Tuesday 10 February 2015

HISTORIA YA KANISA II



MODULI YA KWANZA.
KIPINDI CHA  PERGAMO. KANISA LA KIFAHARI.

A.    UTANGULIZI.
KIPINDI: Toka  patano  amani la mfalme  Kostantino  (313 BK) hadi kuanguka kwa dola ya Rumi  mnamo mwaka 476 BK.

B.    USHINDI WA WAKRISTO
Baada ya miaka miambili ya mateso kanisa liliishinda dola ya Rumi na kupata amani. Mfalme Deokletiani katika utawala wake aliweka watawala  wasaidizi katika majimbo yake kutokana na ukubwa wa dola  ya Rumi.  Baba wa Kostantino alikuwa ni mmoja wa watawala wasaidizi, aliongoza majimbo ya Galia, Uingereza na Hispania, Baada ya kufa kwa watawala wasaidizi kulitokea na kugombea  madaraka baina ya watoto wao.

Baba wa Kostantino alipofariki Kostantino alitangazwa kuwa mtawala badala ya baba yake, na hivyo watoto wa watawala wengine waliamua kuanzisha mapigano ili kuuchukua utawala huo. Miongoni mwa hao waliokuwa na nguvu ni Maksentio, huyu alikuwa ni mtu aliyeshabkia mauaji ya wakristo. Walianzisha mapigano huko Italia maili kumi kutoka Rumi mnamo 28.10.  312 BK
Wakiwa katika eneo la mapigano kabla ya vita kuanza Kostantino aliona alama ya msalaba angani ukiwa umeandikwa maneno  yafuatayo, “Kwa alama hii utashinda”. Kostantino aliitikiakwa sala na akaifanya alama ya msalaba kuwa nembo ya Jeshi lake na walipokuwa vitani Kostantino aliwashinda kabisa maadui zake, adui yake mkuu Maksentio alikufa katika vita hiyo, hivyo Kostantino akawa mshindi.
Kostantino alitambua kwamba msalaba ilikuwa ni alama ya wakristo na hivyo Mungu wa wakristo ndio aliyekuwa amemsaidia katika vita hiyo. Mwaka uliofuata Kostantino alitangaza PATANO LA AMANI na Wakristo, (Edict of Torelant).  Patano hili  lilikomesha mateso juu ya wakristo katika dola yote ya Rumi. Patano hili lililowaletea amani wakristo katika dola ya Rumi lilikuwa na matokeo chanya na hasi katika kanisa.
C.    MATOKEO YA TAMKO LA AMANI
Matokeo ya  patano  la amani yanaweza kuainishwa katika pande mbili ambazo ni matokeo mazuri na matokeo mabaya;
I.                MATOKEO MAZURI,
1.     Mateso juu ya wakristo yalikomeshwa.
2.     Makanisa yaliyokuwa yamebomolewa wakati wa mateso yalijengwa tena kwa fedha ya serikali.
3.     Maaskofu na wachungaji walisamehewa kodi.
4.     Watumishi wa kanisa walianza kufadhiliwa na serikali na hawakutakiwa kuhukumiwa kwa sheria za kawaida.
5.     Wakristo waliruhusiwa kujenga  makanisa mahali popote katika dola ya  Rumi.
6.     Dhabihu za kipagani zilikomeshwa.
7.     Kostantino alijenga makanisa makubwa katika miji ya Yerusalemu, Bethlehemu na katika mji wa Kostantinapoli  ambapo ndio uliokuwa makao makuu yake mapya.
8.     Kusulubiwa kwa wahalifu na desturi  za kuua watoto wasiotakiwa zilikomeshwa.
9.     Watumwa waliachiwa huru.
10.  Siku ya jumapili iliwekwa kuwa siku ya mapumziko kwa watumishi wa serikali.
11.  Alisaidia kuunda umoja wa kanisa kupitia mikutano mbalimbali aliyoiitisha, mfano mkutano wa Naikea mwaka 325 BK.
12.  Alikusudia kuufanya ukristo ukubaliwe na serikali kama dini zingine.
II. MATOKEO MABAYA.
1.     Ilikuwa ni fahali kuwa mkristo, hivyo watu wengi walijiunga na ukristo kwa maslahi binafsi.
2.     Watu walijiunga na ukristo ili waweze kupata vyeo katika kanisa na serikali.
3.     Maadili ndani ya kanisa yalianza kumomonyoka.
4.     Mambo ya kiroho yaliachwa kupewa kipaumbele na badala yake programu mbalimbali zikapewa kipaumbele.
5.     Sherehe na tamaduni za kipagani polepole zilihamia kanisa, kwa kubadilishwa jina na malengo na badhi zilibadilishwa kuwa  sikukuu za kikanisa,  mfano Krismasi.(Kuabudiwa kwa bikira Maria kuliasiliwa kutoka ibada za kipagani za kuabudu miungu , Zeusi, mungu wa uzuri wa warumi na Diana  mungu mwezi).
6.     Katika jimbo la mashariki serikali ililitawala kanisa mpaka likapoteza  nguvu na maisha ya kiroho.
7.     Katika jimbo la magharibi kanisa lilipata nguvu dhidi ya serikali.

Kostantino hakutaka kutumia nguvu katika kuwafanya watu kuwa wakristo, alitaka jambo hili lifanyike taratibu na kwa uchaguzi wa mtu mwenyewe, jambo hili halikufuatwa na watawala waliofuata baada yake.

Baada ya utawala wa Kostantino watawala waliofuatia walikuwa wakali mno walipiga marufuku ibada za kipagani na waabudu dini hizo walihukumiwa kifo na mali zao zilitaifishwa. Walivunja mahekalu ya kipagani, watawala wakristo kwa kutumia jina la ukristo sasa walitumia  njia zilezile mbaya zilizokuwa zimetumia na serikali kulitesa kanisa kuwatesa wapagani.


D.    AINA MBALIMBALI ZA MATESO.
·       Katika kipindi cha Efeso kanisa liliteswa na wayahudi.
·       Katika kipindi cha Smirna kanisa liliteswa na  dola ya Rumi.
·       Katika kipindi cha Pergamo ugomvi ulizuka miongoni mwao wenyewe (wakristo).

E.    UZUSHI NA MAFUNDISHO YA UONGO.
Mafundisho yasiyokubaliana na mafundisho rasmi ya kanisa yaliitwa uzushi na waamini waliamriwa na kanisa kutokuyapokea mafundisho hayo.
Kanisa katika historia yake lilitangaza mafundisho fulani kuwa uzushi kutokana na kutokukubaliwa kwa mafundisho hayo na uongozi wa kanisa.

Si kila mafundisho waliyoyaita uzushi yalikuwa mabaya, kwani kile kilichoitwa uzushi kilikubaliwa baadae na kanisa na kile ambacho kilionekana chema kilikataliwa na kuitwa uzushi baadae. Hoja  au  mawazo  yale waliyoyaita uzushi baadhi yalikuwa na mambo mema ndani yake.
Kanisa halikupambana na mateso tu bali pia na mafundisho ya uongo, sawsawa na unabii uliotolewa na mtume Paulo katika Matendo ya mitume 20:29-30.

·       MAKUNDI YA UZUSHI.
1.     UYAHUDISHAJI.
Hili lilikuwa ni kundi la wakristo wa kiyahudi lililojitokeza wakati kanisa linapanuka katika miji ya wamataifa.  Wayahudishaji hawa walifundisha kwamba wakristo wote walitakiwa kuzifuata sheria za Musa na mapokeo ya dini ya kiyahudi. Waliyakataa maandiko ya mtume Paulo kwa sababu yalipinga mafundisho yao. Kundi hili lilitoweka katika karne ya pili BK.

