Tuesday 10 June 2014

MAOMBI YA UKOMBOZI


Maombi haya ni kwa ajili ya wale ambao wanataka au wanatamani kujiondoa kwenye maagano ya Uharibifu,au maagano na nguvu za giza.Maagano ya Uharibifu yapo kwa ajili ya ya kuharibu tu na si vinginevyo,na kadiri yanavyoendelea kuwepo Uharibifu hauepukiki.Maagano yanayozungumziwa hapa ni yale ya kurithi au yaliyoingiwa na mhusika aidha kwa kujua au pasipo kujua kama anaingia kwenye maagano.Kwa sababu ni maagano ya uharibifu ni muhimu kujiondoa au kuvunja maagano hayo.Ili kuyavunja ni lazima utangaze kuyavunja,na inawezekana maagano mengine yapo hapo muda mrefu,kwa hiyo ni lazima kuomba kwa bidii  [Yakobo 5:16]
Angalizo:Usiombe Maombi haya bila maelekezo,kama huelewi chochote
Aya za kukiri:  Wakolosai 2:14-15, Wagalatia 3:13-14
1.     Ninarudisha mamlaka yote aliyopewa shetani na mababu/mababa ,katika Jina la Yesu.
2.    Nina zilaani roho zote zinazoendelea kutilia mkazo hayo maagano katika maisha yangu na naziamuru kuniachia kwa Jina la Yesu[ Sema mara 3 na anza kusema hivi,”niachie kwa jina la Yesu
3.   Kitu chochote kilichoingizwa kwenye maisha yangu,kwa mkono wa kipepo,ninakiamuru kiachie kwa JIna la Yesu
4.  Kila aina ya sumu iliyopenyezwa kwenye maisha yangu nina iamuru itoke nje sasa,katika jina la Yesu,nina sukuma nje kwa damu ya Yesu.
5.    Ee Bwana Yesu,shusha moto juu ya kila roho ya mauti na kuzimu,iliyoandaliwa kwa ajili yangu,katika jina la Yesu
6.      Nina ponda kichwa na kukanyaga kila mkia wa majoka ya kiroho,katika jina la Yesu
7.      Upanga wa moto,na uanze kukata kila kifungo walichokifunga wazazi,katika jina la Yesu
8.    Ee Bwana,nifunulie agano lolote la siri ambalo shetani amefunga na nafsi yangu au anataka kufunga na nafsi yangu,katika jina la Yesu.
9.   Kila pando,ambalo baba yangu wa mbinguni hakulipanda katika maisha yangu,nina kungo”a katika jina la Yesu.
10.  Baba nina pitisha umeme katika ardhi ya mahali hapa sasa na kila agano na miguu yangu lianze kuvunjika sasa katika jina la Yesu.
11.  Agano lolote la siri ambalo ni la uovu,ninakuvunja katika jina la Yesu
12.  Nina nyunyiza damu ya Yesu kuvunja laana zote
13.  [Imba wimbo huu: Kuna nguvu ya ajabu,damuni mwa Yesu ]
14.  Nina nyunyiza damu ya Yesu kuvunja laana zote za dhambi za wazazi wangu
15.  Ee Bwana,badili laana zote zilizoelekezwa kwangu kuwa Baraka
16.  Kila nguvu ya uovu iliyoelekezwa kwangu,ninakuamuru kurudi moja  kwa moja ,kwa mtumaji katika jina la Yesu.
17.  Ee Bwana Mungu, ninaomba kila alichosema adui kwamba hakitawezekana katika maisha yangu, kikawezekane sasa kwa jina la Yesu.
18.  Nina jiondoa na kujitenganisha katika kambi yoyote ya mateka inayomilikiwa na adui,katika jina la Yesu.
19.  Nina jifungua na kujiondoa kutoka kwenye kila kifungo cha kurithi ,katika jina la Yesu.
20.  Ee Bwana,tuma shoka lako la moto kwenye misingi ya maisha yangu na uharibu/ulikate kila pando ambalo amelipanda adui katika jina la Yesu.
