Sunday 30 November 2014

JINSI YA KUHUBIRI

MPANGO WA KUFANYA NA KUSAIDIA
AFRIKA MASHARIKI NA KATI
CHURCH OF GOD WORLD MISSIONS
MAFUNDISHO YA
MAHUBIRI YA PENTEKOTE
Peter A. Thomas
Translation: Richard M. Sitati, Nairobi, Kenya
2
Yaliyomo
Utangulizi
I. Mhubiri
A. Ufafanuzi
B. Mahitaji ya Mhubiri
1. Mwito wa Mungu
a. Mwito wa Kweli
b. Ushahidi wa Mwito
c. Mwito wa Mungu na Kazi ya Kiulimwengu
2. Mahitaji ya Roho
a. Kujazwa na Roho Mtakatifu
b. Mtu wa Neno
c. Mtu wa Maombi
3. Sifa Nyingine
C. Nafsi ya Mhubiri
1. Halali na Ukamilifu
2. Uhuru kutoka kwa Wivu
3. Nidhamu
II. KUHUBIRI! NI KITU GANI?
A. Kuhubiri na Kufundisha
B. Kuhubiri na Unabii
C. Lengo la Kuhubiri
1. Lengo la Jumla
2. Lengo Halisi
a. Kuhubiri ili Kuleta Mabadiliko
(1) Kuhubiri Msalaba wa Wokovu
(2) Kuhubiri Msalaba kufanya wengi Wanafunzi
b. Kuongoza kwa Shauri
D. Tangaza Ujumbe wa Mungu
E. Neno la Kuonya
III. Andiko
A. Kupata Maandiko na Kupokea Ujumbe
1. Njia ya Kutafuta Andiko Nzuri
2. Ujumbe na Andiko
3. Kukosa Kupata Andiko
B. Nguvu za Mahubiri
1. Kufikiria Mahitaji ya Kiroho
2. Kukaa chini ya Miguu ya Mungu
3. Kuangalia Mambo ya Dunia
4. Kufikiria Safari ya Kiroho ya Mhuduma
5. Kufikiria Kalenda ya Mhuduma
6. Kusudi Kamili la Mafundisho ya Biblia ya Ukristo
7. Uimarishaji wa Daktari
8. Kujaza Akili na Neno la Mungu
3
C. Uangalifu Katika Uchaguzi wa Andiko au Somo
1. Usiahidi kile ambacho hauwezi Kupeana
2. Usichague Maandiko ya Mzaha
3. Muda bora wa Maandiko
4. Andiko na Yaliyomo
5. Kuangalia kwa Hakika
IV. Mambo ya Utafsiri
A. Kuanzisha Maana ya Ukweli ya Maandiko
1. Asili ya Maana ya maandiko
2. Kufikiria Juu
3. Muda, Tabia na Sifa za Andiko
4. Linganisha Andiko naAndiko Lingie
B. Mfano - Kufanyika Kiroho
VII. MAHUBRI MBALIMBALI
A. Maneno Menyewe ya Mahubiri
B. Mahubiri ya Kuonyesha Wazi
C. Mahubiri yanayozungumziwa na Watu
D. Uinjilisti na Mahubiri ya Uchungaji
V. MATAYARISHO YA MAHUBIRI
A. Utangulizi
1. Uwezo wa Utangulizi
a. Anza na (Ma) swali
b. Anza na Jambo la Kusisimua
c. Anza na Andiko
d. Anza na yaliyomo
e. Anza na Muda, Tabia na Desturi
f. Anza na Hadithi au Maelezo
g. Anza na Mambo ya Wakati Uleule
h. Anza na Uteuzi
B. Nafasi ya Mahubiri
1. Mpango ya Nafsi ya Mahubiri
a. Maneno Yenyewe na Mahubiri ya KuonyeshaWazi
b. Mahubiri ya Kuzungumziwa na Watu
2. Mahitaji ya Utaratibu
a. Umoja na Heshima
b. Utaratibu wa Hakika na Kanuni
c. Ulinganifu (Usawa kadiri)
d. Mfululizo au Utiririkaji wa Mahubiri
C. Kuonyesha Wazi Kwa Maandiko
D. Mwisho
1. Njia Mbalimbali za Kumalizia Mahubiri
a. Kurudia Mahubiri kwa Welekevu
b. Kudhihirisha Ubusara
c. Maelezo
d. Linganisha
e. Kusihi kwa Maombi
2. Kumalizia Kwa Urefu
3. Mambo ya Kufanya na Yale Usiyo hitaji Kufanya
4
VI. MAELEZO
A. Sheria za Kutumia Maelezo
1. Urahisi
2. Ukweli
3. Nyumba ya madirisha au madirisha kwa nyumba
4. Madhumuni
B. Mwanzo wa Maelezo
C. Mengi ya Kufikiria
VIII. KUPEANA UJUMBE
A. Kujitayarisha Kuzungumza
1. Maneno ya Kukumbusha na Maandiko ambayo Yameandikwa
2. mahubiri kwa Urefu
3. Ujue Biblia
4. Kutangaza Kiini cha Mahubiri
B. Kuhubiri Ujumbe
1. Umuhimu wa Hotuba Nzuri
2. Kuangalia Umati
3. Kuoyesha kwa Mikono - Mambo ya Kufanya na Yale Ambayo Hatuhitaji Kufanya
4. Mengi ya Kukumbuka
IX. MWISHO
A. Kuweka wakfu
1. Vile Unaweza Kuendeleza
2. Wakati Hakuna Upako
B. Jambo la Muujiza Katika Ibada
C. Huduma wa Madhabahu
D. MWISHO
5
MAFUNDISHO YA MAHUBIRI YA PENTEKOTE
Utangulizi
Kulingana na watetaji wake, mahubiri ya kipentekote yameelezwa kama mapotovu, ya
masikitiko, yasiyo na utabiri, bila shabaha na ya kale. Mahubiri ya kweli ya kipentekosti
yanaelezwa kuwa wakati mwingine yenye sauti ya juu na masikitiko, lakini kwa hakika yasiwe
bila utaratibu na yasiyokubalika. Kwa kuanzia siku ile ya kipentekote ya mwanzoni, mahubiri ya
ukristo ya kiajabu yameelezwa katika Agano Jipya lote, kama yaliyo na utaratibu, na
yanayokubalika, na yenye kusudi fulani. Haya yote yameonekana katika mahubiri ambayo
yameandikwa na pia vile yametajwa katika waraka ambao ni wa mahubiri ya Kipentekote/
kufundisha katika maandiko ambayo yameandikwa. Wahubiri wengine wa kipentekote na
wainjilisti wamesababisha hali ya kutofahamu vema. Kuna wale wanaoamini kwamba mahubiri
ambayo yana upako ni sawa na kuhubiri kwa sauti ya juu, kutetemeka kwa kidevu, kuzungumza
kwa haraka bila kuwa na nafasi ya kupumua sentenzi, kukimbia hapa na pale kanisani, kuruka
kutoka kwa jukwa, na tabia nyingine za kiajabu. Halafu kuna wale ambao wanaamini kwamba
mahubiri ya kipentekote hayahitaji matayarisho kwa sababu Mungu atajaza mdomo wetu kama
tunaweza kuufungua wazi (Zaburi 81:10).
Tunapoendelea kuimarisha mahubiri ya kipentekote ya kiajabu, tutaangalia kwa ufupi imani hizi
nyingine na matendo yake, na kuonyesha mahali wanafanya vibaya. Kusudi kuu la somo hili ni,
kupeana mashauri ya wazi ya kufaa, lengo na kusudi la kuweka mambo sawasawa, mambo ya
kibiblia, mahubiri ya kipentekote. Na kwa hivyo, tunajaribu kupata yafwatayo:
1. Kufikiria sifa na nafsi ya mhubiri wa kipentekote.
2. Kuelezea maana ya kuhubiri na kuanzisha kusudi lake na lengo.
3. Kuonyesha vile tunaweza kutafuta Andiko na ujumbe. Kupeana mashauri vile
tunaweza kupokea mvuto wa mahubiri.
4. Kuonyesha wazi mambo ya msingi ya kutafsiri maandiko (hermenentics).
5. Kuonyesha tofauti na ajabu ya maandiko, kuweka wazi na mahubiri
yanayoshughulisha fikira za watu.
6. Kuelezea ustadi wa matayarisho ya mahubiri, kwa kupeana mashauri ya wazi
vile tunaweza kupeana utangulizi, mwili wa mahubiri na mwisho, pamoja na
kutumia maelezo.
7. Kupeana mashauri ya wazi ya kupeana ujumbe, pamoja na urefu wa mahubiri,
hotuba na ishara.
8. Kuonyesha wazi umuhimu wa upako, nguvu za kiajabu katika ibada na huduma
wa madhabahu, tukifikiria hatari za wazi na udhulumu wa sehemu hizi.
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-..-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.
6
I. Mhubiri
Kuhubiri ni neno la asili katika Agano la Kale, mahali ambapo manabii walitangaza mapenzi ya
Mungu kwa watu wa Israeli, kwa hivyo, walikuja kuwa “wahubiri” wa kwanza. Katika Agano
Jipya, Yohana mbatizaji aliendeleza huduma wao, kama nabii wa mwisho wa Agano la Kale na
pia kama mjumbe wa Mungu wa kwanza wa Agano Jipya. Alifwatiwa na Petro, Yohana,
Yakobo, Paulo na mitume wengine, ambao wote walikuwa wahubiri wa kutangaza au walihubiri
ujumbe wa Mungu. Ingawa kuhubiri kuna asili yake katika Agano la Kale, lakini kunaonyesha
mwanzo wa Agano Jipya, ambao umekuja kuwa sifa ya imani ya mkristo.
Mungu amemchagua mtu mdhaifu kutangaza mapenzi yake. Angewatuma malaika, au kubuni
mpango tofauti wa kueneza ujumbe wake, lakini amewachagua wanaume na wanawake
kutangaza mapenzi yake kupitia huduma wa kuhubiri.
A. Ufafanuzi
Neno mhubiri (Kigriki-Kerux) linatumiwa mara nyingi katika Agano Jipya ambalo
linazungumzia mjumbe akitoa matangazo (Warumi 10:14, 1 Timotheo 2:7, 2 Timotheo 1:11 na 2
Petro 2:5). Kwa hivyo, haikuwekewa mkazo tu kwa huduma fulani, bali inahusika pia kama
mitume, wachungaji, wainjilisti, manabii kama wahubiri, na wale wote wanaotangaza (wajumbe)
ujumbe wa Mungu. Huduma huu wote ukiwa na sifa zake, wote unakuwa chini ya neno moja la
kawaida “mhubiri”. Katikasomo hili, neno hili linatumiwa kwa wale wote wanaopeana ujumbe
wa Mungu bila kujali mwito halisi ambao unaenda pamoja na huduma wao.
Ni jambo la kupendeza kwamba neno la kigriki au kiyunani linalotafsiriwa kumaanisha mhubiri
linaonyesha mtu anayezungumza na nguvu za mamlaka ya juu ambaye ujumbe wake
anautekeleza bila mapatano.1 Anaenda katika hali ya wazi. Kile anachoangaza kiztakuja kuwa
kitendo wakati amekitangaza Mhubiri
1. Mwito wa Mungu
Kufwatiwa kuzaliwa upya, mwito wa utakatifu ni sifa muhimu ya mhubiri. Bila huu mwito,
mhubiri hatakuwa na huduma. Kwa hivyo, ni jambo la muhimu kufahamu mwito wa Mungu na
vile unadhihirishwa.
Mwito wa kuwa shahidi umeenezwa kwa waumini na usichanganywe na mwito kwa huduma.
Lazima ifahamike vyema kwamba si kila muumini ambaye ana mzigo wa kuwaongoza wengine
kwa Kristo au kushuhudia ameitwa bila shaka kuwa mhubiri. Kuhubiri Neno la Mungu ni
zawadi ya mwito wa kuwa shahidi. Ni maamuzi ambayo yanamhusu Mungu pekee yake na si
yetu. Tunaweza kukubali mwito, lakini hatuwezi kuuanzisha.
Mwito wa kuhubiri Neno Lake ni lazima uanzishwe na Mungu na si na mtu au kanisa, haijalishi
ni kadiri gani mtu anataka kuwa mhubiri. Mhubiri wa Injili ni lazima asichague. Wakati
nilipokuwa nikifanya kazi yangu ya huduma katika Kaskazini mwa Ujerumani, nilikutana na
ndugu ambaye alitamani sana kuwa mhubiri. Wakati mwingine, alikuwa na nafasi ya kuhubiri
lakini lilikuwa jambo la kweli kwamba hakuwa ameitwa kuhubiri. Kwa upande wake, lilikuwa
dhibitisho la kweli kwamba upendo wa kutaka kuhubiri Neno hautoshi. Mungu ni lazima atuite.
1 Theologisches Begriffs- Lexikon zum Neuen Testament. (Wuppertal: Brockhauss Verlag, 1977), Uk. 1277.
7
Kwa sababu ya wafanyikazi wachache, kanisa wakati mwingine huchagua wahubiri,ambao
wanachaguliwa kulingana na usimamizi wa njia ya kiulimwengu. Wale wanaoingia katika
huduma kupitia njia ambazo si za kibiblia, wataanguka na watakuja kuwa chukizo kwa mwili wa
Kristo na kwa wao wenyewe. Ni lazima tukumbuke kwamba ufanisi katika kazi ya kiulimwengu
si ufanisi wa haki katika huduma. Yesu hakutuambia kamwe tuwinde wahubiri au wafanyi kazi.
Kuepukana na onyo la kweli ni lazima tufwate maagizo yake ambayo yamepeanwa katika
Mathayo 9:38.
Kwa hivyo, ombeni Bwana wa mavuno awatume wafanyikazi katika mavuno yake.
Kama tutamwomba, atawatuma ! Hii ni ahadi yake. Njia nyingine yeyote haitafaulu. Kuna
tofauti kuu kuwa tu mwajiriwa wa kanisa au “mtu aliyeitwa na Mungu tu” lakini hili jambo
laweza kuleta matokeo yanayotakikana. Tusisahau ya kwamba Mungu hawachagui wale tu
wanaweza, bali huwaongoza wale ambao wameitwa.
a. Mwito wa Hakika
Mhubiri wa Injili ni lazima ajue kwamba bila shaka ameitwa na Mungu. Vile inavyoonekana
mwito huu ni muhimu mno. Kile ambacho ni muhimu ni utendaji wa maarifa ya kuhubiri Neno
la Mungu. Hili hakikisho takatifu litapeana nguvu, faraja na himizo mpya, wakati wa shida. Bila
hakikisho la mwito wa Mungu, mhubiri anaweza kusita na kuondoka hudumani wakati
anapokabiliwa na shida. Vitu havitakuwa tu rahisi na ushuhuda wa ufanisi hautaonekana kila
mara. Katika wakati huu, mhubiri atashikilia thibitisho la mwito wake, la sivyo, ataanguka kwa
imani. Kama Paulo ambaye alijua kwamba huduma wake ulikuwa kwa sababu ya ukaguzi wake
mtakatifu, kwa hivyo, mhubiri ni lazima ajue kwamba Mungu amemwita.
b. Ushuhuda wa kuitwa
Mwito mtakatifu utakuwa ushuhuda, na kuonekana na mwili wa Kristo. Utajidhihirisha
wenyewe katika njia mbalimbali.
(1) Mungu anapoita atapeana nafasi kufuata mwito. Hakuna sababu ya kuitwa na huna
nafasi ya kutekeleza mwito.
(2) Wale ambao wameitwa kuhubiri watagundua utajiri katika Neno la Mungu ambao
hawajawahi kuona. Maandiko yatafunguka na kuwapatia ujumbe kutoka kwa Mungu.
(3) Upako wa Mungu utakuwa ushuhuda katika huduma wa mhubiri. Watu wataona
kitendo kitakatifu maishani mwake. Wale ambao wameitwa watafundisha na kuhubiri
kama Yesu - na mamlaka na si kama Wasudukayo na Mafarisayo (Marko 1:22. Mwili wa
Kristo utatambua mwito kama huo.
(4) Mhubiri wa Kipentekote atashuhudia ukweli wa Marko 16:17-18. Ishara na miujiza
itaonekana katika mahubiri yake.
(5) Mwisho ingawaje si kabisa, mioyo ya thamani itaokolewa na kanisa litatukuzwa
kupitia huduma ambao umepeanwa.
Huenda mwito mtakatifu hautashuhudiwa wakati wa mahubiri machache ya kwanza. Lakini
wakati mtumishi wa Mungu anapojitolea zaidi na zaidi kwa Bwana, thibitisho hili la kweli
litashuhudiwa.
8
2. Mwito wa Mungu na Kazi ya Kiulimwengu
Swali limeulizwa, je, mhubiri anaweza kuajiriwa katika kazi ya kiulimwengu, au ni lazima awe
katika huduma wakati wote? Jambo hili haliwezi kusuluhishwa na jawabu fupi. Kwa kweli,
mhubiri ni lazima apeane wakati wake wote katika huduma ili afaulu vyema. Walakini,
maandiko hayalaumu wale wanaopata mshahara katika kazi za kiulimwengu. Paulo alijisaidia
mwenyewe kwa kutengeneza hema, tunapoangalia jambo hili tunapata suluhisho kwa shida hii.
Anasema kwa kweli kwamba kuna tofauti kupata mshahara ili kuhubiri Injili na kukataa Injili ili
kupata mshahara. Watu wa Mungu watahifadhi mwito na huduma kwanza.2
3. Sifa za Kiroho
Wale ambao wamo hudumani hawaajiriwi katikika “kazi ya kuanzia saa tatu hadi saa kumi na
moja” wakati wanapotekeleza kazi, lakini wanapoondoka ofisini watafuata mambo yao.
Watumishi wa Mungu ambao wameitwa na Mungu ni lazima watimilize matakwa ya huduma
masaa 24 kwa siku kwa sababu kazi yao ni ya kiroho ya asili na hawawezi kukosa kuwa kazini,
hata wakati wa likizo.
Mhubiri ni lazima ajue kwamba ameitwa na mwito mtakatifu. Kwa hivyo, maisha yake yaende
pamoja na mwito wake. Ni lazima awe na jina nzuri miongoni mwa washiriki kanisani na jamii,
hii inamaanisha kwamba atende kile ambacho anahubiri, au awe mwanafunzi wa somo ambaye
anataka kupeana. Hayo yanamfanya mwenye kufaulu. Hii itawezesha kuhubiri na huruma na
upendo, lakini si katika njia ya kudai kisheria.
Mhuduma ni lazima aruhusu Neno analihubiri liendeleze sifa zake, ili awe mtu wa uadilifu
ambaye anafuata Neno lake na anafwata “kazi yake” katika njia ya wema na ubaya. Ni lazima
ajaribu kuwa mfano katika neno na matendo. Mausia ya Paulo ambayo alimpatia Timotheo
yangali thabiti kwa wale wote katika huduma leo.
...uwe mfano kwa wanaoamini, katika usemi wako, mwendo wako, upendo wako, imani
yako na maisha safi 1 Timotheo 4:12.
Matakwa ya juu kwa wale ambao wako katika huduma yameonyeshwa zaidi katika 1 Timotheo
3:1-13. Mungu anawatarajia watumishi wake kuwa na mahitaji haya ili wasiaibike kwa mwito
wao wa juu.
Msemo huu ni wa kweli: kama mtu anatamani kazi ya Askofu, anatamani kitu bora. Halafu
Askofu ni lazima awe mwenye kiasi, mume wa mke mmoja, awe mwenye kiasi, nidhamu na
utaratibu, ni lazima awe mkarimu na anayeweza kufundisha, asiwe mlevi au mtu wa matata, bali
awe mpole, apendaye amani, asiwe mtu wa kupenda fedha,anapaswa kuwa mtu awezaye
kuongoza vema nyumbani mwake, na kuwafanya watoto wake wawe watiifu kwa heshima yote.
Maana kama mtu hawezi kuongoza vema nyumba yake, atawezaje kulitunza kanisa la Mungu?
Mtu ambaye hajakomaa bado katika imani asifanywe kuwa kiongozi katika kanisa, asije akajaa
majivuno na kuhukumiwa kama vile ibilisi alivyohukumiwa.
Wasaidizi (mashemasi) katika kanisa wanapaswa kuwa watu wenye tabia njema na wanyofu,
wasiwe wanywaji mno wa divai au wenye tamaa ya fedha, wanapaswa kuzingatia kwa dhamiri
njema ukweli wa ndani wa imani. Ni lazima kwanza wathibitishwe, na awakionekana kuwa
2 Ray H. Hughes, Mahubir ya Pentekote. Cleveland: Chapa ya Pathway, 1981), uk. 58
9
wanafaa, basi, watoe huduma wao. Wake zao wanapaswa pia kuwa na tabia njema, wasio
wasengenyao watu, wenye kiasi na waaminifu katika mambo yote.
Msaidizi katika kanisa ni lazima awe na mke mmoja tu, na awezaye kuongoza vema watoto wake
na nyumba yake. Maana wasaidizi wanaofanya kazi yao vizuri hujipatia msimamo mzuri na
wanaweza kusema bila hofu juu ya imani yao katika Kristo Yesu.
Maandiko yanaonyesha vyema kwamba mwito wa Mungu ni thibitisho kwa uwezo juu wa
kiroho, ambao unaweza kutekelezwa kwa nguvu na neema ya Roho Mtakatifu.
a. Kujazwa Kwa Roho Mtakatifu
Ukamilifu wa Roho Mtakatifu ulikuwa sababu kuu katika Huduma wa Kanisa la Kale. Hata kwa
wale wanaotumika mezani walitakikana kuwa watu ambao wamejazwa na hekima na Roho
Mtakatifu ( Matendo 6:1-4). Mhubiri wa kipentekote wa wakati ule hakutaka kupungukiwa na
kanuni hii ya Biblia. Ni lazima awe na ujuzi wa kipentekote kabla ya kuwa mnenaji wa kweli
wa Mungu. Hakuna utaratibu, haijalishi ni wema kadiri gani wala ustadi mwema wa uwongozi
au ustadi wa hali ya juu unaweza kushindana na mtu ambaye amejazwa vyema na Roho wa
Mungu.
b. Mtu wa Neno
Mhubiri wa kipentekote atakuwa mtu wa neno. Ataamini katika utendaji wa pumzi wa Biblia na
katika wema wa ukamilifu wake (uhuru kutoka kwa makosa). Ni lazima awe na nafasi si tu
katika huduma wake, bali pia katika maisha yake ya kibinafsi. Kwa upande mwingine, Biblia
isitumiwe kama kitabu tu cha mahubiri. Lazima kilishe mchungaji kabla ya kulisha kondoo
wake.
