Friday, 5 December 2014

HUDUMA YENYE NGUVU


Huduma Yenye
Nguvu
Uhudumu Katika
Nguvu Na
Upako Wa
Roho Mtakatifu
Denzil R. Miller
Imenakiliwa
Maandiko yote ya Biblia yamenukuliwa kutoka kwenye THE HOLY BIBLE
IN KISWAHILI, Union Version, ©United Bible Societies, 1952.
Hairuhusiwi kuchapishwa wala kunakiliwa kwa aina yoyote ile bila kibali cha
kimaandishi kutoka kwa mtunzi kabla ya kuchapisha. Haki zote
zimehifadhiwa.
©2011 Denzil Ray Miller
Springfield, MO, USA
Translated from the author’s book
POWER ENCOUNTER: Ministering in the Power and Anointing
of the Holy Spirit
Kiswahili Version

Yaliyomo
Utangulizi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 1
KIFUNGU I: Kufahamu Huduma yenye Nguvu
Sura ya 1: Huduma yenye Nguvu Iamefafanuliwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 7
Sura ya 2: Huduma yenye Nguvu za Imeelezwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15
Sura ya 3: Huduma yenye Nguvu na Ufalme wa Mungu . . . . . . . . . . . . . 23
Sura ya 4: Huduma yenye Nguvu na Kuhubiri Injili . . . . . . . . . . . . . . . . . 31
KIFUNGU II: Maandalizi ya Huduma yenye Nguvu
Sura ya 5: Mambo Muhimu na Maandalizi ya
Huduma yenye Nguvu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 41
Sura ya 6: Roho Mtakatifu na Huduma yenye Nguvu . . . . . . . . . . . . . . . . 53
Sura ya 7: Kuongozwa na Roho . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 65
Sura ya 8: Silaha za Vita vyetu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 75
KIFUNGU III: Utendaji wa Huduma yenye Nguvu
Sura ya 9: Jinsi ya Kuponya Wagonjwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 87
Sura ya 10: Jinsi ya Kutoa Pepo wachafu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 97
Sura ya 11: Jinsi ya Kupambana na Huwashinda Pepo
Watawala wa “ Maeneo” . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 107
Sura ya 12: Jinsi ya Kuomba na watu Wajazwe Roho
Mtakatifu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 115
Appendix 1 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 125
Appendix 2 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 127
Bibliography . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 129
1
— Huduma Yenye Nguvu —
Utangulizi
Katika miaka ya karibuni kumekuwepo na wito kutoka kwa viongozi wa
makanisa na uongozi wa Ngazi za utawala wa Vyuo vya Biblia katika bara zima
la Afrika wakihitaji kupatikane mafundisho yanayohusu masuala ya huduma za
wachungaji wa Kiafrika, wainjilisti na viongozi wa makanisa. Mafundisho
yanayohusu huduma yenye Nguvu za Kiroho. Wengi wanauliza, “Tunawezaje
kuhudumu katika Nguvu na upako wa Roho Mtakatifu? Tunawezaje kuombea
wagonjwa na kushuhudia uponyaji wao? Tunawezaje kuwaongoza wakristo
waliomo makanisani mwetu katika ubatizo wa Roho Mtakatifu?”
Kitabu hiki kimeandikwa ili kujibu maswali hayo kwa njia tatu tofauti:
Kwanza, kitabu hiki kitaweka msingi wa Biblia kuhusu huduma yenye Nguvu za
Roho Mtakatifu. Ni katika msingi huu imara tu ambapo huduma ya kudumu ya
Roho Mtakatifu inaweza kujengwa. Haya yatajadiliwa katika kifungu cha
kwanza cha kitabu hiki kinachohusu, “Kuielewa huduma yenye Nguvu.” Pili,
kitabu hiki kitaeleza pia matayarisho binafsi ambayo yatahitajika kwa mtu
atakayehitaji kuhudumu katika nguvu za Roho Mtakatifu. Je anahitajika awe mtu
wa namna gani? Je ni mambo gani anahitaji ayapitie katika maisha yake kabla
ya kuingia katika huduma kama hii? Masuala haya yameelezwa katika Kifungu
cha Pili cha kitabu hiki, kinachozungumzia kuhusu “Matayarisho ya Huduma
yenye Nguvu.” Hatimaye tunapenda kutoa ushauri jinsi mtu anavyoweza
kuitenda Huduma yenye Nguvu. Kifungu cha Tatu “Jinsi ya kuitenda Huduma
yenye Nguvu.” Tunategemea kwamba kitabu hiki kitafaa kutoa mafundisho
bayana kwa wale wanaopenda kutii agizo kuu la Bwana Yesu, kuihubiri injili
kwa ishara zitakazofuatana (Marko 16:15-20).
Mapendekezo kwa Ajili ya Kusoma
Endapo mwanafunzi atafaidika na mafunzo ya kozi hii, ni hakika kwamba
haitatokana na usomaji wa kitabu kinadharia pekee. Ni kweli kwamba usomaji
wa kitabu hiki ni muhimu lakini, ili kuwepo na mafanikio mazuri ni vema
kuchanganya nadharia na kujifunza kimatendo. Kumbuka, lengo letu si kufaulu
Utangulizi
2
mitihani tu, bali ni kuona kwamba wanafunzi wetu wanafahamu vema kuhudumu
katika Nguvu na Upako wa Roho Mtakatifu na ishara zikifuata huduma hiyo.
Mafunzo ya Kitaaluma
Baada ya kuyashika haya yote tunatoa mapendekezo yafuatayo kuhusu kozi
hii: Kwanza, mafundisho ya kila somo ni vema baada ya kusoma yafanyiwe kazi
katika maisha ya kila mwanafunzi. Mwalimu anaweza kufanikisha jambo hili
kwa kufundisha vema pamoja na kuwapa wanafunzi vifungu vya kusoma,
majadiliano ya darasani, mitihani ya kuandika na ile ya kuwauliza wanafunzi
maswali darasani n.k. Katika kitabu hiki tumeuliza maswali mengi ili kumsaidia
mwanafunzi afikirie sana masuala yote yanayojadiliwa. Utaona maswali hayo
na alama kama, S 1, S 2, n.k. Maswali hayo yaliyomo katika vifungu vyenye
kivuli chepesi, yanaweza kutumika katika darasa kama maswali ya awali ya
kuanzishia mijadala.
Mafunzo ya Kiutendaji
Kama nyongeza juu ya mafunzo ya darasani, mafunzo ya kiutendaji ni
muhimu. Hili laweza kufanyika kwa njia kadha. Mwalimu anaweza kuchukua
uzito kuamua ni njia gani atatumia kuwafundisha wanafunzi kimatendo. (1)
Mwalimu anaweza kuamua kila juma kuwa na kipindi katika maabara ya
mafunzo, na (2) anaweza pia kuwatia moyo wanafunzi kujihusisha katika
utendaji halisi wa huduma hii katika maeneo mbalimbali wanapokwenda
kuhudumu. Tutaeleza zaidi kuhusu jambo hili.
“Maabara ya Mafunzo”
Kama ilivyopendekezwa awali, njia mojawapo ambayo mwalimu anaweza
kuwasaidia wanafunzi jinsi ya kushiriki na Roho Mtakatifu katika kuitenda
huduma yenye nguvu ni kwa njia ya Maabara ya mafunzo kila juma. Kila juma
wanafunzi wapangiwe kukutana pamoja na mwalimu ili kuabudu, kuomba na
kuamini Mungu apate kutembea katikati yao. Mwalimu awatie moyo wanafunzi
kumsikiliza Roho Mtakatifu, kuombeana endapo yupo anayeumwa katikati yao,
na kumruhusu Roho wa Mungu apate kugawa vipawa katika maisha yao. Ni
vema mwalimu asiwe kama “mtaalam” katika mikutano ya namna hii bali naye
achangamane katika kundi la kujifunza. Anaweza akatamka hivi kwa wanafunzi,
“Tumekuja kujifunza pamoja.” Kwa ruhusa ya uongozi wa chuo mikutano kama
hii yaweza hatimaye kujumuisha wanafunzi wote katika chuo ili kuendeleza
mikutano ya mchana katika “kupokea Roho Mtakatifu” au “Ibada za uponyaji.”
Utangulizi
3
Katika mikutano kama hii walimu na wanafunzi wanaweza kufanyia mazoezi
mambo ambayo wamejifunza madarasani. Kwa jinsi Mungu atakavyotembea na
kubariki ibada hizo, ndivyo ambavyo wanafunzi wataendelea kutiwa moyo.
Mazoezi kwa Vitendo
Namna ya pili ambayo mwalimu anaweza kuwasaidia wanafunzi kuyafahamu
vema mafunzo wanayojifunza darasani ni kuyageuza mafunzo hayo katika
matendo. Jambo hili linaweza kufanyika katika njia mbili. Njia ya kwanza ni
kwa mazoezi. Mwalimu anaweza kuwatuma wanafunzi wawili wawili ili kwenda
kuifanya huduma katika Nguvu za Roho Mtakatifu. Baada ya huduma hiyo
ambayo itahusu kuponya wagonjwa, kutoa pepo, au kuombea wakristo
waliookoka kujazwa na Roho Mtakatifu, wanafunzi watatakiwa kurudi ili kutoa
taarifa kwa mwalimu wa darasa. Majadiliano yatafuata ambapo mwalimu
atawatia nguvu, atawasahihisha na kuwaelekeza vema wanafunzi. Utatambua
kwamba hii ndiyo njia ambayo Yesu alitumia katika kuwafundisha wale sabini,
Luka 10:1-24.
Njia nyingine ambayo mwalimu anaweza kuwaongoza wanafunzi katika
mazoezi ya huduma ni kwa njia ya kwenda nao katika huduma. Anaweza
kuligawanya darasa katika makundi na kwenda na kundi moja kila wakati. Pia
mwalimu anaweza kupanga mipango na makanisa ya jirani kuhusu safari hizo za
huduma katika makanisa hayo. Siku zilizopangwa kwa huduma zifikapo
mwalimu na wanafunzi wanaweza kwenda kufanya huduma, wakiwahudumia
watu katika mahitaji yao.
Mwalimu na darasa pia yawabudi kutumia nafasi zipatikanapo kutoa huduma
katika chuo chenyewe. Je kuna wanafunzi wanaohitaji uponyaji? Je kuna
wanafunzi wanaohitaji kujazwa Roho Mtakatifu? Kama wapo basi huduma ya
nguvu za Roho Mtakatifu yaweza kufanyika katika mamlaka ya Jina la Yesu na
nguvu za Roho Mtakatifu.
4
5
— Kifungu I —
Kuielewa Huduma
Yenye Nguvu
6
7
— Sura Ya Kwanza —
Huduma Yenye Nguvu
Imefafanuliwa
HITAJI LA HUDUMA YENYE NGUVU
Wakati Yesu alipopaa mbinguni hakuacha kanisa nyonge. Alitupa nguvu
yote tunayohitaji kumaliza kazi. Kabla hajarudi kwa Baba yake aliahidi kulipatia
kanisa nguvu ya kuihubiri injili duniani kote (Mdo 1:8). Aliitimiza ahadi hiyo
siku ya Pentekoste (Mdo 2). Kanisa la kwanza lilihudumu katika nguvu kwa
mafanikio makubwa. Ni tamko la kitabu hiki kwamba kanisa leo bado linahitaji
nguvu ile ile kama litahitaji kufanikisha kazi ya kuwahubiri watu wote wa dunia
hii. Kuna sababu kadhaa zinazolifanya kanisa leo kuwa na huduma iliyojaa
nguvu za Mungu. Nitazitaja nne:
Tumo Vitani
Biblia inafundisha wazi kwamba sisi tunaojiita wana wa Mungu tumo katika
vita kubwa ya kiroho. Vita hii tunayopambana ni dhidi ya shetani na wafuasi
wake. Katika Mathayo 13:39 Yesu anatuambia kwamba “adui yetu ... ni
shetani.” (Pia angalia Luka 10:19). Paulo anazungumza kuhusu mapambano ya
kiroho
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na
mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika
ulimwengu wa roho (Efe 6:12).
Paulo anaendelea kusema kwamba lazima tutumie nguvu za silaha za kiroho
ili kupigana vita hii ya kiroho:
Sura Ya Kwanza: Huduma Yenye Nguvu Imefafanuliwa
8
Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata
kuangusha ngome” (2Kor 10:4).
Ngome ambazo mtume ananena habari zake ni ngome za kiroho zilizowekwa
na adui. Kwa hiyo kwanza ya yote lazima tuwe na huduma yenye nguvu kwa
sababu tumo vitani.
Adui anazo Nguvu.
Sababu ya pili inayotufanya tuhitaji huduma yenye nguvu ni kwamba adui
yetu shetani, ni adui mwenye nguvu. Katika Luka 10:19 Yesu anasema kwamba
“Nguvu yote ya adui.” Katika dunia nzima amekusanya jeshi la pepo waliojitoa
kupinga uenezaji wa injili. Kama tutahitaji kumshinda shetani ni lazima
tupambane na nguvu zake kwa nguvu iliyo kubwa zaidi. Tunaweza tu kulitimiza
hili kwa huduma inayotembea katika nguvu za Roho Mtakatifu.
Kazi ni Kubwa
Sababu nyingine inayotufanya tuhitaji huduma yenye nguvu ni kwamba kazi
tuliyonayo ni kubwa kiasi kwamba huduma ya nguvu ni njia pekee ambayo
tunaweza kuimaliza kazi hii. Kazi hiyo niisemayo ni ile ya kulitimiza agizo la
Bwana Yesu kuihubiri injili ulimwenguni pote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote
kabla hajaja tena (Mt 24:14). Leo kumebakia watu wanaozidi 2.5 bilioni katika
dunia ambao hawajapata ushuhuda wa kutosha wa injili. Je tutawafikiaje watu
wengi namna hii. wengi wao wakiishi katika nchi zinazotawala uhuru wa dini na
kupinga kabisa ueneaji wa ukristo? Yesu alituahidi kwamba atatupatia nguvu za
kumaliza kazi hii:
Lakini mtapokea nguvu, akisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa
mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata
mwisho wa nchi” (Mdo 1:8).
Pia alisema kwamba endapo tutakwenda na kuihubiri injili, yeye atalithibitisha
neno lake kwa ishara za nguvu zitakazofuatana nalo. “Akawaambia, enendeni
ulimwenguni mwote mkaihubiri injili kwa kila kiumbe ... Na ishara hizi
zitafuatana na hao waaminio: Kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha
mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa;
wataweka mikono yao juu ya wagonjwa nao watapata afya” (Mk 16:15-18).
Kutokana na Yesu, njia ya kueneza ufalme wake duniani ni kwa nguvu, hii ni,
katika nguvu za Roho Mtakatifu. Silikiza maneno yake:
Sura Ya Kwanza: Huduma Yenye Nguvu Imefafanuliwa
1John Wimber, Power Evangelism, (San Francisco: Harper and Row
Publishers, 1986) uk. 31.
2Ibid, uk. 39.
9
Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa
nguvu, nao wenye nguvu wauteka” (Mt 11:12).
Huduma yenye Nguvu Inafanya Kazi
Sababu ya mwisho inayotufanya tuhusike na huduma yenye nguvu ni kwa
sababu huduma ya namna hiyo inafanya kazi. Mafanikia makubwa ya kanisa la
mitume yanaweza kuwa ni kwa sababu sehemu kubwa ya huduma hiyo ilifanyika
katika nguvu za kimuujiza za Roho Mtakatifu -- na ishara zilizofuatana.
Lile lililofanyika katika kanisa la mitume hakika lawezekana pia kufanyika
leo. Katika kitabu cha Power Evangelism au Uinjilisti wenye nguvu , John
Wimber anaandika, “Katika mapana ya dunia nzima asilimia 70 ya ukuaji wa
makanisa unafanyika katika vikundi vya Kipentekoste na kikarismatiki”1
(charismatic). Vikundi hivi ndivyo vilevile vinavyoamini na kutegemea nguvu
za Roho Mtakatifu katikati yao. Katika kitabu hicho hicho mwandishi
anamnukuu C. Peter Wagner akisema,
Kuna uhusiano wa karibu sana kati ya ukuaji wa makanisa leo na huduma ya
uponyaji ... Injili inapopenyeza eneo, endapo hatutaenda na ufahamu wa matumizi
ya nguvu za miujiza za Roho Mtakatifu, kazi yetu haitakuwa na maendeleo ya
kutosha…2
Kama tunahitaji kuona mafanukio ya huduma ya mitume katika bidii yetu ya
uinjilisti, ni muhimu kuiga njia ambazo mitume walizitumia. Lazima tutumie
nguvu zile zile walizokuwa nazo. Lazima tujifunze kama walivyofanya, jinsi ya
kutembea na kuhudumu katika nguvu za Roho Mtakatifu.
Sura Ya Kwanza: Huduma Yenye Nguvu Imefafanuliwa
3Ibid uk.16 (imenukuliwa kutoka kwa Allen Tipett, People
movements in Southeast Polynesia).
4Opal Reddin, ed., Power Encounter, A Pentecostal Perspective
(Springfield, MO: Central Bible College, 1989) uk. 4.
5Wimber, uk. 16
10
UFAFANUZI WA MANENO
Ili kuwa na ufahamu wa huduma yenye nguvu ni nini, tunahitaji kuifafanua.
Pia tunahitaji kufafanua maneno yanayohusiana na huduma ya kimiujiza.
Mapambano Dhidi ya Nguvu za Giza
Kuna njia mbili ambazo tunaweza kufafanua maana ya mapambano dhidi ya
nguvu za giza: tunaweza kufafanua kwa ufinyu au kwa mapana zaidi.
Tukifafanua kwa ufinyu, mapambano dhidi ya nguvu za giza yanahusu hasa
kupambana na nguvu za giza (mapepo) katika nguvu za Jina la Yesu. Wimber
anamnukuu Allen Tippett ifuatavyo: “Pambano dhidi ya nguvu za giza) ni
pambano la ufalme wa Mungu na ufalme wa giza.”3 Mtaalamu wa mambo ya
utume C. Peter Wagner, kama alivyonukuliwa na Opal Reddin katika kitabu,
Power Encounter, A Pentecostal perspective, (muangalio wa Kipentekoste
kuhusu mapambano dhidi ya nguvu za giza), kitabu hicho kinatoa ufafanuzi
unaofanana: “Mapambano dhidi ya nguvu za giza ni udhihirisho wa wazi kabisa
kwamba Yesu Kristo ni mwenye nguvu zaidi kuliko miungu na mizimu
inayoabudiwa na kuogopwa na mataifa ya watu.”4 Ingawa hatupingani na
ufafanuzi huu, tunaona kwamba ni ufafanuzi mfinyu mno kwa somo hili.
Ufafanuzi kwa upana zaidi, mapambano dhidi ya nguvu za giza ni
udhihirisho wa nguvu za Mungu zikitumika kuendeleza ufalme wake duniani.
John Wimber anafafanua kwa mapana zaidi: “Kila utawala wa nguvu
unapolazimika ushindwe katika ushindani ili injili iweze kuaminiwa ndilo
chimbuko la mapambano dhidi ya nguvu za ibilisi. . .. Kufukuzwa kwa mapepo
katika mapambano dhidi ya nguvu za giza ni sehemu tu ya mapambano ambapo
nguvu za shetani zinajidhihirisha katika hali ya mapepo … Wakati ufalme wa
Mungu unakutana ana kwa ana na ufalme wa dinia hii (wakati Yesu anakutana
na shetani), kunakuwa na pambano (pambano dhidi ya nguvu za giza).”5
Sura Ya Kwanza: Huduma Yenye Nguvu Imefafanuliwa
11
Haduma ya Kuihubiri Kweli
Haduma ya kuihubiri kweli ni mahubiri ya injili ya Yesu Kristo ama kabla
au baada ya mapambano dhidi ya nguvu za giza. Wakati mapambano dhidi ya
nguvu za giza ni mapambano dhidi ya nguvu za shetani, huduma ya kuihubiri
kweli ni mapambano dhidi ya mafundisho ya uongo ya dini au vyama
vinavyowashikilia watu katika utumwa. Ni muhimu ‘kweli’ neno la Mungu
nyakati zote lifuatane na mapambano dhidi ya nguvu za giza. Kichwa cha somo
hili kitazungumzwa kwa urefu katika sura ya 4, “Mapambano dhidi ya nguvu za
giza na kuihubiri injili.”
Huduma yenye Nguvu
Katika kitabu hiki kizima tutatumia maneno, “Huduma yenye Nguvu.” Ni
muhimu basi tufafanue ni jinsi gani tutatumia maneno haya. Huduma yenye
nguvu, kama tutakavyotumia katika somo hili, ni huduma yoyote ya kimiujiza
yenye chimbuko katika Roho wa Mungu, inapotumika kuendeleza ufalme wa
Mungu duniani. Inahusisha ishara, maajabu, uponyaji, na kutoa pepo, huduma
ya karama za Roho, au udhihirisho wowote wa nguvu za Mungu kwa nia ya
kuendeleza ufalme wake.
Nguvu za Uponyaji
Kwa makusudi yetu ya sasa tutapanga uponyaji katika makundi mawili.
Kundi la kwanza tutaliita uponyaji wa agano. Uponyaji wa agano ni uponyaji
kama ulivyotolewa katika kazi ya Kristo msalabani (Isa. 53:4-5). Huu ndio
uponyaji alioutoa kwa watu wote wenye agano na Mungu; hii inamaanisha. Wale
wote waliomfanya Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wao. Katika Mathayo 15:25
Yesu analiita jambo hili “chakula cha watoto.” Pamoja na wokovu, ni sehemu
ya mahitaji ya ajabu ya watoto ambayo kristo aliyatenda msalabani.
Kundi la pili la uponyaji ni uponyaji wa nguvu. Maana yake ni uponyaji
ambao unatumika kama udhihirisho wa uwepo wa ufalme wa Mungu. Hapa mara
nyingi Mungu huponya hata wale wasiomwamini. Namna hii ya uponyaji
inatumika kwa kuambatana na mahubiri ya injili ili kuthibitisha kweli ya yale
yanayohubiriwa. Mara nyingi uponyaji wa namna hii umeitwa “ishara na
miujiza” katika vitabu vya injili na Matendo ya mitume.
Huduma ya Injili
Huduma ya injili yenye nguvu ni matokeo tunapochanganya mapambano
dhidi ya nguvu za giza na huduma ya kuihubiri kweli au neno la Mungu. Naweza
Sura Ya Kwanza: Huduma Yenye Nguvu Imefafanuliwa
6Wimber, uk. 35
12
kuelekeza kimchoro katika chati ifuatayo:
Mapambano dhidi ya nguvu za giza + Huduma ya
kuihubiri kweli = Huduma ya injili yenye nguvu
Kutokana na John Wimber, “(Huduma ya injii yenye nguvu) ni maelezo ya
injili (ambayo) huja kwa udhihirisho wa nguvu za Mungu kwa njia za ishara na
maajabu….. Huduma ya injili yenye nguvu ni uinjiisti ambao unafuatiwa na
uthibitisho wa kimiujiwa wa uwepo wa Mungu.”6 Huduma ya injili yenye nguvu
hufanyika wakati kuna udhihirisho wa nguvu za kimiujiza za Mungu JUMLISHA
mahubiri ya injili yaliyo wazi na yanayozikamata dhamiri za watu na kuwafanya
waikubali injili.
Ishara na Maajabu
Maneno haya yanatokea mara kwa mara katika Agano Jipya “Ishara na
miujiza.” Katika Matendo ya mitume kwanza maneno haya yanaonekana katika
sura ya2, msitari wa 22. Hapa maneno haya yanaelezea kuhusu huduma ya Yesu.
Sehemu ya pili yanatajwa katika sura ya 2, msitari wa 43. Hapa iliyotendeka
kuhusiana na huduma ya kanisa iliyotendeka mara baada ya Siku ya Pentekoste:
Kila mtu akaingiwa na hofu; maajabu mengi na ishara zikafanywa na mitume.
Angalia: Uwe mwangalifu kusoma mistari ifuatayo inayozungumzia
“ishara na ajabu” katika uinjilisti wa Agano Jipya: Matendo 4:29-30;
5:12; 6:8; 14:3; Ru 15;19; Ebr 2:3,4.
Katika maandiko maneno “ishara na maajabu” mara nyingi hutumika
pamoja, ili kuonyesha jinsi mambo hayo mawili yanavyokwenda pamoja.
Ishara ni kitu kinachoonyesha kwenye kitu kingine. “Ishara” katika Agano
Jipya (Kigriki: semeion) ni matokeo ya miujiza yanayoonyesha kwamba
ufalme wa Mungu umekuja na kwamba ujumbe wa injili ni kweli. Katika
Sura Ya Kwanza: Huduma Yenye Nguvu Imefafanuliwa
7Reddin, uk. 238.
13
Marko 16:15 Yesu anafundisha wazi kwamba atayathibitisha mahubiri ya
injili kwa ishara zitakazofuatana nayo. Na katika msitari wa 20 ishara hizi
zinasemekana kuthibitisha ujumbe wa injili kama ulivyohubiriwa na
mitume. Tunapoendelea kuhubiri injili, sisi pia tunaweza kutegemea
Mungu kuthibitisha ujumbe kwa ishara zitakazofuatia.
Neno “ajabu” (Kigriki: tera) linazungumzia kuhusu muujiza wa ajabu
wa Mungu ambao unamfanya mtazamaji kushangaa, kama wakati Yesu
alipomponya kijana aliyepagawa na mapepo katika Luka 9:43:
Wote wakashangaa, wakiuona ukuu wa Mungu (na) walikuwa wakiyastaajabia
mambo yote aliyoyafanya.
Katika Matendo ya mitume hii “ajabu” ya watu ilihusisha mshangao mkubwa
(Mdo 2:7; 3:10); wakaingiwa hofu (Mdo 2:43); wakashangaa wote (Mdo 2:12);
wote alimtukuza Mungu (Mdo 4:21); hofu nyingi (Mdo 5:5,11); ikawa furaha
kubwa (Mdo 8:8); akashangaa (Mdo 8:13) hata imani iokoayo (Mdo 9:42 na
1Kor 2:4-5).
Daktari Jesse K. Moon akizungumza kuhusu makusudi ya ishara na maajabu
katika Agano Jipya:
1. Kuhakikisha Umasihi wa Kristo na kuwafanya watu wamwamini (Mdo 2:22;
Ebr 2:4);
2. Kuwavuta watu wasikilize injili;
3. Kama ushahidi kwamba Kristo yu hai (amefufuka) ni Bwana wa Kanisa;
4. Kuthibitisha neno lililohubiriwa (Mdo 4:29, 30; 14:3; Rum 15:19; Ebr 2:3, 4);
5. Kutambulisha waumini na dini ya kweli (2Kor12:12; Mk 16:15-18);
6. Kukutana na mahitaji ya wanadamu, na
7. Kuendeleza ufalme wa Mungu duniani (Mdo 5:12-14; 8:5-13).7
Sura Ya Kwanza: Huduma Yenye Nguvu Imefafanuliwa
14
Kwa sababu hizo zote yatubidi tuombe sana ili ishara na maajabu viwe
sehemu katika huduma zetu katika kuihubiri injili ya Kristo leo kama ilivyokuwa
katika siku za mitume.
MWISHO
Mahubri yenye upako yakifuatiwa na ishara na maajabu ni ufunguo muhimu
wa kufikia ulimwengu na injili ya Kristo. Lazima tufike katika ufahamu timilifu
kuelewa ni nini maana ya kuhudumu katika nguvu na karama za Roho Mtakatifu.
Tukianza kuwa na ufahamu huo tutaanza kuona matokeo ya Agano Jipya katika
huduma zetu za uinjilisti. Hili ndilo kusudi la kitabu hiki. Ili upate kujaa mambo
haya, unaposoma na kujifunza masomo yafuatayo, ninaomba kwamba kwa njia
ya imani na kujiachilia kwa Roho Mtakatifu, wewe pia utaanza kuhudumu katika
nguvu za kiumitume na matokeo ya huduma zilezile za Agano Jipya.
8London Blitz ilikuwa ni mapigo ya mabomu juu ya mji wa London,
uingereza yaliyoangushwa na ndege za vita za kijerumani katika Vita
Kuu ya pili.
15
— Sura Ya Pili —
Huduma Yenye Nguvu
Imeelezwa
UTANGULIZI
Kuna maelezo mbalimbali ya mapambano dhidi ya nguvu za giza katika
maandiko. Tumechagua mifano michache kutoka kote katika Agano la Kale na
Agano Jipya kwa ajili ya somo hili.
HUDUMA YENYE NGUVU ILIVYODHIHIRISHWA
KATIKA AGANO LA KALE
Katika agano la kale tunaona mifano mizuri ya huduma yenye nguvu.
Tumechagua mifano miwili ili kueleza hoja yetu.
Musa Anapambana na “miungu” ya Misri
Soma habari ya jinsi Musa alivyoshindana na miungu ya Misri katika Kutoka
7-13. Fahamu jinsi Mungu alivyomwambia Musa kwamba mapambano hayo
yote kati yake na Farao ni mapambano kati ya Mungu na “miungu yote ya Misri”
(Kut 12:12). Kutokana na maandiko ya Paulo tunajifunza ya kwamba “miungu
ya Misri” ilikuwa hasa ni majeshi ya pepo wabaya (1Kor 10:20). Katika kitabu
chake, ishara, maajabu, na ufalme wa Mungu, Don Williams anasema, “Kutoka
5-12 inazungumzia matendo makuu ya Mungu, ishara na maajabu yanayoanguka
kama ukungu wa mabomu ya vita yaliyoanguka katika mji wa London.8
Sura Ya Pili: Huduma Yenye Nguvu Imeelezwa
9Don William, sign, wonders and the Kingdom of God (Ann Arbor,
MI: Servant Publications, 1989) uk. 82.
10Fred Haltom, Old Testament Encounters, “Power Encounter, A
Pentecontal Perspective, uk. 103.
16
Hapa tunaona huduma yenye nguvu ikitendeka jambo ambalo ni udhihirisho
wa wazi kabisa kwamba Mungu ana nguvu zaidi kuliko miungu ya Misri. Katika
kila pigo, Mungu alikuwa akipambana na mmoja au zaidi ya miungu ya misri.9
Kutokana na Fred Haltom, Mungu alipeleka mapigo mbalimbali ili kupambana
na kila mmoja katika miungu ya Misri:
Alipeleka mapigo ya damu, vyura, na chawa kama mapigo kwa Nu, mungu wa mto
Naili; Hekt, mungu mke wa nchi ile; na Geb, mungu wa dunia. Alipeleka mapigo ya
Nzi, magonjwa juu ya wanyama, majipu juu ya wanadamu kama mashambulizi juu
ya Scarob, mungu wa wadudu; Apis, mungu ng’ombe; na Thoth, mungu wa ufahamu
na elimu ya uganga. Alipeleka upepo, nzige na giza kama mashambulizi juu ya Ntu,
mungu wa anga; Anubis mlinzi wa mashamba; na Ra, mungu wa jua. Na hatimaye
vifo vya wazaliwa wa kwanza wa Misri kama shambulizi kwa Farao mwenyewe,
mungu-mfalme.10
Kutokana na hayo ya juu, tunaweza kujumuisha kuwa miungu ya Misri
ilikuwa falme na majeshi ya pepo wabaya vikishikilia watu katika utumwa wa
kiroho. Kutoka kwa wana wa Israel katika utumwa wa Misri ilikuwa ni zaidi ya
ukombozi wa kimwili wa watu wa Mungu. Ilikuwa pia ukombozi wa kiroho
kutoka katika utawala wa nguvu za giza,kwenda katika uhuru wa kumwabudu
YEHOVA peke yake.
Eliya Anashindana na Manabii wa Baali juu ya Mlima Karmeli
Katika wafalme wa kwanza 18:20-46 soma habari ya kusisimua kuhusu
mapambano dhidi ya nguvu za giza kati ya Eliya nabii na Baali, mungu wa
Kanani aliyevuviwa na nguvu za mapepo. Merril C. Unger ameandika, “Dalili
ya kuwepo kwa mapepo katika Agano la Kale, kama sio kupagawa, ilikuwa ni
Sura Ya Pili: Huduma Yenye Nguvu Imeelezwa
11Merril C. Unger, Biblical Demonology (Wheaton, IL: Scripture
Press, 1971).
17
namna ya ibada za kipagani za makuhani wa Baali.”11 Kumbuka Eliya hakuwa
tu anapambana na dini ya kuabudu miungu ya Baali, bali alipambana na mapepo
yaliyokuwa nyuma ya dini hiyo, yakiipa nguvu zake.
Tambua kwamba mapambano hayo yalihusisha vyote mapambano dhidi ya
nguvu za giza pamoja na huduma kwa njia ya kuihubiri kweli (1Wafalme 18:21).
Katika mapambano haya YEHOVA, kupeleka moto kutoka mbinguni kuyalamba
maji ilionyesha ukuu wake zaidi kuliko Baali. Wakati huo huo msitari wa 21,
Eliya anawahubiri watu na kuwahamasisha kumfuata Mungu wa kweli aishiye.
Mapambano haya dhidi ya nguvu za giza yalisaidia kuionyesha Israeli na
wapagani ambao Israeli walikutana nao kwamba YEHOVA ni Mungu pekee
astahiliye kutumikiwa na kuabudiwa.
HUDUMA YENYE NGUVU ILIVYODHIHIRISHWA
KATIKA HUDUMA YA YESU
Huduma ya Yesu ilijaa nguvu. Kupitia udhihirisho huo wa nguvu Yesu
alionyesha hakika kwamba alikuwa Ndiye “mpakwa mafuta” aliyetumwa na
Mungu. Pia alionyesha kuwa ufalme wa Mungu ulikuwa umekuja kuupindua
ufalme wa shetani (Lk 11:20). Tunaona huduma yenye nguvu ikiwa
imedhihirishwa kwa njia nne katika huduma ya Yesu: (1) katika makusudi ya
huduma yeke, (2) katika utendaji wa huduma yake, (3) katika mafundisho ya
huduma yake, na (4) katika kukabidhi huduma yake kwa wale waliomfuatia.
Sasa hebu tuangalie katika kila njia mojawapo.
Katika Kusudi la Huduma Yake
Biblia inanena waziwazi kwamba moja ya makusudi ya kuja kwa Yesu
ilikuwa “ni kuziharibu kazi za shetani” (1Yoh 3:8). Hata mapepo aliyopambana
nayo yalielewa ya kwamba Yesu alikuja kuyaharibu:
Na mara palikuwa ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti,
akisema, “Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza? (Mk
1:23-24).
Katika Luka 4:18-19 Yesu alitamka agenda za huduma yake. Huduma yake
Sura Ya Pili: Huduma Yenye Nguvu Imeelezwa
18
ilisimamia juu ya mambo sita:
1. Upako: Alikuja ili kuhudumu katika upako wa Roho Mtakatifu. (“Roho wa
Bwana yu juu yangu kwa maana amenitia mafuta … “)
2. Kuhubiri: Alikuja kuhubiri injili kwa watu waliopotea. (“…kuwahubiri maskini
habari njema”)
3. Kuwaweka wafungwa huru: Alikuja kuwafungulia walewaliofungwa na dhambi
na shetani. (Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao . . .”)
4. Uponyaji: Alikuja kuwaponya wagonjwa. (“…na vipofu kupata kuona tena, …
“)
5. Kuwaacha huru waliosetwa: Alikuja kuwafungulia wale walio
katika utumwa - kiroho, kimwili, kihisia, Kidini, kiuchumi na kijamii . (“ …
kuwaacha huru waliosetwa:)
6. Kutangaza Kuja kwa Ufalme wa Mungu: Alitangaza kuwa wakati umetimia kwa
ajili ya kuja ufalme wa Mungu (“… kutangaza mwaka wa Bwana
uliokubaliwa.”)
Katika Utendaji wa Huduma Yake
Yesu hakutangaza tu kwamba amekuja kupambana na kuziharibu kazi za
shetani, bali pia alidhihirisha jambo hilo katika utendaji wa huduma yake.
Sehemu mbili za mkazo wa huduma ya Yesu zilikuwa: (1)
kuhubiri/kufundisha na (2) uponyaji (angalia: Mt 4:23; 9:35). Mara nyingi
aliyachanganya mambo hayo mawili. Hivyo alichanganya mapambano dhidi ya
nguvu za giza na huduma ya kuihubiri kweli katika mikakati ya huduma yake.
Kuna mifano mingi sana ya mapambano dhidi ya nguvu za giza katika
huduma ya Yesu. Tumechagua mifano minne tu ili kuwakilisha katika somo letu.
