MADA YA TATU
KANISA LA SMIRNA. (KANISA LA MATESO)
A. UTANGULIZI.
Simrna ni mji ambo ulikuwa umbali wa Km 65 Kaskazini mwa Efeso na
ulijulikana kama bandari ya salamakwa wakati ule ukliokuwa katikati ya njia kuu
kutoka rumi kwenda India na Persia(Irani)
Katika moja ya mitaa yake kulikuwa
na hekalu la mungu wa kigiriki alywejulikana kwa jina la zeus Munugu mkuu na
katika upande mwingine wa mji kulikuwa na hekalu la Cybele {mama wa mungu}.
Mji wa Smirna pia ulikuwa ni kituo
cha ibada ya kumwabudu kaisari. Kulikuwa na hekalu ya mfalme wa Rumi Teberio
Kaisari
B. historia ya kipindi cha smirna
inaaminika kwamba siku kumi za mateso yaliyotakiwa kuja juu ya smirna huhusisha
vipindi maalum kumi vya mateso chini ya watawala mbalimbali wa kirumi pia na wao watawala wangekuwa kumi.
Majina ya wafia dini mbalimali
katika kipindi hiki cha Smirna chini ya
wafalme mbalimbali wa Rumi yanaorodheshwa hapa.
1.Klaudi Nero (64-68 AD). Petro alisulubiwa katika
kipindi cha utawala wa Nero. Paulo alikatwa kichwa katika kipindi hiki.
2.Domitiani (90-95 AD) aAlijaribu
kumuua mtume yohana akashindwa na baadae akaamua kumpeleka uhamishoni katika
kisiwa cha Patmo.
3.Trajani(104-117 AD)Simoni ndugu wa
Yesu aliuawa katika kipindi hiki mwaka wa 107.
Askofu wa Ignatious wa
Antiokia aliuawa pia katika utawala
wamfame huyu mwaka 110.Watu wngine waliouawa katika kipindi hiki ni Polikap mwanafunzi
wa Mtume Yohana(155),
4.
Marcus Aurelius.(161-180 AD). Yustini
aliuawa katika utawala huu katika mwaka 165 AD. Pia alifanya mauaji ya
wakristo wengine wengi pia.
5.Septimus Severio.(200-211 AD) alimuua Leonidus baba wa
Origeni mwanatheolojia mkuu., Pia aliwaua na Perpetua na Felistas na ireneos
mwaka 202.AD.
6. Thraker Maximus (235-237
AD).alifanya mauaji lakini hatuna majina ya watu aliowaua.
7.Desiusi .(250-253 AD.)
katika kipndi cha utawala wake matso yaliibuka tena juu ya kanisa na kwa
bahati nzuri utawala wake ulidumu kwa muda mfupi sana nabaada ya kuanguka kwa
utawala wake kipindi kifupi cha amani kilikuja juu ya kanisa.
8. Vareliani (257-260 AD.) Alipanga mauaji lakini
hayakufanyika katika utawala wake.
(270-275 .AD.)Askofu Spriani wa
Kathegi na askofu Sextus wa Rumi waliuawa
C.Mateso ya kitaifa. Tabia za msingi
katika historia ya kanisa katika karne zote mbili yaani karne ya pili naya tatu ni kanisa au wakristo kuteswa
na wafalme wa kirumi. Mateso haya hayakuwa endelevu lakini yalitegemea
mtazamo aliokuwa nao mfalme aliyekuwa
akitawala katika kipindi hicho.Mateso ambayo yalikuwa yakijirudia katika
kipindi hiki yalidumu kwa karibu miaka 200 mpaka mfalme kostantino
alipookoka.na kutangaza tamko la amani.(Edict of costantine) katika mwaka wa
313 AD.
D.
Sababu za kanisa kuteswa.
Imani juu ya Mungu mmoja. Warumi
walikuwa na miungu mbalimbali ambayo walikuwa wakiiabudu pamoja na sanamu zao.
