Friday 5 December 2014

UKOMBOZI

117
Sura ya 10 - Nguvu ya Kupiga mbio katika Mashindano -
Ukombozi
Roho Mtakatifu ni nguvu ya Mungu ya ukombozi katika maisha
yetu. “Alipokuwa katika kumwendea, pepo akambwaga chini, akamtia kifafa.
Yesu akamkemea pepo mchafu, akamponya mtoto, akamrudishia babaye. Wote
wakashangaa, wakiuona ukuu (nguvu)wa Mungu.” (Luka 9:42,43a).
Katika Agano Jipya, Roho Mtakatifu anatajwa mara nyingi kuwa ni
Kidole cha Mungu. “Lakini, ikiwa mimi natoa pepo kwa kidole cha Mungu,
basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia” (Luka 11:20). Yesu alisema
wazi kwamba alitoa pepo kwa Roho Mtakatifu.
Maadui zetu wa kiroho mara nyingi huwazuia waamini wasipige
mbio vizuri na Mungu, kwa kueneza uongo kwamba hawawaathiri Wakristo.
Mara nyingi waamini huzongwa na dhambi na mizigo wanayowekewa na
pepo. Tunakubali kwamba watu wanaomwamini Yesu hawawezi “kupagawa”
na pepo, lakini najua kwamba wanaweza kuonewa na kuathiriwa na pepo.
Haina maana kujua pepo anakaa wapi katika maisha ya mwamini. Suala
muhimu ni kwamba tunahitaji kuwafahamu pepo hao ili tuweze kuwatoa nje ya
maisha yetu, popote pale walipo.
a. Shetani alikuwa malaika mkuu, Nyota ya alfajiri. Alikuwa
kiongozi wakati wa kumwabudu Mungu. Kulingana na Ezekieli sura ya 28 na
maandiko mengine, alikuwa amepakwa mafuta, huenda alikuwa na vyombo
vya muziki ndani ya mwili wake. Alikuwa katika bustani ya Edeni pamoja na
Adamu na Hawa. Alikuwa na sura nzuri. Ana kipaji kikubwa cha kufanya kazi
na biashara. Huenda ndiye aliyeanzisha wazo la kupata utajiri kwa kumiliki
watumwa. Ni mwenye majivuno sana, na anatambua uzuri wake mwenyewe.
Ana akili sana na pia ni mlaghai. Anafanya mambo kwa mipango.
b. Nyota ya alfajiri alimwasi Mungu na kuchukua theluthi moja ya
malaika. Akawapanga katika ngazi za kijeshi na kuiga Ufalme wa Mungu
(Waefeso 6).
c. Shetani sasa ni mkuu wa ulimwengu huu (Yohana 12:31).
d. Baadhi husema kwamba pepo ni malaika walioanguka, na
wengine husema ni majini labda kutoka katika jamii iliyokuwepo kabla ya
Adamu, au labda kutoka kwa mababu zetu. Maandiko hayaelezi hivyo. Lakini,
malaika hawakuumbwa ili wakae ndani ya miili ya wanadamu. Inawezekana
kwamba pepo ni wale wale waliokuwa malaika na ambao sasa wanatawala na
Shetani au pia ni majini yanayoishi ndani ya wanadamu. Sina uhakika juu ya
hayo, ninakisia tu. Hata hivyo, ufafanuzi huo siyo muhimu. Neno au jina
1. Pepo ni nini na Shetani ni nani?
118
jingine linalotumika badala ya pepo ni "daimon." Neno hili lina maana ya
"kujua," au "ajuaye."
