Friday, 30 December 2016

MAOMBI YA KUMALIZA MWAKA 2016 NA KUINGIA MWAKA 2017



https://thumbs.dreamstime.com/t/wood-cross-14796680.jpg        KANISA LA PENTEKOSTE TANZANIA
MLIMA WA     UREJESHO.
MAOMBI YA KUMALIZA MWAKA WA 2016 NA KUINGIA MWAKA WA 2017.
Eee Mungu tunakushukuru kwa rehema zako na upendo wako. Umekuwa mwema sana katika maisha  yetu. Hatujawa wakamilifu vyakutosha mbele zako, Ni kwa neema yako tu Mungu wetu tumefika hapa tulipofika.  Katika mwaka huu wa 2016 Tumekuona ukitulinda, Ukituponya, ukitubarika katika maeneo mbalimbali ya maisha yetu. Hakika wewe ni Ebeneza na Elishadai.
Tuna kila sababu ya kukushukuru baba yetu. Mkono wako umekuwa mwema sana. Tuna kurudishia shukrani, sifa na adhama. Litukuzwe jina lako.
Katika vipindi vigumu tulivyopitia Tuliiona neema yako ikiwa kubwa sana, kutuwezesha kuvuka katika vipindi hivyo. Tulilikumbuka nno lako kama linavyosema katika   katika Yeremia 20:10
Tumekuona ukitimiza ahadi zako kama ulivyosema katika Isaya 54:10
Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa  Asema Bwana akurehemuye
Isaya 55:6
Mtafuteni Bwana, Maadamu anapatikana,
Mwiteni maadamu yu karibu,
Yeremia 23:23
“Mimi ni Mungu aliye karibu, asema.Mimi si Mungu aliye mbali”


1.     Mshukuru Mungu kwaajili ya  wema na fadhili zake alizokutendea mwaka mzima, (shukuru kwaajili ya ulinzi, uponyaji,  uchumi,  n.k) Mwambie  Bwana Asante kwa Yote aliyokutendea katika mwaka wa 2016.
2.     Omba rehema mbele za Mungu katika Maeneo yote ambayo hukwenda kwa ukamilifu mbele zake.
3.     Ombea mwaka 2017 ukawe mwaka wa Baraka na wa  kibali  kwa kila kiumbe. Yeremia 29:9.
4.     Omba Mungu akakutangulie mwenyewe katika kila eneo maishani mwako katika mwaka wa 2017   Kutoka 23:20,      
5.     Omba  Ulinzi wa Mungu ukawe juu yako na familia yako mwaka 2017
6.     Omba wema na Fadhili za Bwana zikawe nawe kwa kiwango cha kupita kawaida katika mwaka 2017
7.     Omba Mungu akainue vipawa na  karama ndani yako katika mwaka huu wa 2017.
8.     Omba Mungu  aachilie upako juu yako.   Matendo ya mitume 1:8
9.     Omba uongozi wa Mungu katika maeneo yote uwe juu yako katika maka 2017.  Isaya 58:11
10.            Omba Mungu akuweke mbali na maonezi ya ufalme wa giza katika mwaka wa 2017 Isaya 54:14
11.            Omba Mungu akupe hazina za gizani na mali  zilizofichwa Isaya 45:3
12.            Omba Mungu akakufundishe mwenyewe mwaka 2017. Isaya 48:17






Karibu Mwaka 2017. Mwaka Wa Kuinuka Na Kusitawi
Isaya 43:18
Asante Mungu kwa kuturidhia kuingia mwaka mpya wa 2017.
Mwaka wa kupokea jambo jipya toka kwako.

By               Rev. Erick L  Mponzi
0762532121





No comments:

Post a Comment