Friday, 5 December 2014

MAOMBI YA KINABII



MAOMBI UA KINABII YA KILA SIKU
 Mwamini Mungu uthibitike, Amini Nabii ufanikiwe (2 Nyakati 20:20) Maombi ya vita ya siku 21 za kinabii za kufunga na kuomba Maombi haya ya kinabii ni ya wiki 21, siku 21 na kila wiki ni siku 1 tu ya kufunga na kuomba. (Ombi la tano 5). Kumbuka maombi haya hutolewa nakala mpya kila wiki. Ni vema kufanya maombi haya kabla ya kulala na baada ya kuamka. Maombi ya kupinga magonjwa, vifo, ajali na uharibifu 1. Baba, katika jina la Yesu, naangusha kila mbinu za kishetani zinazozuia mafanikiao yangu, katika jina la Yesu. 2. Nakataa na kupinga magonjwa ya kila aina katika nyumba yangu na familia yangu, kwa jina la Yesu. 3. Imeandikwa katika Zekaria 2:8 ya kwamba “Yeye anayenigusa mimi anagusa mboni ya jicho la Mungu”, hivyo, ninalisimamia Neno hili na kupinga kila nguvu inayosababisha magonjwa na upotevu wa fedha zangu katika jina la Yesu. 4. Nasimama kinyume na ajali na vifo katika familia yangu na ndugu zangu katika jina la Yesu. 5. Nawafunika watu wa familia yangu, kijiji changu na nje ya kijiji kwa damu ya Yesu. Ninawalinda na kuwaongoza kila mmoja kwa jina la Yesu. 6. Ninaamuru kila kinachoharibu mtaji na biashara yangu kufa mara moja katika jina la Yesu. 7. Ninaificha fedha yangu yote katika damu ya Yesu na kamwe adui hawezi kuigusa. 8. Baba, katika jina la Yesu, nasimama katika Neno kama mtoto wa Mungu niliyeketishwa mahali pa juu pamoja na Kristo, na ninatangaza kuwa mikutano ya kipepo juu ya maisha yangu na fedha yangu haitafanikiwa, katika jina la Yesu. 9. Namfunga kila anayeharibu fedha yangu nyumbani na sehemu yangu ya kazi katika jina la Yesu. 10. Wewe pepo uliyetumwa kuharibu biashara na fedha zangu, ninakufunga na kukutupa kwenye shimo la giza katika jina la Yesu. 11. Ninaamuru moto wa Roho Mtakatifu kumlamba kila mmoja aliyesimama kinyume na biashara na mafanikio yangu katika jina la Yesu. 12. Ewe mlima uharibio, ninakuangusha na nianaamuru usambaratike, katika jina la Yesu. 13. Ninaificha biashara, ofisi, fedha na miradi yangu yote katika damu ya Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai. Amen. 14. Bwana, ninaomba upendeleo wako katika maisha yangu ili niweze kufanikiwa. 15. Upendeleo wako unizunguke kadiri ya Neno lako, katika jina la Yesu. 16. Bwana, naomba kuunganishwa na watu watakaonisaidia kufikia ndoto zangu kwa jina la Yesu. 17. Oh, Bwana, naomba ufanye njia kwa ajili yangu hata pale pasipo na njia katika jina la Yesu. 18. Baba, naomba niunganishe na mtu ambaye atakuwa msaada mkubwa katika kuyafikia mafanikio yangu katika jina la Yesu. 19. Baba ninaamini ya kwamba kila ninapokanyaga ninapamiliki sawasawa na na Neno lako, hivyo naomba univike vazi lako la upendeleo katika jina la Yesu. 20. Asante Bwana Yesu kwa kuwa umefanya sawasawa na nilivyokuomba katika jina la Yesu. Amen. Baada ya kuomba maombi haya tumia dakika saba kumshukuru Mungu Usikose Jumapili hii saa mbili asubuhi. Itakuwa ni ibada maalum ya Urejesho na kuvunja maagano mbalimbali maishani mwako. Ibada hii maalum itafanyika ndani ya Kanisa la RGC Miracle Centre Tabata Chang’ombe. Jinsi ya kufika, Panda magari ya Segerea, shuka Barakuda, pandisha na barabara iendayo Tabata Chang’ombe. Kanisa lipo Chang’ombe mwisho kituoni. Hakika hapo Mungu anaonekana. Kwa mawasiliano, maombi na ushauri 0765-111011 Mimi wako Nabii na Mtume wa Urejesho Peter Nyaga, RGC Tabata Chang’ombe ------------------------------------------------------------------------- Mwamini Mungu uthibitike, Amini Nabii ufanikiwe (2 Nyakati 20:20) Maombi ya vita ya siku 21 za kinabii za kufunga na kuomba Maombi haya ya kinabii ni ya wiki 21, siku 21 na kila wiki ni siku 1 tu ya kufunga na kuomba. (Ombi la Sita 6). Kumbuka maombi haya hutolewa nakala mpya kila wiki. Ni vema kufanya maombi haya kabla ya kulala na baada ya kuamka. Maombi ya kubariki kazi za mikono yetu 1. Mungu wa milele yote “Niko ambaye niko” ninakuabudu na kukutukuza. Uhimidiwe katika jina la Yesu. 2. Bwana, nainua kazi yangu na kuikabidhi kwenye mikono yako. 3. Nawakabidhi wafanyakazi wenzangu na mkubwa wangu wa kazi mikononi mwako. Nipe upendeleo wako mbele yao wote katika jina la Yesu. 4. Imeandikwa katika Isaya 45:2 kwamba “utakwenda mbele yangu na kupasawazisha penye matatizo” kwa hiyo, nakuomba uniandalie njia ya kuinuliwa katika ofisi yangu, katika jina la Yesu. 5. Imeandikwa katika Zaburi 1:3 ya kwamba lolote nitakalolifanya litafanikiwa. Hivyo, Baba nifanye ning’ae katika kazi yangu ili niweze kupandishwa cheo katika jina la Yesu. 6. Baba, nachukua mamlaka dhidi ya falme, mamlaka na nguvu zote za giza katika ofisi yangu, Ninawafunga na kuharibu nguvu zao zote katika jina la Yesu. 7. Wewe pepo wa ukabila ninakufunga na kukutupa nje ya maisha ya bosi wangu na waajiri wote katika jina la Yesu. 8. Kila nguvu za giza katika eneo langu la kazi ambazo hutaka mimi nifukuzwe kazi, ninaziharibu na kuzifuta kabisa katika jina la Yesu. 9. Baba naomba ustawi katika biashara zangu zote katika jina la Yesu. 10. Ninakataa kila namna ya udanganyifu na wizi katika eneo langu la kazi. 11. Bwana, nibariki na kunipa upendeleo katika maisha na kazi zangu kwa jina la Yesu. 12. Imeandikwa “matamanio ya mtu mwema yatatimizwa”. Hivyo, Bwana Yesu nipe matamanio ya moyo wangu katika jina la Yesu. 13. Kila nguvu za giza zilizosimama kinyume nami kuzuia kuinuliwa kwangu na kupandishwa cheo, ninaziharibu na kuziondoa katika jina la Yesu. 14. Wewe pepo unayesimamisha na kurudisha nyuma maendeleo yangu, ninakufunga na kukutupa nje ya kazi yangu na maisha yangu katika jina la Yesu. 15. Bwana, ninaikabidhi biashara yangu mikononi mwako, naomba uitawale, katika jina la Yesu. 16. Bwana, niongoze katika kuitumia pesa yangu na kujua maeneo ya kufungua biashara katika jina la Yesu. 17. Bwana, nipe hekima ya kuendsesha biashara ili niweze kufanikiwa na kustawi katika jina la Yesu. 18. Bwana, naomba upendeleo wako kwenye bidhaa nitakazoziuza ili zipate kibali machoni pa watu katika jina la Yesu. 19. Nisaidie kujua mazingira yangu na kuweza kugundua kazi au biashara unayotaka mimi niifanye ili niweze kufanikiwa katika jina la Yesu. 20. Baba, ninakabidhi fedha zangu zote mikononi mwako, katika jina la Yesu. 21. Bwana ingilia kati na unipe Baraka na hekima ya kufanya biashara itakayozalisha kwa wingi. Amen. Baada ya kuomba maombi haya tumia dakika saba kumshukuru Mungu Usikose Jumapili hii saa mbili asubuhi. Itakuwa ni ibada maalum ya Urejesho na kuvunja maagano mbalimbali maishani mwako. Ibada hii maalum itafanyika ndani ya Kanisa la RGC Miracle Centre Tabata Chang’ombe. Jinsi ya kufika, Panda magari ya Segerea, shuka Barakuda, pandisha na barabara iendayo Tabata Chang’ombe. Kanisa lipo Chang’ombe mwisho kituoni. Hakika hapo Mungu anaonekana. Kwa mawasiliano, maombi na ushauri 0765-111011. Mimi wako Nabii na Mtume wa Urejesho