Sunday 30 November 2014

ELIMU YA KICHUNGAJI

HUDUMA ZA AGANO
JIPYA
Peter A. Thomas
ii
HUDUMA ZA AGANO
JIPYA
Yanayo Husika na Huduma Katika Agano Jipya-
Jinzi ya Kupata Huduma Wetu na Kuutekeleza
Peter A. Thomas
Copy Right:
CEAfrica: Publishers
Nairobi, Kenya
1996
iii
HUDUMA ZA AGANO JIPYA.
UTANGULIZI: 7
I. HUDUMA KUFUATANA NA AGANO JIPYA 9
1. Ufafanuzi wa misamiati 9
2. Mada dhidi ya wajibu wa Kiroho? 10
3. Huduma au kupanda ngazi ya Kanisa? 11
4. Huduma siyo ajira 12
5. Huduma ya pamoja –hakuna watazamaji. 12
6. Kutambua huduma nyingine. 13
HUDUMA ZA KIROHO NA KARAMA ZA KIROHO 17
1. Ufafanuzi wa misamiati 17
1.) Huduma za kiroho 18
2.) Karama za kiroho. 18
2. Asili na tabia za huduma za kiroho. 18
1.) Tambua huduma 19
2.) Sehemu ya kudumu ya maisha ya kiroho 19
3.) Mwamini kutambuliwa na huduma. 20
3. Asili na tabia za karama za Kiroho 20
1.) Karama ya kiroho haihitaji wito 20
2.) Karama za kiroho ni za muda 20
3.) Karama za kiroho hazilingani na huduma. 20
II. HUDUMA ZA UONGOZI. 23
1. Uongozi: - Kwa ajili ya nini ? 23
Mtume 23
1. Viwango vitatu vya utume 24
2. Sifa za utume 24
3. Kazi ya Mtume 25
4. Je kuna Mitume siku hizi? 26
Nabii 28
1. Manabii katika Agano la Kale na Agano jipya. 28
2. Sifa za huduma ya Kiunabii 29
3. Kazi ya nabii 29
4. Mwongozo kupitia manabii 30
5. Huduma ya mahubiri ya nabii 31
6. Kipimo cha nabii. 32
Mwinjilisti 33
1. Kazi na tabia za Mwinjilisti 33
2. Kuanzisha na kushirikiana 34
3. Kufikiria wazo jipya 35
4. Jihadhari na hisia mbaya 35
1.) Dalili ya umaarufu 35
2.) Kususia Uwajibikaji (Majukumu) 36
5. Kutoa nafasi 36
iv
Mchungaji. 37
1. Mchungaji? Wachungaji? –Wazee, Waangalizi au Maaskofu? 37
1.) Matumizi ya neno nje ya mazingira ya Agano jipya. 39
2.) Uongozi wa pamoja / wengi 40
3.) Nafasi au umuhimu wa Mchungaji 41
4.) Sababisho na madhara 42
2. Kazi ya Mchungaji 43
1.) Kutoa uongozi 43
2.) Kutoa chakula cha kiroho 44
3.) Kutoa ulinzi 44
4.) Kutoa faraja na kujali 44
5.) Kanisa kubwa au Kanisa la nyumbani. 45
3. Wachungaji wanaitwa na hawatengenezwi / hawaundwi. 45
MAJADILIANO: - Sifa za Kibiblia kwa uongozi 46
1.) Asiyelaumika 47
2.) Mume wa mke mmoja 48
3.) Mwenye kiasi na busara 48
4.) Mtu wa utaratibu 49
5.) Mwenye sifa njema 49
6.) Mkaribishaji 49
7.) Ajuaye kufundisha 50
8.) Si Mlevi 50
9.) Si mgomvi 50
10.) Asiwe mtu wa kupenda mapato ya aibu. 51
11.) Mvumilivu 51
12.) Si mpiganaji. 52
13.) Ajuaye kuitunza nyumba yake vyema 52
14.) Asiye aliyeongoka karibuni. 53
15.) Kushuhudiwa mema na walio nje 54
.
Mwalimu. 54
1. Chanzo na sifa za huduma . 55
2. Kazi ya Mwalimu 56
3. Siyo maarufu bali ni muhimu 57
4. Neno la tahadhari. 57
III. HUDUMA ZA MASAIDIANO. 59
1. Shemasi –kuhudumu –kutumika 60
1.) Kuteuliwa / kuwekwa kutumika 61
2.) Huduma ya Shemasi 62
3.) Sifa na uchaguzi wa Mashemasi. 62
2. Faraja 64
3. Mtoaji au kutoa. 66
1.) Huduma na haki kwa wote 67
2.) Taratibu kuhusu huduma hii. 68
4. Masaidiano. 69
v
5. Ukarimu 70
1.) Ufafanuzi 71
2.) Inavyotakiwa leo. 71
6. Utawala –Uongozi 72
7. Utawala –Serikali 73
1.) Utawala dhidi ya sheria 73
2.) Eneo la utendaji kazi. 74
8. Kuonyesha rehema. 74
IV. KUTAMBUA SEHEMU YA HUDUMA YETU. 77
1. Jinsi ya kutambua sehemu zetu. 78
2. Jinsi ya kutumika katika huduma zetu 79
1.) Jua / fahamu huduma na kazi ndani ya mipaka yake. 79
2.) Ridhika 79
3.) Miliki mpaka ajapo. 80
3. Jukumu katika huduma yetu 80
1.) Jitoe kwenye, huduma 80
2.) Ishi maisha bora ya utumishi wa Mungu 81
3.) Ujazwe na Roho. 81
4. Kuna nini cha kufanya? 82
HITIMISHO 83
HUDUMA ZA AGANO JIPYA.
UTANGULIZI:
Wakati Kristo aliporudi Mbinguni aliliacha Kanisa lake katika mikono ya Viongozi ambao alikuwa
amewaandaa na kuwatayarisha kuiendeleza kazi yake. Hakuwaita Mitume kumi na wawili tu, bali
yeye mwenyewe aliwafundisha na kuwahakikishia kuendeleza huduma yake. Baada ya kupaa
kwake walitoa huduma muhimu ya uongozi kwa Kanisa la kwanza, katika uwezo wao kama
mitume, kama mwili wa waamini ulivyoendelea kukua na kupanuka, wengine wakishiriki
majukumu ya huduma, hivyo waliongoza, kulinda na kulisha Kanisa changa. Ijapokuwa kiwango
cha Uongozi hakikuwa wazi kama ule wa mitume, hata hivyo huduma zao zilikuwa zimewekwa na
Bwana aliyeinuliwa, bado ni karama zake leo katika mwili wake.
Kama wapentekoste tumezikumbatia karama za Roho kama sehemu ya baraka za Mungu za
mapenzi ya Ki-Mungu katika kanisa lake lililo katika mfumo wa Agano jipya. Hata hivyo, katika
maeneo fulani bado tunafuata mawazo yaliyokuwepo kabla ya kuamka kwa Upentekoste na
kurudi kwa karne. Kwa hiyo, tunatumia mbinu na kufuata mifumo ambayo matengenezo
(reformation) hayakufaulu kubadilisha. Moja ya haya ni kukabiri huduma zetu. Katika sehemu hii
“matengenezo “ hayakufikia malengo, na katika sehemu kuna upungufu kwa pamoja. Kama tokeo
la huduma limebakia kama jambo la wachache wakati wengi wao waliobaki Kanisani
wanahudumiwa”. Tokeo hili limesababisha dhana potofu ambayo imetengeneza huduma kama
sehemu ya kujiinua na kuonyesha cheo chake, na haitumiki tena katika roho ya utumishi. Kamwe
Mungu hakukusudia iwe hivyo.
Ni lazima tufahamu zaidi mtazamo wa huduma wa makanisa wakati huu yameishia katika misingi
ya huduma nne, kwa majina Mchungaji, Mzee wa Kanisa, Shemasi na Mwinjilisti. Katika hali ya
wepesi wa utajiri na upotoshaji wa huduma za Kibiblia, ni lazima kwa namna yeyote kurudi katika
mpango wa asili wa Mungu unaohusu huduma katika mwili wake. Baadaye Kanisa limetambua
huduma zingine za Kibiblia ambazo zilikuwa zimeachwa kwa karne nyingi. Kila moja lazima
itumike ikiwa mwili wa Kristo utakuwa ukitenda kazi yake, kuwapata waliopotea na kuwafanya
waamini kuwa Wanafunzi.
Kwa nyongeza katika mtazamo wa mipaka ya huduma, kanisa lina kabiliana na hali dhaifu ya
maendeleo. Makanisa mengi yamezoelea kutegemea / kumtazama mtu mmoja (one man show)
wakati mchungaji amebeba kila kitu na kubeba mzigo wa huduma zote kanisani peke yake.
Viongozi wengine wanaweza kulinganishwa na mpiga ngoma peke yake kama inavyooneka na
siku zote katika miji ya Ulaya. Ngoma hizi hubebwa na mtu mmoja ambaye huwa anapiga gitaa,
ngoma iliyofungwa mgongoni, mdomoni kuna kinanda ambacho kimefungwa shingoni, na namna
ya zumari ambayo imefungwa Kichwani. Watu kama hawa wanachekesha na kufurahisha
wanavyoonekana. Hata hivyo wale ambao wanawasifia kanisani kwa kufanya kila kitu wao
wenyewe, si kwamba wanachekesha wala kufurahisha, lakini inatisha.
Kristo kamwe hakukusudia kwa mtu mmoja kufanya kazi zote peke yake. Ni mapenzi yake na
mpango wake kwa kila mshirika kutambua huduma yake kupitia hiyo anaweza kuchangia katika
kuujenga na kuukuza mwili wake. Kulingana na Waefeso 4:11 Mungu ametoa huduma tano za
1
uongozi katika Kanisa lake ambazo kazi yake si tu kutoa mwelekeo, amri na uongozi katika mwili
wake, bali ni kumsaidia kila mwanafunzi kutambua wito wa Mungu na eneo mahsusi katika
huduma ambao kwa hiyo amewapaka mafuta wale wote ambao amewakomboa.
Ni amri kwa kila kanisa kufuata mfumo wa Agano jipya kutambua huduma mbali mbali ambazo
zimedhihirishwa, na kutoa nafasi kwa kila mshirika si tu kutambua huduma yake bali aifanyie kazi.
Ni mapenzi ya Mungu kwamba kila mshirika wa mwili wake kutambua, kuelewa na kuzitumia
huduma ambazo amepewa.
Kwa hiyo kusudi na lengo la somo hili ni kama ifuatavyo:-
1. Kutambua maana za huduma ya Kibiblia
2. Kutambulisha huduma zilizoonyeshwa katika Agano jipya.
3. Kuelezea asili na tabia ya kila huduma.
4. Kutambua kazi ya huduma hizi
5. Kutoa mtazamo wa utendaji wa huduma za kiroho.
6. Kuwasaidia hao walioitwa kujua huduma zao za kweli; kuwasaidia kutambua wito wao na
namna ya kufanya kazi ndani ya mipaka yake.
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-
2
I. HUDUMA KULINGANA NA AGANO JIPYA.
Huduma kulingana na Agano jipya inaweza ikabebwa na wale tu wanaoelewa na kufuata
mafundisho ya Yesu Kristo. Mpaka tutakapomruhusu kubadilisha fikra zetu, tabia zetu na
matendo yetu kamwe hatutaweza kuhudumu katika roho ya utumishi na kujitoa dhabihu
wenyewe kama alivyoonyesha mfano. Amri ya Kristo ni kujikana sisi wenyewe, na kubeba
Msalaba wetu kila siku na kumfuata yeye, kuacha kila kitu na kujiweka wakfu sisi wenyewe na
upendo kwake kabla ya familia zetu, ni mhimu na mahitaji ya msingi kwa Watumishi wake.
Kutokuwa mbinafsi na huduma ya kujitoa dhabihu itakuwa dhahiri kwa wale ambao wanafuata
maisha yake na kufuata mafundisho yake.
Mawazo ya huduma ya Agano jipya ni mageni katika ulimwengu, ambapo kujitambua mwenyewe
kujipendelea na kujitukuza ni sheria za siku hizi. Kwa hiyo kabla ya kutazama kwa makini
huduma mbali mbali za Agano jipya ni lazima tujaribu kulielewa vizuri neno “huduma“. Hii ni
muhimu hasa kwa kuwa wazo la Kibiblia limeharibiwa kabisa kwa mitazamo ya kisasa
inayotokea. Kufanya hivyo ni lazima tuwe na hiari kuweka kando mawazo yeyote yaliyokuwepo
kabla kama vile desturi, mila na mtazamo wa kidhehebu lazima tushikilie, na tuyaache maandiko
yazungumze yenyewe. Kwa hiyo mara zote tafsiri binafsi na za Kidini / Kidhehebu zinasomwa
katika Neno la Mungu tunapojaribu kuthibitisha jambo au ushawishi wa mafundisho yetu.
Tunapojaribu kupata maana za kweli za huduma za kibiblia ni lazima tuangalie kwa uangalifu
katika maneno ya asili ya Kiyunani kwa kawaida yametafsiriwa kama huduma. Tafiti hizi ni za
mhimu sana kulielewa somo letu kwa usahihi zaidi. Baada ya hapo tutayaonyesha baadhi ya
mawazo yasiyo sahihi na kuonyesha mawazo ya huduma ya Agano jipya.
Lugha ya kiyunani imetumia maneno yafuatayo ambayo kwa kawaida yametafsiriwa kama
“huduma” au “Mtumishi”.
1. Ufafanuzi wa Neno (Term)
Inafurahisha kutambua kwamba katika Agano jipya neno la kiyunani diakonia, ambalo
limetafsiriwa kama huduma, lina maana ya kutumika na kimsingi lilitumika wakati wa kuonyesha
ofisi ndani ya kanisa. Hata ndani ya desturi za kiyunani za kidunia neno diakonia lilitumika
kuelezea kwa kumaanisha au kutomaanisha kutumika. Neno arche () ambalo linafafanua
ofisi/ huduma ya nguvu / utawala na heshima halitumiki katika ofisi/huduma yoyote ya Agano
jipya, bali linatumika katika serikali ya kiyuda (judaic) na serikali ya wamataifa (Luka 12:11; 20: 20;
Tito 3: 1). Kupitia uchaguzi wa maneno, maandiko huonyesha kwa usahihi kwamba ofisi au
huduma ndani ya mwili wa Kristo haikuwekwa kwa ajili ya nguvu/ madaraka, wadhifa au heshima
wala haionyeshi ukuhani au kazi za upatanishi. Kulingana na hili kuwa mtumishi au kuwa na
huduma kanisani kwa hiyo ni lazima ieleweke kimsingi kama mtumishi (servant). Kwa ukweli wa
jambo neno “huduma” limetumika mara 18katika Agano jipya na diakonia limetumika mara 16
na mara mbili kwa neno Leitourgia likiwa na maana ya kazi ya watu (wazi - Public function)
kama kuhani, kuhudumu, kutumika, anayesaidia maskini (alms giver).1
1 Neno Mtumishi limetumika mara 34.
Mara 14 kama diakonos, (Mathayo 20:26; Marko 10:43; Warumi 13:4 mara mbili; 15:8; Wagalatia 2:17;
Waefeso 3:7; Waefeso 6:21; Wakolosai 1:7, 23, 25; 4:7; I Wathesalonike 3:2; I Timotheo 4:6).
3
2. Mada dhidi ya wajibu wa kiroho.
Mambo haya yanaonyesha wazi ukweli kwamba wazo la huduma halijiingizi lenyewe kwenye
mawazo potofu ambalo linaiona kama sehemu ya cheo cha kujiinua, mahali pa kujiwekea
heshima, na katika nafasi za utawala. Inahuzunisha hasa wakati wapentekoste na Wainjili
(evangelicals) kufuata mfano wa makanisa ya kawaida / yasiyo ya kipentekoste, mahali ambapo
viongozi wanaitwa Maskofu, Maaskofu wakuu n.k; ili kuonyesha “ umuhimu wao. Kanisa lazima
lirudi katika misamiati ya Kibiblia kama vile ndugu, dada, mwanafunzi (disciple) na kutumia
mitindo kama “Askofu “ katika namna sahihi.
Wale ambao wanamnukuu Paulo, ambaye katika nyaraka zake amejitambulisha yeye mwenyewe
kama mtume, wanajihesabia katika akili zao vyeo hawajaelewa umuhimu wa neno. Wakati
alipoandika; “Paulo, mtume wa Yesu Kristo”, alikuwa na maana ya kusema, “Paulo, aliyetumwa
na Yesu Kristo” (Kiyunani apostolos = “aliyetumwa”). Haikuwa inamaanisha cheo. Vyeo, kama
mtume na askofu, kama ilivyotumika katika kanisa la kwanza limeelezwa huduma iliyotolewa kwa
mwamini, na hazikutumika kama alama ya kiroho ya majivuno.
Katika kitabu chake Kelvin J. Conner, the Church in the New Testament, anaelezea kuwa moja
ya sehemu kubwa ambayo inahitaji kuelezewa katika jambo la kuwapa watu “Vyeo vya
udanganyifu” badala ya kuwatambua na kuwakubali katika utendaji wa ofisi na huduma zao.2
Wakati tunapojifunza maandiko tunapata umuhimu wa maelezo ya Conner. Yesu mwenyewe
aliweka wazi kwamba cheo na madaraka ya juu hayana nafasi katika ufalme wa Mungu.
Aliwahukumu wale wanaopenda kukaa katika viti vya heshima katika sikukuu, na viti muhimu
(Chief seats) katika masinagogi, na wale waliotaka kusalimiwa katika sehemu za masoko kwa vyeo
vya kujipachika. Hali yake (Kristo) katika jambo hili bado iko vile vile na itabakia bila kubadilika
katika mafundisho yake yote.
Mathayo 23: 6 –10
Hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi, 7 na kusalimiwa masokoni
, na kuitwa na watu, Rabbi 8 bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni
Mara 8 neno diakoneo kuwa mhudumu, kungojea (mtumishi wa nyumbani au kama mwenyeji), kutumika
linatumia wadhifa wa shemasi, Mathayo 20:28; 25:44; Marko 10:45; Warumi 15:25; Waebrania 6:10; I Petro 1;
12; 4:10; 4:11.
Neno Huperetes limetumika mara 3 - msaidizi wa mpiga kasia, vuta kasia, (hupo = wa chini ya, eretes = piga
kasia) wa chini ya ; msaidizi , mhudumu, ofisa, mtumwa.
Neno Hupereteo limetumika mara moja - wa nchini ya, kutumia, kutumia china ya. Kufanya huduma ya
huperetes.
Neno leitourgos limetumika mara 2 - mtumishi wa watu, atumikaye hekaluni au anayeitumikia injili au mfadhili
wa watu.
Neno leitourgeo limetumika mara moja - mtumishi wa watu kama kuhani.
Neno ergaomai limetumika mara moja - kufanya kazi kwa bidii, tekeleza (kufanya itumike) kufungamanisha
pamoja.
Neno choregeo limetumika mara moja, kuwa kiongozi wa wachezaji, kwa mfano kutoa kumpatia kitu,
mhudumu/mtumishi.
Neno didomi limetumika mara moja - kutoa, fadhili, kuleta, kutenda/kufanya, kukomboa, kutoa,kuridhia, fanya,
toa, kuwa na, sawasawa limetumika katika hali ya upana zaidi
Neno diakonia limetumika mara moja - kuhudumua, msaada, huduma, msaada katika dhiki.
Neno parecho limetumika mara moja - kushikiria kwa karibu, kumudu, kuonyesha hadharani kumpatia mtu kitu,
leta, fanya, toa, tunza, mtumishi, toa.
2 Kevin J. Conner, The Church in the New Testament (Portland: Bible Temple Publishing, 1989), p. 195
4
ndugu. 9 Wala msimwite mtu baba duniani, maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni. 10 Wala
msiitwe viongozi; maana Kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo.
Kama Yesu angelikuwepo duniani leo bila shaka angeliwaambia hawa wapenda vyeo, kama
alivyofanya katika nyakati zake alivyowakemea wale wote waliotaka kuitwa rabi (mwalimu) au
Bwana. Si kwamba angelielezea tu vyeo kama vile: Baba Mtakatifu, Mtakatifu, Mama Mkuu,
Kardinali, Askofu Mkuu bali pia angejumuisha vyeo maarufu vilivyomo katika Wapentekoste na
Wainjili, kama vile: mwenye haki Mheshimiwa wa kuogopwa (Right Honourable Reverend )
muogopwa zaidi; (very Reverend), Daktari (siyo utabibu),Askofu, mpakwa mafuta Mkuu wa
Mungu (Greatly Anointed man of God), n.k. wakati tu wepesi wa kuvikataa vyeo vya Kiroman
Katoliki, wao vile vile waweza kuturudishia kuwa nasi tuko vile vile, kwa kupenda vyeo na
madaraka vimeota mizizi ndani ya moyo wa mwanadamu.
Hivi vyeo vya Kimwili vimechangia sana kuanzisha ngazi za utumishi ambazo zinaugawanya
mwili wa Kirsto katika hali ya juu “na ya chini” na kuwatofautisha waamini, hii ni kinyume na
maandiko.
Ni lazima ielezwe wazi na kukaziwa kwamba ikiwa tunataka kuwa sehemu ya huduma ya ufalme
wa Mungu, mwelekeo wetu ni lazima usahihishwe na nia zetu zisafishwe kutoka kwenye tamaa za
kimwili. Inapendeza sana kuwa waamini wa nyakati za Biblia walijulikana kwa mfumo wa majina
yao ya kwanza. Wanaume na Wanawake katika Neno la Mungu, hata wafalme, manabii, mitume,
waamuzi, wainjilisti, wazee au wengine wametambulikana kwa majina yao ya kwanza. Wengi wao
hatujui hata majina yao ya ukoo. Tunawafahamu kama vile Musa, Yoshua Yusufu, Eliya, Samweli,
Petro, Paulo, Stephano, Luka n.k. Inaonekana hata wahakuwa na tamaa ya vyeo, wala hawakuwa
na fikra za madaraka.3 Kilichowafanya wafanye vizuri zaidi haikuwa vyeo vyao bali ni upako
ambao kupitia huo waliwezeshwa kufanya vizuri katika wito wao wa Ki- Mungu. Hii inadhihirisha
kuwa wito wa Mungu si ule usio na mamlaka na majukumu bali ni ule wa wajibu wa kiroho na
madaraka / mamlaka.
3. Huduma au kupanda ngazi ya Kanisa?
Huduma za Roho Mtakatifu hazipaswi kutumiwa kama hatua za kupandia ngazi kutoka cheo cha
chini kwenda cheo cha juu cha Kanisa (hiarachy). Hata hivyo hutokea kwamba waamini
hupandishwa katika mtazamo wa kishughuli, na kupanda vyeo mpaka nafasi ya juu kadri
iwezekanavyo. Wanaweza wakaanza kama shemasi baadaye wanapandishwa kuwa mzee. Kutoka
hapo wanainuliwa kwenye “cheo” cha mwinjilisti na baadaye mchungaji, na nafasi zingine za
uongozi ambazo zinaweza kufuata. Wengine huenda mbali zaidi hata kufikia “kuwapandisha “
watu na kufikia katika nafasi ya manabii na mitume.
Katika kanuni si vibaya waamini kuthibitisha huduma zao katika kiwango cha chini cha wajibu na
kuwainua kufikia kwenye nafasi ambayo Mungu ameiweka wakfu kwa ajili yao. Kwa namna
yeyote ni kosa kupanda ngazi ya kuinuliwa kwa sababu tu nafasi imejitokeza, ijapokuwa hawana
wito wa huduma iliyotolewa. Vitendo hivyo huelekea katika kushindwa na machafuko. Si Kibiblia
kuziona huduma za Roho Mtakatifu kama nafasi za kupandishwa vyeo. Mtazamo kama huu wa
3 Ibid., p. 209.
5
kimwili ni lazima upingwe kwani utazuia kazi ya Mungu. Kama tunaridhika na wito wetu,
hatutakuwa tuna juhudi kubwa bali pia tutapata urahisi wa kuheshimu huduma za wengine kuliko
zetu wenyewe.
4. Huduma siyo ajira.
Kuhusika kwetu katika ufalme wa Mungu hauko sawa na ajira za kidunia. Wale ambao wanaiona
huduma kama kazi ya kujipatia mapato (nine - to –five) ambapo malipo ya ziada yanaweza
kutegemewa kwa ajili ya masaa ya ziada na kudai kurudishiwa kila kitu tunachofanya, hatujaelewa
asili ya kazi ya Kristo.
Tunajihusisha katika huduma kwa kujitoa na kuwajibika katika wito wa Mungu. Ni yeye ambaye
ametuita, na siyo wanadamu. Haijalishi hata kama tunatumika kama mchungaji, karani wa kanisa,
katibu, mwalimu wa shule ya jumapili au kiongozi wa idara, hii inapaswa kukumbukwa.
Kumtumikia Mungu daima itahusisha kujitoa dhabihu / Mhanga, kujiweka wakfu, kujitoa na
wajibu kwa ajili ya wito wa juu.
Hata hivyo, hii haimanishi masharti ya kazi hayapaswi kuwa mazuri. Yanapaswa kuwa! Bado,
dhehebu ambalo Mungu ametuweka sisi ni lazima kimsingi lionekane kama sehemu kupitia hilo
tuna nafasi ya kuitendea kazi huduma yetu au wito. Kazi zetu ndani ya kanisa lililotolewa kamwe
halipaswi kutazamwa kama mwajiri –uhusiano wa Mwajiriwa. Huduma ya kiroho huonekana
katika kiwango tofauti, kama “Mwajiri” ni Mungu, na siyo mwanadamu.
5. Huduma ya pamoja –hakuna watazamaji.
Baadaye ukuhani wa waamini wote umethibitishwa tena na ukiri mpya kama fundisho la
Kimaandiko. Bado kuna mambo mengi yanayofanyika katika Kanisa la leo ambayo yanamizizi
yake katika historia, tamaduni na mila badala ya Neno la Mungu. Moja ya hayo ni mtazamo
potofu kwamba mchungaji abebe mzigo wote wa kazi na wajibu wa kanisa la mahali pamoja. Hili
wazo potofu limechukuliwa tangu nyakati kabla ya matengenezo na limeelezwa wazi katika
mgawanyiko usiokuwa wa Kibiblia katika mwili wa Kristo katika mchungaji na wasiowachungaji,
kama vile waliosomea kazi / wanaofanyakazi kwa malipo na wasiolipwa. Kama ilivyokwisha
elezewa wazo hilo ni geni katika Agano jipya. Pale tunapata ngazi tofauti za majukumu, kama vile
uongozi n.k., lakini ona kuhusika kwa wote ndani ya kanisa. Watchman Nee anaelezea kwamba
kamwe halikuwa kusudi la Mungu kwamba wengi wa waamini hujiweka wakfu wenyewe bila ya
kazi zao za kitaalamu na kuiacha kazi ya kanisa katika mikono ya wataalamu wa kiroho.4 Hivyo,
mfumo huu wa uchungaji wa mtu mmoja uko katika ulimwengu mzima, bila kujali dhehebu,
kwamba kila mmoja anayeelezea jambo hili au kujaribu kurudi katika mpango wa Agano jipya
anapaswa awe radhi kukabiliana na upinzani mkali.5 Vitabu vingi vya thiolojia ya Kichungaji na
masomo mengi yanayofundishwa katika somo hili katika vyuo vya kikristo na shule za Biblia
yanamuonyesha mchungaji kama ndiye “mtendaji”. Yeye ni mbebaji wa mizigo na mfanyaji kazi
ya huduma, ambayo inamuwekea mzigo ambao sio wa kimaandiko juu ya mtu mmoja, hiyo
4 Watchman Nee, Das Normale Gemeindeleben (Wuppertal: Brockhaus Verlag, 1974), p. 45.
5 Rejea vitabu kama: Pastoring the Smaller Church by John C. Thiessen, au The Ministry of Pastor and
Church by Paul H. Walker
6
inafanya “mdomo wa chupa” (bottle –neck) ambayo inazuia mtiririko wa huduma za Mungu
zenye upako ndani ya kanisa.
Maandiko yanatuonyesha tofauti ya wazo ambalo linapaswa kufuatwa. Ijapokuwa kazi ya
viongozi, haijarishi ikiwa ni sehemu, kiwilaya, kimkoa, kitaifa au ngazi ya kimataifa, ni mhimu na
kazi yao ni kubwa sana hawapaswi kuifanya yote peke yao. Hawakuwekwa kuwaondolea
washirika majukumu yao, ila kuwagawia majukumu na kuwahakikishia kwamba wanatambua
wajibu wao na kufanya kazi kwa bidii.
Inasikitisha kusema huduma mara zote imebebwa na waaminifu wachache wakati wengine
wamekaa tu, kwa ajili ya kuhudumiwa. Kwa sababu yoyote ya kutokuhusika itakavyokuwa,
haiwezi kukubalika Kibiblia. Baadhi ya Waamini kamwe hawaonyeshi wazi kufikiri kuwa Mungu
anawatarajia wao kuhusika barabara. Wanaamini kufanya sehemu yao kwa kukodisha majengo na
kumsaidia mchungaji ambaye anapaswa kufanya kazi. Kwa kawaida ni watu wanaoshutumu
wakati mambo yanapofanyika kinyume na matarajio yao. Wengine wanashindwa kuhusika kwa
sababu hawajui kutambua sehemu ya huduma zao, na hawana uhakika na kile ambacho
kingetarajiwa kwao. kisha kuna wale ambao wanajihisi hawawezi na sio muhimu, na wanashindwa
kufanya kitu chochote. Hata hivyo, haijarishi sababu yoyote itakavyokuwa, hakuna udhuru kwa
kutohusika. Watu ambao wameamua kuwa “watazamaji” lazima watubu utofauti wao, na roho ya
shutuma mara kwa mara, na kuchukua nafasi kuhusika katika huduma. Mara watakapohusika,
watajikuta kama vile kwenye mchezo wa mpira, shutuma zitokanazo na “vyeo” ni tofauti na
shutuma za uzoefu uliopatikana katika “kazi” (utendaji).
Mara zote ni rahisi zaidi kushutumu kama mtazamaji kuliko kuwemo katika mchezo. Na hivyo
ndivyo inavyofanyika Kanisani. Shutuma zinakuwa wazi zaidi, nzuri zaidi na yenye mlingano
wakati watu wanapojihusisha wenyewe binafsi. Wale wanaokaa nyuma, si kwa sababu ya utofauti
bali ni kwa sababu ya kutojua na kuwa na hisia za kujiona duni ni lazima watiwe moyo,
wafundishwe, na wawekwe kwenye huduma zinazowafaa ambazo zitawasaidia kutambua wito wa
Mungu.
Ni muda unaofaa / unaokubalika kwa Kanisa la leo lilipo kuelewa kwamba uhusiano wa
watendaji na watazamaji, kama waigizaji kwa watazamaji hauna nafasi katika kanisa. Kila mshirika
amepewa kazi na wajibu / majukumu katika huo aufanyie kazi. Mtu mmoja alieleza kwa usahihi
kwamba kila mkristo mpya aliyeongezeka katika mwili wa Kristo atatoa kipawa kinachohitajika
kwa ajili ya kufanya kazi.6 Kwa hiyo moja kati ya kazi kubwa ya huduma tano ni kumsaidia kila
mwamini kupata nafasi yake ya kutumika, kutoa fursa kwa ajili ya kuifanyia kazi.
6. Kutambua huduma nyingine.
Kupata mtazamo wa Kibiblia tunapaswa kujifunza kuthamanisha / kutathimini na kuhukumu
matendo yetu, ubora, mila na hisia / fikra kwa neno la Mungu, na kutenda kama tunavyoona bila
kujali kitakachotokea. Agano jipya linaonyesha wazi kuwa huduma ni ya pamoja ya mwili mzima
na siyo amri au siyo faida ya wachache waliochaguliwa. Ni lazima ichukuliwe katika hali ya urahisi
6 Ralph Neighbour, This Gift is Mine (Nashville: Broadman Press, 1974) , p . 27.
7
na siyo katika hali ya kiburi / majivuno kadri kila mshirika aipatapo nafasi yake, kwa hiyo
huchangia katika ukuaji na vita vya kiroho vya kanisa. Hili litafanikiwa ikiwa tutafuata ushauri wa
Paulo.
Warumi 12:3 –5
3 Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyepo kwenu asinie makuu kupita
ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani. 4
kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; 5
vivyo hivyo na sisi tuliowengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.
Upeo kidogo kuhusu wito mwingine kuliko wito wetu ni kuliharibu Kanisa. Hata hivyo, viongozi
wa kiroho mara nyingi hawatambui au kupuuza huduma zingine. Donald Gee ana mtazamo
kwamba wainjilisti wenye kujawa na huruma kwa wale waliopotea wanaweza wakapuuzia
umuhimu wa mafundisho ya imani za Kanisa. Kwao walimu huonekana wakavu na wanaochosha.
Walimu na Wachungaji huwaona wainjilisti kujifanya na kujawa na misisimko. Hata hivyo hawa
wawili wanaweza kukubaliana kirahisi kuwa manabii ni kama walio ehuka, ambao nao huwaona
ndugu zao kama watu wa kimwili.7 Hata hivyo Mungu anamtarajia kila mtumishi kukubali na
kuheshimu wengine wanapozifanyia kazi za huduma zao walizopewa. Badala ya kuonyesha hali ya
kudharauliana tunapaswa kujengana na kuinuana sisi kwa sisi. Tukifanya kazi kwa pamoja
kutalifanya Kanisa kuwa lenye afya.
Si tu tunapaswa kujifunza kuwaheshimu waamini wengine na kuziheshimu huduma zao bali
tunapaswa kuridhika na wito wetu. Hivi ndivyo tutakapoweza kuuweka mwili katika hali ya
umoja. Ukweli huu umewekwa wazi kwa kuufananisha mwili kama Paulo alivyoeleza katika:-
1 Wakoritho 12:12 –27.
Maana kama vile mwili ni mmoja, na unaviungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni
mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. 13 kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili
mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru, nasi
sote tulinyweshwa Roho mmoja. 14 kwa maana mwili si kiung0 kimoja, bali ni vingi;. 15 Mguu
ukisema, kwa kuwa mimi si mkono , mimi sio wa mwili, je! Si kwa mwili kwa sababu hiyo? 16 Na
sikio likisema, kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili, je! Si la mwili kwa sababu hiyo? 17 kama
mwili wote ukiwa jicho ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio kuwapi kunusa? 18 Bali Mungu amevitia
viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka. 19 Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja,
mwili ungekuwa wapi? 20 Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja. 21 Na jicho haliwezi
kuuambia mkono, sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, sina haja na ninyi.
22 Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi. 23 Na vile
viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu
visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana. 24 Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; bali
Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa; 25 Ili kusiwe
na faraka katika mwili bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe. 26Na kiungo kimoja
kikiumia, viungo vyote huumia navyo, na kiungo kimoja kikitukuzwa viungo vyote hufurahi pamoja
nacho. 27 Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake.
Kuna huduma tofauti tofauti bali mwili ni mmoja. Hivyo kila wito unapaswa kutendewa kazi
wakati tukikumbuka uwepo na umuhimu wa washirika wengine. Mbele ya Mungu, umoja ni wa
muhimu zaidi kuliko huduma. Kila kiungo cha mwili kimeunganishwa na kinategemeana na
7 Donald Gee, Die Gaben Christi für den geistlichen Dienst, (Fix Verlag Vahingen Enz, n.d.), p.13
8
kingine katika Kristo. Kama ilivyo katika mwili ambapo macho, yanahitaji masikio, masikio
yanahitaji mikono, mikono inahitaji miguu, Waamini wanahitaji huduma na kujaliana wao kwa
wao. Baadhi ya viungo vya mwili vinaonekana zaidi (more visible) na kupokea usikivu zaidi kuliko
vingine.
Lakini vipo vingine ambavyo siyo dhahiri zaidi kama moyo, mishipa ya damu, ini n.k. mwili
usingefanya kazi. Hivi karibuni nilikuwa na bahati / heshima ya kusaidia katika ujenzi wa jengo la
ofisi la zamani katika sehemu ya kukutania / mkutano katika ya makanisa yetu Ujerumani.
Wakati ukarabati wa jengo ulipomalizika kila mmoja alishangaa / alivutiwa na uzuri wa dari ya
mbao (wooden ceiling ) na sehemu yote kwa ujumla.
Nyaya za Umeme zilichimbiwa kwenye ukuta na ndani ya dari hakukuwa kunaonekana tena lakini
bila ya hizo taa za kwenye dari zisingefanya kazi. Muundo mzima wa Amplifier (amplifaya)
usingekuwa na nguvu, n.k. ijapokuwa kazi iliyofanyika isingeliweza kuonekana hata hivyo ilikuwa
ni muhimu kama vile uzuri ulioonekana katika sehemu ya Mkutano / ya kukutania. Na hivyo
ndivyo ilivyo katika huduma tofauti zilizopo katika mwili wa Kristo. Ingawaje baadhi
hawaonekani kama wengine hata hivyo ni muhimu kufanya kazi katika nafasi zao na wajihusishe
kikamilifu katika Kanisa.
Naomba nitumie mfano mwingine kuelezea ukweli huu. Kama ninavyofundisha semina za
uongozi huwa ninakutana na Waangalizi; Uongozi wa Kitaifa na mtafsiri wangu. Bado,
ninatambua kwamba kuna watu wanaofanya kazi bila kuonekana.
