KANISA LA PENTEKOSTE TANZANIA
JIMBO LA MBEYA
IDARA YA UIJILISTI NA UMISHENI
Jina la idara Idara hii inaitwa idara ya Uinjilisti na
Umisheni.
Maono ya idara(vission)
Kutoa fursa kwa watu wote walioko ndani na nje ya jimbo la Mbeya kusikia
injili ya Yesu kristo, kwa kuanzisha mtembeo wa upandaji wa makanisa
yatakayojizidisha katika kila jamii iliyopo duniani kupitia nyenzo ya uinjilisiti.
Dira
ya idara. (Mission)
Kuhubiri Injili kwa kila kiumbe na kuwafanya watu kuwa wanafunzi
Tunaamini kwamba Injili itahubiriwa kwa haraka pindi tutakapofaulu
kuwafanya waamini kuwa wanafunzi na kama kanuni ya mazidisho itafanya kazi
“kila mmoja kufundisha mwingine”
Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi
wengi hayo uwakabidhi watu waaminifu wataka faa kuwafundisha na wengine. (2Tim 2:2)
Dira ya idara hii ni kuhakiskisha kila mwammini wa kanisa la mahai
anajihusisha na agizo kuu. Kuhamasisha na kutia moyo waaamini kutumbau kwamba
agizo kuu lina mhusu kila mmoja yeye binafsi na kanisa kwa ujumla.
Andiko la idara
Yohana 4:35
,, “Inueni macho yenu myatazame mashamba na kuwa yameshakuwa tayari kwa mavuno”
Kazi za Idara
Malengo ya idara.
Malengo ya idara yamegawanyika katika maeneo mawili ambayo ni
· Malengo ya jumla (general objecive)
Malengo ya jumla yanaelezea kusudi hasa la kuwepo
kwa idara hii na kile kinachpaswa kutekeleza kwa ujumla wake.
· Malengo mahususi(Spesific objective)
Malengo mahususi yanafafanua malengo ya jumla kwa
kuainisha mambo maalumu amabo ni msingi wa uwepo wa idara hii. Malengo mahususi
yanatuwezesha kmatokeo ya muda mfupi na yenye kupimika .
Malengo ya jumla
Idara hii ya uinjilisti na umisheni imeanzishwa kwa kusudi la kuharakisha
utekelezaji wa Agizo kuu la Bwana wetu Yesu Kristo.
Akawaambia “Enendeni ulimwenguni
mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe” Marko 16:14
Maelezo haya ni amri ambayo iko wazi na inadai utekelezaji. Hivyo idara
hii iko kwa kusudi hili la kuhubiri
Injili kwa watu wote na kupanda makansa katika maeneo mbalimbali.
Tunaamini kwamba uinjilisti na
umisheni ndio kipaumbele cha kwanza cha Kanisa . Wosia wa mwisho wa Yesu Kristo
kwa wanafunzi wake ulihusu Agizo kuu yaani Uinjilisti na umisheni. Matendo ya
Mitume1:8
Wosia wa mwisho wa mtu huwa unashikwa na kufanyiwa kazi kuliko kitu
kingine chochote kile. Hivyo kanisa linatakiwa kuupa uzito wa kipekee
wosia huu wa Agizo kuu.
Idara hii inalenga kuhamissha na kutumia rasilimali mbalimbali kuanzia
ngazi ya tawi, parishi na jimbo katika kuhubiri Injili na kupanda makanisa yenye kujizidisha. Tunaamini
raslimali kuu ni watu hivyo wamini wanatakiwa
kufanywa wanafunzi wenye uwezo wa kujizidisha ili kuufikia ulimwengu
wote kwa Injili. Kuhakikisha watu wote wanafikiwa pale walipo kwa Injili ya
Yesu Kristo.
Malengo mahususi
1.
Kuanzisha
idara ya uinjilisi na umisheni kuanzia tawini hadi parishi.
2.
Kuandaa
makongamano ya wahubiri na waimbaji ili
kupeana uzoefu na changamoto katika
huduma ili kuweza kuboresha huduma za waimbaji na wainjilisti walioko ndani ya
KLPT jimbo la Mbeya.
3.
Kunzisha mfuko
wa huduma ya Uinjilisti na umisheni wa jimbo.
· Kupendekeza asilimia tano (5%) ya mapato ya kila
kanisa kuingia katika mfuko wa uinjilisti na umisheni.
· Kundesha halambee kwaajili ya kukuza mfuko wa Injli.
· Kufungua akaunti benki ya uinjilisti na umisheni.
· Kuanzisha miradi mbalimbali mfano shule, gazeti, redio Nk
4.
Kuanzisha
mtandao wa maombi wa Injili na Umisheni.
5.
Kufanya
uinjilisti wa Maandiko
Kuandaa vipeperushi,
majarida na vitini kwaajili ya uinjilisti wa maandiko.
6.
Kufanya Uinjilisti
kupitia vyombo vya habari, mfano Redio, magazeti na luninga.
7.
Kuanzisha
tovuti ya idara
· Kuanzisha tovuti ya idara ambayo itatumika kufaya
uinjilisti kupitia mtandao.
· Kufanya uinjilisti kupitia mitandao mbalimbali ya
kijamii
8.
Kukuza afya ya
kanisa.
Kuhakikisha makanisa yote ya KLPT Jimbo la Mbeya yanakuwa
na vichocheo mbalimbali vitakavyosababisha
kukua kwa vipawa, karama na huduma za waamini wote na kuwafanya
wanafunzi weye kujizidisha kwa kufanya yafuatayo
.
· Kila kansa kuanzisha ibada za maombi na maombezi ya
nguvu kama chambo cha uvunaji.
· Kuboresha mifumo ya ibada. Ibada zisikae kiburudani
zaidi. Ibada kugeuka kuwa ukumbi. Mambo ya kiroho kupewa kipaumbele katika
ibada.
· Uboreshaji wa majego na upatikanaji wa vyombo vya
mziki na injili.
No comments:
Post a Comment