Friday 5 December 2014

UONGOZI BORA

Kitabu Cha
Mafunzo
Ya Uongozi
Kwa
Wanawake
Uongozi Bora
UONGOZI BORA
Uongozi ni uwezo wa kubuni na kuyaweka maono katika vitendo.
-Mshiriki katika Semina ya Mafunzo
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake, kitakuwa chombo muhimu
sana katika kuwawezesha na kuwapa wanawake madaraka ya kumudu maisha yao duniani kote.
Pamoja na kuzingatia mawazo mengi tena mazuri kuhusu uongozi kutoka vyanzo tofauti, kitabu
hiki kinayaweka pamoja mawazo hayo na maono mapya kwa namna ya kipekee inayokiwezesha
kusomwa na kueleweka, na kuwafaa wanawake wote. Kwa hakika, mimi binafsi, sijawahi kuona
kitabu kingine cha mafunzo ambacho ni rahisi kukubalika na kurekebishwa ili kufaa mahitaji na
matumizi ya watu mbalimbali (ikiwa ni pamoja na wanaume), huku kikizingatia tofauti za
mahitaji na mazingira yao. Zaidi ya hayo, mtindo wa kushirikisha uliotumika katika masomo ya
kitabu hiki unaonyesha dhahiri aina ya uongozi unaohimizwa na kitabu chenyewe, yaani uongozi
wa kushirikisha.
-Nancy Flowers, mwandishi na mwalimu wa haki za binadamu
Sasa nimeelewa kawa hata wanawake “wanyonge”wanaweza kuwa viongozi,na hii ndio kuwapa
mamlaka.
-Mwalimu wa masomo katika kituo cha kujifunza kusoma na kuandika
aliyeshiriki katika mafunzo ya uongozi, Morocco
Ikiwa hatujihesabu wenyewe kama viongozi na hatuzungumuzwi katika maandiko na katika
vitabu kama viongozi, ni kwa vipi wengine watatutambua kuwa sisi ni viongozi?
-Mtumishi wa kazi za nyumbani aliyeshiriki katika mafunzo ya uongozi, Jordan
Katika mafunzo haya, nimegundua kwamba nina uwezo wa uongozi ambao kabla ya hapo sikujua
kama ninao.
-Kijana wa kike aliyeshiriki katika mafunzo ya uongozi, Palestine
Ikiwa jamii na raia wanaweza kutambua uongozi kwa jinsi hii na kutathmini na kushirikiana
pamoja na wengine katika kuzunguzumzia jinsi gani uongozi unavyoelekea kwenye ushirikishwaji
na kufanya maamuzi, ndipo matatizo yetu yaliyo mengi yaweza kupata suluhisho.
-Mshiriki wa kiume katika mafunzo ya uongozi, Jordan
Nilitambua ya kwamba nilikuwa na maono ndani yangu ambayo ningeweza fanikisha na hivyo
nilipata msukumo wa kuendelea mbele na hatimaye kufaulu.
-Mwanamke mtetezi aliyeshiriki katika mafunzo ya uongozi, Nigeria
Ninaamini ya kwamba Uongozi Bora ni kitabu muhimu sana ambacho kitaleta mwamko katika
uwanja wa kutetea na kuleta haki za binadamu kwa wanawake na kuwapa mamlaka
wanayostahili …Matarajio yetu ni kwamba kitabu hiki kitakuwa msaada mkubwa si katika kizazi
cha wanawake cha leo tu, bali pia katika vizazi vijavyo ambapo wanawake wataweza kujitambua
wenyewe kama viongozi ndani ya jamii na tamaduni zao. Haya ndio ninapendelea kutimiza kwa
akinamama na mabinti wa Afghanistan kupitia mashirikiano katika kazi na mipango pamoja na
WLP nchini Pakistan…Uongozi Bora kama kilivyotungwa na WLP kwa kushirikiana na
mashirika mengine yasiyokuwa ya kiserikali, ni kifaa maridhawa katika mafunzo ya uongozishirikishi
na ushirikiano katika kujenga ufanisi katika utendaji.
-Sakena Yocoobi, mwasisi wa Taasisi ya Elimu, Afghanistan
ii
KITABU CHA MAFUNZO
YA UONGOZI KWA
WANAWAKE
Mahnaz Afkhami
Ann Eisenberg
Haleh Vaziri
wakishauriana na
Suheir Azzouni
Ayesha Imam
Amina Lemrini
Rabéa Naciri
Kimetafsiriwa na kujaribishwa katika lugha ya Kiswahili na Shirika la Wanawake na Maendeleo
liitwalo:
The Women’s Self-Promotion Movement (WSPM)
Kimehakikiwa na Kuhaririwa na:
Charles Bwenge, Ph.D.
Women’s Learning Partnership for
Rights, Development, and Peace (WLP)
4343 Montgomery Avenue, Suite 201
Bethesda, MD 20814, USA
Tel: 1-301-654-2774/Fax:1 -301-654-2775
Email: wlp@learningpartnership.org
Web: www.learningparnership.org
wakishirikiana na
Association Democratique
des Femmes du Maroc (ADFM)
Secteur les Orangers, Rue Mokla, Villa N° 2
Rabat, Morocco
Tel: 212-37-737165/Fax: 212-37-260813
Email: adfm@mtds.com
BAOBAB for Women’s Human Rights
232A Muri Okunola Street, P.O.Box 73630
Victoria Island, Lagos, Nigeria
Tel/Fax: 234-1-262-6267
Email: baobabab@baobab.com.ng
Women’s Affairs Technical Committee (WATC)
Awad Bldg., Radio Street, 2nd Floor
P.O.Box 2197
Ramallah, Palestine via Israel
Tel: 970-2-298-7783
Fax: 970-2-296-4746
Email: watcorg@palnet.com
Web: www.pal-watc.org
Women’s Self-Promotion Movement (WSPM)
P. O. Box W 78 Parktown
Harare, Zimbabwe
Tel: 263-9191-7392
Email: wspm@yahoo.com,
azimba2002@yahoo.com
© 2003
by Women’s Learning Partnership
for Rights, Development, and Peace (WLP)
ISBN 0-9729395-2-0
Design: Xanthus Design
iv
YALIYOMO
Shukrani i
Dibaji: Sisi ni Akina Nani? iii
Utangulizi: Nguzo, Malengo, Shabaha, na Muundo 1
Misingi ya Ujenzi wa Uongozi: Uongozi kama Shule ya Mawasiliano 5
Mawasiliano Ndani ya Semina: Mwongozo wa Usimamizi 17
Vikao vya Semina
Sehemu ya I: Kukuza Unafsi kwa ajili ya Kufikia Uongozi 27
Kikao cha 1: Kiongozi ni Nani? 29
Kikao cha 2: Jinsi Gani Mimi ni Kiongozi katika Maisha Yangu Mwenyewe? 35
Kikao cha 3: Maono Yangu ni Yapi? 43
Sehemu ya II: Kuwasiliana wa Wengine 49
Kikao cha 4: Jinsi Gani Tunaweza Kuwasiliana? 51
Kikao cha 5: Jinsi Gani Tunaweza Kukidhi Haja na Matakwa Tofauti? 57
Kikao cha 6: Jinsi Gani Tunaweza Kukuza Madaraka kwa Kila Mmoja Wetu? 63
Sehemu ya III: Kuanzisha Ushirika wa Kuelimishana 69
Kikao cha 7: Jinsi Gani Tunaweza Kufikia Lengo la Pamoja? 71
Kikao cha 8: Mpango Wetu wa Utekelezaji ni Upi? 77
Kikao cha 9: Jinsi Gani Tunaweza Kukuza Ujuzi na Vipaji Vyetu? 83
Kikao cha 10: Jinsi Gani Tunaweza Kuhamasisha kwa Ajili ya Utekelezaji? 89
Kikao cha 11:Jinsi Gani Tunaweza Kugawanya Majukumu na Matokeo? 95
Kikao cha 12: Jinsi Gani Tunaweza Kuainisha Shirika Lililopata Mafanikio? 101
Fomu ya Tathmini ya Mshiriki na Msimamizi 107
Viambatisho 111
Kiambatisho A: Matukio Mbadala 113
Kiambatisho B: Mbinu za Usimamizi 127
Kiambatisho C: Usikilivu wa Kushiriki 131
Kiambatisho D: Marejeo Yanayohusiana na Uongozi 133
Kiambatisho E: Mashirika Yanayojihusisha na Masuala ya Uongozi 137
Kiambatisho F: Baraza la Kimataifa la Ushauri 141


i
SHUKRANI
Tunatoa shukrani tele kwa mashirika mbalimbali na watu binafsi waliotusaidia
kufanikisha mradi huu. Tunayashukuru mashirika ya National Endowment for
Democracy, Shaler Adams Foundation, na Tides Foundation kwa msaada walioutoa
katika kuunga mkono jitihada zetu za kubuni na kukuza njia na mbinu za kuimarisha
uwezo wa uongozi kwa wanawake.
Tunawashukuru viongozi waliochangia visa na matukio ya kusisimua kwa ajili ya
kitabu hiki, hususan Zainah Anwar, Thais Corral, Ayesha Imam, Ivy Josiah, Asma
Khader, na Sakena Yacoobi. Viongozi hawa walitupatia hadithi na habari zenye mafao
zinazohusu uzoefu wao binafsi. Pia, tunamshukuru Nancy Flowers aliyepitia na
kuchambua muswada wa kitabu hiki kwa kinaganaga na kuchangia maoni mengi ya
uzoefu na ya kitaalamu kabla ya kuchapishwa.
Shirika la Women’s Learning Partnership for Rights, Development, and Peace (WLP),
lilianzisha mradi huu mnamo tarehe 2 Juni, 2000 wakati tulipofanya mkutano wa kundi
la wataalamu ili kujadili pamoja nasi juu ya njia mpya kuhusu uongozi wa wanawake,
mahitaji ya sehemu zao wanamoishi, na vitu gani vipewe umuhimu katika maendeleo
yao. Tungependa kuwashukuru wafadhili wetu waliowezesha kufanyika kwa mkutano
huu ambao ni pamoja na The General Board of Global Ministries of the United
Methodist Church, The Global Fund for Women, San Francisco Foundation, United
Nations Development Fund for Women (UNIFEM), na United Nations Population
Fund (UNFPA). Walioshiriki katika mkutano huu ni: Alia Arasoughly, Shiva Balaghi,
Janice Brodman, Sylvie Cohen, Thais Corral, Naadia Davis, Nancy Flowers, Leanne
Grossman, Ayesha Imam, Bushra Jabre, Mona Kaidbey, Amina Lemrini, Vivian
Manneh, Pramada Menon, Geeta Misra, Thoraya Obaid, Ayo Obe, Aruna Rao, Najat
Rochdi, Susan Deller Ross, Rahim Sabir, na Sakena Yacoobi. Pia wengi kati ya
wataalamu hawa ni wajumbe wa Baraza la Kimataifa la Ushauri (International
Advisory Council) na wataalamu wa shirika letu ulimwenguni pote (angalia
Kiambatisho F). Tunawashukuru sana kwa mchango na msaada wao waliotupatia
katika kila hatua ya mradi huu.
Tunatoa shukrani kwa Rakhee Goyal, Hanan Kholoussy, na Sian MacAdam kwa
mchango wa maoni yao mazuri na, zaidi ya yote, kushiriki kwao katika kusaidia
maandalizi ya muswada wa kitabu katika hatua zake zote. Vile vile tunatoa shukurani
zetu kwa Maureen Donaghy na Megan Brown kwa ustadi na msaada wao katika
kuandaa na kufanikisha mikutano yetu mbalimbali ya kitaalamu na mikutano ya Baraza
la Kimataifa la Ushauri, pamoja na kuratibu mawasiliano kati washiriki na mashirika
yaliyohusika. Pia tunatoa shukrani za dhati kwa ushirika wa Women’s Self-Promotion
Movement kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kutafsiri kitabu hiki katika Kiswahili na
kuufanyia muswada wa tafsiri majaribio ya kufaa kwake, na kwa Dkt. Charles Bwenge
kwa kuhakiki na kufanya uhariri wa mwisho wa muswada wa toleo la Kiswahili.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
ii
iii
DIBAJI:
SISI NI AKINA NANI
Kitabu hiki kilichapishwa kwa ushirikiano kati ya shirika la Women’s Learning
Partnership for Rights, Development, and Peace (WLP) na washirika wake ambao ni
Association Démocratique des Femmes du Maroc (ADFM), nchini Morocco,
BAOBAB for Women’s Human Rights (BAOBAB), nchini Nigeria, pamoja na the
Women’s Affairs Technical Committee (WATC), nchini Palestine.
Changamoto yetu ilikuwa ni kushughulikia mabara matatu ili kutunga kitabu ambacho
kitakuwa na maono yanayokubalika kwa wote juu ya uongozi wa wanawake,
kitakachozingatia mazingira na mitazamo tofauti, na kinachooanisha malengo ya aina
mbalimbali. Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
kinajumuisha na kuzingatia maoni, mawazo, uzoefu, na ujuzi wa watu kadhaa,
wanawake kwa wanaume wakurugenzi na wafanyakazi wa mashirika yasiyokuwa ya
kiserikali, pamoja na wasomi, viongozi wa siasa, wanasheria na washiriki watendaji
katika sekta ya maendeleo kutoka nchi zaidi ya kumi na tano duniani.
Shirika la WLP lilianzisha mradi huu jijini New York mnamo tarehe 2 Juni, 2000.
Katika miezi kadhaa iliyofuatia WLP liliingia katika mikataba rasmi ya ushirikiano na
mashirika ya ADFM, BAOBAB, pamoja na WATC – yote yakiwa ni mashirika
yasiyokuwa ya kiserikali ambayo malengo yake ni kuimarisha madaraka, ushirika, na
uongozi wa wanawa ke katika jamii zao. Kila moja kati ya mashirika yaliyotajwa hapo
juu, liliweza kupitia na kuchambua kinaganaga muswada wa kitabu hiki katika kila
hatua, na kuchangia katika mpango wa kukikamilisha, umbo lake na maudhui, pamoja
na kufanya tathmini yake kwa kuzingatia utoshelevu na manufaa yake kwa watu wa
tamaduni mbalimbali .
