MBINU ZA
MAZIDISHO.
UTANGULIZI.
Biblia imerekodi habari za kuumbwa Kwa
ulimwengu na mwanadamu wa kwanza (Adamu na Hawa). Amri ya kwanza iliyotolewa na
Mungu kwa viumbe hawa wapya ilikuwa ni kujizidisha.
“Mungu akaumba mtu kwa mfano wake.Kwa mfano wa Mungu
alimwumba mwanamme na mwanamke aliwaumba, Mungu akawabarikia,Mungu akawaambia
zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi na kuitisha”……Mwanzo 1:27-28
Tendo hili la
uzazi halikutakiwa liwe la kimwili pekee, uzidisho wa kimwili (ongozeko) tu
bali pia lilitakiwa kuwa tendo la kiroho yaani uzidisho wa kiroho
Maadamu Adamu na
Hawa wanajizidisha kimwili wangeijaza
dunia na viumbe vingine kama wao. Watu wenye kumjua Mungu na
wenye kutembea katika ushirika na Mungu. Wangekuwa pia wazazi wa kiroho wenye
kuzaa watu wenye kiroho ( wenye uhsiano
na Mungu). Wangezaa kiroho na kimwili pia.
Kuanguka kwa
mwanadamu wa kwanza dhambini kuliathiri tendo hili la uzazi na kujizidisha Mwanzo sura ya 3.
Dhambi ilileta
matokeo ya kifo cha kimwili ambacho
kilirudisha nyuma uzidisho wa kimwili. Pia ilisababisha kifo
cha kiroho ambacho ni kutengana kati
ya Mungu na mwanadamu mwenye dhambi. Mwanzo 2:11. Hili pia liliathiri
tendo la kujizidisha kiroho.
Kwa sababu Mungu
alimpenda sana mwanadamu aliandaa mpango maalumu wa kumuokoa mwanadamu kutokana
na janga hili la kifo cha kiroho (spiritual death) .
Mungu alimtuma
Yesu kristo kufa kwaajili ya dhambi za
wanadamu wote.Yesu alilipa adhabu ya dhambi dhetu kwa kupitia kifo chake
pale msalabani.Kisha aliishinda mauti kwa kufufuka kwake tena kutoka kwa wafu.
Soma Injili ya Yohana sura ya 20.
Hivyo basi kila
mmoj wetu ni lazima achague kukubali mpango wa Mungu wa wokovu kwa kumkubali na
kumpokea Yewsu Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yake na kutubu dhambi
zake.
Ukiwa mwamini
katika Kristo Yesu umesamehewa dhambi zako umeokolewa kutokana na kifo cha
kiroho (mauti ya kiroho) japo kuwa mwili wako siku moja utakufa lakini utaendelea kuishi kiroho na utapokea mwili mpya utakao ishi milele mbinguni. Soma Wakoritho wa kwanza sura ya 15.
Kuokoka ni kuzaliwa kiroho. Unaumbwa upya kiroho.
“Hata
imkeuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipy.a Yakale yamepita tzama yamekuwa mapya. 2 Wakorinto
5:17
Mwanzo wa
uumbaji wa mwanadamu wa kwanza agizo
la Mung kwao lilikuwa ni Kujizidisha.Agizo la kwanza kwa waamini
ni sawa na lile Mungu alilomwagiza Adamu Kujizidisha kiroho.
Tunatakiwa
kujizidisha kiroho na kuijaza dunia kwa kuwaleta watu kwa Yesu Kristo kama sisi
tulivyoletwa na kuwafanya kuwa na
ushirika na Mungu.
Wakati Yesu
alipowaita watu kumfuata ilikuwa ni wito
wa mazidisho.ya kiroho. Luka 5:10
Agizo lake la
mwisho kwa waamini lilikuwa ni kujizidisha
kiroho.Matendo 1:8
Ili kukabiliana
na changamoto yakuwafikia maelfu ya watu wanaokufa katika dhambi bila kuipokea
Injili kila mwamini anapawa kuwa mzazi ( mwenye kujizidisha) . na kujifunza kanuni za mazidisho .
Kozi hii
inafundisha mbinu za ki-Biblia ,uzazi na mazidihs ya kiroho ambazo
zitakuwezesha wewe kujizidisha katika kutii Agizo
la Mungu. Utajifunza jinsi ya kujidizisha kiroho kama wewe binafsi na kushirikiana na waamini wengine katika kanisa la mahali pamoja na makaisa
mengine.
Kama ukifanyia
kazi kanuni za ki-Bibia zilizofundishwa katika kozi hii utajisikia kuwajibika
na kuwaleta maelfu ya watu waliofunzwa na kuandaliwa kwa kazi ya mazidisho. Ukifuata kanuni za ki-Biblia utapata
matokeo ya ki-Biblia.
MALENGO YA KOZI.
Baada ya kumaliza kujifunza kozi hii utaweza:
· Kujizidisha
kiroho kwa kufanyia kazi mbinu na kanuni
za mazidisho.
· Kutoa muhtasari
wa kanuni za mazidisho zilizofundishwa katika Agano jipya.
· Kueleza jinsi
kila mwamini anavyoweza kjizidisha kiroho ili kuweza kuleta maelfu ya watu kwa
Kristo Yesu.
· Kufanya nyumba
yako kuwa kituo cha mazidisho.
· Kuainisha sababu
zinazo kwamisha mazidisho ya kiroho.
· Kuanzisha kituo
cha mazidisho ya kiroho.
SURA
YA KWANZA
WAVUVI
WA WATU.
Malengo ya mada.
·
Baada
ya kumaliza mada hii utaweza:
·
Kuandika
mstari wa ufunguo toka kichwani mwako.
·
Kutambua
agizo la kwanza na la mwisho la Bwana Yesu kwa wanafunzi wake.
·
Kufafanua
maana ya mazidisho.
·
Kueleza
maana ya mazidhisho ya kiroho
·
Kueleza
maana ya mbinu
·
Kueleza
maana ya methodolojia.
·
Kueleza
maana ya methodolojia ya mazidisho kiroho.
