Friday 5 December 2014

UIJILISTI NA MWINJILISTI


2 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
Je Wewe Ni Mwinjilisti?
Usomapo andiko hili utajiuliza wewe mwenyewe ikiwa
kama wewe ni mwinjilisti. Haya ni maswali machache
yakukusaidia katika sala yako ufanyayo ili kuweza kuamua
kama Mungu ndiye anayekuita kuwa mwinjilisti:
1. Je, nina uhakika Bwana amesema nami kwa kuniita au
katika roho yangu kwamba nina wito wa kuwa
mwinjilisti?
2. Je, ninahisi uzito wa maumivu na hali ya kukuza
matumaini iwapatayo watu waliotengana na Kristo?
3. Je, nina mawazo maishani mwangu kuhusu watu
wanaoishi bila Kristo?
4. Je, nina mwamko wa kuwaeleza watu wengine kuhusu
maisha ya Yesu Kristo, kifo chake na kufufuka kwake?
5. Je, nina njaa ya kusoma Neno la Mungu ili kupata
uelewa mpana wa Injili?
6. Je, mawazo ya wanaume na wanawake wanaoishi
umilele wa Jehanamu mbali na Mungu una madhara
makubwa kwangu?
7. Je, ninajisikia kuona kuwa ninahitaji kuhubiri wale
ambao bado hawajaokoka?
8. Je, nimekuwa na ndoto au maono ya kujikuta
ninawahubiri waliopotea na kunihimiza kutaka
kueneza Injili?
9. Je, ninaona maeneo yanayonihitaji mimi kutaka
kusaidia wengine ili kuwaleta kwa Yesu Kristo?
10. Je, ninajisikia kubeba mzigo wowote ninapokutana na
Wakristo wengine ambao hawataki kufikiri au kujali
habari za kuwafikia wasiokoka na ujumbe wa Yesu?
11. Je, kuonesha wengine njia ya kwenda kwa Yesu Kristo
ni kitu muhimu kwangu?
12. Je, nimeandaa mipango yoyote ya kuhubiri au
kushirikiana na wengine Habari Nzuri za wokovu
pekee wa Yesu Kristo?
Unaweza kuwa na majibu ya “Ndiyo” katika sehemu ya
maswali haya. Kama ndivyo ilivyo ni kuwa upo uwezekano
halisi kuwa Mungu anakuita katika kazi ya uinjilisti. Katika
gazeti hili utasoma kuhusu mambo yanayofuata:
• Mwinjilisti ni nani?
• Jadili tabia za kazi ya uinjilisti
• Gundua mwinjilisti na wale wenye wito wa uinjilisti
• Tia moyo, changamoto na fundisha mwinjilisti
• Saidia wachungaji kuwatambua na kuwatia moyo
wainjilisti, kusimama imara katika uinjilisti wao
wenyewe, na pia kusaidia kanisa likue kwa kuwa na
waumini wapya.
• Kutoa msaada wa kimatendo kwa kusaidia uinjilisti wa
viongozi na makanisa yao
MUHIMU
Andiko hili litazungumzia wainjilisti wote wawili,
mwanaume na mwanamke. Sasa na katika historia nzima,
ambao wamekuwa wanatumika katika nafasi ya uinjilisti na
pia wamekuwa wanapokea wito kwa Mungu kuwa wainjilisti.
Utangulizi Wa Mhariri:
Yesu aliwaambia wanafunzi Wake, “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe”
(Marko 16:15). Maandiko yanaonesha kuwa wote wanaomwamini Yesu Kristo wameitwa kushiriki Habari
Zake Njema na wengine (Mathayo 28:18-20; Matendo 1:8). Hata hao ambao wameitwa na kukirimiwa
kama wachungaji katika kanisa la mahali wanaangalizwa kuwa tayari kuhubiri katika nafasi mbalimbali
wanazokutana nazo (2 Timotheo 4:5).
Hata hivyo wapo wale ambao wameitwa kipekee na kuchaguliwa na Mungu kwa kipawa na huduma
kuwa “Wainjilisti” (Waefeso 4:11). Toleo hili la Gazeti la MATENDO litasaidia kueleza wito na kazi za
mwinjilisti kama Maandiko Matakatifu yasemavyo.
Mafundisho haya yatakuwa ya msaada kwa kiongozi yeyote wa kanisa au waumini wa Kristo, kwani
yana mikazo yenye kutia mtu nguvu, kufundisha na pia kukuwezesha wewe na wale unaowaongoza
kuwapata waliopotea ili waje kwa Yesu Kristo.
Sehemu Ya Kwanza
Mwinjilisti Ni
Nani?
Mwinjilisti Na Uinjilisti – Kupeleka Injili Duniani Kote!
NAKALA 14 – NAMBARI 1 –2006 MATENDO/ 3
Mwinjilisti Ni Nani?
Mwinjilisti ni mwanaume au mwanamke aliyechaguliwa
na Mungu kueneza Habari Njema (Injili) za
wokovu wa Yesu Kristo. Mwinjilisti ni mnenaji wa
Mungu. Mwinjilisti hueleza watu habari za Yesu Kristo,
Mwana wa Mungu, Mkombozi. Mwinjilisti huzungumza
kwa maneno habari za Kristo na shabaha ya maisha
Yake, kufa Kwake, na kufufuka.
Mwinjilisti, kwa maneno mengine huhubiri Injili.
Hakuna ujumbe mwingine mkubwa wa kuhubiri
“…Injili … ni uweza wa Mungu uletao wokovu”
(Warumi 1:16).
Habari za Yesu Kristo zimebeba mambo yafuatayo:
alivyokuja duniani; alivyoishi maisha adilifu, hakuwa
na dhambi katika maisha yake; alivyokufa msalabani;
alivyotoka kaburini; na pia anavyoishi milele.
Shabaha ya kifo cha Kristo ilikuwa ni kuchukuwa
hukumu ya Mungu kwa dhambi za watu wote, na pia
kuangamiza nguvu za dhambi. Yesu alishinda mauti
na pia alimshinda ibilisi na nguvu zote za uovu.
Maisha ya Yesu Kristo, kufa, na kufufuka kwake
kunaleta matumaini kwa watu wote na pia kuondoa
woga.
Kama wewe ni mwinjilisti, wewe ni mjumbe wa
Mungu mwenye habari muhimu kuliko habari zote
duniani!
Mwinjilisti Ni Yule Ambaye Ametumwa
Mwinjilisti ni mjumbe - mtu aliyetumwa kutoa
tangazo. Kama Yohana Mbatizaji, mwinjilisti
anamtangaza Yesu kwa watu. “Injili” ni neno lenye
maana “habari njema”. Kwa hiyo mwinjilisti anabeba
ujumbe wa habari njema kwa watu ambao wanataka
kuusikia. Ni habari bora kwa dunia nzima zinazohusu
kifo cha Yesu Msalabani na jinsi alivyojitoa kubeba
ghadhabu ya Mungu kwa ajili ya dhambi zetu na
kutupatia msamaha wa dhambi, na pia kutupa uzima wa
milele.
Yohana Mbatizaji alitumwa na Mungu Mto Yordani
katika jangwa (Mathayo 3:1-12; Yohana 1:6-8,19-34).
Mara nyingi mwinjilisti atatumwa kwenda mahali
ambapo watu hawajui au hawajawahi kusikia habari za
Yesu.
Neno “mwinjilisti” linamaanisha “mtu ambaye
ametumwa mwenye ujumbe”. Mungu aliwachagua
wainjilisti kwenda na ujumbe wa Yesu na kuwaambia
wengine. Uinjilisti ni kazi ngumu - ikiwa ni pamoja na
kulisoma Neno la Mungu, kujitoa dhabihu, kufanya
mipango, kujitia moyo, kusali, na kufunga.
Uinjilisti Ni Kipawa
Soma Waefeso 4:11-12 “Naye alitoa wengine kuwa
mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa
wainjilisti; na wengine kuwa wachungaji na waalimu;
kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya
huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe”.
Mistari hii inatuambia kuwa Yesu amejalia Kanisa
kipawa cha wainjilisti. Zawadi maana yake ni kupokea
kwa shukrani na kuikubali. Mara nyingine wainjilisti
hawakubaliki na wachungaji au na kanisa. Lakini wale
wanaokuja kwa Kristo kupitia katika kazi za mwinjilisti
hushukuru Mungu zaidi na zaidi kwa vipawa
alivyowapa - yeye aliyewaambia habari za Yesu na
kuwaambia namna ya kupata wokovu na maisha mapya
katika Kristo.
Uinjilisti ni mojawapo ya huduma kuu tano za
kiongozi-mtumishi alizotoa Kristo (Waefeso 4:11).
Mwinjilisti ni kipawa kwa Kanisa maana anawaleta
watu kwa Kristo. Watu waliookoka ukweli wanaenda
kanisani na kujifunza namna ya kumfuata na
kumtumikia Mungu.
Mwinjilisti pia ni kipawa kwa watu waliopo
duniani. Mwinjilisti anawaambia watu habari mpya za
maajabu ya Mwokozi Yesu, yeye aliyekufa na
kufufuka tena. Kwa njia ya kuhubiri Injili, watu
husikia namna ya kusameheka kwa dhambi zao na
kuupata uzima wa milele. Kuhubiri Injili ni kiini cha
huduma ya uinjilisti
Wajibu Au Ofisi
Kila huduma katika Waefeso 4:11 inakamilishwa na
watu ambao wameitwa kuifanya kazi ya Mungu.
Mwingine ni mchungaji, mwingine ni mwinjilisti, na
mwingine anaweza akawa mtume.
Baadhi ya watu wanafundisha kuwa vipawa
vilivyopo katika kifungu hiki (Waefeso 4:11) ni kama
ofisi au nafasi za mamlaka. Wanadai eti kipawa hiki
kinawapa wachungaji na wainjilisti ruhusa ya
kuwaamrisha wengine katika Kanisa.
Biblia haitufundishi hivyo. Uchungaji au uinjilisti
siyo kuwa na mfalme juu ya watu wa Mungu. Lakini
Biblia inaweka bayana kuwa mchungaji na mwinjilisti
ni viongozi ambao wanafundisha wengine, kama
Paulo alivyoandika, “kwa kusudi la kuwakamilisha
watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa
Kristo ujengwe” (Waefeso 4:12).
Njia ya Yesu Kristo katika huduma na pia mfano
Wake kwetu sisi ni kuhudumia wengine. “Kwa maana
Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali
kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi”
(Marko 10:45).
Viongozi Ni Watumishi
Yesu alikuwa na mawazo na matendo ya kiutumishi
(Wafilipi 2:4-12). Kuwa kiongozi wa kimungu katika
Kanisa, maana yake ni kuchukuwa njia ya Msalaba,
kutokuwa na tamaa na mipango ya binafsi (soma Luka
9:23; Wagalatia 5:16-25; Wafilipi 2:3-11). Viongozi
wanaofanana na Kristo huishi kama watumishi wa
Mungu kuwatumikia wengine, pamoja na unyenyekevu
wa kweli.
Wachungaji, wainjilisti, waalimu, mitume, na
manabii lazima waoneshe maisha yaliyotengwa ili
kuwatumikia watu. Huduma kuu tano ni kuwa viongoziwatumishi
- ambao wanatumikia wengine kama Yesu
alivyotumika.
4 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
Wito, Na Siyo Cheo
Huduma kuu tano zinazoorodheshwa katika Waefeso
sura ya 4 zinabeba matendo na kazi za hao walioitwa
na si vyeo. Wameitwa kuongoza na kuwafundisha
wafuasi wengine wa Kristo.
Kwa mfano, mchungaji atatunza waumini, kuwalisha
Neno la Mungu, na pia kuwashauri. Wachungaji
wanakirimiwa na kuitwa na Yesu kufanya hivyo.
Mchungaji atajibu kwa Mungu jinsi alivyotunza na
kufundisha ‘kondoo’ wa Mungu.
Mwinjilisti naye ana kazi. Wito wake na huduma
yake vilevile zinatoka kwa Yesu. Ni watu wake ambao
wamechaguliwa kuhubiri habari za Yesu Kristo na
Msalaba wa Yesu. Kila mtumishi-kiongozi awe wa kike
au wa kiume amekirimiwa katika huduma yake kwenye
eneo la huduma. Mchungaji anashughulika na matatizo
na pia mahusiano katika kanisa. Ni lazima ahakikishe
kuwa watu wanakua na pia wawe na afya zao za kiroho.
Anaweza kuwafundisha nidhamu, kama mchunga
kondoo anavyosaidia kundi lake. Hatatumia nafasi yake
vibaya ili kuwa na amri juu ya watu au kufaidika nao ili
atosheleze tamaa zake.
Kwa kawaida wainjilisti wamekirimiwa kuwa na
vipaji vya kupambanua roho na pia ujasiri wa kupingana
na mapepo na roho wabaya zenye kupinga kazi ya Injili
pale ambapo mwinjilisti ametumwa kuhubiri. Wana
uwezo wa kuhubiri Habari Njema kwa nguvu, pamoja
na ishara zitokazo mbinguni huwapa uhakika wa ujumbe
wao. Siku zote wainjilisti hutarajia mafanikio pale
wanapokuwa wanahubiri kwa usikivu kwa Mungu
kwani wanavyofanya hivyo wanakuwa wanafanya kazi
ya wito wao na pia wananena kweli ya Injili (Warumi
1:16).
Siyo Cheo
Watu wanaopenda cheo husisitiza kuheshimika kwa
vyeo vyao. Muda si mrefu wanadhani kuwa wao ni bora
zaidi ya wengine. Lakini Yesu alisema, “Basi, ye yote
ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo
ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni” (Mathayo
18:4). Soma zaidi kuhusu Yesu alivyosema kwa
wafanyakazi na wafuasi wake kuhusu kuwa na utumishi
mnyenyekevu katika Marko 9:33-35 na Yohana 13:3-15.
Wengi wanadhani kwamba kupata cheo kunawastahilisha
kuwaongoza wengine; lakini sivyo. Wengine
wanadhani ni lazima waoneshwe heshima kubwa kama
wana cheo cha “Uinjilisti”. Hata hivyo, wapo wanaume
na wanawake ambao wanampenda Yesu na pia
hushirikisha watu habari za Kristo katika miji na vijiji
vingi. Hawana cheo au kukubalika zaidi, walakini wao
ni wainjilisti wa kweli ambao wanafanya kazi
iliyotakiwa.
Paulo aliwaleta watu wengi Korintho kwa uwezo wa
kuelewa wokovu wa Yesu. Paulo aliwaambia kuwa wao
ni barua yake iliyokubalika. Kazi yake na wito wake
vilioneshwa na watu wengi ambao walimwamini Yesu
Kristo (soma 2 Wakorintho 2:14 - 3:3 na pia
1 Wathesalonike 2:19-20).
Nakala 14 / Nambari 1
TOLEO LA KISWAHILI
YALIYOMO
Mwinjilisti Na Uinjilisti -
Kupeleka Injili Duniani Kote!
Sehemu Ya Kwanza Mwinjilisti Ni Nani? ................... 2
Sehemu Ya Pili Msingi Wa Uinjilisti ....................... 8
Sehemu Ya Tatu Ujumbe Wa Mwinjilisti ................ 14
Sehemu Ya Nne Kazi Ya Mwinjilisti ...................... 17
Sehemu Ya Tano Mfano Wa Mwinjilisti Filipo ....... 19
Sehemu Ya Sita Ishara & Miujiza Na Mwinjilisti .. 22
Sehemu Ya Saba Kuhubiri Ujumbe Ulio Wazi
Wa Injili ........................................ 25
Sehemu Ya Nane Mungu Anavyomuandaa
Mwinjilisti ................................. 32
Wahariri: ...............................................Frank na Wendy Parrish
Wahariri Kimataifa: ................................................ Gayla Dease
Mfasiri wa Kiswahili: .............................................. Anna Makyao
Wahariri wa Kiswahili: .................. Sig Feser & Godson Loshetie
Mhakiki wa Kiswahili: ............................................. Ndelilio Nnko
Gharama za Posta zimelipwa
Chennai - 600 010 India
MAONO NA UTUME
WA GAZETI LA MATENDO
Kuwapatia bure mafundisho ya Bibliana mafunzo ya
huduma viongozi wa makanisa wa nchi za Asia, Afrika, na
Latini Amerika ambao wanafundisha au kuhubiri neon la
Mungu (Biblia) kwa kundi la watu 20 au zaidi angalau
mara moja kwa wiki.
MATENDO (ISSN 0744-1789) hutolewa mara nne kwa
mwaka na World MAP, 1419 North San Fernando Blvd.,
Burbank, CA 91504-4194, U.S.A. Gharama za Posta za
gazeti zimelipwa kule Arcadia, California na katika ofisi
nyingine za Posta. Maswali hupokelewa kwa anwani ya hapo
juu pamoja na Box 4142, Manila, Philippines; Box 942,
White River 1240, South Africa; Box 1037, Kilpauk,
Chennai, 600 010, India.
MKUU WA POSTA: Tafadhali utume mabadiliko ya
anwani kwa ACTS, World MAP, 1419 North San
Fernando Blvd., Burbank CA 91504-4194, U.S.A.
MATENDO ni gazeti linalotolewa bure, ambalo
huchapishwa na kutumwa kwa viongozi wa makanisa.
MATENDO
NAKALA 14 – NAMBARI 1 –2006 MATENDO/ 5
Waraka wa Yakobo unatufundisha kuonesha imani
yetu kwa kazi zetu, na siyo kwa maneno tu (Yakobo
2:14-20). Ni kosa kufikiri kuwa cheo pekee ndicho
kinachokufanya uwe mwinjilisti.
Huduma ambayo Yesu aliitoa siyo cheo. Utumishi ni
huduma. Inamaanisha kufanya kazi ngumu,
kuudhamini wito wako na pia kujitoa kwa Mungu.
Utumishi siyo kupokea cheo ili uheshimike mbele za
watu. Kazi inayofanywa na mwinjilisti ni kazi ya
kumpendeza Mungu na pia inaleta heshima mbele za
Mungu Mwenyewe.
Biblia inafundisha, “Mwingine na akusifu wala si
kinywa chako mwenyewe...” (Mithali 27:2). Acha watu
wakubali kipawa chako kwa kazi yako na matunda yako
na siyo wewe mwenyewe ujipe cheo.
Yesu alisema, “Utawatambua kwa matunda yao”
(Mathayo 7:16). Mchungaji anafahamika kwa utunzaji
na mafundisho yake mazuri kwa kondoo wake;
anaongoza na kulinda watu wa Mungu. Mwinjilisti
anafahamika kwa kuwaongoza watenda dhambi kuja
kwa Kristo na pia kuwaleta katika Kanisa.
Mojawapo Ya Karama Tano Za Uongozi
Uinjilisti ni kazi kubwa na nzuri ya wito. Lakini
hakuna mtu atakiwaye kujivuna kwa wito wake kwani
Yesu ndiye anayetoa kipawa hiki.
Uinjilisti ni mojawapo ya karama tano za uongozi
iliyopewa Kanisa, zikiwa na mpango maalum wa utendaji.
Wachungaji na waumini ni lazima wakubali mwinjilisti ni
kama zawadi, na pia waishi naye vizuri. Wainjilisti, kama
walivyo wachungaji, wapewe heshima na pia wawezeshwe
kifedha (1 Wakorintho 9:14; 1 Timotheo 5:17). Kwa
upande wake mwinjilisti anategemewa awe kiongozi na
kutumika katika nafasi ya uinjilisti.
Wakristo na viongozi ni lazima wakubali kuwa kila
Mkristo ni kiungo muhimu sana katika Mwili wa Kristo
(1 Wakorintho sura ya 12 & 14; Warumi 12:3-8). Kila
Mkristo ni muhimu na pia ana kazi ya kumfanyia
Mungu katika ulimwengu huu.
Ni vizuri kufikiria huduma kuu tano katika kanisa
(Waefeso 4:11-12) kama ni watu wanaofanya kazi kwa
bidii kuitimiliza kazi ya Mungu na mipango yake.
Wanatumika kwa kipawa maalumu maana wanamtii
Yesu. Wanafikia malengo maana wamechaguliwa na
Yesu. Ni vema kuwafikiria hawa viongozi, badala ya
ofisi zao na vyeo vyao na mamlaka yao kueleza wengine
ya kufanya.
Matunda Katika Utumishi
Wachungaji, waalimu, wainjilisti, mitume, na
manabii wanaofanya kazi kwa bidii kutimiliza wito wao
na pia kumfurahisha Mungu watalifanya Kanisa imara
na hai. Ni vizuri kutumika kwa uadilifu na moyo zaidi
badala ya kukumbatia vyeo na kuamini ubembelezaji wa
watu. Yakobo 3:16 anasema, “Maana hapo palipo wivu
na ugomvi, ndipo palipo machafuko, na kila tendo
baya”. Ni mpango wa Mungu kwa walio nao wito
miongoni mwa huduma kuu tano wafanye kazi
pamoja; kila mmoja kwa wito wake, na pia hupata
matunda kwa Mungu.
Tafuta kuzipata roho zinazopotea na pia fanya kazi
na watu wengine, na kila mtu ataelewa kuwa wewe ni
mwinjilisti wa kweli. Kazi yako itatoa ushuhuda wako.
Wachungaji Na Wainjilisti Wanatakiwa
Wasaidiane
Wachungaji na wainjilisti wana kazi tofauti na wana
wito tofauti, lakini wote ni wafanyakazi kwa pamoja
hapa duniani kwa Yesu Kristo. Wachungaji na wainjilisti
ni lazima wathaminiane na kuheshimiana kwa vipawa
vyao na pia wito wao. Wito wa mtu mmoja siyo bora
zaidi ya wito wa mwenzake; wote ni muhimu.
Wachungaji na wainjilisti wana kazi tofauti. Ni
lazima wajitahidi kusaidiana katika kazi ya Injili.
Wengine wamesema mchungaji ni kiongozi muhimu
zaidi katika Kanisa. Hii siyo kweli. Viongozi wote wa
Agano Jipya ni muhimu na pia wana thamani kwa
Mungu na kwa malengo Yake. Kumbuka Yesu
amewaita na kuupa ulimwengu wanawake na wanaume
wenye vipawa vya kiroho. Wakati Yesu akiwa hapa
duniani, alitumika kama mtume, mwinjilisti, mchungaji,
mwalimu, na pia nabii. Na sasa kazi hizo ameziacha
kwa wengine (Waefeso 4:11-12).
Mwinjilisti anamsaidia mchungaji kuwaleta Wakristo
wapya katika Kanisa. Kanisa linaongezeka. Mwinjilisti
anajua kuwa mchungaji atamfundisha muumini mpya na
kumsaidia kuwa imara katika Kristo. Mchungaji
anamsaidia mwinjilisti kwa kumwombea, kuwatia moyo
watu kumsaidia mwinjilisti katika kazi yake, na
kumsaidia kwa msaada wa fedha na mali.
Mchungaji na mwinjilisti ni watu wanaoishi pamoja
tena wanahitajiana tena wanapendana (Warumi 12:10;
Waefeso 4:1-6). Hakuna anayemwambia mwenzake
afanye nini; wote wapo chini ya mamlaka ya Mungu.
Wengine Ni Wachungaji–Wainjilisti
Maeneo mengi watu wanaokolewa kwa muda mfupi.
Wanatakiwa wafundishwe na wakue katika maisha yao
na Yesu. Mwinjilisti anayehubiri ujumbe wa Kristo na
kuwapata waumini anatakiwa kuwatunza hawa kondoo
katika kundi lake Mungu hadi mchungaji apatikane na
pia awatunze hawa waumini wapya.
Wapo wanaume na wanawake ambao “wana miito ya
aina mbili” - kuwaongoza watenda dhambi kwa Yesu na
pia kuwafundisha kama waumini wapya. Ni wito
waliojitia kuwafanya watu wawe waumini wa Kristo.
Unaweza ukawa wewe ni mchungaji ambaye una
wito wa uinjilisti. Kama saa zote wewe unatafuta
waliopotea kwa Yesu, unatunza yale mtume Paulo
aliosema kwa Timotheo kama mchungaji, “Fanya kazi
ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako” (2 Timotheo
4:5). Mungu amekuweka wewe hapo mahali ulipo ili
utunze kondoo, na pia unaweza ukafanya uinjilisti hapo
ulipo. Pengine Mungu anataka uanzishe kanisa lingine
katika mji au jiji lingine. Karama yako ya uinjilisti
itakusaidia kuwapata watu waokoke. Lakini angalia
6 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
usijaribu kuwafundisha wale ambao wana wito wa
wainjilisti wawe wachungaji.
Mwinjilisti Ni Mtaalamu
Mungu amezungumza na wanaume au wanawake
maalumu kuhubiri na pia kueleza ujumbe wa wokovu.
Mwinjilisti atasema “Ndio” kumtumikia Mungu katika
njia hii.
Kila Mkristo ameamriwa kushiriki imani yake katika
Yesu Kristo na wengine
(Mathayo 28:18-20; Marko
16:15; Luka 24:46-48;
Matendo 1:8). Kila Mkristo
anatakiwa kwa furaha aeleze
Kristo ni nani na
amemfanyia nini? Wakristo
wote wanatakiwa wawalete
wengine kwa Yesu Kristo!
Lakini mwinjilisti ana wito
maalumu katika kufanya hivyo.
Mwinjilisti amefundishwa na kuwezeshwa kuwavuta
waliopotea kuja kwa Yesu. Mwinjilisti akapewa wito wa
maisha kuvua wanaume na wanawake kwa Kristo Yesu.
Yesu alimwambia Petro “Njoni mnifuate, nami
nitawafanya kuwa wavuvi wa watu” (Marko 1:17).