Uongozi Bora ni kitabu ambacho kimeundwa kwa namna ya pekee ya kuweza kufaa
kutumika kwa ufanisi katika semina za mafunzo zinazoendeshwa barani Afrika, Asia,
na Mashariki ya Kati. Kwa mfano tayari kimeanza kuzoeleka na kutumiwa katika
semina za mafunzo nchini Morocco, Nigeria, na Palestine. Watu wa aina tofauti
wanashiriki katika mafunzo haya. Baadhi yao ni wafanyakazi na wanachama wa
mashirika yaliyotajwa hapo juu, pamoja na wanafunzi, wanawake wataalamu,
watumishi wa serekali, waalimu, watetezi wa kisiasa, na kadhalika.
Tunayo mipango ya kueneza mafunzo ya uongozi bora kwa wanawake katika nchi zote.
Waratibu wakazi wa mradi wana jukumu la kurekebisha na kuandika kitabu cha
Uongozi Bora kadri ya matakwa na mahitaji ya kila jamii. Miradi hii inaongozwa na
watu wafuatao ambao ni waratibu wa miradi: Amina Lemrini na Rabea Naciri wa
shirika la ADFM, Ayesha Imam wa shirika la BAOBAB, na Suheir Azzouni kutoka
shirika la WATC. Waratibu hawa wanasimamia shughuli zote za majaribio katika jamii
zao, wanafanya tathmini ya kufaa kwa maudhui yake kiutamaduni na wanaibusha
ukuzaji wa taarifa za ziada ambazo ni muhimu na mahususi katika jamii zao. Mwisho,
inatarajiwa kwamba kitabu hiki, Uongozi Bora, kitatafsiriwa na kuchapishwa katika
lugha mbalimbali kufuatana na mahitaji ya wanawake wanaoishi katika nchi tofauti na
hivyo kitakuwa chombo muhimu kitakachotumiwa kubuni, kujenga na kukuza mikakati
ya uongozi bora.
Kwa kuzingatia ujuzi na uzoefu wetu kwa pamoja, shirika la WLP litaweza kusambaza
ushirika wa aina hii katika nchi nyingine za kusini mwa dunia hii.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
iv
Washirika Wetu
Women’s Learning Partnership for Rights, Development and Peace (WLP): WLP ni shirika
la kimataifa lisilokuwa la kiserekali ambalo lengo lake kuu ni kuimarisha uwezo wa wanawake
na wasichana katika nchi za kusini mwa dunia hii kwa njia ya kutafakari juu ya ujenzi mpya wa
madaraka au majukumu yao katika familia na jamii zao, na nchini mwao kwa jumla. WLP
linatimiza shabaha hizi kwa njia ya kushirikiana na mashirika ya wanawake yaliyo katika nchi za
kusini mwa dunia, kwa kuandaa na kukuza mitalaa ya mafunzo ya uongozi na vifaa vya
kufundishia, na pia kuwashirikisha kikamilifu wanawake katika utoaji na utumiaji habari na
maarifa. WLP linatengeneza na kutoa vifaa dhahiri vinavyozingatia tamaduni za kila jamii kwa
ajili ya utangazaji wa habari kwenye radio, video/televisheni, CD-ROM, na katika mawasiliano
ya mtandao wa kompyuta ambavyo huimarisha ushirikiswaji na uongozi wa wanawake katika
ujenzi wa maisha bora ya raia.
Association Démocratique des Femmes du Maroc (ADFM): ADFM ni chama kilichoundwa
mnamo mwaka wa 1985, kikiwa na lengo kuu la kutetea na kuendeleza haki za binadamu za
wanawake, na kuhimiza kuwepo sera na mila zinazozingatia usawa kwa watu wote. Kikiwa ni
mojawapo kati ya mashirika makubwa yasiyokuwa ya kiserekali yanayolenga kutetea haki za
wanawake nchini Morocco, chama cha ADFM kimefanikiwa sana kujenga ushirika na taasisi za
kiserikali na kiraia katika ngazi ya kanda na duniani kote. Shabaha za ADFM ni kuimarisha haki
za wanawake kwa njia ya utetezi, kuamsha ari, utangazaji, kampeni za kujua kusoma na
kuandika, na mkazo katika elimu. Ili kutimiza shabaha zake, ADFM kimeanzisha Chuo cha
Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake, ambacho kinalenga kuongeza ushirikishwaji wa
wanawake katika ngazi zote za maamuzi muhimu yahusuyo jamii.
BAOBAB for Women’s Human Rights (BAOBAB): BAOBAB ni shirika lisilokuwa la
kibiashara na pia lisilokuwa la kiserekali ambalo linajihusisha na utetezi wa haki za binadamu za
wanawake na ufutaji wa sheria zinazowakandamiza wanawake katika misingi ya kidini,
kiserikali, na kimila, hususan zile ambazo zimeelekezwa kwa wanawake Waislamu. BAOBAB
linafanya kazi kwa kushirikiana na wanasheria, viongozi wa serikali, makundi ya haki za
binadamu na haki za wanawake, mashirika mengine yasiokuwa ya kiserikali, pamoja na umma
kwa jumla. Miradi yake inajihusisha na kuendeleza mafunzo ya haki za binadamu, hususan haki
za binadamu za wanawake. BAOBAB linadhamini na kufadhili miradi ya elimu na mafunzo ya
haki za wanawake na ile inayoongeza welewa wa haki za wanawake ambao hatimaye unaweza
kubadilisha sera za kijamii na za serikali.
Women’s Affairs Technical Committee (WATC): WATC ni umoja wa wanawake ambao ni
wanachama au washirika katika vyama vitano vya kisiasa nchini Palestina, vituo sita ambavyo
vinahusika na mafunzo ya wanawake, mashirika ya haki za binadamu ya nchini na ya kimataifa,
na wanawake wengi wataalamu wasiofungamana na vyama maalumu vya siasa. Ukiwa
umeundwa mnamo mwaka wa 1992, umoja wa WATC una shabaha kuu ya kukomesha hali zote
za ubaguzi wa wanawake katika harakati za kujenga jamii imara ya kidemokrasia ambayo
inaheshimu haki za binadamu. Malengo na shabaha za WATC ni pamoja na kukuza ujuzi wa
uongozi kwa vijana wa kike, kuongeza ushirikishwaji wa kisiasa kwa wanawake katika ngazi
zote, na kuviunga mkono, kuvisaidia kwa hali na mali na kuvipa mamlaka vyama vilivyopo vya
haki za wanawake. WATC hutimiza shabaha zake kwa njia ya mafunzo, ushirika, uteteaji,
kampeni, na kuelimisha kupitia vyombo vya habari.
Women’s Self-Promotion Movement (WSPM): WSPM ni ushirika wa wanawake na
maendeleo ulio na msingi wake katika jamii. Ushirika huu uliundwa mnamo mwezi wa Juni,
2001 na akina mama na wasichana wakimbizi pamo ja na raia wenye kipato cha chini nchini
Zimbabwe. Jukumu kubwa la ushirika wa WSPM ni kukuza uongozi, uwezo wa utendaji, na
madaraka ya kiuchumi ya wanawake kwa kuandaa na kuendesha semina za mafunzo ya uongozi
kwa wanawake, programu za kuongeza utambuzi wa haki za kibinadamu za wanawake, na
utetezi. Programu nyingine za WSPM ni pamoja na kampeni na mafunzo juu ya ujenzi wa amani
na usuluhishi wa migogoro, utafiti, uundaji wa ajira, na huduma za mikopo midogo midogo. Sasa
hivi ushirika huu unaendesha kituo cha majaribio cha mafunzo ya kompyuta na mtandao wake
ambayo yamelenga kuimarisha programu ya semina za mafunzo ya uongozi kwa wanawake kwa
kukuza ujuzi wa teknolojia ya kisasa ya habari na mawasiliano ili kuwaongezea wanawake na
wasichana nafasi nzuri ya kupata kazi za kufaa na za kudumu.
v

1
UTANGULIZI:
NGUZO, MALENGO, SHABAHA,
NA MUUNDO
Nguzo
Mawazo na mazoezi ya mafunzo yaliyomo ndani ya kitabu hiki yameegemea katika
nguzo nne. Nguzo ya kwanza ni kwamba katika jamii zilizo nyingi, wanaume
wanafikiriwa kuwa ndio wenye mamlaka na wanawake ni watu wa kutimiza
linalosemwa na wanaume. Fikira hii ni tata kwa sababu dhana kama utawala,
madaraka na uongozi zinaeleweka kwa namna tofauti katika tamaduni na jamii
mbalimbali. Hata katika jamii moja watu wanaweza kuthamini tabia na mienendo
mbalimbali ya binadamu kwa namna tofauti. Kwa mfano, kuamua ugonvi kati ya jirani
wawili kwa kuwatwanga ngumi ya nguvu, kunaweza kuchukuliwa kama kitendo cha
udhaifu kwa mtu anayetwanga ngumi. Lakini katika jamii nyingine au watu wengine,
utumiaji nguvu katika kumaliza ugomvi kunaweza kuchukuliwa kama kitendo cha
uungwana.
Nguzo ya pili ni kwamba sio wanawake pekee, bali ni jamii nzima itanufaika kisiasa,
kiuchumi, na kiutamaduni iwapo kutakuwepo na usawa kati ya wanaume na
wanawake. Utafiti katika nyanja mablimbali kama vile anthropolojia na maendeleo ya
kimataifa umefikia hitimisho moja: kwamba kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya
ushirikishwajia wa akina mama katika maisha ya kijamii na uimarishaji wa maadili,
mitazamo, na mienendo ambayo inaonyesha ushirikiano wa kijamii unaozingatia
misingi ya uhuru, usawa, na uvumilivu. Bila kuwepo uongozi wa wanawake itakuwa ni
vigumu kupata maendeleo thabiti katika nchi zinazoendelea, au katika maeneo yenye
maisha duni ndani ya nchi zilizoendelea. Hata hivyo, ikumbukwe kwamba utaratibu
unaotumika kupima madaraka, kuyagawa au kuyazidisha , na hatimaye kushikiliwa
kwa usawa kati ya wanaume na wanawake utakuwa ni aina ya kipekee katika kila nchi,
jamii, na hata katika familia inayohusika. Kama ambavyo hakuna njia moja pekee
iliyosahihi katika maendeleo ya kiuchumi au ya kisiasa, pia ndivyo ilivyo katika
maendeleo ya wanawake.
Nguzo ya tatu ni kwamba uongozi bora --- uongozi unaotumikia wanawake na
wanaume, maskini na matajiri, na wenye madaraka na wanyonge --- ni ule
unaoshirikisha watu wote. Uongozi huu mpya hujiepusha na fikira potofu ambazo
uwaona baadhi ya watu au baadhi ya tabaka za watu kuwa na haki au mamlaka ya
kuzaliwa ya kufanya maamuzi kwa ajili ya watu wengine. Badala yake, uongozi
unapaswa kujihusisha na kuleta pamoja na kuyafanyia kazi maoni, vipaji na ujuzi wa
watu wengi kadri inavyowezekana na inavyostahili katika sehemu inayohusika. Zaidi
ya hayo, ujuzi katika uongozi hauwezi kutenganishwa na ujuzi katika mahusiano na
watu kwa vile utendaji mwema na ufanisi wa kiongozi unategemea kiwango cha juu
cha ushirikiano alio nao kati yake na washirika, wadhamini, au wafuasi wake.
Ijapokuwa hakuna orodha mahususi ya tabia, mienendo, au ubora inayofafanua sifa za
kiongozi bora katika mazingira yote, kwa jumla kiongozi bora anatarajiwa kuwa na
uwezo wa kufanya maamuzi yaliyo thabiti na mwenye maono, na anayeshirikiana na
wengine kutimiza shabaha za kidemokrasia na uwasa. Kiongozi bora pia hutambua
kuwa njia ambazo anatumia kufikia shabaha hizo, ni muhimu kama zilivyo shabaha
zenyewe.
Nguzo ya nne ni kwamba uongozi wenye kupatanisha na kushirikisha umeundwa
kwenye mawasiliano yaliyo imara. Jinsi wananchi wanavyowasiliana na viongozi
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
2
serikalini, jinsi wazazi wanavyowasiliana na watoto wao, jinsi watumishi
wanavyowasiliana wao kwa wao kazini, na kadhalika --- kila moja ya hali hizi ni
kiwakilishi cha mahusiano ya uongozi katika mazingira mapana. Katika nyakati hizi
ambapo habari ni mojawapo ya bidhaa zenye thamani kubwa duniani na wale watu
wenye uwezo mkubwa wa kuibua na kusambaza habari hizo kuwa na madaraka
makubwa, uongozi wa wanawake unategemea sana uwezo wetu wa kupashana habari,
mawazo, maoni, mitazamo na maono kati yetu sisi kwa sisi na duniani kote.
Mawasiliano thabiti, kama ulivyo uongozi bora, yanahusu jinsi tunavyopashana habari
sisi kwa sisi, tunavyofanya kazi pamoja, na kufanya maamuzi kwa manufaa yetu sote.
Zaidi ya hayo, kadri umuhimu wa teknolojia unavyozidi kuongezeka katika uwanja wa
mawasiliano duniani kote, uwezo wa wanawake kuitumia, kuimudu kwa ufanisi, na
kuimiliki teknolojia hiyo ya mawasiliano kutaleta manufaa makubwa sana katika
kuufanya uongozi wa wanawake kuwa jambo halisi.
