi, Sulemani, Isaya na
Mungu pia alimtumia Samweli kuunda
katiba ya kimonaki. Sauli alitakiwa kuwa mfalme
kwa utii wa sheria ya Mungu lajkini haikutokea hadi wakati wa Daudi.Katiba
iliyoandikwa na Samweli kuongoza ufalme iliitwa kitabu cha mambo ya wafalme 1Samweli 10:25. Kitabu hiki hakikuwa na
maana yoyote kwa Sauli mtu ambaye
hakujua kusoma na kuandika. Katiba hii ilianza kujulikana wakati wa
mfale Daudi mtu aliyekuwa amekulia katika mfumo wa elimu ulioanzishwa na Samweli.
Malme ambaye angeisimamia sheria ya Mungu aliingia kwenye utawala.
Mwandhishi wa kitabu. Mwandishi wa kitabu hiki ni Samweli.
kitabu hiki hakikuandikwa chote na
Samweli kwa bababu kuna matukio yaliyofanyika baada ya kufo cha Samweli yameandikwa katika kitabu hiki. Mfano
kifo cha Samweli mwenyewe katika Sura ya 24. Baadhi ya Sehemu za vitabu hivi
zinadhaniwa kwamba ziliandikwa na watu waliokuwa karibu sana na samweli kama
vile, Gadi mwonaji na nabii Nathani. 1 Mambo ya nyakati 29:29.
Mistari
ya msingi I Samwel
13:13-14 na 1 Samwel 15:22-23.
Muundo wa kitabu .
Kitabu hiki kina sura31 na migawo mitatu
ambayo ni
Mgawo
wa kwanza(sura ya 1-8) Sawmeli mwamuzi wa mwisho wa Israeli
na nabii wa kwanza.
Kitabu hiki kinaziba pengo lilipo la miaka 60 ya historia ya taifa la Israeli kati ya wakati
wa waamuzi na wakati wa wafalme.Baada ya kushindwa kwa kuhani Eli na familia
yake Mungu alimwinua Samweli kuwa mwamuzi wa mwisho na nabii wa kwanza katka
taifa la Israeli. Wakati huu Israeli ilikuwa katika wakati mgumu kwani ni kipindi ambacho Israeli ilikjuwa
ikisumbuliwa sana na wafilisti wailokuwa wameliteka sanduku la agano lilipopelekwa vitani na watoto wa Eli kuhani
wawakati huo. Samweli aliwaongoza wana wa Israeli kuinuka tena walipotubu na kubadili mwnendo wao wa uovu.
Samweli alipokuwa anazeeka alidhihirika
wazi kwamba watoto wake walikuwa na tabia kama za watoto wa Eli mtangulizi
wake na kuwakosesha sifa ya kuwa
viongozi baada ya baba yao kufariki vivyo Israeli walimwomba Mungu kupitia kwa
Samweli awape mfalme kama mataifa mengine. Kwa kufanya hivyo Israeli walikuwa
wanamkataa Mungu asiewe mfalme wao.
Mgawo wa pili: (9-15) Sauli mfalme wa
kwanz wa Israeli.
Mungu akamchagu a Sauli kuwa mfalme na
akamwagiza Samweli amtawaze kuwa mfalme.
Sauli alikuwa ndiye aina ya mfalme ambao Israeli ilifikiri kumpata.
Sauli alistarehe katika ushindi wake wa
mwanzomwanzo katika himaya ya utawala
wake ingawa alishindwa kuwa mwadilifu mbele za Mungu. Kutokana na Sauli kukosa
uadilifu Mungu alimkataa asiew mfalme juu ya Israeli japokuwa alimruhusu
kutawala kwa muda wa miaka 15 hadi wakati wa kifo chake.
Mgawo wa tatu.(16-31) Daudi, mfalme wa
kwanza aliyechaguliwa na Mungu.
Baada ya utawala wa kama miaka 25 hivi wa Sauli Mungu alimchagua
Daudi kuwa mfalme wa Israeli. Daudi alichaguliwa kuwa mfalme akiwa na miaka 15
lakini alianza utawala wake akiwa na maika 30. Umaarufu wa Daudi ulianza wakati
alipomuua Goliathi. Baad a ya Daudi kumuua Goliathi na kupewa
sifda nyingi kuliko Sauli kulizusha wivu na sauli akataka kumuua Daudi kwani
alipoteza usalama moyoni wa kiuongozi.
Daudi alianza kuwindwa na Sauli kama
mnyama ili auawe lakin kwa msaada wa rafiki yake Yonathani kijana wa Sauli na
mke wake Mikali Daudi aliponyoka na kuishi jangwani kama mtoro.