·
Kutoa
mhtasari wa kanuni za asili za uvuvi zinazotumika katika uvuvi wa kiroho.
Mstari wa
ufungo.
“Yesu
akawaambia, njoni mnifuate, name nitawafanya kuwa wavuvi wa watu”. Marko 1:17
Wakati Yesu
alipoanza huduma yake ya hadharani hapa
duniani aliwaita watu kadhaa ili kuwa wanafunzi wake wa awali.
Agizo(amri) lake
la kwanza lilikuwa ni kujizidisha kiroho. Kama wangemfuata, yeye angewafanya wavuvi wa watu.Wangeza kwa kuvua kiroho wanawake na wanaume kama
wao.
Ujumbe wa mwisho
wa Yesu kwa wanafunzi wake ulikuwa ni wito kwa uzazi na mazidisho ya
kiroho.
“Lakini mtapokea
nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho mtakatifu; nanyi mtakuwa ni mashahidi
wangu katika yerusalemu na katika Uyahudi wote na Samaria na hata mwisho wan nchi.
Akiisha kusema hayo;walipokuwa wakitazama akainuliwa wingu likampkea kutoka
machoni pao” Matendo ya Mitume 1:8-9
Ni jinsi gani
wanafunzi wangeweza kutimiza hili agizo kuu walilopewa na Yesu?
Namna gani
kundi hili la watu wangejizidisha na kuufikia ulimwengu wote ?
MBINU ZA MAZIDISHO.
Yesu alifunua
mbinu maalumu ambazo zingewawezesha wanafunzi wake kutimiza agizo kuu. “Kuzaa Kiroho” Mojawapo na muhimu ya
mbinu hizi zilitolewa kama sehemu ya
Agizo kuu katika Matendo ya Mtume 1:8.
Wanafunzi
wangejizidisha kupitia kuvikwa nguvu na
Roho Mtakatifu.Mbinu zingine zilifunuliwa pale wanafunzi walipoanza kujizidisha
na kuufikia ulimwengu kwa Injili. Mbinu
hizi zimeandikwa katika kitabu cha Matendo ya mitume. Na nyaraka katika Agano
jipya.
Kozi hii
inaelezea na kutoa ufafanuzi wa hizi mbinu za mazidisho. Kozi hii inakufundisha wewe jinsi
ya kutumia mbinu hizi ili kuweza kujizidisha kiroho na kuweza kutimiza Agizo
kuu la Mungu.
Lakini kabla ya
yote unapaswa kuelewa maana ya kujizidisha.
Kuzidisha ni kuongezeka mara nyingi kiidadi kwa kujizidisha.Kitu kinapojizidisha huzaa zaidi
na zaidi katika ufanano uleule.Mazidisho ni matokeo ya kuzidisha.
Mfano 3×3 = 9
wakati 3+3 =6. 4×3 maana yake ni
kwamba namba 4 zinatakiwa kuwa tatu,
yaani 4, 4, 4 ambako huleta jawabu la 12. Hivyo kuzidisha huleta jawabu kubwa
kuliko kuongeza. Jambo la msingi hapa ni kwamba namba moja hujirudia katika
mfanano ule.
Katika ulimwengu
wa asili wanawake na wanaume wanazaliana wenyewe kwa kuwa na watoto. Wanajizidisha kimwili.
Mazidisho ya
kiroho yanatokana na kuzaliana kiroho. Mwamini huzaa kiroho kwa
kuwashirikisha Injili watu wengine
wasiomjua Mungu (wasiookoka) kwa
kushuhudia na kuhubiri na kuwaongoza hao aliowashuhudia au kuwahubiri kuwa
waamini na kuwawezesha kuwa wanafunzi
wa Yesu.
Biblia
inadhihirisha mbinu za ki Mungu kwaajili ya mazidisho ya kiroho.
Mbinu ni mpango uliowekwa kwajili ya kufanikisha
lengo fulani mahususi. Au ni hatua zinazowezesha jambo fulani kufanyika kwa
ufanisi kama ilivyokusudiwa.
Methodolojia ni Mkusanyiko wa mbinu mbalimbali zinazowezesha au kufanya kazi kwa pamoja ili
kufanikisha jambo fulani lililokusudiwa.
Methodolojia ya mazidisho ni mkusanyiko wa mbinu mbalimbali
zinazowawezesha waamini kufikia lengo la uzazi wa kiroho kwa njia ya
kujizidisha.
Lengo
halibadilikji. Tunatakiwa kuzaa kiroho na
kuufikia ulimwengu wote kwa Injili ya
Yesu Kristo. Kuna mbinu mbalimbali ambazo
kwazo lengo hili laweza kifikiwa . Mbinu
hizi kwa pamoja huitwa methodolojia ya mazidisho.
Wakati Mwamini
anafanyia kazi mbinu za ki Mungu za
mazidisho matokeo yake huwa ni uzao wa
kiroho.Yaani waamini wapya huzaliwa kiroho katika mji wa mimba ambao ni
kanisa.
WITO KWA MATENDO
Watu ambao Yesu aliwaita kwanza kuwa wanafunzi wake walikuwa ni wavuvi.Walikuwa ni watu wenye
kazi. Hawakukamata samaki kwa wakati
mmoja. Walitumia nguvu kubwa kuvua na kupata samaki wengi wa kila aina.
Wakati Yesu
alipowaita kuwa wavuvi wa watu alidhihirisha mpango wenye kufanana na ile kazi yao ya uvuvi
kwaajili ya mazidisho ya kiroho. Wanafunzi wake walitakiwa kuvua watu toka kila taifa, tamaduni, lugha na makabila
yote. Nyavu zao za kiroho zingejazwa.
Yesu aliwaita watu kwaajili ya kazi .Alisema angewafanya kuwa wavuvi wa
watu.Hawangekuwa watazamaji tu katika mpango wa Mungu.Wangekuwa washiriki
wakuu kwa kuwa wavuvi wa roho za watu.Wito wa Yesu bado ni sawa. Haujabadilika.Tunapaswa kuwa wavuvi wawatu. Kama si wavuvi basi si wanafunzi.
