Friday, 5 December 2014
UONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA
10
9
8
7
6
5
4
3
2
1
11
12
13
v
10
9
8
7
6
5
4
3
2
1
11
12
13
ORODHA YA MAJINA YA KIKUNDI KAZI NA WAWEZESHAJI iii - v
DIBAJI vii - xiii
YALIYOMO Ukurasa
MADA YA KWANZA
SHERIA, MUUNDO NA MFUMO WA UENDESHAJI WA
SERIKALI ZA MITAA 5 - 38
MADA YA PILI
DHANA YA UBORESHAJI WA MFUMO WA SERIKALI ZA MITAA 41 - 45
MADA YA TATU
MUUNDO WA UTUMISHI WA MAAFISA WATENDAJI VIJIJI NA MITAA 49 - 54
MADA YA NNE
KAZI, WAJIBU NA HAKI ZA AFISA MTENDAJI WA KIJIJI NA MTAA 57 - 63
MADA YA TANO
WAJIBU WA AFISA MTENDAJI WA KIJIJI NA MTAA 67 - 76
MADA YA SITA
MBINU ZA MENEJIMENTI NA UONGOZI, SHERIA ZA
KAZI NA USULUHISHI WA MIGOGORO 79 - 89
MADA YA SABA
KANUNI NA TARATIBU ZA UENDESHAJI WA OFISI NA MIKUTANO 93 - 101
vi
MADA YA NANE
KUKUZA UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASKINI 105 - 118
YALIYOMO Ukurasa
MADA YA TISA
UANDAAJI WA MIPANGO SHIRIKISHI 123 - 144
MADA YA KUMI
UANDIKAJI NA USIMAMIZI WA MIRADI 147 - 172
MADA YA KUMI NA MOJA
USIMAMIZI WA FEDHA NA TARATIBU ZA MANUNUZI 175 - 185
MADA YA KUMI NA MBILI
SHERIA NA KANUNI ZA MAADILI YA WATUMISHI WA UMMA 189 - 197
MADA YA KUMI NA TATU
MASUALA MTAMBUKA 201 - 235
KIKUNDI KAZI CHA MAFUNZO
vii
10
9
8
7
6
5
4
3
2
1
11
12
13
KIKUNDI KAZI CHA MAFUNZO YA AWALI KWA MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA
MITAA TANZANIA BARA – APRILI 2004
JINA CHEO TAASISI
Bibi S.S. Musese Mkurugenzi OR-TAMISEMI
Bw. O.P Mtei Kaimu Mkurugenzi OR-TAMISEMI
Bw. E.T. Omuyanja Afisa Ushirika Mkuu Manispaa Dodoma
Bw. E.J. Luvanda Afisa Tawala Mwandamizi OR-TAMISEMI
Bw. F.K. Senge Afisa Miradi Mkuu OR-TAMISEMI
Bw. D.M.Lyakinana Afisa Tawala OR-TAMISEMI
Bw. O.V. Tomeka Afisa Mipango Mkuu OR-TAMISEMI
Dr. R.W.Kisusu Afisa Mipango Mwandamizi OR-TAMISEMI
Bi. M. Macha Afisa Utumishi Mwandamizi Manispaa Dodoma
Bw. M. Tuniga Afisa Ushirika H/W ya Dodoma
Bw.D. Musiba Mkufunzi Mwandamizi IRDP
Bw. G. Ndiwaita Mkufunzi IRDP
Bw. K. Kupa Mhasibu Msaidizi OR-TAMISEMI
Bw. V.F. Kategere Afisa Tawala (Katibu) OR-TAMISEMI
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
viii
KIKUNDI KAZI CHA UBORESHAJI WA KITABU CHA KUFUNDISHIA MAAFISA
WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA - JULAI 2006
JINA CHEO TAASISI
Bibi S.S. Musese Mkurugenzi OWM-TAMISEMI
Bibi M.S. Mbegu Mkurugenzi Msaidizi OWM-TAMISEMI
Bw. V.F. Kategere Afisa Tawala Mkuu OWM-TAMISEMI
Bw. E.J. Luvanda Kaimu Mkurugenzi Msaidizi OWM-TAMISEMI
Bibi. M. Njovu Afisa Utumishi OWM-TAMISEMI
Bi S. Paschal Afisa Serikali za Mitaa OWM-TAMISEMI
Bw. M. Mavura Mchambuzi Kazi OWM-TAMISEMI
Bibi. B.N. Mkina Afisa Elimu Mwandamizi OWM-TAMISEMI
Bw. C.D Zilala Mkurugenzi wa Mafunzo LGTI–HOMBOLO
Bw. J.M.V Swalle Afisa Utumishi Mwandamizi OWM-TAMISEMI
KIKUNDI KAZI CHA MAFUNZO
v
10
9
8
7
6
5
4
3
2
1
11
12
13
KIKUNDI KAZI CHA UBORESHAJI WA KITABU CHA KUFUNDISHIA MAAFISA
WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA - SEPTEMBA 2010
JINA CHEO TAASISI
Bibi Hellen R. Macha Mkurugenzi Msaidizi OWM-TAMISEMI
Bw. Victor F. Kategere Mkurugenzi Msaidizi OWM-TAMISEMI
Bibi. Marietha Njovu Afisa Utumishi Mkuu OWM-TAMISEMI
Bw. Eustadi Ngatale Mwanasheria wa Serikali OWM-TAMISEMI
Bi. Debora Mkemwa A/Serikali za Mitaa OWM-TAMISEMI
Bw. Dastan S. Mboera Afisa Ugavi OWM – TAMISEMI
Bibi. Notburga S. Maskini Afisa Utumishi Mkuu OWM - TAMISEMI
Bw. Emmanuel Nyagawa A/Serikali za Mitaa OWM – TAMISEMI
Bw. Abdulatifu Mkata Afisa Utumishi H/Wilaya Mtwara
Bw. Dauson P. Temu Afisa Mipango H/Wilaya Handeni
Bibi. Samina A. Gulam Afisa Utumishi H/Wilaya Korogwe
Bibi. Cecilia Nzamwita Afisa M/Jamii Mkuu OWM-TAMISEMI
Bw. Denisi Mbilinyi A/Usimamizi wa Fedha OWM-TAMISEMI
Bw. Idris Mtandi Mchumi OWM - TAMISEMI
Bw. Tiberius Mlowosa Mhadhiri Msaidizi LGTI
Bw. Yusuph Mashalla Mhadhiri Msaidizi LGTI
Bibi. Natalia Kalimangási Mhadhiri Msaidizi LGTI
Bw. Geofrey Rwezimula Mhadhiri Msaidizi LGTI
Bibi. Esther Mkenda Mchumi WVBM
Bw. Lazaro S. Bapala Mchumi WKAV
Bw. Paul Botlleberge Mtaalamu Mashauri GTZ – SULGO
Bw. John Millinga Mtaalamu Mshauri GTZ – SULGO
Bi. Nasako Sasaki Mtaalamu Mshauri JICA/LGTI
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
vi
DIBAJI
vii
10
9
8
7
6
5
4
3
2
1
11
12
13
DIBAJI
Tangu mwaka 1984, Serikali iliporejesha Mfumo wa Serikali za Mitaa, jitihada kubwa zimekuwa
zikifanyika katika kujenga mfumo imara wa kitaasisi ili kusimamia na kuratibu shughuli za utawala,
utendaji na maendeleo katika ngazi ya Mkoa, Wilaya Halmashauri, Tarafa, Kata, Kijiji, Mtaa na
Kitongoji. Lengo kuu la kurejesha mfumo huu lilikuwa ni kuwawezesha wananchi kupata fursa ya
kushiriki kwa ukamilifu katika kupanga na kufanya maamuzi yanayohusu maendeleo katika maeneo
yao.
Agenda ya kuziimarisha Serikali za Mitaa iliyoidhinishwa mwaka 1996 ina lengo la kukidhi mahitaji
ya kuwawezesha wananchi kushiriki kwa ukamilifu katika shughuli za maendeleo. Aidha, programu
hii inalenga kutanzua matatizo kadhaa ambayo yamezikumba Serikali za Mitaa kwa muda mrefu.
Matatizo hayo ni pamoja na yale ya kimfumo na kisheria ambayo yamesababisha mwingiliano
wa majukumu pamoja na miundo ya utumishi kutoeleweka na watumishi wahusika wa Serikali za
Mitaa kama vile Maafisa Watendaji wa Kata, Vijiji na Mitaa. Hali hii imesababisha baadhi ya Maafisa
Watendaji wa Kata,Vijiji na Mitaa kutekeleza majukumu na wajibu wao bila melekeo na kuonekana
kama miungu watu ndani ya jamii – jambo ambalo linasababisha kero kwa wananchi na kukosa
imani kwa Serikali yao.
Ni kwa msingi huo, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imeandaa Programu
ya Mafunzo ya Maafisa Watendaji wa Kata, Vijiji na Mitaa. Kitabu cha kufundishia kimefanyiwa
mapitio ili kuweza kuhusisha mambo yote mapya ya muhimu yaliyojitokeza wakati wa kuendesha
Mafunzo. Tayari mafunzo kwa Watendaji wa Kata yamefanyika kote nchini; na sehemu kubwa
ya Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa. Yote haya yanafanyika kwa ajili ya kuboresha utoaji wa
huduma bora kwa Wananchi.
Shabaha au lengo kuu la mafunzo haya ni kuwawezesha Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa
kuelewa na kuzingatia misingi na utaratibu wa utekelezaji wa majukumu yao kulingana na malengo
ya Serikali. Aidha, madhumuni mahsusi ya mafunzo haya ni kuwawezesha Maafisa hao:
• Kuelewa Sheria, Muundo na mfumo wa Uendeshaji wa Serikali za Mitaa;
• Kuelewa dhana ya Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa;
• Kuelewa Muundo wa Utumishi wa Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa;
• Kuelewa Kazi , Wajibu na Haki za Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa;
• Kuelewa Wajibu wa Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa kama Mlinzi wa Amani;
• Kuelewa mbinu za Menejimenti na Uongozi, Sheria za Kazi na Usuluhishi wa Migogoro;
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
viii
• Kuelewa Kanuni na Taratibu za Uendeshaji wa Ofisi na Mikutano, Utunzaji wa Kumbukumbu, na
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano;
• Kuelewa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini, Ujasiliamali na Uanzishwaji wa
Vikundi;
• Kuelewa Utaratibu wa Uandaaji wa Mipango Shirikishi Jamii katika ngazi ya Kijiji na Mtaa;
• Kuelewa Mbinu za Uandikaji na Usimamizi wa Miradi;
• Kuelewa Misingi ya Usimamizi wa Fedha na Taratibu za Manunuzi;
• Kuelewa umuhimu wa kuzingatia Sheria na Kanuni za Maadili ya Watumishi wa Umma katika
utekelezaji a majukumu yao;
• Kuelewa masuala mtambuka yanayohusu Utawala Bora na Demokrasia, Uchambuzi wa Kijinsia
na Makundi yenye Mahitaji Maalumu na Usimamizi wa Majanga (Ukimwi na Hifadhi Endelevu ya
Mazingira).
Mada muhimu zitakazowezeshwa katika mafunzo haya ni:
i. Sheria, Muundo na Mfumo wa Uendeshaji wa Serikali za Mitaa
• Maana, Muundo na Aina za Mamlaka za Serikali za Mitaa na majukumu yake;
• Majukumu ya Mwenyekiti wa Kijiji/Mtaa na Kitongoji;
• Uhusiano wa Serikali za Mitaa na Serikali Kuu;
• Kanuni na Sheria zinazotawala Uendeshaji wa Serikali za Mitaa.
ii. Dhana ya Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
• Dhana ya kupeleka Madaraka kwa wananchi.
• Mahusiano kati ya Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
• Awamu ya Pili ya Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa.
iii. Muundo wa Utumishi wa Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa:
• Maana na Umuhimu wa Muundo wa Utumishi.
• Muundo wa Utumishi wa Maafisa Watendaji wa Vijiji.
• Muundo wa Utumishi wa Maafisa Watendaji wa Mitaa
iv. Kazi, Wajibu na Haki za Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa
• Kazi na Wajibu wa Afisa Mtendaji wa Kijiji
• Kazi na Wajibu wa Afisa Mtendaji wa Mtaa
• Haki za Mtumishi wa Umma
DIBAJI
ix
10
9
8
7
6
5
4
3
2
1
11
12
13
v. Wajibu wa Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa Kama Mlinzi wa Amani
• Dhana ya Mlinzi wa Amani
• Ulinzi wa Amani wakati wa Ukoloni
• Maana ya Ulinzi wa Amani
• Kwa nini kuwe na Ulinzi wa Amani?
• Walinzi wa Amani ni nani?
• Madaraka ya Mlinzi wa Amani
• Msimamizi wa Walinzi wa Amani
• Uwezo wa Maafisa Watendaji wa Vijiji kukamata au Kuagiza Kukamata Watuhumiwa
• Kinga Dhidi ya Mashtaka ya Madai
• Vigezo vya Kutumika
• Ulinzi Shirikishi (Polisi Jamii)
vi. Mbinu za Menejimenti na Uongozi, Sheria za Kazi na Usuluhishi wa Migogoro
• Maana ya Menejimenti
• Misingi ya Menejimenti
• Mbinu za Menejimenti
• Maana ya Uongozi
• Uhusiano kati ya Viongozi na Wanaoongozwa
• Masuala muhimu katika Sheria Mpya za kazi
• Usuluhishi wa migogoro
vii. Kanuni na Taratibu za Uendeshaji wa Ofisi na Mikutano, Utunzaji wa Kumbukumbu,
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
• Taratibu za Kuendesha Ofisi;
• Vitendea Kazi Muhimu;
• Kanuni na Taratibu za Uendeshaji wa Mikutano
• Umuhimu wa kutunza kumbukumbu
• Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
x
viii. Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini, Ujasiriamali na Uanzishwaji wa
Vikundi;
• Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025:
• Ufafanuzi wa Malengo ya Dira ya Taifa 2025
• Maana ya Umaskini
• Viashiria vya Umaskini
• Sera ya Taifa ya kuondoa Umaskini
• Mkakati wa Taifa wa Kuratibu Utekelezaji wa Sera ya kuondoa Umaskini
• Hatua za kuondoa Umaskini
• Vikwazo katika kuwawezesha Wananchi kushiriki katika shughuli za Maendeleo
• Majukumu ya Serikali za Vijiji,Vitongoji na Mitaa katika kupambana na Umaskini
• Ujasiriamali na Uanzishwaji wa Vikundi
ix. Uandaaji wa Mipango Shirikishi Jamii
• Umuhimu wa kushirikisha Wataalam na Wananchi katika Kupanga Mipango ya Maendeleo;
• Umuhimu wa Mipango Shirikishi Jamii
• Dhana ya Mipango Shirikishi Jamii
• Hatua za Upangaji Mipango Shirikishi Jamii
• Uwekaji wa Vipaumbele
x. Uandikaji na Usimamizi wa Miradi
• Muundo wa andiko la Mradi
• Mahitaji na upatikanaji wa Rasilimali
• Usimamizi wa Utekelezaji
• Ufuatiliaji na Tathmini
• Jinsi ya Kupata Fedha za Kugharimia Mradi
• Majukumu ya Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa katika kutafuta vyanzo vya fedha za
kugharimia Miradi ya Maendeleo
DIBAJI
xi
10
9
8
7
6
5
4
3
2
1
11
12
13
xi. Usimamizi wa Fedha na Taratibu za Manunuzi
• Madhumuni ya Kuandaa Bajeti
• Utayarishaji wa Makisio ya Bajeti
• Taratibu za Malipo na Udhibiti wa Ndani
• Utunzaji wa Kumbukumbu za Fedha
• Taratibu za Manunuzi na Udhibiti
• Mchakato wa Manunuzi
• Usimamizi wa Mikataba
xii. Sheria na Kanuni za Maadili ya watumishi Wa Umma
• Maana ya Maadili ya Watumishi wa Umma
• Tabia na Mienendo Ya Kimaadili
• Kutoa Huduma Bora
• Utii kwa Serikali
• Bidii ya Kazi
• Kutoa Huduma bila Upendeleo
• Kufanya Kazi kwa Uadilifu
• Uwajibikaji Kwa Umma
• Kuheshimu Sheria
• Matumizi Sahihi ya Taarifa
xiii. Masuala Mtambuka:
• Utawala Bora na Demokrasia
i) Maana na Misingi ya Utawala Bora;
ii) Maana na Misingi ya Demokrasia;
iii) Nafasi ya Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa katika Kuimarisha Utawala Bora na
Demokrasia
• Uchambuzi wa Kijinsia na Makundi yenye Mahitaji Maalumu
i) Ufafanuzi wa dhana muhimu
ii) Mbinu za Uchambuzi wa Kijinsia
iii) Uchambuzi wa Mmilikaji Mali, Rasilimali na Nyenzo za Kufanyia Kazi
iv) Masuala ya Kijinsia katika Shughuli za Maendeleo
v) Uchambuzi wa Mahitaji ya Makundi Maalumu kwenye Mipango ya Maendeleo
vi) Wajibu wa Maafisa wa Vijiji na Mitaa katika Uchambuzi wa kijinsia na mahitaji ya
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
xii
makundi maalumu.
• Usimamizi wa Majanga (Ukimwi na Mazingira)
i) Maana ya Majanga na Maafa
ii) Vyanzo na aina za majanga
iii) Dhana ya tahadhari dhidi ya Majanga na jinsi ya kudhibiti maafa
iv) Udhibiti wa majanga na maafa yanayosababishwa na vitendo vya watu katika jamii
v) Umuhimu wa Hifadhi endelevu ya mazingira
vi) Njia kuu za maambukizi ya UKIMWI
vii) Athari zitokanazo na UKIMWI
viii) Wajibu wa Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa katika Kuhifadhi Mazingira na
kupambana na Ukimwi
ix) Sera
–– Sera ya Maji
–– Sera ya Elimu
–– Sera ya Barabara
–– Sera ya Kilimo na Mifugo
–– Sera ya Afya
–– Sera ya Ushirika
–– Sera ya Ardhi
–– Rushwa
–– Mwongozo wa Usimamizi wa Fedha ngazi ya Kijiji na Kamati ya Mtaa
–– Taratibu za Manunuzi
–– Uboreshaji wa Miundo
DIBAJI
xiii
10
9
8
7
6
5
4
3
2
1
11
12
13
Kitabu hiki kisingekamilika bila ya michango ya taasisi, Wataalam na watu mbalimbali wa OWMTAMISEMI.
Kwa ajili hiyo, naipongeza Kamati ya Maandalizi ya Mafunzo ya awali ya Maafisa
Watendaji wa Vijiji na Mitaa iliyoainisha hadidu za rejea kwa ajili ya mafunzo haya na kuendelea
kutoa maelekezo ya mara kwa mara pasipo kuchoka wakati wa kufanya mapitio.
Kadhalika, natambua mchango mkubwa wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Chuo Cha
Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma, Shirika la Kimataifa la Maendeleo Japan (JICA) na Shirika
la Kimataifa la Maendeleo la Ujerumani (GTZ – SULGO) kwa mchango wao mkubwa waliotoa
katika maandalizi na hatimaye kupitia na kuboresha Kitabu cha Rejea (Mada) na Mwongozo wa
Kufundishia.
Mwisho, nawapongeza wachapaji wa makala za kitabu hiki na wengine wote waliohusika kwa njia
moja au nyingine kukamilisha uandhishi wa kitabu hiki.
Kattanga, H. A.
KATIBU MKUU
OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MADA YA KWANZA1 10
9
8
7
6
5
4
3
2
1
11
12
13
SHERIA, MUUNDO NA MFUMO WA UENDESHAJI
WA SERIKALI ZA MITAA
2
MADA YA KWANZA
3
10
9
8
7
6
5
4
3
2
11
12
13
1.0 SHERIA, MUUNDO NA MFUMO WA UENDESHAJI WA
SERIKALI ZA MITAA
1.1 UTANGULIZI
Lengo kuu la mada hii ni kuwawezesha Maafisa Watendaji wa Vijiji- na Mitaa kupata uelewa wa
msingi kuhusu sheria, muundo na mfumo wa uendeshaji wa Serikali za Mitaa.
Madhumuni mahsusi ya mada hii ni kuwawezesha Maafisa hao kuelewa:
Maana, muundo na aina za mamlaka na madaraka ya Serikali za Mitaa;
• Uhusiano wa Serikali za Mitaa na Serikali Kuu;
• Uchaguzi wa Wajumbe wa Halmashauri na Ngazi nyingine za Jamii.
• Sheria zinazotawala uendeshaji wa Serikali za Mitaa.
Uelewa huo utawawezesha Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa kutekeleza majukumu yao kwa
kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali za Mitaa bila kuleta kero kwa wananchi na
kuongeza tija na ufanisi katika maeneo yao ya kazi.
1.2 MAANA, MUUNDO NA AINA ZA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA
Maana ya Serikali za Mitaa
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na
marekebisho yake, Ibara ya 145 na 146, Serikali za Mitaa ni vyombo vya wananchi ambavyo vipo
katika ngazi za chini za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vyombo hivi huundwa,
huendeshwa, husimamiwa na kuwajibika kwa wananchi wenyewe. Kwa maana hiyo, Serikali za
Mitaa huwawezesha wananchi kuwa na sauti katika maamuzi mbalimbali ama kwa kushiriki moja
kwa moja au kwa kupitia wawakilishi wao katika shughuli za maendeleo na utawala. Serikali za
Mitaa zinatokana na dhana ya madaraka kwa umma. Dhana na madhumuni ya madaraka kwa
umma ni kuwapa wananchi (wanaume na wanawake) wote uwezo na fursa sawa ya kushiriki
kikamilifu katika masuala ya siasa, uchumi na utawala katika nchi yao. Kwa mujibu wa Ibara ya 8 (1)
(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977), wananchi ndiyo msingi wa mamlaka yote
na Serikali inapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi.
Muundo na Aina za Mamlaka na Ngazi za Serikali za Mitaa
Mwaka 1982 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitunga Sheria Na. 7, 8 na 9 ili kutimiza
maagizo ya Katiba ya Nchi kuhusu uundaji, uendeshaji na usimamizi wa Serikali za Mitaa. Sheria Na.
7 inazungumzia uundaji wa mamlaka za Serikali za Mitaa katika maeneo ya wilaya. Mamlaka hizo ni
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
4
Halmashauri za Wilaya, Mamlaka za Miji Midogo na Halmashauri za Vijiji. Sheria Na. 8 inazungumzia
uundaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika maeneo ya mijini, ambazo ni Halmashauri za Miji,
Manispaa na Jiji. Kifungu Na. 5 cha Sheria Na.7 na 8 kinampa madaraka Waziri mwenye dhamana
ya Serikali za Mitaa kuanzisha Mamlaka za Serikali za Mitaa katika maeneo mbalimbali nchini.
Katika kuanzisha Mamlaka za Wilaya na Miji, Waziri lazima ashauriane na Rais. Sheria Namba 7 na 8
za mwaka 1982 zinafafanua muundo wa mamlaka za Serikali za Mitaa kama ifuatavyo:-
HALMASHAURI ZA WILAYA
[a] Ngazi ya Kitongoji
Kitongoji ni sehemu ya kijiji au Mji Mdogo kama inavyoamriwa na Halmashauri. Kitongoji hakina
idadi maalum ya kaya, hata hivyo idadi ya kaya itapangwa na Halmashauri ya Kijiji na kuidhinishwa
na Halmashauri ya wilaya ambako Kitongoji hicho kimo.Idadi ya vitongoji kwa kila kijiji sio zaidi ya
vitano.
Uandikishaji wa kitongoji
Katika uandikishaji wa kitongoji, hatua zifuatazo lazima zifuatwe;
• Mkurugenzi Mtendaji ataagiza Halmashauri za vijiji ziyagawe maeneo yao katika vitongoji
• Halmashauri zitaangalia maeneo yao na kuamua yagawanywe katika vitongoji vingapi na vya
watu wangapi - kwa kila kitongoji.
• Baada ya kuamua idadi ya vitongoji na ukubwa wake Halmashauri ya kijiji itayapeleka
mapendekezo kwenye Halmashauri ya Wilaya kuthibitishwa
• Mkurugenzi atayapeleka maoni na mapendekezo hayo kwenye Halmashauri yake ili maamuzi
yafanywe na baraza la madiwani.
• Muundo wa Utawala katika Ngazi ya Kitongoji
• Mkutano Mkuu wa Kitongoji (unaowajumuisha wakazi wote wa Kitongoji wenye umri usiopungua
miaka 18 na wenye akili timamu;
• Mwenyekiti wa Kitongoji;
• Kamati ya Kitongoji.
Majukumu na Kazi za Mkutano Mkuu wa Kitongoji
• Kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kitongoji zitakazowasilishwa
na Mwenyekiti wa Kitongoji;
• Kujadili Taarifa ya utekelezaji wa mikakati ya kupambana na umaskini;
• Kujadili hali ya ulinzi na usalama na maendeleo katika eneo la kitongoji;
MADA YA KWANZA
5
10
9
8
7
6
5
4
3
2
11
12
13
• Kuweka mikakati ya kupambana na ugonjwa hatari wa UKIMWI;
• Kupokea maelekezo kutoka kwa Halmashauri ya Kijiji na kuweka mkakati wa utekelezaji wake
katika kitongoji;
Kazi za Mwenyekiti wa Kitongoji
• Kutunza rejesta ya wakazi wa kitongoji na nyaraka nyingine muhimu zinazohusu maendeleo ya
kitongoji kwa jumla ikiwa ni pamoja na kumbukumbu za vizazi na vifo;
• Kusimamia shughuli za ulinzi na usalama wa watu na mali zao waishio katika eneo lote la
kitongoji;
• Kuhamasisha ulipaji wa kodi na ushuru mbalimbali, kama utakavyoamuliwa na kuwekwa mara
kwa mara na Halmashauri ya Kijiji na Wilaya. jJukumu hilo pia linatekelezwa na Mwenyekiti wa
kitongoji kilicho kwenye eneo la Mji, Manispaa au Jiji;
• Kusimamia katika eneo lake suala zima la Hifadhi ya mazingira hususan vyanzo vya maji n.k.;
• Kusimamia suala la afya katika eneo lake ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa kampeni za afya za
Kitaifa, Kimkoa au Kiwilaya dhidi ya magonjwa ya kuambukiza, na hasa, vita dhidi ya UKIMWI;
• Kufuatilia hali ya lishe na uchumi wa wakazi wa kitongoji;
• Kufuatilia na kuhakikisha kuwa kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anapatiwa nafasi na
kushirikiana na viongozi wa shule katika udhbiti utoro shuleni;
• Kuhamasisha elimu ya watu wazima;
• Kusimamia na kuwahamasisha wakazi wa kitongoji katika kutekeleza shughuli za kujitegemea;
• Kusuluhisha migogoro midogo midogo isiyostahili kushughulikiwa na Mabaraza ya Kata au
Mahakama;
• Kuwakilisha kitongoji katika Serikali ya Kijiji;
• Kuwaongoza na kuwahamasisha wakazi wa kitongoji washiriki katika sherehe za Taifa na
mikutano ya hadhara itakayoandaliwa na kuitwa na Serikali au Halmashauri;
• Kutekeleza kazi nyingine atakazopangiwa na Halmashauri ya Kijiji na Wilaya. Jukumu hili pia
linatekelezwa kwa vitongoji vilivyo kwenye Halmashauri za Miji, Manispaa au Jiji.
[b] Mamlaka ya Serikali ya Kijiji
Serikali ya Kijiji huundwa katika kijiji kilichoandikishwa kwa mujibu wa kifungu Na.22 cha sheria
Na.7 ya Sheria za Serikali za Mitaa. Idadi ya kaya katika kijiji siyo chini ya 250 na wakazi wake
hawapungui 1250.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
6
Uandikishaji wa kijiji
Chini ya sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Namba 7 ya mwaka 1982 Serikali ya Kijiji
huandikishwa na Msajili wa Kijiji ambaye huteuliwa na Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.
Ili kuandikisha kijiji taarifa zifuatazo lazima ziwasilishwe kwa Msajili wa vijiji ili kutoa maamuzi.
Taarifa hizi ni
• Mipaka ya eneo la kijiji
• Idadi ya kaya katika kijiji
• Idadi ya watu wanaoweza kufanya kazi
• Kazi au shughuli kuu katika kijiji
• Ukubwa wa eneo la ardhi ya kijiji
• Rasilimali kuu na huduma muhimu katika kijiji
Baada ya kujiridhisha na taarifa hizo Msajili wa vijiji hutoa hati ya kuandikishwa kwa kijiji husika.
MFANO WA CHETI CHA KUANDIKISHA KIJIJI...
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
HATI YA KUANDIKISHWA KWA KIJIJI
(SHERIA NA 7 YA MWAKA 1982)
Imetolewa chini ya kifungu Na. 22
na..........................................................................................................................................
Ninathibitisha rasmi kwa hati hii kwamba kijiji kijulikanacho
kama………...........................................……kilicho katika Wilaya ya
…….........................................……Mkoa wa ……..................……….leo kimeandikishwa kama kijiji kwa
mujibu wa kifungu Na. 22 cha sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Na 7 ya mwaka 1982.
Hati hii imetolewa na kutiwa sahihi na mimi……....................................……..leo
Tarehe……….Mwezi…………..Mwaka…………….
…………………...........……………
Msajili wa Vijiji
MADA YA KWANZA
7
10
9
8
7
6
5
4
3
2
11
12
13
Muundo wa Serikali ya Kijiji
Mkutano Mkuu wa Kijiji ni chombo cha utawala kinachoundwa na wajumbe wafuatao:-
• Wakazi wote wa Kijiji wenye umri usiopungua miaka 18 na wenye akili timamu;
• Mwenyekiti wa Kijiji;
• Wenyeviti wa Vitongoji vyote kijijini;
• Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji ambao ni kati ya 15 na 25;
• Afisa Mtendaji wa Kijiji – Katibu.
Kwa mujibu wa kifungu cha 103 (2) cha sheria namba 7 ya mwaka 1982. Mkutano Mkuu wa Kijiji
huitishwa mara mmoja kila baada ya miezi mitatu.
Kwa mujibu wa kifungu cha 141 cha sheria namba 7 ya mwaka 1982, Mkutano Mkuu ndiyo
Mamlaka yenye madaraka ya juu kabisa kuhusu maamuzi yote ya sera na maendeleo kijijini na
ndiyo yenye wajibu wa kuwachagua na kuwaondoa madarakani wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji
ikiwa ni pamoja na kutekeleza majukumu mbalimbali iliyopewa kwa mujibu wa sheria hii na nyingine.
Wajibu na Majukumu ya Mkutano Mkuu wa Kijiji
• Kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali;
• Kupokea na kujadili mapato na matumizi ya fedha;
• Kupokea na kujadili taarifa za makusanyo ya fedha yakiwamo ya ushuru, ada na mapato
mengine yanayopaswa kukusanywa ndani ya kijiji kwa mujibu wa sheria;
• Kupokea na kujadili taarifa za watu walioomba kupewa ardhi;
• Kupokea na kujadili mapendekezo yatakayotolewa na Halmashauri ya Kijiji au Kitongoji;
• Kupokea maagizo (kama yapo) kutoka ngazi za juu za Serikali na kuweka mkakati wa utekelezaji;
• Kufanya maamuzi yanayozingatia demokrasia;
• Kuchagua Mwenyekiti na Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji;
• Kujadili na kupitisha bajeti na mipango ya maendeleo ya Kijiji;
• Kuidhinisha utungwaji wa sheria ndogo kabla ya kupelekwa kwenye Halmashauri ya wilaya kwa
ajili ya kupitishwa kwa manufaa ya kijiji.
Majukumu ya Mwenyekiti wa Kijiji
• Atakuwa ndiye Mkuu wa Serikali ya Kijiji;
• Atakuwa na wajibu wa kuitisha na kuongoza mikutano yote ya Halmashauri ya kijiji, pamoja na
Mikutano Mikuu ya Kijiji. Lakini endapo Mwenyekiti hayupo katika mkutano wowote, wajumbe
wa mkutano unaohusika wanaweza kuchagua Mwenyekiti wa muda wa mkutano huo;
• Atakuwa mwakilishi wa kijiji kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata;
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
8
• Atawahudumia kwa usawa wanakijiji wote, bila kujali tofauti za Kisiasa, Kijinsia au za Kidini;
• Atakuwa mfano wa uongozi bora na utendaji bora wa kazi, kwa kuwa na shughuli zake
mwenyewe za kujitegemea, ambazo zaweza kuigwa na wanakijiji wenzake.
Halmashauri ya Kijiji
i. Muundo wa Halmashauri ya Kijiji
Halmashauri ya Kijiji huundwa kwenye kijiji kilichoandikishwa kwa mujibu wa Sheria za Serikali za
Mitaa namba 7 ya mwaka 1982. Halmashauri huundwa na wajumbe wasiopungua kumi na tano
na wasiozidi ishirini na tano kama ifuatavyo:-
• Mwenyekiti ambaye huchaguliwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji;
• Wenyeviti wa vitongoji vilivyoko katika eneo la kijiji;
• Wajumbe wanaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji wakiwemo wanawake ambao idadi
yao si chini ya robo ya wajumbe wote wa Halmashauri ya Kijiji;
• Afisa Mtendaji wa Kijiji ambaye atakuwa Katibu wa Halmashauri ya Kijiji.
Halmashauri ya kijiji inatakiwa kukutana mara moja kila mwezi, lakini Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Kijiji anaweza kuitisha mkutano wa dharura wa Halmashauri ya Kijiji wakati wowote kama
ataona inafaa.
ii. Majukumu ya Halmashauri ya Kijiji
• Kuhakikisha ulinzi, amani, utulivu na utawala bora kijijini;
• Kuhakikisha maendeleo ya uchumi na Ustawi wa Jamii kijijini;
• Kupokea na kujadili taarifa kutoka kwenye Kamati mbalimbali za Kudumu za Halmashauri ya
Kijiji;
• Kupokea na kujadili taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za Kijiji ikiwa ni pamoja na
taarifa za makusanyo ya fedha za Halmashauri ya Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji katika Kijiji
hicho;
• Kupokea taarifa ya mambo yaliyojadiliwa katika mikutano ya Vitongoji mbalimbali vya kijiji hicho;
kutokana na kumbukumbu za mikutano hiyo zilizowasilishwa kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji;
• Kujadili maombi ya watu wanaoomba ardhi katika Kijiji;
• Kuzungumzia mambo mengine yoyote ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya Kata na
Halmashauri ya Wilaya;
• Kubuni na kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa madhumuni ya kuinua hali ya
maisha ya wanakijiji;
MADA YA KWANZA
9
10
9
8
7
6
5
4
3
2
11
12
13
• Kupendekeza sheria ndogo zitakazopitishwa na Mkutano Mkuu wa kijiji kwa manufaa ya
kijiji, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria;
• Kuhakikisha kuwa kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi kwa juhudi na
maarifa;
• Kuhakikisha umaskini Kijijini unafutika;
• Kufanya mambo yoyote kama yatakavyoelekezwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji.
iii. Muundo wa Kamati za Halmashauri ya Kijiji
Halmashauri ya Kijiji inapaswa kuunda kamati zifuatazo:-
• Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango;
• Kamati ya Huduma za Jamii na shughuli za kujitegemea;
• Kamati ya Ulinzi na Usalama.
Halmashauri ya Kijiji inaweza kuunda kamati nyingine kwa kuzingatia mahitaji na vipaumbele vya kijiji.
iv. Majukumu na Kazi za Kamati za Halmashauri za Vijiji
(a) Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango
Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango itakuwa na majukumu na kazi zifuatazo:-
• Kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo kijijini;
• Kupendekeza matumizi bora ya ardhi ya kijiji kwa shughuli mbalimbali za kilimo, ufugaji,
ujenzi, viwanja vya michezo n.k.;
• Kuunganisha mipango yote ambayo itatokana na Kamati nyingine Kijijini, au Mipango ya
Kiwilaya au Kitaifa ambayo inatekelezwa Kijijini hapo;
• Kutayarisha makadirio ya mapato na matumizi kwa miradi na shughuli nyingine zote
zinazohitaji matumizi ya fedha za kijiji;
• Kuweka hesabu sahihi za shughuli zote kijijini, na kuhakikisha kuwa fedha za kijiji
zinatumika kihalali na zile ambazo hazijatumika zinawekwa benki katika akaunti ya Kijiji;
• Kusimamia ukusanyaji wa kodi na ushuru wowote uliowekwa na Halmashauri ya Wilaya au
na Serikali ya Kijiji katika eneo la kijiji;
• Kutafuta njia mbalimbali za kuongeza mapato ya kijiji kama inavyoruhusiwa na sheria ya
Fedha za Serikali za Mitaa Namba 9/1982;
• Kuhakikisha kuwa kanuni za kilimo bora, na malengo ya kilimo, ufugaji bora na uvuvi bora
zinafuatwa na kutekelezwa; yaani:-
–– Kutayarisha mashamba mapema;
–– Kuchagua mbegu bora na kuweka mbolea mashambani;
–– Kupanda mapema kwa kufuata mazingira na hali ya hewa;
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
10
–– Kuhifadhi mazao ghalani;
–– Kusafisha mashamba baada ya mavuno;
–– Uvuvi bora unaohakikisha hifadhi ya mazalio ya samaki na mazingira.
• Kuhakikisha kila mwanakijiji anajishughulisha na kupiga vita umaskini.
(b) Kamati ya Huduma za Jamii na Shughuli za Kujitegemea
Kamati ya Huduma za Jamii na Shughuli za Kujitegemea itakuwa na majukumu na kazi
zifuatazo:-
• Kuona kuwa watoto waliofikia umri wa kwenda shule wanaandikishwa na kuhudhuria shule
hadi kumaliza elimu ya msingi.
• Kuona kuwa watu wazima wasiojua kusoma na kuandika wanahudhuria Kisomo cha Watu
Wazima.
• Kuhamasisha ujenzi na ukarabati wa madarasa, visima zahanati, majosho n.k na
kushirikisha wataalam mbalimbali wanaoshughulika na mambo haya.
• Kuhamasisha wanakijiji kuhudhuria kwenye mikutano yote ya kijiji iliyotamkwa katika
sheria.
• Kusimamia utekelezaji wa masharti ya kuzuia mlipuko wa magonjwa pamoja na masharti
ya kuweka mazingira ya kijiji katika hali ya usafi.
• Kuweka taratibu zinazofaa za utekelezaji wa kazi za kujitegemea.
• Kuwahamasisha wakazi wa kijiji kuhudhuria Sherehe za Taifa, Mikutano ya hadhara,
inayoitwa na Serikali, Halmashauri, na viongozi mbalimbali wa kiserikali.
• Majukumu ya Kiafya.
–– Kuchukua hatua za kubaini magonjwa sugu kijijini na kuchukua hatua za kujenga
zahanati/kliniki kama huduma kwa wakazi;
–– Kuchukua hatua za kinga kuzuia maradhi hasa UKIMWI na kutoa ushauri wa watu
ambao wameathirika na ugonjwa huu hatari;
–– Kuweka mazingira ya kijiji katika hali ya usafi;
–– Kuchukua hatua za kutunza mazingira ili kuboresha afya;
–– Kuchukua hatua za kuboresha tija ya chakula na kutumia vyakula vyenye lishe ili
kuboresha afya ya watu wazima na watoto;
–– Kuhamasisha usafi wa mwili na mavazi kwa wanakijiji;
–– Kuchukua hatua za kuelimisha na kuhimiza uzazi wa mpango kwa wanakijiji;
–– Kuchukua hatua nyingine zozote za kuboresha afya kijijini kwa kuzingatia mazingira na
haja za wakati;
–– Majukumu ya Kiujenzi na Miundombinu
MADA YA KWANZA
11
10
9
8
7
6
5
4
3
2
11
12
13
–– Kushughulikia ujenzi wa nyumba bora;
–– Kuwaelimisha na kuwashirikisha wanakijiji katika ujenzi wa nyumba bora;
–– Kusaidia kutafuta vifaa vya ujenzi;
–– Kujenga mabwawa/visima kufuatana na uwezo na mahitaji ya wanakijiji;
–– Kubuni mikakati na mbinu za ujenzi wa nyumba kijijini;
–– Kutafuta ufundi mbalimbali wa viwanda vidogovidogo;
–– Kuona kuwa nyumba za wanakijiji zinajengwa mahali pazuri, mathalani pasipoweza
kuathiriwa na mafuriko, upepo mkali, vumbi na kadhalika;
–– Kuona kuwa nyumba zinajengwa kwa kuzingatia kanuni za afya na ujenzi;
–– Kutayarisha makisio ya kupata fedhana kuwasilisha katika Kamati ya Mipango na
Fedha ili kujadiliwa;
–– Kuweka kumbukumbu ya wanakijiji wenye ujuzi wa kujenga, mfano waseremala,
mafundi uashi na kadhalika na kuwashirikisha katika kazi za ujenzi kijijini;
–– Kutafuta mipango mbalimbali ya usafiri na uchukuzi wa mazao na bidhaa zinazoingia
au kutoka kijijini;
–– Kushirikiana na vijiji vingine vya jirani ili kuanzisha ushirika wa aina mbalimbali, mfano
uchukuzi, kuchimba visima na kadhalika;
–– Kuhakikisha kuwa barabara zinazounganisha kijiji na vijiji jirani zinapitika wakati wote;
–– Kuwashirikisha wanakijiji katika ujenzi na ukarabati wa barabara.
(c) Kamati ya Ulinzi na Usalama
Kamati ya ulinzi na usalama itakuwa na majukumu na kazi zifuatazo:-
• Kuhakikisha mikakati ya ulinzi na usalama inawekwa ili kulinda wananchi na mali zao;
• Kuona kuwa mafunzo ya Mgambo na Sungusungu yanaendeshwa, pamoja na kuhakikisha
kuwa Sungusungu na Mgambo wanaendesha shughuli za Ulinzi na usalama katika kijiji kwa
kuzingatia sheria za nchi;
• Kushirikiana na Kamanda wa Ulinzi na Usalama wa Wilaya katika kupeana taarifa
mbalimbali za uhalifu na nyingine zenye manufaa kwa usalama wa Taifa;
• Kuhakikisha kuwa hakuna magendo au biashara ya magendo inayofanyika katika kijiji,
• Kuhakikisha wananchi wanashiriki kwenye ulinzi shirikishi ;
• Kudhibiti madawa ya kulevya kwa kuchukua hatua mbalimbali kama kuzuia kilimo cha
bangi n.k. katika kijiji.
Kamati zote za kudumu za Halmashauri ya Kijiji zinatakiwa kukutana kabla ya kila mkutano wa
Halmashauri ya Kijiji, ili kila Kamati iweze kutoa taarifa yake katika mkutano huo wa Halmashauri ya Kijiji.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
12
[c] Ngazi ya Kata
Kamati ya Maendeleo ya Kata
Kwa mujibu wa kifungu cha 30 (2) cha sheria namba 7 ya mwaka 1982 kama ilivyorekebishwa na
Sheria Namba 6 ya mwaka 1999, uanzishaji wa Kata huanza kwa Halmashauri ya wilaya kutuma
maombi kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ambaye ndiye mwenye madaraka ya
kuanzisha Kata.
Kifungu Namba 31 cha Sheria Namba 7 ya mwaka 1982 kama ilivyorekebishwa na Sheria Namba 6
ya mwaka 1999 inaanzisha Kamati ya Maendeleo ya Kata kwa kila Kata.
Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kata ni wafuatao:-
• Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata ambaye ni Diwani anayewakilisha Kata;
• Wenyeviti wa Vijiji vyote katika Kata;
• Diwani wa Viti maalum mkazi wa Kata husika;
• Watu walioteuliwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata kutoka Mashirika yasiyo ya Serikali na
vikundi vya kijamii (lakini hawaruhusiwi kupiga kura);
• Afisa Mtendaji wa Kata – Katibu.
Majukumu ya Kamati ya Maendeleo ya Kata
Kwa mujibu wa kifungu cha 32 (1) cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Namba. 7 ya
mwaka 1982 kama ilivyorekebishwa na Sheria Namba 6 ya mwaka 1999 na kifungu 16(1) cha Sheria
ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Na 8 ya mwaka 1982 kama ilivyorekebishwa na Sheria Namba
6 ya mwaka 1999, Majukumu ya Kamati za Maendeleo za Kata ni kama ifuatavyo:-
• Kukuza uanzishaji na uendelezaji wa biashara na shughuli za ushirika katika Kata;
• Uanzishaji wa kazi au shughuli yenye lengo la kuleta ustawi wa jamii wa wakazi katika Kata;
• Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa miradi na programu za Halmashauri ya Wilaya katika Kata;
• Kupanga na kuratibu shughuli na kutoa msaada na ushauri kwa wakazi walio katika Kata ambao
wanajihusisha na shughuli yoyote au biashara (halali ya aina yoyote);
• Kupendekeza kwa Halmashauri ya Kijiji au Wilaya utungaji wa sheria ndogo;
• Kufuatilia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri;
• Kuanzisha na kuendeleza ushirikishwaji wa wananchi katika Maendeleo ya Kata;
• Kusimamia mifuko yote ya fedha iliyoanzishwa na kukabidhiwa kwa Kata;
• Kusimamia maafa na shughuli zinazohusu mazingira; na
• Kuendeleza masuala ya jinsia.
MADA YA KWANZA
13
10
9
8
7
6
5
4
3
2
11
12
13
Kazi na Wajibu wa Afisa Mtendaji wa Kata
Kutokana na Waraka Wa Maendeleo ya Utumishi wa Serikali za Mitaa namba 29 wa Mwaka 2003,
pamoja na sheria iliyofanyia marekebisho Sheria za Serikali za Mitaa namba 13 ya mwaka 2006
kazi za Afisa Mtendaji wa Kata ni:_
• Kumwakilisha na kumsaidia Mkurugenzi wa Halmashauri katika kusimamia shughuli za
maendeleo katika kata;
• Kuandaa mpango kazi kuhusu kazi na wajibu wake na kuuwasilisha kwa Mkurugenzi wa
Halmshauri;
• Kuwasimamia maafisa watendaji wa Vijiji katika kutekeleza majukumu yao ipasavyo;
• Kushiriki na kushauri wakati wa uandaaji wa mipango ya maendeleo ya kata, kuratibu mipango
kazi na taarifa za utekelezaji za Watendaji wa Vijiji katika kata na kuiwasilisha kwa Afisa Tarafa na
kwa Mkurugenzi wa Halmashauri;
• Kushiriki, kushauri na kuwasilisha kwenye kamati ya maendeleo ya kata taarifa kuhusu
utekelezaji wa shughuli ndani ya Kata;
• Kuwa katibu wa kamati ya maendeleo ya kata;
• Kusimamia sheria ndogo zote katika kata;
• Kuhimiza uanzishaji na uendelezaji wa vyama vya ushirika na ujasiriamali na shughuli za ndani ya
kata;
• Kupanga na kuratibu shughuli na kutoa msaada na ushauri kwa wakazi katika kata;
• Kuandaa na kuwasilisha kwa Halmashauri ya kijiji na Halmashauri ya wilaya mapendekezo ya
kutunga sheria ndogo kuhusiana na shughuli za Kata;
• Kusimamia ukusanyaji wa mapato;
• Kuanzisha na kuimarisha maendeleo shirikishi katika kata;
• Kudhibiti majanga ndani ya kata;
• Kuimarisha masuala ya jinsia ndani ya kata;
• Kuwasimamia maafisa watendaji wa Mitaa katika kutekeleza majukumu yao;
• Kuwa mjumbe wa kamati ya maendeleo ya wilaya (DCC);
• Atakuwa kiungo cha uongozi wa Idara zote katika Kata na atashughulikia masuala yote ya
uendeshaji katika Kata chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, Mji,
Manispaa au Jiji;
• Mlinzi wa Amani katika Kata yake;
• Mratibu na Msimamizi, Mpangaji wa utekelezaji wa mipango ya Maendeleo ya Kata;
• Msimamizi wa utekelezaji wa sheria ndogo za Halmashauri katika Kata yake;
• Atafanya kazi zingine zote kama atakavyoagizwa na Mkurugenzi wa Halmashauri.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
14
Kazi na Wajibu wa Diwani
• Kuwakilisha wananchi wote wa Kata yake katika Halmashauri;
• Kusikiliza kero za wananchi na kuzifikisha panapohusika kwa utatuzi;
• Kusikiliza vipaumbele vya wananchi na kuvifikisha mbele ya Halmashauri ili vijumuishwe katika
mipango ya Halmashauri;
• Kuwa kiungo kati ya Halmashauri na ngazi za chini za Serikali za Mitaa (Kata, Vijiji, Mitaa au
Vitongoji);
• Kuhamasisha na kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kulipa kodi, ushuru na mapato
mengine ya Halmashauri ili waweze kupatiwa huduma bora;
• Kufuatilia matumizi ya fedha za Halmashauri kwa lengo la kujiridhisha kuwa matumizi ya
fedha hizo hayavuki bajeti iliyoidhinishwa na kwamba fedha zote zimetumika kwa madhumuni
yaliyowekwa;
• Kuhakikisha kwamba watumishi wote walioko katika eneo la Kata yake wanafanya kazi zao kwa
uadilifu na ufanisi na endapo hauridhishi atatakiwa kutoa taarifa kwenye Kamati husika au kwa
Mkurugenzi wa Halmashauri yake;
• Kuhamasisha na kuelimisha wananchi kuhusu vita dhidi ya umaskini, rushwa na janga la
UKIMWI;
• Kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa maamuzi, mipango na utoaji wa huduma katika Kata yake na
kutoa taarifa kwenye vikao vya Halmashauri au Kamati za Halmashauri endapo kuna kasoro za
msingi za utekelezaji
[d] Ngazi ya Tarafa
Kazi za Afisa Tarafa
Katika kurahisisha mawasiliano Afisa Tarafa ni kiungo kati ya ngazi ya Kata na Halmashauri
kwa upande mmoja na Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kwa upande mwingine, majukumu ya
Afisa Tarafa yameainishwa katika Mwongozo wa Uwajibikaji wa Maafisa Tarafa katika Wilaya
na Halmashauri za Serikali za Mitaa wa tarehe 18 Desemba, 2003 pamoja na Sheria iliyofanyia
marekebisho Sheria za Serikali za Mitaa namba 13 ya mwaka 2006 Majukumu ya Afisa Tarafa ni
kama ifuatavyo:-
• Kumwakilisha Mkuu wa Wilaya katika kutekeleza shughuli za serikali katika Tarafa;
• Kuandaa na kusimamia taarifa au habari kuhusu ulinzi na usalama katika kata zilizomo ndani ya
Tarafa na kuziwasilisha kwa Mkuu wa wilaya na kwa Mkurugenzi;
• Kusimamia utekelezaji wa maamuzi na Sera za Serikali kuu ndani ya Tarafa;
• Kuelimisha na kuwahimiza wakazi ndani ya Tarafa kushiriki katika shughuli za maendeleo;
• Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na wakazi ndani ya Tarafa;
MADA YA KWANZA
15
10
9
8
7
6
5
4
3
2
11
12
13
• Kushughulikia malalamiko ya wakazi ndani ya Tarafa;
• Kuandaa taarifa ya utekelezaji ya Tarafa na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya;
• Kuratibu shughuli zote zinazohusu majanga na dharura ndani ya Tarafa;
• Kushiriki kama mjumbe kwenye vikao vya Kamati ya Maendeleo ya Wilaya DCC;
• Kumwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri na Katibu Tawala wa Wilaya katika kusimamia
maendeleo ya eneo lake;
• Kuandaa ratiba ya kazi yake ili kuonyesha majukumu na muda wa utekelezaji ili kuondoa
mgongano wa majukumu unaoweza kutokea kutokana na maagizo mbalimbali ya ngazi za juu na
kuziwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya/Katibu Tawala wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji;
• Kusimamia utendaji wa shughuli za Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji katika eneo lake;
• Kushiriki na kutoa ushauri kuhusu Upangaji wa Mipango ya Maendeleo katika eneo lake;
• Kuratibu ratiba ya kazi za Maafisa Watendaji Kata wa eneo lake na kuiwasilisha kwa Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji na kwa Mkuu wa Wilaya/Katibu Tawala wa Wilaya;
• Kuhudhuria Mikutano ya Baraza la Madiwani la Halmashauri na kutoa ushauri pamoja na taarifa
za utekelezaji wa shughuli zilizofanyika katika eneo lake;
• Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake kama zitakavyopokelewa
kutoka kwa Watendaji wa Kata na Vijiji na kuziwasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na
nakala kwa Mkuu wa Wilaya/Katibu Tawala wa Wilaya;
• Kuwa Katibu wa vikao vitakavyowahusisha Watendaji Kata, Madiwani na Wataalam waliopo
katika eneo lake;
• Kusimamia utekelezaji wa sheria ndogo za Halmashauri;
• Kufanya kazi nyingine kama atakavyoagizwa na Mkuu wa Wilaya.
[e] Muundo wa Mji Mdogo
Kifungu namba 45 cha Sheria namba 7 ya mwaka 1982 kama ilivyorekebishwa na Sheria Namba 6
ya mwaka 1999 vinabainisha muundo wa Mamlaka ya Mji Mdogo kama ifuatavyo:-
• Mwenyekiti ambaye atachaguliwa miongoni mwa wenyeviti wa vitongoji;
• Wenyeviti wa vitongoji vilivyomo katika eneo la Mamlaka;
• Wajumbe walioteuliwa na Halmashauri ya Wilaya wasiozidi watatu;
• Mbunge anayewakilisha jimbo ambamo Mamlaka hiyo imo;
• Wajumbe viti maalum ambao hawatapungua robo ya wajumbe waliotajwa hapo juu.
• Katibu wa Mamlaka ya Mji Mdogo ambaye ambaye ni Afisa Mtendaji wa Mji Mdogo, lakini
hatakuwa na sifa ya kupiga kura.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
16
Kamati za kudumu za mamlaka ya Mji Mdogo
Halmashauri ya Mji Mdogo huwa na kamati za kudumu zifuatazo;
• Kamati ya kudumu ya fedha, utawala na mipango Miji;
• Kamati ya kudumu ya Elimu, afya na Maji;
• Kamati ya Kudumu ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira.
Majukumu ya Mamlaka ya Mji Mdogo
Mamlaka ya Mji Mdogo utakuwa na majukumu yafuatayo;
• Kudumisha na kuimarisha amani, utulivu na utawala bora ndani ya himaya yake, (eneo lake);
• Kuendeleza uchumi endelevu na ushauri wa jamii kwa wakazi wote walio ndani ya eneo lake;
• Kuanzisha mipango miji kwa maendeleo ya eneo lake;
• Kuhamasisha jamii kupambana dhidi ya maadui umaskini, maradhi na ujinga;
• Kutunga sheria ndogo,
• Kutoza kodi;
• Kutoza ushuru na gharama mbalimbali;
• Kupendekeza makadirio ya mapato na matumizi yake katika Halmashauri ya Wilaya;
• Kukopa fedha.
[f] Muundo wa Halmashauri ya Wilaya
Kwa mujibu wa kifungu cha 35 (1) cha sheria namba 7 ya mwaka 1982 kama ilivyorekebishwa na
Sheria namba 6 ya mwaka 1999 vinafafanua muundo wa Halmashauri ya Wilaya ni kama ifuatavyo:-
• Mwenyekiti ambaye atachaguliwa miongoni mwa Madiwani;
• Diwani kutoka kila Kata iliyomo katika Halmashauri;
• Madiwani viti maalum vya wanawake (wasiopungua theluthi moja ya wajumbe wote);
• Mbunge wa kuchaguliwa;
• Mbunge Viti maalum;
• Mbunge wa kuteuliwa na Rais;
• Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya - Katibu.
MADA YA KWANZA
17
10
9
8
7
6
5
4
3
2
11
12
13
HALMASHAURI ZA MIJI
[a] Ngazi ya Mtaa
Mtaa ni sehemu ya Kata katika eneo la Mamlaka za Serikali za Mitaa
Mijini. Kila Mtaa una kamati yenye Wajumbe 6 -
Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 14A(1) cha Sheria Namba 8 ya mwaka 1982.
Muundo wa Utawala katika Ngazi ya Mtaa
• Mkutano Mkuu wa Mtaa (unaowajumuisha wakazi wote wa Mtaa) wenye umri usiopungua miaka
18 na mwenye akili timamu;
• Mwenyekiti wa Mtaa;
• Kamati ya Mtaa.
Wajibu na Majukumu ya Mkutano Mkuu wa Mtaa
Wajibu wa Mkutano mkuu wa Mtaa ni kupokea na kujadili taarifa kuhusu:
• Miradi inayoendeshwa katika eneo la Mtaa na maendeleo yake;
• Hali ya usalama na ulinzi katika eneo la Mtaa;
• Matatizo ya huduma za Jamii na Hatua zilizochukuliwa;
• Maamuzi ya Kamati ya Maendeleo ya Kata au ya Halmashauri ya Mji, Manispaa au Jiji kupitia
Kamati ya Maendeleo ya Kata yanayoihusu Mtaa;
• Maamuzi ya Kamati ya Mtaa na utekelezaji wake;
• Utekelezaji wa majukumu na kazi za Kamati ya Mtaa;
• Suala lingine lolote linalohusu utoaji wa huduma na maendeleo ya kijamii na kiuchumi;
• Kumwondoa madarakani Mwenyekiti wa Mtaa inapodhihirika kwamba ameshindwa kumudu
madaraka yake. Taratibu za kumwondoa madarakani Mwenyekiti wa Mtaa zimefafanuliwa katika
kifungu cha 14 (4) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Na. 8 ya mwaka 1982.
Majukumu ya Mwenyekiti wa Mtaa
Wajibu wa Mwenyekiti wa Mtaa ni pamoja na:-
• Kuwa Mwenyekiti wa Mikutano yote ya Kamati ya Mtaa na Mkutano Mkuu wa Mtaa;
• Kusuluhisha migogoro midogomidogo ambayo haistahili kuitisha mkutano wa Kamati ya Mtaa au
kupelekwa kwenye Baraza la Kata au Mahakama;
• Kuwa msemaji wa Mtaa;
• Kuwaongoza na kuwahimiza Wakazi wa Mtaa washiriki shughuli za maendeleo, sherehe za Taifa,
Mikutano ya hadhara itakayoandaliwa na Mtaa, Halmashauri ya Mji Manispaa au Jiji na Serikali;
• Kuwakilisha Mtaa kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata;
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
18
• Kutekeleza kazi atakazopewa na Kamati ya Mtaa na Mkutano wa Mtaa na Kamati ya Maendeleo
ya Kata;
• Kusimamia utekelezaji wa kazi na Majukumu ya Kamati ya Mtaa;
• Kusimamia utunzaji wa rejesta ya wakazi wote wa Mtaa.
Muundo wa Kamati ya Mtaa
Muundo wa Kamati ya Mtaa ni kama ifuatavyo:-
• Mwenyekiti wa Mtaa ambaye atachaguliwa na Mkutano Mkuu wa Mtaa;
• Wajumbe wa Mtaa wasiozidi sita watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Mtaa ambao kati yao
wawili wawe wanawake.
