Friday 5 December 2014

UPONYAJI WA ROHO
Dr. Arlin Epperson
Columbia, Missouri USA
573 449 1045
aepperson@ccis.edu
www.healingofthespirit.org
www.healingofthespirit.org/text_only/
2011
Ukurasa1Uponyaji wa Roho - Utangulizi1Kutambua Milango Iliyo Wazi2Kuponywa kwa Dhambi Zetu93Kuponywa kwa Kutosamehe134Kuponywa Dhambi za Zinaa & Viunganishi Nafsi225Kuponywa Kuharibu na Kutoa Mimba316Kuponywa Uchawi337Kuponywa Talaka398Kuponywa Laana419Kuponywa Athari za Ukoo529.1Jedwali la Ukoo - Genogramu6910Kuponywa Ulimi7011Kuyponywa Viapo na Kujitakia Kifo7412Kuponya Vyombo na Mahali7713Uponyaji wa Athari za Kuhusika Bila Kukusudia8514Kuponywa Ufukara8715Kuponywa Kiburi104 Milango ya Uponyaji wa Ndani16Uponyaji wa Maumivu, Hisia na Kumbukumbu10817Kuponywa kwa Kutusiwa Kingono11618Kuponywa kwa Kukataliwa11919Kuponywa kwa Kiwewe13220Kuponywa kwa Mtazamo wetu wa Sura ya Mungu134 Kufunga Milango21Uponyaji Unahitaji Toba14022Kuponywa Kutokana na Athari za Giza14323Sababu za Kutoponywa15624Jinsi ya Kulinda Uponyaji Wako158 Mambo ya Ziada25Nguvu za Uponyaji Kwenye Ushirika Mtakatifu16226Uponyaji wa Mwili16627Kuliweka Kanisa Lako Huru18028Wito wa Makanisa Kuponya19429Mafuta ya Kuwekwa Wakfu19730Maswali Ishirini20031Milango Iliyo Wazi201YALIYOMO
1
#01 Uponyaji wa Roho - Utangulizi www.healingofthespirt.org
Uponyaji wa Roho —Utangulizi
Muhtasari wa Kozi
Nia ya kukitoa kitabu hiki ni kuwaelimisha waumini kuhusu njia kamili ya kupata upo-nyaji wa kiroho. Maandiko yametoa ukweli uliofichika kwa jicho lisilokuwa na ujuzi, ukweli katika maandiko unaokusudia “kutuweka huru” (Yohana 8:31-32). Kama alivyothibitisha Mfalme Daudi, Mungu anataka “kweli ya moyoni” (Zab. 51:7).
Kwa wanaoamini na wanaolijua Neno la Mungu, kufafanua ukweli huu na kuufahamu hutuwezesha kujua vizuri namna ya kutumia mpango wa Mungu katika njia ya kupata uponya-ji. Kama alivyosoma Kristo na kutimiza Isaya 61, alitangaza kwamba Mungu alikuwa amem-tuma (mbali na kazi nyingine) “kuwatangazia mateka uhuru wao.”
Kitabu hiki kinajaribu kuonyesha ukweli wa Mungu kuhusu sehemu nyingi za utumwa ambazo mtu anaweza kujikuta ndani, kisha aweze “kuwekwa huru,” kwa kweli. “Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli” (Yohana 8:36). Kitabu hiki kimekusudiwa kuwa mwongozo ambao mtu anayetaka uhuru kutokana na utumwa, ataweza kukitumia kujisaidia na pia ni kitabu cha mwongozo cha waombezi, wachungaji, na wahudumua wa ukombozi wanao-waombea watu walio utumwani.
Baada ya mtu kumpokea Yesu Kristo kwa moyo wake wote, ni lazima awe tayari kuon-doa maishani mwake kitu chochote kinachoweza kumzuia Roho Mtakatifu kufanya kazi kika-milifu maishani mwake. Kwa hivyo, mtu huyo anatakiwa kujua ni sehemu zipi za maisha yake bado ziko utumwani; hatuwezi kukiweka kitu huru kabla ya kitu hicho kutolewa.
Ukombozi si kufanya kelele! Bali ni kutaka kugundua ni kitu gani kinampa adui mam-laka ya kubaki katika maisha ya mtu huyo. Nia ya Mungu ni kutaka kuwarudisha wanadamu katika mfano wake na sura yake. Neno la Kiebrania na Kigriki linaloeleza “wokovu” lina maa-na ya: usalama, uhifadhi, uponyaji, na timamu.
Mtu akiwa katika utumwa wa kiroho ni sawa na mtu kufungwa na minyoro au kamba. Mnyororo au kamba inawakilisha sehemu mbalimbali katika maisha ya mtu iliyo utumwani. Sababu ya utumwa huo ikigunduliwa, na mtu huyo akanushe miungano hiyo, kamba hizo huka-tika, moja baada ya nyingine. Baada ya kamba au miungano hiyo yote kukatika, pepo hatakuwa na kitu chochote cha kushikilia, hivyo basi ataamriwa kuondoka. Tunaweza kumwamuru kwa kusema, “Miungano hiyo imevunjwa sasa. Lazima uondoke katika jina la Yesu.” Na mtu huyo atakuwa huru kwa utukufu wa Mungu.
Waumini wengi hawajafunzwa, kwa hivyo hawajui kwamba kabla ya kumjua Bwana Yesu, maisha yao—au sehemu ya maisha yao—ilikuwa chini ya bwana mwingine. Waumini hao hawajawahi kuongozwa ili wachukue au wakanushe mamlaka waliyokuwa wamempa adui, ambaye bado anashikilia nafasi yake—kwa kiwango fulani—na ambaye ataendelea kute-tea haki yake kwa dhati wakati wowote inapowezekana, na hivyo basi humkandamiza muumi-ni. Mamlaka yoyote ambayo hayajatolewa kwa Yesu hudaiwa na Shetani. Roho waovu wana-weza tu kuishi mahali ambapo wana mamlaka. Kila mara Shetani husimama upande wetu wa kulia akiwa tayari kutufunga, tukimruhusu kufanya hivyo. Tukibomoa ukuta wetu tutaumwa na nyoka (Mhu. 10:8).
2
#01 Uponyaji wa Roho - Utangulizi www.healingofthespirt.org
Mbona Tuhubiri, Tufunze na Tuhudumu Uponyaji wa Ndani na Ukombozi?
Wakristo wengi hawatambui wala hawajui kwamba wako utumwani, na pia wana ngome na “lango” au “mlango” unaoiruhusu giza kuwaathiri. Wosia uliota-jawa katika Hosea 4:6 bado unatumika hata leo: “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.”
Mojawapo ya kusudi la Kristo kuja duniani lilikuwa ni kuharibu kazi za shetani (I Yohana 3:9-10). Kwanza alikuja “kuwahubiria maskini habari njema” (wanaokandamizwa kiroho, Luka 4:18) na “kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao” (Luka 4:18; Isa. 42:7, 49:9 na 61:1), halafu, pili, “kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa” (Luka 4:19, Isa. 61:2). Utaratibu huo ni muhimu sana.
Kuwa watumwa wa dhambi hututenganisha na Mungu. Utumwa hutupofu-sha na kutuzuia kuona na kusikia Neno la Mungu (Isa. 6:9-10, 42:7-9, 42:18-20, Mat. 13:15, 2 Cor. 4:4), na utumwa hutufanya tupoteze habari njema tuisikiayo (kama ilivyotumika katika Mfano wa Mpanzi, Mat. 13:13-17). Tunapowahudu-mia watu huwa tunawaruhusu kusikia Habari Njema na hivyo basi kuuondoa utumwa, ili Habari jema iweze kupandwa ndani ya ardhi yenye rutuba na itapewa nafasi kubwa ya kukua.
Sababu zengine za kuhubiri, kufunza na kuhudumu ni:
1. Kufukuza mapepo ni ishara ya kwanza iliyotajwa itakayowafuata hao waaminio (Marko 16:17).
2. Tunatakiwa kuufuata mfano wa Kristo, ambapo sehemu moja kwa tatu ya huduma ya Kristo ilidhihirishwa kwa kuwafukuza mapepo.
3. Yesu aliwafukuza mapepo ili aweze kuuleta Ufalme wa Mungu kwa wa-naomtafuta Yesu (rejelea tamko la Yesu katika Mat. 12:28).
4. Yesu aliwafukuza mapepo kuonyesha kwamba Ufalme wa Mungu si ma-neno matupu bali ni nguvu (tazama Mat. 6:13, 28:18, 10:1 na 12:28).
5. Tunahubiri, tunafunza, na kuhudumu ili kuwaweka watu huru, ndiposa wa-pate “taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombo-lezo, vazi la sifa badala ya roho nzito.” (Isa. 61:3).
Falme Mbili
Maandiko yanatufunza kwamba, kabla ya kuchukuliwa mimba tumboni mwa mama ze-tu, Mungu alitujua (Yer. 1:5, Efe. 1:4-5). Mungu anaijua hesabu ya nywele zilizo kichwani mwetu (Luka 12:7). Alituumbwa kwa upendo. Tangu mwanzo Mungu alitaka tuwe wazima: kiroho, kihisia, na kimwili. Pia utaratibu huo ni muhimu kama ilivyotambuliwa hapa chini.
Mungu aliwaumba Adamu na Hawa wakiwa na uzima kamili, kwa mfano wake na sura yake (Mwa. 1:26); akawapa mamlaka juu ya ulimwengu (Mwa. 1:28). Magonjwa na maradhi hayakuwa katika Bustani la Edeni. Mwanadamu alipoumbwa hapo mwanzo, hakuumbwa kuwa mgonjwa wala kufa. Kwa hivyo tunajua kwamba mapenzi kamili ya Mungu ni kututaka tuwe
3
#01 Uponyaji wa Roho - Utangulizi www.healingofthespirt.org
wazima kiroho na kiafya. Isitoshe, katika maandiko, sifa za Ufalme wa Mungu dhidi ya sifa za Ufalme wa Giza zimeonyeshwa.
Ufalme wa Mungu: Ufalme wa Mungu ni wa upendo, kukubaliwa, na msamaha. Yeye hutupa fadhila na neema. Yeye ni Mungu wa tumaini lote. Yeye ni amani yetu. Hata-tuacha kamwe. Yeye ni mkombozi wetu (Rum. 11:26, Mat. 6:13), aliyeziharibu “kazi za giza” (uovu).
Ufalme wa Giza: Shetani alikuja, akaleta kutotii, uasi, dhambi, maradhi, utengano, uchungu, na mateso. Yeye anajulikani kama “mtawala wa ulimwengu huu” (Yohana 14:30). Tunajua kwamba ufalme wa Shetani ni mahali pasipokuwa na upendo, furaha, amani, kukubaliwa, na msamaha; makusudi yake ni kuiba, kuua, na kuharibu (kama ilivyo katika Yohana 10:10 na vifungu vingine). Katika Ufalme wa Giza, kuna kukata-liwa, kuishiwa imani, uharibifu, udanganyifu, mgawanyiko, na kukata tamaa.
Tunajua kwamba kabla mwanadamu hajaumbwa na kuwekwa nchini Ibilisi alifukuzwa mbinguni hadi nchini. Alipofika nchini Shetani akaendelea na uasi wake kinyume cha Mungu kwa kumdanganya mwanadamu amuasi Mungu. Mwanadamu akamtenda Mungu dhambi na kutengwa na uwepo wa Mungu. Hapo basi ikawa mwanadamu amejiweka chini ya mamlaka ya shetani na mapepo wake. Shetani ana mpango wa kuiba, kukua na kukuangamiza nafsi yako (Yohana 10:10). Kwanza anataka kuondoa imani yetu kwa Mungu, lakini akishindwa na hili basi anafanya kila jitihada kuhakikisha hatumjui Yesu kama mwokozi wetu. Akishindwa na hili basi anatafuta njia ya kutatiza huduma yetu ndani ya Kristo.
Ufalme wa Mungu na ule wa uovu unapigania roho na nafsi za wanadamu hapa duniani. Lakini Mungu hapendezewi viumbe vyake vitii nguvu za giza, hivyo basi ametoa njia ya wokovu kwa kumtuma mwanawe wa pekee Yesu ulimwenguni ili atuonyeshe njia. Kupitia kwa ujumbe wa Yesu na kazi yake msalabani tunapata nguvu kinyume cha giza, kukombolewa na kuwekwa huru.
Mamlaka Tuliyopewa na Mungu.
Lazima ushawishike kuhusu ushindi wa kazi ya Kristo msalabani, aliposhinda nguvu za giza (Warumi 8:38-39). Maandiko yanatuambia “Yesu akawajia na kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.. (Math 28:18)
“juu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali na katika ule ujao pia.Naye Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya miguu Yake na amemfanya Yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili ya Kanisa. “ (Efe 1:21-22)
“Mungu akiisha kuzivua enzi na mamlaka, alizifanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuzi-buruta kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba wa Kristo.”. (Kol 2:15)
Yesu aliwapa uweza na mamlaka haya wale (Math 10:1) wale 70 (Luka 10:9,19) na pia kwetu sisi. (Mark 16:17-18) Mamlaka ambayo giza linayo ni yale ambayo wewe au mtu mwingine amelipatia. Kila unachokubaliana nacho unakipa uweza
4
#01 Uponyaji wa Roho - Utangulizi www.healingofthespirt.org
Sisi tunafsi moja ndani ya Kristo, yeye yupo nasi, na ndani yetu. Kuungana kwetu na Kristo kulifanyika tulipopokea wokovu. Ninyi na Kristo ni nafsi moja. (Tazama War 6, 8, Efe 2, 4, Gal 2:20). Tunapaswa kuwa na hakika sisi ni kina nani ndani ya Kristo na kuwa tuna mamlaka kamilifu kinyume cha nguvu za giza tuliyopewa na Yesu Kristo.
Kumbuka kuwa mapepo hawaumbwi tena, hesabu yao ni ile ya tangu awali kama walivyokuwa nyakati za Yesu Kristo ilhali hesabu ya watu ulimwenguni inaongeze-ka kwa mabilioni. Licha ya hayo tunajua kutoka kwa maandiko kwamba kwa kila pepo kuna malaika wawili. Kwa kuwa Yesu ana mamlaka yote , (Math 28:18) sheta-ni anabaki mkono mtupu. Mamlaka yote tumepewa sisi, shetani ana mamlaka yale ambayo sisi tumemruhusu awe nayo.
Ombi la Mamlaka
Mimi ni mwana wa Mfalme, mrithi pamoja naYesu. Kila alicokinunua Yesu na kuki-lipia ni urithi wangu. Nimeunganika na Yesu, nimesulubiwa pamoja na Kristo. Nili-kufa, nikazikwa na kufufuliwa pamoja naye. Sasa nimeketi naye katika mbingu ma-hali palipo juu kuliko mamlaka wala jina katika kizazi hiki na kile kijacho. Ninachu-kua mamlaka ya Kristo juu ya maradhi, dhambi, mapepo na ulimwengu. Mimi ni chumvi na nuru ya dunia. Nashinda giza kwa silaha zote za Munga, nasimama imara nikiwa nimejifunga kweli kiunoni na kuvaa dirii ya haki kifuani, miguu yangu niko tayari kwa Injili ya amani. Nimeitwaa ngao ya imani, ambayo kwayo nitaweza kui-zima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Nimevaa chapeo ya wokovu na kuu-chukua upanga wa Roho, ambao ni Neno la Mungu. Silaha zangu si za mwili bali zina nguvu ya Mungu ili kuvunja viambaza vya giza. Nayaweza yote kwa Kristo-maana yeye aliye ndani yangu ana nguvu kuliko aliye ulimwenguni (imetungwa na Rodney Hogue)
Jinsi Giza Huingia
Adamu na Hawa walisikiliza uwongo wa Shetani na kuruhusu dhambi kuingia katika ulimwengu mzuri wa Mungu, na wakasababisha wanadamu wote kurithi madhara ya dhambi, ukiwemo ugonjwa na kifo.
Kwa vile Mungu alijua tungezaliwa katika ulimwengu ambao mtawala wake (Shetani) ni mwovu, Mungu aliunda “ukuta” wa kiroho (kama inavyoonyeshwa ka-tika Ayubu 1:10) wa kutuzunguka na kutukinga na athari zote za uovu huo (Ayubu 1:10 na 2:4-6). Hata hivyo, Mungu hutupa silaha ya kiroho ili tuweze kujikinga (Efe. 6:13-18). Pia, malaika wa Mungu hutuzingira ili waweze kutuhifadhi na kutu-linda (Zab. 34:7 na 91:10-12).
Sisi sote tumezaliwa na ukuta wa kiroho kama Ayubu, lakini kwa sababu ya dhambi ya kwanza ya Adamu na Hawa (na dhambi zilizofuata), tuna milango wazi katika ukuta wetu inayomruhusu Shetani kututesa, kama alivyomtesa Ayubu. Milan-
5
#01 Uponyaji wa Roho - Utangulizi www.healingofthespirt.org
go hiyo iliyo wazi husababishwa na mambo mengi: sababu za kawaida zimeorod-heshwa hapa chini lakini nyingi zitatajwa katika sehemu zengine za kitabu hiki:
• Dhambi zetu wenyewe (uovu, uwongo, wizi, kiburi, n.k.)
• Kutosamehe
• Kujihusisha na mizungu/ushetani (mambo yasiyoonekana) au shughuli za kipepo
• Dhambi ambazo wengine wametutendea (kimwili, dhuluma ya kimapenzi, kukataliwa, n.k.
• Majeraha na machungu ndani ya roho zetu
• Dhambi za kimapenzi
• Dhambi za kurithiwa au za kizazi: Rejelea Kutoka 20:5 inayozungumza juu ya kuwa-patiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne. Mambo yaliyofanywa na babu zetu yaliyofungua milango ya ukuta wetu kupitia kwa dhambi hizo za kizazi ni:
• Kujihusisha katika mizungu na uchawi
• Utumwa wa aina mbalimbali (ukiwemo ulevi, tamaa, kukataliwa, n.k.)
• Maneno
• Viapo na Kujitakia Kifo
• Dhambi za Kutendewa (kimwili, kutusiwa, ngono, kukataliwa nk)
• Vidonnda na majeraha ndani ya nafsi zetu
• Laana
• Mahali na vyombo najsi
• Mashirika ya kisiri
• Involuntary exposure to darkness
• Ufukara (Africa)
• Kuumizwa, hisia na kumbukumbu
• kukataliwa
• Kiwewe
• Picha yetu ya Mungu
Jee Hufanyikaje?
Dhambi hufungua milango au malango katika ukuta wetu wa kiroho, na kuruhusu ucha-fu wa kiroho kuingia, na kusababisha matatizo ya kiroho—pamoja na ya kimwili. Dhambi in-aweza kutuletea magonjwa—kiroho, kiakili, kihisia, na kimwili. Hakuna “usalama” katika ku-shirikiana na nguvu za giza.
Hata hivyo, Habari Njema ni kwamba Mungu anatupenda na anataka sana kuturudisha katika Ufalme Wake, kiasi cha kumtuma Mwanawe ulimwenguni ili tuweze kusamehewa, kuo-kolewa, kuponywa, na kukombolewa (Isa. 53:5 na 61:1-3) kutokana na kazi za giza. Habari Njema ni kwamba Mungu anataka kuturudisha kwake ili tuweze kutembea katika amani na ulinzi wa mapenzi Yake.
Dhambi, majeraha, na machungu ni vizuizi vinavyotutenga na Mungu na kutufanya tu-hisi kwamba hatujaunganishwa na Mungu. Athari hizo za giza katika maisha yetu (ambayo wa-kati mwingine husababisha utumwa) hutuzuia kurejea katika uhusiano wa haki na Bwana, hu-tuzuia kusikia sauti Yake na kuyajua mapenzi Yake katika maisha yetu. Athari za giza huzuia
6
#01 Uponyaji wa Roho - Utangulizi www.healingofthespirt.org
huduma yetu; hutuweka utumwani na kuzizuia nguvu za Mungu za uponyaji kutenda kazi nda-ni yetu.
Hata hivyo, jua kwamba Mungu anataka kitu chochote kinachotutenganisha naye ki-weze kupona. Anataka kuifunga milango iliyo wazi katika ukuta wetu wa kiroho na kutuweka huru kutokana na athari za giza. Anataka kuiondoa minyororo yote (au kamba) inayowafunga watu katika sehemu mbalimbali za maisha yetu. Habari Njema ni kwamba upendo wa Mungu unaweza kutuponya, unaweza kujenga upya ukuta wetu na kuleta uzima ndani ya roho, hisia, na miili yetu, na unaweza kutubadilisha ili tuweze kupata na kuishi katika hali ya uzima tele kama ilivyoahidiwa kupitia kwa Kristo. Licha ya hayo, Mungu anatutaka turudi kwake katika usafi na hali ya kutokuwa na kosa aliyokuwa nayo Adamu hapo mwanzo.
Jambo la kusikitisha ni kwamba, Wakristo wengi hawaamini kwamba wanaweza kuwa na milango wazi na athari za giza au utumwa—kwa sababu wamebatizwa. Ingawaje ubatizo ni ishara ya kusamehewa dhambi zetu, hauwezi kuondoa matokeo ya dhambi zetu au ya babu ze-tu. Matokeo hayo (yanayopatilizwa kupitia kwa vizazi kama inavyoelezwa katika Kutoka 20:5, na pia katika maandiko mengine) yanaitwa “maovu.” Ni wazi kwamba, dhambi ni sababu na maovu ni matokeo, au athari za dhambi.
Kwa mfano, iwapo unaendesha gari ukiwa mlevi, ukamgonga mtu anayetembea na ukampelekea hospitalini, halafu mtu huyo akapata ulemavu wa kudumu, je, Mungu atakusa-mehe dhambi zako? Ndio; Alifanya hivyo msalabani; lakini, je, atayaondoa matokeo ya dhambi hiyo? La. Dhambi hiyo iko juu ya dereva huyo lakini matokeo ya dhambi hiyo yatampata mtu aliyegongwa. Wakristo wanaweza kutubu kikamilifu lakini bila kujua bado wako chini ya atha-ri za giza katika sehemu fulani za roho yao kwa sababu ya dhambi za hapo awali.
Tatizo liliopo ni la ufahamu. Nitarudia, “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa” (Hosea 4:6). Mtu akiwa mgongjwa na asijue ni mgonjwa hatawahi kwenda kwa dak-tari. Mkristo aliyedhoofika ndani yake, ilhali anadhani kwamba maisha yake yako katika hali ya kawaida, hatawahi kumwambia Mungu amponye; na “hampatii kile mnachotaka kwa saba-bu hamkiombi” (Yak. 4:2). Wakristo wengi hung’ang’ana na mambo makubwa maishani mwao lakini hawajui kwamba ushindi ambao Yesu aliwashindia msalabani unawahakikishia wokovi wa milele na pia una funguo za uponyaji (Isa. 53:5, Mal. 4:2).
Yasikitisha kuwa Wakristo wengi wanaamini kuwa kuokoka kunahifadhi na nguvu za giza. Shetani anafurahia upofu wa kiroho na imani za uongo. Mwandishi wa kitabu amewaombea watu wengi walioathiriwa na nguvu za giza ikiwa tayari wao ni wakristo wa-liookoka. Dhana kuwa wokovu na ubatizo vinatuzuia na athari za giza ni mojawapo ya uongo wa Shetani. Kama fano, mtazame Petro, alikuwa mtiifu na kumfuata Yesu (Math 4:19) alikuwa na uwezo wa kutoa pepo na kuwaponya wagonjwa (Math 10:1), alikuwa na imani ya kutembea juu ya maji (Math 14:29)alikuwapo wakati miujiza ya kuwalisha 5000 (Math 14:21) na 4000 (Math 15:38) na pia aliweza kumtambua Yesu kama Masihi wa Mungu (Matt 16:16). Lakini hata hivyo alipomkemea Yesu asiende Yerusalemu, Jesu alimwambia: “Rudi nyuma yangu, She-tani! Wewe ni kikwazo kwangu. Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.’’ (Matt 16:23). Wengi wanaamini Petro alikuwa ana pepo, ama sivyo Yesu angezungumza na Petro badala ya Shetani.
Tazama usumbufu wa mtume Paulo katika Warumi 6 & 7 Paulo anazungumzia vita ali-vyopigana navyo dhidi ya dhambi. “kwa maana lile ninalotaka kulitenda, silitendi” (Rom 7:15), “Ninapotaka kutenda jema, jambo baya liko papo hapo.” (Rom 7:21) kasha anasema “Ole wangu, mimi maskini!” (Rom 7:24-25). Anataja neno “mimi” mara 40. Lakini katika sura ya 8 anakiri kuwa hawezi kufanya lolote bila ya Roho Mtakatifu na anamtaja Roho Mtakatifu mara 16.
7
#01 Uponyaji wa Roho - Utangulizi www.healingofthespirt.org
Uponyaji wa roho unahusu kuutumia msalaba, damu ya Bwana wetu Yesu, na uzima wa ufufuo na nuru ya Yesu—katika kila kitu kilicho ndani ya roho ya mtu amba-cho hakijakombolewa. Kwa msaada wa Roho Mtakatifu na kwa kusaidiwa na waombezi wenye kumcha Mungu. Waombezi humwomba Mungu atembee katika nyumba yetu ya kiroho, kuutakasa uchafu na uovu na dhambi iliyo katika nyumba hiyo. Wakati mwingi uponyaji wa kimwili hupatikana pamoja na uponyaji wa ndani ya roho.
Ahadi ya Mungu ya uponyaji, na haki za urithi za muumini tulizopewa kwa ajili ya kifo cha Yesu msalabani, ni za watu waliomkubali Yesu mioyoni mwao, waliobatiz-wa, na kuamua kumfuata. Kabla ya kushugulikia baadhi ya milango ya kawaida iliyo wazi katika roho zetu, na namna ya kuyafunga, tunahitaji kuipitia sehemu inayoeleza juu ya “Misingi ya Uponyaji na Maandiko” ili tuweze kuchunguza tunachoamini kuhu-su uponyaji.
Maandiko ya Uponyaji
Katika mwaka wa 1974, Francis MacNutt aliandika kitabu kiitwacho “Healing,” akaorodhesha aina nne za uponyaji. Kuyasoma maandiko mengi yaliyoorodheshwa chini ya kila aina kutakusaidia kuinua imani yako wakati wa uponyaji.
Vilevile, soma Luka 4:18-19 ili ujue sababu sita za Yesu kupakwa mafuta: “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwani amenitia mafuta (#1) kuwahubiria maskini habari njema; amenituma (#2) niwaponye waliovunjika mioyo, (#3) niwatangazie mateka uhuru wao, (#4) na vipofu watapata kuona tena, (#5) niwakomboe wanaoonewa, (#6) kutangaza mwaka wa neema ya Bwana.” Sababu hizo zimetambuliwa hapa chini baada ya kila aina ya uponyaji iliyoainishwa na MacNutt.
Uponyaji wa Roho (kushughulikia toba na msamaha)
(#1—“kuwahubiria maskini habari njema” [katika roho]) (Tazama pia Mathayo 5:3 Hiyo ndiyo Hali ya Heri ya kwanza)
1. Uponyaji, msamaha, na toba ni mambo yanayohusiana.
Mat. 9:2 Marko 2:5 Luka 5:20 na 7:47 Yak. 5:15
2. Msamaha na toba vinahitajika ili kuikamilisha njia ya uponyaji.
Mat. 3:2 na 4:17 Mat. 6:15 Mat. 18:35 Marko 6:12 Marko 11:26 Luka 13:3, 5
Yak. 5:9
Kuiponya Roho Iliyojeruhiwa (kushughulikia uponyaji wa ndani, uponyaji wa hisia, majeraha, na ma-chungu)
(#2—“kuwaponya waliovunjika mioyo” na #5—“kuwakomboa wanaoonewa”)
Meth. 20:27 Is. 61:1-3 Yoh. 13:21
Zab 30:5, 11 na 45:7 Eze. 11:19 na 18:31 1 Kor. 6:20
Zab. 51:10 and 92:10 Eze. 36:26-27 2 Kor. 4:16
Zab. 35:18 and 41:4 Mat. 6:22-23
8
#01 Uponyaji wa Roho - Utangulizi www.healingofthespirt.org
Uponyaji Kutokana na Nguvu za Giza (kushughulikia kitendo cha kufunguliwa kutoka kwa utumwa)
(#3—“kuwatangazia mateka uhuru wao”)
Mathayo Marko Luka Matendo
8:16 1:23-26 4:33-35 5:16
8:28-33 1:32, 34 4:41 8:7
10:1, 8 3:10-12 6:18 16:16-18
12:22 3:14-15 7:21 19:12
12:27-28 3:22 8:2 19:13-16
15:22, 28 3:30 8:27-37
17:15 5:1-14 9:1
6:13 9:28-42
7:25 13:11-13
9:17-26
Uponyaji waMwili
(#4—“na vipofu watapata kuona”)
Mathayo Marko Luka Matendo
4:23 1:31-32, 41-42 4:39-40 3:1-7
8:13, 15-16 2:5-9 5:12-13, 17-18 5:16
9:6, 28-29, 36 5:23, 29, 41-42 6:8, 19 9:33-34, 40
10:1 6:5, 13, 56 7:14-15 14:10
11:5 7:34, 37 8:47, 55 19:12
12:11 8:25 9:1 28:8
14:14 10:46-52 14:4
15:28 18:42-43
20:34 22:51
Yohana 1 Pet. 2:24
4:50 Isa. 53:5
5:5-8
9:6-7
(#6—baada ya hayo aliweza “kutangaza mwaka wa neema ya Bwana”)
Ni ajabu kwamba watu wengi huja kuombewa #4 uponyaji wa mwili. Hii hupewa nafasi ya mbele ijapokuwa Mungu anathamini uponyaji wa roho (toba)
Milango Hufunguliwaje?
Awamu inayofuata itazingatia vile ambavyo milango ya roho zetu hufunguliwa. Tutatalii kwa undani baadhi ya njia ambazo giza huingia ndani yetu. Kuna njia nyingi. Horrobin kwenye ki-tabu chake: Healing through Deliverance (Vol 2, Chosen books, 2003, ISBN 0-8007-9329-3) anaorodhesha namna 49 . Mojawapo wa vitabu vya kwanza kuhusu Ukombozi: Pigs in the Parlor ilichoandikwa na Frank akishirikiana na Ida Mae Hammond (Impact books, 1973) ki-naorodhesha mapepo 258 kwenye makundi 53.
9
#02 Uponyaji Kutokana na Dhambi zetu www.healingofthespirit.org
Uponyaji Kutokana na Dhambi Zetu
Kwa vile sasa tunaelewa umuhimu wa toba kama njia ya kupata uponyaji, hatua inayofuata katika kitendo cha kufunga milango yetu ya kiroho na kuupatanisha uhusiano wetu na Mungu ni kuzi-tambua dhambi zilizo maishani mwetu.
Tunapotenda dhambi, huwa tunasababisha uendeshaji wa nguvu za sheria za kiroho zisizo-badilka. Mojawapo ya hizo ni sheria ya kiroho ya kupanda na kuvuna, ya matokeo na malipo. “Msidanganyike; Mungu hafanyiwi dhihaka:alichopanda mtu ndicho atakachovuna” (Gal. 6:7). Sheria hii huambatana na hakikisho la baraka kwa wanaotii, na vilevile, laana au adhabu kwa wasi-otii.
Kuhitaji toba na msamaha wa dhambi ni kitendo kinachotakiwa kuendelea maishani: “Watu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Rum. 3:23). Kwa hali yoyote, tunawajibika tu kwa Mungu kwa dhambi tunazozijua; kwa hali yake ya fadhili, tunapotembea naye maishani, yeye hututhibitishia dhambi zetu kidogo kidogo kila wakati. Mungu angetuthibitishia dhambi zetu zote mara moja, tungezidiwa na kuhisi kwamba tumeshindwa, na hatungeweza kujaribu kupatana naye. Kwa hivyo, yeye hutufunulia dhambi zetu kidogo kidogo—kama afanyavyo mtu ana-pochambua maganda ya kitunguu. Tunapoendelea kumkaribia Mungu, ndipo tunapoendelea kuziona dhambi zilizo maishani mwetu.
Ili kuyafanya mambo kuwa magumu zaidi, baba wa dhambi—Shetani—hutupofusha na kutu-fanya tusione uchafu wetu, na hivyo basi sisi hukosa kuona dhambi hizo ama sisi hujipa moyo kwa kusema kwamba hatuna shida kubwa. Ingawaje dhambi za matendo yetu (kama vile kudanganya, kuzini, kuiba, kulaani, kuchukia, kulewa, kutotoa fungu la kumi, au kutazama picha za kumtia mtu ashiki) zinatakiwa kuwa wazi kwetu kiasi cha kutohitaji kusadikishwa na Roho Mtakatifu kwamba tunatembea katika kutotii, dhambi za mtazamo (kama vile kiburi, uasi, kutoamini, wivu, ubinafsi, kujitakia makuu, kutawala, kujisimamia, kujitegemea, n.k), ni ngumu kutambua na ngumu kwetu kuziona. Dhambi hizi huonyesha sisi ni watu wa aina gani; hizo dhambi ni sehemu ya urithi wetu wa kiroho, “desturi” zetu binafsi.” Tunahitaji msaada wa Mungu (kupitia kwa neema yake) ili tuzione dhambi hizo na kupata uponyaji. Mungu hawezi kushughulikia “dhambi za mtazamo” mpaka tushug-hulikie “dhambi za matendo” (zilizoorodheshwa hapa ndani).
Si rahisi kujua ni lini hasa tumepata msamaha wa dhambi zetu. Hatuna shaka kwamba kifo cha Yesu Kristo msalabani kilikuwa dhabihu tosha ya kulipia msamaha wa dhambi zote. Lakini msamaha huo hutokea wakati gani katika maisha yetu? Je, ni wakati wa ubatizo wa maji au wakati wa kumpokea Roho Mtakatifu (“kuzaliwa mara ya pili,” Yohana 3:3-6), au unapatikana tu wakati wo-wote, kama neema yake inayopatikana kwa watu wote lakini ni lazima tuombe ili tuweze kuipokea?
Watu wengi hufa kabla ya kumwambia Yesu aingie moyoni mwao; vivyo hivyo, wengi huko-sa kuomba msamaha wa dhambi. Watu wengi hukosa kuomba msamaha wa dhambi, kwa hivyo, ha-wajapokea msamaha huo (Yak. 4:2, “… hamna kitu kwa kuwa hamwombi ”). Tunapokiri, na kutubu na kuomba msamaha, Mungu hutusamehe wakati huohuo. (I Yohana 1:9)
Tusipotubu tunapobatizwa, je, dhambi zetu zitasamehewa eti kwa sababu “tuliloa maji?” La hasha. Vivyo hivyo, je, wakati wa ubatizo sisi husamehewa dhambi tusizozijua na ambazo hatujaom-ba kusamehewa? La hasha. Lakini hatuwajibiki kwa ajili ya dhambi hizi mpaka Bwana atufunulie dhambi zenyewe. Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi za waumini na dhambi za wapagani—wasiojua chochote kuhusu Yesu wala neema yake. Zaidi ya hayo, maandiko yanaunga mkono kwamba tunata-kiwa “kuungama dhambi zetu” ili tuweze kupokea msamaha (Yak. 5:16, 1 Yohana 1:9).
10
#02 Uponyaji Kutokana na Dhambi zetu www.healingofthespirit.org
Tunapoomba ombi la mtenda dhambi (“Bwana, nisamehe dhambi zangu zote”), je, ombi hilo halitoshi? Lazima tuitaje aina ya dhambi. Maombi ya “kujumlisha kila kitu” humtuliza tu mtu kwa kipindi kifupi kutoka kwa giza na utumwa, lakini baadaye mhusika huyo hurudi ili aweze kuombewa kuhusu mambo yale yale.
Kama tulivyotaja mahali pengine katika sehemu hii, lazima tukumbuke kwamba msamaha wa dhambi na matokeo ya dhambi zilizotendwa zamani ni mambo mawili tofauti, na yatahitaji kushughu-likiwa kwa njia mbili tofauti. Watu wengine wanaweza kujua kwamba wamesamehewa, ilhali hisia za hukumu, aibu, hatia zikaendelea kuwatesa. Upande mwingine, kutokana na uzoefu, inapendekezwa kwamba dhambi ambazo mtu ametubu hapo awali (kwa mfano, zile ambazo mtu alitubu alipojitaya-risha kubatizwa) mara nyingi huwa muumni hazikumbuki (kwa ajili ya kuhisi kuwa ana hatia, anao-na aibu, na hukumu). Dhambi hizo alizotubu mtu hufinikwa kwa damu ya Yesu na huwa “hazikum-buki tena.” Kwa hivyo, ni lazima tumtegemee Roho Mtakatifu ili atusaidie kuzitambua dhambi hizo ambazo (kwa sababu yoyote ile) hazijafunuliwa na hatuzijui.
Unapoipitia orodha hii, uwe tayari kusadikishwa na Roho Mtakatifu kuhusu dhambi zilizo ndani ya roho yako ambazo “hazifunuliwa,” na ambazo huzijui. Dhambi zengine ambazo hazijaorod-heshwa hapa huenda zikakujia akilini pia. Zile dhambi zilizotambuliwa “leo” ndizo ambazo Mungu anakutaka uzishughulikie “leo.” Utakaposoma orodha hiyo siku za baadaye, utafunuliwa dhambi zen-gine ambazo hujasadikishwa leo. “mstari baada ya mwingine”” na “agizo baada ya lingine” ni njia anayoitumia Bwana.
Orodha ya Uchunguzi wa Dhambi za Kiroho
Unapopitia orodha ya uchunguzi wa dhambi 72 za mwenendo, omba kwamba Bwana ataku-sadikisha dhambi zozote unazohitaji kukiri na kutubu. Tumia nafasi hii kutambu na kuweka alama (pamoja na tarehe) katika zile dhambi ambazo hujatubu kama utakavyofunuliwa na Mungu. Iwapo huna hakika ya maana kamili ya maneno yafuatayo, ningependekeza utafute maana yake katika ka-musi. (Dhambi hizo za mwenendo ziko katika vifungu vifuatavyo vya maandiko: Kut. 20:1-17, Marko 7:21-22, Rum. 1:29-31, 1 Kor. 6:9-10, Gal. 5:19-21, Efe. 4:28-31 na 5:3-5, 1 Pet. 4:3.)
Dhambi za Mwenendo (mambo tuyafanyayo)
wazinzi washerati waabudu sanamu wanaume kujifanya
kama wanawake
wezi tamaa ulevi wanaojidhulumu
usherehekeaji kupokonya uovu nia mbovu
waliojaa wivu waoga mijadala ulaghai
chuki kuu wavumishaji wasengenyaji wanaomchukia Mungu
wenye inda wenye shaka wenye kujivuna wanaobuni uovu
wasioridhika wasio na fadhili uchafu wasiotii wazazi
ukware ibada ya sanamu uchawi wavunja agano
11
#02 Uponyaji Kutokana na Dhambi zetu www.healingofthespirit.org
kinyongo kuhitilafiana uigaji utoaji mimba
mabishano uchochezi maasi uasi kwa dini ashiki mbovu
Shughuli za ushetani utukanaji hasira upendo usio na mipaka
kujijazia kufuru mizaha mazungumzo machafu
kudanganya kulaghai fikra mbovu jicho la uovu
upumbavu makelele machungu kupenda pesa
unafiki udhalimu ashiki wanaotumia mwili vibaya
wazabizabina wasiosamehe kutoamini picha za kutia ashiki
kuua miungu wengine sanamu za kuchonga kuliita bure jina la Mungu
kutoiweka takatifu siku ya Sabato kutumia pesa kwa njia ya uzembe
kukosa upendo wa kweli kutoheshimu baba na mama
Dhambi za Mtazamo (tulivyo sisi)
Wenye majivuno waasi wanaojitosheleza kujitegemea
kutaka kufanikiwa uzembe ovyo kuwatawala wengine
wa kuridhika kupambana wasioamini wa kujidai
Mwambie Mungu, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akufunulie ikiwa kuna dhambi zengine zisizokuwa katika orodha hii ambazo umesahau ilhali zinatakiwa kushughulikiwa. Dhambi hizo hu-baki katika sehemu ya akili yako iliyofichika kwa kipindi chote cha maisha yako mpaka utakapozi-shughulikia. Maadamu dhambi hizo ziko maishani mwako milango ya kiroho hubaki wazi na Sheta-ni anaweze kuitumia kukutatiza.
Kuwa tayari kukubali njia yoyote ambayo Mungu atachagua kukufunulia mambo. Anaweza kukuonyesha picha ya kitu kilichofanyika hapo awali kinachokuletea hisia na/au mawazo yanayohita-ji kushughulikiwa au jina la mtu linaweza kukujia na kukufanya ukumbuke kitu. Iwapo huelewi kitu chochote, muulize Roho Mtakatifu, Roho wa Kweli, akuwezeshe kuelewa kitu hicho.
Tumia nafasi zilizo hapa chini kutambua dhambi zengine zaidi:
_________________ _________________ _________________
_________________ _________________ _________________
_________________ _________________ _________________
_________________ _________________ _________________
Kwa jumla, hatua zilizo hapa juu zitatambua dhambi katika maisha yako. Katika hali zengine, huenda kukawa na dhambi zilizojificha sana na huenda ukahitaji msaada wa mwombezi aliye na ujuzi akusaidie katika hatua hiyo, ili amwambie Roho Mtakatifu akusaidie kuzitambua.
12
#02 Uponyaji Kutokana na Dhambi zetu www.healingofthespirit.org
Kwa kawaida, sisi hukosa kuona mizigo au “uchafu” wetu: na bila msaada wa Bwana na msaada wa mtumishi wake mwingine, hatuwezi kupokea uponyaji tunaohitaji sana.
Njia ya kutubu dhambi tulizofanya ndiyo hatua rahisi na hatua tuijuayo vizuri katika mazoea ya kuifunga milango iliyo wazi. Njia zengine ni ngumu zaidi na ingawa Yesu alichukua dhambi zetu, hali zengine lazima tujitwalie nguvu za msalaba ili tuweze kuwekwa huru kutokana na dhambi (Ma-tendo 8:23 na 19:18, Efe. 4:28). Njia hii itaelezwa kinagaubaga katika sehemu zinazofuata.
Ombi la Uponyaji Kutokana na Dhambi
Kwa kila dhambi au kikundi cha dhambi kilichotambuliwa, omba ukisema maneno yafua-tayo:
Bwana Mungu, ninakiri na kukubali ______________ kama dhambi katika maisha yangu. Ninasikitika kwa kutenda dhambi hiyo na ninatubu. Ninaikataa dhambi hiyo na kumrudishia Bwana wangu Yesu nafasi ya kiroho. Katika jina la Yesu nimeomba. Amina.
Baadaye, tafuta rafiki mwaminifu au mchungaji kisha umwonyeshe orodha yako-kwa ajili ya kuungama. Hutakiwi kueleza kila kitu kinagaubaga lakini unahitaji kuungama dhambi hizo. Mwam-bie rafiki yako au mchungaji akuombee, ili Bwana akusamehe dhambi zako zote na akuponye; omba kwamba milango yako ya kiroho katika kila sehemu hizi itaponywa na kufungwa. Kisha msifu Yesu.
13
#03 Uponyaji Kutokana na Kutosamehe www.healingofthespirit.org
Uponyaji Kutokana na Kutosamehe, Kuhukumu na Kushitaki
Yesu alisema mambo haya alipokuwa akifunza juu ya siku za mwisho, “Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitianana kuchukiana” (Mat. 24:10). Kutosamehe ku-naweza kuwa kizuizi kimoja kikubwa kinachozuia uponyaji wa roho. Kusamehe kunawe-za kufafanuliwa kwa njia hii, “kitendo cha kumwachilia mtu huru ili asiwajibike kwako—kutokana na kosa alilokufanyia.”
Kwa nini ni lazima tusamehe? (Ufuatao ni wasia kutoka kwa maandiko)
1. Tunaamriwa kusamehe (Law. 19:16, Luka 6:37, Marko11:27, Yak. 5:9, Kol. 3:13, Efe. 4:32).
2. Tusiposamehe, Mungu hatatusamehe; Kifo cha Yesu msalabani hakitakuwa na maana na wokovu wetu utakuwa wa shaka (Mat. 6:12-15 na 18:15).
3. Tusiposamehe, tutakuwa tunakula na kunywa hatia tunaposhiriki katika Ushirika Mtakatifu (1 Kor. 11:28-30).
4. Tusiposamehe, Mungu atatupeleka kwa “watesaji”—machungu na majeraha hu-geuka na kuwa hisia mbaya, kujihurumia, uchungu, maudhi, na hatimaye kinyon-go (Mat. 18:33-34).
5. Uponyaji kutokana na magonjwa na msamaha yanaingiliana sana. Hatuwezi ku-pona mpaka tuamue kusamehe. (Isa. 33:24, Mat. 9:2-6, Marko 2:5-9, Luka 5:20-23, Yak. 5:15).
6. Hatuwezi kumtolea Bwana kitu chochote madhabahuni mpaka tusamehe kwanza na kujaribu kurekebisha mambo na kupatana na wengine (Mat. 5:25, Luka 17:3).
7. Sheria ya The law of the “kuwa na neno juu ya mtu”—“Kila msimamapo na kusa-li, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu ailye mbinguni awasa-mehe na ninyi makosa yenu.” (Marko 11:25).
8. Tunaambiwa tusamehe “saba mara sabini” (Mat. 18:21-22), mpaka tuimarishe hali yetu ya kusamehe.
9. Tukikosa kusamehe tunajiambie wenyewe na pia kumwambia Mungu kwamba, “Nitawashika watu hawa mateka katika hasira yangu mpaka wanilipe, mpaka ni-pokee ninacho wadai (sheria ya kufunga na kufungua iliyo katika Mat. 16:19).
Pia kuna sheria mbili zinazotenda kazi katika kitendo cha kutosamehe: (1) sheria ya hatia (Mat. 5:26, Luka 17:3 na 18:15, Marko 9:40, Kol. 3:13, Efe. 4:32) na (2) sheria ya hukumu (Mat. 7:2, Yohana 7:24).
Kuhusu Makosa
1. Kuna sifa mbili za lazima na muhimu katika kosa: (1) jeraha—kitendo cha kuu-mizwa—na (2) deni au unachonidai—mtu aliyekosewa huhisi kwamba anadai mtu kitu kwa kujeruhiwa. Sisi kama watu waliokosewa, tunamtaka mtu aliyetuko-sea aombe msamaha, aseme kwamba anasikitika, na ayarekebishe maneno aliyo-sema au kitu alichofanya, na aweze kukubali wajibu wa kurekebisha kosa alilo-fanya.
14
#03 Uponyaji Kutokana na Kutosamehe www.healingofthespirit.org
2. Wakati mwingne makosa hutokea kwa sababu ya kutotimiza matarajio. Kwa kumtara-jia mtu awe na mwenendo fulani, tunaweza kuwa tunajitayarisha kuhisi tumekosewa. (Kwa mfano shangazi anayeishi mbali anatuma zawadi ya mtoto na kutarajia kupata shukrani, lakini akakosa “kupokea shukrani” hiyo. Katika hali hii, tarajio zuri la ki-desturi la shangazi huyo la kupewa shukrani linakabiliwa na kule kusahau bila maku-sudi kutoa shukrani.) Tunapokuwa na matarajio fulani kuwahusu watu (yawe ni ma-zuri au la) huwa tunajitayarisha kukosewa kwa kutarajia mwenendo au matendo fula-ni kutoka kwa watu hao. Watu hao wasipotenda mambo tunavyotarajia, tunavyoamini wanatakiwa kufanya, tunaamua kwamba wametukosea, na hatimaye huhisi tumeudhi-ka. Jambo hili mara nyingi hutendeka kati ya wazazi na watoto au kati ya wanandoa. Watu walio na roho wa kutawala watakuwa na tatizo kubwa katika hali hii. Mkosaji hakufanya jambo tulilodhani angefanya, au tulilotaka afanye, kwa hivyo sisi hukose-wa na roho wa hasira hutuingia. s.
3. Makosa pia hutokana na mambo tunayojitarajia ya uwongo, yasiyowezekana, na ya kutiwa chumvi—kama vile kutaka kutambuliwa, kukubaliwa, au kutibithishwa, na jambo hilo halitendeki (roho wa kukataliwa hujitokeza katika mfano huu).
4. Watu waliokataliwa tangu utotoni huwa rahisi kujeruhiwa na makosa ya aina hii.
5. Uhusiano ukiwa wa karibu sana, hisia za kukosewa huwa kubwa zaidi (kama vile ka-tika talaka). Watu unaowajali ndio wanaoweza kuumiza sana.
6. Wakati mwingine sisi huwafikiria vibaya watu wanaotukosea. Makosa mengine huto-kea bila mtu kukusudia, au bila mkosaji kujua, lakini mara nyingi sisi hudhani kwab-ma kosa hilo lilifanywa makusudi.
7. Sis hukasirika na kuudhika. Shetani huona (na kutumia ukweli) kwamba tunayachu-kulia maneno na matendo ya wengine kwa njia “isiyotarajiwa.”
8. Mtu anapodanganywa, yeye “huamini” kwamba mtu huyo anasema ukweli, hata ka-ma sivyo.
9. Kuna aina mbili ya watu waliokosewa: (1) wanaotendewa mambo kwa njia isiyo ya haki na (2) wanaoamini kwamba wametendewa mambo kwa njia isiyo ya haki.
10. Kiburi hutuzuia kukubali hali yetu halisi.
11. Tunapokosewa, sisi hufungwa, na “lo lote utakalolifunga duniani, liatakuwa lime-fungwa mginguni …” (Mat. 16:19). Tunapoudhiwa na mkosaji sisi hujifunga, na vi-levile humfunga aliyetukosea.
12. Tunapokosewa sisi huwa na moyo mgumu—wa kutukinga sisi, nasi hujenga kuta za kuuzingira moyo wetu. Kuta hizo hupunguza majeraha ya makosa ya siku za baa-daye lakini pia hufungia nje upendo wa Mungu, unaotuponya. (Kwa maelezo zaidi kuhusu kuzivunja kuta hizi, tazama sehemu inayoeleza juu ya “Uponyaji Kutokana na Viapo na Matamanio ya Kufa.”)
13. Kwa kawaida watu wanapokesewa wao hujaribu kukana, kusahau, au kulizika katika sehemu ya kufichika akili. Hali hii huwa ya muda tu; makosa hayo hujitokeza tena katika umbo lengine—kama vile magonjwa ya mwilini, kutokuwa na amani, n.k.
14. Baadhi ya hali zinazokuza hali ya mtu kuona amekosewa ni hizi: matusi, mashambu-lizi, kuumizwa, mgawanyiko, kutengana, kuvunjika kwa mahusiano, usaliti, na kurudi nyuma katika wokovu.
15. Tunapoliruhusu kosa libaki moyoni mwetu, jambo hilo husababisha madhara makub-wa kiroho.
16. Mara nyingi sisi huwasaliti watu wanaotukosea—kwa kuwasengenya na kuwakosoa kwa watu wengine (bila wao kujua).
17. Mara nyingi sisi hukusanya makosa mengine kutoka kwa watu hao na kwa watu wen-gine.
15
#03 Uponyaji Kutokana na Kutosamehe www.healingofthespirit.org
18. Makosa ambayo hayajaponywa mara nyingi hugeuka na kuwa chuki, ma-chung, na moyo mgumu.
19. Hatimaye sisi huwa na roho iliyojeruhiwa.
20. Makosa ndiyo sababu inayowafanya watu wengi kuacha ushirika wa maka-nisa yao/au kuiacha imani.
21.Watu wengi huamua kulipiza kisasi. Kwa hali yoyote, maandiko hutushauri, “Msimlipe mtu ovu kwa ovu … Kisasi ni juu yangu; mimi nitalipa, anena Bwana” (Rum. 12:17-19).
22. Machungu hutokana na kisasi ambacho hakijatimizwa; huo ni “mzizi.” Waebrania 12:14-15 inatuonya: “… shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.” Mizizi hiyo ikile-lewa (ikinyunyiziwa maji, ikilindwa, ikilishwa, na kutunzwa), hiyo huzidi kuwa mirefu na yenye nguvu. Hiyo huwa migumu kung’olewa. Na mavuno yake huwa ni hasira, kuudhika, wivu, chuki, mabishano, ugumu wa moyo, na kutokupatana. Tunapokosewa, uwezo wetu wa kuzaa matunda ya haki hukwama.
Kuhusu Kusamehe
Mtu akitendewa dhambi, kwa mfano mtoto (kutusiwa kingono, kupigwa au kutu-siwa), au anapopitia tukio la kutishia uhai wake, kuogofya na hata kumtia taharuki (ama tukio kama talaka), mtendewa hukumbuka wasiwasi, uchungu na hali ya ku-achwa ukiwa na aibu vinavyomfanya kukumbuka mara kwa mara katika mawazo yake.Hali hii ya kukumbuka kitendo hicho huumiza zaidi ya tukio lenyewe. Hali hii huwadhuru 6% ya wavulana na 15% ya wasichana (taza-ma:http://www.medicinenet.com/posttraumatic_stress_disorder/article.htm). Kati-ka matukio haya, kusamehe huwa ni vigumu sana kwa mtendewa pasipo ya kuwa na mwombezi na kupata uponyaji wa ndani.
Makwazo yasiposamehewa, kutosamehe kunakithiri ndani ya nafsi ya mtendewa kiasi cha kufungua mlango kwa roho ya kutosamehe kuingia ndani ya mtendewa. Roho hii ya giza inapopenya hutafuta haki za kumiliki kwa kusham-bulia kumbukumbu ya mtendewa mara kwa mara. Haiwezi kutka hadi mtendewa atoe msamaha kwa Yule aliyemtenda ukatili na kuiamrisha roho hiyo iondoke ma-ra moja.
Mtendewa yapasa atafute uponyaji na kukemea roho ya kutosamehe. Katika kusamehe, mtendewa atoe msamaha kwa dhati yake yote ama sivyo hisia za kutosamehe zitamrudia na hivyo kumfunga tena. Haki zilizotolewa kwa giza lazima zirudishwe kwa Yesu ili uponyaji wa ndani ukamilike. Mada hii imejadiliwa kwa undani katika sura inayoshughulikia: Uponyaji wa Machungu, Hisia na Kumbukumbu. Mambo mengine ya kimsingi ni:
1. Tukitaka kufunga mlango wa kutosamehe na kuwekwa huru, kwanza tu-tambue Kristo alitusamehe dhambi zetu – yaani alilipa madeni yetu, nasi pia yapasa tuwasamehe wanaotukosea (Mat. 6:12, 15; Mat. 18:35).
16
#03 Uponyaji Kutokana na Kutosamehe www.healingofthespirit.org
2. Msamaha si bure. Katika Agano la kale dhabihu zilitolewa kufidia dham-bi. Katika Agano Jipya Kristo aliutoa uhai wake ili tusamehewe dhambi.
3. Msamaha ni sawa na kuwekwa huru na rais hivyo basi mkosaji hapaswi ku-lipa fidia kwa makosa yake.
4. Msamaha ni tendo la hiari sio hisia, hata hivyo baada ya kusamehe mtu hujihisi mwepesi na mchangamfu.
5. Tunapotumia hiari yetu kusamehe, nguvu zote za Mbinguni huja kutusaidia
6. Msamaha unahitaji kumsamehe Mungu pia.
7. Lazima tujisamehe na kupokea msamaha wa Mungu kwa niaba yetu, kama tunavostahili “kumpenda jirani yako kama nafsi yako”(Math 22:39)
8. Jua kwamba punde tunapokiri, Mungu hutusamehe (1Yoh1:9).
9. Iwapo mtenda dhambi ni Mkristo, Mat 5:25-27 anahitajika kupatana na ndugu yake kabla ya kuto dhabihu. Kusamehe hakutegemei kupatana, yaani kusamehewa si lazima kuambatane na kukubali kwa mtesi wako. Hata hivyo Maandiko yanatuusia “tubariki badala ya kulaani” kwa hivyo ombi la Baraka lapasa kusemwa.
10. Shetani atajaribu kukudanganya, ufikiri kuwa ni vigumu kusamehe au hata huchukua muda mrefu.
11. Watu wengi hubeba machungu kinyume cha wafu.Wasamehe wafu pia.
Iwapo mtu ana kinyongo nawe, hiyo ni shida yao sio yako. Wanahitaji kupata-nishwa na Mungu kama ilivyo kwako. Msamaha hauhitaji kupatanishwa. Si shida yako kama wako sawa na Mungu au la, kwa kuwa wewe unasimama peke yako mbele ya Mungu kwa kweli iliyo moyoni mwako.
Mfano wa Mtumishi Asiyesamehe
Katika Mathayo 18, Yesu alifafanua zaidi juu ya utumwa uletwao na dham-bi ya makosa na hatimaye kutosamehe. Mtumishi aliye-“pelekwa kwa watesaji” ni hali inayoendelea kuwepo “mpaka” deni la (kusamehe) liweze kulipwa. Fahamu kwamba wasomi hufafanua neno “watesaji” katika kifungu hiki kuwa na maana ya “roho wachafu” wanaoingia ndani ya mtu kupitia kwa mlango ulio wazi wa kuto-samehe na kusababisha msukosuko, hukumu, machungu, na kukosa amani—hali inayobaki mpaka lile deni lisamehewe.
Kuhusu Hukumu
1. Ingawaje ni kweli kwamba kukosewa na kuwa mtu wa kuwahukumu wen-gine kuna sifa zinazofanana (lakini zisizo sawasawa), matokeo yake ni sa-wa. Mtu akikosewa vikali, mtu huyo huweza kupata “roho wa kutosamehe,” “roho wa chuki,” “roho wa kuhukumu,” na/au “mzizi wa machungu,” naye hukusanya makosa na kuwakosoa watu vikali na kuwahukumu.
2. Tusipolishughulikia kosa hilo upesi, litazaa tunda lililo kinyume na lile linalokuzwa na Mungu—tunda la dhambi, sononeko, hasira, ukatili, wivu, kuudhika, mabishano,
uchungu, chuki, na kijicho, mambo hayo yote huufanya moyo kuwa mgumu, na kumfanya mtu akose kuwa mwepesi kuhisi, na kutia doa ka-tika maono yetu ya kiroho.
17
#03 Uponyaji Kutokana na Kutosamehe www.healingofthespirit.org
3. Shetani akifaulu kutushawishi kutoa hukumu kutokana na (kwa mfano) kuudhika au hasira, au mtazamo wa mbaya wa kukosoa, mara tutaanza kusikia kutoka kwa roho ya ushetani/ mizungu. Roho ya ushetani/mizungu itatwambia “mambo” yote “yasiyo sahihi” na kila tu; itakuja na kutunong’onezea, na pia kutupa maono na ndoto mbaya kuhusu mtu fulani, huduma fulani, n.k. Roho hiyo ya usheta-ni/mizungu huanza kuthibitisha na kuhalalisha hisia zetu mbaya, na kutu-fanya tujione kwamba sisi ni “polisi” wa Mungu”—waliopewa kazi ya kuulaini-sha Mwili wa Kristo.
4. Tunapohukumu, Shetani hutuweka katika eneo lengine la kiroho ambapo itakuwa rahisi kwetu kutawaliwa kwa hila. Tutadanganywa ili tuamini mambo yasiyo sa-hihi; kwa mfano, tutaanza kuchagua kuamini mambo mabaya kuhusu watu wen-gine na matendo yao, na jambo hilo husababisha migawanyiko katika uhusiano. Na pia sisi hujitenga na watu hao kimwili na kihisia. Wakati mwingine roho wa udanganyifu na uwongo hutuingia, ili iweze kutudanganya zaidi na kutufunga.
5. Tukiwa na utumwa chini ya “roho wa kuhukumu,” sisi huwahukumu wen-gine kulingana na vile tunawaona kwa macho yetu ya kimwili wala sio ana-vyowaona Yesu. “… siangalii mambo kama wanavyoyaangalia binadamu; bina-damu huangalia uzuri wan je,lakini mimi naangalia moyoni” (1 Sam. 16:7). Hala-fu sisi “hutenda” kulingana na vile tunavyoona kimwili, jambo ambalo limetiwa doa na roho ya uovu.
6. Wakati mwingine kupitia kwa karama ya Roho Mtakatifu, tunaweza kuona dham-bi ya mtu mwingine. Nasi huweza kuamua kwamba, “kwa vile tunaiona dhambi hiyo, wao pia wanaiona.” Nasi tunaweza kujiuliza ni kwa nini matendo yao haya-kubaliani na mwenendo tunaoamini kuwa sahihi, mwema, wa uadilifu au wa haki. Katika kiwango, ni vyema kukumbuka kwamba si wajibu wetu kuwarekebisha watu hao—urekebishaji, au usadikishaji, ni kazi ya Mungu. Watu walio na ki-pawa cha kupambanua roho mara nyingi huwa rahisi kuingia katika mtego huu wa adui.
7. Sisi huhukumu nia za watu wengine, na kisha kudunisha thamani yao (ambayo ni kuu sana machoni pa Mungu).
8. Wakati mwingine sisi huhukumu makundi ya watu, makabila mengine, au tama-duni fulani. Ilhali hatukubali kwamba “tunabagua,” ilhali hicho ndicho tunachoki-fanya.
9. Wakati mwingine sisi huhukumu uwezo wa mtu mwingine wa kuhudumu kulin-gana na yale tunayo yaona kupitia kwa roho hii ya kuhukumu. Halafu tunakataa kupokea huduma ya mtu huyo, na kuamu kupokea tu huduma ya watu tunaoamini kwamba hali yao ya kiroho “iko katika kiwango cha kawaida” (sawa na chetu au zaidi ya chetu).
10. Tunapokuwa na hali ya kukosoa na kuhukumu, huwa tunamuasi Mungu (Hes. 12:1).
Huu ni wakati mzuri wakutalii maisha yako. Je umewahi kutusiwa, kuonewa, kulau-miwa? Tazama yaliyo ndani ya moyo wako na ujiulize kama umewahi kumuonea, kum-laumu au kutoa ushahidi wa uongo kinyume cha mtu mwingine. Je mimi hutafuta makosa katika maisha ya watu wengine? Wakati mwingine tunawahukumu wengine kwa njia isiyofaa. Twaweza kuwa waaminifu lakini tuishie kuwaudhi wengine. Tunapaswa kuji-hadhari na hali hizi na badala yake kutafuta nafasi ya kutubu na kurekebisha mhusiano yetu na Mungu.
18
#03 Uponyaji Kutokana na Kutosamehe www.healingofthespirit.org
Shina la Uchungu
Tusiposhughulikia kutosamehe na kuwahukumu wengine (Efe 4:26) hali hii ya-weza kuleta machungu. “Angalieni sana mtu ye yote asiikose neema ya Mungu na kwamba shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.”. (Heb 12:15) Uchungu huzaa kisasi, hasira, chuki na hata ukatili unaoishia mauaji (kumharibia mtu sifa au matusi) Ili kuelewa zaidi, tazama: kitabu cha: The Transformation of the Inner Man, Victory House, 1982 ISBN 0-932081-13-4, kurasa 237 – 268 kichoandikwa na John na Paula Sanford
Huenda Tukahitaji Kumsamehe Mungu
Wakati mwingine sisi humkasirikia Mungu, anapokosa kufanya vitu tunavyotara-jia (kama vile kumwacha mtu katika familia yetu afe, anapoacha mambo mabaya yawa-tendekee watu wazuri, n.k.) au anapokosa kutuponya tunapodhani kwamba tuna imani ya kutosha kupokea uponyaji. Tunatakiwa kufahamu kwamba hatuwezi kuuona mpango wa Mungu kutuhusu sisi au kuwahusu wengine. Huenda ikawa tunatoa hukumu isiyo sahihi kabla ya wakati kufika. Ni lazima tumwache Mungu awe Mungu—kuyaachilia mapenzi yetu kwake na matarajio yetu kwake. Katika hali hii, tunahitaji kumwambia Mungu kwamba tunatubu na kuomba msamaha kutoka kwake.
Kwa Nini Tunahitaji Kujisamehe
Shetani kila mara hujaribu kutufanya tuhisi tuna hatia na kuhukumika; yeye huta-fanya tuhisi kwamba tuawajibika kwa dhambi zote tulizotenda. Huenda tuliwatendea wengine mambo yasiyo ya haki, au tuliwaumiza au kuwajeruhi, tulizini, n.k. Kwa kuwa na nia mbovu, Shetani hujaribu kutufanya “tuhisi” kwamba sisi ndio tulikuwa wa kulau-miwa katika kila hali, nasi hatimaye hujihukumu wenyewe. “Kutojisamehe” huzaa hisia za kuona kwamba huna thamani. Uponyaji huauwezi kuja mpaka tujisamehe wenyewe, hata kama Mungu ametusamehe.
Kwa Wale Waliotukosea
Mtu akikukabili na kosa ulilomfanyia, ni lazima ukumbe kunyenyekea. Kiburi hujitetea, lakini unyenyekevu hukubali na kusema, “Ni kweli. Ninatubu kwa kukukosea. Tafadhali nisamehe.” Unaweza kusikitika kwa kwa kufanya kosa hilo. Unatakiwa ku-fanya hivyo hata ukidhani kwamba hujafanya chochote na kwamba umelaumiwa bure.
Uponyaji wa Mahusiano
Ukombozi hauwezi kupatikana iwapo mhitaji ana kasoro katika mahusiano yake na wa-zazi wake.
a. Imetupasa kuwaheshimu (Kutok 20:12) Amri ya 5. Hii ndiyo amri ya kwanza iliyo na ahadi. Tumeahidiwa kuwa tukiwaheshimu baba na mama, tutafanikiwa maishani mwetu.
b. Yatupasa kuwasamehe (Mat. 15:4, Mark 10:19, Eph. 6:2)
c Hatuwezi kuwa wanafunzi tukiwachukia baba na mama zetu (Luka 14:26)
d “Ikiwa mtu atamlaani baba yake au mama yake, taa yake itazimwa katika giza nene.” (Mith 20:20).
Yakupasa kuwapenda (heshimu) baba na mama yako, lakini si lazima kuishi nao. Iwapo jamaa si salama kukaa nao, ni afadhali mtu kujitenga nao. Hii ni kusema waheshimu, na kuwa tayari kuwasaidia. Ni vyema kufuata maagizo yao ikiwa tunaishi chini ya mamlaka yao. Iwapo mhitaji hakupokea upendo wa wazazi au alizaliwa nje ya
19
#03 Uponyaji Kutokana na Kutosamehe www.healingofthespirit.org
ndoa, hali ya kukataliwa yaweza kumfuata. Uponyaji wa ndani waweza kuhitajika iwapo mtu ametusiwa kwa maneno, vitendo au kingono.. Mhuduma atafute majeraha ya kihisia kwa ishara kama hasira, kujidharau, kuhurumia au huzuni isiyo na sababu.
Asili ya kutosamehe katika mahusiano ni ndugu, dada, waajiri, waalimu, wapenzi, na watoto. Unapowahudumia wahitaji waulize juu ya mahusiano ya wazazi wao na kama kuna kutosamehe kulikojificha.
Kuwa Mtu Asiyeweza Kukosewa
Kama watu wazima waliokomaa kiroho, lengo letu linatakiwa kukuza moyo usi-oweza kukosewa, kuwa watu wasioweza kukosewa. Katika sehemu mbalimbali, maandi-ko yanatwambia tuwe watu wasioweza kukosewa (Zab. 119:165, Luka 7:23, Rum. 14:21, 1 Kor. 8:13). Ingawaje hatuwezi kulifikia lengo hili mara moja, mwongozo ufuatao un-aweza kutusaidia:
1. Tunahimizwa kwamba tusikae na hasira kutwa nzima (Efe. 4:26). Tunatakiwa kupatana upesi; tukichelewa kwa muda mrefu itakuwa vigumu kufanya hivyo.
2. Unapokosewa, usimwambie kila mtu makosa uliyofanyiwa; mwendee mtu aliye-kukosea, kama alivyotwambia Yesu tufanye. (Ikiwa unatatizo na ulimi wako, an-galia sehemu inayoeleza kuhusu “Kuuponya Ulimi Wako.”)
3. Samehe—kwani kitendo hicho kinahitajika, lakini hatuwajibiki kumwamini mtu. Kusamehe ni lazima lakini; mtu lazima adhihirishe anaweza kuaminiwa.
4. Usione hatia ikiwa bado unahisi kwamba hutaji kuhusiana na mtu aliyekukosea. Mungu anatutaka tuwapende, lakini si lazima kufurahia kuwa nao.
5. Lengo letu linatakiwa kuwa ni kukuza “tunda la roho” maradufu ili tuweze kuunda ulinzi wa kudumu wa upendo wa kuuzunguka moyo wetu, ili makose ya-siweze kuingia ndani.
Namna ya Kusamehe
1. Mtu atahitaji kufanya juhudi ili aweze kuwa huru kutokana na kutosamehe. Sharti utambue kwamba umeumizwa (kwa kusadikishwa) kisha ukiri.
2. Uwe tayari kufuta madeni yote ya watu waliokukosea.
3. Chukua kalamu na umwombe Mungu ili akuonyeshe mtu yeyote ambaye hujam-samehe. Andika majina ya watu hao hapa chini. Usishangae kuona idadi uta-kayoonyeshwa na Mungu.
_______________ _________________ _______________
_______________ _________________ _______________
_______________ _________________ _______________
_______________ _________________ _______________
4. Shiriki orodha hii (katika kipindi cha kukiri) na rafiki mwaminifu au mchungaji.
5. Muulize rafiki huyo mwaminifu au mchungaji aombe nawe, ili Roho Mtakatifu afkufunulie zaidi mtu yeyote ambaye bado hujamsamehe—ingawaje huenda ukawa umemsahau mtu huyo. (Si rahisi kuyaona “mambo” yetu yote.)
6. Kumbuka, Bwana hakuhitaji upatane na mtu huyo ikiwa mtu huyo hayuko tayari kufanya hivyo. Upatanisho unahitaji msamaha kutoka kwa pande zote mbili. Lakini, jua kwamba Mungu anakuhitaji wewe uwe tayari kupatana.
20
#03 Uponyaji Kutokana na Kutosamehe www.healingofthespirit.org
7. Ikiwa unaona ugumu kumsamehe mtu fulani mwambie Bwana. "Niko tayari ku-fanywa kuwa tayari kwa kitendo cha uwezo wangu na hiari yangu.” Njia hii hufanya kazi kama kuwa na deni. Atakusamehe sasa, na kukuweka huru, unapoji-tahidi kumsamehe mtu uliyekubali kusamehe. Hakikisha umeweza kumsamehe mtu huyo au upate msaada kwa kuwaambia watu wengine wakuombee ili uweze kutimiza lengo hilo.
8. Ikiwa una ugumu wa kumsamehe mtu fulani, mwambie Yesu akujaze na ufa-hamu wake na upendo wake kwa mtu huyo (akufanyie jambo usiloweze kujifa-nyia mwenyewe) na amimine ndani ya moyo wako. Mwambie Mungu akufanye umwone mtu huyo kama anavyomwona yeye.
9. Wakati mwingine kutosamehe huko huwa kuna mzizi wa tukio la hapo awali lililokupa kiwewe au la kudhulumiwa. Katika hali hiyo, hatua ya hapo juu hai-tasaidia katika kumwachilia mtu aliyekukosea na hivyo basi utahitaji msaada wa mwombezi mwenye ujuzi, anayeweza kukuombea ili upate uponyaji wa ndani. (Ikiwa umejaribu kusamehe na kutosamehe kunaendelea kukurudia, labda ombi la uponyaji wa ndani litahitajika.)
10. Kwa imani, omba ombili lililo katika Eze. 36:26, Ukilitanguliza kwa kusema, Bwana, ninaamini ahadi yako katika kitabu cha Ezekieli inanifaa mimi pia.” “Ni-tawapeni moyo mpya na kuweka roho mpya ndani yenu: nitauondoa kwenu moyo mgumu kama jiwe na kuwapa moyo wa utii.”
11. Ikiwa mtu anayetafuta uponyaji ugumu wa kumsamehe mtu aliyemjeruhi, au mwambie mhusika arudie kila kosa alilofanyiwa na kila mkosaji, au anene na mkosaji kama kwamba yuko hapo. Akiendelea kuwa na ugumu zaidi wa kusa-mehe, airisha msamaha huo mpaka mwisho wa ombi la ukombozi baada ya kila milango kufungwa, na roho yake ina nguvu.
Ombi la Uponyaji Kutokana na Kutosamehe
Ikiwa una hasira na Mungu, kwanza mwombe akusamehe kwa kumkasirikia. Ha-lafu, kwa kila mtu uliyeorodhesha hapo juu (kama ulivyofunuliwa na Roho Mtakatifu) omba ombi lifuatalo (limetolewa katika kitabu kiitawacho The Bait of Satan, ukurasa wa 188):
Baba, katika jina la Yesu, ninakubai kwamba nimetenda dhambi kinyume chako kwa kukosa kuwasamehe watu walionikosea. Nimewakosoa na kuwahukumu wengine. Ninatubu. Ninatubu kwa kufanya hivyo na ninaomba unisamehe.
Pia ninakubali kwamba siweze kusamehe bila usaidizi wako. Kwa hivyo, kwa moyo wangu wote, ninaamua kumsamehe ______________ (taja jina la mtu huyo—mweke huru kila mtu mmoja mmoja).
Ninaweka chini ya damu ya Yesu mambo yote waliyonifanyia. Ninawaweka huru ili nisiwadai chochote. Ninawasamehe makosa waliyonitendea.
Baba wa Mbinguni, kama vile Bwana Yesu alikuomba uwasamehe waliomkosea, vivyo hivyo ninaomba uwasamehe walionikosea.
Ninawafungua kutoka utumwani, na ninajua kwamba chochote kinachofunguliwa duniani kitafunguliwa mbinguni pia. Ninaomba uwabariki na uwafanye wawe na uhusia-no wa karibu nawe.
Ninaomba mambo haya katika jina la Yesu. Amina.
21
#03 Uponyaji Kutokana na Kutosamehe www.healingofthespirit.org
Vifaa
1. Rodney Hogue, Forgiveness, 2008, kinapatikana Community of Grace, 380 Elmhurst St. Hayward, CA 94544. 81.
2. John Bevere, The Bait of Satan (Charisma House, 1994). ISBN 0-88419-374-8.
3. Susan Gaddis, Help, I’m Stuck with These People for the Rest of Eternity (Arrow Publications, 2004). ISBN 1886296332.
4. Kathie Walters, The Spirit of False Judgment (Faith Printing, 4210 Locust Hill Road, Taylors, SC 29687, 1995). ISBN 0-9629559-5-7.
22
# 04 Uponyaji Kutokana na Dhambi za Ngono na Miungano ya Nafsi
www.healingofthespirit.org
Uponyaji Kutokana na Dhambi za Kingono, Miungano ya Nafsi, na Kutazama kwa Picha/Sinema Za Watu Walio Uchi
Dhambi za Kingono
Hapo mwanzo Mungu alimuumba Adamu na Hawa na akawataka waungane kama mume na mke. “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye atamba-tana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja” (Mwa. 2:24; angalia pia Marko 10:2-12). Kuwa mwili mmoja kuna maana ya muungano usitenganishwa, kiroho na kimwili. Kili-chounganishwa duniani (kupitia kwa muungano wa ngono) kitaunganishwa kiroho mbinguni.
Mungu hakukusudia kuweko kwa uhusiano wa kingono nje ya ndoa, na kwamba ndoa ya kwanza ingekuwa ndoa pekee. Paulo anasistiza zaidi, akitufunza kwamba kusudi la Mun-gu kuhusu uhusiano kati ya mume na mke unaweza kutumiwa kama picha ya kusudi la Mun-gu kuhusu uhusiano kati ya Yesu na kanisa (Efe. 5:23). Lakini Mungu aliwapa na (kutupa sisi pia) hiari kuchagua. Kisha Shetani, baba wa uwongo ambaye nia yake ni kupotosha na kuharibu, akaingia uwanjani, na amekuwa akifanya kazi ya kugeuza amri na mapenzi ya Mungu tangu wakati huo wa dhambi ya kwanza katiak Bustani la Edeni.
La kusikitisha ni kwamba kuna dhambi nyingi za kingono zinazotendeka katika mwili wa Kristo sawa na zile zinazotendeka nje ya mwili wake. Kwa watu wengi, mafundisho ya Biblia yanaonekana kuwa yasiyofaa au yaliyopitwa na wakati. Siku hizi mambo ambayo wa-tu wanahangaishwa nayo ni hatari za kimwili za kufanya ngono bila kinga, badala ya ku-hangaishwa na mambo muhmu ambayo ni hatari za kiroho—ambazo tunazokosa kuziona.
Fikiria juu ya maandiko yafuatayo kuhusu somo hili:
1. Kutoka 20:14 inasistiza, “Usizini” (inayohusishwa katika kif. Cha 5, ambayo ni “maovu ya baba zao” yatakayopatilizwa wana wao hata kizazi cha tatu na cha nne).
2. Methali 6:32 inaonyesha kwamba mtu yeyote anayezini “anaangamiza nafsi yake.”
3. Malaki 2:13-16 anasema kwamba Bwana aliwaumba kitu kimoja katika mwili na ro-ho (kif. cha. 15).
4. Mathayo 5:32 inaeleza kwamba mtu anayetoka katika ndoa na kuingia katika ndoa nyingine, anazini (Tazama pia Mat. 19:9).
5. 1 Wakorintho 3:16 na 6:19 inathibitisha: mwili wetu ni hekali ya Mungu. Uzinzi hu-chafua hekalu ya Mungu.
6. 1 Wakorintho 5:1-6, ambapo Paulo anazungumza juu ya uzinzi ndani ya Kanisa.
7. 1 Wakorintho 6:16-20 inaonyesha inaeleza kwamba dhambi za kingono zinaelezwa katika kundi tofauti: "Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmo-ja naye? Maana asema, walw wawili watakuwa mwili mmoja.”Dhambi za kingono humfanya mtu atende dhambi dhidi ya mwili wake mwenyewe.
8. Wagalatia 5:21 inasema, “… watu watendao mambo ya jinsi hiyo (dhambi za kingo-no) hawataurithi ufalme wa Mungu.”
9. 1 Wathesalonike 4:3-6 tunapewa shauri “epukeni uasherati”—ni dhambi dhidi ya mwili wetu wenyewe.
10. Galatia 6:8 : Apandaye kwa mwili, katika mwili wake, atavuna uharibifu,
23
# 04 Uponyaji Kutokana na Dhambi za Ngono na Miungano ya Nafsi
www.healingofthespirit.org
Katika vifungu visivyopungua 55, Agano Jipya linashutumu “porneia,” neno la Kigriki lenye maana ya “uovu wa kingono.” Uovu wa kingono unaelezewa kama ngono kabla lya ndoa kwa katika ushauri wa Paulo kwa Wakristo ambao hawajaoana (1 Kor. 7:9). Hakuna majadiliano kuhusu iwapo Mungu anazichukulia dhambi za kingono kuwa mbaya sana. Dhambi za kingono ni nambari tatu ka-tika dhambi zinazochukiwa sana, baada ya (1) “msiwe na miungu wengine ila mimi” (Kumbu. 5:7) na (2) mauaji(Kumbu. 5:17). Fahamuni kwamba dhambi hizi hufungua shimo kubwa sana katika ukuta wetu wa kiroho (marejeleo ya somo hili yanaweza kupatikana katika ukurasa wa 2 katika sehemu yenye kichwa hiki, “Uponyaji wa Roho — Utangulizi”). Fikiria pia matokeo 25 ya kuzini (Tazama Meth. 5:4-2, 6:20-25 na 16-22; 2 Sam. 10:12, 11:4-7, 12:1-7 na 13-14).
Kulingana na Yeremia 3, Mungu anaiita ibada ya sanamu ya aina yoyote, kuwa ni “kuunga-nishwa” kwa Mungu mwingine. Anakiita kitendo hiki uasherati wa kiroho. katika kueleza uasherati wa kimwili kama “kuunganishwa pamoja kusikofaa—iwe ni kabla au baada ya ndoa na katika mahu-siana ya ngono ya jinsia moja (usenge) au kuhusiana na wanyama kingono,” katika amri ya saba (Kut. 20:14) hii ina maana pana zaidi kuliko kitendo kinachofanyika katika “dhambi ya ngono kati ya mume na mke inayotendwa na watu waliooa/olewa.”
Kupitia kwa muungano wa kingono, kuna kuungana kwa roho, nafsi na mwili. Baada ya kitendo cha ngono, miili inaweza kutengana lakini nafsi na roho huwa bado zimeunganishwa pamoja. Kitu fulani katika mwanamume huyo huwa sehemu ya mwanamke huyo, na kitu fulani katika mwa-namke huyo huwa sehemu ya mwanamume huyo. Muungano husababisha “muungano wa nafsi” wa kiroho na kimwili kati ya watu hao wawili. Hii ni ndiyo iliyokusudiwa na Mungu atika muungano na ndoa ya kwanza kati ya mume na mke. Jambo la kusikitisha ni kwamba, watu wanapofanya ngono na watu ambao si “mume au mke wake wa kwanza na wa pekee,” hali ya kiroho ya “mwili mmoja” hu-changanyika, na mpango kamili wa Mungu kwetu huzuiwa, kama vile mpango wake kwa Adamu na Hawa ulizuiwa. Kinachofungwa duniani hugungwa mbinguni. (Mat. 16:19, 18:18)
Tunapoungana kingono na mtu mwingine, sisi huunganishw na mtu huyo kihisia na kiroho. Muungano wa kingono kati ya mume na mke (kama inavyoelezwa katika Mwa. 2:24) huruhusu kule kushiriki pamoja upendo na vipawa vingine vyote kati yao. Muungano wa kingono nje ya mpango wa Mungu kuhusu ndoa (Mwa. 2:24) humfanya mtu apokee mambo yote mabaya kutoka kwa mwenzi wake wa kingono (kama vile roho za giza, kumvutia mtu kwenye mazoea ya tabia mbaya, uovu wote ambao mtu huyo ameupokeakwa ajili ya dhambi zake au dhambi za mababu zake kupitia kwa laana za kizazi, kama ilivyoagizwa katika Kut. 20:5) na matokeo mengine ya dhambi ambazo mwenzi huyo wa ngono aliwahi kutenda (kama vile kujihusisha katika mizungu/ushetani).
Kupitia kwa muungano wa kingono, sisi huwa kitu kimoja na roho ya mtu huyo. Hatuungani tu na mtu tuliyehusiana naye kingono, bali pia tunaunganishwa kwa mfano wa mnyororo na kila mtu ambaye amewahi kushirikiana na mtu huyo kingono. Kufanya ngono nje ya ndoa ni kuuvunjia heshima uumbaji wa Mungu na pia ni tukano kwake, la uasi na upumbavu. Dhambi za kingono hu-wezesha nguvu zozote za giza au mapepo yaliyo ndani ya mtu mmoja kuingia ndani ya mwenzi wake. Na si hilo tu, bali pia humwezesha mwenzi huyo kuingiwa na kila roho ya giza kutoka kwa uhusiano wowote wa awali aliokuwa nao mtu huyo. Hiyo husambaza giza kama vile Virusi vya Ukimwi.
Utumwa na/au Muungano wa Nafsi
Utumwa wa nafsi au muungano wa nafsi hutokana na kuunganishwa pamoja kwa aina yoyote. Utumwa wa nafsi au muungano wa nafsi ni kuunganishwa pamoja kwa mwili, roho, au nafsi katika uhusiano ambao nafsi mbili huunganishwa pamoja na kuwa kitu kimoja. Hii inaweza kufanyika kiroho, kihisia, au kimwili. Fahamu kwamba kuna muungano wa nafsi
24
# 04 Uponyaji Kutokana na Dhambi za Ngono na Miungano ya Nafsi
www.healingofthespirit.org
ulio mzuri (mtakatifu, na unawezeshwa na Mungu) na pia kuna muungano wa nafsi ulio mwovu (usiomtakatifu).
Muungano Unaowezeshwa na Mungu
Muungano unaowezeshwa na kubarikiwa na Mungu ni pamoja na ule ulio halali na mzuri katika uhusiano wa kindoa kati ya “mume na mke”, uhusiano kati ya mzazi na mtoto, uhusiano kati ya ndugu, na uhusiano katia ya jamaa wengine (Mwa. 2:24, Mat. 19:4-9, n.k.). Muungano huo ukivurugwa na kifo, talaka, au uzinzi, kunaweza kuwa na jeraha kubwa sana.
Muungano Usiomtakatifu Unaowezeshwa na Shetani
Muungano usiomtakatifu unaosababishwa na shughuli za uovu wa kingono (na kwa nadhiri za giza, maagano, laana, viapo, na viapo vya siri vya vyama) huwezeshwa na Sheta-ni na ni chukizo kwa Mungu. Dhambi za kingono huzaa muungano wa nafsi usiomtakatifu kiroho na kimwili nazo zinatakiwa kuvunjwa kabla ya uponyaji kupatikana na mfungwa kuwekwa huru.
Muungano Usiosababishwa na Ngono
Muungano usiosababishwa na ndoa hutokea wakati ambapo mtu mmoja humtawala mtu mwingine kwa namna ambayo Mungu hakuipanga. Wakati mwingine muungano mbaya wa nafsi usio wa kiongono hujitokeza na wazazi, washauri au marafiki—watu tunaovutiwa nao au ambao tuna uhusiano wa karibu nao au wa siri. Hii huonekana zaidi katika uhusiano wa kutegemeana.