Uinjilisti Ni Karama
Mungu amewapa wainjilisti karama na vifaa vya
kazi. Mwinjilisti atahubiri kwa mamlaka na nguvu kwa
kuwa ni sehemu ya kipawa chao toka kwa Mungu.
Miujiza hutokea wakati mwinjilisti anahudumu - lakini
ni Injili pekee na siyo miujiza inayookoa (Warumi 1:16;
1 Wakorintho 1:21-24).
Mungu anaweza kumfundisha mwinjilisti namna ya
kuhubiri ili watu waelewe Injili na kuiamini. Kama
wewe ni mwinjilisti, unaweza kumuuliza Mungu akupe
dhana na uelewa wa kuifanya kazi yako vizuri.
Mwinjilisti Ni Muhimu
Katika nchi yetu pasingekuwepo na Mkristo kama
hakuna mtu aliyekuja kuhubiri Injili. Mtume Tomaso
ndiye wa kwanza aliyesafiri kwenda nchi ya India
kueneza Habari Njema. Towashi wa Kushi katika
Matendo ya Mitume sura ya 8 alipeleka Injili Afrika.
Wainjilisti waliweza wakawepo maaskari wa Kirumi na
Wafanyabiashara waliopeleka habari za Yesu Ulaya na
Uingereza.
Watu waliopotea hawawezi kuokolewa pasipo
kufahamu habari za Injili ya wokovu katika Yesu Kristo
(Warumi 10:14-15).
Mwinjilisti Awezeshwe Na Atiwe Moyo
Mwinjilisti ni mtu, mwanaume na mwanamke,
aliyepewa ari ya kueneza ukweli wa wokovu kwa watu
wengi inavyowezekana. Hii inaweza kuleta ugumu kwa
mwinjilisti. Mara nyingi Mungu anatuma mwinjilisti
maeneo ya vijijini au maeneo ambayo Injili inapingwa.
Ibilisi anapingana na kazi ya mwinjilisti wa kweli.
Shetani anapinga uinjilisti kwa sababu anajua nguvu
kubwa ya Injili iwaokoavyo watu kutoka kuzimu,
inabadilisha maisha na kuwaweka huru kutoka dhambi
na nguvu za mapepo.
Mwinjilisti anaombea walio wagonjwa na wale
waliopagawa na pepo na kuwaweka huru. Mwinjilisti
anawaita watu watubu kutoka dhambi na kumtumikia
Mungu aishiye na wa kweli. Wainjilisti wanakwenda
mahali na kuwaleta wengine kwa Yesu na hivyo
kuwawezesha kuanzisha
kanisa.
Wachungaji na makanisa ni
muhimu wawathamini
wainjilisti na kuwawezesha
kufanya kazi yao kwa maombi
na kifedha. Hatutegemei watu
wasiookoka wamlipe
mwinjilisti kwa kuwaleta na
kufahamu Habari Njema ya
Yesu. Ni wajibu wa Wakristo
na makanisa kuwawezesha na kuwatia moyo wainjilisti.
Kanisa linahitaji wainjilisti!
Hata hivyo, kila mhudumu apende kufanya kazi ili
aweze kujisaidia mwenyewe. Mtume Paulo alifanya hivi
kwa kutengeneza mahema (Matendo 18:1-3; 20:34;
1 Wakorintho 4:12). Paulo anaeleza kuwa ni vema
kupokea msaada kutoka kwa wengine kama mhudumu
(1 Wakorintho 9:1-23). Lakini Paulo anasisitiza kuwa
hakutegemea hali hii, “Basi thawabu yangu ni nini? Ni
hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila gharama,
bali kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika
Injili” (1 Wakorintho 9:18). Mwinjilisti, na wahudumu
wote, watumie hekima na waongoze kwa Roho
Mtakatifu katika mambo haya, ili wasipate malalamiko
au changamoto kwa ajili yao au Injili ya Yesu Kristo.
Yesu Alihubiri Injili
Yesu aliposafiri kando kando ya miji ya Galilaya,
watu walikuja katoka maeneo mbalimbali ili waponywe
na kumsikiliza akihubiri na kufundisha.
“Simoni na wenziwe wakamfuata; nao walipomwona
wakamwambia, Watu wote wanakutafuta. Akawaambia,
Twendeni mahali pengine, mpaka vijiji vilivyo karibu,
nipate kuhubiri huko nako; maana kwa hiyo nalitokea”
(Marko 1:36-38).
Yesu alikuwa anahubiri nini? La msingi ni Injili!
Yesu alihubiri Habari Njema: “Hata baada ya Yohana
kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri
Habari Njema ya Mungu, akisema, Wakati umetimia, na
ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini
Injili” (Marko 1:14-15). Yesu alikuwa akihubiri kama
mwinjilisti!
Mwishoni mwa huduma ya Yesu, alikuwa
akifundisha watu na kuhubiri habari kwamba watu
watubu na kumwamini (Yesu) ili waokolewe “Ikawa
siku moja, alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni, na
kuihubiri habari njema, wakuu wa makuhani na
waandishi pamoja na wazee walimtokea ghafula”
Kazi ya kwanza ya
mwinjilisti ni kueleza
watu matendo ya ajabu
ya Yesu Kristo.
NAKALA 14 – NAMBARI 1 –2006 MATENDO/ 7
(Luka 20:1). Mstari huu
unaonesha kuwa Yesu
alikuwa akihubiri kwa
watu wasioamini karibu
na muda wake wa
kwenda Msalabani. Kwa
kuwa Yesu alihubiri Injili
tugundue kwamba
huduma ya uinjilisti ni
muhimu sana.
Mitume Walihubiri
Injili
Yesu alituma mitume
kupeleka Injili “Akaweka
watu kumi na wawili,
wapate kuwa pamoja
naye, na kwamba
awatume kuhubiri”
(Marko 3:14). Baadaye
Yesu aliwatuma 70 zaidi
kwa kazi hii ya
kuwaambia Habari
Njema (Luka 10:1,9).
Paulo Alihubiri
Injili
Safari za Mtume
Paulo zilimpeleka kwa
watu wengi ambao walikuwa hawajasikia habari za
Yesu. Katika safari yake ya pili, Paulo na kundi lake
walikwenda Makedonia kwa sababu ya ndoto aliyompa
Mungu (Matendo 16:9). Katika miji hiyo, alihubiri
kama mwinjilisti kwa watu wasio Wayahudi.
Baadaye, waumini walikusanyika pamoja na Paulo
aliwafundisha kama mchungaji. Kazi yake ya kwanza ni
kuhubiri Kristo kwa wote ambao hawakumjua. Baadaye
makanisa yalikua katika miji hii.
Paulo alikwenda katika miji ya karibu na alihubiri
tena kama mwinjilisti. Hata hivyo Paulo alimtuma
Timotheo, Tito au mtu mwingine katika kundi lake
kufundisha na kuwasaidia wafuasi wapya.
Katika Makedonia, Paulo alikwenda Filipi,
Thesalonike, Beroya, Athene na hatimaye Korintho
(angalia Matendo 16:9 - 18:7). Kila mara, jambo la
kwanza alihubiri kama mwinjilisti. Kitabu cha Matendo
ya Mitume kinaeleza kuwa Paulo alikaa Korintho kwa
miezi 18 kwa amri ya Bwana. Alitenda yote mawili ya
kuhubiri kama mwinjilisti na kufundisha na kuongoza
watu kama mchungaji.
Wanafunzi Wengi Walihubiri Injili
Mariamu Magdalene alitumwa na Yesu kama
mwinjilisti wa kwanza kuwaambia wanafunzi kuwa
amefufuka kutoka kwa wafu (Yohana 20:17-18). Filipo
aliitwa “mwinjilisti” (Matendo 21:8). Wengine
walifanya kama wainjilisti kabla ya kuwa wachungaji.
Petro alihubiri kama mwinjilisti siku ya Pentekoste
Safari za Mtume Paulo zilimkutanisha na watu wengi
ambao bado hawajamsikia Yesu.
(Matendo 2:14-36). Aliwahubiria watu ambao walijua
Mungu wa kweli lakini ambao walikuwa
hawajamwamini Yesu. Mahubiri yake katika Matendo ya
Mitume sura ya 2 yatatupa ukweli wa Yesu na maelezo
ya ukweli kuwa - wakati Yesu alipokufa, ilikuwa na
maana muhimu. Petro aliwaambia watu pia kuhusu
mambo ya kufanya, sasa wanapojua kazi ya Mungu kwa
njia ya Yesu Kristo (Matendo 2:37-39).
Waandishi wanne wa Injili katika Agano Jipya
wana ujumbe ulio wazi wa uinjilisti na makusudi
(Mathayo 28:18-20; Marko 1:1; Luka 1:1-4; Yohana
20:31; 1 Yohana 1:1-4). Mathayo, Marko, Luka, na
Yohana wanatimiza kazi ya uinjilisti kwa sababu
wameandika habari za Yesu ili kila mtu apate kusoma.
Wameandika vitabu vinne vya kwanza vya Agano
Jipya. Wanaeleza jinsi Yesu alivyoteswa,
alivyomwaga damu yake Msalabani, na kufa kwa ajili
ya dhambi za mwanadamu. Injili pia inauambia
ulimwengu jinsi Yesu alivyofufuka kutoka kaburini na
kushinda kifo.
Waandishi wa nyaraka za Agano Jipya wanatimiza
kazi ya uinjilisti. Paulo, Petro, Yakobo, Yohana, Yuda, na
mwandishi wa Kitabu cha Waebrania wanaeleza
umuhimu wa ukweli wa Injili. Kila mwinjilisti (na kila
mwamini) anapaswa ajifunze nyaraka na kupata
ufahamu wa kweli wa Habari Njema za wokovu katika
Yesu Kristo. Maandiko yana nguvu, yasiyo na makosa
na vyanzo muhimu ambavyo Mungu ametoa kwa kila
mtu. 􀂄
8 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
Sehemu Ya Pili
Msingi Wa Uinjilisti
Mwinjilisti Na Uinjilisti – Kupeleka Injili Duniani Kote!
Hii ni sehemu muhimu kwa wachungaji na wainjilisti
kuisoma. Hii itawasaidia katika kufundisha uinjilisti
kwa wengine.
Kila nyumba inahitaji msingi imara. Kama msingi
haujasimama wima, siyo imara, au umejengwa kwa
vifaa vibaya, nyumba inaweza kuanguka, hasa wakati
wa dhoruba (Mathayo 7:24-27). Habari za nyumba
mbili, uliyoelezwa na Yesu inafanyika kwa lolote
ufanyalo kwa Mungu. Huduma, familia, na maisha yako
binafsi lazima ujengwe katika msingi imara ambao
hautatia ufa na hautaoza. Ndiyo ilivyo kazi ya uinjilisti.
Uinjilisti haufahamiki vema kwa viongozi wengi wa
Kanisa. Wengine wanafikiria uinjilisti ni kuwa na
mkutano ya kanisa na kutegemea wasiookoka waje
kanisani na kuitikia Injili.
Wengine wanafanya makosa kwa kuwaambia watu
wafuate taratibu fulani za Kikristo, badala ya
kuwaonesha hitaji la kumpokea na kumfuata Kristo.
Kuwapata watu na kuwaingiza katika hali fulani na
kuwafanya kufuata taratibu zao siyo kuwaleta kwa
wokovu katika Kristo!
Kuwa Mkristo maana yake ni kuwa mmoja anayepokea
na kumfuata Kristo na kuwekwa katika uhusiano mzuri wa
Mungu Baba. Huokolewi kwa kujiunga na kanisa au
kufuata mapokeo ya kidini. Kuokolewa ni kupokea Yesu
aliyefufuka, kutoa maisha yako kwa Yesu, kumtegemea
Yeye na kazi Yake ya kutuokoa Msalabani, na kumfanya
Yeye kuwa Bwana na Mwokozi wako.
Ni lazima kuwakilisha ukweli wote wa Injili ya Yesu
Kristo. Hii ndiyo sababu ni vema kujifunza yale ambayo
Biblia inatufundisha kuhusu uinjilisti na ukweli wa ujumbe
wa Injili. Ujumbe wa uinjilisti usifanywe kuwa ni kitu
kigumu. Uwekwe wazi, uwekwe sawa na rahisi kueleweka
katika kuwakilisha Ukweli wa Yesu kama Maandiko
yasemavyo. Ni muhimu utolewe katika hali itakayomfanya
msikilizaji aelewe. Hii ndiyo kazi ya mwinjilisti.
Injili Ni Kuhusu Mtu – Yesu
Paulo anatoa ujumbe kwa Injili rahisi katika
1 Wakorintho 15:1-5: Yesu Kristo alikufa kama dhabihu
kwa dhambi zetu, alizikwa, na alifufuka toka kwa wafu
na kutupa wokovu na kufanya tuwe na uhusiano na
Mungu. Hii ndiyo Injili iokoayo.
Uinjilisti Ni Kutangaza Injili
Kuwashirikisha Injili maana yake kuwaambia
matendo makuu Yesu aliyotenda. Yesu anawapenda watu
sana hata akafa badala yao na kuchukua mwenyewe
adhabu ya dhambi zao. Wakati Yesu alipofufuka toka kwa
wafu, alishinda dhambi, kifo, kuzimu, na nguvu zote za
uovu. Hii ni habari njema kwa kila mtu dunia yote!
Mambo Yaoneshayo Uinjilisti
Kuelewa na kutumia maneno haya kutakusaidia
kuwakilisha Injili kwa njia iliyo wazi ili kila mtu apate
kuelewa mpango wa Mungu wa wokovu.
Upendo: Mungu anakupenda na alimtoa mwanaye
afe na kuchukua adhabu ya dhambi yako. Upendo wa
Mungu ni upendo wa milele, upendo usio na mipaka au
masharti. Mungu anakupenda pamoja na kuwa una
dhambi na unamchukiza. Hakuna kitu wala yeyote
awezaye kubadilisha upendo wa Mungu kwa ajili yako
(Yohana 3:16; Warumi 5:18; 8:31-39).
Kutubu: Ina maana kubadilisha mawazo,
inayotokana na kubadilisha kusudi na maamuzi. Hivyo,
kutubu ni kuamua kubadilisha dira/mwelekeo - kugeuka
kutoka ubaya na njia ya uovu na kumgeukia Mungu. Toba
si kusema tu samahani; inahusisha kubadili tabia
(Mathayo 3:8). Kutubu ni kukubali kuwa mwenye
dhambi na kuchagua njia ya Mungu badala ya njia zako
mwenyewe (Marko 1:15; Luka 7:44-49; Matendo 26:20).
Kusamehewa: Kila mtu amefanya dhambi na
anahitaji kusamehewa. Kila mmoja anahitaji kujua kuwa
aibu na hatia ya dhambi zinaweza kuondolewa.
Msamaha wa Mungu maana yake Mungu amekuondolea
mzigo wa lile baya lililokuumiza. Amechukua na
amesahau dhambi zako (Warumi 4:6-8; Waefeso 1:7).
Uzima Mpya (Uzima wa Milele): Yesu anatoa uhai
mpya kwa wote wanaomwamini. Unakuwa kiumbe kipya
(2 Wakorintho 5:17). Unapokea maisha mapya, msamaha
NAKALA 14 – NUMBARI 1 –2006 MATENDO/ 9
wa dhambi zako, amani ya moyo wako, upendo wa
Mungu kwa ajili yako na wengine, na kuishi maisha
mapya. Pia utaishi maisha ya milele na Yesu Kristo
mbinguni (Yohana 3:1-6; 10:27-29; 1 Yohana 5:11-12).
Uhusiano: Uhusiano kati ya Mungu na mtu
unawezekana kwa njia ya Yesu Kristo tu. Dhambi zetu
zinatutenga na Mungu Mtakatifu, lakini wakati
tunapokea dhabihu ya Kristo kwa ajili ya dhambi zetu
na msamaha wake, Mungu hatuhesabii tena dhambi
kinyume chetu (soma Warumi 4:4-8). Mungu
anatuhesabia “wenye haki” kwa sababu ya kazi ya
Kristo, na tunaweza kuwa na uhusiano na Mungu na
kumkaribia (Warumi 3:23-24; 5:18-19; 1 Wakorintho
1:30; 2 Wakorintho 5:21).
Wokovu na uhusiano wetu na Mungu hauji kwa
kutunza orodha za sheria “usifanye hiki” na “fanya
hivi”. Ni ukweli kuwa kama tutampenda Mungu,
tutatimiza amri zake (Yohana 14:15). Lakini kazi zetu
haziwezi kutuokoa (Waefeso 2:8-10).
Yesu alimfunua Mungu kwetu sisi kama Baba yetu
(Mathayo 6:9; Yohana 14:7-9). Tunaweza kumfahamu
Mungu na anaweza kutujua sisi (Yohana 17:3;
2 Timotheo 2:19). Ndiyo maisha ya Mkristo - siyo
matambiko matupu, kuishi kwa woga au kutenda mema
kiasi cha kukubaliwa na Mungu.
Kuamini: “Kuamini” ni kuweka tumaini, kuwa na
imani, kushawishiwa kabisa, kutegemea. Kuamini Yesu
ni kuweka tumaini lote kwake na kuwa mfuasi wake.
Hili si jambo la kukubali tu kiakili; ina maana kuyatoa
maisha yako kabisa kwa Yesu (Yohana 1:12). Kuamini
ni kushawishika kuwa utakiri kwa maneno imani yako
kwa Kristo (Warumi 10:9-10).
Kuzimu/Jehanum: Biblia inatoa maelezo ya ziwa la
moto lililopo kwa ajili ya Shetani na malaika zake
(Mathayo 25:41). Yesu alisema kuwa kuzimu kuna “giza
la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”
(Mathayo 8:12).
Wote wanaomkataa Yesu Kristo na kazi zake palepale
wanaamua kutenda dhambi na kufuata njia zao. Mbaya
zaidi, watamfuata Shetani mpaka mahali pa adhabu ya
milele, kuzimu/Jehanum. Mungu hakukusudia hili kwa
watu wake na si kusudi lake yeyote aangamie na
kuteseka milele (1 Timotheo 2:4; 2 Petro 3:9). Lakini
kila mtu ni lazima achague Yesu kuwa mwokozi wake
na kuishi na Mungu au kuteseka milele na kutengwa na
Mungu huko kuzimu.
Mambo Manne Ya Msingi Wa Injili
Injili ina mambo makubwa manne. Wakati wowote
unapohubiri ujumbe, au unapomshirikisha mwingine,
kuandika barua, au kuzungumza na kundi la wanaume
au wanawake, ujumbe muhimu unafanana.
Mambo haya ni: Mpango wa Mungu - Kuasi kwa
Mwanadamu - Kazi ya Yesu ya Kutokoa – Itikio la
Mwanadamu. Jifunze Maandiko yaliyoko chini ili
upate kujifunza zaidi katika kila jambo. [Wachungaji:
Uwafundishe watu wa kanisa lako ili waweze kuwashirikisha
wengine Injili!]
1. Mpango wa Mungu
• Mungu anakupenda (Yohana 3:16; Warumi
8:35-39)
• Mungu amekusudia kukupa maisha tele ya milele
na kuwa na faragha naye (Yohana 10:10; Ufunuo
3:20)
• Mungu amekusudia mema kwa ajili ya maisha
yako (Yeremia 29:11; Warumi 8:28)
• Mungu amekusudia wewe umfahamu (Yohana
7:3)
2. Dhambi ya Mwanadamu
• Dhambi ni uasi dhidi ya Mungu na njia zake
(Yohana 3:19-20; Warumi 5:10)
• Dhambi inatutenga na Mungu (Waefeso 2:12;
4:18)
• Kila mtu ametenda dhambi, imeleta maumivu
makubwa, mateso na kifo katika ulimwengu
(Warumi 3:23; 5:12)
• Haki ya kweli ya Mungu inaleta hukumu kwa
dhambi ya Mwanadamu (Warumi 6:23)
3. Kazi ya Yesu Kristo ya Kutuokoa
• Yesu alikufa Msalabani badala yetu kutulipia
gharama ya dhambi zetu (Wakolosai 2:13-15;
1 Petro 2:24)
• Yesu aliweka njia pekee kwa ajili yetu ili tuweze
kumrudia Mungu (Yohana 14:1-6; Matendo 4:12)
• Yesu alishinda dhambi na kifo na alifufuka toka
kwa wafu (Warumi 1:3-4, 1 Wakorintho 15:20-23)
• Yesu anatupa msamaha wa dhambi, anatupa
amani, upendo, na maisha mapya (Yohana 10:10;
Warumi 5:1)
• Yesu anaishi leo kama Mfalme wa wafalme
(Ufunuo 1:17-18; 19:16)
4. Itikio la Mwanadamu
• Ni lazima niitike lile ambalo Yesu amesema na
kufanya (2 Wakorintho 6:1-2)
• Nikubali dhabihu ya Kristo kwa ajili yangu na
dhambi yangu (Matendo 2:37-41; 16:30-34)
• Nimwambie Yesu anisamehe dhambi zangu na
awe Bwana na Mwokozi wangu (Yohana 3:15-16;
Waefeso 1:7)
• Nigeuke kutoka maisha ya dhambi na kuishi kwa
Neno la Mungu na mpango wake (Warumi sura ya
6; Waefeso 4:17-32)
• Nimfuate Kristo kila siku (Luka 9:23-26;
1 Yohana 1:7)
• Niwashirikishe wengine imani yangu kwa Yesu
(Mathayo 28:19; Marko 16:15)
Kutoa ujumbe mzuri wa Injili – kwa kutumia mambo
haya manne - inaweza kuwa hivi:
“Kuna mmoja mwenye nguvu kuliko wote, Mungu,
ambaye ameumba ulimwengu wote. Yeye ni mkamilifu
mtakatifu na wa haki; mkubwa kuliko chochote au
yeyote. Hakuna kinachoweza kulinganishwa na ukubwa
10 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
na nguvu za Mungu mwenye enzi. Mungu huyu
anakupenda. Amekuumba ili uwe naye. Amekusudia
kuwa na uhusiano na wewe.
“Lakini kuna jambo ambalo limetokea kati yetu na
Mungu. Kuna jambo linakuzuia usiwe na uhusiano na
Mungu na kujua upendo wake na kusudi lake kwa ajili
yako katika maisha haya. Hili linaitwa dhambi. Dhambi
imekuja kati yako na Mungu. Dhambi inaleta shida
nyingi na matatizo katika ulimwengu. Dhambi ni kama
kusema uongo, kudanganya, chuki, kuiba, mawazo
mabaya, mauaji. Biblia inatuambia kuwa moyo wa kila
mwanadamu umejaa dhambi (Yeremia 17:9). Tangu
Adamu na Hawa (Eva)
(wanadamu wa kwanza)
hawakumtii Mungu katika
bustani ya Edeni, kila mtu
amezaliwa na asili ya
dhambi (Zaburi 51:5).
Dhambi ni kama ukuta,
unaokufanya ujitenge na
Mungu. Kwa sababu ya
dhambi ya asili, tunataka
tuishi tutakavyo kuliko
kuishi katika njia ya
Mungu. Watu wote
wamefanya dhambi
(1 Wafalme 8:46; Warumi
3:23). Haki ya Mungu
iliyo timilifu inataka
tuadhibiwe kwa dhambi
zetu.
“Mungu anajua tu wafu
ndani yetu kwa sababu ya
dhambi zetu (Waefeso 2:1;
Wakolosai 2:13).
Amemtuma mwanaye,
Yesu Kristo, achukue
adhabu tuliyopaswa sisi
kwa ajili ya dhambi zetu
na afe badala yetu
Msalabani. Yesu alivunja
ukuta wa dhambi na
kufanya njia yetu ya
kumrudia Mungu. Yesu
alifufuka toka wafu
kuonesha kuwa Yesu ni
Mungu (Warumi 1:4).
Yesu Kristo anaishi milele
kama Mfalme aliye Mkuu
kuliko mfalme yeyote
yule.
“Unaweza kuamini kuwa hii ni kweli kwa kukubali
dhabihu ya Kristo. Unaweza kukubali kuwa wewe ni
mwenye dhambi, mwambie Mungu kuwa najutia
makosa yangu, na kupokea msamaha wa Kristo, na
kuishi kwa amani na Mungu. Uchaguzi ni wako
mwenyewe: Mwamini Kristo na kupokea msamaha,
au kuendelea katika dhambi zako na kuishi katika
uharibifu sasa na hata milele. Je, unachagua
kumwamini Yesu Kristo?”
Kuna njia nyingi za kuzungumza juu ya mambo haya
manne. Kuelezea mambo haya manne ya Injili kutakuwa
rahisi unavyojizoesha kufanya mara kwa mara. Unaweza
kuanza kwa kuyasema kwa sauti mwenyewe; baadaye
jizoeze na Wakristo wenzako; na hatimaye anza
kuwaelezea wasioamini.
Jozi Katika Kupeleka Injili
Hapa kuna “jozi” ambayo inafanya kazi pamoja
wakati wa kupeleka Injili. Jifunze kuitumia; itakusaidia
katika kushirikisha Injili
wazi na kuwaongoza watu
katika kumkubali Kristo.
Jozi Ya Kwanza -
Habari Zako
Mwenyewe & Neno
La Mungu
Waeleze habari zako
au shuhuda au jinsi
ulivyoanza kuamini Yesu
inasaidia watu kumwona
Mungu na kwamba
anapenda kuwasaidia wao
binafsi pia. Ni vema kutoa
neno la shukrani na
kuwaambia wengine
mambo ambayo Mungu
amekutendea (Luka 8:39).
Wakati mwingine
inasaidia unapowaambia
habari za watu wengine.
Ushuhuda wa mambo
ayatendayo Mungu
kugeuza maisha ya watu
ni ushuhuda wenye nguvu
kuhusu uwezo wa Kristo
kubadilisha maisha ya
mtu.