Majukumu na Kazi za Kamati ya Mtaa
Majukumu na kazi za Kamati ya Mtaa ni pamoja na:-
• Kutekeleza sera na maamuzi ya Halmashauri ya Mji, Manispaa au Jiji;
• Kutoa ushauri na mapendekezo kuhusu mipango ya maendeleo na shughuli za Mtaa kwa
Halmashauri ya Mji, Manispaa au Jiji;kupitia kwenye kata.
• Kuishauri Kamati ya Maendeleo ya Kata kuhusu masuala ya ulinzi na usalama katika eneo la
Mtaa;
• Kuweka kumbukumbu sahihi ya Wakazi wa Mtaa;
• Kutekeleza maamuzi ya Kamati ya Maendeleo ya Kata;
• Kusimamia utunzaji wa rejesta ya Wakazi wote wa Mtaa na habari nyingine muhimu zinazohusu
Maendeleo ya Mtaa kwa jumla ikiwa ni pamoja na kumbukumbu za vizazi na vifo;
• Kusimamia ulinzi na usalama wa watu na mali zao katika eneo la Mtaa;
• Kusuluhisha migogoro midogomidogo isiyostahili kushughulikiwa na Baraza la Kata au
Mahakama;
• Kuhamasisha ulipaji wa kodi na ushuru mbalimbali kama zitakavyoamuliwa na kuwekwa na
Halmashauri ya Mji, Manispaa au Jiji na zinazopaswa kulipwa Serikali Kuu;
• Kusimamia suala zima la afya katika eneo lake ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa kampeni za afya
za kitaifa, kimkoa au kiwilaya dhidi ya magonjwa ya kuambukiza;
• Kusimamia uwekaji wa eneo la Mtaa katika hali ya usafi;
• Kushirikiana na Halmashauri ya Mji, Manispaa au Jiji kudhibiti bughudha;
• Kufuatilia na kuhakikisha kuwa kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anapata nafasi ya
kwenda shule na kushirikiana na viongozi wa shule katika kudhibiti utoro;
• Kuhamasisha elimu ya watu wazima;
• Kusimamia na kuhamasisha wakazi wa Mtaa katika shughuli za kujitegemea;
MADA YA KWANZA
19
10
9
8
7
6
5
4
3
2
11
12
13
• Kuwaongoza na kuwahamasisha wakazi wa Mtaa washiriki katika sherehe za Taifa na mikutano
ya hadhara.
[b] Kamati ya Maendeleo ya Kata
Muundo wa Kamati ya Maendeleo ya Kata Mjini _
• Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata ambaye ni Diwani anayewakilisha Kata;
• Wenyeviti wa mitaa na vijiji katika Kata;
• Diwani wa Viti maalum mkazi wa Kata husika;
• Watu walioteuliwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata kutoka Mashirika yasiyo ya Serikali na
vikundi vya kijamii (lakini hawaruhusiwi kupiga kura);
• Afisa Mtendaji wa Kata – Katibu.
[c] Afisa Tarafa
Afisa Tarafa ni kiungo kati ya Kata na Halmashauri ya Mji. Majukumu yake ni kama yalivyofafanuliwa
chini ya kifungu kinachozungumzia majukumu yake katikaHalmashauri za Wilaya.
[d] Afisa Mtendaji wa Kata
Kutokana na Waraka wa Maendeleo ya Utumishi wa Serikali za Mitaa namba 29 wa Mwaka 2003,
pamoja na sheria iliyofanyia marekebisho Sheria za Serikali za Mitaa namba 13 ya mwaka 2006
kazi za Afisa Mtendaji wa Kata ni:_
• Kumwakilisha na kumsaidia Mkurugenzi wa Halmashauri katika kusimamia shughuli za
maendeleo katika kata;
• Kuandaa mpango kazi kuhusu kazi na wajibu wake na kuuwasilisha kwa Mkurugenzi wa
Halmashauri;
• Kusimamia Maafisa Watendaji wa Vijiji wakati wa kutekeleza majukumu yao;
• Kushiriki na kushauri wakati wa uandaaji wa mipango ya maendeleo ya kata;
• Kuratibu mpango kazi na taarifa za utekelezaji za Watendaji wa Vijiji katika kata na kuiwasilisha
kwa Afisa Tarafa na kwa Mkurugenzi wa halmashauri;
• Kuhudhuria, kushauri na kuwasilisha kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata taarifa kuhusu
utekelezaji wa shughuli ndani ya Kata;
• Kuwa katibu wa kamati ya maendeleo ya kata;
• Kusimamia sheria ndogo zote katika kata;
• Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa miradi na mipango ya kata;
• Kuimarisha uanzishaji na uendelezaji wa vyama vya ushirika na ujasiriamali na shughuli za ndani
ya kata;
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
20
• Kupanga na kuratibu shughuli na kutoa msaada na ushauri kwa wakazi katika kata;
• Kuandaa na kuwasilisha kwa Halmashauri ya kijiji na Halmashauri mji, Manispaa na Jiji
mapendekezo ya kutunga sheria ndogo kuhusiana na shughuli za Kata;
• Kusimamia ukusanyaaji wa mapato;
• Kuanzisha na kuimarisha maendeleo shirikishi katika kata;
• Kudhibiti majanga ndani ya kata;
• Kuimarisha masuala ya jinsia ndani ya kata;
• Kuwasimamia maafisa watendaji wa Mitaa katika kutekeleza majukumu yao;
• Kutekeleza majukumu mengine yoyote atakayoelekezwa kufanya na Mkurugenzi wa
Halmashauri;
• Kuwa mjumbe wa kamati ya maendeleo ya wilaya (DCC).
[e] Muundo wa Halmashauri ya Mji
Kwa mujibu wa kifungu namba 19 (1) cha sheria namba 8 ya mwaka 1982, Muundo wa Halmashauri
ya Mji ni kama ifuatavyo:-
• Mwenyekiti atakayechaguliwa miongoni mwa madiwani;
• Diwani wa kuchaguliwa kutoka kila Kata iliyomo katika Halmashauri;
• Madiwani viti maalum vya wanawake wasiopungua theluthi moja ya wajumbe wote;
• Mbunge anayewakilisha jimbo;
• Wabunge wa kuteuliwa na Rais;
• Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji – Katibu.
[f] Muundo wa Halmashauri ya Manispaa
Kifungu namba 19 (2) cha sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) namba 8 ya mwaka 1982
kinafafanua muundo wa Halmashauri ya Manispaa kama ifuatavyo:-
• Meya ambaye huchaguliwa miongoni mwa madiwani;
• Diwani kutoka kila Kata iliyomo katika Halmashauri;
• Madiwani viti maalum vya Wanawake wasiopungua theluthi moja ya wajumbe wote;
• Mbunge wa kuchaguliwa;
• Wabunge wa kuteuliwa na Rais;
• Mkurugenzi wa Manispaa – Katibu.
MADA YA KWANZA
21
10
9
8
7
6
5
4
3
2
11
12
13
[g] Muundo wa Halmashauri ya Jiji
Kifungu namba 19 (4) cha sheria namba 8 ya mwaka 1982 kama ilivyorekebishwa na Sheria Namba
6 ya mwaka 1999 kinafafanua muundo wa Halmashauri ya Jiji la Dar- es -salaam kama ifuatavyo:-
• Meya wa Halmashauri ya Jiji;
• Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji;
• Madiwani watatu wa kuchaguliwa kutoka katika Halmashauri za Manispaa za Kinondoni, Ilala, na
Temeke (mmoja lazima awe ni mwanamke);
• Mameya wote eneo la Halmashauri ya Jiji;
• Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji – Katibu.
• Kwa upande wa Halmashauri ya Jiji la kawaida wajumbe wake kama ifuatavyo:-
• Diwani wa kuchaguliwa kutoka kila Kata iliyomo katika Jiji;
• Madiwani viti maalum vya Wanawake wasiopungua theluthi moja;
• Wabunge wa kuchaguliwa;
• Wabunge wa kuteuliwa na Rais;
• Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji – Katibu.
1.3 MFUMO WA UENDESHAJI WA SERIKALI ZA MITAA
Mfumo wa uendeshaji wa Serikali za Mitaa umegawanyika katika maeneo makuu mawili, yaani
utawala na utendaji. Utawala unaundwa na kuongozwa na viongozi wa kuchaguliwa. Utendaji
unaundwa na kuendeshwa na watumishi wa kuajiriwa.
Aidha, utendaji katika Serikali umegawanyika katika sehemu kuu mbili. Kuna utendaji chini ya
Mamlaka ya Serikali Kuu katika ngazi zake mbalimbali, kwa mfano Taifa (Mkuu wa Nchi/Rais), Mkoa
(Mkuu wa Mkoa), Wilaya (Mkuu wa Wilaya) na Tarafa (Katibu Tarafa). Pia kuna utendaji ambao
uko chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa hususan katika ngazi za Halmashauri (Mkurugenzi wa
Halmashauri), Kata (Afisa Mtendaji wa Kata), Kijiji (Afisa Mtendaji wa Kijiji) na au Mtaa (Afisa Mtendaji
wa Mtaa). Hata hivyo ieleweke kuwa kwa sehemu zote mbili za utendaji kiongozi na Mtendaji Mkuu
ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kitabu hiki cha rejea kitahusika zaidi na ngazi za
Serikali za Mitaa.
Ni vema ieleweke kwamba kimsingi, Kata ni ngazi ya uratibu na siyo ya utawala. Hivyo ndivyo ilivyo
pia kwa ngazi ya kitongoji kijijini na ngazi ya Mtaa mjini. Ingawa viongozi (Wenyeviti wa Vitongoji
na Mitaa) katika ngazi hizi huchaguliwa, wao ni sehemu tu ya utawala katika ngazi ya kijiji au mji na
wala siyo ngazi ya utawala inayojitegemea.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
22
Jukumu kubwa la Kamati ya Maendeleo ya Kata ni kusimamia na kuratibu shughuli zote za
maendeleo ya vijiji au mitaa na kuhakikisha kwamba serikali za vijiji katika Kata husika kwa upande
mwingine, zinatekelezwa ipasavyo. Vielelezo Na. 1A, IB na 1C vinaonesha mfumo mzima wa
uendeshaji (utawala na utendaji) wa Serikali za Mitaa katika ngazi mbalimbali.
KIELELEZO 1A; MFUMO WA UENDESHAJI (UTAWALA NA UTENDAJI) WA SERIKALI
ZA MITAA KATIKA MAMLAKA ZA WILAYA
MADA YA KWANZA
23
10
9
8
7
6
5
4
3
2
11
12
13
Angalizo:
• Kitongoji siyo sehemu halisi ya Utawala bali ni sehemu ya Utawala katika ngazi ya Kijiji.
• Kazi za Mwenyekiti wa Kitongoji ni kumsaidia VEO na Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji.
• Tarafa ni sehemu tu ya utendaji katika ngazi ya Halmashauri na wala siyo ngazi ya utendaji
inayotegemewa katika Serikali za Mitaa.
KIELELEZO 1B: MFUMO WA UENDESHAJI (UTAWALA NA UTENDAJI) WA SERIKALI
ZA MITAA KATIKA HALMASHAURI ZA MIJI
Kisheria bado inaruhusiwa kuwepo Vijiji katika maeneo ya miji. Kwa Halmashauri ambazo zina Vijiji
na Mitaa kwa pamoja angalia Kielelezo IC.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
24
KIELELEZO 1C: MFUMO WA UENDESHAJI (UTAWALA NA UTENDAJI) WA
SERIKALI ZA MITAA KATIKA HALMASHAURI ZA MIJI ZENYE VIJIJI NA MITAA
Sheria za Serikali za Mitaa Na. 7 na 8 za mwaka 1982 sehemu ya IV
inaonesha jinsi uendeshaji wa shughuli za Mamlaka za Serikali za Mitaa unavyopaswa kuwa.
Maelezo kamili kuhusu namna ya kuendesha shughuli hizo yanapatikana katika Kanuni za kudumu
za kila Halmashauri. Kwa kawaida Serikali za Mitaa hufanya maamuzi kwa kupitia kwenye Kamati
zake za Kudumu. Kwa mujibu wa kifungu cha 74 cha Sheria Namba. 7 ya 1982, kifungu cha
42 (1) cha Sheria Namba. 8 ya 1982, Mamlaka za Serikali za Mitaa zina kamati zifuatazo kama
zilivyobainishwa katika Jedwali Na. 1
MADA YA KWANZA
25
10
9
8
7
6
5
4
3
2
11
12
13
Jedwali 1: Kamati za Kudumu za Halmashauri
HALMASHAURI ZA WILAYA HALMASHAURI ZA MIJI, MANISPAA
NA JIJI
Fedha, Uongozi na Mipango Fedha na Uongozi
Elimu, Afya na Maji Uchumi, Afya, Elimu na Huduma za Jamii
Uchumi, Ujenzi na Mazingira Mipango Miji na Mazingira
Halmashauri inaweza kuunda kamati zingine zisizozidi tatu. Kamati hizo ni pamoja na Kamati ya
maadili na kamati ya UKIMWI. Kamati inayohusika na masuala ya fedha hukaa kula mwezi na
Kamati zingine mara nne kwa mwaka. Halmashauri inaweza kukasimu majukumu yake kwenye
kamati husika isipokuwa majukumu yafuatayo:-
• Kutunga Sheria;
• Kutoza kodi;
• Kupitisha makisio;
• Kupitisha miradi ya maendeleo.
1.4 MADARAKA YA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA
Kwa mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa namba 7 na 8 za mwaka 1982 Mamlaka za Serikali
za Mitaa zimepewa madaraka mbalimbali ya kisheria ili kuziwezesha kutekeleza majukumu yake
ipasavyo. Baadhi ya madaraka hayo ni pamoja na:-
(a) Kufanya Maamuzi
Kiutaratibu, Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa au Jiji ndiyo chombo chenye maamuzi ya mwisho
katika ngazi zote zilizoko katika mamlaka za Serikali za Mitaa husika. Hata hivyo, maamuzi hayo
yanatakiwa yafanywe kwa kuzingatia Katiba, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
26
(b) Kutunga Sheria Ndogo
Sheria Ndogo ni sheria zinazotungwa na Mamlaka ambazo siyo Bunge kwa madaraka yanayotolewa
na Sheria zilizotungwa na Bunge ili kurahisisha au kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya mamlaka
husika. Katiba ya Nchi imeliruhusu Bunge kukasimu madaraka ya kutunga sheria kwa mamlaka
hizokutokana na ukweli kwamba:-
• Muda ambao Bunge hukaa ni mfupi na, hivyo, si rahisi kutunga sheria zote au zitakazohusisha
kila kitu;
• Mazingira ya Halmashauri yanatofautiana na hivyo, siyo rahisi kwa Bunge kutunga sheria
zitakazotumika na kufaa nchi nzima;
• Wakati mwingine hutokea matukio ya dharura kama vile ukame, njaa, milipuko ya magonjwa
na mafuriko - mambo ambayo huhitaji maamuzi na utekelezaji wa haraka katika maeneo
yanayohusika;
• Ni njia mojawapo ya kutoa na kupeleka madaraka kwa wananchi kushiriki katika kutunga sheria
zinazowahusu wao wenyewe.
Pamoja na Mamlaka nyingine kuruhusiwa kutunga Sheria, Bunge bado ndicho chombo chenye
mamlaka ya mwisho ya kutoa madaraka hayo na kusimamia utekelezaji wake. Katika kuhakikisha
kwamba sheria ndogo hazitungwi kiholela au kinyume cha sheria za nchi, Bunge hutoa mwongozo
wa jumla katika sheria za nchi ambazo linatunga. Mwongozo huo huonesha taratibu za kufuatwa na
mamlaka husika katika kutunga sheria ndogo. Kwa mfano, katika kifungu cha 155 cha sheria namba
7 ya mwaka 1982 na kifungu cha 80 cha Sheria namba 8 (Mamlaka ya Miji) ya mwaka 1982, Bunge
limezipa Halmashauri hizo madaraka ya kutunga sheria ndogo. Kifungu namba 156 cha sheria
Namba 7 ya mwaka 1982 na kifungu cha 81 cha Sheria namba 8 ya mwaka 1982 vinatoa utaratibu
wa kufuata katika kutunga sheria hizo. Aidha, kwa mujibu wa vifungu namba 163 na 164 vya sheria
namba 7 ya mwaka 1982, Halmashauri
za Vijiji zimepewa uwezo wa kisheria wa kutunga sheria ndogo za vijiji.
Vifungu hivyo pia vinatoa utaratibu unaopaswa kufuatwa na Halmashauri za Vijiji katika kutunga
sheria ndogo kama ifuatavyo:-
Hatua ya Kwanza
Halmashauri ya Kijiji itaitisha Mkutano Mkuu wa Kijiji ili kutoa mapendekezo yake. Mkutano huo
unaweza kupitisha au kutopitisha mapendekezo hayo.
MADA YA KWANZA
27
10
9
8
7
6
5
4
3
2
11
12
13
Hatua ya Pili
Iwapo Mkutano Mkuu wa Kijiji umepitisha mapendekezo ya kutungwa kwa sheria ndogo,
Halmashauri ya Kijiji itawasilisha rasimu ya mswada pamoja na kumbukumbu za Mkutano Mkuu wa
Kijiji kwenye Halmashauri ya Wilaya.
Hatua ya Tatu
Halmashauri ya Wilaya itapitisha sheria hiyo huku ikizingatia maoni yaliyotolewa na Halmashauri
ya Kijiji husika. Sheria hiyo itaanza kutumika kama itakavyoamriwa na kikao cha Halmashauri ya
Wilaya. Mahakama nazo, kwa upande mwingine, zimepewa jukumu la kudhibiti utungaji holela
wa sheria ndogo. Iwapo utaratibu uliowekwa kisheria haukuzingatiwa, basi mtu yeyote ambaye
ameathirika vibaya au hakuridhika na sheria hiyo, anayo haki ya kupeleka ombi lake Mahakamani
akiomba Mahakama ibatilishe sheria ndogo hiyo.
(c) Hadhi ya Kushitaki na Kushitakiwa
Halmashauri kama Mamlaka ya Serikali za Mitaa inachukuliwa kama mtu kisheria. Hivyo, inaweza
kushitaki au kushtakiwa kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria. Taratibu za kufuatwa wakati
wa kufungua madai dhidi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ni kama ifuatavyo:-
(i) Taarifa ya Kusudio la Kutaka Kushitaki
Kwa mujibu wa kifungu cha 183 cha sheria namba 7 ya mwaka 1982 na kifungu cha 97 cha
sheria namba 8 ya mwaka 1982, kabla ya kufungua kesi ya madai dhidi ya Mamlaka ya Serikali
za Mitaa, mlalamikaji anapaswa kupeleka taarifa ya kusudio la kufungua mashitaka ya madai
kwa Mkurugenzi, angalau mwezi mmoja, kabla ya kupeleka madai au kesi yake mahakamani.
(ii) Madhumuni ya Taarifa hiyo ni:-
• Kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kuangalia kama madai hayo ni halali au la!
na kama yatakuwa ni halali basi yalipwe mara moja ili kuepusha gharama zisizokuwa za
lazima.
• Kuwezesha Mamlaka kuweka katika bajeti yake deni husika ikiwa ni maandalizi ya kulipa;
• Kutoa nafasi kwa Mamlaka kushauriana na mdai kwa lengo la kupata mwafaka badala ya
kwenda Mahakamani.
• Kuepusha Mamlaka kushitakiwa kiholela.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
28
(iii) Mambo yanayotakiwa kuzingatiwa katika taarifa ya kusudio ni kama ifuatavyo:-
• Iwe na jina na anwani kamili ya mdai ikiwa ni pamoja na sehemu anayoishi. Taarifa hii
husaidia mamlaka husika kuwasiliana na mdai;
• Ioneshe madai kwa ufasaha pamoja na fidia ambayo mdai anataka;
• Ieleze kuwa mdai au mlalamikaji anatoa siku 30 kwa Mamlaka kulipa madai au kujibu hoja.
Iwapo madai hayakushughulikiwa ipasavyo, basi shauri hilo litapelekwa Mahakamani.
(iv) Taarifa ya kusudio kuwasilishwa na kupokelewa
Taarifa ya kusudio lazima ipelekwe kwenye Mamlaka husika na kupokelewa. Baada ya
kukamilisha utaratibu huu ndipo mdai anaweza kufungua kesi iwapo Mamlaka husika itakaa
kimya tokea kupokea ilani au endapo mlalamikaji hakuridhika na majibu yaliyotolewa na
Mamlaka hiyo. Kwa mujibu wa kifungu cha 194A cha sheria ya marekebisho ya Sheria za
Serikali za Mitaa, mali za Halmashauri hazitakamatwa kwa amri yoyote ya mahakama isipokuwa
Mkurugenzi wa Halmashauri ataweka utaratibu wa kulipa deni lolote lililoamriwa na mahakama
kupitia mapato ya Halmashauri.
(d) Kuingia Mikataba, Kusamehe Kodi, Kukodisha Wakala, Kutwaa Ardhi, Kuwa na Hazina na
Vyanzo vya Mapato na Kuuza na Kumiliki Mali.
Mamlaka za Serikali za Mitaa zina madaraka ya kisheria kuingia katika mikataba, kusamehe kodi,
kukodisha wakala, kutwaa ardhi, kuwa na hazina na vyanzo vya mapato na kuuza na kumiliki mali.
Hata hivyo, matumizi ya madaraka hayo lazima yazingatie misingi, kanuni na taratibu zilizowekwa.
1.5 UHUSIANO KATI YA SERIKALI ZA MITAA NA SERIKALI KUU
Serikali Kuu ni chombo ambacho kwa misingi maalum kimepewa mamlaka ya kuendesha utawala
wa nchi nzima. Maeneo ya Serikali Kuu yanaanzia Taifa, Mkoa, Wilaya na Tarafa. Serikali za Mitaa
ni vyombo madhubuti vya Serikali Kuu katika ujenzi wa utawala bora, demokrasia na kuleta
maendeleo nchini. Kufanikiwa kwa Serikali za Mitaa kunategemea zaidi uhusiano na ushirikiano kati
yake na Serikali Kuu kwa kujenga mazingira mazuri ya kiutendaji. Ibara ya 146 ya Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na marekebisho yake inaweka misingi ya uhusiano kati
ya Serikali za Mitaa na Serikali Kuu. Ili kuwezesha kuwapo na kufanya kazi kwa uhusiano huo, sheria
mbalimbali zimetungwa kuhalalisha uhusiano huo. Sheria hizo ni pamoja na:-
• Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Namba 7 ya mwaka 1982 kama ilivyorekebishwa
na sheria Namba 6 ya mwaka 1999;
MADA YA KWANZA
29
10
9
8
7
6
5
4
3
2
11
12
13
• Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Namba 8 ya mwaka 1982 kama ilivyorekebishwa na
sheria Namba 6 ya mwaka 1999;
• Sheria ya Tawala za Mikoa Namba 19 ya mwaka 1997.
Majukumu ya Serikali Kuu kwa Serikali za Mitaa
Kwa mujibu wa kifungu cha 174A cha Sheria Namba 7 ya mwaka 1982, na marekebisho ya sheria
namba 13 ya mwaka 2006 kifungu cha 54A cha Sheria Namba 8 ya mwaka 1982, majukumu ya
Serikali Kuu kwa Serikali za Mitaa ni kama ifuatavyo:-
• Kuziwezesha Serikali za Mitaa kutekeleza majukumu na mamlaka yake kwa kutambua uhuru
wake kisheria;
• Kubuni na kuweka sera za kitaifa, sheria, kanuni na taratibu kuhusu uendeshaji wa mfumo wa
Serikali za Mitaa;
• Kutoa ushauri wa kitaalam;
• Kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa sera za kitaifa,sheria, kanuni, taratibu, miongozo na viwango
vilivyowekwa kitaifa;
• Kutoa ruzuku kwa Serikali za Mitaa;
• Kuendeleza taaluma;
• Kudhibiti mambo ya kisheria na ukaguzi wa fedha na rasilimali za Serikali za Mitaa. Hii inaweza
kutekelezwa kwa kutoa mafunzo, kutayarisha taratibu na kanuni mbalimbali na kukusanya
takwimu za kitaifa;
• Kuweka mazingira yatakayowezesha mamlaka za serikali za Mitaa kutekeleza majukumu yake
ipasavyo;
• Kuhakikisha watumishi na Mamlaka za Serikali za Mitaa wanatoa maamuzi na miongozo sahihi
wanapotekeleza majukumu yao katika mfumo wa Serikali za Mitaa;
• Kufanya mambo mengine yatakayowezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekelezaji majukumu
yake ya kisheria na majukumu mengine kwa ufanisi na kwa kuzingatia sheria.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
30
Mgawanyo wa Madaraka Kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa
Kwa kuwa utendaji wa Serikali za Mitaa na ule wa Serikali Kuu unafanyika katika maeneo yale
yale inatupasa kuwa na upeo wa kutosha kuhusu mgawanyo wa majukumu kwa ngazi tatu, yaani
Wizara, Mkoa na Wilaya kama ifuatavyo:.
(i) Madaraka ya Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa
Kwa mujibu wa vifungu namba 4 vya sheria namba 7 na 8 za mwaka 1982, majukumu ya Waziri
mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ni kuhakikisha kwamba mamlaka zote za Serikali za Mitaa
zinajengewa uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria. Uwezo huo wa Serikali
za Mitaa unaangaliwa katika fani mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha, utumishi, usimamizi wa
sheria na nidhamu.
(ii) Madaraka ya Mkuu wa Mkoa
Kifungu cha 5 (3) cha sheria ya Tawala za Mikoa Namba 19 ya mwaka 1997 kinaelezea wajibu wa
Mkuu wa Mkoa kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa ni kuziwezesha na kuzijengea mazingira ya
kutekeleza majukumu yao kisheria. Dhana hii ya uhuru wa mamlaka za Serikali za Mitaa inaegemea
katika sharti kuwa, mamlaka hizo zitakuwa zinajiendesha kisheria. Lakini pale itakapobainika kuwa
sheria haifuatwi, basi uhuru huo hautalindwa, bali Serikali Kuu ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Mkoa
itaingilia kati kuona kuwa sheria zinatekelezwa. Msingi huu wa fikra ndio uliosababisha sheria
kumpa Mkuu wa Mkoa uwezo wa kuagiza au kuwaruhusu maafisa wa Serikali Kuu kuchunguza
nyaraka pamoja na kumbukumbu nyingine za fedha za mamlaka za Serikali za Mitaa. Lengo ni
kutaka kugundua endapo kuna ukiukwaji wa sheria au kanuni za fedha. Hatua hizi ni kwa mujibu
wa kifungu cha 44 cha sheria ya fedha za Serikali za Mitaa namba 9 ya mwaka 1982. Kifungu
cha 78A cha sheria namba 8 ya mwaka 1982, kinampa Mkuu wa Mkoa madaraka ya kusimamia
utekelezaji wa sheria za Mamlaka za Serikali (Mamlaka za Miji), ikiwa ni pamoja na kuchunguza
uhalali wa vitendo na maamuzi ya mamlaka hizo na kumuarifu Waziri ikiwa kuna ulazima wa
kuingilia kati endapo vitendo na maamuzi vinakiuka misingi ya sheria.
(iii) Madaraka ya Mkuu wa Wilaya
Kifungu cha 14 cha Sheria ya Tawala za Mikoa Namba 19 ya mwaka 1997, kinampa Mkuu wa
Wilaya majukumu ya kuziwezesha na kuzijengea mazingira mazuri mamlaka za Serikali za Mitaa
zilizomo ndani ya eneo lake ili ziweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Aidha, kifungu cha
78A cha sheria namba 8 ya mwaka 1982, kama vile ilivyo kwa Mkuu wa Mkoa, vimetoa uwezo
kwa Mkuu wa Wilaya kuchunguza uhalali wa vitendo na maamuzi ya Mamlaka za Serikali za
Mitaa katika eneo lake.
MADA YA KWANZA
31
10
9
8
7
6
5
4
3
2
11
12
13
Mkuu huyo anatakiwa kumjulisha Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ikiwa kuna
ukiukwaji na uvunjaji wa sheria na kanuni za nchi katika utekelezaji wa majukumu na maamuzi
ya mamlaka za Serikali za Mitaa. Mkuu wa Wilaya atakuwa Mwenyekiti wa kamati ya ushauri ya
Wilaya (DCC).
(iv) Madaraka ya Afisa Tarafa
Sheria ya Tawala za Mikoa namba 19 ya mwaka 1997 na sheria ya marekebisho ya sheria za
Serikali za mitaa na 13 ya mwaka 2006 zinaeleza kwamba, wajibu wa Afisa Tarafa ni kama
ifuatavyo:-
• Kutekeleza kazi na majukumu ambayo atapewa na sheria hii, au sheria nyingine.
• Kumsaidia Mkuu wa Wilaya katika eneo lake, hivyo ana majukumu ya:-
–– Kusimamia shughuli za Serikali katika Tarafa yake.
–– Kuiwezesha Halmashauri katika eneo lake kufanya na kutekeleza shughuli zake kwa
mujibu wa sheria.
–– Kuwezesha na kusimamia amani na utengamano katika Tarafa yake.
1.6 UCHAGUZI WA WAJUMBE WA HALMASHAURI NA NGAZI NYINGINE ZA JAMII.
Wajumbe wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Jiji huchaguliwa kushika madaraka ya
udiwani kwa uchaguzi huru na wa kidemokrasia unaoendeshwa kuzingatia Sheria ya Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa, Na 4 ya mwaka 1979. Wajumbe wa mikutano ya ngazi za jamii, yaani
za Halmashauri za Vijiji, Kamati za Mitaa na Vitongoji huchaguliwa kwenye uchaguzi ambao
huendeshwa kwa kuzingatia taratibu za uchaguzi zilizoagizwa na Waziri kwa mujibu wa Sheria za
Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Na 7 ya 1982 pamoja na sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka
za Miji) Na 8 ya 1982.
Sifa za Wagombea katika Uchaguzi wa Wajumbe (Madiwani wa Halmashauri) wa Halmashauri
ya Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji.
Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, mtu anaweza kugombea na kuchaguliwa
kuwa mjumbe wa Halmashauri ya Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji kama tu anazo sifa zifuatazo:
a) Ni raia wa Tanzania
b) Anaweza kusoma na kuandika kwa Kiswahili au Kingereza.
c) Amefikia umri wa miaka 21
d) Asiwe ameondolewa haki ya kugombea kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi ya Mamlaka za
Serikali za Mitaa au Sheria nyingine yoyote.
e) Ni mkazi wa kudumu wa eneo lililo chini ya Mamlaka ya Halmashauri husika.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
32
f) Anaishi kwa kipato halali.
g) Ni mwanachama na amedhaminiwa na chama cha siasa kilichosajiliwa chini ya Sheria ya
Vyama vya Siasa.
h) Hayumo katika hukumu ya kifo iliyotolewa na mahakama yoyote nchini au hukumu ya kifungo
kisichozidi miezi sita kilichotolewa na Mahakama; na
i) Asiwe anadaiwa kodi ya Serikali Kuu au Serikali za Mitaa.
Sifa ya kuwa Mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji, Mwenyekiti wa Mtaa au
Mwenyekiti wa Kitongoji.
Mtu atakuwa na sifa ya kugombea kuwa Mwenyekiti au Mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji, Mjumbe
wa Mtaa au Kitongoji iwapo tu anazo sifa zifuatazo:
a) Ni raia wa Tanzania,
b) Anaweza kusoma na kuandika katika lugha ya Kiswahili au Kingereza,
c) Ni mkazi wa kudumu wa Kijiji, Mtaa au Kitongoji
d) Hajawahi kuhukumiwa na Mahakama kwa kosa lolote la jinai wala kuhukumiwa kifo au
kifungo cha zaidi ya miezi sita (6) na
e) Asiwe ameondolewa haki ya kugombea Uchaguzi kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi au
sheria nyingine yoyote.
Sifa za Kupiga Kura katika Chaguzi za Serikali za Mitaa
Mtu atakuwa na sifa za kupiga kura katika Uchaguzi wa kumchagua Mjumbe wa Halmashauri ya
Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji endapo ana sifa zifuatazo;
a) Ni raia wa Tanzania na mkazi wa kudumu wa eneo la Halmashauri husika.
b) Ana umri wa miaka 18 au zaidi
c) Hajaondolewa sifa za kupiga kura kwa mujibu wa sheria hii ya Uchaguzi au sheria nyingine
yoyote.
d) Hana ugonjwa wa akili
e) Hajaondolewa sifa za kuandikishwa kama mpiga kura.
Sifa ya Kupiga Kura katika Uchaguzi wa Halmashauri ya Kijiji, Kamati ya Mtaa na
Mwenyekiti wa Kitongoji
Mtu atakuwa na sifa ya kupiga kura katika Halmashauri ya kijiji, kamati ya Mtaa au Mwenyekiti wa
Kitongoji iwapo tu anazo sifa zifuatazo;
a) Ni raia wa Tanzania
b) Ni mkazi wa kudumu katika Kijiji, Kitongoji au Mtaa husika.
MADA YA KWANZA
33
10
9
8
7
6
5
4
3
2
11
12
13
c) Hajaondolewa sifa za kuwa Mpiga kura chini ya masharti ya sheria za Uchaguzi
d) Ana umri wa miaka kumi na nane (18) au zaidi.
Kuondolewa Ujumbe wa Halmashauri ya Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji
a) Kwa mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa, mjumbe wa Halmashauri ya Wilaya, Mji, Manispaa
au Jiji anaweza kuondolewa ujumbe kwa sababu zifuatazo;
b) Ikiwa amefariki au kujiuzulu kwa maandishi kwa kumuandikia Mkurugenzi wa Halmashauri
c) Ikiwa Halmashauri itavunjwa
d) Ikiwa atashindwa kuhudhuria vikao vitatu vya Halmashauri mfululizo bila ya idhini ya
Halmashauri; hii itakuwa ni pamoja na vikao vya kamati ya kudumu ambapo yeye ni Mjumbe
e) Ikiwa ataajiriwa kwa kazi ya kuwa Mtumishi wa Umma kwenye Halmashauri husika.
f) Ikiwa amehukumiwa kifo au amehukumiwa adhabu kwenda jela kifungo kisichozidi miezi sita
bila kupewa chaguo la kulipa faini na
g) Kutokana na tukio lingine lolote ambalo linamuondolea sifa kwa mujibu wa sheria.
Wajibu wa Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa katika uchaguzi wa viongozi ngazi za jamii:
Watendaji wa Vijiji na Mitaa wanawajibu ufuatao;
• Kuhamasisha wakazi kushiriki ipasavyo kwenye uchaguzi wa viongozi ngazi mbalimbali za
msingi ili:-
–– Wenye sifa za kugombea waombe kugombea nafasi mbalimbali
–– Wenye sifa ya kujiandikisha kupiga kura, wajiandikishe;
–– Waliojiandikisha kupiga kura wajitokeze siku ya kupiga kura.
• Kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri yatakayo wezesha kufanyika kwa uchaguzi
kwa uhuru na haki katika eneo lake.
• Kujiepusha na ushabiki na upendeleo wa aina yoyote.
1.7 SHERIA ZINAZOTAWALA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI ZA MITAA
Lengo la sehemu hii ni kuwawezesha Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa kufahamu sheria za
msingi zinazotawala uendeshaji wa shughuli za Serikali za Mitaa. Sheria hizo ni pamoja na:-
(a) Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Namba 4 ya mwaka 1979
Sheria hii inazungumzia taratibu za Uchaguzi wa madiwani, vipindi vya uongozi, uchaguzi wa
kawaida na uchaguzi mdogo, usajili wa wapiga kura, kupiga kura pamoja na sifa za wagombea
na Wajumbe wa mabaraza ya Mamlaka katika ngazi mbalimbali. Sheria hii pia inaelekeza kuhusu
kampeni za uchaguzi.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
34
(b) Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Namba 7 ya Mwaka 1982.
Sheria hii, pamoja na mambo mengine, inazungumzia Uundaji wa Mamlaka za Wilaya. Aidha,
inazungumzia majukumu na wajibu wa mamlaka hizo, taratibu zinazotakiwa kuzingatiwa wakati
wa kutunga sheria ndogo, wakati wa kuendesha vikao vya Halmashauri na Kamati zake. Sheria
hii pia hutoa maelekezo kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa endapo Halmashauri ya Wilaya
itashindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
(c) Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Namba 8 ya mwaka 1982.
Pamoja na mambo mengine, Sheria hii inazungumzia juu ya Uundaji wa Mamlaka za Miji, ambazo
ni Halmashauri za Miji, Manispaa na Jiji. Wajibu na majukumu ya mamlaka hizo, Kamati za kudumu,
taratibu za kutunga sheria ndogo, pamoja na taratibu zinazozingatiwa wakati wa kuchukua hatua
endapo Mamlaka za Miji zitashindwa kutekeleza majukumu yake.
(d) Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Namba 9 ya mwaka 1982
Sheria hii inahusu fedha za Serikali za Mitaa. Baadhi ya masuala yanayozungumziwa katika sheria
hii ni pamoja na vyanzo vya mapato, taratibu za kutoza kodi na ukusanyaji wa mapato, matumizi
ya fedha, usimamizi wa fedha pamoja na ukaguzi wa vitabu. Kwa ujumla, sheria hii inakazia juu
ya usimamizi na udhibiti wa mali za Halmashauri ambazo zinahusisha fedha taslimu na rasilimali
nyingine.
(e) Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 8 ya mwaka 2002
Sheria hii inafuta sheria ya utumishi wa Serikali za Mitaa Namba 10 ya mwaka 1982. Sheria hii
inaelezea na kufafanua masuala mbalimbali ya utumishi wa umma ikiwa ni pamoja na watumishi wa
Serikali za Mitaa. Masuala hayo ni pamoja na :-
• Mamlaka mbalimbali za ajira;
• Taratibu za ajira na uteuzi;
• Taratibu za nidhamu;
• Taratibu za kupandishwa vyeo.
(f) Sheria ya Tawala za Mikoa Namba 19 ya mwaka 1997
Sheria hii inafafanua mfumo mpya wa utendaji kazi katika Tawala za Mikoa kwa mujibu wa muundo
mpya wa Tawala za Mikoa. Aidha, sheria hii inaweka bayana majukumu mapya ya Sekretarieti za
Mikoa na uhusiano uliopo kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa.
MADA YA KWANZA
35
10
9
8
7
6
5
4
3
2
11
12
13
(g) Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba. 5 ya mwaka 1999
Sheria hii inahusu ardhi ya kijiji na inatoa ufafanuzi juu ya usimamizi wa ardhi ndani ya mipaka ya
kijiji, taratibu za utatuzi wa migogoro ya ardhi kijijini, na vyombo au mamlaka mbalimbali zilizowekwa
kwa lengo la kushughulikia masuala ya ardhi kijijini.
(h) Sheria ya Mabaraza ya Kata Namba 7 ya mwaka 1985
Sheria hii inahusu uundaji wa Mabaraza ya Kata na inafafanua taratibu za kuunda Baraza la Kata,
idadi ya wajumbe wa Baraza, taratibu za uendeshaji wa Baraza la Kata, majukumu ya Baraza, faini
mbalimbali kutokana na makosa yaliyoainishwa, muda/kipindi cha ujumbe wa Baraza na majukumu
ya Kamati ya Maendeleo ya Kata katika usimamizi na uendeshaji wa Baraza la Kata.
(i) Sheria ya mahakama (usuluhisi wa migogoro ya ardhi) namba 2 ya mwaka 2002
Sheria hii inafafanua vyombo au mamlaka zilizowekwa kwa lengo la kushughulikia masuala
ya ardhi. Vyombo hivyo ni pamoja na ;
• Baraza la Ardhi la kijiji
• Baraza la Kata
• Baraza la Ardhi na nyumba la Wilaya
• Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi
• Mahakama ya Rufaa
(j) Sheria ya hifadhi ya mazingira ya mwaka 2004
Sheria hii inahusu hifadhi ya mazingira na inatambua haki ya kila mwananchi kuishi kwenye
mazingira safi ya kiafya na salama.Aidha sheria inasisitiza umuhimu wa kuweka mazingira katika hali
ya usafi na salama.
1.8 HITIMISHO
Mada hii imeelezea maana, muundo na aina za Mamlaka na madaraka ya Serikali za Mitaa,
uhusiano wa Serikali za Mitaa na Serikali Kuu na sheria zinazosimamia uendeshaji wa Serikali za
Mitaa. Uelewa wa mambo haya utawawezesha Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa kutekeleza
majukumu yao kwa kuzingatia muundo, mfumo na sheria za Serikali za Mitaa.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
36
Marejeo
• Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2000) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977
• R. Kinemo na E.J.M. Wiketye (2002) Tafsiri ya Sheria za Serikali za Mitaa, Tathmini, Uzoefu na
Mapendekezo. Chuo Kikuu cha Mzumbe.
• URT (2000) Local Government Laws (Revised 2000)
• Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2003): Mwongozo wa Uwajibikaji wa Makatibu Tarafa
katika Wilaya na Halmashauri za Serikali za Mitaa.
• Kitabu cha Diwani Hatua ya kwanza Somo la Pili wajibu na Majukumu ya Diwani katika
Uongozi na Uendeshaji wa Serikali za Mitaa Julai 2002.
10
9
8
7
6
5
4
3
2
11
12
13
MADA YA PILI 2 DHANA YA UBORESHAJI WA MFUMO WA SERIKALI ZA MITAA
MADA YA PILI
39
10
9
8
7
6
5
4
3
11
12
13
2.1 UTANGULIZI
Dhana ya kupeleka Madaraka kwa wananchi.
Chimbuko la Upelekaji wa Madaraka kwa Umma ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977 na marekebisho yake; katika Ibara ya 8, 145 na 146. Utekelezaji wake unafafanuliwa
kwa kina zaidi na Sera ya Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa ya mwaka 1998. Katika Sera
hii upelekaji wa Madaraka kwa wananchi (ugatuaji) unatafsiriwa kuwa ni kupeleka Madaraka ya
kisiasa, majukumu, rasilimali fedha na rasilimali watu kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo
ni vyombo vya kidemokrasia vyenye wajumbe waliochaguliwa na wanaowajibika kwa wananchi.
Ili kufanikisha ugatuaji huo, Serikali iliamua kuwa na Programu ya Maboresho ya Serikali za Mitaa.
Programu hiyo imetekelezwa kwa awamu mbili, awamu ya kwanza ilikuwa kati ya mwaka 2000-2008
na awamu ya pili imeanza 2009 na itamalizika 2013.
Lengo la mada hii kuwawezesha Maafisa Watendaji wa vijiji na mitaa kuufahamu mpango wa
uboreshaji wa mfumo wa Serikali za Mitaa ili washiriki kikamilifu katika utekelezaji wa sera ya
kupeleka madaraka kwa wananchi kwa lengo la kuongeza ufanisi kwenye Serikali za Mitaa katika
kutoa huduma bora na endelevu.
Mafanikio na changamoto za utekelezaji wa Programu yanaelezwa katika vipengele vinavyofuata.
Lengo la mada hii ni kumuwezesha Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa awe na ufahamu juu ya dhana
ya upelekaji madaraka kwa wananchi ili aweze kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa wahusika
wakuu wa Maendeleo katika maeneo yao kwa kushiriki katika kutoa maamuzi na kusimamia
utekelezaji wa maamuzi yao.
2.0 DHANA YA UBORESHAJI WA MFUMO WA SERIKALI
ZA MITAA
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
40
2.2 AWAMU YA KWANZA YA PROGRAMU
Awamu ya kwanza ya programu ya uboreshaji ya mfumo wa Serikali za Mitaa ilikuwa ni
mwaka 2000-2008. Malengo mahususi ya programu hiyo yalikuwa ni
• Kuongeza ufanisi na tija katika utoaji na upatikanaji wa huduma zinazotolewa au kusimamiwa na
Serikali za Mitaa; -
• Kuwezesha wananchi kuufahamu Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
ili washiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Mpango na kuelekeza misingi ya utawala bora
unaozingatia demokrasia, uwazi,uwajibikaji, ushirikishwaji, utawala wa sheria, usawa na uadilifu;
–– Kuongeza ufanisi kwenye Serikali za Mitaa katika kutoa huduma bora na endelevu;
–– Kuongeza mapato ya Serikali za Mitaa na kuimarisha usimamizi wa fedha za Serikali za
Mitaa;
–– Kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na uwajibikaji wa watumishi;
–– Kuwezesha utungaji wa Sheria za kuongoza utekelezaji wa Mpango;
–– Kujenga uwezo wa Wizara yenye dhamana ya Serikali za Mitaa;
–– Kuratibu maboresho ya kisekta yaliyotekelezwa kwenye ngazi ya Halmashauri.
Mafanikio ya utekelezaji
Katika Awamu ya Kwanza ya Programu kumekuwa na mafanikio katika maeneo yafuatayo-:
2.2.1 Madaraka ya kisiasa
i. Kuongezeka kwa ushiriki wa wananchi katika shughuli za Uchaguzi,
ii. Kuongezeka kwa ari na kushiriki kwa wananchi katika mikutano ya wakazi wa Mitaa,
Vitongoji na Vijiji na kushiriki katika kupanga na kutekeleza, kufuatilia na kutathmini utekelezaji
wa mipango ya maendeleo ya mahali wanapoishi,
iii. Kuongezeka kwa uelewa wa wananchi kuhusu wajibu na haki zao ikiwepo wajibu wa
kuchangia shughuli za maendeleo yao, na
iv. Kuongezeka kwa mwamko wa wananchi kudai kusomewa taarifa za mapato na matumizi ya
Serikali zao za Vijiji. /Mitaa
MADA YA PILI
41
10
9
8
7
6
5
4
3
11
12
13
2.2.2 Madaraka ya kifedha
i. Kuongezeka kwa kiwango cha fedha zinazopelekwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa
njia ya ruzuku isiyokuwa na masharti na
ii. Kuboreshwa kwa Mfumo wa usimamizi wa fedha na utunzaji wa hesabu na hivyo kuboresha
na kuongeza utoaji wa huduma kwa wananchi. Kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali, hali ya usimamizi na utunzaji wa vitabu vya hesabu za fedha
kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa imeendelea kuimarika kama inavyoonekana katika
Jedwali lifuatalo:-
Halmashauri
Mwaka Hati safi Hati yenye shaka Hati chafu
2004/05 62 51 4
2005/06 54 66 4
2006/07 100 24 0
2007/08 72 61 0
2008/09 77 55 1
2.2.3 Madaraka ya Kiutawala
i. Mamlaka za Serikali za Mitaa zina uwezo wa kuajiri, kuendeleza na kudhibiti watumishi wake
wenyewe. Kwa lengo la kufahamu hali halisi ya watumishi, Wizara zimefanya tathmini kuelewa
Ikama za Watumishi katika ngazi mbalimbali. Vilevile Serikali ilikubali kulegeza masharti ya ajira
na baadhi ya Wizara za kisekta zikakubaliwa kuwapangia kazi moja kwa moja wahitimu wa
fani mbalimbali kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa. Jumla ya watumishi 79,458 walipangwa
kwenda kwenye Halmashauri kati ya mwaka 2006/2007 na 2009/2010.
ii. Watumishi wanawajibika kwenye Mamlaka zao za Serikali za Mitaa. Hivi sasa watumishi
wote wanaofanya kazi kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa wanawajibika kwa Mamlaka zao
wakiwemo watumishi wa Shule za Sekondari waliokuwa wanawajibika kwa Wizara mama.
2.2.4 Mahusiano kati ya Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa
i. Wizara za kisekta zimehamisha majukumu na rasilimali watu, vitendea kazi na fedha kwenda
kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa. Katika mwaka 2006/2007 na 2007/2008 Wizara 14
zilifanyiwa upimaji kwa nia ya kubaini majukumu yanayopaswa kuhamishiwa katika Serikali
za Mitaa. Ugatuaji wa majukumu hayo uliwezesha jumla Sh. 286,994,800,000/= kuhamishiwa
katika Bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa mwaka 2007/2008.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
42
ii. Wizara zimebaki na majukumu ya kimsingi ya Kutunga na kusimamia Sera, Viwango,
Ufuatiliaji na Tathmini, kujenga uwezo na kuchukua hatua pale Mamlaka za Serikali za Mitaa
zinaposhindwa kutekeleza wajibu na majukumu yao
iii. Mamlaka za Serikali za Mitaa zimebaki na majukumu yake ya msingi ya kutoa huduma za kijamii
na kiuchumi kwa wananchi na kuwezesha wadau wengine kushiriki katika utoaji wa huduma
hizo.
iv. Mgawanyo wa majukumu kati ya ngazi hizo mbili umeimarishwa. Kila ngazi inatekeleza
majukumu yake kwa mujibu wa Sheria na Sera ya Upelekaji wa Madaraka kwa Wananchi.
2.3 CHANGAMOTO ZILIZOSHUGHULIKIWA
Zifuatazo ni changamoto zilizoendelea kuwepo hata baada ya kumalizika kwa Awamu ya Kwanza ya
Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa: -
i. Mgawanyo usiolingana wa njia za mapato kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa
unaosababisha fedha kutolewa bila kulingana na kazi (za kutekelezwa);
ii. Uhaba wa rasilimali fedha na rasilimali watu ya kuweza kutekeleza majukumu yaliyogatuliwa
kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
iii. Halmashauri kutokupeleka Rasilimali watu, fedha na vitendea kazi kwenye ngazi za msingi.
2.4 AWAMU YA PILI YA PROGRAMU
Programu ya Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa awamu ya Pili
Awamu hii inatekelezwa katika kipindi cha 2009 – 2013 na imeandaliwa kwa kuzingatia changamoto
pamoja na uzoefu uliopatikana katika utekelezaji wa Awamu ya Kwanza. Utekelezaji umehuishwa
katika shughuli za kila siku za OWM - TAMISEMI na pia katika Sekretarieti za Mikoa. Awamu hii
imejikita zaidi katika kujenga uwezo wa watumishi ngazi ya Wizara (OWM – TAMISEMI) na Mikoa
(Sekretarieti za Mikoa) na hivyo kuondokana na dhana ya kuwa na Kitengo Maalum na Ofisi za
Maboresho za Kikanda zinazosimamia maboresho kama ilivyokuwa katika awamu ya kwanza.
Mambo yanayokusudiwa kutekelezwa katika awamu hii ni pamoja na:-
i. Kujenga mazingira ambayo yatawezesha Serikali kutekeleza wajibu wake wa Kikatiba wa
kupeleka Madaraka kwa Wananchi;
ii. Kuzijengea uwezo Serikali za Mitaa kutekeleza majukumu yake katika maeneo ya Uongozi na
Menejimenti Maendeleo ya watumishi kitaaluma, ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa matumizi
ya fedha, uandaaji, utekelezaji, ufuatiliaji, utoaji taarifa za mipango na tathmini za utekelezaji wa
Mipango katika Serikali za Mitaa. Matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika uendeshaji
wa shughuli za uelimishaji na uhamasishaji katika Serikali za Mitaa.
iii. Kuimarisha ushirikishwaji wa wananchi katika kupambana na umaskini kwa kuwawezesha
MADA YA PILI
43
10
9
8
7
6
5
4
3
11
12
13
wananchi kutumia mbinu shirikishi ya Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O & OD) katika
kupanga, kutekeleza na kusimamia miradi ya maendeleo Kuhakikisha kwamba malengo
yaliyokusudiwa yanafikiwa kwa kuwapa wananchi mbinu na stadi shirikishi katika kusimamia
na kufuatilia mapato na matumizi ya fedha za kugharamia utekelezaji wa miradi yao inayolenga
katika kupambana na umaskini; Kuwajengea uwezo Viongozi na Watendaji wa ngazi za Msingi
za Serikali za Mitaa ili wawe chachu ya maendeleo na kuhamasisha wananchi kushiriki katika
shughuli za maendeleo kwa kuzingatia misingi ya Utawala Bora katika maeneo yao; na
iv. Kujenga uwezo wa kitaasisi wa kusimamia na kuratibu utekelezaji wa awamu ya pili ya
Programu katika ngazi zote Serikalini kwa kuzijengea uwezo Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara zingine husika na Sekretarieti za Mikoa ili kuimarisha
usimamizi wa utekelezaji wa maboresho, kuweka mfumo imara wa ufuatiliaji, tathmini na
utoaji taarifa za utekelezaji wa majukumu ya Serikali za Mitaa na kujenga uwezo wa mfumo
wa upashanaji Habari, Elimu na Mawasiliano kuhusu uendeshaji wa Serikali za Mitaa
v. Kuwezesha wananchi katika ngazi zote kushiriki na kudai mambo ya Umma kufanywa kwa
uwazi na pia kudai uwajibikaji wa viongozi na Watendaji
vi. Kuhakikisha utekelezaji thabiti wa ugatuaji wa Madaraka kwa wananchi
2.5 HITIMISHO
Mada hii imeelezea kwa ufupi dhana ya ugatuaji wa Madaraka na utekelezaji wa dhana hiyo kupitia
Mpango wa Uboreshaji wa mfumo wa Serikali za Mitaa awamu ya kwanza na ya pili. Hivyo ni wajibu
wa Maafisa Watendaji wa Mitaa na Vijiji kuielewa dhana hii na kuendelea kuwaelimisha wananchi ili
waweze kushiriki katika kutoa maamuzi juu ya mambo mbali mbali yanayowahusu katika maeneo
yao kwa kuzingatia Sheria Kanuni na Taratibu za nchi hii.
Marejeo
• Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (2006) Kitabu cha kufundishia toleo
la pili, Mafunzo ya kuboresha ujuzi na stadi za kazi kwa Maafisa watendaji wa vijiji na Mitaa
Tanzania Bara
• Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2010) Kijitabu cha Kusaidia Utekelezaji wa Utawala Bora
katika Serikali za Mitaa.
10
9
8
7
6
5
4
3
11
12
13
MADA YA TATU 3 MUUNDO WA UTUMISHI WA MAAFISA WATENDAJI
WA VIJIJI NA MITAA
MADA YA TATU
47
10
9
8
7
6
5
4
11
12
13
3.1 UTANGULIZI
Serikali za Mitaa zilirejeshwa rasmi mnamo mwaka 1982 kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania yamwaka 1977; ibara ya 145 (1) na 146 (2) na Sheria Namba 7 (Mamlaka
za Wilaya) na 8 (Mamlaka za Miji) za Serikali za Mitaa za mwaka 1982. Urejeshaji wa Serikali za
Mitaa uliambatana na uundaji wa vyombo mbalimbali vya sheria ili kuhakikisha kuwa Serikali za
Mitaa zinatekeleza majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu. Hadi kufikia mwaka 1992, shughuli za
Halmashauri katika ngazi ya Kata na Vijiji zilikuwa zikiendeshwa na Makatibu Kata na Makatibu wa
Vijiji ambao pia walikuwa na jukumu la kushughulikia masuala ya Chama cha Mapinduzi.
Baada ya nchi yetu kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya Siasa (mwaka 1992) Serikali iliona
umuhimu wa kutenganisha kofia hizi mbili. Ndipo mwaka 1993 ikaanzishwa Kada ya Maafisa
Watendaji wa Kata na Vijiji. Muundo wa Kada ya Maafisa Watendaji wa Vijiji unaotumika hivi sasa
ulitolewa kwa Waraka wa Tume ya Utumishi wa Serikali za Mitaa wenye Kumb. Na. LGSC/ C.10/3
wa tarehe 30 Mei - 2003. Ngazi ya Mtaa kwa Halmashauri za Jiji, Manispaa na Miji haikuwa na
Muundo wa Kada ya Afisa Mtendaji Mtaa hivyo iliendelea kuwa chini ya usimamizi na uangalizi wa
Afisa Mtendaji wa Kata.
Lengo la uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa pamoja na mambo mengine ni kuimarisha
na kurahisisha upatikanaji na utoaji wa huduma. Kwa kuzingatia lengo hili, Tume ya Utumishi
wa Serikali za Mitaa iliunda muundo mpya wa Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa kwa lengo la
kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na utoaji wa huduma bora.
Lengo la Mada hii ni kuwawezesha Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa kuelewa Muundo wa
utumishi wao pamoja na majukumu yao katika utendaji kazi katika maeneo yao.
3.2 MAANA YA MUUNDO WA UTUMISHI
Muundo wa utumishi ni waraka maalum unaonyesha kazi na wajibu, vyeo na ngazi za mishahara,
sifa na utaratibu wa kuajiriwa na kupandishwa madaraja na masharti ya utumishi kwa kada husika.
Muundo hubadilika kwa kurekebishwa au kufutwa kulingana na mahitaji ya wakati huo. Muundo wa
utumishi humwezesha mwajiri kuwa na habari au taarifa sahihi kuhusu watumishi wake na hivyo
kurahisisha mipango na maamuzi ya utawala na menejimenti yanayohusu utumishi katika taasisi au
asasi husika. Kwa kifupi muundo na utumishi una umuhimu na faida zifuatazo:-
3.0 MUUNDO WA UTUMISHI WA MAAFISA WATENDAJI
WA VIJIJI NA MITAA
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
48
Kwa mwajiriwa humwezesha:-
• Kuelewa sifa anazopaswa kuwa nazo katika ajira husika;
• Kupata picha kamili ya kazi na wajibu wake;
• Kuelewa masharti yake ya kazi;
• Kuelewa ngazi za mshahara wake na taratibu za kupanda kutoka daraja moja hadi lingine na haki
nyinginezo zinazoambatana na ajira yake;
• Kuwa na ari ya kufanya kazi na kujiendeleza ili aweze kupanda cheo na kupata mshahara
mkubwa zaidi.
Kwa mwajiri humwezesha:-
• Kuwa na vigezo rasmi vya kuajiri na kupandisha vyeo watumishi bila upendeleo au kubahatisha;
• Kupanga vizuri safu za watumishi kulingana na mahitaji na malengo ya taasisi au asasi yake;
• Kupanga na kufanya makisio ya mishahara na marupurupu mengine kwa urahisi kwa kuzingatia
madaraja na ngazi za mishahara ya watumishi waliopo na wanaotarajiwa kuajiriwa.
3.3 MUUNDO WA UTUMISHI WA MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI
Muundo mpya wa Maafisa Watendaji wa Vijiji umetolewa kwa Waraka wa Maendeleo ya Utumishi
wa Serikali za Mitaa Na. 30 wa mwaka 2003 wenye Kumb. Na. LGSC/C.10/3. Muundo huu
umeainisha vyeo, majukumu na ngazi za mishahara kwa nafasi zote katika kada hii kama ifuatavyo:-
3.3.1 Vyeo na Ngazi za Mishahara
Chini ya Muundo mpya wa Maafisa Watendaji wa Vijiji, vyeo na ngazi za mishahara vitakuwa kama
ifuatavyo:-
a) Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la III - TGS A/B
b) Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la II - TGS C
c) Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la I - TGS D
d) Afisa Mtendaji wa Kijiji Mwandamizi - TGS E
e) Afisa Mtendaji wa Kijiji Mkuu - TGS F
MADA YA TATU
49
10
9
8
7
6
5
4
11
12
13
3.3.2 Utaratibu wa Kuajiriwa na Kupandishwa Vyeo
Muundo mpya wa Maafisa Watendaji wa Vijiji umeainisha utaratibu wa kuajiriwa na kupandishwa
vyeo kama ifuatavyo:-
Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la III
Sifa ya kuingilia moja kwa moja. Waombaji wenye elimu ya Kidato cha IV na VI waliohitimu
Stashahada katika fani yoyote kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kufaulu usaili
wataajiriwa kwa cheo cha Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la III.
Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la II
Waombaji wenye elimu ya Kidato cha IV na VI waliohitimu Shahada au Stashahada ya juu katika fani
yeyote na kufaulu usaili watapata sifa ya kuajiriwa kwa cheo hiki moja kwa moja;
Kupandishwa cheo Watendaji wa Vijiji Wasaidizi wenye utendaji mzuri na baada ya kupata sifa
zilizotajwa kwenye kipengele b (i) watapata sifa ya kuajiriwa katika cheo hiki wakiwemo kazini.
Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la I
Waombaji wenye elimu ya Kidato cha IV na VI waliohitimu Shahada au Stashahada ya juu katika fani
yoyote na kufaulu usaili watapata sifa ya kuajiriwa katika cheo hiki moja kwa moja;
Kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji mwenye utendaji mzuri kazini kwa mujibu wa sera ya Menejimenti na
Ajira katika utumishi wa umma atapandishwa cheo na kuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la I.
Afisa Mtendaji wa Kijiji Mwandamizi
Waombaji wenye Shahada au Stashahada ya Uzamili katika fani yoyote na ambao watafaulu usaili
wataajiriwa moja kwa moja katika cheo hiki; Kwa Maafisa Watendaji wa Vijiji waliomo kazini ambao
watathibitishwa kuwa na utendaji mzuri kazini watapandishwa vyeo na kuwa Maafisa Watendaji wa
Vijiji Waandamizi.
Afisa Mtendaji wa Kijiji Mkuu
Sifa ya kuingilia moja kwa moja itakuwa ni kwa wale wenye Shahada/Stashahada ya uzamili katika
fani yoyote na waliofaulu usaili; Sifa ya kuingilia waliomo makazini itakuwa ni kwa kupandishwa
cheo Afisa Mtendaji wa Kijiji aliyethibitisha kuwa na utendaji kazi mzuri kazini.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
50
3.4 MUUNDO WA UTUMISHI WA MAAFISA WATENDAJI WA MITAA
Kwa mujibu wa kifungu cha 14 (3) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Namba 8 ya
mwaka 1982, ngazi ya chini kabisa katika muundo wa Serikali ni Mtaa. Kwa msingi huo, Tume ya
Utumishi wa Serikali za Mitaa iliandaa muundo wa utumishi wa kada ya Afisa Mtendaji wa Mtaa
kwenye Halmashauri za Jiji, Manispaa na Miji. Kada hii imeanzishwa ili kuongeza ufanisi katika
utendaji kazi na utoaji wahuduma bora katika maeneo hayo.
Muundo wa Maafisa Watendaji wa Mtaa umetolewa kwa Waraka wa maendeleo ya utumishi wa
Serikali za Mitaa Na. 31 wa mwaka 2003 wenye Kumb. Na. LGSC/C.10/3 wa tarehe 30 Mei, 2003.
Kulingana na sera ya Menejimenti na Ajira katika utumishi wa umma ya mwaka 1999, viwango vya
utendaji kazi na viwango vya kuingilia vimewekwa kwa kuwiana na kada nyingine katika utumishi wa
Serikali za Mitaa zenye sifa, ujuzi wa kazi na majukumu yanayolingana. Muundo huu umezingatia
mfumo mpya wa ngazi za mishahara Serikalini.
3.4.1 Vyeo na ngazi za mishahara
Chini ya muundo huu vyeo na ngazi za mishahara vitakuwa kama ifuatavyo:-
a) Afisa Mtendaji wa Mtaa Daraja la III TGS B
b) Afisa Mtendaji wa Mtaa Daraja la II TGS C
c) Afisa Mtendaji wa Mtaa Daraja la I TGS D
d) Afisa Mtendaji wa Mtaa Mwandamizi TGS E
e) Afisa Mtendaji wa Mtaa Mkuu TGS F
3.4.2 Utaratibu wa kuajiriwa na kupandishwa vyeo
Muundo wa utumishi wa Maafisa Watendaji wa Mtaa umeainisha utaratibu wa kuajiriwa na
kupandishwa vyeo kama ifuatavyo:-
Afisa Mtendaji wa Mtaa Daraja la III
Sifa ya kuingia moja kwa moja katika cheo hiki ni kwa waombaji wenye elimu ya Kidato cha VI
waliohitimu Stashahada katika fani yoyote kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na
kufaulu usaili.
MADA YA TATU
51
10
9
8
7
6
5
4
11
12
13
Afisa Mtendaji wa Mtaa Daraja la II
Sifa ya kuingia moja kwa moja katika cheo hiki ni kwa waombaji wenye shahada ya sanaa yenye
mwelekeo wa Sayansi ya Jamii, Utawala (Public Administration/Local Government Administration)
na wenye shahada ya sheria au sifa nyingine inayolingana na hivyo kutoka Chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali na kufauli usaili;
Watendaji wa Mtaa Daraja la III wenye utendaji mzuri na ambao watapata sifa zilizotajwa kwenye
kipengele 2.2.2. b (i), watapandishwa vyeo na kuwa Afisa Mtendaji wa Mtaa Daraja la II.
Afisa Mtendaji wa Mtaa Daraja la I
Sifa ya kuingia moja kwa moja kwenye cheo hiki itakuwa ni kwa waombaji wenye sifa zilizotajwa
katika kipengele 2.2.2. b (i); Kwa waliomo kazini, Afisa Mtendaji wa Mtaa atapandishwa cheo na
kufikia cheo hiki kwa kuzingatia utendaji mzuri kazini kwa mujibu wa sera ya Menejimenti na Ajira
katika utumishi wa umma.
Afisa Mtendaji wa Mtaa Mwandamizi
Sifa ya kuajiriwa moja kwa moja itakuwa ni kwa waombaji wenye Shahada/Stashahada ya uzamili
katika fani ya Sayansi ya Jamii, Utawala na Sheria, ambao watafaulu usaili; Kwa waliomo kazini,
Maafisa Watendaji wa Mtaa wenye utendaji mzuri kazini watapandishwa vyeo na kufikia Daraja hili.
Afisa Mtendaji wa Mtaa Mkuu
Sifa ya kuajiriwa moja kwa moja itakuwa kama ilivyoainishwa katika kipengele 2.2.2. d (i); Kwa
waliomo kazini, Maafisa Watendaji wa Mtaa watapandishwa vyeo na kufikia cheo hiki kwa
kuzingatia utendaji kazi mzuri kazini.
3.5 UTARATIBU WA KUPANDISHWA VYEO
Ujuzi na masharti yaliyoelezwa katika Muundo wa Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mtaa wa
kumwezesha mtumishi kupandishwa cheo kutoka ngazi moja hadi nyingine ni wa kiwango cha chini
kabisa ambacho italazimu kila mtumishi akipate ili aweze kufikiriwa kupandishwa cheo. Lakini, hii
haina maana kwamba mtumishi akifanikiwa kupata kiwango hicho cha ujuzi lazima apandishwe
cheo. Kupandishwa cheo kutafuata taratibu sawa na za uajiri ambazo zitategemea pia kuwepo kwa
nafasi na fedha za kulipia mishahara.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
52
3.6 HITIMISHO
Mada hii imeelezea muundo wa utumishi na majukumu ya Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa. Afisa
Mtendaji wa Kijiji/Mtaa anapaswa kuyaelewa vema majukumu yake kwa vile yeye ndiye Mtendaji
Mkuu na Mtekelezaji wa majukumu yaliyoelezwa. Maafisa Watendaji wa Vijiji/Mitaa wanapaswa
kuzingatia mipaka yao ya madaraka ili kuondoa migongano kati yao na viongozi wa kuchaguliwa.
Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa anapaswa kuelewa kuwa yeye si mtawala ndani ya Kijiji/Mtaa bali ni
Mtendaji Mkuu wa `shughuli za maendeleo katika eneo lake.
Marejeo
• Waraka wa Maendeleo ya Utumishi wa Serikali za Mitaa Na. 30 wa mwaka 2003, Ofisi ya
Rais,Tume ya Utumishi wa Serikali za Mitaa, Dodoma.
• Waraka wa Maendeleo ya Utumishi wa Serikali za Mitaa Na. 31 wa mwaka 2003 Ofisi ya
Rais,Tume ya Utumishi wa Serikali za Mitaa, Dodoma.
• Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
• Local Government Laws Revised version, 2000.
w
10
9
8
7
6
5
4
11
12
13
MADA YA NNE 4 KAZI, WAJIBU NA HAKI ZA AFISA MTENDAJI
WA KIJIJI NA MTAA
54
MADA YA NNE
55
10
9
8
7
6
5
11
12
13
4.1 UTANGULIZI
Serikali za Mitaa zilirejeshwa rasmi mnamo mwaka 1982 kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977; ibara ya 145 (1) na 146 (2) na Sheria Namba 7 (Mamlaka za
Wilaya) na 8 (Mamlaka za Miji) za Serikali za Mitaa za mwaka 1982. Urejeshwaji wa Serikali za Mitaa
ulifuatiwa na uanzishaji wa vyombo na vyeo mbalimbali vya kisheria vya kuhakikisha Serikali za
Mitaa zinatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya Nchi, Sheria, Kanuni na Sera za Taifa.
Mada hii inaelezea kazi, wajibu na haki za Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa, lakini pia itagusia nafasi
na umuhimu wa Maafisa Watendaji hao katika muundo wa sasa wa Serikali za Mitaa, ikiwa ni
pamoja na sifa na maadili wanayopaswa kuwa nayo.
Lengo la mada hii ni kumwezesha Afisa mtendaji wa Kijiji/Mtaa aweze kujua kazi wajibu na haki
zake ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuondoa migongano ya kimajukumu kati
yake na watumishi wa kuchaguliwa.
4.2 NAFASI NA UMUHIMU WA AFISA MTENDAJI WA KIJIJI NA MTAA
Katika muundo wa sasa wa Serikali za Mtaa, Kijiji na Mtaa ni ngazi muhimu zilizo karibu zaidi na
wananchi kwa minajili ya kusogeza huduma karibu na wananchi. Kimsingi, Kijiji na Mtaa ni kitovu
cha ujenzi wa utawala bora na demokrasia shirikishi. Ngazi ya Kijiji na Mtaa ndiyo kitovu cha jitihada
za Serikali za kukuza uchumi wa soko na kuondoa umaskini.
Hivyo, bila kuwepo Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa, ambae ndio Watendaji na watekelezaji wakuu
wa shughuli za Serikali katika maeneo husika, jitihada za Serikali za ujenzi wa utawala bora na
demokrasia ya kweli, utoaji wa huduma bora na kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi
zitakwama. Kada ya Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa ni kiungo muhimu kati ya wananchi Vijijini na
Mitaani na Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Jiji.
Ni vizuri kujikumbusha kwamba katika mafunzo haya tunasisitiza Utendaji na siyo Utawala.
Tofauti kati ya Utawala na Utendaji ni kwamba Utawala unaundwa na kuongozwa na uongozi
wa kuchaguliwa. Utendaji unaundwa na kuendeshwa na watumishi wa kuajiriwa. Pia ni muhimu
kuelewa kwamba utendaji chini ya Serikali umegawanyika katika sehemu kuu mbili. Kuna utendaji
chini ya Mamlaka ya Serikali Kuu katika ngazi mbalimbali za nchi, kwa mfano, Taifa (Mkuu wa Nchi/
Rais), Mkoa (Mkuu wa Mkoa), Wilaya (Mkuu wa Wilaya na Tarafa (Afisa Tarafa). Aidha, kuna utendaji
4.0 KAZI, WAJIBU NA HAKI ZA AFISA MTENDAJI WA
KIJIJI NA MTAA
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
56
ambao ni chini ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa, hususan katika ngazi za Halmashauri (Mkurugenzi
wa Halmashauri), Kata (Afisa Mtendaji wa Kata), Kijiji (Afisa
Mtendaji wa Kijiji) na Mtaa (Afisa Mtendaji wa Mtaa). Hata hivyo, ni vema ieleweke kuwa kwa
sehemu zote mbili za utendaji, Kiongozi na Mtendaji Mkuu ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
4.3 SIFA ZA AFISA MTENDAJI BORA WA KIJIJI NA MTAA
Ili kuwa na utawala na utendaji bora ni lazima Afisa Mtendaji bora awe na sifa zifuatazo:
a) Awe Mraghbishi
Mraghbishi ni mtu yeyote anayewezesha wananchi kupata ari ya kupenda kujiletea
maendeleo kwa kutumia zaidi ubunifu wao na rasilimali walizo nazo. Mtu huyo anaweza
ama kutoka nje ya jamii au ndani ya jamii yenyewe. Afisa Mtendaji mraghbishi anapaswa
kuwa na sifa zifuatazo:-
Mwadilifu yaani:-
–– Anayejituma na ambaye yuko tayari kufanya kazi bila kujali muda;
–– Mpole na mtulivu;
–– Anayejali watu na kuwa tayari kuishi, kufurahi na kuhuzunika nao;
–– Anayependa uwazi, ukweli na kuwajibika;
–– Anayejiamini na kuamini wengine
–– Mwaminifu (asiyejishirikisha katika wizi, udanganyifu, ubadhirifu na rushwa;
b) Anayeelewa na kuvumilia tabia za watu;
c) Anayesikiliza shida za watu na kuwawezesha kuzitafutia ufumbuzi;
d) Anayewashirikisha watu katika maamuzi bila ubaguzi;
e) Ambaye yuko tayari kujikosoa, kukosoa na kukosolewa;
f) Mwenye upeo mpana wa kupambanua mambo ya maana na upuuzi na asiyetumia lugha ya kihuni;
g) Anayependa kujifunza na kukubali mabadiliko;
h) Anayetoa habari na taarifa ambazo watu wanahitaji na ambazo hawawezi kupata bila msaada
wake;
i) Mwenye tabia ya kupenda kujadiliana na kuzungumza na watu ana kwa ana;
j) Anayependa kufanya kazi za maendeleo na watu wote Vijijini, Vitongojini na Mitaani;
k) Awe na uwezo wa kusimamia utekelezaji wa sheria, kanuni na taratibu bila upendeleo,
huruma wala woga;
l) Awe na uwezo wa kutoa taarifa sahihi zitakiwazo katika ngazi za juu.
m) Asiye toa siri za serikali.
MADA YA NNE
57
10
9
8
7
6
5
11
12
13
4.4 KAZI NA WAJIBU WA AFISA MTENDAJI WA KIJIJI
Kutokana na Waraka wa Maendeleo ya Utumishi wa Serikali za Mitaa Namba
30 wa mwaka 2003, kazi na majukumu ya Afisa Mtendaji wa Kijiji ni kama yafuatayo:-
• Atakuwa Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Kijiji na Kamati zake katika kupanga
mipango ya maendeleo na utekelezaji wa mipango;
• Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Kijiji na atasimamia mapato na matumizi ya Serikali ya Kijiji;
• Atakuwa Mlinzi wa Amani na msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji;
• Ataratibu na kusimamia upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji;
• Atakuwa Katibu wa Serikali ya Kijiji;
• Atatafsiri sera, taratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo za Serikali ya Kijiji;
• Ataratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuziwasilisha
kwenye Halmashauri ya Kijiji na baadaye kwenye Mkutano Mkuu wa Kijiji na Kata;
• Ataratibu vikao vya maendeleo ya Kijiji vitakavyowahusisha wananchi na wataalam waliopo
kwenye eneo lake;
• Atasaidia katika mikakati mbalimbali ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji
mali;
• Atasimamia na kuratibu matumizi bora ya nguvu kazi;
• Atakuwa Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalam katika Kijiji;
• Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi, Wataalam mbalimbali na NGO
zilizopo katika Kijiji.
4.5 KAZI NA WAJIBU WA AFISA MTENDAJI WA MTAA
Kufuatia marekebisho ya Waraka wa Maendeleo ya Utumishi wa Serikali za
Mitaa Namba 31 wa mwaka 2003, kazi na majukumu ya Afisa Mtendaji wa
Mtaa ni kama yafuatayo:-
• Atasimamia utekelezaji wa Sera za Halmashauri;
• Ataishauri Kamati ya Mtaa kuhusu mipango ya maendeleo ya Mtaa;
• Atasimamia utekelezaji wa sheria ndogo pamoja na sheria nyingine zinazotumika katika
eneo la Mtaa;
• Ataishauri Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya ulinzi na usalama;
• Atasimamia utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na umaskini;
• Atakuwa Afisa Mhasibu wa Kamati ya Mtaa;
• Ataandaa na kutunza Rejesta ya wakazi wote wa Mtaa;
• Atakuwa msimamizi wa wataalam wanaofanya kazi katika Mtaa;
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
58
• Atasimamia ukusanyaji wa mapatao ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa
kodi wote;
• Atakuwa Mtendaji Mkuu katika Mtaa;
• Atafanya kazi yoyote atakayoagizwa na Katibu Tarafa au Mkurugenzi wa Halmashauri.
4.6 HAKI ZA MTUMISHI WA UMMA
4.6.1 Mtumishi wa Umma anayeanza kazi
Kwa mujibu wa Kanuni ya 13 (a) na (b) ya Kanuni za Utumishi wa Umma ,Tangazo la Serikali Na.168
la mwaka 2003, mtumishi wa umma anayeanza kazi ana haki ya kupewa;
• Usafiri, yeye,, mwenzi wake, watoto wasiozidi wanne na wategemezi wasiozidi wawili
kutoka kwao hadi katika kituo chake cha kazi.
• Posho ya kuanza kazi kama itakavyopangwa mara kwa mara na Katibu Mkuu (Utumishi)
4.6.2 Muda wa Matazamio na Kuthibitishwa Kazini
Kwa mujibu wa Kanuni ya 14 (1) na (2) (a), (b) na (c) ya Kanuni za Utumishi wa Umma,Tangazo la
Serikali Na.168 la mwaka 2003, na sehemu D.40 na D.43 ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa
Umma za mwaka 2009 mtumishi wa umma anayo haki ya kupata;
• Muda wa matazamio Usiozidi miezi 12
• Msimamizi wa mtumishi wa Umma anapaswa miezi mitatu kabla ya muda wa matazamio
kuisha kuamua kama:-
• Mtumishi athibitishwe kazini, au
• Muda wa matazamio uongezwe, au
• Ajira ivunjwe
4.6.3 Likizo ya mwaka
Kwa mujibu wa sehemu H.1 (1), (2) na (3) ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka
2009 na Kanuni ya 97 (1) na (2) ya Kanuni za Utumishi wa Umma Tangazo la Serikali Na.168 la
mwaka 2003, likizo ya mwaka ni;
• Ni haki ya Mtumishi
• Itakuwa siku 28
• Itatolewa mara moja kila mwaka
• Likizo ya malipo itakuwa kila baada ya mwaka mmoja, ( sehemu H.5 (b) ya Kanuni za
Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009)
• Atakayezuiliwa likizo atalipwa mshahara wa mwezi mmoja kama fidia
MADA YA NNE
59
10
9
8
7
6
5
11
12
13
• Anayeanza kazi kwa mara ya kwanza atapewa likizo ya mwaka baada ya kumaliza miezi
minane
• Malipo ya likizo yatatolewa kwa mtumishi, mwenzi wake, watoto wasiozidi wanne wasiozidi
miaka kumi na minane au wategemezi
• Likizo ya dharura haitazidi siku kumi na nne kwa mwaka
• Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa anaruhusiwa kwenda likizo mahala popote ili mradi
gharama isizidi ile ya kwenda nyumbani kwake.
4.6.4 Likizo ya Uzazi kwa Wanawake
Kwa Mujibu wa sehemu ya H.12 (1-7) ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009,
likizo ya uzazi;
• Itatolewa kwa mtumishi wa umma wa kike kila baada ya miaka mitatu (3)
• Itakuwa ya siku 84 akijifungua mtoto mmoja (1) na siku mia moja (100) akijifungua watoto
zaidi ya mmoja
• Haitaingiliana na likizo ya kawaida ya mwaka
• Ujauzito ukiharibika au mtoto akifariki ndani ya miezi 12 baada ya kujifungua atastahili haki
ya likizo ya uzazi katika ujauzito utakaofuata bila kujali masharti ya miaka mitatu
• Mtumishi atastahili ruhusa ya masaa mawili kabla ya muda wa kumaliza kazi ili kuwahi
kunyonyesha, kwa muda wa miezi sita baada ya kumaliza likizo ya uzazi
4.6.5 Likizo ya Uzazi kwa Wanaume
Sehemu H.13 (a) na (b) ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009, inatamka
kuwa, likizo ya uzazi kwa wanaume;
• Itatolewa kwa mtumishi wa Umma wa Kiume ambaye mkewe amejifungua
• Itatolewa mara moja katika miaka mitatu
• Itakuwa ya siku tano (5)
• Haitaingiliana na likizo ya kawaida ya mwaka
• Itachukuliwa ndani ya siku 7 baada ya mtoto kuzaliwa
4.6.6 Likizo ya bila malipo
Kwa mujibu wa Kanuni ya 99 (1) na (2), ya Kanuni za Utumishi wa Umma tangazo la Serikali Na.198
la mwaka 2003, na sehemu ya H.19 (1) na (2) ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za
mwaka 2009, likizo ya bila malipo kwa Mtumishi Itaombwa kwa Katibu Mkuu Utumishi kupitia kwa
mwajiri wake.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
60
4.6.7 Likizo ya Ugonjwa
Kwa mujibu wa Kanuni ya 100 (1) na (2) ya kanuni za Utumishi wa Umma tangazo la Serikali Na.
168 la mwaka 2003, likizo ya ugonjwa;
• Itatolewa baada ya mapendekezo ya daktari
• Itatolewa na Mamlaka ya Ajira (Mwajiri)
• Itakuwa ya mshahara kamili kwa miezi 6
• Nusu mshahara kwa miezi 6 inayofuata
• Baada ya hapo mtumishi atastaafishwa kazi kwa ugonjwa.
4.6.8 Likizo ya Kustaafu
Kwa mujibu wa kanuni ya 102 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, Mtumishi wa
umma atapewa likizo ya kustaafu kabla ya tarehe yake ya kustaafu.
4.6.9 Kupanda Madaraja ya Utumishi Wa Umma
• Kwa mujibu wa marekebisho ya Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2008 upandaji
wa madaraja utaongozwa na Muundo wa Utumishi na mfumo wa Wazi wa Upimaji wa
Utendaji Kazi wa Watumishi (OPRAS), Mfumo ambao Unazingatia Utendaji Kazi, Ujuzi na
Sifa binafsi.
4.6.10 Matibabu
Kwa mujibu wa kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009, sehemu K.1 (1) and (2),
Matibabu ya Mtumishi yatagharamiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) isipokuwa kwa
magonjwa ambayo hayagharamiwi na mfuko yatagharamiwa na mwajiri.
• Mtumishi atalipwa posho ya kujikimu na nauli anapokwenda kutibiwa nje ya kituo chake
cha kazi.
4.6.11 Uhamisho
Kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, kifungu cha 107 (1)-(5) mtumishi
atapewa uhamisho kwa kuzingatia yafuatayo;
• Endapo ni kwa manufaa ya Umma mtumishi wa umma anaweza kuhamishwa toka kituo
kimoja kwenda kingine
• Maslahi ya uhamisho ni:-
• Posho ya kijikimui kwa siku kumi na nne kwa mtumishi na mwenzi wake na nusu ya
kiwango kwa watoto kwa siku kumi na nne (Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, za
mwaka 2009 sehemu ya L.5 (1) and (2)
MADA YA NNE
61
10
9
8
7
6
5
11
12
13
• Posho ya usumbufu - kwa kiwango cha asilimia kumi (10%) ya mshahara wa mwaka
mzima (Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009, sehemu L.13 (1) na (2)
• Usafirishaji wa mizigo tani tano (5)
4.6.12 Fidia ya Kuumia au Kufa Ukiwa Kazini
Kwa mujibu wa Kanuni ya 110 ya kanuni za Utumishi wa Umma Tangazo la Serikali Na.168 la
mwaka 2003, mtumishi wa umma ana haki ya kulipwa fidia anapoumia au kufariki akiwa kazini.
4.7 HITIMISHO
Mada hii imeelezea kazi, wajibu na haki za Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa. Afisa Mtendaji wa
Kijiji na Mtaa anapaswa kuelewa vema kazi na wajibu wake kwa vile yeye ndiye mtendaji mkuu
na mtekekezaji wa majukumu yaliyoelezwa. Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa anapaswa kuzingatia
mipaka yake ya madaraka ili kuondoa migongano kati yake na viongozi wa kuchaguliwa. Afisa
Mtendaji wa Kijiji na Mtaa anapaswa kuelewa kuwa yeye si mtawala ndani ya Kijiji na Mtaa bali
ni mtendaji mkuu wa shughuli za maendeleo katika eneo lake. Vilevile, Afisa Mtendaji wa Kijiji na
Mtaa anapaswa kusoma na kuzielewa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma kwa ajili ya
kuboresha utumishi wake na kujua haki zake za msingi.
Marejeo
• Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977
• Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma (Standing Orders, 2009)
• Sheria ya Utumishi wa Umma, Na.8, 2002 na kanuni zake za mwaka 2003
• Sera ya Menejimenti na ajira katika Utumishi wa UMMA Toleo la pili, 2008
• Mafunzo ya Awali ya Maafisa (2004)
• Waraka wa Maendeleo ya Utumishi wa Serikali za Mitaa Na. 30 wa mwaka 2003. Ofisi ya
Rais, Tume ya Utumishi wa Serikali za Mitaa – Dodoma.
• Waraka wa Maendeleo ya Utumishi wa Seriakli za Mitaa Na. 31 wa mwaka 2003. Ofisi ya
Rais, Tume ya Utumishi wa Serikali za Mitaa – Dodoma.
• Uongozi Bora kwa Wenyeviti wa Serikali za Vijiji, Vitongoji na Mitaa Tanzania Bara. Ofisi ya
Rais, TAMISEMI-Dodoma.
62
10
9
8
7
6
5
11
12
13
MADA YA TANO 5 WAJIBU WA AFISA MTENDAJI WA KIJIJI NA MTAA KAMA
MLINZI WA AMANI
64
MADA YA TANO
65
10
9
8
7
6
11
12
13
5.1 UTANGULIZI
Mada hii inaeleza wajibu na Maafisa Watendaji wa Vijiji/Mitaa kama walinzi wa amani katika maeneo
yao na dhana ya ulinzi shirikishi. Mada hii ni muhimu sana kwa maafisa hao kwani itawawezesha
kuisaidia jamii kushiriki kikamilifu katika ulinzi na mali zao.
Lengo la mada hii ni kumpatia uelewa Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa kutekeleza wajibu wake kama
mlinzi wa amani katika eneo lake.
5.2 DHANA YA MLINZI WA AMANI
Dhana ya Mlinzi wa amani kama zilivyo dhana nyingine za kisheria hapa nchini ilianzia nchini
uingereza. Dhana hii inahusiana sana dhana ya“Law and Order” ambayo kimsingi ni jukumu la
Polisi. Dhana hii ilianza kutokana na sababu zifuatazo:-
• Kutokuwapo na Polisi wa kutosha wa kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa na kuna utulivu wa
kutosha miongoni mwa wananchi
• Haja ya kuwahusisha wananchi ili wajue umuhimu wa kuzingatia sheria kwa ajili ya kudumisha
amani na utulivu;
• Katika jamii kulikuwapo na watu wa kawaida walioheshimika na kutokana na kuheshimika kwao
ilionekana kwamba watu haowangeweza kupewa mamlaka ya kuwakamata watuhumiwa.
• Pamoja na kupewa mamlaka haya, kulikuwepo na kanuni zamaadili zilizozuia mamlaka haya
kutumiwa vibaya.
Kwa hiyo, mbali na kudumisha sheria na utulivu, walinzi wa amani pia walikuwa na uwezo wa
kusuluhisha mambo madogo madogo. Watu walioheshimika katika jamii ambao walipewa mamlaka
ya ulinzi wa amani walikuwa pia na uwezo wa kutamka kauli ya kuamua kama raia mmoja ni mtu
mwema au la pale uthibitisho huo ulipohitajika.
5.0 WAJIBU WA AFISA MTENDAJI WA KIJIJI NA MTAA
KAMA MLINZI WA AMANI
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
66
5.3 ULINZI WA AMANI WAKATI WA UKOLONI NA WAKATI WA UHURU
• Ulinzi wa amani wakati wa Ukoloni
Wakoloni walipofika hapa nchini hawakuweza kutumia utaratibu wa kumtafuta mtu mwenye
kuheshimika katika jamii ili awe mlinzi wa amani, kwa sababu haikuwa nia yao kuwapa mamlaka
hayo wenyeji. Azma ya wakoloni ilikuwa ni kuweka mamlaka za aina mbalimbali katika chombo
kimoja na kwa hiyo madaraka ya ulinzi wa amani walipewa watawala wa maeneo husika. Huo ndio
ukawa mwanzo wa kuunganisha mamlaka ambayo kwa asili yake ni ya kipolisi pamoja na mamlaka
ya utawala.
• Ulinzi wa Amani wakati wa Uhuru
Wakati wa Uhuru kulikuwa na utaratibu wa kuchanganya mamlaka ya ulinzi wa amani na utawala
unaotumika mpaka sasa.
5.4 MAANA YA ULINZI WA AMANI NA SABABU ZA KUWA NA WALINZI WA AMANI
Walinzi wa Amani ni Maafisa au watumishi wa umma ambao hupewa madaraka na sheria
zilizotungwa na Bunge kufanya kazi kama Polisi na Mahakimu kwa madhumuni ya kulinda amani
katika maeneo ambayo wao ni viongozi wa kiserikali.
Kuna sababu mbili za kuwateua Walinzi wa Amani:
• Kuhakikisha amani na utulivu vinadumishwa katika maeneo yote katika nchi yetu ambako
mara nyingi huwa hakuna Hakimu wala Polisi ambaye anaweza kuchukua hatua mara moja
panapostahili.
• Kusaidia Mahakama za mwanzo wakati Hakimu hayupo au anazungukia Mahakama. Walinzi wa
amani wanawasaidia Mahakimu kwa kuchukua hatua ya kuhakikisha kwamba taratibu za kesi
za jinai na za madai zinakuwa tayari kwa ajili ya kusikilizwa na wahusika wameitwa kuhudhuria
Mahakamani wakati Hakimu atakapokuwepo Mahakamani.
5.5 MLINZI WA AMANI NI NANI
Kwa mujibu wa sheria ya Mahakama za Mahakimu Na. 2 ya 1984 (kif. 51) walinzi wa Amani ni:-
• Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa au Jiji
• Afisa Tarafa
• Maafisa Watendaji wa Vijiji/Mtaa.
MADA YA TANO
67
10
9
8
7
6
11
12
13
5.6 MADARAKA YA MLINZI WA AMANI
• Mlinzi wa Amani anaweza kukamata au kuamrisha kukamatwa kwa yeyote ambaye
anamshuhudia akifanya kosa la jinai.
• Aidha Mlinzi wa Amani anaweza:
• Kupokea malalamiko ya mdomo au ya maandishi toka kwa mlalamikaji. Mlinzi wa Amani
atamchunguza mlalamikaji na kama ataridhika kuwa kuna sababu za msingi atatoa samansi au
hati ya kukamatwa kwa mtu aliyetuhumiwa na mlalamikaji;
• Mlinzi wa Amani hatakiwi kutoa hati ya kukamatwa mtu mpaka aridhike kwamba mtu
aliyeshitakiwa anapaswa kuwekwa rumande ili kusubiri kesi au kama mlinzi wa amani ataona
kuwa mtu huyo hawezi kutii amri ya kuitwa shaurini. Tahadhari: Inasisitizwa kwamba Mlinzi wa
Amani lazima akumbuke kila wakati kuwa kumweka mtu chini ya ulinzi ni kumwondolea uhuru
wake. Kabla ya kumweka mtu rumande au jela mlinzi wa amani lazima kila wakati ajiridhishe
kuwa kuna uwezekano mkubwa wa mtuhumiwa:
• Kutoroka au kukataa kuhudhuria Mahakamani, au
• Kuvuruga ushahidi, au
• Kuwa kero kwa jamii, au
• Ametenda kosa kubwa na uchunguzi utazuiliwa
• Ikiwa mtuhumiwa hakuwekwa chini ya ulinzi.
• Ikiwa hati ya kukamatwa imetolewa na kuelekezwa kwa Afisa wa Polisi huyo anaweza
kuruhusiwa na mlinzi wa amani kumwachia mtuhumiwa kwa dhamana ya fedha maalum.
Tahadhari: Katika maeneo ya vijijini kwa kawaida kunakuwa hakuna Afisa wa Polisi ambaye
anaweza kupewa amri ya kukamatwa; hati ya kukamatwa mara nyingi itaelekezwa na Mhudumu wa
Mahakama au wa Halmashauri, ingawa watu hawa hawajapewa madaraka /uwezo wa kumwachia
mtuhumiwa;
• Kila hati ya kuitwa shaurini au hati ya kukamatwa itakuwa katika fomu maalum zinazopatikana
katika Mahakama;
• Hati ya kuitwa shaurini inapaswa kupewa mtu binafsi anayehusika isipokuwa kama mlinzi wa
amani ataridhika kwamba mtu mwenyewe binafsi hawezi kupatikana au hawezikupatikana bila
kuchelewa, basi ataagiza hati hiyo ipelekwe kwa njia ya rejesta au kwa kuibandika sehemu ya
wazi ya eneo mtu huyo inaposemekana yupo, au kuiacha kwa mtu mzima mwanamume wa
familia yake, au mtumishi mtu mzima wa kiume anayeishi naye;
• Hati ya kuitwa shaurini kwa mdaiwa katika kesi ya madai ieleze kwa kifupi aina ya madai
yanayofanywa dhidi ya mdaiwa;
• Ikiwa kama mtu ataitwa kutoa hati Fulani Mahakamani itatosheleza kama hati hiyo itatolewa hata
kama yeye binafsi asipotokea;
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
68
• Katika kesi zote, za jinai au za madai, ikiwa hati ya kuitwa shaurini imepokelewa na mtu
mwenyewe binafsi lazima nakala moja ya hati hiyo aachiwe mtu huyo na nakala iliyosainiwa na
mtu huyo irudishwe Mahakamani.
Kwa mujibu wa sheria ya Mahakama ya Mahakimu Na. 2 ya 1984 kifungu cha 56 (b) (ii) Mlinzi wa
Amani ambaye ameteuliwa kuwepo Mahakamani haruhusiwi kumweka mtu rumande kwa muda wa
zaidi ya siku saba kwa wakati mmoja lakini ikiwa utaratibu wa kawaida wa mawasiliano kwenda kwa
Hakimu aliye karibu utakuwa umevunjika Mlinzi wa Amani ataweza kumweka mtu rumande kwa siku
zisizozidi ishirini na nane kwa ujumla wake.
5.7 MSIMAMIZI WA WALINZI WA AMANI
Walinzi wa Amani watakuwa chini ya uangalizi wa Hakimu ambaye Mahakama yake iko katika eneo
ambamo Walinzi wa Amani wamepangwa, na chini ya uangalizi wa Hakimu Mkazi Mfawidhi. Walinzi
wa Amani watapaswa kuwatii Mahakimu hao. Maafisa Watendaji wa Vijiji wanatakiwa kuapa kabla
ya kuanza kutekeleza shughuli za ulinzi wa amani. Ieleweke kwamba kabla ya Afisa kuapa hawezi
kutekeleza majukumu ya ulinzi wa amani.
5.8 UWEZO WA AFISA MTENDAJI WA KIJIJI/MTAA KUKAMATA AU KUAGIZA
KUKAMATA WATUHUMIWA
Uwezo wa Maafisa Watendaji wa Vijiji/Mitaa kukamata watuhumiwa mbalimbali unatokana na sheria
mbalimbali kulingana na aina ya madaraka husika. Maafisa Watendaji wa Vijiji wamepewa uwezo wa
kukamata au kuagiza kukamata na Sheria zifuatazo:-
• Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Namba 7 ya mwaka 1982
• Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) namba 8 ya mwaka 1982.
• Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai Namba 9 ya mwaka 1985.
• Sheria ya Mahakama za Mahakimu Namba 2 ya mwaka 1984.
Sheria ya Serikali za Mitaa namba 7 ya mwaka 1982 kifungu 177 (Mamlaka za Wilaya)
Sheria hii inampa uwezo Afisa Watendaji wa Kijiji kukamata watuhumiwa watakaotuhumiwa kuvunja
Sheria Ndogo za Halmashauri au Kanuni zilizotolewa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria.
Kwa mantiki hii, Maafisa Watendaji wa Vijiji wa Mamlaka za Wilaya wana uwezo wakuwakamata.
watuhumiwa wanaotuhumiwa kuvunja Sheria Ndogo za Halmashauri za Wilaya na Vijiji Kifungu
cha 177 (1) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Namba 7 ya mwaka 1982 kinampa
uwezo Afisa Mtendaji wa Kijiji kumkamata mtu yeyote ambaye anatuhumiwa kuvunja Sheria Ndogo
zilizotungwa na Halmashauri ya Wilaya.
MADA YA TANO
69
10
9
8
7
6
11
12
13
Sheria ya Serikali za Mitaa Namba 8 ya mwaka 1982 (Mamlaka za Miji)
Sheria hii inawapa uwezo Maafisa Watendaji wa Kata wa Mamlaka za Miji yaani Halmashauri za
Manispaa, Jiji na Miji wa kukamata mtu yeyote katika Kata yake ambaye anatuhumiwa kuvunja
Sheria Ndogo za Halmashauri (kifungu cha 91 (1). Aidha, kifungu cha 91 (2) kinampa Mkuu wa Mkoa
na Mkuu wa Wilaya uwezo wa kumwagiza mtumishi wa Mamlaka za Miji kukamata mtu yeyote
ambaye anatuhumiwa kuvunja Sheria Ndogo yeyote ya Halmashauri.
Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai Namba 9 ya mwaka 1985 (Criminal Procedure Act
Number 9 of 1985)
Sheria hii inawapa uwezo Maafisa Watendaji wa Vijiji kukamata au kuagizwa kukamatwa kwa mtu
yeyote anayehisiwa kufanya kosa lolote chini ya sheria za Tanzania. Kifungu cha 13 (1) (a) na (b)
kinawapa uwezo Maafisa Watendaji wa Vijiji kama ifuatavyo:-
• Kutoa hati ya kukamata mtu yeyote na kumleta mbele yake ili atoe maelezo kuhusu malalamiko
yaliyotolewa dhidi yake; au
• Kutoa hati ya kuitwa Mahakamani kujibu taarifa ambazo zimetolewa dhidi ya mtuhumiwa huyo.
Masharti na Mipaka Chini ya Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai
Sheria hii inatoa masharti ambayo ni lazima yazingatiwe kabla ya Maafisa Watendaji wa Vijiji kutoa
hati ya kukamata. Masharti hayo ni pamoja na :-
Kuwepo na kiapo kinachoeleza sababu za kutolewa kwa hati hiyo;
Kuwepo kwa maelezo ya kawaida kama itakavyoagizwa na Afisa Mtendaji wa Kata/Kijiji/Mtaa;
• Afisa Mtendaji wa Kijiji lazima aridhike kuwa kuna SABABU ZA MSINGI za kutoa hati hiyo.
• Hati hiyo itakayotolewa lazima ieleze kosa ambalo mtu huyo anatuhumiwa.
• Kuwe na ushahidi au maelezo kuwa mtu huyo hawezi kufika Mahakamani pale atakapohitajika
kufanya hivyo.
• Aidha inasisitizwa katika kifungu cha 12 cha Sheria hii, kuwa haitakiwi kutumia nguvu zaidi ya
zile zinazohitajika kufanikisha kumkamata mtuhumiwa.
Namna ya kumkamata mtuhumiwa
Sheria ya mwenendo wa makosa ya Jinai namba 9/1985 inaeleza namna ya kumkamata mtuhumiwa.
Kifungu cha 11 (1) cha sheria hii kinataka mtu anayemkamata mtuhumiwa kufanya yafuatayo:-
• Kumgusa mtuhumiwa na kumueleza kuwa yuko chini ya ulinzi
• Kumtia pingu na kumpeleka Mahabusu
• Endapo mtuhumiwa atapinga kukamatwa kwa utaratibu wa hapo juu, Basi NJIA ZOZOTE
ZINAZOWEZA KUFANIKISHA KUKAMATWA KWAKE zitatumika ili kufanikisha kukamatwa huko.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
70
Sheria ya Mahakama za Mahakimu Namba 2 ya mwaka 1984
Sheria hii ndiyo inayoanzisha cheo cha Mlinzi wa Amani ambapo Kifungu cha 51 kinampa Waziri wa
Sheria uwezo wa kuteua watu wengine, (mbali ya Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tarafa)
kuwa walinzi wa amani. Waziri kwa kutumia madaraka yake yaliyo katika kifungu hiki amewateua
Maafisa Watendaji wa Vijiji kuwa walinzi wa amani katika maeneo yao.
5.9 KINGA DHIDI YA MASHTAKA YA MADAI
Sheria ya Mahakama za Mahakimu inatoa kinga kwa Mlinzi wa Amani kutotakiwa kulipa fidia au
kuwajibika kwa matendo aliyoyafanya kama Mlinzi wa Amani pale yafuatayo yatakapozingatiwa:-
• Kama Mlinzi wa Amani aliamini au alikuwa na sababu ya kuamini kuwa mtuhumiwa alitenda kosa
ambalo lilisababisha kukamatwa kwake.
• Kama aliagiza kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kwa nia njema (in good faith)
• Kama alifanya hivyo akiwa kazini au akiwa anatekeleza majukumu yake aliyopewa kisheria.
• Kwa walinzi wa amani ambao wameteuliwa kuwepo Mahakamani hawaruhusiwi kumweka mtu
rumande kwa muda wa zaidi ya siku saba kwa wakati mmoja na endapo utaratibu wa kawaida
wa mawasiliano kwenda kwa Hakimu aliye karibu utakuwa umevunjika basi ataweza kumweka
rumande kwa siku zisisozidi 28 kwa jumla.
5.10 VIGEZO VYA KUTUMIKA KUMKAMATA
Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa anapofikiria au kukusudia kumkamata mtuhumiwa anatakiwa kupima
vigezo hivi na kujiuliza kama kweli kuna haja ya kumkamata mtuhumiwa au anaweza kumueleza
mtuhumiwa aende Polisi au Mahakamani yeye mwenyewe. Vigezo hivyo ni kama ifuatavyo:-
• Uwezekano wa mtuhumiwa kukimbia;
• Uwezekano wa mtuhumiwa kukataa kuhudhuria Mahakamani au kufika Polisi pale anapotakiwa
kufanya hivyo;
• Nafasi ya mtuhumiwa akiwa huru kama anaweza kuharibu upelelezi au ushahidi;
• Kama kuna ushahidi kuwa mtuhumiwa akiwa huru anaweza kuleta uvunjaji wa amani;
• Aina ya kosa ambalo anatuhumiwa kulifanya kama ni kubwa mno na kwamba atasababisha
uchunguzi kuharibika.
Tahadhari Kazi ya ulinzi wa amani na madaraka na uwezo wa kukamata au kuagiza kukamatwa kwa
mtuhumiwa ni uwezo uliotolewa kwa mujibu wa sheria hivyo ni lazima masharti ya kisheria yazingatiwe
na kufuatwa katika kutekeleza madaraka haya. Aidha katika kuyatumia madaraka haya suala la haki za
binadamu linatakiwa kuzingatiwa kwa kiwango cha juu. Kwa kuwa madaraka na uwezo huu ni wa kipolisi hivyo
katika kutekeleza jukumu hili la kuwakamata wahalifu, Maafisa Watendaji wa Kata/Vijiji/Mitaa wanapaswa
kuongozwa na kutawaliwa na masharti, miiko na taratibu zinazoongoza na kutawala Jeshi la Polisi.
MADA YA TANO
71
10
9
8
7
6
11
12
13
5.11 ULINZI SHIRIKISHI (POLISI JAMII)
5.11.1 Utangulizi
Ni jukumu la msingi kabisa la Serikali za Mitaa kuihakishia jamii katika himaya yake, usalama wa
maisha, mali, amani na utulivu, ili kujiletea maendeleo na kuinua hali ya maisha. Afisa Mtendaji wa
Kijiji na Mtaa ni kiungo muhimu kati ya wananchi na Serikali.
5.11.2 Dhana ya Ulinzi Shirikishi
Ni mfumo wa utawala unaojikita zaidi kwenye dhana ya mwananchi kulinda nafsi yake, familia yake
na mali zake. Ni mkakati mpya wa utendaji wa Jeshi la Polisi wenye lengo wa kuweka mazingira ya
ushirikiano wa dhati baina ya wananchi na Jeshi la Polisi.
Ni dhana inayopanua malengo ya jeshi la polisi kutoka kwenye mtazamo wa kadri unaolenga
kwenye tukio moja au pengine aina moja tu ya uhalifu kwenda kwenye mtazamo mpana
unaohamasisha jeshi la polisi kulenga kwenye ufumbuzi endelevu wa matatizo ya jamii kwa ujumla
wake; likiwemo uhalifu wenyewe, woga wa kudhurika na uhalifu, vurugu na hali ya wasiwasi ndani
ya jamii na kuzorota au kutojali kwa jamii.
5.11.3 Mpango wa Polisi Jamii/ Ulinzi Shirikishi
Ni mpango unaoelezea mkakati wa mabadiliko ndani ya Jeshi la Polisi nchini ikiwa ni changamoto ya
dhana ya asili iliyotawala fikra za wananchi kwa muda mrefu ya kuhesabu shughuli/jukumu la kuweka
hali ya Usalama na Utulivu katika jamii kuwa ni jukumu la Jeshi la Polisi peke yake, jamii hubakia kuwa
wapokeaji wa maelekezo na miongozo ya Jeshi la Polisi bila ya mchango wao kuhitajika.
Mpango huu unalenga kubadili dhana hii ya asili na kufanya jukumu la kuweka Hali ya usalama na
utulivu katika jamii kuwa ni jukumu la Jamii nzima kwa maana ya kila mwananchi wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania.
5.11.3.1 Misingi Mikuu ya Polisi Jamii/ Ulinzi Shirikishi
• Jeshi la Polisi ni chombo cha kutoa huduma
Msingi mkuu wa kwanza ni mabadiliko katika tafsiri ya Jeshi la Polisi kutoka katika dhana ya
chombo cha mabavu na matumizi ya nguvu na kuwa chombo cha kutoa huduma kwa wananchi.
Namna pekee na sahihi ya kutafsiri mabadiliko haya ni kuwa na miundo ya uongozi na taratibu
zilizobuniwa mahususi za kuruhusu mashauriano baina ya jeshi la polisi na wananchi. Taratibu
hizi huwawezesha wananchi kuchangia mawazo na ufahamu wao katika mipango ya jeshi
la polisi na ikibidi kushiriki katika utendaji wa shughuli za polisi pia kuwawezesha wananchi
kuwaarifu polisi kuhusu kuridhika au kutoridhika kwao na huduma wanayopewa na jeshi la polisi.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
72
• Jeshi la Polisi ni Wawezeshaji
Mabadiliko katika ufafanuzi wa jeshi la polisi tofauti na mtizamo wa zamani jeshi la polisi
katika mpango wa polisi jamii shirikishi ni wataalamu wanao wezesha jamii kutatua matatizo
yao wenyewe na ikibidi kushirikiana na jeshi la polisi badala ya wao yaani jeshi la polisi kuwa
wataalamu wa kupambana na kutoa ufumbuzi wa matatizo. Kwa ufafanuzi huo, kazi za jeshi la
polisi zimekuwa ni kazi za kila mwananchi.
• Jeshi la Polisi na Jamii kupanga mipango ya pamoja
Ni mtizamo madhubuti wa jinsi ya kupanga mipango na mikakati ya utendaji wa jeshi la polisi
kwa imani kwamba jeshi la polisi kwa kufanya kazi pamoja na wananchi kwa pamoja wanaweza
kusaidiana kutatua matatizo yanayo ikabili jamii. Jeshi la Polisi liaandae mazingira ya kuwezesha
ushirikiano huo kwa kuondokana na fikra potofu za kujitenga na wananchi.
5.11.4 Umuhimu wa Ulinzi shirikishi
Faida za kuanzisha na kuendeleza ushirikiano baina ya jeshi la polisi na wananchi ni kama zifuatazo;
• Unasaidia wananchi kupeana habari zinazohusu vitendo vya uhalifu na kuchukua tahadhali
• Unawafanya wananchi kuwa makini kufuatilia kwa karibu nyendo za wahalifu, hivyo Wahalifu
kukosa fulsa au mwanya wa kufanya uhalifu kwenye maeneo ambayo mpango huu umeanzishwa
na kutekelezwa.
• Mpango huu unawaondolea wananchi hofu ya maisha na mali zao, hivyo kuishi kwa amani na utulivu.
• Mpango unasaidia wananchi kupata mafunzo na machapisho mbalimbali yanayohusu ulinzi na
usalama.
• Mpango unawawezesha wananchi;
• Kutoa mchango wa hali na mali katika juhudi za kuzuia uhalifu
• Kujua mbinu mbalimbali za kisasa za kuzuia uhalifu
• Kujua mbinu za kutoa taarifa za uhalifu kwa usahihi
• Kujua mbinu za kutambua mienendo, watu na shughuli zinazoashiria uhalifu
MADA YA TANO
73
10
9
8
7
6
11
12
13
5.11.5 Nafasi ya Afisa mtendaji wa Kijiji na Mtaa katika utekelezaji wa ulinzi
shirikishi
• Kushawishi wananchi katika kijiji/mtaa kuanzisha mtandao wa ulinzi shirikishi kwa kusirikiana na
kamati ya ulinzi na usalama ya kijiji na mtaa.
• Kuratibu shughuli zote za mtandao wa ulinzi shirikishi
• Kuitisha mikutano ya ujirani mwema, kutangaza mpango wa ulinzi shirikishi kwa nguvu zote ili
kila mwananchi aone umuhimu wa kushiriki katika ulinzi na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara
ili kujua maeneo yenye udhaifu ambayo yanaweza kutumiwa na wahalifu.
• Kushirikiana na Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya dola sambamba na askari wa Halmashauri
katika utelezaji wa mikakati ya kuzuia uhalifu na vurugu kwa kuihusisha jamii.
5.11.6 Nafasi ya wananchi katika utekelezaji wa ulinzi shirikishi
Kuna matukio mengi ya uhalifu yanayotokea miongoni mwa jamii na kusababisha madhara au hata
vifo. Baadhi ya matukio hayo ni kama; Unyang’anyi wa kutumia silaha, uvunjaji wa nyumba kwa
wizi, ubakaji, matumizi ya madawa ya kulevya, rushwa, unyanyasaji wa wanawake na watoto, wizi
wa mifugo na vitendo vingine vingi vya uhalifu.
Kutokana na changamoto hizo nafasi ya wananchi katika utekelezaji wa mpango wa ulinzi shirikishi ni;
• Kuwa macho na masikio ya jeshi la polisi kwa saa 24 kila siku
• Kushirikiana na polisi katika kutafuta ufumbuzi endelevu wa matatizo ya kiusalama
yanayojitokeza ndani ya jamii yao
• Kupanga mipango inayotekelezeka ya kujihakikishia usalama wa maisha na mali
• Kufichua wahalifu bila kuwaonea haya wala upendeleo hata kama ni watoto, ndugu au majirani ili
kuleta ufumbuzi endelevu wa tatizo la uhalifu
• Kutoa taarifa za matukio ya uhalifu kwa jeshi la polisi au uongozi wa kijiji na mtaa
• Kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi na kufanya doria katika maeneo yao ili kuhakikisha amani
na utulivu
5.12 HITIMISHO
Serikali za Mitaa zina wajibu wa kufanya shughuli za kipolisi zinazoangukia kwenye mamlaka zao
ili kuzuia vitendo vya uhalifu na vurugu katika jamii. Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa anawajibu wa
kuhakikisha amani, ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao katika neo lake ili kuwezesha ushiriki
wa jamii katika shughuli za maendeleo vilevile kuhamasisha jamii kushiriki katika mpango wa ulinzi
shirikishi.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
74
5.13 MAREJEO
• Sheria ya Mahakama za Mahakimu Na. 2 ya 1984
• Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Namba 7 ya mwaka 1982
• Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) namba 8 ya mwaka 1982.
• Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai Namba 9 ya mwaka 1985.
• Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
• Kipeperushi cha Mpango wa Ulinzi Jirani: Ushirikiano baina ya Jeshi la Polisi na Wananchi
• Polisi kata; Majukumu na mbinu za uwezeshaji wa Jamii, Jeshi la Polisi Tanzania
• Falsafa ya Polisi Jamii/Ulinzi shirikishi, Wizara ya Usalama wa Raia, Jeshi la Polisi Tanzania
• Utaratibu wa Kuanzisha Vikundi vya Ulinzi Shirikishi katika Shehia, Mtaa, Kijiji na Kitongoji, Jeshi
la Polisi Tanzania, 2008
• Jukumu la Kuzuia na Kupambana na Vitendo vya Uhalifu ni letu sisi sote, Jeshi la Polisi
Tanzania.
• Kipeperushi cha Polisi Jamii, Ulinzi Shirikishi; Programu ya Ushirikiano baina ya Jeshi la
Polisi na Wananchi, Jeshi la Polisi Tanzania.
MADA YA SITA 6 10
9
8
7
6
11
12
13
MBINU ZA MENEJIMENTI NA UONGOZI, SHERIA ZA KAZI NA
USULUHISHI WA MIGOGORO
76
MADA YA SITA
77
10
9
8
7
11
12
13
6.1 UTANGULIZI
Mada hii inaelezea kwa muhtasari misingi muhimu ya menejimenti na uongozi, Sheria Mpya za Kazi
pamoja na Usuluhishi wa Migogoro.
Lengo la mada hii ni kuwawezesha Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa ambao ndio wasimamizi
na waendeshaji wakuu wa shughuli za Serikali za Mitaa katika ngazi ya Kijiji na Mtaa, kuelewa kwa
ufupi dhana na Misingi ya Menejimenti na Uongozi, Sheria Mpya za Kazi pamoja na Usuluhishi wa
Migogoro ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
6.2 MAANA YA MENEJIMENTI
Tafsiri nyingi zimetolewa kuhusu maana ya menejimenti. Baadhi yake ni:-
• Breach, E.F.L. katika Kitabu chake “Misingi ya Menejimenti” – (Principles of Management) -
anaelezea Menejimenti kwamba ni uwajibikaji katika usimamizi kazi katika ofisi au kiwanda ili
kufikia malengo fulani.
• Dynier – Katika kitabu chake kinachohusu “Utawala wa Ofisi” – (Office Administration) –
anaelezea Menejimenti kwamba ni utaratibu wa utendaji kazi katika ofisi au kiwanda ili kufikia
malengo fulani.
Kama tunavyoona maelezo/tafsiri zote mbili zina uwiano kwa kiasi kikubwa. Hivyo, Menejimenti
ni utaratibu wa upangaji wa matumizi ya rasilimali zilizopo (watu, fedha, mitambo, majengo, ardhi,
muda na kadhalika), utendaji kazi, usimamizi na uratibu wake ikiwa ni pamoja na uwajibikaji sehemu
za kazi ili kufikia malengo au matarajio yaliyowekwa.
Utaratibu huu hujibu maswali yafuatayo:-
• Nini kitafanyika, lini na ni matokeo gani yanatarajiwa?
• Nani watafanya, watafanyia wapi na watafanya namna gani?
• Watatumia zana, vifaa, malighafi au fedha kiasi gani na zitatoka wapi?
• Usimamizi utafanyikaje na uwajibikaji na uratibu wa shughuli utakuwaje?
• Kila shughuli muhimu itachukua muda gani, na je shughuli nzima itachukua muda gani kukamilika?
6.0 MBINU ZA MENEJIMENTI NA UONGOZI, SHERIA ZA
KAZI NA USULUHISHI WA MIGOGORO
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
78
6.3 MISINGI YA MENEJIMENTI
Misingi ya Menejimenti imegawanywa katika maeneo yafuatayo:
Kupanga
Upangaji wa shughuli zitakazofanyika ni muhimu ili kufikia malengo kikamilifu. Afisa Mtendaji wa
Kijiji au Mtaa lazima aweke mpango mzuri wa kutenda shughuli zake ili malengo yafikiwe.
Kuratibu Watumishi
Ni muhimu kuwa na watumishi wenye ujuzi ili kazi zifanywe kwa ufanisi. Afisa Mtendaji wa Kijiji au
Mtaa sio mwajiri, ni msimamizi tu wa utendaji wa watumishi katika eneo lake ili wote wafanye kazi
kama timu moja. Vivyo hivyo, Watendajihawa inabidi waratibu utendaji kazi wa wananchi ili wafanye
kazi za kujenga Taifa kwa ukamilifu.
Kuongoza
Kuongoza ni kuonyesha njia au mwelekeo. Uongozi mzuri ni ule wenye mwelekeo wenye
kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu. Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa, kama kiungo cha idara
zote za Halmashauri, anatakiwa kuzielewa barabara sifa za kiongozi bora na kuzihusisha na
shughuli zake za kila siku ipasavyo. Uongozi ni mahusiano kati ya viongozi wa ngazi ya juu
na wale wanaoongozwa. Wenye kuongozwa ni vema wapate kiongozi mzuri mwenye uwezo
atakayehakikisha malengo ya ofisi/kiwanda yanafikiwa. Kwa hiyo, Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa ni
lazima awe ni mtu mwenye uwezo wa kuongoza ili malengo ya Halmashauri, Kata, Kijiji na Mtaa
yafikiwe.
Kudhibiti
Udhibiti ni muhimu katika utendaji kazi kwani unasaidia kuona kama kila mtumishi/mfanyakazi
ametekeleza majukumu yake ipasavyo. Udhibiti unasaidia kufikia malengo yaliyowekwa. Mtendaji
wa Kijiji/Mtaa anatakiwa adhibiti watumishi walio katika eneo lake ili kuona kama kila mmoja
anatekeleza wajibu wake ipasavyo.
MADA YA SITA
79
10
9
8
7
11
12
13
6.4 MBINU ZA MENEJIMENTI
Mbinu za Menejimenti hutumiwa kama nyenzo muhimu ya kutekeleza malengo rasmi kwa kutumia
watu na rasilimali nyingine walizonazo. Baadhi ya mbinu hizo ni:-
Kupanga
Hii ni njia ya kujiwekea malengo na taratibu za utekelezaji kwa kutumia rasilimali zilizopo kutekeleza
malengo hayo kwa njia yenye unafuu. Faida yake ni kwamba Mtendaji anapokuwa na tabia ya
kujiwekea utaratibu wa kutenda mambo, na baadaye kwa matumizi bora ya rasilimali zilizopo,
anaweza kupata ufanisi mkubwa zaidi.
Kuunda vikundi
Kuunda vikundi na kuvikabidhi wajibu na majukumu ya kutekeleza malengo fulani. Faida ya mbinu hii
ni kwamba Mtendaji sio lazima afanye kila kitu mwenyewe, bali anaweza kuwatumia watu alio nao.