1. Majaribu yake nyikani. (Soma Luka 4:1-13). Katika majaribu yake
nyikani Yesu alikutana ana kwa ana katika mapambano na shetani. Luka
anasema ya kuwa Yesu aliingia katika mapambano na shetani akiwa “amejaa
nguvu za Roho Mtakatifu” (mstari 1). Hili lilikuwa pambano kuu la kwanza la
Yesu dhidi ya nguvu za giza. Hapa mwanzo tu wa huduma yake, alidhihirisha
nguvu si tu juu ya pepo, bali pia juu ya mfalme wa mapepo, shetani mwenyewe.
Habari za kushindwa kwa nahodha wao bila shaka zilienea haraka katika
ulimwengu wa mapepo, kwa sababu kutokea wakati huo na kuendelea mapepo
yanaonekana kutambua na kuogopa nguvu za Yesu. (Angalia: Mk 1:23-24 kama
mfano.)
2. Muujiza wake wa kwanza katika Marko. (Soma Marko 1:21-27; 34,39;
3:10-11). Muujiza wa kwanza katika injili ya Marko ni mfano halisi wa
Sura Ya Pili: Huduma Yenye Nguvu Imeelezwa
19
mapambani ya Yesu dhidi ya nguvu za mapepo. Kulikuwepo na jambo fulani
kuhusiana na uwepo wa Yesu ambalo liliyatahayarisha mapepo.
Yakitahayarishwa na uwepo wake, yalilia kwa sauti ya woga. Yesu aliyaamuru
mapepo, “Nyamaza” na “Mtoke . . .” Hayakuwa na uchaguzi bali kumtii.
3. Mapambano yake na mtu mwenye pepo katika nchi wa Wagerasi. (Soma
Marko 5:1-20). Hadithi ya Yesu alipomtoa pepo mtu aliyepagawa katika nchi ya
Wagerasi ni mfano mzuri wa mapambano ya Yesu katika kutoa pepo
yaliyoelezwa katika maandiko. Tena kama katika mfano wetu wa mwisho,
mapepo haya pia yanaonekana kutahayarishwa na uwepo wake Yesu. Na tena
mtu aliyepagawa anakombolewa kabisa kutokana na mapepo kwa amri ya Yesu.
4. Alivyomponya kijana aliyepagawa na mapepo. (Soma Marko 9:14-32).
Kijana aliyepagawa katika Marko 9 tena anadhihirisha jinsi Yesu alivyopambana
wazi kabisa na kuzishinda nguvu za mapepo. Kwa mara nyingine tena mapepo
ilibidi yatii amri yake Yesu. Wanafunzi wake walipomuuliza ni kwa nini
hawakuweza kumtoa pepo, Yesu aliwaonyesha upungufu wao katika maombi
kama sababu yao ya kutokuwa na nguvu (mstari 29).
Yesu alifanya ishara, maajabu na miujiza katika huduma yake yote; muda
hautoshi kutuwezesha kuangalia mambo yote haya. Hata hivyo yabidi uifanye
huduma ya Yesu kuwa mafundisho ya maisha yako yote, pia jitahidi kumuiga
yeye katika mambo yote aliyoyasema na kuyafanya. Tunaweza kujifunza mengi
kuhusu kuponya wagonjwa na kushughulika na pepo kwa njia ya mafunzo haya
pamoja na mapambano mengine ya Yesu dhidi ya nguvu za giza.
Katika Mafundisho ya Wanafunzi Wake
Yesu hakuja tu kuziharibu kazi za shetani bali aliwafundisha pia wanafunzi
wake kufanya hivyo hivyo. Ni wazi kwamba, sababu moja ambayo Biblia
inatupatia maelezo mengi na ya kina jinsi Yesu alivyoponya wagonjwa, na jinsi
alivyowakomboa wale waliokuwa katika kifungo, ni ili sisi kama ilivyokuwa kwa
wanafunzi wake kumi na wawili, tuweze kuchunguza jinsi alivyohudumu, na
kama mitume, nasi tumuige.
Nyakati nyingi tunamwona Yesu akiwafundisha wanafunzi wake jinsi ya
kuhudumu katika nguvu za Roho. Katika Luka 9:1-6 na Luka 10:1-23 Yesu
aliwatuma wanafunzi wake katika safari ya mafunzo ya kazi ya utume. Safari ya
pili aliwatuma 70, Yesu alihitaji walete ripoti kwake (mstari 17). Baada ya
kupokea ripoti hiyo, Yesu alichukua muda kuwafundisha. Hapa anawaeleza wazi
kwamba amewapa mamlaka juu “ya nguvu zote za adui” (Luka 10:19).
Katika sura inayofuata (Lk 11:14-26), Yesu anawapa wanafunzi wake
Sura Ya Pili: Huduma Yenye Nguvu Imeelezwa
20
mafundisho zaidi jinsi ya kushughulika na nguvu za mapepo. Sasa waweza
kutaka kusoma kwa utaratibu na kujifunza sehemu hiyo ya maandiko.
Katika Kuikabidhi Huduma yake kwa wale Waliomfuatia
Katika kuikabidhi kazi ya huduma yake kwa wanafunzi wake, Yesu aliweka
wazi ya kwamba watahusika katika huduma yenye nguvu, kama vile yeye
mwenyewe alivyohusika. Katika kuwateua wale mitume kumi na wawili, Yesu
aliwatuma “aliwapeleka wapate kuhubiri tena wawe na amri juu ya pepo”
(Mk.3:14). Ni wazi kwamba walihitajika kuwa na huduma ile ile ya namna mbili
kama alivyoifanya Bwana Yesu, yaani huduma dhidi ya nguvu za giza na
kuihubiri kweli yaani neno la Mungu.
Katika Luka 9:1-2, wakati Yesu alipowatuma wale kumi na wawili “akawapa
uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi. Akawatuma
wautangaze ufalme wa Mungu, na kupoza wagonjwa.” Tena tunaona sehemu
mbili za huduma, huduma ya vitendo na ile ya kulinena neno la Mungu (nguvu
na kuhubiri) vimetiliwa mkazo! Halafu, katika Luka 10 Yesu alipowatuma wale
70 aliwapa nguvu na mamlaka kutoa pepo (Lk 10:1;17-20).
Katika “agizo kuu”, kama ilivyoandikwa katika Marko, baada ya Yesu kutoa
agizo la kuipeleka injili ulimwenguni pote, aliahidi kwamba tunaweza pia
kutegemea ishara zile zile kufuatia huduma zetu kama zilivyo fuatia huduma
yake (Mk 16:15-18). Kutokana na rekodi ya maandiko, wanafunzi wake
walikwenda wakatimiza huduma hiyo ya sehemu mbili yaani huduma yenye
nguvu. (Soma: mistari 19-20). Sisi kama wale waliosikia maneno yale, lazima
tuende katika nguvu za Roho Mtakatifu kuihubiri injili na ishara zikifuatana nasi.
Kitendo cha mwisho cha Yesu cha kuikabidhi huduma yake ya nguvu kwa
wafuasi wake ilikuwa ni kuwapatia nguvu ya upako ule ule uliomwezesha yeye
katika huduma yake duniani (Mdo 10:38). Alifanya hili katika siku ya
Pentekoste “wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha
nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka” (Mdo 2:4). “Nguvu ile ile ya
Kipentekoste” inapatikana kwetu leo, ili sisi nasi tuweze kuzifanya kazi za Yesu
(Linganisha Yn 14:26 na 16:7).
Sura Ya Pili: Huduma Yenye Nguvu Imeelezwa
21
HUDUMA YENYE NGUVU KATIKA
KANISA LA KWANZA
Wakiisha kupokea nguvu za Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste, mitume
walikwenda na kuiga huduma ya Yesu. Kama huduma yaYesu ilivyokuwa,
huduma zao pia zilikuwa kuhubiri neno na vitendo. Hawakuihubiri tu injili, bali
pia kwa njia za miujiza, ishara na maajabu, waliifanya kazi ile ile aliyoifanya
Yesu,wakidhihirisha kuwa ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu kuu.
Uchunguzi Kuhusu Huduma ya Kanisa la Kwanza
Huduma ya kanisa katika kitabu cha Matendo ya mitume ni kuiendeleza
huduma ya Roho Mtakatifu ambayo alimpaka mafuta Yesu ili kutenda kazi.
Tafakari sentensi isemayo “aliyoanza Yesu kufanya na kufundisha” katika
Matendo 1:1:
Kitabu kile cha kwanza nalikiandika, Theofilo, katika habari ya mambo yote
aliyoanza Yesu kufanya na kufundisha (mkazo wa mwandishi).
Maneno haya yana lengo la kusema kwamba, sasa kwamba Yesu
ameisharejea mbinguni, kanisa litaendeleza huduma yake, pamoja na kazi zake
za nguvu. Na haya ndiyo ambayo kanisa la kwanza lilifanya.
Ishara na maajabu vilikuwa msingi wa huduma ya kanisa la kwanza.
Usomaji wa uangalifu wa kitabu cha Matendo ya mitume unadhihirisha kwamba
mitume katika utendaji wa huduma walifuata kanuni ile ile iliyoanzishwa na
Yesu ya kuhubiri Neno na kuidhihirisha kazi ya huduma kwa matendo. Huduma
yao ilihusisha ishara na maajabu, uponyaji, na kutoa pepo, miujiza ya uumbaji wa
asili na masuala ya chakula, ufufuaji wa wafu, kunena kwa lugha, unabii, maono,
na miujiza mingine isiyo ya kawaida.
Matokeo ya kuchanganya ishara na maajabu pamoja na kuihubiri injili yenye
upako, mshangao na ajabu vilionekana katikati ya watu; injili ilihubiriwa kwa
nguvu kubwa ya ushawishi; na maelfu ya watu waliokolewa. Mambo haya haya
yanaweza kutokea leo, endapo sisi, kama mitume, tutafuata utendaji huu wa aina
mbili ambao Yesu alionyesha mfano wake.
Sura Ya Pili: Huduma Yenye Nguvu Imeelezwa
22
Mifano Michache ya Huduma yenye Nguvu Katika Kanisa la Kwanza
Hebu sasa tuangalie mifano michache ya huduma yenye nguvu katika kitabu
cha Matendo ya mitume. Hapa kuna mifano miwili. Unaposoma kila mfano, jibu
maswali manne kuhusu kila huduma yenye nguvu ilipotendeka.
1. Pentekoste. Kwa uangalifu soma Matendo 2:1-41. Sasa jibu maswali
yafuatayo:
a. Je! Ni matendo gani ya nguvu za Mungu yalitendeka katika siku ya
Pentekoste?
b. Je! Makusanyiko ya watu waliitika vipi kwenye matendo hayo ya
udhihirisho wa nguvu?
c. Je! Huduma ya kuihubiri kweli ilitendeka? Kama ndiyo tafadhari eleza
kwa kifupi.
d. Je! Kulikuwa na matokeo gani katika huduma yenye nguvu iliyotendeka
siku hiyo?
2. Uponyaji mbele ya Mlango Mzuri (Matendo ya mitume 3:1-26) Sasa,
kwa uangalifu soma Matendo 3:1-26. Jibu maswali yale yale manne kama
ulivyofanya katika mfano wa awali:
a. Je! Ni udhihirisho gani wa nguvu za Mungu ulitokea mbele ya Mlango
Mzuri wa Hekalu?
b. Je! Muitikio wa makusanyiko ya watu ulikuwaje kutokana na
udhihirisho huo wa nguvu za Mungu?
c. Je! Huduma ya kuihubiri injili ilitendeka? Kama ndiyo, eleza kwa ufupi.
d. Je! Kulikuwa na matokeo gani katika huduma yenye nguvu iliyotendeka
siku hiyo?
12Williams, uk. 107.
23
— Sura Ya Tatu —
Huduma Yenye Nguvu Na
Ufalme Wa Mungu
UFALME WA MUNGU UMEFAFANULIWA
Je! Unafikiri nini unaposikia maneno “ufalme wa Mungu?” Wakristo wengi
wanao ufahamu mdogo sana au hawana kabisa kuhusiana na “ufalme wa
Mungu”. Hii ni hatari, kwa sababu ufalme wa Mungu ni moja ya mambo
makubwa yaliyomo katika Agano Jipya. Ufahamu wa kutosha wa ufalme wa
Mungu ni muhimu sana kwa uinjilisti wenye nguvu.
Utawala wa Mungu
Tunapolifikiria neno “ufalme” katika maana hii ya Agano Jipya, tusifikirie
kuwa ni eneo fulani la kijeografia, bali tufikirie kama ni utawala au sehemu iliyo
chini ya mamlaka ya Mungu, au mamlaka yake juu ya uumbaji wake.
Tunaposema ufalme wa Mungu umekuja, tunamaanisha kwamba Mungu amekuja
kuuweka ufalme au utawala wake duniani.
Maneno Mawili ya Muhimu ya Ufalme
Ufalme wa Mungu unaweza kufikiriwa kuwa upo sasa na pia utakuja
baadaye. Ufalme umekuja na pia utakuja. Tunahitimisha wazo kwa namna hii:
anaandika Don Williams, “Ni kweli ufalme upo hapa, lakini haupo katika
ukamilifu wake. Wakristo waliookolewa basi, wanaishi katika ufalme uliopo na
unaokuja.”12
Sura Ya Tatu: Huduma Yenye Nguvu Na Ufalme Wa Mungu
13Peter Kuzmic, “Kingdom of God,” Dictionary of Pentecostal and
Charismatic Movements, (Grand Rapids: Zondervan Publishing House,
1988) uk. 523.
24
1. Kwa hiyo, ufalme wa Mungu tayari upo. Ulikuja katika na kwa kupitia
kazi ya Yesu Kristo (Lk 17:20-21). Baadaye ulikuja tena wakati Roho
Mtakatifu alipomwagwa katika siku ya Pentekoste (Mk.9:1; Mdo.1:8). Ilikuwa
ni kwa njia ya Pentekoste ambapo Yesu alihamishia huduma yake ya ufalme juu
ya kanisa. Peter Kuzmic anasema, “Watu sasa wanauteka (ufalme wa Mungu)
au unashikwa na wenye nguvu (Mt 11:12-13; Lk 16:16). Mapinduzi ya utawala
wa shetani tayari yamekwisha anza, na nguvu ya ufalme ujao iko tayari ikitenda
kazi katika ulimwengu wa sasa, na baraka za masihi zinapatikana kwa wale
wanaoitikia wito wake.”13
2. Lakini ufalme wa Mungu pia unakuja. Ufalme wa Mungu utakuja katika
utimilifu wake wakati wa kuja kwa Kristo mara ya pili (Ufu 11:15). Kwa hiyo
wakati ufalme wa Mungu umekwisha kuja na uvamizi dhidi ya ufalme shetani
tayari umeshaanza, kunabakia ufalme ujao juu ya nchi. Hili litatokea wakati
Mwana wa Adamu atakapokuja “katika nguvu na utukufu mwingi” (Mt 24:30),
kumshinda shetani na kuuweka utawala wake wa haki duniani.
Kweli hii (kweli ya kwamba ufalme wa Mungu umekwisha kuja, na tena
unakuja) inaeleza hali halisi ya maisha yetu ya sasa. Inaeleza vyote ushindi dhidi
ya shetani upande mmoja, na maendeleo ya mapambano dhidi yake upande wa
pili. Inaeleza kwa nini wengi leo wanapokea uponyaji ghafla wakati ambapo
wengine wengi wanabakia wagonjwa na wanafariki dunia. Inaeleza kwa nini
tuna nguvu dhidi ya mapepo, wakati shetani bado anaendelea kuwatawala watu
wengi katika maeneo mengi ya ulimwengu. Ufalme wa Mungu umekuja kwa
kiasi; ingawaje, siku moja utakuja katika utimilifu wake. Sasa tunazo nguvu na
mamlaka juu ya mapepo, lakini hatimaye nguvu zote za giza zitashindwa kabisa.
Sura Ya Tatu: Huduma Yenye Nguvu Na Ufalme Wa Mungu
14Kuzmic, uk. 522.
25
KUJA KWA UFALME WA MUNGU
Yesu Alikuja Kutangaza utawala wa Mungu
Ujumbe wa ufalme wa Mungu ulikuwa ni msingi wa mahubiri ya Yesu.
Sikiliza maneno yake:
Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia;
maana kwa sababu hiyo nalitumwa (Lk 4:43, mkazo wa mwandishi. Angalia pia: Mt
4:23; Mk 1:14-15; Lk 8:1, 9:11).
Kutokana na Peter Kuzmic, “Swala la ufalme wa Mungu linachukua sehemu
ya umuhimu sana katika mafundisho na utume wa Yesu. “Wazo hili kuu” la
Yesu, kama lilivyoitwa, ni kiini cha mahubiri na ufunguo wa kuielewa
huduma.”14
Yesu alianza huduma kwa kutangaza, “Wakati imetimia, na ufalme wa
Mungu umekaribia… ” (Mk 1:15; angalia pia Mt 3:1). Akianza huduma yake
namna hii, Yesu alikuwa akitangaza kuja kwa utawala wa Mungu duniani.
Alikuwa akisema kwamba ufalme wa Mungu umefika, na ya kwamba ulikuwa
sasa karibu na yeyote atakayetaka kuupokea. “Mwaka wa Bwana uliokubalika”
(Lk 4:19) umekuja. Mungu amekuja katika Yesu Kristo ili kurejesha kile
kilichokuwa chake, na kuleta baraka za mbinguni kwa mwanadamu aliyeko
duniani.
Katika vitabu vya injili, ufalme wa Mungu ulikuwa pia ni msingi wa
mahubiri ya mitume. Mahali popote ambapoYesu aliwapeleka kuhudumu,
aliwaelekeza kuhubiri ufalme wa Mungu na kudhihirisha nguvu yake (Mt 10:7;
Lk 9:2; 10:9, 11).
Kuja kwa Ufalme wa Mungu Kumeleta Vita
Mungu amekuja kwanza katika Kristo, na sasa katika kanisa lake, lililotiwa
nguvu na Roho Mtakatifu, ili kurejesha kile ambacho shetani amekiiba. Amekuja
kwa nguvu kurejesha kile ambacho kwa haki ni chake. Sasa kwa sababu ufalme
wa Mungu umekuja, mapambano yameanza. Shetani aliyewatawala watu
anapingwa vikali na Mungu, kwa hiyo vita kali imeanza. (Angalia Efe 6:12).
Sura Ya Tatu: Huduma Yenye Nguvu Na Ufalme Wa Mungu
26
Kuja kwa Ufalme wa Mungu ni kwa Nguvu
Wakati ufalme wa Mungu unapokuja, hauji kiwoga, wala hauji kwa
kujitetea—unakuja katika nguvu. Paulo alisema, “Kwa maana ufalme wa Mungu
hauwi katika neno, bali katika nguvu” (1Kor 4:20). Kwa kweli, ufalme wa
Mungu hauji katika njia nyingine yoyote. Kwa sababu ya upinzani wa kijeuri wa
shetani dhidi ya ufalme unaokuja, basi ufalme wa Mungu lazima usonge mbele
kwa nguvu. Mvamizi lazima atolewe kwa nguvu. Sikiliza maneno haya ya
Yesu:
Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha
kuwajilia. Ama, awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na
kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo
atakapoiteka nyumba yake” (Mt 12:28-29).
Hivyo, kanisa lazima litembee katika nguvu kama litahitaji kupeleka mbele
ufalme wa Mungu hapa duniani. Siku moja Yesu alizungumzia siku ambayo
wanafunzi wake watauona ufalme wa Mungu ukija katika nguvu:
Amin nawaambia, pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja
mauti kabisa, hata watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu (Mk 9:1).
Wanafunzi walikuwa wameuona ufalme wa Mungu ukitembea katika nguvu
katika huduma ya Yesu; hata hivyo, Yesu alipotoa tamko hili alikuwa
akizungumzia wakati ujao. Na wakati huo alioutaja utatokea wakati ujao lakini
pia ulio karibu. Utatokea kabla ya vifo vya kati ya wale waliokuwepo. Yesu
alikuwa akizungumzia siku ya Pentekoste wakati kanisa lake litakuwa limevikwa
uwezo utokao juu (Lk 24:49). Tunaweza kusema pia kwamba tunauona ufalme
wa Mungu ukija katika nguvu kila wakati tunapomuona mtu amejazwa au
kuguswa na Roho wa Mungu (Mdo 1:8).
Ishara ya Kuja kwa Ufalme
Kati ya vitu vingine, ishara, maajabu na miujiza vinashuhudia ya kwamba
ufalme wa Mungu upo hapa. Hiki ni kivuli kinachoonyesha ni vipi itakuwa
wakati ufalme wa Mungu utakapokuja katika utimilifu wake. Uponyaji leo ni
kivuli cha mwisho wa kuteseka na magonjwa (Ufu 21:4). Kutoa pepo ni ishara
ya uvamizi wa Mungu katika eneo la shetani na ni ishara ya kuharibiwa kabisa
kwa shetani Yesu atakaporudi (Ufu 20:10).
Katika kile kinachoitwa na wengi “sala ya Bwana,” Yesu alifundisha
Sura Ya Tatu: Huduma Yenye Nguvu Na Ufalme Wa Mungu
27
kwamba “Ufalme wako uje” (Mt 6:10), alikuwa akitufundisha kuomba hasa kwa
ajili ya vitu vitatu:
1. Tunatakiwa kuomba kwa ajili ya watu wapate kuokolewa. Ufalme wa
Mungu unakuja kwa mtu binafsi wakati anapokuwa amezaliwa mara ya pili.
Ndivyo Yesu alivyomaanisha aliposema, “...ufalme wa Mungu umo ndani yenu”
(Lk 17:21).
2. Tunatakiwa kuombea watu ili wapate kujazwa na Roho, wapone, na
wakombolewe na uonezi wa mapepo. Ufalme wa Mungu unakuja katika nguvu
wakati watu wanapojazwa na Roho au kuachiwa huru kwa nguvu za Mungu (Mt
12:28 na Lk11:20; Lk10:9).
3. Tunahitaji kuomba ili Yesu arudi tena (Ufu 22:20). Yesu atakapokuja
tena atamshinda shetani na kuusimamisha ufalme wake duniani. Ndipo Ufalme
wa Mungu utakuwa umekuja katika utimilifu wake.
KUHUBIRI INJILI YA UFALME WA MUNGU
Tumeitwa Kuihubiri Injili ya Ufalme
Yesu aliwatuma wanafunzi waende kuhubiri habari njema za ufalme.
Walitakiwa watangaze kwamba Mungu, kwa njia ya Kristo, amekuja
kuusimamisha ufalme wake. Sikiliza maneno yake:
Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kwa ushuhuda kwa
mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja (Mt 24:14).
Katika vitabu vinne vya injili Yesu alisema kuhusu ufalme wa Mungu, au
maneno yanayofanana , ufalme wa mbinguni, karibu mara 90. Katika siku
alizokuwepo baada ya kufufuka, kabla hajarudi mbinguni, tunaambiwa kwamba
alitumia siku 40 na wanafunzi wake “na kuyanena yaliyohusu ufalme wa Mungu”
(Mdo 1:3). Ni vitu gani ambavyo vilihusu ufalme wa Mungu ambavyo
alizungumzia? Kitu kimoja cha muhimu ambacho alizungumzia ilikuwa ni
kujazwa na Roho Mtakatifu (Mdo 1:4-5). Pia alizungumzia kushuhudia katika
nguvu za Roho (Mdo 1:8). Yesu aliwaagiza wanafunzi wake kuihubiri “injili
yaufalme wa Mungu.” Alipowatuma wale thenashara aliwapa maagizo
yafuatayo:
Sura Ya Tatu: Huduma Yenye Nguvu Na Ufalme Wa Mungu
28
Akawaita wale thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na
kuponya maradhi. Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kupoza
wagonjwa” (Lk 9:1-2, mkazo wa mwandishi).
Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, ufalme wa mbinguni umekaribia.
Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; Mmepata bure,
toeni bure (Mt 10:7-8).
Kwa wale sabini aliwapa agizo linalofanana:
Wapozeni wagonjwa waliomo, waambieni, ufalme wa Mungu umekaribia (Lk 10:9).
Kuhubiri kwa ufalme wa Mungu kuliendelea katika kitabu chote cha
Matendo ya mitume. Hapa tunaona kanisa likihubiri na kufundisha injili ya
ufalme. Wakati Filipo alipotelemkia Samaria tunasoma ya kuwa alimhubiri
Kristo (Mdo 8:5), alitenda miujiza (8:6), na “alihubiri habari njema za ufalme wa
Mungu na jina la Yesu Kristo” (8:12).
Katika Efeso Paulo alifundisha kwa muda wa miezi mitatu kuhusu ufalme wa
Mungu (Mdo 19:8; 20:25). Na katika Rumi “alihubiri habari za ufalme wa
Mungu na kufundisha mambo ya Bwana Yesu Kristo” (Mdo 28:30).
Injili ya Ufalme Imeelezwa
Je! Ni nini basi injili ya ufalme ambayo Yesu aliwatuma wao, na sisi pia
kuitangaza. Kumekuwa na ufafanuzi mwingi uliokwishatolewa kuhusu “injili ya
ufalme”. Watu kadha wenye kuchukulia maandiko ya Biblia kuwa yaliandikwa
kuhusu nyakati fulani fulani tu, wanafundisha kwamba injili ya ufalme siyo injili
hii tunayoihubiri leo, bali ni matangazo tu kuhusu kuja kwa Kristo ambayo
yatahubiriwa tu wakati wa dhiki kuu, baada ya kanisa kunyakuliwa. Jambo hili,
kwa kweli, siyo sahihi kwa sababu kama ilivyonukuliwa hapo juu, Yesu
alituagiza kuihubiri injili ya ufalme kabla ya kuja kwake tena (Mt 24:14). Paulo
ametuonya wazi ya kuwa tujihadhari na mtu awaye yote atakayekuja na kuihubiri
“injili nyingine” (Ga 1:6-9) kuliko ile aliyoihubiri yeye.
George Eldon Ladd anafafanua injili ya ufalme kuwa ni “Habari Njema za
ufalme wa Mungu.” Anaendelea kusema, “Injili ya Ufalme ni Injili ambayo
Sura Ya Tatu: Huduma Yenye Nguvu Na Ufalme Wa Mungu
15George Eldon Ladd, “The Gospel of the Kingdom,” Perspectives
on the World Christiam Movement, A Reader (Pasadena, CA: William
Carey Library, 1981), uk. 59.
16Tom Marshall, Foundations for a Healing Ministry, (West Sussex,
ENG: Sovereign World, 1988), uk. 51.
17Williams, uk. 139.
29
ilihubiriwa na mitume katika kanisa la kwanza.”15 Wakati hatutofautiani na
Ladd; tunapenda kuongezea tafsiri yake: Injili ya ufalme ni habari njema
zinazotangazwa kutumia njia zilezile ambazo Yesu na wanafunzi wake
walizitumia. Tom Marshall anatoa tafsiri hii nzuri kabisa ya injili ya ufalme:
“Injili ya ufalme,” anaandika, “ni Injili ya wokovu pamoja na nguvu za zamani
zijazo.”16
Yesu na kanisa la kwanza hawakutangaza tu kuhusu kuja kwa ufalme wa
Mungu, na kupinduliwa kwa ufalme wa shetani, bali pia walidhihirisha nguvu za
ulimwengu ujao kwa kuponya wagonjwa, kutoa pepo, na udhihirisho wa nguvu
za Roho Mtakatifu. Msikilize Yesu akizungumzia jinsi ufalme wa Mungu
utakavyosonga mbele:
Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema za
ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu (Lk 16:16).
Tangu siku za Yohana mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa
nguvu, nao wenye nguvu wauteka (Mt 11:12).
Sisi sio tu watangazaji wa ujumbe wa Yesu, bali pia ni waigizaji wa njia zake
na uthibitisho wa nguvu za ufalme. Don Williams anasema, “Endapo tutashika
agenda ya Yesu ya huduma, tutaomba upako wa nguvu za Mungu, ili tukiwa na
nguvu juu yetu tuweze kuwahubiri maskini, wafungwa kufunguliwa kwao,
vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza ‘mwaka wa
Bwana uliokubaliwa (Lk 4:18-19).”17
Yesu alipowatuma wale Thenashara, “Aliwapa nguvu na mamlaka juu ya
pepo wote na kuponya maradhi, akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu na
kupoza wagonjwa” (Lk 9:1-20). Baadaye alipowatuma wale sabini kutangaza
kuja kwa ufalme wa Mungu aliwaambia:
Sura Ya Tatu: Huduma Yenye Nguvu Na Ufalme Wa Mungu
30
Na mji wowote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula vilivyowekwa mbele
yenu; wapozeni wagonjwa waliomo, waambieni, ufalme wa Mungu umekaribia (Lk
10:8-9).
Hiyo ndiyo maana ya kuhubiri injili ya ufalme. Inamaanisha kuhubiri injili,
lakini inamaanisha pia kufanya hivyo katika nguvu na upako wa Roho Mtakatifu
na ishara zinazofuatana. Tumeitwa na Mungu na kupakwa mafuta na Roho wake
ili kufanya hivyo tu.
31
— Sura ya Nne —
Huduma Yenye Nguvu
Na Kuihubiri Injili
Mapambano dhidi ya nguvu za giza ni sehemu muhimu ya kuhubiri injili ya
kweli. Katika Sura ya 3, “Huduma yenye nguvu na ufalme wa Mungu,”
tulizungumzia kuhusu kuhubiri “injili ya ufalme wa Mungu.” Katika sura hii
tutalipanua somo la kuhubiri injili na jinsi linavyohusiana na mapambano dhidi
ya nguvu za giza. Somo mathubuti kuhusu huduma ya Yesu na mitume
linathibitisha ya kuwa mapambano dhidi ya nguvu za giza ilikuwa sehemu ya
muhimu katika huduma zote mbili. Mapambano dhidi ya nguvu za giza mara
nyingi yaliambatana (au kutanguliwa) na mahubiri ya ujumbe wa injili.
Ushuhuda wenye nguvu kuhusu kweli ya ujumbe wao ulikuwa ndiyo matokeo,
pamoja na watu wengi waliokuwa wakiokolewa.
KUTENDA NA KUTANGAZA: SEHEMU MBILI ZA MUHIMU ZA
USHUHUDA MADHUBUTI WA INJILI
Sehemu mbili madhubuti za ushuhuda wa injili ni kudhihirika kwa utendaji
na kutangaza. Kwa kutangaza tuna maana ya kuihubiri injili. Kwa utendaji tuna
maana ishara, maajabu, na miujiza iliyofuatia mahubiri ya injili. Nguvu ya injili
lazima kwanza ithihirishwe, halafu ndipo kweli inaweza kuhubiriwa. Hii ni
“Kuonyesha na kusema” katika hali yake ya juu. Nguvu za giza lazima kwanza
zishindwe, ndipo ushindi unapoweza kutangazwa.
Kuyafanya Mambo ya Kwanza kuwa ya Kwanza
Katika Mathayo 12:28-29 Yesu alitufundisha ya kwamba lazima mara nyingi
tupambane vita vya kiroho kabla ya injili haijahubiriwa kikamilifu. Sikiliza
maneno yake:
Sura ya Nne: Huduma Yenye Nguvu Na Kuihubiri Injili
32
Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha
kuwajilia. Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na
kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo
atakapoiteka nyumba yake (mkazo wa mwandishi).
Yesu anasema ya kuwa ni muhimu kuyafanya “mambo ya kwanza kuwa ya
kwanza” katika kuihubiri injili. Kwanza, “tunamfunga mtu mwenye nguvu,”
NDIPO “tunaiteka nyumba yake.” Mtu mwenye nguvu katika habari hii ni pepo
kwenye nguvu anayetawala au maisha ya mtu binafsi, au jamii au eneo la mahali
fulani. “Nyumba yake” ni mahali alipoiweka ngome yake. “Vyombo vyake”
inawakilisha Roho ya mhusika, au roho za watu katika jamii au eneo la mahali
fulani ambapo shetani amewaweka watu hao katika hali ya utumwa.
MTU MWENYE NGUVU wa Mathayo 12:28-29
Anapomtawala Mtu Anapotawala jamii au eneo la mahali
fulani
Mtu mwenye Nguvu Pepo mwenye nguvu
anamtawala mtu
Pepo mwenye nguvu akitawala jamii
au eneo la mahali
Nyumba ya mtu
Mwenye Nguvu
mtu chini ya utawala wa pepo Jamii au eneo la mahali chini ya
utawala wa pepo
Vyombo vya mtu
mwenye Nguvu
Roho ya mtu Roho za watu wa jamii fulani au eneo
la mahali fulani
Yesu anatuambia ya kuwa kabla ya kuteka nyumba ya mtu mwenye nguvu
na kuvichukua vyombo vyake, maana yake, kabla hatujampokonya roho za watu
anaowashikilia mateka, lazima tupambane naye na kumshinda. Ninaamini ya
kwamba, ishara ambayo Yesu amewaahidi wale wanaotimiza agizo kuu ni
kwamba “watatoa pepo” (Mk 16:17). Mpangilio wa kwanza wa kazi ni
kuzishinda nguvu za mapepo, ndipo tunaweza kutangaza kwa uhuru wokovu kwa
wale walioshikiliwa mateka.
Nguvu Nyingi!
Kama tulivyokwisha kuona katika sura ya 1, Kristo amekwisha kutupatia
Sura ya Nne: Huduma Yenye Nguvu Na Kuihubiri Injili
33
zana zote zinazotakiwa kuimaliza kazi. Zana mbili alizotupatia ni Roho
mtakatifu na injili. Njia isiyoshindwa katika kutoa ushuhuda wa injili yenye
nguvu na ushawishi ni ifuatayo:
Nguvu za Nguvu Matokeo
Roho Mtakatifu + ya njili = ya Ajabu
Hebu kwa kifupi tuchunguze zana moja moja kati ya hizo.
1. Nguvu ya Roho Mtakatifu. Kwanza, Kristo ametupatia nguvu za Roho
Mtakatifu. Katika Matendo 1:8 Yesu alituahidi ya kwamba tutapokea nguvu
akiisha kutujilia Roho Mtakatifu. Kwa hiyo ni muhimu kwa yeyote yule
anayetegemea kuhusika na kuishuhudia injili kuwa amejazwa na Roho Mtakatifu
(angalia sura ya 6, “ubatizo wa Roho Mtakatifu na huduma yenye nguvu” kwa
utimilifu wa somo hili). Siyo tu lazima tujazwe na Roho, bali ni lazima pia tujue
jinsi ya kuzitumia nguvu hizo za Roho Mtakatifu katika huduma .
(Tutalizungumzia jambo hili baadaye).
2. NGUVU ZAIDI ... Nguvu ya Injili. Tena, Kristo ametupatia injili. Hivyo
ni muhimu sana tuwe na ufahamu mzuri wa nguvu hizo na kujua jinsi ya
kuitumia vema injili. Katika Rumi 1:15-16 Paulo ameeleza uhakika wake katika
injili:
Kwa hiyo upande wangu mimi ni tayari kuihubiri injili hata na kwenu ninyi mnaokaa
Rumi. Kwa maana siionei haya injili, kwa sababu ni uweza wa Mungu uletao
wokovu, kwa kila aaminiye....
Tazama jinsi Paulo anavyoieleza injili ya kwamba “ni uweza wa Mungu
uletao wokovu.” Tena katika Rumi 10:17 Paulo anatuambia ya kwamba injili
inayo ndani yake nguvu inayoumba imani katika maisha ya wale wanaoisikia:
“Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.”
Kwa kuangalia vizuri maana katika mtiririko wa kifungu hicho cha maandiko
ya Paulo, utagundua ya kwamba anazungumzia hasa injili. Anasema ya kwamba
injili , ujumbe wa Kristo, inayo nguvu kubwa ya kuleta imani katika mioyo ya
wasikiao!
Sura ya Nne: Huduma Yenye Nguvu Na Kuihubiri Injili
34
Yesu katika kuzungumzia nguvu hii iletayo imani katika mfano wa kumea
mbegu (Mk 4:26-29). Hapa anafananisha injili na mbegu:
Akasema, ‘ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya
nchi; akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikamea na kukua
asivyojua yeye, maana nchi huzaa yenyewe… (Mistari 26-28a).
Kama mbegu, injili ina nguvu ndani yake ya kutoa mavuno. Jinsi ilivyo na
nguvu injili ya Yesu! Kama tu tutaitangaza, ina nguvu ndani yake yenyewe ya
kutoa mavuno.
Lakini ni nini hasa maana ya kuhubiri injili hii ambayo tunazungumzia? Ni
kuhubiri “neno la Kristo!” (Rum 10:17). Ni ujumbe wa Yesu na yale yote
aliyoyatenda, Yote anayoyatenda, na yote yale atakayoyatenda baadaye. Katikati
ya ujumbe huu wa injili ni kifo, kuzikwa na kufufuka kwa Kristo (soma kwa
uangalifu: 1Kor 15:1-4). Tusije tukashindwa kuhubiri ujumbe wenye nguvu.