Daudi alipata fursa kadhaa za
kujilipizia kisasi juu ya sauli pale Mungu alipomtia Sauli Mikononi mwake,
lakin Daudi alikataa kumdhuru Sauli, aliheshimu mafuta ya kimasihi yaliyokuwa
juu yake Sauli na akakataa kuimwaga dmu ya Masihi wa Bwana. Hakika Daudi
alikuwa na moyo wewnye kumcha Mungu
kwani aliamni kwamba kisasi ni juub ya Bwana mwenyewe.
Hata Sauli alipokufa bado Daudi
hakuingiwa kwenye utawala yeye mwneyewe, japokuwa alijua kuwa nafasi ya ufalme
ilikuwa ni yake. Aliamua kusubiri mpaka atawzwe na Mungu mwenye. Wakati huu wa
dhoruba kali juu ya maisha ya Daudi ndio wakati alioandika Zaburi nyingi.
Watu
muhimu ni , Hana,
Eli, Samweli, Sauli, Daudi, Goliathi, na
Yonathani.
Mitajo
ya Kristo. Daudi.
Mafundisho
muhimu.
· Mungu
anatafuta watu watakao sikiliza sauti yake na kuitii kikamilifu.
· Urejesho
na uamsho huja kwa kupitia toba ya kweli.
· Mungu
wakati mwinhgine hutupa yale tunayoyafikiri kuwa ndiyo tunayoyataka ili
kutuonesha kwamba siyo tunayohitaji.
· Mungu
hutaka utii mtimilifu.
· Imani
hutuwezesha kuona mbali kupita mipaka ya maisha tuliyonayo.
· Tunapaswa
kufuata ushauri wa Mungu na wala sio wa wanadamu.
· Ushindi
hupatikana kwa uweza wa Bwana mwenyewe wala si kwa nguvu za mwili.
· Mungu
huwachagua watrumishi kutimiza kusudi lake na sio makusudi na nia za mioyo wao wenyewe.
· Ukaidi
daima huleta matokep mabaya sana.
·
SAMWELI
II
Miaka
40 ya utawala wa Daudi.
I.
Usuli
wa kitabu.
Kitabu hiki ni mwendelezo wa kitabu cha
Samweli na kiachukua jina lake toka kwa mhusika wake mkuu ambae ni Samweli.
Bila makusudi yoyote ya kuharibu
historia ya ufalme wa Waisraeli 2 Samweli anaendelea kueleza juu ya kuanzishwa
kwa ufalme wa Waisraeli na hata mwanzo wa kifo cha Sauli na inaendelea na
utawala wa Daudi. Na hii imechanganuliwa tangu miaka ya 40 ya utawala wa Daudi
(5:4-5) na inaendeleza utawala huu kupitia ushindi na majonzi ya masikitiko
yanayojumuisha dhambi zake, uuaji na hata matatizo katika jamaa yake na hata
taifa. Kusudi katika 2 Samweli inaonesha utawala wake Daudi, na hii inaweza
kufupishwa “kwa kiasi gani dhambi inabadili furaha hata mafanikio kuwa
shida na huzuni” Taifa lilisimama chini ya Sauli na kupanuka wakati wa
Daudi. Utawala wa Sauli uliimarisha Israeli tangu wakati wa Waamuzi lakini
utawala wa Daudi ulileta kupanuka kwa taifa hili na hata kukua zaidi. Kwa hiyo
tunaweza kusema kuwa hii inatueleza kabisa kibiblia jinsi gani utawala wake
ulikuwa, 2 Samweli inaonesha uzuri na ubaya wa mfalme Daudi.
Baada ya kifo cha Sauli Abneri
kamanda mkuu wa majeshi ya Sauli alimtawaza mmojwapo wa watotowa Sauli kuwa mfalme ambaye
ni Ithiboshethi kutawala sehemu moja ya ufalme (Israeli) kwa
miaka miwili. Yuda ilimkubali Daudi kuwa mfalme wao. Baada y kufa kwa
Ithiboshethi utawala ulitakiwa kwenda kwa motto nojawapo wa Yonathani laki Israeli
yote ilitambuwa kwamba Daudi ndiye aliyetakiwa kuwa mfalme juu yao baada ya
kifo cha Sauli.
II.
Mwanndishi wa kitabu Gadi na
Nathani ndio wanaodhwaniiwa kuwa waandishi wa kitabu hiki. Rejea maelezo ya utangulizi
wa uchunguzi wa kitabu cha 1Samweli.
III.
Tarehe ya kitabu .
Kitabu hiki kinadhaniwa kuwa kimeandikwa kama mwaka wa 1010 KK.
IV.
Kusudi/lengo la kitabu.Kueleza miaka arobaini ya uawala wa Daudi.