Ushuhuda mzuri una
maeneo matatu:
1) Maisha yangu
yalikuwaje kabla ya mimi
kukutana na Yesu?
2) Ilikuwaje
nikakutana na Yesu (ni
mazingira yapi
yaliyonileta kwa Kristo)?
3) Maisha yangu yana tofauti gani tangu nikutane na
Yesu?
Kama utajibu maswali haya matatu utatoa ushuhuda
mzuri unapozungumza. Usiwaambie kila kitu, lakini
chagua yale mambo muhimu. Usiweke mkazo sana
katika mambo mabaya uliyotenda zamani, lakini eleza
uzuri wa Yesu na jinsi alivyobadilisha maisha yako. Ni
vema ukaandika ushuhuda wako. Siyo lazima ushuhuda
Kuhadithia au kutoa ushuhuda wako
juu ya jinsi ulivyoweza kumuamini Yesu
Kristo kutasaidia watu waone kuwa
Mungu anajishughulisha nao pia.
NAKALA 14 – NUMBARI 1 –2006 MATENDO/ 11
wako ukawa mrefu
sana. Unaleta
mafanikio mazuri
kama utaelezwa kwa
habari fupi.
Neno la Biblia lina
uhai na lina nguvu.
Hakuna neno jingine
ambalo ni muhimu
zaidi. Washirikishe
maneno ya Biblia,
kwani Neno la Mungu
lina nguvu kuokoa
wenye dhambi:
“Kwa kuwa
nimezaliwa mara ya
pili; si kwa mbegu
iharibikayo, bali kwa
ile isiyoharibika; kwa
neno la Mungu lenye
uzima, lidumulo hata
milele…. Neno la
Bwana hudumu hata
milele. Na neno hili ni
neno lile jema lililohubiriwa
kwenu”
(1 Petro 1:23-25;
angalia pia Yakobo
1:18).
Biblia ndiyo zana
yetu muhimu. Shuhuda
zetu pia zaweza kuwa
zana muhimu. Tumia zana hizi mbili (jozi) pamoja
wakati unaposhuhudia Yesu au wakati wa kuhubiri.
Jozi Ya Pili – Neno & Roho
Wakati unaposhuhudia au kuhubiri kwa ajili ya
Kristo, tumia maneno ya Biblia. Katika baadhi ya
tamaduni, wana ufahamu mdogo wa elimu. Wanaweza
wakawa hawajui hata kusoma. Maneno uyatumiayo
yawe na mpaka na yawe marahisi. Kama ikilazimu, kwa
uangalifu, chukua neno la Mungu na kulifanya rahisi
kwa wengine kulielewa.
Kwa mfano, unaweza kusema, “Watu wote
wamefanya mambo mabaya na kutokumtii Mungu;
tunapaswa tuadhibiwe, lakini Mungu ametoa msamaha
kwa njia ya Kristo”. Hii ndiyo ukweli unaopatikana
katika Biblia katika Warumi 3:23 na Warumi 6:23,
kwamba umeweka katika maneno marahisi. Lakini uwe
mwangalifu sana usibadilishe kamwe maana ya yale
Biblia inasema.
Roho Mtakatifu ni sehemu ya pili ya jozi hii. Yeye
ameahidi kuwa atakusaidia kuelewa na kukumbuka yale
ambayo alifundisha Yesu (Yohana 14:26; 15:26; 16:13).
Ni Roho Mtakatifu anayemfanya mwenye dhambi
kushawishika na kuongoza wengi wamwamini Yesu
(Yohana 16:8). Pasipo kazi ya Roho Mtakatifu huwezi
kuwaleta watu katika wokovu.
Roho wa Mungu
ameahidi kutupa
uwezo wa kuwa
mashahidi (angalizi:
“Ujazwe na Roho
Mtakatifu” katika
Sehemu ya Saba). Ni
vema umwambie
Roho Mtakatifu akupe
nguvu na ujasiri.
Hubiri kwa kutumia
Neno la Mungu na
amini Roho Mtakatifu
kuleta moyo wa
kupokea. Ni mapenzi
ya Mungu kwa watu
wote waokolewe na
kujua ukweli
(1 Timotheo 2:4);
hivyo Mungu
atakusaidia!
Jozi Ya Tatu –
Maombi &
Maandalizi
Unaweza kupata
mafanikio makubwa
katika kuwaleta watu
kwa Yesu kwa kadri
utakavyokuwa
unawaombea wale
utakaowaendea kuwashirikisha
Injili. Ni muhimu kuwaombea watu na maeneo
ambayo utakwenda kuhubiri. Inawezekana Mungu
atakupa mzigo katika mawazo yako kwa mtu fulani.
Utapaswa kuomba mara kwa mara kwa ajili ya mtu huyu.
Unapaswa pia uwe na maandalio. Maandalio ni
pamoja na:
• kusoma na kujifunza Neno la Mungu
• andaa ujumbe (angalia Sehemu ya Saba katika
gazeti hili)
• jizoeze katika lile utakalosema
• tumia muda mwingi na Mungu katika maombi
Chukua muda na ujiulize, “Nichukue habari ipi ya
kumwendea mtu huyu au kikundi?” Kariri mistari katika
Biblia. Mwombe Yesu akuoneshe njia nzuri ya kuwashirikisha
watu wengine. Kama utachukua tahadhari
nzuri, Mungu atakusaidia ili watu wengi waje na
kumfahamu Kristo.
Jozi Ya Nne – Nenda Mkiwa Wawili
Wawili
Yesu aliona ni muhimu watumishi wake wasiende
mmoja mmoja, bali “wawili wawili”. Kama
unashuhudia katika maeneo ya barabarani, chukua mtu
mwingine atakayekuombea kimya kimya wakati
unazungumza. Hili ni jambo zuri. Kufanya wawili
wawili kunatoa nafasi ya kuelimisha wengine katika
Neno la Biblia ni hai na
lina nguvu.
12 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
kazi ya kushuhudia na uinjilisti. Mnaweza pia kutiana
moyo na kusaidiana.
Katika Nchi ya Afrika Kusini kuna wanaume vijana na
wanawake wanaompenda Yesu Kristo na wanafanya kazi
kila siku kuleta roho za watu kwa Yesu. Wengine ni
wanafunzi na wengine ni wafanyakazi. Hawafanyi kazi ya
uchungaji ya kanisa bali ni wavuvi wa roho za watu. Kila
juma wanatoka na kwenda barabarani au katika nyumba
kuwaambia wengine habari za Yesu. Wamejifunza
mambo manne ya kueneza Injili na wangeelewa zana
muhimu (hii jozi) za kutumia. Wanaomba na kujiandaa
wenyewe ili kuwashuhudia. Mwanamke analeta watu
wawili hadi wanne kila juma anapotembelea mjini wakati
wa chakula cha mchana na kuongea na watu.
Anawaongoza watu kwa Yesu na kuwaleta kanisani.
Haya Ni Mpaenzi Ya Mungu Kwa Kila Mkristo:
Uufahamu ujumbe wa Injili, ujue jinsi ya kupeleka
ujumbe na jinsi ya kuzungumza pasipo woga au aibu.
Kila Mkristo ni muhimu ajifunze jinsi ya kuwashirikisha
wengine Injili kwa njia bora ili upate mafanikio mengi.
Uwe Wazi Wakati Unapoongea
Biblia inasema, “Basi wamwiteje yeye
wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye
wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?”
(Warumi 10:14). Watu wanawezaje kuokolewa pasipo
kuelewa ujumbe wa neno?
Ni muhimu kujifunza jinsi ya kupeleka Injili kwa
njia iliyo rahisi na iliyo wazi ili watu waelewe uamuzi
ambao wanaitwa kuufanya na wauamini katika ukweli
wake. (Angalia Sehemu ya Tatu, Ujumbe Wa
Mwinjilisti.) Wakati mwingine maneno ya kidini
tunayotumia yanaeleweka kwetu, hata hivyo yanasikika
kama lugha mpya kwa mtu asiyeelewa. Epuka kutumia
maneno yasiyoeleweka kwa watu ambao hawana
ufahamu wa Kikristo.
Tumia maneno ya kawaida katika kueneza Injili.
Kama utatumia maneno ya Kikristo uwe na uhakika wa
kuyaelezea na mawazo ya Injili wasiyoyajua. Zaidi ya
hayo yote, hakikisha maneno uyatumiayo yanaeleza
ukweli wa Injili nzima.
Mifano
Vigumu
Kueleweka
“Ni muhimu uokolewe, jiachie kwa Yesu.”
“Haleluya, ndugu maisha ya milele ni kwa
ajili yako.”
“Nimeokolewa na kukombolewa.”
“Nilikuwa mwenye dhambi lakini sasa
nimeokolewa.”
“Ngoja nikuambie ushuhuda wangu.”
Rahisi
Kueleweka
“Unalo hitaji. Kristo alikufa kwa ajili yako
na kuchukua dhambi zako. Mpe maisha
yako.”
“Rafiki yangu, Yesu anataka uwe na maisha
- sasa na milele!”
“Yesu amechukua dhambi zangu na
kuniweka huru.”
“Maisha yangu yalitawaliwa na dhambi.
Baadaye nilikutana na Yesu na
akanisamehe dhambi zangu. Amenipa
maisha yanayonifanya nitake kuishi.”
“Ngoja nikuambie habari zangu jinsi
Yesu alivyoniokoa.”
NAKALA 14 – NUMBARI 1 –2006 MATENDO/ 13
Njia nzuri ya kufuata: Weka maneno yako kuwa
marahisi kueleweka bila kubadilisha ukweli wa Injili.
Njia ya pili: Jaribu kuelewa mazingira ya watu
unaotaka kuzungumza nao. Ukiwaelewa, itakuwa rahisi
kuzungumza nao.
Ni muhimu kwako –
kama mchungaji,
mwinjilisti, au kiongozi
wa kanisa - uelewe jinsi
ya kutoa ujumbe wa Injili.
Ni vema ukajua jinsi ya
kuwakilisha Injili kwa
wazi na kwa njia ya
ukamilifu. Mara unapojua
njia hii, unaweza
kuzungumza habari za
Yesu Kristo kila mahali,
na kwa kila mtu na kwa
njia itakayohitajika wakati
huo.
Mungu anatutaka tutoe
ukweli wa kazi, uhakika,
na kwa uangalifu
(2 Timotheo 2:15). Hii ina
maana zaidi kuliko kuelezea Biblia kwa Wakristo. Hii
ina maana pia tuweze kuleta Injili ya Yesu Kristo kwa
wanaume na wanawake wasiookoka.
Njia Za Kushirikisha Injili
1. Katika uhusiano: Mara nyingine hii inaitwa
“uinjilisti kirafiki”. Kuwa rafiki na mtu fulani. Upate
nafasi ya kumjua mtu huyo kabla ya kumshirikisha
habari za Yesu. Jenga daraja la kuaminika na
kutunzana. Mtu atakuwa tayari kufungua moyo wake
kusikia habari za Kristo kwa kadri unavyopenda na
kuishi maisha yako yawe mfano wa imani mbele ya
wengine.
Katika hali nyingine (kwa mfano, Waislamu), upate
ruhusa ya kuzungumza nao. Watu wanahitaji muda wa
kuona kuwa wewe ni mkweli na mwaminifu.
Njia hii ya uinjilisti inachukua muda. Huu ndio
mwenendo. Ina maana utahusika na maisha ya mtu huyu
na uangalizi wake na furaha, mahangaiko na matumaini
yake, familia na kazi yake.
2. Nafasi moja tu na kuzungumza: Njia hii ya
uinjilisti ni ya haraka na yenye nguvu. Ni kile ambacho
unaweza kushirikisha wakati unakaa katika gari moshi
au basi karibu na mtu, au wakati umekutana na mtu
kando ya barabara. Mara nyingi ni mtu mgeni ambaye
hujabahatika kukutana naye. Hii ni kama kukabiliana.
Waambie mambo manne ya Injili na kama pana
uwezekano muulize kama unaweza kuomba naye ili
ampokee Kristo. Wakati mwingine unaweza kumwachia
Biblia au kipande cha maandiko au tract (vipeperushi).
Unaweza kumwonesha upendo wa Mungu. Mwombe
Mungu akupe ujasiri wa kumshirikisha Injili wakati
ukiwa na nafasi.
3. Tendo la huduma: Hali ya upole au kujitoa
kunazungumza kwa ukubwa zaidi. Kufanya jambo la
kumsaidia mtu kunafungua moyo wa kusikiliza Injili
ya Yesu. Omba na angalia nafasi ya kumshirikisha
habari za Yesu kwa njia
hii. Hili ndilo ambalo
Mungu ametutendea.
Alionesha upendo wake
kwetu kwa kumtuma
Yesu kuja kwa ajili yetu
(Warumi 5:8).
4.Kutamka
hadharani: Aina hii ya
uinjilisti ni kuzungumza
katika mhadhara wa
watu. Wakati mwingine
unahitaji kuwakusanya
watu pamoja ili
uzungumze nao. Nyimbo,
waimbaji, wachezaji, au
tendo ambalo linaweza
kuwavuta watu, na
hatimaye kuwahubiria
habari njema za Yesu.
Huu siyo wakati wa kuhubiri mahubiri marefu. Utoe
Injili kwa muda wa dakika tano au sita. Watu
hawatangoja ili wakusikilize kama utahubiri muda
mrefu. Kumbuka huu si mkutano wa Kanisa! Una muda
mfupi tu kushirikisha habari iliyo muhimu kwa watu
wanaosikiliza. Huu ni muda wa kuwaita watu waombe
nawe ili kumpokea Yesu.
5. Tukio maalum: Kanisa lako na huduma inaweza
kukuwezesha katika tukio au wajibu wa kukusanya
watu. Makanisa mengi katika nchi mbalimbali
wamefanya hivi. Wamekuwa na tamasha la muziki, au
sikukuu, kualika wahubiri maalum, kutoa maigizo,
kuonesha sinema ya Injili, au tamasha la kwaya. Baadhi
ya makanisa wameandaa chakula na kualika wageni
ambao hawajaokoka.
Watu katika kanisa lako wanaweza kwenda kutoa
huduma katika shule au katika hospitali. Hii inaweza
kutoa nafasi ya kuwashirikisha Injili kwa kundi la
watu.
Unatakiwa uweze kuwafanya watu wajisikie
kukaribishwa na wasifungwe katika mipaka ya desturi
za kanisa fulani. Kama unataka kuwafanya wawe
waumini wa kanisa lako, wataweza kuona motisha wa
ubinafsi. Lakini kama unataka kuwatambulisha kwa
Mwokozi Yesu, watapenda kumpokea Kristo. (na
wanaweza kuja katika kanisa lako).
Kuna njia nyingi za kuwafikia watu. Mungu atakupa
hekima ya kujua jinsi ya kuwashirikisha wengine Injili
na kuwaelimisha wengine jinsi ya kufanya hivyo.
Jifunze na kumbuka mambo manne ya Injili. Hivyo
utaweza kufundisha wengine jinsi ya kuwashirikisha
habari za Yesu.
Mungu anatutaka tutoe
ukweli wa kazi, uhakika, na
kwa uangalifu (2 Timotheo
2:15). Hii ina maana zaidi
kuliko kuelezea Biblia kwa
Wakristo. Hii ina maana pia
tuweze kuleta Injili ya Yesu
Kristo kwa wanaume na
wanawake wasiookoka.
􀂄
14 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
Sehemu Ya Tatu
Ujumbe Wa
Mwinjilisti
Mwinjilisti Na Uinjilisti – Kupeleka Injili Duniani Kote!
Ujumbe Muhimu Wa Injili
Kuhubiri Injili ni kueneza habari ya Yesu. Ujumbe
wa mwinjilisti unahusika na maisha, kifo na kufufuka
kwa Yesu.
Kuwa na ufahamu wa ujumbe wa Maandiko ya Injili,
inakupasa usome na ujifunze kwa uangalifu vifungu
vifuatavyo vya Biblia.
Yesu Kristo Alitabiriwa
Mwanzo 3:15
Kumbukumbu 18:15
Zaburi 16:10; 22:1-31; 41:9
Isaya 7:14, 9:6-7; 53:1-12; sura ya 61
Zekaria 11:12-13
Kuja Kwa Yesu Kristo Na Ujumbe Wake
Mathayo 1:21; 7:13-14; 18:11
Marko 1:15; 10:27,45; 16:16
Luka 2:10-11; 9:56; 19:10; 23:33
Yohana 1:12-13; 3:16; 10:10,28; 14:1-7; 20:31
Matendo 2:17-39; 3:19; 4:12
Warumi 3:9-26; 5:1-21; 6:17-23; 8:1-11,15-17
1 Wakorintho 15:1-4
2 Wakorintho 5:18-21
Wagalatia 2:16; 3:13,21-26; 4:4-7; 5:16-24
Waefeso 1:1-14; 2:1-18
Wakolosai 1:13-14
1 Timotheo 2:5-6
1 Petro 1:1-5; 3:18
2 Petro 3:9
1 Yohana 4:9-10
Kurudi Kwa Yesu Kristo
Mathayo sura ya 24
Yohana 14:1-3
Matendo 1:10-11
1 Wathesalonike 4:15-18
2 Wathesalonike 2:1-2
Tito 2:13
Ufunuo wa Yohana 22:1-5,20
Kuhubiri vizuri kwa mwinjilisti ni lazima aeleze habari
za Yesu, kueleza jinsi Biblia isemavyo kuhusu Yesu, na
kuwaita watu ili watubu na kumwamini Yesu.
Soma Matendo sura ya 2. Hapa Petro alihubiri na watu
3,000 walimwamini Yesu Kristo. Petro aliwaambia ukweli
kuhusu Yesu na aliwaelezea watu. Hatimaye Petro
aliwaambia makutano waliosikiliza mambo ya kufanya
kwa kuwa sasa wamepata kuelewa ukweli. Aliwaambia
watubu na kumrudia Mungu na kuamini Yesu na kumfuata.
Hubiri Ukweli
Wewe pia unaweza kuwaona watu wakija kwa Yesu
Kristo; wakati unapohubiri ujumbe wa Injili ya Yesu. Kama
Paulo aandikavyo katika 1 Wakorintho 15:1-4: “Basi, ndugu
zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiria; ambayo ndiyo
mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama, na kwa hiyo
mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri;
isipokuwa mliamini bure. Kwa maana naliwatolea ninyi hapo
Kwa mwinjilisti na kuwaita
watu ili watubu na
kumwamini Yesu... Petro
aliwaambia makutano
waliosikiliza mambo ya
kufanya kwa kuwa sasa
wamepata kuelewa ukweli.
Aliwaambia watubu na
kumrudia Mungu na
kuamini Yesu na kumfuata.
NAKALA 14 – NAMBARI 1 –2006 MATENDO/ 15
mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo
alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;
na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama
yanenavyo maandiko”. Huu ni ujumbe rahisi: Yesu aliishi,
alikufa Msalabani, alizikwa na alifufuka kwa nguvu ya
Mungu (angalia Warumi 1:4).
Eleza Ukweli
Eleza kuwa Yesu alikuja ili kurudisha uhusiano wetu na
Mungu anayetupenda (Warumi 5:1; 2 Wakorintho 5:18-20;
Waefeso 2:11-18; 1 Yohana 4:9-10). Yesu alikuja ili
kutusamehe dhambi zetu (Waefeso 1:7; Wakolosai 1:13-14)
na kutuweka huru kutoka kongwa la dhambi (Warumi
6:17-23). Yesu Kristo alikuja kutupa maisha mapya na safi
(Waefeso 1:3-4; 2:10; Tito 2:13-14). Amemtuma Roho
Mtakatifu wake kutupa nguvu ya kuishi maisha ya haki na
kumpendeza Mungu (Warumi 8:1-11; Wagalatia 5:16-23).
Kwa sababu ya Yesu, tunawezeshwa kustahimili kama wana
wa Mungu Aishiye milele, tuwe warithi pamoja na Yesu
(Yohana 1:12-13; Warumi 8:15-17; Wagalatia 4:4-7). Na
siku moja, wajibu wetu tuliopewa duniani utakapotimilika,
tutakaa katika uwepo wa Mungu milele, kumfurahia Mungu
milele (Yohana 17:3; Ufunuo wa Yohana 22:1-5).
Mara Zote Uwaite Waitikie
Yesu anataka wanaume na wanawake kumwitikia Yeye.
Baada ya Yesu kumponya kipofu, Yesu alimtafuta na
kumtaka amwamini Yeye (Yohana 9:35-38). Katika Injili
ya Yohana mlango wa 4, Yesu alitumia muda kwa kuongea
na mwanamke Msamaria kisimani na kumwita amwamini
Yeye Mwenyewe - kama Mwana wa Mungu.
Mwinjilisti anapenda kuomba itikio la watu mara
upatapo nafasi (isipokuwa, labda kwa sababu maalumu
wanadhani wasingeweza kufanya). Watu wanahitaji
kuusikia ukweli wa Injili na hivyo wafanye jambo fulani
kwa lile walilolisikia.
Katika mji fulani nchini India, kikundi cha Injili
walitembelea gereza kila juma na kuwashirikisha Injili ya
Yesu, lakini hawakutoa nafasi kabisa ya watu kumpokea
Kristo. Mwishoni mwinjilisti mgeni alikuja na
kuzungumza habari za Kristo na kuwaambia watu
umuhimu wa wao kumpokea Kristo. Alisema, “Ni wangapi
kati yetu wanapenda kuomba nami kumpokea Yesu Kristo
kama Mungu wako na Bwana wako?” Wengi wa
wasikilizaji waliitikia na kumpokea Yesu.
Ni muhimu wakaonesha itikio lao wakati wanaposikia
Habari Njema kuhusu mambo ambayo Mungu amefanya
katika Yesu Kristo. Waambie watu jinsi ya kuitikia. Ni
lazima watubu dhambi zao; ni lazima wamrudie Mungu na
kumwomba awasamehe. Ni lazima wapokee kazi ya kafara
ya Kristo na kumkubali kuwa Bwana na Mwokozi wao.
Kumtaka Yesu awe ndani ya mioyo yao, ni muhimu
wakajitoa kumfuata Kristo aliye Bwana.
Ujumbe Wenye Nguvu
Ni muhimu kuamini kuwa Mungu ameagiza, anawapa
nguvu, na kubariki mahubiri ya Neno Lake kuhusu Yesu
(Isaya 55:10-11; Warumi 10:14-17; 1 Wathesalonike 2:13;
2 Timotheo 4:1-5). Amini hivi kwa sababu Yesu alisema
mbegu ya Neno huzaa mavuno na watu wataokolewa
(Marko 4:26-29).
Mungu anaeleza jinsi ujumbe wa neno kuhusu Kristo
ulivyo na nguvu: “Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa
mbegu, iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la
Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. Maana, mwili wote
ni kama majani, na fahari yake yote ni kama ua la majani.
Majani hukauka na ua lake huanguka; bali Neno la Bwana
hudumu milele. Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa
kwenu” (1 Petro 1:23-25; angalia pia Yakobo 1:18).
Ujumbe wa Injili ni habari yenye nguvu kubwa
katika dunia. Linaweza kubadilisha moyo wa mwanaume
au mwanamke; linaweza kubadili familia, mji, au taifa.
Unapohubiri na kushirikisha ujumbe wa Injili wenye
nguvu, unaweza kuvuna roho nyingi kwa Mungu.
Uinjilisti unafafanua kazi ya Yesu,
unaelezea ni nini maana yake kwa
watu leo hii.
Ujumbe wa
Injili ni
ujumbe wenye
habari nzuri
duniani.
􀂄
16 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
MASIMULIZI YA MAMBO YA WOKOVU
􀂄
msalabani - na kuchukua hukumu ya Mungu kwa
ajili ya dhambi zetu
• Aliharibu nguvu ya dhambi
• Alifufuka toka wafu kuonesha kuwa Yeye ni
Mungu
• Anaishi na kutawala milele kama Mfalme wa
wafalme
Jambo ambalo Yesu alilifanya ni kwa
ajili ya wanadamu wote. Kila mtu
amefanya dhambi na anahitaji
kuokolewa kutoka matokeo ya
dhambi zake. Hili linaweza
kufanyika wakati mtu anapoamini
kuwa Yesu Kristo alikuja na kufa
kwa ajili yetu na akafufuka toka
kwa wafu. Kila mtu ni lazima
atubu dhambi zake na kukubali
kafara ambayo Yesu alifanya
ili kutuokoa kutoka kifo.
Wanapofanya hivi, Mungu
anasamehe dhambi zao na
kuondoa adhabu ya kifo kwa
ajili yao. Kwa njia hii
wanaweza kuwa na uhusiano
na Mungu, aliye Baba yetu wa
mbinguni, sasa na mpaka milele.
Watu hawawezi kufanya mema wenyewe kiasi cha
kumrudia Mungu au kupata wokovu. Hata nguvu zetu
bora ni kama takataka ukilinganisha na utimilifu wa
Mungu. Hakuna njia nyingine ya kumjua Mungu
isipokuwa kukubali malipo ya Yesu aliyolipia madeni
yetu ya dhambi.
Tunapomwamini Kristo kama Mwokozi na Bwana
wetu, Roho wa Mungu anakuja katika maisha yetu. Roho
Mtakatifu anatusaidia ili tupate kumjua Mungu na
kufikiri, kuamini na kuishi katika njia ya Mungu. Kwa
kuwa Mungu anataka kila mtu aokolewe, Roho
Matakatifu anatupa nguvu ili tuwe na ujasiri wa kuwashirikisha
wengine Habari Njema za wokovu upatikanao
katika Yesu Kristo.