Kuna wale ambao wanaandaa, kupika, kuweka mazingira kuwa safi, kuandikisha watakaoshiriki na
wengine wengi “hawaonekani”, lakini semina isingefanikiwa bila wao. Hivyo nao ni muhimu
kama wale wanaofundisha na wale wanaohudhuria vipindi vya semina. Hii ndiyo picha halisi ya
huduma ndani ya mwili wa Kristo. Wakati huduma zingine zinaonekana zaidi na nyingine
hazionekani kwa “uwazi” lakini bado ni muhimu kama zile zinazoonekana.
Hadithi ya “Mkutano wa vyombo vya kazi vya seremala, ambayo nimeisikia hivi karibuni
inaonyesha ukweli huu katika hali ya kipekee. Mkutano uliitishwa baada ya Wanachama wa baraza
kumwomba Mwenyekiti bwana nyundo ajiuzuru, ambaye daima alikuwa mpiga kelele. Alikubali
kuyaachia madaraka ikiwa ndugu skrubu (screw) pia naye angeondoka kwa vile alikuwa mdogo na
hakuonekana kuwa muhimu na mara zote / daima ilibidi azungushwe zungushwe ili aende mahali
popote “Nitakwenda” ndugu Skrubu (screw) akajibu, ikiwa bwana randa (plain) pia ataondoka.
Kazi yake haina kina (depth) na huharibu uso wa juu tu (surface). “ikiwa nitaondoka”, bwana
randa alisema, hata bwana rula (ruler) pia naye inabidi afungashe, kwa kuwa kila anachofanya ni
kuonyesha mapungufu ya wengine. Kwa kuwa huduma zake zilikuwa hazikubaliki tena, bwana
rula alikubali kuondoka lakini kwa sharti moja tu, kwamba bwana msasa angelifukuzwa pia, kwa
vile alikuwa mwenye fujo sana na mara zote alikuwa akiwasugua wengine vibaya. Wakati bwana
msasa alipokuwa akionyesha kwa nini bwana msumeno “asifukuzwe” pia, kwa vile alikuwa
akikata kila kitu katika vipande vipande, Seremala wa Nazareth aliingia ndani ya chumba.
Kila kitu kikanyamaza. Kwa mguso wa Bwana wake alichukua vifaa na kuendelea kufanya kazi ya
madhabahu aliyokuwa akiijenga. Kwa mara moja / ghafla kila chombo kilitambua tena kinafaa
9
katika matumizi yake na kukamilisha kazi ya wengine. Aliona hakuna haja ya kumdharau yeyote
kati yao, ijapokuwa mashitaka yao yalikuwa ya kweli, lakini katika mikono yake ikawa ya kufaa,
kama alivyowatumia wote katika muda na sehemu inayofaa.
Lazima tukumbuke haya mawazo ya kimaandiko kuhusu huduma, ambayo tumeyatamka kama
sasa tunapotazama huduma mbalimbali zilizoonyeshwa katika Agano jipya. Haijalishi jinsi
huduma zingine zitakavyoonekana maarufu daima / lazima siku zote zitumike katika utayari wa
kutumika (utumwa)
-.-.-.-.-.-.-.-.-
10
II. HUDUMA ZA KIROHO NA KARAMA ZA KIROHO
Kutimiza / kufanikisha lengo la kanisa, Kristo anatoa mwili wake wenye karama za kiroho tisa na
huduma nyingi za kiroho. Baadhi ya walimu wa Biblia wanaziweka hizi mbili katika aina moja –
“karama za Kiroho”.
Hata hivyo, kwa kufanya hivyo kunaleta dosari/ukungu katika maono kwa tabia mbali mbali na
kujaliwa utajiri wa kiroho kwa pamoja. Ili kuepuka utata tutaziangalia kama karama na huduma
zilizojitenga katika Roho yule yule mmoja. Kwa kueleweka vizuri zaidi zitatofautishwa kama
huduma za kiroho na karama za kiroho. Kwa wakati huo huo lazima tutambue kwamba nje ya
zile zilizoorodheshwa katika Waefeso 4:11 huduma zote zimeonyeshwa kama Charismata, neno lile
lile la Kiyunani limetumiwa kwa ajili ya “karama / vipawa tisa vya kiroho.
1. Ufanunuzi wa maneno.
Karama za Roho katika Warumi 12:6- 8 na 1Wakorintho 12:7-10, 28-31 zimeonyeshwa kama
Charismata, ambazo zimetafsiriwa kama “Vipawa / Karama za neema”8 . Zinapokelewa katika
misingi ya upendeleo na neema ya Mungu kwetu sisi ambao hatukuustahili, na havipatikani kwa
kujitaabisha. Katika 1Wakorintho 12:1. Paulo anaelezea vipawa hivi kama Pneumatikos (tafsiri: za
kiroho, inayofungamana na Roho, au kiroho), ambayo inaonyeshwa katika kiingereza kama
karama za Roho, baada ya hapo anazionyesha moja moja kama kipawa cha neema (Charismata).
Waalimu wengi wa Biblia wanazihusisha / jumlisha huduma za Waefeso 4:11 miongoni mwa
Charismata. Hata hivyo, tunaposoma muktadha (context) huduma hizi hazielezwi kama Charismata
bali domata9 (sura 4:8). Inafurahisha kutambua kwamba orodha tatu ya karama hizi za Uongozi
katika 1Wakorintho 12:28 zilikuwepo kabla ya Paulo kundelea na Charismata. Ghafla ukafuata
mstari ule ule, hivyo hazihusishi miongoni mwa Charismata.10
Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza Mitume, wa pili Manabii, watatu Waalimu,
kisha Miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za Lugha.
Hata vipawa vyote, isipokuwa huduma za uongozi katika Waefeso 4:11 zimeelezewa kama
Charismata, tunahitaji kutofautisha kati ya vipawa tisa vya kiroho vinavyojulikana na vile
vinavyobakia. Sababu ya hii, kama tutakapoona baadaye, imesimamia kwenye ukweli kwamba
karama tisa maalum za kiroho ni msukumo/ matokeo ya muda ya Roho, wakati karama
zilizobakia zinatabirika zaidi, na za kudumu. Zile za mwanzo ni za muda, katika asili na
zinajidhihirisha zenyewe katika wajibu wa uongozi wa Roho na kwa muda (hapo hapo). Na zile
zingine zinakuwa sehemu ya kudumu katika maisha ya Kiroho ya Waamini, kwa hiyo
zimetambuliwa na kuelezewa kama huduma. Hivyo “Karama” inakuwa huduma kama inapokuwa
ya “kudumu”, inayoendelea.
8 Karama (Charisma) itolewayo na Mungu nineno ambalo lipo katika umoja, ambalo limetokana na neno la
charis neno la Kiyunani lenye maana ya Neema.
9 W.E.Vine, An Expository Dictionary of the New-Testament Words. (Old Tappan: Fleming H. Revell,
1966), p. 147. Kufuatana na Vine, doma linakazia zaidi kwenye tabia (silika) inayoonekana ya karama kuliko
wema wake wa asili.
10 Katika I Wakorintho 12:4 Paulo anaeleza kwamba pneumatikes kama ifuatavyo; 1. charismata: karama
kipawa cha neema; 2. diakonia: karama ya utumishi, huduma. 3. energema: karama ya kupendekeza au kufaa
kufanya kazi, nguvu, utendaji kazi.
11
Katika somo hili tutaelezea / onyesha matokeo ya Roho kama “karama za Roho”, na karama
zilizobakia kama huduma za kiroho ambazo tunazigawa katika sehemu mbili, kama huduma za
uongozi na “huduma za Masaidiano”.
(1.) Huduma za Kiroho.
Huduma za Uongozi (huandaa) hutoa maelekezo ndani ya Kanisa na kuuandaa mwili kwa ajili ya
huduma. Wakati huduma za masaidiano hutoa nafasi kwa ajili ya utendaji kwa kumhusisha kila
mshirika, na kuweka huduma za Uongozi huru kwa ajili ya kutangaza Injili.
Jedwali lifuatalo litaturahisishia kuonyesha mchanganuo huo kwa uwazi zaidi.
HUDUMA ZA UONGOZI HUDUMA ZA MASAIDIANO
1. Mtume
2. Nabii
3. Mwinjilisti
4. Mchungaji
5. Mwalimu.
1. Mfariji
2. Shemasi/ Utumishi
3. Masaidiano
4. Utoaji
5. Ukarimu
6. Uongozi
7. Utawala / Serikali
8. Kuonyesha huruma
(2.) Karama za roho.
Karama ambazo zimetajwa katika 1Wakorintho 12 kwa kawaida zimeonyeshwa kama karama za
Roho, madhihirisho ya Roho, au msukumo wa kiroho, na inahusisha yafuatayo, ambayo
imegawanywa katika sehemu tatu.
Karama za Ufunuo Karama za utendaji Karama za kunena /
kusema
1. Neno la hekima
2. Neno la maarifa
3. Kupambanua roho
4. Imani
5. Karama za uponyaji
6. Matendo ya miujiza
7. unabii
8. kunena /lugha
9. tafsiri za Lugha
Karama / vipawa vya udhihirisho vinatofautiana katika mitazamo mbali mbali na zile za huduma
za kiroho. Kwa hiyo ni muhimu kutambua tabia hizi mbili, na kutofautisha upekee wake.
Kushindwa kufanya hivyo kutaleta matokeo ya mawazo potofu / mabaya na hata kuleta
machafuko katika mwli wa Kristo.
2. Asili na tabia za huduma za Kiroho.
Kulingana na tabia za Ki -Ungu, huduma tano za Uongozi zinatambuliwa kirahisi kama huduma
za Kiroho. Hizi zote ni za sauti kwa vile zinahusisha uhubiri wa Neno la Mungu, chini ya upako
wa Roho wake Mtakatifu, kama vile yalivyo matokeo ya Miujiza na maajabu. Wakati huduma za
masaidiano ni huduma za kiroho pia, zinafananishwa na mifano mingi na vipawa vya asili, karama
au uwezo.
12
Kuhusishwa katika huduma kamwe hakuwezi kuwa jambo / matakwa ya mwanadamu, huja kwa
mwitikio wa wito wake (Mungu). Ukweli huu uko wazi tunaposhughulika na vipawa vya uongozi,
bali pia zinatumika katika huduma za mwili, kama vile huduma za masaidiano. Kwa namna
nyingine inaonekana kwamba mtu anaweza akatumia uwezo wake wa asili bila kujihusisha
mwenyewe kama wito wa Kimungu umekwisha pokelewa.
Hata hivyo, maumivu mengi na huzuni hujitokeza katika mtazamo huu. Inasisitizwa na
kushauriwa kuhakikisha kwamba wale walio na sauti ya kupendeza, wapiga vyombo, wanaojua
jinsi ya kutunza pesa, au wanautalaamu na ujuzi ndio haswa Mungu amewakusudia kuwatumia
katika huduma kwa ajili ya hiyo wamepewa vipawa vya asili. Kuwa na uwezo wa namna fulani si
lazima kumaanisha kwamba Mungu amemuita mtu katika eneo la huduma ambalo anaweza
akamtumia katika kipawa chake cha asili au ujuzi aliosomea. Kwa mfano:- mtu anaweza akawa
Mhasibu mzuri sana au mtunza fedha lakini utunzaji wa fedha kanisani unahitaji sifa za ziada. Siku
zote hakuna pesa za kutosha wakati uongozi unapoingia kwenye jambo jipya katika malekezo ya
Mungu. Wale wanaotumia akili zao za kawaida (sishauri kwamba hatupaswi kufanya hivyo kwa
kiwango kikubwa) na kuhesabu tu pesa za kanisa zilizopo, zitazuia kuupanua ufalme wa Mungu.
Kutumia mfano mwingine. Wale waliojaliwa kuwa na sauti nzuri za asili si lazima wawe na upako
wa Mungu kugusa mioyo kwa jumbe za nyimbo. Ralph Neighbour anathibitisha kwamba
tumekosa mafundisho ikiwa tunafikiri kwamba vipawa vya kiroho huonyesha kutumia vipawa
vyetu vya asili kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Vipo wazi zaidi kuliko vipawa vyetu vya asili, au
vipawa vya kimwili.11 Mara nyingi Mungu hutumia vipawa vya asili na huongeza wito wake na
baraka. Wale walioitwa lazima, katika mazingira ya kawaida watatambulikana kwa uongozi wa
kiroho, ambao kazi yao ni kutoa nafasi / muda kwa ajili ya huduma na kuwaandaa wale ambao
huonyesha dalili za wito wa Ki- Mungu katika maisha yao.
Ijapokuwa wanatofautiana katika hali fulani, yote haya mawili, uongozi na huduma za mwili zina
tabia zifuatazo ambazo zinazitofautisha na karama tisa za Roho:-
(1.) Tambua huduma
Vipawa kwa ajili ya huduma huonyesha eneo la utendaji kazi katika mwili wa Kristo. Baada ya
huduma kupokelewa ni muhimu zifanye kazi ndani ya mipaka yake, haijarishi ni jinsi gani mtu
anatamani wito mwingine. Inatisha kwamba baada ya walioitwa kama Wachungaji wanashindwa
kufanya kazi ndani ya mipaka ya wito wao, eti kwa sababu huduma ya uinjilisti inawavutia zaidi.
Inasikitisha sana wakati Mwinjilisti anapofanya kazi kama Mchungaji kwa sababu ya fedha
zinazotolewa na Kanisa la mahali pamoja (local Church). Hali kama hizo zitasababisha kutofanya
kazi kiusahihi na kukatishwa tamaa. Hivyo, kila mwamini lazima ajitambue na kuendeleza karama
ya huduma yake, na afanye kazi ndani ya mipaka yake.
(2.) Sehemu ya kudumu ya maisha ya kiroho
Huduma iliyopokelewa na mwamini katika wakati wa kuitwa kwake inakuwa sehemu ya kudumu
ya maisha yake ya kiroho “Haiji” na “Kwenda” kama karama za Roho lakini hukaa na mwamini
katika msingi wa kudumu. Kwa mfano mchungaji sio tu mchunga kundi wakati akiwa
11 Ralph Neighbour, This Gift is Mine (Nashville: Broadman Press, 1974), pp. 21-22.
13
madhabahuni, lakini lazima aishi, kutenda na kufanya kazi kwa masaa 24 kwa siku nzima. Vilevile
si tu kwa wale ambao wako katika nafasi za uongozi bali ni kwa ajili ya wale wanaofuata wito wa
Mungu.
(3.) Mwamini kutambuliwa na huduma
Waamini watatambuliwa kwa huduma zao maalumu, hasa ikiwa watakuwa wameitwa katika
uongozi kwa hiyo, watu wanaonekana kama wachungaji, wainjilisti, wazee nk. Wakati tunafahamu
ukweli huu tunapaswa kukazia kwamba huduma za kiroho hazipaswi kutumiwa kama vyeo kama
vile daktari, profesa, au mkurugenzi. Wale wanaokazia kuitwa muogopwa/mhofiwa (Reverend),
Mchungaji, Askofu na wengine kama hao, ni lazima ikumbukwe kwamba haya majina huonyesha
huduma ya utumwa katika mwili wa Kristo, na siyo vyeo vya heshima/umaarufu kama
inavyotumika kwenye makampuni na siasa za dunia. Hata hivyo huduma zisizokuwa za sauti au
za usemi haziji kwa umaarufu wa cheo, hata hivyo watu wanajulikana na kutofautishwa ndani
katika mwili wa Kristo, zimesimama katika kipawa cha huduma zao.
3. Asili na tabia za karama za kiroho
Karama tisa za kiroho si za kawaida ni za Ki-Mungu katika tabia zake, na hutegemea katika
utendaji wake katika msukumo, uvuvio na upako wa Roho Mtakatifu. Hazina uhusiano katika
uwezo wa asili, kama baadhi ya huduma za kiroho zifanyavyo kazi. Tabia zake ni kama ifuatavyo:
(1.) Karama ya kiroho haihitaji wito
Karama za Roho zaweza kujidhihirisha kupitia mwamini yeyote wa mwili wa Kristo. Kinyume
chake katika huduma,hakuna wito dhahiri unaohitajika kabla ya karama kuanza kufanya kazi.
Kuna uhusiano mdogo kati ya “nafasi” ya mtu (cheo) kanisani na karama za Roho zinazofanya
kazi kupitia yeye. Udhihirisho wa vipawa hufanya kazi kupitia mshirika yeyote wa mwili wa
Kristo, haitegemei huduma maalumu. Huduma zingine, hata hivyo, hasa zile za uongozi zitakuwa
zikiambatana na karama maalumu za kiroho katika msingi wa kawaida wa kuzungumza na kama
tutakavyoona baadaye.
(2.) Karama za kiroho ni za muda
Karama za kiroho hazitolewi katika msingi wa kudumu. Zinategemea msukumo wa Roho, na
hazimilikiwi na mtu yeyote, anayeweza kuzitumia au kuzitendea kazi kama anavyotaka, kama
ambavyo imekuwa ikifundishwa katika miaka ya karibuni. Hata hivyo, karama nyingine zaweza
kujidhihirisha kwa kujirudia rudia kupitia mshirika huyo huyo, kwa hiyo huonekana kwamba
zinaendelea kuwepo ndani ya maisha ya mtu huyo.
(3.) Karama za kioho hazilingani na huduma
Baadhi ya vipawa vya huduma, hasa zile za uongozi zinaunganishwa na karama fulani za Roho
kama sehemu na ushahidi wa wito wa Ki-Mungu. Kwa mfano, Mwinjilisti kila mara atadhihirisha
karama za uponyaji na karama za matendo ya miujiza. Nabii kwa vyovyote hazilingani na karama
ya unabii, kama tutakavyoona atadhihirisha karama ya unabii, na neno la maarifa. Hata hivyo,
14
udhihirisho wa kipawa cha Roho haumpi mtu huduma kwa ghafla. Hakuna kitu kama hicho
kama huduma ya lugha/kunena, au huduma ya hekima au maarifa. Huduma hizi hutokea kwa
ghafla, udhihirisho wa muda, msukumo wa Roho Mtakatifu, na utendaji wake unategemea Roho
Mtakatifu. Zinakuja na kuondoka kwa msukumo wake na kwa hiyo kamwe haziwezi kuwa
“huduma”, ingawaje zinahudumu katika mwili wa Kristo.
Wakati tunapoendelea kuzitofautisha tabia hizi za huduma za kiroho na karama za kiroho sasa
tutaanza kuziangalia huduma tano za uongozi ambazo pia kwa kawaida zimejulikana kama
huduma tano. Wakati tunafanya hivyo tutachunguza tabia zake, makusudi na kazi yake, uthamani
wake na utendaji wake katika Agano Jipya na katika kanisa la sasa.
Sehemu maalumu ya mazungumzo itatolewa kwa ajili ya kuangalia zaidi sifa za kibiblia kwa kila
mtu aliye na moja ya huduma hizi.
Kabla hatujamaliza kufanya haya yote, tutaanzisha uhitaji kwa ajili ya uongozi katika mwili wa
Kristo na kuangalia kwa ufupi chanzo cha huduma hizi, kazi zao na utendaji kazi kwa mpango wa
Mungu na kwa ajili ya kanisa lake kwa ujumla.
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-
15
III. HUDUMA ZA UONGOZI
Bibilia inaonyesha kwa uwazi kuwa Mungu ameweka huduma tofauti, kama inavyoeleza
“Ametoa” (Waefeso 4:11) Hii haionyeshi tu kwamba huduma ya kiroho huja moja kwa moja
katoka kwa Mungu, lakini pia inathibitisha kuwa uanzishaji wa huduma ni lazima utoke kwake.
Hivyo kutumika katika mwili wa Kristo hukuamuliwi na kanisa wala na mtu yeyote, bali na
Mungu. Maandiko yanakazia zaidi kipawa cha asili, uwezo au nafasi iliyowazi ambayo inahitajika
kujazwa si vigezo kwa ajili ya huduma bali ni wito wa Mungu. Hii inaonekana hasa kwa uwazi
wakati tunapofikiria huduma kwa ajili ya uongozi.
1. Uongozi: - Kwa ajili ya nini ?
Vipawa vya uongozi ambavyo vimetajwa katika Waefeso 4:11 daima vimeonyeshwa kama
huduma tano. Mtu mmoja alielezea makusudi na kazi zake kama ifuatavyo:-
Mtume kutawala, nabii kuongoza, mwinjilisti kukusanya, mchungaji kulinda na mwalimu kukuza.
Mistari inayofuata sura 4:11 inaonyesha kwa uwazi zaidi kwamba huduma tano zimewekwa kwa
ajili ya kuwakamilisha watakatifu, kuifanya kazi ya huduma na kuujenga mwili wa Kristo mpaka
wote wafikie umoja wa imani na kumfahamu sana mwana wa Mungu. Makusudi yake ni
kuwaongoza wanaume na wanawake kwenye utimilifu wa Kristo kupitia mahubiri yao,
mafundisho na ushauri, waamini wanaandaliwa kuutendea kazi upambanuzi wa kiroho ambao
upo kwenye msingi wa Neno la Mungu, hivyo kulinda kundi la Mungu kutofuata kila upepo wa
mafundisho ya kigeni. Huduma tano zinasadia zaidi waamini kukua katika yeye kwa mambo yote,
ili kwamba waweze kuchangia kukua na manufaa ya kanisa, kulingana na uwezo wao kadri
wanavyowezeshwa na Kristo (Waefeso 4:12-16) Kwa hiyo siyo vibaya kuwa na uongozi ndani ya
kanisa, bali ni baraka za Mungu zilizotolewa katika mwili wake. Wale wanaodai kuwa wanaweza
kumwabudu Bwana nyumbani na hawahitaji ushirika wa kanisa hawajaelewa utajiri na utekelezaji
wa huduma hizo zilizotolewa na Mungu.
Hizi huduma tano ni kwa ajili ya kutoa mwongozo, uongozi na nidhamu kwa ujumla, na kwamba
zimeaminiwa na uangalizi wa kiroho juu ya kundi la Mungu, na kumsaidia kila mshiriki kupata
nafasi yake katika huduma. Ni sehemu ya wito kumtia moyo kila mwamini kujitahidi kuelekea
ukuaji wa kiroho na kuishi maisha matakatifu. Zaidi zimewekwa kwa ajili ya kutoa faraja na
kurekebisha lini na wapi inapolazimu, na kuandaa na kufundisha waamini kwa ajili ya kazi
waliyoitiwa. Utendaji bora wa kuziandaa huduma tano unaweza ukapimwa kwa utekelezaji wa
wale ambao wameandaliwa kwa ajili ya huduma.
MTUME
Utaratibu wa kwanza wa huduma katika Agano Jipya ni ule wa Mitume. Neno (mtume)
limetokana na neno la Kiyunani apostolos likiwa na maana “aliyetumwa”au “mjumbe”
(kilatini ni sawasawa na kuwa –Mmishionari) kwa hiyo mtume wa kweli siku zote ni yule
aliyetumwa, kamwe si yule ajipelekaye. Ni huduma inayoambatana na nguvu kubwa / uweza
mwingi na mara zote imesimama juu ya orodha ya huduma zilizotolewa na Mungu. (I
Wakorintho 12:28; Waefeso 4:11).
16
Wengi hufikiri kazi ya ki- utume ilikwisha kamilika, na haina umuhimu tena katika kanisa la leo.
Kulingana na wao walikuwepo mitume kumi na wawili tu, na baada ya kifo chao huduma ya
utume ikakoma, Agano Jipya hata hivyo linaonyesha viwango vya utume. Imewahi kusemwa kwa
ufasaha kuwa kutokaueleweka sana na utata vinaweza kuepukwa kwa kutofautisha kati ya hivi
viwango vitatu vya utume.12
1. Viwango vitatu vya utume.
Katika Waebrania 3:1 Yesu Kristo anaelezewa, “kama mtume na kuhani mkuu wa maungamo
yetu”, kama alivyopelekwa na Baba alifanyika mtume (Kiyunani = aliyetumwa) akiwa na ujumbe
wa Ki- Mungu na kazi ya ukombozi wa mwanadamu. Alipokuwa hapa duniani alifunua
kikamilifu mapenzi na asili ya Baba alinena maneno ya Baba na alikamilisha kazi yake ya
ukombozi. Utume wake ni wa kipekee na wa aina yake.
Kisha kulikuwa na wale kumi na wawili ambao Kristo aliwachagua mmoja mmoja na ambao
aliwaita mitume (Luka 6:13). Kama alivyotumwa na Baba, hivyo naye aliwatuma walipokuwa
wakimfuata Kristo walifanyika kuwa wanafunzi, wakapokea mmlaka kuponya wagonjwa,
walifukuza pepo na kutenda miujiza. Hawa kumi na wawili ni muundo wa kiwango pekee cha
utume, na wanashikilia sehemu maalum katika historia ya kanisa. Baada ya kupaa kwa Kristo
wakachukua uongozi wa kanisa changa. Baadhi yao baadaye, chini ya uongozi na uvuvio wa
Roho mtakatifu, waliandika sehemu kubwa ya Agano Jipya. Watu hawa pia wanaelezewa kuwa
mitume wa mwana kondoo (ufunuo 21:14). Viwango vyao vya utume haviwezi kushikwa na
mwamini yeyote.
Kiwango cha tatu cha utume kinawahusu wale walioitwa mitume lakini hawakuwa katika sehemu
ya wale kumi na wawili. Wengi wao wametajwa kwa majina; Mathiya, aliyechukua nafasi ya Yuda;
Barnaba (Matendo ya Mitume 14:14)
Androniko na Yunia (Warumi 16:7), na hata Paulo. Katika (I wakorintho 15:5-7) tunasoma kuwa
baada ya kufufuka kwake Yesu alionekana na wale kumi na wawili, Yakobo, na baadaye na
mitume wote. Ingawa hatuna uhakika wa mitume wote ni nani, ni wazi kwamba wengine
kuongezea wale kumi na wawili wlitambuliwa kama mitume. Hata hivyo kulikuwepo na mitume
wa uwongo. (2 wakorintho 11:13) ambao walishtumiwa na Paulo, Hii inaashiria kuwa na kundi /
hesabu kubwa ya mitume katika kanisa la kwanza. Vinginevyo hakuna mtu yeyote angeliweza
kujifanya kirahisi kuwa mtume. Wale waliohesabika kuwa miongoni mwa mitume halisi
walitakiwa watimize sifa kadhaa.
Sifa hizi zinawakilisha hasa katika kundi la pili kama ifuatavyo:-
2. Sifa za utume
Kwanza kabisa mtume alipaswa kuwa amemwona Bwana yeye binasfi, na awe shahidi wa kwanza
wa ufufuo wake. Wakati wakijaza nafasi ya Yuda wale kumi na mmoja walikazia kwamba nafasi
yake ilipaswa kujazwa na shahidi wa kwanza wa huduma ya Kristo, kuanzia ubatizo wa Yohana
12 B.E. Underwood, Spiritual Gifts Ministries and Manifestations (Franklin Springs: Advocate Press,
1984), p. 20.
17
hadi wakati wa kupaa kwa Yesu (Matendo ya mitume 1:21 –22). Ijapokuwa Paulo hakuwa
miongini wa mitume kumi na wawili, alitetea utume wake kwa kusema kwamba alikuwa
amemwona Bwana (1 Wakorintho 15:7-9). Pili kazi ya mtume ilihusisha kuweka msingi wa
kwanza wa kanisa kupitia kazi yao ya umishenari na kwa kupokea maandiko ya Agano Jipya
kupitia maneno ya Ki-Mungu yaliyovuviwa. Hivyo wakaweka Msingi wa Imani yetu. Kwa mfano
Paulo anasema kuwa alikuwa hodari “kutojenga juu ya msingi wa mtu mwingine” (Warumi
15:20) bali alihubiri Injili sehemu ambayo walikuwa hawajawahi kuisikia (Waefeso 2:20). Tatu,
walidhihirisha huduma ya Ki- Mungu iliyoonekana wazi zaidi, zaidi ya kupita huduma zingine.
Katika (2 Wakorintho 12:12) Paulo anaonyesha kuwa “kweli ishara za mitume zilitendwa kati
yenu katika saburi yote, kwa ishara na maajabu na miujiza”.
Kutokana na uzoefu wa Paulo mitume pia walizoelea mateso, kukataliwa, dhiki na ugumu. Katika
(2 Wakorintho 11:23-33) inatupa mtazamo wa baadhi ya uzoefu wake.
Wao ni wahudumu wa Kristo (nanena kiwazimu) mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana; katika
vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi. Kwa Wayahudi mara tano
nalipata mapigo arobaini kasoro moja.
Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nlivunjikiwa jahazi;
kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za
wanyang’anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine;; hatari za majini; hatari za
jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo; katika taabu na masumbufu; katika kukesha
mara nying; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi. Baadhi ya
mambo ya nje yapo yanijiayo kila siku, ndiyo maangalizi ya makanisa yote. Ni nani aliyedhaifu, nisiwe
dhaifu nami ? Ni nani aliyekwazwa nami nisichukizwe ? ikinibidi nijisifu, nitajisifu kwa mambo ya
udhaifu wangu. Mungu, Baba wa Bwana Yesu, aliye mtukufu hata milele, anajua ya kuwa sisemi uongo.
Huko Dameski liwali wa mfalme Areta alikuwa akiulinda mji wa Wademeski, ili kunikamata; nami
nikateremshwa ndani ya kapu, katika dirisha la ukutani, nikaokoka katika mikono yake.
Wale wote ambao wamezifikia sifa ambazo zimetajwa hapo nyuma walitambulika kama walioitwa
kweli na Mungu kuifanya kazi ya mtume.
3. Kazi ya Mtume
Mitume walitoa uongozi wenye nguvu na katika mtazamo wa kiroho. Waliweka msingi wa
kanisa na mafundisho ya Kikristo. Hii inaonyesha hasa kwa wale kumi na wawili, ambao
waliitendea kazi mamlaka kuu lakini walikuwa wanyenyekevu na wapole. Inaonekana kwamba
vipawa vyote tisa vya Roho vilikuwa vikifanya kazi katika huduma yao, hasa Petro na Paulo. Siyo
tu huduma ya kiutume iliyodhihirisha karama tisa za Roho, bali ilihusisha huduma nyingine zote
za uongozi. Walifanya kazi ya mwinjilisti, walikuwa walimu wenye uwezo, walitenda kama
manabii na waliwajibika kwa ajili ya, “maangalizi ya makanisa yote (II Wakorintho 11:28), wakiwa
na moyo wa kichungaji. Kwa kuongezea walifanya mikutano, waliadibisha kanisa, walitoa ushauri
na kutia moyo na walijihusisha katika kutoa misaada (Matendo 11:30), hivyo wakashiriki baadhi ya
majukumu ya kusaidia huduma. Hii inaonyesha uvumilivu wao.
Kulingana tena na uzoefu wa Paulo, mitume walianzisha makanisa popote walipokwenda,
wakiyaacha katika muundo mzuri chini ya uangalizi wa wazee ambao waliwaweka. Wakati
mwinjilisti alipoanzisha Makanisa lakini hakuwa na uwezo wa kuongoza zaidi waamini wapya
18
katika imani yao mpya waliyoipata (Matendo 8:5-25) mtume aliacha makanisa katika muundo
kamili na salama baada ya kuwa amekwisha kufanya uinjilisti katika eneo jipya. Kamwe, bado
hawakudai makanisa hayo kama yao wenyewe. Wakati ugomvi ulipoibuka Korintho, Paulo
alikuwa mwepesi kuonyesha kwamba si yeye, au Petro wala Apollo wangeliweza kudai kuwa
kanisa ni lao wenyewe, maadamu kanisa ni mali ya Mungu ambaye alikuwa ameyapatia makanisa
kupitia wajibu wa kazi yao.
Wakati mitume walipokuwa wakishirikiana “majukumu” yale yale, ni lazima tutambue kwamba
wengine waliitwa kuwa mitume wa mataifa mengine (kwa mfano Paulo), na wengine kama Petro
waliitwa kuwa mitume wa Taifa moja. Ijapokuwa Petro alikuwa na uzoefu wa utume katika
mataifa mengine alipoitangaza injili katika nyumba ya Kornelio, ilikuwa vigumu kwake kuachana
na desturi za Kiyahudi. Petro, Yakobo na Yohana waliamua kutumika miongoni mwa Wayahudi,
wakati Paulo na Barnaba waliendelea na Umishenari wao kwa mataifa (Umishenari = Kilatini ni
mtume) kazi kati ya wamataifa.13
Wagalatia 2:9
Tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo,
walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika ili sisi tuende kwa mataifa na wao waende kwa
watu wa tohara;
Ni rahisi kuzitambua tabia zilizojitokeza na kuziweka huduma za kitume zikiwepo katika Agano
Jipya. Lakini majibu kwa maswali ambayo mara nyingi hujitokeza, “Je badokuna mitume katika
siku za leo? Limekuwa likileta utata. Hata hivyo, mtazamo wa kwelikatika kweli za kibiblia kwa
sasa unafanya kuwa urahisi kupata jibu.
4. Je kuna mitume siku hizi ?
Baadhi wanadai kwamba huduma ya kitume ilikoma baada ya karne ya kwanza. Bado katika 1
Wakorintho 12:28 tunasoma kuwa Mungu ametoa huduma hii kwa kanisa. Waefeso 4:11-13
inathibitisha ukweli huu na kuonyesha kwamba ilitolewa kwa ajili ya kusudi maalumu, mojawapo
ya hizo ni kuwakamilisha watakatifu.
Kwa hiyo tunaweza tukathibitisha kwamba mitume waliwekwa na Kristo kama huduma ya
kudumu katika mwili wake (Warumi 11:29), hasa tangu michango yao ya kuwakamilisha
watakatifu inahitajika sana kwa siku za leo. Kwa kuwa na uthibitisho huu tunapaswa kuonyesha
haraka sana kwamba ijapokuwa kuna nafasi kwa ajili ya huduma ya kitume kwa wakati wa leo,
mitume wa siku hizi hawako katika kundi moja kama wale kumi na wawili.
Baadhi ya waalimu wa Biblia wanawaorodhesha watu kama Martin Luther, John Knox, John
Wesley, Hudson Taylor na wengine miongoni mwa mitume wa leo. Inawezekana kuna uhalali
katika kufanya hivyo, kadri walivyotoa uongozi wenye nguvu, walifanikisha mambo makubwa
kwa ajili ya ufalme wa Mungu, walitenda kwa ujasiri mkuu na kutoa mtazamo wa kiroho. Hata
hivyo, kutokuwepo kwa vipawa vya kiroho na madhihirisho ya miujiza yasiyo ya kawaida,
13 See C.P. Wagner, Your Spiritual Gifts Can Help Your Church Grow (Bromley: MARC Europe, 1979),
p. 212.
19
uponyaji na maajabu ambayo kwa kawaida huambatana na wito wa-kitume, ambao unawaweka
katika kundi lao wenyewe. Wale ambao wanahuduma hii leo labda hawajulikani kama “Mitume” .
Bado, kazi zao na matokeo ya huduma zao zineemeshwe (graced) na ushahidi wa huduma ya
kitume. Wakati wanapokuwa hawaweki misingi ya kanisa na mafundisho, hata hivyo watatoa
uongozi ule ule wa kiroho wenye nguvu wakiwa na uzoefu mkubwa usio wa kawaida pamoja na
Bwana, na kuthubutu kwenda katika maeneo ambapo injili ilikuwa haijasikika/haijahubiriwa.
Wanadhihirisha vipawa vyote vya Roho,na kuyaacha makundi mazuri waliyoyaanzisha chini ya
uangalizi wa wazee, baadaye waliendeleza huduma zao, kama watangulizi wao wa mwanzo
walivyofanya.
Wakati tunapotambua uendelezaji wa huduma hii ya Ki-mungu ni lazima tuonyeshe kwamba
utume hutegemea wito wa Ki-mungu, na siyo matokeo ya utaratibu wa “huduma ya mabadiliko”.
Kwa miongo (decade) miwili iliyopita kumekuwa na mwelekeo, hata miongoni mwa
wanauamusho (charismatic), kwa ajili ya viongozi kubadilisha kutoka wachungaji kuwa waalimu,
kuwa manabii hadi kuwa mitume. Katika miaka ya 1970 Mungu aliinua waalimu. Huduma yao
ilikuwa yenye nguvu na yenye upako. Katika miaka ya 1980 wengi wao walijulikana kama manabii
katika miaka ya 1990 walionekana kama mitume. Utaratibu huu wa kutoka ngazi moja hadi
nyingine haukujulikana katika kanisa la Agano Jipya. Mitume wa kwanza walipokea wito wao wa
kitume mwanzoni mwa huduma yao. Hata hivyo Paulo na Barnaba walionekana miongoni ma
manabii na waalimu kabla hawajaamuliwa kuwa kama mitume, wito wao ulikuwa tayari ule wa
utume (linganisha Matendo 9 na Matendo 13:1-3). Hadi wakati wa kuamuliwa kwao, Mungu
aliwaandaa na akawaruhusu wafanye kazi pamoja na huduma zingine.
Tabia za kweli za wito wao, hata hivyo, zimekuwa wazi tokea mwanzo. Kwa hiyo inawezekana,
na mara nyingi inafaa, kwamba wale walioitwa katika huduma ya utume waweza kutumika katika
huduma ambayo huwaandaa kwa ajili ya wito wa msingi unaotolewa na Mungu. Mara ukuaji wa
kiroho unaotakiwa, kuonekana mbele za Mungu atawaruhusu kuingia katika wito wao wa asili
(original), tunaweza kuona mfano ule ule katika maisha ya Filipo na Stephano, ijapokuwa
hawakuwa mitume. Wote wawili walijulikana kwanza kama mashemasi na baadaye kama
wainjilisti.
