Monday, 15 December 2014

KANUNI ZA UONGOZI BORA

1
MPANGO WA KUFANYA NA USAIDIA
AFRIKA MASHARIKI NA KATI
CHURCH OF GOD WORLD MISSIONS
KANUNI ZA ONGOZI WA
KIROHO
2
KANUNI ZA ONGOZI WA
KIROHO
Peter A. Thomas
Harare, Zimbabwe
Translation: Maeda David Gabriel
3
KANUNI ZA UONGOZIWA KIROHO
I. Maana ya Uongozi
1. Uongozi Unaweza Kujifunzwa?
2. Tofauti za Uongozi wa Asili na wa Kiroho
II. Vitu Vya Lazima Kwa Uongozi Wa Kiroho
1. Kuzaliwa Upya
2. Wito wa Kiroho
(1) Umuhumu wa Wito wa Kiroho
(2) Mungu Anavyoita
(3) Kutambua Wito
(4) Kuwa mbunifu mwenyewe kwa asili
3. Roho Mtakatifu Kujaa Ndani Kujawa na Roho Mtakatifu
III. Sifa za Uongozi
1. Mtumishi Mbele za Mungu na Wanadamu
2. Mtu wa Imani na Maono
(1) Maono
(2) Imani
3. Kuwa na Ujasiri Katika Neno na Tendo
4. Kukabili Changamoto ya Kufanya Uamuzi
5. Uhitaji wa Hekima na Uamuzi Bora
(1) Hekima
(2) Uamuzi Bora
(3) Kujifahamu - Binafsi
6. Unyenyekevu - Tabia ya Moyo
7. Ukamilifu
8. Kiongozi na Ucheshi
9. Maisha ya Uanafunzi
IV. Jukumu la Kiongozi - Kutoka Maono Kwenda Katika Utekelezaji
1. Kuwekwa ili Kutawala
2. Umuhimu wa Kuwa na Mipango
(1) Uwekaji wa Malengo
(2) Uchoraji wa Mkakati
(3) Kuamua Muda - Utakaotumika
(4) Swali Juu ya Nguvu - ya Watu Itakayotumika na Fedha
(5) Kupima Ubora/Thamani ya Kazi
4
3. Kufanyia Kazi Mamlaka ya Kiroho
(1) Maana ya Mamlaka ya Kiroho
(2) Jinsi ya Kupata Mamlaka ya Kiroho
a. Kuishi Maisha ya Haki
b. Neno la Kutahadharisha
c. Kuukubali Ubwana wa Yesu Kristo
d. Upako/Kutiwa Mafuta
e. Neno la Tahadhari
f. Maombi na Neno
4. Namna Sahihi za Uongozi Kwa Ajili ya Kulea, Kufariji na Kuadibisha
(1) Kuwaendea - Kidemokrasia
(2) Kuwaendea - Kwa Kuamrisha tu Pasipo Kujadili Amri
(3) Kujenga Uhusiano wa Kibaba/Kuwakaribia Watu
(4) Kiserikali/Kimamlaka
(5) Kwa Muda Usio wa Kudumu/Kujishikiza
(6) Mtindo wa Yesu wa Uongozi
V. Kulipa Gharama - Mtihani/Jaribio la Uongozi
1. Kukubali Malaumu
2. Kujitoa Kikamilifu Kufanya Kazi
(1) Kiongozi Bora - Huwashirikisha Mamlaka Wengine
(2) Jinsi ya Kuwashirikisha/Kuwagawia Wengine Kazi
(3) Kazi Gani Zaweza Kugawiwa Wengine Wazifanye
(4) Faida na Hatari Zilizojificha za Kuwagawia
Wengine Kazi
(5) Kuepuka Kuungua Kabisa
(6) Kiongozi wa Kweli Huhuisha Nguvu Zake
3. Kuchukuliana na Upweke, Kukataliwa na Kukatishwa Tamaa/Vunjwa Moyo
(1) Kukataliwa
(2) Upweke/Kuwa Peke Yako
(3) Kukatishwa Tamaa/Kuvunjwa Moyo
(4) Kuwa Tayari/Kujiandaa Kwa Ajili ya Vita vya Kiroho
VI. Hatari Katika Uongozi wa Kikristo
1. Kupenda Pesa
(1) Kutumikishwa na nia Mbaya
(2) Matumizi ya Pesa Zilizopangwa
(3) Jinsi ya Kutunza Pesa za Binafsi
(4) Usijiuze
(5) Mfano wa Kupenda Pesa
(6) Udanganyifu Katika Kuchangisha/Kutunisha Fedha
2. Wanawake
(1) Hatari Katika Kutoa Ushauri
(2) Hatari Kupitia Kukutana Waziwazi/ Ana Kwa Ana
(3) Hatari Katika Kutembelea Majumbani
(4) Jinsi ya Kujilinda Wenyewe
(5) Ushauri wa McBurney juu ya Ishara za Hatari za nje
(6) Dalili za Hatari za Ndani Asemavyo McBurney
5
3. Umaarufu
(1) Utata Juu ya Upako/Umasia
(2) Tatizo la Umaarufu
(3) Jaribio la Kiburi
(4) Jinsi ya Kuwa Mnyenyekevu
Mwisho
6
KANUNI ZA UONGOZIWA KIROHO
Mojawapo ya mahitaji makubwa kabisa ya Kanisa la leo ni hitaji la uongozi wa kiroho.
Unongozi unaoelewa na kufuata kanuni za utumishi na uanafunzi.
Tunaishi katika wakati ambao watu wa Mungu wanataaabika na ulimwengu kuangamia kwa
sababu hakuna wachungaji wa kiroho. Badala ya kuwaongoza wale ambao Mungu
amewaweka katika uangalizi wao wa kiroho, viongozi wengi wanajipatia mali, cheo na
madaraka katika migongo ya wale wanaopaswa kuwatumikia. Uongozi kama unavyoelezwa
na maandiko, unahitaji tena kurudishwa katika Kanisa kwa sababu ulikuwa umeshaharibiwa
sana na viongozi wanaotafuta kujineemesha na umevurugwa na utumiaji wa njia za uongozi
zilizo tofauti na maandiko yasemavyo. Damazio anagusia kwamba njia hizi za kidunia za
uongozi zinatumika licha ya ukweli kwamba wana-saikologia wana-endelea kupata matatizo
mengi kwa Programu zao za mafunzo ambazo kila wakati wameendelea kuzitafutia
masahihisho ili kuweza kupata njia iliyo bora zaidi. Anaendelea kusema kuwa "Ni pigo
kubwa, wakati Kanisa (Kwa sababu ya kutokuwepo kwa uongozi wa Kiroho) linapochukua
njia zisizo za ki-biblia kwa ajili ya kuwafundishia viongozi wake kutokana na hizi programu
za wanasaikologia zinazobadilika kila siku na za wanasayansi wa kijamii badala ya neno la
mungu.1 Wakati Kanisa litakapotumia njia zisizo za kimaandiko, litakuja kukuta kuwa
viongozi wake wanashindwa kukutana na mahitaji ya kiroho ya Mwili wa Kristo. Kutimiza
malengo ya huduma za kibiblia, viongozi wanahitaji zaidi ya shahada za darasani, majina
makubwa makubwa, na uwezo mkubwa ki-akili. Kukutana na mahitaji ya kiroho ya Kanisa,
viongozi lazima waishi maisha ya utumishi, wawe na tabia ya Kimungu, wamsikilize Mungu
na wawe na upako wa Roho Mtakatifu. Kwa kifupi ni lazima wawe wafuasi wa Yesu Kristo.
Viongozi wanaoji-neemeshaNjia zisiso za Ki-maa-ndiko za Uongozi Zaidi ya shahada, majina
makubwa na usomi mwingi Mafunzo ya Uongozi ni lazima, si kwa sababu tu nadharia ya
uongozi imeharibiwa, bali pia kwa sababu Kanisa litatawanyika na kuangamia bila mafunzo
hayo. Katika Mathayo 9:36-37, Yesu alifananisha kizazi cha binadamu na kondoo. Hili
halikufanyika kuonyesha dharau, bali kuonyesha ukweli mmoja mkubwa. Kama vile ambavyo
kondoo Uli-nganisho kati ya binadamu na kondoo huko Ghana wanahitaji mchungaji,
binadamu pia wanahitaji viongozi. Katika miaka yetu minne huko Ghana kama wamisionari
ulinganisho huu ulileta maana.Mara nyingi tuliwaona kondoo wakizagaa bila waangalizi wa
mchungaji. Wali - "kula" katika majalala ya takataka, karibu na kijiji tulichokuwa tunaishi
wakijishibisha na vinyesi. Wengine waligongwa na magari. Hapakuwepo mtu wa
kuwaongoza kwenye majani mabichi au kuwalinda kutoka kwenye hatari. Watu, katika
namna nyingi wanafanana na kondoo. Wakiachwa wenyewe watazurura huku na huko
wakijishibisha na "takataka" za dunia hii, wakihatarisha roho zao yawezekana kuendelea
milele. Kwa sababu hiyo Kristo aliwaonea huruma. Ulimwengu unahitaji viongozi wa kiroho
watakaosimama kijasiri katika kizazi kilichopotoka (Wafilipi 2:5) wakielekeza, na kuongoza
kwa mfano na kutangaza kikamulifu ushauri wa Mungu.
Yesu aliteua uongozi wa Kanisa (Waefeso 4:11) na aliwafundisha viongozi wake wa mwanzo
yeye Mwenyewe. Inasemekana nkwa usahihi kabisa kwamba Kanisa halijapata tena msukomo
mkubwa wa kiroho kutoka kwa viongozi wake zaidi ya ule wa mitume wa kwanza.2 Ili
kukamilisha kazi yake Kanisa linahitaji kufuata mfano uliowekwa na Bwana wake. Kwa hiyo,
viongozi wa sasa, lazima wamruhusu Bwana kuwatayarisha kwa huduma katika Kanisa na
7
jamii. Ni muhimu kabisa kuelewa na kujiandaa kwa wajibu mkubwa uliopo juu ya viongozi
wa kiroho.
Katika kitabu hiki tutajaribu basi kutimiza yafuatayo:
1. Kuonyesha umuhimu wa uongozi wa kiroho na kuonyesha mambo ya lazima na sifa
zinazohitajika kwa viongozi wa kiroho.
2. Kuonyesha baadhi ya kazi muhimu za viongozi wa kiroho, na pia baadhi ya namna
mbalimbali muhimu za uongozi.
3. Kuonyesha gharama iliyopo ambayo kwayo viongozi wa kiroho `wanajaribiwa'
/wanatahiniwa.
4. Kuonyesha hatari au ugumu katika uongozi wa kiroho na kupendekeza njia
mbalimbali za kushinda majaribu katika huduma (mitego).
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.
8
I. Maana ya Uongozi
Maana rahisi kabisa ya `kiongozi' ni mtu anayeongoza. Ni mtu anayeweza kuelekeza na
kuonyesha wengine njia, kwa sababu yeye mwenyewe alikwisha fika hapo. Ukweli huu ni wa
muhimu kabisa katika mambo ya kiroho. Viongozi waKiKristo lazima waweze kuwaongoza
wengine kukutana na Mungu, kutokana na uzoefu wao wakiroho. Wao wenyewe lazima
wajue maana ya kuzaliwa mara ya pili, au kubatizwa na Roho Mtakatifu kabla ya kuweza
kuwasaidia wengine wanaotafuta mambo hayo. Kiongozi lazima aishi maisha matakatifu.
Lazima ajiepushe na dhambi, Ushirikina na uchawi ili kuwasaidia wengine kuja karibu na
Mungu. Tabia yake lazima kila siku ifinyangwe na Mungu kwani anaweza kuwaongoza
mpaka pale ambapo yeye mwenyewe amefikia.
Kiongozi anajua njia Kuishi maisha Matakatifu
1. Uongozi unaweza kujifunzwa?
Swali linaloulizwa mara nyingi ni "Je uongozi unaweza kufunzwa? Jibu la kawaida ni ndiyo.
Kwa sababu, kama Aultman anavyosema, kukuta "tayari - kwa - kuvaa" viongozi katika
kanisa ni mara chache sana na sio kawaida.3 Hivyo viongozi hawazaliwi bali wanaundwa.
Wanaundwa sio kuzaliwa Kuna sheria na kanuni fulani ambazo zikifuatwa zinaleta mafanikio
mazuri. Kanuni hizo zinaweza kujifunzwa. Hii ni kweli kwa viongozi wa kawaida, na pia kwa
wale wa mambo ya kiroho. Kwa mfano mtu anayekataa kugawa, madaraka na wajibu na
kukazania `kufanya yote' atashindwa mara moja. Sheria na Kanuni za uongozi za kawaida
lazima zifunzwe na viongozi wa kawaida, vilevile na viongozi wa kiroho. Hata hivyo kama
Oswald Sanders asemavyo lazima tusisahau kuwa uongozi wa asili na uongozi wa kiroho
waweza kufanana katika baadhi ya vipengele, lakini kuna namna ambazo unatofautiana. Hii
inaonekana wakati baadhi ya tabia zao zinazotawala zinapopamba nisha.4
Sheria za Uongozi Kujifunzwamambo yanayo-pambana
2. Tofauti za uongozi wa asili na wa Kiroho
Uongozi wakiasili Uongozi wakiroho
Kujiamini Kujiamini katika Mungu
Unawajua watu Pia unamjua Mungu
Fanya maamuzi yako mwenyewe Unatafuta mapenzi ya Mungu
Unajitafutia meendeleo zaidi Usiojitukuza
Unatafuta njia zako mwenyewe Unatafuta na kufuata njia za mungu
Unafurahia kuamrisha wengine Unafurahia kumtii Mungu
Unahamasishwa na kufikiria Unahamasishwa kwa
mwenyewe upendo
Kufikiria mwenyewe Kwa Mungu na binadamu
Unajitegemea Unamtegemea Mungu5
Vitu vya lazima kablaya kuwa kiongozi
Kana ilivyokwisha semwa, watu wanaweza kujifunza kuongoza. Lakini, sifa hizo hapo juu,
upande wa kulia zitaonekana tu katika kiongozi kwenye uhusiano wa ndani kabisa na Yesu
Kristo. Kwa kuangalia tofauti hizo hapo juu, inakuwa wazi kuwa kuna kanuni ambazo lazima
zitimizwe kabla mtu hajaweza kuitwa kiongozi wa kiroho. Wakati tunaangalia vitu vya
9
lazima, lazima tukumbuke kuwa ingawa uongozi unaweza kujifunza, kukata shauri kwa
kawaida hakuwafanyi viongozi wa watu ambao kamwe wasingekuwa hivyo vinginevyo.
II. Vitu Vya Lazima Kwa Uongozi Wa Kiroho
Uongozi wakiroho hauji-kirahisi. Kuna gharama ya kulipa, na baadhi ya vitu vya kutimiza.
Ama sivyo twaweza kuwa viongozi, lakini sio viongozi wakiroho. Kwa wengine vitu hivi
vinaweza kuonekana ni rahisi sana. Hata hivyo uzoefu unaonyesha kuwa hata tabia hizi rahisi
hazipo katika baadhi ya watu walio na nafasi za uongozi katika Kanisa.
1. Kuzaliwa Upya
Kuna wanaoitwa viongozi wa kiroho ambao hawana sifa hii muhimu kabisa. Hata watu
wakubwa kama John Wesley, mwanzilishi wa Kanisa la Methodist alikuwa akihubiri injili
kwa miaka kabla ya kupata wokovu wake mwenyewe. Wakati akirudi kwa meli kwenda
Uingereza, Wamissionari wa Kimoravian walimuuliza Wesley kama alijua kwamba dhambi
zake zimesamehewa. "Mimi ni Kiongozi wa dini aliyebatizwa katika Kanisa la Kianglikana,
alijibu" Lakini wale ndugu wa kimoravian hawakuridhika na jibu lile. Waliendelea na kujibu,
hilo silo swali tulikokuuliza. Umezaliwa mara ya pili? Alisumbuliwa sana na swali hilo hasa
kwa sababu ndio kwanza alikuwa amemaliza huduma ya mahubiri huko Marekani.
Alikabiliwa na swali hili mara kwa mara, alitumia muda wake mwingi katika sehemu
iliyobaki kisafari akisoma Agano Jipya. Jinsi alivyozidi kusoma Neno la Mungu, na jinsi
alivyozidi kuongea na ndugu wa kimoravian, ndiyo alivyozidi kushawishika kuwa hakuwa na
uhakika wa msamaha wa dhambi. Aliweza kushinda kiburi chake, na alipofika nyumbani
kwake Uingereza alikaa mbele za Mungu mpaka alipokuwa na uhakika wa wokuvu, Baada ya
uzoefu (experience) huu muhimu Wesley akawa mmojawop wa wale watu wakuu katika
uamsho.
John Wesley na Wamoravian
Sio kila mtu anayehudumu Injili amepata kushiriki kuzaliwa mara ya pili. Kuna wale walio
katika huduma lakini bado wanaenda kwa wachawi. Na bado, wakati huo huo wanataka kuwa
viongozi wa kiroho. Namjua mchungaji mmoja aliyefukuzwa narafiki yake wa kike, aliyebeba
fimbo, wakati mke wake aliangalia toka kwenye nyumba yao. Biblia inaonyesha wazi kuwa
watu kama hao hawawezi Mifano ya Viongozi ambao hawa-jaokolewa. Vitu Vya Lazima
Kwa Uongozi Wa Kiroho. Kuzaliwa mara ya pili Kusisitizwa kuhesabiwa kuwa wamezaliwa
mara ya pili. Kwa hiyo twahitaji kusisitiza kuzaliwa mara ya pili kama kitu cha kwanza
kabisa kwa uongozi wa kiroho. Kabla ya kuweza kuwaongoza watu kwa Kristo, inabidi
tumjue Yeye kama Mkombozi sisi wenyewe. Kwa bahati nzuri kuna wengi wanaobubiri Injili
na wamezaliwa mara ya pili kweli.
2. Wito Wa Kiroho
(1) Umuhumu wa wito wa Kiroho
Huduma Imtafute Mtu
Uamuzi wa kuhubiri Injili haupo kwetu, bali lazima utoke kwa Mungu. Hata siku moja watu
wasijiunge katika kuhudumu kwa sababu ya kutokujua mambo mengineyo. Kama mtu fulani
alivyosema "Sikufaulu katika mambo mengine yote sasa nataka niwe mhudumu wa Injili".
Halafu kuna wale wanaotaka kuwa wachungaji kwa sababu wanataka lile jina la Mchungaji
(Reverend). Wengine wanaingia katika huduma baada ya Kanisa kuingia katika kugombania
madaraka. Lakini kama Mungu hajaita, hakuna mwenye haki ya kuihudumu Injili. Sanders
10
anasema sawa kabisa kuwa lazima ofisi imtafute mtu, na sio mtu kutafuta ofisi.6 Wengine
wanafikiria kuwa usemi huu unapingana na ushauri wa mtakatifu Paulo anayesema kuwa:
Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya Askofu, atamani kazi njema. 1
Timotheo 3:1.
Lakini wakati tunaangalia kutamani kazi ambapo Paulo anaongelea, baadhi ya vitu lazima
vikumbukwe. Lazima tuelewe usemi huu kwa kuangalia wakati ambao alikuwa anaongelea.
Katika siku za Kanisala Mwanzo, hakukuwa na heshima na fahari iliyoambatanishwa na
uongozi kama tunavyojua leo. Wakati Paulo alivyoandika hali ilikuwa tofauti kabisa. Ofisi ya
mwangalizi au askofu haikutamaniwa na wengi kwa vile mara nyingi ilikuwa na shida au
ugumu, hatari, kukataliwa, kuteswa na wajibu mzito. Mara nyingi viongozi wa Kanisa
walikufa - kama waliojitolea mhanga (martyrs). Hili likiangaliwa, usemi wa Paulo utaonekana
katika mwanga mwingine. Hata hivyo, jinsi hali ilivyoendelea kuwa rahisi kwa Kanisa,
uongozi ulianza kutafutwa na watu wanaotafuta vyeo. Hii ndio sababu tunahitaji kusisitiza
umuhimu wa wito wa kiroho.
Tamaa au matakwa ya kibinadamu haitoshi kwa uongozi wa kiroho. A.W. Tozer anasema:
Kiongozi wa kweli na salama yawezekana kabisa kuwa ni yule asiye
na tamaa ya kuongoza, lakini anasukumwa katika nafasi ya uongozi
na msukumo wa Roho Mtakatifu kutoka ndani, na hali halisi ya
mazingira ya nje ... hii ni kama sheria kabisa, yakuwa mtu mwenye
tamaa ya uongozi hawezi kuwa kiongozi.7
Watu wanaoingia katika nafasi za uongozi kwa sababu ya tamaa zao wenyewe ni hatari kwa
Mwili wa Kristo. Wale wanaopigania kupata vyeo, inabidi waendelee kugombania kukaa
kutika nafasi hizo. Na wakati Mungu akituita, na kututawadha/tia mafuta, Anatusaidia kukaa
hapo. Maisha ya Musa ni mfano mzuri wa ukweli huu. Wakati uwongozi wake ulipojaribiwa
na dada yake mwenyewe Miriam, na kaka yake Aron, Mungu mwenyewe ndiye aliyeingilia
kati.
Usipiganie Cheo
Hata hivyo, lazima pia tueleze kuwa kuna wale wanaokataakataa wito wa Mungu kwa
Utumishi kwa sababu ya kujiona kuwa hawafai au wamepungukiwa. Huu ni unyenyekevu au
kujishusha kusikostahili na haipendezi machodi pa Mungu. (angalia kutoka 4:13-16 na
kuendelea). Inabidi tuitikie wito na tumtumainie Mungu anayewezesha na kurudisha thamani
kwa wale wote anaowatuma. Kukumbuka kutokufaa kwetu ni muhimu lakini kusituzuie
kuitikia wito wa Mungu.
Jihadhari na kujishusha kusi-kostahili
(2) Mungu anavyoita
Katika Agano la Kale na pia katika Agano Jipya tunaona kuwa Mungu aliita kwa njia za
miujiza. Mifano hiyo inaweza kupatikana, pamoja na mingine, katiksa maisha ya Musa (msitu
unaoungua), Samweli (sauti ya kusikika), Isaya (maono), na Paulo (mwanga na sauti).
Njia ya Miujiza
Leo miujiza ya namna hiyo bado inatokea mara chache. Pia, Mungu anaweza pia kuita kwa
kupitia kwenye ndoto, na hata unabii. Hata hivyo, tunahitaji kuwa waangalifu hapa. Kwanza
wito kwa utumishi kwenye ndoto lazima uangaliwe kwa uangalifu kwa vile sio kila ndoto
inatoka kwa Mungu. Pili, zawadi ya unabii yaweza kuthibitisha wito au yaweza kuja kama
11
jibu la moja kwa moja kutokana Ndoto na UnabiiUangalifu unahi-tajika Vitu Vya Lazima
Kwa Uongozi Wa Kiroho
na maombi. Lakini haiwezi kukubalika kama njia ya kwanza ya wito (Matendo 9:5-17 na
matendo 13:2-4). Tunajitahidi kuwa waangalifu wakati hao wanaoitwa manabii wanapoenda
kutoka Kanisa hadi Kanisa wakiwawekea watu mikono na kuwaita katika huduma.
Mzigo mzito kwa kazi fulani Licha ya ukweli kuwa Mungu anaita kwa njia za kimiujiza,
tunahitaji kutambua kwamba, mara nyingi zaidi, Mungu anaita kwa kuweka mzigo wa kazi
fulani katika moyo wa mtu. Mzigo huu hauwezi kuondolewa kirahisi; bali hubaki juu ya mtu
huyu mpaka anapoingia katika hudumu aliyoitiwa. Milango iliyo-funguka hufuata wito
Wito wa kiroho utafuatwa na milango "iliyofunguka" kwa huduma, yaani Mungu atatoa
nafasi za kukamilisha wito. Kamwe haifi, na kuacha kutoa nafasi au uwezo wa kuitenda
huduma nafasi au uwezo wa kuitenda huduma hiyo. Wale wanao "hisi" wito maalum lakini
kamwe wasione milango imefunguka lazima wajiulize.