e. Tabia zao ni chafu kabisa. Kamusi ya Vines inasema, "pepo ni
mawakala wa kiroho wanaojihusisha na kuabudu sanamu. Sanamu yenyewe si
kitu, lakini kila sanamu ina pepo anayejihusisha nayo. Pepo huyo ndiye
anayewashawishi watu kuiabudu sanamu hiyo na kutoa kafara, 1 Wakorintho
10:20-21; Ufunuo wa Yohana 9:20; Isaya 13:21. Pepo hueneza uongo na
kutafuta kuwapotoa watu wanaomwamini Yesu, 1Tomotheo 4:1. Kama roho
zidanganyazo huwadanganya watu waamini kwamba kupitia kwa mtu
anayewasiliana na mizimu wanaweza kuongea na watu waliofariki. Pepo
hutenda kazi chini ya Shetani na wameruhusiwa kutesa kwa magonjwa ya
kimwili, Luka 13:16. Kwa kuwa pepo ni wachafu, huwajaribu wanadamu kwa
mawazo machafu, Mathayo 10:1. Hutofautiana katika viwango vya uovu,
Mathayo 12:45. Watawaendea wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya
kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi, Ufunuo wa Yohana 16:14."
a. Kulingana na Yohana 10:10 huiba na kuchinja (kuua) na kuharibu.
Kila kitu wanachokifanya kipo ndani ya mambo hayo matatu.
b. Kuua. Mauaji yao yanahusiana na laana ya milele na pia kifo katika
maisha haya.
c. Kuiba. Ni wezi. Huiba mapenzi ya Mungu kwako. Huiba Neno la
Mungu katika moyo wako. Huiba ubikira, afya, amani, na mali.
d. Kuharibu. Wanaharibu maisha. Wanaharibu kwa madawa ya
kulevya na magonjwa. Wanaharibu familia. Wanaharibu kwa kutumia nguvu,
udhalilishaji wa kijinsia na mapigo kama vile UKIMWI.
a. Kwa kukujaribu (Mathayo 4:1). Lengo lao ni kukutenganisha na
Mungu, uishi bila kumtegemea Mungu.
b. Husema na mawazo au fikira zako (2 Wakorintho 10:5)
c. Hutoa ishara na maajabu ya uongo. (2Wathesalonike 2:9).
d. Huiba Neno ili kuwafanya Wakristo wawe vuguvugu wasizae
matunda (Marko 4).
e. Huwadanganya watu kwamba mashetani na pepo hawapo. Mara
nyingi huwatumia watu wanaoonekana kuwa hawana hatia, wazuri, na wakati
mwingine hata Wakristo. Nimekutana na watu katika makanisa wanaoonekana
kwa wazi kabisa kwamba wana pepo. Watu hao wakaniambia kwamba hakuna
pepo wala ulimwengu wa roho. Wanadai kwamba pepo wabaya ni matendo tu
yanayofanywa na wanadamu.
f. Hujaribu kukufanya utende dhambi ili waweze kukutawala na
Yesu asipate nafasi. Mshahara wa dhambi ni mauti. (Warumi 6:23).
2. Wanafanya nini?
3. Wanatimizaje malengo yao?
119
g. Husema uongo na kuwashutumu watu wasio na hatia (Yohana
8:44 na 2 Wathesalonike 2:9-10). Walimshutumu pia Yesu kwamba ana pepo.
"Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo." (Mathayo
11:18). "Nao waandishi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasema, ana
Beelzebuli, na, kwa mkuu wa pepo huwatoa pepo."(Marko 3:22).
h. Huchukua mamlaka ya mwathiriwa na kumpa mkosaji.
i. Huwawezesha watu kutumia uwezo au nguvu zao (pepo). Muziki
wa roki, ufalaki, kupiga ramli, na kadhalika.
j. Huwatesa watu kimwili, kihisia na kiakili
k. Hutawala na kuendesha ridhaa ya mtu. Wanadhibiti utashi,
mawazo na mhemuko wa mtu, na kutenda kazi zao kwa njia ya mtu huyo.
Husababisha mtu huyo aseme uongo na kuamini uongo wao.
l. Huchukua mamlaka yasiyo na mpaka, na kukiuka mamlaka ya
kweli.
m. Shetani huigiza kazi nyingi za Mungu. Yeye sio mbunifu, haumbi
kitu chochote, ananakili tu na kupotosha yale anayoyafanya Mungu.
Baadhi ya mambo ya kuigiza anayoyatumia Shetani:
Shetani ana uwezo wa kusababisha miujiza kutokea.
Amesababisha baadhi ya Wakristo kuvutiwa na miujiza hiyo. Amewafanya
wengine kuogopa sana miujiza hiyo kiasi kwamba wanakosa kazi timilifu ya
Roho Mtakatifu.