Uasherati wa Kiroho
Uasherati wa kiroho hutokea (1) wakati ambapo mwenzi wa ndoa humpa mtu mwin-gine kitu ambacho ni cha mwenzi wake pekee (kwa mfano, kuwasiliana na mtu mwingine kwa njia ya siri kutoka moyoni au kuwa na uhusiano wa ndani na mtu mwingine), (2) iwapo moyo wa mwenzi mmoja wa ndoa haujajivunza kukumbatia chanzo cha uume au uuke katika muungano wao wa ndoa (3) unapomwonyesha mapenzi au kumbusu kwa hisia kali mtu asiye mwenzi wako wa ndoa, au (4) unapomwelezea mtu mwingine (ambaye si mshauri) hisia za ndani.
Muhtasari wa Matokeo ya Dhambi za Kingono
1. Dhambi za kingono huuzuia upendo wa Mungu unaotiririka kati ya mume na mke katika hali ya kweli na takatifu inayodhihirika katika hali zetu za kufanya mapenzi.
2. Uzinzi ni uharibifu ambao hatimaye huwa na gharama (sheria ya kupanda na kuvuna hujidhi-hirisha hapa).
3. Dhambi za kingono huzaa mazoea mabaya ya kingono, ukahaba, uzinzi, dhuluma ya kingono, ngono kati ya watu wanaohusiana kidamu, usenge, aibu, haita, na kukosa kujithamini.
4. Uzinzi hauwezi kukaa pamoja na Roho Mtakatifu; uzinzi ukiendelea, Roho Mtakatifu ataon-doka.
5. Katika ngono isiyo ya kiungu, kitu fulani kutoka kwa kila mwenzi huenda kwa mwenzake na kuwa sehemu ya mtu huyo (Tazama mfano katika 1 Kor. 6:16, ambapo Paulo anazungumza juu ya watu “wanaungwa” kwa kahaba kuwa “wao hufanyika kuwa mwili mmoja.”).
25
# 04 Uponyaji Kutokana na Dhambi za Ngono na Miungano ya Nafsi
www.healingofthespirit.org
6. Dhambi ya kingono huwa ni mnyororo wa utumwa ambapo watu, bila kujua huathi-riwa na maisha na sifa za watu ambao wameunganishwa nao kingono.
7. Muungano wa nafsi usio wa kiroho hutoa nafasi ya mambo hayo yote kuhamishwa (kwa mapepo kuhamisha kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine—wakati wa kufanya ngono na wakati mwingine unaofuata): roho za giza, kumvutia mtu kwenye mazoea ya tabia mbaya, uovu wote ambao mtu huyo ameupokea kwa ajili ya dhambi za ma-babu zake kupitia kwa laana za kizazi, Kut. 20:5) na matokeo mengine ya dhambi ambazo mwenzi huyo wa ngono aliwahi kutenda, kama vile kujihusisha katika mi-zungu/ushetani).
8. Watu wenye wenzi wengi wa kimapenzi hupoteza sura yao. Wao huanza kusahau wao ni kina nani.
9. Fikira juu ya matokeo 25 ya uzinzi yaliyotambuliwa katika maandiko (baadhi ya mi-fano hiyo ni Meth. 1:8-20, 5:1-12 na 6:20-32, 2 Sam. 11:4-7, 12:1-14).
10. Mungu anachukia uzinzi. Ndiyo dhambi ya tatu mbaya kuliko ibada ya sanamu na kuua
Neema ya Uponyaji
Habari Njema ni kwamba Mungu wa mbinguni alimtuma Mwanawe Yesu Kristo afu-tie msalabani ili tupate msamaha wa dhambi zetu zote, za kingono na zengine pia, tusafishwe kwa damu ya Yesu, na tuweze kuwa na uhusiano mpya naye kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Bwana alimsamehe mfalme Daudi na yule mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi (2 Sam. 12:13, Yohana 8:11). Atakusamehe wewe pia na kukuweka huru.
Labda ushakiri kwa Mungu dhambi zako za kingono “ulipozaliwa mara ya pili” na ukasamehewa. Kwa hali yoyote, hiyo haikuwezeshi kuepuka matokeo ya dhambi zako. (kwa mfano, ikiwa ulitoa mimba, je, Mungu atasemehe dhambi yako ya kuua? Ndio; alifanya hivyo msalabani; lakini ataweza kuondoa mara moja matokeo ya dhambi hiyo na kukurudi-shia mtoto huyo? La. Dhambi hiyo inabebwa na mama huyo lakini matokeo ya dhambi hiyo yanabebwa na mtoto huyo aliyetolewa. Wakristo wanaweza kutubu kwa moyo wao wote na bila kujua waendelee kuwa chini ya athari za giza katika sehemu ya roho zao kama matokeo ya dhambi walizofanya hapo awali)
Milango iliyo wazi isipofungwa na haki iliyotolewa kwa nguvu za giza kukanushwa na kupewa Mungu, adui anaweza kuendelea kutumia sehemu hiyo ya dhambi ulizotenda awali dhidi yako, hata kama umesamehewa.
Maombi ya dhambi za kingo, muungano wa nafsi, na utakaso ziko hapa chini.
Ombi la Kufanywa kwa ajili ya Dhambi za Kingono
Ombi hili la kuwekwa huru kutoka kwa dhambi za kingono na utumwa (au muungano wa nafsi) inatakiwa kushughulikia sehemu hizi:
1. Omba usamehewe.
2. Omba uwekwe huru na kufunguliwa.
3. Omba ili kuzivunja nguvu za tamaa ya kurithiwa; omba ili umsamehe mtu aliyeingiza dhambi hiyo katika ukoo wa familia.
4. Ombea kuvunjwa kwa muungano wowote wa nafsi kati ya mhusika anayetaka kuom-bewa na watu aliyehusiana nao kingono au na mume wa zamani ambaye hameachana.
26
# 04 Uponyaji Kutokana na Dhambi za Ngono na Miungano ya Nafsi
www.healingofthespirit.org
4a. Omba kwamba upanga wa Roho Mtakatifu utamtenganisha kila mwenzi na ku-vunza kila muungano wa nafsi.
4b. Uweke msalaba wa Yesu kati ya kila mwenzi na kuwafunika na damu ya Yesu.
4c. “Mfungue” kila mwenzi kutoka kwa mapatano yasiyo takatifu.
4d. Katika jina la Yesu, tangaza kutenganishwa kwa roho za watu waliojihusisha ka-tika uzinzi.
4e. Chukua mamlaka (katika jina la Yesu), na uvunje nguvu zozote za kishetani zi-lizo ndani ya maisha ya mtu huyo kwa ajili ya kujihusisha katika ngono isiyo ha-lali, ufungwa usio wa kingono, au uzinzi wa kiroho.
4f. Ikiwa sasa mtu huyo ameolewa kwa mtu ambaye “amezaliwa mara ya pili”, omba kwamba Mungu atatambua muungano huo wa sasa kama inavyosema katika Mwa.2:24 na Marko 10:2-12 kwamba “nao wawili watakuwa mwili mmoja”).
5. Ombea utakaso wa mwili, nafsi na roho.
5a. Ombi ili akili ya mtu hiyo itakaswe kutokana na picha za kumfanya mtu awe na ashiki, matukio ya kingono yasiyo ya kiungu na mawazo yote ya dhambi, mane-no, na matendo.
5b. Ombea utakaso wa macho yaliyotazama vitu ambavyo hayakutakiwa kutazama.
5c. Ombea utakaso wa masikio yaliyosikia mambo yasiyo matakatifu.
5d. Ombea utakaso wa mdomo, ngozi, mikono, na sehemu za siri kwa ajili ya vitu vi-liyovigusa.
6. Omba ukipinga roho za uzinzi, kutazama picha zinazoleta ashiki, desturi za kingono zisi-zo za kawaida, hasa ikiwa mhusika huyo amewahi kufanya ngono na kahaba au mnyama.
7. Ombea mhusika ili aweze kuwekwa huru kutoka ana uvozu huo wote na kutoka kwa ma-tokeo ya dhambi hizo.
8. Omba kwamba Mungu atayaponya matukio hayo yote ili Shetani asiweze tena kuyatumia kwa makusudi ya uovu.
9. Mwombee mhusika huyo ili aponywe kutokana na kila hatia na aibu.
10. Ombea uponyaji wa dhambi hizo zote na muungano wa nafsi, ili mtu huyo aweze kufu-nikwa kwa damu ya Yesu.
11. Kwa watu ambao hawajaingia katika ndoa, omba kwamba “hisia za kawaida za kingono” zitaelekezwa katitka shughuli zinazokubalika na zinazofaa.
12. Mfungue kutokana na uzinzi na ndoa za wake wengi za vizazi vilivyotangulia
Sehemu hii ya dhambi za kingoni inahitaji kumtumia mwombezi. Ni vigumu sana kwa mhusika kujiombea na kufanikiwa kabisa katika sehemu hii. Kwanza mhusika anahitaji kukiri dhambi hiyo na kutubu kwa sauti akimtaja mwenzi wake (au wenzi wake, ikiwezekana, kama anvyoelekezwa na Mungu).
Pia, mhusika anatakiwa kutubu kwa ajili ya matendo ya kingono yasiyo halali na yasiyo ya kawaida pamoja na utazamaji wa picha za kumpa mtu ashiki, ikihitajika kufanya hiyvo. Ana-takiwa kukanusha roho wa tamaa, tamaa ya macho, na kukanusha nafasi ya Shetani, aliyo-pewa hapo awali kwa kufanya matendo hayo yote. Jambo muhimu ni mhusika huyo kuamua kuishi maisha matakatifu au kuoa (1 Kor. 7:1-16).
Ni vigumu kuvunja mwenendo wa kingono wa hapo awali, hasa ikiwa mhusika huyo ni kijana ambaye hajaoa. Katika kila hali, mhusika anatakiwa kuonywa kwamba Shetani atam-tia katika majaribu baada ya kupata uponyaji.
27
# 04 Uponyaji Kutokana na Dhambi za Ngono na Miungano ya Nafsi
www.healingofthespirit.org
Ombi la Kumfungua na Kumweka Mtu Huru
Mwombezi anatakiwakuomba ombi hili:
Katika jina la Yesu, ninaamuru roho yako isahau miungano hii. Katika jina la Yesu umefunguliwa kutoka kwa mtu huyo (au watu hao). Ninatangaza kutenganishwa kwa roho yako kutoka kwa kila mwenzi huyo, na ninauweka msalaba wa Yesu kati yako na kila muungano huo usio mtakatifu. Ninakufunika kwa damu ya Yesu kama ngao ya kukulinda kutokana na athari zozote mbaya zilizokujia kupia kwa miungano ya kingono kati yako na mwenzi (au wenzi) hao.
Ninaiweka roho yako huru ili iambatane na mwenzi wako wa ndoa. Ni-nakuweka huru katika jina la Yesu, ninashukuru kwa ajili ya neno la Mungu li-nalotangaza, “…kila utakachofunga duniani, kitafungwa pia mbinguni; kila utakachofungua duniani, kitafugnuliwa pia mbinguni” (Mat. 16:19). (Endelea kuomba ombi la utakaso, lililo hapa chini.)
Ombi la Utakaso
Kutoka katika Ezekieli 36:25 (“Nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtata-kata uchafu wenu wote na sanamu za miungu yenu yote”) na Matendo 11:9 (“Ile sauti ikasikika tena kutoka mbinguni: usiviite najisi vitu ambavyo Mungu amevitakasa.”) tunaamini tumetakaswa; na kutoka Waebrania 10:10 (“Kati-ka mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.”) tunaamini kwamba kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo, tume-takaswa. Ninaomba kwamba Mungu atayanyunyizia maji yake safi juu ya kila kitu kinachohitaji kutakaswa. (Wakati mwingine Mungu anaweza kukupa pi-cha; omba kuhusu unachoona katika picha hiyo.)
Yesu, tunakuomba sasa umimine mito yako ya maji ya uzima juu ya _____________ na katika kila seli ya mwili wake. Yaache maji hayo yatiririke juu ya kila sehemu ya mwili wake, kicha, mikono, sehemu za siri, miguu, nyayo.
Asante Bwana kwa sababu maji yako ya uzima yanamtakasa mtu huyu “awe mweupe kama theluji,” (“Haya njooni tusemezane, asema BWANA: Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana zitakuwa nyeupe kama theluji; Zijapo-kuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.”—Is. 1:18) kwamba kila sehemu ya kuchafuliwa, aibu, na hatia inaoshwa.
28
# 04 Uponyaji Kutokana na Dhambi za Ngono na Miungano ya Nafsi
www.healingofthespirit.org
Asante Bwana kwa kumsafisha mtu hulyu, ndani na nje. Bwana, sasa un-amwona kuwa safi na mweupe kama alivyokuwa siku ambayo ulimuumba kule mbinguni—umempa mwili mpya katika Yesu, mwili safi na mtakatifu. Asante. Katika jina la Yesu nimeomba. Amina.
Vifaa
1. Doris Wagner, Ministering Freedom to the Sexually Broken (Wagner Publications, 2003). ISBN 1-58502-038-9. (Hiki kitabu kilikuwa kifaa bora zaidi kuhusu somo hili—ambacho mambo mengi yaliyo hapa juu yalitolewa.) (now 4 booklets are combined into one 332 page booklet entitled “How to Minister Freedom”, Wagner, Doris, 2005 ISBN 0830737251, 30 contributors)
2 John & Paula Sandford, Transformation of the Inner Man (Victory House, 1982): 269-94. ISBN 0-932081-13-4.
3. Elaine Rose Penn, Soul Ties (Charisma Training Ministries, PO Box 2410, Albany, NY 12220, 2000). ISBN 0-9700449-0-9.
4 Bill and Sue Banks, Breaking Unhealthy Soul-Ties (Impact Books, 322 Leffingwell Ave., Suite 101, Kirkwood, MO 63122, 1999). ISBN 0-89228-139-1.
Kutazama Sinema/Picha Za Matukio ya Ngono
Neno hili “Ponografi” limebuniwa kutoka katika neno la Kiyunani “porne”asmbalo linaweza kutafsiriwa kuwa na maana ya kahaba wa kike au mtumwa wa kimapenzi. Neno Porneia lina tafsiri ya uzinzi, usherati au uchafu wa kimapenzi. Katika Agano Jipya kuna vi-shiria 26, sita zikiwa kwenye nyaraka za Paulo kwa Wakorintho. Muktadha wake ni kuwa waumini hawapaswi kuhusika katika tamaduni ambazo ziliwazingira waumini wa nyakati hizo. “Lakini mimi nawaambia: kwamba ye yote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” (Math 5:28). Naamini kuwa andiko hili linaashiria picha na sinema za watu walio uchi tunazozitazama kwenye majarida, runinga, filamu, simu, na komputa na hata kuwatazama watu walio uchi. Miili yetu haikuumbwa kwa kutazamwa ikiwa uchi (1Wakorintho 6:13). Yatupasa tuepukane na tabia hii (1Wakorintho 6:18) na kuji-kinga tusije tukaishia kuwa watumwa (1 Wakorintho 7:2). Iwapo tumekita mizizi ndani yake lazima tutubu na kumgeukia Mungu (2Wakorintho 12:21)
Jambo la kusikitisha ni kuwa kule Marekani Serikali inaruhusu kutazama picha hizi kama sehemu ya haki za wananchi za kikatiba. Tukiuangalia mtandao tunagundua kuwa jambo hili limeenea kote na linafanyika kwenye siri za vyumba vya watu. Yafaa itambuliwe kuwa kila kilichofichika hutumiwa na Shetani kutudhuru sisi.
Lipo kundi moja linajiita Wawekaji wa Ahadi lililoanzishwa 1990, katika mojawapo ya mi-kutano yao kwenye halaiki ya watu 60,000 asilimia 60% walikuwa wamejihusisha katika tendo hili. Hawa walikuwa ni washirika wa kanisa na hata viongozi wenye nafasi za kutama-nika kwenye kanisa. Kutokana na mikutano yao kulitokea chombo cha filamu kiitwacho: Personal Holiness in Times of Temptation, kama sehemu ya kujikita kwenye mafunzo ya
29
# 04 Uponyaji Kutokana na Dhambi za Ngono na Miungano ya Nafsi
www.healingofthespirit.org
Biblia iliyoandaliwa na Dr. Bruce Wilkinson. Shida hii inaathiri watu wengi kanisani na nje yake wala haliathiri watu wachache tu.
Tendo hili la ponografi ni uasi kwa Mungu na nafsi yake iliyo ndani yetu. Inaharibu thamani ya kujuana kimapenzi na kuifanya kama chombo cha ubatili. Hudunisha thamani ya mwili wa mwanadamu na ni sumu in-ayoufanya mwili kuwa chombo cha kibiashara. Wanaume wengi wanao-husika katika tendo hili hupoteza hisia zao za kimapenzi na kumdharau mwanamke aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu ili kumkamilisha mwana-mume. Kila mtu anazitazama picha hizo ndivyo anavyodidimia katika utumwa wa kutofurahia tendo la ndoa na mpenzi wake wa halali.
Kama chakula kinavyotumika mwilini ndivyo picha hizi zinavyoathiri mawazo na hisia za mtazamaji. Mwishowe mtazamaji anaweza kufana-nishwa na mtu anayetumia madawa ya kulevya na pombe kali.
Utazamaji huu mwishowe humfanya mtu mtumwa na akawa hawezi kufi-kiri kama Mungu alivyokusudia. Watu wanaotazama picha au filamu hizi mwishowe huanza kutumia vyombo visivyo vya kawaida kukidhi mahitaji yao ya kingono.
Dhambi hizi mtu huzitenda kinyume cha mwili wake mwenyewe (1 Wa-korintho 6:17. Miili yetu inapaswa kuwa makani/hekalu la Mungu (1 Wa-korintho 6:12-20) Tunapojihusisha na matendo yaliyo kinyume ya mapen-zi ya Mungu, tunamuasi Mungu. Roho mtakatifu huumia na anaweza ku-hama kutoka katika nafsi zetu. (Efeso 4:31). Tendo hili linamzuia Roho Mtakatifu wa Mungu kutenda kazi ndani yetu. Na tunweza kufikia mahali ambapo tunaweza kumuudhi roho. (1 Thes 5:19)
Wanadamu wote wameumbwa kwa mfano wa Mungu, ili tumjue, tumpende na kumuabudu Kristo. Tunapaswa kila mara kuishi na kufanana na Mungu ili tufikilie utakatifu.
Ili tuiondokee hii dhambi, ni sharti tutubu na kugeukia tabia hii na pia ku-wahusisha wakristo wengine ili waweze kuwa msaada wa karibu katika kutuhimiza tuondokane na dhambi hii.
Mungu anatuhitaji tuishi katika utakatifu kwenye masuala ya ngono. Hivyo basi kutazama picha za matukio ya ngono au watu walio uchi ni dhambi. Jee kuiga tendo la ndoa kwa kutumia vyombo visivyo vya kibina-damu ni halali? Ijapokuwa Bibilia haisemi chochote kuhusu jambo hili,
30
# 04 Uponyaji Kutokana na Dhambi za Ngono na Miungano ya Nafsi
www.healingofthespirit.org
swala tunalopasa kujiuliza ni: Je tendo hili linanielekeza kwa utakatifu? Wengine hunukuu Mwanzo 38:9: “Lakini Onani alijua kwamba uzao haungekuwa wake, kwa hiyo kila alipokutana kimwili na mke wa ndugu yake, alimwaga chini mbegu za kiume ili asimpatie ndugu yake uzao..” ili kueleza kuwa inakubalika kwenye Bibilia. Lakini tuseme tafsiri hii si sa-hihi. Tendo hilo ni dhambi kwa kuwa mila za Waisraeli zilimtaka ndugu wa kiumu wa mwanamume kumzalia nduguye watoto akikutana na mjane wa nduguye aliyekufa. Mfano huu watuonyesha kuwa Onani hakuwa mtii-fu kwa desturi hii ndiposa Bwana akamuua.
Je tubadili vipi mawazo yetu kuelekea utakatifu? Jawabu ni toba na kutubu. Kila kilichofichika chatuelekeza dhambini na ni mlango wazi kwa adui kuingilia. Haitoshi kuomba msamaha kwa Mungu pekee. Ni vyema kutubu mbele ya wapendwa na Mungu. Pia ni vyema kutubu kwa mchun-gaji na kama sisi ni wachungaji tutubu kwa maaskofu ili tupate kuwajibika anayeweza kutusaidia na kututia moyo tusije tukaanguka tena
Ombi La Uponyaji
Baada ya toba na maombi ya msamaha, mtafutaji asaidiwe kukana tama za mwili, macho na usherati uliokithiri moyoni mwake (Math 5:28). Mwom-bezi amuombe Mungu amletee mtafutaji picha ya tukio lile la kwanza. Ki-sha ombi lifanywe ili Yesu aingie kati ya mtafutaji na tukio. Omba damu ya Yesu imfunike mtafutaji kasha yeye mwenyewe amuombe Mungu afute kumbukumbu ya matukio yote yasioletea Mungu utukufu na kumta-kasa. Mapepo ya uchu, tamaa ya macho na usherati yapasa kukemewa ya-toke
Ilani: Habari hizi zimenukuliwa kutoka kwa kitabu cha William M. Struthers, Wired for Intimacy. How pornography hijacks the male brain. 2010, ISBN 978-0-8308-3700-7.
Nyongeza A ina orodha ya vifaa vilivyo kwenye mtandao ili kumsaidia mtu ku-epukana na Ponografi na ulevi wa ngono. Nyongeza B ina vitabu juu ya namna ya kumsaidia mtu kuepukana na Ponografi na ulevi wa ngono.
31
#05 Kuponya Kuharibu na Kutoa Mimba www.healingofthespirit.org
Kuponya Kuharibu na Kutoa Mimba
Watu wengine wanaweza kuuliza, “Kwa nini uponyaji wa kuharibika mimba na utaoji mimba” umewekwa katika sehemu moja? Moja hutokea bila hiari ya mtu na nyingine kwa chaguo la mtu.” Katika hali zote mbili, maisha hupotezwa, kawaida huwa mazishi hayafanyi-ki, na mara nyingi huwa hakuna ukamilishaji wa jambo hilo kihisia. Huenda mtu akaunga-nishwa na kijusi huyo kiroho na kihisia kwa miaka mingi baada ya kitendo hicho ndiyo maana uponyaji unahitajika.
Kuharibika Mimba
Idadi kamili ya mimba zilizoharibika haijulikani. Hata hivyo, kifo ni kitukilichoingi-lia mpango wa Mungu. Yeye hakukusudia sisi tufe. Dhambi ya Adamu na Hawa iliubadili-sha mpango huo.
Si mapenzi ya Mungu kwa watoto kufa wakiwa tumboni, lakini kwa vile tunaishi kati-ka ulimwengu wenye dosari uliojaa magonjwa, kuharibika mimba hutokea. Kiwewe cha kihi-sia anachopata mama kwa kukipoteza kijusi hicho pamoja na tatizo la fikra za kutojali za kina baba wengi ambao husema, “Tusahau jambo hilo na tuendelee na maisha,” wakati ambapo mama anaomboleza na anahitaji kulikamilisha jambo hili kwa vyovyote vile, kabla ya mama kuwa na amani kutokana na msiba huo, atahitaji kulifunga tukio hilo kiroho na kihisia na ata-hitaji kumwachilia mtoto huyo aende kwa Yesu. (Jambo hili halitakiwa kufanywa na kina mama pekee, lakini tutatumia hali inayompata mama kwa ajili ya maelezo.)
Mara nyingi, mtoto asiyezaliwa huwa hafanyiwi mazishi (au ibada ya ukumbusho) na mara nyingi mama huwa halifungi jambo hilo wala kumwachilia mtoto huyo aende kwa Yesu. Pasipokuwa na kulifunga jambo hilo na kuwachilia, sheria ya kufunga na kufungua itatumika: mama huyo amefungwa duniana na mtoto amefungwa mbinguni.
Uponyaji wa ndani unahitajika ili mama huyo awe na amani. Mama huyo anaweza ku-jilaumu kwa kudhani kwamba alichangia kuharibika kwa mimba hiyo kwa sababu ya kuto-zingatia afya au kwa sababu hana hakika iwapo angefanya jambo lolote kukizuia kitendo hi-cho. Wazo la kudhani kwamba angezuia kitendo hicho ni uwongo kutoka kwa adui ambao mama huyo ameukubali na kuamua kuamini. Huenda mama akaingiwa na uwoga wa kudhani kwamba hataweza kushika mimba tena au mambo mengine kama hayo (uchungu wa kutenga-na au kutokamilisha maombolezi, na hivyo basi kuunganishwa na mtoto asiyezaliwa). Zaidi ya hayo, roho wa kifo anaweza kumuingia mtu kupitia kwa tukio hilo la kuharibika mimba.
Kuombea Kuharibika kwa Mimba (mwombezi anatakiwa kufuata hatua hizi)
1. Peleka tukio hilo mbele ya Bwana.
2. Muulize mama ikiwa huyo tayari kumwachilia mtoto huyo kwa Yesu.
3. Omba ombi la kukubali kuwachilia (kwamba mama huyo atavunja muungano wa nafsi yake na mtoto huyo na atamwachilia mtoto huyo kwa Yesu, na kumkabidhi mtoto huyo kwa Yesu ili afanye apendavyo na mtoto huyo).
4. Omba ili Bwana alete amani kati ya mama na mtoto huyo.
5. Ombea hali yoyote ya kuwa na hatia.
6. Omba ili mama huyo aweze kumwonga mtoto huyo akiwa na Yesu (wakati mwingine Bwana anaweza kumwonyesha mtu jinsi ya mtoto huyo.).
32
#05 Kuponya Kuharibu na Kutoa Mimba www.healingofthespirit.org
7. Wakati mwingine Bwana anaweza kuwafunulia jina la mtoto huyo; la sivyo, amwambie mama ampe mtoto huyo jina.
8. Omba ili baraka iwe juu ya mama na mtoto huyo.
9. Waambie wazazi wote wawili wamwambie Yesu awaruhusu kumpakata mtoto wao.
10. Waambie wazazi wote wawili waombe ombi la kujisamehe. (Wakati wa ombi hili huzuni unaweza kujitokea kama hasira au uchungu mwingi na huenda kukawa na kulia, ambayo ni njia ya kuwachilia.)
Kutoa Mimba
Ni jambo la kusikitisha kwamba karibu 50% za mimba kule Marekani hutolewa. Kwa hali yoyote, Mungu analiona jambo hili kuwa ni mauaji. Toba inahitajika kwa ajili ya kitendo hiki. Kumbuka kwamba, Mungu alimsamehee Daudi alipoua na hivyo basi atamsamehe mhusika huyo pia. Katika njia hii, mara nyingi huwa kuna roho wa kutoa mimba anayetakiwakufukuzwa, pa-moja na roho zengine zinazoambatana na dhambi mbalimbali za ngono.
Kuombea kitendo cha Kutoa Mimba (Fuata hatua hizi)
1. Mwambie mhusika aombe Ombi la Kuungama Dhambi baada ya kufuata hatua ya kuungama, kutubu, na kanusho (kama ilivyoelezwa katika sehemu ya kitabu hiki iliyo na kichwa hiki, “Uponyaji Unahitaji Toba.”
2. Mara nyingi huwa kuna dhambi zengine za ngono zinazotakiwa kushughulikiwa (kama ilivyotajwa hapo awali).
3. Peleka mbele ya Bwana tukio hilo la kutoa mimba.
4. Ombea uponyaji katika hali yoyote ya hatia, aibu, woga, na/au kuchanganyikiwa ambayo huenda ilitokea wakati wa kutoa mimba.
5. Ikihitajika, omba kwamba yesu atajidhihirisha katika tukio hilo
6. Omba ombi la kukubali kuwachilia (kwamba mama huyo atavunja muungano wa nafsi yake na mtoto huyo na atamwachilia mtoto huyo kwa Yesu, na kumkabidhi mtoto huyo kwa Yesu ili afanye apendavyo na mtoto huyo).
7. Omba ili Bwana alete amani kati ya mama na mtoto huyo.
8. Omba ombi la kutakaswa.
9. Omba ili mama huyo aweze kumwona mtoto huyo akiwa na Yesu (wakati mwingine Bwana anaweza kumwonyesha mtu jinsia ya mtoto huyo.).
10. Wakati mwingine Bwana anaweza kuwafunulia jina la mtoto huyo; la sivyo, amwambie mama ampe mtoto huyo jina.
11. Omba ili baraka iwe juu ya mama na mtoto huyo katika jina la Yesu.
12. Waulize wazazi wote wawili wajiombee ombi la msamaha (wakati wa ombi hili kuombo-leza au hasira yaweza kusababisha kilio ambayo ni sehemu ya kufunguliwa).
13. Omba kwa ajili ya utakaso.
33
# 6 Healing from Witchcraft & Polygamy www.healingofthespirit.org
Uponyaji wa Uchawi, Itikadi za Kijamii, Mitishamba na Ndoa za Wake Wengi
Semina za wachungaji za hivi majuzi Afrika zimedhihirisha kuna athari fulani zinazoathiri watu katika mada hii ya ukombozi ambazo ni maalum kwa bara la Afrika.
Uganga , Uchawi na Utabibu wa Kienyeji
Mtu akimwendea au kupelekwa kwa mganga yeye mwenyewe au pamoja na wazazi wake au ikiwa vizazi vilivyotangulia viliwahi kumwendea mganga , mara hiyo huwa amepkoea pepo wa uganga anayeambatana na ufukara na kuji-takia kifo. Mtu huyu husumbuka na kujidunisha, kutojipenda na kukata tama ya maisha. Katika kutibiwa mtu aweza kuchanjwa katika maeneo mbalimbali ya mwili ambapo anafanya mapatano ya damu na giza. Mapatano haya yanamfun-ga mtu na kuzuia kuwekwa huru kwake. Pengine katika tukio lile anatoa kafara ya mnyama na kupewa hirizi au aina ya chombo cha kumlinda. Mganga husema dua fulani au kumuapiza kiapo fulani na kumnywesha dawa au maji fulani ya-liyoandaliwa kwa sababu hiyo.
Matokeo ya vitendo hivyo huleta madhara makuu kama vile utasa, uka-haba,. Kuharibu mimba, kutangatanga, kupoteza ajira kusikoweza kuelezeka, mahusiano yanayotatanisha na hata talaka. Wanaume wanaweza kuonyesha upungufu wa nguvu za kiume, kufilisika, hasira, ukatili na usherati. Laana hii ya kizazi hupokezwa hadi pale toba na kuvunjwa kwake kutakapotekelezwa. (Kutoka 20:6)
Yapasa ieleweke kuwa sababu kuu ya waafrika kuwatembelea waganga ni uhaba wa madaktari waliofuzu. Utapata katika maeneo mengi kuna daktari mmoja kwa watu 5000 na zaidi hasa ukitembelea sehemu za mashambani zilizo mbali na miji mikuu. La ziada ni kuwa ili mtu atibiwe mpaka alipe ada zote za matibabu. Hivyo basi kwa jamii zinazosumbukia mahitaji ya chakula, hii hali huleta uzito mkuu kwa mapato ya jamii.
Mama asiyejua anampeleka mtoto aliye mahututi kwa mganga ambaye humtibu na hali yake kuimarika lakini ndani yake huwa mmeingia roho ya giza. Hali hii huambatana na motto Yule maisha yake yote hadi anapokombolewa. Waganga hawa huwa ni marafiki wa jamii na watu walioheshimika na kuami-niwa kuwa wanatimiza jukumu muhimu. Iwe ni tabibu wa kienyeji au mganga matokeo yote huwa ni kumuingizia giza mtu anayekwenda kutibiwa.
34
# 6 Healing from Witchcraft & Polygamy www.healingofthespirit.org
Kina mama walio tasa hudharauliwa na kutothaminiwa, hali huwaelekeza kwa waganga ambao huwapa madawa ya kunywa na kuwanenea dua fulani ili wa-weze kupata watoto. Baada ya miezi tisa hujifungua mtoto ambaye hubeba laa-na pamoja na mamaye. Utasa ni ishara mojawapo ya kuwepo kwa agano la da-mu na kurogwa.
Tabibu wa kienyeji, manabii na watazamiaji wa kiroho hutafutwa na wa-tu ambao marasdhi yao hayana tiba ya hospitali. Sikitiko ni kuwa utabibu huu huambatana na uchawi na laana zinazomfuata mtu maisha yake yote. Wengine hutumia nguvu za giza ili kuwatoa pepo waliowakalia wateja wao. Mfano wa mama fulani aliyemwendea tabibu wa namna hii aliyemwambia avue mava-zi yote na kumuogesha kwa maziwa na dawa za kienyeji. Mama huyu alilazi-mishwa kuzunguka akitazama pembe nne za nchi huku akitsema dua fulani. Baadaye alipewa mshumaa uliobarikiwa na kuambiwa afanye maombi had mshumaa uishe huku marafiki zake wakipewa chumvi wale eti kuvunja laana walizokuwa nazo. Kwa tendo hili alifungua mlango kwa nguvu za giza kuingia ndani ya roho yake. Pepo hawa hufurahia sana kuchukua mamlaka na kumtawa-la mtu aliyewaruhusu waingie ndani yake. Hata kama mtu hajawahi kuwatem-belea waganga, yawezekana vizazi vilivyotangulia vimefanya hivyo. Hii inam-lazimu mtu kujipeleleza na kutubu kwa niaba ya vizazi vilivyotangulia hasa ikiwa hujui kilichofanyika hapo awali.
Itikadi/Tamaduni za Kijamii
1. Kuzaliwa: mtoto anapozaliwa katika jamii hupitia sherehe ya kupewa jina ambayo inajumuisha kuchinjwa kwa mifugo, matambiko fulani, kunyolewa nywele, kutemewa mate, kuvishwa hirizi au kinga fulani kiunoni au kwenye kidole, kuchanjwa n.k. makaribisho anayopewa mtoto Yule kwenye kabila au jamii yao yaweza kujumuisha itikadi ambazo zinamfunga na kumtia nguvu za kikabila ambazo ni za gi-za.matambiko yote yanayofanyika humtia mtoto Yule katika kifungo asichostahili ikizingatiwa majina anayopewa.
Kupashwa tohara: kipindi cha kubalehe cha mtoto hujumuisha tamaduni za kuwapasha tohara na kuwafundisha mambo fulani ya kimsingi ya jamii yao. Kutahiri kuna kumwaga damu ambalo ni agano na vizazi vilivyotangulia. Baadhi ya vinywaji, mizizi na matambiko yanayofanywa huwa yanaingiza giza katika wale wanaopashwa tohara. Kuchinjiwa mifugo, kutengwa kwa matohara, vinywaji vikali, nyimbo na silaha wanazopewa pamoja na tabia wanazofunzwa zaweza kuleta athari za kipepo ndani ya maisha ya matohara.
35
# 6 Healing from Witchcraft & Polygamy www.healingofthespirit.org
Baada ya kupashwa tohara, matohara huachiwa jukumu la utu uzima kama ku-jumuika katika matendo ya ngono na hata kuwa na wapenzi wengi. Kiburi cha kikabi-la na chuki ya jamii nyingine hukuzwa ndani ya matohara. Mabinti huhusishwa katika maagano yanayowaletea matatizo wakati wa kuolewa na ndani ya ndoa zao.
2. Sherehe za Ndoa: katika tamaduni nyingine wakati wa kuozwa, kuna kuapishwa kwa kutumia vifungo na maneno ya wahenga wali-otangulia. Wengine hutemewa mate na wazee na hata pombe au aina fulani ya maneno kusemwa juu yao ambayo yana athari kubwa kwa ndoa yao na maisha yao ya kijamii weanapoanza ndoa yao. Ushera-ti, utasa na hata kuharibu mimba vyaweza kutokana na vile ambavyo wanandoa wanaingia kwenye nyumba yao na maingiliano ya jamii zao mbili katika sherehe za kitamaduni za ndoa.
3. Wafanyibiashara: baadhi ya wafanyibiashara hupeana biashara yao au baadhi ya vitu watakovyotumia kwenye biashara ili vifa-nyiwe itikadi za kienyeji kuvutia wateja. Sherehe hizi hujumuisha kuchinjwa kwa mifugo kama kafara na maagano ya damu. Wengine hupewa aina fulani ya ulinzi aidha kutumia wanyama au hata vitu vya kipepo ilikunufaisha biashara zao. Kwengineko watu hutoa wa-toto wao au sadaka ya binadamu wengine ili biashara zao zinawiri.
5. Vyombo vya Kienyeji: wengine hupewa mishipi, mavazi, mikufu, ngozi, vikapu,shanga, mifupa au marembo ya kienyeji lakini yaliyo na uhusiano fulani na nguvu za giza. Zawadi za vyombo vya kienye-ji kama viti, vibuyu, marembo ya nyumba, miiko, mikuki, visu na kadhalika vyaweza kuwa na uhusiano usieleweka na ulimwengu wa giza. Watalii hununua vitu vya kuenyeji na kuvipeleka nyumbani bi-la kujua asili yake.
6. Sherehe za kitamaduni/kikabila: kutoka Kenya zinajumuisha ku-toa kafara, ibada ya wahenga ambazo ni kinyume ya mapenzi ya Mungu. Sherehje ya : Nc’wala—inayofanywa na kabila la Wango-ni wa kusini mwa Afrika na Mutomboko—kule Zambia na Zim-babwe na Kuomboka— ya kabila la WaLozi ni baadhi ya sherehe tunazizungumzia hapa.
7. Sherehe za maziko: kutakaswa kwa mfiwa wakati mumewe au mkewe anapokufa kupitia ngono na jamaa wa karibu wa marehemu.
8. majina ya Kurithiwa: kumtaja mtoto jina la mtu alikufa zamani ili arithi tabia na hulka ya jamaa huyo.
36
# 6 Healing from Witchcraft & Polygamy www.healingofthespirit.org
9. Uislamu: mtu aliyekuwa muislamu anapobadili dini yake na kuwa mkristo, huwa ana laana ya uislamu ambayo yapasa ivunjwe kwa ji-na la Yesu. Laana hii yaweza ikawa imejiendeleza kutoka kizazi ki-moja hadi chengine.
Ndoa za Wake Wengi
Ndoa za wake wengi zinakubaliwa Afrika. Hivyo basi si ajabu kwa mtu anayetafuta kuombewa kuwa na chimbuko lake katika jamii ambamo kuna ndoa za wake wengi. Matokeo ya tendo hili ni roho ya kukataliwa, tama, uzinzi, talaka, uyatima, kutangatanga, na utamaushi. Mtafutaji huwa na shida ya kuhifadhi ajira, mahusiano, na tabia kutanga tanga. Wana we-pesi wa kuangukia usherati na hali hii huendelea hadi laana hii ivunjwe.
Uzinzi umeshamiri Afrika na kueneza ukimwi kutokana na watu kuwa na wapenzi wengi. Mke huonekana kama mtumwa au hata mfanyi-kazi badala ya mwenzi. Wanawake wengi hawawezi kupata ajira au ku-pandishwa cheo pasipo kutumiwa kimapenzi.
Kukataliwa
mada ya kukataliwa limershughulikiwa vilivyo kwenye sura nyin-gine, lakini hata hivyo ni vyema kutaja kifupi hapa vile inaathiri waafrika. Kutokana na roho za uchawi na ndoa za wake wengi, roho ya kukataliwa hujidhirisha kwa wengi wanatafuta maombi ya kukombolewa na uponyaji. Roho ya ya kukataliwa huambatana na roho ya ndoa za wake wengi. Roho ya uyatima na kutangatanga pia hujidhirisha kwa kukataliwa.mwanamume anapomtwaa mjakazi, huyo mjakazi huvamiwa na roho ya kukataliwa.
Ufukara
Kwa kuwa kusudi la giza ni kuua, kuharibu na kuiba (Yohana 10:10) si ajabu roho ya ufukara kuambatana na uchawi na ndoa za wake wengi. Tuseme kuwa kabla ya kuzungumzia mada ya ufanisi, lazima roho za giza ziondolewe ili Baraka za Bwana zipate nafasi ya kusambaa kwa mtafutaji. Afrika ina tamaduni ya ufukara, njaa na haja nyingi ambazo ni lazima zishughulikiwe ndio ahadi za Mungu za utele zipatikane.
37
# 6 Healing from Witchcraft & Polygamy www.healingofthespirit.org
Afrika imeshamiri kwa kuwepo kwa umasikini, njaa na haja za kila aina. Hali hii husababishwa na urathi na kuchangiwa na roho ya uchawi, ndoa za wake wengi na kukataliwa. Hata hivyo pepo wa giza wanapotolewa, mhitahi anaweza kuelimishwa kuhusu matakwa ya Mungu yaliyo katika maandiko ili apokee ahadi za Mungu za utele.
Ombi la Uchawi, Tamaduni za Kijamii na Utabibu wa Kienyeji
Maombi ya kufunguliwa kwa wale walioathiriwa na mambo haya yanafana. Kama yalivyo maombi mengine yapasa muombaji amuongoze mtafutaji kuru-dia maombi haya. Mtafutaji aelimishwe juu ya milango iliyo wazi na jinsi ya kuifunga. Mtafutaji achukue nafasi ya vizazi vilivyotangulia, kutubu kwa niaba yao . ombi la kwanza liwe la kuombea uchawi ndipo lifuatwe na lile la ndoa za wake wengi.
Mfano wa Sala:
Bwana Yesu, nashukuru kwa kunifia msalabani. Nilipewa kipawa cha Roho Mtakatifu na damu yake ya thamani kunifinika. Nachukua uweza alionipa kinyume cha nguvu za giza na kusimama kwa nafasi ya vizazi vilivyonitangulia kwa kuhusika katika uchawi, itikadi za kienyeji na utabibu wa kienyeji. Naom-ba msamaha kwa niaba yao kama Daudi alivyotubu kwa niaba ya Sauli (2 Sam 21:1-6). Nakiri kwa niaba yao ili dhambi zao zisamehewe na mimi niwekwe hu-ru kutokana na kifungo hicho. Nifunike na damu yako na uuweke msalaba wa Yesu kati yangu na vizazi vilivyotangulia (Iwapo mtafutaji amewaendea wa-ganga yapasa atubu dhambi zake hapa)
Baba mwenye enzi, Nazikana na kukataa kila roho za giza, uchawi, itika-di za kijamii na utabibu wa kienyeji. Nazichukua haki zote za kiroho na ruhusa niliyompa shetani na kumrudishia Yesu. Nakiri nitamfuata Yesu pekee. Na-chagua nuro maishani mwangu na kuamuru roho za giza zihame katika jina la Yesu. Nadai kuwa huru kwa Jina la Yesu – Amin
Iwapo mtafutaji alichanjwa alipomwendea mganga na kufanya agano la damu itapasa atumie mafuta ya kutia wakfu ili kubadili maagano hayo kuwa na Kristo. Ajipake mafuta na kuomba ombi lifuatalo:
Bwana Yesu, ninakuja kinyume cha maagano yaliyofanywa na shetani. Najipaka mafuta na kudai maagano hayo yabadilishwe na kuwa pamoja na Ye-su. Naomba haya yote kwa jina la Yesu – Amin
38
# 6 Healing from Witchcraft & Polygamy www.healingofthespirit.org
Ombi la Ndoa ya Wake Wengi
Bwana Yesu, nashukuru kwa kunifia msalabani. Nilipewa kipawa cha Roho Mtakatifu na damu yake ya thamani kunifinika. Nachukua uweza alionipa kinyume cha nguvu za giza na kusimama kwa nafasi ya vizazi vilivyonitangulia kwa kuhusika katika ndoa za wake wengi. Naomba msamaha kwa niaba yao kama Daudi alivyotubu kwa niaba ya Sauli (2 Sam 21:1-6). Nakiri kwa niaba yao ili dhambi zao zisamehewe na mimi niwekwe huru kutokana na kifungo hi-cho. Nifunike na damu yako na uuweke msalaba wa Yesu kati yangu na vizazi vilivyotangulia (Iwapo mtafutaji amehusika katika ndoa za wake wengi yapasa atubu dhambi zake hapa)
Baba Mwenye enzi, Nazikana na kukataa kila roho za ndoa za wake wengi. Nazichukua haki zote za kiroho na ruhusa niliyompa shetani na kumru-dishia Yesu. Nakiri nitamfuata Yesu pekee. Nachagua nuru maishani mwangu na kuamuru roho za giza zihame katika jina la Yesu. Nadai kuwa huru kwa Jina la Yesu – Amin
(Iwapo mhitaji amehusika katika ndoa wake wengi, zinaa au uzinzi wa aina yeyote yapasa akiri na kutubu dhambi zake mwenyewe)
39
# 7 Uponyaji Kutokana na Talaka www.healingofthespirit.org
Uponyaji Kutokana na Talaka
Hapo mwanzo, Mungu alimuumba Adamu na Hawa na akakusudia waunganishwe kama mume na mke: “Ndiyo maana mwanamume humwacha baba yake an mama yake, akaambatana na mkewe, nao wawili huwa mwili mmoja. “ (Mwanzo 2:24; vilevile Marko 10:6-9). Paulo anaeleza kwamba kusudi la Mungu katika uhusiano wa ndo katia ya mume na mke linaweza kutumiwa kama picha ya kusudi la Mungu la uusiano kati ya Yesu na kanisa lake (Waefeso 5:23). Zaidi ya hayo, Mungu aliwapa wanadamu hiari; kisha Shetani akaingilia kati na tangu wakati huo amekuwa akifanya kazi ya kuumaliza mpango wa Mungu katika uhusiano wa ndoa.
Masuala Zaidi na Mambo ya Kusikitisha
1. Ndoa ni agano la kiroho kati ya Mungu na wanandoa na ni jambo muhimu sana kwa Mungu. Mungu alikusudia kuwe na aina moja tu ya ndoa (Mwa. 2:24, Mark0 10:6-9). Muungano wa nafsi wa kiungu huundwa kupitai kwa agano la ndoa.
2. Talaka haikua katika mpango wa Mungu wa kwanza, kwa hivyo, Yeye anaiona kuwa dhambi. Sheria za kiroho hukiukwa katika kitendo cha talaka (Mat. 5:32).
3. Kuna mambo hali tatu za kuthibitisha talaka zinazoweza kutambuliwa katika maandi-ko: (1) uzinzi (Mat. 5:32), (2) mwanandoa asiye Mkristo anapomwacha mwenzake (1 Kor. 7:15) au mwanandoa ambaye mwenzake amezini lakini yeye hajafanya dhambi kwa kumpa talaka mwenzake ana uhuru wa kuoa/kuolewa tana bila kutenda dhambi (Mat. 5:32), na (3) ingawaje kuiacha ndoa au dhambi za ngono zilizofanywa na mwenzi mmoja ni thibitisho halisi la talaka, vifungu vingine (kama vile 1 Kor. 7:2-5) vinapendekeza kwamba mwanandoa hayuko chini ya kifungo cha kuendelea kuwa ka-tika ndoa na mtu anayevunja nadhiri ya kumfanyia mtu wema unaostahili.
4. Suala lenyewe—kimaandiko—si “sababu ya talaka” bali ni ikiwa mwanandoa ata-fanya mapenzi na mtu mwingine baada ya talaka, kwani maandiko yanakiita kitendo hicho uzinzi (“Anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini, na mwanamume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.”—Mat. 5:32).
5. Uzinzi unapofanyia, mpango wa Mungu wa “wawili huwa mwili mmoja” (Mwa. 2:24) hutatizwa, huchafuliwa, na kuvunjwa. Mpango huu unapovunjwa, hufungua mwanya wa nguvu za giza kupitia.
6. Mhubiri 5:4-6 inapendekeza kwamba laana ya talaka inaweza kumjia mtu kwa kuvun-ja nadhiri na Mungu (ndoa ni nadhiri).
7. Majeraha ya kukataliwa, hasira, na kuachwa yanaweza kudumu baada ya uhusiano kuvunjika.
8. Muungano wa nafsi huendelea kuweko kati ya wanandoa hao mpaka uvunjwe kiroho
9. Habari Njema ni kwamba, Mungu aliye mbinguni alimtuma Mwanawe Yesu Kristo kutufia msalabani ili tuweze kusamehewa kila dhambi (zikiwemo talaka, dhambi za ngono au uzinzi kwa kuoa/kuolewa tena), kuoshwa kwa damu ya Yesu, na kuwa na uhusiano mpya naye kwa nguvu za Roho Mtakatifu.
10. Jambo linalozingatiwa katika uponyaji kutokana na talaka si kutaka kujua ikiwa dhambi ilitendwa kupitia ka tukio hilo bali ni kuomba msamaha unaostahili na kuku-bali neema na msamaha wa Baba Yetu mwenye upendo.
40
# 7 Uponyaji Kutokana na Talaka www.healingofthespirit.org
Kuombea Uponyaji Kutokana na Talaka
Mhusika anatakiwa kuzifuata hatua hizi:
1. Mwambie Mungu akusemehe kwa sehemu uliyochukua katika talaka (watu wote wa-wili hususika).
2. Mwambie Mungu akusamehe kwa dhambi zozote za ngono zilizotendeka kabla au baada ya talaka.
3. Mwambie Mungu akusamehe kwa ajili ya dhambi zolizosababishwa au kuoa/kuolewa tena.
4. Uponyaji kutokana na talaka unahitaji umsamehe kabisa mwenzi wako wa awali.
5. Omba kwamba sehemu yako iliyobaki na mwenzi wako itaachiliwa huru.
6. Omba ili upate uponyaji wa ndani kutuokana na hisia za kukataliwa, hasira au kua-chwa.
7. Omba na kuvunja kwa upanga wa Roho, muungano wowote wa nafsi ulioletewa na muungano wa awali.
8. Iwapo mtu huyo hajaoa/hajaolewa, omba kwamba ataendelea kuishi peke yake ili asi-tende dhambi za ngono.
9. Iwapo mtu huyo ameoa/ameolewa tena, omba kwamba Mungu atautambua uhusiano huo wa sasa kama mpango wa asili uliopangwa mbinguni pamoja na haki zote na ba-raka za agano la kupatana kwa wawili kuwa mwili mmoja.
10. Omba ili Mungu abariki muungano huo na familia hiyo katika jina la Yesu..
41
# 8 Uponyaji Kutokana na Laana www.healingofthespirit.org
Uponyaji Wa Laana
Ijapokuwa baraka ni kinyume cha laana, kuna mambo yanayofanana katika vitu hivyo. Ni maneno yaliyotajwa, yaliyoamriwa, au kuandikwa katika Biblia kwa nguvu na mamlakao ya kiroh kwa wema (Baraka) au uovu (laana). Tamko hilo huzifanya sheria za ki-roho zianze kufanya kazi ya kuendeleza Baraka za laana kutoka kwa kizazi kimoja hadi kin-gine mpaka itakapovunjwa. Baraka zimetajwa katika Biblia mara 221. Laana zimetajwa mara 230.
Maandiko Yanayozungumza Juu ya Baraka
Mifano miwili ya Baraka ni: (1) Baraka (katika agano) ambayo bwana alimpa Abra-hamu—na vilevile Isaka (Mwa. 22:15-18) na (2) Baraka ambayo Isaka alimpa Yakobo (Mwa. 27:27-29). Tazama vile katika kifungu kinachozungumza juu ya Isaka, Mungu han-geweza “kuondoa” baraka ambayo Isaka alikuwa amempa Yakobo (Mwa. 27:37-40; pia ta-zama Kumb. 28:1-14).
Tunaamriwa “kubariki wala tusilaani” (Rum. 12:14). Zaidi ya hayo, Mungu anatua-hidi katika vifungu vingi vya maandiko kwamba atatubariki tukitii. Mifano mingine ya bara-ka ni hii:
• “Kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia, kwa Mungu mwenye nguvu atakayekubari-ki; upate baraka za mvua toka juu mbinguni, baraka za maji ya vilindi vilivyo chini, ba-raka za uzazi wa akina mama na mifugo” (Mwa. 49:25).
• “Baraka za afya mwilini mwako. Baraka za maisha marefu unapoendelea kumtumikia Bwana Mungu wako. Baka za amani na furaha kwako na kwa familia yako. Utabarikiwa unaporudi nyumban na unapotoka nje. Chochote ambacho mikono yenu itaguza kitafani-kiwa. (Kumb. 28:1-14).
• “Ee, Mungu, nakusihi unibariki na kuipanua mipaka yangu. Mkono wako uwe pamoja name na unlined kutokana na jambo lolote ovu, lisiniumize!” (1 Nya. 4:10, kutoka kwa ombi la Yabezi)
• “Ardhi ya Asheri itatoa mavuno kwa wingi, naye atatoa chakula kimfaacho mfalme.” (Mwa. 49:20). “Asheri abarikiwe kuliko watoto wote wa Yakobo, na upendelewe na ndugu zako wote; na achovye mguu wake katika mafuta. Miji yako ni ngove za chuma na shaba. Usalama wako utadumu maisha yako yote. Hakuna aliye kama Mungu wako, yeye hupitia mbinguni kuja kukusaidia, hupita juu angani katika utukufu wake.” (Kumb. 33:24-26, baraka za Asheri).
Maandiko Yanayozungumza Juu ya Laana
Mungu anaahidi kwamba laana itawafuata wanaokosa kutii (Kut. 20:3-5, Kumb. 27:15 na 28:15-68). Kila mara laana huanza na dhambi. “Nyoka alikuwa mwerevu kuoko wanyama wote wa porini walioumbwa na Mwenyezi-Mungu.”(Mwa. 3:1). Laana zilianza kwa dhambi ya Adamu na Hawa na zinaendelea hadi sasa “(Kwa njia ya mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, nayo ikasababisha [laana ya] kifo, hivo kifo kimeenea katika jumuia yote ya binadamu, kwa maana wote wametenda dhambi”—Rum. 5:12).
42
# 8 Uponyaji Kutokana na Laana www.healingofthespirit.org
Kwa sababu ya kukosa kutii Mungu (1) alimlaani nyoka (Mwa. 3:14-15), (2) alimlaani mwanamke—“Nitakuzidishia uchungu wa kuzaa, kwa uchugu utazaa watoto; utakuwa na hamu na mumeo hata hivyo, naye atakutawala” (Mwa. 3:16; laana hi inaen-dela katika kitendo cha kuzaa na kuendelea na kitendo cha kuwa na hedhi kila mwezi, na (3) alimlaani mwanamume—“Kwa kosa lako ardhi imelaaniwa. Kwa jasho utajipatia humo riziki yako, siku zote za maisha yako. Ardhi itakuzalia miiba na magugu, nawe ita-kubidi kula majani ya shambani. Kwa jasho lako utajipatia chakula mpaka utakaporudi udongoni ulimotwaliwa; maana wewe ni mavumbi na mavumbini utarudi.” (Mwa. 3:17-19). (Pia rejelea Mwa. 4:9-13, mahali ambapo Mungu anamlaani Kaini kwa kumuua Ab-eli.)
Dalili za Laana (mbili au zaidi zikidhihirika pamoja)
1. Wazimu na/au kuchanganyikiwa kwa hisia
2. Magonjwa ya kudumu/yasiyopona
3. Utasa, kuharibika mimba kila mara au matatizo mengine ya wanawake
4. Kuvunjika kwa ndoa na kutengwa na familia
5. Kukosa pesa kila mara
6. “Kupatwa na ajali” kila mara
7. Kuwa na historia ya watu kujiua na kupatwa na vifo visivyo kawaida
8. Kizuizi/ukuta wa kiroho katika ukombozi
Unapomwombea mtu ili apate uponyaji wa kiroho, wakati mwingine dalili iliyo wazi sana ya laana ni ikiwa mhusika huyo hawezei kusikiachochote kutoka kwa Mungu. Kuweko kwa ukuta wa kiroho unaomzuia mhusika na mwombezi kupata utambuzi un-aohitajika ili mtu huyo apate ukombozi. Wakati kama huo ni vyema kuuliza “Katika jina la Yesu, je, kuna laana yoyote juu ya maisha yako?” ikiwa ni kweli, mhusika huyo atazi-badilisha hisia zake ghafla na hiyo itakuwa dalili ya kuonyesha kwamba jambo hio ni kweli.
Laana zote huwa na mahali pa kuingilia, na mahali pa kukaa. Wakati mwingine laana ikielekezwa kwa mtu ambaye ni Mkristo halisi, laana hiyo humwendea mtu mwin-gine katika familia. Laaana za wachawi ni baadhi ya laana zenye nguvu sana. Pepo wa laana ina haki ya kiroho katika nafasi inayokaa ndani ya roho ya mhusika. Mhusika huyo huwa katika kifungo cha kiroho.
Chanzo cha Laana
Kila laana ina sababu (au chanzo); “kadhalika laana asiyostahili mtu haimtui” (Meth. 26:2). Tunapohudumu kwa ajili ya kuleta uponyaji wa ndani na tuamini kwamba kuna laana inayohusika, kuna maswali matatu tunayotakiwa kuuliza: (1) Je, kuna laana? (2) Sababu ya laana hiyo ni ipi? (3) Dawa yake ni nini?
43
# 8 Uponyaji Kutokana na Laana www.healingofthespirit.org
Hapa chini kuna sababu tisa za laana zilizotambuliwa. Wahusika wanweza kuathi-riwa na baadhi yazo wakati mmoja. Ingawaje walihudumu wengine hutenganisha aina za laana za kizazi (Kut. 20:5), ukweli ni kwamba, dhambi zote ambazo babu zetu hawakutu-bu huwa ni laana ya kizazi, hasa dhambi ya kuabudu sanamu..
1. Kukosa Kumtii Mungu Husababisha Laana): Biblia imeorodhesha makundi 37 ya dhambi zinazosababisha laana za kukosa kutii. Laana hizi haziwezi kuon-dolewa bila toba na utii: “… Yeyote asiyeshika na kutimiza yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria yuko chini ya laana” (Gal. 3:10). (Maandiko mengine yanarejelea laana za sheria ni Kumb. 27:15-26 na 28:15-68.) Pitia mambo yafua-tayo:
• Kuabudu sanamu, miungu wa uwongo (Kut. 20:3-5)
• Kutoheshimu wazazi (Yakobo alimdanganya baba yake, alidanganya kwamba yeye alikuwa ni Esau, ndugu yake—Mwa. 27:19-27, ndugu za Yusufu walim-chukia wakamuuza na wakamdanganya baba yao kuhusu kilichomtendekea—Mwa. 37)
• Udanganyifu, ulagahi, au usaliti dhidi ya jirani (Meth. 17:13)
• Kudhulumu au kuwanyima haki wanyonge na wasiojiweza (Meth. 28:27)
• Aina zote za ngono isiyo halali (Lawi. 20:10-16)
• Kuwachukia Wayahudi (Mwa. 12:3 na 27:29)
• Kutegemea nguvu za binadamu (Yer. 17:5-6)
• Kuiba, kosa la kusema uwongo (baada ya kuapa kusema ukweli, n.k. (Zak. 5:1-4)
• Kukosa kutii kifedhaa au kumnyima Mungu: “Je, ni sawa mtu kumdanganya Mungu? ... Mmelaaniwa kwa laana” (Mal. 3:8-9)
• Kuwasahau maskini (Meth. 28:27)
• Matendo ya dini yaliyokufa (Yer. 17:5)
• Kila aina ya kukosa kutii sheria za Mungu
2. Mtu Kutamka Laana kwa Niaba ya Mungu:
• Yoshua kuilaani Yeriko (Yos. 6:26); miaka 525 baadaye, Mfalme Ahabu ali-patwa na laana hiyo (I Fal 16:34)
• Nuhu alimlaani Hamu pamoja na watu wa Kanani (Mwa. 9:25)
3. Watu wenye Mamlaka ya Uhusiano: Watu walio na mamlaka ya kizazi, kiroho, kiserikali juu yetu wanaweza kutulaani, kama ilivyo katika mfano wa Yakobo na Raeli: “Aliyeviiba na afe” (Mwa. 31:32); Raeli ndiye aliyeviiba na alikufa baa-daye. Wakati mwingine hizi huitwa laana zisizo za makusudi (Kwa mfano, ma-
44
# 8 Uponyaji Kutokana na Laana www.healingofthespirit.org
neno ambayo watu hunena dhidi ya wengine—bila kuwa na nia ya kumdhuru mtu huyo inaweza tu kufanyika iwapo kuna muungano wa kuhusiana kati ya anayelaani na mhusika, kama vile uhusiano wa mzazi kwa mtoto, mwalimu, mchungaji au muungao wa nafsi (maneno hayo yanayonenwa huwa ni mabaya na ya kuleta uharibi-fu—na wakati mwingi husemwa kama ombi—na watu walio karibu nasi ambao tu-meungana kinafsi au walio na mamlaka juu yetu, kama vile wazazi au wazee katika ukoo wetu.)
4. Maagano yaliyo Kinyume na Maandiko: kama inavyofanyika katika itikadi za Freemason (Kut. 23:32)
5. Wataalam Wanaotumia Nguvu za Giza Kuwalaani Wengine:
• Laana za makusudi zinazotamkwa na wanaume na/au wanawake, wachawi, au watumishi wa Shetani
• Wachawi, walozi, wenye kutaka kauli kutoka kwa mizimo na mapepo au kutoka kwa wa-fu, n.k. (Kumb. 18:10-12)
• Balamu aliyeambiwa azungumze maneno mabaya (laana) dhidi ya Israeli. (Hes. 22:4-6)
• Mtu anayetumia nguvu za Shetani kuliita jina la Shetani ili kutoa laana huleta pepo wa laana aliye na jina (kwa kawaida mtu yeyote tu hawezi kumchagua mtu mwingine bila mpango maalum na kutamka laana juu ya mtu huyo)
• Ili laana hiyo iweze kutimia, ni lazima kuwe na kitu kinachoweza kuhusishwa na mhusi-ka (kinachoweza kutumiwa kama njia ya kumfikia kama vile bidhaa za mtu huyo au vi-bano vya nywele—ambavyo wakati mwingine huibwa na kutumiwa katika tambiko za kulaani)
• Wakati mwingine kitu kinachomilikiwa na mtu fulani hulaaniwa na kurudishwa kwa mwenyewe ili pepo wa laana aweze kufanya kazi moja kwa moja dhidhi ya mhusika ku-pitia kwa kitu kilicholaaniwa (maelezo zaidi yako chini ya # 7 hapa chini, “Laana ya Vi-tu Vilivyolaaniwa,”—kucha zilizokatwa, nywele zilizokatwa, na damu huwa na nguvu sana zikitumiwa kwa njia hii. Picha na watotao wa bandia hutumiwa pia)
• Kwa kumdunga mtoto wa bandia au picha ya mtu katika sehemu maalum, mchawi huita na kutumia mapepo kuweka alama kama hizo katika mwili wa mhusika.
6. Laana za Maeneo: zikiwemo nyumba, madhabahu, nchi, mikoa, na miji(Dan. 10:13). Se-hemu au nyumba huingiwa na uwepo wa uovu kwa njia mbalimbali. Kupitia kwa laana, kua-budu shetani, uhalifu, vurugu, dhambi zengine zilizofanyiwa mahali hapo, vitu vilivyo na uwepo wa uovu, au uwepo wa uovu ulio ndani ya watu wanaoishi mahali hapo. “Mahali” fu-lani panaweza kuathiriwa na uovu iwapo mtu fulani atajihusisha na mizungu/ushetani (kama vile kushiriki katika uaguzi, ulozi, kuwasiliana na mizimu, ubashiri, n.k) shughuli zengine zi-nazoweza kumtia mtu najisi ni kama vile: uzinzi, matendo potofu ya ngono, ubakaji, mauaji au jaribio la kuua, dhuluma ya kimapenzi, au kufanya ibada ya kishetani.
Kwa vile mambo haya hufanyika kwa uamuzi na vitendo vya mhusika, hiyo hu-zipa nguvu za giza ruhusa au haki ya kiroho ya kudai ardhi hiyo na/au mahali hapo kwa makusudi yake. Hii ni sawa na kile kitendo ambacho hufanyika katika roho zetu za kibi-
45
# 8 Uponyaji Kutokana na Laana www.healingofthespirit.org
nadamu tunapotenda dhambi. Kufanya hivyo humpa mwovu ruhusa ya kuathiri sehemu hiyo ya roho zetu. Kwa kiwango fulani, watu walio na roho waovu huleta uovu na vilevile huwa-cha uovu huo mahali wanapokuwa. Kupatembelea mahali hapo kunaweza kumtia mtu najisi kwa ajili ya laana hiyo.
Licha ya hayo, kwa maelezo zaidi kuhusu laana za maeneo, tazama sehemu inayoele-za juu ya “Kuliweka Huru Kanisa Lako ” na “Vifaa na Mahali pa Uponyaji.”
7. “Laana ya “Vitu Vilivyolaaniwa”: Kuviingiza vitu vya kuchukiza mno au vitu vilivyolaa-niwa (yaani vinavyodhaniwa kuwa chini ya laana.”) ndani ya nyumba (“Msipeleke sanamu zozote katika nyumba zenu ama sivyo, mtalaaniwa kama sanamu hizo. Ni lazima mzichukie na kuzidharau kwa kuwa ni vitu vilivyolaaniwa,”—(Kumb. 7:26). Mtu anaweza kupata laana anapofanya mambo yafuatayo bila kujua:
• Akimiliki vitu kwa kukosa kutii (Yosh. 7:19-25, Akani alikubali kwamba alichukua vazi moja na vitu vingine kutoka vitani na hivyo alileta kifo kwake na kwa familia yake)
• Akichukua kitu kilicholaaniwa na kutengwa kwa madhumuni ya Shetani (Kut. 20:4, Kumb. 27:15—kujitengenezea sanamu, na Kumb. 7:25-26—kupeleka ndani ya nyumba yako kitu kilicholaaniwa)
• Ukichukua kitu kilicholaaniwa, utalaaniwa (Yosh. 6:18; pia pitia sehemu inayoeleza juu ya “Vitu na Mahali pa Uponyaji” ili uone orodha ya vitu vilivyolaaniwa)
• Vitu vilivyolaaniwa vinaweza kuwa vitabu, vitu vya ushetani/mizungu, michezo, vitu vya ukumbusho kutoka katika eneo lililolaaniwa, vitu vya sanaa vilviyoundwa na watu walio na laana, n.k.
• Kuwatembelea mabingwa wa maono, watu wanaowasiliana na mizimu, au wachawi hum-fanya mtu apokee laana. Hakuna usalama wowote katika kuchovyachovya ndani ya ushetani; kufanya hivyo humfanya mtu afungue njia ya kupata laana hata kama hakuwa akiitafuta.
8. Dawa Zengine za Mbadala: Asili ya dawa zengine za mbadala (kwa mfano, Reiki, tiba vi-tobo (acupuncture), n.k) zinatakiwa kuchunguzwa zaidi kabla ya kukubali kuzitumia.
9. Laana za Kujiwekea Mwenyewe: maneno tunayotamka dhidi yetu wenyewe kwa mfano:
• Mwanzo 27:13—Rabeka mke wa Isaka, alisema, “…laana yako na inipate mimi” naye hakumwona mwanawe tena: alikufa kabla ya wakati wake kufika.
• Mathayo 27:20-26—Yesu alipokuwa akishtakiwa , umati ulisema, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!”(Tangu wakati huo Wayahudi wamekuwa wakiteswa ulimwenguni).
• 2 Sam 6:22-23 – Mikali, mkewe Daudi ananena kinyume cha mtiwa mafuta wa Bwana na kuishia kufanywa tasa
• Hesabu 12: Miriamu ananung’unika kinyume cha Musa na kugeuzwa kuwa mwenye ukoma
• Pia tazama sehemu inayoeleza juu ya “Kuuponya Ulimi Wako” na “Uponyaji Kutokana na Viapo na Matamanio ya Kufa”—Viapo ni laana za Kujitakia.
46
# 8 Uponyaji Kutokana na Laana www.healingofthespirit.org
Ifuatayo ni Mifano ya Laana za Maneno za Kujitakia Mwenyewe:
a. Kurukwa na akili na/au kuchanganyikiwa kwa hisia:
“Inanipa wazimu.”
“Siwezi kuvumilia kamwe.”
“Ananipa wazimu.”
b. Magonjwa Yasiyopona:
“Kila kunapotokea virusi mimi huambukizwa.”
“Nimechoka na kuchoshwa . . .”
“Huwa katika familia yetu, nadhani atakayefuata ni mimi.”
c. Utasa, kuharibika kwa mimba kila mara, au matatizo mengine ya wana-wake:
“Sidhani kama nitawahi kushika mimba”
“Najua nitampoteza huyu; hufanyika kila mara.
d. Kuvunjika kwa ndoa na kutengwa na familia:
“Mtabiri asomaye kitanga alisema kwamba mume wangu ataniacha.”
“Nilijua tu kwamba mume wangu angempata mke mwingine.”
“Katika familia yetu tumekuwa tukipigana vita vya paka na panya kila mara.”
e. Kukosa pesa kila mara:
“Siwezi kutimiza mahitaji yangu: Pia babangu alikuwa hivyo.”
“Sina pesa za kutoa fungu la kumi.”
“Nawachukia matajiri. Wao hupata watakacho ilhali mimi sipati.”
f. “Kupatwa na ajali” kila mara”:
“Hunitendekea kila mara.”
“Nilijua kulikuwa na tatizo mbele….”
“Mimi ni goigoi.”
g. Kuwa na historia ya watu kujiua na kupatwa na vifo visivyo vya kawaida:
“Kuna maana gani ya kuishi?”
“… mpaka niwe maiti.”
“Afadhali nife kuliko kuendelea kuishi mambo yakiwa hivi.”
10. Laana za Kifamilia au za Kizazi: Wahusiaka wanaoishi au wanaotoka katika nchi zinazoendelea—kama vile Afrika, India, Latin, au Marekani Kusini—huenda wamepata laana za kifamilia bila kujua. Katika baadhi ya nchi hizo, watoto wanapozaliwa, hufanyiwa sherehe za kukabidhiwa kwa miungu na mapepo kupitia kwa apizo la damu, na vilevile wanapobalehe.
Wakristo wengi hawajui kwamba wao (au babu zao) wamekula kiapo cha damu na mashetani kupitia kwa tamaduni fulani wanayotakiwa kudumisha—ilhali walitakiwa tu kuwatii wazazi wao kwa kuthibitisha tamaduni hizo za kifamilia. Ka-tika hali nyingi, watu hao wangekanwa na familia zao iwapo wangekataa kushiriki katika sherehe hizo za kishetani (kwa kukosa kuwatii wazee wa kabila lao na familia)
47
# 8 Uponyaji Kutokana na Laana www.healingofthespirit.org
ilhali watu hao hawawezi kuzungumza kuhusu mambo hayo au hata hawajui kwamba mambo hayo yalifanyika katika familia zao.
Kwa kurejelea Kutoka 20:5 (na 34:6-7; “Kisha Mwenyezi-Mungu akapita mbele ya Musa akitangaza tena, Mungu, ni Mungu mwenye huruma na neema; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa fadhili na uaminifu. Mimi nawafadhili maelfu, ni-kiwasamehe uovu, makosa na dhambi; lakini kwa vyovyote vile sitaacha kumwadhibu mwenye hatia; nawapatiliza watoto na wajukuu uovu wa baba na babu zao, hata ki-zazi cha tatu na cha nne.”) laana kwa “kizazi cha tatu na cha nne” huendelea katika kila kizazi mpaka kuwe na toba na kuvunjwa kwa laana hiyo. (Kwa mfano) Waa-frika wengi wa Marekani wako katika kizazi cha 4 au 5 kutoka kwa urithi wao wa Afrika, na ingawa wamejitolea kuwa Wakristo, laana ya babu zao wa zamani bado inawafuata.
Watu wengi wanaoishi katika nchi zinazokua wana babu zao wa zamani waliotoka vi-jijini na kwenda kuishi mijini, wakiwa wamebeba mizigo yao ya kiroho.
11. Kuwaroga Wengine: Adui hana haki ya kukuumiza vile atakavyo. Lazima kuweko na milango iliyo wazi kihistoria au katika ukoo wenu ama kutokana na kuasi ukifanya maishani mwako kinyume cha maagano na amri za Mungu. Hakuna awazaye kukuro-ga kwa kukutazama au wewe kuwatazama. Lakini iwapo katika mawazo yako unad-hani mtu anaweza kukuroga kwa kukutazama basi inawezekana. “Kama mtu afiki-rivyo moyoni, ndivyo alivyo” (Mith 23:7).
Kuzivunja Laana
Ili laana iweze kuvunjwa, ni lazima laana hiyo ikanushwe na mtu huyo akubali kuwa katika kiapo cha damu ya Yesu Kristo. Kupitia kwa damu ya Yesu na kazi ya kutu-lipia makosa iliyomalizika Kalvari, mtu anaweza kuwekwa huru kutokana na laana, pamoja na viapo vya damu, uchawi na laana zinazohusiana na kuabudu babu wa zamani. Mungu ali-weza kufanya kazi hiyo kupitia kwa kazi iliyofanywa Kalvari (“Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kujitwalia laana hiyo kwa ajili yetu; maana maandiko yanasema: “Yeyote aliyetungikwa msalabani amelaaniwa. Jambo hili lilifanyika kusudi ile baraka aliyopewa Abrahamu iwashukie watu wa mataifa mengine kwa njia ya Kristo, na ili kwa im-ani, tumpokee yule Roho ambaye Mungu alituahidi.”—Gal. 3:13-14).
Yesu alijitwalia laana kwa ajili ya kila mwanadamu. Alijitwalia laana iliyo juu yetu, (pale msalabani) alijitwalia dhambi zote. Hata hivyo mtu anatakiwa kujitwalia mabadiliko hayo kwa toba ya kweli na kukanusha dhambi za babu wa zamani. Mtu anapofanya hivyo, hufunikwa kwa damu ya Bwana Yesu inayosafisha na baada ya kitendo hicho mwovu hawezi kuwa na haki ya mamlaka ya kiroho ya kuendelea kufanya kazi yoyote ya laana za
48
# 8 Uponyaji Kutokana na Laana www.healingofthespirit.org
kizazi. Laana hizo za kizazi hubatilika kupitia kwa kazi ya Kristo iliyomalizika na kwa aga-no mpya ya damu iliyofanywa na Yesu. Hatua zifuatazo ni muhimu kwa kuzivunja kila aina ya laana:
1. Utambuzi: Ikiwezekana tambua chanzo cha laana hiyo kwa jina. Huenda ikawa mhusika alitoa nafasi ya kiroho—au haki ya kiroho—kwa Shetani. Mwambie Roho Mtakatifu akuonyeshe asili, sababu, au kiungo cha laana hiyo; huenda ikawa ni kitu anachomiliki au kilicho nyumbani mwake.
2. Kujitwalia: Jitwalie—Jichukulie kwa njia maalum na kwa imani, kitendo cha Yesu kutufia (Kumb. 21:23). Yesu alitwikwa laana (Isa. 53:6) aliumizwa kwa sababu ya maovu yetu (Isa. 53:5). Kristo ametukomboa kutokana na laana ya sheria (Gal. 3:13-14). Mwambie mhusika akiri imani yake katika Kristo na katika sadaka aliyotoa kwa niaba yetu; akiri imani yake katika kufa na kufufuka kwa Kristo.
3. Thibitisha Mamlaka ya Kiroho: Toa tangazo la kuthibitisha mamlaka ya kiroho juu ya laana hiyo. (Soma kwa sauti maandiko yafuatayo: Gal. 3:13-14, Efe. 1:7, Kol. 1:12-14, 1 Yoh. 3:8, Luka 10:19).
4. Tubu na Kujitoa: Mwambie mhusika amwambie Mungu kwa sauti kwamba anatu-bu na anajitolea kutii (Yesu alinena na mwanamume aliyeponywa hekaluni—“Sasa umepona; usitende dhambi tena, usije ukapatwa na jambo baya zaidi.” Yohana 5:14; vilevile, alimwambia mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi—“Nenda zako, na tangu sasa usitende dhambi tena.” Yohana 8:11). Mhusika huyo anatakiwa ku-tubu dhambi zote anazozijua (jambo hili ni muhimu sana). Atubu kwa ajili ya dhambi zilizofanywa na babu zake (toba ya kujihusisha) hata kama walifanya hivyo bila ku-jua.
5. Samehe: Mhusika anatakiwa kumsamehe kila mtu ambaye amewahi kumdhuru au kumuumiza, pamoja na mtu aliyemlaani— ikiwa anamjua mtu huyo.
6. Kanusha na Kukemea: Mwambie mhusika akanushe kwa sauti uovu wa kizazi na/au viapo vya damu viliyvonenwa juu ya maisha yake au juu ya maisha ya babu zake wa zamani. Jambo hilo lisipofanywa, adui bado atakuwa na haki ya mamlaka ya kiroho ya kumkandamiza kulingana na agano iliyoandikwa katika Kumbukumbu 27:15-26 na 28:16-19. Mhusika huyo anatakiwa kukanusha uhusiano kati yake na ushetani/mizungu au uliofanywa na babu zake wa zamani na kufuta sehemu na haki yoyote ya kiroho aliyompa Shetani. Mhusika huyo anatakiwa kuvitupa vitu vyovyote, vitabu n.k. vilivyotiwa najisi alivyonavyo kisha amkemee Shetani kwa ajili ya laana hiyo; anatakiwa kumwambia Shetani kwamba halitaki jambo hilo tena, na kwamba akili yake, pamoja na mwili wake ni hekalu ya Bwana Yesu Kristo. Katika hali ngumu, huen-da mtu huyo akahitajika kurudia kanusho hilo mara tatu (Kwa sababu wakati mwingine laana hiyo huwa imefanywa na mchawi aliyefanya kiapo hicho cha damu kirudiwe mara tatu).
7. Ondoa Vitu Vyote Vya Chukizo: Mhusika anatakiwa kuondoa katika nyumba yake vitu vyote vinavyochukiza sana. Pia rejelea sehemu iliyo na kichwa hiki, “Vitu na Mahali pa Uponyaji.”
49
# 8 Uponyaji Kutokana na Laana www.healingofthespirit.org
8. Omba Damu ya Yesu: Ili kuivunja laana hiyo, omba damu ya Yesu iwe katikati ya mtu aliyelaaniwa na aliyemlaani. Ikiwa hii haitoshi amuru laana hiyo itamke jina lake halafu uifu-kuze katika jina la Yesu, kama wanavyofanywa mapepo. Vunja muungano wowote wa nafsi kati mhusika na mtu aliyetamka laana hiyo.
9. Mbariki Mtu Aliyetoa Laana: Luka 6:28 inatwambia, “Wabariki wanaokulaani ….” Wa-rumi 12:14 inasema, “… bariki, wala usilaani.” Kwa kulitii Neno la Mungu, tangaza baraka ya Mungu juu ya mtu aliyetamka laana hiyo.
10. Achilia Huru na Ukatae: Laana za kutotii zinaweza tu kuvunjwa kwa kutii (Mat. 16:12, Yak. 4:7). Kuwa mtiifu.
11. Mafuta ya Kupakwa: Iwapo kuna mafuta ya kupakwa yaliyobarikiwa, ni vyema kumpaka mhusika katika kila sehemu ambazo “mponyaji” alimchanja kama njia ya kuufanya uchawi wake. Iwapo walichanjwa katika sehemu za siri, tia mafuta katika sehemu ndogo ya kitambaa cha mkononi ili mhusika huyo aweze kukitumia kugusa mahali alipochanjwa na mchawi.
12. Utasa: Watu wengi ambao wamewahi kwenda kwa wachawi wanaweza kuwa tasa au kukosa kuwa na nguvu za kufanya mapenzi (waume na/au wake). Fanya ombi maalum la kuvunja laana hiyo ili watu hao waweze kuzaa na uweke wakfu watoto wao kwa Yesu.
13. Rudia Nadhiri za Ubatizo: Katika hali zengine ngumu, huenda mhusika akahitajika kurudia nadhiri zake za ubatizo kwa kuomba, “Ninamgeukia Yesu Kristo sasa na kumkubali awe Mwokozi wangu. Ninaweka imani yangu yote katika neema na upen-do wake. Katika Jina la Yesu ninaomba. Amina.”
14. Dagoni: Ikiwa mhusika atang’ang’ana sana wakati wa kuwekwa huru kutokana na laana baada ya mambo yote yaliyotajwa hapo juu kufanywa, fikiria juu ya kuomba na kuvunja laa-na ya Dagoni (I Sam 5) halafu uombe Ombi la Urudishaji na Ufufuo (nafasi haitoshi kuele-za zaidi juu ya jambo hili. Iwapo ungependa kujua mengi zaidi mtumie mwandishi barua pepe (www.healingofthespirit.org naye atakutumia habari zaidi na nakala ya ombi hilo).
Kabla ya kufanya ombi la kuivunja laana, itakuwa bora kumwambia mhusika asome sehemu inayoeleza juu ya “Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi” na kuyafuata mapendekezo yaliyo katika sehemu hiyo ya kujaza jedwali la ukoo. Jedwali la ukoo linaweza kumsaidia mtu kutambua laana zi-nazoweza kuweko pamoja na chanzo cha laana hizo.
Ombi la Kuzivunja Laana
Bwana Yesu, ninaamini kwamba wewe ni Mwana wa Mungu na njia pekee ya kwenda kwa Mungu, na kwamba ulikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu na ukafu-fuka kutoka kwa wafu.
Ninakataa na kuacha uasi wangu na dhambi zangu zote, na ninajiweka chini yako uwe Bwana wangu wa milele. Ninaungama dhambi zangu zote kwako, kwa unyenyekevu ninatubu na kuomba msamaha wako, hasa kwa dhambi zote zilizonifanya nipate laana. Pia ninaomba uniweke huru kutokana na athari za dhambi za babu zangu wa zamani.
50
# 8 Uponyaji Kutokana na Laana www.healingofthespirit.org
Kwa uamuzi wangu mwenyewe, ninawasamehe wote walionidhuru na kuniumiza, kama ninavyotaka Mungu unisamehe: Hasa, ninamsamehe______________ (taja majina ya watu wote unaohitaji kusamehe ambayo Mungu ataweka akilini mwako).
Ninakanusaha muungano wowote na kitu chochote cha ushetani/mizungu au na viumbe au athari za kishetani na iwapo nina vitu vyovyote vilivyolaaniwa, ninajitolea kuviharibu vyote kadiri utakavyoniwezesha kuvitambua. Ninafuta madai yote ya Shetani dhidi yangu. Kwa moyo wangu wote ninakanusha katika jina la Yesu, laana yoyote iliyowekwa juu ya maisha yangu.
Ninatubu kwa niaba ya babu zangu wa zamani ambao kwa kupenda au kutopenda kwao walijihusisha na viapo vya damu, walishiriki uchawi au waliombewa na “waponya-ji” wa kitamaduni wa aina yoyote. Nami kwa unyenyekevu naomba uwasamehe. Pia ni-nakanusha shughuli zozote za ushetani/mizungu zilizofanywa na babu zangu au nami mwenyewe zilizonifanya niwe na mpatano ya damu na Shetani.
Najitolea kukutumikia na kukutii, Bwana, na hivyo basi ninasimama dhidi ya nguvu zote za giza na uovu ambao umeingia katika maisha yangu, iwe ni kupitia kwa ma-tendo yangu, matendo ya familia yangu, matendo ya babu zangu, au kupitia kwa kitu chengine kikubwa zaidi ninachohusika nacho. Bwana, popote palipo na giza maishani mwangu, au nguvu zozote za uovu, ninakanusha sasa. Ninakataa katakata kuwa chini ya nguvu hizo nami ninadai tena sehemu hii ya kiroho iwe yako Mungu.
Bwana Yesu, ninaamini kwamba pale msalabani ulijitwalia kila laana iliyotakiwa kunijia mimi. Kwa ajili ya kitendo ulichonifanyia, ninaamini kwamba madai ya Shetani dhidi yangu yamefutiliwa mbali. Hivi sasa Bwana, najitolea kwako kikamilifu, na nina-kuomba uniweke huru kutokana na kila laana iliyo juu ya maisha yangu, katika jina lili-lobarikiwa la Yesu Kristo.
Ninaomba kutakaswa kwa damu ya Yesu na kuwekwa huru katika kila hali. Nina-vunja athari ya vitu hivyo juu yangu. Ninazimaliza nguvu za vitu hivyo. Ninatambua kwamba nina haki ya kukataa kabisa kuzipa ruhusa ya kutwala sehemu yoyote katika maisha yangu. Ninaamuru nguvu hizo ziondoke sasa, katika jina la Yesu lenye thamani.
Na katika jina kuu la Yesu, Mwana wa Mungu, ninachukua mamlaka juu ya ngu-vu hizo zote za uovu na ninajiweka huru kutokana nazo. Kwa imani, ninapokea uhuru wangu kutokana na nguvu hizo. Ninaziamuru ziondoke kwangu sasa katika jina lililoba-rikiwa la Yesu. Ninamkaribisha na kumwita Roho Makatifu wa Mungu aingie maishani mwangu ili aweze kuukamilisha ukombozi na uhuru wangu kwani ni Roho wa Mungu pekee anayeweza kufanya hivyo. Bwana asifiwe.
Ninakushukuru Bwana kwa sababu, “Mwana akiwapeni uhuru mtakuwa huru kweli.” (Yoh. 8:36), nami najua kwamba umeniweka huru sasa “huru kweli.”Katika jina la Yesu ninaomba. Amina.
51
# 8 Uponyaji Kutokana na Laana www.healingofthespirit.org
Vifaa
1. Derek Prince, Blessing or Cursing, You Can Choose (Chosen Books, 1990). ISBN 0-8007-9166-5. (Hiki ni kitabu bora zaidi kuhusu mada hii; pia kanda zenye sehemu 3 ni za kufaa sana.)