Utaratibu usio wa kibiblia na usiofaa wa huduma ya kutoka ngazi moja hadi nyingine kama
inavyoonekana leo inachukua nafasi kwa sababu nyingi. Kwanza, kamwe wengi hawajaribu
kutafuta wito wao maalumu. “Wao ni wahubiri wa injili tu”. Pili , wengine hutamani huduma
nyingine kuliko za kwao wenyewe.
Tatu, wengi wanashindwa kujisalimisha kabisa kwa Bwana, na inamfanya asiweze kuwatumia
kulingana na wito wao wa kweli. Hivyo baada ya kusema hivi, tunapaswa kuongeza kuwa
kunaweza kuwa na “hali ya kufaa” au maendeleo ya kawaida kutoka huduma moja hadi nyingine
kama tutakavyoona baadaye. Wale wanaotamani/uchu huduma hii katika siku za leo wanapaswa
kukumbushwa kwamba inatakiwa utayari wa kulipa gharama kubwa kama Paulo anavyoonyesha
katika 2 Wakorintho 11:23-30.
Mungu bado anaita na kuweka watu katika huduma ya utume. Hawa mitume halisi wa sasa
wanatambulika, miongoni mwa vitu vingine, katika unyenyekevu wao wa kweli ambao
20
hauwaruhusu kujiita wao wenyewe kama mitume. Lakini huduma zao zinatoa ushahidi wa wazi
wa wito wao. Itakuwa ni vibaya kutegemea kwa kawaida wazee (grey haired men) na watu wenye
uzoefu kujaza vyeo vya mitume wa sasa, kama ilivyopendekezwa na Peter Wagner.14 Hii inaweza
kuthibitisha kuwa ni kweli katika mambo fulani. Lakini cha kufurahisha zaidi katika Agano Jipya
inaonyesha kuwa umri haukuwa ni kigezo kwa ajili ya kuitwa katika utume, ijapokuwa ilikuwa ni
huduma iliyohitaji wajibu mkubwa. Petro, Paulo na wengine walikuwa vijana wakati Mungu
alipokuwa akiwaweka wakfu kuwa mitume. Kigezo hakikuwa umri wao wa asili, bali ulikuwa ni
upevu wa kiroho na mamlaka.
Kwa matokeo ya huduma zao ikawa huduma yenye nguvu, na yenye upako na mamlaka. Hivyo
hivyo mitume wa sasa hawatajulikana kwa vyeo/madaraka lakini kwa madhihirisho ambayo
yataambatana na huduma ya kitume.
Kama tulivyoonyesha tabia na kazi ya huduma hii inakuwa dhahiri kwamba hii huduma inahitajika
sana katika siku zetu kwa ajili ya kulileta kanisa katika utimilifu, kamili wa upevu / ukuaji wa
kiroho. Bila kujali mapokeo ya kanisa, utume lazima uchukue sehemu yake katika mwili wa
Kristo. Si lazima tuthibitishe tu umuhimu wa huduma hii lakini pia tuzitunze huduma hizi za Ki-
Mungu kwa uangalifu dhidi ya kuzitumia vibaya kwa nguvu na njaa ya vyeo / madaraka kwa mtu
mmoja mmoja.
NABII
Huduma ya nabii, kama ile ya mtume, inatambulikana tu hivi karibuni. Hata hivyo hii, haionyeshi
kwamba hakujakuwepo na watu wenye huduma ya kinabii kwa kipindi chote cha historia ya
kanisa. Ijapokuwa mara nyingi hawakutambuliwa kama manabii. Tukimwangalia Nabii kwa
undani zaidi, itakuwa dhahiri kwamba huduma hii kwa namna fulani imekuwa ikifanya kazi kwa
kipindi kirefu zaidi kuliko ilivyotarajiwa.
1. Manabii katika Agano la Kale na Agano Jipya
Katika Agano la Kale huduma ya Nabii ilikuwa imelengwa zaidi kwa taifa la Israeli. Wakati
mwingine walitoa tu Neno la Bwana kwa mataifa, na baadaye kwa wale tu waliokuwa na
mahusiano na Wayahudi. Kazi na kusudi / malengo ya Nabii wa Agano Jipya hutofautiana kwa
mitazamo mingi na ile ya Agano la Kale. Tunapolinganisha huduma mbili tutatambua kwamba
muonaji / Nabii wa wakati wa Agano la kale aliposimama mbele ya Wafalme na Taifa akiwaita
wamrudie Mungu, Agano Jipya linaleta /onyesha picha ya tofauti. Hapa nabii analiambia kanisa
lakini hana tena huduma kwa taifa na watawala wake.
Tofauti na Israeli, mataifa ya leo hayana urithi wa kidini unaowathibitisha kuwa watu wateule wa
Mungu. Kwa hiyo, huduma ya kinabii ya Agano Jipya inajidhihirisha yenyewe hasa ndani ya
mipaka ya kanisa. Nabii hata hivyo anaweza kutumika kuhudumu kwenye mwili wa Kristo katika
kanisa la mahali pamoja, kimkoa, kitaifa na hata ngazi ya kimataifa. Huduma ya kinabii ya kweli
ya kitaifa na hasa ya kimataifa daima itakwenda sambamba na ufunuo wa Mungu kwa wengine
14 C.P. Wagner, Your Spiritual Gifts Can Help Your Church Grow (Bromley: MARC Europe, 1979), p.
208.
21
ambao wana huduma ile ile. Tunapaswa kuelewa wazi kwamba katika kipindi cha kanisa, Mungu
hadhihirishi tena mipango yake kwa mtu mmoja tu, kama ilivyokuwa katika Agano la kale, bali
katika mwili wake kwa ujumla.
Huduma ya manabii wa Agano la kale inajumuisha utabiri, ambayo iliikuwa sahihi zaidi, kwa
matukio yajayo kuhusu Israeli. Kwa nyongeza, nabii zilitolewa kwa undani zaidi/kinaganaga
kuhusu kuzaliwa, maisha, mateso na kazi ya Masihi. Katika Agano Jipya tabiri za mambo yajayo
siyo sehemu muhimu ya huduma ya nabii. Wakati tabiri za kweli zitakapotabiriwa daima
zitakuwa ndani ya mipaka ya maandiko, zikielezea na kumulika kweli ambazo tayari zilikuwepo.
Kwa hiyo haziwezi kufunua kweli mpya zinazohusu mafundisho na mpango wa Mungu
uliokwisha kuwepo kwa ajili ya vizazi. Hata tabiri zilikusudiwa kwa mmoja mmoja kulingana na
Agano jipya, zilitumika tu kama kuthibitisha au jibu la moja kwa moja la maombi ya mtu binafsi,
kama tutakavyoona baadaye.
2. Sifa za huduma ya kinabii
Nabii wa Agano Jipya ni mtu ambaye ana uwezo wa Ki-Mungu kutafsiri maandiko yanayohusiana
na hali ya kanisa iliyopo. Anaweza akatambua kupungua kiroho, uzushi, na uhitaji wa kutia moyo
kama ule uliofichika na dhambi iliyowazi katika mwili wa Kristo / Kanisa. Mungu anafunua hali
za kiroho za kanisa kama zile za kila mtu, nabii anaweza kuona zaidi ya uwezo wa kawaida wa
kuona.
Watu wengine huchanganya kipawa cha unabii na huduma ya nabii. Kipawa cha nabii,
kimeorodheshwa katika 1 Wakorintho 12, ni sehemu ya huduma ya kinabii, kama neno la maarifa
na vingine. Hivyo, si kila mtu ambaye anaweza kutoa unabii au kupokea neno la maarifa ni lazima
afikiriwe kuwa nabii moja kwa moja. Tunahitaji kukumbuka utofauti kati ya huduma za kiroho na
vipawa vya madhihirisho, kama ilivyoelezwa mapema. Kipawa cha unabii au neno la maarifa
halimwezeshi mtu kuwa nabii. Kwa kawaida nabii atavitendea kazi vipawa hivi, lakini vitakuwa
sehemu kubwa ya huduma. Tunapaswa kuelewa kuwa huduma ya nabii hutegemea wito ambao
umekwisha tolewa kwa “wengine” (Waefeso 4:11). Paulo anasisitiza ukweli huu wakati anapotoa
swali katika 1 Wakorintho 12:29: “Je wote ni Mitume? Wengine wamepokea tu wito wa hizi
huduma. Watu wengi hawaelewi wakati Paulo huyo huyo anawatia moyo waamini wote kutoa
unabii (1 Wakorintho 14:1). Kwa kufanya hivyo hamtii moyo kila mtu kuwa nabii, ila badala yake
kutafuta kipawa cha kuhutubu. Ni lazima isisitizwe kwamba si kila mtu anayetoa unabii ni nabii.
Manabii wa Agano Jipya, pamoja na mitume waliweka msingi wa imani yetu ya Kikristo na
mafundisho (Waefeso 2:20), haki ambayo manabii wa leo hawana, zaidi ya kazi hii maalumu,
huduma ya kinabii ya leo haijabadilika sana katika tabia / sifa na kazi zake.
3. Kazi Ya Nabii
Watu wengine hufikiri kuwa neno nabii ni neno lingine la Mhubiri. Lakini ni zaidi sana ya hilo.
Wengine wanashikilia dhana kuwa nabii anahusika tu na utabiri wa wakati ujao. Lakini utabiri wa
wakati ujao ni sehemu kidogo tu ya huduma yake. Nabii wa Agano jipya si msemaji sana wa
mambo yajayo (fore –teller) bali yeye ni “msemaji wa wakati huo huo na kuendelea (forth –
22
teller). Hutangaza ujumbe alioupokea kutoka kwa Mungu, katika ushawishi wa nguvu na upako,
kwa hiyo huwa mnenaji wa Mungu.
Nabii hutafsiri na kutangaza nia ya Mungu kwa watu wake. Kwa wakati fulani anaweza kutabiri
kama tulivyoona kwa Agabo aliyetabiri kufungwa na mateso ya Paulo (Matendo 21:10,11) na njaa
(Matendo 11:22 –30). Hivyo, wakati mwingi nabii atakuwa mnenaji wa Mungu akifunua mizigo
ya moyo wake kwa watu wake.
Kama tulivyoongalia maisha ya Agabo huduma ya nabii, kama ile ya mtume na mwinjilisti,
huduma ya kwenda sehemu zote, ambayo inahusisha vipawa maalumu vya Kiroho. Miongoni
mwao ni unabii, lugha na tafsiri, kupambanua roho na neno la maarifa. Nyongeza ya hayo ishara
na maajabu ni sehemu ya wito wa Kinabii. Tofauti na huduma ya uinjilisti, madhihirisho ya Ki-
Mungu ya nabii hayalengwi sana kwa wasioamini lakini yanaelekezwa na kuthibitisha
madhihirisho ya Ki-Mungu miongoni mwa watu wake. Ni muhimu, hasa katika siku zetu za jamii
inayojali sayansi, ambayo mara nyingi hukana kuwepo kwa Mungu, kuthibitisha imani zetu katika
utendaji kazi wa miujiza ya Mungu. Ni lazima Kanisa lirudi katika uhalisi wa Kibiblia, na
kuondokana na dhana ya Kisayansi ya vitu vinavyoonekana (Materialism) ambayo inatunza ubaya
wake hata ndani ya makanisa ya Kiinjili na ya Kipentekoste. Huduma ya nabii inatolewa hasa
kusahihisha mwelekeo wa Kidunia ndani ya Kanisa katika mambo ya Mungu.
4. Mwongozo kupitia Manabii.
Manabii wa kale waliendewa kutakwa mashauri katika vipindi vya misukosuko kama “Waonaji”
wa Mungu, kutoa mwongozo kwa taifa na kwa watu binafsi. Watu walitarajia kusikia kutoka kwa
Mungu kupitia wao, na kumuuliza Mungu kwa niaba yao. Katika Agano jipya mfumo huu
ulibadilika. Kila mwamini leo hii anaweza kwenda moja kwa moja kwa Mungu kupitia Yesu
Kristo. Tangu mwanzo wa Kanisa katika siku ile ya Pentekoste Mungu huwaongoza watu wake
kupitia:
1. Neno lake (ambalo limeandikwa au kuhubiriwa)
2. Roho wake (bado sauti ndogo, ndoto, maono, fikra)
3. Uongozi wa kanisa
4. Ushauri wa waamini wenzetu
5. Vipawa vya Roho
6. Mazingira (Milango iliyo wazi au iliyofungwa).
Kwa hiyo hatupaswi kujitoa kwa mtu yeyote ambaye hudai ana neno kutoka kwa Bwana, bila sisi
wenyewe kumuuliza. Unabii ambao unathibitisha uongozi wa Mungu katika maisha yetu
unapaswa kupokelewa / kuthaminiwa, lakini maelekezo kutoka kwa wale wanaojiita manabii
ambao hatuna ushahidi wa ndani binafsi kutoka kwa Roho Mtakatifu wanapaswa kuulizwa, na
kukataliwa.
Waamini wa Agano jipya wanatafuta Uongozi wa Mungu lazima wamwachie yeye, namna
atakavyowaongoza na kuwajibu. Mungu anaweza kutumia nabii kuwaongoza watoto wake, lakini
hii inafanyika kwa hiari yake na siyo kufuatana na matakwa ya mwamini.
23
Wakati Mungu alipotoa maelekezo kupitia kwa Agabo inafurahisha kuonyesha kuwa nabii
hakumwambia Paulo la kufanya, lakini alimuonya hatari iliyo mbele. Wale wanaotoa sababu kuwa
Paulo angelimtii Agabo na kukubali maonyo ya manabii wengine lazima wasisahau kuwa Paulo
alikuwa amekusudiwa na Mungu kusimama mbele ya Wafalme na watawala (Matendo 9:15). Paulo
alijua mapenzi ya Mungu. Yeye alikuwa amemsikia binafsi. Ndiyo sababu hakusita kufuata
mpango wa Mungu kwa maisha yake, hata baada ya kuonywa na Agabo.
Katika kitabu cha matendo tunazidi kuona kuwa huduma ya Kinabii haikutolewa kuongoza
mambo ya Kanisa. Kwa matukio mawili wakati kanisa la kwanza lilihitaji mwongozo wakati wa
misukosuko mikubwa katika Matendo 6 na 15, hawakutafuta mwongozo kupitia manabii, bali
walitatua matatizo kwa kutumia njia mbali mbali. Neno la tahadhari lazima litolewe kulingana na
mwongozo kupitia Manabii au kipawa cha Unabii. Katika baadhi ya Makanisa ya Kikristo
Waamini wanatiwa moyo kuwekeana mikono wao kwa wao , na kutabiriana wao kwa wao. Mtu
mmoja alieleza kwa usahihi zaidi kwamba hii ni hatari, hasa unapotokea kwenye sebule ya mtu,
kwa mfano katika ibada za nyumba kwa nyumba ambazo Mchungaji hazitembelei mara kwa mara.
Huduma ya Kinabii pamoja na kipawa cha Unabii vinapaswa vifanyike kanisani ambapo vinaweza
kupimwa, na ikiwa inawezekana vipigwe marufuku au visahihishwe.
Mwongozo unaotolewa kupitia hiki kipawa au huduma unapaswa kupimwa. Huduma ya nabii
siyo kwamba inakosea na kwa hiyo inahitajiwa kupimwa katika mwanga wa maandiko
(1Wathesalonike 5:19 –21; 1Wakorintho 14:29). Tunahitaji kukumbuka kwamba kila unenaji wa
kinabii, iwe kwa wakati ujao au wakati huu ni lazima iwe ndani ya mipaka ya Neno la Mungu.
Mwongozo uliopokelewa kupitia huduma ya kinabii au kupitia vipawa vya ufunuo vyaweza
kukubalika tu kama uthibitisho kwa mwamini ambacho tayari ameshajua kwa mfano katika
matendo 13:3 wakati manabii walipoweka mikono juu ya Paulo na Barnaba ili kuwatenga kwa ajili
ya huduma ya utume, hawa wawili hawakupokea maelekezo mapya bali ni uthibitisho wa wito wa
Mungu.
Ni lazima tuwe na tahadhari wakati wale wanaojiita Manabii kwa kutumia “huduma” zao
kuonyesha kiroho chao kwa kutoa mafunuo mapya kwa wakati mwingine nje ya mipaka ya
Biblia), au kuwashauri watu kuhusu mambo ya fedha zao, ambapo wakati mwingine inafanyika
kwa ajili ya manufaa ya manabii wao wenyewe. Nabii wa kweli hatajihusisha kwenye usuluhishi;
kutoa maelekezo nani wa kumuoa, uchague kazi gani na uishi wapi. Huduma iliyotolewa na
Mungu kamwe haitolewi kwa ajili ya manufaa ya mtu binafsi, kutosheleza matakwa ya watu, au
kwa kuvutia watu. Badala yake itawaelekeza watu kwa Yesu na kuitukuza kazi yake.
5. Huduma ya mahubiri ya nabii.
Baadhi ya waalimu wa Biblia huthibitisha kwamba nabii huzungumza na kuhudumu katika uvuvio
wa ghafla na ufunuo, bila ya maandalizi ya ustadi wa kuhubiri. Mtazamo huo hutokana na
ufahamu usio sahihi ambao hulinganisha vipawa vya unabii na huduma za Kinabii. Katika unabii
watu hunena katika uvuvio wa ghafla. Huduma ya Mahubiri ya nabii, kwa vyovyote hutegemea
kujifunza na maandalizi kama tu huduma nyingine ambazo zinahusisha kutangaza Neno la
Mungu, kama sivyo hata kwa nguvu/makini zaidi. Mahubiri yake wakati mwingine yanaweza
kuonekana hayana mfumo/utaratibu kutokana na ukweli kwamba hujihusisha zaidi katika
24
kufunua mapenzi ya Mungu kuliko kufuata mwongozo ulio wazi. Bado atajiandaa yeye
mwenyewe kupitia kujifunza na kufuata mwongozo wa stadi za Kihubiri (homiletics). Katika
maandalizi yake na wakati akiwa akihubiri atakuwa / atajiachia wazi kwa uongozi wa Roho
Mtakatifu.
Hivyo, atazieleza hali katika Kanisa ambazo zinahitaji kusahihishwa, kusihi (exhortation), kujenga
au kufariji katika namna maalumu / mahususi na ya kibinafsi, haijulikani kwa huduma ya
mwalimu, Mchungaji au Mwinjilisti.
Ujumbe wa nabii mara zote unafikiriwa kuwa mgumu na mzito. Kwa hii mara nyingi haeleweki;
anatengwa, anateswa na mashitaka ya uongo kwa kuwa kinyume mno. Hata hivyo, moyo wa
nabii, umejawa na huruma kwa ajili ya watu wa Mungu. Jumbe / mahubiri yao si magumu bali
kwa kawaida si ya kujadiliana na kuchoma / kuumiza pamoja na shauku takatifu (holy zeal). Hali
ya utulivu ya wafuasi wa Kristo, uhitaji kwa ajili ya uamsho, utakatifu, na kutembea karibu na
Mungu, na kuwepo kwa mafundisho ya uongo na hali ya kidunia ndani ya Kanisa hutia mzigo
ndani ya moyo wa nabii. Anasumbuliwa na shauku kuu ya kuwa wakilisha watu wa Mungu
wakiwa hawana lawama wala doa lolote mbele ya Kristo.
Maandalizi ya nabii si kujisomea sana maoni ya vitabu mbalimbali (commentaries), bali anatumia
muda wake mwingi katika maombi na kusoma Neno. Anapaswa kusikia kutoka kwa Mungu mara
kwa mara katika njia maalumu, vinginevyo huduma yake itapoteza ubora wake.
Anapokuwa anahubiri, ujumbe wake daima unaweza usiwe wenye mantiki na mtiririko, bali hata
hivyo utachoma mioyo ya wasikilizaji. Hahitaji kuambiwa kuhusu matatizo yaliyotolewa katika
kanisa la mahali pamoja kutoka kwa watu wa mahali pale, kabla hajasimama mimbarini /
madhabahuni. Wakati wa maandalizi yake tayari ameshasikia kutoka kwa Mungu na kwa hiyo
anaweza akayasema matatizo yaliyopo bila kuegemea upande wowote / bila upendeleo. Kuwa
makini / bora hategemei “umbeya” katika kanisa, bali “minong’ono” kutoka Mbinguni,
anapokuwa anandaa ujumbe.
6. Kipimo cha nabii.
Yesu, Paulo na Petro walionya kuhusu manabii wa uongo (Math. 7:15; 1Wakorintho 11:14;
1Petro 2:1). Kwa hiyo hatupaswi kumwamini mtu yeyote anayedai kwamba anahuduma ya
kinabii, bali kuzijaribu roho (1Yohana 4:1–2). Kuna vigezo vingi ambavyo vitatusaidia
kupambanua ukweli. Kutoka kwa walaghai / waongo.
1) Manabii kulingana na utaratibu wa Agano Jipya, wanapaswa kujaribiwa, kama wale
waliokuwa chini ya Agano la Kale wakati walipotambuliwa kama manabii wa Uongo
ikiwa utabiri wao haukutimia (kumbukumbu la Torati 18:20 –22).
2) Manabii wa kweli watatambulikana kwa matunda yao. Watadhihirisha tunda la Roho
(Wagalatia 5:22), na Roho wa Kristo. Hata hivyo manabii wa uongo wakionekana katika
ngozi ya kondoo hawawezi kuficha ukatili wao “kama mbweha” kwa muda mrefu.
3) Manabii wa kweli watakubali kusahihishwa (1Wakorintho 14:29).
4) Watatangaza Neno la Mungu pasipo mjadala, bali katika roho ya huruma.
25
5) Wataelekeza kwa Kristo na kumtukuza yeye. Wale wanaojiondoa kwa Kristo na
msalaba wake kufuata miungu mingine siyo manabii wa Bwana. (Kumb. 13:1 –5).
6) Huduma ya kinabii itakubaliana na maandiko. Ikiwa haielekei kwenye misingi ya
mafundisho, kama vile toba, ubatizo, uanafunzi, kujikana, kuridhika, ushindi wa Kristo
msalabani, ufufuo wake na kurudi mara ya pili, kwa haya machache yaliyotajwa, kwa
hiyo kama ni tofauti na hayo yanapaswa kukataliwa. Zaidi, ikiwa itaongoza watu katika
Kongwa / utumwa wa kiroho, sheria na hofu si ya Kristo. Warumi 8:15 inasema: kwa
kuwa hamkupokea tena roho ya utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa
wana, ambayo kwa hiyo twalia Aba, yaani Baba. Kwa hiyo, ikiwa huduma inaleta
utumwa na hofu badala ya uhuru, si ya Mungu.
7) Wale wanaofurahia mahubiri na nabii za kutisha na hukumu bila kuhusika kwa undani
kwa ajili ya watu kwa hakika hawana sehemu katika huduma hii ya thamani. Huduma ya
nabii ina nafasi muhimu katika utaratibu wa Mungu katika uongozi wa kanisa. Ni
muhimu kulileta kanisa katika ukamilifu na upevu. Hivyo, linapaswa kulindwa kutoka
kwenye matukano na kutumiwa vibaya. Ni lazima tuhakikishe halitumiki kwa ajili ya
hila ambayo hutosheleza matakwa kwa ajili ya burudani ya baadhi ya Wakristo wa
kimwili. Wale ambao ni manabii wa kweli hawatatumia huduma zao kuthibitisha kiroho
chao na ukuu, bali watautumikia mwili wa Kristo katika unyenyekevu.
MWINJILISTI.
Afrika ina Vijana wengi ambao kimsingi hujisikia wameitwa kuwa Wainjilsti. Hii ni lazima
ifurahiwe, kama inavyoeleza kuhusika kwao kwa ajili ya waliopotea. Kwa wakati huo huo, hata
hivyo, kuna upungufu wa Wachungaji kulilinda kundi. Upungufu huu wa uwiano huonyesha
mawazo tofauti ya huduma mbali mbali. Siyo mapenzi ya Mungu kwamba ngazi za Wainjilisti
zifanywe kuwa za thamani kuliko huduma zingine kama vile za wachungaji, walimu au manabii.
Kama tunavyoona kazi na sifa za Mwinjilisti tutajitahidi kushughulikia baadhi ya mawazo potofu,
na kujaribu kusahihisha kutolingana kwa huduma kama inavyoonekana Afrika.
1. Kazi na tabia za Mwinjilisti.
Neno Mwinjilist, lina maana “anayeleta Injili, au anayepeleka habari njema”, imetajwa mara tatu
tu katika Agano jipya (Matendo 21:8; ambapo inamweleza Filipo; Waefeso 4:11 na 2Timotheo 4:5
ambapo inamwelezea Timotheo). Watu katika huduma hii wana ujumbe mmoja ukichoma ndani
ya mioyo yao –Neema ya ukombozi wa Mungu. Wakati wowote wahubiripo, utahusiana na
wokovu. Kila wanaposoma Neno, wote huonekana kupata jumbe zao za wokovu katika
maandiko kwa kubainisha zaidi inapaswa kuonyeshwa kwa wazi kuwa si kila mmoja ambaye
anashauku kushirikiana habari njema pamoja na rafiki yake moja kwa moja anakuwa mwinjilisti.
Mzigo mkubwa kwa ajili ya waliopotea na msukumo mkubwa ulio ndani kumhubiri Kristo
pamoja na marafiki zetu ni lazima iwe tabia ya kila mwanafunzi wa kweli. Kwa ajili ya hiyo
waamini wote ni wainjilisti.
Utekelezaji wa huduma hii unahitajika zaidi kuliko tu kuwa na mzigo mkubwa kwa ajili ya
waliopotea, ukitamkwa wito wa Mungu ulio wazi ambao ni wa lazima kwa ajili ya kila mmoja
kuingia katika huduma hii. Wito kama huo utafuatana / ambatana na kuhubiri habari njema, na
matendo ya miujiza na uponyaji.
26
Moja ya alama ya mwinjilisti wa kweli hatafurahia tu watu wengi kuokoka bali pia atafurahia
kuokoka kwa nafsi moja. Wale ambao kwa kawaida “wemezoelea” kuhubiria makundi makubwa
katika mikutano mikubwa bila ya kuwa na mzigo mkubwa wa kufikia mtu mmoja aliyepotea, ni
lazima wajihoji dhamiri zao. Mfano wa Agano jipya wa mwinjilisti wa kweli huonyesha kuwa
kuokoka kwa Towashi kulikuwa ni muhimu kwa Filipo kama kuokoka kwa watu wengi katika
Samaria, (Matendo 8: 5 –40). Aliufikia umati mkubwa na mtu mmoja mmoja, akiwa na shauku ile
ile ya kiroho. Moyo wa mwinjilisti huchomwa na ukiwa na shauku ya kuwafikia waliopotea
popote walipo. Hivyo, atajihusisha katika maeneo mapya ya uinjilisti akiwafikia waliopotea vijijini
na maeneo ambayo kamwe injili haijasikika. Kwa wakati huo huo atakuwa tayari kufanya uinjilisti
makanisani ambapo humwezesha kuwafikia majirani zake wasioamini. Huiona kama kazi yake
kumfanya Kristo ajulikane kama Mwokozi, kwa kuwaongoza wenye dhambi katika msalaba,
kuwaonyesha upendo na rehema ya Kristo, iwe ni Kanisa la mahali pamoja au hadi kuwafikia
wengine katika maeneo mapya. Kulingana na Agano jipya uponyaji na miujiza ni sehemu za
huduma ya Kiinjilisti . hivyo kila mwinjilisti wa kweli anapaswa kupinga ushawishi matangazo
kama “siku 14 za miujiza tupu”, kama inavyoonekana mara zote. Uponyaji haupaswi kuwa kama
msingi wa kivutio wakati anapoendesha mikutano ya Injili.
Mwinjilisti wa kweli ataangalia zaidi kutangaza habari njema. Kuombea wagonjwa itakuwa ni
sehemu ya huduma yake, lakini kamwe isiwe ndiyo kiini cha kuvutia. Miujiza na uponyaji
hufanyika kama uthibitisho wa Neno la Mungu, na siyo kuvutia. Kutumia madhihirisho haya ya
Ki-Mungu ambayo hatustahili, kama matangazo hayaendi sambamba katika Agano jipya. Hii
inapaswa ikumbukwe wakati mikutano ya injili inapofanyika.
2. Kuanzisha na kushirikiana
Huduma ya Mwinjilisti ina mipaka/inakomea katika kuhubiri habari njema. Kwa kawaida
haihusiki sana kutoa mwongozo, au uangalizi wa kiroho. Hivyo, huduma hii hutegemea kazi ya
waalimu na wachungaji. Katika hali ya kawaida kazi ya mwinjilisti huishia mahali ambapo kazi ya
mchungaji na mwalimu huanzia. Hii ni moja ya sababu kwa nini huduma yake ni ya kwenda kila
mahali. Kwa kadri ahubiripo injili kwa wale ambao hawajafikiwa na injili huduma yake itabakia
kuwa na nguvu. Katika Matendo 8 tunaona mfano wa hii kweli. Baada ya Filipo kuwaleta maelfu
kwa Bwana kule Samaria kupitia hamasa yake ya kiinjilisti, aliomba msaada. Ilikuwa kupitia
maombi ya Petro na Yohana ambao waliitikia ombi lake kwamba waamini wapya walikuwa
wameisha batizwa na Roho Mtakatifu (Matendo 8:26). Filipo alikuwa ameweza kuhubiri kwa
uthibitisho mkuu, kuponya wagonjwa na kutenda miujiza, lakini alitegemea huduma ya wengine
kuwaongoza waamini wapya katika uhusiano wa ndani na Mungu. Pia alipungukiwa hali ya
kupambanua roho kama aliyokuwa nayo Petro ambayo ilimwezesha kuona hali ya kweli ya moyo
wa Simoni mchawi (Matendo 8:13)
Wainjilisti wengi wa leo wanaonekana kuzama zaidi kiroho kuliko Filipo, lakini bado
wanategemea huduma ya wengine, hasa ile ya mchungaji. Matunda yake hayategemei tu
ushirikiano na mchungaji bali pia na hali ya kanisa la mahali pamoja. Ikiwa kusanyiko la mahali
pamoja halina mtazamo wa kiinjilisti na kushindwa kuwafanya waamini / washiriki wapya
27
wajisikie kukaribishwa, mwinjilisti atakuwa anafanya kazi bure. Ili aweze kutumika vizuri,
anapaswa kuwategemea wengine. Anahitaji ushirikiano wa:
1. Watu waombao
2. Makanisa yanayojali
3. Wachungaji na waalimu wanaowalea waamini wapya katika Neno la Mungu
4. Wazee wenye uzoefu katika ushauri
5. Washirika / waamini wanaojua namna ya kuwafanya watu wajisikie kukaribishwa.
Wale waliookoka kupitia huduma hii wanapaswa wapelekwe kwenye nyumba za kiroho, kwa
mfano makanisa yanayoendesha mara kwa mara mikutano ya maombi na masomo ya biblia, na
hasa kufanyika vizuri kwenye vikundi vya nyumba kwa nyumba (home cell groups), vyenye sifa ya
upendo na kujali. Mpango huo utaongeza nafasi ili kwamba tunda la kazi ya mwinjilisti libakie.
Kuziangalia mada za mikutano ya hadhara au kampeni ya uinjilisti hazitoshi. Kunyoosha mikono
1000 haisaidii ikiwa tunda la mkutano halitabaki / halitakaa. Hivyo, inahusisha kanisa lote
kuwafikia waliopotea.
Mwinjilisti anategemea ushirikiano wao. Tunatakiwa kukumbushwa kwamba kazi ya kuwaleta
wasioamini kanisani haimtegemei Mwinjilisti peke yake , bali ni wajibu wa washirika wote.
Wanafunzi wote wanapaswa kuwafikia marafiki zao wasioamini, majirani na ndugu.
3. Kufikiria wazo jipya
Petro Wagner wa shule ya makuzi ya kanisa (church growth school) anashauri kuwa kila kanisa la
mahali pamoja kati ya washirika wake, 10% wana kipawa cha uinjilisti.
Tunahitaji kukumbuka kwamba kuelewa kwake kuhusu kipawa hiki cha uinjilisti ni kinyume na
jinsi tulivyozoea. Wagner, na shule ya makuzi ya kanisa, anathibitisha kwamba huduma hii
hufanya kazi ndani ya kanisa/ kusanyiko la mahali pamoja. Watu walio na kipawa hiki wana
“uwezo” maalumu kunena kwa wasiookoka na kuwaleta kwa Kristo.
4. Jihadhari na hisia mbaya
Miongo miwili (miaka 20) iliyopita imeona nguvu mpya ya kiinjilisti katika ulimwengu wote
kupitia hiyo huduma roho nyingi zimeongozeka katika ufalme wa Mungu. Mavuno haya ya
Kiroho ni matokeo ya ujasiri mpya yaliyofikiwa na wanafunzi wa Kristo, wakiwa na moto wa
shauku/mzigo kwa ajili ya roho. Kigezo kingine kinachochangia sana ni jeshi la wainjilisti,
lililoinuliwa na kutayarishwa na Mungu kwa ajili ya mavuno ya nyakati za mwisho. Kamwe, kabla
kanisa la Yesu Kristo halijaona wengi sana wakijiunga ngazi/nafasi ya wainjilisti. Wakati wengi
wao wamefanya hivyo kwa kutii wito wa Mungu, wengine wamejiunga na nafasi hizi wakiwa na
siri iliyofichika moyoni, kama ifuatavyo:
(1) Dalili ya umaarufu
Wainjilisti kama Osborn, Bonnke, Graham na wengine wamechangia umaarufu katika huduma ya
uinjilisti. Kutochoka kwao na bidii ya matunda yao imesababisha vijana wengi ndani yao wawe
28
kama wao. Wengi wao wamekuwa wainjilisti ili kuwaokoa waliopotea kama wafanyavyo hawa
watu wakuu wa Mungu. Hata hivyo wengine wamejilazimisha wao wenyewe kwenye huduma hii
wakiongozwa na tamaa zao kuhuburi katika mikutano mikubwa, kwa kuwaombea wagonjwa na
kutenda miujiza, ili wakuze majina yao wenyewe. Wametiwa hamasa na umaarufu ambao
unaambatana na huduma hizi za uinjilisti wa kimataifa. Hamasa kama hizi ni za kimwili na si za
Ki-Mungu na zitapelekea kushindwa. Hivyo lazima iepukwe kwa vyovyote vile. Utendaji kazi
mzuri wenye matunda katika huduma unaweza kuongoza katika umaarufu, lakini haipaswi kuwa
nguvu ya ushawishi / kuhamisisha kujiunga kwenye huduma. Kuweka mambo katika mtazamo,
ni vyema kukumbuka kuwa tamaa kwa ajili ya ukuu, mvuto au ushawishi, madaraka, na umaarufu
si tu kwamba vilisababisha shetani kuanguka, bali pia watu wengi wazuri wa Mungu.
(2) Kususia uwajibikaji/Majukumu:
Uwajibikaji ni sehemu ya huduma ya kiroho. Kila mtumishi wa kweli wa injili atakuwa tayari
kutoa hesabu ya fedha alizopewa kwa ajili ya huduma zilivyotumika. Hata hivyo, wengine
huanzisha huduma zao, si kwa sababu zimekuwa na kuzidi mipaka ya dhehebu lao, lakini kwa
sababu wanakataa kuwajibika. “Wajibu wao ni kwa Mungu tu” ambapo mara zote huonyesha
fedha na michango iliyotolewa kwa ajili ya jambo fulani wao hutumia kama waonavyo wao
wenyewe. Huduma ya uinjilisti kwao hutoa nafasi ya kazi bila wao kuwajibika katika kamati ya
kanisa.
Wito wa Ki-Mungu, huambatana na mzigo mkubwa kwa ajili ya roho zilizopotea inaweza ikawa
tu sababu inayokubalika kwa ajili ya kuingia katika huduma ya uinjilisti.
5. Kutoa nafasi
Kazi kubwa ya mwinjilisti ni kulifanya jina la Yesu lijulikane katika ulimwengu unaokufa, kwa
sababu hii hupanua mipaka ya ufalme wa Mungu na wakati huo huo tunavamia/shambulia
himaya ya shetani. Kama ilivyokwisha onyeshwa, ushirikiano na hali ya wachungaji wa mahali
pamoja husaidia kutambua matokeo ya huduma ya mwinjilisti. Wakati wachungaji
wanaposhindwa kutoa nafasi kwa wainjilisti huwawanyimi tu washirika wao huduma ya Mungu
iliyotiwa mafuta/wekwa wakfu, huzuia kukua kwa ufalme wa Mungu, lakini pia huchangia
kutenganisha huduma hizi mbili za muhimu. Viongozi wa mahali pamoja ambao huwatumia
wainjilisti watatambua kwamba si tu wanazileta roho, bali wanawahuisha na kuwahamasisha
waamini kutimiza wajibu wao wa kushuhudia na wavunaji wa roho, kwa sababu hii huchangia
kukua kwa makanisa ya mahali pamoja.
Wachungaji wanaopinga kwamba hawahitaji huduma hii kwa sababu wanampango wao wa
kiinjilisti katika makanisa yao hawajaelewa umaana na umuhimu wa huduma hii kwa ajili ya kanisa
la mahali pamoja.
Ingawaje watu huokoka kupitia huduma ya mchungaji katika ibada ya jumapili ya asubuhi,
mwinjilisti atawafikia wasioamini kwa kiwango kikubwa zaidi. Nyongeza ya hayo, mahubiri
yatachochea nguvu ya kiinjilisti katika kusanyiko. Kushindwa kwa kanisa la mahali pamoja na
mchungaji kumtumia mwinjilisti hakutawanyang’anya tu baraka za rohoni bali waweza
29
kuwawekea wainjilisti mipaka ya kufanya kazi ya mchungaji, kwa sababu hiyo wanapoteza utendaji
wao kwa usahihi.