Ni lazima asisome Biblia tu bali ajifunze kwa manufaa yake na kwa mahubiri yake. Hizi ni njia
tofauti za kujifunza Biblia ambazo zaweza kufwatiwa. Kila mhuduma anaweza kutaka moja au
nyingine. Richard Warren anataja njia kumi na mbili:
(1) Ibada
Chagua sehemu fupi ya Biblia yako na utafakari juu yake kwa maombi hadi Roho Mtakatifu
akuonyeshe njia ya kuhusisha ukweli katika maisha yako. Uandike maombi kibinafsi.
(2) Sura katika Ufupi
Usome sura ya kitabu karibu mara tano, halafu uandike chini kwa ufupi mambo ya kati ambayo
umepata ndani.
(3) Sifa Bora
Chagua sifa bora ambayo unataka kuzungumzia maishani mwako na utafute katika Biblia
inasema nini kuhusu mambo haya.
(4) Kiini
Chagua kiini cha Biblia kusoma. Ufikirie maswali matatu hadi matano ambayo ungeyataka
yajibiwe kuhusu kiini hicho. Usome mambo yote ambayo yanahusu mambo haya makuu na
uandike majibu yako ya maswali.
10
(5) Maandiko ya Habari Kuhusu Mtu
Chagua mtu mmoja wa Biblia na ufanye utafiti wa maandiko kumhusu mtu huyo kwa kujua
maisha yake na tabia. Uandike nia zake, nguvu, na udhaifu. Utumie mambo haya umejifunza
kwa maisha yako.
(6) Jambo la Kufikiriwa
Chagua na ulinganishe mistari yote ambayo unaweza kupata kuhusu jambo fulani. Uangalie
mwisho wake na udokeze vile unaweza kushirikiana na mtu mwingine.
(7) Neno la Kusoma
Usome maneno muhimu ya Biblia. Utafute ni mara ngapi neno hilo linapatikana na vile
linaweza kutumiwa. Tafuta maana ya asili ya neno hili.
(8) Msingi wa Kitabu
Usome vile historia, kijiografia, desturi, kisayanzi na siasa ambayo iligeuza kile ambacho
kilifanyika katika Biblia. Utumie vitabu vya kumbukumbu kwa kuongezea ufahamu wako wa
neno.
(9) Utafiti wa Kitabu
Ufanye utafiti wa kitabu chote cha Biblia kwa kukisoma mara nyingi kwa akupata mambo ya
ndani yake. Usome msingi wa kitabu na utayarishe maneno muhimu ya mambo yaliyomo.
(10) Utafiti wa Sura
Ujue kamili mambo yaliyomo ya sura katika Biblia kwa kuangalia kila msitari kwa undani katika
sura hiyo. Gawanya kila sentenzi neno kwa neno, na uangalie maelezo yote.
(11) Kulinganisha Kila Msitari
Ufupishe yaliyomo na kiini kikuu cha kitabu cha Biblia baada ya kupitia mara nyingi. Utayarishe
habari ndogo ya kitabu (dokezo). Njia hii inafanyika baada ya wewe kutumia kitabu cha njia ya
utafiti na utafiti wa kila sura ya kitabu hicho.
(12) Utafiti wa Msitari hadi Mwingine
Uchague ukurasa mmoja wa maandiko na uangalie katika urefu kwa kuuliza mawali, kwa
kutafuta maneno yanayofanana katika maana, na ueleze kila msitari. Uandike matumizi ya kila
msitari uliojifunza.3
c. Mtu wa Maombi
Mhubiri wa kweli wa kipentekote atakuwa mtu wa maombi. Kupitia maombi, hatapokea tu
nguvu za kuishi maisha yanayostahili kama mtumishi wa Mungu, bali atapokea ujumbe kutoka
kwa Bwana. Ni lazima ajiombee, huduma wake, na wale ambao anawatunza kiroho. Zaidi ya
3 Ibid., kur. 92-94.
11
hayo, ni lazima aombee familia yake na ahakikishe kila siku wanashirikiana Neno la Mungu.
Kwa sababu anaweza kuwaleta wengi kwa Bwana na apokee familia yake kwa sababu ya
mwovu. Mhubiri mara nyingi huwa katika hatari ya huduma wakati wake mwingi na watu
kuliko na Mungu. Hii haimaanishi kwamba awe pekee, bali ni lazima ajue wakati anahitaji kuwa
na Mungu pekee yake. Swali ambalo Yesu aliwauliza wanafunzi wake ni, “je, hamwezi kukaa
nami kwa saa moja?” (Mathayo 26:40) bado inatumika leo, hasa kwa wale ambao ni wahubiri wa
Neno Lake.
3. Sifa Nyingine
Mtu ambaye ameitwa katika huduma asiwe mtu ambaye amekosa kufaulu katika kazi nyingine.
Ni lazima awe mtu wa kufanya kazi nyingine kwa bidii, hodari na mwenye ujuzi. Ni lazima
ajitahidi katika ubora wa kutangaza Neno la Mungu. Wale ambao wanajiimarisha kwa kadiri yao
watapoteza manufaa yao. Mhubiri ni lazima awe imara daima vile anaweza kuutunukia ujumbe
wa Mungu vyema. Ni lazima awe tayari kurekebishwa na hata kuchambuliwa (kulaumiwa).
Ishara zake, hali na hotuba lazima vikamilishe ujumbe na kuongezea ubora wake. Lazima
aongeze maneno yake na asiwe na shaka na matumishi yake. Walakini, ni lazima akae kama
kawaida na kuwa mhubiri halisi. Kitu kinachowaweka watu kando na Neno ni maneno yao
wenyewe na hotuba yao ambayo si ya asili. Uwezo wa kuzungumza wa mhubiri ni muhimu.
Kwa sababu yeye ni mnenaji wa Mungu, ni lazima atunze sauti yake, na vile anavyopeana
ujumbe wake. Zaidi na hayo, ni lazima awe hodari. Hasa ya kulingana na utafiti, saa moja ni
sawa na masaa manne ya kufanya kazi ya mikono. Jambo lingine la kupendeza ni kwamba
kuzungumza katika hadhari kuna uchofu mwingi.
C. Nafsi ya Mhubiri
1. Ukweli na Ukamilifu
Ukweli na ukamilifu ni lazima yawe mambo muhimu katika nafsi ya mhubiri. Ni lazima awe
mtu wa wazi na mnafiki katika tabia zake yaani, akitenda tofauti mahali kuna watu, na pia tofauti
akiwa nyumbani asijihusishe katika mambo ya hila na pia kufuata mambo ya akujitakia manufaa
yake mwenyewe. Huduma wake na nafsi ni lazima vionyeshwe katika matendo yake, uaminifu,
na uadilifu. Uaminifu ni muhimu katika uhusiano wake na watu wa kike au kiume. Hata
kusuhubiana na mwanamke/mwanamme, au kupitia mahali ambapo kuna katibu au mhsiriki
yeyote wa kike wa kanisa haikubaliki kabisa. Shauri la Paulo kwa Timotheo, watendee vijana
kama ndugu zako, wanawake wazee kama mama yako na wasichana kama dada zako kwa usafi
wote. Haya yote ni lazima yafuatiwe na watumishi wa Mungu. Uaminifu unatakikana pia wakati
wa kushughulikia pesa na mali. Ninamjua mhuduma ambaye amekosa sifa hizi za msingi.
Wakati alipokabiliwa na shida ya pesa, aliuza paa la kanisa lake, ambayo upepo ulikuwa
umengóa. Mhubiri mwingine alifanya kanisa lake kama chumba la pombe siku za ijumaa na
jumamosi, kwa sababu ya pesa. Kwa uadilifu, uwepo wa maisha ya kiroho katika watu hawa si
hakika.
2. Kuna Uhuru Kutoka kwa Wivu
Wivu utakufanya kiwete, kuondoa na kuharibu kazi ya mhuduma yeyote. Mhuduma ni lazima
ajitahidi kuwa huru kwa mapigo haya ya ibilisi, ambayo yatamwondoa na kutaka kumlinganisha
na wengine. Wivu mara nyingi utauliza je, kwa nini si kuinuliwa katika cheo badala ya
mhuduma mwenzangu? Kwa nini anapokea mshahara mkubwa kuliko mimi? Kwa nini
alisifiwa nami nikaangaliwa kwa jicho ovu, licha ya kufanya kazi kwa bidii kama yeye? Kwa
nini sitambuliwi kwa kazi yangu ya bidii sa ufanisi? Kwa nini mchungaji mwingine alipatiwa
12
kanisa nzuri, nami ningali ninakutana na watu wangu chini ya mti au darazani? Mtu akiwa na
fikira hizi tele kichwani, zitaonekana katika huduma wake na kuhubiri kwake. Wivu ulirarua
ufalme wa Paulo. Uliharibu familia yake na hatimaye mwenyewe. Kila kitu kilianza watu
walipoimba “Suli aliwauwa maelefu na Daudi aliwauwa elfu kumi”. Hakuweza kukubali ukweli
kwamba Daudi alitumiwa na Mungu zaidi na alipendwa zaidi kumliko.
3. Nidhamu
Hakuna kazi nyingine ambayo hupeana nafasi kuu ya kutenda kitu upendacho na hata kuleta
uvivu, kuliko huduma. Hii ni kwa sababu kwamba mchungaji hana msimamizi wa karibu
ambaye anamsimamia, kwa hivyo ni rahisi kwa mtu kukaa kwa starehe na kudhoofika hudumani.
Baada ya kusoma Neno, kuomba, kutembelea watu na kadhalika, mhuduma anaweza kukaa
kitandani nusu siku, awe na wakati wa kusoma kitabu, kujadiliana na marafiki, kuchukua siku ya
kupumzika, au ashughulikie shughuli zake bila mtu yeyote kujua, ila Mungu pekee yake.
Mhubiri ni lazima ajifunze kujipatia nidhamu mwenyewe. Lazima aamke mapema afanye kazi
kwa bidii na afanye masaa mengi ili kufaulu. Kuna saa za kupumzika na likizo, lakini hizi
sizitawale maisha ya mhubiri. Tunapojipatia nidhamu wenyewe, tutajifunza kufanya mambo
yetu kwa utaratibu. Kitabu kidogo ambamo tumeandika mambo fulani kitaweza kutusaidia kujua
kile tunahitaji kufanya kila siku, kila wiki, kila mwezi, na hata mambo ya kila mwaka. Mambo
ya kuzoea kama haya yatafanya mhubiri kuwa huru kujitolea kwa maombi, kusoma na kazi ya
huduma.
13
MASWALI YA MARUDIO - MHUBIRI
1. Kuhubiri kuna chanzo chake wapi?
2. Jaza katika mapengo:
Hata ingawa kuhubiri kuna ________________________ yake katika _________________
Agano, walakini haionyeshi _________________________ Agano ____________________
ambayo imekuja kuwa _____________________________ imani ya ukristo.
3. Katika sifa za Mhubiri, ni jambo gani kuu ambalo liko karibu na kuzaliwa upya?
4. Ni kitu gani ambacho hakitakikani kuchanganywa na mwito kwa huduma?
5. Ni jambo gani hutendeka tunapokuwa na ukosefu wa wafanyi kazi kanisani?
6. Taja sifa za kiroho tatu .
1) ________________________________________________________________
2) ________________________________________________________________
3) ________________________________________________________________
7. Jaza katika mapengo:
Ukweli na ________________________ ni lazima uwe ___________________ wema
katika wahubiri _________________________.
8. Je, wivu utafanya nini kwa kazi nzuri ya mhuduma?
9. Wivu ulimfanya nini mfalme Sauli?
10. Je, huduma unapeanaje nafasi kuu kwa uvivu?
14
Kuhubiri! Ni Kitu Gani?
II. Kuhubiri ni Kitu Gani?
Kuhubiri ni tangazo la Neno la Mungu. Kwa hivyo, maana yake ni zaidi ya kuweka pamoja
maneno na kusema mawazo makuu na maneno yanayotamkwa kwa sauti dhahiri. Kuhubiri kwa
kweli hupatikana katika uwepo wa Mungu. Hii inamaanisha kwamba unapohubiri ujumbe huu,
utakuwa wa nguvu, na utakuwa ukihukumu na kuleta mabadiliko maishani mwa wasikilizaji.
Biblia inatumia maneno mengi ya kigriki ambayo yanatafsiriwa na kuwa “kuhubiri”. Maneno
ambayo ni muhimu ni Euangelizo na kerusso. neno hili la kwanza linatumiwa mara nyingi kwa
kuzungumzia tangazo la habari njema. Linaonyesha kuletwa kwa habari njema, au kuhubiri
injili.4 Yesu alitumia neno hili katika kitabu cha Luka 4:18-19 ambapo alisema,
Roho wa Bwana yu juu yangu, kwani amenipaka mafuta niwahubirie maskini injili.
amenituma niwatangazie mateka kwamba watapata uhuru, vipofu watapata kuona tena,
kuwaweka huru wanaoonewa , na kuwatangazia mwaka wa neema wa Bwana.
Neno la kwanza linamaanisha mleta habari, au kutangaza katika njia ya kupeana ujumbe mara
nyingi hushauri utaratibu, uzito na mamlaka ambayo ni lazima yasikilizwe na kutiiwa.5 Neno
kerusso linaonyesha kupeana kwa ujumbe zaidi kunakamilishwa kwa mamlaka ya juu. Kile
anachotangaza kitakuja kukubalika punde tu atakapokitangaza. Hili jambo la kuunganisha
linapeana neno la utaratibu na la mwisho.6
A. Kuhubiri na kufundisha
Mara nyingi, kuhubiri kunaelezwa kama habari ya kushawishi na ya uinjilisti, na kufundisha ni la
utaratibu na si la kuchochea, kavu na hata ya kuchosha. Maelezo kama haya hayahusiki na
utendaji wa haki kwa njia moja au nyingine ya mawasiliano ya mkristo. Yote mawili
yanatofautiana katika njia fulani na maneno ya kigriki, na utafsiri sawa unaonyesha (kerusso =
hubiri, didasko = fundisha). Walakini kuhubiri kwa kweli kutakuwa na mambo fulani ya
kuhubiri. Mambo haya mawili hayapingani lakini yanakamilishana. Kufundisha kunaelimisha
na kuchochea moyo, a kuhubiri kutachechea moyo na kuelimisha msilizaji. Ni jambo la
kupendeza kujua kwamba katika amri kuu, Mathayo anazungumzia tangazo la injili ni kama
kufundisha na Marko anasema ni kuhubiri, hii inaonyesha kwamba maneno haya yote
yamesokotana na ni sawa na muhimu kwa kutangaza habari njema ya Yesu Kristo. Uhusiano
wa kuhubiri na kufundisha unaonekana zaidi katika Agano Jipya ambapo unaonyesha Yesu kama
mhubiri mkuu, na pia wakati mwingine, unaonyesha Yesu kama Rabbi au mwalimu.
Kuhubiri na kufundisha kwa kawaida kunatofautishwa kama ifwatavyo. Neno kufundisha
linatumiwa kwa ubusara wa wasikilizaji. Ukweli wa Biblia utaonyeshwa katika neno la kuonya
la utaratibu, likipatia muumini msingi imara wa maandiko kwa imani yake. Hata ingawa iko
katika utaratibu, kufundisha kuzuri kutakuwa na upako wa Roho Mtakatifu. Kwa upande
mwingine, kuhubiri kunaweza kushawishi moyo na maono kwa kuamrisha itikio kwa ujumbe wa
Mungu. Kufundisha ni lazima kufwatiwe na kuhubiri kwa sababu kutaimarisha maono ambayo
4 W. E Vine, Kamusi ya Maonyesho ya Maneno ya Agano Jipya. (Tappana mzee: Kampuni ya Fleming H.
Revell, 1966), uk. 201.
5 Yusufu H. Thayer, Kamusi ya Kigriki Kingereza ay Agano Jipya. (Chumba la Vitabu la Grand Rapids,
1977), uk. 346.
6 Theologisches Begriffs- Lexikon, uk. 127
15
yameshutushwa kwa kupeana msingi imara wa ukweli wa Biblia. Katika mazoezi, mambo haya
yote ya mawasiliano hayawezi kutenganwa kwa urahisi. Jay E. Adams anaonyesha kwamba
neno Didasko ambalo linatafsiriwa kama kufundisha linatoka karibu na neno la wazo la
kufundisha, vile linavyotumiwa leo. Katika njia hii, injili inatangaziwa wale wanaomwamini
tayari.7 Kwa hivyo, anaonyesha tena uhusiano wa karibu wa maneno haya.
Tofauti nyingine hupatikana katika kutoa ukweli wa Biblia. Kufundisha kutapeana wakati wa
kusoma na kutafuta maandiko. Kuhubiri kwa upande mwingine ni kutoa msitari fulani katika
maandiko au kuonyesha andiko bila kuangalia katika Biblia ili utiririkaji wa mahubiri
usitatanishwe.
B. Kuhubiri na Unabii
Kuhubiri na unabii ni njia mbili tofauti ambazo Mungu hutumia kuzungumzia mwanadamu. Ya
kwanza huhusika na matayarisho ya utaratibu wa ujumbe na pili ni “zaidi ya” kimiujiza katika
utendaji. Kwa kuangalia sana kipawa cha unabii, kuhubiri kutaweza kumeza kabisa sifa ya
kimiujiza yake.
Neno kuhubiri katika asili yake (kerygma) liko tofauti kabisa kutoka kwa neno (propheteia)
ambalo linadhibitisha kwamba unabii si kuhubiri na kuhubiri si unabii. Unabii unazungumza na
mtu kimiujiza kutoka kwa ushawishi wa Roho Mtakatifu. Kuhubiri kwa upande mwingine ni
kuzungumza kwa mtu “kwa urahisi” na haimaanishi kwamba haikupuliziwa na Mungu. Tofauti
ni kwamba unabii unapeanwa kwa upuzio wa hali ya juu, na katika kuhubiri, Mungu anapulizia
fikira zetu wakati wa matayarisho, katika hali ndogo - katika wazo muhimu na katika hali ya
lazima ambayo neno hili linapokelewa.
Kuhubiri kwa njia ya kipentekote wakati mwingine kuna mambo ya unabii. Hii inaweza
kutendeka mhubiri anapopokea unabii anapohubiri Neno. Au anaweza kuingia katika nyayo za
huduma wa unabii kwa kuzungumzia dhambi fulani, vile inavyojulikana kwake. Wakati
mwingine, Roho Mtakatifu atamwongoza katika upande mwingine tofauti na vile alivyopanga
mwenyewe kukutana na mahitaji fulani ya mtu katika umati. Jambo hili linapotendeka,
mhuduma ni lazima atekeleze imani yake na afuate mwongozo wa Roho Mtakatifu, hata ikiwa
itamaanisha awache maneno yake ambayo alikuwa ametayarisha. Wakati kama huu utaweza
kukamilisha mambo zaidi ya uzimani kuliko hotuba ambayo imetayarishwa kwa makini.
Ray H. Hughes, akielezea zaidi kuhusu neno la unabii la kuhubiri, anaelezea zaidi kwamba
hakuna jambo lingine la kusisimua kwa mhubiri kujua kwamba Mungu anamwangazia. Katika
wakati kama huu, fikira zinakuja kwa moyo wake na hawezi kuzitamka kabla ya fikira nyingine
kumfikia na kumshauri. Maandiko ambayo yametayarishwa mapema na kufikiriwa kwa undani
yatakumbukwa, na yatakunjuliwa kwa ubusara. Mara tu, mhubiri anahisi mahubiri ya mfano
kama huu, hataridhika na mambo machache. Hii ndiyo sababu ya kuonyesha kufunga kula na
kuomba ni muhimu kwa mahubiri ya kipentekote.8
Jambo la unabii katika mahubiri ya kipentekote linahitajika sana siku hizi, kwa sababu
litarudisha hofu ya Mungu miongoni mwa watu. Dhambi ya siri au shida ambazo zimekuwepo
kwa miaka mingi itafichuliwa kupitia mahubiri ya unabii. Mchungaji rafiki yangu alinisimulia
ya kwamba wakati wa kuokoka kwake, alihudhuria ufufuo wa hema. Mhubiri alitumiwa kwa
nguvu na Mungu na kupitia maneno ya unabii katika mahubiri yake, rafiki yangu aliguzwa kwa
7 Jay E. Adams, Predigen, zielbewußt, Anschaulich, Überzeugent. (Giessen7Basel: Brunnen Verlag, 1991),
uk. 14.
8 Huhges, uk. 133
16
ndani. Ilionekana kila neno ambalo alitumia lilimhusu, likifichua fikira zake za ndani na dhambi
ambayo imefichwa. Wakati ibada ilipomalizika, alimshutumu mamake kwa kumwambia
mhubiri kumhusu. Hii haikuwa ndiyo sababu, lakini Roho Mtakatifu alikuwa amemzungumzia
roho wake na kufichua dhambi zake. Aliitikia thibitisho takatifu la hatia ya makosa na akapeana
maisha yake kwa Bwana. Leo, anahubiri Injili.
C. Kusudi la Kuhubiri
Kwa nini tunahubiri? Kusudi lake ni nini au lengo la mahubiri yetu ni nini? Kila mhubiri ni
lazima awe na jawabu sahihi kwa maswali haya, kwa sababu nyingine, ataanguka katika imani
katika mahubiri yake.