WAVUVI WA WATU
Kwanini Yesu
alitumia mfano wa uvuvi kuwaita wanafunzi wake ?
Kwanza ulikuwa
ni mfano ambao wangeuelewa kwa urahisi.Hawa
watu waliishi kwa shughuli ya uvuvi.
Kazi ya uvuvi ilikuwa ni kitu ambacho walitumia nguvu zao nyingi na muda wao mwingi. Wakati
Yesu alipowaita kuwa wavuvi walielewa
kwamba wangewavua samaki (watu)
katika ulimwengu wa kiroho.
Walielewa pia mahitaji ya wito huo. Uvuvi wa kiroho ungehitaji kujitoa
kikamilifu. Kutoa muda na nguvu.
Pili Yesu
alitumia mfano wa uvuvi kuwaita wanafunzi wake kwa sababu kuna kanuni za uvuvi wa asili zinazoweza kutumika katika uvuvi wa watu (uvuvi wa kiroho).
Baadhi ya kanuni hizo ni:
1.
Unapaswa kwenda
mahali samaki walipo.Kama
unataka kupata samaki unapaswa kwenda samaki walipo. Samaki huishi majini. Huwezi kuwapata samaki kwakuwasubiri ukiwa juu
ya mlima au ukiwa jangwani. Mvuvi wa
watu unapaswa kwenda mahali ambako watu ambao hawajaokoka wanapatikana au
kuishi. Watu ambao hawajaokoka
wanapatikana katikia maeneo mbalimblai huwezi kuwasubiri katika mejengo ya
kanisa ndipouwavue. Nenda mahali
wanakopatikana, mfano
sokoni,mashuleni, hospitalini, magerezani,maofisini majumbani na mahali pengine
popote wanakopatikana na kisha wavue
2. Lazima uchunguze mazingira.
Katika uvuvi wa asili mvuvi anapovua huzingatia mazingira, huchunguza
kina cha maji, aina ya maji, ili kujua kama ni maji ya chunvi au la, namna
upepo unavyopiga. Mambo haya yote kwa kawaida hutoa tathimini ya aina ya mtego
na mbinu unazopaswa kutumia Kuvua. Hizi pia ni mbinu utakazotumia katika
uvuvi wa watu. Kweli hizo hapo juu ni
sawa kabisa katika mambo ya kiroho.
Nilazima uchunguze mazingira
ambamo watu wanaishi. Nini mahitaji yao? (Tambua mahitaji yao) Nini kinaendelea katika maisha yao? Hii itakusaidia wewe kujua mbinu utakazotumia katika kuwavua watu hawa.
Yesu alipokutana
na mwanamke kisimani katika Ijili ya Yohana 4 alichunguza mazingira
aliyomkuta yule mwanamke . Alikuwa anatafuta maji ya kawaida. Yesu alitumia hitaji hili la mwanamke kumsaidia kutambua hitaji lake la kiroho.
Mbinu aliyotumia ilimleta mwanamke katika ufalme wa Mungu.
Kama huchunguzi mazingira katika uvuvi wa kiroho (watu) utajikuta mwenyewe unavua
juu ya mlima. Kwa sababu hujui watu
wanakopatikana na jinsi ya kuwafikia.
3
.Tumia mbinu
mbalimbali.
Mvuvi bora hutumia mbinu mbalimbali katika kuwakamata samaki. Hutumia vitu mbalimbali ili kuwavutia samaki.
Hutumia zana mbalimbali za uvuvi . Aina mbalimbali za samaki huvutiwa na mbinu
mbalimbali za uvuvi. Ndiyo maaana mvuvi
bora hutumia mbinu mbalimbali. Mvuvi aweza kujifunza baadhi ya mbinu hizo katika
vitabu vinavyohusu uvuvi. Anajifunza
mbinu zingine kutokana na uzoefu na uchunguzi wa kina. Mbinu anazotumia
hubadilika lakini lengo daima linabaki kuwa lilelile. Kukamata samaki.
Kama unataka
kuwa mvuvi bora wa watu unapaswa kutumia mbinu mbalimbali. Watu wanatofautiana
hivyo hata vitu vinavyowavutia vinatofautiana.
Wengine huvutiwa na mahubiri au mafundisho aukufarijiwa wakati wa matatizo.
N.k. Mbinu za uvuvi wa kiroho zinatofautiana lakini lengo daima ni lilelile. Kupata roho zilizopotea na kuzileta kwa
Yesu Kristo.
4. Unapaswa kutoa nje na kurudisha tena. Haijalishi
mbinu unayotumia, unapswa kuitupa nyavu majini na kuitoa tena. Katika uvuvi wa kawaida jinsi unavyotega mitego yako majini ni jambo
muhimu sana. Unatakiwa kutega mitego yako kwa umakini sana . Pia unapaswa kuwa
makini katika kuwatoa samaki kwenye mitego baada ya kuwakamata.
Katika ulimwengu
wa rohotumeahidiwa kwamba tukilitoa Neno la Mungu halitaturudia bure.
Litafanikisha lengo katika maisha ya
watu Isaya 55:11.
Unapotumia Neno
la Mungu utakuwa katika shabaha kila wakati
na hatimae litawakamata wanawake na wanaume nakuwaleta katika ufame wa
Mungu.
5. Tambua majira na nyakati.Majira ma nyakati huathiri sana shughuli ya uvuvi katika
ulimwengu wa asili. Baadhi ya samaki huhama na hawawezi kupatikana katika baadhi ya kanda wakati wa majira fulani. Samak wakubwa hukamatwa mapema mchana wanapokuja
katika eneo la juu la uso wa maji ili kupata chakula. Kama utavua katika majira yasiyo sahihi au
muda usio sahihi huwezi kuwakamata samaki wengi. Wakati ni muhimu sana katika uvuvi wa kiroho pia.
Utajifunza
baadae jinsi ilivyo muhimu kuvua maeneo
yenye samaki wengi wakati samaki wanauma kiroho.
