Utangulizi:
Biblia
imeeleza kuhusu nyota ya Yesu ilivyoonekana kutoka mashariki,(Mathayo2:1); Hii
inadhihirisha wazi kuwa kila mtu ana nyota yake. Hivyo katika mfulilizo wa somo
hili tutaona maana ya nyota, kazi ya nyota, nyota yaweza kufunikwa kichawi,
madhara ya kuishi bila nyota, dalili za kuchukuliwa nyota, nyota yaweza
kurudishwa na namna ya kutambua nyota yako. Hapa hatuzungumzii kuhusu kusoma
nyota au utabiri wa nyota bali tunaangalia nyota kama ilivyo katika Biblia.
MAANA
YA NYOTA:
Nyota
katika Biblia inawakilisha kipawa, hatma ya mtu, lengo lililomfanya Mungu
akulete hapa duniani na kusudi lako la maisha. Hivyo tunaposema
nyota yako ipo au imechukuliwa maana yake hayo mambo yamechukuliwa au yapo.
Kimsingi hakuna mtu asiye na maana tangu kuzaliwa kwake, kwasababu kila mtu
aliye duniani amekuja kwa kusudi lake.
Kuna
tofauti kati ya elimu na nyota; elimu sio nyota lakini elimu yaweza kunoa
nyota. Na si kwamba kujifunza kunaleta nyota bali nyota ipo kwa wote lakini
elimu inainoa nyota; na ndio maana ni rahisi kumwona mtu hana elimu lakini
anamafanikio mahali fulani. Ukisoma Mhubiri 9:11 Biblia
inasema wakati na bahati huwapata wote na sio swala la elimu au ujuzi tu.
KAZI
YA NYOTA:
·
Nyota
humfanya mtu kuwa mahiri katika utendaji kazi wake. (Effectiveness)
·
Nyota
huleta ubunifu katika maisha ya kila siku (Creativity)
·
Nyota
inamfanya mtu anatenda kwa ufanisi (Efficiency)
·
Nyota
huleta mvuto kwa watu kutoka mbali ili kuleta vitu kwa ajili yako. (Attraction)
·
Nyota humfanya
mtu awe na maisha yenye mwelekeo na kibali mbele za watu.
(Acceptance and Favor)
·
Nyota
humfanya mtu kusikilizwa katika jamii.
Kuna
vitu ambavyo mtu anaweza kuvipata kwasababu nyota yake imeonekana. Nyota yaweza
kuvuta zawadi yaani vile vitu ambavyo hujavitaabikia, na ndio maana Yesu
alipokuwa mdogo aliletewa zawadi na mamajusi wa mashariki. (Mathayo 2:11)
kwahiyo nyota ikichukuliwa maana sahihi ni kwamba hayo mambo hapo juu yote
hayapo.
Mathayo
2:1-2; Wakati
Yesu anazaliwa kulikuwa na watu wanaitwa mamajusi, ambao walikuwa na uwezo wa
kusoma nyota. Hivyo katika ulimwengu wa roho waweza kuona watawala wajao,
maisha yajayo au yale yatarajiwayo. Na ndio maana Mamajusi wa mashariki
ya mbali waliweza kuifuata nyota ya Yesu.
Nyota
inapoonekana inaweza kufuatwa, yaani watu waona zile kazi zake na kumfuata mtu.
Kimsingi tunaposema mtu hana nyota maana yake umahiri, ufanisi na kibali
vimechukuliwa. Lakini nyota ikionekana maana yake haya mambo yote
yamerudishwa na hapo utamwona mtu anafanikiwa hata kama elimu yake sio kubwa.
NYOTA ILIYOCHUKULIWA/ ILIYOFUNIKWA KICHAWI:
Nyota
ikifunikwa au kuchukuliwa kichawi maana yake mvuto, umahiri, ufanisi na uwezo
unakuwa umechukuliwa au umefunikwa. Na ndio maana kuna watu wanahangaika
kuanzisha kampuni, kujenga nyumba, kulima, au kufanya biashara kama nyota
imefunikwa au kuchukuliwa kichawi huwezi kupokea mafanikio ya sahihi kwenye
maisha. Watu wengi wanahangaika kuonekana au kukubalika lakini kumbe tatizo
lipo kwenye nyota yaani imefunikwa au imechukuliwa kichawi.