Kuna maandiko kadhaa yanayoweza kutusaidia kutofautisha
kazi za Roho Mtakatifu na kazi za mashetani na pepo. Maneno ya Mungu
katika 1 Wakorintho 14:33 yanazungumzia juu ya roho ya machafuko. Roho
Mtakatifu hachezi sarakasi. Yupo ili kumfanya Yesu aonekane wazi katika
maisha yetu. Kazi za Roho Mtakatifu kila wakati hupatana na Neno la Mungu.
Roho Mtakatifu humwinua Yesu kila wakati na siyo “Yesu mwingine” (2
Wakorintho 11:4). Dini za kishetani haziwezi kukubali kwamba Yesu alizaliwa
na bikira, kwamba ni Mungu, kwamba ni Mwana pekee wa Mungu, na
kwamba alifufuka katika wafu. Neno la Mungu katika 1 Yohana 4:2-3
linadhihirisha wazi tofauti hiyo.
a. Yesu alimtoa pepo kwa imani ya mwanamke (Marko 7:29).
b. Yule mtu aliyekuwa na pepo mchafu katika nchi ya Wagerasi
alikombolewa, na pepo wakaingia katika nguruwe (Marko 5:1-20).
c. Katika Mathayo 9:32-33 mtu bubu alianza kuongea baada ya pepo
kutolewa.
d. Katika Mathayo 10:1-8 Yesu aliwapa wanafunzi wake amri ya kutoa
pepo
e. Katika Marko 9:17-29 pepo bubu alikuwa ndani ya mvulana tangu
utoto wake.
4. Baadhi ya mifano ya ukombozi na jinsi pepo wanavyotenda kazi.
120
f. Agano la kale linaonyesha pia kwa kivuli jinsi pepo wanavyotenda
kazi. Soma Zaburi 10, 56, 59, 64 na nyingine nyingi. Mifano mingine mizuri ni
vita wakati wa Agano la Kale, makabila na watu kama Yezebeli na Balaamu.
Soma habari hizo huku ukijua kwamba yale yaliyofanywa na maadui wa wana
wa Israeli yalifanywa na pepo.
a. Dhambi zako. Dhambi zote huwapa nafasi pepo, lakini mojawapo
ya dhambi zilizo mbaya ni zinaa. Zinaa huwaunganisha pamoja watu wawili
kiroho kwa njia ya kipekee.
b. Dhambi za vizazi. Pepo huzifuata familia kutoka kizazi hadi kizazi,
na wana haki ya kuweka ugonjwa ule ule na laana juu ya familia hizo (sheria
ya kurithi). Dini za mashetani zimejengwa juu ya kuabudu mizimu ili
kuendeleza laana na kutawala familia. Hujaribu kuwashawishi watu, na hata
Wakristo, kwamba ni lazima watoe pesa kwa mganga wa kienyeji ili walindwe.
Na baadhi hutoa vitu na mifugo kwa waganga hao wa jadi kwa kusudi la
kupata ulinzi na baraka. Watu hawa huamini kwamba kwa kuwasiliana na roho
za mababu zao watabarikiwa na kulindwa wasipatwe na mabaya. Lakini ukweli
ni kwamba yanayotokea yanakuwa kinyume na matarajio yao. Watu hawa
hugeuka kuwa wafungwa wa adui yao, Shetani!
Sikukuu nyingi kama ile siku ya mwisho kabla ya kuanza Kwaresma
(Mardi Gras) huko Marekani zimepangwa kuendeleza laana juu ya maeneo
kadhaa. Na wakati mwingine hata kukutana kwa familia yote (katika siku
maalum) huweza kutumiwa na pepo kuendeleza laana za kifamilia. Ulozi au
vuudu (voodoo) na ushirikina yote hayo yana sikukuu zake. Pepo hupata nafasi
zaidi katika laana za vizazi na mara nyingi hujaribu kuwateka vijana katika
familia. Ndiyo sababu ukorofi na uasi huonekana kwa wazi zaidi watoto
wanapofikia umri wa ujana. Wasipofanikiwa kuwateka, hujaribu tena baadaye.
c. Dhambi katika ulimwengu. Ulimwengu huu umejaa dhambi na hii
huchochea kazi za pepo.
d. Mizigo, au ukandamizaji unaoweza kuupata kutoka kwa mtu
mwingine. Mbinu ya mara kwa mara wanayoitumia pepo ni kumnyanyasa
kijana kijinsia na hivyo kupata nafasi ya kuingia ndani yake maisha yake yote.
