Friday 3 June 2016

elam historia ya kanisa III




MADA    YA    KWANZA.
UTANGULIZI  JUU YA   HISTORIA    YA   KANISA.
A.UTANGULIZI
Somo hili linaanza na kupaa kwa Yesu Mbinguni katika mlima wa mizeituni kama mwaka wa 30 .AD na linaishia na kurudi kwa Yesu mara ya pili ya pili kupitia kwenye mlima wa mizeituni katika kipindi cha mwisho {ufu 19-16-26, Zek 14:1-9}
Waandishi wahistoria ya kanisa hawakubaliani katika namna ya ugawaji wa vipindi vya historia ya kanisa .Baadhi hugawa vipindi kulingana na matukio muhimu kuhusu watu Fulani maalufu, mfano kutawazwa kwa papa wa kwanza mnamo mwaka 590 A.D, au wakati wa matengenezo ya Martini Luther, alipoandika maandiko {Thesis} yake 95 na kuyabandika katika mlango wa kanisa huko Witenberg Ujerumani mwaka 1517 .
Baadhi pia hupenda kugawa vipindi katika historia ya kanisa kulingana na matukio mbalimbali yalioleta athari katika kanisa mfano kuongoka kwa Kiongozi mkuu wa Dora y aRoma Mfalme Kostantino mwaka 313 AD .Au patano la amani la Westphalia mwaka wa 1646.
Pia wataalamu wengine hugawa vipindi vya kanisa kwa kufuata mtindo wa kinabii kwa kuzingatia orodha ya makanisa saba (7) kama yalivyoainishwa katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana sura ya pili nay a tatu.
 Katika somo hili tutagawa vipindi vya historia  ya kanisa kwa kufuata mhutasari wa makanisa saba yanayopatikana katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana Sura ya pili na ya tatu ambapo vipindi mbalimbali vya kanisa vimeorodheshwa kwa njia ya kinabii.
B. DHANA    YA HISTORIA.
Historia kama somo inafafanuliwa kwamba ni somo linalohusu matukio mbalimali katika vipindi mbalimbali vya maendeleo ya mwanadam.
Baadhi ya wataalamu   wanafafanua kwamba historia ni rekodi za shughuliza binadamu katika vipindi viliyopita. Kwahiyo historia huhusika na kuainisha matukio mbalimbali muhimu yaliyotokea katika vipindi mbalimbali katika jamii ya mwanadamu.
C. MAANA YA HISORIA YA KANISA
 Ni taaluma inayoelezea vipindi mbalimbali ambavyo kanisa limepitia tangu kuanzishwa kwake mpaka Yesu kristo atakapokuja kulichukua kwenda mbinguni .

D. SABABU ZA KUJIFUNZA HISTORIA YA KANISA
 Kuna sababu nyingi ambazo zinatufanya tujifunze historia ya kanisa na kuifanya kuwa mojawapo ya somo linalotakiwa kufundishwa katika shule za Biblia na vyuo vya thiolojia .Baadhi ya sababu hizo ni:-
Historia ya kanisa inatusaidia kutambua jinsi kanisa lilivyoanza na jinsi lilivyokabiliana na changamoto mbalimbali.
Inatusaidia kujifunza misimamo ya kiimani ya mababa wa kwanza wa kanisa na kututia moyo sisi kuitetea imani kama wao walivyoitetea.
Inatusaidia kujua changamoto mbalimbali kanisa lilizopitia tangu kuanzishwa kwake mpaka sasa.mfano changamoto ya mateso wakati wa watawala mbalimbali wa Dola ya Rumi waliyowapata kanisa la kwanza, kama vile kusulubiwa kwa mtume Petro, kunyongwa kwa Mtume Paulo, Kuchunwa ngozi na kutumbukizwa kwenye mafuta yanayochemka motoni Mtume Bathromeyo.
Inatusaidia kujua jinsi wakristo waliotutangulia walivyoitetea imani kwa kuwa tayari kufa bila kuisariti imani mfano John Huss Martini Luther, Porykap, Klement Origen, Urlich Zwingri. N.k
D.MAKANISA SABA YA ASIA NDOGO
Mfalme Domitiani alimpeleka mtume Yohana uhamishoni katika kisiwa cha Patmo kwa sababu ya imani. Akiwa katika kisiwa hiki mtume Yohana alipokea jumbe toka kwa Bwana Yesu Kristo kwa ajili ya makanisa saba yaliyokuwa katika Asia ndogo. Jumbe hizo baadae ziliingizwa kwenye orodha   ya kanuni ya Maandiko na sasa ni kitabu cha Ufunuo wa Yohana. Mtume Yohana alipokea jumbe hizi akiwa na umri wa miaka 90.

Jumbe hizi zilikuwa na matuimizi ya aina nne ambayo ni
1. Zilikuwa ni jumbe maaalum kwaaiili ya makanisa   katika wakati wa mwandishi.
2. Zilidhihirisha na kufunua hai ya kiroho ya kila kanisa lililoandikiwa jinsi ilivokuwa . 3. Zilikuwa ni jumbe kwa waamini wote wa zama zote za kanisa.
 4. zilikuwa ni muhtasari wa kinabii wa historia ya kanisa.



F. MUHTASARI WA MPANGILIO WA MAKANISA SABA YA ASIA NDOGO.UFUNUO 1
KANISA
KIPINDI
MUDA
EFESO
KIPINDI CHA MITUME (Kanisa la Mitume)
Tangu kupaa kwa Yesu Kristo Mbinguni mpaka kifo cha Mtume Yohana.
30 .BK- 100 B.K
SMIRNA
KIPINDI CHA MATESO (Kanisa la mateso).
Tangu kuchomwa moto mji wa Rumi mpaka kuongoka kwa mfalme kostantino.
64. B.K – 313 B.K
PEGAMO
KIPINDI CHA KIHARI (Kanisa la Kifahari)

Tangu kuongoka kwa mfalme Kostantino mpaka kuanguka kwa dola ya  Rumi.
313 B.K -476. B.K
TIATHIRA
KIPINDI CHA KIPAPA (Kanisa la Kipapa)
Tangu kuanguka kwa dola ya Rumi mpaka kuanguka kwa Kostantinopali
476. B.K  - 1453 .
SADI
KIPINDI CHA MATENGENEZO (Kanisa la Matengenezo)

Tangu kuanguka kwa Kostantinopali mpaka patano  la Westphalia
1453.- 1648

FILADELFIA
Kipindi cha umisheni au uinjilisti. (KANISA LA UMISHENARI)
Tangu patano la Westphalia mpaka vita ya kwanza ya Dunia.

1648-1914


LAODEKIA
KIPINDI CHA UONGO (kanisa la uongo/vuguvugu)
Tangu vita ya kwanza ya Dunia mpaka kipindi cha Milenia mpya.
1914…









MADA YA PILI
KIPINDI    CHA   EFESO.
{Kanisa la   Mtume}
A. UTANGULIZI.
 Kanisa la   Efeso  Ufu 2:1-7.
MUDA; Tangu kupaa kwa Yesu Kristo kama mwaka 30.AD.Mpaka kifo cha mtume Yohana kama mwaka wa 100.  B.K.

Efeso ulikuwa mji muhimu katika pwani ya Asia ndogo na ulipewa jina la heshima   la Nuru ya Asia. Waefeso waliabudu miungu ya kiasia ambayo ni Artemi, ambae pia aliitwa Diana. Hekalu la artemi lilihesabiwa kuwa  mojawapo ya maajabu ya dunia ya wakati ule.
 Mahali pengine walipoabudia paliitwa  Augusteum. Mahali hapo walitumia kumwabudu mfalme . kiwango cha kiburudani za kidunia zilikuwa nyingi na inakadiriwa kuwa Ukumbi wa Efeso ulikuwa na uwezo wa kuchukua watu 25,000.
Kipindi hiki kinaitwa kipindi cha mitume kwa sababu mitume wote12 wa mwa nakondoo {Yesu} waliishi katika kipndi hiki. Na kipndi hiki kiliishia na kifo cha Mtume Yohana ambae alikufa kifo cha kawaida akiwa mzee mwenye umri wa kama miaka 100.
Tabia za kanisa la Efeso ni muhimu sana katika kipindi hiki . Kuna walimu wa theologia wanaofundisha kwamba mitume na manabii waliishia katika kipindi hiki. Jambo ambalo si kweli kabisa kwani huduma hizi zimekuwepo katika vipindi vyote vya kanisa japokuwa katika vipindi fulani zilififia. Lakini zimekuwepo katika zama zote za kanisa.
 B.ULIMWENGU WA WAKATI WA MITUME
Mitume walipambana na upinzani mara tu kanisa lilipoanza. Upinzani huo ulitokana  na makundi mbalimbali
 . 1. Wayahudi, Wayahudi walikuwa ni adui namba  moja wa kanisa .walilivamia kanisa wakati lingali changa kwa kushirikiana na mfalme wa kirumi walimsulibisha Yesu Kristo.
 a).  Masafarisayo. Hawa walianza katika kipindi cha Ezra na Nehemia . waliporudi toka uhamishoni Babeli. Wakati ukuhani mpya ulipoanzishwa.  Waliamini ufufuo wa wafu, adhabu ya wenye dhambi , kutokufa kwa nafsi,uwepo wa malaika na huduma zao na kwamba kila kitu kinamtegemea Mungu. Mtazamo wao wa kisiasa ulikuwa ni wa kiyahudi. Na
 Waliogopa kushirikiana na watu wasiokuwa mafarisayo. Mfano Wasamaria, na Wamataifa na kwa namna zote walizishika sheria za Musa na walifanya tohara.
 b.Masadukayo, Hawa jina lao lilitoka kwa Sadoki kuhani mkuu wa wakati wa Daudi toka uzao wa Haruni Kuhani Mkuu. Hivyo walikuwa ni uzao wa kikuhani.Wao hawakuamini ufufuo wa wafu wala uwepo wa malaika.
 2. Dora ya Kirumi,. Mwaka 63 mfalme wa Rumi Julius Kaizari aliivamia na kuishinda Parestina na akaanzisha utawala wa kirumi katika nchi ya parestina . Huu ulikuwa ni ufalme wanne uliokuwa umeishinda na kuitawala Israeli kulingana na unabii wa Danieli . Israeli ilikuwa chini ya utawala wa dola ya Rumi Yesu Kristo alipozaliwa na katika kipindi cha maisha yake hapa duniani.
 a. Upagani, hii ilikuwa ni dini ambayo mianzo yake ni mtawala Nimrodi katika mnara wa Babeli na dini hii baadae ilisambaa katika maeneo mbalimbali yaliyoizunguka Babeli mpaka Misri, Ugiriki na Rumi.Waliabudu miungu ya kigeni {Yer 2:25}. Ilikuwa ni miungu ya zamani sana ya Kibabeli, ilikuwa na majina mbalimbali katika nchi mbalimbali, mfano artemi ,Diana, Osiris, Jupita Appos Zeus. N.K
b.Ibada ya mfalme. .Hii ilikuwani moja wapo ya tamaduni za dola ya kirumi. Baadhi ya wafalme wakirumi walijitangaza kwamba wao ni miungu na wakadai kwamba wananchi wao wanatakiwa kuwaabudu.hivyo Ibada ya kuwaadudu wafalme {makaisari} ilianzishwa. Kukataa kumwabudu Kaisari  kungepelekea mtu kuhukumiwa adhabu ya kifo. Ibada ya kumwabudi mfalme ilikuwa imerithiwa toka kipindi cha babeli.
C.Wanafasalsafa wa Kigiriki. Kulizuka falsafa za kigiriki ambazo zilikuwa zinasisitiza kwamba lengo la maisha ni furaha na anasa. Walisisitiza kwamba maarifa yanaweza kupatikana kwa njia ya kufikiri {Logic}.Waliegemea katika vitu vinavyoonekana tu. Falsafa hizi ndizo ambazo zilikuwa zimeshikiliwa  na watu mbalimbali katika kipindi hiki.
Falsafa hizi zilisisitiza kwamba maisha ni kula na kunywa kwa sababu baada ya kufa mwanadamu alikuwa anaoza na kwamba hakukuwa na maisha baada ya kufa.


C. KUANZA KWA KANISA.
 Kanisa lilianza  Yerusalemu siku aliposhuka Roho mtakatifu katika chumba cha juu katika hekalu la Yerusalem. Baada ya Yesu Kristo kupaa Mbinguni wanafunzi walirudi toka mlima wa Mizeituni mpaka hekaluni na kukaa katika chumba cha juu. Waliomba na kusubiri kuvikwa nguvu. Baada ya siku kumi Roho Mtakatifu alishuka na wote waliokuwemo kwenye chumba cha juu walijazwa na Roho Mtakatifu na kuanza kumwazimisha Mungu kwa Lugha zingine. Kazi ya uinjilisti ilianza papo hapo mtume Petro alihubiri na watu 3000 wakaokolewa na kubatizwa. Hii inahesabiwa kwamba ndio mwanzo wa kanisa la agano jipya.
  Sifa za kanisa   la kwanza.
1.                   Lilikuwa na utii kwa sehemu
2.                    Utendaji. Lilikuwa na hali ya utendaji
3.                   Utendaji lilikuwa na utendaji
Matokeo ya kujazwa Roho Mtakaifu    
1.       Kutiwa nuru. Waamini kwa kwanza walitiwa nuru  katika akili na fahamu zao na wakapata kuyaelewa maandiko matakatifu.
2.      Kutiwa nguvu na ujasiri, wamini hawa walitiwa nguvu na ujasiri na na kuwezeshwa Kulihubiri Neno la Mungu kwa ujasiri.
3.        Kutenda ishara na maajabu. Mitume waliwezeshwaq kutenda miujiza sawasawa na ahadi ya Yesu Kristo Mk 16:15-20.

 D.   WANACHAMA KTIK A KANISA.
 Wanachama katika kanisa la mwanzo walikuwa ni wayahudi {proselytes} ambao twaweza kuwagawanya katika makundi manne. ambayo ni ;
1.      Waebrania . hawa walikuwa ni wayahudi ambao baba zao walikaa Palestina na walikuwa ni uzao wac Kiebrani.
2.        Hellenists, walikuwa ni wayahudi waliokuwa wanakaa katika nchi zingine wengi wao walikaa  Uyunani.
3.        Proselytes.Walikuwa ni watu wamataifa waliokuwa wamefanyika kuwa raia wa kiyahudi, walifuata sheria za kiyahudi na walijiunga na dini ya  Kiyahudi. Pia walitahiriwa kama wayahudi. Mfano Nikolasi {Mdo 6:5}
E.  UONGOZI NA UTAWALA WA  KANISA.
Kanisa la kwanza halikuwa na Mfumo wa uongozi wa kiutawala  kama ilivo sasa. Kila kanisa la mahali pamoja lilikuwa na uongozi wake uliojitegemea. Hakukuwa uongozi uliokuwa unasimamia makanisa  yote. Mitume walikuwa ni waangalizi wa kanisa na hawakujiweka kuwa watawala wa kanisa. Bali watumishi wa kanisa.
F. MAFUNDISHO YA KANISA   LA   KWANZA. Mafundisho ya kanisa la kwanza yalikuwa rahisi, Agano jipya lilikua halijaandikwa. Ujumbe wao ulikuwa na maeneo machache ambayo ni ; Uungu wa Yesu Kristo. Yesu kristo wa nazareti ni mwana wa Mungu na ni nafsi hai. Maelezo haya yalisababisha mateso katika kanisa .
 Ufufuo wa Yesu Kristo. Ufufuo wa Yesu kristo ulikuwa ni kiini cha mahubiri au ujumbe wa kanisa la kwanza.
Kurudi kwa Yesu Kristo mara ya pili. Walihubiri kwamba Yesu Kristo atarudi tena {Mdo 3:20-21, 1The 4;15-17}Hili lilikuwa ni tumaini la Baraka kwa waamini wote.

G.  KUSHINDWA KWA KANISA LA KWANZA.
Kanisa la kwanza lilishindwa kufikia kusudi kwa sababu zifuatazo.
Kukosa maono ya umisheni . Mungu aliliagiza kanisa kwenda kuhubiri Injili ulimwenguni kote MT20:28, Mk 16:16} lakini kanisa la kwanza hawakufanya hivyo bali walijihusisha na umisheni katika Yerusalemu tu.
 Kujihusisha na shughuli za kijamii,   Mitume walianza  kujihusisha na mambo ya kijamii {kiutawala} kwani shughuli zote za kanisa za kila siku zilifanywa na wao.Tunaona Petro aliyekuwa mhubiri anaanza kujihusiha na mambo ya kiutwala.
Mitume walifika mahali wakagundua tatizo hilo na wakachagua wahudumu saba waliotakiwa kushughulikia mambo ya kiutawala ili wao wadumu katika kulihubiri Neno na Kuomba.
 Bwana alilionya kanisa lake “Tubu na ukafanye mambo ya kwanza la sivyo nitakiondoa kinara chako mahli pake. Mungu alitimiza Neno lake kama Tutakavyo ona hapo baadae.
H.  KUENEA KWA KANISA LA KWANZA. Kupanuka kwa kanisa tangu mahubiri ya Stefano {mwaka 35. AD} hadi mkutano wa Yerusalemu {mwka 48. AD}.Mambo ya msingi katika kipindi hiki yalikuwa ni upandaji wa makanisa. Kipindi hiki kifupi kilikuwa na umuhimu mkubwa kwa kanisa. Japokuwa kanisa mwanzo lilikuwa Yerusalemu tu sasa lilipandwa katika  maeneo mengine kama vile Siria na Asia ndogo na kuelekea Ulaya.
Waamini wa kwanza walikuwa ni Wayahudi lakini baada ya kipindi hiki kifupi waamini wengi walikuwa ni wamataifa .
 Mwanzoni Injili ilihubiriwa kwa kiebrani na kwa kiaramu lakini baadae iligundulika kwamba ulimwengu mzima ungefikiwa na Injili kupitia lugha ya Kigiriki kwa sababu kigiriki wakati huo kilikuwa ni lugha ya mawasiliano ya kimataifa kama ilivyo kiingereza kwa dunia nzima ya sasa.
I.                    KUTESWA KWA KANISA   NA VIONGOZI WA KIYAHUDI.
 Yesu aliwaagiza mitume kwenda kuhubiri Injili duniani kote lakini wao walipenda kukaa Yerusalemu .Mungu alikasirika na akaamua kuruhusu mateso katika kanisa .{Mdo 9}
1.      Mahubiri ya Stefano{.Mdo 6:1-4, 7} Kwa sababu ya imani yake kwa Neno la Mungu Stefano alihukumiwa kuuawa na kuwa mfia dini wa kwanza katika imani ya kikristo. Kijana mmoja mfalisayo wa tarso Sauli alishuhudia mauaji ya Stefano na Baadae kijana huyo akawa kiongozi mkuu wa mauwaji ya wakristo katika taifa la wayahudi. 
Kutokana na tukio hili waamini wote walikimbia Yerusaelimu isipokuwa mitume {Mdo 8:1-4}.Waamini hao walisambaa maeneo mbalimbali na kila mahali walipokwenda walilihubiri Neno . Kwa njia hii kwa muda mfupi Injili ilipata kuenea kwa haraka katika maeneo yote yaliyoizunguka Yerusalemu.
2.      Kanisa Linakwenda Samaria,{ Mdo 8}.Wasamaria walikuwa ni chotara ambao asili yao ilikuwa ni  Ashuru ambpo walihamishiwa katika eneo la Kaskazini mwa Israeli. Pale waisraeli  walipochukuliwa kwenda utumwani Ashuru {Irani}. Mchanganyiko wa wageni hao na mabaki ya waisraeli ambao hawakwenda utumwani Ashuru yaliunda kabila la Ashuru kutokana na kuoana .Watoto waliozaliwa walikuwa chotara.
Wasamaria Walikuwa na hekalu lao katika mlima Gelzimu na walivitumia vitabu vitano vya Musa pekee kama Biblia yao. Kwahiyo Wayahudi hawakuchangamana nao.
 Roho Mtakatifu alimwambia Shemasi Filipo kwenda kuhubiri Neno Samaria Mungu alimtumia kufanya ishara na maajabu kwa jina la Yesu huko Samaria. Uamsho mkuu ulitokea  huka Samaria. Watu wa huko Samaria waliokoka na kubatizwa .Mitume walipopata habari hii walikuja kuwaombea ujazo wa Roho Mtakatifu.  Baada ya maombi hayo Wasamaria walijazwa Roho mtakatifu.
  Angalizo. Wasamaria waliokolewa na kubatizwa katika maji chini ya huduma ya Filipo, lakini walikuwa bado hawajabatizwa kwa Roho Mtakatifu . Ubatizo wa Roho mtatifu ni upako maalumu ambao kupitia huo tunapokea nguvu toka kwa Mungu.

3.      Injili inakwenda Afrika {Mdo 8 }. Roho mtakatifu alimtuma mwinjilisti Filipo kwenda kumhubiri Neno Towashi wa Kushi {Waziri wa fedha wa Ethiopia}. Filipo alimwongoza towashi huyu kwa Bwana na kasha akambatiza. Inaaminika kwamba towashi huyu alipeleka injili Afrika . Kwa sabau alikuwa ni mkza wa Barala Afrika katika nchi ya Ethiopia

J.   MTESI WA KANISA ABADILI UPANGA {Mdo 9 }
Sauli wa tarso ambae ndiye aliekuwa mtesi mkuu wa kanisa kwa kipindi hiki aliokoka baada ya kukutana na Yesu Kristo alipokuwa safariki kuelekea Dameski kuwakamata na kuwaua waamini {Mdo 9:20 }. Mara baada ya kuokoka alianza kuihubiri injili {Kumhubiri Kristo Yesu}. Paulo aliweka chini upanga wake wa mauaji na kuchukua upanga wa Neno la mungu Ambao hakuuacha mpka kifo chake.{ 2Tim 4:7}.
 Paulo alikwenda katika jangwa la Arabia kwa miaka Mitatu ambapo alipata mafuo zaidi toka kwa Mungu.  Baada ya hapo alirudi Yerusalemu kuonana na mitume. Baada ya Sauli kukutana na Ndugu alirudi tena Tarso. Kanisa lilipata raha baada ya kuokoka kwa Sauri wa Taso.{Gal 1:16-18, Mdo 9:20-31}.
 5.Injili inakwenda kwa watu wa mataifa{Mdo 10 }. Mtume Petro alitumwa kwenda kumhubiri Kornelio mtu wa Mataifa Injili . Mtume petro ndiye aliyefungu mlango wa Injili kwa wayahudi na kwa Watu wa mataifa.  Petro alihubiri injili kwenye nyumba wote waliokuwa wamekusanyika wakimsikiliza walishukiwa na Roho mtakatifu  na wakaanza kunena kwa Lugha Mpya kisha Petro akawabatiza .Huu ulikuwa ni mwanzo wa Injili au kanisa kuwafikia watu wa mataifa.
 6. Injili inakwenda Asia Ndogo {Mdo 13} Katika sura hii tunaona wito wa wamishenari wawili kwenda kuhubiri katika nchi ya kigeni.   Wito huu na kutumwa huku kulifanyika Antiokia mahali ambapo wanafunzi walipewa jina na kuitwa wakristo kwa mara ya kwanza {Mdo 11:26}.
Balnaba alikuwa ni mchungaji wakati Paulo alipokuja kutoka Dameski. Wanafunzi  wote walimwogopa, Balnaba alimpokea na kumtambulisha kwa kanisa {mitume Yerusalemu} Mdo 9;26-29.
Japokuwa mitume walimtuma Balnaba Antiokia mahali ambapo kanisa lilikuwa na uamsho mkubwa aliamua kufunga safari kutembea zaidi ya KM 150 kwa meli ili kwenda kumtafuta Sauli wa Tarso .Alimpata na kisha akamchukua na kuja nae Antiokia bila kujua kwamba miaka ya mbele sauti ya Bwana ingemwita kupia njia ya unabii
Nitengeeni Balnaba na Sauli kwa kazi niliowaitia.{Mdo 13:1-5 }.
Balnaba na Paulo waliombewa na kanisa na kisha kwenda kwenye umisheni wao kuelekea Asia ndogo mahali ambapo walianzisha makanisa mengi. Kama inavyoainishwa katika Matendo ya Mitume 13 na 14. Baadae walirudi Antiokia mahali ambapo palikuwa ni kituo chao cha umisheni.
K. KUTENGANA KWA WAMISHENARI . Wakati mitume hao {Paulo na Balnaba} walipokuwa wanajiandaa kwaajiliya safari yao ya pili ya umisheni walipishana. Kulitokea kutokuelewana katika jambo moja. Balnaba alitaka kumchua Marko{ ambae aliwaacha katika safari ya kwanza ya umishenari na kurudi Yerusalemu}waende nae katika safari ya pili ya umisheni lakini Paulo alikataa kuambatana nae, hivyo kukatokea mgongano kati yao na kisha wakaamua kutengana. Hapa tunaona moyo wa kichungaji wa Balnaba japokuwa Marko alishindwa katika safari ya kwanza ya umishenari aliamua kumpa nafasi nyingine. tuna mwona Paulo akiwa mtu wa kushikilia kanuni kuliko kumpendeza mtu yeyote. Mtu ambae yuko tayari kuvunja mahusiano na Balnaba kuliko kukubaliana nae. Miaka ilipita na Mtume Paulo akakomaa kiimani. Mtume Paulo ambae alisema katika uchanga wake : mimi si duni kuliko hao mitume wakubwa {2Kor 11:5}. Baadae alisema ‘Mimi ni wa kwanza kwa wenye dhambi {1Tim 1:16}. Paulo alfika mahali pakujitambua, kujisifu kulibadilishwa na kujishusha na upendo ulichukua nafasi mahali pa chuki na kanuni. Katika waraka wake wa pili kwa Wakorintho alisisitiza sana upendo na msamaha. Baadae tunamwona   Mtume Paulo akiwa katika upweke gerezani   akisubiri kunyongwa. Alimwagiza   Timotheo kumleta Marko. Marko huyu huyu ndiye aliyemkataa wakati wanafanya huduma na Balnaba.
Kutokana na hili tunajifunza ya kwamba tusimkatae mtu kutokana na makosa aliyoyafanya kwa sababu twaweza kumhitaji tena baadae.
7. Mkutano wa Yerusalemu. {48.B.K}. Tatizo lilitokana na kuokoka kwa wamataifa na kujiunga   na kanisa. Wakristo wakiyahudi walikuwa na mitazamo tofauti tofauti juu ya hili .Walikuwa na mitazamo ifuatayo:
1. Kundi lenye msimamo  mkali liliamini ya kwamba hakuna wokovu nje ya Israeli . Kwa hiyo ingawa wamataifa wamempokea Yesu Kristo kama masihi wao kwahiyo walipaswa kutahiriwa na kushika Torati ya Musa {Sheria za Kiyahudi}Ili waweze kuokolewa Bila kufanya hivyo wokovu wao ungekuwa ni batili.
Kundi la wenye mabadiliko.Hawa waliamini kwamba wokovu ni kwa njia ya imani katika Yesu Kristo.Bila ya kushika sheria za kiyahudi. Wao waliamini kwamba sheria za kiyahudi haziwahusu watu wa mataifa. Paulo na balnaba walikuwa mojawapo wa watu wenye mtazamo huu. Mkutano uliitishwa Yerusalemu ili kushughulikia jambo hili muhimu la mafundisho kutokana na watu wa mataifa kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wao. Baada ya majadiliano marefu Mitume na Wazee walifikia hitimisho ambalo lilithibitishwa na Roho mtakatifu kwamba Wamataifa hawakuwa chini ya Sheria za kiyahudi na kwamba walichotakiwa kufanya ni kujiepusha na Ibada ya sanamu, kula nyama iliyosongolewa na damu, kujiepusha na uasherati na uzinzi. Barua iliandikwa na mitume na ikapelekwa kwa kanisa la mataifa kwa mikono ya Paulo, Balnaba Yuda na Sila. Walipofika Antikoa walilikusanya kanisa na kuwapa ujumbe wa kikao cha mitume na wazee kilichofanyika Yerusalemu kuhusu tatizo lao. Waamini hawa walifurahi sana kupata ujumbe wenye kuwatia moyo {Mdo 15:30-31}
L. KANISA MIONGONI MWA MATAIFA.
Tangu mauaji ya Stefano (48 B.K) mpaka mauaji ya Paulo   mtume mwaka 68 B.K
Katika kipindi hiki chote tunategemea kitabu cha Matendo ya Mitume, nyaraka za Paulo na mwanzo wa waraka wa kwanza wa Petro. Um isheni wa mtume Paulo na Watendakazi wenzake   ulifanyika katika   dola yote  ya Rumi. Wakati  mitume wengine walikwenda   nchi za mbali zaidi. (hii ni kulingana na  mapokeo).
Idadi ya waamini wa kimataifa ilikua kwa kasi sana wakati idadi ya waamini wa kiyahudi iliendelea kushuka.Wayahudi walianza kukasirika na kufanya  fitina  dhidi ya kanisa  na walikuwa tayari kuanzisha mateso dhidi ya wakristo.

Safari Ya Pili Ya Mtume Paulo
Kwa sababu ya kupisha kwa Balnaba na Paulo, Balnaba alimchukua mpwa wake Yohana(Marko) na kwenda katika nchi ya kwao Kipro, Paulo alimchukua nabii Sila katika safari yake ya pili ya umisheni  na kwenda kuyatembelea makanisa waliyokuwa wameyafungua katika safari ya kwanza walipokuwa na Balnaba.Paulo likusudi kwenda Bithinia lakini Roho Mtakatifu akamkataza. Kisha walielekea Troa mji wa Kaskazini Magharibi ya Asia ndogo.
Injili inakwenda  Ulaya. (Wito wa Makedonia)
Usiku mmoja wakati Paulo na Sila wakiwa Troa mtu wa Makedonia alimtokea kwenye maono akisema “Vuka uje Makedonia utusaidieMara Paulo na Sila walikwenda Makedonia katika bara la Ulaya na wakaanzisha kanisa katika mji wa Filipi, Thesolanike, Beroya, Athene na Korintho.
Tunakumbuka kwamba mwanzoni kila mahali Paulo alipokwenda , aliwaendea Wayahudi kwanza.  Wayahudi toka sehemu mbalimbali zadunia ya wakati ule walikuwepo katika siku ya Pentekoste na walishuhudia kumiminwa kwa Roho Mtakatifu na  ubatizo wa waaini wapya 3,000. Wengi wao walitoka nchi za mbali kuja kusherehekea sikukuu ya Pasaka katika mji wa Yesulasalemu na kurudi nchini kwao. Inawezekana baadhi yao mtume Paulo alikutana nao, kwasababu baadhi yao walionekana kuwa naurafiki zaidi na Paulo.
Wakati wayahudi wengi walipoikataa Injili ya Kristo kama mfufuka mwana wa Mungu, Paulo aliwageukia watu wa mataifa.
Kanisa katika Filipi, Mwamini wa kwanza katika Ulaya alikuwa ni mwanamke aliyeitwa Lidia muuzaji wa rangi za zambarau mwenyeji wa Tiathira.  yeye na nyumba yake walibatizwa na alifungua mlango wa  nyumba yake kwaajili ya watumishi wa Mungu.
Kanisa katika Thesalonike. Pia katika mji huu mtume Paulo alikwenda kwa Wayahudi kwanza kama ilvyokuwa desturi yake. Baadhi ya  Wayahudi na Wayunani waliamini. Wayahudi wasioamini walianzisha ghasia dhidi ya   watumishi wa Mungu, yaani Paulo na watendakazi wenzake.   Kwa hakika washitaki hawa walijua nini cha kusema.  Kama mitume wangekamatwaq kwa kuanzisha dini nyingine  hakuna tatizo ambalo lingetokea kwa watesi kwa sababu Ugiriki ilikuwa ina dini nyingi na k  walizikubali karibu  zote.
Wao walikuja na uvumi mwingine kabisa kwa kusema kwamba “Watu hawa wanadai kwamba kuna mfalme mwingine”.
Inaonekena Wayahudi hao Walianzisha uvumi huo ili serikali iweze kushiriki katika zoezi la kuwadhibiti mitume.
Kanisa katika  Beroya. Injili ilikubaliwa kwa watu wote Wamataifa na Wayahudi Wakati Wayahudi wa Thesalonike waliposikia walikuja tena kufanya ghasia dhidi ya mitume  hivyo  iliwalazimu Paulo na Sila kuondoka mjini hapo, lakini Neno la Mungu  lilikuwa tayari limehubiriwa.
Hakika mitume hawa waliishi sawasawa na Neno la Kristo “Watakapowafukuza katika mji mmoja kimbilieni katika mji mwingine. (Mt 10:23)

Kanisa katika Athene.   Hapa pia mitume hawa waliwaendea Wayahudi , lakini wayahudi hao hawakulipokea Neno. Baadae mtume Paulo aligundua ya kwamba Mungu aliwapofusha macho Waisraeli kwa muda kwa sababu walimsulubisa Kristo Yesu.
Wanafalsafa wa Kigiriki walimpa mtume paaulo changamoto japo kuwa si sana kwa sababu walitaka kulisikia Neno, hawakutubu bali walivutiwa tu na mdahalo.  Walipokuwa hawajui  chakujibu walidhihaki.
Kanisa katika  Korintho.   Pia mahali hapa kama ilivyokuwa kawaida yake mtume Paulo alikwenda kwa Wayahudi  kwanza.  Alikaa na Wayahudi watengeneza mahema(Akila na Prisila). Inadhaniwa kuwa alitengeneza nao mahema ili kujipatia pesa kwaajili ya kujikimu   ili aweze kuhubiri Injili pasipo kumlemea mtu yeyote.(Mdo 20:34). Japokuwa Paulo alikuwa ni Rabi aliyeelimika na Mtume hakudharau kazi ndondogo kwaajili ya kueneza Injili.
Maamuzi Thabiti. Wayahudi waliipinga Injili tena na hii ilileta  kwa huduma ya Injili ya Paulo. Mtume Paulo alisema
Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu mimi ni safi tangu sasa nitakwenda kwa watu wa mataifa.s (Mdo 18:6)
Paulo na Sila walikaa Korintho kwa muda wa miezi kumi na nane (18) wakiwafundisha waamini. Kutoka Korintho mtume Paulo aliandika nyaraka mbili kwa Wathesalonike
Baada ya shambulio linguine lililfanywa na Wayahudi dhidi yake (Paulo) aliamua kuondoka  Korintho na kurejea Antiokia kwa kupitia Efeso na Kaisaria.
m. SAFARI YA TATU YA   UMISHENI YA MTUME PAULO (Mdo 18:23-22:17)
Katika awamu hii mtu aliyeambatana na mtume Paulo ni  Timotheo aliyejiungas katika timu yake katika safari ya pili ya umisheni huko Listra. (Mdo 1-3) na kwa muda mfupi idadi kubwa ya wanatimu walikuwa pamojanae kabla hajamaliza safari hii. Mmojawapo wa watu hao muhimu alikwa ni Dk. Luka.
n. PAULO MTUME KATIKA MINYORORO (Mdo 22:23-28: 31)
 Paulo alitumia miaka kadhaa akiwa gerezani  lakini kamwe hakuacha kufanya kazi ya umisheni. Mazingira hayakubadili kusudi lake. Baada ya safari ndefu Paulo alifika Rumi jiji ambalo alitamini sana kuliona. Alikuwa na uhuru wa kuishi katika nyumba aliyokuwa ameipanga mwenyewe huku akiwa chini ya uangalizi wa askari mageza, japokuwa alikuwa mfungwa bado alileta athari kubwa  katika kanisa huko Rumi. Moja ya mambo makuu aliyofanya ni kuandika  nyaraka kwa Waefeso, Wafilipi, Wakolosai na Filemoni.
Inaaminika kwamba baada ya miaka miwili ya kukaa kifungoni  mtume Paulo aliachiwa huru (Mdo 28:30-31) lakini hakuna rekodi kamili katika kipindi hiki isipokuwa taarifa chache tu.
Mapokeo yanasema kwamba mtume Paulo alikamatwa Nikroporisi Kaskazini  mwa Ugiriki chini ya mtawala wa Rumi aliyeitwa Nero na akarudishwa Rumi  katika kifungo hiki cha pili aliandika nyaraka zifuatazo:- 1&2Timotheo, na Tito. Barua hizi zikikuwa ni barua zake za mwisho mnamo mwaka 68. B.K. Mtume Paulo aliuawa kwa amri ya mfalme Nero.
h. UANDISHI WA  MAANDIKO   MATAKATIFU.
Inadhaniwa kwamba  mpaka kipindi cha Mkutano Yerusalemu mnamo mwaka 48. B.K hakuna hata kitabu  kimoja cha Agano jipya kilichokuwa kimeandikwa, lakini karibu ya mwaka 68.B.K idadi kubwa ya Maandiko ya Agano Jipya yalikuwa tayari yameandikwa, hii ikijumlisha Injili ya Mathayo, marko, Luka, nyaraka za Paulo, Yakobo na 1Petro. Katika kipindi cha miaka ya 68- 100.B.K