1. Kusudi la Jumla
Kusudi la jumla au madhumuni ya kuhubiri ni kumtukuza Mungu. Itaweza kufupishwa zaidi
kama tangazo la mapenzi ya Mungu kwa watu wake na kwa wale wanaohitaji wokovu, kwa
sababu hii ni kuwahimiza kutii amri yake. Mapenzi yake, vile yanavyofunuliwa katika Neno
lake, ni mara mbili. Kwanza hakuna yeyote ambaye anatakikana kuangamia (2 Petro 3:9) na
jambo la pili ni kwamba wale ambao wameokoka watampenda na mioyo yao yote na majirani
kama wenyewe, yaani, kwamba wakubaliane na amri yake kuishi maisha matakatifu kama vile
wanafunzi walivyofanya (1 Wathesalonike 4:3). Mambo haya mawili ni lazima yazungumzwe
katika njia moja au nyingine tunapohubiri injili.
2. Kusudi Dhahiri
Ni lazima tuhakikishe kwamba ujumbe tunaohubiri ukubaliane na nia ya mambo mawili ya
kuhubiri. Ni mara tu wakati kila ujumbe unafaa katika kusudi kuu ndipo mahubiri yatafaa. Kwa
kutimiza haya madhumuni yafwatayo, ni lazima yatekelezwe ukihubiri.
a. Hubiri Kwa kuleta Mabadiliko
Mahubiri yetu ni lazima yaanzishwe kwa Roho Mtakatifu, yakidhihirishwa kwa upendo wake, na
kutangazwa chini ya upako na katika madhubutu ya nguvu zake. Ni lazima yashawishi na yavutie
wasikilizaji kwa kujitolea maisha yao kwa Bwana Yesu Kristo. Lazima yaongoze mtu katika
maarifa ya ndani ya Mungu na kuwa na uhusiano wa ndani wa moyoni naye, ambao matokeo
yake ni upendo kwa Mungu na watu wengine. Kwa ufupi, wale ambao wako katika huduma ni
lazima wawe wafafanuzi bora. Kwa kutimiza haya, ni lazima tuhubiri msalaba. Hii pekee italeta
wokovu na kuzaa wanafunzi.
(1) Kuhubiri Msalaba kwa Wokovu
Ni lazima tuhubiri Kristo aliyesulubishwa, kama vile Paulo alivyofanya. Halafu nafsi itampata
Mungu. Biblia inasema katika 1 Wakorintho 1:18,
Maana ujumbe kuhusu kifo cha Kristo ni jambo la kipumbavu kwa wale walio katika
mkumbo wa kupokea, lakini kwetu sisi tulio katika njia ya wokovu ujumbe huo ni nguvu
ya Mungu.
Kuhubiri msalaba inamaanisha ni kuweka wazi ubaya wa dhambi, kuonyesha haki ya Mungu, na
ukweli kwamba kila dhambi itaadhibiwa na Mungu. Walakini, ujumbe hautamalizika kamwe
17
katika kutokuwa na tumaini au katika njia ya kukana. Baada ya dhambi kuwekwa wazi na
hukumu kutekelezwa na Roho Mtakatifu, msalaba ni lazima uhubiriwe kama mfano wa tumaini
kwa mtenda dhambi, na msingi wa msamaha wake.
(2) Hubiri Msalaba Kufanya Wanafunzi
Kufanya wanafunzi haihusiki tu na utafsiri wa Biblia, bali ni badiliko la maisha la tangazo la
Neno la Mungu. Mahubiri kama haya yatawasaidia watu kukua katika upendo wao kwa Mungu
na watu wengine. Hii itaonyesha wazi jambo linalomaanisha kuchukua msalaba na kumfwata
Yesu.
Mungu hataki tu sisi kupeana ujumbe katika mfano wa mafundisho ya Biblia au makisio. Yeye
anatutaka kupeana mashauri ya wazi kwa watu wake, ambayo yatawawezesha kulitumia neno
lake kwa maisha yao ya kila siku. Kuhubiri kwetu ni lazima kuwe wazi na kufaa, ili kuleta
mabadiliko ya maisha ya kanisa na mwamini binafsi. Kwa maneno mengine, mahubiri ya
kipentekote ni lazima yawe na uhusiano wa maisha.
b. Ongoza kwa Udhabiti au Maamuzi
Mahubiri ya kipentekote katika Agano Jipya yaliamrisha udhabiti. Wale wanaosikiliza kwa
mahubiri ya wanafunzi na mitume, waliuliza, nitafanya nini ili niokoke? Au waliokota mawe ili
wamnyamazishe mhubiri:
Basi, watu waliposikia hayo, walichomwa mioyo, wakawauliza Petro na wale mitume
wenzake, “Ndugu zetu, tufanyeje? Matendo 2:37
Wale wazee wa baraza waliposikia hayo, walighadhibika sana wakamsagia meno kwa
hasira Matendo 7:54.
Katika makanisa mengine kama yale, watu hawaruhusiwi kamwe kuongozwa na kujitolea kabisa
kwa Kristo. Kama tu wanahudhuria kanisa kila mara, mchungaji huonekana ametosheka.
Walakini, kwa kuruhusu mambo kama hayo, mchungaji hafanyi tu hali ya watu wanaohusika
kutofaa, bali hawawezi kuhisi ukamilifu ambao uko katika Yesu, pia hupeana nafasi kwa mambo
ambayo si muhimu kwake mwenyewe na washiriki. Mara nyingi, mikutano hii na kujitolea
vyema ni chanzo cha shida nyingi.
4. Kufuata Mambo Fulani Muhimu
Mhuduma ni lazima ahubiri Neno na ajizuie kuhubiri mahubiri ya kupendeza nafsi yake. Kabla
ya kusimama kwa mimbara, ni lazima awe na hakika na kile Roho Mtakatifu anataka kutenda na
kukamilisha kupitia ujumbe. Asihubiri ikiwa hana hakika na mambo haya. Kujua kusudi halisi
la mahubiri ni muhimu. Jay E. Adams anasema kwamba mhubiri, anaamshwa na mke wake
jumapili asubuhi saa kumi asubuhi na anamuuliza: je, kiini cha ujumbe wako leo ni nini?
Lazima awe tayari kumwambia katika sentenzi bora , jambo kuu la ujumbe wake. Halafu
anaweza kugeuka na kuendelea kulala, kama hakuna chochote kilichotendeka.9 kama tunajua na
kufwata mapenzi ya Mungu, mahubiri yatakuwa ya manufaa.
D. Kutangaza Ujumbe wa Mungu
Kuhubiri ujumbe wa Mungu, si fikira zako au mambo ya elimu yako. Kusudi la kuhubiri ni
kutangazia watu Neno Lake na kwa dunia inayoangamia. Ni lazima kuhubiri kusiwe tu
kuambiana hadithi au kushirikiana ushuhuda. watu wanataka kujua Mungu anasema nini, na
Mungu anataka kujua kile ambacho kiko moyoni mwake.
9 Adams, kur. 37-38.
18
Kuhubiri ni sehemu kuu katika ibada. Wakati mwingine, watu husema kwamba Roho Mtakatifu
alitenda kazi kwa njia ya ajabu hadi mhubiri akashindwa na la kufanya. Kwangu binafsi, nina
shida na jambo kama hili, hasa kama hili jambo laweza kutendeka mara nyingi. Neno ni muhimu
kwa sababu lina nguvu. Biblia inasema katika kitabu cha Waebrania 4:12,
Kwa kuwa Neno la Mungu ni hai na lina nguvu kali zaidi kuliko upanga wenye makali
pande mbili, hukata kabisa hadi mahali ambapo moyo na roho hukutana, hadi pale
vikutanapo viungo vya mwili na mafuta. Neno hilo huchambua nia na fikira za mioyo ya
watu.
Kwa hivyo, kama mhuduma hajapewa nafasi ya kushirikiana na watu Neno la Mungu, ambalo ni
muhimu kwa ugawanyaji wa nafsi na Roho, tuna haki ya kujaribu Roho akitenda kazi, ambayo
huzuia tangazo la Neno Lake.
E. Neno la Onyo
Wakati mwingine, mhubiri anaweza kujaribiwa kutoka kwa mimbara, anapolaumiwa kwa
makosa asiyoyatenda, au anaweza kujaribu kuthibitisha haki katika matendo yake kwa kutumia
hali hii bora. Ni lazima akatae mwelekeo kama huu na atumie tu mimbara kutangaza Neno la
Mungu. Walakini, watu watapoteza heshima na imani katika cheo chake. Unapolaumiwa kwa
makosa usiyo yatenda au kutofahamu, mhubiri ni lazima awe na neema ya kushughulikia mambo
haya kwa Mungu. Ni lazima awe mlinzi wake. Mambo ambayo yanahitaji kuelezwa wazi ni
lazima yashughulikiwe katika hali ya kibinafsi na si kwa mimbara. Kazi ya mimbara ni
kutumiwa kwa kuhubiri Neno Lake tu. Kitu kingine chochote ni lazima kichukuliwe kama
kutotumia mamlaka vyema.
Tunapoangalia kusudi halisila kuhubiri, tunaweza kuzungumzia mahitaji, shida na uwezo wa
watu wa Mungu. Hii itawapa mafundisho yao mema, maombi na faraja (1 Wakorintho 14:3).
Kwa ufupi, kanisa litakuwa na mafundisho mema.
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-
19
MASWALI YA MARUDIO - KUHUBIRI! NI NINI?
1. Jaza katika mapengo:
Kuhubiri ni ___________________________ Neno la Mungu. Kwa hivyo ni
____________ ___________kuliko kusanyiko na matamshi ______________
__________________ na maneno yanayotamkwa vyema.
2. Je, kuhubiri na kufundisha kunaelezewaje mara nyingi?
3. Kwa nini jambo la unabii linahitajika sana katika mahubiri ya kipentekote leo? Toa sababu
mbili.
4. Kusudi kuu la kuhubiri ni nini?
5. Jaza katika mapengo:
Mhuduma ni lazima ahubiri ________________ na ajizuie kutoka kwa mahubiri ya
binafsi _____________ kwake mwenyewe. Kabla ya kusimama kuhubiri kwa mimbara,
ni lazima awe _____________ ya kile ___________________ anataka aseme na kile
____________ _________________ anataka kutimiliza kupitia ujumbe.
20
Makala
A. Kupata Makala na Kupokea Ujumbe
Kupata makala sahihi ni muhimu kwa kutimiza kusudi la kuhubiri. Lakini hili jambo mara
nyingi si rahisi, hasa kwa wachungaji wanaohitaji ujumbe mpya kwa jumapili 52 za mwaka.
Wainjilisti wana bahati ya kuhubiri mahubiri sawa mara nyingi kwa sababu wanahubiria umati
mbalimbali. Mchungaji, hata hivyo, anahubiria watu sawa mara mbili au tatu kwa wiki. Shida
ya kutafuta Andiko nzuri halikuwi jambo la kawaida hata kwa wahubiri wakuu kama Spurgeon.
Alitayarisha mahubiri yake katika mistari mifupi mingi kila jumamosi ambazo angeweza
kuhubiri mwezi mzima, lakini hakuweza kutumia hata mmoja, ila tu ule unaofaa. Wakati
mwingine, aliketi kwa masaa akitafuta Andiko sahihi.10
Uthabiti katika kutafuta Andiko sahihi utaonyesha tofauti ya mhubiri na ujumbe kutoka kwa
Mungu. Hughes anadhibitisha kwamba kuna tofauti kati ya mahubiri na ujumbe. Mtu anaweza
kujifunza vile mahubiri yanawekwa pamoja kupitia masomo kwa mfano wa hotuba, lakini mtu ni
lazima asimame mbele ya Mungu kwa kupokea ujumbe. Kutayarisha ujumbe si jambo rahisi,
lakini litagharimu bidii. Ni uzao wa kiroho, kwa hivyo, mhubiri asiwe “mwindaji wa Andiko”.
Mtu ambaye anatafuta fungu la maneno au maneno ambayo amesikia atakumbukwa mara chache
kwa mahubiri ya kufaa.11 Ni wale tu ambao watapata Andiko linaloenda pamoja na ujumbe wa
Mungu wataweza kupata kusudi la kuhubiri.
1. Jinzi ya Kupata Makala Yanayofaa
Kutafuta Andiko/makala yanayofaa na kupokea ujumbe unaofaa ni muhimu. Mungu anapenda
kutuongoza katika majaribu haya, kwa sababu anajali sana kuhusu watu wake ambao wanahitaji
mahubiri ya kufaa hali yao. Anataka mahitaji yao kushughulikiwa, wasiwasi yao na hofu
kubadilishwa na imani, maisha ayao kurekebishwa na maumivu yao kuponywa. Kwa hivyo,
unapotayarisha mahubiri, unahitaji kuanza na maombi, kuendelea na maombi na kumaliza na
maombi.
Tutajua kwamba tumepata Andiko sahihi wakati msitari au sehemu ya Andiko itaenda pamoja na
roho na haiwezi kutoka fikirani mwetu, lakini huanza kujielezea yenyewe. Maandiko
yanapojifunua na kufichua mali yake, tutaona mambo katika Andiko ambayo hatujawahi kuona
mbeleni, hata ingawa tumeyasoma mara nyingi. Spurgeon alisema kwamba kutafutana na rafiki
wa zamani. Tunamjua tunapomwona.12 Tunaweza kuwa na hakika kwamba Mungu ametupatia
ujumbe tunapohisi mzigo na upako, andiko linapojikunjua. Pohl Anasema kwamba kujikunjua
ni kama Andiko linatutafuta badala ya sisi kulitafuta.13 Wakati mwingine, Andiko “litaruka” na
kuja kuwa hai vile tunavyosoma Neno kwa ibada yetu wenyewe. Jambo hili linapotendeka, si
vigumu kutambua sehemu ya maandiko yanayosema “Mungu ndiye hupeana”, hasa wakati fikira
zinapokuja pamoja na kupeana ujumbe. (Ni lazima tuhimize au tuonyeshe kwamba kusoma
Biblia wakati wetu wenyewe ni lazima usiwe usiwe kwa kusudi la kutafuta Andiko la jumapili,
lakini ifanye tu kwa uendelezaji wa kiroho maishani mwetu). Mwanzo wa maelezo ni lazima
ufwatiwe na utafiti na mambo ya ujasiri ili kuufanya ujumbe kufaa.
10 Charles H. Spurgeon, Ratschläge für prediger. (Wuppertal: Oncken Verlag, 1975), ku. 35
11 Huges uk. 89.
12 Ibid., uk.35
13 Adolf Pohl, Anleitung zum Predigen. (Wuppertal: Onken Verlag, 1976), uk. 11.
21
Wakati mwingine ni lazima tutafute Andiko kwa kuomba muda mrefu kwa kupiga magoti yetu
chini. Hili linaweza kuwa jambo la kuchosha na linahitaji uthabiti. Walakini, hatuwezi
kusimama mbele ya watu wa Mungu bila Neno kamilifu kwa saa moja. Ni lazima tujionyeshe
kama watumishi wa Mungu na watu wake hata kama ni vigumu kutafuta Andiko sahihi na
ujumbe. Kutumika kunamaanisha kufanya kazi na kupinga majaribu ya kutafuta njia rahisi ya
kufanya mambo wakati mambo yanakuwa magumu. Kwa hakika, hatuwezi kupata ujumbe
sahihi kwa kusimama mbele ya maktaba yetu ya binafsi, kwa kusoma sana ufafanuzi tofauti na
vitabu.
Baada ya fungu la maneno ya maandiko kupatikana, yanahitajika “kuchovya” katika maombi!
Mahubiri mengi yamekosa kutimiza kusudi lake kwa sababu yanakosa upako wa kiroho ambao
hupatikana tu kupitia Roho Mtakatifu. Ni jambo la kuhuzunisha ikiwa mahubiri yanahusu wenye
akili, yakienda kutoka fikira moja hadi nyingine lakini yakiwacha nje moyo na roho wa mhubiri
na msikilizaji.
2. Ujumbe na Andiko
Wakati mwingine, Mungu ataweka ujumbe moyoni mwetu, nasi twahitaji kutafuta Andiko
ambalo linafaa. Kwa njia hii, hatutapokea ujumbe kwa kusoma maneno fulani ambayo
tumepewa, bali tutaupata ujumbe huu tukiwa maombini au tunapowasiliana na Mungu labda
wakati tunapoendesha gari letu na kadhalika. Baadaye, mawazo haya yatakuja pamoja kwa
urahisi na kuwa ujumbe kamili, Roho wa Bwana atatuongoza kwa Andiko sahihi ambalo ujumbe
utahusika nalo. Tunaposoma maandiko, mhubiri ni lazima ahakikishe kwamba Andiko ambalo
amesoma linatumiwa kama “chanzo cha ujumbe”. Kwa ujumbe ambao Mungu ameweka moyoni
mwake. Kwa sababu nyingine, wasikilizaji watachanganyikiwa wakati wanapokuwa wakitarajia
ufasiri wa ujumbe kusomwa.
3. Kukosa Kutafuta Andiko
Je, kitu gani kitafanyika kama tutakosa kupokea ujumbe? Hili ni swali ambalo linaulizwa mara
nyingi na liko sawa hivyo, kwa sababu mhubiri kwa hakika atakuwa na wakati kama huu. Haya
yakitendeka , ni lazima aombe tena. Mchungaji ninayemjua alikumbwa na shida kama hii
alipoulizwa kuhubiri katika mkutano wa kimataifa Ujerumani. Hata baada ya kufunga kula,
haikujalisha matokeo yoyote, alienda msituni kabla ya siku ya mkutano wa kimataifa mkuu,
akimlilia Mungu. Alikuwa karibu kukata tamaa alipoupokea ujumbe mara moja. Mahubiri yote
yaliyohubiriwa mkutanoni mwake yalikuwa ndiyo mema. Mungu alikuwa ameitikia uvumilifu
wake. Tunapohubiri makanisani mwetu , tunajaribiwa kutochukua mambo kwa uangalifu vile
inatakikana kama tungeweza kuhubiria maelfu ya watu. Hapa ndipo mahali mhubiri anaweza
kuonyesha uaminifu wake. Wakati kama huu wa kukata tamaa, wewe kama mchungaji mwenye
ujuzi ni muhimu na masomo muhimu ambayo Mungu anapitia kutukumbusha kumtegemea.
Kwa bahati nzuri, utafiti wa Andiko sahihi si mzigo mara nyingi. Mara nyingi ni rahisi
kupatikana, ujumbe huu huja fikira haraka tunaposoma maandiko, na kutangaza ujumbe kwa
ufupi.
B. Nguvu za Mahubiri
Hata ingawa mhuduma hawezi kujifunza kutoka kitabuni vile anaweza kupata andiko sahihi au
ujumbe kwa washiriki wake (umati) mashauri yafuatayo yanaweza kumsaidia kupata nguvu kwa
mahubiri mapya.
22
1. Kufikiria Mahitaji ya Kiroho
Mhubiri ni lazima ajue mahitaji ya kiroho ya washiriki wake, mwili wa Kristo wote, na jamii
ambazo anaishi nazo. Lazima afikirie mambo ya kimwili, mali na mahitaji ya uadilifu ya watu
wake na ya wale anaokutana nao kila siku Anapokuwa maombini, ni lazima awaruhusu
washiriki wake wapite mbele ya macho yake ya kiroho, ili aweze kujua shida ambazo anaweza
kuzungumzia katika mahubiri yake. Utovu na ugumu wa kanisa unaweza kusaidia kudhihirisha
mahubiri. Unapotenda kazi ya uchungaji au kutembelea hospitali, mhudumaanaweza kuona
mahitaji ya ujumbe fulani. Kwa ufpi lazima aangalie kukua kwa kiroho kanisani mwake.
Spurgeon anashauri kwamba dhambi ambayo imeenea kanisani ni lazima izungumziwe.
Anazungumzia watu wa ulimwengu, wa tamaa, ambao hawaombi, mwenye hasira, kiburi, bila
upendo wa undugu, waongo na waovu mwingine.14 Vile vile, mifano ya kuanguka kwa imani,
mafundisho yasiyo ya kweli au shida muhimu inayoingia kanisani lazima ishughulikiwe na
mwelekeo wa Mungu, ili mateso haya yaweze kusimamishwa kabla ya kutenda uharibu wake.
Walakini, tunapofikiria mahitaji na dhambi za watu wetu lazima tuzuie majaribu na
kuyashutumu kutoka kwa mimbara. Spurgeon anasema kwamba mimbara imeitwa “ngome ya
waoga”, ambayo kulingana naye mwenyewe ni jina sahihi kwa mahali hapa, wakati wapumbavu
wanapopanda jukwa na kwa ushupavu wao wanawatukana wasikiliaji wao kwa kushikilia
makosa yao waliyokiri au kutangaza udhaifu wao hadharani.15 Bila uangalifu mhubiri anaweza
kuzungumzia maneno ya kibinafsi na hata ya kuchukiza akiwa mimbarani. Anaweza kusema
vitu ambavyo hatakikani kusema. Ni lazima awe na hakika kujitahidi kuwa na nia sahihi ili
aweze kuzungumza ukweli katika upendo. Neno la Mungu laweza kutenda kazi bila usaidizi wa
kimwili.
2. Kuketi Chini ya Miguu ya Wengine
Wakati mwingine, tunaupokea ujumbe tunapowasikiliza watu wengine wa Mungu au
tunaposoma vitabu vingine vya ukristo. Fikira nyingine zimaweza kujapamoja, na kuanza
kutayarisha ujumbe moyoni mwetu. Rafiki yangu mmoja ameeleza njia hii kama “kukamua
n´gombe ili kutengeneza siagi yetu”. Ni lazima tujizuie kwa majaribu kwa kurudia kuhubiri
mahubiri ya mtu mwingine au ujumbe unaopatikana katika utafsiri mwema au kitabu cha ibada.
Kwa sababu si vibaya kutafsiri neno ambalo tumelipokea katika njia kama hizi na kulifanya
mahubiri, litakuwa jambo lisilo la busara kuhubiri fikira za watu wengine, na kuonyesha fikira
hizi kuwa zetu wenyewe.
Mtu mwingine alisema, kusoma vitabu vizuri ni kama maji makavu - hustawisha fikira zetu.