Mara nyingi wale wanaoitwa “wahubiri wa injili” wanahubiri sehemu ndogo tu
ya injili ya Yesu. Sisi tusishindwe kuhubiri habari njema za Yesu kwa ujasiri,
kwa sababu ni habari hizo tu ambazo zinazo nguvu ya Mungu iwaleteayo watu
wokovu (1Kor 1:18).
3. SAWA SAWA NA ... Matokeo ya Ajabu. Kama kwa uaminifu
tutachanganya zana hizo mbili—nguvu ya Roho Mtakatifu na Nguvu ya Injili—
tunaweza kutegemea matokeo ya ajabu. Hili ndilo lililotokea katika kanisa la
kwanza katika kitabu cha Matendo ya mitume.
Tunaweza kufuatilia ukuaji wa ajabu wa kanisa la Agano Jipya kupitia
mistari kadha katika kitabu cha Matendo ya mitume. Litakuwa ni zoezi la
kufurahisha na la faida kwako kusoma na kuiwekea alama mistari ifuatayo katika
Biblia yako. Unaposoma, tambua jinsi kanisa lilivyokua kutoka waumini 120
hadi maelfu kwa muda mfupi. Tambua pia jinsi ambavyo ukuaji huo wa ajabu
ulivyoletwa kwa kuchanganya nguvu ya Roho Mtakatifu na uaminifu katika
kuihubiri injili.
Ukuaji wa Kanisa la Kwanza katika Kitabu cha
Matendo ya Mitume
----------------------------------------------------
Matendo 1:15; 2:41; 2:47; 4:4; 5:14; 6:1; 6:7; 8:6; 9:35; 9:42; 11:21; 11:24;
11:26; 12:24; 13:49; 14:1; 14:21; 16:5; 17:4; 19:18; 19:20; 19:26
Sura ya Nne: Huduma Yenye Nguvu Na Kuihubiri Injili
35
MAPAMBANO DHIDI YA NGUVU ZA GIZA YALIVYOONEKANA
KATIKA HUDUMA YA YESU NA KANISA LA KWANZA
Yalivyoonekana Katika Mahubiri na Mafundisho ya Yesu
Katika huduma yake Yesu alichanganya kufundisha na kuhubiri injili na
uthibitisho wa nguvu za Roho Mtakatifu (angalia Mt 4:23 na 9:35). Hii
ilisababisha makundi makubwa kuja kusikiliza ujumbe wake na kumfuata (Mt
4:24-25; 9:36).
Katika kuwaagiza (Mk 3:13-15) na baadaye kuwatuma wale thenashara (Lk
9:1-2), na katika kuwatuma wale sabini, Yesu aliwawezesha na kuwaelekeza
kutoa pepo, kuponya wagonjwa, na kuihubiri injili ya ufalme (Lk 10:9).
Hatimaye akitoa agizo kuu la kuhubiri injili ulimwenguni pote, Yesu aliahidi
uwezo wa kimungu ambao ungekuja tu kwa njia ya kujazwa na Roho Mtakatifu.
(Soma kwa uangalifu Mk 16:17-18; Lk 24:48-49; Yn 22:21-22; Mdo 1:8).
B. Yalivyoonekana Katika Mahubiri na Mafundisho ya Kanisa la Kwanza
1. Katika Matendo ya Mitume. Katika Matendo ya mitume, tunaona
waziwazi namna ya kushuhudia. Kanisa la kwanza nyakati zote walichanganya
mahubiri ya injili na udhihirisho wa nguvu za Roho Mtakatifu. Ingawa namna
hiyo ya huduma inaonekana katika kitabu kizima cha Matendo ya mitume,
nitanukuu mifano minne tu kati yake:
a. Pentekoste. Mfano wetu wa kwanza ulitokea siku ya Pentekoste (Mdo 2:1-
41). Hapa kulianzia na matendo makuu ya nguvu za Mungu. Maelfu ya watu
walioingia katika nyua za hekalu ili kuabudu siku ile hawakuwa na wazo wala
hamu ya kusikiliza mahubiri ya wafuasi wa Yesu. Lakini ghafla wakasikia
kutoka mbinguni “uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi” (mstari
2). Katika mshangao wao, waliona “zimewatokea ndimi zilizogawanyika kama
ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao” (mstari 3); ndipo wakawasikia wale
120 wakianza “kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka”
(mstari 4).
Wakati ule ule, “mabadiliko ya imani” makubwa yakatendeka katika mioyo
ya wale walioshuhudia matendo makuu ya nguvu za Mungu na uwepo wake.
Kwa sababu ya miujiza walioishuhudia, mtazamo wao mzima ukawa umebadilika
ghafla. Hawakuwa tena wapitaji wasio na hamu na mambo ya wafuasi wa Yesu;
bali walikuwa sasa washiriki wa mkutano ule wakiwa tayari kuamini na kuipokea
injili. Petro aliposimama kuhubiri, walikuwa tayari wanayo hamu na yale
Sura ya Nne: Huduma Yenye Nguvu Na Kuihubiri Injili
36
aliyotaka kusema. Na, Petro alipomaliza mahubiri yake,watu 3,000 waliitikia.
“Mabadiliko ya imani” wakati wa Pentekoste
Watu kabla ya Watu baada ya
muujiza wa muujiza wa
Pentekoste Pentekoste
Hawakuwa na .....>.....>.....>.....>.....>.....>......>.....>......>......>.....> Walikuwa tayari
hamu Mabadiliko ya Imani kuamini
b. Mlango mzuri. Mfano wetu wa pili ulitokea muda mfupi tu baadaye. Tena
tunaona mitume wakifuata namna ile ile ya kuchanganya udhihirisho wa nguvu
za Roho Mtakatifu na mahubiri ya wazi ya injili ya Kristo. Hii ilitokea kwenye
ingilio la hekalu liitwalo Mlango Mzuri (Mdo 3:1-4:4). Matokeo ya udhihirisho
wa nguvu ya Mungu, mtu aliyezaliwa kiwete anaponywa, kundi lile lile ambalo
awali halikuwa na nia ya kuwasikiliza wafuasi wa Yesu, kwa mara nyingine tena
“imani yao inazidi kubadilishwa.” Ghafla “wakajaa ushangao
wakastaajabia...[na] wakawakusanyikia mbio wakishangaa sana” (3:10-11). Kwa
mara nyingine tena Petro alisimama na kuhubiri injili ya Kristo, matokea yake
yalikuwa kwamba wengi walisikia na kuamini ujumbe wake “Na hesabu ya watu
waume ikawa kama elfu tano” (4:4).
c. Filipo katika Samaria. Tunaona mtiririko huo huo— muunganiko kati ya
utendaji wa nguvu za Roho Mtakatifu na kuhubiriwa kwa injili kukiendelea
katika huduma ya Filipo katika Matendo 8:1-7. Maandiko matakatifu yanasema
ya kuwa “Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, akawahubiri Kristo”
(mstari 5). Pamoja na kuhubiri injili, pia alidhihirisha nguvu za Mungu: “Na
makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo na
walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya” (mstari 6). Ishara hizo za
kimiujiza zilikuwa kutoa pepo, na uponywaji wa wengi waliopooza na viwete.
Matokeo yalikuwaje? Makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale
yaliyosemwa (mstari 6); “...walipomwamini Filipo akihubiri habari njema za
ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo” (mstari 12); na “..ikawa furaha kuu
katika mji ule” (mstari 8).
d. Paulo katika Lystra. Mfano wa mwisho wa namna ambavyo kanisa la
Sura ya Nne: Huduma Yenye Nguvu Na Kuihubiri Injili
37
kwanza lilivyochanganya utendaji wa matendo ya nguvu za Roho Mtakatifu na
mahubiri ya injili unapatikana katika huduma pa Paulo katika mji wa Galatia wa
Lystra (Mdo 14:8-10):
Na huko Lystra palikuwa na mtu mmoja, dhaifu wa miguu, kiwete tangu tumboni
mwa mamaye, ambaye hajaenda kabisa. Mtu huyo alimsikia Paulo alipokuwa
akinena; ambaye alimkazia macho na kuona ya kuwa ana imani ya kuponywa,
akasema kwa sauti kuu, simama kwa miguu yako sawasawa. Akasimama upesi
akaenda.
Kama katika sehemu zote katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Paulo
alitumia nafasi hii kuhubiri ujumbe wa injili (angalia mistari 7; 15-17).
Ikiwa tutahitaji kuona matokeo yale yale katika huduma za Agano Jipya,
lazima basi tutumie mifano hii kama changamoto kwa huduma zetu za uinjilisti.
2. Katika mafundisho ya Paulo. Si tu kwamba tunaona utendaji na mahubiri
vikiwa vimeonyeshwa katika huduma ya Yesu na mitume hapo mwanzo, pia
tunaona mafundisho ya wazi katika barua za Paulo. Katika barua yake ya
kwanza kwa kanisa la Korintho, Paulo, akizungumzia kuhusu mambo katika
huduma yake aliyokuwa ameyafanya katikati yao anaandika,
Maana niliazimu nisijue neno lolote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa. . ..
Neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye
kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, ili imani yenu
isijengwe katika hekima za wanadamu, bali katika nguvu za Mungu” (1Kor 2:2-5,
mkazo wa mwandishi).
Wakati alipokuwa na Wakorintho, huduma ya Paulo ilikuwa na msingi wa
vitu viwili: ujumbe wa “Yesu Kristo aliyesulibiwa,” na “udhihirisho wa nguvu
za Roho.” Katika 2Wkorintho 12:12 aliwakumbusha ya kwamba, alipokuwa nao,
“kweli ishara za mtume -- ishara, maajabu na miujiza -- vilitendwa katikati [yao].
. ..” Katika 1Wakorintho 14:23-26 Paulo analieleza kanisa kuwa litegemee
udhihirisho wa nguvu na uwepo wa Roho wakutanikapo. Alipokuwa akielezea
huduma yake kwa Warumi, Paulo aliwakumbusha ya kuwa huduma yake ilikuwa
na ishara zilizokuwa na udhihirisho wa nguvu za Roho:
Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yangu, mataifa wapate
kutii, kwa neno au kwa tendo—kwa nguvu za ishara na maajabu, katika nguvu za
Roho Mtakatifu; hata ikawa tangu Yerusalemu, na kando kando yake mpaka Iliriko
Sura ya Nne: Huduma Yenye Nguvu Na Kuihubiri Injili
38
nimekwisha kuihubiri injili ya Kristo kwa utimilifu” (Rum 15:18-20, mkazo wangu).
Tambua ya kwamba ujumbe wa Paulo ulikuwa na vyote “yale niliyonena na
kutenda.” Alitenda “ishara na miujiza kwa njia ya nguvu za Roho Mtakatifu,”
na pia “aliihubiri injili ya Kristo kwa utimilifu.”
Hatimaye, katika 1Wathesalonike 1:5 Paulo anawakumbusha Wathesalonike
jinsi injili ilivyowafikia:
Injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali katika nguvu, na katika Roho
Mtakatifu na uthibitifu mwingi.
Tena tunaona namna ile ile ya kuihubiri injili pamoja na utendaji wa nguvu
za Roho, vikileta majibu ya dhahiri na ya kudumu—ambayo ni kanisa la
Thesalonike lenyewe.
MWISHO
Tumeonyesha katika sura hii ya kuwa kuna mambo muhimu mawili katika
huduma ya kweli ya injili ya Kristo. Moja ni udhihirisho wa nguvu za Roho wa
Mungu; na lingine ni kuihubiri injili kwa uwazi. Endapo tutahitaji ushuhuda
wetu kuwa na manufaa, lazima pia tujifunze kutumia njia zilezile ambazo Yesu
na mitume walizitumia.
39
— Kifungu Cha II —
Matayarisho Ya Huduma
Yenye Nguvu
40
41
— Sura ya Tano —
Mambo Ya Muhimu Katika
Matayarisho Ya Huduma
Yenye Nguvu
Katika somo letu la huduma yenye nguvu, sasa tunaanza Kifungu cha II,
“Matayarisho ya Huduma Yenye Nguvu.” Yeyote anayehitaji kuhusika katika
huduma ya uinjilisti wenye nguvu lazima atilie maanani chanzo cha maelekezo
ya huduma yake na matayarisho yake yenyewe. Katika somo hili tutaangalia
mambo yote mawili. Tutajibu maswali yafuatayo: “Je! Ni mambo gani muhimu
katika huduma ya mapambano dhidi ya nguvu za giza? Na “Je ni matayarisho
gani yanahitajika ili kuwa na huduma madhubuti na yenye nguvu?”
MAMBO MUHIMU KATIKA HUDUMA YENYE NGUVU
Yako mambo mengi ambayo yanahusika na ujenzi wa huduma yenye nguvu
katika maisha ya mtenda kazi wa Kristo. Katika somo hili tutashughulikia
mambo matano ambayo tunafikiria ya kwamba ni ya muhimu.
Upako
Jambo la kwanza la muhimu katika huduma ya mapambano dhidi ya nguvu
za giza ni upako. Neno upako tinamaanisha uwepo wa Roho Mtakatifu unaokuja
kukaa juu ya mkristo aliyekwisha kujazwa na Roho mtakatifu anapokuwa yuko
katika huduma. Ipo mifano mingi katika Biblia inayohusu upako. Upako wa
Roho Mtakatifu ulimjia Petro wakati yeye na Yohana walipoitwa mbele ya
baraza la wakubwa na wazee na waandishi ili kueleza tendo lao la kumponya mtu
kiwete na kuhubiri injili katika ua wa hekalu sehemu iliyoitwa tao la Sulemani:
Sura ya Tano: Mambo Ya Muhimu Katika Matayarisho Ya Huduma Yenye Nguvu
18Don Stamps, Full Life Study Bible, New Testament (Deerfield FL:
Life Publishers, 1990), tazama Matendo 4:8 uk. 236.
42
Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia… (Mdo 4:8. Mkazo wa
mwandishi).
Angalia sehemu ya sentensi “akijaa Roho Mtakatifu.” Hii haikuwa mwanzo
wa kujazwa Roho Mtakatifu kwa Petro kule kulikomjia siku ya Pentekoste. Hii
ilikuwa ni uwepo wa Roho Mtakatifu aliyempaka upako ili azungumze katika
nguvu za Roho. Ilikuwa ni utimilifu wa unabii wa Yesu katika Luka 12:11-12.
Mfasiri wa Biblia Don Stamps anaandika kuhusiana na mstari huo: “Petro
alipokea ujazo mpya wa Roho Mtakatifu uliomletea uvuvio mpya, hekima na
ujasiri ambao kwa njia ya huo aliweza kuihubiri kweli ya Mungu.”18 Hivi ndivyo
tunavyomaanisha tunapozungumzia kuhusu upako.
Baadaye siku hiyo hiyo, Petro na Yohana waliporudi kutoa ripoti, upako wa
Roho Mtakatifu ukaja juu ya kikundi chote wakati walipokuwa wakiomba:
Hata walipokwisha kumuomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa,
wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri (Mdo 4:31,
mkazo wa mwandishi).
Tena wote walijazwa na, au kupakwa na Roho Mtakatifu. Hakuna wasiwasi
ya kwamba huo ni upako wa Roho Mtakatifu unaozungumzwa katika mistari
miwili ya baadaye:
Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi na neema
nyingi ikawa juu yao wote (Mdo 4:33, mkazo wa mwandishi).
“Neema nyingi [ikawa] juu yao wote,” ikaleta matokeo ya “nguvu nyingi,”
jambo ambalo kwa mara nyingine lilikuwa ni upako wa Roho Mtakatifu.
Stefano alikuwa ni mtu “aliyejaa imani na Roho Mtakatifu” (Mdo 6:5).
Katika Matendo 6 tunasoma kuhusu yeye kuwa amepakwa na Roho Mtakatifu:
Sura ya Tano: Mambo Ya Muhimu Katika Matayarisho Ya Huduma Yenye Nguvu
19Hugh Jeter, By His Stripes (Springfield, MO: Gospel Publishing
House, 1977), Uk. 173.
43
Na Stefano akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa
katikati ya watu … lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho
aliyesema naye (mistari 8, 10, mkazo wa mwandishi).
Watu waliweza hata kuuona upako wa Roho Mtakatifu usoni mwake alipokuwa
akinena:
Watu wote walioketi katika ile baraza wakamkazia macho yao wakamwona uso wake
kuwa kama uso wa malaika (Mdo 6:15).
Ilikuwa ni upako wa Roho Mtakatifu uliomjia Paulo katika kisiwa cha Kipro
akimdhihirishia hukumu ya Mungu ambayo ilikuwa imwangukie Elima, mchawi.
Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho,
akasema, ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa ibilisi, adui wa haki yote,
huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? Basi angalia mkono wa Bwana u juu
yako, nawe utakuwa kipofu, usione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na
kiza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza
(Mdo 13:9-11, mkazo wa mwandishi).
Kama mtu akihitaji kuhudumu katika nguvu za Roho Mtakatifu kama wale
wakristo wa kanisa la kwanza, yeye pia lazima ajifunze kutembea katika Roho
na kuwa tayari kujitoa na kutii maongozo ya Roho kama vile anavyotaka.
Imani
Imani ni kiungo kingine cha muhimu katika huduma yenye nguvu. Imani
imefafanuliwa katika njia nyingi. “Imani katika Kristo,” anasema mmisionari
mkongwe Hugh Jeter, “ni ujasiri katika Kristo. Ni kuamini ya kuwa yeye ndiye
kama anavyosema mwenyewe, na atafanya yale anayosema atafanya … Imani
yaweza kuwa mfu. Lakini imani nyakati zote hutenda kazi.”19 “Imani,” anasema
mwandishi mwingine “inamaanisha kwamba umeamini kile ambacho Mungu
ameahidi, na kile unachoomba, ni chako, na kwamba umekipokea, (hata kabla
Sura ya Tano: Mambo Ya Muhimu Katika Matayarisho Ya Huduma Yenye Nguvu
20T. L. Osborn, How to Receive Miracle Healing (Nairobi: Evangel
Publishing House, 1955), uk. 169.
44
hujakipokea, hata kabla hujakiona au kukipapasa).”20 Kwa makusudi yetu
tutafafanua imani kama uwezekano wa kumwamini Mungu kwa ajili ya miujiza.
Imani ya jinsi hiyo huangalia kwa Mungu bila kuchoka ili atimize neno lake kwa
ishara. Imani ya jinsi hiyo imeonyeshwa katika ujasiri wa Petro wakati,
akimuona Yesu akitembea juu ya maji, alimwita,
Bwana ikiwa ni wewe niamuru nije kwako juu ya maji. Akasema, njoo. Petro
akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu (Mt
14:28-29).
Imani ya jinsi hii ilikuwa ni ule uchu wa Petro na Yohana wakati
walipomwambia yule mtu mbele ya Mlango Mzuri “tuangalie” (Mdo 3:4).
Walikuwa na kitu alichohitaji, na walikuwa na uchu wa kukitoa! Mtu anayehitaji
kutumiwa katika huduma yenye nguvu lazima, kama Roho anavyoongoza,
ahudumu katika nguvu ya upako wa Roho Mtakatifu.
Ujasiri
Ujasiri ni kujitoa, kuwa tayari, kudiriki kuchukua hatua ya imani, hata kama
kudiriki kuchukua hatua hiyo ya imani kwaweza kuleta kushindwa na kuadhirika.
Ujasiri wa jinsi hiyo umeonyeshwa katika huduma ya Paulo, wakati kule Lystra
alidiriki kufanya kitendo ambacho kingeweza kumletea kushindwa na kuadhirika.
Wakati alipokuwa akihubiri mbele ya kusanyiko la watu, Paulo alihisi moyoni
mwake ya kwamba mtu mmoja kiwete, ambaye alikuwa hajawahi kutembea,
alikuwa na imani ya kupona. Paulo akalia kwa sauti kuu, “Simama kwa miguu
yako sawasawa, akasimama upesi akaenda” (Mdo 14:10).
Je! Ingekuwaje kama mtu huyu asingetembea? Paulo angeweza kuadhirika,
na huduma yake labda ingeweza kuishia Lystra. Hata hivyo, Paulo alikuwa jasiri
wa imani, alikuwa tayari kudiriki kushindwa, matokeo yake uamsho mkubwa
ukatokea katika mji ule. Ujasiri wa jinsi hiyo unaweza kuja tu kutokana na
kujitoa kwa Mungu, imani kuu katika neno lake na kujazwa na Roho Mtakatifu
(Mdo 4:31).
Huduma yenye nguvu inahusisha sana uchukuaji wa hatua za jinsi hiyo.
Sura ya Tano: Mambo Ya Muhimu Katika Matayarisho Ya Huduma Yenye Nguvu
45
Hatupewi uhakika kila wakati tunapoombea wagonjwa kuponywa au kila
tunapokutana na mapambano dhidi ya nguvu za mapepo. Wale ambao kila
wakati wanapenda kujiokoa na fedheha “kwa kujilinda” hawataweza kuwa na
huduma madhubuti na yenye nguvu. Mafanikio yatakuja tu kwa wale
watakaoamua kutenda kwa imani na ujasiri.
Kuongozwa na Roho Mtakatifu
Kuongozwa na Roho Mtakatifu ni jambo la nne muhimu katika huduma
yenye nguvu. Kabla mtu hajahudumu kwa nguvu katika jambo lolote lazima
kwanza apambanue mapenzi ya Mungu katika jambo hilo, akitambua ya kuwa
Mungu hawezi kulibariki jambo lolote lililo nje ya mapenzi yake. Mhudumu wa
Kipentekoste ni lazima nyakati zote ajiulize, “Je! Ni nini mapenzi ya Mungu
katika jambo hili? Je! Mungu anahitaji atembee kwa namna gani? Je! Anafanya
nini? Na Je nawezaje kujipanga sambamba na mapenzi yake?
Yesu mfano wetu mkuu katika huduma, nyakati zote alifanya mapenzi ya
Baba yake. Kamwe hakuhudumu kwa mapenzi yake mwenyewe, bali nyakati
zote alifuata mapenzi ya Baba yake wa mbinguni kwa njia ya Roho Mtakatifu
aliyemjaza. Kwa uangalifu jaribu kufikiria kuhusu mambo yafuatayo katika
huduma ya Yesu:
Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda,
kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo mwana vile vile. Kwa maana
Baba anampenda mwana, naye humwonyesha yote ayatendayo mwenyewe; hata na
kazi kubwa zaidi kuliko hizo atamwonyesha (Yn 5:15-20).
Sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha (Yn 8:28).
Kwa sababu mimi sineni kwa nafsi yangu tu, bali Baba aliyenipeleka, yeye
mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema… . basi hayo ninenayo mimi
kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo (Yn 12:49-50, mkazo wa mwandishi).
Je! Umeona jinsi ambavyo Yesu alisema tu na kufanya yale ambayo Baba
alimwambia kusema au kuyafanya. Siku moja kando ya birika iitwayo Kiebrania
Bethzatha, jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala… . vipofu, viwete, nao
waliopooza (Yn 5:4). Yesu alimponya mmoja wao (mstari 8). Je! Alimchaguaje
huyo tu kumponya? Kutokana na rekodi (Yn 5:19-20), Yesu alimchagua huyo
kwa sababu alikuwa akifuata maelekezo ya Baba yake wa mbinguni. Katika
Roho alimwona alichokuwa akifanya Baba yake, na akafanya hivyo hivyo. Hiyo
Sura ya Tano: Mambo Ya Muhimu Katika Matayarisho Ya Huduma Yenye Nguvu
46
ilikuwa ndiyo siri ya huduma yake kubwa ya uponyaji.
Kama nasi, kama Yesu, tutahitaji kuhudumu katika nguvu, lazima sisi pia
tusikilize sauti ya Baba na tupambanue kwa uhakika ni nini anachokifanya? Ni
nani anayetaka kumponya? Ni kwa jinsi gani anataka kumponya? Ni nini
mwitikio wangu katika Roho katika jambo hili. Haya ndiyo maswali ambayo
lazima yaulizwe na kujibiwa kama tutataka kuhudumu katika nguvu. Maswali
haya yanaweza tu kujibiwa na Baba mwenyewe kwa njia ya Roho aliyetupa.
Mtu mmoja amesema, “Huduma ya nguvu ni nyepesi. Unalohitaji kulitenda
ni kuisikia sauti ya Mungu na kuitii;” Hii ni kweli. Mara tukigundua Baba
anafanya nini, linakuwa ni jambo la kujipanga na mipango yake. Tutajadili
habari ya kuongozwa na Roho Mtakatifu zaidi katika Sura ya 7, “Kuongozwa na
Roho Mtakatifu na Huduma yenye nguvu.”
Unyenyekevu
Unyenyekevu ni uwezo wa kujiona kama vile Mungu atuonavyo, yaani
kujiona kama vile tulivyo. Hili ni jambo la tano muhimu ambalo ni kiungo
muhimu na cha mafanikio katika huduma yenye nguvu. Paulo anazungumzia hali
hiyo katika Rum 12:3 asemapo, “Usinie makuu kupita inavyokupasa kunia, bali
uwe na nia ya kiasi.…”
Anawataka waumini waishi maisha ya unyenyekevu, yaliyo
huru na kiburi, kule kujiona mtu wa maana: “Msitende neno lolote kwa
kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu
mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake” (Fil 2:3).
Anayamalizia mafundisho yake kuhusu unyenyekevu anaposema, “Iweni na
nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu. . ..” (Fil
2:5). Ndipo anapoendelea kuelezea tabia ya Yesu ambayo haikuwa na ubinafsi
kabisa:
Ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa
sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho. Bali alijifanya kuwa hana
utukufu, akatwaa namna ya utumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena
alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti,
naam, mauti ya msalaba!” (Fil 2:6-8).
Hali hiyo ya unyenyekevu ni jambo la muhimu la tano la huduma yenye nguvu.
Jinsi mioyo yetu ilivyovunjwa tena na tena katika miaka hii yote tumekuwa
Sura ya Tano: Mambo Ya Muhimu Katika Matayarisho Ya Huduma Yenye Nguvu
47
tukiona janga linalohusu watu ambao, kwanza walitumika na Mungu kwa namna
kubwa, wakianguka kwa ajili ya roho ya kiburi. Wakisahau maonyo ya wazi ya
maandiko, walianza kujiona na kujifikiria wenyewe kwa hali ya juu na hatimaye
kuanguka kutokana na uzito wa kiburi chao. Ni kweli “Kiburi hutangulia
maanguko” (Mith 16:18).
Nafikiria hakuna namna ya huduma ya Kikristo iliyojaa majaribu ya kiburi
kuliko huduma yenye nguvu. Nguvu inalewesha, na ni rahisi kwa mtumishi
anayetumiwa sana na Mungu kulewa na kile afikiriacho kuwa ni nguvu na
mafanikio yake mwenyewe. Na ni mara nyingi watu wanakuwepo
kumhakikishia umaarufu wake. Kwa kuiona miujiza aifanyayo, watu hufurahia
kumheshimu kama vile ni mungu mdogo “wametushukia kwa mfano wa
wanadamu!” (Mdo 14:11). Fedha na nafasi ya heshima huja kirahisi, na mara
huanza kufikiria na kuamini kwamba baraka za Mungu ni kwa ajili yake.
Mtumishi huyo huwa tayari kwa anguko kubwa.
Kuna sababu ya pili ambayo huwa ni sababu ya kuanguka kwa wengine.
Maanguko haya kuwa siyo kwa ajili ya mafanikio ya huduma yenye nguvu, bali
hutokea kwa kukosa mafanikio hayo. Kwa sababu wengine wanatamani mno
kutumiwa na Mungu kwa namna kubwa au kwa sababu wanatamani sana kule
kuonekana na watu kama watumishi wenye nguvu kubwa wanaighoshi kweli.
Nyakati nyingine wanaanza kuinakili miujiza au kufanya mambo zaidi ya
maandiko. Wanakuwa wako tayari kuridhika na jambo ambalo siyo halisi badala
ya, kwa unyenyekevu kumtegemea Mungu kwa matendo ya kweli. Jinsi
inavyohuzunisha na ilivyo janga kubwa.
Katika kuhudumu katika huduma yenye nguvu, tusije tukasahau ya kwamba
nguvu yote ni ya Mungu na hivyo utukufu wote. Wakati wale sabini na wawili
waliporudi kutoka kwenye huduma, walitoa ripoti kwa Yesu, “Bwana hata pepo
wanatutii kwa jina lako” (Lk 10:17). Yesu alifurahi pamoja nao. Halafu
akawapa onyo “Lakini msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa
sababu majina yenu yameandikwa mbinguni” (Mstari 20). Alikuwa
anawaambia, “Msijiinue kwa yale mliyoyatenda kwa ajili ya Mungu, bali furahini
kwa yale Mungu aliyowatendea.” Unyenyekevu ni jambo muhimu kwa huduma
yoyote ambayo itadumu katika miujiza.
Sura ya Tano: Mambo Ya Muhimu Katika Matayarisho Ya Huduma Yenye Nguvu
48
MATAYARISHO YA HUDUMA YENYE NGUVU
Sasa tuangalie matayarisho ya binafsi kwa ajili ya huduma yenye nguvu.
Kuna mambo matano hasa ambayo mtu lazima ayaangalie wakati wa maandalizi
binafsi kwa ajili ya uinjilisti wenye nguvu.
Chunguza Nia Yako
Kwanza kabisa katika maandalizi ya huduma yenye nguvu mtu lazima
ajichunguze mwenyewe ni kwa nini anataka kujihusisha na huduma ya jinsi hiyo.
Jambo tulitendalo kwa ajili ya Mungu ni muhimu sana; kwa nini tunalitenda ni
muhimu tena zaidi. Lazima tuwe na uhakika kuhusu nia zetu katika kutaka
kutumika na Mungu katika huduma ya uinjilisti wenye nguvu. Katika Matendo,
sura ya 8, Simoni yule mchawi aliitaka huduma yenye nguvu, lakini nia yake ya
ndani haikuwa nzuri. Alitamani sana aonekane kuwa ni mtu mwenye nguvu, hata
akawa yuko tayari kununua kwa gharama kipawa hicho. Petro akitambua nia
zake mbaya, alimkemea akimwambia, “Huna fungu wala huna sehemu katika
jambo hili, kwa kuwa sio moyo wako si mnyofu mbele za Mungu” (Mdo 8:21).
Je! Ni wangapi leo pia wanahitaji huduma ya nguvu kutokana na nia mbaya?
Je! Ni nia gani mbaya au nzuri katika kutaka kujihusisha na huduma yenye
nguvu? Nia mbaya ni pamoja na kiburi, tamaa ya kujinufaisha na kujiendeleza
na hitaji la kutumia nguvu juu ya watu. Nia nzuri katika kutaka kujihusisha na
huduma yenye nguvu ni pamoja na shauku ya kumtukuza Mungu, upendo na
shauku ya kutaka kuwasaidia watu, na nia ya kuendeleza ufalme wa Mungu
duniani.
Imarisha Uhusiano wako na Mungu
Jambo la pili ambalo mtumishi anahitaji alifanye katika matayarisho kwa ajili
ya huduma ya miujiza ni kuimarisha uhusiano wake na Mungu. Lazima atambue
kwamba anaweza tu kuhudumu kwa uhakika kutokana na uhusiano mzuri na
Mungu. Lazima atambue ya kwamba kamwe huduma yake haitaweza kuwa na
nguvu kuliko mshikamano alionao na Mungu. Kama tulivyokwisha kuona awali
katika sura hii, Yesu mwenyewe alihudumu kutokana na uhusiano wake na Baba.
Je! Unakumbuka Yesu alisemaje? “Kwa kuwa Baba ampenda mwana, naye
humwonyesha yote ayatendayo” (Yn 5:20). Ilitokana na uhusiano huu wa
upendo na Baba yake kwamba huduma ya Yesu ilitendeka. Katika hali hiyo
hiyo, manabii walihudumu kutokana na ushirika wao na Yesu, na pia na Baba,
kwa kuwa Biblia yasema kwamba watu “wakawatambua ya kwamba walikuwa
Sura ya Tano: Mambo Ya Muhimu Katika Matayarisho Ya Huduma Yenye Nguvu
49
pamoja na Yesu” (Mdo 4:13). Endapo unatamani kutumika na Mungu katika
huduma ya uinjilisti wenye nguvu, wewe pia, kama Yesu na mitume, lazima
utumie muda wa kutosha kuimarisha uhusiano wako na Mungu kwa njia ya
maombi, kusoma maandiko na kuyatafakari, na kujitoa kabisa ili kufuata mapenzi
yake.
Ongeza Ufahamu Wako
Njia ya tatu ya kujiandaa binafsi kwa ajili ya huduma ya miujiza ni kuongeza
ufahamu wako kuhusu somo hili. Kusoma na kuitumia misingi iliyomo katika
kitabu hiki ni njia ya kwanza nzuri katika kuongeza ufahamu, lakini hii ni
mwanzo tu. Hapa kuna njia nyingine ambazo unaweza kuongeza ufahamu
kuhusu huduma ya kimaandiko yenye nguvu.
1) Kutoka katika Agano Jipya soma na kusoma tena vitabu vya Injili na
Matendo ya mitume. Mwandishi huyu anaweza kushuhudia kutokana na ujuzi
wake binafsi kuhusu jambo hili ya kwamba, ukamilifu wa kusoma kimpangilio,
kusoma tena na tena, kwa vitabu hivi kunaweza kabisa kuyabadilisha maisha
yako. Kumefanya hivyo kwake. Wakati mmoja mhudumu mkongwe aliyekuwa
akitumika sana katika huduma za uponyaji na kutoa pepo aliulizwa na mtumishi
kijana, “Je! Unaweza kunielekeza vitabu vyovyote vizuri katika somo la
uponyaji?” “Ndio” alijibu yule mzee, “Naweza kukuelekeza vitabu vinne vya
ajabu sana.” Kusikia hivyo yule kijana alitoa karatasi na kalamu tayari kuandika.
“Je! Ni vipi hivyo vitabu vinne vya ajabu?” aliuliza, “Lazima nivipate.” Mhubiri
yule mkongwe alijibu, “Mathayo, Marko, Luka na Yohana.” Fanya mazoezi ya
kusoma na kusoma tena vitabu vinne vya Injili na Matendo ya mitume, wakati
wote ukijiuliza maswali kama, “Je! Yesu na mitume walihudumu vipi katika
nguvu? Je! Waliwaponyaje wagonjwa na kutoa pepo? Ni nini ilikuwa siri ya
mafanikio yao? Je! Ninawezaje kuiga maisha na huduma zao?”
2) Pia unaweza kusoma vitabu ambavyo vina masomo ya jinsi hiyo
vilivyoandikwa na watumishi wa Mungu wengine mashuhuri. Lakini angalia:
Siyo kila kitabu kilichoandikwa kuhusu somo hili kina misingi sahihi ya Biblia,
wala si kwamba waandishi wote wa vitabu vya jinsi hiyo ni watumishi wenye sifa
njema na heshima.
Utii
Nne, lazima ujiandae kwa ajili ya huduma yenye nguvu kwa kutii na kufuata
mapenzi ya Mungu. Yesu alijitiisha mwenyewe chini ya mapenzi ya Baba yake
wa mbinguni, na akapokea baraka za Baba yake. Sisi pia, kama tutahitaji
Sura ya Tano: Mambo Ya Muhimu Katika Matayarisho Ya Huduma Yenye Nguvu
50
kupokea baraka za Mungu, lazima tutii na tujitiishe wenyewe chini ya mapenzi
yake. Lazima tusisahau:Mungu atatoa upako kwa mipango yake tu, pia ameahidi
kulithibitisha neno lake kwa ishara zifuatanazo nalo (Mk 16:15-20).
Pata Uzoefu
Hatimate, endapo unahitaji kuhusika na huduma ya uinjilisti yenye nguvu,
lazima upate uzoefu -- wote wa kiroho na wa kiutendaji.
1. Uzoefu wa kiroho. Uzoefu wa kiroho lazima uhusishe kuzaliwa mara ya
pili (Yn 3:3-7). Biblia inatuambia habari ya watu waliojaribu kufanya huduma
yenye nguvu pasipo kuwa wamezaliwa mara ya pili:
Baadhi ya wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja
jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu wakisema, ‘Nawaapisha
kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja
Skewa, myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu,
akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu
aliyepagawa pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata
wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa. (Mdo 19:13-16)
Habari hii na iwe kama onyo kwa wale wanaotaka kujihusisha na huduma yenye
nguvu pasipo kuzaliwa mara ya pili.