2. Dennis Cramer, Breaking Christian Curses (Arrow Publications, 1997). ISBN 1-886296-19-7.
3. Frank Hammond, The Breaking of Curses (Impact Christian Books, 332 Leffingwell Ave., Kirkwood, MO 63122; 314-822-3309, 1993). ISBN 0-89228-109-X.
4. Peter Horrobin, Healing Through Deliverance, Vol. 2 (Chosen Books, 1991, re-printed 2003): 180-194. ISBN 8007-9325-0.
5. Dick Bernal, Curses, What They Are and How to Break Them (1991). ISBN 1-56043-468-6.
70
# 10 Uponyaji wa Ulimi Wako www.healingofthespirit.org
Uponyaji wa Ulimi Wako
Mungu Aliiumba Dunia kwa “MANENO”
Katika kitabu cha Mwanzo, imetajwa mara tisa kwamba Mungu aliumba kwa kunena maneno, kama vile: “Mungu akasema, “Mwanga uwe,” mwanga ukawa. . . Anga liwe kati-kati ya maji. . . Ardhi na itoe aina zote za viumbe hai.” (Mwa.. 1:3, 6, 24). Maneno yana nguvu za ajabu.
Yesu Alibariki, aliponya, alitenda miujiza, na kuwafukuza mapepo kwa “MANENO”
Mfano mmoja ni huu: “naye, kwa kusema neno tu, akawafukuzu hao pepo. (Mat. 8:16). (Pia rejelea: Mat. 9:20-22 na 28-30, Marko 5:33-34 na 41—“inuka.”)
Yesu alitupa nguvu za KUUNDA au KUHARIBU, KUBARIKI au KU-LAANI, kwa MANENO
1. Methali 18:21: “Ulimi una nguvu ya kufanya hai na kuwa, wanaopenda kuutumia watakula matunda yake.”
2. Yakobo 3:2-11: “Maneno ya kubariki na ya kulaani hutoka katika kinywa kimoja. Ndugu zangu mambo haya hayapaswi kuwa hivyo” (kif. 10).
3. Kumbukumbu 11:26-28: “Angalieni, leo hii nawawekea mbele yenu Baraka na laa-na … Baraka, kama mtatii amri za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu … na laana kama hamtatii amzri za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.”
4. Baraka: zinapatikana katika vifungu vingi (Lawi. 26:2-13, Kumb. 28:1-14 na 30:16).
5. Laana: vilevile ziko katika vifungu vingi (Lawi. 26:14-33, Kumb. 28:15-68 na 30:17-19).
6. Baraka zimetajwa mara 221 katika Biblia; laana, mara 230.
7. Warumi 10:10: “na hukiri kwa kinywa” (mema na mabaya).
8. Mathayo 16:19 inathibitisha kanuni ya kufunga na kufungua kwa maneno.
9. Warumi 12:14: “bariki, wala usilaani.” (Pia Tito 3:2 na Yak. 4:11—msilaumiane nyinyi kwa nyinyi).
10. Mathayo 12:37: “Maana kwa maneno yako utakubaliwa kuwa mwadilifu, na kwa maneno yako utahukumiwa kuwa na hatia.” Tunachonena kwa kukiri na kudai) ndicho tutakachopokea.
• Tunapolalamika tunamkosoa Mungu.
• Hatuna haki ya kukosoa au kuhukumu kiumbe yeyote wa Mungu.
• Tunachosema ndicho tutakachokuwa.
• Tunabariki kwa midomo na mikono yetu.
• Bariki wala usilaani.
71
# 10 Uponyaji wa Ulimi Wako www.healingofthespirit.org
Kuhusu Nguvu iliyo Katika Maneno
Chunguza marejeleo yaliyo katika makundi yafuatayo.
1. Maneno huamua majaliwa: Kalebu na Yoshua waliripoti hivi “Twende mara moja tukaimi-liki nchi hiyo. kwa kuwa tunao uwezo sanawa kushinda.” (Hes. 13:26-31), ilhali wale watu wengine kumi walitoa ripoti hii “Hatutaweza kupigana na watu hao: wao wana nguvu kuliko sisi.” Mungu akawajibu “Nitawateneeni yaleyale niliyosikia mkiyasema” (Hes. 14:28). Ne-na na kuomba ahadi, sio matatizo.
2. Ulimi hunena uzima au mauti.. (Rejelea Zab. 34:11-13, Meth. 13:3, 15:4, 21:23, Yak. 1:26.)
3. Ulimi huwakilisha kitokacho moyoni: “… maana kwa maneno yako utakubaliwa kuwa na hatia.” (Mat. 12:33-37; pia tazama Yak. 3:6-13 na 4:11-12).
4. Maradhi ya ulimi ni haya:
4a. Kunena kupita kiasi (Meth. 10:19, Yak. 3:8, Mhu. 5:2-3)
4b. Maneno yasiyofaa (Mat. 5:37 na 12:36)
4c. Udaku (Lawi. 19:16, Meth. 18:8 na 20:19, Zab. 15:1-3)
4d. Uwongo (Meth. 6:16-19 na 12:22, Ufu. 21:8)
4e. Maneno ya Kinafiki (Zab. 12:1-3, Meth. 26:28 na 29:5)
4f. Kuwa mwepesi kunena (Metha. 29:20)
4g. Kunung’unika na kulalamika (Kut. 16:7, Hes. 14:27 na 16:11, Yoh. 6:43, 1 Kor. 10:10)
4h. Kukosoa, kulaumu, au kuhukumu Mat. 7:1-2, Luka 6:37, Yoh. 7:24)
5. Chanzo cha kila tatizo linaloathiri ulimi wetu kiko ndani ya moyo wetu.
6. Makusudi mawili ya ulimi: (1) kumtukuza Mungu: (2) Kuwaambia watu Habari Njema.
7. Umuhimu wa “kuungama”: ina maana ya kusema kama ilivyokuwa.”
8. Sisi “huumba” kwa maneno yetu: “Kila utakachofunga duniani, kitafungwa pia mbinguni; kila utakachofungua duniani, kitafunguliwa pia mginguni” (Mat. 16:19 na 18:18). Vivyo hivyo sisi “huumba” tunapoombea sehemu za mwili ili zipate uponyaji.
9. Mungu huumba kwa kusema kwamba vitu visivyokuweko, viweze kuweko (Rum. 4:17).
10. Tukitoa amri (tukidai, tukiita, tukikiri) kitu fulanitutakipata kitu hicho.
11. Kukiri na kutarajia mabaya matokeo yatakuwa mabaya: Sheria ya kupanda na kuvuna huchochea sheria ya hukumu.
12. Hatuwezi kufanya mambo yanayozidi: “… ila akaamini kwamba mambo yote anayosema yanafanyika, atafanyiwa jambo hilo.” (Marko 11:23).
Maneno yana jukumu la kutekeleza. Yana nguvu. Chochote mnachokubaliana huyapa nguvu. (Math 18:19). Tunapozungumza jambo moja (kukubaliana) sisi huunganishwa. (Mwa. 11, I Kor. 1:10) Tukikubali tunachoambiwa na Shetani au mtu mwingine, sisi hukubaliana na maneno hayo hata kama maneno hayo ni ya uwongo. Ombi la Yesu katika Yohana 17 lilikuwa ni; wawe kitu kimoja. Yeye alijua kwamba iwapo wangeungana na kukubaliana wangekuwa na nguvu nyingi. Isaka alimba-riki Yakobo, Esau alipotaka baraka hiyo, Isaka alimwambia kwamba hangeweza kuifuta baraka aliyompa Yakobo. (Mwa. 27)
Maneno yoyote yanayotoka kinywani mwako yana kazi maalum ya kutekeleza. Maneno hayo yanaweza kufungua mbingu au jehanamu. Ni rahisi kwako kujua iwapo unatamka maneno ya jeha-namu. Maneno hayo huwa kama haya: “Wewe huna thamani, wewe ni kama baba yako, afadhali usingezaliwa, hutawahi kufanikiwa, wewe ni mjinga.” Maneno ya kutoka jehanamu huidunisha tha-mani yako, majaliwa yako na kuzuia uwezo wako wa kuwa unachotakiwa kuwa.
72
# 10 Uponyaji wa Ulimi Wako www.healingofthespirit.org
Maneno ya kutoka mbinguni huwa kama haya: “Unapendwa, umejaliwa kuwa na cheo kikuu, una thamani kuu, utafanikiwa sana katika siku zako za usoni.” Sisi watu wazima tunaweza kukubali au kukataa maneno tunayonenewa. Lakini mtoto akisikia maneno ya aina hiyo yakinenwa juu ya maisha yake na mtu mwenye mamlaka kama vile: mzazi, mwalimu, atayaamini maneno hayo. Watoto hudhani kwamba maneno hayo ni ya kweli ilhali maneno hayo ni ya uwongo. Ukimwambia mtoto kwamba yeye ni mjinga kisha mtoto huyo ayapokee maneno hayo, mtoto huyo atakuwa mjinga, hata kama yeye si mjinga, kwa sababu amekuba-liana na maneno hayo, na Shetani akasema, sasa ninaweza kulitekeleza jukumu hilo, nime-funguliwa mlango, naye atatimiza jukumu la maneno hayo.
Maneno yanaweza kuwa mazuri au mabaya. Tunaweza kuunda mbingu au jehanamu juu yetu kwa maneno tuyanenayo. Tunaweza kuibadilisha hali kwa kukubaliana na/au kuya-pa maneno hayo jukumu jipya.
Ukosoaji, malalamiko, na hukumu ni lugha ya ibada ya jehanamu. Mambo hayo ya-liwazuia Waisraeli kuingia katika Nchi ya Ahadi (Hes. 11). Sisi huyapa mapepo idhini au huwapa malaika idhini. “Basi, nawaambieni, kila neno lisilo maana, watakalolinena wana-damu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. Kwa kuwa kwa maneno yako utahesa-biwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.” (Math. 12:36-37.)
Kukiri na kutarajia mambo mabaya huleta matokeo mabaya: Sheria ya kupanda na kuvuna huichochea sheria ya hukumu.
Luka 6:38 mara nyingi hutumiwa kama maandiko ya kuwahimiza watu kutoa sadaka, lakini hebu tazama muktadha wake katika vifungu vinavyokitangulia kifungu hicho. Vifungu hivyo vinazungumza juu ya kumpenda adui yako, na kuwabariki wanaokulaani. Kifungu cha 38 kinazungumza juu ya kutowahukumu wengine. Kinasema, “wapeni watu (lugha ya mbin-guni) nanyi mtapewa: kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.” Maandiko yanaorodhesha njia tano ambazo kwazo utarudishiwa.
Hivi sasa fikiri juu ya jambo hili. “Nikikosoa, nikihukumu, nitarudishiwa mara tano zaidi,” kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa. . . . . Iwapo malalamiko yana-toka ndani yako, hebu fikiri utakachorudishiwa. Hali ya giza inasema, maneno hayo yalitoka kinywani mwake, kwa hivyo nina haki ya kisheria ya kuwarudishia. Labda baadhi ya laana zinazokukumba zimesababishwa na kile kilichotoka ndani yako. Ukiwabariki watu wengine, fikiri juu ya kile kitakachokurudia mara tano. Wape zawadi wasiyotarajia.
Fikiri juu ya maandiko yafuatayo yanayosema kwamba, ukiacha neno lililo ovu litoke kinywani mwako, utamhuzunisha Roho Mtakatifu. “Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia. Wala
73
# 10 Uponyaji wa Ulimi Wako www.healingofthespirit.org
msimhuzunishe Roho Mtakatifu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi. Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi. (Efe. 4:29-32) Je, utatayarisha mazin-gira ya mbinguni yakuzingire ili malaika watimize majukumu yao au utatayarisha mazingira yatakayowezesha mapepo yatimize majukumu yao?
Nguvu za Maneno Katika Ukombozi
Kwa vile sasa una kiwango fulani cha ufahamu kuhusu nguvu za maneno, hebu sasa tutumie ufahamu huo katika ukombozi wetu.
Tukisha tambua milango iliyo wazi, tunahitaji kuifunga. Tunatakiwa kufanya hivyo kwa kutumia maneno. Mungu anaifahamu mioyo yetu na mawazo yetu pia, lakini Shetani haijui mioyo yetu wala mawazo yetu. Kwa hivyo tunatakiwa kumwambia Mungu mambo fulani kwa sauti ili Shetani aweze kutusikia: (1) kukiri (2) kutubu (3) kukana (4) kuyaondoa mamlaka/idhini ya kiroho iliyouwezesha mlango huo kufunguka. Halafu ni lazima tumwam-bie Shetani aondoke. Mambo hayo yote hufanywa kwa kutumia maneno. Maneno yetu yana jukumu la kumfukuza mpenyezaji asiyetakikana. Maneno hayo yana nguvu tunapoyanena katika jina la Yesu. Hiyo ni kama kwamba Yesu mwenyewe ndiye anayanena maneno hayo. Kifo chake msalabani kilitupa idhini ya kulitumia jina la Yesu. Maneno yetu ni maneno ya Ufalme wa Mungu, kwa kukubaliana na Yesu na Mungu Baba. Maneno hutuweka huru ku-tokana na athari za giza. Bwana Asifiwe.
Ombi la kuuponya ulimi wako
Katika jina la Yesu ninaivunja kila laana ya maneno iliyo dhidi yangu. Ninaliteka nyara kila neno lililonenwa juu yangu, au nililonena juu yangu mimi mwenyewe. Ninavunja nguvu za laana hizo. Ninakemea na kufutilia mbali kila jukumu la giza na ninalirusha ardhini ili lisiwe na athari yoyote. Ninakataa na kubatilisha kila uwongo nilioamini.
Ninaziita baraka zinishukie mahali hapa. Ninaifuta kila laana niliyonena juu ya mtu mwin-gine. Ninayarusha maneno hayo ardhini ili yasiwe na athari yoyote. Ninawabariki watu wote niliowalaani. Yesu alitwaa laana yangu ili niweze kuishi katika baraka. AMINA.
Vifaa
1. Derek Prince, Does Your Tongue Need Healing? (Whitaker House, 1986). ISBN 0-888368-239-7.
74
# 11 Uponyaji Kutokana na Viapo na Matamanio ya Kufa www.healingofthespirit.org
Uponyaji Kutokana na Viapo na Matamanio ya Kufa
Viapo
Kiapo ni kitu kinachosemwa kwa maneno (au akilini) kwa hiari yetu wenyewe ambacho huongoza mwili na akili za mtu kuanzia wakati huo wa kutamkwa. Kiapo ni agizo linalotumiwa kupi-tia kwa moyo na akili hadi mwilini. (“Umejibana kwa maneno yako mwenyewe, umejinasa kwa ahadi uliyofanya.”—Meth. 6:2). Ingawaje akili yenye ufahamu husahau neno hilo, nafsi ya ndani haisahau. Ni uamuzi unaofanywa na akili na moyo kuanzia wakati huo. Agizo hilo hukaa rohoni.
Viapo vya ndani huwa ni utaratibu wa kujilinda navyo hufanya kazi kama utaratibu wa ku-jikinga ili roho zetu zisijeruhiwe wala kuumizwa. Viapo vya ndani hujenga ua la kuuzunguka moyo. Watu wengi ambao huonyesha hisia za kukataliwa wakati mwingine wao huwa na mioyo migumu. Lazima mtu atake mwenyewe kuuondoa ukuta huo na kukanusha viapo hivyo, ili aweze kuuhisi upendo wa Mungu kikamilifu. Viapo humzuia Mungu kuuponya moyo.
Viapo vya ndani vinavyodhihirishwa huwa na maana kwamba sehemu fulani ya maisha yetu itaendeshwa kinyume na mpango na makusudio ya Mungu. Viapo hivyo vitatuzuia kuweza kutumiwa na Mungu na humkaribisha Shetani atutawale katika sehemu fulani. Viapo vya ndani huenda visidhi-hirishwe mara moja katika mienendo yetu lakini hatimaye husababisha hisia kuharibika au kulipuka.
Viapo hivyo vya ndani hufanya kazi ya kuamrisha akili na mwili. Ingawaje nia ya viapo hivyo huwa ni kutuzuia kuumia, viapo hivyo hutufanya tukose kupendwa na Mungu na watu wengine pia. Upendo wetu huwa “baridi””—sisi huonyesha upendo kwa nje tu kwani upendo huo si wa kutoka moyoni.
Mtu yeyote akisema kiapo cha ndani, kiapo hicho kitaingia ndani ya roho, mwili na nafsi ya mtu huyo na roho hufanya kila jambo ili kiapo hicho kidumu. Unapokitamka, roho yako husikia na kukisajili. Roho husema, “Haya ni mapenzi yake, hicho ndicho akitakacho, kwa hivyo lazima nitii.”
Roho yako hulazimishwa kukifuata kiapo hicho. Hata hivyo, pepo anaweza kumuingia mtu kwa sababu ya kiapo cha ndani. Unapotamka kiapo, roho wa kutawala na wa kujitegemea huingia ndani yako ili kiapo hicho kiweze kutimia, “nawe” huwekwa katika kiti cha enzi cha maisha yako (“wewe” huhakikisha kwamba hakuna mtu atakayeweza kukwambia “wewe” unachotakiwa kufanya. “wewe” huwezi tena kuingia katika uhusiano. “Wewe” hujitegemea, “wewe” umeizoesha roho yako kwamba hakuna mtu anayeweza kukwambia “wewe” unachotakiwa kufanya.) Baadhi ya mifano ni:
“Sitawahi tena kumruhusu mtu aniumize au (anitumie) vibaya)”
“Sitajaribu kufanya jambo hilo tena.”
“Sitakataliwa tena.”
“Sitamwamini tena mwanamume (au mwanamke).”
Hutaweza kuuhisi upendo wa Mungu, wala kuisikia sauti yake, ikiwa una ukuta uliouzunguka moyo wako. Lazima umwamini Mungu vilivyo ili uweze kuamini kwamba anaweza kuzivunja kuta hizo. Kuamini kwamba labda Mungu hataweza kutulinda (tukiomba kwa ajili ya kuondoa kiapo hicho) ni suala la kuamini linalopaswa kushughulikiwa. Msaidi-zi anatakiwa kumhakikishia mtu anayetaka uponyaji kwamba Mungu ni mlinzi wake na atamlinda ili mambo hayo yasiudhuru moyo wake: mtu huyo anatakiwa kumwamini Mungu badala ya kujiamini mwenyewe. Kutomwamini Mungu ni kuwa na kiburi.
75
# 11 Uponyaji Kutokana na Viapo na Matamanio ya Kufa www.healingofthespirit.org
Ombi la Kuvunja Viapo
1. Mwambie Mungu akufahamishe viapo vyovyote vinayoweza kuzuia uponyaji wako..
2. Viapo ni dhambi. Mtu huyo anatakiwa kuvikiri kama dhambi kisha aombe msamaha.
3. Mwambie mtu huyo akanushe viapo hivyo katika jina la Yesu; achukue sehemu yoyote aliyotoa kwa mwovu na amrudishie Mungu. Tumia mwongozo huu wa ombi:
Bwana, ninakiri kiapo hiki cha __________ kuwa ni dhambi na ninaomba msamaha. Katika jina la Yesu ninachukua sehemu yoyote nilyopoteza na kukupa wewe Bwana. Ninai-vunja ahadi hii ya ndani ya ______________, najiweka huru kutokana nayo kama kitendo cha kutii. Tafadhali fanya upendavyo ndani ya maisha yangu. Katika jina la Yesu ninaomba. Amina.
Ombi Atakaloomba Mwombezi
Katika jina la Yesu, ninakuweka huru kutokana na kiapo hiki na kukurudisha kwa fu-raha ya mwanzo ya nafsi yako. Ninakuachilia ili uweze kuufungua moyo wako na uwe huru unaposhirkiana na wengine. Asante Yesu kwa kumrudisha ___________ katika hali uliyo-muumba. Katika jina la Yesu ninaomba. Amina.
76
# 11 Uponyaji Kutokana na Viapo na Matamanio ya Kufa www.healingofthespirit.org
Matamanio ya Kufa
Tamanio la kufa ni aina ya kiapo cha ndani. Watu wengi waliodhulumiwa kimapenzi, wenye huzuni, au waliokataliwa vibaya—au wanaoichukia miili yao—mwishowe huwa na matamanio ya kufa. Wengine wao huhisi kujidhania kwamba, “wameshindwa.” Kila wazo la kutaka kujiua huambatana na tamanio la kufa.
Mara nyingi kila tamano la kufa huambatana na hasira kwa ungu kwa “kuniumba kama nilivyo” au kwa kuyaacha mambo yafanyike kama yalivyofanyika. Watoto wengine huja duniani bila kutaka kuzaliwa kwa sababu ya matukio ya uchungu yaliyofanyika walipo-kuwa tumboni.
Mara nyingi watu huwa na matamanio ya kufa wanapokuwa wazee. Matamanio ya kufa hufungua mlango unaoruhusu roho ya kifo na huzuni kuingia ndani ya mtu. Athari hizo za giza humfanya mtu huyo awe na huzuni mwingi na kumshawishi ajiue.
Ombi kwa Ajili ya Matamanio ya Kufa
1. Mtu anayetaka uponyaji anatakiwa kukiri matamanio yoyote ya kufa na kutamani ku-jiua (au jaribio lolote la kufanya hivyo) kuwa ni dhambi na aombe msamaha.
2. Mhusika huyo anatakiwa pia kukanusha mawazo, majaribio, au viapo vyovyote.
3. Mhusika huyo anatakiwa pia kukiri na kutubu hasira aliyo nayo kwa Mungu.
4. Wakati mwingine roho wa kifo huweko na ni lazima afukuzwe.
5. Omba maombi yaliyo katika sehemu inayoeleza juu ya “Kuiponya Picha Tuliyonayo Kuhusu Mungu.”
Vilevile Omba Ombi Lifuatalo:
Bwana, ninakiri kuwa matamanio ya kufa na kutamani kujiua (na jaribio lolote la ku-fanya hivyo) ni dhambi. Ninakanusha mambo hayo katika jina la Yesu. Ninatubu kwa kujika-taa na ninakupa sehemu yoyote ambayo nilikuwa nimempa Shetani. Ninaamuru roho zote za giza za kifo, kujiua, au huzuni ziondoke katika jina la Yesu.
Ninaukubali mwili wangu na kuikubali hali yangu ya sasa na ninakuomba unipata-nishe na nafsi yangu. Nipatanishe na wakati wangu, na mahali na nafsi yangu kamilifu hapa duniani. Ninakuamini Bwana, uniongoze maishani ili niweze kutimiza yote unayonikusudia ili niweze kukutukuza.
Asante kwa kuniokoa kutokana na nafsi yangu. Katika jina la Yesu ninaomba. Amina
77
# 12 Vitu na Mahali pa Uponyaji www.healingofthespirit.org
Uponyaji wa Vitu na Mahali
Watu wengine huwa hawaamini kwamba vitu au mahali panaweza kuingiliwa na athari za uovu. Kwa watu hao wasioamini, itakuwa vigumu kubishana na watu ambao wameishi mahali palipoingiliwa na ambao wamepata kuona matukio mbalimbali yasiyo ya kawaida ambayo ya-mewahi kutokea kupitia kwa nguvu za uovu.
Ripoti ya mambo yasiyo ya kawaida zimewahi kutokea kama vile TV, redio na kompyuta kuzima zenyewe bila mtu kuzizima, picha au chupa za maua kuanguka—bila sababu yoyote. Taa kuwaka zenyewe, sauti za watu wanaotembea au wanaolia zimesikika usiku, n.k. John Sanford aliyeandika kitabu hiki (Deliverance and Inner Healing) na Frances McNutt aliyeandika (Deli-verance from Evil Spirits) wamewahi kuripoti kwamba kompyuta zaozilikataa kufanya kazi au zilionyesha maneno na ishara mbovu walipokuwa wakitayarisha miswada ya vitabu walivyoku-wa wakiandika.
Wakati mmoja niliwahi kupokea ujumbe kupitia kwa barua pepe uliotumwa na athari ya uovu kutoka kwa kompyuta iliyokuwa ndani ya nyumba ya rafiki yangu mmoja ambaye ni ali-kuwa akitatizwa na athari za uovu katika nyumba yake kwa kipindi fulani. Watu wengine wa-mewahi kuripoti kwamba magari yao yalionyesha kwamba mafuta yalikuwa yamejaa kila wakati na breki za magari yao zikakataa kufanya kazi walipokuwa wakiendesha gari na hawangeweza kulizima mpaka walipoomba kwa bidii ili wakombolewe.
Kwa nini mambo hayo hutokea? Kuna angaa sababu nne za kusumbuliwa huku.
1. Huwa kuna vitu vilivyotiwa najisi ndani ya nyumba hiyo
2. Nyumba hiyo huwa imejaa uwepo wa uovu kwa sababu ya dhambi za watu walioishi ka-tika nyumba hiyo hapo awali.
3. Nyumba hiyo imejengwa karibu na au juu ya ardhi iliyotiwa najisi.
4. Zimwi la mtu aliyekufa linahitaji kuachiliwa huru (mapepo huwa yameingia mahali ha-po.)
Vitu Vilivyotiwa najisi
Mambo mengi yameshaandikwa kuhusu athari za uovu zinazojitoa wazi kupitia kwa vitu fulani. Sanamu na vitu vingine vinavyotumiwa kufanya kazi ya ushetani/mizungu vinaweza ku-wa mlango wa kuingilia nguvu za mapepo. Israeli iling’ang’ana na sanamu kwa miaka elfu moja, bila kufuata maagizo ya Bwana: “Teketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga za miungu yao. Msipeleke sanamu zozote katika nyumba zenu, ama sivyo, mtalaaniwa kama sanamu hizo. Ni la-zima mzichukie na kuzidharau kwa kuwa ni vitu vilivyolaanniwa.” (Kumb. 7:25-26 na 12:3).
Waisraeli walionywa kila mara waondoe sanamu, wabomoe nguzo za Ashera, wa-waondoe watu wanaowasiliana na mizimu, na sanamu za nyumbani, na kuharibu madhabahu waliyokuwa wakifanyia ibada. Mara moja moja wafalme walitii (2 Fal. 23:8, 13-15; lakini wengi walikosa kutii, 2 Fal. 15:1-5). Ingawa hatuna hatia ya kuabudu miungu wengine kama walivyofanya Waisraeli, sisi hukosa kutumia hekima ya kujua ni vitu gani tunavyoingiza nyumbani kwetu. Vitu vilivyobuniwa, zawadi, vitu vya ukumbusho, sanamu ndogo za Budd-ha) vyote vinashukiwa kuwa na athari. Hata vipande vya mawe au mchanga kutoka katika sehemu zengine za ulimwengu vinaweza kuwa vimetiwa najisi.
Vitu vilivyotwa najisi vinaweza kututenga na makusudi ya Mungu, ulinzi wake, na nguvu zake. Vitu hivyo humpa adui mlango wa kuingia. Vitu vilivyotiwa najisi huvutia uovu kama vile kinyesi huwavutia nzi. Mlango huo huingiza uchafu wa kiroho ndani ya
78
# 12 Vitu na Mahali pa Uponyaji www.healingofthespirit.org
nyumba. Zaidi ya hayo, roho waovu walio ndani ya watu hupata nguvu kutoka kwa vitu vilivyotiwa najisi vilivyo ndani ya nyumba. Rejelea matumizi, dalili na marejeo yafuatayo:
1. Vitu halisia huwa vyenye maana kiroho.
• Damu (Kut. 12:7-13)
• Hema Takatifu, mapambo yake, vyombo (Kut. 26 na 27)
• Joka la Musa la shaba (Hes. 21:5-9)
• Dhahabu, fedha, vazi (Yosh. 7:10-26), mkuki (Yosh. 8)
• Ubatizo wa Maji (Luka 3:21-22)
• Karamu ya Bwana (Mat. 26:26)
• Vitambaa, aproni za miujiza (Mat. 19:11-12)
• Mafuta ya Uponyaji (Yak. 5:14)
2. Kumiliki vitu vingine kumekatazwa
• Orodha ya vitu vinavyoaibisha Mungu (Kumb. 4:15-19, 23-24)
• Miungu wengine, sanamu, au picha (Kut. 20:3, Kumb. 27:15)
3. Kujihusisha katika shughuli zengine kumekatazwa.
• Uchawi, unajimu (Kumb. 18:9-13; pia tazama sehemu inayoeleza juu ya “Uponyaji Kutokana na Mizungu/Ushetani”)
4. Utumiaji wa kitu fulani unaweza kuimarisha maana ya kiroho ya kitu hicho.
• Vitu vilivyochongwa, sanamu—za kuabudu miungu wengine.
• Madhabahu na/au nguzo za Ashera, vitu vya kipagani, na sanamu (Kumb. 7:5 na 12:3, Amu. 3:7)
5. Dhambi ya mtu mmoja inaweza kusabaisha athari kwa kila mtu katika kikundi .
• Akani alificha dhahabu, fedha, na vazi kutoka vitani (Yosh. 7)
• Israeli iliumia sana kwa ajili ya uamuzi wa wafalme wengi waliokuwa watenda dhambi
• Yona (katika meli, Yona 1:3-15)
6. Dalili za najisi ya kiroho zinazoweza kuweko kutoka kwa vitu:
• Magonjwa ya kudumu kuja ghafla
• Kuendelea kupata ndoto mbaya na/au jinamizi
• Kukosa usingizi au kupata usingizi usio wa kawaida
• Matatizo ya kitabia
• Matatizo ya uhusiano, kupigana kila wakati, kubishana
• Kukosa amani
• Kutotulia, watoto kusumbua
• Magonjwa yasiyoelezeka
• Kuendelea katika utumwa wa dhambi
• Uvundo mbaya usioelezeka
• Uzito katika anga, unaowafanya watu washindwe kupumua
• Kuchafuka moyo kila wakati na kuumwa na kichwa.
• Matatizo ya kifedha
7. Dalili Zinazoweza kuweko za najisi ya kiroho kutoka kwa shughli za mizun-gu/ushetani:
• Pepo mbaya mwenye ghasia (mapepo kuvisongeza vitu vya asili)
• TV, redio, na kompyuta kujiwasha na kujizima
79
# 12 Vitu na Mahali pa Uponyaji www.healingofthespirit.org
• Picha au chupa za maua kuanguka
• Taa kuwaka zenyewe
• Sauti za watu wanaotembea au wanaopiga nduru usiku
8. Vitu vinavyoweza kusababisha najisi:
• Vitu vinavyohusiana na ibada ya kipagani (mwanaserere wa vuudu, vinyago vya mi-zimu, nyoka, mazimwi, ndege wa radi, ndege wa hadithini Uarabuni, n.k.)
• Vitu vinavyohusiana na dhambi za zamani au miungano miovu ya nafsi (mikufu, pete, barua za mapenzi, picha, kitabu cha kumbukumbu za kila siku, majarida)
• Vitu vyenye historia isiyojulikana vinavyoonekana kuwa havina uovu, kama vile sa-namu ndogo za mbao, picha, vitu vya kitalii
• Vitu vyovyote vinavyotumiwa kufanya uchawi au shughuli za bingwa wa maono, kama vile uaguzi, hirizi, chembechembe za mawe, n.k.
• Michezo kama vile “Majoka,” “Mkuu wa Uimwengu.” n.k.
• Mfuasi wa Budha, Baniani, au vitu vingine vilivyobuniwa vya ibada kutoka Mashari-ki
• Vitu au vitabu vinavyohusiana na shetani, uchawi, Dini ya Kizazi Kipya, Nyota za unajimu, mwezi kongo, mipira ya chembechembe za jiwe, piramidi, au sanaa ya vita.
• Vitu au vitabu vinavyohusiana na unajimu, uaguzi, au vilivyoandikwa na waandishi fulani (Edgar Cayce, Jean Dixon, n.k.)
• Gazeti lenye hadithi za katuni, picha kubwa za muziki wa “rock,” na vifaa vilivyo na picha zinazojulikana za giza.
• Vifaa vya kiponografia vya aina yoyote (video, vitabu, magazeti, mawazo ya TV)
• Sanaa yenye michoro ya kimapepo, kama vile nyoka, roho, kifo, fuvu la kichwa, ma-zimwi, n.k.
• Vitu au vitabu vinavyohusiana na vyama vya siri kama vile freemason, Nyota ya Ma-shariki, Mashujaa wa Malta, Fuvu la kichwa na Mifupa.
• Vitambaa vya Kimasoni, vitabu, au pete (ishara za yin-na-yang za Mashariki)
• Vitabu na filamu fulani za watoto kama vile “Harry Potter” (vinavyowahimiza watoto watake kupata nguvu za kiroho zisizokubaliwa na Mungu)
• Sinema zenye ujumbe wa mizungu/ushetani, vurugu kali sana, lugha chafu sana, maudhui waziwazi ya ngono
• Vitu vilivyolaaniwa na watu wengine, (vitu usivyovijua mpaka Mungu akufunulie)
• Vitabu vinavyozingatia kupenda anasa au kifo na uharibifu (Mfalme Steven)
(Orodha iliyo hapo juu imetolewa katika kitabu kiitwacho “Spiritual House Cleaning” kilichoandikwa na Eddie na Alice Smith.)
Inafaa kutambuliwa kwamba watu wapya waliobadili dini katika kanisa la kwanza walivileta vitu vyao na vitabu vilivyotiwa najisi, na vitu hivyo vikachomwa: “Wengi wao waliokuwa wameshughulikia mambo ya uchawi hapo awali, walikusanya vitabu vyao, wakavi-choma mbele ya wote. Walikisia gharama ya vitabu hivyo wakaona yafikia vipande vya fedha hamsini elfu.” (Matendo 19:19).
Vitu vilivyopagawa na mapepo vinaweza kuingia nyumbani mwako bila wewe kujua au kwa kuletwa na watu wengine. Wakati fulani mwanamke mmoja alipokuwa akifanyiwa maombi ya ukombozi, Bwana alitujulisha kwamba nyumbani kwake kulikuwa na vitu kadhaa vilivyotiwa
80
# 12 Vitu na Mahali pa Uponyaji www.healingofthespirit.org
najisi alivyopokea kama zawadi kutoka kwa baba yake. Kwa sababu ya kuwa na hamaki, baba huyo aliwaambiwa waganga wenye nguvu wavilaani vitu hivyo kabla ya kuvituma kwa mwa-nawe. (kwa ajili ya chukizo kwa mke wake aliyekuwa amempa mtu huyo talaka). Mwanamke huyo hangeweza kuwa huru kabisa mpaka vitu hivyo vilipokusanywa na kuteketezwa.
Njia ya Kuvitakasa (vitu vilivyotiwa najisi)
1. Amini kwamba Mungu anataka kutujulisha vitu vyote vilivyotiwa najisi, tukimwomba kwa imani.
2. Ikiwezekana, mwambie mtu aliye na kipawa cha upambanuzi aje kutafuta vitu katika nyumba yako, akiomba na kumwambia Mungu amjulishe juu ya kitu chochote kilichoti-wa najisi.
3. Ikiwezekana teketeza vitu vyote vilivyotiwa najisi vitakavyopatikana (au vitupe ndani ya pipa la takataka).
4. Mwambie Mungu atakase kila mahali palipokuwa na vitu hivyo.
Mahali Palipotiwa Najisi
Mahali na/au nyumba huingiwa uwepo wa uovu kupitia kwa njia kadhaa: laana, ibada ya Shetani, uhalifu, fujo, dhambi zilizotendwa, vitu vilivyo na uwepo wa uovu au kupitia kwa uwe-po wa uovu ulio ndani ya watu wanaoishi mahali hapo. Mahali fulani panaweza kuathiriwa na uovu iwapo mtu aliye mahali hapo atajihusisha na ushetani/mizungu (uaguzi, ulozi, kuwasiliana na mizimu, ubashiri, n.k.) Mambo mengine yanayoweza kufanya mahali fulani patiwe najisi ni pamoja na uzinzi, mazoea potofu ya ngono, ubakaji, mauaji au jaribio la kuua, dhuluma ya kima-penzi, matambiko ya kishetani. Kwa vile mambo hayo hufanyika kwa hiari pamoja na matendo ya watu wanaohusika nayo, nguvu za giza hupewa haki ya kiroho (au ruhusa) ya kumiliki ardhi hiyo na/au mahali hapo kwa makusudi ya uovu. Hii ni sawa na jambo ambalo hufanyika ndani ya roho zetu za kibinadamu tunapotenda dhambi; huwa tunampa mwovu ruhusa ya kuathiri sehemu hiyo ya roho yetu. Kwa kiasi fulani, watu walio na roho waovu huleta uovu fulani mahali na pia wao huacha uovu fulani popote waendapo. Kuna mifano mingi ya matatizo yaliyowapata watu kwa kujihusisha katika shughuli za uovu hapo awali.
Miaka kadhaa iliyopita, mwanamke mmoja aliyekuwa amekodisha nyumba katika mji mwingine aliniambia juu ya athari za uovu katika nyumba yake. Alituomba (timu yetu ya hudu-ma) twende tukaiombee nyumba hiyo. Kwa vile nyumba yake ilikuwa umbali wa karibu maili 50, na hatukutaka kukimbilia mahali ambapo Mungu hakuwa ametutuma, tulikusanya ki-kundi kidogo cha watu waombe ili tujue ikiwa tungemwita aje kukaa nasi kisha tuibariki nyumba hiyo. Tulipokuwa tukiomba, mwanamke mmoja katika kikundi hicho aliyekuwa na kipawa cha kupambanua mapepo aliweza kuiona nyumba hiyo na akaona kwamba wakati mmoja watu wa-naoabudu Shetani waliishi katika nyumba hiyo, na kwamba kafara zilikuwa zimefanyiwa ndani ya gereji ya nyumba hiyo katika sherehe za mizungu/ushetani. Pia tuligundua kwamba mwa-namke huyo aliyekuwa ametuomba tuiombee nyumba yake alikuwa akiishi na mwanamume am-baye hakuwa amemuoa. Alishauriwa kwamba hata kama nyumba yake ingetakaswa kiroho na kubarikiwa, utakaso huo haungedumu kwa sababu ya dhambi ya uzinzi katika nyumba hiyo, am-bayo ingefungua mwanya wa uovu kurudi tena. Mwishowe aliondoka katika nyumba hiyo.
Familia nyingine ilieleza kwamba ilikuwa ikikumbwa na dalili za najisi ya kiroho. Nyumba hiyo ilipokuwa ikitakaswa, watu hao walipata michoro ya ishara za kishetani juu ya paa la nyumba hiyo na katika kuta za gereji. Mifano kama hiyo ni thibitisho kwamba nyumba am-bayo uzinzi umefanyiwa ndani inaweza kupata laana.
81
# 12 Vitu na Mahali pa Uponyaji www.healingofthespirit.org
Kupaponya Mahali Palipotiwa Najisi
Kitendo cha kupatakasa mahali palipotiwa najisi hufanyika hivi:
1. Kwanza ondoa vitu vyote vilvyotiwa najisi.
2. Watakase watu wanaoishi mahali hapo (kwani wanaweza kuleta najisi ya kiroho ndani ya nyumba hiyo)
3. Tafuta mzizi wa tatizo hilo—tafuta kujua vile mahali hapo palitiwa najisi.
4. Takasa nyumba (au mahali hapo) (2 Nyak. 29).
5. Bariki nyumba (au mahali hapo) (1 Nyak. 17:27).
6. Tayarisha Meza ya Bwana katika nyumba (au mahali hapo).
Yafuatayo ni maelezo zaidi kuhusu hatua zinazohusika katika kufanya uponyaji na utakasaji wa mahali palipotiwa najisi:
1. Ondoa vitu vyote vilivyotiwa najisi: Omba ili ufahamishwe juu ya kitu chochote katika nyumba hiyo ambacho kinaweza kuwa kimechafuliwa. Mchague mtu mmo-ja aliye na kipawa cha upambanuzi wa roho ili aweze kuingia ndani ya kila chum-ba cha nyumba hiyo, akimwomba Mungu amfahamishe vitu vyote vilivyotiwa na-jisi. Biblia inasema tuvichome vitu hivyo. (Kumb. 7:5 na 12:3, Matendo 19:19).
2. Watakase watu wanaoishi mahali hapo: Ni muhimu kwa watu wanaoishi ma-hali hapo kumwamini Yesu, kubatizwa na kupata ubatizo wa Roho Mtakatifu. Watu hao wanatakiwa kumtaka Yesu kuliko vile wanavyotaka nyumba yao ita-kaswe. Waambie watumie sehemu hii ya somo kutambua sehemu za athari ya uo-vu walizojiingiza ndani. Omba na kumuuliza Roho Mtakatifu akujulishe aina yoyote ya dhanmbi ambayo haijafanyiwa toba ndani ya maisha ya mtu yeyote anayeishi katika nyumba hiyo, ili milango yote iliyo wazi iweze kufungwa. Kwa vile ni vigumu sana kuuona “uchafu” wetu wenyewe, kuna faida kubwa kwa mtu aliye na imani kuu kuomba nawe na kukuombea.
3. Tafuta chanzo cha tatizo hilo: Iwapo nyumba hiyo imetwa najisi kiroho, anza hatua ya kutafuta chanzo cha tatizo kwa kutaka kufahamu ni kwa nini mahali hapo pametiwa najisi. Uliza maswali kama vile: “Nini kilifanya mahali hapo pawe hivyo?” “Maovu hayo yalianza wakati gani?” “Je, umegundua mkondo wowote maalum?” Wahoji majirani ili upate habari zaidi. Ikiwezekana, fanya utafiti kuhu-su historia ya nyumba hiyo (mahali au ardhi). Nani aliyeishi mahali hapo awali? Shughuli gani zilifanywa mahali hapo? Wakaazi wa awali walijihusisha katika mambo gani? (vitabu, mashirika, n.k.)? Majibu ya maswali hayo yatakuwezesha kufanya uamuzi utakaokufanya ugundue chanzo cha tatizo hilo.
Iwapo kulikuwa na shughuli zozote za uovu zilizofanyika, baadhi ya majirani wana-weza kujua. Zaidi ya hayo, iwapo unamjua mtu yeyote aliye na kipawa cha kupambanua ro-ho, mwambie aje kuomba ili muweze kupata ufunuo wa chanzo cha tatizo hilo. Ni vyema iwapo chanzo cha tatizo hilo kitagunduliwa (kama kilivyo katika hatua ya uponyaji wa ndani) la sivyo, mwanya huo utabaki wazi na kuwezesha athari za kipepo kurudi mahali hapo.
82
# 12 Vitu na Mahali pa Uponyaji www.healingofthespirit.org
4. Takasa nyumba (au mahali hapo): Iwapo chanzo cha tatizo hilo, au kosa lililofa-nywa linaweza kutambuliwa, mwenye nyumba (kwa niaba ya mtu aliyetenda dhambi) anatakiwa kuchukua nafasi ya mtu huyo na kuomba msamaha na kutubu (rejelea se-hemu iliyo na kichwa hiki, “Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi” ili uweze kupata maelezo zaidi ya shughuli hizi.) Iwapo ovu la kwanza ni kujihusisha katika ibada ya Shetani na tambiko la kishetani, kikundi kikubwa cha waombezi wenye ujuzi na wenye imani kuu wanatakiwa kukusanywa kwani nguvu za maombi maalum zitahita-jika ili ziweze kuushinda uovu ulio mahali hapo.
Omba ili Mungu apatakase mahali hapo na ardhi hiyo kutokana na uovu wo-wote. Mwambie Bwana—asiyejua mipaka ya wakati—aifikie historia ya nyumba na ardhi hiyo na aweze kupaponya; omba ili roho zote za kipepo zilizo mahali hapo zi-weze kuondolewa na kwamba mahali hapo paweze kutakaswa kutokana na chuki ya muda mrefu na kila hali ya kutofautiana.
Omba kwamba Bwana atapaosha mahali hapo kwa damu yake na aweze kuteketeza (kwa moto wake) kitu chochote kinachoweza kuwapa mapepo na nguvu za kishetani nafasi ya kutenda kazi. Tumia msalaba, damu, na ufufuo wa maisha ya Yesu kwa kila kitu katika historia ambacho hakijaponywa. Mwambie Bwana ateke-leze msamaha, achukue mamlaka juu ya nyumba hiyo na ardhi hiyo, na uitangaze kuwa ya haki na iliyotakaswa katika jina la Yesu. Kisha iweke wakfu kwa Yesu na kwa makusudi yake.
5. Ibariki nyumba (au mahali hapo): Baada ya nyumba hiyo kutakaswa, ibariki. Tem-bea nje ya nyumba hiyo ukiomba ili malaika wa Bwana wanaohusika na vita waweze kuilinda. Omba kwa sauti Zaburi 91 halafu ingia ndani ya nyumba hiyo na uombe kwamba mwangaza na uzima wa Yesu utaijaza nyumba hiyo. Mwambie Mungu ai-jaze nyumba hiyo na uzuri wake, na nguvu za uwepo wa malaika wake watakatifu. Omba ili amani ya Mungu ishuke juu ya nyumba hiyo (Mat. 10:13, Luka 10:5).
Iweke wakfu nyumba hiyo kwa Mungu. Paka mafuta matakatifu juu ya viunzi vya milango na madirisha kama ukumbusho wa siku ya Pasaka. Iwapo maji matakati-fu hutumiwa katika ushirika wenu, pata kiasi fulani cha maji hayo—au yabariki maji kwa ajili ya kazi hiyo—na unyunyizie kiasi fulani katika kila chumba cha nyumba hiyo. Kumbuka kuomba ombi la shukrani kwa jambo ambalo unajua kwamba Bwana anatenda mahali hapo.
6. Tayarisha Meza ya Bwana katika nyumba (au mahali hapo): Hatimaye tayarisha ibada ya Meza ya Bwana katika nyumba hiyo (kama ilivyoelezwa zaidi katika sehe-mu iliyo na kichwa hiki: “Nguvu za Uponyaji za Ushirika Mtakatifu.”)
Vifaa vya Uponyaji wa vitu na Mahali
1. Eddie na Alice Smith, Spiritual House Cleaning (Regal Books, 2003). ISBN 0-8307-3107-5.
2. Chuck Pierce, Protecting Your Home from Spiritual Darkness (Wagner Publications, 1999). ISBN 0-9667-481-7-4.
3. Francis MacNutt, Deliverance from Evil Spirits (Chosen Books, 1995): 253-68. ISBN 0-8007-9232-7.
4. John and Mark Sandford, Deliverance and Inner Healing (Chosen Books, 1992): 205-40. ISBN 0-8007-9206-8.
83
# 12 Vitu na Mahali pa Uponyaji www.healingofthespirit.org
Ardhi Iliyotiwa Najisi
Athari za uovu haziko katika nyumba na majengo pekee bali pia zinaweza kuwa juu ya mae-neo makubwa. Ardhi iliyotiwa najisi imetajwa zaidi ya mara 15 katika Biblia (rejelea Zab. 106:38, Isa. 24:5, Yer. 2:7 na 3:1). Kama vile mizoga huwavutia tai wa angani, ndivyo ardhi, vitu au mahali palipotiwa najisi huvutia uovu wa kiroho. Mapepo hujaa mahali palipotiwa najisi. Yafuatayo ni marejeleo yanayojulikana:
• Katika Mwanzo 4:10, Mungu ananena na Kaini baada ya kaini kumuua Abeli na Mungu akatangaza “Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.”
• Walawi 18:24-25 inasema kwamba ardhi ya Israeli ilitiwa najisi kwa sababu dhambi za nchi hiyo zilikuwa zimeingia katika ardhi hiyo.
• Yeremiah 4:23-29 inapendekeza kwamba dunia itaomboleza.
Katika hali moja, mwendelezaji mmoja alitaka kukigawa kipande cha ardhi ili ajenge nyumba mpya. Kila Kontrakta aliyempa kazi ya kujenga barabara alipata tatizo la mitambo yake kuharibika. Hatimaye Roho Mtakatifu aliwajulisha kwamba mahali hapo palikuwa mahali pata-katifu, mahali maalum pa mkutano wa densi na sherehe za kiroho za Wenyeji wa Marekani. Wa-hindi hao walikasirika sana walipopokonywa ardhi hiyo mwanzo wa miaka ya 1800 na walikuwa wameilaani.
Hadithi moja katika toleo moja (Oktoba 27, 2000) la Jarida la Wall Street liliripoti juu ya matokeo kadhaa ya athari za uovu yaliyowafuata watalii waliookota mawe meusi ya volkano ku-toka kwa Mbuga ya Kitaifa ya Hawaii Volcanics, iliyokuwa katika kisiwa cha Hawaii. Iliripotiwa kwamba mtalii mmoja kutoka Florida aliokota mchanga mweusi wa volkano akitumia chupa ya soda na akaenda na mchanga huo nyumbani. Aliporudi nyumbani, mnyama wake kipenzi alikufa, mchumba wake akamwacha, wakala wa FBI wakamshika. Aliurudisha mchanga huo na sasa mambo yameanza kuwa mazuri. Yeye anaamini kwamba Pele—ambaye ni mungu wa kike wa volkano za Hawaii—huwaadhibu watu wanaochukua kitu chochote kinachomilikiwa naye. Zaidi ya hayo, Mhifadhi wa Mbuga hiyo huripoti kwamba kila wiki mawe kadhaa kutoka kwa Pele hu-rudishwa na watu wasiojulikana, pamoja na barua ndogo inayosema “bahati mbaya” ilipatikana tangu kuchukuliwa kwa vitu hivi.
Bob Beckett katika kitabu chake kinachoitwa “Commitment to Conquer: Redeeming Your City by Strategic Intercession”, anaeleza juu ya matukio yasiyo ya kawaida yaliyotokea wakati ambapo yeye na familia yake waliishi karibu na ardhi iliyotiwa najisi. Kuna vitabu vingine kad-haa vinavyorekodi na kueleza juu ya athari za uovu zilizotokea katika miji, majiji, na maeneo. Athari hizo huzuia kabisa juhudi za kufanya uinjilisti na zitaendelea kufanya hivyo mpaka se-hemu hizo ziombewe na laana zote kuvunjwa.
Vifaa Vinavyohusu Ardhi Iliyotiwa najisi
1. Ed Silvoso, That None Should Perish (Regal Books, 1994). ISBN 0-8307-1690-4.
2. C. Peter Wagner, Warfare Prayer (Regal Books, 1992). ISBN 0-8307-1513-4.
3. C. Peter Wagner, Breaking Strongholds in Your City (Regal Books, 1993). ISBN 0-8307-1638-6.
4. John Dawson, Taking Our Cities for God (Creation House, 1989). ISBN 0-88419-241-5.
5. C. Peter Wagner, Editor, Wrestling With Dark Angels (Regal Books, 1990). ISBN 0-8307-1446-4. (Hasa Sura ya 3—“Roho za Nchi”)
6. Bob Beckett, Commitment to Conquer: Redeeming Your City by Strategic Intercession (Chosen Books, 1997). ISBN 0800792521.
84
# 12 Vitu na Mahali pa Uponyaji www.healingofthespirit.org
Pia inatakiwa kufahamika kwamba uwezo unaotumiwa na mapepo una nguvu katika sehemu fulani kuliko zengine. Sehemu ambazo ibada ya Shetani na tambiko za kishetani zimefa-nyiwa ni baadhi ya sehemu zitakazokuwa ngumu kutakasa. Vilevile, sehemu ambazo tamaduni zake zinawakubali waganga wa kienyeji, wachawi, na vuduu zitakuwa ngumu kutakaswa. Sehe-mu ambazo zimetumiwa kwa muda mfupi kutenda dhambi (kama vile kutumia chumba cha hoteli kufanya uasherati) huwa rahisi kutakasa.
Kuiponya Ardhi
Kuiponya ardhi hutekelezwa kwa njia sawa na ile inayotumiwa kupaponya mahali (kwa kutumia hatua za 3, 4, 5 na 6 zilizo hapo juu). Hali ya kutambua dhambi za watu walioishi mahali hapo awali, ambao wakati mwingine huwa wamekufa, hujulikana kama uchoraji ramani kiroho. Wakati mwingine utambuzi huo unaweza kupatikana kutoka kwa watu wanaoijua ardhi hiyo, ku-pitia kwa magazeti ya kitambo, au kwa kupata ufunuo wa kiroho. Ardhi hiyo ikiwa kubwa sa-na—na iwapo watu wengi waliishi hapo—nguvu nyingi za maombi zitahitajika.
Kwa mfano katika ardhi isiyo na watu kule Marekani, waombezi wawili au watatu wata-hitajika. Kuuombea mji au jiji zima kutahitaji waombezi wengi na pia muda mrefu. Kuiombea sehemu fulani katika nchi fulani ambayo imeathiriwa na vuduu au uchawi kunatakiwa kufanywa tu kwa kuongozwa na Mungu na kutahitaji woambezi wengi. Kuna mifano mingi ya matokeo ya kufaulu katika vitabu vilivyotajwa hapo juu (vilevile rejelea sehemu inayoeleza juu ya “Kuli-weka Huru Kanisa Lenu” inayoeleza kinaganaga kuhusu kitendo hicho)
85
# 13 Healing from Involuntary Exposure www.healingofthespirit.org
Uponyaji Kutokana na Kuhusika kwa Giza Bila Kukusudia
Katika juhudi za kuhudumia watu kwa miaka mingi, kuna nyakati ambapo mtafutaji anatambua kuwa amehusika na giza ambalo limefungua milango ya nafsi yake pasipo yeye kujua wala kukusudia. Kuna milango mingine iliyo wazi ambayo haiwezi kuorodheshwa kwenye makundi yale mengine yaliyozungumziwa kwenye kitabu hiki. Mahojiano huwa hayawezi kutambua milango hii kwa kuwa mtafutaji haijui. Mifano ifuatayo itasaidia kueleza:
1. Ngono kati ya wapenzi ambao hawajaoana huruhusu roho mchafu kupenya kutoka kwa mpenzi mmoja hadi kwa mwenzake. Hali hii hujumuisha wale wapenzi wengine ambao kila mmoja ameenda nao katika siku zilizopita.
2. Iwapo mtafutaji alikuwa akitumia madawa ya kulevya na vileo vingine na kupoteza fahamu zake basi mapepo walimuingia kwa kutokuwa na uwezo wa kumudu hisia na mawazo yake.
3. Mtafutaji mmoja aligundua kuwa mlango ulifunguliwa alipoenda kula kwenye hoteli ya kihindi iliyokuwa na sanamu ya Buddha mlangoni. Kwa kusoma maneno yaliyoandikwa kwenye bango kando ya sanamu hiyo na kuiinamia, nafsi yake ilifunguka na kuingiwa na pepo.
4. Mwandishi wa kitabu hiki alitazama filamu ya vita vya pili vya dunia akiwa na miaka saba na kuona matukio ya kutisha. Tukio hili l;ilimtia pepo wa hofu aliyekaa ndani yake kwa miaka 35 hadi alipofukuzwa.
5. Mwanamke aliyeombewa akiwa na miaka 57 kwa ajili ya ndoto za kuogofya alitambua kuwa pepo huyu alimuingia wakati alipocheza mchezo wa bao akiwa miaka 7na kuishi na mates ohayo kwa miaka 50
6. Mama mmmoja mwafrika aliyekuwa na mkahawa huko Nairobi alitembelewa na jirani yake aliyemgusa na kumhamishia pepo mchafu.hivyo basi yapasa tujihadhari tunapoguswa na watu tusiowajua kwa kuwa ni rahisi kuhamishimiwa giza kwa tendol kama hilo.
7. Mtafutaji mmoja alikuja na roho asiyeeleweka, baadaye tukatambua alikuwa na mpenzi muislamu na baada ya kuombewa akawekwa huru. Lakini alipomrudia mpenzi wake, yule pepo mchafu alimrudishia kwa kugusana tu.
8. Binti mmoja alitamani sana vipawa vya mke wa mchungaji aliyemmiliki mumewe na washirika wa kanisa lao. Kwa tama hii alipokea roho ya Jezebeli kutoka kwa mke wa mchungaji
9. Watafutaji wengi wamepeanwa kwa Shetani na jamaa zao bila kujua
10.Wakati mwingine kuna pepo wa uchawi katika ukoo wa mtafutaji na maombi ya kawaida hayawezi kumtoa
86
# 13 Healing from Involuntary Exposure www.healingofthespirit.org
11. Watafutaji ambao wameishi katika nchi za mashariki huwa na pepo wengi wasiotambulika kwa urahisi
12. Watafutaji ambao wamekuwa waislamu huwa na pepo ambao hawatambuliki kwa urahisi na mhudumu wa wastani
13. Kundi la waombezi lilikuwa likimuombea mama mmoja lilikumbwa na tukio ambapo mmoja wao alimwambia pepo nionyeshe nguvu zako. Pepo Yule akamhama mtafutaji na kumuingia yuile aliyekuwa akiomba.
14. Kule Kanada mama mmoja alivaa mkufu aliopewa na babake na ikawa vigumu kukopmbolewa hadi alipouvua
15. Mwananamke aliyevunja uchumba na mpenzi wake aliyekuwa tayari ameoa hakuweza kuwekwa huru hadi alipopeana mkufu na picha yake
16. Kule St. Louis kulikuwa na mama aliyekuwa akitolewa kafara na kuhani wa shetani kila siku
17. Mwanamke mwingine alinunua manukato na kila apoyatumia aliugua. Katika maombi Mungu akamjulisha kuwa muuzajo=I wa manukato yale alikuwa mchawi. Manukato na mafuta mengi hutengenezwa na watu wenye nia za kuroga na hivyo kuwaletea watumizi maafa makubwa.
18. Mwanamke mwingine alipewa mavazi na mshirika kanisani lakini Bwanma akamwambia asivae mavazi hayo badala yake ayachome
19. Wengine hukodi au kununua nyumba ambazo zimetumiwa kwa matendo ya giza, kusipofanywa maombi ya utakaso giza huendelea
Mtafutaji anaweza kuhisi giza hata baada ya maombi bila kufahamu litokapo. Kundi la waombezi lapasa kuwa na mtu mmoja mwenye kipawa cha utambuzi wa roho. Majibu huja baada ya kipindi kirefu cha maombi ya kufungua kifungo hicho.
87
# 14 Healing from Poverty www.healingofthespirit.org
Uponyaji wa Roho ya Ufukara
Idadi kubwa ya ulimwengu inaishi katikia ufukara. Katika mataifa mengi, hiyo ni hali ya maisha ambayo imejikitika katika tamaduni za mataifa hayo, na hali hiyo imebaki vivyo hivyo katika vizazi vingi sana. Ufukara hujikita ndani ya mawazo na mitazamo ya watu. Jambo la kusikikitisha ni kwamba, watu hao hawaijui njia nyingine. Kuishi katika ufukara hukubalika na kutarajiwa na watu hao; nayo huwa hali ya kizazi katika tamaduni ya ufukara. Inasikitisha kwamba Wakristo wengi hawatambui kwamba kifo cha Yesu msalabani hukutuletea msamaha wa dhambi na uponyaji wa magonjwa yetu pekee, bali kilituletea uponyaji kutokana na ufukara.
Zingatia vifungu vifuatavyo vya maandiko: “Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kris-to, kwamba ingawa alikuwa tajiri, kwa ajili yenu alikubali kuwa maskini, ili kwa umaskini Wake ninyi mpate kuwa matajiri.”—2 Kor. 8:9, na, “‘‘Anastahili Mwana-Kondoo, Yeye aliyechinjwa, kupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na sifa!’’ –Ufu. 5:12*
Mojawapo ya vizuizi vya kuupokea utele wa Mungu katika maisha yetu ni ukosefu wa kufahamu na kukubali kwamba baraka za ufanisi ni mojawapo ya sababu iliyomfanya Yesu atufie msalabani. Si vigumu kwetu kuamini kwmaba Alizifia dhambi zetu. Na watu wengi hukubali kwamba alikufa kwa ajili ya uponyaji wtu (wa mwili, akili na roho). Kwa nini basi ni vigumu kwetu kuamini kwamba alikufa ili kutuweka huru kutokana na hali ya ufukara? vilevile, tambua kwamba Yesu alikufa kwa ajili ya … (1) dhambi zetu (wokovu), (2) magonjwa yetu (uponyaji wa mwili, akili na roho), na (3) fedha zetu (mahitaji yetu ya kifedha). . Yesu amelipa gharama ili tuwe “tajiri.”
Vivyo hivyo, kifo cha Yesu msalabani kilifidia “laana ya ufukara.” Tazama vile ambavyo ukweli huu umefunuliwa katika maandiko hapa chini:
• Hakuwa amekula kwa masaa 24 (Njaa)
• Alikuwa na kiu (“Nina kiu”) (Kiu)
• Hakuwa na chochote na alivuliwa vazi lake (Uchi)
• Hakuwa na mahali pa kuzikwa (Kuwa na hitaji)
Jambo la kusikitisha ni kwamba, Wakristo wengi hawatambui kwamba, sisi kama watoto wa mfalme na warithi wa ahadi zake, tuna haki ya kupata Baraka za kifedha tulizopokea kwa ajili ya msalaba.
Hatua ya kupokea uponyaji kutokana na laana ya “roho ya ufukara” ni kufahamu na kukubali kwamba vile ambavyo kuna falme mbili zinazofanya kazi ya kung’ang’ania nafsi zetu (Ufalme wa Giza na Ufalme wa Nuru), falme hizo mbili vilevile zinafanya kazi katika hali ya fedha zetu. Falme hizo zinazopingana zina ufalme wa hapa duniani wa Mamoni (au mvuto wa tamaduni—ulio na sifa za mahitaji, ukosefu, kunyimwa, njaa, kutotosheleza, woga na ufukara) kinyume na hali ya Mungu ya uchumi wa mbinguni ya Utele—mawazo na moyo wa Mungu (iliyo na sifa ya utele, maradufu, amani, utoshelezi na uaminifu).
Uchumi wa Mamoni
Mamoni (au uchumi wa ulimwengu) una misingi yake katika ukopaji, deni, haja, fahari, hamu ya ufanisi, shinikizo la kifedha, hofu, uchoyo na tamaa, ambavyo ni aina ya ibada ya sanamu.
Mungu anachukia kila aina ya ibada ya ibada ya sanamu. Ibada ya sanamu ni kitendo cha kuthamini na kuheshimu mtu au kitu fulani kuliko tunavyomthamini na kumheshimu Mungu. Tambua kwamba amri
88
# 14 Healing from Poverty www.healingofthespirit.org
tatu za kwanza (tazama Kut. 20) ni onyo zilizo wazi dhidi ya ibada ya sanamu. Efe. 5:5 inatwambia wazi kwamba, “Kwa habari ya mambo haya mjue hakika kwamba: Mwasherati, wala mtu mwovu, wala mwenye tamaa mbaya, mtu kama huyo ni mwabudu sanamu, ambaye kamwe hataurithi Ufalme wa Kristo na wa Mungu.”
Fedha ni mungu mkuu mpinzani, kwani matumnizi ya fedha kwa ajili ya uchoyo, tamaa na/au kuhodhi ni kinyume na mpango wa Mungu wa kushirikiana, kutoa na ukarimu. Uchoyo ni hamu ya utajiri wa ubadhirifu (usiofaa na wa ubinafsi) na tamaa (katika muktadha huu wa Biblia) inayorejelea kuwa na husuda wa kupita mipaka na usio na kipimo (hali ya kukosa nidhamu) kuhusu vitu tusiovyomiliki. Mungu anachukizwa sana na uchoyo na tamaa. Mamoni ni neno la Kiaramaiki lililo na maana ya utajiri. Katika tafsiri zengine za Biblia neno “Fedha” limeanza kwa herufi kubwa kwa sababu ni jina la kipekee. Mamoni ni mtu wa kiroho katika ulimwengu wa mapepo. Mamoni huleta “roho ya ufukara.” Tamaa na uchoyo ni sifa zinazobainisha mungu wa uwongo anayeitwa Mamoni.
Katika maandiko, Yesu alipomtaja Mamoni, alisema hivyo katika muktadha wa kutoweza kuwatumikia mabwana wawili. Kumtumikia bwana yeyote wa nguvu zinazozidi za binadamu (kama Mamoni) katika ulimwengu wa mapepo kunachukuiliwa kuwa ibada sugu ya sanamu. Shetani anatutaka tuwe katika utumwa na kumtumikia “roho wa ufukara.” Kumbuka kijana tajiri (katika Mat. 19:16-22) aliyemwendea Yesu akimuuliza amwambie alichohitajika kufanya ili kuurithi uzima wa milele. Yesu alipomjibu, akamwambia auze kila kitu alichokuwa nacho na awape maskini fedha hizo…Maandiko yanasema, “alienda zake kwa huzuni: kwani alikuwa na mali nyingi.” Kifungu hiki kinaonyesha ukosefu wa kijana tajiri—upendeleo wa utajiri (Mamoni) ulizidi upendeleo wa Mungu.
Zingatia sifa zifuatazo za ufukara.
• Ufukara ni mtesaji.
• Ufukara huunda mazingira ya kukata tamaa ambapo mbegu za kujitoa uhai huota.
• Ufukara humvua mwanamume au mwanamke ujasiri wake na hali ya kujithamini.
• Ufukara huzima na kudidimiza maono na ndoto.
• Ufukara husababisha mbegu za hasira na kashfa kukua.
• Ufukara ni utumwa (na kutekwa kifedha si jambo la kawaida).
• “roho wa ufukara” atakufanya kuwakashifu wanataka kukuweka huru.
• Ufukara utakufanya uwe na shaka kuhusu ukweli kumhusu Mungu, ambaye ni Asili na Mpaji wako wa kweli.
• Ufukara huzaa woga, na woga hukufanya utake kuhodhi vitu—kunakosababisha ukosefu wa vitu.
• Ufukara si hali ya kifedha pekee ya maisha yako, bali ni hali ya kiroho ya moyo na nafsi yako.
• Ufukara ni pepo wa kutolewa. “Bwana ni… mkombozi wangu …”—Zab 18:2.
• Ufukara ni adui wa kuangamizwa.
Ufukara ni laana (tazama Kumb. 28:15, na sura ya 30) na ni matokeo ya dhambi ya Adamu. Hata hivyo, kifo cha Kristo msalabani kilitimiza masharti yote ya haki ya kuifuta laana ya ufukara (kama inavyodhihirshwa katika kifungu cha Maandiko kinachosema ( “rehema hushinda haki”).
Uchumi wa Mungu wa Mbinguni wa Utele
Ingawa watu wengi hawajui, uchumi wa Mungu una mali isiyo na mwisho. Katika uchumi wa Mungu ha-kuna kuhitaji wala kukosa. Uchumi wa Mungu una sifa za utoshelezi, maradufu na hisia za amani, kuridhika na uaminifu. Kwa upendo, uchumi wa Mungu huyafanya matatizo ya uchumi wa Mamoni yatoweke. Tambua kwam-
89
# 14 Healing from Poverty www.healingofthespirit.org
ba Mungu hutekeleza sehemu yake tunapotekeleza sehemu yetu. zingagtia sifa zifuatazo za uchumi wa Mungu wa mbinguni:
1. Mungu ana mali isiyoweza kuisha—nasi kama warithi wake, tunaweza tukaipata mali hiyo. Kwa mfano:
• Kut. 16—Waisraeli walipokuwa jangwani walilishwa manna kwa miaka 40
• 1 Fal. 17:8-16—Eliya na mjane; mafuta na unga wake havikuisha, “mpaka”…
• 2 Fal. 4:1-7—Ushauri wa Eliya kwa mjane; mtungi mmoja wa mafuta uliijaza mitungi mingi—mafuta hayo yaliuzwa na mjane huyo akayalipa madeni yake yote.
• 1 Nyak. 29:3-28—Ingawa Daudi alizaliwa katika familia ya kimaskini, alitoa mali nyingi ya kulijenga hekalu, kwani alitambua na kukubali kwamba “vitu vyote vinatoka kwa Mungu” (kif. 14)
• Mat. 14:15-21—Yesu aliwalisha wanaume 5000 kwa mikate 5 na samaki 2
• Mat. 15:32-38—Yesu aliwalisha wanaume 4000 kwa mikate 7 na “samaki wadogo wachache,” kulikuwa na mabaki yaliyojaza vikapu 7
• Mat. 17:24-27—Petero na sarafu iliyokuwa ndani ya samaki
• Luka 5:1-11—Simioni Petero alishusha nyavu zake upande mwijngine na nyavu hizo zikaanza kuvunjika kwa sababu ya utele wa uzito wa samaki waliokuwa wamevuliwa
2. Mungu hujumlisha badala ya kuongeza—Katika uchumi wa Mamoni, faida ya 5-10% huonekana kuwa nzuri. Linganisha faida hiyo na faida nyingi ambayo Mungu anatuahidi:
• Mwa. 26:12—Isaka alibarikiwa mara 100
• Mwa. 30:27-30—Labani alikubali kwamba kuongezekakwa mifugo wake kulitokana na kibali alichopata Yakobo kutoka kwa Mungu
• Mat. 13:12 na Marko 4:8—ongezeko la mara 30, 60, au 100; “Kwa maana yule aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele….”
• Maandiko mengine yanayoahidi ongezeko maradufu ni: Mat. 19:29 na Marko 10:28-30.
Sehemu yetu ya kushiriki katika uchumi wa Mungu wa mbinguni ni KWANZA, kufanya uamuzi, ahadi ya kuufuata mpango wa Mungu badala ya mpango wa mwanadamu—yaani, kuandama uhuru na baraka za kifedha badala ya ujinga wa kifedha, kama tunavyoshauriwa katika Kumb. 11:26, “Tazama, leo ninaweka mbele yenu baraka na laana….” Pia, “…nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana. Basi sasa chagueni uzima, ili wewe na watoto wako mpate kuishi”—Kumb. 30:19 na kif. 15 (pia Yos. 24:15). Na kama Math. 6:24 inavyoonya, ‘‘Hakuna mtu ye yote awezaye kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa ama atamchukia huyu na kumpenda yule mwingine, au atashikamana sana na huyu na kumdharau huyu mwingine.”—ni lazima tuchague. Hatuwezi kutenda mambo wakati mmoja katika uchumi wa Mamoni na vilevile katika uchumi wa Mungu wa utele. PILI, ni lazima tuyatimize masharti aliyotaja katika Maandiko yake ya kuzipokea baraka alizotuahidi.
I. Kile Ambacho Maandiko Yanasema Kuhusu Fedha
1. Maandiko yanasema mambo mengi kuhusu fedha, mali na utumishi kuliko mada nyengine. Zingatia yafuatayo:
• Mifano 16 kati ya 38 aliyotoa Yesu ilikuwa juu ya fedha au mali.
• Yesu alinena mambo mengi kuhusu fedha kuliko alivyonena kuhusu mbinguni na jehanamu (zote pamoja).
• 10% ya vitabu vya Injili, vifungu 288 vinazungumza juu ya fedha na mali.
90
# 14 Healing from Poverty www.healingofthespirit.org
• Katika vifungu vya Biblia kuna
—vifungu 500 juu ya maombi
—chini ya 500 kuhusu imani
—zaidi ya 2300 kuhusu fedha, mali na utumishi
Kuna aina nne za maelezo kwa nini fedha na mali vinatajwa mara kwa mara katika mafundisho ya Yesu.
a) Vile tunavyotumia fedha zetu huathiri mahusiano na ushirika wetu na Mungu. Katika mfano wa Yesu katika Luka 16:11, anatuambiwa: “Ikiwa hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewaaminia mali ya kweli?” Aya hii inazungumzia ukweli kwamba hatutaweza kumtumikia Mungu kikamilifu mpaka pale tutakapokuwa waaminifu katika matumizi ya fedha zetu.
b) Mali hupingana na Bwana – kazi na mapenzi yake – maishani mwetu. Mungu anataka mapenzi yake yapate kipaumbele maishani mwetu, hataki tuwe na miungu wengine wanaotutawala wala kung’ang’ania muda na ibada yetu kwake.
c) Awamu kubwa ya maisha yetu inazingirwa na matumizi ya fedha; Mungu kwa hekima yake ametuandaa vilivyo kwa kutupatia mwongozo unaofaa katika maandiko.
d) Fedha na mali ndiyo maeneo ya mwisho ya maisha yetu tunayomuachia Mungu (kama ilivyoelezewa katika mfano wa tajiri—Math. 19:16-22, na mwisho wa uhai wetu).
2. Maandiko Yanaahidi Ufanisi kwa Watiifu. Ijapokuwa baraka na laana zinatofautiana, kuna mfanano kwa kuwa maneno yote mawili yamezungumziwa na kuandikwa kwenye Bibilia kama yaliyo na uwezo wa kiroho na mamlaka ya kuleta mema (Baraka) na uovu (uovu). Neno baraka limetajwa mara 221 ilihali laana limetajwa mara 230. Baadhi ya mifano ya Baraka zi-lizo ahidiwa ni:
Baraka zimetajwa kwenye Kumbu. 28:1-14 (na laana zinafuatia aya. 15-68)
• Tutapandishwa “mahali palipo juu ya mataifa yote nchini.”
• Tutapata baraka “mjini” na “kondeni;” “tuingiapo” na “tutokapo.”
• Tunda la mwili wako litabarikiwa.
• Mazao ya nchi yetu yatabarikiwa.
• Malimbuko ya mifugo yenu yataongezeka.
• “Kikapu” kitabarikwa (chombo kikubwa cha kuhifadhi mazao ya shamba) na “ghala” (chombo cha kukandia, hutumiwa kwa kuhifadhi na kuandaa chakula hasa mkate).
• Maghala yenu yatabarikiwa.
• Kila utakachokigusa kitabarikiwa.
• Adui zetu watashindwa na kutoweka usoni petu.
• Bwana atatuzidishia mali.
• Bwana atatufungulia hazina yake nzuri (mvua ya msimun.k. )
• Tutakopesha mataifa mengi bila kukopa, Bwana atatufanya vichwa wala sio mkia, tu-takuwa juu na sio chini ya mataifa haya.
91
# 14 Healing from Poverty www.healingofthespirit.org
Baraka zilizotajwa kwenye Kumbu. 8:5-18—Tumeahidiwa
• Kula mkate pasipo upungufu wala kukosa
• Kujenga nyumba nzuri
• Kuwa na mifugo mingi
• Kujumlisha fedha na dhahabu
• Kuzidisha kila tulicho nacho
Baraka zilizotajwa kwenye Mal. 3:8-12 (tuleta zaka ghalani)
• Mungu atatufungulia madirisha ya mbinguni
• Bwana atatumiminia Baraka kiasi cha kukosekana chumba cha kuzihifadhi
• Mungu atamkemea aharibuye kwa niaba yetu
• Mharibifu hatoharibu mavuno ya nchi yetu
• Mizabibu yetu haitozaa kabla ya msimu wake
• Mataifa yote yatatuita wabarikiwa
Maandiko Mengine yenye Ahadi ya Utele
• Jos. 1:8 “Usiache Kitabu hiki cha Torati kiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapoifanikisha njia yako na kisha utasitawi sana.”
• Zab. 34:10 “Wana simba wenye nguvu hutindikiwa na kuona njaa, bali wale wamtafutao BWANA hawatakosa kitu cho chote kilicho chema..”
• Zab. 84:11 “Kwa kuwa BWANA ni jua na ngao, BWANA hutoa wema na heshima, hakuna kitu chema anachowanyima wale ambao hawana hatia..”
• Isa. 1:19 “Kama mkikubali na kutii, mtakula mema ya nchi”
• 2 Kor. 8:9 “Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba ingawa alikuwa tajiri, kwa ajili yenu alikubali kuwa maskini, ili kwa umaskini Wake ninyi mpate kuwa matajiri.”
• Filip. 4:19 “Naye Mungu wangu atawajaza ninyi kila mnachohitaji kwa kadiri ya utajiri Wake katika utukufu ndani ya Kristo Yesu.”
• 3 Yoh 2 “Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako kama vile roho yako ifanikiwavyo.”
Kutokana na maandiko haya tunatambua kuwa mpango na nia ya Mungu kwa watu wake ni kuwa na utele. Hakuna uungu wowote kwa mtu kuwa masikini. Ufukara ni laana ambayo lazima ivunjwe, ni roho/kifungo ambacho mtu apasa kuwekwa huru. Ukarimu hushinda ufukara. Si ajabu ku-na wengine ambao wanashangaa kama Bibilia ya Kiafrika inasoma sawa na ile ya Wazungu kwa swala hili. Utapata kwamba mzungu anasoma Bibilia na kuelewa na kuishia kufaidika na ahadi za utele kuli-ko Mwafrika. Lakini ifahamike kuwa Bibilia zote ni sawa.
Ahadi za Mungu ni zile zile iwe ni kwa mwafrika au mzungu na Mungu hasemi uongo. Habari njema ni kuwa Mungu anataka kukuweka huru kutokana na roho wa ufukara na kukuleta katika utele. Mungu ana mpango wa kuzitumia fedha zako na maagizo ya mpango huu yapo ndani ya maandiko. Somo hili linanuia kusaidia kuelewa na kutimiza mpango huo. Ili upate faida ya mpango huu, lazima
92
# 14 Healing from Poverty www.healingofthespirit.org
umaanishe kusoma kila andiko lililoorodheshwa. Hata hivyo ifahamike kuwa mabadi-liko hayatapatikana usiku kucha, lakini pia hayakawia.
Hebu basi tuanze na mafundisho ya kimsingi kuhusu vile ambavyo Mungu anataka tufikirie na kutumia fedha.
II. Mafundisho ya Kimsingi Kuhusu Matumizi ya Fedha
Mpango wa Mungu wa matumizi ya fedha zetu unajikita kwenye misingi saba . Misingi hii ina kiini chake katika maandiko ambayo yanafaa kueleweka, kukubaliwa na kutumika ili ahadi za Mungu zitekelezwe.
1. Mungu Aliumba Vyote—Hapo mwanzo kabla ya kuumbwa kwa chochote: Mungu aliumba vyote (Mwa. 1). Wewe name tulizaliwa bila chochote na tutaiwacha dunia hii bila chochote. Yapasa tutambue kuwa Mungu ndiye mpaji wa vyote tulivyo navyo. Kila tulicho nacho ni chake, sio chetu, sisi ni watumizi, walinzi sio wamilki.
2. Vyote ni mali ya Mungu—vyote vilivyoumbwa na Mungu ni mali ya Mungu . ijapokuwa twaweza kuvichukulia vyote tulivyo navyo kama mali yetu, dhana hii si sawa na ndilo shina la matatizo tunayokumbana nayo tunapomiliki fedha kwa njia ya Kiungu. Maandiko yanatuonyesha kuwa Mungu ni mwenye:
• Nchi Zab. 24:1
• Dhahabu yote na fedha Hag. 2:8
• Vyote vilivyomo mbinguni na duniani 1 Nyakati. 29:11
• Nchi Law. 25:23
• Ng’ombe katika milima elfu Zab. 50:10
• Maandiko mengine yanothibitisha Mungu anamiliki vyote:
Kutok. 9:29 Kumbu. 8:18 Kumb. 10:14 1 Nyakati. 29:12 Zab. 24:1 1 Kor. 10:26
3. Sisi ni Walinzi/Watunzaji – kwa kuwa Mungu ameumba na anamiliki vyote, yapasa ifahamike kuwa sisi sio wenye mali bali ni watunzaji wa mali ya Mungu. Sisi ni walinzi/wasimamizi tu. Wasimamizi hawana haki miliki ila majukumu ya kutunza pekee kwa niaba ya mwenyewe. Ili kufaulu katika kutimiza mpango wa Mungu inapasa mawazo yetu yaende sambamba na jukumu la utunzaji tulilopewa. Hebu yatalii mawazo yafuatayo ili uelewe vizuri jukumu hili:
• Mfano wa wapangaji(mzabibu; Math 21:33-46 na Mark 12:1-12)
• Utamaduni wa wayahudi ulimheshimu Mungu kama mwenye mali, hali ya kumiliki kwa mtu binafsi kulitokana na Warumi.
• 1 Kor. 4:2, “Zaidi ya hayo, litakiwalo ni mawakili waonekane kuwa waaminifu.”
4. Mungu humpa kila mmoja kulingana na mpango wake – licha ya kuwa mwenyewe Mungu anamiliki kila tukio duniani. Yeye ni Mungu wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo sisi tukiwemo. Kulingana na maandiko yeye huinua mataifa na wafalme na
93
# 14 Healing from Poverty www.healingofthespirit.org
kuwaangusha kwa mapenzi yake. Yeye anatupatia rasilmali kulingana na mpango wake kwa kila mmoja wetu. Tazama maandiko yafuatayo:
• Isa 40:15-26—Mungu anamiliki mataifa
• Mat. 25:14-30—mfano wa talanta
• 1 Nya. 29:12—“utajiri na heshima vinatoka kwako unayevitawala vyote”
• Kumb. 8:18—ni Mungu akupaye uwezo wa kupata utajiri…
• Dan. 2:21,44—Mungu huinua na Kuwaangusha wafalme
Ni vyema kujifunza kutosheka na vile alivyotupatia Mungu kama alivyokiri Paulo—“Sisemi hivyo kwa vile nina mahitaji, la! Kwa maana nimejifunza kuridhika katika hali yo yote.”—Filip. 4:11). Neno kutosheka limetajwa mara saba katika Bibilia na katika sita ya hizo inahusiana na fedha. Ukiongezea laana zilizotajwa katika Kumbu. 28:47-48, tunatambua umuhimu wa kuwa na mtazamo wa “kutoa kwa furaha”: “Kwa sababu hukumtumikia BWANA Mungu wako kwa furaha na kwa moyo wakati wa kufanikiwa kwako, kwa hiyo katika njaa na kiu, katika uchi na umaskini wa kutisha, utawatumikia adui ambao BWANA atawatuma dhidi yako. Yeye ataweka nira ya chuma shingoni mwako hadi amekwisha kukuangamiza.”
5. Maandiko yanazungumzia Viwango Vitatu Vya Utoaji—Licha ya hayo Mungu humpa kila mmoja kukingana na mpango wake kwa viwango vitatu viliyotajwa kwenye Biblia. Mpango wake ni kututosheleza au kutupa tele. Je hivi sasa uko kwenye kiwango kipi?
• Katika Ufukara—mhitaji, uchi, njaa na kiu
• Kutosheka—Una kiasi bila ya ziada
• Utele/Wingi—unajitosheleza na kubaki na ziada (sio tajiri)
Tumetaja hapo awali kuwa Yesu alifidia “laana ya ufukara” pale msalabani. Ahadi za Mun-gu za utele hazitakuhamisha kutoka kwenye ufukara hadi utajiri mara moja. Itachukua muda na ju-hudi kuhifadhi maneno ya Mungu moyoni mwako. Hata hivyo Yer 31:33 – inatuambia kuwa atayaandika maneno haya mioyoni mwetu: “Nitaweka sheria yangu ndani yao na kuiandika katika mioyo yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.” Au kama ilivyoandikwa kwenye Ebr. 10:16, “…Nitaziweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika katika nia zao.” ….” (Tazama pia Jos. 1:8, “Usiache Kitabu hiki cha Torati kiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapoifanikisha njia yako na kisha utasitawi sana.”)
Inachukua muda na juhudi kuwa msimamizi mwema juu ya kile alichokipeana Mungu. Ikumbukwe kuwa Mungu sio benki ya mbinguni tunamotoa fedha kila tunapozihitaji. Kwa kawaida Mungu hutupitisha katika kipindi cha kujaribiwa – kwanza hutupa milki ya mambo madogo ili kuona vile tunavyoyasimamia ndiposa atuinue na kutuongezea majukumu.
6. Mungu anataka uwe na fedha kwa sababu—
• Kukimu mahitaji ya jamii yako (1 Tim. 5:8)
• Kutekeleza majukumu yako
94
# 14 Healing from Poverty www.healingofthespirit.org
• Kuwatuma wahuma kote ulimwenguni kuhubiri habari njema (Warum10:15)
• Kulipa ushuru na kumtolea Mungu (Math. 22:21)
• Kulipa zaka na sadaka kwa ajili ya kazi ya Mungu (Lawi. 27:30)
• Kuwaruzuku watoto wako na wale uwapendao (Math. 7:11)
• Kuwafaa wengine waliopungukukiwa
• Kuwasaidia masikini (Mith. 11:24-26, 19:17 and 28:27)
• Kuweza kusuluhisha haja za dharura (Mhu. 10:19b)
• Kuota ndoto kubwa kwa jamii yako na wengine zinazohitajiuwepo wa Mungu
7. Mungu hubariki Watiifu—Mojawapo ya kanuni muhimu za Baraka zilizo ndani ya Bibilia ni ahadi zenye masharti. Wasomi wa Bibilia wameorodhesha ahadi 635 kwa kila mtu binafsi. Ahadi hizi zote zina masharti, yaani Mungu anaahidi kufanya kitu (Baraka) iwapo sisi tutafanya kitu(kutii) .
Kwa mfano ahadi ya wokovu inaelezwa hivi, ijapokuwa Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya wote, ili mtu aokoke itambidi: “Kwa sababu kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba ‘‘Yesu ni Bwana.’’ na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka”—Warum 10:9. Hivyo wote hawawezi kuokoka mpaka kwanza watimize sehemu yao kama ilivyoelezewa kwa aya hiyo.
Mfano mwingine ni ule wa –kuzaliwa mara ya pili. Kuna sharti ambalo linatangulia ahadi hiyo- ‘‘Amin, amin nakuambia, hakuna mtu ye yote anayeweza kuingia katika Ufalme wa Mungu isipokuwa amezaliwa kwa maji na kwa Roho”—Yoh 3:5. Hivyo basi wote hawazaliwi mara ya pili bila ya kuzaliwa kwa maji na Roho.