Wakristo walitangaza kwamba kuna Mungu mmoja tu Mfalme wa rumi alijenga hekalu
ambalo lilipaswa kutumiwa na watu wote kuabudu miungu yao na akawapa wakristo
nafasi na ya kushiriki kumwabudu Mungu wao katika hekalu hilo. Wakristo walikataa fursa hiyo na kusababisha
wao kuonekana kwamba wako tofauti na wananchi wengine. Hivyo mateso yalianza
dhidi yao.
2.kukataa
kumwabudu kaisari. Kama ilivyokwisha elezwa katika
sura iliyopita kwamba makaisari wa kirumin walijitangaza kwamba wao ni miungu
na wakadai waabudiwe na wananchi au raia wao. Hivyo raia wote wa dola ya Rumi
walilazimika kushiriki ibada ya kumwabudu kaisari. Mahekalu ya ibada za kaisari
yalijengwa kila mahali na sanamu za makaisari zikawekwa na watu wakalazimishwa
kumwabudu kaisari na kutoa dhabihu mbele ya
sanamu za kaisari. Hii ilikuwa
mojawapo ya ibada za kitaifa katika dola ya Rumi.
Wakristo walipinga vikali iabada hizona hawakuwa tayari kushiriki ibada
hizo wala kutoa dhabihu mbele ya sanamu za kaisari. Kutokana na asababu hiyo
wakristo waihesabiwa kuwa wasdaliti wa kaisari na dola kwa umjla na hivyo walipaswa
kuhukumiwa kifo. Wakristo walianza kuteswa na dola ya Rumi kwa sababu ya
kukataa kumwabudu kaisari na kumwita Yesu Mfalme(Kurious).
3.Kutojihusisha kwenye ibada za
sanamu. Ibada hizi za sanamu zilikuwa sehemu ya maisha ya kila siku katika dola
ya rumi. Sanamu hizo zilisimamishwa katika kila nyumbba na ziliabudiwa katika
kila sherehe. Dhabihu za vinywaji
zilitolewa kwa sanamu hizo. Hivyo
wakristo walikataa kujihusisha katika shughuliza kilasiku za kijamii zilizohusha
ibada za sanamu(mfano sherehe mbalimbali). Wakristo walipokataa kujihusisha na
hayo mambo walionekana wako kinyume na jamii nzima.Kwa sababu hiyo jamii
iliwahesabu kama maadui.
4.kutambuliwa rasmi kwa dini ya
kiyahudi: Dini ya kiyahudi ilitambuliwa rasmi na dola ya Rumi kama dini ya
kitaifa. Mwanzoni kanisa wakati linaanza lilitambuliwa kama kikundi tu ndani ya
dini ya kiyahudi chenye msimamo mkali na hivyo
kanisa lilipata upendeleo wea serikali kwa namna fulani. Lakini mara
baada ya kuanguka wa Yerusalemu na na kubomolewa kwa hekalu katika mwaka wa 70
AD, kanisa au ukristo ulisimama peke yake na dini ya kiyahudi walikuwa tayari
kushirikiana na serikali kulitesa
kanisa.
Kanisa kufanya mikutano ya faragha.
Kuokana na mateso kanisalilianza kukutana katika maeneo ya siri na hasa wakati
wa usiku. Hii ilipelekea kanisa kuhisiwa vibaya na selrikali kwamba lilikuwa
linafanya njama ya kupindua serikali au kufanya maasi kwa sababu serikali ya
rumi ilipiga marufuku mikutano yote isiyo harali pia mikutano ya usiku ilipigwa
marufuku. Kwa kuogopa kwamba mikutano yote iliyokuwa haina kibali cha serikali
na iliyofanyika vifichoni haikuwa na nia njema kwa dola ya Rumi. Kwa sababu
hiyo wakristo walitazamwa na dola kama waasi. Watu wanopanga njama na maadui
kuleta vurugu na maasi ndani ya dola na hivyo dola ilianzisha mateso juu ya
kanisa.
Usawa katika kanisa. Kanisa
liliwaona watu wote kuwa sawa. Hakukuwa na matabaka katika kanisa. Waliwaona
watu wote kuwa sawa a hawakumwogopa mtu yeote na wala hawakuogopa cheo cha mtu.
Kuokana na sabu hiyo kanisa lilionekana kuwa na dharau, lisilo na heshima na
hivyo kanisalilifanyika adui wa dola.