2.     UNOSTIKI
  Kundi hili waliamini kwamba Baada ya ngazi ya Mungu mkuu kulikuwa na miungu wengine  wengi ambao baadhi wakiwa  wema na wengine  waovu. Unosti ulikuwa na elementi za falsafa za kiyunani na dini za kipagani.

Unostiki ilikuwa ni falsafa iliyojaribu kutumia imani ya ukristo katika kuthibitisha ukweli wake.  Hivyo kanisa lilipinga vikali mno unosti likikana kwamba imani yake si falsafa na wokovu hautegemei falsafa  na mafumbo bali ufunuo wa Yesu kristo.

Wanostiki walipunguza thamani ya maisha na huduma ya Yesu Kristo. Habari nzima juu ya maisha na huduma ya Yesu ilielezwa kwa njia ya mafumbo (allegory). Unostiki ulizuka katika karne ya pili baada ya Kristo na ulishamiri katika karne ya tatu na  ya nne.  

Unostiki hata sasa unajidhihirisha katika karne hii ya ishirini na moja katika  dini mbalimbali hapa ulimwenguni. Hususani kupitia   falsafa ya mpango mpya wa dunia (New World  order Philosophy)

v MAFUNDISHO YA UNOSTIKI.
1.     Maarifa ya pekee hufunuliwa kwa watu wachache tu.
2.     Wokovu si kwa watu wote, ni kwa watu wachachetu  wenye kuyaelewa maarifa yanayofunuliwa.
3.     Ulimwengu huu na vitu vilivyomo ndani yake umeumbwa kwa nguvu isiyo kamili na hii ndio asili ya maovu yote katika ulimwengu.
4.     Yesu si mwanadamu, alikuwa na roho tu. Yesu alikuwa ni roho aliyejifanya aonekane katika umbile la binadamu.
5.     Waliamini kwamba mmoja wa miungu wadogo alikuwa ndani ya Yesu na ndio aliyekuwa asili ya uungu wake.




3.     MARSION
 Huyu alikuwa ni mtoto wa askofu wa Pontus. Alikuja Rumi yapata mnamo  mwaka 138BK.  Alipofika Rumi alijulikana kwa haraka sana kutokana na jinsi alivyojitolea sana katika kanisa kwa mali zake. Pia mafundisho yake yalimpa umaarufu na kumfanya ajulikane sana. Kutokana na umaarufu huo Marsion alipata wafuasi wengi. Mafundisho yake hayakukubaliwa na kanisa hivyo alitangazwa kuwa mzushi na  alitengwa na kanisa mnamo mwaka 144 BK.
Marsioni aliunda chama chake ambacho kiliwaunganisha wafuasi wake wote. Chama chake hakikuongezeka kwa njia ya kuzaliana kwa sababu ya kukataa mambo ya ndoa. Waliongezeka kwa njia ya wanachama wapya kujiunga. Marsion alikuwa ni mtu wa kwanza kutunga  kanuni ya maandiko.
v MAFUNDISHO YA MARSION
1.     Kwa kiasi kikubwa mafundisho yake yalifanana na mafundisho ya wanostiki.
2.     Aliweka sharti la wafuasi wake (wanandoa) kutokutana kimwili na kwamba walitakiwa kuachana na kuishi maisha ya upweke.
3.     Alikaza kwamba wokovu ni kwa watu wote. Wokovu hutegemea Injili ya Yesu na si kwa kufunuliwa mafumbo kifalsafa.
4.     Injili ya upendo wa Mungu inahitaji kusikika zaidi katika kanisa.
5.     Kanisa limeichafua Injili kwa kuichanganya na mambo ya dini ya kiyahudi.
6.     Mungu wa Agano la kale ni tofauti na baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Kwa sababu Mungu wa agano la kale alifurahia dhabihu za damu.
7.     Mungu aliyeumba ulimwengu na watu wake ni Mungu mwovu, Mungu mwingine mwema alijificha hadi wakati wa Yesu Kristo.


4.       UMONTANO.
Kilikuwa ni kikundi kilichoanzishwa na mtu mmoja aliyeitwa Montano mwenyeji wa Frigia. Wafuasi wa kikundi hiki waliitwa wamontano. Kikundi hiki kilienea sana  kuanzia mwishoni mwa karne ya pili na kuendelea kwa karne mbili zaidi.
Wakati wa ubatizo wake Montano alinena kwa lugha nyingine na kutabiri na hivyo akajiita kuwa ni kinywa cha Roho Mtakatifu aliyetabiriwa na Yohana. Alikuwa na wasaidizi wawaili wanawake ambao nao pia walijitambulisha kuwa ni vyombo pekee vya Roho Mtakatifu. Karama za kinabii zilijidhihirisha katika mlengo wa umontano. Kutokana na mikazo yao,  Wamontano walihukumiwa uzushi na kutengwa na kanisa.

v MAMBO MUHIMU YA MONTANO.
1.     Walikaza kwamba wamefunuliwa juu ya mwisho wa dunia uliokuwa karibu sana kutokea.
2.     Baadhi ya wafuasi wa umontano walikataa kulima kwa sababu Yesu angekuja kabla ya msimu wa mavuno.
3.     Baadhi walikataa ndoa kwa kuwa mwisho wa dunia ulikuwa karibu.
4.     Kiongozi wao mmoja wa huko Pontus aliwapeleka washirika wake porini kwenda kumlaki Bwana Yesu wakati anarudi duniani kwa mara ya pili.
5.     Kiongozi mwingine wa huko Shamu aliwakataza washirika wake wasilime kwa sababu Yesu angerudi kabla ya msimu wa mavuno.
6.     Alikataa hali ya kanisa kumezwa na ulimwengu.
7.     Alidai kuwa kanisa lilikuwa limepoa na hivyo lisitarajie kurudi kwa Yesu.
8.     Walipinga suala la uaskofu kuchukua mamlaka katika kanisa. Waliweka mkazo katika huduma ya unabii na ukuhani wa waamini wote.


v KUMEGEKA KWA KANISA CHINI YA UONGOZI WA NOVATIANO NA   DONATO.
Katika karne ya tatu na ya nne kulitokea  na kumegeka kwa kanisa.  Mmeguko huo uliongozwa na Novatiano  katika karne ya tatu na Donato karne ya nne. Kugawanyika huko kulitokana na kurejeshwa kwa  viongozi na wamini waliokuwa wameikana imani katika kipindi cha mateso. Pia makundi haya yalijitenga kutokana na kuona wakristo wengi walikuwa wanaishi maisha machafu kama wapagani waliokuwa wanawazunguka.

v UASI WA NOVATIANI.
 Katika karne y tatu askofu wa Rumi aliyeitwa Kalisto alitangaza kwamba dhambi yoyote ili inaweza kusamehewa kiwa mkosaji anaonesha toba ya kweli.Fundisho hili lilienea sana. Wakristo waliokuwa wameikana imani yao wakati wa mateso walitaka kurudi kanisani na askofu Kalisto alikubali kuwapokea watu hao.
Kiongozi mmoja wa kanisa aliyeitwa Novatiani, hakukubaliana na jambo hilo na alilipinga vikali na akaungwa mkono na wachungaji wengine ambao nao walikuwa kinyume na maamuzi hayo ya askofu. Walijitenga na kanisa    na kuanzisha ushirika wao.  Novatiani alichaguliwa kuwa kiongozi wao.

v UASI WA DONATO.
Mmeguko wa kanisa chini ya uongozi wa Donato ulitokea Afrika ya kaskazini karne ya nne baada ya utawala wa mfalme Deokletiani. Mfalme huyu katika kipindi cha utawala wake alikuwa na mpango wa kufuta ukristo na kuchoma moto Biblia zote. Wakati wakipindi  cha mateso makali baadhi ya viongozi wa kanisa waliasi imani wakaamua kutoa maandiko matakatifu (Biblia) yateketezwe ili kujinusuru na kifo.
Baada ya kipindi cha mateso kumalizika viongozi hao yaani wachungaji na maaskofu walioasi walitaka kurudi kanisani. Kanisa katoliki  lilikuwa limekubali kuwapokea. Kanisa lilikubali kuwarudishaviongozi hao katika sharika zao. Katika mji wa Karthegi waamini wengi sana walikataa kuongozwa na mtu aliye mkana Yesu na kutoa Biblia kwa serikali ili  ziteketezwe.
Donatusi alikuwa kiongozi wa mgomo huo na alipata wafuasi wengi. Watu hao walijitenga na kanisa na kuanzisha huduma yao. Kulikuwa na ugomvi kati ya wakatoliki na wadonato kwa kwa muda mrefu.