Kuweka wasimamizi
Baada ya kuunda vikundi vya kazi lazima kuweka uongozi wenye uwezo na wajibu wa shughuli
hizo ili watoe usimamizi wa karibu. Vile vile, shughuli za usimamizi zinaweza kufanywa kwa
kutumia uandishi wa taarifa za utekelezaji kwa vipindi maalum. Taratibu za usimamizi zinawajibisha
watekelezaji.
Mbinu/Njia za udhibiti
Mipango, ratiba, makisio na taarifa mbalimbali ni mbinu za Menejimenti katika kudhibiti shughuli
za kiongozi. Njia hizi za udhibiti zinawezesha kupima utekelezaji na kulinganisha na malengo
yaliyokusudiwa na kusaidia kueleza sababu za kushindwa kufikia malengo.
Mbinu za Mawasiliano
Mtendaji/kiongozi lazima awasiliane na anaowaongoza kuhusu mambo yaliyokusudiwa kufanyika
na pia lazima apate taarifa za utekelezaji. Mbinu ya mawasiliano inaweza kutumika kuwahamasisha
wanaoongozwa kwa kutumia maelekezo ya mdomo au maandishi. Mtendaji anapaswa kuelewa
kinachotendeka wakati wote na kuwafanya anaowaongoza waelewe kwamba anaelewa
wanachofanya. Mawasiliano ni kigezo cha msingi katika kufanikisha malengo yote ya Serikali.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
80
Ushirikishwaji
Hii ni zana na mbinu ya msingi sana katika kufanikisha majukumu ya umma. Ushirikishwaji zaidi ya
kutegemea kanuni na sheria rasmi hutegemea pia mwenendo wa kiongozi anayehusika. Ni muhimu
pia wanawake washirikishwe kikamilifu katika uongozi , kwa sababu idadi yao ni kubwa na ndio
wazalishaji wakubwa. Mbinu za kuwashirikisha ni pamoja na kuwahamasisha wajitokeze kugombea
nafasi mbalimbali za uongozi na kuwapa majukumu, changamoto na misaada.
Utunzaji na Matumizi ya Takwimu na Kumbukumbu
Takwimu na kumbukumbu zilizoandaliwa na kutunzwa vizuri huwezesha wanakijiji kuandaa mipango
yenye uhakika zaidi.
6.5 MAANA YA UONGOZI
Kuongoza ni msingi mmojawapo wa Menejimenti. Kuongoza ni kuonyesha njia,kutangulia na
kuelekeza katika utekelezaji wa majukumu ya umma. Kuongozani kujenga moyo wa pamoja
miongoni mwa wanaoongozwa na kuwahamasisha ili watekeleze yale yaliyokusudiwa. Ili kiongozi
aongoze, lazima apate wafuasi ambao wanamkubali na kumfuata. Hivyo, ni jukumu la kiongozi
kujenga mazingira mazuri mahali pake ili kuhakikisha kuwa anakubalika.
Tendo la kuongoza ni kuwawezesha watu wamfuate na tendo hilo linahitaji busara. Lakini
inakubalika kwamba tendo hili linahitaji ujuzi pia ambao mtu anaweza kujifunza. Kwa msingi huo,
uwezo wa kuongoza ingawa umefikiriwa kuwa ni kipaji, hivi sasa unaonekana ni jambo linaloweza
kuletwa kwa kujifunza.
6.6 AINA ZA UONGOZI
Uongozi umegawanyika katika aina kuu tatu zifuatazo:
Uongozi wa Ki-imla
Hii ni aina ya uongozi ambapo mkubwa hutoa amri na kutekelezwa na anaowaongoza bila ya wao
kutoa kauli yeyote. Aina hii ya uongozi ambayo uamuzi hutolewa na mtu mmoja bila majadiliano au
ushirikishwaji, ingawa ni wa kizamani, bado unapatikana katika taasisi chache kama vile Majeshi.
Faida ya aina hii ya uongozi ni kuweza kufanikisha malengo kwa muda mfupi na unaweza kutumika
katika dharura. Hata hivyo aina hii ya uongozi inashindwa kujenga nidhamu ya kudumu kwa
wanaoongozwa. Uongozi huu unafanikiwa pale tu ambapo msimamizi yupo na akitoka,
wanaoongozwa huacha kufanya walichokusudiwa.
MADA YA SITA
81
10
9
8
7
11
12
13
Uongozi Huria
Uongozi huria hutoa madaraka makubwa kwa wanaoongozwa kufanya kila watakacho bila ya
maelekezo yoyote kutoka kwa viongozi. Kuwepo kwa uongozi huu, mara nyingi, ni dalili ya kushindwa
kwa kiongozi kuzingatia uwezo mkubwa wa wale wanaoongozwa katika kujisimamia wenyewe.
Uongozi huu una kasoro kubwa za kutofikia malengo na unashindwa kujenga moyo wa uwajibikaji
miongoni mwa wanaoongozwa.
Uongozi wa Kidemokrasia
Uongozi huu umezingatia kwamba wanaoongozwa wanao uwezo wa kujiamulia mambo
yanayowahusu. Kwa hiyo, kiongozi huwashirikisha na kuwashawishi wanaoongozwa wachangie
kwa mawazo na vitendo mambo ya kufanya. Pale ambapo hawajaelewa, kiongozi huwaelimisha na
kuwashauri mpaka watakapokubali.
Uongozi wa kidemokrasia tofauti na ule wa ki-imla, unalaumiwa kwa kufanya mambo polepole
na unachelewesha maamuzi. Uongozi huu una faida kwamba watu wakisha kubaliana na jambo
linalohusika wanalitekeleza hata wakati msimamizi hayupo maana tabia ya kulitekeleza imekuwa
ndani ya mioyo yao.
6.7 SIFA ZA KIONGOZI
Sifa za kiongozi ni nyingi na mara nyingi siyo rahisi kuziorodhesha zote. Kwa mfano, kiongozi awe
mvumilivu, awe na ujuzi juu ya kazi yake, awe mchapa kazi, awe na ushirikiano, jasiri, mwaminifu,
awe na uwezo wa kujieleza, awe mpenda watu na anayekubalika; n.k.
Kimsingi, sio rahisi kumpata kiongozi mwenye sifa zote ambazo, kwa kawaida,anatakiwa awe nazo.
Hata hivyo, kutokuwepo kwa watu walio na sifa zote za uongozi haina maana ya kutowepo na
uongozi bora. Kwa hiyo sifa pekee haziwezi kuzungumzia suala la uongozi.
Hali halisi pia inaweza kutumiwa kuzungumzia suala la uongozi. Hali halisi pia imetambua viongozi
wanapaswa kuwa na sifa kadhaa ambazo hutofautiana toka aina moja ya kazi kwenda nyingne.
Kwa maana hiyo ni kwamba watu wengi wanao uwezo wa kuwa viongozi bora kulingana na jinsi
wanavyozingatia maadili ya kazi zao na kujirekebisha ili kuweza kuwiana na mahitaji ya kazi hizo.
Kwa mfano, mwalimu anapaswa kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kujieleza kuliko mwanajeshi. Hali
kadhalika, mwanajeshi anapaswa kuwa na sifa ya ujasiri zaidi kuliko mwalimu.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
82
6.8 UHUSIANO KATI YA VIONGOZI NA WANAOONGOZWA
Uhusiano Rasmi
Kiongozi yeyote anapaswa kuzingatia kanuni ya uadilifu anapohusiana rasmi na wale
anaowaongoza. Kutekeleza kanuni hiyo kutamwezesha kiongozi kutekeleza kazi yake kwa haki,
nia njema na ufanisi. Kinyume cha uadilifu ni dhuluma, vitisho, rushwa, upendeleo na magendo
ambayo huipa Serikali sura mbaya mbele za wananchi. Uongozi ni dhamana na viongozi hawapaswi
kugeuza madaraka waliyopewa na umma na kuyatumia kwa manufaa yao. Nidhamu ya hali ya juu
inatakiwa kwa viongozi wanapotekeleza wajibu wao.
Uhusiano Usio Rasmi
Uhusiano usio rasmi mahali popote una umuhimu wake, na kuwa hauwezi kupuuzwa na viongozi
wanapotenda shughuli zao.Hivyo, kiongozi ana wajibu wa kutambua kuwepo kwa taasisi zisizo
rasmi na kufanya kila njia kuzitumia katika kunufaisha malengo yake. Kiongozi lazima ajitahidi
kushiriki katika shughuli mbalimbali za wanakijiji/mtaa ili ajenge hali ya kukubalika kwa mfano
mazishi, sherehe mbalimbali, kutambua na kuwaheshimu wazee wenye busara Kijijini, na
kuzungumza na vikundi mbalimbali vya ngoma, ushirika, ufundi na viongozi wa dini.
6.9 SHERIA MPYA ZA KAZI (Masuala Muhimu)
Mnamo mwaka 2004, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitunga Sheria Mpya za Kazi
ili kukidhi mahitaji ya mfumo wa kiuchumi na kijamii tulionao sasa hapa nchini. Sheria hizi ni Sheria
ya Ajira na Mahusiano Kazini, Namba 6 ya mwaka 2004 na Sheria ya Taasisi za Kazi, Namba 7 ya
mwaka 2004. Vipengele katika sheria hizi mbili vinahusika sana na kusimamia haki na wajibu katika
sekta binafsi. Ieleweke kuwa wafanyakazi katika sekta ya umma, ikijumuisha Maafisa Watendaji wa
Mitaa/Vijiji wanaongozwa na Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002. Sheria nyingine
zilizotungwa mwaka 2008 na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Sheria ya Mamlaka ya
Kusimamia Hifadhi ya Jamii Namba 8 ya mwaka 2008 na Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Namba
20 ya mwaka 2008. Sheria hizi zinalenga kuweka utaratibu kwa wafanyakazi kuweka akiba kwa ajili
ya mafao ya uzeeni na kuwa na mfumo utakaowezesha mfanyakazi anayeumia au kupata ulemavu
mahala pa kazi kulipwa fidia.
Lengo la mada hii ni kumuwezesha Afisa Mtendaji wa Kijiji/ Mtaa kujua masuala muhimu yahusuyo
haki stahili, wajibu, taratibu na kanuni zilizoainishwa katika sheria mpya za kazi ambazo kati ya
mambo mengine zimefuta mfumo wa zamani wa kushughulikia migogoro ya kikazi.
MADA YA SITA
83
10
9
8
7
11
12
13
Madhumuni Makuu ya Sheria Mpya za Kazi ni pamoja na:
• Kukuza maendeleo ya kiuchumi, tija na haki za jamii.
• Kutoa mwongozo wa kisheria kwa ajili ya mahusiano mazuri na haki ya ajira na viwango vya
msingi vya mazingira ya kazi
• Kutoa mwongozo wa majadiliano ya pamoja na hiari baina ya waajiri na wafanyakazi
• Kutoa mwongozo wa kutatua migogoro ya kazi kwa njia ya usuluishi, uamuzi na hukumu.
Matumizi ya Sheria
Sheria hizi zinawahusu waajiri na wafanyakazi waliopo kwenye sekta binafsi na za umma Tanzania
Bara isipokuwa Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Jeshi la
Kujenga Taifa. Pamoja na Sheria Mpya za Kazi, Watumishi wa umma, ikiwa ni pamoja na Maafisa
Watendaji wa Mitaa/Vijiji bado wanaongozwa na Sheria nyingine za Utumishi wa Umma ikiwa ni
pamoja na Sheria Na. 8 ya mwaka 2002, Sheria Namba 18 ya mwaka 2007.
Haki za Msingi na Ulinzi
Sheria inakataza ajira za watoto, kazi za shuruti, ubaguzi sehemu za kazi na inaruhusu kuanzisha na
kujiunga na vyama vya wafanyakazi na waajiri. Vile vile inamlinda mwananchi pale anapokuwa hana
nguvu za kupata kipato kwa sababu za umri na ulemavu.
Viwango vya Ajira (Ajira zenye staha)
Sheria imeweka viwango vya ajira (ajira zenye staha) ambavyo ni pamoja na saa za kazi, malipo ya
ujira, kiinua mgongo, likizo mbalimbali, kuacha na kuachishwa kazi na aina ya mikataba ya ajira.
Sheria Mpya za Kazi na Wajibu wa Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa
Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa anao wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa anazielewa na kuzitafsiri
sheria hizi ili zimsaidie katika utendaji wake wa kazi wa kila siku. Hususani kuwaelimisha wananchi
wake taasisi zilizoundwa katika kutatua matatizo yanayohusiana na malalamiko mahali pa kazi.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
84
6.10 USULUHISHI WA MIGOGORO
Maana ya Mgogoro
Mgogoro ni msuguano unaodhihirika kati ya angalau pande mbili zinazohusiana zinapopokea
malengo, motisha hafifu na mwingiliano toka pande nyingine katika kufikia malengo yao. Mgogoro
hudhihirishwa na tofauti katika mawazo, hisia au matendo yanayotokea kati ya watu, makundi ya
watu, taasisi , jumuiya au mataifa yanayoingiliana.
Chanzo cha mgogoro
Migogoro hutokea kila mahali katika maisha. Migogoro hii husababishwa na:
i. Tofauti za uelewa
Tofauti za uelewa husababisha kutokuelewana, kuchanganyana na kusuguana
ii. Tofauti za vipaumbele au uthamanishaji
Mgogoro hutokea pale watu wenye tofauti za vipaumbele au uthamanishaji wanapojaribu
kufanya kazi pamoja.
iii. Tofauti ya matarajio kutokana na kutowasiliana
iv. Kuhofia kupoteza nafasi na heshima
Mgogoro hutokea mara nyingine kutokana upande mmojawapo unapojaribu kulinda cheo,
heshima au nafasi walionayo
Madhara ya Migogoro
i. Migogoro kwa ujumla, husababisha uharibifu wa mali na uhusiano kati ya pande zinazohusika
ii. Migogoro huharibu mrejesho kutokana na:
–– Watu waliopo katika mgogogro hupoteza muda, nguvu na mali katika kufikia lengo
–– Mgogoro wa muda mrefu baina ya watu husababisha hisia hasi na uharibifu wa ustawi wa
jamii,
–– Mgogogro hukwamisha kufikia lengo la taasisi sambamba na kuridhisha matakwa
binafsi.
MADA YA SITA
85
10
9
8
7
11
12
13
Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro
Usuluhishi wa migogoro ni mchakato wa kutambua mgogoro, kudadisi chanzo chake na kutumia
mbinu sahihi ya kutatua tatizo ili wahusika waweze kufikia malengo yao wakati huo huo uhusiano
wao ukiboreka. Baadhi ya mbinu hizi ni:
• Kutawala Maamuzi:
Mbinu hii hutumika pale ambapo maamuzi ya haraka yanatakiwa kufanyika kwa ajili ya ustawi wa
jamii na taasisi kwa kufuata maelekezo ya msuluhishaji.
• Mbinu Shirikishi:
Mbinu hii hukutanisha pande mbili ili kufikia utatuzi wa tatizo na kufikia muafaka ili kukubaliana
malengo na maarifa mapya.
• Kuepuka Suluhu ya Mgogoro:
Mbinu hii hutumika kuahirisha mgogoro bila kutoa suluhisho la kudumu. Hutumika pale ambapo
suluhisho la haraka halihitajiki au kuna jambo lenye utata.
• Kuepusha shari:
Mbinu hii hutumika kutatua mgogoro kwa upande mmoja kujitoa katika madai ili kuepusha shari.
Msuluhishi anajenga mazingira ya kufanya upande mmoja kukubali na kujiondoa katika mgogoro.
• Kukubaliana:
Mbinu hii inalenga kufikia makubaliano ya kumaliza mgogoro, ijapokuwa haitoi suluhisho la
kudumu la tatizo. Mbinu hii hutumika kutoa suluhisho kwa pande mbili zinazokinzana na zenye
nguvu sawa.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
86
Wajibu wa Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa katika Usuluhishi na Utatuzi wa Migogoro
Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa kama Mtendaji Mkuu wa shughuli zote katika eneo lake na pia kama
Mlinzi wa Amani, analojukumu kubwa la kuhakikisha migogoro yote inayojitokeza inashughulikiwa
na kupewa ufumbuzi wa kudumu. Uzoefu unaonesha kuwa katika maeneo mengi kuna migogogro
inayohusiana na:
• Ugomvi kati ya Wakulima na Wafugaji,
• Wananchi na Wawekezaji,
• Koo na Koo,
• Kaya na Kaya
• Kati ya Wananchi na Taasisi za Serikali
• Watumishi na Taasisi binafsi za Mikopo n.k.
Hivyo ni vema Maafisa hawa wakahakikisha kuwa migogoro hiyo inatatuliwa mapema iwezekanavyo
kwa kutumia sheria, kanuni na taratibu zilizopo kwa kushirikiana na taasisi na ngazi za serikali
zilizopo.
6.11 HITIMISHO
Katika mada hii tumejifunza mambo muhimu manne, yaani mbinu za
Menejimenti na Uongozi, sheria Mpya za Kazi pamoja na usuluhishi wa migogoro . Mada hii ni
muhimu sana kwa MaafisaWatendaji wa Vijiji na Mitaa ili kuwawezesha kutenda kazi kwa ufanisi,
kwani wao ndiyo wasimamizi na watekelezaji wakuu wa shughuli za Serikali za Mitaa katika ngazi ya
Kijiji na Mtaa.
Ni muhimu kwa Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa kuelewa na kuzingatia
vema maudhui ya mada hii ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi
wa hali ya juu.
MADA YA SITA
87
10
9
8
7
11
12
13
6.12 MAREJEO
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2004). Mafunzo ya Kuboresha Ujuzi na Stadi za Kazi kwa
Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dodoma.
Breach, E.F.L. Principles of Management.
Thomson, G.(1981): A Textbook of Personnel Management. IFM.Roes, W.D.(1988): The Skills of
Management.
Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Na. 6 ya Mwaka 2004
Sheria ya Taasisi za Kazi Na. 7 ya Mwaka 2004
Neil H. Katz and John W. Lawyer, Communication and Conflict Management Skills
MADA YA SABA7 10
9
8
7
11
12
13
KANUNI NA TARATIBU ZA UENDESHAJI WA OFISI NA
MIKUTANO, UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU, TEKNOLOJIA YA
HABARI NA MAWASILIANO
MADA YA SABA
91
7.1 UTANGULIZI
Watendaji wa ngazi ya Kijiji na Mtaa wana majukumu makubwa. Ili
kutekeleza majukumu yao kwa ukamilifu wanahitaji kuelewa taratibu za menejimenti. Taratibu hizi ni
pamoja na Uendeshaji wa ofisi na mikutano, Utunzaji wa Kumbukumbu, Mawasiliano, Matumizi ya
Teknolojia ya habari na mawasiliano (Teknohama) katika Utunzaji wa Kumbukumbu na Mawasiliano
na vilevile kujua vifaa/vitendea kazi muhimu vinavyotakiwa kuwepo katika ofisi za Vijiji na Mitaa.
Lengo kuu la mada hii ni kuwawezesha Maafisa Watendaji wa Vijiji na
Mitaa kuelewa na kuzingatia kanuni na taratibu za uendeshaji wa ofisi na mikutano, Utunzaji
wa Kumbukumbu, Mawasiliano, Matumizi ya Teknohama katika Utunzaji wa Kumbukumbu na
Mawasiliano.
Madhumuni mahsusi ya mada hii ni kuwawezesha Watendaji
hawa kuelewa:-
• Maana ya ofisi;
• Vitendea kazi muhimu katika uendeshaji wa ofisi na mikutano;
• Kanuni na taratibu za kuendesha ofisi na mikutano.
• Utunzaji wa Kumbukumbu za Ofisi
• Mawasiliano na
• Nafasi ya Matumizi ya Teknohama katika kutunza Kumbukumbu na Mawasiliano.
Kwa madhumuni ya kukidhi malengo hayo, mada hii imegawanyika katika vipengele vifuatavyo:-
• Maana ya ofisi;
• Vifaa vya ofisi;
• Kanuni na taratibu za kuendesha ofisi na mikutano
• Utunzaji wa Kumbukumbu za Ofisi
• Mawasiliano na;
• Nafasi ya Matumizi ya Teknohama katika kutunza Kumbukumbu na Mawasiliano.
7.0 KANUNI NA TARATIBU ZA UENDESHAJI WA
OFISI NA MIKUTANO, UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU,
TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO
10
9
8
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
92
7.2 MAANA YA OFISI
Ofisi ni mahali ambapo shughuli zote za uendeshaji na maamuzi hufanyika. Ofisi huwa ni mahali
maalum palipoteuliwa kwa ajili ya kuendesha shughuli mbalimbali ambazo ni rasmi. Kwa kawaida,
ofisi huendeshwa ndani ya jengo maalum ambalo limejengwa au kukodiwa na Kijiji au Mtaa au
taasisi yoyote inayotambuliwa kisheria.
7.3 VIFAA VYA OFISI
Ofisi ya Kijiji na Mtaa kama zilivyo ofisi nyingine, huwa na vifaa/vitendea kazi mbalimbali ambavyo ni
mali ya Serikali ya Kijiji au Kamati ya Mtaa. Vifaa hivi vinaweza kuwa ni:-
• Meza;
• Viti;
• Kabati;
• Nyaraka muhimu za Serikali ikiwa ni pamoja na Katiba, Sheria, Sera, Kanuni, Taratibu na
miongozo ya Serikali;
• Masijala ya wazi na ya siri;
• Rejesta mbali mbali za Kijiji au Mtaa;
• Shajala;
• Vyombo vya usafiri kama vile baiskeli na pikipiki;
• Taa;
• Bendera ya Halmashauri;
• Bendera ya Taifa;
• Nyenzo nyinginezo ambazo hurahisisha uendeshaji wa ofisi
• Kompyuta, n.k
Kwa matumizi endelevu na utunzaji bora wa vifaa, inashauriwa kuwa vifaa vyote vya ofisi pamoja
na mali nyingine yoyote ya Serikali ya Kijiji au Kamati ya Mtaa iorodheshe katika Daftari Maalumu la
kuhifadhi Vifaa vya Ofisi kwa kuonyesha idadi, thamani yake, tarehe ya kununuliwa au kupokelewa,
mahali ilipopokelewa/nunuliwa. Pamoja na kuwa na orodha ya mali yote ni vizuri kudhibiti matumizi
yake. Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa ni lazima watoe mfano kwa kutotumia mali ya Serikali kwa
manufaa yao binafsi.
MADA YA SABA
93
10
9
8
11
12
13
7.4 KANUNI NA TARATIBU ZA KUENDESHA OFISI NA MIKUTANO
7.4.1 Kanuni na Taratibu za Kuendesha Ofisi
• Utoaji wa Taarifa /Habari za Ofisi
Kwa mujibu wa Kanuni za Serikali za Mitaa (Maadili ya Watumishi) za mwaka 2000 kifungu
cha 3, utoaji wa taarifa maana yake ni pamoja na kutoa ukweli au habari zinazojulikana kwa
mtu yeyote binafsi ambazo zinapaswa kutolewa kwa mujibu wa Kanuni hiyo. Hii ina maana
kwamba taarifa za ofisi hazitolewi kiholela tu.
7.4.2 Kanuni na Taratibu za Kuendesha Mikutano ya Vijiji na Mitaa.
• Kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na.451 la 1995 aya ya 14.2 Mikutano yote ya Serikali ya
Kijiji/Kamati ya Mtaa na Mikutano Mikuu ya Kijiji/Mtaa inaitishwa na Mwenyekiti wa Serikali ya
Kijiji/Kamati ya Mtaa.
• Mkutano wa wakazi wote wa Kijiji unatakiwa kuitishwa angalau mara moja kila baada ya
miezi mitatu (Robo mwaka – Mara nne kwa Mwaka),
• Mkutano wa Halmashauri ya Kijiji hufanyika mara moja kwa kila mwezi na mikutano ya
dharura huitishwa wakati wowote ikionekana inafaa.
• Mkutano wa Wakazi wa Kitongoji hufanyika mara moja kwa mwezi na mkutano wa Wakazi
wote wa Mtaa ni mara moja kila baada ya miezi miwili.
• Mikutano hii hufanyika muda na mahali popote kulingana na maamuzi ya Serikali ya Kijiji/
Kamati ya Mtaa.
• Katibu (Mtendaji wa Kjiji/Mtaa) huwajulisha Wajumbe kuhudhuria mkutano baada ya Mwenyekiti
kukubali mkutano ufanyike;
• Mkutano utafanyika tu endapo akidi ikitimia ambapo kwa mujibu wa Sheria Na. 7 ya Serikali za
Mitaa ya Mwaka 1982 kifungu cha 105, Mikutano ya Serikali ya Kijiji akidi inatakiwa iwe si chini ya
nusu ya wajumbe wote wa Serikali ya Kijiji na kwenye Mkutano wa Kijiji ni angalau asilimia ishirini
(20%) ya Wanakijiji wa Kijiji husika. Vilevile kwa upande wa Kamati ya Mtaa Kikao cha Kamati ya
Mtaa akidi isipunguwe wajumbe Watano na Mkutano wa Wakazi wa Mtaa akidi ni nusu ya Wakazi.
• Mwenyekiti ndiye anafungua na kufunga mkutano;
• Mwenyekiti hana budi kuzingatia muda maalum wa kuzungumza na awape wajumbe nafasi
ya kutosha kuchangia mawazo;
• Maamuzi ya walio wengi yazingatiwe;
• Ikiwezekana kura zipigwe endapo suala linalozungumziwa litaleta utata;
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
94
• Baada ya mkutano Mwenyekiti na Katibu wanalazimika kufuatilia utekelezaji wa maamuzi
kwa muda uliokubaliwa katika mkutano na kuandaa taarifa ya Mrejesho (Yatokanayo) kwa
Mkutano au kikao kijacho.
N.B: Maamuzi ya ngazi za juu ni lazima yatekelezwe baada ya majadiliano katika vikao na kwa
kuzingatia ushauri wa wataalamu.
7.5 UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU
7.5.1 Maana ya Kumbukumbu
Kwa mujibu wa mada hii, kumbukumbu ni taarifa au habari rasmi zilizoandaliwa au zilizofikishwa
ofisini na kuhifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya Ofisi. Bila kuwepo na kumbukumbu za maandishi,
shughuli za Ofisi hazitekelezeki kwa ukamilifu. Hivyo basi, utunzaji mzuri wa kumbukumbu katika
Ofisi ni muhimu sana.
7.5.2 Umuhimu wa Kumbukumbu
• Kuweka uwazi wa Shughuli za Ofisi ya Kijiji/Mtaa
• Kurahisisha mawasiliano ya kiofisi baina ya Serikali ya Kijiji/Kamati ya Mtaa na Wadau
wengine pamoja na Umma
• Kufuatilia na Kutoa tathmini katika utoaji wa huduma na matumizi ya rasilimali kwa ajili ya
maendeleo ya Kijiji/Mtaa
• Kutumika kwa ajili ya mipango ya baadae
• Kutumia ajili ya rejea mbalimbali katika kufanya maamuzi ya masuala mbalimbali yanayohusu
ustawi wa jamii, maendeleo na huduma mbalimbali zinazotolewa na Ofisi husika.
7.5.3 Aina za Kumbukumbu
Kumbukumbu katika ofisi ya Kijiji/Mtaa zinaweza kuwa katika sura ya barua, nyaraka, miongozo,
mihtasari, rejesta, takwimu na vitabu. Vile vile kulingana na maendeleo ya teknohama, kumbukumbu
zinaweza zikawa katika kompyuta kwa njia ya maandishi na picha.
MADA YA SABA
95
7.5.4 Sehemu ya Utunzaji wa Kumbukumbu
Kumbukumbu za Ofisi katika Serikali ya Kijiji/Kamati ya Mtaa hutunzwa katika sehemu maalumu
iliyotengwa kwa shughuli hiyo inayofahamika kama Masijala.
7.5.4.1 Masijala
Hii ni sehemu maalum ambayo kumbukumbu za ofisi hutunzwa.
• Masijala hupokea barua na kumbukumbu mbalimbali zinazoingia na kuzisambaza kwa
wahusika mbalimbali katika ofisi.
• Masijala ni mahali ambapo hutunza na husambaza kwa ufanisi na katika muda unaotakiwa
barua, na mawasiliano mengine yanayopelekwa nje ya ofisi.
• Masijala ndipo ambapo majalada hufunguliwa na huratibiwa kwa kutumia mifumo mbalimbali
ili kurahisisha upatikanaji na matumizi ya kumbukumbu kwa watumiaji.
• Masijala hutunza na kutoa kumbukumbu kwa ajili ya matumizi ya rejea mbalimbali za
uendeshaji wa shughuli za Kijiji/Mtaa
7.5.4.2 Aina ya masijala
Kuna aina mbili za Masijala; Masijala ya Wazi na Masijala ya Siri.
Masijala ya Wazi hutumika kuweka kumbukumbu na barua ambazo zinaweza kutumiwa au
kuonekana na Mtumiaji yeyote aliyeidhinishwa bila kuleta athari kwa ofisi au Jamii.
Masijala ya Siri hutunza kumbukumbu ambazo ni za siri. Kumbukumbu hizi hutumiwa na Afisa
aliyeapishwa ili kuepusha athari inayoweza kutokea kwa jamii, ofisi au Afisa Mhusika iwapo
kumbukumbu hizi zitawafikia watu wasiohusika.
7.5.5 Taratibu na Kanuni za kutumia Kumbukumbu.
Kwa mujibu wa Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma za Mwaka 2005, Watumishi
wa Umma haruhusiwi kufanya yafuatayo:-
• Kutoa kwa watu wasiohusika taarifa za Serikali, ama za siri au za kawaida, ambazo
wamezipokea kutoka kwa watu wengine kwa kuaminiwa tu lakini bila idhini. Kwa kuzingatia
utunzaji wa siri za Serikali, watumishi hawaruhusiwi pia kutoa taarifa za Serikali kwa watu
wasiohusika hata baada ya kuacha kazi katika utumishi wa umma.
• Kupotosha au kuzuia utekelezaji wa sera na mipango ya Serikali kwa kutoa taarifa kwa
watu bila idhini kabla sera na mipango hiyo kutangazwa rasmi kwa umma.
• Kutumia nyaraka au taarifa za Serikali wanazozipata katika kutekeleza wajibu wao kwa
manufaa yao binafsi.
10
9
8
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
96
• Taarifa za Serikali zitatolewa kwa vyombo vya habari na maafisa wenye madaraka ya
kufanya hivyo kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.
• Upelekaji na upokeaji wa barua za wazi na za siri
Ofisi ya Kijiji na Mtaa huwa na mawasiliano ya maandishi kati yake na ofisi na asasi nyingine.
Mawasiliano haya yanaweza kuwa ya wazi au siri. Mawasiliano yoyote; yawe ya siri au wazi ni
mali ya ofisi na hairuhusiwi kufanyika nje ya maeneo ya ofisi. Ni vema ofisi ya Kijiji au Mtaa ikawa
na masijala itakayotumika katika kutunza kumbukumbu zote za Ofisi zikiwemo rejesta maalum
ya kurekodi Mawasiliano yanayotoka nje ya Ofisi na yanayoingia ndani ya Ofisi ili kurahisisha
upatikanaji wa kumbukumbu hizo. Hivyo ni vema Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa wote
wazingatie hilo. Mtendaji wa Kijiji/Mtaa kama Mtumishi wa Umma anatakiwa kuzingatia na kuzifuata
taratibu hizo.
7.6 Mawasiliano
Uendeshaji wa shughuli za utawala katika ngazi ya Kijiji/Mtaa hauwezi kufanikiwa bila kuwepo
mawasiliano madhubuti kati ya viongozi na wananchi na kati ya ngazi moja ya utawala na ngazi
nyingine. Mawasiliano yanakuwa sahihi pale yanapofanyika kwa wakati unaofaa na ujumbe
unaopelekwa ukiwa sahihi na kwa njia sahihi ili kuwaletea maendeleo wananchi katika Mitaa na/au
Vijiji vyao.
7.6.1 Maana ya mawasiliano
Mawasiliano ni mchakato unaohusu uelewa na utoaji wa habari kutoka kwa mtu mmoja kwenda
kwa mtu mwingine ili kuwawezesha wahusika wawili kushirikishana kile wanachokiona au
wanachokifahamu.
7.6.2 Umuhimu wa Mawasiliano
Mawasiliano ni muhimu katika utendaji kazi wenye tija katika ofisi ya Kijiji/Mtaa.
• Mawasiliano hufanyika ndani ya ofisi na katika mazingira ya nje ya ofisi kwa maana ya
umma, taasisi na wadau wengine.
• Kwa mantiki hiyo, mawasiliano ni mbinu inayotumika na ofisi katika kutekeleza kwa ufanisi
majukumu yake.
MADA YA SABA
97
7.6.3 Aina na Mbinu za Mawasiliano
Mtendaji/kiongozi wa Kijiji/Mtaa lazima awasiliane na anaowaongoza kuhusu mambo
yaliyokusudiwa kufanyika na pia lazima apate taarifa za utekelezaji. Katika kutekeleza suala hilo
anaweza kutumia aina za Mawasiliano zifuatazo:-
• Barua,
• Simu za Mkononi,
• Simu za Maandishi (Fax),
• Mikutano,
• Ana kwa Ana,
• Lugha ya Vitendo,
• Vyombo vya habari kama vile Radio, Televisheni na Magazeti.
• Mbinu za Mawasiliano:-
• Michezo
Mtendaji wa Kijiji/Mtaa anatakiwa kuwa na mbinu mbali mbali katika kutumia aina za mawasiliano
ambazo zimeainishwa hapo juu. Mbinu hizo ni kama vile michezo, sanaa za maandishi na
maonesho, na burudani mbali mbali. Katika matumizi ya mbinu hizo, Afiisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa
anatakiwa azingatie dhana ya ushirikishaji jamii kwa kuzingatia makundi yenye mahitaji maalum
kama vile Wanawake, Vijana, Watoto na Walemavu.
7.6.4 Changamoto za Mawasiliano na Mbinu ya Kuziepuka
i. Lugha
Lugha ni nyenzo kubwa ya Mawasiliano. Mara nyingi watu huelewana kwa kutumia lugha
inayoeleweka baina yao. Endapo lugha inayotumika haiendani na Jamii inayohusika, mwitikio wa
jambo linalolikusudiwa utaathirika. Hivyo ni muhimu kutumia lugha inayoeleweka katika mawasiliano
yote ya kiofisi na umma. Kwa mujibu wa kipengele cha C.1 (3) Kanuni za Kudumu za Utumishi wa
Umma, 2009 Lugha ya Kiswahili na Kiingereza ndizo zinazotambulika kwa mawasiliano yote ya
kiofisi.
ii. Uchaguzi wa Mbinu ya Mawasiliano
Uchaguzi wa mbinu ya mawasiliano usio sahihi husababisha walengwa kutoelewa ujumbe
uliokusudiwa. Kwa hiyo mbinu ya mawasiliano ichaguliwe kwa kuzingatia mazingira ya kazi katika
jamii iliyopo.
10
9
8
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
98
iii. Mila na Desturi
Uchaguzi wa lugha ya mawasiliano usioendani na mila na desturi za eneo husika katika mikutano
na maongezi ya anan kwa ana unaathiri maelewano kati ya viongozi na jamii. Maafisa Watendaji wa
Vijiji/Mtaa wanapaswa kuwa makini kwa kusoma na kuzingatia mila na desturi za mahali ili kujenga
maelewano na jamii.
iv. Umasikini
Umasikini ni kikwazo kikubwa kwa Jamii katika kutumia baadhi ya njia za mawasiliano (mfano simu
na magazeti). Hali hii inasababisha jamii kukosa habari kutoka kwenye vyanzo vilivyo nje ya uwezo
wao. Ili kukabiliana na changamoto hii, Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa anapaswa awe makini katika
uchaguzi wa mbinu ya mawasiliano kwa kuzingatia uwezo wa watumiaji.
v. Upatikanaji wa Habari
Mara nyingi habari muhimu kwa jamii hazitolewi kwa mujibu wa taratibu. Afisa Mtendaji wa Kijiji/
Mtaa anatakiwa kuweka wazi taarifa za mapato na matumizi ya Kijiji/Mtaa kwa kipindi husika.
Ahakikishe taarifa mbalimbali zinatolewa kwa umma, kwa wakati na kwa njia rahisi itakayowafanya
walengwa kuzipata kwa urahisi.
7.6.5 Nafasi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Teknohama)
Ili kwenda na wakati kwa lengo la kurahisisha utendaji wa kazi katika Utumishi wa Umma , Afisa
Mtendaji wa Kijiji/Mtaa anatakiwa kuwa na uelewa wa matumizi ya zana za Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano. Teknolojia hii inalenga kuunganisha ngazi zote za utendaji kazi serikalini pamoja na
wadau wengine wote wa maendeleo.
Kutokana na mabadiliko haya ya Teknolojia katika Nyanja ya Mawasiliano na kwa kuzingatia misingi
ya Utawala Bora inayohitaji Serikali kuendesha mambo yake kwa uwazi, Sheria, Sera, Nyaraka,
Kumbukumbu na taarifa mbalimbali za Serikali zitapatikana kwa njia ya mtandao wa Kompyuta kwa
jamii.
7.7 HITIMISHO
Katika mada hii tumeeleza mambo ya msingi kuhusu maana ya ofisi,
vifaa/vitendea kazi muhimu vya ofisi, kanuni na taratibu za kuendesha ofisi na mikutano, utunzaji
wa kumbukumbu, mawasiliano na nafasi ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika utunzaji
wa kumbukumbu na mawasiliano. Inasisitizwa kwamba Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa
washirikiane na Halmashauri za Wilaya au Miji yao pamoja na wananchi kuhakikisha kwamba vijiji na
mitaa yote inakuwa na ofisi nzuri zinazolingana na hadhi ya majukumu na wajibu wao kwa umma.
MADA YA SABA
99
Utunzaji wa kumbukumbu ni eneo mojawapo muhimu sana
katika suala zima la uendeshaji wa Ofisi. Hivyo, Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa hawana budi
kuhakikisha kuwa kumbukumbu zote za Ofisi zao zinatunzwa ipasavyo kwa mujibu wa Sheria,
Kanuni na Taratibu za Serikali.
Katika kuimarisha mawasiliano na jamii na kuzingatia misingi ya utawala bora, Maafisa Watendaji
wa Vijiji/Mitaa wahakikishe kuwa mikutano yote inaitishwa na kuendeshwa kwa mujibu wa Sheria,
Kanuni na Taratibu za Serikali za Mitaa.
7.8 MAREJEO
1. Jamhuri Muungano wa Tanzania: Kiongozi cha Serikali za Vijiji. Ofisi ya Rais TAMISEMI –
DODOMA.
2. Jamhuri Muungano wa Tanzania: Kiongozi cha Timu ya Uwezeshaji ya Kijiji/Mtaa. Ofisi ya Rais
TAMISEMI – DODOMA.
3. Jamhuri Muungano wa Tanzania: Umuhimu wa Kuweka Kumbukumbu katika Serikali za Mitaa.
Ofisi ya Rais TAMISEMI – DODOMA.
4. Jamhuri Muungano wa Tanzania: Registry Procedure Manual – Ofisi ya Rais – Menejimenti ya
Utumishi wa Umma - DAR ES SALAAM
5. Jamhuri Muungano wa Tanzania (2009): Standing Orders, 2009 – OR - MUU
6. Jamhuri Muungano wa Tanzania (1970): Sheria ya Utunzaji wa Siri za Serikali, 1970 - Ofisi ya
Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma - DAR ES SALAAM
7. Jamhuri Muungano wa Tanzania: Kijitabu cha Kusaidia Utekelezaji wa Utawala Bora katika
Serikali za Mitaa - Ofisi ya Rais TAMISEMI – DODOMA.
8. Jamhuri Muungano wa Tanzania (2006): Mafunzo ya Kuboresha Ujuzi wa Stadi za Kazi kwa
Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa Tanzania Bara (2006). Ofisi ya Rais TAMISEMI – DODOMA.
9. Jamhuri Muungano wa Tanzania: Sera ya Taifa ya Habari na Mawasiliano. Wizara ya Habari,
Michezo na Utamaduni
10. Jamhuri Muungano wa Tanzania (2005): Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa
Umma, 2005 - Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma - DAR ES SALAAM
11. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2000) Uongozi Bora kwa Watumishi wa Serikali za Vijiji,
Vitongoji na Mitaa Tanzania Bara. KITABU CHA KUFUNDISHIA OR - TAMISEMI Dodoma.
10
9
8
11
12
13
MADA YA NANE 8 10
9
8
11
12
13
KUKUZA UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASKINI, UJASIRIAMALI
NA UANZISHWAJI WA VIKUNDI
MADA YA NANE
103
8.0 KUKUZA UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASKINI,
UJASIRIAMALI NA UANZISHWAJI WA VIKUNDI
8.1 UTANGULIZI
Tangu tupate Uhuru mwaka 1961, Serikali ya Tanzania imetangaza vita dhidi ya maadui watatu;
umaskini, ujinga na maradhi. Maadui hawa wanakwamisha maendeleo ya wananchi na kufanya maisha
yao yawe duni. Tokea wakati huo Serikali, kwa kushirikiana na wananchi, imekuwa ikibuni na kutekeleza
mikakati na mbinu mbalimbali za kupambana na maadui hawa. Hata hivyo, hali ya umaskini imeendelea
kuwepo kwa kiwango kikubwa. Takwimu zinaonyesha kuwa wananchi wengi wana kipato amabacho
hakikidhi mahitaji yao ya msingi kama vile chakula, malazi, mavazi, elimu na afya.
Pamoja na mikakati iliyokuwepo baada ya uhuru mpaka 1980, maadui hawa waliendelea kuwepo
na hivyo Serikali iliazimia kuangalia upya mikakati ya awali na kuiboresha kwa lengo la kupunguza
kiwango cha maadui hao ili iendana na mabadiliko ya mazingira ya kijamii na kiuchumi kwa wakati
huo. Hivyo, kuanzia mwaka 1986, Serikali ilianza kufanya marekebisho ya kijamii na kiuchumi
ambayo yanaendelea kutekelezwa ili kuhakikisha kuwa marekebisho hayo yanatokana na mwelekeo
wa falsafa ya maendeleo ya muda mrefu na yanaongozwa na wananchi wenyewe.
Hata hivyo, serikali ya Tanzania kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa imeridhia malengo ya
milenia, malengo hayo yamekusudia kupunguza umaskini na kuboresha maisha ya wananchi.
Kwa ujumla, katika utekelezaji wa maridhiano hayo, serikali ya Tanzania ilijiwekea dira ya taifa ya
maendeleo 2025 na kuandika andiko la mkakati wa kupunguza umaskini. Andiko hilo lilisababisha
kuandaliwa kwa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA)
Lengo la Mada
Lengo la mada hii ni kumwezesha Afisa Mtendaji wa kijiji/mtaa awe na ufahamu kuhusu dira ya
Taifa ya Maendeleo, Mkakati wa kukuza, Malengo ya Milenia na Kupambana na Umaskini na
sera mbalimbali za kisekta zinazo saidia katika kukuza uchumi na kupunguza umasikini ikiwemo
ujasiriamali. Ufahamu huu utamwezesha kuhamasisha jamii katika shughuli za kiuchumi na kubuni
mbinu za kujiongezea kipato
8.2 UMASKINI
Umaskini ni hali ya maisha isiyoridhisha. Ni hali ya kuwa na uwezo mdogo wa kumudu mahitaji ya
maisha ya mwanadamu ya kila siku. Hali hii inajidhihirisha; kwa kuwa na kipato duni, kuishi katika
mazingira duni, kusumbuliwa na maradhi na ujinga.
10
9
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
104
8.2.1 Viashiria vya Umaskini
Viashiria vinavyoonyesha hali halisi ya umaskini hapa Tanzania ni pamoja na;
• kutojua kusoma na kuandika,
• Kutokuwa na uhakika wa kupata chakula, mavazi na malazi
• Uhaba wa maji safi na salama,
• Huduma duni za afya,
• Vifo vingi vya wananchi,
• Muda mfupi wa maisha,
• Utapiamlo kwa watoto na watu wazima,
• Uchakavu wa mazingira,
• Ukosefu wa ajira na kipato duni,
• Kutofahamu masuala muhimu ya jamii.
8.3 DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO
Dira ya maendeleo ni kioo kinachoonyesha mwelekeo wa jamii au Taifa kufikia malengo/matakwa
yanayokusudiwa. Malengo/matakwa hayo ni budi yawe chanya, yaeleweke na kukubaliwa na jamii
au Taifa husika kwa muda maalum.
Nchi yetu ina dira ya maendeleo iliyoandaliwa 1999 na inayotoa mwelekeo wa maendeleo ya Taifa
letu kwa siku za usoni. Dira hiyo inajulikana kama Dira ya maendeleo Tanzania 2025 (TDV 2025).
Madhumuni ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ni kuamsha, kuunganisha na kuelekeza juhudi na
fikra zetu na rasilimali za Taifa katika maeneo ya msingi yatakayotuwezesha kufikia malengo ya
maendeleo yetu. Pia, dira itatuwezesha kustahimili ushindani mkubwa wa kiuchumi wa ndani na nje
ya nchi (global economy).
Katika kutekeleza dira hii, inatarajiwa jamii ya Watanzania itakuwa yenye maendeleo ya kuridhisha
na hivyo kuondokana na umaskini unaokabili wananchi kama tulivyoona hapo juu.
Malengo makuu ya dira ya taifa ya maendeleo 2025 ni: maisha bora na mazuri kwa watanzania
wote, uongozi bora na utawala wa sheria na uchumi imara wenye uwezo wa kukabiliana na
ushindani. Kulingana na malengo hayo, Tanzania ya mwaka 2025 inatazamiwa kuwa ni Taifa lenye
sifa zifuatazo:
• Maisha bora na mazuri;
• Amani, utulivu na umoja;
• Utawala na uongozi bora;
MADA YA NANE
105
• Jamii iliyoelimika na inayopenda kujifunza zaidi; na
• Uchumi wenye ushindani na ukuaji wa kudumu kwa maslahi ya watu wote.
8.4 MALENGO YA MILENIA
Tanzania kama mwanachama wa Umoja wa mataifa imeridhia malengo ya maendeleo ya Milenia –
Millenium Development Goals (MDGs) yaliyosainiwa na nchi wanachama wa umoja huo kwa lengo la
kuyatekeleza na kuboresha maisha ya wananchi wa nchi zinazoendelea. Malengo hayo ni pamoja na:
1. Kuondoa umaskini uliokithiri na njaa
2. Kutoa elimu ya msingi kwa wote
3. Kuendeleza usawa wa kijinsia na kuendeleza wanawake
4. Kupunguza vifo vya watoto
5. Kuboresha afya ya uzazi
6. Kupambana na VVU/UKIMWI, Malaria na magonjwa mengine
7. Kuhakikisha mazingira endelevu
8. Kuendeleza ushirikiano wa maendeleo kimataifa
8.5 MKAKATI WA KUKUZA UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASKINI TANZANIA -
MKUKUTA
MKUKUTA ni mkakati wa taifa wa kukuza uchumi utakaosaidia kupunguza umaskini. Umeandaliwa
baada ya matokeo ya mashauriano ya wadau mwaka 2004 na kupitishwa na baraza la mawaziri
mwezi februari, 2005.
MKUKUTA ulipangwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2005/06 hadi 2009/10.
Kuanzia Octoba, 2009 mpaka Machi, 2010, MKUKUTA ulifanyiwa mapitio na matokeo ya mapitio
hayo ni MKUKUTA II.
Pamoja na hayo, MKUKUTA I na II umeandaliwa katika nguzo kuu tatu;
• Ukuaji wa Uchumi na Kupunguza Umaskini wa Kipato
• Kuimalisha Ubora wa Maisha na Ustawi wa Jamii
• Utawala Bora na Uwajibikaji
Nguzo zote tatu za MKUKUTA zina mikakati ya utekelezaji yenye mtazamo unaohimiza matokeo
tarajiwa, mengi kati ya matokeo hayo yatapatikana kupitia kwa utaratibu wa sekta mbalimbali
unaoshirikisha wadau wote katika utekelezaji. Utekelezaji wake unachangia kufanikisha kufikia dira
ya maendeleo ya 2025 na malengo ya millennia.
10
9
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
106
Kielelezo kifuatacho kinaonyesha uhusiano uliopo kati ya nguzo tatu za MKUKUTA.
Kukuza Uchumi na Kupunguza
Umaskini (Mkukuta)
Ukuaji wa Uchumi na
Kupunguza Umaskini
wa Kipato
Maisha Bora na
Ustawi wa Jamii
Utawala Bora na
Uwajibikaji
8.6 SERA ZA SEKTA MBALIMBALI ZINAZOCHANGIA KUKUZA UCHUMI
Sera za sekta mbalimbali zimeandaliwa kuchangia jitihada za taifa za kukuza uchumi na kupunguza
umasikini. Aidha, mikakati ya kutekeleza sera hizo imeandaliwa ili kutoa msukumo kwa wadau
mbalimbali kushiriki kikamilifu katika shughuli za kufanikisha utekelezaji wake. Wadau hao ni
wananchi ambao ndio watakaonufaika moja kwa moja na matokeo ya kisekta ya kukuza uchumi na
hatimaye kupunguza umaskini. Wengine ni watendaji na viongozi wa serikali ngazi zote pamoja na
wadau wa maendeleo wakiwemo Asasi za Kiraia, makampuni binafsi, mashirika ya ndani na nje ya
Tanzania. Baadhi ya sera zinazobainisha hatua mbalimbali ya kuondoa umasikini ni pamoja na sera ya
kilimo na maendeleo ya ushirika, sera ya uvuvi, sera ya kuendeleza baishara ndogo na za kati (SMEs),
sera ya taifa ya biashara, sera ya usafiri na usafirishaji, sera ya ajira kwa vijana nk. Viongozi wa vijiji
na mitaa hususan watendaji wanapaswa kuelewa vizuri sera hizi ili waweze kuwasaidia wananchi
kuzitafakari na kubaini maeneo ya kutoa msukumo wa kiutendaji kulingana na mazingira yao.
MADA YA NANE
107
8.6.1 Sera za Kisekta za Kukuza Uchumi Tanzania
Kama ilivyokwisha elezwa, sera za kisekta zinalenga kukuza uchumi na hatimaye kupunguza umaskini
kwa watanzania hususani asilimia 57 wanaoishi chini ya Dola moja ya Kimarekani kwa siku.
Ili matazamio ya kukuza uchumi yafikiwe, na sera zilizoelezwa hapo juu zitekelezwe, mahitaji ya
utekelezaji wa sera ya elimu, afya, sera ya usafiri na usafirishaji na sera ya ajira ni muhimu sana.
Maendeleo ya taifa letu kiuchumi yatafikiwa iwapo wananchi wengi watakuwa na elimu ya kutambua
kero na kushiriki kikamilifu katika utatuzi wake. Aidha, uboreshaji wa miundombinu ya usafiri na
vyombo imara vya usafiri na usafirishaji kama inavyoonekana kwenye sera ya usafiri na usafirishaji
ndio nyenzo ya kujikwamua katika dimbwi la umaskini.
8.6.2 Mikakati ya Kuratibu Utekelezaji wa Sera za Kisekta za Kukuza Uchumi na
Kupunguza Umaskini
Malengo ya Mikakati ya Taifa ya Kuratibu Utekelezaji wa Sera za sekta mbalimbali za kukuza uchumi
na kupunguza Umaskini ni kutoa Miongozo (guidelines) kwa wadau wote wakiwemo watendaji
ngazi za msingi kushiriki kikamilifu kukuza uchumi na kupunguza umaskini uliokithiri ifikapo mwaka
2025. Wananchi wote kwa pamoja waelewe azma ya serikali wakishirikiana na wadau wengine wa
maendeleo ya kupambana na umaskini na kulifikisha taifa kwenye uchumi wa kisasa na endelevu.
Malengo hayo yatafikiwa kwa kufanya yafuatayo:-
i. Kuweka mfumo wa kuratibu utekelezaji sera za sekta za kukuza uchumi ngazi ya msingi
ambako watendaji wa vijiji na mitaa ndipo walipo
ii. Kuhakikisha kuwa makundi yote kwenye jamii yanashiriki kwa ukamilifu katika jitihada za
kukuza uchumi na kupunguza umaskini
iii. Kufafanua kwa uwazi mgawanyo wa majukumu na wajibu wa wadau wa kutekeleza mipango
na miradi ya kukuza uchumi
iv. Kutoa fursa sawa kwa wanaume na wanawake ya kuwawezesha kushiriki kwenye kazi zenye
tija kwa maendeleo ya uchumi wao, maisha bora na kuongeza tija.
10
9
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
108
Kwa mujibu wa mikakati hii, kila Afisa Mtendaji wa Kijiji au Mtaa, kwa kushirikiana na viongozi na
wataalam, anatakiwa kufanya yafuatayo:-
a) Kuendeleza na kuimarisha misingi ya utawala bora; kwa mfano utawala wa sheria,
uwajibikaji, uwazi na ukweli. Hivyo, anatakiwa kutekeleza yafuatayo:-
–– Kubuni Sheria Ndogo za kusaidia utekelezaji wa miradi ya kukuza uchumi;
–– Kuelimisha umma juu ya shughuli za Serikali na kutoa tafakari ya miongozo inayoletwa na
sekta mbalimbali zikiwemo zinazolenga kukuza uchumi;
–– Kuzingatia masuala ya jinsia katika uongozi, mipango na bajeti za maendeleo;
–– Kufanya mapitio na kuratibu sera na maagizo mbalimbali na kuhakikisha hakuna
migongano katika utekelezaji wake;
–– Kubaini maeneo ya mafunzo yanayolenga kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa watendaji
wa vijiji na mtaa.
b) Kuhamasisha wananchi ili washiriki kikamilifu katika miradi ya kiuchumi kwa kutumia rasilimali
zilizopo katika maeneo yao na kupunguza umaskini;
c) Kubuni njia za kukuza uchumi wa Kijiji/Mtaa na Kuhakikisha kuwa teknolojia sahihi na rahisi
inapatikana na kutumika ipasavyo kwa lengo la kuongeza tija;
d) Kuhimiza wananchi matumizi zaidi ya nyenzo za uzalishaji mali kama vile mboji, samadi na
mali ghafi;
e) Kusimamia mipango ya uzalishaji mali na uwekaji wa akiba ya chakula cha kutosha kwa kila kaya;
f) Kuhimiza hifadhi bora ya mazao ili kupunguza upotevu na uharibifu wa mazao;
g) Kuhimiza kilimo cha umwagiliaji maji pale panapostahili na matumizi bora ya maji;
h) Kusimamia upimaji wa ardhi katika eneo lake ili kuwezesha wananchi kupata Hati miliki;
kusimamia utayarishaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi na kudhibiti uharibifu wa
mazingira.
i) Kuhimiza uendelezaji na uanzishaji wa vyama vya ushirika, kwa mfano, Vyama vya wachimbaji
wa madini pale yanapopatikana, ujenzi wa nyumba bora, kilimo, ufugaji, akiba na mikopo.
j) Kuratibu kazi za jamii za ujenzi na ukarabati wa miundo-mbinu ya mawasiliano hasa barabara
za vijijini na vitongojini na mitaa;
k) Kupanua wigo wa mapato na kusimamia vyema matumizi yake katika miradi ya kukuza
uchumi na kuondoa umaskini;
l) Kusimamia na kuratibu mipango ya kupanua, kuboresha na kuchangia elimu kwenye maeneo
ya watendaji wa mtaa/vijiji
m) Kusimamia na kuratibu mipango ya upatikanaji wa maji ya kutosha, safi na salama kwenye
maeneo yao;
MADA YA NANE
109
n) Kusimamia na kuratibu mipango ya uboreshaji wa huduma za afya na usafi wa mazingira;
o) Kubuni mikakati ya kuongeza ajira kwa vijana na kuzuia ajira za watoto;
p) Kutekeleza Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1997), Sheria za Serikali za Mitaa
zinazohusu Mamlaka za Wilaya/Miji na Sheria ya Nguvu-kazi zinazompa Afisa Mtendaji wa Kijiji,
Kitongoji na Mtaa majukumu aliyonayo.
8.6.3 Hatua za Kupunguza Umaskini
Kitovu cha vita dhidi ya umaskini ni Kaya. Umaskini na hali duni ya maisha vitaweza kumalizika tu
iwapo wananchi wenyewe wataamua kuondokana na hali hiyo kwa kutumia nguvu-kazi iliyopo,
rasilimali zilizopo kwenye maeneo yao na misaada kutoka Serikalini na sehemu nyingine ikiwemo ya
wadau wa maendeleo pale hali inaporuhusu.
Ili kupunguza/kuondokana na umaskini, Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa kwa kushirikiana na
viongozi na wataalam, hawana budi kuhakikisha kuwa hatua zifuatazo zinachukuliwa:-
a) Kuelewa hali halisi ya umaskini katika maeneo yao. Afisa mtendaji anatakiwa kubaini viashiria
vya umaskini, na kutumia viashiria hivyo kuorodhesha kaya maskini;
b) Kuainisha sababu za umaskini kwa ushirikiano na wananchi katika eneo lake;
c) Kuelimisha kila mwananchi aelewe tatizo la umaskini na ajenge azma ya kufanya kazi kwa
bidii na maarifa ili kuondokana nao;
d) Kuelimisha wananchi kutambua fursa zilizopo na uwezo walionao wa kuondokana na
umaskini kwa kutumia fursa hizo;
e) Kuratibu, Kujenga na kuboresha uwezo wa ufundi, maarifa na stadi za kazi ndani ya kaya ili
kuongeza tija;
f) Kuchukua hatua za makusudi za kuziwezesha kaya kuunda vikundi vya uzalishaji mali;
g) Kuimarisha vikundi vya ushirika vya uzalishaji mali na biashara;
h) Kuhamasisha wananchi Kujenga uwezo na utamaduni wa kudunduliza na kuweka akiba
10
9
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
110
8.7 VIKWAZO VINAVYOMKUMBA MTENDAJI KATIKA KUWAWEZESHA
WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO
Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa hukumbana na vikwazo mbalimbali katika uelimishaji wa wananchi
kuhusu shughuli za maendeleo. Hivyo, ni vema kila Afisa Mtendaji akaelewa vikwazo hivi na namna
ya kuvitafutia ufumbuzi. Baadhi ya vikwazo ni pamoja na:
a) Tofauti za Mahitaji na Vipaumbele Miongoni mwa Wananchi: Afisa Mtendaji wa Kijiji au Mtaa
ana jukumu la kubaini tofauti zilizopo miongoni mwa wananchi anaowahudumia na awe tayari
kutumia kila nyenzo zilizopo katika eneo lake la utendaji kurekebisha hali hiyo. Nyenzo hizo ni
utaalam, sheria, kanuni, taratibu na mahitaji ya wananchi walio wengi.
b) Tabia ya Baadhi ya Viongozi na Watendaji Kukumbatia Madaraka: Ufumbuzi wa tatizo hili ni
kwa kila Kiongozi na Mtendaji wa Serikali katika ngazi ya Kijiji, Kitongoji na Mtaa mwenye
tabia hii kuondokana nayo na ahakikishe kwamba anawapatia wananchi fursa ya kuchangia
katika kufanya maamuzi yanayohusu maendeleo yao.
c) Upeo Mdogo wa Elimu na Utaalam: Kila Afisa Mtendaji wa Kijiji au Mtaa abaini utaalam
unaopatikana katika eneo lake la kazi na kuandaa utaratibu wa kuueneza katika jamii nzima.
d) Ubadhirifu na Utawala Mbovu: Ili kuepukana na hali hii, kila Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa
anatakiwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za Serikali ili kujenga imani kwa wananchi
anaowahudumia.
e) Utaratibu Mbaya wa Shughuli za Maendeleo Zifanywazo na Taasisi na Asasi za Serikali na
Zisizo za Serikali: Kila Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa anatakiwa kusimamia na kuratibu vizuri
shughuli zote za maendeleo.