Kuharibu
biashara za sanamu.: Kulikuwa na biashara iliyokuwa inafanywa ndani ya dola ya
Rumi.biasharahiyo ilikuwa ni ya uuzaji wa sanamu. Watu wengi walijipatia faida kutokana na biashara
hiyo.Mitume walipohubiri Injili watu
waliokoka na kuachana na ibada za sanamu . Mitume walifundishwa kwamba sanamu
si kitu na hazipaswi kuabudiwa anaepaswakuabudiwa ni Mungu muumba Mbingu na
nchi pekee. Watu wengi waliacha kununua
sanamu hizo . Kitendo hicho kilisababisha biashara hiyo ya uuzaji sanamu
kudolola. Watengenezaji na wauzaji wa
sanmu hizo walipata hasara na wakaamua
kuanzisha kuja juu na
Kuanzisha ghasia dhidi ya kanisa
kwani walipoteza wateja wao.
E.Hatua za mateso. Kuna mwingiliano
kati ya kipindi cha efeso na Smirna. Kipindi cha Efeso kiliisha na kifo cha
mtume Yohana mwaka 100 AD. Wakati kipindi cha Smirna kilianza wakati wa mateso
ya kitaifa.(dola) wakati mfalme nero alipouchoma mji wa Rumi mwaka 64AD
VIPINDI
KUMI VYA MATESO YA KITAIFA.
MATESO
YA KWANZA Chini ya Kaisari Nero.(54-68 AD.)
Klaudi Nero alikuwa na umri wa miaka
16 alipoingia katika utawala (ufalme) katika mwaka 54 AD. Alikuwa mjukuu mkubwa
wa Agustus aiyetoa amri ya watu wote kuhesabiwa sensa (Lk 2). Nero alikuwa
mfalme wa kwanza katka wafalme kumi kuanzisha mateso dhidi ya kanisa.Alichoma mji wa rumi mwaka
64 AD.Theruthi mbili ya mji wa Rumi iliteketea. Mfalme nero aliwasingizia
wakristo kwamba ndiyo waliohusika na uharibifu huo. Hivyo kaina lililazimika
kuingia kwenye mateso makali. Katika kipindi hiki mtume Petro alisulibiwa miguu juu kichwa
chini mnamo mwaka 67 AD.Pia mtume Paulo alikamatwa na kufungwa Rumi ambapo alihukumiwa kifo na kisha akauawa kwa kukatwa kichwa mwaka 68 AD. Mjini Rumi.
Mfalme Nero alikuwa katkili kuliko
makaisari wote wa dola ya rumi waliomtangulia na waliomfuata. Kwani hajatokea
kaisari katikadola ya Rumi aliyefanya mauaji kama Nero. Mwaka 59 AD. mfalme Nero alimuua mama yake . pia alimuua
mke wake wa kwanza(Octavia)na kisha mkewe wa pili(Pompea) na baadae alimuua
kaka yake na rafiki yake mwalimu Seneka.
Mpaka mwaka wa 64 AD. Rumi ilikuwa
katika ghasia kuu. Mfalme nero alituhumiwa kwamba yeye ndiye aliyehusika na
kuuchoma moto mji wa Rumi. Lakini yeye alikanusha na kuwashutumu wakristo kuwa
ndiyo waliohusika na tukio hilo.Kutokana
na hilo kanisa liliingia katika kipindi cha mateso makali. Maelfu ya wakristo
waliuawa baadhi yao walitupiwa kwenye hifadhi za wanyama ili waliwe na wanyama
wakali na baadhi yao walichomwa moto na mfalme akaendesha gari lake juu yao katika
bustani yake. Bustani ya mfalme ambako tukio hili lilifanyika leo ni eneo la la jiji la Vatikani makao makuu ya papa na kania la MT. Petro.Kaisari Nero alijiua mwenyewe
mwaka68. AD.
KIPINDI
CHA PILI CHA MATESO CHINI YA DOMITIAN. (90-96 AD).
Baada ya nero kujiua mwaka wa 68
ADkatisa lilipata amani mpaka alipoinuka mtawala mwingine ambaye ni Domitiani.