Malengo
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake kimekusudiwa
kutumika kama kifaa cha kujifunzia na utangulizi wa mafunzo ya uongozi. Tofauti na
vitabu vingine vya mafunzo ya uongozi ambavyo huweka msisitizo katika masuala ya
“jinsi gani” ya kugombea nafasi ya uongozi wa kisiasa au kuendesha kampuni, kitabu
hiki kinazungumzia maswala ya kuwezesha na kuwapa madaraka wanawake na mbinu
za mawasiliano. Kimelenga kumwezesha msomaji au mshiriki katika semina ya
mafunzo kubaini yeye mwenyewe na kujenga mbinu bora za kuwasilisha maoni yake,
kusikiliza yanayosemwa na wengine, kuafikiana na wengine, kujenga lengo la pamoja,
na kuendeleza ushirika wa kujifunza katika sehemu za kazi, majumbani, na katika jamii
yake.
Shabaha
Shabaha yetu katika kutunga kitabu hiki ni kuunda kifaa muhimu, ambacho kinaweza
kutumiwa na jamii yoyote ile, kuimarisha ushirikishwaji na uongozi wa wanawake
katika sehemu na ngazi mbalimbali zinazohusu shughuli na maamuzi muhimu ya
kijamii. Lengo letu kuu ni kutoa mchango katika uwekaji wa mazingira mazuri kwa
ajili utendewaji haki na usawa kwa watu wote, wanawake na wanaume, duniani kote.
Uongozi wa wanawake, kama ulivyo ushirikishwaji wa wanawake au madaraka ya
wanawake, haimaanishi kuwa ni ishara ya wanaume kupoteza uongozi, ushirikishwaji,
au madaraka. Uongozi halali huelekea kule ambapo kila mtu anapopewa uhuru wa
kutosha kuchagua na kuamua linalofaa.
Muundo
Sura inayofuatia katika kitabu hiki--- “Misingi ya Ujenzi wa Uongozi: Uongozi kama
Shule ya Mawasiliano”--- inachora ramani ya jumla ya muundo wa katibu hiki, na
kimsingi imekusudiwa kutumiwa zaidi na wasimamizi. Sura hii inajaribu kuweka wazi
misingi ya aina hii mpya ya uongozi ambao unalenga kushirikisha, kujumuisha watu
wote, kuzingatia demokrasia na, muhimu kuliko yote, kuwawezesha wanawake kupata
madaraka na kutimiza majukumu yao kwa ufanisi. Sura inayofuatia---“Kuwasiliana
Ndani ya Semina: Mwongozo wa Usimamizi” --- haitoi mwongozo wa kuendesha
mafunzo ya uongozi kama yanavyoelezwa katika kitabu hiki tu, bali pia inaweza
kutumika kwa jumla kama rejeo muhimu katika kusimamia na kuendesha aina yo yote
ya mkutano. Vikao kumi na viwili vilivyomo katika kitabu hiki vinajihusisha na mada
za ukuzaji wa uongozi kuanzia kwenye mikakati hadi
Utangulizi: Nguzo, Malengo, Shabaha, na Muundo
3
uimarishaji wa vipaji vya uongozi vya mtu binafsi, na hadi masomo juu ya kuanzisha
na kuimarisha taasisi kwa kutumia mifano ya kukuza uongozi jumuishi.
Kama ambavyo hakuna aina moja tu ya ubora au tabia za kufafanua kwa usahihi sifa za
kiongozi bora, vile vile hakuna mbinu moja tu ya kufundisha ujuzi wa uongozi. Katika
kitabu hiki, pamoja na kusisitiza mambo yahusuyo uongozi, mbinu za kufundisha na
kujifunza ambazo ndio msingi wa kitabu hiki, ndio hizo hizo zimewekwa kwa
makusudi ya kuwawezesha na kuwapa madaraka wasimamizi na washiriki wa semina
za mafunzo. Masomo yaliyowasilishwa ndani ya kitabu hiki ni miongozo tu inayoweza
kutumika kwa namna tofauti kulingana na mazingira na mahitaji ya jamii husika. Kwa
mfano, wasifu wa watu mashuhuri na hadithi za mashirika yaliyofanikiwa katika
utendaji wa kazi zao ni mifano tu iliyokusudiwa kuchochea majadiliano na inaweza
kubadilishwa na wasifu na hadithi ambazo zinaeleweka vizuri zaidi katika mazingira ya
kila jamii husika.
Masomo katika kitabu hiki yamegawanywa katika sehemu tatu. Sehemu ya Kwanza,
“Kukuza Nafsi kwa ajili ya kufikia Uongozi”, Kikao cha kwanza kinachunguza tafsiri
mbalimbali za uongozi pamoja na kaida za uongozi zilizozoeleka na mpya. Kikao cha
Pili kinamsaidia msomaji na mshiriki katika semina ya mafunzo kugundua uwezo wake
binafsi wa uongozi. Kikao cha Tatu kinalenga kuonyesha jinsi gani viongozi huanza
na maono ya kipekee, wazo au msukumo wa aina fulani ambao hatimaye hujipa
changamoto wenyewe na kuviweka vitu hivyo katika matendo.
Sehemu ya Pili inazungumzia juu ya “Kuwasiliana na Wengine.” Katika sehemu hii
Kikao cha Nne kinaangalia mbinu za kibinafsi ambazo huleta maarifa ya mawasiliano
kati ya viongozi na washiriki wa Mafunzo. Kikao cha Tano kinaeleza juu ya
umuhimu wa kuwa na maafikiano, maelewano, mashauriano, na mtu kuheshimu
washirika wenzake hata kama mitazamo na maoni yao yanatofautiana ili kuiwezesha
mikutano ya washirika kuzitimiza shabaha zetu, na Kikao cha Sita kinachunguza
mbinu na ambazo zinazoweza kutumiwa kwa kuimarisha madaraka ya utendaji wa
wengine ili juhudi zetu ziwe nzito, kubwa na zenye kudumu daima.
Sehemu ya Tatu inahusu “Kuanzisha Ushirika wa Kuelimishana”. Katika sehemi hii,
Kikao cha saba kinazungumzia jinsi gani wafanyakazi wa shirika fulani pamoja na
wanaushirika wanaweza kuafikiana na kujenga maono yenye mwelekeo mmoja. Kikao
cha Nane kinachunguza njia ambazo zinaweza kutumiwa kwa kuendeleza mipango
madhubuti ya utendaji katika shirika. Kikao cha Tisa kinajihusisha na kutazama njia
ambazo zinaweza kutumiwa kulinda na kuimarisha nguvu za watu pamoja na taratibu
ambazo zinaweza kutumiwa kukuza ujuzi na vipaji vyetu.
Kikao cha Kumi kinazungumzia maarifa na mbinu ambazo zinaweza kutumiwa na
mashirika kuhamasisha wanaushirika kwa ajili ya utekelezaji wa mipango ili kufikia
malengo yao. Kikao cha Kumi na Moja kinazingatia mbinu za kujenga ushirikiano
madhubuti kati ya mashirika katika kuratibu kampeni za kutetea haki za wanawake, na
Kikao cha Kumi na Mbili kinachunguza vigezo tofauti vinavyoweza kutumika
kubaini shirika la mafunzo lililopata mafanikio.
Ili kuwezesha muundo maalumu wa semina za mafunzo kwa ajili ya kikidhi haja za kila
sehemu, viambatisho katika kitabu hiki vinatoa vikao mbadala vilivyozingatia
mazingira maalumu ya kiutamaduni, maoni kwa ajili ya vikao mbadala na mbinu za
kuunda mazoezi, na mikakati ya kuimarisha mawasiliano miongoni mwa washiriki wa
semina za mafunzo. Vikao mbadala viko katika Kiambatisho A vikiwa pamoja na
maelezo yanayopendekeza jinsi gani vikao mbalimbali vinavyoweza kubadilishwa ili
kukidhi mahitaji ya kila sehemu. Kiambatisho B ni orodha ya mbinu zinazotumiwa na
wasimamizi wenye ujuzi kwa ajili ya kuibusha mvuto na majadiliano baina ya
washiriki. Wasimamizi wa semina za mafunzo wanahimizwa kuwa tayari kubadilibadili
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
4
mbinu hizi kufuatana na mazingira wanamosimamia mafunzo, kutumia mbinu na
mikakati ambayo wanaona inaweza kuleta mafanikio katika semina zao na kuachana na
ile ambayo haifai au isiyokuwa muafaka kwa mazingira wanamofanyia kazi.
Kiambatisho C, kikiwa kinajihusisha na usikilivu wa kushiriki, kinatoa mapendekezo
juu ya usikilizaji wenye mafao na mazungumzo yenye maana. Kiambatisho D kinatoa
marejeo yanayohusiana na uongozi na Kiambatisho E kimeorodhesha mashirika
yasiyokuwa ya kiserekali ulimwenguni ambayo yanajihusisha na kuendeleza uongozi
wa wanawake. Kiambatisho F kinayo orodha ya wajumbe wa Baraza la Kimataifa la
Ushauri (International Advisory Council), jumuia ya wataalamu wanaowakilisha
mitazamo mbalimbali ya kitaaluma, kiutamaduni, na kidini ambayo hufuatilia na
kuweka sawa taarifa za kisheria, kisiasa, na kiutamaduni zilizotolewa katika mtalaa wa
uongozi wa WLP.
5
MISINGI YA UJENZI WA UONGOZI:
UONGOZI KAMA SHULE YA MAWASILIANO
Mahnaz Afkhami
Kitabu hiki kinahusu wanawake na uongozi katika enzi hizi za mapinduzi ya
usambazaji wa habari . Tunalenga wanawake kwa sababu (a) ndio wanaofanya sehemu
kubwa ya watu wote ulimwenguni , (b) kwa kiasi kikubwa wamekuwa hawashirikishwi
katika maamuzi ambayo yameathiri maisha yetu katika siku zilizopita, na (c)
wanastahili kupata nafasi kubwa na kufanya mambo mengi kwa ajili ya maendeleo kwa
wakati ujao iwapo tunataka kutengeneza dunia hii kuwa mahali pema kwa ajli yetu
sisi wenyewe na kwa ajili ya watoto wetu. Tunalenga uongozi kwa sababu, kama
viongozi ,wanawake wanaweza kuleta mageuzi na kuelekeza dunia ya kesho kwenye
maisha bora tunayohitaji, kama vile uhuru, usawa, haki, baraka, wingi wa mali, pamoja
na amani kwa wote. Tunalenga teknolojia ya usambazaji habari kwa sababu ndio kani
inayotawala, inayounda miundo na pia kuweka dira ya maendeleo ya kichumi, haki za
watu na uhuru wa kila mtu katika karne hii ya ishirini na moja.
Wanawake, Habari, na Uimarishaji wa Madaraka
Nafasi ya Wanawake Kupata Madaraka ni Ndogo
Kwa muda wa miongo kadhaa iliyopita, wanawake wametokea kuwa wenye juhudi
nyingi katika masuala ya jamii zao. Lakini hadi sasa bado wangali mbali sana na mahali
ambapo wangestahili kuwa iwe ni katika sekta ya binafsi au ya umma. Asilimia ya
wanawake wanaoshikilia nafasi za umeneja na usimamizi katika nchi zilizoendelea ni
karibu 33, barani Afrika ni asilimia 15, na katika bara la Asia na visiwa vya Pacific
ni asilimia 131. Kiwango hiki katika Afrika na Asia- kidogo kama kilivyokinaonyesha
ongezeko maradufu katika kipindi cha miaka Ishirini iliyopita. Kiwango
cha wanawake wanaoshiriki katika maamuzi ya kiuchumi ya ngazi za juu kimeendelea
kuwa kidogo mno, hata katika nchi za Magharibi.
Kati ya kampuni 1000 zilizo maarufu sana nchini Marekani katika mwaka wa 2000, ni
kampuni tatu tu zilizokuwa na wakurugenzi watendaji wanawake 2. Karibuni sehemu
zote za ulimwengu, kazi zimetengwa kwa msingi wa maumbile ya kijinsia. Mara nyingi
wanawake wamejikuta wanaishia kufanya kazi za ukarani, ukatibu muhtasi, uuzaji
dukani, na utumishi wa nyumbani wakati wanaume wakiwa katika kazi za viwandani
na usafirishaji. Kwa wastani duniani kote wanawake hufanya kazi kwa saa nyingi kwa
wiki kuliko wanaume, lakini kazi zao huwa hazilipwi wala kuhesabiwa kuwa za
maana. Hata pale ambapo wanawake wanafanya kazi sawa na kazi za wanaume,
wanawake hulipwa kwa asilimia 30 hadi 40 pungufu ya malipo wanayolipwa wanaume.
Katika Umoja wa Mataifa, wanawake wameshikilia asilimia 9 tu ya vyeo vya ngazi za
juu, na asilimia 21 ya vyeo vya ngazi za uandamizi, lakini wanashikilia asilimia 48 ya
vyeo vya kitaalamu ngazi ya chini katika utumishi wa serikali3. Hadi sasa serekali
zilizo nyingi hazijali wala hazionyeshi nia ya kutaka kukidhi mahitaji ya kazi za
kitaalamu na uongozi kwa wanawake.
1 United Nations, The World’s Women 2000: Trends and Statistics, New York:United Nations. Uk. 130.
2 Kutoka “A Start-Up of Her Own,”Marci Mc Donald, U.S News & World Report, Mei 15,2000.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
6
Utofauti huu wa kijinsia sio matokeo ya kipengee kimoja tu cha utaratibu wa kihistoria
kama vile tabia za kijamii, dini, mahusiano ya kiuchumi au sheria; bali ni matokeo ya
mchanganyiko wa sababu zilizo tofauti. Wanawake wengi wanatambua utata wa
mfumo wa kijamii ambao bila sababu za msingi huwanyanyasa na huwanyima nafasi ya
kukuza na kutumia vipaji vyao. Kwa mtazamo huo huo, wanawake wanatambua kuwa
wao pia ni sehemu ya mfumo huo huo. Sasa wanawake wengi wanatambua kuwa tatizo
lao kubwa sio kushindana na wanaume tu, bali pia ni jinsi gani ya kujenga fikira mpya
na kusaidia kujenga upya mfumo wa kijamii ambao umewafunga watu wote, wanawake
kwa wanaume. Katika karne hii ya ishirini na moja, wanawake watahitajika kubeba
mzigo wa kutafisiri kwa usahihi jinsi gani maisha mema ya kibinaadamu
yanavyostahili kuwa, na kupiga hatua mbele zaidi ya kuweka tafsiri hiyo katika
vitendo, yaani kushiriki kikamilifu kwa vitendo katika dunia hii ambayo inazidi
kuungana na hivyo kuwa tata zaidi. Tunajua kwamba katika baadhi ya jamii— kama
vile Scandinavia— ambako kundi kubwa la wanawake wamejiingiza katika uwanja
wa siasa4, uhusiano wa kijinsia na, kama matokeo ya hili, uhusiano wa kijamii kwa
jumla, umekuwa wa kuzingatia haki na usawa. Kwa hiyo, ili wanawake waweze
kutimiza wajibu wao ipasavyo popote pale walipo, hawana budi wajitahidi kushiriki
kadri wanavyoweza katika masuala ya jamii zao. Ni lazima uwezo na madaraka yao ya
utendaji yaimarishwe.