Baadhi ya wachungaji husita kuwakaribisha wainjilisti kwa sababu ya kutokuelewana huko nyuma
na wengine ambao waliingilia maswala / mambo ya kanisa la mahali pamoja, au waliwaendea
washirika wao kuomba msaada wa fedha bila wao kujua. Mambo hayo yasiyofuata taratibu lazima
yashughulikiwe katika namna inayofaa, ili huduma ya mwinjilisti iweze kutumika katika msingi
ulio wa kawaida. Hili halitalinufaisha tu kanisa, bali kutaiheshimu huduma ambayo ilianzishwa na
Bwana mwenyewe.
MCHUNGAJI
Huduma hii imekuwa maarufu/mashuhuri sana. Neno la Kiyunani kwa mchungaji poimen
limetajwa mara nyingi katika Agano jipya, lakini limetafsiriwa mara moja tu kama “Mchungaji”
imeandikwa katika Waefeso 4:11 katika sehemu nyingine zote pale inapoonekana katika Kiyunani
imetafsiriwa kama “Mchungaji wa Kondoo”. Tunapochunguza zaidi tutagundua kwamba wazo la
kibiblia la huduma hii kiasi fulani laweza kutofautiana kulingana na vile tulivyozoea. Maandiko
yanatuonyesha ukweli kwamba maneno ambayo yametumika kwa ajili ya umaarufu wa kupenda
vyeo siku hizi kama, “Askofu”, lilikuwa sawa sawa na huduma ya Mchungaji katika kipindi cha
kanisa la kwanza. Inazidi kuonyesha kuwa uongozi katika kanisa la mahali pamoja halikuwa jambo
la mtu mmoja, bali lilishirikisha wengine wengi wote waliokuwa wameitwa na Mungu.
1. Mchungaji ? Wachungaji? –Wazee, Waangalizi au Maaskofu?
Katika kanisa la kwanza kazi ya uongozi ndani ya kanisa la mahali pamoja walishirikishana.
Hakuna mahali popote katika kanisa jipya tunapokuta kusanyiko la mahali pamoja likiwa na
kiongozi mmoja tu. Hasa katika kitabu cha Matendo ya Mitume na nyaraka za Paulo zinaonyesha
kuwa uwazi zaidi kwamba mitume waliwachagua wazee (neno la wingi) katika makanisa
waliyokuwa wameyaanzisha. Wakati neno la umoja linapotumika kifungu kinaeleza sifa za
kiongozi huyo (1 Timotheo 3:2, Tito 1:7).
Tunahitaji kutambua kwamba maneno, Mzee, (kiyunani: Presbuteros, kutokana na hilo
limepatikana neno la kiingereza Presbyter), Mwangalizi (kiyunani: episkopos, kutokana na hilo
limepatikana neno la kiingereza episcopal) na Askofu (Kiyunani: episkopos) yanatumika kwa
pamoja, hivyo inaonyesha kwamba maneno tofauti yanatumika kwa ajili ya ofisi/huduma moja.
Sifa za Askofu/mwangalizi zimeorodheshwa katika 1 Timotheo 3:1-7, na zile za mzee, katika Tito
1;6-9,hazina mjadala, zinafanana. Katika 1 Petro 5:1-2 viongozi wanahamasishwa kulisha
(poimaino–linamaana Mchungaji wa kondoo) kondoo na kuwatunza (episkopeo). Katika
Matendo 20 (mstari wa 17 na 28) maneno kama wazee na waangalizi yanatumika kwa pamoja na
neno la Kigriki poimen –Mchungaji wa Kondoo (shepherd) au mchungaji (pastor). Tutazame
haya na katika maandiko mengine.
30
Sifa za Askofu/Mwangalizi Sifa za Mzee
Kiyunani –episkopos
1 Timotheo 3:1-7:
1 Ni neno la kuaminiwa, mtu akitaka kazi ya
askofu, atamani kazi njema. 2 Basi imempasa askofu
awe mtu asiye laumika mume wa mke mmoja mwenye
kiasi na busara, mwenye utaratibu, mkaribishaji,
ajuaye kufundisha, 3 si mtu wa kuzoelea ulevi, si
mpiga watu, bali awe mpole, si mtu wa kujadiliana,
wala asiwe mwenye kupenda fedha, 4 mwenye
kusimamia nyumba yake vyema, ajuaye kutiisha
watoto katika ustahivu, 5 Yaani mtu asiyejua
kusimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje
kanisa la Mungu ? 6. Wala asiwe mtu aliyeongoka
karibuni, asije akajivuna akaanguka katika hukumu
ya Ibilisi. 7. Tena imempasa kushuhudiwa mema na
watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego
wa Ibilisi.
Kiyunani –Presbuterios
Tito 1:5 –9:
5 Kwasababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze
yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji
kama vile nilivyokuamuru’ 6 ikiwa mtu
hakushitakiwa neno, ni mume wa mke mmoja, ana
watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni wafisadi
wala wasiotii. 7 Maana imempasa askofu awe mtu
asiyeshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa
Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe
mwepesi wa hasira, asiwe mlevi wala mgomvi, asiwe
mpenda mapato ya aibu, bali awe mkaribishaji,
mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki,
mtakatifu, mwenye kuthibiti nafsi yake, akilishika
lile neno la imani vilevile kama alivyofundishwa,
apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho
yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga.
1 Petro 5:1-2:
Nawasihi wazee walio kwenu mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na
mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye; 2 lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na
kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya
aibu bali kwa moyo.
Matendo 20:17-28
Toka Mileto Paulo akatuma watu kwenda Efeso, akawaita wazee wa kanisa. 18 walipofika kwake,
akawaambia, ninyi wenyewe mnajua tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa Asia, Jinsi nilivyokuwa
kwenu wakati wote, 19 nikimtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, na kwa machozi, na majaribu
yaliyonipata kwa hila za Wayahudi; 20 ya kuwa sikujiepusha katika kuwatangazia neno lolote liwezalo
kuwafaa, hali naliwafundisha wazi wazi, na nyumba kwa nyumba; 21 nikiwashuhudia Wayahudi na
Wayunani wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo. 22 Basi sasa, angalieni, nashika
njia kwenda Yerusalemu hali nimefungwa rohoni, nisiyajue mambo yatakayonikuta huko; 23 isipokuwa
Roho Mtakatifu mji kwa mji kunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja. 24
Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na
huduma ile ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia habari njema ya neema ya Mungu. 25 Na
sasa tazameni mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowahubiria ufalme wa Mungu, nikienda huko na
huko, hamtaniona uso tena. 26 kwa hiyo nawashuhudia wote siku hii ya leo ya kuwa mimi sina hatia
kwa damu ya mtu awaye yote. 27 Kwa maana sikujiepusha na kuwahubiri habari ya kusudi lote la
Mungu. 28 Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi
kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake
mwenyewe.
Matendo 14:23:
Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga,
wakawaweka katika mikono ya Bwana waliye mwamini.
Yakobo 5:14
Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa, nao wamuombee, na kumpaka mafuta
kwa jina la Bwana.
31
Tito 1:7
Maana imempasa askofu awe mtu asiyeshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu, asiwe mtu wa
kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mlevi wala mgomvi, asiwe mpenda mapato ya
aibu;
Wafilipi 1:1:
Paulo na Timotheo watumwa wa Kristo Yesu kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walioko Filipi,
pamoja na maaskofu na mashemasi
Inaonekana kwamba neno mzee linaonyesha uzoefu wa kukua kiroho na kuwalewa wale
walioelezewa, wakati Askofu au Mwangalizi (kwa pamoja yametafsiriwa kutokana na neno lilelile
la kiyunani; episkopos) huonyesha tabia ya kazi iliyotendeka. Eugene Juhnson anathibitisha
kwamba, Askofu hakuwa na sehemu ya kutawala makanisa au hakuwa na cheo cha kikanisa.15
Kwa mtazamo huu tunahitaji tuchunguze zaidi matumizi ya neno, pamoja na matumizi yake ya
kidunia katika nyakati za Ki-biblia.
(1) Matumizi ya neno (episkopos) nje ya mazingira ya Agano Jipya.
Neno Mwangalizi au askofu (episkopos) yote yanatumika katika ustaarabu wa Kiyunani
(Hellenism) na wa Kiyuda (Judaism). Katika utamaduni wa Kiyunani neno episkopos –
Mwangalizi linapatikana katika maandishi ya Homer ambayo yanaelezea miungu iliyolinda nchi,
watu na masoko. Baadaye neno linatumiwa kuonyesha wafanya kazi wa serikali waliotumwa
kutoka Athene kwenda kulinda amani katika miji iliyokuwa chini ya himaya ya Wayunani.16 Neno
episkopos linaelezwa zaidi kama vile wasimamizi; wahasibu, waweka hazina, watumishi wa serikali
na wapiga mbiu (heralds) ambao walikuwa wakipeleka habari / jumbe.17
Katika uyahudi neno episkopos linaonekana katika Waessene (Essenes) dini/dhehebu la Kiyahudi
la Wakumrani (Qumran) ambao waliongozwa na mebaqqer. Alilinda na kuongoza kwa mamlaka
kama yale ya mfalme (monarch). Kwa upande mwingine kazi yake pia inalinganishwa na ile ya
mchungaji wa kondoo, kama baba akionyesha huruma kwa watoto wake na kuwakusanya wale
waliopotea.18
Katika nyakati za Agano la Kale wazee walikuwa viongozi wa makabila na koo za kifamilia.
(Wazee 70 na Musa –Hesabu 11:16; Kumbukumbu 27:1, nk). Neno Mzee na kazi zao zilifuatwa
na Kanisa la kwanza (Wakizingatia historia ya nyuma ya Wayahudi), wakati neno askofu au
mwangalizi liliongezewa kuonyesha uangalizi wao wa kiroho.
Ijapo kuwa baadhi ya dalili za episkopos za Kidunia zinaweza kuonekana katika mwangalizi /
askofu wa Agano jipya, hata hivyo ni za kipekee na inaonekana hazikuanza kutokana na ushawishi
wa kidunia. Kazi ya Mwangalizi kibiblia haikujua kulazimisha kuwa kwenye uongozi, bali
ulitazamwa katika roho ya undugu, upendo wa Agape na usawa pamoja na waamini wengine
katika mwili. Kwa kuwa neno askofu (episkopos) limetumika katika 1Petro 2:25 kumwelezea
15 Eugene Johnson, Duly and Scripturally Qualified (Cincinnati: Standard Publishing,1975), p. 35.
16 Theologisches Begriffs Lexikon zum Neuen Testament,, (Wuppertal: Brockhaus, 1977), I: 124.
17 Arnold Bittlinger, Im Kraftfeld des Heiligen Geistes. (Marburg: Ökumenischer Verlag, 1976), p. 133.
18 Theologisches Begriffs Lexikon zum Neuen Testament, p. 125.
32
Kristo kama Mchungaji wa Kondoo na Askofu wa roho zetu, tunapaswa kufahamu kwamba
uangalizi wa kiroho, utumishi, upendo na kujikana binafsi ni alama ya kweli ya askofu.
Kulielezea jambo la uongozi wa pamoja katika kiwango cha kanisa la mahali pamoja, hatupaswi tu
kuyatazama maandiko bali turudi nyuma katika historia ya kanisa la kwanza na muundo wa
utamaduni wake.
(2) Uongozi wa pamoja / wengi.
Wazo la uongozi wa pamoja ulijulikana katika jamii ya Yuda, Kiyunani na jamii ya Kirumi. Miji
mingi ya Kiyunani ilikuwa na gerousia, ambalo laweza kutafsiriwa kama baraza la wazee au
presbyterium (presbytery) uongozi wa baraza la wazee mkoa wa kanisa). Mabaraza haya
yalichagua waangalizi watumishi miongoni mwa washirika wao kwa ajili ya kazi mbali mbali.
Baraza kuu la uongozi la Rumi (baraza la wazee) vile vile lilichagua wenye vyeo vya juu
(waangalizi) na wenye vyeo vya chini kutoka miongoni mwao. Kila mmoja wa viongozi hawa
waliwajibika moja kwa moja kwenye baraza kuu ambao walikuwa na mamlaka kamili ya
usimamizi. Hata hivyo, baadaye uongozi huu wa pamoja ulipotea pale uongozi wa utawala wa
kirumi alipojitoa kwenye baraza kuu (senate). Wakati uongozi katika gerousia na wa baraza kuu
kujitoa kwenye baraza la zamani na familia zenye vyeo / daraja la juu, wazee katika masinagogi ya
kiyahudi walichaguliwa na kusanyiko la sinagogi. Hapa tena tunaona uongozi wa pamoja. Hata
hivyo, wazee wa baraza la sinagogi waliteua mwangalizi kwa kila sinagogi –archisynagogos, na
mtumishi wa sinagogi (shemasi).19
Katika Agano jipya tunaona kusanyiko la mahali pamoja liliwekwa chini ya uangalizi wa wazee,
(ambao hawakuchaguliwa bali waliteuliwa na mitume,au wale walioamuliwa kufanya hivyo (Tito
na Timotheo). Kila baraza la wazee lilimtambua mzee kiongozi; ambaye alikuwa kiongozi
miongoni mwa wazee wenzake. Yakobo ambaye alijulikana kama kiongozi wa Kanisa la
Yerusalemu ni mfano mzuri. Alijulikana dhahiri kama kiongozi na mnenaji wa kanisa la mahali
pamoja la Yerusalemu, hata hivyo hakuwa kiongozi mmoja tu. Leo angejulikana kama mchungaji
wa kanisa la mahali pamoja. Aliliwakilisha kanisa nje na miongoni mwa jamii ya Kikristo.
“Malaika” (kiyunani angelo = tarishi) ambaye aliyaandikia Makanisa saba yaliyoko Asia ndogo
(Ufunuo 2 na 3) kwa kawaida inaaminika kuwa ni wazee viongozi au wachungaji wa matawi wa
makanisa haya, kwani haitakuwa na maana kuwaandikia barua malaika / viumbe visivyoonekana.
Kadri muda ulivyozidi kwenda kanuni hii ya Ki-biblia ya kuwa kiongozi miongozi mwa wenzake
ilipotea. Hii ilimaanisha kwamba kanisa likawa na mfumo wa uongozi.
Henry C. Sheldon anaelezea;
Ni rahisi kufikiriwa kwamba ofisi / huduma ya askofu ilikuwa ikikua pole pole ambayo chanzo
chake kilikuwa ni baraza la wazee. Baraza hili katika makanisa mengi kiasili lingekuwa na mzee
kiongozi. Watu wenye nguvu na uwezo mkubwa wangeitwa kujaza hii nafasi. Lengo la umoja na
utawala bora ungelisababisha kugawa / kutoa (delegate) madaraka kwao, mpaka kuja kuwa wakuu
wa makanisa, au maaskofu halisi.20
19 Arnold Bittlinger, Im Kraftfeld des Heiligen Geistes, p. 136.
20 Henry, Sheldon, History of the Christian Church (Peabody: Hendrickson, 1988), p. 245.
33
Barua ya Clement, mmoja wa mababa wa kitume, iliyoandikwa mwishoni mwa karne ya kwanza
inaonyesha kuwa maaskofu na wazee bado walifikiriwa kuwa viongozi wa makanisa ya mahali
pamoja. Mfumo wa utawala wa kiaskofu kwa mfano kiongozi pekee wa Kanisa la mahali pamoja,
na baadaye kiongozi wa makanisa, haukujulikana. Baadaye ulitokea kwenye karne ya nne.21
Kamusi mpya inayoitwa “The New International Dictionary” ya Kanisa la Kikristo inaeleza, kwa
kupotea kwa huduma ya uamsho wenye nguvu, na kutambuliwa kwa kanisa na watawala katika
karne ya nne, askofu mmoja akiwa kiongozi / msimamizi wa jimbo au wa Makanisa ulijitokeza.
Kwa kawaida alikuwa mkuu wa jiji au kanisa la mjini. Zaidi sana, kwa kukubali mgawanyiko wa
kanisa katika utawala pia wakatokea maaskofu ndani ya maaskofu –hii ni papa, Askofu mkuu
(patriarch), Askofu mkuu kwenye jimbo lililo na maaskofu wengi (metropolitan), Askofu mkuu
(archbishop).22
Ijapokuwa wazo la uongozi wa kushirikiana, na kanuni ya kuwa kiongozi miongoni mwa
mwenzake ulipotea kipindi cha historia ya kanisa, hatuna udhuru wa kutufanya tusirudi kwenye
mfano wa kibiblia. Kanisa la Kikristo ni la jumuia, na siyo vikundi vya ushirika wa biashara au
kampuni. Kwa hiyo haliwezi kuendeshwa kwa kanuni zilizopo za kidunia, ambapo maamuzi
yanafanywa na wakurugenzi au mameneja. Kutokana na roho ya umoja, maamuzi yanayofanywa
na uongozi wa kanisa yanapaswa yawe ya pamoja. Ikiwa kama mwafaka hautafikiwa, wazee
wanapaswa kuingia katika maombi ya kufunga kutafuta mapenzi ya Mungu katika jambo hili kwa
kuwa nia ya Mungu ni “moja” tu, ni wajibu wa uongozi kufanya yote yanayotakiwa kupata
mapenzi ya Mungu. Hii inamaanisha kwamba kila mzee anapaswa kuwa radhi kuweka kando
mawazo aliyokuwa nayo, na yasiyoegemea upande wowote, na kujikana, ili Mungu adhihirishe
mapenzi yake kwao. Hakuna nafasi ya ubinafsi/umimi au kuzuia katika uongozi wa kibiblia,
kama ilivyowekwa wakfu kufunua roho ya umoja ya Ki-Mungu na usawa kwa wote.
(3) Nafasi au umuhimu wa Mchungaji
Sasa twaweza kujiuliza, nini umuhimu wa Mchungaji wakati uangalizi wa kiroho upo mikononi
mwa wazee, maaskofu na waangalizi? Kuliweka wazi hili jambo tunapaswa kuelewa kwamba
neno la kiyunani kwa mchungaji ni poimen (Waefeso 4:11), ambalo maana yake ni “mchungaji
wa kondoo” kwa mfano atunzaye aongozaye na alishaye kondoo. Chakufurahisha neno la
kiyunani poimen linatafsiriwa “Mchungaji wa kondoo” mara 17 na mara moja tu (katika Waefeso)
kama Mchungaji.23 Ikiwa kama tukilinganisha Matendo 20:28 na mstari wa 17 tunaona kwamba
madaraka yametolewa kwa wazee au waangalizi ni yale ya Mchungaji wa kondoo
Matendo 20:28
Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi
ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.
Maandiko katika 1 Petro 5:1-2 yanathibitisha hili ambapo wazee wanatiwa moyo kulisha
(Kiyunani poimanate) kondoo. Hata hivyo tafsiri sahihi siyo kulisha bali ni “kuchunga kondoo”,
21 Early Christian Writings, The Apostolic Fathers (London: Penguin Books, 1987), p. 17.
22 The New International Dictionary of the Christian Church, (Grand Rapids:Zondervan, 1981), p. 133.
23 Linganisha : Mathayo 9:36; 25:32, 26:31; Marko 6:34; 14:27; Luka 2:8, 15, 18, 20; Yohana 10:2, 11,
12, 14, 16 Waebrania 13:20; I Petro 2:25.
34
ambayo huonyesha ni zaidi ya kulisha kwa hiyo,kazi ya Mchungaji inapaswa kuonekana inafanana
na ile ya mzee au mwangalizi.
Baada ya kuona maneno yanavyoingiliana, uongozi wa pamoja (plurality of leadership) na
umuhimu wa Mchungaji tunapaswa sasa kutafuta sababu ya utofauti ambao upo kati ya Neno la
Mungu na utaratibu wa sasa.
(4) Sababisho na madhara
Haitoshi tu kuonyesha kuwepo kwa utofauti kati ya maandiko na mazoea, bali tunapaswa kujaribu
kutafuta sababu ya tofauti hii ni kujaribu kutafuta njia ya kuziba ufa. Wakati wa kujifunza
maandiko inakuwa dhahiri kwamba uanzishaji wa makanisa katika kanisa la kwanza unatofautiana
mno na siku zetu/mazoea ya leo. Utaratibu wa sasa umebeba kupeleka injili sehemu zisizofikiwa
na wachungaji, wanatumwa kuangalia / kutunza makundi/makanisa mapya yaliyoanzishwa.
Mtazamo wa Agano Jipya kwa upande mwingine unaonyesha kwamba makanisa mapya
yalianzishwa na mitume ambao waliwachagua na kuwateua wazee katika kusanyiko walilokuwa
wamelianzisha. Hawakuleta wachungaji kwa ajili ya uongozi wa kanisa kutoka mahali pengine.
Ijapokuwa Paulo aliwatumia watu kama Timotheo au Tito ambao walisaidia makusanyiko mapya
yaliyoanzishwa kwa kipindi fulani, hatuna mahali panapoonyesha katika maandiko au historia ya
kanisa kuwa walifanya kazi kama wachungaji wa mahali pamoja wa kudumu katika makanisa
yoyote ambayo Paulo aliyaanzisha katika safari zake za Umishonari.
Hili linatuacha wapi? Kutokana na kutokuwepo kwa huduma ya kitume tumebuni taratibu zetu
wenyewe za kujitoa kuanzisha makanisa na namna ya kupeleka injili katika maeneo mapya.
Tukirudi kwenye mfano wa kibiblia, kitu fulani tunapaswa kufanya, tutapinga vikali mazoea ya
kisasa na mila/desturi. Kukumbatia mawazo ya Agano Jipya haitakuwa rahisi na itatulazimisha
kutafuta suluhu itakayotoa nafasi iliyobora, kwa wakati huo huo tukikubaliana na taratibu za siku
hizi. Ni muhimu kuonyesha matokeo tuliyoyaona katika hali ya kanisa la leo, ambayo
yanapendekeza kuwa:-
1. Kuendelea na uinjilisti wa kufika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma ya “kuagiza”
viongozi wa makanisa kwa wakati ule ule tujitahidi kurudi katika taratibu za kibiblia, wapi na
lini inapowezekana.
2. Kutambua kwamba kamwe halikuwa kusudi la Mungu kuweka mambo ya kiroho ya
kusanyiko katika mikono ya mtu mmoja tu. Nidhahiri kwamba usimamizi/uangalizi wa
kiroho mara zote ulikabidhiwa kwa baraza la wazee.
3. Kutekeleza uongozi wa pamoja kwa mara moja. Wachungaji waliowekwa katika makanisa
mapya wanapaswa kujitahidi kuonyesha ni waamini waliokua kiroho haraka iwezekanavyo na
ambao watashirikiana katika majukumu ya uongozi.
4. Kutunza wazo la “Mzee kiongozi” au Mchungaji wakati wakishirikiana majukumu kwa ajili ya
mambo ya kiroho ya waamini miongoni mwa wazee mahali pamoja.
5. Kulinda dhidi ya dhana potofu ya vyeo vya kibiblia hasa wakati vinatumika kuonyesha
“umuhimu” wetu, hakuna kituchochote isipokuwa kiburi na majivuno ya kiroho. Kutumia,
vyeo vya kibiblia kwa usahihi hata hivyo haipendezi kwamba tunapaswa kuanza kuwaita
viongozi wa mahali pamoja waangalizi au Maaskofu. Neno Mchungaji ni la kimaandiko na
huonyesha kazi iliyotolewa ni ya kufaa.
6. Tofauti ya viwango vya majukumu katika uzee ni lazima utambuliwe katika 1 Timotheo 5:17
tunasoma: “Wazee watawalao vyema na wahesabiwe kustahili heshima mara dufu; hasa wao
wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha.”Hii inaonyesha kwamba si kila mzee ameitwa
35
kuhubiri neno. Kwa nyongeza katika huduma ya kufundisha na kuhubiri maandiko
yanaonyesha kazi zifuatazo za wazee/wachungaji
 Kuliwakilisha kanisa la mahali pamoja (Matendo 11:30; 21:18)
 Kuwajibika kwa ajili ya kanisa la mahali pamoja (Mdo 14:23)
 Kuliongoza kanisa (1 Timotheo 5:17).
 Kuombea wagonjwa (Yakobo 5:14)
 Kutunza mapato ya kanisa na kulifanya kanisa liwe na nidhamu (1 Petro 5:2)
 Kutumika kama mshauri (Matendo 20:28)
7. Wakati tunapowaangalia viongozi kama waangalilzi (waangalizi wa wilaya, mwangalizi wa
kitaifa n.k) hatupaswi kusahau kwamba maandiko yanaeleza hiki cheo kutumika kwa ajili ya
viongozi wa kanisa la mahali pamoja.
Katika kifungu cha maandiko kilichopo katika 1 Timotheo 5:17 inaonesha kwamba viongozi wa
kanisa la mahali pamoja walishirikishana majukumu na kazi zote. Hivyo, wajibu wa kichungaji
kama vile utawala, ushauri, kutembelea wagonjwa hospitalini, utunzaji wa mahesabu, kuhubiri,
kufundisha, n.k. vinapaswa kuangaliwa / kufanywa na kundi la viongozi. Katika kanisa la sasa
Mchungaji mara zote anatarajiwa kufanya vizuri zaidi katika mambo yote haya yaliyotajwa, kitu
ambacho kamwe Mungu hakutarajia iwe hivyo. Huduma itakuwa sanifu zaidi ikiwa Mchungaji
atashirikisha baadhi ya majukumu yake na wazee wenzake bila kuhisi hofu hasa ikiwa wanaweza
kufanya kazi nzuri zaidi yake. Kama makanisa yanayoamini Biblia, tunapaswa kufuata mfano wa
kibiblia, na bila kuvutwa na mwelekeo usio wa kimaandiko ambao unatuzunguka.
2. Kazi ya Mchungaji
Mtu mmoja alieleza, Mwinjilisti ni kama daktari wa uzazi au mkunga, ambaye hushughulika na
kuzalisha watoto wachanga kiroho, wakati Mchungaji ni daktari wa magonjwa ya watoto, ambaye
anajihusisha na kukua, maendeleo na afya ya kiroho ya mtoto mchanga.24 Kwa maneno mengine
kusudi la Mchungaji ni kuwatunza na kuwaimarisha wale waliookoka kupitia uinjilisti. Bado hii ni
moja tu ya kazi zake nyingi, ambayo inakusanya majukumu mengi, kama kazi yake
inavyojumuisha majukumu mengi pamoja na yafuatayo:-
(1) Kutoa uongozi / kuongoza
Mchungaji huonyesha njia. Huweka hatua (pace) na kutoa mwelekeo. Hufanya hivyo kwa kutoa
uongozi wa kiroho kwa ajili ya kusanyiko la mahali pamoja kupitia mfano wake, uthabiti, imani,
maono na hekima. Ni wajibu wake kuwaongoza waamini kuwa na ushirika wa karibu sana na
Bwana, na wale ambao hawajaokoka kuwa na uhusiano ulio hai na Yesu. Kupitia yeye waamini
watakuja kwake kwa ajili ya ushauri na kutiwa moyo.
Kutoa uongozi maana yake ni kuwa msimamizi. Mchungaji anapaswa kugawa madaraka na
kuwahusisha watu wengi kadri iwezekanavyo. Lakini kitu kimoja ambacho hapaswi kugawa
madaraka ni uongozi wake. Kama George Canty anavyoeleza kwa usahihi, kiongozi anapaswa
kuongoza, na siyo kutupa hatamu (reins) kwenye shingo ya farasi. Hapaswi kuendesha ibada kwa
24 B.E. Underwood, Spiritual Gifts, Ministries and Manifestations (Franklin Springs: Advocate Press,
1984), p. 33.
36
kuliruhusu kanisa kutenda kadri mtu yoyote anavyojisikia kutenda. Ibada ya kanisa haipaswi kuwa
huru kwa wote –huyu ana wimbo? Mwingine anahudumu meza ya Bwana, mwengine anaongoza
uimbaji? Mchungaji anatakiwa kutunza utaratibu, ili kila jambo litendeke kwa utaratibu na katika
roho nzuri.25
(2) Kutoa chakula cha kiroho
Moja ya kazi ya msingi ya Mchungaji ni kutoa chakula cha kiroho kwa kondoo zake. Kwa hiyo
anapaswa kuwa mwanafunzi wa neno, kamwe haachi kujifunza na kupanua ufahamu wake wa
maandiko.
Ikiwa atashindwa kuiendeleza huduma yake atapoteza utendaji wake wa kazi polepole. Huduma
yake itanyong’onyea na haitakuwa na ladha. Kulisha kondoo huhitaji maandalizi ya kudumu.
Agizo la Yesu kwa Petro “Lisha kondoo wangu” Limetolewa kwa watumishi wote vile vile.
Lakini wahubiri wengine wanajitoa kidogo kuwawakilisha watu wa Mungu na jumbe zenye upako
zilizopokelewa kutoka kwake. Mahubiri yanayohubiriwa yanapaswa yawe hai, yanayogusa maisha
ya watu, na siyo tu marudio ya kitabu kinavyosema, au kile alichokisoma katika kitabu. Wahubiri
ambao wanatafuta umaarufu na kutambuliwa wanaweza kuwalisha watu wa Mungu jumbe nyepesi
za kubabaisha na jumbe za maarufu (jumbe za kuwapendeza watu zitakazokufanya upendwe na
watu. Imani ya kupita kiasi (hyper-faith) na mafanikio ya kupita kiasi (hyper –prosperity) n.k,
lakini Mchungaji wa kweli atajisikia kuwajibika kutangaza shauri kamilifu la Mungu katika
mahubiri yake na mafundisho yake.
(3) Kutoa ulinzi
Mchungaji wa kweli hujisikia kuwajibika kulilinda kundi lake kutokana na uzushi na mafundisho
ya uongo. Kwa hiyo anapaswa kuwa macho/mwangalifu, kumjua adui yake na kuwa makini
hatari zozote zinazoweza kutokea ambazo zitalidhuru kundi lake. Anatambua kuwa kuna mbwa
mwitu waliojivika ngozi ya kondoo wakitafuta kujifananisha na kondoo, kutawanya na
kuliangamiza kundi la kondoo (Tito 1:11; 2Petro 2:1; Matendo 20:28-32). Hata hivyo kuhusika
kwake hakutamtia katika hali ngumu kuitendea kazi mamlaka bali atawapa uhuru wa kuchagua
wale wanaowalea.
(4) Kutoa faraja na kujali
Uwezo wa mahubiri na mafundisho mazuri hayatoshelezi kumfanya Mchungaji afanikiwe. Kuna
kitu cha ziada kinachohitajika. Ni kama tu Mchungaji wa kondoo, akitunza kundi lake, akiyatibia
majeraha, michubuko na kuviganga viungo vilivyovunjika, kwa hiyo Mchungaji anapaswa kujua
jinsi ya kufariji waliovunjika moyo, kuwatia moyo wenye huzuni na kuwatuliza waliokwazwa.
Atajisikia ndani ya roho yake wakati baadhi ya washirika wake wanateseka.
Kwa kadri anavyoomba kwa ajili yao kila siku, akiyataja majina yao mbele za Bwana, Roho
Mtakatifu anaweza kumfunulia mahitaji yao. Mchungaji wa kweli atakuwa na moyo wa uchungaji
wa kondoo, kama vile Yakobo (Matendo 15:13 21:18) ambaye alipewa jina la utani “magoti ya
25 George Canty,. The Practice of Pentecost (Basingstoke: Marshall Pickering, 1987), p. 154.
37
ngamia” kwa sababu ya usugu wa ngozi katika magoti yake kutokana na kupigamagoti mda
mrefu akiombea kondoo zake.
Katika mitizamo mingi picha ya mchungaji wa mashariki ya mbali inafaa sana kuelezea huduma ya
mchungaji / mchungaji wa kondoo. Hatunzi tu kondoo bali huchukua nafsi / wajibu wa mlinzi,
kiongozi, tabibu na “mkombozi” wa kondoo wake. Kuwalinda kutokana na wanyama wa mwitu
na wezi, hujenga zizi la kondoo ambalo kondoo hutunzwa wakati wa usiku. Wakati kondoo
wakiingia zizini mchungaji husimama langoni akihesabu kondoo kila siku wakati wakipita juu ya
fimbo yake. Hii humwezesha kuchunguza hali zao zilivyo, akiwabagua na kuwahudumia wale
ambao ni wagonjwa au waliochubuliwa, na kutambua yeye mwenyewe kuwa hakuna aliyepotea.
Usiku hulala mlangoni, hivyo yeye huwa “mlango” wa zizi. Kwa hiyo wanyama mwitu hawawezi
kuingia bila ya yeye kushambuliwa kwanza, wala kondoo hawawezi kuondoka bila ya yeye
kugundua/kutambua. Huwalinda huwalisha na huwapenda katika kiwango hata cha kuwajua
majina yao. Mfano huu unapaswa kumvuvia kila mchungaji kuwa mlinzi kiongozi wake.
Itamhamasisha kuhesabu kondoo zake kila siku katika maombi, hivyo huwachunguza hali ya
kiroho chao na kuwahakikishia kuwepo kwao katika kusanyiko lake. Kundi la Mchungaji
limeundwa na watu wasio wakamilifu kutoka kila mahali. Ni wajibu wake kulinda roho zao.
Kufanya hivyo anahitaji awe ni mtu aliyejawa na huruma nyingi kuhubiri Neno, kuthibitisha,
kukemea na kusihi pamoja na uvumilivu na mafundisho yote (2 Timotheo 4:2). Anaweza kutoa
pia ushauri na kusaidia ikiwa kama kuna ulazima. Kwa ufupi yuko pale ka ajili ya kondoo zake
kwa hiari akiyatoa maisha yake kwa ajili ya kondoo wake.
(5.) Kanisa kubwa au Kanisa la Nyumbani (dogo)
Si kila mtu aliyeitwa kwenye huduma ya uchungaji atakuwa mtumishi wa Kanisa kubwa –Kanisa
lenye maelfu ya washirika. Kuongoza makanisa yenye ukuaji usiokuwa wa kawaida na kuhudumu
kazi za kila siku inahitaji kipawa cha nyongeza / ziada. Wachungaji wengine huchunga makanisa
yenye waamini chini ya washirika elfu moja hata chini zaidi ya washirika mia mbili. Inaonekana
kwamba kwa kawaida wameitwa kuwa wasimamizi wa makundi ya nyumbani, ambayo ni sehemu
ya Kanisa kubwa chini ya uongozi, wa kwanza wa “Viongozi waliosawa” mzee. Wachungaji kama
hao ni watenda kazi wazuri wakati wote wanapofanya kazi yao ya huduma ya kichungaji.
Kufundisha –kuhubiri katika ibada za nyumba kwa nyumba (home –cell groups). Kuitwa
kuhubiri hakuna maana ya kuwa siku zote itaonekana huduma ya kuonekana zaidi. Inachukua
ukuaji wa kiroho kutambua na kukubali ukweli huu. Wale wanaoshindwa kufanya hivyo
hawatawavunja moyo tu wale waliochini ya uangalizi wao, lakini hatimaye wanaweza kukata tamaa
wakijiona kuwa wameshindwa. Kwa upande mwingine wako wengi ambao wana uwezo kuchunga
makanisa makubwa bali wanashindwa kujiweka wakfu, kuvumilia, kazi ngumu na uwezekano wa
mafundisho ambayo yanahitajika kuliongoza Kanisa katika kukua.
3. Wachungaji wanaitwa na hawatengenezwi / hawaundwi.
Wakati uwazi wa mafundisho ya Biblia unaweza kuwasaidia wachungaji kufanya vizuri zaidi; hata
hivyo, haiwezi ikawa badala ya wito wa Ki –Mungu. Kwa kuwa, wachungaji wanaitwa na
hawatengenezwi / hawaundwi. Kujiunga kwenye Chuo cha Biblia, kupokea sitashahada au
shahada baada ya miaka mitatu hadi minne ya kujifunza Biblia haimgeuzi mwanafunzi moja kwa
38
moja kuwa mchungaji au mtumishi yeyote wa Injili. Maandiko yanaonyesha wazi kuwa uchungaji
ni kipawa kutoka kwa Mungu kwa Kanisa lake (Waefeso 4:11). Hawawezi kutengenezwa katika
viwanda na vilevile kuwa fundisha elimu ya Kibiblia ya kutunga hotuba (Homiletics) na elimu ya
usemaji (rhetoric). Huduma hii msingi wake upo katika wito wa Ki –Mungu, na si katika wingi
wa mafundisho ambayo mtu anayapokea. Na tukumbuke kwamba Mungu kamwe haiti mtu
ambaye hajampa vipawa vya lazima, kwa mfano huduma.
Na ieleweke kwamba kusudi la kutoa masomo ya Shule ya Biblia au Chuo ni kuwaandaa wale
walioitwa. Watu binafsi ambao wangependa kuendelea na sitashahada au shahada wangefanya
vizuri kama wangelichagua sehemu (kozi) nyingine ya kusomea. Wale wanaohisi kuwa wanahitaji
mafundisho ya utumishi hata hivyo wanahitaji kutiwa moyo kuhudhuria Shule ambazo zina
watumishi / wafanyakazi si tu wakufunzi (scholar), lakini wawe wanatheolojia na watumishi
wenye msimamo wa utendaji kazi vile vile. Mafunzo ya Biblia yanapaswa kuwaandaa viongozi na
watenda kazi kushughulikia maswala ya huduma. Kutoa ushauri kwa mtu anayetaka kujinyonga /
kujiua, kutatua matatizo ya ndoa, kuwatia moyo na kuwashauri wasio na kazi, kuwafariji wasio na
matumaini.n.k. hata hivyo itakuwa muhimu kuonyesha umahiri au ujuzi aliojifunza kutatua /
kufafanua fasihi ya maandiko . Maksi zilizopatikana kwenye majaribio pamoja na karatasi za
uchunguzi (term paper research) havitakuwa na maana anapokabiliwa na matatizo ya kutisha ya
mwanadamu. Vyuo vingi, seminari na Shule za Biblia vimetambua haya na vimefanyia
marekebisho mitaala yao na kufanya mabadiliko katika wakufunzi kwa kuwaongezea walimu
wenye ujuzi wa elimu ya Kichungaji.