Wakristo wengi waliuawa . Mtume Yohana alipelekwa uhamishoni kwenye kisiwa cha
Patmo ambapo ndipo mahali alipopokeas ufunuo amao sasa ni kitabu cha Ufunuo wa
Yohana.
KIPINDI
CHA TATU CHA MATESO CHINI YA TRAJANI 104-107 AD.
Trajani husemekana kuwa mtu
muimusana miongoni mwa watawala wa Rumi. Alikuwa mtawala mzuri kwa nchi yake
lakini aaliwaua wakristo. Mmoja wa mahakimu wake aliyeitwa Plin the younger. Gavana wa behtania
alichunguza maisha ya wakristo na mafundisho yao na kugundua kwamba mafundisho hayo hayakuwa na chochote chenye
kuleta uasi kwa serikali ya Rumi. Alileta ripoti yake mbele ya mfalme Trajani
lakini mfalme alijibu “ Kama watu hawa walioletwa mbele yako wamepatikana na
hatia kwa sababu ya kuwa wakristo na wauawe lakini ikiwa wataikana imani yao ya
kikristo na na ikathibitika kwamba wanaabudu miungu yetu na waachiwe huru.
Katika kipindi hiki waliuawa wakristo mbalimbali kama ifuatavyo.
Simoni mdogo wa Bwana Yesu.
Alisulubiwa katika mwaka wa 107 AD.akiwa na umri wa miaka 110. Alisulubiwa kwa
amri ya mfalme wa Rumi {Trajani}.
Askofu Ignatious wa Antiokia ambaye
aliandika nyaraka mbalimbali kwa makanisa mbalimbali ambazo baadhi yake
zinapatikana katika kitabu kiitwacho “Mababa wa Kitume”{Apostolic
fathers}. Alikuwa tayari kuuawa kwaajili
ya Bwana Yesu. Aliandika barua za kuwafariji wakristo akiwa njiani kuelekea
Rumi ambapo alitumwa katika hifadhi ya
wanyama wakali na akaliwa na wanyama
wakali mnamo mwaka 110.AD
PORIKAP. {69-155 AD} Alikuwa
mwanafunzi wa mwaanfunzi wa mtume Yohana na rafiki wa trajani na mwalimu wa
Irenius. Inadhaniwa kuwa Polikap aliteuliwa na mtume yohana kuwa askofu wa
makanisa saba ya Asia. Alipoamriwa kumkana bwana Yesu Kristo ili kuepukana na
kuuawa yeye alijibu:
“Miaka 86 nimemtumikia Bwana wangu
na hajatenda Jambo lolote baya kwangu, nawezaje kunena vibaya juu ya Bwana
wangu aliyeniokoa? Alichomwa kwenye moto na akafa kifo cha kishujaa kwaajili ya
Imani yake juu ya Yesu Kristo. Aliuawa chini ya utawala wa mfalme Antonius Pius
mwaka 155 A.D.
KIPINDI CHA NNE CHA NNE CHA MATESO
CHINI MARCUS
AURELIUS 161-180 A.D.
Marcus alikuwa alijulikana kam
mfalme borawa nchi yake na mwandishi mwenye maadili. Japokuwa alikuwa mtumzuri
kwa taifa lake alikuwa mtesi wa kanisa. Alifikiri kurejesha maisha ya zamani ya kirumi na dini za zamani.
Kwa wakati huo ukristo ulikuwa na mashiko zaidi.Waamini wengi walikuwa tayari
kufa kwa ajili ya imani yao na wala hawakuogopa kifo. Walikikabili kifo kwa
shangwe na ushindi mkuu. katika kipindi
hiki waaminni wengi waliuawa na wengine walitupwa katika hifadhi za wanyama wakali na wakaliwa na wanyama .
YUSTINI (Justine)Marty 100-165 A.D
alizaliwa na alielimishwa vizuri mpaka kuwa mwanafalsafa na aliendelea
kufundisha hata baada ya kuwa mkristo. Alirejerea kwa manabii wa zamani wa
Kiebrania. Aliandika maneno yafuatayo dhidi ya ukatili na mauaji yaliyokuwa
yanaendelea dhidi ya wakristo. “wanatushitaki, wanatusulubisha
kwenye misalaba na kutupa kwenye hifadhi za wanyama wakali na kwenye moto. Lakini wanapofanya
mabaya zaidi juu yetu ndivyo idadi ya wakristo inaongezeka na kuwa kubwa zaidi.
Mnamo mwaka 165 A.D .alikamatwa na mfalme wa Rumi Marcus Aureliusi na kuuawa.
KIPINDI CHA TANO CHA MATESO CHINI YA
SEPTIMUS. 202-211. A.D.
Baada ya kifo cha Marcus Aurelius
kanisa lilipata amani mpaka alipoinuka mtawala mwingine aliyejulikana kwa jina
la Septimus Severus. Mtawala huyu alimuua Leonides baba wa Origeni
mwanatheologia mkuu. Katika mji wa kathegi Perpetua na mtumwa wake Felistas
walitumwa katika hifadhi ya wanyama poli wakali na wakauawa.
Mfalme Karakala alitoa uraia uraia kwa kila
mtu katika dola yake. Huu ulikuwaq ni uhuru mkubwa kwa wakristo. Watumwa pekee
ndio ambao wangeweza kusulubiwa au kutupwa kwenye hifadhi za wayama poli wakali.
KIPINDI CHA SITA CHA MATESO CHINI YA
THRAKA MAXIMUS
235-237. A.D.
Baada ya kipindi cha amani Thraka alikalia kiti cha enzi cha Rumi.
Alikua mpiganaji na alikusudia kuonyesha huruma zake kwa dini za kipagani kwa
kuwatesa wakristo. Utawala wake ulikuwa mfupi kwa sababu ya kutawala kwake kwa
njia ya udikteta. Maadui zake walitengeneza kikundi ambacho kilifanikiwa
kumuua.
KIPINDI CHA SABA CHA MATESO.CHINI
YA DECIUS 250-253 A.D.
Katika kipindicha utawala wake
mateso makali yaliibuka tena na kwa bahati nzuri kipindi chake cha utawala
kilikuwa kifupi na kanisa lilipata raha kwa kipinda raha na amani kwa miaka 40.
KIPINDI CHA NANE CHA MATESO CHINI YA
VARELIANI. 257-260. A.D.
Askofu Sipriani wa Kathegi aliuawa
pia askofu wa Rumi Sextus aliuawa.
KIPINDI CHA TISA
CHA MATESO. CHINI YA AURELIUS. 270-275. A.D
Mfalme Aurelius alikuwa mwabudu jua
japokuwa hakulitesa kanisa moja kwa moja mwanzoni lakini hakuwapa uhuru wakristo. Hatimae aliamuru kwamba wakristo
wateswa. Kwa bahati nzuri amri yake haikutekelezwa Kutokana na kifo chake cha
ghafla.
KIPINDI CHA KUMI CHA MATESO CHINI YA
DEOCLETIAN 303 3010. A.D
Mfalme Deocletiani na wasaidizi wake
waliwafunga wakristo gerezani. Baadae sehemu ya jingo hili lilibadilishwa na
kuwa Kathedro ya Mtakatifu Petro. Deocletiani aliagiza kuchomwa moto kwa kila
nakala Biblia, makanisa kubomolewa na wakristo wenye msimamo mkali
kunyang’anywa uraia. Akiwa na umri wamiaka 80 deocletiani aliondoka kwenye kiti
cha utawala, lakini wafuasi wake
Galarius na Kostantinusi
waliendeleza mateso mpka mfalme Kostantino
mototo wa Kostantinus alipotoa tamko la amani kwa kanisa mwaka 313 A.
Tamko hili la amani lilisitisha mateso kwa kanisa kwa kipindi cha karne mbili
Siku kumi za kujaribiwa zilizotajwa
katika Ufuno wa yohana 2:10 zilifikia mwisho. Baadae mfalme Deocletiani
alipotambua kwamba yuko karib na kufa alitubu dhambi zake mbele ya askofu wa
mji.. Mwka 337 A.D alibatizwa. Mtu aliyeamini kwamba angeweza kuufuta ukristo
alijikuta yeye mwenyewe anakuwa mkristo.
