MODULI YA
KWANZA.
KIPINDI CHA PERGAMO. KANISA LA KIFAHARI.
A.
UTANGULIZI.
KIPINDI:
Toka patano amani la mfalme Kostantino (313 BK) hadi kuanguka kwa dola ya Rumi mnamo mwaka 476 BK.
B.
USHINDI WA
WAKRISTO
Baada
ya miaka miambili ya mateso kanisa liliishinda dola ya Rumi na kupata amani. Mfalme
Deokletiani katika utawala wake aliweka watawala wasaidizi katika majimbo yake kutokana na
ukubwa wa dola ya Rumi. Baba wa Kostantino alikuwa ni mmoja wa watawala
wasaidizi, aliongoza majimbo ya Galia, Uingereza na Hispania, Baada ya kufa kwa
watawala wasaidizi kulitokea na kugombea madaraka baina ya watoto wao.
Baba wa
Kostantino alipofariki Kostantino alitangazwa kuwa mtawala badala ya baba yake,
na hivyo watoto wa watawala wengine waliamua kuanzisha mapigano ili kuuchukua
utawala huo. Miongoni mwa hao waliokuwa na nguvu ni Maksentio, huyu alikuwa ni
mtu aliyeshabkia mauaji ya wakristo. Walianzisha mapigano huko Italia maili
kumi kutoka Rumi mnamo 28.10. 312 BK
Wakiwa katika
eneo la mapigano kabla ya vita kuanza Kostantino aliona alama ya msalaba angani
ukiwa umeandikwa maneno yafuatayo, “Kwa alama hii utashinda”. Kostantino
aliitikiakwa sala na akaifanya alama ya msalaba kuwa nembo ya Jeshi lake na
walipokuwa vitani Kostantino aliwashinda kabisa maadui zake, adui yake mkuu
Maksentio alikufa katika vita hiyo, hivyo Kostantino akawa mshindi.
Kostantino
alitambua kwamba msalaba ilikuwa ni alama ya wakristo na hivyo Mungu wa
wakristo ndio aliyekuwa amemsaidia katika vita hiyo. Mwaka uliofuata Kostantino
alitangaza PATANO LA AMANI na
Wakristo, (Edict of Torelant). Patano hili
lilikomesha mateso juu ya wakristo
katika dola yote ya Rumi. Patano hili lililowaletea amani wakristo katika dola
ya Rumi lilikuwa na matokeo chanya na hasi katika kanisa.
C.
MATOKEO YA TAMKO
LA AMANI
Matokeo ya patano la amani yanaweza kuainishwa katika pande
mbili ambazo ni matokeo mazuri na matokeo mabaya;
I.
MATOKEO MAZURI,
1.
Mateso
juu ya wakristo yalikomeshwa.
2.
Makanisa
yaliyokuwa yamebomolewa wakati wa mateso yalijengwa tena kwa fedha ya serikali.
3.
Maaskofu
na wachungaji walisamehewa kodi.
4.
Watumishi
wa kanisa walianza kufadhiliwa na serikali na hawakutakiwa kuhukumiwa kwa
sheria za kawaida.
5.
Wakristo
waliruhusiwa kujenga makanisa mahali
popote katika dola ya Rumi.
6.
Dhabihu
za kipagani zilikomeshwa.
7.
Kostantino
alijenga makanisa makubwa katika miji ya
Yerusalemu, Bethlehemu na katika
mji wa Kostantinapoli ambapo ndio uliokuwa makao makuu yake mapya.
8.
Kusulubiwa
kwa wahalifu na desturi za kuua watoto wasiotakiwa
zilikomeshwa.
9.
Watumwa
waliachiwa huru.
10. Siku ya jumapili iliwekwa kuwa siku ya mapumziko kwa
watumishi wa serikali.
11.
Alisaidia
kuunda umoja wa kanisa kupitia mikutano mbalimbali aliyoiitisha, mfano mkutano
wa Naikea mwaka 325 BK.
12.
Alikusudia
kuufanya ukristo ukubaliwe na serikali kama dini zingine.
II. MATOKEO
MABAYA.
1.
Ilikuwa
ni fahali kuwa mkristo, hivyo watu wengi walijiunga na ukristo kwa maslahi
binafsi.
2.
Watu
walijiunga na ukristo ili waweze kupata vyeo katika kanisa na serikali.
3.
Maadili
ndani ya kanisa yalianza kumomonyoka.
4.
Mambo
ya kiroho yaliachwa kupewa kipaumbele na badala yake programu mbalimbali
zikapewa kipaumbele.
5.
Sherehe
na tamaduni za kipagani polepole zilihamia kanisa, kwa kubadilishwa jina na
malengo na badhi zilibadilishwa kuwa
sikukuu za kikanisa, mfano
Krismasi.(Kuabudiwa kwa bikira Maria kuliasiliwa kutoka ibada za kipagani za
kuabudu miungu , Zeusi, mungu wa uzuri wa warumi na Diana mungu mwezi).
6.
Katika
jimbo la mashariki serikali ililitawala kanisa mpaka likapoteza nguvu na maisha ya kiroho.
7.
Katika
jimbo la magharibi kanisa lilipata nguvu dhidi ya serikali.
Kostantino
hakutaka kutumia nguvu katika kuwafanya watu kuwa wakristo, alitaka jambo hili lifanyike
taratibu na kwa uchaguzi wa mtu mwenyewe, jambo hili halikufuatwa na watawala waliofuata
baada yake.
Baada
ya utawala wa Kostantino watawala waliofuatia walikuwa wakali mno walipiga
marufuku ibada za kipagani na waabudu dini hizo walihukumiwa kifo na mali zao
zilitaifishwa. Walivunja mahekalu ya kipagani, watawala wakristo kwa kutumia jina la ukristo sasa walitumia njia zilezile mbaya zilizokuwa zimetumia na
serikali kulitesa kanisa kuwatesa wapagani.
D.
AINA MBALIMBALI
ZA MATESO.
· Katika kipindi
cha Efeso kanisa liliteswa na wayahudi.
· Katika kipindi
cha Smirna kanisa liliteswa na dola ya
Rumi.
· Katika kipindi
cha Pergamo ugomvi ulizuka miongoni mwao wenyewe (wakristo).
E.
UZUSHI NA
MAFUNDISHO YA UONGO.
Mafundisho
yasiyokubaliana na mafundisho rasmi ya kanisa yaliitwa uzushi na waamini waliamriwa
na kanisa kutokuyapokea mafundisho hayo.
Kanisa katika historia yake lilitangaza mafundisho fulani
kuwa uzushi kutokana na kutokukubaliwa kwa mafundisho hayo na uongozi wa
kanisa.
Si kila mafundisho waliyoyaita uzushi yalikuwa
mabaya, kwani kile kilichoitwa uzushi kilikubaliwa baadae na kanisa na kile
ambacho kilionekana chema kilikataliwa na kuitwa uzushi baadae. Hoja au mawazo
yale waliyoyaita uzushi baadhi yalikuwa
na mambo mema ndani yake.
Kanisa halikupambana na mateso tu bali pia na
mafundisho ya uongo, sawsawa na unabii uliotolewa na mtume Paulo katika Matendo
ya mitume 20:29-30.
· MAKUNDI YA UZUSHI.
1.
UYAHUDISHAJI.
Hili lilikuwa ni
kundi la wakristo wa kiyahudi lililojitokeza wakati kanisa linapanuka katika miji
ya wamataifa. Wayahudishaji hawa
walifundisha kwamba wakristo wote walitakiwa kuzifuata sheria za Musa na
mapokeo ya dini ya kiyahudi. Waliyakataa maandiko ya mtume Paulo kwa sababu
yalipinga mafundisho yao. Kundi hili lilitoweka katika karne ya pili BK.
2.
UNOSTIKI
Kundi hili waliamini kwamba Baada ya ngazi ya Mungu
mkuu kulikuwa na miungu wengine wengi ambao
baadhi wakiwa wema na wengine waovu. Unosti ulikuwa na elementi za falsafa
za kiyunani na dini za kipagani.