6. Lazima
uwe mvumilivu.Katika ulimwengu wa asili mvuvi hutakiwa kuwa mvumilivu.Ni
lazima asubiri samaki waingie kwenye mtego aliotega na kukamatwa. Hii pia ni kweli katika ulimwengu wa roho.
“Kwahiyo
ndugu vumilieni hata kuja kwake Bwana. Tazama mkulima hungoja mazao yake ya
nchi yaliyoyathamani, huvumilia kwaajili
yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho” Yakobo 5:7.
KUZAA KIROHO
Katika ulimwengu wa asili samaki hupelekea kutokea
kwa samaki wengine wengi kwa njia ya kuzaliana. Uvuvi katika ulimwengu wa asili
husababisha mazidisho ya samaki .
Uvuvi katika ulimwengu wa roho husababisha mazidisho ya watu katika ufalme wa Mungu. Uzazi wa
kawaida husabisha mazidisho ya watu walio hai. Uzazi wa kiroho husababisha pia mazidisho ya watu kiroho.
Hii haiji
kutokana na programu za kibinadamu. Uzazi
wa kiroho huja kupitia mtiririko wa
maisha ya kiroho toka kwa Mungu. Katika maisha ya kawaida ya binadamu
maisha ya kiumbe kipya huanza katika tumbo la uzazi la mwanamke(uterus) na
seli hai moja . Seli hiyo hujizidisha
hadi mtu kamili anapokuwa amefanyika. kisha
mtoto huzaliwa.
Uzazi wa kiroho
pia ni sawa na huo.Huanza na mtiririko
wamaisha ya ki-Mungu kwa mtu mmoja ,
hujizidisha katika tumbo la kiroho la uzazi
ambalo ni kanisa. Na kisha
mtoto wa kiroho huzaliwa.
Katika mada inayofuata
utajifunza jinsi kuzaliana na
kujizidisha kiroho kunavvoanza.
zoezi
1.
Andika
mstari wa ufungo wa mada hii toka kichwani wako
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
2.Agizo la kwanza
na la mwisho la Bwana Yesu kwa wanafunzi wake lilikuwa ni.
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
3.
Eleza
maana ya mazidisho
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
4.
Ninamna
gani waamini wanavyoweza kuzaa kiroho
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
5.
Eleza
maana ya mbinu.
.......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................…………………
6.
Eleza
maana ya methodolojia
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
7.
leza maaana ya methodolojia ya mazidisho.
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
8.
Toa muhtasari wa kanuni za uvuvi katika ulimwengu wa asili zinazoweza kutumika katika uvuvi wa watu.
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
MADA YA PILI
SIKU YA VITU
VIDOGO
Baada ya kumaliza kujifunza mada
hii utaweza.
· Kuandika
mstari wa ufunguo toka kichwani mwako.
· Kuandika
mhtasari wa kanuni za msingi za mazidisho.
· Kueleza
aina mbalimbali za ukuaji wa kanisa.
· Kuorodhesha
marejeo ya maandiko yanayoonesha kwamba mazidisho ni ki-Biblia.
·
Kubaini
sababu hasi zinazoweka msisitizo wa
kukua kwa kanisa kiidadi pekee.
Mstari wa ufunguo.
“Maana ninani aliyedharau siku ya
mambo madogo ? ” (Zekaria 4:10)
Ukuaji wa mwili wa binadamu
huanza na seli hai moja ambayo ni matokeo ya ushirika kati ya mwanamme na mwanamke kupitia tendo la
ndoa. Seli hiyo hujizidisha katika tumbo la uzazi la mwanamke mpaka kiumbe kingine kimeumbika. Kiumbe hicho
kinapokuwa kimepevuka pia huwa kina
uwezo wa kujizidisha.
Ukuaji wa kiroho huanza na
ushirika wa karibu kati ya mtu mmoja na Bwana Yesu Kristo. Maisha ya kiroho
hutiririka katika roho na nafsi ya mtu
aliyempokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yake.
Aina hii ya uzima hulelewa katika
mji wa mimba wa kiroho ambao ni kanisa, hukua
mpaka mwanafunzi mwingine amezaliwa .
Mwanafunzi huyo anakuwa na uwezo wa kuzaa kiroho kwa kuwaleta watu
wengine kwa Yesu Kristo. Misha huanza na seli hai moja katika wa kimwili au
ulimwengu wa kiroho.
Ndiyo maana Mungu alisema nani
aliyedharau siku ya mambo madogo ? Zekaria 4:10.
Katika mada hii utaanza na mambo
madogo. Utajifunza kanuni za msingi za
mazidisho na aina mbalimbali za ukuaji kiroho. Utajifunza jinsi Mungu
anavyohusika na mazidisho ya kiroho na vigezo vinavyoonesha msisitizo potofu
katika ukuaji wa kanisa kiidadi (numeric growth). Utaanza na mambo madogo
ambayo kwayo ufunuo mkuu umejikita.
Kanuni
za msingi za mazidisho.
Nilazima
uelewe kanuni za msingi za mazidishoya kirohoili uweze kujifunza na kufanyia
kazi . Kanuni za ki-Biblia za mazidisho hazibadiliki
lakini mbinu za uzidishaji zaweza kubadilika lakini lengo daima linabaki kuwa
lilelile. Lengo na kanuni za mazidisho zinabaki kuwa sawa lakini mikakati ya kufikia lengo hilo hubadilika.
Lengo laMungu tangu mwanzo wa
nyakati limekuwa ni :
,,,,”Yaani kuleta madaraka ya wakati
mtimilifu, atavijumlissha vitu vyote katika Kristo,vitu vya mbinguni na vitu
vya duniani pia naam, katika yeye huyo”Waefeso 1:10
Watu wake na hali ya kihistoria
hubadilika kati ya mataifa, Mungu
hubadili mikakati yake ili kufanikisha lengo lake.
Mfano Wakati mababa wa Israeli waliposhindwa
kutekeleza wajibu wao wa kiroho
(kikuhani) Mungu aliinua makuhani. Wakati makuhani walioanza kuwa
wadhalimu aliinua manabii kama viongozi wa kiroho.