Mungu amejifunua Mwenyewe katika nafsi ya Yesu
Kristo. Pia amejifunua Mwenyewe katika njia na mpango
wa wokovu kwa ajili yetu katika Biblia. Biblia ni maneno
ya Mungu ambayo Mungu aliwafunulia watu kuandika
kwa kadri walivyoongozwa na Roho. Biblia
inatufundisha lile lililo kweli. Tunaweza kuliamini na
kulitumaini. Ni lazima tulisome na kujifunza Biblia mara
nyingi kwa kadri inavyowezekana.
Kila mtu atakufa kifo cha mwili. Lakini tunapoamini
Yesu Kristo na wokovu wake, tutakaa katika maisha ya
milele mbinguni na Mungu. Wale wote wanaokataa
mwaliko wa Mungu wa msamaha watatengwa na Mungu
na kuingia Kuzimuni.
Mungu ni wa milele - Yeye hana mwanzo wala
hana mwisho. Yeye ni Mungu Pekee wa kweli,
Mwenye enzi na Ajuaye kila kitu. Anao upendo
mkamilifu, ana huruma, ana samehe, mvumilivu, na
mpole. Mungu ni wa rehema; tena ni Mungu wa haki.
Mungu amejifunua mwenyewe kwetu kama Baba,
Mwana, na Roho Mtakatifu - ni nafsi tatu za Mungu
Mmoja.
Mungu aliumba mbingu na nchi. Katika mfano wake
aliwaumba Adamu na Hawa (Eva). Aliwaweka ili
watawale vilivyoko duniani, na kuwapa Bustani nzuri ya
Edeni kuishi. Mungu aliwaambia wazae na kuongezeka.
Mungu aliwapenda, aliwatembelea na kuzungumza nao.
Shetani alimjia Hawa na Adamu katika mfano wa
nyoka, na kuwashawishi
kuwa kuna mambo mengi
katika maisha kuliko yale
ambayo Mungu aliwajalia.
Huyu muongo, mwizi, na
mharibifu alileta changamoto
kwa Mungu na Neno lake, kama
alivyofanya wakati alipoleta uasi
mbinguni na akafukuzwa na wafuasi
wake. Shetani na mapepo yake bado
wanafanya kazi ya kuwajaribu watu
wamwache Mungu.
Adamu na Hawa wakachagua
kuasi agizo la Mungu la utunzaji
wake na kutokula katika mti ambao
matunda yake yangeweza kuwafanya kuona uovu.
Kutokutii kwao kulifanya dhambi iingie katika
wanadamu. Dhambi ni mawazo, maneno, na matendo
yaliyo kinyume na sheria ya Mungu na kusudi lake la
upendo kwa binadamu. Dhambi inaleta uharibifu na
maumivu kwa binadamu. Dhambi inatutenga na Mungu
na mpango wa Mungu wa maisha yetu sasa na hata
milele.
Haki ya Mungu iliyo kamilifu inatutaka tufahamu
matokeo ya dhambi, ambayo ni kifo – kimwili na kiroho.
Lakini Mungu, katika upendo wake mkamilifu, ameweka
mpango wa kumwokoa mwanadamu kutoka dhambi na
mauti na kutufanya tuwe na uhusiano kati ya Mungu na
mwanadamu ambao dhambi iliharibu.
Katika muda mwafaka katika historia ya
mwanadamu, Mungu alimtuma Mwana Wake wa pekee,
Yesu Kristo, kutimiliza mpango wake wa wokovu kwa
mwanadamu.
Yesu Kristo, alikuwa na ambaye ni Mungu:
• Alizaliwa na bikira, aliishi maisha yasiyo na
dhambi
• Alimfunua Mungu na mpango wake wa
kumwokoa mwanadamu
• Alitoa maisha yake badala ya mwanadamu - akafa
NAKALA 14 – NAMBARI 1 –2006 MATENDO/ 17
Sehemu Ya Nne
Kazi Ya
Mwinjilisti
Mwinjilisti Na Uinjilisti – Kupeleka Injili Duniani Kote!
Wajibu Wa Mwinjilisti
1) Kazi muhimu za mwinjilisti ni:
• kueleza habari za Yesu (Yesu ni nani na Amefanya
nini?)
• kuwaita watu watubu dhambi zao.
• kuwataka wamwamini Kristo
• kuwaambia watu wampokee Kristo kwani ndiyo
njia pekee ya kuwa na uhusiano na Mungu
Wainjilisti wa kweli wengi wanajisikia mzigo kwa
ajili ya giza la kiroho ambalo limewapofusha wanaume
na wanawake wanaowazunguka, na ambao wamepotea
na wanakwenda Kuzimu pasipo Kristo.
Wainjilisti hawajisikii kutosheka kwa kuhudhuria
kanisani. Wanafahamu kuwa Mungu huwatumia ili
kuwaokoa watu kutoka giza walilo nalo sasa, na kutoka
katika maisha ya kuzimu milele, ambayo yameandaliwa
kwa wale waliomkataa Kristo (Wagalatia 1:4; Wakolosai
1:13; 1 Wathesalonike 1:10).
Wainjilisti wanajisikia kusukumwa kuwaombea na
kuwataka watu waliopotea (wanaweza kuwa wa taifa la
mwinjilisti au kutoka maeneo mengine ya dunia). Tena
watakuwa na hamu kubwa kuwaendea watu hawa na
kuwaambia ukweli ili waokolewe. Watu wengine
wanaweza kuwakatisha tamaa wasiende, kuwatia woga
au changamoto nyingine. Lakini pamoja na hayo
wainjilisti watakwenda, kwa sababu wanajua kuwa
Mungu amezungumza nao na wanalazimika kutii. Hizi
ni baadhi ya ishara za wale walio na wito wa uinjilisti.
Mwinjilisti ni lazima ajifunze kuonesha matokeo ya
kuita watu wampokee Yesu na kuwasaidia waweze
kuweka maisha yao yote katika kumfuata Kristo. Ni
lazima ajifunze jinsi ya kutoa mwaliko wa Mungu kwa
watu waliopotea ili wapokee msamaha. Ni lazima
waweze kuwaongoza katika maombi ya kukiri dhambi
zao na kutaka Kristo awe Bwana wa maisha yao.
2) Mwinjilisti aelimishe wainjilisti wengine.
Wainjilisti wengi wameonesha mafanikio makubwa
katika huduma zao. Pamoja na hayo, wameshindwa
kupeleka elimu, ujuzi na uzoefu wao kwa wengine.
Mwinjilisti anaweza kuleta maelfu ya watu, hata
makumi ya maelfu kwa Kristo. Lakini wainjilisti
watakuwa hawajatimiza utume wao kama hawataweza
kuelimisha wainjilisti wapya.
Mpango wa Mungu mara zote kwa viongozi (ambao
ni pamoja na wainjilisti, wachungaji, waalimu, na
wengine) ni muhimu kuelimisha wengine na kuwainua
waweze kuendeleza kazi ya Mungu (Waefeso 4:11-12;
2 Timotheo 2:2). Kwa njia hii kazi ya huduma
inaongezeka kizazi hata kizazi.
Kama wewe ni mwinjilisti, ni yupi unamwinua
katika huduma ya uinjilisti? Ni nani atakufuata katika
kazi yako? Paulo anamwandikia Timotheo, “Na mambo
yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi,
hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa
kuwafundisha na wengine” (2 Timotheo 2:2). Kila
kiongozi anawiwa kufundisha kizazi kinachofuata na
kuwarithisha hekima na uzoefu wao. Hawa walioelimishwa,
wanaume na wanawake, ni muhimu
waelimishe wengine wawe wainjilisti pia.
Uzoefu wako una thamani kwa vijana. Mwongozo
Mwinjilisti anawaandaa wainjilisti
wengine.
18 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
wako, ufahamu wako, na ujuzi vinasaidia kuepuka
makosa na matatizo. Tumia muda wako kuelimisha
wainjilisti ambao Mungu amewaleta ili uwaelimishe.
Nenda nao katika huduma zako. Wape masomo ya
uinjilisti. Wafundishe toka Biblia. Waelimishe jinsi ya
kufanya huduma ya uinjilisti. Kwa njia hii Ufalme wa
Mungu unakua!
Kuna mtu huko Ulaya ambaye ni mchungaji na
mwinjilisti mwenye kazi nyingi. Ana kanisa lenye
waumini maelfu. Bado anatumia siku moja kila juma
kuelimisha watu 12 kwa ajili ya huduma ya Injili.
Anatumia masaa kuongea, kushauri, kusikia, na kuomba
pamoja nao. Anawapa kazi kumsaidia na hata kutoa
huduma, wakati anapowafundisha. Baada ya mwaka au
miaka miwili wanakuwa tayari, anawaacha wakafanye
huduma zao. Kila mmoja kati ya hawa 12 anaanza
kuelimisha 12 wengine. Baada ya miaka 2 tu watakuwa
wameelimishwa watu 144 ili kutumikia Mungu kama
viongozi wa Kikristo. Baada ya miaka miwili mingine
kutakuwa na watu 1728 ambao watakuwa
wameelimishwa na kuendelea! Na inaendelea hivyo.
Hii ndiyo njia ambayo Yesu aliwaelimisha wanafunzi
wake. Ni lazima utumie muda kukaa na wale wanaotaka
kuwa wainjilisti. Wachungaji, ni muhimu utafute
mwinjilisti mwenye uzoefu ambaye ataweza kuelimisha
wengine. Ni vema akawa ni mtumishi mwenzi na rafiki
wako. Wainjilisti wanaweza kuwa baraka kwa kanisa
lako na kwa Ufalme wa Mungu.
3) Mwinjilisti anafundisha waumini jinsi ya
kueneza Injili. Kazi ya tatu ya mwinjilisti ni kuelezea
yaliyoko kwa Waefeso 4:11-12: “Naye alitoa wengine
kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine
kuwa wainjilisti; na wengine kuwa wachungaji na
waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata
kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujenge”.
Elewa kuwa katika mistari hii viongozi wa Mungu,
ni pamoja na wainjilisti, wanafundisha watu katika
Mwili wa Kristo ili watende kazi ya kumtumikia Mungu
katika ulimwengu. Mwinjilisti anaitwa kufundisha na
kuandaa watu kwa kazi hii.
Uinjilisti ni kazi ya kila Mkristo. Mungu amewaita
wainjilisti watoe maisha yao ili kuwashirikisha wengine
Injili. Lakini kila muumini ajitahidi kuwaambia
wengine habari za Kristo na mambo aliowatendea. Ni
jambo linalohitajika kuwa kila Mkristo aelimishwe
kushirikisha imani yake kwa wengine.
Mwinjilisti anawafundisha wengine jinsi ya
kuwaleta watu kwa Yesu na jinsi ya kuwashirikisha
wengine imani ili watu wengi waje katika mpango
wa wokovu wa Yesu Kristo.
Hii ni kazi muhimu kwa mwinjilisti. Mwinjilisti
analeta mwamko wa imani na kuwafanya wengine
wapate hamu kutangaza habari za Kristo.
Kuwafundisha wengine jinsi ya kushirikisha imani
ya Kristo inasaidia wengi kukua na kuimarika. Imani
katika Kristo ni kuwashirikisha wengine. 􀂄
Ni lazima uchukue
muda na wale ambao
wanataka kujifunza
kuwa wainjilisti.
Hayo ndiyo Yesu
aliyofanya.
NAKALA 14 – NAMBARI 1 –2006 MATENDO/ 19
Sehemu Ya Tano
Mfano Wa
Mwinjilisti Filipo
Mwinjilisti Na Uinjilisti – Kupeleka Injili Duniani Kote!
Chukua dakika chache na usome mlango wa 8 wa
Kitabu cha Matendo ya Mitume. Utaelewa kuwa Filipo
alikuwa mtu wa Mungu na mwenye tabia njema. Ndiye
peke yake katika Biblia anaitwa “mhubiri wa Injili”, yaani
mwinjilisti (Matendo 21:8).
Mtu Aliyewatumikia Wengine
Mara ya kwanza tumesoma habari za Filipo katika
Matendo sura ya 6. Ni miongoni wa wahudumu saba waliochaguliwa
na kanisa la Yerusalemu kusaidia watu wenye
mahitaji mbalimbali. Filipo alianza kumtumikia Mungu kwa
kuwasaidia maskini na wajane. Alitumika kwa sababu kanisa
na viongozi walimtaka
afanye kazi hiyo. Filipo
hakukataa kufanya huduma
hii ya ushemasi kwa
sababu, labda, hakujifikiria
kuwa mkuu kuliko huduma
ya shemasi. Alikuwa tayari
kujinyenyekeza na
kutumika pamoja na
kujifunza.
Kama unataka Mungu
akubariki anzia pale
Mungu alipokuweka.
Biblia inaeleza kuwa
Filipo alikuwa miongoni
mwa wahudumu saba
waliokuwa na sifa nzuri
kwa ajili ya imani yao,
hekima zao, na nguvu za
kiroho katika Roho Mtakatifu (Matendo 6:1-6). Sifa hizo
nzuri za kiroho zilimstahilisha kuwapa wajane chakula
mezani!
Filipo alifanya kazi yake kwa bidii, akiwatimizia
mahitaji yao ya kimwili na ya kiroho pia. Tafuta kufanya
kazi kwa uangalifu katika kanisa au katika huduma
mahali ambapo Mungu amekuweka. Uwe macho sana
kuona mahitaji ya watu wanaokuzunguka. Watumikie
wanawake na wanaume ambao Mungu amekuweka juu
yao, kama Filipo alivyotumikia mitume, na viongozi wa
kanisa la Yerusalemu. Jitahidi kujituma mwenyewe na
kuwa mtumishi mwaminifu, na wakati unafanya hivi,
Mungu atakuongezea na kukupeleka maeneo mengine
katika wajibu mkubwa zaidi (Mathayo 25:21; Luka 16:10).
Filipo: Mtu wa Maombi
Katika Kitabu cha Matendo ya Mitume kinaeleza
kuwa Filipo alikwenda kaskazini mpaka Samaria. Kwa
nini Filipo aende mji mgeni? Biblia inatueleza kuwa
alikwenda kwa sababu ya mateso makubwa yaliyoanza
Yerusalemu. Filipo angeweza kutumia muda wake
kuomba na kumsikiliza
Mungu na kumtaka
Mungu amueleze mahali
atakapokwenda
kuhubiri. Filipo pia
angeliweza kuombea
waliokuwa wagonjwa
kwa sababu Biblia
inatuambia kuwa wengi
waliponywa.
Fikira Ya
Kimungu Kwa
Ajili Ya
Waliopotea
Filipo alijisikia
kutumwa na Mungu
kuhubiri Wasamaria.
Hawa walikuwa tofauti
kuliko Wayahudi ambao Filipo aliwafahamu. Filipo
alikwenda kwa watu wageni, ambao waliwachukia
Wayahudi, kuwaambia habari za Yesu. Filipo alikuwa na
mzigo kwa Wasamaria ambao hawakumjua Yesu.
Walimhitaji Kristo pia. Alikwenda kwa sababu Yesu
alimtuma. Alikwenda kuwaambia wengine habari za Yesu
Kristo. Alikwenda kwa sababu alijua fikira ya Mungu kwa
watu waliopotea. Kile ambacho Mungu alikijali, pia Filipo
alikijali. Filipo alianza kuwa na moyo uliofanana na ule wa
Filipo alienda kwa
watu wageni, wale
waliochukua watu
wake, kuwaambia
habari za Yesu.
20 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
Yesu, pengine kwa njia ya maombi na kumsikiliza Mungu
katika maombi. Lakini Filipo hakuomba tu; bali alifanya
kwa vitendo. Alikwenda kuhubiri.
Ujumbe Aliohubiri Filipo Ulikuwa Mrahisi
Wa Kueleweka
Injili yenyewe ni wazi, ujumbe wa kueleweka. Mungu
alituumba sisi na anatupenda sisi. Tumetengwa na Mungu
kwa sababu ya dhambi. Yesu, Mwana wa Mungu, alikuja
duniani katika hali ya mtu; alikufa Msalabani ili
tusamehewe dhambi zetu na kutuwezesha kumrudia
Mungu. Kristo alizikwa na alifufuka kutoka kwa wafu na
kaburi. Dhambi na nguvu za Shetani ziliharibiwa. Yesu
Kristo anaishi leo na ana nguvu zote. Yesu anakutaka
umwamini Yeye na kumpa maisha yako. Hukumu
inawangoja wale wote waliomkataa Mwana wa Mungu;
baraka zisizo na mwisho zipo kwa wale waliofuata Yesu.
Huu ni ujumbe wenye nguvu na ambao unafanya kazi
ya kugeuza watu. Unagusa mioyo migumu na unaleta
tumaini kwa wale walio gizani. Kuwaambia watu
inatakiwa wawe wazuri siyo Injili. Wanaume na
wanawake hawawezi kuwa wazuri wao wenyewe;
wanahitaji nguvu ya Yesu katika maisha yao ili waweze
kushinda uovu na kuishi katika haki.
Ni muhimu kuwaambia watu kuwa Yesu anayo nguvu
na anaweza kuondoa dhambi zao zote, aibu yao kwa ajili
ya dhambi zao. Yesu anaweza kufanya mtu mpya kutoka
mfanya dhambi (2 Wakorintho 5:17). Yeye anaweza kuleta
tumaini kwa waliokata tamaa na nguvu kwa walio
wadhaifu (Isaya 40:29; Warumi 15:13). Anaponya walio
wagonjwa na kutupa mahitaji yetu yote tunayohitaji katika
maisha yetu kwa ajili ya Mungu.
Injili ni ujumbe mzuri, uliojaa matumaini na ahadi!
Kama mwinjilisti mwema, Filipo alijua jinsi ya kuhubiri
ujumbe mwepesi ulioleta maana kwa wasikilizaji – na
wengi waliokolewa.
Filipo Alipewa Miujiza
Miujiza, ishara, na maajabu ni sehemu ya huduma ya
mwinjilisti. Biblia inatuambia kwamba miujiza mikubwa
ilifanyika wakati Filipo alipohubiri (Matendo 8:6-7,13).
Watu waliona miujiza na ishara zilizowafanya wavutiwe
kusikia maneno ya Filipo. “Na makutano kwa nia moja
wakasikiliza maneno yake yaliyosemwa na Filipo
walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya”
(Matendo 8:6).
Ishara ni matendo ambayo si ya kawaida kutoka kwa
Mungu yanayomfunua kuwa wa kweli na mwenye nguvu.
Ishara na miujiza imeahidiwa kwa kila amwaminiye
Kristo; wainjilisti kwa upekee wa mara nyingi wana ishara
na maajabu wakati wakihubiri Injili (soma Marko
16:15-18).
Siku za karibuni mwinjilisti alikuwa akihubiri katika
kijiji msituni. Aliwaambia watu kuwa Mungu amemtuma
kwao na ujumbe. Aliwaambia jinsi Yesu alivyoteswa na
kufa na kufufuka siku ya tatu; na kuwa Yesu anatoa
msamaha wa dhambi. Hatimaye mwinjilisti akasema, “Ili
kuwahakikishia niliyoyasema kwenu ni kweli,
tutawaombea watu wote wagonjwa, na nitamwomba Yesu
awaponye.” Alianza kuwaombea wagonjwa na wakapona.
Mchawi alitubu na alianguka ardhini wakati mapepo
yalipoamriwa kutoka katika Jina la Yesu. Watu walipoona
mambo haya, walimwamini Yesu. Zaidi ya watu ishirini
katika kijiji kile walimpokea Yesu Kristo siku hiyo!
Ipo mifano mingi ya ishara na miujiza. Katika Afrika,
katika kijiji cha Waislamu, kikundi cha wanawake
walipewa ruhusa ya kuwaambia watu habari za Injili.
Kulikuwa na ukame mkubwa kwa muda mrefu. Kila mara
mwinjilisti alipozungumza na mvua ikaanza kunyesha!
Kila mmoja katika kijiji, hata kiongozi wa kijiji, alikubali
kuwa Mungu alikuwa anatuma baraka kwa sababu mvua
inanyesha.
Wainjilisti wanatoa ujumbe wa Injili na miujiza
inatokea wakati wakiomba na kuzungumza. Yesu alisema,
“Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio...” (Marko
16:17).
Kama mwinjilisti, unaweza kumuomba Mungu
miujiza, na kuomba mpaka miujiza itokee. Ombea
wagonjwa katika jina la Yesu wakati unapohubiri na amini
kuwa Mungu atawaponya watu.
Hivyo miujiza na ishara nyingi zilifanyika Samaria na
mji mzima ukataharuki na kufahamu jambo hilo. Biblia
inatuambia kuwa mji wote ukajaa furaha (Matendo 8:8).
Mahali popote ambapo Injili inakwenda panakuwa na
furaha na shauku njema. Injili inapohubiriwa na
kuaminiwa, dhambi zinasamehewa na maisha mapya
yanapatikana; na hiyo ndiyo miujiza ya Mungu ikitenda
kazi! Mara nyingi, kuna mambo ya nyongeza kama
magonjwa yanapona, mapepo yanatolewa, na watu
wanafunguliwa na kufanywa upya. Injili ina nguvu!
Siyo muda mrefu uliopita, mwinjilisti alikuwa
anahubiri katika mji mmoja na mvulana mdogo ambaye
alikuwa kiziwi na bubu aliponywa wakati wakimwombea.
Ujumbe wa matumaini na ahadi ambao
Filipo alihubiri ulikuwa wazi na
mwepesi. Mungu ametuumba sisi na
anatupenda sisi... Kristo alikufa kwa
ajili yetu... Huu ni ujumbe mzito ambao
hufanya kazi ya kubadili watu.
NAKALA 14 – NAMBARI 1 –2006 MATENDO/ 21
Mama yake akaenda kwa
majirani, marafiki, na
familia na wote wakaona
kuwa aliweza kusikia na
alianza kuzungumza.
Usiku uliofuata watu
waliongezeka na mama
alisimama mbele na
kuwaambia watu jinsi
mtoto wake alivyoponywa.
Usiku ule watu wengi
waliyatoa maisha yao kwa
Yesu, pamoja na mama
yake yule mwana. Baada
ya ujumbe wa Injili,
Bwana Mungu anatoa
uponyaji wa aina nyingi.
Watu wengi waliamini kwa
sababu waliona jinsi mtoto
alivyoponywa, na kundi liliendelea kuongezeka kila
mara. Mamia ya watu waliokolewa kwa siku tatu. Ndivyo
ilivyotokea wakati Filipo alipokwenda Samaria!
Filipo Alikuwa Mwepesi Kutii
Yesu anajua mahali ambapo watu wako tayari kusikia
Injili. Alimtuma Filipo Samaria. Baadaye Yesu alimtuma
Filipo kutoka kazi ya uinjilisti yenye mafanikio makubwa
kwenda kuzungumza na mtu mmoja katikati ya jangwa.
Matendo 8:26: “Malaika wa Bwana akasema na Filipo,
akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia
ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni
jangwa.”
Mwinjilisti ni lazima atumie muda wake kuendelea
kujifunza kufahamu kusudi na mapenzi ya Mungu, na kutii
Mungu anapomwongoza. Mipango mizuri ingaliweza
kumhimiza Filipo akae Samaria, ambapo alikuwa amepata
mafanikio mazuri, na watu wengi walikuwa wakimpokea
Yesu Kristo. Lakini Mungu alizungumza na Filipo kwenda
na kuzungumza na mtu mmoja.
Tunaweza kujifunza jambo muhimu sana katika habari
hii. Ni lazima kumtii Mungu. Yeye anajua zaidi mipango
yake. Mungu alijua kuwa mtu wa Kushi aliyekutana na
Filipo angeamini na kuchukua ujumbe wa Injili katika
nchi yake katika Afrika. Alikuwa mtu mashuhuri (alikuwa
na mamlaka chini ya Kandake Malkia wa Kushi). Mtu
huyu mmoja alikuwa muhimu kwa Mungu. Kupelekewa
Injili ulikuwa ni mpango kamili. Mtu wa Kushi angeweza
kuongea na taifa, na Mungu alimtuma mwinjilisti
kuzungumza naye.
Mwinjilisti ni lazima awe mnyenyekevu, awe tayari
kuzungumza na mtu mmoja sawa na kuzungumza na kundi
kubwa. Azungumze na watu waliokataliwa, ambao
wanaonekana hawana umuhimu, hata kwa mtu mmoja.
Mtu mmoja ambaye hathaminiwi na watu wa dunia
anaweza kuwa muhimu sana mbele zake Mungu.
Inawezekana Mungu anachagua kiongozi mmoja ambaye
anaweza kushawishi watu wengi na Mungu anaweza
kukutumia kwake.
Utii amri ya Mungu
akikutuma kwenda na
kuhubiri hata wakati watu
wanazungumza mabaya
kuhusu wewe, au hata
wakati wewe binafsi
huelewi ni kwa nini. Mungu
amejaa hekima na uwezo na
anawabariki wote
Wainjilisti ni lazima
wawe watiifu katika wito
wao ambao Mungu
ameuweka maishani mwao
hata wakati ambao ni
mgumu au wakati
mwingine watu
hawaelewi. Kutii amri ya
Mungu ni muhimu mno
kwa mwinjilisti. Utii amri
ya Mungu akikutuma
kwenda na kuhubiri hata
wakati watu
wanazungumza mabaya
kuhusu wewe, au hata
wakati wewe binafsi
huelewi ni kwa nini.
Mungu amejaa hekima na
uwezo na anawabariki
wote wanaomtii.
Uwe Tayari Kwenda
Mwinjilisti ni lazima awe tayari kwenda mahali popote
ambapo Mungu anamtuma. Mungu anaweza kumtuma
mahali pageni na mahali papya. Mungu anaweza mara
nyingi hututuma kwa watu ambao hawatufanani.
Wasamaria walikuwa hawako sawa na Filipo.
Ingewezekana kuwa ni jambo geni na mahali ambapo
asingejisikia kupapenda yeye mwenyewe. Hata mtu wa
Kushi hakuwa sawa na Filipo. Lakini Filipo alikuwa tayari
kwenda mahali pale Mungu alipomwita. Mwinjilisti ni
lazima wawe tayari kujitoa mwenyewe na kwenda mahali
pale ambapo Mungu anawatuma.
Mwinjilisti mmoja ameeleza jinsi alivyokwenda vijiji
vingi kuhubiri Injili. Katika baadhi ya vijiji alipigwa;
mahali pengine alifungiwa nje ya nyumba. Lakini hata
hivyo alikwenda. Watu wengi walichagua kumwamini
Yesu. Angesema nini kwa Yesu kama hakuwa amekwenda
katika vijiji na watu wangekuwa hawajasikiliza ujumbe?
Watu wengi katika dunia wanaangamia bila kufahamu
habari za Mungu kwa sababu hakuna mtu wa kuwapelekea
Habari Njema za Yesu.
Mwinjilisti huyo alimsifu Bwana kwani Mungu
alimkubali afikwe na mateso kwa ajili ya Yesu - na alimsifu
Mungu kwani wengi watakuwa mbinguni!
Mateso, kukataliwa, maisha magumu, na uovu kama
itikio la watu ni sehemu ya wito wa mwinjilisti. Kila
mwamini ni lazima akutane na mateso wakati anapotaka
kuishi maisha ya kumpendeza Mungu ya kumtii
(2 Timotheo 3:12). Lakini Mungu atakusaidia, atakulinda
na kukuongoza, na kukupa utoshelevu na tuzo katikati ya
mateso na maisha magumu.
Filipo alikuwa na mafanikio ya kweli.
Kwa sababu Filipo alimtii Mungu na alihubiri Injili
kamili, watu wengi waliokolewa. Kila Mkristo ni lazima
amtii Mungu. Usiangalie tu mafanikio mbele ya macho
ya watu; badala yake kila mara jaribu kumfurahisha
Mungu. 􀂄
22 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
Sehemu Ya Sita
Ishara & Maajabu
Na Mwinjilisti
Mwinjilisti Na Uinjilisti – Kupeleka Injili Duniani Kote!
Sababu Za Kumuuliza Mungu Akupe
Ishara Na Miujiza
1. Yesu aliwaahidi wote wamwaminio (Marko
16:17-20; 1 Wakorintho 12:8-11; 13:2-8).
2. Yesu alisema wote wamwaminio watapewa
kufanya mambo makubwa kuliko alivyofanya (Yohana
14:12-13).
3. Kristo aliondoa kazi zote za giza na mapepo
katika Msalaba (Wakolosai 2:15). Aliwapa waaminio
mamlaka juu ya nguvu za giza (Marko 16:17; Yohana
14:12-13). Wakati mwinjilisti anapotumia mamlaka ya
Kristo kutoa mapepo, nguvu za mapepo zinazomtawala
mtu zinavunjika na mtu anafunguliwa. Watu wengi
wamefungwa na nguvu za mapepo na wanahitaji
kuwekwa huru kwa nguvu za Yesu. Wale wote
wanaojikuta katika nguvu za mapepo wanapaswa kujua
kuwa kama Mkristo, hawako chini ya nguvu za giza na
hawapaswi kuishi kwa hofu.
4. Ishara na miujiza inaonesha nguvu ya kweli na
mamlaka ya Yesu Kristo.
5. Ishara na miujiza inasaidia kuifanya Injili iwe na
nguvu pale inapohubiriwa.
6. Paulo aliona miujiza mingi wakati wa huduma
yake (Warumi 15:18-19; 2 Wakorintho 12:12), kama
alivyofanya Filipo. Petro naye aliona miujiza ikifanyika
wakati alipokuwa anahubiri habari za Yesu. Wainjilisti
wengi na wahudumu wa Neno mahali pote duniani
nyakati zote hata siku hizi wanaona Mungu akitenda
miujiza wakati wanapoombea watu. Kama mwanafunzi
na mhudumu wa Kristo, ni vema ukafahamu na kuamini
Mungu kwa ishara na miujiza kama sehemu mojawapo
ya huduma.
Miujiza Yaweza Kuleta Matatizo
Miujiza inawafanya watu wawe na sababu ya
kufurahia na kuamini Injili. Yohana 20:30-31 inaeleza,
“Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu
mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu
hiki. Lakini hizi zimeandikwa; ili mpate kuamini ya
kwamba Yesu ndiye Kristo, mwana wa Mungu; na kwa
kuamini mwe na uzima kwa jina lake.”
Lakini miujiza inayofanywa kwa jina la Yesu
inaweza isilete kila mara itikio lenye mwelekeo mwema.
Yesu alipingwa wakati alipokuwa akifanya miujiza
(Mathayo 12:9-14). Paulo alikutana na shida nyingi
wakati akihubiri Injili na miujiza ikatokea (soma
Matendo 19:9-12,23-41). Shetani anapinga Injili na kila
kitu ambacho kinamtukuza Yesu aliyefufuka; watu
ambao hawajakombolewa hufanya hivyo pia.
Omba na kutaka ulinzi wa Mungu. Mungu
atakusaidia kila mara unapohubiri na kuwaombea
wagonjwa na kukabiliana na mapepo. Kila mara
msikilize Roho Mtakatifu na fanya kwa hakika lile
ambalo Roho Mtakatifu anakueleza ufanye. Usijaribu
kufanya kama watu wengine wafanyavyo au mitindo ya
huduma za wengine. Wewe huna huduma zao. Wewe
una huduma ambayo Mungu amekupa, na inaweza kuwa
na nguvu kwa njia ya Kristo. Fanya kwa imani lile
ambalo Bwana anakuonesha.
Jinsi Ya Kuanza Kuona Miujiza
Moja: Mtii Mungu. Hubiri Injili pale ambapo
Mungu amekutuma. Waambie watu kuwa Yesu anaweza
kuwaponya na wawekee mikono na kuwaombea katika
jina la Yesu; wapake mafuta walio wagonjwa, kulingana
na Maandiko Matakatifu (Marko 6:13; Yakobo 5:14).
Kumbuka, si wewe au karama yako inayowaponesha
watu. Ni nguvu ya Mungu inayoponesha wakati unatii
kuongozwa na Roho Mtakatifu.
Mbili: Neno la Mungu lina nguvu na li hai
(Waebrania 4:12) na linabebwa na mamlaka ya Mungu.
Kariri mistari au milango kadha ya Biblia mara nyingi
kama sehemu ya tabia yako ya Kikristo. Hatimaye,
wakati unapowaombea wengine, nukuu mistari ya
Maandiko ambayo Roho Mtakatifu anaileta katika
mawazo yako.
NAKALA 14 – NAMBARI 1 –2006 MATENDO/ 23
Kwa mfano, kama unamwombea mtu aliye mgonjwa,
unaweza kusema, “Yesu, Neno Lako linatuambia kuwa,
maombi ya imani yataokoa walio wagonjwa, na Bwana
utawainua wewe. Hivyo, sasa hivi, tunakubali maneno
yako na tunakutaka wewe umponye na kumuinua mtu
huyu!” Kuna nguvu wakati Neno la Mungu linapozungumzwa.
Tatu: Uwe na imani katika Yesu Kristo kwamba
Yeye ndiye ambaye Biblia inasema wazi kuwa ni Yeye
Mwenye mamlaka YOTE, na nguvu ZOTE! Wakati
tunatembea katika utii wa kuongozwa na Roho
Mtakatifu na Neno la Mungu, Kristo atafanya kazi
kwa njia yetu katika nguvu zake za mamlaka ya
kutenda mapenzi yake. (Mathayo 18:18-20; Marko
16:17).
Nne: Ni vema ukataka sana karama ya maarifa na
ya hekima na ya utambuzi. (1 Wakorintho 12:8-11). Je,
mtu ni mgonjwa kwa sababu amepagawa na mapepo,
magonjwa ya kimwili au yote mawili? Je, kuna dhambi
katika maisha yake ambayo inasababisha magonjwa?
Je, mtu huyo au familia yake imeshajihusisha na
mambo ya ushirikina? Tegemea zaidi Roho Mtakatifu
kukusaidia katika kutambua sababu za ugonjwa au
matatizo, ili uweze kusema ukweli wa shida katika
maombi. Usiwe na haraka. Katika hali nyingine,
kufunga na maombi ya ziada yatahitajika (Mathayo
17:21).
Tano: Katika muda wako wa maombi, umwombe
Bwana upate kutiwa moyo ili uwe tayari kuona ishara na
miujiza. Omba kwa lugha na jieleze mwenyewe, jenga
imani yako (Yuda 20).
Sita: Mwambie Roho Mtakatifu akufundishe kuhusu
miujiza unaposoma Biblia. Mwambie Mungu akupe
watu wengine ambao watakufundisha na kukusaidia
kukua katika maeneo hayo.
Wakati unapohubiri au kuwashirikisha Habari
Njema wengine, uulize kama kuna mtu mgonjwa kati
yao. Waulize ruhusa kama unaweza kuwaombea.
Waambie kuwa Yesu anaweza kuponya walio
wagonjwa. Omba na amini kuwa Mungu atafanya
miujiza. Hatimaye washirikishe Injili na kuomba nao
ili wampokee Kristo.
Wakati unapoombea wagonjwa, uwe makini katika
Roho Mtakatifu. Msikilize wakati unapohudumu. Ni
jambo muhimu sana kumleta mgonjwa au waliopagawa
na pepo ili waokolewe katika Kristo kwa sababu wanayo
nguvu ya kupinga mipango yote ya kipepo kwa njia ya
Kristo tu (Mathayo 12:43-45; Waefeso 6:10-18; Yakobo
4:7; 1 Petro 5:8-9).
Ishara, Maajabu, Na Miujiza Mara Nyingi
Vinatendwa Na Wainjilisti
Katika masomo yaliyotangulia, tumejifunza kuwa
Filipo alihubiri na aliomba kwa jina la Yesu. Maroho
machafu yaliondoka; watu waliokuwa wagonjwa
walipona.
Haya yote ni ishara zenye nguvu zinazoonesha watu
kuwa Filipo aliwaambia ukweli. Hivyo watu
Omba na mwambie Mungu akupe ulinzi wake. Mungu
atakusaidia kila mara unapohubiri na omba kwa ajili ya
wagonjwa na pia kemea mapepo. Siku zote sikiliza Roho
Mtakatifu na fanya kile ambacho Roho Mtakatifu
amekuambia ufanye.
24 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
walishangaa na kufurahia (Matendo 8:5-13).
Soma tena Matendo 8:5-13, mwambie Bwana
akufundishe. Kama wewe ni mwinjilisti ambaye anamtii
Mungu na anahubiri ujumbe kamili wa Injili, amini
kuwa Mungu atakupa miujiza na ishara zitafuata!
Kundi la wainjilisti katika bara la Afrika waliomba
na walijisikia kuongozwa na Mungu kwenda katika vijiji
viwili kuhubiri Injili. Walikwenda pale na kuhubiri
Injili; watu wengi wakamkubali Yesu Kristo. Wanakijiji
waliwataka wainjilisti waombe mvua, kwani
hapakuwepo na mvua kwa miezi mingi. Baada ya kundi
hili kuondoka na kwenda kijiji kingine, mvua ilinyesha
kwa masaa matatu na nusu! Wanakijiji waliwatuma watu
wafuate kundi hilo na kuwaambia habari hizo. Mungu
aliwapa ishara kijiji kizima kwamba nguvu za Mungu ni
za kweli na kwamba yale ambayo wainjilisti waliyasema
ni kweli.
Miujiza ilifanyika kila mahali Yesu alipokuwa.
Miujiza ilifanyika mahali wanafunzi walipokwenda.
(Warumi 15:19; Matendo 6:8). Filipo alikuwa ni
mwanafunzi na wewe ni mwanafunzi pia. Dunia
imebadilika lakini Mungu habadiliki (Waebrania
13:8). Mwambie Mungu kwa imani akupe karama ya
miujiza ili kuthibitisha nguvu za Mungu na ujumbe
wa Injili.
Sababu Miujiza Isiweze Kufanyika
Moja: Kutokuwa na imani au unashindana na
kutokuamini. Ni muhimu kuwa na imani katika Yesu na
kwamba Yeye ni nani ili nguvu za miujiza ziweze
kuonekana (Mathayo 17:14-20; Waebrania 11:6).
Mbili: Kama huamini kuwa Mungu anafanya
miujiza, au anaweza kukutumia kuwa wewe uombe kwa
miujiza. Mungu hakuahidi nguvu zake kwa watu walio
na elimu, matajiri, wasomi, au kwa watu wasemaji bora.
Yesu aliahidi nguvu zake kwa watu wote, “hao
waaminio” (Marko 16:16-17).
Tatu: Kama maisha yako si safi. Hukumtii Mungu
au unatenda dhambi. Au unakuwa na malengo ambayo
si sawa, kutaka kufanya miujiza ya Mungu ili kujitukuza
mwenyewe na siyo Yesu Kristo (Matendo 8:14-23). Ni
lazima utubu nenda kwa kaka au dada na kukiri
madhaifu yako na waombe kwa ajili yako na
kukuombea (Yakobo 5:16; 1 Yohana 1:9). Wahudumu
wote wa Injili ni lazima waishi maisha maadilifu.
(1 Timotheo 3:2; Tito 1:6).
Nne: Mtu fulani amekufundisha kuwa miujiza
haifanyiki siku hizi. Una habari ambazo si za kweli.
Amua kusoma Neno la Mungu na jifunze ukweli kuhusu
mambo ambayo Yesu alifanya na alivyosema kuhusu
miujiza. Inahitaji imani kuamini Mungu na Neno Lake.
Kumbuka, tunamtumikia Mwokozi aliyefufuka na
asiyebadilika, “Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na
hata milele” (Waebrania 13:8).
Yesu Mwenyewe alisema, “Na ishara hizi
zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa
pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka;
hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa;
wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao
watapata afya” (Marko 16:17-18).
Kuhusu Paulo na Barnaba, inasemekana, “Basi
wakakaa huko wakati mwingi, wakinena kwa ushujaa
katika Bwana, aliyelishuhudia neno la neema yake,
akiwajalia ishara na maajabu yatendeke kwa mikono
yao” (Matendo 14:3). Mwambie Mungu akupe hayo
matendo ya nguvu kwa ajili ya huduma yako ili
Mungu apate kutukuzwa na Ufalme wa Mungu upate
kukua.
Tano: Ingewezekana umekosa taratibu au una
kiburi. Huchukui muda wa kusoma na kujifunza
Biblia au kuijenga imani yako kwa Mungu. Ni mara
chache unahubiri au kuwaambia wengine habari za
Yesu Kristo. Unataka mialiko maalum kwa ajili ya
kuhubiri.
Katika mambo haya yote unatakiwa utubu! Ni lazima
uamue kuwa mwanafunzi mwaminifu, kuomba na
kujifunza. Ni muhimu ukawa tayari kukubali kwenda
mahali ambapo Mungu anakutuma ukahubiri - na kwa
yeyote ambaye hajapata kusikia Habari Njema! Wakati
tunapokuwa waaminifu katika madogo au vitu dhaifu,
ndipo Mungu anatoa zaidi (Mathayo 25:23).
Inachukua muda kwa imani yako kukua katika hali
itakayokufanya uamini Mungu kwa miujiza. Soma
Biblia yako ili ujifunze vizuri ujumbe wa Injili. Soma
sehemu hii ya ujumbe mara nyingi, na masomo mengine
yanayoonesha miujiza. Anza kuamini Neno la Mungu na
mwambie Mungu, “Ninakuamini.” Mungu anapokupa
nafasi kuwashirikisha wengine Injili, omba kwa ajili ya
mahitaji ya mtu au watu wale unaowashirikisha.
Mwombe Mungu akuongoze na kukuelekeza na
kukufundisha. Muda si mrefu utaanza kuona mambo ya
miujiza yakifanyika. Uwe mtii katika yale yote Mungu
anayokuonesha, na hivyo utakua katika ufahamu na
Bwana Yesu atakutumia.
Vifungu Vya Biblia Vioneshavyo Ishara,
Maajabu, Na Miujiza
Chukua muda kusoma, kujifunza, na kuomba kwa
ajili ya mistari kutoka Maandiko ambayo yanakuambia
kuhusu nguvu za Mungu na miujiza, ishara, na
maajabu:
Ayubu 5:9
Yeremia 32:21
Mika 7:15
Mathayo 12:28
Marko 16:16-17,20
Luka 5:17; 10:18-20
Yohana 4:54; 6:14; 12:9-11; 14:12
Matendo 3:16; 4:7-10,16,22; 4:29-30; 8:5-13; 10:38;
14:3; 15:12; 19:11-12
Warumi 15:19
1 Wakorintho 4:20; 12:9,10,28
2 Wakorintho 12:12
Waefeso 1:18-19
1 Wathesalonike 1:5
Waebrania 2:2-4 􀂄
NAKALA 14 – NAMBARI 1 –2006 MATENDO/ 25
Sehemu Ya Saba
Kuhubiri Ujumbe
Ulio Wazi Wa Injili
Mwinjilisti Na Uinjilisti – Kupeleka Injili Duniani Kote!
Ni Mungu, kwa njia ya Roho Mtakatifu Wake,
huwaita watu waje kwake Mwenyewe (Yohana 6:44). Ni
lazima tuombe sana, kumwambia Mungu awalete wote
kwa wokovu wale ambao hawajamjua Yesu.
Lakini tutakuwa tumefanya makosa kama
hatutatambua ushauri mzima wa Neno la Mungu na
maagizo ya Kristo: Pamoja na kuwa Mungu atawavuta
watu, ni lazima sisi tumtii Mungu na kwenda kuhubiri
Injili na kuwaambia watu Habari Njema!
“Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena
wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje
pasipo mhubiri? Tena wahubirije wasipopelekwa?
Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao
wahubirio habari ya mema!” (Warumi 10:14-15).
Ndiyo, Roho Mtakatifu atawavuta watu kwa wokovu.
Lakini kama kifungu hiki kinavyoeleza kwa uwazi
kabisa, watu ni lazima wasikie habari za Yesu kabla ya
wao kumuamini.
Yesu aliwaagiza wanafunzi wake, “Basi, enendeni,
mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza
kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu”
(Mathayo 28:19-20); “Enendeni ulimwenguni mwote,
mkahubiri Injili kwa kila kiumbe” (Marko 16:15).
Kama jambo hili halikuwa muhimu mno kwa watu
kupokea wokovu, hivyo ingekuwa ni zoezi ambalo
halina maana. Ni lazima tuende; ni lazima tutangaze!
Watu wanaangamia kila siku ambao hawajasikia Injili.
Ni kusudi la Mungu kwamba HATA MMOJA
asiangamie, lakini WOTE waje na kutubu (2 Petro 3:9).
Wakristo ni lazima wamtii Kristo, wafuate mfano wake
–waite watu wapate kutubu na kuamini, wahubiri Injili
kwa kila kiumbe kama Kristo alivyotuagiza tufanye!
Na wakati tunapohubiri ujumbe wa Injili, ni muhimu
ukawa rahisi na kueleweka. Tena ujumbe huo ulete
maana kwa wasikilizaji. Ujumbe wa Injili ni lazima
ueleweke ili watu wawe na uhakika na uamuzi ambao
watafanya.
Ujumbe mzuri wa uinjilisti ni wa kipekee kwani ni
kuhusu Yesu ni nani – na siyo jinsi ya kuomba, kusaidia
wengine, au jinsi ya kufanya mambo mema (yale
mafundisho siyo ujumbe wa uinjilisti). Wakati
mwinjilisti anapohubiri, anawaambia watu habari za
Yesu Kristo na kuwaita watu kwa Yesu Kristo kwa toba.
Wahubiri wengi hawajui jinsi ya kuhubiri ujumbe wa
uinjilisti. Ujumbe wa kiinjili ni lazima uwe juu ya Yesu
na kwa nini watu wanahitaji kumpokea Yesu awe Bwana
na Mwokozi wa maisha yao.
Chagua Somo La Biblia Lenye Umuhimu
Wake
Chagua somo la kuhubiri ambalo litaleta maana kwa
watakaolisikia. Hapa ipo mifano michache kutoka Biblia
ya kuhubiri ili kuwafanya watu wamfahamu Yesu Kristo
na wokovu ambao anatoa kwa ajili yao:
• Kondoo aliyepotea (Luka 15:4-7)
• Shilingi iliyopotea (Luka 15:8-10)
• Mtu ambaye Yesu alimfungua kutoka nguvu za
mapepo (Marko 5:1-15)
• Mwanamke aliyemwendea Yesu kwa hitaji lake
(Luka 8:43-48)
• Mwaliko uliokataliwa (Mathayo 22:1-10)
• Je, jina lako liko katika Kitabu cha Uzima cha
Mwanakondoo? (Ufunuo 20:12-15)
• Yesu atakuwa Mchungaji Wako (Yohana
10:2-4,26-29)
• Njia mbili za maisha (Mathayo 7:13-14)
• Kumwita Yesu wakati wa shida (Warumi 10:13)
Kuna vifungu vya Maandiko vingi ambavyo
vitakuwa msingi jinsi ya kutoa ujumbe ulio wazi wa
Injili. Mwambie Mungu akupe mwelekeo wa Biblia na
maisha ya watu ili unapohubiri ueleweke.
Kutoa Injili Ya Upendo
Baadhi ya wainjilisti wanaanza kutoa ujumbe wao
kwa kusema, “Ni lazima uokoke! Utakwenda Jehanam!”
Wanarudia maneno haya tena na tena. Hali hii ya
kuhubiri inawafanya watu wajione hawafai na kujenga
kujihukumu. Baada ya muda, wataacha kusikiliza na
wakaondoka.
Maneno yako ni lazima yawavute watu. Biblia
26 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
inatufundisha ni wema wa Mungu unaotuongoza
tufikie toba (Warumi 2:4). Je, unaweza kuwaambia
watu kwa nini ni lazima waokoke? Je, unaweza
kuwaambia upendo mkubwa wa Mungu, na kafara
kubwa ya Yesu aliotoa kwa ajili yao? Je, unaweza
kuwaambia furaha iliyopo kwa kumjua Yesu? Waambie
mambo watakayokosa kwa kumkataa Yesu. Waambie
mambo ambayo watapata wakimpokea Yesu Kristo!
Hapa kuna mifano michache itakayokusudia
kuelewa mahubiri mazuri ya kiuinjilisti:
Baadhi Wanahubiri...
“Wote ni watenda dhambi na mtakufa!”
“Ni lazima uokoke!”
“Ni lazima uwe Mkristo!”
“Usiwe mdhambi, njoo kanisani.”
“Utakwenda Jehanam!”
“Ni lazima uwe mzuri!”
“Ni lazima ubadilishe maisha yako!”
“Ninajua mengi kuhusu Mungu!”
“Sikiliza mtu mwenye nguvu za
Mungu!”
Mahubiri Mazuri...
“Wote tumefanya dhambi. Hukumu ya Mungu kwa dhambi ni kifo.
Yesu alichukua hukumu hii Mwenyewe. Kama utampokea Kristo na
dhabihu yake kwa ajili yako, Yeye atakusamehe dhambi na kukupa
uzima.”
“Dhambi inatutenga na Mungu na upendo wake. Ndiyo sababu
unamhitaji Yesu - alikufa na kulipia dhambi zako.”
“Unaweza kumfahamu Mungu kwa kumpokea Yesu awe Mwokozi
wako.”
“Je, umechoka na dhambi na kutengwa na Mungu? Yesu peke yake
anasamehe dhambi na kukusafisha na mambo yote yasiyo haki, na
kukuponya madhara yote ya dhambi.”
“Wote wanaompokea Yesu Kristo watafanywa kuwa wa Mungu na
kukaa naye milele. Wale wote wanaomkataa Kristo watatengwa na
Mungu milele, pale Jehanam. Mungu anapenda ukae naye lakini ni
uamue mwenyewe.”
“Wote tumefanya dhambi mbele za Mungu. Lakini Yesu alikufa
Msalabani ili tupate kusamehewa dhambi. Hatuwezi kuwa wema pasipo
msaada wa Kristo.”
“Wengi wetu tunapenda kubadilika, lakini hatuna nguvu kujibadilisha
wenyewe. Yesu anatupa nguvu ya kubadilika, kushinda dhambi, kukataa
ubaya na kuwapenda wengine badala ya kuwachukia.”
“Uwezo wa kumfahamu kiakili tu Mungu au Yesu hauwezi kutuokoa.
Ni lazima upokee msamaha wa Kristo na kumkubali awe Bwana na
Mwokozi.”
“Mimi si mzuri zaidi yako. Mimi ni mkosaji. Lakini nimempokea
Yesu Kristo. Yeye amenisamehe na amenipa Uzima na Roho Wake,
na sasa ninamfahamu Mungu. Niko hapa kukuwezesha nawe upate
nafasi hii.”
Elewa Watu Ambao Unawahubiria
Ni watu gani ambao unapenda kuwashirikisha
Injili? Je, ni wafanyabiashara? Wanawake? Wafanyakazi?
Wanafunzi? Watu muhimu? Waislamu?
Wahindu? Wabudaa? Jitahidi ufahamu desturi zao,
mawazo yao, na imani yao. Jitahidi kuwaelewa na
kwa nini wako kama walivyo.
Unaweza kufanya hivi kwa njia mbili. Moja,
jifunze kila uwezalo kuhusiana na watu hawa.
Wanaishije? Nini kinawaogopesha? Wanaamini nini?
NAKALA 14 – NAMBARI 1 –2006 MATENDO/ 27
Wana wasiwasi na mambo gani? Wana matumaini
gani?