Unostiki ilikuwa
ni falsafa iliyojaribu kutumia imani ya ukristo katika kuthibitisha ukweli
wake. Hivyo kanisa lilipinga vikali mno
unosti likikana kwamba imani yake si falsafa na wokovu hautegemei falsafa na mafumbo bali ufunuo wa Yesu kristo.
Wanostiki walipunguza
thamani ya maisha na huduma ya Yesu Kristo. Habari nzima juu ya maisha na
huduma ya Yesu ilielezwa kwa njia ya mafumbo (allegory). Unostiki ulizuka katika
karne ya pili baada ya Kristo na ulishamiri katika karne ya tatu na ya nne.
Unostiki hata sasa unajidhihirisha katika karne hii
ya ishirini na moja katika dini
mbalimbali hapa ulimwenguni. Hususani kupitia falsafa
ya mpango mpya wa dunia (New World order
Philosophy)
v
MAFUNDISHO YA
UNOSTIKI.
1.
Maarifa
ya pekee hufunuliwa kwa watu wachache tu.
2.
Wokovu
si kwa watu wote, ni kwa watu wachachetu wenye kuyaelewa maarifa yanayofunuliwa.
3.
Ulimwengu
huu na vitu vilivyomo ndani yake umeumbwa kwa nguvu isiyo kamili na hii ndio
asili ya maovu yote katika ulimwengu.
4.
Yesu
si mwanadamu, alikuwa na roho tu. Yesu alikuwa ni roho aliyejifanya aonekane
katika umbile la binadamu.
5.
Waliamini
kwamba mmoja wa miungu wadogo alikuwa ndani ya Yesu na ndio aliyekuwa asili ya
uungu wake.
3. MARSION
Huyu alikuwa ni mtoto wa askofu wa Pontus.
Alikuja Rumi yapata mnamo mwaka 138BK. Alipofika Rumi alijulikana kwa haraka sana
kutokana na jinsi alivyojitolea sana katika kanisa kwa mali zake. Pia
mafundisho yake yalimpa umaarufu na kumfanya ajulikane sana. Kutokana na
umaarufu huo Marsion alipata wafuasi wengi. Mafundisho yake hayakukubaliwa na
kanisa hivyo alitangazwa kuwa mzushi na alitengwa na kanisa mnamo mwaka 144 BK.
Marsioni aliunda
chama chake ambacho kiliwaunganisha wafuasi wake wote. Chama chake
hakikuongezeka kwa njia ya kuzaliana kwa sababu ya kukataa mambo ya ndoa.
Waliongezeka kwa njia ya wanachama wapya kujiunga. Marsion alikuwa ni mtu wa kwanza kutunga kanuni ya maandiko.
v MAFUNDISHO YA MARSION
1.
Kwa
kiasi kikubwa mafundisho yake yalifanana na mafundisho ya wanostiki.
2.
Aliweka
sharti la wafuasi wake (wanandoa) kutokutana kimwili na kwamba walitakiwa
kuachana na kuishi maisha ya upweke.
3.
Alikaza
kwamba wokovu ni kwa watu wote. Wokovu hutegemea Injili ya Yesu na si kwa kufunuliwa
mafumbo kifalsafa.
4.
Injili
ya upendo wa Mungu inahitaji kusikika zaidi katika kanisa.
5.
Kanisa
limeichafua Injili kwa kuichanganya na mambo ya dini ya kiyahudi.
6.
Mungu wa Agano
la kale ni tofauti na baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Kwa sababu
Mungu wa agano la kale alifurahia dhabihu za damu.
7.
Mungu
aliyeumba ulimwengu na watu wake ni Mungu mwovu, Mungu mwingine mwema
alijificha hadi wakati wa Yesu Kristo.
4. UMONTANO.
Kilikuwa
ni kikundi kilichoanzishwa na mtu mmoja aliyeitwa Montano mwenyeji wa Frigia. Wafuasi
wa kikundi hiki waliitwa wamontano.
Kikundi hiki kilienea sana kuanzia
mwishoni mwa karne ya pili na kuendelea kwa karne mbili zaidi.
Wakati wa
ubatizo wake Montano alinena kwa lugha nyingine na kutabiri na hivyo akajiita
kuwa ni kinywa cha Roho Mtakatifu aliyetabiriwa na Yohana. Alikuwa na wasaidizi
wawaili wanawake ambao nao pia walijitambulisha kuwa ni vyombo pekee vya Roho
Mtakatifu. Karama za kinabii zilijidhihirisha katika mlengo wa umontano.
Kutokana na mikazo yao, Wamontano
walihukumiwa uzushi na kutengwa na kanisa.
v MAMBO MUHIMU YA MONTANO.
1.
Walikaza
kwamba wamefunuliwa juu ya mwisho wa dunia uliokuwa karibu sana kutokea.
2.
Baadhi
ya wafuasi wa umontano walikataa kulima kwa sababu Yesu angekuja kabla ya msimu
wa mavuno.
3.
Baadhi
walikataa ndoa kwa kuwa mwisho wa dunia ulikuwa karibu.
4.
Kiongozi
wao mmoja wa huko Pontus aliwapeleka washirika wake porini kwenda kumlaki Bwana
Yesu wakati anarudi duniani kwa mara ya pili.
5.
Kiongozi
mwingine wa huko Shamu aliwakataza washirika wake wasilime kwa sababu Yesu
angerudi kabla ya msimu wa mavuno.
6.
Alikataa
hali ya kanisa kumezwa na ulimwengu.
7.
Alidai
kuwa kanisa lilikuwa limepoa na hivyo lisitarajie kurudi kwa Yesu.
8.
Walipinga
suala la uaskofu kuchukua mamlaka katika kanisa. Waliweka mkazo katika huduma
ya unabii na ukuhani wa waamini wote.
v
KUMEGEKA KWA
KANISA CHINI YA UONGOZI WA NOVATIANO NA
DONATO.
Katika karne ya tatu na ya nne
kulitokea na kumegeka kwa kanisa. Mmeguko huo uliongozwa na Novatiano katika karne ya tatu na Donato karne ya nne.
Kugawanyika huko kulitokana na kurejeshwa kwa
viongozi na wamini waliokuwa wameikana imani katika kipindi cha mateso.
Pia makundi haya yalijitenga kutokana na kuona wakristo wengi walikuwa wanaishi
maisha machafu kama wapagani waliokuwa wanawazunguka.
v
UASI WA
NOVATIANI.
Katika karne y
tatu askofu wa Rumi aliyeitwa Kalisto alitangaza kwamba dhambi yoyote ili inaweza kusamehewa kiwa mkosaji anaonesha toba ya
kweli.Fundisho hili lilienea sana. Wakristo waliokuwa wameikana imani yao
wakati wa mateso walitaka kurudi kanisani na askofu Kalisto alikubali kuwapokea
watu hao.
Kiongozi mmoja wa kanisa aliyeitwa
Novatiani, hakukubaliana na jambo hilo na alilipinga vikali na akaungwa mkono na
wachungaji wengine ambao nao walikuwa kinyume na maamuzi hayo ya askofu. Walijitenga
na kanisa na
kuanzisha ushirika wao. Novatiani
alichaguliwa kuwa kiongozi wao.
v UASI WA DONATO.
Mmeguko wa kanisa chini ya uongozi wa Donato
ulitokea Afrika ya kaskazini karne ya nne baada ya utawala wa mfalme
Deokletiani. Mfalme huyu katika kipindi cha utawala wake alikuwa na mpango wa
kufuta ukristo na kuchoma moto Biblia zote. Wakati wakipindi cha mateso makali baadhi ya viongozi wa kanisa
waliasi imani wakaamua kutoa maandiko matakatifu (Biblia) yateketezwe ili
kujinusuru na kifo.