Tumeelezea baadhi ya dhana inayohitilafiana, na kuonyesha jinsi Mungu alivyokusudia kufanya
kazi katika huduma hii. Ijapokuwa desturi za dini na mila zimeharibu zaidi hii huduma kuliko kitu
kingine chochote, kazi ya kurudi katika mifano ya Kibiblia siyo rahisi. Hata hivyo, tunapaswa
tuwe radhi si tu kuziweka pembeni desturi bali pia tuachane na kiburi nakutafuta madaraka na
mamlaka. Kulingana na maandiko uongozi ulimaanisha kushirikishana na kamwe haukukusudiwa
kuwa jambo la mtu mmoja.
MAJADILIANO:
Sifa za Kibiblia kwa uongozi si kila mtu anaweza kuwa mwangalizi, au kiongozi wa jambo fulani.
Wale wanaothibitisha wito wao wa Ki-Mungu, lazima watimize sifa fulani kama ilivyoonyeshwa
katika 1Timotheo 3:1 –8, na Tito 1:5-9. Wakati sifa hizi zimeunganika na huduma ya Wazee /
Waangalizi / Maaskofu, hatutakosea kusadiki kwamba tabia na maadili yanayohitajika yanapaswa
kuwa ushahidi si tu kwa wazee / wachungaji / wangalizi bali pia vinapaswa kuonyesha maisha na
huduma ya wainjilisti, waalimu, mitume na manabii, na wale ambao wana huduma za juu za
uongozi, pamoja na mashemasi (Tito). Hivyo ni muhimu kwetu kuchunguza masharti haya ya
kimaandiko, hasa kushindwa kukubaliana na viwango hivi ambavyo vimetolewa na Mungu
vimesababisha matatizo mengi.
1Timotheo 3:1 –7:
Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. 2 Basi imempasa askofu awe
mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji,
39
ajuaye kufundisha; 3 si mtu wa kuzoelea ulevi; si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana,
wala asiwe mwenye kupenda fedha, 4 mwenye kuisimamia nyumba yake vyema, ajuaye kutiisha watoto
katika ustahilivu; (5 yaani, mtu asiyejua kusimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la
Mungu?) 6 wala asiwe mtu aliyeongoka karibuni, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.
7 Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa
ibilisi.
Vinafurahisha vyote na ni muhimu kwamba Paulo hakueleza sana kazi za Wazee bali aliangalia
zaidi katika tabia zao. Hivyo “kuwa” ni muhimu zaidi kuliko “kutenda” kwa kufaa kwa ajili ya
uongozi. Mtu mmoja alieleza vizuri zaidi kwamba sifa kwa ajili ya uongozi si za majadiliano, kwa
sababu viongozi walivyo ndivyo watu watakavyo kuwa.26
Asiyelaumika.
Sifa za kiongozi zinapaswa zisiwe na lawama, asiyelaumiwa au asiye na shaka / wakuaminika
(Kiyunani: anepilempton). Neno la kiyunani linaonyesha kama “lazima” inakazia umuhimu wa
ulazima.27 Hii haimaanishi kwamba amefikia kiwango cha kuwa mkamilifu, bali maisha anayoishi
yanapaswa kuwa manyoofu. Ninakumbuka tukio moja ambalo Kiongozi wa Kanisa alishutumiwa
kuwa na ndoa ya nje na mmoja wa washirika wake. Alipokabiliwa na hili shitaka jibu lake lilikuwa,
“sina hatia mpaka ithibitishwe kuwa nimefanya”. Kama angekuwa hana lawama mwitikio wake
ungekuwa wa tofauti. Angekuwa ameomba uchunguzi wa haraka ufanyike ili kuliweka jambo hili
wazi.
John Mac Arthur hueleza kwamba lawama haimaanishi ukamilifu kama ni hivyo wote tusingefaa.
Inamaanisha kwamba kusiwepo na doa/kasoro kubwa katika maisha yake kwamba watu wengine
watakuwa wanaionyesha. Anapaswa awe kielelezo cha utauwa, ili watu wake waweze kufuata
mfano wake, akiwa na uhakika kwamba hatawaongoza katika dhambi. 28 Neno la Kiyunani hasa
linamaanisha: kutoyumbishwa, ambalo huonyesha kwamba shutuma / mashitaka hayatadumu
kwa mtu asiye na lawama.
Arrington anaelezea:
Kutolaumiwa mtumishi hapaswi kuwa na kitu chochote na ambacho kitatumika kwa halali
kukumbushia na kuiwekea maswali tabia yake. Mashitaka yanayofanywa dhidi yake, uchunguzi
hautathibitisha mashitaka dhidi yake. Kwa hiyo atakuwa ni mtu asiye laumika.29
Kiongozi wa kiroho atakuwa chini ya mashambulizi makubwa ya shetani zaidi ya waamini.
Majaribu ambayo anayapata ni makali na si yale tu ambayo shetaani anayakusudia kwake, bali ni
huduma yake anayoitafuta kuidhoofisha na kuiharibu. Mara kiongozi anapoanguka si tu anajiletea
aibu yeye mwenyewe, familia na huduma yake bali anamwaibisha Kristo.
Kwa hiyo uhitaji kwa Mungu kutokuwa na lawama hakupaswi kuchukuliwa kwa mzaha. Kutimiza
sharti hili la kiroho kiongozi lazima alinde mawazo, maneno, matendo yake na kazi zake kwa
26 John F. MacArthur, The Master’s Plan for the Church(Chicago: Moody Press, 1991), pp. 215-216.
27 Bauer, Walter, Gingrich, F. Wilbur, and Danker, Frederick W., A Greek-English Lexicon of the New
Testament and Other Early Christian Literature (Chicago: University of Chicago Press, 1979).
28 John F. Mac Arthur, p. 88.
29 French L. Arrington, Maintaining the Foundations ( Grand Rapids: Baker Book House, 1988), p. 78.
40
uangalifu. Mahitaji yafuatayo kwa ajili ya viongozi ni matokeo ya asili kwa yeye kutokulaumiwa.
Baadhi ya hizi tabia ni madhihirisho ya nje ya kazi ya Roho Mtakatifu katika utu wake wa ndani.
Mume wa mke mmoja.
Maana halisi ya uhitaji huu kwa wazee/waangalizi umejadiliwa na wengi. Usemi huu unaweza
kueleweka kwa njia moja au zaidi. Tunahitaji kuangalia kwa ufupi tafsiri nne za kawaida.
1) Wengine hutumia maandiko kutetea hoja kwamba kiongozi wa kikristo anapaswa kuwa
ameoa, ambavyo ni kinyume na msimamo wa Kanisa la Rumi ambao unatetea useja wa
makuhani. Ikiwa nadharia hii ingekuwa ni kweli; hakuna mtu asiyeowa ambaye angefaa kwa
ajili ya uongozi katika kanisa. Katika jambo hili Paulo angejiondoa mwenyewe katika
uongozi; kama jinsi yeye mwenyewe hakuwa ameoa.
2) Nadharia ya pili inathibitisha kuwa kiongozi wa kikristo hapaswi kuwa na uhusiano na
wanawake wengine nje ya ndoa. Maadili mazuri na uaminifu katika ndoa, na hapaswi kumpa
talaka mke wake, au kutengana naye. Uaminifu wake unapaswa kuwa usio wa kubadilika,
kama vile maandiko yanavyosema.
3) Wengine wanatetea kwamba andiko linaonyesha kwamba kiongozi anayefiwa na mke wake
hapaswi kuoa tena. Hata hivyo, hakuna katika Agano jipya na Agano la kale linalothibitisha
nadharia hii. Kwa upande mwingine linashauri vijana wajane waolewe tena (1Timotheo
5:14). Katika Warumi Paulo anatumia kuoa tena baada ya kifo kama mfano kwa ajili ya kweli
ya kiroho (Warumi 7:3).
4) Hatimaye nadharia ya mwisho, ambayo ni maarufu sana katika Afrika na nchi ambazo
sehemu kubwa ya jamii zinakubaliana kuwa na mitaara (polygamy), hutetea kwamba hakuna
mtu anayepaswa kuwepo katika nafasi ya uongozi ambaye ameoa zaidi ya mke mmoja.
Hivyo ikiwa atajaribu kulirekebisha tatizo kwa kuwafukuza wengine au kwa kuwatunza
vingenevyo, mtu kama huyo anafaa kwa uongozi. Hivyo kanisa linapaswa kuwa makini na
kulinda sifa zake na linapaswa kuwa mfano unaofaa katika jamii.
Miongoni mwa mitazamo hii minne, mtazamo wa pili na wa nne ndio hasa inaonekana kuwa
tafsiri sahihi ya uhitaji kwa ajili ya uongozi. Sio kwamba tu zinaonekana kufaa bali pia zinafaa sana
katika hali ya kanisa la leo. Ikiwa ameoa, kiongozi anapaswa kuwa mume wa mke mmoja. Ikiwa
kama hajaoa moyo wake haupaswi kuwa na tamaa ya wanawake, kwa mfano hatakiwi kuwa
“mwanamume anayependa wanawake”. Usafi wa ngono (Sexual purity) ni jambo la muhimu hapa
na si kwamba tu kiongozi ameoa au hajaoa.
Mwenye kiasi na busara.
Tafsiri ya kawaida ya neno la Kiyunani (nephalios) humaanisha kuwa na kiasi. Humaanisha
kutojihusisha kabisa na kileo, au angalau kutoka katika matumizi yake yasiyo na kiasi.30 Neno la
kiyunani linaonyesha mtu fulani anayekunywa mvinyo nyingi na inaonyesha kwamba mtu huyo
ana tatizo la ulevi. Katika mtazamo wa upana zaidi neno linaonyesha kutafuta starehe.31 Kwa
hiyo, linaonyesha kwamba kiongozi anapaswa kuwa na kiasi katika kuonekana kwake na namna ya
maisha. Anapaswa kuwa mwenye msimamo mzuri na ajizuie kwenye mambo yanayopindukia,
katika maisha yote. Hata hivyo kujizua na ulevi halipaswi kuwa jambo dogo / lisilo na umuhimu,
30 Joseph H. Thayer, Greek-English Lexicon of the New Testament (Grand Rapids: Baker Book House,
1977), p. 425
31 John F. MacArthur, The Master’s Plan for the Churchp. 89.
41
hasa katika ulimwengu ambao umeambukizwa na ulevi ambao huharibu maisha, ndoa, familia na
maisha ya watu wengi.
Mtu wa utaratibu.
Neno la kiyunani (sophron) limetafsiriwa kama mwenye busara, linawakilisha wazo kwamba
kiongozi anapaswa kuwa mwenye akili timamu, na kwamba lazima awe mwenye busara, akili na
awezaye kujitawala. Anapaswa kuonekana mwenye afya na siyo kuwa mtu wa mambo ya kiroho
kupita kiasi katika maisha yake. Kukabiliana kwake na matatizo hakupaswi kuwa kwa haraka bali
kuwe katika hali ya usawa / msimamo. Wehu na washikiliaji sana wa sheria kwa hakika hawana
sifa hii. “wakaidi” ndani ya kanisa wanapaswa kujifunza kukabiliana na matatizo yaliyotolewa bila
upendeleo na kwa utulivu. Kuwa na busara inaonyesha zaidi kuwa makini juu ya mambo ya
kiroho na mambo ya Mungu. Ucheshi ni mzuri, hata hivyo maisha hayapaswi yaonekane na
kuchukuliwa kama utani mkubwa/ mizaha.
Mwenye sifa njema.
Heshima kwa viongozi wa kikristo si ya kulazimisha bali inapaswa kuja yenyewe. Bali wazee
wanategemewa kuishi maisha ya staha na heshima (kosmios –maisha). Kwa matokeo haya
watastahiliwa na kuheshimiwa na washirika wao na jamii yote kwa ujumla. Namna ya maisha
yenye sifa njema ni matokeo ya moja kwa moja ya kazi ya Ki –Mungu ndani ya kiongozi, itakuwa
dhahiri kwa watu na nyumbani. Wale mabwana wanaojifanya wema katika watu (nice guy) bali ni
bahili na hawazithamini familia zao nyumbani, hawafai.
Kosmios linatokana na neno la asili kosmos.32 Ambalo moja ya maana zake inaonyesha mpango wa
ulinganifu au utaratibu. Hivyo tabia nzuri inaonyesha mtazamo wa maisha ambao kwenye mfumo
na mpangilio. Mtu aliye na maadili haya atatimiza wajibu wake mwingi kwa bidii na kwa
kuwajibika. Kama mmojawapo alionyesha kuwa nidhamu ya mawazo hutoa au huzaa matendo
yenye nidhamu –tabia njema. Utaratibu mzuri wa maisha ni muhimu kwa kiongozi yeyote.
Hata hivyo msemo wa ucheshi unaeleza kuwa mtu mwenye kipaji yuko katika kuzuia machafuko,
tunapaswa kukumbuka kuwa viongozi wenye namna ya maisha ya machafuko wanazuiwa katika
utendaji wao. Kutatanika, kuchelewa, na kutokuwa na mipangilio itakuwa kizuizi katika kutimiza
malengo yoyote yaliyowekwa.
Mkaribishaji.
Ukarimu siyo tu unahitajika kwa waangalizi bali pia unafikiriwa kuwa ni moja ya huduma za
Agano jipya ambazo zilifanywa na washirika wa mwili wa Kristo. Baadhi wanadai kwamba
ukarimu ulikuwa muhimu katika ulimwengu wa karne ya kwanza ambapo hapa kuwepo na
nyumba za wageni au mahoteli. Hata hivyo hii imebadilika siyo muhimu tena kuwakaribisha
wahubiri wanaosafiri.33 Hii inaweza ikawa mtazamo wa baadhi ya wale wanaoichambua Biblia na
32 Enhanced Strong’s Lexicon, (Oak Harbor, WA: Logos Research Systems, Inc., 1995). Neno Kosmos:
Utaratibu wa kufaa unaopatana au katiba/ mfumo wa nchi, mpango/ utaratibu, serikali.
33 Arrington, Maintaining the Foundations, p. 80.
42
kuiweka wazi ambao huyaangalia maandiko katika mtazamo halisi wa kimagharibi au wa
Kiamerika. Baadaye katika somo hili tutakapoangalia katika huduma ya ukaribishaji
tutalishughulikia hili jambo kwa ufasaha.
Neno la kiyunani (philoxenos) linatokana na maneno phileo (kupenda, kuonyesha mapendo) na Xenos
(Mgeni). Kwa hiyo tafsiri ya kawaida huonyesha kupenda wageni ambalo huonyesha kwamba sifa hii
haimanishi tu kwamba kuwa mkarimu na upendo kwa marafiki na kwa washirika wa kanisa, bali
pia kwa wageni. Kufanya hivyo tunahitaji hekima na upendo wa Ki-Mungu kujaza fahamu na
mioyo yetu, vinginevyo tutafanywa kuwa faida ya wengine na kwa hiyo tutaumizwa.
Ajuaye kufundisha.
Ijapokuwa moja ya mahitaji kwa ajili ya Wazee / waangalizi ni “kuweza kufundisha” (Kiyunani
didaktikon, tafsiri ya kawaida ni “anafaa kufundisha”) si kila mmoja aliyekuwa katika huduma hii
katika kanisa la kwanza alitimiza hitaji hili. Kulingana 1Timotheo 5:17 wengine walitawala tu
wakati wengine pia walihubiri na kufundisha. Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima
maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. Tafsiri ya kawaida ya kujitaabisha katika
kuhutubu na kufundisha (kiyunani; logo kai didaskalia) haswa inapaswa iwe, kujitaabisha katika
usemi (kuhubiri) na kufundisha. Kwa hiyo, hitaji kwa wazee katika 1Timotheo 3:3 kuweza
kufundisha siyo lazima iwe kuhubiri injili hadharani bali kuelekeza ambacho kinaonekana kwa
mtu. Inaweza ikamaanisha kuwa wazee waweze kueleza na kujibu maswali kwa ufasaha
yanayohusu maandiko, injili na maisha katika Kristo kwa yeyote yule anayetafuta ufafanuzi wa
haya.
Kuweza au kufaa kufundisha inaonyesha zaidi kwamba maisha ya kiongozi yaende sambamba na
mafundisho yake. Msemo, “fanya nisemacho, lakini usifanye kile ninachofanya, “ haikubaliki si
kwa viongozi wa kanisa tu bali kwa waamini wote. Fursa na wajibu wa kuelekeza wengine
unapaswa kufuatwa.
Si mlevi.
Mzee au kiongozi yeyote wa Kikristo hapaswi kujihusisha kwenye ushawishi wa vileo au aina
yoyote ya pombe, kwa vile hii huongoza kwenye upotofu zaidi. Badala yake anapaswa kujawa na
Roho (Waefeso 5:18). Kufikilia tatizo la sasa la ulevi si vyema kwa ajili ya viongozi tu bali ni kwa
ajili ya kila mshirika kujitenga na ulevi, ili kuwa msaada kwa wale wanaohitaji ukombozi kutoka
kwenye mateso ya mwanadamu. Si mlevi “(Kiyunani: paroinos, kwa kawaida kulewa, kutawaliwa na
kileo34) ni usihi wenye nguvu zaidi kufikia katika hali ya umakini kuliko tunavyoona kwenye neno
“kiasi”.
Si mgomvi
Neno la Kiyunani plektes halimaanishi tu “mpiganaji” bali pia linamaanisha muonevu au mgomvi.
Kwa hiyo, kiongozi hapaswi kupigana tu kimwili lakini pia kwa maneno; kwa mfano, kwa maneno
34 Bauer, Walter, Gingrich, F. Wilbur, and Danker, Frederick W., A Greek-English Lexicon of the New
Testament and Other Early Christian Literature (Chicago: University of Chicago Press, 1979).
43
makali, kejeli au kwa mafumbo. Kamwe hapaswi kuwaumiza wengine au asipendelee fujo. Zaidi,
hapaswi kupenda mabishano, asiyependelea kutokubaliana, au kukosoa / kubishana kwenye
mambo yenye utata. Wala tabia yake haipaswi kuwa ya kuogopesha. Watu wanapaswa kujisikia
huru kuwaamini viongozi wacha Mungu. Anapaswa kuweza kuyakabili mambo katika akili ya
utulivu na katika roho ya unyenyekevu.
Asiwe mtu wa kupenda mapato ya aibu.
Neno la (Kiyunani aphilarguros) halielezi tu ulafi wa kuwa na vitu vingi lakini pia inaonyesha
kubania / kutoa kidogo na kujirundikia utajiri. Inamaanisha kuwa na tamaa ya kuwa navyo vingi
zaidi au tamaa ya kutoridhika kwa ajili ya utajiri au kujipatia. Nia ya kiongozi wa kikrsto kwa ajili
ya huduma haipaswi kutabiriwa ikiwa atajiunga kwenye vyeo vya huduma ili awe tajiri. Ikiwa
atajitahidi kuishi maisha ya kuwa navyo vingi na utajiri, huduma yake itashindwa, kwa sababu
moyo wake utakuwa mahali hazina yake ilipo. Hii haimaanishi kuishi katika kiwango cha maisha
ya njaa / shida. Maandiko pia yanatufundisha kuwa mtenda kazi anastahili ujira wake, na wale
ambao wanaohubiri injili wanapaswa kuishi kwa ajili ya injili. Wakati hii inaonyesha stala,
haimaanishi kuwa fukara / maskini.
Yesu alionyesha wale wanaozunguka zunguka na kula katika nyumba za wajane. Tahadhari hii
bado inafanya kazi leo. Mtumishi wa injili anapaswa kupinga jaribu la kuwa rafiki na wajane
wenye uwezo kwa ajili ya kujipatia fedha. Watu wengi walio wazee, wamevutwa sana kwa upendo
na maneno mazuri, wamevutiwa katika kumtolea Bwana, ambavyo kwa namna nyingine
inatafsiriwa kutunisha mifuko ya wahubiri. Kupenda mapato ya aibu kutobuni njia nyingi za kuwa
tajiri ambako hili tendo ni mfano mmoja tu.
John Mac Arthur anaonya kutoweka kibandiko cha bei (price tag) katika huduma zetu, kama
matarajio ya fedha kwa ajili ya huduma inaweza ikamletea ushawishi mbaya na hata kupotosha
huduma ya mtu. Zawadi ya fedha inaweza ikapokelewa kama inatoka kwa Bwana lakini haipaswi
kutafutwa.35 Tahadhari yake imetolewa wakati watumishi wengine bado wanategemea “matoleo
mazuri” ambayo hasa hupelekea kwenye “malipo” ya kima kikubwa kwa kila anapojihusisha
kuhubiri. Kama matarajio yao hayakufikiwa, hukataa mwaliko kwa nia njema. Kwao huduma ni
mtaji / kitu cha kujipatia fedha.
Mvumilivu
Neno la kiyunani (epieikes) linafafanuliwa kama kujizoesha katika uvumilivu uthabiti wa mtu
ambaye yupo upande wa maskini, au kuwa mvumilivu miongoni mwa wacha Mungu wanaobezwa
na kudharauliwa. Zaidi inaonyesha kuwa na huruma, kustahimili, mwenye rehema au mpole. Hii
tabia haipaswi kuonekana tu kwenye nafasi yake yenye mamlaka, bali pia katika maisha yake
binafsi.36 Maelezo yanaweza kuonekana yakitofautiana katika mtazamo wa kwanza. Hata hivyo, ni
maelezo yanayokubalika ya tabia inayobainisha ambayo inahitajika sana katika jamii ambapo
“kiwiko cha mkono” (elbow)” imekuwa kama ishara ya kufanikisha matakwa ya mtu. Saburi mara
35 John MacArthur, The Master’s Plan for the Church, p. 226.
36 Exegetical Dictionary of the New Testament, 3 Vol. (GrandRapids: Eerdmans Publishing Company,
1990), Vol. 2, p. 26.
44
zote imefikiriwa kama udhaifu. Mtu mwenye subira anaonekana kama mtu wa kusukumwa
sukumwa. Lakini namna nyingine uvumilivu unahitaji nguvu ya ndani na humpa kiongozi uwezo
kushikilia kwa udhabiti haki na uthibitisho wake (convictions).
Si mpiganaji
Kiongozi wa kikristo hapaswi kuwa “mpiganaji” (Kiyunani: amachos). Neno hili linaonyesha mtu
ambaye hakuna mtu ambaye anataka kupigana naye, hashindwi, asiyeshindwa na ambaye hapendi
kupigana, mwenye amani.37 Tunaona kuwa kiongozi si mgomvi au mbishi wala kujifanya kama
hashindwi au kama mtu fulani ambaye hawezi kuhimili.38 Anapaswa awe mtulivu na mwenye
kujilinda badala ya kuwa mgomvi na asiyetaka kupatana. Kwa maneno rahisi, ni mkunjufu.
Viongozi wa kikristo ambao wanajaribu kutawala kwa kuamrisha hawampendezi ‘Mungu’.
Ajuaye kuitunza nyumba yake vyema, kuwatiisha watoto wake katika unyenyekevu wote.
Maandiko yanaeleza kuwa wale wasioweza kuzitunza nyumba zao vizuri watashindwa kulitunza
vizuri Kanisa la Mungu. Kwa hiyo, kiongozi anashauriwa “kutawala” nyumba yake vyema. Neno
hli (Kiyunani: proistemi) linaonyesha kuwa anapaswa kutunza vyema mambo ya nyumbani
kwake. Sehemu ya utawala huu mzuri unajumuisha uhusiano wa kiongozi kwa watoto wake na
tabia zao.
Neno la Mungu halikubaliani na mwelekeo wa sasa ambao unawaruhusu watoto kufanya
vyovyote watakavyo. Kinyume chake linawategemea watoto kuwa wanyenyekevu kwa wazazi
wao. Akiwatiisha watoto wake katika unyenyekevu (Kiyunani: hupotage –ambalo kwa kawaida
lina maana kuonyesha heshima na utii) inapaswa kufanyika kwa “unyenyekevu wote” (Kiyunani:
semnotes). Hivyo, haiji kwa kutumia vipimo vigumu vya nidhamu ambavyo hukiuka heshima ya
mtoto. Neno la Kiyunani linaonyesha kwamba nidhamu katika nyumba iwe thabiti bali zisiwe
ngumu. Kwa maneno mengine utiifu haupaswi kuchanganywa na unyanyasaji. “kwa unyenyekevu
wote “ inaeleza zaidi “kuonyesha uaminifu” ambao huonyesha kwamba tabia ya kiongozi
kanisani, pamoja na kutangaza injili inapaswa ikubaliane na tabia / mwenendo wake nyumbani.
Unafiki / uzandiki kwa kiongozi, ambapo mahubiri na matendo hayapatani kwanza yataonekana
na washirika wa nyumbani mwake mwenyewe. Hakuna kitakachodhoofisha mamlaka yake
nyumbani, kuliko ile isiyopatana na tabia yake. Hii haimaanishi kwamba hapaswi kuwa na kasoro
kabisa, bali mnyoofu na mwaminifu. Ataungwa mkono, upendo na heshima katika familia yake
ikiwa atakuwa radhi kukiri mapungufu yake mbele za Mungu na kwa wapendwa wake.
Kabla hatujaenda katika jambo linalofuata tunapaswa kuelewa hitaji, “kuwatiisha watoto. Kuwa
wale ambao wanaeleza kwa usahihi kwamba hatuwezi kutarajia utakatifu kamili kwa watoto,
wakati wengine wanadiriki kumuondolea sifa za uongozi mtu yeyote ambaye watoto wake
hawamfuati Kristo. Maisha ya Samweli yanaweza kutusaidia kuelewa juu ya habari hii. Mwamuzi
huyu na Nabii wa Israeli alikuwa mmoja kati ya wachache ambaye maandiko hayaonyeshi tabia
37 Liddell, H. G., and Scott, Abridged Greek-English Lexicon (Oxford: Oxford University Press) 1992.
38 Joseph H. Thayer, Greek-English Lexicon of the New Testament (Grand Rapids: Baker Book House,
1977), p. 31.
45
yoyote mbaya, au dhambi. Hata hivyo wakati amekuwa mzee Israeli walikataa kutawaliwa na
watoto wake, kwa vile hawakuwa wanafuata njia zake. Ikiwa watoto wa huyu mtu mtakatifu
walishindwa kufuata hatua za baba yao, dai gani linaweza kuwekewa viongozi wa Agano Jipya
kuhusu vijana na mabinti zao?
Wakati utauwa / utakatifu katika wazazi wa kikristo ni wa muhimu sana, ni lazima tutambue
kwamba watoto, kadri wanavyokuwa wanapaswa kujiamulia wao wenyewe ikiwa watamfuata
Kristo. Jinsi baba na mama walivyo wa Kristo, itakuwa ni rahisi kwao (watoto) kufanya uamuzi
sahihi. Lakini kama tulivyoona katika swala la Samweli hii haituhakikishii kuwa wanafanya
uchaguzi sahihi. Wakati wakiwa wadogo na katika miaka ya kukuwa kwao kunapaswa kuwa na
ushahidi wa kuwa “watii” kwa mfano, heshima, kutawaliwa na nidhamu. Ikiwa wataiacha njia
waliyofundishwa wakati watakapokuwa watu wazima nafasi ya kiongozi haihitaji kuharibiwa na
matendo yao.
Jambo jingine linalopaswa kuelezewa ni hali ile ambayo mtu ameokoka wakati mke wake na
watoto bado wanaendelea kuishi maisha ya dhambi. Katika jambo kama hilo, baada ya kuonyesha
kukua kiroho, anaweza akawa mzee au kiongozi kanisani? Sifa zilizotolewa katika 1Timotheo,
zinaonyesha wazi na kuthibitisha kwamba hasitahili kuongoza. Hawezi kuwa mzee / kiongozi,
ambayo haimaanishi kwamba Mungu hawezi kuwa na mipango mingine kwa ajili yake. Wakati
nikifanya kazi pamoja na mtu wa Mungu kwa kipindi fulani, ambaye familia yake haikuonyesha
dalili zozote za wokovu (ndivyo niivyoona, hata hivyo mimi siyo mwamuzi wa mwisho wa jambo
hili), niliona jinsi mke wake na baadhi ya watoto wake hawakusaidia kustahili kwake na sifa zake
na wale walio nje ya kanisa.
Asiye aliyeongoka karibuni.
Maana ya kawaida ni “haikupandwa hivi karibuni” (Kiyunani: neophutes). Kama vile mumea
mchanga unavyochukua muda kutoa mizizi na kukua kabla ya tunda halijatarajiwa, mwamini
mpya anapaswa kupewa muda wa kufundishwa na kuimarishwa katika Imani. Mtu yeyote hapaswi
kufikiriwa katika uongozi ndani ya kanisa ambaye hajaonyesha kukua katika mambo ya Mungu na
katika maisha yake binafsi. Vinginevyo anaweza “kuinuliwa” (Kiyunani: tuphoo –kwa kawaida
kupumua moshi, au kutoona kwa ajili ya moshi) kwa majivuno. Kupandishwa cheo kwa haraka
kutaleta majivuno ya kiroho. Kiongozi anapaswa kujithibitisha mwenyewe. Hapaswi kujiona yeye
ni wa maana. La sivyo maangamizi ya kiroho yatatokea.
Nilikuwa na fursa ya kusikitisha ya kujua ukweli huu mimi binafsi. Baada ya kuokoka kutoka
katika madawa ya kulevya, ulevi na uzinzi ghafla nikajiona mwenye shani/heshima, kadri
nilivyoombwa kutoa ushuhuda wangu katika kila kanisa nililokwenda. Badala ya kukua pole pole
katika maarifa ya Kristo nilipata sifa nisizositahili na kujiona mimi ni bora.
Hata hivyo sikuwa kiongozi, katika hali hii isiyofaa ilinifanya kuwa na kiburi cha kiroho na
nilikaribia kupoteza wokovu wangu. Ilikuwa ni maombi tu uvumilivu, upendo na ushauri wa
waamini waliokomaa ambao ulinirudisha katika njia, hivyo walizuia maangamizi ya kiroho katika
maisha yangu.
46
Wakati mshirika mchanga anaweza kujivuna kirahisi ikiwa atawekwa kwenye uongozi, kiburi kile
kile ambacho kilimsababisha shetani kufukuzwa kutoka mbinguni, kinaweza kuingia moyoni mwa
mtumishi na kiongozi yeyote haijalishi ni muda gani amekuwa akimfuata bwana. Hatupaswi
kushawishika kwamba sisi ni wa muhimu sana au tumefanikiwa, bali tunapaswa kukumbuka
daima bila yeye hatufai. Kiongozi hatapoteza wokovu wake kutokana na kiburi, bali anaweza
kupoteza nafasi muhimu sana aliyo nayo.
Kushuhudiwa mema na walio nje
Ushuhuda (Kiyunani; martyria39) mzuri (Kiyunani kalos) miongoni mwa wasioamini ni sifa
muhimu kwa yeyote aliyepo katika nafasi ya uongozi. Hata hivyo wanafunzi wa kweli; na hasa
viongozi mara zote watakuwa vikwazo kama vile Yesu alivyokuwa amesema(1Petro 2:8), hata
hivyo wanapaswa kutembea kwa uangalifu katika jamii ya wasioamini. Wale walio nje ya Kanisa
wakati mwingine wana utambuzi wa mambo ambayo yanafaa au yasiyofaa kwa wakristo kutenda.
Wakati viongozi wanashindwa kuishi kulingana na sifa hizi hawatapoteza tu utendaji kazi wao
katika jitihada za kuwapata waliopotea, lakini sifa ya kanisa itatiwa doa. Hivyo viongozi
wanapaswa kuhakikisha kwamba maisha yao binafsi, maisha ya familia zao, na maisha yao kwa
watu wengine, pamoja na biashara na mambo yao ya fedha / kulipia madeni kwa wakati na
kutojihusisha kwenye mipango isiyo ya uaminifu) haitatoa sababu yoyote ionekane kuwa una kosa
kwa walio nje.
Kuwa na matokeo kama yale ya Kanisa la kwanza, kutunza roho ya uamsho na kiwango cha
utakatifu ambacho ni cha thamani katika moyo wa Mungu. Viongozi wa leo hawapaswi kukwepa
majukumu ambayo yamewekwa tayari katika 1Timotheo 3 na Tito 1 mfumo unaweza kubadilika,
lakini kiini cha sifa hizi kitabakia vile vile kwa muda wote kwa kila kiongozi aliyeitwa na Mungu.
MWALIMU
Huduma ya mwalimu imepewa umhimu katika kanisa la Agano jipya. Imeorodheshwa katika
maeneo yote matatu ambapo vipawa vya huduma vimetajwa (Warumi 12:6-8; 1Wakorintho 12:28
na Waefeso 4:11). Kifungu katika Waefeso kinaonekana kuonyesha kwamba huduma hii
imeunganishwa na ile ya Mchungaji. Baadhi ya walimu wa Biblia wamebishana kuwa huduma zote
mbili zimeungana kwa mtu mmoja. Kwa sababu hii baadhi wameiorodhesha kama moja,
Mchungaji / mwalimu. Hii tunapaswa kuipinga. Wakati uwezo wa kufundisha ni sehemu ya
huduma ya kichungaji, itakuwa vibaya kukisia kwamba wachungaji wote ni waalimu, na waalimu
wote ni Wachungaji. Maandiko yanaonyesha kwamba kanisa la kwanza lilitambua huduma ya
mwalimu kama huduma moja (Matendo 18:27; 1Wakoritho 3:6; Tito 3:13 na Matendo 13:1 –
waalimu wameorodheshwa pamoja na mitume).
39Kittel, Gerhard, and Friedrich, Gerhard, Editors, The Theological Dictionary of the New Testament,
Abridged in One Volume, (Grand Rapids, Michigan: William B. Eerdmans Publishing Company) 1985. Katika
Kiyunani sanifu neno kaloCEs lilielezea uzuri kama mpangilio mzuri uliokamilika, kuwa na usawa, kuwa na
uwiano ulio wa haki. Kile ambacho ni kizuri na chenye mpangilio mzuri mbele za Mungu ni chema pia. Katiak
uchangaji kaloCEs lina sehemu kubwa ya ufahamu wa filosafia ya "haki/usawa", kwa mpangilio/ utaratibu au
"ubora" uliodhihirika kwenye mambo haya kama tabia ya kweli, mafundisho sahihi, na mtazamo sahihi katika
ulimwengu. Hata hivyo yote haya yana mwelekeo wa kimazingira katika Kristo na injili.
47
Wakati mchungaji anahuduma ya “hapo hapo / kutoondoka” mwalimu anaweza kufanyia kazi
wito wake katika kanisa la mahali pamoja au huduma ya kwenda kila mahali katika makanisa, hasa
wakati huduma yake ya kufundisha imepata kibali, kama tunavyoona katika mfano wa Apollo
(Matendo 18:27; 1Wakoritho 16:12; Tito 3:13). Kwa leo huduma hii pia inapatikana katika shule
za biblia, vyuo au vyuo vikuu vya Kikristo.
1. Chanzo na sifa za huduma.
Hakuna huduma ya Uongozi ambayo imeunganika na ile ya uwezo wa asili kama ile ya huduma ya
kufundisha. Bado maandiko yanaonyesha kwa uwazi kwamba ni ya Ki –Mungu katika asili kama
vile huduma zingine (warumi 12:6 0 7 ; 1Wakorintho 12:28; Waefeso 4:11). Kuna mazoea ya
kulinganisha huduma ya Kibiblia ya kufundisha na kazi ya kufundisha. Hata hivyo mtu hawezi
kuwa mwalimu kanisani eti kwa sababu amekwenda mafunzo ya kawaida ya Kidunia, bali kwa
sababu alipokea huduma yake kutoka kwa Mungu.
Mafundisho maalumu katika ualimu (pedagogy) yanaweza yakaongeza utendaji wake lakini
hayawezi kufidia wito wa Mungu. Zaidi ya ufahamu na mtazamo wa kitaaluma unahitajika
kufanya kazi kwa usahihi kama kiongozi alivyoitwa kuwaandaa watakatifu (Waefeso 4:11). Ikiwa
mwalimu atashindwa kuweka vipaumbele vya taaluma yake sahihi vyaweza hata kuwa kikwazo
katika utendaji wake. Kama George Canty anavyoeleza kwa usahihi, “hatupaswi kusahau kwamba
kusudi la Kristo ni kujenga na siyo elimu.40
Mafundisho ya kikristo mara zote yamefanywa kuwa makavu kwa sababu ya wale ambao, kwa
kawaida wametumia uwezo wao wa asili wa kufundisha ndani ya Kanisa. Lakini, hakuna huduma
inayotendeka katika nguvu na upako wa Roho Mtakatifu inaweza kuitwa huduma kavu. Vijito /
chemi chemi za maji yaliyo hai zitabubujika kutoka kwa mwalimu wa kweli (1Wakorintho 3:6).
