1
Sura ya
Kuumbwa
Upya
Na
A.L. na Joyce Gill
Available from
www.gillministries.com
Swahili – New Creation Image
2
Vitabu vingine vya A.L. na Joyce Gill
Baraka zako za Agano
Ahadi za Mungu kwa Kila hitaji Lako
Kuandaliwa kwa Kutawala
Ondoka! Katika Jina la Yesu
Ushindi juu ya Uwongo
Vitabu katika Mwongozo Huu
Mamlaka ya Mwamini
Njia ya Kuepuka kupata Hasara
Na kuanza Kushinda
Ushindi wa Kanisa
Kupitia Kitabu cha Matendo
Msaada wa Mungu wa Uponyaji
Kupokea na Kuhudumu
Nguvu za Uponyaji za Mungu
Vipawa vya Huduma
Mtume, Nabii, Mwinjilisti,
Mchungaji, Mwalimu
Uinjilisti wa Kimiujiza
Mpango wa Mungu wa Kufikia Ulimwengu
Mbinu za Kuishi
Kutoka Agano la Kale
Sifa na Kuabudu
Kufanyika wenye Kumwabudu Mungu
Maombi
Kuileta Mbingu Duniani
Kuishi Kusiokuwa kwa Kawaida
Kupitia Kipawa cha Roho Mtakatifu
3
Kumhusu Mwandishi
A.L. na Joyce Gill ni wanenaji, waanzilishi na walimu wa Biblia. Huduma ya usafiri ya mitume
imempeleka katika mataifa zaidi ya hamsini ya ulimwenguni, kuwahubiria umati unaozidi laki
moja yeye binafsi na pia kwa mamilioni kwa redio na tuninga.
Vitabu vyao vinavyouzwa na stakabadhi vimeuzwa zaidi ya milioni mbili katika nchi ya
Marekani. Maandishi yao, ambayo yametafsiriwa katika lugha nyingi, inatumika katika vyuo vya
Biblia na pia katika washa mbalimbali duniani.
Kweli zenye nguvu na zibadilishazo katika Neno la Mungu hulipuka katika maisha ya wengine
kupitia mahubiri ya ajabu, mafundisho, maandishi na huduma ya kanda za kuona na kusikiza.
Utukufu wa ajabu wa uwepo wa Mungu unaonekana katika washa za sifa na ibada wakati
waamini wanatambua jinsi kuwa wakweli na karibu wanapomwabudu Mungu. Wengi
wamegundua mbinu mpya na yenye kusisimua ya ushindi na ujasiri kupitia mafundisho yao juu
ya mamlaka ya mwamini.
Waandishi hawa wamewafundisha waamini wengi kupiga hatua na kuingia katika huduma za
Mungu za asili pamoja na nguvu ya uponyaji ya Mungu katika mikono yao. Wengi wamejifunza
kutenda katika karama zote tisa za Roho Mtakatifu katika maisha yao ya kila siku na katika
huduma zao.
A.L. pamoja na Joyce wana shada za katika Jiologia. A.L. pia amejifunza na kupata Udaktari
katika Filosofia kutoka Chuo Kikuu cha Vision. Huduma zao zinaegemea juu ya Neno la
Mungu, huangazia Yesu, imara katika imani na kufundisha katika mamlaka ya Roho Mtakatifu.
Huduma yao huonyesha moyo wa upendo wa Baba. Mahubiri na mafundisho yao huambatana na
upako wa ajabu, ishara na maajabu, na miujiza ya uponyaji na wengi wakiangushwa chini ya
nguvu za Mungu.
Ishara ya uvuvio ukijumulisha kicheko cha kitakatifu, kilio mbele za Bwana na utukufu wa
Mungu na utukufu na nguvu huonekana na wengi wanaohudhuria mikutano yao.
4
Neno kwa Walimu na Wanafunzi
Yesu alisema, “imekwisha!” kazi ya Yesu ya ukombozi ilikamilika. Kwa nini basi, tunawaona
watu wengi wakiishi katika kushindwa? Kwa nini waamini wengi wanaishi katika magonjwa?
Kwa nini watu wake Mungu wako katika utumwa, kufungwa na nguvu za mapepo?
Shetani alituhadaa! Kwa muda fulani, tumepoteza ukweli kuhusu mambo mazuri ambayo
yamejumlishwa katika ukombozi wetu. Mtume Paulo aliandika:
Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama,
yamekuwa mapya. 2 Wakorintho 5:17
Ufunuo wa maisha-yabadilishayo katika masomo haya ya Sura ya Kuumbwa Upya itawaweka
huru waamini kutokana na hisia za kuhukumika, kuangamia, kutojisikia wa maana,
kutoheshimika, na kutotosheleza ili waweze kubadilishwa katika mfano wa Kristo. Itawaachilia
waamini waanze kufurahia, kutenda na kuwa na vyote walivyoumbwa kuwa, na kumiliki.
Masomo haya yataweka wazi kweli zenye nguvu za maana ya kuwa kiumbe kipya katika Yesu
Kristo. Hizi ni kweli za msingi ambazo ni “lazima” kwa kila mwamini.
Kadri unavyoacha kweli za Neno la Mungu zikolee kuhusu kuumbwa upya, ndipo kweli hizi
zitatoka akilini mwako hadi rohoni. Kitabu hiki basi kitatoa mwongozo kwako ili kukitumia
unapowaeleza wengine kweli hizi.
Mifano kutoka maisha ya binafsi inaitajika ili kufundisha vizuri. Waandishi wameacha haya ili
walimu waweze kutumia mifano na ustadi kutoka maishani mwao, au maisha ya watu ambao
wanafunzi watahusiana nao. Ni bora ikumbukwe kuwa ni Roho Mtakatifu ambaye amekuja
kutufundisha mambo yote, na kuwa tunaposoma, au kufundisha, ni sharti tutende katika nguvu
na kuongozwa na Roho Mtakatifu.
Masomo haya ni bora kwa makundi, Shule za Biblia, Shule za Jumapili, na makundi ya
nyumbani. Ni bora kuwa mwalimu na wanafunzi wawe na nakala ya kitabu hiki mkononi
wanapojifunza. Vitabu vinapatikana kwa wingi.
Vitabu bora huandikwa ndani, kutiwa mistari, kutafakari juu yake, na pia kuviwaza. Tumeacha
nafasi kwa ajili ya nakili zako na maelezo. Mpangilio umewekwa ili kujifunza haraka na
kukusaidia kupata msaada tena. Mpangilio maalum humsaidia kila mtu, punde tu wanapojifunza
nakala hii, kuyafundisha wengine yaliyomo.
Paulo alimwandikia Timotheo:
Nayo mambo yale uliyonisikia nikiyasema mbele ya mashahidi wengi, uwakabidhi watu waaminifu
watakaoweza kuwafundisha watu wengine vile vile. 2 Timotheo 2:2b
Masomo haya yameundwa kama masomo ya Biblia yanayohuzisha katika Mpango wa
Kuendeleza Huduma, ambayo ni mbinu ya mpango wa kujifunza. Mawazo haya yanakusudia
kuzidisha maishani, huduma na mafunzo ya wanafunzi ya baadaye. Wanafunzi wa awali, kwa
kutumia nakala hii, wanaweza kuwafundisha wengine masomo haya kwa urahisi.
5
Orodha ya Yaliyomo
Somo la Kwanza Kuumbwa kwa Mfano Wake 7
Somo la Pili Mfano wetu wa Baba 16
Somo la Tatu Mfano wetu wa Mwana 26
Somo la Nne Mfano wa Kuumbwa Upya 37
Somo la Tano Kuibadilisha Sura Yetu ya binafsi ya Zamani 45
Somo la Sita Sura yetu katika Kristo 57
Somo la Saba Haki katika Kuumbwa Upya 68
Somo la Nane Faida za Kuumbwa Upya 75
Somo la Tisa Wahusika Katika Asili ya Kiungu 85
Somo la Kumi Neno la Mungu na Kumbwa Upya 97
Unless otherwise indicated all Scripture
quotations in New Creation Image are taken
from the New King James Version.
Copyright 1979, 1980, 1982,
Thomas Nelson Inc., Publishers
6
7
Somo La Kwanza
Kuumbwa kwa Mfano Wake
Utangulizi
Masomo ya Sura ya Kuumbwa Upya yataleta ufunuo wenye
nguvu kutambua sisi ni nani katika Kristo – maana ya kuwa
kiumbe kipya. Italeta uhuru wa kuwa na hisia ya hukumu,
kustahili adhabu, kutokutosheleza, na kuwa chini.
Itatuingiza kwa ujasiri katika ufunuo wa maisha
yabadilishayo yenye maana ya kuwa katika Yesu Kristo.
Tutagundua kile Mungu alikusudia kwetu katika kazi Yake
ya ukombozi. Tutajikuta tumetambulika kama:
Waliozaliwa mara ya pili
Roho aliyeumbwa tena
Kuumbwa tena upya
Mtume Paulo aliandika maneno haya:
2 Wakorintho 5:17 Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo,
amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama, yamekuwa
mapya.
Kama waamini, sisi tu sehemu ya wanadamu wa ujamaa
mpya, ujamaa wa “waliozaliwa mara ya pili” tukiwa na uhai
wa Mungu ndani yetu. Sisi tu viumbe vipya katika Kristo.
Mara nyingi katika masomo haya, waamini watatajwa kama
“viumbe wapya”
Masomo haya yataleta ufunuo mpya kuhusu Yesu ni nani
nasi ni nani ndani Yake.
Tukiwa na ufunuo huu wenye nguvu sisi kama waamini
tutaanza kutembea katika uhuru, mamlaka, ujasiri, nguvu,
na ushindi maishani mwetu na katika huduma.
Tutajikuta tukitangaza kwa ujasiri:
Ninajua mimi ni nani katika Yesu Kristo!
Mimi ni yule Yeye anasema!
Ninaweza kufanya kile anasema naweza!
Ninaweza kupata kile anasema naweza!
MWANADAMU – ALIUMBWA KWA MFANO WA MUNGU
Ili kuelewa sisi ni nani kama viumbe wapya, ni lazima
tuelewe kile waume na wake walipoumbwa kwanza wawe.
Ni sharti tuelewe kuwa alikuwa na kusudi na mpango
alipowaumba waume na wake kwa mfano Wake na
akawapa mamlaka kamili juu ya ardhi.
Mwanzo 1:26-28 Ndipo Mungu akasema, “Tufanye mtu kwa
mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale juu ya samaki wa
8
baharini na ndege wa angani, juu ya dunia yote, na juu ya viumbe
wote watambaao juu ya nchi.”
Kwa hiyo Mungu alimwumba mtu kwa mfano wake mwenyewe,
kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanaume na mwanamke
aliwaumba.
Mungu akawabariki na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke,
mkaijaze tena dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini,
ndege wa angani na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.”
Sura na Sanamu
Tuliumbwa kwa mfano wa Mungu. Kama viumbe wapya,
tunabadilishwa kwa mfano wa Mwana wake. Mfano ni sura
kamili ya kitu. Kulingana na kamusi “sanamu” maana yake:
Kuiga au kumwasilisha mtu
Kitu kionekanacho au sura ya kitu katika kioo
Mtu kwa mfano wa mwingine; nakili; mwingine; au
mfano wake
Kuwakilisha kikamilifu
Mungu aliumba Adamu kwa mfano wake kweli.
Alimuumba awe kama Mungu mwenyewe – sura
ionekanayo katika kioo ya Mungu katika mwili, katika nafsi
ya Mungu, na katika roho Wake, ambayo ilikuwa hai na
uhai na pumzi ya Mungu.
Mwanadamu aliumbwa ili kuwa mfano na utukufu wa
Mungu hapa duniani.
1 Wakorintho 11:7a Mwanaume haimpasi kufunika kichwa chake
kwa kuwa yeye ni mfano wa Mungu na utukufu wa Mungu.
Kiumbe aliye na Utatu
Mungu alisema, “hebu tumfanye mwanadamu kwa mfano
Wetu.” Alisema “Wetu” kwa sababu Mungu, hata ingawa
yu mmoja, yu katika nafsi tatu tofauti.
Mungu Baba
Mungu Mwana
Mungu Roho Mtakatifu
Waume kwa wake waliumbwa katika mfano Wake pia kama
nafsi tatu.
Sisi tu roho.
Roho wetu ni ufahamu wa Mungu ndani yetu ambayo
inahusika na mambo ya kiroho – sehemu ndani yetu
ambayo inaweza kuwa na uhusiano na ushirika na
Mungu.
9
Sisi ni nafsi.
Nafsi ni sehemu yetu ambayo inahusika na akili zetu.
Hii ni ufahamu, hisia na uwezo wa kuchagua. Hii ni
sehemu yetu inayowaza na kufikiria.
Tunaishi katika Mwili.
Mwili wetu ni sehemu yetu ionekanayo – nyumba
ambamo roho na nafsi zetu huishi.
Jinsi nafsi ya utatu wa Mungu ni tofauti na ya kipekee, hata
hivyo Mungu mmoja, hivyo hivyo roho wetu, na mwili
hujumlisha mtu aliyeumbwa na Mungu.
Mtume Paulo alitaja juu ya nafsi tatu zetu alipoandika,
1 Wathesalonike 5:23 Mungu mwenyewe, Mungu wa amani,
awatakase ninyi kabisa, roho zenu, nafsi zenu na miili yenu,
nanyi mhifadhiwe kikamilifu bila kuwa na lawama katika Bwana
wetu Yesu Kristo.
Tunatakiwa kuwa na ufunuo kuhusu roho zetu zilizoumbwa,
na kupitia ufunuo huo, Mungu atarejesha roho zetu na mili
tena katika ile hali iliyokusudiwa iwe. Kwa kufanya hivyo,
tutakuwa “tumetakasika kabisa” na “kuhifadhiwa bila dosari
kwa kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo.”
Na Uhai wa Mungu
Tunatambua kuwa Mungu, kwa mikono Yake, aliumba
Adamu kwa mfano Wake na akamvuvia pumzi Yake ya
uhai.
Mwanzo 2:7 Bwana Mungu alimwumba mtu kutoka mavumbi ya
ardhi akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, mtu akawa
kiumbe hai.
Uhai wa Mungu ni zaidi ya hali ya kuwa hai. Ni chanzo cha
uhai wote.
Maisha ya Zoe
Kuna maneno mawili ya Kigiriki ya muhimu yatumikayo
badala ya “uhai” katika Agano Jipya. “Psuche” ina
maanisha asili au uhai wa mwanadamu. “Zoe” ina maanisha
uhai na hali ya Mungu Mwenyewe. Ni uhai wa Zoe, uhai na
hali ya Mungu, ambayo imewekwa ndani ya kila mwamini
aliyezaliwa upya.
Hii inafurahisha aje – sisi tu hai na uhai na hali ya Mungu!
Adamu na Eva walipotenda dhambi, walipoteza uhai wa
Zoe lakini tunapozaliwa upya, roho zetu hufanyika hai na
uhai wa Mungu.
Ni uhai wa Mungu tu ndio una nguvu za kuumba. Katika
kumuumba mwanadamu, mavumbi yalifanyika hai kwa
sababu uhai wa Mungu ulivuviwa ndani yake.
10
Yohana 1:3,4 Vitu vyote viliumbwa kwa Yeye, wala pasipo Yeye
hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa. Ndani
Yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya
watu.
Na Nuru ya Mungu
Uhai wa Mungu ni nuru; na nuru hii, au utukufu ung’aao,
ulifanyika nuru ya Adamu na Eva kabla hawajatenda
dhambi.
1 Yohana 1:5 Huu ndio ujumbe tuliosikia kutoka kwake na
kuwatangazia ninyi, kwamba Mungu ni nuru na ndani yake
hamna giza lolote.
Inawezekana baada ya kuanguka, Adamu na Eva walivikwa
na nuru hii kutoka kwa Mungu – utukufu Wake unaong’aa.
Na Ukamilifu wa Mungu
Tunajua mili ya Adamu na Eva ilikuwa na afya
iliyokamilika, mamlaka na nguvu kwani hii ni sehemu ya
uhai wa Mungu.
Uhai na pumzi ya Mungu ilikuwa ndani ya damu kila
sehemu yao, huku ikiwaacha na afya kamili na uzima wa
milele. Adamu na Eva waliumbwa kuishi milele.
Hawangekufa ikiwa wangeendelea kuwa na uhai wa Mungu
ndani yao.
Roho (akili na, hisia) ya Adamu na Eva ilikuwa ya Mungu
katika asili yake. Roho zao zilikuwa na uhai wa Mungu
ndani yao, na akili yao, hisia hiari ilikuwa moja na Mungu.
Roho zao zilikuwa kamilifu – moja na Mungu.
Kupewa Utawala
Kitu cha kwanza Mungu alisema kuhusu Adamu na Eva
baada ya kuwaumba kilikuwa “basi na wawe na utawala!”
Mwanzo 1:26 Ndipo Mungu akasema, “Tufanye mtu kwa mfano
wetu, kwa sura yetu, wakatawale juu ya samaki wa baharini na
ndege wa angani, juu ya mifugo, juu ya dunia yote, na juu ya
viumbe wote watambaao juu ya nchi.”
Mungu aliwapa Adamu na Eva mamlaka na utawala juu ya
dunia. Mungu alibakisha mamlaka na utawala juu ya
ulimwengu wote isipokuwa ardhi. Hapa, alitoa mamlaka
haya kwa kiumbe kipya ambaye aliumba kwa mfano Wake.
Na Uwezo wa Kuumba
Kama vile uwezo wake Mungu uliumba dunia, Adamu na
Eva walipewa uwezo kufikiria, kuamini na kuumba.
Kwa sabau dhamira yao ilikuwa sawa na Mungu, hapakuwa
na hatari ya utumishi mbaya wa hali ya uhai wa uumbaji wa
Mungu ndani yao kwa nia iliyo kinyume. Viumbe vyote vya
11
Mungu duniani vilikuwa kamilifu na bora na walishauriwa
kuzidisha kile ambacho tayari kiliiumbwa kamilifu.
Mwanzo 1:28 Mungu akawabariki na akawaambia, “Zaeni
na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia na kuitiisha. Mkatawale
samaki wa baharini, ndege wa angani na kila kiumbe hai
kiendacho juu ya ardhi.”
Kuwa na Ushirika na Mungu
Mungu alipowaumba Adamu na Eva, walikuwa na ushirika
uliokamilika pamoja naye. Aliongea nao ana kwa ana.
Wangeweza kumwendea Mungu kwa ujasiri. Hawakuwa na
hisia za kuhukumika, lawama, au kuzushwa hadhi.
Walikuwa na uhusiano kamili na Mungu.
Mungu alionyesha kuridhika kwake na Adamu alipowaleta
wanyama kwake ili awape majina.
Mwanzo 2:19 Basi Bwana Mungu alikuwa amefanyiza kutoka
katika ardhi wanyama wote wa porini na ndege wote wa angani.
Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lolote
alilokiita kila kiumbe hai, likawa ndilo jina lake.
Uhuru wa Kuchagua
Mungu pia aliwapa Adamu na Eva uchaguzi – uhuru wa
hiari wa kuchagua. Hakuumbwa kama mashini mfano wa
mtu bila uwezo wa kuchagua kuwa na au dhidi ya Mungu.
Walikuwa na uamuzi wa kutii au kutomtii Mungu.
Uamuzi huu ulitokana na agizo la Mungu kuhusu mti
mmoja katika bustani ya Edeni, mti wa kujua mema na
mabaya. Mungu alisema kuwa ikiwa watakula kwa mti huo,
kwa hakika wangekufa.
Mwanzo 2:16,17 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu
akamwambia, “Uko huru kula matunda ya mti wowote katika
bustani, lakini kamwe usile matunda ya mti wa ujuzi wa mema
na mabaya,kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika
utakufa.”
KUINGIA KWA DHAMBI – MWANADAMU KUPOTEA
Maandiko yanaonyesha kuwa Adamu na Eva walichagua
kutomtii Mungu. Hii ilikuwa dhambi.
Mwanzo 3:6 Mwanamke alipoona ya kuwa tunda la mti huo
lilikuwa zuri kwa chakula na la kupendeza macho, tena
linatamanika kwa kujipatia hekima, basi akachuma katika
matunda yake, akala, pia akampa mumewe, aliyekuwa pamoja
naye, naye akala.
Kupitia kwa dhambi, wanadamu wote walipata mateso sana.
12
Ushirika Kupotea
Mungu katika utakatifu na haki Zake hangeshirikiana na
Adamu na Eva. Dhambi yao ilikuwa kizuizi kati yao na
Mungu. Hukumu na kuangamia kwao kuliwafanya wajifiche
kwa Mungu.
Mwanzo 3:8 Ndipo yule mwanamume na mkewe, waliposikia
sauti ya Bwana Mungu alipokuwa akitembea bustanini wakati
wa utulivu wa jioni, wakajificha kutoka mbele za Bwana Mungu
katikati ya miti ya bustani.
Walipoteza vitu vyao vya dhamana, uhusiano na ushirika
wao uliokamilika na Mungu.
Kupotea kwa Uhai wa Mungu
Wakati Adamu na Eva walikula tunda walilokatazwa,
walikufa kiroho. Hawakuwa na uhai wa Mungu ndani yao.
Warumi 5:12 Kwa hiyo kama vile dhambi ilivyoingia ulimwenguni
kupitia kwa mtu mmoja na kupitia dhambi hii, mauti ikawafikia
watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi.
Nafsi zao zilikufa kiroho. Roho zao hazikufanya kazi.
Pumzi ya roho wa Mungu, ambayo Mungu aliivuvia ndani
ya Adamu, haikuwepo tena.
Kupotea kwa Utukufu wa Mungu
Utukufu wa Mungu ambao ulikuwa umewafunika Adamu
na Eva ghafla ulitoweka.
Warumi 3:23 Kwa kuwa wote wametenda dhambi na
kupungukiwa na utukufu wa Mungu...
Ghafla wakagundua kuwa walikuwa uchi.
Mwanzo 3:7a Ndipo macho yao wote wawili yakafumbuliwa,
wakajiona kwamba walikuwa uchi.
Kupotea kwa Ufahamu wa Kiroho
Adamu na Eva walipokufa kiroho, roho zao hazikuwa hai
tena kwa Mungu. Fikira zao hazikuwa sawa na Mungu tena.
Ufahamu wao ukatoka kwa roho yao, ambayo sasa ilikuwa
imekufa, kwa hiyo wakategemea mili yao ya asili.
Wakaanza kutumia hali yao ya asili kupitia hisia tano za
mwili. Mambo ya kawaida na kweli yakawa ya kuona, sikia,
nusa, onja, au gusa.
Kupoteza Afya Iliyokamilika
Mili ya Adamu na Eva haikuwa na uhai wa Mungu tena.
Sasa wangekuwa na magonjwa, maradhi na kuugua.
Walipotenda dhambi walianza kuzeeka na kufa kimwili.
13
Kupoteza Mamlaka
Adamu na Eva walipoteza mamlaka na utawala juu ya
dunia. Walimpa Shetani. Sasa waliishi katika ufalme wake,
bila tumaini wakiwa chini ya yule alikuja “kuiba, kuua, na
kuharibu.”
Kufanywa Kutokubadilishwa
Mawazo yasiyobadilishwa, na akili ya mwamini ni mawazo
yasiyobadilishwa upya na Neno la Mungu, yaliyo na fikira
za kiovu.
Mithali 6:16,17,18 Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana, naam,
viko saba vilivyochukizo kwake: Macho ya kiburi, ulimi
udanganyao, mikono imwagayo damu isiyo na hatia, moyo ule
uwazao mipango miovu, miguu ile iliyo myepesi kukimbilia uovu
……
Wamejaa vitu ambavyo Mungu anachukia.
Kiburi
Ulimi danganyifu
Kumwaga damu isiyo na hatia
Kupanga mbinu na hisia za uovu
Kukimbilia mambo ya ujanja
Mtume Paulo pia anaeleza kuhusu mtu asiyemja Mungu,
asiye na haki.
Warumi 1:18-22 Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka
mbinguni dhidi ya uasi wote na uovu wa wanadamu ambao
huipinga kweli kwa uovu wao, kwa maana yote yanayoweza
kujulikana kumhusu Mungu mwenyewe ameliweka wazi kwao.
Kwa maaana tangu kuumbwa kwa ulimwengu, asili ya Mungu
asiyeonekana kwa macho, yaani, uwezo wake wa milele na asili
yake ya Uungu, umeonekana waziwazi ukitambuliwa kutokana
na yale aliyoyafanya ili wanadamu wasiwe na udhuru. Kwa
maana ingawa walimjua Mungu wala hawakumshukuru, bali
fikira zao zimekuwa batili na mioyo yao ya ujinga ikatiwa giza.
Ingawa wakijidai kuwa wenye hekima, wakawa wajinga.
AHADI YA MKOMBOZI
Ahadi ya Kwanza
Adamu na Eva walisimama bustani ya Edeni:
Bila tumaini na waliotolewa uhusiano na ushirika na
Mungu
Bila mamlaka yao
Bila ufahamu, hekima na afya
14
Lakini, Mungu alivyonena na shetani, alimwahidi
mwanadamu kurejeshwa kupitia mkombozi atakayekuwa
mbegu ya mwanamke.
Mwanzo 3:15 Nami nitaweka uadui kati yako na huyo
mwanamke, na kati ya uzao wako na wake, huo atakuponda
kichwa, nawe utamgonga kisigino.
Kupitia kwa Mbegu ya Ibrahimu
Ahadi ya mkombozi ilifanywa upya Mungu aliponena kuwa
mataifa yote duniani yatabarikiwa kupitia Abrahimu.
Mwanzo 18:18 Hakika Abrahamu atakuwa taifa kubwa na lenye
nguvu, kupitia kwake mataifa yote ya dunia yatabarikiwa.
Mungu alitaja tena ahadi hii kwa Isaka na Yakobo. Aliahidi
kuwa mataifa yote duniani yatabarikiwa kupitia mbegu yao.
Kulikuwa na Mkombozi anayekuja!
Kupitia kwa Mbegu ya Daudi
Mungu pia alitoa ahadi ya agano na Daudi kuhusu mbegu.
Hii pia ilikuwa katika Mkombozi atakayokuja, Yesu Kristo.
Zaburi 89:34-36a Mimi sitavunja agano langu wala sitabadili lile
ambalo midomo yangu imetamka. Mara moja na kwa milele,
nimeapa kwa utakatifu wangu, nami sitamdanganya Daudi,
kwamba uzao wake utaendelea milele.
Kutabiriwa na Isaya
Isaya alitabiri kuja kwa Mkombozi.
Isaya 9:6,7a Kwa maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
tumepewa mtoto mwanamume, nao utawala utakuwa mabegani
mwake. Naye ataitwa: Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye
Nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa Amani. Kuongezeka kwa
utawala wake na amani hakutakuwa na mwisho. Atatawala
katika kiti cha enzi cha Daudi na juu ya ufalme wake
akiuthibitisha na kuutegemeza kwa haki na kwa adili, tangu
wakati huo na hata milele.
Kwa Niaba Yetu
Dhambi na mauti ilikuwa matokeo ya kuasi kwa Adamu na
Eva. Ni kupitia kwa kuja kwa Adamu wa mwisho tu kwa
niaba yetu, ndipo tunaweza kuwekwa huru kwa gharama
hizi. Isaya 53 inatoa picha ya kuja kwa Mkombozi.
Isaya 53:4,5 Hakika alichukua udhaifu wetu na akajitwika huzuni
zetu, hata hivyo tulifikiri amepigwa na Mungu, amepigwa sana
naye na kuteswa. Lakini alitobolewa kwa ajili ya makosa yetu,
alichubuliwa kwa maovu yetu, adhabu iliyotuletea sisi amani
ilikuwa juu yake, na kwa majeraha yake sisi tumepona.
Kupitia kazi ya ukombozi ya Masiha aliyekuja, vyote
ambavyo Adamu na Eva walipoteza walipoanguka
15
vingerejeshwa. Kwa mara tena wanadamu wangefanyika
viumbe waliotarajiwa kuwa. Kuumbwa upya kutarejeshwa!
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Kwa nini Adamu na Eva walikuwa na tabia ya Mungu walipoumbwa?
2. Je, Adamu na Eva walikuwea na nini ndani yao iliyowafanya kuwa tofauti na wanyama
wengine walioumbwa na Mungu?
3. Orodhesha baadhi ya vitu ambavyo mwanadamu alipoteza alipoanguka ambavyo vitarejeshwa
katika kuumbwa upya.
16
Somo la Pili
Mfano wetu wa Baba
Utangulizi
Ili kuelewa mfano wetu wa kuumbwa upya, ni sharti tuwe
na ufunuo kuhusu Mungu ni nani. Kwa sababu tumeumbwa
kwa mfano Wake, hatuwezi kuelewa tuliumbwa ili kuwa
vipi mpaka tuwe na picha ya Baba.
Mtume Paulo aliandika, jinsi tunao utukufu wa Bwana,
tutabadilishwa katika mfano huo huo. Ufunuo huleta
mabadiliko.
2 Wakorintho 3:18 Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji
tunaakisi utukufu wa Bwana, kama kwenye kioo. Nasi
tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu
mkuu zaidi, utokao kwa Bwana, ambaye ndiye Roho.
Katika somo hili, tutaona utukufu wa Baba. Tutapinga picha
na sura ambazo huenda tumejiwekea kuhusu Baba.
Tutamruhusu Roho Mtakatifu, kwa ufunuo wa Neno la
Mungu, kudhihirisha picha ya kweli ya Baba wetu wa
mbinguni.
Njia Tatu za Utendaji wa Roho
Yesu na Watu
Katika njia ya Yesu na watu, wengi walipokea ufunuo mpya
na walipata uhusiano wa karibu na ushirika na Yesu binafsi.
Msisimuo wa Kufanywa Upya
Katika Msisimuo wa Kufanywa upya, wengi walipata
uhusiano wa karibu na pia ushirika na Roho Mtakatifu
binafsi.
Jinsi watu walivyoelekezwa na Roho Mtakatifu, waliweka
kando mambo ya tenzi na kupata furaha ya Kibiblia ya
kuingia katika sifa kwa Yesu.
Daudi anatueleza haya alipoandika,
Zaburi 100:4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na katika
nyua zake kwa kusifu, mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.
Kumfahamu Baba
Katika mbinu hii mpya ya utendaji wa Mungu kabla ya
kurudi tena kwa Yesu, tutaingia katika uhusiano na ushirika
wa karibu na Baba. Tutafanyika watu wake
wanaomwabudu.
Tukiwa tukiimba, tukiinua mikono yetu, kupiga makofi,
kuruka na kucheza mbele za Bwana. Lakini, sasa kuna
mapendekezo ya kuingia katika uwepo wa Baba ndani ya
Utakatifu wa watakatifu – kuingia ndani ya pazia.
17
Sio tu kuwa tumetosheka kubaki nje kwenye ukumbi, bali
tunatazama kwenye uso wa Baba, kuhisi mikono Yake ya
upendo kwetu, na kuwa karibu Naye katika kuabudu.