Baada ya kipindi cha mateso kumalizika
viongozi hao yaani wachungaji na maaskofu walioasi walitaka kurudi kanisani.
Kanisa katoliki lilikuwa limekubali
kuwapokea. Kanisa lilikubali kuwarudishaviongozi hao katika sharika zao. Katika mji wa Karthegi waamini wengi sana
walikataa kuongozwa na mtu aliye mkana Yesu na kutoa Biblia kwa serikali
ili ziteketezwe.
Donatusi alikuwa kiongozi wa mgomo huo
na alipata wafuasi wengi. Watu hao walijitenga na kanisa na kuanzisha huduma
yao. Kulikuwa na ugomvi kati ya wakatoliki na wadonato kwa kwa muda mrefu.
F.
UMOJA NA UTAWALA
WA KANISA.
Kanisa lililazimka kuwa na umoja kamili
ili liweze kuwa na nguvu ya kukabiliana na mateso yaliyoliandama na uzushi
uliokuwa unajitokeza. Hivyo kanisa lilipambana na maadui wakubwa wawili ambao
ni mateso na mafundisho potofu.
Kutokana na uzushi kutokea, kanisa ilibidi liwe na utambulisho au jina litakalowa tofautisha na makundi ya uzushi, hivyo kanisa lilianza
kijiita Katoliki.
Jina katoliki linatokana na neno la
kiingereza universal, lenye maana “ya popote au ya mahali popote” Kanisa lilianza kutumia jina Katholiki kwa maana
mbili, ambazo ni:
1.
Kanisa
lisilo na mipaka ya majimbo au ya nchi.Kanisa moja lililo katika nchi zote ulimwenguni.
2.
Kanisa
leye mafundisho sahihi.
v
SAABU ZA KANISA
KUHITAJI UTAWALA WENYE NGUVU.
1.
Kutokea
kwa ukiri wa imani.
2.
Kutokea
kwa Kanuni Ya Maandiko Matakatifu.
3.
Kutokea
kwa maaskofu waliopewa mamlaka ya kutunza mafundisho yaliyotokana na mitume wa
kwanza.
v
Ukiri Wa Imani.
Huu
ulikuwa ni ushuhuda mfupi uliotumiwa katika kazi za kawaida sharikani kama vile
ubatizo. Ukiri wa imani ulieleza kwa kifupi kile kanisa linachoamini naa
ulitumika kama kiapo kuwa mtu anakubaliana na taratibu za kanisa hilo hivyo
anastaili kubatizwa na kupokelewa katika kanisa.
v
Kanuni Ya
Maandiko Matakatifu.
Kanuni
ni kwaida inayotumiwa kupima usawa na usahihi wa kitu. Kanuni huelezea vitabu vilivyokubaliwa kupokelewa na kanisa kama
maandiko Matakatifu. Kanisa liliweka kanuni ili kubainisha kati ya vitabu
vilivyokuwa ni neno la Mungu na vile visivyokuwa Neno la Mungu. Mfano wa vitabu
visivyokuwa neno la Mungu ni vile vilivyoandikwa na wanosti.
Makundi
ya uzushi kama vile wanostika na Marsion waliharakisha kutungwa kwa kanuni hii.
Mababa wa kanisa walitumia
kanuni mbalimbali katika kuvibaini vitabu hivyo. Baadhi ya njia hizo ni
kumtambua mwandishi kama alikuwa ni mtume au la, Kupokelewa kwa kitabu na watu walionadikwa kwa mara ya kwanza na
matumizi ya kitabu hicho katika makanisa mbalimbali na mamlaka ya kitabu
chenyewe N.k
v
Haja Ya Kutokea
Kwa Viongozi Wenye Mamlaka.
Maaskofu walitokea kama watu wenye
mamlaka ya kutafasili maandiko na kufundisha wazi mafundisho ya mitume. Neno
askofu maana yake ni mwangalizi/msimamizi. Neno hili hapo awali lilitumiwa na
watu wote na kulikuwa na maaskofu katika idara mbalimbali za serikali, baadae matumizi
ya istilahi hii yalibakia katika Kanisa tu.
Uaskofu
ulisaidia kuleta utawala wenye nguvu na
umoja katika kanisa kupitia mambo mawili ambayo ni mafuatano ya mitume na ibada.
·
Mafuatano Ya
Mitume
Ilidaiwa
kwamba maaskofu walikuwa badala ya mitume.
Kwa namna fulani uaskofu ulitokana na mitume, yaani maaskofu waliwekwa
na mitume kuwa watawala katika kanisa na mamlaka ya utawala wao ilihusisha
kuhubiri na kuitetea Injili.
·
Umoja Wa Ibada
Ibada
mbalimbali zilizokuwa zikifanywa na kanisa kwa pamoja zilisaidia kukuza umoja
wa kanisa na kutokea kwa viongozi wenye mamlaka. Kulikuwa na ibada mbalimbali
ambazo zilifanywa na kanisa, baadhi ya ibada hizo ni ibada ya ubatizo na ibada ya
meza ya Bwana. Pia kanisa liliadhimisha sikukuu mbalimbali ambazo pia kwa namna fulani zilichangia kukuza
umoja wa kanisa.
G.
MABISHANO YA
KITHIOLOJIA.
Mabishano
ya kithiolojia yalisababishwa na mitazamo mbalimbali ambayo wakristo walikuwa
nayo juu ya Yesu Kristo. Baadhi ya mitazamo hiyo ni .
v
Uungu wa Yesu
Kristo.
Wakristo
wa awali walimpa Yesu heshima kwa kumwita majina mbalimbali kama vile
Masihi, Kurios, Kritos na Logos.
Jina
la Logosi lilitokana na falsafa za kigiriki, Kutokana na falsafa hizo Logos
ilikuwa ni njia ya Mungu kufanyika mwili na kukaa na watu hapa duniani. Hivyo wakristo
wa awali walimtambua Yeus kama Mungu.
v
Kristo kama
Logosi.
Katika
kipindi cha karne ya pili na ya tatu karibu wanazuoni wote wa kikiristo
walifundisha kwamba Kristo alikuwa ni Logos.
Kulikuwa na mwanazuoni moja aliye itwa Yustini Shahidi ambae aliweka mkazo kuwa Logos alikuwa ni Mungu wa pili.
Wanazuoni
wengine waliweka mkazo katika umoja wa
Yesu.Walikubali kwamba Logos
amefanyika kuwa mwili katika Yesu Kristo
lakini alikuwa ni Mungu halisi, Mungu mwana ndiye aliyefanyika mwili, si
Mungu wa pili. Kulingana na mtazamo waYustini ni dhahiri kwamba alikana ubinadamu wa Yesu. Yesu kama Logos alikuwa Kweli Mungu na
mwanadamu kweli.
v
Monarchianism. Dhana
ya Mungu mmoja.
Kulikuwa na wanazuoni wengine waliopinga
mafundisho ya kumhusisha Yesu na Logos kwa sababu jambo hili lilielekea kupinga imani yakuwa Mungu ni mmoja. Wanazuoni hao waliona
kwamba dhana ya utatu wa Mungu ilielekea
kuwa ni uzushi wa kuwa na miumngu
mingi.
Wamonarchianism
waligawanyika katika makundi mawili ambayo ni;
1.
Wamonarchianism
wa kimabadiliko, hawa walikuwa na mtazamo wenye kumwona Yesu kama mwanadamu pekee tu,
ambae hakuwa Mungu aliyefanyika mwili. Kundi hili liliongozwa na Askofu Paulo Samosota wa Antiokia.
2.
Wamonarchianism
wa kimfano. Hawa waliona kuwa hakuna tofauti kati ya baba na mwana. Baba ndiye aliye vaa mwili. Kwa hiyo majina haya baba, mwana na Roho
mtakatifu yalitumika kuonesha kwetu njia au hali tatu Mungu alizotumia
kujidhihirisha. Hivyo hakuna nafsi
tatu bali ni nafsi moja. Kundi hili liliongozwa na Sabelio.