Yesu alitumia mbinu mbalimbali katika huduma yake. Hakushugulika na watu wote kwa njia moja. Mbinu zake zilibadilika lakini lengo lake
lilibaki sawa daima. Kugusa na kubadilisha maisha ya watu.
Hizi ni baadhi ya kanuni za msingi unazopaswa kuzielewa ‘ Siku ya mambo madogo’ . Kabla ya kuanz kujihusisha.
Mungu huhusika na mkutano.
Mungu daima amekuwa anahusika na
ulimwengu mzima
“Kwamaana jinsi hii Mungu
aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwana wa pekee ili kila mtu amwaminie asipotee
bali awe na uzima wa milele” Yohana 3:16
,,, bali huvumilia kwenu maana
hapendi mtu yeyote apotee bali wote waifikilie toba” 2 Petro 3:9.
Yesu alilielezea hili aliposema “ Mwana
wa adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea” Luka 19:10
Mungu anahusika na mkutano .
Anahusika na idadi. Anahusika na mazidisho ya waamini watakao zaa na kuieneza
Injili. Unapoanza somo la mazidisho unapaswa kuanza na mtazamo huo alio nao Mungu wa kuufkia
ulimwengu wote kwa ujumbe wa Injili.
Ni Mungu anaetoa au kusababisha ukuaji.
Mazidisho ya kiroho hayawezi kufikiwa
bila Mungu kuhusika. Ni Mngu
anaesababisha ukuaji.
…”mwenye kukuza ni Mungu” 1. Wakorintho 3:
Mwamini nilazima atumie kanuni za
ki Mungu. Kuna kanuni katika Neno la
Mungu zinazoshusika katika maisha ya kila siku
na huduma.Mungu hutenda kazi kupitia watu wanaojua kufanyia kazi kanuni
hizo za kiungu.
Tangu mwanzo wa ulimwengu Mungu
amekuwa akifanya kazi katika dunia hii kwa kupitia mwanadamu. Aliwapa adamu na Hawa kazi ya kutunza
bustani. Alimtuma Nuhu kuokoa maisha hapa duniani wakati wa gharika kuu. Mungu
alimwinua Ibahimu kuunda taifa la Israeliambalo kupitia kwalo angejidhihirisha
kwa mwenyewe kwa mataifa yote ya dunia. Mungu pia aliwatuma manabii, wafalme, na
waamuzi kufanikisha mpango wake katika
Agano la kale.
Katika Agano jipya mtu Yohana
mbatizaji alitayarisha njia ya Bwana Yesu.
Yesu alianza hudumayake na watu wa kawaida. Na alipopaa kwenda Mbinguni aliacha hatima ya
Injili katika mikono ya watu hawa wa kawaida.
Rekodi zote za Biblia zinaonesha Mungu akishirikiana na
mwanadamu au mwanadamu akituia kanuni za
ki Mungu kufanikisha lengo la Mungu. Hii
ni kweli katika mazidisho ya kioho .
Mungu hamtumii mtu yeyote kutangaza Injili . Huwatumia wanawake na
wanaume wanaoelewa na kushiriki kaununi zake za mazidisho.
Paulo alielezakuhusu
ushirikiano “ Nilipanda na Apolo
akamwagilizia maji lakini ni Mungu anaekuza” 1 wakorintho 3:6.
Paulo alieleza umuhimu wa waamini
kutimiliza wajibu wao katika mpango wa Mungu.
“ Kwa kuwa kila atake liitiajinala
Bwana ataokolewa .
“Basi wamwitaje yeye wasiye mwamini? Tena wamwinije yeye wasiyemsikia? Tena
wamsikiaje pasipo mhubiri ?”
Warumi 10: 13-14
Yesu ndiyo lengo la mazidisho. Yesu alisema ;
“Nami nikiinuliwa juu ya nchi nitawavuta wote kwangu” Yohana 12:32
Yesu alikuwa akiionga hapa kuhusu kuinuliwa juu ya
msalaba kufa kwaajili ya dhambi za ulimwengu. Kupitia kifo chake angewavuta
watu wote kupitia nguvu ya Injili.
Unapohubiri Injili tambua kwamba tayari Yesu amekwisha inuliwa. Anpokuwa ameinuliwa juu katika maisha yako n
kanisa lako atu watavutwa na nguvu ya Injili.
Mazidisho ni lazima Yesu anapokuwa anpokuwa ameinuliwa juu.
Neno la
Mungu hubababisha ukuaji. Mathayo 13:1-9
Yes alieleza mfano katika Mathayo 13:18-23 soma habari hii katika
biblia yako. Katika mfano huu mbegu
huwakilisha Neo la Mungu. Mungu
ameahidi kwamba tunapopanda Neno lake halitarudi bure.
“ Ndivyo litakavyo kuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu halitabnirudia bure.
Bali litatimiza mapenzi yangu nalo litafanikiwa katika mambo niliolituma
ISaya 55:11
,,,,Ninaliangalia neno langu ili nipate kulitimiza” Yeremia 1:12
Ni Neno la mungu ambalo huleta mabadiliko katika
maisha ya watu. Mabadiliko hupelekea
ukuaji na mazidisho ambayo yamejikita katika Neno la Mungu.
Roho Mtakatifu
huwezesha mazidisho. Katika ujumbe wa
mwisho wa Yesu kwa wanafunzi wake alisema,
“Lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu
Roho mtakatifu; nanyi mtakuwa ni mashahidi wangu katika Yerusalemu na katika
Uyahudi wote na Samaria na hata mwisho wan nchi” Matendo ya
Mitume 1:8
Nguvu ya roho mtakatifu huwezeshamazidisho. Karama
za Roho Matatifu huwezesha mazidisho. Tunda la Roho la roho mtakatifu
hubababisha kuzaliwa kwa waamini wapya.
Tuachunguzakazi ya Roho Mtakatifu
katika mazidisho katika kozi hii baadae.