Yohana 4:23 Lakini saa yaja, tene ipo, ambapo wale waabuduo
halisi,watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu
wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta.
Baba anawatafuta waabudio wa kweli watakaokuwa na
muda kuabudu katika roho na kweli, watakaoingia mahali
pa Utakatifu wa watakatifu.
BABA WETU HAPA DUNIANI
Sura yetu ya Baba wa mbinguni mara nyingi huonyeshwa
na vitendo vya baba wa hapa duniani. Uhusiano wetu na
baba wetu wa hapa duniani hugusia uhusiano wetu na Baba
wa mbinguni.
Shughuli nyingi
Baba wengi walikuwa na shughuli nyingi kupata muda na
wana wao wanapokua. Hii huenda ni kwa sababu nyingi,
lakini hii imewaacha wengi na hisia kuwa “Mungu ana
shughuli nyingi kando nami.”
Mwenye Kutoa Adhabu kali
Baba wengine wamewapa watoto wao adhabu kali kupitia
nidhamu bila upendo. Watoto hawa mara nyingi wanajihisi
kuwa Baba yao wa mbinguni huwaangalia na adhabu kali,
ni kama anayo fimbo mkononi Mwake akisubiri mtu avuke
ya msitari.
Asiye na upendo
Wengi wamekua katika nyumba ambapo upendo ni haba
mno na pia kusikilizwa na baba yao. Hata kama walijaribu
sana, inaonekana hawakupata pongezi na shukrani kutoka
kwa baba yao.
Kwa haya, sura ya Baba yao wa mbinguni ni moja ya
kutoyakubali na kupuuza maitaji yao. Wanajihisi kuwa
Mungu hawajali kuhusu mafanikio yao na kuwa Yeye kwa
kweli hawapendi.
Umaskini
Wengine walitoka katika jamii ambapo baba zao aidha
hawangeweza, au hawakuta, kukutana na kutosheleza
maitaji ya kijamii katika maisha ya kawaida. Walikua katika
maisha ya umaskini.
Watu hawa mara nyingi wanakuwa na “picha ya umaskini”
ya Mungu. Wanakuwa na tatizo kuona kwamba Mungu
atakutana na maitaji yao maishani.
18
Kunyanyazwa
Watoto wengi wameteswa na baba zao wa duniani. Wengine
wameteswa kihisia, wengine kimwili, na wengine pia
wameteswa kijinsia.
Haya yamewazuia kummwamini kabisa Baba wa mbinguni
au kupokea upendo Wake mkuu. Wajihisi kuhukumika
mbele za Mungu au hukasirika naye, na wanashindwa
kumtegemea maishani kabisa.
BABA WETU WA MBINGUNI
Upendo
Mbali na kuteswa, kukataliwa, au kudhulumiwa tulizopata
kutoka kwa wazazi wetu wa duniani, ni sharti tuwasamehe,
na kupokea uponyaji kutoka kwa Mungu ili tutambue,
kupokea, na kufurahia upendo wa ajabu wa Baba wetu wa
mbinguni.
1 John 3:1a Behold what manner of love the Father has
bestowed on us, that we should be called children of God!
Mtume Paulo aliandika kuwa hakuna kitakachotutenga na
upendo wa Baba.
Warumi 8:38,39 Lakini katika mambo haya yote tunashinda,
naam na zaidi ya kushinda, kwa Yeye aliyetupenda. Kwa maana
nimekwisha kujua kwa hakika ya kuwa wala mauti, wala uzima,
wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo wala
yatakayokuja, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo
chini, wala kiumbe kingine chochote hakitaweza kututenga na
upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Baba anayo furaha kwa ajili Yetu
Badala ya baba asiyejali na mkali, tunaye Baba wa
mbinguni anayetupenda sana mpaka ana furaha kwetu na
pia akiimba.
Nabii Zefania anaeleza kuhusu Mungu kwa njia hii:
Sefania 3:17 Bwana Mungu wako yu pamoja nawe, yeye ni
mwenye nguvu kuokoa. Atakufurahia kwa furaha kubwa,
atakutuliza kwa pendo lake, atakufurahia kwa kuimba.
Neno la Kiebrania la Zefania lililotumika kufurahi lina
maana ya msingi “kuimba” au ‘kuruka kwa furaha” Mungu
ana furaha tele kwetu kama wanawe, Yeye huruka juu na
chini na kucheza katika njia ya kuonyesha furaha kuu.
Je, ni sura tofauti iliyoje ya Baba! Mungu hana shughuli
nyingi hata atusahau. Yeye hakasiriki, mwenye nidhamu
bila upendo. Yeye hataki kutuadhibu. Yeye anayo furaha
juu yetu. Anaruka kwa furaha kwa ajili yetu!
19
Mioyo Hugeuka kwa Baba
Leo, kama vile katika Agano la Kale, Mungu anawatumia
manabii kugeuza mioyo ya watoto kwa baba zao.
Malaki 4:5,6a “Tazama, nitawapelekea nabii Elia kabla ya kuja
siku ile iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana. Ataigeuza mioyo ya
baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba
zao.
Mungu anageuza mioyo ya watoto, waume kwa wake, kwa
baba zao wa duniani na mioyo ya Watoto wa Mungu kwa
Baba wao wa mbunguni.
VIZUIZI VITATU KATIKA USHIRIKA
Dhambi
Adamu na Eva walikuwa na ushirika bora na Mungu hadi
wakati walipotenda dhambi. Mungu mtakatifu na mwenye
haki hangekuwa na ushirika pamoja na dhambi.
Wakati wa wokovu, dhambi zetu husamehewa na
kuondolewa. Uhusiano wetu, na ushirika wetu na Mungu
huanza. Tunapotenda dhambi, hata kama uhusiano wetu na
Mungu huendelea, ushirika wetu Naye huvunjika. Ushirika
huu unaweza tu kurejeshwa tunapokiri dhambi zetu Kwake.
1 Yohana 1:9 Kama tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni
mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha
toka kwenye udhalimu wote.
Kukataliwa
Wengi hukataliwa na baba zao wa duniani. Labda walikuwa
matokeo ya uzazi au mimba isiyopangiwa. Labda baba
alitaka sana mtoto wa jinsia ya kinyume, au kama mtoto,
hawakufikia kiwango cha matakwa ya baba yao.
Mtu awe aliteswa katika kukataliwa au hisia za kukataliwa,
yeye huwa na mawazo tele na kusononeka maishani mwake.
Watu hawa hujihisi kuwa hata Baba yao wa mbinguni pia
huwakataa. Wanakuwa na ugumu kukubali upendo Wake na
kukubalika. Kuna kitu ambacho huwazuia wasifikie
uhusiano wa binafsi na wa karibu na Baba wao wa
mbinguni na kufanyika waabudio Wake wa kweli.
Mtu aliye na hisia za kukataliwa maishani mwake ni lazima
awasamehe waliomkataa na kisha kupokea uponyaji wa
Mungu rohoni mwake.
Hofu
Hofu ya kufika mbele ya Baba imewazuia wengi
kutokufanyika waabudio wa kweli Kwake. Lakini, badala
ya hofu, Mungu ameweka kwetu Roho wa kufanyika Wake
ambapo tunaweza kuja kwake na kumwita Abba.
20
Warumi 8:15 Kwa maana hamkupokea roho ya utumwa
iwaleteayo tena hofu, bali mlipokea roho ya kufanywa wana,
ambaye kwa yeye twalia “Abba,” yaani, Baba.”
“Abba” ni kueleza kupendwa na, uhusiano wa karibu wa
binafsi na Baba. Inaweza kutafsiri “Baba”
2 Wakorintho 6:18 “Mimi nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa
wanangu na binti zangu, asema Bwana mwenyezi.”
Ni kwa upendo mkuu wa Baba ndipo alituchukuwa kuwa
watoto Wake.
1 Yohana 3:1a Oneni ni pendo kuu namna gani alilotupa Baba,
kwamba sisi tuitwe watoto wa Mungu!
Kuelewa juu ya upendo mkuu wake Mungu huondoa hofu
yetu.
Daudi, Mfano Wetu
Daudi alikuwa mtu aliyekuwa akitafuta roho ya Mungu.
Alitafuta kuwa wa karibu sana na Baba yake wa mbinguni
katika kuabudu.
Zaburi 27:4 Jambo moja ninamwomba Bwana hili ndilo
ninalitafuta: niweze kukaa nyumbani mwa Bwana siku zote za
maisha yangu, niutazame uzuri wa Bwana na kumtafuta hekaluni
mwake.
Daudi alitafuta kukaa katika uwepo wa Mungu kila siku
maishani mwake. Alitafuta kuingia katika uwepo wa Baba,
na kutazama urembo wake.
Alitoa Sifa na Kuabudu
Zaburi 27:6b Nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe,
nitamwimbia Bwana na kumsifu.
Daudi alijuwa jinsi ya kuimba sifa na kucheza mbele za
Bwana akiwa “bustanini”. Lakini, alitaka zaidi. Alitaka
kuingia katika uwepo wa Baba na kutafuta uso Wake.
Zaburi 27:8 Moyo wangu unasema kuhusu wewe, “Utafute uso
wake!” Uso wako, Bwana “Nitautafuta.”
Alikuwa na Hofu ya Kukataliwa na Mungu
Hata kama Daudi alitaka kumwabudu Baba, alipoingia
katika uwepo wake Baba katika kuabudu, ghafla alirudi
nyuma kwa hofu ya kukataliwa.
Zaburi 27:9 Usinifiche uso wako, usimkatae mtumishi wako kwa
hasira, wewe umekuwa msaada wangu. Usinikatae wala
usiniache, Ee Mungu Mwokozi wangu.
21
Kukataliwa na Baba wa Duniani
Daudi aliteswa kwa kukataliwa na baba yake wa duniani
akiwa kijana, na sasa hiyo hofu ya kukataliwa ilimuzuia
kuingia mbele ya Baba wa mbinguni bila hofu.
Daudi alipokuwa kijana, nabii Samueli alikuja Bethlehemu
kumpaka mafuta mfalme atakayefuata. Babake Daudi
aliwakusanya watoto wake wote pamoja kwa matumaini
kuwa mmoja wao atatiwa mafuta kama mfalme. Daudi
hakualikwa mbele za Samueli siku hiyo.
Huu ungekuwa wakati ambapo Daudi angejisikia
kukataliwa na babake wa dubiani. Hii iliweka hofu ndani ya
Daudi kuwa atakataliwa na Babake wa mbinguni.
Ingawa alitaka sana kuja mbele za Baba yake wa mbinguni,
kuutafuta uso wake, na kuuona urembo wake, wakati
alianza kuingia katika kuabudu, hofu ya kukataliwa iliishika
roho yake.
Kupata Uhuru Kutokana na Kukataliwa
Daudi aligundua kuwa alikataliwa na baba yake na mama
yake. Aliielewa shida, na kisha akafanya uamuzi dhidi ya
hisia za kukataliwa.
Zaburi 27:10 Hata kama baba yangu na mama wataniacha,
Bwana atanipokea.
Wakati huo, Daudi alitembea kwa ujasiri katika uwepo wa
Mungu. Aliutazama uso Wake na kuhisi upendo na
kukubalika na Baba rohoni mwake
YESU ANAMDHIHIRISHA BABA YAKE
Mojawapo ya kusudi la Yesu hapa duniani ilikuwa
kumdhihirisha Baba Yake. Wakati huduma ya Yesu hapa
duniani ilikaribia kukamilika, punde tu kabla ya Yeye
kushikwa, kujaribiwa na kusulubiwa, Yesu alimtaja Baba
Yake mara hamsini katika Injili kama alivyoandika Yohana,
sura kumi na nne hadi kumi na saba.
Alisema kwa kurudia rudia kwa wanafunzi Wake, “Nataka
mumfahamu Baba yangu!”
“Nifahamu Mimi – Mfahamu Baba Yangu”
Tukimfahamu Yesu, tutamfahamu Baba. Kadri tunapotumia
muda kumjua Yesu kupitia Injili, ndipo tutamjua Baba zaidi.
Yohana 14:7 Kama mngenijua Mimi, mngemjua na Baba pia.
Tangu sasa mnamjua Baba yangu tena mmemwona.
Katika Injili, tunaona upendo na huruma ya Yesu
alipoendelea kuwafikia na kuwagusa watu, kukutana na
22
mahitaji yao, kuponya miili yao na kurejesha mioyo yao.
Hii ilikuwa kielelezo cha upendo wa Baba.
Yohana 14:9b Mtu yeyote aliyeniona Mimi, amemwona Baba.
Upendo Wa Baba
Yesu alipowachukua watoto na kuwashika mikononi,
alionyesha upendo wa Baba kwa watoto Wake.
Mathayo 19:14 Yesu akasema, “Waacheni watoto wadogo waje
kwangu, wala msiwazuie, kwa maana ufalme wa Mbinguni ni wa
wale waliokama hawa.”
Je, ni picha ya ajabu iliyoje ya kuonyesha jinsi Baba
angependa kutuvuta ili tuwe karibu Naye na kuweka
mikono yake kwetu.
Yesu alipowahudumia wale waliokuwa karibu Naye,
alidhihirisha upendo wa Baba Yake.
Yohana 14:23 Yesu akamjibu, “Mtu yeyote akinipenda atalishika
Neno Langu na Baba yangu atampenda, Nasi tutakuja kwake na
kufanya makao Yetu kwake.”
Je, ni ufunuo wa ajabu ulioje. Sema kwa sauti.
Baba yangu wa mbinguni ananipenda!
Anataka aje na Yesu na aishi pamoja nami!
Baba yangu anataka kujenga nyumba Yake pamoja
nami!
Kutoa Kwa Baba
Yesu alisema kuwa tunaweza kumwuliza Baba yetu msaada.
Yohana 16:23b Amin, amin, nawaambia, kama mkimwomba Baba
jambo lolote kwa jina langu, Yeye atawapa.
Hatuulizi katika jina la Yesu kwa sababu Baba anampenda
Yesu na atamfanyia mambo. Tunauliza katika jina la Yesu
kwa sababu kupitia kwa dhabihu ya Yesu ndipo uhusiano
wetu na Baba unarejeshwa.
Nyumba ya Baba
Yesu alituambia kuhusu nyumba ya Baba Yake. Alisema
kuwa ataenda na kutuandalia mahali katika nyumba ya Baba
Yake.
Yohana 14:2 Nyumbani kwa Baba yangu kuna makao, mengi.
Kama sivyo, ningeliwaambia. Nakwenda kuwaandalia makao.
Hapo baadaye, tunatakiwa kuishi katika Nyumba ya Baba.
Hapa ndipo jamii huishi. Tunatakiwa kuwa na uhusiano wa
karibu na Baba wa mbinguni.
“Nitawambia kwa Uwazi”
Yesu anataka kutuambia wazi kuhusu Baba Yake.
23
Yohana 16:25 Nimewaambia mambo haya kwa mafumbo. Saa
yaja ambapo sitazungumza nanyi tena kwa mafumbo bali
nitawaeleza waziwazi kuhusu Baba.
Hapa ni baadhi tu ya mara zile hamsini Yesu alitaja kuhusu
Baba Yake katika sura hizi nne. Yesu alionyesha hamu kuu
kuwa kila mmoja wetu atafika katika uhusiano wa karibu na
Baba Yake.
MWANA MPOTEVU
Mara nyingi mfano wa Mwana Mpotevu hutumika katika
jumbe za kiinjilisti kama mwito wa toba au kurejeshwa
katika ushirika. Tumeelewa kuwa tunaweza kuja kwa Baba
hata kama tumezushwa na kuzama katika hali yoyote.
Katika kuasi, mwana mpotevu alitoka nyumbani na
kuharibu urithi wake wote katika maisha yasiyokubalika.
Kisha ukame mkuu ukaja, akawa akiwalisha nguruwe na
kula makanda waliyokula.
Mwana
Wengi wetu tunakubaliana na mwana. Tumejihisi, au
tunaweza kuhisi, kutengwa na Baba wa mbinguni, hofu ya
kukataliwa, au hisia za kutokuwa wa maana, kutokuwa na
msamaha na kuhukumika.
Luka 15:17-20a “Lakini alipozingatia moyoni mwake, akasema,
“Ni watumishi wangapi walioajiriwa na baba yangu ambao wana
chakula cha kutosha na kusaza, bali mimi hapa nakufa kwa njaa!
Nitaondoka na kurudi kwa baba yangu na kumwambia, “Baba,
nimetenda dhambi mbele za Mungu na mbele yako. Sistahili tena
kuitwa mwanao, nifanye kama mmoja wa watumishi wako.”
Alisema, “Mimi sistahili tena.” Kijana huyu, kama vile
waamini wengi leo, alijisikia hastahili. Aliona sura yake
haifai. Na hata kama alikuwa na sura hiyo, alirudi
nyumbani.
Baba
Mfano huu ni ufunuo wa ajabu kuhusu Baba yetu wa
mbinguni.
Mungu hapendelei.
Yeye si mkali
Yeye hangojei watoto wake waume kwa wake
wamlilie kwa msamaha.
Je, Yesu alisema nini?
Luka 15:20b “Lakini alipokuwa bado yuko mbali, baba yake
akamwona, moyo wake ukajawa na huruma. Akamkimbilia
mwanawe, akamkumbatia na kumbusu.
Badala ya Baba yetu kugeuza uso wake mbali nasi kwa
kukataliwa, Yeye anatusubiri tuje kwake. Anataka kuweka
24
mikono yake kwetu na kutubusu kama ishara ya upendo
Wake mkuu na wa ajabu.
Ms. 21 “Yule mtoto akamwambia baba yake, “Baba, nimekosa
mbele za Mungu na mbele yako. Sistahili kuitwa mwanao tena.”
Baba hata hakujadili kile mwanawe alikuwa amefanya, au
kile alikuwa akisema.
Ms. 22-24 “Lakini baba yake akawaambia watumishi, “Leteni
upesi joho lililo bora sana, mkamvike pete kidoleni mwake na
viatu miguuni mwake. Leteni ndama aliyenona, mkamchinje ili
tuwe na karamu, tule na kufurahi. Kwa maana huyu mwanangu
alikuwa amekufa na sasa yu hai tena, alikuwa amepotea na sasa
amepatikana!” Nao wakaanza kufanya tafrija.
Sura ya Mwana
Baba alijua kuwa ilimbidi aibadili sura ya mwanawe.
Alimvalisha vazi nzuri. Aliiweka pete kwenye kidole na
vyatu vipya miguuni mwake.
Punde tunapompokea Yesu kama mwokozi, Baba yetu wa
mbinguni anatuona kama wanawe waume kwa wake.
Tumevalishwa mavazi Yake ya haki. Tunayo pete ya
mamlaka kwenye vodole vyetu.
Katika upendo, anasema, “jinsi napenda wafahamu wao ni
nani ndani ya Yesu Kristo. Wao ni wamoja na Mwana
wangu! Wao ni haki wa Mungu katika Yesu Kristo.”
Mtume Paulo aliandika haya.
2 Wakorintho 5:21 Kwa maana Mungu alimfanya yeye
asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate
kufanywa haki ya Mungu katika Yeye.
Mfano Wetu wa Kuumbwa Upya
Tunapomruhusu Yesu kudhihirisha Baba yake kwetu, sura
na mifano mibaya tuliyo nayo kuhusu Baba wetu wa
mbinguni itabadilika.
Tutakuwa, kama Daudi, tuuone urembo wa Bwana.
Tutautafuta uso Wake. Tutamwabudu Yeye. Tutahisi
kukubalika kwake. Tunapouona utukufu Wake Bwana, sura
yetu ya Baba itabadilika, na pia sura yetu ya binafsi ya
awali itabadilishwa na kuwa mfano wa kuumbwa upya.
Wengi wamekuwa wakitafuta mkono wa Mungu badala ya
uso Wake. Wametumia muda wao kuja kwa Bwana
wayatosheleze mahitaji yao.
25
Kubadilishwa
Kwa Kumtafuta Baba
Badala yake ni sharti tuje mbele za Mungu na kutumia
muda kuutafuta uso Wake na kuuona utukufu Wake. Kisha,
tutabadilishwa katika mfano wake.
2 Wakorintho 3:18 Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji
tunaakisi utukufu wa Bwana, kama kwenye kioo. Nasi
tutabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu
mkuu zaidi, utokao kwa Bwana, ambaye ndiye Roho.
Mwandishi wa Zaburi Daudi alieleza kama vile mtume
Paulo.
Zaburi 17:15 Na mimi katika haki nitauona uso wako, niamkapo,
nitaridhika kwa kuona sura yako.
Kwa Kumwabudu Baba
Hatubadilishwi kwa mfano wake tunapojitazama na
kutarajia mabadiliko yafanyike maishani mwetu.
Tunabadilishwa kwa mfano wake tunapotumia muda na
Baba yetu katika upendo wa karibu na kumwabudu Yeye
jinsi alivyo.
Tunapoendelea kutumia muda kuutafuta uso wa Mungu,
basi “tunaamka” tukiwa na nyuso zetu ziking’aa na utukufu
wa Mungu. Sisi, kama Musa alishuka baada ya kuutumia
muda wake na Mungu mlimani Sinai, tutang’aa katika
utukufu wa Mungu.
Luka aliandika,
Luka 11:36 Basi ikiwa mwili wako wote umejaa nuru, bila
sehemu yake yoyote kuwa gizani, basi utakuwa na nuru kama
vile taa ikuangazavyo kwa nuru yake.”
Basi, tutakuwa kile ambacho wanadamu waliumbwa wawe
Mungu aliposema, “Hebu na tuumbe mwanadamu kwa
mfano wetu.”
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Je, ni kwa njia gani mfano wetu wa Baba wetu wa mbinguni hubadilishwa na maisha yetu ya
utotoni?
2. Je, mfano wetu wa Baba wa mbinguni unaweza kubadilishwa ili kukubaliana na mfano wa
kweli wa Baba jinsi inavyodhihirishwa katika Neno la Mungu?
3. Kulingana na 2 Corinthians 3:18, je, tunaweza kubadilishwa vipi kwa mfano wa Bwana?
26
Somo la Tatu
Sura Yetu ya Mwana
MWANA WA MUNGU
Ili tuwe na ufunuo kamili kuhusu hali yetu kama viumbe
vipya, ni lazima tuwe na ufunuo kuhusu Mwana wa Mungu.
Mtume Paulo aliandika kuwa Mungu alikusudia, akaandaa
au kututenga ili tubadilishwe katika sura ya Mwana wa
Mungu.
Warumi 8:29a Maana wale Mungu aliowajua tangu mwanzo, pia
aliwachagua tangu mwangu mwanzo, wapate kufanana na mfano
wa Mwanawe.
Tunapobadilishwa kwa sura ya Mwanawe, tutaanza
kutimiza uwezo wetu na kuanza kuishi kama viumbe vipya.
Tunafahamu kuwa Yesu ni mmoja na Baba na Roho
Mtakatifu, na kuwa kila mwenendo walio nao – tunao pia.
Ni Mungu
Mtume Yohana anatuambia mambo manne muhimu kuhusu
Mwana.
Yeye mara yote alikuwepo.
Yeye ni Neno la Mungu aishiye.
Yeye ni muumba wa vitu vyote.
Yeye alifanyika Mwili na akakaa nasi.
Yohana 1:1-3,14 Hapo mwanzo, alikuwako Neno. Huyo Neno
alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Tangu
mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu. Vitu vyote
viliumbwa kwa Yeye, wala pasipo Yeye hakuna chochote
kilichoumbwa ambacho kimeumbwa.
Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu.
Aliwaumba Adamu na Eva
Yohana aliweka wazi kuwa vitu vyote vilumbwa na Mwana
wa Mungu. Adamu na Eva waliumbwa Naye.
Mwanzo 1:27 Kwa hiyo Mungu alimwumba mtu kwa mfano wake
mwenyewe, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanaume na
mwanamke aliwaumba.
Mwanadamu aliyekombolewa ni sharti aumbwe tena, ili
kubadilishwa katika sura ya Mmoja aliyewaumba Adamu na
Eva kwa mfano Wake.
27
MWANA WA ADAMU
Aliziacha haki zake kama Mungu
Yesu alizaliwa kwa bikra hapa duniani kama mwanadamu.
Alikuwa angali Mungu kweli, lakini aliziacha haki zake
kama Mungu na akaja hapa duniani kama mwanadamu.
Alikuwa mwanadamu kweli, lakini hali Yake ya kiungu
haikupotea.
Wafilipi 2:5-8 Tuweni na nia ile ile aliyokuwa nayo Kristo Yesu.
Yeye ingawa alikuwa sawa na Mungu, hakuona kule kuwa sawa
na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho, bali alijifanya si kitu,
akajifanya sawa na mtumwa, akazaliwa katika umbo la
mwanadamu. Naye akiwa na umbo la mwanadamu,
alijinyenyekeza hata mauti, naam, mauti ya msalaba!
Ni muhimu sana kuelewa kuwa Yesu aliziweka kando haki
zake kama Mungu. Alijiweka kama mwanadamu. Yote
aliyofanya Yesu alipoishi na kuhudumu hapa duniani,
alifanya kama mwanadamu, wala sio kama Mungu.
Ufahamu wa Kupotosha
Tukimtazama Yesu alipotembea hapa duniani akitenda
katika nguvu Zake kama Mungu, hatuwezi kuelewa jinsi
tunaweza kubadilishwa katika sura Yake.
“Ndiyo!” tunaweza kusema, “Yesu angeweza kuwaponya
wagonjwa, kukemea mapepo, na kutuliza dhoruba. Hata
hivyo, alikuwa Mwana wa Mungu. Alikuwa mwenye nguvu
zote! Je, haya yanatuhusu vipi?”
Je, Yesu angekuwa mfano au mwongozo katika maisha yetu
ikiwa alitenda kama Mungu? Ikiwa Yesu aliishi na kutenda
katika ulimwengu usio wa kawaida, basi tutasema sisi ni
wanadamu tu.
“Ni tumaini la kipekee tulilo nalo,” tutawaza, “ni kuomba ili
kupata msaada usio wa kawaida kutukomboa kutokana na
mapigo, magonjwa na matatizo ya kifedha.”
Tukichukua sura ya Yesu akitenda hapa duniani – akiziweka
kando haki zake kama Mungu – akija kama mwanadamu
katika mamlaka Mungu alimpa – basi tunaweza kujiona
tukiyatenda mambo yale Yesu alitenda.
Mamlaka Duniani
Yesu alisema,
Yohana 5:24,25 “Amin, amin, ninawaambia, ye yote anayesikia
maneno yangu na kumwamini Yeye aliyenituma, anao uzima wa
milele, naye hatahukumiwa, bali amepita kutoka mautini, na
kuingia uzimani. Amin, amin, nawaambia, saa yaja, nayo saa ipo,
wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, nao
watakaoisikia watakuwa hai.
28
Wale wanaoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, wataishi.
Kisha Yesu akaendelea akisema,
Yohana 5:26, 27 Kama vile Baba alivyo na uzima ndani Yake,
vivyo hivyo amempa Mwana kuwa na na uzima ndani Yake. Naye
amempa Mwanawe mamlaka ya kuhukumu kwa kuwa Yeye ni
Mwana wa Adamu.
Ni wazi kutokana na kifungu hiki kuwa mamlaka Yesu
aliishi na kuhudumu nayo alipokuwa hapa duniani, haikuwa
mamlaka Yake kama Mwana wa Mungu. Yalikuwa
mamlaka Yake kama Mwana wa Adamu.
Yesu ni kielelezo kwetu kama mfano. Kama viumbe vipya
katika Yesu, mamlaka tuliyopewa na Mungu hapa duniani
yamerejeshwa. Ni sharti tutenda katika mamlaka hayo kama
Yesu, Mwana wa Adamu, alivyofanya. Tunapopokea
ubatizo wa Roho Mtakatifu, tunaweza kutenda katika
mamlaka hayo Yesu alitenda baada ya Roho Mtakatifu kuja
juu Yake.
Sasa, tunaposoma Injili, tunaweza kuona kuwa Yesu kwa
kweli alikuwa mfano wetu na mwelekezi. Tunaweza
kutenda katika mamlaka na nguvu zile Yesu alifanya akiwa
hapa duniani. Wanadamu, kama viumbe wapya, wanaweza
kuishi katika mamlaka hayo waliyoumbwa waishi ndani
yake Mungu aliposema, “Hebu na wawe na utawala!”
Was Last Adam
Yesu alikuja kama Adamu wa mwisho.
1 Wakorintho 15:45 Kwa hiyo imeandikwa, “Mtu wa kwanza
Adamu alifanyika kiumbe hai,” Adamu wa mwisho, Yeye ni roho
iletayo uzima.
Kila kitu Adamu aliumbwa kufanya – Yesu alifanya. Mungu
alisema, “Hebu na wawe na utawala” – Yesu alichukua
utawala juu ya mapepo, juu ya viumbe vyenye uhai, juu
vitu. Alitembea katika mamlaka.
Mathayo 7:28,29 Yesu alipomaliza kusema maneno haya,
makutano ya watu wakashangazwa sana na mafundisho yake,
kwa sababu alifundisha kama yeye aliye na mamlaka, wala si
kama walimu wao wa sheria.
Alishiriki katika Ubinadamu wetu
Yesu alishiriki katika ubinadamu wetu kama nyama na
damu.
Waebrania 2:14a Basi kwa kuwa watoto wana nyama na damu,
Yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao.
29
Alipata Majaribu
Alipata majaribu kama vile sisi tunapata.
Waebrania 4:15 Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza
kuchukuliana na sisi katika udhaifu wetu, kwani Yeye
mwenyewe alijaribiwa, kwa kila namna, kama vile sisi
tujaribiwavyo, lakini Yeye hakutenda dhambi.
Hata kama alipata majaribu kama mwanadamu yeyote, Yesu
aliishi bila dhambi kama vile Adamu na Eva waliumbwa
wawe.
Kazi zake – Kazi zetu
Yesu alikuja kuwa na kutenda yote aliyowaumba wanadamu
kuwa na kutenda. Aliziweka kando haki zake kama Mungu
na akaishi na kuhudumu kama mwanadamu hapa duniani.
Yohana 14:12 Amin, amin, nawaambia, ye yote aniaminiye Mimi,
kazi nizifanyazo yeye atazifanya, naam na kubwa kuliko hizi
atazifanya, kwa sababu mimi ninakwenda kwa Baba.
Yesu angesema, “yeye aaminiye atatenda kazi hii na hata
kazi kubwa zaidi” ikiwa hii haikuwezekana.
Nguvu Zake – Nguvu zetu
Kazi zote na huduma ya Yesu ilifanyika katika nguvu za
Roho Mtakatifu.
Luka 3:22a Roho mtakatifu akashuka juu Yake kwa umbo kama
la hua.
Hakuna miujiza ya Yesu iliyoandikwa hadi baada ya Roho
Mtakatifu kuja juu Yake alipobatizwa. Huu ulikuwa
mwanzo wa huduma ya Yesu duniani.
Yesu alisema, alitiwa mafuta na Roho Mtakatifu ili kuhubiri
Injili, kuwaponya wagonjwa, na kuwakemea mashetani.