MADA YA TATU.
  KANISA LA  SMIRNA(KIPINDI CHA MATESO)
 KIPINDI CHA SMIRNA
 A. UTANGULIZI.
Simirna ni mji ambo ulikuwa   umbali wa Km 65 Kaskazini mwa Efeso na ulijulikana kama bandari ya salama kwa wakati ule. Ulikuwa   katikati ya njia kuu kutoka Rumi kwenda India na Persia(Irani)
Katika moja ya mitaa yake kulikuwa na hekalu la mungu wa kigiriki aliejulikana kwa jina la zeus Mungu mkuu na katika upande mwingine wa mji kulikuwa na hekalu la Cybele {mama wa mungu}.
Mji wa Smirna pia ulikuwa ni kituo cha ibada ya kumwabudu kaisari. Kulikuwa na hekalu la mfalme wa Rumi Teberio Kaisari
B. VIPINDI VYA MATESO
Historia ya kipindi cha smirna  Inaaminika kwamba siku kumi za mateso yaliyotakiwa kuja juu ya smirna huhusisha vipindi maalum kumi vya mateso chini ya watawala mbalimbali wa kirumi  pia na wao watawala wangekuwa kumi.
Majina ya wafia dini mbalimali katika kipindi hiki cha   Smirna chini ya wafalme mbalimbali wa Rumi yanaorodheshwa hapa.
1.      Klaudi   Nero (64-68 B.K). Petro alisulubiwa katika kipindi cha utawala wa Nero. Paulo alikatwa kichwa katika kipindi hiki.

2.      .  Domitiani (90-95 B.K) alijaribu kumuua mtume Yohana akashindwa na baadae akaamua kumpeleka uhamishoni katika kisiwa cha Patmo.


3.      Trajani (104-117   B.K) Simoni ndugu wa Yesu aliuawa katika kipindi hiki mwaka wa 107 B.K.  Askofu   Ignatious  wa Antiokia  aliuawa pia katika utawala wa mfame huyu mwaka 110.B.K.  Watu wengine waliouawa katika kipindi hiki ni Polikap mwanafunzi wa Mtume Yohana  (155 B.K),
 4.    Marcus Aurelius. (161-180 B.K). Yustini  aliuawa katika utawala huu katika mwaka 165  B.K. Pia alifanya mauaji ya wakristo wengine   wengi pia.
 5.  Septimus   Severio. (200-211 B.K) alimuua Leonidus baba wa Origeni mwanatheolojia mkuu., Pia aliwaua na Perpetua na Felistas na ireneos mwaka 202 B.K
 6.  Thraker Maximus  (235-237 B.K).alifanya mauaji lakini hatuna majina ya watu aliowaua.
 7. Desiusi. (250-253 B.K. )  katika kipndi cha utawala wake mateso yaliibuka tena juu ya kanisa na kwa bahati nzuri utawala wake ulidumu kwa muda mfupi sana na baada ya kuanguka kwa utawala wake kipindi kifupi cha amani kilikuja juu ya kanisa.
8.      Vareliani   (257-260 AD.) Alipanga mauaji lakini hayakufanyika katika utawala wake.
(270-275  B.K.) Askofu Spriani wa Kathegi na askofu Sextus wa Rumi waliuawa katika kipindi hiki.

C. Mateso ya kitaifa. Tabia za msingi katika historia ya kanisa katika karne zote mbili yaani karne ya  pili na ya tatu ni kanisa au wakristo kuteswa na wafalme wa kirumi.
Mateso haya hayakuwa endelevu   lakini yalitegemea mtazamo   aliokuwa nao mfalme aliyekuwa akitawala katika kipindi hicho.  Mateso ambayo yalikuwa yakijirudia katika kipindi hiki yalidumu kwa karibu miaka 200 mpaka mfalme Kostantino alipookoka  na kutangaza tamko la amani.(Edict of c Torelance) katika mwaka wa 313  B.K
D. SABABU ZA KANISA KUTESWA.
1. Imani juu ya Mungu mmoja. Warumi walikuwa na miungu mbalimbali ambayo walikuwa wakiiabudu pamoja na sanamu zao. Wakristo walitangaza kwamba kuna Mungu mmoja tu Mfalme wa Rumi alijenga hekalu ambalo lilipaswa kutumiwa na watu wote kuabudu miungu yao na akawapa wakristo nafasi na ya kushiriki kumwabudu Mungu wao katika hekalu hilo.  Wakristo walikataa fursa hiyo na kusababisha wao kuonekana kwamba wako tofauti na wananchi wengine. Hivyo mateso yalianza dhidi yao.
2. Kukataa kumwabudu kaisari. Kama ilivyokwisha elezwa katika sura iliyopita kwamba makaisari wa kirumin walijitangaza kwamba wao ni miungu na wakadai waabudiwe na wananchi au raia wao. Hivyo raia wote wa dola ya Rumi walilazimika kushiriki ibada ya kumwabudu kaisari. Mahekalu ya ibada za kaisari yalijengwa kila mahali na sanamu za makaisari zikawekwa na watu wakalazimishwa kumwabudu kaisari na kutoa dhabihu mbele ya  sanamu za kaisari.  Hii ilikuwa mojawapo ya ibada za kitaifa katika dola ya Rumi.
Wakristo walipinga vikali  iabada hizo na hawakuwa tayari kushiriki ibada hizo wala kutoa dhabihu mbele ya sanamu za kaisari. Kutokana na asababu hiyo wakristo waihesabiwa kuwa wasaliti wa kaisari na dola kwa ujumla na hivyo walipaswa kuhukumiwa kifo. Wakristo walianza kuteswa na dola ya Rumi kwa sababu ya kukataa kumwabudu kaisari na kumwita Yesu Mfalme (Kurious).
3.Kutojihusisha kwenye ibada za sanamu. Ibada hizi za  sanamu zilikuwa sehemu ya maisha ya kila siku katika dola ya Rumi. Sanamu hizo zilisimamishwa katika kila nyumba na ziliabudiwa katika kila sherehe. Dhabihu za vinywaji   zilitolewa kwa  sanamu hizo. Hivyo wakristo walikataa kujihusisha katika shughuli za kila siku za kijamii zilizohusiusha ibada za sanamu(mfano sherehe mbalimbali). Wakristo walipokataa kujihusisha na hayo mambo walionekana wako kinyume na jamii nzima.Kwa sababu hiyo jamii iliwahesabu kama maadui.
4.Kutambuliwa rasmi kwa dini ya kiyahudi: Dini ya kiyahudi ilitambuliwa rasmi na dola ya Rumi kama dini ya kitaifa. Mwanzoni kanisa wakati linaanza lilitambuliwa kama kikundi tu ndani ya dini ya kiyahudi chenye msimamo mkali na hivyo  kanisa lilipata upendeleo wea serikali kwa namna fulani. Lakini mara baada ya kuanguka kwa Yerusalemu  na kubomolewa kwa hekalu katika mwaka wa 70  B.K, kanisa au ukristo ulisimama peke yake na dini ya kiyahudi walikuwa tayari kushirikiana na serikali   kulitesa kanisa.
5. Kanisa  kufanya mikutano ya faragha. Kuokana na mateso kanisa lilianza kukutana katika maeneo ya siri na hasa wakati wa usiku. Hii ilipelekea kanisa kuhisiwa vibaya na selrikali kwamba lilikuwa linafanya njama ya kupindua serikali au kufanya maasi kwa sababu serikali ya rumi ilipiga marufuku mikutano yote isiyo harali pia mikutano ya usiku ilipigwa marufuku. Kwa kuogopa kwamba mikutano yote iliyokuwa haina kibali cha serikali na iliyofanyika vifichoni haikuwa na nia njema kwa dola ya Rumi. Kwa sababu hiyo wakristo walitazamwa na dola kama waasi. Watu wanopanga njama na maadui kuleta vurugu na maasi ndani ya dola na hivyo dola ilianzisha mateso juu ya kanisa.
6.      Usawa katika kanisa. Kanisa liliwaona watu wote kuwa sawa. Hakukuwa na matabaka katika kanisa. Waliwaona watu wote kuwa sawa a hawakumwogopa mtu yeote na wala hawakuogopa cheo cha mtu. Kuokana na sabu hiyo kanisa lilionekana kuwa na dharau, lisilo na heshima na hivyo kanisalilifanyika adui wa dola.
7.      Kuharibu biashara za sanamu.: Kulikuwa na biashara  iliyokuwa inafanywa ndani ya dola ya Rumi.Biasharahiyo ilikuwa ni ya uuzaji wa sanamu. Watu wengi  walijipatia faida kutokana na biashara hiyo.  Mitume walipohubiri  Injili watu waliokoka na kuachana na ibada za sanamu .
 Mitume walifundishwa kwamba sanamu si kitu na hazipaswi kuabudiwa anaepaswakuabudiwa ni Mungu muumba Mbingu na nchi  pekee. Watu wengi waliacha kununua sanamu hizo . Kitendo hicho kilisababisha biashara hiyo ya uuzaji sanamu kudolola.  Watengenezaji na wauzaji wa sanmu  hizo walipata hasara na wakaamua kuanzisha  kuja juu  na kuanzisha ghasia dhidi ya kanisa kwani walipoteza wateja wao.



E.HATUA ZA MATESO.
Kuna mwingiliano kati ya kipindi cha efeso na Smirna. Kipindi cha Efeso kiliisha na kifo cha mtume Yohana mwaka 100  B.K. Wakati kipindi cha Smirna kilianza wakati wa mateso ya kitaifa.(dola) wakati mfalme nero alipouchoma mji wa Rumi mwaka 64 B.K.


F. VIPINDI   KUMI VYA MATESO YA KITAIFA.
MATESO YA KWANZA Chini ya Kaisari Nero.(54-68 B.K)
Klaudi Nero alikuwa na umri wa miaka 16 alipoingia katika utawala (ufalme) katika mwaka 54 AD. Alikuwa mjukuu mkubwa wa Agustus aiyetoa amri ya watu wote kuhesabiwa sensa (Lk 2). Nero alikuwa mfalme wa kwanza katka wafalme kumi kuanzisha mateso   dhidi ya kanisa.Alichoma mji wa rumi mwaka 64 B.K .Theruthi mbili ya mji wa Rumi iliteketea. Mfalme Nero aliwasingizia wakristo kwamba ndiyo waliohusika na uharibifu huo. Hivyo kanisa  lililazimika kuingia kwenye mateso makali. Katika kipindi hiki  mtume Petro alisulibiwa miguu juu kichwa chini mnamo mwaka 67 B.K.  Pia mtume Paulo alikamatwa na kufungwa Rumi  ambapo alihukumiwa kifo na kisha akauawa kwa  kukatwa kichwa mwaka 68 B.K  . Mjini Rumi.
Mfalme Nero alikuwa katkili kuliko makaisari wote wa dola ya Rumi waliomtangulia na waliomfuata. Kwani hajatokea kaisari katika  dola ya Rumi aliyefanya mauaji kama Nero. Mwaka 59 B.K .  Mfalme Nero alimuua mama yake . pia alimuua mke wake wa kwanza (Octavia)na kisha mkewe wa pili(Pompea) na baadae alimuua kaka yake na  rafiki yake  mwalimu Seneka.
Mpaka mwaka wa 64  . B.K   Rumi  ilikuwa katika ghasia kuu. Mfalme Nero alituhumiwa kwamba yeye ndiye aliyehusika na kuuchoma moto mji wa Rumi. Lakini yeye alikanusha na kuwashutumu wakristo kuwa ndiyo waliohusika  na tukio hilo.  Kutokana na hilo kanisa liliingia katika kipindi cha mateso makali. Maelfu ya wakristo waliuawa baadhi yao walitupiwa kwenye hifadhi za wanyama ili waliwe na wanyama wakali na baadhi yao walichomwa moto na mfalme akaendesha gari lake juu yao katika bustani yake. Bustani ya mfalme ambako tukio hili lilifanyika  leo ni eneo la  la jiji la Vatikani  makao makuu ya papa na kania la  MT. Petro.  Kaisari Nero alijiua mwenyewe  mwaka68. B.K
KIPINDI CHA PILI CHA MATESO CHINI YA DOMITIAN. (90-96 B.K).
Baada ya Nero kujiua mwaka wa 68 B.K  kanisa lilipata amani mpaka alipoinuka mtawala mwingine ambaye ni Domitiani. Wakristo wengi waliuawa . Mtume Yohana alipelekwa uhamishoni kwenye kisiwa cha Patmo ambapo ndipo mahali alipopokea ufunuo ambao sasa ni kitabu cha Ufunuo wa Yohana.
KIPINDI CHA TATU CHA MATESO CHINI YA TRAJANI 104-107 AD.
Trajani husemekana kuwa mtu muimusana miongoni mwa watawala wa Rumi. Alikuwa mtawala mzuri kwa nchi yake lakini aaliwaua wakristo. Mmoja wa mahakimu wake aliyeitwa  Plin the younger. Gavana wa behtania alichunguza maisha ya wakristo na mafundisho yao na kugundua kwamba   mafundisho hayo hayakuwa na chochote chenye kuleta uasi kwa serikali ya Rumi. Alileta ripoti yake mbele ya mfalme Trajani lakini mfalme alijibu “ Kama watu hawa walioletwa mbele yako wamepatikana na hatia kwa sababu ya kuwa wakristo na wauawe lakini ikiwa wataikana imani yao ya kikristo na na ikathibitika kwamba wanaabudu miungu yetu na waachiwe huru. Katika kipindi hiki waliuawa wakristo mbalimbali kama ifuatavyo.
Simoni mdogo wa Bwana Yesu. Alisulubiwa katika mwaka wa 107 AD.akiwa na umri wa miaka 110. Alisulubiwa kwa amri ya mfalme wa Rumi {Trajani}.
Askofu Ignatious wa Antiokia ambaye aliandika nyaraka mbalimbali kwa makanisa mbalimbali ambazo baadhi yake zinapatikana katika kitabu kiitwacho “Mababa wa Kitume”{Apostolic fathers}.  Alikuwa tayari kuuawa kwaajili ya Bwana Yesu. Aliandika barua za kuwafariji wakristo akiwa njiani kuelekea Rumi ambapo  alitumwa katika hifadhi ya wanyama wakali  na akaliwa na wanyama wakali mnamo mwaka 110.AD
PORIKAP. {69-155 AD} Alikuwa mwanafunzi wa mwaanfunzi wa mtume Yohana na rafiki wa trajani na mwalimu wa Irenius. Inadhaniwa kuwa Polikap aliteuliwa na mtume yohana kuwa askofu wa makanisa saba ya Asia. Alipoamriwa kumkana bwana Yesu Kristo ili kuepukana na kuuawa yeye alijibu:
“Miaka 86 nimemtumikia Bwana wangu na hajatenda Jambo lolote baya kwangu, nawezaje kunena vibaya juu ya Bwana wangu aliyeniokoa? Alichomwa kwenye moto na akafa kifo cha kishujaa kwaajili ya Imani yake juu ya Yesu Kristo. Aliuawa chini ya utawala wa mfalme Antonius Pius mwaka 155 A.D.
KIPINDI CHA NNE CHA   MATESO CHINI   MARCUS
 AURELIUS 161-180 A.D.
           Marcus alikuwa alijulikana kam mfalme borawa nchi yake na mwandishi mwenye maadili. Japokuwa alikuwa mtumzuri kwa taifa lake alikuwa mtesi wa kanisa. Alifikiri kurejesha  maisha ya zamani ya kirumi na dini za zamani. Kwa wakati huo ukristo ulikuwa na mashiko zaidi.Waamini wengi walikuwa tayari kufa kwa ajili ya imani yao na wala hawakuogopa kifo. Walikikabili kifo kwa shangwe na ushindi mkuu. katika kipindi  hiki waaminni wengi waliuawa na wengine walitupwa  katika hifadhi za wanyama wakali  na wakaliwa na wanyama .
YUSTINI (Justine)Marty 100-165 A.D alizaliwa na alielimishwa vizuri mpaka kuwa mwanafalsafa na aliendelea kufundisha hata baada ya kuwa mkristo. Alirejerea kwa manabii wa zamani wa Kiebrania. Aliandika maneno yafuatayo dhidi ya ukatili na mauaji yaliyokuwa yanaendelea  dhidi  ya wakristo. “wanatushitaki, wanatusulubisha kwenye misalaba na kutupa kwenye hifadhi za wanyama  wakali na kwenye moto. Lakini wanapofanya mabaya zaidi juu yetu ndivyo idadi ya wakristo inaongezeka na kuwa kubwa zaidi. Mnamo mwaka 165 A.D .alikamatwa na mfalme wa Rumi  Marcus Aureliusi na kuuawa.