F.     UMOJA NA UTAWALA WA KANISA.
Kanisa lililazimka kuwa na umoja kamili ili liweze kuwa na nguvu ya kukabiliana na mateso yaliyoliandama na uzushi uliokuwa unajitokeza. Hivyo kanisa lilipambana na maadui wakubwa wawili ambao ni mateso na mafundisho potofu.
Kutokana na uzushi kutokea,  kanisa ilibidi liwe na utambulisho au jina litakalowa tofautisha  na makundi ya uzushi, hivyo kanisa lilianza kijiita Katoliki.
Jina katoliki linatokana na neno la kiingereza universal, lenye maana   ya popote au ya mahali popote” Kanisa lilianza kutumia jina Katholiki kwa maana mbili, ambazo ni:
1.     Kanisa lisilo na mipaka ya majimbo au ya nchi.Kanisa moja lililo katika nchi zote ulimwenguni.
2.     Kanisa leye mafundisho sahihi.

v SAABU ZA KANISA KUHITAJI UTAWALA WENYE NGUVU.
1.     Kutokea kwa ukiri wa imani.
2.     Kutokea kwa Kanuni Ya Maandiko Matakatifu.
3.     Kutokea kwa maaskofu waliopewa mamlaka ya kutunza mafundisho yaliyotokana na mitume wa kwanza.

v Ukiri Wa Imani.
Huu ulikuwa ni ushuhuda mfupi uliotumiwa katika kazi za kawaida sharikani kama vile ubatizo. Ukiri wa imani ulieleza kwa kifupi kile kanisa linachoamini naa ulitumika kama kiapo kuwa mtu anakubaliana na taratibu za kanisa hilo hivyo anastaili kubatizwa na kupokelewa katika kanisa.

v Kanuni Ya Maandiko Matakatifu.
Kanuni ni kwaida inayotumiwa kupima usawa na usahihi wa kitu. Kanuni huelezea vitabu vilivyokubaliwa kupokelewa na kanisa kama maandiko Matakatifu. Kanisa liliweka kanuni ili kubainisha kati ya vitabu vilivyokuwa ni neno la Mungu na vile visivyokuwa Neno la Mungu. Mfano wa vitabu visivyokuwa neno la Mungu ni vile vilivyoandikwa na wanosti.

Makundi ya uzushi kama vile wanostika na Marsion waliharakisha kutungwa kwa kanuni hii.
Mababa wa kanisa walitumia kanuni mbalimbali katika kuvibaini vitabu hivyo. Baadhi ya njia hizo ni kumtambua mwandishi kama alikuwa ni mtume au la, Kupokelewa kwa kitabu na  watu walionadikwa kwa mara ya kwanza na matumizi ya kitabu hicho katika makanisa mbalimbali na mamlaka ya kitabu chenyewe N.k

v Haja Ya Kutokea Kwa Viongozi Wenye Mamlaka.
 Maaskofu walitokea kama watu wenye mamlaka ya kutafasili maandiko na kufundisha wazi mafundisho ya mitume. Neno askofu maana yake ni mwangalizi/msimamizi. Neno hili hapo awali lilitumiwa na watu wote na kulikuwa na maaskofu katika idara mbalimbali za serikali, baadae matumizi ya istilahi hii yalibakia katika Kanisa tu.
Uaskofu ulisaidia kuleta utawala wenye nguvu  na umoja katika kanisa kupitia mambo mawili ambayo ni mafuatano ya mitume na ibada.

·       Mafuatano Ya Mitume
Ilidaiwa kwamba maaskofu walikuwa badala ya mitume.  Kwa namna fulani uaskofu  ulitokana na mitume, yaani maaskofu waliwekwa na mitume kuwa watawala katika kanisa na mamlaka ya utawala wao ilihusisha kuhubiri na kuitetea Injili.

·       Umoja Wa Ibada
Ibada mbalimbali zilizokuwa zikifanywa na kanisa kwa pamoja zilisaidia kukuza umoja wa kanisa na kutokea kwa viongozi wenye mamlaka. Kulikuwa na ibada mbalimbali ambazo zilifanywa na kanisa, baadhi ya ibada hizo ni ibada ya ubatizo na ibada ya meza ya Bwana. Pia kanisa liliadhimisha sikukuu mbalimbali ambazo pia kwa namna fulani zilichangia kukuza umoja wa kanisa.



G.   MABISHANO YA KITHIOLOJIA.
Mabishano ya kithiolojia yalisababishwa na mitazamo mbalimbali ambayo wakristo walikuwa nayo juu ya Yesu Kristo. Baadhi ya mitazamo hiyo ni .

v Uungu wa Yesu Kristo.
Wakristo  wa awali walimpa Yesu heshima  kwa kumwita majina mbalimbali kama vile Masihi, Kurios, Kritos na Logos.
Jina la Logosi lilitokana na falsafa za kigiriki, Kutokana na falsafa hizo Logos ilikuwa ni njia ya Mungu kufanyika mwili na kukaa na watu hapa duniani. Hivyo wakristo wa awali walimtambua Yeus kama Mungu.

v Kristo kama Logosi.
Katika kipindi cha karne ya pili na ya tatu karibu wanazuoni wote wa kikiristo walifundisha kwamba Kristo alikuwa ni Logos.  Kulikuwa na mwanazuoni moja aliye itwa Yustini Shahidi ambae aliweka mkazo kuwa Logos alikuwa ni Mungu wa pili.
Wanazuoni wengine waliweka mkazo katika umoja wa Yesu.Walikubali kwamba Logos amefanyika kuwa mwili katika Yesu  Kristo lakini alikuwa ni Mungu halisi, Mungu mwana ndiye aliyefanyika mwili, si Mungu wa pili. Kulingana na mtazamo waYustini  ni dhahiri  kwamba alikana ubinadamu wa Yesu. Yesu kama Logos alikuwa Kweli Mungu na mwanadamu kweli.

v Monarchianism. Dhana ya Mungu mmoja.
 Kulikuwa na wanazuoni wengine waliopinga mafundisho ya kumhusisha Yesu na Logos kwa sababu jambo hili lilielekea kupinga imani yakuwa  Mungu ni mmoja. Wanazuoni hao waliona kwamba dhana ya utatu wa Mungu ilielekea kuwa ni uzushi wa kuwa na miumngu mingi.
Wamonarchianism waligawanyika katika makundi mawili ambayo ni;
1.     Wamonarchianism wa kimabadiliko,  hawa walikuwa na mtazamo wenye kumwona Yesu kama mwanadamu pekee tu, ambae hakuwa Mungu aliyefanyika mwili. Kundi hili liliongozwa na Askofu Paulo Samosota wa Antiokia.
2.     Wamonarchianism wa kimfano.  Hawa waliona kuwa hakuna tofauti kati ya baba na mwana. Baba ndiye aliye vaa mwili. Kwa hiyo majina haya baba, mwana na Roho mtakatifu yalitumika kuonesha kwetu njia au hali tatu Mungu alizotumia kujidhihirisha. Hivyo hakuna nafsi tatu bali ni nafsi moja. Kundi hili liliongozwa na Sabelio.
Baada ya mateso kukoma katika kanisa kulitokea mgogoro mwingine ndani ya kanisa uliohusisha mgongano wa kimafundisho (doctrinal controversals).
Baadhi ya viongozi wa kanisa walianza kuibuka na mafundisho yaliyoonekana kuwa mageni katika kanisa na hivyo walihukumiwa uzushi na kutengwa na kanisa.
Wakristo walitumia muda mwingi kujadiliana wao kwa wao badala ya kuipeleka Injili mbele.  Katika moduli hii tutajadili badhi tu ya mabishano ya kithiolojia  yaliyotokea ndani ya kanisa.