Mazidisho ni
wajibu shirikishi. Katika kanisa la
kwanza (kanisa la karne ya kwanza baada
ya Kristo). Kazi ya kutangaza Injili haikuwa ya wachungaji, wainjhilisti,
waalimu, manabii na mitume pekee. Kila mwamini wa agano jipya aliwajibika
katika kueneza Injili.
Kama tunataka kuufikia ulimwengu wote kwa Injili ni
lazima turudi katika mpango wa agao
jipya wa kila mwamini katika mwili wa
Kristo (kanisa) kuwa mzazi wa kiroho.
Hatuwezi
kuufikia ulimweng, kwa kuacha wajibu wa
kueneza Injili mikononi mwa watu wachache tu. Kuna waamini wa kutosha ambao
wangeweza kuufika ulimwengu wote kwa urahisi kwa Injili ya yesu Kristo.
Kumekosekana watu wenye unuo wa kutambua
kuitikia fursa kwaajili ya mazidisho.
Agizo lililotolewa na Yesu kwa waamini “ Kwenda
ulimwengui mwote na ujumbewa Injili. Hutakiwi kusubiri amri ya kwanza kwa sabau amri imekwisha
kutolewa .
AINA ZA UKUAJI
Biblia imeelezea aina nne za za ukuaji wa kanisa au
mazidisho ya kanisa. Aina hizo ni :
1.
Ukuaji
wa kijografia, Ukuaji huu ulitabiriwa na Yesu Matendo ya Mitume 1:8. Kanisa
lilitakiwa kukua kijografia, yaani kuenea toka eneo moja mpaka eneo jingine,
Toka mji mmoja mpaka mji mwingine, taifa moja hadi taifa jingine.
2.
Ukuaji
wa kiidadi, Kanisa ingeongezeka kiidadi wakati linakuwa kijografia. Kuka
kiidadi kwa kanisa la kwanza kumeelezwa
katika katika kitabu xcha Matendo ya mitume.
Mfano. Kanisa
liliongezeka toka watu 12 hadi watu 120 matendo 1;15
Toka watu 3000
katika matendo 2:41 hadi watu 5000 katika Matendo 4:4.
3.
Ukuaji
wa kimakundi (Ethic growth). Kanisa la
kwanza pia lilikuwa kimakundi .
Injili ilienea nje ya mipaka ya kiyahudi ilifika mpaka Samaria na kwa matafifa yote. Injii ilienea katika
makundi mbalimbali yenye tamaduni tofautitofauti . Toka utamadui wa kiyahudi
mpaka utamaduni wa kisamaria.
4. Ukuaji wa
kiroho. Ukuaji wa kiidadi sio msisitizo pekee wa mazidisho ya kiroho. Kama
utakavyojifunza baadae katika kozi hii. Ukuaji wac kiroho ni muhimu sana.
Wanafunzi wa Yesu ni lazima wakue katika viwango vya ubora wa kiroho na kiidadi.
“Lakini
kueni katika neema na katika kumjua
Bwana wetu na mwkozi Yesu Kristo” .2 Petro 3:18
Shauku ya ungu ni kwamba:
“Tuishike kweli katika upendo na kukua hata
tumfikie yeye katika yote, aliye kichwa Kristo”. Waefeso 4:15.
MSISITIZO WA IDADI
Baadhi ya watu hudharau suala la ukuaji wa kiroho
katika mazidisho ya kanisa na ukuaji wa kanisa kwa sababu wanaamini kwamba kuweka msisitizo wa idadi si sahihi.
MADA YA TATU
KIELELEZO CHA
MAZIDISHO
Baada ya kumaliza mada hii utaweza;
Kuandika mstari wa ufunguo toka kichwani.
Kufafanua maana ya mfano.
Kueleza
sababu kwanini Yesu alitumia mifano.
Kubaini kanuni za mazidisho katika mifano
iliyofundishwa na Yesu.
Msitari wa ufunguo.
……………………………………….Marko 4:33
UTANDULIZI
Mada hii inalenga katika kananu za mazidisho
zilizofundishwa na Yesu katika huduma
yake akiwa hapa duniani. Kielelezo ni habari inayotumia mfano
kutoka katika mazingira asilia ya ulimwengu kuelezea ukweli wa kiroho.
Maana halisi ya neon kielelezo ni kuweka kando ya ,
kulinganisha. Katika vielelezo Yesu alilinganisha mifano asilia na kweli za kiroho. Kielelzo habari ya
kiulimwengu yenye kweli za ki-Mbingu
Kwanibni vieelezo?
Wanafunzi walimuuliza yesu kwanini
alitumia mifano kufundisha kweli za kiroho
“Na wanafunzi wakja wakamwambia, kwanini unaongea
nao kwa mifano?”
Mathayo 13:10.
Yesu akajibu, kwa sababu ninyi mmejaliwa kuzijua
siri za ufalme lakini si wao {kosa}
Mathayo 13:11
Kuelewa kweli zilizofundishwa kwa mifano
kuliwezekana kwa wanafunzi kwa sababu walikuwa
na ufahamu wa kiroho. Waliokuwa hwana ufahamu wa kiroho walisikia mifano
na wakashindwa kuielewa. Kweli za kirohgo zaweza kutambuliwa kwa ufahamu wa
kiroho.
1Kor 2:14
Tmu mwenye ufahamu wa kiroho ni mtu Yule aliyezaliwa
mara ya pili. Wale wqenye ufahamu wa kiroho huelewa kanuni zilizofundishwa katika mifano. Mtu wa
mwili kamwe hawzi kuelewa.
INJILI YA UFALME
Injili unayotakiwa kuihubiri kwa mataifa ni injili
ya ufalme wa Mungu. Ujumbe wake unahusu kuzaliwa kwa Yesu, maisha na huduma
yake.Inahusiaha kifo chake kwaajili ya wenye dhambi na ufufuo wake toka kwa wafu. Unapawa kuwaeleza watu namna
ya kuingia katika ufalme wa Mungu.
MFANO WA
MAZIDISHO.
Yesu alitoa mifano mingi kuhusu ufslme wa Mungu.