Baada
ya mateso kukoma katika kanisa kulitokea mgogoro mwingine ndani ya kanisa uliohusisha mgongano wa kimafundisho
(doctrinal controversals).
Baadhi
ya viongozi wa kanisa walianza kuibuka na mafundisho yaliyoonekana kuwa mageni
katika kanisa na hivyo walihukumiwa uzushi na kutengwa na kanisa.
Wakristo walitumia
muda mwingi kujadiliana wao kwa wao badala ya kuipeleka Injili mbele. Katika moduli hii tutajadili badhi tu ya
mabishano ya kithiolojia yaliyotokea
ndani ya kanisa.
1. Maabishano Baina
Ya Mchungaji Ario Na Askofu
Alexander.
Ario
alimshutumu askofu wake kuwa alikuwa anaweka mkazo sana juu ya uungu wa Yesu
katika mafundisho yake. Alexander alifundisha kwamba mwana ni wa milele sawa na baba. Ario alipinga fundisho hilo yeye
alidai kwamba baba ni wa milele lakini
mwana alikuwa na mwanzo wake. Kuna kipindi ambapo mwana hakuwapo. Askofu Alexander
aliitisha mkutano wa sinodi huko Iskanderia
ili kujadili suala hilo na hatimae Ario alitangazwa
kuwa mzushi na alitengwa na kanisa.
Ario
aliungana na Askofu Euzebio wa Nikomedia na wakaandika nyaraka mbalimbli ambazo zilitetea fundisho lao
na wakazisambaza maeneo mbalimbali ili ziendelee kusomwa na wakristo
mbalimbali.
v
Mkutano Wa
Naikea.
Baada ya nyarakahizo kusomwa majadiliano miongoni
wa viongozi wa kanisa yalipamba moto na kuleta mgawanyiko ndani ya kanisa.
Mfalme Kostantino hakupendezwa na mgogoro huo ulioleta mgawanyiko miongoni mwa
wakristo hivyo aliwaomba viongozi hao wapatane na iliposhindikana kupatana kwa viongozi hao,
mfalme akitumia nguvu ya dola aliamua kuitisha mkutano wa viongozi wote wa
kanisa toka seheu mbalimbali ili aweze kuwapatanisha. Mkutano huo ulifanyika
mwaka 325BK katika mji wa Naikea na hutambulikana kama mkutano wa kwanza wa
kanisa zima, kwa sababu ulihusisha viongozi mbalimbali toka sehehemu mbalimbali.
Katika
mutano huo Askofu alexender alishinda kwa hoja na hatimae Ario alitangazwa kuwa
mzushi na akatengwa na kanisa. Katika kipindi hki kanisa lilitunga ukiri wa
imani ambao ulipaswa kutumiwa na makanisa yote. Ukiri huo ulikweka mkazo katika
uungu wa Yesu kuwa Yedu ni sawa na baba.
Mkutano wa
Naikea
haukuweza kumaliza majadiliano na badala yake uliyachochea kwani majadiliano
hayo yaliendelea kwa muda wa miaka therathini
na tano baada ya mkutano wa Naikea. Baadhi ya viongozi wa kanisa walitiria
mashaka ukiri wa Naikea kwasababu hawakuuzoea.
v Mkutano Wa Kostantipali
Kutokana
na majadiliano hayo ya muda mrefu na makali
kulikuwepo na haja ya kuitisha mkutano mwingine wa kanisa zima. Mkutano hu
uliitishwa katika mji wa Kostantinopoli mnamo
mwaka wa 381 BK. Katika mkutano huu walifanya marekebisho kidogo ya ukiri wa imani wa Naikea.
Mkutano Wa
Efeso.
Baada
ya Apolinari kuhukumiwa uzushi, kuliendelea mabishano makali katika kanisa. Baadhi ya mabishano hayo yalikuwa baina ya askofu Sirilo wa Iskandelia na askofu Nestori
wa Kostantinopoli.
Sirio
alipinga fundisho la Apolinari Aliona
kwamba uungu na ubinadamu wa Yesu kuwa ni hali mbili zisizo weza kutenganishwa
. Alipokuwa anataka kueleza uungu wa Yesu alianza kwa kumwita bikira Maria ‘Theotokos’ yaani mama wa Mungu.
Askofu
Nestori alibaini uzushi katika maelezo ya Sirilo, yeye alipendekeza Mariamu aitwe mama wa Kristo. Maaskofu hao walishambuliana vikali sana kwa
maandishi. Shauli hilo lilipelekwa kwa askofu wa Rumi ili aweze kutoa uamuzi.
Askofu wa Rumi alimpa ushindi Sirilo na kumtangaza
Nestori kuwa mzushi.Hayo yalifanyika katika mkutano wa tatu wa kanisa
uliofanyika katika mji wa Efeso mnamo mwaka 433 BK.
2. Majadiliano
Ya Apolinari.
Apolinari
alkuwa ni askofu wa Laodikia. Askofu
huyu alijaribu kueleza uhusiano uliopo baina ya hali mbili tofauti
alizo nazo Yesu. Yaani hali ya uungu
na hali ya ubinadamu.
Yeye
alikuwa na mtazamo wa kwamba mwili wa Yesu
ni ubinadamu na akiri na roho yake ni Logosi
aliyefanyika mwili. Katika
kueleza fundisho hilo askofu huyu alikaza
uugu wa Yesu uliokana ubinadamu wake.
Kutokana na fundisho hili Apolinari alitangazwa kuwa mzushi katika mkutano wa Kostantinopali mnamo mwaka
381BK.
3. Mabishano Ya Peregia.
Peregia
alikuwa ni mmonaki, mwingereza aliekuja Afrika Kaskazini kwajili ya kuhubiri
Neno la Mungu katika kanisa la Afrika ya Kaskazini.
Peregia
alifundisha kwamba mtu harithi dhambi toka kwa
Adamu, lakini kila mtu ni lazima afanye uchaguzi yeye mwenyewe.
Peregia alipingwa vikali na Agustino mkuu kwa mafundisho yake. Agustino alifundisha
kwamba Adamu alipotenda dhambi alikiwakilisha kizazi chote cha binadamu na
kwamba mtu hawezi kuokolewa kwa uchaguzi wake mwenyewe, bali ni kwa mapenzi ya Mungu na kwamba neema ya Mungu
haiwezi kukataliwa na wanadamu.
Mafundisho
ya peregia yalipingwa vikali na kanisa na kuonekana ni uzushi. Kanisa
lilikubalia na na ya mafundisho ya Agustino mkuu.
H.
KUZUKA
KWA UMONAKI.
Utawa
au umonaki ulianza katika karne ya tatu BK. Kabla ya kipindi hicho wakristo waliishi katika jamii
na familia. Mara baada ya ukristo kushamiri mambo ya dunia yalianza kuingia
kanisani, baadhi ya wacha Mungu hawakuridhika na hali hiyo hivyo waliamua
kujitenga na kukaa peke yao nje ya mji katika mapango au katika nyumba
walizokuwa wamejijengea. Nyumba hizo zilijulikana kama nyumba za watawa maarufu
kama Monastery.
Baadhi ya mambo yaliyochochea kuanzishwa kwa
utawa ni mvuto wa Injili, maovu kukithirikatika kanisa na falsafa ya uovu wa mwili. Kulikuwa na
watu ambao waliuza kila kitu walichokuwa nacho wakawagawia maskini na kisha
wakajitenga na kuamua kuishi maisha ya kimasikini mbali na jamii yao. Baadhi ya watu hao ni;
v Antoni Mtawa Wa Kwanza.
Mtu huyu alikuwa ni mwenyeji wa Misri na ndiye
mwanzilishi wa utawa. Antoni aliuza kila kitu alichokuwa nacho na kuwagawia
maskini mali zake na kisha akaishi nje
ya mji akilima na kuwapatia maskini
chakula alicholima.Baada ya muda alijitenga na
kuishi peke yake pangoni mlimani.