Makubaliano Rasmi ya Kimataifa Yapo kwa ajili ya Mahitaji ya
Kuimarisha Madaraka ya Wanawake
Tumeanzisha Muungano uliokubaliwa na Mataifa kwa ajili ya kuimarisha madaraka ya
utendaji wa wanawake. Makubaliano haya, yaliyofikiwa wakati wa Mkutano wa Nne
wa Umoja wa Mataifa juu ya Wanawake mjini Beijing, mnamo mwaka wa 1995,
yamefafanuliwa zaidi katika waraka wa Beijing Platform for Action. Waraka huu
unasema kwamba:
Tamko la Utendaji la Beijing ni ajenda ya kuimarisha uwezo na madaraka ya
utendaji wa Wanawake. Linalenga kuondoa vizuizi vyote vinavyozuia
wanawake kushiriki kimatendo katika nyanja na ngazi zote za maisha ya
kifa milia na ya umma, kwa kushiriki kikamilifu katika maamuzi ya kiuchumi,
kijamii, kiutamduni, na kisiasa. Hii inamaanisha kwamba kanuni za ugawaji
sawa wa madaraka na majukumu zinastahili ziwekwe kati ya wanawake na
wanaume majumbani mwao, sehemu za kazi, na hata katika ngazi pana za
kitaifa na kimataifa. Usawa kati ya wanawake na wanaume ni suala la haki za
binadamu na sharti la kuwepo haki za kijamii. Na pia ni jambo la lazima na la
msingi katika kuleta usawa, maendeleo na amani. Ushirika uliobadilishwa na
kujengwa upya kwa kuzingatia usawa kati ya wanawake na wanaume ni
sharti muhimu kwa kuleta maendeleo ya kudumu yanayolenga kuboresha
maisha ya watu wote. Bidii imara na ya muda mrefu ni muhimu, ili wanawake
na wanaume waweze kufanya kazi kwa manufaa yao wenyewe, kwa manufaa
3United Nations, The World’s Women 2000: Trends and Statistics , New York: United Nations, uk. 167.
4 Mwaka wa 1995 baraza la mawaziri wa Sweden lilikuwa la kwanza kuwa na idadi sawa ya mawaziri
wanawake na wanaume. Kuanzia wakati huo, sera zilizobadilishwa katika ustawi wa jamii, mazingira, na
matumizi ya jeshi, kwa mfano, ni ishara ya mageuzi mapya katika nguvu ya kisiasa.
Misingi ya Ujenzi wa Uongozi: Uongozi kama shule ya Mawasiliano
7
ya watoto wao, na kwa manufaa ya jamii yao ili kuweza kukabili changamoto
za karne hii ya ishirini na moja.... Tamko la Platform for Action linasisitiza
kwamba wanawake wabadilishane maoni juu ya masuala ambayo yanaweza
kutatuliwa tu iwapo yatafanyiwa kazi kwa kushirikiana na wanaume kulekea
lengo la pamoja la kujenga usawa wa kinjisia duniani kote. Tamko
linaheshimu na kuthamani utofauti uliopo katika hali na mazingira ya
wanawake, na pia kutambua kwamba baadhi ya wanawake wanakabiliwa na
vizuizi vya kipekee katika uimarishaji wa uwezo na madaraka yao ya
utendaji.5
Teknolojia ya Habari Inatawala Mfumo Mpya wa Mahusiano ya
Kiuchumi Duniani
Mapinduzi ya mawasiliano yanabadilisha hali ya madaraka. Habari na maarifa
vimekuwa nguzo za matumizi ya uwezo wa kisasa, vikiwa vinadhibiti njia na
uhusiano wa uzalishaji mali. Mawasiliano ya kisasa---yakiwa yanamudu wakati---
yamepunguza kwa kiasi kikubwa umbali ambapo kila mtu anajiona kuwa jirani wa
mwingine. Teknolojia ya habari imefanya mawasiliano duniani kuwa mepesi kama vile
mtu anavyopiga gumzo na jirani zake kijijini au mtaani, jambo ambalo limezilazimisha
serekali na makampuni kujielekeza yenyewe kutimiza mahitaji ya ushindani wa
kimataifa. Serikali nyingi zimeanza kushurutishwa na matakwa yanayokinzana kati ya
ushindani wa kimataifa na haki za wananchi. Hiki kielelezo-dunia kipya, ambacho kwa
jumla kinaitwa utandawazi (globalization), kinapendekeza sura mpya ya uhusiano na
madaraka. Hakuna awezaye kusema kwa uhakika iwapo hali hii mpya italeta matokeo
mazuri au mabaya kwa binadamu. Hata hivyo, tuna uhakika kwamba tusipoitumia
teknolojia hii mpya ipaswavyo, tutayafikia maisha yaliyo mbele yetu, yaliyojaa neema
tele, tukiwa gizani bila kujua kinachoendelea na hivyo bila udhibiti wetu. Kutokana na
teknolojia za kisasa za habari kubeba chachu za kuibua uwezo na madaraka, karne ya
ishirini na moja inatoa nafasi mpya kwa wanawake lakini pale tu ambapo wanawake
watakuwa wamejiandaa kikamilifu kuzitumia nafasi hizi.
Teknolojia ya Habari ni Tata na Yenye Hatari
Teknolojia ambayo inatawala uchumi wa kisasa duniani ni yenye kujiendesha , yenye
sura nyingi, na tata. Haina mipaka. Inachukua hali na uwezo mpya kadri inavyokua,
na kuleta mambo mapya ambayo yanadai kufanyika kwa marekebisho sambamba kwa
upande wa watu binafsi, jamii, na mataifa. Watu, jamii, au mataifa ambayo yana uzoefu
zaidi wa teknolojia hii na mienendo ya mabadiliko yatakuwa kwenye nafasi nzuri ya
kuvuna matunda yake. Itakuwa vigumu kuingia katika ushindani kwa wale wasiokuwa
na uzoefu na teknoljia hii ya habari na hawafanyi jitihada za kushiriki katika matumizi
yake, utengenezaji wake, au uenezaji wake. Teknolojia hii mpya , ambayo haijali
mateso ya watu, haizingatii mahitaji ya watu ila tu mpaka sisi wenyewe tunaitumia
kikamilifu na kuielekeza itufanyie hivyo. Kwa vile teknolojia hii ya habari huleta
madaraka, haiendani kabisa na udhaifu wa binadamu. Hatutashinda matokeo yake
mabaya kwa kulalamika au kuomboleza. Linalohitajika kwetu ni kugundua njia na
mbinu za kupata uhodari na ujuzi wa kutosha wa kutuwezesha kuitumia teknolojia hii
kwa manufaa yetu. Kimsingi hili ni tatizo la elimu. Hata hivyo, ili kulishughulikia kwa
5 “Ripoti ya Mkutano wa Nne wa Umoja wa Mataifa juu ya Wanawake,” Convenant for the New Millenium:
The Beijing Declaration & Platform for Actionn (Beijing, September 4-15, 1995), Santa Rosa, California:
Free Hand Books, 1996, pp. 7-8.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
8
ufanisi tunahitaji kulikabili kisiasa, yaani kwa kutoa aina ya uongozi ambao unatoa
nafasi ya kushirikisha wanajamii wote katika masuala yanayowahusu na kufikia
maamuzi ya pamoja.
Teknolojia ya Habari Inatoa Mwanya wa Maisha Mazuri ya Baadaye
kwa Wote
Teknolojia ya habari inaweza kutusaidia kupata maarifa, uongozi, na maafikiano
tunayohitajika katika jitihada zetu za kufikia hali ya maisha ambayo tunahitaji.
Teknolojia hii ya kisasa ya habari inaweza kuenezwa katika sehemu zote duniani kwa
gharama ndogo na kusaidia sera za taifa na za kimataifa ambazo zimelenga kuwasaidia
watu na jamii maskini kushiriki kikamilifu katika maamuzi yanayohusu maisha yao.
Karne ya ishirini ilifungua milango kwa maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia.
Matokeo yake ni kwamba ,karne ya ishirini na moja inatarajiwa kuleta maendeleo ya
aina yake katika kuendeleza maisha ya binadamu. Mandeleo ya kisayansi yametupa
uwezo wa kutokomeza magonjwa mengi ya hatari kwa maisha ya binadamu, kuongeza
muda za kuishi, kubadili hali ya utendaji kazini, na kuleta hali ya maisha inayostahili
kwa kila mmoja wetu. Tunawe za sasa kuunda, kukusanya na kutangaza habari na
maarifa ulimwenguni pote kwa haraka sana, na kwa gharama ndogo sana. Tunaweza
sasa kukabiliana na kutatua na matatizo ya kimsingi yalioyokuwa kikwazo katika
juhudi za maendeleo mengi huko nyuma kutokana na kutokuwepo njia za haraka za
mawasiliano na kubadilisha habari.
Haja ya Kupunguza Pengo Katika Umilikaji wa Teknolojia ya Habari
Tumekabiliwa na tatizo la tofauti kubwa ya umilikaji na utumiaji wa teknolojia ya
habari. Tatizo hili linatokana na kutokuwepo nafasi sawa ya kupata na kutumia habari
na maarifa na uwezo usiolingana wa kutumia habari na maarifa hayo kwa ajili ya
maendeleao, na pia kwa ajili ya usawa na uhuru wa kijinsia. Kwa mfano, nchini
Marekani kuna kompyuta nyingi zaidi kuliko idadi ya kompyuta zilizo katika nchi
nyingine duniani zikiwekwa zote pamoja 6. Mahali pote duniani, na zaidi katika nchi
zinazoendelea, nafasi ya wanawake kupata na kutumia teknolojia ya kisasa ni ndogo
kuliko ilivyo kwa wanaume.
Ipo haja ya kuziwezesha nchi maskini kuwa na uwezo wa kumiliki na kutumia
teknolojia hii ya kisasa, na zaidi ya hapo, kuyawezesha makundi ya watu maskini
katika kila nchi hizo kumiliki na kutumia teknolojia hii. Kati ya makundi hayo,
wanawake na wasichana hawana budi kupewa kipaumbele. Tunahitaji kueneza utajiri
huu wa matumizi ya mtandao wa kompyuta katika kila pembe ya dunia hii. Na hii sio tu
mashini za kompyuta zenyewe na mafunzo ya utumiaji, bali pia ubunifu wa nyenzo
muafaka kufuatana na utamaduni, lugha, na jamii husika. Wanyonge na watu
walioachwa nyuma kimaendeleo duniani wasiwezeshwe tu kuwa watumiaji wa habari
zilizoandaliwa mahali pengine, bali pia wawezeshwe kuwa wabunifu wa maarifa
ambayo wao na watu wengine wanaweza kuyatumia. Sote tutakuwa matajiri iwapo
tutazingatia na kuheshimu uzoefu, ujuzi na hekima za binadamu wote duniani kote.
Iwapo tutazingatia changamoto ya kueleza maoni yetu na kusikiliza ya wengine na
kujumuisha yote kwa pamoja, tutakuwa tumetengeneza ulimwengu ambapo kila
binadamu atatambua na kufurahia utu na nafasi yake, baraka, haki, na usawa.
6 United Nations Development Programme (UNDP), Human Development Report 1999, New York: Oxford,
1999, p. 62.
Misingi ya Ujenzi wa Uongozi: Uongozi kama shule ya Mawasiliano
9
Tusipofanikiwa katika changamoto hiyo, tutajikuta tunaishi katika ulimwengu
tusioweza kujivunia.
Uongozi na Jumuia Zilizo Mafunzoni
Wengi miongoni mwetu huishi katika jamii zenye mfumo wa tabaka za madaraka na
taratibu za utawala msonge. Mahali pa utawala huo panaweza kuwa nyumbani, jamii,
uwanja wa siasa, au katika uchumi. Muundo wa tabaka za madaraka hulea na kulelewa
na utamaduni wa utiifu ambao hauchelei kudumisha na kusitiri mpangilio wa madaraja
ya watu kwa kutoa utaratibu wa watu wenye mamlaka. Jukumu la mamlaka hayo ni
kuhalalisha mahusiano ya maagizo kwa kuweka ridhaa. Katika ukosefu wa mamlaka,
yaweza kutokea kila mhusika katika mahusiano ya maagizo kuwa mdhalimu au bwege.
Hii sio aina ya uhusiano wenye mafao ambao tunajaribu kuujenga. Badala yake,
tumelenga katika kujenga aina ya jamii ambamo wanawake na wanaume
wanashirikiana kikamilifu kama viumbe wanaowasiliana na kusikilizana badala ya
mmoja kuwa mtoa amri na mwingine kuwa mtekelezaji amri. Tunaangalia uongozi
katika jumuia zilizo mafunzoni kama njia ya kulea binadamu wenye utu ambao
hushirikiana na kusikilizana kwa ajili ya jamii na maisha yao. Ili tuweze kuelekea
katika ujenzi wa jumuia zilizo mafunzoni, hatuna budi tuanzie hapa tulipo.
Wengi miongoni mwetu, dhana ya “uongozi” huibusha nguvu, ushupavu, na uwezo
unaotumika kufikia lengo lenye mafao. Mtu huhesabiwa kuwa kiongozi, ikiwa
anaweza kuelewesha wengine ili nao waweze kutimiza lile analokusudia kufanya.
Katika tafsiri hii ya dhana, wale watu walio katika mamlaka tayari wamo katika nafasi
nzuri ya kuongoza. Hata hivyo, mambo hayawi hivi mara zote. Tunaelewa sana
kutokana na uzoefu wetu kwamba watu walio katika nafasi za mamlaka ---kwa mfano,
baba, wakuu wa kazi, wamiliki wa ardhi na nyumba, na wataalamu --- sio viongozi.
Kwa upande mwingine, wengi wetu tumekutana na watu ambao hawamo katika nafasi
mahsusi za mamlaka lakini tukahisi ni viongozi kwa jinsi wanavyoathiri watu na vitu
vilivyowazunguka. Je, kama hali ndio hiyo, uongozi ni sifa nafsia za mtu? Je, ni tabia
ambayo baadhi huwa nayo na wengine hawana?
Uongozi sio Nini
Njia mojawapo ya kuanza mjandala juu ya uongozi ni kuweka wazi kile ambacho sio
sehemu ya uongozi. Wengi wetu tutakubaliana kwamba uongozi sio uwezo wa kutumia
nguvu au ushurutishaji. Inawezekana kabisa kulazimisha watu wafanye lile ambalo sisi
tunataka kwa kuwatishia kuwaadhibu. Baba anamtishia kumwadhibu mtoto wake kwa
sababu mtoto huyo ameshindwa kazi ya darasani au ameshindwa kufanya kazi fulani
ndani ya nyumba. Mkuu wa kazi ofisini anatishia kumnyima mfanyakazi bonasi yake
mpaka pale mfanyakazi huyo atakapoongeza ufanisi katika utendaji. Tunaweza
kufikiria kwamba vitendo hivi si vizuri na havikupaswa kutokea katika mazingira kama
haya iwapo uongozi ungekuwa umepewa nafasi. Kwa mfano, baba hahitaji kumpa
adhabu mtoto wake wala mkuu wa kazi kumwadhibu mfanyakazi wake iwapo
pangekuwepo na mawasiliano mazuri ya kuleta maelewano.
Mifano hii inatuonyesha kwamba uongozi sio kama vile mamlaka, yawe ya kimila
kama vile mamlaka ya mzazi juu ya mtoto wake, au yawe ya kisheria kama vile
mamlaka ya mkuu wa kazi katika mfumo msonge wa utawala. Baba anaweza
kumshurutisha mwanae amfanyie jambo fulani na huyo mwana akafanya hivyo tu kwa
hisia kuwa baba yake ana haki ya kumshurutisha. Mfanyakazi wa chini kwa kawaida
hufanya shughuli zake kwa kufuata magizo ya mkuu wake wa kazi alimradi maagizo
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
10
hayo yamo ndani ya mamlaka ya mkuu huyo, na kwa hiyo mtumishi wa chini anahisi
kuwa mkuu wake ana haki ya kumpa maagizo. Hili ndilo kwa kawaida tunamaanisha
tunaposema utumiaji wa mamlaka halali. Mamlaka halali yana faida ya utumiaji nguvu
usiokuwa wa lazima, lakini bado ni kitu tofauti kabisa na uongozi.
Maisha yetu ya kila siku hutufunza kwamba baadhi ya watu wana aina fulani za nafsia
inayoheshimiwa na kukubalika kwa watu wengi. Kwa hiyo wanaweza kuwashawishi
watu wengine kwa urahisi kutokana na haiba (charisma) yao. Hata hivyo izingatiwe
kwamba haiba sio sawa na uongozi. Haiba ni kipaji cha kuzaliwa, na ambacho ni watu
wachache wanacho, na wengi hawana. Wakati uongozi ni kitu kilichofungamana na
mawasiliano, na ambacho kila mtu anaweza kuwa nacho. Wapo watu wengi ambao
hawana kipaji cha haiba, lakini wametokea kuwa viongozi mashuhuri. Kwa hiyo
uongozi si utumiaji nguvu, wala mamlaka ya kimila, kisheria, au kihaiba, ijapokuwa
mojawapo ya sifa hizi inaweza kuwemo katika dhana ya uongozi. Watu walio katika
nafasi za utoaji amri waweza kuwa au wasiwe viongozi. Kwa hiyo hali za uongozi
hazina budi zitofautishwe kidhana kutoka hali za utoaji amri au mifumo ya utawala
yenye taratibu za amri.
Uongozi na Mawasiliano
Kuongoza ni kuwasiliana. Ili uongozi uwepo, tunahitaji walao watu wawili ambao kwa
kiasi fulani wanashirikiana na kuhusiana. Hakuna awezaye kuongoza akiwa katika
upweke. Kwa hiyo, uongozi ni mojawapo ya aina za mawasiliamo. Kuna uhusiano
mkubwa kati ya jinsi mtu anavyoongoza na jinsi anavyowasiliana na wengine. Katika
shirika lenye utaratibu wa tabaka za madaraka, mfumo wa mawasiliano ni amri kutoka
juu kwenda chini. Pia, hivyo ndivyo inavyokuwa kuhusu uongozi wa shirika la aina
hiyo. Mwenye cheo hutoa kazi na maelekezo ya jinsi ya kuifanya, na mwajiriwa aliye
chini yake hutekeleza na kutoa ripoti ya matokeo. Kwa juu juu, mfumo huu huonekana
kuwa thabiti, lakini kiukweli sio thabiti kwa sababu unaelekea zaidi kuendeleza aina ya
uhusiano ambao wengi wetu hatuwezi kuuvumilia.
Mawasiliano katika jumuia zilizo mafunzoni hufuata mkondo tofauti. Sio mkondo wa
juu kwenda chini, bali ni ule wa kuhusisha watu wote. Ni mkondo unaokwenda pande
zote. Haujihusishi na kitu cho chote cha utumiaji nguvu au mamlaka. Hutupilia mbali
mfumo wa tabaka za madaraka. Mara zote hujitokeza katika umbo la mazungumzo,
ambapo kila mhusika hushiriki na kujifunza. Utaratibu wa uongozi katika mfumo huu
hufuata utaratibu ule ule wa mawasiliano. Kila mmoja huonekana na hutarajiwa kuwa
kama kiongozi na mfuasi. Au, kwa maneno mengine, kila mmoja ni kiongozi ambaye
anafanya kazi na viongozi wenzake katika jitihada za kufikia maafikiano kwa pamoja
juu ya suala linalojadiliwa, njia mbalimbali zilizopo za kushughulikia masuala husika,
na maamuzi yanayofanywa. Kila mmoja hufanya jitihada ya kufikia kuona jambo kwa
namna moja, mtazamo wa maisha ambao wote hukubaliana nao.
Dhana hii ya uongozi inaweza kuonekana kama kichekesho inaposikika kwa mara ya
kwanza, lakini sivyo ilivyo. Inaweza kuonekana kama kitu cha kufikirika tu kwa
sababu tumezoea ule mfumo wa mawasiliano ya kutoka juu kwenda chini. Mawasiliano
ya kutoka juu kwenda chini ndio wengi wetu tumeyajua kutokea majumbani, shuleni,
kazini, na katika sehemu za kuabudu. Kwa vile ni kwa njia hii hii tulivyolelewa, hatuna
budi tufanye jitihada kadri tuwezavyo kutokomeza mila hizi za zamani. Ni pale tu
tukiishakubali na kutambua kuwa upo uwezekano wa kujifunza na kuamua pamoja,
tutakuwa tumeanza safari ya kuelekea mwisho mwema kabisa na uhusiano wenye
manufaa wa kuweka misingi ya maisha bora ya siku zijazo.
Misingi ya Ujenzi wa Uongozi: Uongozi kama shule ya Mawasiliano
11
Uongozi Ndani ya Jumuia Zilizo Mafunzoni
Uongozi ni shughuli yenye kuathiri na kuelekeza watu kufikia lengo fulani. Ni shughuli
inayohusu kutoka hatua moja ya maisha kwenda nyingine. Kutoka hatua moja kwenda
nyingine kunahitaji lengo, maono. Kwa hiyo, uongozi unahusu kujenga maono. Maono
si jambo la kuweka malengo tu, bali linahusu ujengaji picha ya wazo zuri juu ya
shughuli tunayotaka kufanya itoe sura gani iwapo tutaifanya vizuri ipasavyo. Kwa
msingi wa hoja hii, uongozi hauwezi kuwepo bila lengo. Uongozi lazima uwe na
mwelekeo, vinginevyo sio uongozi tena. Kwa kuzingatia hayo, linafuatia swali: ni jinsi
gani tunafasili lengo, tunaweka mielekeo, tunaanza utekelezaji, na kubaini vigezo vya
kupima mafanikio? Je, ni lazima shughuli hii ifuate muundo wa tabaka za madaraka?
Kwa vile tunaanza na mazingira ya kijamii yaliyoegemea uongozi shurutishi, inafaa
kuzungumzia mawazo muhimu yanayoweza kutusaidia kuleta mageuzi ya uongozi
katika jumuia zilizo mafunzoni.
Kuongoza Jumuia Zilizo Mafunzoni
Kwa vile uongozi jumuishi umeegemea katika misingi ya kutoa na kupokea,
maafikiano hayaji mpaka jamii yenye maono na mtazamo wenye mafao umefikiwa.
Malengo na njia za kuyafikia vyote viko katika mwendo na mabadiliko wakati wote na
hakuna lengo moja tu linalopewa muhimu au utukufu kwa kiasi cha kutosha
kuhalalisha njia zote. Hii haimaanishi kuwa washiriki hawaamini sana maoni yao au
hawafikirii kwa makini baadhi ya malengo; ukweli ni kwamba wanalikabili suala zima
katika utaratibu ambao ni kinyume kabisa na mfumo wa tabaka za madaraka. Mfumo
wa uongozi katika jumuia zilizo mafunzoni unaweza kujumuisha vipengee vifuatavyo:
Utaratibu Unaotoa Nafasi ya Mabadiliko: Utaratibu wa kujifunza hubadilikabadilika
kadri kujifunza kunavyoendelea. Uongozi unapatikana kadri ya utaratibu
unavyoingiliana na kujifunza kwenyewe---utaratibu unakuwa kujifunza na kujifunza
kunakuwa utaratibu. Kujifunza katika mazingira haya sio tu hali ya utoaji ufundishaji
mawazo na tabia, bali pia ni hali ya urekebishaji wa mahusiano miongoni mwa
washirika wa ushirika. Katika ushirika wa walio mafunzoni, utaratibu sio suala la idadi
ya ofisi zilizounganishwa kwa uhusioano wa mamlaka, bali ni mwingiliano hai na
madhubuti kati ya binadamu halisi.
Mgao Mzuri wa Madaraka: Ili kufikia lengo la utaratibu kuwa kujifunza na kujifunza
kuwa utaratibu, ni muhimu kugawa madaraka katika utaratibu mzuri. Kuondokana na
uhusiano wa tabaka za madaraka haimaanishi vurugu. Kwa hakika, inamaanisha kuwa
utaratibu mzuri wa utendaji unatokana na mahusioano ya watu mtazamo, ujuzi,
shauku, na karama ambazo ufanikisha mazungumzo na kuendeleza jamii yenye mafao
baina ya washiriki.
Kuheshimiana: Uongozi ndani ya jumuia zilizo mafunzoni hutegemea uwezo wa
washiriki kubadilishana maoni kati yao kama binadamu walio sawa na kamili. Uongozi
jumuishi husisitiza kuwepo kwa washiriki wazungumzaji wanaoheshimiana na
kuheshimu maoni ya kila mmoja wao---hata kama maoni hayo yanatofautina na yao.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
12
Makubaliano ya Hiari: Katika jumuia zilizo mafunzoni, mamlaka hayapotei.
Mamlaka uwepo na huchukua jukumu muhimu katika utimilifu maono ya pamoja.
Lakini mamlaka hayo yameegemea katika makubaliano ya hiari, na wala sio
mkusanyiko wa sheria au vitisho vya nguvu. Si mamlaka ya kuamrishwa, bali ni
mamlaka yanayoibuka kadri maongezi na mabadilishano ya maoni yanavyoendelea.
Namna ya Kufikiri : Jumuia zilizo mafunzoni zinatambua ushirikiano uliopo katika
makundi, hata pia mahusiano kati ya makundi na jumuia nzima. Zinabuni na kukuza
mfumo wa kufikiri. Washiriki hujua kwamba utambulisho wao na matendo yao huleta
mafanikio kamili pale tu yanapofikiriwa kama sehemu ya kundi lote kwa jumla.
Utambuzi wa mifumo ya kufikiri uyapa majadiliano sura ya kimkakati. Huhusisha
shabaha na uwezo uliopo katika mazingira ya mabadiliko ya mahali na wakati. Jumuia
zilizo mafunzoni zinaweza kuendeshwa katika mazingira tofauti, ikiwa ni pamoja na
mashirika rasmi. Kwa hakika, viongozi wengi waliofanikiwa ndani mashirika rasmi
hutumia ujuzi wa mawasiliano unaoweza kufananishwa na vipengee vilivyotajwa hapo
juu. Shabaha ni kufungamanisha taratibu za mahusiano rasmi na taratibu za zinazojenga
jumuia zilizo mafunzoni.
Maadili ya Uongozi Ndani ya Jumuia Zilizo Mafunzoni
Tunekwisha sisitiza kwamba uongozi sio kutumia nguvu, mamlaka, au amri. Bali ni
kitu kinachoonyesha jinsi ya kuhusiana na kushiriki na watu wengine katika mazingira
yanayoongozwa na taratibu fulani. Ili kuweza kuleta uongozi katika jumuia zilizo
mafunzoni, tunahitaji kuweka mwongozo unaofaa wa kuleta uongozi huo. Mwongozo
kama huo utajumuisha vipengee tulivyokwishataja hapo juu. Hata hivyo, kuandaa
mwongozo kama huo kunategemea kuwepo kwa mitazamo, v ipaji, na tabia ambavyo
vitasaidia katika kukuza na kudumisha mwongozo, ambapo kwa hakika mitazamo,
vipaji, na tabia hizo zinapaswa kufunzwa. Vinakuwa sehemu ya utaratibu wa
kuendesha kujifunza kama uongozi au, kinyume chake, uongozi kama kujifunza.