(2) Kutambua wito
Tunatambua Mungu AnapoitaKanisa Litatambua WitoUmuhimu wa wito-sio uamuzi wa
binafsi Kujichagua inasaba-bisha matatizo
Bila kujali namna tunavyopokea wito, Mungu anapoita, tunajua. Kama wito ni wa kweli, sio
sisi tu bali hata Kanisa (Mwili wa Kristo) utatambua; hivyo kuwa wakili `aliyetumwa'. Na
bado, kanisa kamwe haliiti! Mungu anaita, na Kanisa linatambua utume wake wa ki-Mungu.
Kanuni hii ya Ki-Biblia lazima ifuatwe (linganisha Matendo 9:3-16) na matendo 13:1-3).
Damazio anahakikisha kuwa Mungu lazima awe ndiye anayeita mtu kwenye huduma, na
kama ameita, basi huduma ya mtu itatambulika na hatahitaji kukazana au kujitahidi ili
ajulikane. Na kwa upande mwingine wale wanaojijua kwa ndani kabisa kwamba wao
wenyewe wamechagua tu kuwa na huduma ya watu, au "kufanya jambo zuri kwa ajili ya
dunia", au "kuwaridhisha wazazi", au kuwasaidia watu na mbinu mpya za "kisaikologia"
wanaweza vilevile wakajiuzulu leo. Wao pamoja na makanisa watafurahi zaidi.8 Wengine
waliotambuliwa na Kanisa mara nyingi huwa wahudumu wa kujichagua na wainjilisti,
wanaosababisha matatizo makubwa kwa mwili wa Kristo. Kutokuwepo kwa baraka za Mungu
katika huduma yao itakuwa ni uhakikisho kuwa Mungu kamwe hakuwaita, bali watu au
Kanisa.
(4) Kuwa mbunifu mwenyewe kwa asili
Wito wa ki-mungu hauhitaji kufanana babisa na wa mhudumu mwingine au na ule wa mtu
mkubwa wa Mungu. Wengine wanatilia mashaka katika wito wao kwa sababu hawajaupokea
kama ndugu fulani alivyopokea Mungu anaita katika njia tofauti kwa kila mtu na si juu yetu
kuamua ni namna gani tunataka kupokea wito. Kama Mungu akiongea nasi, basi na turidhike
na namna ile ambayo imetokea. Baada ya kupokea wito wetu binafsi na tuwe kama tulivyo
(originals). Hakuna haja ya kuiga wengine. Inashangaza uona baadhi ya wachungaji na
wainjilisti wakiwaiga watu wakuu wa Mungu au hata watumishi wenzao. Mungu hajatuita
kuwa T.L. Osborn, Billy Grahama au Reinhard Bonnke anatutaka tumtumikie kama tulivyo.
Kama vilevile ambavyo Daudi alimpiga Goliati kwa njia aliyoijua yeye vizuri, na hivyo hivyo
nasisi tuwe kama tulivyo. Huduma za asili, kama vile michoro ya kwanza (original) ina
maana kubwa zaidi kuliko nakala tu. Mungu anaita kila mtu kwa njia yakeKuwa kama
ulivyoUlivyo kulinga-nisha na kuinga
12
3. Roho Mtakatifu Kujaa ndani
Matendo ya Mitume inaonyesha wazi kwamba huduma kwa Mungu ilianza tu baada ya
wanafunzi kupokea nguvu kutoka juu. Hakuna mhudumu atakayeweza kukabiliana na nguvu
za uharibifu bila nguvu za Roho Mtakatifu. Kama hii hazina ya kiroho ilikuwa lazima kwa
Mitume, ambao walifanya kazi na Bwana wetu kwa zaidi ya miaka mitatu, je ni kiasi gani
wanahitaji wanaofuata nyayo zao leo.
Ku-kabiliana na majitu yenye nguvu Kwa sababu ya ukosefu wa nguvu za kiroho, Kanisa na
mhudumu wake wameshindwa katika vita vingi vy kiroho. Matokeo yake ufalme wa Mungu
haujapanuka kama ambavyo ingetakiwa. Kiongozi kwa hiyo hawezi kupumnzika mpaka
amepokea ahadi ya baba hata kama itakuwa na maana ya kusimamisha huduma, na kujifungia
mpaka amepokea nguvu za Roho Mtakatifu. Lazima iwe ni changamoto kwa kila mhudumu
kusoma, kuwa hata wale wanaohudumu kwenye meza walitakiwa wajazwe na Roho
Mtakatifu (Matendo 6:1-4). Kamwe tulisahu kuwa hakuna mpango, hata uwe mzuri namna
gani, na wala sio namna fulani nzuri ya uongozi, utakaoweza kushindana na kiongozi
aliyejazwa Roho Mutakatifu.
Mipango na njia nzuri haziwezi kushindana. Vitu Vya Lazima Kwa Uongozi Wa Kiroho
Ni baada tu ya kutimiza mambo hayo matatu hapo juu ndipo mtu anapoweza kuingia katika
uongozi wa kiroho. Kwa hiyo ni lazima aonyeshe, na kila siku kukuza sifa zifuatazo
zinazomwonyesha yeye kama kiongozi.
.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-
13
III. Sifa za Uongozi
Wakati tunaangalia sifa za uongozi, tukumbuke kuwa sifa hizi kila siku inabidi zikuwe
kuelekea katika ukamilifu. Hata siku moja huwezi kusema sasa ni mefika. Viongozi wa
kiroho siku zote lazima wajisalimishe kwa Mungu, kama wanataka kubaki mstari wa mbele
kwa wale wanaowaongoza. kuendelea kukua ni muhimu
Sifa za kiroho zifuatazo kwa namna moja au nyingine zina umuhimu ulio sawa. Hata hivyo
tunahitaji kuangalia kwa karibu zaidi katika hii sifa ya kwanza kwani ndiyo ambayo ni ngeni
zaidi kwa tabia ya asili ya mwanadamu. Lakini bila hiyo, kamwe hatutaweza kuwa viongozi
wa kiroho katika ile namna ambayo Mungu angetutegemea kua.
ngeni zaidi kwa asili ya mwanadamu
1. Mtumishi Mbele za Mungu na Wanadamu
Sifa hii, zaidi ya nyingine yoyote, inaonyesha tofauti kati ya uongozi wa asili na wa kiroho.
Umuhimu wa utumishi lilikuwa ni fundisho ambalo wanafunzi waliliona gumu sana
kulielewa. Hata wakati wa karamu ya mwisho walikuwa wanabishana nani mkubwa kati yao
(Luka 22:24-27). Basi walipima ukuu katika ufalme wa Mungu kwa vigezo vya ulimwengu
huu. Mafundisho ya Kristo kuhusu utumishi Lazima. Katika Injili ya Marko na Luka
anaonyesha tofauti kubwa kati ya Uongozi wa kawaida na wa kiroho. Hivyo kuonyesha ukuu
wa kweli kwa kufuata vigezo vya Mungu.
Tofauti kubwa kati ya uongozi wa asili na wa kiroho
Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa
wao huwatumikisha.
Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu,
balimtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumwa wa wote.
Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa bali kutumika, na
kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi. Marko 10:42-45.
Neno lililotumika katika maandishi ya Kigiriki ni diakonos, lenye maana ya mtumishi au
mhudumu. Inamaanisha mtu anayesahau mahitaji yake mwenyewe ili kuwatumikia wengine.
Neno mtumishi pia lilipewa jina lingine lililokuwa na maana ya mtumwa au mtumwa aliye
kifungoni (bondslave) doulos. Mtumwa aliye vifungoni alikuwa ni mtu aliyeishi maisha yake
kabisa kwa utumishi wa wengine.
Mtumishi Mtumwa Sifa za Uongozi
Akawaambia, Wafalme wa Mataifa huwatawala, na wenye mamlaka juu
yao huitwa wenye fadhila, Lakini kwenu sivyo; bali aliye mkubwa kwenu
na awe kama aliye mdogo; mwenye kuongoza kama yule atumikaye. Luka
22:24-27
Kuwa kama wadogo
Mstari wa mwisho ulikuwa mzito sana katika nchi moja ya Afrika Magharibi, ambapo
tulifanya kazi kwa miaka kadhaa. Huko watoto au vijana wadogo walifanya kazi ambazo
hakukuwa na mtu mwingine aliyekuwa tayari kuzifanya. Kama maji yalitakiwa yachotwe
mtoni, mtoto inabidi afanye hivyo. Mara nyingine waweza kuwaona mtu mzima na kijana
mdogo wakitembea njiani. Mtoto alibeba mzigo wakati yule mtu mzima alitembea mikono
mitupu. Sasa hii ilikuwa inatokana na mila, na ngoja niharakishe kusema kuwa hakuna mila
ambayo in mbaya kabisa kabisa. Lakini pale mila inapopingana na mafundisho ya Biblia mila
lazima iinamie chini na kutoa njia kwa Neno la Mungu kushika hatamu. Hii hasa ni kweli kwa
wale ambao ni viongozi wa kondoo wa Mungu.
14
Uongozi sio ubwana
Maandiko yanaonyesha kuwa utumishi ni hatua ya msingi kabla ya Uongozi (Angalia pia
Marko 9:35; Matayo 18:4; 1 Petro 5:1-4). Mistari hiyo iliyotajwa, ikisomwa inaonyesha wazi
kuwa uongozi sio ubwana. Ubwana hauna nafasi katika viongozi wa Kikristo. Ubwana ni wa
Yesu Kristo tu aliye Bwana na Mwalimu wetu. Lakini tuwe watumishi na ndugu kwa ndugu.
Sasa mtu atataka kusema kwamba Neno la Mungu pia linaongelea mamlaka ya viongozi. Hii
ni kweli. Lakini mamlaka haya hayana uhusiano wowote na ubwana. Hebu tuangalie
maandiko ambayo ndiyo mara nyingi yanatumiwa katika habari hii.
Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana waowanakesha
kwa ajili ya roho zenu; Kama watu watakaotoa hesabu ili kwamba
wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua maana isingewataa ninyi.
Waebrania 13:17.
Kutawala ni kuongoza
Tafsiri sahihi ya neno "tawala" lililotumika katika kigriki (hegeomai) ni "kuongoza" hivyo
halihusiani na neno ubwana. Hivyo aya hii ingeweza kufasiriwa hivi:
Watiimi wale wanaowaongoza (wale wanaongoza kwa kuwa mfano,
wanaochunga kama uongozi) na jinyenyekezeni wenyewe katika
wanayowalisha na maonyo ya upendo, maana wakesha kwa niaba ya nafsi
zenu...
Ni salama kusema kuwa Kiongozi wa kweli, ni yule anayetumia mamlaka katika nguvu ya
utumishi. Uongozi wa Kiroho kamwe haulazimishi, bali mfano mkubwa unaongoza. Yesu
mwenyewe ni mfano mkubwa kuliko wote wa uongozi anaposema ... mwana wa Adamu
alikuja sio kutumikiwa bali kutumikia ...
mfano mkubwa kabisa wa kutumikia wengine
Wale wanaotawala kundi na kutaka utii wote, baada ya muda si mrefu hugeuka kuwa beberu
(katili). Viongozi wa aina hii mara nyingi wamejisukuma katika vyeo kwa kupitia katika siasa
za Kanisa, au wamejiingiza tu katika kundi kwa njia nyingine. Kwa hiyo ushirikiano toka kwa
wale wafuasi wao kuwa haudumu siku zote inawabidi kukazana kuonyesha vyeo na mamlaka
yao kwa sababu hakupewa na Mungu. Kiongozi wa kiroho, kwa upande mwingine, hahitaji
kuwakumbusha wale walio chini yale kuwa yeye ndiye mwenye madaraka kwa sababu
kuwatumikia wengine kuwafungulia mamlaka.
kuwatumikia wengine kuwa-funglia mamlaka
Kiongozi mmoja mashuhuri wa kidini, aliyekuwa anafundisha juu ya uhusiano "mzuri" kati
ya Mchungaji na watu alisema kwa anaamini kuwa walikuwa pale kumtumikia yeye maneno
yake kabisa yalikuwa hivi: "Ninapotaka nyumba yangu ipakwe rangi, naita tu baadhi ya wana
kuundi na wanapaka rangi kwenye nyumba. Ninapotaka uwanja wangu Ulimwe, naita tu
baadhi ya wana kundi na wanalima Uwanja wangu".9 Ralph Mahony anaonyesha wazi na
sawa kabisa kuwa watu katika Kanisa hawapo pale kutumukia Uongozi.10 Ni bahati mbaya
kuwa baadhi ambao wamemua Mungu na kutembea katika njia yake wanadai utumishi wa
mtumwa kwa wafuasi wao. Mungu katika Ezekieli 34:1-10 anasema kwa sauti na kwa
ufasaha kwamba aina hiyo ya Uongozi sio wa kwake na LAZIMA UEPUKWE!
washarika hawapo ili kuutumikia uongozi Biblia inatoa anyo tahadhari
Neno la Bwana likanijia kusema, mwanadamu, toa Unabii juu ya
wachungaji wa Israeli, toa Unabii, uwambia, naam, hao wachungaji,
Bwana MUNGUasema hii; ole wao wachungaji wa Israeli, wanaojilisha
15
wenyewe; je haiwapasi wachungaji kuwalisha Kondoo? Wagonjwa
hawakuwatia nguvu, wala hawakuwaponya wenye maradhi, wala
hamkuwafunga walivunjika, wala hamkuwarudisha waliofukuzwa, wala
hamkuwatafuta waliopotea; bali kwa nguvu na kwa ukali mmewatawala.
Nao wakatawanyika kwa sababu hawakuwa na Mchungaji; wakawa
chakula cha wanyama mwitu, wakatawanyika. Kondoo zangu
walitangatanga katika milima yote, na juu ya kilima kirefu, naam Kondoo
zangu walitawanyika juu ya uso wote wa dunia; wala hapakuwa na mtu
aliyewaulizia wala kuwatafuta. Basi enyi wachungaji, lisikilizeni neno la
Bwana; Kama mimi niishivyo asema Bwana Mungu, kwa sababu kondoo
zangu walikuwa mateka, kondoo zangu wakawa chakula cha wanyama
mwitu wote, kwa sababu hapakuwa na mchungaji, wala wachungaji
wangu hawakuwalisha kondoo zangu;
Kwa sababu hiyo, enyi wachungaji, lisikieni neno la bwana; Bwana
Mungu asema hivi; Tazama mimi ni juu ya wachungaji; nami nitawataka
kondoo zangu mikononi mwao, nami nitawaachisha hiyo kazi ya
kuwalisha kondoo; nao wachungaji hawatajilisha wenyewe tena; nami
nitawaokoa kondoo zangu vinywani mwao, wasiwe, wasiwe tena chakula
chao.
Tabia ya jinsi hii ya ubinafsi na iliyo kati ya nafsi lazima ingeongoza kwenye tukiola matatizo
makubwa yaliyotokea miaka michache iliyopita katika Marekani ya Kusini - Guyana.
Mhudumu wa Injili aitwaye Jim Jones aliwakusanya mamia ya watu kumzunguka. Mambo
yaliendelea vyema mpaka akadai utii kamili hii iliongoza kufikia mahali ambapo alikusanya
vitabu vya Pasi za kusafiria na vitabu vya kutunzia fedha benki. Aliendelea kutangaza ndoa
zote kuwa zimefutwa. Watu wangeweza tu kuolewa, tembeatumbea na kutumia pesa
atakapoidhinisha/ruhusu hivyo. Wale walioasi dhidi aliwaadhibu vibaya sana. Bado watu
waliendelea kumpenda sana/kumwabudu yeye. Jambo baya la kuhusunisha/maafa lilitukia
alipowahudumia wafuasi wake wakati wa kushiriki meza ya Bwana/ushirika mtakatifu, kitu
fulani kilichosababisha kufa kwa mamia ya watu katika kipindi cha siku moja.
Kiongozi wa Kikristo lazima kamwe asitafute mamlaka Tunapohudumu/tumikia wengine
katika roho ya Kristo, mamlaka yataingizwa kwetu na aliyesema "nguvu zote au mamlaka,
nimewapa mimi mbinguni na duniani". Mahoney anathibitisha kwamba kiongonzi
aliyewekwa na Mungu ni yule atafutaye majukumu/kuwajibika. Kiongozi asiye na Mungu ni
yule atafutaye mamlaka. Viongozi wa Kimungu wanakubali kuchukua majukumu kwa ajili ya
kundi la Mungu sawa na mchungaji afanyavyo kwa ajili ya kondoo. Kiongozi mwema/mzuri
wa kiroho daima atakumbuka kwamba kondoo ni mali ya Mungu. Kiongozi mbaya hudai
kondoo ni mali yake binafsi/mwenyewe. Mtume Petro asema:
Lichungeni kundi la Mungu lililoo kwenu, na kulisimamia si kwa kulazimis
hwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu,
bali kwa moyo. Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali
kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi. 1 Petro 5:2-3.
Hakuna haja ya kuwa na hofu kwamba wataipoteza heshima yao watakapoongoza katika hali
ya kama mtumwa. Hivi ndivyo shetani atakavyo tuamini. Bali Kristo ndiye mfano mkuu
kwamba usemi huo siyo kweli. Kinyume cha usemi huo ndicho hutukia. Hakuna kiongozi
awaye yoyote duniani aliye na mamlaka kupita Kristo na wakati huo huo hajawepo aliye
mtumishi mkuu kupita YEYE KRISTO.
16
2. Mtu wa Imani na Maono
(1) Maono
Kiongozi wa kweli hana budi kuwa mtu mwenye maono. kwa lugha rahisi, kuwa na maono
kunamaanisha, kuwa na lengo na mpango wa kujenga nyumba ni lazima kwanza awe na wazo
au "maono" jinsi nyumba hiyo itakavyoonekana. Kwa maneno mengine anahitaji awe na
michoro kamili. Michoro hii kamili lazima ionyeshe wazi nyumba itakuwa ni ya mviringo,
mraba au mstatili, ghorofa moja au mbili. Pia ni lazima ionyesha idadi ya vyumba na
mpangilio wake. Ni bayana kwamba mchoro kamili huhitajika kila tutakapo kujenga. Hivyo
katika kujenga Ufalme wa Mungu yaani Kanisa, utakuta wengi hujenga pasipo kwanza kuwa
na mipango. Neno la Mungu lingali likisema kwamba kukosa maono husababisha ...
maangamizo. Pasipo maono watu huangamia. Mithali 29:18.
Mtu wa Maono Haja ya Mchoro Kamili, Endapo mtu angetuuliza ni nini mipango yenu juu ya
Kanisa? Au mnatarajia Mungu kufanya nini katika Kanisa? Wengine wetu wangeweza kujibu
"twataka tuwafikie walio- Haja ya Maono MaalumuMaono kupitia Maombi
potea dhambini tunataka Mungu atubariki. Lakini majibu kama haya hayatoshelezi. Tunahitaji
kuwa na maono ya wazi juu ya yale tutakayo Mungu atutendee. Maono ya jinsi hii yaweza
atakapoweka mioyoni mwetu mambo atakayo kuyafanya kupitia maisha na huduma yetu.
Pamoja na hayo twaweza kutambua mahitaji kadhaa yanayohitaji kushughulikiwa katika
Kanisa. Pengine twaweza kuongozwa kufanya mikutano ya wazi ya Injili, semina, au
kuendesha mafundisho maalumu na muhimu kwa ajili ya ukuaji wa Kanisa. Lazima
tumruhusu Mungu atupe maono katika maeneo yafuatayo.
(1) Kwanza kabisa twahitaji maono kwa ajili ya maisha yetu binafsi.
Lazima tupange malengo ya maisha yetu wenyewe. Katika kipindi cha
mwaka inatubidi tusibakie vile tulivyokuwa awali.Yapo maeneo
kadhaa katika maisha yetu ambayo hayana budi kuendelea kukua
wakati wote.
(2) Pili: Twahitaji maono kwa ajili ya Makanisa yetu. Lazima tudhamirie
ni watu wangapi tunaotaka tuwafikia kwa Injili, na ni watu wangapi
tunaotaka tuwapokee kama washirika kufikia mwisho wa mwaka n.k.
(3)Tatu: Twahitaji maono kwa ajili ya madhehebu yetu katika ngazi ya
wilaya na hata Kitaifa. Nilazima tumruhusu Mungu kutupa maono kwa
ajili ya maeneo haya yote. Hata hivyo ni lazima iwe na maana halisi
pia ndani ya mipaka ya Imani yetu.
Mtazamo wa ImaniUwezo kuona zaidi kupita
Maono tunayoyazungumzia hapa, yanaweza kuitwa "mtazamo wa Imani". Mtazamo huo wa
Imani hutusaidia kuona zaidi kupita hali halisi iliyopo inavyoonekana, Unaweza kuona
utulivu penye machafuko, uvunaji wa kiroho wa nafsi penye utasa wa kiroho. Hutusaidi
kuona uwezekano wa mtu ambaye bado ni mlevi au kahaba kufanywa mtakatifu. Kiongozi
mwenye maono huona mabadiliko yatakayotokea Mungu atendapo kazi.
Tofauti kati ya kanisa lililokufa na linalokua ni yale maono ya uongozi wake.12 Tofauti kati
ya ibada mfu na hai ni yale maono ya kiongozi wa ibada hiyo. Tofauti kati ya Kanisa lenye
nguvu kifedha na lile dhaifu ni yale maono ya uongozi uliopo. Kuwa na maono yaliyo sahihi
ni ufunguo mkuu kwa ajili ya kukua kwa Kanisa na hata kiroho kwa ujumla. Tofauti ya kufa
na Uzima
17
Pia kuwa na maono juu ya kitu fulani haimaanishi kwamba mambo yote yatafanya kazi
pasipo shida na matatizo. Maono yatajaribiwa kwa dhiki nyingi. Watakuwepo
watakaotwambia kwamba maono hayatoki kwa Bwana. Wengine wanaweza kuinuka kinyume
nasi tunajaribu kuyatekeleza.
Mungu ataruhusu majaribu kama haya ili kuimarisha imani yetu. Hivyo, maono na imani
havina budi kwenda pamoja. Mfano dhahiri wa kibiblia unaonyesha "kujaribiwa kwa maono"
unaonekena katika maisha ya Nehemia. Maono yake yalijaribiwa vilivyo, hakujikunja katika
dhiki hizi zote zilizomkabili. Adui zake hawakufanikiwa kumkatisha tamaa. Badala yake
alimtafuta Mungu katika maombi.
Kujaribiwa kwa MaonoMfano Nehemia
(2) Imani
Kamwe lazima maono yasizidi imani ya mtu. Kama ilivyokwisha kutamkwa awali, tabia hizi
mbili za uongozi huambatana pamoja. Kiongozi mwennye maono kazima awe na imani ili
maono yapate kudhihirika, vinginevyo hatageuka kuwa kivuli kidanganyifu imani
itamwezesha kiongozi kusimama imara katika maono aliyopewa na Mungu, hata ujapotokea
upinzani na dhiki. Habari za Yongi Cho, mchungani wa Kanisa kubwa kuliko yote duniani
lenye washirika zaidi ya 600,000, zashuhudia juu ya ukweli huu. Mwanzoni Mungu
alipompatia maono kujenga Kanisa lenye uwezo wa kukaa watu zaidi ya 10,000 alitii. Kama
angeshindwa kuami ni kwa imani iliyo zaidi ya imani ya kawaida jengolingekuwa
halijakamilika mpaka sasa kupitia imani aliyopewa na Mungu Cho aliweza kushinda vikwazo
vingi, na leo analiongoza kongamano moja kubwa zaidi kuliko yote ulimwenguni. Imani hudhihirisha
MaonoYongi Cho Kazi ya Ufalme wa Mungu mara zote itakutana na upinzani na
magumu mengi. Kwa ajili hii kiongozi Mkristo lazima afanye kila kazi yake kwa imani.
Maisha yake ya imani.