Habari za maisha za watu wakuu wa Mungu pamoja na ibada za kusifu zimeweza pia kuwa
chanzo cha upuzio wa mhubiri.
3. Kuchunguza Mambo ya Ulimwengu
Mhubiri ni lazima ajijulishe na mambo yanayofanyika ulimwenguni -kupitia magazeti ya habari
au kwa kusikiliza habari za kila siku. Kwa sababu mambo yanayofanyika ulimwenguni
yatashawishi fikira za washirika wake, mhuduma wa injili ni lazima ayaonyeshe kwa maelezo
kamili na katika upana ambao umepenwa na Neno la Mungu
4. Kuangalia Safari ya Kiroho ya Mhuduma
14 Charles H. Spurgeon, Lectures to my Students. (Granda Rapids Baker House, 1977), uk. 91
15 Ibid., uk. 92
23
Mahubiri mengine yana chanzo chake katika ujuzi wa kiroho wa mhuduma. Mahubiri yake
yatakuwa ya ndani mno na ya upendo atakapoweza kuhubiri kuwa na ushahidi ni juu ya chukizo,
ubadilisho na shida kutokana na ujuzi wake mwenyewe wa kibinafsi.
5. Kufikiria Kalenda ya Mkristo
Hata ingawa kama wapentekote tunaamini katika kuongozwa na roho, wakati wa kutangulia siku
kuu ya kuzaliwa kwa yesu Kristo, Krismasi, Pasaka, Kupaa na Pentekote inaweza kupeana
msingi kwa mahubiri muhimu. Tunaweza pia, kuhubiri ujumbe wa pasaka katika Krismasi,
ikiwa tumeongozwa na roho wa Mungu sana, lakini itakuwa vyema sana kufikiria kwa.kufaa.
6. Kuangalia shauri Kamili la Mafundisho ya Biblia ya Wakristo
Mhubiri ni lazima ajiulize mwenyewe kila mara ikiwa anatangaza kamili mausia ya Mungu, au
kama amewacha nje mafundisho muhimu ya Biblia. Kama yeye si mwangalifu, anaweza
kuangalia kwa urahisi mambo yasiyo muhimu. Hadithi inaambiwa ya mhubiri ambaye mara
nyingi alihubiri kuhusu ubatizo wa maji hadi wakati washiriki wake walipomchagulia Andiko,
ambalo lilikuwa Mwanzo 1:1, “Mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi”. Baada ya kusoma
Andiko, alisema mwanzoni Mungu aliumba na nchi. Kwa sababu nchi ilikuwa na asili mia 70 ya
maji, na hii inatuonyesha tena umuhimu wa ubatizo wa maji. Ujumbe wetu wa kupendeza labda
hautaweza kuwa ubatizo wa maji bali huenda imani, miujiza, mwisho wa mambo, kuwa
mtumishi na kadhalika. Mbali na mambo haya, ni lazima tuwapatie watu wetu chakula cha
kiroho chenye kila kitu. Mahubiri yetu yahusike kila wakati na mahubiri makuu ya Biblia kama
utatu, maongozi ya Mungu, ufunuo, kuja kwa Yesu mara ya pili, na kugeuzwa kwa Yesu katika
mwili, pentekote na mengine. unapoyaweka mambo haya pamoja kuwa mahubiri, ni lazima
ujumbe ubaki wa kufaa. Ukweli muhimu usihubiriwe kama masikio tu lakini uonyeshwe kwa
maisha ya kisasa.
7. Ustaarabu wa Daftari
Wote, Blackwood16 na Evans17 wanashauri ustaarabu wa daftari. Kila mara,fikira yoyote,
maelezo, uangalifu au majadiliano ambayo yanampendeza mhuduma, lazima ayaandike chini.
Uangalizi huu unaweza kufanyika anapokuwa akisoma Neno la Mungu au wakati wake nje ya
chumba cha kusoma. Evans anasema kwamba wakati mwingine ambapo ni vigumu kupata
Andiko, yeye hurudi katika daftari na hupata moja pale ambayo imepigwa msitari. (Kwa hivyo
ni jambo la busara kwamba dokezo la fikira yake lishughulikiwe). Na kama anajihisi bila
ujumbe, anaweza kuupata kutoka kwa hii manna. Katika njia hiii, atakuwa na akiba imara ya
ujumbe, na hataweza kukosa cha kuhubiri.18 Wengine wanapokea fikira mpya, wanapoenda
matembezini, wengine wanapokuwa wakioga au wanapokuwa wakisafiri kwa basi. Mimi
mwenyewe hupata ujumbe wa kuhubiri ninapokuwa nikiendesha gari safari ndefu. Hasa wakati
kuna msongamano mdogo wa magari, fikira zangu ziko huru kusikia kutoka kwa Mungu. Katika
njia hii, ni vyema kuwa na utepe wa ujumbe au fikira zetu. Kila mhubiri aandike chini masomo
tofauti yanapokuja mara kwa mara. Fikira nyingi nzuri zimepotezwa kwa sababu tumekosa
kuziandika chini.
16 AndrewW. Blackwood, Matayarisho ya Mahubiri. (Nashville: Abingdon, 1948), uk. 39.
17 Williams Evans, Jinzi ya kutayarisha Mahubiri. (Chicago: Mooody Press, 1980), uk. 26.
18 Ibid., uk. 27.
24
8. Kujaza Fikira na Neno la Mungu
Ni lazima tutafute kila mara ujumbe mpya. Lazima roho yetu iwekwe katika hali ya utendaji. Ni
majonzi kwa mchungaji anayepoteza wakati wake. Mhubiri anayechukua mambo kuwa rahisi
kutoka jumatatu hadi jumamosi anahitaji kuhisi aibu. Hawezi kumtarajia Mungu kumpatia
ujumbe jumamosi jioni baada ya kupoteza nafasi yake wiki nzima. Atapokea “ujira” kwa
uzembe kama huo anaposimama mbele ya watu na hana chochote cha kusema.
Baada ya kuorodhesha “nia za mahubiri”, ni lazima iwekwe mkazo kwamba mwongozo wa Roho
Mtakatifu ni mkuu zaidi katika utafutaji wetu wa ujumbe au Andiko. Tunapoishi katika uwezo wake
kila mara na mwongozo wake, hatutakosa hata kodogo ujumbe kutoka kwake kwa watu wake.
Wakati mwingine, tunajihisi tunaongezwa kuhubiri ujumbe ambao tumeshahubiri siku nyingine.
Hii hufanyika hasa tunapokaribishwa kuhudumia umati ambao haujatusikia hata kidogo
tukihubiri. Mimi mwenyewe ninapendelea kufuata shauri la Spurgeon, alisema kwamba mahubiri
yanaweza kuwa mazuri baada ya kuhubiri mara 10. Walakini, tusichukue kila mahubiri ambayo
yamehubiriwa na Mungu wakati mwingine na kurudi kuhubiri. Matokeo yatakuwa maangamizo.
Yatakosa nguvu, uhai na upako. Kabla ya mahubiri kurudiwa kuhubiriwa, ni lazima yatakazwe
na yafufuliwe katika maombi.
C. Uangalifu Katika Uchaguzi wa Andiko au Somo
Tunapochagua Andiko, ni lazima tuchukue uangalifu fulani ili tuepukane na hangaiko lisilofaa
na uharibifu kutoka kwa kusudi la ujumbe. Maongozi yafuatayo yatatusaidia kufanya hivyo.
1. Usiahidi Kile Usichoweza Kupeana
Tusihubiri mambo ambayo hayawezi kuwazika, na ambayo yanakosa umuhimu, kama njia za
adhabu, mbingu ya tatu na kadhalika. Evans anaonyesha kwamba fikira kuu kama hizi zaweza
kuwekwa pamoja na kuwa mahubiri, lakini hazitatengeneza mahubiri mazuri yao wenyewe.19
2. Usichague Maandiko Hafifu
Mhubiri ni lazima ajizuie kutumia maandiko asiyoyajua sana, au ambayo ni hafifu. Mfano wa
jambo hili la kwanza utakuwa miti katika kitabu cha Ufunuo au kundi la nzige. Mfano wa
Andiko huenda utakuwa “kwa maana alikuwa mfupi wa kimo” (Luka 19:2), au “kisha mbwa
wakalamba damu yake” (1 Wafalme 22:38).
3. Muda Unaofaa wa Maandiko
Wahubiri wengine wanapendelea maandiko marefu, na wengine hupenda mafupi. Kwa kawaida
hakuna sheria ambayo inatusaidia kujua ni gani kati ya mambo haya mawili ni mazuri. Walakini,
maneno machache yanaweza kukumbukwa kwa urahisi, hasa kwa sababu yanamwezesha
mhuduma kuyarudia anapohubiri. Jambo kuu la kuonyesha kuhusu uchache wa maneno lisiwe
chaguo letu bali lazima lihusike na mwongozo wa Roho Mtakatifu. Kama maandiko mengi ni
muhimu kwa kupata lengo ambalo ametupatia, halafu ni lazima tutulie kwa mahubiri ya maneno
marefu. Na kama maandiko mafupi yatatimiliza kusudi lake, basi maandiko yatakuwa mafupi.
19 Ibid., uk. 30.
25
4. Andiko na Yaliyomo
Andiko laweza kuwa na maana tofauti wakati linatumiwa tofauti na maneno mengine ambayo
hudhihirisha maana yake. Kuzungumzia kando na maana ya yaliyomo inamaanisha ni kuliondoa
maana halisi ya maandiko, au kutumia sehemu ya msitari kama “hakuna Mungu”, ukiwacha nje
“mpumbavu amesema moyoni mwake” (Zaburi 14:1). Mfano huu wa kwanza ni uvunjaji wa
maandiko kwa sababu hugeuza maana yake, na wa pili huiba asili ya kusudi lake. Kwa mfano
kutumia Yohana 3:4, kama maandiko ya toba (ubatizo) ni uvunjaji wa utafsiri wa mambo ya
maandiko.
5. Kuangalia kwa Wema
Maandiko kwa kawaida ni hakika na si kinyume, kwa hivyo tutende hivyo katika kuhubiri kwetu.
imeshauriwa kwamba tunapohubiri kutoka kwa Zaburi 1 ni lazima tutumie muda wetu mwingi
tukizungumzia kuhusu mti wenye mazao kuliko mausia ya wasio wa Mungu. Tunapohubiri
kuhusu nyumba mbili ambazo zimetajwa katika mahubiri ya mlimani, lazima tuwekee mkazo
nyumba ambayo ilisimama wakati wa dhoruba, na si ile ambayo ilianguka.20 Unahitaji kutumia
msitari halisi wa maandiko kuliko ule unaozungumzia kinyume. Kwa mfano, mhubiri ni lazima
aweze kupata Andiko lingine kuliko, “sasa huyu mtu alinunua uwanja na ujira wa dhambi,
akaanguka chini akapasuka na matumbo yake yakamwagika nje” (Matendo 1:18), unapohubiri
juu ya mshahara wa dhambi.
20 Blackwood, uk. 51.
26
MASWALI YA MARUDIO - MAKALA (MAANDIKO)
1. Ni jambi gani la muhimu sana la kutimiza kusudi la kuhubiri?
2. Ni tofauti gani italetwa na uvumilifu katika kutafuta Andiko sahihi?
3. Ni kitu gani kinahitajika kufanywa baada ya kupata Andiko sahihi?
4. Taja mambo manane ambayo yanaweza kukusaidia kupata shawishi kwa ujumbe mpya.
1) __________________________________________________________
2) __________________________________________________________
3) __________________________________________________________
4) __________________________________________________________
5) __________________________________________________________
6) __________________________________________________________
7) __________________________________________________________
8) __________________________________________________________
5. Ni jambo gani kuu linaonyesha urefu wa maneno ya maandiko?
27
Kanuni za Utafsiri
IV. Kanuni za Utafsiri
Baada ya Andiko nzuri la kanuni la utafsiri wa maneno kupatikana (Kanuni za Utafsiri wa
Maandiko) ni lazima zitumiwe kuonyesha maana halisi ya Andiko lililochaguliwa. Gottfried
Adams anasema vyema kwamba kabla ya utafsiri mzuri wa maandiko kufanyika, mkalimani
lazima apende kuweka kando mafundisho ya madhehebu na mawazo aliyowaza mbeleni.21 Ni
hapo tu ataweza kuanzisha maana ya ukweli wa maandiko. Mara tu mhubiri atakapopenda
kukaribia maandiko kwa haki maana ya maandiko yafahamika kwa kutumia kanuni zifwatazo na
utaratibu.
A. Kuanzisha Maana ya Kweli ya Maandiko
1. Maana ya Mwanzoni ya Maandiko
Jambo kuu miongoni mwa kanuni la utafsiri wa maandiko ni kugundua maana ya asili ya andiko
kupitia “exegesis” maana yake ni kuchora nje, maana ya maneno moja hadi lingine na yote kwa
jumla.22
Njia bora ya kupata maana ya kweli ni kusoma maandiko katika lugha yake ya asili. Hii itaweza
kuwa ngumu kwa wahuduma wengi katika Afrika. Walakini wale ambao hawawezi kusoma
maandiko katika labda lugha ya kigriki au Kihebrania ni lazima wasikate tamaa, bora tu
wanafahamu kingereza. Kuna maongozi mengine ya masomo ambayo yaweza kumsaidia mhubiri
kusoma maana ya asili ya Andiko. Maongozi mengine ni kutoka kwa “kamusi ya mzabibu ya
kuelezea maneno ya kiyunani”, wuest ya masomo ya Kiyunani.
2. Kuwazia Maneno Yaliyomo
Maneno yaliyomo ni maandiko kabla na baada ya maneno chini ya wazo la uangalifu. Mara
nyingi mtu hahitaji kusoma tu mistari michache ambayo inafuatana na maandko, bali anahitaji
kusoma sura nzima au sura nyingi ili kujua yaliyomo. Wahubiri wengi wanapuuza unganisho la
maandiko wanapochagua msitari wa maandiko. Wanachagua nje ya utaratibu wake, kwa hivyo,
huharibu maana yake ya kweli. Ni lazima kwa mhubiri kusoma maandiko katika hali yake ikiwa
anataka kutafuta ujumbe wake wa kweli. Kama sivyo mtu anaweza kwa urahisi kuhubiri
mahubiri juu ya “si vizuri mwanamume kuoa” ambayo yanapatikana katika 1 Wakorintho 7:1.
Ukweli ni kwamba hii si amri kutoka kwa Mungu lakini ni ushauri kutoka kwa Paulo. Mapenzi
ya Mungu kuhusu ndoa yameelezwa katika kitabu cha Mwanzo ambapo anasema si vyema mtu
kuishi pekee yake.
3. Wakati, Njia na Desturi ya Maandiko
Je, mwandishi anataka kueleza nini? Alimwandikia nani? Walikuwa watu wa mataifa, waroma
au Wayahudi? (Kitabu cha Wagalatiakwa mfano kiliandikwa hatarini ya kufungwa katika sheria.
Kitabu cha Waebrania kiliandikiwa waumini Waebrania, na kadhalika. Je! vitabu vya Waraka
viliandikiwa kikundi fulani au mtu binafsi? (Filemoni, Tito, 1&2 Timotheo, viliandikiwa watu
binafsi). Je! maandiko yanaonyesha tabia na desturi ya wakati wake? Kama ni hivyo, je,
maandiko yana maana sawa kwetu, kama yalivyofanyika kwa watu katika siku za Biblia, au
21 Gottfried Adam, Einführung in die Exegetischen Methoden. (Grünewald: Kaiser, 1979), uk. 11.
22 Ibid., uk. 52.
28
yalikuwa yao tu? Haya ni maswali sawa lazima yaulizwe tunaposoma maandiko. Biblia
hudhihirisha historia na msingi wa desturi wa maandiko yanaweza kutafsiriwa vibaya. Gordon
Fee anasema kwamba habari kama hiyo ni ya kuonya kwa kufahamu maandiko mengi.23 Kwa
mfano, jambo la wanawake kufunga vichwa vyao vitambaa linafahamika bora wakati jambo hili
linatekelezwa ambalo hutoa habari ya msingi kwa barua ya kwanza kwa Wakorintho.
Siyo tu ufahamu sahihi wa desturi ya Biblia utaweza kuendeleza ufahamu wetu wa maandiko,
bali pia ni kuruhusu maandiko kuwa hai. Kwa mfano, tunapozungumzia kuhusu mfano wa
mpanzi, mhubiri anaweza kuongezea mahubiri yake mambo mengine mazuri kuhusu hali ya
shamba ambayo yalijulikana kwa mkulima wa Galilaya. Katika Israeli, mashamba yako
mlimani, madogo kwa kiwango, na karibu yote yamefunikwa na mawe. Watu hutengeneza kitu
kama daraja ya mawe na kutembelea juu yake. Mchanga wa juu hauki ndani kabisa, na kwa
hivyo, mizizi ya miiba humea ndani ya ardhi sana. Kama unataka kuiangamiza kabisa, mkulima
anahitaji kulima au kuchimba ndani ya ardhi karibu sentimita arobaini (40 cm). Lakini
ilichomwa tu, na tena ilimea. Mkulima wa Galilaya alifahamu msemo huu wa Bwana, aliposema
kwamba mbegu nyingi ziliharibiwa. Walijua kwamba mpanzi hakuwa mzembe katika upandaji
wake, lakini alikuwa amehesabu hasara kabla ya kuanza.
Kusoma nyakati za Agano la Kale na Agano Jipya kutatupatia mwanga bora wa maana ya
maandiko. Kwa mfano, ni muhimu kufahamu kwamba nyumba katika Israeli zilikuwa na paa
laini na wakati wa miezi ya jua kali, watu walilala juu yake, kwa sababu ndani ya nyumba
kulikuwa na joto jingi sana. Kwa sababu mambo haya tunaweza kufahamu vile marafiki wanne
wangeweza kubeba mwanaume kiwete juu ya nyumba na hataimaye kumteremsha ndani ya
nyumba ili Yesu amponyeshe. Tunakubaliana kwa mshangao wa Paulo, “maskini miye! nani
atakayeniokoa kutoka katika mwili huu unaonipeleka kifoni?” (Warumi 7:24) ikiwa twaweza
kufahamu adabu ya kuogovya ambayo Paulo anazungumzia. Mhalifu alipomwua mtu mwingine,
alihukumiwa kifo kwa kufungwa na nyororo kwa mwili wa yule ambaye alimwua. aliachwa pale
kupumua harufu ya mwili huo kwa kuwa karibu nao hadi wakati yeye atakufa pia.
Vitabu vya maelezo ya Biblia, vinafafanua na nakili zingine zitatusaidia kwa msingi wa kusoma
Biblia.
4. Linganisha Andiko na Andiko
Ni muhimu sana kujua maana ya maandiko kwa kulinganisha andiko na lingine. Kama si hivyo,
twaweza kwa urahisi kuanguka katika makosa na hata katika hatari ya mafundisho yasiyo ya
kweli. Kwa mfano ujumbe wa manufaa haungekosekana kama waenezaji wake wangeweza
kutambua maandiko kwa njia hii. Zaidi na hayo, “sisi ni miungu” jambo ambalo ni asili ya
Yohana 10:35 halingeanzishwa kama waendelezaji wake wangekuwa wamesoma Neno katika
Zaburi 82:6, maneno ambayo Yesu alitaja. Kama wangekuwa wamelinganisha maandiko na
mengine, wangejua kwamba waamuzi ambao si wa haki walionyeshwa kama miungu, walikuwa
kwa kweli wamewekewa wakfu kutekeleza haki kwa niaba ya Mungu. Lakini Mungu pia
aliwaweka kwa sababu walikosa kutoa uamuzi na kutawala katika utakatifu. Kwa hivyo, Yesu
alipozungumzia kuhusu msitari huu wa maandiko, hakujaribu kuanzisha jambo kwamba sisi ni
miungu, bali alikuwa anaonyesha kwamba Mafarisayo hawana haki ya kumhukumu, kwa sababu
waamuzi wasio wa haki waliitwa miungu. Pia, kama waendelezaji wa jambo hili wangefikiria
mausia ya maandiko na mafundisho yake kuhusu asili ya dhambi ya mtu, hawangejitangaza kuwa
miungu. Vivyo hivyo, wale wanaoamini katika kizazi cha ubatizo ni lazima walinganishe
Yohana 3:5 na maandiko mengine ambayo yanaonyesha waziwazi kwamba maji hayawezi
23 Gordon D. Fee, New Testament Exegesis. (Philadelphia: Wetminister Press, 1983), uk. 94
29
kuosha dhambi za mwanadamu, bali ni damu ya Yesu. Mifano mingine mingi inaweza
kupeanwa, ambayo inaweza kutumiwa kwa mambo ya uadilifu, lakini wakati na nafasi
haviruhusu.
Ni muhimu zaidi kukusanya maandiko mengi iwezekanavyo kwa somo ambalo twahitaji
kuhubiri, kwa hivyo, tutaweza kuonyesha mausia yote ya maandiko kwa somo hili.
B. Fumbo la Maneno - Kwa Kufanya Kiroho
Matumizi ya fumbo la maneno ambayo yanafanya kiroho maandiko fulani yameshutumiwa na
wengi. Walakini, mimi mwenyewe ninapenda kukubaliana na Spurgeon ambaye anasema
kwamba, kama tungeweza kulalamikia baraza la ushauri la ubusara, lenye wahubiri waliofaulu,
ambao si wenye elimu tupu, bali watu ambao wako kiwanjani kwa ajili ya kazi hii, tungekuwa na
kura za wengi wa kutuunga mkono kutumia fumbo la maneno.24 Kwa sababu twahitaji kupinga
jambo la kufanya maandiko kiroho, tusidharau walekevu wake kabisa, ikiwa tu yako katika
mipaka ifuatayo.