Pia, ili kuhudumu katika nguvu mtu lazima ajazwe na Roho kama
walivyokuwa wale mitume wa karne ya kwanza (Mdo 2:4). Ubatizo wa Roho
Mtakatifu ulikuwa ndiyo chimbuko la nguvu ya ajabu ya kiroho katika kanisa la
Matendo, na unabakia kuwa chanzo cha kiroho kwetu pia. Tutajadili kuhusu
utendaji wa nguvu hii katika sura ya 6, “Roho Mtakatifu na huduma yenye
nguvu.”
2. Uzoefu wa kiutendaji. Kama ilivyo katika kazi yoyote, ujuzi katika
huduma ya nguvu hupatikana kwa kupitia uzoefu wa kiutendaji. Mtu anayehitaji
kuwa mzoefu katika eneo la huduma hii, lazima afanye hivyo kwa kupitia
mazoezi halisi ya kiutendaji. Uzoefu huu unapatikana kwa ubora zaidi, kwa
kufanya na mhudumu mwenye uzoefu. Hivi ndivyo wale thenashara, chini ya
uongozi wa Yesu, walivyopata uzoefu. Jinsi tunavyojihusisha katika huduma
yenye nguvu na kujizoeza katika vyote, mafanikio na kushindwa, tunajifunza
zaidi kuwa wahudumu hodari wa Kristo.
51
MWISHO
Kama hitimisho, yeyote anayetaka kutumika katika huduma yenye nguvu
lazima atilie maanani kweli kweli kuhusu matayarisho yake binafsi. Asisahau ya
kuwa tunahudumu, si kwa njia ya nguvu zetu, bali kutokana na nguvu zitokazo
kwa Mungu.
52
21Don Stamps, “Baptism in the Holy Spirit,” Full Life Study Bible
New Testament, uk. 228.
53
— Sura ya Sita —
Roho Mtakatifu Na
Huduma Yenye
Nguvu
Kabla mtu hajahusika na huduma yenye nguvu, ni lazima afahamu na
abatizwe na Roho Mtakatifu. Hii ni kawaida kwa wakristo (wote katika Agano
Jipya na pia leo), na ndiyo chanzo cha nguvu za kiroho katika maisha ya mtu na
katika huduma. Katika somo hili tutaangalia swala hili. Pia tutaangalia karama
za Roho Mtakatifu jinsi zinavyohusiana na huduma yenye nguvu.
UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU NA
HUDUMA YENYE NGUVU
Ubatizo wa Roho Mtakatifu Umefafanuliwa
Tunaweza kusema mambo mengi kuhusu kufafanua maana ya ubatizo wa
Roho Mtakatifu; hata hivyo, tutataja mambo matano tu:
1. Lengu kuu la utume wa Kristo duniani. Kulingana na mfafanuzi wa Biblia,
Don Stamps, “moja ya lengo kuu la huduma ya Yesu duniani lilikuwa ni
kuwabatiza wafuasi wake katika Roho Mtakatifu.”21 Kutokea mwanzo mpango
wa Yesu haukuwa tu kupata wafuasi, ili kuwa na kundi lionekanalo mbele za
watu. Mpango wake ulikuwa kuushinda ulimwengu, kwa kutumia watu
waliofundishwa vema na kupewa zana. Zana hizo ni Roho Mtakatifu. Yohana
Mbatizaji mwanzoni mwa huduma ya Yesu alisema, “Yeye ambaye utamwona
Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu”
(Yn 1:33). Kwa hiyo kutokea mwanzo Yesu aliamua kuwabatiza wafuasi wake
Sura ya Sita: Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
54
kwa Roho Mtakatifu. Lilikuwa ndilo lengo la huduma yake.
2. Kuzamishwa na kujazwa na Roho Mtakatifu. Ubatizo wa Roho Mtakatifu
unaweza kuelezwa kuwa ni kuzamishwa, na kujazwa, na Roho Mtakatifu.
Katika Matendo 1:4-5 Yesu aliita kitendo cha ubatizo ni kuzamishwa katika
Roho Mtakatifu:
Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalem, bali waingoje ahadi
ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu; ya kwamba Yohana alibatiza kwa
maji, bali ninyi mtabatizwa na [kuzamishwa ndani ya] Roho Mtakatifu (mkazo wa
mwandishi).
Siku kumi baadaye, siku ya Pentekoste, Roho akaja. Biblia inasema ya kwamba
wote wakajazwa Roho Mtakatifu:
Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho
alivyowajalia kutamka (Mdo 2:4, mkazo wa mwandishi).
Kama chombo kilicho wazi kinaweza wakati huo huo, kuzamishwa na
kujazwa na maji, ndivyo ilivyokuwa kwa wakristo hao siku ya Pentekoste. Na
ndivyo inavyoweza kuwa kwa watu wote wa Mungu.
3. Utendaji wa Roho Mtakatifu katika kumbatiza mtu ni tofauti na ni pekee
na kule kumzaa mtu upya kiroho. Ubatizo wa Roho Mtakatifu hautendeki wakati
sambamba na wokovu kama watu kadha wanavyotaka tuamini. Ni utendaji wa
tofauti na pekee kutoka kile kitendo cha awali cha wokovu. Kama vile wale
thenashara walivyookoka kwanza (Yn 20:22), na baadaye wakajazwa na Roho
Mtakatifu (Mdo 2:4). Pia kama watu wa Samaria walivyookoka kwanza (Mdo
8:12, 14), na baadaye “wakampokea Roho Mtakatifu” (Mdo 8:17), ndivyo ilivyo
kwetu leo. Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni utendaji wa Roho Mtakatifu katika
maisha ya mkristo tofauti na pekee na kuzaliwa mara ya pili.
Je! Umezaliwa mara ya pili? Je! Wewe u mwana wa Mungu? Kama ndivyo,
basi unaweza kutafuta kujazwa na Roho Mtakatifu kama ilivyokuwa kwa
wakristo wa kanisa la karne ya kwanza.
4. Kuvikwa uweza utokao juu. Katika Luka 24:49 Yesu alielezea ubatizo
katika Roho Mtakatifu kama “kuvikwa” na nguvu kutoka juu: “Na tazama
nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe
uweza utokao juu.”
Picha Yesu anayoionyesha hapa ni ile ya mtu anayevikwa na nguvu za
Mungu, na akiisha kuvikwa, yuko tayari kufanya kazi ya Mungu. Yesu aliahidi
Sura ya Sita: Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
55
wazi nguvu kama hiyo kwa wafuasi wake baada ya Roho Mtakatifu kuwajilia juu
yao. “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia Roho Mtakatifu juu yenu” (Mdo
1:8). Neno la kiyunani hapa lililotafsiriwa “kuwajilia juu yenu” (eperchomai) ni
neno lilelile lililotumika katika Luka 1:35 likielezea Roho Mtakatifu kuja juu ya
Maria kabla ya kuzaliwa Yesu: “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu
zake aliye juu zitakufunika” (Lk 1:35).
Ni wazi maana yake hapa, kama katika Matendo 1:8 ni ya kuzungukwa
kabisa, nakuzingirwa kabisa kwa nguvu za Mungu. Ndivyo inavyotokea kwa
mkristo aliyebatizwa katika Roho Mtakatifu.
5. Ahadi ya wakristo wote walioamini. Kila mkristo aliyezaliwa mara ya pili,
anaweza na anatakiwa kubatizwa katika Roho Mtakatifu. Kuhusu wale 120
waliokusanyika siku ya Pentekoste, Biblia inasema “wote walijazwa Roho
Mtakatifu.” Haisemi ya kuwa 119 walijazwa, na mmoja hakujazwa. Inasema
wote walijazwa.
Kutokea mwanzo Mungu alitaka tuyafahamu mapenzi yake kuhusu swala la
kubatizwa na Roho Mtakatifu. Ni mapenzi yake kuwa kila mtu aliyeamini
ajazwe na Roho Mtakatifu. Petro aliweka jambo hili wazi aliposimama siku ya
Pentekoste akasema kuhusu “Karama ya Roho Mtakatifu”: “Kwa kuwa ahadi hii
ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali na kwa
wale watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie” (Mdo 2:39).
Kwa hiyo ahadi ya ubatizo katika Roho Mtakatifu, na nguvu ambazo
zinaletwa na ubatizo huo, ni kwa “wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu
wamjie.” Hii inamaanisha, rafiki yangu, kuwa ahadi hiyo ni kwa ajili yako pia.
Je! Unaweza kumwita Bwana leo, na kumuomba akujaze na Roho wake
Mtakatifu?
Umuhimu wa Ubatizo wa Roho Mtakatifu Katika Huduma yenye Nguvu
Hata kama ni jambo la wazi, lakini tutalisema hata hivyo: Kabala ya kuingia
katika huduma ya uinjilisti wenye nguvu, ni lazima kujazwa na nguvu za Roho
Mtakatifu. Ujazo huo wa nguvu huja kwa njia ya ubatizo katika Roho Mtakatifu
ambao tumekuwa tukijadili (angalia Mdo 1:8). Umuhimu wa jambo hili katika
huduma yenye nguvu umeonyeshwa katika njia mbili:
1. Ubatizo katika Roho Mtakatifu ni agizo katika maandiko. Kwanza,
umuhimu wa ubatizo katika Roho Mtakatifu ni jambo dhahiri kwa sababu ni
agizo kutokana na maandiko. Katika barua yake kwa wakristo wa Efeso, Paulo
anawaagiza waumini hao maagizo mawili. Tunategemea kuyatii yote: “Tena
msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho” (Efe 5:18).
Katika agizo lake la mwisho kwa wanafunzi wake kabla ya kupaa kwake
Sura ya Sita: Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
56
kwenda mbinguni, Yesu aliwaagiza kujazwa na Roho, (Mdo 1:4-5). Wakati wa
siku zake arobaini baada ya kufufuka, Yesu aliwaagiza wafuasi wake wasianze
kushuhudia watu hadi watakapokuwa wamebatizwa katika Roho Mtakatifu (Lk
24:49; Mdo 1:4, 5, 8). Yesu alielewa wazi ya kwamba huduma aliyowaitia
wanafunzi wake ilikuwa ni kubwa kuliko uwezo wa kibinadamu. Walihitajika
wasithubutu kuifanya kwa nguvu zao wenyewe. Lazima kwanza “wavikwe na
uweza utokao juu.”
Jambo hilo ni kweli hata leo. Kabla hatujajaribu kuingia katika huduma
yoyote, zaidi huduma yenye nguvu, sisi pia lazima tujazwe nguvu za Roho
Mtakatifu. Tutakuwa ni wajinga endapo tutawaza vinginevyo!
2. Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni chimbuko letu la nguvu. Umuhimu wa
ubatizo wa Roho Mtakatifu katika huduma ya nguvu pia unadhihirika kwa sababu
Roho Mtakatifu ni chimbuko letu la nguvu za huduma ya jinsi hiyo. Ilikuwa
hivyo kwa wote, Yesu na kanisa la kwanza, na ndivyo ilivyo kwetu leo.
Nguvu ya Yesu kwa ajili ya huduma ilikuja kwa ajili ya upako wa Roho
Mtakatifu. Upako huo kwanza ulitokea wakati wa ubatizo wake katika mto
Yordani (Lk 4:22). Ilikuwa hadi baada ya kupakwa mafuta na Roho Mtakatifu
ndipo alipoingia katika huduma yake ya umasihi. Sikiliza maneno haya ya
mtume Petro kuhusu huduma ya Yesu:
Habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na
nguvu; naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote
walioonewa na ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye (Mdo 10:38).
Ingawa tunaamini kwa uthabiti ya kwamba Yesu alikuwa, na hakuisha kuwa
mwana wa Mungu wa milele, pia tunajua ya kwamba alipokuwepo hapa duniani,
aliamua kuhudumu chini ya upako wa Roho Mtakatifu. Alifanya hivi ili aweke
ramani ya huduma kwa ajili yetu kuifuata.
Ni muhimu kutambua ya kwamba Yesu hakuweza kumponya hata mgonjwa
mmoja, hakutoa hata pepo mmoja, wala hakufanya muujiza wowote hadi
alipokwisha kupakwa mafuta ya Roho Mtakatifu wakati wa ubatizo wake. Hata
hivyo, baada ya upako wake na Roho, mara moja alianza kuhudumu sehemu
mbalimbali katika nguvu. Usomaji wa uangalifu wa mistari ifuatayo kutoka
katika injili ya Luka utaelezea kwa wazi jambo hili: Lk 4:1-2; 4:14; 18:21, 5:17;
6:19. Kama upako huo wa Roho ulikuwa ni wa muhimu kwa Yesu katika
kuitenda huduma yake, si zaidi utakuwa ni wa muhimu kwetu pia leo!
Ni wazi pia kutokana na usomaji wa kitabu cha Matendo, ya kwamba ubatizo
wa Roho Mtakatifu ulikuwa ni msingi wa huduma ya kanisa la Agano Jipya.
Sura ya Sita: Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
57
Kitabu hiki cha Agano Jipya kinarudia tena na tena kusisitiza ya kuwa ubatizo
wa Roho Mtakatifu ni zawadi ya Mungu kwa kanisa. Zawadi hii imetolewa kwa
kanisa ili lipate kuiendeleza kazi ya Yesu na ili kanisa tilimize utume wake wa
kupeleka injili hadi miisho ya nchi (Mdo 1:8).
Karibu sehemu kama sita katika Matendo tunaambiwa kuhusu watu
kubatizwa, au kujazwa na Roho (Mdo 2:4; 4:33; 8:17; 9:17-18; 10:44-46; 19:6).
Matendo makuu ya nguvu za Mungu yaliambatana na kumwagwa huko kwa
Roho Mtakatifu na matokeo yake kuingizwa kwa idadi kubwa ya watu katika
ufalme wa Mungu. Pia tunaona katika Matendo ya kwamba upako uliofuatana
na vitendo hivyo vya kubatizwa na Roho ilikuwa ndiyo chanzo cha nguvu ya
miujiza katika kanisa. Ilikuwa ni baada ya kumwaga kwa Roho (Mdo 4:31)
kwamba tunapata rekodi hii, “Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake
Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote” (Mdo 4:33).
Kwa hiyo, unaona ya kuwa Roho Mtakatifu alikuwa chanzo cha nguvu kote
katika huduma ya Yesu na ya kanisa la Agano Jipya. Kwa walrostp wa kitabu
cha Matendo ya mitume nguvu hii ilikuwa ni matokeo ya kubatizwa kwa Roho
Mtakatifu. Nguvu kama hiyo ingalipo leo pia kwetu endapo sisi pia tutajazwa
na Roho.
Je! Unawezaje Kupokea Roho Mtakatifu Leo
Katika sehemu hii ya somo letu swali linaibuka, “Je! ni kwa jinsi gani
tunaweza kubatizwa na Roho Mtakatifu leo:” Ni matumaini yetu ya kwamba
baada ya kusoma maelekezo haya rahisi, utapokea karama iliyoahidiwa ya Roho
Mtakatifu.
1. Masharti ya upokeaji wa Roho Mtakatifu. Yako masharti mawili muhimu
kabla mtu hajabatizwa na Roho Mtakatifu. Kabla mtu hajajazwa na Roho
Mtakatifu (1) ni lazima awe amezaliwa mara ya pili kweli kweli, na (2) ni lazima
yeye mwenyewe awe na shauku ya kujazwa na Roho.
a. Kuzaliwa upya. Biblia inafundisha waziwazi ya kwamba kabla mtu
hajabatizwa na Roho Mtakatifu ni lazima awe amezaliwa mara ya pili. Yesu
mwenyewe alituambia “ulimwengu hauwezi kumpokea” Roho wa kweli, yaani,
Roho Mtakatifu, “kwa kuwa haumwoni wala haumtambui” (Yn 14:17). Ni wale
tu ambao kweli wamezaliwa kwa Roho wa Mungu (Yn 3:5-17) ndio wanaoweza
kumpokea Roho Mtakatifu. Jambo hili linahusu imani binafsi katika Yesu Kristo
kama mwokozi, kujitoa na kutumainia kabisa mapenzi ya Mungu na toba,
ambayo ni kule kugeuka kutokana na jambo lolote linalomuudhi Mungu. Je!
Umezaliwa mara ya pili kweli kweli? Kama bado, kwa nini usimgeukie Kristo
sasa hivi katika imani na toba.
Sura ya Sita: Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
58
b. Shauku ya kujazwa. Sharti la pili muhimu kabla ya kubatizwa na Roho
Mtakatifu ni ile shauku ya kujazwa. Yesu alisema, “Heri wenye njaa na kiu ya
haki, maana hao watashibishwa” (Mt 5:6). Watashibishwa na nini?
Watashibishwa na haki ya Mungu ambayo huja kwa utakaso wa Roho mtakatifu
(1Kor 6:11, Rum 16:15). Ili kujazwa na Roho mtu ni lazima awe na shauku na
Mungu kuliko vitu vyote. Yesu bado anatuita, “Mtu akiona kiu, na aje kwangu
anywe. . .” (Yn 7:37). Je! Unayo kiu kwa ajili ya Mungu? Kama ndivyo, basi
umekutana na jambo la pili muhimu kabla ya kujazwa Roho Mtakatifu.
2. Jinsi unavyoweza kumpokea Roho Mtakatifu. Sasa, kama utahitaji kujazwa
na Roho Mtakatifu, fanya mambo haya matatu:
a. Mwombe Mungu ili ujazwe na Roho Mtakatifu leo. Yesu amekwisha
kutupatia ahadi ya ajabu ya kumpokea Roho. Sikiliza manene yake: “kwa kuwa
kila aombaye hupewa!” (Lk.11:10). Je! Umesikia tamko hilo? Kila aombaye
hupewa. Sasa sikiliza maneno haya tena:
Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vilivyo vyema,
Je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao!
(Mstari 13).
Je! Unahitaji Mungu akujaze na Roho Mtakatifu? Mwombe tu sasa; Yeye
yuko tayari kukujaza leo.
b. Karibia “kiti cha neema” kwa ujasiri. Ujapo kujazwa na Roho Mtakatifu
yakubidi ukaribie kiti cha neema kwa ujasiri. Maandiko yanatuambia, “basi na
tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri” (Ebr 4:16). Tunaweza kuja mbele za
Mungu bila woga tukiwa tumejaa ujasiri kwa sababu tunajua ya kuwa tunakuja
sawa sawa na mapenzi yake. Unapokuja kujazwa na Roho Mtakatifu, uje kwa
ujasiri ukifahamu ya kuwa Mungu anakukaribisha katika uwepo wake.
c. Msifu Mungu kwa imani yenye tumaini. Sasa anza kumsifu Mungu kwa
moyo wako wote, na ufanyapo hivyo tegemea ya kwamba atakujaza kwa Roho
Mtakatifu. Hili ndilo wale 120 walilofanya kabla ya siku ya Pentekoste. Biblia
inasema, “Nao walikuwa daima ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu” (Lk 24:53).
Waangaliaji walipoona ya kuwa wale 120 wamejazwa Roho katika siku ya
Pentekoste, waliwasikia wakimsifu Mungu katika lugha zao, sikiliza maneno yao:
“tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu!” (Mdo
2:11). Unatakiwa kufanya vile vile kama mitume wa kwanza. Msifu Mungu kwa
moyo wote. Unapomsifu, fanya hivyo kwa imani yenye matumaini.
Unapoendelea kumuabudu, tegemea ya kuwa Mungu atatimiza ahadi yake.
Mtegemee kukujaza na Roho Mtakatifu. Na utegemee kunena kwa lugha kama
Sura ya Sita: Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
22Kuna ishara nyingine nyingi au matokeo ya kujazwa na Roho wa
Mungu. Hapa tunataja zile tu zinazohusiana moja kwa moja na huduma
yenye nguvu.
59
Roho atakavyokuwezesha!
3. Ushahidi wa Kubatizwa kwa Roho Mtakatifu. Ukiisha tu kujazwa na Roho
hutakuwa kamwe mtu yule yule tena. Tegemea ishara nyingine kufuatia kujazwa
kwako.
a. Ishara ya kwanza. Ishara ya kwanza ya kujazwa kwako na Roho Mtakatifu
itakuwa ni kunena kwa lugha nyingine kama Roho atakavyokuwezesha (Mdo
2:4). Hii ilikuwa ndio ishara iliyotokea mara kwa mara kwa waumini katika
kitabu cha Matendo, na ndiyo “ishara ya awali” ya kubatizwa na Roho Mtakatifu.
Soma mwenyewe Biblia katika Matendo ya mitume 2:1-4; 10:47-47; na 19:1-6.
Utajua wazi utakapojazwa na Roho, kwa sababu utaanza kunena kwa lugha
nyingine!
b. Ushahidi mwingine wa kimaandiko unaohusiana na huduma yenye nguvu.
Jinsi unavyoendelea kujifunza kutembea katika Roho ishara za namna nyingi
zitafuata. Chini nimeandika namna nane zinazohusiana na huduma ya uinjilisti
wenye nguvu:22
• Nguvu ya kuwa shahidi (Mdo 1:8)
• Ujasiri (Mdo 2:14-41; 4:31)
• Nguvu ya kufanya kazi za Yesu (Yn 14:16; 16:14)
• Udhihirisho wa huduma mbalimbali za Roho (1Kor 12:1-11)
• Kuongezeka kwa hisia kutambua dhambi zinazomhuzunisha Roho
Mtakatifu (Yn 16:7-11)
• Shauku kubwa na uwezo wa kuomba na kuombea
wengine (Rum 8:26-29)
• Kuongezeka kwa ufahamu wa kutambua uwepo wa
Mungu katika maisha (Yn 14:16-18)
• Upendo mkuu kwa Mungu na kwa watu (Rum 5:5).
KARAMA ZA ROHO NA HUDUMA YENYE NGUVU
Ufahamu sahihi wa karama za rohoni na hasa karama tisa za rohoni (au
“udhihirisho wa Roho”) zilizoorodheshwa katika 1Kor 12:8-10 ni muhimu kwa
Sura ya Sita: Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
60
huduma yenye nguvu. Tutatoa dibaji fupi kwa ajili ya karama hizo na sehemu
yake katika huduma yenye nguvu.
Karama za Roho Zimefafanuliwa
Karama za Roho zimefafanuliwa katika njia mbalimbali. Kwa ajili ya kusudi
letu tutatumia maelezo yafuatayo: Karama za Roho ni upako wa kimiujiza
waliopewa wakristo waliojazwa Roho Mtakatifu ili kulitimiza kusudi la Baba.
Hebu tuchukue muda mfupi kuchunguza ufafanuzi wa sentensi hii kipengele kwa
kipengele.
Kwanza, tumesema karama za Roho ni “ upako wa kimiujiza.” Kwa hili tuna
maana ya kuwa karama za Roho zina chimbuko, si katika uwezo wa
mwanadamu, bali katika Roho wa Mungu. Huja kama “upako”. Kwa maneno
mengine zinatenndeka chini ya upako wa Roho Mtakatifu, na karama zinatolewa
wakati Roho anapotembea juu ya mtu aliyejitoa maisha yake kwa Bwana.
Pia tulisema katika ufafanuzi wetu, ya kwamba karama za Roho “zinapewa
kwa wakristo waliojazwa na Roho Mtakatifu.” Hizi ni “karama,” kwa hiyo
zinatolewa si kwa ushindi au tuzo fulani, bali kama utoaji tu wa neema ya Mungu
ya bure. Tusemapo zinatolewa, hatuna maana ya kwamba zinatolewa kama mali
ya kuhodhi binafsi bali tuna maana zinatolewa kwa watu binafsi ili kutimiza
mahitaji kadha wa kadha kulingana na kazi ya Mungu. Zinatolewa kupitia
wakristo “waliojazwa na Roho”. Kwa kusema wakristo waliojazwa na Roho tuna
maana wale waliobatizwa na Roho Mtakatifu (Mdo 2:4) na wanaendelea
kutembea “katika Roho” (Ga 5:25).
Ufafanuzi wetu pia unasema ya kwamba karama za Roho zinatolewa “na
Roho Mtakatifu.” Ni Roho Mtakatifu ndiye mtoaji wa karama hizi (1Kor 12:4-6),
na zinatenda kazi, si kutokana na mapenzi ya mtu, bali kutokana na mapenzi ya
Roho (1Kor 12:11). Sababu ambayo karama zinatolewa na Mungu si kwa ajili
ya kutimiza mipango na mapenzi ya mtu yeyote. Zinatolewa ili “kutimiza
mapenzi ya Baba” na kuendeleza ufalme wake duniani.
Karama za Roho zimetambuliwa
Sasa tutaangalia kwa karibu katika 1Wakorintho 12:7-10 na tutazitambua zile
“karama” tisa za Roho zilizoorodheshwa. Wakati tukitambua ya kwamba kuna
orodha nne zingine za karama za Roho katika barua za Paulo (kama Rum 12:6-8;
1Kor 12:28; 1Kor 12:29-30, Efe 4:11), pia tunaamini ya kwamba karama hizi tisa
zina sehemu ya kipekee kabisa katika huduma ya uinjilisti wenye nguvu. Hebu
na tuangalie basi karama hizi:
Sura ya Sita: Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
23Karama hii ingeweza kuitwa “kazi za nguvu” au kwa Kiebrania
(Greek: energemata dunameon) “utendaji wa kazi za nguvu.”
61
Karama Tisa za Roho (1Kor.12:7-11)
1. Karama za Mafunuo
(Zimetolewa ili kutambua mawazo ya Mungu)
• Neno la Maarifa ufunuo wa kimuujiza wa ufahamu wa Mungu
• Neno la Hekima ufunuo wa kimuujiza wa hekima ya Mungu
• Kupambanua Roho ufunuo wa kimuujiza wa kutambua ni roho gani
anayejidhihirisha au ni roho gani aliye nyuma ya tendo
fulani.
2. Karama Unabii
(Zimetolewa ili kuyanena maneno ya Mungu)
• Karama ya Unabii kunena kwa muujiza ujumbe utokao kwa Mungu
katika lugha ijulikanayo na mzungumzaji.
• Karama ya aina za kunena kwa muujiza ujumbe au sala
Lugha kutoka kwa Mungu katika lugha isiyoeleweka na
mzungumzaji.
• Karama ya Tafsiri kunena kwa muujiza maana ya
za Lugha ujumbe uliotolewa kwa lugha.
3. Karama za Nguvu
(Zimetolewa ili kuzitenda kazi za Mungu)
• Karama za uponyaji wa magonjwa kimiujiza
Kuponya
• Karama ya msukumo wa kimuujiza wa imani ili
Imani kuitimiza kazi fulani ambayo inakuwa
imetolewa na Mungu
• Karama ya tokeo la nguvu ya kimiujiza ili kuitimiza ya Mungu
Matendo kaziya miujiza23
Sura ya Sita: Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
62
Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. Maana mtu mmoja
kwa Roho apewa neno la hekima na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho
yeye yule; mwingine imani kwa Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya
katika Ruho yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza, na mwingine unabii,
na mwingine kupambanua Roho; mwingine aina za lugha, na mwingine tafsiri za
lugha. (1Kor 12:7-10)
Karama hizi tisa zinaelekea kujipanga kiasili katika makusudi matatu. Kundi
la kwanza tunaliita “karama za mafunuo.” Karama hizi za mafunuo zimepewa
“ili kusudi tupate kuyatambua mawazo ya Mungu.” Paulo anaita karama hizi tatu
kama neno la maarifa, neno la hekima, na kupambanua Roho. Kundi la pili
tunaliita “karama na unabii.” Hizi zimepewa “ili tuweze kunena maneno ya
Mungu.” Karama hizi zinajumuisha, karama ya unabii, karama ya aina za lugha,
na tafrisi za lugha. Kundi la tatu tunaliita “karama za nguvu.” Hizi zimetolewa
“ili tupate kuzitenda kazi za Mungu.” Hizi tatu ni karama za kuponya, karama
ya imani, na matendo ya miujiza (au kazi za nguvu). Hebu sasa tujaribu
kufafanua kila karama mojawapo katika karama hizi.
Karama za Roho na Huduma yenye Nguvu
Tujadili sasa ni jinsi gani karama hizi zinahusiana na huduma ya nguvu.
1. Karama za Mafunuo na huduma yenye nguvu (Zimetolewa ili kutambua
mawazo ya Mungu). Karama za mafunuo ni muhimu katika huduma yenye
nguvu. Katika Matendo ilikuwa hasa neno la Maarifa, au kupambanua roho,
ambavyo vilianzisha mlolongo wa matokeo yaliyofanya hatimaye karama ya
nguvu itokee (angalia Mdo 14:8-10; 16:16-18). Kabla hatujafanya kazi za
Mungu ni lazima tujue mawazo ya Mungu, hii ina maana, ni lazima tutambue
yakini ni nini mapenzi ya Mungu katika swala fulani tunalolishughulikia. Yesu
mwenyewe hakuenda tu ovyo akiponya wagonjwa. Kila wakati alisikia kutoka
kwa Baba yake wa mbinguni. Sikiliza vizuri maneno yake: “Mwana hawezi
kutenda neno lolote mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa
maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo mwana vile vile” (Yn 5:19).
Yesu hakufanya lolote pasipo kwanza kuyajua mapenzi ya Baba yake
kuhusiana na jambo lalote. Vi vyo hivyo, ni muhimu kwanza tupokee ufunuo
wa Mungu kuhusiana na jambo tulilonalo.
Ni muhimu sana pia kwamba karama ya kupambanua Roho itendeke mwanza
kabla hatujajua jinsi ya kuiendea huduma fulani ya uponyaji. Ni lazima kwanza
tutambue siyo tu endapo mtu ni mgonjwa, bali pia ni kwa nini ni mgonjwa. Je!
Ugonjwa huo umeletwa na matatizo ya asili au umesababishwa na uonevu wa
Sura ya Sita: Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
24Stanley Horton, What the Bible says about the Holy Spirit
(Springfield, MO: Gospel Publishing House, 1976), uk. 144.
63
mapepo? Kuna habari iliyosimuliwa inayomhusu Smith Wigglesworth, ambaye
alikuwa akiombea watu wawili viziwi. Kwa yule wa kwanza alisema, “Pokea
uponyaji!” na mtu yule alipona mara ile ile. Kwa wa pili alisema, “Mtoke mtu
huyu wewe pepo wa uziwi.” Masikio ya mtu huyu pia yalifunguliwa mara.
Baadaye alipoulizwa ni kwa nini alimhudumia kila mtu kwa namna tofauti
alisema, “Huhitaji kuponya mapepo, ila kuyaamuru kutoka.” Bwana
Wigglesworth asingeweza kufahamu namna ya kumhudumia kila mtu vema
pasipo utendaji wa karama ya kupambanua roho. Ni mara ngapi tumejaribu
“kuponya pepo” na kukemea ugonjwa utoke, wakati tulistahili kufanya tofauti
ya hivyo: Kuanza kutenda karama ya mafunuo huwezesha utendaji wa karama
za nguvu kufuatia.
2. Karama za unabii na huduma yenye nguvu (Zimetolewa ili kuyanena
maneno ya Mungu). Karama za unabii ni za muhimu katika uinjilisti wenye
nguvu. Karama ya unabii mara nyingi itatangulia au kufuatia utendaji wa nguvu
za Mungu. Ndivyo ilivyokuwa siku ya Pentekoste wakati Petro alipohubiri
“mahubiri” madhubuti ya Pentekoste. Kwa kweli mahubiri hayo hayakuwa
mahubiri ya kawaida, bali yalikuwa matamko ya unabii yakiwa yamezungumzwa
chini ya upako wenye nguvu za Roho Mtakatifu24 Matokeo ya kuona na kusikia
miujiza ya Pentekoste (udhihirisho wa nguvu), na kusikia matamko ya unabii wa
Petro (kweli ya neno), watu walichomwa dhamiri kwa ajili ya dhambi zao (Mdo
2:37) na 3,000 waliokolewa na kubatizwa siku ile ile (mstari 41).
Paulo anatufundisha katika (1Kor 14:22) ya kwamba ndimi ni ishara kwa
wasioamini ya kwamba Mungu anafanya kazi katikati ya kusanyiko la wakristo.
Pia anasema ya kwamba kwa njia ya unabii mwenye dhambi anapata kutambua
kuhusu uwepo wa Mungu. Matokeo yake atajiona dhahiri ya kuwa “ni mwenye
dhambi,… na siri za moyo wake huwa wazi; Na hivyo atamwabudu Mungu
akianguka kifudifudi…” (mistari 24-25). Kutimilika kwa unabii kama
ilivyotokea katika manabii wa Agano Jipya, Agabo, yaweza pia kuwa ni
ushuhuda wenye nguvu ya uwepo wa Mungu katika kanisa (Mdo 11:27; 21:10).
3. Karama za nguvu na huduma yenye nguvu (Zimetolewa ili kutenda kazi
za Mungu). Karama za nguvu kwa kawaida huwakilisha matumizi ya karama za
Roho katika uinjilisti wenye nguvu. Kwa njia ya karama za uponyaji na imani
watu huponywa, nguvu na uwepo wa Mungu hudhihirika, watenda dhambi
Sura ya Sita: Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
64
huletwa macho kwa macho na ukweli wa Mungu aliye hai, na mioyo yao huwa
tayari imeandaliwa kusikiliza na kuipokea injili. Katika uponyaji wa Ainea
tunaona kitu kama hicho kikitokea:
Hata Petro alipokuwa akizunguka-zunguka pande zote akawatelemkia na watakatifu
waliokaa Lida. Akamwona mtu mmoja huko, jina lake Ainea, mtu huyo amelala
kitandani miaka minane; maana alikuwa amepooza. Petro akamwambia, Ainea, Yesu
Kristo akuponya; ondoka, ujitandikie. Mara akaondoka. Na watu wote waliokaa
Lida na Sharoni wakamwona wakamgeukia Bwana. (Mdo 9:32-35)
Kwa njia ya karama ya kuponya, uamsho mkubwa ulilipuka katika eneo lile lote.
Karama nyingine ambayo ni ya muhimu katika huduma ya nguvu ni karma
ya matendo ya miujiza (yaani, “utendaji wa kazi za nguvu”). Utendaji wa karama
hii unaonekana kufungulia nguvu za kimungu zinazoleta uponyaji na matokeo ya
miujiza (Lk 5:17; 6:19; Mk 5:30). Kutokana na “Full Life Study Bible,” (toleo
la Biblia lenye mafunzo” “Hizi [karama za matendo ya nguvu za miujiza] ni
matendo ya nguvu za miujiza yanayobadilisha kanuni za asili. Hujumuisha
matendo makuu ambayo kufanya ufalme wa Mungu kushinda ufalme wa shetani
na mapepo … hii hujumuisha kutoa mapepo” (angalia pia Lk 11:20).
MWISHO
Nguvu za Roho wa Mungu ni muhimu kwa ajili ya huduma yoyote ya nguvu.
Nguvu hizi zinatolewa wakati mtu akibatizwa na Roho Mtakatifu. Zinaanza
kufanya kazi kwa kupitia karama za Roho. Ni muhimu kwa hiyo, kwamba kila
mkristo atakayetaka kutumika na Mungu katika eneo hili la uinjilisti wenye
nguvu awe amebatizwa na Roho Mtakatifu. Pia, ni lazima, ajifunze kutembea
katika Roho ili kusudi hitaji linapotokea na jinsi Roho apendavyo, karama ziweze
kutenda kazi katika huduma yake. Kama hujabatizwa na Roho Mtakatifu ni
vema uanze kutafuta kujazwa sasa hivi kwa kumuomba Mungu akujaze kwa
Roho wake.
65
— Sura ya Saba —
Kuongozwa Na Roho
Mtakatifu Na Huduma
Yenye Nguvu
UMUHIMU WA UONGOZI WA ROHO MTAKATIFU
KATIKA HUDUMA YENYE NGUVU
Ilikuwa ni Muhimu Katika Huduma ya Yesu
Uchunguzi wa uangalifu wa vitabu vinne vya injili unaonyesha ya kwamba
kila tendo la huduma ya Yesu lilifanyika chini ya uongozi na uangalizi wa Baba
yake wa mbinguni. Yesu alikuwa na ushirika nyakati zote na Baba. Kama
tulivyokwisha elekeza awali katika Sura ya 5, “Mambo muhimu na Matayarisho
ya Huduma yenye Nguvu,” wakati wote alitenda kama Baba alivyoelekeza.
Soma kwa uangalifu na kwa kutafakari maneno yafuatayo ya Yesu kama
yanavyopatikana katika Yohana 5:19, 20:
Amin Amin nawaambia, mwana hawezi kutenda neno mwenyewe, ila lile ambalo
amwona Baba analitenda; Kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo
mwana vile vile. Kwa kuwa Baba ampenda mwana, naye humwonyesha yote
ayatendayo” (mkazo wa mwandishi, angalia pia Yn 8:28-29 na Yn 12:49).