Peter Nyaga, RGC Tabata Chang’ombe. -------------------------------------------------------------- MWAMINI MUNGU UTHIBITIKE, AMINI NABII UFANIKIWE (2 NYAKATI 20:20) Maombi ya vita ya siku 21 za kinabii za kufunga na kuomba: Ombi la tatu. Maombi haya ya kinabii ni ya wiki 21, siku 21 na kila wiki ni siku 1 tu ya kufunga na kuomba (Ombi la Tatu 3).Kumbuka maombi haya hutolewa nakala mpya kila wiki. Ni vema kufanya maombi haya kabla ya kulala na baada ya kuamka Jinsi ya kuomba maombi ya kuugua na kulia Sio rahisi kabisa kuomba maombi ya kuugua na kulia, hata tunapoomba mambo ya rohoni kama uamsho, watu wote waokolewe, Bwana azidi kumtumia vema mchungaji , kuombea ibada ya siku ya matendo makuu ya miujiza, mkutano wa injili nk.Ni rahisi kufanya maombi ya kulia na kuugua hasa tunapomwomba Mungu atuponye magonjwa yetu mabaya, atupe kazi kimiujiza, ashughulikie mume/mke anayetutesa nk. lakini sio rahisi tunapoombea mambo ya rohoni kama ifuatavyo. Kutiisha mwili Miili yetu ni rahisi sana kulia na kuugua tunapopata msiba au mateso ya kimwili, lakini linapokuja suala la kulia na kuugua kwa mambo ya rohoni, miili yetu hupingana nasi kabisa na kutufanya tusione maana ya kulia na kuugua katika maombi ya jinsi hiyo, pamoja na shetani kuwa adui yetu mkuu, miili yetu pia ni maadui zetu wakubwa wanaopingana na kila jambo la rohoni tunalotaka kulifanya Wagalatia 5:17 na kwa sababu mwili hutamani ukishindana na roho na roho hushindana na mwili kwa maana hizi zimepingana hata hamuwezi kufanya mnayotaka. Hatuna budi kuutiisha mwili ili tufanye mambo ya rohoni kinyume na hiyari yake (Warumi 8:6-8;19-21; 2Wakorintho10:4-5). Tukiunganisha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kiinukacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka kila fikra ipate kumtii Kristo. Kwa hiyo kabla ya kuingia katika maombi ya rohoni ya kuzama kwa kina yaani ya muda mrefu, ambayo tunataka yawe ya kulia na kuugua, sharti tuutiishe mwili na kuuamuru kuwa chini ya roho zetu na kukemea kila mipango ya shetani ya kutuzuia kuomba kwa kuugua. Kuomba tupewe roho ya neema ya kuomba Hatuwezi kufanya maombi ya kuugua na kulia mpaka pale tunapopewa au kumwagiwa roho ya neema na kuomba Zakaria 12:10, “nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba nao watamtazama yeye ambaye walimchoma, nao watamuombolezea kama vile mtu amuombolezeavyo mwanawe wa pekee nao wataona uchungu kwa mzaliwa wake wa kwanza”.Hivyo baada ya kuutiisha mwili, hatuna budi kuwa na kipindi cha kutosha kuomba tumwagiwe roho ya neema na kuomba, kipindi hiki hakina budi kuchukua muda upatao dakika 20, na kile cha kwanza cha kutiisha mwili hakina budi kuchukua muda upatao dakika 10. Baada ya dakika hizi ndipo tunaweza kuomba maombi yanayoweza kumfanya Mungu ashuke, hata hivyo kuna utata kidogo. Je roho ya neema ni nini? Roho ya neema na kuomba Kwanini hatuna budi tumwagiwe roho ya neema? Ili tujue ni kwa nini hatuna budi kuelewa na kujikumbusha maana ya neema, kwa ufupi na kwa urahisi wa kuelewa ni msaada utokao mbinguni wa kutuwezesha kufanya yale ambayo tusingeweza kufanya kwa nguvu au jitihada zetu wenyewe (Waebrania 4:16; 1Wakorintho 15:10) “basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji”.Kwa msingi huu wanadamu wote ni dhaifu sana katika maombi ndio maana wengi utawasikia wakisema NAPENDA SANA KUOMBA LAKINI NAJIKUTA SIWEZI KUOMBA nitakavyo. Roho Mtakatifu yeye hana tatizo hilo tulilonalo, la