V.
Ujumbe wa kitabu.
Tunavuna tunchopanda. Kila mwanadamu akifanyacho ni mbegu na kitatoa mavuno
kutokana na aina ya mbegu iliyopandwa.
VI.
Mistari ya msingi.
2Samweli 7:16 na (2Samweli 24:24).
VII.
Muundo wa kitabu.
·
Kitabu hik kina sura 24 na
·
Migwanyo mikuu mine 4.
Mgawanyo
wa kwanza
(1-10) Kuinuka kwa Daudi.
Baada ya kifo cha
Ssauli daudi alitawazwa kuwa mfalme wa Yuda katika mji wa Hebroni ambako kulikuwa
na makabila mawili ya kusini. Makabila kumi
ya Kaskazini hayakmtambua Daudi kuwa mfalme yalimfuata Ish bosheth (mwana pekee wa Sauli aliyekuwa amesalia )kuwa
mfalme .
Kutokana na jambo hili kulikuwa navita ya
wenyewe kwa wenyewe kwa muda wa miaka saba na nusu. Daudi na amiri jeshi wake
Yoabu walimshinda Ish bosheth na amiri jeshi wake Abneri. Na wote wawili
waliuawa.
Daudi
aliendelea kumngoje Mungu aili amuweke kuwa mfalme na baada ya kutimiza miaka
30 Mungu alimuweka Daudi kuwa mfalme wan chi nzima. Daudi alitawala taifa zima
kwa muda wa miaka 30, kipindi hiki kilikuwa ni kipndi cha furaha mno kwa kuwa
Daudi
Daudi
aliufanya mji wa Yesrusalemu kuwa mji mkuu wa kisiasa na kidini.
·
Alirudisha lile sanduku la agano yerusalemu.
·
Alifanuikiw kiuchumi, kisiasa na kivita
·
Alileta uadilifu na haki nchini.
·
Daudi alikuwa n nia ya kumjengea Bwana hekalu lakini Bwana alimkataza na kumwambia
mwanae Sulemani ndiye angehusika na ujenzi huo.
·
Mungu alimwahidi daudi kwamba mbali yake itaishi milele na
kwamba kutakuwa na mfalme na kiti cha enzi kutoka kwenye ukoo wa Daudi. Ahadi hii hujulikana kama agano la Daudi na hatimae
ilitimizwa katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Soma 2Samweli 7:8-17 na Luka 1:26-33.
Mgawanyo
wa pili
(11-12) Kuanguka kwa Daudi.
Anguko la Daudi
lilitokea wakati wa kipindi chake cha mafanikio makuu na ustawi. Anguko hilo
lilitokana na sababu zifuatzo.
Kukosa kazi kwa Daudi. Daudi hakuwa
mahali alipotakiwa kuwa na hivyo akajihusisha na dhambi. Tunakuwa mawindo
rahisi kwa shetani tunapokosa kujihuisisha na kazi ya Mungu.
Kama Daudi
angekwenda vitani na majeshi yake tkio hilo la dhambi lisingetokea.
Daudi aliacha kujali (unconern). Kwa hakika kipindi hiki kilikuwa
ni kipindi cha vita na Daudi aliamua kutokwenda vitani na kukaimisha mtu
mwingine nafasi yake. Kwa sababu kipindi hiki kilikuwa ni cha mafanikio hivo
Daudi hakujisikia kuwajibika yeye mwwenyewe. Tusipokuwa waagalifu wakati wa Mafanikio waweza kuwa ni wakati mzuri kwa adui
kutuangusha katika dhambi.
Kutokana na Daudi kutokuwa katika nafasi yake
aliiruhusu dhambi kutafuna maisha yake. Daudi alizini na Bethsheba na kumpa
mimba, kisha akajaribu kuificha dhambi yake kwa kumrububi uria ili alale na
mkewe Betsheba ili ionekane kwamba ni mimba ya Uria, lakini mpango huo
ukashindikana. Baada ya kushindikana
mpango huo Daudi akaamua kufanya dhambi ya maauaji. Akamwamuru amiri jeshi wake
mkuu (Yoabu) kumuweka Uria kwenye mstari wa mbele vitani ili uria auawe, mpango
huo ukafanikiwa Uria asiye na hatia
akauawa. Hayo yote Daudi anayanya ili kufunika dhami yake.Dhambi inazaa dhambi na
kisha mauti. Kutokuwa kwenye nafasi+ Tamaa= uzinzi+ uongo= mauti.
Dhambi inabakiwa
kuwa dhambi hata ipakwe rangi nzuri kiasi gani na dawa yake ni toba tu.
Unapojaribu kuficha dhambi utajikuta unaongeza dhambi juu ya dhambi. Hivyo toba
ndiyo dawa pekee ya dhambi.