1.     Maabishano Baina  Ya Mchungaji  Ario Na Askofu Alexander.
Ario alimshutumu askofu wake kuwa alikuwa anaweka mkazo sana juu ya uungu wa Yesu katika mafundisho yake. Alexander alifundisha kwamba mwana ni wa milele sawa na baba. Ario alipinga fundisho hilo yeye alidai kwamba baba ni wa milele lakini mwana alikuwa na mwanzo wake. Kuna kipindi  ambapo mwana hakuwapo. Askofu Alexander aliitisha mkutano wa sinodi huko Iskanderia ili kujadili suala hilo na hatimae Ario alitangazwa kuwa mzushi na alitengwa na kanisa.

Ario aliungana na Askofu Euzebio wa Nikomedia na wakaandika  nyaraka mbalimbli ambazo zilitetea fundisho lao na wakazisambaza maeneo mbalimbali ili ziendelee kusomwa na wakristo mbalimbali.
v Mkutano Wa Naikea.
 Baada ya nyarakahizo kusomwa majadiliano miongoni wa viongozi wa kanisa yalipamba moto na kuleta mgawanyiko ndani ya kanisa. Mfalme Kostantino hakupendezwa na mgogoro huo ulioleta mgawanyiko miongoni mwa wakristo hivyo aliwaomba viongozi hao wapatane na  iliposhindikana kupatana kwa viongozi hao, mfalme akitumia nguvu ya dola aliamua kuitisha mkutano wa viongozi wote wa kanisa toka seheu mbalimbali ili aweze kuwapatanisha. Mkutano huo ulifanyika mwaka 325BK katika mji wa Naikea na hutambulikana kama mkutano wa kwanza wa kanisa zima, kwa sababu ulihusisha viongozi mbalimbali toka sehehemu mbalimbali.

Katika mutano huo Askofu alexender alishinda kwa hoja na hatimae Ario alitangazwa kuwa mzushi na akatengwa na kanisa. Katika kipindi hki kanisa lilitunga ukiri wa imani ambao ulipaswa kutumiwa na makanisa yote. Ukiri huo ulikweka mkazo katika uungu wa Yesu kuwa Yedu ni sawa na  baba.
Mkutano wa Naikea haukuweza kumaliza majadiliano na badala yake uliyachochea kwani majadiliano hayo yaliendelea kwa muda wa miaka therathini na tano baada ya mkutano wa Naikea. Baadhi ya viongozi wa kanisa walitiria mashaka ukiri wa Naikea kwasababu hawakuuzoea.

v Mkutano Wa Kostantipali
Kutokana na majadiliano hayo  ya muda mrefu na makali kulikuwepo na haja ya kuitisha mkutano mwingine wa kanisa zima. Mkutano hu uliitishwa katika mji wa Kostantinopoli mnamo mwaka wa 381 BK. Katika mkutano huu walifanya marekebisho kidogo ya ukiri wa imani wa Naikea.

Mkutano Wa Efeso.
Baada ya Apolinari kuhukumiwa uzushi,  kuliendelea mabishano makali katika kanisa.  Baadhi ya mabishano hayo yalikuwa baina ya askofu Sirilo wa Iskandelia na askofu Nestori wa Kostantinopoli.
Sirio alipinga fundisho la Apolinari  Aliona kwamba uungu na ubinadamu wa Yesu  kuwa ni hali mbili zisizo weza kutenganishwa . Alipokuwa anataka kueleza uungu wa Yesu alianza kwa kumwita bikira Maria ‘Theotokos’ yaani mama wa Mungu.
Askofu Nestori alibaini uzushi katika maelezo ya Sirilo, yeye alipendekeza  Mariamu aitwe mama wa Kristo. Maaskofu hao walishambuliana vikali sana kwa maandishi. Shauli hilo lilipelekwa kwa askofu wa Rumi ili aweze kutoa uamuzi. Askofu wa Rumi alimpa ushindi Sirilo na kumtangaza Nestori kuwa mzushi.Hayo yalifanyika katika mkutano wa tatu wa kanisa uliofanyika katika mji wa Efeso mnamo mwaka 433 BK.



2.      Majadiliano Ya Apolinari.
Apolinari alkuwa ni askofu wa Laodikia.  Askofu huyu  alijaribu kueleza uhusiano uliopo baina ya hali mbili tofauti alizo nazo Yesu.  Yaani hali ya uungu na hali ya ubinadamu.
Yeye alikuwa na mtazamo wa kwamba mwili wa Yesu ni ubinadamu na akiri na roho yake ni Logosi aliyefanyika mwili. Katika kueleza fundisho hilo askofu huyu alikaza uugu wa Yesu  uliokana ubinadamu wake. Kutokana na fundisho hili Apolinari alitangazwa kuwa mzushi  katika mkutano wa Kostantinopali mnamo mwaka 381BK.

3.     Mabishano Ya Peregia.
Peregia alikuwa ni mmonaki, mwingereza aliekuja Afrika Kaskazini kwajili ya kuhubiri Neno la Mungu katika kanisa la Afrika ya Kaskazini.
Peregia alifundisha kwamba mtu harithi dhambi  toka kwa Adamu, lakini kila mtu ni lazima afanye uchaguzi yeye mwenyewe.
 Peregia alipingwa vikali na Agustino mkuu  kwa mafundisho yake. Agustino alifundisha kwamba Adamu alipotenda dhambi alikiwakilisha kizazi chote cha binadamu na kwamba mtu hawezi kuokolewa kwa uchaguzi wake mwenyewe, bali ni kwa  mapenzi ya Mungu na kwamba neema ya Mungu haiwezi kukataliwa na wanadamu.
Mafundisho ya peregia yalipingwa vikali na kanisa na kuonekana ni uzushi. Kanisa lilikubalia na na   ya mafundisho ya Agustino mkuu.



H.     KUZUKA KWA UMONAKI.
Utawa au umonaki ulianza katika karne ya tatu BK. Kabla ya  kipindi hicho wakristo waliishi katika jamii na familia. Mara baada ya ukristo kushamiri mambo ya dunia yalianza kuingia kanisani, baadhi ya wacha Mungu hawakuridhika na hali hiyo hivyo waliamua kujitenga na kukaa peke yao nje ya mji katika mapango au katika nyumba walizokuwa wamejijengea. Nyumba hizo zilijulikana kama nyumba za watawa maarufu kama  Monastery.
 Baadhi ya mambo yaliyochochea kuanzishwa kwa utawa ni mvuto wa Injili, maovu kukithirikatika kanisa na falsafa ya uovu wa mwili. Kulikuwa na watu ambao waliuza kila kitu walichokuwa nacho wakawagawia maskini na kisha wakajitenga na kuamua kuishi maisha ya kimasikini  mbali na jamii yao. Baadhi ya watu hao ni;
v Antoni Mtawa Wa Kwanza.
 Mtu huyu alikuwa ni mwenyeji wa Misri na ndiye mwanzilishi wa utawa. Antoni aliuza kila kitu alichokuwa nacho na kuwagawia maskini mali zake na kisha akaishi  nje ya mji  akilima na kuwapatia maskini chakula alicholima.Baada ya muda alijitenga na  kuishi peke yake  pangoni mlimani. Watu mbalimbali walimwendea huko pangoni ili kujifunza na kisha alifanikiwa kupata wafuasi ambao nao waliamua kuungana nae kuishi maisha ya utawa. Alipat wafuasi karibuni elfu mbili. 