kushindwa kuomba, ni mwombaji wa kipekee kama alivyo Yesu. Huyu ndiye msaidizi wetu Yohana 14:26. “lakini huyo msaidizi huyo Roho Mtakatifu ambaye Baba atampeleka kwa jina langu atawafundisha yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia kwa kuwa yeye ni mwombaji asiyefananishwa, hutupa roho ya neema au roho inayotusaidia udhaifu wetu na kutufanya tuombe jinsi inavyotupasa kuomba” . Bila roho hiiiya neema au ya msaada huu sisi hatuwezi kuomba itupasavyo (Warumi 8:26) “kadhalika roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo lakini roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa “ jitihada zetu pekee haziwezi kumlazimisha Mungu ashuke. Roho ya kuomba Roho ya kuomba ni roho inayomwagwa kwetu na kutuwezesha kuomboleza au kulia na kuugua katika maombi (Zekaria 12:10) “nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba nao watamtazama yeye ambaye walimchoma, nao watamuombolezea kama vile mtu amuombolezeavyo mwanawe wa pekee nao wataona uchungu kwa mzaliwa wake wa kwanza”Roho Mtakatifu huomba kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, hutupa neema au msaada wa kutuwezesha sisi nasi kuomba kwa kulia na kuugua kunakoweza kumfanya Mungu ashuke. Bwana atupe neema ya kuyakumbuka haya na kuyatendea kazi kabla ya maombi marefu. Hakika tukifanya hivyo tutamwona Mungu akishuka kati yetu (Yohana 13:17).“mkiyajua haya heri ninyi mkiyatenda” tegemea kupokea upako huu wa neema maishani mwako. Ni matumaini yangu neno hili litakaa ndani ya moyo wako na utalifanyia kazi. Kumbuka siri kubwa ya kuhifadhi maombi maishani mwako ni kuogopa kutenda dhambi na kuacha dhambi kabisa Yohana 15:7; Kumb. 28:1-2. Tia bidii kusikiliza neno na kulitendea kazi. Maombi 1. Baba katika jina la Yesu natubu dhambi zangu zote leo, pia naomba uweza wa Roho Mtakatifu unisaidie ili nisirudie tena. 2. Bwana Yesu nakuja tena kwako wewe Bwana wa msamaha ili nipate kusamehewa dhambi zangu zote nilizorithi na kufanya, baba unisamehe (tamka dhambi ulizofanya, chukua kama nusu saa ni bora zaidi). 3. Baba najiachilia kwa damu yake Yesu damu takatifu, damu iliyomwagika kalvari, damu ya thamani, damu ya ushindi, damu ya uweza wa kumiminika juu yangu, na kunitakasa katika jina la Yesu Kristo. 4. Wewe Yesu umesema, njooni kwangu ninyi wenye dhambi, wenye mizigo nitawapumzisha (Mathayo11:28). Bwana Yesu naja mbele yako unipe pumziko nimechoshwa na maisha ya dhambi, na maisha ya kuanguka. 5. Unisafishe Bwana, sikia kilio changu mimi mkosefu nakuja kwako sasa nipokee kama nilivyo. 6. Ee Bwana Yesu wewe umejaa neema na rehema tele, chunguza nafsi yangu, chunguza mwenendo wangu ili upate kunisamehe. 7. Unishike mkono wako Bwana, ukiniacha peke yangu nitaanguka maana shetani ananitafuta kwa kasi sana usiku na mchana, Bwana nahitaji msaada wako kwa haraka sana tena sasa hivi. 8. Mungu wa mbinguni naomba usamehe dhambi za babu zangu, Bwana unifundishe kila siku kusamehe walionikosea na kuanzia leo nawasamehe kwa moyo wangu wote walionikosea, kwa mabaya yote waliyonitendea, baba nawasamehe nakuomba pia uwasamehe katika jina la Yesu Kristo. 