KIPINDI   CHA  TANO CHA MATESO   CHINI YA SEPTIMUS. 202-211.  A.D.
Baada ya kifo cha Marcus Aurelius kanisa lilipata amani mpaka alipoinuka mtawala mwingine aliyejulikana kwa jina la Septimus Severus. Mtawala huyu alimuua Leonides baba wa Origeni mwanatheologia mkuu. Katika mji wa kathegi Perpetua na mtumwa wake Felistas walitumwa katika hifadhi ya wanyama poli wakali na wakauawa.
 Mfalme Karakala alitoa uraia uraia kwa kila mtu katika dola yake. Huu ulikuwaq ni uhuru mkubwa kwa wakristo. Watumwa pekee ndio ambao wangeweza kusulubiwa au kutupwa kwenye  hifadhi za wayama poli wakali.
KIPINDI CHA SITA CHA MATESO CHINI YA THRAKA MAXIMUS
 235-237. A.D.  Baada ya kipindi cha  amani Thraka alikalia kiti cha enzi cha Rumi. Alikua mpiganaji na alikusudia kuonyesha huruma zake kwa dini za kipagani kwa kuwatesa wakristo. Utawala wake ulikuwa mfupi kwa sababu ya kutawala kwake kwa njia ya udikteta. Maadui zake walitengeneza kikundi ambacho kilifanikiwa kumuua.

KIPINDI CHA SABA CHA MATESO.CHINI YA   DECIUS 250-253 A.D.
Katika kipindicha utawala wake mateso makali yaliibuka tena na kwa bahati nzuri kipindi chake cha utawala kilikuwa kifupi na kanisa lilipata raha kwa kipinda raha na amani kwa miaka 40.
KIPINDI CHA NANE CHA MATESO CHINI YA VARELIANI. 257-260. A.D.
Askofu Sipriani wa Kathegi aliuawa pia askofu wa Rumi Sextus aliuawa.
KIPINDI CHA  TISA  CHA MATESO. CHINI YA  AURELIUS. 270-275. A.D
Mfalme Aurelius alikuwa mwabudu jua japokuwa hakulitesa kanisa moja kwa moja mwanzoni lakini hakuwapa uhuru  wakristo. Hatimae aliamuru kwamba wakristo wateswa. Kwa bahati nzuri amri yake haikutekelezwa Kutokana na kifo chake cha ghafla.
KIPINDI   CHA KUMI CHA MATESO CHINI YA  DEOCLETIAN 303 3010. A.D
Mfalme Deocletiani na wasaidizi wake waliwafunga wakristo gerezani. Baadae sehemu ya jingo hili lilibadilishwa na kuwa Kathedro ya Mtakatifu Petro. Deocletiani aliagiza kuchomwa moto kwa kila nakala Biblia, makanisa kubomolewa na wakristo wenye msimamo mkali kunyang’anywa uraia. Akiwa na umri wamiaka 80 deocletiani aliondoka kwenye kiti cha utawala, lakini wafuasi wake Galarius na Kostantinusi waliendeleza mateso mpka mfalme Kostantino mototo wa Kostantinus alipotoa tamko la amani kwa kanisa mwaka 313 A. Tamko hili la amani lilisitisha mateso kwa kanisa kwa kipindi cha karne mbili
Siku kumi za kujaribiwa zilizotajwa katika Ufuno wa yohana 2:10 zilifikia mwisho. Baadae mfalme Deocletiani alipotambua kwamba yuko karib na kufa alitubu dhambi zake mbele ya askofu wa mji.. Mwka 337 A.D alibatizwa. Mtu aliyeamini kwamba angeweza kuufuta ukristo alijikuta yeye mwenyewe anakuwa  mkristo.
G. UONGOZI KATIKA KANISA   KATIKA KIPINDI HIKI.
Wakati mitume wakiwa hai uongozi ulionekana ni utumishi yaani kutumikia au kuwajibika. Wakati Luka alipoandika kitabu cha matendo naPaulo alipoandika nyaraka zake tuna kuta maneno askofu na wazee yakiwa na maana sawa yaani yakimaanisha ofisi moja. Lakini katika miaka ya 125’s tunakuta maaskofu wamekuwa watawala katika maeneo yao. Katika baraza la yerusalemu mwaka 48 A,D {Mdo 15}  mitume wote na wazee walihusika. Lakini katika baraza la mwaka 150 A.D waliohusika ni maaskofu pekee. Hii inadhihirisha kwamba kanisa liliondoka taratibu kwenye mafundisho halisi ya mitume. Huduma ya mitume ilizimwa na ikachukuliwa na maaskofu . Maaskofu walijifanya watawala wa kanisa. Hii ndio sababu inayosababisha baadhi ya wataalam kuamini kwamba kipindi cha mitume kiliishia na kifo cha mtume Yohan, jambo ambalo si kweli. Huduma za mitume, manabii, waalimu wachungaji na wainjilisti kama zinavyoelezwa katika waefeso 4:11 ziliendelea kuwapo katika kipindicha mitume na vi[pindi vingine vyote vya kanisa, japokuwa zimekuwa  zikikataliwa na katika vipindi fulani ilionekana kama zimetoweka lakini  kwa uhakika zimekuwapo  na bado zimekuwa  zikifanya kazi katika kanisa hata sasa.
H. SHULE ZA THEOLOGIA.
Shule ya  Alexandria. Ilianzishwa  mwaka 180. A.D  na Pantaenusi ambaye alikuwani mwanafalsafa wa kigiriki na baadae akwa mkristo. Kisha alikwenda India, irani na Saudi Arabia katika huduma. Alikufa mwaka 200.A.D .
Klementi wa   Alexandria. Alikkuwa mwanafunzi wa Pantaenus  na alimsaidia katika uendeshaji wa shule. Alikuwa ni mkuu wa shule hadi alipoondolewa kwenye wadhifa huo katika kipindi cha mateso cha septimus Severusi mwaka 2002. A.D. Baadhi  ya vitabu vyake mpka sasa vipo.
Origeni (185-254 A.D). Alikuwa ni mwanatheologia mkuu. Baba yake Alikuwa ni motto wa Leonidas. Baba yake aliuawa kutokana na imani yake katika Kristo chini ya utawala wa mfalme Severus katika mwaka wa 2002 A.D. Wakati huo Origeni alikuwa na umri wa miaka 17. Origeni aliisdaidia familia yake kwa kufundisha falsafa ya kigiriki pamoja na fasihi. Aliianzisha kwa upya shule ya Biblia iliyokuwa imefungwa kutokana na kuondoka kwa Klementi. Baadae alikuwa ni mwandishi wa vitabu vya dogma na thiologia. Baadae alikwenda Kaisaria na alianzisha shule nyingine ya Biblia ambapo alikuwa ni kiongozi wa shule hiyo kwa karibu zaidi ya miaka 20.  Alifungwa jela chini ya mateso Deciani na alikufa kutokana na kutendewa kinyama akiwa gerezani.alikufa akiwa na umri wa miaka 69 mnamo mwaka 254. A.D.
Shule ya Asia ndogo. Shule hii haikuwa katikamji wowote ilikuwa ni shule ya masafa (mobile Bible School). Ilihusisha waalimu wa thiolojia na waandishi. Baadhi yao ni Ireneus(130-202A.D) aliyezaliwa Smirna. Alipata  elimu yake ya awali ya Biblia chini ya Porkap. Kansa la Asia ndogo lilimpeleka Ufaransa kama mmisionari. Aliuawa wakati wa mateso ya Severusi mwaka wa 202 A.D.
Shule ya kathegi: Shule hii ilikuwa kaskazini mwa Afrika na ilifanya vizuri kuliko shule zingine kubadili imani ya Kithiologia katika Ulaya. Watu wakuu katika katika shule hii walikuwa ni Tetullani  na Sipriani. Tetullani (160-200 A.D) Alikuwa ni mteteaji shujaa wa imani ya kikristo dhidi ya dini ya kiyahudi na mafundisho potofu  alijiunga na umontano na alitumia kalamu na mahubiri kuthibitisha kile alichofikiri ni mambo ya kidunia na  mabishano katika kanisisa.
Sipriani Askofu wa Kathegi (195-258 A.D) Alikuwa ni motto wa afisa wangazi ya juu wadola ya Kirumi. Alikuwa mkristo wakati wa ujana wake. Mambo matatu yaliyomtukia mpaka kuwa mkristo ni Maandiko ya tetullani, mafundisho ya Cellius toka Rumi na Maandiko matakatifu (Biblia).
Mwaka mmoja baada ya kuwa mkristo alikuwa askofu na kiongozi mkuuwa makanisa ya Afrika Kaskazini mwaka 248 A. D.  Mnamo Mwaka 257 A.D. Mfalme Valentine alimfungia kufanya huduma mwaka   na mwaka 258 aliuawa.

Kanisa la karne ya pili lilipambana na mambo makuu mawili ambayo ni Mateso na uzushi(Heresy) yaani mafundisho potofu. Mtume Pulo alitabiri ya kwamba:
“ Najua mimi yakuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa mwitu wakali wataingia kwenu wasilihurumie kundi. Tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao”
I.                    UZUSHI NA MAFUNDISHO YA  UONGO.
Mafundisho yasiyokubaliana na mafundisho rasmi ya kanisa yaliitwa uzushi na waamini waliamriwa na kanisa kutokuyapokea mafundisho hayo.
Kanisa katika historia yake lilitangaza mafundisho fulani kuwa uzushi kutokana na kutokukubaliwa kwa mafundisho hayo na uongozi wa kanisa.

Si kila mafundisho waliyoyaita uzushi yalikuwa mabaya, kwani kile kilichoitwa uzushi kilikubaliwa baadae na kanisa na kile ambacho kilionekana chema kilikataliwa na kuitwa uzushi baadae. Hoja  au  mawazo  yale waliyoyaita uzushi baadhi yalikuwa na mambo mema ndani yake.
Kanisa halikupambana na mateso tu bali pia na mafundisho ya uongo, sawsawa na unabii uliotolewa na mtume Paulo katika Matendo ya mitume 20:29-30.





J.  MAKUNDI YA UZUSHI.
1.     UYAHUDISHAJI.
Hili lilikuwa ni kundi la wakristo wa kiyahudi lililojitokeza wakati kanisa linapanuka katika miji ya wamataifa.  Wayahudishaji hawa walifundisha kwamba wakristo wote walitakiwa kuzifuata sheria za Musa na mapokeo ya dini ya kiyahudi. Waliyakataa maandiko ya mtume Paulo kwa sababu yalipinga mafundisho yao. Kundi hili lilitoweka katika karne ya pili BK.

2.     UNOSTIKI
 Unostiki ilikuwa ni falsafa iliyojaribu kutumia imani ya ukristo katika kuthibitisha ukweli wake. Kundi hili waliamini kwamba Baada ya ngazi ya Mungu mkuu kulikuwa na miungu wengine  wengi ambao baadhi wakiwa  wema na wengine  waovu. Unosti ulikuwa na elementi za falsafa za kiyunani na dini za kipagani.

.  Hivyo kanisa lilipinga vikali mno unosti likikana kwamba imani yake si falsafa na wokovu hautegemei falsafa  na mafumbo bali ufunuo wa Yesu kristo.

Wanostiki walipunguza thamani ya maisha na huduma ya Yesu Kristo. Habari nzima juu ya maisha na huduma ya Yesu ilielezwa kwa njia ya mafumbo (allegory). Unostiki ulizuka katika karne ya pili baada ya Kristo na ulishamiri katika karne ya tatu na  ya nne. 

Unostiki hata sasa unajidhihirisha katika karne hii ya ishirini na moja katika  dini mbalimbali hapa ulimwenguni. Hususani kupitia   falsafa ya mpango mpya wa dunia (New World  order Philosophy)

MAFUNDISHO YA  UNOSTIKI.
1.     Maarifa ya pekee hufunuliwa kwa watu wachache tu.
2.     Wokovu si kwa watu wote, ni kwa watu wachachetu  wenye kuyaelewa maarifa yanayofunuliwa.
3.     Ulimwengu huu na vitu vilivyomo ndani yake umeumbwa kwa nguvu isiyo kamili na hii ndio asili ya maovu yote katika ulimwengu.
4.     Yesu si mwanadamu, alikuwa na roho tu. Yesu alikuwa ni roho aliyejifanya aonekane katika umbile la binadamu.
5.     Waliamini kwamba mmoja wa miungu wadogo alikuwa ndani ya Yesu na ndio aliyekuwa asili ya uungu wake.



4.      MARSION
 Huyu alikuwa ni mtoto wa askofu wa Pontus. Alikuja Rumi yapata mnamo  mwaka 138BK.  Alipofika Rumi alijulikana kwa haraka sana kutokana na jinsi alivyojitolea sana katika kanisa kwa mali zake. Pia mafundisho yake yalimpa umaarufu na kumfanya ajulikane sana. Kutokana na umaarufu huo Marsion alipata wafuasi wengi. Mafundisho yake hayakukubaliwa na kanisa hivyo alitangazwa kuwa mzushi na  alitengwa na kanisa mnamo mwaka 144 BK.
Marsioni aliunda chama chake ambacho kiliwaunganisha wafuasi wake wote. Chama chake hakikuongezeka kwa njia ya kuzaliana kwa sababu ya kukataa mambo ya ndoa. Waliongezeka kwa njia ya wanachama wapya kujiunga. Marsion alikuwa ni mtu wa kwanza kutunga  kanuni ya maandiko.

v MAFUNDISHO YA MARSION
1.     Kwa kiasi kikubwa mafundisho yake yalifanana na mafundisho ya wanostiki.
2.     Aliweka sharti la wafuasi wake (wanandoa) kutokutana kimwili na kwamba walitakiwa kuachana na kuishi maisha ya upweke.
3.     Alikaza kwamba wokovu ni kwa watu wote. Wokovu hutegemea Injili ya Yesu na si kwa kufunuliwa mafumbo kifalsafa.
4.     Injili ya upendo wa Mungu inahitaji kusikika zaidi katika kanisa.
5.     Kanisa limeichafua Injili kwa kuichanganya na mambo ya dini ya kiyahudi.
6.     Mungu wa Agano la kale ni tofauti na baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Kwa sababu Mungu wa agano la kale alifurahia dhabihu za damu.
7.     Mungu aliyeumba ulimwengu na watu wake ni Mungu mwovu, Mungu mwingine mwema alijificha hadi wakati wa Yesu Kristo.


4.       UMONTANO.
Kilikuwa ni kikundi kilichoanzishwa na mtu mmoja aliyeitwa Montano mwenyeji wa Frigia. Wafuasi wa kikundi hiki waliitwa wamontano. Kikundi hiki kilienea sana  kuanzia mwishoni mwa karne ya pili na kuendelea kwa karne mbili zaidi.
Wakati wa ubatizo wake Montano alinena kwa lugha nyingine na kutabiri na hivyo akajiita kuwa ni kinywa cha Roho Mtakatifu aliyetabiriwa na Yohana. Alikuwa na wasaidizi wawaili wanawake ambao nao pia walijitambulisha kuwa ni vyombo pekee vya Roho Mtakatifu. Karama za kinabii zilijidhihirisha katika mlengo wa umontano. Kutokana na mikazo yao,  Wamontano walihukumiwa uzushi na kutengwa na kanisa.

v MAMBO  MUHIMU YA MONTANO.
1.     Walikaza kwamba wamefunuliwa juu ya mwisho wa dunia uliokuwa karibu sana kutokea.
2.     Baadhi ya wafuasi wa umontano walikataa kulima kwa sababu Yesu angekuja kabla ya msimu wa mavuno.
3.     Baadhi walikataa ndoa kwa kuwa mwisho wa dunia ulikuwa karibu.
4.     Kiongozi wao mmoja wa huko Pontus aliwapeleka washirika wake porini kwenda kumlaki Bwana Yesu wakati anarudi duniani kwa mara ya pili.
5.     Kiongozi mwingine wa huko Shamu aliwakataza washirika wake wasilime kwa sababu Yesu angerudi kabla ya msimu wa mavuno.
6.     Alikataa hali ya kanisa kumezwa na ulimwengu.
7.     Alidai kuwa kanisa lilikuwa limepoa na hivyo lisitarajie kurudi kwa Yesu.
8.     Walipinga suala la uaskofu kuchukua mamlaka katika kanisa. Waliweka mkazo katika huduma ya unabii na ukuhani wa waamini wote.


v KUMEGEKA KWA KANISA   CHINI YA  UONGOZI WA NOVATIANO NA   DONATO.
Katika karne ya tatu na ya nne kulitokea  na kumegeka kwa kanisa.  Mmeguko huo uliongozwa na Novatiano  katika karne ya tatu na Donato karne ya nne. Kugawanyika huko kulitokana na kurejeshwa kwa  viongozi na wamini waliokuwa wameikana imani katika kipindi cha mateso. Pia makundi haya yalijitenga kutokana na kuona wakristo wengi walikuwa wanaishi maisha machafu kama wapagani waliokuwa wanawazunguka.

v UASI WA  NOVATIANI.
 Katika karne y tatu askofu wa Rumi aliyeitwa Kalisto alitangaza kwamba dhambi yoyote ili inaweza kusamehewa kiwa mkosaji anaonesha toba ya kweli.Fundisho hili lilienea sana. Wakristo waliokuwa wameikana imani yao wakati wa mateso walitaka kurudi kanisani na askofu Kalisto alikubali kuwapokea watu hao.
Kiongozi mmoja wa kanisa aliyeitwa Novatiani, hakukubaliana na jambo hilo na alilipinga vikali na akaungwa mkono na wachungaji wengine ambao nao walikuwa kinyume na maamuzi hayo ya askofu. Walijitenga na kanisa    na kuanzisha ushirika wao.  Novatiani alichaguliwa kuwa kiongozi wao.

v UASI  WA DONATO.
Mmeguko wa kanisa chini ya uongozi wa Donato ulitokea Afrika ya kaskazini karne ya nne baada ya utawala wa mfalme Deokletiani. Mfalme huyu katika kipindi cha utawala wake alikuwa na mpango wa kufuta ukristo na kuchoma moto Biblia zote. Wakati wakipindi  cha mateso makali baadhi ya viongozi wa kanisa waliasi imani wakaamua kutoa maandiko matakatifu (Biblia) yateketezwe ili kujinusuru na kifo.