Mistari ya juu inatuonyesha ya kwamba Yesu alihudumu na kutenda kazi za
miujiza chini ya uongozi wa Baba yake wa mbingini. Alifanya yale tu
“aliyomwona Baba akifanya.” Hivyo kwa njia ya Roho aliyekaa ndani yake
alikuwa nyakati zote na ushirika na Mungu. Kila muujiza alioufanya ulikuwa
umeandaliwa kabla na Mungu. Nyakati zote alifanya yale ambayo Baba yake
Sura ya Saba: Kuongozwa Na Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
66
alimwambia ayafanye.
Hapo awali kulikuwepo mtu ambaye Mungu mara nyingi alimtumia kuponya
wagonjwa. Siku moja mtu mmoja alimpa changamoto, “Kama una karama ya
kuponya, kwa nini usiende hospitali na kumponya kila mtu pale?” Mtu yule
alimjibu, “Yesu alipokwenda hospitali hakumponya kila mtu pale.” Ni lini kwani
ambapo Yesu alikwenda hospitali?” Yule mtu wa kwanza alimwuliza. “Aliwahi
kwenda “hospitali ya “Bethzatha,’” alimjibu. “Soma mwenyewe katika Yohana
5:1-15. Ingawaje palikuwa na ‘namba kubwa ya watu wasiojiweza … vipofu,
viwete na waliopooza” pale, Yesu alimponya mmoja tu kati yao.
Nyakati nyingine Yesu aliwaponya wote waliokuwa wagonjwa mahali fulani
(angalia: Mt 4:23, 24; 8:16). Nyakati nyingine alimponya mmoja tu, kama
kwenye birika la Bethzatha kama ilivyoelezwa juu. Kwa nini Yesu alimponya
mmoja tu pale Bethzatha? Katika mistari ifuatayo (mistari 19-20), Yesu alijibu
hili swali yeye mwenyewe: “Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile
ambalo amwona Baba analitenda.” Yesu alimponya mtu mmoja tu pale
Bethzatha kwa sababu Baba yake wa mbinguni alimwelekeza amponye huyo
mmoja tu. Kama nyakati zote, alifanya lile alilomwona Baba yake akilifanya.
Utendaji huu, ninafikiri, ni ufunguo muhimu katika huduma yoyote ya
mafanikio, na hasa huduma yenye nguvu. Sisi tunaotamani kutumika katika
huduma kama hiyo ni lazima tujifunze mfano kutoka kwa Yesu. Kama vile
huduma ya Yesu katika neno na tendo ilivyokuwa chini ya uongozi wa Baba
yake, sisi pia, kama tutatumika katika nguvu na mafanikio makubwa, lazima
tuzitende huduma zetu chini ya uongozi wa Baba wa mbinguni. Njia pekee
kwetu sisi ya kupata kuhudumu katika nguvu ni kuisikiliza na kuitii sauti ya
Mungu. Kama ilivyokuwa kwa Yesu, sisi pia tunaweza tu kulitenda lile
tumwonalo Baba akilitenda—siyo zaidi, wala siyo pungufu.
Kama hivi ni kweli, fikiria tu ilivyo muhimu kuweza kusikia na kutambua
sauti ya Baba. Pasipo uwezo huo ni mambo madogo sana katika huduma
yatafuatia.
Ilikuwa ni Muhimu Katika Huduma ya Kanisa la Kwanza
Mitume walijifunza jinsi ya kuhudumu hasa kwa kuangalia na kuiga huduma
ya Yesu. Kama yeye. wakati wote walitafuta na kupokea maelekezo katika
kutenda huduma zao.
Sura ya Saba: Kuongozwa Na Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
25John Wimber, Power Evangelism.
67
Yesu na mitume mara nyingi walishuhudia, kwa kutumia maneno ya John
Wimber, “kwa mpango kamili wa Mungu.”25 Kwa maneno mengine, Mungu
alipanga tayari ule wakati wao wa kushuhudia, ndipo akawaongoza kupafikia
mahali ambapo walijikuta wapo penye uwezekano wa kushuhudia. Tutataja
mifano mitatu katika Agano Jipya wa kwanza unamhusu Yesu, wa pili unamhusu
Filipo, na wa mwisho unamhusisha mtume Petro.
1. Yesu na mwanamke msamaria. Katika Yohana 4:1-42 soma kuhusu
uamsho wa ajabu uliotokea mji wa Samaria uitwao Sikari. Uamsho huo ulianza
kutokana na ushuhuda wa Yesu kwa mwanamke huyo wa Samaria.
Alimshuhudia, na kumpata mwanamke aliyekutana naye katika kisima cha kijiji.
Lakini ni kwa nini Yesu alikwenda Samaria? Alikwenda kwa sababu Baba yake
wa mbinguni alimwelekeza aende pale. Katika mstari wa 4 Biblia inasema,
“Naye alikuwa hana budi kupita Samaria.” Kwa nini ilikuwa ni muhimu hivyo
kwa Yesu kupita Samaria? Kwa sababu Baba alikuwa ameshaipanga safari hiyo.
Kulikuwa na mwanamke aliyemhitaji Yesu, na pia mji ule ulikuwa tayari
umewiva kwa ajili ya uamsho.
2. Filipo na towashi wa Kushi. Habari ya Filipo na towashi wa Kushi ni
mfano mmojawapo wa kanisa la kwanza jinsi lilivyohudumu kwa kufuatilia
“mpango halisi wa Mungu.” (Angalia Mdo.8:26-40). Katika mstari wa 26 Biblia
inasema, “Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, ondoka ukaende
upande wa kusini hata njia ile - itelemkayo kutoka Yerusalem kwenda
Gaza—nayo ni jangwa.” Mungu alikuwa tayari amepanga makutano kati ya
Filipo na mwafrika mmoja aliyekuwa ana njaa ya kumjua Mungu aishiye.
Alipomwona mtu huyo amepanda gari lake la farasi akisoma kutoka Isaya 53:7-8,
Roho wa Bwana akasema na Filipo, “Sogea karibu na gari, ukashikamane nalo”
(mstari 30). Alipokaribia gari lile, Filipo alimsikia mtu yule akisoma kwa nguvu
kutoka katika kitabu cha Isaya. Filipo akaanza mazungumzo na mtu yule
yaliyomfanya hatimaye aokolewe. Hapa tena tunaona waziwazi umuhimu wa
Filipo kuweza kuisikia sauti ya Roho. Kama tutahitaji kuwa na huduma yenye
mafanikio, sisi pia ni lazima tuweze kuisikia na kuifahamu sauti ya Roho.
3. Petro na nyumba ya Kornelio. Mfano wa mwisho wa kuhudumu kwa
“mpango halisi wa Mungu” unapatikana katika Matendo 10:1-48. Katika habari
hii Mungu mwenyewe alipanga mkutano baina ya Kornelio, askari wa Kirumi na
mtume Petro. Akiwa tayari amepanga mahali pa kukutania, ndipo Mungu
Sura ya Saba: Kuongozwa Na Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
68
akaanza kuzungumza na wote Kornelio na Petro kwa njia ya maono (mistari 3-4;
10-11). Pia Alisema wazi kwa Petro kwa njia ya Roho wake (mstari 19). Soma
habari hii ya ajabu wewe mwenyewe katika Biblia yako. Tena utauona umuhimu
wa kuweza kusikiliza na kutii sauti ya Roho.
Kwa kuhitimisha, kama sisi, kama ilivyokuwa kwa Yesu na mitume,
tutahudumu chini ya uongozi wa Roho, lazima tujifunze kuisikiliza na kuifahamu
sauti ya Mungu. Hii inatuleta kwenye swali la muhimu, “Je! Mtu anawezaje
kusikiliza sauti ya Mungu?” Tutajaribu kujibu swali hili katika sehemu ifuatayo
ya sura hii.
JINSI YA KUISIKIA SAUTI YA MUNGU
Kama utahitaji kuisikia sauti ya Mungu, fahamu na kuitumia misingi sita
ifuatayo:
Tambua ya Kwamba Mungu Anazungumza na Wewe
Kwanza, ni lazima utambue ya kuwa Mungu huzungumza na watoto wake
leo. Kusema kweli, anazungumza na wewe leo! Mungu, kwa asili yake, ni
Mungu asemaye, na kama Baba yeyote mwenye upendo, anazungumza na watoto
wake nyakati zote. Endapo wewe huisikii sauti ya Mungu, si kwa sababu
hazungumzi na wewe bali bila shaka ni kwa sababu wewe mwenyewe hujui jinsi
ya kumsikiliza yeye.
Wakati fulani mtunza bustani alikuwa akitaka kumwagilia maji katika bustani
yake. Alisumbuliwa kwa sababu maji yalikuwa hayatoki kwenye mpira wa
kumwagilia. Kwa hasira alimpigia kelele mtunza bustani mwenzake, “Maji
hayatoki katika mpira huu. Nilikuambia fungulia maji katika bomba ili yapate
kutoka!” Alipewa jibu hili: “Rafiki, maji yamekwisha kufunguliwa, lakini kuna
mkunjo katika mpira wako, kiasi kwamba maji hayawezi kutoka.” Ndivyo mara
nyingi ilivyo kwetu. Mungu anasema nasi, lakini sisi hatusikii. Tuna mkunjo
katika mpira wetu.
Fahamu Jinsi Mungu Asemavyo
Kama tutahitaji kuisikia sauti ya Mungu ni lazima tufahamu jinsi Mungu
anavyozungumza nasi. Yesu alisema, “Kondoo humsikia sauti yake
[(mchungaji]… wanaijua sauti yake” (Yn.10:3-4). Zipo njia nne ambazo Mungu
anazungumza nasi leo. Tunaweza kuziita (1) kwa njia ya msingi, (2) kwa njia ya
Sura ya Saba: Kuongozwa Na Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
69
ana kwa ana, (3) kwa njia ya kawaida, na (4) kwa njia yakuthibitisha.
1. Njia ya msingi ambayo Mungu husema nasi. Njia ya msingi ya Mungu
kusema na mwanadamu leo ni kwa njia ya Neno lake, Biblia Takatifu. Kama
unataka kujua ni nini Mungu anasema kwako, unaweza kuona katika Biblia. Hii
ni njia pekee ya msingi tuliyonayo katika kusikia sauti ya Mungu. Njia nyingine
yoyote lazima ipimwe na kuhakikishwa na njia hii ya msingi.
2. Mungu pia husema kwa njia ya ana kwa ana. Zaidi ya Neno lake, Mungu
pia huzungumza na watoto wake kwa njia ya ana kwa ana. Katika Biblia njia hizi
ni pamoja na ndoto, maono, malaika pamoja na kunena kwa sauti ya kusikika.
Ni kweli Mungu anaweza kufanya mambo hayo yote leo, ingawa onyo lazima
litolewe hapa. Nyakati zingine watu kadhaa wasio wakiroho, wakitaka
waonekane kuwa ni wa kiroho mbele za wengine, hujifanya eti Mungu
amezungumza nao kwa njia kadha, matokeo yake watu wengi wa kiroho huamua
kuachana na maswala ya jinsi hii,ya ndoto na maono. Je! Mwangalio wetu uweje
katika maswala haya? Kwanza, lazima tufahamu ya kuwa hizo sio njia peke yake
ambazo Mungu alitumia kusema na watu wake katika Biblia. Njia muhimu
aliyotumia ilikuwa ni kwa njia ya Roho wake katika roho zao. (Tutajadili jambo
hili baadaye). Hata kama njia hizo za ndoto na maono siyo njia peke yake
ambazo Mungu alinena na watu wake, pia ni kati ya njia anazotumia. Njia pekee
ya kufanya ni kule kutokukazania kuzitafuta njia hizo tu. Hata hivyo kama
Mungu atachagua kusema nasi kwa njia hizo basi hapo tusiwe na shaka lolote.
3. Njia ya kawaida ambayo Mungu hutumia. Kama tulivyokwisha
kuzungumza hapo juu, njia ya kawaida sana ambayo Mungu hutumia kusema na
watoto wake ni kwa njia ya Roho wake katika roho zetu. Mistari miwili ya
Agano la Kale inatusaidia kuelezea njia hii. Mmoja ni mfano wa nabii Eliya.
Hakuisikia sauti ya Mungu katika hali ya ana kwa ana (k.m. kama upepo mkali,
tetemeko, au moto), bali alisikia sauti yake kama “sauti ndogo ya utulivu” (1Fal
19:12-13). Mfano mwingine ni ushuhuda wa nabii Isaya. Aliielezea sauti ya
Mungu kwa namna hii: “… na masikio yako yatasikia neno nyuma yako
likisema, ‘Njia ni hii ifuateni’” (Isa 30:20).
Swala hili ya kwamba Mungu hunena na watumishi wake Roho kwa roho
limewekwa wazi katika Agano Jipya. Katika Rumi 8:14 mtume anasema, “Kwa
kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.”
Halafu katika mstari wa 16 anaendelea, “Roho mwenyewe hushuhudia pamoja
a roho zetu, ya kuwa sisi tu wana wa Mungu.” Angalia hapa Paulo anasema ya
kuwa Roho wa Mungu husema moja kwa moja na roho za watu waliookoka. Hii
ndiyo njia ya kawaida sana ambayo yatupasa kutegemea Mungu kusema nasi leo.
Sura ya Saba: Kuongozwa Na Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
70
Mtume Paulo anaendeleza jambo hili katika 1Wakorintho 2:9-13. Hebu
chukua muda kidogo usome kwa uangalifu na kuyafikiria maneno haya. Hapa
Paulo anaweka njia tatu ambazo Mungu hutumia kusema na roho zetu. Kabla
ya yote anaeleza ya kwamba Mungu hutufunulia kweli yake kwetu kwa Roho
wake:
Lakini kama ilivyoandikwa, mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio
halikuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo
Mungu aliwaandalia wampendao - lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana
Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu. (mistari 9-10, mkazo wa
mwandishi)
Halafu, Paulo analinganisha kati ya roho ya mtu na Roho wa Mungu.
Anasema kwamba roho ya mtu ndani yake inayatambua mawazo yake. Katika
hali hiyo hiyo Roho wa Mungu huyatambua mawazo ya Mungu:
Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu
iliyo ndani yake? Vivyo hivyo mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa
Mungu. (mstari 11)
Hatimaye, Paulo anaelekeza matumizi ya ukweli huu. Anasema ya kuwa
kwa kuwa Roho wa Mungu anayajua mawazo ya Mungu, nasi tumempokea Roho
wa Mungu, tunaweza kwa namna hiyo tukayajua mawazo ya Mungu. Roho wake
atayatambua na kuziambia roho zetu:
Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi
tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena si kwa maneno
yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu bali yanayofundishwa na Roho.…
(Mistari 12-13a pia angalia mstari 16)
Njia ya kawaida ya Mungu katika kuzungumza na watoto wake ni kwa Roho
wake na roho zetu. Kama mwana wa Mungu unaweza kutegemea mara nyingi
kuisikia sauti ya Mungu ikisema nawe kwa njia hii.
4. Mungu husema kwa njia ya kuthibitisha. Njia ya mwisho ambayo
tunaweza “kuisikia” sauti ya Mungu ni kwa njia ya kile kinachoitwa “njia ya
kuthibitisha.” Tofauti na zile njia tatu tulizozungumzia hapo juu, njia za
kuthibitisha si njia za moja kwa moja za kumsikia Mungu kama zile za ana kwa
Sura ya Saba: Kuongozwa Na Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
71
ana. Katika njia hii Mungu hutumia matukio au watu wengine kusema nasi. Njia
mojawapo katika hizo ni matukio ambayo hutumwa na Mungu mwenyewe. Hii
ina maana ya kuwa ni yale matukio ya maisha ambayo Mungu huyapanga moja
kwa moja kwetu ili kutuonyesha mapenzi yake.
Njia nyingine ya kuthibitisha ambayo Mungu hutumia kusema nasi ni kupitia
wakristo wengine waliojazwa Roho Mtakatifu. Kwa maneno mengine, Mungu
atasema mapenzi yake kwetu kupitia wakristo mwingine. Mara nyingine mtu
huyu atajua kuwa ule ujumbe ambao mwenzake anazungumza unatoka kwa
Mungu, nyakati nyingine atasema maneno ambayo hayaelewi vizuri, lakini
Mungu atayafanya yaeleweke mioyoni mwetu.
Wakati mwingine Mungu atasema nasi kupitia matamko ya unabii ambayo
huzungumzwa katika hali ya upendo katika kusanyiko la wakristo. Matamko
haya ya unabii huwa ni pamoja na jumbe za lugha na tafsiri pamoja na unabii wa
upako. Tena, lazima tutoe onyo kali hapa. Wengi wetu tumekwisha kuona njia
hii ikitumika vibaya na wakristo wachanga ambao wana mori wa kupita kiasi.
Wengine wamepotolewa na kukwazwa na “manabii wa uongo” wa jinsi hii.
Kumbuka mambo haya mawili unapojisikia ya kwamba Mungu anaweza kuwa
anasema kwako kupitia wengine: 1) Linalozungumzwa ni lazima likubaliane
kabisa na Neno la Mungu. Kama sivyo, ulikatae mara moja kama vile halitoki
kwa Mungu. 2) Linalozungumzwa ni vema lihakikishe na jambo ambalo tayari
Mungu amekwisha kusema, au atasema, moja kwa moja kwenye roho yako.
Kamwe, narudia kamwe usimruhusu mtu akuambie Mungu amesema hivi pasipo
kupima na kuhakikisha kwa uhakika yake yaliyosemwa. Mara zote mtafute
Mungu wewe mwenyewe hadi amezungumza nawe moja kwa moja, kwa Roho
wake ndani ya roho yako.
Tayarisha Moyo Wako Kuisikia Sauti ya Mungu
Sababu mojawapo ambayo inatufanya tushindwe kuisikia sauti ya Mungu
anaposema ni kwa sababu mioyo yetu haijatayarishwa vema kumsikiliza. Ni
sasasawa na redio ambavyo inatakiwa ichomekwe kwenye nguvu ya umeme na
pia iyapate masafa ya stesheni inayorusha matangazo kabla haijaweza kupokea
taarifa kutoka kwenye stesheni ya redio ya matangazo, sisi pia ni lazima tuyapate
masafa ya Roho Mtakatifu kabla hatujaweza kuisikia sauti ya Mungu.
Ninaposema ni lazima tuchomekwe kwenye nguvu ya umeme ninamaanisha ya
kwamba ni lazima tuzaliwe mara ya pili. Ni kwa njia ya kuzaliwa mara ya pili
ndipo roho zetu zinapokuwa zimeunganishwa na nguvu za mitambo ya mbinguni,
yaani Roho wa Mungu. Paulo anasema katika 1Wakorintho 6:17, “Lakini yeye
Sura ya Saba: Kuongozwa Na Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
26Kwa majadiliano ni vipi unaweza kujazwa na Roho Mtakatifu,
angalia sura ya 6, “Roho Mtakatifu na Huduma yenye nguvu.”
72
aliyeungwa na Bwana ni Roho moja naye.” Roho zetu “zimeungana” na Roho
wa Mungu. Ni pale “tukizaliwa katika Roho” (Yn.3:5) ambapo Roho Mtakatifu
anaingia ndani yetu, ndipo tunapofanyika kuwa “viumbe vipya” katika Kristo
(2Kor.5:17). Ndiyo maana Yesu alisema ya kwamba mara mtu akizaliwa mara
ya pili ndipo anapoweza “kuuona ufalme wa Mungu” (Yn.3:3). Paulo alisema
“Mwanadamu wa tabia ya asili… hayapokei [mambo ya Roho wa Mungu],
maana kwake hayo ni upuuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa
yatambulikana kwa jinsi ya Rohoni” (1Kor.2:14).
Zaidi ya kule kuzaliwa mara ya pili, “kuchomekwa” katika nguvu ya
mitambo ya mbinguni kunahusu pia kubatizwa na Roho Mtakatifu. Kama
tutahitaji wakati wote kusikia sauti ya Roho, ni lazima tujazwe na Roho
Mtakatifu.26 Kujazwa na Roho kutatuongezea uwezo wa kusikia sauti ya Roho.
Inaweza kulinganishwa na kuongezea nguvu zaidi katika redio au kuinua waya
mrefu zaidi wa mapokezi ya mawimbi ya hewa katika redio. Kwa kujazwa na
Roho utapokea nguvu zaidi na pia unakuwa na hisia zaidi katika Roho.
Sio tu lazima tuunganishwe na Roho wa Mungu, lazima pia tuunganishe
mitambo yetu na sauti yake. Haitoshi tu redio iungane na chanzo cha mitambo
ya nguvu. Kabla ya kupokea ujumbe kutoka kwenye kituo cha kurushia
matangazo, ni lazima pia iunganike na kupata masafa yanayohusika.
Tunaunganisha masafa yetu na Mungu kwa njia ya kujitoa kwa Mungu na kwa
mapenzi yake timilifu kwa maisha yetu. Biblia inatuonya, “Kwa hiyo kama
anenavyo Roho Mtakatifu: Leo kama mtaisikia sauti yake, msifanye migumu
mioyo. . ..” (Ebr 3:7-8). Tunahitaji kuiweka mioyo yetu wazi na laini mbele
zake. Wepesi wa hisia wa namna hiyo kwa Roho wa Mungu waweza kupatikana
tu kutoka mioyo yenye unyenyekevu na utii. Hii yaweza kuja kwa njia ile tu ya
maisha ya kumtumaini, pamoja na muda mwingi unaotumika katika maombi ya
kulitafakari neno.
Jifunze Jinsi ya Kuitambua Sauti ya Mungu
Kama tutahitaji nyakati zote na kwa uwazo kuisikia sauti ya Mungu ni lazima
tujifunze kuisikia wakati anaposema. Yesu alisema, “Kondoo kumsikia
[mchungaji] sauti yake… na … huijua sauti yake” (Yn 10:3-4). Uwezo wa
namna hiyo wa kuijua sauti ya mchungaji, unakuja tu kwa njia ya mazoezi
Sura ya Saba: Kuongozwa Na Roho Mtakatifu Na Huduma Yenye Nguvu
73
(angalia Ebr 5:14). Jinsi tunavyofanya mazoezi ya kuisikia na kutii sauti ya
Roho, tunajifunza vema zaidi kuitambua sauti yake asemapo.
Ijaribu Sauti ili Kuhakikisha Kama Kweli ni ya Mungu
Neno la maonyo ni muhimu hapa. Ni muhimu kwamba tunajifunza
kuzijaribu sauti “tunazozisikia” ili tuweze kuzitambua kama kweli ni sauti za
Mungu. Biblia inatuambia ya kwamba kuna “sauti za namna nyingi duniani
(1Kor 14:10). Sauti hizi ni pamoja na sauti za binadamu, vyote sauti yetu ya
ndani (mawazo yetu), na sauti zanje (watu wengine). Sauti hizi pia ni pamoja na
sauti za kiroho pamoja na mawazo ambayo yanaweza kupandikizwa katika
mawazo na Mungu au na Roho wachafu. Ni muhimu kujua jinsi ya kupima sauti
hizi, ili kujua kama zinatoka kwa Mungu au hapana. Kama hazikubaliani na
neno la Mungu lazima zikataliwe.
Kwa Imani Fanya Mazoezi ya Kuitii Sauti ya Mungu
Msingi wa mwisho ambao lazima tuufahamu ni huu: Kama tutahitaji
kujifunza namna ya kuipambanua sauti ya Mungu, lazima kwa imani tuanze kutii
sauti yake tunapoisikia. Tunayo sababu moja nzuri ya kusikia sauti ya Mungu:
Tunaisikiliza sauti ya Mungu ili tupate kuitii. Je! Tufanye nini basi? Ni lazima
tutegemee kuwa Mungu atasema, na atakaposema, sisi lazima tumtii. Jinsi
tunavyomtii na kumfuata, tunajifunza kuipambanua sauti ya Mungu vema.
MWISHO
Uwezo wa kujua na imani ya kutii sauti ya Mungu ni mahitaji muhimu kwa
huduma yenye nguvu. Tunahitaji tufanye kuwa ndiyo shabaha yetu kujifunza
jinsi ya kuyafanya yote.
74
75
— Sura Ya Nane —
Silaha Za Vita Vyetu
UTANGULIZI
Katika sura ya 3, “Huduma yenye nguvu na ufalme wa Mungu.” tulijifunza
ya kwamba Kristo alikuja kuanzisha ufalme wa Mungu duniani. Anaendelea
kufananisha malengo yake kwa njia ya kanisa, na upako wa Roho Mtakatifu.
Kwa sababu shetani anapinga maendeleo ya ufalme wa Mungu, vita kuu ya
kiroho imeanza. Sasa, ikiwa tunapenda au la—ikiwa tunafahamu au
hatufahamu—kanisa limo katika vita kubwa dhidi ya ufalme wa shetani (angalia
Efe 6:12). Katika vita hii Kristo ametupatia nguvu na mamlaka dhidi ya adui,
shetani. Sikiliza yale aliyosema Yesu katika Luka 10:19-20:
Nilimwona shetani akianguka kutoka mbinguni kama umeme. Tazama nimewapa
amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu
kitakachowadhuru.
Ili vita yoyote ipate kupigwa vema, inahitaji silaha. Ni hivyo hivyo, vita vya
kiroho vita tunavyopigana vinahitaji silaha za kiroho. Sisi kama jeshi la kiroho
la Kristo tumepewa zana zote za kiroho tunazohitaji kumshinda shetani. Katika
2Wakorintho 10:3-5, mtume Paulo anazungumzia kuhusu silaha hizo za kiroho:
“Maana silaha za vita vyetu si za mwili bali zina uwezo katika Mungu hata
kuangusha ngume.”
Katika sura hii tutazitambua silaha hizi za kiroho na kujadili jinsi ya
kuzitumia ili kushinda vita dhidi ya shetani na majeshi yake ya mapepo.
Sura Ya Nane: Silaha Za Vita Vyetu
27The New Testament in the Translation of Ronald Knox
76
SILAHA ZOTE ZA MUNGU
Katika Waefeso 6:10-18 tunaambiwa tuvae silaha zote za Mungu, au kama
Ronald Knox alivyotafsiri sehemu hii, “Unahitaji uvae silaha zote zilizomo katika
bohari ya Mungu ya silaha”27 Tumeambiwa ya kwamba tuzichukue silaha za
Mungu ili tukabiliane na shetani. Je! Ni nini basi maana ya “silaha zote za
Mungu” kama ilivyoandikwa katika Waefeso sura ya 6, na tunaweza kuzitumia
vipi ili kumshinda shetani? Hili ndilo tutakalojadili katika sehemu ya kwanza ya
sura hii.
Chanzo cha Nguvu ya Vita
Lazima tukumbuke ya kwamba chanzo cha nguvu zetu za vita si za kimwili,
bali za kimungu. Hapa katika maandiko haya Paulo anatuambia tuwe “hodari
katika Bwana na “katika uwezo wa nguvu zake” (mstari 10). Tunatakiwa
tusiangalie katika nguvu zetu, au silaha zetu ili kupigana vita hii ya kiroho.
Tunatakiwa kumwangalia Mungu na nguvu zake na silaha zake. Ingawa
hatuangalii katika nguvu zetu, kuna jambo, hata hivyo, ambalo lazima tulifanye:
Lazima sisi wenyewe “tuvae silaha zote za Mungu [tupate] kuweza kuzipinga hila
za shetani.”
Makusudi ya Silaha Zote za Mungu
Paulo anatueleza makusudi ya silaha za kiroho. Zipo mbili:
Kwanza, kwamba tunaweza kusimama kinyume cha mashambulizi ya adui
(mstari 13), na pili, kwamba tusiangukie katika mtego wa “hila” za shetani
(mstari 11). Neno lililotafsiriwa “Hila” katika mstari wa 11 lina asili ya neno la
kiyunani, “methodeia.” ambalo limetafsiriwa kwa kiingereza katika namna
nyingi, pamoja na “njia,” “mbinu,” “ujanja,” “hila,” na “mitego.” Hivyo,
tunahitaji kuwa tumejiandaa kwa vyote mashambulizi ya adui na mbinu zake
mbalimbali.
Sehemu Mbalimbali za Silaha Zote za Mungu
Paulo sasa anatumia mavazi ya silaha za askari wa Kirumi kama njia ya
Sura Ya Nane: Silaha Za Vita Vyetu
77
kuelekeza sehemu mbalimbali za silaha za mkristo za kiroho. Sikiliza maneno
yake:
Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
sehemu za kufungiwa miguu utayari tupatao kwa injili ya amani; zaidi ya yote
mkitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye
moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chepeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao
ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho,
mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote (Efe 6:14-
18, mkazo wa mwandishi).
Utatambua ya kwamba tulitilia mkazo maneno saba ya muhimu na sehemu
za sentensi katika kifungu cha maneno yaliyopo juu. Kila neno au sehemu ya
sentensi inazungumzia silaha yenye nguvu ya mkristo. Tutaangalia kwa kifupi
kila silaha:
1. Kujivika silaha ya kweli. Sisi, kama askari wa kikristo, tunahitaji kujivika
silaha ya kweli. Kujivika kweli viunoni maana yake ni kwamba tujivike silaha
ya Neno la Mungu, ambalo ni kweli (Yn 17:17). Tuijaze mioyo yetu na mawazo
yetu na Neno la Mungu. Pia inaweza kumaanisha tujivike na kusema ukweli
ambao ni uaminifu wote na tabia njema.
Kutokana na mstari wetu, tunatakiwa tujivike silaha hizi zote ile tuweze
kukabiliana na mashambulizi na hila za shetani. Hebu fikiri pamoja nami kwa
kitambo. Je! Ni dhidi ya hila zipi za shetani silaha hii ya kweli inaweza
kutumika? Inaweza kutumika dhidi ya uongo wa shetani! Kumbuka ya kuwa
yeye ni mwongo na baba wa huo (Yn 8:44). Moja ya silaha zenye nguvu za
shetani ni uongo. Tunaweza kukabiliana na uongo wake kwa kuihubiri kweli ya
Neno la Mungu na kwa kuishi maisha ya ukweli na heshima mbele za Mungu na
wanadamu.
2. Kuvikwa silaha ya haki. Katika vita vyetu na shetani, tunatakiwa tusijivike
silaha ya kweli tu, bali pia lazima tujivike silaha ya haki. Haki inaweza
kufafanuliwa kama uhusiano mzuri na pia maisha mema. Tunaweza tukawa
kweli watu wa haki kama tuna uhusiano mzuri na Mungu kwa njia ya Yesu
Kristo. Kutokana na matokeo yauhusiano huu tunatakiwa sasa kufanya mazoea
ya kuishi maisha mema; hii inamaanisha kuishi maisha masafi na matakatifu. Ni
lazima tujue namna ya “kusema ‘hapana’ kwa ubaya na tamaa za kidunia, na
tuishi maisha kwa kiasi na haki na utauwa katika ulimwengu huu wa sasa” (Tit
2:12). Hivyo kwa kuvaa dirii ya haki, tutaweza kuizima mishale yote ya shetani
Sura Ya Nane: Silaha Za Vita Vyetu
28Kwa majadiliano zaidi kuhusu nguvu ya injili angalia Sura ya 4,
“Huduma yenye nguvu na kuihubiri injili.”
78
na hila zake ambazo zimewashinda wengi.
3. Kujivika utayari. Tena Paulo anatuambia ya kwamba tujivike na utayari.
Kwa maneno mengine, tunahitaji tubakie katika hali ya kuwa tayari na wakati
wote tuwe macho kwa mashambulizi ya adui. Petro anatuonya, “Muwe na kiasi
na kukesha, kwa kuwa mshitaki wenu ibilisi, kama simba aungurumaye,
huzunguka-zunguka, akimtafuta mtu ammeze” (1Pet 5:8). Lazima tujiweke
tayari dhidi ya ujanja na mashambulizi ya adui.
Tambua ya kuwa Paulo anasema ya kwamba utayari huu unaletwa na injili.
Ni kuhubiriwa kwa injili kunakoleta utayari, maandalizi na kuwavika silaha watu
dhidi ya mbinu za maadui.28
4. Kujivika silaha ya imani. Silaha nyingine ambayo tunahitaji “tuichukue”
katika vita vyetu na shetani ni silaha ya imani. Imani ambayo tunahitaji
tuichukue ni lazima kwa hakika ichangamane na imani iokoayo, hii inamaanisha
ule msingi wa kumwamini Mungu na wokovu wake kupitia kifo cha Yesu
msalabani. Hata hivyo, silaha hii ya imani lazima iende zaidi ya imani ile
iokoayo. Ni lazima pia ichangamane na imani yenye nguvu zaidi ijinyoshayo
na kuyafikia yale ambayo Mungu ameyaahidi. Imani ya jinsi hiyo inaweza
kutumika kama ngao ya “kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu” (Efe
6:16). Kwa silaha hii tunaweza kushinda kila shambulizi la adui. Mashambulizi
haya yanaweza kuchanganya mawazo machafu, tamaa na ukaidi, maamuzi ya
ukaidi, tamaa na woga.
Sio tu kwamba imani ni silaha madhubuti ya kujikinga, kama ilivyotajwa
hapo juu, pia ni silaha yenye nguvu katika mashambulizi. Yaweza kutumika
kumshinda adui. Tumia muda kusoma Waebrania, sura ya 11. Katika “sura hii
mashuhuri ya imani” utaona jinsi wanaume na wanawake wa zamani
walivyoitumia imani kama silaha yenye nguvu ya mashambulizi. Kwa imani
“walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi” (mstari 33). Kwa
imani “walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni” (mstari 34).
Kwa kweli Biblia nzima imejaa watu kama hao ambao walitumia imani kama
silaha yenye nguvu ya kuusukuma mbele ufalme wa Mungu duniani. Nasi pia,
lazima tutumie silaha za kiroho zenye nguvu.
Sura Ya Nane: Silaha Za Vita Vyetu
79
5. Kujivika wokovu/ukombozi. Silaha ya tano katika silaha za mkristo dhidi
ya shetani ni silaha ya wokovu. Hapa tunahitaji kutafsiri wokovu katika mapana.
Hapa tunazungumzia sio tu wokovu kutoka dhambini na jehanamu, bali pia
wokovu wowote, au ukombozi, utokao kwa Mungu. Hii yaweza kuchanganya
wokovu, au ukombozi, kutokana na mapepo, hatari, ugonjwa na kifo. Pia
hujumlisha ukombozi kutoka kwa shetani na mitego yake iliyofichika.
Wokovu huu unaweza tu kuja kutoka kwa Mungu. Tunalohitaji kulitenda
ili kuupokea ni kuliitia jina la Bwana (Rum 10:13). Tunapokuwa
tumedanganywa na adui na “ kuchukuliwa mateka wa vita,” ni lazima tukumbuke
ya kwamba hatujapoteza mambo yote. Tunaweza kumwita Mkombozi wetu
mwenye nguvu za ajabu, atatuokoa!
6. Kujivika Neno la Mungu. Moja ya silaha za kiroho zenye nguvu ni Neno
la Mungu, katika maandiko limeelezwa kwamba ni “upanga wa Roho.” Ninaona
uwezekano wa aina mbili wa matumizi ya neno hili kwa mtumishi mkristo
“kuchukua . . .neno la Mungu.” Kwanza, ina maana kujivika silaha ya Biblia.
Kujivika Biblia lazima tusome, tukariri, tuchambue, tutumie, na tuhubiri Neno
la Mungu.
“Neno la Mungu” katika mstari huu pia linaweza kumaansha “neno” la
binafsi ambalo tunaweza kulipokea kutoka kwa Mungu. Watafsiri wengine wa
Biblia hulieleza neno hili kutoka kwa Mungu kama “neno la rhema” wakielezea
neno ambalo limetokana na lugha ya Kiebrania. Hili “neno la rhema” laweza
kuwa sehemu fulani ya maandiko ambalo Mungu husema na moyo wako ili
kukutana na hitaji fulani binafsi. Pia inaweza kuwa ufunuo fulani wa binafsi
utokao kwa Mungu ambao una nia ya kukutana na hitaji fulani hii inaweza
kujumuisha maneno ya maarifa na hekima.
Kwamba ni ushauri mzima wa Mungu (Biblia nzima), au ni mstari fulani wa
maandiko, silaha hii inaweza kutumika kwa njia zote mbili, kushambulia na
kujikinga katika mapambano. Inaweza kutumika kama silaha ya mashambulizi
wakati neno linahubiriwa na kufundishwa chini ya upako wa Roho Mtakatifu.
Inaweza pia kutumika kama silaha ya kinga ili kujikinga na mashambulizi ya
shetani. Shetani anapotujia na uongo wake tunaweza kumrushia ahadi za Mungu
usoni kwake. Atarudi nyuma tu dhidi ya mapambano kama haya.