Mojawapo ya mifano hiyo ulihusu jinsi ufalme wake ungeenea duniani kote. Mifano ifuatayo kuhusu kuka kwa ufalme inadhihirisha nanuni za msingi
za mazidisho. Tazama marejeo yotwe katika biblia yako.
·
Kondoo
aliyepotea Mathayo 18:12-14; Luka
15:4-7
·
Sarafu ilyopoteLuka 15:8-10
·
Mwana
mpotevu: Luka
15:11-32
Mifsno
hi inadhihirisha jinsi Mungu anavyohusika na waiopotea na uharaka wa unaotakiwa kuufanya ili kuwaleta katika ufalme wa Mungu. Haijalishi
kwanini wamepotea. Kondo walikuwa wanatangatanga, sarafu ilipotea kwa uzembe.
Mwana alipotea kutokana na uasi wake mwenyewe. Unatakiwa kufanya kila jitihada
kuwatafuta waliopotea dhambini. Unatakiwa kuwaendea kule walipo na
siokuwasubiri waje kwako.
Mungu
hajihusishhi na jinsi gani watu walivyopotea bali jinsi wanavyoweza kupatikana.
Empty
Banguet table
Sherehe
tupu Luka 14:15-23
Mazidisho ayapaswi kusimama eti
kwa aababu baadhi ya watu wanakataa kuitikia mwito wa Injili. Unatakiwa
kuwatafuta watu walio na njaa ya kiroho na kuwaleta katika sherehe
iliyoandaliwa na Bwana.
Mtini usiozaa matunda Luka 13:6-9
Yesu alitoa mfano wa mtini usio
zaa. Mtini ni kiwakilishi cha taifa la
Israeli. Mungu aliwainua Israeli kama taifa
ambalo kwalo angeudhihrisha ufalme wake kwa ulimwengu kwa kupitia taifa
hili. Mungu alitarajia mtini Israeli kuza matunda kutoka kwa mataifa ya
kipagani ya luimwengu kwa kuwashirikisha Injili. Lakini Israeli walibaki tasa
na wasio na matunda.
Sasa Mungu ameliinua kanisa kwaajili ya kusudi hili. Mungu anawalea
waamini na kuwaanda kuwa wazalishaji
kama alivyofanya kwa taifa la Israeli. Kusudi lake ni lilelile.
Tunatakiwa kuleta matunda toka kwa mataifa yaani kuwaleta watu kwa Yesu kw
kuwahubiri Injili ya Ufalme wa Mungu. Mungu hapendezwi na mti usio zaa matunda.
·
Talants: Mathayo 25:14-30; Luka
19:11-27
·
Msafiri : Marko 13:34-37
·
Mtumishi: Mathayo 24:43-51; Luka 12:39-46
·
Mtumishi anayetazama: Luke 12:36-38
·
Wakili mwaminifu: Mathayo 25:14-30
Mfao
wa mtumishi unasisitiza uwakili wa hekima katika Injili ambao waamini
wamekabidhiwa. Kila mwamini amepewa talanta au kipawa fulani cha kutumia katika
kuieneza Injili. Unatakiwa kutumia talanta uliyopewa katika kuieneza Injli bila
kujali talanta yako ni kubwa au ndogo kiasi gani. Kila mwamini anapaswa
kujizidisha. Yesu atakaporudi tena atawatuza wale waliotumia vizuri talanta
zao.
Wale
wasiozalisha wanaitwa kuwa sio waaminifu.
Luka (Matthew
16:27)
Yesu
alitambua kuwango cha uzalishaji kanika hatua za mazidisho.
Luka 12:48
……………………………………………………………………………………………..
Ufalme wa mungu huenezwa kwa hekima kwa kutumia
vipawa ya kiroho tulivyopewa na Mungu.
Ukitumia kile Mungu alichokupa thawabu yako inaongezeka. Usipotumia utapoteza
hata kile ulichonacho.
Mpanzi Mathayo
13:3-8; Mark 4:3-8; Luka 8:5-8
Ufalme wa Mungu unaenezwa kwa
kupanda mbegu ya neno la Mungu. Hakuwezi kuwa na mazidisho pasipo Neno la
Mungu. Matunda hutegemea uzima ulio katika
mbegu (Neno la Mungu) na mwitikio wa udongo (mwitikio wa mtu kwa neon la
Mungu). Kutakuwa natofauti ya mwitio kwa Neno lililopandwa.
Wajibu wako ni kupanda. Kwa kadli unavyopanda mbegu
ya Neno la Mungu baadhi ya ardhi ikotayari na kutoa mavuno. Sehemu nyingie ya
ardhi ni duni vivyo inatoa matunda kidogo. Hata yesuy alikabiliana na tatizo la udongo usio na mwitikio katika
huduma yake hapa duniani.
Marko5:56…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..
Kwa kadli unafanya kazi ya kuuzidisha ufalme wa
Mungu kwa kuwaleta watu kwa yesu shetani
atajaribu kuleta pingamizi. Atajaribu kupanda watu wanaoitwa magugu miongoni
mwa mbegu njema ya Mungu.
Baadhi ya watu wanokiri na kuija kanisani si
waaminifu ni magugu yaliyopandw na
shetani. Yesu hatakiwa wewe kutumia muda mwingi na nguvu nyingi kushughulika na
magugu. Anataka uweke mkazo katika kupanda mbegu njema kazi ya kutenganisha ni
yak wake mwenyewe.
Uvuvi
Yesu alilinganisha kukua kwa ufalme wa Mungu na
nyavu kubwa iliyorushwa baharini. Kila aina ya samaki waliingia, lakini nyavu
inapotolewa majini kuletwa nchi kavu samaki wavuri hutengwa na samaki
wabaya.
Ufalme utawaleta wanaume na wanawake kutoka katika
mataifa mbalimbali. Wengi wataingia. Baadhi watakuwa waaminifu na baadhi sio. Katika siku ya mwisho ya hukumu Yesu ataporudi wema na wabaya watatenganishwa . Hujaitwa
kutenganisha umeitwa kuvua.