Zana potofu nyingine ambayo inapaswa kusahihishwa ni wazo kwamba huduma ya kufundisha
inapaswa kuchukuliwa katika msisimko mdogo au kutokuwa na msisimko / mguso. Hata hivyo,
mwalimu ambaye hajaitwa na Mungu ataweza kukana hisia zake wakati mwanga wa Roho wa
Mungu unamulika mawazo yake, na kuvuvia midomo yake anaponena. Kwa hiyo mafundisho ya
Kikristo yanapaswa kuwa na upako na shauku ya kuhubiri Neno.
Huduma ya kufundisha inafanya kazi katika viwango tofauti vya mawasiliano kuliko vile vya ujuzi
wa Kidunia. Ni makusudi, lakini pia inafurahisha. Haikusudiwi tu katika mawazo, bali pia katika
moyo (hata hivyo, siyo katika hisia tu) ili kuleta mabadiliko katika tabia na namna ya maisha ya
wale wanaofundishwa. Maelekezo ya mawazo / ufahamu ni muhimu kwa vile huchochea moyo
na hisia kwa njia ya nabii au mwinjilisti. Kwa kuwa wakristo wanaushinda ulimwengu kwa
kufanywa upya nia, (Warumi 12:2) na siyo tu kuchochea hisia (1Petro 4:1; 1Petro 1:13; 2Petro 3:1;
Wafilipi 2:5; 2Timotheo 1:7). Maelekezo ya nia yanakuwa muhimu sana, ili iweze kuwekwa katika
njia ya Kristo. Charles Conn anaeleza wazi kwamba haitoshi kuomba mpaka tumekuwa na hisia
nzuri, bali, nia zetu zinapaswa kujawa na ukweli wa Kristo. Inapaswa kujihusisha na kujitoa katika
maisha ya utakatifu na haki.41
40 George Canty, The Practise of Pentecost, p. 160.
41 Charles Conn, A Balanced Church, p. 164.
48
Huduma ya kufundisha haitolewi kwa kufikisha habari tu au kutoa ufahamu wa kina wa
maandiko, bali kuwaongoza, watu katika utii kwa Mungu, hivyo kubadilisha maisha ya wasikilizaji
katika sura ya Kristo. Peter Wagner anaeleza kwamba anawatarajia wale ambao anawafundisha
kujifunza, kama vile Billy Graham anavyotarajia watu kuinuka na kuja mbele ya madhabahu baada
ya kuhubiri.42 Dhana yake inakubalika. Kila mwalimu anapaswa kutarajia watu kujifunza na
kubadilika ( ambavyo inaonyesha kwamba ufahamu umetendewa kazi na siyo tu kusikia), kama tu
vile mwinjilisti anavyotarajia watu kuokoka kwa kuitikia ujumbe wake. Mafundisho ya kweli ya
kiroho ni zaidi ya kutoa au kusikia mafundisho, kadri yanavyofanya kazi ndani ya moyo wa
mwanafunzi.
2. Kazi ya mwalimu.
Kristo aliweka waalimu katika mwili wake kutafsiri ujumbe wa zamani wa maandiko kwa ajili ya
Kanisa la leo. Wakati ni kweli kwamba ukweli kamwe haubadiliki; hata hivyo tunapaswa
kutambua kwamba hutafuta ufafanuzi mpya katika kila muda wa kipindi. Mwalimu kupitia Roho
Mtakatifu anawezesha kutoa mwanga katika vifungu vigumu na kuelezea yanayohusu muda wao
wa leo. Mtazamo wa ndani anaoupata unawakirishwa na kupangwa kwa mantiki, wakati huduma
hii haitakuwepo, ukweli wa Agano jipya utatafsiriwa katika hali ya Kisheria, bila kujali utamaduni
wake uliomo katika maandiko. Hivyo sehemu ya kazi ya waalimu ni kuhakikisha kwamba
maelekezo na sheria za kanisa la kwanza zinaeleweka, zimetasiriwa bara bara na kufafanuliwa
katika siku na karne yetu. Kama hii haitatendeka maswali na mambo kama vile ya wanawake
kufunika nywele zao kwa mfano, mara zote itakuwa chanzo cha ugomvi.
Kristo hakutuamuru tu kuwahubiri wenye dhambi bali kuwafundisha, kama vile kuwafanya
wanafunzi (Mathayo 28:19 –20). Waalimu wanasehemu muhimu katika jitihada hii ya kufanya
mwanafunzi. Kwa hiyo, mwalimu atafanya zaidi kuliko kuelezea vifungu vyenye utata / vigumu.
Katika mafundisho yake anapaswa kuhakikisha kwamba anatafsiri maandiko kulingana na namna
ya utendaji wa maisha. Kamwe hapaswi kuwa na msimamo wa kutojali maneno yenye msingi
zaidi ya Kristo, kwa mfano:-
 Kumpenda Mungu kwa moyo wako wote; akili na kwa roho na jirani yako kama
unavyojipenda mwenyewe.
 Kuubeba msalaba wake na kumfuata Kristo kila siku.
 Kumpenda Kristo zaidi ya baba, mama, mke, watoto na maisha yako mwenyewe.
Huduma ya kufundisha inajidhihirisha yenyewe katika njia nyingi. Mbali na sehemu yake ndani ya
huduma tano za uongozi itawawezesha wale walioitwa kuwakilisha kweli ya kiroho kwa watoto,
vijana, mabinti au makundi mengine maalumu kama vile wazee au ambao hawajaoa au kuolewa.
Kuongeza utendaji wake wa kazi mwalimu hapaswi kuwa mwanafunzi wa Neno tu, bali anapaswa
kujihusisha yeye mwenyewe kujifunza na kutumia mbinu tofauti za kufundisha, njia na mitindo ya
kufundisha. Kama vile Yesu alivyo tumia njia mbali mbali za kuwakilisha kweli ya kiroho, kwa
hiyo mwalimu anapaswa kutumia njia na mbinu tofauti tofauti. Vielelezo vya kufundishia, mifano,
mjadala katika vikundi, maigizo n.k. ni baadhi ya njia atakazotumia.
42 C.P. Wagner, Your Spiritual Gifts Can Help Your Church Grow (MARC: Europe Press, 1979), p. 128.
49
Kujifunza kwa makini hutendeka wakati wanafunzi wanapewa nafasi ya kuuliza maswali na kutoa
maoni. Kwa hiyo, waalumu wanapaswa kutengeneza mazingira ambayo yatawawezesha
wanafunzi, kujifikia huru kuuliza swali au kutoa maoni; ambayo inamaanisha kuwa hawapaswi
kudhalilishwa kutishwa au kuwafanya wajione wapumbavu.
Kufundisha mwili wa Kristo hakuhitaji tu ufahamu bali kuwa makini. Kadri mwalimu
anavyokumbuka kumtegemea Mungu atakuwa na uwezo wa kupinga majaribu ya kuonyesha
elimu au kuonyesha ubora wake kuliko wengine, hivyo huleta athari katika maisha ya kiroho kwa
wale anaowafundisha.
3. Siyo maarufu bali muhimu.
Kwa kuwa kufundisha kunaonekana si kwa muhimu sana kuliko vipawa vingine vya uongozi, si
wengi wanaotamani huduma hii. Ijapokuwa haitakuwa ya kuvutia sana si kwamba ina umuhimu
mdogo. Kwa kuwa Mungu anapenda kulithibitisha neno lake haijarishi ni kupitia huduma ipi
inayotangazwa, kupitia yeye mwalimu ataona watu wakiokoka na kuponywa pia.
Wengine wanarejea katika 1Yohana 2:27 na kubisha kwamba huduma ya mwalimu si ya lazima
kwa kuwa Roho Mtakatifu atawaongoza waamini katika kweli yote. Hata hivyo, wale wanaotetea
hoja kama hiyo wameshindwa kugundua kanuni mbili za msingi za hermeneutics/elimu ya
kutafsiri maandiko. Kwanza kabisa wamechukua maandiko nje ya mazingira ya andiko, na pili,
wameshindwa kutafsiri andiko kulingana na maandiko mengine katika mada hiyo, kama vile
Waefeso 4 na 1Wakorintho 12. Wakati kanuni za Hermeneutics (kanuni na mbinu za utafsiri wa
biblia) zimetumiwa vizuri tutaona kwamba:
(1.) Huduma ya ualimu imetolewa na Mungu kwa ajili ya kulijenga kanisa lake (Waefeso
4:11 “Alitoa”).
(2.) Roho Mtakatifu haifanyi huduma ya mwalimu kuwa haihitajiki bali huikamilisha
huduma aliyoianzisha.
(3.) Roho wa Mungu hufundisha waamini kupambanua mafundisho ya uongo na
mafundisho potofu(1Yohana 2;26).
Ikiwa 1Yohana 2 inasomwa yote tutaona kwamba 1Yohana 2:27 kwa njia yoyote ile haionyeshi
kutohitajika kwa huduma ya kufundisha.
4. Neno la tahadhari.
Ujuzi mwingi katika maswala ya kiroho huleta kiburi cha kiroho (1Wakorintho 8:1). Kwa hiyo
unyenyekevu ni ishara / dalili ya mwalimu wa kweli. Moja ya matukio mazuri katika kanisa la
kwanza ni lile la Apollo ambaye alikuwa hodari katika maandiko (matendo 18:24 –26) lakini hata
hivyo alikaa chini ya miguu ya watengeneza mahema wawili kupata mafundisho. Wakati mwalimu
anapokataa kufundishika na kukataa kusikiliza maarifa na nuru ambayo wengine wamepokea, au
kukataa kukosolewa kwa mafundisho yake, yuko katika nafasi ya hatari ambayo inaweza ikasitisha
huduma yake au ataishia kwenye mafundisho potofu / uzushi.
50
Migawanyiko mingi katika ufalme wa Mungu ililetelezwa na watu waliodai kulazimisha kwamba
kuelewa kwao kuhusu mafundisho fulani ya kanuni, au tafsiri zao za maandiko ndiyo tu zilikuwa
sahihi. Wanaeleza maoni yao kama ni ya imani pekee ambayo yamesababisha madhara makubwa
katika mwili wa Kristo.
Wakati tunahitimisha somo letu la mwalimu tunafanya vyema kama tutatilia maanani onyo la
George Canty.
Kuwepo kwa usafiri wa haraka, kanda za redio na mawasiliano mengine ya haraka katika ulimwengu
vimeleta mawazo mengi mapya. Siamini Mungu ananipa ujumbe, kila wakati ninapohubiri, nusu ya
watu wa ulimwengu husikia kwa kanda ya redio, lakini ni maalumu kwa ajili ya Kampuni ambayo
nimetafuta uongozi wa dhahili kwa kila ambacho ninataka kusema. Watumiaji wa kanda hizo
inawezekana kuwa kama kusikiliza wa siri mazungumzo ya watu kwa kile nisemacho mbele ya watu
walioko mbele yangu, ikiwa ni mafundisho ya kweli katika mtazamo ambao nimeueleza … Vinginevyo
itakuwa habari za kawaida, mdomo kwa sikio badala ya moyo kwa moyo.43
Wazo la Canty limekubalika vizuri. Kupitia matumizi ya vyombo vya habari mafundisho
yameenea kwa haraka sana duniani. Kinachofanya mambo yawe mabaya zaidi ni kwamba
vielelezo na kanda za video vina mafundisho potofu yanayoenea kwa kiwango kile kile. Hata
kama waalimu wa Kimataifa wanaofahamika wanafahamu mafundisho potofu ambayo waliyatetea
wakati huo, kiwango hiki cha uharibifu kimesababishwa kupitia kwa uenezaji wa haraka wa
mafundisho yao hauwezi kurejeshwa nyuma kirahisi. Kwa mifano mingi kubadilika kwa mawazo
/ maoni yao hakuenezwi kwa makini kama mafundisho yao potofu ya awali. Baada ya kusema hili
tunapaswa kuonyesha haraka kwamba licha ya hatari hizi, kuna kanda (za vielelezo au video)
zinazosambaswa zikiwa na mafundisho ya kawaida ambayo yanaweza kuwa baraka kwa waamini
mahali popote hapa ulimwenguni. Ikiwa hii haikuwa kweli, tungeweza kusitisha usambazaji wa
vitabu vya kufundishia au fasihi pia. Hata hivyo, maoni ya Canty anatutahadharisha sisi kufanya
kwa tahadhari kwa kutumia mtindo huu wa mawasiliano.
Kama tulivyoona huduma ya ualimu katika agano jipya haitegemei mafunzo ya ujuzi wa kidunia
bali katika wito wa Mungu. Wakati inapotumika katika upako wa Roho Mtakatifu inaburudisha
akili na nafsi, na inamsaidia mwamini kuushinda ulimwengu kupitia kufanywa upya kwa nia.
Inaweza isiwe maarufu, lakini hata hivyo inasehemu muhimu sana katika mpango wa Mungu kwa
muda wote.
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-
43 George Canty, The Practise of Pentecost, p. 164.
51
IV. HUDUMA ZA MASAIDIANO.
Kuna huduma zaidi zimeorodheshwa katika Agano jipya kuliko zile ambazo zimetajwa katika sura
ya nne ya Waefeso. Warumi 12:6 –8 na 1Wakorintho 12:28 inatupatia orodha ya nyongeza mbili
za huduma hizi si kwa ajili ya Uongozi, hata hivyo zimetolewa na Kristo katika Kanisa lake, kwa
hiyo ni muhimu kama zingine zilivyo.
Sehemu ifuatayo ya huduma za masaidiano imekusudiwa kusaidia waamini wale ambao wanafikiri
“kwa kuwa siwezi kuhubiri sitafanya chochote” tambua huduma zao. Kama wanafunzi wa Kristo
tunafanya vizuri kukumbuka mfano wa talanta (Mathayo 25:14 –30). Kwa hiyo, tuonyeshe na
tutumie vipaji vyetu ijapokuwa ni kimoja tu.
7
Warumi 12:6–8.
Basi kwa kuwa tuna karama
zilizo mbali mbali, kwa kadri
ya neema tuliyopewa, ikiwa ni
unabii, tutoe unabii kwa
kadri ya imani, 7 ikiwa
huduma tuwepo katika
huduma yetu mwenye
kufundisha, katika
kufundisha kwake, 8 mwenye
kuonya, katika kuonya
kwake; mwenye kukirimu,
kwa moyo mweupe, mwenye
kusimamia kwa bidii, mwenye
kurehemu, kwa furaha.
1 Wakorintho 12:28
Na Mungu ameweka wengine
katika kanisa, wa kwanza
mitume, wa pili manabii, watatu
walimu, kisha miujiza, karama
za kuponya wagonjwa na
masaidiano, na maongozi, na aina
za lugha.
Vifungu hivi viwili vya maandiko vinafunua utajiri mwingi na huduma mbalimbali ambazo
zilifanya kazi katika kanisa la kwanza. Katika Warumi 12:6-8 tunaona nyongeza katika vipawa
viwili vya uongozi ambavyo ni nabii na mwalimu, vipawa vya huduma, kuonya, kukirimu,
kusimamia na kurehemu.
Tunaporudi katika 1 Wakorintho tunaona huduma za masaidiano na kusimamia.
Tunapoziangalia huduma hizi moja baada ya nyingine, tunahitaji kukumbuka tena kwamba si za
uwezo wa asili, bali kwa asili ni za kiroho. Hii inaonyesha hasa wakati tunaangalia huduma ya
ukarimu, masaidiano au kutoa/kukirimu.
Wakati tunajifunza hizi huduma tutatambua kwamba si zote zinaonekana sawa. Kama vile mwili
ulivyo na sehemu za ndani na za nje, hivyo ndivyo kanisa lina huduma zinazoonekana na
zinazoonekana kidogo. Maandiko yanaonyesha hili kwa uwazi zaidi katika 1 Wakorintho 12.
Ingawa sehemu za ndani kama vile moyo, ini, figo, mishipa ya damu nk. Havionekani, hata hivyo
ni mhimu kama vile mikono, miguu, macho, masikio nk. Vyote hivyo ni muhimu kwa ajili ya
mwili kufanya kazi kikamilifu.
52
1. Shemasi –kuhudumu –kutumika
(1 Timotheo 3:8-13; Wafilipi 1:1; Warumi 12:8; 1 Wakorintho 12:8)
Shemasi ni nini? Kwa uhakika kila dhehebu litajibu swali kulingana na historia ya ushawishi wa
mafundisho yao. Alexander Strauch anaeleza kwamba miongoni mwa makanisa yanayoamini
Biblia (bila kufikira makanisa yasiyo ya kiroho) sifa mbili zinazotofautiana sana zinaendelea
kutishia wazo la Agano Jipya mengine kuhusu ushemasi.44 Wakati makanisa mengine
wanawapandisha kimakosa mashemasi katika nafasi ya kuwa mjumbe katika kamati kuu ya
utendaji, wengine huwapunguzia / huwashusha na kuwa katika hadhi ya kulinda,
mlango/bawabu, watunze mazingira na watu wanaokarabati majengo.45 Bado wengine wanampa
wadhifa wa shemasi kama ishara ya heshima, kama vile mhofiwa (Reverend), lakini kwa watu wa
kawaida.46 Kwa hiyo, ni lazima kwetu kuitambua huduma ya ushemasi kulingana na nafasi zao
katika maandiko. Kufanya hivyo tunapaswa kutambua kwamba Kiyunani jina (noun) diakonia,
kuhudumu au huduma, na tendo (verb) kwa kiyunani diakoneo, kutumika, linaonekana mara nyingi
katika Agano Jipya ambapo yanatumika katika mtazamo wa kutumika kwa pamoja.47
Neno diakonia hata hivyo linaweza kutumika kwa upana kwa ajili ya huduma zote kanisani (1
Wakorintho 12:5). Kwa nyongeza neno diakonos, mtumwa, limetumiwa na Paulo wakati akijieleza
yeye mwenyewe kama mtumwa wa Kristo (2 Wakorintho 6:4) mtumwa wa injili (Waefeso 3:7), na
mtumwa wa kanisa (Wakolosai 1:25).48 Katika matukio matatu tofauti neno diakonos linatumika
kuonyesha anayeshikilia ofisi maalumu ya shemasi (1 Timotheo 3:8,12; Wafilipi 1:1).
Maneno ya Kiyunani, yaliyotumika katika Wafilipi 1:1 na 1Timotheo 3:8,12-13 hayaonyeshi tu
watumwa, au anayetoa huduma, bali ni watumishi katika kanisa ambalo walikuwa wanatambuliwa
kikamilifu na mitume. Paulo katika waraka wake kwa Wafilipi anawataja kwa pamoja na wazee
(sura 1:1), hivyo anaonyesha kwamba nafasi ya utumishi wao katika kanisa la kwanza
iiunganishwa na huduma kwa wenye mahitaji na usimamizi wa misaada.
Orodha ya kipawa katika Warumi 12:6-8 inataja kutumika ni kama moja ya karama za huduma.
Tafsiri ya King James inaonyesha maana hiyo hiyo na neno la Kiyunani (–diakonia)
kama huduma.49 Kwa kuwa diakonia imeorodheshwa miongoni mwa vipawa na huduma za
kiroho kama vile kufundisha, kuonya na uongozi/kusimamia inaonekana kuonyesha kwamba
inataja huduma ya shemasi.
44 Alexander Strauch, Minister of Mercy The New Testament Deacon (Littleton: Lewis and Roth
Publishers, 1992), p. 157.
45 Ibid., p.10.
46 John F. MacArthur Jr. The Master’s Plan for the Church, p. 201.
47 Neno diakoneo huonekana mara 36 katika Agano Jipya Linapatikana mara 21 katika Injili na katika
kitabu cha Matendo ya Mitume (zaidi sana limetumika katika mifano ya Yesu), mara 3 katika kitabu cha
Yohana, mara 8 katika nyaraka za Paulo, mara moja katika waraka wa Waebrania, na mara 3 katika waraka wa
kwanza wa Petro. Jina diakonia linaonekana mara 33 katika Agano Jipya linapatikana mara moja katika vitabu
vya injili (Luka 10:40), mara 8 katika cha Matendo ya Mitume, mara 22 katika Nyaraka za Mtume Paulo, mara
moja katika Nyaraka wa Waebrania na mara moja katika kitabu cha Ufunuo. Kwa maelezo zaidi rejea:
Exegetical Dictionary of the New Testament, Grand Rapids: Eerdmans Publishing, 1990, I:307.
48 Neno diakonos - Sawa sawa na mtumwa linapatikana mara 29 katika Agano Jipya, ambapo neno hili
limetumika mara nane katika vitabu vya Injili na mara 21 katika Nyaraka za Paulo
49 Hii kwa kawaida ipo katika msingi wa Vulgate (Tafsiri ya Agano Jipya katika Kilatini) ambapo neno
dia konia ni sawasawa na mtumwa ambavyo limetafsiriwa kama mtumishi (rejea Mathayo 20: 26-27)
53
(1) Kuteuliwa/kuwekwa kutumika
Wengi wanasema watu saba walichaguliwa kuhudumu mezani katika Matendo 6:1-6 kama
Mashemasi wa kwanza wa kanisa. Stefano na Filipo wakawa mashuhuri. Hata neno hivyo
shemasi halionekani hapa. Hata hivyo kifungu kina maneno mengi ambayo yanatokana na neno
lile lile kundi kama shemasi (diakonos). Katika mstari 1 neno la Kiyunani diakonia, kuhudumia
chakula kila siku (KJV inalionyesha kama utumishi) inatumika wakati katika mstari wa 2
diakoneo, kuhudumu mezani limetumika.
Matendo 6:1-6
1 Hata siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manung’uniko ya
Wayahudi wa Kiyunani juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika huduma ya
kila siku. 2 Wale thenashara wakawaita jamii ya Wanafunzi, wakisema, haipendezi sisi kuliacha neno
la Mungu na kuhudumu mezani. 3 Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa
kuwa wema, wenye kujawa na roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili; 4 na sisi tutadumu
katika kuomba na kulihudumia lile neno. 5 Neno hili likapendeza machoni pa mkutano wote;
wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro na Nikanori, na
Timoni, na Permena, na Nikolao muongofu wa Antiokia; 6 ambao wakawaweka mbele ya mitume, na
walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao.
Kwa kuwa Matendo 6 kidesturi imekubalika kama ya kwanza kutaja Mashemasi katika Agano
jipya. Tunahitaji kukumbuka kwa nini huduma hii ilianzishwa. Kanisa la kwanza halikufuata
mfano wa Kristo tu na kuwahubiri maskini (Mathayo 11:5) bali pia liliwatunza wajane na yatima
(Yakobo 2:5). Baadhi ya wajane hawa waliotokea katika ustaarabu wa Kiyunani, na ingawa
walikuwa wayahudi kwa kuzaliwa, walizungumza kiyunani na walijiweka wazi zaidi kwenye
utamaduni wa kiyunani kuliko wa kwao. Katika jamii ya Kiyahudi walionekana kuwa kundi tofauti
la kijamii. Wayahudi waliofuata mila na mapokeo hawakuficha dharau zao kwa Wayunani, mazoea
ambayo yaliingia Kanisani.50 Kiasi fulani wajane wenye asili ya Kiyahudi wa kiyunani walipuuzwa
na Wakristo wa kiebrania. Upendeleo wa ndugu na ukabila ulikuwa karibu kutokea kwa sababu ya
chuki ya kikabila. Mitume, mara moja waligundua usumbufu huu, na wakaukabiri kwa hekima
ambayo Mungu aliwapa. Baada ya kuwaita waamini pamoja, maelekezo yao ilikuwa kuchagua
watu saba ambao wamejazwa na Roho Mtakatifu, hekima na imani kuhudumu mezani ili
kuliondoa tatizo. Kukabidhi kwa jukumu hili haikuwa kwa sababu hawakuwa na huruma kwa
wajane wa Kiyunani, wala kwa sababu mitume walijifikiria wao ni bora zaidi. Kwa hakika
hawakufikiria jukumu kama lile la unyenyekevu kwao, bali walitambua tu kwamba kuwajali
maskini haukuwa wajibu wa kwanza katika huduma yao, bali kumhubiri Kristo. Kipaumbele cha
kwanza kwao ilikuwa kuomba na kuhudumu Neno. Labda walihisi ulazima wa kuchagua wale
saba baada ya kuwa wamehusishwa katika kugawa fedha kabla ya hali iliyokuwepo. Walifahamu
kutokana na uzoefu kwamba tatizo lililopo lingeweza kuwavuruga tena kutoka katika kazi yao
kuu, ambapo ingezuia utendaji bora wa huduma yao. Katika Matendo 4:32 –35 tunasoma:
Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja;wala hapana mtu mmoja aliyesema
ya kuwa kitu chochote alichonacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika. 33 Na
mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi; na neema nyingi ikawa juu yao
50 Alfred Endersheim, The Life and Times of Jesus the Messiah (McLean: Mac Donald Publishing
Company, n.d.), p. 7. Pia rejea William Fairweather, The Background of the Gospels, Judaism in the Period
between the Old and New Testament (Minneapolis: Klock & Klock Christian Publishers, 1977).
54
wote. 34 wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote
waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa; 35 Wakaiweka
miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadri alivyohitaji.
Kadri walivyotambua ukweli wa maneno ya Bwana wao: “kwa maana siku zote mnao maskini
pamoja nanyi:” (Mathayo 26:11). Mitume walitoa kwa ajili ya huduma ya kudumu kwa wale
ambao hawakuwa na kitu katika jamii ambao walikuwa sehemu ya mwili wa Kristo. Wale saba
walichaguliwa na Kanisa, na kikazi waliwekwa na mitume. Wawili wao walipokea wito kama
wainjilisti; hata hivyo hayakuwa matokeo ya moja kwa moja ya ushemasi wao. French Arrington
anaeleza kuwa kila mmoja wa hawa saba alikuwa na jina la Kiyunani, ambavyo hata hivyo
anashindwa kuthibitisha kwamba walikuwa Wayunani, maana wayahudi wengi walikuwa na
majina ya Kiyunani kwa kuwa wale saba inawezekana walizungumza Kiyunani, kwa hiyo
waliandaliwa si kiroho tu bali pia katika lugha (lingustically) kushughulikia tatizo. Kuteuliwa kwa
wale saba ilikuwa ni kuwahakikishia wale waliokuwa wakinung’unika kwamba wajane waamini
waliokuwa wakizungumza Kiyunani wasije wakapuuzwa katika siku za mbeleni. Hii ilikuwa
muhimu hasa kwa vile wanawake wachache tu ambao waume zao walikuwa wamekufa walikuwa
na uwezo wa kujisaidia wao wenyewe.51
(2) Huduma ya shemasi.
Kazi ya msingi ya shemasi ni kuwaangalia / kuwatunza maskini, wajane na ambao hawana maisha
mazuri, kama vile walemavu, wasio na makazi (pamoja na watoto wa mitaani), wasio na kazi,
wazee, wafungwa, wakimbizi, waliokumbwa na ukame, na wenye njaa. Maandishi ya wakristo wa
kwanza katika karne tatu za mwanzo yanashuhudia kwamba jukumu kubwa la shemasi ilikuwa ni
kuwahudumia waamini wenye mahitaji kanisani. Hii ni kinyume na matendo ya makanisa ya sasa
ambayo yamejihusisha kuwasaidia wengine walio mbali / ng’ambo wakati wakipuuza ndugu zao
walio nyumbani. Tusisahau kuwa mashemasi waliwekwa kuwatunza washirika wa mwili wa
Kristo. Wakati kanisa linapaswa kusaidia watu wa namna mbali mbali ni jukumu lake la kwanza
kuwaangalia / kuwatunza wenye uhitaji hasa wale wa jamii ya waaminio.
Wagalatia 6:10
Kwa hiyo kadri tupatavyo nafasi tuwatendee watu wote mema; na hasa jamii ya waaminio.
Watu katika huduma hii hawaangalii tu mahitaji ya vitu vinavyoonekana, bali pia wanajihusisha
kukutana na mahitaji kivitendo. Wanaweza kutumika kwa mfano kama wahudumu kukusanya
sadaka / matoleo au kujihusisha katika kazi zinazofanana ambazo zinahitaji uajibikaji na uaminifu.
Baadaye, wakati tutakapochunguza huduma za masaidiano na usimamizi tutaona kwamba
huduma ya shemasi inaingiliana sana na huduma hizi mbili.
(3) Sifa na uchaguzi wa mashemasi.
Si kila mtu anaweza kujiunga na wadhifa wa shemasi. Wale waliochaguliwa kuwaangalia wenye
mahitaji walitakiwa kuwa na sifa fulani kama zile zinazolingana na za wazee (linganisha
1Timotheo 3:8 –13 na 1Timotheo 3:1,2 vile vile Tito 1:7 na Matendo 6:3), ambazo zingeweza
kuonekana sana katika huduma hii.
51 French L. Arrington, The Acts of the Apostles (Peabody: Hendrickson Publishers,1988), p. 66.
55
1Timotheo 3;8 –13
Sifa za mashemasi:
- Wawe wastahivu
- Si wenye kauri mbili
- Si watu wa kutumia mvinyo sana
- Si watu wanaotamani fedha ya aibu
- Wakishika siri ya Imani katika dhamiri safi
- Wajaribiwe kwanza
- Wasio kuwa na hatia
- Waume wa mke mmoja
- Wakiwasimamia watoto wao vizuri na
nyumba zao.
Sifa kwa wake zao:
- Wake zao wawe wastahivu
- Si wasingiziaji
- Wa kiasi.
- Waaminifu katika mambo yote
1 Timotheo 3:1 –4
Sifa za wazee:
- Asiyelaumika
- Mume wa mke mmoja
- Mwenye kiasi na busara
- Mtu wa utaratibu
- Mwenye sifa njema
- Mkaribishaji
- Ajuaye kufundisha
- Asiye zoelea ulevi
- Si mpiga watu
- Asiyependa mapato ya aibu bali awe
mvumilivu
- Si mgomvi / si mwenye mabishano
- Si mwenye kupenda fedha
- Mwenye kuisimamia nyumba yake vyema,
ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu
- Asiye mtu aliyeongoka karibuni
- Mwenye kushuhudiwa mema na walio nje.
Mashemasi walipaswa kuwa na tabia njema na uaminifu kwa vile walihusika na mambo ya fedha
na ugawaji wa vitu. Watu wasio waaminifu na wachoyo wangesababisha madhara makubwa.
Ijapokuwa sifa za ofisi / huduma hizi mbili zinafanana lakini zinatofautiana sana katika
majukumu yake na mtazamo wa huduma. Hii imekuwa wazi tayari katika usimikaji wa huduma
hizi. Wakati wazee waliteuliwa na mitume kwa ajili ya uongozi wa kanisa (Matendo 14:23; Tito 1:5
–9), mashemasi walichaguliwa na kusanyiko na baadaye walisimikwa kwa ajili ya jukumu la
uongozi wa kanisa la mahali pamoja (Matendo 6:1-3). Ijapokuwa mitume waliwachagua saba kwa
ajii ya huduma, walifanya hivyo kama viongozi wa kanisa la mahali pamoja katika Yerusalem, na
siyo katika uwezo wao kama viongozi wa kidunia wa kanisa.
Kuwachagua mashemasi katika kanisa la leo mambo yafuatayo yanapendekezwa:
1. Mchungaji anaweza akaliuliza kusanyiko kumpendekeza mtu mmoja au zaidi ambao wana
uwezo na wanaofaa katika huduma hii. Hii inaweza kufanyika kupitia kura za siri. Baada
ya kufikiri kwa makini, kanisa linaweza kuonyesha wagombea wapi wameonyesha mfano
wa maadili na tabia nzuri na wanafaa kwa ajili ya kutumika katika nafasi hii.
2. Mchungaji mwenyewe anaweza kupendekeza watu wanaofaa kwa ajili ya ushemasi. Ikiwa
tutafuata mfano wa Kibiblia hawa watu watathibitishwa na kanisa baadaye.
3. Baada ya kuchaguliwa, mashemasi wanapaswa kusimikwa mbele ya kusanyiko la kanisa
katika maombi na kuwekewa mikono na mchungaji / Wazee.
Uchaguzi huu ufanyike tu baada ya maombi ya muda mrefu na kuwa wazi katika uongozi wa
Roho Mtakatifu. Ikiwa hakuna mtu mwenye uwezo na wito, ni vyema kusubiri. Kuhusu kusimika
watu wachanga kwenye huduma Paulo anatuonya: usimuwekee mtu mikono kwa haraka
1Timotheo 5:22.
56
Namba / wingi wa mashemasi katika kanisa la mahali pamoja unategemea ukubwa na wingi wa
kazi ambazo zinaweza kufanyika. Kanisa la Yerusalemu lilikuwa na mashemasi saba. Makanisa
madogo yanaweza yakahitaji shemasi mmoja au wawili tu. Ingawa tumeweka mashemasi katika
kazi / huduma tunapaswa kukumbuka kuwa kila mshirika katika mwili wa kristo anapaswa
kutumika na kujitoa kufanya kazi katika ufalme wake. Baadhi ya watoa maoni wa biblia
wanaruhusu wanawake kujiunga na nyadhifa za mashemasi; kulingana na Warumi 16:1 ambayo
inasema “Namkabidhi kwenu Fibi, ndugu yetu aliye mhudumu wa Kanisa lililoko
Kenkrea”. Neno lile lile la Kiyunani kwa “Mtumishi” limetumika hapa ambapo limetumika
kuonyesha huduma au kazi ya shemasi katika Wafilipi 1:1 na 1Timotheo 3:8, 12.
Kwa kuhitimisha tunahitaji kukumbuka kwamba hatupaswi kujiwekea mipaka kuwatunza wale
wasiojiweza nyakati za Krismasi kwa kawaida watu wanapokumbuka wajibu wao kusaidia wasio
na vitu. Kuwatunza wahitaji inapaswa iwe na sehemu ya kudumu katika kila kusanyiko la mahali
pamoja katika mipango ya kila siku. Kwa hiyo, Mungu katika hekima yake alilipa kanisa lake
huduma ya mashemasi kuiendeleza huduma hii muhimu ya kutangaza ujumbe wa injili. Wale
walioitwa katika huduma hii ya thamani wanapaswa kufanya hivyo katika moyo safi na nia njema.
Kama mashemasi wameitwa kuhubiri na wamejitoa katika huduma yao tutakuwa na matokeo yale
yale kama ilivyo katika matendo ambapo tunasoma: Neno la Mungu likaenea na hesabu ya wanafunzi
ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile imani.
2. Faraja
(Warumi 12:8)
Huduma ya faraja (Paraklesis) ni kuwezeshwa Ki-Mungu katika kuhudumu, kutia moyo na
kuwapa tumaini waamini wengine katika mwili. Hii inaweza ikatokea kuwa mtu mmoja mmoja au
katika mfumo wa ujumbe/mahubiri. Muundo wa jina (noun) wa neno hili (kiyunani Parakletos)
linatumika kwa ajili ya Roho Mtakatifu (Yohana 14: 16,26) ambalo kwa kawaida lina maana,
ameitwa badala ya mwingine, kwa mfano kumsaidia mtu. Lilikuwa ni neno la kisheria lililotumika
mahakamani. Lilionyesha mshauri wa Sheria, mwanasheria msaidizi, Wakili wa utetezi, au Wakili,
anayemtetea mtu mwingine katika jambo lake.52 Neno faraja (paraklesis) lina maana sawa na
neno paraklete, ambalo lina maana ya mfariji au Msaidizi. Hivyo ikiwa faraja ina usahihi, itakuwa
ni kwa faida ya mtu anayehudumiwa. Kwa hiyo faraja ya kweli siku zote itaendelea na kutia moyo
na tumaini.
Imependekezwa kwa usahihi kwamba huduma ya faraja imeunganishwa na huduma ya ushauri,
ambapo mshauri hutenda kama mfariji na Wakili ambaye anamtetea mtu mwingine. Huduma ya
faraja inampa mshirika wa mwili wa Kristo uwezo wa Kiungu kuchukuliana na walioumia,
aliyekata tamaa, dhaifu, wenye mashaka na watu wenye mafadhaiko na kutoa ushauri ambao
utawatia nguvu, utawafariji kutoa mwelekeo na kuwa na moyo wa imani. Hata hivyo, faraja kama
vile kushauri haitasamehe makosa. Hutafuta kusahihisha lakini wakati huo huo huwatia moyo
wale ambao ni wadhaifu na ambao waweza kuanguka.
52 W.E. Vine, An Expository Dictionary of New Testament Words (Old Tappan: Fleming H. Revell
Company, 1966), p. 208.
57
Mimi mwenyewe binafsi nimekutana na waamini wenye huduma hii maalumu. Baada ya kusema
nao, mmoja anaondoka akiwa ametiwa moyo na tumaini jipya. Hawataweza kukatishwa tamaa
kwa urahisi na watu, ijapo kuwa wengine wote walibaki na mambo yao bila matumaini. Peter
Wagner anaeleza kwamba Waamini walio na huduma hii wanajihusisha na mambo ya kiroho ya
ndugu au dada kwa kipindi kinachohitajika kumsaidia huyu mtu, ndipo wataondoka kwa
mwingine ambaye anahitaji kutiwa moyo na wao.53
Habari za Barnaba, Paulo na Marko ni mfano bora wa kimaandiko. Baada ya Yohana Marko
kuacha safari ya kwanza ya umishenari bila kukamilika, Paulo alikataa kumchukua katika safari yao
ya pili ya umishenari. Hata hivyo, Barnaba ambaye alikuwa ameuona uwezo ndani ya kijana,
alijisikia kwamba angeweza kupewa fursa nyingine kujithibitisha mwenyewe. Kwa bahati mbaya,
Paulo na Barnaba hawakukubaliana / hawakuafikiana katika mawazo yao hivyo waliachana. Baada
ya tukio hili Barnaba hakutajwa tena wakiwa pamoja na Paulo. Wengine wanafikiri kwamba
Barnaba alimpendelea Yohana Marko kwa sababu alikuwa ndugu yake.