Watu mbalimbali walimwendea huko pangoni ili kujifunza na kisha alifanikiwa
kupata wafuasi ambao nao waliamua kuungana nae kuishi maisha ya utawa. Alipat
wafuasi karibuni elfu mbili.
v Pokomeo Mwanzilishi Wa Nyumba Za Utawa.
Huyu alikuwa mdogo wa Antoni na ndie aliyeanzisha nyumba za utawa. Yeye alijenga boma kubwa ambalo wafuasi wake
waliishi ndani wakijitenga na mambo ya ulimwengu. Watawa hawa walijishughulisha na ibada na kazi,
utawa huu ulikaza ushirika na ulipendwa na watu wengi.
v Faida Za Utawa.
1.
Ulifanyika
kuwa vituo vya wakimbizi.
2.
Walitoa
msaada kwa watu wenye mahitaji , mfano kusaidia maskini na wasiojiweza.
3.
Walileta
mchango mkubwa katika kuinua kilimo.
4.
Walikuza
elimu kwani watawa walitumia muda mwingi katika kusoma na kuandika maandiko
mbalimbali.
5.
Walipeleka
wamishenari katika mataifa mbalimbali kueneza Injili.
6.
Walitoa
viongozi bora katika jamii na katika kanisa.
7.
Walitafsiri
Mandiko katika lugha mbalimbali.
v Madhaifu Ya Utawa.
1.
Mkazo
wa juu ya kuishi maisha ya useja.waliwakataza wafuasi wao wasioe wala kuolewa.
2.
Upendeleo
na anasa. Baada ya utawa kupata umaarufu, walianza kuishi maisha ya anasa na
kukwepa kulipa kodi.
I.
KUKUA KWA DOLA
YA RUMI
Mfalme
Kostantino mara baada ya kuingia katika utawala alihamishia mako makuu ya dola
ya Rumi katika mji wa Kostantinopoli. Tutatazama namna Rumi ilivyokuwa makao makuu ya kanisa.
Wakati kanisa la Orthodox la mashariki lilikuwa likitawaliwa na serikali, Patriaki
wa Rumi alidai kuwa na mamlaka katika
kanisa lote la ulimwengu wa magharibi, ambao ulikuwa kupitia kanisa la Katoliki
la Rumi. Hii iliwezekana kwa sababu
kadhaa, badhi zikiwa ni;
Kufanana
kiutawala.
Kulikuwa na mazoea kuongoza kanisa kwa mfumo wa kiserikali ambapo kunakuwa na
kiongozi mkuu mmoja anaetakiwa kusikilizwa . wakati huu kulikuwa na maaskofu karibu kila
mji, ambao katika miji mikubwa waliitwa Patriaki
(patriarch) yaani baba mkubwa. Kulikuwa na mapatriaki katika miji ya Yerusalemu, Antiokia, Iskanderia, Rumi na Kostantinopali.
Kulikuwa na mashindano ya kugombea ukuu
miongoni mwa mapatriaki. Swali lilikuwa nani angekuwa kiongozi mkuu wa kanisa
lote ulimwenguni. Rumi ikiwa imetengeneza njia ya kuwa makao makuu ya kanisa
ilikuwa na viongozi bora. Kwa muda mrefu kanisa la Rumi lilikuwa imara.
Lilisimama kidete kupinga mafundisho potofu. Kanisa la Rumi liliihudumia Jamii
kiroho na kimwili kwa kuanzisha kazi za kijamii dunia nzima ya wakati ule. Nyumba za utawa, shule na hospitali
zilianzishwa katika maeneo mbalimbali,
jambo hili lililipa umaarufu kanisa la Rumi. Wamishenari walitumwa katika
ulimwengu mzima wa wakati ule kueneza Neno la Mungu.
Wakati nguvu ya kanisa ilikuwa inakua, nguvu
ya dola iliendea kuzolota, nguvu ya kisiasa ya Rumi ilizidi kuporomoka.
Kwa
muda mrefu wa utawala wake dola ya Rumi ilikuwa imetajirika sana. Maadui
zake waliokuwa wanaishi jirani nae waliutamani utajiri wa wake. Maadui hao waliivamia Rumi ambayo sasa haikuwa
na uzoefu wa kivita. Baadhi ya maadui walioivamia Rumi na kuishambulia dola ya Rumi ni wavisigothi, wasaksoni, wavandali,
, wahuni, wabarigandiana na wafaransa.
Uvamizi wa mataifa haya ulipunguza nguvu ya dola ya Rumi.
Janga lingine lilikuwa ni vita ya wenyewe kwa
wenyewe, baina ya wanachama wa seneti . kugombania kiti cha utawala Kabila la
kijerumanilililojulikana kama Herulisi
liliivamia na kuishinda dola ya Rumi mnamo mwaka 476 BK.
MODUI
YA PILI.
KIPINDI
CHA THIATIRA; KANISA LA NYAKATI ZA GIZA.
KIPINDI.
Tangu kuanguka kwa dola ya Rumi hadi kuanguka kwa Kostantinopoli.
A.
UTANGULIZI
Katika kipindi
cha Pergamo tuliona jinsi Patriaki wa Rumi alivyochukua mamlaka ya uongozi wa kanisa na kuinuka kwa
Rumi kuwa makao makuu ya kanisa. Tuliona jinsi mafundisho potofu pamoja mambo ya kipagani yalivyoingia
kanisani
Haikutoshga kwa
Patriaki wa Rumi kuwa Askofu mkuu wa kanisa lote duniani na kuwa na mji wa Rumi
kama makao makuu ya kanisa lote duniani, baada ya hapo alijitangaza kuwa
kiongozi wa mataifa kwa njia ya kukuza
upapa katika karne kumi za kipindi cha giza. Kipindi
cha giza kilikuwa na hatua tatu ambazo ni, kukua, kusitawi na kuanguka.
1.
Kukua.
Gregori
I alipokuwa kijana aliteuliwa kuwa msimamizi wa majengo na vyakula katika Mji wa Rumi. Baada ya kifo cha baba yakeAliamua
kutoa kwa kanisa mirathi ya babaye. Mnamo mwaka 578 BK Gregori I aliteuliwa na papa
kuwa balozi wake katika mji wa Kostantinopoli. Mwaka 585 hadi 590 BK alikuwa msaidizi wa papa huko Rumi na kiongozi
mkuu wa Monastery. Baada ya papa Pelegio II kufariki dunia kwa ugonjwa wa tauni
mwaka 590 BK, Grogori I aliteuliwa na umati
wa watu huko Rumi kuwa Askofu badala ya Peregio II.
Kukua kwa nguvu ya upapa kulianza baada ya Gregori
I kushika wadhifa wa upapa katika
mwaka wa 590 BK. Mfumo wa kubadilisha
majina mtu alipokuwa anaingia katika nafasi ya upapa ulianza katika kipindi
hiki. Gregori aliitwa mkuu kwa sababu ya mafanikio yake ambayo baadhi ni,
1.
Alitumia
uwezo wa kikanisa katika kuwasaidia
watu, (kuwapa chakula na nguo).
2.
Serikali
ilipolega aliimarisha ulinzi katika mji wa Rumi.
3.
Alimtambua
papa wa Rumi kuwa na mamlaka juu ya
viongozi wengine wote wa kanisa.
4.
Alilipatia
kanisa nguvu ya kisiasa na kidini.
5.
Alitengeneza
dogma ya kanisa.
Kutokana
na misaada ya kijamii aliyokuwa
anaitoa papa Grogori I, wanachi wa Rumi
walianza kumheshimu na kumhesabu kama
kiongozi wao. Hivyo basi Gregori Mkuu aliimarisha nguvu ya upapa katika mambo
ya kidini na kisiasa pia.
v Sababu za kukua kwa upapa
Mbali na mchango wa Gregori Mkuu katika kukuza
nguvu ya upapa kulikuwa mambo mengine kadhaa yaliyopelekea kukua kwa upapa
katika kipindi hiki. Baadhi ya sababu hizo ni:
1.Nguvu ya haki, kanisa liliwatetea raia dhidi ya watawala
dharimu hivyo likapendwa na watu.