Kanuni inaambatana na Baraka pamoja na ahadi za utele. Hatuwezi kuwa na matarajio ya kupokea ahadi na Baraka za mungu bila ya kutimiza masharti ambayo Mungu ameweka katika neno lake. Iwapo hatutii badala ya ahadi tunaangukia laana.
Katika Bibilia kuna makundi 37 ya dhambi za uasi zinazosababisha laana. Ili mtu aepukane na laana hizi inampasa atubu na kutii. “kama hutamtii BWANA Mungu wako na kuzishika kwa bidii amri zake zote na maagizo ninayokupa leo, laana hizi zote zitakuja juu yako na kukupata:”—Kumbu. 28:15 (Tazama pia 8:10-20; 27:15-26 and 28:15-68).
Kwa kuwa Baraka zilizotajwa kwenye maandiko haya ni za masharti, hufikiliwa tu na wale wanaotii. Hakuna ahadi kwa waasi, badala yake ni laana zilizoahidiwa. Ukitaka kitu kutoka kwa Mungu - fanya vile Mungu asemavyo.
III. Masharti ya Kupokea Baraka na Ahadi za Utele
Hebu tutazame masharti yaliyo kwenye maandiko ya kupokea Baraka na ahadi za
95
# 14 Healing from Poverty www.healingofthespirit.org
utele:
1. Kulipa Zaka na Kutoa Sadaka—kulipa zaka ni jambo la lazima kama inavyoamrishwa katika Kumbu 4:22. Yapasa tuelewe kuwa zaka ni takatifu na ni ya Bwana (Law. 27:30). Zaka ni kodi yetu ya mbinguni kwa maskani na mali ya Mungu tunayomiliki. Ni deni tulilo nalo kwa Mungu.
Kila utoapo zaka Mungu atakubariki na kufungua madirisha ya mbinguni kwako. Usipolipa zaka fedha zako zitalaaniwa na mharibifu ataharibu mazao yako. Mal. 3:10 ndicho kifungu cha pekee ambacho kinatupa changamoto ya kumjaribu Mungu. Hebu tafakari yafuatayo juu ya zaka:
• “Kutoa zaka na sadaka ndio ushahidi wa pekee wa upendo wetu( kama inavyodhi-hirishwa na Yoh 3:16)
• Tendo la kulipa zakani ishara ya kuwa hatuna choyo.
• Tusipolipa zaka , tunamuibia Mungu kile ambacho ni chake (Mal. 3). Kulipa zaka na sadaka ilikuwa ishara kuwa Israeli inatambua uongozi wa Mungu kwamba wao na kila walicho nacho ni mali yake. Ktolipa zaka ni kukaa utawala wa Mungu na kuasi kama alivyofanya shetani tangu awali.
• Kulipa zaka huvunja laana ya kifedha iliyo juu ya maisha na jamii yetu (Mal. 3).
• Tendo la kulipa zaka ni kuthibitisha imani yetu kwa Mungu.
Hebu tutalii vile Agano la Kale linasema kuhusu zaka:
Zaka katika Agano la Kale
Ijapokuwa tunajua zaka ni 10%, kulikuweko na aina tatu za zaka ambazo Mungu aliamrisha na sherehe zake zilidumu kwa siku 7 ambapo sadaka nyingine zilitolewa kama ilivyoorodheshwa hapa chini:
• Zaka ya Kwanza (Mwa. 14:17-24)—Abrahamu alitoa zaka kwa Melchizedeki; hakuchukua malimbuko. Maandiko kadhaa yanaerleza kuwa wana Waisraeli waliamriwa kutoa sehemu moja kwa kumi ya kila maongeo (Law. 27:30 na 32; Kumbu. 14:22)
• Zaka ya Walawi (Hes. 18:21-24)—zaka hii ilikuwa kwa ajili ya kuwakimu walawi ambao pia ilwapasa kutoa sehemu moja ya kumi kwa makuhani
• Zaka ya Utunzaji (Kumb. 26:12-13)—ililipwa kila baada ya miaka mitatu ilikuwakimu masikini
• Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu (Kuto. 12:17)—ilikuwa kumbukumbu la Pasaka
• Sikukuu ya Mavuno (Kuto. 23:16 na Kumbu. 16:10)—matunda ya kwanza/malimbuko yalitolewa kumshukuru Mungu aliyepeana mavuno
• Sikukuu ya Tarumpeta ya Kuandama kwa Mwezi (Zab. 81:3)—kuikumbuka sauti ya Mungu mkuu
• Sikukuu ya Upatanisho (Law. 23:27-28 na Hes. 29:12)—kusherekea ondoleo la dhambi
• Sikukuu ya Mahema (Law. 23:34 na Kumb. 16:13-14)—sherehe iliyofanywa mwisho wa mwaka baada ya kukusanya mavuno
96
# 14 Healing from Poverty www.healingofthespirit.org
Wasomi wa Bibilia wanakadiria kuwa zaka na sadaka hizi zote zingefika 23.3% kwa mwaka. Matoleo haya yalikuwa kama kodi ambayo ilikuwa lazima ilipwe.
Hebu tutazame masharti yaliyomo katika Mal. 3:8-11: “Je, mwanadamu atamwibia Mungu? Hata hivyo mnaniibia. ‘‘Lakini mnauliza, ‘Tunakuibia kwa namna gani?’ ‘‘Mnanii-bia zaka na dhabihu. Mko chini ya laana, ninyi taifa lote, kwa sababu mnaniibia mimi. Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu. Nijaribuni katika hili,’’ asema BWANA Mwenye Nguvu, ‘‘nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na ku-wamwagieni baraka nyingi mpaka mkose nafasi ya kutosha au la. Nami kwa ajili yenu nitam-kemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu, wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake,’’ asema BWANA Mwenye Nguvu..”
Ijapokuwa Mungu anazungumza na taifa la Israeli, tunajua kuwa Maandiko yote ni kwa faida ya mwanadamu (kama ilivyoandikwa kwenye 2 Tim. 3:16, “Kila andiko, lililovuviwa na Mungu lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na kuwafundisha katika haki”). Hivyo basi katika aya hizi (Mal. 3:8-11), Mungu ananena nasi pia na kutupatia kanuni za kuwa mwangalizi au msimamizi. Hii ni kusema kama mtu hakulipa zaka wala kutoa sadaka, yeye ni mwizi na yuko chini ya laana (yaani atamwachilia mharibifu mlangoni kwako). Laana hii inaambatana na kuasi na haijalishi ni maombi kiasi gani mtu ataomba hawezi kuwekwa huru isipokuwa kurudia maisha ya utiifu (kulipa zaka na kutoa sadaka kwa uaminifu. Baada ya Mungu kutangaza kuwa tumemuibia, anatuambia katika aya ya 10 namna ya kurekebisha kosa hili: “Leteni zaka kamili ghalani,…” (Kumbuka ni kwenye Mal 3:10 pekee ambapo Mungu anasema: “Nijaribuni”
Hebu tazama ni Baraka kiasi gani anazoahidi kwa wale waaminifu katika Mal. 3:10-11: “. . . nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka nyingi mpaka mkose nafasi ya kutosha au la. 11Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu, wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake,’’” Ahadi iliyoje! La kusikitisha ni kuwa wakristo wengi wachungaji wakiwemo hawalipi zaka au hata wakilipi hawafanyi hivyo kwa uaminifu. Hii ndiyo sababu halisi ya watu kuendeleakuishi katika ufukara. Hali hii itaendelea hadi wamrudie Mungu kwa uaminifu. Ukitaka ithibati ya Baraka hizi, tazama 2 Nyakati 31:7-12. Katika tajriba yangu sijawahi kumpata mtu ambayeamekuwa muaminifu kwa kulipa zaka ambaye amejuta wala kukosa kulipa.Mungu atakubariki kuzidi kiwango cha zaka utakazotoa.
Kwa kusisitiza, ieleweke kuwa zaka ni sehemu ya Mungu na kodi ya nafasi unamokaa duniani na yale ambayo Mungu amekupa. Ijapokuwa kutoa sadaka ni hiari ya mtu, zaka ni lazima, ni deni ambalo kila mmoja wetu lazima alipe. Mungu anataka nyongeza (Kumbuka Mfano wa Talanta). Usipolipa zaka utalaaniwa, ukiitumia kwa kusudi jingine unamuudhi Mungu.
2. Toa sadaka ya “mazao ya kwanza” (yaani tunda au mavuno ya kwanza ya nafaka kila
97
# 14 Healing from Poverty www.healingofthespirit.org
mwaka- hutolewa kwa Mungu kama shukrani.)
Mith.3:9-10 yatuhimiza, “Mheshimu BWANA kwa mali zako na kwa malimbuko ya mazao yako yote, ndipo ghala zako zitakapojaa hadi kufurika, viriba vyako vitafurika kwa mvinyo mpya.” Mungu anahitaji tulipe zaka na kutoa sadaka kwanza kabla ya kuingia kwenye matumizi mengine ya fedha au mavuno. Tukingojea hadi mwisho wa mwezi kulipa zaka na kutoa sadaka, ni nadra kupata ma-salio ya fedha za kulipa zaka kamili, hali inayotulazimu kumpa Mungu masalio. Tutoapo pindi tunapo-lipwa huwa tunamheshimu Mungu kwanza hivyo basi kuishia kupokea Baraka za kujitosheleza.
Maandiko kuhusu Mazao ya Kwanza Maandiko Kuhusu Baraka za Utiifu
Kut. 22:29 na 23:19 2 Nyak. 31:5-8 (kutia moyo viongozi)
Law. 23:10-11 Neh. 13:31 (Bwana atakukumbuka)
Hes. 18:12 Pro. 3:9-10 (maghala yatajazwa pomoni)
Kumb. 18:4 na 26:2 Ez. 20:40-41 and 44:30 (ili “Baraka ya amani ikae nyumbani mwako”)
Neh. 10:35-37 na 12:44
3. Wape Masikini—tafakari maandiko yafuatayoambayo yanatuhimiza kuwashughulikia masikini. Masikini na wajane wana mahali maalum katika mpango wa Mungu. Mungu hubariki wote wanaowakimu masikini na wajane
• Kumbu. 15:7-11 Amri kutoa kwa masikini na wahjitaji.
• Zab. 41:1-3 Kuna Baraka tunapowakumbuka masikini.
• Mith. 19:17 “Yeye amhurumiaye maskini humkopesha BWANA,naye q atamtuza kwa aliyotenda.”
• Mith. 21:13 “Kama mtu akizibia masikio kilio cha maskini, yeye pia atalia wala ha-tajibiwa.”
• Mith 22:22-23 “Usiwadhulumu maskini kwa hila kwa sababu ni maskini, wala kumd-hulumu mhitaji mahakamani, kwa sababu BWANA atalichukua shauri lao naye atawateka wao waliowateka”
• Mith. 28:27 “Yeye ampaye maskini hatapungukiwa na kitu cho chote, bali yeye awafumbiaye maskini macho hupata laana nyingi.”
• Mith. 29:7 “Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini, bali mwovu hajishug-hulishi na hilo.”
• Eze. 16:49 Mojawapo ya sababu za kuangamizwa kwa Sodomu ilikuwa kutowajali masikini.
4. TOA—Tutavuna tulichopanda—Mbali na kuwasaidia masikini, wajane na mayatima, Mungu hutupatia nafasi za kutoa – ili tuvune kwa wingi.
• Luka 6:38—“ Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa;… hata kumwagika ….”
• Mith. 11:25—“ yeye awaburudishaye wengine ataburudishwa mwenyewe”
• 2 Kor. 9:6—“… Ye yote apandaye kwa uchache pia atavuna kwa uchache, naye apandaye kwa ukarimu pia atavuna kwa ukarimu.”
• 2 Kor. 9:10— “atawapa na kuzidisha mbegu zenu za kupanda.”
Kanuni za Mungu za utele zinategemea kupanda kwa imani na kuvuna Baraka za kifedha. Kuna kanuni nyingine iitwayo “mbegu ya imani.” Nafasi hairuhusu kuwa na mjadala huu kwa
98
# 14 Healing from Poverty www.healingofthespirit.org
ukamilifu lakini kanuni hizi zitasaidia.
• Mungu aliamuru kila alichokiumba kuzaana na kuongezeka (Mwa. 1:11, 20 na 22).
• Kilicho ndani yako kinaihtaji nyongeza
• Kila mbegu ina masharti ya kuongezeka na kuzaa aina yake
• Kadri upandapo mbegu iliyo mkononi mwako ndivyo Mungu huachia kilicho mkononi mwake
• Mbegu ndogo yaweza kuleta mavuno makuu
• Unapozuia kilicho mkononi mwako Mungu naye huzuia kilicho mkononi mwake
• Unapoongeza idadi ya mbegu zako ndivyo Mungu anakuza mazao yako (2 Kor 9:6)
• Mbegu isipopandwa haiwezi kuleta mavuno
• Kila ulicho nacho ni mbegu, ukiizuia basi unazuia mavuno
• Hakuna mwingine awezaye kukupandia mbegu yako
• Unapoipatia mbegu yako masharti fulani, imani hukuzwa (1 Falme 17:13-16)
• Tambua mbegu (kipawa, talanta, fedha, upendo) uliyopokea kutoka kwa Mungu na umshukuru (kutii amri ya shukrani)
• Shukrani ni nguvu, kanuni ya maisha, pasipo shukrani hakuna mavuno
• Wakati ni sarafu ardhini na unaweza kutoa kile ambacho fedha haziwezi kununua
• Kuna kipindi cha kupanda, kikipita hakuna mavuno
• Panda mbegu uliyopewa usilalamikie ile usiyo nayo
• Upandapo weka imani yako kwenye mbegu yako, mbegu yako ndiyo itakojumlishwa, lakini imani yako ndiyo sababu ya kujumlishwa huko
• Mungu hatambui mahitaji bali hutambua imani
• Mbegu ya imani ni kupanda uliyo nayo ili upate uliyoahidiwa
• “ … Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa”—Luka 6:38.
• Kuomba ni ufunguo wa kupokea (Math. 7:7-8 na Yak. 4:2-3).
• Imani huhitaji kuelekezwa – kitu kamili (matokeo).
• Unapotoa ahadi ya mbegu ya imani unaingia kwenye agano kati yako na Mungu. Usigeuke na kuvunja ahadi uliyomwekea Mungu
• Dharura huzaa miujiza lakini hofu huwa pingamizi
• Subira ni msimu uliosahaulika kati ya kupanda na kuvuna
• Baraka kuu huja baada kipindi kirefu cha subira
• Unapoichimbua mbegu yako kuona kama imezaa, kwa pupa zako hutaweza kupata mavuno
• Utavuna kulingana na kiasi cha mbegu ulizopanda.
• Okoa zaka yako kutoka kwa shetani, usipompa Mungu itachukuliwa na shetani.
• Mkristo asipowekwa katika eneo la fedha hawezi kupokea mpango kamilifu wa Mungu.
• Kukiri kwako ndiko mavuno yako, utavuna unachokiri (Yak. 3:3-6).
99
# 14 Healing from Poverty www.healingofthespirit.org
Kwa mengi kuhusu “mbegu ya imani,” tazama 31 Reasons People Do Not Receive Their Financial Harvest, The Covenant of 58 Blessings, au 7 Keys to 1000 Times More (Mike Murdock, P.O. Box 99, Denton, TX 76202; 1-888-947-3661; www.thewisdomcenter.tv), or Seed-Faith 2000 by Oral Roberts (at Amazon.com).
5. Kama msimamizi, kuwa mkurugenzi mwema wa mali ya Mungu—(“ Zaidi ya hayo, litakiwalo ni mawakili waonekane kuwa waaminifu”—1 Kor. 4:2.)
Kumiliki kitu sio sawa na kuwa mwenyewe. Ikiwa twaamini kuwa Mungu ndiye mwenye vyote, basi yapasa tuchukue jukumu letu kama watunzaji na wakurugenzi. Pitia mfano wa shamba la mizabibu (Marko 12:1-9 na Luka 20:9-16). Tukimtambua Mungu kama mwenye vyote tulivyo navyo basi hata maamuzi ya namna ya kutumia vile alivyotupatia itabidi tumhusishe kama ifuatavyo::
a) Ishi na Kanuni ya 10-10-80 . Kutoka kwenye mapato wasimamizi wema hulipa zaka 10% kama malimbuko,kuweka akiba 10% na kutumia 80% inayobaki.
b) Ratibu mapato na matumizi yote.
c) Usikope na ufanye juhudi ya kulipa madeni yote uliyo nayo. Uchumi wa Mammoni umejikita katika kukopa na kukopesha. Ijapokuwa maandiko hayasemi kukopa ni dhambi, tunashauriwa katika sehemu kadha tuepukane na kukopa (tazama katika Mith. 11:15, 17:18 na 22:26-27). Kukopa kunakubaliwa ikiwa kile unachotaka kukinunua kitaongeza thamani yake kama vile shamba au nyumba. Lakini tuseme kuwa kila tunapokopa sisi huwa mateka na kupoteza uhuru wa kutumia rasilmali zetu vile ambavyo Mungu angependa tufanye. Kukopa kwaweza kuchelewesha mpango wa Mungu kwa maisha yako na hata kutatiza kukua kwako kiroho. Tazama maandiko yafuatayo:
• Kumbu. 15:6 and 28:12 “… hutakopa….”
• Mith. 22:7 “Tajiri humtawala masikini na mkopaji mtumwa wa Yule amkopeshaye.”
• Warumi 13:8 “Usiwe mdeni wa awaye yote….”
d) Gharimika kwa mahitaji wala sio kila utakalo. Uchumi waMammoni husukumwa na tamaa ya kujipatia kila utakalo (sio mahitaji) Kuishi katika uchumi wa Mungu kwahitaji kuangalia kila haja na kutambua tofauti ya hitaji badala ya utakalo (kama ilivyo katika 1Tim. 6:8). Tutilie mkazo nidhamu ya kukuza utele kwa utukufu wa Mungu.
e) Muulize Mungu kabla ya Kuanza biashara . iwapo huna fedha za kutekeleza kile unachonuia, pengine Mungu anakwambia usubiri. Ukiwaza kuwa Mungu ananena nawewe kuhusu kuwekeza kwenye biashara fulani tafuta ushauri wa kufaa kabla kuanza. Tafuta ushuhuda wa watu wawili kabla ya kuendelea na mpango wako. Hakikisha ni Mungu anayenena nawewe wala sio mawazo yako mwenyewe.
6. Uaminifu kwa Mambo Madogo—Luka 16:10-12 yatuambia: “Ye yote aliye mwaminifu katika mambo madogo, pia ni mwaminifu hata katika mambo makubwa, naye mtu ambaye si mwaminifu katika mambo madogo pia si mwaminifu katika mambo makubwa. Ikiwa hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewaaminia mali ya kweli? Nanyi kama hamkuwa waaminifu na mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?”
100
# 14 Healing from Poverty www.healingofthespirit.org
Mojawapo ya sababu ya wewe kutokuwa na utele ni kwa kuwa Mungu haja-fikia kiwango cha kukuamini na utele wa mbinguni. Kabla ya Mungu kukuruhusu kuwa msimamizi wa mali yake, kwanza yapasa uonyeshe uaminifu katika usima-mizi wa mali iliyo chini yako kama ilivyoelezewa katika andiko hili: “Yesu akam-jibu, “Ni yupi basi wakili mwaminifu na mwenye busara ambaye bwana wake atamfanya msimamizi juu ya nyumba yake yote, naye awape watumishi wengine chakula chao wakati unaofaa? Itakuwa ni furaha kwa mtumishi yule ambaye bwa-na wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. Amin nawaambia, atampa mamlaka juu ya vyote alivyo navyo. Lakini ikiwa yule mtumishi atawaza moyoni mwake, ‘Bwana wangu anakawia kurudi,’ akaanza kuwapiga wale watumishi wa kiume na wa kike na kula na kunywa na kulewa, bwana wake yule mtumwa atakuja siku asiyodhani, na saa asiyoijua. Huyo bwana wake atamkata vipande vipande na kumwekea fungu lake pamoja na wale wasio waaminifu. “Yule mtumishi anayefa-hamu vema mapenzi ya bwana wake na asijiandae wala kufanya kama apendavyo bwana wake, atapigwa kwa mapigo mengi. Lakini ye yote ambaye hakujua laini akafanya yale yastahilio kupigwa atapigwa kidogo.Ye yote aliyepewa vitu vingi, atadaiwa vingi na ye yote aliyekabidhiwa vingi kwake vitatakiwa vingi. ”—Luka 12:42-48. Maandiko kadhaa yanatuhitaji kuwa wasimamizi waaminifu. Sisi ni ma-wakala wa Mungu. Wakala ni mtu anasimamia matakwa ya mwenye rasilmali. Jinsi unavyotumia fedha zako ni ishara ya uhusiano wako na Mungu.
IV. Laana za Uchawi, Madawa ya Kienyeji na Itikadi za Kijamii
Katkia miji mingi Afrika, laana ya ufukara huingia kutokana na waumini kuhusika na uchawi, kywaendea waganga, kutumia mitishamba, madawa ya kienyeji, ndoa za wake wengi na usherati. Hali hii husababisha laana kupitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Hatua za kuwekwa huru zilizoorodheshwa kwenye sehemu hiyo yapasa zifuatwe kabla ya ukombozi kutoka kwa roho ya ufukara kuombewa. Hata kama mtu ameombewa maombi tunayopendekeza hapa, ni muhimu aanze kwa kutalii sehemu hizi ili kusisalie giza lolote linaloweza kuathiri maisha yake baadaye.
Nilipokuwa najiandaa kwa Semina nilizofanya huko Zambia , katika maombi yangu Bwana alinihimiza kuwa roho ya ufukara yapasa kuombewa sawa na vile tunavyoombea roho za giza. Hatua zenyewe ni (1)Kukiri, (2)Toba, (3) kuchukua ruhusa ya kiroho iliyopewa kwa roho ya ufukara na kumrudishia Yesu na kisha, (4) kuamuru mapepo hao watoke.
Omba ombi hili baada ya kuombea uhuru kutokana na uchawi, madawa ya kienyeji, itikadi za kijamii na ndoa za wake wengi.
Ombi la Kufunguliwa Kutoka kwa Roho ya Ufukara
101
# 14 Healing from Poverty www.healingofthespirit.org
Bwana Yesu naja kwako kukombolewa na roho ya ufukara. Nakiri kuwa nime-poteza faida ya ufalme wa mbinguni ili kutimiza haja za moyo wangu na tamaa za mali ya dunia.
Bwana natubu kwa kusumbukia maisha, chakula na mavazi. Natubukwa kuweka hazina duniani ambako nondo na kutu huharibu na wezi kuiba. Natubu kwa kupenda fedha, kutumikia fedha na utajiri, kwa choyo na tamaa ambayo ni ibada ya sanamu.
Natubu imani kuwa pesa ni jawabu la kila haja maishani. Natubu kwa kukusa-hau wewe uliye asili ya uhai wangu na kujiletea madhara mimi na wengine. Natubu kwa kuchagua kujitajirisha na kujaza maisha yangu giza, utumwa na usumbufu. Natu-bu kwa kutokuwa na msimamo tabithi.
Nachagua kukupenda wewe kwa moyo wangu wote na kuweka hazina yangu moyo wangu ulipo katika ufalme wa mbinguni. Nitumie upendavyo.
Natambua na kukiri dhambi zangu za kumuibia Mungu kwa kutotoa zaka na sa-daka kamili, kutowakimu wajane, mayatima, masikini na kutokuwa mwaminifu kwa kidogo. Bwana nisamehe kwa dhambi hizi zote na uniondolee laana hii katika jina la Yesu.
Vizazi Vilivyotangulia
Naja kwa niaba ya vizazi vilivyotangulia kutubu kwa kumuibia Mungu zaka na matoleo ya yote uliyowapa. Natubu dhambi zangu na zile za vizazi vilivyotangulia kwa kuifanya mioyo yao migumu na kuzuia mkono wangu kuwasaidia waliokuwa na mahitaji.. Naomba msamaha ili niwekwe huru.
Natubu kwa moyo wangu wote kwa kiburi cha vizazi kung’ang’nia fedha na dhahabu na kutafuta utajiri wa dunia hii. Natafuta utajiri wa mbinguni wa Bwana wan-gu Yesu Kristo. Natubu kwa kujali mali ya dunia hii na kuiabudu.
Mtazamo wa Ufukara
Bwana, shetani ameamuru kifo na uharibifu juu yangu, anataka niisi katika uma-sikini na utamashaushi. Kwa niaba yangu na vizazi vilivyotangulia, natubu kwa kuwa na mtazamo wa ufukara, kukubali umasikini na kuishi maisha ya ubinafsi, uchoyo na kutojali mwili wa Kristo. Natubu na kugeukia uongo kuwa uungu ni kuishi maisha ya ufukara. Baba, katika rehema zako, niweke huru na vizazi vijavyo kutokana na uongo huu. Sifa na utukufu ni zako kwa Baraka tele ulizoniwekea me na jamii yangu.
Kutoa
Bwana natubu kwa kufanya zaka na kutoa kwangu jukumu badala ya tendo la upendo. Niondolee sheria na kuwajibika kwake. Nipe kuishi chini ya neema yako.
102
# 14 Healing from Poverty www.healingofthespirit.org
Kama neno lako lisemavyo roho ya ukarimu itashibishwa naye awatiliaye wengine maji atamiminiwa mwenyewe. Kila apandaye kwa wingi atavuna kwa wingi-kipimo kamili-kimefinyiliwa na kumwagika. Bwana, nachukua ruhusa ya kiroho niliyopeana kwa roho ya ufukara na kukurudishia wewe.
Tangazo
Natangaza kuwa Yesu alikuja tupate maisha ya utele. Nachagua kuamini, kukubali na kusadiki Mungu atanipa kila haja yangu na kunipa urithi mimi na vizazi vijavyo ili asiweko hata mmoja atakayeishi katika ufukara. Nachagua kupokea kutoka katika chemichemi ya uhai ambapo Mungu anapeana utajiri katika ufalme wake. Nitafungua mkono na moyo wangu kwa wahitaji na kuwashirikisha mali yangu kadri utakavyoniongoza ili asiweko mhitaji hata mmo-ja.
Bwana nakuomba uangamize mizizi iliyoko kati yangu na mali ya dunia hii, najihusi-sha na wewe peke yako. Nakupa kila nilicho nacho, wewe ndiwe mwenye vyote nilivyo navyo. Niruhusu kuishi chini ya neema na utoaji wako. Natubu kwa kutokuamini unaweza kunitosheleza. Nitakutumainia wewe kukutana na kila hitaji langu. Nitatosheka na kile unipa-cho kama ni ujira au fedha.
Bwana nakushukuru kwa kunipa uwezo wa kupanda mbegu. Roho Mtakatifu nifun-dishe namna ya ya kupanda na kuvuna kwa makusudi ya kiungu. Nakiri kuwa nitakula mkate wa uhai na kufurahia wingi wako. Fungua macho yangu nione fedha kwa macho ya kiroho na kujua kuwa zinatoka kwako na zafaa kutumika kwa makusudi yako. Achilia kila rasilmali ambayo adui amenyakua kutoka kwangu na kwa jamii yangu. Bwana vunja kila laana ya ku-panda mbegu nyingi na kuvuna kidogo, kula na kutotosheka, kupokea mshahara na kuuweka kwenye mfuko ulio na matundu. Rudisha mavuno yaliyoliwa na nzige. Asante Bwana.
Natubu kwa niaba ya jamii yangu kwa kutopokea urithi uliotuahidi: kufungua madiri-sha ya mbinguni na kumimina Baraka mpaka tushindwe kuipokea. Naahidi kutimiza masharti uliyoweka ili nipokee Baraka na urithi huu. Naomba Baraka hizi zije kwa wingi kiasi cha kuwaachia watoto na wajukuu wangu. Bwana Yesu nakiri ifuatavyo:
• Naamini Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya ufukara wangu.
• Naamini upatanisho wake ulinipa utele.
• Naamini Yesu alichukua laana ya ufukara kwa niaba yangu
• Naamni kuwa ijapokuwa Yesu alikuwa tajiri, lakini kwa ajili yangu alifanywa masikini ili mimi niwe tajiri (2 Kor. 8:9).
• Naamini Mungu ndiye mweye vyote nchini namini ni msimamizi tu, kila nili-cho nacho ni mali yake.
• Naamini Mungu ndiye mwenye fedha na dhahabu na ng’ombe walio katika mi-lima elfu, na kuwa ana utajiri wote mbinguni.
• Naamini Yesu atakutana na kila hitaji langu kutoka kwa hazina yake mbinguni
103
# 14 Healing from Poverty www.healingofthespirit.org
• Naamini ahadi za Mungu zina masharti.
• Naamini Bibilia inaahidi utele nikitimiza masharti yaliyowekwa.
• Naamini Mungu atanitimizia mahitaji yangu yote kwa kadri ya utajiri wa utuku-fu ndani ya Kristo (Filip4:19).
• Naamini ni sharti nilipe zaka na sadaka ili kupokea utele wa mbinguni.
• Naamini nikiwa mwaminifu, Mungu ataniondolea mharibifu mlangoni mwan-gu.
Ahadi
Na sasa, ee Bwana, Naahidi mbele yako na mashahidi hawa:
• Nitalipa zaka na sadaka kwa yote nitakayopokea
• Nitotao malimbuko ya yote unipayo
• Nitatoa kumkimu mchungaji wangu, wajane, mayatima , masikini na wahitaji
• Nakutumainia kwa mahitaji yangu
• Nitazingatia kanuni ya 10-10-80 uliyonifundisha
• Nitakungojea unifungulie milango ya kazi na biashara
• Nakushukuru kabla ya Kupokea na kukupa utukufu wote
Neno Lako
Nakiri Kuwa neno lako linasema:
Utatupatiahazina za mbinguni na utajiri uliofichwa kwenye mali pa siri. Wewe ndiwe utupae uwezo wa kutajirika ili utimize agano lako ulilowaahidia mababu zetu hapo awali.
Yesu naachilia upako wa kuwa mshindi- kupa kina. Baba, mimi na vizazi vitakavyo-kuja baada yangu hatutokuwa chini; bali juu. Tutakuwa kichwa sio mkia. Mimi nimebarikiwa na kupendwa na Bwana.
Baba nipe moyo uliotahiriwa ili ufungue hazina zako kutoka mbinguni. Utuongezee zaidi na zaidi mimi na watoto wangu. Nakusihi, nitumie ufanisi katika jina la Yesu.
Nasimama kinyume cha roho ya ufukara na Mammoni nakuwaamuru watoke. Nake-mea roho ya ufukara itoke mfukoni mwangu, kwenye hazina yangu, jamii yangu, biashara zangu na kanisa langu. Natangaza kwamba sina maagano na roho hizi!
Naomba roho ya kupokea na kutoa iingie ndani ya maisha na himaya yangu. Bwana, naomba unirudishie kile ambacho nzige wamekula, kile kilichoibiwa na kupotea. Nirudishe kwenye mahali pa urithi wa utele wa ufalme wa Mungu. Utukufu na sifa zote ni zako unapo-nifungulia utele katika jina la Yesu. Amin
104
# 15 Healing from Pride www.healingofthespirit.org
Uponyaji wa Kiburi
Bwana ananihimiza niwaambie kuhusu dhambi ya kiburi cha kiroho. Ijapokuwa wachungaji wengi wameondokea dhambi za kimwili ambazo zimejaa duniani, ajabu ni kuwa wao hubadili mtazamo wao na kuiga utu wa kiroho ambaoi ni hatari zaidi unaojidhirisha kimwili. Kila aliyeteuliwa kuwatumikia watu wa Mungu ana athari za vishawishi vingi. Kiburi ndicho chanzo kikuu cha matatizo kanisani na huishia kusinyaa kwa washirika kiroho na kijumla.
Hili ndilo lango kuu ambalo shetani huingilia kwenye mioyo ya wale wenye bidii ya kukuza dini … ndilo kiingilio cha moshi kutoka katika shimo lisilo na kina ili kupotosha maamuzi na kuwatia katika mikono ya shetani watauwa kwa kuzuia kazi ya Mungu.
Kiburi hutatiza kazi ya Mungu kwa kuifungia roho katika giza na kumzuia mtu kutubu dhambi ya kiburi. Kiburi cha kiroho ni dhambi iliyojificha kiasi cha kutoweza kutambulika kwa urahisi.
Mtu awaeza kuuliza: jee tunawezaje kukitambua kiburi cha kiroho? Ni nadra kwa wale wenye kiburi cha kiroho kutambua wanacho. Tabia yao huwa na namna ya utauwa inayowahadhaa wao wenyewe na wengi ijapokuwa kuna wachache wanaoweza kukiona kiburi hicho cha kiroho. Kiburi huambatana na roho ya udini ili kumfanya mchungaji na usharika wake kuwa na mfano wa uungu.
Kibinadamu sisi hupokea motisha na nguvu tunapojisifu wenyewe. Kiburi ni dhambi hatari inayomfanya mtu kuonekana mtakatifu ilhali yeye si mtakatifu akijawa uongo, ulaghai na tabia za kupotosha. Mtu mwenye kiburi hutafuta kuonekana, kutambulika na kukubaliwa.
Yafaa ikumbukwe kwamba ni dhambi ya kiburi iliyomfanya Ibilisi afukuzwe mbinguni. Hata mitume walionekana kuwa na kiburi katika matukio mawili: “Kukazuka mabishano miongoni mwa wanafunzi kuhusu ni nani miongoni mwao atakayekuwa mkuu kuliko wote” (Luka 9:46) na tena: Pia yakazuka mabishano katikati ya wanafunzi kwamba ni nani anayeonekana kuwa
mkuu wa wote miongoni mwao,” (Luka 22:24) Wakati mwingine tunafunzwa kiburi na wazazi wetu: Kisha mama yao wana wa Zebedayo akamjia Yesu pamoja na wanawe, naye akiwa amepiga magoti mbele yake, akamwomba Yesu amfanyie upendeleo.(Mathayo 20:20)
Musa
Tukimtazama Musa tunaambiwa katika Bibilia ya kuwa alipoanza huduma yake alikuwa: … mtu mnyenyekevu sana, mnyenyekevu kuliko mtu mwingine ye yote katika uso wa dunia (Hesabu 12:3) Naam , Musa mwenye utukufu aliianza huduma yake huku amejawa unyenyekevu na upole mwingi. Hata hivyo hatima ya huduma yake hakuingia kwenye nchi ya agano kwa kuadhibiwa kutokana na kiburi cha kiroho kwa kutompa Mungu utukufu. Ni huyuMusa aliyewaongoza wana Waisraeli kuvuka bahari ya Shamu kutoka Misri hadi jangwani wakielekea Kanani. Alimtii Mungu akafanya miujiza mingi safarini. Mojawapo ilikuwa kuupiga mwamba watu walipohitaji maji jangwani. Mungu alimwambia aupige mwamba na humo kukatoka maji yaliyowaburudisha watu.
Bibilia yatujulisha kuwa ule mwamba ulikuwa picha ya Kristo – “Mwamba wenye Imara”(I Wakorintho 10:4). Kwa mpango wa Bwana huu “Mwamba wenye Imara” ulipigwa ili yale maji ya uzima yabubujike kutoka kwa Yesu kwa ajili ya kizazi chote cha
105
# 15 Healing from Pride www.healingofthespirit.org
Adamu ili kiwe wana Waisraeli watokao Misri – yaani ulimwenguni – kwenye dhambi- kutoka katika ufalme wa adui na kuingia kwenye utiifu na ushirika na Bwana. Hivyo basi Musa huku akikaidi agizo la Bwana aliuendea ule mwamba na kuupiga mara mbili kwa fimbo yake huku akiwapigia watu mayowe: “enyi waasi, je, ni lazima tuwatoleeni maji kutoka katika mwamba huu?’’ (Hesabu 20:1-12)
Maskini Musa! Alikuwa akijilimbikizia utukufu yeye mwenyewe badala ya kumpa Bwana. Punde Musa akatambua kosa kubwa alilotenda, yaweza kusemekana kuwa hili ndilo kosa la pekee alilofanya lakini Bwana alimnyima starehe ya kuingia Kanani kwa ajili yake. Musa aliuona mji wa Kanani kwa mbali kutoka kwenye ufuo wa mto wa Yordani ambako alizikwa
Ishara za Kiburi cha Kiroho:
Soma orodha ifuatayo na usikize kama Bwana ananena nawewe kuhusu maisha yako:
• Kujiinua nafsi yako kuliko wengine.
• Kujivunia matukio ya kiroho kama kufunga na kuomba kwa muda mrefu
• Kutofundishika, kujidai una majibu ya maswala yote ya kiroho.
• Kujiona kuwa umekomaa kiroho kuliko wengine wote.
• Kujiona kwamba Mungu hujibu maombi yako na maombi yako yana nguvu kuliko ya wengine
• Kutaka kuwaombea wote wanaohitaji uponyaji bila kuwahusisha wengine
• Kupenda kuhubiri wakati wote na kufikiri kuwa unahubiri bora kuliko wengine
• Kujivuna eti unajua zaidi kwa ajili ya elimu uliyo nayo.
• Mungu akiongea nawewe unaanza kujikweza kama mtu wa maana.
• Kutaka kujulikana kwa mavazi sanifu kama kuvaa suti panapo joto kali
• Kuchukulia muda wako kuwa muhimu kuliko watu wengine
• Kupenda kuheshimika kila wakati
• Asiyeweza kukubali kukosolewa ama hata kukubali ana udhaifu au maradhi fulani yanayomtatiza
• Kupenda nafasi ya kwanza chakulani
• Kupenda kula kwenye meza kuu
• Hukaa kwenye viti vya fahari na meza kubwa mbele yao.
• Huwakashifu wengine na kuwatoa makosa kila mara
• Wanajivunia kutobadilika kwao eti wao ni wastahiki zaidi
• Huwaingilia wengine wanapokuwa katikati ya kunena
• Hawamudu maombi ya kina
• Huwaza maoni yao ni bora kuliko ya wengine
Ishara za Mtu Mnyenyekevu:
Tafakari juu ya ishara zifuatazo za watu wanyenyekevu:
• Hujivika utulivu, unyenyekevu, upole wa moyo na tabia
• Mkimya, msikivu, mwenye
• Hana machungu au ukali
• Hufanya mtu kuwa kama mtoto mdogo, mpole kama mwanakondoo
• Kuzungumza naye kuna wema na huruma kwa wanadamu wote
• Huwaheshimu wengine kuliko nafsi yake mwenyewe
106
# 15 Healing from Pride www.healingofthespirit.org
• Amejawa na shukrani
• Unyenyekevu sio kujidunisha bali kujishushambele ya wengine
Bibilia Inasema nini Kuhusu Unyenyekevu na Utumishi
Soma vile Bibilia inavyosema kuhusu kiburi na majivuno. Bwana hawasikii wanajivuna. Majivuno ni laana (Zaburi 119:21), ni chukizo mbele za Bwana (Mithali 16:5), pia ni mojawapo ya dhambi saba anazozichukia Mungu (Mithali 6:7). Kiburi kimejumuishwa na dhambi za uzinzi, na uovu (Warumi 1:30, 2 Timotheo 3:2-3). Tazama maandiko (Zab Ps 74:14,104:24-25, Isa 27:1
Zab 9:12 “Kwa maana yeye alipizae kisasi cha damu hukumbuka, hapuuzi kilio cha wanaoonewa.”
Mithali 16:19 – “Ni afadhali kuwa mnyenyekevu katika roho miongoni mwa walioonewa kuliko kugawana nyara pamoja na wenye kiburi.”
Zab 119:21 “Unawakemea wenye majivuno, waliolaaniwa waendao mbali na amri zako.
Mith 6:17 Macho ya kiburi, ulimi udanganyao, mikono imwagayo damu isiyo na hatia,”
Mith 15:25 “BWANA hubomoa nyumba ya mtu mwenye kiburi, bali huilinda mipaka ya mjane isiguswe...”
Mith 16:5 “BWANA huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyoni. Uwe na hakika kwa hili: “Hawataepuka kuadhibiwa.”
Mith 21:4 “Macho ya kudharau na moyo wa kiburi, ni taa ya waovu, navyo ni dhambi!”
Mith 28:25 “Mtu mwenye tamaa huchochea fitina, bali yule amtegemeaye BWANA atafanikiwa.”
Jer 50:32 “Mwenye majivuno atajikwaa na kuanguka wala hakuna ye yote atakayemuinua, nitawasha moto katika miji yake, utawakaoteketeza wote wanaomzunguka.””
Math 18:4 “Kwa hiyo mtu yeyote ajinyenyekezaye kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni.
Math 23:11 “Yeye aliye mkuu kuliko ninyi nyote miongoni mwenu atakuwa mtumishi wenu...
Math 23:12 “Kwa kuwa ye yote anayejikweza atashushwa, na ye yote anayejinyenyekeza atakwezwa.
Marko 10:44 “na ye yote anayetaka kuwa wa kwanza, hana budi kuwa mtumwa wa wote.”
Marko 9:35 “Akaketi, akawaita wote kumi na wawili akawaambia: ‘Kama mtu ye yote akitaka kuwa wa kwanza hana budi kuwa wa mwisho na mtumishi wa wote.”
War 1:29-30 “Wakiwa wamejawa na udhalimu wa kila namna, uasherati, uovu, tamaa mbaya na hila. Wamejawa na husuda, uuaji, ugomvi, udanganyifu, hadaa na nia mbaya. Wao pia ni wasengenyaji, wasingiziaji, wanaomchukia Mungu, wajeuri, wenye kiburi na majivuno, wenye hila, wasiotii wazazi wao
107
# 15 Healing from Pride www.healingofthespirit.org
2 Tim 2:24 “Tena haimpasi mtumishi wa Bwana kuwa mgomvi, bali inampasa awe mwema kwa kila mtu, awezaye kufundisha, tena mvumilivu.”
2 Tim 3:2-3 “Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kumkufuru Mungu, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio watakatifu, wasio na upendo, wasiopenda kupatanishwa, wasingiziaji, wasiozuia tamaa zao, wakatili, wasiopenda mema,.”
Yak 4:6 “Lakini Yeye hutupatia neema zaidi. Hii ndiyo sababu Maandiko husema: ‘‘Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.’’
1 Pet 5:6 “Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati Wake.”.
Uponyaji wa Dhambi ya Kiburi
Wale walio na kiburi wanapokaidi kujithathmini na kutubu, Bwana huwaadhibu kwa manufaa yao wenyewe katika maswala ya kifedha, kiafya na hata mahusiano yao na wengine. Zipo jinsi kadhaa ambazo wachungaji na viongozi wa kanisa wanaweza kujikinga na kiburi:
1. kupeleleza nafsi na moyo wako kwa makini. Maandiko tofauti yanatuamuru kufanya hivyo (Zab 19:12, 13 51:10, 139:23, 141:4)
2. Unapotambua kiburi, ungama mbele za wengine na utubu kwa Mungu
3. Wajibika kwa mhuduma mwingine ambaye anaweza kukueleza unpaoanza kupotoka. Kumbuka ni rahisi kwa wengine kutambua kiburi kilicho ndani yako kuliko wewe mwenyewe.
108
#16 Uponyaji wa Machungu, Hisia na Kumbukumbu www.healingofthespirit.org
Uponyaji wa Machungu, Hisia, na Kumbukumbu
Kumbukumbu zinaweza kuumiza, kulemaza, na kuwafunga watu. Watu wengine husema kwamba kuumizwa huku huwa kunasababisha nyufa katika nafsi zetu. Aina hii ya kuumizwa inaweza pia kutuweka kifungoni, na kuzuia nguvu ya Mungu ya uponyaji kufanya kazi ndani yetu, na kutufanya tuwe wagonjwa kimwili. Kwa hali yoyote, upendo wa Mungu unaweza kutubadili (kugeuza na kurekebisha) hisia—na kumbukumbu zetu pia—kutuweka huru na kutuwezesha kuishi maisha teletele kupitia kwa Yesu Kristo. Mungu anayetaka “unyofu wa ndani” (Zab. 51:7), humruhusu Roho wake Mtakatifu (roho wa kweli) atufunulie ukweli na kuufanya upendo wake uifunike kila hali ili uponyaji uweze kutokea.
Sehemu hii inashughuilkia uponyaji wa ndani kwa jumla. Sehemu zengine zinaeleza kwa kina vitu dhahiri vinavyosababisha kuumia kwa kumbukumbu, kama vile kukataliwa, talaka, dhuluma, n.k.
Ufafanuzi
"Ugonjwa wa roho husababishwa na mambo tuyafanyayo, ilhali ugonjwa wa hisia kwa jumla husababishwa na mambo tunayofanyiwa. Hukua kutokana na machungu tufanyiwayo na mtu mwingine au tukio fulani lililotupata hapo awali. Machungu hayo hutuathiri wakati huu, kwa umbo la kumbukumbu mbaya, na hisia dhaifu au zilizoumizwa. Mambo hayo hutuongoza kutenda aina mbalimbali za dhambi, majonzi, kuhisi kwamba huna thamani au wewe ni kitu duni, uwoga na wasiwasi usio na sababu, magonjwa ya kiakili, n.k. Jambo lengine linalotokea hapa ni madhara yanayowapata watoto nyakati hizi kwa sababu ya dhambi za wazazi wao. Yaani uponyaji wa machungu yaliyopita unagusia hisia, kumbukumbu na, watu wenye ukoo wa kidamu" (kama inavyoelezwa katika kitabu cha John Wimber, “Power Healing”).
Uponyaji wa Ndani (Mambo ya Kufahamu)
1. Toba haiwezi kuziponya kumbukumbu za mambo yaliyokuletea uchungu au maumivu. Mtu huyo hakufanya kosa bali alikosewa.
2. Aina nyingi za uponyaji wa ndani zinatuhitaji tuwasamehe watu waliotukosea au waliotudhulumu; pia tunahitaji ombi la uponyaji wa kumbukumbu za machungu na maumivu ya tukio hilo zilizo ndani yetu.
3. Hatuwezi kuwa na amani na furaha ya ndani na upendo kamili wa Mungu ikiwa bado tuna machungu moyoni. Watu wengi wenye machungu huhisi woga au woga wa kukataliwa, kukataliwa, kujikataa mwenyewe, na/au kutojithamini.
4. Hitaji letu kubwa ni kupendwa na ikiwa tutanyimwa upendo huo tukiwa watoto wachanga au wadogo (hali inayojulikana kama upungufu wa upendo), wakati fulani katika maisha yetu tutaathirika na kukosa amani—ya kuweza kuwapenda na kuwaamini wanadamu na/au Mungu.
5. Machungu haya yanaweza hata kuweko kabla ya kuzaliwa (huenda yalitokea mtoto akiwa ndani ya tumbo—kama itakavyoelezwa katika sehemu nyingine baadaye. Mtoto anaweza kuhisi kukataliwa akifahamu kwamba wazazi wake hawakumtaka au wakati wake wa kuzaliwa haukufurahiwa.
6. Machungu hayo ya ndani yanaweza kuwa chanzo kikubwa cha matatizo ya kimwili.
7. Mara nyingi roho za uovu hujiingiza katika hisia hizo na kufanya uponyaji kuwa mgumu.
8. Mahitaji mengine ya uponyaji wa ndani yanaweza kuwepo kwa sababu ya dhambi za watu waliotutangulia (kama ilivyojadiliwa katika sehemu inayoeleza juu ya “Uponyaji Kutokana
109
#16 Uponyaji wa Machungu, Hisia na Kumbukumbu www.healingofthespirit.org
na Athari za Kizazi”).
9. Jambo la kimsingi ni hili: kwa vile “wakati” ni kitu kisichokuweko kwa Mungu wa mbinguni, basi Yesu (ambaye ni yule yule jana, leo na hata milele) anaweza kukifikia kile tunachokijua kuwa wakati na kuyaponya machungu, maumivu, na kumbukumbu za mambo yaliyopita ili ziache kutuletea machungu. Kisha Yesu huujaza upendo katika kila sehemu iliyo ndani yetu iliyopata uchungu, maumivu na iliyo tupu.
10. Wakati wa kupata uponyaji wa ndani huwa tunamwambia Yesu aurudie ule wakati ambao mtu huyo aliumizwa, alikataliwa, au alidhulumiwa, na amweke huru kutokana na athari za kuumizwa huko “wakati huu” kwa kumfunulia vitu vilivyomuumiza na kumwomba Mungu aziponye athari za hali katika maisha ya zamani ya mtu huyo zilizoleta machungu na zinazomfunga. Katika hali nyingi, kila hali inatakiwa kuombewa moja moja.
11. Tatizo kubwa si tukio, bali ni hisia zinazojitokeza baada ya tukio lililosababisha tatizo hilo (kuendelea kuwa na uchungu) na kumruhusu Shetani aingie.
12. Sehemu fulani za roho (ya mtu anayeona uchungu) hazijawekwa wakfu kwa Mungu (na chochote kisichomilikiwa na Yesu, humilikiwa na Shetani)
13. 80% ya matatizo ya watu wanaotembelea “Kliniki ya Mayo” huwa wana magonjwa yanayosababishwa na matatizo ya akili, bali si ya mwili.
Dalili Zinazoweza Kuonyesha Kwamba Mtu Anahitaji Uponyaji wa Ndani
1. Wao hujitenga na maisha, na kufanya mambo kama kwamba wanataka kujificha
2. Wao huwa na soni na huwa hawako tayari kutumia karama zao
3. Wao huonyesha au husema kwamba wanahisi kukataliwa
4. Wao huonyesha ugumu wa kukua kiroho
5. Wao hung’ang’ana na mazoea ya tabia mbaya, kusamehe, kuona uchungu, n.k.
6. Wao huonyesha mwenendo au hisia tupu na wakati mwingine huwa hawaonyeshi hisia zozote.
7. Wao huonyesha kwamba wana upweke mkubwa
8. Wao huonyesha matendo ya kuhisi kwamba wanateswa, wanasumbuliwa, au wanaumizwa
9. Wao huonyesha ishara za kuhisi kwamba wamepotea kabisa na kukosa maana ndani yao lakini nje wao hufanya mambo kama kwamba kila kitu kiko sawa.
10. Wanaweze kupata kizunguzungu wakati wa kupakwa mafuta na Bwana
11. Wana matatizo ya kutoweza kusoma vizuri
12. Wao huonyesha hisia na matendo ya woga na kutofurahia wakati wa kipindi cha ibada
13. Wao huhisi kwamba roho yao iko kifungoni
14. Wakati mwingine wao hulia kwa njia isiyoweza kuzuilika
15. Wao hushangaa na kudhani kwamba wanarukwa na akili
16. Wao huonyesha hisia za kuwa na hatia na aibu
Orodha ya Uponyaji wa Ndani
Maswali yafuatayo yanaweza kukusaidia kutambua sehemu za maisha yako zinazohi-taji uponyaji. Maswali haya pia yanaweza kupendekeza sehemu zilizo wazi katika “ukuta wako wa kiroho” ambazo adui anaweza kutumia kuingia. Tafuta mahali palipotulia, fanya matayarisho ya kiroho kwa muda mfupi, halafu muulize Mungu afungue akili yako na aku-saidie kuyakumbuka majibu ya maswali yafuatayo.
110
#16 Uponyaji wa Machungu, Hisia na Kumbukumbu www.healingofthespirit.org
1. Je, umewahi kupewa talaka? Uhusiano kati yako na mwenzi wako wa zamani uko vipi? Je, ndani yako kuna hali ya kutosamehe? Je, amekuumiza sana na kukukataa?
2. Je, umewahi kuishi na mtu mwingine “muhimu” maishani mwako halafu mkawachana?
3. Orodhesha watu wote ambao wamewahi kukuumiza vibaya (na bado unahisi uchungu huo).
4. Je, umewahi kubakwa au kudhulumiwa (kimapenzi, kimwili, au kihisia), ni nani aliye-fanya hivyo? Je, umemsamehe mtu huyo?
5. Je, mimba yako imewahi kuharibika au umewahi kutoa mimba au kumtunga mwanamke mimba na mimba hiyo ikatolewa au ikaharibika? Je, umewahi kulipia utoaji wa mimba au kumpeleka mtu akatoe mimba?
6. Baba yako alikuwa mtu wa aina gani? Mlihusiana vipi? Je, alikupenda? Aliwahi kukuo-nyesha mapenzi kwa kukubeba na kukwambia maneno ya upendo?
7. Mama yako alikuwa mtu wa aina gani? Mlihusiana vipi? Je, alikupenda? Aliwahi kukuo-nyesha mapenzi kwa kukubeba na kukwambia maneno ya upendo?
8. Je, siku za utoto wako zilikuwa za furaha? Je, wewe ni mtoto wa kupanga au ulitunzwa na wazazi wa kupanga?
9. Je, baba na mama yako walikufa ukiwa mdogo, au mmoja wao alitoka nyumbani kwa sababu ya wao kutengana au kupeana talaka?
10. Orodhesha majina ya watu wote waliokukataa au waliokufanya uhisi kwamba huna tha-mani.
11. Je, umewahi kufikiria juu ya kujiua?
12. Je, umewahi kupatikana na ugonjwa wa kiakili au kulazwa hospitalini kwa ajili ya kupo-kea ushauri wa matibabu ya kiakili?
13. Je, umewahi kutamka kiapo chochote, kama vile “sitamruhusu mume aniumize?”
14. Je, una hofu nyingi na/au uoga usio na sababu? Je, kuna kitu maalum unachoogopa?
15. Je, kuna sanamu zozote maishani mwako—vitu unavyovithamini sana kuliko Mungu au mambo unayofanya kwanza kabla ya kufanya kazi ya Mungu?
16. Je, kuna mtu ambaye amejaribu kukutawala? Umewahi kujitahidi sana kumfurahisa mtu fulani bila kufaulu? Je, kuna mtu yeyote mnayetegemeana?
17. Je, uliwahi kuaibishwa vibaya sana ulipokuwa mtoto au kijana?
18. Je, unaweza kutambua utaratibu wa matukio ya kuumiza yaliyoanza utotoni, na kuen-delea?
19. Je, umewahi kutamani uwe mtu mwingine? Je, unajichukia? Je, umewahi kudhani kwam-ba heri usingezaliwa?
20. Je, una tatizo la kutoweza kusoma vizuri lililogunduliwa ulipokuwa mtoto? Je, una aina nyingine ya upungufu wa kimwili?
21. Je, unawachukia watu wa jinsia nyingine au wa jinsia sawa na yako?
22. Je, wewe hujikuta kwamba unakasirika kwa njia isiyo ya kawaida unapoambiwa kitu au unapofanyiwa kitu (wewe hukasirika kupita kiasi)?
23. Je, wewe hukumbuka kila mara tukio la zamani lililokuumiza? Je, unasikia vibaya unapo-fikiria juu ya tukio hilo?
24. Je, kuna watu usioweza kuwasamehe? Je, huwa unaona vigumu kumwambia mtu mwin-gine akusamehe?
25. Je, wewe huwa na hisia kali za hatia au aibu?
111
#16 Uponyaji wa Machungu, Hisia na Kumbukumbu www.healingofthespirit.org
26. Je, wewe huona ugumu mkubwa kukubali kwamba umefanya makosa? Je, huwa unatafuta mtu wa kulaumu kila wakati mambo yanapokwendea vibaya maishani mwako?
27. Je, wewe huhisi hasira ndani yako kila wakati? Je, wewe huwakosoa watu katika mazungumzo au mawazo yako kila wakati?
28. Je, una ulimwengu wa ndoto ambao wewe huukimbilia?
29. Je, una ugonjwa wa mwili ambao chanzo chake hakijulikani?
30. Je, umewahi kupatikana kuwa wewe si mwepesi wa kuelewa mambo, mtu anayefurahi na kuhu-zunika kupita kiasi, kuwa na ugonjwa wa bi-pola?
31. Je, wewe huwa na tatizo la majonzi au huwa na majonzi kwa kipindi kirefu?
32. Je, wewe hupata jinamizi au hutatizwa na ndoto mbaya mara kwa mara?
33. Je, una uchovu wa mwili au wa akili kwa ajili ya kung’ang’ana na matatizo ya ndani?
34. Je, huwa unaona ugumu kulala au hutaka kulala kupita kiasi?
35. Je, wewe huwa na tatizo kubwa la kutotulia na/au kuwa “mbioni” kila wakati? Je, wewe hu-shindwa kuketi na kutulia kwa kipindi fulani?
36. Je, wewe hufanya kazi kupita kiasi? Je, wewe huona hatia unapokosa kufanya kitu kinachoweza kusababisha mambo mazuri? Je, wewe hujitahidi kuwafurahisha wengine?
37. Je, ulifikia umri wa utu uzima kabla ya kuhisi kwamba unapendwa na mtu mwingine?
38. Je, wewe hujifananisha na watu wengine na hatimaye kuhisi kwamba hustahili na ukavunjika moyo?
39. Je, wewe huwa na hitaji kubwa la kutaka kuonyeshwa upendo au wewe huchukia sana kitendo cha kuguswa?
40. Je, wewe huhisi kwamba huna usalama, au huhisi kwamba hupendwi, au hukubaliki
41. Je, ni vigumu kwako kuamini kwamba Mungu anakupenda na anakukubali?
42. Je, wewe huona ugumu kupenda na kupendwa?
Je, wewe hujiona vipi? (Tia mviringo katika maelezo yanayohusika)
Kuwa na thamani ya chini Kutokuwa salama Nafsi ya kujitenga
Kujihukumu Kujichukia Kuwafurahisha wengine
Jidunisha mtu wa kushindwa kuteseka sana moyoni
kujiona mtu wa chini kuhoji sura yangu Sura ya unafiki
kuhitaji sana upendo mzinzi mwenye shaka
asiyestahili kuogopa kukataliwa sijijui
kutafuta kibali kujikataa kuhisi umeachwa
kujishutumu huwezi kupokea upendo mwenye majonzi
huwezi kupenda uchungu/maumivu ya ndani huwezi kupenda mwenzio
hakuna uhusiano unaodumu kuwa mwema au kutaka kukubaliwa
Ombi la Uponyaji wa Ndani
1. Kwa kawaida, ombi hili hufanyiwa mahali pa siri kukiwa na watu wawili pekee katika timu ya maombi. Baadhi ya kumbukumbu zinaweza kumfanya mtu ahisi ana hatia au aone aibu.
2. Kila mara ombea uponyaji wa ndani kabla ya kufanya ombi la ukombozi. Kumbukumbu ya asili ikiponywa, roho za giza zitaondoka.
112
#16 Uponyaji wa Machungu, Hisia na Kumbukumbu www.healingofthespirit.org
3. Kwa kawaida mtu huyo huulizwa, kwa kusaidiwa na Roho Mtakatifu, apige picha kichwani ya tukio lililomuumiza. Halafu tutamwambia Yesu Kristo aingie katika pi-cha hiyo iliyo kichwani—sio kwa ajili ya kuibadilisha, bali aondoe uchungu na maumivu na kuweka upendo ndani ya picha hiyo.
Hebu tutumie mfano huu. Msichana mdogo anadhulumiwa kimapenzi na baba, ndugu au mtu wa ukoo wake. Wakati wa tukio hilo, mlango hufunguliwa na roho chafu za tamaa, woga, maumivu ya mwili, na kuchanganyikiwa (iwapo mtu huyo ni baba yake) humwingia. Kwa kawaida, uponyaji hauwezi kufanyika mpaka msichana huyo alilete tukio hilo akilini mwake na amwambie Yesu aingie katika picha hiyo na aondoe hisia zenye maumivu alizohisi wakati wa kitendo hicho, ha-lafu alete uponyaji katika tukio hilo.
Wakati mwingine sisi (waombezi) tutahitajika kuomba kwamba msalaba wa Yesu uwekwe katikati ya mdhulumu na mtu anayetaka uponyaji, na jambo hi-lo likitendeka katika picha iliyo akilini mwake kutakuwa na mwangaza upande wake wa msalaba na giza litakuwa upande mwingine wa msalaba. Wakati mwin-gine Yesu huja na kusimama katikati ya mdhulumu na mtu anayetaka uponyaji. Kwa vyovyote vile, tukio lililosababisha hisia za kiwewe huponywa kwa upendo wa Yesu na kwa mhusika anayetaka uponyaji kukubali kumsamehe mdhulumu wake na kumpa Yesu hisia za kiwewe zilizokuweko wakati huo.
Sisi (waombezi) tutafukuza au kuamuru roho chafu ziondoke na kum-womba Yesu aliponye tukio hilo. Hatimaye uponyaji huja, na ingawaje mhusika huyo atalikumbuka tena tukio hilo katika siku za baadaye kama tukio la kihisto-ria, tukio hilo halitamletea tatizo la Ugonjwa wa Dhiki Unaojitokeza Baada ya Hali ya Kiwewe, kama ilivyotambuliwa hapo awali.
4. Iwapo nguvu za Roho Mtakatifu ziko mahali hapo, mtu huyo ataweza (1) kumwona Yesu katika picha hiyo, (2) kuuhisi wema na upendo wa Yesu, au (3) kujua kile ambacho Yesu angefanya (hii sanasana hutokea kwa watu wenye akili ya kuhakiki).
5. Iwapo hawawezi kumwona Yesu katika picha hiyo na picha hiyo ina giza, huenda ikawa kuna roho za uovu au laana inayouzuia mwangaza wa Yesu kuingia katika picha hiyo.
6. Ombi linaweza kufanywa la kuuweka msalaba wa Yesu katikati ya mdhulumu na mdhulumiwa.
7. Mhitaji aeleze hisia alizo nazo
8. Muulize mhitaji kama anamuona Yesu kwenye taswira/picha hiyo
9. Mwambie mhitaji amkabidhi Yesu hisia za machungu waliyo nayo
10. Muulize mhitaji iwapo anataka Yesu amkumbatie
11. Mhitaji akiwa tayari , muombe Roho Mtakatifu amwelekeze katika tukio jingine
12. Ombi la aina hii huchukua vikao zaidi ya kimoja na kuambatana na kulia kwingi
13 Kitendo hiki kitahitaji muda mwingi usio na haraka. Sikiliza, penda, na kuomba lakini usitoe ushauri. Huna majibu yoyote; ni Mungu pekee aliye na majibu.
113
#16 Uponyaji wa Machungu, Hisia na Kumbukumbu www.healingofthespirit.org
Ombi Sikivu
Ombi mbadala kwa lile la kawaida huitwa ombi la usikivu au “kuona na kuonekana”. kusudi la ombi hili ni kumpa mtafutaji nafasi ya kuutazama uso wa Yesu na kuonekana na kukumbatiwa mikononi mwa Yesu. Ombi hili humsaidia mfatutaji kumpata Yesu mahali pa salama badala ya kumtafuta kwenye matukio ya kusikitisha. Yesu humpa utulivu, faraja, ujasiri na ahadi kuwa anaweza kuingia kwenye maeneo ya kutisha. Inamruhusu mwombezi kuelewa vile mtafutaji anavyosikia, kuona na kumhisi Yesu. Tunamchukua Yesu kwa neno lake:
““Njoo!’’ Naye asikiaye na aseme, “Njoo!’’” (Ufu 22:17) “Tazama, nasimama mlangoni nabisha. Kama mtu ye yote akisikia sauti Yangu na kufungua mlango, nitaingia ndani na kula pamoja naye,naye pamoja nami.” (Ufu 3:20) “…naye atakuwa pamoja nawe, kamwe hatakuacha wala hatakutupa. Usiogope wala usifadhaike.’’. (Kumbu 31:8) na maneno ya mwisho aliyonena Yesu kwa wanafunzi wake “Hakika Mimi niko pamoja nanyi sikuzote, hadi mwisho wa nyakati.” (Math 28:20)
Utaratibu wa maombi sikivu ni kama ifuatavyo:
1. Mwombezi anamuuliza Yesu swali.
2. Yesu anajibu mtafutaji.
3. Mtafutaji anaeleza jibu alilopewa na Yesu.
Hatua za Ombi Sikivu
1. Maskani ya Mkutano – Mtafutaji anamuuliza Yesu akutane nao mahali salama. Kila mtu ana mahali ambapo ni salama kukutana na Yesu moyoni mwake. Mungu ana mahala pake pa usalama hata katika nafsi za wanawe waliovunjika moyo.
Mwombezi anaomba: Asante Yesu kwa kuumba mahali salama ndani ya nafsi ya kila mtu ambapo twaweza kuanza hatua hizi za uponyaji. Naomba hivi sasa utuonyeshe mahali hapo katika maisha ya mtu huyu.
Muulize mtafutaji kile Yesu anachomuonyesha.
Mwombezi anaomba: Yesu muonyeshe __________ (jina la mtafutaji) jinsi unavyomuona. (taswira inayokuja kwa kawaida ni ile ya mtoto na mzazi ampendaye. Amani yaweza kupatikana)
2. Kutambua asili ya vidonda – Mwombeszi anaomba: “Bwana tuonyeshe asili ya vidonda unavyotaka kuponya.” Mungu anapomuongoza mtafutaji kutambua asili ya majeraha yake, huwa ni kumbukumbu ya tukio la hapo awali au kisa fulani cha taharuki. Nyakati hizo majeraha hutokea na jumbe kujikita katika mioyo. Hata baada ya kusahau matukio yenyewe, tunaishi maisha huku tukirudia hisia za majeraha hayo. Tunajifunza kuwa na hasira, hofu na kutamauka tukiwa bado wachanga .
Wakati mwingine anaweza kumshika mkono mtafutaji na kumpitisha kutoka kwenye chumba cha uchafu hadi kwenye majeraha. Nyakati nyingine hututangulia ili atuhakikishie kuna
114
#16 Uponyaji wa Machungu, Hisia na Kumbukumbu www.healingofthespirit.org
usalama. Mara nyingi Yesu huwaelekeza kwenye kumbukumbu na kuwahakikishia atakuwa nao hata kama hawawezi kumuona mara hiyo. Mtafutaji lazima ahisi tukio kadri wanapolikumbuka ili waone majera waliyoyapata.
3. Kiri – Kwa mtafutaji “ Una hisia gani katika tukio hili, uchungu, hofu, kuchanganyikiwa, hasira? Mwambie Yesu vile unavyosikia.” Mtafutaji akiwa wazi, Yesu huhuingia haraka kumsaidia.
4. Ufunuo wa Yesu. (tazama) “Bwana, neno lako latuambia hutatuwacha wala kutusahau . Umeahidi kuwa nasi wakati wote. Hebu fungua macho ya mioyo yetu? Tuwezeshe kukupata katika kumbukumbu hii.” Yesu ajapo hutakasa hisia maumivu, uongo, viapo ambavyo mtafutaji ameapa, udhalimu, aibu na masikitiko. Anatukaribisha kumpatia shida zetu zote (Zab 55:22, I Pet 5:7) Huifanya mioyo misafi na kutakasa miili yetu na maji safi (Heb 10:22)
5. Kuona - Tunapompata Yesu katika taswira ya kumbukumbu, tunamuuliza aingie kati ya mtafutaji na Yule aliyesababisha maumivu hayo au tukio lenyewe . Kisha tunamuuliza mtafutaji “Jee unataka Yesu akukumbatie?” Yaweza kuchukua muda kwake kuitikia, lakini maumivu yote yanapotoweka, wao hukimbilia mikono iliyo wazi ya Yesu.
Wanapokuwa kwenye mikono ya Yesu, subiri kwa muda kisha muulize mtafutaji “Je unataka kuangalia uso wa Yesu uone upendo alio nao kwako?” Mpe dakika chache kasha umhimize, anapotazama, muulize “Unaona nini usoni mwa Yesu?
6. Uponyaji wa Mtazamo wa Nafsi - Baada ya mtafutaji kutazama uso wa Yesu, muulize “Hebu muulize Yesu – unaona nini ukinitazama? Watafutaji wengi huwa na mtazamo mbaya wa kibinafsi unaohitaji kuponywa. Mada hii itazungumziwa kwa urefu kwenye sura yake.
7. uponyaji wa kumbukumbu inayofuatia – rudi kwenye eneo la mkutano na umuulize Yesu kumletea mtafutaji kumbukumbu nyingine inayofaa kuponywa. Fuata utaratibu ule ule uliozungumziwa hapo juu kwa kila kumbukumbu atakayoileta Yesu.
Vifaa (kulingana na kipaumbele)
1. Norma Dearing, The Healing Touch (Chosen Books, 2002). ISBN 0-8007-9302-1.
2. John and Paula Sanford, Healing the Wounded Spirit (Victory House, 1985). ISBN 0-932081-14-2.
3. John and Mark Sandford, Deliverance and Inner Healing (Chosen Books, 1992). ISBN 0-8007-9206-8Charles Kraft, Defeating Dark Angels (Servant Pub., 1992). ISBN 0-89283-773-X.
4. Ruth Stapelton, Gift of Inner Healing (Bantam, 1997). ISBN 0553102915.
5. Matthew and Dennis Linn, Healing of Memories (Paulist Press, 1974). ISBN 0809118548.
6. Barbara Shlemon Ryan, Healing Prayer (Servant Books, 2001). ISBN 1-56955-262-2.
115
#16 Uponyaji wa Machungu, Hisia na Kumbukumbu www.healingofthespirit.org
7. Charles Kraft, Deep Wounds, Deep Healing (Servant Publications, 1993). ISBN 0-89283-784-5.
8. David Seamands, Healing of Damaged Emotions (Chariot Victor Books, 1991). ISBN 0896939383.
9. Betty Tapscott, Inner Healing Through Healing of Memories (Box 19827, Houston, TX 77024, 1977).
10. Francis MacNutt, Healing (Bantan Books, 1974): 161-73. ISBN 0-87793-074-0. (Muhutasari mzuri katika kurasa chache)
11. Agnes Sanford, Healing Gifts of the Spirit (Lippincott Publishers, 1966, reprinted 1974). ISBN 087-981056-4.
12. John and Paula Sandford, Transformation of the Inner Man (Victory House, 1982). ISBN 0-932081-13-4.
13. John Wimber, Power Healing (Harper & Row, 1987). ISBN 0-06-069533-1.
14. Francis MacNutt, Deliverance From Evil Spirits: A Practical Manual (Chosen Books, 1955). ISBN0-8007-9232-7.
15. Brad Jersak, Can You Hear Me? (FreshWind Press 2003) ISBN 0-9833586-0-2 (Much of the information on Listening Prayer is taken from this resource)
116
# 17 Uponyaji Kutokana na Dhuluma ya Kimapenzi www.healingofthespirit.org
Uponyaji Kutokana na Dhuluma ya Kimapenzi
Inakadiriwa kwamba mwanamke mmoja kati ya wanne amewahi kudhulumiwa kima-penzi au kubakwa. Isitoshe, idadi hiyo inazidi kuongezeka. Dhuluma ya kimapenzi ni moja-wapo ya matukio yanayoleta uharibifu na kujeruhi hisia. Wahasiriwa hufadhaika sana kihisia na hubaki wazi kwa athari za giza kwa njia nyingi. Matukio kama hayo huharibu picha waliyo nayo kuhusu Mungu na husababisha kila aina ya matatizo ya kihisia, kiroho, na kimwili (kwa mfano, 50% watakuwa na majonzi, 33% watajaribu kujiua, 20% watatumia madawa ya ku-levya).
Unapoitia orodha ifuatayo, weka alama katika hali iliyokupata maishani.
Madhara Yanayotokana na Dhuluma ya Kimapenzi
1. Kuanza kuchanganyikiwa na kupoteza sura
2. Woga na wasiwasi mbalimbali kuonekana
3. Utumwa wa nafsi kuonekana
4. Unaanza kujiuliza ni kwa nini Mungu aliruhusu jambo hilo lifanyike
5. Unakuwa na hasira kwa wazazi na/au kwa Mungu, kwa sababu hawakukulinda
6. Kukataliwa hutokea, iwapo mhasiriwa hataaminiwa na wazazi
7. Mhasiriwa huhisi kwamba amesalitiwa iwapo mzazi alijua bali hakufanya jambo lolote
8. Uzinzi, au dhambi zengine za kimapenzi hujitokeza
9. Ugumu wa kuhusiana na kimapenzi na mwenzi wa ndoa huonekana
10. Ndoa zilizokosa kufaulu huonekana
11. Kila mara mhasiriwa hujihisi kwamba yeye ni mchafu na huona haya
12. Mhasiriwa huuchukia mwili wake
13. Mhasiriwa huamini kwamba yeye ndiye alisababisha kitendo hicho au makosa yalikuwa yake
14. Jinamizi hutokea
15. Kukata tamaa na/au majonzi hujitokeza
16. Hasira isiyoweza kudhibitiwa pamoja na ghadhabu hudhihirika
17. Tamaa huanza kujitokeza
18. Mhasiriwa huhisi upweke na/au kuachwa
19. Mhasiriwa hutaka kukimbia, kujitenga, kujificha
20. Mhasiriwa huhisi kwamba amepoteza usafi wake
21. Mhasiriwa huwa na hisia za hatia, kusalitiwa, na kuhukumiwa
22. Mhasiriwa huhisi kuwa ametumiwa vibaya na amekuwa mchafu
23. Mhasiriwa huonyesha hisia kinzani k.m kupenda pamoja na kuchukia wakati mmoja
Mambo Yanayohitajika Ili Kupata Uponyaji Kutokana na Dhuluma ya Kimapenzi (Fahamu kwamba uponyaji wa ndani unaweza kuhitajika kwanza kabla ya mtu kuweza kusamehe.)
1. Kumsamehe mdhulumu/wadhulumu
2. Kusamehe mzazi/wazazi kwa kutomlinda
3. Kumsamehe Mungu
4. Kumsamehe mtu yeyote aliyekataa kuamini kwamba jambo hilo lilifanyika
5. Kujisamehe
6. Mwombe Mungu amsamehe mdhulumu na uombe msamaha kwa niaba ya mdhulumu huyo
7. Omba na kuvunja viapo vyovyote vilivyotamkwa na mtu huyo kuhusu kutowaruhusu wa-naume (au watu wa jinsia moja na mdhulumu) kusonga karibu na mhasiriwa huyo
8. Soma Zaburi 139, kumlazimisha mtu huyo kufahamu kwamba tumeumbwa kwa njia ya ajabu
117
# 17 Uponyaji Kutokana na Dhuluma ya Kimapenzi www.healingofthespirit.org
Ombi la Uponyaji wa Ndani kwa ajli ya Dhuluma ya Kimapenzi (fuata hatua zifuatazo)
1. Omba ukimwambia Yesu alete akilini tukio linalohitaji uponyaji
2. Mwambie Yesu awe katika tukio hilo
3. Weka msalaba wa Yesu katikati ya mdhulumu na mdhulumiwa
4. Ngoja mpaka Yesu amshikilie mhasiriwa
5. Mpe Yesu hisia zote
6. Kwa kutumia upanga wa Roho, iweke huru roho ya mhasiriwa kutoka kwa mtu aliyemdhulumu, vunja mapatano ya nafsi
7. Omba ili hisia zote zilizojeruhiwa ziweze kuponywa
8. Omba ili ukweli uweze kujulikana badala ya uwongo
9. Omba ili kuwe na uponyaji kutokana na woga, hofu, kuchanganyikiwa, maumivu, ku-jeruhiwa, hasira, hatia, aibu, na uchafu.
10. Fukuza roho zote zinazohusika (kwa mfano, kiwewe, tamaa, woga, hasira, chuki, ku-kataliwa, kujikataa, kujichukia, roho ya kumchukia mwanamume au mwanamke, roho ya kumchukia Mungu, picha za kumpa mtu ashiki, kutokuwa na thamani—na hali ikiwa mbaya zaidi, ukahaba, kutoa mimba, kifo, kujiua, usenge, usagaji)
11. Omba kwamba dhuluma hiyo itakoma katika ukoo wa kizazi chenu (kwa mfano, watu wanaodhulumiwa hudhulumu: watu walioumizwa huwaumiza wengine)
Ombi la Kupata Uponyaji Kutokana na Dhuluma ya Kimapenzi (imetolewa ili kutumiwa kwa wanawake lakini inaweza kugeuzwa iwapo kuna haja ya kufanya hivyo)
Mwombezi anatakiwa kuomba hivi:
Bwana, asante kwa kumpenda _______________ na kwa kutaka sana kumweka huru. Ulihuzunika aliposumbuliwa kwa njia isiyo ya haki na umeubeba uchungu wake na masikitiko yake moyoni mwako kwa miaka hii yote.
Bwana, tunakualika hivi sasa ili uingie ndani ya moyo wake ambapo nafsi yake ya msi-chana mdogo iliyohisi kwamba ana uoga mwingi, ni mchafu sana, ametumiwa sana, na ameai-bishwa. Mimina upendo wako kamilifu ndani ya moyo wake ili kuondoa woga wote. Nena na moyo wake ili aweze kujua kwamba unamkubali na unampenda vile alivyo, na kwamba hakuna anavyoweza kuupoteza upendo huo. Bwana, chukua uchungu wake wote pamoja na aibu, na uyafunike majeraha yake yote kwa mafuta yako ya uponyaji. Katika jina la Yesu ninaomba. Amina.
Baada ya maombi ya kuliponya tukio hilo na kufukuza roho wa giza kufanyika, huenda watu wengi wakaendelea kuhisi kwamba wao ni wachafu; katika hali hiyo mhusika anatakiwa kusomewa maandiko yafuatayo halafu umwombee ombi la utakaso.
Maandiko ya Utakaso
• “Nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtatakata uchafu wenu wote na sanamu za miungu yenu yote” (Eze. 36:25).
• “…Usiviite najisi vitu ambavyo Mungu” (Matendo 11:9).
• “… sisi tunatakaswa dhambi [kufanywa watakatifu] zetu kwa ile dhabihu ya mwili wake aliyotoa mara moja tu, ikatosha” (Ebr. 10:10).
118
# 17 Uponyaji Kutokana na Dhuluma ya Kimapenzi www.healingofthespirit.org
• Ombi ili Mungu amnyunyizie mtu huyo maji safi (wakati mwingine Bwana atakuonyesha picha—omba kuhusu unachoona katika picha hiyo).
Ombi la Kutakaswa Kutokana na Dhuluma ya Kimapenzi
Mwombezi anatakiwa kuomba kwamba:
Bwana Yesu, tunakuomba sasa uyamimine maji yako ya uzima juu ya ____________ na katika kila chembe ya nafsi yake. Tunaomba maji hayo yamiminike juu ya kila sehemu: kichwa, mikono, mwili, sehemu za siri, miguu, na nyayo.
Asante Bwana kwa sababu maji yako ya uzima yanamsafisha ili awe “mweupe kama theluji”—na kwamba kila hali ya unajisi, aibu, na hatia inasafisha na kuondolewa. Asante kwa kumfanya kuwa safi ndani na nje.
Bwana, sasa unamwona kuwa safi na mweupe kama alivyokuwa siku uliyomuumba mbinguni. Sasa ana mwili mpya ndani ya Yesu, amefanywa kuwa safi na mwenye kukosa doa. Katika jina la Yesu ninaomba. Amina.
Vifaa
1. Paula Sandford, Healing Victims of Sexual Abuse (Victory House, 1988). ISBN 0-932081-21-5.
2. Doris Wagner, Ministering Freedom to the Sexually Broken (Wagner Publications, 2003). ISBN 1-58502-038-9.
3. Jan Frank, Door of Hope (Nelson Books, 1995). ISBN 0785279660.
4. www.gospelcom.net/mlm/index.htm (healing sexual brokenness)
119
# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa www.healingofthespirit.org
Uponyaji Kutokana na Kukataliwa
Kukataliwa ni mojawapo ya mitindo ya Shetani ya ukandamizaji. Kukataliwa kunaweza kumzuia mwenye dhambi kumjia Mungu ili apate wokovu na kumzuia Mkristo kuufikia uwezo wake wa kuwa ndani ya Mungu; hudhoofisha, huvunja, na kuzuia uhusiano mwema kati ya watu wa familia moja, wanandoa, wafanyakazi, na marafiki. Pia huibadilisha sifa ya Mungu kama baba wa mbinguni mwenye upendo anayetupenda na kututakia mema.
Kamusi ya Kiingereza inaeleza kwamba Kukataliwa “ni kitendo cha kutupa au kuacha mtu au kitu” inayoonyesha kwamba mtu au kitu hicho kilichotupwa hakina thamani. Kwa hivyo, kukataliwa hutufanya tuhisi kwamba hatuna thamani au hatustahili.
Kunyimwa upendo—ambayo ni hali nyingine ya kukataliwa—huwa ni kiini cha kukataliwa. Kukataliwa(kunakotendeka au kusikotendeka wazi, kwa kweli au kwa kudhania) humnyima Yesu Kristo nafasi yake halali katika maisha ya watoto wake na huwazuia waumini kuhisi uchangamfu na thamani ya maisha inayoweza kutolewa na Yesu pekee.
Kukataliwa husababisha majeraha moyoni—wakati mwingine huwa na uchungu mwingi mpaka akili ikakataa kuushughulikia, nasi huuzika katika akili yetu iliyofichika. Baadaye, jambo hilo hujitokeza katika njia zengine zinazotuletea matatizo. Kukataliwa ni maradhi yasiyotambuliwa na pia yasiyotibiwa kwa urahisi katika Mwili wa Kristo siku hizi. Jambo la kusikitisha ni kwamba, idadi kubwa ya watu wanaoenda kuombewa huwa na tatizo la hisia za kukataliwa.
Dalili za Kukataliwa
Je, wewe hujiona vipi? (Tia mviringo katika maelezo yanayohusika)
kuwa na thamani ya chini kutokuwa salama nafsi ya kujitenga
kujihukumu kujichukia furahisha wengine
duni naamini nimeshindwa kuteseka sana moyoni
kujiona mtu wa chini kuhoji sura yangu kuonyesha sura ya unafiki
kuhitaji sana upendo mzinzi mwenye shaka
asiyestahili kuogopa kukataliwa sijijui
kutafuta kibali kujikataa kuhisi nimeachwa
kujishutumu kutokubali upendo mwenye majonzi
siwezi kupenda uchungu/maumivu ya ndani siwezi kumpenda mwenzi
hakuna uhusiano unaodumu kufanya bidii ili niweze kukubaliwa
Chanzo cha Kukataliwa (Muhtasari)
Kiini kinachosababisha kukataliwa kinaweza kupatikana kutoka kwa asili moja au ziaid kati ya hizi zilizoorodheshwa hapa chini (maelezo kamili ya kila mojawapo yametolewa):
1. Kukataliwa kwa urithi
2. Kukataliwa kwa kizazi
3. Wakati na hali ya kushika mimba
4. Matukio na mtazamo wa mama au baba wakati wa mimba
4A. Hali inayoweza kusababisha kukataliwa mtoto akiwa tumboni
4B. Matokeo ya kukataliwa yanayojitokeza ndani ya mimba
5. Kukataliwa kunakosabibishwa na aina ya kuzaliwa
120
# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa www.healingofthespirit.org
6. Mtoto kukosa kuunganishwa na mama au baba yake
7. Sababu za kukataliwa baada ya kuzaliwa
7A. Dalili za kukataliwa baada ya kuzaliwa
8. Mtoto wa kupangwa, au kulazimishwa kuishi na watu wa ukoo wako au katika nyumba ya kukuza watoto, au kuishi katika tamaduni tofauti.
8A. Uponyaji kutokana na athari za kitendo cha kumpanga mtoto
9. Hali inayosababisha kukataliwa wakati wa utotoni
10. Matatizo shuleni yanayosababishwa na walimu au wanafunzi (yanayoweza kusababisha ku-kataliwa)
11. Sababu nyingi za kukataliwa zinazojitokeza baadaye maishani
12. Hali zinazosababisha kukataliwa katika ndoa
1. Kukataliwa kwa urithi: Shetani ni baba wa kukataliwa. Kukataliwa kulianzishwa na kitendo cha Shetani kumjaribu Hawa na hatimaye Adamu. Hakukuwa na Kukataliwa kabla ya maja-ribu ya shetani, kwani "… Mungu akaona kila kitu alichofanya kuwa ni chema kabisa" (Mwa. 1:31). Kwa kukubali pendekezo la Shetani la kula tunda walilokatazwa, Adamu na Hawa walimkataa Mungu na wakaingia katika uasi na dhambi. Walikuwa na tamaa (ya kile kitu wa-lichoambiwa na Shetani kwamba Mungu alikuwa amewanyima) na ukaidi (kwa kufanya kitu walichokuwa wamewekewa mipaka na Mungu).
Kutokana na hayo, walikataliwa na Mungu, wakalaaniwa, na wakaamriwa kuondoka katika Bustani. Hawa (na wanawake wote) waliahidiwa kwamba kwa uchungu watazaa wato-to na watatawaliwa na waume zao. Mungu aliilaani ardhi na akamwambia Adamu kwamba angeipata riziki yake kwa jasho (Mwa. 3:16-19). Mungu hakuwasiliana nao tena kama ali-vyofanya hapo awali.
Adamu na Hawa walitenda kitu kinachojulikana kwa jumla kama dhambi ya kwan-za. Kwa hivyo, watoto wote waliozaliwa nao (na vizazi vyao) walirithi dhambi hiyo kama ukoo wa kiroho, na hivyo basi kuigeuza dhambi ya kwanza kuwa dhambi ya urithi. Kuto-kea hapo, kizazi chote cha wanadamu kimekuwa na hali hiyohiyo ya dhambi; vilevile, laana ya kukataliwa na adhabu ya kifo cha kiroho imerithishwa kwa njia ya kushika mimba na kuzaliwa (Rum. 5:12).
Kaini, aliyekuwa mtoto wa kwanza kuzaliwa, alikuwa wa kwanza kupokea laana ya “dhambi ya urithi.” Alikuwa mkaidi, mbishi, na hakutoa sadaka inayofaa, kama alivyohitaji Mungu. Alimkataa Mungu na Mungu akamkataa Kaini. Kwa sababu Kaini “aliongozwa na yule mwovu” (1 Yohana 3:12). Iwapo tutafikira juu ya vile Shetani anaweza kuwatawala wa-nadamu kwa hila ili wahisi kwamba wamekataliwa ni lazima tuanze na Kaini.