Baada ya kipindi cha mateso kumalizika viongozi hao yaani wachungaji na maaskofu walioasi walitaka kurudi kanisani. Kanisa katoliki  lilikuwa limekubali kuwapokea. Kanisa lilikubali kuwarudishaviongozi hao katika sharika zao. Katika mji wa Karthegi waamini wengi sana walikataa kuongozwa na mtu aliye mkana Yesu na kutoa Biblia kwa serikali ili  ziteketezwe.
Donatusi alikuwa kiongozi wa mgomo huo na alipata wafuasi wengi. Watu hao walijitenga na kanisa na kuanzisha huduma yao. Kulikuwa na ugomvi kati ya wakatoliki na wadonato kwa kwa muda mrefu.

K.  HALI YA KANISA KATIKA KIPINDI CHA   MWISHO WA KARNE YA PILI:
Kanisa lililotakasika. Mateso yaliwaondolea mbali wale ambao hawakuwa waaminifu katika imani yao. Wale ambao hawakuwa na imani kamilifu na waliojiunga na kanisa kwa masilahi yao binafsi.
Mafundisho yenye  mfumo mmoja. Japokuwa kanisa lilihusisha watu wa tamaduni , rangi na jamii mbalimbali bado lilikuwa na umoja wa imani wa ajabu katika kanisa lote. Walifuata mafundisho ya mtume Paulo, Petro na wengine. Mdo 2:42.
Kanisa lenye muundo: kazi iliyofanya na Paulo ya kuweka viongozi wa Kanisa katika kila mji ilileta ufanisi. Viongozi hao walikutana katika mikutano   na kujadili  mambo mbalimbali muhimu kuhusu kanisa. Hii ilisababisha kutokea kwa ushirikiano imara wa kimataifa.(International Fellowship) ambao umekuwepo mpaka  sasa.
Kanisa lenye  kusitawi {kukua}. Licha ya mateso yaliyolikumba kanisa, kanisa liliendelea kukyua kwa kasi. Kanisa lilikumbana na mateso makali chini ya watawala mbalimbali wa Kirumi, lakini kanisaliliendelea kukabiliana na mateso hayo na likawa tayari kuwapelekea watesi hao Injili ya uzima.
Hakika Malango ya kuzimu hayakulishinda kanisa
KUANDIKWA  KWA AGANO JIPYA. Hatuwezi kueleza kwa udhahiri au kikamilifu   kwamba ni lini hili lilifanyika. Baadhi ya vitabu   kama  vile nyaraka za Paulo zilikubaliwa kila mahali, wakati vingine kama vile Waebrania, Yakobo na Ufuno wa Yohana vilikubaliwa Mashariki peke yake na kukataliwa Magharibi.
Kanisa la mashariki lilikubali baadhi ya vitabu  ambavyo havipo katika Biblia. Baadhi ya vitabu  hivyo  ni  Waraka wa Balnaba, Mafundisho ya mitume kumi na wawali  na Ufunuo wa mtume  Petro. Mabaraza yalikutana mara kwa mara ili kutambua ni vitabu gani vilivyokuwa vimevuviwa  na vipi havikuvuviwa. Inadhaniwa  kwambaAgano jipya halikutambuliwa rasmi mpka baada ya mwaka 300 B.K



















MADA YA NNE
KIPINDI CHA  PERGAMO

 KANISA LA   KIFAHARI/KITAIFA.

A.    UTANGULIZI.
KIPINDI: Toka  patano  amani la mfalme  Kostantino  (313 BK) hadi kuanguka kwa dola ya Rumi  mnamo mwaka 476 BK.

B.    USHINDI WA WAKRISTO
Baada ya miaka miambili ya mateso kanisa liliishinda dola ya Rumi na kupata amani. Mfalme Deokletiani katika utawala wake aliweka watawala  wasaidizi katika majimbo yake kutokana na ukubwa wa dola  ya Rumi.  Baba wa Kostantino alikuwa ni mmoja wa watawala wasaidizi, aliongoza majimbo ya Galia, Uingereza na Hispania, Baada ya kufa kwa watawala wasaidizi kulitokea na kugombea  madaraka baina ya watoto wao.

Baba wa Kostantino alipofariki Kostantino alitangazwa kuwa mtawala badala ya baba yake, na hivyo watoto wa watawala wengine waliamua kuanzisha mapigano ili kuuchukua utawala huo. Miongoni mwa hao waliokuwa na nguvu ni Maksentio, huyu alikuwa ni mtu aliyeshabikia mauaji ya wakristo. Walianzisha mapigano huko Italia maili kumi kutoka Rumi mnamo 28.10.  312 BK

Wakiwa katika eneo la mapigano kabla ya vita kuanza Kostantino aliona alama ya msalaba angani ikiwa imeandikwa maneno  yafuatayo, “Kwa alama hii utashinda”. Kostantino aliitikiakwa sala na akaifanya alama ya msalaba kuwa nembo ya Jeshi lake na walipokuwa vitani Kostantino aliwashinda kabisa maadui zake, adui yake mkuu Maksentio alikufa katika vita hiyo, hivyo Kostantino akawa mshindi.
Kostantino alitambua kwamba msalaba ilikuwa ni alama ya wakristo na hivyo Mungu wa wakristo ndio aliyekuwa amemsaidia katika vita hiyo. Mwaka uliofuata Kostantino alitangaza PATANO LA AMANI na Wakristo, (Edict of Torelant).  Patano hili  lilikomesha mateso juu ya wakristo katika dola yote ya Rumi. Patano hili lililowaletea amani wakristo katika dola ya Rumi lilikuwa na matokeo chanya na hasi katika kanisa.

C.    MATOKEO YA TAMKO LA AMANI
Matokeo ya  patano  la amani yanaweza kuainishwa katika pande mbili ambazo ni matokeo mazuri na matokeo mabaya;
I.                MATOKEO MAZURI,
1.     Mateso juu ya wakristo yalikomeshwa.
2.     Makanisa yaliyokuwa yamebomolewa wakati wa mateso yalijengwa tena kwa fedha ya serikali.
3.     Maaskofu na wachungaji walisamehewa kodi.
4.     Watumishi wa kanisa walianza kufadhiliwa na serikali na hawakutakiwa kuhukumiwa kwa sheria za kawaida.
5.     Wakristo waliruhusiwa kujenga  makanisa mahali popote katika dola ya  Rumi.
6.     Dhabihu za kipagani zilikomeshwa.
7.     Kostantino alijenga makanisa makubwa katika miji ya Yerusalemu, Bethlehemu na katika mji wa Kostantinapoli  ambapo ndio uliokuwa makao makuu yake mapya.
8.     Kusulubiwa kwa wahalifu na desturi  za kuua watoto wasiotakiwa zilikomeshwa.
9.     Watumwa waliachiwa huru.
10.  Siku ya jumapili iliwekwa kuwa siku ya mapumziko kwa watumishi wa serikali.
11.  Alisaidia kuunda umoja wa kanisa kupitia mikutano mbalimbali aliyoiitisha, mfano mkutano wa Naikea mwaka 325 BK.
12.  Alikusudia kuufanya ukristo ukubaliwe na serikali kama dini zingine.

II. MATOKEO MABAYA.
1.     Ilikuwa ni fahali kuwa mkristo, hivyo watu wengi walijiunga na ukristo kwa maslahi binafsi.
2.     Watu walijiunga na ukristo ili waweze kupata vyeo katika kanisa na serikali.
3.     Maadili ndani ya kanisa yalianza kumomonyoka.
4.     Mambo ya kiroho yaliachwa kupewa kipaumbele na badala yake programu mbalimbali zikapewa kipaumbele.
5.     Sherehe na tamaduni za kipagani polepole zilihamia kanisa, kwa kubadilishwa jina na malengo na badhi zilibadilishwa kuwa  sikukuu za kikanisa,  mfano Krismasi.(Kuabudiwa kwa bikira Maria kuliasiliwa kutoka ibada za kipagani za kuabudu miungu , Zeusi, mungu wa uzuri wa warumi na Diana  mungu mwezi).
6.     Katika jimbo la mashariki serikali ililitawala kanisa mpaka likapoteza  nguvu na maisha ya kiroho.
7.     Katika jimbo la magharibi kanisa lilipata nguvu dhidi ya serikali.

WATAWALA WALIOFUATA BAADA KOSTANTINO

Kostantino hakutaka kutumia nguvu katika kuwafanya watu kuwa wakristo, alitaka jambo hili lifanyike taratibu na kwa uchaguzi wa mtu mwenyewe, jambo hili halikufuatwa na watawala waliofuata baada yake.

Baada ya utawala wa Kostantino watawala waliofuatia walikuwa wakali mno walipiga marufuku ibada za kipagani na waabudu dini hizo walihukumiwa kifo na mali zao zilitaifishwa. Walivunja mahekalu ya kipagani, watawala wakristo kwa kutumia jina la ukristo sasa walitumia  njia zilezile mbaya zilizokuwa zimetumiwa na serikali kulitesa kanisa kuwatesa wapagani.


D.    AINA MBALIMBALI ZA MATESO.
·       Katika kipindi cha Efeso kanisa liliteswa na wayahudi.
·       Katika kipindi cha Smirna kanisa liliteswa na  dola ya Rumi.
·       Katika kipindi  cha Pergamo ugomvi ulizuka miongoni mwao wenyewe (wakristo).

F.     UMOJA NA UTAWALA WA KANISA.
Kanisa lililazimka kuwa na umoja kamili ili liweze kuwa na nguvu ya kukabiliana na mateso yaliyoliandama na uzushi uliokuwa unajitokeza. Hivyo kanisa lilipambana na maadui wakubwa wawili ambao ni mateso na mafundisho potofu.
Kutokana na uzushi kutokea,  kanisa ilibidi liwe na utambulisho au jina litakalowa tofautisha  na makundi ya uzushi, hivyo kanisa lilianza kijiita Katoliki.
Jina katoliki linatokana na neno la kiingereza universal, lenye maana   ya popote au ya mahali popote” Kanisa lilianza kutumia jina Katholiki kwa maana mbili, ambazo ni:
1.     Kanisa lisilo na mipaka ya majimbo au ya nchi.Kanisa moja lililo katika nchi zote ulimwenguni.
2.     Kanisa leye mafundisho sahihi.


v SABABU  ZA KANISA KUHITAJI UTAWALA WENYE NGUVU.
1.     Kutokea kwa ukiri wa imani.
2.     Kutokea kwa Kanuni Ya Maandiko Matakatifu.
3.     Kutokea kwa maaskofu waliopewa mamlaka ya kutunza mafundisho yaliyotokana na mitume wa kwanza.

v Ukiri Wa Imani.
Huu ulikuwa ni ushuhuda mfupi uliotumiwa katika kazi za kawaida sharikani kama vile ubatizo. Ukiri wa imani ulieleza kwa kifupi kile kanisa linachoamini naa ulitumika kama kiapo kuwa mtu anakubaliana na taratibu za kanisa hilo hivyo anastaili kubatizwa na kupokelewa katika kanisa.

v Kanuni  Ya Maandiko Matakatifu.
Kanuni ni kawaida inayotumiwa kupima usawa na usahihi wa kitu. Kanuni huelezea vitabu vilivyokubaliwa na kupokelewa na kanisa kama maandiko Matakatifu. Kanisa liliweka kanuni ili kubainisha kati ya vitabu vilivyokuwa ni neno la Mungu na vile visivyokuwa Neno la Mungu. Mfano wa vitabu visivyokuwa neno la Mungu ni vile vilivyoandikwa na wanosti.

Makundi ya uzushi kama vile wanostika na Marsion waliharakisha kutungwa kwa kanuni hii.
Mababa wa kanisa walitumia kanuni mbalimbali katika kuvibaini vitabu hivyo. Baadhi ya njia hizo ni kumtambua mwandishi kama alikuwa ni mtume au la, Kupokelewa kwa kitabu na  watu walionadikwa kwa mara ya kwanza na matumizi ya kitabu hicho katika makanisa mbalimbali na mamlaka ya kitabu chenyewe N.k

v Haja Ya Kutokea Kwa Viongozi Wenye Mamlaka.
 Maaskofu walitokea kama watu wenye mamlaka ya kutafasili maandiko na kufundisha wazi mafundisho ya mitume. Neno askofu maana yake ni mwangalizi/msimamizi. Neno hili hapo awali lilitumiwa na watu wote na kulikuwa na maaskofu katika idara mbalimbali za serikali, baadae matumizi ya istilahi hii yalibakia katika Kanisa tu.
Uaskofu ulisaidia kuleta utawala wenye nguvu na umoja katika kanisa kupitia mambo mawili ambayo ni mafuatano ya mitume na ibada.

·       Mafuatano Ya Mitume
Ilidaiwa kwamba maaskofu  walikuwa badala ya mitume.  Kwa namna fulani uaskofu  ulitokana na mitume, yaani maaskofu waliwekwa na mitume kuwa watawala katika kanisa na mamlaka ya utawala wao ilihusisha kuhubiri na kuitetea Injili.

·       Umoja Wa Ibada
Ibada mbalimbali zilizokuwa zikifanywa na kanisa kwa pamoja zilisaidia kukuza umoja wa kanisa na kutokea kwa viongozi wenye mamlaka. Kulikuwa na ibada mbalimbali ambazo zilifanywa na kanisa, baadhi ya ibada hizo ni ibada ya ubatizo na ibada ya meza ya Bwana. Pia kanisa liliadhimisha sikukuu mbalimbali ambazo pia kwa namna fulani zilichangia kukuza umoja wa kanisa.


G.   MABISHANO YA KITHIOLOJIA.
Mabishano ya kithiolojia yalisababishwa na mitazamo mbalimbali ambayo wakristo walikuwa nayo juu ya Yesu Kristo. Baadhi ya mitazamo hiyo ni .

v Uungu wa Yesu Kristo.
Wakristo  wa awali walimpa Yesu heshima  kwa kumwita majina mbalimbali kama vile Masihi, Kurios, Kritos na Logos.
Jina la Logosi lilitokana na falsafa za kigiriki, Kutokana na falsafa hizo Logos ilikuwa ni njia ya Mungu kufanyika mwili na kukaa na watu hapa duniani. Hivyo wakristo wa awali walimtambua Yeus kama Mungu.

v Kristo kama Logosi.
Katika kipindi cha karne ya pili na ya tatu karibu wanazuoni wote wa kikiristo walifundisha kwamba Kristo alikuwa ni Logos.  Kulikuwa na mwanazuoni moja aliyeitwa Yustini Shahidi ambae aliweka mkazo kuwa Logos alikuwa ni Mungu wa pili.
Wanazuoni wengine waliweka mkazo katika umoja wa Yesu.Walikubali kwamba Logos amefanyika kuwa mwili katika Yesu  Kristo lakini alikuwa ni Mungu halisi, Mungu mwana ndiye aliyefanyika mwili, si Mungu wa pili. Kulingana na mtazamo waYustini  ni dhahiri  kwamba alikana ubinadamu wa Yesu. Yesu kama Logos alikuwa Kweli Mungu na mwanadamu kweli.

v Monarchianism. Dhana ya Mungu mmoja.
 Kulikuwa na wanazuoni wengine waliopinga mafundisho ya kumhusisha Yesu na Logos kwa sababu jambo hili lilielekea kupinga imani yakuwa  Mungu ni mmoja. Wanazuoni hao waliona kwamba dhana ya utatu wa Mungu ilielekea kuwa ni uzushi wa kuwa na miumngu mingi.
Wamonarchianism waligawanyika katika makundi mawili ambayo ni;
1.     Wamonarchianism wa kimabadiliko,  hawa walikuwa na mtazamo wenye kumwona Yesu kama mwanadamu pekee tu, ambae hakuwa Mungu aliyefanyika mwili. Kundi hili liliongozwa na Askofu Paulo Samosota wa Antiokia.
2.     Wamonarchianism wa kimfano.  Hawa waliona kuwa hakuna tofauti kati ya baba na mwana. Baba ndiye aliye vaa mwili. Kwa hiyo majina haya baba, mwana na Roho mtakatifu yalitumika kuonesha kwetu njia au hali tatu Mungu alizotumia kujidhihirisha. Hivyo hakuna nafsi tatu bali ni nafsi moja. Kundi hili liliongozwa na Sabelio.
Baada ya mateso kukoma katika kanisa kulitokea mgogoro mwingine ndani ya kanisa uliohusisha mgongano wa kimafundisho (doctrinal controversals).
Baadhi ya viongozi wa kanisa walianza kuibuka na mafundisho yaliyoonekana kuwa mageni katika kanisa na hivyo walihukumiwa uzushi na kutengwa na kanisa.
Wakristo walitumia muda mwingi kujadiliana wao kwa wao badala ya kuipeleka Injili mbele.  Katika moduli hii tutajadili badhi tu ya mabishano ya kithiolojia  yaliyotokea ndani ya kanisa.