21.  Nina ipitisha Damu ya Yesu,katika mifumo yote ya mwili wangu[mfumo wa damu,wa fahamu,wa chakula,wa upumuaji,wa takamwili n.k] na kuisafisha mabaki yote ya urithi wa vitu viovu katika jina la Yesu.
22.Damu ya Yesu na moto wa Roho mtakatifu,unisafishe kila kiungo cha mwili wangu [Figo,moyo,mapafu,macho,masikio,n.k] katika jina la Yesu
23.   Nina vunja mikataba yote ya kiukoo na kikabila inayonihusisha mimi katika jina la Yesu.
24.   Nina jiondo/ninajivua/vunja laana zote za kikabila na kiukoo katika jina la Yesu
25.   Nina tapika chakula chochote cha uovu nilicholishwa katika maisha yangu,katika jina la Yesu
26.  Mapepo,majini,mizimu na wachawi manao fuatilia maisha yangu,na mpararaizi[mpooze] sasa katika jina la Yesu.
27.  Shambulio lolote lilopangwa juu ya familia yangu,ninalibatilisha kwa ajili yangu katika jina la Yesu
28.  Nina vunja matoke mabaya yote kwa ajili ya jina la kiuovu,lilipachikwa kwenye nafsi yangu katika jina la Yesu
29.Nina batilisha laana zote,mikosi,majanga,ajali,maradhi yote yaliyoelekezwa kwenye maisha yangu katika jina la Yesu.
30.  Muombe Mungu aondoe laana zote alizo ziachilia kwenye maisha yako kwa sababu ya kutotii neon lake[kumb 28:]
31.   Pepo lolote lililo jipachika kwenye laana yoyote inayonihusu mimi,toka,katika jina la  Yesu
32.   Laana zote katika maisha yangu,badilika na kuwa Baraka,katika jina la Yesu
33.Utakapokuwa unataja laana zilizoorodheshwa hapo chini,sema kwa kumaanisha “vunjika,vunjika ,vunjika” katika jina la Yesu.Nina jitenganisha na nyinyi katika jina la Yesu.
·         Laana zote za udhaifu wa kiakili na kimwili
·         Laana zote za kushidwa katika kila ninalofanya
·         Laana zote za umaskini
·         Laana zote za kuvunjika kwa familia
·         Laana zote za kuonewa na kudharauliwa
·         Laana zote za Uharibifu wa mtu binafsi,kama vile kujinyonga n.k
·         Laana zote za magonjwa sugu
·         Laana zote za kishirikina
·         Laana zote za kuharibikiwa mambo ya uzazi na viungo vya uzazi
·         Laana zote za kufanya kazi kwa bidii pasipo kuiona faida
·         Laana zote za kulowea mambo ya uovu kama vile zinaa,pombe,sigara n.k
34.Jitamkie maneno ya Baraka wewe mwenyewe,kwa mfano kwa kusema “hakutakuwa na umaskini tena,magonjwa tena n.k katika maisha yangu katika jina la Yesu.
35.  Nina jifungua na kujitenganisha na vifungo vya madhabahu zote za giza katika jina la Yesu.Sema mara kadhaa ukifuatiwa na maneno yafuatayo “nina jitenganisha” katika jina la Yesu.Tumia muda kidogo kwenye hilo.
36.   Nina tapika sumu zote za mashetani nilizozimeza katika jina la Yesu.
37.[Weka mikono yako juu ya kichwa chako] Nina vunja kila mamlaka za giza katika maisha yangu,katika jina la Yesu.Rudia “nina vunja katika jina la Yesu.