Ingawaje Kaini na Abeli walizaliwa na hali ya kukataliwa kwa urithi, Kaini ndiye aliyeathiriwa sana. Mungu alizungumza na Kaini ili amhimize kufanya uamuzi bora: "Mwe-nyezi Mungu akamwambia Kaini…Je, ukitenda vyema hutakubaliwa?” (Mwa. 4:7). Kaini alipewa nafasi nyingine lakini aliikataa.
Kutokana na uamuzi wa Kaini na hatimaye kitendo cha kumuua ndugu yake, Mungu alimkataa na akamlaani, ndiyo maana watu wengine huita kukataliwa “Dalili za Ugonjwa wa Kaini.” Kujihurumia kwa Kaini, kumlaumu Mungu eti alitenda mambo kupita kiasi, kuogopa kukataliwa, uonevu, kifo, na kuachwa (Mwa. 4:13-14) kunatusaidia kuelewa kadiri ya dalili za watu wengi wenye tatizo la kukataliwa katika nyakati hizi. (Kwa maelezo zaidi ya “Dalili za Ugonjwa wa Kaini.” Soma kitabu hiki, “Excuse Me, Your Rejection is Showing,” ambacho mambo mengi katika sehemu hii yametolewa humo.)
121
# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa www.healingofthespirit.org
2. Kukataliwa kwa kizazi: Kutokana na kifungu kilicho hapo juu tunaona kwamba vizazi vyote vya Adamu na Kaini vinaelekea kuwa na kukataliwa kwa urithi. Kwa hali yoyote, sio watu wote hurithi roho wa kukataliwa. Sadaka ya Abeli ilikubaliwa na Bwana. Kama tutaka-vyoona katika sehemu za baadaye, laana zote zina masharti. Tukikosa kutii laana zote zi-lizoahidiwa hutufuata (Kumb. 28 na 30). Kaini alipokea laana ya kukataliwa (kwa sababu ya uwezekano wa kuweko kwa kukataliwa kwa urithi na dhambi yake ya kukosa kutii na ukaidi) ilhali Abeli hakufanya hivyo.
Dhambi ya kizazi imejadiliwa kinaganaga katika sehemu inayoeleza juu ya “Uponya-ji kutokana na Athari za Kizazi.” Tuseme kwamba mababu zetu wa zamani walipokosa kutii, walipata laana (kukataliwa) nayo inaendelea kupitishwa kama laana ya kukataliwa kwa wa-toto wote kwa kizazi cha tatu na hata cha nne, kama ilivyotajwa katika Kutoka 20:5 " . . . mimi Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana maovuya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao."
Watu ambao huja kuombea wanapopitia dalili za mababu zao, wengi woa hugundua kwamba mama na baba zao, babu/nyanya au shangazi na wajomba pia hudhirisha dalili za kuwa na laana ya kukataliwa.
(Maelezo yaliyo hapo juu ni habari ya kimsingi kuhusu vile kukataliwa huanza.)
3. Wakati na hali ya kushika mimba: Zifuatazo ni njia maalum ambazo kukataliwa kunaweza kuanza katika mtu fulani. Omba ili Bwana akuonyeshe chanzo cha kukataliwa katika maisha yako. Weka alama katika maelezo yote unayodhani yanakuhusu wewe:
3a. Mzazi wangu mmoja au wote wawili hawakutaka mimba
3b. Wazazi wangu hawajaoana
3c. Kushika mimba kulitokea baada ya kitendo cha “kufanya mapenzi mara moja kwa mara ya kwanza” au kupitia kwa kitendo cha kuzini
3d. Mama alikuwa mdogo sana na hakuwa amejitayarisha kuwa mama
3e. Hakukuwa na pesa za kutosheleza mahitaji ya mtoto
3f. Dhuluma ya kimapenzi, ubakazi, kujamiiana kati ya watu wenye uhusiano wa kida-mu.
4. Matukio na mtazamo wa mama au baba wakati wa mimba: Katika kitabu kiit
wacho “The Secret Life of the Unborn Child” (Thomas Verney, MD ISBN 0-440 50565-8), mwandishi wa kitabu ananukuu utafiti kuhusu mambo ambayo watoto walio tumboni wana-weza kufanya:
4a. Kusikia
4b. Kupendelea muziki fulani
4c. Kuhisi upendo au kutopendwa na mama
4d. Kujua sauti ya baba na ya mama
4e. Kuwa na wasiwasi mama akivuta sigara
4f. Kuonyesha hisia fulani mama akijaribu kufikiria juu ya sigara.
4g. Kuwa na uwezo wa kukumbuka
4h. Kufanya uamuzi wa vile atatenda mambo baada ya kuzaliwa (kama vile kukataa kuunganishwa na mama)
4i. Kukumbuka kiwewe chochote alichopata kabla ya kuzaliwa au wakati wa kuzaliwa
4j. Kuwa na msimamo na tabia zake binafsi
4k. Kukataa kunyonya (kwa sababu ya kukataliwa alipokuwa tumboni)
122
# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa www.healingofthespirit.org
4l. Kuonyesha hasira kubwa (iwapo baba yake alitoweka nyumbani au mama alifanya uzinzi na watu wengine, au mtoto huyo alikuwa ni tokeo la kitendo cha kufanya ma-penzi nje ya ndoa)
4m. Huhisi kukataliwa ikiwa baba hayuko au haonyeshi dalili za kujali
4n. Woga wa mama hupitishwa kwake
4o. Huona hatia kuwa ndani ya tumbo
4p. Huwa mtu wa kutekeleza mambo (kupata haki ya kuishi)
4q. Kuwajibika kwa ajili ya matatizo ya mimba ("nikikua, huenda nikamuumiza mama")
4r. Kufanya jambo fulani (kugeuka tumboni) ili awe chini ya mkono wa mama akiuweka juu ya tumbo.
4A. Hali inayoweza kusababisha kukataliwa mtoto akiwa tumboni
1. Jaribio la kutoa mimba
2. Mama hakutaka kupata mimba
3. Utumiaji wa madawa ya kulevya, pombe, au tumbako mama akiwa na mimba
4. Kufanya mpango wa kumpeleka mtoto ili awe mwana wa kupangwa
5. Wazazi kuoana kwa sababu mama ameshika mimba
6. Mtoto angetolewa tumboni (iwapo sheria ingehalalisha kitendo hicho)
7. Mama kuwa chuki na kuudhika kwa vile alikosa nafasi fulani kwa ajili ya kuwa na mimba
8. Mama kuwa mgonjwa akiwa na mimba
9. Mama alikuwa na ajali au jeraha akiwa na mimba
10. Mama kumpoteza mpendwa wake akiwa na mimba
11. Kuwa na matatizo wakati wa kujifungua au kujifungua wakati kuna tukio la kusaba-bisha kiwewe
12. Mama alimtaka mtoto wa jinsia fulani na akapata wa jinsia tofauti
13. Hisia kinzani (wakati mbaya, kutokuweko na pesa, baba kuwa katiak jeshi, mama akiwa shuleni, n.k.)
14. Mama na baba wakiwa na uhusiano mbaya
4B. Matokeo ya kukataliwa yanayojitokeza ndani ya mimba
1. Kulia bila kukoma
2. Kuwa na hamaki wakati wa kutumia chombo cha mtoto cha kwendea haja
3. Kukataa kunyonya
4. Kukataa kuliwazwa na mama
5. Kuona hatia kwa kuwa ndani ya tumbo
6. Anahisi “mimi sitakiwi; mimi ni mzigo”
7. Hujitahidi ili aweze kutekeleza mambo (“lazima niwaonyeshe kwamba ninaweza; la-zima nipate upendo wao”)
8. Kila mara hujitahidi kuwafurahisha watu
9. Hukataa kupendwa
10. Hutamani asingezaliwa
11. Huwa na matatizo ya kuungana na watu wengien kirafiki
5. Kukataliwa kunakosabibishwa na aina ya kuzaliwa
5a. Kuwa na maumivu marefu
5b. Muda wa mimba kuzidi kiasi
5c. Kupasuliwa wakati wa kuzaa
123
# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa www.healingofthespirit.org
5d. Watoto kuzaliwa na wanawake ambao hawakujua wana mimba
5e. Maumivu ya kulazimishwa au kumlazimisha mtoto kutoka
6. Mtoto kukosa kuunganishwa na mama au baba yake
6a. Mtoto kukosa kubebwa au kupendwa vilivyo na mzazi mmoja au na wazazi wote wawili
6b. Mama kuwa mgonjwa mtoto akiwa bado mchanga
6c. Kulazwa hospitalini
6d. Ugonjwa au afya mbaya ya mtoto
6e. Mama kuwa na mashaka kuhusu uwezo wa kuwa mama
6f. Kufanyiwa dhuluma ya kimwili
6g. Ugonjwa wa kimatibabu unaosabisha matatizo ya kula
7. Sababu za Kukataliwa baada ya Kuzaliwa
7a. Kukosa upendo
7b. Kufananishwa na mtoto mwingine
7c. Kutohisi kwamba yeye ni mzuri kiasi cha kutosha
7d. Dhuluma ya aina yoyote
7e. Ukosoaji
7f. Woga
7g. Mtoto kupangwa
7h. Kuchekwa na watoto shuleni, majirani, n.k.
7i. Ulemavu wa kimwili
7j. Kujaribu kupata upendo kwa kufanya mambo fulani
7k. Kujua kwamba mama aliitoa mimba ya ndugu ya mtoto huyo au kulikuwa na kuhari-bika kwa mimba
7l. Mtoto kuhisi kwamba hastahili; hakuna anayemjali mtoto
7m. Mmoja wa wazazi au wazazi wote wawili kutokuweko
7n. Wazazi kutengana
7o. Mzazi mmoja kuiacha familia
7p. Tukio la Vitaa Vikuu vya Pili vya Dunia lilionyesha:
• Uingereza ilijenga nyumba za mayatima kwa watoto ambao mama na baba zao walikufa katika vita hivyo.
• Theluthi moja ya watoto hao walikufa bila sababu yoyote au kwa sababu mioyo yao iliwacha kupiga.
• Wengine hawakuweza kukua, hawakuweza kula, au vichwa vyao vilikua lakini miili haikuweza kukua.
• Watoto hao walionekana kama wazee wadogo, waliokuwa na ngozi ya kijivu.
• Walikosa upendo; wanawake wachanga Uingereza walialikwa kuwabeba, kuwa-bembeleza na kuwalisha.
• Tukio hilo lilithibitisha kwamba ni kweli hitaji letu la upendo ni kubwa kuliko hitaji la chakula na hali ya kuendelea kuishi.
7A. Dalili za kukataliwa baada ya kuzaliwa
1. Kuamini uwongo wanaoambiwa na watu wengine na wanaojiambia wenyewe.
2. Hisia za umasihi ("Lazima nimpendeze Mungu la sivyo hatanipenda.")
3. Huwa hawakubaliwi vile walivyo—bali wao hukubaliwa tu kwa sababu ya mambo ambayo waliyotimiza, kwa yale waliyofanya.
4. Husifu bila kukubali: wao huzingatia mambo ambayo mtu amefanya bali sio kuzinga-tia mtu mwenyewe
124
# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa www.healingofthespirit.org
5. Wengi huona haya kwa ajili ya miili yao.
6. Wengi huishia kutawaliwa na ubaya au kufanya vitu vinavyobadilisha hali ya moyo (kula, TV, kazi, mazoezi, dini, pombe)
7. Wengi hujichukia, hulaani sehemu zao zengine, au huongeza uzito ili wasiweze ku-wavutia wanaume
8. Wengine hutaka kusifiwa kila wakati au hutaka kutimiza makubwa.
8. Mtoto wa kupangwa, au kulazimishwa kuishi na watu wa jamii yake au katika nyumba ya kukuza watoto, au kuishi katika tamaduni tofauti.
8a. Husababisha hisia za kuachwa na kukataliwa pia pamoja na kuogopa kukataliwa.
8b. Watoto wanaotoka katika kabila fulani kupata malezi katika tamaduni iliyo tofauti
8c. Kupelekwa katika shule ya bweni
8d. Hufungua mwanya wa roho ya kuachwa, uzururaji, kukataliwa, na ya kuchanganyi-kiwa kumwingia mtu huyo
8A. Athari za kitendo cha kupanga mtoto
1. Huenda watoto wa kupanga wasijue habari nyingi kuhusu wazazi wao au maisha yao ya utotoni; tumia habari uliyonayo na umtegemee Roho Mtakatifu ajaze mapengo.
2. Katika kila hali, watoto wa kupangwa hujaa hisia za kukataliwa, hukosa kujithamini, huwa na hasira, na masuala ya kuachwa.
3. Wao wametekwa na vitu vyote vilivyo katika mazingira yao (woga, hangaiko, wasi-wasi, hatia, aibu, kuchanganyikiwa, chuki, hasiri, na uchungu wa mama yao).
4. Wao hukosa usalama, hukosa kutunzwa na kusaidiwa vilivyo.
5. Watapoteza sifa zao na watakuwa wakijiuliza iwapo wana haki ya kuishi.
6. Wao hudhani kwamba wana kasoro fulani.
7. Wao huamini uwongo (kwa mfano, “Mimi nina sura mbaya, mimi ni ovyo, mimi ni kosa lililofanyika….”).
8. Wao hukabiliana na maisha kwa kutumia hasira na uasi au kwa woga na kujitenga.
9. Maombi ya kuwaombea watu waliofanywa wana wa kupangwa yanatakiwa kuwa na uvunjaji wa kifungo na muungano wa nafsi kati ya mtu huyo na mamake mzazi.
9. Hali inayosababisha kukataliwa wakati wa utotoni
9a. Mtoto anayekosolewa, anayeadhibiwa kupita kiasi, anayeonewa, anayepuuzwa, au anayependelewa (au aliye katika familia moja na ndugu anayependelewa)
9b. Wazazi kukaripiana mara kwa mara mbele ya watoto wao
9c. Mazungumzo ya kutengana au kupeana talaka, ambayo humfanya mtoto ajilaumu kwa kuwaletea wazazi wake shida
9d. Wazazi wanaowasiliana kupitia kwa watoto pekee
9e. Kuwa na baba mkali, mwenye sheria nyingi na anayeadhibu kupita kiasi
9f. Kina baba wasio kuwa na msimamo thabiti, wasiojali, na wanaotawaliwa na wake zao
9g. Baba au mama mlevi
9h. Kuwa na ndugu wa kiume au wa kike aliye mgonjwa na anayehitaji kushughulikiwa kila zaidi
125
# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa www.healingofthespirit.org
9i. Kusikia maoni ya yanayoumiza (kwa mfano, “Hata sikukutaka wewe” au “Wewe ni mjinga.”)
9j. Dhuluma ya kimwili, kimazungumzo, au kimapenzi inayofanywa na wazazi, marafi-ki, au watu wengine wanaoonekana katika mazingira ya nyumbani mara kwa mara
9k. Mtoto kudanganyiwa kuwa amefanya kitu ilhali kilifanywa na ndugu yake, n.k. (sua-la la uaminfu hutokea)
9l. Kulazimishwa kufaulu kimasomo (hongo ya kufaulu kimasomo)
9m. Kupatikana na moto au tetemeko la ardhi linaloharibu nyumba ya familia yenu
9n. Kuhukumiwa au kufungwa kwa mtu wa familia yenu
9o. Kushuka kwa kiwango cha maisha ya familia yenu—kulikosababishwa na kichwa cha familia kufutwa kazi, kufilisika, n.k.
9p. Kuwa na kipindi kirefu cha upweke kwa sababu ya wazazi kutojali
9q. Kutokuweko kwa wazazi katika shughuli zisizo za kimasomo za shule ya mtoto
9r. Ugumu wa lugha ya nchi ya uhamiaji
9s. Ugonjwa
9t. Kujaziwa mno majukumu ya kinyumbani
9u. Adhabu kali au ya kikatili
9v. Mzazi mmoja au wote walitaka mtoto wa jinsia tofauti na yule waliyempata
10. Matatizo shuleni yanayosababishwa na walimu au wanafunzi (yanayoweza kusababisha kukataliwa)
10a. Ulemavu wa mwili unaomfanya mtoto kutochaguliwa katika shughuli za timu au ku-zuiwa kujihusisha na michezo
10b. Matatizo ya kuzungumza, kasoro alizozaliwa nazo mtu, kitembe
10c. Ulemavu wa kimasomo
10d. Kuchokozwa, kuonewa, kusumbuliwa kimapenzi
10e. Kufukuzwa shuleni kabisa
10f. Kubandikwa jina la uchokozi
10g. Kutoaminiwa na walimu
10h. Kuonewa na walimu
10i. Rekodi ya kimasomo ya ndugu au dada mkubwa kutumiwa dhidi yako
10j. Matatizo ya kusikia au kuona
10k. Kuona aibu kwa ajili ya jinsi yako
11. Sababu nyingi za kukataliwa zinazojitokeza baadaye maishani
11a. Umaskini katika familia
11b. Matukio ya kimapenzi yasiyostahili yanayofanyika mapema maishani
11c. Kutoa mimba (kulikopangwa au kulikolazimishwa)
11d. Kujikataa mwenyewe (kunakofanyika kwa sababu ya kuona aibu kwa ajili ya sehemu za mwili zisizopendeza, unene, n.k.)
11e. Kukataliwa katika uhusiano au kuvunjika kwa uchumba
11f. Kuwa mgonjwa au kuwa mgonjwa kitandani kwa muda mrefu
11g. Matatizo mengi ambayo mtu hawezi kuyavumilia
11h. Kujihukumu mwenyewe baada ya kufanya mambo mabaya
126
# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa www.healingofthespirit.org
12. Hali zinazosababisha kukataliwa katika ndoa
12a. Mwenzi wa ndoa kukosa maadili (au kutokuwa mwaminifu)
12b. Mwenzi mmoja au wote wawili kutokuwa na uwezo wa kuwasiliana vizuri
12c. Mwenzi mmoja kuwa mtawala au kuwa mchoyo kifedha
12d. Mzazi mmoja kumtetea mtoto (dhidi ya mzazi mwingine)
12e. Mwenzi mmoja kukataa uhusiano wa kingono
12f. Mwenzi mmoja akiugua kwa muda mrefu (kama vile kansa)
12g. Kifo cha mwenzi mmoja au mtoto
12h. Talaka au kutengana
12i. Kutoweza kupata watoto
12j. Mume kufa bila kuandika wosia
Sababu moja kuongezea kwa nyingine
Si rahisi kuwa na sababu moja pekee ya kukataliwa katika kuumizwa kwa mtu. Watu wengi huumizwa kwa njia mbalimbali, njia moja ikiongezea juu ya uchungu na maumivu yaliyoko. Kwa hivyo, mtu huyo huwa na kukataliwa kuliko ongezwa juu ya kwingine, na hivyo kuongeza shida iliyoko. Kwa hali yoyote, huwa kuna mzizi unaotakiwa kutambuliwa kabla ya kufanya ombi la upo-nyaji. Ingawaje watu wengi wanaofika kuombewa huwa wana kukataliwa kunakotokana na vizazi vilivyopita (kwa ajili ya athari za giza zilizojadiliwa hapo awali), mara nyingi huwa kuna sababu nyingine iliyokuweko kabla, wakati wa, au muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Roho ya Kukataliwa yenye sehemu nyingi
Ni nadra sana kwa laana ya roho ya kukataliwa kutambuliwa ikiwa pekee yake, kwani mara nyingi huwa imeambatana na na roho mmoja au roho nyingi za kujikataa mwenyewe, kuogopa kuka-taliwa, kuogopa kuachwa, woga, na kukataliwa kunakotambulika. Katika hali nyingi, mhusika huwa amewakataa wazazi wake, au watu wengine (pamoja na kujikataa yeye mwenyewe na Mungu), kwa kukosa kufanya jambo lolote la kuzuia maumivu na uchungu waliopata utotoni. Mhusika aliyejeruhi-wa huuzingira moyo wake kwa kujenga ukuta wa kihisia naye huapa, kwa kusema, “hakuna mtu ata-kayeniumiza tena” (viapo vimeelezwa kinaganaga katika sehemu iliyo na kichwa hiki, “Uponyaji ku-tokana na Viapo na Matamanio ya Kufa”). Watu wanaokuwa na aina mbaya ya kukataliwa wakati mwingine huwa na sifa mbalimbali au hubadili nafsi kama njia moja ya kujikilinda kihisia.
Dhihirisho wazi au dalili za kukataliwa (pamoja na roho zinazohusiana) humfanya mtu afanye mambo makuu mawili: (1) kuwa na uchokozi (kunakodhihirika kwa uasi, uzinzi, kujitoshele-za, hasira, kuwakataa wengine, uwongo, na/au kutojali) au (2) kutenda mambo kwa kutoonyesha hisia (kunakodhihirisha hali ya kutafuta kibali, kunyenyekea, upweke, na/au majonzi.)
Kuiponya hali ya Kukataliwa
kuna mifano mingi ya kukataliwa iliyoonyeshwa katika Biblia. Yesu alikataliwa kuliko mtu yeyote aliyewahi kuishi duniani. Alizaliwa horini mwa ng’ombe maili 70 mbali na nyumbani kwao. Alizaliwa na mama aliyekuwa ameposwa—na hakuwa ameolewa—bikira. Alipokuwa mdogo, waza-zi wake walikimbilia Misri ili asiuwawe. Wazazi wake walikosa kumwelewa alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, na ndugu zake wa kambo walimtatiza. Mafundisho yake yalikataliwa na watu waliokuwa katika mji wake na aliweza tu kuwaponya wagonjwa wachache katika mji huo. Watu wa mji huo walijaribu kumuua. Viongozi Wayahudi wa kidini na kisiasa walimkataa. Umati wa Kiyahudi ulimkataa. Wasimamizi wa Kirumi pia walimkataa, na pia wengi wa wanafunzi wake walimkataa na kumwacha. Isaya 53:3 inasema, “Alidharauliwa na kukataliwa na watu.”
127
# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa www.healingofthespirit.org
Maandiko mengine pia yananena juu ya kukataliwa kwa Yesu (Mat. 21:42, Zab. 118:22-23, Luka 9:22, Marko 8:31, Luka 17:25). Hata alipokuwa msalabani, inasemekana kwamba Yesu ali-muuliza Baba yake kwa nini alikuwa amemkataa, kama alivyosema katika maneno yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” (Mat. 27:46). Alizaliwa katikati ya mifugo, akasulubiwa katikati ya wahalifu, alizungukwa na umati uliokuwa katili. Lakini Yesu, Mwana wa Mungu, aliwa-wezesha “wana wa mwanadamu” wafanyike kuwa “wana wa Mungu” kwa Kufa kwa ajili ya dhambi zetu, magonjwa yetu, huzuni yetu, mateso yetu, na kudharauliwa na kukataliwa kwetu na wanadamu. “Hata hivyo alivumilia majonzi yetu, na kubeba huzuni zetu. Sisi tulifikiri amepata adhabu, amepig-wa na Mungu na kuteswa. Lakini alijeruhiwa kwa sababu ya dhambi zetu, aliumizwa kwa sababu ya maovu yetu. Kwa kuadhibiwa kwake sisi tumepata uhai; kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” (Isa. 53:4-5).
“Kwa kupigwa kwake” tumepona, pia tumepona kutokana na kukataliwa. Hiki ni kipawa kilichowezesha na kifo chake msalabani—sawa na msamaha wa dhambi zetu, uponyaji wa magonjwa yetu, na kupewa mamlaka juu ya adui. Nacho hupokewa kwa imani, sawa na ahadi zake zote.
Kinyume cha “kukataa” ni “kukubali.” “Ametujalia katika Mwanae mpenzi” (Efe. 1:6). Ka-tika Kigriki, neno kujaliwa (kama lilivyotumiwa hapa) lina maana ya “anayependwa sana." Tuna-poenda kwa Mungu kupitia kwa Yesu, huwa tunajaliwa au tunakubaliwa na kupendwa sana kama ndugu yetu Yesu.
(Kwa mafunzo zaidi kuhusu kukataliwa, soma na kufikiri juu ya maandiko yafuatayo: Zab. 22:9, 27:10, 29:9-10, 68:5-6, 127:3-5, 139:13-16 na 23-24, Yer. 1:5, Efe. 2:10.)
Matayarisho Kabla ya Kuomba
1. Iwapo mhusika anayetaka uponyaji amewakataa wazazi wake (au watu wengine ambao wa-memkataa) anahitaji kukiri dhambi hii na kuomba msamaha.
2. Ni lazima mhusika huyo awasamehe wazazi wake kwa kukosa kumtaka (kumkataa), aondoe hukumu yoyote aliyotoa kwa wazazi wake, na hatimaye awabariki wazazi wake.
3. Mhusika huyo anatakiwa kuwasamehe na kuwaweka huru watu wote ambao wamewahi kumuumiza au kumjeruhi. Mhusika huyo asiposamehe na kuamua “kumheshimu baba na mama” (amri ya 5), huenda asipokee uponyaji.
4. Ingawaje mhusika huyo ameteseka kwa kukataliwa, anawajibu kwa vile ambavyo alishughu-likia, na vile alidhihirisha kukataliwa huko (kama vile kuwa na hasira, kuwa na kiburi, uasi, na kujisikitikia, n.k.) Even though the seeker has suffered rejection, they are still accountable for the ways in which they have handled, dealt with, and expressed their rejection (such as in anger, rudeness, rebellion, self-pity, etc.). These injurious behaviors need to be confessed and forgiveness requested from God.
5. Shiriki nao maandiko yanayozungumza juu ya kukataliwa (Zab. 27:10, 29:9-10, 109:22, 127:3-5, 139:13-16 na 23-24, Jer. 1:5, Efe. 2:10).
6. Mwambie mhusika anayetaka uponyajia asome ukweli unaomhusu yeye mwenyewe katika sehemu inayoeleza juu ya “Kuiponya Picha Tuliyonayo Kuhusu Mungu” na akanushe uwongo alioamini hapo awali kumhusu yeye mwenyewe.
7. Mwambie mhusika aseme kwa kinywa chake mwenyewe kwamba ameamua kuyaondoa “ma-tunda mabaya” ambayo kukataliwa kumezaa ndani ya maisha yake (kama vile machungu, kuudhika, chuki, na uasi).
128
# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa www.healingofthespirit.org
8. Mwambie mhusika huyo atamke kwa kinywa chake mwenyewe kwamba anajikubali, hata kama ni vigumu kufanya hivyo. Aahidi kwamba hatawahi tena kujidunisha au kujikosoa (Efe. 2:10) na hatuna haki ya kukikosoa kitu kilichoumbwa na Mungu.
Ombi la Uponyaji
Omba mambo yafuatayo kwa niaba ya mhusika huyo (kuanzia alipokuwa tumboni). Sistiza kwamba Mungu anataka “kweli ya ndani” (Zab. 51:7). Ikihitajika, soma maneno hayo ukiomba na macho yako yakiwa wazi.
1. Uzima si kosa
2. Mungu alikuumba kwa upendo
3. Mungu alikuumba ili uwe; ulikuwa wakati unaofaa na mahali panapofaa
4. Mungu alitayarisha njia
5. Mungu alikupa uzima
6. Wewe ni faida kubwa na furaha pia, wala si mzigo au
7. Ninaomba kuondoa uwongo ambao mtoto huyu amekubali
8. Ninaleta msalabani mtazamo au matarajio yoyote ya kudhuru
9. Mwone Mungu akimimina upendo juu ya mtoto huyu
10. Puliza pumzi safi ya uzima ndani ya roho yake
11. Mkaribishe mtoto huyu kukua katika uzima kamili
12. Mwambie mtoto wa ndani awasamee watu wote waliomjeruhi
13. Mwambie mtoto wa ndani ajisamehe kwa kutenda mambo kinyume na kuwa na mtazamo mbaya
14. Omba ili upendo wa Mungu unaoleta uponyaji uweze kumiminwa ndani ya roho hiyo iliyoje-ruhiwa
15. Mwambie Yesu ampe mhusika huyo karama ya uaminifu, pumziko, na amani
16. Ombi ili nafsi yote ya mhusika iweze kupata ukamilifu na amani
17. Omba ili nguvu za mwenendo na mitindo yote isiyo ya haki iweze kuvunjika
18. Amuru (katika jina la Yesu) kwamba dhambi zote za kizazi zitakomeshwa
19. Amuru (katika jina la Yesu) kwamba kila roho ya uovu na laana inayotokana na familia ya mtoto huyu
Kama ilivyotajwa hapo awali, mbinguni hakuna wakati. Omba ili Bwana aweze kurejelea ku-rasa za maisha ya mtu huyo na aponye kila hali aliyokuwa na hali ya kutojithamini au alipohisi kwamba hatakikani, amekataliwa, au alipokuwa na woga wa kukataliwa. .
20. Mwambie mhusika afumbe macho yake na aweze kujiona akiwa mbele ya kiti cha enzi, ahisi ukuu, upendo, na mazingira ya amani na furaha.
21. Mwambie mhusika adhani kwamba yeye ni mtoto, anakipokelewa na Yesu, na mikono ya Bwana ikizunguka mabega yake na kuweka taji juu ya kichwa chake—mwambie ajione aki-wa anakua mikononi mwa Yesu
22. Haribu nguvu zote za matukio yoyote ya hisia zilizotegwa.
23. Weka msalaba wa Yesu katikati ya mtoto huyo na wazazi wake
24. Omba kwamba urithi wake wote utachujwa kupitia kwa msalaba
25. Amuru (katika jina la Yesu) kwamba kila laana itakomeshwa
129
# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa www.healingofthespirit.org
26. Omba kwamba mtu huyo atazungukwa na upendo wa Mungu—tangaza kwamba hakuna kitu chochote kitakachomdhuru na uombe kwamba athari zozote za giza hazitaweza kuwafikia
27. Omba kwamba mwangaza utaingia katika maisha ya mtoto huyo
28. Omba kwamba ugumu wowote wa moyo utayeyushwa
29. Omba kwamba macho ya moyo wao yatafunguka
30. Omba kwamba mtoto huyo atafunguliwa milango mizuri, itakayomuingiza katika majaliwa yake ya milele
31. Omba kwamba mtu huyo atamiminiwa faraja ya uponyaji wa Bwana—utakaomshikilia mpa-ka atakapoweza kupata pumziko katika moyo wa Baba
32. Omba kwamba ukweli kuhusu mtu anayestahili kuwa utaandikwa moyoni mwake
33. Nena kwa mtu wake wa ndani ili aweze kumkumbatia kwa mikono yote mtu anayemkaribi-sha katika uzima tele
34. Omba ili upendo na uzima wa Yesu unaoponya utaingia katika roho iliyojeruhiwa
35. Omba ili mtu huyo achague sura mpya na umwambia aombe akijua:
• Mimi ni mtoto wa Mungu I am a child of God
• Mungu ananipenda God loves me
• Nimechaguliwa I am chosen
• Ninapendwa I am loved
• Mimi ni wa thamani I am precious
• Sihitaji kufanya kazi ili kumfanya Mungu anipe kitu
• Mimi ni zawadi kutoka kwa Mungu I am God's gift
• Sitapoteza chochote I can't lose it
• Mungu ameitayarisha njia God has prepared the way
• Mungu ameyahifadhi maisha yangu God has preserved my life
• Mungu ananitaka nitembe kwa utulivu katika maisha yangu mapya
Hebu sasa muone Bwana akija na upanga wa kweli kumtenganisha mhusika na hali yake ya zamani … (sahishi mambo yafuatayo kwa kutumiwa kiwakilishi cha mtu huyo ukiomba):
• Aongozwe katika majaliwa na makusudi yake kamilifu
• Awekwe huru ili awe jinsi anavyotakiwa kuwa
• Ugumu wowote wa moyo uyeyushwe na macho na moyo wake uweze kufunguka
• Apate ulinzi
• Atimize majaliwa yake
• Msalaba uwekwe katikati ya mtoto huyo na wazazi wake
• Hatimaye, baraka iwe katika maisha yake katika jina la Yesu
• Roho zote za kukataliwa, kujikataa, uwoga wa kukataliwa, kuachwa, kutengwa, upweke, kudanganyiwa, hatia, na aibu zitaondoka.
Ombi la Uponyaji wa Ndani
Rudia makala ya uponyaji wa ndani kutoka katika sura iliyotangulia . Iwapo mwom-bezi anaweza kutambua ni lini kukataliwa kulipoanza katika mahojiano au apokee jibu kuto-ka kwa Mungu, itasaidia kuombea uponyaji wa ndani ili Yesu aingie na kubadili tukio la kwanza la kukataliwa. Hii ni muhimu kwa watoto wa kupanga au waliotengwa na mzazi mmoja au wote wawili.
130
# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa www.healingofthespirit.org
Ombi la kuombwa na Mhusika Anayetaka Uponyaji
Mwambie mhusika atamke ombi lifuatalo kwa sauti.
Bwana Yesu Kristo, ninaamini kwamba wewe ni Mwana wa Mungu na wewe ni njia pekee ya kumfikia Mungu baba. Ulikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu na ukafufuka kutoka kwa wafu.
Ninatubu dhambi zangu zote na kuwasamehe wengine, kama ninavyotaka Mungu anisamehe. Ninawasamehe watu wote walionikataa, walionijeruhi, waliokosa kunionyesha upendo, na ninaamini kwamba wewe pia utanisamehe na kuwasamehe watu hao.
Bwana, ninaamini kwamba umenikubali. Hivi sasa, kwa ajili ya kile ulichonifanyia msalabani, ninakubali kwamba ninakubaliwa. Ninapendwa sana. Ninatunzwa na wewe. Un-anipenda sana. Unanitaka. Baba yako ni Baba yangu. Mbinguni ni makao yangu ya milele. Mimi ni mmoja wa familia ya Mungu, familia iliyo bora zaidi ulimwenguni. Asante! Asante, Bwana!
Jambo lengine, Bwana; ninajikubali kuwa ulivyoniumba. Mimi ni kazi ya mikono yako na ninakushukuru kwa kuniumba hivi. Ninaamini kwamba umeanza kazi nzuri ndani yangu na utaikamilisha (Fil. 1:6, 1 Tes. 5:24).
Bwana, ningependa msamaha wako uweze kuwa na matokeo mema maishani mwan-gu, ndiposa ninajisamehe sasa kwa kufanya mambo yote niliyoleta mbele yako kwa maombi, na ninaachilia hisia zote nilizokuwa nazo hapo awali za kuona hatia na kurejelea mara kwa mara mambo ya zamani baada ya kukuomba msamaha.
Ninavunja utumwa wa kujihukumu kwamba sikubaliki kwako na kwa wengine. ni-weke huru kutoka kwa mawazo hayo ya kudhuru, katika jina la Yesu.
Hivi sasa, ninafunga roho wa kukataliwa, kujikataa, kukataliwa kunakoonekana, na uwoga wa kukataliwa, katika jina la Yesu Kristo lenye baraka. Ninavunja nguvu za adui ka-tika maisha yangu na kuziamuru ziondoke katiak jina la Yesu. Ninachukua sehemu yoyote niliyokuwa nimempa na sasa kwa furaha ninamrudishia Mungu.
Ninatangaza kwamba nimewekwa huru kutkana na roho zote za giza na uovu zilizo-tumia majeraha yaliyokuwa katika maisha yangu. Ninaiachilia roho yangu ili ifurahie ndani ya Bwana. Katika jina la Yesu, ninaomba. Amina.
Ombi la Kuwekwa Huru Kutokana na Kukataliwa kwa Kizazi
Mwambie mhusika atamke ombil hili kwa sauti.
Mwenyezi Mungu wa Milele, unayenuia kuvirejesha vitu vyote kwa Mwanao mpendwa, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana, ninakushukuru kwa watu wote wa vizazi vilivyopita walioniachia amani, upendo, na nafasi ya kukujua wewe na Mwanao, Yesu Kristo.
Tafadhali tuma mwangaza wa Mwanao Yesu Kristo katika sehemu zote za dhambi na zina-zoumiza za vizazi vya zamani vya mstari wa familia yangu, kwa watu wote waliotatiza na kukataliwa, kujikataa, kuogopa kukataliwa, kujihukumu, kukosa kujithamini, kuogopa kutofaulu, upweke, kukata-liwa kulikoonekana, au hisia za kuachwa. Tafadhali tuma nuru na damu ya Yesu (iliyomwagwa msa-labani ili tupate msamaha) katika sehemu zote zilizojaa uchungu na utupu katika mioyo ya watu wa familia yangu na uwaponye katika Jina Takatifu la Yesu.
Waliokuwa katika vizazi vilivyopita wamenikosea na kuniumiza kwa kushirikia katika mie-nendo, shughuli, na matendo yaliyosababisha kukataliwa pamoja na hisia zote zilizotajwa hapo awali na yanayohusiana na hali hii isiyotakatifu. Hivi sasa, Ee Bwana, ningependa kuja mbele ya kiti chako cha enzi kwa niaba yao na kuomba msamaha kwa niaba yao. Bwana, wasamehe kwa sababu kwa hali nyingi, hawakujua walichokuwa wakifanya. Tafadhali wasamehe na uvunje madhara yoyote yaliyoni-
131
# 18 Uponyaji Kutokana na Kukataliwa www.healingofthespirit.org
jia mimi. Ee Bwana, waachilie watu wote walio mahali hapa kutoka kwa dhambi za mababu na nyanya zao wa zamani, hata kwa kizazi cha tatu na cha nne, kama ilivyoandikwa katika Maandiko Matakatifu. (Kut. 20:5). Nifunike kwa damu yako iliyomwagika Kalvari.
Ninatuma upendo na msamaha wako kwa watu wote walioniumiza au waliowaumiza watu wengine walio katika mstari wa familia yangu. Ninakuomba uwasamehe na kuwawezesha kuwa wa-kamilifu na wawe na maisha mapya ndani yako. Niondolee maumivu na uchungu wote niliopitia ku-tokana na maneno ya kukosoa niliyoambiwa ambayo yamefanya nihisi kwamba sipendwi na sitakika-ni.Wasamehe watu katika familia yangu ambao wamekosoa umbo langu na uwezo wangu wa kiakili na kimwili, na wa watu wengine pia.
Ninakuomba unisamehe kwa kila hali ya kutenda dhambi kama walivyotenda mababu zangu. Nisamehe na kunirudisha katika hali nzuri ya maisha kwani wewe pekee ndiwe uwezaye kufanya hivyo.
Mungu Mwenyezi, ninaomba unijulishe sehemu zozote katika mstari wa familia yangu zina-zohitaji kuombewa zaidi, ili kuvunja utumwa wa dhambi na ujinga na kunirudisha mimi na wengine katika urithi halisi ndani yako. Wahurumie watu wote walio katika msari wa kizazi change. Waweke huru, ili waje mbele yako wakiwa na hakika ya upendo na msamaha wako. Tuma upendo wa Mwanao Yesu Kristo katika kila mahali penye giza na panapoumia katika vizazi vya zamani, vya sasa, na vi-javyo ili viweze kujifunza kuishi kikamilifu kimwili, kiakili, na kiroho kwa utukufu wa milele wa Jina lako takatifu, kupitia kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Ninaomba mambo haya yote katika jina lenye thamani la Yesu. Amina.
Vifaa (kulingana na umuhimu wake)
1. Noel and Phyl Gibson, Excuse Me, Your Rejection Is Showing (Sovereign World Publishers, PO Box 777, Tonbridge, Kent TN 11 0ZS, England, 1997, reprinted 2004). ISBN 1-85240-110-9. (Available in the US through the Arsenal Bookstore, 11005 Voyager Parkway, Colo-rado Springs, CO 80921.)
2. John and Paula Sandford, Healing the Wounded Spirit (Victory House, 1985). ISBN 0-932081-14-2.
3. Norma Dearing, The Healing Touch (Chosen Books, 2002). ISBN 0-8007-9302-1.
4. Charles Kraft, Deep Wounds, Deep Healing (Servant Pub., 1993). ISBN 0-89283-784-5.
5. Derek Prince, God's Remedy for Rejection (Whitaker House, 1993). ISBN 088368-864-6.
6. Francis and Judith MacNutt, Praying for Your Unborn Child (1989). ISBN 0-38523-2829. (Available from www.Christianhealingmin.org, 904-765-3332.)
7. Thomas Verney, MD, The Secret Life of the Unborn Child (Summit Books, 1981).
132
# 19 Healing from Trauma www.healingofthespirit.org
Uponyaji wa Athari Za Kiwewe
Kiwewe hutokana na matukio tuliyopitia katika maisha yetu ambayo hatukuwa na uwezo wa kuyazuia. Tukio la kiwewe laweza kusababishwa na tendo lolote kama vile ajali ya barabarani, kuanguka, kudhulumiwa kingono na hata kupokea habari za kifo. Mifano mingine ni kifo kwenye jamii, talaka, kufutwa kazi, wazazi kutengana, ajali ya barabarani, kufiwa na mpenzi, mtoto au jamaa wa karibu, kunajisiwa, kujeruhiwa, hofu ya mauti au hata vita.
Wapo wengi Afrika ambao wamepitia matukio ya kiwewe kutokana na mapigano ya kikabila (Rwanda) na machafuko ya uchaguzi (Kenya). Haya ni matukio ambayo hatukupanga wala nafsi zetu hazikuyatajia kutokea
Watu wanapokumbwa na kiwewe kuna hatari ya kwamba nafsi zao huwa wazi kwa adui kuingia ndani ya roho zao. Mfano mzuri ni wakati mama anapomuuguza mwanawe ambaye amehusika katika ajali ya barabarani na kuishia kumuona akifa hospitalini. Roho wa kifo anapata nafasi ya kupenya ndani ya mama huyu. Tukio kama hili hata hivi haliathiri watu wote kwa njia sawa. Wengine wanakubali tukio la kifo kama jambo la kawaida. Lakini utapata kwamba wengine wanaathirika na tukio hilo kwa namna ambayo inabadili mkondo wa maisha yao kikamilifu.
Mungu alituumba tukiwa na roho, nafsi na mwili. Tukio la kiwewe linaathiri sehemu zote za uhai wetu bila kuacha nje mojawapo. Uharibifu hutokea kwa nafsi yetu (roho na vionjo) kupitia kwa majeraha au maumivu ya kimwili. Tabibu wa hospitali hushughulikia kuutibu mwili bila ya kujali athari zilizofanyika ndani ya roho zetu. Hali hii inaweza kusababisha kutatizika kwa vionjo vya kibinadamu, mtu kuwa na matatizo ya mawazo/fikira za kujitoa uhai na hata kuishia kulemaa kimwili.
Mojawapo wa huduma za Yesu kama inavyodhihirika katika Isaya 61:1 ni: Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo (kuwaponya). Peter Horrobin (tazama mwisho wa ibara hii) anapendekeza kuwa waliovunjika mioyo ni wale waliovunjika vipande vipande. Ni kusema kuwa sio tu miili yetu iliyovunjika bali hata mioyo yetu imepondeka wakati mmoja. Roho ya udhaifu yaweza kutufanya kuwaza kuwa tumelemaa kimwili kwa kuwa imepenya ndani yetu wakati tulipokumbwa na kiwewe hivyo basi ikafungiwa ndani yetu. Tunafikiri kuwa tumelemazwa na ajali, kumbe ni roho wa giza aliyeingia ndani yetu wakati wa tukio la kiwewe ili kutupatia majeraha ya kimwili. Kiwewe kilichoingia na kujifungia ndani ya nafsi hutambulika, kufunguliwa na kuponywa pindi roho za hofu na udhaifu zinapokemewa. Mara hiyo zile ishara za ulemavu wa kimwili hutoweka. (nukuu kutoka: Ministering Freedom to the Emotionally Wounded, tazama Sura ya 5—“Jinsi Kiwewe Kinavyomdhuru Mtu Mzima” Imeandikwa:Peter Horrobin).
Matokeo ya matukio haya yanajumuisha roho ya kifo, hofu kuu ama hata kuingia kwa roho ya udhaifu. Hali hii husababisha ndoto mbaya usiku, maumivu, mawazo mabaya ama hata wasiwasi usioweza kueleweka. Tukio la maonevu au kufanyiwa madhambi kwa motto akinyanyaswa kimapenzi, kupigwa ama kutusiwa au anapohusika kwa tukio la kuhatarisha uhai linaloleta hofu au taharuki ya talaka. Yule aliyefanyiwa dhuluma hizi hukumbuka wasiwasi, uchungu, matusi, dhuluma, kukataliwa, kuwachwa, aibu na hatia hii humsababishia kukumbuka tendo hilo mara kwa mara katika mawazo yake. Tendo hili la kumbukumbu lina athari
133
# 19 Healing from Trauma www.healingofthespirit.org
kubwa sana kuliko hata kulemaa kimwili ama maumivu anayoyapata mtu wakati wa tukio
lenyewe. Kumukumbu hii wasemavyo wanasayansi hugandisha tukio hilo ndani ya akili ya
mtu. Hatima hii huwakumba asilimia sita ya watoto wa kiume na aslimia kumi na tano ya
watoto wa kike. Ili kuelimika zaidi tazama tovuti ifuatayo:
http://www.medicinenet.com/posttraumatic_stress_disorder/article.htm).
Iwapo kumbukumbu imedhurika vilivyo yaweza kusababisha mtu kugawanyika katika
haiba kadhaa ambako tajriba na nafsi yake inavunjika vipandevipande. Hii inadhihirika kwa
wale waliohusishwa na dhuluma za itikadi za kishetani ama Satanic Ritual Abuse (SRA).
Ili kuelewa mada hii kwa ukamilifu, tazama: Deliverance from Evil Spirits (Francis
MacNutt, kurasa 223-235) kuwahudumia watu waliokumbwa na hali hizi kunahitaji ujuzi wa hali ya
juu na elimu ya ndani katika somo hili. Watu walioathiriwa na hali hizi yafaa waelekezwe kwa
washauri wa kikristo ambao wana ujuzi wa mada ya uponyaji wa ndani na huduma ya ukombozi.
Maombi ya uponyaji wa ndani yanahitajika sana na yamejadiliwa katika sura inayoshughulikia
Uponyaji wa Mawazo. Mtafutaji anakaribishwa kukumbuka matukio hayo ya kuumiza na kisha
mhuduma atamuombea akimwuliza Yesu aingie ndani ya picha hiyo na kumuondolea mtafutaji
hatari ya tukio hilo. Kisha mtafutaji hupewa fursa ya kupeana matukio yote ya dhuluma kwa Yesu.
Mhuduma anapoomba, Mungu huponya matukio hayo na kasha kukemea kila roho zinzohusiana na
maumivu/machungu yaliyotajwa.
134
#20 Kuiponya Picha Tuliyo nayo Kuhusu Mungu www.healingofthespirit.org
Kuiponya Picha Tuliyonayo Kuhusu Mungu
Picha tuliyonayo kuhusu Mungu ni mojawapo ya kizuizi kikubwa cha kupata uponyaji wetu. Mara nyingi huwa hatujui vizuri kwamba Mungu anatupenda kwa hivyo angependa kuleta baraka na uponyaji ndani ya maisha yetu. Ili kuimarisha imani yako katika jambo hili, jibu maswali yaliyo hapa chini na uyasome maandiko yanayoandamana na maswali hayo.
Je, unajua kwamba Mungu anakupenda? Je, unajua kwamba Mungu anakupenda na anataka kukuponya na kukubariki? (N, L)) Soma marejeleo yafuatayo:
a. “Kisha Mungu akasema, “Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu:… Mungu akaona kila kitu alichofanya kuwa ni chema kabisa” (Mwa. 1:26-31).
b. “Maana Mungu aliupenda ulimwengu hivi hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).
c. “Kila mtu anayekiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu anaishi katika muungano na mtu huyo, naye anaishi katika muungano na Mungu. … Mungu ni pendo; na kila mtu aishiye katika upendo, anaishi katika muungano na Mungu, na Mungu anaishi katika muungano naye” (1 Yohana 4:15-16).
d. “…Kristo anaishi ndani yangu. Maisha haya ninayoishi sasa naishi kwa imani, imani katika Mwana wa Mungu, aliyenipenda hata akayatoa maisha yake kwa ajili yangu” (Gal. 2:20).
Badala ya kumwona Mungu kuwa ni baba mstahamilivu, anayependa, mkari-mu, na anayesamehe, watu wengine humwona kuwa ni baba mkali, asiye na huruma, anayeweka hesabu ya dhambi tuzifanyazo na aliye mwepesi kutuadhibu kila tunapo-fanya kosa. Labda unadhani kwamba Mungu anakungoja tu ufanye kosa na kwamba Kitabu cha Uzima kina kurasa mbili pekee (upande wa “mazuri” na upande wa “ma-baya”), na kwamba utahukumiwa kulingana na alama utakazopata kwa mambo hayo mawili.
Wakati mwingine huwa hatudhani kwamba tunastahili baraka za Mun-gu—na hivyo kutenda mambo kama inavyostahili. Kusema kweli, wakati mwin-gine matendo yetu hudhihirisha mawazo yetu ya ndani, vile inavyoelezwa katika Mi-thali 23:7, “Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo” Na iwapo tuna baba mza-zi asiye na huruma, ambaye hutuadhibu kwa kikatili, au labda aliyekosa kututunza, akatuwacha, au aliyetudhulumu (kimwili, kwa maneno, au kimapenzi), jambo hilo hu-tufanya tushindwe kuyageuza mawazo yetu na kumkubali baba wa Mbinguni ambaye tunatakiwa kuamini kwamba ni mzuri, mwenye upendo, mkarimu, mwenye kusa-mehe, n.k.
135
#20 Kuiponya Picha Tuliyo nayo Kuhusu Mungu www.healingofthespirit.org
Iwapo Yesu angekuja kuketi mbele yako na akutazame machoni, ungekuwa na hisia zipi? …hofu au kutaka kukwepa?…Woga? …furaha ya matarajio? Je, Yesu akiangalia ndani ya nafsi yako, unadhani anaiona takataka yako pekee (udanganyifu wako, mawazo yako machafu, udhaifu wako na uchafu)? Labda wewe hutumia muda mwingi—kujaribu kukumbuka kwa uchungu—mambo yote uliyotakiwa kufanya lakini hu-jafanya, mambo ambayo wewe huyapuuza au hukosa kuyafanya, au wewe huwa na hatia ku-husu mambo mabaya ambayo umeyatenda. Labda umetubu kwa kufanya makosa hayo lakini mawazo ya kuwa na hatia na kutojisamehe huendelea kujitokeza akilini mwako. Kisha wewe huamini na kukubali kwamba Yesu hajaridhishwa nawe, na hilo huzihalalisha hisia hizo za kujiona una hatia.
Labda wewe kila mara hupigana na habari na mawazo yasiyo mazuri. Mawazo hayo yote hurekodiwa akilini mwetu. Nayo huturudia kwa njia za kushangaza sana. Kumbuka kwamba, mpango wa adui ni kujaribu kutufanya kila wakati tuicheze kanda hiyo ya mambo yote mabaya tuliyoyapitia katika maisha yetu: “Muwe macho,kesheni! Maana adui yenu, Ibilisi, huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mawindo” (1 Pet. 5:8). Tuna-takiwa kukabiliana na mawazo hayo mabaya kwa njia hii “Muwe macho, kesheni!”
Habari Njema ni kuwa, tukipeleka msalabani hayo mawazo mabaya yasiyostahili, na ambayo mara nyingi huwa si kweli, Mungu husamehe na kuyasahau mambo hayo; hataya-kumbuka tena. Msalaba una nguvu za kutusafisha ili tukisimama mbele ya Mungu, tutasi-mama tukiwa watakatifu wakati huo: safi, waliosamehewa, na wapya kabisa. Dhambi zote za hapo awali huwa zimesamehewa na kusahauliwa.
Jua kwamba Mungu hatuhukumu (Yoh. 3:17, “Maana Mungu hakumtuma Mwanae ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu; bali aukomboe.”) Hatia, aibu, na majuto, havitoki kwa Mungu. (Kumbuka vile Adamu alimjibu Mungu alipokuwa amejificha katika Bustani la Edeni, “Nani aliyekwambia kwamba uko uchi?”—Gen. 3:11.) Moyo wa Mungu huwa mzito kwa sababu sisi humwambia mara kwa mara atusamehe ilhali tayari ametusamehe. Mpango wa Mungu kwetu hauwezi kutambulika mpaka tuwe tayari kujua na kusema, “Mimi ni mtoto wa Mungu.”
Iwapo hujui kwamba Mungu anakupenda, iwapo huamini vilivyo kwamba umeumb-wa kwa mfano wake (ndani) na sura (nje; angalia Mwa. 1:26), na iwapo huamini kwamba anakukubali vile ulivyo, basi endelea na somo lililo hapa chini na uombe ombi lililo mwisho wa somo hili.
Tambua na kuweka alama (K) kando ya sentensi unazoamini kuwa kweli kati ya hizi:
(a) Nina tatizo la kuamini kwamba Mungu ananipenda.
(b) Huwa ninamtambua Baba yangu wa mbinguni kwa zile ishara ambazo nimeona kwa baba yangu wa hapa duniani, ambazo hazikuwa za malezi mema wala afya.
(c) Baba yangu wa hapa duniani alinidhulumu kihisia, kimwili, kimapenzi—(tumia mviringo kuonyesha moja au zaidi ).
(d) Mimi hufikiria Mungu ni hasibu, anayejumlisha hesabu ya mazuri na mabaya.
(e) Ninafikiri ninatakiwa kufanya juhudi ili niweze kupata upendo na baraka za Mungu..
(f) Ninafikiri sistahili Baraka za Mungu kwa sababu ya dhambi zangu.
(g) Nimemkasirikia Mungu kwa sababu alikubali mambo fulani yanitendekee mimi/au watu niwapendao.
136
#20 Kuiponya Picha Tuliyo nayo Kuhusu Mungu www.healingofthespirit.org
(h) Sina hakika ikiwa Mungu ananipenda au la. Yeye huwa hajibu maombi yangu.
(i) Ni vigumu kwangu kuamini kwamba Mungu ananipenda.
(j) Nina hasira kwa Mungu.
(k) Ninahisi nina hatia, haya, na hukumu, na ninafikiri haya yanatoka kwa Mungu.
(l) Sijipendi bali ninajichukia, kwa hivyo sioni ni vipi ambavyo Mungu anaweza kunipenda.
(m)Nimejaribu kubadilika ili niwe mtu mzuri lakini nimeshindwa. Siamini kwamba Mungu ananijali.
(n) Wazee wa kanisa wameniombea lakini hakuna jambo lililotendeka.
(o) Nina tatizo la kuamini kwamba Yesu alikuja kuniponya au kuniweka huru.
Watu wengi wameamini uwongo wa shetani na wameamua (kwa kusaidiwa na Shetani) kwamba Mungu hawapendi. Watu wengi hawaijui minyororo inayowafunga. Katika huduma yake ya uponyaji, Yesu aliwachukulia watu waliokuwa na machungu kuwa ni waathiriwa na akawaweka huru.
Yesu alikuja kuwafungua waliovunjika moyo na kuwaweka huru mateka (Isa. 61:1 na Luka 4:18). Mwaliko wa Yesu ni, “… Njooni kwangu… nanyi mtatulizwa rohoni mwenu…” (Mat. 11:28-30). Waumini wengi hawajapata uhuru wa kweli; labda wanaelewa kwamba wana-takiwa kupata wokovu lakini hawaishi katika uzima tele (John 10:10) wenye uhuru (Yoh.8:31-32) walioahidiwa na wanaoweza kuupata. Bibilia inasema: “Huchunga kundi lake kama mchungaji wa mifugo: Hukusanya wanakondoo katika mikono yake na kuwachukua karibu na moyo wake, huwaongoza taratibu wale wanyonyeshao”. (Isa 40:11), “BWANA Mungu wako yu pamoja nawe, yeye ni mwenye nguvu kuokoa. Atakufurahia kwa furaha kubwa, ata-kutuliza kwa pendo lake, atakufurahia kwa kuimba.’’ (Zeph 3:17)
Kuna namna mbili za kubadili vile ambavyo mhitaji anawaza Mungu anamuona
1) Hatua ya kuona na kuonekana inafanya kazi vizuri hapa. Tunamuuliza mhitaji aombe “Yesu ni nini unachoona ukitazama ndani yangu?” Yesu hutokea katika picha kwenye mawazo yao na kuondoa kila dhana ya kujidunisha na chuki. Mhimize mhitaji amuombe Mungu amguse. Kipindi cha kukaa mikononi mwa Yesu huleta uponyaji wa ajabu. Hata iwapo wamemkasirikia Mungu, yeye huwatwaa mikononi mwake na kuwakumbatia kwa upendo.
2) Kutia kweli ya neno la Mungu nafsini na moyoni. Soma maandiko yafuatayo kila siku hadi Mungu akuhakikishie upendo alio nao kwako
Maandiko yanatwambia ukweli huu kuhusu Mungu:
• Rafiki mwema anayehusika nasi (Zab. 139:1-18)
• Mwenye rehema, mwenye neema, na mwenye huruma (Zab. 103:8-14)
• Anayetukubali na aliyejaa furaha na upendo (Zeph. 3:17, Rum. 15:7)
• Mwema na mwenye moyo wa kupenda (Isa. 40:11, Hosea 11:3-4)
• Yuko nami kila wakati; anatamani kuwa nami Yer. 31:20, Ebr. 13:5)
• Mstahimilivu, mvumilivu, asiyekasirika upesi (Kut. 34:6, 2 Pet. 3:9)
• Mwenye upendo, mpole, na anayenilinda (Zab. 18:2, Yer. 31:3, Isa. 42:3)
• Mwaminifu, anayetaka kunipa uzima kamili (Omb. 3:22-23, Yoh. 10:10)
• Mwingi wa neema na rehema (Luka 15:11-23, Ebr. 4:15-16)
137
#20 Kuiponya Picha Tuliyo nayo Kuhusu Mungu www.healingofthespirit.org
• Wa huruma na wa kusamehe; moyo wake na mikono yake iko wazi kila wakati (Zab. 130:1-4, Luka 15:17-24)
• Anataka nikue na anaona fahari kubwa juu yangu (Rum. 8:28-30, 2 Kor. 7:4)
4. Maandiko yananiambia kwamba katika Kristo:
• Ninakubalika na ninapendwa (Mwa. 1:26-27)
• Mimi ni chumvi na mwanga wa ulimwengu (Mat. 5:13-14)
• Mimi ni mtoto wa Mungu (Yoh. 1:12)
• Mimi ni mtoto wa Mungu na mwovu hawezi kunidhuru (1 Yoh. 5:18)
• Mimi ni tawi la mzabibu wa kweli, njia ya Uzima wake (Yoh. 15:1, 5)
• Mimi nimechaguliwa na kutumwa nizae matunda (Yoh. 15:16)
• Mimi ni shahidi wa Kristo (Mate. 1:8)
• Mimi ni rafiki ya Kristo (Yoh. 15:15)
• Nimefanywa kuwa mwadilifu (Rum. 5:1)
• Nimejiunga na Bwana na ni roho moja naye (1 Kor. 6:17)
• Nimenunuliwa kwa bei kubwa; mimi ni wa Mungu (1 Kor. 6:20)
• Mimi ni kiungo cha mwili wa Kristo (1 Kor. 12:27)
• Mimi ni mtakatifu (Efe. 1:1)
• Nimefanyika kuwa mwana wa Mungu (Efe. 1:5)
• Ninaweza kumwendea baba moja kwa moja kupitia kwa Roho Mtakatifu (Efe. 2:18)
• Nimekombolewa na kusamehewa dhambi zangu zote (Kol. 1:14)
• Nimekamilika katika Kristo (Kol. 2:10)
• Hakuna hukumu kwangu (Rum. 8:1-2)
• Ninajua kwamba katika mambo yote Mungu hufanya kazi ili nipate mambo mema (Rum. 8:28)
• Siwezi kutenganishwa na upendo wa Mungu (Rum. 8:35-39)
• Mimi ni hekalu la Mungu (1 Kor. 3:16)
• Nimeimarishwa, nimewekwa wakfu, na kutiwa muhuri na Mungu (2 Kor. 1:21-22)
• Mimi ni mhuduma wa upatanisho (2 Kor. 5:17-20)
• Mimi ni mfanyakazi pamoja na Mungu (2 Kor. 6:1)
• Ninatawala pamoja na Kristo mbinguni (Efe. 2:6)
• Mimi ni kiumbe wa Mungu (Efe. 2:10)
• Ninaweza kumwendea Mungu kwa uhuru na ujasiri (Efe. 3:12)
• Nimefichwa pamoja na Kristo katika Mungu (Kol. 3:3)
• Nina hakika kwamba Mungu aliyeanza kazi hii njema ndani yangu ataiendeleza mpaka ikamilike (Fil. 1:6)
• Mimi ni raia wa mbinguni (Fil. 3:20)
• Naweza kuikabili kila hali kwani Kristo hunipa nguvu (Fil. 4:13)
• Roho niliyepewa na Mungu si wa kunifanya niwe mwoga; sivyo, ila ni Roho wa kunijalia upendo na nidhamu (2 Tim. 1:7)
• Mimi ni mwana wa Mungu na mwovu hawezi kunidhuru (1 Yoh. 5:18)
• Ninaweza kupokea neema na fadhili wakati wa shida (Ebr. 4:16)
138
#20 Kuiponya Picha Tuliyo nayo Kuhusu Mungu www.healingofthespirit.org
Kauli za kweli na Imani: Baada ya kuomba ombi lililo mwisho wa sehemu hii (kwa sauti ya juu ukiwa na rafiki), soma (kila siku kwa sauti ya juu) Kauli hizi kumi na moja za “Kweli na Imani” mpaka picha uliyo nayo kuhusu Mungu ibadilike na kuwa ile ya kweli—kama ilivyopendekezwa katika Warumi 12:2, “… mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu….”
a. Ninafahamu kwamba kuna Mungu mmoja pekee wa kweli na aliye hai anayeishi kama Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu (Kut. 20:2-3, Kol. 1:16-17).
b. Ninafahamu kwamba Yesu Kristo ni Masiha, Neno aliyefanyika mwili akakaa kwetu, na kwamba Alikuja ili azivunje kazi za ibilisi (Yoh 1:1 na 14, Kol. 2:15, 1 Yoh. 3:8).
c. Ninaamini kwamba Mungu amethibitisha kwamba ananipenda, kwa sababu nilipokuwa bado mwenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yangu (Rum. 5:8). Ninaamini kwamba ameniokoa kutoka kwa nguvu za giza, na kunileta salama katika ufalme wake, kwake nimekombolewa, yaani dhambi zangu zimeondolewa (Kol. 1:13-14).
d. Ninaamini kwamba mimi ni mwana wa Mungu na ninatawala pamoja na Kristo mbinguni (Efe. 2:6). Ninaamini kwamba nimeokolewa kwa neema ya Mungu kwa njia ya imani na jambo hili si matokea ya juhudi zangu, bali ni zawadi ya Mungu (Efe. 2:8-9, 1 Yoh. 3:1-3).
e. Ninaamua kuwa imara katika kuungana na Bwana nikisaidiwa na nguvu zake kuu. Situmaini katika nguvu za mwili, maana silaha tunazotumia katika vita vyetu si silaha za kidunia, ila ni nguvu ya Mungu yenye kuharibu ngome zote (2 Kor. 10:4). Ninavaa silaha ninazopewa na Mungu na kuamua na kusimama imara katika imani na kuzipinga mbinu mbaya za ibilisi (Efe. 6:10-20, Fil. 3:3).
f. Ninaamini kwamba bila Kristo siwezi kufanya chochote (Yoh. 15:5), kwa hivyo ninakiri kwamba ninamtegemea vilivyo. Ninaamua kukaa ndani yake ili niweze kuzaa matunda mengi. (Yoh. 15:6-8) na kumtukuza Baba yangu. Ninamtangazia Shetani kwamba Yesu ni Bwana wangu (1 Kor. 12:3). Ninakataa kila aina ya vipawa bandia au kazi za shetani katika maisha yangu.
g. Ninaamini ukweli utaniweka huru (Yoh 8:32) na kwamba Yesu ni ukweli (Yoh 14:6). Yesu akiniweka huru, nitakuwa huru kweli (Yoh 8:36). Ninatambua kwamba kutembea katika nuru (1 Yoh 1:3-7) ni njia pekee ya kuwa na ushirika wa kweli na Mungu na mwanadamu. Kwa hivyo, ninaharibu hoja zote za uongo wa Shetani kwa kuziteka fikira zote na kuzifanya zimtii Kristo (2 Kor. 10:5). Ninatangaza kwamba Biblia ndicho kiwango pekee chenye mamlaka ya kuyaongoza maisha (2 Tim. 3:15-17).
h. Ninaamua kumtolea Mungu mwili wangu kama dhabihu iliyo hai, takatifu na kuitoa nafsi yangu yote kwa Mungu kwa ajili ya uadilifu (Rum. 6:13). Ninaamau kuzigeuza fikira zangu kwa kusoma na kukubali neno la Mungu lililo hai ili niweze kuyajua mapenzi ya Mungu na kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu (Rum. 12:1-2). Ninavua hali ya kale na uovu wake na kuivaa hali mpya (2 Kor. 5:17, Kol. 3:9-10) inayopatikana kupitia kwa Yesu Kristo. Ninatangaza kwamba mimi ni kiumbe kipya katika Kristo.
i. Kwa imani, ninaamua kujazwa na Roho Mtakatifu (Yoh. 16:13) ili niweze kuelekezwa katika ukweli wote. Ninaamua kuongozwa na Roho ili nisifuate tena tamaa za kidunia. (Gal. 5:16, Efe. 5:18).
j. Ninakanusha malengo yote ya kibinafsi na kuamua kufuata lengo la upendo. Ninaamua kuzitii amri mbili kuu: kumpenda Bwana Mungu wangu kwa moyo
139
#20 Kuiponya Picha Tuliyo nayo Kuhusu Mungu www.healingofthespirit.org
wangu wote, kwa roho yangu yote na kwa akili yangu yote, na kumpenda jirani yangu kama ninavyojipenda mimi mwenyewe (Mat. 22:37-39, Marko 12:33, 1 Tim. 1:5).
k. Ninaamini kwamba Bwana Yesu ana mamlaka yote juu mbinguni na hapa duniani (Mat. 28:18) anatawala juu ya kila cheo kiwezacho kutajwa katika ulimwengu huu (Efe. 1:19-23); nimepewa uhai kamili katika kuungana naye (Kol. 2:10). Ninaamini kwamba Shetani na mapepo wake wako chini yangu katika Kristo (Yak. 4:7) kwa vile mimi ni kiungo cha mwili wa Kristo. Kwa hivyo ninatii amri ya kumnyenyekea Mungu na kumpinga ibilisi, na ninamwamuru Shetani aondoke mbele yangu katika jina la Yesu Kristo.
Ombi la Kuiponya Picha Niliyo nayo Kuhusu Mungu
Bwana, ninaamini kwamba uliniumba kwa mfano wako na sura yako. Ninajua kwamba siwe-zi kuzipokea baraka zote ulizonitengea mimi mpaka niweze kuelewa kwamba unanipenda vile nilivyo na kwamba sitakiwi kufanya juhudi zozote ili nizipokee baraka hizo. Yesu alitufikia tukiwa bado wenye dhambi kwa hivyo ninajua kwamba unanipenda vile nilivyo.
Bwana, ninatubu kwa kuamini uwongo wote kuhusu hali yako na hali yangu ndani yako. Ni-nakataa na kukanusha uwongo huo. Ninaomba msamaha kwa hasira na uchungu wowote nilionao kwako. Ninaamua kukupa nafasi unayostahili moyoni mwangu na maishani mwangu.
Bwana, ninajua kwamba siwezi kuwa na haki mbele yako mpaka niweze kupatana na wazazi wangu. Nisaidie kuwasamehe kwa mambo yote mabaya waliyonitendea na niweze kuwapenda kama unavyowapenda.
Iponye picha isiyo halisi ambayo nimekuwa nayo kukuhusu wewe Bwana, na uibadilishe ili iwe picha yako halisi, ya upendo, huruma, uponyaji, na baraka. Niwezeshe kujua bila shaka yoyote kwamba umenikubali, mimi ni mmoja wa watoto wako maalum na wa thamani. Ninaomba baraka hizo katika jina la Yesu. Amina.
Vifaa
1. Neil Anderson, Victory Over the Darkness (Regal Books, 1990). ISBN 0830713751.
2. Neil Anderson, The Bondage Breaker (Harvest House, 2000). ISBN 0-7369-0241-4. (Much of the material for this section was taken from this book.)
3. Brad Jersak, Can You Hear Me? Fresh Wind Press, 2003) ISBN 0-9733586-0-2
140
# 21 Uponyaji Unahitaji Toba www.healingofthespirit.org
Uponyaji Unahitaji Toba
Kwa nini tunahitaji kutubu?
Mbali na kujua kwamba tunafunzwa na tunaamriwa kutubu, maelezo yafuatayo yanatuonye-sha faida zengine zinazotokana na kitendo cha toba.
1. Dhambi “hufungua” tundu katika ua au silaha inayotukinga, ilhali toba “huziba” tundu hizo. Tunapotenda dhambi, au mtu akitukosea, mlango katika ua letu la kiroho hufunguka (Ayubu 1:10) na roho ya giza inaweza kuingia ndani ya roho zetu (na kuruhusu utumwa uin-gie ndani). Njia pekee ya kufunga milango ya kiroho iliyo wazi na kunyakua tena “nafasi” tu-liyompa shetani ni kutubu na kumwambia Mungu afunge na kuuponya mlango huo ulio wazi. Haiwezekani kuifunga milango hiyo na kupokea uponyaji kamili wa roho au hisia, au upo-nyaji kutokana na giza, bila kitendo cha toba. Pia ni vigumu kupokea uponyaji wa miwli bila kitendo cha toba.
2. Mungu anaona kwamba toba ni muhimu sana. Chochote utakachotaka kuamini… amini kwamba toba si kitu cha hiari. Neno tubu (au toba) limetumika karibu mara 126 katika Bib-lia. Mungu alijua kwamba tunatakiwa kukumbushwa mara kwa mara kuhusu kanuni hii. Kila mara kumbuka kwamba Mungu anataka “unyofu wa ndani” (Zab. 51:7). Mara nane (na Yesu mwenyewe alinena mara mbili) maandiko yanatuamuru, “Jihadharini [ikiwa na maana ya, “kuwa waangalifu”] (Kut. 19:12, Kumb. 4:23 na 11:16, Yer. 17:21, Luka 17:3 na 21:34, Mate.5:35 na 20:28). Sisi wenyewe tunatakiwa kukifanya kitendo hicho cha toba.
3. Kila uhusiano tulionao na Mungu unategemea hali yetu ya toba. Iwapo dhambi haiko, hakuna haja ya kutubu. Kwa hali yoyote, maandiko yanatuonyesha kwamba Mungu hawezi kusikia maombi yetu tusipotubu (Zab. 66:18, 1 Pet. 3:12). Vivyo hivyo, Yohana Mbatizaji alihubiri“ubatizo wa kutubu ili kusamehewa dhambi” (Marko 1:4; tazama pia Luka 24:45-47). Mpango wa Mungu wa kutupatanisha naye huanza kwa kitendo cha toba “ili kusame-hewa dhambi.”
4. Mungu anatuamuru tusafishwe na kutakaswa ili tuweze kuingia katika uwepo wake. Kitendo cha kusafishwa na kutakaswa hutegemea toba; kuna vifungu vingi vinavyonena ku-husu hitaji letu la kusafishwa (Zab. 51 na 139:23-24, Mat. 23:26, 2 Kor. 7:1, Yak. 4:8, 1 Yoh. 1:9, Lawi. 11:44).
5. Kufanywa upya pamoja na uhuisho huanza kwa toba. Uchunguzi kuhusu uhuisho mkuu wa kidini unaonyesha kwamba uhuisho huo ulianza kwa toba.
6. Afya yetu ya kihisia na kimwili inategemea toba. “Ungamanieni dhambi zenu…ili mpate kuponywa” (Yak. 5:16). Kuna uwezekano wa milli yetu kukosa kuponywa tukikosa kuun-gama na kutubu dhambi.
7. Kushiriki katika Ushirika Mtakatifu “kwa njia isiyostahili” kunaweza kuleta matatizo makubwa. Kuhusu kitendo cha kutubu kabla ya kushiriki katika Ushirika Mtakatifu, 1 Wakorintho 11:25-30 in-atuonya: “… Basi kila mtu ajichunguze mwenyewe kwanza, ndipo ale mkate huo na anywe kikombe hicho; maana anayekula na kunywa bila kutambua maana ya mwili wa Bwana anakula na kunywa hu-kumu yake yeye mwenyewe. Ndiyo maana wengi kati yenu ni dhaifu na wagonjwa, na wengine kad-haa wamekufa.” Kujichunguza sisi wenyewe na kutubu dhambi zetu (kwa ajili ya kujitayarisha ku-shiriki katika Ushirika Mtakatifu) ni juhudi la kufanywa kila siku maishani.
141
# 21 Uponyaji Unahitaji Toba www.healingofthespirit.org
Hatua za Kufanya Toba
Ikiwa toba ni muhimu sana, tunatakiwa kuifanya vipi? Kuna hatua sita zina-zohusika katika kitendo cha toba.
1. Kuhukumika: ni kusadiki au kujua moyoni mwako kwamba kuna kosa mahali. Mojawapo ya kazi za Roho Mtakatifu ni kuwasadikisha watu. Se-hemu kubwa ya kitabu hiki imetayarishwa ili ikusaidie kutambua sehemu katika maisha yako zinazohitaji toba. (Soma maandiko yafuatayo ili uone hali mbalimbali za kusadikisha: Zab. 51:3, Yoh 8:9, Yoh 16:8, Mate. 2:37 na 5:38, 2 Kor. 7:9-10).
2. Kuungama—kwa Mungu na kwa ndugu zako: Watu wengi huwa wako tayari kuungama dhambi zao kwa Mungu lakini huwa hawataki kuungama dhambi zao kwa ndugu zao. Katika Yakobo 5:16 tunashauriwa, “Ungama-nieni dhambi zenu…ili mpate kuponywa.” La kusikitisha ni kwamba, iki-wa hutaki dhambi zako ziletwe katika “nuru,” milango iliyofunguliwa huenda isiweza kuzibwa. Shetani hufanyia kazi gizani. Mungu anatutaka tuungame ili tuweze kupokea msamaha wa dhambi. Bila shaka, tunahitaji kuwa na ujasiri: hatutakiwi kujisahau na kusimama juu ya jukwaa na kuanza kumtukuza shetani kwa kushuhudia juu ya kila jambo baya tulilofanya, la-kini tusikose kuungama sehemu fulani katika ushuhuda wetu ikiwa Mungu atatwambia tufanye hivyo (hii huenda ikamfaidi mtu mmoja au watu kadhaa ambao Mungu amewachagua waweze kusikia ushuhuda huo). (Soma maandiko yafuatayo: Marko 1:4, Yak. 5:16, 1 Yoh.1:9.)
3. Toba: Mwambie Mungu kwa sauti kwamba unatubu dhambi ulizofanya. Mungu anajua kwamba unatubu kwa sababu anaujua moyo wako, lakini sa-babu ya kukiri “kwa sauti” ni kwamba Shetani anatakiwa kusikia una-chosema. Yeye haujui moyo wako wala hawezi kujua kilicho akilini mwa-ko. Wakati mwingine ni lazima umwambie Mungu unatubu kwa dhambi fu-lani ulizotenda wakati fulani na mahali fulani. Wakati mwingine unaweze kukusanya dhambi hizo pamoja na kumwambia Mungu kwamba unatubu kwa wakati wote uliotenda dhambi hizo, kwa mfano, uwongo (rejelea Zab. 38:18, 2 Kor. 7:9).
4. Kukanusha: Katika hali zinazohusu dhambi nzito, kama vile kujihusisha na mizungu/ushetani, utahitaji kuchukua hatua nyingine ya kukanusha dham-bi hiyo, ukimwambia Shetani kwamba unachukua idhini ya kiroho (au nafa-si) uliyokuwa umempa (Isa. 55:7).
5. Kugeuka: Kugeuza au kubadilika, au kuacha kutenda mabaya na kuamua kutii uadilifu wa Mungu na mapenzi yake, ni masharti mengine ya to-ba. Ukimwambia Mungu unatubu ilhali unaendelea katika mwenendo
142
# 21 Uponyaji Unahitaji Toba www.healingofthespirit.org
uleule, mlango utabaki wazi na hutaweza kupokea uponyaji. Toba ya kweli inahitaji mabadiliko kamili katika mtazamo na mwenendo (Tazama Luka 15:11-24, Yoh. 4:7-29 na 8:11).
6. Kurudisha: Huenda ukahitajika kurudisha ulichochukua iwapo Mungu atakwambia ufanye hivyo. Fanya unavyoelekezwa na Mungu (Lawi. 6:5, Luka 19:8—Mfano wa Zakayo wa kuwarudishia watu vitu vyao mara nne; 2 Kor. 7:9-10).
Namna ya Kutubu
Toba ni njia inayohitaji kuzingatiwa kila mara kwa mara. Sehemu zifuatazo katika kitabu hiki zitakusaidia kutambua dhambi zilizo katika maisha yako na milan-go iliyo wazi katika ua lako la kiroho inayohitaji kuzibwa na kuponywa; shughulikia sehemu zinazokuhusu pekee.
Hatua ya kwanza ya toba ni kusadiki kwamba umefanya kosa, kutambua kitu unachohitaji kutubu. Kwa hivyo, tengeneza orodha ya dhambi ambazo Mungu ataku-onyesha unapopitia sehemu zifuatazo na unapotumia mfano wa orodha uliyopewa. Baada ya kutambua vitu ambavyo Mungu anataka viachiliwe na kuponywa, omba ombi lifuatalo la kuungama dhambi.
Ombi la Kuungama Dhambi
Kwa kila dhambi au kikundi cha dhambi ulizotambua, omba kwa kutumia mis-tari ya maneno yafuatayo:
Bwana Mungu, ninaungama na kukubali _________________ kama dhambi katika maisha yangu. Ninasikitika kwa kufanya dhambi hizo na ninatubu. Ninakanu-sha dhambi hiyo na kumpa Baba wa Mbinguni nafasi yote ya kiroho. Katika jina la Yesu ninaomba. Amina.
Baadaye, tafuta rafiki mwaminifu au mchungaji halafu umwonyeshe orodha yako-kwa ajili ya kuungama. Hutakiwi kueleza kila kitu kinagaubaga lakini unahitaji kuungama dhambi hizo. Mwambie rafiki yako au mchungaji akuombee, ili Bwana akusamehe dhambi zako zote na akuponye; omba kwamba milango yako ya kiroho katika kila sehemu hizi itaponywa na kufungwa. Kisha msifu Yesu.
143
# 22 Uponyaji Kutokana na Athari za Giza www.healingofthespirit.org
Kufunga Milango - Uponyaji Kutokana na Athari za Giza
Zaidi ya thuluthi moja ya huduma ya Yesu ya uponyaji ilihusu kuwaweka watu huru kutokana na nguvu za giza. Sisi ambao ni wanafunzi wake, je, tunatarajia kwamba huduma “yetu” ya uponyaji itakuwa tofauti?
Wakristo wengi hawaamini kwamba Wakristo wanaweza kukandamizwa na athari za giza. Tatizo lililo hapa ni la ufahamu: “Watu wengi wameangamia kwa kukosa maarifa.” (Hosea 4:6). Mtu ambaye ni mgonjwa na hajui ni mgonjwa hawezi kwenda kwa daktari. Mkristo aliye na ulemavu ndani yake—au aliyefungwa na athari za giza anayedhani kwamba maisha yake, ni “ya kawaida,” hatawahi kumwambia Mungu amponye: na “Hampati kila mnachotaka kwa sababu hmkiombi” (Yak. 4:2).
Wakristo wengi hung’ang’ana na masuala makubwa maishani mwao lakini hawajui kwamba ushindi aliowashindia Yesu msalabani unawahakikishia wokovu wa milele na vilevile unawapa ufunguo wa kuwekwa huru, na vile nanma ya kupata uhuru kutokana na wapenyezaji wa kipepo pamoja na nguvu za giza. Yesu tayari ametupa msamaha lakini wapenyezaji hao hubaki—mpaka tuwape notisi ya kuondoka.
C. Peter Wagner na wengine wameainisha “vita vya kiroho” katika viwango vitatu tofauti, kama iliyo-tajwa hapa chini:
1. Kiwango cha chini au cha mtu binafsi: ambapo kuyafukuza mapepo kutoka kwa mtu fulani (kunakojulikana sana kama ukombozi) hufanywa. Utaratibu wa kufanya hivyo umeelezewa kwa ma-pana katika sehemu iliyo na kichwa hiki: “Uponyaji Kutokana na Athari za Giza.”
2. Kiwango cha Ushetani/Mizungu: kinachohusu shughuli za kipepo zinazofanyika ndani ya vitu, kama inavyofanyika katika ushetani, uchawi, ushamoni, curandero, na freemason (kama ilivyoeleza katika sehemu zengine zilizo ndani ya kitabu hiki.)
3. Kiwango cha Eneo: hivi ni vita vya kiroho vinavyohusiana na nguvu kuu na nguvu zinazotawala nyumba, makazi ya eneo fulani, jiji eneo, mikoa, na mataifa (nayo imeelezwa zaidi katika sehemu in-ayeleza juu ya “Kuliweka Huru Kanisa Lako”).
Falme Mbili
Biblia inaeleza juu ya falme mbili tofauti. Ufalme wa Mungu (Mbinguni) na ufalme wa Shetani (Jehanamu). Katika vifungu vitano, Shetani ameitwa “mungu”—au mfalme—wa “dunia hii” (Yoh. 12:31, 14:30, 16:11, Efe. 2:2). Shetani alimuasi Mungu hata kabla wanadamu hawajaingia duniani. Baba alimtuma Yesu aharibu kazi za ufalme wa Shetani. Tunaishi katikati ya kipindi cha ushindi dhidi ya kifo ambapo Shetani alishindwa katika msalaba, kifo na kufufuka kwa Yesu, na mwisho wa kuharibiwa kwa ufalme wake, Bwana atakaporudi tena. Hivyo basi; tuko katika vita vya kiroho mpaka Kristo atakaporudi.
Mpango wa Shetani Kuhusu Ufalme Wake
1. Kutuzuia kumwamini Mungu na Yesu
2. Kutuzuia kumjua Yesu Kristo.
3. Kutuzuia kumtumikia Yesu Kristo vizuri.
Kanuni Saba za Somo la Mapepo
Kuna nadharia nne za mawazo kuhusu asili ya mapepo—hatutazipitia hapa; hata hivo, kuna makubaliano kuhusu kanuni zifuatazo kama ilvyoorodheshwa hapa chini (zilitambuliwa na C. Peter Wagner):
1. Kuna viumbe viitwavyo mapepo au roho waovu.
2. Mapepo ni viumbe vilivyo na sifa za mwanadamu—lakini havina mwili; kwa mfano vina tabia, hiari, hisia (kama vile hasira na wivu), ufahamu, kujitambua, na uwezo wa kuzungumza.
3. Mapepo hutenda mambo miongoni mwa binadamu na hutaka kuingia ndani ya wanadamu na wanyama ili yaweze kuidhihirisha hali yao.
4. Nia ya kila pepo ni uovu—kusababisha mateso mengi iwezekanavyo katika maisha ya sasa na maisha ya baadaye.
144
# 22 Uponyaji Kutokana na Athari za Giza www.healingofthespirit.org
5. Mapepo yamepangwa chini ya mfumo wa ngazi za madaraka ya viongoz, wakuu, mamlaka, na Shetani ndiye kiongozi mkuu.
6. Mapepo yana nguvu fulani zinazopita uwezo wa wanadamu ambazo hutumiwa nayo kutenda maovu wayatakayo.
7. Mapepo yameshindwa kwa damu ya Yesu na hivyo basi yanaweza kukabiliwa (kwa uwezo wa nguvu za Roho Mtakatifu anayefanya kazi kupitia kwa waumini).