Ya pili, omba na kutaka Mungu akufunulie mahitaji
yao. Mngojee Mungu naye atakuelekeza kwa njia ya
maneno, mitazamo, au kwa njia ya picha katika mawazo
yako. Tayari Roho Mtakatifu anajua maisha yao na
atakusaidia jinsi ya kuzungumza nao. Atakusaidia.
Kuhubiri mahitaji muhimu ya binadamu ni njia yenye
nguvu katika mahubiri ya kiuinjilisti.
Wathamini Watu Ambao Unawahubiria
Mara nyingi utawahubiria wanaume, wanawake na
watoto pamoja. (Hata watoto wadogo sana wanaweza
kuelewa Injili na kumpokea Yesu!) Ni lazima useme
kwa kuheshimu na ukweli (1 Petro 3:15). Wainjilisti
hawakuitwa kuwahukumu watu (Yohana 3:17). Ni
lazima kuwa wanyenyekevu na kukumbuka kuwa kila
mtu (pamoja na sisi) tumefanya dhambi na tunamhitaji
Yesu - kwani hakuna aliye bora zaidi ya mwingine.
Wasaidie watu watambue upendo wa Mungu kwa ajili
yao; waite katika tumaini lipatikanalo kwa Yesu Kristo.
Kama ukiwaonesha watu upendo wa kweli na heshima,
kwa vyovyote watapenda kusikiliza ujumbe ulio nao.
Kuzungumza Kwa Kujiamini
Wewe kama mtu binafsi huna lolote unaloweza
kusema ili kubadilisha maisha. Lakini ni muhimu
kukumbuka kuwa ni Yesu anayekutuma. Wewe ni
mtumishi wa kusema ujumbe wa Mtu Mwingine
ambaye ni Mkubwa kuliko wewe mwenyewe. Wewe ni
mtumishi kufanya mapenzi ya Bwana wako. Ameahidi
kukusaidia. Jinsi utakavyohubiri zaidi, ndivyo utakavyojijenga
katika kujiamini. Kila mwinjilisti anafanya
makosa, lakini unaweza kujifunza kutokana na makosa
ili kufikia mhubiri bora. Wakati ambapo hujafanya
vizuri, omba na mwambie Yesu akufundishe jinsi ya
kufanya vizuri. Kwa njia ya mazoezi mengi utakuwa
mhubiri wa Injili vizuri.
Ujazwe Na Roho
Yesu alikuwa mfano wa aliyejazwa Roho, Roho
alimtia nguvu (Matendo 10:38). Yesu alihubiri kwa
mamlaka, akitoa pepo, akiponesha walio wagonjwa, na
kuwafungua waliofungwa na kuwaacha huru (Mathayo
4:23; Luka 4:14-19). Yesu alikuwa mkamilifu, Mwana
wa Mungu asiye na dhambi. Hata hivyo kuna wakati
kabla ya kuanza huduma yake ambapo Roho Mtakatifu
alikuja na kumjaza (Luka 4:1; Yohana 1:32-33).
Yesu aliweka wazi kuwa wanafunzi wake – wale
ambao walikuwa tayari wanamwamini – walihitaji pia
Roho Mtakatifu kuwajaza ili waweze kuwa mashahidi
wenye nguvu (Luka 24:45-49; Matendo 1:5,8).
Ubatizo wa Roho Mtakatifu umetolewa na Yesu
(Mathayo 3:11). Ubatizo huu wa Roho Mtakatifu
unatenda mambo makuu katika mahubiri ya Petro na
wanafunzi wengine. (Matendo 2:14-47; 3:11-26;
4:23-31), na utakusaidia wewe pia kuhubiri Injili kwa
ujasiri zaidi.
Wakati mtu anampokea Kristo, anazaliwa upya kwa
kazi ya Roho Mtakatifu. (Yohana 3:5-6). Roho
Mtakatifu anakuja na kuishi ndani yake (Warumi
8:9-11). Hata hivyo, Kristo anajua kuwa tunahitaji
nguvu Yake ili tuweze kukamilisha mapenzi Yake katika
dunia hii. Hivyo, Yesu ametuahidi kujazwa na Roho
Mtakatifu na kufurika (Yohana 7:38-39) ili tuweze
kupakwa mafuta katika huduma (Luka 24:49; Matendo
1:8).
Ubatizo wa Roho Mtakatifu ulitokea kwa waumini
wale waliokwisha kumwamini Kristo kama Mwokozi
wao (Matendo 2:1-4). Haya yalitokea baadaye kwa
wengine pia, ambao walimpokea Kristo na kubatizwa
kwa maji, lakini walikuwa bado Roho Mtakatifu
hajawajilia juu yao. “Na mitume waliokuwako
Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria
imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na
Yohana; ambao waliposhuka, wakawaombea
wampokee Roho Mtakatifu; kwa maana bado
hajawashukia mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa
jina lake Bwana Yesu. Ndipo wakaweka mikono yao juu
yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu” (Matendo
8:14-17).
Je, Roho Mtakatifu amekushukia kwa nguvu? Je,
unataka kuwa na ujasiri zaidi wakati unapohubiri na
kuzungumza juu ya Yesu? Kama Yesu Kristo ni Bwana
na Mwokozi wako, hivyo karama ya Roho Mtakatifu iko
kwako (Matendo 2:37-41). Nguvu ikuwezeshayo kuwa
na ushuhuda ufaao wa Yesu inakuja wakati unapokea
ubatizo wa Roho.
Kupokea Roho Mtakatifu
Unapokeaje Roho Mtakatifu? Kwanza, hakikisha
kuwa maisha yako ni safi mbele za Mungu. Kiri dhambi
yoyote inayofahamika na kutubu mbele za Mungu.
Mwombe Mungu akuchunguze, na kwa njia ya maombi
yakiri mambo yote aliyokuonesha.
Baadaye mwambie Yesu akujie kwa njia ya Roho
Mtakatifu na kwa nguvu. Anza kumsifu Yesu Kristo.
Biblia inatufundisha kuwa unaweza kuanza kwa
kusema kwa lugha nyingine ambayo hujapata
kujifunza, kama ilivyotokea kwa wanafunzi (Matendo
2:1-4; 10:44-46). Usikatishwe tamaa kama itatokea
kuwa huanzi kusema mara moja. Chukua muda
umwabudu Bwana Yesu na mwambie akupe Roho
Wake Mtakatifu.
Kama unamjua mtu ambaye ameshajazwa na Roho
Mtakatifu, mwambie mtu huyu aweke mikono juu yako
na kukuombea (Matendo 8:14-17). Mungu anajibu
maombi! Ni Yesu alituambia kuwa tunahitaji kupewa -
hivyo omba nawe utapokea kama Yeye Mwenyewe
alivyoagiza.
Uendelee Kujazwa Na Roho Mtakatifu
Tunahitaji kujazwa Roho Mtakatifu kila mara na
kwa upya. Biblia inaelekeza waumini kuwa, “...bali
mjazwe Roho; mkisemezana kwa zaburi na tenzi na
nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia
28 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba
sikuzote…” (Waefeso 5:18-20). Ni wazi kwamba
maelekezo haya siyo jambo la wakati mmoja, lakini ni
jambo la wakati wote. Ni lazima liwe linatokea mara
kwa mara. Neno la asili la Kiyunani (Kigriki) la
“kujazwa” limetafsiriwa “kuendelea kujazwa” - jambo
linaloendelea na kufanywa upya kwa njia ya Roho
Mtakatifu na Mungu.
Tunahitaji Roho
Mtakatifu akae ndani
yetu kama Wakristo -
ili atupe faraja,
atuongoze, na
kutufundisha.
Tunahitaji pia Roho
Mtakatifu atujie na
kutupa nguvu katika
huduma yetu. Na
tunataka Roho
Mtakatifu kuendelea
kutujaza - ili kutupa
upya na kutusaidia
kuiwezesha mioyo
yetu na midomo
kujazwa na sifa,
nyimbo, na shukrani!
Kuamini Mungu
– Tumia
Karama Zako
Mwinjilisti mzuri
anategemea nguvu za
Mungu na hekima
zitende kazi ndani
yake. Matokeo
mazuri ya uinjilisti
hayatokani na uwezo
au kipawa chetu cha
kiasili. Mungu
anatumia mambo
yetu ya kawaida,
lakini Mungu anataka umwamini Yeye - kwani ni Roho
Mtakatifu peke yake awezaye kuleta ushawishi kwa
watu (Yohana 16:8). Wajibu wa mwinjilisti ni kuwa
mwaminifu kuwashirikisha Injili, hivyo atalazimika
kumwamini Bwana kwa matokeo yake.
Mungu anatoa karama na vipawa kwa watu na
wahubiri wenye hekima wanaovitumia kwa utukufu wa
Mungu (1 Wakorintho 10:31). Mungu anatutazama
tutumie vipawa kwa uwezo tulio nao (Mathayo
25:14-28). Mungu amefanya kila mtu na upekee wake.
Analo kusudi la kutuumba sisi kwa jinsi tulivyo na
hakuna anayeweza kufanya kama tufanyavyo. Siyo
jambo la hekima kuiga wahubiri wengine; wanao wajibu
wao wenyewe wa kutimiza. Hata hivyo, unaweza kupata
mawazo kutoka kwa wahubiri wengine na kuyatumia
katika ujumbe wako, utumie njia zako, unapowashirikisha
ukweli wa Yesu.
Hubiri Kwa Ajili Ya Toba
Ni muhimu kwa mwinjilisti kuwaambia wanaume na
wanawake kwamba ni lazima wabadilishe mwelekeo wa
maisha yao. Wanatembea katika njia ya uharibifu; ni
lazima wageuke na kumfuata Yesu (Mathayo 7:13-14).
Waite watu wabadilishe mwelekeo (watubu), kutoka
kufuata njia zao wenyewe na kufuata njia za Mungu.
Hubiri na kuweka ujumbe wazi kwa watu kwamba ni
lazima waamue ni
nani wanataka
wamfuate. Kuna
uchaguzi wa aina
mbili tu: kumpokea
Yesu Kristo na
kutembea katika njia
zake; au kuchagua
ubinafsi wao ambao
utawafikisha katika
uharibifu wa milele.
Hubiri Ili
Kugusa Mioyo
Yao
Maisha ni
magumu, makatili
kwa watu wengi.
Ujumbe wa Injili una
tumaini la kweli na
la amani na Mungu,
ana msamaha wa
dhambi. Watu
wanahitaji kufahamu
kuwa Mungu
atatembea nao katika
maisha yote kama tu
watamgeukia Yeye
kwa wokovu. Hubiri
na kutoa upendo wa
Mungu, wokovu wa
Kristo, na faraja ya
Roho Mtakatifu.
Hubiri ukiwaambia watu jinsi ya kumfuata Kristo.
Watu wanahitaji kujua pia kuwa kuna hukumu na
adhabu kwa ajili ya dhambi. Elezea kifo cha Yesu cha
Msalaba, misumari iliyopigiliwa katika miguu na
mikono yake, damu ilivyochuruzika katika mwili wake,
Waambie jinsi Yesu alivyotundikwa juu ya Msalaba kwa
masaa akiwa katika maumivu makali, jinsi alivyoteseka
- kwa ajili ya kafara ya dhambi zetu, akachukua adhabu
yetu juu yake mwenyewe. Elezea matukio yote; chora
picha kwa maneno yako mwenyewe. Waangalize kuwa
hii siyo hadithi - ni Ukweli! Waambie Yesu alifufuka
toka kwa wafu kwa nguvu ya Mungu na Yeye ni hai
sasa. Watie moyo wafikie uamuzi wa kumchagua Kristo!
Hubiri Kuendana Na Wasikilizaji Wako
Njia nyingine ya kuhubiri ni kuwakilisha hoja
yenye kufikirisha na kuitikisha hadi mwisho. Mtume
Shiriki ukweli wa Yesu!
NAKALA 14 – NAMBARI 1 –2006 MATENDO/ 29
Paulo alifundisha hivi wakati mwingine (Matendo sura
ya 17).
Unataka kuwashawishi watu waone mpango sahihi
wa Kristo (2 Timotheo 4:2) na ukweli wa uamuzi wa
kumfuata Kristo. Unafikiri na wao na kuwaleta kwa
uamuzi ulio sahihi.
Unaweza kuwaambia habari za faida za rohoni
(lakini watu wasije wakaambiwa kumfuata Kristo kwa
baraka zake tu). Kuna sababu nzuri ya kuogopa hukumu
ya mwisho; ni uamuzi mzuri kumfuata Kristo. Mtu
anaweza kumfuata Kristo ili aondolewe aibu na hatia
yake kwa sababu ya dhambi zake huko nyuma na pia
kuondoa dhamiri kujishtaki. Kumwamini Yesu kwa
kutubu kunaondoa dhambi, na hii ndiyo sababu nzuri ya
kumfuata Kristo.
Kwa mfano nikijua mtu ambaye anaingia katika
safari ya hatari na pengine kufa, ningependa kufikiri
naye kuhusu uamuzi wake. Nitampa sababu kwa nini
asiende: mvua itanyesha sana na kuosha barabara
nzima; kuna wanyama wakali; kuna wezi na silaha kila
mahali - kuna hatari. Nitamwambia yote ambayo
yatampoteza katika safari yake; jinsi ambavyo familia
yake itakavyoteseka, na mengineyo. Na huu ni ujumbe
muhimu.
Ni sawa na wakati ambao unahubiri habari za
kumkubali Kristo. Safari ya maisha ni hatari na ina
uangalifu mdogo sana. Maovu na mabaya hutokea pale
ambapo mwanadamu anachagua njia ya dhambi.
Mwanadamu anaweza kupoteza kitu muhimu sana
katika maisha yake na tena anaweza kupoteza nafsi
yake. Je? Unaona jinsi ambavyo sababu hii inasaidia
mwanadamu kuweza kuona wazi maisha yake yalivyo
kama jinsi ambavyo hakumfuata Mungu na njia Zake.
Kwa mahubiri aina hii utakuwa umeweka wazi
mawazo ya uongo yanayofanya watu wafikiri kuwa
wanaweza kuishi bila Kristo. Unatakiwa ueleze usalama
wa kitambo tu wa maisha yao, pengine ipo katika fedha,
familia, mafanikio, au tambiko fulani katika dini.
Sisitiza kuwa kila mtu ana uwezo wa kuchagua juu ya
maisha yake, na pia kuwa matokeo ya milele katika
chaguo afanyalo. Kama wanakataa kuchukua uamuzi ni
kuwa wamekwisha kumkataa Kristo kwa kutokupokea
wokovu anaoutoa.
Tumia Picha Na Hadithi Katika Mahubiri
Unapohubiri unaweza ukatumia picha za maneno za
maisha ya kila siku zenye kuhusiana na watu
unaozungumza nao. Yesu alifanya hivyo alipokua
anazungumza katika mifano na mafundisho yake. Neno
“mfano” maana yake ni “kulinganisha”, kuchukua kitu
kimoja mbele ya kingine na kuonesha jinsi
vilivyofanana.
Yesu alizungumzia mashamba, wanyama, fedha,
kula chakula, kazi za shambani, watoto wakicheza
(Mathayo 11:16-19; 13:1-32; 20:1-16; 22:1-14;
25:14-30; Luka 15:4-7). Wakati Yesu anasema, “Mimi
ndimi mlango” (Yohana 10:9), kila mmoja alimuelewa
ana maana gani. Waliweza kuona mlango katika
mawazo yao. Yesu alitumia vitu vinavyoeleweka kama
picha kuonesha kuwa alikuwa Yeye ni njia pekee
kumfikia Mungu.
Kuna mifano mingi, habari, na picha katika Biblia
zinaweza kuchora ujumbe kwa wasikilizaji wako, zenye
kuonesha upendo wa Mungu, hali ya watu kupotea, na
ukweli wa wokovu:
• Shilingi iliyopotea (Luka 15:8-10)
• Msamaria Mwema (Luka 10:30-37)
• Nyumba mbili (Mathayo7:24-27)
• Njia nyembamba na njia pana (Mathayo 7:13-14)
• Mwanamke aliyefumaniwa (Yohana 8:3-11)
• Mwizi aliyetubu akiwa msalabani (Luka
23:39-43)
Mifano hii na mingine mingi itakusaidia kuhubiri
kwa picha na hadithi. Itawasaidia wasikilizaji wako
waelewe upendo wa Mungu na matumaini yake ya
kuwaokoa watu.
Hubiri Kwa Huruma NA Juhudi
Vipo vitu vitatu ambavyo Mwinjilisti anahitaji.
Kwanza, ni jambo la muhimu kutambua upendo
mkubwa wa Mungu kwa watu wake. Mungu
anawapenda watu unaowahubiria! Amewafanya Yeye
Mwenyewe kwa ajili Yake, na kuchagua kuwapenda
wote. Hapendi watu hawa waishi katika dhambi, kuishi
katika maisha ya giza na maumivu, kuitumikia miungu
ya uongo, na kutengwa na Yeye katika maisha haya hata
milele. Siyo mapenzi Yake hata mmoja aangamie
(2 Petro3:9).
Upendo wa Mungu kwa wasikilizaji wako uujaze
moyo wako. Mungu aliangalia umati kwa huruma kwa
sababu aliona jinsi walivyopotea na hali waliyo nayo
(Mathayo 9:36-38). Hii ndiyo huruma ya Mungu.
Huruma ni pale mhubiri anapoguswa kwenda katika
kina kumsaidia aliyepotea. Ni zaidi ya kusikia huruma.
Ni hali ya kuona kuwa rehema za Mungu zinapatikana
kwa ajili yetu ambao hatukustahili. Unatakiwa uwe na
upendo wa namna hiyo kwa watu waliopotea na
wanaoangamia.
Pili, unahitaji mawazo ya Kristo (1 Wakorintho
2:11-16). Yesu anajua nini kuhusu watu hawa? Yeye
anajua wanachohitaji, jinsi ya kuwasaidia ili waweze
kumjua Yeye. Yesu alizungumza kuhusu mambo ya
ndani kabisa moyoni mwa mwanamke kisimani.
Alijieleza hali yake na akamwambia yale anayohitaji
kuyasikia ili kumleta katika wokovu (Yohana 4:7-42).
Yesu atakusaidia ujue unayohitaji kuyasema. Anajua
mahitaji ya watu na wanachotaka, madhaifu yao na hofu
zao. Muulize Mungu akupe hekima kwa sababu anatoa
kwa wote wanaotaka (Yakobo 1:5).
Tatu, kila mwinjilisti anahitaji nguvu na juhudi za
Roho Mtakatifu (angalia “Kujazwa na Roho Mtakatifu”
hapo juu). Wanahitaji nguvu na juhudi ya Mungu rohoni
ili kuhubiri Habari Njema.
Juhudi ni kujisikia kwa uzito, kuwa na mzigo,
upendo usio na mpaka, na matakwa makali. Kuwa na
juhudi kwa ajili ya mambo ya Mungu kunamfanya
30 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
muumini amfuate Mungu na awe tayari kutenda
makusudi ya Mungu. Hali hii ni kama moto wakati
mwinjilisti anatumia muda wake kuomba na kuwa
katika uwepo wa Mungu, na anapojifunza Neno la
Mungu.
Unapokuwa na juhudi kwa Injili, unakuwa na ujasiri
wa kueneza ukweli kuhusu Yesu na mambo yaliyopo
yanaouzunguka ulimwengu. Unashawishika kuwa lile
ulisemalo ni kweli na muhimu.
Roho Mtakatifu atakupa nguvu na uhai katika
kuhubiri kwako, na kukujaza na mzigo wa huduma kwa
ajili ya waliopotea. Tafuta huruma za Mungu kwa ajili
ya watu na hii itakusaidia kuwa mnyenyekevu na kuwa
tayari mbele za Bwana.
Wakati mwingine mwinjilisti lazima aongee kwa
ushujaa na bila woga kuwatangazia watu kwamba
wamepotea katika dhambi. Lakini kila wakati kumbuka
kwamba huruma na upendo wa Mungu umekugusa na
kukuokoa wakati ulipokuwa mdhambi. Neema ni
upendeleo wa Mungu ambao haupatikani au hatustahili.
Tunapewa bure. Toa neema na huruma hiyo kwa
wasikilizaji wengine wa Habari Njema. Uwe shujaa, bila
woga katika Mungu, na mwombe Mungu akujaze
huruma kwa ajili ya wanaokusikiliza.
Toa Mwaliko
Mwinjilisti huhubiri Injili, akiwaita watu watubu na
kumfuata Yesu. Kila wakati maliza mahubiri kwa
kuwatia moyo wanaokusikiliza ili wafanye uamuzi juu
ya wanachosikia. Huu ni mwaliko wa wasikilizaji
kuitikia katika ujumbe wa Injili.
Mwitikio unaweza usiwezekane; lakini kama
unaweza, uwaombe wasikilizaji kuamua kama
watakaomkubali Kristo. Wakati unahubiri umati wa
watu au katika chumba kilichojaa watu, mwinjilisti
aweza akasema:
• Ni wangapi wameelewa ujumbe wa Mungu?
• Ni wangapi kati yenu wanataka kuomba Yesu
msamaha wa dhambi zao?
• Wapo watakaotoa maisha yao kwa Yesu na kuishi
naye?
• Nani atatubu dhambi na kumkubali Yesu Kristo?
• Nani anataka kumpokea Yesu Kristo kama Bwana
na Mwokozi wake?
• Ni nani atachagua kumfuata Yesu?
Waweza kuwaambia kuonesha matumaini yao kwa
kunyoosha mikono, kusimama, kuja mbele, au kutoa
maamuzi yao kwa waliokaa karibu. Waambie wachukue
hatua ya kuonesha wanajitoa kwa Yesu. Neno
huwashauri wanaoamini kutokuwa na aibu kukiri wazi
na kumfuata Yesu Kristo (Mathayo 10:32-33; Warumi
10:9-13).
Waume na wake lazima wajue kwamba wanafanya
maamuzi; lazima wapaswa kujua wafanye nini. Uwe
wazi kabisa, hivyo hawatachanganyikiwa na kufikiri
kwamba labda wanajiunga tu na kanisa au wanatoa
sadaka aina fulani za kidini. Elezea wazi nini maana ya
kumpokea Kristo kama Mwokozi wao.
Wakati Wote Omba Na Wale Wanaoitika
Wakati watu wanaonesha kutamani kumpokea Yesu,
kumkubali Yesu kama Mwokozi na Bwana, waombe
wasali pamoja nawe. Ni vizuri wasali kwa sauti,
wakirudia sala yako. Hii yaweza kuwa ngumu kwa
wengine, lakini watie moyo kushiriki. Ni rahisi kwako
kusali kwanza na kuwaambia warudie maneno yako.
Tumia sentensi rahisi na ufanye sala zako kwa kifupi.
Huu ni mfano wa sala unayoweza kusali na wale
wanaoitikia ujumbe wa Injili:
“Mpendwa Bwana Yesu, naamini wewe ni Mwana
wa Mungu. Naamini ulikufa Msalabani kwa ajili yangu,
ili uondoe dhambi zangu. Naamini ulifufuka katika
wafu. Mimi ni mdhambi. Natubu dhambi zangu zote.
Natubu kwa kuishi maisha yangu kwa mapenzi yangu
mwenyewe. Naomba unisamehe na uondoe dhambi
zangu zote. Nioshe na unitakase. Niokoe, Yesu Kristo,
na unipe maisha mapya. Ingia moyoni mwangu, na
unifanye niwe Wako. Asante kwa kuniokoa. Nakuchagua
uwe Bwana wangu, nikufuate Wewe siku zote za maisha
yangu. Nashukuru kwa uwezo wa kumjua Mungu.
Asante kwa kunipa Roho Mtakatifu Yako. Niwezeshe
niishi kila siku kukupendeza Wewe. Amina.”
Baada Ya Watu Kumkubali Kristo
Tumia muda kuwasaidia watu kuelewa walichofanya
kwa kumkubali Kristo. Waambie, “Sasa mmekuwa wa
Yesu. Mmekuwa sehemu ya familia ya Mungu. Yesu
atawawezesha kuishi maisha hayo. Yesu yupo karibu
nawe kila wakati. Unaweza kuongea naye kwa sala na
maombi, kama tulivyofanya hapa. Hakikisha kwamba
unapata Biblia na kuisoma kila siku. Hii itakusaidia
kujifunza juu ya Mungu na jinsi ya kuishi naye.”
Katika mikutano mengine au makanisa, baada ya
watu kumpokea Yesu kama Mwokozi na Bwana wao, ni
vizuri kuchukua muda kidogo na kuwaombea. Watubu
kwa maneno yao wenyewe. Wakatae uhusiano na
mambo maovu, vitendo, au watu - kama uchawi,
kuabudu mashetani, au kujihusisha na dini za uongo.
Kukataa maana yake ni kuacha kutii au kuacha kufuata
jambo. Wakati watu wamekataa maovu katika maisha
yao, unaweza kuwaombea na kuamrisha nguvu za giza
kutoka, katika Jina la Yesu. Ombea ulinzi wa Mungu
katika maisha yao.
Mifano ya sala hizo:
Muumini Mpya: “Yesu Mpendwa, nakataa dhambi
ya ____________ (uchawi au dhambi zingine). Nakataa
kushiriki katika nguvu za giza na nachagua kukutumikia
Wewe kama Mwokozi na Bwana wangu. Tafadhali
nifanye huru katika maovu sasa nikikuita. Asante Yesu.”
Mwinjilisti: “Baba Mungu, natumia mamlaka yako
kupitia Yesu kuamrisha kila nguvu ya kuzimu na roho
wachafu kumwacha mtu huyu na nyumbani kwake,
familia yake na maisha yake yote. Nasema kwamba
damu ya Yesu Kristo imemfanya huru. Nakuomba
uwalinde katika njia zote. Asante, Baba, katika Jina kuu
la Yesu. Amina.”