Ikabili kila kazi kwa imani Kwa sababu daima mara nyingi hataweza kuona mipango yake
yote ikiendelea kikamilifu mwanzoni. Katika matukio mengi panakuwapo vidhibitisha
vichache vya mafanikio. Uwezekano wa kutofaulu kabisa mara zote hufifia. Hata hivyo,
kiongozi wa kweli huchukua hatua katika imani na akiwa na maarifa au ufahamu kuwa
Mungu yu upande wake.
Imani kwa wakati wa matatizo
Ni jambo la muhimu kabisa kwa kila kiongozi kuwa na kiwango kikubwa cha imani zaidi ya
wafuasi wa wastani. Wakati wa matatizo unapojiinua, kiongozi Mkristo lazima atende katika
imani. Twaona hivi waziwazi katika maisha ya watu mashuhuri katika biblia. Mfano Musa
katika bahari nyekundu ya Shamu au Joshua mbele ya Jeriko. Katika mazingira ya jinsi kama
hiyo imani huwa muhimu sana katika kuyatekeleza yale ambayo Mungu ametuamuru
tuyafanye. Vinginevyo tutakuwa kama wajumbe wale kumi waliorudi Israeli wakitoa taarifa
kwamba majitu ni makubwa mno. Wawili tu miongoni mwa kumi ma wawili walikuwa
wenye maono muhimu na imani ili kuimiliki nchi.
3. Kuwa na Ujasiri Katika Neno na Tendo
Sanders anasema, kiongozi wa kiroho anapaswa kuwa na ujasiri kwa mpangilio ulio bora
zaidi kuliko. Siyo ujasiri katika kuendelea tu bali hodari katika mwili pia.13
Inatakiwa ujasiri kunena dhidi ya dhambi na zinaa, pia dhidi tabia ya unafiki. Yesu aliuweka
katika matendo ujasiri aliokuwa nao alipokuwa akiwahutubia mafarisayo. Petro na Yohana
walijawa na ujasiri mkuu waliposimama mbele ya baraza la Sanhedri.
Sanders anatukumbusha kuwa Martin Luther mleta matengenezo ya Kanisa mkuu alikuwa ana
sifa hii muhimu kwa kipimo kikuu aliposimama pekee dhidi ya dola yote ya Kanisa la Kirumi
18
la Kikatoliki. Kwa sababu ya ujasiri na uhodari Mungu angeweza kuleta mabadiliko makubwa
katika historia ya Kanisa Rafiki yake alipomtahadharisha asiende Worms alisema "Lazima
nitakwenda Worms ingawaje kuna mashetani wengi kama vigae juu ya mapaa." Alipoulizwa
na mtawala wa dola ili akanushe alitangaza "Kwa mabaraza au Papa siwezi kuwa tofauti ya
hayo kwani mara nyingi wamekuwa wakikosea.
Dhamiri yangu ni mfungwa kwa neno la Mungu. Hapa ninasimama; siwezi kufanya
kinginecho chochote. Mungu nisaidie. Siku chache kabla ya kifo chake, akilikumbuka tukio
hilo Luther alisema: "Sikuogopa chochote, Mungu aweza kumfanya mmoja kuwa jasiri sana.
Sikujua endapo ningeweza kububujika furaha sasa."14
Ujasiri wa jinsi hiyo hauji kwa watu pasipo kushughulikiwa. Vivyo hivyo Mungu huwaamuru
viongozi katika kazi yake kuwa na ujasiri mwema. Wangalikuwa hawana hofu, amri hii isinge
kuwa na maana yeyote. Joshua alipokea ujasiri huu (Joshua 1:6,7,9). Petro na Yonana
iliwapasa kumtafuta katika maombi pamoja na Kanisa, baada ya kutishiwa na wajumbe wa
baraza la Sanhedri (Matendo 4:24-32).
Ujasiri wa kiongozi huonyeshwa pia kimatendo katika kukubali kwako kuzikabili kweli zisizo
za kumpendeza na mazingira katika utulivu, na ndipo huchukua hatua ya kutenda kwa uthabiti
katika huru ya kweli hizi, ingawaje yaweza kumaanisha kuyakabili madhara binafsi au
kutokutambulika sana.15 Kiutendaji ujasiri huhitajika ili kuwashughulikia washarika wa
Kanisa wenye kufanya mambo yawe magumu na wenye ushawishi, au kusema wazi dhidi ya
dhambi ndani ya jumuiya au Kanisa.
Ujasiri unahitajika ili manabii watamke waziwazi tabia zisizo za utawa na ukengeufu. Nathan
mbele ya Daudi, au Elia mbele ya Ahabu na Yohana Mbatizaji mbele ya Herode, wote
walithibitisha ujasiri wa Kimungu. Ujasiri wa jinsi hiyo hauhitajiki kwa ajili ya kutamka wazi
yaliyo mabaya tu, bali kama Sanders asemavyo, "watu huwatarajia viongozi kutenda kwa
ujasiri na kupoteza vichwa vyao, lakini siyo wao. Huwatia nguvu wafuasi wao katikati ya
mazingira ya kuwavunja vipande vipande.16
Ujasiri wahitajika ili kuwa Mkristo katika ulimwengu unaooza. Pia wahitajika ujasiri zaidi ili
kuwa Kiongozi Mkristo.
4. Kukabili Changamoto ya Kufanya Uamuzi
Kiongozi wa Kiroho mara kwa mara hukabiliwa na mambo yanayohitaji jibu lake katika
matukio mengi atajaribiwa kuchelewesha kufikia uamuzi. Toa jawabu la mambo Hasa
anapoyakabili matatizo na mazingira mabaya hata hivyo hushindwa kutoa jawabu
hakutakuwa kufa tu kwa uongozi wake bali kutaharibu na kufanya kazi anayoiongoza
isiendelee kukua. Kuchelewesha kutoa jibu mara kwa mara kutaleta madhara ya kudumu
kwake na kwa Kanisa.
Usiepuke maamuzi yasiyo-furahisha Kuna watu ambao huhamishia majukumu yao kwa
wengine ili kuepuka maamuzi mabaya. Kazi inapokamilika watu hao wanataka wapokee sifa
ya ushindi. Tabia ya jinsi hii huharibu Uongozi wao kufuatana na asemavyo Sanders alama ya
kiongozi wa kweli ni kufanya maamuzi haraka na yaliyo waziwazi. Wakati kweli zote
zimepatikana. Punde kiongozi wa kiroho awapo na uhakika wa mapenzi ya Mungu, mara
atachukua hatua ya kutenda pasipo kujali yatakayotokea. Hata anapotenda lazima akubali
Uajibikaji kikamilifu kwa kushindwa au kufanikiwa na asiziweke lawama kwa mwingine
awaye yeyote yele.17
Lipa gharama iliyo-husika
Kawaida, uamuzi wa dhati uliokosewa ni bora zaidi kuliko kutokuwa na uamuzi wowote.
Katika maamuzi mengi sehemu iliyo ngumu si katika kujua nini tunapaswa tufanye, bali
19
afadhali kulipa gharama inayotakiwa. Orodha hii huenda ikamsaidia Kiongozi katika hatua za
kufanya uamuzi.
Usifanye uamuzi katika kuelemewa na mizigo mizito. Ni hafadhali
kuchelewesha uamuzi kuliko kufanya uamuzi wakati una hasira,
umechanganyikiwa au uwapo chimi ya mgandamizo mkuu.
Usifanye maamuzi ya kufumba na kufumbua. Maamuzi ya mara/haraka ni
ubunifu tu mpaka yatengamazwe na taarifa za kutosha.
Usioburuza miguu yako. Uamuzi lazima ufikiwe wakati fulani. Kuzimisha
kufikia uamuzi, kawaida huleta matokeo ambaayo ni nyongeza kwa
rasilimali iliyojaa tele ya biashara ambayo haijamaliziwa.
Shauriana na wengine, hasa wale ambao uamuzi wako utagusa mambo yao
Usijaribu kufurahia mwanzoni kila kitu. Kamwe hutakuwa na kweli zote,
hivyo itakubidi uwe na msingi thabiti wa matendo katika kweli hizo
zipatikanazo wkati uamuzi wako unahitajika.
Usiogope kufanya uamuzi usio sahihi. Hakuna mtu anayejua kila kitu.
Kuna hatari kuhusika katika kila uamuzi.
Punde uamuzi unapofikiwa, endelea na jambo jingine. Hupati chochote
kwa kuyahofia maamuzi ya wakati uliopita na wapoteza uwezo wa kutoa
kikamilifu usikivu usiokuchukiza kwa maamuzi mwngine muhimu.18
5. Uhitaji wa Hekima na Uamuzi Bora
Nyakati nyingine kiongozi wa kiroho anakabiliwa na mambo magumu na mazingira
yasiyoeleweka bayana, yanayotaka jibu na hatua atakayochukua. Endapo hatua atakayochua
itakosa hekima na uamuzi bora, matokeo yatakuwa machafuko mabaya sana
(1) Hekima
Hekima hufanya tabia zote zilizotamkwa awali kufanya kazi, ilizipate kuleta matokeo zaidi.
Hekima itatusaidia kuongoza katika hali ya kutumika kama mtumwa kwa jinsi ambayo
wafuasi wetu hawataipoteza heshima yao kwetu. Itatusaidia kuona vipi tuyaweke katika
matendo maono yetu, na kuwa na ujasiri pasipo kuelemewa zaidi kuliko mambo. Kupitia
hekima-tutafanya maamuzi sahihi.
Hekima humaanisha kufanya kazi
Hekima pia huhitajika kwa ajili ya mikutano ambamo mazingira magumu au matatizo
hujadiliwa vivyo hivyo katika ugumu wa uhusiano baina ya watu. Hekima ni zaidi ya maarifa
au ufahamu. La mwishoni ulimbikizaji wa kweli, la awali ni kuwa na huru katika moyo wa
mambo hivyo hutusaidia sisi kuwa wenye hekima kwa wakati sahihi.
(2) Uamuzi Bora
Uamuzi bora ni Hekima katika tendo. Sifa hii humpa kiongozi ulinganifu wa uzito ulio
muhimu afanyapo maamuzi. Inamsaidia yeye kuona nyuma ya yaliyo dhahiri na kwa makini
kabisa kupima mambo ambayo yanawezekana. Kiongozi lazima aweze kuamua mazingira na
pia uwezo na ushindani wa wale anaowaongoza, kabla ya kuwapatia kazi na majukumu. Ili
20
kufanya uamuzi bora kwa matendo lazima asiwe mwenye maoni aliyokwishapokea pembeni,
upendeleo na asiwe mwenye kusimamia yale yaliyo katika ufahamu wake mwenyewe.
Hekima ikifanya kazi Kuona yasiyo dhahiri
(3) Kujifahamu - Binafsi
Binafsi kufahamu udhaifu na nguvu zako Kiongozi wa kiroho atashindwa katika maamuzi
yake na hataweza kufanya uamuzi bora endapo hajifahamu binafsi. Lazima awe mwenye
uwezo wa kuangalia nyuma na kuchambua upya hatua alizokwisha chukua na hisia zake
hatika hali ya ukweli kabisa. Ni muhimu kwakutambua udhaifu na nguvu zake. Neema ya
kukubali kushindwa kwake pasipo kujisikia kudhalilishwa, lazima iwe sehemu ya tabia yake.
Kwa wakati huo huo lazima aweze kuchukua hali ya mafanikio pasipo kiburi kuchipuka ndani
yake.
Katika Warumi 12:3-6 Paulo anasema:
Kwa kuwa ninasema, kupitia Neema niliyopewa namwambia kila mtu
aliyeko kwenu, asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya
kiasi, kama Mungu alivyomgawia kiasi, cha imani ... tuna karama zilizo
mbalimbali, kwa kadri ya neema tuliyopewa; ...
Ulinganifu sahihi wa tulivyo Maandiko hapo hututia moyo sisi tuwe na mtazamo wenye
ulinganifu sahihi kuhusu sisi wenyewe, jinsi gani tulivyo na vitu gani tunavyo. Haitupasi
kujifikiria zaidi kuliko au upungufu kuliko vile tulivyo binafsi.
6. Unyenyekevu - Tabia ya Moyo
Utumwa na unyenyekevu havitenganishwi daima. Unyenyekevu wa kweli huleta matokeo ya
utumwa, na utumwa hutokana na unyenyekevu. Tabia hizi ni muhimu bayana kwa kila
kiongozi Mkristo.
Unyenye-kevu alama ya Kiroho cha kweli Katika mizani ya Mungu ya uthamani
unyenyekevu umesimama katika nafasi ya juu sana. Katika siku zetu kuna kujitangazabinafsi.
Lakini maana rahisi ya Kristo kuhusu uongozi inahusisha upole wa binafsi katika
kuwafundisha wanafunzi wake kwa ajili ya kuongoza baadaye, Kristo alikazia mara kwa mara
tena umuhimu wa tabia hii ya utu wema. Unyenyekevu wa Kiongozi, kama hali ya kiroho
yapaswa kuwa sifa inayokuwa daima. Kama Yohana Mbatizaji, tabia ya kiongozi lazima iwe
"Lazima aongezeke, ila mimi lazima nipungue" matatizo mengi ambayo yana mizizi katika
watu binafsi wenye mapambano yanayoendelea ili watambulike na kujiinua wenyewe.
Wengine wamekanyagwa na kutumiwa katika kujitafutia faida za binafsi. Haikumaanishwa
iwe hivyo na mwanzilishi wa Kanisa, Kristo Yesu. Kwake yeye unyenyekevu ilikuwa alama
ya kiroho ya kweli.
Mungu awatumiapo wanaume na wanawake waweza kuonekana wakuu sana machoni pa
watu. Kwa ajili hii, ni muhimu tujikumbushe wenyewe kwamba hakika sisi si chochote pasipo
yeye. Hasa tukizingatia asili ya mwanadamu iliyo na kawaida ya kujitukuza. Inatupasa
kuzingatia katika ufahamu wetu kwamba shoka hiiwezi kujivuna kwa ajili ya miti iliyokatwa
ikaanguka. Haliwezi kufanya chochote kwa afanyaye shughuli za mbao. Alilinoa, na alitumia.
Punde anapolitupa kando, hufanyika chuma la zamani tu. Huwa vivyo hivyo kwetu na
huduma.
Mwelekeo wa kujitukuza Hivyo kiongozi wa kiroho wa leo, kwa vyevyote vile atakuwa yule
ambaye alionyesha unyenyekevu jana kwa kufanya kazi kwa furaha na uaminifu katika hatua
ya pili.19 Bahati mbaya wachache sana wako tayari kufanya hivyo.
21
7. Ukamilifu
Kwa maneno rahisi, ukamilifu ni kuwa mkweli kimsingi. Kuwa na ukamilifu humaanisha
kutogawanyika katika neno na matendo. Vile kiongozi anasema na kufanya lazima iwe
taswira ya kweli ya ushawishi uliopo moyoni mwake. Lazima awe mtu mwenye kusimamia
neno lake asemalo, akizitunza ahadi zake na majukumu aliyopewa kuyasimamia. Endapo
ukamilifu wake utakuwa na walakini watu watapoteza tumaini lao thabiti katika uongozi
wake. Kiongozi mwenye ukamilifu pia atakuwa mtu mwenye ujasiri.
Taswira ya ushawishi wa moyoni Zaidi ya hayo ukamilifu ni kung'ang'ania kwa dhati
uthamani wa tabia humpatia kiongozi tabia inayoonekana wazi hadi ndani. Hakuna agenda
yenye kufichwa. Hatajificha nyuma ya "kinyago" ili kuwatumikisha wengine kwa faida yake.
Mafarisayo walikosa tabia hii njema ya kiroho. Hii ndiyo sababu walipewa changamoto na
kukemewa vilivyo na Bwana wetu.
Hakuna agenda zilizo-fichwa
8. Kiongozi na Ucheshi
Valvu ya Usalama Ucheshi mzuri ni alama ya kiongozi wa kiroho. Uthamani wake waweza
kutokuelezeka, kwa vile ufanyavyo kwa ajili yake, na kwa kutumia katika huduma yake.
Kiongozi mmoja Mkristo wakati fulani alisema: "Kamwe sijakutana na kiongozi asiye
mcheshi Uwezo huu wa kusimama nje ya nafsi ya mtu na yanayomzingira, kuona mambo
katika mtazamo fulani na kucheka. Ni valvu ya usalama." Kamwe hutawaongoza wengine
mbali bila furaha ya Bwana na viambata vyake, ucheshi.20
Kiongozi wa kiroho lazima awe na uwezo wa kucheka ajifikiriapo mwenyewe, na asijichukue
mwenyewe katika hali ya kununa sana. Njia za kucheka ni alama bora zaidi ya imani, ndipo
njia hufuatia njia ya kujali na kutokuwa na mzaha. Mbali na umuhimu wa ucheshi, twahitajika
mambo manne.
(1) Kamwe tusiruhusu watu wayacheke mambo matakatifu.
(2) Ucheshi wetu lazima uwe safi
(3) Kipimo chema cha ucheshi wetu mahali unapostahili ni iwapo twaingoza hali
hiyo au inatuangoza.
(4) Tusifanye au tusitamke mizaha katika mambo yaliyogharimiwa na wengine.
Mambo haya yazingatiwapo ucheshi utafanyika kitendea kazi kwa kiongozi wa kiroho.
9. Maisha ya Uanafunzi
Kwa kumalizia pasipo kupunguza umuhumu wake, Kiongozi wa kweli atakuwa mfano bora
wa maisha ya mwanafunzi. Kuishi kiuanafunzi na kiutumwa ni sifa mbili za kudumu za
kiongozi wa kiroho.
Tatizo linalolikabili Kanisa la wakati huu linasababishwa na kweli kwamba wapo viongozi
wengi ambao hushindwa kuonyesha alama au sifa za mwanafunzi wa kweli. Maisha yao
huonyesha kuwa ni watu wa tabia za mwilini, wanaonuia - nyadhifa tu na ubinafsi kwa
kufanya hayo wanasababisha matatizo makubwa katika Mwili wa Kristo. Hawaongozwi na
Roho bali hufanya maamuzi yaliyo matakwa yao wenyewe. Hawana alama za wanafunzi
22
ambazo zipo katika makundi mawili. Yakiitwa: (1) upendo usio wa ghoshiwa kwa Mungu na
wengine na (2) Maisha ya kujikana-mwenyewe ambayo yatauruhusu msalaba ufanye kazi ya
mageuzi katika maisha yao, ili matendo ya mwili yapate kufishwa. Maandiko yanatamka hivi
yakifafanua; Ni pale tu upendo kwa Mungu na wengine utakapotulazimisha sisi na pale
tutakapotaka kubeba msalaba wetu kila siku yaani kufa nafsi, tunafanyika wanafunzi wa
kweli.
Siyo wanafunzi wengi Yesu aliamuru kuwafanya watu kuwa wanafunzi wake. Kama viongozi
wa kiroho watashindwa kuishi kama wanafunzi wenyewe, hawataweza kuutimiliza mwito
mkuu. Uanafunzi wataka vielelezo kiuwajibikaji. Kufundisha na kuhuburi juu ya uanafunzi
haitoshi. Mifano katika matendo huhitajika. Wafanye Wanafunzi kwa kuwa Mwanafunzi
.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.
23
Kazi/Jukumu la Kiongozi
IV. Jukumu la Kiongozi
Sifa za uongozi mbazo zimetamkwa tayari zina umuhimu hakika. Lakini hazitoshi pekee ili
kazi ifanyike. Kiongozi lazima ajue kuchukua hatua toka maono kwenda katika utekelezaji.
Lazima ashihirishe ustadi wa uongozi ufuatao. Pasipo ustadi aweza kutambulika mtu wa
rohoni tu ila hatakuwa kiongozi. Kutoka Maono hadi utendaji Kutoka Maono Kwenda Katika
Utekelezaji
1. Kuwekwa ili Kutawala
Pasipo utawala wenye nguvu ya kufanya kazi ya kusimamia maono na hali ya kiroho ya
kiongozi hivi vitashindwa kutimiliza chochote kile. Kupita kutoka maono kwenda katika
matendo kunahitaji kupangilia kwa makini, ambayo huhusishwa upangaji malengo, kufuatana
na upewaji kipaumbele chake, usimamizi na thamani; kwa maneno mengine wahitajika
utawala mwema. Utawala mwema wahitajika
Agano Jipya katika 1 Wakorintho 12:28 linasema moja ya karama za huduma kama karama
ya kutawala (NIV). Karama hii haitolewi ili kuifanya kazi ya Mungu iwe ngumu au ya
kuchosha balikutoa utaratibu sahihi, kuunganisha na kutoa nguvu ya kufanya kazi katika
mwili wake. Hampatia Kiongozi mwelekeo muhimu ili kwamba aweze kuwafanya watu
wafanye hivyo huifanya kazi na kuwaongoza kuelekea lengo maalumu, kwa kufanya hivyo,
huifanya kazi iwe ya ufanisi zaidi. Utawala wa kawaida mara nyingi huonyesha ukandamizaji
na kuandaa kunako pita kiwango. Uwezo wa kutawala kiroho hata hivyo, utatoa nafasi kwa
ajili ya Roho Mtakatifu na utaendeshwa katika hali ya unyenyekevu na upole katika nidhumu.
Mwelekeo na utendaji kazi
Kila aliitwa na Mungu kuingia katika uongozi atakuwa na ujuzi fulani wa kutawala kwa kadri
ya wito ulivyo mkuu ndivyo uweza wa kutawala utakavyokuwa mkuu.
Kiongozi katika kanisa kijijini hahitaji ujuzi kwa kiwango zaidi ya mtu atawalaye katika ngazi
ya Wilaya, Taifa, Bara au Kimataifa mara nyingine watu hutaka uongozi ambao si sawa na
kiwango cha uwezo wao kutawala. Ngazi tofauti tofauti
Hii itasababisha machafuko na kuchanganyika, kukosa mwelekeo na hata mugawanyiko
mkubwa wa shirika baadaye. Mungu hatatuita tushike nyadhifa fulani pasipo kutupatia
"karama" muhinu za kutekeleza jukumu hilo. Wahusishe wengine wenye ujizi unaohijika
Kutawala haimaanishi kuwa mtu awe "Jeki" ya biashara zote. Wachache sana watakuwa na
maarifa katika maeneo yote yanayoangukia chini ya utawala. Kwa ajili hiyo Kiongozi atafute
ushauri wa hekim katika maeneo ambayo yeye mwenyewe hana maarifa juu yake,
hakufundishwa, na hana uzoefu. Kujitenga wenyewe kutoka ushauri na masahihisho ya walio
na ujuzi imamaanisha kuyaendea mambo mabaya. Kama hatuna maarifa ya kujenga majumba
na tunajaribu kujenga Kanisa, au twawajibika kupanga matumizi ya fedha nyingi na pasipo
kuwa na maarifa juu ya jinsi ya kutumia fedha lazima tuwe wanyenyekevu vya kutosha ili
tukubali kutokuweza kwetu, na kutafuta msaada katika maeneo haya. Mahoney anasema,
mashirika ya Kikristo mara nyingi hayana mpango mzuri wa matumizi ya fedha
zinazohitajika kwa ajili ya mradi fulani. Hata hivyo, watu wanapouliza juu ya ukosekanaji wa
mipango, haumbiwa, "Ndugu wewe huelewi. Hatuendeshi shirika hili kama biashara,
tunaendesha kwa imani mara nyingine huwafanya watu wakope zaidi ya wanavyoweza kulipa
kwa viwango vya riba kubwa sana na malipo halisi. Huduma nyingi njema za Kikristo
24
zimeshindwa kwa sababu Kiongozi ameukataa ushauri juu ya kutawala kutoka kwa ndugu
aliye na uzoefu.21 Kama Kiongozi ana kiwango fulani tu cha uwezo wa kutawala lazima
awaruhusu wale walio na vipaji vinavyohitajika ili kuleta utaratibu na ufanisi. Kama
ukosekanaji wa ujuzi wa kutawala hautasemwa wazi wazi na mhusika, shughuli zitaacha
kukua na kuendelea. Kupuuzia alama za tahadhari itatuongoza kuvunjika kwa Shirika.