Kwanza, ni lazima tunapohubiri, tuonyeshe ukweli wa dhahiri na kuwekea mkazo maana ambayo
imepewa ya maandiko. Fumbo la maneno ni lazima lisiruhusiwe kuchukua mahali pa maana pa
kweli pa maandiko. Kwa mfano unapohubiri kuhusu safari ya Eleaser kumtafutia mchumba
mwana wa Ibrahimu, ni lazima tuonyeshe jambo la hakika la kihistoria. Hapo ndipo maandiko
yanaweza “kufanywa kiroho”, kwa kuelewa kwamba, Ibrahimu alipokuwa akimtafutia mwanawe
mchumba, Baba wetu wa mbinguni anamtafutia mwanamke mchumba. Kwa sababu Rabeka
alihitaji kuhitimu mambo fulani kuwa mchumba, kwa hivyo pia mchumba wa Kristo ni lazima
awe na sifa fulani. Rabeka alipomfwata Eleasar kwa kupenda kwake, vivyo hivyo mchumba wa
Kristo ana watu wa “kujitolea”. Rabeka alikuwa anapenda kuolewa na Isaka hata kama alikuwa
hajawahi kumwona hata kidogo. Vivyo hivyo, kanisa halijamwona Bwana, lakini linajitayarisha
kumwona. Tunapofanya mfano wa msamaria mwema kiroho, ni lazima tuelezee jambo muhimu
la hadithi, ambalo jukumu lake ni kuwasaidia wale ambao wana haja.
Pili, tusilazimishe maana ya kiroho kwa maandiko ambayo hayawezi kutuelekeza katika njia hii.
Fumbo la maneno lisiende kinyume cha fikira ya kawaida. Spurgeon anapeana mfano wa
mhubiri ambaye alitumia maandiko. “Nilikuwa na vikapu vitatu vyeupe kwa kichwa changu”,
kutokana na ndoto ya mwogaji mkate wa Farao. Kuhusu maandiko haya, alitoa mahubiri kuhusu
utatu. Kusema kweli, njia hii inafanya jambo la kufanya maandiko kiroho mbali.
Tatu, ikiwa tu fumbo la maneno litakuwa katika hali ya haki ya Biblia, picha na mifano inaweza
kutumiwa. Kwa mfano, Waebrania 10:1 inatuambia sheria ya Wayahudi si picha kamili ya
mambo yale halisi, ni kivuli tu cha mema yanayokuja. Zaidi ya hayo, tunapata fumbo la maneno
ambalo linatumiwa na waandishi wa Agano Jipya ili kuelezea mfano wa kweli wa Kristo. Kwa
mfano, kulingana na kitabu cha Waebrania 8-10, ni mfano wa ukweli wa Agano Jipya. Na mti
wa mzabibu ni mfano kwa Israeli. Paulo anasema zaidi kwamba Waisraeli ni mifano ambayo
iliandikwa kwa manufaa yetu.
Basi, mambo yaliyowapata wao ni kielelezo kwa wengine, na yaliandikwa ili kutuonya
sisi ambao mwisho wa nyakati unatubariki. 1 Wakorintho 10:11
Kama unaongozwa na ubusara huenda fumbo la maneno mazuri yanaweza kutumiwa. Kwa
kweli itawashawishi wasikilizaji na kuwaweka imara. Walakini, kufanya maandiko kiroho ni
24 Ibid., uk. 103.
30
lazima itumiwe kiasi. Ikiwa mhubiri amepewa nafasi atumie maandiko ili yawe na maana yake
ya asili. Kwa kutumia maneno haya ya uadilifu, tunafwata onyo la upole la Paulo ambaye
alishauri kugawanya katika unyofu “Neno la ukweli” (2 Timotheo 2:15). Tunapofwatana na
sheria hizi ndipo tunaweza kutayarisha mahubiri mema.
-.-.-.-.-.-.-.-..-.-.-.-.-.-..-.-.-.-.-.-.-.-.-..-.-.-.-.-.-.-.-.-.-
31
MASWALI YA MARUDIO - MAFUNDISHO YA UTAFSIRI
1. Je, ni kitu gani lazima kifanywe kabla ya utafsiri wa maandiko kufanyika?
2. Ni jambo gani la kwanza miongoni mwa mambo ya utafsiri wa maandiko?
3. Tunamaanisha nini kwa kusema “mambo yote yaliyomo”?
4. Jaza katika mapengo:
Si tu ______________ ufahamu wa desturi ya Biblia itaendeleza ____________ yetu
_______
ya ________________, bali itaruhusu pia maandiko kuja kuwa _______________.
5. Kwa nini ni muhimu sana kujua maana ya maandiko kwa kulinganisha maandiko na
mengine?
32
Aina Mbalimbali za Mahubiri
Kuna aina mbalimbali za mahubiri ziitwazo, kiini cha maneno, ufasiri na mambo yanayo
fikiriwa. Kila moja ni tofauti na ya kiajabu. Ni lazima tupate ufahamu wa kila njia na vile
inatumiwa. Wahubiri hupenda kutumia njia moja, ambayo wanaipenda sana. Mhuduma mwema
hujifunza kutumia kila njia ya kuhubiri kila mara. Kama njia moja imetumiwa sana, watu
watapoteza moyo wa kupenda kutusikiliza.
A. Kiini cha Maneno ya Mahubiri
Kiini cha maneno ya mahubiri ni msingi wa ujumbe. Neno Andiko limepatikana kutoka kwa
neno la Kirumi “teytus” au “teyta” ambalo linaonyesha kitu ambacho kimefumwa au kusokotwa.
Linaweza pia kutafsiriwa kama “vifaa vilivyosokotwa”. Kulingana na utafsiri huu, ni rahisi
kumalizia na kusema kwamba ujumbe wa kiini cha maneno ni kitu “kilichosokotwa” kutoka kwa
maandiko.
Mahubiri ya kiini cha maneno yanahusika na usomaji wa uangalifu wa maneno mafupi. Njia hii
huchanganua maandiko na haiitumii tu kama mambo ya kurukia kwa somo fulani. Itawaongoza
wasikilizaji katika maandiko na sio mbali na maandiko, vile mahubiri ya kufiria yanavyofanywa.
Hata kama kiini cha maneno ya kuhubiri kinachanganua msingi na maana ya asili ya maneno,
hakitaonyesha matumizi ya maandiko.
Maandiko hupeana umbo na utaratibu wa mahubiri. Yanahusika na maana halisi ya ujumbe. Hii
itafanya mambo rahisi kwa washiriki kufuata. Ujumbe ukijikunjua, msikilizaji ataongozwa
kupitia mahali ambapo pamedokezwa na maandiko. Nji ya mahubiri ya kiini cha maandiko
haijiongozi yenyewe kwa maandiko yanayoshawishi ujumbe. Kama mhubiri si mwangalifu,
anaweza kutumia njia ya mahubiri kama haya vibaya. “Blackwood mwenye cheo cha Uhauri
(Exhorter) ambaye alihubiri kutoka katika kitabu cha Mwanzo 5:24 Enoka akaenenda pamoja na
Mungu, naye akatoweka; maana Mungu alimtwaa. Badala ya kushughulikia maana ya dini ya
mtu kama urafiki wa ndani na Mungu”, alichagua njia ya utambaazi wake mwenyewe. Katika
mfano wa mahubiri wa kiini cha maaandiko, alizungumzia kwanza kutembea kwa Enoka na
Mungu, na kisha juu ya maneno, “Hakukuwa”: “Enoka hakukuwa kanisa lenye kuamriwa na
maaskofu, kwa sababu alitembea, hakucheza danzi. Enoka hakuwa mbatizaji, kwa sababu
alitembea, hakuogelea, Enoka hakuwa mtu wa kusadiki kwamba makasisi watosha katika kanisa
wala hakuna haja ya maaskofu, kwa sababu alitembea na Mungu. Enoka hakuwa mfwasi wa
mafundisho ya Yohana Wesley, kwa sababu Mungu alimchukua”.25 Mfano kama huu ni wa
kuchekesha, lakini usiigwe. Mifano ya mahubiri haya iko katika mwisho wa somo hili.
B. Mahubiri ya Ufasiri
Mahubiri ya kiini cha maneno na mahubiri ya ufasiri yana uhusiano wa karibu. Yote mawili
yanafanana. yote ni maelezo ya maandiko, lakini hutofautiana kwa wingi wa maneno ambayo
yamechaguliwa. Mahubiri ya ufasiri huelezea kwa urefu, mahubiri ya kiini cha maneno kwa
upande mwingine ni maelezo ya maneno katika ufupi. Aina hizi zote za kuhubiri hutukuza
maandiko, kwa sababu yanafanya juhudi kuonyesha maana ya maandiko, na matumizi yake sasa.
Mahubiri ya kiini cha maneno yanaweza kugeuzwa na kuwa mafundisho kwa sababu yanahusika
na utafiti mwingi wa andiko moja maneno mafupi. Mahubiri ya ufasiri, walakini, huwekea
mkazo kuhubiri. Mhubiri wa mahubiri ya ufasiri yanahusika sana na njia ya kukutana na
mahitaji ya mwanadamu kuliko kuelezea maana ya maneno ya kigriki na ya kihebrania.
25 Adams, uk. 75.
33
Mambo yaliyotendeka ya kihistoria na masimulizi katika Agano la Kale na Agano Jipya ni
maelezo kamilifu kwa mahubiri ya ufasiri. Maisha ya hadithi ya Musa, Yusufu, Ibrahimu, Daudi,
Samsoni, Samweli, Ruthu, Ester, Yesu, Paulo, Petro na wengine hupeana hakikisho ya maisha
kamili, mambo ya kuigizwa na mashauri, ambayo yanaweza kutumiwa katika mahubiri ya
ufasiri. Mwenye kueleza kwa mfano anaweza kutumia wazo lake akielezea, kwa kustawi,
kuanguka na ushindi wa Samsoni. Hadithi ya Yesu na mtu mwenye pepo wa Gadarene, na
maombi ya kuishi ya Jairo na uthabiti wa kitendo cha imani cha mwanamke mwenye shida ya
kutokwa na damu katika kitabu cha Marko 5, huonyesha jambo ambalo ni maridadi kwa
mahubiri ya ufasiri chini ya kichwa “Jinzi ya kuhisi Yesu” walakini, mahubiri ya ufasiri yaweza
pia kuchukuliwa kutoka katika waraka au sehemu nyingine za Biblia, ikiwa tu yanahusu sura ya
kitabu fulani au sehemu ndefu ya maandiko.
Hata ingawa mahubiri ya ufasiri yanahusika na maneno mengi yasiwe tu na wazo moja la msingi,
ambalo linaweza kuangaziwa kila upande tofauti. Lazima yawe na lengo la kati ambalo lina
utaratibu. Mtu anaweza kuhubiri kitabu chote ikiwa tu wazo la msingi linafuatwa. Ikiwa
tunahubiri kuhusu “kumjengea Mungu” tukitumia kitabu cha Nehemia, maneno yote ambayo
yametumiwa ni lazima yadumishe shabaha yetu ya kawaida. Tunaweza kuanza kwa kuonyesha
umuhimu wa kuwa na mzigo kabla ya kuanza kujenga (sura ya 2). Kutoka pale tuonyeshe
kwamba Mungu hutengeneza njia ya kutimiza maono. Tunaweza kuonyesha vile tunaweza
kujenga, kwa kuhesabu uharibifu (sura ya 2) na pia kwa kufanya kazi katika umoja upande kwa
upande. Katika sura ya 6 tunaona kwamba wale ambao wanamfanyia Mungu kazi watakutana na
mambo magumu au shida, lakini hatimaye watamaliza kazi.
Uzuri wa mahubiri ya ufasiri ni kwamba yako dhahiri. Njia hii haigeuzi maandiko lakini huenda
pamoja na maandiko. Kwa hivyo, wasikilizaji wanaojua njia watakuwa imara katika neno, na
kuongeza maarifa yao ya Biblia.
Mahubiri ya ufasiri yana ubaya wake. Ikiwa mhubiri hawezi kuwa mwangalifu anaweza kuwa
mvivu katika matayarisho yake. Kuna hatari ya kusoma msitari baada ya msitari mwingine wa
maandiko ambayo yamechaguliwa, na kupeana maelezo machache au kwa kutoa maono
machache kuyahusu, halafu mahubiri yanakuja kuwa mafafanuzi tu badala ya kuwa tangazo la
ukweli ambalo limo ndani ya maandiko.26 Kwa kurudi kuambia hadithi ya maandiko haitoshi.
Mhubiri ni lazima ajaribu kuwaonyesha wasikilizaji wake welekevu wa kufaa. Imeshasemwa
kwamba “mahali ambapo welekevu unaanzia ndipo mahali mahubiri yanaanzia”. Ubaya
mwingine ni kusoma maandiko mengi. Watu wengi kwa kawaida hupendelea maandiko mafupi
kuliko maandiko marefu. Si tu yanapokelewa haraka, bali yanakumbukwa kwa urahisi.
Aina hii ya mahubiri inahitaji matayarisho zaidi kuliko mahubiri mengine yoyote. Mhuduma si
lazima tu asome maandiko yote, bali kila fungu la maneno, sentenzi, usemi wa maneno ili kupata
maana sahihi. Ikiwa matayarisho yatafanywa vyema, njia hii haiwezi kuruhusu uvivu.
Blackwood anasema, mahubiri ya ufasiri, kama kazi moja ya mimbara, mahubiri yanaweza
kuonekana ya kustahili kulingana na muda, uangalifu na maombi ambayo yamehusishwa.27
C. Mahubiri ya Kiini cha Maandiko
Imeshasemwa kwamba katika historia ya kuhubiri, mahubiri ya ufasiri yameshinda mahubiri
mengine. Miongoni mwa ujumbe ambao umekuja kuwa wa maarufu kila mmoja amekuja kuwa
katika sehemu hii.28
26 Evans, uk. 56.
27 Ibid., uk. 89.
28 Ibid., uk. 90
34
Mahubiri ya kiini cha maandiko yana sifa muhimu ya mahubiri ya ufasiri au mahubiri ya
kuchungua maneno, lakini yanakosa utafiti wa asili. Hayaelezi maana ya maandiko fulani bali
huelezea kiini cha habari. Hata ingawa hilo jambo si la uchanguo wa maelezo ya mahubiri lakini
ni la mwongozo wa Biblia, kama mahubiri wengine.
Mahubiri kama haya yanahusu masomo fulani, shabaha au kiini fulani cha maneno. Somo
linaonyesha maana ya mahubiri na si maandiko. Ujumbe wa kiini cha habari unamruhusu
mhuduma kuhubiri kwa kila somo ambalo anafikiria ni muhimu kwa kondoo wake. Ikiwa
anaona umuhimu wa ufufuo, msamaha, ukarimu na kadhalika. Katika kanisa anaweza
kuzungumzia kwa urahisi ukosefu wa kiroho kupitia maneno ya kiini cha mahubiri. Pia
inamwongoza mhubiri zaidi kuchunguza sana kwa makini maarifa ya somo lolote.
Hashurutishwi na uchache wa maandiko lakini anaweza kuchagua mistari mingi ya maandiko
kuwekea nguvu ujumbe ambao unawaka moyoni mwake. Mahubiri kuhusu uwanafunzi,
utumishi, unyenyekevu, zaka, utawala wa Mungu, kuja kwake Yesu mara ya pili na kadhalika,
mahubiri haya yote yako chini ya mahubiri ya kiini cha maandiko, yakiruhusu kuenda ndani ya
somo.
Mahubiri ya kiini cha maandiko yanaweza kutumiwa vibaya kwa urahisi, kwa sababu
yanafungua njia kuzungumzia maneno ya kiulimwengu, na umuhimu wa kiroho au bila.
Yanaweza kutumiwa kujadilia mazingara, usalama wa dunia, usawa wa binadamu, uchaguzi wa
kisiasa ujao, jambo lingine lolote la muhimu, linalohusu maoni yetu na ushawishi. Mambo ya
kijamii na umuhimu wake hayawezi kuridhisha mahitaji ya kiroho na nafasi. Masomo ambayo ni
ya kiulimwengu hayana nafasi katika mimbara. Hii haimaanishi kwamba tusishughulikie mambo
ya kijamii, kama ni muhimu, lakini kuhubiri kwetu lazima kuwe na umuhimu wa kiroho.
Wale wanaotumia njia hii wanaweza kuwa “wasimulizi wa mimbara” kwa kuzungumzia kwa
jambo lolote kuhusu jamii, siasa, mazingira na uendelezaji wa kiroho. Ninakumbuka mhuduma
mmoja ambaye alitumia njia hii pekee yake. Hakuna haja kusoma magazeti ya habari au
kusikiliza habari katika wiki kwa sababu alitumia karibu habari yote katika mahubiri yake katika
jumapili.
Hata ingawa mahubiri ya kiini cha maandiko yana ubaya wake lazima tuendelee kutumia njia hii
ya mahubiri kila wakati. Kama itatumiwa vyema itamsaidia mtu wa Mungu kushirikiana ujumbe
ambao umakuja kutoka kwa Mungu, kwa wakati unaofaa. Kwa hivyo, mahubiri ya kiini cha
maandiko yatakuwa “hali ya maisha” ya kuhubiri.
Kwa kumalizia tumesema kwamba tena hakuna njia ambayo inatakikana kutumiwa pekee. Kila
njia, ikiwa ya uchangzi ya maneno, kiini cha maandiko au ya ufasiri ina mahali pake pazuri. Njia
moja ya kuwapendeza washiriki wetu na kile tunahitaji kusema katika njia tofauti ya mahubiri.
D. Mahubiri ya Uinjilisti na Uchungaji
Mahubiri ya uinjilisti na uchungaji yameweza kuwa mahubiri ya kiini cha maandiko, uchanguzi
wa maandiko au ufasiri. Kusudi la ujumbe wa uinjilisti ni kuongeza mioyo kwa Yesu. Mahubiri
ya uchungaji kwa upande mwingine shabaha yake iwe ya kuwafanya wale ambao wameletwa
kwa Bwana wanafunzi. Sangster anadhibitisha kwamba jambo kuu la mahubiri ya ukristo ni
kuwaleta wanaume na wanawake kwa sharti la Kristo na kukua kiroho katika yeye.
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.
35
MASWALI YA MARUDIO - AINA MBALIMBALI ZA MAHUBIRI
1. Kwa jumla kuna aina tatu za mahubiri. Ni zipi?
1) __________________________________________________________
2) __________________________________________________________
3) __________________________________________________________
2. Elezea kwa ufupi mahubiri ya uchanguzi wa maandiko.
3. Mahubiri ya uchanguzi wa maandiko na ya ufasiri yanatofautianaje?
4. Katika historia ya kuhubiri, ni mahubiri gani yanashinda mengine na ni kwa nini?
5. Mahubiri ya kiini cha maandiko yanaweza kutumiwaje vibaya kwa urahisi?
36
Uundaji wa Mahubiri
Kila mahubiri mazuri hujigawanya mwanzoni katika sehemu tatu muhimu, ambazo ni utangulizi,
mwili na mwisho. Sehemu tatu ni lazima zionyeshe umoja, utaratibu, ulinganifu na ufungamano.
Kuangalia kinaganaga kwa sehemu hizi tatu za mambo ya mahubiri ni muhimu.
A. Utangulizi
Utangulizi umeelezwa kwa haki kama mlango au ukumbi. Hutumiwa kwa kusudi fulani la
kujulisha wasikilizaji ujumbe utakaofwata.
Utangulizi mzuri utafanya watu kuwa na usikifu kutoka mwanzoni. Utawashawishi watu na kile
ambacho tunahitaji kusema. Kwa hivyo, sentenzi za kwanza tatu za mahubiri ni za maana sana.
Ni lazima ziwe na utaratibu, na za kuvutia na pia za kushawishi usikifu. Kama tunaweza kukosa
usikifu mwanzoni, wasikilizaji watakata tamaa wakati wote uliobaki wa ujumbe. Wengi huja
kanisani na shida na mambo yanayohusika na mahali pa kazi zao na nyumbani fikirani mwao.
Kwa hivyo, utangulizi wa ujumbe ni lazima uwalete karibu na uwaongoze maisha yao ya kila
siku. Mwanzo wa ujumbe ni lazima uwe wa kupendeza sana ili wasikilizaji wasiwe na la
kufanya ila tu kutusikiliza kile tunahitaji kusema.
Utangulizi mzuri hautaleta tu karibu kupenda ujumbe, bali utaweka mwongozo mhubiri
atakaofuata. Kwa kufanya hivyo, mkutano unapatiwa maono mara moja ya jambo ambalo
litafwatiwa. Ni lazima iwe maono madogo na si maono kamili. Kwa maneno mengine, mhubiri
asijaribu kuhubiri mahubiri yake katika utangulizi.
Kwa sababu wahubiri wengi wanahubiria watu sawa kila wiki, utangulizi ni lazima uwe tofauti.
“Milango” tofauti ni lazima itumiwe kwa kuanzia ujumbe, la sivyo, watu watapoteza imani.
Kuna uwezekano kadhaa wa utangulizi.
1. Uwezekano wa Utangulizi
a. Anza na (Ma) swali
Wahubiri wengi huanza mahubiri kwa kusema, “Biblia inasema...... na watu wanakosa la kusema
kwa sababu njia hii imetumiwa mara nyingi. Ni bora kuanza kwa kuuliza maswali kama, je,
unajua kwa hakika vile waweza kumpendeza Mungu? Wengine wanafikiri wanaweza
kumpendeza Mungu kwa kuomba, kwa kushujudia au kusoma Biblia. Lakini je, twaweza
kumpendeza Mungu kwa kufanya hayo? Baada ya kuuliza haya maswali, tunasoma Waebrania
11:6 kama maandiko yanayosema, “Bila imani haiwezekani kumpendeza Mungu”. au twaweza
kuuliza, “Je, tutafanyaje tunapokumbwa na shida? Unalalamika, unalia au unashtuka kwa ukali
au ujeuri? Wafilipi 1:12-18 inatuonyesha jinzi Mungu anataka tutende”.
b. Anza Jambo la Kushitusha
Katika chumba hiki, kuna mwuuaji! Alimuuwa mtu jana tu. Alifikiri hakuna mtu yeyote
aliyemwona, lakini matendo yake ya kutisha yalijulikana. Nimeandika dhibitisho la uuaji wake .