Kile Ambacho Roho Wachafu Hufanya
Kuna mapepo yasiyoweza kuhesabika, kila moja hulingana na kila dhambi. Kitabu kimoja kiitwacho “Pigs in The Parlor” kinaorodheshwa zaidi ya mapepo 250. Baadhi ya sifa za roho wachafu ni:
1. Huendelea kuwajaribu watu ili watende dhambi (Mwa. 3:1-6)
2. Huumiza na kuharibu (Ayubu 2:3-6)
3. Hupinga malaika wa Mungu (Zak. 3:1)
4. Hunena na kulia (Math. 8:29-31, Luka 4:41 )
5. Hukaa moyoni mwa wanadamu na wanyama (Mat. 8:28-32)
6. Huiba ukweli kutoka akilini mwetu (Mat. 13:19)
7. Huwaangusha watu (Luka 4:35)
8. Huwatesa watu (Luka 6:18)
9. Huwatoa watu povu kinywani (Luka 9:39)
10. Hujaribu kudhihirisha hali yao (Mat. 17:15)
11. Huiba neno la Mungu kutoka katika mioyo ya watu (Luka 8:12)
12. Huifunga miiili ya watu (Luka 13:16)
13. Hupinga, husumbua, na kuzuia kazi ya watumishi wa Mungu (Luka 22:31, 2 Kor. 12:7)
14. Huwajaribu watu wa Mungu ili watende dhambi (Luka 22:31)
15. Huweka mawazo na mipango miovu ndani ya akili za watu (Yoh. 13:2, Mat. 5:3)
16. Hutia mawazo machafu ndani ya watu (Yoh 13:2, Mat 5:3)
17. Huwafunga watu kimwili (Luka 13:16)
18. Hujeruhi watu (Luka 9:39)
19. Huwajaribu watu wa Mungu kutenda dhambi (luka 22:31)
20. Huenda kinyume, kuwatesa na kuzuia kazi ya Mungu (Luka 22:31, 2 Kor 12:7)
21. Huingia ndani ya watu na kuwatawala—vile Shetani aliingia ndani ya Yuda(Yoh.13:27)
22. Uwongo (Mate. 5:3)
23. Huiga vitu halisi (Mate. 8:9-11)
24. Husababisha magonjwa na kuteseka (Luka 13:11)
25. Huwashambulia watu (Mate. 19:16)
26. Huwajaribu waumini ili wafanye mambo yasiyo ya kimaadili (1 Kor. 7:5)
27. Huziba akili za watu ili wasiujue ukweli wa injili (2 Kor. 4:4)
28. Hujifanya malaika wa nuru (2Kor 10:4)
29. Hutumia unyonge wa watu (2 Kor. 2:11)
30. Hupanga kazi ya mapepo (Efe. 6:11-12)
31. Huzuia ueneaji wa injili (2 Thes. 2:1-10)
32. Hutega mitego ili waumini waweze kutenda dhambi (1 Tim. 3:7)
145
# 22 Uponyaji Kutokana na Athari za Giza www.healingofthespirit.org
33. Huhimiza kuweko kwa dini za uwongo na mambo ya roho kwa kutumia kanuni za mapepo (1 Tim. 4:1-3)
34. Hushambulia kwa ukali (1 Pet. 5:8)
35. Huchochea mateso dhidi ya Wakristo (Ufu. 2:10)
36. Huwadanganya watu wote (Ufu. 12:9)
37. Huwashitaki na kuwakashifu waumini (Ufu. 12:10)
Unavyoweza Kujua Iwapo Kuna Mapepo
Mambo mengi yameandikwa kuhusu maneno yanayoweza kufafanua au kuainisha kiwango ambacho mtu huathiriwa na mapepo, kama vile athari, kandamizo, au kupagawa. Kwa vile watu hawawezi kukubaliana kabisa kuhusu ufafanuzi wa maneno haya na kwa vile tunaamini kwamba badala ya kiwango cha athari, huenda ikawa ni hali ya daraja ya athari (kuanza kuathiriwa polepole hadi kuathiriwa vikali), hatutatumia maneno hayo lakini ni muhimu sana kujua iwapo mapepo wako.
Zifuatazo ni njia tunazoweza kutumia kujua ikiwa mapepo wako, kwa kupata habari moja kwa moja au kwa kutathmini dalili:
1. Mungu humwambia mhusika anayetaka uponyaji kwamba kuna pepo
2. Mhusika ataeleza uwezekano wa pepo kuweko kwa kutumia uchunguzi, orodha, au kidadisi
3. Kupitia kwa vipawa vya ujuzi, kutambua roho, au roho wa ufunuo
4. Mungu humwambia mwombezi
5. Kutokana na uzoefu (kujua na kutambua vile yanafanya kazi)
6. Kuwa na mtu mwenye amani atakaye uliza iwapo mapepo yako (nayo yakikubali kwamba yako).
7. Pepo kujitoa wazi wakati wa ibada au wakati wa ombi la ukombozi
8. Kwa pepo kunena kupitia kwa mtu au kwa kuziona tabia za mtu zisizoweza kuzuiwa.
Dalili za Uwezekano wa Mapepo Kuwa na Makazi Ndani ya Mtu Kutoka kwa Daraja ya Chini Hadi ya Juu
1. Kutotulia kunakoonekana wakati wa ibada
2. Kujaribu kila kitu
3. Kutokuwa na usingizi mzuri
4. Kuhisi kulazimishwa bila sababu
5. Tabia za kupita mipaka
6. KUlazimishwa kufanya kitu kisicho cha kawaida
7. Woga, wasiwasi, au chuki ya kudumu—bila sababu yoyote
8. Uzito kifuani
9. Kuhisi msamaha wa masharti
10. Mapendekezo yasiyo ya kawaida
146
# 22 Uponyaji Kutokana na Athari za Giza www.healingofthespirit.org
11. Kuchukia kitu chochote kinachohusiana na dini na/au Ukristo
12. Kutosoma maandiko au kukosa kuomba (kabisa)
13. Kutoenda kanisani.
14. Kutoweza kusoma maandiko kwa muda wowote.
15. Kujitenga na watu wa kanisa
16. Kutoweza kuomba
17. Kutoweza kulitaja jina la Yesu
18. Kuhisi kwamba kuna kitu ndani ya mtu, kinachotawala matendo na/au mazungumzo yake.
19. Kusikia sauti akilini zikinena na mtu huyo
20. Kudhihirisha uigaji wa vipawa vya kiroho
21. Kuwa na mawazo ya kujiua
22. Kujaribu kujiua
23. Kujikatakata
24. Kukausha macho au kutazama mahali pamoja kwa muda mrefu
25. Ikiwa mazungumzo afanyayo si yake; kuna kubadilika kwa sauti (au sauti nyingi) au sauti za paka
26. Alama kutokea ghafla mwilini
27. Kuzungumza na viumbe visivyonekana
28. Tabia zisizo za kawaida; kufanya mambo kama wanyama, kutoweza kutulia, ishara ya mikono au kichwa isiyo ya kawaida, mikunjo ya mwli isiyowezekana kwa urahisi.
29. Macho yake kuwa meupe, hali isiyo ya kawaida, yenye kuchukiza; kuweko kwa harufu mbaya sana
30. Vitu kuanza kutoka puani au mdomoni
31. Mtu huyo hurushwa na nguvu zisizoweza kuonekana
32. Ugonjwa wa ghafla wa muda mfupi na kutokwa na povu mdomoni
Orodha ndefu zaidi iko katika kitabu cha Horrobin kiitwacho “Healing & Deliverance” (kurasa za 55-84) na katika kitabu cha Wallace kiitwacho “The Occult Trap” (kurasa za 211-216), na katika vitabu vingine vingi vilivyo mwisho wa sehemu hii.
Mambo ya Kuzingatia Katika Huduma
Si ajabu kwamba sehemu hii iko mwisho wa somo hili. Mhusika anayetaka uponyaji akifuata mfululizo wa taratibu ya sehemu iliyoorodheshwa katika ukurasa wa “Yaliyomo” wa kitabu hiki, huenda hakutakuwa na haja yakufanya ukombozi rasmi. Mhusika akianzia sehemu hii atang’ang’ana sana kuyaondoa mapepo hayo..
Pepo anaweza tu kuingia ndani ya mtu ikiwa ana haki ya kiroho ya kufanya hivyo, pamoja na kupata nafasi ya kufanya hivyo. Ni jambo la kimsingi sana kuziondoa haki hizo ili ukombozi bora na wa kudumu uweze kupatikana. Mwombezi anapozungumza na mhusika, anatakiwa kutambua shida inayojitokeza na mzizi wa shida hiyo.
Kujua vipi na lini pepo huyo aliingia ni muhimu kwa ajili ya kuufikia mzizi wa tatizo hilo na kutasaidia sana wakati wa ukombozi. Mlango wa kiroho ukishafungwa kwa njia ya kutubu, kusamehe, na uponyaji wa ndani, nafasi au haki ya kiroho ya pepo kudumu ndani ya mtu huyo huondolewa. Kwa hivyo pepo huyo ni lazima—na wakati mwingine huondoka bila maombi kufanywa; ndiyo maana ni
147
# 22 Uponyaji Kutokana na Athari za Giza www.healingofthespirit.org
muhimu kila mara kuombea uponyaji wa kiroho na uponyaji wa ndani kwanza.
Waombezi wengine huamini kwamba litakuwa jambo la msaada ikiwa mhusika atajaza fomu ya uchunguzi au orodha kwanza, ili kutambua ngome za sehemu za utumwa. Kuna vifaa maalum vilivyoorodeshwa mwisho wa sehemu hii katika vitabu vya watu hawa: Wagner, Gibson and Wallace
Mbinu za Kufanya Huduma ya Ukombozi
Kuna zaidi ya wanachama 150 wa Shirika la Kimataifa la Wahuduma wa Ukombozi na wengine wengi walio na kipawa hiki ambao wanahudumu katika kusanyiko za mashinani. Kila mhuduma hutumia mbinu ya ukombozi anayoiona kuwa bora na ambayo inaweza kutofautiana na zengine. Mbinu hizo zinaweza kuwekwa katika makundi matano makuu, kulingana na ujuzi na uzoefu wa mhuduma, nguvu za Roho Mtakatifu zilizo ndani ya mhuduma wakati huo, na iwapo mhitaji anaonyesha wazi (ishara).
1. Kujikomboa: Kulingana na uzito wa athari hiyo, mhitaji anaweza kusoma vitabu mbalimbali kama kitabu hiki, kuomba sala ya kufunguliwa na kuwekwa huru. Mbinu hii haitumiwi sana.
2. Kitendo cha Mungu cha Enzi: Wahitaji wengine hukombolewa moja kwa moja kwa mkono wa Mungu. Mtume Paulo ni mfano mzuri. Mhitaji huyo huwa anaomba na kumsihi Mungu amweke huru. Kufunguliwa huko kunaweza kutokea kwa njia nyingi tofauti na mahali mbalimbali.
3. Kukabiliana: njia hii inaweza kutumika mara nyingi iwapo mtu ataonyesha wazi ishara katika mikutano mikubwa ya injili, au katika mikutano ya ibada. Mara nyingi kitendo hicho huwa hakitarajiwi na huwa kinamshangaza mtu huyo. Waombezi huyaamuru mapepo yajitambue kwa majina, na pia yaeleze nafasi yao ya kiroho ya kuwa ndani ya mtu huyo. Katika mazingira ya mkutano mkubwa wa injili, mlango ulio wazi unaweza kuwa ni ngome iliyokuwa ikivunjwa na mhubiri mtu huyo alipoanza kuonyesha wazi ishara. Wahuduma wanaweza kuyaambiwa mapepo hayo yataje majina yao, na yaeleze haki waliyonayo ya kubaki ndani ya mtu huyo. Huenda pepo huyo akaendelea kujidhihirsha wakati huo. Wakati mwingine njia hiyo huwa ya kelele, yenye sarakasi, ndefu, na mara nyingi inaweza kumdunisha mtu anayehudu-miwa—na wao humzingatia pepo huyo badala ya kumzingatia Yesu. Baada ya nafasi hiyo kuchukuliwa na Mungu (kwa njia ya toba na maombi yanayofaa), pepo huyo huamriwa aondoke. Nilazima kufahamu kwamba katika kila hali isipokuwa moja (Math. 8:29-32, Marko 5:1-13, Luka 8:27-33), Yasu alikataa kuzungumza na mapepo na akayaamuru yanyamaze (Marko 1:23-25, Marko 3:11-12, Luka 4:33-36, Luka 4:41). Ikiwa tutafanya kile alichofanya Yesu,” hatutakiwi kuzungumza na mapepo mpaka iwe ni lazima kufanya hivyo. Hata hivyo, ikiwa kuzungumza na mapepo ndiyo njia pekee tunayojua ya “kuwafukuza,” au ikiwa hatuna imani katika njia nyingine, itatubidi tutumie njia hiyo na kutarajia kwamba atatubariki tunapofanya juhudi hizo.
148
# 22 Uponyaji Kutokana na Athari za Giza www.healingofthespirit.org
Hata hivyo, tukifanya ukombozi kwa njia hii pekee, bila kumhudumia mtu uponyaji wa ndani, mapepeo yanaweza kutoka tu kwa muda mfupi, kisha yarudi tena kwa sababu mlango wa kuingilia bado uko wazi (kwa vile kuumizwa, machungu, maumivu, n.k hayajapona).
Mhuduma anapozidi kuwa na imani na uzoefu, atajifunza kumtazamia Mungu ili amjulishe ni mapepo gani yapo ndani ya mtu na yanawezaje kuondolewa. Mtu mmoja katika timu ya waombezi aliye na kipawa cha kutambua roho husaidia sana wakati wa uponyaji wa ndani
4. Ukombozi Unaoamriwa na Bwana: Wakati mwingine, Bwana atatambulisha roho mchafu kwa mhuduma halafu ammpe imani na nguvu za kumfukuza kwa amri moja pekee, kama alivyofanya Yesu. Lakini kuna wahuduma wachache sana wanaofanya hivyo mara kwa mara.
Sijawahi kuona kitendo hiki kikifanyika katika miaka 30 niliyofanya huduma ya ukombozi.
5. Maombi katika mistari ya uponyaji, kuwaita watu madhabahuni au wakati wa huduma. Wahitaji wengine ambao huja mbele ya madhabahu kuombewa hukombolewa kutokana na nguvu za giza, mazoea ya ubaya huondolewa mara moja, na miili yao hupata uponyaji.
6. Ukombozi wa Kikundi Wakati wa Mikutano: Upako mkuu wa Roho Mtakatifu ukishuka katika mkutano wakati wa kuabudu na kuhubiri, wakati mwingine watu hukombolewa bila kuguzwa na mtu yeyote wala kuombewa. Wakati mwingine jambo hilo hufanyika wanapopumzika ndani ya roho pengine wakiwa wamelala juu ya sakafu. Jambo hilo hutendeka katika ibada za makanisa ya uhuisho lakini halitendeki katika makanisa ya kitamaduni. Mbinu hii ndiyo hutamanika sana na, ni ya haraka, nayo humtukuza Mungu.
7. Mpango wa Hatua-Kumi wa Pablo Bottari: Kwa miaka mingi Pablo Bottari alisimamia hema la ukombozi la mikutano mikubwa ya injili ya Carlos Anacondia’s nchini Argentina. Akiwa huko alisimamia huduma ya ukombozi kwa maelfu ya watu naye mwenye alishiriki katika ukombozi wa zaidi ya watu 30,000. Aliunda mfano huu wa hatua kumi wa ukombozi uliomtulivu na wa kufaa. (Kitabu cha Pablo Bottari kinachoitwa “Free In Christ” (Creation House, 2000, ISBN 0884196577) Mengi kuhusu njia hii yameelezwa hapa chini.
Kubainisha kati ya Ishara Wazi za Mapepo na za Roho Mtakatifu
Ishara wazi za nguvu za giza na za Roho Mtakatifu wakati mwingine huonekana kama kwamba zinafanana. Ishara wazi ikianza kuonekana mhubiri au mmoja wa kikundi cha huduma anaomba kwa mamlaka makuu dhidi ya ukandamizaji wa mapepo, ishara zilizo wazi zinaweza kudhaniwa kuwa zinasababishwa na uwepo wa mapepo. Kwa upande wa pili, ishara wazi zinapoanza mhubiri au mmoja wa kikundi cha huduma anapoombea Baraka, au mwongozo, au kwa ajili ya kupewa vipawa vya kiroho, ishara hizo wazi huwa zinatokana na kazi ya Roho Mtakatifu
Iwapo hali hizo hazionyeshi chochote, kuna vidokezo hapa.
1. Mtu akionyesha ishara wazi za mapepo, mara nyingi yeye huanguka chini au hukimbia ndani ya chumba hicho akipiga nduru, na kutakuwa na ishara zengine za mwili kama vile kuukunja mwili, kuukunja uso, sauti kubadilika ghafla, kukataa kuwaangalia wahuduma, macho kubingirika, povu kutoka mdomoni, nduru, kufanya vitendo vya uhasama. Ishara zengine zilizo wazi ni kama vile
149
# 22 Uponyaji Kutokana na Athari za Giza www.healingofthespirit.org
kuumwa na kichwa ghafla, kupata kichefuchefu, matendo ya ukali wa ghafla, au matendo ya uharibifu, kama vile kuwapiga watu mateke au kuvunja samani/fanicha, kutoa sauti kama ya nyoka, kutaka kuwakwaruza watu kwa makucha.
2.Iwapo mtu anaonyesha ishara wazi za Roho Mtakatifu, anaweza kulia kwa sauti, kutoa machozi bila kizuizi, na anaweza kuanguka juu ya sakafu.
3. Iwapo mshirika aliye katika kundi la huduma ana kipawa cha utambuzi wa mapepo, ni vyema kumwambia athibitishe ni roho gani aliye ndani ya mtu huyo.
4. Iwapo mtu huyo “yuko macho”, muulize. Mara nyingi anaweza kujua iwapo ana amani moyoni mwake (ishara ya kuonyesha ni Roho Mtakatifu), au iwapo ana woga na fadhaiko.
5. Iwapo mtu huyo yuko “chini,” halafu mtu aliye na mamlaka ya kiroho aweke mkono wake juu ya kichwa cha mtu huyo, au aiweke Biblia juu ya tumbo la mtu huyo, au auweke msalaba juu ya kichwa cha mtu huyo, mtu anayetawaliwa na mapepo atakuwa na mkali na atajaribu kugeuka na kujipinda kuuondoa. Iwapo mtu anatawaliwa na Roho Mtakatifu hawezi kufanya matendo yaliyotajwa hapo juu.
6. Iwapo mtu huyo anatoa machozi bila kizuizi, au anaomba, bila shaka mtu huyo anaongozwa na Roho Mtakatifu.
Wahitaji huja kutafuta ukombozi kwa njia moja kati ya hizi mbili.
(1) Mhitaji huonyesha ishara wazi katika mkutano mkubwa wa injili, wakati wa mkutano, au wakati wa kuwaombea wagonjwa (njia ya kuonyesha hisia na huwa inamshangaza mtu huyo), AU
(2) Mhitaji hujua kwamba ana nguvu za giza na huja kuombewa kabla ya kujitokeza kwa ishara wazi, (njia ya utendaji wa kutangulia). Njia hii inapendelewa zaidi. Anza na hatua ya 2 iliyo hapa chini.
Hatua zifuatazo ni muhtasari kutoka kwa njia ya Hatua-Kumi ya Pablo Bottari
Hatua ya 1: Pepo akionyesha ishara wazi katika mkutano mkubwa wa injili, katika mkutano, au wakati wa maombi.
Mtu akianza kuonyesha ishara wazi katika mkutano kisha apoteze fahamu (mapepo huwa yanautawala mwili na sauti ya mtu huyo na hayawezi kumwacha atende atakavyo), usikemee mapepo hayo kwanza (huwa si pepo mmoja pekee) kwani kufanya hivyo kutavuruga mapepo hayo na kumfanya mtu huyo awe na woga. Ni lazima kila mara tumwoneshe mtu huyo upendo wenye huruma; ingawa amepoteza fahamu, mara nyingi mtu huyo huwa anaweza kusikia tunachosema kwa hivyo kuyakemea mapepo kunaweza kuzidisha woga ndani ya mtu huyo.
Kwanza, tambua iwapo ishara hizo wazi ni za kipepo, au Roho Mtakatifu kwa kutumia mwongozi ulio hapo juu. Kikundi cha waombezi kiwe tayari kumpeleka mtu huyo mahali patulivu iwapo ishara hizo zinavuruga ibada.
Mtu mmoja pekee azungumze na mtu huyo kimyakimya. Usipige kelele. Roho Mtakatifu na mapepo husikia. Ikigunduliwa kwamba ishara hizo ni za Roho Mtakatifu, mwache alie kwa kipindi fulani. Mwambie maneno ya upendo na amani. Waambie waombezi waombe kimya-kimya.
Tahadhari unaposema. Iwapo mtu huyo anaonyesha ishara za mapepo, au za Roho Mta-katifu, anaweza kusikia usemayo. Usimzidishie woga kwa kuzungumza juu ya mapepo
150
# 22 Uponyaji Kutokana na Athari za Giza www.healingofthespirit.org
akikusikia.
Baada ya kumpeleka mtu huyo mahali pa faragha itabidi mtu huyo azuiliwe kitandani au sakafuni ili asijiumize wala kumuumiza mtu yeyote katika timu hiyo ya huduma. Yafunge mapepo hayo kimya kimya kwa kusema, “Lazima unyenyekee chini ya jina la Yesu. Tulia.”
Baada ya mapepo hayo kufungwa na mtu huyo kutulia, tutamwambia mtu huyo ainuke polepole: “Katika jina la Yesu, nachukua mamlaka juu ya akili na mwili wako. Pata fahamu sasa. Fumbua macho yako.” Mwambie kwa upole kwamba Mungu anampenda halafu muulize ikiwa yeye ni muumini au la. Mwambie kwamba ana tatizo la kiroho na ungependa kumsaidia. Mwambia hivi “chukua mamlaka “utawale mwili wako sasa na usimame.”
Ikiwa mapepo hayo hayatamruhusu mtu huyo kuamka au kusimama, akiwa mahali palipotulia endelea kunena na mapepo hayo ukiyaambia mapepo hayo “yabaki chini,” na uiambie roho ya mtu huyo iinuke. Usianze kuhudumu mpaka utulie ndani ya chumba cha maombi na mtu huyo apata fahamu tena. Endelea kumwonyesha upendo. Mtu huyo anatakiwa kuhisi upendo, kukubaliwa na kuhimizwa. Endelea kumwambia mtu huyo kwamba Yesu anaweza kumweka huru. Mwambia kwamba Yesu anampenda.
Lazima uweze kuzungumza na mtu anayehudumiwa, kwa sababu ni lazima aweze kushirikiana nawe ili ukombozi huo uweze kufanikiwa.
Iwapo mtu ataonyesha ishara wazi ndani ya mkutano, lakini aendelee kuwa na fahamu, mpeleke mahali patulivu na uanze kumhudumia kwa kuanza na hatua ya 2.
Hatua ya 2: Hakikisha mtu huyo amemkubali Yesu kuwa Mwokozi na Bwana wake, na mtu huyo angependa kuwa huru.
Mhitaji akija kuombewa ombi la ukombozi, au akiletwa, lakini awe yuko na fahamu, muulize kuhusu uhusiano wake na Mungu. Je, ameisikia injili? Je, ameokoka, Ikiwa hajafanya hivyo, anatakiwa kuelewzwa kuelezwa kuhusu injili kisha akaribishwe kumpa Kristo maisha yake. Anatakiwa kubatizwa na kupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu. Kumwombea mtu asiyeamini ombi la ukombozi ni jambo gumu sana, na mhitaji huyo hataweze kudumisha ukombozi huo bila kuwa na Roho Mtakatifu. Huenda kukawa na shawishi la kuomba ombi la ukombozi mara moja. Hata hivyo, huenda ikawa mapepo hayo yamekuwa ndani ya mtu huyo kwa muda mrefu, kwa hivyo hakuna haja ya kuomba mara moja. Mtu huyo atafaidika iwapo kwanza atazaliwa mara ya pili. Kufanyla hivyo kutarahisisha ukombozi huo baadaye.
Iwapo mhusika huyo ni mtu anayeamini na amebatiwa na anajua kwamba ana gia ndai yake, kwanza muulize ikiwa angependa kuwa huru (watu wengine huwa hawako tayari.) Muulize, “je una hakika?” mfunze vile mapepo hingia ndani ya watu na vile mapepo huondolewa. Mpe maandiko asome ili imani yake iongezeke. Mwambie akujulishe atakapokuwa tayari. Mwache asome nakala ya kitabu hiki iwapo kinaweza kupatikana.
Hatua ya 3: Mhoji mhitaji ili ugundue milango iliyo wazi iliyomtia kwenye utumwa.
Hatua ya kwanza katika uponyaji wa ndani na ukombozi ni kutambua milango iliyo wazi. Jambo hili hufanywa kwa (1) kumwambia mhusika akisome kitabu hiki na kujaza orodha za uponyaji wa ndani, au (2) kumwambia kiongozi wa kundi la maombi afanye mahojiano ya mdomo mhitaji huyo akija kuombewa. Iwapo mhitaji huyo hajapata mafunzo kuhusu ukombozi, mhuduma atahitajika kuchukua muda wa kumfunza mtu vile milango hufunguliwa.
151
# 22 Uponyaji Kutokana na Athari za Giza www.healingofthespirit.org
Anza mahojiano haya kwa kumuuliza mtu huyo akamwambie kila ambacho Bwana, au muulize akwambie “hadithi” yake. kufanya hivyo kutakuwezesha kujua milango iliyo wazi. Hawataweza kujua milango yote iliyo wazi. Kwa hivyo kiongozi wa kikundi cha maombi anatakiwa kuwa na wakati wa kumuuliza mhitaji maswali, na ayasikilize majibu na vilevile amsikilize Mungu. Kwani anaweza kuwa na milango mingine iliyo wazi na ambayo haijaorodheshwa. Huenda ikawa mhitaji alitambua mlango mmoja au zaidi katika darasa au mahubiri fulani, au aliambiwa na Mngu, au alifahamisha kutoka mahali pengine. Hapa chini kuna mwongozo wa mahojiano.
1. Ikiwezekana, mwambie mhusika ajaze “Orodha ya Uponyaji wa Ndani” iliyo hapo juu.
2. Njia bora ya kuanza mahojiano hayo ni kuuliza, “Mungu amekuwa akikwambia nini?” au “Niambie hadithi yako.”
3. Sikiliza pale ambapo mtu huyo atasema anaumizwa sana (kimwili, kihisia, au kiroho)
4. Sikio moja limsikilize mhusika, na sikio lengine limsikilize Bwana.
5. Tambua iwapo tatizo hilo ni tatizo linalojitokeza au ni mzizi wa tatizo. (Tatizo linalojitokea ni tatizo linalojirudia ambalo ni ishara ya mzizi wa tatizo. Kwa mfano, mtu anakuja kuombewa akiwa na tatizo linalojitokeza la kuumwa na kichwa. Chanzo cha tatizo hilo ni kwamba hapo awali katika maisha yake alimwendea mbashiri na akafungua mlango wa mizungu/ushetani. Katika hali hiyo, kukiombea kichwa kinachouma hakutaleta uponyaji; kwani hiyo ni ishara tu ya mzizi mkubwa wa tatizo hilo. Mzizi unaosababisha tatizo ni lazima utambuliwe na ukishapona, kichwa hicho kitawacha kuuma.)
6. Hali zinazoweza kuwa na hitaji kubwa la uponyaji wa ndani ni:
• Kukataliwa (kumeelezwa katika sehemu inayoeleza juu ya “Uponyaji Kutokana na Kukataliwa”
• Talaka
• kukataliwa ulipokuwa mtoto
• kufanyiwa mzaha
• kuwa na woga kupita kiasi
• kutoa mimba
• kifo cha mtu wa ukoo wa karibu katika familia (au mtu unayempenda sana)
• kujihusisha na laana
• kutopendwa kama mtoto au mke
• Kupigwa au kudhulumiwa (kwa maneno, kimwili, au kimapenzi)
7. Yaliyomo ni orodha bora ya uchunguzi ya kujua milango inayoweza kuwa wazi. Inaanza kwa milango inayoweza kutambuliwa kwa urahisi (kwa mfano, dhambi za mtu binafsi—kama vile kudanganya, kuiba au kulaghai, kutosamehe, na kujihusisha na mizungu/ushetani).
8. Mwanzoni mwa kipindi cha mahojiano, uliza ikiwa kuna kutosamehe kokote; mara nyingi huwa kuna kutowasamehe watu waliowaumiza.
9. Iwapo kuna magonjwa ya mwili yanayohitaji uponyaji, swali muhimu la kuuliza ni, “Ugonjwa huu ulianza lini?” Iwapo ulianza wakati wa tukio la kiwewe, uchunguzi zaidi wa kiroho utahitajika.
152
# 22 Uponyaji Kutokana na Athari za Giza www.healingofthespirit.org
10. Uponyaji wa ndani na ukombozi unatakiwa kuombewa kwanza, kabla ya uponyaji wa mwili. Matatizo mengine ya mwili husababishwa na matatizo ya kiroho au ya kipepo.
11. Andika vidokezo vya milango iliyo wazi. Ombea orodha hiyo na umwambie Bwana akuonyesha ni milango unayotakiwa kuiombea kwanza. Mara nyingi yeye atakupa mwelekeo.
12. Kipindi cha mahojiano hakitakiwi kuchukua muda mrefu sana (dakika 15-20) la sivyo upako wa maombi unaweza kutoweka. Fahamu kwamba mapepo yanaweza kumfanya mhusika atoe majibu marefu
13. Mwambie Mungu akuonyeshe “vizuizi au milango iliyo wazi” asiyoijua mhusika.
14. Hakikisha umewauliza wengine walio katika timu ya huduma iwapo Mungu amenena nao kuhusu milango mingine.
15. Waulize watu wengine katika kikundi iwapo Mungu amenena nao kuhusu milango mingine zaidi.
16. Tambua ni milango ipi inahitaji ukombozi, na ipi inahitaji uponyaji (ile ambayo mhitaji hakutenda dhambi, lakini wengine walimkosea.)
Hatua ya 4: Ombi la Uponyaji.
1. Anza kwa ombi la kuabudu ambapo kila mtu katika kikundi atakubali atatambua kwamba anamtegemea Mungu. Muulize mhitaji iwapo angependa kuomba. Mwambie mhitaji aombe kwa sauti au kimoyomoyo.
2. Amua mpangilio wa kuishughulikia milango hiyo iliyo wazi.
3. Mwambia mhitaji kwamba Mungu atanena naye na kumpa majibu akilini mwake.
4. Mwongoze mhitaji kuomba ombi la toba. Mwambie mhitaji amfuate kiongozi huyo katika maombi hayo. Tazama maelezo ya maombi maalum kuhusu milango iliyo wazi yaliyo katika kila kitengo cha kitabu hiki ili yaweze kukusaidia. Ombi la kila mlango ulio wazi linatakiwa kuyahu-sisha mambo yafuatayo:
a) kumsamehe mtu aliyemjeruhi au aliyemwongozo katika mwenendo mbaya.
b) kukiri na kutubu kwa ajili ya kila dhambi ya mhitaji
c) kuikana dhambi hiyo katika jina la Yesu
d) kuichukua tena idhini ya kiroho (haki) aliyonayo pepo huyo na kumpa Yesu (wa-kati mwingine hiyo huitwa “haki ya kiroho”).
e)kutubu kwa ajili ya babu za mtu huyo iwapo mlango ulio wazi unatokana na dham-bi ya kizazi.
f) kumuahidi Bwana kwamba mtu huyo hatarudia dhambi hiyo
5. Funga mapepo na hisia na uzifukuze katika jina la Yesu.
6. Mwombe mhitaji huyo ili apate uponyaji wa ndani kutokana na majeraha, vidonda, dhuluma, na kukataliwa ambako hakutenda dhambi yoyote. Weka msalaba wa Yesu katikati ya mhitaji huyo na mdhulumu wake.
7. Omba ili Bwana ampe moyo mpya
8. Omba ili Mungu aliponye tukio hilo
9. Rudia hatua hiyo katika kila mlango ulio wazi mpaka na/au mhitaji ajisikie yuko huru
10. Zaidi ya hayo, usizungumze na mapepo wala kuyaruhusu yazungumze nawe. Kristo hakuyaruhusu mapepo hayo kuzungumza. Yakizungumza, usiyakemee mapepo, bali sema, “Ni lazima mnyenyekee chini ya jina la Yesu. Tulia.”
11. Endelea kuomba mpaka ujue kwamba milango yote imefungwa
153
# 22 Uponyaji Kutokana na Athari za Giza www.healingofthespirit.org
12. Mwambie Mungu akuonyeshe milango yoyote iliyo wazi. Muulize kila mshirika wa kikundi akwambie.
13. Maliza tu baada ya watu wote katika kikundi kukubali kwamba hakuna kazi nyingine inayohitajika kufanywa.
Hatua ya 5: Mwambie mhitaji amsifu na kumshukuru Yesu kwa ukombozi wake.
Sheria ya kushukuru inatumika mahali hapa. Kushukuru kutamfanya mhitaji adumishe ukuombozi wake. Vilevile, muulize ikiwa yuko tayari kushuhudia kuhusu uponyaji wake. Ushuhudia pia husaidia katika kudumisha ukombozi.
Hatua ya 6: Omba ili mhitaji ajazwe na Roho Mtakatifu moyoni mwake na katika kila sehemu iliyokuwa imetawaliwa na nguvu za giza.
Usisahau hatua hii muhimu, mhitaji anafaa kujazwa na Roho Mtakatifu ili kuudumisha ukombozi wake. Jumuisha maombi ya kinabii kwa faida ya siku za usoni na mwenendo wake na Mungu.
Utajuaje Kwamba Roho Wachafu Wameondoka?
1. Mungu humweleza mhusika na mhusika huyo anaweza kulihisi giza likiondoka (yeye huhisi furaha au ushindi)
2. Mungu humwambia mtu mmoja katika timu (kupitia kwa kipawa cha ujuzi na ufunuo au kwa kupambanua roho)
3. Ishara za hapo awali hutoweka (hata hivyo, wakati mwingine roho hujificha na kukosa kuondoka).
4. Uliza kila mshirika wa timu ikiwa amemaliza. Endelea kuomba mpaka kila mtu akubali kwamba mapepo hayo yameondoka.
5. Wakati mwingine huwezi kujua— bali unahitajika tu kungoja na kujionea.
Kuwaita Watu Madhabahuni Wakati wa Huduma
Makanisa mengi ya Marekani na Afrika yana kipindi cha kuwaita watu madhabahuni na wakati wa huduma baada ya kuhubiri Neno. Mara nyingi kipindi hiki huwa cha kelele nyingi ambapo kikundi hca sifa na kuabudu huendelea kuimba na mchungaji huchukua kipaza sauti na kuenda katika kila mstari na kumwombea kila mtu upesiupesi kwa sauti ya juu naye wakati mwingine huwatarajia watu “waanguke chine” kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Ni wazi kulingana na maagizo yaliyotolewa hapo juu kwamba mbinu hii haifaa kwa ajili ya kufanya ombi la ukombozi, au ombi la uponyaji wa mwili, kama tutakavyoona katika vitengo vitakavyofuata. Huku ni kupoteza wakati. Kitendo hicho humtukuza mchungaji, lakini hakimsaidi sana anayetaka uponyaji. Iwapo kutakuwa na maombi ya kuiombea idadi kubwa ya watu baada ya ibada, kwanza kabisa, kanisa linatakiwa kuwa tulivu kadri iwezekanavyo. Kikundi cha huduma kinatakiwa kumsaidia mchunguji. Kisha mahitaji yatakayohitaji muda mrefu na mahojiano yaweze kuhairisha. Sisi humwalika Yesu asafishe, apake mafuta na kuweka bendeji juuu ya vidonda (vya mwili au vya kiroho) halafu tunapanga wakati mwingine wa kufanya upasuaji.
154
# 22 Uponyaji Kutokana na Athari za Giza www.healingofthespirit.org
Kumwombea Mtu Aliyefanya Matambiko ya Kishetani
Ingawaje kitabu hiki hakiwezi kuishughulikia mada hii kwa kina, ni vyema kuwa na utangulizi wa maelezo mafupi.
Kuna ushahidi mwingi wa kuridhisha unaoonyesha kwamba makundi ya wafuasi wa Shetani huwasumbua watu, sanasana watoto. Wao hudhulumiwa na kuteswa na baba zao, hubakwa, na kulazimisha kushiriki katika aina nyingi ya ibada za Shetani zinazodhihaki mateso na kusulubiwa kwa Yesu, kwa kuwachinja wanyama, watu wasio na hatia, sanasana watoto wachanga au vijana wadogo.
Kutokana na matukio hayo, mara nyingi nafsi za watoto hujigawa katika nafsi nyingi ili waendelee kuishi kisaikolojia, ili mtoto huyo aweze kudumu baada ya tukio la kihisi lisiloweza kuvumiliwa. Kudhania kwamba mambo hali hiyo ni roho zinazotakiwa kuondole-wa ni kosa kubwa sana linaloweza kusababisha madhara ya kudumu. Kwa mfano, mtoto akilazimishwa kumtesa au kumua mtu fulani, kuna uchungu mwingi sana kwa mtoto huyo kuamini kwamba yeye ni mtu anayeweza kufanya matendo kama hayo. Kwa hivyo sehemu kuwa “muuaji” ndani yake inaweza kujigawa na kuleta nafsi ya ukatili ya kumwezesha kutekeleza kitendo hicho kiovu. Jambo hilo huitwa Ugonjwa wa Nafsi Nyingi.
Nafasi haitoshi kutoa maelezo ya namna ya kumwombea mtu aliye na tatizo hilo. Lazima mtu awe mwangalifu sana. Vitabu vifuatavyo vinaweza kukusaidia.
Deliverance from Evil Spirits, by Frank MacNutt, Chap 17 pages 223 – 235 Chosen Books, ISBN 0-8007-9232-7
Ritual Abuse, Margaret Smith, Harper Collins 1993
Uncovering the Mystery of MPD, Case Studies by James Friesen (Here’s Life Publish-ers) 1991
Multiple Personality Disorder, by Paul Cooprider www.pullingdownsrongholds.com 863 648 2568. Booklet 34 pages
Bob Larson’s book of Spiritual Warfare Chap 30 pages 372-386. Thomas Nelson ISBN 0-7852-6985-1 479 pages
Kundi la Waombezi
Kundi la waombezi linatakiwa kuwa wafuatao:
1. mtu aliye na imani kuu na nguvu za kiroho (atakayefanya mazungumzo yote)
2. mtu aliye na kipawa cha kutambua roho
3. mwombezi mwingine mmoja au wawili (ni lazima kuwa na mwakilishi wa kiume na wa kike katika timu)
4. mtu mmoja pekee anayenena (au anayemwombea) mhusika
155
# 22 Uponyaji Kutokana na Athari za Giza www.healingofthespirit.org
5. Kila mshirika wa kundi la maombi anatakiwa kuwa amepitia wakati wa uponyaji na ukombozi yeye mwenyewe kabla ya kushiriki katika timu ya huduma.
6. Ni kiongozi pekee anayepaswa kumgusa mhitaji. Muulize kabla ya kumgusa.
Vifaa Vilivyopendekezwa Kuhusu Ukombozi
Kuna vifaa vingi vizuri vinavyopatikana siku hizi, lakini vifuatavyo ni bora zaidi kwa sasa:
1. Charles Kraft, Defeating Dark Angels (Servant Pub., 1992). ISBN 0-89283-773-X.
2. Peter Horrobin, Healing Through Deliverance, Vol. 1 (Chosen Books, 2003). ISBN 0-8007-9325-0.
3. Noel and Phyl Gibson, Freedom in Christ (New Wine Press, 1996). ISBN 1-874367-53-1.
4. Noel and Phyl Gibson, Evicting Demonic Intruders (New Wine Press, 1993). ISBN 1-874367-90-4.
5. Ed Murphy, Handbook for Spiritual Warfare (Nelson Pub., 1992, reprinted 2003): 623. ISBN 0-7852-5026-3.
6. Doris Wagner, How to Cast Out Demons (Wagner Books, 1999). ISBN 1-58502-002-8.
7. James S. Wallace, The Occult Trap (Wagner Books, 2004). ISBN 1-58502-040-0.
8. John and Mark Sandford, Deliverance and Inner Healing (Chosen Books, 1992). ISBN 0-8007-9206-8.
9. Frank Hammond, Pigs in the Parlor (Impact Books, 332 Leffingwell Ave., Suite 101, Kirkwood, MO 63122, 1973). ISBN 0892280271.
10. Francis MacNutt, Deliverance from Evil Spirits (Christian Healing Ministries Inc., PO Box 9520, Jacksonville, FL 32208, 904-765-3332, 1995). ISBN 0-8007-9232-7.
11. Derek Prince, They Shall Expel Demons (Chosen Books, c/o Baker Book House, PO Box 6287, Grand Rapids, MI 49516-6287, 1998). ISBN 0800792602.
156
#23 Sababu Zinazoweza Kuzuia Uponyaji www.healingofthespirit.org
Sababu Zinazoweza Kuzuia Uponyaji
Tunaamini kwamba ni mapenzi ya Bwana kuwaponya watu wote wanaomjia wakita-ka uponyaji—katika jina la Yesu. Imani hii inaungwa mkono katika maandiko yote. Hata hivyo, kunaweza kuwa na vizuizi katika mwili wa kanisa nyakati za sasa, vinavyoweza kuu-zuia uponyaji wa miili yetu na roho zetu.
Tumia habari ifuatayo kama orodha ya uchunguzi ili upitie sababu zinazokufanya usipokee uponyaji. Omba kwanza ili Mungu akufunulie sehemu zozote zilizotajwa hapa chini (au zengine ambazo hazijaroodheshwa) zinazozuia baraka za uponyaji katika maisha yako.
1. Picha tuliyonayo kuhusu Mungu huenda isiwe ya Baba mwenye upendo na mwenye kusa-mehe. Kwa hivyo, tunadhani au tunaamini kwamba hatustahili kupata uponyaji kutoka kwake au kujibiwa maombi yetu. Hatuna hakika kwamba tunatakiwa kutafuta baraka za Mungu.
2. Hatujui (moyoni mwetu) kwamba Kifo cha Kristo kilifanyika kwa ajili ya magonjwa na dhambi zetu (Isa. 53).
3. Hatuna maarifa “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa” (Hosea 4:6)—maarifa ya:
• Jinsi ya kuomba
• Aina ya maombi ya kutumia
• Kazi za nguvu za giza
• Hitaji la uponyaji wa kihisia
• Vipawa vya uponyaji vya Roho
4. Tuna dhambi maishani mwetu ambazo hatujawahi kuungama (Yak. 5:16, Zab. 66:18).
5. Hatujawasamehe wengine (Mat. 5:23-25, 6:14-15 na 18:34-35; Ayubu 42:10-13).
6. Dhambi ambazo wengine—wametutendea—tunatakiwa kupata uponyaji wa ndani kwa ajili ya majeraha yetu na kumbukumbu zetu.
7. Tunapata utambuzi usio sahihi halafu tunaombea uponyaji usio sahihi. Tunaweza kuwa tu-naombea ugonjwa (Yohana 5:5) ilhali roho ya ugonjwa (Luka 13:11-12) ndiyo inayotusum-bua. Vilevile, sisi huombea uponyaji wa dalili tulizonazo badala ya kuombea chanzo cha ta-tizo lenyewe (kwa mfano, kuombea kichwa kinachouma badala ya tatizo/matatizo ya ndani, kwa kushughulikia athari za mizungu/ushetani).
8. Sisi hukosa imani ya kutosha, hutumia mantiki, hushuku, au huwa na tashwishi (Mat. 8:26, 14:31, 16:8 na 17:19-20; Marko 6:5-6, Luka 16:19-31).
9. Sisi hukosa nguvu za kutosha (Luka 24:49).
10. Sisi hukosa kujitayarisha vilivyo (hali yetu huenda ikahitaji kuomba na kufunga kama ili-vyoelezwa katika Mat. 17:21).
11. Sisi hukosa kutoa shukrani ya kutosha (Zab. 149:5-9, kulingana na sheria ya shukrani).
12. Sisi hupata matokeo mabaya ya mambo tunayokiri kwa vinywa vyetu, kwa njia ya kula-lamika na kunung’unika (Hes. 21:4-5, Zab. 78:18-20 na 32-33; Meth. 12:14 na 18, 15:4 na 18:20-21; pia rejelea sehemu inayoeleza juu ya “Kuuponya Ulimi Wako”).
13. Tukiwa chini ya laana fulani (Kumb. 28:45-46; rejelea sehemu inyaoeleza juu ya “Uponyaji Kutokana na Laana”).
14. Tukiwa chini ya athari za dhambi za kizazi bila kujua (Kut. 20:5; pia rejelea sehemu inayoe-leza juu ya “Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi”).
157
#23 Sababu Zinazoweza Kuzuia Uponyaji www.healingofthespirit.org
15. Tunadhani (tunaamini) kwamba ni mapenzi ya Mungu sisi kuwa wagonjwa (inayotambuliwa kama “mateso ya kuokoa”).
16. Huenda tunajaribu kumweleza Mungu “vile” anatakiwa kutuponya. Huenda tunahisi kwamba hatatuponya moja kwa moja, au huenda tukakimbilia kupata msaada kutoka kwa madaktari kwanza kabla ya kumwomba Mungu atuponye.
17. Sisi huzingatia sana “chombo” cha uponyaji ambacho Mungu anatumia (kwa mfano, mwom-bezi) kuliko kumzingatia Mungu mwenyewe.
18. Tukiwa vuguvugu katika uhusiano wetu na Kristo—"Afadhali ungekuwa kimojawapo: baridi au moto" (Ufu. 3:15). Kumbuka kwamba Mungu huwatuza wale wanaomtafuta kwa moyo wote.
19. Uponyaji huchukua muda. Watu wengi hutaka kupata muujiza wa haraka nao humwekea Mungu mipaka ya miujiza.
20. Watu wengine hufifia katika imani yao kwa kutazama (kuzingatia) dalili walizonazo. Watu hao huzifanya “hisia” zao kuwa msingi wa imani yao badala ya kuwa na tumaini katika Neno la Mungu.
21. Mazoea mabaya ya chakula na/au ya afya yanaweza kuwa kikwazo kwa nguvu za Mungu za uponyaji (kwa mfano, unene, kutofanya mazoezi,n.k.).
22. Sisi huamua kuamini ushahidi wa daktari kuliko kuamini uwezo wa Mungu na haja yake ya kutuponya.
23. Ingawaje uponyaji umeahidiwa, umetambuliwa, na kuthitibishwa katika maandiko, jambo la kusikitisha ni kwamba haukubaliki sana katika ushirika wa kanisa. Sisi huwa wepesi kukubali uamuzi wa madaktari bila kufikiria juu ya mapenzi ya Mungu katika tathmini zetu.
24. Huwa tunasahau kutegemea baraka za Mungu za hapo awali (Zab. 78:41).
25. Wasiwasi, woga, na mahangaiko huzuia kutendeka kwa jambo hilo (Mat. 6:25-34, Fil. 4:6).
26. Kiburi huzuia uponyaji (2 Fal. 5:10-11). Sisi hudhani, “Tunaweza kujifanyia wenyewe.”
27. Huenda ikawa tunasistiza kwamba ni lazima Mungu atuponye moja kwa moja, na hivyo basi kukataa kwenda hospitalini. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tunadhihirisha roho ya dini na mtazamo mbaya (Mat. 11:16-17, Luka 11:54, 2 Tim. 3:5); na hatutakuwa tunakubali kwamba Mungu anaweza kuzitumia njia zengine asilia za uponyaji—kupitia kwa dawa na/au madakta-ri. Tunamtaka Mungu atuponye tu kimiujiza.
28. Tukiwa na nia mbaya (Yoh. 6:26, Yak. 4:3, 1 Yoh. 5:14-15); tunataka uponyaji kwa sababu zisizo sahihi).
29. Tukiwa na mitazamo isiyo ya kiungu kuwahusu viongozi wa kanisa au kulihusu shirika la kanisa (Hes. 16:1-3 na 31-33, 12:1-2 na 9-10).
30. Tukiwa na “moyo mgumu” (Ezek. 12:1-2, Marko 8:15-18, Zab. 78:8-11, Ebr. 3:8-11). Tuki-puuza juhudi za Mungu za kutaka tumsikilize; tukikataa kusadiki.
31. Tukiwasahau maskini (Meth. 21:13, Is. 58:7-8) na “kumwibia Mungu” (Mal. 3:8). Inajulika-na vizuri sana miongoni mwa watu wanaohubiri na kufunza kuhusu kupokea baraka zinazoto-lewa kutoka kwa Mungu kwamba kutoa sadaka kwa maskini kunahitajika ili mtu aweze kupokea baraka za kupewa: “Mungu amezipokea sala na sadaka zako kwa maskini wala ha-tazisahau”(Mat. 10:4; tazama vif. 1-4). Watu wachache sana wanafahamu kwamba kutoa sadaka kwa maskini huathiri baraka za uponyaji tunazotafuta.
158
# 24 Utunzaji wa Baadaye (Jinsi ya Kudumisha Uponyaji Wako)
www.healingofthespirit.org
Utunzaji wa Baadaye (Jinsi ya Kudumisha Uponyaji Wako)
Lengo la uponyaji wa ndani pamoja na huduma ya ukombozi si kuwekwa huru kuto-kana na athari za giza pekee—bali pia ni kuirudisha nafsi na mwili wa mhusika kwa uzima wa kiroho ili mtu huyo aweze kuwa mtu ambaye Mungu anamtaka awe. Mhusika huyo asi-pofanya chochote baada ya tukio la uponyaji, hali yake inaweza kuwa mbaya kuliko hapo awali. (Tazama Mat 12:43-45, Luka 11:24-26) Yafuatayo ni mapendekezo ya kuzingatiwa baada ya kipindi cha maombi makuu kumalizika.
1. Peleleza na upeleleze tena: Muulize Mungu mara tatu akufunulie giza lengine lolote linaloweza kuwepo au milango iliyo wazi inayohitaji kufungwa na kuponywa. Muul-ize kila mtu katika kikundi cha maombi ikiwa anahisi kwamba uponyaji huo umeka-milika.
2. Peleleza kutoka kwa mhusika: Muulize mhusika anajisikia vipi na ikiwa kifua au moyo wake unahisi kuwa ni mwepesi; tayari anajua vile alikuwa akihisi giza lilipo-kuweko, ataweza kuhisi au kujua giza likiondoka.
3. Kujazwa Roho Mtakatifu: Mwombee mhusika huyo ili ajazwe Roho Mtakatifu. Mpake mafuta juu ya kichwa chake. Anatakiwa kujua kwamba mwili wake ni hekalu ya Roho Mtakatifu. Mkabidhi Kristo kila sehemu ya mwili wa mtu huyo (Rum. 6:12-13).
4. Kurudisha nguvu mwilini: Mweleze mhusika kwamba atahitaji kurudisha nguvu mwilini. Kwa mfano, huenda akahitaji kulala kwa masaa 12 au zaidi. Huenda ana kiu au njaa na hivyo basi atahijitaji vinywaji zaidi na chakula.
5. Majeraha na uchungu: Iwapo mhusika “alidhihirisha mapepo,” anaweza kuamka siku ya pili bila kukumbuka vizuri tukio hilo lakini ataona majeraha na uchungu uta-kuwa mahali alipokuwa akishikwa wakati wa kudhihirisha mapepo.
6. Mpango wa kuhifadhi maandiko moyoni: Wakolosai 3:16 inatushauri, “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote….” Mwambie mhusika huyo aanze mpango wa kuhifadhi maandiko moyoni na kusoma Biblia kwa makini, hasa iwapo alikuwa na milango wazi ya tamaa, upotovu, mazoea ya tabia mbaya, na aina zengine za tamaa ya mwili katika maisha yake. Wakolosai 2:6-7 inashauri, “Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye: Wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani….” Jifura-hishe kwa Neno na ahadi za Mungu kila mara.
7. Mafundisho ya Biblia: Warumi 12:2 inaeleza, ““Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu….” Ukweli unaofunuliwa kutoka kwa Neno la Mungu ni muhimu kwa kitendo cha mgeuzo. Iwa-po kulikuwa na uasi, uchawi, uasi wa kidini, au kushiriki katika dini za uwongo kati-ka maisha ya mtu huyo, pendekeza mafundisho ya Biblia yenye imani halisi, yata-kayomwezesha kukua vizuri na kuimarika, na kupata ulinzi kamili.
8. Zingatia mambo mazuri: ushuhuda wa uponyaji aliopata mhusika huyo unatakiwa kuzingatia mambo mazuri ya kuipata nuru ya Yesu, bali usizingatie maelezo mengi ya kuiacha giza.
9. Fikira zinazotiwa akilini: Elimisha mhusika kuhusu haja ya kutofautisha kati ya “kuisikia sauti ya giza ikijaribu kumwathiri kutoka nje ya mwili wake” dhidi ya “ku-hisi uwepo wa giza ndani yake.” Yeye yuko huru, lakini nguvu za giza zitajaribu kumdanganya na kumfanya aamini kwamba hajapokea uponyaji. Sauti hizo
159
# 24 Utunzaji wa Baadaye (Jinsi ya Kudumisha Uponyaji Wako)
www.healingofthespirit.org
mbili zinaweza kufanana, na mhusika huyo huenda asiweze kubainisha tofauti hiyo kwa urahisi. Huenda mhusika huyo akaanza kuamini uwongo unaosema kwamba ha-japona (Bob Larson analiita jambo hilo “fikira za kishetani zinazotiwa akilini”). Mweleze mhusika kwamba sauti hiyo ya giza itanyamaza baada ya muda fulani.
Mwambie mhusika mambo yafuatayo,“Umepata upasuaji mkuu wa kiroho. Mungu amekumulikia nuru yake. Ametimiza sehemu yake nawe ni lazima utimize sehemu yako. Usipokuwa makini na mwangalifu, ni rahisi sana kuirejelea mienendo na mpangilio wa ma-wazo ya zamani, kujaribiwa unaposhirikiana na marafiki zako na mambo ya zamani, na ku-sababisha uponyaji uliopokea “utoweke.” Fahamu kwamba nguvu za giza zitajaribu sana (kwa muda fulani) kurudi mahali ambapo zilikaa kwa starehe hapo awali. Zitajaribu kukuridhisha kwamba hukuponywa na kwamba hukusamehewa kabisa, ingawaje ulisamehe-wa—ulipoomba msamaha mara ya kwanza. Simama imara kwa ahadi hii: “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” (1 Yohana 1:9).
Isitarajiwe kwamba Roho Mtakatifu akikubariki na uponyaji wa ndani, mambo yote yamekamilika, na kwamba hakuna haja zaidi ya kuudumisha uponyaji. Ni hatari sana kufi-kiri kwamba “utunzaji wa baadaye” hauhitajiki. Kumbuka, Yesu alionya: “Angalia umeku-wa mzima, usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi” (Yohana 5:14). Soma Luka 11:24-26, inayoeleza juu ya jambo linaloweza kutendeka baada ya Bwana kuisa-fisha “nyumba” yako ya kiroho usipohakikisha kwamba sehemu iliyosafishwa inapata mwanga wa kiroho, kwa kumwambia Yesu aingie ndani ya moyo wako na roho yako, badala ya kuiacha nyumba hiyo iwe tupu (na giza liweze kurudi ndani). Kuna mambo kadhaa un-ayotakiwa kufanya ili uweze kudumisha uponyaji wako na kuendelea mbele katika safari ya-ko na Yesu.
Uponyaji ni njia, bali si kikomo cha safari au tukio linalofanyika mara moja pekee. Mtu akirudia mazoea ya dhambi, au kurudia mazoea yoyote yaliyokatazwa au vitu vya kipe-po alivyoacha, anaweza kuupoteza uhuru wake na kutawaliwa tena na athari za giza na utumwa, kwa hali mbaya sana kuliko ile ya awali. Don Basham ameandika, “Kuyaondoa mambo mabaya katika maisha yetu ni nusu ya mapambano: kila hali ya kuondoa inatakiwa kufuatwa na hali ya kuongeza.” Mapendekezo yafuatayo yatakusaidia kudumisha uponyaji ambao Mungu amekupa:
1. “Enenda zako, wala usitende dhambi tena” (Yohana 8:11): Kutubu kuna maana kwamba tunasikitika kwa mabaya tuliyotenda na tunataka kuishi katika haki ya Bwana; tunaamua kuwacha kutenda mambo tunayofahamu kuwa mabaya mbele za Mungu na tunaamua kufanya mambo yaliyo haki machoni pake. Vile Wakolosai 3:2 inashauri, “Yafikirini yaliyo juu siyo yaliyo katika nchi,” tunashika njia mpya na hatukumbuki tena dhambi zetu za zamani (na vile tulivyoishi) (kama alivyosema Paulo katika Fil. 3:13-14). Tunakumbuka na kufurahia kwamba Mungu ametusamehe. Kisha tunakuwa “Wenye shi-na na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani …” (kama tunavyo-shauriwa katika Kol. 2:7).
2. Usikae na dhambi kwa muda mrefu: Tunatakiwa kutii na kutotenda dhambi, lakini tukitenda dhambi, tunatakiwa kumkabidhi Bwana dhambi hiyo mara moja kwa kukiri na kutubu. Hata ukijikwaa, usibaki chini; inuka na uendelee kutembea ndani ya Bwana (1 Yohana 1:5, 9 na 2:1). Kumfuata Kristo kuna maana ya kuamua kuyatii mafundisho yake.
160
# 24 Utunzaji wa Baadaye (Jinsi ya Kudumisha Uponyaji Wako)
www.healingofthespirit.org
3. Toa ushuhuda wako wa uponyaji: Kutoa ushuhuda wako wa uponyaji kutaisaidia imani yako kukua na kutakufanya umzingatie Yesu Kristo; utakuwa baraka na ushu-huda kwa wengine.
4. Fahamu hali yako ya mawazo: Vita kati ya mema na maovu huanzia akilini. Usiyakubali mawazo maovu au mabaya. “Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtaka-poweza kuyajua mapenzi ya Mungu na kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu.” (Rum. 12:2).
Shambulio la mawazo maovu likizidi kuwa tatizo, afadhali useme, “Mungu, silitaki wazo hili,” kuliko kumkemea shetani na kumzingatia. Kumbuka, “Mpingeni Shetani naye atawakimbia”(Yak. 4:7). Mtu anayegawa vitu (Shetani) akileta kifuru-shi katika mlango (wa mawazo yako) kikiwa kimeandikwa jina lako, si lazima ukiku-bali. Kuwa makini ili uweze kujua mitego yoyote ambayo shetani anataka kukutega nayo. Kisha “mkimtwika yeye fadhaa zenu zote….” (1 Pet. 5:7), Baba yako wa Mbin-guni atakujibu mara moja na kukupa ushindi.
5. Ijaze akili na roho yako kwa mawazo mazuri ya Yesu: Wafilipi 2:5 inatushauri, “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu….” Kwa maombi, kiri kwa shukrani sehemu za maisha yako ambazo umepokea uhuru. Sikiliza muziki na nyimbo zenye ujumbe mzuri wa Kikristo. Kumbuka, “Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, ... haki, … sa-fi,… yenye kupendeza ,.. yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.” (Fil. 4:8).
6. Omba kila siku: Maombi ni silaha bora zaidi ya kulishinda giza. Kila wakati, dumi-sha mawasiliano na Mungu. Kuwa na wakati wa kutulia na kuisikiliza sauti yake (Yoh. 15:7, 1 Kor. 14:14, 1 Thes. 5:17).
7. Soma Biblia na sala za kila siku: Roho nzuri ndani yako inahitaji chakula cha kiro-ho kila siku. Usipoilisha roho yako vizuri, itapata ugonjwa. Ukiwa mgonjwa mwilini halafu ushindwe kula chakula cha mwili, daktari atalazimisha chakula mwilini mwa-ko ili ayaokoe maisha yako. Ingawaje huenda usiwe na njaa ya chakula cha kiroho, unatakiwa kujilazimisha kula chakula cha kiroho ili uyaokoe maisha yako ya kiroho. Soma ushuhuda wa kuhimiza kutoka kwa watu wengine na vitabu vya kutia moyo vya mashujaa wa imami; fanya shughuli zinazojenga, zinazokuza, na kuimarisha.
8. Msifu Bwana katika hali zote: “Furahini katika Bwana siku zote; tena nasema, fu-rahini.” Jumuisheni sheria ya shukrani (Fil. 4:6-7). Maneno ya vinywa vyetu yana-weza kumwalika Yesu au kualika giza. Jieupushe na kulalamika, kunung’unika, ku-sema kichinichini, kutafuta makosa, au kuhukumu, kwani hayo yote hupanda mbegu ya giza.
Paulo anapendekeza na kutuarifu “Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni ma-penzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.” (1 Thes. 5:18).
161
# 24 Utunzaji wa Baadaye (Jinsi ya Kudumisha Uponyaji Wako)
www.healingofthespirit.org
9. Jifunze kusimama imara (kwa imani) katika ahadi za Yesu Kristo: soma na kuji-funza Biblia ili uweze kujua ahadi zake ni zipi—zitumie na kuzitangaza kuwa ni zako wewe.
10. Tafuta ushirika wa kanisa na uweze kujiunga nao: Hudhuria kila mara. Unda au jiunge na kikundi kinachoweza kukusaidia kuwajibika na kitakachoomba nawe na pia kukuombea. Tahadhari usije ukadhani kwamba huwahitaji watu wengine na kwamba unaweza ukafaulu ukiwa peke yako.
11. Shiriki katika sakaramenti kadiri uwezavyo: Unapojitayrisha kwa ajili ya Ushiri-ka Makatifu, fuata ushauri wa maandiko wa kujichunguza (1 Kor. 11:27-32). Uki-fanya kosa, kiri na kutubu, halafu nenda katika Ushirika Mtakatifu kwa moyo wa ku-sherehekea. Ukiwa mgonjwa, waite wazee wa kanisa “Je, yuko mgonjwa kati yenu? Anapaswa kuwaita wazee wa kanisa, nao watamwombea na kumpaka mafuta kwa ji-na la Bwana” (Yak. 5:14).
12. Mtafute mshauri wa kiroho wa Kikristo: Mwombe mshauri aliye na uzoefu akuongoze (kama mkurugenzi wa kiroho) katika safari yako ya kiroho na uweze kutii uongozi na ushauri wao.
13. Tamani kujazwa Roho Mtakatifu: Jisalimishe kwa Roho Mtakatifu. Umemsikia akinena nawe ulipopokea uponyaji. Atanena nawe tena kila mara ukimwomba na ku-jitayarisha.
14. Gundua vipawa vyako vya kiroho na mahali unapoweza kutumika katika mwili wa Kristo: Mwambie Roho Mtakatifu akuongoze na kukuwezesha, na kukutayarisha kufanya huduma bora. Kisha jitoe kutumika.
15. “Vaeni silaha zote za Mungu” kila siku: Vaa silaha iliyotajwa katika Efe. 6:10-18.
16. Mpe Bwana Yesu mawazo yako yote, haja zako, na mipango yako: Ukifanya hivyo, ataendelea kukuongoza na utashangazwa na vitu vingi vilivyojaa ukarimu na baraka atakavyokufunulia na kukufanyia. Ameahidi kukudumisha kama shamba lililo na chemichemi ya maji. Ukimtumaini, ukimtegemea, na kumkiri katika mambo yote, “atazinyosha njia zako” (Meth. 3:5-6).
17. Enenda katika Msamaha: Kusamehe haraka ni muhimu.
18. Lipa ulicodhulumu au kumwibia mtu: Iwapo umemdhulumu mtu, mlipe. Ukihitaji-ka kuomba msamaha, fanya hivyo.
Vifaa
1. Bob Larson, Larson’s Book of Spiritual Warfare (Thomas Nelson, 1999): 455-61. ISBN 0-7852-6985-1.
162
# 25 Nguvu za Uponyaji za Ushirika Mtakatifu www.healingofthespirit.org
Nguvu za Uponyaji za Ushirika Mtakatifu
Ushirika Mtakatifu wa Kwanza
Ushirika Mtakatifu wa kwanza ulioandikwa katika Biblia ulifanyika baada ya Abra-hamu kurudi nyumbani baada ya kumkomboa Lutu mpwa wake, familia ya Lutu na mali yake. Melkisedeki alimpa Abrahamu mkate na divai na akambariki. Naye Abrahamu akampa Melkisedeki sehemu ya kumi ya vitu vyote alivyokuwa navyo. Vifungu hivi (Mwa. 14:18-20) vinaonyesha kuweko kwa uhusiano kati ya Ushirika Mtakatifu, baraka na fedha (ingawa kipengele cha “fedha” hakitashughulikiwa katika sehemu hii).
Pasaka na Ushirika Mtakatifu
Chakula cha Pasaka (kilichorekodiwa katika Kut. 12:1-14) kilikuwa aina ya Ushirika Mtakatifu, na kilisherehekewa kwa mara ya kwanza usiku ambao watu wa Mungu walikom-bolewa kutoka katika utumwa wa Misri. Tukio la Pasaka lilikuwa ishara ya mambo kadhaa.
1. Ukombozi: Kitendo cha Waisraeli kutoka Misri kinawakilisha ukombozi wao uliosababish-wa (uliotayarishwa) na Kristo)—ambaye ni “Mwanakondoo aliyechinjwa tangu mwanzo wa ulimwengu” (Ufu. 13:8), kama sehemu ya kazi ya Yesu ya kutufia. Ukombozi wao kutoka Misri ulikuwa wa kiroho na wa mwili pia.
2. Mwanakondoo Mwanakondoo asiye na kilema chochote ni dalili na aina ya kusulubiwa kwa Yesu (wakati huo kitendo hicho hakikuwa kimefanyika). Waisraeli walitakiwa kuwa na “mwanakondoo” miongoni mwao, na “damu” juu yao.
3. Damu: Damu iliyokuwa juu ya miimo iliwakilisha damu ya Yesu iliyomwagwa Kalvari kwa msamaha wa dhambi na kwa ajili ya wokovu wetu.
4. Kujitayarisha: Kula chakula cha Pasaka “mkiwa mmejifunga mikanda viunoni mwenu, mmevaa viatu na fimbo zenu mikononi” (Kut. 12:11) ilikuwa ishara ya Mungu kutaka siku zote kuwaongoza watu wake kote ulimwenguni kutoka utumwani ili waingie katika maisha mapya.
5. Damu juu ya miimo: Damu iliyokuwa juu ya miimo iliwakilisha ulinzi wa Mungu dhidi ya malaika wa kifo.
6. Mkate Usiotiwa Chachu: Kula mkate usiotiwa chachu kuliwakilisha kuchukua jukumu la kuwachana na dhambi (pia rejelea Mat. 16:11-12, kuhusu chachu—au “mafundisho” ya uwongo—ya Wafarisayo na Wasadukayo).
7. Vitu vya kupewa: “Mali” ya Wamisri ilitolewa kwa Waisraeli kama ishara ya Mungu ku-wapa vitu walivyohitaji wakati wote (Kut. 12:35-36).
8. Uponyaji “Hakuna hata mmoja wao aliyejikwaa” miongoni mwa Waisraeli milioni 2 au 3 (Ps. 105:37) walioondoka na Musa. Tukio hilo ni ishara ya nguvu na ahadi ya Mungu ya kui-ponya miili yetu. “Ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Kristo kutoka wafu anaishi ndani yenu, basi huyo aliyemfufua Kristo kutoka wafu ataipa uhai miili yenu yenye hali ya kufa; atafanya hivyo kwa njia ya Roho wake akaaye ndani yenu” (Rum. 8:11). Miili yetu hupewa uhai (hu-changamshwa) tunapokumbuka na kusherehekea Ushirika Mtakatifu.
9. Sherehe: Chakula cha Pasaka kilikuwa wakati wa kusherehekea, karamu—wakati wa kushe-rehekea ushindi (sio wakati wa kulia na kukumbuka machozi ya zamani). Divai pia ni ishara ya sherehe. Ushirika Mtakatifu unatakiwa kusherehekewa kama chakula cha furaha. Tunata-kiwa kuingia katika sherehe hiyo kwa furaha.
163
# 25 Nguvu za Uponyaji za Ushirika Mtakatifu www.healingofthespirit.org
10. Kumbukumbu: Mungu aliwaamuru Waisraeli waadhimishe Sikukuu ya Pasaka kama kum-bukumbu na agizo la milele (Kut. 12:14). Sikukuu ya Pasaka ilitakiwa kuwa wakati wa ku-kumbuka; sherehe yake inatakiwa kuwa kumbukumbu ya kuzikwa na kufufuka kwa Bwana.
11. Tangazo: Tukio la Pasaka lilikuwa tangazo kwa adui za Mungu pamoja na Shetani kwamba Mungu atawaongoza watu wake. Pia ulikuwa wakati wa kushindwa kwa Shetani.
12. Ushirika Mtakatifu: Ushirika Mtakatifu ni wakati wa familia kukusanyika katika Meza Ta-katifu. Kama alivyoonyesha Yesu, Yeye na wanafunzi wake walishirikiana pamoja kama fa-milia ya Mungu. Kila mtu aliweza kuifikia Meza kwa njia sawa. Kila mtu, akiwemo Yuda, alikaribishwa na Yesu kula chakula cha Pasaka.
Kama ilivyokuwa katika Sikukuu ya Pasaka, kwenda katika Meza ya Ush irika Mta-katifu kunatakiwa kuhusisha kujitwalia ukombozi kutokana na nguvu za dhambi na kifo na kujitwalia nguvu za mwili, uponyaji, na kupokea vitu kwa njia ya imani yenye matarajio—kwa kula (mkate) mwili wa Bwana, ambaye kwa mapigo yake tulipata uponyaji. Kuondoka Mezani bila kuomba (na kujitwalia) baraka za kiroho na za mwili ni kukataa mambo tuliyo-pewa kupitia kwa kifo cha Kristo, kitendo alichotufanyia sisi.
Yohana 6 inasema, Yesu mwenyewe ni “mkate wa uhai” utokao mbinguni. Maelezo hayo yalikuwa tofauti na mkate ambao Waisraeli walipewa walipokuwa jangwani. Mana (mkate) waliopata ulililisha taifa zima kwa safari yao yote ya miaka 40. Hivyo basi tunaweza kuamini kwamba mkate wa uhai utokao mbinguni (ambao mana ilikuwa mfano wake) ume-tolewa kwa ajili ya kutuendeleza kimwili na kiroho. Kwa hivyo tunaweza kuja Mezani tu-kiwa na tarajio la kupata nguvu za mwili na uponyaji. Kifungu hiki katika Yohana 6 pia kinataja, “Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu, akaa ndani yangu, nami nakaa nda-ni yake” (kif. 56). Tunapokula na kunywa nembo hizo, sisi hufanya hivyo kwa kuhakikishi-wa kwamba Yesu anakaa ndani yetu.
Mat. 15:22-28 inanena juu ya “mkate wa wana.” Mkate ni kitu muhimu sana katika maisha ya binadamu. Kumnyima mtu mkate ni kumnyima kitu muhimu cha uhai. Katika hali hii, Yesu alipouita uponyaji “mkate wa wana,” alikuwa akitangaza kwamba uponyaji ni ki-tu cha msingi sana tunachopewa na Mungu. Ni jambo la kufurahisha kwamba, Yesu ali-sema pia, “Je, kuna yeyote miongoni mwenu ambaye mtoto wake akimwomba mkate, atampa jiwe?” (Luka 11:12, Mat. 7:9). Tunapomwomba Baba Yetu wa Mbinguni uponyaji, tunata-kiwa kufanya hivyo kwa ujasiri kwa sababu yeye anapenda sana kutupa tunachoomba.
Tunapoikaribia Meza ya Bwana, kuna mambo mawili yaliyo muhimu kwa uponyaji: (1) Yesu ni mkate wa uhai utokao mbinguni, anayetupa uhai wake wa kiungu kwa njia ya Roho, na (2) mkate kama “mkate wa wana”—ulio na maana ya uponyaji.
Kwanza, Meza ni mahali pa urafiki wa karibu ambapo tunaweza kuhisi uwepo wa Bwana kupitia kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Tunaweza kumtarajia Yesu adhihirishe uwepo wake katika Meza hiyo, na hilo ndilo jambo tunalotakiwa kuzingatia. Tunapoula mkate huo, kwa imani—tunapokea uhai na nguvu za Mungu kwa njia ya Roho. Kama vile mkate uli-okuwa jangwani uliwalisha Waisraeli kila siku, na kuwapa nguvu za kuwadumisha, vivyo ndivyo Yesu, ambaye ni mkate utokao mbinguni, hutupa nguvu za kiroho, kihisia, na kimwi-li. Yeye huja kutupa sisi vitu alivyotoa bure kupitia kwa kifo chake cha mhanga.
Ni lazima tuje Mezani tukiwa tumejitayarisha vilivyo, baada ya kuyachunguza mai-sha yetu mbele ya Mungu. Mbali na kutushauri tujichunguze wenyewe kabla ya kushiriki,
164
# 25 Nguvu za Uponyaji za Ushirika Mtakatifu www.healingofthespirit.org
I Wakorintho 11:23-31 inahusisha “dhaifu na wagonjwa” na kutostahili kwetu, kutotambua kwetu vile tunavyostahili kuikaribia Meza hiyo na mwili na damu ya Bwana wetu (ambapo kuna uponyaji mkuu tunaposhiriki katika Ushirika Mtakatifu kwa imani na kwa kutambua vilivyo maana yake).
Ushirika Mtakatifu ni sakaramenti takatifu sana, sherehe takatifu inayohusu ishara za sadaka ya Kristo na agano yetu—kuonyesha mapatano kati ya Mungu na wanadamu. Kila mara huwa tuna hiari ya kumchagua Mungu au utajiri. Katika Mwanzo 14:18-20, Abrahamu aliamua kulipa sehemu ya kumi ya vitu vyote na akapewa mkate na divai, badala ya kuchu-kua utajiri wa Mfalme wa Sodoma.
Wakati wa matayarisho ya ndoa ya Kiyahudi, baada ya wazazi kujadiliana juu ya ma-hari (pesa ambazo mwanamume anayetaka kuoa hukubali kumlipa baba ya msichana kwa kumtoa binti yake), bwana arusi humpa bibi arusi kikombe na kumwambia, “Ninakupenda na ninakupa uhai wangu. Je, utakubali kuolewa nami?” Mwanamke huyo akinywa kutoka kwa kikombe hicho huwa anasema, “Ndiyo, nitaolewa nawe.” Vivyo hivyo, Yesu alipoinua ki-kombe hicho na kuwapa wanafunzi wake (na anapoendelea kutupa kikombe hicho siku hizi), alikuwa akiwaomba waungane naye katika agano—wawe bibi arusi wake (mwili wake), ka-ma inavyotajwa: “Kisha akatwaa kikombe cha divai, akamshukuru Mungu, akawapa; wote wakanywa kutoka kikombe hicho. Akawaambia, “Hii ni damu yangu inayothibitisha agano la Mungu, damu inayomwagwa kwa ajili ya watu wengi” (Marko 14:22-24, Mat. 26:26-28, Lu-ka 22:19-20).
Katika Meza hiyo tunafanyika kuwa mwili mmoja na Kristo. Yeye ni mkate wa uhai na chemichemi ya maji ya uzima. Wanaokuja kwake hawawezi kuona njaa wala kuona kiu.
Ushirika Mtakatifu ni Zawadi Ambayo ni Yeye Mwenyewe.
Meza hiyo ni mahali pa kupokea msamaha. Divai inatunenea juu ya damu yake, iliyomwagwa kwa ajili ya msamaha wa dhambi. Damu yake ilifungua “njia mpya ya uhai” ya kuingia katika uwepo wa Baba. Ushirika Mtakatifu pia hutupa nafasi ya kupokea msamaha na uponyaji katika ukoo wetu, ingawa jambo hili huwa halitiliwi maanani; kuna jedwali la ukoo lililotolewa kwa ajili ya uponyaji na baraka za urithi wetu wa kiroho. Wakati wa kushi-riki katika Ushirika Mtakatifu kwa njia hiyo, uponyaji wa ajabu hufanyika na watu wengi huwekwa huru kutokana na athari mbaya za kizazi za hapo awali. (Rejelea sehemu inayoele-za juu ya “Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi” kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii.)
Ombea Mambo Yafuatayo katika Ekaristi (Karamau Takatifu)
1. Msamaha
2. Kupata kusamehewa na wengine (Tunaweza kuwafunga wengine kwa kutowase-mehe, nao wanaweza kutufunga pia; hii ni kuachilia sehemu ya “wanaweza kutufun-ga” katika sheria ya kiroho ya kufunga na kufungua.)
3. Faida za agano ya kufa na kufukufa kwa Yesu
4. Sehemu yetu ya “mkate wa wana” ya uponyaji
5. Uponyaji wa mwili, afya, na nguvu
6. Ulinzi dhidi ya malaika wa kifo
7. Yesu adumu ndani yetu
8. Fadhila na wema wa Mungu
9. Kupewa vitu tunavyohitaji
165
# 25 Nguvu za Uponyaji za Ushirika Mtakatifu www.healingofthespirit.org
Ombi
Bwana, tunajua kwamba Ushirika Mtakatifu unawakilisha nafasi ya kuweza kuunga-na Yesu, kwani unawakilisha kukutana na Bwana kiroho na kimwili. Tunajua kwamba maandiko yanatwambia, “Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu, akaa ndani yangu, nami nakaa ndani yake.”
Tunapoula mkate huo na kuinywa divai hiyo, tunakula chakula cha kiroho, na tunafa-nyika “mwili mmoja” na Yesu Kristo. Ishara hizo ni zawadi yako ya thamani sana kwetu. Wewe ni mkate wa uzima na maji ya uzima. Mwili wako uliojeruhiwa umetupa afya ya mwi-li na uponyaji. Damu yako iliyotiririka imetupa msamaha na uponyaji wa kiroho.
Bwana, tunakuja kwako leo tukihitaji uponyaji wa roho zetu pamoja na miili yetu, na kukumbuka agano tuliyofanya nawe tulipobatizwa. Kwa kitendo hiki cha imani tunajitwalia damu ya Yesu iliyomwagwa kwa ajili yetu, na tunaomba nguvu kamili za Ushirika Mtakatifu zitumike kwetu na kwa familia zetu.
Tunakushukuru, Bwana Yesu, kwa baraka ulizotupa katika jina lako la thamani.
Amina.
Vifaa
1. John Hampsch, The Healing Power of the Eucharist (Servant Pub., 1999). ISBN 0-56955095-6.
2. Ken and Lorna Matthews, The Healing Technician’s Manual (Rapha Christian Minis-tries, P.O. Box 817, Grandview, MO 64137, 1996). (Sehemu kubwa ya habari iliyo hapo juu ilitolewa katika kitabu hiki.)
166
# 26 Healing of the Body www.healingofthespirit.org
Uponyaji wa Mwili
Utangulizi
Kila muumini yapampasa ajibu swali hili: “Je uponyaji wa kiroho ni sehemu yangu?” Uponyaji wa kiroho ni tendo la Mungu la neema linalofanywa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Uponyaji huu unajumuisha kuukomboa mwili kutoka kwa ma-radhi na kuurudishia afya na uhai. Uponyaji huu ni haki yako – ni mapenzi timilifu ya Mungu kwako na tendo la upatanisho kupitia kwa damu iliyomwagika ya Yesu.
Maradhi hayana haki ya kuishi mwilini mwako kama mgeni alivyo na haki kumiliki nyumba ya mtu mtu mwingine. Si haki kwa ugonjwa kukutawala wewe, kuukubali ni kufanya urafiki na adui wa Mungu ambaye amehukumiwa. Yesu Kristo amekukomboa kwa kufufuka kutoka kwa wafu. Ni haki yako kuponywa, kukombo-lewa na kuwa mshindi. Mungu ameahidi afya kwa kila mtu (Mith. 4:22; 1 Pet. 2:24). 1 Peter 2:24 sio tu ahadi bali ni thibitisho (kamailivyo Math 8:17); inatambua tendo lililokamilika na kuhakikishwa na Yesu.
Hakuna yeyote anayefurahia ukamilifu wa Roho na ajuaye ukombozi anaye-faa kusumbuka kimwili awe ameshiba au amelala. Yafaa unapoishi duniani usiwe na maumivu yoyote. Huduma ya uponyaji ya Yesu yadhihirisha kwamba ametukomboa kutoka kwa maradhi na ugonjwa. Yesu hakuja tu kuokoa roho zetu bali pia kuponya mwili unaougua. Hivyo basi alimwuliza mtu aliyepindika “… lipi rahisi kusema, Dhambi zako zimesamehewa au InukaUende?”—Math 9:5. Huduma ya Kristo ili-nuia kuleta ukamilifu wa roho, nafsi na mwili.
Mungu siku zote ni mponyaji na ataendelea kuwa mponyaji milele. Uponyaji wako upo. Kumbuka Yesu aliwaponya wote waliomjia wala hakumfukuza mtu yeyote. Hakuna wakati ambapo yesu alisema si mapenzi ya Mungu kumponya mtu au kwamba ilikuwa mapenzi ya Mungu mtu aendelee kuugua. Hakuna ugonjwa un-amfunza mtu wala kumsaidia mtu kukua kiroho. Yesu aliwaponya wote waliomjia na hivyo kudhihirisha mapenzi ya Mungu yasiyobadilika ni kuponya kila mgonjwa.
Kiini cha Magonjwa
Maradhi ni chanzo cha kifo, nacho kifo ni mshahara wa dhambi. Kumbuka hakukuwa na magonjwa hadi Adamu alipotenda dhambi. Hakuna maradhi katika ufalme wa Mungu. Magonjwa yanatokana na dhambi ya asili. Kama dhambi hain-gekuweko, maradhi nayo hayangekuweko.
167
# 26 Healing of the Body www.healingofthespirit.org
Elewa kuwa maradhi yanatoka kwa shetani. "… Jinsi Mungu alivyomtia Yesu wa Nazareti mafuta katika Roho Mtakatifu na jinsi alivyokwenda huku na huko akitenda mema na kuponya wote wali-okuwa wameonewa na nguvu za Shetani, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye.."—Mat 10:38.
Tuongeze kuwa udhaifu pia unatoka kwa shetani “Wakati uo huo akaja mwanamke mmoja aliyekuwa na pepo mchafu, naye alikuwa amepinda mgongo kwa muda wa miaka kumi na minane, wala alikuwa hawezi kunyoka wima. Yesu alipomwona, akamwita akamwambia, “Mwanamke, uwe huru, umepona ugonjwa wako.” Yesu alipomwekea mikono Yake, mara akasimama wima akaanza kumtukuza Mungu”—Luka 13:11-13. Yesu alikuwa akifanya mapenzi ya Baba na kwa kufanya hivyo akiharibu kazi za shetani (Ebr. 2:14 na 1 Yohn 3:8).
Tazama maandiko uone jinsi ambavyo maradhi yanaelezewa kuwa kazi ya shetani. Tangu siku ile "Basi Shetani akatoka mbele za BWANA naye akampiga Ayubu kwa majipu mabaya tangu nyayo za miguu yake hadi utosi wa kichwa. " (Ayu 2:7) hadi wakati mkombozi alikuja na kumfungua "Je, huyu mwanamke, ambaye ni binti wa Abrahamu, aliyeteswa na Shetani akiwa amemfunga kwa miaka yote hii kumi na minane, hakustahili kufunguliwa kutoka katika kifungo hicho siku ya Sabato?” " (Luka 13:16), Yesu aliziharibu kazi za shetani—“Basi kwa kuwa watoto wana nyama na damu, Yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao, ili kwa kifo chake, apate kumwangamiza huyo mwenye nguvu za mauti, yaani, Shetani "—Ebr. 2:14.
Tangu mwanzo wetu, shetani amekuwa akishurutisha kizazi chetu kuvuna mazao ya ma-radhi, maumivu, na kuharibika. Watu wa Mungu mara nyingi hudanganywa na adui hadi kukubali magonjwa kama sehemu yao badala ya kutafuta afya na ukombozi.
Upatanisho wa Kristo ulifunika Maradhi Yetu
Mojawapo ya sababu za kuja kwa Kristo ilikuwa kuwakomboa watu kutoka katika uongo na utawala wa shetani ikiwemo maradhi ya kiakili na kimwili. Yesu alituokoa kutoka kwa maradhi na dhambi zetu: “…Lakini alitobolewa kwa ajili ya makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu, adhabu iliyotuletea sisi amani ilikuwa juu yake, na kwa majeraha yake sisi tumepona”—Isa 53:5.
Utakumbuka kuwa Mungu alimwambia Musa atengeneze nyoka wa shaba kama aina ya Kristo (Hesabu 21:8-9) ili kuwaokoa watu kutoka kwa mauti. Iwapo uponyaji wa mwili haupati-kani, kwa nini Wanawaisraeli waliokuwa wakifa walihitajika kumtazama nyoka wa shaba ili wai-shi –(uponyaji wa mwili). Kama ilivyoondolewa laana yao kwa kumtazama nyoka, ndivyo in-avyoondolewa laana yetu kwa kumtazama Kristo aliyeinuliwa.
Kifo cha Yesu kilitupatia wokovu na uponyaji: "akusamehe dhambi zako zote na kuponya magonjwa yako yote, aukomboa uhai wako na kaburi, na kukuvika taji ya upendo na huruma…”Zab. 103:3-4. Uponyaji ni dhihirisho la Upatanisho wa Kristo: "“Mwenyewe alitwaa udhaifu wetu na alichukua ma-gonjwa yetu.’’ "—Math 8:17.
Petro anasema hivi kuhusu kifo cha Yesu: “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu kati-ka mwili wake, juu ya mti, ili kwamba,tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tupate kuishi katika haki. Kwa kupigwa kwake, ninyi mmeponywa”—1 Pet. 2:24. Kumbuka ushuhuda wa Petro juu ya upako wa Yesu wa uponyaji kakia Matendo 10:38: "Jinsi Mungu alivyomtia Yesu wa Nazareti mafuta katika Roho Mtakatifu na jinsi alivyokwenda huku na huko akitenda mema na kuponya wote waliokuwa wameonewa na nguvu za Shetani, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye."
Uponyaji kaika Agano Jipya
Yesu alihudumia wagonjwa: "Yesu akapita katika Galilaya yote, akifundisha katika masi-nagogi yao, akihubiri Habari Njema za Ufalme wa Mungu, akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi miongoni mwa watu.. "—Math 4:23. Tafakari yafuatayo:
168
# 26 Healing of the Body www.healingofthespirit.org
• 20% ya jumbe zote kwenye Injili ni juu ya uponyaji.
• Maandiko 41 katika Injili yanazungumzia uponyaji uliofanywa na Yesu
• Mara 19 Bibilia inaelezea idadi ya watu walioponywa na Yesu.
• Yesu aliwatuma wanafunzi wake kuponya (Luka 9:1-2 na 10:1, 9).