8.8 MAJUKUMU YA SERIKALI ZA VIJIJI NA MITAA KATIKA KUPAMBANA NA
UMASKINI
Kutokana na kuwa karibu sana na watu, Serikali za Vijiji na Mitaa zina nafasi maalumu na ya pekee
katika utekelezaji wa sera za kupunguza umaskini. Kwa sababu hiyo, Taasisi hizi zitakuwa na
majukumu yafuatayo:-
a) Kupendekeza Sheria Ndogo zitakazosaidia kupunguza umaskini kwa mfano, Sheria Ndogo za
kuhifadhi mazingira, ushirikishaji jamii katika shughuli za kujitegemea, ushuru; n.k.
b) Kuelimisha wananchi kuhusu matumizi sahihi ya nguvu kazi;
c) Kutambua mahitaji ya wananchi na kuweka mipango ya maendeleo kulingana na umuhimu na
mazingira ya sehemu husika;
d) Kubuni na kupendekeza miradi ya kijamii na kiuchumi;
MADA YA NANE
111
e) Kuratibu ukusanyaji wa rasilimali, fedha, mali na nguvu-kazi kwa ajili ya kutekeleza mipango
ya Kijiji au Mtaa, na kutambua pengo lililopo katika kiwango cha rasimimali hizo;
f) Kuratibu na kusimamia shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali kwenye maeneo yao.
8.9 UJASIRIAMALI NA UANZISHAJI WA VIKUNDI VYA KIUCHUMI
8.9.1 Maana ya Ujasiriamali
Ujasiriamali umetafsiriwa kwa maana nyingi kama ifuatavyo:
• Ni uthubutu, utafiti na ubunifu wa kutumia fursa na rasilimali zilizopo kwa njia tofauti na
ilivyozoeleka au inavyofanyika katika maisha ya kila siku.
• Kuunganisha dhana, kujituma na kubadilika kutokana na mabadiko ya kimazingira na
kitekinolojia na inahusika pia na kufikia mahitaji ya masoko.
• Ni uwezo wa kufanya jambo tofauti na kila mtu anavyofikiria.
8.9.2 Maana ya Mjasiriamali
• Mjasiriamali ni mtu ambaye ana uwezo wa kugundua dhana na rasilimali katika mazingira
anayoishi na kuiboresha kutokana na mahitaji ya wananchi, serikali au taasisi husika.
• Mjasiriamali ana uwezo wa kutumia fursa zilizopo katika masoko, rasilimali au tekinolojia na
hamasa kutoka ndani ili kuweza kufikia hitaji husika.
• Mjasiriamali ni mtu ambaye angependa kujiongoza mwenyewe na kuvuka mipaka iliyozoeleka na
kufanya mambo kwa njia tofauti zaidi.
Aidha Mchumi Joseph Schumpteter ameendelea kuchambua maana ya mjasiriamali kama mtu
mwenye ubunifu katika:
• Kuzalisha bidhaa hiyo hiyo ila kwa kutumia njia rahisi zaidi au kwa gharama nafuu.
• Kugundua fursa zilizopo kwa upande wa masoko.
• Kuwa na taasisi inayoongozwa katika mtazamo tofauti zaidi.
10
9
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
112
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya kiuchumi na kitekininolojia ambayo
yamepelekea jamii nyingi duniani ikiwemo Tanzania kubadilisha mfumo wa maisha na uzalishaji mali
kutoka kwenye kutegemea kilimo na ajira rasmi na kuhamia kwenye shughuli nyingine zikiwemo
ujasiriamali na biashara. Watu wengi wamekuwa wakitumia mjasiriamali na mfanyabiashara
kama watu wanaofanya shughuli za aina moja lakini tafsiri zilizopo zinaonyesha utofauti kama
inavyoonekana:
• Wafanyabiashara wadogo hufanya bishara ili waweze kupata mahitaji muhimu wakati
mjasiriamali anafanya biashara ili kuongeza mtaji na kukua.
• Wafanyabishara wadogo hufanya biashara hiyohiyo kwa muda mrefu wakati mjasiriamali hukua
na kuanzisha biashara nyingine zenye tija zaidi
• Mjasiriamali ana uthubutu na ubunifu wa kufanya maamuzi magumu ambayo yanaweza kuathiri
ujasiriamali wake wakati mfanyabiashara anaweza asiwe tayari kuyakabili.
8.9.3 Sera ya Taifa ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo SME (Small and
Medium Enterprises) ya Mwaka 2003.
Dira ya maendeleo ya Taifa, inalenga ifikapo mwaka 2025, Tanzania iwe imejenga uchumi wenye
nguvu, imara, endelevu na wenye kuhimili ushindani na changamoto za maendeleo na mabadiliko
ya soko na tekinolojia katika uchumi wa kikanda na dunia kwa ujumla. Kwa kuzingatia hayo jukumu
la serikali na wadau wote ni kuhamasisha wananchi kutumia rasilimali kwenye maeneo yao na
zinazopatikana kutoka nje ili kuweza kufikia lengo hilo. Serikali kupitia wizara ya Viwanda Biashara
na Masoko imeandaa sera ya viwanda vidogo na biashara ndogo ya mwaka 2003 na andiko la
mkakati wa utekelezaji wake ambao unatoa jukumu la kila mdau.
Maana ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo (SMEs):
• Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo ni shughuli za kiuchumi zisizo za kilimo zinazobainishwa kwa
ukubwa wake. Kutegemeana na hali ya nchi na makubaliano. ukubwa huu huwekewa vigezo vya
ajira, mitaji au mapato ya Tasnia(Enterprise) kwa Tanzania tunatumia vigezo vya mitaji na ajira.
• Kimsingi tafsiri ya taifa ya Viwanda na Biashara Ndogo inahusika na sekta rasmi ingawa imekuwa
vigumu kuachana na sekta isiyo rasmi, hii nikutokana na wananchi wengi wamejiajiri katika
viwanda na bishara ndogo zenye ufanisi mdogo. Ili kukabialiana na changamoto zinazowakabili
kundi la wananchi waliojiajiri kwenye sekta hii moja ya mkakati wa utekelezaji wa sera ni
urasimishaji wa shughuli za hizo za kiuchumi.
MADA YA NANE
113
Rejea jedwali linaloonyesha
Makundi ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo
KUNDI LA JASIRIAMALI
IDADI YA
WAFANYAKAZI
MTAJI WA UWEKEZAJI MASHINE
(Tsh Shillingi – Tshs)
Viwanda vidogo na Biashara ndogo
Sana
1 - 4 Hadi Millioni 5
Viwanda vidogo na Biashara ndogo 5 - 49 Million 5 hadi millioni 200
Viwanda na Biashara za Kati 50 – 99 Million 200 hadi million 800
Viwanda na Biashara Kubwa 100 na zaidi Zaidi ya Millioni 800
8.9.4 Maeneo Mahususi ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara
Ndogo
• Kuboresha mfumo wa taratibu za kisheria
• Kuimarisha miundo mbinu na maeneo ya kufanyia kazi
• Uimarishaji wa ujasiriamali na masoko ya huduma za uendelezaji wa Biashara (BDS)
• Mafunzo ya Biashara (Taarifa, Technolojia, Fursa za masoko)
• Kuboresha fursa za upataji wa fedha kwa viwanda vidongo na Biashara Ndogo.
• Kuimarisha uwezo wa wadau katika kutekeleza programu za sera hii.
• Masuala ya mtambuka (Mazingira, Kuimarisha viwanda vijijini,
Jinsia na makundi maalum VVU na UKIMWI.
8.9.5 Uanzishaji wa Vikundi vya Kiuchumi
8.9.5.1 Maana ya vikundi na faida za uanzishaji wa vikundi vya biashara:
Maana ya vikundi
Kikundi/Vikundi ni mkusanyiko wa watu wawili au zaidi wanaofahamiana wenye lengo moja la
kufikia. Mara nyingi kikundi/Vikundi huanzishwa kutokana na uhitaji kama vile mikopo, kupata
elimu, n.k. Watu waliopo katika kikundi wanaweza wasiwe kwenye sekta inayofanana mfano
vikundi vya kufarijiana, kukopeshana n.k.
Jumuiya – huu ni mkusanyiko wa watu ambao ni mpana zaidi kulingana na vikundi na mara
nyingi hujumuisha watu waliopo kwenye sekta inayofanana. Dhumuni la kuanzisha jumuiya
linaweza kuwa la kibiashara au maendeleo mbalimbali yakiwemo ya kitaaluma au kitasnia mfano
jumuiya ya wasindikaji chakula, wahandisi, n.k
10
9
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
114
8.9.5.2 Jinsi ya kuanzisha Kikundi/Vikundi vya kiuchumi
Vikundi huanzishwa kutokana na uhitaji, ambapo wajumbe hukubaliana sifa, wajibu, na haki za
kila mmoja wao ili kikundi kiweze kuwa endelevu.
Kuna umuhimu wa kusajili vikundi kisheria ili viweze kupata fursa zinazoto kutokana na
kutambulika huko.
Baadhi ya sehemu zinazosajili vikundi ni
• Afisa Biashara wa wilaya
• Afisa ushirika wa wilaya
• BRELA ( Kusajili wa jina na Biashara)
• Wizara ya Mambo ya Ndani.
Aidha, sehemu ya kwenda kusajili kikundi hutegemea dhumuni la kikundi husika.
8.9.5.3 Faida za vikundi vya kiuchumi
• Kujenga ufahamu wa pamoja juu ya mambo mbalimbali,
• Inarahisisha mawasiliano na kupeana taarifa hasa za masoko.
• Kuwa na sauti ya pamoja katika kutatua changamoto zinazowazunguka
• Kuwa na nguvu moja ya ushawishi na mashauriano.
• Ni rahisi kufikiwa na watoa huduma (BDS Providers ) kama vile Benki, SIDO n.k
8.9.6 Changamoto za Wajasiriamali na Jinsi ya Kukabiliana Nazo
i. Ufinyu wa mtaji
Kutokana na ugumu wa upatikanaji mitaji watu wengi hufanya biashara wakiwa na mtaji mdogo
ambao hauwezi kukidhi uendeshaji wa biashara husika. Tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa kuongeza
mtaji kwa njia ya kukopa fedha au bidhaa au kupata ufadhili kutoka kwa ndugu, jamaa au marafiki.
ii. Kukosa ujuzi na mbinu za kuuza na kufanya biashara
Tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa kujifunza mbinu kutoka kwa wafanyabiashara wenzako
waliotangulia hasa kama yupo katika kikundi kimoja. Vilevile unaweza kujifunza kutoka kwa
wataalamu wa biashara hasa SIDO na watoa huduma wengine.
iii. Kukosa ujuzi wa masuala ya fedha
Ukifanya biashara unajihusisha moja kwa moja na masuala ya fedha . hivyo, kama mfanyabiashara
lazima ujue namna ya kutunza fedha masuala ya kibenki na kuweka akiba, kukopa na uwekezaji.
MADA YA NANE
115
iv. Ukosefu wa ujuzi wa mambo ya uongozi
Mjasiriamali ni mtu ambaye anatakiwa kujiongoza mwenyewe na kuwa na juhudi katika utekelezaji
wa mambo yake katika biashara. Na ikibidi kutafuta ushauri wa kitaalamu kuhusu mambo ya
uongozi kwani ni sehemu muhimu katika maendeleo ya biashara.
v. Matatizo ya utafutaji wa masoko
Kama haukufanya utafiti kuhusu soko la bidhaa zako unaweza ukajikuta unakosa soko la kuuzia.
Namna ya kukabiliana nayo ni kufanya utafiti wa kina kabla ya kuanza biashara kwa kujifunza kutoka
kwa waliotangulia na wataalamu wa masuala ya biashara.
8.9.7 Nafasi ya Maafisa Watendaji katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini
• Kuelewa dira ya maendeleo ya nchi na kuifafanua vizuri kwa wananchi
• Kuelewa mikakati na sera mbalimbali za kukuza uchumi na kuwaelimisha wananchi ili itumike
kujiletea maendeleo
• Kushirikiana na wataalam na viongozi waliopo kufanya tathmini uwezo wa kiuchumi wa kaya na
kutumia tafiti hizo kubaini mahitaji yao na namna ya kupata mahitaji hayo.
• Kuainisha shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazofanywa na wananchi katika maeneo yao ili
kujua mapato na uwezo uliopo katika kuboresha maisha na hatimaye maendeleo ya jamii.
• Kujua orodha ya wajasiriamali na vikundi vya kiuchumi vilivyopo katika maeneo yake
• Kuhamasisha na kupendekeza maeneo ya uanzishaji na uendelezaji wa mitaa ya viwanda na
vituo vya biashara yakiwemo maeneo ya masoko
• Kujifunza kutokana na mifano mizuri ya uendeshaji wa shughuli za kifedha wa kijadi wa
kukopeshana na kuiboresha kwa madhumini ya kutumika kuendeleza jasirimali na biashara
ndogo kwenye maeneo yake.
• Kuhamasisha ubunifu katika utoaji wa huduma mbalimbali za kifedha hii ikiwa ni pamoja na
huduma za ukopeshaji wa mitambo, utoaji mikopo maalum ya kununulia malighafi, mikopo kwa
ajili ya ununuzi wa hisa na kuendeleza utaratibu wa kuweka na kukopa.
• Kusaidia na kuhimiza uanzishaji na uimarishaji wa vyama na jumuiya za wenye viwanda vidogo,
wajasiriamali na biashara ili iwe rahisi kwao kupata taarifa na utaalamu wa kuboresha shughuli zao.
10
9
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
116
8.10 HITIMISHO
Ili kukuza uchumi na kupunguza umaskini kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anapaswa
kufanya kazi kwa juhudi na maarifa. Hivyo, kila Afisa Mtendaji wa Kijiji au Mtaa hana budi
kuhakikisha kwamba kila mtu mwenye nguvu na uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi ipasavyo.
Kufanya kazi ni haki na ni wajibu wa kila mtu mwenye afya njema na akili timamu. Kamwe kwenye
kijiji/Mtaa asiruhusiwe mtu kuzurura ovyo au kutumia muda mwingi katika shughuli ambazo hazina
manufaa wala tija kama vile ulevi, kucheza bao na kamari. Afisa mtendaji wa Kijiji/Mtaa ahamasishe
jamii kufanya kazi kwa bidii ikiwemo ujasiriamali na kuanzisha vikundi vya kiuchumi.
8.11 MAREJEO
• Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2001) Mafunzo ya Viongozi katika Ngazi ya Kijiji, Mtaa na
Kitongoji. Ofisi ya Rais, TAMISEMI – Dodoma.
• Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2000) Uongozi Bora kwa Wenyeviti wa Serikali za Vijiji,
Vitongoji na Mitaa. Ofisi ya Rais, TAMISEMI – Dodoma
• Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2002): Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, Ofisi ya Rais, Tume
ya Mipango Dar es Salaam.
• Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2003): Mfumo wa Upangaji
• Mipango Shirikishi Jamii wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo,
• Ofisi ya Rais, TAMISEMI- Dodoma.
• Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2003): Mafunzo ya Kuboresha Ujuzi na Stadi za Kazi kwa
Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji
• (Toleo la nne). Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dodoma.
• Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(2006): Rejea ya mwezeshaji Ngazi ya Kijiji/Mtaa, TAMISEMIDodoma.
• Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2003). Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Viwanda vidogo na
Biashara ndogo, Wizara ya Viwanda na Biashara.
10
9
11
12
13
10
9
11
12
13
MADA YA TISA 9 UANDAAJI WA MIPANGO SHIRIKISHI JAMII
MADA YA TISA
121
10
11
12
13
9.1 UTANGULIZI
Kwa kipindi kirefu tangu nchi yetu ilipopata uhuru mwaka 1961 suala la upangaji mipango ya
maendeleo lilikuwa likifanywa na wataalam kutoka Serikalini na Mashirika yasiyo ya Kiserikali.
Wataalam hao walipewa majukumu ya kubaini matatizo ya wananchi, kubaini njia za ufumbuzi na
kuamua nini kifanyike kwa lengo la kuondoa kero/shida za wananchi. Upangaji huo wa mipango
kutoka juu kwenda chini haukutoa fursa kwa Walengwa kuweza kutoa mawazo na mapendekezo
yao juu ya nini kifanyike katika kutatua matatizo yanayowakabili. Utaratibu huu wa upangaji
uliwanyima wananchi haki yao ya ki-katiba ya kushiriki katika mipango na shughuli za utekelezaji
wa maendeleo katika sehemu zao kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 145 ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Miradi mingi iliyobuniwa kutokana na utaratibu huu wa upangaji mipango, haikujali vipaumbele
vya wananchi. Kutokana na mapungufu hayo miradi mingi haikuwa endelevu. Kwa miaka ya
hivi karibuni Serikali imeongeza juhudi zake za kuwawezesha wananchi kuwa na kauli kubwa
juu ya maamuzi yanayohusu maisha yao kwa kuweka msukumo mpya wa kutaka mipango ya
maendeleo iandaliwe na wananchi wenyewe. Kwa sababu hiyo, Serikali imebuni mfumo wa upangaji
mipango unaowataka wananchi kubaini kwanza fursa walizonazo ambazo kama wakizitumia
ipasavyo zitaiwezesha jamii kujiletea maendeleo na pia wananchi wabaini vikwazo vya maendeleo
vinavyoweza kupelekea fursa zilizopo zisiweze kutumika ipasavyo.
Mfumo huu wa upangaji mipango kwa kuzingatia FURSA na VIKWAZO kwa MAENDELEO ndio
unaopewa msukumo na Serikali ikishirikiana na mashirika na taasisi mbalimbali nchini.
Lengo la mada hii ni kuwawezesha maafisa watendaji wa vijiji na mtaa kuwa na uelewa wa kutosha
juu ya upangaji mipango ya maendeleo ulioshirikishi. Uelewa huo wa Maafisa Watendaji wa Vijiji
na Mitaa utawawezesha kuandaa mipango ya maendeleo iliyo endelevu na shirikishi na kwa hiyo
kuwarahisishia usimamizi na uratibu wa shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
9.0 UANDAAJI WA MIPANGO SHIRIKISHI JAMII
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
122
9.2 UMUHIMU WA MIPANGO SHIRIKISHI JAMII
Mfumo wa upangaji mipango wa fursa na vikwazo katika ngazi ya Kijiji, Mtaa na Kata huiwezesha
jamii kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa kuandaa mpango. Aidha, mfumo huu
umechaguliwa na Serikali kutokana na sababu zifuatazo:-
• Ni mfumo wa upangaji mipango unaobadili utaratibu wa upangaji mipango kutoka juu kwenda
chini na kufanya Kijiji na Mtaa kuwa kitovu na chanzo cha upangaji mipango;
• Ni mfumo unaoanza kwa kuibua FURSA za maendeleo zilizopo ndani na nje ya jamii husika hivyo
kujenga fikra za kujitegemea tofauti na mbinu shirikishi nyingine zinazoanza kwa kuibua matatizo
na hivyo kujenga fikra za utegemezi;
• Ni mfumo unaolenga kuleta maendeleo endelevu na kuondoa umaskini kulingana na maelekezo
ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025;
• Ni mfumo unaotekelezeka katika ngazi zote za Kijiji na Mtaa;
• Ni mfumo unaoleta uwazi na uwajibikaji wa shughuli za jamii kila siku;
• Ni mfumo ambao unaziwajibisha Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kushauri na kusimamia mambo
yaliyoamuliwa na wananchi wenyewe.
• Ni mfumo unaotoa nafasi kwa wananchi kumiliki Mipango na Miradi ya Kijiji na Mtaa na hivyo
kuwa na maendeleo endelevu.
9.3 DHANA YA MIPANGO SHIRIKISHI JAMII
9.3.1 Maana ya mpango shirikishi jamii
Mpango shirikishi jamii ni mfumo ambao unaiwezesha jamii kushiriki kutoa maamuzi sahihi katika
mchakato wa uchambuzi, upangaji, utekelezaji, na usimamizi wa shughuli zao za maendeleo.
Ni utaratibu ambao hutayarishwa na jamii yenyewe kwa mpangilio rasmi unaoonyesha shughuli
ambazo zinatarajiwa kufanyika kwa lengo la kuboresha maisha ya jamii inayolengwa. Mpango wa
maendeleo huambatana na ratiba ya utekelezaji ambayo huonyesha muda, wahusika mbalimbali,
usimamizi wa utekelezaji, ufuatiliaji na matokeo ya utekelezaji huo.
9.3.2 Programu
Ni jumla ya miradi tofauti ambayo inawiana au kutofautiana na hubuniwa na kutekelezwa kwa lengo
la kutatua tatizo moja au zaidi. Programu ni sehemu ya mpango.
MADA YA TISA
123
9.3.3 Mradi
Mradi ni jumla ya shughuli zilizobuniwa kutekelezwa kwa lengo la kutatua tatizo fulani lililojitokeza
ndani ya jamii katika kipindi maalum.
Kielelezo Namba 9.1 kinaonyesha mahusiano yaliyopo kati ya Mpango,
Programu na Mradi.
MPANGO
PROGRAMU
MIRADI
Kuboresha hali ya maisha
1. Uhai, Ulinzi na maendeleo ya wanawake, na
makundi maalumu
2. Kuongeza rutuba ya udongo na tija ya Kilimo
3. Kuandaa mazingira mazuri ya uwekezaji
1. Kinga ya magonjwa ya mama na mtoto
2. Uhakika wa chakula katika kaya
3. Ufuatiliaji wa maendeleo ya mama na mtoto
4. Mikopo ya mbolea na pembejeo
5. Hifadhi na utunzaji wa mazingira
6. Elimu ya biashara kwa wajasiriamali
9.3.4 Fursa
Fursa ni rasilimali zilizopo katika jamii ambazo ama zinatumika kikamilifu au hazitumiki kabisa.
Mfano kuwepo kwa zahanati, shule, misitu, ardhi, barabara ndani ya jamii ni fursa zinazoweza
kuiletea jamii maendeleo iwapo zitatumika kikamilifu.
10
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
124
9.3.5 Vikwazo
Vikwazo ni vizuizi vinavyosabisha fursa za maendeleo zisiweze kutumika kikamilifu kwa manufaa ya
wananchi husika, mfano:
• Vikwazo vya kijamii kama vile mila na desturi zilizopitwa na wakati;
• Vikwazo vya kiuchumi kama vile ukosefu wa mitaji ya uwekezaji na uendeshaji;
• Vikwazo vya kisiasa kama vile tofauti za itikadi;
• Vikwazo vya kiufundi kama vile ukosefu wa wataalam wenye ujuzi unaohitajika.
9.3.6 Ufumbuzi
Ufumbuzi ni mikakati na hatua zitakazochukuliwa ili kukabiliana na vikwazo kwa maendeleo.
9.4 HATUA ZA UPANGAJI MIPANGO SHIRIKISHI JAMII
Kulingana na mwongozo na maelekezo ya Kitaifa kuhusu mfumo wa upangaji mipango shirikishi
jamii, kuna hatua mbili za kufuata kama mpango unaoandaliwa na kijiji na mtaa utaandaliwa kwa
mara ya kwanza, kaa ifuatavyo;
• Hatua ya kwanza ni ya maandalizi ya awali na
• Hatua ya pili ni upangaji mpango Shirikishi Jamii kwa vitendo.
9.4.1 Sehemu ya kwanza: Maandalizi ya Awali:
Maandalizi muhimu yanayofanyika ni pamoja na:-
• Uongozi wa Kijiji na Mtaa kufanya mikutano na wananchi kwa lengo la kuwahamasisha na
kuwaeleza juu ya kuwepo kwa zoezi la kuandaa Mpango Shirikishi Jamii;
• Kuandaa timu ya upangaji Mpango Shirikishi Jamii itakayojumuisha wananchi, wataalam na
viongozi;
• Uongozi wa Kijiji na Mtaa kuwasiliana na uongozi wa Kata, Tarafa na Wilaya ili kupata msaada
wa kitaalam;
• Wataalam wa Wilaya hufanya ziara ya awali ambapo hukutana na Serikali ya Kijiji na Kamati
ya Mtaa kwa lengo la kufahamiana, kufafanua lengo la zoezi la upangaji mipango shirikishi na
kukubaliana tarehe ya kuanza kwa zoezi hilo.
9.4.2 Sehemu ya Pili: Upangaji Mpango Shirikishi Jamii
Hatua zifuatazo hufuatwa katika upangaji mpango shirikishi:-
• Mkutano Mkuu wa kijiji na Mtaa kwa lengo la kufafanua madhumuni ya zoezi la upangaji Mpango
Shirikishi Jamii na ufafanuzi wa kazi zitakazofanyika;
• Kukusanya takwimu na habari mbalimbali na uchambuzi wa hali halisi ya jamii;
MADA YA TISA
125
• Kuweka vipaumbele;
• Kuweka malengo, shabaha na kubaini mikakati ya ufumbuzi;
• Kupitisha na kuthibitisha rasimu ya mpango;
• Kuweka taratibu za utekelezaji wa mpango;
• Ufuatiliaji na tathmini.
9.5 UKUSANYAJI WA TAKWIMU
Takwimu ni taarifa iliyokusanywa kwa njia mbalimbali kwa ajili ya madhumuni fulani. Katika kuandaa
Mpango Shirikishi Jamii, hatua ya ukusanyaji wa takwimu ni muhimu kwa sababu ubora na uthabiti
wa mpango unaoandaliwa hutegemea sana usahihi wa takwimu na habari mbalimbali zilizokusanywa
zinazoihusu jamii inayoandaa mpango huo. Kuna takwimu za aina mbalimbali kama vile:-
• Takwimu za kitaalam;
• Takwimu za mazingira;
• Takwimu za nyakati; na
• Takwimu za kijamii na kiuchumi.
9.5.1 Takwimu za Kitaalam
Takwimu hizi hukusanywa kutoka kwenye rejesta ya Kijiji na Mtaa, majalada, taarifa za kitaalamu,
utafiti na uchunguzi uliowahi kufanywa ndani ya Kijiji na Mtaa.
9.5.2 Takwimu za Mazingira
Takwimu za mazingira hukusanywa na wananchi wenyewe kwa kutumia zana shirikishi zifuatazo:-
• Ramani ya Kijiji na Mtaa
• Kataa ya Njia (matembezi mkato).
9.5.2.1 Ramani ya Kijiji na Mtaa
Ramani ya kijiji na Mtaa huchorwa na kikundi cha wananchi kilichoteuliwa katika mkutano mkuu
kuunda timu ya upangaji mpango shirikishi. Ramani huchorwa kwanza ardhini kwa kutumia
rasilimali zilizopo kama vile vijiti, mkaa, mawe, n.k.na kisha huhamishiwa kwenye karatasi au
daftari. Ramani ya Kijiji na Mtaa huonyesha mambo yafuatayo:-
• Mipaka ya Kijiji na Mtaa;
• Mipaka ya vitongoji;
• Eneo la makazi;
• Taasisi zilizopo;
• Raslimali zilizopo;
10
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
126
• Miundo mbinu; na
• Dira
Kielelezo 9.2 Mfano wa Ramani ya Kijiji: Ramani ya Kijiji cha Nrao Kisangara
9.5.2.2 Kataa ya Njia
Kataa ya njia hufanywa na kikundi cha wananchi kilichoteuliwa kwa kutembea kutoka pembe
moja ya Kijiji hadi nyingine (mfano kutoka kaskazini hadi kusini mwa kijiji). Matembezi haya
hufanyika kwa lengo la kuhakiki fursa na vikwazo vilivyoonyeshwa katika ramani ya Kijiji na Mtaa.
Matembezi haya hugawanywa katika ukanda unaofanana. Kielelezo cha Kataa ya njia huonyesha
mambo yafuatayo katika ukanda husika:-
• Matumizi ya ardhi;
• Aina ya udongo;
• Fursa za maendeleo zilizopo;
• Vikwazo vya maendeleo vilivyopo.
MADA YA TISA
127
Mchoro wa kataa ya njia:
9.5.3 Takwimu za Nyakati
Takwimu hizi hukusanywa kwa kutumia zana shirikishi zifuatazo:-
• Matukio Muhimu ya Kihistoria ya Kijiji na Mtaa
• Kalenda ya Msimu.
9.5.3.1 Matukio Muhimu ya Kihistoria
Hizi ni taarifa ambazo huonyesha matukio muhimu yaliyowahi kutokea katika jamii katika siku za
nyuma. Matukio haya yanaweza kuwa ya njaa, magonjwa, ukame, mafuriko, mavuno mengi n.k.
Katika kuainisha matukio haya faida/athari zilizowahi kutokea hubainishwa na hatua au mbinu
za ufumbuzi zilizochukuliwa kukabiliana na matukio hayo huwekwa wazi. Hii huiwezesha jamii
kutumia mbinu kama hizo endapo tatizo linajirudia tena. Jedwali Namba 5.1 linaonyesha namna
ya kuweka kumbukumbu za matukio muhimu Kijijini na Mtaani.
10
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
128
Jedwali Na. 9.1 Historia ya Matukio Muhimu katika Kijiji cha Kona
MWAKA TUKIO SABABISHO UFUMBUZI
1970 Njaa kali (Mmerika) Mabadiliko ya hali ya
hewa (mvua kidogo)
Kununua chakula kutoka vijiji
vya jirani
Msaada toka Serikalini
1980 Mlipuko wa ugonjwa
wa kipindupindu
Kaya kutotumia vyoo
Watu kutotumia maji
salama
Kila kaya kuchimba choo,
Kila Kaya kuchemsha maji ya
kunywa na kuweka mazingira
safi
9.5.3.2 Kalenda ya Msimu
Kalenda ya msimu ni zana inayotumika kuwezesha jamii kutambua shughuli mbalimbali
zinazofanyika katika jamii katika kipindi maalum. Kalenda ya msimu vile vile huisaidia jamii
kutambua ni kipindi gani cha matatizo au faraja katika mwaka wenye matukio ya kawaida. Ni
muhimu kuhakikisha kuwa kalenda ya msimu inatayarishwa kwa kipindi ambacho jamii inafikiria
kuwa ni mwaka wa kawaida. Jedwali Namba 5.2 linaonyesha mfano wa kalenda ya msimu.
MADA YA TISA
129
Jedwali Na. 9.2 Kalenda ya Msimu Kijiji cha Kona
MAELEZO J F M A M J J A S 0 N D
1. Mvua
2. Shughuli za kilimo
A. Kilimo cha mahindi
Kulima
Upandaji
Upaliliaji
Mbolea
Kuvuna
B. Kilimo cha kahawa/ ndizi
Kupalilia
Kukata matawi
Kupiga dawa
Kuvuna
C. Kilimo cha matunda na mboga
Nyanya
Parachichi
Mchicha
Kabichi
3. Shughuli za utawala
4. Nguvu kazi
5. Upatikanaji wa chakula
6. Magonjwa ya Binadamu
Malaria
Kichomi
Kuharisha
10
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
130
9.5.4 Takwimu za Kijamii na Kiuchumi
Takwimu za kijamii na kiuchumi hukusanywa na jamii husika kwa kutumia zana Shirikishi zifuatazo:-
• Uchambuzi wa taasisi;
• Ramani ya rasilimali kijinsia;
• Shughuli za kutwa kijinsia; na
• Tathmini ya uwezo wa Kaya.
9.5.4.1 Uchambuzi wa Taasisi
Taasisi ni chombo chenye uongozi na madhumuni maalum kinachotoa huduma kwa jamii.
Uchambuzi wa taasisi hufanywa na jamii husika pamoja na wawezeshaji kutoka nje ya Kijiji na
Mtaa kwa madhumuni yafuatayo:-
• Kuzitambua taasisi na kazi ambazo zinafanya;
• Kuzitambua taasisi ambazo zinashirikiana na jamii katika nyanja mbalimbali za maendeleo;
• Kufahamu uhusiano uliopo baina ya moja na nyingine katika kuihudumia jamii;
• Kuzitambua taasisi ambazo haziko ndani ya jamii, lakini zina umuhimu ndani ya jamii.
Mahusiano baina ya taasisi na jamii, taasisi na taasisi ndani ya jamii huonyeshwa kwenye mchoro
wa chapati kama inavyoonekana katika Vielelezo 9.2, 9.3 na 9.4.
Kielelezo Na. 9.2 Mahusiano Baina ya Jamii na Taasisi
Kanisa
Klabu ya Mpira wa Miguu
Shule
Sungusungu
Serikali ya Kijiji/Kata
Msikiti
Kijiji/Kata
MADA YA TISA
131
Chapati ya taasisi yenye mahusiano mazuri na Jamii itakuwa karibu sana na kitovu/katikati ya Jamii
na ile yenye mahusiano madogo itakuwa mbali na katikati. Zitolewe sababu za wazi za hali ya
mahusiano na ziandikwe. Ile isiyo na mahusiano mazuri na Jamii itakuwa mbali na kitovu na ile iliyo
na mahusiano mazuri itakuwa karibu sana na kitovu.
Kielelezo Na. 9.3 Mahusiano ya Taasisi na Taasisi
Kanisa
Klabu ya Mpira wa
Miguu
Shule
Serikali ya Kijiji
Msikiti
Kielelezo Na. 9.4 Mahusiano baina ya Jamii na Taasisi zilizo Nje ya Kijiji/Mtaa
Hospitali
Ofisi
ya Kata
Sekondari
Soko
Kielelezo Namba 9.4 kinaonyesha kuwa kadiri mshale wa taasisi unavyokuwa karibu na kitovu cha
duara, ndivyo taasisi hiyo ilivyo muhimu kwa jamii.
10
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
132
9.5.4.2 Ramani ya Rasilimali Kijinsia
Ramani ya rasilimali Kijinsia ni zana shirikishi inayoiwezesha jamii kubaini mapengo ya kijinsia
juu ya umilikaji mali, utoaji wa maamuzi na utumiaji wa rasilimali hizo katika Kaya. Uchambuzi juu
ya umilikaji Mali kijinsia huiwezesha jamii kupanga mikakati ya kuondoa mapengo yaliyopo na
hatimaye kuwa na mipango inayozingatia masuala ya jinsia. Matokeo ya zoezi la uchambuzi wa
ramani ya rasilimali kijinsia huwekwa katika jedwali kama inavyoonekana katikaJedwali Namba 9.3
Jedwali Namba 9.3 Umilikaji wa Rasilimali Kijinsia
Rasilimali Wanaume Wanawake
Umilikaji Maamuzi
Kutumia Kumiliki Kutumia Kumiliki
Ng,ombe √ √ √ X
Nyumba √ √ √ X
Shamba √ √ √ x
Redio √ √ √ √
Vyombo vya kupikia √ x √ √
Kuku √ x √ √
Baiskeli √ √ √ x
Ufunguo: Alama ya √ inamaanisha “Ndiyo”.
Alama ya X inamaanisha “Hapana”.
Matokeo ya zoezi hili yanaonyesha kuwa wanaume wanamiliki mali nyingi na zenye thamani kubwa
wakati wanawake wanamiliki vitu venye thamani ndogo.
Hii inaonyesha mgawanyo usio sawa ambapo jamii inapaswa kuchukua hatua za makusudi
kurekebisha hali kama hiyo.
9.5.4.3 Shughuli za Kutwa Kijinsia
Zana hii shirikishi huiwezesha jamii kuangalia mgawanyo wa kazi kati ya wanawake na wanaume
katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Aidha, upungufu wa uwajibikaji kijinsia huweza
kubainishwa. Zoezi hili hufanyika katika makundi ya wazee, wanawake, wanaume na vijana
na kuonyesha shughuli zote zinazofanywa na makundi haya tangu wanapoamka mpaka
wanapokwenda kulala.
MADA YA TISA
133
Mfano wa jedwali la shughuli za kutwa kijinsia kwa wanawake umeonyeshwa katika Jedwali Namba 5.4
Jedwali Namba 9.4 Shughuli za kutwa kijinsia
Muda Baba Mama
Mtoto wa
kiume
Mtoto wa kike
11.00 Amelala Ameamka na
kutayarisha mlo wa
asubuhi
Amelala Ameamka
11.00 – 12.00 Amelala Amefuata maji Amelala Amefuata maji
12.00 – 01.00 Ameamka • Anafanya kazi za
usafi wa mazingira
• Kuchemsha maji ya
kuoga
• Kuandaa kifungua
kinywa
Ameamka Anasafisha vyombo
01.00 – 01.30 Kifungua kinywa Kifungua kinywa Kifungua
kinywa
Kifungua kinywa
01.30 – 07.00 Kufanya kazi za
shambani
Kufanya kazi za
shambani
Kwenda shule Kwenda shule
07.00 – 08.00 Shambani Anatafuta mboga/ kuni Shule Shule
08.00 – 09.00 Kurudi nyumbani Kurudi nyumbani akiwa
na mzigo wa kuni
Kurudi
nyumbani
Kurudi nyumbani
09.00 – 10.00 Amepumzika Anaandaa chakula Amepumzika Anamsaidia mama
kuandaa chakula
10.00 – 10.15 Anakula Anakula Anakula Anakula
10.30 – 04.00
usiku
Burudani na
chakula cha
usiku
• Kufua nguo
• Kuosha vyombo
• Kuangalia mifugo
• Kuogesha watoto
• Chakula cha usiku
na anatandika
kitanda
Anacheza na
chakula cha
usiku
Anaosha vyombo
Chakula cha usiku
04.00 – 11.00
asubuhi
Amelala Anaanda mlo wa
asubuhi
Amelala Amelala
Masaa ya
kufanya kazi
7:30 13:30 8:30 13:30
9.5.4.4 Tathmini ya Uwezo wa Kaya
Zoezi la tathmini ya uwezo wa kaya huiwezesha jamii kutambua hali ya uwezo wa kiuchumi kwa
jamii inayoandaa mpango shirikishi jamii. Hii huiwezesha jamii kutambua kaya zenye hali nzuri,
hali duni na zile zenye hali nafuu, na hivyo kuweza kupanga mikakati ya namna ya kupambana
na umaskini kwa kaya pamoja na jamii yote.
10
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
134
Zoezi la tathmini ya uwezo wa kaya hufanyika katika ngazi ya Kitongoji na Mtaa. Washiriki
huweka vigezo vya uwezo wa kujikimu kwa kaya zenye hali nzuri, nafuu na duni. Matokeo ya
tathmini ya uwezo wa kujikimu ya kaya hujumuishwa na kupata tathmini ya uwezo wa Kitongoji
na Mtaa. Matokeo ya kila Kitongoji na Mtaa hukusanywa na kujumuishwa na hivyo kupata
matokeo ya kijiji.
Mfano wa tathmini ya jumla ya uwezo wa Kijiji na Mtaa unaonyeshwa katika Jedwali Namba 9.5.
Jedwali Namba 9.5: Tathmini ya Uwezo wa Kijiji na Mtaa
Na. Kitongoji/ Mtaa Kaya zenye hali
Duni Nafuu Nzuri Jumla ya kaya
1 A 30 10 5 45
2 B 52 27 13 92
3 C 67 22 10 99
4 D 43 17 9 69
Jumla 192 76 37 305
Asilimia 63 25 12 100
9.6 UWEKAJI WA VIPAUMBELE
Vipaumbele huwekwa ili kujua ni suala gani linapewa umuhimu wa kwanza, na lipi linafuatia hadi la
mwisho. Vipaumbele huwekwa katika makundi yanayojumuisha wazee, wanawake, wanaume na
vijana. Baada ya kujumuisha matokeo ya kila kundi, vipaumbele vya jumla huweza kupatikana na
hivyo kuiwezesha jamii kupanga mpango wake kutokana na vipaumbele hivyo. Njia tatu hutumika
katika kuweka vipaumbele ambazo ni:-
• Kuweka vipaumbele kwa kupiga kura,
• Kuweka vipaumbele kwa utashi, na
• Kuweka vipaumbele kwa mlinganisho kijozi.
Njia ya mlinganisho kijozi ni njia bora zaidi ya kuweka vipaumbele kwa kutumia jamii nzima. Njia hii
hutoa fursa ya kulinganisha njia moja ya ufumbuzi na nyingine hadi njia zote za ufumbuzi zikamilike.
Aidha, njia hii huhitaji uwezo mzuri wa mwezeshaji.
MADA YA TISA
135
Mfano wa Jedwali la Mlinganisho Kijozi umeonyeshwa katika Jedwali Namba 5.6 lenye njia tofauti
za ufumbuzi kwa shabaha ya kufikia lengo la kujitosheleza kwa chakula.
Jedwali Na. 9.6. Vipaumbele kwa kutumia njia ya Mlinganisho Kijozi
UFUMBUZI MBEGU B/SHAMBA SOKO GULIO KIWANDA BARABARA KUFYEKA JOSHO DUKA ALAMA NAFASI
MBEGU MBEGU SOKO GULIO KIWANDA BARABARA MBEGU JOSHO MBEGU 3 6
B/SHAMBA SOKO GULIO KIWANDA BARABARA B/SHAMBA JOSHO DUKA 1 8
SOKO GULIO SOKO BARABARA SOKO SOKO SOKO 6 3
GULIO GULIO BARABARA GULIO GULIO GULIO 7 2
KIWANDA BARABARA KIWANDA KIWANDA KIWANDA 5 4
BARABARA BARABARA BARABARA BARABARA 8 1
KUFYEKA JOSHO DUKA 0 9
JOSHO JOSHO 4 5
DUKA 2 7
Mwisho kila njia ya ufumbuzi huhesabiwa na kuwekewa alama na hatimaye kupewa nafasi kuanzia
ya kwanza hadi ya mwisho. Katika mfano ulioonyeshwa kwenye Jedwali Namba 9.6, kipaumbele
cha kwanza kilikuwa ni ukarabati wa barabara, ikifuatiwa na kuanzishwa kwa gulio. Kipaumbele cha
mwisho kilikuwa ni kufyeka msitu na kuanzisha mashamba mapya.
9.7 KUWEKA MALENGO, SHABAHA NA KUBAINI MIKAKATI YA UFUMBUZI
Uchambuzi wa takwimu na habari zilizokusanywa huiwezesha jamii kubaini fursa za maendeleo
zilizopo na vikwazo au matatizo yanayoikabili jamii. Kwa kuzingatia vipaumbele vilivyowekwa na
jamii, timu za upangaji mipango shirikishi kutoka ngazi ya Kata na Wilaya hazina budi kushirikiana
na wananchi katika kuweka malengo, shabaha na kubaini njia mwafaka za kutatua matatizo ya
wananchi. Aidha, kwa kila lengo linalowekwa na jamii, ni vema kuainisha fursa zilizopo, vikwazo
vilivyopo, sababu ya kuwepo kwa vikwazo hivyo na njia sahihi za utatuzi wa vikwazo hivyo. Jamii
vile vile hujiwekea hatua za utekelezaji, nani atakayehusika, mahitaji halisi, gharama na awamu za
utekelezaji.
Baada ya kukamilisha uchambuzi na kuainisha malengo shabaha na shughuli muhimu jamii
ikisaidiwa na timu ya upangaji shirikishi hukamilisha jedwali la mpango na kutathimini uwezekano
wa utekelezaji wake. Mfano wa jedwali la Mpango Shirikishi Jamii wa Fursa na Vikwazo huonekana
kama Jedwali Namba 5.7 linavyoonekana. Rasimu ya mpango wa kijiji na Mtaa itawasilishwa
na Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa katika kikao maalum cha Kamati ya Maendeleo ya Kata ili
10
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
136
kutoa ushauri kwenye rasimu ya mipango ya miaka mitatu ya Vijiji na Mitaa. Maoni na ushauri wa
Kamati ya Maendeleo ya Kata yatajumuishwa kwenye rasimu na kuwasilishwa kwenye Mkutano
Mkuu Maalum wa kijiji ili kujadiliwa na kupitishwa. Baada ya kupitishwa, Mpango utawasilishwa
katika ngazi ya Halmashauri. Aidha, nakala ya Mpango itawasilishwa pia kwenye Kata ili Kuandaa
muhtasari wa shughuli za utekelelzaji kisekta.
Jedwali Namba 9.7 Mpango Shirikishi Jamii wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo
Kijiji cha…………………
Kata ya:………………….
Wilaya ya:…………………
Mkoa wa:………………………
Lengo Kuu: Maisha Bora na Mazuri
Lengo: Kujitosheleza kwa Chakula na Kuwa na Uhakika wa Upatikanaji Wake
Lengo
mahususi
Fursa Vikwazo Sababisho Ufumbuzi
Hatua za
utekelezaji
Mahitaji
Gharama
Viashiria
Ndani Nje
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
Kuongeza
uzalishaji wa
zao la mahindi
kutoka
magunia 10
kwa sasa
hadi kufikia
magunia 15
kwa ekari kwa
mwaka ifikapo
mwaka 2008
Upatikanaji
wa
pembejeo
za kilimo
(mbegu,
mbolea na
madawa)
Upungufu
wa
huduma za
ugani
Kuwepo kwa
mtumishi
mmoja tu wa
ugani anaye
hudumia Vijiji
vitano
Uboreshaji
wa huduma
za ugani
Kutoa usafiri
kuwa na
vishamba
darasa
Pikipiki
mafuta
mbegu
posho 50,000
150,000
50,000
75,000
Idadi ya
magunia ya
mahindi
MADA YA TISA
137
9.8 MAPITIO NA UWEZESHAJI
9.8.1 Maana ya mapitio na uwezeshaji
Mapitio ni mchakato wa kupitia/kuhuisha mipango iliyokwisha pangwa kwa kuzingatia matokeo ya
Ufuatiliaji na Tathmini ya kila mwaka. Mapitio yanafanyika ili kuangalia mabadiliko ya mahitaji ya
Jamii pamoja na sera za kitaifa. Mipango iliyopangwa kwa kutumia mfumo wa Fursa na Vikwazo
kwa Maendeleo sharti izingatie dhana hii ya Mapitio ili kuifanya mipango iwe endelevu.
Uwezeshaji ni mchakato unaofanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuijengea uwezo Jamii katika
shughuli za maendeleo. Uwezeshaji unasaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kuainisha mahitaji halisi
na vipaumbele vya Jamii.
Uwezeshaji hufanyika kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu, (kisanduku 1.1 kuhusu ushauri wa
kitaalamu) na upelekaji wa taarifa zinazohusu sera na miongozo ya kisekta kwa Jamii wakati wa
kufanya mapitio kwa ajili ya kuhuisha mpango, kutekeleza na kufanya Ufuatiliaji na Tathimini
Shirikishi. Wakati ushauri unatolewa, na taarifa mbalimbali zinasambazwa kwa Jamii ni muhimu
Mamlaka za Serikali za Mitaa kutilia mkazo suala la umiliki wa mipango na kuzijengea Jamii uwezo.
Kisanduku 1.1: Ushauri wa Kitaalamu
Ushauri wa kitaalamu unahusisha
1. Teknolojia zilizopo
2. Vifaa na zana bora
3. Makadirio ya gharama halisi
4. Mifano ya shughuli zinazolandana
5. Vyanzo vya fedha vinavyowezekana na kufanya ufuatiliaji na tathimini shirikishi
6. Sera za kitaifa, miongozo na viwango vya kisekta 10
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
138
9.8.2 Wahusika katika mchakato wa mapitio na uwezeshaji
Wahusika wa Mapitio na Uwezeshaji wamegawanyika katika ngazi ya Jamii na Wilaya. Wakati wa
kuanza Mapitio na Uwezeshaji (mwaka wa 1) usambazaji wa miongozo ya Mapitio na Uwezeshaji na
utoaji wa mafunzo ya namna ya kufanya mapitio hufanyika na kuratibiwa na OWM – TAMISEMI.
9.8.2.1 Ngazi ya Jamii
Katika ngazi ya Kijiji, Mkutano Mkuu wa Kijiji ndio wenye mamlaka ya utoaji wa maamuzi juu ya
miradi mbalimbali ya maendeleo. Halmashauri ya Kijiji ina wajibu mkubwa wa kufanya Mapitio
na Uwezeshaji katika kutambua shughuli za kiuchumi na za kijamii. Halmashauri ya Kijiji lazima
ifahamu vizuri dhana ya Mapitio na Uwezeshaji na vilevile iwezeshe na kuhamasisha Jamii
kufanya Mapitio.
Katika ngazi ya Mtaa, Kamati ya Maendeleo ya Kata ina wajibu mkubwa katika kufanya Mapitio
na Uwezeshaji kuhusiana na shughuli za kiuchumi na kijamii chini ya uwezeshaji wa Mamlaka
za Serikali za Mitaa. Kamati ya Maendeleo ya Kata ni lazima ifahamu vizuri dhana ya Mapitio na
Uwezeshaji pamoja na kuwezesha na kuhamasisha Jamii kufanya Mapitio.
Aidha, Maafisa Ugani wa Kata kwa kushirikiana na Afisa Mtendaji wa Kata/Mtaa/Kijiji, watashiriki
kikamilifu katika kuwezesha Mapitio katika ngazi ya Jamii.
9.8.2.2 Ngazi ya Wilaya
Katika ngazi ya Wilaya/Manispaa/Mji/Jiji, Baraza la Madiwani lina majukumu yafuatayo:
• Kuandaa, kuratibu na kusimamia utekelezaji wa mipango yote katika eneo la utawala la
kisheria na
• Kuzingatia, kurekebisha na kuratibu mipango ya maendeleo, miradi mbalimbali na mipango
ya vijiji katika eneo la utawala la kisheria
Kutokana na uwezo huu, Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM) zinaweza kufanya mapitio na
uwezeshaji kuhusiana na shughuli za kiuchumi na kijamii katika eneo lake. Katika kutekeleza
haya mafunzo ya wawezeshaji ngazi ya Wilaya na ngazi ya Kata ni muhimu kufanyika ili kuwapa
ujuzi wa kuweza kuiwezesha Jamii kufanya Mapitio ya mipango yao ya maendeleo.
Katika ngazi ya Kata, Kamati ya Maendeleo ya Kata , pamoja na majukumu mengine, ina
majukumu yafuatayo kisheria;
• Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa miradi na mipango ya Halmashauri za Wilaya/
Manispaa/Mji/Jiji ndani ya Kata husika.
MADA YA TISA
139
• Kupanga na kuratibu shughuli zote kwa kutoa ushauri kwa wakazi wa Kata husika katika
kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.
• Kuhamasisha na kuchochea maendeleo shirikishi katika Kata
9.8.3 Umuhimu wa Mapitio
Ili Mamlaka za Serikali za Mitaa ziweze kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma ni lazima
kuzingatia mchakato wa kufanya mapitio kama msingi muhimu katika uandaaji wa mipango yake.
Mapitio yanayofanywa na Jamii ni muhimu kwa sababu yanawezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa
kubainisha mahitaji ya Jamii katika mipango iliyohuishwa.
Endapo mipango ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa haitatokana na mipango ya Jamii iliyohuishwa,
mipango hiyo haitakuwa na umuhimu kwa Jamii kwa vile haitakuwa na vigezo vinavyotokana na
mgao wa bajeti na hivyo kusababisha matumizi ya fedha yasiyokuwa ya manufaa na yasiyo ya wazi
kwa Jamii kwa sababu hayatokani na mahitaji ya Jamii hiyo.
9.9 UTAYARISHAJI WA BAJETI
9.9.1 Maana ya makisio
Makisio ni matarajio ya mapato na matumizi katika kipindi maalum kwa shughuli zinazohusiana na
fedha.
9.9.2 Maana ya Bajeti
Bajeti ni mpango wa ukusanyaji wa mapato na matumizi katika kipindi maalum. Bajeti ni
sehemu ya mchakato wa upangaji mipango ambayo inahusisha mgawanyo wa rasilimali chache
katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Ni dhahiri kwamba Mpango na Bajeti ni dhana
zinazotegemeana kwani mpango bila bajeti hauwezi kutekelezeka hata kama ni mzuri kiasi gani.
9.9.3 Madhumuni ya Kuandaa Bajeti
• Kuwawezesha wananchi kupanga, kutekeleza, kutathmini na kusimamia rasilimali zao;
• Kuwawezesha wananchi kuchangia katika kutoa mawazo na nyenzo kwa ajili ya maendeleo ya
sehemu zao;
• Kuwawezesha wananchi kujenga ari ya kujiendeleza na moyo wa kuwajibika katika utekelezaji
wa mipango yao kwa kuongozwa na mpango wa mapato na matumizi.
10
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
140
9.9.4 Faida ya Makisio/Bajeti
• Kuongeza ukusanyaji wa mapato na utumiaji wa mapato yaliyokusanywa;
• Kurahisisha ufuatiliaji wa ukusanyaji wa mapato na kudhibiti matumizi;
• Nidhamu katika ukusanyaji wa mapato na matumizi yake hujenga moyo wa walipa kodi
kuendelea kulipa kodi, ada na ushuru mbalimbali; na
• Kuwezesha kujua vyanzo muhimu na visivyo muhimu ili kusaidia wakati wa kufanya maamuzi.
9.9.5 Utayarishaji wa Makisio ya Bajeti
Makisio ya bajeti hutayarishwa kutokana na vyanzo vya mapato vinavyoeleweka na gharama
ambazo Kijiji na Mtaa vinatarajia kulipia katika utoaji wa huduma mbalimbali. Makisio ya bajeti
yamegawanyika katika sehemu kuu zifuatazo:-
9.9.5.1 Mapato
Sheria namba 9 ya mwaka1982 imeorodhesha vyanzo vya mapato ya kijiji kama ifuatavyo:-
a) Mapato ya Ndani
• Mapato ya kutokana na shughuli, biashara na huduma;
• Ushuru wa mazao;
• Ushuru wa ada mbalimbali kutokana na pombe, maliasili, madini, minada n.k;
• Mapato mengineyo kama vile faini na tozo mbalimbali zinazotokana na utekelezaji wa sheria
ndogo za vijiji.
b) Mapato ya Nje
• Ruzuku kutoka Halmashauri;
• Mikopo kutoka Taasisi za Fedha;
• Misaada kutoka Mashirika ya hiari;
• Misaada au mikopo kutoka Taasisi za Maendeleo za Kimataifa;
• Misaada na mikopo kutoka kwa watu binafsi ; na
• Mapato na mikopo kutoka vyanzo vingine.
9.9.5.2 Matumizi
a) Matumizi ya Kawaida
• Mishahara na posho;
• Gharama za safari; na
• Matumizi mengineyo yatakayokubalika katika vikao.
MADA YA TISA
141
b) Matumizi ya Maendeleo
• Matumizi kwa ajili ya ukarabati na matengenezo ya mali za kudumu kama vile majengo,
mashine, meza, kabati na trekta;
• Matumizi kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa huduma za jamii kama vile Elimu, Afya, Maji,
Kilimo, Mifugo, Barabara n.k.
• Matumizi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kiuchumi; na
• Matumizi kwa ajili ya ujenzi wa vitega uchumi na biashara.
Mfano wa Muundo wa Bajeti ya Kijiji na Mtaa ni kama unavyoonekana katika Kielelezo Namba 9.5
Kielelezo Namba 9.5: Mfano wa Muundo wa Bajeti ya Kijiji na Mtaa
MAELEZO KIASI (TSHS)
MAPATO
(a) Mapato ya ndani
Ada 30,000
Ushuru wa mazao 100,000
Faini 20,000
Ushuru wa masoko 100,000
Jumla ndogo 250,000
(b) Mapato ya nje
Halmashauri 500,000
Misaada (TASAF na AFRICARE) 1,000,000
Jumla ndogo 1,500,000
JUMLA KUU YA MAPATO 1,750,000
MATUMIZI
(a) Matumizi ya kawaida
Posho ya wakusanyaji mapato 50,000
Huduma za ofisi 100,000
Usafiri 50,000
Jumla ndogo 200,000
(b) Matumizi ya maendeleo
Ukarabati wa zahanati 550,000
Ujenzi wa darasa 1,000,000
Jumla ndogo 1,550,000
JUMLA YA MATUMIZI 1,750,000
10
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
142
9.10 HITIMISHO
Mada hii imeelezea mwelekeo wa sasa wa Serikali wa kubadili mfumo wa upangaji mipango ya
maendeleo ya Kijiji na Mtaa kutoka ule wa juu kwenda chini kuwa wa kuanzia chini kwenda juu kwa
kuwashirikisha wananchi. Mada pia imeelezea umuhimu wa kufanya Mapitio ya Mipango ya Jamii
kila mwaka ili kuendana na mabadiliko ya vipaumbele vya jamii na pia sera za kitaifa. Aidha, taratibu
za uandaaji wa bajeti ya kijiji na umuhimu wa kutayarisha bajeti hiyo vimefafanuliwa. Maafisa
Watendaji wa Vijiji na Mtaa hawana budi kuzielewa taratibu hizo ili waweze kutayarisha makisio ya
mapato na matumizi ya Mitaa na Vijiji vyao kwa ufanisi wa hali ya juu.
9.11 MAREJEO
URT (2000): “Brief on Opportunities and Obstacles to Development Planning (O &OD
Participatory Planning) Presidents Office – Regional Administration and Local Government,
Dodoma”;
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2004): Mafunzo ya Kuboresha Ujuzi na Stadi za Kazi kwa
Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Dodoma, Tanzania;
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2003): Mfumo wa Upangaji Mipango Shirikishi Jamii wa
Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo; Kitabu cha Rejea Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa, Dodoma;
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2000): Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977.
MADA YA KUMI10 10
11
12
13
UANDIKAJI NA USIMAMIZI WA MIRADI
MADA YA KUMI
145
10.1 UTANGULIZI
Mada hii inaelezea kwa muhtasari namna ya kuandaa andiko la mradi na jinsi ya utekelezaji wake.
Aidha, mada pia inafafanua njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika kupata fedha za kugharamia
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotokana na andiko la mradi.
Lengo la mada hii ni kumwezesha Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa ili aweze kuelewa namna ya
uandaaji wa andiko la mradi na kuibua vyanzo mbalimbali vya fedha za kugharamia utekelezaji wa
miradi ya maendeleo inayotokana na ubunifu wa andiko la mradi. Uelewa wa uandishi wa andiko la
mradi na uibuaji wa vyanzo vya mapato utasadia Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa kuwa mstari wa
mbele katika kuandaa maandiko ya miradi na kutafuta vyanzo vya fedha za kugaharamia miradi hiyo
badala ya kukaa na kusubiri Serikali pekee kutekeleza jukumu hilo.
10.2 MUUNDO WA ANDIKO LA MRADI
Kila andiko lazima liwe na maelezo mafupi kuhusu mradi. Andiko la mradi litaratibiwa na VEO/
MEO akishirikiana na kamati ya uwezeshaji ya kijiji. Pamoja na mambo mengine muhimu, maelezo
yatatolewa kwa ufupi juu ya mambo yafuatayo;
• Mahali mradi ulipo, (Mfano mradi utatekelezwa katika Kata/Kijiji/Wilaya – taja jina la eneo husika
na umbali toka makao makuu ya wilaya kama ni mradi wa kikundi/jamii).