Hapa kumeandikwa, kila anayemchukia ngudu yake ni muuaji (1 Yohana 3:15).29 Mshangao
kama huu utumiwe kwa kiasi. Pia ni muhimu kuwa mwangalifu jinzi unavyotumiwa.
c. Anza na Maandiko
29 Blackwood, kur. 61-62.
37
Hii ni njiia labda inayotumiwa mara nyingi katika utangulizi. Baada ya kusoma maandiko,
mhubiri anaweza kuuliza swali au aseme jambo ambalo lina uhusiano na maandiko. Utangulizi
unaweza kutayarishwa kutoka kwa matayarisho ya maandiko, au kutokana na kutofahamu
maandiko. Ujumbe katika 1 Yohana 3:6 Basi, kila aishiye katika muungano na Kristo hatendi
dhambi, lakini kila mtu atendaye dhambi hakupata kamwe kumwona, wala kumjua Kristo,
inaweza kuelezea utangulizi ambao unaonyesha kutofahamu maandiko. Mhubiri anaweza
kuonyesha kwamba neno dhambi, linaonyesha maisha ya dhambi na si mtu asiyetakikana bali
kitendo cha dhambi, kinachofanywa na mwamini.
d. Anza na Maneno ya kutangulia
Utangulizi wa kupendeza unaweza kutayarishwa kwa kutumia maneno yanayotangulia ya
maandiko. Mistari inayofwata au inayotangulia maandiko, mara nyingi hupeana utangulizi
mzuri. Kwa mfano, unapohubiri, mwanamke aliyetokwa na damu, ni lazima aonyeshe ni kwa
nini watu walimzingira Yesu.
e. Anza na Wakati, jinzi na Desturi
Wakati na historia ya Waisraeli iliwaongoza wenyewe katika utangulizi unapohubiri kuhusu
maono ya Isaya. Utawala wa mfalme Uziah, uthabiti ambao alitoa kwa taifa, majivuno yake
ambayo yalileta hukumu wake, kifo chake na kutokujua nani ataongoza au kutawala taifa baada
yake yeye, hutoa msingi mzuri wa mwanzo wa mahubiri. Ni katika mipango hii ambayo nabii
anamwona Mungu katika maono akiketi katika kiti cha enzi.
Unapohubiri, “chukua msalaba wako na unifwate” asilil na kusudi la msalaba ni habari yenye
mapambo ambayo yanaweza kutumiwa kwa urahisi kama utangulizi.
Zaidi ya hayo, tabia za jamii ya nchi za mashariki, hali ya maisha yao, mtindo wa mavazi yao, na
mahali ambapo wanaishi hupeana mambo ya kuendeza ya utangulizi. mambo ya ajabu kwa
waandishi na wapokeaji tofauti (makanisa au watu binafsi) yanaweza kutumiwa kuanza ujumbe.
f. Anza na Hadithi au Maelezo
Njia hii mara nyingi ilitumiwa na Bwana. Unapotumia hadithi au unapotumia maelezo, ni
lazima tuhakikishe kwamba yanastahili mahubiri yetu. Tusiseme hadithi tu kwa sababu
tunaipenda, au kwa sababu tumeisikia hivi karibuni. Kusudi la maelezo kama haya ni kufanya
watu wapende mahubiri na si zaidi na haya. Hadithi na maelezo yataweza kuwa ya kustahili
ikiwa ni mafupi, mazuri (matamu) na yako kamili.
g. Anza na Mambo ya Wakati Huo Huo
Kusoma gazeti au habari, kusikiliza habari au kufuata mazungumzo katika basi yanaweza
kutuelekeza kwa utangulizi mzuri. Unapotumia njia hii, shida au jambo linaelezwa na baadaye
linaunganishwa kwa maandiko ambayo umesoma. Njia hii ya mfano wa mwanzo wa utangulizi
hupeana uwezo mwingi.
h. Anza na Msitari wa Andiko
Mahubiri yanaweza kuwa ya kustahili unapoyaanza na msitari wa maandiko ya kuchoma moyo
wa mambo fulani yanayojulikana. Neno kuu la chuchill ni “usikat etamaa” ni mojawapo ya
mifano mingi.
38
Unapotumia mfano mmoja wa mahubiri ambao umetajwa, ni lazima tukumbuke kwamba
utangulizi mzuri unahitaji matayarisho mazuri. Usiuwache kando kidogo kwa mda fulani.
Mawazo ya kwanza ni mawazo ya kudumu. Kwa hivyo, mhubiri ataweza kufanya vyema kwa
kuandika mwanzo wa mahubiri yake kabisa. Hii itaweza kufanyika baada ya mahubiri
kukamilika. Wakati huu anaweza kujua wazo kuu la ujumbe wake, na vile utangulizi unaweza
kumwongoza kwa kiini cha kati cha ujumbe. Utangulizi ni lazima uonyeshe wazo kuu.
Utangulizi mzuri hauwezi kuwa mrefu, au wa sauti kubwa au wa kitisho. Hautaahidi zaidi
kuliko kile mhubiri anaweza kupeana. Kuishi watu kwa upande kuja kwa madhabahu
kutafwatiwa baadaye lakini si katika mwanzo wa ujumbe. Dakika tatu au tano ya utangulizi ni
muda mrefu wa kutosha kwa mahubiri ya dakika arobaini. Utangulizi mrefu utawafanya
wasikilizaji kuchoka. Kama hatuwezi kuwashawishi wasikilizaji wetu na kuwafanya kusisimka
wakati huu, tunaweza kufikia mwisho wa mahubiri yetu.
B. Mwili wa Mahubiri
Maneno ya kueleza, maandiko au kichwa cha mahubiri yanatengeneza mwili wa mahubiri.
Sehemu hii ya ujumbe imeitwa pia ni majadiliano au maongezi. Kwa sababu ni sehemu kuu ya
wakati wa mahubiri na lazima tuchukue muda wetu kuyafikiria.
Mwili wa mahubiri ni lazima uelezee, usimulie, ujadilie na uelezee kwa mfano ukweli ambao
twahitaji kuzungumzia. Kabla ya haya kufanyika, ni lazima tujue somo kwa hakika. Kwa
maelezo mazuri wakati wa maneno au maana ya asili ya maneno. Lazima tupeane ushahidi wa
ukweli ambao umehubiriwa. Neno la Mungu hupeana msingi bora wa majadiliano. Mambo
mengine ni ushahidi wa kibinafsi, (kwa mfano tunapohubiri kuhusu uponyaji, tunaweza kutumia
ujuzi wetu wenyewe au wale wengine kama thibitisho) ukweli kutoka historia na sayanzi.
1. Kutayarisha Mwili wa Mahubiri
Unapotayarisha mwili wa mahubiri, ni lazima tujiulize wenyewe maswali manne ya msingi
wenyewe. Je, nataka kusema nini? Kwa nini ninataka kusema? Nitasemaje? Kutoka hapa,
tunahitaji kuuliza somo kuhusu maandiko au somo?
a. Mahubiri ya Kuchagua Maneno na Ufasiri
Tunaposhughulikia maandiko au somo, ni lazima tuulize, kwa nini? Nini? Jinzi gani? Lini?
Wapi? Kitu gani kilitendeka kabla na baada? Hali ya mambo yalikuwaje? Matokeo yalikuwa
nini? Nani alikuwepo? Kwa nini walikuwa hawako? Walifanya nini? Je, hii inaonyesha nini
leo? Sasa ilimaanisha nini? na kadhalika. Majibu kwa maswali haya yatatuwezesha kudokezea
maandiko. Yatatusaidia kuandika sehemu zetu kuu na vijisehemu. Wacha tutumie Luka 16:19-
31 kama mfano.
Kwanza kabisa ni lazima tutambue ni nani anahusika: Lazaro, mtu tajiri ambaye hana jina, na
mbwa. Jambo la pili ni kutafuta mahali mbalimbali ambapo vitu hivi vilitendeka, lango ambalo
Lazaro aliketi, nyumba ya tajiri, Jehanamu, kifua cha Ibrahimu au mbinguni. Kisha tunataja
matukio au hali ya mambo mawili. Lazaro : Maskini sana, mgonjwa, mwombaji, anayetegemea
wengine, akitamani kula mabaki, vidonda vyake vililambwa na mbwa. Mtu tajiri: tajiri sana,
aliyevalia nguo za rangi ya zambarau bivu, aliyeishi maisha ya anasa kila siku. Je, jambo gani
lilitendeka kwa wao wote. Wote walikufa. Ni nini lilikuwa jawabu? Mtu tajiri: Alikuwa na
maziko (kilio). Lazaro: Hakuna maziko ambayo yametajwa. (Hapa tunaweza kufikiria ni nini
kilisemwa katika masishi.) Baada ya kifo, Mtu tajiri: Katika Jehanamu si kwa ajili ya utajiri
39
wake, bali kwa sababu ya kukosa kumjua Mungu, anateseka katika uchungu. Lazaro:
Anafarijiwa kifuani mwa Ibrahimu, si kwa sababu ya umaskini wake bali kwa sababu ya kumjua
Mungu. Kitu gani kilifanyika tena? Mtu tajiri: katika uchungu, anamwomba Ibrahimu
ameogopa, anawafikiria wengine, anafikiria mioyo ya wengine, Ibrahimu anakataa maombi yake.
Je, hii inaonyesha nini? Baada ya kifo, tunakutana na mwisho (Shimo kubwa linatengenezwa).
Kwa hivyo, ni lazima tutayarishe shauri sahihi ambalo litadhihirisha maisha yetu ya nje,
tunapokuwa tungali hai. Kuomba kutosheka na kidogo ambacho uko nacho, kuwa ma moyo wa
kufikiria wengine, kuwa tu na fikira ya uinjilisti haitatusaidia katika jehanamu. Tuko na sheria
na manabii na Agano Jipya, ni bora tusikilize kile wanachotuambia kabla ya mwisho wa wakati.
Utajiri mzuri unadhihirishwa baada ya kifo. Kuwa na mali nyingi na pesa nyingi havitatusaidia
maisha yajayo.
Ukweli huu wote utatengeneza dokezo kwa urahisi. Baada ya sehemu zetu kuu na mambo haya
yawe na wajibu wa mahitaji fulani. Kabla ya kuangalia mambo haya kwa makini, tunahitaji
kufikiria maneno yanayotengeneza mambo yanayoshughulika na fikira za watu.
b. Mahubiri ya Maneno ya Kufikiria
Sehemu ya kwanza ya mahubiri ya maneno ya kufikiria ni lazima ielezee somo ambalo mhubiri
anashughulika nalo. Kwa mfano, kama tunahubiri kuhusu imani, sehemu ya kwanza ni lazima
ielezee maana ya jambo hili. Hii inaweza kufanyika kwa kudhibitisha maono sahihi na
kushughulikia mambo ya kutoeleweka ya kawaida. Kabla ya mtu kuelezea somo lolote, ni
lazima kwa kweli awe na ufahamu sahihi mwenyewe. Ili kuelezea shabaha yetu, tunaweza
kutumia maelezo fulani, mifano au kutofautisha.
Umuhimu na ukweli wa yale ambayo yameonyeshwa katika sehemu ya kwanza ni lazima
yathibitishwe katika sehemu ya pili. Pale, mwalimu atapeana majadiliano kwa ujumbe wake, na
kuonyesha umuhimu wake. Unapohubiri kuhusu imani na matokeo yake. Hii inaweza kufanyika
kwa kutumia maandiko na ushuhuda wa watu wakuu wa Mungu, au hata kwa kutumia ushuhuda
wa kibinafsi. Sehemu hii ya mahubiri ni lazima imshawishi msikilizaji kukua katika imani.
Sehemu ya tatu inaonyesha thibitisho la imara la ukweli. Kwa hivyo, itaonyesha sehemu ya
Mungu katika jambo hili na jukumu la mtu. Sehemu hii itaongoza hadi kwa welekevu wa
ukweli. Kwa kutumia mfano wa imani tena, sehemu hii ya mwili wa mahubiri itaonyesha vile
imani ya kibinafsi itaweza kudhihirishwa na vile tunaweza kukua katika imani.
Mahubiri mengine, kama ni mahubiri ya kuchangua maneno, mahubiri ya ufasiri na mahubiri ya
kushughulisha fikira za watu yote yatajieleza kwa welekevu baada ya kila jambo na si kwa
mwisho. Kwa sababu hii, welekevu wa jambo katika mwisho usiwe mfupi na kutumiwa kama
muhtasari ambao unaleta ujumbe katika mwisho unaofaa.
2. Mahitaji ya Utaratibu
a. Umoja na Mapatano
Utaratibu wa mahubiri ni lazima uonyeshe umoja na mapatano. Kwa kutayarisha, vipande vya
mahubiri havitafanya mahubiri kuwa mazuri. Kila sehemu ni lazima iwe na uhusiano na
nyingine. Lazima zote ziwe sehemu za ukweli mkuu, shabaha na kusudi. Umoja wa ujumbe
utaongezwa nguvu zaidi kutoka sehemu moja hadi nyingine, kwa sababu ya matayarisho mazuri.
Kila sehemu ni lazima itayarishwe kibinafsi, ionekane kama iko pekee yake, lakini, unapohubiri,
tusiwe na ujumbe ambao umesimama, hautiririki kutoka sehemu moja hadi nyingine.
40
b. Utaratibu wa Hakika na Mpango
Sehemu tofauti za ujumbe ni lazima zifuatane katika utaratibu wa hakika. Ni kama kujenga
mjengo, jiwe moja linalowekwa juu ya lingine. Sehemu kuu ni lazima ipangwe katika mfano
kwamba, wazo kuu lionyeshwe wazi. Wahubiri wengine wanatatanisha wasikilizaji wao kwa
sababu ya kukosa mpango wa utaratibu. Wanatangatanga wakijua wanatoka wapi na kuenda
wapi.
Kanuni na mpango sahihi utafanya kazi ya kuhubiri rahisi. Mahubiri yanaonyesha utaratibu wa
hakika ni rahisi watu kuyakumbuka. Watu wanapenda kufuata wazo kuu la mahubiri. Ujumbe
usiokuwa na mpango mzuri hufanya utaratibu huu kutowezekana. Imesemekana kwamba,
wahubiri wengine wanamwiga Ibrahimu, aliyeondoka akijua mahali ambapo alikuwa akienda.
Wahubiri kama hawa wakiulizwa ni kwa nini wanakosa kanuni, mara nyingi wanasema “Lakini
ninaongozwa na Roho Mtakatifu, ndugu yangu”. Singizio kama hilo halikubaliki. Wachungaji
kama hawa mara nyingi pia watasema: “Nilipoenda katika mimbara asubuhi hii, sikujua
nitafundisha nini.” Ni muhimu kwa wao kufahau kwamba hili si dhibitisho la kiroho bali ni
mfano wa uvivu, hasa jambo likifanyika mara kwa mara.
c. Ulinganifu (Usawa wa Sehemu)
Jambo la tatu linahusika na ulinganifu, ambao unaonyesha ulinganifu wa sehemu tofauti ya
mahubiri. Kila sehemu kuu ni lazima ipokee wakati fulani ambao ni hitaji muhimu. Hii
haimaanishi kwamba sehemu zote ziwe na wakati mmoja.
Hasa waanzilishi hutumia wakati mwingi kwa wakati mmoja na kutojali sehemu nyingine
zinazobaki. Walakini, kila sehemu ya mahubiri ni lazima ishughulikiwe kwa uasawa na lazima
itayarishwe vyema. Hatuwezi kuingia katika mimbara na wazo ambalo halijakamilika kuhusu
somo letu. Ni lazima tuwe na hakika na kile ambacho tunahitaji kusema, na muda ambao
tunahitaji kutumia kwa kila sehemu. Hatuwezi kuacha sehemu yoyote ya ujumbe hali ya
kutoeleweka. Kama si hivyo, itasababisha hali ya kutokuwa na maana kamili.
d. Mfufululizo au Kutiririka kwa Mahubiri
Hitaji la nne linataka mfululizo au mtiririko wa mahubiri. Ni lazima tuwe na maendeleo na
mwendo, kwa ujumbe kufikia mwisho wake. Mahubiri ni lazima yatimize kusudi lake. Lazima
tusiwache nje shabaha na kusudi, ambalo tulihitaji mwanzo wa ujumbe.
e. Kudokezea Mahubiri
Njia rahisi na bora ya kudokezea mahubiri ni kutengeneza mfano wa “mifupa” ya binadamu,
ambayo yanaonyesha mambo makuu na madogo. Ni mfano wa sanamu ya wazo letu. Baada ya
sanamu hii ya mifupa kutengenezwa, sasa tunaweza kuweka “nyama” juu yake, hii ni kusema,
kuongezea maelezo zaidi ya maandiko. Hii “nyama” kwa kawaida ina mawazo ambayo Roho
Mtakatifu ameongoza (upuzio) wakati tunakuwa tukisoma maandiko. Maneno mengine
yanaweza kuja kutoka kwa mambo ambayo mhuduma anayakusanya. Evans anasema kwamba
ikiwa anakusanya mambo wakati tu anapotayarisha mahubiri, watu watapokea mawazo ambayo
hayakamiliki.30
Mwili wa mahubiri ni lazima utayarishwe. Mtu mmoja alisema kwamba mahubiri ambayo
yanakosa utaratibu yanatukumbusha mambo ya mwanzo ya uumbaji katika kitabu cha Mwanzo
30 Ibid., uk. 94.
41
sura ya 1, “nchi ikiwa ukiwa, tena patupu”.Kwa hivyo, tunahitaji mpango, ambapo ni rahisi
ambao hautatizi na ambao una mambo makuu na madogo, kama katika mifano itwatayo:
Utangulizi
I. Jambo Kuu la Kwanza
1. Sehemu Ndogo ya Jambo
2. Sehemu ya pili Ndogo
(1) Sehemu ya kwanza Ndogo ya Ndogo sana
(2) Sehemu ya Pili Ndogo ya Ndogo sana
3. Sehemu ya Tatu Ndogo sana
II. Jambo la Pili Muhimu
1. Sehemu ya Kwanza Ndogo
2. Sehemu ya Pili Ndogo sana
3. Sehemu ya Tatu Ndogo sana
(1) Sehemu ya Kwanza ya Sehemu Ndogo sana
(2) Sehemu ya Pili ya Sehemu Ndogo sana
4. Sehemu ya Nne Ndogo sana
III. Jambo la Tatu la Muhimu
1. Sehemu ya Kwanza Ndogo sana
2. Sehemu ya Pili Ndogo sana
Mwisho
Sheria ya zamani huweka masharti matatu ya kuelezea maneno. Walakini vifaa vya kutumia
katika mahubiri vinaweza kupangwa katika njia tofauti. Kama ujumbe unahitaji sehemu tano au
saba, basi ni lazima igawanywe iwezekanavyo.
Wahubiri wengine wana tabia ya kutangaza nambari ya kila sehemu. Hii hupeana hakikisho na
utaratibu, kwa sababu hii humwezesha msikilizaji kufuata ujumbe zaidi kwa urahisi. Ubaya ni
kwamba, matumizi ya kutoa nambari ya kila sehemu yaweza kutatanisha kutiririka kwa ujumbe
katika mimbara. Nambari inaweza kutangazwa na walimu wa Neno lakini haiwezi kuwasaidia
vyema kwa kuhubiri. Kama tunataka watu kufuata mwendo wa ujumbe tunaweza kuonyesha kila
sehemu kwa kuwaza kidogo, kwa kufupisha sentenzi ya kwanza au kwa kuwekea mkazo kiini
cha ujumbe, lakini si kutumia nambari.
Lazima “tuchimbue” ndani ya maandiko. Tunapokuwa tukitayarisha, ni lazima tutofautishe
mahubiri ya watu wasio okoka na wale ambao wameokoka, na wale ambao wamezaliwa upya
katika Kristo au mama na baba katika Kristo.
D. Mwisho
Wengi wanafikiria dakika tano za mwanzoni za ujumbe ni sehemu moja nzuri ya mahubiri, na
kwa kweli ni hivyo. Bila mwisho mzuri na mahubiri mazuri yanaweza kukosa ukamilifu.
Sehemu ya kumalizia au mwisho wa ujumbe mara nyingi haipatiwi muda wa kutosha wakati wa
kutayarisha. Mhubiri anaweza kuwa katika tahamaki kuhusu ujumbe wake na anaweza kukosa
kutayarisha mwisho unaofaa. Mahubiri mazuri ni kama safari ya kuenda kwa ndege nzuri
ambayo mtu hawezi kutabiri mwanzo ila tu baada ya “kutua”.
Katika kuhubiri, kuanza vyema na ujumbe wa kupendeza ni lazima kusifwatiwe na “kutua”
kubaya. Mwisho mara nyingi huungana na sehemu ya mwisho wa mwili wa mahubiri. Ni juhudi
42
ya mwisho ambayo huamua “mapambano”31. Na baadaye, umbo lake na shabaha ni lazima
vitayarishwe vyema. Maneno mengi ya kumalizia hayako na umuhimu, hayana maana na ni ya
kutatanisha, kwa sababu hii hupunguza na hata huharibu ujumbe ambao unafuata. Mwisho wa
ujumbe ni lazima uwe na nguvu na wa kweli, ukimpatia msikilizaji awe na fikira ya ukamilifu.
Lazima aweze kukusanya mambo mengine ambayo yamebaki.32
Kwa kumalizia mahubiri, kuna mambo tofauti yanayohitajika kama katika utangulizi. Kuna
karibu njia tano tofauti za kumalizia ujumbe.