Kuzolota kwa
serikali,
Wakati serikali inazolota kanisa lilizidi kujiimarisha, kiuchumi na kijeshi
hivyo viongozi dhaifu walihitaji msaada wa kanisa katika kupambana na adui zao hivyo kanisa likazidi kuwa na mamlaka
na nguvu ya ushawishi.
2.
Ulaghai, Kanisa
lilitumia kigezo cha ujinga wa watu
kujipatia mamlaka. Kanisa lilitengeneza nyaraka mbalimbali zenye kulipa
mamlaka ya kiutawala na kudai kwamba ziliandikwa na wahusika walioandikwa kumbe
sivyo. Zifuatazo ni baadhi ya nyaraka hiz
v Waraka wa mfalme Kostantiono kwa askofu
Silvesta (314-335 BK). Huu ulikuwa ni waraka uliogushiwa na kanisa kwamba uliandikwa
na Kostantino kumpa mamlaka ya kiutawala
askofu wa Rumi (Silvesta) juu ya wafalme wote wa Ulaya na Ulaya nzima.
v Tamko la uongo la Isodore(850 BK).
Kulikuwa na maandiko yaliyokuwa yanadai kwamba askofu wa Rumi alikuwa amepokea
waraka toka kwa mitume uliokuwa
unamtangaza asofu wa rumi kuwa askofu wa kanisa dunia nzima na kwamba
kanisa lilitangazwa kuwa huru (yaani kanisa kutokuwa chini ya serikali).
2
KUSITAWI KWA
UPAPA (1073- 1216 )
Nguvu
ya upapa ilifikia kilele chake katika utawala wa Gegori VII ambaye pia alijulikana kama Hildebrand. Katika kipindi hiki upapa ulikuwa na nguvu kamili kikanisa na kiserikali katika mataifa yote ya
kule Ulaya.
1.
Papa
Gregori VII alifanya matengenezo ya ukreli na kukataza ndoa kwa wakreli.
2.
Aliliondoa
kanisa chini ya utawala wa serikali, kanisa likaanza kujitawala, alifuta suala
la maaskofu kuteuliwa na watawala wa serikali (wafalme).
3.
Alilifanya
kanisa kuwa juu ya selikali.
v
Papa Innocent
Iii (1198
-1216).
Huyu alikuwa ni papa mwingine mwenye nguvu
kubwa. Katika siku yake ya kutawazwa kuwa papa alitoa usemi wenye maneno yafuatayo.
“ Mahalifa wa mtakatifu Petro wako katikati ya Mungu na watu; wadogo kuliko
Mungu lakini wakubwa kuliko watu, wenye
uwezo wa kuwahukumu watu wote lakini wasioweza kuhukumiwa na yeyote”
Katika
barua yake ya kiofisi aliandika “ papa hajapewa mamlaka kwa kanisa pekee bali kwa ulimwengu mzima.
Akiwa na haki ya kuwaondoa na kuwaweka
watawala katika uongozi. Papa innocent III alijitwalia mamlaka ya serikali ya
mji wa Rumi akijifanya yeye mwenyewe
kuwa bwana kwa kuanzisha nchi ndani ya
nchi ijulikanayo kama nchi ya
Vatikani.hivyopapa akawa kiongozi wa kidini na kiserikali.
3
KUANGUKA KWA
UPAPA.
Kuanguka
kwa upapa kulianza wakati wa papa Bonifasi
VIII katika mwaka 1303. Jambo hili
lilisababishwa na kuanza kuibuka kwa roho ya utaifa miongoni mwa nchi
mbalimbali. Jambo hili lilileta mtikisiko dhidi ya Bonifasi VIII. Watu walianza
kuwaheshimu viongozi wa nchi zao kuliko kumheshimu papa. Amri na maagizo
mbalimbali ya papa yalipuuzwa na viongozi wa nchi. Baada ya mfalme wa ufaransa
kukata kutii maagizo ya papa, papa Alianzsha
vita na mfalme wa ufaransa na hatimae Bonifasi
VII akashindwa vita hiyo na kuwekwa kizuizini mpaka mauti ilipomfika.
B.
KUINUKA KWA
UISLAMU
Kanisa lilipata mashambulizi makuu katika
karne ya saba kutoka kwa waislamu. Dini ya Uislamu ilianzishwa na kijana mmoja
aliyeitwa Mohamed. Kijana huyo alizaliwa
mnamo mwaka 570 BK katika mji wa Maka. Alianza kazi yake kama nabii na mwana matengenezo kwa kuanzisha dini yake mnamo mwak 610 BK
katika mji aliozaliwa. Kutokana na kutokukubaliwa na watu wa mji huo aliamua
kuhamia katika mji wa Madina katika mwaka wa 622 BK. Kipindi hicho kinaitwa Hajira. Kalenda
ya Waislamu inaanza wakati huo wa kuhama kwa Mohamed toka Maka kwenda Madina.
Ndani ya kipndi cha miaka miambili waislamu
walikuwa wameisha zishinda sehemu mbalimbali za dunia na kuanzisha dini yao ya
uislamu, Uanzishaji wa dini hiyo ulienda sambamba na uanzishaji wa dola ya
Kiislamu katika maeneo yoyote waliyoyashinda. Baadhi ya maeneo waliyokuwa
wameyashinda na kuanzisha utawala wao ni
nchi za Mashariki ya kati, Afrika ya Kaskazini, Asia ndogo. Mouhamedi na
wafuasi wake walieneza dini yao kwa kutumia upanga, mahali popote watu
walipokataa kuipokea dini hiyo walilazimika kutumia vita na nguvu ya kijeshi.
Maeneo
yoyote waliyofanikiwa kuyateka hatua ya kwanza ilikuwa ni kufuta dini zingine
zote zilizokuwa maeneo hayo na kuwalazimisha raia wote kujiunga na dini hiyo.
Kuinuka
kwa dini ya Uislamu kulichangia katika kuanguk kwa upapa na kuzoofisha nguvu ya
kanisa kwa ujumla. Kwa mfano Afrika kaskazini kanisa lilizoofika na hatimae
likafifia kabisa.
C.
KUTENGANA KWA
KANISA LA KATOLIKI.
Kanisa
la katoliki la mashariki lile la magharibi
yalitengana rasmi mwaka 1054 BK, japokuwa kihuduma yalitengana tangu zamani. Daima kulikuwa na kushindania
madaraka ya kwambani nani aliyekuwa mkuu
kati ya papa wa Rumi na Patriaki wa Kostantinopoli. Hatimae katika mwaka 1054
BK makanisa haya yalitengana ramsi.
v
SABABU
ZA KUTENGANA
Kutofautiana
kimafundisho, Kuhusu asili ya Roho mtakatifu. Kanisa la
magharibi lilidai kwamba Roho mtakatifu alitoka kwa baba na kwa mwana wakati
lile la mashariki lilidai kwamba Roho
mtkatifu alitoka kwa baba pekee.
Ndoa kwa
makuhani. Kanisa la magharibi lilikataza makuhani kuoa wakati la kanisa la
mashariki liliruhusu makuhani kuoa.
Sababu ya kisiasa, Baada ya kuanguka kwa dola ya Rumi mataifa ya magharibi yalitaka kuwa chini ya
Kostantinopoli.
Kuabudu sanamu.Kanisa la
magharibi lilianzisha matumizi ya sanamu katika ibada wakati kanisa la
mashariki lilipinga matimizi ya sanamu.
Kugombea ukuu,
Madai ya kanisa la mashariki
ya kuwa ni kanisa la kitawala.
D.
KUSITAWI
KWA UTAWA.