7. Kujivika maombi katika Roho. Silaha ya mwisho iliyotajwa katika
Waefeso 6:18 ni “maombi katika Roho.” Je! Inamaanisha nini maombi katika
Roho? Ina maana ya aina yoyote ya maombi yenye upako wa Roho au
yanayoongozwa na Roho. Pia ninaamini, ni kunena hasa katika lugha. (Angalia
1Kor 14:14 na Rum 6:26). Kuomba katika Roho ni silaha ya kiroho yenye nguvu
Sura Ya Nane: Silaha Za Vita Vyetu
80
sana mikononi mwa wakristo waliojazwa na Roho Mtakatifu. Paulo anatuambia
kwamba kamwe tusije tukaiweka silaha hii chini; ila “tuombe kila wakati katika
Roho” (mstari 18). Askari wa kiroho anapoomba katika Roho baraka nyingi
hufuata: akili yake inafanyika upya, maisha yake ya kiroho yanatiwa nguvu
(1Kor 14:4), imani yake hujengwa (Yuda 20), na maombi yake yanakuwa ni
sawasawa na mapenzi ya Mungu (Rum 8:27).
SILAHA ZA KIROHO NANE ZENYE NGUVU ZAIDI
Jinsi tunavyoendelea na sura hii ya silaha za vita vyetu, sasa tutaeleza kwa
kifupi silaha nane za kiroho na zenye nguvu ambazo amepewa muumini.
Nyingine kwa sababu zimejadiliwa kwa marefu mahali pengine katika kitabu
hiki, tutazielezea kwa kifupi tu. Hata hivyo tunaona ni vema kuziweka zote
mahali pamoja katika sura hii. Hii ni kumsaidia msomaji ili apate kuona ni silaha
ngapi ambazo tayari anazo katika vita vyake dhidi ya shetani.
Silaha ya Maombi
Tumetaja sasa hivi maombi katika Roho kama silaha ya kiroho, lakini tazama
tena Paulo anavyosema katika Waefeso 6:18: “Kwa sala zote na maombi mkisali
kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea
watakatifu wote” (mstari 18, mkazo wangu). Tazama hapa Paulo anasema
“Mkisali kila wakati,” na tunatakiwa tufanye hivyo “kwa sala zote na maombi.”
Maombi ya namna nyingi ni silaha lubwa lakini isiyotumika mara nyingi katika
mikono ya askari wa kiroho. Hivyo tusishindwe kutumia silaha hii yenye nguvu.
Silaya ya Kufunga
Silaha nyingine yenye nguvu ambayo tunayo ni silaha ya kufunga. Kufunga
kunatakiwa kutumika pamoja na silaha ya maombi. Katika Marko Sura ya 9 ni
habari ya kijana aliyepagawa. Katika habari hii wanafunzi wa Yesu wanajaribu
kumtoa pepo kwa kijana; hata hivyo bidii yao haina mafanikio. Baba wa kijana
huyo anamwona Yesu akija, anamkimbilia, anamuomba aje amtoe pepo. Yesu
anakubali na kumtoa yule pepo na kijana anakuwa huru. Baadaye wanafunzi wa
Yesu walimuuliza, “Mbona sisi hatukuweza kumtoa?” Yesu aliwajibu, “Namna
hii haiwezi kutoka kwa neno lolote isipokuwa kwa kuomba na kufunga” (Mk
Sura Ya Nane: Silaha Za Vita Vyetu
29NKJV - Tafsiri mojawapo ya Biblia katika Kiingereza.
81
9:29, NKJV).29 Ninaamini ya kwamba “Pepo wa namna hii” bado angalipo na
maombi na kufunga ndiyo njia pekee ya ushindi dhidi yapepo wa namna hii.
Maandiko yanataja njia nne ambazo tunaweza kutumia silaha ya kiroho ya
kufunga:
1. Kusaidia kuingia katika uwepo wa Mungu (Ezra 8:23).
2. Kuwafungulia wafungwa huru (Isa 58:6).
3. Kupata hekima na ufahamu (Dan 9:2-3, 21-22).
4. Kupata mapenzi ya Mungu katika jambo fulani (Mdo 13:2).
Tumia muda wa kutosha kuangalia mistari hiyo na kutafakari katika kila
mstari. Itakusaidia kuelewa nguvu ya ajabu ya silaha ya kufunga.
Silaha ya Sifa
Silaha nyingine ambayo hatujaitaja ni silaha ya sifa. Hata kama sifa huwa
haifikiriwi kuwa ni silaha ya kiroho, hata hivyo iko nguvu kubwa ya kiroho
inayotokea katika sifa iliyo na upako wa Roho. Wana wa Israeli walipopiga
kelele ukuta wa mji ulianguka (Yos 6:16-20). Wakati waimbaji wa Yehoshafati
walipoanza kuimba na kusifu uzuri wa utakatifu wa Mungu, Mungu alishuka na
akaweka waviziao dhidi ya majeshi ya wana wa Amoni, na wana wa Moabu, na
hao wakaao Mlima Seiri na waliangamizwa (2Nyak 20:1-26). Kama Paulo na
Sila walivyoomba na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu usiku wa manane katika
jela ya Kirumi, nguvu ya Mungu ilidhihirika: “Ghafla pakawa tetemeko kuu la
nchi hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka,
vifungo vya wote vikafunguka” (Mdo 16:26).
Tunapomsifu Mungu, uwepo na nguvu zake huja na kutawala mahali iliyopo
sifa (Zab 22:3), ndipo adui yetu huchanganyikiwa na kushindwa. Sifa ni silaha
nyingine yenye nguvu mikononi mwa muumini.
Silaha ya Upendo
Upendo ni moja ya silaha zetu za kiroho na yenye nguvu. Upendo wa kweli
una nguvu za ajabu katika kuwaongoza watu kwa Kristo. Wengine ambao
hawawezi kumwamini Yesu kwa njia ya majadiliano yetu, au kwa njia ya
utendaji wa nguvu wa matendo makuu ya Mungu, wanaweza kuja kwa Kristo
Sura Ya Nane: Silaha Za Vita Vyetu
30Kwa maelezo ya kina kuhusa karama hii angalia sura ya 6, “Roho
Mtakatifu na Huduma Yenye Nguvu”
31Kwa maelezo kamili ya asili na matumizi ya karama za Roho
katika huduma ya nguvu angalia Sura ya 6, “Roho Mtakatifu na
Huduma yenye nguvu.”
82
kwa njia nyepesi ya udhihirisho wa upendo wa kweli. Sauli wa Tarso alimgeukia
Kristo kwa sababu ya udhihirisho wa upendo aliouona katika ushuhuda wa
Stefano. Kwa jinsi mawe yalivyompiga Stefano na kuuondoa uhai wake,
aliomba, “Bwana usiwahesabie dhambi yoyote” (Mdo 7:60). Udhihirisho huo
wa upendo ulikuwa na nguvu sana kwenye ufahamu wa Sauli, na ukamtayarisha
kukutana kwake na Kristo aliyefufuka katika njia ya Dameski. Baadaye, katika
Warumi 12:17, 20-21, Paulo anatuambia jinsi ambavyo sisi pia tunaweza kutumia
silaha hiyo ya upendo:
Msimlipe mtu ovu kwa ovu, angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote… ‘lakini
adui yako akiwa na njaa mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe, maana ufanyapo hayo,
utampalia makaa ya moto kichwani pake.’ Usishindwe na ubaya bali uushinde ubaya
kwa wema.
Hivyo, uovu unaweza kushindwa na wema, na wanaume na wanawake
wanaweza kumjia Kristo kwa silaha ya upendo.
Ubatizo wa Roho Mtakatifu
Katika Matendo 1:8 Yesu alisema ya kuwa wafuasi wake watapokea nguvu
baada ya kuwajilia Roho Mtakatifu. Alikuwa akizungumza habari ya kubatizwa
na Roho Mtakatifu (Mdo 1:4). Jambo hili ni silaha muhimu sana ya vita vya
kiroho.30
Karama za Roho Mtakatifu
Sababu mojawapo kwa nini karama za Roho zilitolewa kwa kanisa (hasa zile
karama tisa za Roho zilizoandikwa katika 1Kor 12:8-10) ni kwa ajili ya vita za
kiroho. Kwa kupitia karama hizi jeshi la Mungu, kanisa, linaweza kupokea amri
na maelekezo kutoka kwa Kamanda wake mkuu (karama za ufunuo); silaha hiyo
inaweza kunena maneno yenye nguvu kutoka mbinguni (karama za unabii); na
kuweza kudhihirisha nguvu za Mungu dhidi ya adui (karama za nguvu).31
Sura Ya Nane: Silaha Za Vita Vyetu
32Kwa maelezo kamili ya asili na matumizi ya karama za Roho
katika huduma yenye nguvu angalia Sura ya 6, “Roho Mtakatifu na
Huduma yenye Nguvu.”
83
Silaha ya Jina la Yesu
Yesu ametupatia Jina lake kama silaya ya kiroho ya kutumika dhidi ya
majeshi ya uovu. Mamlaka yote ya mbinguni inasimama nyuma ya Jina la Yesu.
Na, tutumiapo Jina lake kama alivyoelekeza, sisi pia tunakuwa tunazungumza na
mamlaka ya mbinguni. Nguvu zote za kuzimu lazima zitii Jina ambalo ni juu ya
kila jina (Fil 2:9-11). Sikiliza maneno ya Yesu kuhusu matumizi ya Jina lake:
Amin Amin nawaambieni, yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye
atazifanya; naam na kubwa kuliko hizi atazifanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
Mkiniomba neno lolote kwa jina langu, nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya
mwana. Mkiniomba neno lolote kwa jina langu nitalifanya (Yn 14:12-14).
Tena siku ile hamtaniuliza neno lolote, Amin Amin nawaambia, mkimwomba Baba
neno lolote atawapa kwa jina langu, hata sasa hamkumwomba neno kwa jina langu;
ombeni nanyi mtapata furaha yenu iwe timilifu (Yn 16:23-24).
Mitume mara nyingi walitumia jina la Yesu kuponya wagonjwa, kutoa pepo,
na kuzitenda kazi za Yesu (Mdo 3:6). Sisi pia tunaweza kutumia silaha hii ya
kiroho na yenye nguvu ili kutimiza mambo yale yale.
Silaha ya Injili. Injili, ambayo ni ujumbe wa Kristo, ni silaha kubwa na
yenye nguvu. Katika Warumi 1:16 Paulo anaiita “nguvu ya Mungu iletayo
wokovu kwa kila mtu aaminiye.” Katika mioyo ya wale waisikiao ikihubiriwa.
Injili inapohubiriwa nguvu ya Mungu huachiliwa. Jinsi ilivyo silaya ya ajabu,
kuhubiriwa kwa Kristo!32
MWISHO
Mungu ametupa silaha za kiroho nyingi zenye nguvu ili tuzitumie katika
kupambana na kuzishinda nguvu za shetani. Sisi kama mashujaa wake wa
kiroho, tunahitaji kujifunza jinsi ya kuitumia vema kila silaha.
84
85
Kifungu Cha III
Utendaji Wa Huduma
Yenye Nguvu
86
87
— Sura Ya Tisa —
Jinsi Ya Kuponya
Wagonjwa
UTANGULIZI
Sasa tunaanza kifungu cha tatu na cha mwisho cha mafunzo haya,
kinachoitwa “Namna ya” kuifanya huduma yenye nguvu. Makusudi ya kifungu
hiki ni kukusaidia wewe ujue namna ya kutumia misingi uliyokwisha jifunza
katika vifungu viwili vilivyotangulia. Katika somo la kwanza la kifungu hiki
tutajifunza jinsi ya kuponya wagonjwa; sehemu ya pili tutaangalia jinsi ya kutoa
pepo; katika sehemu ya tatu tutajadili jinsi ya kupambana na kuyashinda
“mapepo ya maeneo”’ na katika somo la mwisho tutajadili jinsi ya kuwaongoza
watu kubatizwa kwa Roho Mtakatifu. Nia yetu ni kujifunza masomo haya vema,
kisha tutaenda kuyatenda yale tuliyojifunza. Mungu akubariki unapoendelea
katika vipindi hivi vitatu vya kuburudisha.
Kama ulivyosoma hapo juu, makusudi ya somo hili ni kutoa maelekezo jinsi
ya kuponya wagonjwa. Njia ambayo tutapendekeza hapa ni ya kimaandiko na
kichungaji. Tunasema ni ya “kimaandiko” kwa sababu inatokana na jinsi
walivyofanya Yesu na mitume. Tunasema ya kwamba ni ya “kichungaji kwa
sababu tutaanza maelekezo kutoka muangalio wa kuchungaji. Tofauti na
mwinjilisti wa mikutano ya nje, mchungaji mara nyingi anahusika na kuomba,
si kwa makundi ya watu kwa ujumla bali kwa mtu mmoja kwa wakati. Mtu
anayemwombea ni mtu anayemfahamu, anayempenda, na anayehusiana naye
katika maisha ya kila siku. Mchungaji wa kweli anahusika sana na mahitaji na
hali ya yule anayemhudumia. Lengo lake ni kwamba,kwa vyovyote vile katika
kumhudumia mtu huyo nia yake ni kumfanya ajisikie na kuona ya kuwa
anapendwa zaidi na Mungu, anapendwa zaidi na kanisa kuliko ilivyokuwa kabla
ya kuanza huduma hiyo kwake. Mchungaji hawezi kumwingia au kufanya
kipapara kwa mtu, wala hawezi kumlaumu au kumlaani kwa kutokuwa na imani,
Sura Ya Tisa: Jinsi Ya Kuponya Wagonjwa
88
bali, kama Yesu atamhudumia siku zote katika upendo huku akijali sana hisia ya
mtu yule.
MATAZAMIO YA AWALI
Kabla hatujajadili mambo mbalimbali yanayohusika na kuponya wagonjwa,
tutaelekeza umuhimu wa matazamio ya awali. Kabla ya yote tutajadili kile
tunachoita “mazingira ya uponyaji.”
Mazingira ya Uponyaji
Kwa kusema “mazingira ya uponyaji” tunakuwa tunazungumzia hali ya
kiroho inayozunguka mahali pa huduma hiyo. Huduma hiyo inaweza kujumuisha
kuponya wagonjwa, kutoa pepo au huduma yeyote inayohitaji udhihirisho wa
nguvu za Roho. Mhudumu anapokaribia kuanza huduma na namna hiyo ni
muhimu kutambua pia swala hilo la mazingira ya uponyaji.
Katika injili yake, Luka alizungumzia habari ya mazingira hayo ya uponyaji
ambayo ilikuwepo katika huduma ya uponyaji ya Yesu. Sikiliza maneno yake:
“Wakakutanika makutano wengi wamsikilize na kuponywa magonjwa yao… Na
uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya” (Luka 5:15, 17). Tambua hapa
kwamba Yesu alihudumu uponyaji katika mazingira yaliyojaa uwepo wa
kimungu: “nguvu ya Mungu ilikuwapo.”
Wakati fulani, alipotoka kumfufua binti Lazaro kutoka kwa wafu,
tunamwona Yesu akijihusisha na mazingira ya kiroho yaliyoizunguka huduma
yake:
Alipokwisha kuingia, akawaambia, mbona mnafanya ghasia na kulia, kijana hakufa,
amelala tu, wakamcheka sana. Naye alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa
babaye wa yule kijana na mamaye, na wale walio pamoja naye, akaingia ndani
alimokuwamo yule kijana, akamshika mkono kijana, akamwambia, ‘Talitha, kumi!
… Mara akasimama yule kijana akaenda.’ (Mk 5:39-42, msisitizo omeongezewa)
Tambua hapa ya kwamba kabla Yesu hajafanya muujiza ule, kwanza
aliwaweka nje wale wote waliokuwa hawaamini na ni kinyume na huduma yake.
Sura Ya Tisa: Jinsi Ya Kuponya Wagonjwa
33Soma Matendo 9:40, utaona Petro akifanya jambo la jinsi hiyo
hiyo alipomfufua Dorkasi kutoka kwa wafu.
34Kwa ajili ya mifano mingine ya uwepo wa Mungu angalia Kutoka
3:1-6; 2Nyakati 7:1-3; Luka 2:8-9; Matendo 2:1-13; Matendo 4:31 na
1Wakorintho 14:22-25.
89
Alikuwa kwa maneno mengine, anatengeneza mazingira ya kiroho.33
Taarifa mbili za injili zinaeleza ya kuwa wakati fulani Yesu alizuiliwa
kuitimiza huduma yake kwa sababu ya mazingira ya kutokuamini. Biblia
inasema kwamba ilikuwa ni nyumbani kwa ke Nazareti,
Wala hakuweza kufanya muujiza wowote huko, isipokuwa aliweka mikono
yake juu ya wagonjwa wachache akawaponya. Akastaajabu kwa sababu ya
kutokuamini kwao. (Mk 6:5-6: Mt 13:58)
Kutokana na matukio haya tunaweza kusema ya kuwa yapo mambo mawili
yanayotujulisha mazingira ya uponyaji:
1. Uwepo wa Mungu. Kwanza, mazingira ya uponyaji yanatambulikana kwa
uwepo wa Mungu. Hapa hatusemi kuhusu tabia ya Mungu kwamba yupo kila
mahali nyakati zote, bali hapa tunasema jambo tofauti kidogo. Tunamaanisha
uwepo wa Mungu unaodhihirika wazi. Uwepo wa jinsi hiyo ulizungumzwa
katika Luka 5:17 hapo juu: “uwepo wa Bwana ulikuwapo apate kuponya.”34
2. Imani yenye Matumaini. Jambo lingine, mazingira ya uponyaji
yanategemea uwepo wa imani yenye matumaini. Imani hii yenye matumaini ni
namna ya imani iliyodhihirika kwa yule mwanamke katika Marko 5:28,
aliposema: “Nikiyagusa mavazi yake tu nitapona.” Imani yenye matumaini ni
imani inayokuwepo wakati watu wanapotegemea muujiza kutoka kwa Mungu.
Mhudumu mwenye hekima anaweza, akahubiri ujumbe wa injili huku akisisitiza
kuhusu imani na uponyaji, akasaidia kuumba imani yenye matumaini katika
mioyo ya watu.
Maandalizi ya Binafsi ya Mtumishi
Hata kama katika Sura ya 5 tumezungumzia kwa ujumla kuhusu matayarisho
kwa ajili ya huduma yenye nguvu, tunaona ni muhimu kuzungumza tena hapa
kuhusu maandalizi kwa ajili ya huduma ya uponyaji. Yapo mambo sita ambayo
Sura Ya Tisa: Jinsi Ya Kuponya Wagonjwa
90
mtu anaweza kuyafanya ili kujiandaa kwa ajili ya huduma hiyo.
1. Omba kwa ajili ya ujazo mpya wa Roho Mtakatifu. Omba hadi
unapousikia upako wake.
2. Jikumbushe Yesu ni nani, amefanya nini na amekuagiza ufanye nini.
Usisahau kwamba ni kwa njia ya Yesu tu, na imani katika yeye, kwamba
ushindi unaweza kuja.
3. Angalia ya kwamba umejishusha “ubinafsi.” Kumbuka ya kwamba,
wewe mwenyewe huwezi kutenda neno lolote (Yn 15:5).
4. Jaribu kuondoka katika mawazo yako mwenyewe kuhusu uponyaji au
ukombozi ambao utatokea. Tambua ya kwamba hakuna huduma mbili
zilizofanana, uponyaji ulikuwa tofauti katika huduma hizo.
5. Muulize Mungu, Je! Unataka nifanye nini? (Angalia: Yn 5:19-20).
Ukiisha tu kugundua mapenzi ya Mungu katika jambo, jitoe kikamilifu
katika mapenzi yake. Ndipo sasa unaweza kuendelea katika ujasiri wa
imani.
6. Mara zote omba katika Roho Mtakatifu, ukisikiliza nyakati zote sauti
yake inavyokuelekeza.
Jinsi Upako wa Huduma Unavyokuja
Katika Sura ya 6, “Roho Mtakatifu na Huduma yenye Nguvu”, tulisema
karama za Roho, hujumuisha karama tatu za nguvu, na huja kama “upako” wa
Roho Mtakatifu. Je! Upako huo unakujaje juu ya mtu kwa ajili ya huduma”
Wengine wameshuhudia uwepo wa nguvu kutoka ndani, au nguvu ijayo kwa
ghafla, “joto,” au “msisimko”. Wengine wanasema upako huja kwa hali ya
huruma nyingi kwa ajili ya yule anayehudumiwa, au uhakika mkubwa ya
kwamba kazi itafanyika. Katika vitabu vya injili mara nyingi tunamwona Yesu
“akijawa na huruma” kabla ya kuponya wagonjwa (Mk l 1:41). (Tutaangalia
somo hili baadaye). Bado wengine hushuhudia ya kwamba pamoja na hisia hizo
za ndani mara nyingine huja “ufahamu” kwamba Mungu anataka uponyaji
ufanyike, au imani ya ghafla yenye uhakika ya kwamba Mungu ataponya au
kutenda muujiza. Hata hivyo upako ukikujia binafsi utahisi katika roho yako
kwamba Roho wa Mungu anatenda kazi katika jambo hilo.
Sura Ya Tisa: Jinsi Ya Kuponya Wagonjwa
91
JINSI YA KUPONYA WAGONJWA
Tunapendekeza hatua tatu za mtindo wa kichungaji wa kuponya wagonjwa.
Hii ni njia ya kawaida ambayo inafanana na huduma ya uponyaji ya Yesu na
mitume. Njia hii inahitaji kujibu maswali matatu ya muhimu kuhusu huduma ya
uponyaji: Je! Ni nini hasa hitaji la mtu? Je! Nitaitendaje huduma? Je!
Nitamshauri vipi mtu huyu baada ya huduma kutendeka:
Hatua Tatu za Mtindo wa kichungaji wa Kuponya Wagonjwa
1. Hatua ya 1: Mahojiano. Hatua ya kwanza katika huduma ya uponyaji ni
kugundua hitaji kamili la mtu. Mara nyingi huwa tunaanza mara moja kuomba,
hata bila kufahamu tuombee jambo gani. Jambo hili ni ujinga na pia ni hatari,
kwa sababu mara nyingi tunaombea jambo lisilohusu tatizo, na matokeo yake mtu
huondoka pasipo kutatuliwa tatizo lake. Kwa hivyo ni lazima tuanze huduma ya
uponyaji kwa kuuliza maswali.
Swali zuri la kuanzia kwa mtu aliyekuja kwa ajili ya hitaji la uponyaji ni “Je!
Ungehitaji Mungu akutendee nini?” Baada ya kuuliza swali hilo, ni vema
tusikilize kwa makini sana jibu la mtu huyo. Tunahitaji kusikiliza kwa njia nne:
kwa masikio yetu, kwa macho yetu, kwa moyo na kwa roho zetu. Kwa masikio
yetu tunamsikiliza vema mtu huyo anasema nini, kwa macho yetu tunaangalia
kama Mungu tayari anatenda nini, na jinsi gani mtu anaonyesha dalili za uitikio
kwa Mungu. Kwa mioyo yetu tunajisikia maumivu yake na tunahisi imani yake;
na roho zetu tunasikiliza kwa makini sana kama Roho wa Mungu anatuambia
nini.
Kabla ya kuendelea na huduma lazima tufanye maamuzi ya aina mbili.
Kwanza, lazima “tutoe uamuzi wa kiuganga,” yaani tuamue tatizo ni nini.
Halafu lazima tufanye “uamuzi wa huduma”; yaani ni kwa jinsi gani tutaendelea
na huduma.
a. Uamuzi wa kiuganga. Katika uamuzi wa kiuganga tunaamua ni nini tatizo
la mtu huyo na ni nini chanzo cha tatizo lake. Kabla ya kuanza huduma ya
uponyaji tunahitaji kujua ni wapi mtu anapoumia, kwa nini ana hali hiyo, na ni
kwa jinsi gani tutaendelea na huduma. Je! Chanzo cha ugonjwa ni cha asili au
ni mapepo. Jibu la maswali hayo litasaidia kuelekeza ni kwa jinsi gani tuendelee
na huduma.
b. Uamuzi wa huduma. Baada ya hapo lazima tuamue tutaendeleaje na
huduma. Jiulize mwenyewe, “Je! Ninahitaji kutoa mapepo au kuomba maombi
ya imani? Kama nitahitaji kuendelea na huduma, nitumie njia gani ya
Sura Ya Tisa: Jinsi Ya Kuponya Wagonjwa
35Mfano wa Yesu alipotoa maelekezo baada ya maombi angalia Yn
5:14; Mk 5:19; na Yn 9:35-39.
92
kimaandiko?” Hapa ni muhimu sana tuendelee kuwa na hisia kali kwa uongozi
na sauti ya Roho Mtakatifu.
2. Hatua ya 2: Kuhusika na Huduma. Hatua inayofuata katika huduma ya
uponyaji ni ile tunayoiita “kuhusika na huduma.” Sasa tunatenda kutokana na
uamuzi wa kiganga na uamuzi wa huduma. Katika hatua hii tunaweza kuendelea
kwa kumwomba Roho Mtakatifu aje na kudhihirisha uwezo wake. Sasa ndipo
tunapohudumu uponyaji kwa njia ya kuweka mikono, maneno ya imani, amri ya
imani, matamko, maombi, mafundisho na uachiliaji wa nguvu, maombi ya
mapatano, kufunga na kufungulia au njia nyingine za Biblia. (Tutajadili kati ya
njia hizi katika sura ijayo).
Ni muhimu kukumbuka ya kwamba tunapoendelea na huduma, ni lazima
tuendelee wakati wote kuwa macho ya kile Mungu anachofanya. Uwe macho
kwa dalili zozote za utendaji wa Roho. Jiulize,”Je! Mungu anafanya nini sasa
hivi katika swala hili?” Unaweza kumuuliza anayehudumiwa kwamba
“Unajisikiaje? Je! Maumivu yametoka, au je! Unahisi kuwa jambo lolote
linatokea?” Jinsi unavyogundua nini Mungu anafanya kwa mtu huyo endelea
kuhudumu, kufuata uongozi wa Roho.
Ni muhimu tusisimame mapema katika huduma hiyo ya uponyaji. Wakati
mwingine uponyaji huchukua muda mrefu (Mk 8:22-25). Endelea kuomba hadi
mtu amepona au unahisi mtiririko wa Roho umesimama.
3. Hatua ya 3: Maelekezo baada ya Maombi. Huduma yetu inakuwa
haijamalizika hadi tumetoa maelekezo baada ya huduma hiyo ya maombi kwa
mtu tuliyemwombea. Yesu pia alifanya hivyo.35 Kama mtu amepokea uponyaji,
mtie moto aendelee katika imani na utii. Kama amepona kwa sehemu tu -- na hii
ndivyo ilivyo mara nyingi --mtie moyo amwamini Mungu kwa ajili ya utimilifu
wa uponyaji huo. Kama hapokei uponyaji, mhakikishie kuwa upendo wa Mungu
na nguvu ya uponyaji wa Yesu vinaendelea. Mhakikishie ya kuwa utaendelea
kumwombea na unaamini Mungu pamoja naye kwa uponyaji wake. Pia unaweza
kumwambia arudi tena kwa kipindi kingine cha maombi.
Sura Ya Tisa: Jinsi Ya Kuponya Wagonjwa
36Jim Miller, “Jinsi ya kuponya wagonjwa, (maandiko
yasiyochapishwa), uk.3.
93
Jinsi Yesu Alivyoponya Wagonjwa (Njia ya Biblia ya Kuponya Wagonjwa)
Je! Yesu aliwaponyaje wagonjwa? Hili ni swali la muhimu kwa sababu Yesu
ndiye mfano wetu kwa ajili ya huduma. Tukiichunguza huduma ya uponyaji ya
Yesu, hiyo inakuwa ndio mfano wa huduma zetu za uponyaji.
Kuhusu huduma ya uponyaji ya Yesu, Jim Miller amesema: “Jambo la
muhimu ambalo linajionyesha lenyewe unapochunguza njia ambazo Yesu
aliponya wagonjwa: Hakuwaponya wagonjwa kwa namna ile ile mara mbili.
Hata hivyo pia ni muhimu kuona ya kwamba alitumia njia kadha tu, hakutumia
zaidi ya njia kumi mbalimbali”36 Katika ratiba zake mbili, “Huduma ya Uponyaji
ya Kristo na “Njia Zilizotumika na Kristo katika Huduma yake ya Uponyaji,”
Miller anaandika ya kwamba vitabu vya injili vinaonyesha rekodi 41 tofauti za
uponyaji wa Yesu (kadhaa zikiwa za uponyaji zaidi ya mmoja). Sehemu kubwa
ya maandiko yanayofuata yalipatikana kwa njia ya kuzisoma ratiba hizo (Angalia
hitimisho ! Na 2)
1. Kusema neno. Njia mojawapo ya Yesu katika kuponya wagonjwa ilikuwa
ni kwa njia ya kutamka neno kwa yule aliyekuwa akiponywa.
• Wakati mwingine hii ilikuwa ni amri kwa mtu mgonjwa kufanya jambo
fulani:
“Simama ujitwike godoro lako, uende” (Yn 5:8);
“Nyosha mkono wako” (Mk 3:5);
“Akasema, kijana, nakuambia, inuka” (Lk 7:14).
• Nyakati nyingine ilikuwa ni amri kwa mapepo:
“Fumba kinywa, mtoke!” (Mk 1:25);
“Ewe pepo mchafu mtoke mtu huyu!” (Mk 5:8);
“Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru mtoke huyu,
wala usimwingie tena: (Mk 9:25).
• Nyakati nyingine alisema moja kwa moja kwa ule ugonjwa au hali ile:
“Nataka takasika!” (Mt 8:3; Mk 8:41);
Sura Ya Tisa: Jinsi Ya Kuponya Wagonjwa
94
“Upewe kuona” (Lk 18:42);
“Funguka!” (Mk 7:34).
• Nyakati nyingine neno lake lilikuwa ni kuitikia kwa ajili ya imani ya
mpokeaji uponyaji:
“Imani yako imekuponya” (Mt 9:22);
• Au tamko rahisi lililoonyesha ya kuwa uponyaji umetokea:
“Umefunguliwa katika udhaifu wako” (Lk 13:12);
“Mwanao yu hai” (Yn 5:50).
2. Kugusa na kuweka mikono. Njia nyingine ya kawaida ambayo Yesu
alitumia kuponya wagonjwa ilikuwa kugusa au kuwawekea mikono wagonjwa:
“Akamgusa mkono, homa ikamuacha” (Mt 8:15);
“Yesu… akawagusa macho yao; mara wakapata kuona. . .” (Mt 20:34);
“Yesu akatia vidole masikioni mwake...akamgusa ulimi. Mara masikio yake
yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikafunguka. . .” (Mk 7:33-35);
“Akaweka mikono yake juu ya kila mmoja, akawaponya” (Lk 4:40).
3. Imani. Nyakati nyingine Yesu alijibu ili kuonyesha ya kuwa imani ilikuwa
ndiyo kiungo kilicholeta uponyaji.
• Nyakati nyingine alitambua imani ya mpokeaji wa uponyaji:
“Enenda… imani yako imekuponya” (Mk 10:52); “Mama, imani yako
ni kubwa, na iwe kwako kama utakavyo.” (Mt 15:28).
• Nyakati nyingine alitambua imani za wengine: “Naye Yesu alipoiona
imani yao [rafiki za aliyepooza]” (Mk 2:5).
4. Huruma. Kama ilivyoandikwa hapo juu, maandiko mara nyingine
huonyesha wazi ya kuwa huruma ni kiungo cha muhimu katika kuponya
wagonjwa:
“Akawahurumia akawaponya wagonjwa wao (Mt 14:14); “Naye
akamhurumia akanyosha mkono wake akamgusa” (Mk 1:41-42);
“Bwana alipomwona alimwonea huruma… akaligusa
jeneza. . .yule maiti akainuka, akaketi akaanza kusema” (Lk 7:13-15).
Sura Ya Tisa: Jinsi Ya Kuponya Wagonjwa
95
5. Kuachilia Nguvu. Biblia inaonyesha waziwazi ya kuwa Yesu alifanya kazi
zake zote katika nguvu za upako wa Roho Mtakatifu (Mdo 10:38; Lk 5:17).
Miujiza yake mingi ilitendeka kutokana na uachiliaji wa nguvu iliyotiririka
kutoka kwake hadi kwenye miili ya wagonjwa na kuleta uponyaji:
“Uweza ulikuwa ukimtoka ukiwaponya wote” (Lk6:19); “Kuna mtu
amenigusa; ninajua kwa sababu nguvu imenitoka” (Lk 8:46).
6. Jina la Yesu. Ulinganifu makini wa uponyaji uliofanywa na mitume katika
kitabu cha Matendo unaonyesha ya kuwa wao pia waliiga njia zake za uponyaji;
hata hivyo, kulikuwepo na ongezeko moja la muhimu. Wao walifanya katika jina
la Yesu (Mk 16:17-18; Mdo 4:10). Leo, sisi pia inatubidi tuige njia za Yesu
pamoja na ongezeko hili la muhimu kabisa—lazima tufanye katika nguvu kuu ya
Jina la Yesu!
MWISHO
Sisi kama watumishi wa Kristo, tumepewa agizo la wazi. Tunatakiwa
tuhubiri injili, na kuponya wagonjwa. Pia , Yesu ametupa mfano mzuri wa jinsi
ya kufanya hivyo. Kazi yetu ni kutoka kwa imani na utii, tukiiga njia zake na
kumtegemea yeye kulihakikisha neno lake kwa ishara zitakazofuatana.
96
97
— Sura Ya Kumi —
Jinsi Ya Kutoa Mapepo
UTANGULIZI
Kanisa linapokwenda duniani na injili, moja ya agenda zake za kazi ni
kupambana na kuzishinda nguvu za giza katika jina la Yesu. Inafurahisha kuona
ya kuwa muujiza wa kwanza wa Yesu ulioandikwa katika injili ya unahusu kutoa
pepo (Mk 121-27), na pia ishara ya kwanza itakayofuatana na watu walioamini
iliyonenwa katika agizo kuu katika Marko (16-15-18) ni “kwa jina langu watatoa
pepo...” (Mstari 17). Katika Sura ya 3, “Huduma yenye Nguvu na Ufalme wa
Mungu,” tulizungumzia jinsi kuja kwa ufalme wa Mungu duniani kutakavyoleta
mapambano na shetani na majeshi yake ya mapepo. Majeshi haya ya uovo
yatapinga kuja kwa ufalme wa Kristo iwe katika eneo la mahali au katika maisha
ya mtu binafsi. Kwa hiyo mapepo ni lazima yapingwe na kutolewa popote pale
yatakapoonekana na mhudumu wa injili
Katika sura ijayo tutazungumzia jinsi ya kushindana na kuyashinda mapepo
yanayowaonea na kuwaweka katika hali ya utumwa watu wa eneo la mahali
fulani. Katika sura hii tutazungumzia jinsi ya kuyatoa mapepo yaliyopagaa miili
na maisha ya watu tunaokutana nao katika huduma ya injili. Hata hivyo, kabla
hatujajadili jinsi ya kuyatoa mapepo, tutaangalia kwanza kwenye Biblia ili
tugundue jinsi mapepo yalivyo, na jinsi yanavyowapagaa na kuwatesa mateka
wao.
Sura Ya Kumi: Jinsi Ya Kutoa Mapepo
37William O. Donovan, Jr., Introduction to Biblical Christianity
from an African perspective. (Ilorin, Nigeria: Nigeria Evangelical
Fellowship, 1992), uk. 235.
98
KUWAELEWA MAADUI ZETU
Mapepo ni Nini
1. Chanzo cha kuwepo kwa mapepo. Watafsiri wa Biblia wa kiinjili mara
nyingine hukataa kukubaliana kuhusu chanzo cha mapepo. Wengine husema ni
roho wasio na miili wa kizazi kilichokuwepo kabla ya kuumbwa Adamu;
wengine wanabishia na kusema kutokana na ushahidi wa Biblia, mapepo bila
shaka ni wale malaika waliotenda dhambi wakaanguka pamoja na shetani katika
uasi wake dhidi ya Mungu (Mt 25:41; Ufu 12:9). Jambo moja ambalo tunaweza
kuwa na uhakika nalo ni uwepo wa mapepo yenyewe. Biblia, na hasa injili nne,
hazina shaka kuhusu uwepo huo. Pia tuna uhakika wa kazi zake. Kazi hizo
kutokana na Wilbur Odonovan ni pamoja na kuwapa “nguvu watu watenda
dhambi (kama wachawi) wanaotafuta nguvu za kimiujiza dhidi ya watu
wengine.”37 Yesu mara nyingi alipambana na kuyatoa mapepo. Halafu
akatuambia sisi, kanisa lake, tutahusika katika huduma ya jinsi hiyo hiyo (Mk
16:17; Lk 9:1-2).