1. Njia mbalimbali za kumalizia Mahubiri
a. Tazamo la Nyuma
Kufupisha kile ambacho kimesemwa ni njia moja (uwezo) ya kumalizia mahubiri. Ni tazamo la
nyuma la fikira ambalo limeelezwa na ukweli kupanuliwa. Fikira muhimu ambazo zimeelezwa
katika mwili zitarudishwa katika sentenzi zilizochaguliwa vyema, zilizoelezwa vyema, kweli,
zitatushauri. Wazo la kati na shabaha ya ujumbe inafupishwa.
b. Matumizi ya Kufaa ya Binafsi
Ujumbe ambao unazungumzia sehemu halisi za maisha ya ukristo ni lazima imalizie na
matumizi ya kufaa ya binafsi. Aina hii ya mwisho husaidia wasikilizaji kuona kile Mungu
anataka kutoka kwake. Humpatia mashauri vile anahitaji kutumia ujumbe maishani mwake.
c. Maelezo
Mahubiri mengine, hasa yale ambayo yana shabaha ya kiinjilisti, yanamalizwa na hadidhi au
maelezo. Njia hii inaweza kuwa ya kustahili. Walakini, kama hadithi haielezwi vyema, inaweza
kuharibu malimwengu na matarajio ambayo mahubiri yamesababisha. Kuambia hadithi, au
kutumia maelezo, havitoshi. Ni lazima iwe ya kufaa na kuchangia ukamilifu wa ujumbe.
d. Linganisha
Mahubiri kuhusu nyumba juu ya mwamba na nyumba juu ya mchanga yanaweza kumalizwa na
kuonyesha mambo dhahiri na mambo ya kukanusha ya njia ya majengo mawili. Kwa kuonyesha
upande wa ukweli na upande usio wa kweli au upande wema na ubaya, msikilizaji anapatiwa
muda mzuri kufanya uchaguzi bora.
e. Himizo la Kuonyesha
Kupitia himizo la kuonyesha, akili ya matendo na vile umati unaweza kuzungumziwa, labda
kama kikundi au njia ya kuzungumzia mtu mmoja mmoja. Njia hii inajulikana katika mikutano
ya kiinjilisti, ambayo inaongoza watu kukata shauri kwa Yesu. Inaweza pia kutumiwa katika
mikutano ya ufufuo. Himizo la kuonyesha watu njia linafuatiwa na kuwaita watu kuja kwa
madhabahu.
2. Urefu wa Mwisho
Maneno yoyote ambayo yanaweza kuchukua muda zaidi ya dakika tatu na tano yanaweza
kuharibu mwisho wa kufaa. Wahubiri wengi wana tabia mbaya ya kusema mara nyingi “na sasa
katika mwisho” kabla ya wao kumaliza ujumbe wao kweli. Wengine wanarudia kile ambacho
31 Ibid., uk. 75.
32 Ibid., uk. 101.
43
wameshasema, kwa sababu hawajafikiria ya kutosha kuhusu mwisho wa mahubiri yao. Baada ya
kufikia mwisho! usiendelee na mambo mengine. Tunaposema ni mwisho, wacha uwe mwisho.
Kitu kizuri ni kujizuia kutangaza wazo letu la kumalizia ujumbe lakini umalizie katika njia moja
ambayo imeelezwa.
C. Mambo ya Kufanya na yale ya Kutofanya
Utayarishe mwisho mfupi na rahisi, lakini si fupi sana au mwisho wa ghafla. Usimalize kwa
kusema tu: “na Mungu ayabariki maneno haya yote”.
Kama sheria, tumaalizie na jambo la kufaa. Hakuna ubaya au nadhara ya kuhubiri kuhusu
Jehanamu na matokeo ya dhambi. Walakini, ni lazima tumalizie na msalaba na msamaha wa
dhambi. Hakuna kitu ambacho chaweza kuwabadili watu haraka kuliko wahubiri wa mauti
ambao wanakosa kuonyesha njia ya kutoka utumwani.
Usiongezee kitu chochote kipya katika mwisho wa ujumbe. Kusudi la mwisho ni kumaliza na si
kuongezea wazo mpya. Lengo kuu lazima lihifadhiwe na kusudi la ujumbe. Kitu chochote
kisiondolewe. Hakuna nafasi kwa ushauri katika mwisho unaweza kutumiwa mwanzoni au
katikati ya mahubiri bali si mwishoni hata kidogo. Kwa sababu tunajaribu kuwaongoza
wasikilizaji kukata shauri katika mambo ya kiroho, shauri haliwezi kuhesabiwa haki katika
harakati ya kumalizia ujumbe.
Kila mwisho ni lazima umalizwe na mwito au hitaji la badiliko. Lazima utuongoze kwa shauri
kamilifu la kuwa mwanafunzi bora wa Yesu Kristo.
44
MASWALI YA MARUDIO _ MATAYARISHO YA MAHUBIRI
1. Ni sehemu gani tatu ambazo mahubiri mazuri yanajigawanya?
1) __________________________________________________________
2) __________________________________________________________
3) __________________________________________________________
2. Ni kusudi gani halisi ambalo utangulizi unatumikia?
3. Utangulizi mzuri utafanya nii kutoka mwanzoni?
4. Jaza katika mapengo:
Utangulizi mzuri hautatoa tu _____________________ bali uta________________
mwongozo wa mhubiri ambao utafuata.
5. Taja uwezekano nane wa utangulizi:
1) _________________________________________________________
2) _________________________________________________________
3) _________________________________________________________
4) _________________________________________________________
5) _________________________________________________________
6) _________________________________________________________
7) _________________________________________________________
8) _________________________________________________________
6. Mwili wa Mahubiri utafanya nini?
45
7. Ni maswali gani manne ya msingi ambayo tunahitaji kujiuliza wenyewe kabla ya kutayarisha
mwili wa mahubiri?
1) _________________________________________________________
2) __________________________________________________________
3) __________________________________________________________
4) __________________________________________________________
8. Taja maswali mengine ambayo tunaweza kuuliza tunaposhughulikia soo hili?
9. Je, sehemu ya kwanza ya mahubiri ya jambo linaloshughulisha fikira za watu ni lazima lifanye
nini?
10 Mahitaji mane ya utaratibu ni nini?
1) _______________________________________________________________
2) _______________________________________________________________
3) _______________________________________________________________
4) _______________________________________________________________
11. Njia rahisi na bora ya kudokeza mahubiri ni gani?
12. Kwa nini zile dakika tano za mahubiri ni muhimu?
13. Taja njia tano tofauti za kumalizia mahubiri
1) __________________________________________________________
2) __________________________________________________________
3) __________________________________________________________
4) __________________________________________________________
5) __________________________________________________________
14. Je, twahitaji kufanya nini tunaposema “mwisho”?
15. Kila mwisho umalizwe vipi?
46
Maelezo
Sehemu ya mahubiri ambayo itakumbukwa ni maelezo. Mimi binafsi ninaweza kukumbuka
maelezo mengi yaliyoelezwa vyema, lakini ninakumbuka mahubiri machache. Bwana wetu
alionyesha mfano wake wa matumizi na thamani ya kutumia mahubiri ya picha. Watu hufurahia
kusikiliza maelezo. Wale wanaotaka ukamilifu katika matumizi yake mara nyingi watasikilizwa.
Maelezo ni dirisha kwa mahubiri. Yanaonyesha mwanga wa somo. Ujumbe mwingi ni kama
nyumba ambazo hazina madirisha. Waweza kuwa na msingi mzuri na ukuta thabiti, lakini
ujumbe hauruhusu nuru kupita. Maelezo ni lazima yatimize kusudi la kuruhusu nuru katika
ukweli wa Biblia. Maelezo haya yasije kuwa katika mwisho wake yenyewe, bali yachangie
ukamilifu wa mahubiri.
Sheria fulani ni lazima zikumbukwe wakati tunapotumia maelezo.
A. Sheria za Kutumia Maelezo
1. Urahisi
Kila mtu, hata mtoto ni lazima aweze kufahamu Yasiwe magumu au ya kutatiza. Mafafanuzi
mengine yanayoonekana kuwa yanahitaji kuelezwa kwa urefu, kabla ya kufahamika. Kristo
alipotumia mfano wa madirisha, ulikuwa mfano wazi na rahisi na wasomiwa Biblia (Mafarisayo
na Wasudukayo), na wakulima na wavuvi. Unaposhughulika na wafanyikazi wa kiwanda,
wakulima wake wa nyumbani tusijaribu kutumia uvumbuzi katika sayanzi, elimu ya nyota,
masomo ya hesabu na mambo mengine. Wasikilizaji wengi watakuwa watu ambao hawana
elimu ya chuo kikuu bali watu rahisi wa kawaida.
2. Ukweli
Hadithi ya kubuni au hadithi ambayo sisi wenyewe tumewazia, tunaweza kuitumia, kama
tunaweza kuionyesha. Ni lazima tusijifanye kwamba hadithi kama hizi ni kweli. Matukio
kutokana na maisha ya watu wengine yasitumiwe katika hali ya kuonyesha tuliyashuhudia
wenyewe. Haya yanaweza kuonekana ya kupendeza lakini uwongo haumpendezi Mungu.
3. Nyumba ya Madirisha au Madirisha kwa Nyumba
Ni vile tujuavyo kwamba nyumba haina madirisha tu, kwa hivyo mahubiri yasiwe tu na maelezo.
Kuna wahubiri ambao wana kipawa cha kusimulia na watu wanawapenda kuwasikiliza.
Walakini, Yesu hakutumia kusimulia hadithi bali kulihubiri Neno Lake. Maelezo ni lazima
yakamilishe kuhubiri kwa Neno na si kuchukua mahali pake. Kila hubiri lisiwe na zaidi ya elezo
moja kwa kila jambo kuu. Kama sivyo, mahubiri yote yatakuwa “madirisha bila kuta”.
4. Dhamira
Maelezo huongoza ujumbe. Humsaidia mhubiri kupata kusudi au azimio la mhubiri.
Tusisimulie hadithi kwa kupenda tu. Maelezo huongoza mahubiri si mahubiri kuongoza
maelezo.
B. Chanzo cha Maelezo
Kristo alitoa maelezo yake kutoka kwa mambo ya asili, vyombo vya nyumbani, (mshumaa,
chumvi, shindano, jicho na kadhalika). Ulimwengu wa biashara (wadai, wadeni wavu za uvuvi
na kadhalika). Kila mara, alitumia mifano ya maisha ya kila siku. Aliona ukweli wa kiroho wa
47
mambo ya dunia karibu naye. Mhubiri mwema anayestahili ataufwata mfano wake. Mara nyingi
atakuwa akiangalia vitu na mambo ambayo anaweza kutumia kama mifano. Litakuwa jambo la
busara kuwa na kitabu kidogo ambacho ataweza kuweka mambo haya.
Ni lazima tujiepushe kwa kutumia vitabu vya maelezo, au hadithi ambazo wengine
wameshatumia. Hakuna mtu anayependa kusikia maelezo kama hayo mara ya pili, hata kama ni
mazuri. Kwa hivyo, tuwache macho yetu wazi na tutafute na maelezo ya asili katika magazeti,
habari binafsi ya watu wakuu, uvumbuzi, maarifa ya ujenzi (Yesu alizungumzia misingi ya
nyumba mbili), na sehemu nyingine za maisha ya kila siku. Kila maelezo mazuri ni lazima
yaandikwe chini na kuwekwa kwa utaratibu. Maisha ya watu wa Agano la Kale na Agano Jipya
yatumiwe kuelezea ukweli wa kiroho. Tunaweza pia kutumia mambo ya ujuzi wetu. Walakini,
tunapofanya hivyo, tujiepushe na kujitukuza na kujivuna. Wale wanaotafuta maelezo
wanapokuwa wakitayarisha mahubiri watakosa hadithi nzuri.
C. Mengi ya Kufikiria
Kabla ya kupeana maelezo, ni lazima tuyafahamu bora. Lazima tuwasaidie watu wahisi, waone
na kujua kile tunachowaambia. Ikiwa hatushawishiwi na kuguzwa na hadithi, pia wasikilizaji
wetu hawatafanywa hivyo. Uchache wa maneno ni ufunguo wa kusimulia hadithi. Lazima uwe
hakika na si wa ghafla. Unaposoma injili, tunaweza kujifunza kutoka kwa Yesu, ambaye ni
mkuu wa hadithi.
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-..-.-.-.-.-.-.-.
48
MASWALI YA MARUDIO - MAELEZO
1. Je, maelezo ni nini na yanafanya kazi gani?
2. Matumizi manne ya maelezo ni yapi?
1) ________________________________________________________________
2) ________________________________________________________________
3) ________________________________________________________________
4) ________________________________________________________________
3. Jaza katika mapengo:
Maelezo _________________ ________________. Yanasaidia mhubiri ku
___________ _____________ ya mahubiri.
4. Ni kwa nini tujiepushe na kutumia vitabu vya maelezo na hadithi ambazo watu wengine
wametumia?
5. Ni lazima tufikirie nini tunapotumia ujuzi wetu wenyewe kama maelezo?
49
Kupeana Ujumbe
A. Kujiandaa Kunena
1. Maneno na Mahubiri yaliyoandikwa
Wale wanaoanza katika huduma hufanya vyema wanapoandika mahubiri yao kamili. Mazoea
kama hayo yatamsaidia mhubiri katika njia tofauti. Yatamfundisha kuweka fikira zake pamoja
katika utaratibu wa kiakili. Yatasaidia pia kusema shabaha halisi ya mahubiri yake, na kuifwata
katika matayarisho yake. Nidhamu hii itaongeza maneno yake ya fikirani, na kuendeleza
matumishi yake na kumsaidia kujidhihirisha barabara na sarufi nzuri. Mara tu mahubiri
yameandikwa, itakuwa rahisi kutayarisha msitari wa kuonyesha umbo la mahubiri katika
mimbara. Wale wanaofikiria mahubiri ambayo yameandikwa kwa misitari isiyo ya kiroho
wanahitaji kukumbuka kwamba wahubiri wakuu kama Jonathani Edwards, alisoma mahubiri
yake kwa ukamilifu. Ujumbe wake unaojulikana “wenye dhambi mkononi mwa Mungu mwenye
ghadhabu” alikuwa na nguvu na upako na watu walishilia vitu kanisani wakiogopa kwamba
ardhi itaweza kufunguka na kuwameza. Alipokuwa akisoma mahubiri yake, aliwaleta karibu na
uso wake kwa sababu ya udhaifu wa macho.
Wengi huhubiri kutoka kwa mahubiri ya maneno mafupi bila umati kugundua. Wengine
wanajifanya kuwa wanahubiri kutoka kwa ufahamivu wao, lakini wao huwa na kijikaratasi
ambacho kina mahubiri mafupi, na yamefichwa katika Biblia. Ni lazima tusiwadanganye watu.
Ikiwa unatumia mahubiri ambayo umeandika kwa karatasi katika mimbara, usifiche jambo hili.
Wale ambao wanafikiri jambo la kuweka mahubiri mafupi kwa karatasi si jambo la kiroho.
Watafanya vyema kwa ustadi, hasa kama watawacha watu wao wakishangaa mwisho wa
mahubiri, kuhusu kile kisomwa. Kuenda katika mimbara kama umejitayarisha vyema,
haimaniishi ni kutokuwa na imani, au kutoongozwa vyema na Roho Mtakatifu. Kwa upande
mwingine, inaonyesha tunachukua mwito wetu kuwa wa maana na hatupendi kusimama mbele
ya umati au washiriki bila cha kusema.
Msemo wa zamani unasema kwamba, mhubiri ni lazima awe tayari kwa mambo matatu:
Kuhubiri, kuomba na kukufa. ili kutimiliza hitaji la kwanza kwamba kila mhuduma ni lazima
awe na mahubiri mafupi kwa karatasi kila mara. Hii itamwezesha kuhubiri, ikiwa ameulizwa
kufanya hivyo kwa muda mfupi.
2. Urefu wa Mahubiri
Urefu wa mahubiri ni lazima uchunguzwe kabla ya kusimama katika mimbara. Uchunguzi
umefanywa katika nchi ya Marikani na umeonyesha kwamba watu kupoteza usikivu wao baada
ya dakika 20. Hata kama hatuwezi kukubaliana na matokeo ya uchunguzi huu, tunaweza
kufanya vyema kukumbuka kwamba tunaweza kufahamu kama miili inastahimili. Watu
wanapokalia viti vya mbao ambavyo ni vigumu na havifai, fikira zetu haziwezi kufahamu zaidi.
Walakini, wakati ujumbe una upako na wa kupendeza, watu hupenda kustahimili mateso fulani
kwa miili yao, “kwa manufaa ya nafsi zao”. Na kama ujumbe si wa kupendeza na hauna upako,
kila dakika ambayo itaongozwa itakuwa mateso kwa mwili, nafsi na fikira. Je, ni muda gani
ujumbe unahitaji kuchukua? Kama sheria, utangulizi hautachukua muda wa dakika tatu au tano.
Sehemu kuu inaweza kuchukua dakika ishirini na tano hadi thelathini (25-30) na dakika 5-5
zitakuwa za kutosha kwa kufikia mwisho wa mahubiri. Ujumbe wote kwa jumla usiwe aiu
usichukue zaidi ya dakika 40-45. Kama si hivyo, utawapoteza watu.
50
3. Ujue Biblia
Mhubiri ni lazima ajue vitabu vyote vya Biblia na mahali vinapatikana. Ni lazima afahamu kiini
cha kila kitabu. Kwa mfano ajue kwamba kitabu cha Mwanzo huzungumzia mwanzo wa
ulimwengu, Nuhu, Ibrahimu ha kadhalika. Anaposikia neno “Wagalatia”, wasioamini, sheria ya
Musa na tunda la Roho lazima vimjie fikirani mwake mara moja.
4. Kutangaza Somo la Mahubiri
Je, tunahitaji kutangaza somo la Mahubiri la ujumbe wetu au tunahitaji kusoma maandiko na
kuanza kuhubiri? Kutangaza shabaha yetu kutatusaidia kujipatia nidhamu. Kuna wengine
wanaofikiri kwa kuanza na jina la somo. Si desturi jambo hili la kiroho. Wanapinga na kusema
desturi kama hii inakubalika wakati wa hotuba wa kisiasa, mafundisho na kusoma karatasi za
habari, lakini hawaoni kama ni bora katika mimbara. Walakini, tabia ya kutangaza somo letu
itasababisha mambo mawili. Hufanya mhubiri kuzungumzia somo lake bila kwenda nje, na
huwasaidia wasikilizaji kufuata ujumbe wake. Kama tunatangaza shabaha yetu, kama “Mungu
wa milima na Mungu wa mabonde” ujumbe ambao uko katika kitabu cha 1 Wafalme 20,
tunawapatia wasikilizaji jambo la kuwazia. Hili jambo litawasaidia kufuata fikira kuu hasa
tunapotumia mifano ya Agano la Kale na watu wa Agano Jipya ambao walishuhudia Mungu na
si Mungu wa milima (wakati mzuri tu), bali Mungu wa mabonde, yule ambaye yuko nao wakati
wa shida.
Wengi huhubiri kutoka kitabu cha Mwanzo hadi kitabu cha ufunuo. Wanaguza jambo lolote na
kila kitu. Kutangaza shabaha itazuia tabia kama hii kabla ya kusoma somo, lazima tujue shabaha
ya ujumbe wetu kabisa.
B. Kuhubiri Neno
1. Umuhimu wa Hotuba Nzuri
Mahubiri mazuri hutegemea ujumbe sahihi au mzuri na upako wa Roho Mtakatifu. Jambo la pili
ni umuhimu wa hotuba nzuri. Hii inaenda pamoja na matumishi sahihi ya maneno na maelezo
mazuri ya sarufi. Wengi wana shida katika sehemu hizi. Njia moja ya kushinda upungufu huu ni
kusoma vitabu kwa sauti. Tukisoma vitabu zaidi, sauti yetu itakuwa safi.
Tunaposoma maandiko, ni lazima tuyaelewe kabisa. Jisomee maandiko kwa sauti kwa wakati
mfupi kabla ya kuyasoma katika ibada, hasa kama yana maneno ya kihebrania au maneno
mengine magumu. Kwangu mimi mwenyewe, sijisikii vyema mtu anapofanya makosa kila mara
anaposoma maandiko mwanzoni. Kumbuka kwamba unahitaji kuhubiri Neno, kwa hivyo, watu
wanahitaji kujua kwamba uelewe unachotaka kusema.
Unapohubiri, uhakikishe kwamba hatutemi na kusimamasimama. Ni jambo la kuchukiza kama
watu wanaoketi mbele ya kanisa watakapofungua miavuli yao kuonyesha kwamba kuna shida
katika sehemu hii. Kitulizo ni kwamba kuenda na kikombe cha maji katika mimbara na kunywa
kidogo ikiwezekana. Hili litaweza kuwa jambo la kufadhaisha kidogo lakini ni bora kidogo
kuliko zamaha ya miavuli. Wazo kando na kikombe cha maji linaweza kutubu shida.
Mhubiri aanze katika sauti ya kawaida. Ni bora kuanza katika sauti ya chini (si chini sana -
katikati) kuliko kuanza kwa sauti ya juu. Sauti yetu itabadilika yenyewe bila kujua
tunapoendelea na mahubiri. Tukianza kwa sauti mwanzoni, kuzungumza kwetu kutaweza kuwa
hakupendezi masikioni mwa wasikilizaji.
51
Ni muhimu zaidi kwamba hotuba yetu si ya kuchosha. Tunapohubiri, ni lazima tusiwe kama
injili ambayo inaenda kwa mwendo wa juu. Badilisha sauti yako, mwendo wa na ukubwa.
Lazima tujifunze sauti zetu katika njia tofauti. Lazima tuwe na manon´gonezo na sauti kama ya
mngurumo wa radi, na mpangilio mzuri wa sentenzi na mkazo wa pole wa hotuba, wakati na
mahali ambapo ni muhimu. Jambo hili kwa kweli ni lazima litendeke kwa njia ya kawaida.
Watu wanapohitajika kuwa na usikivu bora, ni lazima tubadilishe sauti yetu. Ni lazima wahisi
kwamba tunawasiliana nao. Kama tunasema Yesu Kristo anawataka wote waokoke, ni lazima
tuzungumze, “je, hutaki kumkubali?” Lazima tuzungumze kwa sauti ya chini na ya siri. Sauti
nzuri katika mahali pazuri ni bora. Ninamjua mhubiri mmoja ambaye anajaribu sana kutumia
sauti yake katika njia tofauti na sauti yake si ya asili. Wacha tukumbuke kwamba hakuna kitu
chochote ambacho kinaweza kuchukiza wasikilizaji kuliko hotuba ambayo si ya siri.