v Pokomeo Mwanzilishi Wa Nyumba Za Utawa.
 Huyu alikuwa mdogo wa Antoni  na ndie aliyeanzisha nyumba za  utawa.  Yeye alijenga boma kubwa ambalo wafuasi wake waliishi ndani wakijitenga na mambo ya ulimwengu. Watawa hawa walijishughulisha na ibada na kazi, utawa huu ulikaza ushirika na ulipendwa na watu wengi.


v Faida Za Utawa.
1.       Ulifanyika kuwa  vituo vya  wakimbizi.
2.     Walitoa msaada kwa watu wenye mahitaji , mfano kusaidia maskini na wasiojiweza.
3.     Walileta mchango mkubwa katika kuinua kilimo.
4.     Walikuza elimu kwani watawa walitumia muda mwingi katika kusoma na kuandika maandiko mbalimbali.
5.     Walipeleka wamishenari katika mataifa mbalimbali kueneza  Injili.
6.     Walitoa viongozi bora katika jamii na katika kanisa.
7.     Walitafsiri Mandiko katika lugha mbalimbali.

v Madhaifu Ya Utawa.
1.     Mkazo wa juu ya kuishi maisha ya useja.waliwakataza wafuasi wao wasioe wala kuolewa.
2.     Upendeleo na anasa. Baada ya utawa kupata umaarufu, walianza kuishi maisha ya anasa na kukwepa kulipa kodi.



I.      KUKUA KWA DOLA YA RUMI
Mfalme Kostantino mara baada ya kuingia katika utawala alihamishia mako makuu ya dola ya Rumi katika mji wa Kostantinopoli. Tutatazama  namna Rumi ilivyokuwa makao makuu ya kanisa. Wakati kanisa la Orthodox la mashariki lilikuwa likitawaliwa na serikali, Patriaki wa Rumi alidai kuwa na  mamlaka katika kanisa lote la ulimwengu wa magharibi, ambao ulikuwa kupitia kanisa la Katoliki la Rumi. Hii iliwezekana kwa  sababu kadhaa, badhi zikiwa ni;

Kufanana kiutawala. Kulikuwa na mazoea kuongoza kanisa   kwa mfumo wa kiserikali ambapo kunakuwa na kiongozi mkuu mmoja anaetakiwa kusikilizwa .  wakati huu kulikuwa na maaskofu karibu kila mji, ambao katika miji mikubwa waliitwa Patriaki (patriarch) yaani baba mkubwa. Kulikuwa na mapatriaki katika miji ya Yerusalemu, Antiokia, Iskanderia, Rumi na Kostantinopali.
 Kulikuwa na mashindano ya kugombea ukuu miongoni mwa mapatriaki. Swali lilikuwa nani angekuwa kiongozi mkuu wa kanisa lote ulimwenguni. Rumi ikiwa imetengeneza njia ya kuwa makao makuu ya kanisa ilikuwa na viongozi bora. Kwa muda mrefu kanisa la Rumi lilikuwa imara. Lilisimama kidete kupinga mafundisho potofu. Kanisa la Rumi liliihudumia Jamii kiroho na kimwili kwa kuanzisha kazi za kijamii dunia nzima ya wakati ule.  Nyumba za utawa, shule na hospitali zilianzishwa  katika maeneo mbalimbali, jambo hili lililipa umaarufu kanisa la Rumi. Wamishenari walitumwa katika ulimwengu mzima wa wakati ule kueneza Neno la Mungu.

 Wakati nguvu ya kanisa ilikuwa inakua, nguvu ya dola iliendea kuzolota, nguvu ya kisiasa ya Rumi ilizidi kuporomoka.
Kwa muda mrefu wa utawala wake dola ya Rumi ilikuwa imetajirika sana.   Maadui zake waliokuwa wanaishi jirani nae waliutamani utajiri wa wake.  Maadui hao waliivamia Rumi ambayo sasa haikuwa na uzoefu wa kivita. Baadhi ya maadui walioivamia Rumi na kuishambulia  dola ya Rumi ni wavisigothi, wasaksoni,  wavandali, , wahuni, wabarigandiana na wafaransa. Uvamizi wa mataifa haya ulipunguza nguvu ya dola ya Rumi.

 Janga lingine lilikuwa ni vita ya wenyewe kwa wenyewe, baina ya wanachama wa seneti . kugombania kiti cha utawala Kabila la kijerumanilililojulikana kama Herulisi liliivamia na kuishinda dola ya Rumi mnamo mwaka 476 BK.









 
MODUI YA PILI.
KIPINDI CHA THIATIRA;   KANISA LA NYAKATI ZA GIZA.
KIPINDI. Tangu kuanguka kwa dola ya Rumi hadi kuanguka kwa Kostantinopoli.


A.    UTANGULIZI
Katika kipindi cha Pergamo tuliona jinsi Patriaki wa Rumi alivyochukua   mamlaka ya uongozi wa kanisa na kuinuka kwa Rumi kuwa makao makuu ya kanisa. Tuliona jinsi mafundisho potofu   pamoja mambo ya kipagani yalivyoingia kanisani 
Haikutoshga kwa Patriaki wa Rumi kuwa Askofu mkuu wa kanisa lote duniani na kuwa na mji wa Rumi kama makao makuu ya kanisa lote duniani, baada ya hapo alijitangaza kuwa kiongozi wa mataifa  kwa njia ya kukuza upapa katika karne kumi za kipindi cha giza.  Kipindi cha giza kilikuwa na hatua tatu ambazo ni, kukua, kusitawi na kuanguka.
1.     Kukua.
Gregori I alipokuwa kijana aliteuliwa kuwa msimamizi wa majengo na vyakula katika  Mji wa Rumi. Baada ya kifo cha baba yakeAliamua kutoa kwa kanisa mirathi ya babaye. Mnamo mwaka 578 BK Gregori I aliteuliwa na papa kuwa balozi wake katika mji wa Kostantinopoli. Mwaka 585 hadi 590  BK alikuwa msaidizi wa papa huko Rumi na kiongozi mkuu wa Monastery. Baada ya papa Pelegio II kufariki dunia kwa ugonjwa wa tauni mwaka 590 BK, Grogori I aliteuliwa  na umati wa watu huko Rumi kuwa Askofu badala ya Peregio II.

 Kukua kwa nguvu ya upapa kulianza  baada ya Gregori I  kushika wadhifa wa upapa katika mwaka wa 590 BK.  Mfumo wa kubadilisha majina mtu alipokuwa anaingia katika nafasi ya upapa ulianza katika kipindi hiki. Gregori aliitwa mkuu kwa sababu ya mafanikio yake ambayo baadhi ni,
1.     Alitumia uwezo  wa kikanisa katika kuwasaidia watu, (kuwapa chakula na nguo).
2.     Serikali ilipolega aliimarisha ulinzi katika mji wa Rumi.
3.     Alimtambua papa wa Rumi kuwa na mamlaka juu  ya viongozi wengine wote wa kanisa.
4.     Alilipatia kanisa nguvu ya kisiasa na kidini.
5.     Alitengeneza dogma ya kanisa.
Kutokana na misaada  ya kijamii aliyokuwa anaitoa  papa Grogori I, wanachi wa Rumi walianza kumheshimu  na kumhesabu kama kiongozi wao. Hivyo basi Gregori Mkuu aliimarisha nguvu ya upapa katika mambo ya kidini na kisiasa pia.

v Sababu za kukua kwa upapa
Mbali  na mchango wa Gregori Mkuu katika kukuza nguvu ya upapa kulikuwa mambo mengine kadhaa yaliyopelekea kukua kwa upapa katika kipindi hiki. Baadhi ya sababu hizo ni:
1.Nguvu ya haki,  kanisa liliwatetea raia dhidi ya watawala dharimu  hivyo likapendwa na watu.