38.  Taja mambo yafuatayo kwa mamlaka na sema “vunjika kwa jina la Yesu.
·         Mamlaka zote za mizimu na miungu ya familia,ukoo,na kabila
·         Mamlaka zote za roho za kichawi zilzopo ndani ya familia,ukoo,kabila
·         Mamalaka zote zilizoshika rimoti za kudhibiti familia,ukoo,kabila
·         Mamlaka zote ovu ndani ya Familia,ukoo,kabila nk
39.  Kila mmiliki wa mzigo niliobebeshwa beba mzigo wako katika jina la Yesu[Mzigo unaweza kuwa ugonjwa,mikosi wabebeshe wamilki]
40.  Nina zipoodhesha/nina zipararaizi madhabahu zote za giza  katika jina la Yesu
41.  Nina zilaani madhabahu zote za uovu zilizoelekezwa zidi yangu katika jina la Yesu
42.  Nina agiza nyundo ya  Mungu aliyeumba mbingu na nchi,iponde kila madhabahu ya giza zilizoelekezwa kwenye maisha yangu katika jina la Yesu.
43.  Ee Bwana tuma moto wako na uteketeze madhabahu zote za giza zinazoinuka dhidi ya maisha yangu,
44.  Makuhani wote wa madhabahu zote za giza wanaocheza na maisha yangu,wakutane na upanga  wa roho mtakatifu. Katika jina la Yesu.
45.  Mkono wowote unaotaka kunikamata na kuniteka kwa ajili ya Maombi haya ninayoomba kauka katika jina la Yesu.
46.  Nina waamuru makuhani wa madhabahu za giza kunyweni damu wenyewe katika jina la Yesu
47.  Nina rudisha urithi wangu ulioibiwa na madhabahu za giza katika jina la Yesu.
48.  Ninafuta/ninaliondoa jina langu kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu
49.  [Weka mkono wako mmoja kifuani] Ninaziondoa Baraka zangu kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu
50.  [Weka mkono mmoja kifuani na mwingine kichwani] Ninaondoa kitu chochote kile kinachoniwakilisha mimi [kama vile nguo] kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu.
51.  [Taja kiungo chochote katika mwili wako ambacho akifanyi kazi ipasavyo au kama ni mwili wote taja mwili] na useme maneno yafuatayo “nina kuondoa kwenye madhabahu za giza” katika jina la Yesu.Tamka hivyo mara saba.
52.  Nina jitenganisha kutoka kwenye maagano yote ya damu na nguvu za giza katika jina la Yesu
53.  Damu ya Yesu na unene kwa ajili yangu dhidi ya maagano yote na nguvu za giza
54.  Nina tamka Uharibifu dhidi ya roho chafu zote katika maisha yangu.Katika Jina la Yesu.
55.  Nina jitenganisha na laana zote za maagano katika jina la Yesu
56.  Nina jitenganisha mimi na familia yangu kutoka katika kila agano la damu katika jina la Yesu.
57.  Ninajitenganisha na kila agano la damu la kurithi katika jina la Yesu.
58.  Nina iondoa damu yangu kwenye madhabahu za giza  katika jina la Yesu
59.  Nina iondoa damu yangu kutoka kwenye benki za damu kwenye ulimwengu wa giza katika jina la Yesu
60.  Nina vunja kila agano la damu la kutokukusudia kwa  jina la Yesu
61.Ee bwana ,damu ya mnyama yeyote iliyomwagika kwa niaba yangu,Naipoteze nguvu ya agano sasa,kwa jina la Yesu