9. Bwana Yesu kama maandiko matakatifu yashuhudiavyo, katika kitabu cha Isaya 59:1-3 naamini sasa na pia najua ya kwamba mkono wako si mfupi kushindwa kuniokoa, wala wewe si kiziwi usisikie ila maovu yangu yameufanya uso wako ugeukie upande mwingine, Bwana naomba uniangazie ili nipate kupenya kimaisha na kupata wokovu wa milele katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti. 10. Bwana Yesu nakushukuru kwa kusikia kilio changu, nakushukuru kwa kunisamehe dhambi zangu zote, nakushukuru kwa kuwasamehe walionikosea, nakushukuru sana kwa kunikubali tena, kwa kunipokea katika mikono yako mitakatifu, jina lako lizidi kuinuliwa katika jina la Yesu Kristo. 11. Ubarikiwe Bwana wa majeshi uinuliwe mara saba kwa mara sabini, jina lako lizidi kuabudiwa kila siku mahali popote. 12. Nakuja kinyume na falme na mamlaka zilizo kinyume na harusi yetu katika jina la Yesu. 13. Nafunga kila pepo lililoandikwa kufunga ndoa yetu katika jina la Yesu. Baba ifanye harusi yetu kuwa yenye mafanikio. Pokea utukufu katika jina la Yesu. 14. Ngome ya moto inizunguke popote niendako katika jina la Yesu. 15. Baba Mungu mbingu na ifunguke mvua ya neema inyeshe Baraka za rohoni zinifikie mahali popote nipatikanapo katika jina la Yesu Kristo. 16. Asante Mungu baba na Bwana Yesu kwa ajili ya neema na rehema zako kwa kunijibu maombi yangu haya katika jina la Yesu Kristo ninaomba. Amen Baada ya kuomba maombi haya tumia dakika saba kumshukuru Mungu Usikose Jumapili hii saa mbili asubuhi. Itakuwa ni ibada maalum ya Urejesho na kuvunja maagano mbalimbali maishani mwako. Ibada hii maalum itafanyika ndani ya Kanisa la RGC Miracle Centre Tabata Chang’ombe. Jinsi ya kufika, Panda magari ya Segerea, shuka Barakuda, pandisha na barabara iendayo Tabata Chang’ombe. Kanisa lipo Chang’ombe mwisho kituoni. Hakika hapo Mungu anaonekana. Kwa mawasiliano, maombi na ushauri 0765-111011 Mimi wako Nabii na Mtume wa Urejesho Peter Nyaga, RGC Tabata Chang’ombe Mwanamaombi namba ……………… -------------------------------------------------------------------------------------------- Mwamini Mungu uthibitike, Amini Nabii ufanikiwe (2 Nyakati 20:20) MAOMBI YA VITA YA SIKU 21 ZA KINABII ZA KUFUNGA NA KUOMBA Maombi haya ya kinabii ni ya wiki 21, siku 21 na kila wiki ni siku 1 tu ya kufunga na kuomba. (Ombi la nne 4). Kumbuka maombi haya hutolewa nakala mpya kila wiki. Ni vema kufanya maombi haya kabla ya kulala na baada ya kuamka Maombi ya kuvunja laana za Umaskini 1. Katika jina la Mungu Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, ninavunja kila laana ya Baba na mama yangu iletayo umaskini maishani mwangu, katika jina la Yesu. 2. Ninakataa kuteseka na umaskini maishani mwangu kutokana na laana za wazazi katika jina la Yesu. Amen. 3. Leo kwa uweza wa Mungu aliye juu ninavunja kila aina ya laana ya umaskini maishani mwangu kwa jina la Yesu. 4. Kama ilivyoandikwa katika Mathayo18:18 natangaza katika maisha yangu ya kwamba umaskini sio sehemu yangu katika jina la Yesu. 5. Mungu wangu nifanye nisione umaskini wala kunukia harufu yake katika maisha yangu na familia yangu kwa jina la Yesu. 6. Sikubaliani na roho ya umaskini na kamwe haitaambatana nami wala familia yangu katika jina la Yesu. 7. Napokea upako wa Roho Mtakatifu na laana za wazazi kamwe hazitanifanya kuwa maskini katika jina la Yesu. Amen. 8. Mungu wangu na Bwana wangu, navunja kila laana na vyama vya siri walivyoninyunyizia kwa jina la Yesu 9. Chochote ambacho wazazi wangu na marafiki walikifanya kupitia vyama vya siri na wachawi nakivunja kwa jina la Yesu. 10. Uchawi wowote wa manuizo, maeneo waliyonilaani na kuniita nijiunge nao, nayadhoofisha na kuyaangamiza kwa jina la Yesu. Amen. 11. Roho chafu na mapepo yanayoshughulika na chama cha wachawi na kazi zao ninazivunja jina la Yesu. Amen. 12. Ile laana ya utasa maishani mwangu, na katika familia yangu naivunja katika jina la Yesu. 13. Laana za utasa wa utajiri, watoto na biashara nazivunja kwa jina la Yesu 14. Navunja laana za utasa maishani mwangu, nilizorithi kutoka kwa wazazi wangu katika jina la Yesu. 15. Ninajiweka huru mimi na familia yangu yote kutoka katika laana za utasa, nilizolaaniwa na maadui kwa jina la Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai. 16. Adui wa afya njema kwa familia yangu nakuvunja, nakufunga minyororo na kukuharibu kwa jina la Yesu. 17. Navunja laana za utasa maishani mwangu. Nilizorithi toka kwa wazazi wangu kwa jina la Yesu. 18. Najiweka huru mimi na familia yangu yote kutoka katika laana za utasa ambazo maadui walinilaani nazo kwa jina laYesu. 19. Utasa katika familia yangu uwe umetoka kwa marafiki zangu, au walionitakia mema, ninauharibu sasa kwa jina la Yesu. 20. Laana zote za utasa katika biashara kutoka kwa shetani nazivunja sasa na zisirudi tena katika jina la Yesu. 21. Laana ya utasa kwenye maisha yangu, familia yangu, biashara na vinginevyo iwe imetoka kwenye maroho machafu, watu, sehemu ninayoishi au kazini kwangu, naivuinja na kuilaani sasa kwa jina la Yesu Amen. 22. Laana za utasa katika familia yangu na mababu zangu nazikataa sasa na kuzivunja kwa jina la Yesu. Amen Baada ya kuomba maombi haya tumia dakika saba kumshukuru Mungu Usikose Jumapili hii saa mbili asubuhi. Itakuwa ni ibada maalum ya Urejesho na kuvunja maagano mbalimbali maishani mwako. Ibada hii maalum itafanyika ndani ya Kanisa la RGC Miracle Centre Tabata Chang’ombe. Jinsi ya kufika, Panda magari ya Segerea, shuka Barakuda, pandisha na barabara iendayo Tabata Chang’ombe. Kanisa lipo Chang’ombe mwisho kituoni. Hakika hapo Mungu anaonekana. Kwa mawasiliano, maombi na ushauri 0765-111011 Mimi wako Nabii na Mtume wa Urejesho Peter Nyaga, RGC Tabata Chang’ombe ----------------------------------------------------------------------------------------------------------- MAOMBI MAALUM YA VITA YA KIL;A WIKI OMBA KILA SIKU MAOMBI HAYA YA KINABII Mwamini Mungu uthibitike, Amini Nabii ufanikiwe (2 Nyakati 20:20) Maombi ya vita ya siku 21 za kinabii za kufunga na kuomba (Ombi la pili 2) Maombi haya ya kinabii ni ya wiki 21, siku 21 kila wiki ni siku 1 tu ya kufunga na kuomba. Hakikisha umekuja kupakwa mafuta ya upako ili upokee neema ya Mungu. Siku ya kufunga ni tarehe …………………………… Njoo saa moja asubuhi. Soma maandiko haya kabla ya maombi. Amen Kumbukumbu 28:1-14; “Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;” Nehemia 13:2, Luka 18:1; Isaya 43:18-19; 1. Baba wa mbinguni katika jina la Yesu Kristo naomba 2. Baba wa mbinguni jina lako litukuzwe duniani kama huko mbinguni katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti Mwana wa Mungu aliye hai. 3. Nakushukuru wewe Simba wa Yuda kwa kunipatia nafasi katika siku hii ya tatu ya maombi yangu kwa njia ya vita vya kiroho, jina la Bwana libarikiwe sana. 4. Ahsante kwa kunitia nguvu tangu siku ya kwanza ya maombi hadi leo, kweli jina lako libaeikiwe sana. 5. Bwana Yesu, kama ulivyokuwa nami tangu siku ya kwanza ya maombi, leo naingia katika siku ya kuvaa silaha za vita vya kiroho kwenye maombi yangu katika jina la Yesu. 6. Baba Mungu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti naomba ukanitie nguvu zitokazo juu, ili nipate kupambana na kumshinda huyu mwovu shetani, nipe ujasiri mwingi wa kuwashinda kabisa mapepo wote wanaofuatilia mafanikio yangu ya kiuchumi. 