1.     Mabishano Baina  Ya Mchungaji  Ario Na Askofu Alexander.
Ario alimshutumu askofu wake kuwa alikuwa anaweka mkazo sana juu ya uungu wa Yesu katika mafundisho yake. Alexander alifundisha kwamba mwana ni wa milele sawa na baba. Ario alipinga fundisho hilo yeye alidai kwamba baba ni wa milele lakini mwana alikuwa na mwanzo wake. Kuna kipindi  ambapo mwana hakuwapo. Askofu Alexander aliitisha mkutano wa sinodi huko Iskanderia ili kujadili suala hilo na hatimae Ario alitangazwa kuwa mzushi na alitengwa na kanisa.

Ario aliungana na Askofu Euzebio wa Nikomedia na wakaandika  nyaraka mbalimbli ambazo zilitetea fundisho lao na wakazisambaza maeneo mbalimbali ili ziendelee kusomwa na wakristo mbalimbali.
v Mkutano Wa Naikea.
 Baada ya nyarakahizo kusomwa majadiliano miongoni wa viongozi wa kanisa yalipamba moto na kuleta mgawanyiko ndani ya kanisa. Mfalme Kostantino hakupendezwa na mgogoro huo ulioleta mgawanyiko miongoni mwa wakristo hivyo aliwaomba viongozi hao wapatane na  iliposhindikana kupatana kwa viongozi hao, mfalme akitumia nguvu ya dola aliamua kuitisha mkutano wa viongozi wote wa kanisa toka seheu mbalimbali ili aweze kuwapatanisha. Mkutano huo ulifanyika mwaka 325BK katika mji wa Naikea na hutambulikana kama mkutano wa kwanza wa kanisa zima, kwa sababu ulihusisha viongozi mbalimbali toka sehehemu mbalimbali.

Katika mkutano huo Askofu alexender alishinda kwa hoja na hatimae Ario alitangazwa kuwa mzushi na akatengwa na kanisa. Katika kipindi hiki kanisa lilitunga ukiri wa imani ambao ulipaswa kutumiwa na makanisa yote. Ukiri huo ulikweka mkazo katika uungu wa Yesu kuwa Yedu ni sawa na  baba.
Mkutano wa Naikea haukuweza kumaliza majadiliano na badala yake uliyachochea kwani majadiliano hayo yaliendelea kwa muda wa miaka therathini na tano baada ya mkutano wa Naikea. Baadhi ya viongozi wa kanisa walitiria mashaka ukiri wa Naikea kwasababu hawakuuzoea.

v Mkutano Wa Kostantipali
Kutokana na majadiliano hayo  ya muda mrefu na makali kulikuwepo na haja ya kuitisha mkutano mwingine wa kanisa zima. Mkutano hu uliitishwa katika mji wa Kostantinopoli mnamo mwaka wa 381 BK. Katika mkutano huu walifanya marekebisho kidogo ya ukiri wa imani wa Naikea.

Mkutano Wa Efeso.
Baada ya Apolinari kuhukumiwa uzushi,  kuliendelea mabishano makali katika kanisa.  Baadhi ya mabishano hayo yalikuwa baina ya askofu Sirilo wa Iskandelia na askofu Nestori wa Kostantinopoli.
Sirio alipinga fundisho la Apolinari  Aliona kwamba uungu na ubinadamu wa Yesu  kuwa ni hali mbili zisizo weza kutenganishwa . Alipokuwa anataka kueleza uungu wa Yesu alianza kwa kumwita bikira Maria ‘Theotokos’ yaani mama wa Mungu.
Askofu Nestori alibaini uzushi katika maelezo ya Sirilo, yeye alipendekeza  Mariamu aitwe mama wa Kristo. Maaskofu hao walishambuliana vikali sana kwa maandishi. Shauli hilo lilipelekwa kwa askofu wa Rumi ili aweze kutoa uamuzi. Askofu wa Rumi alimpa ushindi Sirilo na kumtangaza Nestori kuwa mzushi.Hayo yalifanyika katika mkutano wa tatu wa kanisa uliofanyika katika mji wa Efeso mnamo mwaka 433 BK.



2.      Majadiliano Ya Apolinari.
Apolinari alikuwa ni askofu wa Laodikia.  Askofu huyu  alijaribu kueleza uhusiano uliopo baina ya hali mbili tofauti alizo nazo Yesu.  Yaani hali ya uungu na hali ya ubinadamu.
Yeye alikuwa na mtazamo wa kwamba mwili wa Yesu ni ubinadamu na akiri na roho yake ni Logosi aliyefanyika mwili. Katika kueleza fundisho hilo askofu huyu alikaza uugu wa Yesu  uliokana ubinadamu wake. Kutokana na fundisho hili Apolinari alitangazwa kuwa mzushi  katika mkutano wa Kostantinopali mnamo mwaka 381BK.

3.     Mabishano Ya Pelegio.
Pelegio alikuwa ni mmonaki, mwingereza aliekuja Afrika Kaskazini kwajili ya kuhubiri Neno la Mungu katika kanisa la Afrika ya Kaskazini.
Peregia alifundisha kwamba mtu harithi dhambi  toka kwa Adamu, lakini kila mtu ni lazima afanye uchaguzi yeye mwenyewe.
 Pelegio alipingwa vikali na Agustino mkuu  kwa mafundisho yake. Agustino alifundisha kwamba Adamu alipotenda dhambi alikiwakilisha kizazi chote cha binadamu na kwamba mtu hawezi kuokolewa kwa uchaguzi wake mwenyewe, bali ni kwa  mapenzi ya Mungu na kwamba neema ya Mungu haiwezi kukataliwa na wanadamu.
Mafundisho ya pelegio yalipingwa vikali na kanisa na kuonekana ni uzushi. Kanisa lilikubalia na na   ya mafundisho ya Agustino mkuu.



H.     KUZUKA KWA UMONAKI.
Utawa au umonaki ulianza katika karne ya tatu BK. Kabla ya  kipindi hicho wakristo waliishi katika jamii na familia. Mara baada ya ukristo kushamiri mambo ya dunia yalianza kuingia kanisani, baadhi ya wacha Mungu hawakuridhika na hali hiyo hivyo waliamua kujitenga na kukaa peke yao nje ya mji katika mapango au katika nyumba walizokuwa wamejijengea. Nyumba hizo zilijulikana kama nyumba za watawa maarufu kama  Monastery.
 Baadhi ya mambo yaliyochochea kuanzishwa kwa utawa ni mvuto wa Injili, maovu kukithirikatika kanisa na falsafa ya uovu wa mwili. Kulikuwa na watu ambao waliuza kila kitu walichokuwa nacho wakawagawia maskini na kisha wakajitenga na kuamua kuishi maisha ya kimasikini  mbali na jamii yao. Baadhi ya watu hao ni;
v Antoni Mtawa Wa Kwanza.
 Mtu huyu alikuwa ni mwenyeji wa Misri na ndiye mwanzilishi wa utawa. Antoni aliuza kila kitu alichokuwa nacho na kuwagawia maskini mali zake na kisha akaishi  nje ya mji  akilima na kuwapatia maskini chakula alicholima.Baada ya muda alijitenga na  kuishi peke yake  pangoni mlimani. Watu mbalimbali walimwendea huko pangoni ili kujifunza na kisha alifanikiwa kupata wafuasi ambao nao waliamua kuungana nae kuishi maisha ya utawa. Alipat wafuasi karibuni elfu mbili. 


v Pokomeo Mwanzilishi Wa Nyumba Za Utawa.
 Huyu alikuwa mdogo wa Antoni  na ndie aliyeanzisha nyumba za  utawa.  Yeye alijenga boma kubwa ambalo wafuasi wake waliishi ndani wakijitenga na mambo ya ulimwengu. Watawa hawa walijishughulisha na ibada na kazi, utawa huu ulikaza ushirika na ulipendwa na watu wengi.

Jerome (Hironimo)
Utawa ulienea sana sehemu ya magharibi kwa njia ya Jerome. Mtu huyu alikuwa na uwezo mkubwa kufasiri Maandiko na alifanywa kuwa katibu wa Papa wa Rumi kwa kipindi kirefu. Aliishi maisha ya kujikana. Alisema “ Mtu asieoa hujipatia sifa ya pekee mbele a Mungu. Alikiri kuwa kwa wazi kabisa kwamba  “ Maisha ya utawa hayawezi kuondoa majaribu yote”  Alidai kwamba alipokaa katika boma la utawa huko mlimani bado aliwaza  juu ya wasichana wa Rumi.
Jerome alikuwa fundi wa Maandiko na elimu. Alitafsiri Biblia kwa lugha ya Kilatini iliyojulikana kwa jina la Vulgate. Tafsiri inayopendwa sana na wakatoliki wa Rumi mpaka sasa.
Yeye alishirikiana na wanawake watawa kutunza yatima Huko Bethrehemu na Palestina. Walikuwa na nyumba mbili za watawa, moja ikiwa ya watawa wa kiume na nyingina ya watawa wa kike.



Benedikto   Mwanzilishi Wa Kanuni Za Utawa.
Benedikto wa Nusia alianzisha shirika la utawa huko Monte Kasino Italia.  Yeye aliweka mkazo katika umoja. Aliweka uongozi uliosimamia nyumba zote za utawa. Aliona kuwa kila nyumba ya utawa ni jeshi la Yesu waliotayari kumtumikia wakati wowote.
Kiongozi wa kila nyumba ya utawa aliitwa Aboot, na watawa wote walipaswa kumtii. Aliweka mpangilio mzuri wa saa za ibada, sala na kusoma. Nyumba za kanuni za Benedikto zilikuwa mahali pa kuu pa elimu na kilimo. katika majimbo mengi Ulaya.


v Faida Za  Utawa.
1.       Ulifanyika kuwa  vituo vya  wakimbizi.
2.     Walitoa msaada kwa watu wenye mahitaji , mfano kusaidia maskini na wasiojiweza.
3.     Walileta mchango mkubwa katika kuinua kilimo.
4.     Walikuza elimu kwani watawa walitumia muda mwingi katika kusoma na kuandika maandiko mbalimbali.
5.     Walipeleka wamishenari katika mataifa mbalimbali kueneza  Injili.
6.     Walitoa viongozi bora katika jamii na katika kanisa.
7.     Walitafsiri Mandiko katika lugha mbalimbali.

v Madhaifu Ya Utawa.
1.     Mkazo wa juu ya kuishi maisha ya useja.waliwakataza wafuasi wao wasioe wala kuolewa.
2.     Upendeleo na anasa. Baada ya utawa kupata umaarufu, walianza kuishi maisha ya anasa na kukwepa kulipa kodi.




I.       KUANGUKA  KWA DOLA YA RUMI
Mfalme Kostantino mara baada ya kuingia katika utawala alihamishia mako makuu ya dola ya Rumi katika mji wa Kostantinopoli. Tutatazama  namna Rumi ilivyokuwa makao makuu ya kanisa. Wakati kanisa la Orthodox la mashariki lilikuwa likitawaliwa na serikali, Patriaki wa Rumi alidai kuwa na  mamlaka katika kanisa lote la ulimwengu wa magharibi, ambao ulikuwa kupitia kanisa la Katoliki la Rumi. Hii iliwezekana kwa   sababu kadhaa, badhi zikiwa ni;

Kufanana kiutawala. Kulikuwa na mazoea kuongoza kanisa   kwa mfumo wa kiserikali ambapo kunakuwa na kiongozi mkuu mmoja anaetakiwa kusikilizwa .  wakati huu kulikuwa na maaskofu karibu kila mji, ambao katika miji mikubwa waliitwa Patriaki (patriarch) yaani baba mkubwa. Kulikuwa na mapatriaki katika miji ya Yerusalemu, Antiokia, Iskanderia, Rumi na Kostantinopali.
 Kulikuwa na mashindano ya kugombea ukuu miongoni mwa mapatriaki. Swali lilikuwa nani angekuwa kiongozi mkuu wa kanisa lote ulimwenguni. Rumi ikiwa imetengeneza njia ya kuwa makao makuu ya kanisa ilikuwa na viongozi bora. Kwa muda  mrefu kanisa la Rumi lilikuwa imara. Lilisimama kidete kupinga mafundisho  potofu. Kanisa la Rumi liliihudumia Jamii kiroho na kimwili kwa kuanzisha kazi za kijamii dunia nzima.  Nyumba za utawa, shule na hospitali zilianzishwa katika maeneo mbalimbali, jambo hili lililipa umaarufu kanisa la Rumi. Wamishenari walitumwa katika ulimwengu mzima wa wakati ule kueneza Neno la Mungu.

 Wakati nguvu  ya kanisa ilikuwa inakua, nguvu ya dola iliendelea kuzorota, nguvu ya kisiasa ya Rumi ilizidi kuporomoka.
Kwa muda mrefu wa utawala wake dola ya Rumi ilikuwa imetajirika sana.   Maadui zake waliokuwa wanaishi jirani nae waliutamani utajiri wa wake.  Maadui hao waliivamia Rumi ambayo sasa haikuwa na uzoefu wa kivita. Baadhi ya maadui walioivamia Rumi na kuishambulia  dola ya Rumi ni wavisigothi, wasaksoni,  wavandali, , wahuni, wabarigandiana na wafranka. Uvamizi wa mataifa haya ulipunguza nguvu ya dola ya Rumi.

 Janga lingine lilikuwa ni vita ya wenyewe kwa wenyewe, baina ya wanachama wa seneti  kugombania kiti cha utawala. Kabila la kijerumanilililojulikana kama Herulisi liliivamia na kuishinda dola ya Rumi mnamo mwaka 476 BK.















MADA YA TANO
KIPINDI CHA THIATIRA;    KANISA   LA NYAKATI ZA GIZA.
KIPINDI. Tangu kuanguka kwa dola ya Rumi hadi kuanguka kwa Kostantinopoli.


A.    UTANGULIZI
Katika kipindi cha Pergamo tuliona jinsi Patriaki wa Rumi alivyochukua   mamlaka ya uongozi wa kanisa na kuinuka kwa Rumi kuwa makao makuu ya kanisa. Tuliona jinsi mafundisho potofu   pamoja mambo ya kipagani yalivyoingia kanisani 
Haikutosha kwa Patriaki wa Rumi kuwa Askofu mkuu wa kanisa lote duniani na kuwa na mji wa Rumi kama makao makuu ya kanisa lote duniani, baada ya hapo alijitangaza kuwa kiongozi wa mataifa  kwa njia ya kukuza upapa katika karne kumi za kipindi cha giza.  Kipindi cha giza kilikuwa na hatua tatu ambazo ni, kukua, kusitawi na kuanguka.

1.     Kukua.
Gregori I alipokuwa kijana aliteuliwa kuwa msimamizi wa majengo na vyakula katika  Mji wa Rumi. Baada ya kifo cha baba yake aliamua kutoa kwa kanisa mirathi ya babaye. Mnamo mwaka 578 BK Gregori I aliteuliwa na papa kuwa balozi wake katika mji wa Kostantinopali. Mwaka 585 hadi 590  BK alikuwa msaidizi wa papa huko Rumi na kiongozi mkuu wa Monastery(nyumba za utawa). Baada ya papa Pelegio II kufariki dunia kwa ugonjwa wa tauni mwaka 590 BK, Grogori I aliteuliwa  na umati wa watu huko Rumi kuwa Askofu badala ya Peregio II.

 Kukua kwa nguvu ya upapa kulianza   baada ya Gregori I  kushika wadhifa wa upapa katika mwaka wa 590 BK.  Mfumo wa kubadilisha majina mtu alipokuwa anaingia katika nafasi ya upapa ulianza katika kipindi hiki. Gregori aliitwa mkuu kwa sababu ya mafanikio yake ambayo baadhi ni,
1.     Alitumia uwezo   wa kikanisa katika kuwasaidia watu, (kuwapa chakula na nguo).
2.     Serikali ilipolega aliimarisha ulinzi katika mji wa Rumi.
3.     Alimtambua papa wa Rumi kuwa na mamlaka juu  ya viongozi wengine wote wa kanisa.
4.     Alilipatia kanisa nguvu ya kisiasa na kidini.
5.     Alitengeneza dogma ya kanisa.
Kutokana na misaada   ya kijamii aliyokuwa anaitoa  papa Grogori I, wanachi wa Rumi walianza kumheshimu  na kumhesabu kama kiongozi wao. Hivyo basi Gregori Mkuu aliimarisha nguvu ya upapa katika mambo ya kidini na kisiasa pia.

v Sababu za kukua kwa upapa
Mbali   na mchango wa Gregori Mkuu katika kukuza nguvu ya upapa kulikuwa mambo mengine kadhaa yaliyopelekea kukua kwa upapa katika kipindi hiki. Baadhi ya sababu hizo ni:
1.Nguvu ya haki,  kanisa liliwatetea raia dhidi ya watawala dharimu  hivyo likapendwa na watu.