62.  Kila tone la damu linalotamka mabaya dhidi yangu,na ikae kimya sasa, kwa damu ya Yesu
63.  Ninajifungua na kujiondoa kutoka kwenye kila agano la damu la kifamila,kiukoo,kabila katika jina la Yesu.
64.  Nina jitenganisha na kila agano la damu nililoingia kwa kujua au kutojua kwa jina la Yesu
65.  Ee Bwana kila agano la damuna nguvu za giza lipoteze nguvu na uhalali wake juu yangu katika jina la Yesu.
66.  Damu ya agano jipya la Bwana na Mwokozi wangu Yesu Kristo,naiikemee  damu ya agano na nguvu za giza ilijipanga kinyume name.Kwa jina la Yesu
67.  Nimepewa mamlaka  ya kubatilisha haki zote zilizopo kwenye maagano yote ya damu na nguvu za giza .kwa jina la Yesu.
68.Agano lolote la damu na nguvu za giza lililofungwa kwenye kiungo chochote kwenye mwili wangu,nalivunjike sasa.Kwa jina la Yesu
69.  Ninapokea vitu vyote vilivyoibiwa au kuchukuliwa  na adui kupitia maagano na nguvu za giza.Kwa jina la Yesu.
70.  Nina vunja agano lolote la damu na nguvu za giza kwenye damu yangu .Kwa jina la Yesu

maombi ya ukombozi



MAOMBI YA UKOMBOZI

UTANGULIZI
Maana ya Ukombozi inaweza kuwa:
·        Kufunguliwa kutoka katika kifungo Fulani
·        Kumtoa pepo mchafu kutoka kwa mtu
·        Kufunga nguvu za giza zinazosababisha uharibifu Fulani
·        Kutoa mapepo kwa aliyepagawa
·        Kuvunja maagano na mikataba iliyofungwa inayowatesa watu
·        Kuvunja vifungo vya shetani
·        Kung’oa mizizi ya mbegu ya uharibifu iliyopandwa na ibilisi
·        Kuondoa mizigo isiyoonekana ambayo watu wamebebeshwa bila kujua.
·        Kuisafisha njia
·        Kuharibu kazi za shetani
·        Kumweka mtu huru kutoka nguvu za shetani
Unaweza ukaendelea kuyataja mengi zaidi. Pia zipo njia za kufanya hivyo ila la msingi ni kuwa kwa uhakika inahusu yafuatayo:
1.     Mtu kufunguliwa na kuishi maisha mapya
2.     Kugundua adua alipojificha
3.     Kumng’oa adua alipojificha
4.     Kung’oa vitu vyote vya adui na kuponya yale yaliyoharibiwa na adui.
5.     Kumfunika mtu kwa ulinzi wa Mungu kusudi adui asiweze kurudi tena.
NJIA ZINAZOTUMIKA
1.     Kuziamuru zijitokeze zilikojificha katika Jina la Yesu – hii inaweze kuchukua muda mwingi.
·        Maombi
·        Nyimbo za Damu ya Yesu  
·        Neno la Ushindi
·        Wakati mwingine kutumia mafuta
2.     Wafungue mapepo; bila fujo kwa kuyaamuru bila mahojiano “Mtoke mtu huyu katika Jina la Yesu” Marko 5:8 – 9;9:25 – 27; Luka 8:27 – 33
3.     Haribu Vifaa vyote vya adui
4.     Toba kwa yale yaliyosababisha kupagawa wewe mwenyewe, wazazi au wengine.
5.     Ikibidi shughulikia mababu – Walawi 26; Daniel 9
6.     Mkatae shetani na kazi zake na dai eneo lote lililotekwa. Ukitafakari uweza uliopo katika  1 Yohana 3:8 inayosema Yesu amekuja kuzivunja nguvu za ibilisi.
7.     Bomoa kila ngome yake iliyokuzunguka.
8.     Jisalimishe kwa Mungu na mkatae shetani. Yak. 4:7
UKOMBOZI
-         Kukomboa
-         Kukinunua tena kitu kilichokuwa chako
Bibilia inaonyesha jinsi ambavyo ukombozi wa wana wa Israel kutoka utumwani Misri ulivyokuwa.
Tendo hilo lilitingisha dunia lakini hata hivyo ilikuwa ni alama tu ya tendo kuu ambalo Mungu alikusudia kwa mwanadamu.
Israel ilikombolewa na Mungu mwenyewe, sio wao waliojikomboa
Mu
Posted by Fredrick Kweka at 2:09 A