Ukuaji huzuiliwa Kujifunza Kanuni muhimu
Ukosefu wa utawala sahihi mara nyingi huzuia ukuaji wa Makanisa yetu na mashirika.
Inasemekana kuwa asilimia themanini na tano ya makanisa yote Marekani yana watu pungufu
zaidi ya washarika mia mbili. Kinachosababisha hali kuwa hivi ni kwamba katika matukio
mengi uongozi hautambui uhitaji wa utawala. Mtu mmoja hawezi katika hali ya ufanisi
kuwaongoza zaidi ya watu mia moja sabini na tano. Kwa ajili hii, Makanisa machache hufikia
zaidi hatua hiyo kwa sababu kiongozi anashindwa kutoa utawala unaohitajika.22 Kila
kiongozi hana budi kujifunza kanuni muhimu zaidi za kimsingi za utawala kama anataka
afanikiwe.
2. Umuhimu wa Kuwa na Mipango
Utekelezaji wa maono huhitaji kupangilia kwa makini. Kiongozi lazima awe na mpango ili
apate kufikia malengo yake. Hawezi kupanga mpango wakati ameendelea katika utekelezaji.
Kila mjenzi mwelevu ana michoro kabla hajaanza ujenzi. Vivyo kiongozi mwelevu atakuwa
na mpango kwa ajili ya utekelezaji wa maono yake. Kupangilia mambo ni hatua ambayo kwa
kuipitia hatua muhimu huorodheshwa. Kupangilia kwa makini ni muhimu Kiongozi lazima
apange shughuli zake za kiwiki, kimwezi na kimwaka. Tunapoanda mpango makini lazima
tujiulize maswali yafuatayo:
(1) Nini tunataka kufanye (Kutayarisha malengo)?
(2) Kwa njia gani tutayafanya (kuelezea
hatua - mbinu)
(3) Wakati gani tutaanza na tutamaliza
(4) Wafanyakazi gani na fedha kiasi au mali
kiasi gani (Eelezea aina ya wafanyakazi
na mahitaji ya kifedha)
(5)Vifaa gani vitatumika kupima thamani au gharama.
Kuwahamasisha na kuwatia ari watu, hata kuufanya mradi uanze kwa kasi haitoshi. Mpango
wa uhakika wahitajika kama mradi hautaishia katika kuleta machafuko au matatizo. Yesu
alisema:
Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi
kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? Asije
akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao
wakaanza kumdhihaki, wakisema, mtu huyu alianza kujenga, akawa hana
nguvu za kumaliza. Luke 14:28-30.
Kupanga siyo jambo jipya lililoanza siku hizi. Katika Angano Jipya twaona Paulo alifuata
mpango maalumu. Mkakati wa Paulo Alipoliamzisha Kanisa, aliweza kwenda ndani ya mji
uliopangiliwa kimikakati (Warumi 15:18-24). Hapo aliihubiri Injili na kutenda miujiza, kwa
25
kadri Roho Mtakatifu alivyomwezesha (Mstari 19,20) Mara nyingi alianza kwendea sehemu
nyinginezo kwa kuanzia hekaluni, hapo alihubiri habari za Yesu. Kisha akawaendea mataifa
katika mji ule. Baada ya kundi la waumini wa Kristo kuanzishwa aliwaacha mikononi mwa
wazee wa Kanisa ili waendelee kuwatunza, au mmoja miongoni mwa watendakazi pamoja
naye angaliweza kubaki mpaka kundi hilo la waumini liwe na nguvu kiasi cha kutosha na
tayari kuwa na uongozi kutoka miongoni mwao wenyewe. Baada ya kuondoka Paulo
aliendelea kuwasiliana na Makanisa kwa nyaraka zake. Kadri muda ulivyoendelea yeye au
mtendakazi miongoni kwa watendakazi pamoja naye aliweza kurudi ili kuwatia moyo. Kama
Paulo, Mtume Mkuu aliufuata mpango maalumu wenye kueleweka kwa kuieneza Injili,
hatupasi sisi nasi kufanya vivyo?
Kuwa Mshirika na Mungu Mipango lazima ifanywe katika hali ya maombi na kutafakari.
Lazima tuutafute ulinzi na hekima ya Mungu, kama twataka tufanikiwe. Mpaka tufanyike
washirika na Mungu, vinginevyo na mahitaji haya muhimu na ya lazima, mipango huanza na
kuweka malengo.
(1) Uwekaji wa malengo
Lengo hupimika, hugusika, hufikiwa au hupatikana , ni hatua hakika isaidiayo katika
kutekeleza maono tuliyopatiwa na Mungu.23 Bila uwekaji wa malengo maono yataendelea
kubaki kama wazo tu. Malengo lazima yawekwe kimpangilio katika imani, maombi na
kufunga. Yanachangizo katika yale yanayotakiwa kufanywa na yale yatakayopatikana.
malengo kulingana na umuhimu wake
Baada ya malengo kutambulika lazima yawekwe katika utaratibu kufuatana na umuhimu
wake zaidi ya jinginelo. Viongozi wengi hufanya kazi kwa kiwango cha wastani badala ya
kiwango kuzidi sana. Moja ya sababu ni kwa sababu wanashindwa kutoa kipaumbele kwa
malengo yanayostahili. Kutoa kipaumbele humaanisha kuyachimbua kwa makini yale tu
ambayo tungepaswa kuyafanya endapo ingetulazimu kuacha vitu vingine vyote. Upo uhitaji
wa kuzigawanya kazi nyinginezo katika vipengele vitatu, vikiitwa (1) Muhimu sana (2)
Muhimu (3) Si muhimu sana. Mara ifanyikavyo hivi yatupasa kuweka alama chini ya kila
kipengere sawasawa na umuhimu au ulazima wake. Lazima tuamue nini ni cha kupewa
kipaumbele na tukifanye namba moja katika orodha yetu. Baada ya kufanya hivyo tuamue
namba mbili, na kisha kuendelea. Kutoa kipaumbele ni hidhamu iliyo muhimu zaidi kuliko.
Mungu huwatafuta wanaume na wanawake ambao wanaweza kupanga utoaji wa kipaumbele
kwa tendo litakiwalo na kufanya mtiririko wenye maana ambao wataufanyia kazi.
(2) Uchoraji wa Mkakati
Jinsi gani yabidi ufanyike? Hatua gani zabidi zichukuliwe ili kufikia lengo? Majibu kwa
maswali haya yatatoa mkakati unaohitajika. Hata hivyo, kufafanua kila hatua kunahitaji muda
mwingi na kazi ngumu. Bali gharama hii lazima ilipwe kwani mafanikio ya mpango au mradi
wowote yanahusiana moja kwa moja na muda atumiao mtu kufafanua jinsi gani malengo yake
yatapatikana.
Muda na kazi ngumu huhitajika
(3) Kuamua muda - utakaotumika
Muda wa mwisho wa kukamilisha lazima upangwe, mara inapoamuliwa uelekeo gani
tuaelekea. Lazima tujaribu tufanye mahesabu na kupanga muda unaohitajika kwakila hatua.
Kwa kufanya hivyo tutaweza kuamua kama mradi unaendelea vyema sawasawa na
ilivyopangwa.24 Kuweka muda wa mwisho Kwa mfano: Kama tunapanga kufanya mkutano
26
wa hadhara, lazima tupange tarehe utakapofanyika. Muda uliopangwa lazima uruhusu
maandalizi ya kiroho kufanyika (maombi na kufunga), kuwafunza washauri, uchapishaji wa
matangazo na barua za mwaliko na kazi nyinginezo za uhusiano na watu. Zaidi lazima
pawepo muda wa kutosha kuandaa na kuvijaribu vyombo muhimu vitakvyotumika na kupata
vibali vinavyostahili kutoka serikali ya sehemu ile n.k. Wanenaji au wahubiri na kwaya
zitakazoshiriki lazima wapatiwe taarifa mapema kabla ya wakati. Mialiko mara nyingi
hutupwa kapuni kwa sababu imetalewa kwa kipindi kifupi.
(4) Swali juu ya Nguvu - ya watu itakayotumika na Fedha
Kuwahusisha wengine Kiongozi wa kweli kamwe hatajaribu kafanya mambo yote peke yake.
Atawahusisha wengine, na atafanya mambo au shughuli zifanyike kupitia wao. Baada ya
kuamriwa na Roho kuhusu mtu fulani alivyo na ujuzi zaidi ya wengine atamwendea awe
msaidizi wa kutazamiwa. Kama ataafiki kusaidia Kiongozi atampatia taarifa muhimu na
mafunzo, ndiposa atasimamia maendeleo yao na utendaji kazi yao. Amua kiasi cha fedha
kitakacho-husika
Iliyo mingi, kama si mipango au miradi au miradi yote huhitaji zaidi ya nguvu za mtu mmoja.
Inahitaji pesa. Itagharimu nini?, ni swali ambalo huulizwa mara tu mpango/mradi
unapoanzishwa. Kuamua kuhusika kwa fedha mtu lazima atazame hatua tofauti za kimkakati
na kukisia gharama za binafsi na za jumla. Hata hivyo, kujua gharama iliyotumika siyo
mwisho wa tatizo. Gharama zinapokuwa juu kuliko bajeti ilivyo sasa au imani yetu
inavyoruhusu, lazima tupitie upya mipango yetu na tuone wapi twaweza kupunguza matumizi
yasiyo na umuhimu. Wengi kwa sababu walihuia zaidi kuliko uwezo wao wa kifedha au
imani yao ilivyoruhusu.
(5) Kupima ubora/thamani ya kazi
Ukaguzi wa kazi ina vyoendeleaKurekebisha mipango Mpango wetu unapofanyiwa kazi
wahitaji kukaguliwa mara kwa mara. Kwa ajili hiyo, mfumo wa kupima thamani ya kazi/kitu
ambacho utakagua maendeleo, ya mpango lazima uanzishwe. Ukaguzi wa maendeleo ya kazi
waweza kufanywa kupitia mikutano ya Kamati, taarifa ya mdomo au iliyoandikwa, taarifa ya
takwimu, simu toka kwa kiongozi, na kwa kuona mwenyewe kwa macho. Ni muhimu kuona
wapi panahitaji marekebosho au kufanya mabadiliko hata kubadilisha jinsi ya kufikia.
Kurudisha taarifa mara kwa mara kuliko kwema ni muhimu ili upimaji wa thamani au ubora
upate kufanyika vyema. Mtu fulani ametamka kwamba ni jambo lisilo la kawaida au ni jambo
la kipekee kuliko kanuni kwamba malengo yatafikiwa pasipo kurekebisha mpango au pasipo
kukabiliwa na matatizo na vikwazo.25 Kwa ajili hii upimaji wa thamani au ubora wa mara
kwa mara utaonyesha kama mradi/mpango unalengwa vilivyo, kama malengo yalifikiwa, na
kama maono yametimilizwa hadi mwisho. Upimaji thamani/ubora huhakikisha uwajibikaji
kutao hesabu jambo ambalo lipo kwenye mzizi wa maisha ya Ukristo.25 (Mathayo 25:15-30).
3. Kufanyia Kazi Mamlaka ya Kiroho
Kupitia upentekoste, na hasa uamsho wa kiroho kwa madhehebu yasiyo ya Kipentekoste
katika miaka ya hivi karibuni, ufahamu mpya kuhusu mamlaka ya kiroho umekuja ndani ya
Kanisa. Wahudumu wa Injili hata watu wa kawaida wana shauku ya mamlaka hii, kamwe
haijawahi kuwa hivi kabla. Swali ni, yawezekana vipi kupatikana? Pasipo kuzitimiza kanuni
zilizokwisha kuwekwa kwa ajili ya viongozi wa kiroho, na pasipo kuwa na sifa za kiongozi
ambazo zimekwisha tamkwa mbeleni, mamlaka ya kiroho haitadhihirishwa katika huduma ya
27
Kiongozi. Tabia hizi mbili ni za msingi/muhimu sana. Ili kupata mamlaka ya kiroho zaidi ya
hizo zingali zahitajika.
Ufahamu mpya juu nguva za KirohoZaidi zahitajika
(1) Maana ya Mamlaka ya Kiroho
Ralph Mahoney anelezea mamlaka ya kiroho hivi ifuatavyo:
Tunapozungumzia kuhusu mamlaka ya kiroho, hatuzungumzii
kuhusu kuwaendesha watu wala kuwatawala kimabavu. Lakini
tunamaanisha kuweka katika matendo mamlaka katika
mambo/maswala ya rohoni, katika ulimwengu wa maisha ya kiroho
ya watu.27
Tunapozungumzia kuhusu mamlaka ya kiroho hatuzungumzii kuhusu mambo ya walawi, au
mamlaka ya Kanisa. Mafarisayo walikuwa na mamlaka kuu ya ki-ulawi, lakini hawakuwa na
mamlaka ya Kiroho. Mafarisayo hawakuweza kukemea pepo na kumtoa au kuponya
wagonjwa. Hii ndiyo sababu Yesu alijibu wakati fulani walimshutumu kwa kutoa pepo:
"Kama mimi nikitoa kwa Beelzebuli; je wana wenu huwatoa kwa nani?" (Mathayo 12:27).
Hapo aliwaonyesha kwamba wao wenyewe hawakuweza na hata kwa wakati ule
wasingeweza kutoa pepo.28
Hivyo basi Mamlaka ya Kiroho, yaweza kufafanuliwa kama "Nguvu ya kusimama katika jina
na mamlaka ya Yesu Kristo ili kutii mapenzi yake juu ya nguvu za Kiroho na za Kimwili au
mazingira."29
(2) Jinsi ya Kupata Mamlaka ya Kiroho
Baadhi ya mafundisho katika miaka ya karibuni yamewaongoza watu kuamini, kwamba
waweza kuzunguka wakifanya miujiza. Wakati wowote na mahili popote wanapotaka. Lakini
Biblia yatuonyesha sisi waziwazi sivyo mambo yapaswa kuwa. Kwa wakati huo huo Mungu
atutakapo tutendee kazi mamlaka ya Kiroho, kuna kanuni za kutimiza kwanza. Tusipotimiza
kanuni hizi, tutashindwa kama wanafunzi, katika Mathayo sura 17:14-19, ambao hawakuweza
kutoa pepo lililowakabili wao. Au tutakuwa kama wana wakiume wa Skewa katika Matendo
19, ambao waliachwa wakiwa wamepigwa, uchi na walijeruhiwa. Kwa ajili hii swali ni vipi
twapokea mamlaka ya kiroho?
Kuishi Maisha ya Haki
Hatua ya kwanza na muhimu zaidi ni kuishi maisha ya haki. Pasipo haki hatuwezi kuyapata
mamlaka ya Mungu.
Aina mbili za hiki Tunapozungumzia kuhusu haki twazungumzia kuhusu aina mbili za haki.
Ya kwanza ni haki isiyoondosheka. Ya pili ni haki ile tuifanyayo kwa njia ya matendo. Katika
haki isiyoondosheka Mungu atutamka kuwa tu wenye haki kwa sababu tumeikubali na
kuitumia dhabihu ya Yesu kwa ajili ya ondoleo la dhambi, kwa niaba yetu. Aina hii ya haki
hutuhakikishia msamaha wetu. Hatuendelei kuhukumiwa tena ila tumekubaliwa machoni pa
Mungu.
Kwa vyovyote vile, kama tunataka kutendea kazi mamlaka ya kiroho haki yetu yahitajika
kuwa zaidi kupita hatua hiyo. Wokovu huanza kwa kupewa isiyoondoshwa haki au hiki
28
itokanayo na tuyafanyayo. Lakini ndipo matunda ya haki lazima yaanze kukua. Hii ndiyo
tunaita haki ya kimatendo au haki iliyotimizwa (Warumi 8:2-4).
Wakristo wengi sana husisitiza juu ya kuokolewa kwa neema (Waefoso 2:8-9) na hupuuzia
kweli muhimu kwamba tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu tutende matendo mema,
ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo. (Waefeso 2:10). Hatuokolewi
kwa njia ya matendo, bali twaokolewa ili tuzae na kuzalisha kazi njema, kupitia maisha ya
Roho Mtakatifu ndani yetu. Jukumu la Kiongozi Kwa maneno mengine yatupasa kuishi
maisha ya haki. Mahoney amasema baadhi ya watu wamewapatia changamoto waumini wakipentekoste
na wana-uamsho katika makanisa yasiyo ya kipentekoste kwamba wao ni sawa
na kundi la watu ambao waweza kuruka futi 10 juu, lakini ambao wakati waigonapo ardhi tu
hawawezi kutembea wakiwa wina.30 Bahati mbaya kuna kweli fulani ndani yake.
Katika mizungu ko ya uamsho wa kiroho kwa waumini wasio wapentekoste tuna milipuko
mingi ya hisia pasipo kujitoa kwa dhati kwa Bwana. Mahubiri mengi kuhusu nguvu pasipo
mahubiri mengi kuhusu usafi wa moyo. Lakini kama tunataka mamlaka ya kiroho, yatupasa
tuishi kitakatifu.31 Mahoney anaendelea kukazia usemi huu kwamba:
Kulipuka hisia pasipo kujitoa kwa dhati Kama hatuwezi kuyashika na
kuyasimamia maagano, kama watu, hawatutegemei, kama watu
hawatutumainii, kama hatulipi bili tunazodaiwa, kama hatujiingizi
kwenye kadi zetu siku kazini kuna kuwa wakweli kwa ajili ya
mishahara yetu, na kama hatuweki imani yetu katika matendo
hatutapata/kuwa na mamlaka ya Kiroho.32
Kama hatuishi impendezavyo Mungu, Mungu hataachilia mamlaka yake kupitia sisi. Neno la
Mungu lasema: "Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake hukielekea kilio
chao." (Zaburi 34:15) kama twataka tusikilizwe na kutumiwa na Mungu lazima tuishi maisha
ya haki.
Mungu huwasikia wenye haki Kama wahudumu wa Injili yatupasa tutambue kwamba kuishi
maisha ya haki kunahusisha ya jamaa zetu. Endapo ndoa zetu ni viwanja vya mapambano,
hapatakuwa na mamlaka ya Kiroho. Hii imeelezwa vyema katika 1 Petro 3:7, tunaposema
kwamba hata maombi yetu huziiliwa wakati uhusuano wetu na wenzi wetu haupo katika hali
nzuri. Ndoa ya Kiongozi ndipo mahali ambapo shetani hudondoshea baadhi ya mashambulizi
mabaya zaidi kuliko. Yaweza kutikia kwamba muda mfupi tu kabla mkutano kuanza ugomvi
utazuka kati ya kiongozi na mkewe. Twawajibika kuangalia kwa tahadhari eneo hili la
ushambulizi. Endapo itatukia hivyo mara kwa mara, twaweza kuwa na uhakika kuwa shetani
ndiye asababishaye hayo.
ndoa za viongozi ni uwanja wa ma-shambulizi kurejesha haki zetu mbele za Mungu.
a. Tukiri makosa yetu kwa Mungu
b. Tengeneza mambo inapowezekana (Lika 19:5). Hii sikatika
kurudishavitu vilivyoibiwa tu bali inahusisha vitu vilivyoibiwa tu bali
inahusisha ujengaji upya wa uhusiano zilizovunjika. (Mathayo 5:23-
24).
c. Toa msamaha dhidi ya wale ambao wamwkuumiza/jeruhi maandiko
yanasema kushindwa kusamehewa kutamfungia Mungu nje ya maisha
yetu (Mathayo 6:14-15)
d. Jitoe kabisa kwa yaliyo mapenzi bayana ya Mungu, ukimtumainia Roho
wake kufanya kazi muhimu ndani yetu.
29
Neno la Kutahadharisha
Mamlaka pasipo uhusiano sahihi Kitu cha kutisha ni kwamba kuna nyakati ambapo twatumia
mamlaka ya Kiroho pasipo kuwa na uhusiano ulio sahihi na Yesu. Hii imewaongoza walio
wengi kuamini kuwa kwa sababu waliweza kutendea kazi karama fulani za Roho, au kunena
kwa lugha kwamba maisha yao ni sahihi. Lakini hii si lazima iwe hvyo. Maisha ya Samsoni
na Maandiko katika (Mathayo 7:22-23 yanaeleza yakifafanua:
Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina
lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza
mingi? ndipo mitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe, ondokeni
kwangu, ninyi mtendao maovu.
Kiongozi aishiye dhambini akililiana na pepo Hivyo inatubidi tumruhusu Roho Mtakatifu
ayakague maisha yetu mara kwa mara, na kutuonyesha wapi tulipokosea, ili tuweze kufanya
masahihisho muhimu na kuyaleta makosa hayo chini ya damu ya Kristo. Lazima kamwe
tusisahau kuwa mapepo yanajua hali yetu ya kiroho vizuri sana. Endapo tunataka kutoa pepo
wachafu, pasi pokuwa na haki inayotakiwa tuwe nayo, tutakuwa katika matatizo mabaya sana.
ilikuwa na fursa ya kuhuzunisha kushuhudia jinsi mapepo yalivyotaja dhambi za kiongozi wa
Kanisa aliyetaka kuzitoa pepo hizo. Alikabiliana na mamlaka za Kiroho katika ulimwengu wa
giza bila kuvaadirii ya haki kifuani mwake. Katika tukio jingine nimeona jinsi pepo wachafu
walivyomshambulia na kumbwaga chini mtumishi, kwa sababu aliomba pamoja na mtu
aliyepagawa pepo pasipo kuishi maisha ya haki. Hatuwezi kukabiliana na mamlaka za kiroho
na nguvu za giza kwa kuzipuuzia. kwa sababu hii Paulo alitutahadharisha sisi tuvae silaha za
rohoni. Majawapo ya silaha hizo ni dirii ya haki kifuani. Yatupasa kuwa watu watakatifu
kama twataka tuwe na mamlaka juu ya nguvu za mapepo na shetani mwenyewe.
Kuukubali Ubwana wa Yesu Kristo
Hatutaweza kufanya chochote kiroho kwa ufanisi mpaka tuwe tumeyaweka maisha yetu,
malengo na matakwa yetu kwa kiwango cha ujumla chini ya mamlaka ya Neno la Mungu, na
Ubwana wa Yesu Kristo. Kristo aliweza kutenda kazi mamlaka zaidi ya mamlaka ya kawaida
kwa sababu ya alivyokuwa amejitoa kwa ujumla kwa mapenzi ya Babaye. (Mathayo 26:42;
Luka 22:42; Yohana 4:34). Vivyo hivyo twawajibika kufanya hivyo. Pasipo kutii kwa kipimo
cha jumla hapawezi kuwa na mamlaka ya kiroho. Kristo Kielelezo/ mfano wetu Tusitarajie
kutumiwa na Mungu kama mara kwa mara twaenenda tukitafuta njia zetu wenyewe,
twajifanyia maamuzi yetu wenyewe na kamwe hatuulizi yaliyo mapenzi ya Mungu. Ni mpaka
tu tuwe chini ya Ubwana wa Kristo, tukiwa na uhusiano na yeye kama mzabibu na matawi
yake ndipo tutakapoweza kuwa na uwezo dhidi ya magonjwa, mapepo na mazingira. Si
kinginecho chochote kile ila uhusiano huu wa karibu utafungulia mtiririko wa nguvu zake na
mamlaka ndani ya maisha yetu, kutoka pale ambapo utaweza kuwagusa na kuwasaidia
wengine.
Chini ya Ubwana wa Kristo kikamilifu Kiwango cha kujitoa kwetu kwa mapenzi ya Mungu
mara nyingi hujaribiwa/hutihaniwa wakati Mungu anapotutaka tufanye kitu/jambo fulani
ambalo ni kinyume kabisa na mipango yetu na mapenzi yetu. Anaweza hata kutuomba
tumtolee dhabihu, kile ambacho twajua kuwa ni mapenzi yake, sawa na tukio la Abrahamu na
Isaka. Kujaribiwa/kutihaniwa kwa jinsi hiyo itaonyesha ni kwa kiasi gani twakubali
kuyaweka mawazo, maono, mipango, matakwa na mapenzi yote hivi vipate kuwa sawa
na/kuyatii yaliyo mapenzi ya Mungu. Huku kujitiisha chini ya mapenzi ya Mungu mana kwa
30
mara, ndicho kitu kinachohusu uongozi wa kweli na uanafunzi wa kweli kwa ujumla. Kwa
kiwango/kipimo kile kile, tunachojitoa kwa Kristo na kuendelea kutii
Jukumu la Kiongozi kutii/kujitiisha chini ya Neno la Mungu tutakuwa na mamlaka katika
ulimwengu wa Kiroho.