Kuzolota kwa serikali, Wakati serikali inazolota kanisa lilizidi kujiimarisha, kiuchumi na kijeshi hivyo viongozi dhaifu walihitaji msaada wa kanisa katika kupambana na  adui zao hivyo kanisa likazidi kuwa na mamlaka na nguvu ya ushawishi.
2.     Ulaghai, Kanisa lilitumia kigezo cha ujinga wa watu  kujipatia mamlaka. Kanisa lilitengeneza nyaraka mbalimbali zenye kulipa mamlaka ya kiutawala na kudai kwamba ziliandikwa na wahusika walioandikwa kumbe sivyo. Zifuatazo ni baadhi ya nyaraka hiz
v Waraka wa mfalme Kostantiono kwa askofu Silvesta (314-335 BK). Huu ulikuwa ni waraka uliogushiwa na kanisa kwamba uliandikwa na Kostantino kumpa mamlaka ya kiutawala  askofu wa Rumi (Silvesta) juu ya wafalme wote wa Ulaya na Ulaya nzima.

v Tamko la uongo la Isodore(850 BK). Kulikuwa na maandiko yaliyokuwa yanadai kwamba askofu wa Rumi alikuwa amepokea waraka toka kwa mitume uliokuwa  unamtangaza asofu wa rumi kuwa askofu wa kanisa dunia nzima na kwamba kanisa lilitangazwa kuwa huru (yaani kanisa kutokuwa chini ya serikali).




2       KUSITAWI KWA UPAPA (1073- 1216 )
Nguvu ya upapa ilifikia kilele chake katika utawala wa Gegori VII ambaye pia alijulikana kama Hildebrand. Katika kipindi hiki  upapa ulikuwa na nguvu kamili  kikanisa na kiserikali katika mataifa yote ya kule Ulaya.
1.     Papa Gregori VII alifanya matengenezo ya ukreli na kukataza ndoa kwa wakreli.
2.     Aliliondoa kanisa chini ya utawala wa serikali, kanisa likaanza kujitawala, alifuta suala la maaskofu kuteuliwa na watawala wa serikali (wafalme).
3.     Alilifanya kanisa kuwa juu ya selikali.

v Papa Innocent III  (1198 -1216).
 Huyu alikuwa ni papa mwingine mwenye nguvu kubwa. Katika siku yake ya kutawazwa kuwa papa alitoa usemi  wenye maneno yafuatayo.
  Mahalifa wa mtakatifu Petro  wako katikati ya Mungu na watu; wadogo kuliko Mungu lakini wakubwa kuliko watu,  wenye uwezo wa kuwahukumu watu wote lakini wasioweza kuhukumiwa na  yeyote”

Katika barua yake ya kiofisi aliandika “ papa hajapewa mamlaka  kwa kanisa pekee bali kwa ulimwengu mzima. Akiwa na haki ya  kuwaondoa na kuwaweka watawala katika uongozi. Papa innocent III alijitwalia mamlaka ya serikali ya mji wa Rumi  akijifanya yeye mwenyewe kuwa bwana kwa kuanzisha  nchi ndani ya nchi  ijulikanayo kama nchi ya Vatikani.hivyopapa akawa kiongozi wa kidini na kiserikali.



3       KUANGUKA KWA UPAPA.
Kuanguka kwa upapa kulianza wakati wa  papa Bonifasi VIII katika mwaka 1303.  Jambo hili lilisababishwa na kuanza kuibuka kwa roho ya utaifa miongoni mwa nchi mbalimbali. Jambo hili lilileta mtikisiko dhidi ya Bonifasi VIII. Watu walianza kuwaheshimu viongozi wa nchi zao kuliko kumheshimu papa. Amri na maagizo mbalimbali ya  papa yalipuuzwa na  viongozi wa nchi. Baada ya mfalme wa ufaransa kukata kutii maagizo ya  papa, papa Alianzsha vita na  mfalme wa ufaransa na hatimae Bonifasi VII akashindwa vita hiyo na kuwekwa kizuizini mpaka mauti ilipomfika.


B.    KUINUKA KWA UISLAMU
 Kanisa lilipata mashambulizi makuu katika karne ya saba kutoka kwa waislamu. Dini ya Uislamu ilianzishwa na kijana mmoja aliyeitwa  Mohamed. Kijana huyo alizaliwa mnamo mwaka 570 BK katika mji wa Maka. Alianza kazi yake kama nabii na mwana matengenezo   kwa kuanzisha dini yake mnamo mwak 610 BK katika mji aliozaliwa. Kutokana na kutokukubaliwa na watu wa mji huo aliamua kuhamia katika mji wa Madina katika mwaka wa 622 BK.  Kipindi hicho kinaitwa  Hajira. Kalenda ya Waislamu inaanza wakati huo wa kuhama kwa Mohamed toka Maka kwenda Madina.

 Ndani ya kipndi cha miaka miambili waislamu walikuwa wameisha zishinda sehemu mbalimbali za dunia na kuanzisha dini yao ya uislamu, Uanzishaji wa dini hiyo ulienda sambamba na uanzishaji wa dola ya Kiislamu katika maeneo yoyote waliyoyashinda. Baadhi ya maeneo waliyokuwa wameyashinda na kuanzisha utawala wao ni  nchi za Mashariki ya kati, Afrika ya Kaskazini, Asia ndogo. Mouhamedi na wafuasi wake walieneza dini yao kwa kutumia upanga, mahali popote watu walipokataa kuipokea dini hiyo walilazimika kutumia vita na nguvu ya kijeshi.
Maeneo yoyote waliyofanikiwa kuyateka hatua ya kwanza ilikuwa ni kufuta dini zingine zote zilizokuwa maeneo hayo na kuwalazimisha raia wote kujiunga na dini hiyo.
Kuinuka kwa dini ya Uislamu kulichangia katika kuanguk kwa upapa na kuzoofisha nguvu ya kanisa kwa ujumla. Kwa mfano Afrika kaskazini kanisa lilizoofika na hatimae likafifia kabisa.



C.    KUTENGANA KWA KANISA  KATOLIKI.
Kanisa la katoliki la mashariki lile la magharibi  yalitengana rasmi mwaka 1054 BK,  japokuwa kihuduma yalitengana  tangu zamani. Daima kulikuwa na kushindania madaraka ya kwambani nani  aliyekuwa mkuu kati ya papa wa Rumi na Patriaki wa Kostantinopoli. Hatimae katika mwaka 1054 BK   makanisa haya yalitengana ramsi.


v SABABU ZA KUTENGANA
Kutofautiana kimafundisho,  Kuhusu asili ya Roho mtakatifu. Kanisa la magharibi lilidai kwamba Roho mtakatifu alitoka kwa baba na kwa mwana wakati lile la  mashariki lilidai kwamba Roho mtkatifu alitoka kwa baba pekee.
Ndoa kwa makuhani.  Kanisa la magharibi  lilikataza makuhani kuoa wakati la kanisa la mashariki liliruhusu makuhani kuoa.
 Sababu ya kisiasa,   Baada ya kuanguka kwa dola ya Rumi  mataifa ya magharibi yalitaka kuwa chini ya Kostantinopoli.
Kuabudu sanamu.Kanisa la magharibi lilianzisha matumizi ya sanamu katika ibada wakati kanisa la mashariki lilipinga matimizi ya sanamu.
Kugombea  ukuu,   Madai ya kanisa la mashariki  ya  kuwa ni kanisa la kitawala.

D.     KUSITAWI KWA UTAWA.
Mashirika mbalimbali ya kitawa yalisitawi katika kipindi hiki na yakajitolea kusaidia jamii katika maeneo mbalimbali. Baadhi ya mashrika hayo ni :
Wabenedectino walianza mwaka 529 BK
Wasisteri mwaka 1098.
Wafransiska  mwaka 1209.
Wadomeni mwaka 1215.

Kipindi cha karne za katikati kulichangia sana katika ustaarabu wa ulimwengu, hasa katika mambo ya elimu, maandiko, na mambo ya ufundi, katika kipindi hiki zilijengwa kathedro kubwa . kuna baadhi ya vyuo vikuu vikubwa vilivyojengwa wakati huu, mfano wa vyuo vikuu hivyo ni Chuo  kikuu cha Parisi huko Ufarasnsa, Chuo Kikuu cha Kambridge,   Chuo Kikuu cha Oxford, nacho vyote iwili vikiwa  huko Uingereza. Kuanzishwa kwa vyuo vikuu hivi kulipelekea elimu kukua na kuleta mtazamo mpya katika jamii kama tutakavyoangalia baadae katika kipindi kitakachofuata.


E.    WATANGULIZI WA MATENGENEZO YA KANISA.
Katika mwaka wa 1229 kanisa la Rumi  lilikataza  waumini wa kawaida wasisiome Biblia isipokuwa makuhani tu. Lugha ya kilatini iliteuliwa kuwa lugha takatifu na hivyo mtu yeyote asiyejua kilatini alizuiliwa kuhubiri.

1.     PITA WALDO.
 Katika miaka ya 1970  alitokea  mfanya biashara  mmoja aliyeitwa Pita waldo  mwenyeji wa Loyona Ufaransa. Mtu huyu alipenda kujua mambo yaliyo katka Biblia lakini hakuweza kwa sababu hakufahamu kilatini hivyo aliwaajiri  mapadri wawili wamtafsirie  Biblia katika lugha ya kifaransa.  Baada ya kusoma neno la Mungu alivutiwa nalo sana hivyo akauza kila kitu alichokuwa nacho na akala kiapo cha umaskini, akajitoa kikamilifu kuhubiri neno la Mungu.

Pita Waldo Alianzisha timu iliyoitwa  watu maskini. walianza kuhubiri, lakni walipingwa na papa. Mwaka 1184 walijitenga na kanisa  kwa sababu hawakukubali kitendo cha wao kuzuiwa kuhubiri,
Waldo alipinga baadhi ya mafundisho ya kanisa la Katoliki. Baadhi ya mambo aliyoyapinga ni    mafundisho kuhusu toharani,  misa na kwaajili ya wafu na kumwabudu Mariamu mama wa Yesu.
Watu hawa waliamini kwamba kili mtu alitakiwa kuwa na Biblia katika lugha yake ya asili na  ya kwamba Biblia ilitakiwa kuwa mamlaka ya mwisho na iliyokuu katika mambo ya imnani na maisha. Kanisa lilianzisha mateso dhidi ya wawadeni yaani wafuasi wa Waldo. Kadili walivyokuwa wanateswa  ndivyo walivyokuwa wakiongozeka. Mnamo  mwaka 1211 wawadeni themanini   walichomwa moto huko Ujerumani.  Pita waldo alisaidia kuleta matengenezo ya kanisa kwani alisaidia kupatikana kwa Biblia katika Lugha zingine na kuhamasisha kila mtu kusoma Biblia. Waldo anajulikan kama mmoja  wa  wanamatengezo ya kanisa watangulizi.


2.     JOHN WIKRIF.
Huyu alikuwa mwalimu wa Chuo kikuu cha Oxford. Mnamo mwaka 1378 Wikrif alitaka kuleta matengenezo katika kanisa kwa kuwaondoa watumishi wa kanisa waliokuwa dharimu,na kuwanyang’anya mali ambazo aliamini kwamba ndizo zilizokuwa chanzo cha watumishi hao kuwa dharimu. Alichapisha andiko lililoeleza maadili wanayotakiwa kuwa nayo watumishi wa kanisa.
Alifundisha kwamba wakati viongozi wa kanisa wanapokuwa mafisadi serikali ilitakiwa kuchukua mali zao na kuwapa watu wengine wenye nia ya kumtumikia Mungu. Katika mwaka wa 1379 alianza kupinga dogma ya kanisa  kwa kutoa madai yafuatayo;
Ø  Yesu pekee ndiye aliyekuwa kiongozi mkuu wa kanisa na si papa.
Ø  Biblia pekee ndio yenye mamlaka kuu na ya mwisho kwa waamini na si kanisa wala papa.
Ø  Kanisa lilitakiwa kuiga mfano wa kanisa la  agano jipya.
Ø   
John Wikrif kwa msaada wa tajiri Lord Cobham alitafsiri Biblia  katika lughaya kiingereza na kuisambaza katika maeneo mbalimbali . Alianzisha chama cha Wahubiri maskini na wakaanza kuzunguka katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo wakihubiri watu neno la Mungu.

Mwaka 1382 alipinga fundisho la mageuzo ya maumboya mwili na damu ya Yesu linalojulikana kama transubstan-tiation. Mawazo yake yalipingwa vikali na kanisa na serikali na akafukuzwa ukufunzi.  Mwaka 1402  Bunge La Uingereza  lilipitisha sheria ya hukumu ya kifo  kwa watu wanohubiri mafundisho kinyume na yale yaliyokubaliwa na kanisa. Wahubiri maskini waliteswa vikali sana, baadhi walifungwa nakuchomwa moto na kufukuzwa nchini. Viongozi wa kanisa walijaribu kuchoma moto Biblia zote  za Kiingereza. Wikrif alifariki mnamo mwaka 1384.
Shujaa huyu anakumbukwa sana katika historia ya kanisa kwa mchango wake wa kutafsiri Biblia katika Lugha ya kiingereza. Wikrif ndiye mtu wa kwanza kutafsiri Biblia kwa lugha ya kingereza.


3.     JOHN HUS
Huyu alikuwa ni mkuu wa chuo kikuu cha Plague huko Bohemia, mtawa  na padre wa kanisa  la Rumi la katoliki. Mwaka 1401 John Hus alipata upadrisho.  Padri huyu alipendezwa na maandiko ya John Wikrif na hivyo alianza kuhubiri  mafundisho ya mtangulizi wake Wikrif.
Alipinga mafundisho mbalimbali  yasiyo ya kiBiblia ya kanisa la Romani katoliki na akasisitiza watu kuishi maisha matakatifu. Alisisitiza kwamba Biblia ndiyo mamlaka ya mwisho  kwa mwamini na katika huduma za kanisa.
Katika kitabu chake alichoandika juu ya kanisa, alifasili kwamba kanisa ni mwili wa Kristo, na  Yesu Kristo pekee akiwa kiongozi wake mkuu. Alitetea nafasi ya ukuhani na kudai kwamba   Mungu pekee ndiye aliyekuwa na uwezo wa kusamehe dhambi. Alieleza kwamba hakuna mamlaka ya kanisa inayoruhusiwa kuanzisha mafundisho (doctrine) yaliyo kinyume na Biblia na kwamba Waamini hawatakiwi kutii  maagizo yasiyo ya kimaandiko.
John Hus Alipinga mambo yafuatayo, udharimu wa  mapadri, kuuzwa kwa vyeti vya msamaha, kuondolewa kikombe cha divai kwa walei. Baada ya mashambulizi hao mazito dhidi ya mafundisho ya kanisa  Hus alifukuzwa upadri  na akaambiwa abadilishe msimamo wake kwa kufuta kauli, jambo ambalo Hus hakukubaliana nalo. Hatimae Hus alihukumiwa kifo na akachomwa moto.  Hus akiwa anachomwa moto  alitoa unabii kwa kusema “leo mnaniua mimi lakini miaka miamoja ijayo Mungu atamwinua mtu mwingine ambaye matengenezo  yake hayaatweza kuzimwa” Kweli baada ya kipindi hicho Mungu alimwinua Martini  Luther mwana matengenezo mkuu kama tutakavyoona hapo baadae.




4.     JEROME SAVANAROLA.
Alizaliwa Ferrara Italia mnamo mwaka 1452, alikuwa ni mtawa wa shiriki la  wadominiko.Alijaribu kuleta matengenezo katika kanisa na serikali. Alipinga uovu uliokuwa unafanywa na mapapa.  Alisomea mambo ya  ubinadamu na utabibu. Kufikia mwaka 1491 alikuwa mhubiri maarufu kule Frolence.
Alitabiri kwamba papa  na mfalme wa Naples wangekufa siku moja, jambo ambalo lilitokea  kama alivyotabiri. Katika mahubiri yake alitabiri hukumu kubwa ambayo ingekuja  juu ya mji ikifuatiwa na kipindi  chema ambapo Frolence ingewaunganisha watu wote wa Itali. Utimilizo wa unabii huu ulionekana kuwa ni kuvamiwa  kwa Itali na mfalme Charles VIII. Ambaye mwaka  1494 aliuondoa utawala dhalimu wa Frolence.
Baada ya kuanzishwa kwa serikali mpya Saravano alipaata umaarufu sana pale Frolence kupitia mahubiri yake na alileta mabadiliko mengi katika jamii. Alianzisha matengenezo ya kodi, Kusaidia maskini na   matengenezo katika mahakama.  Aliubadilisha mji kutoka katika maisha  ya kimwili na kuishi maisha ya kiroho.
Kutokana na mabadiliko hayo kila mtu katika mji alikwenda kanisani na matajiri waliwapa misaada masikini.Wafanya biashara walirudisha vitu walivyokuwa wamewatapeli wateja wao. Waimbaji waliacha kuimba nyimbo za kidunia na kuanza kuimba nyimbo za kumsifu Mungu. Waliachana na  maisha maovu, walichoma moto mawigi, vinyago, vitabu vya kipagani,  picha za ngono na kila kitu walichodhani kuwa ni kiovu. Hakika uamsho mkuu ulitokea kama alivyokuwa ametabiri.
Jerome alitabiri kwamba angehubiri kwa miaka nane tu pale Florence na  kisha angeuawa. Katika mwaka 1498 Jerome  alimshutumu papa Alexander VI kwa kutangaza hadharani maovu aliyokuwa anayafanya yeye na wasaidizi wake. Baada ya mkasa huo Alexander VI  aliamua kumwekea vikwazo na kisha baadaye akamnyonga na kuuchoma moto mwili wake mnamo  mwaka huohuo wa  1498. Maneno yake ya mwisho akiwa anauawa alisema “ Bwana Aliteseka sana kwaajili yangu”. Mapambano yake dhidi ya papa yalimfanya kuwa shujaa na  kuwa mtangulizi wa matengenezo ya kanisa. Alikuwa tayari kuitetea imani kwa gharama yoyote.
Wanamatengenzo watangulizi walionyesha ushujaa katika kuitetea imani. Hawakukubali kusalimu amri kwa uongozi wa kanisa au serikali na hawakuwa tayari kunyamaza kimya na kuacha hali mbaya kuendelea kulitafuna kanisa, walikubali kulipa gharama katika kuitetea imani na kupinga uovu. Walitengeneza njia ambayo ilifuatwa  na wanamatengenezo wakuu baadae kidogo  katika kipindi cha kanisa la Sardi yaani kanisa la matengezo.
Kuna mengi ambayo twaweza kujifunza kwa watu hao   kutokana na vile kila mmoja alivyosimamia kusudi lake kwa ujasiri na imani kuu. Kama tutajifunza na kutetea imani kama wao tunaweza kuleta matengenezo katika kanisa vuguvugu la wakati huu wa utandawazi.