Kuzolota kwa serikali, Wakati serikali inazolota kanisa lilizidi kujiimarisha, kiuchumi na kijeshi hivyo viongozi dhaifu walihitaji msaada wa kanisa katika kupambana na  adui zao hivyo kanisa likazidi kuwa na mamlaka na nguvu ya ushawishi.
2.     Ulaghai, Kanisa lilitumia kigezo cha ujinga wa watu  kujipatia mamlaka. Kanisa lilitengeneza nyaraka mbalimbali zenye kulipa mamlaka ya kiutawala na kudai kwamba ziliandikwa na wahusika walioandikwa kumbe sivyo. Zifuatazo ni baadhi ya nyaraka hiz
v Waraka wa mfalme Kostantiono kwa askofu Silvesta (314-335 BK). Huu ulikuwa ni waraka uliogushiwa na kanisa kwamba uliandikwa na Kostantino kumpa mamlaka ya kiutawala  askofu wa Rumi (Silvesta) juu ya wafalme wote wa Ulaya na Ulaya nzima.

v Tamko la uongo la Isodore(850 BK). Kulikuwa na maandiko yaliyokuwa yanadai kwamba askofu wa Rumi alikuwa amepokea waraka toka kwa mitume uliokuwa  unamtangaza asofu wa rumi kuwa askofu wa kanisa dunia nzima na kwamba kanisa lilitangazwa kuwa huru (yaani kanisa kutokuwa chini ya serikali).




2       KUSITAWI KWA UPAPA (1073- 1216 )
Nguvu ya upapa ilifikia kilele chake katika utawala wa Gegori VII ambaye pia alijulikana kama Hildebrand. Katika kipindi hiki  upapa ulikuwa na nguvu kamili  kikanisa na kiserikali katika mataifa yote ya kule Ulaya.
1.     Papa Gregori VII alifanya matengenezo ya ukreli na kukataza ndoa kwa wakreli.
2.     Aliliondoa kanisa chini ya utawala wa serikali, kanisa likaanza kujitawala, alifuta suala la maaskofu kuteuliwa na watawala wa serikali (wafalme).
3.     Alilifanya kanisa kuwa juu ya selikali.

v Papa Innocent Iii (1198 -1216).
 Huyu alikuwa ni papa mwingine mwenye nguvu kubwa. Katika siku yake ya kutawazwa kuwa papa alitoa usemi  wenye maneno yafuatayo.
  Mahalifa wa mtakatifu Petro  wako katikati ya Mungu na watu; wadogo kuliko Mungu lakini wakubwa kuliko watu,  wenye uwezo wa kuwahukumu watu wote lakini wasioweza kuhukumiwa na  yeyote”

Katika barua yake ya kiofisi aliandika “ papa hajapewa mamlaka  kwa kanisa pekee bali kwa ulimwengu mzima. Akiwa na haki ya  kuwaondoa na kuwaweka watawala katika uongozi. Papa innocent III alijitwalia mamlaka ya serikali ya mji wa Rumi  akijifanya yeye mwenyewe kuwa bwana kwa kuanzisha  nchi ndani ya nchi  ijulikanayo kama nchi ya Vatikani.hivyopapa akawa kiongozi wa kidini na kiserikali.



3       KUANGUKA KWA UPAPA.
Kuanguka kwa upapa kulianza wakati wa  papa Bonifasi VIII katika mwaka 1303.  Jambo hili lilisababishwa na kuanza kuibuka kwa roho ya utaifa miongoni mwa nchi mbalimbali. Jambo hili lilileta mtikisiko dhidi ya Bonifasi VIII. Watu walianza kuwaheshimu viongozi wa nchi zao kuliko kumheshimu papa. Amri na maagizo mbalimbali ya  papa yalipuuzwa na  viongozi wa nchi. Baada ya mfalme wa ufaransa kukata kutii maagizo ya  papa, papa Alianzsha vita na  mfalme wa ufaransa na hatimae Bonifasi VII akashindwa vita hiyo na kuwekwa kizuizini mpaka mauti ilipomfika.

B.    KUINUKA KWA UISLAMU
 Kanisa lilipata mashambulizi makuu katika karne ya saba kutoka kwa waislamu. Dini ya Uislamu ilianzishwa na kijana mmoja aliyeitwa  Mohamed. Kijana huyo alizaliwa mnamo mwaka 570 BK katika mji wa Maka. Alianza kazi yake kama nabii na mwana matengenezo   kwa kuanzisha dini yake mnamo mwak 610 BK katika mji aliozaliwa. Kutokana na kutokukubaliwa na watu wa mji huo aliamua kuhamia katika mji wa Madina katika mwaka wa 622 BK.  Kipindi hicho kinaitwa  Hajira. Kalenda ya Waislamu inaanza wakati huo wa kuhama kwa Mohamed toka Maka kwenda Madina.

 Ndani ya kipndi cha miaka miambili waislamu walikuwa wameisha zishinda sehemu mbalimbali za dunia na kuanzisha dini yao ya uislamu, Uanzishaji wa dini hiyo ulienda sambamba na uanzishaji wa dola ya Kiislamu katika maeneo yoyote waliyoyashinda. Baadhi ya maeneo waliyokuwa wameyashinda na kuanzisha utawala wao ni  nchi za Mashariki ya kati, Afrika ya Kaskazini, Asia ndogo. Mouhamedi na wafuasi wake walieneza dini yao kwa kutumia upanga, mahali popote watu walipokataa kuipokea dini hiyo walilazimika kutumia vita na nguvu ya kijeshi.
Maeneo yoyote waliyofanikiwa kuyateka hatua ya kwanza ilikuwa ni kufuta dini zingine zote zilizokuwa maeneo hayo na kuwalazimisha raia wote kujiunga na dini hiyo.
Kuinuka kwa dini ya Uislamu kulichangia katika kuanguk kwa upapa na kuzoofisha nguvu ya kanisa kwa ujumla. Kwa mfano Afrika kaskazini kanisa lilizoofika na hatimae likafifia kabisa.



C.    KUTENGANA KWA KANISA LA KATOLIKI.
Kanisa la katoliki la mashariki lile la magharibi  yalitengana rasmi mwaka 1054 BK,  japokuwa kihuduma yalitengana  tangu zamani. Daima kulikuwa na kushindania madaraka ya kwambani nani  aliyekuwa mkuu kati ya papa wa Rumi na Patriaki wa Kostantinopoli. Hatimae katika mwaka 1054 BK   makanisa haya yalitengana ramsi.


v SABABU ZA KUTENGANA
Kutofautiana kimafundisho,  Kuhusu asili ya Roho mtakatifu. Kanisa la magharibi lilidai kwamba Roho mtakatifu alitoka kwa baba na kwa mwana wakati lile la  mashariki lilidai kwamba Roho mtkatifu alitoka kwa baba pekee.
Ndoa kwa makuhani.  Kanisa la magharibi  lilikataza makuhani kuoa wakati la kanisa la mashariki liliruhusu makuhani kuoa.
 Sababu ya kisiasa,   Baada ya kuanguka kwa dola ya Rumi  mataifa ya magharibi yalitaka kuwa chini ya Kostantinopoli.
Kuabudu sanamu.Kanisa la magharibi lilianzisha matumizi ya sanamu katika ibada wakati kanisa la mashariki lilipinga matimizi ya sanamu.
Kugombea  ukuu,   Madai ya kanisa la mashariki  ya  kuwa ni kanisa la kitawala.

D.     KUSITAWI KWA UTAWA.
Mashirika mbalimbali ya kitawa yalisitawi katika kipindi hiki na yakajitolea kusaidia jamii katika maeneo mbalimbali. Baadhi ya mashrika hayo ni :
Wabenedectino walianza mwaka  529 BK
Wasisteri mwaka 1098.
Wafransiska  mwaka 1209.
Wadomeni mwaka 1215.