UONGOZI KATIKA KANISA KATIKA KIPINDI HIKI.
Wakati mitume wakiwa hai uongozi
ulionekana ni utumishi yaani kutumikia au kuwajibika. Wakati Luka alipoandika
kitabu cha matendo naPaulo alipoandika nyaraka zake tuna kuta maneno askofu na
wazee yakiwa na maana sawa yaani yakimaanisha ofisi moja. Lakini katika miaka
ya 125’s tunakuta maaskofu wamekuwa watawala katika maeneo yao. Katika baraza
la yerusalemu mwaka 48 A,D {Mdo 15}
mitume wote na wazee walihusika. Lakini katika baraza la mwaka 150 A.D
waliohusika ni maaskofu pekee. Hii inadhihirisha kwamba kanisa liliondoka
taratibu kwenye mafundisho halisi ya mitume. Huduma ya mitume ilizimwa na
ikachukuliwa na maaskofu . Maaskofu walijifanya watawala wa kanisa. Hii ndio
sababu inayosababisha baadhi ya wataalam kuamini kwamba kipindi cha mitume
kiliishia na kifo cha mtume Yohan, jambo ambalo si kweli. Huduma za mitume,
manabii, waalimu wachungaji na wainjilisti kama zinavyoelezwa katika waefeso
4:11 ziliendelea kuwapo katika kipindicha mitume na vi[pindi vingine vyote vya
kanisa, japokuwa zimekuwa zikikataliwa
na katika vipindi fulani ilionekana kama zimetoweka lakini kwa uhakika zimekuwapo na bado zimekuwa zikifanya kazi katika kanisa hata sasa.
SHULE ZA
THEOLOGIA.
Shule
ya Alexndria. Ilianzishwa mwaka 180. A.D na Pantaenusi ambaye alikuwani mwanafalsafa
wa kigiriki na baadae akwa mkristo. Kisha alikwenda India, irani na Saudi
Arabia katika huduma. Alikufa mwaka 200.A.D .
Klementi
wav Alexandria. Alikkuwa mwanafunzi wa
Pantaenus na alimsaidia katika
uendeshaji wa shule. Alikuwa ni mkuu wa shule hadi alipoondolewa kwenye wadhifa
huo katika kipindi cha mateso cha septimus Severusi mwaka 2002. A.D. Baadhi ya
vitabu vyake mpka sasa vipo.
Origeni(185-254
A.D). Alikuwa ni mwanatheologia mkuu.
Baba yake Alikuwa ni motto wa Leonidas.
Baba yake aliuawa kutokana na imani yake katika Kristo chini ya utawala wa mfalme
Severus katika mwaka wa 2002 A.D. Wakati huo Origeni alikuwa na umri wa miaka
17. Origeni aliisdaidia familia yake kwa kufundisha falsafa ya kigiriki pamoja
na fasihi. Aliianzisha kwa upya shule ya Biblia iliyokuwa imefungwa kutokana na
kuondoka kwa Klementi. Baadae alikuwa ni mwandishi wa vitabu vya dogma na
thiologia. Baadae alikwenda Kaisaria na alianzisha shule nyingine ya Biblia
ambapo alikuwa ni kiongozi wa shule hiyo kwa karibu zaidi ya miaka 20. Alifungwa jela chini ya mateso Deciani na alikufa kutokana na
kutendewa kinyama akiwa gerezani.alikufa akiwa na umri wa miaka 69 mnamo mwaka
254. A.D.
Shule
ya Asia ndogo. Shule hii haikuwa katikamji wowote
ilikuwa ni shule ya masafa (mobile Bible School). Ilihusisha waalimu wa
thiolojia na waandishi. Baadhi yao ni Ireneus(130-202A.D) aliyezaliwa Smirna.
Alipata elimu yake ya awali ya Biblia chini ya Porkap. Kansa la Asia ndogo
lilimpeleka Ufaransa kama mmisionari. Aliuawa wakati wa mateso ya Severusi
mwaka wa 202 A.D.