Mzigo sio dhambi uliyotenda ila ni ukandamizwaji unaofanyiwa kwa dhambi
ya mtu mwingine.
e. Kwa njia ya sanamu katika maisha yako. Sanamu inaweza kuwa
kitu chochote unachokipa umuhimu kuliko Mungu. Inaweza kuwa mtu, tabia,
desturi, au hata dhehebu.
f. Kuasi mamlaka. Kama mtu hataki kumpokea Yesu kuwa Bwana
wake, mtu huyo, atakuwa chini ya utawala wa kiumbe kingine. Hawa
alidanganywa na Shetani, na yeye akamdanganya Adamu. Adamu angeweza
kutumia mamlaka yake dhidi ya Shetani lakini hakufanya hivyo. Kwa kweli,
Hawa alipokea mamlaka yasiyokuwa ya kawaida na Adamu naye hakutumia
mamlaka aliyopewa. Dhambi ya asili inaonyesha jinsi dhambi na mamlaka
5. Jinsi wanavyopata nafasi katika maisha yako.
121
yalivyoungana pamoja. Ni wazi, kwamba wote wawili wangepaswa kutii
mamlaka ya Neno la Mungu (Mti wa Uzima).
g. Wakristo wanaweza kudhurika (baadhi ya watu wanapinga
jambo hili). Kama mtu ana pepo kabla ya kumpokea Yesu, muda unaweza
kupita kabla ya kupokea ukombozi. Baadhi ya watu hawapokei ukombozi kwa
sababu hawataki kujiachia kikamilifu mikononi mwa Yesu. Ni kweli kwamba
Mkristo hawezi kupagawa na pepo, lakini anaweza kabisa kuathiriwa. Jambo
muhimu siyo istilahi gani tutumie: kupagawa, kuathiriwa, au kuonewa? Kitu
muhimu ni kujua jinsi ya kushinda kazi za pepo katika maisha yetu.
Maandiko yafuatayo yanaonyesha kwamba bado tunaweza
kudhurika hata baada ya kuamini. "Basi Roho ananena waziwazi ya kwamba
nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho
zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani" (1 Tomotheo 4:1). "Mwe na kiasi
na kukesha; kwa kuwa mshtaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye,
huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze" (1 Petro 5:8). "Lakini nachelea;
kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu
fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. Maana yeye ajaye akihubiri
Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine
msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana
naye!" (2 Wakorintho 11:3-4).
Baadhi ya watu husema kwamba damu ya Yesu huwalinda
Wakristo. Ndiyo na hapana. Damu ya Yesu hutulinda tunapokuwa tu Wakristo
watiifu. "Kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na
roho, hata mkapata kutii na kunyunyiziwa damu ya Yesu. Neema na amani na
ziongezwe kwenu" (1 Petro 1:2). Wakristo wanahitaji ukombozi.
Shetani alipowashawishi Adamu na Hawa wafanye dhambi, alipata
nafasi ya kuwatawala, na kuwatawala wanadamu wote. Ana nguvu kuliko
binadamu wa kawaida. Dhambi isiposhughulikiwa, Shetani anakuwa mtawala.
Yesu alichukua dhambi zetu pale msalabani akalipa adhabu ya mwisho.
Tukiujua ukweli huo na kuwa watii, tutakuwa huru mbali na Shetani na pepo.