Baada ya watu kumpokea Yesu ni vizuri kuwaombea
NAKALA 14 – NAMBARI 1 –2006 MATENDO/ 31
kujazwa na Roho Mtakatifu (angalia “Kujazwa na
Roho” hapo juu). Kama tulivyojifunza, Roho Mtakatifu
huja na kukaa kwa kila mmoja anayekiri Yesu Kristo
kama Bwana na
Mwokozi wake.
Lakini Yesu ametoa
kwa kila anayeamini
kipawa cha Roho
Mtakatifu
kuwashukia na kuwa
mashahidi wake.
Waombee wapokee
hiki kipawa.
Wanaweza wakasali
katika lugha
wasizozijua.
Waelekeze waelewe
ni vizuri kusema
katika lugha mpya.
Ubatizo Wa
Maji
Biblia
inamwamuru kila
muumini katika
Kristo abatizwe
katika maji (Mathayo
28:19; Matendo
2:38). Mtie moyo
kila anayekubali
kumpokea Kristo
abatizwe katika maji.
Hii inaweza
kufanyika kanisani
au mahali popote
penye maji (mtoni,
baharini, bwawani
n.k.). Unaweza
ukawabatiza au
ukamtumia
mchungaji au
kiongozi wa kanisa unayemwamini kuwa anaweza
kuwabatiza waumini wapya katika maji.
Kanisa Kama Familia
Mwisho, utawaongoza watu hawa katika kanisa
ambalo litawafundisha na kuwatunza. Kama hakuna
uwezekano unatakiwa uwafundishe hadi mchungaji au
mwalimu aje. Paulo alifanya hivi katika Matendo
14:20-23. Watakuwa pia wanahitaji Biblia kusoma na
kujifunza kwayo. Jitahidi uwape waumini wapya Biblia
yao wenyewe, angalau Agano Jipya.
Mtumaini Mungu Katika Matokeo
Amini kuwa Mungu atawaleta watenda dhambi kwa
Yesu. Bwana alisema kwa Paulo, “...Usiogope, bali
nena, wala usinyamaze …kwa maana mimi nina watu
wengi katika mji huu” (Matendo 18:9-10). Amini nguvu 􀂄
Chukua muda kumgojea Bwana!
za Roho Mtakatifu aliyeko ndani. Uamini ukweli na
uhakika wa Neno la Mungu na Injili ya Yesu Kristo. Ni
neno lililo hai na lenye nguvu! Kumbuka kuwa ni
Mungu pekee ndiye
anayeokoa; wewe ni
mhudumu unayebeba
ujumbe wake katika
maagizo ya Yesu
Kristo. Mungu
anatamani watu wote
waokoke na pia
wamwamini Yesu
zaidi ya jinsi wewe
unavyotamani
(2 Petro 3:9).
Kunapokuwa na
matokeo kidogo
unaweza kufanya
mambo mawili.
Kwanza kabisa, nenda
kwa Mungu kwa
maombi na zungumza
naye kwa hali
uliyonayo. Chukua
muda wa kusubiri
Mungu. Mwache
akushtue kama kuna
jambo ambalo
anatamani wewe
ulielewe. Pili,
mwambie Mungu
akufundishe, jinsi
anavyopenda wewe
uhubiri Injili yake.
Mungu atakaponena
nawe, uitikie! Mungu
atakufundisha, na pia
atakupa waalimu.
Unapofanya mapenzi
ya Mungu kwa uweza
wako wote, mtumaini
kwa mafanikio. Wakati mbegu zinapoingia ardhini zinazaa
matunda. Unaweza au usiweze kuyaona mafanikio yake.
Jambo muhimu ni kumwamini Mungu na Neno Lake.
Haimaanishi matokeo uyaonayo, msifu Mungu na
kumpa shukrani. Mungu anastahili sifa zetu zote na
heshima yako, muda wote, kila mara. Watu wataitikia
ujumbe wako, mpe Mungu sifa. Ni Mungu anawakarimu
wainjilisti; ni Neno la Mungu linaloleta uzima; ni Roho
wa Mungu ndiye analeta watu kutubu. Mwinjilisti ni
kama mhudumu mtiifu kwa kazi hii kubwa ya Mungu!
Ni heshima gani ambayo Mungu ametuitia kuihubiri
Injili na kushiriki kuleta ukweli wa Yesu Kristo kwa
wengine. Wale wanaojitwika utukufu (kujisifu) wao
wenyewe ni wanyonge na pia ni wajinga ambao
wamekumbatia dhambi ya majivuno. Ni Mungu pekee
ambaye anamwokoa mwanadamu. Hivyo mpe Mungu
sifa ZOTE (Zaburi 115:1)!
32 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
Sehemu Ya Nane
Mungu
Anavyomuandaa
Mwinjilisti
Mwinjilisti Na Uinjilisti – Kupeleka Injili Duniani Kote!
Mungu Anataka Ujitoe Moja Kwa Moja
Wakati Yesu anapokuwa Bwana wa maisha yako,
anakuwa Bwana wa kila kitu. Mipango yako, vipawa
vyako na ujuzi, mawazo yako, kujisikia kwako, familia
yako, mwili wako, maisha yako - vyote hivi ni vya Yesu
Kristo na si vyako. Kama hujampa Yeye mambo yote na
kila kitu, kutoka katika moyo wako, afanye kama
atakavyo, fanya hivyo leo. Mwambie Mungu kwa njia
ya maombi.
Hivyo kila siku omba Roho Mtakatifu akuchunguze
na aletaye kukusadikisha.
Mwache Mungu akuoneshe
mambo unayoyahitaji kupata au
kuacha ili uweze kujiachia kwa
Mungu kikamilifu. Ukiri na
kutubu pale unapotambua kuwa
umefanya dhambi au makosa,
ubinafsi au tamaa za mwili.
Uwe na nidhamu na mwili wako
ili uweze kuwa mwanafunzi wa
Yesu mwenye nguvu. Biblia
inatuambia, “Basi nyenyekeeni
chini ya mkono wa Mungu ulio
hodari...” (1 Petro 5:6).
Mambo yafuatayo
yatakusaidia kujipima katika
maisha yako. Hizi si sheria au
mambo ya nje ya kujihakiki. Hii
ni njia ya uaminifu ya
kujitathimini maisha na huduma
yako kutoka katika moyo.
Maswali haya yana lengo la
kukusaidia ukue katika maisha
yako na kuwa chombo kizuri
katika mikono ya Mungu. Uwe
mwaminifu mwenyewe; na zaidi
sana, uwe mwaminifu kwa
Mungu. Hatuwezi kumdanganya
Mungu. Anajua yaliyomo
moyoni na anaona kila kitu katika maisha yetu. Ni vema
kila wakati kumkaribia Mungu kwa unyenyekevu,
kumtaka akusaidie kwa neema ili tuweze kukua na kuwa
imara na kuwa mtumishi mwaminifu Kwake.
Kama baadhi ya mambo hayo si ya kweli kwako,
lakini unataka yawe yako, mtake Mungu akusaidie. Na
chukua hatua ya kuyatenda! Inasemekana kuwa
inatupasa tutoe muda kwa mambo yenye umuhimu.
Kama mambo haya ni muhimu kwako, ni lazima uanze
kutoa muda kwa ajili hiyo.
NAKALA 14 – NAMBARI 1 –2006 MATENDO/ 33
Mambo Yamfanyayo Mwinjilisti Kukua
• Je, mnatumia muda muafaka kwa maombi na
kujifunza somo la Biblia kila siku?
• Je, ninachukua muda wa kumsikiliza Mungu,
kungoja ili azungumze na kuyafunua mawazo yake
na mpango kwa ajili yangu?
• Je, ninamwomba Roho Mtakatifu achunguze
maisha yangu? Je, ninakiri dhambi zangu kila
mara?
• Je, ninajifunza Biblia na kupanga vizuri hubiri
ambalo nitalifanya?
• Je, ninajaribu kusahihisha mazungumzo,
muonekano, elimu ya Biblia, na ujuzi wangu?
• Je, nitakapokwenda kuhubiri, nina waumini
wengine pamoja nami?
• Je, nimemwomba Mungu aongeze huduma
aliyonipa kwa upako na nguvu?
• Je, nimejazwa na uwezo wa Roho Mtakatifu
kama ilivyo katika Matendo ya Mitume sura ya 2?
• Je, ninao watu wanaoniombea kila siku katika
huduma yangu na kwa ajili yangu, kipekee wakati
ninapokwenda kuhubiri au kuwashirikisha wengine
Injili?
• Je, ninaomba kwa ujasiri ili kuwa mhubiri mzuri
wa Kristo?
• Je, mmefunga na kuomba kwa mwezi huu?
• Je, ninajua Biblia isemavyo kuhusu kuomba na
kumwamini Mungu kifedha, ili Mungu aweze
kutoa mahitaji kwa familia yangu NA huduma
yangu?
• Je, ninaye mshauri kunisaidia? Je,
nimemwambia Mungu anipe mtu wa kunifundisha?
• Je, kuna mwanaume au mwanamke ambaye
naweza kumwomba anisaidie kwa muda wake na
kunisaidia katika huduma yangu?
• Je, nimeomba na kumwambia Mungu anioneshe
mwanaume au mwanamke ambaye naweza
kumuandaa na kumsaidia katika uinjilisti? Kama
ndivyo, ilivyo je, ninafanya nini katika hilo?
• Je, nina nidhamu nzuri katika njia zangu au
mimi ni mvivu?
• Je, ninatumia muda wangu vizuri na mwenzi
wangu na watoto?
• Je, ninachelewesha kuanza kazi au ninafanya
kazi kwa bidii, kutunza wito wangu na kuheshimu
neno langu?
• Je, mawazo yangu ni mazuri? Je, mawazo yangu
yapo kwa Mungu?
• Je, ninasoma Biblia na vitabu vingine vya
Kikristo kunisaidia mimi kukua?
• Je, ninafanya kazi na wachungaji, kuwasaidia
kulijaza kanisa au kuanzisha kanisa lingine?
• Je, nimesoma na kuelewa - na pia ninafuata -
yasemayo Maandiko kuhusu wale walioitwa katika
uongozi katika kanisa la Kikristo (1 Timotheo
3:1-13; Tito 1:5-9)?
Tumia mistari hii kujisaidia wewe - na wainjilisti
wengine - jikumbushe na pia kutia moyo.
Dhamani Ya Kuwa Mwinjilisti Mzuri
Siyo rahisi kuwa katika huduma, bali zawadi ya utii
wa wito wa Yesu Kristo ina thamani kuliko dhiki.
Kuwaona watu wanakuja kwa Kristo ni zawadi kubwa
tunayoweza kuwa nayo duniani. Biblia inatufundisha
kuwa “mwenye hekima huvuta roho za watu” (Mithali
11:30).
Zipo zawadi za kipekee za milele zinazowasubiri
walio watiifu na wenye imani katika Kristo. Kwa wale
wanaowashawishi wengine kwa ajili ya haki, Daniel
12:3 anasema, “Na walio na hekima watang’aa kama
mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda
haki watang’aa kama nyota milele na milele.”
Tunda la Injili na kuwaambia wengine habari za
Kristo ni tunda la milele ambalo litadumu milele.
Mungu siku zote atawafariji na kuwazawadia wale
wanaomtumikia na imani na utiifu wa moyo.
Yesu anaelewa vizuri, na zaidi ya wengine wote,
majaribu na vikwazo ambavyo tunakutana navyo katika
maisha tukiwa wafuasi Wake. Lakini tuna mfano Wake
mzuri na tutashinda, “tukimtazama Yesu, mwenye
kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa
ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili
msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa
kuume wa kiti cha enzi cha Mungu” (Waebrania 12:2).
Furaha ya Kristo inajumuisha uelewa kuwa kifo chake
kitaturudisha katika uhusiano wa Mungu, aliye Baba –
Baba yetu wa mbinguni! Sisi waumini ni furaha kwa
Kristo, ni Bibi Arusi mtarajiwa kwa hamu kubwa
(Waefeso 5:25-27; Ufunuo 19:7-9). Kuwaleta wengine
kwa Yesu ili waokoke kupitia Yesu Kristo kutuletee
furaha pia.
Kukamilisha wito wa Mungu maishani mwako
kutakugharimu sana. Kila muumini ana gharama zake:
kuacha utajiri, uchoyo, na matendo ya mwili - na
kubadilishwa tufanane na Yesu.
Unapotoa maisha yako kuishi maisha ya sadaka kwa
ajili ya Kristo, utafanya zaidi ya yale ambayo Baba
anafanya. Utaona nguvu zaidi za Mungu na uwepo wake
kwako. Unapoendelea kuwa mwenye nidhamu na
mwenye imani, utakuwa mwenye ujuzi wa kuziokoa
roho zinazopotea na kuwa mvuvi wa watu (Mathayo
4:19). Utakua katika hekima, na kuwa tajiri katika
mambo ya Mungu. Kumtumikia Mungu kwa maisha
yako kuna thamani kuliko gharama yoyote
(1 Wakorintho 9:19-22)!
Maisha Ya Binafsi Ya Mwinjilisti
Mwinjilisti – kama muumini yeyote, anajitahidi
kuishi maisha safi na yenye mwelekeo mbele zake
Mungu. Ni lazima awe na uhusiano mwema na familia
yake na jamii yake. Matunda ya mwili kama hasira au
kuhukumu, itaonesha vibaya wakati unapohubiri.
Kumtendea mkeo au watoto mambo yasiyo mema
halimfurahishi Mungu, na linaathiri ushuhuda wako kwa
wengine. Kudanganya mtu kunatoa jina mbaya kwa ajili
ya Kristo, ambaye unamwakilisha. Kusema nitafanya
jambo fulani na hatimaye usifanye si jambo la uaminifu
34 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
na si la Kimungu. Tabia yako ya kutenda dhambi ni
lazima ishughulikiwe ili uweze kumwakilisha Kristo
kama alivyo na mambo yatendwayo na nguvu yake ya
kukomboa!
Mwinjilisti apende Biblia na aisome na kujifunza.
Atafute nafasi itakayomwezesha
kuwashirikisha
ukweli wa
Bwana, lakini asiache
wajibu wake wa kutunza
familia au kazi yake ya
asili. Mwinjilisti
anaomba sana - katika
basi, anapotembea, akiwa
katika jumuia ya watu,
au akiwa peke yake,
daima ni vema kuomba
na kumsikiliza Mungu.
Moyo wa mwinjilisti
ni lazima uwe laini na wa
kufundishika. Wakati
unapomngojea Mungu,
atakusaidia umfahamu
zaidi. Wakati unapokua
katika kumjua zaidi,
utakuwa mwinjilisti
mzuri kwa sababu
unamfahamu Baba yako.
Yesu alifanya tu yale
aliyofanya Baba; alisema
tu yale Baba aliyosema
(Yohana 5:19; 8:26).
Shabaha yetu kama wahudumu ni kumjua Mungu kwa
karibu ili tuweze kuongozwa kwa sauti yake na kujua
mapenzi yake.
Kama umeolewa ni lazima umwangalie mwenzi
wako kama ambavyo Yesu angemwangalia, na
kuwapenda kama alivyolipenda Kanisa (Waefeso 5:25).
Mtunze mkeo kwa upole na kwa ufahamu (1 Petro 3:7)
Mjali mumeo kwa heshima na utii (Waefeso 5:33).
Kama hujaolewa lazima uwe na mawazo mazuri na
mwili safi (1 Wathesalonike 4:3-5). Bwana anajua yote
uyatendayo kwa siri zaidi ya masikio na macho ya watu
wengine. Mhudumu ambaye hajaoa au kuolewa
anapaswa kuwa na mawazo na matendo maadilifu. Ni
lazima wakiri makosa yao na kujiweka mbali na vifungo
vya tabia ya dhambi.
Katika mahusiano ya kibiashara, kifamilia, kikanisa,
au kirafiki ni lazima yasiwe na lawama ili kazi ya Yesu
isiwe na kipingamizi au isemwe vibaya. Wengi wetu
tumesikia watu wakipinga wokovu wa Yesu kwa sababu
ya muumini wanayemfahamu hakuwa mpole, haaminiki,
au si mwaminifu. Wamekuwa “kikwazo” kwa sababu ya
matendo ya dhambi ya waumini (1 Wakorintho
10:32-33).
Kama mhudumu unamwakilisha Mfalme wa
wafalme. Maneno yako lazima yawe kweli; ni lazima
utende yale yote uliyoyaahidi. Kama huwezi kwa
maneno yako, na badala yake unatoa udhuru, inaweza
kuwa kikwazo kwa wengine, na kuwafanya wampinge
Kristo. Mnawakilisha Yesu kila dakika katika kila siku,
siyo tu wakati unahubiri, lakini katika kila tendo.
Maneno yako yawe ya kutia moyo, na siyo yaliyojaa
lawama (Waefeso
4:15,29; Wakolosai 4:6).
Mungu anatamani
tuwe vyombo vya
heshima (2 Timotheo
2:21). Huwezi
kuwaandalia wageni
wako katika vyombo
vichafu. Ungependa
uwape chakula katika
vyombo safi. Mungu
anapokea heshima
wakati wewe ni msafi
kiroho na kuwa tayari
kuwa chombo chake.
Kama dhambi, kusema
mabaya, au tabia mbaya
ya maisha yako
hautakuwa unafaa kwa
kazi ya Mungu.
Chukua muda sasa wa
kumtaka Roho
Mtakatifu achunguze
moyo wako. Wakati
anapozungumza nawe,
ukiri, utubu kwa njia ya
maombi, na umruhusu
Yesu aondoe mambo yote machafu. Utakuwa huru na
utatumika kwa Bwana wako. Tubu mbele za Mungu
mara kwa mara. Chukua hali ya chini ili Mungu apate
kukuinua na kukuweka katika makusudi makubwa.
Katika maombi yako, toba na kukiri iwe sehemu ya kila
siku: Mtake Mungu akuchunguze; mwombe akusamehe,
mwombe Mungu akupe uzima.
Ni Lazima Ujifunze Neno La Mungu,
Yaani, Biblia
Biblia ni chanzo chako cha Ukweli. Ni lazima
uisome kila siku, jifunze na kukariri mistari ili uweze
kukua na kukomaa na ufundishe na kuhubiri vizuri.
Usihubiri jambo lolote ambalo haliwezeshwi na
Maandiko yote. Mafundisho ya uongo yamekuwepo
sana siku hizi. Biblia inatuonya juu ya waalimu wa
uongo na mafundisho ya uongo yatatokea siku za
mwisho na wengi watapotoka. Wakati unapojifunza,
chunguza Maandiko kila siku ili kuhakikisha kuwa lile
unalolisikia ni kutoka kwa Neno la Mungu (Matendo
17:11).
Mtu ambaye hajui maneno ya Mungu hawezi kutoa
ushauri mzima wa Kimungu kwa watu. Bwana
anaelekeza, “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na
Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari,
ukitumia kwa halali neno la kweli” (2 Timotheo 2:15).
Chukua muda sasa hivi kumwomba
Roho Mtakatifu kuupeleleza moyo
wako. Wakati anapozungumza na
wewe, ungama, tubu katika sala, na
mruhusu Yesu aondoe uchafu wote.
Utakuwa huru na pia utatumika zaidi
kwa Bwana wako.
NAKALA 14 – NAMBARI 1 –2006 MATENDO/ 35
Kuna mwinjilisti nchini India alikuwa anakariri
mistari ya Biblia kila juma. Watoto wake nao pia
walikariri mistari kila juma. Alikariri maelfu ya mistari.
Alipohitajiwa kuhubiri au kushauri au alipohitaji
hekima, alikuwa ameweka maneno ya Mungu katika
moyo wake. Mtu huyu aliye na nguvu ya Neno la
Mungu ambalo laweza kugeuza watu na kumlinda
mwenyewe kutoka nguvu za uovu (Zaburi 119:11).
Ni Lazima Uwe Ni Mtu Wa Maombi
Maombi katika maisha ya mhudumu au mwanafunzi
wa Yesu hayana uchaguzi - ni agizo la msingi, na
linapatikana katika Maandiko yote! Uwe ni mtu wa
maombi.
Anzisha tabia nzuri ya maombi. Omba katika muda
uliojipangia kila siku. Omba wakati unapotembea au
unapokaa. Omba kila wakati wa usiku na mchana
(1 Wathesalonike 5:17). Omba kwa roho na ufahamu
(1 Wakorintho 14:15). Kufunga na kuomba kunavunja
vifungo vyote walivyofungwa navyo watu na maeneo.
Mwinjilisti mmoja katika Afrika aliyataka makanisa
mbalimbali kufunga na kuomba pamoja. Mikutano hii
iliwasaidia kuunganisha makanisa kwa kusudi maalum
na kuzidisha matokeo ya kiroho. Kazi ya ibilisi
imezuiliwa wakati watu wanapokutana pamoja.
Makanisa yamebadilika na watu wengi wamekuja kwa
Kristo kwa sababu makanisa na wainjilisti wameomba
na kufanya kazi pamoja.
Huwezi kuwa mhudumu au mwinjilisti ambaye
Mungu amekusudia pasipo kuwa ni mtu wa maombi.
Katika maombi unapata uhuru, msamaha, nguvu, na
mwongozo unaoutaka.
Chukua muda wako wa kuomba na timu yako au na
kiongozi mwingine. Tafuta mwombezi na kuwataka
wakuombee kila siku. Chukua muda uombe kila siku na
wenzako na pia omba peke yako, ombea nchi na watu
ambao utawahubiria.
Endelea Kuwa Mwanafunzi
Inaweza kutokea kuwa hakuna uwezekano wa
kujiunga na Chuo cha Biblia au Seminari. Tafuta
mapenzi ya Mungu katika jambo hilo na kulifuata kwa
imani. Kama pana uwezekanao, hudhuria mafundisho
yatolewayo katika semina au masomo ya Biblia katika
eneo lako.
Chukua nafasi uongee na wahudumu wengine na
wainjilisti. Jifunze kutoka kwao, na jitolee utumike nao.
Wako tayari, kutenga muda wa kuwauliza maswali.
Nenda uwasikie wakihubiri. Wasikilize, watathimini, na
jifunze.
Baadhi ya wanaume na wanawake waliofanikiwa
hawakupata elimu ya masomo ya Biblia, hata hivyo
walifanya mambo makubwa kwa Mungu. Wahudumu
wazuri sana ni wale wanaojifunza Biblia kwa uaminifu
na kuendelea kujifunza kwa kadri iwezekanavyo, na
kuyaweka kwa vitendo yale waliyojifunza. Kujifunza ni
zaidi ya kuingia darasani. Kujifunza ni jambo ambalo
linafanyika kwa maisha yote.
Tafuta Mshauri Katika Kristo; Uwe
Mshauri Kwa Wengine
Omba na kumtaka Mungu akupe mwalimu, mshauri
katika Bwana. Huyu ni mtu ambaye amekomaa katika
Mungu, atakayekusaidia kukua. Mshauri anatoa
ushauri wakati anakuangalia katika maisha yako.
Katika nchi nyingi, mtu ambaye ni mchanga kiimani
anamtaka mtu aliyekomaa awe “baba wa kiroho” wake.
Hii inafanyika pia kwa wanawake wanaohitaji “mama
wa kiroho”.
Wajibu wa mtu aliyekomaa ni kumwongoza na
kumfundisha yule aliye mchanga kiimani, awe ni
msaidizi atakayempa hekima. Paulo alikuwa na
uhusiano na Timotheo (1 Timotheo 1; 2 Timotheo 1:2).
Ni jambo la uhakika kuwa Paulo alimpenda Timotheo
na alimtaka Timotheo mzuri. Paulo alikuwa tayari
kujitoa na kuchukua muda kumsaidia na kumfundisha
Timotheo.
Walio wachanga kiimani ni lazima waheshimu
wazima na uzoefu wa wale waliokomaa kiimani. Ni kwa
njia hii hawa wachanga wanapata ujuzi muhimu kwa
njia ya uzoefu na hekima ambayo wengine wamejifunza
kwa miaka mingi. Ni njia ya Mungu kuelimisha
viongozi wa vizazi vijavyo.
Ni lazima uanze kuangalia mtu au watu wawili wa
kuelimisha, ambao watapata faida kutokana na uzoefu
na mafunzo yako (2 Timotheo 2:2). Omba na Mungu
atakuonesha ni nani umwelimishe na kumshauri.
Kukataliwa Na Kujaribiwa
Kazi ya mwinjilisti inamweka katika hali ya
kukutana na watu ambao watakubali au watamkataa
Kristo. Wale watakaomkataa Kristo watamkataa
mwinjilisti pia.
Siyo kila mtu alimkubali Yesu na ujumbe Wake
wakati alipohubiri. Baadhi ya watu watakuwa na hasira
nawe na kukuchukia kwa sababu unaleta Habari Njema.
Baadhi ya wainjilisti watapigwa na kutishiwa maisha
yao kwa kumhubiri Kristo. Hata baadhi ya wanafamilia
wanaweza kuwa kinyume nawe. Yesu alituambia
tutateswa kwa sababu Yake (Mathayo 10:16-20).
Watu watazungumza yasiyofaa na pia kutoa hukumu
za uongo. Ni muhimu usifanye moyo wako kujishitaki
au kukua katika uchungu, kwani utajichafua wewe na
wengine (Zaburi 37:38; Waebrania 12:15). Usije
ukawalaumu watu wengine wanapokushitaki. Usije
ukapenda kulipiza kisasi. Huu siyo mpango wa Mungu
wa kushughulika na majeruhi ya rohoni (Warumi
12:17-21). Hasira ya mwanadamu siku zote haitengenezi
haki ya Mungu (Yakobo 1:20).