Hata hivyo, inaonekana kwamba hakukata tamaa juu ya Marko kwa sababu ya huduma yake ya
kufariji. Kama isingelikuwa kwa ajili ya Barnaba na huduma yake, tusingeweza kumsikia Marko
tena, na labda tusingeweza kufurahia injili kulingana na Marko kama sehemu ya maandiko ya
Agano jipya. Kwa sababu ya huduma ya Barnaba, baadaye Paulo aliweza kutuma habari kwa huyu
“mtoro” akimuona yeye mwenyewe na huduma yake inafaa (2Timotheo 4:11). Huduma ya
Barnaba ya kutia moyo ilianza kabla ya tukio hili. Kwa hakika Paulo alinufaishwa na huduma ya
Barnaba kabla ya Yohana Marko. Wakati wanafunzi wengine walikuwa na hofu na walisita
kumkaribisha mgeni ambaye mambo yake yalikuwa ya mashaka/ yasiyoaminika, Barnaba
alimchukua mtesaji wa awali wa kanisa chini ya kivuli chake na akamtambulisha Paulo kwa
viongozi wa Yerusalemu.
Matendo: 9:26 –28
26 Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi, na walikuwa wakimuogopa wote,
wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi. 27 Lakini Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume,
akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema naye, na jinsi alivyohubiri kwa
ushujaa katika Dameski kwa jina la Yesu. Naye akawa pamoja nao katika Yerusalemu akiingia na
kutoka.
Barnaba hakumtambulisha tu Paulo kwa Uongozi bali alitambua wito wake na uwezo mkubwa
kwa ajili ya huduma. Hivyo, wakati wa uamsho ulipotokea kule Antiokia Barnaba alienda
kumtafuta Paulo ili aungane naye baada ya kuwa ameamriwa na mitume aende naye huko, hivyo
alitoa nafasi kwa Paulo kuhudumu na kushiriki katika Uongozi.
Matendo 11:19 –26:
19 Basi wale waliotawanyika kwa sababu ya ile dhiki iliyotukia kwa habari ya Stefano; wakasafiri hata
Foinike na Kipro na Antiokia, wasilihubiri lile neno ila kwa Wayahudi peke yao. 20 Lakini baadhi yao
walikuwa watu wa Kipro na Krene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wayahudi wa Kiyunani,
wakihubiri habari njema za Bwana Yesu. 21 Mkono wa Bwana ukawa pamoja nao watu wengi
wakaamini, wakamwelekea Bwana. 22 Habari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa Kanisa
lililokuwako katika Yerusalemu; wakamtuma Barnaba, aende hata Antiokia.23 Naye, alipokwisha
53 C.P. Wagner, Your Spiritual Gifts Can Help Your Church Grow, pp. 153 - 154.
58
kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la
moyo. 24 Maana alikuwa mtu mwema amejaa Roho Mtakatifu na imani, watu wengi wakaongezeka
upande wa Bwana. 25 Kisha akatoka akaenda Tarso kumtafuta Sauli, 26 hata alipokwisha kumuona
akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na
kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.
Vijana wengi wanao ianza kazi ya Bwana wanahitaji baba na mama wa Kiroho katika upande wao
kupitia hao (baba na mama) ambao huduma hii ya faraja inafanya kazi. Hawa ndio wanatazama
zaidi ya mwanzo wa kujaribu kusita sita, kutambua wito uliotolewa na Mungu na wenye nguvu.
Wanasimama kati kwa maombi na kutia moyo mpaka ushahidi wa wito wa Mungu unakuwa wazi
kwa wote. Ikiwa isingekuwa kwa waamini wenye uwezo huu wa Ki-Mungu, mimi binafsi
nisingekuwa mhubiri wa injili leo.
Huduma hii inahitajika ulimwenguni kote, hasa Afrika, ambapo wachungaji wazee wanaona
vigumu kuwatia moyo na kuwainua vijana wa kike na wa kiume. Badala ya kutambua uwezo wao
wanawaona watumishi wanainuka kama tishio kwa nafasi na madaraka yao. Tofauti ipi ilikuwa
kwa Barnaba ambayo shauku yake kubwa ilikuwa ni kwa maswala ya kanisa na si kwa ajili ya
wadhifa wake. Ijapo kuwa alitambua kuwa Paulo alikuwa amemshinda katika uwezo na nguvu
aliachia uongozi wake bila wivu / kinyongo. Mdogo akawa mkubwa. Msaidizi akawa kiongozi.
Mdogo akawa mkubwa. Msaidizi akawa Kiongozi.
Haikuwa tena “Barnaba na Paulo” bali “Paulo na Barnaba”. Ujasiri huu baadaye ulimfanya
Barnaba asikubaliane kabisa na Paulo wakati alipokataa kumpa Yohana Marko fursa / nafasi
nyingine. Kama mwingine anavyosema, Paulo alifikiria kazi ya Barnaba. Huduma ya Barnaba
ilimfanya ajitenge na Marko kwa ajili ya safari za umishenari pamoja na Paulo kwa ajili ya siku za
baadaye. Lazima ilikuwa ni huruma hii ambayo iliwashawishi mtume kumpa Yose jina lake jipya
Barnaba – “mwana wa faraja”. Ingawa Barnaba hakuandika maandiko, aliwatia moyo Paulo na
Marko, akiwa nao wakati wa majaribu, hivyo alichangia kiasi kikubwa katika kuandika Agano
jipya. Leslie Flynn anaeleza kwa usahihi kwamba kama isingelikuwa kwa ajili ya Barnaba na
huduma yake ya kutia moyo tungekosa nusu ya vitabu vya Agano jipya.54
3. Mtoaji au kutoa
(Warumi 12:8)
Fedha ni mada inayogusa miongoni mwa wakristo. Wahubiri wengi hawajisikii vizuri
kuzungumzia au kuhubiri juu ya fedha, kwa kuhofu kwamba wataeleweka vibaya, na matokeo
yake watu wataacha kutoa kabisa. kama mmoja alivyosema. Neva (nerve) zinayohisi haraka sana
katika mwili wa mwanadamu ni ile inayoelekea kwenye mfuko / fedha.55 Chakufurahisha,
wakufunzi wa Biblia wamesema kuwa Yesu alizungumzia sana juu ya fedha kuliko kitu kingine
chochote. Kwa hiyo ikiwa Bwana wetu alizungumzia juu ya fedha bila kusita, kwa nini sisi
tusifanye hivyo. Tunapozungumzia maswala ya fedha tunafanya vizuri kukumbuka maandiko
yafuatayo:
54 Leslie B. Flyn, Nineteen Gifts of the Spirit (Wheaton: Victor Books, 1974), p. 88 kama ilivyonukuliwa
na C.P. Wagner p. 154.
55 Ibid., p.116.
59
Luka 6:38:
Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwa sukwa hata
kumwagika ndicho watu watakachowapa kifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho
mtakachopimiwa.
2 Wakorintho 9:6
Lakini nasema neno hili; apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.
Kwa nyongeza kwamba wakristo wote wanapaswa kutiwa moyo kutoa (2Wakorintho 9:7), kuna
huduma maalumu ya utoaji. Ralph Neighbour anaeleza kwamba hiki siyo kitendo cha asili, bali ni
uongozi wa Ki-Mungu wa Roho Mtakatifu ambaye huongoza kushiriki kwa imani anachoamuru.56
Neno la Kiyunani (metadidous) kwa kawaida linamaanisha; “Mtu anayegawia “ wengine.
(1) Huduma na haki kwa wote.
Baadhi wanaona utoaji kama uovu. Kwa bahati nzuri kuna wale ambao wameiona kama huduma
yao ya kutoa ni zaidi kuliko mwamini wa kawaida. Utoaji, katika kanisa la kwanza ni huduma
iliyotambulikana sawa sawa na ile ya kufundisha au kuponya, na ilifanyika kupitia neema ya Roho
Mtakatifu. Wale waliokuwa na hali nzuri walikuwa mawakili wa mali zao ili kusaidia kazi ya
Mungu. Barnaba, mwana wa Faraja anatumika kama mfano. Aliitikia hitaji la fedha la kanisa la
kwanza kwa kuuza mali, na kuweka mapato miguuni mwa mitume (Matendo 4:36 –37). Lilikuwa
ni tendo la hiari. Hakuna aliyelazimisha. Tunaposoma Matendo 5:4 tunaona kwamba Petro
alimkemea Anania na Safira kwa kulidanganya kanisa na Roho Mtakatifu na si kwa ajili ya
kushindwa kutoa kanisani. Aliwakumbusha kwamba kiwanja kilikuwa ni chao na baada ya kuisha
kukiuza fedha zilikuwa zao. Hakuna aliyekuwa amewaambia kutoa kanisani. Wakati Barnaba na
wengine walihamasika na huduma ya utoaji, Anania na Safira ambapo walihamasishwa na uchoyo
na kiburi. Katika kiburi chao walitaka kujulikana kuwa ni watu wakarimu. Hata hivyo katika
uchoyo wao walitamani sehemu ya mapato kwa ajili yao.
“Mtoaji” wa kweli atatoa katika ukarimu waKi-Mungu, anajua kutoa kwa wakati unaofaa, na
mahali au watu anaopaswa kuwapa. Anatambua kirahisi hitaji halisi. Huduma hii haikutolewa
kwa washirika wa mwili wa Kristo wenye uwezo/mali tu, bali pia kwa wale wenye kipato cha kati
au wale wenye kipato cha chini. Rafiki yangu Mmishenari wa karibu amethibitisha ukweli huu
mara nyingi. Kwa pato lake la kawaida amesaidia kampeni za kiinjilisti, alinunua kiwanja na vitu
vya kanisa, amewasaidia watumishi mahali pamoja na kupata njia na namna ya kuwasaidia wengi
wenye mahitaji, katika kiwango kwamba watu wanaamini kuwa yeye ni tajiri, kitu ambacho siyo
hivyo. Kimsingi anamruhusu Mungu kumtumia kama njia ya baraka zake, hivyo ndivyo
inavyotenda kazi huduma ya utoaji.
Wale wanaofikiri kutoa zaka zao kama maelezo ya huduma hii wanapaswa kujua kwamba kutoa
zaka ni kiwango cha kawaida ambacho ni cha Mungu (Malaki 3:8-10). Ni mahali pa kuanzia kwa
ajili ya utoaji na siyo mwisho wake. Baada ya kutoa zaka zetu tunapaswa kukumbuka kwamba
90% inayo bakia si yetu bali ni yake vile vile. Sisi ni mawakili tu na si “wamiliki”. Kwa ubinafsi
56 Ralph W. Neighbour, Jr. This Gift is Mine (Nashville: Broadman Press, 1974), p. 46.
60
90% inayobakia kama yetu inazuia baraka za Mungu katika maisha yetu. Ralph Neighbour
anaeleza kuwa tutashindwa kukua katika neema ikiwa tutaendelea kutoa zaka ya mapato yetu tu.57
(2) Taratibu kuhusu huduma hii
Maandiko yanaeleza kwa uwazi kwamba huduma ya utoaji inapaswa ichukuliwe kwa urahisi
(Warumi 12:8) maneno yalitumika katika kiyunani cha ki-koine (haplotes na haplous) yana maana
pana zinazowiana. Maana ya msingi ni, ingawa kwa urahisi kuonyesha usafi, isiyochanganywa na
isiyoghoshiwa. Kwa matumizi zaidi maalumu inaonyesha isiyo na hila.58 Kwa hiyo, wale
wanaoitendea kazi hudma hii wanapaswa kutoa kwa fadhili, kwa mawazo safi, bila kuwa na nia
iliyofichika, na bila kujifanya. Kristo alitumia msemo kama huu. Mkono wako wa kushoto usijue
ufanyalo mkono wako wa kuume, (Mathayo 6:3), likimaanisha kutoa bila kupima/kufikiria kiasi
gani utarudishiwa.
Watu wanaofanya kazi katika huduma hii hawatatumia mali zao kulitawala kanisa. Wale
wanaojaribu kulitawala kanisa na kutumia uongozi kwa hila kwa utajiri wao hawana kipawa hiki.
Watafanya vema kubaki na fedha zao. Waamini ambao wanatoa kiukweli kwa Mungu watajitiisha
wao wenyewe kwa uongozi, na hawatatarajia heshima isiyostahili au kuhudumiwa kipekee zaidi
ya washirika wengine. Nia zao hazipaswi kuonekana, kutambuliwa au kupendelewa kama
mafarisayo, bali wakitoa kwa upendo kwa ajili ya Mungu, asili yake na watu. Hawajionyeshi katika
kutoa kwao kama mafarisayo.
Yesu aliwatahadharisha wanafunzi wake kuwa waangalifu na watu ambao “wanapiga tarumbeta
mbele yao wenyewe” ili wengine waone utoaji wao wa masaidiano. Katika msemo wa siku hizi hii
inamaanisha kwa wale ambao hawatatoa mpaka majina yao yawe yameandikwa kwenye ukuta wa
jengo, bamba la taarifa. Watu kama hao hawajaelewa kanuni ya utoaji wa Kibiblia, huduma hii
siyo ya wazi / ya kuonekana, kama inavyotendeka bila kuonekana na watu, bali na Mungu.
Kutoa si lazima tu kuwe kwa siku maalumu za sikukuu au za majira ya mwaka. Kama mtu mmoja
alivyosema: kutoa baada ya Krismasi –hiyo ni huruma ya kweli. Waamini wanaitenda kazi katika
huduma hii watakuwa na muda wa kutosha kwa mwaka mzima kutoa kwa mambo yanayofaa na
kusaidia wale walio na uhitaji wa kifedha. Watatoa kwa moyo mkunjufu na siyo kwa kinyongo.
Wale wanaotoa pasipo kulazimishwa wanafurahia kuiona kazi ya Mungu inakua, na mahitaji
binafsi yatapunguzwa kupitia zawadi zao wanazozipata. Mara tu mambo ya maana yanapotajwa
hutaka kutoa. Hata hivyo hawatambagua yeyote atakayehitaji / kuomba msaada, bali wamruhusu
Roho wa Mungu kuwaongoza kutoa kwa uangalifu. Wakati huduma hii inatoa vitu au vyanzo vya
fedha Kanisani na kwa watu binafsi kwa furaha na kwa ukarimu, tunapaswa kukazia kuwa utoaji
kama huo unapaswa kuwa katika mipaka ya uwezo wetu. Hatupaswi kutoa katika kiwango
ambacho tunajikuta sisi wenyewe tupo katika madeni. Ikiwa tutakopa kutoka kwa watu wengine
ili kusaidia au ikiwa familia yetu inateseka sana katika uhitaji kwa ajili ya kutoa kwetu, makusudi
yetu mazuri yanavuka mpaka ambao Mungu ameukusudia. Wakati mwingine tunaweza kukaukiwa
na raslimali zetu kwa ajili ya kumsaidia mwingine. Hata hivyo kadri tutakavyofanya chini ya
57 Ralph W. Neighbour, This Gift is Mine, p. 45.
58 Exegetical Dictionary of the New Testament, Volume 1: p. 123.
61
uongozi wa Mungu, ataongezea kurudishia vitu vyetu ili tuweze kuendelea kutoa wakati na sisi
mahitaji yetu yanatimizwa.
Kwa kuhitimisha tunapaswa kuthibitisha kuwa hakuna mwamini ambaye ameondolewa kutoka
kwenye nafasi hii ya utoaji. Wale ambao wanasema: “sina huduma hii, hivyo sihitaji kutoa”,
hawijiibii tu wao wenyewe baraka nyingi bali wanaacha mashaka juu ya wokovu wao. Hii ni kweli
hasa wakati maandiko yanaeleza wazi, “maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda
fedha”(1Timotheo 6:10). Kama mmoja alivyosema, kuna pochi / mifuko mingi ambayo
haijaokoka na kubatizwa leo Kanisani.
4. Masaidiano
(1Wakorintho 12:28)
Neno lililotumika katika kiyunani antilempsis likimaanisha masaidiano, msaada au kusaidia.
Huduma ya masaidiano ina sehemu muhimu katika kila kanisa lenye nguvu. Kama huduma hii
haitakuwepo uongozi utaingia kwenye kazi nyingi zisizo za lazima, zikiwazuia katika wito wao wa
kweli na huduma (Matendo 6:1 –7). Wale waliobarikiwa na Roho hii ya uwezo wa kutoa
wanalitumikia Kanisa kwa kulisaidia katika utendaji majina yao yanaweza yasitajwe mara kwa mara
madhabahuni, na wakati mwingine inaweza ikaonekana hawachangii michango ya “kiroho” katika
ufalme wa Mungu, lakini hata hivyo wanasaidia kwa furaha mahali popote na wakati wowote
inapohitajika. Ingawa masaidiano yamewekewa mipaka katika kusaidia kivitendo, hata hivyo ni
huduma ya kiroho ya utoaji, kwa hiyo haipaswi kuchukuliwa kama ya kawaida au hata isiyo ya
kiroho. Inaweza ikajumuisha majukumu yafuatayo:
Kusaidia ofisini:-
1) Kufanya kazi kama Katibu mhitasi (PS)
2) Utunzaji wa kumbukumbu / masijala
3) Kusaidia kama mtunza mahesabu
4) Rudufu (duplicating), nakili (copying) na utunzaji wa majarada (filing)
5) Kupeleka barua.
Usimamizi
1. Kupanga viti kwenye mikutano
2. Kuhakikisha kwamba chaki zinapatikana kwenye darasa lililotolewa.
3. Kuhakikisha kwamba ubao unafutwa kabla ya kuanza kipindi kingine.
4. Kuandaa usafifi kwa ajili ya wahubiri maalumu, wachungaji n.k
5. Kupika na kuandaa chakula kwa wanasemina.
6. Kutoa vifaa kwa ajili ya mchungaji, kanisa au wamishenari.
7. Kusimamia na kuwa kiongozi wa malazi wakati wa mkutano n.k.
Uhusiano.
1) Kuweka matangazo kwa ajili ya mikutano maalumu
2) Kuwasiliana na vituo vya Redio n.k.
3) Matangazo kanisani
4) Kukaribisha wageni kanisani
5) Kuandaa video au kuonyesha vielelezo vya picha (slide)
Kukarabati jengo.
1) Utunzaji wa vifaa vya Kanisa –kukarabati n.k.
2) Kufanya kazi kama mjenzi
3) Kusafisha jengo la kanisa na mazingira yote.
4) Msimamizi wa mapambo –maua n.k.
62
Vifaa
1) Kurekodi jumbe kwenye kanda za redio au video, hivyo hufanya jumbe ziwepo kwa
wafungwa kama wagonjwa, wazee au wale ambao hawakuwepo kwenye ibada ya siku ile.
2) Kuonyesha sinema za kikristo.
3) Kutumika kama mpiga picha.
Watumishi wengine wanajaribu kufanya haya yote wao wenyewe, na kwa hiyo hawatafanya vizuri
katika wito wao. Hakuna mchungaji anayeweza kufanya kila kitu. Mungu kwa hekima yake
amelibariki Kanisa lake na huduma ya masaidiano.
Ijapokuwa huduma hii haivutii sana, hata hivyo ni muhimu sana, kwa sababu inatoa msaada wa
kiutendaji katika Kanisa la Mungu. Itahakikisha maendeleo mazuri ya kusanyiko la mahali pamoja
na kanisa kwa ujumla. Ni huduma ya Ki-Mungu na wala si ya uwezo wa asili, ingawaje haihudumii
tu mtu wa kiroho. Hata hivyo inahudumia katika mtazamo wa Kiutendaji na mahitaji ya kimwili
ya wengine huendeleza kukubali kwao kwa ajili ya huduma ya kiroho. Tabia yake ya kiroho
inaonekana vizuri katika namna ambayo kazi inavyofanyika, pasipo manung’uniko na malalamiko
bali kwa furaha kama kwa Bwana.
5. Ukarimu
(1Petro 4:9 –10)
Maandiko huwatia moyo waamini wote kuwa wakarimu, kuwakaribisha wageni, na kuorodhesha
ukarimu kama sifa maalumu kwa Wazee / waangalizi (Warumi 12:13; 1Timotheo 3:2; Tito 1:8).
Unatoa maelezo ya wengi ambao walitenda ukarimu na wale walioupokea. Miongoni mwao
alikuwa Bwana wetu, ambaye alikaribishwa katika nyumba ya Mariamu na Martha. Kupitia huo
pia tunajua kwamba Paulo na Wasafiri wanzake walipokea ukarimu wa Lydia , Fibi, Gayo, na ule
wa mwanafunzi wa zamani kwa jina aliitwa Mnasoni, kwa kuwataja tu wachache (Matendo 16:15,
Warumi 16:1-2; Warumi 16:23; Matendo 21:16). Tunasoma zaidi katika Matendo ya Mitume
kuwa Mtume Petro alikaa siku nyingi na Simoni Mtengeneza ngozi (Matendo 9:43).
Wakati tunaposoma katika Agano Jipya, na hasa kitabu cha Matendo ya Mitume tunaona kuwa
ukarimu ulikuwa ukitendeka kwa kawaida katika kanisa la kwanza. Hii inawezekana ilikuwa ni
mwendelezo wa desturi ya Agano la Kale kwa huo Waisraeli walikaribisha wageni waliowakuta
kwenye malango ya mji na kuwakaribisha ndani ya nyumba zao. Hata hivyo historia inatuambia
kuwa ukarimu ulilchukua maana mpya katika mfumo wa utamaduni wa kanisa la kwanza. Wakati
unasafiri katika dola ya Kirumi kwa urahisi kwa sababu ya mabarabara mazuri, na amani ya
Warumi iliyokuwepo, nyumba za wageni zilionekana kuwa na matatizo kwa vile migahawa/
mahoteli mengi yalikuwa madanguro, na mandhari za ulevi na uovu. Hii ndiyo sababu Waamini
walifungua nyumba zao hasa kwa wanafunzi na Wainjilisti wasafiri. Gayo alisifiwa kwa sababu
alifuata tendo hili (3 Yohana 5-8). Yeye na wenzake walitoa nafasi nzuri ambapo wasafiri
wangelikaa. Hata hivyo ukaribisho kama huo haukufanyika kwa walimu wa uongo, hili
ingelisaidia kueneza mafundisho yao ya uongo.
63
2 Yohana 10 –11
10 Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho yao, msimukaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe
salamu. 11 maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu.
Kwa nyongeza katika hili tendo la kawaida la kanisa la kwanza kutoa nyumba za wageni kwa ajili
ya wasafiri walio kuwa wamechoka. Wafasiri wengi wa biblia wameorodhesha ukarimu ni kama
vipawa au huduma nyingine. Katika mazingira ambamo mtume Petro anautamka ukarimu
anashauri kwamba, ijapokuwa haijatamkwa katika orodha mbili za Paulo.
1 Petro 4:9-11
9 Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung’unika; 10 kila mmoja kwa kadri alivyopokea karama,
itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbali mbali za Mungu. 11 Mtu akisema
na aseme kama mausia ya Mungu; Mtu akihudumu na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili
Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na
milele. Amina.
Kulingana na maandiko ya Kale ya Kristo, ukarimu haukupaswa kuzidi zaidi ya siku mbili. Baada
ya hii mgeni alipaswa kufanya kazi kwa ajili ya kujikimu yeye mwenyewe, ili asiishi kwa uvivu kati
yao. Ikiwa atakataa mpango huo alipaswa achukuliwe kama mtu anayelitumia jina la Kristo kwa
manufaa yake mwenyewe (Christ –Monger) 59
(1) Ufafanuzi
Huduma ya ukarimu (Kiyunani philoxenos = ukarimu kwa wageni, kujitoa kwa ukarimu,
kuwapenda wageni) ni uwezo wa Ki-Mungu kutoa nyumba au chakula kwa wale wenye uhitaji,
katika njia hiyo wanajisikia ukaribisho wa kweli. Ukarimu kama huo ni wa tofauti na ule wa
kukaribiswa tu, kwa sababu “ kukaribisha” hudai ukamilifu na hutafuta kuwapendezesha wengine
na mali, ujuzi wa kupika na mambo mazuri ya kijamii, ambayo huweka mkazo katika vitu kuliko
watu.60 Ukarimu wa kimaandiko hautafuti kupendezesha bali kuhudumia wale wanaohitaji
nyumba ambao wako mbali na kwao. Inathibitisha kuwa vitu vyetu pamoja na makao yetu ni vya
Mungu na vinapaswa kutumika katika huduma yake. Ni huduma ambayo kwa furaha na fadhila
huwasaidia wale wenye mahitaji ya chakula na malazi bila kutegemea kurudishiwa chochote.
Ukubwa wa chumba au nyumba inasehemu ndogo tu katika huduma hii ambayo imetolewa na
Mungu. Wale ambao wanayo hii huduma wanajua jinsi ya kuwafanya watu wajisikie
wamekaribishwa vizuri kwa kutoa mahali pa kupumzikia safi na pazuri. Kwa moyo wa ukarimu
wakishirikiana katika nyumba zao, chakula na ushirika pasipo kulazimishwa, ambayo huruhusu
faragha inapohitajika, kumfanya mgeni ajisikie huru na amani. Prisila na Akwila (1 Wakorintho
16:19) na Nimfa (Wakolosai 4:15) na Filemoni (Filemoni 2) ni mifano zaidi katika biblia ya watu
na huduma hii. Chakufurahisha, Yesu anaonyesha kuwa ukarimu utakuwa na sehemu muhimu
katika hukumu (Mathayo 25:35)
(2.) Inavyotakiwa leo
Wengine wanatoa hoja kuwa ukarimu ulikuwa ni muhimu katika ulimwengu wa karne ya kwanza
wakati hapakuwa na mahoteli kama tunavyoyajua leo. Hata hivyo, kwa kuwa hii imebadilika siyo
59 The Didache, (Paulist Press: Mahawh, 1948), p. 23.
60 B.E. Underwood, Spiritual Gifts, Ministries and Manifestations, p.46.
64
muhimu tena kuwakaribisha wahubiri wanaosafiri katika nyumba zetu.61 Hii inaweza ikawa ni
mitazamo wa baadhi ya wafafanuzi wa Biblia ambao hutazama maandiko kutokana na mtazamo
halisi wa kimagharibi au mtazamo wa Kimarekani, lakini kwa uhakika hautumiki katika nchi za
ulimwengu wa tatu ambapo waamini wasafirio hawawezi kukaa katika mahoteli ya gharama
kubwa. Nyumba za wageni ambazo ni za bei ya chini mara nyingi ni sehemu chafu / kama vile
katika siku za Biblia. Kwa hiyo katika nchi nyingi huduma ya ukarimu bado ina sehemu kubwa
katika maisha ya kanisa. Ulimwengu wa magharibi ungelifanya vizuri kama ungelirudi katika
utendaji huu wa Kibiblia, kwa sababu ni chanzo kikubwa cha baraka kwa wale wanaoutenda na
wale wanaopokea ukarimu. Hustawisha / hutajirisha maisha ya hawa wote. Biblia inaeleza kuwa
wale walioitendea kazi huduma hii waliwahudumia malaika pasipo wao kujua (Waebrania 13:2).
Huduma ya ukarimu inaweza ikajieleza yenyewe zaidi katika utawala na kuendesha nyumba za
wageni na za kikristo kama inavyoonekana katika nchi za ulimwengu wa tatu. Wale
wanaosimamia hizo taasisi wanatakiwa wawe na neema ya kutosha ukarimu, na uchangamfu
kuwafanya wengine wajisikie kukaribishwa. Katika matukio mengi mimi mwenyewe binafsi
nimekuwa na fursa ya kuishi katika sehemu kama hizo wakati wa safari zangu katika Afrika. Ni
baraka gani iliyo nzuri na ya kirafiki baada ya kuwa umechoka wakati ukiwa mbali na nyumbani.
6. Utawala - Uongozi
(Warumi 12:8)
Neno la Kiyunani Proistemi linalotumika katika Warumi 12:8 linatafsiriwa kama tawala au utawala
likiwa na maana: Kuelekeza, kuwa juu ya, kutawala, kutunza, kuhusika na, kusimama mbele ya, kuongoza,
na kuhudumia.62 Pia inatafsiriwa kama uongozi. Neno hili limetumika mara mbili katika 1
Timotheo ambapo inaonyesha moja ya sifa za wazee, “yaani mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake
mwenyewe atalitunzaje kanisa la Mungu”? (sura 3:5), na katika sura ya 5:17 ambapo inaonyesha
wajibu wa wazee, “Wazee watawalao vyema na wahesabiwe kustahili heshima mara dufu hasa wao
wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha”.
Kipawa cha huduma hii kinafanya kazi kwa pamoja na huduma zozote za uongozi
zilizoorodheshwa katika Waefeso 4:11. Pia itajidhihirisha kwa viongozi wanaosimamia mipango
fulani au idara za kanisa katika matawi, wilaya, taifa, bara au katika ngazi ya kimataifa. Huwapa
maono, malengo na mipango jinsi ya kutimiza kama ilivyopangwa. Mara kiongozi anapotambua
mahitaji ya kufanyika anasonga mbele na kuelekeza kwa wale wanaofuata. Tumaini lake ni katika
Mungu, imani na uwezo wake kwa kawaida kuhusiana na wale ambao wako pamoja naye
kutaonyesha uongozi wake. Kwa hiyo utawala wake hautalazimishwa, au kufanywa kwa nguvu,
wala kutawala kwa hila. Wale wanaomfuata watafanya hivyo kwa hiari yao.
Kama ilivyoonyeshwa tangia mwanzo wa somo, huduma ya kiroho, na katika uongozi huu,
haifanyi kazi katika dhana ya utemi au ya ukuu (boss). Kuwezeshwa huku kwa Ki-Mungu hakutoi
ngazi kwa wale wanaotaka kutumikiwa, wanaotaka kuwa na huduma hii kwa njia yao, na wale
wanaofurahia kuwatawala wengine.
61 Arrington, Maintaining the Foundations, p. 80
62 Exegetical Dictionary of the New Testament, p. 156. Also W.E. Vine, An Expository Dictionary of
New Testament Words, p. 307
65
Kutetea mamlaka na kutafuta umaarufu siyo kanuni za Agano Jipya, bali hudhihirisha mitizamo
ya kidunia, uchoyo na mambo kama hayo. Hata hivyo, lazima tutambue kwamba licha ya usawa
wa waamini wote, na wazo la uongozi kama mtumwa, Mungu ametoa kwenye kanisa lake wale
walio na huduma ya “utawala” kwa mfano wale wanaoongoza. Ingawa biblia inafundisha ukuhani
wa waamini wote ni dhahiri kwamba kanisa haliwezi kufanya kazi bila viongozi. Mwelekeo katika
makundi mengine ya kanisa kwa kila mmoja kuongoza siyo tu ya kibiblia, bali hatimaye
husababisha uharibifu mkubwa. Kuongoza humaanisha kutendea kazi mamlaka ya kiroho kwa
hekima na uvumilivu na kuongoza kwa mfano.
Wakati huduma ya uongozi inatenda kazi kanisa litakuwa na mwelekeo na litakuwa na utaratibu.
Litazidi kuhakikisha linaendesha mikutano ya kanisa na ya bodi vizuri. Utatoa wenyeviti wa
kamati mbalimbali walio na uwezo, na kulisaidia kanisa kuendelea mbele kwa mipango
madhubuti. Huona utekelezaji wa mipango hii na kutathimini utendaji kazi wao. Mwishowe
hushirikisha mzigo wa kazi na kujua namna ya kuwahamasisha na kujihusisha kwa kadri
inavyowezekana. Huduma ya utawala au uongozi inahitajika katika kila ngazi ya kanisa. Yeyote
ambaye anahusika na kikundi cha watu anapaswa awe na kipawa hiki. Si lazima tu kwa viongozi
wa kimataifa ambao wanafanya maamuzi,bali pia kwa wale wanaosimamia matawi ya kujifunza
biblia katika sehemu za majumbani, au kwa waalimu wa madarasa ya shule ya watoto ya Jumapili.
7. Utawala –Serikali
(1 Wakorintho 12:28)
Huduma ya utawala au serikali (Kiyunani kubernesis) limetolewa na Mungu siyo kukataza au
kuzuia kazi yake, bali kutoa amri, kusudi, uratibu na kuhakikisha utendaji kazi mzuri katika mwili
wake. Unampatia mtu ulazima wa maono na mwongozo, ili aweze kuandaa na kuongoza hadi
kufikia kwenye malengo maalumu, hivyo kufanya kazi ya kanisa kuwa nzuri zaidi. Katika neno la
kidunia la kiyunani jina lilitumika kumwelezea rubani (mtu anayeshikilia usukani) wa meli,
kuiongoza kwa usalama kupita katika dhoruba mpaka bandarini. Tafsiri ya King James inatafsiri
neno la kiyunani kama serikali wakati tafsiri ya NIV inaonyesha kama utawala.
(1) Utawala dhidi ya sheria
Wengi wanaiona huduma ya uongozi na utawala kama zinafanana. Hata hivyo, ukweli
unaonyesha kwamba si wote ambao ni viongozi wenye nguvu ni lazima wawe watawala wazuri
kwa hiyo kiongozi mwenye busara atatafuta wenye uwezo, wanaume na wanawake wanaoaminiwa
kuongoza mambo ya kanisa katika maeneo ambapo hana utaalamu nayo. Viongozi wazuri
hawatajifanya kujua kila kitu bali watajitambua na kukiri uwezo wao.
Maisha ya kanisa la leo linafunua zaidi kwamba huduma ya utawala haiambatani moja kwa moja
na uwezo unaohitajika kwa ajili ya uongozi. Wataalamu wanazifanya kazi walizopewa kwa
mpangilio sahihi, na wanajua jinsi ya kuratibu lakini si, ya watu. Kuhamasisha watu kunahitajika
zaidi ya kupanga mipango. Inahitaji hekima, mbinu, huruma, faraja na imani, kitu fulani ambacho
kiongozi anacho. Watu hawatafuti mipango mikubwa tu bali kwa ajili ya kuwa vielelezo ambao
huongoza katika kutekeleza malengo yaliyowekwa.
66
(2) Eneo la utendaji kazi
Ni wazi kwamba huduma hii imekusudiwa kwa ajili ya makanisa makubwa ambapo wachungaji
wanahitaji msaada wa utawala kuhakikisha uendeshaji mzuri wa kanisa. Watawala wanahitajika
katika usimamizi wa makanisa makubwa. Lakini ni jinsi gani kipawa hiki kinafanya kazi chenyewe
katika kanisa la mahali pamoja ? Je ina maana kwa ajili ya taasisi kubwa tu au makusanyiko
makubwa tu ? Chakufurahisha, kanisa la kwanza kwa uhakika halikuwa na kanisa lolote kubwa,
wala biblia haionyeshi kuwepo kwa vyombo vikubwa vya taasisi. Kwa hiyo kuna uhusiano gani
wa huduma hii ndani ya kanisa la mahali pamoja ? Kwa uhakika viongozi wa kanisa la mahali
pamoja wanapewa kipawa cha utawala kutimiza huduma zao za kuhubiri. Ni wasimamizi wa
shughuli zote zinahusiana na wafanyakazi wa kanisa, kuandaa au kuandika barua, kutunza
mahesabu, kupiga simu, na kusimamia mipango yote kwa ujumla, hivyo husaidia kanisa kufanya
kazi kwa urahisi zaidi. Katika hatua hii tunapaswa kukumbuka kwamba mfano wa Mungu kwa
ajili ya uongozi ni kushirikishana Majukumu na mamlaka. Kulingana na maandiko uongozi wa
kanisa la mahali pamoja siku zote ni wa wote. Hivyo, mambo ya utawala wa kanisa hayapaswi
kuwekwa kwa mtu mmoja peke yake.
Kama tulivyoona mwanzo, kanisa la kwanza lilikuwa na wazee ambao walitawala na wazee ambao
walifundisha na kuhubiri (1 Timotheo 5:13). Katika makanisa yaliyoanzishwa hivi karibuni, na
katika makusanyiko madogo watu walio na huduma hii waweza kuwa wachache, hata hivyo
watakuwepo ikiwa mchungaji kiongozi atakuwa radhi kuwashirikisha majukumu yake. Baadhi ya
majukumu ya kiutawala ya kila siku, kama vile kupiga simu, kuchapa barua, kukusanya, kufungua
na kutuma barua yanaweza kufanywa na katibu wa kanisa. Maamuzi ya kiutawala ni muhimu
zaidi, kupanga, hayo yanapaswa kufanywa na kundi la uongozi ambalo lina huduma hii.
Utawala pia unajihusisha na utunzaji wa fedha. Wale walio na kipawa kwa ajili ya huduma hii
watazitunza fedha kwa uaminifu, na hawazuiliwi katika maono yao na mazingira ya fedha
yaliyopo. Watakubaliana na miradi, ingawa fedha zitakuwa hazitoshi wakati mradi
unapoanzishwa. Kwa imani wanatazama mbele ya hali iliyopo na kutambua kwamba Mungu
atatoa. Hata hivyo, hawataingia kwenye miradi bila ya kuwa na uhakika wa ndani kwamba mradi
uliotolewa ni wa Mungu.
Mtawala wa kweli hataweka mipango zaidi ya uwezo alio nao, bali ataacha nafasi kwa ajili ya
utendaji wa Roho Mtakatifu. Sifa hii itaonyesha kama utawala wake ni wa uwezo wa asili /
kawaida au ni matokeo ya wito wa Kimungu.