Mashirika
mbalimbali ya kitawa yalisitawi katika kipindi hiki na yakajitolea kusaidia
jamii katika maeneo mbalimbali. Baadhi ya mashrika hayo ni :
Wabenedectino
walianza mwaka 529 BK
Wasisteri
mwaka 1098.
Wafransiska mwaka 1209.
Wadomeni
mwaka 1215.
Kipindi
cha karne za katikati kulichangia sana katika ustaarabu wa ulimwengu, hasa
katika mambo ya elimu, maandiko, na mambo ya ufundi, katika kipindi hiki
zilijengwa kathedro kubwa . kuna baadhi ya vyuo vikuu vikubwa vilivyojengwa
wakati huu, mfano wa vyuo vikuu hivyo ni Chuo kikuu cha Parisi huko Ufarasnsa, Chuo Kikuu cha Kambridge, Chuo
Kikuu cha Oxford, nacho vyote iwili vikiwa
huko Uingereza. Kuanzishwa kwa vyuo vikuu hivi kulipelekea elimu kukua
na kuleta mtazamo mpya katika jamii kama tutakavyoangalia baadae katika kipindi
kitakachofuata.
E.
WATANGULIZI WA
MATENGENEZO YA KANISA.
Katika
mwaka wa 1229 kanisa la Rumi
lilikataza waumini wa kawaida
wasisiome Biblia isipokuwa makuhani tu. Lugha ya kilatini iliteuliwa kuwa lugha
takatifu na hivyo mtu yeyote asiyejua kilatini alizuiliwa kuhubiri.
1.
PITA
WALDO.
Katika miaka ya 1970 alitokea
mfanya biashara mmoja aliyeitwa Pita waldo mwenyeji wa Loyona Ufaransa. Mtu huyu alipenda
kujua mambo yaliyo katka Biblia lakini hakuweza kwa sababu hakufahamu kilatini
hivyo aliwaajiri mapadri wawili
wamtafsirie Biblia katika lugha ya
kifaransa. Baada ya kusoma neno la Mungu
alivutiwa nalo sana hivyo akauza kila kitu alichokuwa nacho na akala kiapo cha
umaskini, akajitoa kikamilifu kuhubiri neno la Mungu.
Pita
Waldo Alianzisha timu iliyoitwa watu
maskini. walianza kuhubiri, lakni walipingwa na papa. Mwaka 1184 walijitenga na
kanisa kwa sababu hawakukubali kitendo
cha wao kuzuiwa kuhubiri,
Waldo
alipinga baadhi ya mafundisho ya kanisa la Katoliki. Baadhi ya mambo aliyoyapinga
ni mafundisho kuhusu toharani, misa
na kwaajili ya wafu na kumwabudu
Mariamu mama wa Yesu.
Watu
hawa waliamini kwamba kili mtu alitakiwa kuwa na Biblia katika lugha yake ya
asili na ya kwamba Biblia ilitakiwa kuwa mamlaka ya mwisho na iliyokuu katika mambo ya
imnani na maisha. Kanisa lilianzisha mateso dhidi ya wawadeni yaani wafuasi
wa Waldo. Kadili walivyokuwa wanateswa ndivyo walivyokuwa wakiongozeka. Mnamo mwaka 1211 wawadeni themanini walichomwa moto huko Ujerumani. Pita waldo alisaidia kuleta matengenezo ya
kanisa kwani alisaidia kupatikana kwa Biblia katika Lugha zingine na
kuhamasisha kila mtu kusoma Biblia. Waldo anajulikan kama mmoja wa
wanamatengezo ya kanisa watangulizi.
2. JOHN WIKRIF.
Huyu
alikuwa mwalimu wa Chuo kikuu cha Oxford. Mnamo mwaka 1378 Wikrif alitaka
kuleta matengenezo katika kanisa kwa kuwaondoa watumishi wa kanisa waliokuwa dharimu,na
kuwanyang’anya mali ambazo aliamini kwamba ndizo zilizokuwa chanzo cha
watumishi hao kuwa dharimu. Alichapisha
andiko lililoeleza maadili wanayotakiwa kuwa nayo watumishi wa kanisa.
Alifundisha
kwamba
wakati viongozi wa kanisa wanapokuwa mafisadi serikali ilitakiwa kuchukua mali
zao na kuwapa watu wengine wenye nia ya kumtumikia Mungu. Katika mwaka
wa 1379 alianza kupinga dogma ya kanisa
kwa kutoa madai yafuatayo;
Ø Yesu pekee ndiye
aliyekuwa kiongozi mkuu wa kanisa na si papa.
Ø Biblia pekee
ndio yenye mamlakua kuu na ya mwisho kwa waamini na si kanisa wala papa.
Ø Kanisa
lilitakiwa kuiga mfano wa kanisa la
agano jipya.
Ø
John
Wikrif kwa msada wa tajiri Lord Cobham
alitafsiri Biblia katika lughaya
kiingereza na kuisambaza katika maeneo mbalimbali . Alianzisha chama cha Wahubiri maskini na wakaanza kuzunguka katikia
maeneo mbalimbali ya nchi hiyo wakihubiri watu neno la Mungu.
Mwaka
1382 alipinga fundisho la mageuzo ya
maumboya mwili na damu ya Yesu
linalojulikana kama transubstan-tiation. Mawazo yake yalipingwa vikali na kanisa na serikali na akafukuzwa ukufunzi.
Mwaka 1402 Bunge La Uingereza lilipitisha sheria ya hukumu ya kifo kwa watu wanohubiri mafundisho kinyume na yale
yaliyokubaliwa na kanisa. Wahubiri maskini waliteswa vikali sana, baadhi
walifungwa nakuchomwa moto na kufukuzwa nchini. Viongozi wa kanisa walijaribu
kuchoma moto Biblia zote za Kiingereza.
Wikrif alifarikia mnamo mwaka 1384.
Shujaa huyu anakumbukwa sana katika historia ya kanisa
kwa mchango wake wa kutafsiri Biblia katika Lugha ya kiingereza. Wikrif ndiye mtu
wa kwanza kutafsiri Biblia kwa lugha ya kingereza.
3. JOHN HUS
Huyu
alikuwa ni mkuu wa chuo kikuu cha Plague huko Bohemia, mtawa na padre wa kanisa la la Rumi la katoliki.
Mwaka 1401 John Hus alipata upadrisho.
Padri huyu alipendezwa na maandiko ya John Wikrif na hivyo alianza
kuhubiri mafundisho ya mtangulizi wake
Wikrif.
Alipinga
mafundisho mbalimbali yasiyo ya kiBiblia
ya kanisa la Romani katoliki na akasisitiza watu kuishi maisha matakatifu. Alisisitiza
kwamba Biblia ndiyo mamlaka ya mwisho
kwa mwamini na katika huduma za kanisa.
Katika kitabu
chake alichoandika juu ya kanisa, alifasili kwamba kanisa ni mwili wa Kristo, na Yesu Kristo pekee akiwa kiongozi wake mkuu.
Alitetea nafasi ya ukuhani na kudai kwamba Mungu
pekee ndiye aliyekuwa na uwezo wa kusamehe dhambi. Alieleza kwamba
hakuna mamlaka ya kanisa inayoruhusiwa kuanzisha mafundisho (doctrine) yaliyo
kinyume na Biblia na kwamba Waamini
hawatakiwi kutii maagizo yasiyo ya
kimaandiko.
John Hus
Alipinga mambo yafuatayo, udharimu
wa mapadri, kuuzwa kwa vyeti vya msamaha, kuondolewa
kikombe cha divai kwa walei. Baada ya mashambulizi hao mazito dhidi ya
mafundisho ya kanisa Hus alifukuzwa
upadri na akaambiwa abadilishe msimamo
wake kwa kufuta kauli, jambo ambalo Hus hakukubaliana nalo. Hatimae Hus
alihukumiwa kifo na akachomwa moto. Hus
akiwa anachomwa moto alitoa unabii kwa
kusema “leo mnaniua mimi lakini miaka miamoja ijayo Mungu atamwinua mtu
mwingine ambaye matengenezo yake hayaatweza
kuzimwa” Kweli baada ya kipindi hicho Mungu alimwinua Martini
Luther mwana matengenezo mkuu kama tutakavyoona hapo baadae.