Upako/kutiwa mafuta
Pasipo upako wa Roho wa Mungu huduma iwayo yeyote ile itakuwa kavu na isiyozaa
matunda. Upako ni wa muhimu sana katika kuyatendea kazi mamlaka ya Kiroho.
Utatuwezesha kuangusha chini ngome za Kiroho:
Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata
kuangusha ngome (2 Wakorintho 10:4)
... nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta (Isaya 10:27).
Yesu alitiwa mafuta apeta kuhudumu Yesu mwenyewe alitiwa mfuta ili apate kufanya
huduma, kama tuonavyo katika Luka 4:18-19. Ikiwa ilikuwa ni muhimu kwa Bwana wetu
kutiwa mafuta/kupokea upako, je ni kwa kiasi gani zaidi sisi twahitaji? Hakuna kiongozi
awezaye kutoa changamoto kwa mamlaka za kiroho pasipo kuwa amepokea upako. Wengi
wangali wakifanya hivyo. Hii ndiyo sababu kwanini, sawa sawa na uchunguzi 50% ya
wamishionari wanarudi nyumbani kwao baada ya muhula wao wa kwanza kwisha wakiwa
wamevunjika, wametekewa nguvu na wameshindwa katika huduma yao. Kamwe hawarudi
kwenye uwanja/maeneo yao ya kazi tena.33 Walikabiliana na nguvu za mapepo pasipo kuwa
na upako.
Yesu alikusudia kwamba Injili isitolewe kwa njia ya maneno matupu tu bali katika
udhihirisho wa Roho na nguvu (tazama 1 Wakorintho 2:4-5). Kamwe hakutarajia
ulimwengu uamini Injili isiyo na nguvu. Hii ndiyo sababu aliahidi kwamba ishara
zitaambatana na wale waaminio (Marko 16:15-20). Kwa Wakristo wa kwanza mamlaka ya
kiroho likuwa ukweli uliodhihirika. Katika Warumi 15:19 Paulo aliandika: "Kwa nguvu za
ishara na maajabu, katika nguvu za Roho Mtakatifu" ... Aya hii humaanisha kuwa Injili
haitakuwa mmehubiriwa kikamilifu mpaka tu nguvu yake idhihirishwe kwa ishara na miujiza.
Ishara na miujiza vikia-mbatana Lazima tujichunguze/peleleze wenyewe. Je ishara, maajabu
na miujiza hutendeka katika huduma yetu? Kama hapana, kwanini hapana? Mungu anataka
midhihirisho ya kimiujiza itukie. Hili ndilo kusudi lake. Tungali bado tunatakiwa kulipa
gharama ili iwe hivyo? Yesu aliwaambia wafuasi wake kuendelea kusubiri katika mji wa
Yerusalemu mpaka watakapokwisha pokea nguvu (Luka 24:49). Wengi hushindwa katika
huduma kwa sababu hawana nguvu ileile ambayo Kristo aliiahidi; hii imeongoza waaminio
kwenye mtazamo usio bora: bali waminio ndio wanazifuata ishara na miujiza. Huenda toka
mkutano mmoja mkubwa na kuendea mwingine kwa ajili ya kuona miujiza tu. Hata hivyo
Kristo anataka kumtia mafuta kila kiongozi kwa Roho wake, ili uthibitisho wa nguvu zake
usiendelee kuwa bidhaa adimu miongoni mwa watu wake.
Neno la Tahadhari
Wengi wanapendelea wawena ushindi wa haraka tangia mwanzoni mwa huduma yao. Kabla
ya kufikia kukamilika kwa huduma iliyotolewa, miaka ya maandalizi kwa ujumla hutangulia,
katika muda huo tabia huundwa. Kama tutakimbilia kuingia kwenye huduma pasipo
kumruhusu Bwana kuyaumba maisha yetu na kutuandaa tayari kwa yale ambayo ametutia,
31
tutakuwa tunayaelekea matatizo makubwa. Pasipo tabia imara ya Kiroho upako utakuwa na
nguvu sana, na hatimaye utaharibu maisha yetu! Kuna mifano mingi ya kweli hii
yakusikitisha. Hii ndiyo sababu maandiko yanatushauri katika 1 Timotheo 3:6 Kwamba mtu
aliongoka karibuni asiruhusiwe kushika nafasi ya uongozi katika Kanisa. Mungu aliwandaa
watumwa wake katika Agano la Kale na Agano Jipya, mpaka walipokuwa tayari "kupanda
kwenye kiti cha enzi". Yusufu alisubiri karibuni miaka 14 hivi kabla hajaanza kuona ahidi ya
Mungu ikitimizwa. Kabla Daudi hajavikwa taji kuwa Mufalme juu ya Israeli na Yuda, kwa
ajili yake alitiwa mafuta alipokuwa kijana mdogo, zaidi ya miaka kumi na mitao ilipita. Paulo
kwa njisi hiyo hiyo, alipitia miaka 14 ya kutengenezwa kabla hajaachiliwa kuingia katika
huduma ya utume, Mungu alimwita kuingia katika huduma hii tangia alipobadilishwa/zaliwa
mara ya pili (Matendo 9:13). Viongozi wengi wangelalamika endapo ingewabidi watumie
miaka 30 katika maandalizi kwa ajili ya huduma ya miaka 3 1/2 kama Bwana wetu
alivyofanya. Viongozi wengi wanapendelea zaidi watumie muda wa miaka 3 1/2 katika
maandalizi na miaka 30 katika huduma mafanikio/ushindi katika huduma pasipo kuundwa
tabia
Hatari mbili kuhusu Upako Twatakiwa tuzitambue hatiari mbili zinazosababisha matatizo
makubwa katika Mwili wa Kristo. Kuna wale ambao wametiwa mafuta lakini hawafanyi
chochote katika huduma zao (2 Timotheo 1:6). Wametiwa mafuta kwa ajili ya huduma za
kuinjilisti au huduma nyinginezo, lakini kamwe hawafanyi kazi sawa sawa na wito wao.
Tatizo la pili husababishwa na wale ambaowanajaribu kufanya kazi katika huduma
mbalimbali ambazo hawakuitiwa mafuta kwa ajili ya hizo, pale hupita mpaka wa wito wake.
Matokeo mara nyingi huwa ni vurugu za usimamizi na kifedha, mara nyingine kushindwa
moja kwa moja katika huduma. Natuone jinsi hiyo lazima wajifunze kutokana na kosa la
Sauli. Sauli aliondolewa kutoka kiti cha Enzi cha Israeli kwa sababu alijaribu kufanya kazi
katika ofisi ya mtu mwingine. Lazima tujibane wenyewe na kufanya kazi ndani ya mipaka ya
wito wetu. Damazio anathibitisha kwamba dhiki nyingi, wivu na jeraha vyaweza kuepukwa
kama viongozi wa Mungu hawataona tu bali watakubali huduma zao na kubakia ndani ya
mipaka yao.34
Ili kuwa na mamlaka ya kiroho inatupasa tutiwe mafuta. Kama tulivyoona, Mungu humtia
mafuta kiongozi yule tu aishiye katika haki na akubaliye Ubwana wa Yesu katika maeneo
yote ya maisha.
Kiongozi lazima azamishe ujumbe wake Kuna watu wengi ambao wanaishi kwa ujuzi
waliokwisha upata wakati uliopita na mafundisho pasipo kupokea neno jipya au Mguso toka
kwa Bwana Huduma yao ni kama maji yasiyotembea, yasiyo na ladha na yabebayo
magonjwa. Kwa ajili hiyo kiongozi lazima aendelee daima azamishe kwa kina kirefu jumbe
zake na uhusiano wake na Mungu katika maombi. Kama mchungaji wa kiroho ataendelea
daima kuwalisha kondoo wake masomo yale yale watu huwa wembamba kiroho. Njaa kwa
ajili ya chakula zaidi cha kujenga cha kiroho itawaongoza kwenye malisho ya majani mabichi
yaani huduma ya mchungaji mwingine katika Kanisa tofauti. Kama Kiongozi anataka kundi la
kondoo wake alilishe vizuri, lazima awe amejitoa sana/kufanya/kwa maombi na kulisoma
Neno kwa bidii. Ni rahisi sana. kwa kiongozi kushughulikia mambo mengi, hata yaliyo
matakatifu, huendelea kufanya hivyo hata hupuuzia nidhamu hizi mbili za uongozi wa kiroho.
Lakini mamlaka ya kiroho pamoja na uongozi wa Kiroho huja tu kwa kupitia maombi na
usomaji wa Neno. Imani yetu itaimarishwa na mamlaka itaachiliwa ije kwetu tunapomkaribia
Mungu.
Wakati uchunguzi ulipofanyika miongoni mwa wahudumu, ilifahamika kwamba mhudumu
wa wastani hakuomba zaidi ya dakika tano kwa siku moja. Kabla hatujahukumu; kwa kuwa
32
wakweli lazima tuulize: Ni muda kiasi gani minatumia mbele za Bwana katika maombi ya
kuzama ya kila situ 20. Maombi hufungua mikondo ya mbinguni ya mahitaji yetu. Kama
maisha yetu ya maombi yapo chini kwenye kiwango cha chini kabisa cha utupu, twahitajika
tuongoze muda wetu wa kukaa mbele za Mungu. Wale ambao wamejizoeza kufanya maombi
ya mara kwa mara, maombi ya kuzama/kwenda ndani zaidi yatayaendeleza zaidi, hapa
tukumbuke kwamba ni neema ya Mungu iliyotusaidia sisi kufikia hapa tulipo leo. Mtu wa
asili huyapinga maombi. Hataki atumie muda mwingi akiomba tu. Lakini kama tunataka
mamlaka ya kiroho lazima tujitie nidhamu wenyewe katika kufanya maombimarefu ya mara
kwa mara. Kwa kweli tupu kuwa Kiongozi inabidi aombe mara nyingi kina kile kikubwa cha
shughuli/mambo aliyonayo ya kufanya.
Matokeo ya uchunguzikujia-dibisha katika kuwa mwombaji
Miongozo hii ifuatayo yaweza ikatusaidia kwa muda wetu wa kukaa
mbele za Mungu/Bwana:
Umuulize Bwana akuonyeshe akilini mwako dhambi zozote ambazo
hujaziungama. Mwambie Mungu dhambi hizi naomba pokea msamaha
wake na kusafishwa/utakaso (1 Yohana 1:9,10).
Kisha tumia muda wa kutosha kwa kumshukuru na kumsifu Mungu kwa
vile alivyo na kwa yale amefanya (Zaburi 100).
Ikabidhi siku kwa Mungu. Mwambie Mungu kwa kiwango gani unahitaji
uongozi na ulinzi wake. Omba ulinzi wake na utii maelekezo yote Mungu
akupatiayo uwapo katika dhambi.
Omba kwa ajili ya mwenziwako, watoto na walio wa jamaa yako. Ombea
washarika wako na viongozi. Ombea waumini wa Kristo.
Katika sehemu nyinginezo ulimwenguni. Ombea yatima na wajane.
Ombea viongozi wa taifa lako. Ombea viongozi wako wa kiroho. Ombea
makundi ya watu wa lugha au makabila mbalimbali katika sehemu uishiyo
ambao wangali wanahitaji Injili. Ombea wahudumu wa Injili wenzako na
Wamishionari na kwa ajili ya Uinjilisti wa nchi nyinginezo. Katika
maombi haya yote ruhusu kazi ya Roho Mtakatifu aje juu yako na omba
kwa lugha/nena kwa ndimi. Andika picha unazohisi zimekujia kutoka kwa
Bwana wakati ulipokuwa katika kuomba. Chukua hatua ya utii sawasawa
na chochote Mungu akupatiacho wewe katika maombi.35
Biblia isiwe kitabu tu cha kuandalia ujumbe Maombi lazima yachanganyike na usomaji wa
Neno la Mungu. Mamlaka ya kiroho itaachiliwa kutujia wakati Neno lake lisomwapo,
linapotiiwa na kuwekwa katika tendo. Lazima kamwe tusifikie mahali ambapo twafungua
Biblia ili tutafute sehemu ya kusoma kwa ajili ya ujumbe utakaotoa kipindi kifuatacho. Neno
la Mungu litulishe sisi kwanza kabla ya sisi kulitumia kuwalisha wengine. Wtumishi Wauu
wa Mungu katika historia ya Kanisa kama Wesley, Martin Luther, Finey n.k walikuwa watu
wa kitabu kimoja - Biblia. Kama twataka tuwe viongozi wa kiroho wa kweli wanaoweza
kutendea kazi mamlaka ya kiroho, twahitajika kuwa watu wa KITABU kimoja vivyo hivyo
kiitwacho KITABU! - BIBLIA!
Hamkuweza kukesha saa moja Kuna wale ambao wanahangaika juu ya muda unaohitajika
kutumiwa kwa ajili ya maombi ya kila siku na usomaji wa Neno. Kwa upande wa kimwili
33
twajua vyema wakati gani tumekula chakula cha kutosha. Mambo yote shwari, hakuna wa
kutuambia wakati wa kuacha kuendelea kula. Kwa jinsi hiyo hiyo twaweza kujua hakika
wakati nafsi zetu zimelishwa, na wa wakati gani tumemgusa Mungu. Bahati mbaya wengi
huinuka toka "mezani" pa kiroho kabla hawajatoshelezwa. Wale wapendao waambiwe muda
una unaohitajika lazima wazingatie swali Yesu alilowauliza wanafunzi wake: "Je hamkuweza
kukesha pamoja nami hata saa moja. (Mathayo 24:40). Kwa kuongezea, pamoja na ule muda
maalumu wa saa moja utengwao kila siku, inatubidi kudumu katika kuwasiliana na Bwana
pasipo kukoma. Tunapoendesha gari, tunapo tembea barabarani, au tufanyapo kazi/majukumu
karibu na nyumbani, twaweza kuendelea kuwasiliana na Baba yetu.
Jukumu la Kiongozi
Haijulishi ni muda gani twautumia katika maombi ma Neno daima yawezekana pawepo
ongezeko. Tuwapo na mambo mengi yakufanya ndivyo yatupaswa pia kutumia muda mwingi
katika maombi na Neno. Hii ilikuwa ni tabia ya Martin Luther aliyetumia hadi masaa manne
kuomba kila siku. Ni bahati mbaya sana kwamba mara nyingi kazi inapotuzidia sisi,
twapuuzia kitu kile ambacho ndicho kitakachotuwezesha kutimiza/kufanya kazi yetu kwa
mafaniko. Natumtafute Bwana zaidi kuliko ambavyo tumewahi kumtafuta awali, kwa sababu
mavuno yako tayari na yaweza kuvunwa na watu wenye mamlaka ya kiroho tu Angalia kazi
zisi-kuzidie
4. Namna Sahihi za Uongozi kwa ajili ya kutunza, kufariji na kuadibisha
Kazi hasa ya uongozi lazima ifanyike kwa upendo na huruma. Viongozi lazima wawe tayari
kutoa maisha yao kwa ajili ya kondoo zao (1 Yohana 3:16). Lazima watoe/onyesho mwelekeo
kwa mfano na ushauri, na kutunza kupitia mafundisho. Huku ndiko kuliongoza kundi
kuliongoza kundi. Viongozi wa kiroho lazima wawe na uwezo wa kushughulikia mahitaji ya
watu pamoja na kufariji kila inapohitajika. Wao ni walinzi, walindao, wahifandhio na
kuliadibisha kundi la Mungu katika upendo. Kufanya haya yote kiongozi hana budi kuwa na
maarifa ya kina juu ya Mungu, na pia awe na ufahamu juu ya mahitaji muhimu na tabia halisi
ya binadamu. Baadhi ya mahitaji hayo ni (1) Kutaka kupendwa, (2) Kujisikia kuwa sehemu
ya jumuia aliyopo (3) Kujisikia kukubalika, (4) kutaka kutambuliwa (5) Kujisikia salama na
kuhitajika, (6) Kuwa na fursa ya kujieleza na kushirikishwa.
Kuelekeza kwa mfano ushauri na mafundisho Ili kuongoza kwa ufanisi kiongozi lazima
atumie mbinu za aina mbalimbali za uongozi au mitindo, sawa sawa na hali inavyohitaji.
Lazima akubali kubadilisha mbinu kikamilifu kila inapobidi, pasipo kupoteza mg'ang'anio
wake. Mtindo sahihi wa uongozi hutokana na mazingira yaliyopo. Mathalani, Idara ya
Zimamoto au Jeshi haliwezi kuendesha shughuli zake pasipo kuwaendea wanaoongozwa kwa
jinsi ya kuwatawala au kuwafanya wazitii amri. Hakuna muda kwa ajili ya kukaa chini na
kujadili jinsi ya kupambana na mtoto au jinsi ya kumkataa/rudisha nyuma adui. Katika
matukio kama haya ya hatari/dharura mitindo ya Uongozi sawa sawa na hali halisi kiongozi
anawajibika kutoa amri na miongozo itakayofuatwa. Baadaye wakati tukio la dharura/hatari
linapokoma mambo yaweza kujadiliwa na kupimwa kwa ajili ya tukio jingine wakati
utakaofuata. Hata hivyo kama kiongozi atakuwa mwenye kuwaamuru tu mara kwa mara wale
anaowaongoza, na si katika mazingira ya hatari uongozi wake punde utageuka kuwa utawala
wa mabavu ulio mzigo wa kuwaelemea watu.
Maendeleo ya Kanisa Kila shirika la Kikanisa hupita hatua tofautifofauti. Wakati utendaji
kazi kwa kufuata malengo fulani unapoanzishwa, mwanzilishi mara kwa mara huwa mtu
ambaye hutenda pasipo kujadiliana sana. Sawa sawa na maono yake, anajua nini huhitaji
kufanyika, na vipi lazima kifanyike. Hata hivyo, sawa na kazi inayoendelea na kupanuka
mtindo tofauti wa uongozi huhitajika. Utakaoruhusu wengine kuchangia mawazo yao na
34
kushiriki kwao kimatendo. Hivyo kiongozi mwenye hekima/mwerevu kila mara atazingatia
upi miongoni mwa mitindo ya uongozi wafaa kutumika ilivyotayari.
(1) Kuwaendea –kidemokrasia
Kishiriki kutoa maamuzi Kuwafikia watu ili kuwaongoza kwa mtindo huu huwahamasinsha
wengine kwa kuwaruhusu kushiriki katika hatua mbalimbali za kufanya uamuzi. Kiongozi
atatumia mtindo huu anapohisi kuwa kwa kiwango kikubwa kazi zitafanywa kwa njia ya
kufanya kazi pamoja na wengine na kwa kushirikishana maamuzi. Mfumo huu wa "serikali"
ni kwa ajili ya watu na kutoka watu. Itaruhusu kila mtu kutoa maoni yake na kushiriki pia
kiutekelezaji, ili maamuzi yatakayochukuliwa yawe maamuzi ya kundi la watu. Hata hivyo
kuwaendea - kidemokrasia siyo jibu kwa kila hali ingawaje ni mfumo unaotumika sana, wa
kawaida wa uongozi. Yamkini udhaifu wake mkuu mi kuchelewa katika kutenda/chukua
hatua wakati wa hatari.
(2) Kuwaendea - kwa kuamrisha tu pasipo kujadili amri
Viongozi waongozao kwa kutawala kimabavu na kuamrisha hudhani kana kwamba watu
hawatafanya kitu chochote kile mpaka waambiwe ndipo hufanya. Wautumiao mtindo huu
hujiona wenyewe kama peke yao ndiyo wenyekujua nini huhitajika kufanywa na vipi
kitafanyika. Engstrom anasema kwamba viongozi watawalao kwa mabavu na kuamrisha
pasipo kujadiliana na wengine mara nyingi huendelea mbele pasipo kutegemea hisia za
mwanadamu. Wanatumia watu ili kuongeza mammlaka yao. Kuungwa mkono kwa maamuzi
yao kusimamia katika kuutumikisha na kulazimisha kwa kutishia. Hakuna chombo cha
kukagulia na mizani ya kupimia udhaifu wa kiongozi au awaendeavyo watu.36 Katika kipindi
cha historia ya ueneza ji wa Ukristo mtindo huu mbaya wa unongozi umepata nafasi ndani ya
Kanisa mara kwa mara. Hivi karibuni umeingizwa tena tafsiri zilizopita mpaka za mafundisho
ya "mchungaji" katika mafundisho hayo washirika/wanachama hawaruhusiwi kufanya uamuzi
wowote ule mpaka tu, ukubaliwe na kupitishwa na "uongozi". Fikra kama hiyo hata hivyo ni
kinyume cha mafundisho yatokanayo na maandiko na lazima yapatiwe changamoto.
Mafundisho juu ya uchungaji Viongozi watawalao kwa mabavu na kuamrisha kila jambo
mara kwa mara nidhaifu katika utu wao na hujisikia kuogopeshwa kirahisi na nguvu za
wengine kuongoza wakijitegemea wenyewe. Ili kulipiza sehemu ya udhaifu wake anaamua
kuamrisha badala ya kuongoza. Mara kwa mara huweka mafanikio ya mradi/mpango wake
juu zaidi ya ule wa watu wengine. Kwake yeye kufanikisha malengo yake ni muhimu zaidi
kulikoni uhusiano baina ya mtu na mtu. Tafsiri ya hali ya juu ya mtindo huu ni udikteta.
Pamoja na maana yake nyinginezo mbaya kuwaendea watu kwa mtindo huu kunahitajika
katika matukio ya dharura/hatari au hali mbaya. kuamuru badala ya kuongoza
(3) Kujenga Uhusiano wa Kibaba/Kuwakaribia Watu
Viongozi watumiao mtindo huu hujitambulisha pamoja kundi. Ana shaukuya kuwafanya watu
wake wafurahi na kwa hiyo mara nyingine wataona ni vigumu kudumisha nidhamu.
Kuyaweka mambo katika mpangilio mzuri mara nyingi kunahitaji kuvumilia, kwa sababu
hatua Kali za kukataza na maamuzi dhabiti haikubaliani na mbinu hii ya uongozi. Watu
huanza kumtegemea na kiongozi huyu aondolewapo shirika hufa. Pampja na hayo hakuna
mtindo mwingine utawakaribia watu na mahitaji yao kama huu. tamani kuwafanya watu
wafurahi
35
(4) Kiserikali/Kimamlaka
kufikiri kwa utaratibukupangilia kupita Kiasi Kiongozi huyu, hufurahi. Kutazama
sheria/kanuni, taratibu na katiba ya shirika. Huchukulia kwamba matatizo yote yaweza
kutatuliwa kama kila mtu atafuata/ng'ang'ania. Anapangilia mambo zaidi ya kawaida.
Kutokuzidisha mikutano ya masuala ya biashara ni moja ya mikazo yake ya nguvu.
Huwaendea watu kiakili na kiujuzi naye hufuata njia za kibunge. Udhaifu wa mbinu/ni
upuziaji wa uhusiano baina ya watu, na hali ya kukubaliana na asiyoyakubali ili awapate
walio wengi kwa uamuzi muhimu. Usemi ulio kanuni "toa kidogo chukua kidogo" ni wa
kufuatwa mara kwa mara.
(5) Kwa Muda Usio wa Kudumu/Kujishikiza
Kuwaongoza watu hivi hutumiwa na viongozi ambao wengine wanajua kwamba uongozi wao
ni wa muda mfupi tu. Hutumiwa na wale ambao wamewekwa kusimamia kwa muda fulani tu
wakisubiriwa wastahilio nyadhifa hizo, au wale ambao huwa mbali na mashirika yao mara
kwa mara. Kiongozi wa jinsi hii hufanya kazi ya matengenezo/ukarabiti na kuruhusu kila
kitu/jambo kufuata njia yake iliyoandikiwa awali.
(6) Mtindo wa Yesu wa Uongozi
usipende-lee, uwe mkweli, sukumwa na upendo, pasipo unafiki, ubinafisi
Kamwe hajawahi kuwapo kiongozi mkuu zaidi ya Bwana wetu. Jinsi alivyowaongoza watu
lazima ifuatwe na wote ambao watakao kuwa viongozi wazuri wa Kiroho. Kristo alisukumwa
na upendo.
Katika kutenda kwake hakuwa na unafiki, hakuwa mbinafsi, kujipenda mwenyewe, alikuwa
wazi/mkweli, alitenda haki hakupendelea, alikuwa na huruma, alikuwa mtakatifu na mwenye
haki maisha yake yalikuwa makamilifu. Maneno yake na matendo yake havikupingana
kamwe. Alikuwa karibu na watu, (mtindo wa kuwakaribia watu) lakini aliendelea kudumisha
nidhamu na heshima alikuwa mkali na mwenye kusukumwa moyoni wakati alipolisafisha
hekalu (mtindo wa kuamrisha). Bado alikuwa mpole na mnyenyekevu, alipenda
kuwashirikisha wengine alipo-watuma kwenda kuhubiri, kuponya wagonjwa na kutoa pepo
(mtindo wa kimamlaka). Lakini hakusita
kuwaongoza lilipotokea tatizo/walipokwama. Alifurahia kuishika sheria (mtindo wa
kiserikali/mamlaka/lakini kamwe hakuruhusu sheria za kibinadamu zisizo na msingi katika
Mungu kuendelea kuwepo. Kuwasaidia watu na kuwaingiza katika ufalme wa Mungu ilikuwa
jambo la muhimu zaidi kwake kuliko sheria zilizowafunga watu. Alitambua kuhusu muda wa
uongozi wake uliokuwa ni muda mfupi tu hapa dumiani (mtundo wa kujishikiza). Lakini
hakushindwa kuwaandaa wanafunzi wake kuendeleza kazi yake katika uongozi wake. Yesu
alikuwa kiongozi mkamilifu. Katika uongozi wake alionyesha kimatendo nguvu ya kila
mtindo wa uongozi, lakini kamwe hakukubali/toa nafasi kwa ajili ya madhaifu ya mitindo
hiyo. Roho Mtakatifu yule aliishi ndani ya Bwana wetu, akimsadia yeye kuweka mfano kwa
vizazi vyote anataka kuishi ndani yetu pia. Lililobakia kwetu ni kujitoa kwake kama
twataka/tamani kuongoza kama Yesu alivyoongoza.
Yesu alionyesha nguvu za kila mtindo wa uongozi
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-
36
Kulipa Gharama - Mtihani/Jaribio la Uongozi
Uongozi wa kweli hata unapowekwa katika matendo/fanywa na watu wazima/waliopevuka na
wasio fuata milipuko ya hisia mara zote husababisha makelele juu ya anayeongoza. Kama
mtu fulani alivyosema "jambo/kitu chochote kinachostahili kufanywa kina gharama/bei
iliyoandikwa juu yako". Oswald Sanders anasema kwa jinsi hiyo hiyo "Mtu awaye yote yule
asitamani kukwea kwenye uongozi katika kazi ya Mungu kama mtu huyo hajajiandaa kulipa
gharama zaidi ya wengine wenye madaraka yafananayo na yake kwa wakati huo huo na
watendakazi pamoja naye, walivyotayari kulipa.37 Kukubali/kuwa tayari gharama/bei ni
mtihani/jaribio la uongozi. Hivyo natufikiria baadhi ya gharama. Uongozi mara kwa mara husababisha
makelele
1. Kukubali Malaumu/juu yake kuwepo.
Ni mpja ya jaribio/mtihani mkuu ambao kiongozi hana budi kuuvumilia. Unyenyekevu wake
hauwezi kuonekana sawa sawa mahali penginepo popote kuliko katika jinsi anavyokubali na
kujibu shutuma/maalaumu, Sanders athibitisha kwamba shutuma yaweza kuyafanya
mambo/kazi zote kufikia mwisho mwema, kama kiongozi anaweza kuikubali.38 Hata hivyo
asili ya mwanadamu huwa na hali ya kukataa/tupilia nje sahihisho au shutuma ya maandishi.
Kwa asili watu ni wenye kiburi na hawapendi kukubali makosa waliyoyafanya.
Moja ya Mtihani Mkuu Mahali sahihi ambapo twaweza kujifunza kukubali shutuma ni
nyumbani. Twachukua hatua gani/tunajibu vipi wakati wenzi wetu au wengineo katika jamaa
yetu wanapoonyesha madhaifu yetu. Kama hatuwezi kukubali/kuchuliana na shutuma ya
kimaandishi katika kiwango hicho, kwa kiwango gani pungufu zaidi tutaikubali katika
huduma, hasa wakati inakuja kutoka watu ambao wamekubali tuwaongoze.
Jifunzie Nyumbani Kusikiliza vile watu wengine wanasema kuhusu sisi kutatusaidi
kujitambua/jua wenyewe. Mara nyingi hatujui tunakutana na watu mpaka watuambie.
Mashoga/walagai hutusaidia kujisikia vizuri kuhusu sisi wenyewe, lakini hawajatufaidia kitu.
Inaonekana kwamba kama hatuwezi upokea shutuma toka kwa watu (ambao twawaona),
uwezekano mkubwa upo kwetu kushindwa kupokea sahihisho/rekebisho watetaji pigo
majungu hawasaidii
Neema ya kupokea Shutuma Pima hili ilivyo nyenyekea chini ya makosa kutokakwa Mungu
(ambaye hatumuoni). Badiliko halisi na ukuaji kihisia huja kwa kuukubali udhaifu na kasoro
za kiutu sawa na zinavyoonekana na wengine. Hi ni bei/gharama ya uongozi. Spurgeon
aliyekuwa miongoni mwa wahubiri wakuu/mashuhuri alipokea barua zikimshutumu baada ya
kila ujumbe aliohubiri. Neema ya kupokea shutuma bado alikuwa nayo. Kiongozi aliyepevuka
anaweza kupokea shutuma na kujirekebisha na kujisahihisha. Anaweza kujinyenyekeza
mwenyewe chini ya makosa yake, na kupima matendo yake mbele za Mungu. Katika maombi
ataona kama shutuma ya maandishi ilikuwa ya kweli kisheria. Kama ilikuwa ya kweli,
atajirekebisha, kama haikuwa ya kweli ataiweka kando, pasipo kushika/kuinua magongo, na
ataendelea na kazi yake. Dunia/walimwengu huuona uwezo wa jinsi hiyo ni udhaifu, lakini
machoni pa Mungu ni alama ya ukuu wa kiroho na kupevuka.
Ku-undishika Twatakiwa tujiulize wenyewe, je watu hujisikia huru kuonyesha makosa yetu,
au wanaogopa kutujua sisi? Mungu hivi karibuni alisema: "Mimi mwili wangu
haupatani/unaathiriwa na shutuma". Tabia kama hiyo ni mbaya sana. Moja ya sifa
njema/wema wa kiongozi ni kukubali kwake kufundishika, hii ni sehemu ya unyenyekevu wa
kweli. Daudi angeweza kujinyenyekeza chini ya dhambi zake wakati Jothani alimwambia:
37
"Wewe ndiwe mtu yule". Tungefanya nini katika hali kama hiyo? Kukubali kusahihishwa na
shutuma ni somo la kujifunza. Mpaka tujifunze, vinginevyo kamwe hatutakuwa viongozi
wafanyao kazi ya uongozi vizuri.
2. Kujitoa Kikamilifu Kufanya Kazi
"Dunia inaendeshwa na watu waliochoka". Kwahali hii yaweza kupatiwa changamoto lakini
yawezekana kuna kitu halisi ndani yake. Kuna kutaka kunakoongezeka daima kutoka kwa
kiongozi, kunakochukua nguvu zake za ufahamu/akili na kuweza kumaliza/chakaza nguvu
nyingi. Kiongozi bora hanabudi kukubali kuamka mapema na kusoma kwa muda mrefu,
kusimama baadaye na kufanya kazi kwa bidii kuliko viongozi wenzake wenye shughuli kama
zake kwa wakati huo huo. Kama kiongozi hayuko tayari kulipa gharama ya uchovu/kuchoka
uongozi wake daima utakuwa si mbaya na wala si mzuri.39
Bahati mbaya wengi wamejiunga na vyeo vya viongozi wa Kikristo katika kutafuta mtindo
rahisi wa maisha. Nataka kukwepa kazi halisi, na kufikiri wanaweza kufanya hivyo kwa kuwa
wahudumu wa Injili. Lazima tumtilie wasiwasi mtu awaye yeyote yule
anayeng'ang'ania/anayepigania kuwa kiongozi lakini kamwe hajaweza kufanikiwa katika
wito/kazi ya kawaida. Yatupasa tujue vipi "tufanye kazi kwa mikono yetu", kama twataka
kuona tunda katika huduma. Mara moja nilikutana na kijana aliyeniambia aliitwa awe
Mwinjilisti. Kwa kuwa alikuwa akipita kwenye matatizo makubwa ya kifedha nilimshauri
atafute kazi kidogo ya kufanya mpaka huduma yake itakapoweza kumtegemeza/kumsaidia
kifedha; vile vile kama Paulo alivyofanya. Yule mvulana alinijibu; "Nimeitwa nihubiri na
siyo kufanya kazi". Haihitajiki kusema kwamba ilibidi Jumuiya ya Kikristo iwajibike juu ya
maisha yake. Alichokuwa akikitafuta kilikuwa ni kuishi maisha kirahisi rahisi pasipo kufanya
kazi. Watu wa jinsi hiyo hawafai kwa huduma. "Itwa kuhubiri siyo kufanya kazi"
Wanafunzi wa Yesu walikuwa watu wenye kazi. Petro Yakobo, Yohana na Andrea walikuwa
wavuvi. Mathayo ingawaje kazi yake haikujulikana sana katika siku zake alikuwa mtoza
ushuru. Paulo Mtume mkuu alifanyakazi kama mtengenezaji wa mahema kwa muda fulani ili
apate mahitaji yakera ya wengine. Katika Agano la Kale twaona mtindo huu pia. Mungu
aliwaita watu wakaziacha kazi zao. Amosi alikuwa mchungaji wa kondoo/mifugo, Daudi
vivyo hivyo na Elisha alikuwa mkulima, kwa kutaja tu wachache.
Kutokana na ukosefu wa uongozi wa moja kwa moja, huduma ya Kikristo hutoa jaribu kubwa
la kuwa mvivu/wavivu Katika kazi za kawaida twakumbushwa mara kwa mara juu ya
kuwajibika kwetu kutoa hesabu kwa njia ya wasimamizi waliopo kila siku. Lakini sivyo
ilivyo Kiongozi Mkuu/Mwangalizi/Askofu yuko mbali, kwa ajili hii hakuna mtu aonaye nini
tunachokifanya. Kwa sababu hiyo baadhi hawatilii maanani huduma zao. Huendelea kulala
sana hata kuchelewa kuamka asubuhi na moja kwa moja kuziendea shughuli/kazi zao
mbalimbali. Ili kuwa kiongozi wa Kikristo nidhamu ya kila mtu binafsi yahitajika. Nidhamu
ya binafsi ya jinsi hii huwani ya lazima kwa wote walio katika nafasi za uongozi kujifunza.
Jaribu la kuwa mvivu Kudumisha Kazi ngumu jasho na kupaniakuishi katika nusukustaafupaa
livujalo Ni wale tu wanaodumisha maisha yenye nidhamu wataweza kufanya
jambo/kitu fulani kwa ajili ya Mungu. Inainua maono yanapopokelewa. Ni vyema
inavyosikika na yapendeze sana. Twafikiri juu yake usiku na mchana na twafurahishwa sana
juu ya mambo/vitu vitakavyopatikana. Lakini tunapoaanza "kuzaa" kwa maono hayo, tutaona
kwamba kazi nyingi ngumu, kujitoa, jasho na kudhamiria kwahitajika.
Mahoney, habadili usemi kwamba kuna wachungaji wengi ambao kamwe hawajajifunza
kufanya kazi. Wanaishi katika nusu kustaafu au kusitaafu kamili, ingawaje bado hawajafikia
38
umri wa kufanya hivyo.40 Viongozi kama hao hawajui hata ina maanisha ninikupokea
maono, na kwa upungufu zaidi jinsi ya kuyatekeleza. Bado wangali hatahivyo wanashangaa
kwanini hakuna kinachotukia/tendeka katika huduma yao. Wakati hakuna kuwajibika,
uwezowa kufanya na kukubali/kutaka kufanya kazi ufalme wa Mungu utaathirika. Sawa sawa
na mtu fulani alivyosema, watu kama hao wataitazama paalinalovuja na kusema "Kwa nini
tutengeneze/zibe paa? Jua linawaka, mvua hainyeshi sasa" Ndipo mvua itakaponyesha
watasema, "siwezi kutengeneza/ziba paa ivujayo sasa kwa sababu mvua inanyesha.41
Kufanya kazi zaidiya saa 2-11 kwa siku Maono yanapotakiwa kuwekwa katika matendo, mtu
fulani anapaswa afanye kazi. Kuzungumzia kuhusu maono haitoshi. Wale ambao wamesikia
kutoka kwa Mungu na ambao hufanya mambo/vitu vifanywe si watu ambao hufanya kazi
kuanzia saa mbili hadi kumi na moja (wakiwa na masaa mawili ya mapumnziko kwa ajili ya
chakula) kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, lakini ni wanaume na wanawake watakaotafuta
fursa/wakati kwa ajili ya kumtumikia Bwana wao. Watu wenye maono watamtolea/watampa
Bwana kila walichonacho. Wanapoyatoa maisha, muda na nguvu Mungu atazineemesha
nguvu za ili kwamba wavune mavuno ya kiroho. Masaa hayo ya kazi sitini, sabini, themanini
majuma yatazaa/leta matunda kwa ajili ya ufalme wa Mungu.
kujitoa kwa moyo hutoa wafanyakazi na fedha Wakati kiongozi anapojitoa kwa kazi yake
ataona kwamba wengine watafanyakazi pamoja naye. Watakuwa tayari kutoa dhabihu. Kwa
njia hii ya kumtegemeza/saidia kifedha, muda, na nguvu-ya kibinadamu ili kuwasaidia
viongozi wao kupata kuyafikia malengo waliyopewa na Mungu. Lakini lazima akubali kulipa
gharama/bei, kuongoza njia na kufanya kazi kwa bidii. Mara ajuapo nini Mungu anataka na
kuanza kuyatekeleza maono yake, watu watakaribia kumzunguka na kufanya kazi pamoja
naye. Baada ya maono na kupokelewa na malengo kuelezewa na kupokelewa, waumini
watajiunga katika juhudi za kufanya yatukie kimatendo. Matokeo yatakayofuata yatazidi
matarajio yetu.
Baada ya kusema haya yote lazima tuharakishe kuonyesha kwamba kuna viongozi wengi
ambao ni wenye bidii na wanakaribia kuteseka kutokana na uchovu kuliko uvivu. Viongozi
hawa lazma wakumbuke usemi wa kale: "Kama shetani hawezi kukuzuia wewe, atakushika
mkono na atakimbia nawe". Kwa ajili hii hawanabidi kujifunza mambo matatu.
(1) Kiongozi Bora - Huwashirisha mamlaka wengine
Kwa nini baadhi ya watu mara kwa mara huchoka ni kwa sababu ya kutokutaka/kubali kwao
kushirikisha wengine majukumu yao. Ni watu wasemao, "Ninaifanya mwenyewe". Badala ya
kuwagawia na wengine madaraka yao, wanataka watunze kila kitu wenyewe. Hebu kwa
kifupi tuangalie kwa nini baadhi ya viongozi wameshindwa kushirikisha wengine mzigo wa
kazi zao.
ninafanya mwenyewe
(1) Baadhi hawawagawii wengine kwa sababu wanafikiri kwamba hakuna
mtu awezaye kuifanya vizuri vya kutosha. Ni watu wenye kutaka
kufanya vitu kwa ukamilifu ambao hawaamini/tumaini katika uwezo
wa wengine.
(2) Wengine wameshindwa kushirikisha wengine mzigo wa kazi zao kwa
sababu hawajui vipi wanashirikisha watu.
(3) Kisha wapo wale ambao hawatawagawia wengine sehemu za
mamlaka/kazi yao kwa hofu ya ushindani na kukosa kujulikana. Kama
39
mtu fulani anaweza kufanya vyema zaidi kulikoni wao, huenda
wakaachishwa kazi, hivyo wanafikiri.
(4)Mwishoni kuna wale ambao wanashindwa kupata muda wa kukaa
kufikiria, kuchambua na kuorodhesha kazi zinazoweza kufanywa na
wengine. Wana hisi kwamba mzigo wa kazi walizonazo kwa sasa ni
nzito sana, na hawabakishi muda wa kuwandaa/tayarisha wengine
kushirikiana kazi zao.
kugawia wengine kazi hulinda Kuwa wengine kazi mbalimbali, pamoja na mamlaka na
kuwajibika, itamlinda Kiongozi kutoka uchovu usiona ulazima kuwepo. Makanisa yanayokua
yanaongozwa na viongozi wanaojua jinsi gani ya kuwashirikisha na kuwahusisha wengine.
(2) Jinsi ya Kuwashirikisha/Kuwagawia Wengine kazi.
kugawia wengine kaziPinga kuingilia Kabla hatujawagawia wengine kazi zetu yatupasa tujue
nini lazima kifanyike. Kwa ajili hii Kiongozi ataandaa orodha yenye vitu vyote
vinavyohitajikufanywa. Kisha hukagua kipi/kitu gani yaweza kutekelezwa kwa
kuwashirikisha wengine na kazi gani yahitaji kuhusika kwake binafsi. Kisha ataonyesha jinsi
gani kazi yapasa ifanywe na wakati gani yahitaji kukamilishwa. Baada ya kufanya hivyo
anawahusisha watu sahihi kwa kazi hiyo. Kuwashirikisha wengine kunataka uchaguzi wa
makini wa watu wawezao wenye ujuzi zaidi kulikoni wengine kwa wakati ule ule kazi
iligawiwa wengine ikifanya kiongozi hana budi kupewa taarifa za maendeleo yake. Mara kazi
inapokuwa imegawiwa wengine lazima apinge jaribu la kuingilia maendeleo ya kazi ya
aliyegawiwa. Vinginevyo kwa urahisi maelezo haya yataweza kumfaa:
Jumatatu anamuita aliyechini yake anamwelezea tatizo na kumwambia
kuanza kulishughulikia mara; Jumanne analigawa kwa mwingine;
Jumatano anafanya kazi peke yake na bila kumwambia awaye yeyote yule
kati yao kuwa amefanya.42
Tabia kama hiyo huchanganya akili. Kazi iliyogawiwa mtu lazima amimwe, lakini pasipo
kuingiliwa. Mpaka tu iwe imebaimika kwamba kazi itaharibika.
(3) Kazi gani zaweza kugawiwa wengine wazifanye
Ujuzi wa kugawia wengine kazi/majukumu sio kitu kilichoanza siku hizi. Tayari ujuzi huu
ulikuwa unatumika na kutndewa kazi kwa mafanikio katika Agano la Kale na Agano Jipya
pia. Ushauri wa Jethro kwa mkwewe Musa nn moja ya mifano mizuri ya kugawia wengine
kazi katika Angano la Kale (Kutoka 18:1-27 Baada ya wana wa Israeli kutoka Misri Musa
alikabiliwa na maamuzi mengi.
Utawala wake ulikubaliwa na watu sawa na utawala wa Mungu. Kile mtu katika Israeli
alimwendea kwa ajili ya kupata ushauri na kupatiwa makazi kisheria. Jethro alibaini kuwa
mkwe wake hataweza kusimama iana hii ya kubanwa/kusongwa nakazi nyingi kwa muda
mrefu. Kwa ajili hii alimpatia ushauri wenye hekima ili awageuze wazee walio na ujuzi zaidi
kuliko wengine kazi/shughuli za kisheria, wakati yeye mwenyewe akiendelea
kuyaangalia/shughulikia mambo magumu zaidi. Jethro alitambua kwamba kuna mipaka
katika nguvu za mtu za kimwili, kiakili na kiroho. Sawa na fundisho la Jethro aliweza
kuongeza nguvu katika kufanya/shughulikia maswala muhimu zaidi ya kiroho ya ofisi yake.
Katika matendo sura ya sita twasoma kwamba fundi kulani la wajane walijisikia
wamesahauliwa katika kuhudumiwa. Jambo hili lilipokewa Mitume walishughulikie.
Walielekeze watafutwe watu saba, waliojazwa Roho Mtakatifu na Hekima, ambao watadumu
40
katika kuwahudumia wajane. Badala ya kuhusika wenyewe katika kuwahudumia. Vinginevyo
ungemaanisha waache kuhubiri, kusoma Neno na kujitoa kwa maombi waliamua kuwagawia
kazi na kuwahusisha wengine (Matendo 6:4). Hii haimainishi kwamba Mitume hawakukubali
kushughulishwa na kazi nyonge/ihitajiyo kushuka na kunyenyekea ya kuandaa meza/chakula.
Hii inaonyesha zaidi kwamba walijiweka huru wenyewe kwa ajili ya kazi/shughuli muhimu
zaidi.
Mitume na WajaneKujiweka huru kwa kazi muhimu Kabla kiongozi hajawagawia wengine
kazi, lazima ahakikishe kuwa nia ya moyo wake ni njema/sahihi. Kugawia wengine kazi,
kusiwe ni njia ya kuzikwepa kazi fulani ambazo anahisi ni za chini kulinga na heshima yake
anayostahili. Sawa na Mahoney anavyothibitisha, "Kiongozi Salama haogopeshwi na kazi za
mikono/zitumiazonguvu ya mwanadamu au majukumu manyonge/yanahitaji kujinyenyekesha
na kuvunjika"43 Anoendelea kusema, Siyo kukwepa kazi fulani
Mtu ambaye hajajiandaa kusafisha/deki choo (kama hali yahitaji) bado
hajajiandaa kuchukua uongozi wa kiroho. Kufikiri kwamba kazi
isiyopendwa kama hiyo hailingani/ni pungufu kuliko na heshima yetu
tunayostahili kuikosa maana yote ya uongozi kama haupo usalama wa
kutosha ndani ya Mungu kufikia mahali pa kukubali kusafisha njia/bomba
la maji machafu ya choo lililoziba basi shetani kwa urahisi kabisa
atakutoa/ng'oa kutoka nafasi ya uongozi.44
kutambua mipakaKazi zisizo za kupendeza zisigawiwe wengine
Mara nia ya kiongozi iwapo sahihi anapaswa kugawa kazi za kila siku na vitu ambavyo yeye
mwenyewe hana muda wa kuvifanya. Lazima pia afahamu mipaka yake, hapo akigawia kazi
wengine ambao wana ujuzi zaidi katika maeneo fulani kulikoni yeye alivyo. Kila kiongozi
lazima aweze kufanya hivi pasipo kujisikia kuwa na upungufu. Zaidi kazi zake
zinavyoongezeka, zaidi hana budi kuwagawia wengine. Kwa vyovyote vile maamuzi makuu
lazima yafanywe na kiongozi
kazi zisizopendeza watu/mbaya au ngumu pia zisigawiwe watu wengine, katika hali hiyo
kiongozi lazima apinge jaribu la "mpite paa" yaani kutafuta njia rahisi ya kutokea.
Wakati kazi inapokuwa imekwisha gawiwa wengine lazima tupatiwe taarifa juu ya maendeleo
yake. Engstrom na Dayton walishauri hatua hizi zifutazo katika utoaji wa taarifa.