Kipindi cha karne za katikati kulichangia sana katika ustaarabu wa ulimwengu, hasa katika mambo ya elimu, maandiko, na mambo ya ufundi, katika kipindi hiki zilijengwa kathedro kubwa . kuna baadhi ya vyuo vikuu vikubwa vilivyojengwa wakati huu, mfano wa vyuo vikuu hivyo ni Chuo  kikuu cha Parisi huko Ufarasnsa, Chuo Kikuu cha Kambridge,   Chuo Kikuu cha Oxford, nacho vyote iwili vikiwa  huko Uingereza. Kuanzishwa kwa vyuo vikuu hivi kulipelekea elimu kukua na kuleta mtazamo mpya katika jamii kama tutakavyoangalia baadae katika kipindi kitakachofuata.


E.    WATANGULIZI WA MATENGENEZO YA KANISA.
Katika mwaka wa 1229 kanisa la Rumi  lilikataza  waumini wa kawaida wasisiome Biblia isipokuwa makuhani tu. Lugha ya kilatini iliteuliwa kuwa lugha takatifu na hivyo mtu yeyote asiyejua kilatini alizuiliwa kuhubiri.

1.     PITA WALDO.
 Katika miaka ya 1970  alitokea  mfanya biashara  mmoja aliyeitwa Pita waldo  mwenyeji wa Loyona Ufaransa. Mtu huyu alipenda kujua mambo yaliyo katka Biblia lakini hakuweza kwa sababu hakufahamu kilatini hivyo aliwaajiri  mapadri wawili wamtafsirie  Biblia katika lugha ya kifaransa.  Baada ya kusoma neno la Mungu alivutiwa nalo sana hivyo akauza kila kitu alichokuwa nacho na akala kiapo cha umaskini, akajitoa kikamilifu kuhubiri neno la Mungu.

Pita Waldo Alianzisha timu iliyoitwa  watu maskini. walianza kuhubiri, lakni walipingwa na papa. Mwaka 1184 walijitenga na kanisa  kwa sababu hawakukubali kitendo cha wao kuzuiwa kuhubiri,
Waldo alipinga baadhi ya mafundisho ya kanisa la Katoliki. Baadhi ya mambo aliyoyapinga ni    mafundisho kuhusu toharani,  misa na kwaajili ya wafu na kumwabudu Mariamu mama wa Yesu.
Watu hawa waliamini kwamba kili mtu alitakiwa kuwa na Biblia katika lugha yake ya asili na  ya kwamba Biblia ilitakiwa kuwa mamlaka ya mwisho na iliyokuu katika mambo ya imnani na maisha. Kanisa lilianzisha mateso dhidi ya wawadeni yaani wafuasi wa Waldo. Kadili walivyokuwa wanateswa  ndivyo walivyokuwa wakiongozeka. Mnamo  mwaka 1211 wawadeni themanini   walichomwa moto huko Ujerumani.  Pita waldo alisaidia kuleta matengenezo ya kanisa kwani alisaidia kupatikana kwa Biblia katika Lugha zingine na kuhamasisha kila mtu kusoma Biblia. Waldo anajulikan kama mmoja  wa  wanamatengezo ya kanisa watangulizi.


2.     JOHN WIKRIF.
Huyu alikuwa mwalimu wa Chuo kikuu cha Oxford. Mnamo mwaka 1378 Wikrif alitaka kuleta matengenezo katika kanisa kwa kuwaondoa watumishi wa kanisa waliokuwa dharimu,na kuwanyang’anya mali ambazo aliamini kwamba ndizo zilizokuwa chanzo cha watumishi hao kuwa dharimu. Alichapisha andiko lililoeleza maadili wanayotakiwa kuwa nayo watumishi wa kanisa.
Alifundisha kwamba wakati viongozi wa kanisa wanapokuwa mafisadi serikali ilitakiwa kuchukua mali zao na kuwapa watu wengine wenye nia ya kumtumikia Mungu. Katika mwaka wa 1379 alianza kupinga dogma ya kanisa  kwa kutoa madai yafuatayo;
Ø  Yesu pekee ndiye aliyekuwa kiongozi mkuu wa kanisa na si papa.
Ø  Biblia pekee ndio yenye mamlakua kuu na ya mwisho kwa waamini na si kanisa wala papa.
Ø  Kanisa lilitakiwa kuiga mfano wa kanisa la  agano jipya.
Ø   
John Wikrif kwa msada wa tajiri Lord Cobham alitafsiri Biblia  katika lughaya kiingereza na kuisambaza katika maeneo mbalimbali . Alianzisha chama cha Wahubiri maskini na wakaanza kuzunguka katikia maeneo mbalimbali ya nchi hiyo wakihubiri watu neno la Mungu.

Mwaka 1382 alipinga fundisho la mageuzo ya maumboya mwili na damu ya Yesu linalojulikana kama transubstan-tiation. Mawazo yake yalipingwa vikali na kanisa na serikali na akafukuzwa ukufunzi.  Mwaka 1402  Bunge La Uingereza  lilipitisha sheria ya hukumu ya kifo  kwa watu wanohubiri mafundisho kinyume na yale yaliyokubaliwa na kanisa. Wahubiri maskini waliteswa vikali sana, baadhi walifungwa nakuchomwa moto na kufukuzwa nchini. Viongozi wa kanisa walijaribu kuchoma moto Biblia zote  za Kiingereza. Wikrif alifarikia mnamo mwaka 1384.
Shujaa huyu anakumbukwa sana katika historia ya kanisa kwa mchango wake wa kutafsiri Biblia katika Lugha ya kiingereza. Wikrif ndiye mtu wa kwanza kutafsiri Biblia kwa lugha ya kingereza.











3.     JOHN HUS
Huyu alikuwa ni mkuu wa chuo kikuu cha Plague huko Bohemia, mtawa  na padre wa kanisa la la Rumi la katoliki. Mwaka 1401 John Hus alipata upadrisho.  Padri huyu alipendezwa na maandiko ya John Wikrif na hivyo alianza kuhubiri  mafundisho ya mtangulizi wake Wikrif.
Alipinga mafundisho mbalimbali  yasiyo ya kiBiblia ya kanisa la Romani katoliki na akasisitiza watu kuishi maisha matakatifu. Alisisitiza kwamba Biblia ndiyo mamlaka ya mwisho  kwa mwamini na katika huduma za kanisa.
Katika kitabu chake alichoandika juu ya kanisa, alifasili kwamba kanisa ni mwili wa Kristo, na  Yesu Kristo pekee akiwa kiongozi wake mkuu. Alitetea nafasi ya ukuhani na kudai kwamba   Mungu pekee ndiye aliyekuwa na uwezo wa kusamehe dhambi. Alieleza kwamba hakuna mamlaka ya kanisa inayoruhusiwa kuanzisha mafundisho (doctrine) yaliyo kinyume na Biblia na kwamba Waamini hawatakiwi kutii  maagizo yasiyo ya kimaandiko.
John Hus Alipinga mambo yafuatayo, udharimu wa  mapadri, kuuzwa kwa vyeti vya msamaha, kuondolewa kikombe cha divai kwa walei. Baada ya mashambulizi hao mazito dhidi ya mafundisho ya kanisa  Hus alifukuzwa upadri  na akaambiwa abadilishe msimamo wake kwa kufuta kauli, jambo ambalo Hus hakukubaliana nalo. Hatimae Hus alihukumiwa kifo na akachomwa moto.  Hus akiwa anachomwa moto  alitoa unabii kwa kusema “leo mnaniua mimi lakini miaka miamoja ijayo Mungu atamwinua mtu mwingine ambaye matengenezo  yake hayaatweza kuzimwa” Kweli baada ya kipindi hicho Mungu alimwinua Martini  Luther mwana matengenezo mkuu kama tutakavyoona hapo baadae.

4.     JEROME SAVANAROLA.
Alizaliwa Ferrara Italia mnamo mwaka 1452, alikuwa ni mtawa wa shiriki la  wadominiko.Alijaribu kuleta matengenezo katika kanisa na serikali. Alipinga uovu uliokuwa unafanywa na mapapa.  Alisomea mambo ya  ubinadamu na utabibu. Kufikia mwaka 1491 alikuwa mhubiri maarufu kule Frolence.
Alitabiri kwamba papa  na mfalme wa Naples wangekufa siku moja, jambo ambalo lilitokea  kama alivyotabiri. Katika mahubiri yake alitabiri hukumu kubwa ambayo ingekuja  juu ya mji ikifuatiwa na kipindi  chema ambapo Frolence ingewaunganisha watu wote wa Itali. Utimilizo wa unabii huu ulionekana kuwa ni kuvamiwa  kwa Itali na mfalme Charles VIII. Ambaye mwaka  1494 aliuondoa utawala dhalimu wa Frolence.
Baada ya kuanzishwa kwa serikali mpya Saravano alipaata umaarufu sana pale Frolence kupitia mahubiri yake na alileta mabadiliko mengi katika jamii. Alianzisha matengenezo ya kodi, Kusaidia maskini na   matengenezo katika mahakama.  Aliubadilisha mji kutoka katika maisha  ya kimwili na kuishi maisha ya kiroho.
Kutokana na mabadiliko hayo kila mtu katika mji alikwenda kanisani na matajiri waliwapa misaada masikini.Wafanya biashara walirudisha vitu walivyokuwa wamewatapeli wateja wao. Waimbaji waliacha kuimba nyimbo za kidunia na kuanza kuimba nyimbo za kumsifu Mungu. Waliachana na  maisha maovu, walichoma moto mawigi, vinyago, vitabu vya kipagani,  picha za ngono na kila kitu walichodhani kuwa ni kiovu. Hakika uamsho mkuu ulitokea kama alivyokuwa ametabiri.
Jerome alitabiri kwamba angehubiri kwa miaka nane tu pale Florence na  kisha angeuawa. Katika mwaka 1498 Jerome  alimshutumu papa Alexander VI kwa kutangaza hadharani maovu aliyokuwa anayafanya yeye na wasaidizi wake. Baada ya mkasa huo Alexander VI  aliamua kumwekea vikwazo na kisha baadaye akamnyonga na kuuchoma moto mwili wake mnamo  mwaka huohuo wa  1498. Maneno yake ya mwisho akiwa anauawa alisema “ Bwana Aliteseka sana kwaajili yangu”. Mapambano yake dhidi ya papa yalimfanya kuwa shujaa na  kuwa mtangulizi wa matengenezo ya kanisa. Alikuwa tayari kuitetea imani kwa gharama yoyote.
Wanamatengenzo watangulizi walionyesha ushujaa katika kuitetea imani. Hawakukubali kusalimu amri kwa uongozi wa kanisa au serikali na hawakuwa tayari kunyamaza kimya na kuacha hali mbaya kuendelea kulitafuna kanisa, walikubali kulipa gharama katika kuitetea imani na kupinga uovu. Walitengeneza njia ambayo ilifuatwa  na wanamatengenezo wakuu baadae kidogo  katika kipindi cha kanisa la Sardi yaani kanisa la matengezo.
Kuna mengi ambayo twaweza kujifunza kwa watu hao   kutokana na vile kila mmoja alivyosimamia kusudi lake kwa ujasiri na imani kuu. Kama tutajifunza na kutetea imani kama wao tunaweza kuleta matengenezo katika kanisa vuguvugu la wakati huu wa utandawazi.

F.     KUANGUKA KWA KOSTANTINOPALI.
 Wanahistoria wengi wana tazama kuanguka kwa  Kostantinopoli kama mpka wa kipindi cha karne za katikati na nyakati hizi zetu. Waislamu toka Uturuiki waliivamia Kostaninopoli na kuishinda  mnamo mwaka 1453. Hekalu zuri liliojengwa na mfalme Kostantino lililojulikana kama Saint Sophia liligeuzwa na kuwa msikiti. Huu ndio uliokuwa mwisho wa kipindi cha giza au mediaval Period.







MODULI YA TATU.
KIPINDI CHA SARDI  KANISA LA MATENGENEZO
KIPINDI : Tangu kuanguka kwa Kostantinopoli hadi Patano la Amani la Westpharia.


A.    SABABU ZA KUZUKA KWA MATENGENEZO YA KANISA.
Kitendo cha Kanisa la Rumi   kutokuwa  tayari  kupokea mabadiliko yaliyokuwa yanapendekezwa na watu wema kama vile, Wikrif na Hus, viongozi wa baraza la matengenezo na mengine mengi kulipeleka  kuanza kwa nguvu  wimbi kubwa la matengenezo.

Hadi kufikia miaka 1500 misingi wa jamii ya kipindi cha giza ilikuwa  inabadilika kutokana na mabadiliko ya  kielimu, kisiasa na kidini, kiuchumi. Kanisa la  ulimwengu lilianza   kupoteza  nguvu  na kanisa la kitaifa likaanza kuchukua nafasi 
Kupanuka kijiografia  kulileta mabadiliko mengi katika kufiiri. Kwa kifupi kulikuwa na sababu mbalimbali zlizopelekea wimbi la matengenezo ya kanisa kutokea,  baadhi ya sababu hizo ni;

1.     Kukua kwa utaifa(nationalism).
Kila nchi ilianza kuweka mkazo kujijenga yenyewe, hivyo nchi mbalimbali zilianza kujitenga na ushirikiano wa kimataifa,  Hii ilipelekea kanisa la ulimwengu kokosa nguvu kwani utaifa ulisababisha kuanza kwa kanisa la kitaifa kila mahali.

2.     Kuvumbuliwa kwa mashine za uchapishaji.
Johann Guthenberg alivumbua mashine ya uchapaji  mwaka 1456. Mpaka wakati huu vitabu vyote viliandkwa na kunakiliwa kwa mkono.  Kuvumbuliwa kwa mashine hii kulisababisha  Biblia na maandiko mengine kuchapwa na kusambazwa katika maeneo mbalimbali. Kusambazwa kwa maandiko haayo kulipeleka kuamsha akiri za watu na kutambua hitaji la kuwepo kwa mabadiliko katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kanisa.

3.     Kuzuka kwa mwamko wa kujifunza. (Renaissence)
Hiki kilikuwa ni kipindi ambacho  ulizuka  mwamko mkubwa
 wa kujifunza . Kipindi hiki kilianza huko Ulaya Italia karne ya 14  na kuendelea hadi karne ya 17. Wasomi wengi waliibuka  katika kipindi hiki. Watu walianza kufikiri mambo kwa upya kutokana na elimu waliyokuwa wamepata. Kutokana na elimu hiyo watu walihitaji mabadiliko katika maeneo mbalimbali ili kuweza kuleta maendeleo. Hivyo kanisa nalo likajikuta linahitaji mabadiliko japo kuwa halikuwa tayari kwaajili ya mabadiliko hayo.

B.    VIONGOZI WA MATENGENEZO YA KANISA.
Katika kipengere hiki tutawatalii baadhi ya wana matengenezo ya kanisa, yaani tutawachunguza watu ambao Mungu aliwasimamisha  kuleta kweli ya neno la Mungu katika kanisa lililokuwa limepotoka na lisilokubali matengenezo kwa hiali. Tutawatalii wanamatengenezo wafuatao, Martn Luther, John Calvin, Ulrich Zwingli na John Knox.

1.Martin Luther

No comments:

Post a Comment