Wachawi
wanaweza kuona nyota ya mtu na kuifunika ili isionekane; na kwa namna hii watu
wengi wanaonekana hawana mafanikio katika maisha kumbe nyota zao zimefunikwa.
Hivyo ni muhimu kupambana Kwa Jina la Yesu ili nyota yako ionekane.
MADHARA YA KUISHI BILA NYOTA YAKO:
·
Kwa kuwa nyota ndiyo inamwezesha mtu
kuwa na kila kitu, ndio kusudi la mtu, upendeleo wa mtu; hivyo madhara ya
kutokuwa na nyota ni kutokuwa navyo vyote vile.
·
Siku zote unakuwa unatenda chini ya
kiwango (Under performance). Na kwa namna hiyo hakuna mtu anakubali kile
unachotenda; yaani elimu na maarifa yote yakuwa chini ya kiwango.
·
Utapata na kuibiwa; unapata kazi
baadaye unaibiwa au unapata mchumba baadaye anaibiwa. Kimsingi huwezi kudumu na
haya mambo.
·
Unapata lakini anatumia mtu
mwingine.
DALILI
ZA NYOTA ILIYOFUNIKWA:.
·
Maisha kukosa mwelekeo; mtu akikosa
nyota hata kama akiwa na elimu kama nyota haipo lazima mtu huyo atakosa
mwelekeo.
·
Kukwama kibiashara na kuishi maisha
kwenye madeni.
·
Unafanya kazi lakini hupati
maendeleo. Yaani mtu anapata mshahara mzuri lakini anakosa mafanikio halisi
kwasababu ya nyota iliyofunikwa au kuibiwa.
·
Wewe ni kiongozi lakini jamii
haikutambui.
·
Ukichangia hoja za mijadala
mbalimbali hakuna anayekusikiliza.
·
Umesoma lakini hupati kazi, na
ukipata kazi haiendani na elimu yako
·
Maisha ya upweke na hakuna
anayekujali katika familia.
·
Unatenda kazi kwa bidii lakini
hupandi cheo.
·
Kama ni binti sifa zote
lakini hakuna anayekuchumbia maana huonekani.
·
Kuandamwa na mabalaa na mikosi.
·
Kupotelewa na watu wa muhimu
NYOTA
YAWEZA KURUDISHWA:
Hatua
ya kwanza kama hujaokoka unatakiwa kuokoka; kuokoka ni kumpokea Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha
yako ili upate uwezo wa kushindana, hivyo ukigundua nyota imechukiliwa
unatakiwa umpokee Yesu ndani ya moyo wako. Ni kitu cha kushangaza kuhitaji
msaada wa Yesu halafu yeye humtaki kimsingi kuokoka ni hatua ya kwanza ya
kurudisha nyota.
Hatua
ya pili ni kushindana kwa maombi;
kama mtu anayetaka kurudisha nyota yake ni lazima achukue hatua ya
kushindana katika maombi. Hivyo baada ya kuokoka hatua inayofuata ni kushindana
ili nyota irudi. Nyota yaweza kurudishwa kwa kuomba katika Jina la Yesu Kristo.
UTAJUAJE
NYOTA YAKO NI IPI:
Usithubutu
kwenda kwa mganga wa kienyeji au kusoma kwenye magazeti ili kujua nyota
yako. Ni muhimu kujua kilichoibiwa ni kipi katika maisha yako.
Isaya 47:13 “Umechoka kwa wingi wa
mashauri yako; basi, na wasimame hao wajuao falaki, wazitazamao nyota,
watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata.” FALAKI
ni elimu juu ya mambo ya nyota; biblia inataja kuwa kuna watu
wanaojishughulisha na usomaji wa nyota. Lakini kuna mambo kadhaa yanayoweza
kukuonyesha nyota yako ni ipi:-
Moyo
wako, akili zako na mawazo yako yanakuwa katika hilo jambo AMBALO NI NYOTA
YAKO. Mfano kama nyota yako ni biashara basi utakuta moyo wako upo kwenye
biashara, basi lazima nyota yako ni k biashara. Kama nyota ni kuimba au siasa
lazima moyo utakupeleka kwenye kuimba na siasa. Hivyo tambua kuwa kwenye nyota
yako ndipo kuna Baraka zako.