Punje ya
haradali Mathayo 13:31-32; Marok 4:31-32; Luka 13:19
Ufalme wa mungu uajizidisha kama
punje ya haladari.Punje ya haladari huwa ndogo sana mwanzoni. Lakini hukua hata
kufikia kuwa kama mti. Ufalme wa Mungu
duniani mara nyingi huwa na mwanzo mdogo.Yesu aliporudi Mbinguni baadfa ya
hudumsa yake hapa duniani aliacha
kikundi kidogo cha waamini kuieneza Injli.Kikundi hicho kidogo cha
waamini kilijizidisha na kuwa maelfu ya waamini
katika mataifa mbalimbali.
Mathayo13:33;
Luka 13:21
Ufalmw wa Mungu utajizidisha na kuenea kupitia
Mzabibu na matawi yake Yohana 15:1-16
Mfano huu unaeleza mahusiano yaliyopo kati ya Yesu na
hatua za kuzaa matunda. Yeye ni mzabibu wa kiroho na sisi ni matawi yake. Huwezi kuzaa matunda peke yako. Unakuwa na
uwezo wa kuzaa matunda kwa kadri unavyokuw umeungamanishwa na Yesu. Yesu
anataka kuondoa katika maisha yako kila kitu kinachoweza kukufanya usizae
matunda ili uweze kuzaa matunda bora.
Mavuno Mathayo 9:37-38, Luka 10:2
Katika mfano huu shamba ni
ulimwengu. Mavuno ni wanawake na wanaume waliotayari kuiitikia Injili ya
ufalme. Mavuo makubwa ya kiroho yako tayari yakisubiri kuvunwa na watendakazi
wa kiroho.
Kanuni nyingine za Mazidisho.
Yesu alifundisha kanuni nyingine
za mazidisho katika maelezo mafupi.
Nuru ya ulimwengu Mathayo
5:14-16; Luka 8:16
Ufalme wa Mungu utajizidisha
wakati waamini wanatokea kama nuru katika mji ulio juu ya kilima ambayo inaweza kuonekana kutka maili nyingi. Tunatakiwa kuuangazia
nuru ya Ysu ulimwengu uliojaa giza.Ufalme
wa Mungu utazidishwa kwa kadri watu wengi wanavyoijia nuru.
Chumvi ya dunia.Luka 13:4
Katika wakati wa Biblia chumvi
ilipakwa katika nyama ili kuzuia isioze. Waamini ni chumvi inayotakiwa kupakwa
kwa ulimwengu kwa ujumbe wa uhifadhi
yaani wokovu. Ufalme wa Mungu utazidishwa
wakati watu wanaokolewa kutoka kwenye uozo wa dhambi.
Hazina ya mbinguni Matthew 6:19-21; Luke 12:15.
Waamini hawatakiwa
kujishughulisha zaidi na kutafuta hazina za duiani kuliko kutafuta hazina ya
Mbinguni. Tumeitwa kwaajili ya maizidisho ya kiroho. Kwadili unawashirikisha
watu ujumbe wa Injili hazinayako Mbinguni itakuwa inazidishwa.
Mlango mpana Mathayo 7:14
Huwezi kuhukumu njia sahihi kwa
kigezo cha idadi.Njia ya upotevuni inabeba watu wengi wakati njia ya kuelekea
uzimani inabeba watu wachache.
Kazi nyingi Mathayo 7:22
Kazi nyingi za ajabu zitafanywa
na watu wengi katika hali ya nje
kutakuwa na mazidisho na ukuaji. Lakini kufanya kazi nyingi za ajabu si
lazima kuwe ni kufanya mapenzi ya
Mungu na kulitimiza kusudi. Kazi ya
Mungu inatakiwa kufanywa na watu wa Mungu kwa njia ya Mungu.
Kidogo ni bora Mathayo 10:42; Mathayo 14:15-21
Kila kitu kinachofanywa kwa Jina
la Yesu hata kama kinaoonekana kidogo ni cha thamani.Muujiza wa Yesu kulisha
watu zaidi ya 5000 kwa samaki
na mkate michache unaelezea jinsi Mungu anavyozidihsa kwa kutumia kidogo
tulichonacho.
Kukua kunahitaji badiliko Marko 2:21-22; 7:13
Makuzi mapya yanahitaji
mabadiliko. Huwezi kuweka kitu kipya katika kitu cha kale chenye mfumo wa
maisha ya dhambi. Uwezo mkuu wa nguvu za
Mungu huzuiwa na waamini
wanaoishi maisha ya kale na hawaitaji
mabadiliko.
Pata
kwa kupoteza Marko 8:34-37; 10:29-30
Pokea
kwa kutoa : Luke
6:38.
Kanuni za ulimwengu zinafundisha
kwamba unapata kwa kupokea zaidi na zaidi . Yesu alifundisha kwamba unapata
kila kitu unapokuwa umepoteza kila kitu. Kile kinachotokea kupota katika
ulimwengu wa asili kinapatikana katika
ulimwengu wa Roho.
Kifo huleta uzima Yohana 12 :24
Kupitia kifo cha Yesu watu wengi
waepata uzima wa milele. Ili mbegu iweze kuzaa ni lazima ife.Kupitia kifo huja
uzima . Ili kuwa mwamini mwenye kuzaa ni lazima ufe kwa mapenzi yako mwenyewe.
Ni lazima ufe kwa dhambi. Nilazima uache njia yako na kufuata njia ya Yesu
Krsito.
Kanisa katika mwamba Mathayo 16:18
Ufalme Wa Mungu umejengwa juu ya
mwamba ambao ni Yesu Kristo. Hakuna
ukuaji bila Yesu kuhusika. Yesu alisema
“nitalijenga kanisa langu” Alisema hakuna mtu angeweza kuja kwake bila kuvutwa na baba yake (Mungu).
Yohana 6:44
Upinzani ungetarajiwa lakini malango ya kuzimu hayangeushina mpango wa Mungu wa ukuaji wa ufalme wake.
No comments:
Post a Comment