• Hali iliyopelekea kubuniwa kwa mradi - elezea tatizo lililosababishwa kubuniwa kwa mradi kama
mbinu ya utatuzi - (mfano mradi wa maji umebuniwa na wanakijiji/Kata /Wilaya ili kuwawezesha
wanajamii kupata maji katika umbali wa mita 400 au kuongeza uzalishaji).
• Malengo ya mradi – elezea hali inayotarajiwa kufikiwa kwa kipindi cha mradi husika ukizingatia
malengo mahsusi ambayo yataelezea hatua mbalimbali za utekelezaji ili kufika lengo kuu. (Tumia
mti wa malengo/matumaini)
• Kazi zitakazofanyika kufikia malengo hayo- elezea kazi zote zitakazotekelezwa katika kipindi
husika kwa mtirirko wake, (mfano kuchagua eneo la kuchimba bwawa/lambo/kisima, Kutayarisha
vitabu vya tenda, kutangaza tenda, kuchagua mkandarasi, kusafisha eneo, kupata mafunzo n.k.
• Gharama za mradi - elezea mradi utagharimu jumla ya shilingi ngapi mpaka utakapomalizika, pia
elezea mchango utakaotolewa na jamii na wahisani mbalimbali.
(Mfano Mradi huu utagharimu jumla ya Tshs. 41,079,000/=. Mchango wa Serikali ni 80% sawa Na
Tsh.35, 000,000/= ambapo kati ya hizo Tshs 5,000,000/= ni kwa ajili ya kutujengea uwezo
wakuendesha mradi wetu wa bwawa, na zilizobaki ni za kutekelezea mradi. Jamii itatoa mchango
wa Tshs. 6,079,000/= zikiwa ni nguvu kazi).
10.0 UANDIKAJI NA USIMAMIZI WA MIRADI
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
146
• Muda wa utekelezaji – mradi utatekelezwa kwa muda gani – hapa unaweza kutoa maelezo kwa
kutumia miezi/miaka, (Mfano - Mradi huu tunatarajia kuutekeleza kuanzia mwezi Julai 2010 hadi
June 2011).
• Manufaa yanayotarajiwa – elezea jinsi ambavyo jamii itanufaika baada ya mradi kukamilika
(mfano - jamii itapata maji ya kutosha karibu na makazi yao, mifugo itapata maji ya kunywa, kijiji
kitaongeza mapato kutokana na ufugaji wa samaki/kilimo cha mbogamboga).
Ili kuhakikisha kuwa mambo yote muhimu yameelezwa, muhtasari utayarishwe baada ya sehemu
zote za andiko kukamilika. Muhtasari wa andiko la mradi usizidi kurasa mbili. Ikibidi Jedwali la bao
mantiki linaweza kuwekwa mara tu baada ya maelezo ya muhtasari. (Mfano wa Bao Mantiki (Logical
Frame work).
MADA YA KUMI
147
Jedwali 10.1: Bao Mantiki la Mradi wa Ujenzi wa Bwawa Kijiji cha Mazingara
SHUGHULI VIASHIRIA NJIA ZA KUHAKIKI DHANIO
Lengo kuu
Uzalishaji wa mazao ya kilimo na
mifugo umeongezeka katika kijiji cha
Mazingara ifikapo Juni 2011.
1. Kilimo cha umwagiliaji wa
mazao kimetekelezwa
2. Ufugaji kwa kutumia aina bora
za mifugo umefanyika.
1. Taarifa ya kamati ya mradi wa
Jamii
2. Taarifa za mtaalam wa kilimo na
mifugo
Malengo Mahsusi
1. Kufanya savei ya bwawa.
2. Kuchimba bwawa.
3. Kupata mafunzo juu ya utunzaji
wa bwawa na hifadhi ya mazingira
miundo mbinu ya kuhifadhi maji.
1. Utafiti wa bwawa umefanyika
2. Bwawa limechimbwa
3. Mafunzo juu ya utunzaji wa
bwawa na hifadhi ya mazingira
yametolewa
1. Taarifa ya kamati ya mradi wa
Jamii
2. Taarifa za mtaalam wa kilimo/
mifugo
Matokeo
1. Bwawa limepatikana
2. Uzalishaji wa mazao ya kilimo
umeongezeka.
3. Kipato kimeongezeka
1. Bwawa 1 limechimwa ifikapo
Juni 2008
2. Kanuni za kilimo/ufugaji bora
zimezingatiwa
3. Mahitaji muhimu yanapatikana
katika kaya
1. Kutembelea na kuona bwawa
2. Taarifa ya kamati ya mradi wa jamii
3. Taarifa ya Serikali ya kijiji.
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
148
10.3 UTANGULIZI
Toa maelezo mafupi kuhusu mchakato uliopitiwa katika kuibua na kuandaa mradi. Utangulizi pia
utajumuisha taarifa na takwimu muhimu kuhusu jamii/kijiji/mtaa/Kata/wilaya au kikundi husika.
Taarifa na takwimu hizo (tazama O&OD mada ya tisa) ni kama vile eneo la kijiji, miundo mbinu
iliyopo, matumizi ya ardhi, hali ya uzalishaji wa mazao na mifugo, upatikanaji wa malisho, upatikanaji
na mtawanyiko wa mvua, hali ya joto, idadi ya kaya, idadi ya kaya zenye mifugo, idadi ya wakazi
wenye uwezo wa kufanya kazi na idadi ya wanakikundi. Pia namba ya akaunti ya benki iwapo mradi
utatoa fedha moja kwa moja kwa jamii itabidi kuwe na akaunti ya benki inayotambuliwa na kijiji/
Mtaa/Kata/Halmashauri / Manispaa. Taarifa na takwimu hizi zitategemea aina na asili ya mradi.
Kwa mfano si lazima kwa kikundi kuonyesha idadi ya watu katika kijiji, eneo la kijiji, idadi ya watu
wenye uwezo wa kufanya kazi n.k. Kama ni mradi wa ufugaji ni lazima kuonyesha idadi ya mifugo na
eneo la malisho lililopo.
Taarifa zingine zitahusu taasisi zilizopo na miradi mingine inayotekelezwa, fursa zingine zilizopo
zinazoweza kusaidia utekelezaji wa mradi.
(Mfano kuwepo mabonde yanayoweza kuhifadhi maji muda mrefu, kuwepo kwa mifugo, ardhi yenye
rutuba, mazao ya kilimo ya chakula na biashara yanayostawi vizuri, kuwepo kwa nguvukazi ya
kutosha).
Elezea matatizo yatakayotatuliwa na mradi yatakayotokana na mti wa matatizo - Mti wa matatizo
uambatanishwe kama (Kiambatanisho Na.10. I).
MADA YA KUMI
149
Kutokutumia
mbolea
Kulima zao
moja muda
mrefu
Bei kubwa
ya mbegu
ya mahindi
Ukosefu wa
elimu ya
matumizi ya
mbegu bora
Uwezo
mdogo
wa udongo
kuhifadhi
maji
Uhaba wa maji
ya umwagilia
Mashambani
Mashamba
machafu
Matumizi
duni ya
viuatilifu
Elimu duni
ya kilimo
cha
mahindi
Ukosefu wa
miundo
mbinu ya
maji
Kilimo cha
kuparua
Maduka ya
mbegu bora
yako mbali
Ukosefu wa
mawakawa
mbegu
Ukosefu wa
elimu ya
matumizi ya
mbolea
Maduka ya
mbolea
kuwa mbali
Elimu duni
ya kilimo
mseto
Kuwa mbali
na huduma
za kitaalam
Ukosefu
wa mitaji
Matumizi ya
zana duni
Ukosefu wa
mawakala
wa mbolea
Wadudu na wanyama
waharibifu wa mahindi
Upungufu wa unyevunyevu
Mashambani
Matumizi ya mbegu
duni ya mahindi
Upungufu wa
Rutuba mashambani
HALI DUNI YA MAISHA
KIPATO DUNI
KUTOKUWA NA
UHAKIKA WA CHAKULA
UZALISHAJI MDOGO WA
MAHINDI GUNIA 5 KWA EKA
Kiambatanisho 10.2 Mti wa Matatizo – Kilimo
Kila kipengele kitaandikwa katika aya ya peke yake. Taarifa hizi zinategemewa kupatikana kutoka katika ripoti ya O&OD ya kijiji/jamii husika na tafiti nyingine
zilizowahi kufanyika katika jamii/kijiji husika kama zipo.
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
150
10.4 MALENGO YA MRADI
Malengo ya mradi yatokane na mti wa malengo/matumaini uliotayarishwa wakati wa zoezi la O&OD. (Kiambatanisho Na. 2)
Kiambatanisho 10.2 Mti wa Matumaini – Kilimo
UZALISHAJI WA MAHINDI
UMEONGEZEKA GUNIA 15 KWA EKA
HALI NZURI YA MAISHA
Wadudu na
wanyama
waharibifu wa
mahindi
wamedhibitiwa
BWAWA
POWER TILLER
KIPATO KIMEONGEZEKA
KUWA NA UHAKIKA
WA CHAKULA
Unyevunyevu
mashambani
umeongezeka
Mbegu bora za
mahindi
zimetumika
Rutuba
imeongezeka
mashambani
Matumizi
sahihi ya
viuatilifu
Mashamba
yame
paliliwa
Maji ya
umwagiliaji
Mashambani
yamepatikana
Uwezo wa
udongo
kuhifadhi maji
umeongezeka
Elimu ya
matumizi
ya mbegu
bora
imetolewa
Mbegu ya
mahindi
Inauzwa
kwa bei nzuri
Mbolea
imetumika
Kilimo Mseto
kinatumika
Elimu ya kilimo
bora cha
mahindi
imetolewa
Ukosefu wa
miundo mbinu
ya maji
Kilimo cha
Kutifua
kimetumika
Maduka ya
bora yako
karibu na
wakulima
mbegu
Mawakala
wa mbegu
bora
wamepatikana
Elimu ya
matumizi
ya mbolea
imetolewa
Maduka ya
mbolea
yako karibu
Elimu ya
kilimo
mseto
imetolewa
Ukosefu wa
mawakala
wa mbolea
Zana bora
zimetumika
Huduma za kitaalam
zimepatikana
ya kilimo cha mahindi
Mitaji
yapatikana
kujenge
miundombinu
MADA YA KUMI
151
10.4.1 Lengo kuu
Ainisha hali nzuri tarajiwa ya muda mrefu kidogo baada ya utekelezaji wa mradi. Kwa kawaida
lengo kuu ni matokeo ya muda mrefu ya mradi (mfano - Upatikanaji wa maji safi kwa jamii katika
umbali wa mita 400 ifikapo mwaka 2013, uzalishaji wa mahindi umeongezeka kutoka gunia 15
kwa eka ifikapo 2013). Kwa kawaida lengo kuu ni hali nzuri inayotarajiwa kupatikana baada ya
kutatua tatizo kuu katika jamii/kikundi husika. (Angalia mti wa malengo/matumaini)
Malengo Mahsusi
Ainisha matokeo ya muda mfupi yanayotarajiwa kupatikana kutokana na kufanikiwa kwa utekelezaji
wa mradi. Maelezo haya yatajumuisha matokeo mahususi yatakayotokana na utekelezaji wa
shughuli mbali mbali zilizopangwa kutekelezwa katika kipindi cha utekelezaji wa mradi.
(Mfano - Bwawa limechimbwa, maji yanapatikana, mazingira yamehifadhiwa. Kama ni mradi wa
kilimo – mbegu bora za mahindi zimetumika, unyevunyevu mashambani umeongezeka, rutuba
imeongezeka, wadudu waharibifu wamedhibitiwa).
Mti wa malengo uambatanishwe kama (Kiambatanisho Na.10. 2)
10.5 Maelezo ya Mradi
Toa maelezo kuhusu teknolojia iliyochaguliwa na jamii au kikundi kama ufumbuzi wa kitaalam wa
matatizo yao. (Mfano uchimbaji wa bwawa)
Pia maelezo mafupi yatolewe kuhusu teknolojia mbadala zilizojadiliwa lakini hazikuchaguliwa kwa
sababu moja au nyingine. Sababu za kutochagua teknolojia mbadala zielezwe.
(Mfano - Uchimbaji wa visima ni teknolojia mbadala ambayo haikuchaguliwa kwa sababu
utunzaji wake una gharama zaidi kuliko bwawa).
Pia kipengele hiki kitaeleza kwa kina kazi zote zitakazofanyika katika kipindi chote cha utekelezaji
ikiwa ni pamoja na mafunzo na huduma za kitaalam zitakazohitajika. Maelezo haya yatahusu hasa
aina ya kazi, muda wa utekelezaji wake, na jinsi ambavyo kazi hizi zitasaidia katika kufikia malengo
yaliyokusudiwa. Mpango wa kazi shirikishi jamii utaambatanishwa kama Kiambatanisho Na. 10.3.
(Angalia mfano)
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
152
Kiambatanisho 10.3 (Mfano wa mpango kazi shirikishi jamii)
Na Tatizo Visababishi Ufumbuzi Mhusika Msimamizi Muda wa utekelezaji Rasilimali zinazohitajika
Kuanza Kumaliza Ndani Nje
1. Uhaba wa
maji ya
umwagiliaji
mashambani/
mabondeni
Ukosefu wa
miundombinu ya
umwagiliaji
Kujenga
majaruba na
mifereji
Wanakijiji
Serikali
Kamati ya
mradi
Oktoba
2006
Februari
2006
Nguvukazi
Fedha
Eneo
Fedha
Utaalamu
Vifaa
Uharibifu wa
mazingira
Kutoa elimu
ya hifadhi ya
mazingira
Wanakijiji
Serikali
Serikali ya kijiji
Kamati za
miradi
Oktoba
2006
Februari
2006
Nguvukazi Utaalam
Vifaa
Ukosefu wa
mitaji
Kupata mitaji Serikali
Serikali ya kijiji
Kamati za
miradi
“ “ Nguvukazi
Fedha
Fedha
Ukataji wa miti
ovyo
Kupata elimu
ya hifadhi ya
miti
Serikali ya kijiji
Wataalam
Kamati za
miradi
“ “ Nguvukazi
Utaalam
Ufugaji wa
mifugo kiholela
Kupata elimu
ya ufugaji
bora.na
kudhibiti
Serikali ya kijiji
Wataalam
Kamati za
miradi
“ “ Nguvukazi Utaalam
Pia mpango wa utekelezaji unaoonyesha muda wa utekelezaji wa kazi mbali mbali uambatanishwe kama Kiambatanisho Na. 10.4. (Angalia Mfano)
MADA YA KUMI
153
Kiambatanisho 10.4 Mfano - Mpango wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa
bwawa
Na Shughuli Mhusika
Kipindi cha utekelezaji
Anza Maliza
Kusafirisha mtambo kwenda
eneo la kazi na kurudisha
Kamati
Mtaalam
May 2010 May 2011
Kusafisha eneo la kuchimba
bwawa
Kamati
Mtaalam
June 2010 June 2011
Kupima eneo la tuta na mtaro
Kamati
Mtaalam
June 2010 June 2011
Kuchimba msingi
Kamati
Mtaalam
June 2010 June 2011
Kurudisha udongo wa
mfinyanzi katika msingi
Kamati
Mtaalam
June 2010 June 2011
Kuchimba mtaro wa kulazia
bomba
Kamati
Mtaalam
June 2010 June 2011
Kuchimba udongo wa
kujengea tuta umbali wa mita
100
Kamati
Mtaalam
June 2010 June 2011
Kuchimba lambo kwa upana
wa mita 20
Kamati
Mtaalam
June 2010 June 2011
Kujenga vihunzi
Kamati
Mtaalam
June 2010 June 2011
Kusafirisha mawe
Kamati
Mtaalam
June 2010 June 2011
Kumimina zege la
mchanganyiko
Kamati
Mtaalam
June 2010 June 2011
Kujenga tuta kwa mawe na
saruji
Kamati
Mtaalam
June 2010 June 2011
Kujenga chemba 2 katika
bomba (mainholes)
Kamati
Mtaalam
June 2010 June 2011
Kujenga kisuwusu (intake)
Kamati
Mtaalam
June 2010 June 2011
Kujenga kituo cha maji (DP)
na viungo vya mabomba
Kamati
Mtaalam
June 2010 June 2011
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
154
10.6 MAHITAJI NA UPATIKANAJI WA RASILIMALI
Eleza aina na kiasi cha rasilimali au nyenzo zitakazohitajika katika kutekeleza kazi za mradi.
Rasilimali hizi ni kama vile nguvu kazi, nyenzo za kilimo, pembejeo, vifaa vya ujenzi, utaalam
n.k. Eleza mahali ambapo rasilimali hizi zitapatikana.
(Mfano - maduka ya pembejeo, maduka ya vifaa vya ujenzi n.k)
Pamoja na utaratibu utakaofuatwa katika kununua au kuzipata rasilimali hizo ni muhimu katika
kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali kwa wakati muafaka. Mwongozo wa serikali wa manunuzi
utatumika katika kuchagua utaratibu utakaotumiwa na jamii au kikundi katika kupata rasilimali
zinazohitajika.
(Mfano - kununua kwa zabuni, kununua katika duka moja tu linalouza vifaa vinavyohitajika,
kuoanisha bei kutoka katika maduka mbalimbali na kuchagua bei ambayo ni sahihi n.k).
10.7 GHARAMA ZA MRADI
Kila andiko lazima lionyeshe makadirio ya gharama ya rasilimali zote zinazohitajika ikiwemo nguvu
kazi. Makadirio ya gharama yatajumuisha asilimia 10 ya gharama za mradi kama tahadhari ya
ongezeko la bei au mahitaji ya rasilimali. Makadirio yafanywe kwa kuzingatia gharama halisi za
mradi na si kwa lengo la kutumia fedha zote zinazotolewa na Serikali (Kupitia ufadhili).
Toa maelezo kuhusu jinsi ambavyo jamii au kikundi kitachangia katika gharama za mradi. Kiasi
cha fedha zinazoombwa kutoka Serikalini (Wafadhili) pia zinatakiwa kuonyeshwa. Jamii na vikundi
vinatakiwa kuzingatia asilimia za uchangiaji gharama kama zinavyoelezwa katika miongozo ya
mradi.
Kwa miradi ya jamii, mchango wa jamii utakuwa wa hali na mali (nguvu kazi, mali, fedha tasilimu)
kwa kiasi kisicho chini ya asilimia 20 ya jumla ya gharama za rasilimali na Serikali (Kupitia wafadhili)
itachangia asilimia 80 ya gharama hizo hadi kiwango cha juu cha shilingi milioni thelathini
(30,000,000/=) kwa kila kijiji.
Serikali (Kupitia wafadhili) pia itatoa shilingi milioni tano (5,000,000/=) kwa kila kijiji kwa ajili ya
mafunzo na huduma za kitaalam, ambazo si lazima jamii kuchangia. Kwa hiyo, jumla ya mchango
wa Serikali (Kupitia wafadhili) ni shilingi milioni 35 kwa kila kijiji. Mchango huu utatolewa kwa muda
wa mwaka mmoja hadi mitatu kutegemea na shughuli za mradi.
MADA YA KUMI
155
Kwa miradi ya vikundi, Serikali (Kupitia wafadhili) itachangia asilimia hamsini (50%) ya gharama
za pembejeo kama vile mbegu, mbolea, na viatilifu hadi kufikia shilingi 25,000 kwa kaya kwa
msimu. Mchango huu utatolewa kwa miaka au misimu miwili. Aidha, Serikali (Kupitia ufadhili)
itachangia asilimia themanini (80%) ya jumla ya gharama za teknolojia nyingine tofauti na matumizi
ya pembejeo za aina iliyotajwa hapo juu. Vile vile, mradi utatoa shilingi laki saba na elfu hamsini
(750,000/=) kwa kila kikundi chenye kaya 40 sawa na shilingi 18,750/= kwa kila kaya kwa ajili ya
mafunzo na huduma za kitaalam.
Muhtasari wa gharama na utaratibu wa uchangiaji utakuwa kama ilivyoonyeshwa katika Jedwali Na.
10.2 na Jedwali Na. 10.3. Mchanganuo wa mahitaji ya rasilimali na gharama zake utaambatanishwa
kama Kiambatanisho Na. 10.5. Pia mpango wa uchangiaji gharama za mradi uambatanishwe kama
Kiambatanisho 10.6 (a).
Mfano - Jedwali Na. 10.2 Muhtasari wa gharama na utaratibu wa uchangiaji
Na. Aina ya kazi/Shughuli Kiasi cha gharama (Shilingi)
Jumla
Mwaka 1 Mwaka 2
1 Maandalizi ya ujenzi 3,860,000.00 0.00 3,860,000.00
2 Uchimbaji wa lambo 18,773,000.00 0.00 18,773,000.00
3
4 Kufunga bomba la mm 75 kipenyo
class B PTH
45,000.00 0.00 45,000.00
5 Kusafirisha mawe na kujenga tuta 3,830,000.00 0.00 3,830,000.00
6 Kujenga kituo cha maji, mbauti na
chemba katika bomba na kisuwusu
(intake) katika lambo
3,287,205.00 0.00 3,287,205.00
7 Kufanya savei 2,122,000.00 0.00 2,122,000.00
Jumla 31,917,205.00 31,917,205.00
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
156
Jedwali Na. 10.3 Muhtasari wa Mpango wa Uchangiaji gharama
Chanzo cha mchango
Kiasi cha mchango(Shilingi)
Jumla
Mwaka 1 Mwaka 2
Jamii 6,079,000 6,079,000
Halmashauri ya Wilaya 1,750,000 1,750,000
Wafadhili 35,000,000 35,000,000
Jumla 42,829,000 42,829,000
MADA YA KUMI
157
11
12
13
Kiambatanisho 10.5: Mfano wa Mchanganuo wa gharama
Na Shughuli Mhusika Aina ya
Rasilimali
Kipimo Idadi Bei kwa
Kila
kipimo
Jumla
(Tsh)
Mchango
wa HW
Mchango
wa Jamii
ASDP
1 Kuchimba msingi (Hard core) kwa kina cha
mita 1.50 hadi kuupata udongo mzuri kwa
kiini cha lambo na kwa mwishilio wa tuta
kila upande kina kisipungue 0.5 m
Mtaalam Caterpillar M3 462 2,000 924,000 0.00 0.00 924,000
2 Kurudishia udongo wa mfinyanzi katika
msingi kwa tabaka la sm 15-20 na
kuushindilia hadi usawa wa ardhi
Mtaalam Mtambo M3 462 2,000 924,000 0.00 0.00 924,000
3 Kuchimba mtaro wa kulazia bomba kwa
vipimo 0.5 x 0.5 x mita 37 eneo la tuta na
kuelekea upande wa chini mita 63 ikiwa
imenyooka kwa mteremko wa 1:100 na
kurudishia udongo na kushindilia
Mtaalam M 100 2,000 200,000 0.00 0.00 200,000
4 Kuchimba udongo wa kujengea tuta umbali
wa mita 100 kwa upande wa juu na mita
50 upande wa chini wa kujenga tuta kwa
kushindilia udongo kwa mtambo, tabaka
kabla ya kushindilia lisizidi sm 30 – 50 kwa
kimo mita 5
Mtaalam M3 13,000 1,185 15,405,000 0.00 0.00 15,405,000
5 Maandalizi ya kusafirisha mtambo kwenda
eneo la kazi na kurudisha
Kamati
Mtaalam
Jumla 2,500,000 0.00 0.00 2,500,000
6 Kusafisha eneo la lambo kwa kuondoa
udongo wa juu mm 150 na eneo la ujenzi
wa tuta sm 30 kwa mtambo
Kamati
Mtaalam
Caterpillar M2 70 18,000 1,260,000 0.00 0.00 1,260,000
7 Kupima eneo la tuta na utoro kwa kupigilia
mambo urefu wa mita 1.20 na kufuatilia
mwenendo wa kuanza
Kamati
Mtaalam
Jumla 100,000 0.00 0.00 100,000
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
158
Mchango wa Serikali (Kupitia ufadhili) na wadau wengine kwa kila mwaka wa utekelezaji ufanyiwe mchanganuo kwa kuzingatia mpango wa
utekelezaji na kuambatanishwa kwenye andiko kama Kiambatanisho Na. 6 (b). Hii itarahisisha utoaji wa fedha kwa wakati unaotakiwa.
8 Kujenga wigo katika kituo cha
kuchotea maji kwa miti kuwezesha
nidhamu ya kuchota maji
Mtaalam Nguvukazi Md 10 3,000 30,000 30,000 0.00 0.00
9 Kukusanya mawe kwa ajili ya
kujengea eneo la usawa katika
mlambo
Kamati Jamii Nguvukazi Trip 210 10,000 2,100,000 2,100,000 0,00 0.00
10 Kugonga kokoto kwa ajili ya ujenzi
wa eneo sawa la mlambo – control
section
Kamati Jamii Nguvukazi Trip 190 10,000 1,900,000 1,900,000 0.00 0.00
11 Kusimika bango (placard) la
kuonyesha ilani ya uchotaji na
matumizi ya maji na uwepo wa
sheria ndogo ndogo
Mtaalam L/S - - 80,000 80,000 0.00 0.00
12 Kukusanya mawe ya kujengea
mbauti
Kamati Jamii Nguvukazi Trip 160 10,000 1,600,000 1,600,000 0.00 0.00
13 Kutengeneza barabara hadi
kwenye eneo la kuchota maji
Kamati Jamii Nguvukazi Md 11 10,000 110,000 110,000 0.00 0.00
MADA YA KUMI
159
10.8 USIMAMIZI WA UTEKELEZAJI
Toa maelezo bayana kuhusu majukumu ya wanakamati wa kamati ya mradi, wanakikundi/wanajamii,
serikali ya kijiji, Halmashauri ya Wilaya na watekelezaji wengine watakaoshiriki. Pia maelezo
yatolewe usimamizi wa mafunzo na huduma za kitaalam zitakazohitajika.
Kiambatanisho 10.6 Mfano wa Mgawanyo wa Majukumu
Majukumu Mhusika
1. Kusimamia na kuratibu shughuli zote za mradi
2. Kusimamia rasilimali zote zitakazopatikana wakati wa
utekelezaji
3. Kutoa taarifa ya matumizi ya fedha na utekelezaji wa
shughuli zote wakati wa uchimbaji wa bwawa
4. Kufanya mawasilino na wataalam
Kamati ya mradi
1. Kuona kama shughuli za mradi zinatekelezwa kulingana na
ratiba
2. Kupitia taarifa za utekelezaji wa mradi
3. Kupitisha bajeti ya mradi
4. Kutatua migogoro ya wanakiji kama itajitokeza
Serikali ya Kijiji
1. Kuandaa na kuhakikisha kuwepo kwa timu ya wawezeshaji
2. Kuwezesha timu ya Wilaya kutekeleza majukumu yake
3. Kupitisha andiko la mradi wa jamii
4. Kupokea na kuingiza fedha kwenye akaunti ya mradi
Halmashauri ya Wilaya
10.9 Ufuatiliaji na Tathmini
Maelezo ya kina yatafafanuliwa kuhusu utaratibu utakaofuatwa katika kufuatilia na kutathmini
shughuli za mradi. Muhtasari wa maelezo haya utatolewa kwenye jedwali la mpango wa ufuatiliaji
na tathmini ya shughuli za mradi na kuambatanishwa kama Kiambatanisho Na. 10.7. Utaratibu
wa ufuatiliaji na tathmini utakaopendekezwa lazima uwe shirikishi na uhusishe kwa kiasi kikubwa
ushiriki wa wanakikundi na wanajamii wenyewe.
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
160
Mfano wa ufuatiliaji wa utekelezaji mradi
Kiambatanisho 10.9: Mpango wa Hifadhi ya Mazingira na Jamii – Kijiji cha …………… Mradi wa Jamii – Uchimbaji wa
Bwawa
LENGO/
SSHUGHULI
KIASHIRIA/
KIGEZO
JINSI YA
KUPATA
TAARIFA
VIPINDI
VYA
TAARIFA
GHARAMA/
NYENZO
MHUSIKA WA
KUKUSANYA
TAARIFA
NANI
ATATUMIA
NINI KITAFANYIKA
KWA TAARIFA HIYO
DHANIO MAELEZO
Kutafuta eneo
la kuchimba
bwawa
Eneo la
kuchimba
bwawa
limepatikana
Taarifa ya
kamati ya
mradi
Mara moja - Kamati ya mradi
wa jamiii
Serikali ya kijiji
Serikali ya kijiji
Jamii H/Wilaya
Mdau mwingine
Kupata uhakika wa
kutekeleza mradi wa
ujenzi wa bwawa
Kufanya savei
ya eneo la
kuchimba
bwawa
Eneo la
kuchimba
bwawa
limefanyiwa
savei
Taarifa ya
kamati ya
mradi na
Mhandisi
Mara moja Fedha, vifaa
vya kufanyia
savei,
Mhandisi
Kamati ya mradi
wa jamiii
Serikali ya kijiji
Serikali ya kijiji
Jamii
H/Wilaya
Mdau mwingine
Kuhakikisha matumizi
ya fedha,
Kumbukumbu
ya matumizi ya
baadaye.
MADA YA KUMI
161
10.10 MATOKEO YA UTEKELEZAJI
Toa maelezo kuhusu matokeo yanayotajiwa kupatikana kutokana na kutekeleza mradi. Vigezo vya
kupima matokeo viainishwe bayana (Angalia Bao Mantiki katika Kipengele cha Muhtasari).
Kwa miradi inayolenga kuongeza uzalishaji kwa mfano; (moja ya matokeo inaweza kuwa ongezeko
la uzalishaji litakalopatikana). Kipengele hiki pia kieleze upatikanaji wa masoko na utaratibu
utakaotumika katika kuuza ziada ya uzalishaji. Hali kadhalika matumizi ya matokeo yataelezwa
bayana.
10.11 MANUFAA YA MRADI
Eleza manufaa ya kifedha, kiuchumi, kijamii pamoja na mazingira yatakayopatikana kutokana na
kutekeleza mradi. Pia maelezo mafupi yatolewe kuhusu jinsi ambavyo mradi utachangia katika
mkakati wa Taifa wa kupunguza umasikini.
Manufaa ya mradi ndiyo yatakayothibitisha uhalali wa mradi na hivyo kuongeza utashi wa wahusika
katika kuutekeleza. Manufaa ya kifedha na kiuchumi ni tathmini ya matokeo ya mradi ikilinganishwa
na gharama za utekelezaji wake
(Mfano; Ongezeko la uzalishaji wa mazao ya mifugo na kilimo, Ongezeko la kipato cha wanajamii
hivyo kuongeza mzunguko wa fedha katika kijiji). Manufaa ya kifedha na kiuchumi yatahusu hasa
miradi ya uzalishaji ambayo hesabu za faida zinaweza kufanyika. Jedwali la tathmini ya kifedha na
kiuchumi litaambatanishwa kama kiambatanisho Na. 10.8.-(not reflected)
10.12 UPATIKANAJI WA SOKO
Kwa miradi ya uzalishaji, toa maelezo kuhusu upatikanaji wa soko la mazao ya kilimo na mifugo
yatakayopatikana na jinsi ya kuongeza ubora wa mazao haya ili kuvutia wanunuzi na kupata bei
nzuri. Bei za kuuzia ili kupata faida na manufaa pia zielezwe.
10.13 TATHMINI YA ATHARI YA MAZINGIRA
Shughuli za uzalishaji mara nyingi zina athari kwenye mazingira (mfano; miradi ya kilimo, ujenzi
wa mabwawa au malambo). Kipengele hiki kitaeleza athari zinazoweza kutokea endapo mradi
utatekelezwa kama ulivyopangwa na mbinu thabiti za kuzuia athari hizo. Fomu itatumika
kama mwongozo wa kuwakumbusha wanajamii juu ya mambo ya kuzingatia ambayo ikijazwa
itaambatanishwa kama Kiambatanisho Na 10.9.
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
162
Kiambatanisho 10.9 MPANGO WA HIFADHI YA MAZINGIRA NA JAMII – KIJIJI CHA
…… MRADI WA JAMII – UCHIMBAJI WA BWAWA
JINA LA MRADI ________________________
MASWALI YA DODOSO
MAELEZO
NA JE MRADI UTAPELEKEA: NDIYO HAPANA YA ZIADA
Matumizi ya mbolea za asili?
Mahitaji ya ziada ya maji?
Kupoteza ardhi kwa watumiaji wa sasa?
Matumizi ya madawa mapya ya kilimo?
Kuongezeka kwa chumvi kwenye udongo?
Uchafuzi wa vyanzo vya maji?
Manufaa kwa wanawake na wanaume?
Kuibuka kwa wadudu wapya waharibifu?
Upimaji wa udongo?
Ufahamu wa mafunzo ya mbinu husishi ya
udhibiti wa wadudu waharibifu (IPM) kwa jamii?
Ufuatiliaji wa udongo, maji na wadudu
waharibifu?
Kukubalika kwa mbinu husishi ya udhibiti wa
wadudu waharibifu (IPM)
MADA YA KUMI
163
Kuendelea miradi maalumu ya PMP?
Kuainishwa kwa athari za matumizi ya madawa
ya kilimo?
Mbinu za PMP’s kulenga IPM zilizopo?
Maoni ya DFO: ………………………………………………………………………..
Nashauri andiko: ………………………………………………………………………..
Sahihi: (DFO): ………………………………… Tarehe: ……………………….
DODOSO LA ATHARI ZA MAZINGIRA KUHUSIANA NA MRADI
JINA LA MRADI ________________________
MASWALI YA DODOSO
MAELEZO
NA JE MRADI UTAPELEKEA: NDIYO HAPANA YA ZIADA
Kuna mtu yeyote anayeishi na aliyekaribu na
Eneo la mradi, au anayelima, kutumia eneo kwa
Malisho au kunywesha mifugo au kwa matumizi
Mengine?
Kuanzisha migogoro na jamii za wafugaji?
Kuongezeka kwa samadi?
kuwa na mifugo mingi?
Uwezekano wa binadamu kupata magonjwa
yatokanayo na mifugo?
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
164
Kuongezeka kwa sumu zitokazo na madawa
ya mfiguo (Majosho)?
Mpangilio wa malisho ni wa mzunguko?
Kuna mpangilio wa mfumo wa uhifadhi wa
samadi na madawa?
Maoni ya DFO: ………………………………………………………………………..
Nashauri andiko: ………………………………………………………………………..
Sahihi: (DFO): ………………………………… Tarehe: ……………………….
MADA YA KUMI
165
FOMU YA MAOMBI YA MRADI
Fomu hii ijazwe baada ya wanufaishwa wa mradi kumaliza pendekezo la (Mradi)
Wanufaishwa wapeleke fomu iliyojazwa kwa afisa wa Wilaya na nakala kwa Halmashauri ya kijiji.
1. Jina la mradi _____________________
2. Mahali: Kijiji _____________________ Kata ______________ Wilaya ____________
3. Wanufaishwa wa Mradi: Kaya __________ Wanaume _________ Wanawake _______
4. Nani aliwezesha mchakato wa ushirikishwaji: timu ya Wilaya/ timu ya Kata/ NGO’s/ Wengineo
________
5. Shughuli kuu ambayo itafanywa na mradi: ___________________________________
6. Faida / Manufaa yanayotarajiwa kutoka kwenye mradi: _________________________
7. Makadirio ya gharama ya mradi: Tsh _____________________________
8. Michango ya wanufaishwa: Taslimu ______________
Vitu/ bidhaa/ nguvu kazi ________________
9. Mchango wa Serikali __________________________
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
166
Orodha/ wadhifa Jina Jinsia (me/ke) Sahihi/Saini
Mwenyekiti
Katibu
Mweka Hazina
Mjumbe
10. Sahihi/ Saini ya mwenyekiti wa kijiji na afisa Mtendaji wa Kijiji
Mwenyekiti _______________ Afisa Mtendaji wa Kijiji wa Kijiji _________________
Tarehe __________________ Tarehe _________________
10.14 UENDELEVU WA MRADI
Kipengele hiki kitaeleza mbinu na mipango thabiti ya uendelevu wa mradi kwa faida ya kizazi cha
sasa na baadaye
(Mfano: mradi wa ujenzi wa bwawa utakuwa endelevu kwa sababu ni mradi wa kudumu kwani
utakapokuwa umekamilika hatua zitakazochukuliwa za kuhakikisha uendelevu wa mradi ni pamoja
na kuwa na michango kutoka kwa kila mwanajamii (wakati wa kununua maji) ambayo itasaidia
ununuzi wa vifaa na gharama za ufundi).
Kama ni mradi wa uzalishaji kila mwanakikundi atachangia sehemu ya mavuno ili kutunisha akaunti
ya kikundi ambapo fedha zinaweza kutumika kununulia pembejeo kwa wanakikundi wote).
Orodha ya Viambatanisho
1. Mti wa matatizo.
2. Mti wa malengo.
3. Mpango wa kazi wa jamii (CAP)
4. Mpango wa kazi wa Mradi wa kikundi/Jamii.
5. Mchanganuo wa mahitaji ya rasilimali na gharama za mradi.
6. Mpango wa utekelezaji.
MADA YA KUMI
167
7. Mpango wa ufuatiliaji na tathmini.
8. Makadirio ya manufaa na faida ya mradi.
9. Fomu ya tathmini ya mazingira.
10.15 JINSI YA KUPATA FEDHA ZA KUGHARIMIA MRADI
Ili mradi uweze kutekelezwa unahitaji rasilimali watu na rasilimali fedha. Ni muhimu kwa Afisa
Mtendaji wa Kijiji na Mtaa baada ya kufahamu namna ya kuandaa andiko la mradi afahamu pia njia
mbalimbali za kupata fedha za kugharimia utekelezaji wa mradi husika. Afisa Mtendaji wa Kijiji na
Mtaa hana budi kushirikisha jamii namna bora ya kupata fedha za kugharimia miradi kwa maendeleo
yao.
Zifuatazo ni baadhi ya njia mbalimbali za namna ya kupata fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi
husika:
10.15.1 Vyanzo vya Fedha
1. MICHANGO YA WANANCHI
Wananchi wanaweza kuhamasishwa kuchangia rasilimali fedha au nguvu kazi zao katika
kutekeleza miradi mbalimbali kwa maendeleo yao.
2. RUZUKU TOKA SERIKALINI
• Serikali kuu
Serikali kuu inaweza kufadhili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile Ruzuku
ya miradi ya maendeleo (CDG)
• Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa/Jiji
Halmashauri ya wilaya/Mji/manispaa/Jiji inaweza kugharamia miradi ya maendeleo katika ngazi
ya kijiji na mtaa kwa kutumia fedha zilizokusanywa kutoka katika vyanzo vyake vya ndani
3. WAHISANI BINAFSI
Wahisani binafsi huweza pia kugharimia miradi ya maendeleo. Kabla ya kufikiria kuomba fedha
kutoka kwa mtu binafsi ni vizuri kumwelewa mvuto unaweza kuwa ni nini.
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
168
4. MIKOPO KUTOKA TAASISI ZA FEDHA
• Bodi ya mikopo ya Serikali za mitaaa
Bodi ya mikopo ya Serikali za mitaa ni chombo kilichoundwa ili kutoa mikopo katika Halmashuri
ya Wilaya/Mji/Manispaa/Jijij kugharamia shughuli mbalimbali ikiwemo ya maendeleo. Kwa kuwa
kijiji ni shirika mtu, kinaweza kukitumia chombo hiki kupitia Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa/
Jiji kupata mkopo. Hata hivyo mtaa hauna sifa hii kisheria.
• Mabenki (CRDB, NMB, NBC, POSTAL BANK, DCB, n.k)
Mabenki huweza kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu kufadhili utekelezaji wa miradi ya
maendeleo. Kwa kuwa kijiji ni shirika mtu, kinaweza kukopa benki. Hata hivyo kijiji kinatakiwa
kupata msaada wa kitaalam kuhusu utaratibu sahihi wa kufuatwa kutoka Halmashauri ya Wilaya/
Mji/Manispaa/Jiji husika kabla ya kukopa. Mtaa hauna sifa hii kisheria.
5. MASHIRIKA YA KIDINI
Baadhi ya mashirika ya kidini huweza kutoa misaada katika kuchangia utekelezaji wa miradi ya
maendeleo. Mashirika hayo ni kama TCRS n.k
6. MISAADA YA KIMATAIFA NA FEDHA ZA KULETA MAENDELEO
Misaada ya kimataifa iko katika sehemu zifuatazo:
• Misaada toka mashirika ya maendeleo ya kimataifa kama vile: FAO, ILO, UNICEF, UNDP,
UNESCO, UNFPA, UNHCR, UN HARBITAT n.k
• Misaada ya ngámbo toka programu za Serikali mfano USAID, EU,DFID
• Misaada ya ngámbo toka mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (mashirika haya hupata fedha
toka kwa wananchi) kwa ajili ya shughuli za kimaendeleo. Aidha, mashirika haya hutumika
kama wakala kwa ajili ya mashirika ya kimataifa. Mifano ya mashirika haya ni : VSO (UK),
peace corps (USA), OXFAM, Save the Children n.k
7. MIFUKO YA UFADHILI
Kuna vyombo mbali mbali vinavyotoa misaada inayotokana na fedha zilizowekwa na watu
wanaopenda kuchangia, Mfano: Benjamin William Mkapa foundation (BMAF), Mfuko wa fursa
sawa kwa wote (TEOF), Wanawake na maendeleo (WAMA), Aga Khan Foundation n.k
MADA YA KUMI
169
8. MICHANGO /FEDHA KUTOKA KWENYE MAKAMPUNI
Unapoomba fedha toka kwenye makampuni jitahidi kuonyesha ni jinsi gani nao watanufaika-
Asante, kutambulika, jina zuri, kutangaza shughuli zao kwenye taarifa za mwaka n.k makampuni
hayo ni kama vile : TBL, COCACOLA, IPP, SBL, VODACOM, ZAIN, TIGO, ZANTEL
10.15.2 MAJUKUMU YA AFISA MTENDAJI WA KIJIJI NA MTAA KATIKA KUTAFUTA
VYANZO VYA FEDHA ZA KUGHARAMIA MIRADI YA MAENDELEO
• Kufanya utafiti wa wahisani wanaoweza kukubali maombi ya fedha za kugharamia mradi
• Kuishirikisha Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa/Jiji hatua zote zinazohusu utafutaji wa
fedha za kugharimia miradi
• Kuhakikisha kuwepo kwa ushiriki wa washika dau wote katika kutafuta vyanzo vya fedha za
kugharamia miradi
• Kusoma na kuelewa vizuri kanuni na masharti ya wahisani kabla ya kutia sahihi mkataba na
kuhakikisha kuwa masharti hayo yanafuatwa kikamilifu.
• Kuandaa utaratibu mzuri unao endana na masharti ya utoaji taarifa kama utaratibu huo
umetolewa na wahisani.
10.16 HITIMISHO
Mada hii imefafanua kwa kina namna ambavyo Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa anavyoweza
kuhamasisha na kushirikisha jamii katika kuandaa andiko la mradi na utekelezaji wake. Aidha, mada
pia imefafanua njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika kupata fedha za kugharamia utekelezaji
wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotokana na andiko la mradi. Hivyo inatarajiwa kwamba
baada ya kupata ufahamu huu, Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa watakuwa mstari wa mbele
katika kuandaa maandiko ya miradi na kutafuta vyanzo vya fedha za kugharamia miradi hiyo badala
ya kukaa na kusubiri Serikali pekee kutekeleza jukumu hilo.
11
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
170
10.17 MAREJEO
1. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2003): Kitabu cha mwongozo wa uandaaji wa miradi ya
Kilimo na Mifugo.
2. URT (2000): “Brief on Opportunities and Obstacles to Development Planning (O & OD).
Participatory Planning, President’s Office – Regional Administration and Local Government,
Dodoma”;
3. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2007); Kiongozi cha Mchakato wa Mapitio na uwezeshaji
4. The United Republic of Tanzania (2003); Ministry of Agriculture and Food Security, Project
Operational Manual.
5. URT (2003); Training Module 2: Preparation and Appraisal of Subporjects.
6. Monitoring and Evaluation Course for World Vision Tanzania (2002); Nzomo Mwita.
7. Managing Project Risk (2002); ‘’Business risk management for Project Leaders’’ Yen Yee Chong
and Evelyin May Brown.
8. Agricultural Project Planning in Tanzania (2001); (Ahandbook on Cycles and Sequences,
Participation, Identification, Planning and design, Economic and Financial analysis and
Environmental assessment of Agricultural Projects). David J.B. Howlett and Joseph Nagu.
9. Project Cycle Management Tool for Development Assistance (1999); (Foundation for Advanced
Studies on International Development, Kudan – Minami Chidoya, Tokyo Japan.
10. General Guidelines for the Analysis of Agricultural Production Projects (1991); A.R. Ayazi.
KUMI NA MOJA MADA YA 11
11
12
13
USIMAMIZI WA FEDHA NA TARATIBU ZA MANUNUZI
MADA YA KUMI NA MOJA
173
11.1 UTANGULIZI
Usimamizi na udhibiti wa fedha na taratibu za manunuzi ni muhimu sana katika Mamlaka za Serikali
za Mitaa ambazo kwa sasa zinapewa na Serikali Kuu mamlaka ya kujiamulia mambo yao wenyewe.
Bila kuwepo na mfumo mzuri wa usimamizi na udhibiti wa fedha pamoja na taratibu za manunuzi,
Mamlaka za Serikali za Mitaa haziwezi kufikia malengo ya utoaji huduma bora kwa wananchi na pia
hazitaweza kutoa taarifa zilizo sahihi na zenye uwazi.
Lengo la mada hii ni kuwawezesha maafisa watendaji wa Kijiji na Mtaa wakiwa kama watendaji
wakuu katika kijiji na mtaa kuelewa masuala muhimu yanayohusu usimamizi wa fedha kama
ilivyoainishwa katika Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa namba 9 ya Mwaka 1982; na sheria ya
manunuzi namba 21 ya Mwaka 2004 pamoja na kanuni za manunuzi za Serikali za Mitaa za Mwaka
2007 ili kuongeza udhibiti na uwajibikaji katika kusimamia fedha katika ngazi ya kijiji na mtaa.
11.2 USIMAMIZI WA FEDHA
11.2.1 Uandaaji wa Bajeti
11.2.1.1 Maana ya makisio
Makisio ni matarajio ya mapato na matumizi katika kipindi maalum kwa shughuli zinazohusiana
na fedha.
11.2.1.2 Maana ya Bajeti
Bajeti ni mpango wa ukusanyaji wa mapato na matumizi katika kipindi maalum. Bajeti ni
sehemu ya mchakato wa upangaji mipango ambayo inahusisha mgawanyo wa rasilimali chache
katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Ni dhahiri kwamba Mpango na Bajeti ni dhana
zinazotegemeana kwani mpango bila bajeti hauwezi kutekelezeka hata kama ni mzuri kiasi gani.
11.2.1.3 Madhumuni ya Kuandaa Bajeti
• Kuwawezesha wananchi kupanga, kutekeleza, kutathmini na kusimamia rasilimali zao;
• Kuwawezesha wananchi kuchangia katika kutoa mawazo na nyenzo kwa ajili ya maendeleo
ya sehemu zao;
• Kuwawezesha wananchi kujenga ari ya kujiendeleza na moyo wa kuwajibika katika utekelezaji
wa mipango yao kwa kuongozwa na mpango wa mapato na matumizi.
11.0 USIMAMIZI WA FEDHA NA TARATIBU ZA
MANUNUZI
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
174
11.2.1.4 Faida ya Makisio/Bajeti
• Kuongeza ukusanyaji wa mapato na utumiaji wa mapato yaliyokusanywa;
• Kurahisisha ufuatiliaji wa ukusanyaji wa mapato na kudhibiti matumizi;
• Nidhamu katika ukusanyaji wa mapato na matumizi yake hujenga moyo wa walipa kodi
kuendelea kulipa kodi, ada na ushuru mbalimbali; na
• Kuwezesha kujua vyanzo muhimu na visivyo muhimu ili kusaidia wakati wa kufanya maamuzi.
11.2.1.5 Utayarishaji wa Makisio ya Bajeti
Makisio ya bajeti hutayarishwa kutokana na vyanzo vya mapato
vinavyoeleweka na gharama ambazo Kijiji na Mtaa vinatarajia kulipia katika utoaji wa huduma na
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Makisio ya bajeti yamegawanyika katika sehemu
kuu zifuatazo:-
a) Mapato
Kwa mujibu wa kifungu cha 9(1) cha Sheria ya fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa namba 9
ya mwaka 1982 kama ilivyorekebishwa na Sheria namba 6 ya Mwaka 1999 inaainisha vyanzo vya
mapato ya kijiji kama ifuatavyo:-
Mapato ya Ndani
• Mapato ya kutokana na shughuli, biashara na huduma;
• Ushuru wa mazao;
• Ushuru na ada mbalimbali kutokana na pombe, maliasili, madini, minada n.k; na
• Mapato mengineyo kama vile faini na tozo mbalimbali zinazotokana na sheria ndogo za vijiji.
Mapato ya Nje
• Ruzuku kutoka Halmashauri ya Wilaya;
• Mikopo kutoka Taasisi za Fedha;
• Misaada kutoka Mashirika ya hiari;
• Misaada au mikopo kutoka Taasisi za maendeleo za Kimataifa;
• Misaada na mikopo kutoka kwa watu binafsi ; na
• Mapato na mikopo kutoka vyanzo vingine.
MADA YA KUMI NA MOJA
175
b) Matumizi
• Matumizi ya Kawaida
–– Mishahara na posho;
–– Gharama za safari; na
–– Matumizi mengineyo yatakayokubalika katika vikao.
• Matumizi ya Maendeleo
–– Matumizi kwa ajili ya ukarabati na matengenezo ya mali za kudumu kama vile majengo,
mashine, meza, kabati na trekta;
–– Matumizi kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa huduma za jamii kama vile Elimu, Afya, Maji,
Kilimo, Mifugo, Barabara n.k.
–– Matumizi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kiuchumi; na
–– Matumizi kwa ajili ya ujenzi wa vitega uchumi na biashara.
Mfano wa Muundo wa Bajeti ya Kijiji na Mtaa ni kama unavyoonekana katika
jedwali lifuatalo:
MAELEZO KIASI (TSHs)
MAPATO
(a) Mapato ya Ndani
Ada
Ushuru wa Mazao
Faini
Ushuru wa masoko
30,000/-
100,000/-
20,000/-
100,000/-
Jumla Ndogo 250,000/-
(b) Mapato ya nje
Halmashauri ya Wilaya
Misaada (TASAF na AFRICARE)
500,000/-
1,000,000/-
Jumla Ndogo 1,500,000/-
JUMLA KUU YA MAPATO 1,750,000/-
MATUMIZI
(a) Matumizi ya kawaida
Posho ya wakusanyaji mapato
Huduma za Ofisi
Usafiri
50,000/-
100,000/-
50,000/-
Jumla Ndogo 200,000/-
(b) Matumizi ya Maendeleo
Ukarabati wa zahanati
Ujenzi wa darasa
550,000/-
1,000,000/-
Jumla Ndogo 1,550,000/-
JUMLA YA MATUMIZI 1,750,000/-
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
176
11.2.2 Ukusanyaji wa Mapato
Ni muhimu kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri
ndani ya eneo lake kwa sababu mapato yanayokusanywa na Halmashauri hutumika katika mamlaka
hizo kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Ili kuwezesha usimamizi thabiti wa ukusanyaji wa mapato na uandaaji wa taarifa zilizo sahihi,
Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa anatakiwa kutunza daftari la mapato ambalo litaainisha vyanzo
vyote vya mapato na mwenendo wa ukusanyaji wa mapato kutoka katika kila chanzo husika. Ni
wajibu wa Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa kuhakikisha kuwa mapato yote yanakusanywa kama
yalivyoorodheshwa katika daftari la mapato.
Kila Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa atatakiwa kuhakikisha kuwa makusanyo ya mapato yanafanyika
kwa kutumia stakabadhi halali na kuwasilishwa katika akaunti ya benki au Mamlaka husika kwa
wakati kwa mujibu wa taratibu za ukusanyaji wa fedha. Hii itasaidia kupunguza tabia ya watu
wachache wanaokaa na fedha kwa lengo la kuzitumia kabla ya kuziwasilisha.
11.2.3 Taratibu za Malipo na Udhibiti wa Ndani
Kila Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa atahakikisha kwamba malipo yanafanyika kwa mujibu wa
Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa.
Hati za malipo zitaidhinishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Mipango na Uchumi au Mjumbe
wa Kamati atakayechaguliwa na Halmashauri ya Kijiji na Kamati ya Mtaa.
Wanaoidhinisha malipo wazingatie yafuatayo:
• Kwamba matumizi yote ni halali, yameidhinishwa na yana viambatanisho vyote muhimu.
• Kwamba kuna fedha za kutosha kulipia gharama hizo katika akaunti ya Kijiji. Kuwekuwa
(kuidhinisha malipo zaidi ya fedha zilizopo) hakutaruhusiwa.
• Kwamba matumizi yanafanyika kulingana na makisio yaliyoidhinishwa.
• Kwamba umakini na uangalifu utiliwe maanani katika usimamizi wa matumizi.
• Aidha kamati za usimamizi wa miradi mbalimbali zihusike kikamilifu katika uidhinishaji na
ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za miradi hiyo.
11.2.3.1 Kutia Saini Hundi
Kutakuwa na watu wawili watakaohusika kutia saini hundi, mmoja kutoka kundi A na mwingine
kundi B. Haitaruhusiwa wajumbe wawili wa kundi moja kutia saini kwa wakati mmoja.
MADA YA KUMI NA MOJA
177
Kundi A
Halmashauri ya Kijiji na Kamati ya Mtaa itachagua wajumbe wawili waadilifu ambao si wajumbe
wa Halmashauri ya Kijiji na Kamati ya Mtaa. Watakaochaguliwa ni lazima wathibitishwe na
Mkutano Mkuu wa Kijiji/Mkutano wa wakazi.
Kundi B
i. Mtendaji wa Kijiji / na Mtaa
ii. Mtaalam aliyeko Kijijini na katika Mtaa atakayechaguliwa na Halmashauri ya Kijiji na Kamati ya
Mtaa ambaye si mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Kamati ya Mtaa.
Angalizo:
• Hatua za kinidhamu na kisheria zichukuliwe na Halmashauri ya Kijiji na Kamati ya mtaa
kwa yeyote atakayeidhinisha malipo kiholela bila kuzingatia vipengele vilivyotajwa hapo juu
pamoja na kanuni na taratibu za fedha zilizopo.
• Akaunti ya Kijiji na Mtaa itumike tu kwa shughuli rasmi za Kijiji na Mtaa
• Hakuna akaunti ya Benki itakayofunguliwa kwa jina la Kijiji na Mtaa bila idhini ya Mkutano
Mkuu wa Kijiji/Wakazi. Hii itahusu pia akaunti ya miradi iliyofadhiliwa katika Kijiji/Mtaa
• Malipo yoyote kwa watu wa nje yafanyike kwa hundi iliyofungwa
11.2.3.2 Ukaguzi wa Ndani
• Kwa mujibu wa kifungu 45(3) cha Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa ya Mwaka 1982,
Mkaguzi wa ndani atateuliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa/Jiji.
Kazi ya ukaguzi wa ndani ifanywe kwa makini na kwa kufuata mpango wa ukaguzi.
• Ni wajibu wa Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa kuhakikisha kuwa mapendekezo yote
yatakayotolewa katika taarifa ya ukaguzi yanafanyiwa kazi kikamilifu na kwa wakati.
• Taarifa za ukaguzi wa ndani zijadiliwe katika kikao cha Halmashauri ya Kijiji na Kamati ya Mtaa
• Wanakijiji na wakazi wa Mtaa wahamasishwe vizuri ili wawe wadhibiti wa shughuli za Kijiji na
Mtaa.
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
178
11.2.4 Utunzaji wa Kumbukumbu za Fedha
Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa akiwa kama Afisa Mhasibu atahakikisha kunakuwepo na utunzaji
mzuri wa kumbukumbu zote za fedha ikiwa ni pamoja na;
• Stakabadhi za mapato,
• Hati za Malipo,
• Daftari mbili za fedha ambapo moja litatumika kwa ajili ya mapokezi na matumizi ya fedha za
matumizi ya kawaida na daftari la pili kwa ajili ya mapokezi na malipo ya fedha za matumizi ya
maendeleo
• Nyaraka zote zitunzwe katika majalada (file) maalum.
11.2.5 Uandaaji na Uwasilishaji wa Taarifa za Fedha
Kila Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa anawajibika kutoa taarifa za mapato na matumizi kwa mujibu
wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Na. 9 ya mwaka 1982. Utoaji wa taarifa za fedha na
mambo mengine utasaidia pia kutoa maamuzi ya maendeleo kwa wakati na wananchi kujenga
imani kwa Serikali yao.
Taarifa za fedha zitaandaliwa kutokana na muhtasari wa daftari la fedha. Mtendaji wa Kijiji na Mtaa
atatengeneza kila mwezi taarifa za fedha zifuatazo ambazo zitathibitishwa na Halmashauri ya Kijiji
na Kamati ya Mtaa na kuwasilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Kijiji na Mkutano wa wakazi kila
baada ya miezi mitatu:
• Taarifa ya mapokezi na malipo ya fedha (taarifa ya mapato na matumizi)
• Usuluhisho wa benki
• Orodha ya wadai na wadaiwa.
• Tathmini ya bajeti
• Orodha ya mali za kudumu na mali za muda mfupi
11.3 TARATIBU ZA MANUNUZI
Chini ya sera ya sasa ya Serikali ya ugatuaji wa madaraka, fedha nyingi zinaelekezwa moja kwa
moja katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Sehemu kubwa ya fedha hizo hutumika katika masuala
ya manunuzi. Pia kumekuwa na miradi mingi ya maendeleo katika ngazi ya Kijiji na Mtaa. Hivyo
basi usimamizi na udhibiti wa taratibu za manunuzi ni muhimu sana katika ngazi ya Kijiji na Mtaa ili
kuhakikisha kuwa manunuzi yanayofanyika yanakuwa yenye kuleta tija.
MADA YA KUMI NA MOJA
179
11.3.1 Taratibu za Manunuzi na Udhibiti
• Mahitaji ya vifaa na huduma yawekwe wazi kwa maandishi au hati maalum kutoka kwa watumiaji
• Kamati ya Fedha, Mipango na Uchumi ichambue na kuidhinisha mahitaji yaliyotolewa na kufanya
mpango wa manunuzi
• Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa atafute bei kutoka kwa wauzaji wasiopungua watatu tofauti
• Kamati ya Fedha, Mipango na Uchumi ilinganishe ubora na bei ya vifaa/huduma na kufanya
tathmini
• Kamati ya Fedha, Mipango na Uchumi iteue mzabuni mwenye bei nafuu na ambaye vifaa au
huduma yake ina ubora unaohitajika
• Malipo yafanyike kwa kutumia hundi iliyofungwa
• Kuwepo na daftari litakaloonesha kumbukumbu za vifaa vilivyonunuliwa, vifaa vilivyotumiwa na
vifaa vilivyopo. Daftari hiili liwe na sehemu ya kuonesha jina la kifaa, mgawaji, idadi, bei na thamani.