Shule ya kathegi: Shule hii ilikuwa
kaskazini mwa Afrika na ilifanya vizuri kuliko shule zingine kubadili imani ya
Kithiologia katika Ulaya. Watu wakuu katika katika shule hii walikuwa ni
Tetullani na Sipriani. Tetullani
(160-200 A.D) Alikuwa ni mteteaji shujaa wa imani ya kikristo dhidi ya dini ya
kiyahudi na mafundisho potofu alijiunga
na umontano na alitumia kalamu na
mahubiri kuthibitisha kile alichofikiri ni mambo ya kidunia na mabishano katika kanisisa.
Sipriani Askofu wa Kathegi (195-258
A.D) Alikuwa ni motto wa afisa wangazi ya juu wadola ya Kirumi. Alikuwa mkristo
wakati wa ujana wake. Mambo matatu yaliyomjutia mpaka kuwa mkristo ni Maandiko
ya tetullani, mafundisho ya Cellius toka Rumi na Maandiko matakatifu (Biblia).
Mwaka mmoja baada ya kuwa mkristo
alikuwa askofu na kiongozi mkuuwa makanisa ya Afrika Kaskazini mwaka 248 A.
D. Mnamo Mwaka 257 A.D. Mfalme Valentine alimfungia kufanya huduma
mwaka na mwaka 258 aliuawa.
Kanisa la karne ya pili lilipambana
na mambo makuu mawili ambayo ni Mateso na uzushi(Heresy) yaani mafundisho potofu. Mtume Pulo alitabiri ya
kwamba:
“ Najua
mimi yakuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa mwitu wakali wataingia kwenu
wasilihurumie kundi. Tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema
mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao”
Baadhi ya makundi ya
uzushi………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
HALI YA KANISA KATIKA KIPINDI
CHA MWISHO WA KARNE YA PILI:
Kanisa lililotakasika. Mateso
yaliwaondolea mbali wale ambao hawakuwa waaminifu katika imani yao. Wale ambao
hawakuwa na imani kamilifu na waliojiunga na kanisa kwa masilahi yao binafsi.
Mafundisho yenye mfumo mmoja.
Japokuwa kanisa lilihusisha watu wa tamaduni , rangi na jamii mbalimbali bado
lilikuwa na umoja wa imani wa ajabu katika kanisa lote. Walifuata mafundisho ya
mtume Paulo, Petro na wengine. Mdo 2:42.
Kanisa lenye muundo: kazi iliyofanya
na Paulo ya kuweka viongozi wa Kanisa katika kila mji ilileta ufanisi. Viongozi
hao walikutana katika mikutano na
kujadili mambo mbalimbali muhimu kuhusu
kanisa. Hii ilisababisha kutokea kwa ushirikiano imara wa
kimataifa.(International Fellowship) ambao umekuwepo mpaka sasa.
Kanisa lenye kusitawi{kukua}. Licha
ya mateso yaliyolikumba kanisa, kanisa liliendelea kukyua kwa kasi. Kanisa
lilikumbana na mateso makali chini ya watawala mbalimbali wa Kirumi, lakini
kanisaliliendelea kukabiliana na mateso hayo na likawa tayari kuwapelekea
watesi hao Injili ya uzima.
Hakika
Malango ya kuzimu hayakulishinda kanisa
Kuandikwa kwa agano jipya. Hatuwezi
kueleza kwa udhahiri au kikamilifu
kwamba ni lini hili lilifanyika. Baadhi ya vitabu kama
vile nyaraka za Paulo zilikubaliwa kila mahali, wakati vingine kama vile
Waebrania, Yakobo na Ufuno wa Yohana vilikubaliwa Mashariki peke yake na
kukataliwa Magharibi.
Kanisa la mashariki lilikubali
baadhi ya vitabu ambavyo havipo katika
Biblia. Baadhi ya vitabu hivyo ni Warakawa Balnaba, Mafundisho ya mitume kumi
na wawali na Ufunuo wa mtume Petro. Mabaraza yalikutana mara kwa mara
ili kutambua ni vitabu gani vilivyokuwa vimevuviwa na na
vipi havikuvuviwa. Inadhaniwa kwambaAgano jipya halikutambuliwa rasmi mpka
baada ya mwaka 300. A.D
No comments:
Post a Comment