Utaratibu huu na matokeo yake hujulikana kama “maadili ya uongozi” katika jumuia
zilizo mafunzoni.
Hebu tuanze kwa kuangalia mawazo haya ya kawaida. Baadhi ya watu huamini
kwamba kimsingi watu ni wavivu, na kwamba bila kuwalazimisha au
kuwadanganyadanganya hawawezi kufanya kazi wala kuzaa matunda yoyote. Na
wengine ufikiria kwamba kiasili watu ni wabunifu na wazalishaji na hupenda kufanya
kazi. Kitu wanachohitaji tu ni mazingira mazuri ambamo hamna vikwazo vya kuzuia
ubunifu wao. Tofauti za fikira hizi ni zaidi ya mtindo wa kufikiria. Ni mitazamo miwili
inayokinzana katika kuangalia ulimwengu huu. Mtazamo wa kwanza unatetea uongozi
shurutishi katika mfumo wa tabaka za madaraka. Na mtazamo wa pili unatetea
utaratibu wa kushirikisha watu kwa njia ya mazungumzo na mawasiliano. Bila ya shaka
yo yote, ushirika wetu ulio mafunzoni ni lazima uhimize sifa nafsia ambazo huibua na
kudumisha mtazamo wa pili iwapo tumedhamiria kukuza maadili ya uongozi katika
jumuia zilizo mafunzoni. Jinsi gani twaweza kuhimiza mtazamo wa pili? Ni vipengee
vipi vya maadili ya uongozi tunavyovitafuta?
Mitazamo juu ya Wengine: Mitazamo tunayokuwa nayo juu ya watu wengine ni ya
muhimu sana. Tunahitajika kujifunza kuona watu wengine kama binadamu
waliokamilika kabisa na walio na dhamira ya kutenda yanayofaa. Ni muhimu tujenge
fikira kwamba wanataka kujifunza kuwa binadamu wenye maisha bora, na
wanapendelea kufanya kazi sio, kimsingi, kwa ajili ya kupewa mishahara au
kutukuzwa, bali ni kwa ajili ya kupata maelimisho ambayo yanatiwa msukumo na kazi
zao. Zaidi ya yote, wanapendelea kutambuliwa kama binadamu katika ujumla wake na
Misingi ya Ujenzi wa Uongozi: Uongozi kama shule ya Mawasiliano
13
aliyekamilika. Mtazamo wetu hauwezi kuwafanya watu wengine wawe kama walivyo
kikweli, lakini unaonyesha sisi wenyewe ni watu au tungependa kuwa watu wa aina
gani. Tunahitaji kujiangalia mbali zaidi ya hali zetu wenyewe, kujijua wenyewe, kuwa
wenye unyeyekevu, kuwa wazi, tunaofundishika na kutoshikilia njia moja tu.
Kulinda Maadili: Tunapaswa kulea maadili yanayofaa na kuyalinda. Kusema “maadili
yanayofaa” tuna maana ya mambo yote bora yanayotuwezesha kwenda nje yetu sisi
wenyewe na kufikia imani katika uwezekano wa kwamba tunaweza kushirikiana na
wengine na kwa pamoja tukaweza kugeuza dunia hii kuwa mahali pema kwa watu wote
kuishi. Kushikilia maadili kunaipa maana kubwa kazi yetu ya ushirika zaidi ya shughuli
yenyewe tunayokuwa tunaifanya kwa kuunganisha matokeao ya kazi yetu na shabaha
kuu inayojumuisha watu wote. Kwa kifupi, kushikilia maadili kunatuwezesha kutetea
suala la watu wote zaidi ya masuala yetu ya binafsi.
Kutambua Mahitaji ya Wengine: Maadili ya uongozi katika jumuia zilizo mafunzoni
huwa hayashurutishi kutumikia watu wengine tu, bali la muhimu kuliko yote ni
kujisikia kupenda kutumikia wengine. Hali hii wakati mwingine inaitwa “ uongozitumishi”(
servant leadership)7. Lakini haitoshi kujitoa tu kutumikia wengine, bali pia ni
muhimu kujifunza jinsi gani ya kutambua mahitaji ya wengine. Tunahitaji kukuza
uwezo wetu wa kutambua hisia za watu wengine, kujiweka katika nafasi za wengine,
kuona dunia kupitia katika macho yao. Ili tuweze kufanikiwa katika hili tunapaswa
kuondokana na chuki bila sababu dhidi ya wengine na uhasama, kuachana na
kuepukana na hukumu kali dhidi ya wengine, kujifunza kuachana na kulazimisha maoni
yetu kwa wengine, kukubali tofauti za aina mbalimbali, kudhibiti hasira zetu, kuzipa
uzito sifa nzuri walizonazo wengine, kutambua vipaji, na kusamehe.
Upimaji wa Mafanikio kama Maendeleo ya Binadamu: Maadili ya uongozi katika
jumuia zilizo mafunzoni huthamini sana mafanikio. Kwa hiyo, huhesabu kwamba kazi
imefanyika kwa ufanisi iwapo mwongozo unaoelekeza uongozi kama kujifunza
umeimarishwa. Yanapima mafanikio na tija (productivity) katika misingi ya ongezeko
la thamani kwa kukuza na kuendeleza karama za mwanadamu. Maadili hayo
yanasisitiza uamin ifu na kusadiki kwamba utendaji kwa kuzingatia uhalisi, ukweli, na
shauku miongoni mwa wanaushirika ni njia bora ya kuongeza tija.
Uvumilivu na Ustahamilivu : Maadili ya ya uongozi katika jumuia zilizo mafunzoni
husisitiza juu ya umuhimu wa kuvumilia. Mtu hawezi kujifunza au kufundisha kama
hana uvumilivu. Ili kujenga mtazamo sahihi wa uongozi katika jumuia zilizo mafunzoni
lazima tujifunze jinsi ya kupambana na matatizo na kukomaa kimaisha kupitia katika
shida. Ushupavu, uvumilivu, ujitoaji mhanga, ustahamilivu--- hizi ni baadhi ya sifa
zinazohitajika kwa mafanikio kama kiongozi.
Kufanyakazi Kama Timu: Maadili ya uongozi katika jumuia zilizo mafunzoni
yanashurutisha kwamba washiriki wafanye kazi, wawasiliane, na kuendelea kama timu.
Kazi ya kundi kama timu ndio msingi wa jumuia zilizo mafunzoni. Kufanya kazi kama
timu huhusisha kuheshimiana, kuthamini utofauti, na ukarimu katika ngazi la mtu
binafsi, uwezo wa kumaliza ugomvi, kushirikisha kila mwanaushirika katika maamuzi
na utekelezaji wake, na kuanzisha makundi katika ngazi za ushirika. Lakini, zaidi ya
hayo ni kwa kufanya kazi kama timu ambapo tunajifunza misingi ya uongozi katika
jumuia zilizo mafunzoni.
Mafunzo ya Kundi : Wajibu wa kimafunzo wa kazi ya kundi katika jumuia zilizo
mafunzoni ni kusaidia washiriki katika kuendeleza “funguo za kielimu” ambazo
7 Soma Larry C. Spears, ed. Insights on Leadership, Service, Stewardship, Spirit, and Servant Leadership,
New York: John Wiley, 1998.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
14
huwawezesha kufikia kwenye masikilizano kwa njia ya mafunzo ya kundi. “Funguo za
kielimu” ni “picha, mawazo, na hadithi ambazo huweka akilini mwetu kuhusu sisi
wenyewe, watu wengine, taasisi au mashirika, na kila kipengee cha maisha hapa
ulimwenguni.”8 Zinafanya kazi kama kioo ambamo tunapitia kuona ulimwengu.
Funguo hizi ni msingi wa mtazamo wetu wa kiutamaduni unaounganisha matendo,
maadili, na mapenzi yetu. Kwa sababu sisi ni matokeo ya tamaduni zile zilizojengeka
katika misingi ya tabaka za madaraka kihistoria, wengi kati yetu tunakuwa na funguo za
kielimu ambazo si mwafaka kwa miongozo inayofikiriwa kuwa msingi wa jumuia
zilizo mafunzoni. Kwa hiyo ipo haja kubwa ya kukuza funguo hizi, na pale
inapowezekana kuzibadilisha. Hata hivyo, sio jambo rahisi kwa maana funguo hizo
zimeishajikita ndani kabisa katika akili zetu, na hatukai tukizifikiria na wala kuzifanyia
uchambuzi. Kazi nzuri ya kundi inaweza kutusaidia kuzileta katika ufahamu wetu na
hivyo kuweza kuzichambua na kuzifanyia mabadiliko au kuzirekebisha pale
inapolazimu. Mafunzo ya kundi husika na aina za mazungunzo ambayo huwezesha
kuwepo kwa umoja imara, yaani, uratibu, umoja, na ushirika ambao matokeo yake ni
mazuri kuliko yale yatokanayo na ka zi ya mtu pekee au ya kibinafsi. Dhana ya umoja
haina maana kuwa kila mmoja anakubaliana na kila kitu kinachosemwa na mwingine.
Bali inamaanisha kwamba kwa vile washiriki wa kundi wameishajifunza kuthamini na
kuheshimu watu wengine na maoni yao, basi wote wanaweza kuchangia katika
majadiliano yatakayoleta matokeo ambayo washiriki wote watajivunia kuwa ni yao.
Mwongozo wa Uongozi Katika Jumuia Zilizo Mafunzoni
Yale ambayo yamekwishajadiliwa hadi sasa yanaweza kuandikwa kwa kifupi kama
mwongozo wa kukuza na kuendeleza uongozi katika jumuia zilizo mafunzoni. Uongozi
kama kujifunza ni:
Kuhusisha Watu wa Jinsia Zote: Kiukweli ni kwamba wanaume na wanawake
hushirikiana katika kufasili, kufafanua, kutenda na kutimiza shabaha ambazo
huwanufaisha wote. Lengo la kitabu hiki ni kuonyesha kwamba ushirika wa aina hiyo
unawezekana, na hauna budi utekelezwe iwapo tunataka kufanikiwa katika ujenzi wa
mifumo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa ambayo itatufikisha kwenye maisha bora na
yenye kuendelea. Pia, inaonyesha kwamb a karibu kila mtu anaweza kuwa kiongozi
ikiwa dhana ya uongozi imeundwa akilini mwetu kwa mtazamo wa kuleta maendeleo.
Kwa hiyo, hata ikiwa kitabu hiki kinasisitiza zaidi na hali za wanawake, kinawafaa
sana wanaume pia. Kwa kweli, kitakuwa na mafanikio ma kubwa ikiwa wanaume nao
pia wanashiriki katika kukipa umbo na umuhimu unaostahili.
Mawasiliano: Watu huzungumza juu ya masuala wanayofikiria kuwa ni muhimu.
Mazungumzo ya namna hii ni yenye kufaa na kujenga. Kila mtu analo la kuchangia na
kila tendo la kuchangia linakuwa tendo la uongozi. Lengo mojawapo la kitabu hiki ni
kuonyesha ya kwamba inawezekana kugeuza mkusanyiko wa watu usiokuwa na
mwelekeo kuwa jamii yenye kuwa na mawasiliano kwa kuielimisha juu ya faida za
mawasiliano, na kwamba njia hii huainisha na kudhihirisha sifa za uongozi.
Kuwa na Lengo: Jukumu kubwa la jamii yenye mawasiliano ni kufasili na kufafanua
lengo au shabaha. Shughuli ya kufasili na kufafanua lengo ni shughuli ya kushiriki
katika kujifunza, na kwa hiyo ni shughuli inayomshirikisha mhusika katika utumiaji wa
madaraka. Sura na njia za kufasili lengo au shabaha hutueleza mengi kuhusu nyendo za
8 Peter M. Senge, Art Kleiner, Charlotte Roberts, Richard B. Ross, and Br yan J. Smith, The Fifth Discipline
Fieldbook: Strategies and Tools for Building a Learning Organization, New York: Currency Doubleday,
1994, p. 235. Kwa mjadala wa kina, pia soma Warren Bennis and Joan Goldsmith, Synchronicity: The Inner
Path of Leadership by Joseph Jaworski, San Francisco: Barrett-Koehler, 1998, and Learning to Lead: A
Workbook on Becoming a Leader, Cambridge: Perseus, 1997.
Misingi ya Ujenzi wa Uongozi: Uongozi kama shule ya Mawasiliano
15
kisiasa. Hutueleza iwapo mfumo wa siasa ni wa kidemokrasia au wa kimabavu, wenye
kuwekea mkazo usawa au wenye kutetea matabaka ya wenye madaraka. Lengo
mojawapo la kitabu hiki ni kutofautisha kati ya njia hizi mbili zinazohusiana na kufasili
na kufafanua shabaha au lengo.
Demokrasia na Usawa: Katika jumuia yenye kuwekea mkazo mawasiliano na
mashirikiano, washiriki hueshimiana na kuthaminiana kama binadamu katika ujumla
wake.Njia ambamo kuheshimiana kwao kunajitokeza kadri wanavyofasili na kufafanua
malengo, pia ndimo humo humo hali na ubora wa uongozi hufasiliwa na kufafanuliwa.
Moja kati ya shabaha za kitabu hiki ni kutusaidia kuelekea kwenye misingi ya
kidemokrasia na usawa katika kudhihirisha malengo yetu, hata pale ambapo tamadumi
zetu zinaelekea kwenye kuenzi mfumo wa tabaka za wachache wenye madaraka na
utawala wa kushurutisha.