Luka 4:18,19 “Roho wa Bwana yu juu Yangu, kwa sababu
aminitia mafuta kuwaletea maskini habari njema. Amenituma
kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao na vipofu kupata
kuona tena, kuwaweka huru wanaoonewa na kutangaza mwaka
wa Bwana uliokubarika.”
Wakati Yesu alijiandaa kuondoka hapa duniani,
Alizungumza juu ya kuja kwa roho Mtakatifu, na alisema
kuwa Roho Mtakatifu atawapa wafuasi Wake nguvu.
Matendo 1:8a Lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu
Roho Mtakatifu.
Tunayo nguvu hiyo iliyokuwa katika maisha ya Yesu
alipofanya huduma duniani.
Luka aliyatumia maneno – “nguvu” na “Roho Mtakatifu” –
alipoandika juu ya maisha ya Yesu.
30
Matendo 10:38 Jinsi Mungu alivyomtia Yesu wa Nazareti mafuta
katika Roho Mtakatifu na jinsi alivyokwenda huku na huko
akitenda mema na kuponya wote waliokuwa wameonewa na
nguvu za shetani, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye.
Yesu Alikuja
Kumdhihirisha Baba
Yesu, Mwana wa Mungu, ni sura kamili ya Baba.
Yesu alisema,
Yohana 10:30 Mimi na Baba Yangu tu Umoja.
Yeye pia alisema,
Yohana 14:6,7 Yesu akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na
uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia
kwangu. Kama mngenijua Mimi, mngemjua na Baba pia. Tangu
sasa mnamjua Baba Yangu tena mmemwona.”
Mwandishi wa kitabu cha Waebrania alisema kuwa Yesu
alikuwa sura ya Mungu kamili.
Waebrania 1:3a Mwana ni mng’ao wa utukufu wa Mungu na
mfano halisi wa nafsi Yake ……
Paulo aliandika kuwa Kristo alikuwa sura ya Mungu
asiyeonekana.
Wakolosai 1:15 Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa
wa kwanza wa viumbe vyote.
Yesu alikuwa mzaliwa wa kwanza kwa sura a Jesus was the
first-born in the image of His Father to be over all creation.
We are born again to be conformed to His image as new
creations.
Kutenda Mapenzi ya Baba
Yesu alipokuja hapa duniani, aliacha mapenzi yake kwa
Baba. Alipotembea hapa duniani, alifanya mapenzi ya Baba
Yake.
Yohana 6:38 Kwa kuwa nimeshuka kutoka mbinguni si ili
kufanya mapenzi yangu, bali mapenzi yake Yeye aliyenituma.
Kuharibu Kazi za Shetani
Popote Yesu alihudumu, aliharibu kazi za shetani. Yohana
anatuambia kuwa hii ilikuwa mojawapo ya kazi muhimu
Alikuja hapa duniani.
1 Yohana 3:8b Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa
ili aziangamize kazi za Ibilisi.
31
YESU – BADALA YETU
Adhabu ya Dhambi
Dhambi ya Adamu na Eva iliwatenga na Mungu mtakatifu
ambaye hangehuzishwa na ndambi. Mungu hangeamua,
katika upendo, kuipuuza dhambi, kwa sababu Mungu pia yu
mkamilifu katika haki. Kwa kuwa Mungu ni mtakatifu na
mwenye haki, hangevumilia dhambi.
Mungu alisema,
Mwanzo 2:17b … Kwa maana siku utakapokula matunda yake,
hakika utakufa.
Adamu na Eva walipoteza uhusiano wao na Mungu. Roho
wa Mungu ndani yao hangekaa walipotenda dhambi.
Adamu na Eva hawangewapa watoto wao kile wasicho
kuwa nacho. Asili ya Mungu ndani yao ilitoweka, na asili
ya dhambi ilitawala. Asili ya dhambi ya Adamu ilipitishwa
kwa vizazi vyake.
1 Wakorintho 15:22 Kwa maana kama vile katika Adamu watu
wote wanakufa, vivyo hivyo katika Kristo wote watafanywa hai.
Asili ya dhambi hupitishwa kutoka kizazi hadi kikingine
kupitia kwa mbegu ya Baba. Kwa kuwa kila mtu hapa
duniani ana baba, mtume Paulo aliandika,
Warumi 3:23 Kwa kuwa wote wametenda dhambi na
kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
Adhabu ya dhambi ni mauti ya kiroho, na hii ilisababisha
mauti ya kimwili.
Warumi 6:23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali
karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana
wetu.
Warumi 5:12 Kwa hiyo kama vile dhambi ilivyoingia ulimwenguni
kupitia kwa mtu mmoja na kupitia dhambi hii, mauti ikawafikia
watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi....
Kuzaliwa Kwa Yesu
Yesu alikuja hapa duniani, akapajikwa kwa Roho Mtakatifu
na kuzaliwa na bikra, ili kufanyika badala yetu. Kwa sababu
ya kupajikwa kwake kwa kimiujiza, Yesu hakuwa na asili
ya dhambi. Alikuwa na asili ya Mungu ndani Yake, ambayo
mwanadamu alikuwa amepoteza.
Mathayo 1:20b “Yosefu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua
Maria awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa
uweza wa Roho Mtakatifu.
32
Mathayo 1:23 “Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa
mwana, nao watamwita jina lake Imanueli,” maana yake,
“Mungu pamoja nasi.”
Mipango ya Mungu ya Upendo
Upendo wa Mungu kwa wanadamu haulinganishwi! Yohana
na Paulo waliandika kuhusu hii.
Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu
hata akamtoa mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye
asipotee, bali awe na uzima wa milele.”
Warumi 5:8 Lakini Mungu aliudhihirisha upendo Wake kwetu
kwamba: Tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa
ajili yetu.
Mpango wa upendo mkuu wa Mungu kwa wanadamu
ulihuzisha kumtuma Mwana Wake wa pekee, Yesu, kuishi
kama mwanadamu aliyekamilika, na kisha kwa Mwana
Wake kuibeba adhabu ya dhambi za wanadamu.
1 Petro 3:18 Kwa kuwa Kristo naye aliteswa mara moja tu,
mwenye haki kwa ajili ya wasio na haki, ili awalete ninyi kwa
Mungu. Mwili wake ukauwawa, lakini akafanywa hai katika
Roho.
Yesu alichukua nafasi yetu. Hukumu yote iliyokusudia
kwetu, aliibeba. Alifanyika dhambi kwa ajili yetu ili
tupokee haki Yake. Alizibeba dhambi zetu ili tusibebe sisi
wenyewe.
2 Wakorintho 5:21 Kwa maana Mungu alimfanya yeye
asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate
kufanywa haki ya Mungu katika Yeye.
Alichukua magonjwa yetu, maradhi na maumivu ili tusibebe
sisi wenyewe.
Isaya 53:4,5 Hakika aliuchukua udhaifu wetu na akajitwika
huzuni zetu, hata hivyo tulifikiri amepigwa na Mungu, amepigwa
sana naye na kuteswa. Lakini alitobolewa kwa ajili ya makosa
yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu, adhabu iliyotuletea sisi
amani ilikuwa juu yake, na kwa majeraha yake sisi tumepona.
YESU – MKOMBOZI WETU
Katika maandiko ya Agano la Kale, Ayubu alitoa unabii
kuhusu Mkombozi atakayekuja.
Ayubu 19:25 Ninajua kwamba mkombozi wangu yu hai, naye
kwamba mwishoni atasimama juu ya nchi.
Daudi aliandika,
33
Zaburi 19:14 Maneno ya kinywa changu na mawazo ya moyo
wangu, yapate kibali mbele zako. Ee Bwana, Mwamba wangu na
Mkombozi wangu.
Isaya aliandika kuhusu Mkombozi mara kwa mara.
Isaya 44:6 “Hili ndilo asemalo Bwana, mfalme wa Israeli na
Mkombozi, Bwana mwenye Nguvu: Mimi ni wa kwanza na Mimi
ni wa mwisho, zaidi yangu hakuna Mungu.”
Kukombolewa kutoka kwa Utumwa
Katika Agano la Kale, mtu akiwa katika matatizo ya
kifendha angeweza kujiuza au jamii yake katika utumwa.
Mtu huyu, au watu, angeweza kuwekwa huru ikiwa
“angekombolewa” na jamaa au wao wenyewe iwapo
wangepata fedha za kutosha. Wakati mwingine
wangewekwa huru baada ya miaka ya kuhudumu, au kwa
sababu ya tendo la ujasiri wangetenda.
Maandiko yanamtazama mwanadamu asiye na ukombozi
kama mtumwa asiye na matumaini katika dhambi na
shetani, bwana wao.
Kwa Damu Yake
Mwanadamu hangekombolewa na vitu vyovyote vyenye
uasi. – si kwa fedha au dhahabu – si kwa tendo lolote
wangetenda. Gharama ya ukombozi wao ilikuwa damu ya
Mwana wa milele wa Mungu aliyefanyika mwili. Ilikuwa
damu ya gharama ya juu mno, damu iliyo na uwezo mkuu
mno hata kuziosha dhambi za wanadamu wote.
1 Petro 1:18,19 Kwa maana mnafahamu kwamba mlikombolewa
kutoka katika mwenendo wenu usiofaa ambao mliuridhi kutoka
kwa baba zenu, si kwa vitu viharibikavyo, yaani, kwa fedha na
dhahabu, bali kwa damu ya thamani ya Kristo, kama ile ya
Mwana kondoo asiye na dosari wala doa.
Kuwekwa Huru
Neno la Kigiriki la tafsiri “kukombolewa” katika msitari
huu ilikazia kitendo cha kuweka huru au kurejeshwa kwa
kununuliwa. Sisi, tulikuwa Wake katika kuumbwa, sasa
tumekuwa wa mkombozi kwa kununuliwa.
Yohana 8:36 Hivyo mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli
kweli.
Yesu si tu alitukomboa, alituweka Huru! Alitununua kwa
damu yake ya dhamani. Tulifanyika mali yake, na alikuwa
na haki kisheria kutuweka huru.
Ili Kufanyika Wafalme na Makuhani
Neno la kiasili “agorazo” tafsiri yake “kukombolewa”
katika msitari unaofuata maana yake ni “kwenda sokoni
34
kununua.” Yesu alitununua kutoka kwa utumwa ili
kufanyika wafalme na makuhani ndani Yake.
Ufunuo wa Yohana 5:9,10 Nao wakaimba wimbo mpya
wakisema: “Wewe unastahili kukitwaa kitabu na kuzivunja lakiri
zake, kwa sababu ulichinjwa na kwa damu Yako ukamnunulia
Mungu watu kutoka katika kabila, kila lugha, kila jamaa na kila
taifa. Wewe umewafanya hawa wawe ufalme na makuhani wa
kumtumikia Mungu wetu, nao watamiliki katika dunia.”
Hadi Milele
Neno la kijumla la, “exagorazo” tafsiri yake
“kukombolewa” katika Wagalatia 3:13, maana yake
“kununua kutoka kwa ili isirudishwe tena kamwe.”
Wagalatia 3:13a Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya
sheria ...
Kwa kazi ya ukombozi ya Kristo kwa ajili yetu,
tulinunuliwa kutoka kwa utumwa katika dhambi, kwa
ukamilifu kabisa, hata tunaweza kuwa na ujasiri
tusirejeshwe soko ya utumwa tena.
Hii hasa ilieleweka katika nyakati na siku za Kirumi ambao
wangeuzwa kila mara kwa mnada na mabwana zao.
YESU – KITAMBULISHO CHETU
Kuunganishwa Pamoja Naye
Wakati tulipoweka imani yetu katika Yesu kama Mwokozi
wetu, muujiza ulifanyika. Mungu Roho Mtakatifu
alituunganisha pamoja Naye. Tulifanyika Mwili Wake.
1 Wakorintho 12:13 Kwa maana katika Roho mmoja wote
tulibatizwa katika mwili mmoja, kama ni Wayahudi au Wayunani,
kama ni watumwa au watu huru, nasi sote tulinyweshwa Roho
mmoja.
Zababu ya kazi ya ukombozi wa Yesu haikuwa tu kuwa siku
moja tuwe Naye mbinguni. Petro aliandika kuwa Yesu
alitoa njia tunayoweza kuishi katika haki.
1 Petro 2:22,24 “Yeye hakutenda dhambi, wala udanganyifu
haukuonekana kinywani mwake. Yeye mwenyewe alizichukua
dhambi, tupate kuishi katika mwili wake, juu ya mti, ili kwamba,
tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tupate kuishi katika haki.
Kwa kupigwa kwake, ninyi mmeponywa.
Alifanyika Dhambi Kwetu
Katika kazi ya ukombozi Yake kwa ajili yetu, Yeye
“alifanyika” dhambi kwetu. Alizibeba dhambi zetu juu ya
mwili wake msalabani.
35
2 Wakorintho 5:21 Kwa maana Mungu alimfanya yeye
asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate
kufanywa haki ya Mungu katika Yeye.
36
Alifanyika Laana Kwa Ajili Yetu
Yesu alichukuwa laana iliyokuja kwa mwanadamu kwa ajili
ya dhambi.
Wagalatia 3:13 Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria
kwa kufanyika laana kwa ajili yetu, (kwa maana imeandikwa,
“Amelaaniwa yeye aangikwaye juu ya mti.”)
Alizibeba Dhambi Zetu
Msalabani, Yesu alifanyika “mwanakondoo wa Mungu
aondoaye dhambi za ulimwengu.” Alizichukua dhambi zetu
zote hadi chini ardhini ili sizikumbukwe na Mungu kamwe,
daima.
Yohana 1:29 Siku iliyofuata, Yohana alimwona Yesu akimjia
akasema, “Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye
dhambi ya ulimwengu!”
Zaburi 88:3,6,7 Kwa kuwa nafsi yangu imejaa taabu, na maisha
yangu yanakaribia kaburi.
Umenitupa kwenye shimo lenye kina kirefu sana, katika vina vya
giza nene. Ghadhabu imekuwa nzito juu yangu, umenigharikisha
kwa mawimbi yako yote.
Tuliunganishwa pamoja Naye katika mauti Yake.
Warumi 6:6 Kwa maana twajua kwamba utu wetu wa kale
ulisulibiwa pamoja naye ili ule mwili wa dhambi upate
kuangamizwa, nasi tusiendelee kuwa tena watumwa wa dhambi.
Kufanyika Hai
Baada ya kuzichukuwa dhambi zetu chini ya ardhi,
Alifufuka kwa ushindi katika mauti, jehanamu, na kaburini.
Alifanyika “mzaliwa wa kwanza katika kifo.”
Wakolosai 1:18 Yeye ndiye kichwa cha mwili, yaani, kanisa, naye
ni mwanzo na mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, ili Yeye
awe mkuu katika vitu vyote.
“Alifanyika hai” katika Roho.
1 Petro 3:18 Kwa kuwa Kristo naye aliteswa mara moja tu,
mwenye haki kwa ajili ya wasio na haki, ili awalete ninyi kwa
Mungu. Mwili wake ukauwawa, lakini akafanywa hai katika
Roho.
Wakati Yesu alipofanyika hai, tulifanywa hai pamoja naye.
Waefeso 2:5,6 Hata tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu,
alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu, yaani, (mmeokolewa
kwa neema). Mungu alitufufua pamoja na Kristo na kutuketisha
pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu,
Wakati Yesu alipofanyika hai, alirejeshwa katika uhai
kamili wa Baba. Alifanyika tena katika haki.
37
Warumi 3:26 Alifanya hivyo ili kuonyesha haki yake wakati huu,
ili yeye awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yule
anayemwamini Yesu.
Alifanyika Haki kwetu
Wakati wa wokovu, tulipewa haki ya Yesu. Tufanyika
wenye haki kama vile Yesu alivyo mwenye haki.
Paul wrote,
2 Wakorintho 5:21 Kwa maana Mungu alimfanya Yeye
asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate
kufanywa haki ya Mungu katika Yeye.
Na sasa sisi tuliofanyika haki basi na “tuishi kwa haki.”
Petro aliandika,
1 Petro 2:24a Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika
mwili wake, juu ya mti ili kwamba, tukiwa wafu kwa mambo ya
dhambi, tupate kuishi katika haki.
Kama viumbe wapya katika Kristo Yesu, sisi si wenye
dhambi tena. Tumefanyika wenye haki!
2 Wakorintho 5:17 Kwa hiyo kama nmtu akiwa ndani ya Kristo,
amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama, yamekuwa
mapya.
Kamwe hatutaishi katika hukumu na lawama. Tumefanyika
wenye haki!
Basi hatuko tena katika mawazo ya dhambi. Bali tuwe na
mawazo ya haki.
Basi tusimruhusu tena shetani kutuweka chini na
kutushinda.
Tunatambua kuwa “sisi ni haki ya Mungu katika Yesu
Kristo.” Sisi tuko huru kutokana na lawama na hukumu.
Warumi 8:1 Kwa hiyo, sasa hakuna hukumu ya adhabu kwa wale
walio ndani ya Kristo Yesu, wale ambao hawaenendi kwa
kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho.
Sisi tu viumbe vipya katika Kristo Yesu! Roho zetu ni zenye
haki kama vile Mungu ni mwenye haki. Kila siku, roho zetu
na miili yetu inabadilishwa katika sura ya Mwana Wake!
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Kulingana na Yohana 5:24-27, ni kwa mamlaka gani Yesu alihudumu alipokuwa hapa
duniani?
2. Eleza kazi ya Yesu kama Mkombozi wetu.
3. Je, tunawezaje kufanyika “wenye haki ya Mungu” katika Kristo?
38
Somo la Nne
Sura Ya Kuumbwa Upya
KATIKA KRISTO
Kulingana na mtume Paulo, tunampokea Kristo kama
Mwokozi wetu, tunakuwa ndani ya Kristo. Tumefanyika
viumbe vipya. Mambo yote yanafanyika upya maishani
mwetu.
2 Wakorintho 5:17 Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo,
amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama, yamekuwa
mapya.
Punde tu tunapopokea Yesu kama Mwokozi wetu, Roho
Mtakatifu anatuunganisha kwa Yesu Kristo.
Tunaunganishwa pamoja Naye milele.
Mambo ya Zamani Yalipita
Tunapofanyika “katika Kristo,” mambo ya zamani yanapita.
Hii inamaanisha sehemu ya wengine wetu iliyokuwepo
awali, haipo tena. Zile sehemu zilizotajwa kama “vitu vya
zamani” hufa. Lakini pia, kunakuwa na kuzaliwa upya –
mtu mpya wa kiroho huzaliwa.
Vitu Vyote hufanyika Upya
Mwamini mpya si yule mtu aliyekuwa awali. Yule mtu wa
zamani hayupo tena. Yule mtu amepita. Vitu vyote
vimefanyika upya.
Je, lingeshangaza vipi wakati tunasherehekea mtoto
aliyezaliwa kisha mtu akauliza, “Vipi kuhusu maisha ya
zamani ya mtoto huyu?”
Ungejibu, “Mtoto huyu amezaliwa vihi sasa. Hana maisha
ya zamani!”
Ni vivyo hivyo ibilisi anapotukumbusha kuhusu kushindwa
na dhambi za awali kabla ya kuzaliwa upya. Sehemu hiyo
ya maisha yetu ya zamani imepita. Haipo tena! Kama
viumbe vipya, hatuna zamani ambayo ibilisi anaweza
kujenga mashtaka dhidi yetu. Paulo aliandika, “vitu vya
zamani vimepita! Vitu vyote vimefanyika vipya!”
Kuzaliwa Mara ya Pili
Yesu aliponena na Nikodemo, Alisema ni lazima uzaliwe
mara ya pili.
Yohana 3:7 Kwa hiyo usishangae ninapokuambia huna budi
‘kuzaliwa mara ya pili’.
Kwanza, Nikodemo alifikiri kuwa Yesu anazungumzia
kuhusu mwili wake kuzaliwa tena. Kisha, Yesu akaeleza
39
kuwa sehemu ya mwili wa mwanadamu wa kupata kuzaliwa
upya si mwili bali ni roho. Ilikuwa roho ya mwanadamu.
Yohana 3:5,6 Yesu akamwambia, “Amin, amin nakuambia,
hakuna mtu yeyote anayeweza kuingia katika ufalme wa Mungu
isipokuwa amezaliwa kwa maji na kwa Roho. Mwili huzaa mwili,
lakini Roho huzaa roho.
Roho Mpya
Wakati wa wokovu, roho yetu mpya huwa kamilifu. Kamwe
haitakuwa kamilifu au haki zaidi ya wakati huu.
Roho ni sehemu ndani yetu itakayoishi milele. Ni sehemu
inayojali uwepo wa Mungu. Roho ya mwamini ni sehemu
inayoshirikiana na Mungu kwa sababu ni ya haki kama vile
Mungu ni mwenye haki.
“Roho ngumu” imeondoka! Mungu amutupatia “roho ya
mwili.” Ametupatia Roho isiyo gumu, nyepesi na yenye
upendo. Ametupatia roho anayejali kuishi katika haki.
Ezekieli 11:19 Nitawapa moyo mmoja na kuweka roho mpya
ndani yao, nitaondoa kutoka ndani yao moyo wa jiwe na kuwapa
moyo wa nyama.
Roho zetu zimekamilika katika Yesu. Mungu angependa
kurejesha roho zetu kwa kuyafanya upya mawazo yetu.
Mungu angependa kurejesha miili yetu katika afya kamili.
Wakati wa wokovu, tulifanyika viumbe vipya. Mwili
(mifupa, nyama, na damu) na roho (fikira, uwezo wa
kuchagua, na hisia) havikubadilishwa kabisa, bali roho
alifanyika upya na kamilifu wakati wa wokovu.
Paulo aliandika maneno ya kusisimua kwa Wafilipi –
“Tenda wokovu wenu kwa kuogopa na kutetemeka.”
Wafilipi 2:12 Kwa hiyo, wapenzi wangu, kama vile ambavyo
mmekuwa mkitii sikuzote, si tu wakati nikiwa pamoja nanyi, bali
sasa zaidi sana nisipokuwapo. Utimizeni wokovu wenu kwa
kuogopa na kutetemeka.
Tunajua kuwa wokovu ni bure; na msitari huu unahitilafiana
na mingine hadi tunapoelewa kuwa wakati huo wa wokovu,
roho zetu zimekamilika katika Kristo. Kutoka wakati huo,
roho zetu hufanya kazi na Roho Mtakatifu ili kuyabadilisha
mawazo na miili yetu katika sura ya Kristo. Inabadilishwa
kila siku. Wokovu wetu unafanya kazi katika mawazo na
miili yetu.
Paulo aliendelea,
Wafilipi 2:13 Kwa maana Mungu ndiye atendaye kazi ndani yenu,
kutaka kwenu na kutenda kwenu kwa kulitimiza kusudi lake
jema.
Roho – Fedha – Afya
40
Ni vyema kuwa na ufunuo juu ya roho katika utu ni nini
hasa katika Kristo Yesu. Ni bora tuelewe kuwa roho
aliyeumbwa upya ni kamili na yenye haki kabisa machoni
pa Mungu.
Kwa ufunuo huu na katika ufahamu wa kazi ya ukombozi
ya Yesu kwa ajili yetu, tutaanza kutembea kwa afya katika
roho na miili yetu.
Roho zetu zitaendelea wakati mawazo yetu yanafanywa
upya kwa kusoma, kusikia, kutafakari, kuamini, kunena, na
kulitenda Neno la Mungu.
Warumi 12:2 Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali
mgeuze kufanya upya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na
kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema,
yanayopendeza machoni pake na ukamilifu.
Wakati roho zetu zinabadilishwa – kufanana na sura Yake –
tutafaulu, na mili yetu itakuwa na afya. Yohana aliandika
kuhusu haya.
3 Yohana 1:2 Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo yote na
kuwa na afya yako kama vile roho yako ifanikiwavyo.
HAKI YAKE MUNGU
Je, Mungu ni Mwenye Haki kiasi gani?
Yeye ni wa haki katika kuwa na katika njia zake zote.
Haki Yake ni zaidi ya ukosefu wa dhambi au uwezo
wa kutokutenda dhambi.
Ni wema wa hali ya juu na usiokuwa na kifani amabo
hauwezi kutazama dhambi au kuikaribia dhambi.
Mungu hana uwezo wa kutenda dhambi.
Mungu katika haki yake hangeweza kuipuuza dhambi ya
Adamu na Eva na vizazi vyao, hata katika upendo Wake,
angependa.
Warumi 3:25,26 Yeye ambaye Mungu alimtoa awe dhabihu ya
upatanisho kwa njia ya imani katika damu Yake. Alifanya hivi ili
kuonyesha haki Yake, kwa sababu kwa ustahimili Wake
alizichukua zile dhambi zilizotangulia kufanywa. Alifanya hivyo
ili kuonyesha haki Yake wakati huu, ili Yeye awe mwenye haki
na mwenye kumhesabia haki yule anayemwamini Yesu.
Haki yake Mungu inaonekana katika imani.
Warumi 1:17 Kwa maana katika injili haki itokayo kwa Mungu
imedhihirishwa, haki ile iliyo kwa njia ya imani hadi imani. Kama
ilivyoandikwa: “Mwenye haki ataishi kwa imani”.
Haki Zetu
41
Hatuwezi kufanywa haki kwa matendo yetu wenyewe.
Nabii Isaya anatoa picha nzuri ya haki zetu.
Isaya 64:6a Sisi sote tumekuwa kama mtu aliye najisi, nayo
matendo yetu yote ya uadilifu ni kama matambaa machafu.
Chochote tufanyacho, hata tujaribu kwa bidii zote, bado
itakuwa matambaa machafu machoni pa Mungu. Matendo
yetu mema tuliyotenda kabla ya kuumbwa upya iliongeza tu
matambaa machafu.
Haki Iliyoletwa
Yesu alipokufa msalabani, Alizichukua dhambi zetu zote –
kukosekana kwa haki juu yake. Badala yake alitupatia haki
yake. Je, ni ubadilishanaji ulioje!
Dhambi zetu zimewekwa Kwake.
Haki Yake kamili imewekwa juu yetu.
Wakati tulipoweka imani yetu juu ya Yesu Kristo kama
Mwokozi wetu, roho zetu zilifanyika “haki ya Mungu.”
Warumi 3:22 …haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa Yesu
Kristo kwa wote wamwaminio.
Neno “amini” ina maana kutegemea, kuegemea, na
kutumainia kazi ya ukombozi ya Yesu kwa ajili yetu.
Paulo alitaja kuwa tulipozaliwa upya na kuumbwa tena,
tulifanyika haki ya Mungu katika Yesu.
2 Wakorintho 5:21 Kwa maana Mungu alimfanya Yeye
asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate
kufanywa haki ya Mungu katika Yeye.
Tulipofanyika haki ya Mungu, si kuwa hatuwezi kutenda
dhambi tu. Si kwa kuwa dhambi zetu zote zimesamehewa –
hata kama inafurahisha hivyo. Tunapofanyika katika haki ya
Mungu, ina maana kuwa roho zetu ni zenye haki kama vile
Mungu mwenyewe ni mwenye haki.
Tumetangazwa kuwa wenye haki.
tumepokea haki kutoka kwa Mungu.
Sura ya Zamani ya Ukosefu wa Haki
Kuwa tuko na haki kama vile Mungu ni mwenye haki, ni
vigumu kwa wengine kukubali. Tumefundishwa kwa
utofauti sana na waalimu-wenye busara.
Wakristo wengi huishi maisha yao yote kwa kupigwa na
kotosamehewa na lawama, bila kutambua kuwa wako ndani
ya Kristo Yesu.
Kwa imani tunatakiwa kukubali na kuamini kuwa sisi ni
haki yake Mungu. Tunapotambua zaidi kuhusu Mungu,
tunakuwa tukitambua haki badala ya kutambua dhambi.
Hatuko tena Katika Dhambi
42
Tusijione tena kamwe kama “wenye dhambi waliookolewa
kwa neema.” Sisi si wenye dhambi tena! Sisi ni viumbe
vipya!
Wakristo wengi hujikuta wakitenda dhambi kwa sababu
wao huambiwa ni wenye dhambi.
Wamesikia mafundisho kuhusu dhambi mara kwa mara.
Mawazo yao yameegemea dhambi kila mara. Hawajapokea
ufunuo kuhusu haki, kwa hivyo dhambi bado inatawala
maishani mwao. Kwa kupitia ufunuo wa haki yake Mungu,
tunafanyika wenye ufahamu wa haki. Tunajiona kama vile
Mungu anavyotuona. Tunajiona kama wenye ufahamu wa
haki yaake Mungu kama vile Alivyo na haki. Kwa hivyo,
dhambi haitawali tena miilini mwetu. Basi hatutendi dhambi
tena kwa mazoea.
Tunaiona dhambi kama vile Mungu anaiona. Imepoteza
mvutio kwa sababu tumepata ufunuo wa haki yake Mungu.
KWA KUBADILISHWA KWA SURA YAKE
Tunapoendelea kutembea katika ufunuo wa haki yake
Mungu kama viumbe vipya katika Kristo Yesu, basi
tunabadilishwa kwa kuyafanya upya mawazo yetu. Ni
mafuatano ya mambo. Tunabadilishwa kila siku katika sura
ya Mwanawe.
Warumi 8:29 Maana wale Mungu aliowajua tangu mwanzo, pia
aliwachagua tangu mwanzo, wapate kufanana na mfano wa
Mwanawe, ili Yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa
ndugu wengi.
Kukiri Dhambi
Sisi kama Wakristo tukitenda dhambi, tusiishi katika
kushindwa, lawama na hukumu katika maisha yetu yote.
Punde tu tukigundua kuwa tumetenda dhambi, ni sharti
tukiri dhambi hizo kwa Mungu, na kwa imani, kupokea
msamaha Wake. Kisha tunaweza kuendelea kutembea
katika haki, tukiwa huru kutoka kwa kutosamehewa na
lawama.
1 Yohana 1:9 Kama tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni
mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha
toka kwenye udhalimu wote.
Kukiri maana yake ni kukubaliana na Mungu kuhusu
dhambi. Sisi, kama Mungu, lazima tuichukie dhambi.
Tunakokaribia Mungu, ndipo tunapotembea katika ufunuo
wa haki, basi tutaweza kujaribiwa mara chache kutenda
dhambi.
Jifunze Kurejea
43
Tunapokosea katika sehemu fulani maishani mwetu, no
sharti tujifunze kurekebisha na kurejea haraka. Kama bondia
anapopigwa na kuanguka mkekani, tusilale hapo na kujihisi
kushindwa. Bali, tujifunze kuruka toka kwenye mkeka kwa
miguu yetu. Turejee na kuendelea mbele.
Tunapotenda dhambi, tusikubali mawazo ya hukumu,
lawama, na kushindwa. Bali, kwa haraka tutubu dhambi
zetu na kupokea msamaha. Kama bondia anayeshinda,
tuamke na kuelekea katika ushindi.
Uweze Kubadilishwa
Roho zetu zina haki ya Mungu, lakini tutoe miili yetu kwa
Mungu kila siku kama kafara inayoishi.