Jambo
ambalo ni nyota yako utalitenda bila kupambana; Yaani hutatumia nguvu kwenye
kulitekeleza jambo hilo.
MAOMBI
YA KURUDISHA NYOTA:
Kurudisha nyota Iliyoibiwa:
Baba
katika Jina la Yesu, nimetambua kuwa nyota yangu yaweza kufunikwa na kuibiwa;
na leo ninaamua kuirudisha kwa Jina la Yesu kila nyota yangu iliyoibiwa, nyota
ya kukubaliwa, ufanisi, umahiri, biashara, kazi au nyota ya hatma njema naamuru
irudi kwa Jina la Yesu Kristo. Ninaamuru nyota yangu ikombolewe kwa damu ya
Yesu, ninaamuru iachiliwe katika Jina la Yesu.
Kufunua
nyota iliyofunikwa:
Katika
Jina kuu la Yesu ninasafisha nyota yangu iliyofunikwa; nyota ya mafanikio
ninaisafisha kwa Jina la Yesu. Katika torati kila kitu husafishwa kwa Damu nami
natumia Damu ya Yesu kusafisha nyota yangu katika Jina la Yesu. Ninatakasa
nyota yangu iliyochafuliwa katika Jina la Yesu. Ninang’arisha nyota yangu
katika Jina la Yesu.
Kuangamiza
wasimamizi wa nyota:
Ninasimama
kinyume na kila mashetani, wachawi na waganga wa kienyeji wanaoshikilia nyota
yangu katika Jina la Yesu. Waliofunika nyota ninawaangamiza katika ulimwengu wa
roho, ninateketeza wote walioiba nyota yangu kwa Jina la Yesu. Katika Jina la
Yesu niharibu kazi na utawala wa mashetani wanaoiba nyota yangu katika Jina La
Yesu.
:
Biblia imeeleza kuhusu nyota ya Yesu
ilivyoonekana kutoka mashariki,(Mathayo2:1); Hii inadhihirisha wazi
kuwa kila mtu ana nyota yake. Hivyo katika mfulilizo wa somo hili tutaona maana
ya nyota, kazi ya nyota, nyota yaweza kufunikwa kichawi, madhara ya kuishi bila
nyota, dalili za kuchukuliwa nyota, nyota yaweza kurudishwa na namna ya
kutambua nyota yako. Hapa hatuzungumzii kuhusu kusoma nyota au utabiri wa nyota
bali tunaangalia nyota kama ilivyo katika Biblia.
MAANA YA NYOTA:
Nyota katika Biblia inawakilisha
kipawa, hatma ya mtu, lengo lililomfanya Mungu akulete hapa duniani na kusudi lako la maisha. Hivyo
tunaposema nyota yako ipo au imechukuliwa maana yake hayo mambo yamechukuliwa
au yapo. Kimsingi hakuna mtu asiye na maana tangu kuzaliwa kwake, kwasababu
kila mtu aliye duniani amekuja kwa kusudi lake.
Kuna tofauti kati ya elimu na nyota;
elimu sio nyota lakini elimu yaweza kunoa nyota. Na si kwamba kujifunza
kunaleta nyota bali nyota ipo kwa wote lakini elimu inainoa nyota; na ndio
maana ni rahisi kumwona mtu hana elimu lakini anamafanikio mahali fulani.
Ukisoma Mhubiri 9:11 Biblia inasema
wakati na bahati huwapata wote na sio swala la elimu au ujuzi tu.
KAZI YA NYOTA:
- Nyota humfanya mtu kuwa mahiri katika utendaji kazi wake. (Effectiveness)
- Nyota huleta ubunifu katika maisha ya kila siku (Creativity)
- Nyota inamfanya mtu anatenda kwa ufanisi (Efficiency)
- Nyota huleta mvuto kwa watu kutoka mbali ili kuleta vitu kwa ajili yako. (Attraction)
- Nyota humfanya mtu awe na maisha yenye mwelekeo na kibali mbele za watu. (Acceptance and Favor)
- Nyota humfanya mtu kusikilizwa katika jamii.