4. JEROME SAVANAROLA.
Alizaliwa
Ferrara Italia mnamo mwaka 1452, alikuwa ni mtawa wa shiriki la wadominiko.Alijaribu kuleta matengenezo
katika kanisa na serikali. Alipinga uovu uliokuwa unafanywa na mapapa. Alisomea mambo ya ubinadamu na utabibu. Kufikia mwaka 1491
alikuwa mhubiri maarufu kule Frolence.
Alitabiri kwamba
papa na mfalme wa Naples wangekufa siku
moja, jambo ambalo lilitokea kama
alivyotabiri. Katika mahubiri yake alitabiri hukumu kubwa ambayo ingekuja juu ya mji ikifuatiwa na kipindi chema ambapo Frolence ingewaunganisha watu wote
wa Itali. Utimilizo wa unabii huu ulionekana kuwa ni kuvamiwa kwa Itali na mfalme Charles VIII. Ambaye
mwaka 1494 aliuondoa utawala dhalimu wa
Frolence.
Baada ya kuanzishwa
kwa serikali mpya Saravano alipaata umaarufu sana pale Frolence kupitia
mahubiri yake na alileta mabadiliko mengi katika jamii. Alianzisha matengenezo
ya kodi, Kusaidia maskini na
matengenezo katika mahakama.
Aliubadilisha mji kutoka katika maisha
ya kimwili na kuishi maisha ya kiroho.
Kutokana na
mabadiliko hayo kila mtu katika mji alikwenda kanisani na matajiri waliwapa
misaada masikini.Wafanya biashara walirudisha vitu walivyokuwa wamewatapeli
wateja wao. Waimbaji waliacha kuimba nyimbo za kidunia na kuanza kuimba nyimbo za
kumsifu Mungu. Waliachana na maisha
maovu, walichoma moto mawigi, vinyago, vitabu vya kipagani, picha za ngono na kila kitu walichodhani kuwa
ni kiovu. Hakika uamsho mkuu ulitokea kama alivyokuwa ametabiri.
Jerome alitabiri
kwamba angehubiri kwa miaka nane tu pale Florence na kisha angeuawa. Katika mwaka 1498 Jerome alimshutumu papa Alexander VI kwa kutangaza
hadharani maovu aliyokuwa anayafanya yeye na wasaidizi wake. Baada ya mkasa huo
Alexander VI aliamua kumwekea vikwazo na
kisha baadaye akamnyonga na kuuchoma moto mwili wake mnamo mwaka huohuo wa 1498. Maneno yake ya mwisho akiwa anauawa
alisema “ Bwana Aliteseka sana kwaajili yangu”. Mapambano yake dhidi ya
papa yalimfanya kuwa shujaa na kuwa
mtangulizi wa matengenezo ya kanisa. Alikuwa tayari kuitetea imani kwa gharama yoyote.
Wanamatengenzo
watangulizi walionyesha ushujaa katika kuitetea imani. Hawakukubali kusalimu
amri kwa uongozi wa kanisa au serikali na hawakuwa tayari kunyamaza kimya na
kuacha hali mbaya kuendelea kulitafuna kanisa, walikubali kulipa gharama katika
kuitetea imani na kupinga uovu. Walitengeneza njia ambayo ilifuatwa na wanamatengenezo wakuu baadae kidogo katika kipindi cha kanisa la Sardi yaani
kanisa la matengezo.
Kuna mengi
ambayo twaweza kujifunza kwa watu hao
kutokana na vile kila mmoja alivyosimamia kusudi lake kwa ujasiri na
imani kuu. Kama tutajifunza na kutetea imani kama wao tunaweza kuleta
matengenezo katika kanisa vuguvugu la wakati huu wa utandawazi.
F.
KUANGUKA KWA KOSTANTINOPALI.
Wanahistoria wengi wana tazama kuanguka
kwa Kostantinopoli kama mpka wa kipindi
cha karne za katikati na nyakati hizi zetu. Waislamu toka Uturuiki waliivamia
Kostaninopoli na kuishinda mnamo mwaka
1453. Hekalu zuri liliojengwa na mfalme Kostantino lililojulikana kama Saint Sophia liligeuzwa na kuwa
msikiti. Huu ndio uliokuwa mwisho wa kipindi cha giza au mediaval Period.
MODULI YA TATU.
KIPINDI CHA
SARDI KANISA LA MATENGENEZO
KIPINDI
: Tangu kuanguka kwa Kostantinopoli hadi
Patano la Amani la Westpharia.
A. SABABU ZA KUZUKA KWA MATENGENEZO YA KANISA.
Kitendo
cha Kanisa la Rumi kutokuwa tayari kupokea mabadiliko yaliyokuwa yanapendekezwa na
watu wema kama vile, Wikrif na Hus, viongozi wa baraza la matengenezo na
mengine mengi kulipeleka kuanza kwa
nguvu wimbi kubwa la matengenezo.
Hadi
kufikia miaka 1500 misingi wa jamii ya kipindi cha giza ilikuwa inabadilika kutokana na mabadiliko ya kielimu, kisiasa na kidini, kiuchumi. Kanisa
la ulimwengu lilianza kupoteza
nguvu na kanisa la kitaifa
likaanza kuchukua nafasi
Kupanuka
kijiografia kulileta mabadiliko mengi
katika kufiiri. Kwa kifupi kulikuwa na sababu mbalimbali zlizopelekea wimbi la
matengenezo ya kanisa kutokea, baadhi ya
sababu hizo ni;
1.
Kukua kwa utaifa(nationalism).
Kila
nchi ilianza kuweka mkazo kujijenga yenyewe, hivyo nchi mbalimbali zilianza
kujitenga na ushirikiano wa kimataifa, Hii ilipelekea kanisa la ulimwengu kokosa
nguvu kwani utaifa ulisababisha kuanza kwa kanisa la kitaifa kila mahali.
2.
Kuvumbuliwa kwa
mashine za uchapishaji.
Johann
Guthenberg alivumbua mashine ya uchapaji
mwaka 1456. Mpaka wakati huu vitabu vyote viliandkwa na kunakiliwa kwa
mkono. Kuvumbuliwa kwa mashine hii
kulisababisha Biblia na maandiko mengine
kuchapwa na kusambazwa katika maeneo mbalimbali. Kusambazwa kwa maandiko haayo
kulipeleka kuamsha akiri za watu na kutambua hitaji la kuwepo kwa mabadiliko
katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kanisa.
3.
Kuzuka kwa
mwamko wa kujifunza.
(Renaissence)
Hiki kilikuwa ni
kipindi ambacho ulizuka mwamko mkubwa
wa kujifunza . Kipindi hiki kilianza huko
Ulaya Italia karne ya 14 na kuendelea
hadi karne ya 17. Wasomi wengi waliibuka
katika kipindi hiki. Watu walianza kufikiri mambo kwa upya kutokana na elimu
waliyokuwa wamepata. Kutokana na elimu hiyo watu walihitaji mabadiliko katika
maeneo mbalimbali ili kuweza kuleta maendeleo. Hivyo kanisa nalo likajikuta linahitaji
mabadiliko japo kuwa halikuwa tayari kwaajili ya mabadiliko hayo.
B. VIONGOZI WA MATENGENEZO YA KANISA.
Katika
kipengere hiki tutawatalii baadhi ya wana matengenezo ya kanisa, yaani
tutawachunguza watu ambao Mungu aliwasimamisha
kuleta kweli ya neno la Mungu katika kanisa lililokuwa limepotoka na
lisilokubali matengenezo kwa hiali. Tutawatalii wanamatengenezo wafuatao, Martn Luther, John Calvin, Ulrich Zwingli
na John Knox.
1.Martin Luther
No comments:
Post a Comment