Warumi 12:1 Kwa hiyo, ndugu zangu, nawasihi kwa rehema zake
Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu na
inayompendeza Mungu, hii ndiyo ibada yenu yenye maana.
Roho zetu zinayo haki ya Mungu, lakini mioyo yetu ni
sharti ibadilishwe kwa kuyafanya upya mawazo yetu katika
ufunuo wa Neno la Mungu.
Warumi 12:2 Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali
mgeuze kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na
kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema,
yanayopendeza machoni pake na ukamilifu.
Kuwa Na Ujasiri
Kwa ufunuo wa haki ya Mungu katika kuumbwa upya,
tunaweza kwenda mbele ya kichi cha enzi cha Mungu kwa
ujasiri. Tunajua kuwa Mungu atatusikia.
Waebrania 4:16 Basi na tukikaribie kiti cha rehema kwa ujasiri,
ili tupewe rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa
mahitaji.
Tunaweza kuja kwa Mungu kwa ujasiri bila shaka kwa
sabau tunaielewa neema Yake. Tunatambua kile Yesu
amefanya kwa niaba yetu. Tunajua kuwa tumesamehewa.
Tunatambua kuwa sisi tu viumbe vipya katika Yesu Kristo.
Tunajua kuwa sisi ni haki ya Mungu.
Uwe Hai
Kama viumbe vipya, tunayo maisha mapya ndani yetu.
Maisha haya mapya ni maisha yale ya Kristo mwenye.
Waefeso 2:4,5a Lakini Mungu, kwa upendo wake mwingi kwetu
sisi, ambaye ni mwingi wa rehema, hata tulipokuwa wafu kwa
ajili ya makosa yetu alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu….
Ubinafsi wa awali uliotembea kulingana na njia ya
ulimwengu huu haupo tena. Mtu mpya wa ndani amewekwa
hai.
44
Waefeso 2:1-3 Kwa habari zenu, mlikuwa wafu katika makosa na
dhambi zenu, ambazo mlizitenda mlipofuatisha namna ya
ulimwengu huu na za yule mtawala wa ufalme wa anga, yule
roho atendaye kazi ndani ya wale wasiotii. Sisi sote pia tuliishi
katikati yao hapo zamani, tukifuata tamaa za mwili na mawazo
yake. Nasi kwa asili tulikuwa wana wa ghadhabu , kama mtu
mwingine ye yote.
Ujazwe
Kama viumbe vipya, roho zetu zimejazwa na wema wa
Mungu. Yote Alivyo – imetujaza. Utajiri Wake wote katika
kipimo imefanyika yetu.
Waefeso 3:19 Na kujua upendo huu kwamba unapita fahamu, ili
mpate kujazwa na kufikia kipimo cha ukamilifu wa Mungu.
Katika Biblia ya Ufafanuzi inasema,
... kuwa ujazwe (kila mahali ndani yako) kwa wema wote wa
Mungu – [maana yake] ili upate utajiri kamili wa Uwepo wa
Mungu, na kufanyika mwili uliojazwa kamili na kufurika na
Mungu mwenyewe!
Kama viumbe vipya, hatuko na utupu tena. Badala yake,
tumejazwa na Mungu! Tumefurika na Yeye.
Tunapoendelea katika njaa na kiu kwa ajili ya haki Yake,
tutajikuta tumejazwa na haki zake Mungu hata katika roho
na miili yetu.
Mathayo 5:6 Ni heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao
watatoshelezwa.
Kupokea Upendo Wake
Ni ufunuo mkuu ulioje kutambua kuwa Mungu hajakasirika
nasi! Anatupenda! Hata tulipokuwa adui zake, alitupenda.
Yohana 15:12,13,14 Amri Yangu ndio hii: Mpendane kama mimi
nilivyowapenda ninyi. Hakuna mtu mwenye upendo mkuu kuliko
huu, mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. Ninyi ni rafiki
zangu mkifanya ninayowaamuru.
Kama viumbe vipya tukiwa na roho mpya ya nyama,
tunafanya kwa haraka kile anatuamuru kufanya.
Kuwa Rafiki wa Mungu
Je, ni furaha iliyoje kujua kuwa Mungu hakasiriki nasi. Sasa
anasema, “ninyi ni marafiki zangu!” Sisi ambao awali
tulikuwa adui Wake, tumerejeshwa Kwake katika Kristo.
Sisi sasa tu rafiki zake na Yeye ni Rafiki yetu. Kama rafiki
za Mungu, tunayo huduma ya kuunganishwa. Tungependa
wengine wakutane na Rafiki wetu, na kama sisi, wafanyike
marafiki wake Mungu.
Kurejeshwa Kwake
Kama viumbe vipya tumerejeshwa Kwake.
45
2 Wakorintho 5:17,18 Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo,
amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama, yamekuwa
mapya. Haya yote yanatokana na Mungu, ambaye
ametupatanisha sisi na nafsi yake kwa njia ya Yesu Kristo na
kutupatia sisi huduma ya upatanisho.
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Je, nini maana ya kuumbwa kipya?
2. Eleza kwa kinaga ubaga haki Yake Mungu.
3. Eleza kwa kinaga ubaga haki ya kuumbwa upya.
46
Somo La Tano
Kuibadili Sura Yetu ya Kimwili ya Zamani
Uamuzi ni Wetu
Tunajifunza masomo haya, tutafika mahali ambapo itatubidi
kufanya uamuzi. Je, tutaamini ufunuo wa Neno la Mungu,
au tutashikilia mafundisho ya zamani ambayo tumepokea
kwa miaka mingi?
Je, tutakubaliana na mtume Paulo alipoandika,
Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe
kipya, ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya. (2
Wakorintho 5:17)
Tumejifunza kuhusu jinsi tulivyoumbwa tuwe, kuhusu
upendo wetu, Baba wa mbinguni, na kuhusu kazi ya
ukombozi ya Yesu Kristo kwa niaba yetu. Sasa ni wakati wa
kufanya uamuzi wa busara na kuingia katika yote ambayo
Mungu ametuwekea.
Kuweka Kando Sura yetu ya Kimwili ya Zamani
Ni muhimu kuwa na sura nzuri ya kibinafsi. Tusimruhusu
ibilisi kutupotosha kuwa hatufai kupokea baraka za Mungu.
Tukifanya hivyo, tutapitia maisha bila ushindi. Tukiishi
maisha ya kushindwa, hatutaweza kupigana na kuyanshinda
mapepo. Hatutaweza kuishi katika maisha ya ushindi kama
Wakristo na kuhudumu wengine vyema.
Kwa wengi wetu, lazima kuwe na wakati wa kuvua mtu wa
zamani – mitindo ya zamani – na kuvaa sura ya kuumbwa
upya kwa kuyafanya upya mawazo yetu.
Paulo aliandika kuhusu kuvua mtu wa zamani. Kitendo cha
uamuzi.
Waefeso 4:22,23 Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa
zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake za
udanganyifu. Mfanywe upya roho ya nia zenu.
Kufaa Iliyo Mpya
Tunapovua mtu wa zamani, lazima tubadili mawazo yetu.
Kufanya upya kutakuja tu ikiwa tutayabadili mawazo yetu
kwa imani katika ufunuo wa Neno la Mungu.
Paulo aliendelea kusema katika msitari unaofuata.
Waefeso 4:24 Mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawa sawa na
mfano wa Mungu katika haki yote na utakatifu.
Tunapovua mtu wa zamani, sura ya kimwili ya zamani, na
kufanya upya mawazo yetu katika ufunuo wa Neno la
Mungu, tunavaa mtu mpya, kiumbe kipya.
47
Kiumbe kipya hajapungukiwa kwa kile ambacho anachoona
katika hisia zile tano ufunuo mpya huishi katika imani.
Kiumbe kipya hutambua kuwa yeye ameumbwa upya,
ameumbwa kulingana na Mungu, katika haki na utakatifu.
Viumbe wapya hawajioni tena kama wenye dhambi.
Wanatambua kuwa roho zao ni zenye haki na takatifu kama
Mungu. Wanajua kuwa mioyo yao na mili inabadilishwa
kwa sura ya Mwana katika haki ionekanayo na utakatifu
katika matembezi yao kila siku.
NGOME ZA ZAMANI
Wakati wa kukua, Shetani aliweka ngome mbalimbali
mawazoni mwetu. Sasa, hata tukiwa wazima, tunafikiri
kuwa hatuwezi kufanya kitu fulani kwa sababu tuliambiwa
tulipokuwa watoto kuwa hatuwezi. Maneno yanayoharibu
yaliyonenwa kwa muda yamekuwa ngome inayotakiwa
kuvunjwa.
Kutokutosheleza
Labda uliambiwa, “Aah, usijaribu kufanya hiyo; kakako
mkubwa atalishughulikia.” Ulianza kuwaza, “Mimi sina
uwezo kama kakangu.”
Kutokuwa wa Maana
Labda mwalimu alisema “Sielewi ni kwa nini hili ni tatizo
kwako, wengine darasani hawana shida nalo.” Wazo lako la
kwanza likawa “Mimi si mwerevu kama wengine darasani.”
Mtindo Ukufaao
Labda tumeamini yale wengine wamesema kuhusu asili yetu
kijamii au kuhusu kundi la watu fulani tunaotambulika nao.
Mambo haya ya kijumla huenda imekuwa mitindo itufaayo
maishani mwetu.
Iwapo una nywele nyekundu, labda umesikia, “wenye
vichwa vyekundu kila wakati wana hasira ya haraka.”
Mtindo mwingine labda ni, “Mama yangu alijawa na shaka
kila wakati, kwa hivyo hivi ndivyo mimi nlivyo.”
Labda tulisikia na kuamini mambo mengi kuhusu utaifa au
asili ya ujamaa wetu ambayo imetufanya kuamini kuwa
hatuwezi kuwafikia wengine karibu nasi. “Wajerumani kila
mara…” au Waholanzi kila mara…”
Ufunuo wa kuumbwa upya utatuweka huru kutokana na
mawazo ya kutokuwa na maana au kutosheleza ambayo
yameweka uvuli maishani mwetu hapo awali.
48
Chuki au Kupendelea
Ufunuo wa kuumbwa upya utatuweka huru kutokana na
chuki ya utaifa. Tutaanza kuona waamini wenzetu wa kila
taifa kama viumbe wapya katika Kristo.
Katika msitari unaofuata ufunuo wa Paulo kuhusu kuumbwa
upya, aliandika,
2 Wakorintho 5:16a Hivyo tangu sasa hatumwangalii mtu ye yote
kwa mtazamo wa kibinadamu.
Paulo pia aliwaandikia Wagalatia,
Wagalatia 3:26-28 Kwa maana ninyi nyote mmekuwa watoto wa
Mungu katika Kristo Yesu kwa njia ya imani. Kwa maana wote
mliobatizwa ndani ya Kristo, mmemvaa Kristo. Wala hakuna tena
Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala
mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo
Yesu.
Ni lazima tujione pamoja na waamini wengine wote kama
vile Mungu anavyotuona. Kama roho walioumbwa tena, sisi
hatuko tena na utaifa wetu wa zamani au kundi la jamaa
letu. Tumezaliwa katika jamii mpya, jamii ya Mungu. Basi
hatutamtazama mtu mwingine kulingana na rangi ya ngozi
yake. Tutajikubali wenyewe na wengine, kama viumbe
wapya katika Yesu Kristo.
KUZIANGUSHA NGOME
Shetani angependa kuzitumia hisia za zamani za
kudharauliwa, kutokuwa wa maana, na chuki kutushika
katika utumwa. Sasa ni wakati wa kuziharibu ngome hizo.
Ziharibu
Ikiwa Mungu amedhihirisha ngome mawazoni mwako
wakati wa mafundisho haya, unaweza kuzivunja sasa hivi.
Sema kwa sauti,
Shetani, nakufunga katika jina la Yesu.
Nakataa ngome hii ya ~ (itaje) ~ sasa,
katika jina la Yesu.
Sitaikubali iendelee. Natoa fikira zozote na mawazo
ambayo ni kinyume na ufunuo kutoka kwa Neno la
Mungu kunihusu mimi,
kile naweza kutenda au kile naweza kupata
kama kiumbe kipya katika Yesu Kristo!
Itachukuwa muda kuivunja tabia ya kuwaza au kusema
mawazo ya zamani ya kinyume. Lakini, kila mara mawazo
haya yanakuja mawazoni mwetu, lazima punde tuzikatae,
tusizushe chini, na kuendelea kutangaza kile Neno la
Mungu linaonyesha kuhusu kuumbwa upya. Kwa kufanya
hivyo, tabia hiyo itavunjwa na utakuwa huru. Anza kuwaza
na kusema,
49
Neno la Mungu linasema mimi ni kiumbe kiumbe kipya
mimi ni katika jamaa ya Mungu na kuwa
hakuna_____________ katika jamaa ya Mungu.
Vitu vya zamani vimepita.
Mimi mtu mpya katika Kristo!
Vunja Laana
Shetani huenda alishinda alipoweka laana juu ya jamii
kupitia dhambi katika vizazi vilivyopita. Kwa mfano, mtu
anapojitia kitanzi, roho wa kujiua husalia katika jamii hiyo
hadi ivunjwe katika nguvu ya jina la Yesu.
Mtu anapoua mtu mwingine, kuna roho za uuaji
zinazosumbua jamii hiyo kila kizazi.
Kuna laana za kizazi au roho wa kurithi ambayo hufungua
mlango wa magonjwa aina fulani zinazojishikilia katika mili
yetu. “Aah, ndiyo, matatizo ya moyo hupita katika jamii
zetu.” Au “Wanawake wote katika jamii yetu hupata
saratani.”
Laana ya kizazi ni rahisi kuivunja kama ngome katika akili
zetu. Sema,
Shetani, nakufunga katika jina la Yesu!
Ninavunja laana ya ____________, __________
na ________________!
Ninaamuru laana zote za kizazi na kila roho mwovu
wa kurithi ili kuvunjwa juu ya maisha yangu sasa hivi.
Mimi ni kiumbe kipya! Mimi ni mtoto wa Mungu!
mimi ni sehemu ya jamii mpya!
Mimi ni sehemu ya jamii ya Mungu!
na hakuna tena utumwa,
hakuna laana, hakuna magonjwa katika Jamii ya
Mungu!
Wakati mawazo au dalili za utumwa huo, laana, au
magonjwa hujaribu kukuja kwako, zikemee! Ikiwa
umekuwa ukikubali dalili, zikemee mara moja na uanze
kutangaza kwa ujasiri kile ambacho Neno la Mungu
linasema kuhusu uhuru wako.
KUIBADILI SURA YA ZAMANI YA KIMWILI
Kuendelea kushikilia sura yetu mbaya ni dhambi. Hatutaki
kuwa kama wale mtume Paulo alieleza.
Warumi 1:21,22 Kwa maana ingawa walimjua Mungu,
hawakumtukuza Yeye kama ndiye Mungu wala
hawakumshukuru, bali fikira zao zimekuwa batili na mioyo yao
ya ujinga ikatiwa giza . Ingawa wakijidai kuwa wenye hekima,
wakawa wajinga.
50
Sisi ni wale Mungu anasema tuko. Kwa sababu Yesu alikufa
ili kutuweka huru kutokana na vitu hivi, kuendelea
kuvishikilia ni matusi kwa Mungu.
Kutokuwa Wa Maana
Waamini wengi wanakuwa na ukosefu wa usalama kuhusu
uwezo wao. Wanaugua kutokana na hofu mbaya ya
kushindwa. Neno la Mungu lasema,
Wafilipi 4:13 Naweza kuyafanya mambo yote katika Yeye
anitiaye nguvu.
2 Timotheo 1:7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali roho
ya nguvu, ya upendo na moyo wa kiasi.
Ni sharti tutangaze bila kukosa,
Ninaweza kutenda mambo yote katika Kristo
anitiaye nguvu.
Ninajua Mungu amenipa roho wa nguvu,
wa upendo na akili iliyo timamu.
Umbo la Nje
Wengi hujihisi kukosa usalama kuhusu umbo lao, wakiwaza
na hata kusema, “Mimi niko mnene sana,” “Mimi ni
mwembamba sana,” kama ttu nywele yangu ingekuwa rangi
tofauti,” “ningependa sana iwe nyofu.” Wao wana aibu au
huwazia sana juu ya umbo lao.
Utafiti unaonyesha kuwa karibu warembo wengi
wanaoshindana katika mambo ya urembo na wanaotawala
katika sinema huhusi kuwa kuna kitu wangependa
kubadilisha kuhusu umbo lao.
Katika maeneo yetu, kuna mkazo juu ya umbo la nje. Lakini
Neno la Mungu linadhihirisha kuwa sisi ni nafsi za kiroho
tulioumbwa katika sura ya Mungu. Tuliumbwa ili
kuonekana kama Mungu. Urembo wetu upo ndani ya roho
ya mtu – mwu mwenyewe – roho wetu aliye ndani yetu.
Tunaweza kuinu vichwa vyetu na kuachilia urembo na
mng’aro wa Yesu kuonekana usoni mwetu.
Wakati nabii Samueli alipokuja Bethlehemu kumpaka
mmoja wa watoto wa Yesse ili awe Mfalme atakayefuata,
alistaajabika sana na urembo wa mtoto wa kwanza. Nafasi
za heshima mara nyingi zilienda kwa mtoto wa kwanza wa
kiume, na basi mara tu aliona kuwa yeye huenda achakuliwe
na Mungu awe mfalme. Lakini Bwana alimzuia.
1 Samweli 16:7 Lakini Bwana akamwambia Samweli,
“Usitazame sura yake wala kimo chake, kwa kuwa nimemkataa.
Bwana hatazami katika vile vitu mwanadamu avitazamavyo.
Mwanadamu hutazama katika sura ya nje, lakini Bwana
hutazama moyoni.”
Kukosa Elimu
51
Wengine hujihisi kukosa usalama wanapokosa elimu; lakini,
Neno la Mungu linaonyesha kuwa katika Kristo, tumepata
hazina ya hekima na maarifa. Maarifa ya kweli ni kumjua
Mungu.
Wakolosai 2:2,3 …kusudi langu ni kuwa watiwe moyo na
kuunganishwa katika upendo, ili wapate kujua ulivyo utajiri wa
ufahamu kamili, waijue siri ya Mungu, yaani, Kristo mwenyewe,
ambaye ndani Yake kumefichwa hazina yote ya hekima na
maarifa.
Hisia za Kukataliwa
Ni kwa nini tunawaona waamini wengi leo wanaoteseka
katika kukataliwa, na hisia za kukataliwa, wakiwa na
majeraha ya kimawazo rohoni mwao?
Mungu alisema,
Waefeso 1:5-7 …alitangulia kutuchagua tuwe wanawe kwa njia
ya Yesu Kristo kwa furaha Yake na mapenzi Yake mwenyewe.
Kwa hiyo tunamsifu Mungu kwa huruma zake kuu alizotumiminia
kwa sababu sisi ni wa Mwanae Mpendwa. Katika Yeye tunao
ukombozi kwa njia ya damu Yake, yaani msamaha wa dhambi,
sawasawa na wingi wa neema Yake.
Ikiwa “tumekubalika katika Wapendwa,” basi tusiruhusu
hisia za kukataliwa kutujia. Basi lazima tuwe na ulinzi
katika maarifa yetu ya kukubali katika Yesu Kristo.
Mungu Baba anatukubali na upendo ule kama vile
anavyokubali Mwana Wake mwenyewe, Yesu. Lazima
tuyaweke chini mawazo ya kukataliwa na kutafakari juu ya
Neno hadi tuwe na hakikisho la kukubalika kwetu. Kwa
sababu Mungu anatukubali, tunaweza kuwakubali wengine.
Unyenyekevu wa Uongo
Mara nyingi kuna kiburi cha kiroho ambacho kimejitokeza
kwa miaka mingi ambacho kimakosa kimeitwa
kunyenyekea.
Tunaimba nyimbo kwa maneno kama”Mimi ni mwenye
dhambi aliyepotea na kuokolewa kwa neema.” Hiyo si
kweli. Mara tu tukiookoka hatuko tena wenye dhambi
waliopotea”!
Kwa miaka tuliimba maneno ya wimbo maarufu wa zamani
uliokuwa na msemo “kwa mdudu kama mimi.” Hivi sivyo
Mungu anavyotuona! Hii ni kinyume na Neno la Mungu.
Sisi si wadudu maskini wa mavumbi. Sisi ni viumbe wapya!
Tu ndani ya Kristo! Sisi tunabadilishwa kwa sura Yake.
Sura ya kibinafsi isiyo na maana kama vile kiburi inaweza
kuleta kushindwa maishani mwetu.
Kuwaza jinsi tusivyo na maana inaweza kuwa kielelezo cha
unyenyekevu, lakini inajenga ngome za kushindwa juu ya
52
maisha yetu ambayo hutuzuia kugundua uwezo wetu katika
Yesu Kristo.
Unyenyekevu Wa Kweli
Unyenyekevu wa kweli unatokana na kuitambua neema ya
Mungu. Unyenyekevu ni kutambua kuwa katika siku za
awali, tulipokuwa maadui wa Mungu, tusiostahili upendo
Wake mkuu, Alitukomboa ili tufanyike wale Alivyotuumba
tuwe.
Unyenyekevu wa kweli ni kuwaza mema kuhusu Mungu. Ni
kutambua kuwa yote tuliyo na yote tutendayo ni kwa ajili ya
neema Yake kuu na rehema juu yetu.
Ni kweli kuwa hatutakiwi “kuwaza juu yetu zaidi ya vile
tunaitajika,” na hata hivyo tusiwaze juu yetu wenyewe china
ya vile tunaitajika kuwa.
Ikiwa tutajiona kama Yesu na kutenda kazi ya Yesu, ni
lazima kwanza tuizushe chini ile sura ya zamani ya
kutokuwa wa maana, “siwezi tenda” na kuzibadili na sura za
kuumbwa upya.
KUIBADILI SURA YA UTUMWA
Wengi wanayo sura ya utumwa. Wanajiona wakiishi katika
ufukara ya mtumwa. Hajajiona wakipokea baraka na mali
kwa Mungu. Hajajiona kama wana wa Mfalme.
Mfano wa Wana wa Israeli
Misri, wana wa Israeli hawakujua chochote kando na
utumwa kwa mamia ya miaka. Kama wana wa Mungu
waliokombolewa, waliitaji ufunuo kuhusu wao ni nani kama
wana wa Mungu wa agano.
Dhahabu, Fedha
Mungu alitaka kuibadili sura yao ya binafsi kutoka
umaskini ya mtumwa hadi ile ya viumbe wapya ya wana wa
Mungu waliokombolewa. Aliwaamuru waulize Wamisri
dhahabu na fedha na vitambaa na vipuli vyenye gharama ya
juu.
Hawakutakiwa kuviweka dhahabu na fedha mbali katika
masanduku. Hawakutakiwa kuweka vitambaa vyenye
urembo na kwa ajili ya kuvitenga viwe salama waliposafiri
katika jangwa. Mungu aliwaamuru waweke fedha, na
dhahabu, na vitambaa juu ya watoto wao.
Kutoka 3:21,22a “Nami nitawapa hawa watu upendeleo mbele ya
Wamisri, kwa hiyo mtakapoondoka nchini hamtaondoka mikono
mitupu. Kila mwanamke Mwisraeli atamwomba jirani yake
Mmisri na mwanamke ye yote anayeishi nyumbani kwake ampe
vyombo vya fedha, dhahabu na nguo, ambavyo mtawavika wana
wenu na binti zenu.”
53
Wana Waisraeli – watu wa Mungu waliochaguliwa –
hawakutoka nje ya Misri wakiwa na matambara ya utumwa.
Mavazi na vyatu, ambavyo havikuisha wakiwa njiani
kuelekea nchi ya ahadi, yalikuwa mavazi na johari ya mali
nyingi.
Mungu aliibadili sura ya binafsi ya zamani. Alikuwa
akiivunja sura yao ya utumwa ya zamani.
Kupata Zaidi
Baadaye, wakati ulipofika wa kujenga mahali patakatifu,
palikuwa na dhahabu na fedha nyingi mikononi mwa wana
Waisraeli hata na kuwa walitoa vingi mno. Wakamwuliza
Musa kuwazuia wasotoe zaidi.
Kutoka 36:5-7 Ili kuja kumwambia Musa, “Watu wanaleta zaidi
kuliko mahitaji kwa ajili ya kazi hii ambayo Bwana ameagiza
ifanyike.”
Ndipo Musa akatoa agizo, nao wakapeleka neno hili katika kambi
yote: “Mtu ye yote mwanaume au mwanamke asilete tena kitu
chochote kwa ajili ya sadaka ya mahali patakatifu.” Hivyo watu
wakazuiliwa kuleta zaidi, kwa sababu walivyokuwa navyo tayari
vilitosha na kuzidi kuifanya kazi yote.
Katika njia hiyo hiyo Mungu aliibadili sura ya wana
Waisraeli wenyewe, anataka kuibadili sura yetu ya zamani
ya umaskini na utumwa katika dhambi. Angependa tupate
furaha ya wokovu.
KUYAZUSHA CHINI MAWAZO
Je, tunawezaaje kuiondoa sura ya zamani ambayo
haimpendezi Mungu?
Je, tunaweaje kukiondoa kifungo cha kutokuwa wa maana,
kukosa usalama, hisia za kutokutosheleza, lawama, hukumu
na kutokuwa wa dhamana?
Je, vipi tunaeweza kuyashughulikia mawazo haya ya
kudhania katika maisha yetu?
Neno la Mungu linatupa jibu.
2 Wakorintho 10:5 Tukiangusha mawazo na kila kitu
kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka
nyara kila fikira ipate kumtii Kristo.
Mawazo ya kudhania yapo akilini mwetu. Ni sharti
tuyaongoze mawazo yetu na kuzusha chini kila wazo
ambalo ni kinyume na Neno la Mungu.
Vita vipo akilini mwetu – katika roho zetu, katika fikira zetu
na katika uwezo wa kuchagua. Ni katika sehemu hizi ndipo
tutashinda vita au kushindwa. Mawazo yetu ni sharti
yafanywe upya kwa Neno la Mungu.
54
Ni sharti tuzilete kwenye utumwa kila wazo na kulifanya
kumtii Yesu. Ni sharti tuchukue uongozi na kuyafanya
mawazo yetu kutii ufahamu wa sisi ni nani katika Kristo.
Kama Nyoka
Ikiwa nyoka wa sumu kali angeanguka kutoka mtini na
kujikunja mkononi mwetu, hatutasimama hapo na
kumwangalia anapojiandaa kutuuma na kuweka sumu ndani
yetu. Hapana! Tutarusha mkono wetu mara moja na kwa
haraka tuwezavyo. Litakuwa jambo la ghafla, la uamuzi,
kitendo cha haraka. Tutamvuta chini nyoka huyo kabla
aume.
Vivyo hivyo, ni lazima, kwa dharau, tuyavute mawazo
yanayodhania chini ya sura ya zamani. Lazima tupige
kelele, “nakataa wazo hilo katika jina la Yesu!”
Wakati mawazo yetu ya zamani inaposema,
“Huwezi kufanya hilo wewe ni mwoga sana.”
Tunasema
“Nakataa wazo hilo katika jina la Yesu.
Ninaweza kufanya mambo yote katika Kristo anitiaye
nguvu.”
Wakati akili zetu za zamani zinaposema,
“Wewe una saratani.”
Tunasema,
“Nalikataa wazo hilo katika jina la Yesu.
Neno la Mungu linasema,
Hakuna pigo litakuja karibu na makao yangu.
Ninajua kuwa kwa mapigo ya Yesu mimi nimepona.”
Silaha Kuu
Tunazo silaha kuu za kuvunja ngome juu ya maisha yetu.
Mtume Paulo aliandika,
2 Wakorintho 10:4a Silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina
uwezo katika Mungu…
Tunasizusha na kukataa fikira zinazodhania na ambazo ni
kinyume na ufahamu wa Mungu, tunaziharibu nguvu zake
juu yetu.
55
KUIVUA SURA YA BINAFSI YA ZAMANI
Njia ya kuivua sura ya binafsi ya zamani inaelezwa na
mtume Paulo kama katika kitabu cha Wakolosai.
Wakolosai 3:9,10 Msiambiane uongo kwa maana mmevua kabisa
utu wenu wa kale pamoja na matendo yake, nanyi mmevaa utu
mpya unaofanywa upya katika ufahamu sawasawa na mfano wa
Mwumba wake.
Baadaye, kwa ufunuo wa Neno la Mungu, “kuvua mtu wa
zamani” na “tunavaa mtu mpya,” ambaye anafanywa upya
ufahamu katika sura ya Muumba.
Kuyafanya Upya Mawazo Yetu
Hatuwezi kuibadili jinsi roho yetu inavyofanya kazi kwa
hisia zetu wakati wa wokovu. Hiyo ni hatua ya kwanza tu.
Tunayafanya upya mawazo yetu na kubadilishwa katika
sura ya muumba tunapotafakari juu ya Maandiko.
Warumi 12:2 Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali
mgeuze kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na
kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema,
yanayopendeza machoni pake na ukamilifu.
Paulo aliandika kuwa mwanadamu ni sura na utukufu wa
Mungu.
2 Wakorintho 3:18 Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji
tunaakisi utukufu wa Bwana, kama kwenye kioo. Nasi
tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu
mkuu zaidi, utokao kwa Bwana, ambaye ndiye Roho.
Ikiwa tuliumbwa katika mfano wa Mungu, na kama viumbe
vipya tumerejeshwa katika sura ya Mungu, basi ni matusi
kwa Mungu kuendelea kusema mambo yaliyo kinyume
kutuhusu.
Tusiongee juu yetu kama vile tumefanya awali. Sisi ni
viumbe vipya. Tunabadilishwa kutoka utukufu hadi utukufu.
KUZUSHA CHINI SURA YA PANZI
Sura ya “Naweza-Kutenda”
Ikiwa tutaishi maisha ya Kikristo yenye ushindi,
yanayofaulu, inatupasa kuyabadili sura yetu ya “siwezitenda”
na ile ya “naweza-kutenda.” Ni bora kuelewa kuwa
tunaweza kutenda kile Neno la Mungu linasema tunaweza
kutenda.
56
Mfano wa Majasusi Kumi na Wawili
Mungu aliahidi kuwapa wana Waisraeli nchi ya Kanani.
Siku ikafika ambapo Mungu alisema atumwe mtu mmoja
kutoka kwa kila kabila kuitembelea nchi na kuleta taarifa.
Mwisho wa siku arobaini, wakarudi na taarifa yao.
Hesabu 13:27,28a,30-33 Wakampa Musa taarifa hii: “Tuliingia
katika nchi uliyotutuma, nayo inatirika maziwa na asali! Hili
hapa tunda lake.
“Lakini watu wanaoishi huko niwenye nguvu na miji yao ina
ngome na ni mikubwa sana.”
Sisi Tunaweza
Kisha Kalebu akawanyamazisha watu mbele ya Musa na
kusema, “Imetupasa kupanda na kuimiliki nchi, kwa maana
hakika tunaweza kufanya hivyo.”
Sisi Hatuwezi
Lakini watu waliokuwa wamepanda pamoja naye wakasema,
“Hatuwezi kuwashambulia wale watu, wana nguvu kuliko sisi.”
Wakaeneza taarifa mbaya miongoni mwa Waisraeli kuhusu nchi
walioipeleleza. Wakasema, “Nchi tulioipeleleza hula watu
waishio ndani yake. Watu wote tuliowaona huko ni majitu.”
“Tuliwaona Wanefili huko (wazao wa Anaki wanatokana na
Wanefili.) Tulijiona kama panzi machoni petu wenyewe, nao
ndivyo walivyotuona.”
Tofauti Ni Mungu
Kalebu na Yoshua walikuwa na ufunuo kuhusu Mungu
alikuwa nani. Walinena kama watu walio viumbe wapya
wanatakiwa kunena. Walisema, “hebu na twende mara moja
na kuinyakuwa nchi na mali, kwa maana tunaweza
kuishinda.”
Waliendelea,
Hesabu 14:8,9 Ikiwa Bwana anapendezwa nazi, atatuongoza
kuingia katika nchi ile, nchi itiririkayo maziwa na asali, naye
atatupa nchi hiyo.
Ila tu msimwasi Bwana. Wala msiwaogope watu wa nchi hiyo,
kwa sababu tutawameza. Ulinzi wao umeondoka, lakini Bwana
yupo pamoja nasi. Msiwaogope.
Watu wengine kumi waliona hali hiyo hiyo kama vile
Kalebu na Yoshua. Wao, hata hivyo, hawakuyaweka macho
yao kwa ukuu wa Mungu. Walitazama uwezo wao wa
kawaida na kujiona kama panzi. Wao walijiona kuwa na
“sura ya panzi.”
57
Uamuzi Wetu
Leo, tunaitajika kuzusha chini sura yetu ya panzi na
kuibadilisha na sura ya kuumbwa upya. Kama Kalebu na
yoshua, ni lazima tuweke imani yetu katika ukuu wa Mungu
na kuanza kusema, “tunaweza kabisa kuichukua nchi yetu!”
Kwa wengi, sura yetu ya zamani imekuwa kizuizi kikuu
kinachotuzuia kuwa, kupata, na kutenda yote Mungu
amekusudia kwetu kama viumbe vipya.
Nilazima kwa ujasiri tunene kwa mlima wa hali tofauti na
kusema, “Na uondoke na kutupwa baharini!”
Mathayo 21:21 Yesu akawajibu, “Amin, amin nawaambia, kama
mkiwa na imani wala msiwe na shaka, si kwamba mtaweza
kufanya tu yale yaliyofanyika kwa huu mtini, bali hata
mkiuambia huu mlima, ‘Ng’oka, ukatupwe baharini,’ nalo
litafanyika.
Silaha za vita vyetu ni kuu katika Mungu na kuvuta chini
ngome. Ngome za sura yetu ya binafsi ambayo itaporomoka
na kuanguka. Tutafanyika wale ambao Mungu amesema
tuko. Kama viumbe vipya, sura ya binafsi ya zamani itapita
na vitu vyote, na pia sura yetu tuliyogundua mpya,
itafanyika upya.
2 Wakorintho 5:17 Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo,
amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama, yamekuwa
mapya.
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Je, nini baadhi ya ngome za zamani za sura ya kibinafsi ambazo ume “yavuta chini” baada ya
masomo haya?
2. Eleza njia iliyotajwa katika Wakolosai 3:9,10 kama kuvua mtu wa zamani na kuvaa mtu
mpya.
3. Je, tunawezaje kuyafanya mawazo yetu upya kama ilivyotajwa katika Warumi 12:2?
58
Somo La Sita
Sura Yetu Katika Kristo
JAMII YETU KATIKA KRISTO
Kuzaliwa Upya
Wakati tunapokea Yesu Kristo kama Mwokozi,
“tumezaliwa mara ya pili” katika jamii ya mpya ya Mungu.
Yesu alimwambia Nikodemo,
Yohana 3:7 Kwa hiyo usishangae ninapokwambia huna budi
‘kuzaliwa mara ya pili.’
Yesu alimfafanulia Nikodema kuwa Yeye hakuwa
akizungumzia kuzaliwa kimwili, bali “kuzaliwa tena”
maana yake ni kuzaliwa katika roho.
Yohana 3:5,6 Yesu akamwambia, “Amin, amin nakuambia,
hakuna mtu yeyote anayeweza kuingia katika Ufalme wa Mungu
isipokuwa amezaliwa kwa maji na kwa Roho. Mwili huzaa mwili,
lakini Roho huzaa roho.”
Kabla ya kupokea Yesu kama Mwokozi, wakati tulikuwa
hai katika miili yetu (mifupa, nyama na damu) na nafsi
(akili, hangaiko la moyo na uwezo wa kuchagua) tulikuwa
tumekufa kiroho. Wakati wa wokovu “tulizaliwa mara ya
pili” kiroho. Roho zetu zilifanyika hai. Tulifanyika viumbe
wapya katika Yesu Kristo.
Tulizaliwa katika jamii mpya, jamii ya Mungu.
Tulipozaliwa katika jamii ya Mungu, tulifanyika Wana
wake.
Wana wa Mungu
Mtume Yohana aliandika,
1 Yohana 3:1a Oneni ni pendo kuu namna gani alilotupa Baba,
kwamba sisi tuitwe watoto wa Mungu!
Tukielewa kuwa tu watoto wa kiume na wa kike wa yule
aliye na nguvu sana, aliye na maarifa, Baba mwenye hekima
nyingi duniani, basi tutagundua kuwa maisha yetu, vyeo,
haki, manufaa, na mambo ya baadaye yamebadilika kabisa.
Kuelewa uhusiano wetu wa kijamii kama wana wa wa
Mungu inaweza kuibadili jinsi tunavyowaza kutuhusu.
Paulo aliandika,
Warumi 8:14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa
Mungu hao ndio watoto wa Mungu.
Tunapompokea Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi,
tunafanyika wana wa Mungu.
59
Yohana 1:12 Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa
kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio Jina Lake.
Neno “haki” maana yake mamlaka. Mara tu tunapoamini,
tunapata mamlaka kisheria kufanyika mwana wa kiume au
wa kike wa Mungu.
Wana wa Urithi wa Mungu
Mungu hajatufanya tu watoto Wake, pia ametupatia urithi
pamoja na zawadi kama vile Yesu. Sisi ni warithi pamoja na
Kristo.
Warumi 8:17a …basi ikiwa sisi ni watoto, basi tu warithi, warithi
wa Mungu, warithio pamoja Naye Kristo….
Mali na vitu vya Baba ni zaidi ya kipimo, na vyote alivyo
navyo Baba ni vya Mwana.
Je, linastaajabishaje kugundua kuwa sisi, baada ya kuzaliwa
katika jamaa ya Mungu, tumefanyika warithi pamoja na
Yesu Kristo. Urithi Wake wote umefanyika urithi wetu.
Utajiri wote wa mbinguni ni wa Yesu, na kwa sababu sisi tu
warithi pamoja Naye, basi utajiri wote mbinguni ni wetu.
Waefeso 1:3 Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu
Kristo aliyetubariki sisi kwa baraka zote za rohoni, katika
ulimwengu wa roho ndani ya Kristo.
Kupata Kushika Urithi Wetu
Kwa imani katika Yesu, tumezaliwa katika jamaa ya
Mungu, na kufanyika wana wa Mungu. Kama wana wa
Mungu, tunapokea urithi wa ahadi.
Wagalatia 3:26 Kwa maana ninyi nyote mmekuwa watoto wa
Mungu katika Kristo Yesu kwa njia ya imani.
Ezekieli 46:16 “Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: ‘Ikiwa mkuu
atawalaye atatoa zawadi kutoka kwenye urithi wake na kumpa
mmoja wa wanawe, hiyo zawadi itakuwa pia kwa wazao wake,
itakuwa mali yao kwa urithi.”
Kama viumbe wapya, ni lazima tunyakue vitu vyetu.
Lazima tupate kushika vyote vilivyo vyetu katika haki.
Kupokea Ufadhili Wetu
Ni jambo la kustaajabisha mno kugundua juu ya fadhili zetu
kama wana wa kiume na wa kike wa Baba wa mbinguni. Je,
ni furaha ilioje kugundua kuwa si lazima tungoje mpaka
tutakapofika mbinguni ndipo tuanze kufurahia urithi wetu.
Mtume Paulo aliandika,
Wafilipi 4:19 Naye Mungu wangu atawajaza ninyi kila
mnachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu ndani ya
Kristo Yesu.
60
Tunaweza kuanza kufurahia urithi sasa kama viumbe
wapya, kwani tayari “tumezaliwa upya” “katika jamaa ya
Mungu.”
Kama viumbe wapya, watoto wa Mungu, na warithi pamoja
na Yesu Kristo, hatustahili kulia na kumwomba Mungu
kujibu maitaji yetu hapa duniani. Vyote alivyonavyo Mungu
ni tayari vyetu. Kile tu tunaitajika kufanya ni kutambua jinsi
ya kupokea utajiri wa Mungu kwa imani na kutii.
Nguvu ya Kupata Utajiri
Musa alinena maneno haya kwa wana Waisraeli,
Kumbukumbu La Torati 8:18 Lakini kumbukeni Bwana Mungu
wenu, ndiye ambaye huwapa uwezo wa kupata utajiri na hivyo
kulithibitisha agano lake ambalo aliwaapia baba zenu, kama
ilivyo leo.
Asili ya Kutoa
Ni asili ya Baba kutoa.
Yohana aliandika,
Yohana 3:16a Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu
hata akamtoa ……
Kwa sababu tu watoto wa Baba, ni bora iwe ndani yetu asili
mpya ya watoaji.
Yesu alisema,
Luka 6:38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa. Kipimo cha kujaa
na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho
watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile
mpimacho, ndicho mtakachopimiwa.
Nyumba ya Uekezaji Baraka
Tunapotoa kwa Mungu kwa imani na kutii, tunampa Mungu
kipimo cha kutumia kutubariki. Kwa hivyo maitaji yetu yote
yanajibiwa kutoka kwa nyumba ya uekezaji ya urithi wetu
wa milele.
Katika kitabu cha Malaki tunasoma,
Malaki 3:10 “Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula
katika nyumba yangu. Nijaribuni katika hili, asema Bwana
Mwenye Nguvu, nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya
mbinguni na kuwamwagieni baraka nyingi mpaka mkose nafasi
ya kutosha au la.”
Je, ni furaha ilioje kujuwa kuhusu kupokea baraka zetu
kama viumbe vipya wana wa Mungu wa kiume na wa kike.
MWILI WA KRISTO
Kama viumbe wapya, sisi hatufanyiki tu sehemu ya jamii ya
Mungu, bali kwa muujiza wa kuzaliwa upya, tunafanyika
sehemu ya mwili wa Kristo.
61
Mtume Paulo aliandika,
1 Wakorintho 12:27 Sasa ninyi ni mwili wa Kristo na kila mmoja
wenu ni kiungo.
Waamini wote, kwa jumla, wanajumlisha mwili wa Kristo.
Sisi, kila mmoja, ni washirika wa mwili huo.
Sisi ni Sehemu ya Muhimu
Mungu anayo nafasi kwa kila mwamini katika mwili Wake.
Anayo kazi itambulikayo tuikamilishe.
Ms. 18 Lakini kama ilivyo, Mungu ameweka viungo katika mwili,
kila kimoja kama alivyopenda.
Tunawaitaji Wengine
Kila mwamini katika mwili wa Kristo anawaitaji wengine.
Ms. 21,22 Jicho haliwezi kuuambia mkono, “Sina haja nawe!”
Wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu, “Sina haja na
ninyi!”Lakini badala yake, vile viungo vya mwili vinavyoonekana
kuwa dhaifu, ndivyo ambavyo ni vya muhimu sana.
Ms. 26 Kama kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia
pamoja nacho, kama kiungo kimoja kikipewa heshima, viungo
vyote hufurahi pamoja nacho.
Kila sehemu ya mwili wa Mungu ni muhimu! Kama vile
mwili wa mwanadamu ulivyo na uwezo wa kulinda,
kusaidia, na kuumba, basi pia mwili wa Kristo.
NAFASI YETU KATIKA KRISTO
Wakati wa wokovu, Roho Mtakatifu alitubatiza katika Yesu
Kristo. Kwa muujiza kwa kuzaliwa upya, tulifanyika wa
katibu na Yesu. Tuliunganishwa pamoja Naye.
1 Wakorintho 12:13 Kwa maana katika Roho mmoja wote
tulibatizwa katika mwili mmoja, kama ni Wayahudi au Wayunani,
kama ni watumwa au watu huru, nasi sote tulinyweshwa Roho
mmoja.
Neno Ubatizo maana yake ni:
Ni kutambulika kabisa na
Wakati wa wokovu, tunatambulika na Yesu Kristo.
Wakati kipande cha kitambaa cheupe kinapowekwa katika
rangi nyekundu, kitambaa huchukua rangi hiyo.
Inakubaliana na rangi hiyo kwa sababu “inabatizwa” ndani
yake. Katika hali hiyo hiyo, roho zetu huchukua hali ya
Mwana wa Mungu tunapobatizwa ndani Yake na Roho
Mtakatifu wakati wa wokovu. Tunatambulika Naye kabisa –
kushikamana Naye kwa karibu-sehemu ya mwili Wakepamoja
Naye.
62
Yote alivyo Yesu, sisi tupo!
Vyote alivyo navyo Yesu ni vyetu!
Yote tulivyo na kuwa navyo ni
kwa sababu tu ndani Yake.
Kama inavyofundishwa katika Waefeso
Paulo alitaja nafasi zetu na vilivyo vyetu “katika Kristo”
mara nyingi katika sura tatu za mwanzo katika barua yake
kwa Waefeso.
Kubarikiwa na Baraka za Kiroho
Aliandika kuwa tumebarikiwa na kila baraka ya kiroho
katika Kristo.
Waefeso 1:3 Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu
Kristo aliyetubariki sisi kwa baraka zote za rohoni, katika
ulimwengu wa roho ndani ya Kristo.
Baraka zote za mbinguni zenye utajiri, utukufu, na
zinazotosheleza zipo kwa ajili yetu ili tupokee na kufurahia
maishani mwetu kila ziku.
Kuchaguliwa ndani Yake
Baba alimchagua Yesu. Yeye ni yule Aliyechaguliwa. Kwa
sababu sisi tu ndani Yake, basi tunashiriki katika
kuchaguliwa Kwake.
Waefeso1:4 Kwa maana alituchagua katika Yeye kabla ya
kuumbwa ulimwengu ili tuwe watakatifu na bila lawama mbele
Zake.
Mungu hakutuchagua kwa ajili ya sura zetu, uwezo, au
umuhimu wetu wa kibinafsi. Alituchagua kwa sababu mile
tangu, alituona katika Kristo.
Kutengwa Ndani Yake
Tunashiriki katika Mwisho Wake kwa sababu tu ndani
Yake.
Waefeso 1:5 Kwa upendo alitangulia kutuchagua tuwe wanawe
kwa njia ya Yesu Kristo kwa furaha Yake na mapenzi Yake
mwenyewe.
Hatujatengwa ili tuwe na Mungu milele kwa sababu Yeye
anatupenda zaidi ya vile anawapenda wengine. Baba
angetazama katika vizazi na kutuona katika Kristo.
Alituchagua kwa sababu alimchagua Kristo, nasi tu wamoja
Naye.
Urithi wetu na kutengwa kwetu ni kwa sababu ya nafasi
yetu katika Yesu Kristo.
Waefeso 1:11 Katika Kristo sisi nasi tumepata urithi, tukiisha
kuchaguliwa sawasawa na kusudi la Mungu, Yeye ambaye
hufanya mambo yote kulingana na mapenzi Yake.
Kukubalika ndani Yake
63
Tumekubalika katika Mpendwa. Kukubalika kwetu na Baba
ni kwa sababu tuko ndani ya Kristo.
Waefeso 1:6 Kwa hiyo tunamsifu Mungu kwa huruma zake kuu
alizotumiminia kwa sababu sisi ni wa Mwanae Mpendwa.
Kukombolewa kwetu, kusamehewa, na utajiri wote wa
neema Yake ni kwa sababu tuko ndani Yake.
Waefeso 1:7 Katika Yeye tunao ukombozi kwa njia ya damu
Yake, yaani, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa
neema Yake.
Tumefunikwa ndani Yake
Tumewekwa na mhuri wa Roho Mtakatifu kwa sababu
alituunganisha, na milele kutufanya moja na Yesu Kristo.
Waefeso 1:13 Ninyi pia mliingia ndani ya Kristo mliposikia Neno
la kweli, Injili ya wokovu wenu. Mkiisha kuamini, ndani yake
mlitiwa muhuri, kwa yule Roho Mtakatifu wa ahadi
mliyeahidiwa.
Kuketi Pamoja Naye
Kwa sbabu tu moja Naye, tumeketi pamoja Naye mbinguni.
Waefeso 2:6 Mungu alitufufua pamoja na Kristo na kutuketisha
pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu.
Hata kama tunaishi katika mili yetu hapa duniani, katika
Kristo tumeketi mbinguni. Yesu alipokamilisha kazi Yake
ya ukombozi, aliketi katika mkono wa kuume wa Baba.
Zaburi 110:1 Bwana amwambia Bwana wangu: “Keti mkono
wangu wa kuume, mpaka niwafanye adui zako kuwa mahali pa
kuweka miguu yako.”
Paulo alidhihirisha kuwa tumeketi Naye mahali.
Tunafurahia faida zote ya kazi Yake iliyokamilika hapa
duniani. Sisi, kwa imani, tunafurahia kila wakati pumziko
lipatikanalo kwa kila mwamini, hata katika dhoruba
maishani.
Kazi Nzuri ndani Yake
Tumeumbwa katika Kristo Yesu kwa kazi nzuri.
Waefeso 2:10 Kwa maana sisi ni kazi ya mikono ya Mungu,
tulioumbwa katika Kristo Yesu, ili tupate kutenda matendo
mema, ambayo Mungu alitangulia kuyaandaa tupate kuishi katika
hayo.
Adamu na Eva waliumbwa kwa kusudi, nasi katika Kristo
tumeumbwa kwa kusudi hilo pia. Tumeumbwa kutenda kazi
Yake hapa duniani. Sisi ni mwili wa Kristo utendao kazi
hapa duniani mahali Pake.
Yesu alipokuwa hai na akihudumu dunaiani, aliwaambia
waamini Wake,
64
Yohana 14:12 Amin, amin, nawaambia, ye yote aniaminiye Mimi,
kazi nizifanyazo yeye atazifanya, naam na kubwa kuliko hizi
atazifanya, kwa sababu Mimi ninakwenda kwa Baba.
Kama waamini katika Kristo, sisi tu mwili wa Yesu. Sisi tu
miguu Yake, nyayo, na mikono Yake hapa duniani. Kama
mwili wa Yesu sisi tunaendelea kutenda kazi Yake leo.
Mwili wa Kristo:
Huwakilisha Kristo ulimwenguni
Huleta upendo wa Mungu ulimwenguni
Huleta uponyaji wa Mungu na ukombozi
Huleta watu katika ufahamu wa Mungu uokoao
Kufanywa Kumkaribia
Sisi, tuliokuwa adui wake na mabali sana Naye,
“tumefanywa karibu” kwa damu Yake kwa sababu tu ndani
Yake.
Waefeso 2:13 Lakini sasa katika Kristo Yesu, ninyi ambao hapo
kwanza mlikuwa mbali na Mungu, sasa mmeletwa karibu kwa
njia ya damu ya Kristo.
Sasa tunaweza kufurahia, ushirika wa karibu unaoendelea
pamoja Naye.
Kufanyika Moja
Tunapoumbwa ndani Yake, uadui wote kati yetu na Mungu
uliondolewa. Sisi wawili ghafla tukafanyika moja.
Waefeso 2:15 Kwa kuibatilisha ile sheria pamoja na amri zake na
maagizo yake alipoutoa mwili wake, ili apate kufanya ndani yake
mtu mmoja mpya badala ya hao wawili, hivyo akifanya amani.
Mtu aliyeumbwa upya hawezi kutenganishwa na Yesu na
amani Yake, kadri anapoendelea kuwa ndani Yake.
Hekalu Takatifu
Ndani Yake, tunajengwa pamoja kama hekalu takatifu,
kama pahali anapokaa Mungu Mwenyewe.
Waefeso 2:20-22 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na
manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ndiye jiwe kuu la pembeni.
Ndani Yake jengo lote limeshikamanishwa ili kuwa hekalu
takatifu katika Bwana. Katika Yeye ninyi nanyi mnajengwa
pamoja ili mpate kuwa makao ambayo Mungu anaishi ndani yake
kwa njia ya Roho Wake.
Je, ni furaha ilioje kugundua kuwa Mungu amechagua
kukaa nasi hapa duniani. Amechagua kuishi ndani yetu kila
mmoja na kuishi ndani yetu kama kanisa Lake.
65
Ujasiri – Katika Uhuru ndani Yake
Kwa sababu tu ndani Yake, pamoja Naye, kuunganika
kabisa Naye, kama viumbe wapya tunashiriki katika yote
alivyo na vyote Alivyo navyo..
Haki Yake imefanyika haki yetu. Mwisho Wake
umefanyika mwisho wetu. Uhai Wake umefanyika uhai
wetu.
Wakati tulipokea ufunuo wa kuzaliwa upya, tunaweza
kusema kwa ujasiri,
Ninajua mimi ni nani katika Kristo!
Nnimefanyika pamoja Naye!
Sasa nina shiriki haki Yake,
Ajali Yake, na uhai Wake!
Mimi ni kiumbe kipya!
Mambo ya zamani yamepita!
Vitu vyote vimefanyika vipya!
Waefeso 3:12 Yeye ambaye ndani Yake na kwa njia ya imani
katika Yeye tuweze kumkaribia Mungu kwa ujasiri na kwa uhuru.
Tunaweza kuja kwenye uwepo Wake kwa ujasiri kwa uhuru
kwa sababu tu ndani Yake, basi hatuko tena katika hukumu
au lawama. Sisi ni viumbe vipya. Sisi ni haki Yake Mungu
katika Yesu Kristo.
Wana wa Mwanga
Yesu alikuwa Mungu katika mwili. Yesu alitumwa katika
dunia hii ya giza la kiroho kama nuru ili kuonyesha upendo
wa Mungu na nguvu kwa wale watakaoamini ndani Yake.
Yohana 8:12 Kisha Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi
ni nuru ya ulimwengu. Mtu ye yote akinifuata hatatembea gizani
kamwe bali atakuwa na nuru ya uzima.”
1 Wathesalonike 5:5 Ninyi nyote ni wana wa nuru na wana wa
mchana. Sisi si wana wa giza wala wa usiku.
Waamini waishi kama wana wa mwanga. Inawapasa waishi
katika ushindi kulingana na nuru ya ufunuo wa Neno la
Mungu. Paulo anatuagiza kwa kusema,
Waefeso 5:8 Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, lakini sasa
ninyi ni nuru katika Bwana. Enendeni kama watoto wa nuru.
Kuoshwa, Kutakaswa, kuthibitishwa
Kama viumbe wapya, tumewekwa huru kutoka kwa dhambi.
Tumeoshwa, kutakaswa, na kuthibitishwa.
1 Wakorintho 6:10,11 …wala wezi, wala wenye tamaa mbaya,
wala wafiraji, wala walafi, wala walawiti, wala wanaodhihaki,
wala wanyang’anyi. Baadhi yenu mlikuwa kama hao. Lakini
66
mlioshwa, mlitakaswa, mlihesabiwa haki kwa jina la Bwana
Yesu Kristo na katika Roho wa Mungu wetu.
Kuoshwa, ni kufanywa safi. Mungu hataruhusu uchafu
mbele ya uwepo Wake. Haki kamili haiwezi kukaa na
dhambi.
1 Yohana 1:7 Lakini tukienenda nuruni, kama Yeye alivyo nuruni,
twashirikiana sisi kwa sisi na damu yake Yesu, Mwana Wake
yatasafisha dhambi yote.
“Kutakaswa” hueleza uhusiano watu wanaweza kupata kwa
Mungu kwa imani katika Kristo. Ina maana kuwa
tumewekwa mbali na uovu, na kutengwa kwa ajili ya
Kristo. Tumetengwa na ulimwengu, na tuna uhusiano na
Mungu unaotokana na haki Yake ndani yetu.
Tumeoshwa na kutakaswa. Pia tumefanywa haki.
Kuthibitishwa ina maana kutangazwa kisheria kuwa haki na
Mungu. Tu wenye haki; roho zetu ni kamilifu mbele za
Mungu. Katika Kristo sisi tu viumbe wapya. Dhambi za
awali zimetoweka – zimeoshwa katika damu ya Yesu.
Warumi 3:28 Kwa maana twaona kwamba mwanadamu
huhesabiwa haki kwa njia ya imani wala si kwa matendo ya
sheria.
Warumi 8:31b,33 Ikiwa Mungu yuko upande wetu, ni nani
awezaye kuwa kinyume chetu?
Ni nani atakayewashtaki wale ambao Mungu amewachagua? Ni
Mungu mwenyewe ndiye mwenye kuwahesabia haki.
Wakati Shetani na umati wake wanapokuja na
kutukumbusha yaliyopita, lazima tuseme,
Sahau hayo, Shetani,
Nimeoshwa, kutakaswa, na kuthibitishwa!
Mimi ni kiumbe kipya!
Mambo ya zamani yamepita!
Vitu vyote vimefanyika upya!
URAIA WETU MPYA
Haki Zetu
Kama viumbe wapya, tunao uraia mpya.
Raia wa nchi amehakikishiwa haki fulani za kitaifa chini ya
katiba ya taifa. Katiba ni sheria tamati ya nchi. Sheria
zingine zote za taifa hutegemea haki za kimsingi za
kikatiba. Tusipojua haki zetu, tunaweza kunyanyaswa na
watu wapotovu.
Kama viumbe wapya, tumepewa haki za kitaifa nyingi,
lakini tunaweza kunyanyaswa na shetani. Tunaweza
kuteseka bila sababu. Kuwa kiumbe kipya haimaanishi
67
kuwa tutafurahia baraka zetu zote za kiroho, lakini hutupatia
haki kisheria kuziagiza.
Silaha Zetu
Katika dunia hii, Shetani amenyakuwa haki zetu kama
viumbe wapya. Lakini, Mungu ametupatia silaha za kiroho
tunazoitaji kurejesha haki hizo.
Paulo aliandika kuwa silaha zetu si za hapa duniani, na
kuwa zina nguvu za kiungu, zenye nguvu hata kuvuta
ngome chini.
2 Wakorintho 10:4 Silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina
uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome.down strongholds...
Ngome ni kama eneo lililotengwa kama boma. Inashikilia
sana juu ya hali zote, fikira, watu au mashirika. Inaweza
kuwa ngome ambayo Shetani amejenga juu ya afya au
fedha. Hata iwe ngome ya aina gani, tuna silaha za kuizusha
chini!
Ili Kutekelesha Kikamilifu
Hakuna silaha iliyo kamili iwapo haitatumika.
Iwapo adui angemshambulia mtu aliyejihami, bado
atamwumiza ikiwa mtu huyo hatatumia silaha zake. Mtu
aliyeshambuliwa anaweza kujihami toka kichwani hadi
vidole miguuni, lakini asipotumia silaha zake, anaweza
kushindwa.
Ni vivyo hivyo kwetu sisi kama viumbe wapya. Tunaweza
kufikia silaha tutakazoitaji kumshinda adui, lakini lazima
tuzitambue na pia jinsi ya kuzitumia.
Kueleza kwa Wazi
Paulo alieleza silaha na sana za vita kwa kiumbe kipya
katika kitabu cha Waefeso.
Waefeso 6:11-17 Vaeni silaha zote za Mungu ili kwamba mweze
kuzipinga hila za Shetani.
Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali
dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya
pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Kwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kushindana siku
ya uovu itakapokuja nanyi mkiisha kufanya yote, simameni
imara.
Kwa hiyo simameni imara mkiwa mmejifunga kweli kiunoni na
kuvaa dirii ya haki kifuani, nayo miguu yenu ifungiwe utayari
tuupatao kwa Injili ya amani. Zaidi ya haya yote, twaeni ngao ya
imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye
moto ya yule mwovu. Vaeni chapeo ya wokovu na mchukue
upanga wa Roho, ambao ni Neno la Mungu.
Silaha Moja Ya Kupigana
68
Kuna silaha aina mbili za kawaida, za kujikinga na
kupigana. Baadhi ya silaha ni za kujikinga
tunaposhambuliwa, na moja ni kwa ajili ya kumshambulia
adui.
Upanga wa Roho – Neno la Mungu – ni silaha ya kupiga
iliyotajwa katika kifungu hiki cha maelezo. Tunaponena
Neno la Mungu kwa imani, ibilisi lazima aachilie. Yeye
hana kinga dhidi ya silaha hii.
Mungu ametupatia silaha hii, lakini lazima tujifunze
kuitumia. Kama viumbe wapya, lazima tunene Neno la
Mungu kwa hali ambazo zinajaribu kutuvuta chini.
Kumalizia
Tunayo sura Mpya katika Kristo.
Kwa muujiza wa kuzaliwa upya, tumezaliwa katika jamii ya
Mungu. Kama wana wa Mungu wa kiume na wa kike,
tumefanyika warithi pamoja na Kristo. Vyote vilivyo vyake
sasa ni vyetu kushiriki.
Tuko ndani Yake, na kwa sababu ya cheo chetu kipya,
tumebarikiwa na baraka zote za kiroho, kuchaguliwa,
kukusudiwa, kukubalika, kufunikwa, na kuketi pamoja
Naye.
Tumeumbwa katika Kristo kutenda matendo Yake mema
hapa duniani. Sisi, tuliokuwa adui Wake wakati fulani,
tumeruhusiwa kuwa na ushirika wa karibu pamoja Naye.
Sisi ni hekalu Lake takatifu. Tuna ujasiri mpya na uhuru
kwa sababu ya imani yetu ndani Yake.
Sisi tuliokuwa gizani sasa tunaelezwa kuwa watoto wa nuru.
Tumeoshwa, kutakaswa, na kuthibitishwa. Tunazo haki za
utaifa kama viumbe wapya. Lazima tuvae silaha kamili ya
Mungu ili kurejesha urithi wetu, faida zetu, na haki zetu
kama viumbe wapya katika Yesu Kristo.
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. je, ni nini maana ya kuzaliwa upya?
2. Je, ina maana gani kwako “ndani ya Kristo”?
3. Je, ina maana gani kwako kuwa sehemu ya watoto wa nuru?
69
Somo La Saba
Haki za Kuumbwa Upya
KAMA WATOTO WA IBRAHIMU
Mtume Paulo aliandika kuwa ikiwa sisi ni wa imani, sisi ni
watoto wa Ibrahimu. Hii ni ya muhimu kwa sababu kama
watoto wa Ibrahimu, tunazo haki nyingi na fursa za kihaki.
Wagalatia 3:6,7 … Kama vile Abrahamu, “Yeye alimwamini
Mungu ikahesabiwa kwake kuwa haki.” Hivyo basi mjue kwamba
wale wanaomwamini Mungu hao ndio watoto wa Abrahamu.
Haki ya Ibraham
Mungu alimtazama Ibrahimu kama mwenye haki sio kwa
sababu ya matendo yake mema, maisha ya kipekee, au faida
yake kuu, bali kwa sababu Ibrahimu alikuwa na imani.
Ibrahimu hakuwa amekamilika, lakini alikuwa mwenye haki
kwa ajili ya imani yake.
Si lazima tuwe tumekamilika ili kuwa na haki yake Mungu.
Hata hivyo, lazima tumwamini Mungu na kupokea haki
Yake kwa imani, kama vile Ibrahimu alifanya.
Katika ulimwengu wa unaoonekana, sisi ni wa baba wetu
wa hapa duniani, kuzaliwa katika jamii inayolibeba jina
lake. Tunapozaliwa tena katika imani, tunazaliwa katika
jamii ya imani na tunayo haki ya kutumia jina la jamii –
jamii ya Ibrahimu.
Ahadi Zake Mungu kwa Ibrahimu
Mungu alipomwita Abramu (baadaye akaitwa Ibrahimu)
kutoka Haran, alimpa ahadi nyingi; na kwa sababu tu katika
jamii ya Ibrahimu, tunaweza kushiriki katika ahadi hizi.
Mwanzo 12:1-3 Bwana akawa amemwambia Abramu, “Ondoka
katika nchi yako, waache watu wako na nyumba ya baba yako,
uende mpaka nchi nitakayokuonyesha.”
“Mimi nitakufanya taifa kubwa na nitakubariki, Nitalikuza jina
lako, nawe utakuwa baraka. Nitawabariki wale wanaokubariki,
ye yote akulaaniye nitamlaani na kupitia kwako mataifa yote
duniani yatabarikiwa.”
Sisi tumehesabika katika baraka za Ibrahimu! Tunaweza
kuzichukua ahadi hizi kuwa zetu.
Ukoo Wake
Mungu alimwahidi Ibrahimu idadi kubwa ya uzao. Mbegu
yake ingekuwa kama nafaka ya mavumbi duniani – kwa
kuguzia mbegu yake ya kimwili.
70
Mwanzo 13:16 Nitaufanya uzao wako uwe mwingi kama
mavumbi ya nchi, hivyo kama kuna ye yote awezaye kuhesabu
mavumbi, basi uzao wako utahesabika.
Mungu pia alimwambia Ibrahimu kuwa ukoo wake
watakuwa wengi kama vile nyota angani – kuguzia mbegu
yake ya kiroho kwa imani.
Mwanzo 15:5 Akamtoa nje na kusema, “Tazama juu kuelekea
mbinguni na uhesabu nyota, kama hakika utaweza kuzihesabu.”
Ndipo akamwambia, “Hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.”
Agano Linalodumu Milele
Mungu aliweka agano la kudumu na Ibrahimu na ukoo
wake. Kwa imani, sisi ni ukoo wake na tu sehemu ya agano
hili la kudumu.
Mwanzo 17:7 Nitalithibitisha agano langu kama agano la milele
kati yangu na wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo
niwe Mungu wako na Mungu wa wazao wako.
Yesu, mbegu ya Ibraham
Tukiwa ndani ya Yesu, sisi ni warithi katika ahadi za baraka
ya Mungu kwa Ibraham. Sisi tu warithi katika agano la
Ibrahamu.
Wagalatia 3:16 Ahadi zilinenwa kwa Abrahamu na kwa mzao
wake. Maandiko hayasemi, “Kwa wazao,” likimaanisha watu
wengi, bali “Ni kwa mzao wako”, yaani mtu mmoja, ndiye Kristo.
Wagalatia 3:29 Nanyi mkiwa ni mali ya Kristo, basi ninyi ni wa
uzao wa Abrahamu na warithi sawasawa na ile ahadi.
BARAKA ZETU KATIKA IBRAHAMU
Sisi ni watoto wa Ibrahamu – ukoo wake wa kiroho – na
kwa imani tunaweza kupokea baraka. Ikiwa ni lazima
tupokee baraka hizi kwa imani, ni lazima tuzitambue.
Orodha ya Baraka
Kumbukumbu La Torati 28:1-14 Kama ukimtii Bwana Mungu
wako kwa bidii na kufuata amri zake zote ninazokupa leo kwa
bidii, Bwana Mungu wako atakuweka juu ya mataifa yote katika
dunia. Baraka hizi zote zitakuja juu yako na kukupata, kama
ukimtii Bwana Mungu wako:
Utabarikiwa mjini na utabarikiwa mashambani. Utabarikiwa uzao
wa tumbo lako, mazao ya nchi yako na wanyama wako,
wachanga wa kufugwa, ndama wa makundi yako ya ng’ombe na
wanakondoo wa makundi yako. Kapu lako na vyombo vyako vya
kukandia vitabarikiwa. Utabarikiwa uingiapo na utabarikiwa
utokapo.
71
Bwana atakujalia adui wainukao dhidi yako watashindwa mbele
yako. Watakujia kwa njia moja lakini watakimbia mbele yako
kwa njia saba.
Bwana ataagiza baraka juu ya ghala zako na juu ya kila kitu
utakachogusa kwa mkono wako. Bwana Mungu wako
atakubariki katika nchi anayokupa.
Bwana atakufanya kuwa taifa lake takatifu kama alivyokuahidi
kwa kiapo, kama ukishika maagizo ya Bwana Mungu wako na
kwenda katika njia zake. Kisha mataifa yote ya dunia wataona
kuwa unaitwa kwa jina la Bwana, nao watakuogopa.
Bwana atakupa kustawi kwa wingi, katika tunda la uzao wa
tumbo lako, wanyama wachanga wa mifugo yako na mazao ya
ardhi yako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwapa.
Bwana atafungua mbingu, ghala zake za baraka, kukupa mvua
kwa majira yake na kubariki kazi zako zote za mikono yako.
Utakopesha mataifa mengi lakini hutakopa kwa ye yote. Bwana
atakufanya kichwa, wala si mkia. Kama utazingatia maagizo ya
Bwana Mungu wako ninayokupa siku hii ya leo na kuzifuata kwa
bidii, daima utakuwa juu, kamwe hutakuwa chini. Usihalifu amri
zangu zo zote ninazokupa leo, kwa kwenda kuume au kushoto,
kwa kufuata miungu mingine na kuitumikia.
Zimepewa Kwetu
Ahadi hizi alipewa Ibrahimu kwanza, kisha kwa ukoo wake
wa kimwili, na kisha zikapewa ukoo wake wa kiroho – wale
ambao ni wa imani.
Wagalatia 3:6,7,14 …. Kama vile Abrahamu, “Yeye alimwamini
Mungu ikahesabiwa kwake kuwa haki.” Hivyo basi mjue kwamba
wale wanaomwamini Mungu hao ndio watoto wa Abrahamu.
... ili kwamba baraka aliyopewa Abrahamu ipate kuwafikia watu
Mataifa kwa njia ya Kristo Yesu, ili kwa imani tupate kupokea ile
ahadi ya Roho.
Kwa Leo
Gundua kuwa ahadi alizopewa Ibrahimu ni za sasa, sio
tutakapofika mbinguni. Ni za leo.
Hebu tuchukue muda kumshukuru Mungu kwa ajili ya
baraka zetu za kuumbwa upya.
Baba, nakushukuru kuwa nimebarikiwa jijini
na kubarikiwa mashambani.
nimebarikiwa popote nilipo.
Nakushukuru kuwa matunda ya uzao wangu
imebarikiwa,
watoto wangu wamebarikiwa.
Nakushukuru Bwana
kuwa mifugo wangu wamebarikiwa nawe.
72
Nakushukuru Bwana
kuwa kikapu changu kimejaa
kuwa nina chakula cha kila siku.
Nakushukuru Bwana kuwa nimebarikiwa
ninapoingia na kubarikiwa ninapotoka nje.
Ninajua kuwa adui anapojaribu kuja
dhidi yangu, tayari ameshindwa.
Atakuja dhidi yangu kutoka upande mmoja,
lakini atatimuka katika pande saba.
Bwana,nakushukuru kuwa yote nifanyayo itadumu.
Ninaenda kutembea katika njia zako,
kesho, na kila siku ya maisha yangu.
Nakushukuru Bwana kuwa watu wataona
jinsi ulivyo mkuu maishani mwangu.
Nakushukuru Bwana kuwa utanipa
maendeleo makuu.
Nakushukuru Bwana kuwa umefungua
nyumba ya baraka mbinguni,
na kuwa ninaweza kuipokea hapa duniani.
Nakushukuru Bwana kuwa numenifanya
niwe kichwa na si mkia –
umeniweka juu na wala si chini.
Ewe Baba, nakushukuru kwa baraka zako zote!
Sitaacha kukufuata, Bwana.
sitawatumikia miungu wengine.
Nitaziweka amri zako.
Katika jina la Yesu, Amina
UHURU KUTOKANA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI
Kuokolewa kwa Neema
Paulo alitaja kuwa dhambi haina tena mamlaka ya kisheria
juu ya wale wanaokiri Yesu kama Bwana na Mwokozi wao.
Basi hatuishi tena chini ya sheria. Tumeokoka –
kukombolewa – si kwa sheria, bali kwa neema.
Warumi 6:14 Kwa maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu
yenu, kwa sababu hampo chini ya sheria, bali chini ya neema.
Waefeso 2:8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya
imani, wala hii si kwa matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka
kwa Mungu.
Maelezo ya neema ni kuwa ni kupewa usichositahili – kitu
tunachopewa tusichostahili.
Sio tu kuwa hatukustahili mapenzi ya Mungu, tulistahili
kinyume cha hii. Waume kwa wake hawangeweza kuitimiza
73
sheria; na kwa hiyo, haingewaletea wokovu – ingeleta tu
mauti.
Kuokolewa maana yake kuokolewa kutoka kwa kitu au
kukombolewa kutoka kwa kitu. Je, tumekombolewa kutoka
kwa kitu gani?
Huru Kutokana na Laana
Basi hatuko tena chini ya sheria ya dhambi na mauti, na
hatuko tena chini ya laana ya sheria. Tumekombolewa
kutokana na laana ya sheria; hata hivyo, tusipotambua haki
zetu kama viumbe wapya, wakati Shetani au roho wa pepo
wake wajapo kuweka laana juu yetu, tunaweza kushindwa.
Lakini, tunapotambua haki zetu za kuumbwa upya,
tunaweza kushinda kila vita.
Wakati mambo haya yanakuja dhidi yetu yakionekana kama
sehemu ya laana, tunaweza kusema kwa ujasiri,
Nimekombolewa kutoka kwa laana ya sheria.
Yesu Alifanyika Laana
Yesu alifanywa laana hii kwa ajili yetu! Yeye alichukua
laana hizi juu ya mwili Wake kwa niaba yetu ili
kutukomboa kutoka kwa laana hizi! Alituweka huru
kutokana na kila aina ya laana hizi za kisheria alipolipia
adhabu yetu msalabani.
Wagalatia 3:13 Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria
kwa kufanyika laana kwa ajili yetu, (kwa maana imeandikwa,
“Amelaaniwa yeye aangikwaye juu ya mti.”)
Yesu pekee ndiye aliyeweza kuiweka sheria kikamilifu.
Aliishi maisha makamilifu chini ya sheria na akafanyika
kafara iliyokamilika.
Kukombolewa Kutoka kwa Laana
Ni muhimu kufahamu yanayojumlishwa chini ya laana. Je,
Yesu alibeba nini kwa ajili yetu? Je, laana ya kisheria ni
nini? Tunapojifunza sehemu hii, tutagundua kuwa
tumekuwa tukikubali vitu kutoka kwa Shetani ambavyo
haitupasi kupokea.
Musa aliorodheshwa kuwa vitu vilivyo sehemu ya laana
katika Kumbukumbu la Torati 28:15-68. (Itakuwa bora
kusoma sehemu hii yote) Musa pia aliorodhesha laana
zitokanazo na kutokutii na ifuatayo ni kwa kifupi.
Kumbukumbu La Torati 28:15,20 Hata hivyo, kama hutamtii
Bwana Mungu wako na kuzishika kwa bidii amri zake zote na
maagizo ninayokupa leo, laana hizi zote zitakuja juu yako na
kukupata:
Bwana ataleta laana juu yako, fadhaa na kukaripiwa katika kila
kitu unachokigusa kwa mkono wako, mpaka umeangamia na
74
kuharibika ghafula kwa ajili ya maovu uliyoyafanya kwa
kumwacha yeye.
Je, laana za sheria ni zipi? Je, adhabu ya kutokutii sheria ni
ipi?
Maradhi
Homa, inayowasha
Joto kuu na kiangazi
Uharibifu kwa mimea
Anga ya shaba
Ardhi ya chuma
Mvua hugeuka vumbi na majivu
Kushindwa
Miili hufanyika chakula cha ndege na wanyama
Ngozi kuwasha, upele, na maradhi ya ngozi
Wazimu, upofu, kuchanganyikiwa akili
Kushindwa katika yote tufanyayo, kuteswa, kuibiwa
Kupoteza Wapendwa, nyumba, matunda ya kikazi
Kupoteza mali, watoto
Huu ni mwanzo tu wa orodha!
Kuangalia katika Maisha ya kawaida
Sasa, chukua muda usome laana za kisheria katika
Kumbukumbu la Torati tena, lakini wakati huu kumbuka
kuwa Yesu amekukomboa kutokana na laana ya sheria na
uongeze maneno, “Yesu amenikomboa kutoka kwa
____________ . Kwa mfano,
Yesu amenikomboa kutokana na magonjwa.
Yesu amenikomboa kutokana na maradhi yanayoua.
Yesu amenikomboa kutokana na homa na mwasho.
Yesu amenikomboa kutokana na jua kali na joto
Yesu amenikomboa kutokana na...
Tafuta katika Kumbukumbu la Torati 28 mambo ambayo
Shetani ameweka juu yako. Hivi ni sehemu ya laana ya
sheria na Yesu amekukomboa kutoka na laana hiyo!
Anza kukubaliana na Neno la Mungu,
Nimekombolewa na Yesu
kutokana na laana ya _______ .
Yesu alilipa adhabu ya dhambi.
ninaamuru kila dalili
ya laana hii kuniacha sasa!
Wakati Yesu alitundikwa msalabani, alifanyika laana kwetu
ili tufanyike wenye haki. Yeye hakutupatia uzima wa milele
75
tu bali, Yesu alitupatia vyote ambavyo tunaitaji kuwa
washindi katika maisha haya.
Wakati Shetani anapojaribu kuleta mojawapo ya laana hizo,
tunasema,
Eeh, hapana Shetani!
Yesu ametukomboa kutokana na laana hiyo!
Uhuru juu ya Mambo ya Kale
Mara nyingi Shetani hutunasa katika kukubali mojawapo ya
laana kwa kukubali kuwa tumetenda dhambi, na kuwa laana
hii ni ya adhabu yetu kwa ajili ya dhambi hiyo. Tunaanza
kuwaza kuwa tunastahili kile anaweka juu yetu.
Shetani husema kweli anapotwambia kuwa laana huja kwa
ajili ya dhambi. Lakini Shetani hatukumbushi kuwa Yesu
tayari alilipa adhabu ya dhambi hiyo, ili tusibebe dhambi
hiyo tena au laana hiyo inayokuja baada ya dhambi hiyo.
2 Wakorintho 5:17 Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo,
amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama, yamekuwa
mapya.
Kuishi Katika Ushindi
Kama viumbe wapya, tuko huru kutokana na sheria ya
dhambi na mauti. Tumekombolewa kutoka kwa kila
dhambi, kila adhabu, na kila laana.
Warumi 8:2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima katika Kristo
Yesu imeniweka huru mbali na sheria ya dhambi na mauti.
Ikiwa tutatenda dhambi, lazima tukiri na kupokea msamaha.
1 Yohana 1:9 Kama tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni
mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha
toka kwenye udhalimu wote.
Tunapokiri dhambi zetu, mara moja tunawekwa huru tokana
na dhambi hiyo juu yetu. Tumeoshwa kutoka kwa wasio na
haki. Shetani hawezi tena kutushinda katika mashtaka ya
hukumu na laana.
Dhambi, laana zake, na sheria ya dhambi na mauti, haina
haki ya kisheria kutushinda. Tunaweza kuishi na baraka za
viumbe wapya maishani mwetu.
Tukiwa na Uwezo Kushinda
Ibrahamu alikuwa na imani na ikaesabika kwake kuwa
mwenye haki. Kwa imani, tunaweza kupokea baraka
alizopewa yeye.
Yesu alikuja na kuchukua laana ya sheria juu Yake
mwenyewe. Kwa imani, tunapokea wokovu wetu. Kwa
imani, tunaweza kuyashinda mambo ya ulimwengu huu.
Imani inatupatia uwezo wa kushinda!
76
1 Yohana 5:4 Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu huushinda
ulimwengu. Huku ndiko kuushinda kuushindako ulimwengu,
yaani, hiyo imani yetu.
Kama viumbe wapya, tunakiri nguvu ya Mungu yenye
ushindi ndani yetu. Uamuzi ni wetu kuruhusu nguvu hizi
kutenda kazi ndani yetu au hapana. Tunaweza kuamua na
kuliamini Neno la Mungu, au tunaweza kuamini hali na
mazingira yetu.
Nguvu ya Mungu yenye ushindi inaachiliwa tunapoamini na
kuachilia Neno Lake na kunena kwa ujasiri. Ni imani yetu
katika Neno Lake ndiyo huleta ushindi kwetu.
Shetani hutuambia kuwa sisi tu wenye lawama, wenye
dhambi wasio na manufaa, na kwamba hatuwezi dhidi ya
magonjwa, maumivu, umaskini, na kuhangaika ambayo ni
sehemu ya laana.
Mungu anasema sisi ni viumbe wapya, tukiwa huru
kutokana na lawama, hukumu, na laana ya kisheria.
Mungu anasema sisi tu warithi katika baraka za ahadi
za Ibrahimu.
Mungu anasema kama washindi, tunaweza kutembea
katika baraka Zake tele.
Tunaweza kuwa, tenda, na kuwa na vyote ambavyo Mungu
ametoa kwetu kama waamini katika Yesu Kristo.
Ni lazima tuamue kumwamini Mungu badala ya
uongo wa Ibilisi.
Ni lazima tuamue kujiona kama vile Mungu
anavyotuona.
Lazima tuanze kutangaza yote ambayo Mungu
amesema juu yetu.
Kisha tunaweza kufurahia haki zetu kama viumbe wapya
katika Yesu Kristo!
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Je, kwa nini ni muhimu kufahamu kuwa sisi tunatoka katika jamii ya Ibrahimu?
1. Taja baadhi ya ahadi za agano Mungu aliweka na Ibrahimu ambazo ni muhimu kwako.
3. Kwa kutumia Kumbukumbu la Torati 28:15-68, andika ukurasa wa kutangaza ukitaja uhuru
wako kutokana na laana za kisheria.
77
Somo La Nane
Faida Ya Kuumbwa Upya
Utangulizi
Ufunuo wa kuumbwa upya na haki yetu katika Yesu huleta
faida nyingi kwa mwamini katika Yesu Kristo.
Zaburi 68:19a Sifa apewe Bwana, Mungu Mwokozi wetu,
ambaye siku kwa siku hutuchukulia mizigo yetu.
USHIRIKA NA MUNGU
Mojawapo ya faida kuu ya kuumbwa upya ni kuwa
tunaweza kutembea na Mungu kwa ujasiri na bila aibu
katika uwepo Wake wa utukufu. Tunaweza kutembea
pamoja Naye. Tunaweza kuwa na ushirika wa karibu Naye.
1 Yohana 1:3-7 Twawatangazia lile tuliloliona na kulisikia ili
kwamba nanyi mwe na ushirika wetu hasa ni pamoja na Baba na
Mwanawe Yesu Kristo. Tunaandika mambo haya ili furaha yetu
ipate kuwa timilifu.
Huu ndio ujumbe tuliosikia kutoka kwake na kuwatangazia ninyi,
kwamba Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza lo lote. Kama
tukisema kwamba twashirikiana naye huku tukienda gizani,
twasema uongo, wala hatutendi lililo kweli. Lakini tukienenda
nuruni, kama Yeye alivyo nuruni, twashirikiana sisi kwa sisi na
damu yake Yesu, Mwana Wake yatusafisha dhambi yote.
Ukiristo ni tofauti na dini zingine kwa kuwa tunampokea
Kristo, tunaweza kuwa na uhusiano wa binafsi (kuwa
sehemu ya jamii ya milele ya Mungu) na ushirika (wa
karibu sana kila siku) na Mungu.
Kusudi la Mungu katika ukombozi ilikuwa kurejesha
uhusiano Wake na mwanadamu, na kurejesha ushirika
Naye.
Kufafanua
Kulingana na Kamusi (Webster’s Unabridged Dictionary),
baadhi ya maelezo ya ushirika ni:
Hali ya kuwa mwenza
Uhusiano wa karibu kati ya watu wenye matakwa ya
sawa na kirafiki
Kuwa karibu sana
Kuambatana pamoja
Kufahamiana sana
Kushirikiana kwa karibu
78
Mwito
Tumeitwa kushirikiana na Mungu.
1 Wakorintho 1:9 Mungu ni mwaminifu ambaye mmeitwa naye ili
mwe na ushirika na Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu.
Ni wazo la jabu lililoje. Mungu ametuita katika ushirika
pamoja Naye. Mungu anataka kuwa na ushirika pamoja
nasi!
Ushirika wetu wa karibu na Mungu ni bora utuelekeze kwa
kiwango cha ushirika na ndugu na dada zetu katika jamaa ya
Mungu. Mtume Yohana aliandika,
1 Yohana 1:3,4 Twawatangazia lile tuliloliona na kulisikia ili
kwamba nanyi mwe na ushirika nasi na ushirika wetu hasa ni
pamoja na Baba na Mwanawe Yesu Kristo. Tunaandika mambo
haya ili furaha yetu ipate kuwa timilifu.
Huleta Furaha
Furaha ni matokeo ya ushirika wa karibu na Mungu usio na
kizuizi, na pamoja na waamini wenzetu katika Yesu Kristo.
Zaburi 16:11 Umenijulisha njia ya uzima, utanijaza furaha katika
uwepo wako, pamoja na furaha za milele katika mkono wako wa
kuume.
Hakuna furaha iliyo kuu kuliko ile ipatikanayo katika
ushirika wa karibu na Mungu Mwenyewe kupitia kwa Neno
Lake. Yeremia aliandika,
Yeremia 15:16 Maneno yako yalipokuja, niliyala, yakawa
shangwe yangu na furaha ya moyo wangu, kwa kuwa nimeitwa
kwa jina lako, Ee Bwana Mungu, Mungu Mwenye Nguvu.
Mwamini, aliyepata ufunuo wa kuwa kiumbe kipya katika
Yesu, amepata furaha.
Punde tu wale ambao waliosumbuliwa na mawazo ya
kutokusamehewa, kuhukumiwa, na kutokuwa wa maana,
wanapotambua ufunuo wa haki, wao hufunguliwa kutokana
na utumwa hadi furaha iliyo kuu.
Ni wale tu ambao wana ustadi katika ufunuo wa kuumbwa
upya wanaweza kupata furaha isiyo kifani ya ushirika wa
karibu na Mungu bila hofu ya hukumu.
Daudi aliandika kuhusu furaha hii.
Zaburi 32:1,2 Heri mtu yule ambaye amesamehewa makosa yake,
ambaye dhambi zake zimefunikwa. Heri mtu yule ambaye Bwana
hamwesabii dhambi na ambaye rohoni mwake hamna
udanganyifu.
79
Uhusiano Uliovunjika
Tunapotenda dhambi, uhusiano wetu na Mungu hauvunjiki.
Tungali watoto Wake.
Kupitia dhambi, ushirika wetu Naye huvunjika. Kwa mara
nyingine, dhambi imekuwa kizuizi kati yetu na Mungu.
Lakini, kwa ajili ya rehema zake, Mungu alipata njia kwa
ushirika wetu pamoja Naye urejeshwe mara moja.
Yohana aliandika,
1 Yohana 1:8-10 Kama tukisema kwamba hatuna dhambi,
twajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu. Kama
tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki,
atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha toka kwenye udhalimu
wote. Kama tukisema hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye
kuwa mwongo na Neno lake halimo ndani yetu.
“Kukiri” maana yake ni kutaja. Tunaitajika kutaja dhambi
zetu na wala si tujidanganye, kujaribu kuficha au kukataa
kuwa tumetenda dhambi. Badala yake, kwa haraka tukubali
na pia kwa Mungu kuwa tumetenda dhambi machoni pake
na machoni petu.
Neno “dhambi” ina maana “kukosea alama”. Tunatenda
dhambi mara tu tunamokosea alama ya Mungu ambayo ni
ukamilifu katika haki katika mawazo na matendo yetu.
The moment we recognize that we have “missed the mark,”
we must immediately confess our sin and receive God's
forgiveness and cleansing from that unrighteousness.
Kutumia vibaya Neema ya Mungu
Wengi wasio na ufunuo wa haki, wametumia vibaya neema
ya Mungu. Wachukulia kimakosa kuwa ina maana
wanaweza kutenda dhambi wanapotaka bora tu wakiri
baadaye na kupokea msamaha wa Mungu.
Yohana aliweka wazi, alipoendelea katika msitari ufwatao,
kuwa tusikubali dhambi iingie maishani mwetu.
1 Yohana 2:1 Watoto wangu wapendwa, nawaandikieni haya ili
msitende dhambi. Lakini kama mtu ye yote akitenda dhambi,
tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo Mwenye haki.
Mwito wetu kwa Mungu ni mwito mbali na dhambi.
80
MAFANIKIO
Faida nyingine ya mwamini aliyezaliwa mara ya pili -
kiumbe mpya – ni ili tuwe na mafanikio ya kweli. Kuna aina
mbili ya mafanikio, ile ya nafsi, na katika sehemu ya
kifedha.
Kupitia mtume Yohana, Mungu aliandika kuwa anataka
tufanikiwe na tuwe na afya nzuri – hata wakati nafsi zetu
zinafanikiwa.
3 Yohana 1:2 Uzima huo ulidhihirishwa, nasi tumeuona na
kuushuhudia, nasi twawatangazieni uzima wa milele, ambao
ulikuwa pamoja na Baba, nao ukadhihirishwa kwetu.
Je, nini Mungu angependa zaidi ya yote? Kuwa tutafanikiwa
na kuwa katika afya nzuri, hata wakati nafsi zetu
hufanikiwa.
Je, nini maana “wakati nafsi yako hufanikiwa?”
Mafanikio ya Nafsi
Nafsi zetu ni fikira zetu, hisia zetu na uwezo wa kuamua
kwetu. Mafanikio ya nafsi – mafanikio ya fikira na
mafanikio ya hisio – hutokana na kujitolea kwetu maishani
kama dhabihu inayoishi kwa Yesu, na kuyafanya upya
mawazo yetu katika Neno la Mungu. Mafanikio ya nafsi ni
mwanzo wa mafanikio na afya ya kimwili.
Warumi 12:1,2 Kwa hiyo, ndugu zangu, nawasihi kwa rehema
Zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu na
inayompendeza Mungu, hii ndiyo ibada yenu yenye maana.
Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuze kwa
kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha
ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza machoni
Pake na ukamilifu.
Mungu anawataka watu Wake, viumbe Wake wapya,
kufanikiwa katika nafsi na mwili. Viumbe wapya kamwe
hawataishi katika mtindo wa ulimwengu huu. Wanatakiwa
kufwata mtindo wa Neno la Mungu.
Ni Njia
Viumbe wapya wako katika njia ya kubadilishwa na
mabadiliko haya huja wakati mawazo yao hufanywa upya
kwa kuendelea kusoma, kusikiliza, kutafakari, kuamini, na
kutenda Neno la Mungu.
Hatua ya kwanza ya muhimu kuelekea kwa afya kamili na
mafanikio ni kufika katika ufunuo wa kuumbwa upya.
Ufunuo huu utamuweka huru mwamini kutokana na
mawazo ya lawama, hukumu, na kutokuwa wa maana, ili
81
yeye aweze kupokea faida ya kuumbwa upya, na kuanza
kutembea katika mafanikio na afya kamili.
Imefafanuliwa
Mtoto wa Mungu “aliyefanikiwa” kwa kweli ameelezwa
katika sehemu ya kwanza ya Zaburi.
Zaburi 1:1-3 Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu
waovu, wala hafuati njia ya wenye dhambi au kukaa katika
baraza la wenye mizaha. Lakini huifurahia sheria ya BWANA,
nayo huitafakari mchana na usiku. Mtu huyo ni kama mti
uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao huzaa matunda yake
kwa majira na majani yake hayanyauki. Kila afanyalo
hufanikiwa.
Mtu aliyefanikiwa kwa kweli ni yule:
anatembea katika imani na utiifu kwa ufunuo wa
Neno la Mungu
anatembea katika upendo na anao ustadi katika
ushirika wa karibu na Mungu na pia waamini wenza
anao ustadi wa amani ya Mungu na kutosheka katika
yote anayotenda
anaendelea katika huduma kwa Bwana na kwa maitaji
ya wengine
maitaji yake ya kifedha yamejibiwa ili awe
“ameandaliwa bora kwa kazi nzur”
anaweza kutoa kwa ukarimu kwa Bwana na kwa
maitaji ya wengine
Mafanikio ya Kifedha
Kinyeme na vile tumefundishwa, pesa si uovu. Ni kupenda
fedha ndio mwanzo wa uovu.
Fedha ni muhimu sana katika kutimiza Agizo Kuu. Ni
lazima tutambue jinsi ya kupokea mafanikio ya Mungu ya
kifendha ili tuwafikie waliopotea hapa duniani na injili ya
Yesu Kristo.
Yohana alituonya kuwa ni sharti tuwe macho tusipende vitu
vya hapa duniani. Tuendelee kuwa waangalifu dhidi ya
uwongo katika utajiri, au kiburi katika maisha ambacho
huleta tamaa juu ya vitu, au heshima ya wanadamu.
Mungu alisema tukitafuta kwanza ufalme wa Mungu na
haki Yake, atatubariki na vitu.
Mathayo 6:33 Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki
yake na haya yote mtaongezewa.
Mtu wa aliyeumbwa upya alikuwa na ufunuo wa haki,
atapanua ufalme wa Mungu na haki yake Mungu juu ya
82
maitaji yake mwenyewe. Atamtafuta Mungu na haki Yake,
na Mungu atampa “vitu hivi vyote.”
Kumtolea Mungu
Mungu hatafuti mahali pa kuhifadhi baraka Zake za kifedha.
Badala yake, anatafuta mito, wale ambao ni watoaji katika
ufalme Wake.
Yesu alisema,
Luka 6:38 “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa . Kipimo cha kujaa
na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho
watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile
mpimacho, ndicho mtakachopimiwa.”
Tunapojitolea katika imani na utiifu kwa Mungu, Yeye
ataizidisha kwetu ili tuendelee kuitoa Kwake.