Kutambua Njia Sahihi: “ Lengo halihalalishi njia ya kulifikia” ni kanuni ya kimaadili
inayojulikana sana duniani kote. Kanuni hii ina maana ya kwamba watu waadilifu huwa
hawatumii njia zisizo halali kufikia lengo hata kama ni la muhimu au haraka kiasi gani.
Kwa upande mwengine, kuna uhusiano wa karibu sana kati ya lengo na njia za
kulifikia. Malengo ya kweli hayawezi kuwekwa bila ya kwanza kufanya tathmini na
maelezo kamili ya uwezo wa washiriki au vifaa ambavyo vipo au vinaweza kuwepo ili
kutumika kufikia malengo hayo. Kwa kutofanya tathmini na melezo ya kweli kuhusu
njia tunazoweza kutumia kunaweza kutuelekeza kuweka malengo yasiyotimizika
kamwe.
Uongozi Hujengeka ndani ya “Jumuia iliyo Mafunzoni”: Katika kitabu hiki
hatukusudii kufafanua kinaganaga tuna maana gani tunaposema “jumuia iliyo
mafunzoni”. Kwa jumla tunaweza kusema kwamba “jumuia iliyo mafunzoni” ni
mwongozo wa kukuza na kuendeleza “uongozi kama kujifunza” na unavyo vipengee
vya msingi vilivyoorodheshwa hapo juu. Jinsi gani vipengee hivi vinaundwa na
kutumika, kutategemea zaidi utamaduni wa jamii ambapo ukuzaji na uendelezaji, na
utumiaji wa uongozi kama huu unajaribiwa katika vitendo.
Jukumu kuu la kitabu hiki ni kutualika sisi sote kuchunguza kwa makini na kwa
ubunifu suala la uongozi kama kujifunza, na ufahamivu wa aina mbalimbali
wanaoupata wanawake kutokana na dhana hii. Dhana hii ya uongozi kuhusiana na
kujifunza imejumuishwa na kuambatanishwa kistadi ndani ya vikao vyote vilivyo
katika kitabu hiki.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
16
Mawasiliano Ndani ya Semina: Mwongozo wa Usimamizi
17
Mawasiliano Ndani ya Semina:
Mwongozo wa Usimamizi
Mwongozo huu umekusudiwa kukusaidia wewe, msimamizi/mratibu wa semina au
warsha, kuelewa shabaha za sehemu na vikao vya semina au warsha, na kwa kufikia
shabaha zako kwa kusimamia na kuongoza majadiliano na mazoezi. Kama msimamizi,
wajibu wako ni kufuatililia kwa karibu sana kazi na kuongoza kila kikao cha mafunzo.
Tofauti na waalimu wa kawaida au wakufunzi, wajibu wako sio kuongoza kundi
kufikia mahitimisho au makubaliano maalumu. Bali, jukumu lako ni kuandaa na
kuweka mazingira yanayofaa ambamo washiriki wa semina, ikiwa ni pamoja na wewe,
wanaweza kujifunza kutokana na mawazo na uzoefu wa wengine, kutokubaliana bila
kugombana, na kufanya kazi pamoja ili kufikia maafikiano. Utatengeneza mazingira
hayo kwa kufanya maandalizi makini ya kupanga chumba cha semina na vifaa
vinavyohitajika mapema kabla ya kipindi chenyewe kuanza, pamoja na kufikiria kwa
makini mbinu za usimamizi ambazo zinahimiza kuheshimiana, majadiliano yanayoibua
fikira, na hali ya kushirikiana.
Shabaha za Mafunzo
Uongozi wenye kujihusisha, wenye kushirikisha na unaojumuisha watu wote huegemea
kwenye uwezo wa kutumia baadhi ya mbinu za uongozi, ambapo mbinu zilizo muhimu
ni pamoja na mawasiliano, kusikiliza, ujenzi wa maafikiano, kujenga mtazamo
unaokubalika kwa wote, na kuendeleza ushirika katika kujifunza. Mbinu hizi ni baadhi
ya zile zinazozungumziwa katika vikao vya semina. Katika hatua mbalimbali wakati wa
semina unaweza kuchagua kujadali maana na umuhimu wa dhana hizi kwa undani
zaidi.
Mawasiliano: Uongozi wo wote ule huanza na mawasiliano bora. Viongozi
wanahitajika kuwa na ujuzi wa kuwasilisha mawazo na shabaha zao kwa wengine.
Viongozi bora wana ujuzi wa kuchunguza, kusikiliza, kujieleza kwa ufasaha, na
kuwasiliana na wengine. Kwa sababu hii, vikao vyote vya semina hii vinasisitiza juu
ya kuimarisha ujuzi wa mawasiliano. Vikao vya mwanzo vimelenga ujuzi wa mtu
binafsi wa kuwasiliana na wengine, na vile vya mwisho vinazingatia mawasiliano
ndani ya makundi na kati ya shirika na shirika.
Kusikiliza: Viongozi wanaimarishwa kwa njia ya kusikiliza maoni na shabaha za
wengine. Kusikiliza sio tendo linaloishia tu kusikia yanayosemwa na msimamizi wa
kazi, mfanyakazi mwenzako, au mshindani wako, bali pia hujumuisha kutathmini na
kuyapatia nafasi inayostahili mapendekezo na maoni yao. Msikilizaji bora, kama alivyo
kiongozi bora, ni yule anayejifunza kutokana na anayosikia.
Ujenzi wa Maafikiano: Kuleta maafikiano ni hatua muhimu sana ya shughuli nzima ya
kufanya maamuzi katika uongozi bora. Kwa njia ya mazungumzo, watu katika
makundi, timu, au shirika kubwa hutokea wakaelewa hoja wanazokubaliana nazo wote.
Maamuzi hufikiwa kulingana na welewa wa wote juu ya kuwepo njia na uwezekano wa
aina mbalimbali. Pale ambapo tofauti za maoni zinaendelea kuwepo, hakuna hatua yo
yote inayochukuliwa na kundi. Ijapokuwa wakati mwingine kazi ya kuleta maafikiano
inaweza kuleta hali ya kukata tamaa na upoteaji wa muda mwingi, inaelekeza kundi
katika maamuzi yanayokubaliwa ambayo kila mshiriki atayaheshimu, kuyaunga
mkono, kuyatetea, na kuyatekeleza.
Kujenga Maoni ya Pamoja: Makundi madogo na mashirika makubwa yanaweza
kufaidika kupitia uundaji wa maoni ya pamoja. Kupitia mazungumzo, ujenzi wa
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
18
maafikiano na uzoefu wa pamoja maadili na kanuni za msingi hutokea ambamo kila
mshiriki kwa kiasi chake ameweza kushiriki katika uundaji wake na pia kuendelea
kuchangia na kunufaika. Maoni ya pamoja ni njia rahisi na nyepesi kwa kuwezesha
upangaji wa shabaha ambao hufuatana na umbo la kundi na wakati. Kundi linapounda
maoni ya pamoja, kila mshiriki hushughulika kufuatana na mwongozo wa kundi
ambamo anashrikiana na wengine kumiliki na kutimiza majukumu na malengo ya
kundi.
Kuendeleza Ushirika wa Elimu: Matokeo ya ushirika huonyesha mawazo na shughuli
za washiriki wake. Shirika ambalo wanachama wake hutekeleza maelekezo kwa ufanisi
halitakuwa ushirika wa kujielimisha iwapo washiriki wake hawapati nafasi ya kuuliza
faida au maana ya shughuli zao, kutathmini uwezo wao kwa ajili ya kuuboresha, au
kubadilishana maoni juu ya mafunzo waliyojifunza. Kuendeleza ushirika wa elimu ni
mbinu ya kujenga shirika lote kwa jumla kwa kujitathmini na kushirikiana katika
kujifunza. Mbinu hii inahusisha kujitambua na kujitathminini kama mtu binafsi na pia
kama kikundi kwa jumla kwa ajili ya washiriki kutekeleza shabaha na shughuli zao.
Kwa hiyo, ushirika wa mafunzo ni ushirika ambamo ushirikiano wa washiriki huleta
kujiangalia, tathmini, na maarifa ambayo huongeza au kuchochea nguvu za kufikia
shabaha za ushirika. Ushirika wa mafunzo hujenga mazingira mazuri ya kazi
yanayochochea moyo wa kushirikiana na kuongeza bidii kubwa ya kazi ambamo kila
mtu huongeza maarifa wakati akijifunza kuboresha uwezo wake mwenyewe na uwezo
wa ushirika kwa jumla 9.
Majukumu ya Msimamizi
Msimamizi bora husikiliza na kujifunza pamoja na washiriki wengine wa semina.
Juku mu lako ni kufanya maandalizi ya vikao na kuongoza washiriki katika mazoezi ya
semina. Hauhitajiki kuwa mtaalamu katika masuala ya uongozi au kufahamu majibu
yote. Majadiliano yanayofaa yatakuja kama matokeo ya maoni yote kutoka kwa
washiriki wote ndani ya kikundi.
Kuongoza Maongezi: Wakati mwingine unaweza kupendelea kuongoza mazungumzo
ya kundi ili yafuate mwelekeo mpya unaohimiza uulizaji maswali au udadisi makini.
Kazi yako sio kuongoza matokeo ya mazungumzo, bali ni kuongoza mwelekeo wa
majadiliano huku ukizingatia maanani kuwa hakuna maoni yaliyo sahihi au bora zaidi
kuliko mengine. Kwa njia hii unaweza kuhakikisha kwamba kila mshiriki atatoa
mchango katika mafunzo na katika kubadilishana maarifa. Msimamizi mzuri hujenga
uaminifu, mazingira yasiyoegemea upande mmoja ambamo kila mtu hujiona ni salama
na huru kutoa maoni yake bila kuhukumiwa au kushambuliwa na wengine. Hii husaidia
washiriki kujisikia kwamba wana uhuru wa kutosha wa kutokubaliana na wengine kwa
njia ya kuelimishana na kuheshimiana. Usitishike iwapo patatokea kuwepo kimya cha
muda mrefu kati ya watoaji maoni. Vipindi kama hivi ni wakati ambapo washiriki
wanaweza kupima maoni yao na kujenga moyo wa kujiamini kabla ya kuyasema.
Ibusha Majadiliano: Katika vipindi vyote vilivyomo ndani ya kitabu hiki, maswali
yamewekwa kwa namna ya kuibua majadiliano na malumbano. Maswali hayo
9 Kwa mjadala wa kina, soma Peter M. Senge, Art Kleiner, Charlotte Roberts, Richard B. Ross, and Bryan J.
Smith, The Fifth Discipline Fieldbook: Strategies and Tools for Building a Learning Organization, New
York: Currency Doubleday, 1994.
Mawasiliano Ndani ya Semina: Mwongozo wa Usimamizi
19
yamekusudiwa tu kutumika kama mwongozo unaoweza kuliongoza kundi kuvumbua
na kujadili mada mbalimbali za uongozi. Alimradi kundi linaendelea na majadiliano
yenye maana na faida, jisikie huru kuachia mazungumzo kwenda nje au kinyume na
maswali yaliyotolewa hapa. Zaidi ya hayo, unaweza kuamua kutumia njia tofauti kwa
kuandaa mazoezi au mbinu za kuuliza maswali mengine zaidi ya haya
yaliyokwishaandikwa katika kitabu hiki (kwa mapendekezo zaidi, angalia Kiambatisho
B). Kama umegundua washiriki ambao wana aibu au woga wa kuongea, unaweza
kupendekeza maoni yako na kisha mwombe mmoja kati yao aeleze maoni yake juu ya
ulichosema. Alimradi unaendelea kuzingatia kwa makin i mahitaji ya kila mshiriki na
yale ya kundi zima kwa jumla, na kutumia busara pamoja na kufanya jukumu la
kujifunza kuwa la wote, unakuwa umeimarisha usimamizi bora.
Kuheshimu agenda: Msimamizi anaweza kuongoza majadiliano vizuri kwa
kuhakikisha kila shughuli inafanyika katika muda uliopangwa na mara kwa mara
kuwakumbusha washiriki juu ya ajenda ya somo. Ijapokuwa makundi ya semina
yatatofautiana kwa ukubwa, ni jambo la kufaa sana kuwahimiza washiriki kusema
maoni yao kwa ufupi, usitoe nafasi kwa mtu mmoja au watu wachache kutawala
mazungumzo. Suala hili ni muhimu zaidi katika mazoezi yale yanayohusu kila mshiriki
kutoa maoni yake au kusimulia kisa chake. Njia ya kidiplomasia ambayo unaweza
kutumia kuwakumbusha washiriki wasizungumzie masuala yaliyo nje ya ajenda, ni
kuelekeza mawazo na maelekezo yako kwa kundi lote badala ya kuyaelekeza kwa mtu
mmoja tu. Pia, usikose kuwahimiza washiriki kusikiliza kwa makini yale ambayo
wengine wanasema na kuzingatia maoni yaliyokwishatolewa na wengine hapo nyuma.
Kugawanya Wajibu: Ingawa ni wajibu wako kuongoza kila kikao cha semina tokea
mwanzo hadi mwisho, sio lazima uwe msimamizi katika kila shughuli au kusimamia
kila majadiliano. Kugawanya wajibu kunaweza na ni muhimu kuwe sehemu halisi ya
usimamizi wa vikao vya semina. Njia rahisi ya kufanya hivi ni kuwapa moyo washiriki
kujitolea kuandika yale yanayojadiliwa katika kundi, kusoma kwa sauti maelekezo au
maelezo yaliyo katika kitabu hiki, na/au kusimamia majadiliano. Kumwakikishia
mshiriki kuwa asiwe na hofu juu ya makosa ya herufi iwapo amejitolea kuandika au ya
matamshi iwapo amejitolea kusoma kwa sauti, kunaweza kumsaidia sana kujenga moyo
wa kujiamini na pia kutia moyo wengine kujitolea.
