UONGOZI WA Chuo cha Biblia cha Elam Christian Harvest
Seminary (ECHASE) unayofuraha kuwatangazia Watendakazi na Viongozi wa Kanisa Nafasi za
kujitolea kufundisha katika chuo hiki.Tunaamini
kuwa Wako watumishi wa Mungu nchini wenye elimu ya Huduma na Theolojia wanaoweza kufundisha watumishi
wengine.
Elam Christian Harvest
Seminary ni Taasisi ya Kikristo inayofanya kazi na madhehebu yote katika
kuwaanda watendakazi na Viongozi wa Kanisa
kwaajili ya Mavuno ya nyakati za mwisho.
Tunaamini kuwa
Watendakazi wanapaswa kuandaliwa katika uwanja wa Mavuno, kama alivyofanya
Bwana wetu Yesu Kristo katika kuwaandaa wanafunzi wake kwaajili ya kazi ya
Mavuno
Tunakusudia kuwaandaa
watendakzi na viongozi wa Kanisa wengi wenye kujaa maarifa ya Neno la Mungu na
Upako wa Roho Mtakatifu kwaajili ya kuingia katika Mavuno ya Kiroho ili kuondoa changamoto ya
uhaba wa watendakazi kama alivyosema
Bwana Wetu Yesu Kristo kwamba “Mavuno ni Mengi lakini Watendakazi ni Wachache
(Luka 10:2)
Tunakusudia kuanzisha Vituo vya mafunzo katika Maeneo mbalimbali katika mikoa na wilaya Nchini Tanzania. Vituo hivyo vitaendesha
Mafunzo ya wiki moja hadi wiki mbili kwa
mwezi. Hivyo tunahitaji kuwa na Wakufunzi wengi ili kuweza kutimiza mkakati huu.
Biblia inasema katika 2Timotheo 2:2
Na
mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu
waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine
Tunatoa ombi la kujitolea kufundisha katika vituo
hivi vitakavyoanzishwa katika Maeneo mbalimbali nchini.
SIFA ZINAZOTAKIWA.
Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-
1. Awe
amezaliwa mara ya pili (awe ameokoka)
2. Awe
na Huduma mojawapo ya zile huduma tano za Uongozi (Mtume,Nabii,Minjilisti,
mchungaji au mwalimu)
3. Mhitimu wa Chuo cha Biblia katika fani ya Theolojia, Huduma au uongozi wa Kiroho ngazi ya Shahada, Stashahada ya Uzamili au Shahada ya
Uzamili.
4. Awe
Mshiriki katika kanisa la Mahali Pamoja (a member of a local Church).
5. Awe
anajua kuongea na kuandika vizuri Kiswahili au Kiingereza.
Jinsi
ya Kutuma Maombi
Mtumishi yeyote
aliyetayari kujitolea kufundisha
katika Seminari hii awasiliane na uongozi
wa Seminari kwa simu namba 0762532121/0765992774
au kwa barua pepe elamseminary@gmail.com
Mwisho wa kupokea
maombi ni tarehe 25/
Tangazo hili limetolewa
na
Rev.Dr. Erick L Mponzi
MKURUGENZI
MKUU
No comments:
Post a Comment