Friday, 12 January 2018

NAFASI YA KAZI YA KUFUNDISHA CHUO CHA BIBLIA

 
UONGOZI WA   Chuo cha Biblia cha Elam Christian Harvest Seminary (ECHASE)   unayofuraha kuwatangazia  Watendakazi na Viongozi wa Kanisa Nafasi za kujitolea kufundisha  katika chuo hiki.Tunaamini kuwa  Wako watumishi wa Mungu  nchini wenye  elimu ya Huduma   na Theolojia wanaoweza kufundisha watumishi wengine.
Elam Christian Harvest Seminary ni Taasisi ya Kikristo  inayofanya kazi na madhehebu yote katika kuwaanda watendakazi na Viongozi wa Kanisa  kwaajili ya Mavuno ya nyakati za mwisho.
Tunaamini kuwa Watendakazi wanapaswa kuandaliwa katika uwanja wa Mavuno, kama alivyofanya Bwana wetu Yesu Kristo katika kuwaandaa wanafunzi wake kwaajili ya kazi ya Mavuno
Tunakusudia kuwaandaa watendakzi na viongozi wa Kanisa wengi wenye kujaa maarifa ya Neno la Mungu na Upako wa Roho Mtakatifu kwaajili ya kuingia katika  Mavuno ya Kiroho ili kuondoa changamoto ya uhaba wa watendakazi  kama alivyosema Bwana Wetu Yesu Kristo kwamba “Mavuno ni Mengi lakini Watendakazi ni Wachache (Luka 10:2)
Tunakusudia kuanzisha  Vituo vya mafunzo katika  Maeneo mbalimbali katika mikoa na wilaya  Nchini Tanzania. Vituo hivyo vitaendesha Mafunzo ya wiki  moja hadi wiki  mbili kwa   mwezi. Hivyo tunahitaji kuwa na Wakufunzi wengi  ili kuweza kutimiza mkakati huu.
Biblia inasema  katika 2Timotheo 2:2
  Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine
Tunatoa  ombi  la kujitolea kufundisha   katika vituo  hivi  vitakavyoanzishwa   katika Maeneo mbalimbali nchini.



SIFA ZINAZOTAKIWA.
           Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa  zifuatazo:-
1.     Awe amezaliwa mara ya pili (awe ameokoka)
2.     Awe na Huduma mojawapo ya zile huduma tano za Uongozi (Mtume,Nabii,Minjilisti, mchungaji au mwalimu)
3.      Mhitimu wa Chuo cha Biblia  katika fani ya Theolojia, Huduma  au uongozi wa Kiroho ngazi ya   Shahada, Stashahada ya Uzamili au Shahada ya Uzamili.
4.     Awe Mshiriki  katika kanisa  la Mahali  Pamoja (a member of a local Church).
5.     Awe anajua kuongea na kuandika vizuri Kiswahili au Kiingereza.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Mtumishi yeyote aliyetayari  kujitolea kufundisha katika  Seminari  hii awasiliane na   uongozi wa Seminari  kwa simu namba 0762532121/0765992774 au kwa barua pepe elamseminary@gmail.com
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 25/
Tangazo hili limetolewa na



Rev.Dr. Erick L Mponzi
MKURUGENZI MKUU