2. Tabia za Mapepo. Je! Mapepo yakoje? Je! Asili yao na tabia zao zikoje?
Biblia inafundisha mambo yafuatayo kuhusu asili na tabia ya mapepo:
a. Ni viumbe vilivyo hai (Mdo 16:16-17; Lk 4:33-35; 8:28-31; Yak 2:19).
Sio tu nguvu zisizo na uhai, zilizopo au zinazofikiriwa. Ni viumbe halisi vilivyo
hai vyenye ufahamu, utashi
b. Ni roho (Mwa 3:1; Ufu 16:13). Ni roho ambao hawana miili wanatafuta
kuishi katika miili ya wanadamu.
c. Wana nguvu. Wana ufahamu, uwezo na nguvu (Lk 8:29; Mdo 16:16-17;
2Thes 2:9). Lakini hata kama wana nguvu, wakati huo huo nguvu hizo zina
kipimo tofauti na Mungu, ambaye ni mwenye nguvu zote na hakuumbwa, wakati
mapepo yameumbwa na nguvu kiasi. Hayana uwezo kwa namna yoyote wa
kumlingana Mungu.
d. Ni maovu. (Mk 1:23; Efe 6:12). Yana tabia iliyo ya kiwango cha chini
kabisa, ni maovu kupita kiasi, makatili tena yaliyobobea katika kila uovu.
3. Malengo ya Mapepo. Kama wakristo wanavyopenda kutimiza mapenzi
ya Baba yao wa mbinguni, mapepo pia yanatafuta kutimiza mapenzi ya baba yao,
Sura Ya Kumi: Jinsi Ya Kutoa Mapepo
99
shetani. Inaonekana ya kwamba moja ya malengo ya kwanza kabisa ya shetani
ni kujaribu kupambana na Mungu na kumletea madhara ya kumuumiza, mapepo
pia yanashiriki kusudi hilo. Yakijua ya kuwa hayawezi kushindana na Mungu
wala kumdhuru moja kwa moja, shetani na mapepo yake wanajaribu kumdhuru
Mungu kwa njia ya kuwaumiza na kuwatia uwete wale ambao Mungu
anawapenda—kizazi cha wanadamu. Kwa hiyo kusudi la msingi la mapepo ni
kumshambulia mwanadamu (hivyo kinyume cha Mungu) kwa kuiingilia miili ya
wanadamu, nafsi na roho. Hufanya hayo kwa njia kama tatu hivi:
a. Kwa kutafuta wanadamu wayaabudu (1Kor 10:19-21). Mapepo yanataka
abudu ambayo Mungu anastahili.
b. Kwa kutafuta kumweka mtu katika utumwa wa woga, ugonjwa na tabia
mbalimbali zinazomfunga. Kwa namna hii yanaharibu ule mfano wa Mungu
katika mwanadamu.
c. Kwa kumtia upofu mwanadamu katika kweli ya injili (Ebr 2:14; Mdo
10:38; 2Kor 4:4; 2Tim 2:25). Kwa namna hiyo yanamwondoa mwanadamu
katika ushirika na Mungu kwa wakati uliopo na katika umilele.
Katika kitabu chake Introduction to Biblical Christianity from an African
perspective,’ Wilbur O’Donovan, Jr. ameorodhesha shughuli mbalimbali ambazo
mapepo yanajihusisha nazo. Hapa nimeorodhesha kati ya shughuli hizo pamoja
na maelezo yake:
• Udanganyifu. Kwa njia ya uongo mapepo yanaleta chuki, dini za
uongo, na hata mafundisho ya uongo kanisani (Yn 8:44; 1Tim 4:1;
2Pet 2:21).
• Fujo na mauaji. Kama yakiachiwa kutimiza mapenzi yao mabaya
mapepo huleta fujo, madhara, na hata vifo kwa mateka wao (Yn 8:44).
• Mateso. Mapepo hutesa watu na kuwapiga upofu, ububu (Mt 12:22),
uharibifu wa viungo (Lk 13:11-17); ugonjwa (Ayu 2:7; Mdo 10:38),
na kuharibikiwa akili (Lk 8:27-29).
• Zinaa. Biblia mara nyingi huzungumzia jambo la “pepo wachafu”
kuelezea uchafu wao kizinaa na ambavyo yanawasha tamaa za watu
ambao yamewapagaa (Mt 10:1; Mk 1:23; 3:11).
• Kizuia kazi ya Injili. Kama tulivyokwisha kutaja hapo juu, mapepo
hukazana kupinga maendeleo ya injili wakati wowote yapatapo nafasi
(1Thes 2:18; Efe 6:12).
• Kuwavuruga watu wa Mungu (Lk 22:31; 2Kor 12:7). Mapepo hutafuta
njia ya kuwavuruga, kuleta matatizo, kusumbua na kuwakatisha tamaa
Sura Ya Kumi: Jinsi Ya Kutoa Mapepo
38O’Donovan, kurasa 231-235.
100
watu wa Mungu popote yanapoweza.
• Kuendeleza uchawi na kuabudu sanamu (Kumb 32:16-17; 1Sam
15:23). Mara nyingi huwa ni mapepo yanayokuwa nyuma yakiongoza
na kutia nguvu uchawi, na kuabudu mababu kama tunavyoona duniani
leo (1Kor 10:19-20).38
Kupagawa na Mapepo
Mapepo yanatafuta kuwaandama na kuwatawala mateka wao katika njia
kadhaa. Njia kuu ya shambulio la mapepo linaitwa “kupagawa na mapepo”
katika Biblia zetu. Wakati pepo (au mapepo) yanapompagaa mtu, yanamwingia
mtu na kuyatawala maisha yake. Kumtawala huku kunaweza kuwa ni kumtawala
kwa sehemu tu au kumtawala kabisa. Kunaweza kuwa ni kwa muda au kwa
wakati wote. Kupagawa kwa pepo humdhuru mtu katika hali mbaya sana,
zifuatazo ni kati ya hali hizo:
1. Mabadiliko ya mtu, au wingu linalompunguza ufahamu (Mk 9:26).
2. Mamlaka nyingine huzungumza katika mtu aliyepagawa (Lk 8:28-30).
3. Nguvu Nyingi mwilini (Lk 8:29).
4. Elimu isiyoelezeka, au nguvu za kichawi (Mdo 16:16-17).
5. Usumbufu katika mwili (Mk 1:26), ni pamoja na uziwi na upofu (Mt
12:22-30; 9:32-34).
6. Kujidhuru au kujiua (Mk 9:22, 5:5).
7. Kuhamasika au woga wa Kristo na jina lake (Mk 1:24).
Wengine husema ya kwamba mkristo anaweza kupagawa na pepo. Wengine
wanakataa jambo hili. Je! Ukweli ni upi? Je! Mkristo anaweza kupagawa? Jibu
ni, sivyo, mkristo hawezi kupagawa na pepo. Hata kama mkristo anaweza
kujaribiwa, kudanganywa, kushambuliwa na hata kuonewa na mapepo kwa hali
ya nje ya mwili wake, haiwezekani kwa mkristo kupagawa (pepo kuishi ndani
yake/au kutawaliwa ufahamu wake) na pepo. Zipo sababu nne zinazokubaliana
na jibu hili. Kwanza kabisa katika Agano Jipya hakuna rekodi ya mkristo
aliyezaliwa mara ya pili kupagawa au kutolewa pepo. Pili, katika maandiko kuna
sababu kamili za kuamini ya kuwa ukombozi kutokana na mapepo mara nyingi
Sura Ya Kumi: Jinsi Ya Kutoa Mapepo
39Tambua hasa maelezo ya Biblia kuhusu uamsho wa Filipo kule
Samaria katika Matendo 8:5-8.
101
ulitokea wakati wa mtu kuokoka.39 Tatu, hatuoni popote katika nyaraka
kupagawa kukiwa tatizo la wakristo au wakristo wakionywa kuhusiana na jambo
hilo. Na hatimaye, tunahitaji tukumbuke ya kuwa, ingawa mkristo hawezi
kupagawa na pepo, kupagawa kunawezekana kwa mkristo aliyerudi nyuma au
aliyeikana imani. Wengi, katika uzoefu wangu, ambao wanasema ya kuwa
wamewahi kushughulikia “mkristo aliyepagawa na pepo” walikuwa kwa kweli,
wanashughulika na wakristo waliorudi nyuma au walioikana imani.
Shetani, Adui Aliyeshindwa
Katika kushindana na mapepo ni muhimu kushika ukweli wa namna mbili.
Kwanza, lazima tusije tukasahau ya kwamba nguvu ya shetani katika nyakati hizi
imezuiliwa vikali sana na Roho Mtakatifu (2Thes 2:7). Kwa njia ya nguvu za
Roho tunazo nguvu za kumwamuru shetani. Pili, lazima tusije tukasahau ya
kwamba, nguvu za shetani na mapepo yake zilivunjwa kabisa pale Kalvari (Yn
12:31). Sikiliza maneno haya ya mtume katika Kol 2:15: “Akiisha kuzivua enzi
na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika
msalaba huo.”
“Nguvu na mamlaka” zilizozungumzwa katika mstari huu ni nguvu za shetani
na mapepo duniani. Msalabani Yesu alivunja mgongo wa shetani. Shetani na
mapepo yake sasa ni maadui walioshindwa kwa sababu ya kazi kuu ya Yesu pale
msalabani.
JINSI YA KUTOA PEPO
Sasa tunaelekea katika kichwa cha kutoa mapepo. Kabla hatujasema kuhusu
jinsi ya kutoa mapepo, lazima kwanza tuzungumze kuhusu mhudumu mwenyewe
wa ukombozi huo.
Sura Ya Kumi: Jinsi Ya Kutoa Mapepo
102
Mhudumu wa Kutoa Mapepo
Kuna mambo ya muhimu ambayo mtu yeyote anayehitaji kuhusika katika
huduma ya ukombozi anahitaji kufahamu jinsi ya kufanya. Hapa chini
yameorodheshwa mambo matano ya muhimu kwa mhudumu wa ukombozi huo:
1. Lazima atambue kuwa kutoa pepo ni vita kamili na ya uhakika, dhidi ya
shetani, hivyo asichukulie vita hiyo kirahisi tu.
2. Kwa sababu vita ni ya kiroho, ni muhimu sana awe amejazwa na Roho
Mtakatifu.
3. Lazima pia awe amejitoa kabisa kuwa chini ya mapenzi ya Mungu
(Yak.4:7).
4. Lazima awe na ufahamu kamili juu ya silaha za vita vyake (Efe 6:10-18)
na pia lazima afahamu jinsi ya kutumia silaha hizo katika vita vyake.
5. Lazima awe na imani iliyo hai katika ushindi wa Kalvari, damu ya
Kristo, na ushindi uliomo katika Kristo.
Kuhudumia Ukombozi Kutokana na Mapepo
Sisi kama watumishi wa Kristo, tumetumwa na kuvikwa silaha ili kuhudumu
ukombozi kwa wale ambao wameonewa na nguvu za mapepo. Kumbuka, Yesu
ni mfano wetu na kiongozi wa vita hivyo vya kiroho Angalia: Luka 4:18-19; 31-
37) na ametuagiza tumfuate katika vita hivyo (Marko 16:15-18).
Sio tu kwamba Yesu ametuagiza, bali pia ametupatia silaha za kuhudumu
ukombozi kwa walioonewa. Kwa njia ya kujazwa karama za Roho Mtakatifu
(yaani karama za ufunuo, hasa ile ya kupambanua roho) tumepewa uwezo wa
kuwatambua na kuwaweka wazi mapepo. Pia tumepewa nguvu na mamlaka ya
kuwaamuru na kuwatoa mapepo (Luka 9:1-2; 10:17-19).
Jinsi ya Kutoa Mapepo
Kutoa mapepo na kuvunja vifungo vya mapepo ni kazi ya Mungu kwa njia
ya Roho Mtakatifu. Ni ishara ya uwepo wa ufalme wa Mungu na pia ni
udhihirisho wa nguvu na ubwana wa Yesu juu ya dunia hii. Kama ilivyo katika
uponyaji wa wagonjwa, mambo matatu yafuatayo yanahusika katika ukombozi:
1. Mahojiano (uvumbuzi). Endapo mahojiano yanawezekana -- ingawa huwa
siyo hivyo mara nyingi -- basi hapo itakuwa ndiyo hatua ya kwanza katika
shughuli ya ukombozi. Ni katika hatua hii ya kutaka kugundua tatizo ambapo
kwa njia ya karama ya kupambanua ruho, tunaweza kugundua uwepo wa kazi ya
mapepo. Pia mara nyingine mapepo yakihamakishwa na uwepo wa Mungu,
Sura Ya Kumi: Jinsi Ya Kutoa Mapepo
103
hujidhihirisha yenyewe kama yalivyofanya katika huduma ya Yesu (Mk 1:23;
5:6-7).
Kabla ya ukombozi kuanza, mara nyingi ni vema, inapowezekana kumhitaji
yule anayehitaji kukombolewa kujikabidhi kwa Mungu. Mwongoze kwa njia ya
maombi, sala ya toba na kuzitubia dhambi zake, hasa dhambi zile ambazo
zinakaribiana au kuhusiana na kufungwa kwake mapepo. Hapa ni lazima azikane
kwa ujasiri pia ayakatae mapepo, na kazi zote za mwili katika maisha yake.
2. Utendaji wa huduma. Kufikia sehemu hii mhudumu anaweza sasa kuingia
katika huduma yenyewe ya mapambano dhidi ya nguvu za mapepo. Anaweza
kuamua kuanza kuliitia jina la Yesu na kuja kwa Roho Mtakatifu. Mara
anapohisi uwepo wa Mungu anaweza kuendelea kutoa pepo. Moja au zaidi ya
njia moja kati ya zifuatazo zaweza kutumika:
• Anaweza kuyafunga mapepo katika jina la Yesu (Mt 16:17-19; 18:18).
• Anaweza kuyaamuru mapepo yatoke, au yamwachilie mtu huyo (Lk
4:35).
• Anaweza pia kuyaamuru mapepo yasimrudie mtu huyo tena (Mk 9:25).
Nyakati nyingine huwepo mapambano na kukatalia kwa mapepo (Lk 8:29;
11:14). Katika hali kama hizo mhudumu lazima akakamae kwa imani hadi
ushindi utakapokuja. Ukombozi mara nyingi huandamana na udhihirisho wa
mapepo kwa aina nyingi (Lk 4:33-35; 9:42; Mk 7:30). Katika hali kama hizo
mhudumu anatakiwa asitahayari wala asiyumbishwe na mbwembwe za namna
hiyo, bali aendelee na mapambano katika nguvu za Roho, ili kuyanyamazisha
mapepo (Mk 1:25;34), na katika mamlaka aliyonayo katika Kristo, kuyaamuru
yatoke na kwenda (Mk 9:25).
Full Life Study Bible (tafsiri mojawapo ya Biblia), katika “Nguvu dhidi ya
shetani na mapepo” imetoa hatua zifuatazo kuchukuliwa katika kuwakomboa
watu kutokana na vifungo vya mapepo:
• Tambua ya kuwa hatumo katika mapambano dhidi ya damu na nyama
bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili (Efe 6:12).
• Ishi mbele za Mungu ukiwa umejitoa katika kweli na haki (Rum 12:1-2;
6:14).
• Uwe na imani kwamba nguvu za shetani zinaweza kuvunjwa katika
sehemu yoyote ile ya ufalme wake (Mdo 26:11; Efe 6:16; 1Thes 5:8),
Pia utambue ya kwamba mkristo ana silaha za kiroho na zenye nguvu
Sura Ya Kumi: Jinsi Ya Kutoa Mapepo
40Full Life Study Bible, New Testament, “Power over Satan and
Demons”, uk. 81.
41Angalia Sura ya 12, “Jinsi ya kuomba na watu wajazwe na Roho
Mtakatifu.”
104
ambazo Mungu amezitoa kwa ajili ya kuharibu ngome ya shetani (2Kor
10:4-5).
• Tangaza injili ya ufalme katika nguvu za Roho Mtakatifu (Mt 4:23; Lk
1:15-17; Mhu 1:8, 2:4; 8:12; Rum 1:16; Efe 6:15).
• Pingana na shetani ana kwa ana kwa kuamini katika jina la Yesu (Mdo
16:16-18). Kwa kutumia neno la Mungu (Efe 6:17), kwa kuomba katika
Roho (Mdo 6:4; Efe 6:18). Kwa kufunga (angalia Mt 10:1; 12:28;
17:17-21; Mk 16:17; Lk 10:17; Mdo 5:16; 8:7; 16:18; 19:12; . . .).
• Omba hasa ili Roho Mtakatifu aihukumu mioyo ya walipotea kuhusu
dhambi, haki na kuja kwa hukumu (Yn 16:7-11).
• Omba na uwe na shauku ya udhihirisho wa Roho kwa njia ya karama za
uponyaji, lugha, miujiza, ishara na maajabu (Mdo 4:29-33; 10:38; 1Kor
12:7-11).40
3. Maelekezo baada ya maombi. Hatua ya mwisho katika ukombozi wa
mapepo ni maelekezo baada ya maombi na ushauri. Mara nyingi mtu anapokuwa
chini ya kutawaliwa au chini ya nguvu ya mapepo, ushauri na msaada wa
maombi baada ya huduma ni vitu vya muhimu. Mtu huyo anahitaji maombi
mengi, ushauri na misaada mingine ya kumjenga. Huu badi sio muda wa
kumwacha tu mtu huyo; ni wakati wa kumwonyesha kumjali kwa upendo. Pia
ni muhimu mara moja kupima hali yake ya kiroho. Kama hajaokoka au kuzaliwa
mara ya pili, basi ni vema aongozwe mara moja katika hatua za wokovu. Lazima
pia tumwongoze mtu huyo katika hatua za kubatizwa katika Roho Mtakatifu.41
Yesu alionya kwa vikali jambo la kuzembea mambo haya muhimu:
Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa
kupumzika asipate. Halafu husema, nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata
akija, aiona tupu, imefagiwa na kupambwa. Mara huenda akachukua pamoja naye
pepo wengine saba walio waovu kuliko mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na
mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. (Mat 12:43-45a)
Sura Ya Kumi: Jinsi Ya Kutoa Mapepo
105
Hivyo ni muhimu kwamba hali ya kiroho ya mtu ishughulikiwe baada tu ya
ukombozi dhidi ya mapepo. Mhudumu lazima abakie na mawasiliano ya karibu
na mtu huyo hadi akombolewe kabisa kutokana na kifungo.
MWISHO
Kama wahudumu wa injili tumeamriwa kutoa mapepo. Lazima tufanye
hivyo katika nguvu na upako wa Roho na katika njia ambayo inaonyesha upendo
na heshima kwa watu wale tunaowahudumia.
106
42Kwa sababu wengi wa roho hao wachafu wamepangiwa kutawala
sio tu maeneo ya kijiografia, bali pia watu, jamii, mara nyingine huitwa
“mapepo watawalao” au mapepo ya jamii.”
107
— Sura Ya Kumina Moja —
Jinsi Ya Kupambana Na
Kuyashinda Mapepo
Na Maeneo
MAPEPO YA MAENEO NI NINI?
Tunapotumia neno “mapepo ya maeneo” tunazungumzia kuhusu mapepo
kama tulivyozungumza katika Sura ya 10; ingawa katika hali hii tunazungumzia
mapepo yenye maagizo ya namna nyingine na yale yanayowaonea wanadamu.
Tunazungumzia kuhusu mapepo yanayotawala na kuhusika na tabia mbalimbali,
sio za watu binafsi, bali juu ya maeneo fulani, makundi ya watu, au jamii.42
Mapepo Yana Ngazi na Vyeo
Biblia inafundisha wazi ya kwamba mapepo fulani yana vyeo mbalimbali na
kazi mbalimbali:
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na
mamlaka, juu wa wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika
ulimwengu wa roho (Efe 6:12, angalia pia Kol 2:15).
Uchunguzi zaidi wa Biblia unatuonyesha ya kwamba kati ya mapepo hayo
yanayotawala yamepangiwa maeneo fulani, jamii, watu, vikundi, makabila, n.k
katika dunia nzima. Kutokana na C. Peter Wagner, “shetani hupanga au kutoa
Sura Ya Kumina Moja: Jinsi Ya Kupambana Na Kuyashinda Mapepo Na Maeneo
43C. Peter Wagner, “Territorial Spirits,” Wrestling with Dark
Angels, ed., C. Peter Wagner and F. Douglas Pennoyer, (Ventura
California: Regal Books, 1990), uk. 77.
44Wesley Deuwel, “Touth the World Through Prayer, (Grand
Rapids, MI: Francis Asbury Press, 1986), kurasa 104-105.
108
mamlaka ya juu kwa mapepo yake ya ngazi za juu kutawala nchi, mikoa, miji,
watu, vikundi, vitongoji na sehemu za starehe za jamii ya watu katika dunia
nzima.”43
Katika kitabu chake, “Touch the World through Prayer,” Wesley Beuwel
amesema kuhusu ngazi za vyeo vya mapepo:
Jinsi shetani alivyoyapanga mapepo katika ufalme wake hatuwezi kufahamu.
Maandiko yanatumia majina kadhaa kwa mapepo hayo, katika njia inayoonyesha
yako chini ya utawala wa shetani. Hapa kuna kati ya majina hayo katika Kiyunani
pamoja na sehemu ambapo maneno hayo yametumika katika Biblia:
Maneno haya yanaweza kuelezea ngazi mbalimbali za mamlaka au vyeo mbalimbali chini
ya shetani. Jambo la muhimu ni kwamba hao wote wanazo nguvu za kiasi tu, ufahamu,
na pia maeneo ya shughuli. Wahusika wa ngazi hizo zote walishindwa na Kristo
msalabani. Na wote wanafahamu kuwa wanasubiri hukumu yao ikatayofuatiwa na
hukumu ya milele (Mt 8:29).”44
archa wafalme (1Kor 15:24; Efe 1:21; 3:10; 6:12; Kol
1:6; 2:10, 15)
exousiai mamlaka (1Kor 15:24; Efe 1:21; 3:10; 6:12; Kol
1:16)
dunameis nguvu (Rum 8:38; 1Kor 15:24; Efe 1:21)
kuriotes usultani (Efe 1:21; Kol 1:16)
ubwana
throni viti vya enzi (Kol 1:16)
archontes watawala (1Kor 2:6)
kosmokratores wafalme wa dunia (Efe 6:12)
Sura Ya Kumina Moja: Jinsi Ya Kupambana Na Kuyashinda Mapepo Na Maeneo
45George Otis, Jr., The Last of the Giants, (Tarrytown, NY: Chosen
Books Publishing, 1991), uk. 88.
46Ibid, uk. 94.
109
Shetani ni Kamanda Wao Mkuu Hawa pepo watawala wako chini ya uongozi
wa kamanda wao mkuu, shetani, kwa kuwa Biblia inasema, “Twajua … dunia
yote pia hukaa katika yule mwovu: (1Yn 5:19). Kwa neno “dunia yote
(Kiyunani, kosmos) Biblia hapa inazungumzia kuhusu mitindo yote
inayoendeshwa kidunia, hii ni pamoja na tawala za siasa, dini, elimu, jamii,
uchumi n.k. Kutokana na George Otis, Jr., “Lengo la shetani… ni kuupata
utawala juu ya maisha ya wanadamu kwa kutawala njia zote za dunia—siasa,
uchumi na dini—ambazo wamezitengeneza.”45
Shetani hutawala kwa kupitia mtandao wenye nguvu wa mapepo “falme” …
mamlaka… wakuu wa giza hili … na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu
wa roho (Efe 6:12). Otis anaendelea kusema kuhusiana na mtandao huo wa
utawala wa mapepo:
Leo mpangilio wa mapepo ya uovu umetanda juu ya dunia nzima ili kutawala
maeneo na watu walio tayari chini ya utawala wa shetani na kupiga vita dhidi ya
wale ambao bado hawajawa chini ya utawala huo. Katika maandiko ‘watu wenye
nguvu’ (mapepo yenye ngazi za juu) yanatajwa majina kufuatana na maeneo ambayo
yanashikilia. Hii ni pamoja na ufalme wa Uajemi (Daniel 10:13), mkuu wa Uyunani
(Daniel 10:20, mfalme wa Tiro (Ezekiel 28:12), Babeli mkuu (ufu 17:3-5). Sehemu
nyingine mtawala wa giza ametumia jina la miungu ya eneo fulani kama Beli katika
Babeli (Yer 51:44), Baal-Zebubu wa Ekroni (2Waf 1:2-3), na Apolioni wa kuzimu
(ufu 9:11).46
Katika hitimisho, mapepo ya maeneo ni mapepo ya ngazi za juu yaliyopewa
kutawala maisha ya watu kwa kutawala maeneo au jamii ambapo wanakaa.
JE NI NINI KAZI NA SHUGHULI ZA
MAPEPO YA MAENEO?
Kazi za Mapepo ya Maeneo
Kama ilivyotajwa hapo juu, kazi ya awali ya mapepo ya maeneo ni
kuyashikilia maeneo fulani na kuwaweka watu katika utumwa. Pia yanawatia
Sura Ya Kumina Moja: Jinsi Ya Kupambana Na Kuyashinda Mapepo Na Maeneo
47F. Douglas Pennoyer, “Dungeons of Collective Captivity,
Wrestling with Dark Angels, (City: Publisher, Date), uk 250.
110
watu ugumu wa kutoiamini injili na kuokoka (2Kor 4:4). Njia mojawapo
wanayofanya ni kutawala au kuwa na uwezo juu ya viongozi na serikali (angalia
Ufu 16:14). F. Douglas Pennoyer amezungumzia juu ya “utumwa wa pamoja,”
uliowekwa juu ya watu na mapepo ya ngazi za juu. Njia moja ambayo mapepo
hayo yanaweza kutawala eneo au jamii, anasema, ni kwa kuwatawala na
kuwaongoza watu wa jamii hizo:
…mapepo yanapofanya kazi kupitia watu yanaweza kutawala jamii na kutumia
uongozi wa mahali pale kuzuia injili kupenya katika maisha ya jamii ile… Lengo la
mapepo ni kuwaweka wawe watumwa katika vifungo vya shetani, katika namna ya
utumwa wa pamoja unaokatisha tamaa watu binafsi kujikomboa kwa kupasua katikati
ya ufungwa huo hadi kwenye ufalme wa nuru.”47
Kazi za Mapepo ya Maeneo
Je! Mapepo haya yanazuiaje jamii kutoka katika nuru? Njia moja ni kwa
kuwafunga watu kutokana na kweli ya injili:
Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani
yao mungu wa dunia hii amepofusha fikra zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili
ya utukufu wake Kristo aliye sura ya Mungu (2Kor 4:3-4).
Shetani anawezaje kupofusha fikra za ufahamu wa watu billioni tano dunia
nzima? Akiwa ni kiumbe aliyeumbwa hawezi kufanya hivyo peke yake; lazima
afanye hivyo kupitia mtandao wa utawala na uongozi wa mapepo.
Njia nyingine ambayo shetani anatawala maeneo na jamii ni kwa njia ya asili
ya dhambi iliyo katika watu wote kwa kuwafanya wazame katika hali ya dhambi.
Watu na jamii wanavyozidi kushuka kiwango chao cha utu pia watazidi
kufungwa. Hiyo ndiyo njia yatumiayo mapepo ya maeneo.
JINSI YA KUPAMBANA NA KUYASHINDA
MAPEPO YA MAENEO
Sawasawa na mapepo yote, mapepo ya maeneo yanaweza kupingwa katika
nguvu na mamlaka ya Jina la Yesu. Kuna njia tatu ambazo tunaweza kupambana
Sura Ya Kumina Moja: Jinsi Ya Kupambana Na Kuyashinda Mapepo Na Maeneo
111
na kuyashinda mapepo haya yatawalayo ili injili iweze kupenya maeneo
yasiyofikiwa.
Kwa “Vita Kali ya Maombi”
Njia ya kwanza ambayo tunaweza kupambana na kuyashinda mapepo ya
maeneo ni kwa kile kilichoitwa “vita kali ya maombi.” Katika namna hii ya
maombi tunakuja kinyume cha mapepo haya tawala katika jina la Yesu na katika
nguvu ya Roho Mtakatifu. Kama vile tunavyoamuru mapepo yanayowatesa
watu, tunayaamuru mapepo haya pia kuachilia utawala wao juu ya maeneo na
jamii. Tunapofanya hivyo tunaita pia nguvu za Roho Mtakatifu kuleta uamsho
katika maeneo hayo ya watu. Uwepo wa Roho Mtakatifu utafanyika kizuizi kwa
nguvu za mapepo (2Thes 2:7). Maombi ya jinsi hiyo mwisho wake utakuwa
“milango iliyofunguka” kama mara nyingi inavyotajwa katika maandiko.
(Angalia 1Kor 16:9, 2Kor 2:12; Kol 4:3; Ufu 3:8). Kabla ya kuingia nchi, eneo,
mji, kitongoji, au kijiji kuihubiri injili, ni hekima kwamba tupange muda kamili
kwa ajili ya vita kali ya maombi ya jinsi hii.
Kwa Kumfunga Mtu mwenye Nguvu
Njia ya pili ambayo tunaweza kupambana na kuyashinda mapepo ya maeneo
ni kwa njia ya “kumfunga mtu mwenye nguvu.” Yesu alisema kuhusu kutumia
silaha hii ya kiroho katika Mathayo na Luka:
Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha
kuwajilia. Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na
kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo ataviteka
vitu vyake (Mt 12:28-29).
Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake ni
salama; lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda
amnyang’anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea na kuwagawa mateka yake
(Lk 11:21-22).
Je! Ni nani mtu huyu “mwenye nguvu” ambaye Yesu anazungumzia katika
sehemu hii ya maandiko? Ni pepo mwenye nguvu anayetawala au mtu binafsi,
jamii au eneo fulani. Tambua kuwa Luka 11:21 anazungumzia pepo huyu
mwenye nguvu akiwa “amejifunga silaha.” Nyumba ya mwenye nguvu yaweza
kuwa au mwili wa mtu ambamo roho huyo hukaa au eneo fulani analotawala.
Vitu vyake ni roho za wanaume na wanawake aliowashikilia mateka.
Sura Ya Kumina Moja: Jinsi Ya Kupambana Na Kuyashinda Mapepo Na Maeneo
112
Kutokana na mistari hii miwili ya maandiko, tunajifunza namna mbili
muhimu kuhusu kupambana na kuyashinda mapepo ya maeneo.
1. Kwanza tunajifunza ya kuwa mapepo ya maeneo yanatolewa kwa Roho
wa Mungu (Mt 12:28). Katika Luka 11:21 Yesu anaelezea Roho wa
Mungu kama “mmoja mwenye nguvu zaidi” kuliko pepo ambaye ni mtu
mwenye nguvu. Ni kwa njia ya nguvu za Roho tu ndipo tunaweza
kuyashinda hayo mapepo yenye nguvu.
2. Tena, tunajifunza ya kwamba tunamshinda mtu mwenye nguvu kwa
kuingia nyumbani mwake na “kumfunga.” Tunafanya hivyo kwa
kuingia katika eneo la mapepo na kuyaamuru na kuyafunga katika jina
la Yesu na katika nguvu ya Roho Mtakatifu. Katika jina la Yesu
tunaamuru yaachilie utawala juu ya watu yanaowashikilia mateka. Kwa
njia ya nguvu ya Roho na upako, tunayanyang’anya silaha na
kuyamaliza nguvu.
Kwa Njia ya Kuitangaza Injili katika Nguvu ya Roho
Njia ya tatu ya kupambana na kuyashinda mapepo ya maeneo ni kwa
kuitangaza injili katika nguvu ya Roho. Kama tulivyojifunza katika Sura ya 5,
kuna nguvu nyingi mno katika injili ya Kristo. Hakika ni “nguvu ya Mungu
iletayo wokovu.” Watu wanaposikia na kuamini injili, nguvu ya mapepo
kushikilia watu huachilia. Jinsi nuru ya injili inapong’aa zaidi na zaidi katika
mahali, giza linaondolewa na watu wanawekwa huru.
Maelekezo Sita Muhimu ya Kupambana Katika Vita za Kiroho Dhidi ya
Mapepo ya Maeneo
Tunafunga sura hii kwa kupendekeza maelekezo matano muhimu katika
kupambana vita za kiroho dhidi ya mapepo ya maeneo:
1. Uwe na uhakika ya kuwa una uhusiano mzuri na Mungu. Kabla mtu
hajadiriki kupambana na Roho hawa wa giza ni lazima kwanza atambue ya kuwa
ni kweli amezaliwa mara ya pili. Lazima ajue ya kuwa ana maisha mazuri ya
maombi, na pia ya kuwa ana uhusiano wa karibu na Mungu. Kumbuka,
tunahudumu kutokana na uhusiano na Mungu. Ni wale tu ambao kweli
“wanamjua Mungu wao,” watakuwa “hodari na kutenda mambo makuu.” Ili
kupambana na mapepo ya giza mtu ni lazima ajue hasa kumtegemea Mungu.
2. Ukiri na kuziacha dhambi zote uzijuazo. Mtu hawezi kuingia katika
mapambano ya vita vya kiroho bila kuzitubia dhambi zake. Kumbuka Isaya 59:1-2:
Sura Ya Kumina Moja: Jinsi Ya Kupambana Na Kuyashinda Mapepo Na Maeneo
113
Tazama mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa; wala sikio lake si
zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu
wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.”
Kama inawezekana, yeyote atakayepanga kufanya vita ya kiroho lazima
kwanza atafute ukombozi wake binafsi kutokana na dhambi katika maisha yake
mwenyewe. Dhambi yoyote au matendo ya mwili (Angalia: Gal 5:19-21)
yanayoendelea kujitokeza maishani mwa mtu ni mpenyo kwa shambulizi la
mapepo, na ni lazima yashughulikiwe na kuyashinda. Tafuta ukombozi na
uponyaji kabla ya kuanza vita vya kiroho.
3. Jivike silaha zote za Mungu. Katika Waefeso 6:10-18 tumeambiwa
“tujivike silaha zote za Mungu” kabla ya kuhusika katika vita vyovyote vya
kiroho. Kusiwe na askari mjinga ambaye ataingia katika mapambano bila
kwanza kujivika silaha zote za Mungu.
4. Ujazwe na Roho Mtakatifu. Tunatoa mapepo kwa njia ya Roho wa Mungu
(Lk 11:20). Hivyo kabla mtu hajaingia katika mapambano ya kiroho, ni lazima
kwanza abatizwe na Roho Mtakatifu. Zaidi ya hili, lazima pia atembee daima
katika uwepo na nguvu za Roho.
5. Uwe tayari kudumu katika maombi hadi ujapo ushindi. Kama katika kila
vita, ushindi haupatikani katika vita moja. Kama Daniel lazima tuwe tayari
kuvumilia katika maombi hadi ushindi upatikane (Angalia: Dan 10:2:12).
6. Changanya maombi na mahubiri ya injili yenye upako yakifuatiwa na ishara na
maajabu ya kibiblia. Hatimaye, lazima tufahamu ya kuwa wokovu na ushindi vyaweza
kuja tu katika eneo lililo chini ya uonezi wa mapepo wakati maombi yakichanganywa na
mahubiri ya injili katika nguvu za Roho ikifuatana na ishara na maajabu.
114
115
— Sura Ya Kumi na Mbili —
Jinsi Ya Kuomba Na Watu
Ili Wajazwe Na Roho
Mtakatifu
UTANGULIZI
Katika Sura ya 6, “Roho Mtakatifu na Huduma yenye Nguvu,” tulizungumzia
umuhimu wa kubatizwa katika Roho Mtakatifu inavyowiana na huduma yenye
nguvu. Tulisema kwamba kabla mtu hajajihusisha na huduma yenye nguvu,
lazima aelewe na kubatizwa katika Roho Mtakatifu. Katika sura ile ile
tulizungumzia jinsi mtu anavyoweza kujazwa na Roho wa Mungu. Katika somo
hili tutazungumzia jinsi ambavyo tunaweza kuwaongoza wengine katika jambo
hili la muhimu la kikristo.
Katika sura hii tutaelekeza kwa vitendo “namna ya” kuomba na watu
wanaohitaji kubatizwa na Roho Mtakatifu. Mwandishi ametumia njia hii ya
kuombea watu kote marekani na Afrika, na binafsi ameshuhudia mamia ya watu
wakijazwa na Roho.
Wengine wameuliza endapo ni vyema kuwaelekeza watu jinsi ya kujazwa na
Roho Mtakatifu. Katika kitabu kiitwacho Pneumatology Stanley Horton anasema
kuhusiana na swala hili: “Je! Unaweza kusema ni vibaya kuwapatia watu
maelekezo kuhusu kumjia Kristo Mbatizaji na kumwelekezea imani zao?”