Kuna vitu ambavyo mtu anaweza
kuvipata kwasababu nyota yake imeonekana. Nyota yaweza kuvuta zawadi yaani vile
vitu ambavyo hujavitaabikia, na ndio maana Yesu alipokuwa mdogo aliletewa
zawadi na mamajusi wa mashariki. (Mathayo
2:11) kwahiyo nyota ikichukuliwa maana sahihi ni kwamba hayo mambo hapo juu
yote hayapo.
Mathayo 2:1-2;
Wakati Yesu anazaliwa kulikuwa na watu wanaitwa mamajusi, ambao walikuwa na
uwezo wa kusoma nyota. Hivyo katika ulimwengu wa roho waweza kuona watawala
wajao, maisha yajayo au yale yatarajiwayo.
Na ndio maana Mamajusi wa mashariki ya mbali waliweza kuifuata nyota ya
Yesu.
Nyota inapoonekana inaweza kufuatwa,
yaani watu waona zile kazi zake na kumfuata mtu. Kimsingi tunaposema mtu hana
nyota maana yake umahiri, ufanisi na kibali vimechukuliwa. Lakini nyota
ikionekana maana yake haya mambo yote
yamerudishwa na hapo utamwona mtu anafanikiwa hata kama elimu yake sio kubwa.
NYOTA ILIYOCHUKULIWA/ ILIYOFUNIKWA KICHAWI:
Nyota ikifunikwa au kuchukuliwa
kichawi maana yake mvuto, umahiri, ufanisi na uwezo unakuwa umechukuliwa au
umefunikwa. Na ndio maana kuna watu wanahangaika kuanzisha kampuni, kujenga
nyumba, kulima, au kufanya biashara kama nyota imefunikwa au kuchukuliwa
kichawi huwezi kupokea mafanikio ya sahihi kwenye maisha. Watu wengi wanahangaika
kuonekana au kukubalika lakini kumbe tatizo lipo kwenye nyota yaani imefunikwa
au imechukuliwa kichawi.
Wachawi wanaweza kuona nyota ya mtu
na kuifunika ili isionekane; na kwa namna hii watu wengi wanaonekana hawana
mafanikio katika maisha kumbe nyota zao zimefunikwa. Hivyo ni muhimu kupambana
Kwa Jina la Yesu ili nyota yako ionekane.
MADHARA YA KUISHI BILA NYOTA YAKO:
- Kwa kuwa nyota ndiyo inamwezesha mtu kuwa na kila kitu, ndio kusudi la mtu, upendeleo wa mtu; hivyo madhara ya kutokuwa na nyota ni kutokuwa navyo vyote vile.
- Siku zote unakuwa unatenda chini ya kiwango (Under performance). Na kwa namna hiyo hakuna mtu anakubali kile unachotenda; yaani elimu na maarifa yote yakuwa chini ya kiwango.
- Utapata na kuibiwa; unapata kazi baadaye unaibiwa au unapata mchumba baadaye anaibiwa. Kimsingi huwezi kudumu na haya mambo.
- Unapata lakini anatumia mtu mwingine.
DALILI ZA NYOTA ILIYOFUNIKWA:.
- Maisha kukosa mwelekeo; mtu akikosa nyota hata kama akiwa na elimu kama nyota haipo lazima mtu huyo atakosa mwelekeo.
- Kukwama kibiashara na kuishi maisha kwenye madeni.
- Unafanya kazi lakini hupati maendeleo. Yaani mtu anapata mshahara mzuri lakini anakosa mafanikio halisi kwasababu ya nyota iliyofunikwa au kuibiwa.
- Wewe ni kiongozi lakini jamii haikutambui.
- Ukichangia hoja za mijadala mbalimbali hakuna anayekusikiliza.
- Umesoma lakini hupati kazi, na ukipata kazi haiendani na elimu yako
- Maisha ya upweke na hakuna anayekujali katika familia.