• Yesu aliaagiza wanafunzi wake kuponya (Mark 16:15-18).
Kwa nini Yesu Aliponya?
1. Kutimiza unabii na kushuhudia Ufalme ujao wa Mungu (Math. 8:16-17)
2. Kuthibitisha yeye alikuwa Masihi (Matendo 2:22-24)
3. Kudhihirisha uwezo wake kusamehe dhambi (Math 9:1-8)
4. Kuonyesha kazi za Mungu (Yoh 9:13-25)
5. Kumtukuza Mungu (Yohn 11:4)
6. Kuwaleta watu kwenye imani (Yoh 20:30-31)
7. Kwa ajili ya huruma na uendo wake kwa watu (Math 20:34)
Je Uponyaji ni Kwa Wote?
Je wote huponywa? “La.” Je Yesu alikufa kuokoa wenye dhambi wote? “Ndio.” Kila mwenye dhambi ana haki ya kuokolewa lakini si wote wanaokoka. Kad-halika na uponyaji wa mwili, kupokea kipawa sio jambo la lazima bali ni hiari ya mtu mhitaji. Kuna watu wengi wagonjwa ambao hawajui wala kuamini kuwa ni haki yao kuponywa.
Miili yetu ni Hekalu la Mungu
“Je, hamjui ya kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu, akaaye ndani yenu, ambaye mmepewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe, kwa maana mmenu-nuliwa kwa gharama. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu na katika roho ze-nu ambazo ni mali ya Mungu.”—1 Kor. 6:19-20. Mwili wako ni jengo takatifu la Mungu, ndio sehemu muhimu sana duniani anapotaka kuishi Mungu. Tunapobatizwa tunawekwa wakfu kwa Mungu na kusudi lake. Baadaye tunaachilia mawazo maovu yaingie na kuishi ndani yetu hata kusababisha maradhi. Lazima tujue kuwa kila waka-timiili yetu ni mali ya Mungu na inatupasa tufanye kila jambo kwa utukufu wake
(Warum12:1).
Uponyaji na Miujiza
Uponyaji wa kimwili ni zaidi ya kurudi uhai katika viungo vinavyougua na kuondoa maumivu. Uponyaji huchukua muda – wakati mwingine haraka na mwingine polepole. Ili uponyaji ukamilike, wakati mwingine inabidi kufanyike awamu kadha za maombi. Wakati mwingine muujiza unafanyika kwa haraka. . Wale wanaotafuta upo-nyaji hutaka muujiza – kuponywa mara hiyo papo hapo lakini Mungu aweza kutumia mwelekeo wa uponyaji wa majira kidogo kila siku mpaka kufikia ukamilifu.
Ni rahisi kwa mtu kuhifadhi uponyaji wake kuliko kutafuta uponyaji. Pindi im-ani ya uponyaji ipatikanapo na kanuni zake kueleweka, tusitarajie kuugua. Mungu ali-
169
# 26 Healing of the Body www.healingofthespirit.org
powatoa Waisraeli kutoka Misri(milioni 5-6) “hakuwepo mdhaifu hata mmoja kati yao”(Zab 105.37) uponyaji timilifu hudumu kadri tunvyomsongelea Mungu.
Uponyaji na Dawa
Wengine husema “Kama ni mapenzi ya Mungu kuniponya, kuna haja gani kutumia dawa na madaktari” Ni kweli kuwa Isaya alimwambia Hezekia achukue matunda ya mtini na kuyaweka kwenye jipu (2 Fal 20:7), lakini pia tunda la mtini halikumponya. Hata hivyo aya ya 1 yatujulisha kuwa Hezekia alikuwa na “ugonjwa wa kufisha”, aya ya 5 yatuelekeza kuwa Mungu alisema “ni-takuponya”. Kama Yesu alivyochukua udongo akampaka kipofu machoni, twajua kuwa udongo haukuleta uponyaji maana alimwamuru akanawe uso.hakuna kisa kingine ambapo udongo ulitu-mika kama dawa ya kuponya upofu. Badala yake alichanganya mate na udongo kama tendo la ku-tii kwa Yule kipofu(Yoh 9:6). Kutii kwake ilikuwa ishara ya imani. Kisa cha Naamani (2 Fal 5:1-27) aliyedhani maagizo ya kwenda kujitosa Yordani mara saba (aya ya 10 – kwa uponyaji wake) ilikuwa ni kitendo cha kumdunisha/dharau. Sawa na Yule kipofu, wote walitii na kupokea Baraka ya uponyaji.
Pia imenakilwa na Timotheo “mvinyo kidogo” (1 Tim. 5:23) ulipendekezwa kwa ajili ya maumivu ya tumbo. Hivyo basi matumizi ya dawa chini ya maagizo yafaayo ni sawa kwetu.
Yafikirie maandiko yafuatayo kuhusu matumizi ya dawa na kuwaona madaktari:
1. “hakuna dawa ya kidonda chako, wewe hutapona"—Yer. 30:13.
2. “Lakini umetumia dawa nyingi bila mafanikio, huwezi kupona. …"—Yer. 46:11.
3. “…ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote! "—Ayu 13:4.
4. “Asa alipatwa na ugonjwa kwenye miguu yake. Ingawa ugonjwa wake ulimzidia sana, ha-ta katika kuugua kwake hakutafuta msaada kutoka kwa BWANA bali kwa matabibu tu”—2 Nya. 16:12.
5. “Hapo palikuwa na mwanamke aliyekuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa miaka kumi na miwili. Mwanamke huyu alikuwa ameteseka sana kwa mikono ya matabibu wengi na kutumia kila kitu alichokuwa nacho lakini badala ya kupona hali yake ilizidi ku-wa mbaya …"—Mark 5:25-26.
Mungu amewapa madaktari busara na elimu na kuumba vitu ambavyo hutumiwa kutenge-neza madawa ambayo madaktari hutumia kutibu maradhi. Ijapokuwa madaktari wana ujuzi wa kusaidia katika matukio ya ajali, kuzama au dharura ambapo mtu hawezi kujisaidia, yapasa ikum-bukwe kujwa Mungu ndiye anayeponya. Kutumia dawa na madaktari sio dhambi na inakubalika na Mungu lakini sio njia ya pekee wala mapenzi timilifu ya Mungu. Kumuona daktari ni muhimu hadi imani ifikie upeo kwa muumini kupokea uponyaji wake kutoka kwa Mungu.
Mateso ya Ukombozi?
Je maradhi ni mapenzi ya Mungu? La, hasha! Maradhi hayatoki kwa Mungu, huja tu kama majaribu yanavyoruhusiwa kuja kwetu. Mungu anaweza kuruhusu maradhi kuja kama alivofanya kwa Ayubu lakini hatumi maradhi. Iwapo maradhi ni Baraka na mapenzi ya Mungu, basi ni dhambi na kinyume cha mapenzi ya Mungu kuombea uponyaji.
Kuna tofauti kati ya (1) ugonjwa na kuugua, na (2)majaribu, mtihani, adhabu, kurudiwa, mateso, na mashaka.Mungu anaahidi kuwa tutakumbwa na mashaka, taabu, majaribu, mateso, na usumbufu (Ebr. 11:37-40; 1 Pet. 4:12; Yohn 16:33; Mat 14:22; 2 Kor. 1:6; Zab 34:19; 2 Tim. 3:12 na 4:5)—kutakasa nafsi, kukuza utu wa kiroho na uhusiano wetu na Mungu. Hii si sawa na ma-radhi au udhaifu.
170
# 26 Healing of the Body www.healingofthespirit.org
Wakati mwingine Mungu hutumia maradhi na ugonjwa kutuelekeza kiroho, lakini hasababishi maradhi haya kutujia wala sio kusudi lake kuyatumia kutukuza sisi kiroho. Hata hivyo kuna uhusiano kati ya dhambi na maradhi, na wakati mwingine Mungu hatatu-ponya mpaka tuachane na dhambi zetu(Luka 5:20 na 7:47-48; Yak. 4:14-16 na Zab 66:18).
Tazama aina ya usumbufu uliotajwa katika maandiko yafuatayo. Yote hayaambata-ni na maradhi (2 Kor. 6:4-5, 11:23-28 na 12:10-11):
masaibu mahitaji matatizo viboko
kifungo vurugu kazi kukesha
uchovu kufunga maumivu ya mwili
uchi njaa kiu kuweweseka
maradhi kuzomewa mateso
mapigano kupigwa mawe kuzama
wezi nyikani ndugu bandia uchovu
baridi uvumilivu
mateso shida za baharini kuteswa na jamaa zako
Neno “mateso” limeandikwa mara 54 katika Agano Jipya na hujumuisha mateso, usumbufu, njaa au hukumu ya mwisho lakini sio maradhi. Neno “sumbuka” limeandikwa mara 65 katika Agano Jipya ambapo ni mara moja tu ambapo linazungumzia ugonjwa am-bao umesababishwa na shambulizi la kishetani sio ugonjwa wa kawaida. Kwa nini basi tu-sumbuke?
• Kukuza na kujaribu imani yetu Yak. 1:24
• Kubadili uasi na dhambi 1 Kor. 11:30; Yak. 5:13-15
• Kujifunza utiifu Ebr. 5:8
• Kukuza unyenyekevu 2 Kor. 12:7 (Mwiba wa Paulo)
• Kumtukuza Mungu 1 Pet. 4:13-14
Tazama tofauti iliyoko hapa: (1) Yak. 5:13, “Je, mtu ye yote miongoni mwenu amepatwa na taabu? Basi inampasa aombe.,” kasha inafuatwa na, (2) Yak. 5:14, “Je, ku-na ye yote miongoni mwenu aliye mgonjwa? Basi inampasa awaite wazee wa kanisa wamwombee na kumpaka mafuta kwa Jina la Bwana.” Yakobo anaeleza tofauti ya ugonjwa na kupatwa na taabu.
Mwiba wa Paulo mwilini haujazungumziwa katika Bibilia nzima isipokuwa kama mfano. Kwengineko katika Bibilia neno mwiba linapotumika tunaona mwiba wenyewe ukitajwa. Katika Hesabu 33:55, “Musa aliwaelekeza Wanawaisraeli kabla ya kuingia kati-ka mji wa Kanani, Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wakaao katika nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama miiba kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi.’’ " Mwiba huu utakuwa usumbufu ka-tika nchi mtakayoishi- usumbufu wa kila mara. Paulo anaeleza kuwa malaika wa shetani alimtesa. Mwiba wa Paulo haukuwa maradhi.
Twaweza kutarajia majaribu na mateso ya kila aina Mungu anapoijaribu imani yetu na kutukuza katika mwendo wetu naye. Lakini hatufai kufikiria kuwa maradhi ni mapenzi ya Mungu au kuyakubali kama chombo cha ukombozi. Yapasa tuwe waangalifu tunapo-
171
# 26 Healing of the Body www.healingofthespirit.org
muombea mtu aliye majaribuni au kwenye mateso. Iwapo majaribu au mateso yanatekele-za kusudi la Mungu wakati huo nasi tuombe yakome itakuwa tunakwenda kinyume na ma-penzi ya Mungu.
Ni vigumu kutambua tofauti kati ya majaribu na mateso yatokanayo na yafua-tayo:
• Maisha ya ulimwengu yenye uasi kwa wale wasiomjua Kristo
• Dhambi na uasi kwale wanaomjua Kristo
• Laana na athari za vizazi vilivyotangulia
• Hofu na utovu wa imani kwa wale wanaomjua Kristo
• Majaribu na Mateso ya wale wanaotembea na Kristo
Kuna tofauti za ndani ambazo zaweza kujulikana tu na wale walio na kipawa cha kupam-banua roho au ufunuo. Kadri mnapoomba kwa Baba juu ya matukio ya maisha yako , Mungu ata-toa jawabu na kubainisha ukweli ulipo.
Ponya Roho Kwanza
Mnamo 1976, Francis MacNutt aliandika kitabu kiitwacho “Healing” ambamo aliorodhe-sha aina nne za uponyaji: (1) Uponyaji wa Roho, (2) Uponyaji wa hisia na mioyo iliyovunjika, (3) uponyaji kutokana na athari za giza, na (4) uponyaji wa miili yetu. Watu wengi huja na hitaji la kuponywa mwili kwanza kabla ya kutafuta uponyaji wa roho. Mungu anhusika na uponyaji wa roho(toba) na hufurahia uponyaji wa roho ndiposa mwili ufuatie. Kwanza tunatakasa chombo cha ndani(roho na nafsi) ndipo kuwe na nuru itakayoruhusu uhai wa Yesu kuingia mwilini kwetu. Pin-gamizi kubwa ya uponyaji ni pepo mchafu.
Kuna uhusiano unaobainika kati ya dhambi na ugonjwa na mara nyingi Bwana hatuponyi maradhi mpaka tutubu (Zab 66:18, Luka 5:20; Luka 7:47-48; Yak. 4:14-16;). Mungu hakuahidi kuharibu kazi za shetani iwapo tunazingatia matendo ya giza. Dhambi ambayo haijaungamwa hu-zuia rehema za Mungu kutufikia. Kumbuka, "Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa,
bali ye yote aziungamaye na kuziacha
hupata rehema. "—Mith. 28:13.
Ugonjwa ni “roho ya maradhi”. Ukiponywa ndani ya nafsi yako hata mwili wako utapona. Shida yote iko inasababishwa na usafi au uchafu wa roho. Uponyaji hugusa maeneo matatu: roho, nafsi na mwili. Jua kuwa mwili wako huathiriwa na roho yako ("Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako kama vile roho yako ifanikiwavyo "—3 John 2). Huwezi kupo-kea uponyaji wa mwili kabla ya kupokea uponyaji wa roho.
Uhusiano kati ya Maradhi na Dhambi
Tazama hatua ya dhambi na maradhi katika maandiko yafuatayo. “3akusamehe dhambi zako zote
na kuponya magonjwa yako yote,”.(Zab 103:3) and “naomba ufanikiwe katika mambo yote na ku-wa na afya yako kama vile roho yako ifanikiwavyo”. (3 Yohn 2). Kuna uhusiano kati ya maradhi na dhambi. Maradhi yote ni matokeo ya:
a) kutengwa na Mungu (uasi)
b) kutengwa kwa nafsi (kujichukia)
c) kutengwa na wengine (kutosamehe, hasira, majeraha)
172
# 26 Healing of the Body www.healingofthespirit.org
Utafiti waonyesha kuwa 80% ya magonjwa yanaathiri akili, yaani hutokana na mawazo, hisia na matatizo katika roho zetu wala sio magonjwa yenyewe. Mwili unaitikia hali iliyoko kwenye nafsi na roho. Adui huleta yafuatayao:
kujichukia kutosamehe hofu
hukumu chuki kiwewe
kujikataa machungu wasiwasi
hofu ya kukataliwa hasira kujisukuma
kujikana maudhi kujipenda
kujihukumu farakano kwenye jamii
kujidunisha
miili yetu nayo inaitikia na chembe za damu zinaanza kuugua. Chembe zinazozuia marad-hi zinaharibika na hivyo basi wewe unaanza kuwa mgonjwa. Unapohisi au kusema mambo yaliyo hapo juu, roho ya kuugua inapata kibali cha kuingia ndani yako. Roho hii inaanza kuumiza mwili mpaka uishie kuwa na maradhi yafuatayo:
mizio kuzimia
ugonjwa moyo, mshipa kifafa
kasi ya damu kisukari
kuvunda kwa damu saratani
Kuvunjika mifupa
Utengano unapoponywa (yaani kujichukia, kutosamehe, kujikataa) chembe chembe za damu zinazopigana na maradhi huanza kufanya kazi kama zilivyokusudiwa. Ili kujifunza zaidi, tazama: Henry W. Wright A More Excellent Way, Be in Health, ISBN 0-9678059-2-9.
Uponyaji Kanisani
Kuna aina mbili za uponyaji kanisani: (1) huduma inayofanywa na wachache wenye vipawa na (2) uponyaji unaofanywa kanisa zima kwenye ibada za uponyaji au vi-pindi vya huduma baada ya ibada.
Huduma ya Uponyaji
Fuata hatua zifuatazo kuanzisha huduma ya uponyaji kanisani:
1. Mfano – kuwa na vipindi na kanuni za uponyaji kwa kuzoea kuhubiri na kufun-disha juu ya uponyaji ili uongozi na washirika wawe na uzoefu wa kuponya na kukuza imani katika huduma hii ya uponyaji.
2. Fundisha na kutia hima ushirika kuhusika na uponyaji katika mafundisho na mahubiri ukitumia wahuduma waalikwa wenye vipawa vya kufundisha na kutoa mifano ya uponyaji.
173
# 26 Healing of the Body www.healingofthespirit.org
3. Tambua walio na vipaji vya uponyaji na wale wanaotamani kujifunza, kuponya na kuendeleza vipaji vyao.
4. Funza na kuwapa vifaa vikundi vya huduma chini ya viongozi muafaka.
5. Tuma vikundi vya huduma kwenye maeneo kila juma ili waweze kuimarisha huduma yao.
6. Wape wahuduma nafasi ya kukuza vipaji na uwajibikaji.
7. Rudia hatua hizi na vikundi vipya vinapojiunga na huduma ya uponyaji
Tazama kitabu: How to Have a Healing Ministry in Any Church, na C. Peter Wagner
(kinapatikana kupitia Amazon.com)
Ibada za Uponyaji Kanisani
Kuna upako mkuu ndani ya ibada zilizopangwa maalum kwa ajili ya uponyaji kuliko kati-ka maombi ya mtu binafsi nyumbani. Kuna aina sita ya matukio ambamo Mungu huponya kwenye ibada hizi:
1. kwenye ibada ya sifa na kuabudu
2. watu wanaposhuhudia uponyaji kwenye mikutano au filamu za video
3. watafutaji wanapopumzika katika roho
4. katika maneno ya utambuzi
5. kiongozi anapoombea kundi zima
6. watafutaji wanapoombewa na kundi la waombezi wa huduma ya ukombozi
Tambua matukio matatu ya hapo juu ni matendo ya neema ya Mungu pasipo nguvu za mwanadamu kuhusika. Uponyaji huu ni bora kwa kuwa Mungu pekee hupokea utukufu. Tukio la mwisho peke yake ndilo linalohusisha kuwekewa mikono. Mungu huitikia sifa, ibada na imani. Kila ibada ya uponyaji yapasa kuanza na kipindi cha sifa na ibada.
Iwapo kundi halijafundishwa juu ya huduma ya uponyaji, mafundisho ya maandiko ya-paswa kufanywa kabla ya huduma kuanza ili watu wafahamu haki zao za uponyaji kutokana na upatanisho wa Kristo. Pia yafaa kujenga imani kwenye maandiko na mifano ya uponyaji na nam-na ambavyo Mungu huponya. Shuhuda na filamu za video zaweza kutumika iwapo zinapatikana.
Kabla ya mkutano mchungaji aamue iwapo atafanya maombi yote au atasaidiwa na kundi la waombezi. Hata hivyo ieleweke kuwa mchungaji anapofanya maombi yote anaweza kuzuia wengine walio na kipaji cha uponyaji kukitumia.
Maneno ya Utambuzi
Neno la utambuzi ni ufunuo unaotolewa na Roho Mtakatifu. Paulo alipokeamaneno haya ya utambuzi kupitia ufunuo (1 Kor. 2:12-13). Roho Mtakatifu hutoa ufunuo kuhusu haja ya mhi-taji ya uponyaji.. hii ni ishara kuwa Mungu anataka kumponya mtu huyo. Uponyaji huu hutimilika
100% kwenye matukio haya.
174
# 26 Healing of the Body www.healingofthespirit.org
Kufuata mapenzi ya Mungu hukuza imani ya uponyaji kwa mhitaji na muombezi. Maneno ya utambuzi huja ifuatavyo:
1. hisia – maumivu, uchungu msukumo
2. kuona – taswira ya eneo la mwili
3. kusoma – kuona kwenye mawazo neno lililojiandika kwenye uso/kipaji
4. Mawazo – hali ya kuwaza (akilini) mtu ana hali fulani
5. Maneno – katika kuomba au kuongea na mtu, mara maneno yanakuja kinywani juu ya hali ya mtu unayemuombea
6. Ndoto – kumuona mtu kwenye shida fulani ndotoni
7. Maono – kuwa na maono unapotulia kana kwamba unaota
Pindi mtu mwenye hali iliyotambuliwa anapojitokeza, aombewe alipo au aletwe mbele ya mkutano.
Hofu ya kufanya makosa ni pingamizi ya maneno ya utambuzi. Kuuliza maswali kwa mfa-no: “Kuna mtu anaumwa na mkono” kuliko kusema: “Mungu ameniambia kuna mtu mwenye maumivu mkononi” ni rahisi kwa kumtambua aliyekusudiwa na neno la utambuzi. Mara nyingi maneno ya utambuzi huwajia washirika walio na kipawa hiki kwa hivyo ni sawa kuuliza katika ibada kama kuna mtu aliye na “neno la utambuzi”.
Watu wengine wana kipawa cha utambuzi kinachoweza kutumika kuwavutia watu kwa Kristo. “maneno” yapokewayo mtaani au sokoni yanaweza kuhusisha hali ya muuzaji au mhudu-mu bila ya kuandamana na uponyaji wa mwili. Yanaposemwa maneno haya mtu hutambua kuwa yamesemwa kwa kusudi la Mungu ili apate kuokoka
Ombi la Uponyaji kwa Kumwekea Mtu Mkono
1. Anza na Mahojiano- Uliza maswali yafuatayo:
• Jina lako ni nani?
• Unataka kuombewa kwa jambo gani?
• Je umekuwa na hali hii kwa muda gani?
• Unajua sababu ya shida hii?
• Je umetafuta ushauri wa daktari, uchunguzi wake ulisema shida ni nini?
• Ninin kilichokuwa kikifanyika maishani mwako hali hii ilipoanza?
• Je ulikuwa na tukio la taharuki au kiwewe hali hii ilipoanza?
Mahojiano yawe mafupi dakika 2-3, usichukue muda mrefu kuzungumzia ishara za shida kwani huondoa imani.
2. Utambuzi wa shida – iwapo unaelewa chanzo na sababu ya hali uliyohadithiwa, endelea na hatua ya 3, iwapo hujui usimuulize mhitaji, omba Roho Mtakatifu akuonyeshe chanzo cha hali hii. Jiulize je ni shida ya kimwili (Yoh 5:5) au kiroho (Luka 13:11)?” katika jawabu mhitaji ameelezea ishara au hisia zake au kiini? Tambua iwapo inatokana na kutosamehe, hasira au dhambi za mhitaji?
3. Uchaguzi wa Maombi
175
# 26 Healing of the Body www.healingofthespirit.org
• Mtie mafuta kichwani iwapo inakubalika.
• Ikikubalika ombi linapoendelea gusa eneo la maumivu, lakini kwanza muulize mhitaji ikiwa ni sawa. Wakati mwingine ni rahisi kumwambia mhitaji agues eneo la maumivu halafu wewe uweke mkono wako juu ya mkono wake
• Kwanza muulize Roho Mtakatifu awepo. Omba roho amshukie na kumhudumia mhitaji maana ni roho aponyae.
• Omba ombi la baraka: “Nakubariki katika jina la Yesu, pokea Roho Mtakatifu, Yesu anakupenda na kukugusa sasa”
• Omba ombi la kudai: “Baba katika jina la Yesu, naomba umfungue macho mhitaji.”
• Omba ombi la kuamrisha“Katika Jina la Yesu , naamuru uvimbe huu kutoweka” au “Katika jina la Yesu maumivu yaishe, zungumzia sehemu iliyo na udhuru ipone”
• Omba kinyume cha roho ya kuugua au udhaifu: hii inafaa iwapo umeongozwa na Roho Mtakatifu.
• Wakati mwingine waweza kuhisi ni sawa kusitisha maombi
• Mara nyingi anza kwa kuombea mahitaji ya kiroho kabla kuombea mahitaji ya kimwili.
• Roho anapoanza kumgusa mhitaji, mtumainie Mungu kutoa siri zilizo ndani ya moyo wake (1Kor. 14:25).
• Omba ikiwa macho yako wazi ili uweze kuona kile Roho Mtakatifu anachofanya. Mwambie mhitaji atulie wala asiombe badala yake afunge macho nakumakinika kwa Yesu.
Kawaida katika kuombea uponyaji wa mwili, maombi ya kudai na kuamuru hutumika. Yapasa useme kwa uwazi unapoamuru.
4. Kuingiliana na Kupokea Majibu—hatua hii inahusisha kumuuliza maswali mhita-ji ili uelewe kinachoendelea.
Unapomuona Roho Mtakatifu akimjia mtu, mshukuru Mungu na uulize uwe-po wake uongezeke. (Mheshimu Mungu kwa kila anachofanya, naye atatenda men-gi zaidi. Mshukuru kwa matendo yake.)
Baada ya dakika 2-3 za maombi, mhoji kwa kuuliza: “wajisikiaje sasa?” Je kuumwa kichwa kumisha? Kama bado kinagonga, omba tena na uulize swali hili tena. Yapasa kubaini kama kuna tofauti yoyote. Francis MacNutt huomba mara ta-tu. Muulize mhitaji kama anahisi uwepo wa Roho Mtakatifu (joto, kutekenywa); muulize “Je Mungu anaongea na wewe?” Watu wengi hujua vile roho anavyodhihi-rika ndani ya miili yao. Waweza kuwasaidia kuelewa iwapo hawajui. Maombi yawe mafupi kama ya Yesu yalivyokuwa. Ombi la dakika 20-30 laweza kuhitajika au uombe mara 2-3. Maumivu hutoweka kwanza, kisha mtu anaanza kutembea na mwishowe tofauti za hisia hudhihirika.
Wakati mwingine waweza kuona ushahidi wa Roho Mtakatifu kama vile ku-lia, kupepesa macho, baridi, joto, kutetemeka, uzito, kuanguka, amani, kicheko au hata kuonekana kama mlevi. Ishara hizi hubainisha uponyaji unafanyika.
176
# 26 Healing of the Body www.healingofthespirit.org
Mhitaji akianza kulia, mpe muda hadi amalize, hii ni ishara uponyaji unaendelea kufanyika. Usitafute ishara, wengi huponywa pasipo na ishara za kuonekana
5. Matendo ya Imani -imani huongeza uponyaji. Waulize wafanye kitu amacho hawakuweza kufanya kabla ya kuombewa kwa mfano – kuinama, kutembea?
6. Kuhitimisha Maombi—uponyaji usipopatikana, usihubiri au kupeana ushauri. Mtie moyo mhitaji kuendelea kuomba huku akimngojea Mungu na kurudi wakati mwingine kwa maombi ya ziada. Mhitaji atahadharishwe kuwa anaweza kupata shambulizi baada ya kuponywa, hivyo basi awe tayari kukemea katika jina la Yesu. Kipindi hiki kiwe kifupi.
Maombi na Unabii
Kutoa unabii kwa wagonjwa kwenye maombi huleta matatizo mengi. Usifanye hivyo pasipo Roho Mtakatifu kukuelekeza. Pia usimhubirie mhitaji katikati ya maombi au baada ya maombi.
Mapenzi yako Yatendeke
Wakristo wanapaswa kujua ni mapenzi ya Mungu kuponya isipokuwa wakati am-bapo mtu ameishi kiasi cha miaka yake aliyopangiwa na Mungu.
Tunapoomba “mapenzi yako yatendeke” tunaweka jukumu la uponyaji kwa Mungu bila kuhukumika wasipopokea uponyaji. Kama hatujui mapenzi ya Mungu kwa mtu basi hakuna sababu ya kuwaombea uponyaji. Yafaa tuombe kwanza kujua mapenzi ya Mungu na punde tupatapo jawabu ndipo tuwaombee uponyaji. Tabu ya mtu haipo mbinguni, bali ipo hapa duniani.
Katika mafundisho ya Yesu ni nadra kupata swala la kuuliza “kama ni mapenzi ya-ko” Yesu hakupendekeza kwa maneno yake wala matendo kuwa dhambi, maradhi au kifo ni mapenzi ya Mungu. Yapasa nyakati zote kujua kuwa uponyaji ni mapenzi ya Mungu. Yesu alimwambia Yule mtu aliyeugua ukoma: “ninataka takasika” - Math. 8:3.
Sala ya Bwana yasema, "… Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe. Ufalme wako uje. Mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni "—Mat. 6:9-10. Mapenzi ya Mungu mbinguni ni kutuponya na kupitia katika ufalme wake anatutakia hali hiyo hapa duniani kama huko mbinguni ambako hakuna maradhi wala usumbufu.
Mapendekezo ya Ziada
• Usimuombee mtu pasipo kujua upendo wa Mungu kwao.
• Muombe Mungu akupe upendo alio nao kwa mtu huyo.
• Omba uweze kumuona huyo mtu kama vile Mungu anavyomuona.
• Kumbuka kwamba hauna jibu lolote wala si wewe uponyae.
• Mshirikishe upendo wa Mungu kwanza.
• Omba na usifu kwanza.
• Muulize Mungu anataka kumponya vipi.
• Muulize kuhusu uhusiano wake na Mungu.
177
# 26 Healing of the Body www.healingofthespirit.org
• Pitia sehemu inayozungumzia “Pingamizi kwa Uponyaji.” Tazama kama kuna lolote am-balo Mungu ananena na wewe kwenye sehemu hii.
• Tambua ni taswira gani ya Mungu walio nayo kwa kuwauliza juu ya mahusiano waliyo nayo na baba yao – je ni mkarimu, mwenye upendo au mkatili? Waonyeshe upendo, wasik-ize, waombee bila na kuwashauri. Kumbuka taswira ya Mungu si sawa na yako.
Waponyaji
Marko 16:15-18 na Yakobo 5:13-16 yapendekeza kuwa wanafunzi wote wameitwa ili kuombea uponyaji. Kwa swala la vipawa vya kiroho, 1 Kor. 12:9 inasoma “vipawa vya uponya-ji”— hii inadhihirisha kuwa kuna aina zaidi ya moja ya vipawa vya uponyaji. Watu wengine wa-tapata kuwa wana wepesi wa kuombea aina fulani ya uponyaji kuliko wengine. Kuna wale walio na karama ya kuponya magonjwa ya moyo na wengine kuweka huru waliotekwa na nguvu za giza. Wengine wana karama ya kuombea uponyaji wa ndani, hivyo basin i muhimu tutambue ni aina gani ya karama ya uponyaji tuliyo nayo.
Waponyaji (wenye karama ya uponyaji) wana sifa fulani zinazowatambulisha: pendo na huruma kwa wengine. Ili kuwa bomba la uponyaji wanahitaji kuwa na upendo thabiti, huruma na rehema. Huruma ni zaidi ya hisia, ni tendo la neema linalomfanya mtu kuugua na mwenzake (ta-zama - Math. 9:36, 14:14, 15:32 na 20:34; Marko 1:41, 5:19, 6:34, 8:2 na 9:22; Luka 7:13, 10:33 na 15:20).
Waponyaji wanapaswa kuwa na roho safi kabla ya kuwaombea wengine ili wakawe mfere-ji inayofaa kupitisha nuru na uhai wa Yesu kwa mtafutaji. Waponyaji makini huonyesha kuwa ka-ribu na Mungu kwa kulitalii neno lake, kuomba na matendo ya utauwa. Huweza kumakinika kwqa Mungu kuliko nafsi zao wenyewe.
Pingamizi za Uponyaji
Sio wote wajao kuombewa uponyaji watapona. Yesu ameshinda maradhi lakini bado haya-jaondolewa duniani. Hii ni siri ya ufalme ambayo hatuwezi kuieleza ama kuithibiti. Shetani anata-futa kutukasirisha na kututia machungu kinyume cha Mungu kwa kuhakikisha kuwa hatuponywi ili atutenganishe na asili ya uponyaji. Utengano huwa chimbuko la uchungu, kutoamini na uasi mioyoni mwetu. Jawabu muafaka kwa swali la kwa nini uponyaji haupatikani ni: “ Sijui kwa nini hukuponywa; lakini inapasa tumwulize Mungu?’
Baadhi ya yafuatayo yaweza kuwa sababu ya uponyaji kutofanyika:
• Kutosamehe
• Hasira, uchungu
• Kutoshughulikia uponyaji wa ndani kwanza
• Kuwa chini ya laana
• Atahari za Ukoo/Vizazi
• Kuhusika katika ibada ya shetani/ushetani
• Kutokuwa na haja na uponyaji kwa dhati
• Kutokuamini kuwa Mungu anaweza kuponya leo
• hofu
• hukumu na dhambi ambayo haijaungamwa
• uasi
• viapo ambavyo hayajavunjwa
178
# 26 Healing of the Body www.healingofthespirit.org
• vifungo nafsi visivyo vya kiungu
• imani kuwa mateso ni sehemu ya ukombozi
• dhambi maishani
• kuwepo kwa pepo au utesi
• hisia za kutokuwa na thamani
• taswira mbaya ya Mungu
• kutoelewa kuwa kifo cha Yesu kilikamilisha upatanisho kwa maradhi na dhambi zetu
• dhambi za wengine dhidi yetu zinazohitaji uponyaji wa kumukumbu
• kutotambua maradhi sawa
• kuombea ishara badala ya kiini cha ishara hizo
• utovu wa imani/kutoamini
• nguvu zisizotosha
• kutoshukuru
• kukiri kusikolingana na uponyaji unaohitajika
• dhana kuwa Mungu anaponya kwa kutumia madawa/madaktari pekee
• kuzingatia chombo cha uponyaji badala ya Mungu
• kutafuta muujiza wa papo hapo
• kuzingatia ishara za maradhi na kuanza kuzikubali kwa misingi ya hisia badala ya kuamini neno la Mungu
Mbona Wengine hupoteza uponyaji wao?
Baadhi ya wale wasiohifadhi uponyaji wao huwa ni kwa sababu ya kutozingatia na kuendelea na mafundisho. Wengine wanayarudia maisha na mazingira ya kale na kupoteza imani yao iliwaletea uponyaji. Utovu wa shukrani, kutokukuza roho kunafanya mbegu iliyopandwa kusinyaa na kukosa kina. (Math. 13:6 na 26). Wengine huvunja maagano waliofanya na Mungu, kuingia na tashwisi, kurudi nyuma katika amani na kutotembea ka-tika nuru. Uponyaji mwingine huhitaji muda na imani ili kukamilika katika kutii. Kuna baadhi ambao wanatafuta suluhisho la haraka kwa mwili na kusahau kuwa kusudi la Mun-gu la uponyaji ni kuleta utakaso.
Kutoponywa kwa wengine kunaweza kusababishwa na utafyamlo na kutozingatia masharti ya kukuza afya bora. Mtu asipotunza afya yake huwa anavunja kanuni zilizo-wekwa na licha ya hilo atake uponyaji wa Mungu, yafaa akumbuke kuwa kukiuka kanuni za afya ni kuasi sheria ya Mungu. Hivyo basi kila mtu yampasa azingatie lishe bora, kula kiasi ili asiangukie maradhi kama kisukari, uzito kupita kiasi, maumivu ya tumbo n.k. am-bayo yanaweza kuzuia uponyaji kukamilika.
Baada ya Mungu kujitambulisha kama Jehova-Rapha mponyaji wetu,masharti ya-liwekwa ili watu waweze kuwajibika kwa uponyaji na afya yao. Kuna nyakati ambapo wa-gonjwa wasiojua namna ya kutumia lishe bora na maelekezo mengine wanahitaji ushauri wa msomi aliye na ujuzi huo. Baraka inayotafutwa huja kupitia kuzingatia ushauri huo.
179
# 26 Healing of the Body www.healingofthespirit.org
Vifaa
1. F. F. Bosworth, Christ The Healer (Revell Publ., 1973). ISBN 0-8007-5124-8.
2. Morton Kelsey, Healing & Christianity (1995). ISBN 0-8066-2776-X.
3. Jonathan Graf, HEALING: The Three Great Classics of Divine Healing, (Christina Publi-cations, 3825 Hartzdale Drive, Camp Hill, PA 17011). ISBN 0-87509-491-0 1992.
4. Agnes Sanford, The Healing Light (1972)
5. John Wimber, Power Healing (Harper & Row, 1987). ISBN 0-06-069533-1.
6. Francis MacNutt, Healing (1974). ISBN 0-87793-074-0.
7. Francis MacNutt, Power to Heal (Ava Maria Press, 1977). ISBN 0-87793-133-X.
8. Francis MacNutt, Prayer That Heals (Ava Maria Press, 1981). ISBN 0-37793-219-0.
9. Barbara Shlemon, Healing Prayer, (Ava Maria Press, 1975).
Uponyaji katika Agano Jipya (inajumuisha uponyaji wa mwili na kuwekwa huru kutoka kwa roho za giza)— Baadhi ya matukio ya uponyaji yamenakiliwa katika Injili zaidi ya moja, kwa hivyo Injili ya kwanza ambamo imenakiliwa ndiyo iliyoorodheshwa.
Mathayo 4:23; 8:2-3, 5-6, 14-15, 16, 28-32; 9:2, 18-19, 20-22, 23-25, 27, 32-33, 35; 12:10, 13, 15, 22; 13:58; 14:14, 35-36; 15:22-28, 30-31; 17:14-18; 19:2; 20:30-34; 21:14
Marko 1:34; 7:32-35; 8:22-24
Luka 5:15; 7:14-15; 8:2; 13:11-13, 32; 14:1-4; 17:12-14; 22:50-51
Yohana 4:46-51; 5:8-9; 9:1; 11:43-44
Matendo 3:1-9; 5:16; 9:1-9, 32-35, 38-41; 14:8-9; 28:3-9.
180
# 27 Kuliweka Huru Kanisa Lako www.healingofthespirit.org
Kuliweka Huru Kanisa Lako
Kwa nini utake Kuliweka kanisa lako huru?
Kusanyiko nyingi zina— lengo la uinjilisti la kutekeleza tume kuu—kama mojawapo ya kazi yao maalum (Mat. 28:19, Marko 16:15). Zaidi ya hayo, kusanyiko nyingi hazijaweza kufaulu katika juhudi hizo. Sababu ya matokeo haya haba huenda ikawa ni ya kiroho badala ya kimwili: “Kwa maa-na kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho” (Efe 6:12). Hata hivyo, “…maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu kuangusha ngome” (2 Kor. 10:4).
Fikiria juu ya mifano hii ya kweli:
1. Kule Adrogue, Brazil, Kanisa la Baptist lilikuwa na washirika 70 pekee baada ya miaka 70 ya juhudi za uinjilisti: kanisa hilo lilikuwa kaburi la waanzilishi wa kanisa hilo. Isitoshe, kati ya washirika hao 70, hakuna yeyote aliyekuwa mkazi wa Adrogue. Halafu katika mwaka wa 1974, Eduardo Lorenzo akawa mchungaji huko. Kufikia mwaka wa 1987 kulikuwa na washi-rika 250; kufikia mwaka wa 1990 wakawa 600; kufikia mwaka wa 1991, 1000; kufikia mwa-ka wa 1993, 2000. Alipoulizwa ni kitu gani kilitendeka katika mwaka wa 1987, Mchungaji Lorenzo alisema kwamba yeye alianza tu kutumia maombi ya vita vya kiroho.
2. Mtu mmoja aliyeitwa Carlos Annacondia (aliyemiliki kiwanda cha kutengeneza nati na ko-meo katika mji mdogo uliokuwa nje ya Buenos Aires, Brazil) alipatwa na tukio la kiroho na akaamua kuiacha biashara yake na kuwa mwinjilisti. Carlos akaanza kujifunza na kutumia kanuni za maombi ya vita vya kiroho kama alivyofanya Mchungaji Lorenzo (na wengine), ambaye kazi yake ya kiinjilisti husistiza juu ya vita vya kiroho (kupambana na falme na mamlaka) na utangazaji wa injili—sio tu kwa watu pekee bali kwa askari jela wa kiroho wa-naowashika mateka watu hao. Yeye huanza kwa kuiombea miji baada ya kutangaza injili ma-hali hapo. Akishahisi kwamba nguvu za kiroho zilizo juu ya sehemu hiyo zimetekwa ndipo ataanza kuhubiri injili.
3. Kanisa la Olivus Baptist la Mchungaji Albarto kule Argentina (kwa miaka mingi) lilikuwa limekwama na washirika 50 pekee. Baada ya kuhudhuria mkutano mkubwa wa Annacondia, Mchungaji Alberto na viongozi wake wa kawaida walifanya mkutano wao wenyewe. Baada ya ibada ya kwanza, aliwakaribisha watu kwenda mbele. Hakuna aliyeenda. Alipokuwa aki-sumbuka sana moyoni mwake kuhusu ukosefu wa nguvu na kutoitikia kwa watu hao, alisikia sauti ya ndani ikimwambia, “Jaribu kuffanya vile Annacondia hufanya.” Alipokuwa karibu kukata tamaa, aliamua kujaribu njia hiyo. Aliomba ombi lenye nguvu la vita vya kiroho na kukemea mapepo waziwazi, kama alivyomwona Carlos Annacondia akifanya. Baada ya kuyafunga mapepo kwa mamlaka aliyokuwa amepewa na Yesu Kristo, aliwaalika tena watu waende mbele. Wakati huo watu 15 waliinuka kutoka katika viti vyao na uelekea mbio mbele ya kanisa kumpokea Kristo awe Mwokozi wao. Baada ya kipindi kifupi, kanisa hilo li-likua na likawa na washirika 900 na likaanza kusanyiko za setilaiti za washirika 2,100. Len-go lake sasa ni kuwa na washirika 20,000.
4. Mchungaji Steve Nicholson alihubiri injili kule Evanston, Illinois, kwa miaka sita bila kupata matunda yoyote. Yeye na washirika wa kanisa lake waliwaombea wagonjwa na watu wa-chache wakapata kupona. Ushirika wake wa Vineyard Christian haukuwa ukikua. Nicholson akaanza maombi ya bidii pamoja na kufunga. Kiumbe cha ajabu kisicho cha kawaida ki-limtokea na kung’uruma, “Kwa nini unanisumbua?” Kilijitambulisha kama pepo ya uchawi iliyokuwa na mamlaka juu ya sehemu hiyo ya kijiografia. Katika harakati ya vita hivyo, Ni-cholson alizitaja barabara zilizokuwa katika sehemu hiyo. Roho hiyo ikajibu vikali, “Sitaki
181
# 27 Kuliweka Huru Kanisa Lako www.healingofthespirit.org
kukupa sehemu hiyo yote.” Katika jina la Yesu, Nicholson aliiamuru roho hiyo kuondoka mahali hapo. Katika miezi mitatu iliyofuata, idadi ya watu katika kanisa hilo iliongezeka ma-ra mbili kutoka watu 70 hadi 150, wengi wa watu hao walikuwa wameokoka na kuachana na uchawi. Karibu waumini wote wapya walihitaji kukombolewa kutokana na mapepo.
5. Kathie Walters (mwandishi wa kitabu kiitwacho The Spirit of False Judgment) anaripoti kati-ka ukurasa wa 32: “… tulipokuwa tukiishi mahali fulani, Mungu alitufahamisha kuhusu ro-ho ya nuru ya uwongo na umaskini iliyokuwa juu ya sehemu hiyo. Biashara ilianguka na watu wengi walikuwa waking’ang’ana kifedha na kiroho. Ilikuwa vigumu sana kwa watu ku-okoka. Hawakuona wema wa Mungu (unaowafanya watu watubu). Tulikifunga kitu hicho na kukitupilia mbali tukiwa chini ya upako. Baada ya miaka mitatu sehemu hiyo ilifanikiwa sana. Biashara ikaanza kunawiri, majengo mazuri yakajengwa, na watu wakafanikiwa na wa-kaokoka. Makanisa mazuri yakajengwa mahali hapo.”
Mambo matatu yanaweza kutambuliwa kutokana na mifano iliyo hapo juu (na kutoka kwa mifano mingine mingi ambayo haikutolewa):
• Mbinu na juhudi zote za kiinjilisti duniani zitazaa matunda machache sana iwapo ushin-di hautapatikana katika vita vya kiroho kwanza.
• Tunatakiwa kuzingatia kipimo cha kiroho cha ukuaji wa kanisa, bali si mpango na mbinu.
• Watu wengi ambao hawajampokea Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wao hawajafanya hivyo kwa kuwa hawawezi—hawawezi tu kwa sababu Shetani amewapofusha na kuwa-shika mateka (2 Kor. 4:4).
Katika mwaka wa 1976, mwinjilisti na mhuduma Derick Prince, aliyejulikana katika mataifa mengi aliripoti, “Kwa miaka mingi nimeamini kwamba, katika kila jiji kuu la taifa lolote lile, Shetani ameweka ‘mtu wa nguvu’—nguvu ya kiroho isiyoonekana inayosababi-sha upingaji wa makusudi ya Mungu na watu wa Mungu katika sehemu hiyo.” (Fall, 1976 newsletter).
Makanisa ya Latin na Marekani Kusini yanaonekana kuwa yanaongoza katika kipimo cha kiroho cha ukuaji wa kanisa, vilevile ukuaji kama huo unafanyika Marekani Kaskazini. C. Peter Wagner anaonyesha vile washirika wameongozeka katika makanisa ambayo yame-kubali njia hizi za “kutumia vipaji” za kufanya uinjilisti na huduma, kama inavyoonyeshwa hapa chini:
Kanisa la Kutumia Vipaji Kusanyiko la Mungu
Ukuaji Ukuaji
1965 milioni 50 milioni 1.6
1985 milioni 247 milioni 13.2
1991 milioni 391 Kubwa zaidi duniani (makanisa 2400
Katika Sao Paulo, Brazil,
pekee)
Kutokana na mifano hiyo, ni wazi kwamba makanisa hayo yanafahamu vyema kwamba vita vya kweli vya uinjilisti ni vya kiroho. Ishara na miujiza, kukombolewa kuto-kana na nguvu za giza, uponyaji wa kimuujiza, ibada za kuendelea zenye shauku kubwa, un-
182
# 27 Kuliweka Huru Kanisa Lako www.healingofthespirit.org
abii, na maombi ya vita vya kiroho huchukuliwa na huduma hizi kuwa matendo ya kawaida ya Ukristo.
Vita vya kibiblia visipoeleweka, kutakuwa na kuvunjika moyo, hasira, kuchanganyi-kiwa, na huduma isiyo na nguvu katika kusanyiko. Hata kama ni kuratibu burudani ya muziki wa Kikristo, kuanzisha kanisa, au kufanya kazi ya uinjilisti, kanuni ni ile ile: tunatakiwa kumfunga “mtu wa nguvu” na kupata mamlaka juu ya Shetani kabla ya kuyaona ma-tunda kamili ya kazi yetu.
Kuyaweka makanisa huru kutokana na athari za giza zinazowapinga, kunahitaji aina mbili za imani ya msingi: (1) kuamini kwamba roho za giza hukaa ndani ya watu na mahali (vita vya kiroho vya kiwango cha chini katika ardhi) na (2) dhambi za watu huleta laana juu ya ardhi, na kuzipa roho fulani za giza haki ya kisheria ya kukaa mahali hapo au katika ardhi hiyo mpaka roho hizo zifukuzwe (vita vya kiroho vya taifa fulani au vya kimkakati).
Ukandamizaji wa kiroho unaohusika katika mifano iliyo hapo juu huwa na umbo mbalimbali. Fikiria juu ya mifano mingine miwili iliyo hapa chini:
1. Miaka michache iliyopita, katika jiji la Guadalajara, Mexico (jiji lenye watu milioni 6), kulikuwa na makansia 160 pekee ya kiinjili, na hiyo ilikuwa chini ya 0 .5% ya idadi ya watu wote—ilhali katika nchi za Latin America kulikuwa na 10-20%. Ng’ambo nyingine ya mpaka wa nchi hiyo, 30% ya idadi ya watu ilihudhuria makani-sa ya kiinjili. Kwa nini kulikuwa na ukinzai huo? Iligunduliwa kwamba upinzani wa kiroho ulitokana na jumba lenye soko lililoitwa Kona ya Shetani, ambapo dira iliyoundwa kwa marumaru, iliyokuwa na alama iliyoelekea kaskazini, kusini, masha-riki, na magharibi; Shetani alikuwa ametumia ishara hiyo kulichukua jiji hilo kwa ku-tumia ukandamizaji wa kiroho.
2. Victor Lorenzo aligundua kwamba jiji la La Plata, Argentina, lilikuwa limeanzishwa zaidi ya miaka 100 iliyopita na mtu mmoja aliyekuwa na cheo cha juu katika Freema-son, alilipanga jiji hilo kwa kutumia ishara za Umasoni na tarakimu. Maiti kadhaa iliyotiwa mumiani ilizikwa katika sehemu mbalimbali ili kuhakikisha kwamba jiji hi-lo litaendelea kuwa chini ya utawala wa kipepo uliotaka kumiliki kwa hila. Jumba hi-lo lenye soko la Moreno lililokuwa mbele ya kanisa kuu lilikuwa na sanamu nne za shaba za wanawake warembo, kila sanamu iliwakilisha laana fulani juu ya jiji hilo.
Athari hii ya giza inawezaje kutokea (mamlaka na nguvu katika umbo la roho za nchi fulani)?
Fikiria juu ya mfano wa kanisa ambalo liko Mallakka, Malaysia, ambalo halikuweza kukua pamoja na makanisa mengine yote katika jiji hilo. Nabii mmoja kutoka Uingereza akaenda katika jiji hilo; akaisoma historia ya awali ya Francis Xavier—matukio yaliyompata mmisionari huyo wa Kikatoliki miaka 400 iliyopita. Nabii huyo aligundua kwamba watu wa-likataa kumsikiliza Xavier, kwa hivyo Xavier alipanda juu ya mlima na kukung’uta vumbi kutoka kwa miguu yake—kitendo hicho kilileta laana. (Tazama Marko 6:11) Nabii huyo alipeleka kikundi cha wachungaji juu ya mlima huo na wakatubu kwa niaba ya jiji la Mallak-ka kumkataa mtumishi wa Mungu miaka 400 iliyopita. Laana hiyo ilivunjwa, na tangu siku hiyo makanisa ya Mallakka yalianza kukua.
Roho za Maeneo
183
# 27 Kuliweka Huru Kanisa Lako www.healingofthespirit.org
Mtu yeyote ambaye ametembelea nchi hizi: India, Navajoland, Cameroon, Haiti, Ja-pan, Morocco, Peru, Nepal, New Guinea, na China anaweza kushuhudia kwamba aliona mfumo wa ngazi za madaraka ya miungu na roho, inayochukuliwa kuwa mambo ya kawaida katika maeneo hayo. Viumbe hivyo vinadhaniwa kuwa vinatawala nyumba, vijiji, miji, ma-bonde, mikoa , na nchi, viumbe hivyo hutumia nguvu zisizo za kawaida kutawala mie-nendo ya watu wa nchi hizo.
Jacob Loewen, mwana anthropolojia na mshauri wa ufafanuzi wa Biblia , anaonelea kwamba Agano la Kale linasadiki kuweko kwa roho za kipepo zinazotawala nchi fulani, am-bazo mara nyingi huitwa “miungu.” Anaripoti kwamba katika Marekani ya Kati na Kusini, roho zinachukuliwa kuwa “wamiliki” wa mambo ya kijiografia au mandhari ya nchi. Waha-mahamaji wa Kihindi hawawezi kusafiri kutoka katika nchi moja kwenda kwa nchi nyingine bila kuomba ruhusa kutoka kwa roho ya nchi inayotawala eneo wanalotaka kuingia ndani..
Vernon Sterk, mmisionari wa Kanisa la Reformed la Marekani ambaye amefanya ka-zi katika nchi ya Mexico kwa zaidi ya miaka 20 anasema kwamba kila mtu katika makabila ya Tzotzil anaweza kutambua miungu dhahiri kwa majina ya miungu hiyo. Aligundua kwamba roho za uovu na roho za uangalizi zina vyeo na majukumu ya taifa. Roho zote zina mipaka ya kijiografia ambayo nguvu zao zinaweza kufikia, ingawaje nguvu za roho za uovu zinaweza kufika mbali kuliko roho za uangalizi au roho za mababu.
Habari iliyo hapa juu inazua maswali kadhaa. (1) Je, maandiko yana maelezo kuhu-su kuweko kwa roho za nchi? (2) Iwapo mamlaka na nguvu—katika umbo la roho za nchi—zina athari mbaya kwa kazi ya makanisa, huwa zinajitokeza vipi? (3) Zinawezaje kutambuliwa? (4) Zinawezaje kufukuzwa au kuondolewa?
Maandiko yafuatayo yanapendekeza kuwepo kwa ngazi za mamlaka za roho za kipe-po, pamoja na ukweli kuhusu hali ya roho hizo, n.k.
1. Shetani ni mtawala wa dunia hii (Yoh. 12:31, 14:30, 16:11, 2 Kor. 4:4).
2. Kristo alipojaribiwa na Shetani, hakupinga uwezo wa Shetani kumpa “nitakupa milki zote za ulimwengu na fahari yake” (Mat. 4:8-9).
3. Shetani hunaibisha nguvu zake kwa mamlaka, nguvu, na watawala wa giza (Efe. 6:12). Kunaweza kuwa na milioni kadhaa za roho za giza za aina mbalimbali. Marko 5:9 inapendekeza kwamba jina la roho hiyo lilikuwa “Legioni,” kufikia 6,000.
4. Roho zengine za uovu (au mapepo) hukaa ndani ya watu, ilhali zengine zinazoitwa roho za uangalizi au za mababu hukaa katika maeneo ya kijiografia.
5. Maandiko mengine yanayoeleza juu ya ngazi za mamlaka ya Shetani ni haya:
Kumb. 12:2-3 na 32:17 1 Fal. 20:23 1 Kor. 15:32
Amu. 3:7 2 Fal. 17:16, 29-31 Ufu. 12:6-10
1 Sam. 7:3-4 Dan. 10:13 Ufu. 20:8, 10
6. Shetani ana mapepo, malaika wa giza, mamlaka, nguvu, watawala wa giza (Efe. 6) waliopewa kazi katika viwango vifuatavyo na kila kiwango kina mamlaka yanayozidi kiwango kilicho chini yake: Nchi, Mikoa, Jiji, Maeneo, Mahali pa kuabudu sanamau, Mahali pa kazi, Makanisa, Nyumba, Watu Binafsi.
184
# 27 Kuliweka Huru Kanisa Lako www.healingofthespirit.org
7. Roho zengine (kama vile mapepo) zinaweza kubadilika kwa urahisi zaidi. Roho zen-gine (kama vile roho za mababu au uangalizi) zimewekewa mipaka ya kijiografia ka-tika uwezo wa nguvu zao.
8. Katika hali zengine, roho hizo huwa imara katika nyumba fulani, mto, au eneo la kiji-ografia, na kusababisha kila mtu anayeishi karibu na sehemu hiyo kuathiriwa na ma-gonjwa, magonjwa ya akili, au mashambulizi makali.
9. Roho ya uovu ikiwa na cheo cha juu, nguvu nyingi za kiroho zitahitajika ili roho hiyo iweze kufungwa.
10. Usiwahi kuingilia uwanja wa shetani bila kupewa maagizo kamili na Bwana. Kuna msemo wa zamani unaokubali kwamba, “Hakuna mahali salama kuliko kuwa ndani ya mapenzi ya Mungu; hakuna mahali hatari zaidi kuliko kuwa nje ya mapenzi hayo.” Usipokuwa na ulinzi wa kiroho, giza hilo linaweza kuishinda hali hiyo pamoja na watu wanaohusika katika hali hiyo.
11. Ondoka katika eneo la adui iwapo vita hivyo vinakuzidi.
12. Baadhi ya maarifa na uzoefu katika sehemu hii umetoka kwa watu wanaohudumu ka-tika juhudi za kiinjilisti. Wao hupata ushindi katika juhudi za kiinjilisti baada ya ku-zivunja nguvu za adui zilizo juu ya kanisa, makazi ya watu, au jiji.
13. Ulimwengu usioonekana wa roho za giza, kama unavyoelezwa katika kitabu cha Frank Peretti (This Present Darkness and Piercing the Darkness), unakaribia kueleza ukweli kuhusu ulimwengu huo.
Je, maandiko yanaeleza juu ya kuweko kwa roho za nchi?
Yafuatayo ni maandiko yanayotaja miungu wa nchi:
1. Mwanzo 11:9: Katika Mnara wa Babeli, kulikuwa na ziggurat—jengo la zamani lili-lojulikana sana na lililokuwa limetengenezwa kwa ajili ya kufanya mambo ya mizun-gu/ushetani (Mungu aliliharibu kwa kuzivuruga lugha zao).
2. 1 Wafalme 11:5: Sulemani alimtumikia Ashtarothi—mungu wa kike wa Wasidoni, na alimfuata Milkomu—chukizo la Waamoni.
3. 1 Wafalme 20:23: Wapinzani wa Waisraeli waliogopa kwamba wao walikuwa na “miungu ya milimani,” iliyokuwa na nguvu kushinda zao.
4. 2 Wafalme 17:9-18 and 29-31: Israeli iliunda miungu yao na kuabudu sanamu.
5. 2 Wafalme 21:3: Manasseh aliunda sanama na akaabudu na kutumikia vitu vyote vya mbinguni.
6. Waamuzi 8:33: Mara baada ya kifo cha Gideoni, Waisraeli waliirudia miungu ya Baali na wakamfanya Baal-berithi kuwa mungu wao.
7. Yeremia 50:2-3: Yeremia anatoa unabii na kusema; “Beli ameaibishwa na Merodaki amefadhaishwa; sanamu zake zimeaibishwa, vinyago vyake vimefadhaishwa.”
8. Danieli10:13-20: inazungumza juu ya Malaika Mlinzi wa Persia.
9. Matendo 19:23-41: watu wa Efeso waliabudu mungu wa kike Diana.
10. Ufunuo 9:11: Abadoni alitambulika kama malaika (pia “mfalme”) wa kuzimu.
Ardhi iliyotiwa najisi imetajwa zaidi ya mara kumi na tano katika Biblia (Zab. 106:38, Isa. 24:5, Yer. 2:7 na 3:1).
185
# 27 Kuliweka Huru Kanisa Lako www.healingofthespirit.org
Maandiko yanayowaamuru wana wa Israeli “mtaziharibu sanamu zao zote za mawe na za kusubu na kupabomoa kila mahali pao pa ibada” (kama vile katika Hes. 33:52) ni mengi sana hatuwezi kutaja yote. Mpango uliotolewa kwa Waisraeli wa Amri Kumi hauku-fanyika kiajali (kwanza, msiwe na miungu mingine ila mimi, na pili, msijifanyie sanamu ya miungu); katika siku zote za historia yao, Waisraeli walikuwa na tatizo la kutii amri hizo mbili.
Kwa nini roho za maeneo hutokea?
Ardhi na mahali panaweza kubarikiwa au kulaaniwa kutokana na matendo ya watu wanaoishi mahali hapo. (Tazama Mwa. 4:10-11, wakati ambao Mungu ananena na Kaini akimwambia “Umefanya nini? Damu ya ngugu yako yanililia kutoka udongoni. Sasa wewe umelaaniwa! Hutailima tena ardhi yenye rutuba ambayo kama kinywa imeipokea damu ya nduguyo uliyemuua.” na Yesu alipoingia Yerusalemu siku ya Jumapili ya Matawi alisema, “`Nawaambieni kama hawa wakinyamaza, hakika hayo mawe yatapaaza sauti” (Luka 19:40).
Maandiko hayo na mengine yatakayofuata yanaonyesha kwamba ardhi ina roho. Ni vipi ambavyo nguvu za giza huunda ngome za nchi fulani? Hufanya hivyo kupitia kwa ardhi iliyotiwa najisi, kupitia kwa dhambi za watu, ibada ya miungu na sanamu, na desturi za mi-zungu/ushetani. Kama vile mizoga ya wanyama huwavutia tai wa angani, ndivyo ardhi iliyo-tiwa najisi huuvutia uovu wa kiroho. Mapepo hukusanyika mahali ambapo ardhitiwa na-jisi.
Ni kitu gani hudumisha mapepo? Mapepo huendelezwa iwapo desturi na imani na dhambi zilezile, mitazamo, na utamaduni wa zamani utaendelea. Kama inavyofanyika kwa wanadamu, mapepo huendelea kuwako kama laana za kizazi mpaka ziondolewe kwa damu ya Yesu..
Hata hivyo, roho zinazotawala hazina mamlaka ya kwenda katika sehemu nyingine bila ruhusa. Hali fulani zimezipa roho hizo mamlaka ya kuunda msingi wa ufalme wao, un-aotumiwa kuwatawala watu wa sehemu hiyo. Hali hizo mara nyingi huitwa “ngome.” Watu waliotenda dhambi wakiingia katika nchi fulani na kukaa hapo, nchi hiyo hutiwa najisi, na roho hizo za nchi hupata haki za kiroho za kubaki mahali hapo, na kuwafanya wakazi hao kuwa mateka.
Maandiko mengi yanaeleza juu ya nchi kutiwa najisi na laana zilizoingia katika nchi hizo kutokana na dhambi za watu walioishi katika nchi hizo. Walawi 18:25 inasema kwam-ba, “ nchi yao ilitiwa najisi: nami nikaiadhibu, nayo ikawakataa wakazi wake.” Pia, Ezra 9:11 inasema, “Nchi mnayoiendea na ambayo itakuwa mali yenu ni nchi iliyo najisi yenye uchafu wa wakazi toka nchi mbalimbali”
Tusidanganyike kwamba uvunjaji wa amri ya kwanza na ya pili pekee ndiko kutai-chafua ardhi. Dhambi za kikundi, kama hizi zifuatazo, zinaweza kuleta matokeo hayo.
Kuhukumu
Uovu
Kukosoa
Kutosamehe
Ufuasi wa madhehebu
Mafundisho ya uwongo
Migongano
Uvuguvugu
186
# 27 Kuliweka Huru Kanisa Lako www.healingofthespirit.org
Migawanyiko
Haki ya kujidai
Kuwa na mawazo finyu
Majisifu
Ngome za tamaduni
Hali ya kutojali au Kuridhika mno
Ushikiliaji mno wa sheria
Kiburi
Hali ya kutoijali dini
Kutawala
Uchoyo wa kifedha
Usimamizi mbaya
Ubinafsi katika mambo ya roho
Kuamini masengenyo na uvumi
Kukataa kueneza injili
Kukataa kuipinga dhambi
Dhambi za Marekani zinazojulikana vizuri ni:
• Dhambi dhidi ya Wahindi wa Marekani (zaidi ya mikataba 350 ilivunjwa)
• Utumwa
• Kuwatesa Wayahudi kwa kutowapendelea Wasemiti
• Kuwazika Wajapani wa Marekani wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia
• Kiburi cha watu wa Marekani
• Tamaa ya vitu
Roho za maeneo hutambuliwa vipi?
Unawezaje kuhudumu uhuru ndani ya shirika la mwili wa kanisa? … kwa njia ile ile unayotumia kuhudumu uhuru kwa mtu mmoja: tafuta njia iliyotumiwa na pepo/mapepo kuingia halafu uifunge kwa kutubu.
Utatambuaje vitu ambavyo Mungu anataka kuponya katika kanisa lako au ardhi ye-nu? Utafanya hivyo kupitia kwa aina ya uchunguzi wa kiroho au ujasusi wa kiroho, utakao-kupa habari utakayotumia kuomba kwa umaizi dhidi ya ngome ambazo dhambi ya kikundi ilitumia kuingia. Watu wengine huiita njia hiyo, uchoraji ramani ya kiroho—au kuona na macho ya kiroho nguvu za kiroho na ngome zinazotuzuia kuyafikia makusudi ya Mungu, ni kama “kuipiga hali ya mbinguni x-ray ya kiroho” na pia katika kanisa. Rejelea Ezekieli 4:1-2 kama mfano wa uchoraji ramani ya kiroho, ambapo Ezekieli aliagizwa na Mungu achore ramani ya mji wa Yerusalemu juu ya tofali, kisha "uzingire mji huo.” Jambo hili linarejelea vita vya kiroho (bali si vya kawaida).
Itakuwa faida kwetu kumjua mtu mwenye nguvu ni nani ili tuweze kumfunga sa-wasawa na kumnyang’anya mali yake (Mat. 12:29, Marko 3:27, Luka 11:21-22). Uchoraji wa ramani ya kiroho hutusaidia kumtambua mtu mwenye nguvu. Katika hali zengine, njia hii itatupa mfululizo wa sifa zitakazotuongoza moja kwa moja hadi kwa mtawala wa nchi fulani. Katika hali zengine tunaweza kujikuta tunakabiliana na mtu wa kawaida aliye na nyama-na-damu anayetumiwa na Shetani. Vilevile katika hali zengine, tunawea kujikuta tu-nakabiliana na muundo wa kijamii uliojaa uovu.
Njia hiyo ya uchoraji ramani ya kiroho inaweza kutimizwa kwa kuzifuata hatua kad-haa muhimu, kama inavyoonyeshwa hapa chini:
1. Fanya uchunguzi na utafiti kuhusu historia na urithi wa ardhi ambayo kanisa liko juu yake (na maeneo yaliyo karibu). Wakati fulani kipande cha ardhi ya kanisa kilipatikana kwa kugawa-
187
# 27 Kuliweka Huru Kanisa Lako www.healingofthespirit.org
nywa kwa sehemu kubwa ya ardhi. Fanya utafiti katika maktaba na katika rekodi za maha-kama na magazeti ya zamani. Hasa tafuta vitu vinavyotia najisi, kama vile: umwagaji da-mu, uvunjaji wa mikataba, uvunjaji wa maagano, na ubaguzi wa rangi.
2. Katika dhehebu lako, fanya juhudi ya kujua historia ya kusanyiko lako. Majaribu yao yaliku-wa gani na yalitokea vipi. Je, kuna ishara zozote zinazoonyesha kwamba dhambi za mtu fula-ni au za kikundi fulani zilisababisha ukandamizaji unaoonekana wakati huu?
3. Kusanya kikundi cha viongozi wa kusanyiko ili muweze kuwa na wakati wa kuomba na kupata upambanuzi. Tafuta msaidizi kutoka nje akisaidie kikundi hicho kujadili juu ya vi-pawa vya ukombozi (uwezo) vya kusanyiko pamoja na sehemu zenye ngome za giza (udhai-fu) zinazoweza kuweko (katika wakati uliopita na wakati wa sasa) katika kusanyiko hilo. Mtarajie Roho Mtakatifu awape utambuzi. Fahamau kwamba Mungu ana shauku kubwa ya kuliweka kanisa lako huru kuliko shauku uliyo nayo wewe. (Kitabu kiitwacho “Setting Your Church Free” kinaweza kusaidia sana katika kulishughulikia jambo hili.)
4. Waambie watu walio na kipawa cha uombezi na upambanuzi waliombee kusanyiko lako kwa ajili ya kusaidia kutambua ukandamizaji wowote ulioko. Watu hao wanaweza kuwa washiri-ka wa kusanyiko lako au la. La sivyo, wakaribishe katika mikutano yenu mnapofanya mambo hayo.
5. Ukipambanua kwamba kuna roho chafu juu ya ardhi ya kanisa au kusanyiko, itakuwa bora kuyajua majina ya roho hizo (kama vile, Kali, Iara, Pele) na/au majina yanayowakilisha kazi zao—yanayosistiza wanachofanya (kwa mfano, roho ya mgawanyiko husababisha mga-wanyiko, n.k.). Watu wanaowaombea wengine ili kuwakomboa kutokana na ukandamizaji wa mapepo wamejifunza kwamba, huwa kuna matokeo mazuri roho zikitambuliwa kwa ma-jina na kuamriwa kuondoka katika jina la Yesu, badala ya kuhudumu kwa ombi lisilo wazi kama hili “Bwana, iwapo kuna roho zozote hapa, tunaziamuru zote kutoka katika jina lako.”
Mwongozo wa Kutumia katika juhudi za utambuzi
1. Onyesha sehemu ya kijiografia uliyo na mamlaka ya kiroho yake—uwanja wa kanisa, au sehemu inayozunguka mahali ambapo jengo la kanisa limesimama (tazama onyo zilizojadiliwa hapa chini katika kidokezo cha 11, cha “Muhtasari”).
2. Omba ili ujue mpango wa Mungu kuhusu mashambulizi na wakati ufaao.
3. Hakikisha kuna umoja kanisani au kati ya viongozi wa kusanyiko.
4. Onyesha picha kamili, kwa kutambua kwamba hitaji hili ni la mwili wote bali si la viongozi pekee.
5. Hakikisha viongozi wamejitayarisha kiroho kwa kutubu, kunyenyekea, na kuwa wa-takatifu (rejelea kidokezo cha 1, “Toba ya Mtu Binafsi,” kilichotajwa hapa chini).
6. Fanya utafiti wa hali ya kihistoria ya awali.
7. Fanya kazi na waombezi walio na kipawa cha huduma hii.
8. Tambua:
• Vipawa vya ukombozi vya kanisa
• Ngome za Shetani katika sehemu hiyo
• Roho za nchi zilizowekwa katika mwili wa kanisa au ardhi
• Dhambi ya shirika—ya zamani na ya sasa
• Umaizi wa kiroho (unaotakiwa kuthibitisha unachokijua kupitia kwa utafiti)
188
# 27 Kuliweka Huru Kanisa Lako www.healingofthespirit.org
Mungu atalielimisha kundi hilo kuhusu tathmini la kweli la udhaifu wao kabla ya wao kuzirithi ahadi hizo. Mungu huondoa kabla ya kuzidisha. Lazima kitu kife ili kiweze kufufuliwa.
Namna ya Kuondoa Athari za Kiroho Zinazokandamiza
Vita vya kiroho huanzia kwa kiwango cha mtu binafsi na kuendelea kuwa ngumu, ku-toka kwa mtu binafsi na familia hadi kwa maisha ya kanisa na kuendelea hadi kwa mji na nchi. Njia ya kuondoa athari hizo inatakiwa kuanza kwa kukiri na kutubu kwa mtu binafsi na inatakiwa kutangulia “Mwongozo wa kutumia katika Juhudi za Utambuaji” ulio hapo juu.
1. Toba ya Mtu Binafsi: Roho za uovu hutaka kuitawala nafsi au mwenendo wa mtu. Roho hizo huweza kuingia katika maisha ya mtu kupitia kwa laana na dhambi za vi-zazi vilivyopita, dhambi na maovu ya sasa, kuabudu sanamu, uonevu, vitu au desturi za mizungu/ushetani, kiwewe wakati wa utotoni, kutosamehe, na aina za kujichafua, kama vile uovu. Mambo hayo yakifanyika, mlango hufunguka katika ua la kiroho li-nalomlinda mtu (rejelea Ayubu 1:6-12) na kuruhusu athari za giza kuitawala sehemu hiyo ya roho yetu au nafsi yetu. Mara nyingi mtu huyo huwa hafahamu kwamba kuna mlango uliofunguliwa au anaathiriwa kwa sababu Shetani hutuziba macho ili tusi-weze kuziona dhambi zetu wenyewe kwani Shetani hukaa na kufanya kazi ndani ya giza. Hivyo basi roho zetu hupata “najisi ya kiroho” sawa na ile iliyozungumziwa kuhusu makanisa na ardhi. Lazima sisi wenyewe tuwe safi kabla ya kutarajia kuli-safisha kanisa letu na ardhi ya kanisa.
Njia ya kufanya hivyo ni moja katika dhambi za mtu binafsi na dhambi za shi-rika:
• Kutambua dhambi yenyewe.
• Kukiri na kutubu dhambi hizo kwa Mungu na kwa ndugu zetu (1 Yohana 1:9).
• Kuomba ili milango ya ua letu iweze kufungwa.
Njia hii ni geni kwa washirika wengi wa makanisa na msaada utahitajika ku-toka kwa msaidizi mwenye ujuzi na uzoefu ili jambo hili liweze kutimizwa kikamili-fu. Tayarisha warsha ya masaa 3-5 kwa ajili ya madhumuni haya kabla ya kujaribu kutambua ngome za shirika—la sivyo tutazibwa macho na kukosa kuziona shughuli za Shetani na pia hatutaweza kuisikia sauti ya Bwana (kwani kutakuwa na “takataka” nyingi za kuzuia).
Dhambi zetu wenyewe hutuzuia kuona na kusikia kiroho. (Kifaa bora ki-nachozungumzia suala hili kiko katika Sehemu ya 1 ya kitabu kinachoitwa ‘Setting Your Church Free,’ kilichoandikwa na Neil Anderson; hata hivyo, yeye hashughulikii sana suala la kuwafukuza roho waovu wanaokaa ndani ya watu, hilo ni kosa kub-wa.) Katika kiwango hiki, jitayarishe kwa upinzani dhidi ya adui.
Zaidi ya hayo, Wakristo wengi hawaamini kwamba wanaweza kuathiriwa na roho waovu wala roho hao kukaa ndani yao. Kutokana na mambo tuliyoona katika vipindi 400 vya maombi ya ushauri, ilibainika kwamba 90% ya watu waliotujia wali-kuwa na athari za giza zilizokuwa zikiwakandamiza ndani ya nafsi zao. Kwanza, viongozi wanatakiwa kunyenyekea kwa kukiri makosa yao. Mara nyingi ibada ya ghafla hutokea baada ya kipindi hiki cha toba.
189
# 27 Kuliweka Huru Kanisa Lako www.healingofthespirit.org
Mafanikio hayawezi kuonekana mpaka kauli ya maafikiano (kulingana na uhusiano wenye mpangilio mzuri) itumike. "Ikiwa utawala mmoja umegawanyika makundimakundi yanayopingana, utawala huo hauwezi kudumu” (Marko 3:24). Fa-hamu kwamba mamlaka ya kiroho hubainika tu iwapo kuna uhusiano wenye mpangilio mzuri miongoni mwa waumini wanaofanya kazi kutimiza lengo moja.
2. Fanya Ombi la Kumfunga Mtu Mwenye Nguvu: Hatua hii inaweza kutimizwa vizuri kati-ka mkutano wa shirika na inaweza kuendeshwa vizuri kupitia kwa uongozi wa msaidizi aliye na uzoefu (mapendekezo ya mada hii yako katika Sehemu ya II ya kitabu kiitwacho; ‘Setting Your Church Free’). Anza kwa kuomba na kudai ulinzi wa Zaburi 91. (Hii inaweza kufanywa na watu kadhaa, mmoja baada ya mwingne, au kwa kutumia mtindo wa kule Korea, ambapo watu wote huomba kwa sauti wakati mmoja; wakati mwingine kwa sauti ya juu sana. Pia re-jelea Mat. 12:28-29, Marko 3:27, Luka 11:21-22.)
3. Toba ya Kujishirikisha: Baada ya utakasaji wa mtu binafsi kufanyika na ngome kutambuli-wa na kuvunjwa, kikundi kitakuwa tayari kuingia katika hatua ya toba ya kujishirikisha. Ha-tua hii hufanyika mtu anapotambua dhambi za shirika za kizazi hiki au kilichopita hala-fu awe tayari kusimama kwa niaba yao na kutubu dhambi zao (kusamehe dhambi hizo). Kumbuka, “Mkiwasamehe watu dhambi zao, wamesamehewa; msipowasamehe, hawasame-hewi.” (Yoh. 20:23).
Dhambi inatambuliwa kuwa na sehemu mbili: dhambi yenyewe na maovu au mato-keo ya dhambi hiyo. (Kwa mfano, dereva mlevi akisababisha ajali na amuumize mtu, dhambi hiyo itakuwa juu ya dereva huyo mlevi lakini matokeo ya dhambi hiyo huonekana kwa mtu aliyejeruhiwa au aliyeuwawa.)
Kutoka 20:5 inatuarifu, “… nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha hao wanichukiao.” Katika kifungu hiki cha maandiko, wana hawakuten-da dhambi—lakini matokeo ya dhambi za baba zao huwafuata kupitia kwa laana ya kizazi mpaka toba ifanywe kwa ajili ya dhambi hiyo ya kwanza na dhambi hiyo ifunikwe kwa da-mu ya Yesu. Hi i si kusema kwamba kila mtu hawajibiki mwenyewe mbele za Mungu kwa dhambi alizofanya mwenyewe! Yesu alijitwalia dhambi zetu na akatufia msalabani ili tuweze kuwa huru. Sisi pia tunaweza kusimama kwa niaba ya mtu mwingine (mtu mmoja au kikundi, aliye hai au aliyekufa) na kuomba ili waweze kusamehewa, na kuomba kwamba matokeo ya dhambi ya kwanza yaondolewe. Tazama mifano ya kitendo hiki iliyo hapa chini:
a. 2 Samueli 21:1, 3: “Wakati mmoja kulitokea njaa kali nchini Daudi akiwa mfalme. Njaa hiyo ilidumu miaka mitatu mfululizo. Daudi alimwomba Mwenyezi-Mungu shauri. Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Sauli na jamaa yake wana hatia ya kum-waga damu kwa sababu aliwaua Wagibeoni.”…. Daudi akawauliza Wagibeoni, “Niwatendee nini? Nitalipaje kwa maovu mliyotendewa ili mpate kuibariki nchi hii na watu wake Mwenyezi-Mungu?”
b. Danieli 9:5-7: Danieli alitubu kwa niaba ya babu zake na akaomba kwa ajili ya dhambi ya shirika.
c. Nehemia 1:6-7: Nehemia aliungama dhambi za Israeli. Pia, “… watu wa Israeli wa-likuwa wamejitenga mbali na watu wa mataifa mengine wakasimama na kuungama dhambi zao na maovu ya babu zao” (Neh. 9:2).
d. Rejelea maandiko mengine yanayoeleza juu ya toba ya kujishirikisha (Ezra 9:5-15 na Yer. 3:25, 14:7 na 20).
190
# 27 Kuliweka Huru Kanisa Lako www.healingofthespirit.org
4. Ungama dhambi za shirika: Mtu mmoja au wengi (mmoja baada ya mwingine) anaweza kusimama na kuungama dhambi za shirika. Iwapo mwakilishi wa kikundi kilichokosewa yuko hapo, ni vyema kuungama kwa mtu huyo na kuomba msamaha mbele ya watu wote, kama vile katika hali ya ukabila, ubaguzi, au dhambi zilizoten-dewa Wahindi wa Marekani. Iwapo hali ya kutosamehe ipo miongoni mwa washirika wa sasa, ni vyema kuomba msamaha mbele ya watu wote.
Wakati wa kuomba msamaha wa dhambi, Nehemia na Danieli waliungama dhambi zao wenyewe pamoja na dhambi za shirika za babu zao. Watu wanaosamehe dhambi za wengine wasisahau kujishirikisha na dhambi zilizofanywa au zinazofa-nywa, hata kama wao wenyewe hawana hatia ya dhambi hizo.
5. Omba ili Dhambi hizo Zisamehewe: Kwa kuelekezwa na kiongozi, mtu mmoja mmoja katika kikundi ataomba dhambi hizo zisamehewe au watu wanaweza kuomba pamoja wakati mmoja. Ngome zozote au dhambi za shirika zinatakiwa kutambuliwa na kuombewa.
Tukishatambua shughuli ya mamlaka yenye sifa fulani, tunatakiwa kukuza sifa iliyo kinyume—sio tu kwa kuyapinga majaribu lakini kwa kuonyesha kitendo halisi. Je, adui anatuletea majaribu ya kuwa watu wa kutisha na wachoyo? Tunataki-wa kuipinga tamaa hiyo kwa ukarimu wa ajabu. Tunaweza kukishinda kiburi kwa kuwa wanyenyekevu na kuishinda tamaa ya mwili kwa kuwa watakatifu; tunaweza kuushinda woga kwa kuwa na imani, na kuushinda uchovu kwa kuwa na bidii.
Mbali na kuyapinga majaribu kwa kufanya kitendo halisi, tuna wajibu wa ku-ziachilia nguvu za Mungu tunapolitangaza Neno lake kwa sauti. Katika haki yetu ya mamlaka kuna faida kubwa ya kunena ili kusudi la Mungu lifanyike kama anavyo-tufunulia mawazo yake. Tunanena katika jina la Yesu, kupitia kwa nguvu za Roho Mtakatifu, kwa sababu ya damu ya Yesu iliyomwagika, kwa upanga wa Roho, am-bao ni Neno la Mungu.
6. Kuweka Nguzo katika Jengo au Ardhi: Kwa kutumia Isaya 33:20-23 neno kwa neno, kusanyiko zengine zimepata msaada mkubwa kwa kuweka nguzo halisi katika kona za jengo au ardhi yao. Tafuta nguzo (2" x 2") kwa kila kona ya jengo au ardhi hiyo halafu andika juu ya nguzo hizo maandiko, kama vile, “Mpingeni Shetani naye atawakimbia” (Yak. 4:7). Kipeleke kikundi katika kila kona na kuomba maombi ya ulinzi; itisha nguvu za damu ya Yesu na uwekaji wakfu wa ardhi hiyo. Pandeni ngu-zo hizo ardhini kama ishara ya kujipatia “paa la kiroho” na kuweka mpaka katika ardhi iliyowekwa wakfu kwa Mungu. Mtangazie adui kwamba vitu vyote vilivyo ka-tika ardhi hiyo vimekabidhiwa kwa Mungu, na vile vile watu walio katika ardhi hiyo.
Kwa Muhtasari
1. Ufalme wa Shetani ni ngazi ya mamlaka iliyo na mipaka ya roho waovu, iliyo na mpango, mamlaka, na viwango vya amri.
191
# 27 Kuliweka Huru Kanisa Lako www.healingofthespirit.org
2. Falme, mamlaka na nguvu za ulimwengu wa roho (Efe. 6) hutaka kutawala sehemu za kijiografia, miji, watu, na makabila.
3. Neno la Mungu linawaambia waumini wasizipuuze nguvu hizo, vilevile linatuamuru tuziteke, tumfunge mtu mwenye nguvu, tuteke nyara mali yake, na kuvunja utawala na mamlaka ya mwovu aliye katika eneo letu la mamlaka (Tazama onyo zilizojadili-wa hapa chini katika kidokezo cha 11)
4. Sisi tulio waumini, tumepewa mamlaka ya kumshinda adui kutokana na ushindi wa Yesu.
5. Tunatakiwa kutumia Neno na nguvu za Mungu kwa hekima kulingana na utambu-zi wa milki isiyoweza kuonekana.
6. Tunatakiwa kumshinda mwovu kabla ya kutumia mbinu za huduma kwa watu.
7. Juhudi zetu zinatakiwa kuwa na kiwango kikubwa cha kusifu na kuabudu. Kati-ka enzi za Mfalme Yehoshafati (2 Nyak.20), Mungu aliwashinda adui za Yuda kwa njia ya kumsifu Mungu wala si kwa vitendo vya kijeshi: “… akawaweka wale wata-kaomwimbia BWANA, ... na kusema, Mshukuruni BWANA; kwa maana fadhili zake ni za milele. Wakati walipoanza kuimba na kusifu BWANA aliwavuruga akili wanajeshi wa Amoni, Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja kupigana na Yuda. Na wanajeshi hao wakashindwa” (2 Nyak. 20:21-22). Njia ya kweli ya kuliondoa giza ni kuleta nuru. Imarisha uwepo wa Bwana miongoni mwa watu wake kwa njia ya kusifu (Zab. 22:3).
8. Vumilia uchungu mpaka uzae. Mafaniko ya ushindi wa kiroho ya kanisa lako ya-taathiriwa na hali mbili za kiroho: nguvu za hamu yenu na kipimo cha imani yenu. Kitu chochote kinachowazwa na Mungu hatimaye hutimia. Dumisha usugu mta-katifu unapoomba ushindi. Kipindi cha kuvuna kitakuja. Huduma mpya zitazaliwa. Hata hivyo, vitu hivyo havitafanyika mara moja. Mpango wa Mungu huwa mrefu kuliko mpango wetu.
9. Kumbuka, vita vya kiroho siyo lengo lenyewe bali ni kifaa cha kufanya uinjilisti na huduma kwa njia inayofaa. Lengo letu si kuzifichua tu ngome za kishetani na kufunga mamlaka na nguvu; balilengo letu ni kuurejesha utukufu wa Mungu kwa vitu vyote vilivyoumbwa na pia kuvirejesha kwa makusudi yake. Vita vya kweli vya kuwa na uinjilisti na huduma inayofaa ni vita vya kiroho.
10. Fanya mpango wa siku za baadaye. Kanisa lako lina shirika lililopita, la sasa, na la baadaye. Sehemu yenu ya familia ya Mungu ina kipawa, ahadi, na eneo la kuchukua. Ni muhimu kwenu kufahamu kile ambacho Mungu ameliita kusanyiko lako kuwa na kufanya, iwapo mtafaulu kukamilisha neno ambalo Mungu amewapa watu wenu na kanisa lako.
11. Kuna maonyo mawili ya kuzingatia:
a. Usithubutu kufanya mambo yanayozidi kiwango chako cha athari ya kiroho na mamlaka, bila kupata mwongozo maalum kutoka kwa Mungu. Kufanya hivyo hukuondoa katika paa la kiroho la ulinzi na kukuhatarisha kwa silaha za adui. Pia kufanya hivyo huleta dhambi ya kuthubutu—ya kujaribu kuendeleza
192
# 27 Kuliweka Huru Kanisa Lako www.healingofthespirit.org
Ufalme wa Mungu bila mwongozo maalum kutoka kwake. Una mamlaka ya ku-liombea kanisa lakini huna mamlaka ya kuuombea mji au ngome za mji (kama vile maduka ya picha za kutia ashiki) mpaka Mungu akuongoze ku-fanya hivyo (soma kitabu hiki “Needless Casualties of War” kilichoandikwa na John Paul Jackson).
b. Usizingatie giza sana kuliko nuru. Ingawa tunatakiwa kufikiria juu ya nguvu za giza wakati wa kufanya mambo hayo, tukizifikira sana zitapata nguvu zai-di.