F.     KUANGUKA KWA KOSTANTINOPALI.
 Wanahistoria wengi wana tazama kuanguka kwa  Kostantinopoli kama mpka wa kipindi cha karne za katikati na nyakati hizi zetu. Waislamu toka Uturuiki waliivamia Kostaninopoli na kuishinda  mnamo mwaka 1453. Hekalu zuri liliojengwa na mfalme Kostantino lililojulikana kama Saint Sophia liligeuzwa na kuwa msikiti. Huu ndio uliokuwa mwisho wa kipindi cha giza au mediaval Period.




MADA YA SITA
KIPINDI CHA SARDI   KANISA LA MATENGENEZO
KIPINDI : Tangu kuanguka kwa Kostantinopoli hadi Patano la Amani la Westpharia.


A.    SABABU ZA KUZUKA KWA MATENGENEZO YA KANISA.
Kitendo cha Kanisa la Rumi   kutokuwa  tayari  kupokea mabadiliko yaliyokuwa yanapendekezwa na watu wema kama vile, Wikrif na Hus, viongozi wa baraza la matengenezo na mengine mengi kulipeleka  kuanza kwa nguvu  wimbi kubwa la matengenezo.

Hadi kufikia miaka 1500 misingi ya jamii ya kipindi cha giza ilikuwa  inabadilika kutokana na mabadiliko ya  kielimu, kisiasa, kidini na kiuchumi. Kanisa la  ulimwengu lilianza   kupoteza  nguvu  na kanisa la kitaifa likaanza kuchukua nafasi 
Kupanuka kijiografia  kulileta mabadiliko mengi katika kufikiri. Kwa kifupi kulikuwa na sababu mbalimbali zilizopelekea wimbi la matengenezo ya kanisa kutokea,  baadhi ya sababu hizo ni;

1.     Kukua kwa utaifa(nationalism).
Kila nchi ilianza kuweka mkazo kujijenga yenyewe, hivyo nchi mbalimbali zilianza kujitenga na ushirikiano wa kimataifa,  Hii ilipelekea kanisa la ulimwengu kokosa nguvu kwani utaifa ulisababisha kuanza kwa kanisa la kitaifa kila mahali.
Mgogoro  wa kanisa katika karne ya 14 na 15.(Utumwa wa Babeli. Kugombania madaraka yaupapa.)(Great Schism)


2.     Kuvumbuliwa kwa mashine za uchapishaji.
Johann Guthenberg alivumbua mashine ya uchapaji  mwaka 1456. Mpaka wakati huu vitabu vyote viliandkwa na kunakiliwa kwa mkono.  Kuvumbuliwa kwa mashine hii kulisababisha  Biblia na maandiko mengine kuchapwa na kusambazwa katika maeneo mbalimbali. Kusambazwa kwa maandiko haayo kulipeleka kuamsha akiri za watu na kutambua hitaji la kuwepo kwa mabadiliko katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kanisa.

3.     Kuzuka kwa mwamko wa kujifunza. (Renaissence)
Hiki kilikuwa ni kipindi ambacho  ulizuka  mwamko mkubwa
 wa kujifunza . Kipindi hiki kilianza huko Ulaya Italia karne ya 14  na kuendelea hadi karne ya 17. Wasomi wengi waliibuka  katika kipindi hiki. Watu walianza kufikiri mambo kwa upya kutokana na elimu waliyokuwa wamepata. Kutokana na elimu hiyo watu walihitaji mabadiliko katika maeneo mbalimbali ili kuweza kuleta maendeleo. Hivyo kanisa nalo likajikuta linahitaji mabadiliko japo kuwa halikuwa tayari kwaajili ya mabadiliko hayo.

Ø  Mgogoro  wa kanisa katika karne ya 14 na 15.(Utumwa wa Babeli. Kugombania madaraka ya upapa.)(Great Schism)
Ø  Rushwa.
Ø  Kanisa kutojali maisha ya kiroho ya watu na kujikita katika mambo ya kiuchumi.
Ø  Kuuzwa kwa vyeti vya msamaha
Ø  Upendeleo. (Mtu mmoja kuwa na vyeo vingi kwawakati mmoja) 
Ø  Mapapa kukosa maadili.
Ø  Mapadri kuwa na elimu duni.
Ø  Kuzuka kwa falsafa  ya Mantiki.

B.    VIONGOZI WA MATENGENEZO YA KANISA.
Katika kipengere hiki tutawatalii baadhi ya wana matengenezo ya kanisa, yaani tutawachunguza watu ambao Mungu aliwasimamisha  kuleta kweli ya neno la Mungu katika kanisa lililokuwa limepotoka na lisilokubali matengenezo kwa hiali. Tutawatalii wanamatengenezo wafuatao, Martn Luther, John Calvin, Ulrich Zwingli na John Knox.



ULRICH ZWINGLY
Alikuwa ni mwanamatengenezo wa kanisa wa kiswisi asiyejulikana sana kama Martn Luther na John Calvin lakini aliye na mchango mkubwa katika mategenezo ya kanisa.
Alizaliwa mwaka 1484,  na kuelimishwa katika  Chuo kikuu cha Basel na Vienna akisomea fani ya ubinadamu. Alifanya kazi kama  Padre wa Parish Huko Glarus Uswisi mwaka 1512. Katika mwaka wa 1515 Ulrich alianza kuyatilia shaka mafundisho ya Kanisa la Katoliki na alianzisha kile kilichoitwa matengenezo ya Zurich. Alihubiri jumbe za kiBiblia na kufanikiwa  kulibadilisha baraza la mji kuwa na mtazamo kama wa kwake.
Baraza hili liliufanya mji kuwa ngome ya Uprotestant.  Hoja 67 za Zwingli ziliasiliwa na kufanywa Mafundisho rasmi ya mji na mji uliweza kubadilika kwa haraka sana. Mahubiri na mafundisho yalifanywa mara kwa mara, sanamu ziliondolewa , mapadre waliruhusiwa kuoa, Watawa walihamasishwa  kutoka katika makao yao yaliyowatenga na jamii na kuja kuishi na jamii. Nyumba za kitawa zilivunjika na wakatumia mali zao katika kufadhili elimu na misaada kwa maskini.
Mwaka 1525 Zwingly alijitenga na kanisa la katoliki, na akaanzisha mlengo wake.
Mnamo mwaka 1450 baada ya kuongoka Zwingly alianza kuwakusanya wanafunzi waliopenda kujifunza,kigiriki, baadhi ywa wanafunzi hawa waliongoka na wakavutiwa sana na Biblia.
Katika mdahalo wa mji uliofanyika katika ukumbi wa mji Zwingly aliwasilisha hoja 67 Mnamo Februari1523  ambamo aliambatisha mamlaka ya  Kanisa la Romani Katoliki. Mamlaka ya papa, kuwabudu watakatifu, wokovu kwa matendo mema, mifungo, sikukuu, hija,  oda ya watawa, useja kwa mapadre, Uuuzaji wa vyeti vya msamaha, adhabu na toharani. Viongozi wa mji walivutiwa sana na hoja za Zwingli.
Katika mdahalo mwingine wa Oktoba 1523 Zwingli alishambulia matumizi ya sanamu na akataka kuiondoa Krismas. Viongozi wa mji hawakukubaliana na jambo hili na hivyo zwingly  alikaa kimya. Zwingry aliwaogopa watawala.
Kutolizishwa kwa wanafunzi wake.
Baadhi ya wanafunzi wake waliokuwa wamemsaidia katika kuhitimisha hoja zake zote mbili walijisikia kwamba wamesalitiwa na Zwingli. Kwa kuacha kushughulikia swala la Sakramentili kuwapendeza watawala. Walikuwa wamefundishwa na yeye mwenyewe kufuata mafundisho ya Biblia hivyo wakatambua kwamba Zwingly alianza  hakuwa anawaongoza katika mwelekeo sahihi. Hivyo wakaamua kuanza kujisimamia wenyewe.
Vijana hawa walikuwa ni  Conrad Grebel na Felix Manz. Conrad alikuwa ni mwanazuoni wa kigiriki na Felix alikuwa ni mwanazuoni wa kiebrania.  Kwa pamoja vijana hawa waliongoza kikundi cha watu katika kujifunza kikailifu mafundisho ya Biblia juu ya ubatizo.
Mwaka 1524 walihitimisha kwamba ubatizo usifanywe kwa watoto wadogo.  Walifundishwa kwamba watu waliompokea Yesu kama Bwana na mwokozi wao ndio wanaostahili kubatizwa. Pia alitengeneza mawazo mapya kuhusu kanisa wakiamini kwamba kanisa la kweli lilikuwa linahusiha watu wale walibatizwa baada ya kukiri.
Vijana hawa walijaribu kumshawishi mlezi wao wa zaani akubaliane na mawazo haya, 

kwa kiasi fulani Zwingli alikubaliana na mawazo haya, japo  shauku yake ya kuwapendeza watawala kulisababisha, kuwakataa na kuwpinga mawazo ya hawa wanafunzi wake wa zamani.
Katika mdahalo wa  Januari 18-19 – 1525 vijana hawa walibishana Zwingli kuhusu suala la ubatizo wa watoto, Kiongozi wa mji alimtangaza Zwingly kuwa mshindi wa mdahalo huo na akatangaza ya kwamba yeyote ambaye  hangefanya ubatizo wa watoto wadogo au  angebatiza   ubatizo wa waamini alitakiwa ama kutubu au kuondoka Zurich ndani ya siku nane.
Kuanzisha kwa kanisa huru la kwanza.
Katika nyumba ya Colad Grebel walikusanyika watu wachache  ili kujadili nini  walitakiwa kufanya.  Baada ya majadiliano hayo walifikia uamuzi wa kwamba wanatakiwa kubatizwa upya kwa kwa sababu wote walibatizwa wakiwa watoto katika kanisa la Katoliki. Conlad alimbatiza George Blaurock ksa sababu   mtu huyu alikuwani padre. Hivyo baada ya kubatizwa kwake alipewa jukumu la kuwabatiza wengine. Kwa sababu hii walianza kuitwa wanabatisti,  maana yake ikiwa ni wabatizwa upya.
Hii ilikuwa ni moja ya mapinduzi  ya matengenezo.  Mapinduzi haya yalianzisha kanisa jipya. Watu hawa walianza kukutana kwaajili ya ibada na wakaanza kueneza kanisa lao katika maeneo mbalimbali.Kikundi hiki pia kiliitwa undugu wa uswisi.
Baada ya mlango huu kukua na kuenea, ulishambuliwa na kupingwa sana karibu katika Ulaya nzima. Kanisa la Romani Katoliki, pamoja na wanamatengenezo yaani Martin Luther pamoja na John Calvin walihusika katika kuwaua Wanabatisti.  Zaidi ya wanabatisti 4000 walinyongwa.
Mnamo mwaka 1529 wanamatengenezo walikutana katika mji wa  Marbag ili kuweza kuimalisha umoja wao. Wanamatengezo hao walikubaliana katika mambo kadhaa, lakini kulitokea kutokukubaliana katika jambo moja ambalo ni meza ya Bwana. Zwingli alisema kwamba mkate na divai ni kielelezo tu cha ukumbusho wa mauti ya Yesu, wakati Luther alikaza kwamba kwa namna fulani Yesu alikuwa katika mkate na divai kwa njia ya fumbo. Jambo hili lilileta utegano mkubwa baina ya wanamatengenezo hawa.
Kulizuka vita baina ya Kanisa la Romani katoliki  Waprotestant, katika vita hiyo Zwingly aliuawa, hii ilikuwa mwaka 1531.
MARTNI LUTHER.
 Martin Luther alizaliwa mnamo mwaka 1483.  Baba yake aliitwa Hans  na mama yake aliitwa magareth. Alizaliwa katika  familia ya kimsikini, baba yake alikuwa mfanyakazi  katika mgodi wa madini.   kujiunga Martin alisoma Theolojia katika vyuo vikuu vya Erfurt na Edburg. Mnamo mwaka 1505 alitunukiwa shahada ya kwanza katika falsafa na katika mwaka 15012  alipata shahada ya pili ya udaktari katika Theolojia. Baada ya masomo yake alianza kufundisha Biblia katika Vyouo Vikuu  vya Erfurt na Witternberg 
Mnamo mwaka 1507 alipata ubarikio na kuwa padre. Mnamo mwaka 1510,  Martn na mmonaki mwingine mmoja walisafiri kwenda Rumi kwaajili ya shughuli za Chama chao cha umonaki. Akiwa Rumi alishangaa kuona udharimu uliokuwa ukifanywa na mapdre huko Rumi. Martin akiwa mmonaki alipata mabishano makubwa moyoni mwake, na alijiuliza namna gani ambavyo angeweza kupata rehema za Mungu. Alijipiga, Alifunga na kujitesa kwa muda mrefu ili aweze kusamehewa dhambi zake. Alipata majibu ya maswali yake yote baada ya kusoma Waraka wa Warumi 1:16-17. Ukiwa na maneno mwenye haki ataishi kwa imani.
Wakati huo huo  papa Leo X aliwatuma wawakilishi wake katika nchi mbalimbali kukusanya fedha kwajili ya ujenzi wa kanisa la Mt Petro.  Walikusanya fedha hivyo kwa njia ya kuuza vyeti vya msamaha. Wakristo waliweza kununua vyeti kwajili yao wenyewe na kwaajili ya ndugu zao waliokwisha kufariki ili waweze kupata msamaha.
Luther alipinga vikali jambo hili pamoja na mambo mengine ambayo  yalikuwa kinyume na Maandiko matakatifu kwa kuandika hoja 95 na kuzibandika katika mlango wa kanisa kule Huko Wittenberg. Marafiki  Luther walipiga kopi hoja hizo na kuzisambaza katika maeneo mbalimbali ya nchi ya ujerumani ili ziweze kusomwa na watu wote. Kwa muda mfupi nakala hizo ziliweza kuenea na mafundisho ya Luther yakaenea  katika maeneo mbalimbali.
Baada ya hoja hizo kuenea Luther aliitwa na Kardinali, Cajetan katika mji wa Dusgbarg( 1518). Kardinari huyo alimtaka Luther kukiri makosa yake lakini Luther alipinga swala hilo.
Papa Leo wa kumi alimwandikia Luther barua ya kumtishia kumtenga na kanisa iwapo hangekiri makosa yake.  Baada ya Luther  ya kuipata barua hii aliichoma hadharani mbele ya watu wengi.
 Mnamo mwaka 1521.Luther alitengwa rasmi na kanisa Katoliki.
Luther aliitwa katika mkutano  uliofanyika katika mji wa worms ulioitishwa na kaisari Charles V, ili aweze kusikilizwa na kumaliza mgogoro. Katika  mkutano huo Luther alitakwa kukiri makosa  yake kuhusu vitabu alivyokuwa ameviandika na kuvisambaza.. Luther alikataa kubadili msimamo  wa  kuyakana maandishi yake, na hatimaye kaisari  na wafalme wake walitangaza hukumu ya kifo dhidi ya Luther. Katika mkutano huo kulitokea fujo na hatimae Luther alitoroka na kuokolewa na mfalme Fredrick wa Saksoni na kupelekwa katika boma lake la Wartburg. Akiwa huko alijificha kama mfungwa na alibadilishwa jina na kuitwa Jorg na kupelekewa nguo zingine. Alibadili sura yake  kwa kufuga ndevu.
 Akiwa katika boma hilo alianza kazi ya kutafsiri Biblia katika lugha ya kijerumani.  Katika muda huu  wa kukaa mafichoni Luther alifanya kazi kubwa ya matengenzo kuliko wakati mwingine kwake wote.
 Mnamo mwaka 1529 Wafalme walibadili msimamo wao wakaamua  ya  kupigana dhidi ya wanamatengenezo. Wafalme 19 walipinga uamuzi huu, na hivyo wakaitwa waprotestanti. Hivyo neno hilo wakapewa watu wale waliokubali matengenezo  ya kanisa.  Martin Luther alifariki dunia mnamo m 17,  Februari, 1546. Na kuzikwa katika kanisa alikobandika zile hoja 95 kule wartnbarg.