Ni lazima kusamehe wale ambao wamekukosea na
kukuudhi (Mathayo 18:21-35). Njoo kwa Mungu kama
ungemjia Baba mpendwa ambaye anakujali na
kukukubali (Warumi 15:7; Waefeso 1:6). Unaweza
kuyatoa majeruhi yako kwa Mungu na pia kumwambia
akuponye (Zaburi 42:4; 62:8). Acha Baba yako wa
mbinguni akufariji, akutengeneze na pia kukujenga
katika majaribu.
36 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
Kama hupendi Mungu ayachukue majeraha yako ya
kukataliwa, ibilisi atayatumia majeraha yako kukuumiza
wakati unahubiri Injili. Utajaribiwa kubadili ujumbe
wako ili upate kushawishi watu wakunje mkono. Biblia
inaita mtego huu kuwa ni “kuwaogopa wanadamu”
(Mithali 29:25).
Kuwa makini pia na
mtego wa mafanikio.
Mafanikio katika uinjilisti
yatakufanya uanze
kujihesabia ushindi na
kuanza kujitwalia utukufu.
Unaweza ukaanguka
katika dhambi ya kujivuna
na kuanza kuhudumu
kimwili. Angalia sana
majivuno (Mithali 11:2;
16:18; 1 Petro 5:5-9).
Lazima tuwe wapole
kwa Mungu pamoja na
majeraha tuliyonayo, tubu
kwa uchoyo na kiburi,
samehe waliokukosea na
umwombe Mungu kwa
uponyaji katika maisha
yetu.
Unapomruhusu Mungu
akuponye utakuwa na
uhakika wa Mungu zaidi
na upendo. Utagundua
kuwa anakupenda na pia
wewe ni muhimu Kwake.
Baadaye utakuwa na uwezo wa kuwapenda
wanaokukataa na kuchukia, katika nafasi uliyonayo
katika Kristo - ambapo ni mahali pa nguvu ya kushinda
na kukubaliwa bila sharti lolote.
Kuwa Na Mpangilio Na Huduma
1) Maono (Dira) Kwa Ajili Ya Huduma
Je, unajua huduma yako inaenda wapi? Je, unayo dira
kutoka kwa Mungu kwa ajili ya kazi yako maishani?
Kama huna, unaweza kumwambia Mungu akupe dira na
mwelekeo katika maisha yako. Kama amekuita na
kukupa kazi ya huduma yake, anapenda kukuonesha
ufanye nini ili kufanikisha hilo!
Katika maono ya pekee, Isaya aliyaona maono ya
Bwana (Isaya sura ya 6). Isaya alikubali hali yake ya
dhambi na alitubu na alibadilishwa. Mungu alimwita
kuwa nabii na kufunua njia na shabaha katika maisha ya
Isaya. Maono kama hayo siyo ya kawaida, na yametokea
kwa watu maalum katika Maandiko ambao Mungu
aliwapa mwito wa pekee (kama Isaya; na Sauli [Paulo]
katika Matendo 9:1-19).
Lakini Mungu amekuita katika huduma yako. Ana
mpango maalum kwako ili uutimilize. Kama
unavyomtafuta kwa bidii na kutumia muda katika sala,
Mungu atakusaidia uweze kuona mapenzi yake katika
maisha yako. Atakupa ndoto au maono. Tena
atazionesha njia zako unavyomtegemea na kumkubali
siku hadi siku (Mithali 3:5-6; Mathayo 6:33).
Yesu alifanya tu yale ambayo Mungu alimfunulia.
Alisema, “Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila
lile ambalo anamwona Baba analitenda; kwa maana
yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile
vile” (Yohana 5:19-20).
Yesu alifanya yaliyo
mapenzi ya Baba.
Hakufanya wala kusema
kila kitu isipokuwa lile
ambalo Baba alimfunulia.
Yesu amekuwa ndiye
ametuonesha mfano wa
kumtegemea Baba kabisa.
Mungu amejifunua
Mwenyewe na makusudi
yake katika Biblia nzima.
Njia mojawapo nzuri sana
ya kumtambua Mungu na
makusudi Yake, ni kusoma
Neno la Mungu mara
nyingi uwezavyo. Biblia ni
“mwanga wa njia yangu”
(Zaburi 119:105). Mwanga
unatuangaza njia zetu,
unatusaidia kuona jinsi ya
kutembea. Mruhusu
Mungu akuoneshe kwa
upya ukweli mtimilifu wa
Maandiko ili akuongoze
katika njia zake.
Mungu aweza pia kukupa mwelekeo maalum,
kuhusu majukumu ya huduma. Je, unataka kuufikia mji
fulani ili watu wapate kumjua Kristo? Je, umeomba na
kumtaka Mungu akupe mpango wake? Je, umetaka
Mungu kama anayo njia ambayo ingewezesha uinjilisti
kufanyika? Au jinsi ya kuanzisha kanisa? Wakati
mwingine Mungu anakupa hatua za wazi kabisa za
kufuata ili kuyafanya mapenzi yake.
Mruhusu Roho Mtakatifu azungumze nawe na
kukuongoza katika kufanya maamuzi – kama ni mahali
gani pa kuhubiri, ni jambo gani la kusema, ni nani
atafanya kazi nawe? Usiwe na hamu ya kujenga
yafuatayo au kuwa na sifa uwe mkuu. Usiwe na hamu
ya kujenga huduma yako au kuwa na “mafanikio”.
Tunafanya kazi kwa matunda ya milele (Yohana 15:16),
si ili tupate thawabu hapa duniani (Mathayo 6:1-4).
Uwe na utayari wa kwenda na kufanya kazi - wakati
na mahali pale Roho akuelekeza, kwa utukufu wa
Mungu. Kila mji au jinsi ni tofauti; hivyo njia ya kufikia
mahali au kundi la watu inaweza kutofautiana.
Mtume Paulo alipewa jinsi ya kufikisha utume wake.
Aliwahubiri Wayahudi kwanza; ndipo akaenda kwa
wasio Wayahudi. Katika safari yake ya pili ya misheni,
alitaka kwenda kaskazini na mashariki; lakini Mungu
akamkataza. Alipata ndoto ambayo mtu kutoka
Makedonia (Ulaya) alikuwa anamwita aende na
Je unajua mtazamo wa
huduma yako?
DIRA
NAKALA 14 – NAMBARI 1 –2006 MATENDO/ 37
kuwasaidia (Matendo 16:9-10). Paulo alikuwa anataka
kuyafanya mapenzi ya Mungu, lakini alikuwa karibu na
kwenda mwelekeo mbaya. Mungu alitaka Paulo na timu
yake kwenda magharibi, Ulaya na kuipeleka Injili.
Paulo, alipofika Makedonia, alimkuta Lidia ambaye
ndiye wa kwanza kuongoka Ulaya (Matendo 16:12-15).
Lidia alikuwa mfanyabiashara, alimpa Paulo nyumba
yake aitumie kwa kazi yake, na kuwa ndilo kanisa la
kwanza Ulaya. Nyumba hii ikawa pia msingi wa
uinjilisti maeneo ya Ulaya. Lidia na wenzake
walimsaidia Paulo katika kueneza Injili. Mungu alikuwa
na mpangilio ulio wazi, lakini Paulo alihitaji kufahamu
mpangilio utakaomsaidia kutimiza kusudi la Mungu.
Mngoje Bwana, mwombe na kujitoa mbele Zake.
Mwimbie Yesu; msifu; mwaga moyo wako wote Kwake;
na hatimaye ngoja umsikie Yeye. Mungu ataachilia
kusudi lake kwako. Mungu anaweza kukupa maono
maalum au mpangilio, au kuyafunua mapenzi yake
katika picha za kiakili au kwa maneno na kuziweka
katika mawazo yako. Yaandike yote, pamoja na tarehe,
Mungu aliyokuambia na kukuonesha. Yaombee haya
yote na yaweke yote mbele ya watu wa kiroho ambao
unawaamini. Anza sasa kuchukua hatua ya imani
kufanya yale ambayo Mungu amekuonesha uyafanye!
2) Maelezo Ya Taswira
Mara unapoanza kuona mwelekeo na dira, inasaidia,
ukiandika maelezo ya taswira. Maelezo ya taswira
yanakueleza kwa kifupi lile ambalo umeitwa kwalo.
Maelezo haya yanasaidia sana kama yatatolewa kwa
ujumla kuliko kuwa na mambo madogo madogo. Kwa
mfano, badala ya kuandika “Tutaanzisha makanisa
matano na nyumba za yatima mbili na kuwa na
mikutano mwaka huu”, ingekuwa vizuri kama
ungeandika, “Tutaeneza Injili kwa kuanzisha makanisa
na kufanya kazi za kijamii kama Mungu atakavyotuelekeza,
ili Yesu atukuzwe.”
Tenganisha maeneo ya kazi na kuyawekea malengo
maalum na yaandike yote. Kwa mfano, kama Mungu
amekupa wito wa kuanza shule, iweke kwenye maelezo
yako pia.
3) Malengo
Baada ya kuandika maelezo kwa njia ya maombi,
elezea kimaandishi jinsi ya kufikia dira na taswira ili
zifanyike. Je, una mpango wa kuifanya? Andika
malengo yote ambayo unakusudia kukamilisha. Huo
ndiyo wakati wa kuwa na mambo madogo madogo
zaidi.
Kwa mfano: “Baada ya muda wa miaka miwili
tutaelimisha wachungaji wawili na kuanzisha makanisa
mawili katika eneo hili; baada ya miaka mitano
tutakuwa na makanisa matano zaidi.” Au, “Kundi letu
litahubiri Injili kwa kila kijiji katika eneo hili - katika
kijiji kimoja kwa mwezi, kwa miaka mitatu inayofuata.”
Au, “Tutasambaza vipeperushi 10,000 katika miji kwa
miezi sita ifuatayo. Pia tutakuwa na mikutano ya
uinjilisti katika maeneo yote manne ya mji kila juma.”
Kuwa na utaratibu mzuri unasaidia kuwezesha kazi
kufanyika kwa vizuri. Kwa njia ya maombi na
kumsikiliza Bwana, utajua mpango wake kwa ajili
yako. Mungu atakupa njia ya kusaidia makanisa
waweze kufanya kazi ya uinjilisti kwa pamoja.
Maelezo ya taswira yako na malengo yako ni
muhimu yaeleweke kwako, katika mawazo yako, na uwe
tayari kumwambia mtu yeyote atakayekuuliza. Ni
muhimu kuombea maandiko haya mara kwa mara na
kuwa na nia ya kubadilisha au kurekebisha ifanyike
hivyo kama ni lazima.
Kumsikia Mungu na kufanya mambo yote kwa imani
itakufanya uwe na mafanikio katika kukamilisha kusudi
la Mungu kwako. Wengine wataona ni rahisi kuelewa na
kukuwezesha na kazi yako.
Kujenga Timu Ya Uinjilisti
Yesu alijenga kundi la watu kumi na wawili. Yesu
aliwatuma watende kazi yake wawili wawili nao;
walikuja tena kutaka maelekezo na mahusiano, na
kwenda tena. Mtume Paulo alijenga pia timu zake.
Wakati mwingine alikwenda mwenyewe, lakini
alipendelea kufanya kazi kwa timu.
Kila mtu katika timu yake atakuwa na karama tofauti
na wewe. Hii itaongeza mafanikio zaidi katika huduma.
Mwinjilisti mmoja alikuwa na mwanamke katika
timu yake aliyekuwa na karama ya kuponya. Mtu huyu
mara nyingi aliona nguvu ya Yesu na kutenda miujiza ya
kuponya katika mikutano yao. Watu wengi
wanafunguliwa katika Injili wakati wanapomuona Yesu
akiponya watu kwa njia ya huduma ya mwanamke huyu.
Mwanamume mwingine katika timu alikuwa na uwezo
wa kuandaa mikutano mikubwa ya kiroho katika miji.
Mwinjilisti huyu aliwaelimisha wainjilisti wengine
katika timu yake. Kulikuwa na wainjilisti watatu katika
timu hii ambao walikuwa wakihubiri katika magulio,
wanaotembelea wafungwa vifungoni au hospitali, au
walifanya mambo ambayo yalihitajika katika kuwashirikisha
wengine ujumbe wa wokovu.
Kuwainua na kuwatia moyo wafanyakazi inasaidia
kuiwezesha Injili kufikia wengi na kuwa na mafanikio
makubwa. Timu inakuwa kama familia ambako mahitaji
yote yatumike na malengo ya taswira yanatimilizwa.
Kuwa Mtumishi Wa Ufalme
Mungu hamuiti mtu yeyote awaye yote kujenga
huduma yake mwenyewe. Mungu amekuita kwa
makusudi yake, na amekuruhusu wewe kuwa mbia wake
kama Yesu anavyojenga Ufalme wa Mungu!
Viongozi wengi wa kanisa wanataka kumtumikia
Mungu, lakini wanataka watengeneze jina kubwa kwa
wao wenyewe. Wanadharau na kukatisha tamaa viongozi
wengine na wahudumu. Ni wachoyo na hawataki
kuwatumikia wahudumu wengine kama mbia.
Wanafikiri utumishi wao ni mzuri zaidi, na kazi yao
ndiyo kazi pekee muhimu. Na hii ni chukizo kwa dunia
na Kanisa! Kiongozi wa namna hii hulenga zaidi
maslahi yake mwenyewe na siyo mahitaji ya wengine,
38 / MATENDO NAKALA14 – NAMBARI 1 – 2006
na pia siyo kwa Ufalme wa kweli wa Mungu. Hii siyo
Roho ya Kristo.
Kushiriki na watu wengine na wahudumu wengine
kunaleta utukufu mkubwa kwa Mungu na ufanisi mzuri
zaidi katika kazi. Kutia moyo na kuwasaidia wahudumu
wengine kunaleta baraka kubwa za Mungu katika
utumishi wako. Unapotoa, unapokea (Luka 6:38).
Wakati unapopoteza maisha yako (na matakwa yako)
kwa ajili ya Kristo, utapata maisha ya kweli (Mathayo
16:25). Wakati unapochukua “nafasi ndogo” ya
kutumikia wahudumu
wengine na huduma
zingine, Mungu
atakupandisha cheo (Luka
14:10-11).
Maono yako yanatakiwa
yawe na uwezo wa kufanya
kazi na makundi mengine,
makanisa, na huduma
mbalimbali. Hii ni kujenga
Ufalme mkubwa wa
Mungu na siyo kanisa
moja, dhehebu au huduma
moja. Wakati wahudumu
wanapofanya kazi pamoja,
watu wanaona umoja wa
Mwili wa Kristo na baraka
za Mungu zinakuja (Zaburi
133:1-3). Wainjilisti
wanajikusanya pamoja na
kufanya kazi katika
makanisa yaliyo mengi
katika miji na kuleta baraka
nyingi katika mji huo.
Tenga Muda
Kupumzika
Wafanyakazi wengi wamechoka kama ukuni katika
moto maana hawakuchukua muda wa kupumzika. Miili
yao huugua; mawazo yao huchoka; roho zao hufifia; na
pia kushindwa kuhimili majaribu. Mungu ameamuru
kuwa tupumzike siku moja kwa juma. Sote tunahitaji
mapumziko.
Kila muhudumu - na kila mtu - anahitaji mapumziko
angalao mara moja kwa juma kujirudisha upya kwa
Mungu na kupumzisha mwili wake, mawazo yake na
roho yake.
Kuna wakati ratiba yako inahitajika sana zaidi ya
kawaida. Utumike lakini ni lazima utenge muda wa
kupumzika na utafute matendo ambayo yanaburudisha
mwili wako.
Wakati Yesu na wanafunzi wake walipohudumu,
watu wengi walikuwa wanaingia na kutoka hata wakati
mwingine Yesu na wanafunzi wake hawakuwa na muda
wa kula. Yesu aliwambia, “Njooni ninyi peke yenu kwa
faragha, mahali pasipokua na watu, mkapumzike
kidogo” (Marko 6:31).
Mara kwa mara Yesu alikuwa na muda wa 􀂄
Shirikiana na watu pia wahudumu
wengine kuleta utukufu mkubwa kwa
Mungu na ufanisi mzuri wa kazi.
kupumzika na pia kufanya sala. Yeye ni mfano kwetu
kuwa hakuna asiyeruhusiwa na Mungu kupumzika.
Chombo Cha Heshima
Kumbuka kuwa watu watapokea zaidi uyasemayo
endapo watakuheshimu wewe kama ulivyo na
unavyoishi katika maisha yako. Kujiweka chini ya
maongozi ya Ufalme wa Mungu ni jambo la muda
mrefu. Unatakiwa siku zote ukue, ujifunze, na pia ujitoe
kwa kazi ya Mungu inayolenga kwako.
Mwinjilisti, Mungu
amekuita kuubeba ujumbe
Wake wa ukombozi kwa
watu wengine. Unaweza
ukawa mfano hai wa
mabadiliko mazuri
ambayo ujumbe wa
Mungu unaweza kufanya
katika maisha ya mtu.
Chunga sana maisha yako
yawe safi na pia angalia
mwelekeo na tabia yako.
Mungu anajishughulisha
na mabadiliko ya maisha
yako kwa jinsi ambavyo
wewe unajishughulisha na
kutafuta msaada Wake.
Atakupenda na
kukuwezesha wewe na
kazi yako kwa
kukubadilisha wewe
kutoka ndani. Ni lazima
utii na kulifuata Neno
Lake. Jipe muda wa
kutosha kujichunguza
mbele za Mungu na
kuitikia maneno Yake na
kuyaacha yafanye kazi katika maisha yako na familia
yako. Kwa kufanya hivyo utakuwa mwinjilisti na
mhudumu mzuri wa Injili aliye chombo cha heshima na
amfaaye Bwana wake!
Mambo Yaliyo Muhimu Zaidi
Tabia yako – itakavyokuwa ni kitu muhimu sana
mbele za Mungu zaidi ya kitu chochote ungefanya kwa
ajili yake. Mungu anajali zaidi jinsi ulivyobadilishwa
kufanana na Yesu zaidi, kuliko kiasi cha kazi
unachoweza kumfanyia.
Utii na kujitoa kwako kwa Mungu ni kitu muhimu
sana kwake zaidi ya mikutano mingi yenye mafanikio na
wingi wa watu. Mwamko wa kumwonesha Yesu katika
utukufu wake, nguvu, uweza wake ni muhimu kuliko
kujitengenezea sifa. Yaweke mawazo hayo akilini
mwako kila siku katika huduma yako. Miongozo hii na
mafundisho haya yanalenga kukusaidia wewe uwe mtu
mwenye uwezo kwa Kristo Yesu Bwana wetu. Tumia
wewe mafundisho haya na umwamini Mungu akutumie
kwa malengo na utukufu wake!
Unahitaji Kufanya Upya Kibali Chako Cha MATENDO?
Hapa ni maelezo ya kujua:
Angalia katika kibandiko kilicho juu ya bahasha ya MATENDO. Juu kabisa upande wa kulia wa
kibandiko ni TAREHE (mwezi/mwaka) wa kumalizika baada ya neno "EXPIR".
Ikiwa tarehe hiyo ni CHINI YA MIEZI SITA tangu sasa, basi, huu ni wakati wa kufanya upya!
Hupaswi kuandika kila mara unapopokea toleo la MATENDO; unatakiwa kujaza tu IWAPO kibali
chako cha miaka miwili kitaishia katika miezi sita ijayo.
Jinsi ya kufanya upya kibali chako cha MATENDO cha miaka 2:
• Kata kipande cha "Fomu Ya Kuomba Kuendelea Kupokea Gazeti La Matendo" hapo chini
(au nakili kwenye karatasi nyingine);
• Fuata maelekezo YOTE katika hiyo fomu (zungushia duara majibu ya NDIYO au HAPANA);
• Jibu maswali YOTE yaliyomo kwenye fomu - andika vizuri kwa herufi kubwa; na
• Utume bila kuchelewa fomu uliyojaza kwa ofisi ya World MAP.
ANGALIZO:
Gazeti la MATENDO sio "Masomo kwa njia ya Posta".
Hutapokea "cheti" au "stashahada" baada ya kusoma
MATENDO. Ni tumaini na maombi yetu kuwa unapokea
kilicho bora zaidi. Mafundisho yaliyo ya kiBiblia na
mafunzo ya huduma kivitendo! Hili litakutayarisha
wewe kuwa na ufundishaji ulio mzuri, kuhudumia na
kuwahubiria wengine. MATENDO hutumwa bure kwa
viongozi wa kanisa wanaoomba kulipokea katika Asia,
Afrika na Latini Amerika. Viongozi wa kanisa watapokea
MATENDO kwa miaka miwili; kisha wanatakiwa kujaza
upya kibali chao ili kuendelea kupokea MATENDO kwa
miaka miwili zaidi.
1. Kwa kuwa kibali changu cha gazeti la MATENDO kitamalizika katika muda wa miezi sita ijayo, ninahitaji kuomba upya
kibali changu: (Zungushia duara kwenye jibu lako.) NDIYO HAPANA
2. Namba yangu ya kibandiko cha MATENDO ni LABL NO: _____ _____ _____ _____ _____ _____
(Namba hii inapatikana sehemu ya juu, upande wa kushoto wa kibandiko kilichoko juu ya bahasha ya MATENDO, baada ya "LABL NO".)
Tarehe ya kumalizika kwa muda wa kupokea gazeti la MATENDO ni: EXPIR ______ / ______
(Tarehe hii inapatikana sehemu ya juu, upande wa kulia , baada ya "EXPIR".) mwezi mwaka
3. Mimi ni kiongozi wa kanisa katika Afrika na ninahubiri au kufundisha neno la Mungu kutoka kwenye Biblia kwa kundi la
watu wapatao 20 au zaidi kila wiki. (Hii ni LAZIMA iwe ni kweli ndipo uweze kupokea Gazeti la MATENDO au kitabu
cha Fimbo ya Mchungaji.) (Zungushia duara kwenye jibu lako.) NDIYO HAPANA
4. Je, unayo nakala ya (kitabu cha) Fimbo ya Mchungaji katika lugha yoyote? (Zungushia duara kwenye jibu
lako.) NDIYO HAPANA
5. Unaomba nakala ya (kitabu cha) Fimbo ya Mchungaji? (Zungushia duara kwenye jibu lako) NDIYO HAPANA
6. TAFADHALI ANDIKA JINA NA ANWANI YAKO HAPA CHINI. ANDIKA ISOMEKE VIZURI, KWA HERUFI KUBWA.
Jina:
__ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __
Anwani:
__ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __
__ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __
Mkoa/Jimbo:
__ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ Nchi: __ __ __ __ __ __ __ __
Wadhifa (au wajibu) wangu katika kanisa ni:__ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __ __
Sahihi/saini yangu:: ________________________________________ Tarehe ya leo: _________________________
7. Nakala hii ya MATENDO ilikuwa: ___rahisi kueleweka ____ngumu kueleweka ___inasaidial ___ haisaidii
Tuma fomu yako kwa: WORLD MAP, PO BOX 721, ARUSHA, TANZANIA
Hakikisha umeomba
upya kibali chako
mara moja baada ya
kila miaka miwili ili
usikae na kungojea na
kujiuliza: "Nakala
yangu ya gazeti la
Matendo iko wapi?"
FOMU YA KUOMBA KUENDELEA KUPOKEA GAZETI LA MATENDO / FIMBO YA MCHUNGAJI - zungushia duara NDIYO/HAPANA
SW 14/1
Omba kupatiwa nakala
yako ya zana ya mafunzo
yenye uwezo kutoka
World MAP!
Fimbo ya Mchungaji - yenye
kujulikana kwa wengine kama
"Shule ya Biblia katika
Kitabu" -- ni kitabu chenye
kurasa 1000 kilichotayarishwa
kwa kusudi la kuwafunza na
kuwaandaa viongozi wa kanisa.
Kimejaa maandiko ya waandishi
wengi yaliyojaa upako wa
Roho, na yenye msingi wa
kiBiblia. Kitabu hiki kimeandikwa
kwa kusudi la kukidhi
mahitaji maalum ya viongozi
wa kanisa wafanyao kazi Asia,
Afrika na Latini Amerika.
NDANI ya kitabu hiki kimoja, yaani Fimbo ya Mchungaji, utapata:
[1] Kitabu Kidogo Cha Malezi Ya Waamini Wapya ambacho kinakupatia masomo yote ambayo inapasa
uwafundishe watu wote wapya wanaookoka.
[2] Mwandani Wa Biblia wenye maelfu ya rejea za Biblia zinazoshughulikia masomo makuu 200 katika
Biblia. Sehemu hii katika Fimbo Ya Mchungaji, itakusaidia katika kufundisha wengine Biblia.
[3] Mwongozo Wa Kufunza Viongozi chenye masomo mazuri mno ya kufunza viongozi yaliyochapishwa
na World MAP kwa zaidi ya miaka thelathini.
Yote hayo na zaidi yamo katika kitabu kiitwacho Fimbo Ya Mchungaji.
Ili kuweza kupokea nakala yako ya kitabu hiki cha mafunzo ya uongozi yenye uwezo, yaani Fimbo Ya
Mchungaji, soma kwa makini na ujaze Fomu ya Maombi iliyoko nyuma ya ukurasa huu wa mwisho (au
andika vizuri kwa HERUFI KUBWA maswali hayo yote katika karatasi ya pembeni iwapo hutaki kukata
gazeti lako).
Mara baada ya kujibu kila swali, na kuandika mwitikio wako kwa wazi kama iwezekanavyo, tuma fomu
hii kwa ofisi ya World MAP iliyo karibu. (Anuani imeoneshwa kwenye Fomu ya Maombi.) Utapokea
nakala yako ya Fimbo Ya Mchungaji upesi iwezekanavyo (lakini kwa kuwa wakati mwingine usafirishaji
ni wa polepole, tafadhali ruhusu kama miezi 6 hivi ili Fimbo Ya Mchungaji ikufikie.) Asante sana.
For private circulation

No comments:

Post a Comment