Ifanye - usitoe taarifa (Mamlaka kamili)
Ifanye - toa taarifa mara ile ile
Ifanye - toa taarifa mara kwa mara
Ifanye - toa taarifa. Uamuzi utafanywa na kiongozi45
(4) Faida na Hatari Zilizojificha za kuwagawia wengine kazi/majuku
Hatari zilizo-jificha za kugawa kazi Mtu anayewagawia wengine kazi lazima atahadhari dhidi
ya hatari zilizojificha zinazoonekana kwa mwanga wa kufifiafifia. Baadhi yake
zimeonyeshwa na Engstrom (1) Watu hujuchukulia madaraka zaidi ya waliyoyapewa. (2)
Watu wanashindwa kutoa taarifa, jambo linalomsababisha kiongozi apoteze/ashindwe
kuongoza kwa usahihi (3) Kazi haitafanyika sawa sawa kabisa na jinsi ingepaswa kufanyika,
jambo ambalo husababisha kutatulia moyoni kwa upande wa Kiongozi.46 Tunapogawia
wengine kazi lazima tuepuke kutumia watu wale wale kila mara, inaeweza ikatuletea matokeo
ya kinyume/mabaya. Kutokuitazama/ kupuuzia mtazamo huu hakutajenga chuki na ugomvi tu
41
bali kutatuoongoza kwenyekuwabebesha mzingo mkubwa zaidiya uwezo wao mfanyakazi
mwenye kutaka kufanya kazi.
Faida za kuwagawia wengine kazi ni nyingi. Mojawapo ni hii inamuweka huru kiongozi kwa
kazi inayostahili kupewa kipaumbele zaidi. Pia inawahusisha wengine katika kazi-iliyotolewa.
Wakati wanapofanya kazi zao ujuzi wao na uwezo wao vyaweza kupimwa. Kwa kuongezea
hayo watajisikia sehemu ya kundi.
(5) Kuepuka kuungua kabisa
Kama viongozi wanaishi wakiwa na misukumo inayoendelea ya kuzingwa na kazi nyingi
pasipo kuwa na muda wa kupumzika/pata burudani, watapoteza baada ya muda mfupi uzuru
wa jinsi wawezavyo kutumiwa na ufanyaji kazi wao. Engstron anasema usemi/maneno haya
mafupi. Ni afadhali niungue kabisa kwa ajili ya Bwana kulikoni nishike kutu kwa ajili ya
shetani, inasikika kama inavutia na kweli ya kidini, na kujitoa kwa kiongozi lazima kukaribie
kauli hii. Lakini kama mtu ataweza kujipumzisha na kuto yitanua sana, ufanyaji wa kazi yake
utaongezeka. Kama mtu ataungua kabisa, mchango wake wa kuhamasisha hufikia
mwisho/hukoma.47 Imesemekana kwamba Mtume Yohana mara moja aliulizwa vipi
angeweza kucheza na mbwa mdogo, jibu lake lilikuwa "stara ya meli ambayo iko katika
nguvu ya mvutano na mkandamizo itavunjika baada ya muda simrefu".
(6) Kiongozi wa Kweli Huhuisha Nguvu Zake
Kiongozi wa Kikristo mara kwa mara hanabudi kuhuisha nguvu zake za ndani. Kazi
aifanyayo haiwezi kufanywa kwa njia nyingineyo yeyote ile Paulo aliifahamu siri hii.
Alisema,
Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, ili neema hiyo iongezwe sana,
kwa hao walio wengi shukrani izidishwe, na Mungu atukuzwe. Kwa hiyo
hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa; lakini utu wetu wa
ndani unafanywa upya siku kwa siku (2 Korintho 4:15-16).
3. Kuchukuliana na Upweke, Kukataliwa na Kukatishwa Tamaa/Vunjwa moyo.
Jaribio/mtihani mwingine wa kiongozi ni jinsi anavyochuliana na kukataliwa au upweke.
(1) Kukataliwa
Yesu aliipitia njia hii ya kukataliwa. Mandiko yanatuambia kwamba,” alikuja kwa walio wake
lakini walio wake hawakumpokea “(Yoh 1:11). Ili kuchukuliana na hali ya mahitaji mtu
mwenye nguvu za ndani na anayejiona mwenyewe kuwa ni wa thamani na mwenye
kuheshimiwa na Mungu. Kila mwanadamu wa kawaida anahitaji kupendwa. Kushinda hali hii
ya kukataliwa, kiongozi lazima ajifunze kujiegemeza kwa Yesu. Ili kushindana au kukabiliana
na hisia hizo/kujisikia huko lazima awe amesukumwa na Upendo wa Mungu kama nguvu ya
kumhamasisha afanye matendo/kazi zake. Kama nia ya ndani ya kiongozi inategemea/msingi
katika kukubalika au kukataliwa na wengine huduma yake itashindwa kuendelea.
Wakati kukataliwa kunapopata/chukua nafasi yatupasa mara zote tujiulize wenyewe kwanini
tunakataliwa. Yawezekana ni kwa sababu kadha wa kadha.
42
(1) Yamkini ni kwa sababu tu Mabwana juu ya kundi, na siyo watumwa
au wachungaji wema.
(2) Yamkini ni kwa sababu tunafanya maamuzi yetu wenyewe pasipo
kwanza kupata ushauri toka kwa Mungu au wengine.
(3) Yamkini ni kwa sababu inatupasa tufanye kazi nyonge/zisizopendeza
ambazo ni za muhimu. Kama vile kuwaandaa wale ambao hawafanyi
vyema kufikia viwango vinavyostahili.
Mpaka tu pale kukataliwa kunakotutesa kumapotokana na sababu ya mwisho iliyotajwa,
hatuna budi kubadilisha mtindo wa maisha yetu. Lakini kama twakataliwa kwa sababu
twafanya vile tunavyofahamu kuwa ni sahihi, na kwa sababu Mungu anatutaka tufanye hivyo,
yatupasa tuchukulie hiyo kama gharama ya uongozi. Kiongozi lazima akubali/atake kulipa
gharama hii kwa ajili ya kazi na ufalme. Hii haitakuwa rahisi hasa tukijua kuwa ntu wetu wa
asili hutamani sifa kutoka kwa wengine.
(2) Upweke/Kuwa peke yako
Kwa kawaida, mara nyingi kiongozi lazima awe mpweke. Daima lazima awe mbele ya
wafuasi wake. Sander anathibitisha kwamba kwa kawaida mwanandamu hutamani ushirika,
na ni jambo la kawaida kutaka kushirikisha wengine mizigo ya majukumu/kazi na utunzaji
bora. Mara nyingi ni vigumu kufanya maamuzi yafikiayo umuhimu wa mbali utakaogusa
maisha ya wafanyakazi uwapendao-Hii ni moja ya gharama nzito ya kulipwa.48 Kwa
upande/mwingine lazima kiongozi aweze kukaribisha urafiki. Lazima awe kaka/ndugu
miongoni mwa wandugu. Lakini kwa upande/mkono mwingine anapaswa awe amepevuka/
kwa kiwango cha kutosha na awe na nguvu za kumtosha kusimama - peke yake, hasa wakati
panapokuwepo na upiinzani mwingi afanyapo kazi/shughuli/majukumu yake.
Mtazamo mwingine wa upweke unataka utayari wa kiongozi kwenda mbali kutoka
makutano/kundi na kuwa faraghani/peke na Baba. Yesu alifanya hivi katika huduma yake.
Katika kujifisha/kujitenga kwa jinsi hiyo tutapokea nguvu mpya ma amri mpya, pia na
ujumbe kutoka kwa Bwana! Bado kiongozi hapaswi kamwe kuwa "Mpweke". Anatakiwa awe
na faragha/peke wakati mwingine, lakini kwa wakati huo huo hanabudi kuwa mtu wa
watu/mwenye kuwaendea watu, kwa sababu kiroho chaweza kufikiwa. Peke yako na
MunguNguvu mpya, taratibu na jumbe
(3) Kukatishwa Tamaa/Kuvunjwa Moyo
Hali halisi na mazingira vitainuka katika huduma na maisha ya kiongozi vitajaribu kumvunja
moyo na kumkatisha tamaa. Mara nyingi kuvunjika moyo huja wkati hakuna kidhibiti
kionekanacho na kushikika cha tunda katika huduma yake. Katika nyakati kama hizo
nguvu/juhudi zote, muda wote, kazi ngumu na dhabihu huonekana kuwa ni bure. Anaweza
pengine kujisikia kama Elia, kwamba ni yeye tu peke yake aliyejitoa kwa Mungu
kikamilifu/kabisa. Hali zenye kuvunja moyo Tofuta kutiwa moyo kutoka Mungu
Katika nyakati kama hizo lazima ajifunze kutafuta kutiwa moyo kutoka kwa Bwana, na si
kwa jinsi watu wanavyokubaliana naye. Lazima afuate mfano wa Elia (1) chukua muda
kuhuisha nguvu za kimwili. Katika nyakati za kuchoka/kutekewa nguvu - kimwili watu huwa
chombo/wazi kwa kukatishwa tamaa/kuvunjwa moyo. Kwa ajili hiyo, Mungu alimwambia
Elia "Inuka, ule na unywe" (1 Wafalme 19:5,6). (2) Chukua muda kumtafuta Mungu.
Hakuna mtu mwenye ujuzi bora zaidi katika kujitia moyo zaidi ya Bwana wetu. Mwaliko
wake kwa wote wenye kulemewa na mizigo mizito na nira nzito hasa unawafaa/ni kwa ajili ya
43
viongozi wake. Kama Elia alivyokaa mbele za Mungu siyo maisha yake ya kiroho
yaliyoamshwa tu, bali alipokea ujumbe mpya kutoka kwa Mungu pia.
4. Kuwa Tayari/Kujiandaa kwa ajili ya Vita vya Kiroho
Tayari kwa pambano la upinzani wa kiroho. Kiongozi ambaye hajajiandaa/hajajiweka tayari
kupambana vita vya kiroho atashindwa/hatafanikiwa katika huduma. Kila mtu anayehusika
katika kuupanua. Ufalme wa Mungu lazima awe tayari kwa mapambano ya upinzani wa
kiroho. Hata kama vita vitafanyika katika ulimwengu wa kiroho, mara kwa mara hujionyesha
vyenyewe katika ulimwenguni wa asili, kwa njia ya ugomvi na upinzami kutoka kwa watu.
Kutimia kikamilifu silaha za Kiroho. Shetani anajaribu kila anachoweza kuzuia kuhubiriwa
kwa Injili, kukua kwa muumini binafsi na kukua kwa Kanisa kwa ujumla. Hivyo lazima
kiongozi atumie kikamilifu/kabisa silaha zake zote za rohoni sawa na ilivyotamkwa katika
Waefeso 6:8-10. Kamwe, silaha za asili na za kimwili havitashinda vita. Wale tu
wanaojifunza kutumia silaha za kiroho inavyostahili wataweza kuongoza vyema katika
uongozi wao.
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-
44
Hatari katika uongozi wa Kikristo
Kama viongozi wa kiroho tunisahau ya kwamba tuko katika vita vya kiroho. Na katika
mapambano yetu dhidi ya shetani, tunasababisha hasara kubwa sana kutika ufalme wote. Kwa
upande wake, hutushambulia katika maeneo muhimu matatu yajulikanayo:
Ma-shambulizi ya shetani
1. Kupenda pesa/ fedha
2. Wanawake
3. Kujulikana/ umaarufu
Yapo matatizo katika sehemu zote hizi, lakini hatari inayomkabili kiongozi wa kiroho ni
mbaya zaidi. Huwa anatembea "juu ya kamba" hii, na kwa vile ameyaweka macho yake
kumtazama Yesu na Neema yake, ndipo tu ataweza kukwepa hatari hizi zote zinazomkabili.
Hatari mbaya zaidi
Watumishi wema wa Mungu, wakubwa kwa wadogo, waliosimama katika mstari wa mbeli
katika vita vya kiroho wameanguka katika mtego wa shetani kwa jinsi moja au zote katika
majaribu haya matatu. Madhara na kuchanganyikiwa kwa waamini na wasioamini kufuatia
maanguko kama haya ni makubwa. Hivyo ni vyema kabisa kwamba Kiongozi wa kikristo
anapaswa kujiangalia akijilinda asianguke kwenye mtego wa mdanganyaji, ili kuzuia
kuchanganyikuwa, kuumizwa na hata kuangamizwa kabisa dunia ya Wakristo.
Jilinde na mdanga-nyaji
Wengine wetu wanaweza wawe wamewahi kumsikiliza A.A. Allen, (Mtumishi wa Mungu)
alipoanza uponyaji wao kwenye mikutano yake, kwa bahati mbaya sana kufikia mwisho wa
huduma yake alikuwa anaishi dhambini. Alipokuja, alikutwa kwenye nyumba isiyoeleweka
vizuri akiwa amezungukwa na chupa tupu za pombe. Habari hizi zilipoenea, wengi
waliokuwa wamempokea Yesu katika mikutano yake waliposikia waliaacha imani.
Mandiko pia yanatoa ushuhuda kama huo juu ya watumishi wa Mungu walioanza huduma
zao vizuri kabisa lakini wakamalizia huduma na maisha yao katika matatizo ya kutisha. Kwa
mfano Samsoni aliyebeba lango la mji wa Gaza kwa nguvu za Mungu wakati alipokuwa
tayari anaishi dhambini. (Waamu zi 16:1-3). Miujiza na mafanikio katika huduma A.A. Allen
visitumike kamwe kupima maisha ya mtu, bali Utakatifu. Hivyo tunahitaji kuwa macho na
yale maaeneo/majaribu matatu yaliyotajwa.
1. Kupenda Pesa
Nia njema Kiongozi wa kweli wa Kikristo asihubiri kamwe kwa ajili ya kupata fedha. Kama
hili litakuwa ndio lengo lake huduma yake basi anatanguliwa na maanguko. Hata hivyo hii
haina maana kwamba mhudumu wa Injili asiishi kama watu wengine na kuwa na hakika ya
pato. Lakini tu pesa zisiwe ndiyo nia ya kuhudumu kwake.
(i) Kutumikishwa na mia mbaya
Mtumishi wa Mungu au mtumwa wa watu Kama kiongozi yuko kwenye huduma kwa ajili ya
pesa, ni wazi kuwa anawajibika kwa wale wanaomlipa. Kuwajibika kwa namna hiyo,
kwaweza kumzuiya kutangaza neno kamili la Mungu kwani ataogopa kuwaudhi wahisani
wake wanaomsaidia. Hivyo, hatakuwa tena mtumishi wa Mungu bali amekuwa mtumwa wa
watu.
45
Jaribu la Kifedha huo huo Matumaini ya kipesa hayana budi kuwa ya umuhimu wa chini kwa
mtumishi wa Kiroho. Damazio anathibitisha haya kwa kusema wazi kwamba, moja ya
majarubio ya kweli aliyowekewa mtu aliyetawadhwa na Mungu ni kule kuwa kwa hali ya
kawaida, atapendelea na wakati wane akitumika katika wito wake kwa muda wake
mwenyewe bila kuangalia kuhusu msaada wa kifedha.49 Hivyo wale wanaotegemea
kujifunza huduma wakubaliwe tu ikisha hakikishwa kuwa wako tayari kuhudumu pasipo
namategemeo ya pesa au cheo.
(2) Matumizi ya Pesa Zilizopangwa
Siyo tu kwamba kiongozi mkristo awe nania njema kuhusu huduma, ila pia awe mwaminifu
katika kutunza fedha zinazopitia au kutunzwa naye. Niaamini kuwa, Mungu anataka
tuwafundishe wahudumu wanayoechipukia juu ya uaminifu katika sehemu ihusuyo fedha.
Anayojifunza somo hili toka hatua ya mwanzo, Mungu anaweza kumwamini kwa makubwa
zaidi baadaye. Bahati mbaya wengine hawajifunzi somo hili na hivyo wamekumbana na
mikasa, na hata
kuanguka kwenye huduma zao. Jaribu kubwa ni kushindwa kutunza pesa zilizopangwa kwa
kazi maalumu na kufanyia kazi zake mwenyewe kinyume na mpango uliokuwepo.
Ninamjua mwinjilisti ambaye alipokuwa nchi za ng'ambo aliwashirikisha watu ufunuo wake
juu ya kujenga shule Biblia nchini kwake. Dada mmoja Mkristo aliguswa sana na hitaji hili
akauza nyumba yake na kutoa pesa nyingi sana kwa Mwinjilisti huyu pamoja na gari mbili ili
huyu mwinjilisti aweze kuifanya kazi ya Bwana kwa kujenga shule ya Biblia atakaporudi
nyumbani kwao. Dada yule aliposhindwa kupata habari na barua toka kwa yule mwinjilisti
baada ya kurudi nyumbani, dadaaliamua kununua tiketi ya ndege ili aje kuona mradi ule
unaendeleaje. Jambo la kukatikasha tamaa kabisa, yule dada alikuta kwamba hapakuwepo na
shule ya Biblia. Hata hakikuwepo kiwanja/eneo la kujengea. Alikaa sebuleni petu karibu kulia
na bila tumaini. Alikaribia hata kuacha imani. "shule ya biblia"
(3) Jinsi ya Kutunza Pesa za Binafsi
Tunahitaji pia kuwa waangalifu jinsi ya kutunza fedha zetu wenyewe. Baadhi ya viongozi
huandika hundi wakati akaunti zao benki hazina pesa za kutosha. Siyo kwamba hufaya hivi
makusudi bali wameshindwa kuweka kumbukumbu halisi za matumaizi Kama hundi
zitakuwa zinarudishwa rudishwa, basi wahudumu (minister) watapoteza heshima zao na hata
baadaye kupoteza huduma yake kabisa. Hii inafanana pia na ile tabia ya wanaokopa pesa na
kushindwa kurejesha kama ilivyokubaliwa. Ikiwa sisi viongozi wa kiroho, tunakuwa ma
madeni ambayo tunashindwa kuyarudisha, hundi zenye kurudishwa mara kwa mara, au
kushindwa kutunza fedha au kudanganya watu kuhusu pesa zao, tutaipoteza huduma yetu.
Tazama salio la akiba yako Benki
(4) Usijiuze
Moja ya vitu vibaya kuliko vyote kinachoweza kumtokea mhudumu/mtumishi wa Mungu ni
kujiuza mwenyewe kwa mnunuzi mkuu kuliko wote. Tunapaswa kumtumikia Mungu katika
Kanisa alimotuweka, na sio dhehebu ambalo `litatulipa' vizuri zaidi. Vinginevyo tukakuwa
"makahaba wa kiroho", tukijiuza wenyewe pale tutakapopata malipo zaidi. Kujiuza kwa
Mnunuzi Mkuu
46
(5) Mfano wa Kupenda Pesa
Demos Shakarian Moja ya mifano mizuri juu yayale yanayaweza kumpata mtumishi
anayependa pesa, ni ule unaosimuliwa na Demos Shakaria, mwanzilishi wa Full Gospel
Business Men International. Anaeleza kuhusu mwinjilisti waliyemwalika kwenda kuhubiri
kwenye mkutano wao mmoja wa hadhara. Kila jioni baada ya huduma huja kuuliza juu ya
sadaka iliyokusanywa. Hakuna hata siku moja aliyoridhika na kiasi kilichokusanywa. Kila
mara alikuwa akimwaambia wahudumu, "Mngeweza kupata zaidi. Hamuifanyi kazi vizuri.
Lazima uguse mioyo ya watu ili watoe zaidi". Mwinjilisti anayesafiri Pamoja na udhaifu huu
katika tabia zake, hawakuwahi kupata msemaji mwingine aliyekuwa na upako zaidi katika
kuhubiri. Na hawakuwahi kuona miujiza zaidi, watu wakisogea mbele kumpokea Yesu kama
walivyoona katika mikutano yake. Mkutano wa mwisho ulikuwa siku ya Jumapili alasiri.
zaidi ya watu elfu kumi walihudumia mkutano. Mwinjilisti akahubiri maneno mazito
yaliyogusa na kuchochea mioyo ya watu, Lakini kabla hajaamalizia ujumbe wake alisema:
"Baraka kuu kuliko zote toka kwa Mungu hazitakushukia rafiki mpaka utakapompa vyote.
Toa kila kitu kwenye mifuko yenu ili aweze kuwajazeni na baraka zote za mbinguni." Hata
kama kusingekuweko kukusanya sadaka siku ya mwisho, aliendelea kusema, "Ni nani atakaye
kutoa? Toa mpaka Mungu afunue mikono yake kukupa wewe". Dada mmoja alianza kwa
kusimama akaenda madhabahuni na kumpa kitu fulani, "Mungu akubariki dada", alisema.
"Mungu atakubariki sana kwa zawadi hii". Wengine wakafuatia. Ikaendelea hivi kwa muda
wa saa moja au zaidi. Kuja mbele na kutoa pesa ilikuwa ndio ushuhuda wa kujitoa kikamilifu.
Kuja mara ya pili au ya tatu ndiko kujiweka wakfu kusikoonekana kwa kawaida. Baada ya
kama masaa mawili na nusu, aliacha kuomba pesa. Mara alipomaliza tu sala ya mwisho,
wahudumu waliharakisha kuchukua zile sadaka kwenda kwenye chumba cha kuhesabia
matolea. Walipoanza tu kuhesabu, yule Mwinjilisti alivamia chumba ghafla, huku
anatetemeka mwili nzima. "Hizi ni zangu" alisema akijawa na hasira. "Kila kitu ni changu",
na kwa kusema hivyo alizichota pesa zote kwenye mfuko mkubwa ambao alikuwa amekuja
nao. Pamoja na upinzani kwa wahudumu/wasaidizi Shakarian alimruhusu mtu huyo
kuendelea, huku akilisema "pesa hizi zako", kwa sababu Mungu hataki njia zile ziletazo
maswali mengi za jinsi hii kutunisha mfuko wa fedha", Mwinjilisti alimwita mpumbavu na
akaondoka pale chumbani akiwa na fedha zote. Kwa majuma sita aliishi pamoja familia ya
shakanani na kusema alipokuwa akiondoka. Hakuweza hata kusema ahsante baada ya miaka
sita kupita, asubuhi moja mtu mbayambaya alifika ndani ya ofisi ya Shakarian. Alikuwa ni
mwinjilisti yule yule, ameishiwa kabisa, alielezea habari za kuhuzunisha juu yake mwenyewe,
aliomba apewe fedha ili aende Detroit, Shakarian alimpatia fedha hizo. Mwishowe miaka
mitatu baadaye alikufa.50 Kupenda fedha hakukumharibia huduma yake na jamai tu, bali
kulimharibia hata maisha yake.
6) Udanganyifu Katika Kuchangisha/Kutunisha Mfuko wa Fedha
Pasipo viungo vya mwili wa Kristo kuutegemeza ufalme wa Mungu kifedha kazi ya Mungu
haiwezi ikofanyika. Biblia yatupatia mafundisho wazi kuhusu njia iliyo sahihi ya utoaji.
Katika Mathayo 6:2-4 tunasoma:
Fuata Fundisho la Biblia
"Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki
wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. Amin
nakuambieni, wamekwisha kupata thawabu yao.
Bali wewe utoapo sadaka, hata mkomo wako wa kushoto usijue ufanyalo
mkono wako wa kukuume; sadaka yako iwe kwa siri na Baba yako aonaye
sirini atakujazia.
47
ma pia twasoma katika 2 Wakorintho 9:7.
“Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake si kwa huzuni,
wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa
ukunjufu.”
Mbali na maandiko haya baadhi ya wahubiri wa Injili hutumia njia/maneno ya udanganyifu
katika kuchangisha matoleo. Rafiki yangu mwema aliniambia kwamba alihudhuria mkutano
mahali ambapo mhudumu aliliambia kusanyiko kwamba sasa watakwenda kumtolea Mungu
zawadi. Hakuna udanganyifu wa maneno ya kushawishi Hivyo akawaelekeza watoe sarafu ya
fedha toka mifukoni mwao. Na kuitiksa mbele za Bwana kama sadaka/toleo lao. Kisha
akaendelea kwa kuuliza: "Kwa vipi wampatia zawadi mtu mwingine? Unaifunga! Unaifunga
kwa kutumia nini! Kwa kipande cha karatasi zuri! Kwa jinsi hiyo hiyo chukueni vijikaratasi
vizuri vya noti za fedha mfungie sarafu kwa ajili ya Bwana".
Kiongozi wa kweli wa kiroho kamwe hatatumia njia hizo katika kuchangisha/kutunisha fedha
kwa ajili ya ufalme wa Mungu.