- Unatenda kazi kwa bidii lakini hupandi cheo.
- Kama ni binti sifa zote lakini hakuna anayekuchumbia maana huonekani.
- Kuandamwa na mabalaa na mikosi.
- Kupotelewa na watu wa muhimu
NYOTA YAWEZA KURUDISHWA:
Hatua ya kwanza kama hujaokoka unatakiwa kuokoka; kuokoka ni kumpokea Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha
yako ili upate uwezo wa kushindana, hivyo ukigundua nyota imechukiliwa
unatakiwa umpokee Yesu ndani ya moyo wako. Ni kitu cha kushangaza kuhitaji
msaada wa Yesu halafu yeye humtaki kimsingi kuokoka ni hatua ya kwanza ya
kurudisha nyota.
Hatua ya pili ni kushindana kwa maombi; kama mtu anayetaka kurudisha nyota yake ni lazima achukue
hatua ya kushindana katika maombi. Hivyo
baada ya kuokoka hatua inayofuata ni kushindana ili nyota irudi. Nyota yaweza
kurudishwa kwa kuomba katika Jina la Yesu Kristo.
UTAJUAJE NYOTA YAKO NI IPI:
Usithubutu kwenda kwa mganga wa
kienyeji au kusoma kwenye magazeti ili kujua nyota yako. Ni muhimu kujua kilichoibiwa ni kipi katika
maisha yako. Isaya 47:13 “Umechoka kwa wingi
wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wajuao falaki, wazitazamao nyota,
watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata.”
FALAKI ni elimu juu ya mambo ya nyota; biblia inataja kuwa kuna watu
wanaojishughulisha na usomaji wa nyota. Lakini kuna mambo kadhaa yanayoweza
kukuonyesha nyota yako ni ipi:-
Moyo wako, akili zako na mawazo yako
yanakuwa katika hilo jambo AMBALO NI NYOTA YAKO. Mfano kama nyota yako ni
biashara basi utakuta moyo wako upo kwenye biashara, basi lazima nyota yako ni
k biashara. Kama nyota ni kuimba au siasa lazima moyo utakupeleka kwenye kuimba
na siasa. Hivyo tambua kuwa kwenye nyota yako ndipo kuna Baraka zako.
Jambo ambalo ni nyota yako
utalitenda bila kupambana; Yaani hutatumia nguvu kwenye kulitekeleza jambo
hilo.
MAOMBI YA KURUDISHA NYOTA:
Kurudisha nyota Iliyoibiwa:
Baba katika Jina la Yesu, nimetambua
kuwa nyota yangu yaweza kufunikwa na kuibiwa; na leo ninaamua kuirudisha kwa
Jina la Yesu kila nyota yangu iliyoibiwa, nyota ya kukubaliwa, ufanisi, umahiri,
biashara, kazi au nyota ya hatma njema naamuru irudi kwa Jina la Yesu Kristo.
Ninaamuru nyota yangu ikombolewe kwa damu ya Yesu, ninaamuru iachiliwe katika
Jina la Yesu.
Kufunua nyota iliyofunikwa:
Katika Jina kuu la Yesu ninasafisha
nyota yangu iliyofunikwa; nyota ya mafanikio ninaisafisha kwa Jina la Yesu.
Katika torati kila kitu husafishwa kwa Damu nami natumia Damu ya Yesu kusafisha
nyota yangu katika Jina la Yesu. Ninatakasa nyota yangu iliyochafuliwa katika
Jina la Yesu. Ninang’arisha nyota yangu
katika Jina la Yesu.
Kuangamiza wasimamizi wa nyota:
Ninasimama kinyume na kila
mashetani, wachawi na waganga wa kienyeji wanaoshikilia nyota yangu katika Jina
la Yesu. Waliofunika nyota ninawaangamiza katika ulimwengu wa roho,
ninateketeza wote walioiba nyota yangu kwa Jina la Yesu. Katika Jina la Yesu
niharibu kazi na utawala wa mashetani wanaoiba nyota yangu katika Jina La Yesu.
No comments:
Post a Comment