8. Kuonyesha Rehema
(Warumi 12:8)
Kuishi katika moja ya miji mikubwa ya Afrika iliyo na baadhi ya maeneo makubwa ya maisha ya
hali ya chini katika bara hili inaleta maana mpya kwenye huduma ya kuonyesha rehema. Wakati
inapokabiliwa na hali ngumu na uhitaji wa kutisha unaoenea katika maeneo haya ufukara na
sehamu za kuishi za hali ya chini na katika hali duni, unajiuliza, tunaanzia wapi na inaishia wapi.
Ni kazi kubwa na yenye nguvu kuwasaidia watu katika hali hizo au mtu yeyote anayeishi katika
hali ya umaskini. Hata hivyo wenye rehema hawashindwi kirahisi. Kupitia Roho wa Mungu
67
wanatambua wazi mipaka yao na kuhusika kwao. Kadri wanavyofuata uongozi wa Mungu
hawapokei tu yale anayoyatoa, anawawezesha kusaidia, bali wanavumilia katika upendo wao na
huruma kwa wale wasio na vitu katika jamii.
Neno la Kiyunani (eleeo) linaonyesha kama ifuatavyo huruma, wema au nia njema kwa wenye
taabu na wenye mateso, wakishirikiana kwa nia ya kuwafungua na utayari wa kuwasaidia wale
waliopo katika mateso.63 Inaweza kutafasiriwa zaidi; kuonea huruma kwa ajili ya mateso ya mtu
mwingine, huruma ambayo inajidhihirisha wenyewe katika utendaji, kuhurumia, kuwa na huruma
juu ya, kuonyesha fadhila.64 Kwa hiyo, huduma hii ni zaidi ya kujisikia huruma au kusikitika kwa
ajili ya wasiokuwa na mahitaji. Huenda zaidi ya hisia zozote na kujihusisha kabisa kujaribu
kuondoa taabu ya aliye na mateso. Huweka huruma ya kweli isiyokuwa na ubinafsi, ambayo
hububujika kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu kupitia kwa mwamini hadi kwa wengine
wenye uhitaji wa pendo na uangalizi wa Mungu. Wale waliompazia sauti Yesu “tuhurumie”
walihitaji zaidi ya hisia za kawaida. Walihitaji kitendo. Walimtegemea yeye azuie na kuingilia
mateso yao. Ndivyo ilivyo hata leo. Kuonyesha huruma au kuhurumia hakutoshi. Maandiko
hutegema kuonyesha rehema katika utendaji, kama Yakobo anavyoonyesha katika sura 2:15-16:
Ikiwa ndugu mwanaume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, 16 na mtu wa kwenu
akamwambia, enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili
yafaa nini ?
Kama vile huduma ya utoaji, kuonyesha huruma vinapaswa vitendeke chini ya uongozi wa Roho
Mtakatifu, vinginevyo atashindwa na mahitaji yanayotuzunguka. Paulo anasihi “tuwatendee watu
wote mema, na hasa jamaa ya waaminio” ni ushauri mzuri (Wagalatia 6:10). Katika mwili wa
Kristo kuna wengi wenye dhiki, vilema, wasiopendwa, watu wenye jazba wanasubiri rehema na
huruma ionyeshwe kwao. Hawa tunapaswa kuwasaidia kwanza. Hata hivyo hii haina maana
kwamba hatupaswi kuwafikia wale walioachwa na jamii, masikini, walioathirika, ombaomba,
wasio na kwao, makahaba, wasiopendwa, na wale wote walio katikati ya mji ambao hawana
makao. Lakini kama methali isemavyo:- “wema wa mtu huanzia kwao”. Ni wema gani ikiwa
tutaonyesha rehema kwa wale walio nje ya mwili wa Kristo na kupuuza mahitaji ya ndugu na dada
zetu walio katika Kristo.
Kuonyesha rehema, ni kama tu huduma ya masaidiano ni tendaji katika asili. Wakati
“masaidiano” humfungua kiongozi wa kiroho kutoka kwenye kazi mbalimbali za kiutendaji, na
kumkamilisha katika utendaji wake kwa kumsaidia katika maeneo ambapo anaweza akawa na
ufahamu kidogo au hana kabisa, huduma ya rehema imeelekezwa kwa Watakatifu waliokwenye
shida. Imeelekezwa katika mwili wote wa Kristo, na wakati inapokuwa inatendeka, inatumika
zaidi katika kiwango cha kiroho.
Baada ya kuzitambua huduma katika Agano Jipya, zile huduma zote kwa ajili ya uongozi na zile za
asili za kiutendaji zaidi sasa itakuwa muhimu kuona ni jinsi gani tunaweza kuwasaidia wale
waliojitoa katika uangalizi wetu kutambua sehemu za huduma yao na eneo la kazi. Kabla
63 Joseph H. Thayer, Greek - English Lexicon of the New Testament,, p. 203.
64 W.E. Vine, An Expository Dictionary of New Testament Words, p. 60. Also Leslie Flyn, 19 Gifts of
the Spirit, p. 133.
68
hatujaenda katika sehemu ya mwisho ya somo hili tukumbuke tena kwamba huduma zote ni za
muhimu. Wakati huduma nyingine zinaonekana zaidi na ni wazi kuliko nyingine, zote ziko sawa
na ni muhimu mbele za Bwana. Hebu sasa tuangalie baadhi ya kweli muhimu kuhusu huduma za
Agano Jipya, baadhi yake tumekwisha kionyesha.
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-
69
IV. KUTAMBUA SEHEMU YA HUDUMA YETU
Wale walioitwa kuhubiri hivi karibuni au baadaye; kwa ushahidi wa huduma yao, watatambua
huduma ambayo watatumika. Wachache kama mtume Paulo watajua huduma zao maalumu
katika kipindi cha wito wao. Hakuwa na uhakika tu wa wito wake kuhubiri bali alijua kwamba
alitengwa kuipeleka injili nje ya mipaka ya Israeli. Hata hivyo Paulo alionekana miongoni mwa
manabii na waalimu kule Antiokia (Matendo 13:1) kabla hajapata kibali cha kazi ya mtume.
Wengi wa wahubiri; eneo dhahiri la huduma litakuwa wazi tu kadri utendaji kazi wao
utakapokuwa wazi wakati wakifanya uinjiilisti, wanachunga, wanafundisha, kuanzisha makanisa au
kutangaza mapenzi ya Mungu kama nabii. Hivyo, wito wa kawaida wa kuhubiri hubadilika kuwa
wito maalumu.
Huduma tano za kuhubiri au za uongozi huvuka mipaka ya vipawa vya asili / kawaida. Hawawezi
kufanya kitu chochote bila uwezo wa kawaida /asili uliotakaswa kwa sababu ni wa tabia ya Ki-
Mungu kabisa na zinaambatana na wito wa Ki-Mungu halisi. Kwa upande mwingine, huduma za
masaidiano mara zote zinahusiana na uwezo wa asili / kawaida. Vipawa kama vile kuimba,
ufundi useremala, uashi nk.), kuandika na vingine ambavyo Mungu aweza kuvitumia na
kuvitakasa wakati tunapojikabidhi kwake. Vipawa kama hivyo wanavyo waliookoka na
wasiookoka vilevile. Hata hivyo, hivi vipawa vitakuwa huduma kama Mungu ataongeza upako na
baraka zake.
Wale wasiokuwa na wito wa kuhubiri inawezekana wasijue nafasi zao katika mwili wa Kristo,
kama vile huduma ya wale walioitwa kutangaza injili. Hata hivyo, wana shauku kubwa ile ile ya
kumtumikia Mungu na kufanya mapenzi yake, na kumsubiri aseme nao moja kwa moja.
Wanapaswa kukumbuka kwamba katika mambo mengi zaidi Mungu huwaongoza kwa urahisi
zaidi wale ambao wamekwisha anza katika sehemu zao walizoteuliwa katika shamba lake. Wale
wanaoshindwa kujihusisha kwa sababu hawajui huduma zao, inawezekana wasijue wako katika
huduma gani. Kwa upande mwingine wale wanaouliza ni kitu “gani kinahitajika kifanyike”
watapata sehemu zao kwa urahisi zaidi. Kadri tunavyojitoa kwa Mungu atatusadia kupata sehemu
ya kazi zetu. Kuhakikisha kuwa tumeipata inawezekana kama ifuatavyo:
(1) Utendaji kazi, kama Mungu aongezavyo baraka zake.
(2) Kanisa kuitambua huduma/wito
(3) Nafasi hupatikana kufanya kazi katika huduma
(4) Ushahidi wa kuwezeshwa Ki-Mungu kuitendea kazi huduma aliyopewa.
Peter Wagner anashauriwa kwamba tunapaswa kuzijaribu huduma mbalimbali mpaka tumeipata
ile ambayo Mungu anatutaka tuitumikie.65 Wakati hii inaweza kutupeleka mbali sana, tunapaswa
kutambua ukweli kwamba hata Stefano na Filipo walihudumu mezani kabla ya kupokea wito wao
kama wainjilisti. Hata hivyo, kwao halikuwa ni jambo la kuzijaribu huduma mbalimbali, bali
walikuwa tayari kwa Bwana. Mungu hutoa nafasi mbali mbali za kupata sehemu zetu za kufanyia
kazi, tukimuuliza katika maombi. Badala ya kuzifanyia majaribio karama nyingi, kama
inavyoshauriwa na Wagner, ninaamini kabisa kwamba utafiti wa muda mrefu na wa kukatisha
65 C.Peter Wagner, Your Spiritual Gifts Can Help Your Church Grow, pp 119-120
70
tamaa unaweza ukaepukwa au angalau ukafupishwa ikiwa tutamtafuta Mungu kwa bidii kuhusu
nafasi zetu katika ufalme wake.
1. Jinsi ya kutambua sehemu zetu
Mungu anataka kila mwamini ajihusishe kikamilifu katika ufalme wake. Ili kujua sehemu zetu
tunapaswa kuwa makini katika sauti na uongozi wake, na tunapswa kuwa katika utendaji. Kama
vile gari litembealo linaweza kuongozwa katika mwelekeo wowote, vilevile Mungu huongoza wale
ambao ni watendaji na wale waliotayari kuongozwa. Hii ina maana kwamba kuwa tayari kwa kazi
yoyote ambayo itajitokeza kanisani. Wanapopewa kazi inaposwa ichukuliwe katika maombi, kwa
kumuuliza Bwana ikiwa hii inaweza ikajitokeza kuwa huduma. Uaminifu, uvumilivu, kuangalia
mahitaji yanayopaswa kufanyika na kutafuta mahitaji ya wengine na kanisa litatusaidia kutambua
sehemu zetu na eneo la huduma. Kwa nyongeza, tunapaswa kutambua kuwa wachungaji
wanashikilia funguo kwa ajili ya kuwasaidia washirika kujua sehemu zao. Sio tu wanapaswa
kuwatahadharisha tofauti mbalimbali kupitia mafundisho, bali pia kwa kutoa nafasi kwa ajili ya
huduma.
Mara waamini watakapokuwa wamefundishwa na kujua maeneo yao ya kazi, viongozi watavuna
faida. Mzigo utashirikishwa kwa watu wenye uwezo na kanisa litakua. Uratibu mzuri wa
huduma katika kiwango cha kanisa la mahali pamoja kimsingi humtegemea mchungaji. Anapaswa
kuhakikisha kuwa na ushirikianao wa pamoja wa washirika wote.
Waamini wanateseka na “dalili za kiroho za kipepeo” ambazo huwachukua kutoka kanisa hili hadi
lingine, wakitafuta maono ya siku za leo na misisimko ya kiroho, itakuwa vigumu kutambua
sehemu zao za kufanya kazi katika mwili wa Kristo.
Uwajibikaji hupewa nafasi ya juu katika orodha ya vipaumbele vya Mungu. Kwa hiyo wale
wanaotembelea kanisa baada ya jingine na dhehebu baada ya lingine hawawezi kuwa na kiwango
hiki cha Ki-Mungu, ambacho ni sehemu muhimu ya kila huduma. Ni wale tu wanaojihusisha
katika kusanyiko la mahali pamoja, wakiwa hapo na kuwa washirika wa siku zote na wa
kutumainiwa watatambua sehemu zao za kazi.
Wengine wanahofu kujitoa wao wenyewe kwa ajili ya huduma kwa sababu wana mawazo potofu
kwamba kutenda mapenzi ya Mungu ni sawa na kuwa na taabu na kutokuwa na furaha. Wazo la
kwamba la kufurahia maisha, na katika huduma ya furaha, ni kinyume na mapenzi ya Mungu,
ambayo mizizi yake ni katika uchaji wa Mungu, na imevuta mawazo ya wengi. Lakini kumtumikia
Mungu kunachekesha ! hata kazi ambazo wengine wangezifikilia kwamba hazipendezi zinaweza
zikafanyika kwa moyo alioujaza na furaha.
Peter Wagner anaonyesha jambo la maana anapoelezea, Mungu anajua kila kitu cha hali ya miili
yetu, na nafsi zetu. Anajua hisia zetu na anafahamu kwamba ikiwa tunafurahia kufanya kazi
tunafanya kazi njema, kuliko ikiwa hatuifurahii kwa hiyo sehemu ya mpango wa Mungu
inaambatana na kipawa cha kiroho ambacho hutupatia pamoja na hisia zetu katika njia ambayo
tunajisikia vizuri kuitumia. Mtazamo wake unaungwa mkono na maandiko kama Zaburi 37:4
“Nawe utajifurahisha kwa Bwana, naye atakupa haja za moyo wako”.Ambayo inaonyesha kwamba
71
kibiblia hakuna kutokubaliana kati ya kujifurahisha sisi, wenyewe na kumpendeza Mungu.66 Ikiwa
huduma yetu zitaendela kukauka, itasababisha kutopata usingizi na “itapokelewa kama kitu
kisicho faa kwa wengine, tunaweza kuwa na uhakika kwamba hatufanyi kitu ambacho Mungu
alikusudia tukifanye.
2. Jinsi ya kutumika katika huduma yetu
Waamini ambao wametambua maeneo yao ya huduma na wanahusika katika huduma wanapaswa
kufuata miongozo fulani ili kuwa watendaji kazi wazuri. Kwa hiyo ni muhimu kufikiri yafuatayo:-
(1) Fahamu huduma na kazi ndani ya mipaka yake
Kwa sababu ya upungufu wa watendakazi katika kanisa watu mara zote wamejihusisha katika
huduma ambazo hawakuitiwa. Hata hivyo ulazima unaonyesha kuhitaji kwa wakati, haipaswi
kamwe kuvumiliwa kwa wakati wote. Kadri tutakapokuwa tunatenda ndani ya wito wetu tu
tunaweza tukazaa matunda. Kwa mfano wale walioitwa kama Mchungaji hapaswi kufanya kazi
kama mwinjilisti kwa muda wote na si vinginevyo. Mtu mmoja alisema, “ Unaweza ukatumia
Koleo (pliers) kupigilia msumari kwenye ukuta, lakini nyundo yaweza kufanya kazi vizuri zaidi”.
Ndivyo ilivyo katika ulimwengu wa kiroho. Ikiwa mtu ni mwinjilisti anaweza akafanya kazi ya
kichungaji kwa muda, lakini kamwe hawezi kufanya kazi vizuri kama mchungaji. Hivyo ndivyo
ilivyo kwa huduma nyingine zote.
Kitu kibaya zaidi ambacho kinaweza kutokea ni kwamba mtu mmoja anategemea kufanya kazi
vizuri zaidi kama mwinjilisti, kwa wakati uleule anakuwa mtawala bora sana, mshauri mzuri,
mwalimu mzuri, na vilevile mchungaji mashuhuri na hata nabii mwenye upako. Kwa nyongeza
anategemewa kufanya miujiza, kuponya wagonjwa, kuongoza uimbaji na kukusanya sadaka. Hii
inaonekana imevuka mpaka, lakini inakuwa karibu na kila kinachotendeka katika baadhi ya
makanisa. Mtu aliye katika hali hiyo hawezi kamwe kufanya haki katika matakwa haya yote. Kwa
wakati huo huo yatamzuia kufanya kazi katika huduma aliyoitiwa. Hivyo, atashindwa kufanya
kazi vizuri katika wito wake wa kweli. Wakati mwingine tunaweza kujaza nafasi ijapokuwa hatuna
kipawa kwa huduma hiyo. Kwa vile huduma hii ni ya muda kwa sababu ya hali ya dharura
hakuna madhara yatakayotokea. Hata hivyo, ikiwa tutashindwa kurudi kwenye eneo ambalo
tuliloitiwa tutapoteza utendaji kazi wetu na usioleta matunda.
(2) Ridhika
Kuwa na wivu katika huduma nyingine kuliko huduma zetu hakutasababisha tu kukatishwa tamaa
na kutoridhika bali kunaweza kutuongoza katika hukumu ya Ki-Mungu. Katika 1 Samweli 13, na
2 Mambo ya Nyakati 26:16-20 tuna mifano miwili ya kibiblia ambayo watu hawakuridhika na wito
wao. Uzia na Sauli wote walinyoosha mikono yao katika huduma ya mtu mwingine, matokeo
yakawa ukoma kwa Uzia na kwa Sauli alipoteza ufalme. Tunapaswa kukumbuka kwamba hatuna
uchaguzi bali tuikubali huduma ambayo ametupatia (Waefeso 4:11). Mungu hafanyi makosa wito
wake unazingatia nafsi zetu, uwezo na kukua kiroho. Kwa hiyo hakuna haja kwetu kuona wivu
bali kufanya vizuri katika huduma ambayo tumeipokea.
66 Peter Wagner, Your Spiritual Gifts Can Help Your Church Grow, pp. 123-124.
72
(3)Milki mpaka ajapo
Mfano wa talanta unatupa onyo kali tusichukulie huduma kiurahisi, bali ni kumiliki (kushikilia au
kujaza nafasi, kutwaa mali na kudumisha utawala au kujaza nafasi, kutwaa mali na kudumisha
utawala au kama vile kwa kushinda au kujishughulisha, 67) mpaka ajapo (Luka 19:13 –25). Ukweli
ni kwamba Yesu alisema mfano huu ukionyesha kwamba watu wengine ambao walipokea wito
kwa mfano huduma haikuendelea kwa sababu wao wenyewe walishindwa kujitoa katika huduma.
Hujishughulisha wao wenyewe na mambo ya kidunia na kushindwa kuvitumia vipawa vyao kwa
sababu vinaonekana havina maana kwao. Kama wanafunzi wake tunapaswa kukumbuka kwamba
hatutatoa tu hesabu ya maneno na matendo yetu bali pia ya fedha ambazo tumekabidhiwa
kuzilinda. Wakati tunaposimama mbele ya hukumu ya Kristo atatuona tu wema na watumwa
waaminifu.
Luka 19:13-30
13 Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, fanyeni
biashara hata nitakapokuja. 14 lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata
na kusema hatutaki huyu atutawale. 15 Ikawa aliporudi ameupata ufalme wake aliamuru waitwe wale
watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake. 16 Akaja wa kwanza
akasema, Bwana fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi. 17 Akamwambia, vema, mtumwa
mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi. 18
Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida. 19 Akamwambia huyu
naye, Wewe uwe juu ya miji mitano. 20 Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo
nililiweka akiba katika leso. 21 Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mugumu; waondoa
usichoweka, wavuna usichopanda. 22 Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa
mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda; 23 basi,
mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake ? 24
akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi. 25
Wakamwambia, Bwana anayo mafungu kumi. 26 Nawaambia, kila aliye na kitu atapewa, bali yule
asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho. 27 Tena wale adui zangu, wasiotaka niwatawale,
waleteni hapa muwachinje mbele yangu. 28 Na alipokwisha kusema hayo, alitangulia mbele akapanda
kwenda Yerusalemu. 29 Ikawa alipokaribia Bethfage na Bethania, kwenye mlima uitwao wa mizeituni,
alituma wawili katika wale wanafunzi, 30 akisema, Nendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na
mtakapoingia ndani mtaona mwanapunda, amefungwa, ambaye hajapandwa na mtu yeyote bado,
mfungueni mkamlete hapa.
3. Jukumu katika huduma yetu
Huduma katika mwili wa Kristo una sehemu mbili, moja ya Ki-Mungu na nyingine ni ya
kibinadamu. Wajibu wa Mungu ni kuita na kuwawezesha wale anaowachagua. Kwa upande
mwingine sisi tunapaswa kuonyesha kuwajibika kwa kujitoa kwake na kwenye huduma
tulizopokea, kuishi maisha yanayofaa ya watumishi wake, na kujazwa na Roho wake. Huduma ina
gharama ! inahitaji kujiweka wakfu na kujitoa.
(1) Jitoe kwenye huduma
Mara tutakapojua eneo letu la huduma tunapaswa kujitoa sisi wenyewe kwenye huduma.
Huduma haijitokezi tu yenyewe. Tunapaswa kujitoa sisi wenyewe katika huduma ambayo
67 The American Heritage® Dictionary of the English Language, Third Edition copyright © 1992 by
Houghton Mifflin Company. Electronic version licensed from InfoSoft International, Inc. All rights reserved.
73
inahusisha maombi, kufunga, maandalizi na utii. Changamoto ya maandiko “kutembea katika
Roho”hutendeka hasa kwa wote ambao wanatendea kazi na kufuata wito wao. Uzembe
unaweza kuingia/kuonekana katika kazi nyingine ya ujuzi/utaalamu ijapokuwa hii ni tofauti, bali
si katika huduma, kwa kuwa hatuwafanyii kazi wanadamu bali Mungu. Kujitoa na kujiweka
wakfu sisi wenyewe ni muhimu sana kwa vile vipawa haviwezi kufanya kazi bila ya kuhusika
kwetu. Kushindwa kufanya hivyo kutatambuliwa na wale ambao tunapaswa kuwatumikia. Hii
inaonyesha kwamba kwa mfano nabii anapaswa kutumia muda mwingi kwa uhusiano wa karibu
na Mungu, mwalimu anapaswa kutumia muda mwingi kujifunza na kuandaa.
(2) Ishi maisha bora ya utumishi wa Mungu
Kila aliyepokea huduma ana wajibu mkubwa kwa Mungu na kwa wenzake. Si tu anapaswa
kuitunza imani yake kwa nguvu (Warumi 12:6-8), bali anapaswa kutimiza tabia na sifa fulani kama
ilivyoelezwa mapema. Paulo anaonyesha kirahisi, bidii na furaha, na kuonyesha kwamba haijalishi
sana kila tunachofanya, kama kwa jinsi tunavyofanya. Kumtumikia Mungu hakukufanyi moja
kwa moja kuwa mtakatifu, bali huhitaji zaidi sharti la mwanzo. Kwa hiyo, watu katika nafasi za
uongozi wanapaswa siku zote wajitahidi kuishi maisha ya Kiungu. Kuonekana zaidi huhitaji
sifa/tabia bora. Hii haionyeshi kwamba wengine ambao wanatumika katika mwili wa Kristo
katika huduma zinazoonekana kidogo kama vile wasaidizi, watoaji, au wakarimu hawapaswi
kutimiza sifa zile zile. Kila mshirika anapaswa kuonyesha asili ya Kristo.
(3) Ujazwe na Roho
Kristo aliwaagiza Wafuasi wake kusubiri Yerusalemu mpaka wamepokea nguvu ya Roho
Mtakatifu. Ndipo tu wangepaswa kupeleka injili pande zote za ulimwengu. Leo tunakabiliana na
ukweli kwamba wengi wapo katika huduma bila ya kuwa na ubatizo wa Roho Mtakatifu, hasa
walio nje ya upentekoste na makundi ya wanauamsho. Ni wazi kwamba kuna wachungaji wengi
wa kweli, waalimu na wainjilisti huitendea kazi huduma yao bila ya kuwa na Roho Mtakatifu.
Hata hivyo upotofu huu wa kutoka kwenye maandiko, haupaswi kupokelewa kama kanuni.
Vinginevyo tunapaswa kujitahidi kurudi katika mfano wa kibiblia. Kutokubatizwa na Roho
Mtakatifu kutakuwa na baadhi ya matokeo yafuatayo:-
(1) Bila ya ubatizo wa Roho Mtakatifu huduma itakuwa na upungufu mkubwa na itakuwa
na vikwazo kwa vile hukosa nguvu na upako ambao Mungu ametoa kwa kila
aliyemwita. Wachungaji, Wainjilisti nk. Wanaohudumu bila ya ujazo wa Roho
Mtakatifu wataweza kutumika kwa sababu Mungu amewaita, lakini hawatatenda vizuri
zaidi kama Mungu alivyowakusudia wawe. Kwa kusema hivi moja kwa moja maswali
yanajitokeza. Je ni vipi Wainjilisti wakubwa na waliofanikiwa nje ya upentekoste na
wana uamsho ? Swali hili laweza kujibiwa tu kwa swali jingine. Je ni makosa kufikiria
kuwa huduma yao ingelikuwa nzuri zaidi ikiwa wangelikuwa wamebatizwa kwa Roho
Mtakatifu?
(2) Huduma ya kitume na ya kinabii, na kwa kiwango fulani huduma ya mwinjilisti
haiwezekani kufanyika bila ya ubatizo wa Roho Mtakatifu, kwa sababu huduma hizi
zinaingiliana sana na madhihirisho ya vipawa na zinategemeana sana.
74
Katika Matendo 6 tunasoma kwamba hata wale saba, walichaguliwa kuhudumu mezani, walipaswa
kuwa wamejazwa kwa Roho. Kwa hiyo ikiwa ilikuwa ni sifa ya kufanya hata kazi za kawai-da,
kila mmoja anayejihusisha kutangaza Neno la Mungu anapaswa kujitahidi kwa ajili ya ule u-jazo
wa Roho mtakatifu. Kwa muda mrefu mwili wa Kristo umeruhusu desturi za dini kutoa masharti/
amri kwa ajili ya sifa katika huduma. Ni wakati unaofaa kurudi katika masharti ya kibiblia
ambayo kwa huo ujazo wa Roho ni mhimu sana. Hakuna mafunzo ya kielimu, digrii, ujuzi wa
kuitawala na mipango iliyoandaliwa vizuri inaweza ikasimama badala ya hitaji hili la Kimungu.
Ujazo wa Roho huleta asili za Ki-Mungu katika huduma. Ndani ya huduma ya kitume, kinabii na
vilevile ya kiinjilisti hii inaweza kutambulikana kirahisi. Katika huduma ya kichungaji na
kufundisha inaweza isiwe dhahiri, na hata inaonekana kidogo katika huduma za masaidiano, kutoa
utawala nk. Bali ipo na inaweza kutambulika kwa vile ni sehemu muhimu ya upako wa watumishi.
Kila huduma itakuwa na asili ambayo haiwezi kupatikana katika uwezo wowote wa asili. Inaweza
kuwa ni vigumu kuifafanua, bali wale walio wa Kiroho watatambua, ingawaje hawataweza
kuielezea. Asili ya Ki-Mungu katika huduma za masaidiano zitatambulikana hasa jinsi
zinavyoendeshwa. Wale walioitwa hawataiona kama kutimiza tu wajibu bali kama huduma kwa
mfalme. Kwa sababu ya ishara za Marko 16:17-18 haziishii tu katika vipawa vya uongozi, watu
ambao huwahudumia wasafiri katika nyumba zao, huonyesha rehema, kutoa, kutawala,
masaidiano vitaonyesha nguvu ya uponyaji wa Mungu na miujiza itaonekana katika kujibu
maombi yao, na kama sehemu ya huduma zao.
4. Kuna nini cha kufanya?
Kabla ya Kristo kurudi Mbinguni hakuliacha Kanisa na Uongozi tu bali aliliacha na huduma
nyingi mbali mbali. Kwa hiyo hakuna udhuru kwa yeyote kushindwa kujihusisha kuweka hali ya
kuzitambua huduma, na kumsaidia kila mshirika kuelewa huduma yake. Kwa upande mwingine
kila mwamini anapaswa kujitoa yeye mwenyewe kwa Mungu na kuwa tayari kwa ajili ya “uteuzi”.
Orodha ifuatayo inaweza kutusaidia kuona baadhi ya huduma mbali mbali zinazowezekana katika
kanisa la leo, zikitenda kazi kulingana na mfumo wa Agano jipya.
Kiroho
 Kuwa kiongozi wa Kanisa la nyumbani
 kuwa kiongozi wa sifa katika kanisa la
nyumbani
 Kufikia vikundi vidogo kama vile vya
jamii ya Ki –Asia, jamii ya Kizungu, moja
ya makabila madogo yanayoishi katika
eneo lako.
 Huduma za Wanawake
 Huduma za wababa
 Huduma za Vijana
 Huduma kwa watoto (wa umri tofauti)
 Huduma Vijana wa miaka 13 –19
 Huduma kwa Wazee
 Kupiga vyombo –gitaa, kinanda, ngoma
Utendaji
 Kuwa na Kanisa la nyumbani kwako
 Fanya kazi kama ujenzi
 Msimamizi wa miradi ya ujenzi
 Kuwa bwana mipango / mpangiliaji
 Kusaidia kiutendaji kama fundi umeme,
fundi magari, fundi seremala n.k.
 Kuwa mtoaji
 Mgawaji wa misaada
 Kiongozi wa kugawa misaada
 Huduma ya fedha –kusaidia
 Kuhesabu sadaka, kutunza kumbukumbu za
mahesabu ya fedha.
 Kuwa mtawala
 Kuwa Katibu
75
 Kuwa sehemu ya kikundi cha sifa
 Kuwa kiongozi wa kikundi cha sifa
 Maombezi
 Kuwa sehemu ya kikundi cha uinjilisti
 Kuanzisha makanisa
 Huduma katika watoto wa mitaani
 Huduma kwa wakimbizi
 Kuwa Shemasi
 Kuwa Mzee
 Kuwa mshauri
 Huduma ya kukaribisha wageni
 Huduma ya kutembelea
 Anayeshirikisha meza ya Bwana.
 Kusaidia kama mtaalamu wa kompyuta
 Huduma ya mabasi
 Kutumika kama dereva wa kanisa au
 uongozi wake
 Ukarimu
 Kutoa malazi kwa wageni
 Kupika kwa ajili ya mikutano, semina au
mikutano mingine maalumu.
Orodha hii siyo kwamba imekamilika kwa vyovyote vile, lakini inaweza ikatoa wazo la uwezekano
wa huduma. Wale ambao wanamtafuta Mungu kwa bidii kwa ajili ya huduma zao katika ufalme
wake waweza kuhakikishiwa kwamba atawasaidia kutambua na kuona eneo la huduma yao.
Hitimisho
Waamini ambao wanasubiri huduma “ziwatafute” inawezekana kabisa wasijihusishe katika
kupanua ufalme wa Mungu. Wengine ambao wanasubiri kazi ambayo huwapa umaarufu, heshima,
madaraka na hali ya kuridhisha ya kazi kabla hawajawa watendaji wazuri hawajaelewa kanuni za
huduma ya Agano jipya. Hata hivyo, ikiwa tutaiendea huduma tukiwa na utayari wa kutumika na
kuwa wazi mbele za Mungu kutoongoza, kwa uhakika tutatambua huduma yetu katika ufalme
wake, kuzaa matunda, watendaji kazi wazuri na kuwa baraka kwa wengine.
Tutakapokuwa tuna uhakika wa sehemu zetu katika huduma, na tufanye vizuri kwa kujitoa kwa
Bwana na kujitoa sisi wenyewe kwa moyo wote katika huduma. Katika sehemu yoyote tutakayokuwepo
katika ufalme wake hebu tuitendee kazi huduma kwa kusudi moja. Kumtukuza Bwana
wetu na mwokozi Yesu Kristo kwa ajili ya kuupanua ufalme wake na kulijenga Kanisa lake.
-.-.-.-.-.-.-.-.-
76
BIBLIOGRAPHY
Ancient Christian Writers. The Didache. New York: Paulist Press, 1948.
Arrington, French, L. Divine Order in the Church. Grand Rapids: Baker Book House, 1978.
_____________. The Acts of the Apostles. Peabody: Hendrickson Publishers, 1988.
_____________. Maintaining the Foundations. Grand Rapids: Baker Book House, 1982.
Austin-Sparks, T. Prophetic Ministry. London: Billing & Sons, 1973
Bauer, Walter.; Gingrich F. Wilbur.; and Danker, Fredrick W. A Greek-English Lexicon of the New
Testament and Other Early Christian Literature. Chicago: University Press. 1979.
Bittlinger, Arnold. Im Kraftfeld des Heiligen Geistes. Marburg: Ökumenischer Verlag, 1976.
Canty, George. The Practice of Pentecost. Basingstoke: Marshall Pickering, 1987.
Conn, Charles W. A Balanced Church. Cleveland: Pathway Press, 1975.
Conner, Kevin J. The Church in the New Testament. Portland: Bible Temple Publishing, 1989
Damazio, Frank. The Making of a Leader. Eugene: Church Life Library, 1987.
Early Christian Writings. The Apostolic Fathers. London: Penguin Books, 1987.
Endersheim, Alfred. The Life and Times of Jesus the Messiah. McLean: Mac Donald Publishing
Company, n.d.
Enhanced Strong’s Lexicon. Oak Harbor: Logos Research Systems, 1995.
Exegetical Dictionary of the New Testament. 3 Vol. Grand Rapids: Eerdmans Publishing Company,
1990.
Fairweather, William. The Background of the Gospels, Judaism in the Period between the Old and New
Testament. Minneapolis: Klock & Klock Christian Publishers, 1977.
Fee, Gordon. The First Epistle to the Corinthians. Grand Rapids: Eerdmans Publishing Co., 1984.
Dictionary of the Christian Church. Grand Rapids: Zondervan Publishing House, 1984.
Dobbins, Gaines S. A Ministering Church. Nashville: Broadman Press, 1960.
Family Encyclopedia of the Bible. Grand Rapids: Eerdmans Publishing Co., 1978.
Flynn, Leslie B. 19 Gifts of the Spirit. Wheaton: Victor Books, 1974
Freeman, James M. Manners and Customs of the Bible. Plainfield: Logos International, 1972.
Gaus, Hollis R. The Preaching of Paul, A Study of Romans. Cleveland: Pathway Press, 1986
Gee, Donald. Die Gaben Christi für den geistlichen Dienst. Stuttgart: Henkel Druck, n.d.
77
Hodge, Charles. Ephesians. London: Marshall Pickering, 1991.
Horton, Harold. The Gifts of the Spirit. North Glenoaks: World Map, 1979.
Jefferson, Charles. Der Hirtendienst. Erzhausen: Schönbach Druck GmbH, 1979.
Johnson, Eugene. Duly and Scripturally Qualified. Cincinnati: Standard Press, 1975
Knospe, Dieter. “Diakone und Älteste, Ihre Biblische Unterscheidung, der Weg in Ihrem Dienst,
Das Ziel Ihres Auftrages.” Paper presented at Minister’s Meeting of Gemeinde Gottes
Germany, Kniebis, November 1987.
Lange, J.P. Commentary on the Holy Scriptures. Grand Rapids: Zondervan Publishing House, 1976.
Lexikon zur Bibel. Wuppertal: Brockhaus Verlag, 1977.
Liddell, H.G.; and Scott. Abridged Greek-English Lexicon. Oxford: Oxford University Press, 1992.
Lim, David. Spiritual Gifts, A Fresh Look, Commentary & Exhortation from a Pentecostal Perspective.
Springfield: Gospel Publishing House, 1991.
Lindsay, Gordon. Apostles, Prophets and Governments. Dallas: Christ of the Nations Inc., 1982.
MacArthur, John. Spiritual Gifts, 1Corinthians 12. Chicago: Moody Press, 1983
____________. The Master’s Plan for the Church.Chicago: Moody Press, 1991.
Mason, Steve. Josephus and the New Testament. Peabody: Hendrickson Publishers, 1992.
Murray, John. The Epistle to the Romans. Grand Rapids: Eerdmans Publishing Co., 1968.
Nee, Watchman. Das Normale Gemeindeleben. Wuppertal: Brockhaus Verlag, 1974.
Neighbour, Ralph W. This Gift is Mine. Nashville: Broadman Press, 1974.
Preuschen, Erwin. Griechisch-deutsches Taschenwörterbuch zum Neuen Testament. Berlin: Walter de
Gruyten, 1976
Richards O. Lawrence & Martin, Gib A Theology of Personal Ministry, Spiritual Giftedness in the Local
Church. Grand Rapids: Zondervan Publishing House, 1981
Rienecker, Fritz. Sprachlicher Schlüssel zum Griechischen Neuen Testament. Gießen: Brunnen Verlag,
1977.
Sheldon, Henry. History of the Christian Church. 5 Vol. Peabody: Hendrickson, 1988.
Simpson, James D. The Pentecostal Evangelist. Cleveland: Pathway Press, 1988.
Stevenson, J. A New Eusebius. Documents Illustrating the history of the Church to AD 337. Cambridge:
University Press, 1987.
Strauch, Alexander. Minister of Mercy, The New Testament Deacon. Littleton: Lewis and Roth
Publishers, 1992.
78
Thayer’s Greek-English Lexicon of the New Testament. Grand Rapids: Baker Book House, 1977.
The New International Dictionary of the Christian Church. Grand Rapids: Zondervan Publishing
House, 1978
Theologisches Begriffslexikon zum Neuen Testament. Wuppertal: Brockhaus Theologischer Verlag, 1977
Underwood, B.E. Spiritual Gifts, Ministries and Manifestations. Franklin Springs: Advocate Press,
1984.
Ulonska, Reinhold. Geistesgaben in Lehre und Praxis. Erzhausen: Leuchter Verlag, 1983.
Vine, W.E. An Expository Dictionary of New Testament Words. Old Tappan: Fleming H. Revell, 1966.
Wagner, Peter C. Your Spiritual Gifts Can Help Your Church Grow. Marc Europe Press, 1979.
Walker, Paul L. The Ministry of Church and Pastor. Cleveland: Pathway Press, 1965.