Kuomba Dhidi ya Roho za Maeneo
1. Soma vitabu kumi kuhusu mada hii kabla ya kufanya chochote. Kitabu cha kwanza kinatakiwa kuwa ‘Engaging the Enemy’ (kilichoandikwa na C. Peter Wagner; soma sehemu iliyo katika ukurasa wa 145 iliyochangiwa na Vernon Sterk).
2. Kiwango cha ushindi wa kiroho kitategemea (1) nguvu za hamu yenu na (2) kipimo cha imani yenu.
3. Usijaribu (peke yako) kuomba dhidi ya roho za nchi; kwa kawaida jambo hilo li-nahitaji kufanywa na kanisa nzima (au kundi la makanisa katika sehemu maalum) ili kuwe na nguvu za kiroho za kutosha kulishinda giza hilo.
4. Kujua jina/majina ya roho hizo katika kiwango chochote si jambo la maana sana laki-ni ni muhimu kufahamu hali halisi au aina ya kandamizo.
5. Kiwango cha roho fulani kikiwa kikubwa sana, nguvu zaidi za kiroho zitahitajika kui-funga roho hiyo.
6. Ni lazima tuanzishe kitendo. Kila kifungu katika Biblia kinachoeleza juu ya ombi la vita vya kiroho kinaonyesha kwamba kitendo huanzia duniani.
7. Ombi la vita vya kiroho hufanywa vyema na makundi ya waombezi wenye motisha na wa kiroho.
8. Muulize Bwana majina au hali ya roho inayokandamiza.
9. Tubu na kuungama kwa ajili ya dhambi za watu walioishi na kufa hapo awali katika sehemu hiyo.
193
# 27 Kuliweka Huru Kanisa Lako www.healingofthespirit.org
Vifaa
Vya Kukusaidia Sana:
1. Bob Beckett, Commitment to Conquer: Redeeming Your City by Strategic Interces-sion (Chosen Books, 1997). ISBN 0800792521.
2. C. Peter Wagner, Breaking Strongholds in Your City (Regal Books, 1993). ISBN 0-8307-1638-6.
Vya Kukusaidia Kiasi:
3. C. Peter Wagner, Warfare Prayer (Regal Books, 1992). ISBN 0-8307-1513-4.
4. C. Peter Wagner, Engaging the Enemy (Gospel Light Publications, 1995). ISBN 0830717692
5. John Dawson, Taking Our Cities for God (Creation House, 1989). ISBN 0-88419-241-5.
6. Cindy Jacobs, The Voice of God (Regal Books, 1995): 229-51. ISBN 0-8307-1773-0.
7. Cindy Jacobs, Possessing the Gates of the Enemy (1991): 222-47. ISBN 0-8007-9223-8.
8. Kathie Walters, The Spirit of False Judgement (Good News Fellowship Ministries, 1995). ISBN 0926955957.
9. John Paul Jackson, Needless Caualties of War (Streams Publications, 1999). ISBN 158483-000X.
10. Neil F. Anderson and Charles M. Mylander, Setting Your Church Free, (Regal Books, 1994). ISBN 0830716556. Kitabu hiki kina sehemu mbili—moja ni ya kuleta uhuru kwa washirika wa kusanyiko na nyingine ni ya kuleta uhuru katika kanisa kupi-tia kwa hatua 7: (1) Nguvu za kanisa letu, (2) Udhaifu wetu, (3) Kumbukumbu, (4) Kutambua na Kutubu kwa ajili lya dhambi za shirika, (5) Kutambua Ushambulizi wa Kiroho kutoka kwa Adui Kwa Sababu ya Kile Ambacho Kanisa Linafanya Wakati Huu, (6) Ombi la Mpango wa Utekelezaji (7) Mikakati ya Uongozi. Kitabu hicho ha-kizungumzi juuu ya mamlaka na nguvu au vita vya kiroho, ambalo ni kosa)
194
# 28 Churches Call to Heal www.healingofthespirit.org
Wito wa Makanisa Kuponya
Uponyaji ni sehemu ya injili na jukumu la waumini wote.
Uponyaji umekuwa nadra kanisani. Tunapasa kupatia uponyaji kipaumbele. Hatuwezi kuhubiri injili (neno) pasipo uponyaji (matendo). Lazima haya mawili yaende sambamba
Kristo alihubiri"UFALME WA MBINGU UMEKARIBIA"
"UFALME WA SHETANI UNAANGAMIZWA"
Ili kutimiza hili yapasa tuwaponye wagonjwa na kutoa pepo.
Kwa nini Yesu aliponya?
1. Kutimiza unabii Math 8:17
2. Kuthibitisha yeye ni Messia Matendo 2:22
3. Kusamehe dhambi Math 9:1-8
4. Kutenda Kazi ya Mungu Yohana 9:13
5. Kumpa Mungu utukufu Yohana 11:4
6. Kuleta Imani kwa watu Yohana 20:30-31
7. kuhurumia na Kupenda watu Math 20:34
Kupitisha Uwezo wa Kuponya
1. Yesu alikuwa na uwezo wote Math 28:18
2. Yesu aliwaita mitume 12 na kuwapa nguvu za kuponya Luka 9:1-2, 10
3. Yesu aliwaita 70 na kuwapa uwezo Luka 10:1,9
4. Yesu aliwaita waumini wote na kuwapa nguvu akisema " Nazo ishara hizi zitafuatana na wale waaminio: Kwa Jina Langu watatoa pepo wachafu, watasema kwa lugha mpya, 18watashika nyoka kwa mikono yao na hata wakinywa kitu cho chote cha kuua, hakitawadhuru kamwe, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona.” . . . Mark 16:17-18
5. Hatua ya kupitisha uwezo wa kuponya kwa waumini wote unaelezewa katika Yohana 15-17.
• Kwanza wawe watumishi
• Watambue asili ya nguvu hizi ni Baba
• Watambue Yesu ndiye anayeelekeza uwezo huu
• Unahitaji utiifu “Nitatenda lile Baba alilonituma”
• Njia ya nguvu hizi ni Roho Mtakatifu
• Yesu aliwaombea wanafunzi watakaswe
• Yesu aliwaombea wanafunzi wampokee Roho Mtakatifu na nguvuYohana 20:22
• Yesu aliwaambia wake wangoje hadi Roho Mtakatifu awajilie. (Luka24:49)
 Nguvu hizi zatufanya mashahidi wema (Matendo 1:8)
 Alitupa nguvu kushuhudia (Math 28:18)
6. Wanafunzi katika Kanisa ya awali waliamriwa waponye watu.
Wakati mnapokwenda, hubirini mkisema, ‘Ufalme wa Mbinguni umekaribia.’ Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo wachafu. Mmepata bure, toeni bure. Math 10:7-8
195
# 28 Churches Call to Heal www.healingofthespirit.org
“Je, mtu ye yote miongoni mwenu amepatwa na taabu? Basi inampasa aombe. Je, kuna ye yote mwenye furaha? Basi na aimbe nyimbo za kusifu. Je, kuna ye yote miongoni mwenu aliye mgonjwa? Basi inampasa awaite wazee wa kanisa wamwombee na kumpaka mafuta kwa Jina la Bwana. Kule kuomba Kwa imani kutamwokoa huyo mgonjwa, naye Bwana atamwinua Na Kama ametenda dhambi, atasamehewa. Kwa hiyo ungamianeni makosa yenu ninyi kwa ninyi na kuombeana ili mpate kuponywa. Maombi ya mwenye haki yana nguvu tena yanafaa sana: Yakob 5:13-16
Andiko hili laelezea kuwa uponyaji wa kikristo sio kipawa maalum ambacho Mungu huwapatia wachache bali ni haki ya kila aaminiye.
7. ili uponyaji usipotee kanisani, umeorodheshwa katika vipawa tisa vya Roho Mtakatifu. “Maana mtu mmoja kwa Roho hupewa neno la hekima na mwingine neno la maarifa kwa Roho huyo huyo. Mtu mwingine imani kwa huyo Roho na mwingine karama za kuponya. Kwa mwingine matendo ya miujiza, kwa mwingine unabii kwa mwingine kupambanua roho, kwa mwingine aina mbali mbali za lugha, kwa mwingine tafsiri za lugha: (I Kor 12:8-10)
8. Amri ya Kristo kwa waaminio wote: “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Ye yote aaminiye na kubatizwa ataokoka. Lakini ye yote asiyeamini atahukumiwa. “Nazo ishara hizi zitafuatana na wale waaminio: Kwa Jina Langu watatoa pepo wachafu, watasema kwa lugha mpya, watashika nyoka kwa mikono yao na hata wakinywa kitu cho chote cha kuua, hakitawadhuru kamwe, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona "Mark 16:14-20
Uponyaji ni njia Uinjilisti
1. Kristo aliponya kudhihirisha Neno, Je sis?
2. “Uinjilisti wa Nguvu”
• Dhihirisha kasha utangaze, tendo kasha neno
• Mungu hunena ndipo nitende
• Mungu hutumia vipawa vya kujua, kuponya, ukombozi, unabii, ndimi ili kufungua akili za wale wasiookoka kwa njia maalum
• Ugumu wa kupokea neno unavunjwa na kudhihirishwa kwa nguvu za Mungu
• Taz:POWER EVANGELISM, na John Wimber, Harper & Row, 1986
• Taza HOW TO HAVE A HEALING MINISTRY IN ANY CHURCH by C. Peter Wagner, Regal 1988, Chap 3 Power Evangelism Today
Huduma ya Uponyaji Makanisani
Matatizo
1. ombi la uponyaji hufanywa kama desturi
2. ombi la uponyaji hufanywa kisiri
3. ombi la uponyaji hufanywa na wazee wa kanisa
4. kanisa halitambui vipawa vya washirika.
5. ombi la uponyaji hufanywa uponyaji wa mwili pekee.
6. ombi la uponyaji kwa kawaida hufanywa na mchungaji.
196
# 28 Churches Call to Heal www.healingofthespirit.org
Mapendekezo
1. Fanya uponyaji sehemu ya msingi ya Injili.
2. Hubiri na kufundisha uponyaji
3. Andaa warsha ya “Kutambua Vipawa Vya Kiroho” ili kila muumini atambue ni vipawa gani vya kiroho alivyo navyo.
4. Fanyeni ibada za uponyaji
5. Toeni nafasi za maombi na huduma kwa wagonjwa baada ya ibada.
6. Tengeni makundi ya uponyaji kadri ya vipawa vinavyohitajika na mwongozo wa Mungu.
7. Yafanyie mafundiso makundi ya uponyaji kuhusu aina 4 za maombi ya uponyaji na namna ya kuyatumia.
8. Kila kundi la uponyaji lifanyiwe maombi kabla ya kuwaombea wengine.
9. Tumia utaratibu ulioelezewaia kitabu “ HOW TO HAVE A HEALING MINISTRY IN ANY CHURCH” kilichoandikwa na C. Peter Wagner, Regal Books, 1989
10. Badili vile unavyoendeleza Kanisa lako ukitumia maandiko yafuatayo kama mwongozo:
• I Wakorintho 14:26-33 Efe 5:19-21
• Kol 3:16-17 Matendo 2:42-46
11. Yesu alitumia thuluthi moja ya muda wake katika uponyaji, thuluthi nyingine katika ukombozi, na nyingine kwenye mafundisho na mahubiri. Kwanini makanisa yetu yasifuate mfano huu?
12. Fuata utaratibu ulioelezewa katika kitabu cha Brad Jersak “Can You hear Me? (Fresh Wind Press 2003) ISBN 0-9733586-0-2 Sura 10 Ombi Sikivu Kanisani ukurasa 195-214.
Masharti ya Kulikuza Kanisa
Yapo mambo matatu yanayaohitajika kufanyika ili kanisa likue.
1. Mchungaji anapasa kupeana huduma na washirika kutoa uongozi.
Katika makanisa mengi kule Marekani na Afrika mchungaji hufanya huduma zote, kuombea wagonjwa na walionyanyaswa. Mchungaji ameitwa kuwa kiongozi sio mtendaji wa huduma zote. Hakuna kanisa linaloweza kufaulu lisipoelewa na kutumia vipawa vya kiroho.
2. Washirika Kama “ukuhani wa waumini wote” (I Peter 2:5, 9) yapasa wapewe mamlaka na motisha ya kufanya huduma ya kufundisha, kuhubiri, uponyaji na ukombozi. Wanapaswa kufundishwa namna ya kutambua vipawa vyao vya kiroho na kuvitumia kanisani. “kila mtu ana kipawa chake kutoka kwa Mungu” (I Kor 7:7) Wakorintho wa kwanza sura ya 12 haiwezi kusomwa bila kueleweka kama kusudi la Mungu kwa kila mshirika kunwa na mahali na huduma ya kutekeleza katika mwili wa Kristo. Iwapo mchungaji hapeani nafasi kwa washirika kufanya huduma, jukumu hilo litamuangukia yeye. Kitabu cha C Peter Wagner, “Your Spiritual Gifts Can Help Your Church Grow” ISBN 0-8307-1681-5 kina maelezo mufaka kwa hoja hii.
3. Wake za wachungaji wanastahili kupewa nafasi kuwa watenda kazi pamoja na waume zao badala ya kuwa watumwa wa wachungaji na kanisa. Wake hawa wana vipawa vinavyoweza kukuza huduma za waume wao na makanisa yao. Hivyo basi wasipohusishwa katika huduma ya kanisa ni kwqenda kinyume cha mafundisho ya Roho Mtakatifu anayehitaji vipawa vilivyo ndani yao vitumike kwa ukamilifu.
197
#29 Anointing Oil www.healingofthespirit.org
Mafuta ya Kutawaza
Watu wanapowatembelea waganga na tabibu wa kienyeji na kuchanjwa, Yule tabibu hufanya agano la damu kati ya mgonjwa na mizimu. Ili kuvunja agano hili na kuondoa athari zake, matumizi ya mafuta ya kutawaza kwa kila sehemu iliyochanjwa na tabibu yahitajika. Kwa ajili ya umuhimu wa mafuta ili kuvunja maagano ya damu yapasa tujadili mada hii kwa undani zaidi.
Mafuta ya Kawaida
Zipo aina mbili za mafuta zilizotajwa kwenya Bibilia. Kwanza ni mafuta ya kawaida yaliyotumika kama ifuatavyo:
• Kuhifadhi ngano na mifugo, yalinunuliwa na kuuzwa sokoni
• Nishati kwa kuwasha taa – tazama mfano wa wanawali kumi
• kupikia
• kuchanganywa na unga kama dhabihu ya nyama
• kuchanganywa na unga kupika mkate usiotiwa chachu
• kutumika kama sehemu ya dhabihu ya kupeperushwa
• kupakwa kwa siko la kulia, gumba la kuia, kidole cha kulia na mkono wa mkosaji kwa utakaso
• alimwagiwa Esta kwa kumuandaa kwa utakaso wa nafasi mpya
• aina ya pesa au hata utajiri
• fungu la kumi
• kupakwa usoni ili kung’arisha uso
• kupakwa usoni wakati wa maombolezo
• kumwagwa kutoka kwenye kiriba au chungu
• Elija 1Falme 17:12 kisa cha Elija na mjane
• Elisha 1Falme 4:6 Elisha na muujiza wa mjane aliyeuza mafuta ili kulipa madeni
• Kuandaa mwili kwa ajili ya kuzikwa
• Kukanda miguu kuondoa maumivu (Mariama na Yesu)
• Kupaka majeraha kwa uponyaji (Msamaria)
Mafuta ya Kutawaza
Mafuta ya kutawaza yalikuwa maalum. Yalikuwa na viungo maalum ndani yake. “Mtu ye yote atakayetengeneza manukato kama hayo na ye yote atakayeyamimina juu ya mtu ye yote ambaye si kuhani atakatiliwa mbali na watu wake.’ ’’ Kisha BWANA akamwambia Mose, “Chukua vikolezi vyenye harufu nzuri vifuatavyo: natafi, shekelethi, kelbena na uvumba safi vyote vikiwa na vipimo sawa, pia tengeneza mchanganyiko wa uvumba wenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. Utiwe chumvi ili upate kuwa safi na mtakatifu.” (Kutoka 30:33-35)
198
#29 Anointing Oil www.healingofthespirit.org
Maandiko yafuatayo yanaeleza matumizi tofauti ya mafuta ya kutawaza:
• Kutoka 29:7 mafuta ya kutwazwa kutiwa kichwani pake.
• Kutoka 29:21 Haruni alimiminiwa damu na mafuta katika mavazi yake na yale ya wana wake ili awe ametengwa
• Kutoka 30:25 mafuta ya kutawaza
• Kutoka 30:31 mafuta ya kutawaza kwa vizazi vyenu vyote.
• Kutoka 35:15 mafuta ya kutawaza katika malango ya madhabahu
• Kutoka 40:9 kutawaza sanduku la agano na kila kilichomo ndani yake pamoja na vyombo vyote vilivyotakaswa na kutengewa Mungu
• Lawi 21:12 mafuta ya kutawaza kumiminiwa kuhani mkuu
• Zab 45:7 mafuta ya furaha
• Isa 61:3 mafuta ya raha kwa waombolezao
• Marko 6:13 aliwatia mafuta wengi waliokuwa wagonjwa na kuwaponya.
• Yakobo 5:14 kuwatia mafuta.
Matumizi ya mafuta ya kutawaza yanaweza kusemwa kuwa ni:
• kutakasa
• kutenga
• kuweka wakfu
• kumtengea Mungu
• Kuponya
Ni nani aliyetiwa mafuta?
• Sanduku la Agano, vyombo viliyomo, madhabahu
• Makuhani
• Makuhani wakuu
• Wafalme
• Wazawa wa Kiume
• Wagonjwa Marko 6:13, Yakobo 5:13
• Kitambaa cha mkono na vazi la uponyaji
Kutawazwa Kulifanyika Wapi?
• Kichwani
• Mavazi
• Mwili (Marko 6:13 na Yakobo 5:13 haisemi ni sehemu gani ya mwili)
• Alinitia mafuta Kichwani (Zab 23:5)
199
#29 Anointing Oil www.healingofthespirit.org
Muhtasari
Bibilia haikubali matumizi ya mafuta kwa sababu zingine zozote. Kuwatia mafuta wanyama, stakabadhi, mashamba au hata kunywa mafuta haya haikubaliki kimaandiko.
Katika Agano la Kale ni makuhani na makuhani wakuu pekee ambao waliruhusiwa kuwamiminia watu mafuta. Katika agano jipya baada ya Kristo, waaminio wote ni ukuhani wa kifalme (IPetro 2:9). Ruhusa ya nani atakayemimina mafuta ni uamuzi wa dhehebu. Katika Marko 6:13 tunaambiwa kuwa ni mitume 12 waliotimiza jukumu hili. Katika Yakobo 5:13 ni wazee waliopewa jukumu hilo.
Ingawa Agano la Kale lapendekeza mafuta yapaswa kutia kichwani na kwenye mavazi, maandiko ya Agano Jipya hayatoi mwelekeo wa sehemu ya mwili ambapo mafuta yafaa kutumiwa. Jambo hili limeachiwa madhehebu kuamua. Wengine hutia mafuta kichwani pekee , wengine hutia kwenye maeneo yanayohitaji uponyaji. Sioni kama Yesu angetatizwa na swala hili.
Katika Agano la Kale milango na vyombo viliyokuwemo hemani vilitiwa mafuta. Siku hizi wengine huweka wakfu makao yao ili kuyahifadhi kutokana na athari za giza. Hili pia ni jambo ambalo Yesu hangelipinga.
Mafuta yaliyotumiwa katika Agano la Kale yalikuwa na viungo maalum ambavyo vina gharama ya juu sana leo. Katika madhehebu mengi, mafuta ya mizeituni hutumika, hata hivyo maji hayakubaliki kwa kutia wakfu kwa kuwa si mafuta.
Ilieleweke wazi kuwa mafuta ni ishara ya Roho Mtakatifu na upendo wa Mungukwa watoto wake. Yanaashiria uwepo wa Mungu na kutambua haja ya mwanadamu kwa msaada wa Mungu. Yanatukumbusha kwamba Mungu ni Muumba na Baba wa wote aliye tayari kila wakati kujibu maombi ya imani. Yanatukumbusha rehema za Mungu katika kuiponya miili, nafsi na roho zetu. Mafuta yenyewe hayana nguvu/uwezo wa kuponya.
Kwenye agano jipya, mafuta ya mizeituni yanageuka kuwa wakfu kwa maombi ya Baraka, utakaso na kutengwa na mchungaji au mhuduma huku akifungua kifuniko na kukielekeza juu mbinguni. Baada ya kuwekwa wakfu hayawezi kutumika kwa mambo ya kawaida.
Lifuatalo ni mfano wa ombi la kuweka mafuta wakfu
Baba yetu uliye mbinguni, twakijongelea kiti chako cha neema kuomba ubariki na kutakasa mafuta haya ili yatumike kama ilivyoandikwa. Bwana twatambua upungufu wetu na haja yetu ya msaada wako. Mafuta haya yawe kumbukumbu ya rehema za Mungu kutumiminia Roho Mtakatifu na upendo wa Baba. Twaomba Baraka hii kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, AMIN.
201
# 29 Twenty Questions www.healingofthespirit.org
Maswali ya Kumuuliza Mtafutaji wakati wa Mahojiano
Jee Ameokoka? Uhusiano wako na Mungu ukoje? Jee umempa Bwana maisha/uhai wako? Jee umezaliwa mara ya pili kwa maji, damu na Roho Mtakatifu?
Jee unataka kuwa huru? Una hakika ya hili? Akiwa anasita, ahirisha kikao hiki
Milango iliyo wazi? Nieleze hadithi ya maisha yako, Mungu anakunenea nini?
1. Maovu yao – umefanya dhambi gani? Uongo, wizi, ulaghai?
2. Kutosamehe – Je kuna mtu ambaye hujamsamehe? Una maudhi au uchungu na mtu yeyote? Je umemkasirikia Mungu?
3. Dhambi za Ngono- Umewahi kuzini tangu uokoke? Jee kuna viunganishi nafsi ambavyo vyahitaji kuvunjwa? Umewahi kuaribu au kutoa mimba?
4. Uganga – Umemtembelea mganga, mpiga ramli au tabibu wa kienyeji?
5. Ndoa za wake wengi – Jee wewe au jamii yako imehusika katika ndoa za wake wengi?
6. Sherehe, tamaduni na itikadi za kijamii – Jee wewe au jamii yako imehusika katika sherehe za kitamaduni? Kuchanjwa, kuvaa hirizi, kufanya kafara?
7. Talaka – Jee umehusika katika kisa cha talaka?
8. Laana – Jee kuna laana maishani mwako?
9. Laana zitokanazo na athari za vizazi – matukio yanayokuathiri kutoka kwa vizazi vilivyotangulia kama laana, uchawi, kuo wake wengi ama itikadi za kijamii ulizorithishwa
10. Ulimi – Jee ulimi wako wahitaji uponyaji?
11. Viapo, Kukijakia kifo- jee umeapa kujiua au kusalimisha roho yako?
12. Vitu vilivyonajisi – Je una vyombo vilyonajisiw au vichafu? Makao yako ni safi?
13. Kuhusika na giza bila Kukusudia- Jee umehusika na matendo ya giza bila kukusudia. Jee ipo milango iliyo wazi ambayo roho anakushuhudia hivi sasa?
14. Ufukara – Jee wahitaji uponyaji kutokana na ufukara? Jee unatoa fungu la kumi?
15. Kiburi– Jee unahitaji uponyaji kutokana na kiburi?
16. Machungu na Vidonda – Jee umeumizwa au kuudhiwa na wengine? Wewe ni motto wa kupanga?
17. Matusi– Umewahi kutusiwa kimwili, kunajisiwa, au kuumizwa kihisia?
18. Kukataliwa– Umewhahi kukataliwa na wazazi, mpenzi au wenzio shuleni au hata nyumbani?
19. Kiwewe – Umehusika katika kisa na kuponea chupuchupu, unaogopa kifo?
20. Nafsi Hafifu – Unajidharau? Unafahamu kuwa Mungu anakupenda?

52
# 9 Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi www.healingofthespirit.org
Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi
Hali na Chanzo cha Dhambi ya Kizazi
Mojawapo ya njia ambazo Shetani hutunyanyasa ni kutumia athari za uovu kupitia kwa “milango” iliyo wazi katika ua linalotukinga. (rejelea Ayubu 1:10) kwa ajili ya dhambi zilizotendwa na babu zetu. Mungu anatwambia hayo katika vifungu kadhaa vya maandiko (Kut. 20:5 na 34:7, Hes. 14:18, Kumb. 5:9, Yer. 32:18).
Watu wachache sana wanaweza kupinga kuwepo kwa urithi wa maumbili—njia ya halisia ya kurithisha sehemu ya DNA inayorithisha tabia au umbile fulani kwa watoto wetu, ambayo huwafanya watoto wetu wawe na sifa za kimaumbile na hali ya wazazi wao na babu zao (kurejelea “mwili”). Pia, wachache wanaweza kupinga kuwepo kwa kuelekeza kwa ku-rithisha watoto matatizo ya kiakili ya wazazi wao (kwa mfano, huzuni, wasiwasi, dukudu-ku,— kurjelea “nafsi”). Vilevile, kuna urithi wa kiroho tunaopokea tukiwa tumboni mwa mama zetu (kurejelea “roho”). Tunalijuaje jambo hili?
Katikati ya kifungu cha tano cha Kutoka 20 (Amri kumi) tunapata maneno haya ku-toka kwa Mungu: “kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wi-vu. Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha hao wani-chukiao. Lakini nawafadhili maelfu ya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.” (Kut. 20:5-6). Mzizi wa dhambi ya asili ulianzishwa na Adamu na Hawa katika Bustani la Edeni. Ingawaje walitenda dhambi, baadaye walimfuata Mungu na kumtii. Adamu na Hawa waliwa-rithisha watoto wao—kupitia kwa urithi wa kiroho—dhambi ya kuasi na kuabudu sanamu na vilevile baraka za rehema (kif. 6).
Abeli aliamua kutii na hivyo basi akapokea rehema. Kaini aliamua kuasi na akatenda dhambi ya kuabudu sanamu na kuua. Kwa ajili ya kitendo hicho watoto wa kaini walilaaniwa hadi sasa. Kurithisha huku kwa baraka au laana (kulikoanza na Adamu na Hawa) kunaende-lea mpaka sasa katika sheria ya kiroho ya urithi.
Kwa nini Mungu amelishikilia sana jambo hili? Hebu tuchunguze kwa makini Amri Kumi, kwanza kupitia kifungu ambacho amri hii iliandikwa, kinachofuata amri za kwanza tatu (zinazohusu dhambi ya kuabudu sanamu) Anza na kifungu cha 2: “Mimi ndimi Mwe-nyezi-Mungu, Mungu wako, niliyekutoa nchini Misri, ambako ulikuwa mtumwa” (Kut. 20:2). Katika kifungu hiki Mungu anawakumbusha Waisraeli kwamba wao ni wake. Ali-waumba, aliwatoa Misri, aliteseka nao walipokuwa wakitoka Misri na kwa miaka 40 waliyo-zurura jangwani kwa sababu ya kuasi. Vifungu vifuatavyo vinasema:
• “ 3Usiwe na miungu mingine ila mimi.”
• “4Usijifanyie sanamu ya miungu wa uwongo, au kinyago chochote kilicho mbinguni, ka-tika nchi au majini chini ya ardhi.”
53
# 9 Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi www.healingofthespirit.org
• “5 Usiisujudie wala kuitumikia: kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu. Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha hao wanichukiao;”
• “6 Lakini nawafadhili maelfu ya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.”
Vifungu vitatu vya kwanza vilivyoonyeshwa hapo juu vinazungumza juu ya dhambi ya kuabudu sanamu. Si ajali kwamba vifungu hivyo vinatangulia katika orodha ya amri zote kumi.
Katika kitabu cha C. Peter Wager “Hard Core Idolatry”, anafafanua kwamba kuabudu sanamu ni “kuabudu, kutumikia, kuahidi, kutii, kufanya matendo ya kuinamisha kichwa, kutoa heshima kuu, kufanya ushirikiano na, kufanya agano na, kutafuta nguvu kutoka kwa au kwa njia yoyote ile kutukuza kiumbe yeyote wa roho pasipo Mungu.” Kwa hivyo, kuabudu sanamu kunahusu kuabudu vitu vya ulimwengu usioonekana (watawala wakuu wa kiroho, nguvu, n.k.), Kufanya hivyo humfanya mtu aweze kuvitambua kwa njia maalum (au kuabudu) vitu halisi kati-ka ulimwengu unaoonekana (magari, nyumba, nguo, pamoja na sanamu, n.k.) kuabudu sanamu ni kukipa kitu kingine (kama vile kazi zetu, pesa zetu, watoto wetu) uangalifu, nafsi, na kipaumbele ambacho Mungu anastahili kupewa. Uaminfiu wetu unatakiwa kumwendea Mungu kwanza (mi-pango yake, makusudi, sheria, n.k.) Katika maisha yetu tunatakiwa kwanza kumfuata Mungu na haki yake.
Ingawaje uzinzi wa kimwili ni mbaya katika mfumo wa maadili ya Mungu, uzinzi wa ki-roho (ambao ni kuabudu sanamu) ni kitu cha kuchukiza mno. Mungu anachukia dhambi za kua-budu sanamu kuliko dhambi zengine zote. Yeye aling’anga’ana kwa uvumilivu na wana wa Israeli kwa miaka 2500 walipofanya dhambi za kuabudu sanamu. Watu waliokuwa wakiishi ulimwenguni walichagua “uovu.” Mungu akawaangamiza (isipokuwa Nuhu na familia yake) ka-tika gharika.
Hata hivyo, Waisraeli hawakupata funzo kutokana na mambo yaliyofanyika hap awali. Musa alipotoka mlimani na amri za kwanza. (Amri Kumi), Waisraeli—wakiongozwa na Haru-ni—walipatikana wakiabudu sanamu ya ndama ya dhahabu, na watu 23, 000 walifanya dhambi za ngono na karamu ya ulafi, ulevi na uasherati (I Kor. 10:8).
Mtu anapotenda dhambi kwake binafsi au dhambi dhidi ya mwenzake, au anposhiriki katika aina yoyote ya ushetani, tukio hilo la dhambi hukita mizizi ndani ya roho yake, na kufun-gua mlango katika ua lake la kiroho. Mtu huyo asipotubu (kwa kuufuata mpango wa Mungu), dhambi hiyo huzama katika mawazo na mwenendo wake; dhambi hiyo huwa siri (ikiwezekana) na hurudiwa kwa njia rahisi. Mtu huyo huacha kumzingatia Mungu na mpango wake na kuanza kuizingatia dhambi hiyo, inayomwakilisha shetani na ufalme wake wa giza.
Hata kama ilitendeka vipi, mtu huyo amekiruhusu kitu kichukue nafasi ya kwanza katika moyo wake. Ameacha kuzifuata njia za Mungu moyoni mwake. Mtenda dhambi huyo huanza “kuifuata miungu mingine,” kama alivyofanya Hawa alipoamua kula tunda walilokatazwa. Mun-gu hukichukulia kitendo hicho kuwa ni kuabudu sanamu, na hivyo basi sheria ya urithi wa kiroho huanza kufanya kazi.
Dhambi hii ambayo mtu hajatubu hugeuka na kuwa laana ya kizazi, na waandishi wengi na waombezi hutumia tukio hilo kuifafanua dhambi ya urithi. Ili kuelewa zaidi vile uovu huu huendelea kutoka kizazi kimoja hadi kingine, soma (pamoja na somo la sehemu hii) sehemu in-ayoeleza juu ya “Uponyaji Kutokana na Laana.” Ningependa kusema hivi, tunaweza kupoteza
54
# 9 Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi www.healingofthespirit.org
nguvu zetu kwa kujaribu kupata uponyaji ilhali kinachotuzuia kupata uponyaji wetu ni laa-na—mzizi wa dhambi ya kizazi uliopandwa miongo mingi iliyopita. Kufanya hivyo ni kama kujaribu kupigana na adui ilhali mikono yetu imefungiwa nyuma yetu. Dhambi ya kizazi huchochea angaa sheria nne za Mungu kama inavyoonyeshwa hapa chini.
1. Sheria ya Mungu ya Baraka na Laana: Kumbukumbu 28 inazungumza juu ya ba-raka na laana. Katika kumbukumbu 28:1-2, Mungu anasema kwamba wanoitii sauti ya Mungu na kuzingatia kwa uangalifu amri zake zote watapewa baraka zilizoorod-heshwa katika vif. 3-14. Lakini wasiotii sauti yake au kuzingatia sheria zake zote anaahidi kuwaletea laana zilizoorodheshwa katika vif. 15-48 na 58-61. (Tazama pia Kumb. 27:15-26.)
2. Sheria ya Mungu ya Kupanda na Kuvuna: “Alichopanda mtu ndicho atakachovu-na.” (Gal. 6:7). Babu zetu walipokumbana na hali ngumu, au walipopatwa na maja-ribu, shida, na vishawishi, wengine waliendelea kushirikiana na Mungu kwa njia ya karibu na kumgeukia ili awasaidie; walitubu dhambi zao, wakaomba baraka walipo-pata majaribu na shida, na kuomba ili wapate uponyaji kutokana na machungu na ma-jeraha waliyopata. Walipanda “mbegu nzuri,” na wote katika vizazi vyao vya baadaye waliweza kuvuna upendo, furaha, na baraka kutokana na uamuzi bora waliofanya ba-bu zao.
Lakini babu zetu wengine walitenda mambo kinyume na hayo walipopatwa na majaribu, shida na hali ngumu. Waliumizwa, wakajeruhiwa au wakadhulumiwa na kusumbuka, na hawakumgeukia Mungu awasaidie. Badala yake, walimwacha Mungu na wakakosa kusamehe, wakawa na hasira, wakakosa kutii n.k. Wengine walijaribu kutatua matatizo yao wenyewe. Wengine wakaendelea kuwa na hasira na chuki, na wakakosa kuyaona makusudi ya Mungu katika maisha yao. Walipowasamehe wen-gine, walipokea neema ya Mungu na wakasamehewa. Walipokosa kusamehe na kutu-bu, waliirejelea sheria ya Agano la Kale ya jicho-kwa-jicho.
Kutokana na milango hiyo iliyofunguliwa, roho waovu waliganda juu ya matendo hayo maovu na wakaweza kuingia katika vizazi vilivyofuata. Roho hao waovu walipanda mbegu za tamaa, kukataliwa, dhuluma, kumwabudu Shetani na kila aina ya uovu na watu waliposhiriki katika matendo hayo, vizazi vilivyofua-ta vilivuna laana za kihisia , kiroho na magonjwa ya kimwili, na vilevile kuvuna utengano wa watu na utengano wa jamii. Vizazi hivyo vya baadaye vilivuna laana na roho waovu ( na kusababisha hali ya maisha isiyofaa kwa watu wenyewe na kwa familia zao za baadaye, ambazo mara nyingi zilijihusisha katika vitendo vya uchungu na vya kuzoea tabia mbaya ya kujamiiana kwa maharimu. Hali hiyo ya mambo huendelea kuwa mbaya zaidi kila kizazi kinapoendelea kukosa uponyaji. Si ajabu jamii inaendelea kuwa na hali mbaya katika afya ya (mwili, akili na roho) tunayoiona wakati huu!
Bila kujua kwamba shida zilizoko sasa za kihisia, kimwili na kiroho zilian-zia katika vizazi vilivyotangulia (kutokana na tukio la kiwewe au dhambi mbaya ya kuhuzunisha) watu wengi sasa wanavuna mavuno ya huzuni, dukuduku, uwo-
55
# 9 Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi www.healingofthespirit.org
ga, pamoja na shida mbalimbali. Wakristo wengi katika kizazi cha sasa hushangaa ni kwa nini (katika maisha yao ya kiroho) hawawezi kumsikia au kumwona Mun-gu, na pia hushangaa ni kwa nini wana kung’ang’ana kwingi.
3. Sheria ya Mungu ya Kufunga na Kufungua: “Nitakupa funguo za ufalme wa mbinguni; kila utakachofunga duniani, kitafungwa pia mbinguni; kila utakachofungua duniani, kitafunguliwa pia mbinguni.” (Mat. 16:19). Babu zetu walipotenda dhambi, walivifunga vizazi vyote vya baadaye kwa athari au matokeo ya dhambi hiyo. Yesu pekee ndiye anayeweza kufungua mikanda hiyo.
Wahusika wengine huwa wanajiuliza iwapo chanzo cha dhambi yao ya urithi kilikuweko kitambo kuliko vizazi vinne vilivyopita. Jambo hili huulizwa sana na Waafrika wa Marekani—ambao babu zao walikuwa watumwa, vilevile Wahindi wa asili ya Marekani au watu wanaotoka katika mataifa mengine kama vile (Japan na Ujerumani).
Watu wengine hudhani kwamba dhambi hiyo ikishapita vizazi “vinne” vili-vyotajwa, watoto wanaozaliwa huwa wamewekwa huru kutokana na laana hiyo bila masharti, wakidhani kwamba laana hiyo hurudiwa tu kwa vizazi vinne halafu ikaisha. Hiyo si kweli. Kwa kila kizazi kisichotubu, utaratibu wa kizazi cha kwanza huanza upya. Laana hujirudiarudia mpaka toba ifanyike. Watoto wakishatubu, basi wao huwa katika kf. 6 Lakini nawafadhili maelfu ya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.”
Kutoka 20:5 inatumia neno maovu. Kuna utata kuhusu tofauti iliyoko kati ya neno ‘dhambi’ na ‘uovu’. Hiyo ni rahisi kueleza, dhambi ni chanzo na maovu ni matokeo. Mzazi akitenda dhambi (kama vile kujihusisha katika ushetani/mizungu au dhambi ya ngono), hiyo huleta laana. Mzazi alitenda dhambi lakini laana hiyo husa-babisha maovu ya kizazi au udhaifu unaorithishwa kizazi cha mtu huyo. Mazoea ma-baya ya kiafya, au kupata ugonjwa wa zinaa mtu akiwa mja mzito, kunaweza kusaba-bisha ulemavu katika mwili wa mtoto. Dhambi ya kiroho husababisha ugonjwa wa ki-roho mara moja ndani ya mtu aliyeitenda, nayo husababisha maovu ya ugonjwa wa kimwili/au ulemavu katika vizazi vitakavyofuata. Tusielewe vibaya, msamaha wa dhambi umetolewa kupitia kwa kifo cha Yesu msalabani. Hatuwajibiki kwa dhambi zilizotendwa na vizazi vilivyopita, lakini Mungu hakuahidi kwamba tutaepuka mato-keo ya dhambi zao bila nguvu za kiungu kuingilia kati. Ukweli ni kwamba alisema, “Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne.(Kut. 20:5 na 34:7, Hes. 14:18, Kumb. 5:9.
4. Sheria ya Mungu ya Kuzidisha: “Nyingine zilianguka penye udongo mzuri, zikaota, zikazaa; nyingine punje mia moja, nyingine punje sitini na nyingine thelatini.” (Mat. 13:8). Chochote tupandacho kitazidi. Tukipanda mbegu ya tufaha, tutavuna mti mzi-ma uliojaa matufaha. Tukipanda (halafu mwaka uwe mzuri) kipimo kimoja cha mbegu za ngano, tutavuna vipimo 30 vya ngano.
56
# 9 Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi www.healingofthespirit.org
Hebu fikiria juu ya mifano hii ya kisasa inayoonyesha vile sheria hii inafanya kazi.
Uchunguzi ulifanywa na Idara ya Ustawi ya Jimbo la New York kumhusu Mag (mwanamke aliyeishi katika miaka ya 1900), mhamiaji wa Amerika ambaye aligeuka na kuwa kahaba. Katika kipindi cha miaka 70 walipata watu 1200 waliotoka katika uzao wa Mag na wakagundua mambo yafuatayo: 280 walikuwa maskini waliopata msaada kutoka kwa taifa, 148 walikuwa wahalifu waliofungwa jela. Jimbo hilo liligharimika (kwa kutu-mia kiasi cha kubadilisha fedha cha mwaka wa 1903) $1,308,000.
Uchunguzi ulifanywa miongoni mwa watu 1 200 wa uzao wa familia ya Jukes. Max alikuwa mkanaMungu aliyemwoa mwanamke asiyemjua Mungu na wakawa na wa-tu wa uzao wao 560: 310, walikufa wakiwa maskini, 150 walikuwa wahalifu, 7 walikuwa wauaji, na 100 walikuwa walevi. Zaidi ya nusu ya wanawake hao walikuwa makahaba. Gharama kwa serikali ilikuwa $ milioni 1.5 kwa kutumia kiasi cha kubadilisha fedha cha karne ya 19.
Jonathan Edwards aliishi wakati wa Max Jukes. Alikuwa Mkristo aliyemwoa mwanamke mcha Mungu. Kati ya watu 1,394 wa uzao wake, 295 walihitimu na shahada ya chuo, 13 wakawa maraisi wa vyuo na 65 wakawa Maprofesa. Watatu walichaguliwa katika bunge ya Amerika. Watatu wakachaguliwa kuwa magavana wa jimbo, na wengine walikuwa mawaziri katika nchi za kigeni. Thelatini walikuwa mahakimu, 100 walikuwa mawakili, na mmoja alikuwa mkuu wa kitivo katika Chuo kimoja cha Utabibu, sabini na watano wakawa maofisa wa jeshi la nchi kavu na la maji, Mia moja walikuwa wamisho-nari waliojulikana sana, wahubiri na waandishi. 80 walikuwa na vyeo katika ofisi za umma. Mmoja wao alikuwa Mdhibiti Fedha wa Hazina ya Marekani na mwingine akawa Makamu wa Raisi wa Marekani. Hayo yote hayakuigharimu serikali chochote.
Fikiria juu ya Andrew Murray aliyekuwa mmishonari wa Afrika kusini. Alikuwa na watoto 11: 5 wakawa wahuduma, 4 wakawa wake wa wahuduma, wajukuu 10 waka-wa wahuduma, na wajukuu 13 wakawa wamishonari katika nchi za kigeni.
Uchunguzi uliofanywa na Dk. D. H. Scott ulionyesha kwamba kulikuwa na hatari ya 237% ya kumpata mtoto aliye na kasoro za kimwili na kihisia iwapo mama ya mtoto huyo yuko katika uhusiano ulio na matatizo au katika ndoa yenye matatizo wakati wa mimba ya mtoto huyo.
Kasisi Marshall Lowell—kuhani wa kanisa la Episkopo—alitoka katika familia iliyokuwa na mpangilio wa mtoto mmoja wa kiume katika kila kizazi kufa. Katika umri fula-ni mmoja alikufa akiwa na umri wa miaka 65, aliyefuata akafa tena na umri wa miaka 42, hali hiyo ikaendelea hivyo. Alimwomba Mungu ili avunje laana hiyo na akaendelea kuishi.
Uchunguzi uliofanywa mwaka wa 1978 katika Chuo Kikuu cha Loyola ulionyesha kwamba wagonjwa kadhaa walijaribu kujiua katika tarehe fulani ya kila mwaka.Iligunduliwa kwamba tarehe hizo zilikuwa tarehe zilezile ambazo mama zao walijaribu kutoa mimba watu hao walipokuwa tumboni. Pia mbinu walizotumia kujaribu kujiua zilifanana na zile ambazo mama zao walitumia kujaribu kuzitoa mimba hizo.
Molly—mwanamke wa miaka 30 mwenye afya nzuri na mwenye akili nyingi alipat-wa na kitu alichokieleza kuwa hofu kuu ya kuaibisha, woga wa kusafiri mahali popote karibu na maji. Iligunduliwa kwamba mjomba yake aliyezama wakati wa mkosi wa Titanic “haku-kabidhiwa kwa Bwana . Hakukuwa na nafasi ya ufungaji (kama inavyofanyika katika mazi-shi). Ufungaji ulipofanyika, woga huo uliondoka kabisa.
57
# 9 Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi www.healingofthespirit.org
Margaret alikuwa na umri wa miaka 73 alipoanza “kushambuliwa” na—milipuko mikali ya kukasirika na ugomvi usiosababishwa na chochote. Mama yake (aliyekuwa amefa-riki miaka minne iliyopita akiwa na umri wa miaka 96) alikuwa na tabia kama hiyo. Zaidi ya hayo, iligunduliwa kwamba katika vizazi sita vilivyopita, mtoto wa kwanza wa kike alikuwa ameonyesha tabia kama hizo za kutatiza. Iligunduliwa kwamba tabia hiyo ilikuwa imeanza karibu miaka 150 iliyotangulia, mtu mmoja wa familia hiyo alipojiua. Baada ya kitendo hi-cho, katika mkondo wa familia hiyo, mtoto wa kwanza wa kike aligeuka na kuwa mlevi sugu, na kuwa na tabia sawa na zile zilizoelezwa hapo juu. Margaret alipata uponyaji wake kupitia kwa maombi.
Mwalimu mmoja alikuwa akipata jinamizi mara kwa mara. Katika kila jinamizi ali-jiona akiwa amesimama kando ya “lindi kubwa jeusi.” Iligunduliwa kwamba, alipokuwa na umri wa miaka miwili, baba yake alifia juu ya nyambizi, iliyozama wakati wa vita. Baada ya kuombewa, jinamizi hizo hazikuonekana tena.
Alletah Nagako—mwanamke wa Kiafrika wa umri wa miaka 33—alikuwa na “pembe” ya urefu wa inchi 1.5 iliyokuwa imeota juu ya kichwa chake kwa kipindi cha miaka minne iliyopita. Aligundua kwamba baba ya baba ya babu yake alikuwa mchawi naye pia ali-kuwa na pembe juu ya kichwa chake.
Mwandishi mmoja anayeitwa Noel Gibson amegundua kitu anachokiita ulevi sugu wa urithi, unaoweza kusababisha aina sita za kutawaliwa na ubaya kujidhihirisha bila mtu anayetawaliwa na ubaya huo kuwa na hamu yoyote ya pombe. kutawaliwa na ubaya kunawe-za kukiruka kizazi kimoja kabla ya kurudia tena kuwatawala watu. Aina nyingine ya kutawa-liwa na ubaya ni: madawa ya kulevya, nikotini, kamari, mazoezi ya kupita kiasi, chakula na kufuja pesa (Kitabu kiitwacho “Freedom in Christ,” ukurasa wa 233).
Fikiria Juu ya Uchunguzi Huu wa Nyakati Hizi
1. Watoto waliokuwa na nyanya waliovuta sigara wana uwezo mara mbili wa kutawaliwa na ubaya huo, hata kama mama zao hawakuvuta sigara.
2. Watoto wana uwezo mara mbili wa kufanya uzinzi katika ndoa zao ikiwa mama au baba zao walifanya uzinzi, hata kama hawakujua kitendo cha wazazi wao cha kutokuwa waaminifu.
3. Watoto wa wazazi waliotengana wana kiasi mara kumi, cha kujiua.
4. Watoto wa kike kutoka katika ndoa zilizovunjika wana kiasi mara 5 cha kuvunja ndoa kuliko kiwango wastani cha nchi.
5. Watoto wa kiume kutoka katika ndoa zilizovunjika wana kiasi mara 3 cha kuvunja ndoa kuli-ko kiwango cha wastani cha nchi.
6. Watoto wa walevi sugu wana uwezo mara 3-5 wa kuwa walevi sugu, homoni zao ni tofauti na zile za watoto waliozaliwa na wazazi wasio walevi. Wanaweza kunywa pombe nyingi bila kulewa.
7. Kuna hatari ya 237% ya kumpata mtoto aliye na kasoro za kimwili na kihisia iwapo mama ya mtoto huyo yuko katika uhusiano ulio na matatizo au katika ndoa yenye matatizo wakati wa mimba ya mtoto huyo.
8. 80% ya watu walio katika jela au wale ambao ni makahaba walidhulumiwa kimapenzi wali-pokuwa watoto.
9. 22% ya watoto wote hudhulumiwa kimapenzi.
58
# 9 Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi www.healingofthespirit.org
Mifano ya Dhambi za Kizazi Katika Biblia
1. Abrahamu aliwadanganya wafalme wawili kwamba Sara alikuwa “dada” yake. Baa-daye Rabeka (mtoto wa ndugu ya Abrahamu na mamake Yakobo) walipanga njama na mwanawe (Yakobo) kumdanganya Isaka, babake Yakobo. Imeandikwa kwamba alikufa bila kuwapata watoto wengine; utasa ulikuwa laana ya aibu katika Israeli (Mwa. 27).
2. Kwa vile watu wawili wa familia ya Musa walitenda dhambi kwa kunung’unika dhidi yake, familia za Kora, Dathani na Abramu zilikufa pamoja na watu wengine 250 (Hes. 16:35).
3. Watoto wa Akani walikufa na baba yao kwa sababu ya dhambi yake (Yosh. 7:1-26).
4. Eli alipokosa kuwarekebisha watoto wake waliokuwa na utovu wa heshima, alisaba-bisha laana kuwekwa juu ya vizazi vyake vya baadaye (I Sam. 3:13-14 na 2:32-33).
5. Gadhabu ya Mungu ilimjia mkuu wa watu wa Yuda vizazi viwili baada ya Manase, ingawaje Manase alitubu na Yosia akawa mfalme mwenye haki kuliko wote (2 Fal. 23:26-27).
6. Yeroboamu alipoabudu sanamu laana iliwajia watoto wake na taifa lake ((1 Fal. 14:9-11).
7. Daudi alikubali kwamba, “Mimi ni mkosefu tangu kuzaliwa kwangu; mtenda dhambi tangu tumboni mwa mama yangu.” Yeye alikuwa ni uzao wa Rahabu, aliyekuwa ka-haba (Mat. 1:5-6) naye aling’ang’ana na uzinzi na ndoa ya wake wengi. Mtoto wake aliyeitwa Amnoni alimtamani dadake na akafanya mapenzi naye. Sulemani, mwana wa Daudi alikuwa na wanawake 600 na mahawara (wengine wao walitoka Misri) nao walileta sanamu na miungu wa uwongo katika nchi ya Israeli.
8. Yoshua, alidanganywa akafanya agano na watu wa Gibeoni (Yosh. 9:7) miaka 430 baadaye Daudi aliomba na kumuuliza Mungu kwa nini kulikuwa na njaa, Mungu akamwambia Daudi kwamba ni kwa sababu Sauli alikuwa ameivunja agano hiyo kwa kuwaua watu wengi wa Gibeoni (2 Sam. 21:1-6). Daudi alikubali dhambi ya Sauli na watu wa Gibeoni wakawataka watoto saba wa Sauli wanyongwe ili kulipia makosa hayo ndiposa njaa ikome.
9. Yesu alipokuwa akisulubiwa, umati ulisema, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu! (Mat. 27:25). Wayahudi wameteseka sana tangu wakati huo.
10. Yesu aliwaambia wakuu wa sheria, “Matokeo yake ni kwamba kizazi hiki kitaadhibi-wa kwa sababu ya damu ya manabii wote iliyomwagika tangu mwanzo wa ulimwen-gu.” (Luka 11:50).
Dhambi inaweza kusafiri kupitia kwa vizazi katika makundi ya kidini au ya kisiasa, na pia kupitia kwa familia (Mat. 23:29-36). Katika kifungu cha 31 tunapata kwamba “… nyinyi ni watoto wa watu waliowaua manabii, “ na katika kifungu cha 35, “Hivyo lawama yote itawapateni kwa ajili ya damu yote ya watu wema iliyomwagwa juu ya ardhi. Naam, tangu kumwagwa damu ya Abeli am-baye hakuwa na hatia, mpaka ile ya Zakaria, mwana wa Barakia, ambaye mlimuua hekaluni kati ya patakatifu na madhabahu, na katika kifungu cha 36, “Nawaambieni kweli, kizazi hiki kitapata adha-bu kwa sababu ya mambo hayo.”
59
# 9 Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi www.healingofthespirit.org
Maandiko Mengine Yanayoshughulikia Hali ya Urithi na/au Hukumu ya Dhambi za babu ni:
Lawi. 26:39-40 Hes. 14:18 1 Fal. 22:52 2 Fal. 5:27
2 Fal. 23:26-27 Neh. 9:2 Zab. 106:6 Yer. 2:9 Yer. 3:25 Yer. 14:7 and 20 Omb. 5:7 Dan. 9:1-20 Mik. 7:6 Mat. 27:25 Luka 19:42-44 Luka 11:47-52
Luka 23:28 Yoh 5:25 Yoh 9:2 1 Pet. 3:19
I Pet 4:6
Ombi la Uponyaji Kutokana na Dhambi Iliyorithiwa
Habari Njema
Habari Njema ni kwamba mtu aliye katika kizazi cha sasa akimgeukia Yesu amsaidie, upen-do wake wa kuponya na kusamehe unaweza kutiririka hadi kwa vizazi vilivyopita na kukiponya chanzo cha tatizo hilo, na kuyafanya “maovu” hayo yakose kuwa na madhara yoyote. Anaweza ku-tuweka huru kutokana na utumwa wetu wa zamani na kuyageuza matokeo ya mbegu iliyopandwa.
Mhusika akimgeukia Mungu na kumwomba amponye kutokana na tatizo alilonalo, Mungu huleta nguvu na nuru yake, uzima wake na msamaha katika kila sehemu ya mkondo wa familia hiyo inayoumia. Matukio ya uchungu ya siku zilizopita hukatwa, na kuruhusu uponyaji na afya njema ku-furahiwa na watu wa familia ya sasa. “Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kujitwa-lia laana hiyo kwa ajili yetu; maana Maandiko yanasema: “Yeyote aliyetundikwa msalabani amelaa-niwa.” Jambo hili lilifanyika kusudi ile baraka aliyopewa Abrahamu iwashukie watu wa mataifa mengine kwa njia ya Kristo, na ili kwa imani, tumpokee yule Roho ambaye Mungu alituahidi.” (Gal. 3:13-14). Yesu alizifia laana zilizolimbikiziwa watoto wetu.
Hatuwezi kueleza kabisa vile uponyaji wa athari za kizazi hufanyika lakini ni sawa na maele-zo ya vile kifo cha Yesu msalabani kililipia dhambi zetu, na pia hatuwezi kueleza kwa nini kukiri na kutubu huondoa silaha ambazo Shetani anaweza kutumia dhidi yetu, wala hatuwezi kueleza kwa nini kufunga kula kuna faida kubwa. Hizi ni siri ambazo tumepewa kupitia kwa neema ya Mungu.
Tunajua kwamba mbinguni hakuna wakati. Mungu anaweza kulifikia tukio lolote wakati wowote katika maisha ya mtu fulani ya kizazi kilichopita—ili alete uponyaji, kama anavyo-fanya kwa watu wa kizazi cha sasa kupitia kwa uponyaji wa ndani. Yeye haibadilishi hali hiyo bali huleta mabadiliko tunapoitikia, ili auwezeshe upendo, neema, rehema na uponyaji utiririke katika hali hiyo.
Maombi ya Kibiblia ya Kumweka Mtu Huru Kutokana na Dhambi ya Kizazi
Uwezo (katika maisha yetu wenyewe) wa kutambua na kutubu dhambi za babu zetu ni wazo geni kwa Wakristo wengi. Sembuse kuomba (tukitubu) kwa ajili ya dhambi za watu waliokufa kitam-bo—jambo linalohitajika ili tuweze kupona? Kuziombea dhambi za watu waliokufa kunajulikana ka-
60
# 9 Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi www.healingofthespirit.org
ma toba ya kujihusisha—kuomba na kutubu kwa niaba ya babu zetu ili tuweze kujiweka huru. Fiki-ria juu ya mifano hii katika maandiko:
1. Ezra na Waisraeli waliomba msamaha kwa ajili ya dhambi za babu zao (Neh. 1:6 na 9:5-15).
2. Daudi aliomba na kumwambia Mungu asikumbuke maovu ya zamani (Zab. 79:8).
3. Daudi aliomba na kuungama dhambi za babu zake (Zab. 106:6).
4. Daudi alitubu kwa ajili ya dhambi za Sauli alipowaua watu wa Gibeoni (2 Sam. 21:1-5).
5. Yeremia alikubali uovu wa babu za Israeli (Yer. 3:25, 14:7 na 20, na 32:18).
6. Danieli aliungama dhambi zake na dhambi za wafalme wa watu wake (Dan. 9:1-20).
7. Nehemia aliziombea dhambi za Israeli (Neh. 1:4-11 na 9:1-4).
Kuombea Uponyaji wa dhambi za urithi kunahitaji hatua tatu:
• Kwanza, ni lazima tutambue dhambi na laana hizo.
• Pili, ni lazima tuombe maombi ya toba ya kujihusisha na kumwomba Mungu awasamehe watu waliotenda dhambi hiyo ya kwanza.
• Tatu, ni lazima tuombe na kumwambia Mungu atuweke huru kutokana na laana hizo za kizazi ili tuweze kuwekwa huru.
Kutambua Dhambi na Maovu ya Kizazi
Kuna njia mbili za kutambua dhambi na maovu ya kizazi yanayoathiri maisha yako ya kutembea na Mungu. Njia moja ni ya kumwambia mtu aliye na kipawa cha utambuzi wa mapepo na aliye na uzoefu katika uwanja huu akuombee. Mara nyingi waombezi hao wana-weza kutambua majina ya dhambi hizo na vizazi vilivyotenda dhambi hizo. Kwa hali yoyote, waombezi walio na vipawa na uzoefu huo ni wachache sana. Hata kama wako, matumizi ya jedwali la ukoo yatawasaidia sana.
Ikiwa watu walio na vipawa hivyo hawako, kutumia jedwali la ukoo na kuzifuata ha-tua zifuatazo kunaweza kukusaidia kutambua dhambi za kizazi za babu zako. Wakati mwin-gine utaweza kupata dokezo kuhusu aina ya dhambi hiyo kupitia kwa ishara za dhambi hizo katika maisha yako (kwa mfano, kukataliwa, tamaa, uzinzi, kukosa kujienzi, kutazama picha za kutia ashki, kukosa kiasi, n.k.) Ili kutambua dhambi za kizazi, fuata hatua hizi.
1. Lifuate jedwali la ukoo lililo mwisho wa sehemu hii, weka majina ya babu zako ma-hali ulipoonyeshwa. Kadiri unavyoweza kuyakumbuka. Ikihitajika pata usaidizi kuto-ka kwa babu zako walio hai.
2. Tumia orodha iliyo hapa chini ili utambue babu ambao walihusika katika mkondo wa tabia hiyo, kama ilivyoonyeshwa. Andika dhambi zao katika jedwali ya ukoo kando ya majina yao. Matatizo mengine yanaonekana wazi lakini mengine yanajulikana kwa Mungu pekee na yanaweza kutambuliwa tu kwa usaidizi wa Roho Mtakatifu. Usijali
61
# 9 Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi www.healingofthespirit.org
kuhusu kitu usichokijua. Yesu atakufunulia unachotakiwa kujua, na akikufunulia kitu ataleta uponyaji katika hali hiyo.
3. Tafuta mkono unaojitokeza katika ukoo wa kizazi hicho. Wakati mwingine laana hiyo humwathiri tu babu mmoja pekee katika kizazi fulani—wakati mwingine huathiri ba-bu wote. Wakati mwingine laana hiyo hukiruka kizazi kimoja au zaidi kisha ikarudi baadaye. Matatizo mengine huwafuata watu kutoka juu hadi chini (kutoka kwa babu hadi kwa baba) ilhali mengine huja kutokea upande mmoja hadi mwingine (kutoka kwa shangazi hadi kwa shangazi au kutoka kwa binamu hadi kwa binamu).
4. Tumia masomo ya sehemu za awali katika somo hili ili uweze kuondoa—kwa kutam-bua, kutubu, na kusamehe—dhambi zote zinazojulikana katika maisha yako.
5. Ikiwezekana, pata usaidizi kutoka kwa mwombezi aliye na uzoefu wa kuombea athari za kizazi. Iwapo mtu huyo hawezi kupatikana, wasilisha orodha hiyo wakati wa Meza ya Bwana.
Orodha ya Uchunguzi #1—Tambua tatizo lolote la kiroho lililotokea kati ya matati-zo yafuatayo:
1. Shughuli za mizungu/ushetani: rejelea orodha inayohusu mada hii katika sehe-mu inayoeleza juu ya “Uponyaji Kutokana na Mizungu/ushetani”
2. Kifo kisicho cha kawaida, cha fujo au cha ghafla: majonzi ya ghafla ambayo hayajatatuliwa, mauaji, jaribio la kujiua, kujinyonga, au mkondo katika ukoo wa mwanamume wa kufa wakiwa na umri mdogo.
3. Vifo visivyo na mazishi: watu waliokufa lakini wakakosa kufanyiwa mazishi vi-zuri au (waliokosa kukabidhiwa) kwa Bwana, waliokufa vitani, waliopotelea ma-jini, mimba zilizotolewa, mimba zilizoharibika, n.k. vilevile waliofia katika taasisi za magonjwa ya akili, nyumba ya kuwauguzia watu, au katika jela; watu ambao hawakufanyiwa mazishi ya Kikristo, pamoja na kufanyiwa ibada ya ukumbusho au maombi, au wale ambao (kwa sababu zozote zile) walizikwa lakini watu hawa-kuomboleza.
4. Dhambi za Ngono:
• Uzinzi
• Ukahaba
• Usenge/ubasha
• Kujamiiana kwa maharimu
• Picha za kutia ashiki
• Upotofu wa kingono, kama vile uhayawani wa kuingilia mnyama
• Ngono ya ovyo ovyo,
• Tamaa ya ngono
• Kutawaliwa na ubaya kingono
• Mazoea yasiyo ya kawaida yanayohusu utumwa, uchungu, n.k..
5. Dhuluma: ya kimapenzi, ya maneno, au ya hisia.
62
# 9 Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi www.healingofthespirit.org
6. Mwenendo wa kutawaliwa na ubaya: mazoezi ya kupita kiasi, kutawaliwa na kazi au ufujaji wa pesa, madawa ya kulevya, chakula, kamari, ngono, pombe, kutawaliwa na nikotini, n.k.
7. Dhambi za kurudiwarudiwa: uwongo, udanganyifu, wizi, masengenyo, kukosoa, n.k.
8. Kutawaliwa na utumwa wa nafsi: mtu aliye kufa ambaye ulikuwa ukimtegemea alipokuwa hai (kwa mfano, mzazi mmoja aliyekuwa wa kutawala na mwingine aliye-kuwa mtiifu)
9. Mikondo miharibifu au isiyo ya kawaida katika uhusiano: talaka, kuachwa, mtu anayevutiwa na watu walio na shida au matatizo.
10. Historia ya kiwewe katika familia: mauaji ya kinyama, baa, utumwa, kutekwa nya-ra, masuala ya asili ya kabila (yanayohusiana na historia ya kabila lao)
11. Historia ya kidini: dini zisizo za Kiyahudi au za Kikristo, hasa dini za Mashariki
12. Uchungu aliopata mtu akiwa tumboni: Uchunguzi umeonyesha kwamba watoto wanaweza kukumbuka mambo yaliyorekodiwa ndani ya akili iliyofichika tangu mimba hiyo ilipotungwa (wengi wanaweza kukumbuka hadi wakati ambao mimba hiyo ilikuwa na miezi minne) Kuna mifano ifuatayo:
• Mtoto aliyetungwa mimba kutokana na tamaa au ubakaji
• Mimba nje ya ndoa
• Mzazi aliyefikiria juu ya kumtoa mtoto wake awe wa kupangwa au kumwacha mtoto wake
• Mama ambaye mimba yake iliharibika au aliyetoa mimba kabla ya mhusika anayetaka uponyaji kutungwa tumboni mwa mama huyo.
• Woga/wasiwasi (mama alikuwa na ugumu wa kubeba mimba hiyo mpaka wakati wa ku-zaliwa mtoto)
13. Tukio la kiwewe na/au kukataliwa utotoni kwa njia zifuatazo:
• Hisia kinzani au kukataliwa na mzazi mmoja
• Kumpoteza mama au baba
• Mama au baba kupatwa na ugonjwa wa kuhatarisha maisha.
• Mtoto kupata ugonjwa wa kuhatarisha maisha
• Baba au mama kuiacha familia
• Mtoto aliyepangwa au aliyetumwa kuishi na jamaa zake wengine
• Woga usio wa kawaida wa mzazi au wa jamaa wengine
14. Kukataliwa na kukosa kujithamini: Njia za kawaida ambazo mizizi ya dhambi za zamani za kizazi inaweza kuonekana ni kwa njia ya kukataliwa, kujikataa mwenyewe, kuogopa kukataliwa, kukosa kujithamini na huzuni—vitu hivyo vyote vina sifa nyingi zinazofanana (pia rejelea sehemu inayoeleza juu ya “Uponyaji Kutokana na Kukataliwa”):
—nafsi ya mtu ya kujitenga —kujitahidi kuwafurahisa wengine
—maumivu makubwa moyoni —kuwa na sura ya kinafiki
—kutamani upendo —kuwa na shaka, kujidunisha
—hisia za kutokuwa na thamani —kujichukia
—hisia za kuachwa —kujilaumu
63
# 9 Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi www.healingofthespirit.org
—kutokuwa na uhusiano wa kudumu —hakubali kupendwa au kupenda
—majeraha na uchungu wa ndani —hajijui
—hawezi kukubali upendo wa wengine
—mwelekeo wa kutaka kukubaliwa na wengine —mwelekeo wa kufanya
kwa kuwa mzuri au kwa kujitahidi sana mapenzi kwa njia ovyo
Orodha ya Uchunguzi #2—Tambua mambo unayofikiria kuwa ni “mikondo ya dham-bi” katika ukoo wa familia yenu (ongeza mengine kila unapoyatambua):
hamaki wivu kuwa na kinyongo ulafi
kutosamehe kulipiza kisasi kuwa na hasira kiburi
kupenda mali ukaidi kuwa baridi katika upendo
Orodha ya Uchunguzi #3—Tambua matatizo ya kiafya yanayojitokeza sana katika fa-milia yenu (jisikie huru kuongeza mengine katika orodha hii):
saratani ugonjwa wa sukari duwaza
kuumwa kichwa matatizo ya moyo maradhi ya kiakili
kusahau vidonda vya tumbo matatizo ya ngozi
kuharibika akili matatizo ya kupumua magonjwa ya kiakili
matatizo ya kisaikolojia shinikizo la damu
Ombi la Uponyaji wa Dhambi na Moavu ya Kizazi
Dhambi na maovu ya kizazi ya Agano la Kale yanaonekana tena katika magonjwa ya wakati huu yasiyo na tiba. Habari Njema ni kwamba, kwa vile Yesu alichukua dhambi na maovu yetu, tu-naweza kuwekwa huru. Ingawaje hiyo ni kweli, bado tunatakiwa kujitwalia nguvu hizi za msala-ba wakati mwingine kwa njia maalum sana ili tuweze kupokea uhuru tunaotaka (Matendo 19:18-19, Waefeso 4:28) Kwa njia ya maombi mhusika anayetaka uponyaji anatakiwa kufanya mambo haya:
1. Kukubali imani yako kwa kile ambacho Kristo alikufanyia msalabani; mshukuru kwa baraka ya neema, msamaha wa dhambi, damu ya Yesu na mafuta ya Roho Mtakatifu.
2. Rudia tena nadhiri zako za ubatizo; mkubali Yesu awe Bwana na Mwokozi wako na umwambie aingie tana moyoni mwako. Ahidi kumfuata na kumtii kama Bwana wa-ko.
3. Tubu dhambu zozote za kuabudu sanamu (unazozijua na usizozijua).
4. Mwambie Mungu akuonyesha mahali ambapo dhambi ya kwanza (chanzo kikuu) ilianzia. Mwambie akuwezeshe “kuliona” tukio hilo na watu waliohusika.
5. Ungama dhambi za babu zako: “Ninakiri dhambi za babu zangu, wazazi wangu na zangu mwenyewe za _________” (tubu kila dhambi ya kizazi).
64
# 9 Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi www.healingofthespirit.org
6. Msamehe mtu wa kwanza kutenda dhambi hiyo (huenda hawakujua athari ya kitendo wa-lichokuwa wakifanya—kama vile Yesu aliwaombea msamaha watu waliomtesa, alipo-kuwa msalabani (Luka 23:34).
7. Kwa niaba ya watu wote wa familia yako, msamehe mtu wa kwanza kutenda dhambi hiyo. “Ninaamua kumsamehe na kumwachilia huru__________ kwa dhambi na athari ya _________ (taja jina la dhambi), ndani ya maisha yangu na ndani ya maisha ya watu wa-liomtangulia.”
8. Mwambie Mungu akusamehe kwa “matunda” yoyote ya sasa au ya zamani ya dhambi hizi katika maisha yako mwenyewe au katika maisha ya watu wa familia yako ya karibu. “Ninakuomba Bwana unisamehe, kwa dhambi hizi—kwa kuziruhusu zinitawale na kwa laana zilizoletwa kwangu na kwa watu wa familia yangu.”
9. Mwombee mtenda dhambi huyo na umwombe Mungu amsamehe (kama alivyofanya Ye-su—na anaendele kutufanyia). Iwapo Bwana ameweka akilini mwako picha ya watu wa-liotenda dhambi hiyo ya kwanza ya urithi, mwambie Yesu aingie ndani ya picha hiyo iliyo akilini mwako. Endelea kuomba mpaka uwaone watu hao wakimwendea Yesu kwa utiifu au mpaka sura yao igeuke kutoka kwa giza hadi kwa nuru au uwaone wakipiga magoti mbele ya Mungu na kuomba msamaha.
10. (Ikiwezekana) omba kwamba watu hao wataweza kumfahamu Bwana Yesu Kristo, wa-kiamua kufanya hivyo.
11. Iwapo kuna watu waliokufa katika familia yenu na hawakufanyiwa mazishi, omboleza kwa ajili yao, na umwombe Mungu awapokee, Kwa upendo wakabidhi kwa Mungu na umwambie awapokee. Waombee watu ambao wamekuwa na majonzi kwa ajili ya watu hao waliokufa ili waweze kufarijika kwa kujua kwamba wafu hao sasa wako na Bwana. Omba ili wao pia waweze kuwaachilia huru watu hao waliokufa.
12. Omba maombi yaliyo katika sehemu inayoeleza juu ya, “Uponyaji Kutokana na Laana” ili uvunje laana zozote zilizokujia. Halafu mbariki mtu aliyesababisha laana hiyo.
13. Katika jina la Yesu, kanusha athari zozote za ushetani/mizungu.
14. Omba kwamba msalaba wa Yesu utawekwa katikati ya dhambi hiyo na watu wa famili yako (wa sasa na wa zamani) na kwamba dhambi hiyo itafunikwa kwa damu ya Yesu.
15. Omba kwamba mhusika anayetaka uponyaji pamoja na watu wote katika ukoo wa familia yake watawekwa huru kutokana na dhambi hiyo na maovu yanayotokana nayo.
16. Omba ili utumiwe kama chombo cha kupitishia upendo na nguvu za Mungu ili watu wote wa ukoo wa familia yako waweze kuwekwa huru kutokana na utumwa, uchungu au dhambi yoyote.
17. Kwa niaba ya watu wote wa familia yako wanaoishi na waliokufa, tuma msamaha kwa watu wa vizazi vilivyopita.
18. Omba msamaha kwa njia yoyote ambayo tulianguka katika majaribu ya dhambi hiyo —kama vile vizazi vya zamani vilianguka katika majaribu.
19. Pitia maelezo juu ya maagano ya damu katika sehemu inayoeleza juu ya “Uponyaji Ku-tokana na Laana.” Mwombe Mungu na umwambie avunje kila viapo, viapo vya damu au laana za uchawi zilizowekwa juu ya maisha ya kila mtu katika vizazi vya ukoo wako.
20. Omba kwamba watoto wote wa watu wa familia yako wanaoishi sasa watawekwa huru pia.
21. Mshukuru Mungu kwa uponyaji huo.
65
# 9 Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi www.healingofthespirit.org
Enda kwa athari ya kizazi inayofuata (mwenendo) ambayo Mungu anataka kuiponya. Utahi-tajika kurudia njia iliyoelezwa hapo juu. Kwa kila athari ya uovu. Huenda ikachukuwa muda mrefu lakini itakuwa ya manufaa sana.
Mwalimu wa Biblia Paul Cox amefaulu kuomba dhidi ya idadi yoyote ya dhambi za kizazi kwa kutumia Isaya 59—inayoeleza juu ya tando za buibui na mayai ya joka (yanayohusiana na udaku na kashfa) ya hukumu ya kukosoa, kijicho, mabishano, kushikilia makosa, lawama na wivu. Paulo na kikundi cha watu wengine wameunda ombi la magonjwa yasiyopona ya kizazi na ya kiroho, kihi-sia na kimwili, la kumweka mtu huru (kutokana na ukoo wa kizazi) la mambo yafuatayo: uwongo, kumkana Mungu, kunena lawama dhidi ya Mungu, kutunga na kunena uwongo moyoni, kunena dhu-luma na uasi. Kwenda katika uchawi, machungu, ghadhabu, hasira, mizozo, na kashfa, pamoja na kila aina ya nia ya kuwadhuru wengine. Anasema ombi hilo ni la manufaa sana.
Nafasi haituruhusu kujadili Isaya 59 au ombi hilo (ambalo lina kurasa kadhaa). Lakini ikiwa ungependa nakala ya ombi hilo wasiliana na mwandishi wa kitabu hiki naye atafurahi kukutumia kwa njia ya barua pepe.
Ombi la Kuzivunja Laana za Kizazi za Mizungu/ushetani
Bwana,
Naja mbele yako leo nikitaka kusafishwa na kuwekwa huru kutokana na laana hizi za kizazi za kua-budu ngono, ndoto na tamaa, na laana zengine zozote za kizazi.
Ninakanusha uhusiano wote na athari ya kitu chochote cha ushetani/mizungu au cha Kishetani sasa na katika urithi wangu. Ninafuta madai yote ya Shetani dhidi yangu kulingana na Kumb. 7:26 na II Kor 6:14-15.
Ninatambua na kutubu kwa ajili ya babu zangu waliovunja Amri zifuatazo.
Kut. 20:3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
Kut. 20:4 Usijifanyie sanamu ya miungu wa uwongo, au kinyago chochote kilicho mbinguni, katika nchi au majini chini ya dunia.
Kut 20:5 Usiisujudie wala kuitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu. Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha hao wani-chukiao;
Kut. 20:13 Usiue.
Kut. 20:14 Usizini.
Ninatambua kwamba kuabudu miungu wa uwongo katika kizazi cha urithi wangu ni kama gugu lili-lopandwa katika maisha yangu, linaloniunganisha na nguvu za kishetani zilizoachiliwa katika vizazi vya hapo awali na watu waliovunja ahadi hizo kimakusudi na wengine pia. Gugu hilo lina mizizi mi-refu inayoenea mpaka kwa vizazi vijavyo na linawakilisha uovu na athari inayoendelea ya babu zan-gu walioabudu miungu wa uwongo. Ni kama uzinzi wa kiroho.
66
# 9 Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi www.healingofthespirit.org
Ninaukata mzizi huu katika jina la Yesu kulingana na Mat 15:13 inayosema, Kila mmea am-bao Baba yangu aliye mbinguni hakupanda, utang’olewa.
Katika jina la Yesu,, ninakuomba sasa uniweke huru kutokana na kila laana iliyo juu ya mai-sha yangu kulingana na Gal 3:13-14 inayosema. “Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kujitwalia laana hiyo kwa ajili yetu; maana Maandiko yanasema: “Yeyote aliye-tundikwa msalabani amelaaniwa.” Jambo hili lilifanyika kusudi ile baraka aliyopewa Abra-hamu iwashukie watu wa mataifa mengine kwa njia ya Kristo, na ili kwa imani, tumpokee yule Roho ambaye Mungu alituahidi.”
Ninatubu kwa ajili ya dhambi ya uasi iliyofanywa na babu zangu kulingana na I Sam 15:23 “ni kama dhambi ya uchawi.” Hili ni dhihirisho la uasi wao dhidi ya Mungu, kutawala kwa hila, kuogofya, na kuamuru Wakristo wengine.
Bwana, kama vile Mwanao Yesu Kristo alitubu kwa niaba yangu alipomwaga damu msala-bani na kufa, ninaomba msamaha na kutubu kwa niaba ya babu zangu wa zamani waliotenda dhambi hizi mbaya. Ninaomba kwamba kupitia kwa damu ya Yesu, athari yao juu ya maisha yangu itafutiliwa mbali. Ninawasamehe kwa yale waliyotenda, na kutumai kwamba siku mo-ja kwa njia fulani wataweza kufahamu na kusadikishwa juu ya dhambi hizi na kukubali toba na msamaha kwao wenyewe.
Ninawabariki wote katika ukoo wa babu zangu waliosababisha laana kuja juu yangu kulinga-na na Luka 6:28 inayoniamuru: “Watakieni baraka wale wanaowalaani, na waombeeni wale wanaowatendea vibaya.”
Ninakiri imani yangu kwa Yesu Kristo na sadaka aliyotoa kwa niaba yangu kulingana na (Ebr. 3:1, Ebr. 11:6, Marko 9:23, Mat. 17:19-21).
(Rudia ombi hili mara tatu.)
Bwana Yesu Kristo, ninakiri kwamba nimetenda dhambi dhidi yako, na ninakuomba unisamehe kwa dhambi zangu zote. Ninaamini kwa moyo wangu wote kwamba wewe ni Mwana wa Mungu. Uliacha kiti chako cha enzi mbinguni ukawa mwanadamu. Uliishi katika ulimwengu huu na ukajaribiwa katika kila hali kama sisi, ilhali huku-tenda dhambi. Halafu, ukaenda msalabani na ukayatoa maisha yako. Damu yako ya thamani ilimwagika ili niweze kukombolewa. Ulifufuka na ukaenda mbinguni. Utaru-di tena katika utukufu wako wote. Ninakupa maisha yangu na ninakuomba uingie ndani ya moyo wangu kikamilifu, ili niweze kuishi na wewe milele. Katika jina la Ye-su. Amina.
67
# 9 Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi www.healingofthespirit.org
Katika jina la Yesu, ninakanusha kila aina ya kuabudu sanamu, vitu vyote vilivyotu-miwa kuwakilisha miungu wa uwongo, na kazi zote za Shetani katika ibada ya kishe-tani.
Ninavunja mikataba yoyote ambayo babu zangu walifanya na Shetani kwa damu na kwa maneno. Ninakanusha na kuvunja wakfu wowote wa watoto katika mstari wa kizazi changu iliyofanywa kwa Shetani, iliyoniathiri mimi na kunizuia kumwabudu na kumtumikia Kristo nipendavyo.
Kwa jina la Baba, la Mwanao Yesu Kristo, na la Roho Mtakatifu, ninavunja kila muhuri wa kiroho unaonifunika, na kuzuia roho waovu na laana zozote kuvunjwa katika maisha yangu. Nimewekwa huru kwa upanga wa Roho Mtakatifu.
Ninakanusha matambiko ya kishetani ya kudhihaki kaida ya Ushirika Mtakatifu, ya kutoa sadaka ya wanyama na ya watu, ukiukaji wa kingono, ubakaji, uasherati, uzinzi, karamu ya uasherati, na kusaliti upendo na uaminifu.
Ninakanusha metendo yote ya dhuluma ya kihisia, kimwili, na kimapenzi yaliyofanyika wakati wa matambiko ya kishetani ya ukoo wa babu zangu, kudhihaki kwa sherehe za Kikristo, sherehe za ku-wafanya watu wazae, zinazotokana na matambiko ya zamani ya kipagani, matambiko yote ya kutoa sadaka na sherehe zinazodhihaki kifo cha Yesu msalabani, ya misa giza au ushirika unaotumia vitu visivyotakatifu kama nembo na vitu visivyo takatifu au miili iliyo uchi hutumiwa katika vituo vya ibada.
Ninakanusha kule kudhihaki mateso na kusulubiwa kwa Yesu, kwa kuwachinja wanyama au wana-damu wasio na hatia, matendo ya matambiko ya mauaji na mateso, ya desturi potofu za kingono, na matambiko ya dhuluma ya kimapenzi kutukuza tamaa na uharamishaji wa mwili wa binadamu na amri ya Yesu ya kuwapenda wengine.
Ninakanusha njia aliyotumia Shetani ya kupotosha akili za waathiriwa ili kumbukumbu yao ya she-rehe na matukio ya dini inawafanya wawe na mawazo ya tamaa ya mwili.” Ninakanusha kila mawa-zo machafu na uwezo wa kubuni picha akilini na ninatamani niwe na mawazo mazuri kichwani mwangu.
Katika jina la Yesu Kristo, ninakanusha na kupinga roho ya Kushikilia, na roho ya Amadeus (ta-maa). Ninakanusha na kukataa roho mwovu wa Succubus iliyoweza kusababisha mawazo machafu, ndoto, au uwezo wa kubuni picha akilini. Ninakanusha kila aina ya picha mbovu zilizonijia kwa kuji-husisha na michezo kama vile “Majoka.”
Shetani, ninachukua nafasi yoyote ya kiroho ambayo huenda ulipewa na babu zangu au nami mwe-nyewe. Huna haki maishani mwangu wala mamlaka juu yangu. Mimi ni wa Mungu na nitamtumikia yeye pekee. Kwa mamlaka ya Bwana wangu Yesu Kristo, ninavunja nguvu ya kila laana iliyonishu-kia. Ninaamuru kila pepo wa laana aondoke maishani mwangu sasa. kila laana za Kizazi, pepo za laa-na ya uchawi, laana iliyorithiwa ya kuabudu uasherati, uwezo wa kubuni picha akilini, na tamaa ni lazima ziondoke sasa katika jina la Yesu Kristo. AMINA
Nguvu za Uponyaji za Ushirika Mtakatifu
68
# 9 Uponyaji Kutokana na Athari za Kizazi www.healingofthespirit.org
Baada ya kufanya maombi ya kuvunja athari za kizazi, jedwali la ukoo lililokamilishwa lina-takiwa kutolewa wakati wa sakaramenti ya Ushirika Mtakatifu ambayo ni mojawapo ya njia muhimu ambazo Bwana hutupa uponyaji.
Kifo cha Yesu kilikuwa kitendo cha nguvu sana katika historia yote. Wakati huo, Shetani ali-shindwa kabisa. Kupitia kwa msalaba, tunajitwalia faida zote za kuteseka, kufa na kufufuka kwa Ye-su—za kuponya majeraha yote ya babu.
Watu wanapopokea nembo wakati wa Ushirika Mtakatifu, nguvu za kiungu za Bwana aliye-fufuka zitakuweko ili ziweze kuponya machungu na dhambi ambayo imeusumbua ukoo wa familia yenu, utumwa ambao umekuwa katika ukoo wa familia hiyo kwa karne nyingi—hatimaye huvunjwa. Dhambi husamehewa na watu wakawekwa huru kutokana na machungu yao, hisia na kumbukumbu. Tunaporudia kusema Sala ya Bwana kama sehemu ya sakaramenti hiyo, sisi husema, “Ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike duniani, kama huko mbinguni … utuokoe na maovu,” na kumwambia Mungu awaweke huru watu walio hai na waliokufa, kutokana na utumwa wa kuwa chini ya mwovu.
Katika Ushirika Mtakatifu, tunaomba kwamba kupitia kwa damu ya Yesu (inayowakilishwa kwa divai ya Ushirika Mtakatifu) Yesu Kristo atatakasa ukoo huo (wa watu walio hai na waliokufa) kutokana na mambo yote yanayoleta kizuizi katika maisha ya kimwili na ya kiroho, hasa kwa kuvunja kila vifungo vya urithi na laana, kwa kufukuza kila aina ya mapepo. (zingatia mapendekezo mengine yaliyo katika sehemu inayoeleza juu ya “Nguvu za Uponyaji za Ushirika Mtakatifu.”)
Mhusika anayetaka uponyaji anashauriwa kusoma vitabu katika orodha iliyo hapa chini, vili-vyoandikwa na McAll na Smith vinavyohusu nguvu za sakaramenti hii katika uponyaji wa athari za kizazi.
Vifaa
1. Kenneth McAll, Healing the Family Tree (Sheldon Press, London, 1982). ISBN 0-85969-532-8. (upigaji chap wa kitabu hiki umekoma.)
2. Kenneth McAll, A Guide to Healing the Family Tree (Queenship Pub., 1996). ISBN 1-882972-64-3.
3. Patricia Smith, From Generation to Generation (Jehova Rapha Press, PO Box 14780, Jack-sonville, FL 33238-1470, 1996). ISBN 1-888871-24-5.
4. John Hampsch, Healing Your Family Tree (Our Sunday Visitor, Huntington, Indiana 46750, Library of Congress, 1989). ISBN 087973437X.
5. Noel and Phyl Gibson, Evicting Demonic Intruders (New Wine Press, 1993): 99-120. ISBN 1-874367-09-4.
6. Noel Gibson, Freedom in Christ (New Wine Press): 233. ISBN 1874367531.
7. http://claretiantapeministry.org/ (kuuponya ukoo wako)

1 comment:

  1. Je! Unatafuta mkopo kuanza biashara, kulipa bili yako, tunatoa mkopo wa $ 3,000 hadi $ 500,000,000.00, tunatoa au aina ya mkopo hapa na 2%. Ninatarajia sasisho lako kuhusu suala hili. Asante kwa muda wako na uelewa! Kwa hiyo kurudi kwetu ikiwa una nia .. Tafadhali wasiliana nasi kwenye barua pepe yetu: Fredjosephloans@gmail.com

    ReplyDelete