Kanuni ya biblia
Neno kanuni kietimolojia ni neno la kiarabu lenye asili yaya kiebrania lijulikanalo kama keneh .lekiwa na maana ya fimbo nyofu ya kupimia .Katika kigiriki kanon likiwa na maana ileile fimbo nyofu ya kupimia
Maana ya Ki biblia, ni kanuni zinazo tumika kupima vitabu vinavyo stahili kuhesabiwa kama Neno la Mungu
1. Sababu ya kuwa na kanuni ,
2. Zinatusaidia kujua vitabu vinavyostahili kuwa katika Biblia.
3. Zinatusaidia kutambua kati ya kitabu cha kweli na cha uongo .
4. Zinatusaidia kuwa na imani thabiti.
5. Zinatusaidia kutambua mafundisho potofu
1. Aina za vitabu vinavyo paswa kupimwa
2.
3. Vitabu vilivyo katika biblia yetu vya
4. Vitabu vilivyopotea vinavyo tajwa katika agano la kale,
5. Vitabu vya apokrifa
Uingazaji wa vitabu kwenye orodha ya Biblia
Uingizaji wa kitabu kwenye orodha ya biblia ni kitendo ambacho
vitabu vya Biblia hupokea ibali cha mwisho na kupokelewa na viongozi wa
kanisa.Njia nyingi zilitumika katika kutambua vitabu vinavyo stahili
kupokelewana kuingizwa katika orodha ya maandiko matakatifu yaani
Bilbia,Watu wa Mungu walilazimika kutafuta ishara Fulani za ki –Mungu
KANUNI ZILIZOTUMIKA
Mamlaka
ya kitabu; Je kitabu kinadai kuwa ni Neno la Mungu? Kila kitabu katika
Biblia hubeba dai la kuwa na mamlaka ya ki-Munguy.Maneno yafuatayo mara
nyingi yalitumika.kuthibitisha ;Asema Bwana wa majeshi ,Neno la Bwana
lilinijia kusema.Katika vitabu vya historia maonyo humaanisha zaidi na
matangazo ya mamlaka i kuhusu kile Mungu amefanya katika historia ya
watu wake.
Kama mamlaka ya ki Mungu ilikosekana katika kitabu ,hakikufikiliwa kuwekwa kwenye orodha ya maandiko matakatifu na kilkataliwa kuingizwa katika orodha ya maandiko.
Mamlaka ya kiuandashi ; Kitabu kiliandikwa kwa mkono wa mtu gani ? Nabii,Mtume ;au mtu alieagizwa na mungu au mtu alietembea na mitume kwa karibu sana kama Marko na Luka.
Kama
vitabu hivyo havikuandikwa na watu waliotajwa hapo juu ilibidi
vikataliwe. Kutokana na maonyo ya mtume Paulo ilbidi kutopokea kitabu
toka kwa mtu ambae kwa udandanyifu alijiita mtume.(2the 2 :2, 2kor 11 ;13 na 1Yoh 2 ;18-19 ;4 ;1-3) Hivyo ilikuwa ni muhimu kutambuamwandishi wa kitabu.ili kuamua kama kitabu kikubaliwe au kikataliwe.
Uhakika wa kitabu ;je kitabu kina ukweli ?kinasema ukweli kuhusu Mungu,mwanadamu,dhambi ,wokovu .nk.Alama nyingine maalumu ya uvuvio ni ukweli
au uhakika wa kitabu Kitabu chochote chenye makosa ya kukosa ukweli
(kutokana na ufunuo uliopita)kisingevuviwa na Mungu.kwani Mungu hawezi
kusema uongo.mungu na neno lake ni wamoja. Kutokana na kanuni hii
Waberoya waliyapokea mafundisho ya paulo ya Paulo na kuchunguza maandiko
ili kuona kama kile kilichofundishwa na mtume Paulo kilikuwa kweli na kilikubaliana na ufunuo wa Mungu katika Agano la kale au la. (Mdo
17 :11)Kuhitilafiana na ufunuo uliotangulia kungeonesha wazi kwamba
fundisho halikuvuviwa.Sehemu kubwa ya mafundisho ya apokrifa yaliyo
dhaniwa kuwa na uvuvio yalikataliwa kutokana na kanuni hii ya uhakika kitabu.
Asili ya kitabu kuwa na nguvu ;Je kitabu kina nguvu ya Mungu ?kina nguvu inayo weza kubadilihsa maisha
ya mwanadavumu ? Kipimo hiki hakikuwa wazi kama baadhi ya vingine,
kipimo hiki kilihusu uwezo wa kitabu adili maisha ya mtu.
Mana Neno la Mungu li hai tena lina ngu…Ebr 4 :12. kwa sabau hii linaweza kutumika .
….kwa mafundisho,na kwa kuwaonya watu makosa yao na kwa kuwaongoza na
kwa kuwaadibisha katika haki….2Tim 3 ;16-17. Mtume Paulo anathibitisha
kuwa uwezo wa maandiko yaliyovuviwa kubadili maisha ya watu ulihusika
katika kupokelewa kwa maandiko yote.vitabu vingine vilikataliuwa
kutokana na kukosa sifa hii.
Kupokelewa
kwa kitabu ;je kitabu kimepokelewa n kukubaliwaa watu ambao kwanza
kiliandikwa kwaajili yao ?walikitambua kwamba kilitoka kwa Mungu.Chapa
na muhuri wa mwisho wa maandiko yewenye mamlaka ni kukubaliwa
kwake na watu wa Mungu ambao kwanza maandiko hayo yalitolewa kwao.Neno
la Mungu lililotolewa kupitia nabii wake pamoja na ukweli wake lazima
litambuliwe na watu wake walioandikiwa. Katika utaratibu wa kuviingiza
vitabu kwenye orodha mababa wa kanisa walitumia kanuni hii.Kwa sababu
kama kitabu kilipokelewa,kikakusanywa, na kikatumika kama Neno la Mungu
na wale ambao kilitolewa kwao kwanza basi kiliingizwa katika orodha ya
vitabu vya Biblia .
Rev.Dr.Erick L M Mponzi
Mkurugenzi Mkuu
ELAM CHRISTIAN HARVEST SEMINARY
No comments:
Post a Comment