• Kanuni za udhibiti wa ndani zizingatiwe ili kuweka wazi mgawanyo wa majukumu. Kwa mfano,
mtu anayetunza na kuandika daftari la vifaa asihusike kuidhinisha na/au kutoa vifaa.
• Kulingana na viwango vya usalama, vifaa vinunuliwe tu vinapohitajika na kwa kiasi
kinachohitajika ili kuondoa uwezekano wa kulundikana vifaa stoo ambavyo vinaweza kuharibika,
kupotea au kuibiwa.
11.3.2 Mpango wa Manunuzi na Makisio
• Mpango wa manunuzi utayarishwe kuonesha mahitaji husika. Mpango huo utoe maelezo kwa
kuonesha vipengele vya ununuzi kwa kipindi cha miezi 12 ijayo.
• Mpango wa manunuzi uoneshe vifaa vitakavyonunuliwa na kupangwa kwa kipaumbele
• Manunuzi yaoneshwe kwa kila tarehe na fedha zitakazohitajika
• Mpango wa manunuzi utumwe kwenye mamlaka kwa ajili ya kusimamia mikataba ya ujenzi na
mingineyo yenye kuhitaji wataalam/ washauri kutoka Halmashauri husika
11.3.3 Mchakato wa Manunuzi
• Kuhakiki mahitaji na kupata idhini kutoka Kamati ya Fedha, Mipango, na Uchumi
• Kutafuta bei kutoka kwa wauzaji wasiopungua watatu tofauti
• Kulinganisha ubora na bei ya vifaa/huduma.
• Kununua kutoka kwa muuzaji mwenye bei nafuu na ubora unaohitajika
• kufanya malipo kulingana na makubaliano
• Malipo yote yafanyike kwa hundi iliyofungwa 12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
180
11.3.4 Mapokezi ya Vifaa
• Mali au vifaa vilivyonunuliwa vikaguliwe kabla ya kupokelewa ili kuhakikisha ubora, idadi ya vifaa
kulinganisha na maelezo kwenye hati ya ununuzi (Local Purchase Order), hati ya madai (Invoice)
na hati ya kukabidhi mali (Delivery note).
• Matatizo yoyote katika mali au vifaa vilivyopokelewa yatolewe taarifa
11.3.5 Utunzaji wa Kumbukumbu za Manunuzi
• Mtunza bohari aingize katika daftari la vifaa, kumbukumbu zote za mali na vifaa vilivyopokelewa
kwa idadi, bei na thamani ya mali na vifaa.
11.3.6 Usimamizi wa Mikataba
Katika usimamizi wa mikataba kuna nyaraka za makubaliano rasmi ambazo zinatoa ushahidi wa
makubaliano ambazo hujumuisha mikataba ya manunuzi na mikataba mingine ya kisheria. Nyaraka
hizi huonesha mamlaka zinazohusika kutoa au kupokea huduma kama ifuatavyo: Maelezo kamili
ya huduma, bei, ubora, gharama halisi ya kutoa huduma, muda wa kutolewa huduma, masharti
ya kutoa huduma na malipo, tarehe ya kutolewa, majina na saini za waliotoa idhini na mashahidi
pamoja na mhuri wa mamlaka husika. Wakati wote nyaraka za malipo ya madai yanayotokana na
makubaliano hayo, ziambatanishwe na nyaraka husika za makubaliano.
• Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa/Jiji ashirikishwe katika maandalizi/uhakiki
wa mikataba mikubwa kabla ya kusainiwa na pande mbili husika.
• Marekebisho na mabadiliko katika viwango vya mikataba, kiasi cha gharama na muda yapate
kibali cha Halmashauri ya Kijiji na Kamati ya Mtaa.
11.3.7 Ongezeko la Muda wa Mkataba
Kama kuna sababu maalum za kuongeza muda wa mkataba zitolewe na mjenzi kimaandishi katika
kipindi cha siku 28 za kubainika kwa sababu hizo.
11.3.8 Kusimamisha Mikataba
Kama mzabuni ameshindwa kuzingatia masharti ya mkataba bila sababu za msingi, mkataba
unaweza kufutwa kwa maandishi.
MADA YA KUMI NA MOJA
181
11.3.9 Usimamizi wa Badiliko la Gharama
Kamati ya Fedha, Mipango na Uchumi itasimamia kikamilifu utekelezaji wa mkataba kwa kuzingatia
masharti yafuatayo:
• Kukagua muda wa mkataba na kuhakikisha kwamba kazi inakamilika katika muda muafaka na
kwa ubora unaokubalika.
• Kuhakiki hatua za kupata ongezeko sahihi katika gharama kutokana na mkataba
• Kuhakiki wajibu katika makubaliano umezingatiwa kwa pande zote
11.3.10 Utaratibu wa Kuhesabu Mali
• Kila ifikapo mwisho wa mwaka, Kamati ya Fedha, Mipango na Uchumi isimamie zoezi la
kuhesabu vifaa vyote vitakavyokuwemo bohari pamoja na mali za kudumu
• Kutakuwepo na fomu maalum zitakazotumika wakati wa zoezi la kuhesabu mali za kudumu
zitakazotolewa na Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa/Jiji.
• Tofauti zozote zitakazojitokeza zichunguzwe na kutolewa taarifa kwa Halmashauri ya Kijiji na
Kamati ya Mtaa.
11.3.11 Utunzaji wa Daftari la Kumbukumbu za Mali
Kila Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa anatakiwa kutunza daftari la mali za kudumu. Daftari hilo litaonesha
mambo yafuatayo:
• Aina ya mali ya kudumu, hali na mahali ilipo,
• Jina la mmiliki,
• Gharama ya mali ya kudumu,
• Tarehe ya kununuliwa mali ya kudumu,
• Ongezeko la thamani ya mali ya kudumu,
• Mauzo na taarifa nyingine kuhusu mali ya kudumu; na
• Kila aina ya mali itaandikwa kwenye ukurasa wa peke yake
Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa atakapotayarisha taarifa za fedha za mwisho wa mwaka, aoneshe
orodha ya mali za kudumu zinazomilikiwa na Kijiji na Mtaa na zile zinazomilikiwa na Halmashauri husika.
Kwa udhibiti wa mali mzuri, mali za kudumu zikaguliwe na kuhesabiwa chini ya usimamizi wa kamati
ya Fedha, Mipango na Uchumi angalau mara moja kwa mwaka.
12
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
182
11.3.12 Taarifa ya Manunuzi
Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa atatoa taarifa ya ununuzi na upatikanaji wa bidhaa na huduma kila
robo mwaka kwa kipindi cha mwaka wa fedha husika kwenye Mkutano Mkuu wa Kijiji na Mkutano
wa Wakazi ikieleza kwa uwazi vipengele vifuatavyo:
• Mahitaji ya bidhaa na huduma iliyokusudiwa katika mipango ya kipindi cha robo mwaka
• Taratibu zilizozingatiwa katika ununuzi
• Aina ya bidhaa na huduma zilizonunuliwa:
–– Maelezo ya huduma na bidhaa, majina ya wazabuni waliopata mkataba na thamani ya
mkataba
–– Maelezo ya njia zilizotumika kuchagua na kuteua wazabuni
–– Kiasi cha bidhaa zilizonunuliwa kama dharura na kama kuna ununuzi wenye utata
• Gharama za mradi na uhalali wake. Gharama za mradi ni zile zilizoko katika mkataba na
ongezeko, kama lipo. Maelezo ya kina yatolewe kama kuna ongezeko la gharama
• Kama Kamati ya Fedha, Mipango na Uchumi imezingatia taratibu na kanununi za manunuzi
zilizopo na matumizi mazuri ya rasilimali na kwamba kanuni za uwajibikaji na uwazi zilitumika
katika ununuzi
• Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa atatoa taarifa kama Sheria na taratibu zimezingatiwa na
kumbukumbu muhimu zimetunzwa katika ununuzi na upatikanaji bidhaa na huduma zote na
kwamba matumizi yote ya ununuzi yameidhinishwa na vifaa vimetumika kama ilivyokusudiwa.
11.4 HITIMISHO
Mada hii imeelezea misingi muhimu ya kuzingatia katika usimamizi wa fedha na taratibu za
manunuzi katika ngazi ya Kijiji na Mtaa. Kwa kifupi mada imeongelea uandaaji wa bajeti, ukusanyaji
wa mapato, malipo na udhibiti wa ndani, utunzaji wa kumbukumbu na uandaaji wa taarifa
mbalimbali za fedha. Aidha, masuala muhimu yanayohusu manunuzi na usimamizi wa mikataba
yameelezwa kwa kina. Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mtaa hawana budi kuzielewa taratibu hizo ili
waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
MADA YA KUMI NA MOJA
183
11.5 MAREJEO
• Mafunzo ya Kuboresha Ujuzi na Stadi za Kazi kwa Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dodoma, Tanzania; Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania (2006):
• Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na Marekebisho yake ya Mwaka
2008.
• Mwongozo wa Usimamizi wa Fedha Ngazi ya Halmashauri ya Kijiji na Kamati ya Mtaa, Ofisi ya
Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (2009)
• Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004
• Sheria ya fedha ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982 na Marekebisho yake ya Mwaka 2000
• Randama ya fedha za Serikali za Mitaa,ya mwaka 1997, Ofisi ya Waziri Mkuu
• Kanuni za Manunuzi katika Serikali za Mitaa za mwaka 2007
• International Public Sector Accounting Standards IPSASs)
12
13
KUMI NA MBILI MADA YA 12
12
13
SHERIA NA KANUNI ZA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA
MADA YA KUMI NA MBILI
187
12.0 SHERIA NA KANUNI ZA MAADILI YA UTUMISHI WA
UMMA
12.1 UTANGULIZI
Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma zimetungwa na Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa katika
kifungu cha 34 cha Sheria Na. 8 ya Utumishi wa Umma ya Mwaka 2002 pamoja na Kanuni ya 65 (1)
ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003.
Kwa mujibu wa Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma ya mwaka 2008, Ufafanuzi
wa Fasili ya Utumishi wa Umma katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni utumishi katika moja
ya makundi ya utumishi yafuatayo:-
• Utumishi katika Serikali Kuu
• Utumishi wa Sheria na Mahakama
• Utumishi wa Serikali za Mitaa
• Utumishi wa Afya
• Utumishi wa Walimu
• Utumishi wa Polisi, Magereza, Uhamiaji na Zimamoto
• Utumishi wa Kisiasa
• Utumishi wa huduma za kawaida
• Utumishi wa Taasisi na Wakala Tendaji za Serikali zinazojitegemea na vyombo vingine vya Umma
• Utumishi wa Bunge
Kwa makusudi, Utumishi wa Jeshi haukujumuishwa katika fasili hii.
Kwa kutambua na kuzingatia kwamba hivi sasa Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa ni Watumishi
kamili/halali wa Serikali za Mitaa, shabaha ya mada hii ni kuwawezesha.
Maafisa hawa kujifunza Kanuni za Maadili ya Watumishi wa Umma ili waweze:-
• Kuelewa maana ya maadili ya Watumishi wa Umma kwa jumla;
• Kuelewa umuhimu na kubadili tabia na mienendo yao kwa mujibu na Kanuni za Maadili ya
Watumishi wa Umma;
• Kuelewa namna ya kutekeleza wajibu wa majukumu yao kwa uadilifu na kuzingatia utawala wa
Sheria, haki na usawa;
• Kubaini mbinu sahihi ambazo zitasaidia kujenga na kuimarisha imani ya wananchi kwa Serikali yao.
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
188
Kwa kifupi, mada hii inaelezea juu ya mambo muhimu yafuatayo:-
• Tabia na Mienendo ya Kimaadili
• Kutoa Huduma Bora
• Utii kwa Serikali
• Bidii ya Kazi
• Kutoa Huduma Bila Upendeleo
• Kufanya Kazi kwa Uadilifu
• Kuwajibika kwa Umma
• Kuheshimu Sheria
• Matumizi sahihi ya Taarifa
Lengo la mada hii ni kumwezesha Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa kuzijua Sheria na Kanuni za
Maadili ya Utumishi wa Umma ili aweze kufanya kazi zake vizuri na kuihudumia jamii kwa uadilifu.
12.2 MAANA YA MAADILI YA WATUMISHI WA UMMA
Maadili ya Mtumishi wa Umma maana yake ni tabia, mienendo na miiko inayokubalika katika
Utumishi wa Umma.
12.3 KANUNI ZA MAADILI YA UTENDAJI KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma zimeainishwa kwa mujibu wa , Tangazo la
Serikali Na. 168 la mwaka 2003. Kanuni hizo zimenukuliwa kama ifuatavyo hapa chini:-
12.4 TABIA NA MIENENDO YA KIMAADILI
Kwa mujibu wa Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma Kanuni ya 1 ni kwamba ili
Utumishi wa Umma uwe wenye ufanisi na wa kuheshimika, watumishi wanapaswa kuzifuata Kanuni
za Maadili ya Utumishi pamoja na kuwa na tabia na mwenendo unaozingatia mambo yafuatayo:
• Kutoa Huduma Bora
• Utii kwa Serikali
• Bidii ya Kazi
• Kutoa Huduma Bila Upendeleo
• Kufanya Kazi kwa Uadilifu
• Kuwajibika kwa Umma
• Kuheshimu Sheria
• Matumizi sahihi ya Taarifa
MADA YA KUMI NA MBILI
189
Kimsingi, mtendaji wa Kijiji/Mtaa anatakiwa kuzingatia utu na maslahi ya umma katika utekelezaji
wa majukumu yake.
12.4.1 Kutoa Huduma Bora
Kwa mujibu wa Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma Kanuni ya 2, Watumishi wa
Umma wanapaswa kutambua kwamba wana wajibu wa kutoa huduma bora kwa umma.
Katika kutimiza wajibu wao, wanapaswa pia kuzingatia yafuatayo:
a) Kuifahamu vema na kuiheshimu Kanuni hii ya Maadili.
b) Kuweka malengo halisi ya kazi ili kuwawezesha kufikia kiwango cha juu kabisa katika utendaji
wao wa kazi.
c) Kuwa wabunifu, wavumbuzi na siku zote kujibidiisha kuongeza viwango vya utendaji kwa
kujiongezea maarifa na ujuzi.
d) Kutumia misingi ya haki, badala ya upendeleo, katika utoaji wa huduma.
e) Kuwa msafi na kuvaa nguo za heshima zinazokubalika mahali pa kazi
f) Kujitahidi kudumisha uhusiano mzuri mahali pa kazi na utendaji kazi wa pamoja kwa:
i) Kutoa maelekezo ambayo ni wazi; sahihi na ya kueleweka;
ii) Kuepuka kufanya vitendo viovu au kutamka maneno yanayolenga kuwaaibisha
watumishi wa ngazi moja, za chini yao au wa vyeo vya juu;
iii) Kuepuka matumizi ya lugha mbaya, matusi, utani na hasira katika utendaji wa kazi;
iv) Kutafakari ipasavyo maoni rasmi yanayotolewa na watumishi wengine na hata walio
chini yao;
v) Kufanya mikutano ya watumishi mara kwa mara;
vi) Kuhakikisha kwamba watumishi walio chini yao wanaweka malengo halisi ya kazi,
kufuatilia utendaji wao mara kwa mara na kuwa himiza kuongeza uwezo na ujuzi wao
katika utendaji;
vii) Kutoa taarifa za tathmini ya utendaji kwa watumishi bila upendeleo;
viii) Kutoa sifa au tuzo kwa watumishi wenye utendaji bora na kuwaadhibu wenye utendaji
duni;
ix) Kuwaheshimu watumishi wenzao pamoja na kuheshimu haki zao, hasa haki za faragha
wanaposhughulikia taarifa zao za siri na binafsi
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
190
12.4.2 Utii Kwa Serikali
Kwa mujibu wa Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma, Kanuni ya 3
a) Watumishi wa Umma wanapaswa kuitii Serikali iliyopo madarakani.
b) Kwa hiyo, Watumishi wa Umma wanatakiwa kutekeleza sera na maelekezo halali
yanayotolewa na Mawaziri na viongozi wao wengine wa Serikali.
12.4.3 Bidii Ya Kazi
Kwa mujibu wa Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma Kanuni ya 4. Watumishi
wa Umma wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ya hali ya juu. Vilevile, wanapaswa
kuonyesha kwamba wanaheshimu na kujali wajibu wao kwa kufanya yafuatayo:
a) Kutumia maarifa, ujuzi na utaalamu wao ili kupata ufanisi wa upeo wa juu katika utendaji wao
wa kazi;
b) Kutimiza wajibu wao na kwa kufanya kazi kwa ufanisi wa kiwango cha juu na kuzikamilisha
katika muda unaotakiwa;
c) Kuepuka mwenendo mbaya ambao utaathiri ufanisi katika utendaji kazi;
d) Kuwa tayari kufanya kazi katika kituo chochote cha kazi atakachoopangiwa; na
e) Kufika sehemu ya kazi kwa muda uliopangwa na kuzingatia muda rasmi wa kufanya kazi.
12.4.4 Kutoa Huduma bila Upendeleo
Kwa mujibu wa Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma Kanuni ya 5.
a) Watumishi wa Umma wanayo haki ya Kidemokrasia ya kuwa wanachama chochote cha
siasa. Vilevile, wanayo haki ya kuvipigia kura vyama vyao pamoja na viongozi wao wakati wa
uchaguzi mkuu.
b) Watumishi wa Umma wanaweza kushiriki katika masuala ya siasa katika vyama vyao ili mradi
kwa kushiriki kwao hawataonyesha upendeleo katika utendaji wao wa kazi.
c) Hata hivyo, Watumishi wa Umma wanapaswa kuzingatia masharti yaliyowekwa katika ushiriki
wao katika masuala ya siasa:-
i) Hawaruhusiwi kufanya wala kujihusisha na masuala ya siasa wakati wa saa za kazi au
mahali pa kazi;
ii) Kutoa huduma kwa upendeleo kutokana na msimamo wao wa kisiasa; na
iii) Kutumia taarifa au nyaraka za kiofisi wanazopatakutokana na utumishi wao kwa umma
kwa manufaa ya vyama vyao.
MADA YA KUMI NA MBILI
191
d) Watumishi wa umma wanayo haki ya kuwasiliana na viongozi au wawakilishi wao wa kisiasa
ilimradi wanazingatia yafuatayo:
i) Waepuke kutumia ushawishi wa kisiasa kuingilia mgogoro wa kikazi baina yao na
Serikali;
ii) Waepuke kutumia ushawishi wa kisiasa kwa manufaa yao binafsi ambayo sio sehemu
ya sera za Serikali.
e) Watumishi wa Umma wanayo haki ya kuabudu na kushiriki dini yoyote wanayoipenda ilimradi
kwa kufanya hivyo hawavunji sheria zilizopo. Hata hivyo, kwa kuwa Serikali haina dini,
hairuhusiwi kuhubiri imani za dini wakati wa kazi na mahali pa kazi.
12.4.5 Kufanya Kazi kwa Uadilifu
Kwa mujibu wa Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma Kanuni ya 6. Ya mwaka 2003
c) Watumishi wa Umma wanapaswa kutumia madaraka waliyokabidhiwa kwa kuzingatia
mipaka ya madaraka yao na hawapaswi kutumia madaraka hayo kwa manufaa yao binafsi,
kuwapendelea marafiki na jamaa zao au kuwakandamiza wengine.
d) Watumishi wa Umma wanapaswa kusimamia vizuri fedha na mali ya umma waliyokabidhiwa
na ni wajibu wao kuzuia uharibifu, upotevu au ubadhirifu usitokee kutokana na uzembe au
manufaa ya mtu binafsi au kundi fulani.
e) Watumishi wa Umma wanapaswa kutumia rasilimali za umma kwa manufaa ya umma.
Rasilimali za umma ni pamoja na mitambo, vifaa vya ofisi, simu, kompyuta, mashine za
kunakili kwa picha, huduma za umma (kama vile umeme, maji, usafiri n.k.), majengo na vifaa
vinginevyo vilivyonunuliwa kwa fedha za Serikali au kutolewa msaada kwa Serikali. (Gharama
anazorejeshewa mtumishi na Serikali au gharama za huduma za nyumbani kwa baadhi ya
watumishi kama vile: simu, maji, umeme huhesabiwa kama ni sehemu ya mali ya umma).
f) Watumishi wa Umma wanapaswa kuwa waaminifu na kutumia muda wa kazi kutekeleza
wajibu wao. Hawaruhusiwi kutumia muda wa kazi kwa shughuli zao binafsi au kwa
mapumziko isipokuwa kama wamepewa idhini ya kufanya hivyo.
g) Watumishi wa Umma hawaruhusiwi kuwaomba au kuwaagiza watumishi walio chini yao
kuwafanyia kazi zao binafsi ambazo hazina uhusiano na kazi zao za utumishi wa umma.
h) Watumishi wa Umma wanatakiwa, kwa utaratibu uliowekwa, kuwa tayari kutangaza kwa
waafiri wao au mamlaka yoyote halali mali walizonazo, za waume au wake zao na mali za
ndugu wanaowategemea endapo watatakiwa kufanya hivyo.
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
192
i) Watumishi wa Umma wanapaswa kuepuka tabia ambayo inavunja heshima ya utumishi wao
kwa umma hata wanapokuwa nje ya mahali pa kazi. Tabia inayoweza kuvunja heshima ya
utumishi wa umma ni pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya, ulevi, kukopa kwa kiwango
ambacho hawawezi kurejesha, mwenendo mbaya na kujihusisha na vitendo vyovyote viovu
mbele ya jamii.
j) Watumishi wa Umma wanapaswa kuepuka kutoa zawadi zisizo halali, kuomba,
kulazimisha au kupokea rushwa kutoka kwa mtu yeyote ambaye waliwahi kumhudumia,
wanayemhudumia au wanayetarajia kumhudumia ama kwa kufanya hivyo wao wenyewe au
kwa kumtumia mtu mwingine.
k) Kwa mujibu wa Kanuni hii, rushwa ni mapato yasiyo halali ambayoyamepatikana kutokana na
matmizi mabaya ya ofisi au madaraka aliyokabidhiwa mtumishi.
l) Watumishi wa Umma au familia zao wanapswa kuepuka kuomba, kupokea au kutoa zawadi
ambazo zitaoneka kwamba zinalenga kuathiri uadilifu wao.
m) Watumishi wa Umma wanapaswa kuepuka kutoa zawadi kwawatumishi wenzao
n) Kwa mujibu wa Kanuni hii, vitu vifuatavyo havihesabiwi kama zawadi yenye mwelekeo wa
rushwa:-
i) Vitu vidogovidogo vyenye thamani ambavyo vimetengenezwa mahususi kwa kutolewa
kama zawadi. Vitu hivyo ni pamoja na kadi za salamu, vikombe vya washindi wa
mashindano mbalimbali, kalenda, vitabu vya kumbukumbu za kila siku (shajara),
kalamu n.k.
ii) Kitu chochote ambacho mtumishi wa umma analipia au kufanya marejesho kulingana
na thamani yake;
iii) Kitu chochote ambacho kimelipiwa na Serikali.
o) Zawadi yoyote ambayo haipo kwenye maelezo yaliyotangulia hapo juu, inapaswa
kukabidhiwa kwa mwajiri na mtumishi aliyepokea kwa maandishi. Mwajiri anapaswa kukiri
kupokea zawadi kutoka kwa mtumishi na kuingiza katika rejesta ya zawadi zilizokabidhiwa
kwake. Serikali itatoa sawadi hizo kama hisani kwa jumuiya au shirika lolote.
p) Watumishi wa Umma wanaoacha kazi au kustaafu katika utumishi wa umma, wanapaswa
kuepuka kutumia madaraka waliyokuwa nayo walipokuwa katika utumishi wa umma kwa
kuomba au kupokea huduma ya upendeleo katika utumishi wa umma kwa faida yao binafsi
au watu wengine.
q) Mtumishi aliyeacha kazi au kustaafu aepuke kuwakilisha mtu au shirika lake Serikalini ili
apewe huduma kwa masuala ambayo yalikuwa chini ya madaraka yake alipokuwa katika
utumishi.
MADA YA KUMI NA MBILI
193
12.4.6 Uwajibikaji kwa Umma
Kwa mujibu wa Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma Kanuni ya 7 ya mwaka
2003
a) Watumishi wa Umma wanapaswa kuwahudumia wateja wao na watumishi wenzao kwa
heshima. Vilevile, wanapaswa kuwahudumia kwa makini zaidi wananchi wenye mahitaji ya
pekee kama vile wazee, wanawake, watoto, maskini, wagonjwa, wenye ulemavu na kundi
lolote la watu ambao wapo katika hali ngumu.
b) Watumishi wa Umma ambao wanaombwa na wananchi kutoa ufafanuzi au maelekezo juu
ya masuala yatokanayo na sheria, kanuni na taratibu za Serikali wanapaswa kushughulikia
mahitaji ya wananchi hao karaka kwa uwazi na bila upendeleo.
c) Watumishi wa Umma wanapaswa kutekeleza wajibu wao wakijihesabu kwamba wao ni
watumishi wa umma
12.4.7 Kuheshimu Sheria
Kwa mujibu wa Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma Kanuni ya 8 ya mwaka
2003
a) Watumishi wa Umma wanapaswa kuzifahamu, kuzizingatia na kuzifuata ipasavyo sheria,
kanuni na taratibu za kazi.
b) Watumishi wa Umma wanapaswa kutumia sheria, kanuni na taratibu zilizopo katika
kutekeleza wajibu wao na wakati huo huo kutambua kasoro ambazo zinahitaji marekebisho.
c) Watumishi wa Umma wanapaswa kuepuka kumnyanyasa mwananchi au mtumishi mwenzao
kwa misingi ya jinsia, kabila, dini, itikadi za kisiasa, utaifa, utamaduni, kuoa au kuolewa au
ulemavu.
d) Waepuke kuwa na mahusiano yoyote ya kimapenzi mahali pa kazi na wakati wa kazi. Vilivile,
wanapaswa kuepuka tabia yoyote ya unyanyasaji wa kijinsia. Matendo ya unyanyasaji wa
kijinsia ni pamoja na:-
i) Kulazimisha mahusiano ya kimapenzi au upendeleo wa kimapenzi na mtu yeyote;
ii) Vitendo vya kubaka, kunaji au shambulio lolote la aibu;
iii) Vitendo vya makusudi ambavyo havikubaliki kama vile kugusana, kufinyana,
kupapasana, kusuguana au kushina kwa nguvu sehemu yoyote ya mwili, nywele au
hata nguo;
iv) Kutoa masengenyo, ishara, sauti fulani fulani, utani, matamshi yoyote yanayo lenga jinsi
au kiungo chochote cha mwili wa mtu.
v) Kusaidia au kupokea upendeleo, ahadi au sawadi kutokana na kukubali kuwa na
uhusiano wa kimapenzi;
13
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
194
vi) Kuangalia, kuonyesha au kugawa vit kama vile picha, filamu, machapisho katika
vijarida ambayo huonyesha matukio au vitendo bayana vya mahuusiano ya kimpenzi au
ambayo huvunja maadili mema sehemu ya kazi au wakati wa kazi.
g) Watumishi wa Umma ambao wanaombwa na viongozi wao wa kazi kuvunja Sheria au
Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma au Kanuni za Maadili ya Kazi za
Kitaalamu wanapaswa kutoa taarifa kwa kutumia taratibu za Serikali zilizopo za kushughulikia
malalamiko. Iwapo mtumishi ataona vigumu kutumia taratibu zilizopo katika sehemu yake ya
kazi, malalamiko yanaweza yakaelekezwa moja kwa moja kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambaye atashughulikia malalamiko hayo ipasavyo.
12.4.8 Matumizi Sahihi ya Taarifa
Kwa mujibu wa Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma, Kanuni ya 9 ya mwaka
2003
a) Watumishi wa Umma hawaruhisiwi kutoa kwa watu wasiohusika taarifa za Serikali, ama za siri
au za kawaida, ambazo wamezipokea kutoka kwa watu wengine kwa kuaminiwa tu lakini bila
idhini. Kwa kuzingatia utunzaji wa siri za Serikali, watumishi wahawruhusiwi pia kutoa taarifa
za Serikali kwa watu wasiohusika hata baada ya kuacha kazi katika utumishi wa umma.
b) Watumishi wa Umma hawaruhusiwi kupotosha au kuzuia utekelezaji wa sera na mipango ya
Serikali kwa kutoa taarifa kwa watu bila idhini kabla sera na mipango hiyo kutangazwa rasmi
kwa umma.
c) Watumishi wa Umma hawaruhusiwi kutumia nyaraka au taarifa za Serikali wanazozipata
katika kutekeleza wajibu wao kwa manufaa ya binafsi.
d) Taarifa za Serikali zitatolewa kwa vyombo vya habari na maafisa wenye madaraka ya kufanya
hivyo kwa mujibu wa taratibu zilizoowekwa.
e) Watumishi wa Umma watatoa taarifa za Serikali wanazotaka zipelekwe kwenye vyombo vya
habari kupitia kwa maofisa wao wa habari, mawasiliano na elimu au kupitia kwa wakuu wao
wa kazi.
MADA YA KUMI NA MBILI
195
12.5 HITIMISHO
Mada hii imeainisha na kuelezea kanuni za maadili ya utendaji katika utumishi wa umma. Ni
mategemeo ya Serikali kwamba kuanzia sasa kila Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa atazingatia na
kutekeleza ipasavyo kazi na wajibu wake kwa kuzingatia kwa ukamilifu sheria, kanuni na taratibu
miongozo iliyopo na kutoa huduma bora kwa wananchi kwa ufanisi na kwa viwango vya hali ya juu
vya uadilifu, uwazi, uwajibikaji na heshima. Kwa mujibu wa Waraka wa Utumishi wa Umma na. 3 wa
mwaka 2007 kuhusu Mavazi kwa Watumishi wa Umma wenye Kumb. Na. EG.45/86/01/”A”/2 wa
tarehe 12/9/2007
Inasisitizwa watumishi wa Umma kuvaa mavazi ya heshima wakati wote kwa kuwa mavazi yasiyo
ya heshima, licha ya kumshushia hadhi mvaaji, pia yanashusha hadhi ya Serikali machoni mwa
wananchi tunaowahudumia.
12.6 MAREJEO
• Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kanuni za Maadili ya Utendaji kaika Utumishi wa Umma -
Januari 2005 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma S.L.P. 2483 Dar
es Salaam
• Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ofisi ya Rais, Tume ya
• Utumishi wa Umma Rejea za Sera, Sheria, Kanuni na Nyaraka Mbalimbali Kuhusu Masuala ya
Ajira Katika Utumishi wa Umma – Oktoba 2004
• Waraka wa Utumishi wa Umma na 3 wa mwaka 2007 kuhusu Mavazi kwa Watumishi wa Umma
wenye Kumb. Na. EG.45/86/01/”A”/2 wa tarehe 12/9/2007
• Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma, toleo la pili (2008)
13
KUMI NA TATU MADA YA 13
13
MASUALA MTAMBUKA
MADA YA KUMI NA TATU
199
13.0 MASUALA MTAMBUKA
13.1 UTAWALA BORA NA DEMOKRASIA
13.1.1 UTANGULIZI
Katika muundo wa sasa wa Serikali za Mitaa nchini, Vijiji, Vitongoji na Mitaa ni ngazi muhimu
zilizo karibu na wananchi. Ngazi hizi ndipo mahali pa mwanzo wa Serikali na ambapo mikutano
inayowajumuisha wananchi wote hufanyika kwa lengo la kuwapa wananchi nafasi ya kushiriki
kikamilifu katika maamuzi yanayohusu ustawi na maendeleo yao wenyewe na ya eneo wanamoishi.
Ujenzi wa Utawala Bora unaoambatana na upanuzi wa wigo wa demokrasia ni eneo mojawapo
muhimu sana katika utekelezaji wa Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
ulioanzishwa na Serikali mwaka 1999.
Lengo la Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa ni kuziimarisha Serikali za Mitaa
na kuziwezesha kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia misingi ya Utawala Bora. Ngazi ya
Kijiji, Kitongoji na Mtaa ndiyo kitovu cha ujenzi wa Utawala Bora na Demokrasia shirikishi hapa
nchini. Kwa misingi hiyo, ni dhahiri kwamba lengo la Serikali la kuziimarisha Serikali za Mitaa nchini
linategemea sana ubora wa utawala na utendaji katika ngazi ya Kata, Kijiji, Mtaa, na Kitongoji.
Serikali yenye uwezo mkubwa wa utendaji katika ngazi hizi ndiyo inayoweza kufikisha huduma bora
kwa jamii, kukuza uchumi wa soko na kuondoa umaskini uliokithiri kwa wananchi wake. Kamwe
jitihada za kukuza uchumi wa soko na kuondoa umaskini haziwezi kufanikiwa bila ya Mfumo wa
Utawala bora unaozingatia pamoja na mambo mengine, sheria, kanuni na taratibu zinazoleta
ushindani wa haki na udhibiti unaolinda maslahi na haki zote za binadamu.
Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa ndio wasimamizi na watekelezaji wakuu wa shughuli za Serikali
katika maeneo yao. Ili Watendaji hawa waweze kutoa huduma bora kwa wananchi hawana budi
kuelewa maana, dhana na misingi ya Utawala Bora na Demokrasia.
Lengo la mada ni kumwezesha Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa kuelewa na kuzingatia maana, dhana
na misingi ya Utawala Bora na Demokrasia ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
200
13.1.2 MAANA YA UTAWALA BORA
Katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa, Utawala Bora unatafsiria kuwa ni matumizi ya uwezo
(mamlaka) wa kiserikali katika kusimamia rasilimali za nchi katika jitihada za kuongeza na kutumia
rasilimali hizo ili kuboresha maisha ya wananchi. Aidha, Utawala Bora unaelezwa kuwa ni utaratibu
wa uongozi wa kisiasa kutokana na ridhaa ya wananchi unaolenga kuleta amani, utulivu, ushirikiano
na maendeleo ya wananchi kijamii na kiuchumi bila ubaguzi kwa misingi ya jinsia, kabila, dini, mila
na desturi au hali ya mtu.
Uongozi unaofuta misingi ya Utawala Bora hufanya kila jitihada za kujenga heshima, kuthamini na
kukuza uhuru na utu wa wananchi wote kwa namna ambayo inawezesha utumiaji wa rasilimali na
nguvu kazi kwa makini na ufanisi ili kuhakikisha kuwa wananchi au raia wote wanapata mahitaji yao
ya msingi. Mahitaji hayo ya msingi ni kama vile chakula, mavazi bora, elimu, afya njema na maji safi
na salama.
Hivyo, kimsingi Utawala Bora ni utaratibu wa utumiaji wa madaraka ya umma katika kusimamia
rasilimali za nchi katika jitihada za kuinua hali ya maisha ya wananchi. Utumiaji huo wa madaraka
huambatana na ushirikishwaji wa wahusika wote katika
kuhakikisha kuwa shughuli za umma zinaendeshwa kwa kuzingatia mawazo na maslahi ya wengi,
utawala wa sheria, haki, usawa, uwazi na uwajibikaji.
13.1.3 MISINGI NA MALENGO YA UTAWALA BORA
Chimbuko la misingi ya Utawala Bora na chanzo cha utumiaji wa madaraka na mipaka yake ni
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) na Sheria zilizotungwa na Bunge. Misingi ya
Utawala Bora imeainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
ikisomwa pamoja na marekebisho yake, Sura ya kwanza, sehemu ya 2 na ya 3 ambayo inaeleza
misingi mikuu na malengo muhimu yanayoongoza uendeshaji wa shughuli za Serikali katika ngazi
zake zote. Kwa kifupi, malengo na misingi hiyo ni kama ifuatavyo:-
a) Misingi ya Utawala Bora
• Utawala wa kidemokrasia
• Utawala wa sheria
• Ushirikishwaji wa Umma
• Haki na usawa kwa watu wote
• Uwajibikaji katika Utendaji
• Uwazi katika uendeshaji shughuli
MADA YA KUMI NA TATU
201
• Uadilifu
• Kukidhi matakwa ya wananchi
a) Malengo ya Utawala Bora
• Wananchi ndiyo chimbuko la mamlaka na madaraka ya Serikali;
• Katiba inashika hatamu;
• Utawala wa sheria;Usawa mbele ya sheria na kuwepo na kutokuwepo na ubaguzi;Mgawanyo wa
madaraka;
• Heshima kwa haki za Kulinda haki za binadamu na utu wa mtu;
• Uwajibikaji kwa wnanchi;Ushiriki wa wananchi katika vyombo vya dola;
• Utumiaji wa utajiri na vyanzo vya utajiri vya nchi kwa faida na ustawi wa jamii;
• Maendeleo ya watu na uondoaji wa umaskini, ujinga na maradhi;
• Wajibu wa dola kuhakikisha kwamba utajiri na njia muhimu za uchumi haviingii katika mikono ya
watu wachache binafsi, na
• Wajibu wa vyombo vya dola na Watendaji wake kuondoa ukandamizaji, vitisho, upendeleo,
ubaguzi na rushwa.
Kwa kuzingatia misingi na malengo makuu ya uendeshaji wa shughuli za Serikali
kama ilivyofafanuliwa hapo juu, Misingi ya Utawala Bora inaweza kufafanuliwa
kama ifuatavyo:
Utawala wa Sheria
Sheria ni utaratibu ambao umewekwa na watu ili kuwaongoza kwa namna mbalimbali za kufikia
malengo yao katika jamii au kati ya jamii fulani na nyingine. Katika utawala wa sheria kila mtu
anapaswa kuzingatia na kuongozwa na Katiba ya nchi (ambayo ndiyo sheria mama na sheria
nyingine zote zinapata uhalali kutoka kwenye Katiba), sheria, kanuni na taratibu zilizopo katika
kuendesha maisha yake mwenyewe, katika uhusiano na watu wengine na katika utekelezaji wa
majukumu mbalimbali.
Utawala bora ni ule ambao unafuata sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa ili kuongoza shughuli
za Serikali za kulinda haki za msingi za wananchi na kudhibiti vitendo visivyotakiwa au kukubalika
katika jamii.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
202
Uwazi na Uwajibikaji
Watendaji wa Serikali za Mitaa na Viongozi wa Kuchaguliwa katika ngazi mbalimbali wapo kwa
minajili ya kuwahudumia wananchi na sio kuwatawala na kuwaburuza. Maamuzi na vitendo vyote
vya Watendaji katika ngazi mbalimbali kuhusu utekelezaji wa majukumu yao lazima yafanywe kwa
uwazi bila kificho.
Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa anasimamia na kuratibu shughuli za vyombo vya wananchi ambavyo
vinaundwa, vinasimamiwa, vinaendeshwa na kuwajibika kwa wananchi. Hivyo, Afisa Mtendaji wa
Kijiji/Mtaa anapaswa kuwajali na kuwajibika ipasavyo kwa wananchi wake wote anaowatumikia
katika eneo lake la kazi bila kujali tofauti za rangi, dini, kabila, jinsi na itikadi.
Ulinzi na Usalama
Utawala bora ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa Taifa pamoja na usalama wa raia
na mali zao. Jukumu la ulinzi na usalama linategemea sana ushirikiano kati ya vyombo vya
dola, watendaji wa serikali na wananchi wote kwa ujumla. Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa
wanapaswa kuhakikisha kuwa shughuli za ulinzi na usalama katika maeneo yao zinaimarishwa kwa
kujadiliana na viongozi pamoja na wananchi kuhusu mbinu na mikakati ya kutekeleza jukumu hilo.
Kupiga Vita Rushwa
Rushwa ni adui wa haki na haina budi kupigwa vita na kila mpenda haki. Maafisa Watendaji wa Vijiji
na Mitaa ni lazima wahakikishe kuwa wanapambana na vitendo vyote vya rushwa katika maeneo
yao ili kufanikisha ujenzi wa Utawala Bora nchini.
Utoaji wa Huduma Bora
Utawala bora ni pamoja na Serikali katika ngazi zote kuwawezesha wananchi kuondokana na
umaskini, ujinga na maradhi kwa kuwapatia huduma bora za kiuchumi na kijamii. Huduma hizi ni
pamoja na:-
• Uimarishaji wa huduma za elimu, maji, afya na usafi wa mazingira
• Ujenzi na uimarishaji wa miundo mbinu ya mawasiliano na uchukuzi
• Ushauri wa kitaalam kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na wafanyabiashara ndogo ndogo.
• Kurahisisha utaratibu wa upatikanaji wa viwanja na hati za kumiliki ardhi
• Kulinda usalama wa wananchi na mali zao
MADA YA KUMI NA TATU
203
Demokrasia
Demokrasia ni msingi muhimu sana katika ujenzi wa Utawala Bora. Kutokana na
umuhimu huo, demokrasia nayo ina misingi yake.
13.1.4 Demokrasia
13.1.4.1 Maana, Dhana ya Demokrasia
Neno Demokrasia limetokana na lugha ya kigiriki.”Demos” ikiwa na maana ya watu na “Kratos”
ikiwa na maana ya utawala. Kwa kifupi, demokrasia maana yake ni Utawala wa watu walio
wengi ambapo msingi wa mamlaka yote ya nchi ni wananchi wenyewe. Kwa maneno mengine,
Serikali ya Kidemokrasia ni ile inayoundwa na watu wenyewe kwa ajili ya maslahi yao. Serikali ya
kidemokrasia huchaguliwa na wananchi wenyewe kwa kura za hiari na hivyo, uhalali wa Serikali
na viongozi wake hutokana na ridhaa ya wananchi wenyewe. Tanzania ilikwishaamua kuwa
Serikali zitawekwa na kuondolewa madarakani kwa kauli ya wananchi peke yao, kupitia kura
zao huru na za haki zitakazopigwa katika vipindi vya miaka mitano mitano. Kanuni mojawapo ya
demokrasia ni kwamba Chama kinachoshinda uchaguzi kinaunda Serikali kwa miaka mitano na
Ilani yake ya uchaguzi inaongoza utendaji wa Serikali hiyo.
Tanzania iliamua rasmi kuingia kwenye Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa mnamo mwaka 1992.
Lengo la mfumo huu ni kuleta ushindani wa ufanisi katika kuwahudumia wananchi na kupanua
wigo wa uwazi, ukweli, uwajibikaji na utawala bora kwa jumla na siyo vinginevyo. Miongoni
mwa taratibu zinazopaswa kufuatwa katika ujenzi wa demokrasia ya kweli ni pamoja na watu
kujijengea utamaduni wa:-
• Uvumilivu na staha kwa mitazamo na maoni tofauti ya kisiasa;
• Kufuata na kuheshimu mawazo ya walio wengi na pia kusikiliza na kukubali mawazo ya
wachache iwapo yana manufaa na umuhimu mkubwa kwa Kitongoji au Mtaa, Kijiji, Kata
Wilaya, Mkoa au Taifa kwa ujumla;
• Kutumia nguvu za hoja na siyo hoja za nguvu;
• Kupingana bila kupigana; na
• Kujikosoa na kukosoana bila kuleana.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
204
13.1.4.2 Misingi ya Demokrasia
(a) Ushirikishaji wa wananchi
Maendeleo endelevu ya watu huletwa na watu wenyewe. Katika demokrasia ya kweli wananchi
wanayo haki ya kushiriki katika kutoa mawazo, kupanga, kutekeleza na kutathmini mambo
yote yanayohusu maendeleo yao wenyewe. Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mtaa wanapaswa
kuwashirikisha wananchi kikamilifu katika maamuzi yote yanayohusu ustawi na maendeleo yao.
(b) Kujikomboa
Demokrasia ya kweli inalenga katika suala zima la wananchi kujikomboa kutokana na umaskini,
ukandamizwaji, uonevu, unyonywaji na unyanyaswaji wa kijinsia.
(c) Madaraka kwa umma
Lengo la msingi huu ni kuwapa wananchi wote uwezo wa kisiasa, kiuchumi na kiutawala. Katika
demokrasia ya kweli, msingi wa mamlaka yote ya nchi ni wananchi wenyewe. Madaraka ya
umma hayawezi kupatikana kama wananchi wote au baadhi yao hawana uwezo na fursa sawa
ya kushiriki kwa ukamilifu katika masuala ya siasa, uchumi na utawala wa nchi.
(d) Uchaguzi Huru na wa Haki
Katika demokrasia ya kweli, Serikali halali ni ile ambayo viongozi wake huchaguliwa kwa ridhaa
ya wananchi wenyewe. Hivyo ni vema kila Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa akahakikisha kuwa
msingi huu unazingatiwa kwa makini na vyama vyote vya siasa nchini.
(e) Uhuru wa binafsi
Uhuru binafsi ni pamoja na kila mtu katika jamii kuwa na :-
• Haki ya faragha na usalama
• Uhuru wa kwenda atakako
• Uhuru wa mawazo
• Uhuru wa kuamini dini atakayo
• Uhuru wa kushirikiana na watu wengine
• Uhuru wa kushiriki katika shughuli za Umma
MADA YA KUMI NA TATU
205
(f) Haki za Binadamu Na Wajibu (sura ya kwanza sehemu ya Tatu (12-25) ya Katiba ya
Jamhuri ya muungano wa Tanzania 1977
Demokrasia ya kweli ni pamoja na Serikali na raia kulinda na kuheshimu haki zote za msingi za
binadamu ambazo ni pamoja na :-
Haki Ibara
• Haki ya usawa; (12-13)
• Haki ya kuishi; (14-17)
• Haki ya uhuru wa mawazo; na (18-21)
• Haki ya kufanya kazi. (22-24)
Wajibu
Wajibu wa Jamii (Ibara ya 25)
(g) Mgawanyo wa Madaraka na Vyombo Vikuu vya Uongozi wa Nchi
Demokrasia ya kweli ni pamoja na kuwa na Katiba ya nchi inayofafanua kwa uwazi mgawanyo
na mipaka ya madaraka ya vyombo vikuu vya uongozi wa nchi yaani Bunge, Mahakama na
Utawala. Vyombo hivyo ndivyo mafiga matatu ya uongozi wa nchi yeyote ya kidemokrasia na
hivyo ndivyo ilivyo katika Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
13.1.5 Nafasi ya Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa Katika Kuimarisha Utawala
Bora na Demokrasia
Kwa kuwa Serikali ipo katika mchakato wa kuziimarisha Serikali za Mitaa kwa kuziwezesha
kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia misingi ya Utawala Bora na Demokrasia, Afisa Mtendaji
wa Kijiji na Mtaa anayo nafasi kubwa ya kuhakikisha kuwa wigo wa utawala bora na demokrasia
unapanuliwa ili kurahisisha utekelezaji wa sera na mikakakti mbalimbali ya serikali kwa ufanisi.
Katika kutekeleza misingi ya Utawala Bora na Demokrasia suala la rushwa, ushirikishwaji na haki za
binadamu lazima lipewe kipaumbele ili jamii iweze.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
206
13.1.6 Hitimisho
Mada hii imeelezea maana, dhana na misingi ya Utawala Bora na Demokrasia. Maafisa Watendaji
wa Vijiji na Mitaa hawana budi kuhakikisha kuwa utendaji kazi wao unazingatia misingi ya Utawala
Bora na Demokrasia. Hii itawawezesha Maafisa hawa kutoa huduma bora kwa wananchi kwa ufanisi
wa viwango vya hali ya juu vya uwazi na ukweli, uwajibikaji, uadilifu, heshima nanidhamu na hivyo
kufanya utumishi wao kuwa wa kutukuka.
13.1.7 Marejeo
• Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2001). Mafunzo ya Viongozi katika ngazi ya Kijiji, Mtaa na
Kitongoji; Ofisi ya Rais, TAMISEMI – Dodoma.
• Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2004): Mafunzo ya Kuboresha Ujuzi na Stadi za Kazi kwa
Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji, toleo la nne Ofisi ya Rais , TAMISEMI – Dodoma
• Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2000): Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977.
MADA YA KUMI NA TATU
207
13.2 UCHAMBUZI WA KIJINSIA NA MAKUNDI YENYE MAHITAJI MAALUMU
KWENYE MIPANGO YA MAENDELEO
13.2.1 Utangulizi
Mada hii imeeleza uchambuzi wa kijinsia na makundi yenye mahitaji maalum. Masuala ya Kijinsia
na makundi yenye mahitaji maalum yamekuwa yakisahaulika wakati wa kupanga mipango ya
maendeleo kwenye vijiji na mitaa na kusababisha utekelezaji wa mipango au programu zisizokidhi
mahitaji halisi ya makundi yote kwenye jamii. Ni dhahili kuwa watu wote wakishiriki kikamilifu kuibua
kero na kupanga mikakati ya kutatua kero hizo watashiriki utekelezaji wake. Aidha katika jamii zetu
makundi haya yamekuwa yakikosa nafasi hii muhimu na kupelekea kuwa na mipango ya maendeleo
isiyowakilisha mahitaji ya watu wote wakiwemo wanawake, wazee, watoto, vijana na watu wenye
ulemavu na hivyo kubaki nyuma kimaendeleo
Lengo la mada hii ni kuwawezesha maafisa watendaji wa vijiji na mitaa kuelewa misingi na tofauti
za kijinsia na makundi yenye mahitaji maalum kwenye mipango ya maendeleo. Uelewa huu
utawasaidia wakishirikiana na wataalam kwenye maeneo yao, kuweka mikakati ya kuondoa vikwazo
vilivyopo na kusimamia uandaaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo
13.2.2 Ufafanuzi Wa Dhana Muhimu
(i) Jinsi
Jinsi hutumika kuelezea maumbile ya mtu kama ni mwanamke au mwanaume. Wanawake ni
binadamu wenye via vya uzazi vya kike na wanaume ni binadamu wenye via vya uzazi vya kiume.
Kwa hali hii jinsi ya mtu hutokana na maumbile yake kibaiolojia na haibadiliki,, ni hali ya kuwa
mwanamke au mwanaume.
(ii) Jinsia
Jinsia ni mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume yaliyojengwa na yanayoendelea kujengwa
na jamii. Dhana ya Jinsia inatambua mgawanyo wa kazi kijinsia ambao umejikita kwenye
majukumu ya uzalishaji mali, kwa kuangalia ushiriki wa wanawake na wanaume, mgawanyo wa
mapato na rasilimali, fursa sawa kushiriki katika siasa na uongozi , mila na desturi na katika ajira
rasmi na isiyo rasmi. Tofauti hujitokeza katika ushiriki wa wanawake na wanaume katika nyanja
mbalimbali za maendeleo. Hivyo basi, jinsia inahusu mitazamo, uzoefu, mila na desturi katika jamii
kuhusiana na wanawake na wanaume ambayo hubadilika kulingana na wakati.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
208
(iii) Majukumu ya Kijinsia
Huu ni mgawanyiko wa majukumu katika jamii kwa kufuata mila na desturi za jamii husika. Kwa
mfano, katika jamii ya Kiafrika, upishi, usafi wa nyumba ni kazi ya kike wakati uwindaji na ujenzi ni
kazi ya kiume.
(iv) Masuala ya Kijinsia
Haya ni yale yahusuyo mgawanyiko wa majukumu, mgawanyo wa rasilimali, mahitaji ya wanawake
na wanaume katika jamii. Kwa mfano, si utamaduni wetu mwanaume kupika au kufagia na si jadi
yetu mtoto wa kike kurithi ardhi au mali. Mgawanyiko huu ndio husababisha ubaguzi na unyanyasaji
wa wanawake na unapaswa kupigwa vita kwani kwa mahitaji ya sasa humrundikia mwanamke
majukumu mengi kuliko mwanaume na kumnyima fursa za kimaendeleo.
(v) Mipango ya Kijinsia
Utaratibu wa upangaji mipango unaolenga kubadilisha mahusiano ya kijinsia katika jamii ili kuelekea
kwenye usawa na kupata haki stahili.
(vi) Mahitaji ya Kijinsia
Kwa vile wanawake na wanaume wanafanya kazi tofauti, na wanatofautiana kupata rasilimali za
kuwawezesha kufanya kazi, mahitaji yao pia ni tofauti.
Kwa msingi huo, mipango ya maendeleo inayopangwa lazima izingatie mahitaji ya kijinsia na ilenge
kuongeza ufanisi ili kazi zinazotekelezwa zilete mabadiliko chanya kwenye jamii. Mahitaji ya kijinsia
yamegawanyika katika sehemu mbili:
a) Mahitaji muhimu ya kila siku
Haya ni mahitaji yanayolenga kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi yoyote ile inayofanywa na
mwanamke na mwanaume, kulingana na mgawanyo wa kazi kijinsia.
b) Mahitaji mbinu
Mahitaji mbinu yanaangalia mila na desturi zinazowakandamiza wanawake na wanaume na
kuwanyima haki za kushiriki kikamilifu katika kutekeleza majukumu yao. Mabadiliko ya mahitaji
mbinu huchukua muda na wakati mwingine huwa vigumu kuyabadilisha kwa kuwa yanahusu
mabadiliko ya kifikra na mawazo yaliyopo miongoni mwa jamii.
MADA YA KUMI NA TATU
209
(vii) Makundi yenye Mahitaji Maalum
Makundi yenye mahitaji maalum kwenye jamii hususan vijijini na mitaani ni pamoja na watu wenye
ulemavu, wazee na wasiojiweza, watoto na wale wanaoishi kwenye mazingira hatarishi na vijana
13.2.3 Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia
Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2002) inatambua kuwa maendeleo ya wanawake ni
duni katika nyanja mbalimbali kama vile afya, elimu, uchumi na ndiye wanaobeba vikwazo vyote
vya maendeleo vya sekta hizi. Sera pia inasisitiza kuwa na mkakati wa uhamasishaji wa wanawake
kujiunga kwenye vikundi vya maendeleo na kuwaelimisha kuhusu haki na sheria mbalimbali
zinazowalinda. Mfano, Sheria ya Makosa ya Kujamiiana Namba 4 ya mwaka 1998. Sheria hii
inatamka makosa ya jinai yakiwemo: ukeketaji wa wanawake na watoto wa kike, kuwaingiza watoto
wadogo katika biashara ya mapenzi na kumdhalilisha mwanamke.
Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba 5 ya mwaka 1999 inawapa watu wote haki sawa ya kumiliki ardhi
ikiwa ni pamoja na haki ya kuiendeleza au kuuza. Sheria hii inazuia mume kuuza ardhi na mali zilizo
katika ardhi bila idhini ya mke. .
13.2.4 Uchambuzi Wa Kijinsia
13.2.4.1 Mbinu za Uchambuzi wa Kijinsia
Uhusiano wa kijinsia katika jamii unaweza kubainika kwa kuchambua kwa kina masuala
yafuatayo:-
• Mgawanyo wa majukumu baina ya wanawake na wanaume katika jamii na uchambuzi wa
sababu za mgawanyo huo;
• Utumiaji na umilikaji wa rasilimali na nyenzo zilizopo;
• Mahitaji ya wanawake na wanaume katika kumudu maisha yao na kutekeleza majukumu yao;
• Matumizi ya muda kama rasilimali miongoni mwa wanawake na wanaume katika jamii.
a) Mgawanyo wa Majukumu
Majukumu wafanyayo wanawake na wanaume yamegawanywa na jamii husika kijinsia. Hata hivyo,
katika jamii nyingi duniani ikiwemo Tanzania, mgawanyo huu hauzingatii haki na usawa. Majukumu
yanayohusu wanawake na wanaume katika jamii yanaweza kugawanywa katika sehemu kuu nne:
uzazi, utunzaji wa jamii, uzalishaji mali,siasa na uongozi. Kwenye majukumu haya wanawake
huhusika sana na majukumu matatu, yaani uzazi, uzalishaji mali na utunzaji wa jamii. Jukumu
la siasa na uongozi linafanywa zaidi na wanaume. Yafuatayo ni maelezo kuonyesha ushiriki wa
wanawake na wanaume kwenye majukumu:-
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
210
(i) Jukumu la Uzazi
Jukumu la uzazi linahusu kubeba mimba, kuzaa na kutunza watoto ili kuongeza idadi ya watu
watakaohusika na uzalishaji na kuendeleza jamii siku zijazo.
Katika kutekeleza jukumu hili mwanaume huhusika mwanzo kwenye mchakato wa uzazi na
kulea watoto wakubwa. Kazi ya kutunza mimba, kujifungua na kutunza watoto hadi wakue ni ya
mwanamke. Ni vyema kukiri kuwa jukumu la kutunza mimba na kujifungua haliwezi kubebwa na
wanaume kwani ni la kimaumbile ya mtu mke (kibaologia).
(ii) Utunzaji wa Familia
Jukumu hili hufanywa na wanawake. Mbali na majukumu ya uzazi, wanawake hutakiwa kuwa
waangalizi na watunzaji wa familia kwa kuzingatia mahitaji yao ya kila siku kama vile chakula,
maji, kutunza wagonjwa, wazee na watoto, usafi wa nyumba pamoja na kufua nguo za baba na
watoto.
(iii) Uzalishaji Mali
Shughuli hii hufanywa na jinsi zote (wanawake na wanaume) kwa pamoja. Kufuatana na mila na
desturi za jamii zetu, wanawake hufanya kazi nyingi zaidi na kwa muda mrefu kwa siku kuliko
wanaume. Aidha, inafahamika kuwa katika jamii nyingi duniani ikiwemo Tanzania, wanawake
wako kwenye kundi la watu wenye uwezo wa kufanya kazi na ni wengi kuliko wanaume. Kwa
mantiki hii, ni wazi kuwa mchango wa wanawake katika uzalishaji mali ni mkubwa zaidi kuliko
ule wa wanaume japo kuwa hawana mamlaka juu ya rasilimali na nyenzo zinazotumika katika
uzalishaji mali. Pamoja na kukosa mamlaka haya, hawapati mafao yanayolingana na mchango
wao katika uzalishaji mali.
(iv) Siasa na Uongozi
Pamoja na kuwa jukumu la kuongoza na kufanya maamuzi ni la watu wote kikatiba, uzoefu
umeonyesha kuwa jukumu hili hufanywa na wanaume zaidi kuliko wanawake katika mfumo rasmi
wa uongozi na utawala. Wanawake wengi hawashiriki katika uongozi kutokana na mila na desturi
au kutokuwa tayari kutokana na mazingira yanayowazunguka kama vile elimu duni, majukumu
mengi ya nyumbani na kutokukubalika kama viongozi katika jamii.
Hali inayojitokeza ni kuwa hata maamuzi yanayohusu jamii au masuala ya wanawake hufanyika
katika vikao bila uwakilishi wao. Mgawanyo wa majukumu ya vijiji na mitaa unaweza kuwekwa
wazi kwa kuiwezesha timu ya upangaji mipango shirikishi iweze kubaini majukumu kijinsia
wakizingatia shughuli mbalimbali wafanyazo wananchi katika makundi maalum kama yale ya
MADA YA KUMI NA TATU
211
uzazi, uzalishaji na utunzaji jamii. Zoezi hili laweza kufanyika wakati wa kusaili kaya moja moja.
Utaratibu wa kufuata kukamilisha zoezi hili ni kama ifuaavyo:-
• Jadili shughuli mbalimbali zinazofanywa na kaya kwa mwaka mzima.
• Tumia kalenda ya msimu na kazi za kila siku na matokeo ya usaili katika kujadili.
• Orodhesha shughuli zinazofanyika na tumia vitu maalum kama vile mbegu, mawe au vipande
vya miti, ili washiriki waweze kuchambua na kuonyesha shughuli zinazofanywa na mwanamke
au mwanaume.