2. Wanawake
Karibu na walio kinyume cha maumbile yetu Yamkini wahudumu wengi wa Injili
wameanguka katika eneo hili kulikoni katika lingine miongoni mwa mengineyo. Kupitia
huduma mara nyingine tunakuwa karibu na wanawake/wanaume wenye kuumbwa tofauti na
sisi tulivyoumbwa zaidi ya kazi nyinginezo zote za ujuzi isipokuwa madakatari wa tiba.
(1) Hatari Katika Kutoa Ushauri
Wanawake watakujia katika ushauri wa kiroho. Baadhi yao kwa sababu ya matatizo katika
ndoa zao. Nyumbani mwao wanawaona waume zao wabaya wanaowatendea
kiunyama/kikatili. Kwa wakati huo huo wanamjua Mhudumu yule mtanashati ambaye
wanamuona mara moja au mara mbili kwa wiki na anayeonekana kuwa mwenye tabia nzuri
na rafiki kwa kila mtu.
Mchungaji tazama ndoa yako
Kama dada wale wangeweza tu kumwona mchungaji yule nyumbani mwake, ingali wasaidia
kufahamu kwamba ni kama mtu mwingine tu, mwenye makosa vilevile, mtu na siyo malaika
wanayedhania kuwa: Kwasababu ya matatizo yao wanakuja kwa ajili ya kupata ushauri.
Mchungaji mwenyewe aweza kupitia kipindi kigumu/kibaya cha mikwaruzo katika ndoa yake
mwenyewe. Kwa hali hiyo hiyo jukwaa linaandaliwa kwa ajili ya uhusiano baina ya mshauri
na mshauriwa. Ambalo baada ya muda mrefu utawaongoza kwenye uzinzi na kuvunjika kwa
ndoa, hapondipo huwa mwisho wa huduma na ndoa ya mchungaji.
(2) Hatari Kupitia Kukutana Waziwazi/Ana kwa Ana
Mara nyingi kiongozi anajihusisha katika dhambi ya aina hii pole pole, na mara kwa mara
hajijui. Lakini anaweza pia kukabiliwa na jaribu sawa na ilivyotokea kwa rafiki yangu.
Aliporudi nyumbani baada ya Ibada ya jioni na kuufungua mlango wa chumbani chake, pale
alilala kitandani mwake msichana kijana aliyefunikwa na blanketi. Kwa haraka kabisa alitoka
nje ya chumba akafunga mlango na akamwomba Mungu ampe hekima. Mara ile ile wazo
likamjia akaenda akachukua gongo, akafungua mlango tena na kumwambia binti:
"Nitahesabu hadi tatu na kama utakuwa hujatoka hapa chumbani kufikia hapa, ndipo
nitakusaidia kukutoa nje mwenyewe kwa fimbo hii". Kabla hajafikia kusema mbili, binti
tayari alikuwa amekwisha chopoka kitandani na kutoka nje: Alifanya kitu sahihi katika hila
48
hiyo. Ingaliweza kumharibia huduma yake kama Mungu asingelimpatia yeye maelezo kuhusu
nini afanye.
Kukutana ana kwa ana
(3) Hatari Katika Kutembea Majumbani
Tunaweza kuingia kwenye hatari sana kama hatukuwa waangalifu wakati wa kutembelea
majumbani. Kuitwa na watu wenye matatizo ni jambo la kawaida katika uwajibikaji
kihuduma. Lakini bado, jambo la kufanana na lililompata Mhudumu mwingine, alipokuwa
akitembelea Mkristo mchanga laweza kutokea. Mara alipoweka gari yake nje ya nyumba
akawa anaomba kwa ajili ya uelekezo wa Mungu, alijisikia hali isiyokuwa ya kawaida. Amani
ambayo hujisikia siku zote haikuwepo. Hata hivyo alishuka kwenye gari na kugonga kengele
mlangoni pale. Yule msichana alifungua, akionekana mrembo zaidi ya siku zilizopita, akiwa
amevalia vazi linaloonyesha ndani kuliko nguo za kawaida alizokuwa akivaa aendapo
Kanisani. Alipokaa penye kochi msichana yule alisogea na kukaa karibu sana naye.
Alipomuuliza juu ya matatizo yake, yule msichana alimwambia kuwa toka ameokoka mume
wake hana tena hamu ya maisha ya mapenzi kama walivyokuwa nayo. Akaendelea
kumwambia yule mchungaji kuwa anafikiri huenda hamvutii tena mume wake. Alijisogeza
karibu zaidi na yule mchungaji na kuulizauliza: "Je vipi wewe? Je unafikiri mimi navutia?
Kushindwa kujizuia Mchungaji alimwona anavutia sana na hivyo akaanza kushindwa kujizuia
mwenyewe. Ndipo hapo aliposikia sauti ikimwambia atoke nje ya nyumba hii wakati bado
anaweza. "Ninaondoka sasa" alisema huku akisimama na kuelekea mlangoni. "Kwani haraka
hivyo" yule msichana aliuliza; "mume wangu hatarudi mapema, bado saa moja nzima hivi".
Yule mchungaji alipojisikia mkono wa msichana juu ya bega lake alisisitiza "Nakwenda"!!
Yule msichana akasema "Kama unakwenda, afadhali uondoke sasa hivi", mara ghafla akawa
amegeuka kuwa adui. "Mara ya kwanza nilipokusikia ukihubiri", akaendelea; "niliamua
kuiharibu huduma yako! Unadhani kwamba nilimpokea Kristo kama Bwana na Mwokozi
kweli? Yule mchungaji alikimbilia mlangoni kwa haraka alivyoweza na kuondoka. Mara
alipolifikia tu gari lake, alipeleka maombi kwa Mungu kumshukuru kwa sauti YAKE
iliyomwonya.51
ushauri wa jinsi ya kutenda
(4) Jinsi ya Kujilinda Wenyewe
Wakati tukiiendea miito itokayo majumbani lazima tuangalie yafuatayo: usikae kwenye
kitanda cha mgonjwa, hasa mgonjwa awapo wa maumbile (mume au mke) tofauti na wewe.
Wekea mikono penye paji lake la uso wakati wa kumwombea. Hapana haja ya kuweka
mikono mahali popote pengine katika mwili wake hata kama mahali hapo pawe panauma
kiasi gani.
Njia nzuri kuliko zote kujilinda dhidi ya hatari za wanawake zinazoweza kuathiri huduma
zetu ni pamoja na:
(1) Kuyathibiti na kuyaweka maumbile yetu chini ya msalaba. Kama
hatuwezi kuyathibiti, basi tunahitaji kumwona ndugu yeyote mwenye
mamlaka ya kiroho ili atuombee na kufunga nguvu hizi zinazojaribu
kuharibu maisha na huduma zetu.
(2) Tunatakiwa kuwa na wake/waume zetu katika kutembelea watu. Kama
dadahatakubaliana na hali hii, acha kwenda kumshauri, kwa sababu
kutakuwepo hatari. Kama mhudumu (minister) hajaoa zipo njia tatu
49
anazoweza kufuata: Kwanza anaweza kulipeleka au kumwachia
mchungaji aliyeoa tatizo (wito) huo (lakini ni baada ya mwenye tatizo
kukubali); au kuwachukua mhudumu mwingine aandamane naye, au
mwisho anaweza akafanya ushauri mahali pa wazi ambapo kila mtu
anaweza kuona kinachoendelea pale. Kama mtu anayehitaji ushauri
akikataa njia hizi zote - Jihadhari sana!
(5) Ushauri wa McBurney juu ya Ishara za Hatari za nje.
Mashauri ya Kimaisha ya Louis McBurney's katika kutoa ushauri yafaa kutiliwa maanani na
kila kiongozi. Ameorodhesha dalili za hatari, wakati wanawake wahitajipo ushauri.
Kuongezeka Kutegemewa
Dalili ambayo ni ya kawaida sana ni kule kuomba kwao ili uongeze muda wa vipindi vya
kufanya ushauri.
Malalamiko Kuhusu Upweke
Anayeshauriwa anapoanza kukiri kwamba upweke wake ni mbaya sana kwani sasa
amefahamu jinsi ushirika wa ndoa unavyofananana. Mushauri ndiye nayekuwa pekee ambaye
ameweza kupata kumsaidia.
Mgusano wa Kimwili
"Hii huanza polepole kwa migongano kidogo kidogo ya miili katika kumbi zenye
msongamano wa watu au kwa miguso ya kupapasa mikono yake, lakini huweza kuzidi hata
kufikia kumkumbatia kwa shukrani au `busu takatifu' ambalo huzidisha mawasiliano zaidi ya
yale ya dada katika Bwana. Tukio linalotokea kawaida ni mwanamke kusema, "Umenisaidia
sana, Mchungaji. Je naweza kukumbatia kwashukrani?" busu takatifukukumbatiana kiudada
Tabia Zingine za Kushawishi
Jinsi mwanamke anavyovaa, labda marashi, au ushauri hatari wa kumtembelea wakati mume
wake hayupo, au kuhusu kupeleka ujumbe utakaojulikana kama `bendera Nyekundu' kwa ajili
ya usalama wetu.52 mavazi na manukato
(6) Dalili za Hatari za Ndani Asemavyo McBurney
Kwa nyongeza, baada ya dalili za nje zinavyoonekana, McBurney anataja pia dalili za hatari
toka ndani ya mtu.
Kumfikiria Mwanamke
kutoka tatizo kwenda kwa mtu
Awali hili linaweza kuchukuliwa tu kama kuhusudu sana kujishughulisha namatatizo ya mtu.
Lakini mwelekeo utaanza kubadilika pole pole na kuanza kumfikiria mtu mwenyewe. Hisia
zenye kukupendeza zitaanza kujijenga juu ya uhusiano huu mpya.
Kumlinganisha na Mke Wako/Wake zetu
mzuri kuliko mke
Huyo mwanamke mwingine ataonekana mzuri kuliko mke wako: Atakuwa yeye ni mpya,
tofauti, na anaonekana kuwa mrembo mzuri kuliko yeyote. Anaonekana kutawishwa vizuri,
hahitaji sana, hucheka kila mnapotaniana na kuonekana kama kapendeza sana. Mara, Kasoro
za mke wako zitaonekana kubwa sana. Na punde unaweza kumwambia au kutaka kuwa mke
wako awe kama Mama Jones kwa njia moja au nyingine!
50
Kutafutia Visingizio ili Kuwa Pamoja na Huyo Mwanamke
ukali kwa wake zetu
Hili litaanzia wakati tupo kama kundi. Na kawaida nafasi nyingi zitatokea kumwona katika
shughuli za Kanisa.
Kuanza kuona ashiki/kuwaka tamaa za kimapenzi juu yake
Kuanza kuona ashiki juu yake. Hili laweza kutokea hata tuwapo fisini au tunapomtazama
wakati wa ibada.
Kutafuta Njia Jinsi ya Kukutana Wenyewe Peke yenu:
Hii huanzia kwenye kumdanganya mke wa mtu fulani au karani ofisini. Halafu kufuatiwa na
kuwachukia wake zetu au kuwaamuru juu ya mambo yetu au kuonyesha kuwashukushuku.
Wake zetu wako macho sana kuelewa kuhusu kuhusian kwetu na wanawake wengine kuliko
sisi wenyewe. Tukijifunza kuwasikiliza wake zetu, wangeweza sana kutuokoa na uhusiano
wowote kabla ya kuendelea kwenye uharibufu.
Kwamba kila kitu kinawategemea wao. Wanamini kwamba hayupo mtu alivuviwa kama wao.
Lakini haipo nafasi katika mpango wa Mungu kwa ajili ya walio na utata wa Upako kama
hawa. Kati yetu hayupo wa kujitumainia mwenyewe. Twatakiwa kubakia wanyenyekevu na
kutambua wakati wote kuwa tu vyombo mikononi mwa Bwana. Mungu anaweza kutuacha na
kuwatumia wengine ikiwa tutausahau ukweli huo wa muhimu.
mtu wa Mungu kwa wakati huu
Kutaka Kumshirikisha Mteja Juu ya Matatizo katika ndoa
Kiasi tutakavyozidi kulalamika juu ya wenzi wetu, ndivyo tutakavyozidi kukosa anuani juu ya
ndoa zetu, na ndivyo huyo mwanamke mwingine atakavyozidi kuonekana wa kufaa. Hali
huwa mbaya zaidi, kama huyu mwanamke, mwingine atakapojitahidi kutujali. Ni mazingira
ya upotovu.53
kuongezeka kuomba kwa dhati
Tuwapo macho dhidi ya uwezekano wa matatizo, kuzitunza na kuzipa umuhimu ndoa zetu, na
kuziangalia sana dalili za hatari, ndipo tu tutakapoweza kuyathibiti mashambulizi ya shetani
katika ndoa na huduma zetu.
kaa macho
3. Umaarufu
Hatari anazozikabili kiongozi wa Kikristo, si majaribu ya kimwili tu, bali lazima pia ajilinde
menyewe na wale wadanganyao katika ulimwengu wa roho. Ni lazima ajue kuwa shetani
atatumia kila nafasi itakayopatikana katika maisha yake.
majaribu ya roho
Ukweli wenyewe kuwa mwanadamu ameinuka kufikia nafasi ya uongozi na heshima
inayofuata kutokana na nafasi hiyo, huleta kujipendeza mwenyewe na kiburi, ambavyo kama
hakitakaguliwa, vitamfanya asifae kwa kuendelea kutumiwa katika Ufalme wa Mungu.
Maandiko yanasema kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa Bwana (Mithali 16:5).
(1) Utata Juu ya Upako/Umesia
Viongozi wenye mafanikio, wataona shetani akiwaambia kuwa wao ndio `mtu wa Mungu wa
wakati huu'. Wakifikiri kuwa pasipo wao hakuna litaweza kufanikiwa bila uongozi wao. Watu
kama hawa hujiona kuwa ndio Billy Graham au Reinhard Bonnke, T.L. Osborn (n.k) wa taifa
lao.
51
(2) Tatizo la Umaarufu
tahadhiri juu ya kutaka kujulikana binafsiElekeza Upendo/-Mapenzi kwa YESU
Mara Mungu amtumiapo mtu kwa jinsi ya pekee, umaarufu utaleta matatizo. Bahati mbaya mi
kwamba Wakristo wengi hawajakomaa vizuri Kiroho, kutambua kwamba kupenda kujulikana
kibinafsi ni hatari kubwa kwa kiongozi yeyote. Zitakuwepo wakati wote nafsi zilizo na
heshima zitakazotofautisha isivyo viongozi wao wa Kiroho. Ukweli ni kwamba, "inapasa
waheshimiwe sana katika upendo kutokana na kazi zao". Lakini heshima hii isibadilike na
kuwa "kumwabudu" kiongozi. Hivyo kiongozi wa kweli atajifunza kuelekeza upendo wa
wafuasi wake kwa Kristo kulikoni kwake wenyewe. Anaweza kutiwa moyo kutoka kweli
kwamba kazi yake imezaa matunda na watu wameshukuru na kuifurahia, lakini lazima akatae
kuabudiwa kama sanamu. Stephen Neill siku moja alisema: "Uamaarufu ni hali inayofikirika
ya kiroho iliyo hatari zaidi, kwani huongoza kirahisi kwenye kiburi cha kiroho ambacho
huwaingiza/tia watu katika majaribu.54
(3) Jaribio la Kiburi
Kiburi ni dhambi ambayo huja mara ka mara kwa sababu ya umaarufu/kujulikana mahali
mahali. Mara nyingi aliyeathiri wa/ye na dhambi hii ya kiburi huwa hafahamu kama ipo.
Oswald Sanders katika kitabu chake uongozi wa kiroho anashauri/pendekeza
majaribio/mitihani mitatu ambayo kwayo kiburi chaweza mara kugundulika.
Jaribio la Kipaumbele
Twajibu/tunatenda vipi wakati mtu mwingine achaguliwapo kwa ajili ya kufanya zoezi/kazi
tulioitarajia au mwingine apewapo ofisi tuliyokuwa na shauku sana kuimiliki? Wakati mtu
mwingine anopopandishwa cheo na tunapopuuziwa?
Jaribio la Shutuma
Je shutuma huamsha ukali na chuki/donge mioyoni mwetu na kusababisha kurukia kwenye
kujihesabia haki wenyewe. Je twafanya haraka kuwashutumu walitushutumu/hukumu.55
Jaribio la Ukweli wa Hali ya Moyo Wote
Katika wakati wa kuwa na kweli tukijishutumu wenyewe tutasema mambo mengi kuhusu sisi
wenyewe, na twamaanisha kweli tulivyosema. Lakini twajisikia/hisi vipi wakati wengine hasa
wapinzani wetu wanaposema vitu/mambo hayohayo kuhusu sisi.
Jaribio la "Kujiona Bora Zaidi Kulikoni Wengine" au Wivu
Tunajibu/fanya nini wakati mwingine anang'ara zaidi kuliko/kushinda katika karama na
utimilizaji kazi? Wakati huduma yake inafanikiwa zaidi ya yetu. Wakati anapoziongoza roho
nyingi zaidi kwa Bwana, na atumiapo kiuwezo mkuu zaidi katika kufanywa ishara na miujiza.
(4) Jinsi ya kuwa Mnyenyekevu
Hadithi/habari imeeleza juu za mfalme ambaye wakati alipokuwa sehemu mbalimbali chini ya
ufalme wake alimwona masikini/fukara mwombaji ameketi kando ya njia. Alisukumwana
huruma aliamua kumsaidia mtu huyu kubadilisha njia zake za maisha zilizokuwa mbaya sana
kwa kumpatia kazi katika jumba lake la kifalme. Mwombaji masikini alionyesha kwa
kiwango kikubwa kufanya kazi kwa bidii katika kazi ndogo alizopatiwa ili baada ya kitambo
kifupi apate kumpandisha cheo. Kwa mara nyingine tena mwombaji maskini alionyesha kwa
kiwango cha juu kuwajibika kwake na uaminifu wake, mpaka baada ya kupandishwa cheo
mara kadhaa na miaka ya kutumika aliishia kuwa mtunza hazina/fedha wa mfalme. Kila siku
alionekana ndani ya kichumba aliendelea na kazi yake. Siku moja mtu mmoja akatambua,
52
baada ya kuwa na masaa ya kukaa pamoja na mtunza hazina wa mfalme alitokomea katika
chumba kidogo ambamo alijifungia mlango nyuma yake. Taarifa ya tukio hili ilipelekwa
mfalme pamoja na madai kwamba mtunza hazina, ambaye amekuwa akionyeshwa
kupendelewa sana ametumia wadhifa/cheo chake kufuja fungu la fedha alilokabidhiwa
alitunza. Pasipo kuchelewa mtunza hazina alifikishwa mbele ya mtawala kusomewa shitaka,
mfalme hakuweza kuamini kwamba mtumwa wake mwaminifu amekana/ametenda kinyume
cha kutumainiwa kwake. Mfalme na Maskini Mwombaji Nyakati za Hatari Katika Uongozi
wa Kikristo
Baada ya madai kusomwa, kwa moyo mzito maskini mwombani alijibu "Vitu/mambo kama
hayo ee mfalme vitakuwa mbali nami, baada ya vibali vyote kuja mbele yake upendeleo wote
ambao umemuonyesha mtumwa wako. Ingawa ni kweli kwamba baada ya kufanya kazi katika
ofisi yako ya hazina, nikiitunza mali/utajiri wako, ninajitoa kwenda katika kijichumba kidogo.
Pale nimeficha kasha ambalo ndani mwake nimeweka nguo zilizokuwa nikivaa kama
mwombaji maskini. Baada ya kugusa utajiri/mali zako zote za ajabu na kupendeza huenda na
kuzigusa nguo hizi na hapo ndipo ninajikumbusha mwenyewe wapi, nilitokea, ili kamwe
nisisahau rehema na neema vilivyonyoshwa kunifuatia mimi".
Maandiko yaonyesha kwamba Yesu aliondoka miongoni mwa wanafunzi wake, baada ya
kuhudumu kwa muda mrefu, ili awe pekee/na faragha na Baba yake. Katika Luka 9:10
twasoma:-
Basi wale mitume waliporudi walimweleza mambo yote waliyoyatenda;
akawachukua akaenda nao faraghani mpaka mji mmoja uitwao
Bethsaida.
kuchuku-liana na mafanikio Sasa walipofahamika sana habari zao, Yesu akawachukua
pembeni. Hapo aliwapatia fursa ya kuchukuliana na mafanikio yao kihuduma Yesu alitaka
watambue kwamba huduma yao ilikuwa kwa utukufu wa Mungu. Hauna budi kujifunza
kutoka hayo! Shughuli za huduma zinapoanza mara kwa mara twashindwa kujitoa na kwenda
kando ili kupata kujua jinsi ya kutoa kipaumbele kwa usahihi, na kusikia hutoka kwa Mungu
tena.
Mwisho
uhitaji mkubwa wa viongozi wa KirohoRoho Mtakatifu atafanya sehemu yake
Viongozi wa kiroho wanahitajika sana. Mungu anawatafuta wanaume na wanawake
watakaoweza kuuongoza ulimwengu unaokufa kwa Yesu, na waumini wa Kristo Yesu
kuingia katika ushirika wa karibu zaidi na Bwana wao. Je tuko tayari kusimama mahali
palipobomoka? Je tupo tayari kulipa gharama? Je twamruhusu Roho Mtakatifu mara kwa
mara azifanye kuwa bora zaidi sifa zetu za uongozi? Na je twajilinda wenyewe dhidi ya
maonguko/vitu viwezavyo kutuangusha katika huduma. Sawa na mtu mmoja alivyosema
Kanisa linao tayari viongozi wa kutosha wanaostahili sifa zote, wanaokwepa kazi zote na
wanaondaa kwao na kuwawekea wengine malaumu yote. Kwa ajili hii Kanisa lahitaji
viongozi ambao wako tayari kutimiza kanuni zilizotajwa juu. Hapo tutapata uongozi ambao
Kanisa linauhitaji, na dunia inautafuta. Mara tunapokubali kulipa gharama, Roho Mtakatifu
atakayefanya haya ndani na kupitia sisi, akitupatia mamlaka ya kiroho, muda wote tujitoao
kwake Yeye.
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-
53
BIBLIOGRAPHY
Aultman, Donald S. Learning Christian Leadership, Cleveland: Pathway Press, 1960
Cho, Yongi. The Forth Dimension, New Jersey: Logos International, 1979.
Damazio, Frank. The Making of a Leader, Eugene: Church Life Library, 1987.
Engstron, Ted W. The Making of a Leader, Grand Rapids: Zondervan Publishing House,
1978.
Engstrom, Ted W., Dayton Edward R. The Art of Managementfor Christian Leaders, Waco:
Word Books Publisher, 1982.
Handbuch für Führungsaufgaben im Christlichen Dienst, Lahn: Druckerei Grimm, 1976.
Lindsay, Gordon. The Charismatic Ministry, Dallas: Christ for the Nations, 1986.
Mahoney, Ralph. "Spiritual Authority" Acts Magazine, nd.
______. The Making of a Leader, Gleanoaks: World Missionary Assistance Plan, 1985.
______. "The Use and Abuse of Authority", Acts Magazine, 11 (4) 1983.
McBurney, Louis. "Avoiding the Scarlet Letter", Leadership, 4 (3), 1985.
Minirth, Frank. Before Burn Out, Chicago: Moody Press, 1990.
Richards, Lawrence O. Hoeldtke, Clyde. A Theology ofChurch Leadership, Grand Rapids:
Zondervan Publishing House, 1980.
Sanders, Oswald. Spiritual Leadership, Chicago: Moody Press, 1967.
________. Verantwortung Leitung Dienst, Wuppertal: Brockhaus Verlag, 1980.
Shakarian, Demos. The Happiest People on Earth, London: Hodder and Stroughton, 1973.
The Pentecostal Minister, "Warning Voice", 4, 1985.
Thomas, Griffith W.H. Leben und Arbeit im geistlichenDienst, Marburg: Verlag der Franke
Buchhandlung, 1979.

No comments:

Post a Comment