Mafanikio ni mojawapo ya ahadi zilizoahidiwa kwa kiumbe
kipya. Mungu ameweka agano la baraka za kifedha kwa
watu Wake wanaomtii.
AFYA NA UPONYAJI
Faida nyingine ya kuumbwa upya ni mapato ya Mungu ya
uponyaji ya mwili wake.
Ufunuo wa haki ya kuumbwa upya utawaweka huru baadhi
ya wale waliofungwa na hisia za lawama, hukumu, na
kutokuwa wa maana, ili waweze kupokea kwa ujasiri
uponyaji wao kutoka kwa Mungu.
Katika kazi ya ukombozi ya Yesu kwa niaba yetu, Yeye
alitoa kwa ajili ya wokovu wetu milele, na pia alitoa
uponyaji kwa ajili ya mili yetu.
Kuponywa kwa Mapigo Yake
Katika unabii mkuu wa Isaya kuhusu kuja kwa Masiha,
alinena kwa uwazi juu ya uponyaji wetu.
Isaya 53:5 Lakini alitobolewa kwa ajili ya makosa yetu,
alichubuliwa kwa maovu yetu, adhabu iliyotuletea sisi amani
ilikuwa juu yake, na kwa majeraha yake sisi tumepona.
Petro alikubali ujumbe wa Isaya kuwa kweli alipoandika
kuhusu kazi ya ukombozi ya Yesu akitumia yale maneno.
1 Petro 2:24 … yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika
mwili wake, juu ya mti, ili kwamba, tukiwa wafu kwa mambo ya
dhambi, tupate kuishi katika haki. Kwa kupigwa kwake, ninyi
mmeponywa.
Yehova Rafa
Punde tu baada ya wana wa Israeli walipotoka nje ya Misri,
Mungu alijitokeza kama Yehova Rafa, Mungu aliye
mponyaji wao.
83
Kutoka 15:26 Mungu akasema, “Kama mkisikiliza kwa bidii sauti
ya BWANA, Mungu wenu na kuyafanya yaliyo sawa machoni
pake, kama mkiyatii maagizo yake na kuzishika amri zake zote,
sitaleta juu yenu ugonjwa wo wote niliowaletea Wamisri, kwa
kuwa Mimi ndimi BWANA, niwaponyaye.”
Mungu kamwe habadiliki. Uponyaji ni wa leo!
Neno la Mungu huleta Uponyaji
Mfalme Suleimani anatuambia kuwa uhai na afya kwa
mwili wote wa mwanadamu utoka kwa Neno la Mungu.
Mithali 4:20-22 Mwanangu, yasikilize kwa makini yale
ninayokuambia, sikiliza kwa makini maneno yangu. Usiruhusu
yaondoke machoni pako, yahifadhi ndani ya moyo wako, kwa
sababu ni uzima kwa wale wanaoyapata na afya kwa mwili wote
wa mwanadamu.
Ikiwa tutaligeukia Neno la Mungu na kulitafakari juu ya
kile anasema juu ya kuishi katika afya, hili litakuwa jambo
la kweli kuhusu afya inayoishi, litakuwa kweli maishani
mwetu. Wakati akili zetu zinafanyika upya, mili yetu pia
itakuwa.
Wakati ufunuo huu utaelekeza roho zetu akilini mwetu,
tutaweza kunena kwa ujasiri Neno la Mungu kwa imani, na
uponyaji na afya itakuwa ya kweli.
Kumbuka: Ili kupata mafunzo ya ndani kabisa juu ya uponyaji,
soma God's Provision For Healing nao A.L. and Joyce Gill.
NGUVU YA MUNGU
Faida nyingine kuu ya kuumbwa upya ni uwezo wa
kuachilia nguvu za Roho Mtakatifu kutoka ndani yetu.
Pingamizi Za Kinyume
Waamini wengi waliojazwa Roho Mtakatifu wameshindwa
kuachilia nguvu za Mungu ambazo ziko ndani yao kwa
sababu wameshikwa na mawazo ya kinyume na sura zao.
Wengi, wasio na ufunuo wa haki yake Mungu
inayopatikana katika kuumbwa upta, wamezuiliwa kwa
kukubali dhambi maishani mwao. Wamekuwa na hisia ya
dhambi badala ya hisia ya haki. Wao wamejiona kama
wenye dhambi, na kamwe hawajaweza kupata ushindi
maishani mwao. Wameruhusu Roho Mtakatifu kuhuzunika,
au kuzimwa maishani mwao.
Paulo aliandika,
Waefeso 4:30,31 Wala msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa
Mungu, ambaye kwa huyo mlitiwa muhuri kwa ajili ya siku ya
ukombozi. Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu, hasira, makelele
na masingizio pamoja na kila aina ya uovu.
84
Mtu aliye macho juu ya dhambi ataendelea kutenda dhambi,
na kwa sababu hii, atamhuzunisha Roho Mtakatifu na kuishi
maisha yasiyo na nguvu na yenye kushindwa.
Ufunuo wa Haki
Waamini wenye ufunuo wa kuumbwa upya, watajiona kuwa
wenye haki. Watajiona kama walivyoumbwa kuwa.
Watajiona wakitenda kazi ya Yesu. Watajiona kuwa wenye
haki, wakiwa na ushirika na Mungu, na kutumiwa Naye
katika kuwahudumia wengine.
Watajiona wenyewe wakihudumu na upako wake Mungu
unaoonekana maishani mwao. Kama vile Yesu alisema,
mito ya maji ya uhai itatiririka bila pingamizi maishani
mwao na katika huduma.
Yesu alisema,
Yohana 7:38 “Ye yote aniaminiye Mimi, kama maandiko
yasemavyo, vijito vya maji ya uzima vitatiririka ndani mwake.”
Nguvu ya Kushuhudia
Yesu alisema kuwa kusudi la nguvu, inayokuja baada ya
kupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu, ni kutufanya tuwe
mashahidi kamili wa Yesu Kristo.
Matendo 1:8 “Lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu
Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika
Yerusalemu, Uyahudi kote na Samaria, hadi miisho ya dunia.”
Ishara na Miujiza
Mpango wa Mungu wa kuwafikia waliopotea ni miujiza ya
uinjilisti. Ishara, maajabu, na miujiza kila wakati
itakubaliana na Neno la Injili wakati tunashiriki au
kulihumiri.
Maneno ya mwisho ya Yesu kwa waamini Wake kabla ya
kuondoka hapa duniani kulingana na kitabu cha Mariko
yalikuwa,
Marko 16:15-20 Akawaambia, “Enendeni ulimwenguni mwote,
mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Ye yote aaminiye na kubatizwa
ataokoka. Lakini ye yote asiyeamini atahukumiwa.
“Nazo ishara hizi zitafuatana na wale waaminio: Kwa Jina Langu
watatoa pepo wachafu, watasema kwa lugha mpya, watashika
nyoka kwa mikono yao na hata wakinywa kitu cho chote cha
kuua, hakitawadhuru kamwe, wataweka mikono yao juu ya
wagonjwa, nao watapona.”
Baada ya Bwana Yesu kusema nao, alichukuliwa juu mbinguni na
kuketi mkono wa kuume wa Mungu.
Marko 16:20 Kisha wanafunzi Wake wakatoka, wakahubiri kila
mahali, naye Bwana akatenda kazi pamoja nao na kulithibitisha
neno Lake kwa ishara zilizofuatana nalo. Amen.
85
Kupitia kwa ufunuo wa kuumbwa upya, waamini wataweza
kushuhudia kwa ujasiri kwa Yesu Kristo katika nguvu za
Roho Mtakatifu.
Huru Kutokana na Hofu
Wao hawatazuiliwa tena na hofu ya mwanadamu.
Watasema kwa ujasiri,
2 Timotheo 1:7,8a Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali
roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi. Kwa hiyo usione
haya kushuhudia kuhusu Bwana Wetu …
Waamini walio na ufunuo wa kuumbwa upya hatakuwa na
hofu na bila haya ya kushuhudia kwa Yesu.
Wataweza kusema kwa ujasiri,
Wafilipi 4:13 Naweza kuyafanya mambo yote katika Yeye
anitiaye nguvu.
Nguvu Isiyozuiliwa
Mwamini aliye na ufunuo wa kuumbwa upya atairuhusu
nguvu ya Mungu isiyozuiliwa ionekane katika ishara,
maajabu, na miujiza ya uponyaji.
Lawama na hukumu kamwe haitamzuia katika kuzikemea
pepo au kuwekelea mikono yake juu ya wagonjwa na
kuziachilia nguvu za Mungu katika maisha yao.
Mtu aliye na ufunuo wa kuumbwa upya atapata faida ya
ushirika na Mungu: furaha, uponyaji na afya, mafanikio, na
nguvu isiyozuiliwa ya Mungu. Faida hizi si kwa ajili ya
kumfurahisha mwamini pekee. Ni sharti zitiririke nje kwa
waliopotea na ulimwengu unaoangamia.
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Eleza jinsi hisia ya lawama, hukumu, na kutokuwa na maana kunaweza kuzuia ushirika katika
ya mwamini na Mungu.
2. Ni kwa njia gani ufunuo wa kuumwa upya na haki unaweza kumweka huru mtu ili aweze
kupokea uponyaji wake kutoka kwa Mungu?
3. Ni kwa njia gani ufunuo wa kuumbwa upya na haki unaweza kumweka huru ili awe na ujasiri
na kushuhudia Yesu?
86
Somo La Tisa
Wanaoshiriki katika Hali ya Kiungu
HALI YA MUNGU
Tunampokea Yesu binafsi kama mwokozi wetu, tunafanyika
kiumbe kipya. Tunapokea hali mpya kabisa. Ni hali ya
Mungu Mwenyewe. Je, ni jambo la kufurahisha kukundua
kuwa sisi tunashiriki katika hali Yake Mungu.
2 Petro 1:4a Kwa sababu hiyo, ametukirimia ahadi Zake kuu na
za thamani kupitia hayo mpate kuokoka na upotovu ulioko
duniani …….
Je hali ya Mungu ni ipi?
Kuna sehemu ya hali ya kiungu, sifa zake Mungu, ambazo
zimehifadhiwa kwa Mungu pekee. Nazo ni:
Milele – bila mwanzo au mwisho
Asiyebadilika – kamwe habadiliki
Mwenye nguvu – nguvu zote
Anapatikana kote – yupo kila mahali
Imewekwa kwetu
Lakini, kuna hali fulani za Mungu ambazo zimewekwa
kwetu wakati wa wokovu. Hizo hufanyika sehemu ya
muhimu sana ya kuumbwa upya ndani yetu. Sisi tumepewa:
Haki
Utakatifu
Upendo
Wema, Neema, na rehema
Sehemu hizi za hali yake Mungu zimewekwa ndani ya roho
wetu mpya wakati wa wokovu.
Imedhihirishwa na Ahadi Zake
Petro aliandika kuwa kwa nguvu za Mungu tumepewa vitu
vyote mbavyo ni muhimu maishani na katika mambo ya
Mungu. Tunafanyika washiriki katika hali ya kiungu kwa
ufunuo wa Neno la Mungu. Haya yametolewa kwetu na
ahadi zile kuu na zilizo bora.
2 Petro 1:2-4 Neema na amani iwe kwenu kwa wingi katika
kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu. Uwezo Wake wa uungu
umetupatia mambo yote tunayohitaji kwa ajili ya uzima wa
uchaji wa Mungu, kwa kumjua Yeye aliyetuita kwa utukufu
Wake wa wema Wake mwenyewe. Kwa sababu hiyo,
ametukirimia ahadi Zake kuu na za thamani kupitia mambo haya,
87
ili kwa kupitia hayo mpate kuokoka na upotovu ulioko duniani
kwa sababu ya tamaa mbaya.
Kufanyika Washiriki
Inawezekana kupata hali yake Mungu ndani ya roho zetu
bila kufanyika mshiriki katika hali Yake katika ustadi wetu.
Mtume Paulo aliandika,
Wafilipi 2:12,13 Kwa hiyo, wapenzi wangu, kama vile ambavyo
mmekuwa mkitii sikuzote, si tu wakati nikiwa pamoja nanyi, bali
sasa zaidi sana nisipokuwapo. Utimizeni wokovu wenu kwa
kuogopa na kutetemeka, kwa maana Mungu ndiye atendaye kazi
ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu kwa kulitimiza
kusudi Lake jema.
Wakati wa wokovu, tunapokea sifa hizi za Mungu ndani ya
roho zetu, lakini ni kupitia muda ndipo zinafanya kazi na
kuwa sehemu ya akili na mili yetu. Waamini wote
wamefanyika washiriki katika hali Yake ya kiungu ndani ya
roho zao. Lakini, ni kupitia tu ufunuo wa kuumbwa upya
ndipo tunaweza kuwa washiriki katika hali Yake ya kiungu
katika nafsi na mili yetu.
Waamini wanaweza kuwa washiriki na kufurahia kile
amabcho tayari ni chao kwa ufunuo wa kweli ambao
huonyesha tayari wamepokea hali ya kiungu ya Mungu.
Ni wakati tunapotafakari juu ya Neno la Mungu, na kwa
imani kudai ahadi za Neno Lake, ndipo tunaweza kuwa
washiriki katika hali Yake Mungu katika nafsi na mili yetu.
Wakati roho zetu mpya zimepokea hali yake Mungu, katika
somo hili tutajifunza jinsi ya kuwa washiriki katika hali
Yake katika sehemu ya nafsi na mili yetu.
KUFANYIKA KAMA YEYE
Tumetengwa na Kristo ili tubadilishwe katika sura Yake.
Warumi 8:29a Maana wale Mungu aliowajua tangu mwanzo, pia
aliwachagua tangu mwanzo, wapate kufanana na mfano wa
Mwanawe ….
Roho wa kuumbwa upya imeumbwa katika mfano na sura
ya Mungu, na Wakristo wako katika mpango wa
kubadilishwa kwa sura katika sehemu ya mili na nafsi zao.
Mbinu Inayobadilisha
Mtume Paulo aliandika kwa Warumi,
Warumi 12:1,2 Kwa hiyo, ndugu zangu, nawasihi kwa rehema
Zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu na
inayompendeza Mungu, hii ndiyo ibada yenu yenye maana.
Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuze kwa
kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha
88
ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza machoni
Pake na ukamilifu.
Kama viumbe wapya, basi hatuwezi kubadilishwa na
ulimwengu huu. Ni sharti tuishi katika mbinu ya
kubadilishwa wakati tunabadilishwa kwa sura ya Mwana wa
Mungu.
Kutoa Mili Yetu
Tunaanza mbinu ya kubadilishwa kwa kukata shauri ya mili
yetu kwa Mungu kabisa. Mili yetu ni hekalu la rRoho
Mtakatifu na inatupasa kuitoa kama “dhabihu inayoishi kwa
Mungu.”
Ili kufanyika mshiriki katika hali ya kiungu ambayo tayari
tunayo katika Yesu, ni lazima tuyatoe maisha yetu kwa
uongozi wa Yesu Kristo kila siku.
Kuyafanya Upya Mawazo Yetu
Hata wakati mili yetu hubadilishwa, nafsi zetu ni lazima
zibadilishwe kwa mbinu inayoendelea iitwayo kuyafanya
upya mawazo.
Mbinu hii ibadilishayo hufanyika wakati tunaendelea
kusoma, kusikia, kutafakari juu ya, kuamini, na kulitenda
Neno la Mungu. Ni kazi ya ajabu ya Roho Mtakatifu.
Kwa mbinu hii ya ajabu, mili na nafsi zetu hushiriki katika
hali ya kiungu.
Mungu Kufanya Kazi ndani Yetu
Paulo aliomba, pamoja na hali ya mama anapojifungua
mimba, kwa waamini Wagalatia kuwa Kristo atafanyika
ndani yao.
Wagalatia 4:19 Watoto wangu wapendwa, ambao kwa mara
nyingine ninawaonea utungu, ninatamani kwamba Kristo
aumbike ndani yenu…
Aliwaambia waamini Wafilipi kuwa Mungu alikuwa
akitenda kazi ndani yao.
Wafilipi 2:13 Kwa maana Mungu ndiye atendaye kazi ndani yenu,
kutaka kwenu na kutenda kwenu kwa kulitimiza kusudi Lake
jema.
Mungu anaendelea kutenda kazi katika maisha ya viumbe
Wake wapya, hadi wabadilishwe na kuwa sura ya
Mwanawe.
Kadri tunapomuruhusu kutenda kazi Yake ndani yetu, ndipo
tunakuwa kama Kristo.
Kumbukumbu Maalum: Tumejifunza tayari juu ya haki yake
Mungu na jinsi ilivyowekwa kwetu. Haki ni mojawapo ya sifa zake
Mungu. Katika somo hili, tutachukua kuwa unaelewa juu ya haki
Yake na jinsi imewekwa kwetu wakati wa wokovu na kuendelea
kwa sifa zake Mungu zingine.
89
KUSHIRIKI KATIKA UTAKATIFU WAKE
Mungu ni Mtakatifu
Utakatifu wa Mungu ni wa ajabu, wenye usafi kabisa na
ukamilifu usioweza kuelezwa. Huleta kutengwa kabisa
kutokana na dhambi na uchafu.
Mungu ni mtakatifu kabisa katika hali yake na katika njia
zake zote. Malaika wana tangaza utakatifu wake.
Isaya 6:3 Nao walikuwa akiitana kila mmoja na mwenzake:
“Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni BWANA Mwenye Nguvu,
Dunia yote imejaa utukufu wake.”
Amri ya Kuwa Watakatifu
Roho wetu mpya wa kuumbwa upya ni mtakatifu kama vile
Mungu mwenyewe ni mtakatifu.
Mtume Paulo aliandika,
Waefeso 1:4 Kwa maana alituchagua katika Yeye kabla ya
kuumbwa ulimwengu ili tuwe watakatifu na bila lawama mbele
Zake.
Kumbuka, mili yetu na nafsi zetu ziko katika mbinu ya
kubadilishwa kwa mfano wa Kristo. Ni lazima tuchague na
kuwa watakatifu katika maisha yetu ya kila siku. Huu ni
utakatifu katika ustadi wetu.
Mambo Ya Walawi 19:2b ‘Iweni watakatifu kwa sababu Mimi ni
Mtakatifu, BWANA wenu niliye mtakatifu.’
Ni lazima tuchague kuwa watakatifu katika mienendo yetu.
Ni lazima tuyaweke maisha yetu kama vyombo vitakatifu
kwa Mungu. Ni lazima tujiangalie kama wafu kwa dhambi
na hai kwa Yesu.
Huu ni ustadi wa kutakaswa, mbinu ya kutengwa na
mipango ya hapa duniani na kwa Yesu Kristo Mwenyewe.
Ni kufanyika kama Yesu katika maisha na mienendo yetu
kila siku.
1 Petro 1:15,16 Bali kama Yeye aliyewaita alivyo mtakatifu,
ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote, kwa
maana imeandikwa: “Mtakuwa watakatifu, kwa kuwa Mimi ni
mtakatifu.”
Tumeamuriwa kuwa watakatifu na tunaweza kufanya haya
kwa kushiriki katika hali ya utakatifu Wake Mungu.
90
KUAHIRIKI KATIKA UPENDO WAKE
Mungu ni Upendo
Mungu katika hale Yake ni Upendo. Yeye ni chanzo cha
upendo wote.
1 Yohana 4:16 Hivyo nasi twajua na kuutumainia upendo wa
Mungu alio nao kwa ajili yetu. Mungu ni Upendo. Kila akaaye
katika upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani
yake.
Njia kuu ambayo Mungu alionyesha upendo Wake kwa
mwanadamu ilikuwa kupitia kwa zawadi ya Mwanawe wa
dhamana.
Warumi 5:8 Lakini Mungu anaudhihirisha upendo Wake kwetu
kwamba: Tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa
ajili yetu.
Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu
hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye
asipotee, bali awe na uzima wa milele.”
Aina Nne za Upendo
Kwa sababu katika dunia ya kisasa neno “upendo” mara
nyingi huelezwa vibaya, itakuwa bora kufahamu maneno
manne yanayotumika katika lugha ya Kigiriki.
Erosi
“Erosi” ni pendo kati ya mke na mume. Haipo katika agano
Jipya. Inagusia upendo kati ya mke na mume kama
inavyoelezwa katika Wimbo Ulio Bora. Imepingwa na
Mungu nje ya mapenzi kati ya mume na mke.
Upendo wa kijamii
“Storge” ni upendo wa kijamii. Inatokana na maelezo ya
kuvutiwa na. katika ya watu wa jamii moja
Warumi 12:10 Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa kidugu.
Waheshimuni na kuwatanguliza wengine.
Storge is the affection that family members show for one
another both within natural families and within the family of
God.
Marafiki
Huu ni upendo wa ndani sana kati ya mtu mmoja na
mwingi. Pia unagusia kubusu. Upendo mkuu wa joto na wa
kuvutia.
Yohana 5:20a Baba ampenda Mwana na kumwonyesha yale
ambayo Yeye Baba mwenyewe anayafanya.
Upendo wa marafiki (Philia) ulitumika kueleza upendo wa
uhusiano kati ya Yesu na Lazaro.
91
Yohana 11:3 Hivyo hawa dada wawili walituma ujumbe kwa
Yesu kumwambia, “Bwana, yule umpendaye ni mgonjwa.”
Pia kuna neno “Philos,” mbalo ni mtu fulani aliye mpendwa
sana kwa hisia za upendo kwa mtu mweingine.
Yohana 15:13 Hakuna mtu mwenye upendo mkuu kuliko huu, mtu
kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.
This is the intimate type of love that a husband and wife
have for one another (philandros) .
In addition to the close and warm love relationship that
Jesus had for Lazarus, it is also seen in the love relationship
between David and Jonathan. It is a special love limited to a
few very close relationships between two people.
Upendo wa Mungu
Upendo (agape) huu wa Mungu ambao unatolewa kama
tunda la Roho Mtakatifu katika maisha ya mwamini.
Wagalatia 5:22,23 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani,
uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi. Katika
mambo kama haya hakuna sheria.
Upendo wa agape ni wa ajabu, ni upendo wa Mungu
unaoletwa na Roho Mtakatifu mioyoni mwetu, katika
maisha yetu na vitendo vyetu kwa wengine.
Kwa sababu upendo huu unatoka kwa Mungu, ni upendo
ambao ulimwengu unaweza kupata tu katika kuumbwa upya
– kupitia kwetu. Ni upendo kwa jirani zetu, marafiki wetu,
na hata kama ni la ajabu kwa ulimwengu, na kwa adui wetu.
1 Yohana 3:16 Kwa namna hii twaweza kulijua pendo la Mungu,
kwa sababu Yesu Kristo aliutoa uhai Wake kwa ajili yetu. Nasi
imetupasa kuutoa uhai kwa ajili ya hao ndugu.
Kwa Ufupi
Erosi imepimwa na sheria za Mungu kwa mke au mume tu.
Storge imewekwa kwa jamii wa kawaida au wa kiroho.
Philia umewekwa kwa ajili ya mke au mume na pia rafiki
wa karibu.
Lakini, katika kuumbwa upya, upendo mkuu wa Mungu
unaonyeshwa kwa wote, hata kwa adui wetu.
Upendo wa Mungu katika Kutenda
Pendana mmoja kwa mwingine
Kwa kujazwa hali Yake Mungu ndani yetu, na kama tunda
la Roho, viumbe wapya wanakuwa na upendo mmoja kwa
mwingine.
92
Warumi 13:8 Msidaiwe kitu na mtu ye yote, isipokuwa
kupendana, kwa maana yeye ampendaye mwenzake, ameitimiza
sheria.
Yesu alisema,
Yohana 13:34,35 “Amri mpya nawapa: Mpendane kama Mimi
nilivyowapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi mpendane. Kama
mkipendana ninyi kwa ninyi, kwa njia hii, watu wote watajua
kuwa ninyi ni wanafunzi Wangu.”
Kitu juu ya mengine yote ambacho huwatofautisha
wanafunzi wa Yesu ni upendo walio nao mmoja kwa
mwingine.
Mwanafunzi wa Upendo
Mwanafunzi ni yule aliye chini ya nidhamu ya Yesu. Yeye
ni zaidi ya Mkristo. Yeye ni, ambayo kwa imani na kutii,
anabadilishwa kwa hali ya upendo na sura ya Yesu.
Mwanafunzi atasema pamoja na mtume Yohana,
1 Yohana 4:7 Wapenzi na tupendane, kwa kuwa upendo watoka
kwa Mungu. Kila apendaye amezaliwa na Mungu naye anamjua
Mungu.
Viumbe wapya, wale ambao ni washiriki katika hali ya
kiungu, watatembea katika upendo (agape) wa Mungu.
Warumi 5:5b … Mungu amekwisha kumimina pendo Lake mioyoni
mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ametupatia .
Upendo umeamuriwa na Sheria
Sheria ya Musa iliamuru kuwa tupende mmoja kwa
mwingine.
Mambo Ya Walawi 19:18 Usijilipizie kisasi wala kuwa na
kinyongo dhidi ya mmoja wa jamaa yako, lakini mpende jirani
yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe …
Waume kwa wake wasiobadilishwa hawakuweza kutimiza
sheria. Wao wenyewe hawangependa jirani wao kama
wenyewe.
Yesu alitoa amri mpya ya upendo kwa viumbe Wake
wapya.
Warumi 13:9 Kwa kuwa amri hizi zisemazo, ‘Usizini,” “usiue,”
“usiibe,” “usitamani,” na amri nyingine zote, zinajumlishwa
katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.”
Sheria Kutimizwa na Upendo
Upendo ni timizo la sheria.
Warumi 13:10 Upendo haumfanyii jirani jambo baya. Kwa hiyo
upendo ndio utimilifu wa sheria.
Paulo aliwaandikia Waglatia,
93
Wagalatia 5:14 Kwa maana sheria yote hukamilika katika amri
moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.”
Kupenda Adui Wetu
Mungu, katika hali Yake ya upendo mkuu, alitupenda
tulipokuwa adui wake. Kama viumbe wapya, nasi pia tuko
na hali ya upendo wa Mungu. Nasi pia ni lazima tuwapende
waliopotea hapa duniani na kushiriki nao upendo mkuu
Wake Mungu na pia huruma zake.
Kwa sababu sisi tu viumbe wapya, tunashiriki katika hali ya
upendo wake Mungu. Kwa Roho Mtakatifu, tunaweza na ni
lazima tuwapende hata wale ambao ni adui wetu.
Mathayo 5:44 Lakini mimi ninawaambia: Wapendeni adui zenu na
waombeeni wanaowatesa ninyi.
Yesu hangetuamuru kutenda jambo ambalo haliwezekani
kwetu kutenda. Tunaweza na ni lazima tuwapende adui
wetu kwa upendo wa mungu.
Kuonyesha Upendo mkuu
Yesu aliwaagiza wafuasi Wake jinsi ya kuonyesha upendo
mkuu kwa wengine – hata pia kwa adui zao.
Luka 6:27-30 “Lakini nawaambia wale wanaonisikia, wapendeni
adui zenu. Watendee mema wanaowachukia. Wabarikini wale
wanaowalaani, waombeeni wale wanao watendea mabaya.
Kama mtu akikupiga shavu moja mgeuzie na la pili. Mtu
akikunyang’anya koti lako , usimzuie kuchukua joho pia. Mpe kila
akuombaye na kama mtu akichukua mali yako usitake
akurudishie.
Mtume Paulo aliandika,
Warumi 12:20 Badala yake: “adui yako akiwa na njaa, mpe
chakula, akiwa na kiu, mnyweshe. Maana ukifanya hivyo,
utampalia makaa ya moto yanayowaka kichwani pake.”
Mfano wa Upendo Mkuu
Stefano alikuwa mfano mkubwa wa upendo wa ajabu katika
vitendo alipokuwa akipigwa mawe na adui zake.
Matendo 7:59,60 Walipokuwa wakimpiga mawe, Stefano
aliomba, “Bwana Yesu, pokea roho yangu” kisha akapiga magoti,
akalia kwa sauti kubwa akasema, Bwana usiwahesabie dhambi
hii.” Baada ya kusema haya akalala.
Mtu anayeishi kwa hisia zake kamwe hataona ustadi wa
upendo huu. Inaweza tu kuonekana na kuonyeshwa na wale
ambao wamepata ufunuo wa Mungu ndani yao.
Kuchagua Kupenda
Kwa sababu kupenda adui zetu ni kinyume na hisia zetu na
nafsi zetu za kawaida, sisi tulio na ufunuo wa upendo Wake
94
Mungu ni lazima tuchague kupenda kama vile Mungu
apendavyo.
1 Petro 1:22 Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii
ile kweli kwa njia ya Roho kwa kuwapenda ndugu zenu kwa
upendo wa kweli, pendaneni kwa dhati kutoka moyoni.
Wanaompenda Mungu
Wale ambao wamepata ufunuo wa kuumbwa upya na kuwa
wako ndani ya Kristo, na wamefanyika washiriki katika hali
Yake ya kiungu, basi, juu ya yote, watakuwa wapenzi wa
Mungu.
Watatenda yote wakimfurahisha Mungu kwa kutii Neno
Lake. Watakuwa waabudu wa Mungu.
Viumbe wapya wataendelea kumsifu Mungu kwa baraka
Zake zote za jabu. Watamsifu Mungu kwa jinsi alivyo. Sifa
zake Mungu zitaendelea kuwa juu ya vinywa vyao.
Viumbe wapya watakuwa na upendo wa ndani na wa karibu
zana na Mungu.
Zaburi 42:1,2 Kama vile paa aoneavyo shauku vijito vya maji,
ndivyo nafsi yangu ikuoneavyo shauku, Ee Mungu. Nafsi yangu
inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai. Ni lini nitaweza kwenda
kukutana na Mungu?
Viumbe wapya watatembea katika upendo mkuu wa Kristo
kwa waamini wenza, adui zake, na kwa Mungu Mwenyewe.
KUSHIRIKI KATIKA WEMA NA REHEMA ZAKE
Mungu Ni Mwema
Mungu katika hali Yake ni mwema.
Zaburi 52:1b Wema wake Mungu unavumilia kuendelea.
Wema Wake Mungu ni moja ya ukamilifu kabisa. Wema
Wake unaonyeshwa kwa viumbe Wake wote kwa rehema na
neema Zake.
Rehema na Neema Zake Mungu
Rehema Zake Mungu kwa wanadamu wenye dhambi
zilionyeshwa kwa wazi na kamili wakati alimtoa Mwanawe
ili afe kwa niaba yetu. Mojawapo ya maelezo ya rehema ni:
kuvvumilia kutokutoa adhabu kwa anayevunja sheria
Rehema zake Mungu ni wema wake Mungu uonekanao
katika mahitaji yetu. Mungu amejawa na rehema!
Waefeso 2:4 Lakini Mungu, kwa upendo Wake mwingi kwetu
sisi , ambaye ni mwingi wa rehema...
Mungu anaitwa Baba wa rehema.
95
2 Wakorintho 1:3 Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu
Yesu Kristo, Baba wa huruma na Mungu wa faraja yote.