Ukombozi haumaanishi kila wakati kukemea kwa nguvu na kuwekewa
mikono kichwani, ingawa hilo linawezekana na linatokea mara nyingi. Zipo
njia nyingine ambazo kwazo sisi tunaweza kukombolewa.
a. Uwe mwaminifu. Ungama dhambi zako. Enenda katika uaminifu
na ukweli kwa gharama yoyote. Unaposema uongo unamfanya Shetani awe
baba yako.
b. Kataa kuwa na uhusiano au mawasiliano yoyote ya kipepo
uliyokuwa nayo kama vile: muziki, picha au maandishi yenye kutia ashiki
(ponografia), televisheni, sinema, madawa ya kulevya, ushirikina, uaguzi,
kupiga ramli, ubashiri, michezo ya kadi (karata) na kadhalika.
6. Jambo unaloweza kufanya
122
c. Kataa uhusiano wowote wa kiukoo unaoweza kutumiwa kueneza
laana. Tunaweza kuwa na heshima kwa ndugu zetu katika ukoo bila kupokea
laana zao.
d. Kaa karibu na Yesu kwa njia ya maombi, Neno lake, marafiki
wazuri na washirika wa kanisa. Hakikisha moyo wako umejaa mambo ya
kiroho. Moyo wako ni uwanja wa mapambano.
e. Uwe tayari kukombolewa kwa njia yoyote ile anayotaka Mungu.
Uwe na haja ya kuwa huru. Usimuwekee mipaka Mungu. Anazo njia nyingi za
kukuweka huru. Kazi yake ni kukuweka huru (Luka 4).
f. Mara nyingine watu huwekwa huru mbali na pepo lakini
hawajishibishi kwa Neno la Mungu na pia hawaishi maisha matakatifu. Kwa
njia hiyo pepo huwarudia tena watu hao na hali zao huwa mbaya sana. Ni
vizuri kupata ushauri wa kiroho baada ya kukombolewa. “Pepo mchafu
amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika;
asipoona, husema, nitairudia nyumba yangu niliyotoka. Hata afikapo, akaona
imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio
waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali
yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza” (Luka 11:24-26).
Hata hivyo, kuna njia ya salama na ya kiutendaji ya kuwekwa
huru. Neno la Yesu liliwatoa pepo katika Mathayo 8:16. Linaweza kufanya
vivyo hivyo kwa ajili yako leo. Mimi binafsi nimeshuhudia njia hiyo ikifanya
kazi. Kama ukijaza maji kwenye ndoo kabla ya kuyamwaga maji
yaliyokuwemo, hakuna hatari ya kuwa na nafasi tupu itakayokaliwa na kitu
kingine. Kwa sababu hiyo kama Neno la Mungu likijaa ndani yako, siyo tu
kwamba pepo watatoka, bali pia hakutakuwa na nafasi iliyoachwa wazi ya wao
kurudi.
“Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo
kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi” (Mathayo 8:16).
Kujaza Neno ndani yako kutawatoa pepo katika maisha yako.
Ningependa kumualika kila msomaji akubali sasa kutumia njia hii.
Hata kama huamini kwamba una tatizo lolote, huwezi kujua kwa uhakika.
Fanya hivi. Dhamiria moyoni mwako kwamba Neno la Mungu lijae
kwa wingi ndani yako na kufurika. Na hapo sasa unaweza kulimimina Neno
kwa njia yoyote unayopenda. Soma Biblia, sikiliza kanda za Neno la Mungu,
kariri Maandiko, yaweke mdomoni mwako, yatafakari mchana na usiku. Litii
Neno. Tenda yale ambayo limesema. Neno litatoa nje kila roho katika maisha
yako isiyo takatifu.
g. Ujazwe Roho Mtakatifu ili uwe na nguvu ya kushinda (Matendo ya
Mitume 1:8).
h. Yesu alitupatia nguvu na mamlaka ya kutoa pepo (Marko
16:17).
i. Tunaweza kuwagundua pepo katika maisha yetu tukikaa karibu
na Yesu. Hata hivyo sio kwamba mabaya yote na magonjwa yote yanatokana
na pepo, la hasha. Ugonjwa unaweza kusababishwa na matatizo ya kimaumbile
123
au masuala ya kimaisha. Mwenendo mbaya unaweza kuwa “mwili” wetu. Hata
hivyo kama matatizo haya yasipotatuliwa yanaweza kuwa mlango wa kuingilia
pepo. Tunapaswa kujihadhari na mwenendo mbaya, tabia tusizoweza
kuzishinda, tamaa mbaya, hofu na hisia za kukandamizwa. Usiruhusu hali ya
huzuni au mfadhaiko iendelee bila kupata msaada. Usikubali kutawaliwa na
hisia za kujiua, uharibifu au mauaji. Wala usifiche hisia za ubasha na zinaa.
