Tuesday, 22 October 2019

USAJIRI WA ELAM CHRISTIAN HARVEST SEMINARY


Bwana Yesu apewe sifa.
Chuo cha Biblia cha Elam Christian Harvest Seminary kimekuwa kikitoa mafunzo kwa kushirikiana na Chuo cha Biblia cha Great Commission Bible College tangu kuanzishwa kwake mnano mwaka 2014 mpaka sasa
Chuo hiki kimekuwa kikitoa mafunzo kuanzia ngazi ya Astashahada hadi ngazi ya Shahadada ya uzamivu.
Watu wengi wamekuwa wakiuliza kuhusu usajiri wa  Chuo hiki
Napenda kuwajulisha wanafunzi, wadau wa  Elam Seminary na watu wote kuwa ujumla kuwa  chuo cha Biblia cha Elam Christian Harvest Seminary  ni mwanachama na Kimesajiriwa na Bodi ya  Kimataifa ya Usajiri wa Vyuo vya Biblia na Theolojia iliyoko nchini Marekani Inayojulikana kwa jina la THE ASSOCIATION OF INDEPENDENT CHRISTIAN COLLEGES AND SEMINARIES (AICCS)
Chuo cha Biblia cha Elam   Christian Harvest Seminary kimepewa mamlaka na bodi  kutoa mafunzo kuanzia ngazi ya cheti hadi ngazi ya uzamivu katika fani za Elimu ya Kikristo.
Hivyo  wadau wote na wanafunzi msiwe na shaka Elam  Seminary ni mahali sahihi kwaajili ya yako. Hakika hutajuta kusoma katika chuo hiki.
Ni mimi ndugu katika Kristo Yesu
Rev.Dr. Erick L. Mponzi
MKURUGENZI MKUU
ELAM CHRISTIAN HARVEST SEMINARY

No comments:

Post a Comment