Anajibu swali lake mwenyewe: “Wakristo wengi wanafikiria kuwa hakuna jambo
lolote baya kuhusu kuwapatia watu maelekezo ya jinsi ya kuokoka, Kwa
Sura Ya Kumi na Mbili: Jinsi Ya Kuomba Na Watu Ili Wajazwe Na Roho Mtakatifu
48Stanley M. Horton, Pneumatology, A Study Guide (Irving, TX:
ICI University, 1993), kurasa 241-242.
116
nini basi tusiwasaidie watu kubatizwa?”48 Kweli ukihitaji kuwaona watu
wakijazwa na Roho katika huduma yako, itakuwa ni muhimu kwako
kuwafundisha na kuhubiri juu ya somo hili mara nyingi. Kabla hatujazungumzia
dondoo kuhusu jinsi ya kuomba na mtu ili ajazwe na Roho, kwanza
tutashughulika na matazamio ya awali.
MATAZAMIO YA AWALI
Kabla mshauri wa kiroho hajaomba na mtu ili ajazwe na Roho yapo mambo
mawili muhimu ambayo ni vizuri ayaelewe. Lazima afahamu ni nani ambaye
anaweza kujazwa na Roho na pia ni nani astahiliye kuombea wengine wapate
kujazwa na Roho. Lazima pia aelewe mambo manne muhimu yanayohusika
katika mtu kujazwa na Roho Mtakatifu.
Ni Nani Anayeweza Kujazwa na Roho Mtakatifu?
Kabla ya yote, lazima ufahamu kuwa yeyote aliyezaliwa mara ya pili kweli
anastahili na anatakiwa mara moja ajazwe na Roho. Jambo hili sio la watu fulani
tu waliofikia ngazi fulani ya “utakatifu” au kukua kiroho katika maisha yao ya
kikristo. Wala sio kwa ajili ya daraja fulani la watu ambao ni wa kanisa fulani
au dhehebu. Ni ahadi ya wakristo wa nyakati zote (Mdo 2:17, 18; 38, 39).
Je! Ni Nani Wanaostahili Kuombea Wengine Ili Wajazwe na Roho?
Tena, mshauri wa kiroho inabidi aelewe ya kuwa yeyote ambaye yeye
mwenyewe amejazwa na Roho anaweza kumuongoza mwingine katika jambo
hili. Hitaji kubwa kwa ajili ya kuombea wengine wapate kujazwa na Roho ni ile
shauku ya kweli ya kutaka kuona wengine wakibarikiwa na kutumika na Mungu.
Hatua Zinazohusika katika Kupokea Roho Mtakatifu
Zipo hatua nne za muhimu zinazohusika kwa mtu yeyote anayejazwa na
Roho Mtakatifu: Shauku, imani, sifa na kujitoa kwa Mungu. Hebu tuangalie kwa
kifupi moja ya kila hatua hizi.
1. Shauku. Tumekwisha kuzungumzia shauku au nia kuhusiana na kubatizwa
Sura Ya Kumi na Mbili: Jinsi Ya Kuomba Na Watu Ili Wajazwe Na Roho Mtakatifu
117
katika Roho Mtakatifu katika Sura ya 6. Unaweza kutaka kurejea mazungumzo
yale wakati huu. Biblia mara nyingi huwekea mkazo na umuhimu wa kiu au
shauku katika kupokea baraka za Mungu. Wakati mmoja alipokuwa akifundisha
jinsi ya kujazwa na Roho, Yesu alisema, “tafuta [yaani, “endelea kutafuta”] nawe
utaona” (Lk 11:9). Kutafuta bila kuchoka ni tunda la kiu au shauku. Mungu
ametuambia, “nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu
wote (Yer 29:13). Mwelekeze mtafutaji ya kuwa lazima awe na shauku kwa
moyo wake ili kujazwa na Roho Mtakatifu.
2. Imani. Imani ni jambo muhimu sana katika kupokea lolote kutoka kwa
Mungu—pamoja na Roho Mtakatifu. Katika Wagalatia 3:2 Paulo
anawakumbusha wakristo wa Galatia ya kuwa walimpokea Roho Mtakatifu, sio
kwa matendo ya sheria, bali kwa kuyaamini yale [waliyo] yasikia.” Nia moja ya
mtu atakaye kuwaongoza wengine katika ubatizo wa Roho ni kujenga imani
katika mioyo ya watafutaji. Tutazungumzia zaidi kuhusu hili baadaye.
3. Sifa. Katika kila wakati watu waliokuwa wanajazwa kwa Roho katika
kitabu cha Matendo tunawaona wakiwa na juhudi na furaha wakimsifu Mungu.
Biblia inatufundisha kuwa kabla ya siku ya Pentekoste mitume “walikuwa daima
ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu” (Lk 24:53). Biblia pia inatufundisha
kwamba, “Mungu [huketi] juu ya sifa za Israeli” (Zab 22:3). Tunapomsifu
Mungu anadhihirisha uwepo wake katikati yetu (2Nyak 7:1-3; Mdo 4:31). Njia
nyingine ya mtu atakaye kuwasaidia wengine wajazwe na Roho ni kuwafanya
wamtukuze na kumsifu Mungu kwa furaha na imani yenye matumaini.
4. Kujitoa kwa Mungu. Kujitoa kwa Mungu ni jambo jingine la muhimu
katika kumpokea Roho. Mtu atakaye kujazwa na Roho ni vema aelekezwe jinsi
ya kujiachilia kabisa kwa Mungu. Kujiachilia huku kuhusishe roho yake,
mawazo yake na mwili wake (Rum 6:13; 12:1). Ni kwa njia hiyo ndipo Roho
Mtakatifu atatawala mawazo ya mtu pamoja na viungo vyake vya sauti na kuanza
kunena kwa njia yake kwa lugha nyingine.
NJIA: JINSI YA KUOMBA NA MTU ILI AJAZWE
NA ROHO MTAKATIFU
Kama tulivyofanya katika sura za kuponya wagonjwa na kutoa mapepo,
tutafuata njia ya hatua tatu, inayohusisha, mahojiano, maombi, na maelekezo
baada ya maombi.
Sura Ya Kumi na Mbili: Jinsi Ya Kuomba Na Watu Ili Wajazwe Na Roho Mtakatifu
49Kujenga uhusiano na mtu ni kule kuanza joto la uhusiano wa
ujirani watu wawili wakutanapo.
50Kumtia moyo mtu ni kutamka maneno kadhaa kwake
yatakayomfanya ajisikie vizuri yeye mwenyewe au kwa yale
aliyofanya.
118
Hatua ya 1: Mahojiano
Katika hatua ya kwanza ya mahojiano tutajaribu kutimiza mambo manne:
Kwanza tutajaribu kujenga uhusiano na mhusika. Halafu tutajaribu
kumhakikishia na kujenga ujasiri wa imani. Tatu, tutajaribu kugundua hali yake
ya kiroho na kumpenda Mungu. Hatimaye, tutajaribu kumueleza mhusika
afanyeje ili ajazwe na Roho Mtakatifu.
1. Kujenga uhusiano. Nia ya kwanza katika hatua ya mahojiano ni kujenga
uhusiano49 na mhusika. Kama tayari unamfahamu mtu huyo, hili linakuwa halina
umuhimu. Lakini endapo humfahamu kabisa mtu huyo, anza kujitambulisha
mwenyewe kwake. Sema, “Ndugu, jina langu ni fulani, je! Jina lako mwenzangu
ni nani?” Mwangalie machoni (kama jambo hili halina matatizo kijamii), halafu
sikiliza kwa makini kwa yale atakayojibu. Rudia jina lake kwake, halafu tumia
jina lake wakati wote wa kumhudumia.
2. Kumtia Moyo. Halafu, tafuta kumtia moyo50 mtu na kumjenga imani.
Unaweza kusema, “Nimefurahi sana kwamba umekuja; umefanya jambo jema.”
Unaweza pia kusema, “Hii yaweza kuwa siku kubwa katika maisha yako. Mungu
analo jambo la muhimu na la kipekee sana kwako leo.” Kumbuka, mtu huyo
anaweza kuwa bado ana woga hadi muda huu. Maneno ya jinsi hii yanaweza
kumsaidia kuondoa woga na kuuandaa moyo ili kupokea.
3. Uvumbuzi. Lengo moja hapa ni kutafuta ni kwa nini mtu anayehitaji
kujazwa Roho amekuja mbele, na kutambua wazi yupo mahali gani kiroho.
Unaweza kumuuliza maswali kama yafuatayo:
• Je! Unataka Mungu akutendee nini leo?’ au “je! Umekuja ili ujazwe na
Roho Mtakatifu leo?” Usichukulie tu kwamba amekuja kujazwa na Roho.
Anaweza kuwa amekuja kwa sababu nyingine. Kama amekuja kujazwa,
ni vema aseme mwenyewe hivyo. Kwa kusema hivyo kutamtia nguvu
uamuzi wake wa kujazwa.
Sura Ya Kumi na Mbili: Jinsi Ya Kuomba Na Watu Ili Wajazwe Na Roho Mtakatifu
51Mengi ya maelekezo haya yanaweza kutolewa katika mahubiri
kabla ya muda wa huduma.
119
• “Je! Umewahi kujazwa kabla?” Kama amewahi kujazwa kabla anaweza
akahitaji kutiwa moyo tu ili ajazwe tena. Kama hajawahi kabisa kujazwa,
anahitaji maelezo zaidi.
• “Je! Umewahi kumwona mtu yeyote akiwa amejazwa na Roho?” Kama
amekwisha kuwaona wengine wakiwa wamejazwa na Roho anaweza kuwa
na ufahamu ni nini kitatokea kwake. Kama hajawahi, atahitaji maelekezo
ya kina.
Ukisha uliza maswali haya, sikiliza sana majibu yake. Ugunduzi huo utakusaidia
jinsi ya kuendelea hatua inayofuata.
4. Maelekezo. Katika sehemu hii katika mahojiano kunakuwa na malengo
mawili:
• kuhamasisha imani yenye matumaini katika moyo wa mhusika; na
• kumleta katika ufahamu kamili wa kuelewa anatakiwa afanya nini na ni
nini anategemea kitokee.51
Njia moja ya kuinua imani ni kumkumbusha mhusika juu ya ahadi za Mungu
kuhusu Roho Mtakatifu. Mhakikishie ya kuwa kama kweli amezaliwa mara ya
pili Mungu yuko tayari sasa kumjaza Roho Mtakatifu. Mkumbushe ahadi ya
Yesu katika Luka 11:10, “kwa kuwa kila aombaye hupokea.” Lazima aamini ya
kuwa Mungu anaweza, muda anapomwomba, kumjaza kwa Roho Mtakatifu. Hii
ndiyo tunayoiita “imani yenye matumaini” au “imani ipokeayo.” Hivyo
ategemee kujazwa, na pia kunena kwa lugha kama Roho atakavyomjalia
kutamka. Na awe tayari kutenda sawa na matumaini yake.
Tena, jaribu kumleta katika ufahamu halisi kuhusu afanye nini ili ajazwe, na
ni nini ategemee kutokea. Anahitaji kufahamu ya kuwa kujazwa na Roho
Mtakatifu sio kitu kigumu au kisicho cha kawaida kwa mkristo. Ni jambo la
kawaida kufanyika. Hatajazwa na “Roho Mtakatifu mwingine” bali Roho
Mtakatifu yule yule akaaye ndani yake tokea wakati wa kuzaliwa mara ya pili.
Unaweza kumwambia mhusika, “Kumpokea Roho Mtakatifu ni rahisi! Ni kitu
cha kawaida kufanya. Kwa mtu aliyeokoka ni rahisi kama vile kupumua.” Na
ni kweli! Unakumbuka Yesu alivyofanya na kuwaambia wanafunzi wake katika
Sura Ya Kumi na Mbili: Jinsi Ya Kuomba Na Watu Ili Wajazwe Na Roho Mtakatifu
120
Yohana 20:22? “Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia akawaambia, pokeeni
Roho Mtakatifu.”
Kwa maneno mengine, kupokea Roho Mtakatifu ni kama kuvuvia
(kupumua). Kama kupumua kulivyo ni kitendo cha kawaida mtu kufanya,
kupokea Roho Mtakatifu pia ni kitu cha kawaida kwa mwana wa Mungu.
Halafu, mfanye mhusika ajue wazi ya kuwa ni kitu gani anatazamia kufanya na
pia ni nini kitatokea kwake. Unaweza kusema kama hivi:
Kwanza, tutaomba pamoja. Hatafu, nitakuongoza katika sala ambayo
tutamwomba Mungu atujaze kwa Roho Mtakatifu. Bwana atasikia na kujibu
maombi yetu. Ninajua atajibu kwa sababu tutaomba katika mapenzi yake (1Yn
5:14). Baada ya hapo, nitakuhitaji uchukue hatua ya imani na upokee Roho
Mtakatifu. Nitakuongoza katika sala nyingine fupi. Itakuwa kama hivi, “Bwana
sasa hivi, katika Jina la Yesu, ninapokea Roho Mtakatifu.” Ndipo nitakuomba
uanze kumsifu Bwana kwa moyo wako wote. Unapofanya hivyo, tegemea
Bwana kukujaza kwa Roho wake. Utahisi uwepo wake ukikujaza, na kisha
utaanza kunena katika lugha ambayo hujawahi kujifunza. Usiogope, wewe
uendelee tu kunena. Je! Uko tayari kujazwa na Roho? Je! Una swali lolote?
Endapo mhusika ana mawali, yajibu. Kama hana maswali endelea
kumwombea.
Maombi
Katika maombi yakujazwa Roho Mtakatifu tutafanya mambo mawili:
• tutamwongoza mhusika katika maombi ya kujazwa na Roho Mtakatifu; na
• tutamwongoza mhusika katika hatua ya imani ili kupokea Roho Mtakatifu.
1. Mwongoze mhusika katika maombi. Kama ambavyo unavyoweza
kumwongoza mwenye dhambi katika sala ya toba, sasa mwongoze mkristo mpya
katika kuomba ili ajazwe na Roho. Sala inaweza kuendelea kama ifuatavyo,
mhusika akirudia kila mstari:
Bwana ninakuja sasa nijazwe kwa Roho Mtakatifu …Sasa hivi, hakuna lolote
maishani mwangu ninalohitaji zaidi …Umeahidi ya kuwa mtu yeyote aombaye,
hupokea. . . Ninaomba; kwa hiyo, nategemea kupokea …Ninapoanza kukusifu
nitaachilia imani yangu … Nitaanza kuomba kwa lugha kama Roho atakavyoniwezesha
…Sitaogopa.
Sura Ya Kumi na Mbili: Jinsi Ya Kuomba Na Watu Ili Wajazwe Na Roho Mtakatifu
121
Baada ya kuomba, mhakikishie mhusika ya kuwa Mungu amesikia maombi yake,
na Mungu yuko tayari sasa kumjaza kwa Roho.
2. Mwongoze mhitaji katika hatua ya imani. Sasa mwambie mhitaji wa
kujazwa Roho Mtakatifu anyanyue mikono yake yote miwili na aombe sala fupi
pamoja na wewe, “Bwana sasa hivi, katika jina la Yesu, ninapokea Roho
Mtakatifu.” Sala hii inaruhusu muda kamili ambapo anaweza kuelekeza imani
yake kwa Mungu ili kupokea Roho Mtakatifu. Sasa mtie moto ili aanze
kumwabudu Mungu kwa moyo wake wote. Mara nyingi katika hatua hii mhitaji
atajazwa mara moja na Roho na kuanza kunena kwa lugha kama Roho
atakavyomwezesha. Kama hataanza kunena kwa lugha mara moja, mtie moyo
aendelee kumsifu Bwana. Unaweza kuabudu pamoja naye, wewe pia
ukimruhusu Mungu kukujaza tena kwa Roho Mtakatifu. Hii mara nyingi humtia
moyo mhusika kumsifu Mungu hadi yeye pia amejazwa.
Kama mhitaji ana tatizo la kuweka mawazo yake kwa Bwana, ni vema
kurudia tena hatua ya kwanza kama ilivyoonyeshwa hapo juu. Unapofanya
hivyo, mwelekeze vema zaidi jinsi anavyoweza kujiachilia kwa Roho Mtakatifu.
Akiisha kuanza kunena katika lugha, mtie moyo aendelee. Baki naye wakati
wote anapoendelea kuomba katika Roho.
Ni vema pia nyakati nyingine kumwelekeza mhitaji ya kuwa, wakati ni
muhimu atafute kipawa cha Roho, ni muhimu zaidi amtafute mtoaji wa Roho
mwenyewe. Hivyo anatakiwa aweke mawazo yake kwa Yesu na sio kujawa tu
na fikra za kupokea kipawa cha Roho na kunena kwa lugha kiasi kwamba
anamsahau Bwana ambaye ndiye mtoaji wa vipawa hivi.
Maelekezo Baada ya Maombi
Kama ilivyo katika maombi ya wagonjwa na katika ukombozi dhidi ya
mapepo, ni muhimu kwamba ushauri baada ya maombi utolewe kwa mhusika.
Kama amejazwa na Roho Mtakatifu utatoa ushauri wa aina moja, endapo
hajajazwa utatakiwa kumpa ushauri wa aina nyingine.
1. Kama amejazwa na Roho. Kama mhusika amejazwa na Roho na kunena
kwa lugha, ushauri ufuatao ni muhimu: Mwambie ya kuwa kupokea Roho si
mwisho wa mambo yote; bali ni njia ya kuendea mwisho. Kusudi la kupokea
Roho ni ili kwamba tupokee nguvu kwa ajili ya maisha ya utumishi. Unaweza
kusema, “Huu sio mwisho; ni mwanzo tu. Mungu sasa ataanza kukutumia katika
hali mpya ya nguvu. Tegemea kuwa na nguvu mpya maishani mwako. Nenda
sasa hivi ukamshuhudie mtu habari za Yesu.” Unaweza kutaka kuongeza,
Sura Ya Kumi na Mbili: Jinsi Ya Kuomba Na Watu Ili Wajazwe Na Roho Mtakatifu
122
“Unahitaji pia kutumia muda fulani kila siku ukiomba katika Roho (yaani
kuomba kwa lugha). Hii itakupatia nguvu na itakukumbusha uwepo wa Roho
maishani mwako.”
2. Kama hajajazwa na Roho. Kama hajajazwa na Roho, unaweza kumpa
ushauri ufuatao pamoja na kumtia moyo: Mwambie asikate tamaa kwa sababu
hajapokea Roho Mtakatifu wakati huo. Mhakikishie ya kwamba ahadi ya Yesu
ingali ni kweli -- “Yeyote aombaye hupokea” (Lk 11:10). Mwambie aendelee
kuomba atapokea, aendelee kutafuta ataona, na aendelee kubisha atafunguliwa
mlango (Tafsiri ya Luka 11:9). Unaweza kumuuliza endapo anahitaji kuomba
tena. Kama anataka, rudia tena kama ilivyoelekezwa hapo juu, mtie moyo atende
kwa imani.
MAMBO MENGINE MUHIMU
Tunapomalizia sura hii tutataja kwa ufupi mambo mengine matatu ambayo
ni muhimu tunapohitaji kuwaongoza wengine katika ubatizo wa Roho Mtakatifu.
Fahamu Biblia Inasema Nini kuhusu Somo Hilo
Kwanza, endapo mtu atahitaji awasaidie wengine kujazwa na Roho
Mtakatifu, ni wazi anahitaji atafute mambo yote anayoweza kuyapata juu ya
somo hilo. La muhimu zaidi, lazima asome Neno la Mungu, hasa kitabu cha
Matendo ya mitume, ili kuona kinasema nini kuhusu somo hili. Pia anaweza
kusoma vitabu vingine vizuri kuhusu somo hilo. Jinsi mtu anavyoelewa zaidi
kuhusu Roho Mtakatifu na utendaji wake katika maisha ya watu, ndivyo
atakavyokuwa katika hali nzuri zaidi ya kuwasaidia wengine ili wazipokee
baraka za Mungu.
Usiachilie Uvivu wa Kiroho Ukufanye Ushindwe
Jambo la pili, kama utahitaji kuwasaidia watu kupokea Roho wa Mungu,
usije ukaachilia roho wa uvivu akufanye ushindwe. Kwa sababu ni vigumu mara
nyingi kuombea watu wajazwe na Roho, wengine wanakwepa kuhubiri kuhusu
somo hili au kuwaongoza wengine katika baraka hii kubwa. Kama jambo hili
ndivyo lilivyo kwako, tubia uvivu wako wa kiroho, halafu ujitoe kwa moyo wako
wote kwa ajili ya huduma hii muhimu.
Sura Ya Kumi na Mbili: Jinsi Ya Kuomba Na Watu Ili Wajazwe Na Roho Mtakatifu
123
Angalia Kiwango cha Ujazo Wako
Hatimaye, unapoomba na mtu ili ajazwe na Roho Mtakatifu, ni muhimu
uangalie kiwango cha ujazo wako. Kwa hili nina maana uwe na ujazo wa juu
unapoomba nao. Uachie ujasiri wako katika kudhamiria jambo hili kuonekana
wazi! Wakati huo huo ni vema pia usiwe msukumaji mno wa mambo. Hekima
itakuonyesha kiwango chema cha kutendea kazi hii na kuwatia moyo watu
wajazwe na Roho.
MWISHO
Katika somo hili tumezungumzia jinsi ya kuwa hodari kuwaongoza watu
katika ubatizo wa Roho Mtakatifu. Tumezungumzia mambo muhimu katika
kumpokea Roho, na jinsi unavyoweza kufanya ili kuwatia moyo wengine
wapokee. Tunategemea ya kuwa sasa utajitoa kwa ajili ya kazi hii ya kuwasaidia
wengine wajazwe na Roho. Hakuna jambo la kuridhisha kuliko kusaidia watu
katika kupokea baraka hii ya Mungu.
124
125
Appendix 1
Huduma Yauponyaji Ya Yesu
Vitabu Vitatu Vya Injili
Tendo ya Uponyaji Mt Mk Lk Njia iliyotumika
1. Mtu mwenye pepo mchafu 1:23 4:33 Kutoa pepo kwa neno.
2. Mama mkwe wa Petro 8:14 1:30 4:38 Kugusa, neno.
3. Makusanyiko 8:16 1:32 4:40 Kugusa, neno, imani
4. Mapepo mengi yatolewa 1:39 Kuhubiri, kutoa pepo
5. Mwenye ukoma 8:2 1:40 5:12 Kugusa, neno, imani
ya mwenye ukoma,
huruma,
6. Makusanyiko 5:15 Kuitikia uhitaji.
7. Mwenye kupooza 9:2 2:3 5:17 Neno, imani ya
marafiki
8. Mtu mwenye mkono 12:9 3:1 6:6 Neno,
uliopooza utii, imani.
9. Makusanyiko 12:5 3:10 Kugusa, imani, kutoa
pepo.
10. Mwenye pepo wa nchi ya 8:28 5:1 8:26 Neno, kutoa
Wagerasi pepo.
11. Kufufuliwa Binti Yairo 9:18 5:22 8:41 Neno, kugusa, imani
ya baba yake.
12. Mwanamke aliyetokwa damu 9:20 5:25 8:43 Kugusa, kuachilia
nguvu.
13. Wagonjwa wachache 13:58 6:5 kugusa, (Alizuiliwa
kwa kutokuamini
kwao).
14. Makusanyiko 14:34 6:55 Kugusa, kuachilia
nguvu
15. Binti ya mwanamke 15:22 7:24 Kuikubali
Msirofoinike imani yake
16. Kiziwi na mwenye utasi 7:37 Kugusa, neno.
17. Mtu kipofu 8:22 Kugusa, (kupona
polepole).
18. Kijana mwenye roho 17:14 9:14 9:38 Neno,
mchafu kugusa,
imani ya baba yake.
19. Bartimayo kipofu 20:30 10:46 18:35 Neno, kugusa,
huruma, imani.
20. Mtumwa wa Akida 8:5 7:2 Kuitikia kwa imani.
Appendix 1
126
Huduma Yauponyaji Ya Yesu
Vitabu Vitatu Vya Injili
Tendo ya Uponyaji Mt Mk Lk Njia iliyotumika
21.Vipofu wawili 9:27 Neno, kugusa.
22. Mwenye pepo, kipofu na bubu 12:22 11:14 Kutoa pepo.
23. Mtu bubu na mwenye pepo 9:33 Kutoa pepo.
24. Makusanyiko (magonjwa na 4:23 6:17 Kufundisha,
udhaifu wa kila namna) kuhubiri, kuponya
25. Makusanyiko (magonjwa na 9:35 Kufundisha,
udhaifu wa kila namna) kuhubiri, kuponya
26. Makusanyiko 11:4 7:21 Ushuhuda wa Yohana
27. Makusanyiko 14:14 9:11 Huruma
28. Makutano mengi (vipofu 15:30 Imani ya marafiki
vilema na mabubu)
29. Makusanyiko makubwa 19:2 Haikutajwa
30. Vipofu na viwete hekaluni 21:14 Kuitikia hitaji la watu
31. Mwana wa mjane wa Naini 7:11 Neno, kugusa, huruma
32. Mariamu Magdalena 8:2 Kutoa pepo
na wengine
33. Mwanamke mwenye pepo 13:10 Neno, kugusa
wa udhaifu
34. Mtu mwenye ugonjwa wa 14:1 Kugusa.
Safura
35. Kumi wenye ukoma 17:11 Amri.
36. Sikio la Malko 22:49 Kugusa
Injili ya Yohana
37. Mwana wa Chiwani Yohana 4:46 Neno, imani ya baba
yake.
38. Mtu aliyekuwa hawezi Yohana 5:2 Neno, imani yake.
39. Mkutano mkuu Yohana 6:2 Huruma
40. Mtu aliyezaliwa kipofu Yohana 9:1 Neno, kugusa
41. Lazaro afufuliwa kutoka Yohana 11:1 Amri Kwa wafu
Tambua: Orodha Hii Imenakiliwa Kutoka Orodha Nyingine Ya Jim
B. Miller.
127
Appendix 2
Njia Za Uponyaji Za Yesu
Utaona katika orodha iliyotangulia njia kadha za uponyaji za
Yesu pamoja na mstari wa kwanza wa Biblia, mahali na namna
mbalimbali za jinsi Yesu anavyotumia njia fulani za kuombea.
Huduma ya uponyaji ya Yesu ilifanyika ili pia iwe kama mfano wetu
wa kufuata (Yn 20:21; 1Pet 2:21; 1Kor 11:1).
KUTAMKA NENO: Njia ambayoYesu alitumia mara nyingi katika uponyaji wa wagonjwa
ilikuwa ni kwa kusema neno tu. Mara nyingine hili neno lililotamkwa ilikuwa ni amri kwa
mtu aliye mgonjwa afanye tendo fulani. Wakati mwingine ilikuwa ni amri ya mapepo
kutoka. Kuna wakati Yesu alitamka moja kwa moja kwa ule ugonjwa. Wakati mwingine
neno lake lilikuwa ni la kuikubali imani ya mpokeaji uponyaji, au tamko la kuonyesha ya
kuwa uponyaji umekwisha tendeka. Usomapo mistari ifuatayo ya matukio utamwona
Yesu akitamka neno na kuponya wagonjwa:
(Mk 1:23; Lk 4:33); (Mt 8:14, Mk 1:30, Lk 4:38); (Mt 8:16; Mk 1:32, Lk 4:40); (Mt 8:2, Mk
1:40, Lk 5:12); (Mt 9:2, Mk 2:3, Lk 5:17); (Mt 12:9, Mk 3:1, Lk 6:6); (Mt 8:28, Mk 5:1, Lk
8:26); (Mt 9:18, Lk 9:38); (Mt 20:30, Mk 10:46, Lk 18:35); (Mt 9:27); (Lk 7:11); (Lk
13:10); (Lk 17:11); (Yn 4:46); (Yn 5:2); (Yn 9:1); (Jn 11:1).
AMRI YA IMANI: Njia mojawapo ambayo Yesu aliitumia mara kwa mara kuponya wagonjwa
ilikuwa amri ya imani kama ilivyotajwa hapo juu. Aliweza kuamuru ugonjwa upone,
mapepo yatoke na wagonjwa kuitika kwa tendo la imani. Hapa ipo mifano kwa ajili yako
ili uisome:
(Mt 8:14, Mk 1:30, Lk 4:38); (Mt 9:2, Mk 2:3, Lk 5:17); (Mt 12:9, Mt 3:1, Lk 6:6); (Mt
9:18, Mk 5:22, Lk 8:41); (Mk 7:32); (Mt 20:30, Mk 10:46, Lk 18:35); (Mt 9:27); (Lk 7:11):
(Lk 13:10); (Lk 7:11); (Yn 4:46); (Jn 5:2); (Yn 9:1); (Yn 11:1).
KUGUSA: Yesu mara nyingi aliwagusa watu na kuwaponya. Kugusa huku kulikuwa ni
kuuchukua mkono wa mtu, kumgusa mgonjwa mahali alipohitaji uponyaji utendeke, na
namna zingine za miguso. Soma mistari ifuatayo ili kuona jinsi Yesu alivyotumia kugusa
katika kuponya wagonjwa:
(Mt 8:14, Mk 1:30, Lk 4:38); (Mt 8:16, Mk 1:32, Lk 4:40); (Mt 8:2, Mk 1:40; Lk 5:12); (Mt
9:18; Mk 5:22, Lk 8:41); (Mt 13:58, Mk 6:5); (Mk 7:32); (Mk 8:22); (Mt 17:14), (Mk 9:14,
Lk 9:38); (Mt 20:30; Mk 10:46, Lk 18:35); (Mt 9:27); Lk 13:10); (Lk 14:1); (Lk 22:49); (Yn
9:1).
128
Appendix 2
Njia Za Uponyaji Za Yesu
IMANI YA MPOKEAJI: Yesu mara nyingine aliponya alipoona imani ya mtu inahitaji
uponyaji. Hapa ipo kati ya mifano:
(Mt 8:2, Mk 1:40, Lk 5:12); (Mt 12:15, Mk 3:10); (Mt 9:20, Mk 5:25, Lk 8:43); (Mt 20:30,
Mk 10:46, Lk 18:35); (Mt 9:27); (Yn 5:2).
IMANI YA WENGINE: Nyakati nyingine Yesu aliponya alipoona imani ya marafiki au
familia ya mtu aliyehitaji uponyaji:
(Mt 8:14, Mk 1:30, Lk 4:38); (Mt 8:16, Mk 1:32, Lk 4:40); (Mt 9:2, Mk 2:3, Lk 5:17); Mt
9:18, Mk 5:22, Lk 8:41); (Mt 14:34, Mk 6:55); (Mt 15:22, Mk 7:24); (Mk 7:32); (Mk 8:22);
(Mt 7:14, Mk 9:14, Lk 9:38); Mt 8:5, Lk 7:2); (Yn 4:46).
KUTOA MAPEPO: Mara nyingi Yesu aliwaponya wagonjwa kwa kutoa mapepo ambayo
yalisababisha ugonjwa:
(Mk 1:23, Lk 4:33); (Mt 12:15, Mk 3:10); (Mt 8:28, Mk 5:1, Lk 8:26); (Mt 9:32); (Mt 12:22,
Lk 11:14); (Lk 8:2); (Lk 13:32).
HURUMA: Huruma kwa ajili ya wagonjwa na wenye mateso kilikuwa ni kiungo
kilichopatikana katika huduma ya uponyaji ya Yesu. Huruma yake ilimfanya awafikie na
kuwaponya kama ifuatavyo:
(Mt 8:2, Mk 1:40, Lk 5:12); (Mt 20:30, Mk 10:46, Lk 18:35); (Mt 14:14, Lk 9:11, Yn 6:2);
(Lk 7:11).
UTHIBITISHO WA KUHUBIRI AU KUFUNDISHA: Uponyaji mara nyingi ulifanyika ili
kuthibitisha ujumbe aliofundisha au kuhubiri, kama mistari ifuatayo inavyothibitisha:
(Mk 1:39); (Mt 4:25, Lk 6:17); (Mt 9:35); (Mt 11:4, Lk 7:21).
MATENDO YA AJABU: Wakati mwingine Yesu aliponya kwa kutumia matendo ya ajabu
kama ifuatavyo:
(Mt 9:20, Mk 5:25, Lk 8:43); (Mt 14:34, Mk 6:55), (Mk 8:22); (Yn 9:1).
---------------------------------------------------
Tambua: Orodha hii imenakiliwa kutoka orodha nyingine
iliyotengenezwa na Jim B. Miller.
129
Bibliography
Bennett, Dennis and Rita Bennett. 1971. The Holy Spirit and You.
Plainfield, NJ: Logos`International.
Bonnke, Reinhard. 1994. Mighty Manifestations. Eastbourne, UK:
Kingsway Publication.
Bosworth, F. F. 1973. Christ the Healer. Old Tappan, NJ: Revell.
Carter, Howard. 1968. Spiritual Gifts and Their Operation.
Springfield, MO: Gospel Publishing House.
Duewel, Wesley. 1986. Touch the World Through Prayer. Grand
Rapids, MI: Zondervan.
Evans, W.I. 1954. This River Must Flow. Springfield, MO: Gospel
Publishing House.
Exley, Richard. 1988. Perils of Power: Immorality in the Ministry.
Tulsa, OK: Honor Books.
Fitzpatrick, Graham. 1987. Miracles, Faith, and God’s Will. N.S.W.,
Australia: Spiritual Growth Publications.
Gramenz, Stuart. 1986. How You Can Heal the Sick. Chichester,
UK: Sovereign World.
Haltom, Fred. 1989. “Old Testament power encounters.” in Power
Encounter, A Pentecostal Perspective, ed. Opal Reddin, 94–122.
Springfield, MO: Central Bible College.
Horton, Stanley M. 1993. Pneumatology. Irving, TX: ICI University.
———. 1976. What the Bible Says About the Holy Spirit.
Springfield, MO: Gospel Publishing House.
Jeter, Hugh. 1977. By His Stripes. Springfield, MO: Gospel
Publishing House.
Bibliography
130
Kuzmic, Peter. 1988. “Kingdom of God.” In Dictionary of
Pentecostal and Charismatic Movements, ed. Stanley Burgess,
Gary McGhee, and Patrick Alexander, 521–526. Grand Rapids,
MI: Zondervan.
Ladd, George Eldon. 1981. “The Gospel of the Kingdom.” In
Perspectives on the World Christian Movement, A Reader, ed.
Ralph D. Winter and Steven C. Hawthorne, 51–69. Pasadena,
CA: William Carey Library.
Marshall, Tom. 1988. Foundations for a Healing Ministry. West
Sussex, England: Sovereign World.
Miller, Jim. n.d. “How to Heal the Sick.” Unpublished manuscript
(available through the author).
Moon, Jessie K. 1989. “Power Encounter in Evangelism.” In Power
Encounter, A Pentecostal Perspective, ed. Opal Reddin,
232–255. Springfield, MO: Central Bible College.
O’Donovan, Jr., William. 1992. Introduction to Biblical Christianity
From An African Perspective. Ilorin, Nigeria: Nigeria
Evangelical Fellowship.
Osborn, T. L. 1955. How to Receive Miracle Healing. Nairobi:
Evangel Publishing House.
Otis Jr., George. 1991. The Last of the Giants. Tarrytown, NY:
Chosen Books.
Pennoyer, F. Douglas. 1990. “Dungeons of Collective Captivity.” In
Wrestling with Dark Angels, ed. C. Peter Wagner and F.
Douglas Pennoyer, 249–279. Ventura, CA: Regal.
Pyches, David. 1985. Spiritual Gifts in the Local Church.
Minneapolis: Bethany House Publishers.
Bibliography
131
Stamps, Don. 1992. “Acts 4:8, Peter Filled with the Holy Spirit.” In
The Full Life Study Bible, 1651. Grand Rapids, MI: Zondervan
Publishers.
———. 1992. “Baptism in the Holy Spirit.” In The Full Life Study
Bible, 1642–1643. Grand Rapids, MI: Zondervan Publishers.
———. 1992. “Power over Satan and Demons.” In The Full Life
Study Bible, 1484–1485. Grand Rapids, MI: Zondervan
Publishers.
Summerall, Lester. 1979. Demons, the Answer Book. South Bend,
IN: LeSEA Publishing.
Unger, Merril C. 1971. Biblical Demonology. Wheaton, IL:
Scripture Press.
Wagner, C. Peter. 1990. “Territorial Spirits.” In Wrestling with dark
angels, ed. C. Peter Wagner and F. Douglas Pennoyer, 73–91.
Ventura, CA: Regal.
Williams, Don. 1989. Signs, Wonders, and the Kingdom of God.
Ann Arbor, MI: Servant Publications.
Wimber, John. 1986. Power Evangelism. San Francisco: Harper and
Row.
________. 1987. Power Healing. San Francisco: Harper & Row.
132

No comments:

Post a Comment