Mungu hakukubaliana
na kile Daudi alichokifanya aliamua kumkabili mfalme Daudi kwa kupitia nabii
Nathani.Daudi baada ya kukabiliwa na Mungu akatubu na Mungu akamtangazia
hukumu. Mtoto wa kwanza wa kiume ambaye
angezaliwa na Daudi kwa Betsheba angetakiwa kufa na upanga usingetoka katika
nyumba ya Daudi kwani aliwapa Adui za Bwana nafasi ya kukufuru.
Baada ya Yule motto wa kwanza wakiume kufa Mungu alimjalia Daudi
kupata mtot mwingine wa kiume kwa
Betsheba mtot hyu aliitwa Sulemani ambaye
ndiye aliyekuwa mrithi wa kiti cha ufalme cha Daudi baba yake.
Mgawanyo wa tatu (13-20)Maafa ya
Daudi.
Mungu ni mwingi wa rehema alimrehemu na kumsamehe Daudi
alipotubu, lakini sababu alikuwa amepanda kanuni ya kupanda na kuvuna ilikuwa
haina budi kutenda kzi, hivyo Daudi aliiltete familia yake balaa badala ya Baraka.
Sura hizi zinaeleza kwa undani matokio ya dhambi ya Daudi na hkumu zake. Japokuwa Mungu alimsamehe
Daudi lakini Daudi alitakiwa kuyapokea matokeo ya dhambi yake. Mikasa ilianza katika watoto wa daudi, Amnoni
akambaka ndugye Tamari dada wa Absalomu, Absalomu anamuua Amnoni na kisha
anampindua baba yake na kujitangazia utwala. Daudi anakimbia kama mkimbizi toka
ikulu akiwa peku huku akilia, Absalomu anauawa na kisha Daudi anarejea tena
Yerusalemu kwenye utawala ingawa hakuwa
na utukufu kama ule wa mwanzo.
Dhambi ilileta pigo
kubwa katika maisha ya Daudi.
Mgawanyo wanne (21-24) Ujasiri wa
Daudi.
Sura hizi zinafanya nyongeza ya kihistoria ya kitabu cha Samweli
II. Zinatoa taaarifa maalumu ya mbambo yaliyotokea wakati wa utawala wa Daudi. Daudi
alitenda dhambi nyingine machoni pa Mungu ya kuwahesabu askari wake katika
kuonesha nguvu yake ya kijeshi. Mungu akaleta tauni lakini Daudi akaomba
rehema na tauni ikakoma. Toba yake Daudi na dhabihu aliyoitoa katika mlia Moria
kuliipoozesha tauni. Daudi akanunua
mahali ambapo hekalu lingejengwa na Kristo angetjioa dhabihu yeye mwenye miaka
1000 baadaye.
VIII.Watu muhimu Daudi, Yoabu, Abneri, Ish boshethi, Mefibosheti,
Betsheba, Uria, Nathani na Absalomu.
Mafundisho makuu ya
kitabu.
Dhambi huleta matukio mabaya
Dawa ya dhambi ni toba pekee.
Dhambi yoyte ile inamatokeo ambayo mtenda dhambi hana budi
kuyavuna.
Mungu hana upendeleo na hukumu zake ni za haki.
Mungu ni lazima aiadhibu dhambi.
Mungu husamehe husamehe dhambi tunapotubu.
Dhabihu ya thamani mbele za Mungu ni ile inayogharimu.
Matokeo y dhambi yanaathili jamii nzima.
1 Wafalme.
Usuli wa kitabu.
1 na 2 Wafalme kwa asili yake ni kitabu kimoja kama vile
Samweli na hata Mambo ya Nyakati . Kiliitwa
Wafalme kwa Kiyahudi (Melechim). Viliitwa hivyo tangu historia ya Wafalme wa
Israeli na Yuda tangu zama za Sulemani na hata kuelekea kwa mateka wa Babeli.
Na 1 Wafalme inaishia kwa kueleza mwanzo wa utawala wa Mfalme Ahazia 853 K.K. Vitabu hivi vinaelezea historia ya kipindi cha
miaka karibu 400
Muda wa Kuandikwa:
Ni kama 550 K.K. Kuachiliwa
kwa Yehoakimu toka gerezani ilichukuliwa katika 2 Wafalme kama tukio la mwisho.
Na hii ilifanyika miaka ya 37th kufungwa kwake (560 K.K.). Kwa hiyo 1 na 2
Wafalme yamkini ilikuwa bado haijaandikwa kabla ya tukio hilo. Inaonekana
kabisa kuwa kurudi kwa mateka toka Babeli
No comments:
Post a Comment