96
Kuokolewa kwa Neema
Maelezo ya neema ni:
Ni upendo wa Mungu kwa kuwajali wanadamu.
Ni njia nyingine ya kuonyesha upendo Wake mkuu.
Waefeso 2:5,8 Hata tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu,
alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu, (yaani, mmeokolewa
kwa neema)...
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, wala hii
si kwa matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Kiti cha Enzi cha Neema
Sasa, kama viumbe wapya, tunaweza kuja kwa ujasiri mbele
ya kiti cha enzi cha neema.
Waebrania 4:16 Basi na tukikaribie kiti cha rehema kwa ujasiri,
ili tupewe rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa
mahitaji.
KUSHIRIKI KATIKA MSAMAHA WAKE
Mungu Anasamehe
Njia kuu ya kuonyesha neema na rehema zake Mungu
inapatikana katika msamaha Wake. Msamaha Wake
umeelekezwa kwa kila wenye dhambi wanapompokea Yesu
kama mwokozi wao – kwa niaba yao binafsi.
Waefeso 1:7 Katika Yeye tunao ukombozi kwa njia ya damu
Yake, yaani, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa
neema Yake.
Msamaha Wake umeelekezwa kwa waamini wanapokiri
dhambi zao.
1 Yohana 1:9 Kama tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni
mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha
toka kwenye udhalimu wote.
Katika Agano Jipya, msamaha ina maana:
kupeleka mbali na
kulipa deni au dhambi kwa kuifutiliwa mbali kabisa
kuweka upendo au kujali, kwa kuziachilia kutokana
na, kuachilia au kupuuza dhambi au kuruka mipaka.
Mungu anasamehe na kusahau! Msamaha Wake unaegemea
kazi ya ukombozi ya Yesu, ambayo mbali na kulipa adhabu
ya dhambi zetu, pia alizibeba dhambi zetu hadi chini ya
ardhi, zisije zikakumbukwa au kuhesabiwa dhidi yetu tena.
Waebrania 8:12 “Kwa kuwa nitasamehe uovu wao, wala
sitazikumbuka dhambi zao tena!”
97
Ni Lazima Tusamehe
Kama washiriki katika hali Yake Mungu, sisi kama viumbe
wapya, tutatembea katika rehema na neema za Mungu kwa
wengine. Tutasamehe kama vile Mungu husamehe.
Waefeso 4:32 Iweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa
ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo
alivyowasamehe ninyi.
Endelea Kusamehe
Hata kama mtu ataendelea kutenda dhambi dhidi yetu, ni
lazima tuendelee kusamehe.
Mathayo 18:21,19 Ndipo Petro akamjia Yesu na kumwuliza,
“Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Je,
hata mara saba?”
Yesu akamjibu, “Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara
sabini.”
Kama viumbe wapya, tunaweza kusamehe kwa sababu tu
washiriki katika asili Yake Mungu. Tunaweza na ni lazima
tusamehe kwa sababu Yesu alisamehe.
Chagua Kusamehe
Msamaha ni chaguo. Ni tendo la kumtii Mungu. Tusisubiri
kusamehe hadi tujihisi hivyo. Ni lazima tumtii Mungu na
kufanya uamuzi wa kusamehe kwa sababu Mungu katika
rehema na neema Zake ametusamehe.
Yesu alitundikwa msalabani mbele ya adui Zake.
Walimpiga, kumtemea, kumdhihaki, kusema uwongo juu
Yake, kuweka taji la miba kichwani Mwake, na hata
kumsulubisha. Na bado, hata alipokuwa msalabani,
aliwasamehe.
Luka 23:34a Yesu akasema, “Baba, wasamehe, kwa maana
hawajui walitendalo!”
Yesu ni mfano wetu. Kwa sababu alisamehe na yu ndani
yetu, nasi pia tunaweza kusamehe.
Samehe Ili Usamehewe
Huyu Yesu alisema,
Marko 11:25 Nanyi kila msimamapo kusali, sameheni, mkiwa na
neno na mtu ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi
makosa yenu.
Kama viumbe wapya katika Yesu Kristo na tukiwa na asili
ya upendo Wake Mungu, rehema, na neema, nasi pia
tunaweza kuwasamehe wote waliotenda dhambi dhidi yetu
au dhidi ya wapendwa wetu. Tumeamuriwa kusamehe ili
tusamehewe.
98
Kumalizia
Kama viumbe wapya, tunao uhai na asili ya Mungu ndani
ya roho zetu. Nafsi na mili yetu hushiriki katika asili ya
Mungu kama vile tunabadilishwa katika sura ya Mwanawe.
Sehemu yetu ni kuleta mili yetu kama dhabihu inayoishi
kwa Mungu, ili kutumia muda katika Neno la Mungu, na
kuwasikiliza walimu Wake ili nafsi zetu zibadilishwe kwa
ufunuo wa Neno la Mungu.
Ni sharti tuwe washiriki katika haki Yake Mungu, upendo,
na wema Wake. Tunashiriki katika rehema na neema Zake
hadi sisi, kama Yeye, tuwe wanaowasamehe wengine.
Kama viumbe wapya, roho zetu hupokea asili Yake Mungu
ndani yetu. Nafsi zetu na mili yetu hushiriki katika sili ya
kiungu kwa kubadilishwa kwa nguvu ya Neno la Mungu
maishani mwetu.
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Eleza njia ambayo tunaweza kuwa washiriki katika asili Yake Mungu.
2. unapofanyika mshiriki katika asili Yake Mungu, ni mabadiliko gani unayotarajia katika
mienendo yako, uhusiano, na vitendo kwa wengine?
3. Ni kwa nini ni muhimu kuwasamehe wote waliotenda dhambi dhidi yetu?
99
Somo la Kumi
Neno la Mungu na Kuumbwa Upya
NENO LA MUNGU
Utangulizi
Ufunuo wa kuumbwa upya unapatikana katika Neno la
Mungu. Neno Lake linaweka wazi Yesu na nafasi yetu
ndani Yake. Mabadiliko ya roho na mili yetu inawezekana
tu kwa kufanya upya mawazo yetu katika nguvu ya Neno la
Mungu.
Mmbinu hii ya mabadiliko huja tu tunapotafakari juu ya
Neno la Mungu, na kujiona kama vile Mungu anavyotuona.
Tunapoanza kutangaza Neno la Mungu mara kwa mara
kwetu wenyewe, fikira zetu zitaanza kuwa kama mfano wa
Mungu. Imani yetu, itaachiliwa na tutaanza kujiona tukiwa,
kutenda, na kuwa na yote Mungu anasema kutuhusu kama
viumbe wapya katika Mwana Wake.
Yesu, Neno Linaloishi
Yesu na Neno ni moja. Kulijua Neno Lake ni kumjua Yeye.
Yohana 1:1,14 Hapo mwanzo, alikuwako Neno. Huyo Neno
alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu… Neno
alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu
Wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba,
amejaa neema na kweli.
Yesu ni Neno la Mungu, na Neno ni ufunuo wa Yesu. Yesu
anaonekana katika kila kitabu cha Biblia. Kutafakari juu ya
Neno ni kama kuwa na yesu.
Wakati Yesu anaonekana kwetu, tutakuwa kama Yeye!
1 Yohana 3:2 Wapenzi, sasa tu watoto wa Mungu, lakini bado
haijadhihirika tutakavyokuwa, lakini twajua ya kwamba, Yeye
atakapodhihirishwa, tutafanana naye, kwa maana tutamwona
kama alivyo.
Ni kwa kulielewa Neno la Mungu ndipo tunagundua ufunuo
ubadilishao maisha wa kuumbwa upya.
Limetolewa kwa Kuvuviwa
Biblia imeanzishwa na Mungu. Sio tu mkusanyiko wa
vitabu vilivyoandikwa na watu tofauti katika nyakati nyingi,
limetiwa pumzi na kuvuviwa na Mungu.
2 Timotheo 3:16,17 Kila andiko, lililovuviwa na Mungu lafaa kwa
mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na
kuwafundisha katika haki ili mtu wa Mungu awe kamili,
amekamilishwa apate kutenda kutenda kila kazi njema.
100
Maneno ya asili ya tafsiri “kuvuviwa na mungu” maana
yake ni “kutiwa pumzi na Mungu.”
Mungu alipopumua pumzi Yake kwa Adamu, Adamu
alifanyika roho anayeishi. Adamu alikuwa na uhai ule wa
Mungu mwenyewe ndani yake.
Kwa njia hiyo hiyo, Mungu alipumua pumzi Yake kwa
Neno Lake. Neno la Mungu halina makosa na limekamilika
kwa sababu limevuviwa kwa Roho Mtakatifu.
2 Petro 1:20,21 Awali ya yote, yawapasa mjue kwamba hakuna
unabii katika Maandiko uliofasiriwa kama apendavyo mtu
mwenyewe. Kwa maana unabii haukuja kamwe kwa mapenzi ya
mwanadamu, bali watu walinena yaliyotoka kwa Mungu
wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Linaishi na Lenye Uwezo
Neno la Mungu li hai na uhai wa Mungu. Neno la Mungu ni
kuu katika kuyabadilisha maisha yetu kwa uwezo wa Roho
Mtakatifu.
Waebrania 4:12 Kwa maana Neno la Mungu li hai tena lina nguvu
tena lina makali kuliko upanga uwao wote wenye makali kuwili,
tena linachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, viungo na
mafuta yaliyo ndani yake, tena li jepesi kuyatambua mawazo na
makusudi ya moyo.
Lina Uhai wa Mungu
Uhai wa Mungu, ambao ulivuviwa katika Neno la Mungu,
bado u hai katika upewo wa Mungu na uwezo kama vile ile
siku lilivyoandikwa. Uhai wa Mungu, ulio katika Neno
Lake, unaendelea katika maisha ya wale wanaotumia muda
katika uhai huo.
Mithali 4:20-22 Mwanangu, yasikilize kwa makini yale
ninayokuambia, sikiliza kwa makini maneno yangu. Usiruhusu
yaondoke machoni pako, yahifadhi ndani ya moyo wako, kwa
sababu ni uzima kwa wale wanaoyapata na afya kwa mwili wote
wa mwanadamu.
Kuishi kwa Neno
Kiumbe kipya huishi kwa Neno la Mungu.
Mathayo 4:4 Lakini Yesu akajibu, “Imeandikwa, ‘Mtu haishi kwa
mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.”
Kuumbwa upya ni kuishi katika Neno, kulitegemea usiku na
mchana.
Yoshua 1:8 Usiache kitabu hiki cha Torati kiondoke kinywani
mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, ili upate
kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote
yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapoifanikisha njia yako na
kisha utasitawi sana.
101
Neno Linalodumu
Tunaposoma, kutafakari, kuamini, kukiri, na kulitenda Neno
la Mungu, litashinda kama vile lilishinda katika mji wa
Efeso.
Paulo alifundisha Neno la Mungu kila siku katika shule ya
Tirana.
Matendo 19:10-12 Jambo hili likaendelea kwa muda wa miaka
miwili, kiasi kwamba Wayahudi na Wayunani wote walioishi
huko Asia wakawa wamesikia neno la Bwana.
Mungu akafanya miujiza mingi isiyo ya kawaida kwa mkono wa
Paulo, kwamba leso au vitambaa vilivyokuwa vimegusa mwili wa
Paulo viliwekwa juu ya wagonjwa, nao wakapona magonjwa yao
na pepo wachafu wakawatoka.
Paulo alipoendelea kufundisha na kuhubiri Neno kule Efeso,
mambo makubwa yaliendelea kutendeka.
Matendo 19:17-20 Habari hii ikajulikana na Wayahudi wote na
Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawajaa wote, nalo jina la
Bwana Yesu likaheshimiwa sana. Wengi wa wale waliokuwa
wameamini wakati huu wakaja na kutubu kuhusu matendo yao
maovu waziwazi. Idadi kubwa ya wale waliofanya mambo ya
uganga wakaleta vitabu vyao na kuviteketeza kwa moto
hadharani. Walipofanya hesabu ya thamani ya vitabu
vilivyoteketezwa ilikuwa drakamu 50,000 za fedha. Hivyo neno
la Bwana likaenea sana na kuwa na nguvu.
Ikiwa tutadumu katika Neno la Mungu, kulisoma na
kutafakari kila siku, kuamini, kulinena, na kutenda kwa
ijasiri, ufunuo wa Neno la Mungu utakua sana na kushinda
maishani mwetu na miji yetu kama vile Efeso katika Asia.
UMUHIMU WA NENO MAISHANI MWETU
Hulisha Roho Zetu
Neno la Mungu huweka imani ndani ya roho zetu, na
hujenga upendo wetu kwa Mungu na mmoja kwa mwingine.
Neno la Mungu, kulisha roho wa kiumbe kipya, ni muhimu
zaidi ya kula chakula cha kawaida ili kulisha mwili.
Ayubu 23:12 Sijaziacha amri zilizotoka midomoni mwake, bali
nimeyathamani maneno ya kinywa chake kuliko chakula changu
cha kila siku.
Yeremia 15:16a Maneno yako yalipokuja, niliyala, yakawa
shangwe yangu na furaha ya moyo wangu.
Mathayo 4:4 Lakini Yesu akajibu, “Imeandikwa, ‘Mtu haishi kwa
mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.”
102
Huleta Kukubalika
Mungu anatutazamia kujifunza na kufahamu Neno Lake
kama vile Paulo alimwamuru Timotheo kutenda.
2 Timotheo 2:15 Jitahidi kujionyesha kwa Mungu kuwa
umekubaliwa na Yeye, mtenda kazi asiye na sababu ya kuona
aibu, ukilitumia kwa usahihi neno la kweli.
Hujenga Imani yetu
Imani huja kwa kulisoma na kusikia Neno la Mungu.
Warumi 10:17 Basi, imani chanzo chake ni kusikia na kusikia
huja kwa Neno la Kristo.
Wakati imani inakuja kwa kulisikia Neno, imani hiyo
itaanza kunena, kukiri, na kutangaza Neno la Mungu kama
kweli.
KUTAFAKARI JUU YA NENO LA MUNGU
Ni muhimu kuwa tutafakari juu ya Neno la Mungu, si kwa
asili yetu, upunguvu wetu, kukosa uwezo, hali mbalimbali,
au matatizo. Ikiwa tutaendelea kuweka mawazo yetu juu ya
vitu hivi vya kinyume, mawazo yetu haiwezi kufanywa
upya.
Wafilipi 4:8,9 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya
kweli, yo yote yaliyo na sifa njema, yo yote yaliyo na haki, yo
yote yaliyo safi, yo yote ya kupendeza, yo yote yenye staha,
ukiwako uzuri wo wote, pakiwawepo cho chote kinachostahili
kusifiwa, tafakarini mambo hayo. Mambo yote mliyojifunza au
kuyapokea au kuyasikia kutoka kwangu, au kuyaona kwangu,
yatendeni hayo. Naye Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.
Kutafakari juu ya Neno la Mungu ni muhimu kwa
kubadilishwa kwetu kwa kuyafanya mawazo yetu upya.
Zaburi 1:1-3 Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu
waovu, wala hafuati njia ya wenye dhambi au kukaa katika
baraza la wenye mizaha. Lakini huifurahia sheria ya BWANA,
nayo huitafakari mchana na usiku. Mtu huyo ni kama mti
uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao huzaa matunda yake
kwa majira na majani yake hayanyauki. Kila afanyalo
hufanikiwa.
Wakati mtu aliyeumbwa upya anatafakari juu ya Neno la
Mungu usiku na mchana, mabadiliko huja maishani mwake.
Mstari wa tatu hutaja matokeo yatakayokuja wakati mtu
anaendelea kutafakari juu ya Neno la Mungu.
Ustawishaji – Mizizi yao itapata maji ya uzima
isiyokatika.
103
Kutoa Matunda – Watazaa matunda kwa wakati
unaofaa.
Kutegemea – Tawi lao halitanyauka.
Mafanikio – Chochote wafanyacho kitafanikiwa
Kwa Kuyafanya mawazo yetu Upya
Tunapotafakari juu ya Neno la Mungu, basi “tunabadilishwa
kwa kuyafanya upya mawazo yetu.”
Warumi 12:2a Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali
mgeuze kwa kufanywa upya nia zenu....
Kwa kutafakari juu ya Neno la Mungu, mabadiliko
hufanyika. Nafsi zetu (fikira, hisia, na uwezo wa kuamua)
hubadilishwa na kuwa kile roho zetu huwa wakati wa
wokovu.
Mfalme Suleimani aliandika,
Mithali 23:7a ... Jinsi anavyofikiri moyoni mwake, ndivyo alivyo.
Tunapotafakari juu ya Neno la Mungu, mabadiliko ya ajabu
hufanyika. Nafsi zetu za awali hubadilishwa na kuwa
kipepeo chenye urembo, na kuwa katika mfano wa Kristo
Mwenyewe.
Mbinu za Kutafakari
Fwatilia kwa Makini
Tunapotafakari juu ya Neno la Mungu, tunafuatilia kwa
makini maneno ambayo Mungu amenena. Tunayarejelea
kila mara kwetu wenyewe.
1 Timotheo 4:15 Uwe na bidii katika mambo haya, jitolee kwa
ajili ya mambo hayo kikamilifu, ili kila mtu aone kuendelea
kwako.
Leta Katika Ufahamu
Tunapoendelea kutafakari juu ya Neno la Mungu, tunaanza
kuwa na picha na ufahamu kuumbwa upya. Tunaanza
kujiona kama vile Mungu anavyotuona,
kuwa kile Anasema tuko
kutenda kile Anasema tunaweza kutenda
kuwa na kile anasema tunacho
Mtume Paulo alimwandikia Timotheo kuwa alipotafakari
juu ya Neno, maendeleo yake yataonekana kwa wote.
1 Timotheo 4:15 Uwe na bidii katika mambo haya, jitolee kwa
ajili ya mambo hayo kikamilifu, ili kila mtu aone kuendelea
kwako.
Yoshua aliandika kuwa kwanza tunaitajika kutafakari juu ya
Neno mchana na usiku, na pia kutenda linavyosema, na
mwisho njia yetu itakuwa na mafanikio na tutakuwa na
ushindi bora.
104
Yoshua 1:8 Usiache kitabu hiki cha Torati kiondoke kinywani
mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, ili upate
kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote
yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapoifanikisha njia yako na
kisha utasitawi sana.
Tunapoanza kumwona Yesu jinsi alivyo, kufahamu kuwa
sisi tu viumbe wapya ndani Yake, tutaanza kujiona kama
vile Yeye alivyo. Yohana aliandika kuwa tutakuwa kama
Yeye. Je, ni ahadi ya ajabu iliyoje!
1 Yohana 3:2 Wapenzi, sasa tu watoto wa Mungu, lakini bado
haijadhihirika tutakavyokuwa, lakini twajua ya kwamba, Yeye
atakapodhihirishwa, tutafanana naye, kwa maana tutamwona
kama alivyo.
Tunapotafakari, tutaanza kunena kile Neno la Mungu
linasema kutuhusu kila wakati hadi lifanyike kweli ndani
yetu.
Kulisema kwa Upole
Neno la Kieburania kutafakari ni “kusema kwa upole”.
Tunaposema kwa upole, au kutangaza Neno la Mungu kila
mara kwetu wenyewe, linaachilia nguvu za Neno la Mungu
katika vitendo maishani mwetu.
Isaya 59:21 “Kwa habari yangu mimi, hili ni agano langu nao,”
asema BWANA “Roho wangu, aliyeko juu yenu na maneno yangu
ambayo nimeyaweka katika vinywa vyenu hayataondoka
kinywani mwenu, wala kutoka vinywani mwenu mwa watoto
wenu, wala kutoka vinywani mwa wazao wao kuanzia sasa na
hata milele,” asema BWANA.
Wazia Dhania
Tunapoendelea kutafakari juu ya kweli za kuumbwa upya za
Neno la Mungu, linaachilia dhamira zetu ili kufanya sura za
kiungu. Tunaanza kuwaza mawazo ya Mungu na kujiona
kama viumbe wapya katika macho ya Mungu.
Isaya 55:8,9 “Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu, wala
njia zenu si njia zangu,” asema BWANA. “Kama vile mbingu
zilivyo juu kuliko dunia, ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia
zenu na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
Kufahamu
Tutaanza kutafakari au kuelewa hekima na ufunuo wa
Mungu.
Waefeso 1:17,18 Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu
Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awajalieni ninyi roho ya hekima
na ya ufunuo, ili mpate kumjua zaidi. Ninaomba pia kwamba
macho ya mioyo yenu yatiwe nuru ili mpate kujua tumaini
mliloitiwa, utajiri wa urithi wa utukufu Wake kwa watakatifu.
Neno la Mungu
105
Kuna maneno mawili ya muhimu katika Agano Jipya la
Kigiriki ambayo hutumika kueleza Neno la Mungu.
La kwanza ni Logosi (lililoandikwa), ambalo ni Neno la
Mungu lililoandikwa. La pili ni Rhema, ambalo ni Neno la
Mungu linalonenwa.
Logosi
Logosi ni jina litumikalo katika Biblia yote. Ni maneno ya
jumla ya Mungu yaliyotolewa kwa watu Wake wote.
Rhema
Rhema ni Neno la Mungu linenwalo kwangu mimi binafsi.
Rhema ni ufunuo wa ajabu ambao huja kwetu binafsi kwa
ufunuo wa Roho Mtakatifu tunapotafakari juu ya Neno
lililoandikwa.
Wakati Neno la Rhema huja, kama nuru huingia katika roho
zetu. Tunajua kuwa Mungu amenena kwetu Yeye binafsi.
Ni Neno la Rhema, neno la Logosi linenalwo kwetu kwa
Roho Mtakatifu, ambalo huachilia imani yetu.
NGUVU YA KUTANGAZA NENO LA MUNGU
Mtume Paulo aliandika kuwa imani huja kwa kulisikia na
kwa kusikia Neno la Mungu. Tunalisikia Neno la Mungu
kwa kulisoma sisi wenyewe, kulirudia sisi wenyewe, na kwa
mafundisho mazuri.
Ikiwa kuna hitaji fulani maishani mwetu, tunatakiwa kupata
mistari katika Neno la Mungu ambayo hujibu hitaji hilo na
kisha kuyasoma huku ukiyarudia, punde hayo hufanyika
kweli zaidi kwetu kuliko hali hiyo. Imani imefika.
Neno la Logosi hufanyika Neno la binafsi la Mungu au
Neno la Rhema kama linavyodhihirishwa na kunenwa kwa
roho zetu kwa Roho Mtakatifu. Mara tunapopokea ufunuo
huo, imani huingia katika roho zetu.
Warumi 10:17 Basi, imani chanzo chake ni kusikia na kusikia
huja kwa Neno la Kristo.
Wakati ufahamu wetu huangaziwa na Rhema la Mungu,
tutafikia ufahamu kuhusu ukweli juu yetu katika Yesu.
Tutabadilishwa na kuwa viumbe wapya.
Kulitangaza Neno la Mungu
Kitendo cha kutangaza Rhema la Mungu inaitwa pia kukiri
Neno la Mungu. Neno la Kigiriki ambalo tafsiri yake ni
kukiri ni “homo-logeo.” Kukiri Neno la Mungu ina maana:
Kunena kitu kile kile
Kukubaliana na
Kukuwa katika hali kukubaliana
106
Hii ndiyo ilifanyika kwa kila mmoja wetu wakati tulipokea
ufunuo wa neno la Rhema la Injili. Tulipokea na kukiri
kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, kuwa alikufa kwa niaba
yetu, na kuwa alifufuka kutoka kwa wafu.
Warumi 10:9,10 Kwa sababu kama ukikiri kwa kinywa chako
kwamba “Yesu ni Bwana,” na kuamini moyoni mwako kwamba
Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka. Kwa maana kwa
moyo mtu huamini na hivyo kuhesabiwa haki, tena kwa kinywa
mtu hukiri na hivyo kupata wokovu.
Ninaamini – Ninanena
Wakati tunaamini, tunaitajika kunena, kukiri kile
kimedhihirishwa kwetu. Kuna roho ya imani na inasema,
ninaamini, basi ninanena!
2 Wakorintho 4:13 Imeandikwa, “Niliamini, kwa hiyo nimesema.”
Kwa roho yule yule wa imani pia tuliamini na hivyo tukasema.
Kuelewa Vibaya juu ya Kukiri
Wengi wamekosea juu ya ukweli huu na wamejaribu kukiri
mara kwa mara kitu ambacho wametaka. Wametafuta
maandiko kwa ajili ya neno ambalo linaangazia
mapendekezo yao katika kumlazimu Mungu ili
awatosheleze wao wenyewe.
Ni Rhema, kile Mungu amenena na kuweka wazi Yeye
binafsi kwetu, ambalo litaachilia imani yetu ili kukiri na
kudai kwa ujasiri kile kilicho cha haki kwetu. Ni Rhema,
ambalo sisi kama viumbe wapya, tunaweza kutangaza kwa
ujasiri. Tunaponena maneno haya ya Mungu, mambo yenye
nguvu huanza kutendeka.
Mungu Aliumba kwa Kunena
Tumeumbwa kwa mfano wa Mungu. Mungu ni Muumba na
aliumba kwa kunena maneno.
Waebrania 11:3 Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu
uliumbwa kwa neno la Mungu, vitu vyote vinavyoonekana
viliumbwa kwa vitu visivyoonekana.
Tunaona nguvu ya Mungu katika uumbaji ikitenda kazi
katika sehemu ya kwanza ya Mwanzo ambapo kifungu “Na
Mungu akasema,” imerudiwa mara nyingi.
Tunaumba kwa Kunena
Sisi, kama viumbe wapya, pia tunaumba kwa maneno
tunayosema.
Mithali 18:20 Tumbo la mtu litajaa kutokana na tunda la kinywa
chake, atashibishwa mavuno yanayotakana na midomo yake.
Nguvu katika Ulimi
Maneno yetu yanaweza kuwa maneno yaletayo laana juu
yetu, au yanaweza kuwa maneno ya uhai.
107
Mithali 18:21 Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi, nao
waupendao watakula matunda yake.
Kama viumbe wapya, walioumbwa kwa mfano wa Mungu,
tunaumba kwa maneno. Kwa nguvu ya ulimi, tunaachilia
aidha maneno ya uhai au ya mauti.
Kama viumbe wapya, ni lazima tuchunge midomo yetu na
kuwa waangalifu kuhusu kile tunasema. Labda tunaitajika
kubadili njia ya mazungumzo yetu. Kamwe tusiyaachilie
maneno ya kifo au uovu kutoka vinywani mwetu.
Kulitangaza Neno
Tunapotafakari juu ya Neno la Mungu, imani itaruka ndani
ya roho zetu; na Mungu atadhihirisha Neno Lake kwetu.
Kisha tutatangaza kwa ujasiri kile Mungu amenena kwatika
Neno Lake.
1 Petro 4:11a Ye yote asemaye hana budi kusema kama mtu
asemaye maneno ya Mungu mwenyewe.
Sema kwa Mlima
Yesu alionyesha umuhimu wa imani inayonena, hulitangaza
Neno la Mungu.
Marko 11:22-24 Yesu akawajibu akawaambia, “Mwaminini
Mungu. Amin, amin nawaambia, mtu ye yote atakayeuambia
mlima huu ‘Ng’oka ukatupwe baharini,’ wala asione shaka
moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yametukia,
yatakuwa yake.”
Kwa sababu hiyo nawaambia, yo yote myaombayo mkisali,
aminini ya kwamba mmeyapokea nayo yatakuwa yenu.
Neno la Mungu na Kumbwa Upya Wakati tunapokea
ufunuo wa neno la Rhema la Mungu katika roho zetu za
kuumbwa upya, tutaamini kuwa tunapokea kile Mungu
amenena kwetu. Tutaanza kuambia mlima wa hali maishani
mwetu. Mtu aliye kiumbe kipya atapata kile anasema.
MATANGAZO YA KUUMBWA UPYA
Wale ambao wamepokea ufunuo wa kuumbwa upya
wataanza kutangaza haki zao za kuumbwa upya.
Tangaza kwa Ujasiri
Ninajua mimi ni nani katika Yesu Kristo!
mimi ni kiumbe kipya!
Mambo ya kale yamepita!
Mambo yote yamekuwa mapya!
Mimi ni haki Yake Mungu katika Yesu Kristo!
basi hakuna tena lawama sasa
kwa sababu niko ndani ya Kristo Yesu!
108
Mimi ni mbegu ya imani ya Ibrahimu.
baraka zote za ahadi za Ibrahimu ni zangu.
Mungu hajanipa roho wa hofu,
lakini wa nguvu, na upendo, na wa akili timamu!
Ninaweza kutenda mambo yote katika Kristo anipaye
nguvu! Kazi ambayo Yesu alitenda, Naweza pia
kutenda!
Furaha ya Bwana ni nguvu yangu!
Neno linasema, “hebu na mnyonge aseme, mimi nina
nguvu.” Basi, mimi ni mwenye nguvu!
Hakika, Yesu alibeba magonjwa yangu, na maumivu,
na basi sitaitajika kuzibeba tena!
Kwa mapigo ya Yesu nimeponywa!
Sitashikwa na magonjwa yoyote kati ya haya!
Ni mapenzi ya Mungu juu ya vyote kuwa nitafanikiwa
Nitafanikiwa na kuwa katika afya!
Mungu wangu atakutana na maitaji yangu yote
kutokana na utajiri Wake katika utukufu!
ni Mungu ambaye amenipa nguvu na mali!
Nimemtolea Mungu,
na atazidisha mafanikio ya kifedha kwangu katika hali
ya ukamilifu na yenye kufurika! Chochote
nilichopanda, kile ndicho pia nitavuna!
Nimebarikiwa ninapoingia
na nimebarikiwa niendapo nje!
Chochote ninaweka mikono yangu kufanya
kitabarikiwa na mungu!
Sitashindwa!
Mimi ni kiumbe kipya katika Yesu Kristo!
Kumalizia
Tunaposoma, kusikia, kujifunza, na kutafakari juu ya Neno
la Mungu, imani hujengwa ndani ya mioyo yetu. Kama
viumbe wapya, tunaanza kuachilia nguvu ya Neno la
Mungu lijengalo. Kwa imani, tunatangaza neno hilo
tunaponena.
Neno la Mungu linaishi na lina nguvu. Linao uhai wa
Mungu. Tunapotangaza ufunuo wa kuumbwa upya,
tunakuwa washiriki katika asili Yake Mungu.
Tunapoendelea kutangaza Neno la Mungu, tunajikuta kama
viumbe wapya,
Kuwa yote ambayo Mungu amesema tuko,
kutenda yote ambayo Mungu amesema tunaweza kutenda,
Kuwa na vyote ambavyo Mungu amesema tunaweza kupata.
ufunuo wa kuumbwa upya
hufanyika kweli maishani mwetu.
109
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Eleza jinsi tunaweza kutafakari juu ya Neno la Mungu.
2. Eleza tofauti kati ya Neno lililoandikwa na linalosemwa.
3. kwa nini ni muhimu kutangaza, kusema au kukiri Neno la Mungu kutoka kwa kinywa chako?
No comments:
Post a Comment