2. Uangalie Wasikilizaji
Watu wanataka kuangaliwa. Wale wanaoangalia juu ya paa ya nyumba, sakafu ya nyumba, au
nje ya dirisha wanaweza kuhubiri vyema, lakini watawapoteza wasikilizaji wao. Lazima
tuangaliane jicho kwa jicho. Wakati mwingine, jambo hili si rahisi, hasa tunapokuwa na watu
wanaokufanya kuwa na hofu katika mkutano. Nyuso zao zikionekana kama “majonzi makuu”.
Fahamu kwamba hili ni jambo la makusudi. Wao walijikuta katika hali kama hii. Ni lazima
tuwaonyeshe nyuso za kufanya urafiki wale tunaoangaliana na macho. Na kuchagua mtu mmoja
kila upande na mmoja katikati ya mkutano. Kama tunazungumzia umati mkubwa, ni lazima
tuchague mtu mmoja mbele na mwingine nyuma. Kila mara tunapowaangalia watu hawa, wale
ambao wako karibu nao wanajisikia kwamba tunawaangalia pia. Uwe mwenye kufanya urafiki,
la sivyo, watu wataogopa kukuangalia. Uwe mwenye furaha.
3. Ishara - Jambo la Kufanya na la Kutofanya
Ishara ambayo haifai au ya ujinga huondoa ubora wa mahubiri. Mhuduma ni lazima awe na
utulivu, mwenye ujasiri, nyuma ya mimbara. Wengine wanaonekana ovyo kwa sababu ya
kuogopa au uwoga. Mwongozo ufwatao utaweza kustawisha ishara yetu.
a. Tumia mikono vizuri iwezekanavyo. Usiiweke mfukoni na usipitanishe mikono kwa kifua
unapozungumza. Wacha mikono kuningínia upande wako au ushikilie mimbara. Usipeperushe
mikono yako hewani bila mpango, bali uitumie wakati mzuri. Usishike mapua yako.
b. Uwe mwangalifu kwa vitendo vyako kama hauwezi kupata maneno mazuri. Wengine huanza
kuvuta tai zao. Wengine huanza kushikanisha nywele na vidole vyao. Wengine husugua macho
yao au wanainamisha mwili wao kila upande hadi wanapata neno sahihi. Ni lazima pia tusifuate
mfano wa mhubiri mmoja ambaye aliuangalia mkono wake wa kike na kujaribu na mkono wake
wa kuume kupata maneno. Pia kuna wale wanaopiga kichwa chao, au wanajikuna kichwa wakati
neno linakataa kuja.
c. Usiiname katika mimbara unapohubiri. Unaweza kufanya hivyo kwa muda mfupi unapotaka
kuzungumza kwa ujasiri kwa mkutano. Lakini usihubiri katika hali hiyo. Simama imara na
uongee kama mwanaume. Usiangalie kama swali (?), bali kama alama ya kushangaa (!). Watu
lazima wajisikie kwamba tuna ujumbe muhimu wao.
d. Uhakikishe kwamba ishara zako zinalingana na kile unachosema. Usishikanishe mikono
unaposema wokovu ni kwa kila mtu, lakini kunjua mikono. Tunaweza kuzungumza kwa
kutumia mikono yetu, kuhakikisha, kufukuza, kutisha na kadhalika. Wengine wanaonekana
kama wanakata kuni au nyama, au wanaonekana kama wanaponda fu-fu, sadza au ensima au
52
ugali. Wengine wanatumia mikono kama watu ambao wanakamua nguo. Kweli kama ishara
hizi zinafaa katika mahubiri, ni lazima zitumiwe.
Mbali na haya yote, uwe mtu wa kawaida. Usishughulishe mwili wako katika vitendo
mbalimbali, kwa sababu utakuwa mtumwa wa mambo haya. Mke wetu au rafiki anaweza
kutusaidia katika kuendeleza ishara zetu, kwa kusema mahali ambapo tunahitaji sahihisho.
Walakini hii inahitaji uvumilifu sehemu yetu. Lazima tutende kulingana na jukumu letu. Wale
ambao wana tabia ya utulivu ni lazima wasijaribu kukimbia juu na chini kanisani wanapohubiri.
Na wale watu ambao wamejazwa na Roho wasijilazimishe kusimama kama kuni nyuma ya
mimbara.
4. Mengi ya Kukumbuka
Uhakikishe kwamba umetumia maandiko sahihi. Wasikilizaji wetu watajua kwa kweli maandiko
na hawatakubaliana nasi tukienda kando ya maandiko. Unapozungumzia maandiko fulani,
uhakikishe umetumia maandiko bora kutoka kitabuni, sura na msitari.
Ni jambo la busara kuwekea mkazo mambo ambayo tunasema kupitia maandiko. Njia kama hii
itafanya ujumbe wetu kuwa na nguvu. Hapa tunaweza kujifunza kutoka kwa Bily Graham
ambaye anajulikana kwa kusema, “Biblia inasema”.
Ujiepushe na mazoea mabaya ya hotuba. Usizungumzie kupitia mapuani mwako, na usiwe
ukisafisha koo lako kila mara kwa kukohoa. Ni jambo lakachukiza kumsikiliza mtu ambaye
anasafisha koo lake baada ya kila sentenzi.
Ni lazima tuhakikishe zaidi kwamba hatuna maneno fulani kwa muda mrefu, wala katika
kuhubiri au katika maombi ya hadhara. Ni jambo la kuchukiza wahubiri wanapotumia maneno
kama “unaona sasa”, bada ya kila sentenzi, au wanaposema, “Bwana” baada ya kila maneno
machache katika maombi yao.
Jambo lingine ambalo wahubiri wa kipentekote wamezoea kufanya ni kulazimisha umati au
mkutano kusema “Amina”. Hii inafanyika kwa kupasa sauti “Halleluyah” au “Amina” katikati
ya sentenzi kila mara, ili kutayarisha itikio kutoka kwa wasikilizaji. Ni jambo la kutia moyo
mhubiri anapozungumzia watu wanaoitikia, lakini itikio kama hili ni lazima liwe la kushawishi
na wala si la lazima.
Unaposimama kuhubiri, usiwekee mkazo mahubiri kama haya, bali umtarajie Bwana ambaye
anawawezesha wale ambao ni wanyenyekevu na wenye moyo safi kukusaidia. Ungana na watu
kwa kuabudu na furahia uwepo wa Bwana. Kama tunafikiria sheria za kuzungumzia hadharani
nyuma ya mimbara, tutakuja kuwa watu ambao si wa kawaida. siku ya pili, tuketi chini,
tuchunguze maneno na tuone ni mahali gani tunahitaji mabadiliko. Kama wahubiri wangetumia
wakati wao sana katika kuzungumza kama mkimbiaji katika mazoezi yake ya kukimbia,
wataweza kuwa bora sana kuliko vile wanatakikana kuwa.
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-
53
MASWALI YA MARUDIO - KUPEANA UJUMBE
1. Je, mazoea ya kuandika chini mahubiri yatamsaidiaje mhubiri? Elezea kwa ufupi.
2. Je, ni kitu gani tunahitaji kukumbuka kuhusu urefu wa mahubiri?
3. Kwa nini ni vyema kutangaza somo la mahubiri?
4. Hotuba nzuri inasikika na nani?
5. Je, tujiepushe na kitu gani tunapokosa kupata maneno sahihi? Peana mfano.
54
Mwisho
A. Upako
Upako wa ujumbe na mhubiri ni jambo la manufaa la mahubiri. Bila upako Mtakatifu,
hatutakuwa na huduma wa kweli. si uchanguzi kwa cheo cha uongozi bali upako wa Roho
Mtakatifu ni matokeo ya ufanisi wa huduma.
Watu wengine wanafikiri kwamba upako ni sawasawa na kupasa sauti au kuzungumza haraka na
mhubiri hawezi kuwa na nafasi ya kupumua katikati ya sentenzi. Wengine wanaendeleza upako
wa Roho Mtakatifu kwa kupasa sauti na kusema “Amina” nyingi na Halleluyah ambayo mhubiri
anapenyeza kati ya fikira zake. Ni jambo ambalo haliwezekani kwa mhubiri ambaye ana upako
kuonyesha mtindo au tabia sawa na hii, lakini hili jambo lisiwe la kutatanisha na upako ambao
utawezesha ujumbe wa wahubiri kuleta kitendo cha kusadiki sana kwa undani, kutia moyo na
kujitolea maisha yako kwa Mungu, kuwa mwanafunzi bora.
Upako unapeanwa kwa msingi wa neema. Wale ambao Mungu anawaita, yeye huwapaka mafuta
kwa kuhubiri vyema. Katika siku za zamani, Mungu aliwachagua wafalme, makuhani na
manabii ambao aliwapaka mafuta kwa ajili ya huduma. Ilikuwa mapenzi yake wao kuwa
watumishi wake na vyombo vya nguvu zake. Leo upako wake ungali unapeanwa hivyo- hivyo.
Ingawaje upako wa Roho Mtakatifu hauwezi kuwa kama msamaha, walakini tunahitaji kuutunza.
Wale ambao wana upako, wataishi maisha matakatifu, wataomba, watasoma Neno, watafunga
kula, watatii mapenzi yake, na kutembea katika imani.
1. Jinzi ya Kuihifadhi
Wakati mwingine inaonekana kwamba ujumbe wetu hautiririki vyema. Ni kama unatoka juu ya
ukuta wa jiwe. Kuna sababu nyingi kwa jambo hili:
(a) Huenda tunatazamia mengi zaidi kutoka kwa wasikilizaji, haswa wale ambao wako na nyuzo
sisizo za kirafiki. Wengine wanaonekana wakatili sana ili kwamba unapoteza fikira zako
ukiendelea kuwatazama.
(b) Kuelezea jambo moja kwa muda mrefu au kuenda kwa jambo lingine haraka kunaweza
kupunguza upako wa Roho Mtakatifu. Ni lazima tuende kwa jambo lingine na “mawingo” kama
watoto wa Israeli jangwani.
(c) Kuwa tayari na katika hali nzuri ni mchango mwema wa upako wa kupeana ujumbe. Mwili
na fikira zikiwa katika hali nzuri, zinaitikia vyema kwa Roho wa Mungu kuliko mwili ambao
umekuwa mlegevu.
(d) Wakati mwingine, nguvu za kishetani zinaweza kutatiza mtiririko wa Roho Mtakatifu
kupitia mhuduma. Kwa hivyo, kuomba na kufunga ni lazima kwa kila mhuduma, hasa kwa wale
wanaoanzisha makanisa mapya katika sehemu za mashambani katika Afrika. Nguvu za shetani
ni lazima zipingwe na zifungwe katika maombi kabla ya kuanza kuhubiri. Wahubiri wanaoenda
mahali papya wanakutana na waganga na nguvu zao za kimiungu. Upako utatuwezesha kuvunja
chini nguvu hizi za kiroho na kuonyesha ushahidi wa Kristo katika uwepo maana silaha
tunazotumia katika vita vyetu si silaha za kidunia, ila ni nguvu za Mungu zenye kuharibu ngome
zote. Tunaharibu hoja zote za uwongo , 2 Wakorintho 10:4.
55
Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake
shingoni mwako nayo nira itaharibika, kwa sababu ya kutiwa mafuta Isaya 10:27
(e) Usiwe mfungwa wa maneno yako bali uwe wazi kwa mwongozo na mwenendo wa Roho
Mtakatifu. Uwe tayari kuwacha ujumbe wako ikiwa unahisi kwamba Roho Mtakatifu
anakuongoza tofauti.
(f) Umsikilize Roho Mtakatifu. Usipeane maelezo au usimulie hadithi ambayo umetayarisha,
kama hauna uhuru wa ndani , fanya hivyo. Uongozwe na Roho Mtakatifu. Lazima hadithi
sizisimuliwe kuwa na wazo au kufurahisha masikio ya wasikilizaji, bali itumiwe kwa kusudi la
ujumbe.
(g) Usifanye mahubiri yako kuwa marefu bila umuhimu. Kama Mungu amemaliza kuzungumza
baada ya dakika 15, ni lazima tufanye hivyo. Si lazima tufundishe kwa saa moja ili tuwe kiroho.
Kuwa kiroho kunapeanwa kwa kupenda kutii Roho Mtakatifu, na si kwa urefu au mambo mengi
ya mahubiri yetu.
(h) Usiwaruhusu watu kusimama na kuimba na kukatiza ujumbe wako, vile inavyofanyika
mahali pengine. Neno la Mungu lina ukuu.
2. Wakati ambapo hakuna Upako
Wakati mwingine tumefunga kula, tumeomba, tumetumia masaa na siku kadha kutayarisha
ujumbe, tumefuata sheria zote na tunakosa ujumbe kamili. Jambo kama hili ni la manufaa mara
nyingine. Litatuwezesha kumtegemea Mungu. Lakini likitendeka kila mara lazima tumtafute
Mungu na kujua ni mahali gani tumekosea.
B. Jambo la Kimiujiza katika Ibada
Hebu tupeane nafasi kwa hali isiyo ya asili katika kila ibada, hasa wakati wa asili ya kipentekote.
Na wakati huo tujaribu kuepukana na mshtuko. Kama tutafuata utaratibu wa kanisa la Agano
Jipya, tutapeana nafasi kwa unabii, uponyaji, ukombozi na vipawa vingine vya Roho. Mambo
haya yote yafanywe kwa utaratibu.
Wahuduma wa injili wasifanye makosa ya kuonyesha vitu vitakatifu. Usijifanye kwamba
umesikia kutoka kwa Mungu na ni uwongo. Usiseme, “Mungu amenionyesha” wakati yeye
hajafaya hivyo. Hii hufanyika kwa sababu wahubiri wanataka kujenga jina au kwa sababu
wanataka kujulikana kama “mtu wa Mungu”. Watu wakikosa kuponywa au wakijazwa na Roho
Mtakatifu baada ya kuwaombea, usiwalazimishe kutoa ushuhuda, ili kuinua sifa nzuri yako.
Watu wakiponywa kwa kweli, usiwalazimishe kushuhudia, wenyewe watakuja kwa hiari yao na
kushuhudia kile Mungu amewafanyia. Yesu hakuwalazimisha watu kushuhudia kuhusu uponyaji
wao au ukombozi. Kwa upande mwingine, aliwakataza kuwaambia wengine kile amewafanyia.
Mwinjilisti mwingine Mmarikani alizoea kumtuma mkewe na watu wengine kutoka kwa kikundi
chake kabla ya ibada kuanza, na kila mmoja alikuwa na kitu cha kupasa sauti ambacho
kimefungiwa kwa mwili wao. Hawa watu wangewauliza watu majina yao na shida ile walikuwa
nayo. Ikiwa wagonjwa walitaka kujua wamekuwa wagonjwa kwa muda gani, na vile ugonjwa
wao ulivyoanza na kadhalika. Wakati wa maombi, mwinjilisti huyu angesema kwamba “Mungu
amenionyesha kwamba kuna mwanamke kwa jina fulani. Amekuja kutoka mahali fulani, naye
56
ana shida fulani au ugonjwa ambao amekuwa nao kwa muda wa miaka fulani. Na kila mtu
alifikiri ni mtu wa ajabu wa Mungu, lakini kwa kusema kweli alikuwa mtu mdanganyifu.
Kama tunahitaji mambo ya miujiza kufanyika katika ibada zetu, ni lazima tukatae kabisa
majaribu ya udanganyifu ili kuwavutia watu. Kuwa mwuuaji katika Roho limekuwa jambo la
kawaida katika wafuazi wengine. Kama jambo hili laweza kufanyika kupitia Roho Mtakatifu,
hakuna pingamizi. Maisha ambayo yamebadilika au mwili ambao umeponywa kabisa
utathibitisha ukweli kwamba mambo haya kwa hakika yalitendeka kwa utakatifu. Walakini,
mara nyingi watu huwekewa mikono vichwani na kusukumwa kwa nguvu kidogo nyuma.
Wanaposimama na macho yao yamefungwa na vichwa vimeinamishwa nyuma, mtu hawezi
kuchukua nguvu nyingi kuanguka nyuma, hasa akijua kuna mtu mwingine amesimama nyuma
yake ambaye atamshika. Jambo hili la dhihaka la utakatifu linakuwa la kuchukiza unaposikia
kuhusu seminari ambazo zina mafundisho yanayoitwa “wasukumaji na washikaji”. Mimi
mwenyewe nina shida na mambo haya ambayo watu wanatenda, kwa kuwafanya wengine
kuanguka. Mambo haya yanapofanyika, ni lazima mara nyingi tujiulize, je, jambo hili ni lile
ambalo Yesu au mitume wangefanya? Je, hii inaleta utukufu? Je, hii inabadilisha ya yule
ambaye ameombewa? Kama maswali haya hayawezi kujibiwa kwa uthabiti, basi, dhihirisho la
“muujiza”ni lazima likataliwe, kwa maana labda ni kazi ya mtu au ya pepo wadanganyifu. Yesu
aliahidi ishara na miujiza kufuata kuhubiriwa kwa Neno Lake, kwa hivyo, ni lazima turuhusu
mambo haya kufanyika. Labda wakati huu utakuwa wakati wa mahubiri au katika mimbara,
ambao utakuongoza kwa jambo la pili.
C. Huduma wa Madhabahu
Tusijitayarishe tu kwa mahubiri, bali tutafute mwongozo kutoka kwa Mungu kuhusu ibada ya
madhabahu. Anaweza kupeana mwongozo halisi kwa kile tunahitaji kufanya baada ya ujumbe
kupeanwa (kwa kweli ujumbe wake si wetu). Atatuongoza kuombea watu, kuwa wanyenyekevu
kwake,au na kuruhusu wakati wa binafsi wa kuomba. Lazima tusiwache sehemu hii muhimu ya
ibada kuwa ya kubahatisha! Mungu anawataka watu kuitikia ili ajidhihirishe mwenyewe kwao.
Kwa hivyo, ni lazima tujitayarishe ili Mungu atende kazi. Kabla ya kuenda katika mimbara, ni
lazima tujue kile tunahitaji kujua baada ya mahubiri. Lazima liwe jambo la kawaida kwetu
kumtafuta Mungu kuhusu mapenzi yake kwa ibada ya madhabahu. Hii lazima iwe sehemu yetu
ya matayarisho ya mahubiri.
D. Mwisho
Kuhubiri kuzuri hakuji kwa urahisi. Si jambo ambalo linafanyika tu, bali ni jambo ambalo lina
mambo ya hakika tofauti. Kama vile tumeona, huanza na mwito wa mhubiri na sifa zake, na
huhusika na matayarisho ya utaratibu na kusoma zaidi. Kilele ni wakati wa kupeana ujumbe na
matokeo haya. Mahubiri ambayo yametayarishwa vyema yatakuwa ujumbe tofauti kwa neema.
Mungu anapotakasa kazi yetu, mahubiri ya kufaa ya kipentekote yatakuwa na matokeo.
Mahubiri ya kipentekote ya kufaa yatakuwa na matokeo. mambo haya mara nyingi si ya wazi,
lakini tutaweza kuwa na ishara kwamba Mungu ameyatumia kubadilisha maisha. Mahubiri ya
kufaa yatamtukuza Mungu, yataongoza mioyo kwa msalaba (Kalvari) na katika hali ya kufanya
wengi kuwa wanafunzi. Mungu anaweza kutusaidia kila wakati ili mahubiri yetu yasiwe ya bure.
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-..-.-.-.-.-.-.-.-..-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-
57
MASWALI YA MARUDIO - MWISHO
1. Jaza katika mapengo:
Si katika uchanguzi kwa cheo cha uongozi lakini _______________ wa Roho Mtakatifu
________________ katika huduma __________________.
2. Taja sababu tatu ni kwa nini tunaweza kuwa hatutekelezi vyema ujumbe wetu.
3. Je, kitu gani kitafanyika wakati watu wanaponywa kwa kweli?
4. Jaza katika mapengo:
Kama tunataka miujiza kufanyika katika ibada zetu, ni lazima ______________ majaribu
________________ ili ______________ umati .
5. Kwa nini tujitayarishe kwa huduma wa madhabahu?
58
WATUNGAJI VITABU
Adam, Gottfried. Einfürhrung in die exegetischen Methoden, Grünewald: kaiser, 1979.
Adams, Jay E. Predigen, Zielbewußt, Anschaulich, Überzeugend, Giessen7Basel: Brunnen
Verlag, 1991.
Blackwood, Andrew W. Matayarisho ya Mahubiri Nashville: Abingdon, 1948
Blackwood, Andrew W. Hilfen Zur Predigtvorbereitung, Erzehausen: Leuchter Verlag, 1976.
Evans, Williams. Jinzi ya kutayarisha Mahubiri, Chicago: Moody Press, 1980.
Fee, Gordon D. New Testament Exegesis, Philadelphia: Westminister Press, 1983.
Fisher, Robert E. Mabishano ya Huduma, Cleveland: Pathway Press, 1977
Hughes, Ray H. Mahubiri ya Pentekote, Cleveland: Pathway Press, 1981.
Jentsch, Werner. Predger und Predigt, Gütersloh: Gütersloher Verlagshaus, 1978.
Koller, Charles W. Mahubiri ya kufichua Bila Nakili, Grand Rapids: Baker Book House, 1984.
Pohl, Adolf. Anleitung zum Predigen, Wuppertal: Oncken Verlag, 1976.
Sangster, W. E. Uchoraji wa Utungaji wa Mahubiri, Southampton: Camelot Press, 1985.
Spurgeon Charles H. Ratschläge für Prediger, Wuppertal: Oncken Verlag, 1975.
Thayer, Joseph H. Lexicon ya Thayer ya Kingereza Kigriki ya Agano Jipya, Grand Rapids:
Baker House, 197.
Theologisches Bergriffs- Lexikon zum Neuen Testament, Wuppertal: Brockhaus Verlag, 1977.
Vine, W. E Kamusi ya Ufichuo ya Maneno ya Agano Jipya, Old Tappan: Fleming H.
Kampuni ya Revell, 1966.

No comments:

Post a Comment