7. Ndani yako ninalizamisha kila gari au chombo nitakachotumia safarini kibiashara au vinginevyo, pia nawafunika madereva na abiria wote kwa damu ya Yesu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti (tamka mara 3). 8. Adui zangu wote nawatosa ndani ya moto wa Roho Mtakatifu wakakose amani mpaka watakapotubu na kuliita jina la BWANA wa majeshi. 9. Kwa ngao ya imani nazuia kila mshale unaorushwa na adui na kuuamuru umrudie aliyeurusha na kumdhuru kabisa katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti. Roho Mtakatifu mwenye nguvu zote kwa nguvu zako nikomboe na kuniweka huru kabisa katika jina la Yesu. 10. Ninamwagia damu ya Yesu juu ya kila kioo cha kichawi wanachotumia kuniwinda na ninaamuru moto wa radi kutoka mbinguni ukakivunje vunje katika jina la Yesu (rudia mara saba). 11. Kwa nguvu ya damu ya Yesu ninafuta madhara yote ambayo yameandaliwa kuzimu kwa ajili yangu mwaka huu nayakanyaga katika jina la Yesu. 12. Nafunga roho ya vizuizi vya kiuchumi, nafunga roho ya kukopakopa, nafunga roho ya madeni, nafunga roho ya chuma ulete, nafunga na kusimamisha roho ya kupoteza pesa na mali katika mazingira ya kutatanisha, nafunga na kuvunja roho ya matumizi ya hovyo hovyo, nafunga roho zote za kufikiria na kuamua kufanya biashara au kazi yoyote isiyokuwa na faida na pia nafunga roho zote za kutapeliwa zinazotoka kuzimu katika jina la Yesu. 13. Wewe pepo la umaskini na ujinga, piga kelele na uondoke pamoja na roho zote za kutofanikiwa katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti. Baada ya kuomba maombi haya tumia dakika saba kumshukuru Mungu Tarehe ya kuja kupokea maombi mengine na maelekezo ya kinabii ni ………………………. saa moja asubuhi ukiwa umefunga ili upakwe mafuta. Ukimtii Nabii wa Mungu utafanikiwa. Mimi wako Nabii na Mtume wa Urejesho Peter Nyaga, RGC Tabata Chang’ombe. Simu. 0756-863528. Amen. Mwanamaombi namba …………… ----------------------------------------------------------------------------------------- MWAMINI MUNGU UTHIBITIKE, AMINI NABII UFANIKIWE (2 NYAKATI 20:20) MAOMBI YA VITA YA SIKU 21 ZA KINABII ZA KUFUNGA NA KUOMBA Maombi haya ya kinabii ni ya wiki 21, siku 21 na kila wiki ni siku 1 tu ya kufunga na kuomba. (Ombi la kwanza 1). Hakikisha umesoma maandiko haya kabla ya maombi. Amen Kumbukumbu 28:1-14; Waefeso 6:10-18; Yeremia 1:10; Ayubu 42:2-10; Mathayo 7:7; Luka 18:1; Nehemia13:2; Zaburi 103:1-5. 1. Baba Mungu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti naomba, 2. Nikiinua macho yangu ili nipate kibali kutoka kwako wewe uliye Bwana wa majeshi, Mwamba wa milele, nikikusifu na kukuabudu wewe, Nakuheshimu wewe ni katika jina la Yesu. 3. Siku ya leo ni ya hatari sana, ni siku ambayo nahitaji nguvu zako na ulinzi wako kutoka juu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti. 4. Naliinua jina lako wakati huu ninapopigana vita hii takatifu katika jina la Yesu 5. Tamka moto wa Roho Mtakatifu (rudia mara 7), Damu ya Yesu (rudia mara 7). 6. Baba Mtakatifu katika jina laYesu ninakuja kwako na kupokea damu ya Yesu ikatakase nafsi yangu na mwili wangu. 7. Kama ilivyoandikwa katika Isaya 54:17 kuwa kila silaha itakayofanyika juu yangu haitafanikiwa, natamka kwamba silaha yoyote ya kichawi iliyo kinyume nami ishindwe na kuharibika katika jina la Yesu Kristo. 8. Mishale yote yenye moto ya yule muovu iliyotengenezwa kwa ajili yangu ikamrudie na kumharibu aliyetuma katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti. 9. Ninawafunga, kuwavunja na kuwaharibu kabisa mapepo wote waliotumwa mwaka huu kwa ajili ya kusababisha ajali mbalimbali (tamka mara 3). 10. Popote ambapo jina langu limefichwa kichawi, kimashetani, natuma moto usio wa kawaida mahali hapo na popote ambapo fedha zangu na mali zangu zimezuiliwa katika ulimwengu wa roho, natuma moto Roho Mtakatifu ateketeze nira na vifungo vyote katika jina la Yesu Kristo (rudia mara 2). 11. Kama ilivyoandikwa katika Mithali 18:10 kuwa jina la BWANA ni ngome imara na mwenye haki huikimbilia na kuwa salama, natamka usalama ulio katika Kristo Yesu popote niingiapo, popote nitokako na popote nilipo. 12. Tena ninawafunga wachawi wote wanaoshambulia maisha yangu, fedha yangu na mali zangu katika jina la Yesu. 13. Nakuita Ee Mungu wa Eliya uliyejibu kwa moto, sasa tawala mahali popote penye uchumi, na mali zangu zilipofichwa na kukaliwa vikao vya kichawi juu yangu katika jina la Yesu. 14. Ndani yako ninalizamisha kila gari au chombo nitakachotumia safarini kibiashara au vinginevyo, pia nawafunika madereva na abiria wote kwa damu ya Yesu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti (tamka mara 3). 15. Adui zangu wote nawatosa ndani ya moto wa Roho Mtakatifu wakakose amani mpaka watakapotubu na kuliita jina la BWANA wa majeshi. 16. Kwa ngao ya imani nazuia kila mshale unaorushwa na adui na kuuamuru umrudie aliyeurusha na kumdhuru kabisa katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti. 17. Roho Mtakatifu mwenye nguvu zote kwa nguvu zako nikomboe na kuniweka huru kabisa katika jina la Yesu. 18. Ninamwagia damu ya Yesu juu ya kila kioo cha kichawi wanachotumia kuniwinda na ninaamuru moto wa radi kutoka mbinguni ukakivunje vunje katika jina la Yesu (rudia mara saba). 19. Kwa nguvu ya damu ya Yesu ninafuta madhara yote ambayo yameandaliwa kuzimu kwa ajili yangu mwaka huu nayakanyaga katika jina la Yesu. 20. Nafunga roho ya vizuizi vya kiuchumi, nafunga roho ya kukopakopa, nafunga roho ya madeni, nafunga roho ya chuma ulete, nafunga na kusimamisha roho ya kupoteza pesa na mali katika mazingira ya kutatanisha, nafunga na kuvunja roho ya matumizi ya hovyo hovyo, nafunga roho zote za kufikiria na kuamua kufanya biashara au kazi yoyote isiyokuwa na faida na pia nafunga roho zote za kutapeliwa zinazotoka kuzimu katika jina la Yesu. 21. Wewe pepo la umaskini na ujinga, piga kelele na uondoke pamoja na roho zote za kutofanikiwa katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti. Baada ya kuomba maombi haya tumia dakika saba kumshukuru Mungu Tarehe ya kuja kupokea maombi mengine na maelekezo ya kinabii ni …………………… saa 2 asubuhi ukiwa umefunga ili upakwe mafuta. Ukimtii Nabii wa Mungu utafanikiwa. Mimi wako Nabii na Mtume wa Urejesho Peter Nyaga, RGC Tabata Chang’ombe. Simu. 0756-863528. Amen.

Make Money at :
http://bit.ly/copy_win

1 comment:

  1. Maombi Ombi

    Ndugu Marafiki katika Kristo!
    Mimi ni hivyo kushukuru milele kwa wale ambao wanaweza kusema sala kwa Sundayschools hapa katika Nordmøre katika Norway. Tunataka wazazi kuchukua jukumu na kupeleka watoto wao makusanyo yetu. Mwombe Mungu kutuma uamsho kwetu.
    Niombeeni mimi pia na familia yangu! Mungu akubariki wanaoomba!
    Asante!
    Ndugu wenu katika Bwana, Hans Orset
    Waziri wa 45 SundaySchools.

    ReplyDelete