Jedwali Na. 1 Mgawanyo wa Majukumu Baina ya Wanawake na Wanaume
KAZI WANAUME WANAWAKE
Utunzaji watoto xx xxxxxxxxxxxxxxx
Kusafisha Shamba xxxxxxxxxxxxxxxx
Kulima (kutifua) xx xxxxxxxxxxxxxxxx
Kupanda xxxxxxxxxxxxxxxx
Kupalilia xxxxxxxxxxxxxxxx
Kuvuna xx xxxxxxxxxxxxxxxx
kuuza xxxxxxxxxxxxxxxxxxx xx
(b) Uchambuzi wa Mmilikaji Mali, Rasilimali na Nyenzo za Kufanyia Kazi
Tofauti za umilikaji wa rasilimali, mali na nyenzo baina ya wanawake na wanaume ni kikwazo katika
shughuli za maendeleo. Hii inatokana na wanawake kubaguliwa katika kupata na kumiliki rasilimali
zilizo nyingi na hivyo, kutotumia uwezo na ubunifu wao kwa ukamilifu. Ni vyema watendaji wa
vijiji na mitaa waelewa hali ya umilikaji na kasoro zilizopo ili washirikiane na wataalam waliopo na
viongozi kuweka mikakati ya kurekebisha hali hii. Uchambuzi ufanyike kuhusu:-
• Mahitaji ya rasilimali kwa ajili ya wanawake na wanaume katika kutekeleza majukumu
waliyonayo;
• Hali ya umilikaji mali, rasilimali na vitendea kazi ili kubaini upungufu uliyopo;
• Nafasi ya wanawake na wanaume katika matumizi ya rasilimali hizo;
• Hali ya mgawanyo wa mafao kwa wanawake na wanaume kama yanalingana na jasho lao;
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
212
Jedwali Na. 2 Mgawanyo wa Mali, Rasilimali na Nyenzo Baina ya Wanawake
RASILIMALI
WANAUME WANAWAKE
KUTUMIA KUMILIKI KUTUMIA KUMILIKI
Baiskeli xxxxx xxxxx xxxxx x
Nyumba xxxxx xxxxx xxxxx
Fedha xxxxx xxxxx xx xx
Majembe xxxxx xxxxx xxxxx xxxxx
Ng’ombe xxxxx xxxxx xxxxx
Ardhi xxxxx xxxxx xxxxx
(c) Uchambuzi wa Matumizi ya Muda katika Kaya
Suala la matumizi ya muda kwa wanawake na wanaume kwenye jamii halionekani kuwa kipingamizi
cha maendeleo. Mara nyingi wanawake hutumia muda wao mwingi kufanya kazi kuliko wanaume,
lakini kwa kiasi gani na ni athari zipi hujitokeza, hii haionekani kama hoja. Ni vyema kuwa na
utaratibu wa kujua mpangilio wa kazi za wanawake na wanaume katika majira mbalimbali ya mwaka
ili kuleta ufanisi wa kushiriki katika shughuli za maendeleo. Upangaji wa maendeleo endelevu
unaozingatia jinsia unahitaji kuwa na taarifa kuhusu:
• Mahali shughuli mbalimbali zinapofanyika na watu wanaohusika;
• Muda unaotumiwa na wanawake na wanaume katika kutekeleza shughli hizo.
Uchambuzi wa matumizi ya muda kwa Kaya unaweza kufanyika ukifafanua nani mhusika kwenye
kazi (wazee, vijana, wanawake, wanaume, watu wenye stadi maalum) na itafanyika lini, kwa muda
gani, mara ngapi na ugumu wake. Uchambuzi wa aina hii husaidia kubaini vikwazo na fursa na
kutafuta njia za ufumbuzi. Michoro rahisi inaweze kutumika kufanya uchambuzi huu. Hatua muhimu:
• Wanakaya waombwe kuorodhesha kazi zao kwa siku za kawaida tangu kuamka hadi kulala usiku.
• Muda maalum unaotumika kwa kila kazi sharti ujulikane.
• Kazi zinazotajwa zibainishwe kama ni za siku hiyo, za kuendelea za msimu au siku moja moja tu.
• Kazi mahsusi zibainishwe. Kazi zinazofanyika kwa wakati mmoja na zile zinazojirudia kwa siku
zijulikane.
• Kazi ngumu na zinazohitaji nguvu nyingi zipimwe na kuandikwa kwa kutumia alama maalum
ambazo wanakaya watachagua.
MADA YA KUMI NA TATU
213
Jedwali Na. 12.3 Uchambuzi wa Matumizi na Muda katika kaya
MUDA KAZI ZINAZO FANYIKA NA WATU
WAZIMA
KAZI ZINAZOFANYIKA NA
WATOTO
WANAWAKE WANAUMME WAVULANA WASICANA
11.00 Alfajiri Kuamka kulala Kulala Kuamka
11.00-11.30 Kuchota maji Kulala Kulala Kuosha vyombo
11.30-12.10 Kupika chai, kuosha
vyombo
Kulala Kuamka Kupika chai
12.00-12.30 Kuamsha watoto,
kufagia
13.2.4.2 Athari kwa Wanawake Kutokana na Uchambuzi wa Majukumu
Zifuatazo ni athari zinazojitokeza kwa wanawake kutokana uchambuzi wa kijinsia:
• Kukabiliwa na kazi nyingi kama wazalishaji mali na watunzaji wakuu wa familia na hivyo
kuonekana wakihangaika sana;
• Kufanya kazi muda mrefu zaidi na hivyo, kukosa muda wa kutosha wa kupumzika; hali
ambayo inaweza kuathiri afya na maendeleo yao;
• Kutokuwa na madaraka au fursa ya kufanya maamuzi juu ya huduma, vitendea kazi na
rasilimali wanazohitaji ili kutekeleza majukumu hayo na kutofaidi matunda ya kazi zao
ipasavyo.
13.2.5 Masuala ya Kijinsia katika Shughuli za Maendeleo
Usawa wa kijinsia hauwezi kufikiwa kama mfumo mzima na taratibu za uandaaji na utekelezaji
wa mipango ya maendeleo hauzingatii tofauti zilizopo na kuchukua hatua za kuziondoa katika
programu zinazobuniwa na kutekelezwa. Jitihada zichukuliwe na jinsi zote kuhakikisha kuwa
ufumbuzi wa kasoro hizo unapatikana.
Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa wana wajibu wa kuhakikisha kuwa mipango na miradi
inayobuniwa katika maeneo yao inatatua matatizo ya wananchi. Aidha, masuala ya jinsia hayana
budi kuwa katika ajenda ya vikao mbalimbali vinavyofanyika katika ngazi ya vijiji na mitaa.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
214
13.2.6 Uchambuzi Wa Mahitaji Ya Makundi Maalum Kwenye Mipango Ya
Maendeleo
Mahitaji ya makundi maalum kwenye mipango ya maendeleo ni ya aina mbili:
• Mahitaji ya msingi
• Mahitaji yanayogusa kila kundi Maalum
a) Mahitaji ya Msingi
Ili binadamu yeyote aishi anahitaji chakula, malazi na mavazi. Pia anahitaji kupata elimu na huduma
ya afya. Mahitaji haya ni muhimu na ni haki kwa makundi maalum. Jukumu la kutoa mahitaji haya
kwa makundi maalum ni la familia, jamii na serikali. Kila familia au kaya ina wajibu wa kufanya kazi
na kupata mahitaji ya msingi kwa ajili ya watu wanaoishi kwenye familia hiyo wakiwemo wasio na
uwezo wa kuzalisha. Aidha, ni jukumu la familia, jamii na serikali kuhakikisha watu wote wanapata
elimu na huduma za afya ili kujenga jamii iliyoelimika na yenye afya nzuri. Taifa lolote lisilotoa
kipaumbele kukidhi mahitaji ya makundi maalum halina maendeleo.
a) Mahitaji ya kila kundi
i) Watu wenye ulemavu
Watu hawa wana mahitaji maalum yanayotofautiana na yale ya wasio na ulemavu. Watu wenye
ulemavu wakitimiziwa mahitaji yao na haki zao wengi wao wanaweza kushiriki kwenye mchakato wa
kujiletea maendeleo na ya jamii kwa ujumla. Mahitaji na haki za watu wenye ulemavu ni pamoja na:
• Kuboreshewa miundombinu
• Huduma zinazoendana na aina ya ulemavu
• Kushiriki kutoa mawazo na kusikilizwa
Kuboreshewa miundombinu
Watu wenye ulemavu wanatumia miundombinu tofauti na wasio na ulemavu. Wakati wa
mchakato wa kupanga mipango ya maendeleo ni vizuri kwanza kuwafahamu watu wenye
ulemavu kwenye vijiji na mitaa na ni ulemavu aina gani walionao. Pia kujua mahitaji yao kwa
kuwashirikisha kueleza kama wanauwezo wa kujieleza, kuwauliza na kushirikisha watu wa
karibu yao (wazazi) na wataalam. Waafisa watendaji wawe na orodha ya watu wenye ulemavu
kwenye vijiji na mitaa na kufanya mchanganuo wa mahitaji ya miundombinu yao na kuiingiza
kwenye mipango ya maendeleo. Mfano katika ujenzi wa shule au zahanati mipango ya vyoo
wanavyoweza kutumia watu wenye ulemavu wa viungo izingatiwe.
MADA YA KUMI NA TATU
215
Huduma zinazoendana na aina ya ulemavu
Uandaaji wa mipango ya maendeleo ya utoaji huduma za jamii uweze kuainisha huduma
wanazohitaji watu wenye ulemavu. Mfano, huduma ya kupeleka vifaa vya shule au afya kwenye
vijiji au mitaa inayowapa nafasi watu wenye ulemavu kuvitumia vifaa hivyo (mashine za kuandikia
watu wasioona, fimbo nyeupe n.k)
Kushiriki kutoa mawazo na kusikilizwa
Watu wenye ulemavu wa viungo wana nafasi ya kushiriki kuleta maendeleo yao na ya jamii.
Aidha, wahusishwe kwenye mchakato wote wa kuainisha kero zao na za jamii nzima na upangaji
wa vipaumbele kwenye mipango ya maendeleo.
ii) Wazee na wasiojiweza
Wazee kama ijulikanavyo kuwa wazee ni hazina kwa taifa kutokana na kujua historia ya jamii na
kuirithisha kwa watu wengine, uzoefu, ujuzi na maarifa waliyopata kwa kufanya kazi muda mrefu,
ni budi waheshimiwe na kuwajali wanapofikia kupungukiwa na nguvu za kufanya kazi. Kuwajali ni
pamoja na kuona kama wanapata mahitaji yao na kuendelea kuishi.
Maafisa watendaji wa vijiji na mitaa wana jukumu la kupata takwimu ya wazee wote kwenye maeneo
yao na kuainisha mahitaji yao ili yawekwe kwenye mipango ya maendeleo. Mfano, kuwahakikishia
upatikanaji wa matibabu bure, chakula, na makazi bora.
Watu Wasiojiweza
Katika vijiji na mitaa kuna kundi la watu wasiojiweza, nao wana mahitaji ambayo yakipatikana
yanaweza kuwafanya watu hawa waondokane na utegemezi na kuchangia maendeleo yao na ya
jamii. Ni vizuri wafahamike na kujua sababu zinazowafanya washindwe kupata mahitaji ya msingi
ili yawekwe kwenye mipango ya maendeleo. Mfano kutojiweza kutokana na kukosa fursa za
maendeleo na kubaki kwenye umaskini wa kipato na wa kifikra ambao unaweza kutatuliwa kwa
kutoa elimu ya kuanzisha biashara na kutoa fursa za mikopo. Maafisa watendaji wa vijiji na mitaa
wawe na ubunifu wa kuweza kuwahamasisha kufanya kazi na kutumia wataalam waliopo kupata
ushauri wa kuboresha kazi zao.
iii) Watoto
Watoto ni tegemeo kubwa kwa maendeleo ya taifa lolote, wanahitaji ulinzi na kutimiziwa mahitaji
na haki zao. Kwenye vijiji na mitaa kuna watoto wenye mahitaji mengi na kutokana na umri,
mila, desturi na mfumo uliopo, sauti zao hazisikiki. Japokuwa kuna taasisi zinazofanya kazi za
kuwaendeleza watoto na kuwatetea, mchango wao ni mdogo kwani hazijafika nchi nzima. Aidha,
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
216
kuna mitazamo tofauti kwenye jamii kuhusu kumshirikisha mtoto kutoa mawazo yake. Mahitaji ya
watoto kama maeneo ya michezo, shule jirani na wanakoishi n.k havitiliwi manani kwenye mipango
ya maendeleo na hivyo kuathiri makuzi na maendeleo yao. Mfano kwenye mitaa mingi hakuna
maeneo yaliyotengwa kwa watoto kucheza na upatikanaji wa vifaa vya kuchezea, hakuna shule
za kutosha za awali vijijini, shule za sekondali za kata zimejegwa mbali na kuwalazimu watoto
kutembea umbali mrefu, n.k. Maafisa watendaji wa vijiji na mitaa wana jukumu la kuelewa vizuri
mahitaji ya watoto kwenye maeneo yao na kushirikiana na wataalam na wazazi kuweka mikakati ya
kuwezesha upatikanaji wake.
iv) Watoto walio katika mazingia hatarishi
Tanzania imekuwa ikiripotiwa kuwa na watoto wengi waishio kwenye mazingira hatarishi kusini mwa
jangwa la sahara. Inakadiliwa kuwa zaidi ya milioni mbili ya watoto wanaishi kwenye mazingira hayo.
Hii imechangiwa na umaskini wa kipato na matokeo ya ganga la UKIMWI. Watoto hawa maisha
yao yako hatarini kwa kukosa mahitaji ya msingi na haki zao ili waweze kuwa tegemeo la taifa kwa
siku zijazo. Maafisa watendaji wana jukumu la kuwafahamu watoto hawa, kuainisha mahitaji yao
na kuwashirikisha wale wanaoweza kuchangia mawazo kwenye vikao vya upangaji mipango ya
maendeleo. Aidha, kuwakutanisha na taasisi zinazotoa misaada.
v) Vijana
Vijana ni nguvu kazi ya taifa kwani wana nguvu za kufanya kazi na ni wepesi wa kutoa maamuzi.
Vijijini na mitaani kuna vijana wengi wenye mahitaji tofauti japo kubwa zaidi ni ukosefu wa ajira.
Ni jukumu la watendaji wa vijiji na mitaa kuwa na takwimu zao na kuweka mazingira mazuri ya
kuwashirikisha kwenye maandalizi ya mipango na utekelezaji wa maendeleo. Vijana wanaweza
kupata ajira kwenye miradi inayofanyika kwenye maeneo yao au jirani hasa ile inayohitaji nguvu kazi
za watu kama ya ujenzi wa barabara, shule n.k. Vijana wengi wamekuwa wakikimbilia mijini kutafuta
kazi, mijini wanajikuta wakiishi kwenye mazingira magumu na kushindwa kupata kazi kutokana na
kukosa ujuzi. Wengi wamejiingiza kwenye vitendo vya wizi ili wapate riziki. Ni jukumu la watendaji
ngazi ya msingi wakishirikiana na serikali kuu na wadau wa maendeleo kuandaa mipango ya
maendeleo endelevu ya kuweka mazingira mazuri vijijini ili vijana wasipate ushawishi wa kuondoka
badala yake kujiajiri huko.
MADA YA KUMI NA TATU
217
13.2.7 Wajibu wa Maafisa wa Vijiji na Mitaa katika Uchambuzi wa kijinsia na
mahitaji ya makundi maalumu
Maafisa Watendaji ngazi za msingi wana nafasi na wajibu wa kuratibu na kuondoa kasoro za kijinsia
na mahitaji ya makundi maalum.Uratibu huo unaanzia kwenye ushirikishaji wa jinsi zote na makundi
maalum kwenye uandaaji wa mipango ya maendeleo. Wajibu mahsusi wa Watendaji ni:-
• Kubaini, kutambua na kukubali upungufu uliopo kijinsia ambapo wanawake wamebebeshwa
mzigo mkubwa wa kazi na wawe tayari kuelimisha jamii kubadilika na kuondoa upungufu huo;
• Kushirikiana na wataalam kupata taarifa za mgawanyo wa majukumu na uzito wa kazi kijinsia na
mahitaji ya makundi maalum ili kubaini maeneo ya kurekebisha na kuweka mikakati yake
• Kutambua walengwa halali katika mipango mbalimbali inayoandaliwa na ni kwa jinsi gani
wanawake na wanaume na makundi yenye mahitaji maalumu watashiriki kutekeleza
• Kuelewa tofauti za umilikaji wa rasilimali zilizopo ili kuratibu mipango na miradi ya maendeleo
inayogusa mahitaji ya kijinsia na makundi maalumu,
• Kufahamu sheria na sera mbalimbali zilizotolewa kuzuia unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsia
na makundi yenye mahitaji maalum ili kulinda haki za watu wote
• Kusimamia utelezaji wa miongozo kuhusu ushiriki wa wanawake na makundi yenye mahitaji
maalumu katika kamati mbalimbali za uongozi wa vijiji na mitaa.
• Kukusanya na kuweka takwimu na kumbukumbu zenye mchanganuo wa kijinsia na makundi
yenye mahitaji maalum.
• Kubaini mila na desturi zinazochangia kuwafanya watu wa jinsi tofauti na wenye mahitaji
maalum wasishiriki kujiletea maendeleo kama kuwaficha wenye ulemavu ndani na kuelimisha
jamii kuachana na mila na desturi hizo.
13.2.8 Hitimisho
Mada hii, imeonyesha namna ya kufanya uchambuzi kuhusu tofauti za kijinsia zilizopo kati ya
mwanaume na mwanamke katika kutekeleza majukumu yao, mgawanyo na umilikaji wa rasilimali
na matumizi ya muda, tofauti zinazosababishwa na mila, desturi na mfumo wa kijamii. Mada hii pia
imetoa mchango wa namna ya kufanya uchambuzi wa mahitaji ya makundi maalum. Imewataja
watu wanaoingia kwenye kundi hili na jinsi ya kuwatambua kwenye vijiji na mitaa.
Aidha, mchango wa kuainisha mahitaji kwa kila kundi na jinsi ya kutumia takwimu hizo kwenye
uandaaji wa mipango ya maendeleo. Hivyo, maafisa watendaji wa vijiji na mitaa wana jukumu la
kuelimisha jamii kuona kuwa watu wenye mahitaji maalum wanaweza kujiletea maendeleo na ya
jamii nzima. Hivyo, washirikishwe kutoa mawazo, kuandaa na kutekeleza mipango ya maendeleo.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
218
13.2.9 Marejeo
• Moser C. and Levy (1981), A Theory and Methodology of Gender Planning, Meeting Women’s
Practical and Strategic Needs Policy Unit Gender and Planning Working Paper II. Boserup E.
(1989), Women’s Economic Development, London George, Allen and Unwin (New edition 1989,
London: Earthscan Publications;
• Dey J. (1984) Women in Food Production and FoodSecurity in Africa, Rome; Kisekka M. (1998)
Gender Mainstreaming:
• A paper presented at a TOT Workshop on Integrating Population Variables in
• Development Planning held at Sokoine University of Agriculture July, 1998.
• Rao A. (eds) 1991) Gender Analysis in Development Planning, New York: Kumarian Press.
• UTR (1992) Policy on Women in Development in Tanzania. Ministry of Community Development,
Women Affairs and Children, Dar es Salaam.
• Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2002) Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia. Wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Dar es Salaam.
• Jamhuri ya Muungano wa tanzania (1996), Sera ya Maendeleo ya Vijana. Wizara ya Kazi, Vijana
na Michezo
• Jamhuri ya Muungano wa tanzania (2004), Sera ya Maendeleo ya watu wenye Ulemavu. Wizara
ya Maendeleo ya Vijana na Michezo
• Jamhuri ya Muungano wa tanzania (2003), Sera ya Maendeleo ya Wazee. Wizara ya Kazi, Vijana
na Ustawi wa Jamii
• Jamhuri ya Muungano wa tanzania (2010), Draft ya Mwongozo wa Dawati la Jinsia. Wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
• J. Mbilinyi (2009), Uingizaji wa masuala jinsia katika ufuatiliaji na tathmini za shughuli za
mashirika yasiyo ya kiserikali iliyowasilishwa kwa bodi ya taifa ya uratibu wa mashirika yasiyo ya
kiserikalikwenye ukumbi wa chuo cha maendeleo ya wananchi singida. Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na watoto (paper presented)
• C.A. Nzamwita (2007), Enhancement of young Vulnerable Children: A case of Kimara Ward
(Project Paper).
MADA YA KUMI NA TATU
219
13. 3 USIMAMIZI WA MAJANGA NA MAAFA
13.3.1 Utangulizi
• Lengo la mada hii ni kuwaongezea uelewa Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa kuhusu dhana
ya tahadhari dhidi ya majanga na jinsi ya kupambana na athari zinazotokana na majanga katika
jamii. Aidha Watendaji wataweza kuelewa vyanzo vya majanga ikiwemo matetemeko ya ardhi,
Mafuriko, Ukame, Vimbunga, Wadudu/Ndege/Wanyama waharibifu wa mazao, Vita/mapigano,
Kuharibika kwa mazingira, Magonjwa – hususani Ukimwi na kipindupindu. Umuhimu wa dhana
hii unatokana na ukweli kuwa majanga huathiri maisha na miundo mbinu ya kiuchumi na kijamii.
13.3.2 Maana ya Majanga na Maafa
Maneno “Majanga” na “Maafa” hutumiwa na watu wengi kana kwamba yana maana moja. Lakini
kimsingi maneno haya yana maana tofauti japokuwa yanawiana.
13.3.2.1 Majanga
Ni matukio yanayotokea (mara nyingi) bila kutarajiwa na kusababisha matatizo kwa jamii.
Yanaweza kuwa ya kiasili (kwa mfano vimbunga, mlipuko wa volkano, mafuriko, ukame) au
yanayosababishwa na shughuli za binadamu ndani au nje ya jamii husika (kwa mfano vita). Kwa
maana nyingine vitendo vya watu katika jamii moja vinaweza kusababisha janga au majanga kwa
jamii nyingine.
13.3.2.2 Maafa
Ni matokeo baada ya kuwepo kwa janga au majanga. Matokeo haya huathiri jamii au kundi fulani
la watu katika jamii. Mfano wa athari hizo ni:
• Kuleta dhiki na huzuni ndani ya jamii,
• Matumizi makubwa ya rasilimali;
• Watu kupoteza maisha au kuumia;
• Kupoteza au kuharibiwa kwa mali na miundombinu;
Majanga huleta dhiki na huzuni ndani ya jamii, pamoja na matumizi makubwa ya rasilimali.
Majanga husababisha watu kupoteza maisha au kuumia, na kupoteza au kuharibikiwa na mali
zao. Matokeo ya hali hizi ni kudumaza au kufifia kwa kasi ya mapambano dhidi ya umaskini.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
220
13.3.3 Vyanzo Na Aina Za Majanga
Vyanzo vya majanga
Kuna vyanzo vikuu viwili vya majanga.
• Majanga yanayotokana na matukio ya kiasili, Mfano: Matetemeko ya ardhi, Mafuriko, Ukame,
Vimbunga, Wadudu/Ndege/Wanyama waharibifu wa mazao.
• Majanga yanayotokana na shughuli/vitendo vya binadamu katika jamii. Mfano: Vita/mapigano,
Kuharibika kwa mazingira, Magonjwa – hususani Ukimwi na kipindupindu.
13.3.4 Dhana ya Tahadhari Dhidi ya Majanga na Jinsi ya Kudhibiti Maafa
Kueleweka vema kwa dhana ya tahadhari dhidi ya majanga ndiko kutakuwa msingi wa kupanga
mikakati ya kuchukua ili kudhibiti na kupunguza kiwango cha athari za majanga yatakayoweza
kutokea.
13.3.4.1 Dhana ya Tahadhari dhidi ya majanga
Kwa kuwa majanga ni matukio, upo uwezekano wa kuyadhibiti yasitokee au kudhibiti kiwango
cha athari zake pindi yanapotokea.
Ingawa majanga yanayotokana na matukio ya kiasili siyo rahisi kwa jamii kuyazuia. Lakini
inawezekana kabisa kupunguza kiwango au ukubwa wa athari zake kwa jamii.
Kwa upande wa majanga yanayotokana na shughuli/vitendo vya binadamu, jamii ina uwezo
mkubwa wa kuyazuia na hivyo kupunguza athari zake pindi yanapotokea.
13.3.4.2 Mambo ya kuzingatia
Mambo ya kuzingatia katika tahadhari dhidi ya majanga ni
• Jamii kutambua uwezekano wa kutokea kwa janga au majanga;
• Jamii kufanya maandalizi yaliyo ndani ya uwezo wake kuzuia yasitokee au kupunguza
kiwango cha athari zake yanapotokea
• Maandalizi yanayotakiwa kufanywa na jamii ni pamoja na;
• Kubaini na kuainisha janga au majanga yenye uwezekano mkubwa wa kutokea kiasili au
kutokana na vitendo vya watu katika jamii husika.
• Kubuni mbinu na mikakati ya kuzuia majanga yasitokee kabisa au kupunguza nguvu zake.
• Kubuni mbinu na mikakati ya kupunguza kiwango cha athari za majanga yatakayotokea
• Kubaini na kuainisha rasilimali za kutumia na kugawa majukumu kwa vyombo vya kijamii
na kiutawala, vya kushughulikia maafa yanayoweza kusababishawa na majanga ya aina
mbalimbali yanayoweza kutokea.
MADA YA KUMI NA TATU
221
• Kuwa na utaratibu wa kudumu wa kudhibiti vitendo vya watu vinavyoweza kusababisha
majanga kutokea katika jamii husika.
Maandalizi yoyote yanayofanywa na jamii kama tahadhari dhidi ya majanga na maafa yanalenga
kuyadhibiti majanga na maafa yake. Hivyo maandalizi hayo ni hatua ya kwanza kabla ya
kutekeleza udhibiti wenyewe kwa vitendo. Afisa mtendaji anahusika sana na maandalizi haya.
13.3.4.3 Udhibiti wa majanga na maafa
a) Katika kuchukua tahadhari dhidi ya majanga, kuna hatua mbili muhimu za kuchukua.
Hatua ya kwanza
Kubuni taratibu, mbinu na mikakati ya kuzuia majanga ili yasitokee au kupunguza athari zake
pindi yanapotokea.
Hatua ya pili
Kuiwezesha jamii kufuata taratibu zote za kutekeleza mbinu na mikakati ili kujenga uwezo wa
jamii wa kudhibiti majanga yasitokee au kupunguza athari zake.
b) Udhibiti wa majanga na maafa yanayotokana na matukio ya kiasili.
Baadhi ya majanga na maafa ya kiasili ambayo yamewahi kutokea kwa baadhi ya maeneo
ya mamlaka ya serikali za mitaa ni Mafuriko, Ukame, Vimbunga na Wadudu/ndege/wanyama
waharibifu. Matukio hayo yana uwezekano mkubwa wa kutokea tena katika sehemu hizo au
sehemu nyingine. Udhibiti wa majanga na maafa yanayosababishwa na matukio ya kiasili au
shughuli/vitendo vya binadamu, unafanana kwa baadhi ya maeneo na kutofautiana kwa maeneo
mengine. Kwa sababu hii tutajadili tofauti za udhibiti wa majanga na maafa kwa kuzingatia aina
mbili za vyanzo vyake.
Njia za kudhibiti majanga mbalimbali ya kiasili
i. Mafuriko
Mafuriko ni matokeo ya mvua nyingi ambazo husababisha mikondo ya kawaida ya maporomoko
ya maji ya mvua kujaa kupita kiasi.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
222
Njia kuu za kudhibiti athari za mafuriko ni pamoja na zifuatazo:
• Utabiri mzuri wa hali ya hewa, ili kuweka mapema tahadhari za kuchukuliwa na kuwawezesha
watu kuhama mapema toka sehemu zinazoweza kupata athari kubwa.
• Kuepuka kupima na kujenga makazi katika maeneo yanayoweza kuathirika kwa urahisi na
mafuriko. Mfano mabondeni, kandokando ya kingo za mito, maeneo ya tambarare yaliyo
kandokando ya kingo za mito, , bahari au maziwa hasa maeneo ambapo mito inamwaga
maji baharini/ziwani. Maeneo ya aina hii yatambulike kwa jamii na kuwekewa matangazo ya
tahadhari za mafuriko.
• Kuchimba mifereji mikubwa na imara ya kuongoza maji ya mvua kutoka katika makazi na
mashambani kuelekea mitoni.
• Kutengeneza matuta ya kingo imara za kutenganisha makazi au mashamba na sehemu za
mito ambazo hujaa wakati wa mafuriko.Katika sehemu za mijini, ujenzi holela katika sehemu
za miinuko na milimani udhibitiwe ili kuzuia maporomoko ya udongo yanayosababisha mitaro
na mifereji na maji ya mvua sehemu za chini kujaa udongo.
ii. Ukame
Ukame ni hali ya upungufu au ukosefu wa mvua ambao husababisha unyevu wa ardhi kushuka
chini ya kiwango cha mahitaji ya mimea. Kutokana na hali hiyo, vyanzo vya maji kama mito,
visima na chemichemi hupungua maji au kukauka kabisa.
Ukame unaweza kuwa wa muda mfupi au muda mrefu. Ukame unaathiri watu na viumbe hai
vyote yaani mimea, wanyama, ndege na wadudu.
Njia kuu za kupambana na ukame katika mazingira yetu ni pamoja na zifuatazo:
• Kupunguza mifugo au kufuga kwa uwiano wa hifadhi ya ardhi kwa malisho.
• Kutumia kilimo cha umwagiliaji kwa kadri inavyowezekana bila kuathiri mazingira.
• Kutumia malisho makavu yaliyokusanywa na kuhifadhiwa karibu na makazi ili kupunguza
kuhamahama kwa wafugaji/wachungaji wakati wa kiangazi.
• Upandaji miti ili kuvuta mawingu na kuwezesha mvua kunyesha.
• Kuweka akiba ya chakula kila mwaka baada ya mavuno kwa tahadhari ya baadaye
kunapotokea ukame. Hii iwe tabia kwa ngazi ya familia na ngazi ya jamii kuanzia Kijiji/mtaa
hadi Halmashauri.
• Kutumia teknolojia ya uvunaji wa maji ya mvua kwa kujiwekea akiba ya maji kwa matumizi ya
nyumbani au kwa ajili ya kilimo cha mbogamboga.
MADA YA KUMI NA TATU
223
iii. Vimbunga
Majanga ya aina hii husababishwa na upepo wa kasi kubwa hasa sehemu za Pwani ya Bahari ya
Hindi na katika Visiwa na sehemu zinazopakana na maziwa makubwa kama Victoria, Tanganyika
na Nyasa.
Njia kuu za kudhibiti athari za vimbunga ni pamoja na;
• Utabiri mzuri wa hali ya hewa na mwenendo wa pepo katika majira mbalimbali ya mwaka na
kutahadharisha watu mapema.
• Kutoa tahadhari kwa jamii kwa wakati muafaka juu ya mabadiliko ya tabia za hali ya hewa ili
wasitishe usafiri baharini na katika maziwa nyakati za hatari.
• Kupanda miti inayofaa kwa kinga za pepo karibu na maeneo ya makazi katika vijiji
vinavyopakana na bahari au maziwa ili kupunguza nguvu za pepo kabla ya kuingia katika
makazi.
iv. Wadudu, Ndege na Wanyama waharibifu wa mazao
Wadudu kama nzige, panzi, na viwavi-jeshi husababisha maafa ya njaa kwa kushambulia mimea
ya chakula hususani nafaka.
Ndege aina ya kweleakwelea pia hushambulia mazao ya nafaka na kusababisha njaa miongoni
mwa jamii.
Wanyama kama panya, tembo na nyani huweza kushambulia mazao na kusababisha uharibifu
mkubwa. Panya pia wanaweza kueneza ugonjwa mbaya wa tauni.
13.3.4.4 Udhibiti wa majanga na maafa yanayosababishwa na vitendo vya watu katika jamii
Katika sehemu hii tutajadili matukio matatu ambayo yanatokea katika Mamlaka za Serikali za
Mitaa ijapokuwa kwa viwango tofauti.
Matukio haya ni:
• Vita/Mapigano katika jamii.
• Uharibifu wa mazingira
• Janga la UKIMWI na milipuko ya kipindupindu.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
224
I. Mapigano katika Jamii
Katika kipengele hiki hatuzungumzii vita kati ya nchi na nchi, tunazungumzia mapigano baina
ya jamii ndani ya mamlaka za serikali za mitaa. Mifano ni kama: mapigano kati ya wakulima na
wafugaji, mapigano kati ya koo katika baadhi ya makabila, na kati ya wachimbaji wadogo wa
dhahabu na wawekezaji wakubwa. Mapigano mengine ni Wavuvi wadogo na wavuvi wakubwa.
Njia kuu za kudhibiti mapigano katika jamii ni pamoja na zifuatazo:
• Kuimarisha Utawala Bora katika ngazi zote katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, yaani ngazi
za vijiji, mitaa, kata na Halmashauri zenyewe.
• Kuhamasisha uelewa kuhusu misingi ya utawala bora katika ngazi zote. Vyombo vya utawala
na watendaji wake waheshimu na kulinda haki za jamii hasa katika Nyanja ya uchumi
• Kujenga umoja wa kuheshimiana na kushirikiana kati ya makundi mbalimbali katika jamii
moja, kwa mfano makundi yanayohusika na shughuli mbalimbali za kiuchumi katika mazingira
yaleyale, kama wakulima na wafugaji
• Kujenga umoja kwa kuheshimiana na ushirikiano kati ya uongozi na jamii za vijiji au kata jirani
zilizo ndani ya mamlaka moja ya Serikali za Mitaa.
Jamii zielimishwe kujenga utamaduni wa kuvumiliana na kupokea matatizo na kutumia njia za
kujadiliana kwa uwazi na kwa kuaminiana ili kupata suluhisho na maridhiano kwa maslahi ya
pande zote husika. Waelimishwe kutambua kuwa matumizi ya nguvu hayasuluhishi tofauti na
badala yake huongeza chuki na mafarakano ya muda mrefu.
II. Uharibifu wa Mazingira
• Hiki ni chanzo cha pili katika orodha ya majanga na maafa yanayosababishwa na
vitendo vya watu
Maendeleo yoyote ya kijamii na kiuchumi hutegemea hali ya ustawi wa mazingira. Hali ya hewa
pia hutegemea sana mazingira. Aidha shughuli za uzalishaji mali katika sekta za kilimo, mifugo
na maliasili hutegemea mazingira asilia. Kwa hiyo, kuharibika kwa mazingira ni janga kubwa kwa
jamii linaloathiri sana ustawi na maendeleo ya jamii.
Licha ya kuikosesha jamii mahitaji muhimu, uchafuzi wa mazingira ambacho ni chanzo kikuu cha
kuharibu mazingira husababisha magonjwa mengi hasa magonjwa ya kuambukiza, kama vile
milipuko ya kipindupindu na magonjwa mengine ya kuhara.. Umuhimu wa hifadhi ya mazingira
umefafanuliwa katika vipengele vifuatavyo;
MADA YA KUMI NA TATU
225
• Umuhimu wa Hifadhi endelevu ya mazingira
Upo uhusiano wa karibu kati ya umaskini na uharibifu wa mazingira, uharibifu wa mazingira
husababisha kuenea kwa umaskini katika jamii. Hivyo hivyo umaskini katika jamii huchangia
kwa kiasi kikubwa kuharibika kwa mazingira. Hii ni kwa sababu watu maskini hawana mipango
mbadala na rahisi ya kutumia na kusimamia rasilimali kutoka kwenye mazingira yao kwa mfano
umaskini katika jamii husababisha kilimo duni kutokana na kushindwa kulipia gharama za zana
za kisasa za kurahisisha kazi na kuongeza mavuno. Matokeo yake ni kilimo cha kuhamahama,
ambacho huambatana na kufyeka miti hovyo na kuchoma nyasi, kulima sehemu za vyanzo
vya maji, kufuga mifugo mingi katika eneo dogo au kuhamahama kutafuta malisho hata katika
sehemu za hifadhi za misitu n.k. Hivyo kuelimisha jamii kuhusu hifadhi ya mazingira ni moja ya
mikakati inayowezesha au kuondoa au kupunguza umaskini.
• Maendeleo na mazingira endelevu
Maendeleo na mazingira endelevu hutegemea sana, shughuli za maendeleo kama vile za
uzalishaji mali katika viwanda, kilimo, ufugaji, uvunaji wa maliasili, (kama uchimbaji wa madini,
uvuvi na bidhaa zitokanazo na misitu) hutegemea hali nzuri ya mazingira wakati huo huo shughuli
hizo huweza kuchangia katika kuchafua na kuharibu mazingira. Mazingira yanapoharibika au
kuchafuliwa sana husababisha kushuka kwa uzalishaji mali. Uzalishaji unapopungua huathiri
maendeleo na ustawi wa jamii husika, kwa mfano, uzalishaji kutokana na kilimo, ufugaji, uvuvi,
mazao ya misitu, utalii katika mbuga za wanyama, kunaathirika kutokana na kuharibika au
kuchafuka kwa mazingira aidha udongo hupoteza rutuba inayohitajiwa na mazao na wakati huo
huo mifugo na wanyama pori hukosa malisho na hata maji kutokana na ukame unaosababishwa
na kufyeka na kuchoma ovyo mbuga na misitu. Uchafuzi wa mazingira, mito na hata pwani ya
bahari kutokana na takataka na kemikali za viwanda, ama husababisha samaki kupungua au
aina fulani ya samaki kutoweka kabisa.
III. Janga la Ukimwi
a) Maana ya Ukimwi
UKIMWI ni upungufu wa kinga mwilini. Virusi vya UKIMWI ni viini vinavyoshambulia kinga ya
mwili kupigana na magonjwa. Virusi vya UKIMWI hushambulia na kuharibu uwezo wa mwili
kujikinga na magonjwa. UKIMWI hauna tiba wala chanjo.
b) Njia kuu za maambukizi ya UKIMWI ni kama zufuatavyo:
• Kujamiiana na mtu ambaye amekwishaambukizwa;
• Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua na kunyonyesha;
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
226
• Kuwekewa damu ya mtu aliyekwishaambukizwa virusi vya UKIMWI;
• Kuchangia vifaa vyenye ncha kali na mtu mwenye maambukizi ya VVU.
• Kugusana kwa damu au majimaji ya mwili na mtu mwenye maambukizi endapo utakuwa na
jeraha
c) Njia ambazo zinaweza kutumika kupunguza janga la UKIMWI ni hizi zifuatazo:
• Kuacha ngono zembe;
• Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu;
• Matumizi sahihi ya kinga (Kondomu za kiume/kike);
• Kuacha utumiaji wa madawa ya kulevya;
• Kuepuka kushirikiana miswaki, nyembe, vifaa vya kutogea masikio na pua na vifaa vya
kutahiri;
• Kuacha tabia ya kurithi wajane;
• Kuwashauri wanawake walioambukizwa UKIMWI kuepuka kushika mimba.
d) Athari zitokanazo na UKIMWI ni pamoja na:
• Kupungua kwa nguvu kazi. Kundi la vijana ndilo liko hatarini zaidi kwani vijana wengi
hujihusisha na ngono mara tu baada ya kupata balehe/kuvunja ungo. Wengi wa vijana hawa
hawatumii kinga zozote. Ongezeko la vijana wanaopatwa na UKIMWI unapunguza nguvu kazi
katika ngazi ya Kaya, Kijiji/Kitongoji Mtaa na hata Taifa kwa ujumla;
• Kutengwa na jamii.
Mara nyingi watu walioathirika na UKIMWI hutengwa na jamii;
• Kuongozeka kwa familia tegemezi. Idadi ya familia ambazo ni tegemezi inazidi kuongezeka
kutokana na janga hatari la UKIMWI. Hivyo husababisha umaskini katika jamii kuongezeka.
MADA YA KUMI NA TATU
227
13.3.5: Hitimisho
Mada hii imezungumzia kwa ufasaha majanga na maafa, athari zake na jinsi athari hizo zinavyoweza
kuzuiwa au kupunguzwa. Mtendaji wa Kijiji na Mtaa anatakiwa kuhakikisha kuwa jamii inapata
uelewa wa majanga na maafa, na kushiriki katika kuainisha na kutekeleza mbinu za kupunguza
athari za maafa au kuzuia maafa yasitokee.
Marejeo
• Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (2002) Kitabu cha kufundishia
Madiwani.
• Ministry of Health and Social Welfare: National Training for Comprehensive Management of HIV
and AIDS; Participant Manual for Health Workers Module A.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
228
13.4 MADA YA UKUZAJI AJIRA
13.4.1 Utangulizi
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inahimiza na kuongeza matumaini ya kukuza uchumi na ukuaji
wa ajira ili kufikia mahitaji na matazamio ya watanzania wote ya kupata maendeleo na kuondoa
umaskini. Sera ya Taifa ya Ajira, 2008 inaelezea majukumu ya wadau wakuu wakiwemo Serikali
Kuu, Serikali za Mitaa, Vyama vya Waajiri na Wafanyakazi na inapendekeza kuwepo mfumo wa
kitaasisi utakaoratibu suala la ukuzaji ajira. Mfumo wa kitaasisi katika Serikali za Mitaa utaanzia kwa
Watendaji wa Mitaa au Vijiji.
Lengo la mada hii ni kuwaelimisha Watendaji wa Mitaa/Vijiji juu dhanaya ukuzaji ajira ili kusaidia
kuwaelimisha wananchi kuibua fursa mbalimbali katika maeneo wanayoishi zitakazopelekea
kuongeza vyanzo vya ajira (ikiwemo ajira binafsi au za kuajiriwa). Vilevile kuwafahamisha watendaji
wa mitaa/vijiji kuhusu kuwepo kwa mfumo wa kitaasisi ambao unaanzia kwenye mitaa/vijiji na
majukumu yao kwenye taasisi hizo.
Katika miaka ya karibuni sekta ya umma imekuwa ikiajiri idadi ndogo ya nguvu kazi inayoingia
katika soko la ajira, hivyo msisitizo unatakiwa uwekwe na wadau mbalimbali wakiwemo watendaji
wa mitaa/vijiji katika kuchochea ukuzaji ajira kupitia sekta binafsi ambayo imeonekana kukua na
kuzalisha ajira nyingi katika miaka ya karibuni.
Mtendaji wa Mtaa/Kijiji akiwa kama mtaalamu katika eneo analoongoza, atahusika katika kamati
hii kama mratibu na pia atahusika katika kuunganisha Kamati ya Ukuzaji Ajira katika mtaa au kijiji
chake na Kamati za Ukuzaji Ajira za ngazi za juu kama vile Kamati za Ukuzaji Ajira za Kata, Wilaya
au hata Mkoa.
13.4.2 Ufafanuzi wa Dhana mbalimbali za Ajira
a) Ajira
Ajira hutafsiriwa kama shughuli yoyote halali inayofanywa iliyo ndani ya shughuli za kiuchumi za
taifa. Shughuli hiyo hutakiwa kuwa yenye staha na ambayo hutoa kipato kinacholingana na kima
cha chini cha mshahara katika sekta husika
MADA YA KUMI NA TATU
229
Mtu aliyeajiriwa hutafsiriwa kama mtu anayefanya shughuli yoyote halali inayotambulika kwa mujibu
wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au sheria yoyote ya nchi, na anafanya shughuli
hizo kwa malengo yafuatayo:
i. Kupata mshahara kwa fedha taslimu au malipo mengine badala ya fedha
ii. Kujiajiri au kuajiriwa na akifanya shughuli hiyo kwa faida au kipato chake au kwa ajili ya familia
yake kwa mfumo wa fedha taslimu au malipo mengine badala ya fedha. Hii pia huhusisha
watu ambao wako nje ya kazi zao kwa muda.
Mtu asiye na ajira maana yake ni mtu aliyekosa ajira.
Mtu aliyeajiriwa chini ya kiwango ni yule ambaye anafanya kazi chini ya masaa yaliyokubalika
kisheria, na ambaye bado anaendelea kutafuta ajira ya ziada.
b) Ajira yenye Tija
Ajira yenye tija hutafsiriwa kama ni ajira inayozalisha pato linalolingana na rasilimali zilizotumika
katika uzalishaji. Inapotokea uzalishaji kutolingana na rasilimali zilizotumika ajira hiyo huhesabiwa
kama ajira isiyo na tija.
c) Ajira yenye Staha
Ajira yenye staha ni ajira inayozalisha na inayotoa kipato kwa mtu na inayozingatia mazingira
yanayoheshimu haki mahali pa kazi, majadiliano kati ya mwajiri na mwajiriwa na inayotoa kinga ya
jamii
d) Sekta isiyo Rasmi
Sekta isiyo rasmi maana yake ni shughuli yoyote isiyo ya kilimo, yenye mtaji mdogo, na muundo
rahisi wa kiutawala ambao inatumia teknolojia rahisi. Hapa Tanzania na kwingineko duniani, tatizo
la ukosefu wa ajira, ajira isiyo na staha na ajira zisizo na tija linawakumba sana vijana, wanawake
na watu wenye ulemavu. Hali hii husababishwa na makundi haya kuachwa nyuma katika kumiliki
rasilimali kama vile ardhi, mitaji na ukosefu wa ujuzi.
13.4.3 Umuhimu wa Ajira
Ajira huwa na umuhimu ufuatao:-
• Ni haki ya kila mtu kufanya kazi na kuwa na ajira;
• Ustawi wa ajira ni msingi wa maendeleo na ukuaji wa kiuchumi wa taifa na
• Hupunguza umaskini na kuondoa hali ya watu kuona wametengwa katika jamii husika.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
230
Madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na ukosefu wa ajira kuwa kiwango cha juu ni zifuatazo:-
a) Wananchi hujiona wametengwa na mfumo wa uchumi wa nchi yao. Hii huwafanya wananchi
kujiona wapweke ndani ya nchi yao;
b) Husababisha watu kujihusisha na shughuli zisizo halali (kama vile ukahaba, wizi n.k.) hii
inaweza kupelekea ukosefu wa amani katika nchi na
c) Huchochea kushuka kwa maadili miongoni mwa jamii kutokana na jamii kuamua kujihusisha
kwenye shughuli zisizo halali kwa lengo la kupata mahitaji yao ya kila siku.
13.4.4 Matamko ya Jumuia za Kimataifa Kuhusu Umuhimu wa Ukuzaji Ajira
Tanzania ikiwa mwanachama mmojawapo katika jumuia mbalimbali za Kimataifa imeridhia matamko
mbalimbali yanayohusu ukuzaji ajira. Baadhi ya matamko hayo ni Malengo ya Maendeleo ya Milenia
2015 na Azimio la Ougadougou.
Utekelezaji wa matamko haya umepelekea kuundwa kwa taasisi, kubuniwa kwa mipango na
mikakati mbalimbali kwa ajili ya kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hapa nchini. Vilevile Serikali
imeunda Wizara kwa ajili ya kuratibu utekelezaji wa ukuzaji ajira hapa nchini Kwa ujumla Serikali
inapambana na tatizo la ukosefu wa ajira kupitia malengo na viashiria vilivyomo kwenye Mkakati wa
Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA), Mpango wa Taifa wa Kukuza Ajira, 2007 na
mipango na sera nyinginezo za kisekta.
13.4.5 Hali ya Ajira nchini Tanzania
Kufuatana na Utafiti wa Nguvu Kazi wa mwaka 2005/06, nguvu kazi ya Tanzania inakadiriwa kufikia
watu milioni 18.8. Nguvu Kazi hii inakadiriwa kukua kwa asilimia 4.1 ambayo ni sawa na watu
800,000 kila mwaka. Asilimia 75.1 ya nguvu kazi inakadiriwa kuajiriwa kwenye sekta ya kilimo
(mazao, ufugaji, uvuvi, na misitu), sekta ambayo huchangia zaidi ya asilimia 50 ya pato la taifa. Kwa
muda wa miaka mitano kuanzia mwaka 2001 hadi 2006, sekta isiyo rasmi imekua kwa asilimia 19.3
Kiwango cha ukosefu wa ajira kitaifa ni asilimia 11.7. Ukosefu wa ajira ni mdogo maeneo ya vijijini
kwa asilimia 7.5% ; ambapo kwa upande wa mijini ukosefu wa ajira ni asilimia 16.5, jiji la Dar es
Salaam linaongoza kwa kuwa na ukosefu wa ajira unaokadiriwa kuwa asilimia 31.5.
Takwimu hizi zinalenga kutoa picha na hadhari kwa Serikali na wadau wengine kuandaa sera na
mipango inayohakikisha kuwa nguvu kazi inayoingia kwenye soko la ajira inaajiriwa na zinapunguza
tatizo la ukosefu wa ajira kwa makundi maalum hususani vijana, wanawake, watoto na walemavu.
MADA YA KUMI NA TATU
231
13.4.6 Mapendekezo ya Maeneo ya Ukuzaji Ajira nchini Tanzania
Mpango wa Taifa wa Ukuzaji Ajira mwaka, 2007uliandaliwa na Serikali ili ifikapo mwaka 2010 ajira
zinazozidi milioni moja ziweze kupatikana. Mpango huu ni endelevu kwa kuwa umeshauri njia
mbalimbali za ukuzaji ajira nchini Tanzania
Mpango wa Taifa wa Ukuzaji Ajira, 2007 umependekeza maeneo makuu manne ambayo yanaweza
kusaidia katika ukuzaji ajira hapa nchini. Maeneo hayo ni haya yafuatayo:-
• Ukuzaji ajira unaochochewa na kusaidiwa na uwekezaji binafsi katika biashara/viwanda vya
ngazi zote, viwanda vidogo vidogo, vya kati na viwanda vikubwa;
• Kukuza ajira kupitia uwekezaji wa umma pekee au kwa kushirikisha sekta binafsi;
• Kukuza ajira kwa kuendeleza maendeleo ya rasilimali watu kwa mfumo wa maarifa na maendeleo
ya ujuzi na
• Kukuza ajira kwa njia ya uendelezaji mifumo ya kitaasisi ambayo ni muafaka kwa kusimamia
mfumo wa taarifa ya soko la ajira.
13.4.6.1. Kukuza Ajira Kupitia Uwekezaji Katika Sekta Binafsi
Uwekezaji katika sekta binafsi kwa njia ya viwanda huweza kukuza ajira (Sekta binafsi imekuwa
ni mwajiri mkubwa na inaendelea kuwa hivyo kwa miaka mingi ijayo katika mfumo wa sera za
kiuchumi zilizopo sasa.
Ili sekta hii iweze kuendelea kuajiri watu wengi juhudi zifuatazo zinatakiwa kufanyika:-
a) Kutoa mafunzo kwa wananchi juu ya viwanda vidogo vidogo ili kuinuana kukuza biashara zao;
b) Kuwapatia mikopo ya kuendeleza viwanda vidogo kupitia mabenki na vyombo vya fedha;
c) Kujengea uwezo mabenki na vyombo vya fedha vinavyohusika na utoaji mikopo kwa viwanda
vodogo;
d) Kujengea uwezo wakopaji ili waweze kukopa kwa ajili ya kuendeleza viwanda vidogo;
e) Kuendeleza maeneo maalum ya uwekezaji;
f) Kuvijengea uwezo vyama vya ushirika na vyama vya wakulima
g) Upatikanaji wa mikopo kwa wakulima;
h) Kuongeza shughuli za kuongeza thamani ya mazao ya wakulima;
i) Kukuza soko la ndani na la kimataifa la bidhaa zitokanazo na mifugo na mazao ya mifugo;
j) Kuongeza soko la mazao ya utalii, kuongeza uwekezaji katika utalii na kujengea uwezo
biashara za utalii;
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
232
k) Kujengea uwezo juu ya upatikanaji wa mazao ya misitu na uvuvi;
l) Kukuza na kuwalinda wachimbaji madini wadogo;
m) Kuwaunganisha wachimbaji madini wakubwa na wafanyabiashara wa madini wa ndani;
13.4.6.2. Ukuzaji Ajira kupitia Mfumo wa Mipango ya Uwekezaji wa Umma
Uwekezaji wa umma ni muhimu siyo tu unaboresha miundo mbinu, afya, elimu, maji bali
pia upanuzi wa miradi inayowekezwa na umma inaweza kusaidia katika ukuzaji ajira kama
inavyoelekezwa hapa chini:-
a) Uwekezaji katika miradi ya ujenzi wa barabara kwa kutumia wafanyakazi wengi
Njia hii ya ukuzaji ajira huwezeshwa wananchi walio karibu na miradi hiyo kupata kipato
ambacho huwawezesha kuanzisha miradi itakayowawezesha kuongeza vipato vyao
b) Kuwepo kwa miradi ya umwagiliaji vijijini
Kwa kupanua miradi ya umwagiliaji. Vijiji vinavyofaidika huwa na maeneo mengi na makubwa
yanayoweza kulimwa katika kipindi kirefu cha mwaka.
Kipato kinachopatikana kutokana na kilimo endelevu huwasaidia wakulima kuwa na uhakika wa
chakula na hata kufungua miradi mingine ambayo huchochea ajira zao binafsi au ajira kwa jamii
inayowazunguka
c) Skimu za Makazi.
Kuruhusu wananchi walio katika maeneo yenye watu wengi kama vile Kilimanjaro, Mbeya n.k.
ambao wana nia ya kuendeleza kilimo wanaruhusiwa kuhamia maeneo mengine kama vile
Mtwara, Lindi, Morogoro n.k. kwenda kufungua miradi ya kilimo katika maeneo hayo.
d) Ajira mpya katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa
Katika miaka ya karibuni kama mbinu ya kuboresha utendaji wake, Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania imekuwa ikitoa fursa nyingi kwa watu wahitimu wa shule na vyuo kujaza
nafasi wazi katika serikali kuu au serikali za mitaa katika sekta za kilimo, afya, elimu n.k.
e) Upanuzi wa Miradi ya Kuboresha makazi ya mijini
Upanuzi wa mifumo ya utupaji taka katika maeneo ya mijini ni chanzo kizuri cha kuongeza ajira
kwa kaya nyingi hapa nchini. Njia hii huwezesha ukuzaji ajira kwa kuwapatia vipato wananchi
walio katika maeneo yanayozunguka eneo la mradi ambao baadaye huweza kutumia vipato
walivyopata katika kufungua miradi mingine kujiajiri wenyewe au kuajiri wengine.
MADA YA KUMI NA TATU
233
13.4.6.3 Kukuza Ajira kwa kuendeleza Rasilimali watu kwa Mfumo wa Maarifa na
Maendeleo ya Ujuzi
Katika sekta ya rasilimali watu/elimu ajira zitatengenezwa kupitia maendeleo ya ujuzi kwa
kupanua mafunzo ya ufundi stadi, hususani katika eneo la Teknolojia na Habari na Mawasiliano
(TEKNOHAMA). Vilevile kuboresha ujasiriamali katika sekta mbalimbali hapa nchini italeta
maendeleo makubwa ya kiuchumi
Katika mada hii yafuatayo yanapendekezwa ili kuweza kuongeza ajira katika sekta ya rasilimali
watu/elimu
a) Upatikanaji wa elimu na mafunzo kuanzia ngazi ya elimu ya msingi hadi chuo kikuu na
kuifanya elimu ipatikane kwa wote kwa gharama nafuu.
b) Elimu ya shule, mafunzo ya ufundi stadi na elimu ya juu yanaendeleza maarifa ya ujasiriamali
na mafunzo yanayohusiana nayo
c) Kutenga fedha kwa ajili ya kuendeleza dhana ya kujiajiri miongoni mwa wahitimu wa shule,
vyuo na elimu ya juu
13.4.6.4 Kuongeza Ajira Kupitia Muundo Wa Kitaasisi Kwa Ajili Ya Kuratibu Ukuzaji Ajira
Kazi za taasisi za ukuzaji ajira ni pamoja na kutoa nasaha za ajira, taarifa ya soko la ajira,
ushauri wa shughuli halali za kuongeza kipato, na ukuzaji wa ajira binafsi. Changamoto iliyopo
ni kwamba maafisa waratibu wa ukuzaji ajira waliopo makao makuu au katika ngazi za wilaya
hawatoshelezi, wana ukosefu wa mafunzo stahiki na upungufu wa vitendea kazi. Kuna haja
ya kuboresha mfumo wa kitaasisi wa kuratibu kwa ufasaha dhana ya ukuzaji ajira. Mojawapo
ya taasisi zinazoshauriwa kuundwa ili kuratibu suala la ukuzaji ajira ni Kituo cha Stadi za Ajira.
Kituo hiki kitahusika na uratibu utekelezaji wa sera mbalimbali ambazo zinaathiri ukuzaji ajira na
upatikanaji wa ajira.
13.4.7 HITIMISHO
Mada hii imeelezea dhana nzima ya ajira. Mtendaji wa Mtaa/Kijiji ni muhimu katika kufanikisha azma
nzima ya ukuzaji ajira kwa kuwa wao wanaishi na kuongoza wananchi wa ngazi ya chini katika jamii.
Uelewa wao kuhusu dhana hii utasaidia kuwaelimisha wananchi kuziona na kuibua fursa mbalimbali
zinazoweza kuchangia ukuzaji ajira katika mitaa au vijiji vyao.
Katika mada hii imeonesha kwamba sekta ya umma inaajiri idadi ndogo ya nguvu kazi inayoingia
kwenye soko la ajira kila mwaka. Msisitizo mkubwa kwa wadau mbalimbali ni utengenezwaji wa
ajira kupitia sekta binafsi.
MAFUNZO YA KUBORESHA UJUZI NA STADI ZA KAZI KWA
MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA MITAA TANZANIA BARA
234
Kwa hiyo ni muhimu kwa Mtendaji wa Mtaa/Kijiji kuelewa dhana nzima ya ajira ili aweze kutekeleza
majukumu yao ya kila siku hususani katika kuelimisha wanachi na kuratibu kazi ya ukuzaji ajira
katika Kamati za Ukuzaji Ajira katika maeneo yao.
Pia ikumbukwe kuwa ukuzaji ajira ni suala mtambuka linalohusisha watanzania wote, Wizara, Idara
na Wakala za Serikali, Serikali za Mitaa, Sekta binafsi, Vyama vya Waajiri na Wafanyakazi, Vyama vya
Kiraia na Asasi zisizo za Serikali. Inashauriwa kuwa sekta binafsi, waajiri, asasi za kiraia na wadau
wengine wanashirikiana kwa karibu na kwa dhati kuhakikisha tatizo la ukosefu wa ajira, ajira isiyokidhi
viwango na ajira isiyo na tija linapatiwa ufumbuzi kwa wananchi wa makundi na matabaka yote.
Marejeo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sera ya Taifa ya Ajira, 2008, Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo
ya Vijana, S. L. P. 1422, Dar es Salaam.
United Republic of Tanzania, National Employment Creation Programme, 2007 Ministry of Labour,
Employment and Youth Development, P.O. Box 1422, Dar es Salaam.
Danish Government, African Commission Report, 2009.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Utafiti wa Nguvu Kazi, 2006, Shirika la Takwimu la Taifa, Dar es
Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment