Sunday 30 November 2014

KUANDAA JUMBE ZA BIBLIA

Kuandaa Jumbe za
Biblia.
Kitabu cha ufafanuzi wa Biblia.
Wayne McDill
Southeastern Baptist Theological Seminary
Wake Forest, North Carolina USA
Kiswahili Editor, Joel M. Njoroge
ii
© 2002 Wayne McDill
All rights reserved
Permission to duplicate granted upon request.
Contact sebts.edu
iii
YALIYOMO.
Jinsi ya kutumia Kitabu hiki.
v
Somo la 1 Mjumbe wa Mungu.
1
Somo la 2 Neno Lililoandikwa.
7
Somo la 3 Kuchagua Kifungu cha Biblia.
13
Somo la 4 Kunakili Kifungu kwa Mkono.
19
Somo la 5 Kutafuta Maneno ya Kitendo.
25
Somo la 6 Kuwekea Alama Maneno ya Muhimu.
31
Somo la 7 Kuandika Kile Unachokiona.
37
Somo la 8 Kuorodhesha Viini vya Biblia.
43
Somo la 9 Kutengenezea Sentensi Wazo Kuu.
49
Somo la 10 Kuwekea Mpaka Somo.
55
Somo la 11 Kutafuta Sehemu.
61
Somo la 12 Kutengenezea Kifungu Pointi Kuu.
67
Somo la 13 Kuwafikiria Watu.
73
Somo la 14 Kutengeneza Picha za Maneno.
79
Somo la 15 Kusimulia Hadithi za Kweli.
85
Somo la 16 Mwito wa Kubadilika.
91
Somo la 17 Kukusudia kwa Imani.
97
Somo la 18 Kudokeza Ujumbe.
103
Somo la 19 Kupangilia Mahubiri Yako.
109
Somo la 20 Kuujenga mwili
115
Ushauri kwa Mwalimu.
121
iv
v
Jinsi ya kutumia Kitabu hiki.
Kuandaa Jumbe za Biblia ni kitabu chenye masomo 20 ya njia za mahubiri na mafundisho ya Biblia. Kinaweza kusomwa na mtu binafsi. Lakini pia kinaweza kutumiwa kama kitabu cha kufundishia katika darasa la mahubiri ya Biblia.
Watendakazi wa Kikristo wanaotaka kuandaa jumbe za Biblia zenye manufaa wataona ya kwamba kitabu hiki kiliandikwa kwa ajili yao. Hawahitaji kuwa na elimu ya juu. Hawahitaji kwenda shule. Hawahitaji kununua vitabu vingine vya ziada vya kujifunzia. Hawahitaji hata kuwa na mwalimu.
Kitabu cha kujifunzia kwa somo hili ni Biblia. Kusudi la somo ni kuweka njia ya kutumia vifungu vya Biblia kama msingi wa jumbe za Kikristo. Mtazamo wa andiko pia upo katika msingi wa Biblia. Mtazamo wa kanisa msingi wake ni Biblia. Mtazamo wa mjumbe wa Mungu msingi wake ni Biblia.
Ikiwa unapenda kusoma kitabu hiki, fanya hivyo ukiwa na Biblia yako mkononi. Utahitaji pia penseli au kalamuI na karatasi. Ufunguo wa mafanikio katika kujifunza utakuwa ni muda unaotumika katika kujifunza vifungu vya Biblia. Unaweza kusoma masomo yote katika kitabu hiki na bado usipokee faida yoyote ile kutoka humo. Ni pale tu unapochukua kalamu yako mkononi na kuorodhesha vifungu vya Biblia ndipo mafundisho yatakapo kuwa ya msaada.
Masomo ni mafupi. Muda mwingi utawekwa katika kukamilisha mazoezi rahisi mwishoni mwa kila somo. Kadiri unavyorudirudia masomo haya na vifungu mbalimbali, ndivyo haraka utakavyokuwa stadi katika njia hii ya kuandaa jumbe za Biblia.
Njia bora ya kukisoma ama kujifunza kitabu hiki ni kwa kushirikiana na wanafunzi wengine. Ushirika utasaidia kila mwanafunzi ahusike. Wale wanaotafuta kulitangaza neno la Mungu watachochewa na kutiwa moyo kwa kushirikiana.
Usiharakishe katika somo hili. Uwe mvumilivu unapofanyia kazi masomo haya. Usife moyo ikiwa masomo haya si rahisi. Kuandaa jumbe za biblia hakutazamiwi kuwa rahisi. Ni kazi iliyo ya umuhimu wa juu zaidi aifanyayo mtumishi wa Mungu. Maisha na kazi ya kanisa vinategemea sana kunenwa kunakofaa kwa kweli ya andiko.
Ikiwa somo hili ni la msaada kwako, wafikishie habari na wengine pia. Unaporidhika na njia hii, utaona kwamba wengine watataka kufuata mfano huo. Waeleze ni wapi wanaweza kupata kitabu hiki. Labda uchukue wajibu wa kuwafundisha watenda kazi wengine wa Kikristo.
vi
1
Somo la 1
MMjjuummbbee wwaa MMuunngguu..
Wewe u mjumbe wa Mungu.Ikiwa amekuita upeleke habari njema za Yesu Kristo kwa wanaopotea, wewe ni mjumbe wake. Ikiwa amekuita kupanda makanisa mapya, wewe ni mjumbe wake. Ikiwa amekuita kuwafundisha watu wake mahali popote waamini wanapokusanyika na kumwabudu, wewe ni mjumbe wake.
Mawakala Wanadamu.
Nyakati zingine Mungu amezungumza kupitia malaika (Waamuzi 6:20). Nyakati zingine Mungu amezungumza kupitia ndoto (Mwanzo 41:25).Mungu amezungumza pia na sauti ndogo(1 Wafalme 19:12) na kwa sauti ya ngurumo (Yohana 12:29). Wakati fulani Mungu alizungumza hata kupitia punda. (Hesabu 22:28). Lakini njia ya kawaida ya Mungu ya kuzungumza na Mwanadamu ni kupitia watumishi wake aliowachagua. Amezungumza katika vizazi vyote kupitia manabii wake kufanya mapenzi yake yajulikane. (Waebrania 1:1).
Mungu anawaita wajumbe wake kunena neno lake kwa majirani zao. Nyakati zingine anawaita kwenda sehemu za mbali kuzungumza kwa ajili yake. Yesu alisema, “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri injili kwa kila kiumbe.” (Marko 16:15). Anawaamuru, “Hubiri neno! Mwe tayari kwa wakati unaofaa na usiofaa.Karipia, onya, kemea kwa uvumilivu wote na mafundisho” (2 Timotheo 4:2).
Ni ukweli wa ajabu namna gani: Mungu anatumia wajumbe wanadamu kutoa ujumbe wake kwa wanadamu. Wajumbe wake mara nyingi wanahisi hawastahiri kwa kazi hiyo. Kama Musa,
“Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?” Warumi 10:14
Somo la 1
Mungu anawaita na kuwawezesha wajumbe wanadamu kutangaza neno lake kwa watu.
2
wanaweza wakalalamika,” Ee BWANA, mimi si msemaji,…. Maana mimi si mwepesi wa kusema na ulimi wangu ni mzito.” (Kutoka 4:10) Au kama Yeremia, wanaweza wakasema, “Aa Bwana Mungu, Tazama siwezi kuongea; maana mimi ni mtoto.” (Yeremia 1:6).
Mungu hazikubali sababu hizi. Hawaiti wale wanaoweza; Anawawezesha wale anaowaita. “Ni nani aliyefanya kinywa cha Mwanadamu?” Alimuuliza Musa, “Je si mimi Bwana?” (Kutoka 4:11). Alimwambia Yeremia, “Usiseme mimi ni mototo; maana utakwenda kwa kila mtu nitakaye kutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalo kuamuru. Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe” (Yeremia 1:7, 8). Japo wajumbe wa Mungu ni dhaifu na binadamu wasiokamili, wanabeba ujumbe wenye nguvu na uliovuviwa. Nyakati zingine wajumbe wa Mungu wanaona ni ngumu kuingia katika wito huu wa kiungu. Si jambo dogo kuzungumza kwa niaba ya Mungu. Paulo alisema, “ Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uweza iwe ya Mungu, wala si yetu.” ( Wakorintho 4:7).Ujumbe wa Mungu ni wa thamani lakini sisi tu vyombo vya udongo. Mungu anasitahili kupokea utukufu kwa kutumia vyombo hivi visivyo vya thamani.
Ujumbe pasipo Maneno.
Mjumbe wa Mungu si msemaji tu wa Mungu, ni msikilizaji pia wa neno la Mungu. Hatangazi kile asichokiamini. Ujumbe wa Mungu upo kwanza katika mawazo yake mwenyewe na moyo wake halafu katika midomo yake. Watu wanapoangalia nia na tabia yake, wanaona anavyoishi ndivyo anavyohubiri. “Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote,” Paulo aliandika, Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu,( Wakolosai 3:16, 17).
Maneno ya mjumbe wa Mungu yatasikika ikiwa tu maisha yake ni aminifu pia.Ni ujumbe wa ukimya wa mtazamo wake na tabia inayofanya ujumbe wake unaonenwa uaminike.
3
Maneno ya mjumbe wa Mungu yatasikika ikiwa tu maisha yake mwenyewe yanaaminika pia. Ni ujumbe wa ukimya wa nia na tabia yake unaofanya ujumbe wake ulionenwa uaminike. Hapaswi kuhubiri ujumbe mwingine na akaishi vingine. Maneno yake na matendo yake ni lazima yawe kitu kimoja.
Yesu alisema,Nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni” (Mathayo 5:16). Angalia jinsi nuru ya shuhuda zetu inawafanya watu kuangalia kwa ukaribu matendo yetu mema. Siku zote hilo ndilo swala. Ikiwa unasema wewe ni wa Yesu, watu wataangalia kuona ikiwa maisha yako yanazungumza kimya kimya kuhusu yeye( Yesu) pia.
Ikiwa tabia ya mtu ni nzuri, lakini hajulikani kama ni wa Kristo, watu watasema kuwa yeye ni mtu mwema, na watashindwa kuona kwamba Mungu ndiye anayemfanya kuwa mwema. Ikiwa maneno yake yanahusu Yesu, lakini haishi maisha ya mwamini, watamwita “mnafiki”. Ni pale tu maneno yake yanapoeleweka na matendo yake ni mazuri, watu watamwangalia na kumtukuza Mungu kwa ajili ya Maisha yake.
Nia ya Mjumbe wa Mungu kuhusu wito wake utaambukiza ujumbe wake kwa watu. Anaweza akajivuna. Anaweza akajidhania kuwa yu bora kuliko watu wengine. Badala ya huduma ya Yesu Kristo kupitia kwake. anaweza akadhani mwito wake kama huduma yake mwenyewe.
Ikiwa tabia zake haziko katika msingi wa kweli ya Biblia, wale wanaomsikiliza akihubiri watajua. Haitawezekana kutenganisha tabia yake na hali yake kutoka katika mahubiri yake.
Kielelezo Cha Mjumbe
Paulo alimsihi Timotheo, kijana wake katika huduma, kuwa “kielelezo katika usemi na mwenendo, katika upendo, katika roho,
“Basi wewe umfundishaye mwingine, je! Hujifundishi mwenyewe? Wewe uhubiriye kwamba mtu asiibe, waiba mwenyewe? Wewe ujisifuye katika torati, wamvunjia Mungu heshima kwa kuiasi torati?”
Warumi 2:21, 23
4
katika imani, na katika usafi” (1Timotheo 4:12). Hata kama Timotheo alikuwa ni kijana, angeweza kuwaonesha wengine jinsi ya kuishi kwa kielelezo chake yeye mwenyewe. Angeweza kuwa mwaminifu kwa ujumbe wake wa kimya wa maisha yake. Ndipo wangekuwa rahisi kupokea ujumbe wa injili ulionenwa. Mjumbe wa Mungu ni lazima aishi vile anavyohubiri.
Agizo hili kwa muhubiri linaweka mwelekeo kwa nia yake mwenyewe. Inataja sifa za muhimu kwa tabia zake. Lakini ni zaidi ya hilo. Ndicho kitu ambacho kusanyiko linachokihitaji ili wawe na heshima kwa mjumbe na ujumbe wake. Kielelezo ni kitu bora cha kufuata. Je inawezekana kwa mtumishi kijana kuwa kielelezo kwa waamini wazee? Ndio inawezekana. Katika kiwango chochote cha kukomaa kwako kwa sasa, unaweza kuwa kielelezo chema. Hata kama utaendelea kukua, unaweza kujiletea heshima na kutengeneza njia kwa wengine kufuata. Kumbuka hili: Huwezi kuwa mtu wa aina Fulani na ukawa muhubiri wa aina nyingine. Mstari huu unataja sifa sita ambazo muhubiri anatakiwa kuweka nyayo za kufuatwa na wengine. Chunguza pointi hizi za kielelezo kwa ukaribu zaidi pamoja na mi. Kwanza, mjumbe wa Mungu awe kielelezo “katika neno”. Watu hawataangalia kile unachokisema tu wakati wa mahubiri, wanasikiliza kile unachokisema katika usemi wako wa kila siku. Wanachunguza ikiwa usemi wako unafuata onyo la upole la Paulo, “Neno lolote lile lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililojema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.” (Waefeso 4:29). Usemi wetu uwajenge wasikilizaji ili kwamba maneno yetu yahudumu neema ya Mungu kwao.
Kumbuka hili: Huwezi kuwa mtu wa aina Fulani na muhubiri wa aina nyingine.
5
Pili, Mjumbe wa Mungu awe kielelezo katika “mwenendo”. Hii ni tabia na namna ya maisha. Watu wanategemea Mjumbe wa Mungu kuishi maisha yasiyo na shutuma, mbele za macho ya waamini na wasioamini vilevile ( 1Timotheo 3:7). Kusanyiko linaangalia jinsi gani muhubiri anavyoitendea jamaa yake, heshima yake kwa mkewe, anavyowatunza watoto wake. Wanaangalia mwenendo wake. Wanaangalia nia yake.
Tatu, Ni lazima awe kielelezo “katika upendo.” Upendo wa kikristo si kitu cha kujisikia tu kwa wengine. Ni swala la uamuzi na kitendo. Upendo wa kikristo hutafuta mambo ya wengine, kuwapa wengine mazuri ambayo Mungu angetaka kwa ajili yao. Watu wengine ni wagumu kupenda, lakini mjumbe wa Mungu anapaswa kuwapenda. Anajua kuwa upendo “huvumilia na hufadhiri” kwamba hauhusudu, hautakabari, haujivuni” na kadharika (1 Wakorintho 13:4).
Tafsiri zingine zimeweka pia “katika roho” katika kifungu hiki. Hii inaweza kumaanisha nia ya mjumbe wa Mungu. Njia moja ya kuonesha nia ni moyo wake wa bidii na juhudi kwa ajili ya kazi ya Mungu na Neno lake. Watu watasikia mafundisho na mahubiri ya Mtumishi wa Mungu kulingana na bidii ya moyo wake na ujumbe wake. Ikiwa muhubiri ni mtu aisye na shauku kubwa kuhusu ujumbe wake, je watu watauchukulia kwa uzito ujumbe wake? Jinsi muhubiri anavyonene na kuwashilisha ujumbe wake ndicho kitakachoamua ikiwa wasikilizaji wanasikiliza kile anachokisema.
Mjumbe wa Mungu awe kielelezo pia “katika Imani.” Katika sifa zote zinazohitajika kwa muhubiri na kwa watu, Imani ndicho kitu cha muhimu zaidi. Imani ndiyo shabaha ya kila mahubiri. Kutoka katika Imani thabiti hutoka Utii. Mjumbe wa Mungu hakika
“Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.”
1 Timotheo 4:12
6
aamini neno la Mungu. Hakika anaamini kuwa Mungu hufanya yale yote aliyoyaahidi. Hivyo basi anakuwa mfano sahihi na kielelezo kwa watu, katika umri wake wowote ule na kukomaa kwake. Sifa ya mwisho iliyotajwa katika mstari ni “Katika usafi.” Mjumbe wa Mungu awe ni kielelezo katika uaminifu wake wa uadilifu. Hakuna nafasi ya uchafu wa dunia katika kanisa. Utaona kumomonyoka kwa maadili katika sehemu zote zinazokuzunguka katika jamii yako. Lakini mjumbe wa Mungu ni lazima aepuke hata muonekano wa ovu. Hatajihusisha na hali ambayo inaleta taswishi juu ya tabia zake. Mtumishi anaweza kuheshimiwa ikiwa tu ana unyofu wa maisha. Yako mambo mengi yakusema juu ya nia na sifa za muhubiri. Lakini ukweli ni rahisi: Huwezi kuwa mtu wa aina moja na muhubiri wa aina nyingine.
Mazoezi ya Somo.
1. Rudia mawazo makuu ya somo hili: Mungu amewaita wanadamu wapeleke ujumbe wake kwa wengine. Mungu hawaiti wale wanaoweza; anawawezesha wale anaowaita. Ujumbe wetu wa kimya wa maisha yetu ndio unaoamua ikiwa maneno yetu tunayoyazungumza yatasikilizwa.
2. Soma wito wa Mungu kwa Isaya, Yeremia, Wafuasi wa kwanza wa Yesu, na Paulo. Andika kile unachokiona kama ishara za mwito wa Mungu. (Isaya 6:1-10; Yeremia 1:4-10; Mathayo 4: 18-22; Matendo 26:12-18).
7
Somo la 2
Mungu ametoa neno lake lililoandikwa katika Biblia ili kwamba ujumbe uweze kuhubiriwa kwa uaminifu katika kila kizazi.
Somo la 2
NNeennoo LLiilliillooaannddiikkwwaa..
Ikiwa mjumbe wa Mungu anataka kuwa mwaminifu kwa wito wake, atajuaje cha kusema? Je Mjumbe aseme mawazo yake mwenyewe? Je aseme tamaduni za watu? Au aseme kile ambacho amewasikia wengine wakikisema katika mahubiri yao? Je aombe kupata ujumbe mpya ambao haujasikika? Je aondoke nyumbani kwake na kwenda shuleni kujifunza cha kusema?
Maswali haya yote yanaweza kujibiwa kwa swali lingine: Je mjumbe wa Mungu ana Biblia ambayo anaweza kusoma kwa Lugha yake yeye mwenyewe? Ikiwa anayo, anaweza kuhubiri Neno la Mungu. Wale walio na elimu ya juu wanaweza wakaielewa Biblia kwa urahisi zaidi. Mjumbe wa Mungu atahitaji kupata mafunzo yote awezayo. Lakini wale wanaoweza kuisoma tu Biblia kwa maana yake ya wazi wanaweza pia kuielewa .
Kwa hivyo mjumbe wa Mungu anaweza kuhubiri Neno la Mungu ikiwa atasema ujumbe wa wazi wa andiko la kifungu. Katika somo hili, tutafikiri juu ya umuhimu wa neno la Mungu lililoandikwa.
Kitabu cha Mungu.
Kitabu cha Mungu si kitabu kama kitabu kingine chochote. Ni kitabu cha Vitabu. Ndani yake kuna vitabu 66, 39 katika Agano la Kale na 27 katika Agano jipya. Vitabu katika Biblia vinahusisha historia, shairi, nyimbo, unabii, nyaraka, na mahubiri. Biblia inaeleza hadithi za dunia ya Mungu kuanzia kabla ya uumbaji hadi baada ya mwisho wa mambo yote. Mungu amejionesha mwenyewe kwa mwanadamu kupitia vizazi vingi sana. Mkusanyiko wa ufunuo huo ndio sasa Biblia yetu.
BWANA akamwambia Musa, Andika maneno haya; kwa kuwa mimi nimefanya agano nawe, na pamoja na Israeli, kwa mujibu wa maneno haya." Kutoka 34:27.
8
Mahubiri lazima yasiwe kuhusu mashujaa wa zamani wa dini na jinsi gani tunaweza kuwa kama wao. Mahubiri lazima yawe kuhusu Mungu na jinsi gani tunaweza tukamwamini.
Mungu aliwatumia waandishi wanadamu kuweka ufunuo wake katika maandishi. Kila mmoja aliishi kwa wakati wake na akaandika katika lugha yake. Kila mmoja aliandika kwa maneno yake mwenyewe kwa wasikilizaji wa wakati wake. Japo ujumbe ulinenwa kwa maneno ya mwanadamu, ujumbe ulikuwa pia ni mawazo ya Mungu . Kila mwandishi wa Biblia aliandika kile Mungu alichomvuvia kukisema.
Mila mbalimbali kutoka mashariki ya kati zinaonekana katika maandiko haya – kutoka Mesopotamia, hadi Palestina ya zamani, hadi Misri, na kurudi mpaka Palestina. Watu wengi, miji mingi na wafalme wengi na vita vinatajwa kama watumishi wa Mungu walivyoshughulika navyo. Waandishi wa Biblia waliandika jinsi Mungu alivyojishughulisha nao katika maisha yao wenyewe. Japo Biblia inaeleza habari za watu wengi wa zamani, kimsingi inahusu Mungu. Mapango mkuu wa Mungu kwa ulimwengu na kwa mwanadamu unaonekana kupitia vizazi. Mpango wa Mungu unakamilishwa katika Kristo wa Nazarethi, Mwana wa Mungu. Kifungu chochote kile na kiini chochote kile, hadithi ya Yesu ndio ufunguo. Habari ya Yesu inaitwa Injili. Hii ina maana “habari njema.” Paulo anatafsiri injili, “Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara”(1 Wakorintho 15:3-5). Kifo cha Yesu msalabani kilikuwa ni kwa ajili ya dhambi za wanadamu. Mungu alimtoa mwana wake kama sadaka kwa ajili ya dhambi ili kwamba tupata nishwe naye. Hizo ni habari njema.
Kwa sababu biblia inahusu hasa Mungu, muhubiri atahitaji kuangalia kile kila kifungu kinachomwambia kuhusu Mungu. Mahubiri ni lazima yasiwe kuhusu mashujaa wa dini wa zamani na jinsi gani tunaweza kuwa kama wao. Mahubiri ni lazima yawe kuhusu Mungu na jinsi gani tanavyoweza kumwamini. Si kuhusu sheria ya Mungu tu. Inahusu pia neema ya Mungu ambayo kwayo alipokea na akatuwezesha kuishi kwa ajili yake. Mahubiri ni lazima yawe jinsi ya
9
kumjua Mungu kupitia Yesu Kristo na kuishi kama watumishi wake katika Ulimwengu huu wa giza.
Neno la Mungu ambalo limeandikwa.
Kwa sababu Mungu ametupa ujumbe wake katika neno lililoandikwa la maandiko, kila mjumbe lazima aende katika Biblia kujifunza nini cha kusema. Mungu hakudhani kama ingekuwa vizuri kupitisha tu ujumbe wake kwa mtu mmoja baada ya mwingine, kutoka kinywani kwenda sikioni. Badala yake alitaka liandikwe ili kwamba maneno yabaki kuwa yale yale. Alitaka ujumbe kuwa wa kweli na unaoeleweka kwa vizazi vyote.
Tusingekuwa na Biblia kama neno la Mungu lililoandikwa, wale waliokuwa wa kwanza kulipokea neno lake wangelipitisha kwa wengine, na wengine, na wengine. Mpaka wakati ambapo neno lililozungumzwa lingetufikia, lisingekuwa sahihi kama jinsi ambavyo lilivyokuwa neno la mwanzo. Mungu alimpa Musa maneno yake na akamwambia ayaandike. Mungu alimpa maneno yake Yeremia na akamwambia ayaandike. Mungu aliwaambia wanafunzi wake wa mwanzo kuandika habari za Yesu.
Unaukumbuka mchezo wa watoto wa kupitishiana ujumbe? Watoto wanakaa katika duara. Mmoja anafikiria ujumbe na anaunong’oneza kwa anayefuata, Halafu huyo naye anaunong’oneza ujumbe kwa anayefuata. Na kuendelea, mpaka ujumbe unafika katika duara zima. Mwishoni mtoto wa mwisho anatangaza ujumbe ambavyo ungekuwa. Mara nyingi atakuwa hana uhaki ka. Baada ya kusema kile anachodhani kuwa amekisikia, mtoto aliyeanza kusema ujumbe anasema kile ambacho kilichokuwa kinamaanishwa. Kila mmoja hucheka jinsi ambavyo ujumbe ulivyobadilishwa.
Isingekuwa kituko leo hii ikiwa ujumbe wa Mungu ungekuwa umepotoshwa kwa sababu ya kupitishwa kutoka mtu mmoja baada ya mwingine. Mungu alitaka watu wake kuusikia ujumbe ulio wa kweli kutoka kwake. Njia moja tu ambayo tunaweza kufanya hivyo sisi kama
“Haya, enenda sasa, andika neno hili katika kibao mbele ya macho yao, lichore katika kitabu ili liwe kwa ajili ya majira yakayokuja, kwa ushuhuda milele.” Isaya 30:8.
10
wajumbe wake ni kuwapa watu kile alichokisema katika Neno lake lililoandikwa, Biblia. Baadhi ya wajumbe wanaosema wanazungumza kwa ajili ya Mungu hawatoi neno kutoka katika kitabu Chake. Wahubiri na Waalimu hawa wanasema kile walichosikia wengine wanakisema. Wasema kuhusu ndoto zao. Watoa mawazo ya dini zao wenyewe. Nyakati zingine wanachanganya dini zao za zamani na imani zao mpya ndani ya Yesu. Wanaweza kuzungumza kwa ujasiri nakudai mamlaka ya Mungu, lakini ujumbe hautoki kwenye kitabu cha Mungu. Ni kwa kiasi gani kile wanachokisema kinatoka kwa Mungu? Tutajuaje kwamba ujumbe umetoka kwa Mungu? Je Muhubiri anachukua kitabu kitakatifu cha Mungu na kuelezea kinasema nini kwa watu? Na kama hafanyi hivyo, je ni mjumbe mwaminifu?
Wajumbe Waaminifu.
Kama mjumbe aliyetumwa na Mfalme na ujumbe wa muhimu kwa watu wake, Wajumbe wa Mungu ni lazima wazungumze. Ni lazima tutunze mahubiri hata tunapolemewa. Ni lazima tutunze mahubiri hata tunapotishwa. Ni lazima tupeleke ujumbe wa mfalme vinginevyo watu hawatasikia. Ni lazima tuuseme kwa makini, kile tu mfalme anachotaka tukiseme. Hatupaswi kutoa ujumbe wetu wenyewe. Sisi ni wajumbe, lakini ujumbe si wetu. Ni wa Mungu. Chetu sisi ni huduma ya Neno la Mungu. Mungu amezungumza na tunayo maneno yake katika Biblia. Katika Biblia tunajifunza jinsi ya kuweka imani yetu katika Yesu kama mwokozi wetu. Katika Biblia tunajifunza jinsi ya kuishi kama watu wa Mungu katika ulimwengu huu uliopotoka. Katika Biblia Mungu ametuahidi msamaha wake. Ametuahidi nguvu zake. Ametuahidi makao ya mbinguni.
Kama Mungu asingetuambia katika neno lake, tusingejua juu ya mwokozi wetu. Kama Mungu asingetuambia katika neno lake, tusingejua kuwa Mungu anatupenda, kwamba Mungu anawapenda
“Maana ijapokuwa naihubiri injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri injili!”
1 Wakorintho 9:16
11
watu wote na anawaita kuwa watoto wake. Mungu asingetuambia katika neno lake, tusingejua namna ya kufurahi katika shida zetu.
Pasipo neno la Mungu katika Biblia,tusingejua kuomba ipasavyo. Tusingejua kupendana sisi kwa sisi. Tusingejua jinsi ya kuishi maisha matakatifu. Kweli hizi za ajabu hazingekuja katika mawazo ya mtu yeyote yule kama Mungu asingemwambia. Na anatueleza katika Biblia.
Waamini wapya wanapoweka imani yao kwa Kristo, hawaelewi maisha ya imani. Mawazo yao bado yamejazwa na fikra za wasioamini. Hawajui jinsi ya kuomba. Hawajui jinsi ya kumtii Mungu. Hawajui jinsi ya kuwa nuru katika ulimwengu wa giza. Nani atawafundisha mawazo ya Mungu? Mungu anawaita na anawajalia wajumbe wake kwa kazi hiyo.
Kuwa wajumbe waaminifu, ni lazima kwanza tupokee ujumbe tunaotakiwa kuuutoa. Hii ina maana kwenda katika maandiko na kuchunguza kile Mungu alichokisema. Ndipo tutakapo hakikisha masomo au mahubiri yetu yanasema kile Mungu alichosema. Tunaweza kukielezea katika kizazi hiki. Tunaweza kukihusianisha na uzoevu wa maisha ya wasikilizaji wetu. Lakini ni lazima tusiubadilishe ujumbe au kuuwasilisha ujumbe ulio wetu.
Mawazo ya kidini ya muhubiri mwema yanaweza kuwa ni msaada. Anaweza kudhani kuwa yanasikika kuwa ni ya kihekima na ya changamoto.Lakini mawazo yake mwenyewe hayatakuwa na matokeo mazuri kwa wasikilizaji wake kama jinsi ambavyo ujumbe wa moja kwa moja wa neno la Mungu lililoandikwa ungekuwa. “‘Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyojuu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.” (Isaya 55:8, 9).
Changamoto kwa Muhubiri sasa ni hii, kwamba ujumbe wa andiku la Biblia uwe ujumbe katika mahubiri na mafundisho. Huko ndiko kuhubiri kwa uaminifu.“Maana neno la Mungu li hai, tena lina
Changamoto ya muhubiri sasa ni hii, kuwa na ujumbe wa kifungu cha Biblia, kukifanya ujumbe wa mahubiri. Hiyo ndiyo kuhubiri kwa uaminifu.
12
nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.” (Waebrania 4:12). Ujumbe wa kifungu unapokuwa ni ujumbe wa mahubiri, watu hulisikia neno la Mungu. Katika kitabu hiki, utajifunza jinsi ya kuyaruhusu mawazo ya Mungu kutoka katika Biblia yazungumze kupitia ujumbe unaoutoa kwa watu. Hiyo ndio kazi yako kama mjumbe wa Mungu. Unatakiwa uzungumze ujumbe wa Mungu. Hata kama ujumbe ni kupitia sauti yako, utakuwa ni ujumbe wa Mungu, Hata kama ujumbe utakuwa katika Lugha yako, utakuwa ni ujumbe wa Mungu. Hata kama utauelezea kulingana na maisha ya watu, utakuwa ni ujumbe wa Mungu.
Mazoezi ya Somo.
1. Rudia mawazo makuu ya somo hili: Biblia ni kitabu cha Mungu na kinaeleza jinsi Mungu anavyoshughulika na watu kupitia vizazi vingi. Biblia inahusu Mungu, hasa kuhusu Mwana wake, Yesu Kristo, Mwokozi wa Ulimwengu. Waamini wanaweza kujua mawazo ya Mungu na kuelewa imani ya Kweli kutoka katika Biblia tu. Mjumbe mwaminifu ataamua mawazo yake mwenyewe kwa kutumia mawazo kutoka katika Biblia na kufundisha Watu Mungu anasema nini.
2. Soma vifungu hivi kuhusu neno la Mungu na andika mawazo makuu ndani yake. Unajifunza nini kuhusu neno la Mungu ambacho haukukijua?(Kumbukumbu 4:1-8; Zaburi 119:9-16; Isaya 55:8-11; Waebrania 4:12).
13
Somo la 3
KKuucchhaagguuaa kkiiffuunngguu cchhaa BBiibblliiaa..
Jukumu la kwanza katika kuandaa ujumbe wa Biblia ni kuchagua kifungu. Katika somo hili, tutakuonesha kwamba, kila ujumbe wa Biblia unaweza kujengwa katika mawazo ya kifungu Fulani. Badala ya kufundisha mawazo yake mwenyewe, Mjumbe wa Mungu atafundisha mawazo ya Mungu kutoka katika kifungu cha Biblia.
Kifungu ni sehemu ya maandiko kilichochaguliwa kwa ajili ya kufundishia au kuhubiria. Kinaweza kuwa kidogo kama vile mstari mmoja au kikubwa kama vile sura kadhaa. Tafsiri za kisasa za Biblia, mara nyingi sana huzionesha sehemu hizi za maandiko kwa msomaji. Japokuwa mjumbe wa Mungu anaweza kuchagua kutokufuata vipande hivi katika tafsiri yake, mara nyingi huwa ni vya msaada.
Kifungu ni lazima kiwe kirefu kutosha kuwa chanzo cha mahubiri na kifupi kinachotosha kutumika katika muda uliopo. Katika nyaraka za Agano Jipya, kifungu kinaweza kuwa ni mistari michache tu. Hii ni kwa sababu nyaraka zinaweza kusema mengi sana katika maneno hayo machache. Angalia Warumi 12:1 na 2. Hata hivyo katika habari za Agano la Kale, kifungu kinaweza kuwa zaidi ya sura moja. Angalia wito wa Musa katika Kutoka 3 na 4.
Mjumbe wa Mungu atachagua kifungu kinachokidhi mahitaji ya wasikilizaji wake. Ataomba na kumwambia Mungu amuongoze katika kifungu sahihi. Mungu atamuongoza mjumbe wa Mungu katika vifungu vya Biblia na viini ambavyo watu wengi wanahitaji kuvisikia.
Somo La 3
Jukumu la kwanza katika kuandaa ujumbe wa Biblia ni kuchagua kifungu maalum
Kuandaa Ujumbe Chagua kifungu Nakili kifungu Maneno ya kitendo Maneno ya muhimu Machunguzi Viini vya Biblia Wazo kuu Kiini cha mpaka Mawazo saidizi. Pointi kuu Watu Picha za maneno Kusimulia hadithi Matumizi Kukusudia kwa imani Kuorodhesha
14
Kwa nini kuchagua kifungu?
Ikiwa Mjumbe wa Mungu anahitaji kuwafundisha watu kweli ya Mungu, ataamuaje nini cha kusema? Anaweza kuzungumzia juu ya mawazo yake mwenyewe ya kidini. Anaweza kuzungumza juu ya yale aliyoyasikia waalimu na wahubiri wengine wakiyasema. Anaweza kusimulia hadithi zake mwenyewe za jinsi anavyomfahamu Mungu. Anaweza kuwaambia watu jinsi wanavyopaswa kuishi. Maneno haya yote yanaweza kuwa msaada, lakini mjumbe wa Mungu ni lazima afikishe ujumbe wa Mungu.
Mungu ametoa ujumbe wake kwa mwanadamu katika kitabu tunachokiita Biblia. Alifanya hivyo kwa sababu alitaka neno lake litunzwe kutoka katika mabadiliko na mapotovu yote. Alitaka kweli yake isomwe na vizazi vyote hadi Yesu atakaporudi. Hakuna kitabu kama Biblia. Ni zawadi ya thamani ya Mungu kwa Watu wake. Imani ya Kikristo haiwezi kueleweka mbali na maneno ya Biblia.
Kuchagua kifungu kunamlinda mjumbe wa Mungu kutokuzungumzia mambo mengi kwa wakati mmoja. Ni bora kuwafundisha watu kuhusu kweli moja kuu kutoka kwa Mungu katika somo moja. Wakati mwingine wahubiri wanazungumzia mambo mengi sana yanayokuja akilini wakati wanapoongea. Hawana ujumbe mmoja mzuri unaoeleweka kutoka kwa Mungu na watu wanachanganyikiwa. Muhubiri mwenye kifungu kimoja cha kuelezea anaweza kuzungumzia ujumbe mmoja wa kifungu hicho.
Kuchagua kifungu kutoka katika Biblia kunampa mjumbe wa Mungu mamlaka ya kuzungumza. Ujumbe wake unapotoka katika kitabu cha Mungu, watu watasikiliza kwa sababu wanasikiliza kutoka kwa Mungu. Mamlaka ya mtumishi wa Mungu yamefungamanishwa sana na ujasili wake katika Biblia na mahubiri yake kutoka katika Biblia. Watu watamwamini kama kiongozi kwa sababu anajishusha katika neno la Mungu.
Kuchagua kifungu maalum kwa ajili ya somo au mahubiri kunawapa watu kufuatilia mafundisho yake katika Biblia zao wenyewe.
Hakuna kitabu kama Biblia. Ni zawadi ya thamani kutoka kwa Mungu kwa watu wake. Imani ya Kikristo haiwezi kueleweka mbali na maneno ya Biblia.
15
Ikiwa watu hawana Biblia, muhubiri anaweza akawaonesha maneno katika Biblia yake. Ikiwa wana Biblia, wana weza wakayaangalia maneno na kuhakikisha mjumbe wa Mungu anawasilisha kile Mungu anachokisema. Hii inawaruhusu watu kukusanyika pamoja katika maandiko pamoja na mtumishi wa Mungu na kusikia kutoka kwa Mungu kwa pamoja.
Aina mbalimbali za Vifungu.
Wakati muhubiri anachagua kifungu kwa kila ujumbe, mara tu atajifunza kwamba Biblia ina aina nyingi za maandiko. Baadhi ya vitabu vya Biblia ni vya historia. Vingine ni makusanyo ya sheria za Mungu. Vingine ni mashairi. Vingine ni vya kinabii. Vingine ni vya Maisha ya Yesu. Vingine ni vya Nyaraka. Vingi kati ya vitabu hivi vina mchanganyiko wa aina nyingi za maandiko. Kila kifungu kina muundo wake.
Sehemu kubwa ya Biblia imeandikwa kama hadithi. Hadithi hizi zinazungumzia juu ya historia ya Israeli. Zinazungumzia juu ya Abrahamu, Isaka na Yakobo, mababa wa imani. Zinaeleza juu ya mashujaa wakubwa kama Yusufu, Gidioni, Daudi, na Danieli. Hadithi za Biblia zinaeleza juu ya makabila na mataifa, mapigano na vita, utukufu na janga. Katika Agano Jipya, hadithi zinahusu Yesu na wanafunzi wake. Zinahusu kukua na masumbuko ya kanisa la kwanza.
Hata kama baadhi ya hadithi zinaeleza juu ya watu halisi na matukio halisi , ni mambo yanayohusu Mungu kabisa. Mpango mkuu wa Mungu kwa miaka mingi ya historia na umilele upo katika hadithi. Upendo wa Mungu kwa mwanadamu katika dhambi zake umeelezewa. Kuja kwa mwana wa Mungu kulipa gharama kwa ajili ya dhambi za mwanadamu ndio hadithi kuu, injili. Neno “Injili” maana yake ni “habari njema”. Habari ya Yesu ni habari njema kwa wote wanaoamini.
Hadithi zingine katika Biblia si za watu halisi na matukio halisi. Lakini ndani yake zina ukweli wa Mungu. Yesu alizungumza mafumbo
“Maagizo yako hunitia hekima kuliko maadui zangu, Kwa maana ninayo siku zote.
Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo.”
Zaburi 119:98, 99.
16
kwa wanafunzi wake ili kuwasaidia kuelewa ukweli wa Mungu. Alijua kwamba watu watakumbuka hadithi zaidi kuliko sheria. Alijua kwamba wataelewa mafundisho yake zaidi ikiwa atatumia neno la picha ambalo wanaweza wakaona katika mawazo.
Aina nyingine za vifungu katika Biblia ni nyimbo na mashairi. Kitabu cha Zaburi ni shairi. Imetengenezwa kwa wimbo ili iimbwe. Ni kitabu cha kuabudu cha Biblia.
Unabii ni aina nyingine ya muhimu ya maandiko ya Biblia. Manabii wa Agano la Kale waliwahubiria watu kuhusu kile Mungu alichokitazamia kutoka kwao. Wengi wao pia waliandika mahubiri yao. Walieleza pia juu ya maisha yao.
Biblia ina nyaraka pia ndani yake. Japo kuna nyaraka chache katika Agano la Kale, nyingi zimo katika Agano Jipya. Nyaraka hizi ziliandikwa awali na wafuasi wa karibu wa Yesu baada ya kuwa amerudi mbinguni. Ziliandikwa ili ziwafundishe watu nini wakiamini na jinsi gani ya kuishi.
Kupanga Mahubiri yako.
Kupanga huduma yako ya kuhubiri sanasana ni swala la kuchagua na kuvisoma vifungu vya Biblia ambavyo utavitumia. Mara utakapokuwa umechagua kifungu, kuandaa mahubiri hasa huwa ni kukisoma kifungu hicho. Mipango unayoweka ya kuhubiri itategemea na nafasi ulizonazo na asili ya wasikilizaji wako.
Ikiwa unaanzisha makanisa mapya, mahubiri yako na mafundisho yako yataundwa kuwalenga wasiowaamini kwa Imani ya Kikristo. Ikiwa unatumika katika kanisa lililokwisha kuanzishwa, utahitaji kuwalisha kondoo hao na kweli ya Mungu. Kumbuka, mjumbe wa Mungu anakuwa mwaminifu pale tu anapotoa ujumbe wa Mungu kutoka katika neno lake lililoandikwa.
Ikiwa hauja andaa mahubiri kwa kusoma kwa makini kifungu, utahitaji kuanza kwa vifungu vilivyo na mistari michache. Hapa kuna baadhi ya vifungu vifupi ambavyo huwa ninavipenda.
“Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.
Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.
Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.”
Zaburi 119:9-11.
17
Luka 21:1-4 – Senti ya Mjane. Mathayo 7:24-27 – Fumbo la wajenzi. Isaya 66:2 – Yule Mungu anayemwangalia. 1 Petro 1:3-5 – Urithi wa Mbinguni. Warumi 12:1, 2 – Kuyajua mapenzi ya Mungu. Luka 9:57-62 – Watatu ambao wangekuwa wafuasi. Warumi 3:21-26 – Haki katika Kristo. Yakobo 1:12-15 – Jinsi majaribu yanavyofanya kazi. Yeremia 2:9-13 – Birika lililovunjika. 1Yohana 2:15-17 – Msiipende Dunia. Marko 4:35-41 – Yesu anakemea dhoruba. Luka 6:43-45 –Mti unajulikana kwa matunda yake. Isaya 40:27-31 – Wale wamngojao Bwana. Marko 10:46-52 – Kuponywa kwa Batimayo. Zaburi 15:1-5 –Mweye Haki.
Katika kusanyiko lililowekwa tayari, utahitaji pia kupanga mfululizo wa mahubiri. Kufanya hivi unaweza kuhubiri kupitia kitabu cha Biblia. Lakini pia unaweza kuhubiri kupitia kipengele, kama vile mahubiri mlimani katika Mathayo sura ya 5 – 7. Unaweza kuhubiri pia aina nyingine za mfululizo katika tabia mbalimbali za Biblia, katika Amri Kumi za Mungu, au katika mafundisho ya Biblia kuhusu masomo Fulani. Hata hivyo, kwa namna yoyote ile, chukua kifungu kwa ajili ya mafundisho yako na ukisome kwa umakini kulingana na ujumbe wake uliokusudiwa.
Nimehubiri mfululizo wa masomo 18 kutoka katika nyaraka ya Yakobo. Kwa kuanza, nilikigawa kitabu katika vifungu vya kuhubiria. Halafu nikapanga tarehe ya kila somo. Somo la kwanza lilikuwa ni picha nzima ya kitabu chenyewe. Hapa kuna vifungu vingine 6 na vichwa vyake vya habari kutoka katika sura ya 1 ya Yakobo: Yakobo 1:2-4 Kuitikia tatizo. Yakobo 1:5-8 Kuomba ufahamu. Yakobo 1:9-11 Utukufu wa maisha.
“Kisha Yeremia akamwita Baruku, mwana wa Neria; naye Baruku akaandika katika gombo la chuo maneno yote ya BWANA, yaliyotoka kinywani mwa Yeremia, ambayo BWANA amemwambia.”
Yeremia 36:4
18
Yakobo 1:12-15 Jinsi majaribu yanavyofanya kazi. Yakobo 1:16-20 Kupata unachokitaka. Yakobo 1:21-27 Kupita kusikia mpaka kufanya.
Kuhubiri kupitia vitabu vya Biblia ina uthamani mkubwa sana, kwa muhubiri na kwa wasikilizaji.Tutaangalia jinsi ya kupanga aina hii ya mahubiri katika somo la 9.
Katika somo letu lijalo, tutajifunza jinsi ya kuanza kusoma kifungu kwa makini kwa ajili ya maana iliyonacho.Nimechagua Yohana 3:1- 8 kama kifungu maalum cha kujifunzia. Kifungu hiki ni cha muhimu sana katika kuelewa maisha ya Kikristo.
Mazoezi ya Somo.
1. Rudia mawazo makuu ya somo hili: Ujumbe unaolenga kifungu maalum cha maandiko, unamuhakikishia mjumbe wa Mungu kwamba somo lake linatoa mawazo ya Mungu. Kuchagua kifungu kimoja, kinamuweka mjumbe katika kulenga wazo moja kutoka katika Biblia. Kuhubiri kutoka katika kifungu, huleta mamlaka ya Mungu katika ujumbe. Kuhubiri kutoka katika kifungu, huwatia moyo watu kusoma neno la Mungu.
2. Angalia tena orodha ya vifungu katika somo hili. Soma vyote unavyodhani vitakuwa vizuri kwa mahubiri na mafundisho yako. Ni aina gani ya kifungu watu wanahitaji?
19
Somo la 4
KKuunnaakkiillii KKiiffuunngguu kkwwaa MMkkoonnoo..
Umechagua kifungu chako. Kwa hivyo, unatakiwa ukisome sasa kwa makini ili uuelewe ujumbe wakifungu.Hii ndio kazi ya kwanza ya mjumbe wa Mungu. Unakisoma kifungu kujifunza kinasema nini. Mwandishi alikuwa na ujumbe kwa wasikilizaji wake mwenyewe wakati kifungu kilipoandikwa siku nyingi zilizopita. Ujumbe huo una mawazo ya Mungu ndani yake kwa kizazi chetu pia.
Katika somo hili, tutaanza kazi nyingi za muhimu katika kazi ya kusoma maneno ya kifungu chako. Kazi zote hizi zinapaswa kufanyika kwa kuangalia kwa makini katika kifungu. Hatuanzi kwa kupanga ujumbe wetu kwa kufikiri mawazo yetu. Hatuanzi kwa kumuuliza mtu tunapaswa kusema nini. Hatuanzi kwa kuhubiri yale ambayo wengine wameyasema. Tunaanza kwa kuchagua kifungu kama Mungu anavyotuongoza na kuangalia kwa makini kila maelezo ya kifungu hicho.
Kufanya kazi na kifungu.
Kwa kuanza somo letu katika somo hili,Nimechagua kifungu cha muhimu ambacho utahitaji kuhubiri kwa watu wako. Hii ni habari ya Nikodemo aliyekwenda kwa Yesu usiku kuongea naye kuhusu miujiza yake. Ni mahali hapa ambapo Yesu anatangaza, “Ni lazima uzaliwe mara ya pili”. Katika Biblia yako, kifungu hiki kitaonekana hivi:
Yohana 3:1-8
1. Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi.
2. Huyu alimjia usiku akamwambia, “Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu
Lesson 4
Kuandika kifungu kwa mkono, kifungu kwa kifungu inaweza kukusaidia kuona maelezo ya muhimu ya kifungu
Kuandaa ujumbe Chagua kifungu Nakili kifungu Maneno ya kitendo Maneno ya muhimu Machunguzi Viini vya Biblia Wazo kuu Kiini cha mpaka Mawazo saidizi Pointi kuu. Watu Picha za maneno Kusimulia hadithi Matumizi Kukusudia kwa imani. Kuorodhesha
20
awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye."
3. Yesu akajibu, akamwambia, “Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.”
4. Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5. Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu.
6. "Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.”
7. "Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.”
8. "Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho”
Soma kifungu hiki mara kadhaa kwa uangalifu. Angalia kwa ukaribu maneno na vifungu vya maneno. Anagalia jinsi hadithi inavyofahamisha. Unakuwa kama daktari anayemchunguza mgonjwa kugundua nini kinachomfanya augue. Unaangalia katika kila kidokezi katika kifungu kuhusu maana iliyokusudiwa na mwandishi. Kumbuka hautafuti mahubiri wakati huu. Unajaribu kuelewa kifungu kinasema nini kama jinsi mwandishi na Roho Mtakatifu walivyokikusudia tangu awali.
Unapokisoma kifungu, angalia pia sehemu zilizoko kabla na baada tu ya kifungu ulichokichagua. Utakielewa vizuri kifungu chako ulichokichagua utakapoona nini zaidi mwandishi alichokisema na jinsi gani kifungu chako kinavyopatuna na mawazo yake.
Andika kifungu kwa Mkono.
Njia bora na rahisi kuchunguza kila neno katika kifungu ni kunakili kifungu kizima kwa mkono wako mwenyewe. Ninashauri ukinakili kwa herufi kubwa chini ya upande wa kushoto wa karatasi yako. Baadae utaandika notsi katika upande wa kulia wa karatasi. Kunakili kifungu kwa mkono itakusaidia kukifahamu kifungu vizuri zaidi. Utayachukua maneno ya kifungu kutoka katika Biblia na
Unakuwa kama daktari anayemchunguza mgonjwa kugundua nini kinachosababisha augue. Unaangalia dalili zote katika kifungu kama maana iliyokusudiwa na mwandishi.
21
kuyaweka katika karatasi yako mwenyewe. Utayaweka pia katika mawazo yako mwenyewe. Unapoyaandika maneno ya kifungu katika karatasi yako, ndipo unapoweza kuyawekea alama, kama jinsi nitakavyoshauri katika somo hili. Mara kwa mara utaweza kuyarudia maneno hayo ya kifungu kutoka moyoni mwako utakapokuwa umeyaandika na kuyawekea alama.
Utagundua kwamba, kunakili kifungu kwa mkono inawezesha neno kuzungumza moja kwa moja kwako. Ni lazima ukisome, na vizuri zaidi kwa sauti. Halafu unakinakili neno kwa neno na kifungu kwa kifungu. Ni lazima ukikague pia kuhakikisha kuwa unacho kwa usahihi. Katika Kila hatua unalishikilia neno la Mungu. Katika Kila hatua anaweza kuzungumza na wewe kwa utajiri walo neno. Hata kama haupangi ujumbe, njia hii ya kusoma maandiko inaweza kubadilisha maisha yako.
Unaponakili kifungu neno kwa neno kutoka katika Biblia, utatakiwa keundeleza kilaneno. Jambo hili litakufanya uyaangalia maneno kwa makini. Utagundua kwamba mwandishi alichagua maneno yake kukisema kile tu alichokikusudia kukisema. Maneno aliyoyachagua yanaonekana katika tafsiri ya Biblia yako katika lugha yako. Maneno ya asili ya Biblia yalikuwa katika Kiebrania, Kiyunani na kiaramaiki. Kile unachokisoma katika lugha yako ni halisi katika maana ya maneno ya asili.
Unaponakili kifungu kwa mkono, utayaona pia makundi ya maneno yanayokwenda pamoja. Tunapozungumza, hatusemi neno moja kwa wakati mmoja kutoa maana yetu. Tunasema makundi ya maneno, yanayoitwa vifungu. Njisi mamneno haya yanavyokwenda pamoja ni muhimu sana katika kuelewa kwetu kifungu cha Biblia. Kulisema neno moja tu lenyewe mara nyingi halitoi maana inayoeleweka. Lakini makundi ya maneno kwa pamoja yanafanya wazo lieleweke.
Unaponakili maneno ya kifungu, yaandike katika makundi. Vifungu hivi vinatengeneza sehemu ndogondogo za kifungu.
“Maneno haya yote nikuagizayo yote yatunze na kuyasikia, ili upate kufanikiwa na watoto wako baada yako milele, hapo uyafanyapo yaliyo mema na kuelekea machoni pa BWANA, Mungu wako.”
Kumbukumbu 12:28
22
Vinaeleza pia maneno gani yanayokwenda pamoja. Usishughulike sana na jinsi ya kuvitenganisha vifungu. Viandike tu kama jinsi vinavyoelezewa katika lugha yako.
Hapa kuna kifungu kutoka Yohana kama mfano.
Yohana 3:1-8
1. Basi palikuwa
na mtu mmoja wa
Mafarisayo, jina
lake Nikodemo,
mkuu wa wayahudi.
2. Huyu alimjia
usiku,akamwambia,
Rabi, twajua yakuwa
u mwalimu,umetoka
kwa Mungu; kwa maana
hakuna mtu awezaye
Kuzifanya ishara
hizi uzifanyazo
Wewe, isipokuwa Mungu
yu pamoja naye.”
3. Yesu akajibu, akamwambia,
Amin, amin, nakuambia,
Mtu asipozaliwa mara ya pili,
Hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
4. Nikodemo akamwambia,
Awezaje mtu kuzaliwa akiwa mzee?
Aweza kuingia tumboni mwa mamaye
Akazaliwa?”
5. Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia,
Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho,
Hawezi kuingia ufalme wa Mungu.
6. "Kilichozaliwa kwa mwili
ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho,
ni roho.
7. "usistaajabu kwa kuwa nilikuambia,
hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
“Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.“
2 Wakorintho 5:17
23
8. "Upepo Huvuma upendako,
na sauti yake waisikia,
lakini hujui unakotoka wala unakokwenda;
kadhalika na hali kila
mtu aliyezaliwa kwa Roho.”
Unaponakili kifungu hiki wewe mwenyewe, unaweza ukakigawanya katika njia tofauti. Hakuna njia moja tu ya kufanya hivyo. Kisome kifungu kwa sauti na uone ni jinsi gani maneno yanavyoweza kuwekwa katika mafungu unapozungumza. Huo utakuwa ni utengenezaji wa vifungu ambao utakuwa ni wa asili kwa wasikilizaji wako. Nakili kifungu katika vifungu hivyo vya maneno.
Tayari utaona kuwa kunakili kifungu kwa mkono inakusaidia wewe kuona nini mwandishi anachokisema. Fikiri juu ya jinsi baadhi ya vifungu vya maneno vinavyoungana na vifungu vingine vya maneno. Katika mstari wa kwanza, kifungu “wa Mafarisayo” ksinasema juu ya “mtu” katika kifungu cha maneno cha juu yake. Halafu, “aliyeitwa Nikodemo” inaeleza zaidi kuhusu mtu. Kifungu, “mkuu wa Wayahudi,” kinaeleza zaidi kuhusu mtu mwenyewe.
Kumbuka kwamba kusudi lako ni kuelewa maana iliyokusudiwa na mwandishi wa kifungu. Kuona jinsi vifungu vya maneno vinavyohusiana kimoja hadi kingine itakuonesha vizuri zaidi mwandishi anasema nini. Maneno madogo ya kiunganishi katika vifungu vingi vya maneno vinakusaidia katika hatua hii, maneno kama vile wa, na, kwa, na isipokuwa.Tutayajadili tena zaidi maneno haya ya viunganishi baadae katika somo letu.
Hapa kuna kifungu kingine tena kama utaweza kukinakili kwa mkono.
Mathayo 5:13-16
13 "Ninyi ni chumvi
ya dunia; Lakini chumvi
ikiwa imeharibika,
16 “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
2 Timotheo 3:16, 17.
24
Itatiwa nini hata ikolee?
Haifai tena kabisa, ila
kutupwa nje na kukanyagwa
na watu.
14 "Ninyi ni nuru ya ulimwengu.
Mji hauwezi kusitirika ukiwa
juu ya mlima.
15 "Wala watu hawawashi
taa na kuiweka chini ya
pishi, bali juu ya kiango;
nayo yawaangaza wote waliomo
nyumbani.
16 "Vivyo hivyo nuru yenu
na iangaze mbele ya watu,
wapate kuyaona matendo yenu mema,
wamtukuze baba yenu aliyeko mbinguni.
Katika masomo mawili yajayo, tutaendelea kushughulikia nakala yako uliyoiandika kwa mkono ya kifungu hiki. Usijali sana kama mwandiko wako si mzuri. Notsi zako za kujisomea ni kwa matumizi yako. Ili mladi tu unaweza kuzisoma, basi zina msaada.
Mazoezi ya Somo.
1. Rudia mawazo makuu ya somo hili: Vidokezi vya maana ya kifungu vipo katika maelezo ya maneno ya kifungu. Ni lazima tujifunze kuangalia kwa makini vitu vidogo vidogo katika kifungu ikiwa tunataka kupata picha kamili. Tunaweza kuona vizuri maelezo ya kifungu ikiwa tunakili kifungu kwa mikono yetu wenyewe, kifungu kwa kifungu.
2. Kabla ya kuhamia katika somo linalofuata, angalia vifungu vingine pia kama jinsi tulivyofanya hapa. Vinakili kwa mkono, kifungu kwa kifungu. Ninapendekeza usome Zaburi 1 na Warumi 12:1,2. Usifanye haraka. Chukua muda unaouhitaji.Jinsi unavyojifunza vifungu vingi, ndivyo jinsi utakavyoweza kuvifanyia kazi kwa haraka.
25
Somo la 5
KKuuttaaffuuttaa mmaanneennoo yyaa KKiitteennddoo..
Sasa umekwisha kuchagua kifungu chako. Halafu umeandika pembeni kifungu kwa mkono wako kwa kifungu. Hatua inayofuata ni kugundua maneno yote ya vitendo katika kifungu na kuyapigia mstari katika nakara yako uliyoiandika kwa mkono. Maneno haya yatakuwa ya muhimu sana katika kufungua maana ya kifungu kwako.
Katika kujifunza lugha, maneno haya ya kitendo yanaitwa vitenzi. Hata kama hatukusudii kujifinza matuumizi ya lugha katika kozi hii, jinsi aina mbalimbali za maneno zinavyofanya kazi zake zitakuwa ni za muhimu sana kwetu. Tunataka kuelewa maana halisi iliyokusudiwa na mwandishi wa awali wa kifungu. Kuangalia kwa makini katika maneno yake ndio njia pekee ya kugundua nini alichokusudia kusema.
Kupigia Mstari Vitenzi.
Sasa wekea alama nakara yako ya kifungu uliyoiandika kwa mkono, kwa kupigia mstari maneno yote ya kitendo. Ni ya muhimu katika kifungu chochote kwa sababu yanatueleza kitendo gani kinachoalifiwa katika kifungu. Mara nyigi maneno ya kitendo huwa ni ufunguo katika kuelewa maana ya kifungu.
Nimepitia nakara yangu niliyoiandika kwa mkono ya Yohana 3:1-8 na nikapigia mstari maneno ya kitendo. Je, Nimeacha kitu chochote?
Yohana 3:1-8
1. Basi palikuwa na mtu mmoja
Somo la 5
Kuwekea alama maneno yote ya ktitendo katika kifungu, itakusaidia kuona nini mwandishi wa kifungu alikusudia kusema.
Kuandaa Ujumbe. Chagua Kifungu. Nakili kifungu. Maneno ya kitendo. Maneno ya muhimu. Vilivyochunguzwa. Viini vya Biblia. Wazo Kuu. Kiini cha mpaka. Mawazo saidizi. Pointi kuu. Watu. Picha za maneno. Kusimulia Hadithi. Matumizi. Kukusudia kwa Imani. Kuorodhesha.
26
wa mafarisayo, jina lake Nikodemo, Mkuu wa Wayahudi. 2. Huyu alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye." 3. Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.”
4. Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? 5. Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. 6. "KIlichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. 7. "Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.”
9. "Upepo huvuma upendako, na sauti
yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho." Tayari unaweza kuona, katika kupigia mstari vitenzi kwamba kifungu kinafungua maana yake kwako. Je, uligundua maneno ambayo yanajirudia mara kwa mara? Nimehesabu mara 8 kwamba neno “kuzaliwa” limetumika. Hii inaniambia kwamba swala la kuzaliwa mara ya pili ni la muhimu sana. Kuandika kifungu pembeni kwa mkono na kupigia mstari vitenzi kunafanya wazo la kuzaliwa lionekane.
Aina za Vitenzi.
Hata kama tunayaita “maneno ya kitendo,” vitenzi vingine havioneshi tendo lolote lile. Vinatuambia tu kwamba mtu alikuwepo.
“ Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa macho yao, wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.”
Mathayo 13:15.
27
Hivi vinaitwa “vitenzi visaidizi”. Angalia katika Yohana 3:1-8 kwamba kitendo cha kwanza ni “palikuwa”. Mstari wa kwanza unasema “Basi palikuwa na mtu….” Neno hili halielezei mtu kufanya kitu chochote kile au kufanya kitendo chochote kile. Kinasema tu kwamba alikuwepo. Palikuwa na mtu wa hivyo. Kitendo kingine cha namna hiyo ni katika mstari wa 2, wakati Nikodemo aliposema, “Wewe ni mwalimu…..” Hata kama hakuna tendo lolote linalohusishwa, pigia mstari pia vitenzi hivi visaidizi.
Vitenzi vingine ni vya kutendewa. Hii ina maana mtu mwingine anafanya kitu kwa mtu anaye husika. Angalia tena mstari wa 1 wa Yohana 3. Hapo mwandishi anasema kwamba mtu huyo aliitwa Nikodemo. Hakujiita mwenyewe. Labda baba yake na mama yake ndio walimuita hivyo. Hata kama kitendo hakikufanywa na Nikodemo, lakini kilimuhusu. Hiyo ni kutendewa, ikiwa na maana kwamba, mtendewa alipokea au aliathiriwa na kitendo.
Vitendo vingine ni maneno ya kitendo. Hii inamaanisha, mtu anayeelezewa katika sentensi alifanya kitendo. Nikodemo hakujiita mwenyewe jina hilo. Kwa hivyo “aliitwa” ni kutendewa. Lakini katika mstari wa 2 tunasoma kwamba “alikuja” kwa Yesu na “akamwambia”.Hivi ni vitenzi vitenda. Hivi ndivyo nikodemo alivyotenda.
Vitenzi vingine vinaelezea juu ya matendo yaliyotendeka wakati mwingine. Tunasoma kwamba Nikodemo alikwenda kwa Yesu. Hiki ni kitendo kilichopita. Kitendo kilichotokea siku nyingine ambayo imepita. Si kwamba bado kinatokea. Kimekwisha. Vitenzi hivi vilivyopita vinatumika mara nyingi sana kusimulia hadithi, ikiwa ni za kweli au za kutunga.
Vitenzi vinavyozungumzia kile kinachotekea sasa, vinaitwa, vitenzi vya wakati uliopo. Katika mstari wa 2 Nikodemo alisema,
“Musa akaenda akawaambia watu maneno yote ya BWANA, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote yaliyonenwa na BWANA tutayatenda‟” Kutoka 24:3.
28
”Tunajua….” Anamaanisha kusema kwamba bado wanajua wakati huo anaozungumza. Vitenzi vingine pia vinaeleza yale ambayo bado hayajatokea; hivi ni vitenzi vya wakati ujao. Hakuna vitenzi vya wakati ujao katika Yohana 3:1-8.s Lakini angalia katika Zaburi 1. Mstari wa 3 unasema juu ya mwenye haki kwamba “lolote afanyalo litafanikiwa.” Huu ni wakati ujao. Inatabiri nini kitatokea baadaye. Mwandishi wa Zaburi anasema katika siku zijazo mtu huyu atazaa matunda katika kila hali. Angalia aina mbalimbali za vitenzi juu ya nini vinakuambia kuhusu maana ya mwandishi. Tumeona kwamba kuna vitenzi visaidizi, vitenzi vitendewa, na vitenzi vitenda. Vitenzi vinaweza pia kutueleza wakati wa kitendo, ikiwa ni wakati uliopita, uliopo, au ujao. Zipo aina azingine maalumu za maneno ya kitendo, lakini hatuta jishughulisha navyo katika somo hili.
Kujifunza kuhusu Mungu na Mwanadamu.
Vitenzi katika Biblia vinatusaidia zaidi kwa kutueleza kuhusu Mungu. Muhimu pia ni kuwa vinatueleza kuhusu mwanadamu. Zamani katika Biblia, katika Mwanzo 1:1,tunaambiwa, “Mungu aliziumba mbingu na nchi.” Tunajifunza katika Mwanzo 1:27 kwamba “Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake” Halafu Mungu akamwambia mwanadamu kuwa aweza kula matunda ya miti yote isipokuwa mmoja, ambao hatakiwi kuula. Katika 2:22 kifungu kinatuambia kuwa Mungu alimfanya mwanamke na akamleta kwa mwanamume. Katika Mwanzo 3:6 Biblia inatuambia kwamba mwanamke alichuma tunda la mti uliokatazwa, akampa mume wake naye akala. Halafu wakaogopa na kujificha kutoka kwa Mungu (Mwanzo 3:10).
Matendo haya, ya Mungu na ya mwanamume na mwanamke, yanatueleza zaidi kuwahusu wao. Yanatueleza
“ Mungu ambaye alisema zamani na baba zetu katiika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi anasema na sisi katika Mwana,” Waebrania 1:1, 2
29
kwamba Mungu ni muumbaji wa vyote. Yanatueleza kwamba alimuumba mwanamume na mwanamke. Yanatueleza kwamba aliwapa vyote walivyohitaji kula. Lakini tunajifunza pia aliwakataza kula mti mmoja. Halafu tunajifunza katika matendo kwamba walikula mti huu waliokatazwa. Kuanzia hapo walimuogopa Mungu na kujificha kutoka kwake.
Unapoangalia katika kifungu chochote kile cha Biblia, vitenzi vitakuwa ni vya muhimu sana katika kuelewa ujumbe wake. Ujumbe huo mara nyingi utakuwa unamuhusu Mungu. Angalia ni nini maneno ya kitendo yanakueleza kuhusu Mungu. Kwa sababu Mungu wakati wote anafanya kwa jinsi asili yake, Matendo yake yanafunua tabia zake.
Ujumbe unaweza pia kuwa unahusu mwanadamu, na maneno ya kitendo yatakueleza zaidi kuhusu yeye. Wakati wote Mwanadamu hawezi kuenenda kama jinsi asili yake halisi ilivyo. Anaweza kuwa mnafiki. Lakini hawezi kuificha tabia yake ya kweli. Matendo yake yatamuelezea.
Vitendo vinatumika kutueleza jinsi ya kumtii Mungu. Mara nyingi amri hizi zinatueleza ni nini tusichopaswa kufanya. Angalia Amri Kumi katika kutoka 20. Nane kati ya Amri hizo zinatuambia nini tusichopaswa kufanya na mbili kati ya hizo zinatuambia nini cha kufanya. Maneno haya ya kitendo ni muhimu kutueleza nini Mungu anategemea kutoka kwetu. Agano Jipya pia linatumia maneno mengi sana ya kitendo kuwaeleza wasomaji kwa uwazi kabisa jinsi gani ya kuenenda.
Katika 1 Wakorintho 15, Paulo anatoa maelezo mafupi juu ya Injili ya Yesu. Angalia maneno ya kitendo katika mistari ya 3-8. Yanatuleza kwamba Yesu alitkufa kwa ajili ya dhambi zetu, kwamba akazikwa, kwamba akafufuka tena, na kwamba akaonwa
“Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye, busara aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.” Mathayo 7:24
30
yu hai na watu wengi. Je, umegundua kuwa pana maneno mawili ya utendewaji katika kifungu hiki. Katika somo linalofuata, tutaangalia pia aina nyingine ya maneno. Kumbuka, tunayatafiti maneno ya kifungu kama wanasayansi, kugundua nini tunaweza kujifunza. Hatukisomi kifungu kwa ajili ya wazo la mahubiri ya haraka. Tunakisoma kugundua nini mwandishi aliyevuviwa alichokuwa anakisema. Halafu tunaweza kuufanya ukweli wa kifungu hicho ukweli wa ujumbe wetu kwa watu.
Mazoezi ya Somo.
1. Rudia mawazo makuu ya somo hili: Vitenzi ni maneno ya kitendo yanayotusaidia kuona nini mwandishi alikusudia kusema. Kupigia mstari vitenzi katika nakara yako uliyoiandika kwa mkono itakufanya uangalie kitendo katika kifungu. Kuna aina nyingi za vitenzi, vikiwemo vitenzi visaidizi, vitenzi vitenda na vitendewa, na nyakati nyingi mbalimbali. Vitenzi mara nyingi vinaelezea matendo ya Mungu na kutusaidia sisi kuelewa tabia zake na kazi zake za uweza. Vitenzi pia vinafunua tabia za mwanadamu kwa kuelezea matendo yake.
2. Angalia kwa makini maneno ya kitendo katika vifungu viwili vilivyotajwa hapo mwisho katika somo hili: Kutoka 20:1-17, Amri Kumi za Mungu na 1 sWakorintho 15:1-8, Injili. Chunguza pia Mathayo 9:35-38 kuona kitendo gani Yesu alikichukua kwa watu na kitendo gani alikitaka kwa wanafunzi wake.
31
Somo la 6
KKuuwweekkeeaa AAllaammaa MMaanneennoo MMaakkuuuu..
Maneno yanabeba maana. Baadhi ya maneno yanabeba maana nzito, kama vile gari la mizigo lililobeba mazao ya sokoni. Maneno mengine katika kifungu cha Biblia si ya muhimu sana, lakini yanasaidia kushikilia maana pamoja. Maneno mengine ya Biblia ni misingi ya imani yetu kuhusu Mungu. Haya ni maneno ya muhimu sana. Maneno yote ya kifungu yana uthamani wake katika kuelewa kwako.
Utasoma kwa makini sana maneno ya kifungu. Mwandishi wa kifungu ameweka mawazo yake katika maneno haya. Sasa ni lazima uyafungue maneno na ugundue ujumbe wa mwandishi kwa kizazi chake.Ni pale tu utakapo uelewa ujumbe wake kwa watu wake, ndipo utakapoweza kuusema Ujumbe wa Mungu kwa watu wako.
Kutafuta Maneno ya Muhimu.
Katika somo hili, Tutatafuta maneno makuu katika kifungu. Maneno haya yamejazwa na ukweli wa Mungu. Yanatoa majina kwa mawazo ya muhimu ya imani ya Kikristo. Yanabeba maana ambayo ni lazima itolewe kwa watu wa Mungu. Mjumbe wa Mungu atajifunza maneno haya ya muhimu ili kwamba aweze kuwafundisha watu kwa uaminifu kile ambacho Mungu anachokisema.
Tumepigia mstari vitendo. Mara nyingi haya ni maneno ya kitendo. Ni ya muhimu sana katika kuuelewa ujumbe wa kifungu.
Somo la 6
Kutambua na kuwekea alama maneno makuu katika kifungu, itafungua maana yake kwako kwa ujumbe wako kwa watu.
Kuandaa ujumbe. Kuchagua kifungu. Nakiri kifungu. Maneno ya kitendo. Maneno ya muhimu. Vilivyochunguzwa. Viini vya Biblia. Wazo kuu Kiini cha mpaka Mawazo saidizi. Pointi kuu. Watu. Picha za maneno. Kusimulia hadithi. Matumizi. Kukusudia kwa imani. Kuorodhesha.
32
Tunapowekea alama maneno yale ya muhimu sana katika kifungu chetu, tutawekea alama tena vitendo vingi. Tunatafuta maneno ambayo ni ya muhimu kwa ujumbe wa mwandishi. Ziko aina tatu za maneno ambazo mara nyingi zinabeba uzito wa juu katika kuleta mawazo ya mwandishi kwa msomaji. Baadhi ya maneno haya ni maneno ya majina. Ni ya muhimu kama vile maneno ya kitendo tuliyoyaona katika somo lililopita. Mbali na maneno ya majina na maneno ya kitendo , aina ya tatu ni maneno maelezi ( Maneno yanayoelezea).
Unapoendelea kupitia kifungu, utapata maneno mengi sana ya majina. Katika lugha ya kujifunzia, tunaweza kuyaita nomino . Maneno haya yanatoa majina ya mahali, watu, na vitu. Yanaweza kutoa majina ya mawazo na hisia pia. Kama vile jinsi ambavyo mtu anakuwa na jina, tunavipa majina pia vitu vingine ili kwamba tuweze kuvizungumzia. Nitaonesha baadhi ya maneno ya majina katika vifungu. Maneno mengine ni maneno ya kueleza. Yanaeleza zaidi kuhusu watu, sehemu na vitu. Yanaeleza pia kuhusu matendo. Katika Lugha ya kujifunzia, maneno haya yanaitwa vielezi. Tutayaona baadhi ya maneno haya katika vifungu vya hapa chini.
Kuwekea Alama Maneno ya Muhimu.
Hebu sasa, rudi nyuma tena katika nakara yako uliyoiandika kwa mkono ya Yohana 3: 1-8. Sasa hivi wekea alama maneno yanayoonekana kubeba uzito wa maana katika kifungu. Ni bora kuwekea alama maneno mengi sana kuliko kuwekea alama maneno machache sana. Unaweza kuwekea alama vyovyote vile unavyopenda. Mara nyingi, huwa ninayazungushia duara tu.
Hapa kuna nakara yangu niliyoiandika kwa mkono ya kifungu cha Yohana 3:1-8 ikiwa na maneno ya muhimu yaliyowekewa kivuli. Nimewekea alama maneno kama vile
“Ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni na duniani, na vya chini ya nchi.”
Wafilipi 2:10
33
“Mafarisayo”, “Mkuu”, “Yesu”, “usiku” na mengine. Maneno haya yote hayana uzito sawa wa maana. Lakini kwa pamoja yatakusaidia kuangalia katika ujumbe wa mwandishi. Je, utapenda kuchagua mengine ya tofauti? Au labda niliacha neno ambalo ni la muhimu?
Yohana 3:1-8 1. Basi palikuwa na mtu mmoja wa mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. 2. Huyu alimjia usiku, akamwambia, “Rabi,twajua kuwa u mwalimu,umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi
uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu; yu pamoja naye.” 3. Yesu akajibu, akamwambia,
“Amin, amin, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.”
4. Nikodemo akamwambia, “Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?”
5. Yesu akajibu, “Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu.” 6. "Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. 7. "Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.” 8. "Upepo huvuma uendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; Kadhalika na hali kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.”
34
Maneno mengi tuliyoyawekea alama ni maneno ya majina “Nikodemo” ni jina la mtu aliyekuja kwa Yesu. “Mafarisayo” ni jina la kikundi cha kidini ambacho Nikodemo alikuwemo. “Yesu ametajwa katika kifungu. Mtu huyu alimwendea Yesu “usiku”. Hili ni jina tunaloliita katika wakati wa giza wa siku. Lakini linaelezea pia wakati gani mtu huyu alimwendea Yesu. “ Mwalimu” ni cheo ambacho Nikodemo alimpa Yesu.
Hatupati maneno mengi sana ya kueleza katika kifungu hiki. Lakini kumbuka kwamba Nikodemo alijieleza mwenyewe kwamba ni “mzee”. Alizungumzia tumbo la “mama yake”. Yesu alizungumzia “maji”, “mwili”, na “roho” kuelezea aina mbalimbali za kuzaliwa. Maneno yote haya yanatumika kwa kuelezea katika kifungu hiki. Hata kama wahubiri na waalimu tofauti watawekea alama maneno tofauti, maneno mengi ya muhimu yatawekewa alama. Ni maneno haya yanayoleta maana ya kifungu kama jinsi mwandishi alivyokusudia. Yanatuonesha pia maana ya kifungu kwa wasikilizaji wetu. Angalia sasa jinsi ambavyo kifungu kingine kinavyoweza kuandikwa kwa vifungu na kuwekewa alama. Hapa kuna nakara yangu ya Zaburi 1 ikiwa imepigiwa mstari vitendo na maneno makuu ya aina yote yamewekewa alama. Umegundua nini kuhusu kifungu hiki? Zaburi 1:1-6 1 Heri mtu yule asiye kwenda katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia yawakosaji;Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. 2 Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
“Unifundishe akili na maarifa, Maana nimeyaamini maagizo yako.
Kabla sijateswa mimi nalipotea, Lakini sasa nimelitii neno lako.”
Zaburi 119:66, 67
35
3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake
kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; na kila alitendalo litafanikiwa. 4 Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. 5 Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki. 6 Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya mwenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea.
Baadhi ya maneno ya muhimu sana katika kifungu hiki ni maneno ya kitendo. Mwenye haki amesemwa asiye “kwenda” katika shauri la wasio haki, na wala “hakusimama” katika njia ya wakosaji, wala “hakuketi” barazani pa wenye mizaha. “Huitafakari” sheria ya Bwana. Anafananishwa na mti “uliopandwa” kandokando ya vijito vya maji, “uzaao” matunda yake, “Haunyauki”. “Atafanikiwa” katika kila kitu. Tofauti na wasio haki walio kama makapi, yapeperushwayo na upepo. “Hawata simama” katika hukumu. “Watapotea”
Angalia katika kifungu maneno mengi ya kifungu yaliyotumika. Katika swala hili, maneno ambayo mara nyingi yanatumika kwa kuelezea, yanatumika kama majina ya watu Fulani. Wengine wanaitwa “Wasio haki”, “wakosaji”, na “wenye mizaha” katika mstari wa kwanza. Kuna picha ya kushangaza ya mwenye haki katika mstari wa 3, analinganishwa na mti uzaao. Wale Mungu anaowapenda wanaitwa “wenye haki” katika mstari wa 5. Kifungu kinatoa tofauti ya waziwazi kati ya “mwenye haki” na “asiye haki”.
“Ni nani atakayepanda mlima wa BWANA? Ni nani atakaye simama katika patakatifu pake? Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, asiyeinunua nafsi yake kwa ubatili, wala hakuapa kwa hila.”
Zaburi 24:3, 4
36
Katika somo letu linalofuata, tutatengeza notsi za kile tunachokiona katika kifungu kinachosaidia kuelewa maana yake. Hii itahitaji jicho la umakini sana katika maelezo ya maneno ya kifungu.
Mazoezi ya Somo.
1. Rudia mawazo makuu ya somo hili: Kuwekea alama maneno makuu katika kifungu itayafungua mawazo ya mwandishi kwako. Zaidi ya maneno ya kitendo, tutaangalia maneno ya majina na maneno ya kuelezea. Baadhi ya maneno ya Biblia ni msingi wa imani yetu kuhusu Mungu.
2. Kabla ya kuhamia katika somo linalofuata, soma vifungu vingine kama jinsi tulivyofanya hapa. Vinakili kwa mkono, kifungu baada ya kifungu. Halafu pigia mstari vitendo. Mwisho, wekea alama maneno ya muhimu, yanayobeba maana ya kifungu. Ninashauri ukisome kifungu cha Mathayo 5: 13 – 16. Usifanye haraka. Chukua muda unaouhitaji. Unaposoma vifungu vingi utaweza kufanya kazi kwa haraka.
37
Somo la 7
KKuuaannddiikkaa kkiillee uunnaacchhookkiioonnaa..
Kadiri unapokiangalia kifungu kwa uangalifu zaidi, ni jinsi hiyo unavyokiona vyema zaidi. Sasa umeandika kifungu pembeni kwa mkono, unaanza kuona mambo ambayo hukuyaona mwanzoni. Kupigia mstari vitendo na kuwekea alama maneno ya muhimu imefungua pia kifungu kwako. Hatua inayofuata ni kutengeneza notsi zako mwenyewe kuhusu nini unachokiona katika kifungu. Rudi tena katika nakara yako uliyoiandika kwa mkono na andika vile unavyoviona.
Kutafuta na Kuangalia.
Umewahi kwenda kwa tabibu kwa ajili ya uchunguzi? Uliona jinsi anavyokushughulikia? Ikiwa unaumwa, anakuuliza unajisikiaje, au unasikia maumivu yako wapi. Anauliza pia dalili zingine. Umepungukiwa pumzi? Unalala vizuri? Unapata hamu ya kula vizuri? Anaweza kusikiliza pia moyo wako na jinsi unavyopumua. Anaweza kukuangalia mdomoni, machoni na masikioni. Anatafuta dalili za Ugonjwa wako.
Katika ulimwengu wa asili, vitu vidogo vdogo ni vya muhimu sana. Mvuvi mahili ataangalia muonekano wa maji na muda wa siku. Muwindaji mahili ataangalia kijiti kilichovunjika, alama ndogo sana za miguu na mavi ya wanyama. Mkulima mahili anaangalia mizunguko ya wadudu, madoa katika majani ya miti yake, mabadiliko ya hali ya hewa.
Somo la 7
Kuandika kile unachokiona katika kifungu, itakuandaa katika kupambanua maana ya mwandishi.
Kuandaa Ujumbe. Chagua kifungu. Nakili kifungu Maneno ya kitendo. Maneno ya muhimu Vilivyochunguzwa Viini vya Biblia. Wazo kuu Kiini cha mpaka Mawazo saidizi Pointi kuu Watu. Picha za neno. Kusimulia hadithi. Matumizi. Kukusudia kwa Imani. Kuorodhesha.
38
Askari mtafiti mahili ni mwepesi katika habari ndogo ndogo.Anaangalia mikwaruzo katika kufuri. Anaangalia alama za miguu zilizofifia chini ya dirisha. Anaangalia uzi uliochanika katika nguo ya mtu. Ni kwa kupitia dalili hizi anaanza kuelewa nini kilitokea katika tukio la uhalifu. Vile wanavyovikosa wengine, mtafiti anaviona. Pasipo kuona dalili ndogo ndogo, hawezi kufanya kazi yake. Watafiti wote hawa makini ni kama mwanasayansi ambaye ni lazima aone na aandike habari ndogo sana za kazi yake.
Unaweza kushangaa kwamba kazi za hawa watafiti wote mahili zinamsaada gani kwa mjumbe wa Mungu katika kujifunza kifungu cha Biblia. Zina msaada mkubwa sana. Unaposoma na kujifunza kifungu chako, kazi yako kubwa ni kuangalia kwa makini maelezo katika uandishi. Hautafuti mahubiri ya haraka haraka. Unatafuta nini mwandishi wa kifungu alichokisema na alikisemaje. Unatafuta dalili zote katika maana yake. Wahubiri wengine wanatumia vifungu vya Biblia kama msaada kwa mawazo yao. Tayari wanajua nini wanachotaka kusema. Wanatafuta mstari wa Biblia wa kwenda nao ili kwamba ujumbe wao uonekane kuwa na mamlaka ya Kibiblia. Lakini mjumbe mwaminifu wa Mungu haisomi Biblia yake kwa namna hiyo. Badala yake anakwenda katika kifungu kupokea nini kinachosema. Anataka kuuutoa ukweli wa Biblia kwa watu anapozungumza nao. Kuelewa kifungu kinasema nini, ni lazima tukisome kwa makini. Ni lazima tutafute kila taarifa inayowezekana. Ni lazima tufikiri juu ya taarifa hizo zinamaanisha nini. Maneno kwetu ni kama kiwimbi katika maji kwa mvuvi, au kijiti kilichovunjika kwa muwindaji. Yatatuongoza mpaka kwenye maana ya kifungu. Ndipo tunapoweza kuuwakilisha ujumbe huo kwa watu na wakalisikia Neno hasa la Mungu.
Hautafuti wazo la haraka la mahubiri. Unatafuta kile mwandishi wa kifungu alichosema na jinsi gani alivyokisema.
39
Kuandika notsi zetu.
Hebu sasa turudi tena katika nakara yetu tuliyoiandika kwa mkono ya Yohana 3:1-8. Kwa sababu uliinakiri katika upande wa kushoto wa karatasi yako, unayo nafasi upande wa kulia kwa notsi zako. Nimeandika baadhi ya notsi zangu hapa. Yanawezakuwa mambo ambayo hayafanani na yale utakayoyaandika. Lakini unaweza kuangalia kutoka kwenye notsi zangu, jinsi gani kuangalia maneno kwa umakini kunaweza kutusaidia kuelewa kifungu.
Yohana 3:1-8
1.Basi palikuwa na mtu mmoja
wa mafarisayo, jina lake Nikodemo,
mkuu wa Mafarisayo.
2.Huyu alimjia usiku,akamwambia,
Rabi, twajua kuwa u mwalimu,
Umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna
Mtu awezaye kuzifanya ishara hizi
Uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu
Yu pamoja naye.
3. Yesu akajibu, akamwambia, Amin,
amin, nakuambia,Mtu asipozaliwa
mara ya pili,hawezi kuuona ufalme
wa Mungu.
4.Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu
kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia
tumboni mwa mamaye mara ya pili
akazaliwa?
5. Yesu akajibu, Amin, amin,
nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji
na kwa Roho,hawezi kuingia ufalme
wa Mungu.
6. Kilichozaliwa kwa mwili ni
mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
7. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia,Hamna
budi kuzaliwa mara ya pili.
8. Upepo huvuma uendako, na sauti yake waisikia
lakini hujui unakotoka wala unakokwenda;
kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho
Vivyo hivyo mtu hawezi kumzuia roho wa Mungu anayetoa kuzaliwa upya.
Nikodemo alikuwa mkuu wa wayahudi
Alitaka kuongea na Yesu.
Alikuja usiku. Je Alikuwa anaogopa?
Tayari alikuwa anafahamu kitu kuhusu Yesu kwa kuona baadhi ya miujiza yake.
Alifikiri Mungu yu pamoja na Yesu.
Alifikiri ni mtu kutoka kwa Mungu tu anayeweza kufanya ishara hizi.
Yesu alionekana kubadilisha somo.
Neno “Kuzaliwa” limetumika mara 8 katika kifungu hiki.
“Kuzaliwa mara ya pil” inaonesha kuzaliwa kwa mwili, lakini inaelezea maisha mapya ndani ya Kristo.
Yesu amerudia “Ufalme wa Mungu” mara mbili, “kuona” na “kuingia”
Nikodemo hakuelewa jinsi Yesu alivyotumia “kuzaliwa mara ya pili”
Alikuwa mzee.
Anachukulia kuzaliwa mara ya pili kwa hali halisi badala ya kama picha.
Yesu anazungumzia “maji” ya kuzaliwa kwa mwili na “roho” kwa kuzaliwa upya.
Ufalme wa Mungu ni watofauti na Falme za binadamu.
Yesu anatofautisha kuzaliwa kwa mwili na kuzaliwa kwa roho.
Japo tunaona na kusikia dalili za upepo, hatuwezi kuuendesha/ kuuzuia.
40
Kuangalia Maelezo katika Kifungu.
Hata kama Wahubiri na waalimu mbalimbali wanaweza wakafanya uchunguzi tofauti, bado wanaacha kifungu kiamue nini wanachokiona. Hii ni muhimu sana. Tunakusudia kufundisha Biblia badala ya mitazamo yetu wenyewe ya kidini. Mungu anawatumia wajumbe wanadamu, lakini anawataka kualifu ujumbe kwa uaminifu.
Uwe mwangalifu na notsi zako kubaki na dalili za kifungu. Usianze kuhisi juu ya mawazo ambayo kifungu hakikupi. Kwa mfano, waalimu wengine wamesema “maji” katika mstari wa 5 yanamaanisha maji ya ubatizo, lakini Yesu anazungumzia juu ya kuzaliwa. Maji yanaweza kuwa yanamaanisha sawa na yale maji yanayotoka wakati mototo anapozaliwa. Yanawakilisha Kuzaliwa kwa mwili. Ubatizo unazungumziwa katika maandiko mengine mengi, lakini labda si katika kifungu hiki. Kila alama unayoweka ni lazima yawepo maneno katika kifungu unayoweza kuonesha kuwa yana elekea hilo. Usijibu, “Ninaona nini hapa?” kwa kujaribu kufikiri juu ya baadhi ya mawazo ya kidini. Badala yake jibu swali hilo kwa kuangalia kwa makini maneno ya kifungu. Kumbuka kwamba unajaribu kuelewa maana iliyokusudiwa na mwandishi wa awali wa kifungu. Haujaribu kutengeneza maana unayoipendelea. Hebu angalia sasa uchunguzi niliouona. Maelezo gani katika kifungu tuliyoyaona? Hebu tutengeneze Orodha. Tupate baadhi ya uchunguzi wetu utusaidie kuelewa kifungu.:
1. Neno “kuzaliwa” limetumika mara 8 katika kifungu. Marudio yanatufanya tufikiri kwamba wazo hili ni la muhimu.
2. Yesu analinganisha uzowefu wa kuweka Imani kwa Mungu na mototo kuzaliwa. Vyote hivi ni mwanzo mpya.
“Umtendee mtumishi wako ukarimu, Nipate kuishi, nami nitalitii neno lako. Unifumbue macho yangu nami niyatazame Maajabu yatokayo katika sheria yako.”
Zaburi 119:17, 18
41
3. Nikodemo alikuwa mzee, mkuu wa wayahudi, na alikuja usiku. Labda aliogopa kuonwa na Yesu.
4. Yesu anazungumza juu ya “kuona” na “kuingia” ufalme wa Mungu, ufalme wa roho mwanadamu hawezi kuuona.
5. Nikodemo hakuelewa “kuzaliwa mara ya pili” kama picha ya maisha mapya ya kiroho.
6. Yesu anatofautisha kuzaliwa kwa mwili na kuzaliwa kwa roho kumsaidia Nikodemo kuelewa.
7. Yesu anatumia picha ya upepo kuelezea kisichoonekana lakini asili halisi ya kuzaliwa upya.
Unaweza kuona kwamba uchunguzi wote huu katika kifungu ni mgumu sana kuuona. Usikate tamaa ikiwa hauta ona dalili nyingi katika kifungu kwa mara ya kwanza. Unapoendelea kuisoma Biblia yako jinsi hii, utaviona zaidi na zaidi vitu vidogo vidogo katika kifungu vitakavyokuwezesha kukielewa.
Kumbuka unapoangalia kile unachkiona, uchunguzi wako unaweza kuwa wa aina yoyote. Unaweza kuwa wa kihistoria, unaweza kunakili kile unachokiona kuhusu lugha. Unaweza kuona maelezo ya mila yanayopendeza. Hata hivyo kusudi lako kuu wakati wowote ni Thiolojia. Biblia iliandikwa kuwasilisha ujumbe wa Mungu na njia zake pamoja na uumbaji wake. Huo ndio ujumbe wa Kithiolojia. Na huo ndio tunaopaswa kufundisha watu.
Katika somo letu linalofuata, tutaangalia tena katika notsi zetu na maneno yaliyowekewa alama katika kifungu. Kusudi litakuwa ni kuorodhesha viini vyote vya Biblia tunavyoviona katika kifungu. Viini hivi vitatuongoza katika wazo kuu kwa ujumbe wetu.
Mazoezi ya Somo.
1. Rudia mawazo makuu ya somo hili:
Wajibu wako mkuu/ wa kwanza wakati wote ni thiolojia. Biblia iliandikwa kuwasilisha ujumbe kuhusu Mungu na njia zake pamoja na viumbe vyake.Huo ndio ujumbe wa kithiolojia. Na huo ndio tunaopaswa kuwafundisha watu.
42
Mwalimu au Muhubiri wa Biblia ni kama mwanasayansi anayeona maelezo katika sehwemu dogo dogo na kuelewa zinamaana gani. Mjumbe anayefundisha Biblia ataangalia kwa makini katika kifungu kwa ujumbe wake. Japo wajumbe tofauti tofauti wanaweza kuona vitu tofauti katika kifungu, bado wanakiangalia kifungu kwa ajili ya ujumbe wao. Mjumbe mwaminifu anajaribu kuelewa maana iliyokusudiwa na mwandishi wa kifungu.
2. Umekwisha kuandika Zaburi 1 na Mathayo 5:13-16 na kuwekea alama maneno ya ufunguo. Sasa pitia na uandike notsi ya kile unachokiona katika maelezo ya vifungu hivyo. Usiogope kuandika mawazo yako. Lakini hakikisha kuna uthibitisho wa mawazo yako katika kifungu. Usiache kifungu nyuma na kuanza kuweka fikra zako mwenyewe kuhusu somo.
43
Somo la 8
KKuuoorrooddhheesshhaa VViiiinnii vvyyaa BBiibblliiaa..
Tunamaanisha nini juu ya Viini vya Biblia? Ni mawazo yanayopatikana katika Biblia nzima.Haya ni masomo ambayo ni lazima tuyazungumzie ikiwa tunazungumza kuhusu mafundisho ya Biblia. Mara nyingi viini hivi vya Biblia vinawakilishwa na maneno fulani. Kwa hiyo neno linapoonekaka katika kifungu, mwanafunzi wa Bilbia anajua kwamba kiini kipo hapo.
Viini vya Biblia tunavyovitafuta ni vya Kithiolojia. Hii inamaanisha ni maneno kumuhusu Mungu na jinsi anvyoshughulika na Ulimwengu wake. Viini hivi vya Kithiolojia havina mwisho wa wakati. Ni vya muhimu kwa wasikilizaji wako kama vile jinsi vilivyokuwa vya muhimu kwa watu wa zamani wa Biblia. Thiolojia ni ujumbe wa kweli wa Bilbia. Lugha, historia na mila za Biblia vinatusaidia kuitafsiri thiolojia.
Katika kifungu chochote tunatarajia kupata kiini kimoja ambacho ni wazo kuu la kisehemu kile. Japo viini vingine vipo pia. Hivi vinasaidia wazo kuu na kulifanya lieleweke zaidi. Viini tunavyovipata katika vifungu vya Biblia vipo katika Biblia yote lakini katika muunganiko tofautitofauti. Kila kifungu lazima kitafsiliwe katika namna ya jinsi ambavyo viini vinaonekana ndani yake. Kadiri unavyoisoma Biblia, ndivyo jinsi ambavyo utakuwa unaelewa kuwa viini vya Biblia ni vya muhimu sana katika kumuelewa kwetu Mungu na njia zake na watu.
Kuyapa Majina Mawazo.
Katika somo la 6, tulisema kwamba maneno tofauti katika kifungu yanafanya kazi katika njia tofauti. Maneno mengine ni maneno ya kitendo tunaita vitendo. Mengine yanaelezea maneno tunaita mageuzi. Maneno mengine ni maneno ya majina na haya yanaitwa
Somo la 8
Unaweza kufungua ujumbe wa kifungu kwa kugundua na kuorodhesha viini vilivyoelezwa katika kifungu.
Kuandaa Ujumbe. Chagua kifungu. Nakili kifungu Maneno ya kitendo Maneno ya muhimu Vilivyochunguzwa Viini vya Biblia Wazo kuu Kiini cha mpaka Mawazo saidizi Pointi kuu. Watu Picha za neno Kusimulia hadithi. Matumizi Kukusudia kwa Imani Kuorodhesha.
44
nomino. Maneno mengine mengi yanashikilia maana pamoja katika kifungu, lakini hayabebi viini vya Biblia. Maneno ya kitendo mara nyingi yanafunua viini vya Biblia katika kifungu. Unapopigia mstari maneno ya kitendo katika kifungu chako, utaona baadhi ya viini vikuu. Tumekwisha kuona kwamba neno “Kuzaliwa” linajitokeza mara 8 katka Yohana 3:1-8. Hii intuambia kwamba hiki ni kiini cha muhimu kwa kifungu hiki. Neno hili linabeba kiini cha Biblia cha “Kuzaliwa Upya.”
Maneno mengine ya kitendo yanawezakusaidia unapolitafsiri. Moja ni “Kujua”, kwamba Nikodemo alidhani anajua chochote kuhusu Yesu. Neno lingine la kitendo ni “Kuingia”, limetumika kimaandishi kwa kuingia mara ya pili katika tumbo la mama yake na kutumika kwa picha kwa kuingia katika ufalme. Maneno ya jina katika kifungu pia yanaweza yakafunua viini vyake. Maneno haya yanatoa majina kwa watu, kwa mahali na kwa vitu. Lakini pia yanatoa majina ya mawazo na hisia na sifa za tabia. Tulipoangalia katika Yohana 3:1-8 tuliona kwamba maneno ya majina yanabeba maana pia. Hapa kuna “Nikodemo”,“Yesu”, “Mwalimu”,“Ishara”,“Ufalme”,“roho”,”mwili”, na Upepo”. Hebu tufikiri kama hivi vinaweza kuwa viini vya Biblia. “Nikodemo” si kiini cha Biblia. Ni jina la mtu zaidi kuliko wazo la kithiolojia. “Yesu”, hasa, ni kiini kikuu cha Biblia. Ni jina alilopewa Masihi katika huduma yake ya duniani. Majina ya watu hayawezi kuwa mawazo kwa viini vya Biblia. Jina la Yesu ni la pekee. Yesu anaitwa “mwalimu”. Wazo la kufundisha ni Kiini cha Biblia. Neno “Ishara” linaonesha pia kiini cha Bilbia cha Miujiza. “Ufalme wa Mungu” ni kiini kinachoonekana katika Biblia nzima pia. “Roho” ni kiini kinachomaanisha Roho Mtakatifu. Au inaweza kumaanisha roho ya binadamu. “Nyama,” inamaanisha ngozi ya asili au mwili wa binadamu, ni kiini kingine ncha muhimu cha Biblia. Mara nyingi pia inamaanisha kitu kingine tofauti na ngozi au mwili wa binadamu. Inaweza kumaanisha ufupisho wa uhai na udhaifu wa binadamu. Neno “nyama” limetumika na Paulo kumaanisha uasilia wa dhambi wa binadamu. Neno hili kwa mwili wa Binadamu limekuwa kielelezo cha tatizo la ndani la asili ya anguko la binadamu. Hii ndio tunayita lugha ya picha.
“Likumbuke neno ulilomwambia mtumishi wako, Kwa sababu umenitumainisha. Hii ndio faraja yangu katika taabu yangu, Ya kwamba ahadi yako imenihuisha.”
Zaburi 119:49, 50
45
Viini vya Picha.
Viini vya Biblia mara nyingi vitakuwa katika namna ya picha. Hii ina maana maneno yanatambulisha mambo ya kawaida katika ulimwengu wa asili, lakini yanasimama kwa ajili ya mawazo ya kiroho. “Upepo” si kiini cha Biblia, badala yake linapotumika katika namna ya picha kumaanisha masumbufu ya maisha au Roho Mtakatifu. Kama jinsi tulivyosema, “Kuzaliwa mara ya pili” ni picha tu. Haimaanishi kurudi tena tumboni mwa mama yako na kuzaliwa. Inamaanisha kubadilishwa kiroho unapoweka imani yako kwa Kristo. Unapoandika viini unavyoviona katika kifungu, mara nyingi vitakuwa katika picha.
Moja ya vifungu ulivyovifanyia mazoezi katika somo la 4 kilikuwa ni Mathayo 5:13-16. Kifungu hiki kuhusu “chumvi na nuru” ,kinafahamika kwa wakristo wengi. Kwa mara ya kwanza, utagundua kwamba maneno haya ni ya picha. Yesu hamaanishi chumvi hii ya kawaida, ambayo unawezakutumia kukolezea chakula chako. Hamaanishi nuru hii ya kawaida, kama ile inayotoka kwenye taa. Anamaanisha kitu kingine. Anamaanisha jinsi wakristo wanavyohusiana na ulimwengu wao.
Mathayo 5:13-16
13 "Ninyi ni chumvi
ya dunia; Lakini chumvi
ikiwa imeharibika,
Itatiwa nini hata ikolee?
Haifai tena kabisa, ila
kutupwa nje na kukanyagwa
na watu.
14 "Ninyi ni nuru ya ulimwengu.
Mji hauwezi kusitirika ukiwa
juu ya mlima.
15 "Wala watu hawawashi
taa na kuiweka chini ya
pishi, bali juu ya kiango;
nayo yawaangaza wote waliomo
nyumbani.
16 "Vivyo hivyo nuru yenu
na iangaze mbele ya watu,
“Haya, enenda sasa, andika neno hili katika kibao mbele ya macho yao, lichore katika kitabu ili liwe kwa ajili ya majira yatakayokuja, kwa ushuhuda hata milele.”
Isaya 30:8.
46
wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze baba yenu aliyeko mbinguni. Kwa hivyo tunapoandika viini kutoka katika kifungu hiki, tutaorodhesha maneno haya ya picha: “chumvi”, “radha”, “kukolezwa,” “kutupwa nje,” “kukanyagwa,” “nuru,” “taa,” “pishi,” “kiango,” “nyumbani” na “kuangaza.” Baadhi ya viini ni viini vya kawaida vya Biblia. Vingi ya hivyo si vya kawaida. Ni matendo na mambo yanayotumika kuwakilisha mawazo ya kiroho. Ni lazima uvitafsiri kutoka katika hali ya picha kuingia katika mawazo yanayowakilisha.
Hadithi nyingi za Yesu zinatumia lugha ya picha kama hivi. Anazungumza kuhusu “mbegu” na “udongo”. Anazungumza kuhusu uvuvi, kilimo, utunzaji wa nyumba, kuuza na kununua, ujenzi wa nyumbani, harusi, karamu, hali ya hewa, miti, ndege, maua, na mambo mengine mengi ya namna hiyo ya maisha. Anatumia hivi vitu vya kawaida sana kuelezea mambo ya kiroho. Tukitaka kuelewa kile anachozungumzia, ni lazima tutafsiri picha hizo kwenda kwenye maana halisi iliyowazi. Vingi vya Biblia.
Biblia inafunua viini vingi vikuu. Viini hivi ni mawazo yanayohusu Mungu na mapenzi yake. Baadhi ya viini katika Biblia yanatueleza kuhusu Mungu mwenyewe. Hivi ni viini kama vile uweza wa Mungu, upendo wa Mungu, ufahamu wa Mungu, na neema ya Mungu. Viini haya haya makuu kuhusu Mungu yanapatikana katika sehemu nyingi za maandiko, katika Agano la Kale lote na Agano jipya lote. Viini vingine vyatwambia kile Mungu alichofanya na kile atafachofanya. Mungu aliumba vyote vilivyopo. Mungu huvihifadhi viumbe vyote. Mungu huangalia vyote umba. Mungu anajali viumbe vyake vyote.
Viini vingina vya Biblia vyanatueleza kuhusu binadamu. Aliumbwa katika mfano wa Mungu. Alijaribiwa kutenda dhambi .
"Hayo nimesema nanyi kwa mithali; saa yaja ambapo sitasema nanyi tena kwa mithali, lakini nitawapa waziwazi habari ya Baba.”
Yohana 16:25
47
Akaanguka katika jaribu na akaasi. Dhambi zake zikamleta chini ya ghadhabu ya Mungu . Hukumu inakuja kwa watu wote. Lakini Mungu amemtoa mwokozi kwa binadamu, mwana wake. Sasa mwanadamu anaweza kusamehewa dhambi zake na kupata ahadi ya makao mbinguni. Anaweza kuwa na maisha mapya.ndani ya Kristo. Hivi ni vya ajabu sana katika Biblia.
Inaonekana kuwa mna viini zaidi katike biblia kuliko vile ambavyo tunaweza tukavihesabu. Mambo haya ndiyo hasa Mungu anataka watu wake wayajue. Yanaonekana sehemu nyingi sana katika Biblia. Nyakati zingine viini vya Biblia vinaelezwa kwa uwazi kabisa katika kifungu. Vingi kati ya viini hivi vikuuu vina maneno maalum ya kibiblia ili kuvitambua. Haya ni maneno kama dhambi, wokovu, imani, neema, hukumu, kuzaliwa upya, msamaha, mbingu na jehanam. Tunapoyaona maneno haya katika kifungu, tunajua kwamba kiini ndicho kinachozungumziwa.
Wakati mwingine neno maalum kwa ajili ya kiini linaweza lisiwepo katika kifungu. Hii ni kweli hasa wakati ambapo kifungu kitakuwa na lugha ya picha. Panaweza kuwa na maneno kama “chumvi” na “nuru” ambayo ni lazima yatafsiliwe kulingana na maana zake. Kumbuka kwamba, kiini ni lazima kiwe cha kithiolojia. Kwa mfano, Mwanzo 3:1-8 haitumii neno “Jaribu”. Lakini habari ya Adam na Eva kula tunda walilokatazwa kwa hakika inahusu Jaribu.
Orodha ya Viini Vyetu.
Tumekwisha kuorodhesha viini tulivyoviona katika Mathayo 5:13-16. Kifungu chetu kingine cha kufanyia kazi kilikuwa Yohana 3:1-8. Hebu sasa tuandike orodha yetu ya viini ambavyo vinaonekana pale. Tumekwisha viona vingi katika somo hili. Orodha yangu ni hii hapa. Yako je, iko tofauti?
Mwanadamu
Mafarisayo
Mkuu
Ujuzi
Mwalimu kutoka kwa
Kuzaliwa mara ya pili
Ufalme wa
Kuzaliwa kwa mwili
Kuzaliwa kwa
“Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje,ndugu zetu?”
Matendo 2:37
48
Yesu Usiku
Mungu Ishara Mungu pamoja nasi
Mungu Kuzaliwa Kuzaliwa kwa Maji.
roho Kustaajabu Lazima
Kama jinsi nilivyosema, maneno mengine yanayoonekana katika kifungu hayafai kuwa katika orodha ya viini. Nimeacha “Nikodemo” kwa sababu alikuwa ni mtu na asingeweza kuwa kiini cha kithiolojia. Nimeacha “Wayahudi” kwasababu ni watu, na si wazo. Lakini nikaweka “usiku” kwa sababu nyakati zingine ni picha ya dhambi na kutofahamu. Orodha hii ya viini inaturuhusu kwenda kwa hatua inayofuata. Sasa tutachagua kutoka miongoni mwa viini hivi kiini kimoja kikuu. Tutajibu swali, “Mwandishi anazungumzia nini?” kwa kutumia somo hilo moja kuu.
Mazoezi ya Somo.
1. Rudia mawazo makuu ya somo hili: Viini vya Biblia ni mawazo yanayopatikana katika Biblia nzima. Tunatarajia kupata katika kifungu chochote kiini kimoja ambacho ni wazo kuu la kisehemu hicho. Viini vingine katika kifungu vitakuwa ni saidizi vya kiini kikuu. Viini vingine vinaelezewa kinaganaga, na vingine kwa picha.
2. Rudi tena katika Zaburi 1 na Warumi 12:1,2 tena. Sasa hizi orodhesha viini vyote vya kithiolojia unavyoviona hapo. Unapoangalia katika lugha za picha, jaribu kutambua ni maana gani ya kithiolojia iliyokusudiwa katika kila maelezo.
“Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi”
Matendo 2:40
49
Somo la 9
KKuutteennggeenneezzeeaa sseenntteennssii wwaazzoo kkuuuu..
Somo letu la kifungu sasa limeingia katika sehemu ya kuvuka kutoka katika kifungu kwenda kwenye hubiri. Tumekwisha andika kifungu kwa mkono. Tumegundua maneno makuu katika kifungu. Na sasa tutachagua kutoka katika viini, katika kifungu, somo moja ambalo ndilo kiini cha habari cha mwandishi alichokikusudia. Wazo hilo litakuwa somo la ujumbe wetu..
Uwezo wa Maneno.
Maneno yana uwezo. Neno la Mungu linanguvu haswa.”Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.” (Waebrania 4:12). Kama wajumbe wa Mungu, tunataka kulitangaza neno lake kwa uaminifu. Tunataka maneno yetu yatoe ukweli wake kwa Watu.
Mawasiliano mengi ya binadamu yanahitaji maneno. Inawezekana kuzungumza kwa ishara za mikono au uso. Viziwi hutumia lugha za ishara. Lakini kwa kawaida, unapotaka kuleta ujumbe kutoka katika kitabu cha Mungu, utatumia maneno ya kuzungumza. Jukumu la muhimu sana katika kujifunza Biblia yako ni kugundua ujumbe alioukusudia mwandishi wa Kifungu. Halafu ni lazima utafute maneno sahihi kuutoa ujumbe huo kwa watu.
Rafiki yangu mmoja alikuwa fundi wa mbao. Alipenda kufanya kazi na mbao. Alifurahia uzuri wa mbao. Alifurahia muundo na harufu ya mbao. Aliweza kutengeneza saa, trei,na sahani za mbao
Somo la 9
Uchaguzi wa umakini wa neno nzuri la kuita wazo kuu la kifungu,inakusaidia kutoa ujumbe unaoeleweka kwa watu.
Kuandaa ujumbe Chagua kifungu. Nakili kifungu Maneno ya kitendo Maneno ya muhimu Vilivyochunguzwa Viini vya Biblia. Wazo kuu Kiini cha mpaka. Mawazo saidizi Pointi kuu. Watu Picha za maneno Kusimulia hadithi Matumizi Kusudia kwa Imani. Kuelezea.
50
za kuwapa marafiki. Sehemu nyingi za dunia kuna watu mafundi wa mbao ambao wanaweza kutengeneza vizuri mbao. Wanatengeneza miundo ya wanyama, wanatengeneza vitu vya dhahabu. Wanatengeneza mapambo mazuri ya kasa kwa ajili ya watunza hazina.
Je mjunbe wa Biblia anaweza kuwa fundi mzuri? Ninaamini lazima awe. Wajibu wake ni wa muhimu sana kuliko ule wa mafundi mbao. Badala ya mbao, Mjumbe wa Mungu anafanya kazi kwa maneno. Ni lazima ajue nguvu ya maneno na udhaifu wake. Ni lazima apende uzuri wa maneno, muundo wake na sauti yake. Ni lazima afanye kazi ya kuwa fundi mzuri wa maneno kadiri kipawa chake kinavyoruhusu. Ujuzi wowote unaoweza kuwa nao, ninatumaini utakusudia kuwa mjuzi mzuri wa matumizi ya lugha. Lugha hujumlisha maneno yetu na jinsi tunavyoyatumia kuzungumza sisi kwa sisi. Kwa kutumia Lugha tunaweza kuelezea mazoea yetu. Tunaweza kuelezea matakwa yetu, tunaweza kuelezea hisia zetu, Tunaweza kuelezea mawazo yetu. Nyakati zingine mawazo ni magumu kuyaweka katika maneno. Mjumbe wa Mungu ni lazima awafundishe watu mawazo kuhusu Mungu, kuhusu sheria yake, kuhusu ahadi zake. Mwandishi wa kibiblia ni lazima aweke mawazo yake kuhusu Mungu katika maandishi. Tunayasoma maneno hayo ili tuyaelewe. Halafu ni lazima tuchague maneno yetu wenyewe kuwafundisha watu kile Mungu anachokisema. Tunaweza kutumia maneno kutoka kwenye Bilbia, Lakini ni lazima tutumie maneno kutoka sehemu zingine pia kuelezea maana ya kifungu. Kwa maneno yetu tunajaribu kuelezea kile kilichoko katika mawazo yetu. Tunataka watu wayaelewe maneno na wawe na mawazo sawa. Ndipo tutakapo kuwa tumeridhika kuwa tumewapa watu ujumbe wa Mungu.Kama jinsi mawazo ya mwandishi wa kifungu ya siku nyingi yanakuja kutumika kupitia maneno yake, mawazo hayohayo kutoka kwa Mungu yatakuja kwa watu kupitia maneno yetu.
Mjumbe wa Mungu anafanya kazi katika maneno.Anapaswa kujua nguvu na udhaifu wa maneno. Anapaswa kupenda uzuri wa maneno,muundo wake,sauti yake,Afanye kazi kuwa fundi mzuri wa maneno kadiri ya kipawa chake kinavyoruhusu.
51
Kuorodhesha viini vya Kifungu.
Katika somo Fulani, tulifanyia kazi kuandaa orodha ya viini tunavyovipata katika Yohana 3:1-8 na Mathayo 5:13-16. Sasa tutaipitia orodha hiyo na tupate kiini kimoja kikuu kwa ajili ya kila kifungu.
Yohana 3:1-8 1. Basi palikuwa na mtu mmoja wa mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa wayahudia 2. Mtu huyu alimjia Yesu usiku akamwambia, “Rabbi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu;
Kwa maana hakuna mtu awezaye Kuzifanya Ishara uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye." 3. Yesu akajibu akamwambia,Amin, Amin, nakuambia, mtu asipozaliwa Mara ya pili, hawezi kuuona ufalme Wa Mungu.”
4. Nikodemo akamwambia, awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5. Yesu akajibu, Amin, amin, nakua mbia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu. 6. “Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni
roho. 7. "Usistaajabu kwa kuwa nilikwambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili. 8. "Upepo huvuma upendako, na sauti yake
Viini vya kifungu
mtu
mkuu
wayahudi
Yesu
Usiku
Kujua
Kufundisha
Kutoka kwa Mungu
Ishara
Mungu pamoja nasi
Yesu
Kuzaliwa mara ya pili.
Kuona
Ufalme wa Mungu
Kuzaliwa
Uzee
Kuzaliwa kwa upya
Mama
Kuzaliwa
Kuzaliwa kwa Roho.
Kuzaliwa kwa maji
Kuzaliwa kwa Roho.
Kuingia
Ufalme wa Mungu
Kuzaliwa kwa mwili.
Utokako
Uendako
Kuzaliwa kwa Roho.
Staajabu.
Umuhimu,kuzaliwa upya
Upepo,utasikia
Utokako
Uendako
52
waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadahalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho." Nimeorodhesha kila kiini nilichoweza kukiona katika kifungu. Baadhi ya viini hivi vinataja mafundisho ya muhimu ya Biblia. Na vingine havina umuhimu. Utakuta viini hivi vinahusiana katika njia tofauti tofauti katika vifungu vingine vingi tu.
Sas kazi yetu ni kuchagua neno moja kukipa jina kiini kikuu cha kifungu.Hilo litakuwa neno moja la somo la ujumbe wako kwa watu. Hapa kuna njia za kuchagua ujumbe huo. Jibu swali hili kwa neno moja,”Mwandishi wa kifungu anazungumzia nini?” Katika kifungu hiki, Yesu anazungumza na Nikodemo. Yohana anaandika kutueleza mazungumzo yao. Kiini kikuu kinapaswa kuwa katika neno moja kama inawezekana, au mawili kama itahitajika. Angalia maneno yanayojirudia. Katika kifungu hiki neno, “kuzaliwa” limetumika mara 8. Angalia kama somo ulilolichagua linafaa kwa mistari yote katika kifungu. Hata kama mistari miwili ya mwanzo haisemi “Kuzaliwa”, inaeleza matembezi ya Nikodemo kwa Yesu kwa ajili ya mazungumzo haya. Gundua maana ya lugha ya picha katika kifungu. Neno “Kuzaliwa” linamaana mtu kutoka katika mwili wa mama yake kwenda kwenye mikono ya jamaa yake. Yesu anatumia neno la picha kumaanisha mtu kuwa na maisha mapya kupitia imani katika Mungu.
Unafikiri somo la kifungu ni nini? Kwangu inaonekana kwamba somo ni “Kuzaliwa mara ya Pili” au “Kuzaliwa Upya”. Hicho ndicho kitu Yesu anchozungumzia na Yohana anakialifu. Kwa hivyo ikiwa kifungu
“Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.”
Yohana 20:31
53
kinahusu “Kuzaliwa Upya”, ujumbe wangu kwa watu utakuwa “Kuzaliwa Upya”.
Hebu tuangalie sasa Mathayo 5:13-16 na viini vilivyomo.
Mathayo 5:13-16 13 "Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tene kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. 14 "Ninyi ni nuru ya ulimwengu, mji hauwezi kusitirika ukiwa
juu ya mlima. 15. "Wala watu hawawashi chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo Yawaangaza wote waliomo nyumbani. 16 "Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Kwanza, tunauliza, “Yesu anazungumzia nini?” hatuna uhakika kwa sababu maneno yake mengi ni lugha ya picha. Tutafute maneno yanayojirudia, tunaona “chumvi” mara mbili, pamoja na “radha” na “Kukolezwa”. Baadae katika kifungu tunaona, “nuru” mara nne, pamoja na “taa”, “kiango” na “kuangaza. Si “chumvi” wala “Nuru” inayofaa katika mistari yote, lakini zinakwenda sambamba kwa wazo moja. Wazo moja ni nini? Ufunguo katika kifungu hiki utakuwa katika kugundua maneno haya ya picha, “chumvi” na “nuru” yalikusudiwa kumaanisha nini.
Viini vya kifungu
chumvi
dunia
chumvi
ladha
kukolezwa
wema, kwa bure
kutupwa nje
kukanyagwa
watu
Nuru
ulimwengu
mji,kufichwa
nuru,taa
funika,kiango
nuru,nyumba
nuru zenu ziangaze
watu,ona,
matendo mema
kumtukuza Mungu Baba
mbinguni
“Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.” Mathayo 7:24
54
Katika kifungu hiki, “chumvi” inawakilisha mwamini anavyohusiana na “ulimwengu”. “Nuru” inawakilisha mwamini anavyohusiana na “ulimwengu.” “Radha” ya mwamini inatoa kikolezo kwa dunia. Nuru ya mwamini inapaswa kuangaza ili itoe nuru kwa ulimwengu. Picha hizi mbili zinaonesha kuzungumzia juu ya mvuto wa(athari ya) mkristo kwa watu wanaomzunguka. Chumvi huathiri kila kitu inachogusa. Mwanga huathiri kila kitu pale inapoangaza. Ikiwa tutaita jina la somo la kifungu hiki “Mvuto(Ushawishi, Athari)” je, itatufungulia kifungu? Itafanya kazi katika mistari yote? Je itafanya ujumbe wa kifungu kueleweka? Tunaweza sasa kuwafundisha watu kifungu kinasema nini kwa uwelewa wao? Katika somo letu linalofuata, tutaendelea kuuupa jina ujumbe kw akulikamilsha zaidi somo. Tutachagua neno lingine kuwekea mipaka upeo wa somo letu.
Mazoezi ya Somo.
1. Rudia mawazo makuu ya somo hili: Mjumbe wa Mungu ni lazima achague maneno sahihi. Mjumbe wa Mungu ni lazima awe ni fundi mzuri anapofanya kazi na maneno. Kutoka katika maneno ya mwandishi wa kifungu, muhubiri anaweza akachambua somo moja kuu la mawazo ya mwandishi.
2. Kufanyia mazoezi kazi ya somo hili angalia tena katika Zaburi 1 na Warumi 12:1,2. Umekwisha orodhesha viini kutoka katika vifungu hivi. Utachagua somo gain kutoka katika viini hivi kwa kila kifungu. Je, unasababu za kueleweka kwa kuchagua somo hilo.
"Haya ndiyo maneno BWANA aliwaambia mkutano wenu wote mlimani kwa sauti kuu toka kati ya moto, na wingu, na giza kuu; wala hakuongeza neno. Akayaandika juu ya mbao mbili za mawe, akanipa.”
Kumbukumbu la Torati 5:22.
55
Somo la 10
KKuuwweekkeeaa MMppaakkaa SSoommoo
Tumekwisha vitambua viini vya Biblia katika kifungu. Halafu tukachagua kutoka katika viini hivyo kimoja ambacho kilionekana kuwa somo kuu la kifungu. Sasa tunaendelea na mtiririko huo kwa kulifafanua somo kwa makini zaidi. Kwa kazi hii, tutakiangalia tena kifungu na kugundua jinsi gani mwandishi wa kifungu alivyowekea mipaka upeo wa maelezo yake katika somo.
Kukielewa Kifungu.
Njia bora ya kutafsiri kifungu chochote kile cha maandiko ni kwa kusoma vifungu vingine vinavyozungumzia somo hilo hilo. Mawazo katika Agano Jipya, mizizi yake iko katika Agano la Kale. Manabii walihubiri kanuni kutoka katika sheria ya Mungu. Mafundisho ya Yesu yako juu ya msingi wa kweli wa Agano la Kale. Nyaraka za Agano Jipya zinaelezea maisha na mafundisho ya Yesu kutoka katika Injili.
Vifungu vikuu vya Biblia ni vipana sana kuelezewa kikamilifu katika kifungu kimoja. Mawazo haya kutoka kwa Mungu yamefumwa katika namna ya Biblia nzima. Yanaweza kupatikana katika Agano la Kale au katika Agano Jipya. Yatazungumza katika Zaburi na katika Nyaraka za Agano Jipya. Yapo katika Vitabu vya Sheria na katika Injili.
Usilete kiini katika kifungu kutoka katika mawazo yako mwenyewe. Usijaribu kugeuza na kuunda kifungu kilingane na mawazo yako. Usitafute kifungu kinachoonekana kuthibitisha mtazamo wako. Usikisome katika namna ya jinsi kinavyoonekana
Somo la 10
Kufuata mawazo ya kifungu, utachagua neno lingine lililooneshwa pale kuwekea mpaka upeo wa somo lako
Kuandaa ujumbe. Chagua kifungu Nakili kifungu Maneno ya Kitendo Maneno ya muhimu Uchunguzi. Viini vya Biblia Wazo kuu Kiini cha Mpaka Mawazo Saidizi Pointi kuu Watu Picha za maneno Kusimulia Hadithi Matumizi Kukusudia kwa Imani Kuorodhesha
56
kusaidia mawazo yako. Badala yake utakiacha kifungu kijisemee chenyewe. Utakisoma kifungu kwa ujumbe uliokusudiwa. Mjumbe mwaminifu wa Mungu atafikiria kifungu kinachohitajika na watu wake. Anaweza kutafuta kifungu cha Biblia kinachozungumzia kiini hicho. Lakini wakati wote atakisoma kifungu kwa makini kuyaruhusu mawazo ya mwndishi wa kifungu yazungumze. Kazi yake ya kwanza atakayoifanya ni kugundua nini mwandishi wa kifungu na Roho Mtakatifu walichokusudia kukisema.
Ni muhimu sana kutoyafungia mahubiri na mafundisho yako kwa hekima zako mwenyewe. Ni kifungu cha maandiko tu kilicho na mashauri kamilifu ya Mungu. Unaweza kuwa mcha Mungu. Unaweza kuwa na miaka mingi ya uzoefu. Unaweza kuwa na ufahamu mzuri wa Biblia na hekima kubwa katika kweli za Mungu. Lakini bado ni lazima ulisome neno la Mungu lililoandikwa kwa ujumbe wake kwa watu. Hapo tu ndipo utakapokuwa mjumbe mwaminifu wa Mungu.
Wazo kamili la Kifungu.
Mjumbe wa Mungu atatafuta kugundua kiini kimoja ambacho anakichukua kuwa somo lililokusudiwa na mwandishi wa kifungu. Katika kazi hii anakusudia kujibu swali, “Mwandishi wa Kifungu anazungumzia nini?’ Halafu atatafuta neno lingine katika kifungu liwe kiini cha mpaka ambacho kitafupisha upeo wa somo. Kwa kiini hiki cha pili atauliza, “Mwandishi wa kifungu amefupishaje upeo wa somo lake katika kifungu hiki?” Katika somo la Yohana 3:1-8, tumependekeza kwamba mwandishi alikusudia kushughulika na somo la “Kuzaliwa Upya.” Wazo hili ni la muhimu sana katika kuelewa maisha ya Kikristo. Tunajifunza katika wazo hili kuwa Wakristo “”wanazaliwa mara ya pili.”
Kifungu hiki ndio kifungu kikuu katika “Kuzaliwa Upya” Nyakati zingine huwa tunaliita wazo hili “Kuzaliwa mara ya Pili”. Somo hili limetajwa pia katika 1Petro 1:23 na Tito 3:5. Hata kama Yohana 3:1-8
Ni muhimu sana kwamba usifungie mahubiri na mafundisho yako kwa hekima zako mwenyewe. Ni kifungu tu cha maandiko ndicho chenye mafundisho/ maonyo kamili ya Mungu.
57
ndio kifungu kikuu kaika somo hii, hakitoi taarifa yote ya Biblia kuhusiana na “Kuzaliwa Upya.”
Unaposoma kifungu chochote kile cha Biblia, unataka kugundua wazo kuu katika kifungu hicho. Hata kama kiini au somo linaweza kuelezewa katika maneno mawili au matatu, bado linaweza kuwa si wazo kamili. Ni pana sana. Ni kubwa sana kwa kifungu hiki kimoja. Ni lazima tuangalie katika kifungu tena kwa makini kuona njia halisi ambayo mwandishi ameitumia kufupisha upeo wa kile anachokisema kuhusu somo hilo.
Katika Yohana 3:1-8, mwandishi hasemi kila kitu ambacho kingeweza kusemwa kuhusiana na Kuzaliwa Upya. Lakini badala yake anataarifu mazungumzo yaliyohusu somo hili. Katika mazungumzo haya, Yesu alikuwa anazungumza mawazo kwamba Mungu alikuwa anapendezwa naye. Hakufikiri alihitaji kubadilisha. Yesu alimtaka afahamu kwamba mambo yake yote ya kidini yasingeweza kuubadilisha moyo wake. Alihitaji kuzaliwa mara ya pili.
Angalia kifungu. Angalia Yesu alimwambia kwamba asingeweza kuuona wala kuuingia ufalme wa Mugu kama asingezaliwa mara ya pili. Kifungu cha maneno kikuu kinaonekana kuwa katika mstari wa 7 ambapo anasema, “Ni azima uzaliwe mara ya Pili.” Anaweka wazi kwamba kuzaliwa mara ya pili ni “lazima” anaposema “Ni lazima uzaliwe mara ya pili.” Anaweka wazi kwamba kuzaliwa mara ya pili ni “lazima” katika ufalme wa Mungu.
Wazo hili la umuhimu ndio shabaha halisi ya mafundisho ya Yesu hapa katika kuzaliwa upya.
Ninashauri kwamba wazo la kifungu hiki ni “Umuhimu wa Kuzaliwa Upya.” Kwa kusema kwamba kifungu kinahusu “Kuzaliwa Upya” ni pana sana kwa makusudi halisi ya mwandishi. Yesu alizingatia juu ya “umuhimu” wa kuzaliwa upya. Hiyo inafupisha upeo wa maelezo. Inasaidia pia kuelezea wazo kamili.
“Ninao ufahamu kuliko wazee, Kwa kuwa nimeyashika mausia yako. Nimeiepusha miguu yangu na kila njia mbaya, Ili nilitii neno lako.”
Zaburi 119:100, 101
58
Kutafuta Kiini cha Mpaka.
Utagunduaje hiki kiiini cha mpaka katika kifungu chako? Ngoja nishauri hatua za kuchukua:
1. Orodhesha viini vyote vya Biblia ulivyovigundua katika kifungu.
2. Chagua kiini kimoja ambacho ni somo kuu la kifungu.
3. Angalia kiini kingine cha pili kinachojitokeza katika kifungu.
4. Kijaribu kiini hiki cha pili kama kifungo cha somo kuu.
5. Weka viini vyote viwili pamoja kuelezea wazo la Kifungu.
Hebu tupitie hatua hizi kugundua kiini cha mpaka kwa Mathayo 5:13-16.
Hatua ya kwanza ni kugundua na kuorodhesha viini vyote vya Biblia vilivyoko katika kifungu. Hapa kuna orodha yetu ya viini kutoka Mathayo 5:13-16:
Chumvi dunia chumvi radha kukolezwa wema bure
kutupwa kukanyagwa watu nuru ulimwengu mji kufichika
nuru taa funika kiango nuru nyumba
angaza nuru yenu watu ona matendo mema tukuza Mungu mbingu
Tumechagua kiini kimoja ambacho ndicho somo kuu la kifungu. Hata kama neno halionekani katika kifungu, matumizi ya picha ya “chumvi” na “nuru” yanaeleza wazi kwamba Yesu anazungumzia kabisa kuhusu “mvuto”. Somo hilo linaonekana kutumika vizuri katika mistari yote ya kifungu.
Sasa tunaangalia kiini kingine kilichojitokeza katika kifungu ambacho kinaweza kutumika kama kiini cha mpaka. “Chumvi” na “Nuru” ni lugha za picha kwa somo kuu, “ushawishi.” Kwa jinsi nilivyokisoma kifungu hiki, nimeona kwamba neno “watu” limeonekana mara mbili. Mbali na hilo, “dunia” na “ulimwengu” vimeonekana kumaanisha kitu kimoja, watu waliokaribu na mwamini. Kifungu, “wote waliomo nyumbani,” inaonesha pia watu wengine tunaowafahamu.
“Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele, Maana ndizo changamko la moyo wangu. Nimeuelekeza moyo wangu nizitende amri zako, Daima, naam, hata milele.”
Zaburi 119:111, 112
59
Kutokana na alama zote hizi, nimeamua kuwa kiini kizuri cha pili ni “wengine,” au “ulimwengu wako,” au “watu.”
Kiini kingine ambacho kinaweza kuwa cha mpaka kinaoneshwa kwa matumizi ya “ninyi” na “yenu” katika kifungu. Yesu anasema, “Ninyi ni chumvi ya dunia.” Anasema, “Ninyi ni nuru ya ulimwengu.” Anasema, “Nuru yenu na iangaze” na anazungumzia “matendo yenu mema” na “ Baba yenu wa mbinguni.” Inaonekana wazi kabisa kwamba Anazungumza na waamini.
Kiini kingine kinachoweza kuwa cha mpaka ni “Kristo.” Hata kama “Yesu” au “Kristo” haonekani katika kifungu, tunajua kwamba Yesu ndiye anayezungumza. Tunajua pia kuwa ushawishi wa mwamini si wake mwenyewe, lakini ni kwa ajili ya Kristo. Tunaweza tukalichukulia tu kuwa neno “Kristo” lazima litakuwa sehemu ya wazo.
Kwa hiyo, tuna viini vitatu, ambavyo vinaweza vikatumika kama kiini cha mpaka kwa ajili ya kifungu. Je unakiona kingine? Unaweza kuona kama jinsi tulivyojaribu kufanyia kazi hatua hizi, kwamba unapaswa uyaweke macho yako katika kifungu. Lakini ni lazima pia uangalie katika sehemu kubwa, kwa swala hili mahubiri mlimani katika sura ya 5-7. Kukua kwako kwa kuyaelewa maandiko itakusaidia kutafsiri kifungu.
Hatua yetu inayofuata ni kiini cha mpaka kinachowezekana kwa kukiunganisha na somo kuu. Je kiini “wengine” kitawekea mpaka vizuri somo la “mvuto?” Vyote vinaonekana kuleta maana vinapounganishwa na somo, “mvuto.”
Hatua yetu ya mwisho ni kuyaweka maneno hayo mawili pamoja kama sentensi ya wazo la Kifungu. Kwa pamoja yanapaswa kueleze wazo kamili. Mathayo 5:13-16 inazungumzwa na Yesu kwa wanafunzi wake. Kwa hivyo tunaweza kuona wote “waamini” na “Kristo” kama sehemu ya muhimu ya wazo la Kifungu chochote kile. Tungeweza kusema kwamba Wazo la Kifungu ni “Kuwavuta wengine kwa Kristo.” Au tungeweza kukiita “Mvuto wa Mwamini kwa Kristo.” Vyote hivi vinaonekana kutumika kwa Wazo la Kifungu.
“Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui zangu, Kwa maana ninayo siku zote. Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, maana shuhuda zako ndizo nizitafakarizo.”
Zaburi 119:98, 99
60
Tunawezaje kutulia katika kiini kimoja tu cha mpaka? Angalia hii. Kwa sababu “waamini” wanaeleweka kuwa hao ndio Yesu anaowaambia, tuliache wazo hilo kwa mazungumzo mlimani. Onyesha pia, unapofundisha kifungu hiki kuwa mvuto wetu wetu uwe kwa ajili ya Kristo. Kiini cha Mpaka cha msaada zaidi ni “wengine,” kikioneshwa na maneno “dunia,” “ulimwengu,” na “watu” katika kifungu.
Nilipohubiri kifungu hiki, nilikiita, “Kuuvuta Ulimwengu wako kwa Kristo.” Kwa “Ulimwengu wako,” Nilikuwa namaanisha watu wengine wote wanaotuzunguka kila mmoja wetu ambao wanaguswa na maisha yetu na ushuhuda wetu. Hiyo inaonekana kuwa kile Yesu anachozungumzia. Anatumia chumvi na nuru kama mifano kwa sababu vinaathiri kila inavyovigusa. Kwa namna hiyo hiyo, Mkristo ayaguse maisha ya kila anaowagusa. Jaribio kwa Wazo letu la Kifungu litakuwa ikiwa kifungu kinataka kuzungumza kwa somo hili. Katika somo letu lijalo, tutaona kinasemaje kwa kuangalia jinsi mwandishi alivyoshughulika na somo lake. Tutauliza, “Mwandishi anasema nini kuhusu wazo hili.”
Mazoezi ya Somo.
1. Rudia mawazo makuu ya somo hili: Viini vikubwa vya Biblia ni vipana sana kuelezewa katika kifungu kimoja. Tunategemea kupata katika kifungu chochote kile kiini kimoja ambacho ni wazo kuu la sehemu ile na kiini kimoja kuwekea mpaka upeo wake. Kiini kinaweza kudhihirika katika kifungu hata kama neno halionekani pale.
2. Soma Zaburi 1 na Warumi 12:1,2 kwa swala la mpaka, kufupisha upeo wa somo kuu kwa kila kifungu. Kumbuka kwamba neno unalotumia linaweza kuwa limependekezwa tu na kifungu.
“Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.”
Waefeso 5:17
61
Somo la 11
KKuuttaaffuuttaa sseehheemmuu
Mpango ulio wa zamani mno wa hubiri la Biblia ni ule wa kupitia andiko mstari kwa mstari. Muhubiri anayetumia njia hii hawezi kujaribu kulingamua somo la mwandishi au jinsi gaini alivyoliwekea mipaka somo hilo katika andiko hili. Yeye anaelezea tu maandiko kila mstari kwa wakati wake. Ijapo njia hii ni nzuri, niinataka nikuoneshe njia iliyo bora zaidi. Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kusoma kifungu kwa njia ambayo mwandishi wa kifungu amelionesha somo lake.
Kile Anachokiseme
Tumekwisha chunguza maneno ya mwandishi wa maandiko ili kwa kuyapata mawazo yake. Halafu tukaorodhesha mawazo haya kama viini vinavyoonekana katika maandiko. Katika viini hivi, tukachagua kile kinachofaa sana kama somo kuu la mwandishi katika andiko lile.
Wakati huu tutaorodhesha jinsi mwandishi alivyoshughulika na somo lake katika kifungu bado hatuzungumzii muundo wa mahubiri. Bado tunalisoma somo kuhusu nini mwandishi anasema. Tumeuliza maswali mawili kuhusu maneno ya mwandishi wa kifungu. Swali la kwanza lilituongoza kwa somo la mwandishi, Tuliuliza, “Mwandishi wa kifungu anazungumzia nini?” Halafu tukauliza swali kutuongoza katika kiini cha mpaka kinacholenga somo la kifungu. Tuliuliza, “Jinsi gani mwandishi amewekea mpaka upeo wa kile anachozungumzia?”
Sasa tunalo swali la tatu la kuuliza. Hili limenuiwa kutuongoza sisi katika mawazo ya mwandishi yanayotia nguvu katika somo lake. Tunauliza, “Mwandishi ana nini cha kusema kuhusu somo lake?” Kwa swali hili, tunagundua kwamba mwandishi anaweza kuwa`ameonesha
Somo la 11
Utaanza hatua ya kufafanua kwa kuangalia katika kifungu kuona mwandishi ana nini cha kusema kuhusu somo lake.
Kuandaa Ujumbe Chagua kifungu Nakili kifungu Maneno ya vitendo Maneno ya muhimu Uchunguzi Viini vya Biblia Wazo kuu Kifungu cha mpaka. Mawazo saidizi Pointi kuu Watu Maneno ya picha Kusimulia hadithi/ habari Matumizi. Kukusudia kwa Imani. Kuelezea/Kuorodhesha.
62
namna nyingi ya somo lake katika kifungu. Kabla hatujaamua jinsi ya kupanga mahubiri kutoka katika kifungu hiki, tunataka kuona jinsi mwandishi alivyopanga mawazo yake mwenyewe.
Mjumbe wa Mungu anataka kuhubiri kile ambacho Mungu amekisema katika neno lake lililoandikwa. Kufanya hivyo anataka kufuata mawazo ya mwandishi wa kifungu. Si kwamba tu anataka kufikisha kwa watu somo la kifungu, anataka pia kuwapa mawazo saidizi kwa somo hilo kama jinsi yalivyofunuliwa katika kifungu.
Kuangalia maelezo katika kifungu
Kumbuka kwamba somo lako linahitaji uchunguzi wa makini sana. Ni kama mpimaji anayetafuta sababu katika tukio la uhalifu. Ni kama mtafiti anayeandaa maelezo(notsi) ya nini vithibitisho vinakufundisha. Ni kama muwindaji katika msitu anayeangalia alama za lini mnyama amepita njia hii na alikuwa ni wa aina gani. Je unalo jicho kwa maelezo hayo? Tumegundua kwamba katika aina nyingi za kazi jicho la utaalamu kwa maelezo linahitajika. Mkulima anaweza kuona katika ardhi, katika anga, na katika mmea wake, dalili zitakazo msaidia kupanga kazi yake. Karani anaweza kuona katika vyumba vya namba habari ya biashara. Mwalimu anaweza kuona katika sura za wanafunzi wake ikiwa wanajifunza au wanahitaji msaada maalum zaidi. Mwalimu wa Biblia pia lazima awe na uwezo wa kuangalia katika kifungu chake maelezo yatakayo msaidia kuelewa maana ya kifungu. Tunapoangalia jinsi mwandishi wa kifungu anavyoshughulika na somo lake, Tunajikuta tunafanya kama wachunguzi tena. Hapa kuna baadhi ya ishara ambazo unahitaji kuziona: Angalia maneno ya kitendo na maneno ya jina katika kifungu. Angalia maneno yanayojirudia katika kifungu na angalia kama yanaleta wazo la muhimu. Angalia maneno ya kuunganisha kama vile, na, lakini, wakati na kwamba. Maneno haya yanaonesha uhusiano katikati ya mawazo.
Si tu kwamba anahitahji kuwaeleza watu somo la kifungu, Anahitaji kuwapa mawazo saidizi kwa somo hilo kama yalivyofunuliwa katika kifungu..
63
Angalia maneno ya picha ambayo yanaelezea ukweli wa Biblia kwa njia ya maisha ya kawaida ya duniani au kitu. Angalia maneno ya kusimulia ambayo yanakueleza zaidi kuhusu watu na mawazo katika kifungu. Angalia jinsi maneno mbalimbali yanavyofanya kazi pamoja.
Umuhimu wa kuzaliwa Upya
Tuangalie pamoja katika Yohana 3:1-8 jinsi gani mwandishi (Yohana) na mzungumzaji (Yesu) wanasema kuhusu kuzaliwa upya. Nimependekeza kwamba somo la mwandishi ni “kuzaliwa upya” na kigezo cha mpaka ni “umuhimu”. Hii ina maana tunachukua somo kuu la mwandishi kuwa “Kuzaliwa Upya” Tunaona kwamba anafunga maelezo yake ya kuzaliwa upya kwa wazo la “Umuhimu.” Kwa hiyo somo la kifungu tunatumia ni “Umuhimu wa Kuzaliwa Mara ya Pili”
Hatua inayofuata ni kuchukua somo letu la kifungu tulilolipendekeza kupitia kifungu cha maneno, mstari kwa muda. Tunaangalia mawazo halisi kuhusu umuhimu wa kuzaliwa upya. Haya ni mawazo yanayotia nguvu kukusaidia kuelezea kuwa kuzaliwa upya ni muhimu. Tunalenga kujibu swali, “Nini mwandishi wa kifungu anasema kuhusu somo lake?”
Mistari miwili ya mwanzo inafungua hadithi na kumtambulisha Nikodemo haionekani kusema kitu chochote maalum kuhusu umuhimu wa kuzaliwa mara ya pili.
Mstari wa kwanza unaoeleza waziwazi uhusiano wa “umuhimu” na “kuzaliwa upya” ni mstari wa 3. Hapa Yesu anasema, “mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu”. Yesu anamwambia Nikodemo kwamba ni lazima azaliwe mara ya pili ili “kuuona” ufalme wa Mungu. Hii inaonekana kuwa jibu kwa Nikodemo kwa kule kutaja ishara katika mstari wa 2. Anafikiri kabisa kwamba anamuona Mungu akifanya kazi.
Katika mstari wa 5, Yesu anasema, “Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu.” Yesu anaonekana kujibu swali la Nikodemo kuhusu “kuingia” kwenye tumbo la mama
“Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazia asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli”.
2 Timotheo 2:15
64
yake akiwa mzee. Nikodemo anaonekana kuchanganyikiwa na lugha hii ya picha. Anazungumza katika mstari wa 4 kuhusu kuzaliwa kwa mwili. Yesu anatumia “kuzaliwa” kuwakilisha mabadiliko ya kiroho. Hivyo, Yesu anatofautisha kati ya “Kuzaliwa kwa maji” na “kuzaliwa kwa roho”
Mstari wa 6 unaonekana kuwa na maelezo zaidi juu ya tofauti kati ya “kuzaliwa kwa mwili” na “kuzaliwa kwa roho.” Kuingia ufalme wa roho, lazima mtu awe na uzima wa roho kwa Roho Mtakatifu. Kuzaliwa kwa mwili kunamfanya mtu awe mwanadamu. Ili mtu awe hai kiroho, ni lazima azaliwe kwa roho. Sasa tunakuja katika mstari wa 7 na 8. Sehemu hii ni ngumu kuielewa. Hapa Yesu anatoa neno lingine la picha anapozungumzia “upepo.” Anaacha picha ya “Kuzaliwa” na anaingia katika neno la picha “upepo.” Upepo ni kama Roho Mtakatifu. Kama vile ambavyo upepo huvuma kuelekea unakokutaka, ndivyo Roho afanyavyo kama jinsi apendavyo. Kama vile jinsi ambavyo unaweza kuuhisi upepo kwa sauti yake, ndivyo ambavyo unaweza kuhisi mwendo wa Roho kwa namna fulani. Kama jinsi ambavyo huwezi kusema upepo ulikotoka au unakokwenda, ndivyo usivyoweza kutabiri kutembea kwa Roho. Hivyo mtu aliyezaliwa kwa mwili, hawezi kumutawala Roho Mtakatifu. Hawezi kuwa na hakika ametoka wapi au anakwenda wapi. Lakini mtu aliyezaliwa mara ya pili anaweza kuhisi uelekeo wa Roho. Anaweza nkuona kazi za Roho katika maisha yake. Uzoefu wetu katika picha ya upepo, ni mfano wa uzoefu wetu katika Roho. Tafsiri yangu katika kile Yesu alichokuwa anakisema ni hii.
Nikodemo alikuwa mwanadini sana, ambaye alitafuta kumpendeza Mungu kwa kutunza na kufuata taratibu za dini. Alijaribu kutengeneza uhusiano wake na Mungu kwa shughuli za kidini. Yesu alikuwa anamwambia kuwa, uhusiano wake na Mungu ni lazima uwe ni wa namna nyingine. Badala ya kujaribu kumpendeza Mungu kwa
“Hata walipokwisha kumuomba Mungu,Mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, Wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.”
Matendo 4:31
65
shughuli za kidini, anapaswa kutambua kazi kuu za Mungu. Katika hili ninaona wazo la tatu kuhusu “ umuhimu wa Kuzaliwa Upya”. Mtu lazima azaliwe tena ili ahusiane Vyema na Mungu kama Roho. Katika somo linalofuata, tutaangalia tena kifungu hiki. Kumbuka, katika hatua hii tunalenga kuchunguza jinsi mwandishi anavyozungumza kuhusu somo lake. Huu si muhtasari bado kwa somo ama mahubiri.
Warumi 12:1, 2
Angalia jinsi muundo unavyooneshwa katika kifungu kingine. Tumekwisha kuonesha umuhimu wa “maneno ya kitendo” katika kifungu chochote. Vitendo hivi mara nyingi ni funguo kwa mawazo ya mwandishi. Hakikisha unaangalia vitendo kwa ukaribu unapojibu swali “Mwandishi anasema nini kuhusu somo lake?”
Fungua Biblia yako katika Warumi 12:1, 2. Kifungu hiki kinatoa mfano mzuri sana wa umuhimu wa maneno ya kitendo. Vitendo katika kifungu hiki cha maneno vinaonesha mpangilio wa kifungu. Soma mistari hii na angalia vitendo hapo:nawasihii, itoeni, msifuatishe, mgeuzwe, kujua. Unapoangalia nini Paulo “anachowasihi” wasomaji kufanya, mara moja unaweza kuona muundo rahisi: Jitoweni kwa Mungu Msifuatishe namna ya dunia Mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu.
Neno la mwisho ni Kujua. Maneno yenyewe ni “mpate kujua”. Neno kwamba hapa lina maana ili kwamba au kwa ajili ya.Hivyo kifungu kinasema kwamba waamini wanapaswa kuchukua matendo haya matatu ili kwamba wapate kujua mapenzi ya Mungu, kwamba ni “mema” na “yakupendeza” na “kamili”.
Hivyo, matendo katika kifungu yanatueleza kwamba matendo yote ni kwa ajili ya kujua mapenzi ya Mungu. Mwandishi(Paulo) anasema kwamba mwamini anapaswa kufanya matendo haya ili kujua mapezi ya Mungu. Haya ni mambo muhimu sana kufundisha watu. Maneno mengine katika kifungu yanasaidia maneno haya ya kitendo kwa kutoa maelezo ya ziada.
Muundo wa somo letu unapaswa kufuata muundo wa mwandishi wa kifungu. Lakini mara kwa mara tutachagua namna tofauti tofauti za maneno tunapofikisha wazo lile lile kwa watu katika kizazi hiki.
66
Unaweza kufundisha kifungu hiki cha maneno kwa kutumia maneno ya mwandishi tu kama maelezo yako ya kweli.Hata hivyo katika somo letu linalofuata tutazungumzia jinsi ya kupanga maneno yenyewe ya mawazo haya ili kwamba wanaokusikiliza waelewe vizuri mafundisho haya. Tutaendelea kushughulika na muundo wa kifungu,inapokuwa muundo wa ujumbe.
Mazoezi ya Somo.
1. Rudia mawazo makuu ya somo hili: Tumeangalia majibu ya swali “Mwandishi anasema nini juu ya somo lake.” Tuliweka fikra zetu kwa uangalifu juu ya nini mwandishi anasema katika kifungu. Tunatafuta maelezo zaidi katika kifungu. Tunatafuta kifungu cha mawazo ya mwandishi ambacho kinasaidia somo lake. Tunaona kwamba vitendo vinaweza kutuongoza katika muundo wa mwandishi.
2. Soma Zaburi 1 na mathayo 9:35-38 kugundua jinsi mwandishi alivyo shughulika na somo lake katika kila kifungu. Angalia mawazo saidizi yanayo kamilisha ujumbe mkuu.
“Usiliondoe neno la kweli kinywani mwangu kamwe, Maana nimezingojea hukumu zako. Nami nitaitii sheria yako daima, Naam milele na milele. Nami nitakwenda panapo nafasi, kwa kuwa nimejifunza mausia yako.”
Zaburi 119:43-45
67
Somo la 12
KKuutteennggeenneezzeeaa kkiiffuunngguu ppooiinnttii kkuuuu..
Sasa tunaingia kwenye daraja kupitia kwenye pengo. Umbali ni mkubwa sana kutoka kwenye ulimwengu wa zamani wa Biblia na wa wasikilizaji wako. Wakati wako ni wakati wa tofauti, wa utamaduni tofauti, na lugha tofauti.Utachukuaje wazo la kifungu katika kizazi hiki kama ujumbe wa Mungu kwa leo? Hiyo ndiyo changamoto ya somo hili.Hapa tutaondoka kutoka katika uchambuzi wa kifungu mpaka katika kutengeneza maneno yenyewe ya mawazo ya mahubiri.
Ni mawazo ya namna gani ambayo tunapaswa kuyaleta kwa watu wetu wa leo kutoka katika kifungu? Je, wanahitaji kujua historia ya Biblia? Labda. Je, wanahitaji kujua utamaduni wa watu wa Biblia? Labda. Je, wanahitaji kujua mazingira ya nchi za Biblia? Labda.Lakini kuna aina moja ya elimu ya Biblia wanahitaji kuipokea pasipo kukosa. Ni elimu ya tabia na sifa za Mungu (Thiolojia). Huu ni ujumbe wa maandiko kuhusu Mungu na anavyohusika na uumbaji wake.
Changamoto yetu ni kupata ujumbe huu wa kithiolojia kutoka katika kifungu cha mandiko kupitia. Pengo la urefu wa wakati utamaduni na lugha. Kufanya hivyo tumechukua hatua nyingi sana katika usomaji wetu wa kifungu. (1)Tumekwisha tambua viini vikuu katika kifungu. Halafu (2) Tukachagua kiini kimoja ambacho tulikichukuwa kuwa somo la mwandishi wa kifungu Kulenga somo hilo, tulichagua kiini kingine kutoka katika kifungu kuweka mipaka ya somo. Changamoto yetu ni kupa ujumbe wa kithiolojia kutoka katika kifungu kupitia katika umbali huu wa muda, na mila na lugha. Kufanya hivyo tumechukua hatua nyingi sana katika usomaji wetu wa kifungu.
Somo la 12
Mawazo ya mwandishi wa Kifungu kwa namna ya somo lake, yanaweza yakatengenezewa sentensi nzuri katika kifungu kwa umakini kwa ajili ya pointi kuu katika ujumbe.
Kuandaa ujumbe. Chagua kifungu Nakili pembeni kifungu. Maneno ya vitendo. Maneno ya muhimu. Mambo uliyoyachunguza Viini vya Biblia Tengenezea sentensi wazo kuu. Wekea mipaka somo. Mawazo saidizi. Pointi kuu. Watu. Picha za maneno. Hadithi Matumizi Kukusudia kwa imani Kuorodhesha.
68
(1)Tumekwisha tambua viini vikuu katika kifungu. Halafu, (2) Tulichagua kiini kimoja ambacho tulichukua kuwa somo la mwandishi wa kifungu. Kulenga somo hili, (3) tulichagua kiini kingine kutoka katika kifungu kuweka mipaka ya somo. (4) Halafu tumegundua tena mawazo saidizi anayotoa mwandishi katika somo lake.
Kazi yetu sasa ni kutengenezea sentensi mawazo hayo kwa umakini kwa ajili ya wasikilizaji wetu. Hii itatuwezesha kupata ujumbe wa kithiolojia kwa watu kutoka katika kifungu. Hebu turudi sasa katika vifungu ambavyo tumekuwa tukivisoma na tuone ni jinsi gani tunaweza kuzitengenezea sentensi jumbe zake kwa wakati huu.
Umuhimu wa Kuzaliwa Upya.
Angalia tena kifungu katika Yohana 3:1-8. Kama ungetakiwa kusema wazo la kifungu katika sentensi, ungesemaje? Mimi nimetengenezea sentensi hivi, “Kuzaliwa upya ni muhimu katikam ufalme wa Mungu” Viini viwili vinavyotengeneza wazo ni “kuzaliwa upya” na “umuhimu”. Tunavipata viini hivi ndani ya kifungu. Kimojsa tunakiita Somo na kingine tuliita kiini cha mpaka. Baada ya kuchunguza kwa umakini maneno yote ya kifungu, tunachukua viini hivi kuwa kile mwandishi alichotaka kukisema. Anazungumza juu ya Somo lake “Kuzaliwa upya” na anawekea mpaka mazungumzo yake Katika “Umuhimu” wa kuzaliwa upya. Kwa hivyo tunaweka viini vyote hivi viwili pamoja kupata wazo kamili, “Umuhimu wa Kuzaliwa Mara ya Pili.” Katika wazo letu kama sentensi, tutajumlisha pia kiini “ufalme wa Mungu” kama Yesu alivyofanya katika kifungu. Tunauliza “Ufalme wa Mungu ni nini?” Ni mahali ambapo Mungu anatawala kama Mfalme.Ni ufalme wa Kiroho usioonekana ndani ya mioyo ya watu.Ni wale tu waliozaliwa mara ya pili ndio wanaweza kuuelewa au kuuingia. Nikodemo, kama kiongozi wa dini, kwa hakika alidhani kwamba yumo katika ufalme wa Mungu. Lakini Yesu anamwambia kuwa pasipo kuzaliwa mara ya pili hawezi kuuona wala kuuingia ufalme huo.
Kwa hivyo tunayokanuni ya kuelezea wazo la ujumbe wetu kama sentensi.Tunajumlisha mchanganyiko huu: Somo,Kiini cha mpaka,na viini vingine vya ufunguo vya kifungu.
69
Hivyo tunayo kanuni ya kueleza wazo la ujumbe wetu kama sentensi. Tutajumlisha mchanganyo huu: Somo, kiini cha mpaka, na viini vingine vya ufunguo vya kifungu kama “Mungu”, “Kiroho” au “ufalme wa Mungu” Viini hivi vingine vinaweza kutumika katika kifungu au kulezewa vizuri zaidi. Vinaonesha kuwa ujumbe ni wa Kithiolojia.
Maelezo ya Mwandishi wa Kifungu.
Swali la tatu tulilouliza tulipo kuwa tunasoma viini vya kifungu lilikuwa ni hili, “Mwandishi anasema nini juu ya somo lake?” Tunajua kwamba anaweza kulieleza somo lake katika njia nyingi. Haya ndiyo maelezo ya mwandishi kwa somo lake.
Mara nyingi tunafanya hivi katika mazungumzo yetu. Unaweza kusema , “Ninao farasi wazuri”. Halafu unaweza kusema zaidi kuhusu farasi wako, “Farasi mmoja mzuri ni mweupe” . Farasi mwingine mzuri ni mweusi. Na farasi mwingine mzuri ana madoa madoa. Farasi mwingine mzuri ni wa kahawia”. Hivyo wazo lako kuu ni “farasi wazuri”. Hata hivyo, unasema kuwa pana Mweusi, mweupe, wamadoa madoa na wa kahawia.
Katika somo la 11, tulichambua kifungu kulingana na nini mwandishi anasema kuhusu somo lake. Hebu sasa tuangalie tena mawazo hayo na tuone maelezo ya kithiolojia ambayo tunataka kuyafanya katika ujumbe wetu kwa ajili ya kizazi hiki.
Tumeona katika maneno yake kwamba Yesu anazungumzia juu ya “Umuhimu wa Kuzaliwa Upya”. Halafu tukagundua katika mstari wa 3 Anamwambia Nikodemo, “Mtu asipozaliwa mara ya Pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu”.Hivyo basi, hii ni moja kati ya sababu katika kifungu hiki kwamba kwa nini kuzaliwa upya ni muhimu.
Nikodemo alidhani kuwa ameuona mkono wa Mungu katika matendo ya miujiza ya Yesu. Lakini hakuelewa kuwa Yesu alikuwa ni Masihi. Hakuelewa maana ya kile alichokiona. Aina hiyo ya kuona kwa kiroho kunaweza kuja kwa yule tu aliyezaliwa mara ya pili, na hivyo kuweza kuona ufalme wa Mungu.
“Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili;si kwa miili iharibikayo,bali kwa ile isiyoharibika;kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.”
1 Petro 1:23.
70
Ujumbe wetu katika kifungu hiki tunaweza kusema, Kuzaliwa upya ni muhimu katika kuuona ufalme wa Mungu.Sentensi hii haimtaji Nikodemo. Haizungumzi juu ya wakati uliopita. Ni ukweli wa wakati wote na kwa watu wote.
Mstari wa 5 imeelezwa vizuri sana katika kifungu kama mstari wa 3.Hapa Yesu anazungumza na Nikodemo,”Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, Hawezi kuingia ufalme wa Mungu” Yesu anajibu tena juu ya kile Nikodemo alichosema kuhusu kuzaliwa wakati akiwa mzee. Yesu alitaka ajue kwamba anazungumza kwa mafumbo. “Kuzaliwa kwa maji” kuna maana kuzaliwa kwa mwili. “Kuzaliwa kwa Roho kuna maana kuzaliwa kwa Roho. Hivyo kuzaliwa kwa upya hakuna maana ya kurudi tena kwa mama yako. Si “kuingia” tena katika mwili wake kwa mara ya pili Badala yake ni kuzaliwa mara ya pili kiroho na “kuingia” ufalme wa Mungu Ujumbe wetu katika kifungu hiki tunaweza kusema, “Kuzaliwa upya ni muhimu ili kuingia ufalme wa Mungu” Hii inatoa sababu ya pili ya kuwa kuzaliwa upya ni muhimu katika ufalme wa Mungu. Sehemu ya kifungu inayofuata ni katika mstari wa 7na 8. Katika mistari hii Yesu anaendelea kuzungumza juu ya mfano wa “Kuzaliwa”. Lakini anatumia pia kielelezo ama mfano wa “upepo”. Kama vile jinsi ambavyo mwamini alivyouzoea na na upepo, ndivyo hivyo ambavyo anaweza kumzoeana Roho Mtakatifu, lakini tu ikiwa amezaliwa mara ya pili. Nikodemo alimwendea Mungu kupitia kanuni na taratibu zake za dini. Mfano huu wa upepo unaeleza kwamba tunapaswa kuhusianishwa naye kwa uhusiano wa Kiroho. Katika hatua hii, maelezo mengi yanaweza kutumika kutoa sehemu hii ya ujumbe wako kwa watu. Unaweza kusema. “Kuzaliwa upya ni muhimu ili kumuona Roho wa Mungu.” Je unafikiri juu ya mambo mengine ya kithiolojia ambayo yanaelezwa na mfano huu wa “upepo”? Tutaiangalia hii tena katika somo letu lijalo. Hebu turudi sasa katika Warumi 12:1,2 na tuone ni jinsi gain ambavyo tunaweza kutengenezea sentensi ukweli wa kifungu hicho.
“Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi…..Wote wakajazwa Roho mtakatifu”
Matendo 2:2, 4
71
Kuyajua Mapenzi ya Mungu.
Katika kuchunguza kifungu hiki katika somo lililopita, Tuligundua kwamba, matendo katika kifungu yanadokeza japo kwa ufupi tu mawzo ya mwandishi. Tuliona maneno unganishi, “kwamba” ambayo yalikuwa ni ya muhimu sana katika kuelewa kifungu. Matendo matatu ya waamini ambayo Paulo anayataka ni “Ili mpate kujua” mapenzi ya Mungu. Hapo tunaweza kusema kwamba hoja ni “Mapenzi ya Mungu”. Kiini cha mpaka ni “Kujua”. Hii ina maana “ Kutoa ushuhuda” au “Kuthibitisha”. Paulo anaelezea jinsi ambavyo mkristo anaweza kuthibitisha, kulingana na uzoefu wake kwamba mapenzi ya Mungu ni “Mema” na “kupendeza”, na “Kamilifu”.
Hivyo matendo matatu anayoyataja ni njia ya kujua mapenzi ya Mungu katika maisha ya Mtu binafsi. La kwanza ni “ Itooeni miili yenu iwe thabihu iliyo hai.” Tunaweza kusema, “Mkristo anaweza kuyajua mapenzi ya Mungu kwa kujitoa kikamilifu kwa Mungu” Tendo la pili linalotajwa katika kifungu ni, “Msifuatishe namna ya dunia hii” Tunaweza kusema, “ Mkristo anaweza kuyajua mapenzi ya Mungu kwa kukataa ushawishi wa kiovu wa dunia.”
Onyo la tatu la upole la Paulo katika kifungu ni, “Mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu” Kutokana na wazo hili, katika ujumbe wetu tunaweza kusema, “Mkristo anaweza kujua mapenzi ya Mungu kwa kujiweka chini ya nguvu ya uweza wa kubadilisha ya neno la Mungu “ Kufanya upya kwa nia kunaweza kuja pale tu unapoguswa na ukweli neno la Mungu.
Maelezo zaidi ya Binafsi.
Maelezo zaidi ya mawazo katika vifungu hivi yanaweza kufanyika binafsi zaidi wakati unapo zungumza moja kwa moja na wasikilizaji. Badala ya kusema, “Kuzaliwa Upya ni muhimu” unaweza kusema, kama Yesu alivyofanya, “Ni lazima uzaliwe mara ya pili” Ndipo sentensi zetu tatu ni:
1. Ni lazima uzaliwe mara ya pili ili kuuona ufalme wa Mungu.
2. Ni lazima uzaliwe mara ya pili kuingia ufalme wa Mungu.
“Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui zangu, Kwa maana ninayo siku zote. Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo.”
Zaburi 119:98, 99.
72
3. Ni lazima uzaliwe mara ya pili kumuelewa Roho wa Mungu.
Kwa kifungu cha Warumi 12 tunaweza kubadilisha ufupisho wa kifungu hicho na kukifanya kulenga maisha ya mtu binafsi moja kwa moja. Hivyo badala ya kusema “Mkristo anaweza kuthibitisha mapenzi ya Mungu” unaweza kusema “ Unaweza kuyajua mapenzi ya Mungu” Tunaweza kupata sentensi tatu kama ifuatavyo:
1. Unaweza kuyajua mapenzi ya Muingu kwa kujitoa kikamilifu kwa Mungu
2. Unaweza kuyajua mapenzi ya Mungu kwa kukataa ushawishi wa uovu wa kidunia.
3. Unaweza kuyajua mapenzi ya Mungu kwa kujiweka chini ya uweza wa neno la Mungu libadilishalo.
Vifungu hivi viwili vimeonekana kuwa na mawazo saidizi matatu kila kimoja. Hii haimaanishi kwamba ujumbe wako utakuwa na pointi tatu. Mawazo saidizi katika kifungu yanaweza kutofautiana kiidadi kati ya kifungu na kifungu. Ujumbe wako utafuata kifungu kwa mtazamo huo.
Mazoezi ya somo.
1. Rudia mawazo makuu ya somo hili: Lengo letu lilikuwa ni kuchagua kwa makini maneno tunayoweza kuyatumia kutoa mawazo kutoka katika kifungu kwa wasikilizaji wetu. Mjumbe wa Mungu anatoa thiolojia kutoka katika kifungu chake. Mjumbe wa Mungu anatakiwa awe stadi wa kuchunguza maelezo katika kifungu. Kutoka katika maneno ya mwandishi wa kifungu, tunaweza kupata mawazo saidizi juu ya somo lake.
2. Lengo lako katika zoezi hili ni kutengenezea maneno mawazo saidizi katika kifungu katika njia ambayo yataeleweka kwa wasikilizaji wako.Angalia kila mwandishi anasema nini wazo lake kuu katika Zaburi 1 na Mathayo 9:35-38. Andika mawazo saidizi ya kithiolojia kama jinsi ambavyo ungewapa watu.
73
Somo la 13.
KKuuwwaaffiikkiirriiaa WWaattuu..
Katika upande mmoja, mjumbe wa Mungu atashughulika kwa makini sana na neno la Mungu lililoandikwa. Na katika upande mwingine, atajitahidi kuwaelewa kwa makini watu wanaousikiliza ujumbe wake. Mara nyingi, Mtumishi wa Mungu atamtumikia Mungu kati ya watu watu wa jamii yake. Atawaelewa kwa sababu ametoka kwao. Lakini Mungu amewaita werngine kwenda kwa watu wa lugha na mila tofauti na zao. Hivyo itambidi ajifunze na ayaelewe mawazo yao na desturi zao.
Kwa maana moja, watu wote mahali popote wanafanana. Mungu aliwaumba wote. Wote wameanguka katika dhambi. Wote wanamuhitaji mwokozi. Lakini kwa maana nyingine, watu wote ni tofauti, wanazungumza sauti tofauti, wanahusiana kwa njia tofauti, wanafuatisha historia zao kwa usimulizi ulio tofauti tofauti, wanaabudu miungu tofauti. Hivyo ,mjumbe wa Mungu anajua kuwa watu sehemu wa mahali popote wako tofauti na pia wanafanana.
Kitu cha kuangalia Mjumbe.
Somo letu hasa katika kitabu hiki limekuwa juu ya kuelewa kifungu cha maandiko. Tunataka kujua juu ya maana ya mwandishi wa awali. Kwa hivyo, tunasoma maneno yake, sentensi zake, picha zake na hadithi zake. Tunafanya hivi ili kugundua mawazo ya kithiolojia katika maneno yake na tutumie maneno yetu ili tuyafanye yaeleweke zaidi kwa watu. Tunasoma ujumbe wa mwandishi wa kifungu kwa kizazi chake na tunachukua humo ujumbe wa Mungu kwa vizazi
Somo la 13
Kama jinsi ambavyo mjumbe wa Mungu anavyolisoma neno lililoandikwa kwa umakini, atawasoma pia watu watakaoenda kulisikiliza.
Kuandaa Ujumbe. Chagua kifungu. Nakili kifungu Maneno ya kitendo. Maneno ya muhimu Mambo yaliyochunguzwa Viini vya Biblia. Wazo kuu. Kiini cha mpaka. Mawazo saidizi. Pointi Kuu. Watu Picha za maneno. Kusimulia Hadithi. Matumizi Kukusudia kwa imani Kuelezea.
74
vyote. Lengo letu limekuwa juu ya kifungu juu ya kifungu katika maelezo yake yote.
Muhubiri ni lazima awaangalie watu ambao watakwenda kusikiliza ujumbe wake. Kwa upande mmoja ameshikilia Biblia yake, Neno la Mungu lililoandikwa. Na kwa upande mwingine anaenda kugusa watu ambao wanahitaji kusikia ujumbe wa Mungu. Mjumbe wa Mungu ni msemaji wao kwa ufalme wa Mungu. Ni mleta habari ya neeme ya Mungu katika Kristo. Kama vile ambavyo mjumbe wa Mungu anakisoma kifungu kilichoandikwa katka maelezo yake yote, vivyo hivyo atawasoma watu wake pia. Anajua kwamba watausikia ujumbe wake ikiwa tu atazungumza kwa namna yao. Ni lazima atumie lugha yao. Ni lazima afanane na desturi zao. Ni lazima ajue historia yao. Ni lazima aunganishwe na wao katika namna ya jinsi wanavyoishi maisha yao. Ili azungumze nao kwa njia hii, itambidi awesome watu hao kama jinsi anavyokisoma kifungu. Unafikiri Moyo wa Mungu unakuwa wapi wakati mjumbe wake anapozungumza na watu? Roho Mtakatifu anafanya kazi katika kila kitu kuhusu ujumbe. Lakini kwa hakika moyo wake uko kwa watu ambao Kristo aliwafia. Mchungaji mwema mara nyingi yuko makini kwa kondoo wake. Ikiwa Roho Mtakatifu anawaangalia watu, Mjumbe wa Mungu ni lazima afikiri juu ya watu. Hata kabla hajanza masomo yake ya kifungu, mjumbe wa Mungu anayomahitaji ya watu katika mawazo yake. Anaposoma hawezi kusaidia kufikiri juu ya wasikilizaji atakaokutana nao kupitia ujumbe huu. Anapopanga maneno yake, atakuwa anaziona nyuso za watu katika mawazo yake. Kama vile ambavyo Moyo wa Mungu uko kwa watu, hivyo ndivyo ulivyo moyo wa Mjumbe.
Kuwasoma Watu.
Ikiwa mjumbe wa Mungu anafanya kazi na watu wa nchi yake, basi atakuwa anawafahamu vizuri. Hata hivyo bado atahitaji kujifunza juu ya mitazamo yao na ufahamu wao ama uzoevu wao, atahitaji
Kwa mkono mmoja anashikilia biblia yake,Neno la Mungu lililoandikwa.Kwa mkono mwingine, anatoka kuwagusa watu wanaohitaji kusikia ujumbe wa Mungu.Mjumbe wa Mungu ni msemaji wao kwa ufalme wa Mungu.
75
kugundua ni kwa kiwango gani wana utayari wa kumpokea Mungu na neno lake.
Ikiwa mjumbe wa Mungu ataitwa kuhu dumu kwa watu ambao ni tofauti na watu wa nchi yake, atahitaji kujifunza hali ya watu hao kwa makini sana. Wanaweza wakawa na desturi za tofauti, miiko na historia tofauti. Kadiri anavyowaelewa watu hawa ndivyo jinsi ambavyo atakuwa na uwezo wa kuueleza ukweli wa Mungu kwao.
Jifunze mitazamo yao ya kidini: Ikiwa unahubiri ujumbe wa Mungu, utatia changamoto mitazamo ya kidini ya watu. Itakuwa ni muhimu sana kwako kuelewa dini yao, hasa ikiwa hawamwamini Kristo. Utaupanga ujumbe wako kwa umakini ili uweze kupata upenyo katika mawazo yao kwa ajili ya ukweli wa Mungu.
Jifunze Lugha Yao: Lugha ya watu wowote wale itaeleza kwa nini wanaishi vile wanavyoishi vile wanavyofanya. Sikiliza kwa makini mambo wanayoyasema. Jifunze maneno yao. Chunguza jinsi vijana wanavyozungumza na wazee na jinsi gani wanaume na wanawake wanazungumza wao kwa wao. Jifunze maneno maalum ambayo ni viunganishi vya lugha katika kabila.
Jifunze hali yao ya kiuchumi:. Ni aina gain ya kazi watu wanayoifanya. Je kwa ujumla watu ni wachapa kazi (Wanafanya kazi kwa bidii) na wanajitegemea? Au wanasubiri msaada kutoka kwa mtu mwingine. Unapopanga ujumbe wako, utahitaji kuzungumza nao kulingana na hali zao za kiuchumi. Utahitaji kutumia picha inayofahamika katika kazi zao.
Jifunze desturi zao za kijamii: Historia ya kimila na kiutamaduni, itachangia sana vile ambavyo watu watausikia ujumbe wako. Eneo la muhimu sana katika mila yoyote ni maisha ya familia. Wajibu wa wanaume na wanawake unatofautiana katika desturi tofauti. Jinsi ambavyo wazee wanatendewa ni muhimu sana. Angalia pia desturi za ndoa, sherehe za wakati ambapo mototu anakomaa au avanabalehe, na tamaduni za kuwaheshimu wafu.
“Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote; na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa sababu yeye aliyajua yaliyomo ndani ya mwanadamu.”
Yohana 2:24, 25
76
Jifunze maisha yao ya Kimaadili Nyakati zingine maisha ya watu ya kimaadili yanaweza kuwa na mambo ama mafundisho mazuri ambayo unaweza kuyaendeleza kwa kuwatia moyo na kuwasifia. Makundi mengi ya watu wana kanuni madhubuti kuhusu wizi na uaminifu katika ndoa. Wengine hawana. Unaweza kusema neno zuri la kusifia kuhusu baadhi ya mambo yao mazuri ya kimaadili. Lakini utapaswa kuwapa kanuni zingine kutoka katika neno la Mungu katika maeneo mengine ya maadili yao. Jifunze upokeaji wao wa neno la Mungu:. Utayari wa watu katika neno la Mungu unaweza kutofautiana kwa sababu ya hali zao za kimaisha. Mara nyingi wakimbizi huwa wanautayari kuliko wafanyabiashara matajiri. Wale ambao wamekuwa na utaratibu wa kujishughulisha sana na kufikilia juu ya elimu ya kidunia utayari wao huwa ni mdogo kuliko wale ambao wamezoea mambo ya dini. Utahitaji kuzielewa hali hizi unapoandaa jumbe zako.
Mawazo ya Kifungu na Mahitaji.
Changamoto ya mjumbe wa Mungu ni kuuleta ujumbe wa Mungu usiobadilika kutoka kwa maandiko na kuwafikia wasikilizaji fulani ambao atawakabili wakati anapounena ujumbe huo. Ujumbe wake wapata kuwa daraja ya ukweli wa Mungu kwa watu. Unafanyika kuwa sauti kwa ufunuo wa Mungu kwa watu. Mtumishi wa Mungu ni lazima awe mwaminifu kwa maandiko na kwa watu. Kila wazo la biblia linalingana na hititaji la mwanadamu. Kila mtu anavutiwa kulingana na matatizo na mahitaji yake binafsi.Ujumbe wowoete unaozumgumbia haja hizo utapata kusiki lizwa. Hitaji lolote la mwanadamu linaweza kuambatanishwa na ahadi ya neema katika Maandiko. Mjumbe wa Mungu anaweza kuunganisha mawazo ya kibiblia na mahitaji ya wasikilizaji wake.
Ukihubiri “Ni lazima uzaliwe mara ya pili” kutoka katika Yohana 3, unajua kwamba watu wanahitaji mwanzo huu mpaya na Mungu. Wamekufa kiroho. Wako nje ya ufalme wa jamaa ya Mungu. Hawazihisi kazi za Roho katika maisha yao. Mahitaji haya ya kiroho
Hitaji lolote la binadamu, linaweza kuangaliwa katika ahadi ya neeme iliyoko katika maandiko.Mjumbe wa Mungu anaweza kuunganisha mawazo ya Biblia na mahitaji ya wasikilizaji wake.
Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji.
Mathayo 9:36
77
yanasababisha matatizo binafsi na maumivu ambayo yanaweza kuwa sehemu ya mawasiliano ya kuanzia ya muhubiri.
Unaweza kuhubiri kutoka katika Zaburi 1. Hapa mtu wa Mungu anayakataa mashauri ya wasio wa Mungu. Watu wanasikiliza kupita kiasi watu wasiokuwa wa Mungu. Hawajui wapi pa kwenda. Waambie juu ya mtu wa Mungu: “Hufurahishwa na sheria ya Bwana, na huitafakari mchana na usiku”. Waoneshe jinsi ambavyo watakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya maji na wenye matunda.
Unaweza kuhubiri kutoka 1Yohana 1:9 kuhusu msamaha. Unajua watu wanahukumu kwa ajili ya dhambi zao. Unajua wnajutia maisha ya uchaguzi usio sahihi. Unganisha maumivu yao na ahadi ya Mungu juu ya msamaha. Waonyeshe jinsi Yesu alivyotoa baraka hii ya ajabu kupitia damu yake iliyomwagika (1Yohana 1:7). Waelezee kwamba wanahitaji kukiri tu, ili kupokea msamaha wa Mungu katika Kristo.
Kuwaombea Watu.
Mawazo ya muhimu sana juu ya watu yatakuwa pale unapowaombea. Mjumbe wa Mungu ni lazima awe na nguvu ya Mungu anapolitangaza neno la Mungu.
Jiombee mwenyewe kama mjumbe wa Mungu . Mwambie Mungu ausafishe moyo wako wa dhambi (1 Yohana 1:7). Mwambie akujaze kwa Roho ( Wagalatia 5:16). Mwambie akufunulie siri za maandiko ( Yohana 16:13). Mwambie awashe moto wa shauku ya ujumbe ( 1Wakorintho 9:16). Mwambie akupe maneno mazuri ya kuwasaidia watu waelewe ( 1Wakorintho 2:4). Mwambie akufanye jasiri kwa kweli yake ( Matendo 4:29).
Kiri nguvu ya uweza wa neno la Mungu. Thibitisha kwamba neno la Mungu “Li hai na lina nguvu, lenye makali kuliko upanga ukatao kuwili” (Waebrania 4:12). Mshukuru Mungu kwamba neno lake halitarudi bure, bali litatimiza yale aliyokusudia (Isaya 55:11). Thibitisha kwamba neno la Mungu lafaa kwa mafundisho, kwa kuonya, kwa kuongoza na kwa kuadabisha katika haki( 2Timotheo 3:16).
“Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jisi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo.”
Waefeso 1:18
78
Omba watu wawe wazi katika neno la Mungu. Mwambie Mungu awawezeshe kulisikia kwa furaha ( Marko 6:20). Omba Roho Mtakatifu aweze kuteka upofu wao wa Kiroho ( 2 wakorintho 4: 3-6) Omba macho yao yafunguke ili waweze kugeuka na kutoka katika giza na kuelekea katika nuru (Matendo 26:18). Omba kwamba mioyo yao iwe kama udongo mzuri ambao hupokea neno na kuzaa matunda, kwamba wawe na “Masikio ya kusikia” kile Mungu anachokisema (Mathayo 13:8,9) Omba kwamba Roho Mtakatifu aweze kuwashawishi wasioamini juu ya dhambi, juu ya haki na juu ya hukumu ( Yohana 16:8). Kili kuondolewa kwa ngome zozote dhidi ya elimu ya Mungu ( 2Wakorintho 10:4-5) Omba Kristo ainuliwe katika Ujumbe.. Thibitisha Ubwana wa Kristo katika maisha ya watu (Wafilipi 2:9-11). Omba roho Matakatifu amfunue Kristo kwa wasikilizaji wako (Yohana 15:26). Omba kwamba katika ujumbe wa msalaba, Kristo ainuliwe juu na kuwavuta watu kwake. (Yohana 12:32). Omba kwamba Roho amtukuze yesu katika ujumbe ( Yohana 16:14).
Mazoezi ya Somo
1. Rudia mawazo makuu katika somo hili: Mahali popote watu wafanana sana kama binadamu na wako tofauti sana katika mila zao. Mjumbe wa Mungu atakuwa makini mahali ambapo moyo wa Mungu upo, pamoja na watu. Mjumbe wa Mungu atajifunza kusoma kadori awezavyo kuhusu watu anaowahudumia. Mjumbe wa Mungu ataunganisha ukweli wa Biblia na mahitaji ya watu. Mjumbe wa Mungu atawaombea watu.
2. Chunguza tena vifungu ambavyo tumekuwa tukivisoma. Anagalia mawazo ya kithiolojia na jaribu kuyaunganisha kila moja na mahitaji ya watu wako. Fikiri jinsi ambavyo utayaelezea mahitaji hayo.
“Usiliondoe neno la kweli kinywani mwangu kamwe, Maana nimezingojea hukumu zako. Nami nitaitii sheria yako daima, Naam, milele na milele. Nami nitakwenda panapo nafasi, kwa kuwa nimejifunza mausia yako.”
Zaburi 119:43-45
79
Somo la 14
KKuutteennggeenneezzaa PPiicchhaa
zzaa MMaanneennoo..
Unapopanga mahubiri yako, utahitaji kuhubiri na kufundisha kama Yesu.Utafikiri juu ya njia mbalimbali ambazo zitafanya mawazo ya Biblia yaeleweke vizuri kwa watu kutokana na uzoefu wao wa maisha yao ya kila siku.Kwa hivyo mawazo ya kifungu na mawazo saidizi hayawezi yakasimama yenyewe tu kama ujumbe wako. Yako mambo mengine ambayo utahitaji kupanga.
Tutamfuata Yesu kama mfano wetu wa jinsi ya kutumia picha za maneno kufundisha ukweli wa Mungu. Unapofundisha au kuhubiri, hakikisha unatumia vielelezo vilivyoko katika kifungu. Usivipitie tu, bali chukua picha kamili kwa maneno yako mwenyewe. Wawezeshe watu kuona vielelezo hivyo katika mawazo yao.
Mawazo na Uzowefu.
Tumezungumza juu ya mawazo yanayoelezewa katika kifungu. Ukweli huu kutoka kwa Mungu, unamfaa kila mtu, katika kila kizazi, mawazo haya bado ni ya kweli. Katika kila kabila, mawazo haya bado yanaweza kufanya kazi. Mtu yeyote katika Dunia hii anayesikia mawazo haya anaweza kuona kwamba yanamfaa. Lakini mawazo haya wakati mwingine yanakuwa ni magumu kueleweka. Yanaonekana kuwa juu na mbali na shughuli za kila siku za maisha.
Kwa kila wazo kutoka katika kifungu utazungumza juu ya mazoea ya kila siku, ili kwamba watu wandoke na ujumbe ndani ya mioyo yao. Mawazo ya Mungu ni lazima yaelezwe katika namna ya mazoea ya kila siku ya binadamu.
Somo la 14
Mawazo ya kibiblia yataeleweka kwa watu ikiwa tu, yatawasilishwa katika lugha ya waliyoyazoea.
Kuandaa Ujumbe Chagua kifungu Nakili kifungu Maneno ya kitendo Maneno ya muhimu. Yaliyochunguzwa Viini vya Biblia Wazo kuu Kiini cha mpaka Mawazo saidizi Pointi kuu. Watu. Picha za maneno. Kusimulia hadithi Matumizi Kukusudia kwa Imani. Kuelelzea.
80
Watu wanaishi maisha yao kila siku kama mazoea si kama mawazo. Wanaelewa kazi, kucheza, familia, marafiki, kula na kulala. Lakini pia wanakutana na woga, furaha, huzuni na kukata tamaa. Haya ndiyo mazoea ya maisha ya kiila siku ya maisha. Ikiwa tutazungumza nao kuhusu mawazo tu, tunaweza tukakosa fikra zao. Mawazo yetu yote ni lazima tuyaeleze katika hali ya mazoea ya kila siku ya maisha.
In the text we have been studying, Jesus explained the new life of a believer in terms of being “born again.” He used a familiar experience of life to picture how a person has new life in Christ. Everyone understands about “birth.” They can grasp “spiritual birth” or “new birth” as well. Mjumbe wa Mungu ni lazima aoanishe picha za maneno yake na watu anaozungumza nao. Ikiwa anazungumza na watu skijijini, atatumia mifano ya maisha ya kila siku ya kijijini. Vielelezo vingi vya Yesu vinalenga mazoea ya watu wa kila sehemu. Tutakapokuwa tunavipitia, utona kwamba watu wengi wanaweza wakavielewa maana yake. Unaposoma Biblia yako, chunguza Yesu alifundushaje. Mara zote alifungamanisha mawazo na maisha ya kila siku. Alizungumza juu ya upendo wa Mungu kwa watu wote kwa kusimulia hadithi ya kondoo mmoja aliyepotea. Alizungumza juu ya imani mpya katika dini ya zamani kwa kuwaonya juu ya kuweka Divai mpya katika vyombo vya zamani. Alizungumza juu ya upokeaji wa neno la Mungu kwa watu kwa kueleza juu ya mpanzi aliyepanda mbegu katika udongo tofauti tofauti.
Picha za maeno alizozitumia Yesu.
Hebu tuangalie baadhi ya vielelezo vya Yesu. Tunapoendelea kufanya, fikiri juu ya jinsi gain ambavyo utapanua picha za maneno yake kuwasaidia watu wako kuona wazo katika akili zao. Fikiri pia jinsi gain unavyoweza kupanga vielelezo hivyo hivyo kutokana na mazoea yako ya kila siku. Baadhi ya picha za maneno za Yesu ni hadithi. Hizi
Watu wanaishi kulingana na mazoea, si kama mawzo. Ikiwa tutazungumza nao kama mawazo. Tunaweza tukazikosa fikra zao. Mawazo yetu yote ni lazima yawasilishwe kwa nama ya mazoea.
81
tutaziaangalia katika somo lijalo. Lakini kwa sasa tutashughulika sana na vielelezo rahisi ambavyo havielezei hadithi yoyote.
Picha nyingi za maneno za Yesu zimetoka katika namna mbalimbali za maisha ambazo watu wanazijua. Unapopanga picha za maneno za ujumbe wako, fikiri juu ya Mazoea haya ya kila siku ya maisha.
Mambo ya Nyumbani. Maisha ya kila siku ya nyumbani yalimpa Yesu picha nyingi za maneno zinazofahamika:taa inayotoa mwanga(Mathayo 6:22, 23); Kushona kiraka katika vazi kuu kuu.(Mathayo 9:16); Divai mpya katika viriba vikuu kuu(Mathayo 9:17); Mtu mwenye nguvu ailindaye nyumba yake.(Mathayo 12:29); Mbwa wa kufugwa.(Mathayo 15:26, 27); Kuchuja Mmbu(Mathayo 23:24); Kuku na vifaranga(Mathayo 23:37); Tundu la sindano(Luka 18:25); Kupepeta ngano.(Luka 22:31).
Kula na Kunywa. Kila mtu anaelewa kula na kunywa, Kwa hivyo Yesu aliitumia sana picha hii: Mtu hataishi kwa mkate tu (Mathayo 4:4); njaa na kiu (Mathayo 5:6); chakula cha watoto (Mathayo 15:26): kutiwa chachu kwa mkate (Mathayo 16:6,11,12);kunywea kikombe (Mathayo 20:22,23); Kuonja (Marko 9:1); kunywa maji ( Yohana 4:13-15); kutambua majira (Marko 9:46); chakula kiharibikacho (Yohana 6:27); mkate wa uzima (Yohana 6:32-35); kula na kunywa (Yohana 6:52-59)
Kilimo:. Yesu alitumia mifano mingi sana ya picha kutoka katika kilimo: Kukusanya matunda(Mathayo 7:16-20);Mavuno mengi(Mathayo 9:37, 38);Nira ya maksai(Mathayo 11:29); Miti na matunda(Mathayo 12:33);Watenda kazi wachache kwa ajili ya mavuno(Luka 10:2); mmoja anapanda na mwingine anavuna(Yohana 4:35-38); Jinsi mbegu inavyoota(Yohana 12:24); Mzabibu na matawi(Yohana 15:1-8).
Mchungaji na Kondoo. Moja kati ya picha za maneno nyingi na zinazofahamika sana ilikuwa ni kondoo na uchungaji wa kondoo: Mbwa mwitu katika vazi la kondoo ( Mathayo 7:6); Kondoo wa Israeli aliyepotea(Mathayo 10:6): Kondoo kati ya mbwa mwitu (Mathayo
“Kwa sababu mambo yake yasiyooonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake…..”
Warumi 1:20
82
10:16); zizi la kondoo, mlinzi wa kondoo na mchungaji (Yohana 10:1); Kondoo wanaomfuata mchungaji ( Yohana 10:4,5); sauti ya mchungaji (Yohana 10:3,27); mwizi, mtu wa mshahara na mchungaji (Yohana 10:10-14); kulisha na kutunza kondoo (Yohana 21:15-17).
Nuru na Giza . watu wamezoea sana hali ya Nuru na giza katika mchana na usiku. Waliweza kuelewa Yesu alipotumia hali hii: Nuru ndani yenu (Mathayo 6:23); Nuru huonesha kile kilichoko katika giza (Luka 12:2,3); Nuru, kutembea katika giza (Yohana 8:12); kujikwa usiku (Yohana 11:9,10); Nuru, kuishi katika giza (Yohana 12:46). Ulimwengu wa asili. Uumbaji wa Mungu ulisaidia kutoa mifano ya Yesu: Ndege wa angani (Mathayo 6:26);Maua ya shambani (Mathayo 6:28, 29); majani ya shambani (Mathayo 6:30); mbwa na nguruwe (Mathayo 7:6); mbweha na ndege (Mathayo 8:20); wajanja kama nyoka na wapole kama huwa (Mathayo 10:16); mashomoro (Mathayo 10:29-31); unyasi nyikani (Mathayo 11:7); kutabiri hali ya hewa(Mathayo 16:2, 3); nyoka na majoka (Mathayo 23:33); kumulika kwa umeme (Mathayo 24:27); Tai katika mzoga (Mathayo 24:28);jua, mwezi na nyota (Mathayo 24:29); mawingu (Mathayo 24:30); upepo (Yohana 3:8). Mwili wa Binadamu . Tunafahamu kila kitu kuhusu miili yetu. Yesu aliutumia mfano huu unaofahamika sana: Jicho linalokosesha(Mathayo 5:29); mkono usababishao dhambi (Mathayo 5:30); jicho zuri au baya(Mathayo 6:22, 23); kimo cha mwili. (Mathayo 6:27); kibanzi katika jicho (Mathayo 7:1-5); afya na ugonjwa (Mathayo 9:12); nywele za vichwa vyenu (Mathayo 10:30); mkono au mguu (Mathayo 18:8); Mifupa ya mtu aliyekufa (Mathayo 23:27); mwili na damu (Mathayo 26:26-28). Mbali na namna hizi za maisha, Yesu alitumia mingine pia. Alitumia lugha za vielelezo kuhusu mabwana na watumishi (Mathayo 6:24). Alizungumzia juu maisha ya familia (Mathayo 7:9, 10), watoto(Mathayo 11:16, 17), desturi za harusi (Mathayo 9:15), maisha ya vita (Mathayo 10:34), siasa (Mathayo 12:25),wezi na wanyang’anyi (Mathayo 12:29), milango na funguo (Mathayo 16:19; Luka 13:24, 25).
Mambo ya maisha ya kawaida kwa picha za maneno.
Mambo ya nyumbani
Kula na kunywa.
Kilimo
Mchungaji na kondoo
Nuru na Giza.
Ulimwengu wa asili.
Mwili wa binadamu.
Watumishi na Mabwana.
Maisha ya familia.
Watoto.
Desturi za Ndoa.
Maisha ya vita.
Siasa.
Wezi na wanyang’anyi.
Milango na Funguo.
83
Ni ngumu kutenganisha picha hizi za maneno na ile mifano ya hadithi za mafumbo ambayo Yesu aliisema. Katika somo linalofuata tutaziangalia hadithi hizo za mafumbo, zinasimulia hadithi, wakati ambapo mambo yaliyoelezwa hapo ni mifano tu.
Jinsi ya kupanga picha za maneno.
Kutumia picha za maneno ni muhimu sana katika ujumbe wako, kama hautatumia picha( pamoja na maneno) na kusimulia hadithi katika mahubiri yako, watu hawatasikiliza, na pia hawatajifunza. Unaweza kuwafundisha mawazo yote ya biblia kwa njia ya picha zinazofahamika sana ambazo zitawasaidia kujua unamaanisha nini. Unapofanya hivi utakuwa unahubiri na kufundisha kama yesu
Ngoja nipendekeze hatua unazoweza kuchukua ili kupanga picha za maneno yako kwa ajili ya masomo ya Biblia na mahubiri.
1. Kwanza eleza wazo kutoka katika kifungu kwa kueleweka na kwa urahisi kadiri uwezavyo. Moja kati ya wazo katika Yohana 3:1-8 lilikuwa, “ Kuzaliwa upya ni muhimu ili kuuona ufalme wa Mungu”. Maneno ya ufunguo katika sentensi hiyo ni “Muhimu kuuona”
2. Fikiri juu ya mambo yakawaida yaliyozoeleka ambayo ni “muhimu ili kuona”. Tunapaswa kuwa na nini ili tuweze “kuona?” Andika baadhi mambo uliyoyaona au unayoyafahamu ambayo umekuwa nayo.
3. Angalia makundi ya picha za maneno aliyoyatumia Yesu. Kuna mambo ya nyumbani, kilimo, na mengine. Andika ni jinsi gani ilivyo “muhimu kuona” inavyoweza kuonekana katika kila kundi. Kwa mfano, Taa inaweza kuwa muhimu kwa kuona katika nyumba yenye giza. Au, jicho makini la mchungaji ni muhimu katika kumuona mbwa mwitu anayenyatia kondoo wake.
4. Elezea picha ya maneno ili kwamba watu waweze “kuona” uhalisia katika mawazo yao. Waweze “kuona” nyumba yenye giza na mtu akiwasha taa. Waweze “kuona” kondoo wenye hofu mchungaji mlinzi na mbwa mwitu anyemeleaye. Kufanya hivi unatakiwa kuwa makini sana na mwenye maneno mazuri yanayoweza kueleza vizuri.
Unaweza kuwafundisha mawazo yote ya Biblia kwa namna ya picha zinazofahamika ambazo zitawasaidia kujua unamaanisha nini. Unapofanya hivi utakuwa unahubiri na kufundisha kama Yesu.
84
5. Unganisha picha ya neno nawazo la Biblia. “ Kama vile jinsi ambavyo taa inavyoonesha kilichoko katika chumba chenye giza, ndivyo jinsi ambavyo kuzaliwa mara ya pili hufungua macho yetu katika ufalme wa Mungu”
Nyakati zingine unaweza kutumia mifano inayoeleweka kwa watu hata kama hawajakutana nayo katika maisha yao binafsi.Hii ni sawa kabisa unapotumia mifano iliyotolewa katika maandiko ya kifungu. Labda watu wanaweza kuwa hawafahamu kuhusu kondoo, lakini kwasababu Yesu alitumia mfano huo, unaweza kutumia pia. Hata hivyo hakikisha unaufafanua vizuri. Piacha zingine za maneno zinafahamika sana kiasi kwamba kila mmoja anazielewa. Yesu alitumia jina “Baba” kumaanisha Mungu. Haijalishi watu wanaishi wapi, wanajua hilo liamaanisha nini. Hata kama mtu hamjui baba yake, anafahamu baba yukoje. Anajua baba mbaya na baba mzuri anakuaje.
Mazoezi ya Somo.
1. Rudia mawazo makuu ya somo: Kila wazo katika kila ujumbe linatakiwa liwakilishwe katika hali ya mazoea ili kwamba watu waweze kulielewa. Watu huishi maisha yao kila siku kama mazoea, si kama mawazo. Mfano ni picha ya neno lilnalolinganisha kitu kimja na kingine. Picha za maneno ya Yesu zilitoka katika namna tofauti tofauti za maisha ambazo watu walizijua.
2. Chagua baadhi ya vifungu vya maneno vilivyoorodheshwa katika somo hili vyenye picha cha maneno ya Yesu. Je unaweza kutumia picha hizo kwa wasikilizaji wako?
3. Buni picha yako ya maneno kutoka katika kila kipengele Alichokitumia Yesu.
“Jitahidi kujionesha kwamba umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.”
2 Timotheo 2:15
85
Somo la 15
KKuussiimmuulliiaa hhaaddiitthhii ZZiilleennggaazzoo kkwweellii..
Kuulezea vizuri ukweli wa kithiolojia katika kifungu ndio mwanzo kwa ujumbe wako. Kama jinsi tulivyojifunza katika somo lililopita, Mjumbe wa Mungu ni lazima ayageuze mawazo hayo katika lugha ya mazoea ya kila siku.Watu wanaishi maisha yao duniani kutokana na mazoea yao ya maisha. Wanaelewa mazoea. Kwa hivyo, ni lazima tuyaeleze mawazo katika namna ya mazoea ya kawaida.
Tunafuata tena mfano wa Yesu. Mara zote aliwapa wasikilizaji wake kanuni na sheria. Lakini pia aliwasimulia hadithi kufafanua ukweli huo wa kiroho. Mjumbe wa Mungu anaweza kufanya hivyo pia. Anaweza akasimulia hadithi za Biblia kwa ufasaha. Lakini pia anaweza kusimulia hadithi za hivi sasa ambazo zinabeba maana ya ukweli wa Mungu. Katika somo hili tutaangalia nguvu ya hadithi na jinsi gain ya kuzitumia katika ujumbe wa Biblia.
Uwezo wa Hadithi.
Kusimulia hadithi ni sehemu ya kawaida kabisa ya maisha karibu ya kila mila. Tangu zamani sana, watu wamekuwa wakikaa kuuzunguka moto na kusimulia hadithi za mababa. Leo hii, katika makabila mengi, watu bado wanaendelea kukaa wakiuzunguka moto na kusimulia hadithi zile zile. Katika mila zingine, wanaume hukaa mbele ya moto katika mkutano, au katika maboma ya kuvulia samaki, au katika mikusanyiko ya familia na kusimulia hadithi ambazo zinatafsili maisha kwa kundi.
Wanawake pia ni wasimuliaji wa hadithi. Ikiwa mila haiwajumlishi katika duara la wazee, wanasimuliana hadithi zao katika shughuli zao za ushonaji. Au wanakusanyika kwa ajili ya chai na
Somo la 15
Kusimulia hadithi kuelezea mawazo ya mahubiri, kutaufanya ukweli wa Biblia kuwa mzuri zaidi na unaoeleweka.
Kuandaa Ujumbe. Chagua kifungu Nakiri kifungu Maneno ya kitendo. Maneno ya muhimu. Vilivyochunguzwa. Viini vya Biblia. Wao kuu. Kiini cha mpaka. Mawazo saidizi. Pointi kuu. Watu Picha za maneno. Kusimulia hadithi. Matumizi. Kukusuduia kwa Imani. Kuelezea.
86
kutafakatri matukio ya maisha na yana maana gani. Wanawaeleza watoto nini kilitokea kabla hawajazaliwa. Wanaeleza maana ya majina yao na familia na watu. Nyakati zingine hadithi tunazosimulia zinaweza kuwa ni kwa ajili ya kuburudisha tu. Nyakati zingine ni kwa ajili ya kuelimisha. Nyakati zingine ni kwa ajili ya mazungumzo tu. Hata hivyo, mara kwa mara, Hadithi tunazosimulia zimebeba maana ya maisha. Zinakipa kizazi kipya hali ya kujitambua na kujua watokako.
Sehemu kubwa ya biblia iko katika namna ya hadithi. Matendo makuu ya nguvu za Mungu yanaelezwa katika hadithi. Matendo ya waamini wa kale yako katika hadithi. Ukweli wa muhimu kuliko wote, Injili ya Yesu Kristo, uko katika namna ya hadithi. Mungu allikusudia kuufanya ukweli wake ujulikane kwa watu katika njia ambayo wataikumbuka vizuri. Alitupa Hadithi.
Hadithi katika Ujumbe Wako.
Muhubiri wa neno la Mungu mwenye hekima atakuwa pia ni msimuliaji wa hadithi. Atayafanya matendo ya nguvu ya Mungu kuwa hai tena kwa wasikilizaji wake. Atawaeleza juu ya mashujaa wa imani wa zamani kwa furaha na majonzi yao, ushindi wao na kushindwa kwao, Imani zao na kuogopa kwako. Katika hadithi zote hizi mjumbe wa Mungu mwaminifu atawakilisha ukweli mkuu wa nguvu za neno la Mungu katika njia ya kweli na ya kusisimua. mwenye busara Mjumbe wa Mungu ataeleza pia hadithi za watu wake. Atawakilisha kwao matukio na hali za wakati wao kama jinsi zinavyonekana kwa macho ya imani. Ukweli mkuu wa Biblia ni wa kweli kwa vizazi vyote. Mjumbe wa Mungu atauweka ukweli huo katika matukio na hali za kizazi chake na kuwaonesha watu jinsi Mungu anavyozungumza nao.
Watu hawajui mambo yote ya hadithi zao. Wanazikosa sehemu za muhimu sana. Lakini mjumbe wa Mungu atawapatia mambo haya yanayokosekana. Atawaeleza kutoka katika neno la Mungu lililoandikwa jinsi gain yalivyokuja kuwa katika dunia hii. Atawaeleza makusudi ya Mungu katika maisha yao. Atawaeleza juu ya maisha ya
Muhubiri wa neno la Mungu mwenye busara, atakuwa msimuliaji pia wa hadithi. Atayafanya matendo makuu ya Mungu yawe hai tena kwa wasikilizaji wake.
87
baada ya kufa. Atawaeleza jinsi ya kuzishinda nguvu za uovu ndani na nje yao.
Kila mtu anayatafsiri maisha yake kulingana na jinsi hadithi zinaelezea kuwa yeye ni nani. Mjumbe wa Mungu anaweza kumwambia mwamini hadithi yake mwenyewe kama kiumbe kipya ndani ya Kristo. Yeye ni sehemu ya jamii mpya ya watu iliyookoka. Yeye ni sehemu ya familia mpya ya Imani. Wajibu wake katika Dunia umebadilika. Kuyaelewa yote haya, anahitaji kusikia hadithi kuu za imani kutoka katika Biblia. Anahitaji pia kusikia hadithi za mafumbo zilizoandaliwa katika kizazi hiki zinazo fafanua neno la Mungu.
Kwa mara nyingine, Yesu ni mfano wetu katika kutumia hadithi za mafumbo kuufanya ukweli wa Mungu ueleweke kwa Watu. Katika somo lililopita, tuliangalia picha nyingi za maneno ya Yesu kuona ni jinsi gani zilivyobeba ukweli wa kiroho katika picha za asilia. Mifano ya mafumbo ya Yesu ni picha za maneno ngumu sana ambazo zinasimulia hadithi. Katika matumizi ya Yesu ya hadithi za mafumbo, mjumbe wa Mungu anaweza kuona ni jinsi gain anaweza kutumia hadithi kufanya ujumbe wa Mungu ueleweke.
Kitu gain kinachofanya Hadithi nzuri?
Hadithi alizozisimulia Yesu kuelezea mawazo yake wakati wote zilikuwa ni za kweli katika maisha. Ziliwasilisha mambo yanayofahamika kwa watu. Zilikuwa zinaaminika. Wakati ambapo ukweli wa kufikilika tu, ungeweza kusahaulika kirahisi, hadithi hizi za mafumbo zilipata makao katika kumbukumbu za watu. Hadithi unazozitumia katika ujumbe wako zinaweza kuwa na ubora kama ule wa hadithi za mafumbo za Yesu.
Unaweza kusimulia hadithi katika ujumbe wako ambazo ni za kweli katika maisha. Hadithi za Agano la Kale na Jipya zinaonesha picha ya mambo ambayo tunayo leo. Wahusika katika Biblia ni watu halisi, wakati mwingine ni wenye hekima na wakati mwingine ni wapumbavu. Hadithi za mafumbo za Yesu zilikuwa pia ni za kweli katika maisha. Hebu fikiria juu ya habari ya mwana mpotevu, baba
Kila mmoja hutafsiri maisha yake mwenyewe kwa namna ambavyo hadithi zinavyoelezea yeye ni nani. Mjumbe wa Mungu ni lazima amwambie habari yake mpya kama kiumbe kipya ndani ya Kristo.
88
aliyesubiri na kaka mkubwa (Luka 15:11-32). Tunawaelewa. Unaweza kusimulia hadithi za kizazi hiki ambazo ni za kweli pia katika maisha.
Hadithi za mafumbo za Yesu zinaelezea pia mambo yanayofahamika. Alielezea juu ya mpanzi aliyetoka kwenda kupanda mbegu zake shambani. (Mathayo 13:3-9, 18-22). Mbegu zilianguka katika udongo wa aina mablimbali na zikazaa matunda yanayotofautiana. Yesu alitoa mfano wa udongo wa aina mbalimbali kuonesha utofauti wa mioyo ya binadamu katika kupokea neno la Mungu. Wasikilizaji wake waliwahi kumuona mpanzi mara nyingi na wanafahamu mashamba. Unapowasimulia watu hadithi unaweza kuwaeleza pia mambo ambayo yanafahamika kwao. Hadithi za Yesu zilikuwa pia na mambo ynayoaminika. Hadithi ya Yesu ya kondoo aliyepotea (Mathayo 18:10-14) ilikuwa imebeba mambo yana yofahamika sana kwa wasikilizaji wake. Mchungaji anahesabu kondoo wake na angundua kuwa mmoja hayupo. kwa hivyo anamtafuta kila mahali. Na anapompata anafurahi sana. Hadithi zako zinaweza kueleza pia aina ya mambo ya changamoto ambayo watu wako waifahamu vizuri. Hadithi unayosimulia inaweza kuwa pia ni ya kukumbukwa. Yesu alisimulia juu ya bwana mmoja aliyepata mgeni ambaye hakumtarajia, lakini hakuwa na kitu cha kumlisha (Luka 11:5-8). Ni jambo la kusikitisha sana kutoweza kulisha mgeni wako. Kwa hivyo akamwamsha jirani yake na kumsisitiza amkopeshe mkate. Bwana huyu alikuwa na bidii sana, kama jinsi tunavyotakiwa kuwa katika maombi yetu. Wale waliosikia hadithi hii waliweza kuiona ikijifunua katika mawazo yao. Wasingeweza kuisahau kirahisi.
Mipaka ya Hadithi.
Hadithi zinaweza zikafaa sana katika kuelezea ukweli wa Biblia. Mungu amechagua kutumia hadithi kuwasilisha ujumbe wake kwa binadamu. Lakini mjumbe wa Mungu ni lazima awe makini sana, kwa sababu hadithi zina mipaka yake. Kusimulia tu hadithi inaweza isitoshe kama huduma ya kutangaza.
Hadithi nzuri
Kweli katika maisha.
Mambo yanayofahamika
Mambo yanayoaminika.
Inayokumbukwa.
89
Hadithi pasipo maana ya kithiolojia inayoeleweka inaweza isifae. Wahubiri wengine wanadhani kwamba hadithi za Biblia zinaweza kusimuliwa pasipo hata maelezo. Masimulizi mazuri ya vifungu bila shaka yananguvu. Na mara nyingi watu wanaweza wakaelewa wazo la kithiolojia pasipo hata ya maelezo. Mjumbe wa Mungu hapaswi kudhani tu kwamba watu wote wanaelewa. Atahakikisha kwamba hadithi zote za Biblia anazosimulia na mifano yake mwenyewe zinaeleweka katika maana zake.
Hadithi zinazobuniwa kuburudisha tu, mara nyingi zinabeba maana kidogo. Mjumbe wa Mungu anapenda kusikilizwa na watu anaowahubiria. Anapaswa kufanya kazi kuhakikisha kuwa kile anachokiwasilisha kinawapendeza. Lakini ni lazima awe makini juu ya kuridhika tu kwamba wanamsikiliza. Wahubiri wengine wanasimulia hadithi ambazo ni kama magari makubwa tu ambayo yako tupu, hayajabeba mzigo. Kuropoka kwao husikilizwa, lakini wanatoa msaada kidogo. Kama zilivyo hadithi za Yesu, Hadithi zetu pia ni lazima zibebe ukweli mzito wa Mungu.
Hadithi zilizo na maelezo yasiyo ya muhimu mara nyingi zinachanganya. Hadithi zinaweza kuwa ndefu sana na pia zikawa na maelezo mengi sana. Wahubiri wengine wanapenda sana kurefusha hadithi zao kwa maelezo ambayo si ya lazima sana katika pointi. Wasikilizaji huondolewa katika pointi kwa maelezo ya ziada. Kumbuka kwamba, hadithi ni kielelezo kumsaidia msikilizaji kulipata wazo la Biblia kiundani zaidi. Weka kichwani wazo hilo unaposimulia hadithi.
Sehemu kubwa ya Biblia haipo katika mfumo wa Hadithi. Kuzisimulia tena hadithi za Biblia ni njia nzuri ya kuhubiri, ikiwa tu maana inaeleweka. Lakini sehemu za Biblia kama vile amri, zaburi, unabii na barua haziko katika hali za hadithi. Mtindo wa uandishi wa Biblia umuongoze mjumbe. Ikiwa hakuna hadithi katika kifungu, haiwezi kufundishwa kama hadithi. Hata hivyo, hadithi zinaweza kusaidia kama Vielelezo.
Mjumbe wa Mungu anapenda kusikilizwa na anaowahubiri. Lakini ni lazima awe makini na kuridhishwa na usikilizwaji tu.
90
Hadithi kuu za Yesu.
Taa chini ya kikapu.- Math. 5:14-16 Wajenzi wenye busara na wapumbavu.—Math. 7:24-27 Mpanzi—Math. 13:3-9, 18-22 Ngano na Magugu—Math. 13:24-30, 36-43 Mbegu ya haladari—Math. 13:31, 32 Lulu ya thamani kubwa—Math. 13:45, 46 Nyavu ya kuvulia—Math. 13:47-50 Kondoo aliyepotea—Math. 18:10-14 Mtumwa asiyesamehe—Math. 18:21-25 Wafanya kazi katika shamba la mzabibu—Math.20:1-16 Watoto wawili—Math. 21:28-32 Wakulima waovu—Math. 21:33-40 Sherehe ya arusi—Math.22:2-14 Mtini—Math. 24:32, 33 Watumwa waaminifu na waovu—Math. 24:45-51 Wanawali wenye busara na wapumbavu—Math. 25-1-13
Vipawa—Math. 25:14-30 Kondoo na mbuzi—Math. 25:31-46 Kupanda mbegu—Marko 4:26-29 Watumwa wakeshao—Marko 13:33-37 Mkopeshaji wa pesa.—Luka 7:41-43 Msamalia mwema—Luka 10:30-37 Rafiki muhitaji—Luka 11:5-8 Tajiri mpumbavu—Luka 12:16-31 Mtini usiozaa—Luka 13:5-9 Kiti cha nyuma.—Luka 14:7-14 Karamu kubwa—Luka 14:16-24 Kujenga mnara—Luka 14:27-30 Mfalme wa Vita.—Luka 14:31-33 Shilingi iliyopotea—Luka 15:8-10 Mwana mpotevu.—Luka 15:11-32 Wakili mwenye busara—Luka 16:1-8 Lazaro na Tajiri.—Luka 16:19-31 Bwana na mtumwa—Luka 17:7-10 Mjane mwenye bidii—Luka 18:2-8 Mafarisayo na watoza ushuru.—Luka 18:10-14
Mazoezi ya Somo.
1. Rudia Mawazo makuu ya somo hili. Ili kueleweka, mawazo ya kithiolojia ni lazima yaelezewe katika namna ya mazoea ya halisi. Muhubiri wa neno la Mungu mwenye busara ni lazima awe msimuliaji wa hadithi pia. Hadithi unazozitumia katika ujumbe wako zinaweza kuwa na ubora kama ule wa hadithi za Yesu. Mjumbe wa Mungu ni lazima awe makini, kwa sababu hadithi zina mipaka yake.
2. Kufanyia mazoezi ujuzi katika somo hili, angalia katika kila hadithi kuu za Yesu. Panga jinsi ya kuzielezea katika njia ambayo ni halisi. Fikilia sasa ni jinsi gani unaweza kuvisha wazo la biblia katika hadithi mpya kwa kizazi hiki.
91
Lesson 16
MMwwiittoo wwaa KKuubbaaddiilliikkaa..
Swala msingi kuhusiana na ujumbe wa Mungu ni jinsi gani ya kuitikia. Wakati Petro alipohubiri katika Pentekoste, taarifa inasema, “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na Mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?” (Matendo 2:37). Hilo ndilo swali linalokusudiwa. Baada ya kusikia neno la Mungu limehubiriwa, Tufanye nini?
Hili ndilo swali la kufanyia kazi. Ukweli wa maandiko unahitaji mwitiokio. Lazima kitu kifanyike. Mjumbe wa Mungu atandaa sehemu ya mwitikio kama sehemu ya muhimu katika ujumbe wake kwa ajili ya kufanya kitu juu ya kweli ya Mungu. Tunapoangalia matumizi katika somo hili, tuta fuata tena mfano wa Yesu
Uhitaji wa matumizi.
Baadhi ya waalimu na wahubiri wa Biblia wanadhani matumizi maalum hayahitajiki kwa mjumbe wa Mungu. Wanasimamia mawazo ya kuwa, tunapaswa kuhubiri tu mawazo ya kifungu cha maandiko na tuwaache watu wafanye matumizi yao wenyewe.Wanaamini kwamba Roho Mtakatifu atatibua mioyo ya watu kuuitikia ujumbe. Wahubiri na Waalimu wengine wanashikilia kwamba matumizi ndio sehemu ya kiini cha ujumbe. Wanadhani kwamba mahubiri halisi hayaanzi mpaka utakapoanza matumizi.
Katika Biblia nzima kuna dhana kwamba kulisikia neno la Mungu kunahitaji kuitikia. Katika Agano la kale mwitiko wa pekee wa neno la Mungu uliosawa ni kutii. “Musa akaenda akawaambia watu maneno yote ya BWANA, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu
Somo la 16
Matumizi mazuri katika ujumbe wa Biblia yanahitaji mpango wa umakini, kwa kusoma kweli za kiifungu na wasikilizaji.
Kuandaa ujumbe Chagua kifungu. Nakiri kifungu Maneno ya kitendo. Maneno ya muhimu. Machunguzi. Viini vya Biblia. Wazo kuu Kiini cha mpaka. Mawazo saidizi. Pointi kuu. Watu PIcha za maneno Kusimulia hadithi Matumizi Kukusudia kwa imani Kuorodhesha
92
kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote aliyonena BWANA tutayatenda.” (Kutoka 24:3). Alipokuwe akimalizia mahubiri yake ya mlimani, Yesu aliwaambia mfano wa mjenzi mwenye Busara na mpumbavu. Mmoja alijenga nyumba yake juu ya mwamba. Na mwingine alijenga nyumba yake katika mchanga. Upepo haukuweza kuharibu nyumba moja, lakini uliharibu nyumba nyingine. Ponti yake ilikuwa wazi. Alisema, “ Basi kila asikiaye haya maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba” (Mathayo 7:24).Alisema mtu asiye tii mafundisho yake ni kama yule aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga.
Yakobo alitoa uhusiano halisi kati ya kulisikia neno la Mungu na kulitii. Aliandika, “Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikilizaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.” (Yakobo 1:25). Akaendelea kuunganisha nguvu ya imani ikiwa pamoja na matendo ya mwamini. Aliandika,”Nioneshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.” (Yakobo 2:18)
Jinsi Yesu Alivyoweka Mafundisho kwa Matumizi.
Tutaangalia tena njia ya Yesu. Tunapochunguza njia ya Yesu ya matumizi katika Agano Jipya, tunaweza kujifunza wenyewe jinsi gani ya kuitumia. Angalia uchunguzi mbalimbali kama njia ya Yesu ya matumizi. Mara nyingi Yesu alitoa sababu za mafundisho yake.Watu hawakusikia tu nini cha kufanya, waliweza kujua pia kwa nini wanapaswa kufanya hivyo. Aliwasihi watu kutokujilimbikizia mali duniani, kwa sababu yanaweza kupotea kwa Njia ya ufisadi na wizi (Mathayo 6:19).
Badala yake, aliwataka kujihifadhia mali zao mbinguni, ambako hakuna upotevu. Katika kuwaambia hatari ya duniani ya rushwa na wizi, aliwapa sababu ya onyo hili. Halafu akaongezea sababu ya kina
“Pokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu. Lakini iweni watendaji wa neno wala si wasikiaji tu. Hali mkijidangaya nafsi zenu.”
Yakobo 1:21, 22
93
zaidi, “Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.( Mathayo 6:21).
Yesu alihusisha amri zinazojulikana na akawapa maana za kina. Alitoa baadhi ya mafundisho kwa maneno haya, Mmesikia watu wa kale walivyowaambia” Mathayo 5:21,27,31,38,43). Halafu akaichukua amri kwa maana yake ya kimsingi. Au akaipa maana ya ndani, akaifanya kuwa swala la moyo. Akaichukua amri juu ya kuua kwa undani, kuijumlisha hasira (Mathayo 5:22)
Yesu aliyahuzisha matumizi yake mengi na mifano aliyotoa. Katika karamu, Yesu alichunguza jinsi gani wageni wanavyojichagulia viti vya mbele. Akawaambia mfano kuhusu kwenda katika karamu na kuudhiwa wakati mwenye karamu anapowaambia kuchukua viti vya nyuma
Halafu akawapa mafundisho yake:” Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma” (Luka 14:10).Alitabiri kwamba mwenye karamu angewaambia kuchukua viti vya mbele. Pointi ya Yesu ilikuwa wazi, “Kila ajikwezaye atadhiriwa, naye ajidhirie atakwezwa.” (Luke 14:11).
Yesu alitabiri matukio au hali ambazo watu wangekutana nazo na cha kufanya katika hali hizo. Alitaka watu wawe tayari kabla hawajakutana na hali hizi. Akasema, “Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamuonye, wewe nayeye peke yenu.” (Mathayo 18:15). Akaendelea na hatua zingine mbili zaidi za kufanya kwa ndugu anayekukosea: chukua mashahidi pamoja nawe, na baadae lipeleke kanisani. Yesu alijua kuwa watu wengi wangekutana na ugomvi huo.
Yesu alitumia matukio au hali halisi kufundisha masomo yake..Yesu alikuwa mgeni katika nyumba ya Simoni mfalisayo. Ghafla akaja kahaba na kuanza kulia huku akiiosha miguu ya Yesu na kufuta kwa nywele zake.( Luka 7:36-50). Alipolaumiwa kwa kumuacha mwanamke huyu amguse, akalitumia tukio hilo hilo kufundisha somo. Akasema kuwa mwenyeji wake hakumuosha miguu wakati alipoingia. Pointi ilikuwa kwamba yule asamehewaye sana hupenda sana.
Matumizi ya Yesu.
Sababu kuhusu maelekezo.
Maana ya ndani ya Amri.
Kutumia mifano kwa ajili ya matumizi.
Hali ambazo watu wanaweza kukutana nazo.
Matukio halisi yanayotumika kufundishia masomo.
Kuelezea tabia mbaya kwa uwazi.
Kutumia mifano halisi kwa ajili ya kulinganisha vitu/mambo.
Watake wasikilizaji kujitoa.
Kutumia Lugha ya ziada.
94
Yesu alionesha tabia isiyo kubalika na akaielezea kwauwa zi. Alikuwa mwenye msimamo juu ya wanafiki. Angalia katika Mathayo 23 maneno yake kwa waandishi na mafarisayo. Kwa mfano alisema walikuwa makini kujiosha kwa nje, lakini wakiacha mioyo yao michafu. Alisema “ kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote.(Mathayo 23:27).
Yesu alitumia mifano ya ulinganifu wa vitu ili kwamba matumizi ya maana yake ieleweke na iaminike. Kwa mafano, Yesu aliwataka watu kutokuogopa au kuwa na wasiwasi kwasababu Mungu agewajali. Kufanya maana hii ieleweke, alitumia mfano wa ndege wa anga na maua ya kondeni. (Mathayo 6:26-30). Alieleza kwamba ndege hawapandi wala hawavuni. Akaelezea kuwa maua hayajisokotei nyuzi yenyewe ili kujifanyia nguo. Hoja yake ilikuwa kwamba, Ikiwa Mungu huvitunza viumbe hivi visivyo na thamani, Angeweza kututunza pia hata sisi. Nyakati zingine Yesu aliwataka wasikilizaji wake wawe wanayatendea kazi yale wanayoyakili kuwa wanayafanya. Kiongozi mmoja alimjia yesu akamuliza jinsi ya kuurithi uzima wa milele. (Luka 18:18-22). Alijisema kuwa amezishika amri zote kumi za Mungu. Kwa kweli alikuwa amejitolea, akitaka kujua kitu gani kingine ambacho amepungukiwa. Yesu alimwambia aende na kuuza vyote alivyokuwa navyo na kuwafa Masikini. Ndipo amfuate. Bwana yule alikwenda akiwa amehuzunika. Kujitoa kwake kote kukaonekana kuwa ni kwa uongo.
Yesu alitumia Lugha ya ziada kutengeneza pointi yake.Jesus used exaggerated language to make his point. Aliiichukua amri juu ya uasherati kwa undani sana, kuijumlisha na kumwangilia mwanamke kwa kumtamani. Halafu akalifundisha kusanyiko lake,”Jicho lako la kulia likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe” Akaendelea zaidi, “Mkono wako wa kuume ukikukosesha ukate na uutupe mbali nawe” (Mathayo 5:29,30). Kwa maana ya kawaida Yesu hakumaanisha
“Unifahamishe njia ya mahusia yako;Nami nitayatafakari maajabu yako. Unifahamishe nami nitaishika sheria yako, Naam nitaitii kwa moyo wangu wote.”
Zaburi 119:27, 34
95
wajiharibu miili yao wenyewe. Na wala hakumaanisha kuwa jicho au mkono ndio sababisho la dhambi. Alitumia lugha hii ya ziada kusisitiza umuhimu wa moyo safi.
Jinsi ya kupanga Matumizi.
Hapa kuna baadhi ya njia ambazo unaweza kuchukua kupanga matumizi yako. Nitakuonesha pia baadhi ya mambo yanayofanana kwa matumizi ambayo utapaswa kuyaepuka. Kumbuka kwamba kuwaambia watu jinsi ya kuitikia ni muhimu kama vile kuwapa ukweli wa Mungu.
1. Angalia kwa makini katika kifungu cha somo kuona ikiwa yapo matumizi mahali hapo. Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Wapendeni adui zenu” (Mathayo 5:43, 44). Halafu akawaambia jinsi ya kufanya, Wabarikini wale wote wanaowalaani, wafanyieni mema wale wanaowachukia, waombeeni wale wanao waudhi.” Unapofundisha kifungu hiki, usiache matumizi maalum ya amri ya kuwapenda adui zetu. Eleza vizuri kwa watu katika hali ya mazoea yao.
2. Eleza waziwazi ieleweke wazo la biblia unalotaka kutumia katika kizazi hiki. Unajibu swali,”Tufanye nini?” Au labda matumizi yako yanajibu swali hili, “Tutampendezaje Mungu katika jambo hili?” Kweli za kithiolojia katika mahubiri yako zahitaji mwitikio. Kuna tofauti kati ya kanuni na mwitikio ambao watu wanapaswa kufanya. Ikiwa kifungu kinahusu mwitikio tu (kama ilivyo katika Mathayo 6:1-21), unaweza kuunganisha matendo haya na kanuni nyuma yake. Epuka matumizi ambayo hayaunganishi moja kwa moja na ukweli wa kifungu.
3. Pitia orodha ya hatua tisa za Yesu kwa matumizi. Angalia kama kila kanuni inaweza kutumika katika moja ya njia hizi. Fikiri juu ya njia nyingi uwezavyo kwa ajili ya kutumia katika kila kanuni. Kwa Warumi 12:1,2 tulielezea kanuni kama hivi: “Mkristo anaweza kuyatambua mapenzi ya Mungu kwa kujitoa mwenyewe kikamilifu kwa Mungu.” Unaweza kuitumia hii kwa kuelezea maana ya ndani ya kuwa sadaka iliyo hai, au kwa kuelezea hali ambayo unaweza kutaka kurudi
96
nyuma kutoka katika mapenzi ya Mungu, au kwa kutumia mfano halisi wa sadaka ya hekalu kuonesha kujitoa kwa ukunjufu. 4. Chagua kimoja kati ya matumizi yako yanayowezekana kimoja kinachoelezea wazo la Biblia na kinachowafaa zaidi wasikilizaji wako.Epuka kuibua zaidi matumizi ya “kidini” ambayo yanalenga zaidi katika matendo mema badala ya imani. Ufunguo wa mwitikio wetu wakati wowote ni kujitoa kwa imani kwa Mungu. 5. Toa matumizi katika njia inayoeleweka na ya kivitendo. Watu hawapaswi kutokuwa na uhakika juu na matendo ambayo wanaweza kuyachukua ili kufanya kanuni za Kibiblia kufanya kazi katika maisha yao. Epuka kutumia matumizi ya kiujumla sana ambayo hayalengi moja kwa moja mwitikio maalum.
Mazoezi ya Somo.
1. Rudia mawazo makuu ya somo hili: Katika Biblia nzima kuna dhana kwamba kusikia neno la Mungu kunahitaji mwitikio. Matumizi ya Yesu ya matumizi ya Somo, yanamuonesha mjumbe wa Mungu njia nyingi za kuwatia changamoto watu wake kuutumia ukweli wa Mungu. Mjumbe wa Mungu anaweza kuchukua hatua kupanga matumizi maaalum kwa kila ukweli wa Biblia katika kifungu chake.
2. Angalia tena vifungu ulivyovisoma katika kitabu hiki. Panga jinsi utakavyozitumia kila kweli hizi, ukitumia baadhi ya mbinu alizozitumia Yesu.
97
Somo la 17
KKuukkuussuuddiiaa IImmaannii..
KIla ujumbe wa Biblia unapaswa kutimiza kitu Fulani. Lakini mahubiri mengi yanatolewa kwa kutoeleweka kwamba nini yanapaswa kufanya. Jumbe ziingine zinatolewa “kuwaongoza” watu. Zingine zinakusudia toba. Zingine zina malengo ya kiinjilisti. Jumbe zingine zinakusudia kuwafariji na kuwatia moyo watu. Na zingine kufundisha misingi mikuu ya imani ya dini.
Mjumbe wa Mungu anahitaji kuona jambo likitimia kama matokeo ya ujumbe wake. La sivyo, kwa nini afundishe na ahubiri? Mjumbe wa anaweza kuwa na wazo la kile anachotumaini kama matokeo ya mahubiri yake. Lakini anaweza akawa hana uhakika jinsi ya kupanga nini atakachosema kufikia lengo hilo. Anaweza akahubiri tu kwa sababu ameitwa na Mungu. Anahisi Roho wa Mungu anamsukuma kuhubiri neno.
Uangalifu wa ukaribu wa Maandiko yote utaonesha kwamba lengo kubwa la mahubiri yote na mafundisho yote ni kuamsha imani katika Mungu.
Umuhimu wa Imani.
Mwitikio mmoja wa muhimu sana kwa Mungu ni kumwamini yeye. Ufunuo wake unatolewa kwa mwanadamu kuamsha imani yake. Hata kama mara kwa mara tunafikiri utii kama mwitikio sahihi kwa Mungu, Imani huja kwanza. Imani na utii ni pande mbili za mwitikio mmoja. Panaweza kuwa hakuna utii unaokubalika pasipo imani. Na imani ambayo haileti utii si imani ya kweli.
Katika Agano la Kale, Mungu alijifahamisha mwenyewe ili watu waweze kumwamini. Imani hiyo ingeweza kupelekea utii. Katika miaka ya leo, kusudi ni lile lile. Mungu amezungumza “kwa nyakati mbali
Somo la 17
Kusudi kuu la kuhubiri kote neno la Mungu ni kutoa ukweli wa muhimu wa mwitikio wa Imani wa wasikilizaji.
Kuandaa Ujumbe Chagua kifungu Nakili Kifungu Maneno ya kitendo Maneno ya muhimu. Machunguzi Viini vya Biblia. Wazo kuu Kiini cha mpaka. Mawazo saidizi. Pointi kuu. Watu. PIcha za Maneno. Kusimulia hadithi. Matumizi. Kukusudia kwa imani. Kuorodhesha
98
mbali na kwa njia mbali mbali kwa Manabii” (Waebrania 1:1). Lakini neno hilo lililokuwa likihubiriwa kwao halikuwanufaisha wengine, maandiko yanasema, “halikuchangamanika na imani ndani yao waliosikia.” (Waebrania 4:2). Kusikia Neno la Mungu, pasipo imani, ni bure.
Leo Mungu anajifahamisha kupitia neno lake lililoandikwa. Wajumbe wake wanatangaza kweli ya ujumbe ulioandikwa. Kusudi la tangazo hili ni kuwataka wasikilizaji kuamini katika Mungu. Paulo anaandika, “Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo muhubiri?” (Warumi 10:14). Kuhusiana na mahubiri, wanahitaji kusikia, kuamini, na kumwita Mungu. Imani ni muhimu katika hatua hii. Katika Biblia nzima, Imani imeambatanishwa sana na neema ya Mungu. Kwa wakati huo huo, Imani imetofautishwa na matendo yanayolenga kupata kukubaliwa na Mungu. Kosa kubwa kabisa la Kidini ni mtazamo kwamba mtu anapata msimamo sahihi na Mungu kwa juhudi zake mwenyewe za Kidini. Paulo ameliweka sawa hili anapoandika, “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu; ni kipawa cha Mungu, wala si kwa Matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.” (Waefeso 2:8,9) Imani ni ya muhimu katika kila namna ya maisha ya Kikristo. Imani huleta neema ya Mungu. Kila kitu na kiwe kwa Imani. “Lakini ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa neema . Lakini ikiwa ni kwa matendo, hapo si neema tena; au hapo kazi si kazi tena” (Warumi 11:6). Kwa hivyo katika kila kitu wanachokifanya, waamini wanapaswa kuishi kwa imani, wakihesabu neema ya Mungu. Sehemu nne tofauti toafauti katika maandiko tuasoma, “Mwenye haki ataishi kwa Imani ( Habakuki 2:4; Warumi 1:17; Wagalatia 3:11; na Waebrania 10:38).
Jukumu la mjumbe wa Mungu ni la muhimu sana katika kutaka Imani. Imani si kitu dhahaniwa cha kiroho kilichopandwa ndani ya mkristo. Ni mwitikio hai kwa neno kutoka kwa Mungu linalowezeshwa
Mungu anajifahamisha mwenyewe kupitia neno lake lililoandikwa leo.Wajumbe wake wanatangaza ukweli wa neno lililoandikwa. Makusudi ya kutangaza hivi ni kuwataka wasikilizaji kuamini katika Mungu.
99
na Roho Mtakatifu. Katika hatua hiyo, Neno la Mungu ndio kichanganyo muhimu. Paulo anaandika, “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Mungu” (Warumi 10:17). Ni pale tu mjumbe wa Mungu anapotangaza neno la Mungu ndipo imaniinapochochewa katika mioyo ya wasikilizaji.
Kuchochea Imani
Mjumbe wa Mungu anapaswa kuhubiri na kufundisha kiasi cha kuchochea Imani. Mwitikio pekee uliosahihi wa neno la andiko ni kumwamini Mungu. “Lakini pasipo Imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yupo, na kwamba huwapa dhawabu wale wamtafutao. Hapa kuna vipengele vinavyoweza kusaidia kuwasilisha ujumbe wa kuchochea imani.
Mara zote hubirir kweli ya Mungu kutoka katika andiko. Chukua kifungu cha Biblia na acha mawazo yake yaje kupitia ujumbe wako. Kama jinsi ambavyo tulivyotaja awali, wahubiri wengi wameonekana kutoa mawazo yao na hadithi zao wenyewe tu. Usidhani kwamba mitazamo ya dini yako inatosha kwa somo. Waache watu wafungue Biblia zao ikiwa wanazo. Waache wafuatilie katika kifungu. Ukweli wa Neno la Mungu hutibua imani katika wasikiaji Roho Mtakatifu anapolidhibitisha.
Tafsiri kifungu kama jinsi Mungu alivyokusudia na si kama mwanadamu alivyokusidia. Wasaidie watu kuona ya kwamba maisha ya Kikristo si juu ya kile tunaweza kufanya kwa ajili ya Mungu. Ni juu ya kile Mungu anachofanya katika ulimwengu. Wokovu wetu si kuishi maisha safi ili kumpendeza Mungu. Lakini ni Mungu kuwakubali wenye dhambi na kuwafanya wenye haki pamoja naye kupitia Kristo. Mzigo wa wajibu si wetu tu kuubeba peke yetuo. Yesu alisema, “NIra yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi” (Mathayo 11:30).
“Yesu alisema, „Nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa na uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwapo neno lisilowezekana kwenu.”
Mathayo 17:20
100
Weka uwiano wa ujumbe wako kwa sheria na injili.. Biblia ina vifungu vingi sana vinavyotoa sheria ya Mungu. Vifungu hivi vinatueleza jinsi gani ya kuishi kitabia. Vifungu vingine vinaelezea dhambi za mwanadamu zisizompendeza Mungu. Sharti hili la kitabia ndio jambo kuu la maisha ya kikristo. Lakini pamoja na sheria(sharti la kimaadili) Biblia ina injili (habari njema ya neema). Kifungu chochote kile unachohubiri, jaribu kufanya uwiano unapokielezea kwa watu. Kila kifungu cha sheria kinataja neema. Na kila kifungu katika neema kinataja sheria. Tafuta kuishi kwa Imani wewe mwenyewe na hubiri kutoka Imani yako mwenyewe. Si sawa kwamba mjumbe wa Mungu achochee imani ndani ya watu ikiwa yeye mwenyewe si mwamini thabiti. Kila sehemu ya maisha ya kikristo imejengwa katika uhusiano wetu na Kristo kwa Imani. Haijalishi hali gani tunakutana nazo, swali la Yesu kwetu linaeleweka,“Utaniamini mimi katika hili?” Analiweka kwa yule kipofu katika maneno haya, “Je unaamini kwamba ninaweza kufanya hili?” (Mathayo 9:28). Ikiwa unamwamini Bwana kikamilifu, huduma yako ya mahubiri na mafundisho itatia moyo pia kwa watu wengine. Tumia lugha ya imani katika jumbe zako. Imani katika Mungu ina maana ninamwamini yeye kwa kila kitu. Yesu alisema kwa yule bwana ambaye mwanae alikuwa na pepo mchafu, “Ukiweza kuamini, yote yawezekana kwake aaminiye.” (Marko 9:23). Unapohubiri, tumia lugha ya kuwezekana badala ya lugha ya sharti. Sharti linasema, “Nilazima,” “Tunapaswa,” na “Tunataka,” Kila wiki muhubiri anaendelea kusema “Tunataka” kanakwamba hakuna matumaini ya kupata malengo hayo.
Lugha ya Imani ni lugha ya matumaini. Ni lugha ya uhakika kuhusiana na Mungu ni nani na atafanya nini. Lugha ya imani ni “Mungu ana,” “Mungu ame,” “Mungu ata,” na “Mungu anaweza”. Ni lugha ya kuwezekana kwa neema ya Mungu. Kwa mwamini
Kuchochea Imani Hubiri neno la Mungu Tafsiri kifungu kama Mungu alivyokusudia Weka usawa kati ya sheria na injili. Tafuta kuishi kwa imani. Tumia lugha ya imani.
101
tunasema “Tunaweza,” badala ya “Tunahitaji.” Hakuna kitu ambacho Mungu anakihitaji kwetu kitakosa neema yake. Kila nachoamuru tunaweza kufanya kwa nguvu zake. Huo ndio uhalisia wa imani.
Tutaangalia zaidi swala la kuhubiri kwa imani katika somo la 20 tunapozungumzia juu ya Kuujenga Mwili wa Kristo.
Chumvi na Nuru.
Jambo muhimu hasa katika changamoto la kuhubiri kwa imani ni kana kwamba mahubiri ni ya ubinadamutu au yamejengwa juu yake Mungu. Kila kifungu kinaweza kutafsiriwa katika hali ambayo msisitizo ni juu ya nini wasikilizaji wanapaswa kufanya kwa ajili ya Mungu Au inaweza kutafsiliwa juu ya kile Mungu amefanya na anafanya kwa waamini na kupitia wao. Biblia imeandikwa kumfunua Mungu na mapenzi yake kwa uumbaji wake. Kila kifungu kinapaswa kutafsiliwa katika nuru ya ujumbe huo mkubwa wa Biblia.
Angalia tena Mathayo 5:13-16 kuhusu “chumvi na nuru”. Yesu anaanza kwa kuwaambia wasikilizaji wake, “Ninyi ni chumvi ya ulimwengu” Tumegundua kuwa matumizi yake ya chumvi hapa yanamaana ya mvuto. Hii inaonekana kuwa ya kibinadamu sana. Kwa hiyo mjumbe wa Mungu anaweza akaitafsiri hiyo peke yake kwa watu katika namna ya tabia zao wenyewe. Anaweza akawalaumu kwa kutokuwa wenye haki kama jinsi ambavyo wangepaswa kuwa. Anaweza akawaamuru juu ya jukumu kuu la kuwavuta majirani zao kwa Kristo.
Namna hiyo inaweza kueleweka. Lakini tunauliza sasa “Kuna nini pale kuhusu Mungu na mapenzi yake yanayofanya mvuto huu uwe wa muhimu?” Tutajaribu kuona kifungu kama sehemu ya kubwa ya hadithi ya haja ya Mungu kuwaleta watu kwake mwenyewe. Tutagundua pia njia ya Mungu ni kutumia mwakala wakibinadamu kufanya kazi yake duniani. Kwa hivyo sasa tunakiona kifungu katika nuru ya tofauti. Si juu ya mwamini na ushawishi mvuto wake tu. Ni juu ya upendo wa Mungu na kusudi lake katika ulimwngu.
Kwa hivyo sasa tumeanza kukiona kifungu katika mwanga wa tofauti. Si tu kuhusu mwamini na ushawishi wake. Ni kuhusu Upendo wa Mungu na makusudi yake katika ulimwengu.
102
Haubadirishi maana ya kifungu. Lakini unakielezea kwa watu katika namna pana zaidi. Hii inaonesha ni jinsi gani mvuto wao ni wamuhimu kwa watu wanaowafahamu. Hii inwaonesha pia ni kazi ya Mungu. Si mzigo mzito sana ambao wanapaswa kuubeba kwa nguvu zao wenyewe. Wamao upendeleo wa kuwa mawakala wa Mungu katika dunia kwa neema yake. Wanaweza wakawasha “taa” zao, wakijua kuwa Mungu ndiye anayetoa mwanga huo. Kila Mtu katika Kristo ni kiumbe kipya.Ni Mungu ndiye aliyetufanya “chumvi” na “nuru” katika ulimwengu. Ni Mungu anyefanya kazi kupitia sisi kushughulika na uasi na giza la dunia. Mjumbe wa Mungu anaweza akawatia moyo watu kuwa wajasili kuwasha nuru zao. Wao ni mwakala wa Mungu aliye hai. Wao ndio nuru ya Kristo katika dunia hii ya giza. Yeye ni nuru ya ulimwengu (Yohana 8:12 na Yohana 9:5) na tunaweza kuifanya nuru hiyo iwake kupitia kwetu.
Mazoezi ya Somo.
1. Rudia mawazo makuu ya somo hili: Mwitikio mmoja wa muhimu kwa Mungu na Dunia yake ni kumwamini yeye. Mjumbe wa Mungu anaweza akafuatisha miongozo maalum kwa ajili ya kutia moyo imani kupitia jumbe zake. Kila kifungu ni lazima kitafsiliwe katika nuru ya ujumbe mkubwa wa Biblia wa Mungu ni nani na anafanya nini.
2. Rudi nyuma katika vifungu mbalimbali tulivyovisoma katika masomo haya. Orodhesha katika upande mmoja mawazo yanayotolewa na kifungu ikiwa yatatafsiliwa katika namna umuhusuyo mwanadanu. Katika upande mwingine, andika mawazo katika tafsiri imuhusuyo Mungu.
3. Angalia katika viorodhesho vya mahubiri yako kwa lugha unayoitumia. Je ni Lugha ya kidini au ni lugha ya Imani?
103
Somo la 18
KKuuaannddiikkaa MMuuhhttaassaarrii
wwaa UUjjuummbbee..
Katika somo la 12 tulianza kuelezea jinsi ya kupanga ujumbe wako kulingana na umbo la kifungu. Ujumbe wako utafanana na mawazo ya mwandishi, ukielezewa kama somo lenye kiini cha mpaka. Utafuata pia mawazo yake saidizi kama yalivyoelezewa katika kifungu. Mawazo haya yanaweza kusemwa kuwa kama ramani kuu ya ujumbe wako. Sasa tutaangalia jinsi gani unaweza kupanga kile ambacho ungekisema kwa watu kuwasaidia kuupokea ujumbe.
Sehemu za Muhtasari.
Muhtasari si ujumbe. Ni mpango kwa ajili ya kuwakilisha ujumbe. Utapanga jinsi gani ujumbe utao nekana katika wakati utakaotakiwa kuzungumza kwa watu. Mpango mzuri utajumlisha vipengele funguo vingi.
Wazo kuu la ujumbe wako ni sawa na wazo kuu la kifungu. Ni wazo la kithiolojia. Linazungumzwa katika sentensi kamili. Linajengwa katika somo na neno la mpaka. Katika kusoma Yohana 3:1-8 tulisema “Kuzaliwa upya ni muhimu katika ufalme wa Mungu” Hilo ndilo wazo kuu la kifungu. Ni wazo kuu pia la ujumbe wetu kutoka katika kifungu hiki.
Sehemu nyingine ya Muhtasari wowote itakuwa mawazo saidizi. Tumejaribu kugundua nini mwandishi alikuwa anasema kuhusu wazo lake kuu. Haya ndio mawazo saidizi ambayo nyakati zingine tunayaita pointi za mahubiri. Yanatoa maelezo zaidi kuhusiana na wazo kuu la kithiolojia.
Kwa Yohana 3:1-8, tulisema mawazo saidizi yalikuwa matatu:
Somo la 18
Panga ujumbe wako kulingana na muundo wa kifungu katika namna ambayo mwandishi ametoa mawazo yake.
Kuandaa ujumbe Chagua kifungu Nakili kifungu kwa mkono Maneno ya kitendo Maneno ya muhimu Machunguzi Viini vya Biblia Tengenezea sentensi wazo kuu Wekea mpaka somo Mawazo saidizi Pointi kuu Watu Picha za maneno Kusimulia hadithi Matumizi Kukusudia kwa Imani. Kudokeza.
104
Kuzaliwa upya ni muhimu kuuona Ufalme wa Mungu ( 3). Kuzaliwa upya ni muhimu kuingia Ufalme wa Mungu. 5). Kuzaliwa upya ni muhimu kumuona Roho Mtakatifu 7, 8)
Nyakati zingine Mtumishi atadhani kwamba ikiwa ana mawazo matatu au manne kama hivi, yuko tayari kuhubiri. Anaweza hata asichukue “pointi” hizi kutoka katika kifungu cha Biblia. Lakini yapo mambo mengi ya ziada katika kidokezo kuliko hili. Hapa kuna vidokezi vitano zaidi ambavyo utapanga katika muhtusari wako.
Kila mawazo katika ujumbe wako yanahitaji maelezo. Hii inatumika katika wazo lako kuu na katika mawazo saidizi. Baada ya kulisema wazo la kithiolojia, utahitaji kulielezea kwa watu. Hata kama umechagua sentensi zako kwa makini kwa ajili ya wazo, unaweza kutumia maneno mengine kuhakikisha kuwa inaeleweka. Unaweza kuonesha mahali ambapo wazo linaoneshwa katika kifungu. Unaweza kupitia mambo mbalimbali ya mstari au mistari katika swali. Mawazo yanahitaji pia maelezo. Hii ina maana unahitaji kutumia picha za neno na hadithi kusaidia watu kuona wazo katika namna ya mazoea ya kibinadamu. Angalia tena masomo katika somo hili juu ya picha za maneno na hadithi. Jaribu kutumia baadhi ya namna ambazo Yesu alizitumia, kama tulivyoona katika somo la 14. Tumia pia hadithi kama zake kama tulivyosema katika somo la 15. Tafiti kifungu kwa ajili ya lugha za picha na hadithi unazoweza kutumia tena. Panga kutumia mifano inayofaa katika kila wazo katika ujumbe. Mawazo katika ujumbe wako yatahitaji pia matumizi. Tumekwisha kuona aina nyingi za matumizi kutoka katika mafundisho ya Yesu. Angalia tena katika somo la 16 na panga matumizi yako katika moja ya njia nyingi Yesu alizotumia matumizi yake. Panga matumizi yako kwa kila wazo katika mahubiri kwa moja au zaidi ya hizi. Hakikisha kwamba watu wanaelewa jinsi ya kuuweka ukweli wa kifungu kufanya kazi katika mazoea yao wenyewe.
Kipengele kingine cha kidokezo chako ni sehemu ya ufunguzi. Mara nyingi tunakiita “Utangulizi”. Hiyo ni kwa sababu ni kwa ajili ya
Kutokeza vipengele Wazo kuu la ujumbe kutoka katika kifungu Mawazo saidizi yanayofunuliwa katika kifungu Maelezo ya kila wazo katika ujumbe Kielelezo kwa kila wazo katika ujumbe Matumizi kwa kila wazo katika ujumbe. Sehemu ya ufunguzi kutambulisha wazo. Sehemu ya kufunga kuita mwitikio
105
kulitambulisha somo. Lakini ni lazima ufanye zaidi. Sehemu yako ya ufunguzi wa ujumbe lazima uwasiliane na wasikilizaji. Ni lazima iwasaidie kuona kwanini ujumbe huu ni wa muhimu kwao. Ni lazima uunganishe wazo kuu na maisha na mazoea ya watu. Kwa hivyo sehemu ya ufunguzi inatambulisha somo, lakini inafanya zaidi.
Kipengele cha mwisho katika kidokezo chako ni sehemu ya kufunga. Hii nyakati zingine inaitwa “hitimisho”. Kwa ujumbe wa Biblia sehemu hii imetengenezwa kuita mwitikio. Kwako huu si ujumbe wakichwani tu, yaani kitu cha kufikilia. Itakuwa hiyo. Lakini ni lazima iwe zaidi. Ni lazima imlete msikilizaji uso kwa uso na matakwa ya Mungu juu ya maisha yake. Ni lazima itoe mabadiliko katika uelewa wake, mtazamo wake, na tabia yake. Unaweza kuaita watu kuitikia kwa wakati huohuo mwito wa Kristo.
Kutumia Notsi unapozungumza.
Muhtasari waku ni mpango kwa ajili ya ujumbe utakaouleta kwa watu. Kwa sababu hii ndio umepanga kufuata kwa ajili ya mahubiri yako,Unaweza kufikiri kwamba ni vizuri kwenda na ramani yako unapozungumza. Ngoja mimi nishauri kwamba usifanye hivyo. Ni vizuri zaidi kuwa na Biblia yako tu unapotoa ujumbe wako. Hii inawaambia watu kuwa ujumbe unatoka katika maandiko. Na inawaambia pia kuwa unakifahamu vizuri na unazungumza kutokana a fuliko wa usomaji wako wa Biblia.
Kwa sababu muhtasari wako unafuatisha vizuri kifungu, hautahitaji kuchukua notsi uende nazo utakapokuwa ukizungumza. Utakuwa na Biblia yako kukukumbusha mpango wako. Wazo kuu la ujumbe wako linatoka katika kifungu. Mawazo saidizi yanatoka katika kifungu Maelezo zaidi yanatoka katika kifungu. Kwa maana hii, Biblia yenyewe inatoa notsi ya kile unachokihitaji unapozungumza.
Nimeona kuwa inakuwa ni msaada kuwekea alama kwa rangi maneno ya muhimu na vifungu katika kifungu. Wazo langu kuu na mawazo saidizi yamefungwa katika lugha maalum katika kifungu. Maneno haya yananikumbusha mimi kiurahisi juu ya pointi
“Naye Ezra Kuhani . . . akasoma . . . tangu mapambazuko hata adhuhuri. . . na masikio ya watu wote wakasikiliza kitabu cha torati . . . Nao wakasoma katika kitabu, katika torati ya Mungu, kwa sauti ya kusikilika; wakaeleza maana yake,hata wakayafahamu waliyoyasoma.”
Nehemia 8:3, 8
106
ninazozitaka kuzitoa. Maneno yangu yaliyowekewa alama yananisaidia kujua sihitaji kuogopa kusahau mawazo yangu. Ninaangalia tu katika kifungu kukumbuka nini kinachofuata ninachotaka kuwaambia watu.
Utaona kwamba kuzungumza bila ya kutumia notsi inafanya ujumbe wako kuwa wenye kufaa zaidi kwa watu. Utakuwa huru kuwangalia watu, kuona mwitikio wao, kuitikia vitu ambavyo wanavipenda au wasivyokuwa na uhakika navyo hata wakati unapozungumza. Watu wataweza kuona vizuri sura yako inavyoonekana na lugha ya mwili wako utakapokuwa haujishughulishi na kusoma kutoka katika notsi. Mahubiri yanakuwa na uhai pale tu yanapotolewa. Hata hivyo kupanga vizuri kidokezo chako, ni mango tu. Utahitaji kuwa wazi kwa Roho unapozungumza. Utakiweka kile unachokisema kulingana na changamoto za wakati ule. Unaweza kufanya hivyo bila notsi.
Mafundisho au Mahubiri?
Katika somo letu lote hili, tumesisitiza kwamba mjumbe wa Mungu anapaswa kusoma kifungu cha Biblia kwa makini. Sababu ya kusoma huko kwa makini ni kutoa ujumbe wa Mungu kwa watu. Nimeuchukua ujumbe wako kama “mafundisho” au ‘mahubiri.” Ninakufikiria kama “mwalimu” au “muhubiri”. Unauonaje wito wako? Unafikiri juu ya kile unachokifanya kama “mafundishi” au “mahubiri?” Katika mawazo ya wakristo ambao wamesikia ujumbe wa andiko kwa muda, kuna tofauti kati ya “mahubiri” na “mafundisho”. Hebu tuchunguze tofauti hii na tuone ikiwa inaathiri jinsi ya kuwakilisha ujumbe wako.
Panaweza kuwa na tofauti katika makusudi ya kuhubiri na kufundisha. Sababu ya kwanza ya kufundisha ni kuweka maar lifa. Wakati sababu ya kwanza ya kuhubiri ni kuchochea mwitikio. Wakati mwa limu anatumaini kuwa watu wataondoka wakiwa na ufahamu mzuri, muhubiri anatumaini kuwashawishi wabadilike. Haswa, ni lazima pawe na mafundisho katika kila mahubiri. Mtu hawezi kuitikia
Kuzungumza pasipo notsi. Ujumbe unaeleweka kutoka katika Biblia. Ujumbe unatakana na kujifunza kwa wingi. Kifungu cha Biblia kinafanyika notsi. Ujumbe unawafaa sana watu. Mjumbe anaweza kujiza-wazisha kulingana na wasikilzaji. Mjumbe anaweza kumwitikia Roho Mtakatifu.
107
kwa imani ujumbe wa Mungu ikiwa hauelewi. Mahubiri lazima yatoe kweli ya neno la Mungu lililoandikwa ili kwamba kila mmoja ajifunze kutoka katika ujumbe. Hawawezi kumwitikia Mungu kwa tabia Mpya ikiwa hawajifunzi Mungu anataka nini.
Mwalimu mzuri wa Biblia anatumaini pia kuwa mwishoni masomo yake yatasabaisha mabadiliko katika maisha. Imani yake ni kwmba ikiwa watu watasikia na kuelewa Neno la Mungu, mara watafanya maamuzi juu ya kile wanachopaswa kufanya kuhusu neno hilo.
Tunachokiita “mafundisho” na “mahubiri” vinaweza kutofautiana katika kuwahusisha wasikilizaji. Mwalimu huwa anawaacha watu wajadili mawazo ya somo. Hata hivyo, muhubiri, mara nyingi anatoa ujumbe wake pasipo maoni ya wasikilizaji. Wanaweza kusema “Amina,” lakini labda hawaulizi maswali au kufanya ushauri mwingine.
Matumizi yanaweza kuwa njia nyingine tunayotofautisha kati ya “mafundisho” na “mahubiri”. Muhubiri anawatia changamoto wasikilizaji wake juu ya hatua wanayopaswa kuchukua kumwamini na kumtii Mungu. Anaweza akatoa hatua na kuhitaji mwitikio. Hata hivyo, mwalimu, anaweza asiweke matumizi sana katika somo lake. Labda anaweza asiite mwaliko katika kufunga somo lake.
Tofauti nyingine kati ya “Mafundisho” na “mahubiri” inaweza kuwa yaliyomo katika ujumbe. Mwalimu wa Biblia huwa anatoa historia nyingi na kusimulia hadithi za Biblia. Hata hivyo, muhubiri, anaweza asiridhike kutoa historia tu. Anataka kuzungumzia kanuni za maandiko na jinsi gani tunavyoweza kuziweka kufanya kazi katika matendo yetu.
Nyakati zingine namna ya uwasilishaji ni tofauti katika somo na mahubiri. Mwalimu huwa mkimya sana na anayefikiria sana katika namna yake. Lakini muhubiri mara nyingi anakuwa ni mtu anaye igiza sana na mwenye shauku. Lugha wanazotumia zinaweza kuonekana kama somo au mahubiri. Lugha za matendo na matumizi ya notsi zinaweza kueleza ikiwa ujumbe una namna ya mahubiri au mafundisho.
Kuhubiri au Kufundisha? Tofauti katika malengo ya ujumbe. Tofauti kataka kuwashilikisha wasikilizaji. Tofauti katika matumizi ya ujumbe. Tofauti katika maana ya ujumbe. Tofauti katika namna ya kuuwasilisha ujumbe.
108
Ninatumaini kutachukulia kwa uzito sana tofauti tunayoiona kati ya kuhubiri na kufundisha. Watu wanaweza wakakuambia kwamba ujumbe wako ni kama huu au mwingine. Hii itategemea sana na kile walichokizoea na kile wanachokipendelea. Vyovote vile ni vizuri ujumbe ukitolewa kikamilifu.
Mazoezi ya Somo.
1. Rudia mawazo makuu ya somo hili: Vipengele saba ni muhimu katika kidokezo kinachofaa kwa kupanga ujumbe wa Biblia. Utumiaji wa notsi katika uwasilishaji wa ujumbe wa Biblia unaweza kuzuia kufana kwa ujumbe. Ha kama ujumbe unaweza kuonekana mafundisho au mahubiri, njia zote zina weza kuwa ni za kufaa.
2. Rudi nyuma katika vifungu vingi ulivyokuwa ukivifanyia kazi. Panga kidokezo kwa kila kifungu kikiwa na vipengele vya muhimu kwa uwasilishaji unaofaa.
“Maana ijapokuwa naihubiri injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili.”
1 Wakorintho 9:16
109
Somo la 19
KKuuppaannggiilliiaa MMaahhuubbiirrii YYaakkoo..
Huduma ya kuhubiri na kufundisha ya mjumbe wa Mungu ni zaidi ya hubiri ama hotuba moja. Nafasi ya kutoa ujumbe wa neno la Mungu inaweza kuja katika namna nyingi. Mahubiri ya Jumapili katika ibaada, mafundisho ya Biblia nyumbani, mahubiri ya kiinjilisti uwanjani, mafundisho maalum kwa wanaume, au wanawake, au vijana- namna na mitindo ya kuhubiri Biblia haina mipaka.
Kila ujumbe utaupanga kwa makini. Lakini pia unaweza kupanga mafungu ya mahubiri. Unaweza kupanga kwa matukio maalum. Unaweza kupanga kwa mahitaji na hali maalum katika jamii. Unaweza kupanga kuzungumza juu ya udhaifu wa kiroho miongoni mwa watu. Unaweza kufundisha kweli kuu za Biblia. Unaweza ukashughulika na matatizo ya kimaadili ndani ya kanisa. Katika njia zote hizi unaweza ukahubiri mafungu ya mahubiri ambayoyanaweza kufanya, kitu ambacho ujumbe mmoja tu hauwezi kufanya hivi.
Kuwafahamu Watu.
Katika somo la 13 tuliangalia umuhimu wa watu katika uaandaaji na utoaji wa jumbe za Biblia. Sasa tutaangalia tena watu watakao sikia jumbe zako.Jinsi unavyowafahamu itaguza mpango wako katika njia nyingi. Ikiwa ni kundi la watu wa lugha na desturi yako, tayari unawafahamu vizuri. Ikiwa ni kundi la watu ambao ni wa wageni kwako, utapaswa uwasome vizuri kwanza.
Ikiwa mtumishi anafika katika eneo jipya, atakuwa mwenye busara kusikiliza na kujifunza kadiri awezavyo juu ya historia ya watu.
Somo la 19
Mjumbe wa Mungu atapanga huduma ya mahubiri na mafundisho yake kujumlisha mtiririko wa mahubiri kutoka vitabu vya Biblia.
110
Watumishi wanakuwa wazungumzaji. Hata katika mazungumzo ya binafsi, wanajisikia kuzungumza kitu kuhusu dini. Lakini wanaweza kuwa wenye busara kuuliza maswali kuhusu mila na desturi za watu. Hapo ndipo watakapojifunza historia na mioyo ya watu.
Mambo mengi sana kuhusu watu yataathiri upangaji wako wa jumbe za Biblia. Je wanaishi katika jamii ya mjini au kijijini? Dini gani kuu iliopo katika eneo hilo? Hali yao kiuchumi iko vipi? Je, Watu wameelimika? Kundi la kabila gani lilikuwa la kwanza mahali pale? Nini hasa historia ya kabila la wasikilazaji wako? Ni aina gani ya kazi watu hao wanafanya? Unaweza ukauelezea vipi wepesi wa upokeaji wa mambo ya kiroho? Mjumbe wa Mungu anaweza kuwa mmishonari, mwinjilisti, mpandaji wa makanisa, mwalimu, mchungaji au aina nyingine ya mtumishi. Jukumu lolote lile analoweza kuwa nalo, anahitaji kuwa na moyo wa Kichungaji. Kama Yesu, atakuwa anachukuliwa na huruma kwa hali ya makusanyiko. Hali yao ya kimwili itagusa hisia zake. Hali zao za kiroho zitatibua pia moyo wake. Anapohubiri, watu watajua kuwa anawapenda.
Kupanga mfululizo wa Mahubiri.
Mchungaji anaye zungumza na kusanyiko lile lile kila wiki, atahitaji kupanga mfululizo wa mahubiri. Asili ya Biblia inahitaji makundi ya mahubiri yanayofundishwa kwa wiki au miezi mingi. Biblia inakuwa katika Vitabu. Ni kitabu cha Vitabu. Vitabu hivi vimebeba mambo ya historia, mashairi, mafundisho ya kinabii, maono yajayo, nyaraka na mengine. Ujumbe mmoja kutoka katika kifungu cha mistari mingi kinatoa uonaji wa mara moja wa kweli ya andiko. Ili Watu waelewe kitu juu ya thiolojia ya Biblia, mjumbe wa Mungu atapaswa kuhubiri kutoka katika vitabu vyote. Katika kufanya hivyo atashughulika na masomo ambayo penginevyo asingeyachagua. Atapitia zaidi funguo za misingi mikuu ya imani kuliko vile ambavyo anavipenda zaidi.
Hali zao za kimwili zitagusa hisia zake. Hali zao za kiroho zitatibua moyo wake pia. anapohubiri , watu watajua kuwa anawapenda.
111
Atakutana na mahitaji ya watu ambayo inawezekana kabisa kwamba alikuwa hayafahamu. Zaidi ya yote, ataiacha Biblia izungumze zaidi yenyewe katika njia iliyopangwa.
Mfululizo wa msingi wa jumbe utatoka katika kitabu kimoja au sehemu ya kitabu. Ngoja nishauri hatua unazoweza kuchukua kupanga mtiririko huo.
Soma kitabu kizima mara kadhaa. Ikiwa unapanga mtiririko kutoka katika kitabu kifupi kama vile Yakobo, Yuda, au wafilipi, unaweza kutengeneza mtiririko wako utakaochukua kitabu kizima. Ikiwa unachukua sehemu tu ya kitabu, kama vile mahubiri Mlimani (Mathayo 5-7), unaweza ukaweka umakini zaidi katika sura hizo. Lakini pia utahitaji kusoma injili nzima ya Mathayo.
Chunguza jinsi mwandishi anavyotoa mawazo yake. Njia yake itategemea na aina ya kitabu ilivyo. Unapokisoma, utaona kitani ya mawazo ikijifunua. Chunguza jinsi mwandishi anavyoanza hotuba yake na ponti zake kuu ni zipi. Ikiwa anahoji juu ya wazo, chunguza aina za hoja anazozitumia. Angalia lugha zake za picha na tambua maana yake. Acha kitabu kizima kikuvutie mpaka moyoni.
Zigawe sehemu ulizozichagua katika vifungu vya mahubiri. Kila ujumbe katika kitabu utahitaji kifungu maalum. Inawezekana Biblia yako ikawa na kifungu kilichogawanywa katika vifungu vingi. Vifungu hivi vya kusoma mara zote vitakuwa ni njia nzuri ya kupanga mfululizo wako. Nyakati zingine utatumia mahubiri mawili katika kifungu kimoja . Nyakati zingine, unaweza kutumia vifungu viwili au vitatu katika mahubiri ya wakati mmoja. Katika sehemu za masimulizi kifungu cha mahubiri kinaweza kuwa kirefu kuliko kile cha Nyaraka za Agano Jipya.
Panga kalenda za mfululizo wa jumbe. Unaweza kuwa unazungumza kila wiki kwa kusanyiko lile lile. Ikiwa ndio hivyo utaweza kuandaa kalenda kwa ajili ya wiki zijazo. Ikiwa unakuwa katika kikundi kwa nyakati Fulani tu, bado unaweza kuendelea na
Kupanga mtiririko. Soma kitabu cha Biblia. Chunguza mtiririko wa mawazo ya mwandishi. Igawe habari katika vifungo vya kifungu. Andaa chati ya mtiririko. Panga tarehe za mtiririko
112
mfululizo. Zinapotokea siku kuu au matukio maalum, utahitaji kuuingilia mfululizo kwa ajili ya tukio hilo.
Andaa Chati ya Mfululizo.
Kupanga mfululizo wako katika kalenda ni njia moja wapo ya kuuleta mbele yako kwa karatasi. Kabla hauja ifikia kalenda, unaweza kupanga chati ya mfululizo wote, ikiwa na notsi kwa ajili ya kila kifungu.
Hapa kuna Chati niliyoitengeneza kupanga mfululizo kutoka katika mahubiri ya mlimani Nilipitia sehemu nzima (Mathayo 5– 7) na nikakigawa kifungu katika sehemu kwa kila ujumbe. Chati hii inashughulika na sura ya kwanza tu ya sura hizo tatu. Katika hiyo nimeorodhesha namba ya ujumbe, kifungu, kiini cha kifungu, na kichwa cha habari cha mahubiri yangu. Nimeongeza pia uchunguzi wangu kuhusu kifungu, lakini hakuna nafasi hapa kwa hayo yote.
Mathayo 5 Mfululizo wa mahubiri ya Mlimani.
1
5:1 & 2
Utangulizi wa mfululizo.
Alama za ufalme wa mwanadamu.
2
5:3 - 6
Heri, sehemu ya 1
Hali inayokubadilisha
3
5:7-12
Heri, sehemu ya 2
Njia za ajabu kupitia.
4
5:13-16
Chumvi na Nuru.
Kushawishi Ulimwengu wako.
5
5:17-20
Yesu ana timiza sheria
Kutimiza maadili ya sheria ya Mungu
6
5:21-26
Kuua ndani ya Moyo
Sumu ya hasira
7
5:27-32
Uasherati na ndoa.
Nguvu ya usafi wa kujamiana
8
5:33-37
Yesu anazua viapo
Kuzungumza ukweli rahisi
9
5:38-42
Kwenda maili ya pili
Kutoa msamaha wa ukarimu
10
5:43-48
Kuwapenda adui zako.
Kuwapenda wale usiowapenda.
"Kwa maana, amini, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yoda moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.”
Mathayo 5:18
113
Angalia kwamba nimezigawa heri kwa jumbe mbili. Zinaonekana kuchukua sehemu kubwa sana kiasi kwamba sikuweza kuishughulikia yote hiyo katika kipindi kimoja. Mgawanyo ulifanya kazi vizuri nilipoupa kila ujumbe kichwa chake cha habari.
Angalia kwamba vichwa vimeandikwa kuwaelezea wasikilizaji kulingana na mazoea yao wenyewe. Si vichwa vya misingi mikuuu ya Imani, hata kama ujumbe unatoa ukweli wa kithiolojia. Mahubiri ni hotuba ya mjumbe kwa wasikilizaji wake. Inachukua ukweli wa Biblia na kuwapa watu kwa aina yao. Kuhubiri ni kwa kizazi hiki ujumbe ni kwa ajili ya hali zao wenyewe za maisha.
Umuhimu wa Mfululizo.
Utaona faida nyingi sana katika kupanga jumbe zako kwa mfululizo kupitia kitabu cha Biblia. Hapa kuna baadhi ya faida hizi.
Utaisoma Biblia yote kwa undani wewe mwenyewe. Katika kitabu hiki unajifunza njia zinazochukua Biblia kwa dhati. Mjumbe wa Mungu anakuwa mwaminifu pale tu anapotoa ujumbe wa Mungu kutoka katika Neno la Mungu lililoandikwa. Jumbe za Biblia zinazofaa zinahitaji usomaji wa kifungu kama jinsi kilivyoandikwa. Kukifahamu kitabu chote kitasaidia kuleta maana ya kila sehemu.
Utaepuka kujifunga mwenyewe katika masomo unayoyapendelea. Wahubiri huwa wanashughulika sana na viini wanavyovipenda katika mahubiri yao. Nyakati zingine wamekuwa wakihubiri ujumbe ule ule tena na tena na tena, haijalishi wanasoma kifungu gani. Mjumbe mwaminifu atashughulika kwa makini na ujumbe wa asili wa kifungu. Kiini cha ujumbe ndicho kitakachokuwa kiini cha mahubiri yake.
Hauhitaji kutafuta ujumbe katika dakika za mwisho. Wachungaji wana shughuli nyingi, kama walivyo wapandaji wa makanisa, wainjilisti na wamishonari.Kupanga mfululizo wa jumbe kutoka katika kitabu zinaweka kifungu na kiini kwa kila tukio. Hakuna haja ya kutafuta ujumbe katika dakika za mwisho.
Faida za mtiririko. Soma Biblia kikamilifu zaidi. Epuka kuwekea mipaka masomo unayopendelea Usitafute kifungu dakika ya mwisho. Watu wanakuwa wanaifahamu Biblia Watu wanavutiwa kuisoma Biblia
114
Watu watafahamu mafundisho ya vitabu vyote. Kwa waamini wengi Biblia ni siri. Wamejichimbia hapa na pale kusoma kifungu wanachokipenda.Hawawezi kuona inavyokwenda yote pamoja. Hawana ufahamu wa hadithi kubwa ya andiko. Kuhubiri kupitia vitabu kutawaweka watu katika sehemu kuu za hivyo vitabu. Wataanza kuona picha kubwa. Watu watatiwa shauku zaidi ya kusoma Biblia wao wenyewe. Nimetembelea makanisa mengi sana ambayo washilika hawaji na Biblia kwenye Ibaada. Hawazihitaji kwa sababu Mchungaji hafuati kifungu. Hawakuhamasishwa kuisoma Biblia pamoja na mchungaji. Na wala hawakuhamasishwa kuisoma wao wenyewe. Mahubiri ya kufafanuliwa kupitia vitabu yatasaidia katika swala hili la muhimu.
Mazoezi ya Somo.
1. Rudia mawazo makuu ya somo hili: Mjumbe wa Mungu anaweza akapanga mafungu ya jumbe kutoka katika kitabu kwa ajili ya kuhubiriwa katika mfululizo. Mahitaji na hali za watu zitamsaidia kuamua mfululizo gani wa kupanga. Anaweza akachukua hatua maalum ambazo zitamfungulia kitabu cha Biblia kwa ajili ya kupanga mfululizo unaofaa. Kuhubiri kupitia vitabu vya Biblia kuna faida nyingi sana kwa mtumishi na watu vilevile.
2. Chagua kitabu au sehemu ya kitabu unachotaka kuhubiri kwa watu wako. Chukua hatua zilizoshauriwa katika somo hili katika kusoma kwako kitabu. Panga mfululizo katika chati kama ilivyo katika chati ya hapo juu. Usijali ikiwa hauna uhakika ikiwa unavyo fanya ni sahihi au la. Kadiri unavyofanyia kazi hili, ndivyo jinsi ambavyo hatua hii itakavyoeleweka.
115
Somo la 20
KKuuuujjeennggaa MMwwiillii..
Sasa tumefika katika somo letu la mwisho katika kujifunza jinsi ya kuandaa jumbe za Biblia. Msisitizo wetu katika somo zima umekuwa ni kwmba Mjumbe wa Mungu ni lazima ahubiri na kufundisha kutoka katika Neno la Mungu lililoandikwa. Hapo ndipo atakapo kuwa mwaminifu katika wito wake. Na ni hapo tu ndipo watu wa Mungu “watakapobadilishwa” mawazo yao yanapofanywa upya kwa kweli ya Mungu (Warumi 12:2).
Katika somo hili tutafikiri juu ya kanisa. Mjumbe wa Mungu analo jukumu Maalumu juu ya afya na kazi ya kanisa. Anapolitangaza neno la Mungu, atatumiwa na Mungu kuwaleta wasikilizayi kwa ukomavu katika Kristo.
Kanisa ni nini?
Biblia imetumia picha nyingi sana kuzungumza juu ya kanisa. Kila moja wapo wa picha hizi zinatusaidia kuelewa jukumu la kanisa katika ulimwengu. Watu wa Mungu wasipojielewa wao ni nani, hawatakuwa waaminifu kumtumikia Mungu katika ulimwengu. Hapa kuna baadhi ya picha hizi:
Kanisa ni “mwili wa Kristo” (1Wakorintho 12:27). Yesu hayupo kimwili duniani leo. Lakini waamini ndio mwili wake hapa. Wao ni mikono yake kuwahudumia wengine. Wao ni sauti yake kutangaza habari njema. Wao ni miguu yake kwenda ulimwenguni kote. Wao kwa kila mtu bihafsi ni mwili mmoja wakihudumia kulingana na vipawa vyao.
Kanisa ni “hekalu takatifu” (Waefeso 2:21). Wao ni nyumba ya kiroho, ukuhani mtakatifu, kutoa sadaka za kiroho zinazokubalika kwa
Somo la 20
Mjumbe wa Mungu ni wakala wa Mungu kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo kwa huduma ya neno.
116
Mungu kupitia Yesu Kristo” (1Petro 2:5). Hii inafanyika kwa ibaada ya watu wa Mungu. Haifanyiki kwa majengo ya kanisa. Watu wenyewe ni hekalu kwa ajili ya kuabudia. Na kila mwili wa mwamini ni “hekalu la Roho Mtakatifu” (1Wakorintho 6:19). Popote wanapokusanyika kwa ajili ya Ibaada panafanyika hekalu halisi la Mungu.
Kanisa ni “watu wa Mungu” (1 Petro 2:10). Mwanzo hawakuwa watu, lakini sasa ni “kizazi kiteule, ukuhani mkuu, taifa takatifu, watu wake maalum” (1 Petro 2:9). Kati ya makabiia na lugha zote za duniani, hakuna aliye na wadhifa huu. Wanayo kazi maalum: “kutangaza sifa zake yeye aliyewaita kutoka katika giza kuingia katika nuru yake ya ajabu” (1 Petro 2:9). Wanapaswa kuuambia ulimwengu kile ambacho Mungu amefanya kwako kupitia Kristo. Kanisa ni “kondoo wa Mungu” (1 Petro 5:2). Wao ni kondoo na Yesu ni mchungaji mwema (Yohana 10:11). Mtumishi wa Mungu ni mchungaji chini ya “Mchungaji mkuu” (1 Petro 5:4). Yeye si “mgeni,” “mwizi,” au “mtu wa mshahara” (Yohana 10:1-14). Huduma yake ni kuwalisha kondoo na kuwatunza wanakondoo. Anawaongoza, anawalinda, na kuwalisha. Picha zote hizi za kanisa katika dunia zinawaelezea watu wa Mungu. Hazihusu majengo ya kanisa au vifaa vya kanisa. Zinahusu viumbe hai na si mipangilio. Mjumbe wa Mungu ni lazima awe mwangalifu asizingatia vifaa vya kanisa badala ya watu.
Kuwatayarisha Watakatifu
Mjumbe wa Mungu anaweza akatumika katika kazi mbalimbali, kulingana na wito na vipawa vya Mungu. Paulo anaandika kwamba “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu, kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe.” (Waefeso 4:11) kumbuka kwamba kusudi la haya yote ni “kujenga mwili wa Kristo.” Hii ina maana kuwajenga watu wa Mungu.
Picha za Kanisa
Mwili wa Kristo Hekalu Takatifu Watu wa Mungu Kondoo wa Mungu
117
Kama ilivyo katika kujenga jengo, Mjumbe wa Mungu anapaswa kuujenga mwili wa kanisa. Haswa hii inawalenga zaidi wachungaji. Hii haimaanishi kujenga jengo la Kanisa. Ina maana kulitia nguvu kusanyiko. Mstari wa juu unaendelea, “hata na sisi wote tutakapo ufikia umoja wa imani na kumfahamu sana mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo.” (Waefeso 4:13)
Je, “Kujengwa huku” kunakamilishwaje? Kifungu kinasema kwamba Mungu alitoa watumishi hawa wenye vipawa “kwa ajili ya kuwatayarisha watakatifu kwa ajili ya kazi ya huduma” (Waefeso 4:12). Kuwakamilisha huku kuna maana “kuwaandaa” au kuwakamilisha”. Ina maana pia “kurekebisha.” Mtumishi wa Mungu anapaswa kuwatumikia watu wa kanisa katika njia ambazo zitakazowafanya wawe tayari kwa ajili ya kazi yao.
Kazi ya waamini inaeleweka pia katika mistari hii. Mtumishi wa Mungu anapaswa kuwatayarisha kwa “kazi ya huduma.” Wanatayarishwa kumtumikia Mungu. Wanapaswa kufanya kazi ya huduma katika kanisa na katika ulimwengu.Wale wanaoitwa na Mungu kuwa ni watumishi si wale tu wanao fanya kazi ya huduma. Ni “watakatifu,” waamini ambao wapo kanisani. Wanapaswa kufanya kazi ya Mungu katika ulimwengu, wakiwa na watumishi wa Mungu wakiwaongoza na kuwatayarisha.
Matokeo yapo pia katika mstari. Watu wanapaswa kuwa katika umoja. Wanapaswa kuwa pamoja katika njia fulani za muhimu. Kazi ya Watumishi walioitwa na Mungu ni kuwaleta katika umoja huo. Umoja wao unatakiwa kuwa katika maeneo mawili maalum. Wanatakiwa kuwa wamoja katika “imani” na wamoja katika ufahamu wa mwana wa Mungu” (Waefeso 4:13). Ni kupitia mafundisho pekee ya Neno la Mungu lililoandikwa ndio watu watakapokuja katika mtazamo mmoja wa imani yao, kweli kuu wanazoziamini. Hawatakuja kamwe katika umoja katika uhusiano wao na Kristo Mbali na kulijua Neno la Mungu.
Kama vile ujenzi wa kawaida, Mjumbe wa Mungu anapaswa kujenga mwili wa kanisa. Hii haimaanishi kujenga jengo la kanisa. Inamaana kulipa nguvu kusanyiko.
118
Tafsiri ya Ki-Mungu.
Kuna kusudi moja katika kuhubiri ambalo linafunika zingine zote. Lengo kuu la mahubiri yote ni kuamsha mwitikio wa imani katika Mungu. Haijalishi kifungu gani kimetumika, mjumbe wa Mungu ni lazima aelekeze kwake (Mungu) na kuwataka watu wamwamini Yeye. Hii inahitaji mahubiri na mafundisho ambayo ni ya Ki-Mungu (yanayomuhusu Mungu) na si ya Ki-binadamu (yanayomuhusu mwanadamu).
Unaweza kukitafsiri kifungu chochote kile kwa njia ya ki-binadamu au ya Ki-Mungu. Wahubiri wamekuwa wanaupendeleo kwa tafsiri ya Ki-binadamu. Kwa watumishi wengi lengo kuu la kuhubiri ni kubadilisha tabia na nia za watu. Mara zote matokeo yamahubiri kama hayo yanakuwa ni kurekebisha maadili tu. Lakini ni lazima tukumbuke kwamba mabadiliko yanayohitajika kwa mtu si ya kimaadili tu. Msikiaji anahitaji kumwamini Kristo kwa mabadiliko yatakayomfanya kuwa “kiumbe kipya” (2 Wakorintho 5:17). Mabadiliko ya kimaadili tunayoyatafuta yatakuja katika kumwamini Mungu kiundani. Ikiwa Mtu anatafuta kujibadilisha yeye mwenyewe pasipo imani, anaanguka kutoka katika neema. (Wagalatia 5:4). Anajitenga kutoka kwa Kristo kwa sababu anatafuta kuwa haki kwa sheria. Muhubiri yeyote asisitize kumwendea Mungu ambako hakuhusishi neema yake pekee. Mahubiri yamuhusuyo Mungu yanasisitiza ukweli wa Mungu kwa watu. Kila kifungu kinachukuliwa kulingana na kile kinavyofunua kuhusu Mungu. Mjumbe wa Mungu anatafuta kifungu chake kwa ajili ya ukweli kuhusu tabia ya Mungu, nguvu ya Mungu, lengo la Mungu na uaminifu wa Mungu kwa wakati uliopita. Kifungu kinapotafasiliwa katika kuonyesha Mungu yu nani na anaweza kufanya nini, watu wataingia katika imani. Mtazamo ni kwa Mungu.
Wahubiri wengine watakuwa na mashaka na njia hii ya kuhubiri. Wanaona hitaji kubwa la watu kuacha maisha yao ya zamani ya dhambi na kulitii neno la Mungu kama wakristo wa Kweli. Hawana uhakika jinsi gani mahubiri kuhusu Mungu ni nani itakamilisha hilo.
Mjumbe wa Mungu anatafuta kifungu chake kwa ajili ya ukweli kuhusu tabia ya Mungu, nguvu ya Mungu, makusudi ya Mungu na uaminifu wa Mungu wakati uliopita.
119
Lakini kumbuka kwamba maono ya Mungu siku zote huelekeza katika toba.
Picha inaeleweka – maono ya utakatifu wa Mungu yanaamsha toba na kukili. Katika maono ya hekaluni Isaya alimuona Mungu “ameinuliwa juu” (Isaya 6:1) Mwisho, mwitikio wake ulikuwa kulia kuhusu uchafu wake. (Isaya 6:5). Angalia pia mwitikio wa Petro kwa Yesu alipouona uweza wake kwa kukamata samaki. Alianguka magotini kwake na kumlilia Yesu, “Ondoka kwangu, maana mimi ni mwenye dhambi, Ee Bwana!” (Luka 5:8)
Jinsiukionavyo Kifungu
Asili ya ubinadamu ya muhubiri mwenyewe inaweza kusababisha pia upendeleo unaoweza kuathiri mahubiri yake. Anaweza kuwa mkinzani sana wa watu kwa ajili ya udunia wao. Anaweza kuwa si mvumilivu kwamba watu ni wapole sana kujifunza. Anaweza kukatishwa tamaa na wale aliokuwa anawatumaini kuwa waaminifu. Anaweza akashughulika kwa kushidwa kwake na vikwazo vyake. Hisia zote hizi na mitazamo hii inaweza kuonekana katika mahubiri. Mjumbe siku zote anaacha alama zake katika ujumbe, hata kama haigundui hiyo.
Hebu nishauri kwamba ujiulize tafsiri ya ki-mungu ingekuwa ipi kwa kile kifungu. Vifungu vingine havina kitu cha kusema juu ya sifa za Mungu. Lakini utahitaji kuvitafsiri vifungu hivi katika nuru ya ujumbe mzima wa Biblia. Kila amri katika andiko iko katika msingi wa tabia za Mungu. Kila kifungu kinachoonesha dhambi mizizi yake ni katika asili ya Mungu. Kila kifungu kinachoelezea wokovu tulionao katika Kristo kinaonesha asili ya Mungu. Ukweli wote kuwa thihirishotu Pale unapoliona jambo hili.
Unapokisoma kifungu, unaweza ukakiangalia kwa makini juu ya kile kinachosema na kugundua ujumbe wa Ki-Mungu uliopo pale. Angalia kila wazo katika kifungu juu ya tabia na mapenzi ya Mungu. Ikiwa kifungu kina maelekezo, jiulize kwa nini Mungu angeyatoa. Ikiwa kifungu kinashughulika na dhambi, jiulize hapo pana nini juu ya Mungu
Asili ya ubinadamu ya muhubiri mwenyewe inaweza pia kusababisha upendeleo ambao una athiri mahubiri yake. Mjumbe siku zote anaacha alama yake katika ujumbe, hata kama haugundui
120
kwamba akatae tabia hiyo. Kuelezea muunganiko huu kwa kusanyiko utafungua kweli ya kifungu kwako katika njia bora zaidi.
Mjumbe wa Mungu ameshikamana sana na wito wake kiasi kwamba anaweza kufikiri kazi ya kanisa inamzunguka yeye. Lakini ni kanisa la Mungu. Ni kazi ya Mungu. Ni kusudi la Mungu. Kazi ya huduma kabisa hainihusu mimi wala wewe kama watumishi wa Mungu. Ni juu ya kile Mungu anachofanya. Tumepata nafasi kwa neema kuitwa katika huduma yake. Na tunatarajiwa kuwa waaminifu. Lakini tunajua kuwa ni “lazima tumtazame Yesu, yeye aliyemwanzilishi na mtimizaji wa imani yetu” (Waebrania 12:2). Na lazima tuwaelekeze watu kwake.
Mazoezi ya Somo.
1. Rudia mawazo makuu ya somo hili: Agano Jipya linatumia picha nyingi za maneno kuelezea kanisa. Mjumbe wa Mungu ameitwa “kulijenga” kanisa kwa “kuwakamilisha” waamini kwa ajili ya kazi ya huduma. Mahubiri ya Ki-Mungu yatakuwa yanafaa zaidi kuliko ya Ki-binadamu katika kuongeza imani za watu.
2. Angalia vifungu ambavo tumekwisha kuvisoma. Fikiri juu ya jinsi gani vinaweza kuwa msaada katika “kuwatayarisha watakatifu” na “kuuandaa mwili wa Kristo.” Inachukua nini kuwatia ngvu na kuwalisha kondoo wa Mungu?
“Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyo mpasa kunia; bali awe na nia ya kiasi kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi.”
Warumi 12:3
121
Kwa Mwalimu.
Kitabu cha Kuandaa jumbe za Biblia kiliundwa kwa matumizi binafsi. Kwa muongozo mdogo sana, mtenda kazi mkristo anayejuu kusome anaweza kuelewa na kutumia ujumbe uliotolewa katika somo hili.Walengwa wa kwanza kabisa wa somo hili walikuwa ni wapandaji wa makanisa na wachungaji mastadi. Kwa sababu hiyo kiwango cha elimu kinachohitajika kutumia kitabu hiki kiliwekwa katika kiwango cha msingi. Tafsiri katika baadhi ya lugha zinaweza kuandikwa katika kiwango kigumu zaidi kutokana na historia ya elimu na taaluma katika kundi la lugha hiyo.
Kitabu cha msingi cha kujifunzia katika somo hili ni Biblia. Somo limeundwa kumsaidia mwanafunzi kutumia njia maalum kwa ajili ya kuandaa jumbe za Biblia. Sehemu ya kwanza ya njia hii ni usomaji wa umakini wa kifungu maalum cha Biblia ili kugundua maana ya kithiolojia iliyokusudiwa ya kifungu hicho. Sehemu ya pili inahusisha maelezo ya kweli hizo za kithiolojia na mawazo saidizi kwa ajili ya wasikilizaji wa wakati ule. Sehemu ya tatu ya kuandaa ujumbe wa Biblia inahusisha kufuata mfano wa Yesu katika matumizi ya matumizi na vielelezo. Kwa vipengele hivi katika kuangalia mjumbe wa Mungu ataweza kupanga kidokezo cha ujumbe wake katika namna inayofanana na maana ya kifungu na wahusika wa wakati ule waliokusudiwa.
Lengo kuu la somo hili ni kumfanya mwanafunzi ajifunze njia hii. Hata hivyo, lengo mahususi, ni kwa ajili ya watenda kazi wa kikristo kushughulika na wajibu wao wa kuhubiri na kufundisha kwa kuiacha Biblia izungumze kupitia vifungu vyake mbalimbali. Somo halikuundwa kwa ajili ya kujikumbusha mawazo mbalimbali katika kitabu. Ilitengenezwa kwa ajili ya kushughulika na kifungu maalum cha Biblia kwa kutumia mbinu maalum za kusoma. Mwanafunzi akumbushwe kwamba atapanua ujuzi wake katika kutumia mbinu hizi pale tu atakapokuwa akizitumia mara kwa mara kwa vifungu husika vya andiko.
Hata kama usomaji wa kibinafsi unaweza kufaa, njia inayopendelewa zaidi ni ya kutumia kitabu hiki kwa kuwa na wanafunzi katika makundi. Makundi ya wanafunzi watatu au wane watajifunza kwa haraka zaidi wakisaidiana kila mmoja katika kusoma.Wanafunzi dhaifu watapokea kutoka kwa wanafunzi waelevu. Ile hali ya kuwajibika na kusaidiana itafanikisha kujifunza. Hata kama darasa kubwa litakuwa likikutana mara kwa mara kupitia masomo, makundi madogo madogo ya watu watatu au wane yaendelee kufanya pamoja mara kwa mara kadili wawezavyo.
Mbunifu wa somo hili anatumaini kuwa wamishonari, wachungaji, viongozi wa dini, na watendakazi wengine wa kikristo walio na uzoefu watachukua wajibu wa kuwafundisha wengine watakao furahishwa. Wajumbe walioitwa na Mungu hawapokei wito wao pamoja na ufahamu unaohitajika kwa kutafsiri Biblia kikamifu. Wanahitaji mafunzo. Haiwezekani na haishauriwi kuwachukua watenda kazi kutoka katika maeneo yao kwa ajili ya mafunzo ya ngazi za juu. Wale
122
walioitwa kusoma vyuo na seminari za mafunzo na wafanye hivyo. Lakini kundi kubwa la watenda kazi wa Kikristo ulimwenguni kote wataendelea kuwa wazoefu zaidi pasipo hata na elimu hiyo ya juu. Wakiwa na Biblia mkononi na uelewa wa jinsi ya kutangaza kweli yake, wanaweza “kuwaandaa watakatifu kwa kazi ya huduma” katika njia inayofaa. (Waefeso 4:12). Ikiwa shughuli za upandaji wa makanisa duniani kote zingetakiwa kusubiri elimu ya juu. Ingeishia katika kuchechemea. Mungu anainua watumishi wake katika makundi ya watu katika ulimwengu wote kuwafikia watu na habari njema za Kristo na kuwakusanya katika makanisa ya Agano Jipya. Makanisa haya mapya yaliyopandwa lazima yawe na mafundisho thabiti ya Biblia ili kuendelea kukua, na kuwa makanisa yanayojizalisha. Mwalimu katika somo hili anahitaji kufahamu tu na kutumia njia hii katika huduma yake mwenyewe ya mahubiri. Atakapo kuwa akihudumia Neno la Mugu katika njia hii yeye mwenyewe, anaweza akafundisha pia njia hii kwa wengine. Haijalishi anafanya kazi na mwanafunzi mmoja tu, au kumi na mbili, anaweza kuizidisha huduma yake.
Kitabu hiki ni bure, ila kwa gharama ya uchapishaji wa ndani. Wayne McDill imefanya kitabu inapatikana kwenye line kwa ajili ya wote ambao wangependa kutumia. Unaweza kwenda kwenye tovuti kwa ajili ya kitabu na magazeti kama wengi kama unataka (www.waynemcdill.net). Wayne McDill Southeastern Baptist Theological Seminary Wake Forest, North Carolina USA

No comments:

Post a Comment