Tafuta msaada!
Inamaanisha nini tunaposema Mungu alimharibu Ibilisi? Ni kwa
vipi damu ya Yesu inatupatia nguvu?
“Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo
hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na
nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba maisha yao
yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa” (Waebrania
2:14,15).
“Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi
pamoja naye; tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena,
wala mauti haimtawali tena. Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi
mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu. Vivyo hivyo
ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika
Kristo Yesu” (Warumi 6:8-11).
Mistari hiyo inasema kwamba Shetani “aliharibiwa.” Hiyo inamaanisha
nini hasa? Inaonekana anazunguka zunguka akifanya kazi ya kuwaharibu
wengine.
Kuharibu maana yake ni kufanya nguvu za Shetani ziwe dhaifu -
zisifanye kazi. Yesu alifanyaje hivyo? Ibilisi bado anazunguka zunguka
akiwaharibu wengine. Yesu alipofufuka alikuwa mzaliwa wa kwanza wa jamii
mpya kabisa. Yesu aliweka utu mpya ndani yako siku ulipozaliwa mara ya pili.
Utu huu mpya uko juu kabisa kuliko pepo na mashetani. Walikwisha ua jamii
ya kwanza ya Adamu, katika Yesu pale msalabani. Shetani na pepo hawana
kabisa mamlaka juu ya jamii hii mpya, wanachoweza kufanya tu ni kutuambia
uongo. Yesu alipofufuka, pepo hawakuwa na nguvu tena juu yake. Aliweka
maisha hayo ndani yako.
Neno kuharibu limeelezwa katika Itifaki ya Strongs kama
ifuatavyo:
1) kugeuza kitu kisifanye kazi, kikose kazi, kilegee, kisitumike.
1a) kumfanya mtu au kitu kisiwe na ufanisi tena.
1b)kunyang’anya nguvu, uwezo wa kuathiri na mamlaka
7. Mungu alimharibu Ibilisi
Ufuatao ni mfano wa kuchekesha lakini unaweza kutusaidia
kukumbuka na kupata picha inayoelezea maana ya neno “kuharibu”
124
Hebu jifanye kuwa paka. Sasa mbwa mkubwa anayemuwakilisha
Shetani anakunyanyasa, na kukufanya ukimbie kimbie tu na kujificha. Anaiba
chakula chako na hata kuharibu mahali ulipojificha. Hatimaye mbwa huyu
anakuua.
Kisha kwa ghafla, kwa njia ya muujiza, wewe, paka, unafufuliwa
kutoka kwa wafu. Safari hii wewe sio paka tena. Umegeuka kuwa simba! Sasa
mbwa yule yule anakuja kwako, anakuangalia halafu anakimbia kwa sababu
anajua unaweza kumuua! Mbwa ameharibiwa (amegeuzwa asifanye kazi,
amekosa kazi, amelegea, hatumiki, hana ufanisi, amenyang’anywa nguvu,
uwezo wa kuathiri na mamlaka)!
Hebu jaribu kuwaza sasa kwamba mbwa yule amepanga mpango
fulani. Anakuja kwako na kukushawishi uamini kwamba wewe bado ni paka
hujawa simba kweli kweli. Itakuwaje sasa mbwa huyo akifaulu kukufanya
uishi na kutenda mambo kama paka? Hivyo ndivyo mbwa Shetani anavyofanya
kwa Wakristo wengi.
Jaribu kuwaza tena kwamba Yesu alikuwa “paka” yule aliyekufa.
Lakini muda mfupi kabla ya kufa kwake alipata “ujauzito” pamoja na wewe na
mimi katika Bustani ya Gethsemane. Alipokufa na kufufuka, akawa mzaliwa
wa kwanza katika wafu. Tunapozaliwa mara ya pili, tunakuwa pia simba.
“Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni
mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote”
(Wakolosai 1:18).
Tunahitaji kila wakati kusoma Neno na kumtazama Yesu ili tuweze
kuitunza kweli hiyo katika mioyo yetu. Tukiacha kufanya hivyo, tutachukuliwa
upesi sana na uongo wa dunia hii na kisha tunaweza kudhurika.
“Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa
mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako,
na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo
nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi
mtendao maovu!” (Mathayo 7:21-23).
Yafuatayo yamenukuliwa kwa kiasi fulani kutoka katika kitabu kiitwacho “They Shall Expel
Demons”(Watatoa Pepo), ukurasa wa 215, kilichoandikwa na Derek Prince.
“Bwana Yesu Kristo, nakiri kwamba wewe ni Bwana wangu.”
1. Tamka kwa dhati imani yako katika Kristo. “Bwana Yesu Kristo,
naamini kwamba wewe ni Mwana wa Mungu na njia pekee ya kutufikisha kwa
8. Kumjua Yesu ndilo jambo muhimu
Maombi kwa ajili ya ukombozi
125
Mungu – na kwamba ulikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu na kufufuka
tena ili nisamehewe na kupokea uzima wa milele.”
2. Jinyenyekeze. “Nakataa kiburi na kujihesabia haki kidini na
heshima yoyote isiyotoka kwako. Sistahili rehema yako ila nashukuru tu
kwamba ulikufa badala yangu.”
3. Ungama kila dhambi unayojua kwamba umetenda. “Naungama
dhambi zangu mbele zako na sitaki kuficha dhambi yoyote.” (Sasa orodhesha
dhambi zote na kuungama).
4. Tubu dhambi zote. “Natubu dhambi zangu zote. Naziacha kabisa
na kukugeukia Bwana, unirehemu na kunisamehe.”
5. Wasamehe watu wengine wote. “Kwa uamuzi wangu mwenyewe,
nawasamehe bure wote waliowahi kuniumiza na kunikosea. Naweka mbali
nami uchungu wote na hasira na kinyongo.”(Sasa orodhesha dhambi zote na
kuungama).
6. Vunja uhusiano wako na mambo ya kishirikina na dini zote za
uongo. “Nakata mawasiliano yote niliyokuwa nayo na watu wanaojihusisha na
ushirikina au na dini za uongo. Nakataa kazi zote za Ibilisi, Shetani na pepo
wengine wachafu katika maisha yangu. Naungama na kukataa matendo yangu
yote ya kishirikina na dhambi kuwa ni machukizo mbele zako, Mungu
mtakatifu na mwenye haki. Nakataa kuathiriwa na laana kutoka kwa mababu
zangu.” (Sasa orodhesha dhambi zote na kuungama).
7. Jiandae kuwekwa huru mbali na kila laana katika maisha yako.
“Bwana Yesu, nakushukuru kwamba pale msalabani ulifanyika laana, ili
nikombolewe kutoka katika kila laana na kurithi baraka za Mungu. Nakataa
kila laana kutoka kwa mababu zangu. Na kwa msingi huo nakuomba uniweke
huru na kunipatia ukombozi.”
8. Simama na Bwana. “Nasimama na wewe Bwana, kinyume na pepo
wote wa Shetani. Najiweka mikononi mwako, Bwana, na ninampinga Ibilisi.
Amen!”
9. Toa pepo. “Sasa namkemea kila pepo aliye na utawala juu yangu
(wakemee moja kwa moja pepo hao). Nawaamuru mtoke katikati yangu sasa.
Katika Jina la Yesu, nawatoa! Naomba kwamba kila nguvu za giza zilizopo
katikati yangu, au zilizonionea au kunimiliki, ziharibiwe kabisa na kuondoka
kwangu. Najiweka mimi mwenyewe, mwili wangu, moyo wangu, nafsi yangu,
hisia zangu, na utu wangu kwa ujumla mikononi mwa Bwana Yesu Kristo awe
Bwana na Mwokozi wangu. Naomba haya katika Jina kuu la Yesu, nikiamini
kwamba nimekombolewa.”

No comments:

Post a Comment