Kushiriki : Ni juu yako mwenyewe kuamua iwapo unapendelea kushiriki katika
majadiliano au la. Lakini kumbuka kwamba kwa vile wewe unasimamia kila kikao na
kwa kiasi kikubwa wewe ndiye “mdhibiti”, washiriki watayapa maoni/mawazo na
mapendekezo yako uzito wa ziada. Kwa hiyo ni muhimu kujizuia kuingilia kati ya
majadiliano mara kwa mara, na unapoamua kutoa maoni yako basi hakikisha
unayaweka kwa namna ambayo washiriki wengine watayaelewa kuwa ni maoni yako
binafsi na sio mtazamo pekee au jibu la mwisho juu ya suala linalojadiliwa 10.
Jiburudishe: Kumbuka ya kwamba na wewe pia unashiriki katika semina hii ili upate
maarifa na kuburudika. Jiburudishe!
Majukumu ya Washiriki
Washiriki wanakuja kushiriki kwenye semina hizi kwa sababu nyingi na tena zilizo
tofauti, pamoja na fikira na matarajio mbalimbali juu ya kitu gani kitakuwa
kinafanyika. Bila kujali kiwango chao cha ujuzi au uzoefu au utaalamu, jukumu la
washiriki ni kuchukua nafasi zote mbili za uanafunzi na ualimu, yaani kijifunza na
10 Kwa ajili ya orodha nzuri ya usimamizi ni nini na sio nini, soma “Part I: Facilitating Learning,” katika In
Our Own Words, by Nancy Flowers, Bethesda: Sisterhood is Global Institute, 1999.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
20
wakati huo huo kubadilishana maarifa na wengine. Vikao vya semina vinafanikiwa
sana ikiwa washiriki wanasikiliza kwa makini, wanauliza maswali, na kuhoji maoni na
fikira. Washiriki wana wajibu wa kutoa mchango wa maoni yao katika majadiliano,
kufanya kazi kwa kushirikiana katika vikundi vidogo vidogo au kama sehemu ya kundi
zima, na kutathmini mwendo na maendeleo ya vikao. Kila mmoja anayeshiriki katika
semina atanufaika kwa kuchangia katika kujenga mazingira ya furaha, kuelimishana,
na kuheshimiana wakati wa mafunzo .
Maandalizi ya Vikao
Ni muhimu uje kwenye vikao vya semina ukiwa umejiandaa. Pitia na soma kwa
makini sehemu zitakazojadiliwa katika kikao kabla ya kikao chenyewe ili kuhakikisha
kuwa unaelewa vizuri shabaha zilizokusudiwa katika kitabu hiki na malengo yako
mwenyewe unayotaka kufikia katika semina hii na katika kila kikao. Jiulize na amua ni
vifaa gani unahitaji kuwa navyo na hakikisha umejiandaa kuwa na vifaa vya kutosha
kwa kila shughuli. Vikao vya semina hizi vinaweza kufanyika ofisini, katika majengo
ya umma, nyumbani kwa watu binafsi, au po pote pale ambapo pana utulivuna
faragha, na ambapo washiriki watajisikia vizuri.
Unaweza kuwaomba washiriki kuleta kalamu na karatasi zao, au unaweza kuwasaidia
kuwapa vifaa hivyo wewe mwenyewe. Kutegemeana na hali ya chumba cha kikao na
vifaa vingine vilivyomo, unaweza kuleta chaki kwa ajili ya kutumia ubao wa kuandikia
au peni za wino mzito kwa ajili ya kutumia karatasi kubwa za kuning’iniza. Vinginevyo
unaweza kuleta vipande vikubwa vya karatasi ambavyo utabandika kwenye ukuta kwa
kutumia gundi ya karatasi au misumari midogo. Ubao wa kuandikia, karatasi kubwa za
kuning’iniza, au vipande vikubwa vya karatasi vinafaa sana kwa kuandika maoni
yanayotolewa na dhana kuu zinazotokea ambapo vinaweza kutumiwa na washiriki kwa
urahisi kama kumbukumbu kadri majadiliano yanavyoendelea. Kuandika pointi
muhimu zinazozungumzwa katika karatasi ni kuzuri zaidi kwa sababu maandishi hayo
yanaweza kuwekwa na kutumiwa kama marejeo katika vikao vinavyofuatia, yaani
maoni na mawazo ya kundi yanaweza kuwa kumbukumbu katika vikao vya baadaye.
Miongoni mwa mazoezi katika kitabu hiki, kuna baadhi ambapo washiriki wanahitajika
kujigawa katika makundi madogo madogo ili kufanya shughuli maalumu. Ikiwa si kila
mshiriki ana nakali ya kitabu hiki, basi unaweza kutoa fotokopi ya maelekezo
yanayohusika kwa ajili ya kila kikundi kidogo. Kama fotokopi haiwezekani, basi
unaweza kuandika maelekezo hayo katika karatasi kubwa kwa kutumia herufi kubwa
na kuibandika ukutani ili kila mmoja aweze kuona na kusoma bila shida.
Vikao vilivyo vingi vinahitajika kuchukua muda wa masaa mawili na nusu hadi saa
tatu. Unaweza kupendelea kuwapa washiriki vinywaji au vitafunio ili kuwafanya
wajisikie kwamba wako huru na raha. Njia nyingine ni kuwaomba washiriki wenyewe
kujitolea kuleta vitafunio. Yote haya ni juu yako mwenyewe kuamua ni lipi linafaa
zaidi ya jingine. Kama huna uhakika juu ya kipi washiriki wanakipenda au
wanakitarajia, basi waulize wenyewe juu ya upendeleo wao katika kikao cha kwanza.
Lililo muhimu kuliko yote ni kufanya maandalizi mapema kabisa kabla ya vikao
vyenyewe ili uweze kujua ni lipi litahitajika na jinsi gani vikao vitaendeshwa.
Mawasiliano Ndani ya Semina: Mwongozo wa Usimamizi
21
Kikao cha Kwanza cha Semina
Unapowasili
Fanya juhudi ya kuwasili mapema kabla ya wengine katika kikao cha kwanza ili upate
muda wa kutosha kuhakikisha kuwa chumba cha semina kimo katika mpangilio mzuri
kama unavyopenda. Angalia kama kuna mwanga wa kutosha, joto la kutosha, na/au
hewa nzuri. Angalia iwapo unaridhika na mpangilio wa viti. Ijapokuwa si kitu cha
lazima, ukaaji wa mduara ni mzuri kuliko yote katika kufanikisha majadiliano ya
semina. Ukaaji wa mduara hutoa nafasi nzuri na iliyo sawa kwa kila mshiriki kuona
washiriki wenzake katika kundi na yeye kuonwa na kusikilizwa vizuri na wengine.
Washiriki Wanapowasili
Washiriki wanapoanza kuwasili wafanye wajione na kujisikia wanakaribishwa. Hili ni
muhimu sana hasa ikiwa washiriki hawajafahamiana. Ikiwa bado hawajakufahamu,
hakikisha unajitambulisha na waeleze kuwa wewe ndiye msimamizi au mratibu wa
semina. Kama kuna vitafunio, wakaribishe kwa kuwaeleza wajisikie huru kuchukua
wanachopenda na kisha kuchukua nafasi ya kukaa kila mmoja karibu na mwingine na
kuanza kutambulishana.
Kujitambulisha: Wakati kila mtu amekwishawasili, mara nyingi inakuwa vema
kumwomba kila mmoja kujitambulisha rasmi kwa kundi zima. Iwapo washiriki
wanafahamiana kabla ya hapo, basi unaweza kuwaomba kila mmoja aeleze kwa kifupi
sababu zilizomsukuma kuhudhuria semina hii na matarajio yake. Na wewe pia ni
muhimu ushiriki katika mazoezi haya ya awali ya kutambulishana. Sababu kubwa ya
kushiriki kwako ni kuwawezesha wanakikundi kuanza kuzoeana na kujenga moyo wa
kujiamini kuzungumza mbele ya wengine.
Baadhi ya Vifaa Utakavyohitaji
·  Kalamu na/au Kalamu za risasi
·  Karatasi
·  Karatasi kubwa ya kuandikia mawazo muhimu
·  Ubao wa matangazo
·  Peni za wino mzito za rangi tofauti
·  Chaki
·  Nakala za maelekezo
·  Saa ya ukutani yenye mikuki inayoonekana
·  Vinywaji na vitafunio
·  Vikombe, sahani, taulo za karatasi za mezani
·  Gundi ya karatasi au vijusumari vidogo
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
22
Maelezo: Anza kikao cha kwanza kwa kuwapa washiriki maelezo mafupi juu ya nini
kitakachoendelea, kujadiliwa, na hatimaye watakachojifunza katika kipindi chote cha
semina, na mambo ya msingi katika kila kikao (angalia chini). Linaweza kuwa jambo
na kufaa sana ukiweza kuwaeleza shabaha kuu za mafunzo haya kama
zilivyokwishajadiliwa hapo awali: mawasiliano, kusikiliza, ujenzi wa maafikiano,
kujenga maono ya pamoja, na kuendeleza ushirika wa kujifunza. Njia nyingine,
unaweza ukawauliza jinsi gani wanavyozielewa dhana hizi. Zaidi ya hayo unaweza
kuamua:
·  Kuwataarifu kuwa kila kikao cha semina kitachukua muda wa kati ya masaa
mawili na nusu na masaa matatu.
·  Waeleze mfano wa muundo wa kikao, ikiwa ni pamoja na wakati wa
mapumziko.
·  Waeleze kwamba wataombwa kujitolea kusaidia katika shughuli kadhaa kama
vile kuandika mambo yanayojadiliwa, kutunza muda, kusoma kwa sauti
vifungu katika kitabu hiki, na kisimamia majadiliano.
Muundo wa Vikao: Vikao vilivyoelezwa ndani ya kitabu hiki vimegawanywa katika
sehemu tatu: Sehemu ya Kwanza inahusu “Kukuza Nafsi kwa ajili ya Kufikia
Uongozi”; Sehemu ya Pili ni juu ya “Kuwasiliana na Wengine”; na Sehemu ya Tatu
inazingatia “Kuanzisha Ushirika wa Kuelimishana”. Vikao vya semina ya uongozi
vimepangwa katika utaratibu wa kutoka hatua ya kukuza nafsi kwenda hatua ya kukuza
kundi au timu, hadi hatua ya kuimarisha uongozi bora katika ngazi ya shirika. Mwanzo
wa kila sehemu kuna maelezo mafupi ya utangulizi na madhumuni ya vikao. Linaweza
kuwa jambo la kufaa kuanza kikao cha kwanza kwa kusoma au kufafanua utangulizi wa
Sehemu ya Kwanza. Mwishoni mwa kikao hakikisha kuuliza iwapo kuna mtu mwenye
swali.
Taratibu za Kila Kikao
Vikao vyote vina taratibu zile zile za msingi. Hata hivyo, kila kikao kina shughuli
zake tofauti kingine. Kutegemeana na madhumuni yake, kikao kinaweza kujumuisha
vipengele vifuatavyo:
Dondoo la Utangulizi: Katika ukurasa ulio mkabala na kila kikao kuna dondoo kutoka
katika sura ya utangulizi yenye kichwa cha habari “Misingi ya ujenzi wa uongozi”.
Dondoo linatoa mwanga juu ya mada ya kikao kinachohusika, na linaweza kutumika
kama kitu cha kukumbushia maoni muhimu yanayojitokeza katika sura ya “Misingi ya
Ujenzi wa Uongozi” na pia kutumika kama kichocheo cha majadiliano.
Madhumuni ya Kikao: Kila Kikao kinaanza na orodha ya madhumuni ambayo
yamekusudiwa kuwasaidia washiriki kuelewa lengo lililokusudiwa katika mazoezi na
mswali ya kikao husika, na pia kuwasaidia katika mwelekeo mzuri wa majadiliano juu
ya wasifu (biografia) na visa. Ni juu yako mwenyewe kuamua kuwasomea washiriki
madhumuni ya kikao ama mwanzoni au mwishoni mwa kikao, au kutowasomea kabisa.
Kabla ya Kuanza: Katika Vikao 1, 9, na 12 kuna miongozo iliyowekwa katika
visanduku ili kuwasaidia wasimamizi. Miongozo hii inatoa mapendekezo na
vikumbusho ambavyo vimekusudiwa kuwaongoza wasimamizi katika hatua za
mwanzo, kati, na mwisho wa kila semina kamilifu.
Maoni ya Usimamizi: Kila Kikao kina mapendekezo ya usimamiaji ambayo
yanaeleza mazoezi ya kikao na shabaha za maswali yanayofuatia. Vidokezo kuhusu njia
na mbinu za usimamizi vimewekwa katika visanduku vilivyotangulia maelezo halisi ya
Mawasiliano Ndani ya Semina: Mwongozo wa Usimamizi
23
kila kikao. Visanduku hivi pia vinamrejesha msomaji katika Kiambatisho B kwa ajili ya
maelezo ya ziada.
Mazoezi: Kila kikao kina zoezi moja au zaidi ambamo washiriki wa kila kundi
wanashiriki kuyafanya pamoja kama timu. Shabaha ya mazoezi haya ni kusisitiza
baadhi ya mbinu za uongozi na mawasiliano. Kulingana na muundo wa kundi la
semina na tathmini yako juu ya mahitaji ya washiriki, unaweza kuendelea kutumia
mazoezi kama yalivyo au kuyarekebisha ili yafae kundi lako. Kama ilivyo wazi kuwa
hakuna makundi mawili ya semina yanayotumia kitabu hiki kwa namna ile ile, pia ni
muhimu kwako kuwa tayari kufanya marekebisho unayoona yatafaa zaidi kufikia
malengo na mahitaji ya kila kundi. Maswali kwa ajili ya majadiliano yanafuatia kila
zoezi.
Maswali ya Majadiliano: Maswali ya majadiliano yametungwa ili kuwashawishi
washiriki kutoa mawazo yao juu ya masuala maalumu. Kila swali limejengeka kwa
kuzingatia swali lililolitangulia ili kuongoza mjadala kusonga mbele. Ikiwa ni mara
yako ya kwanza kusimamia semina ya uongozi, basi litakuwa ni ja mbo la kufaa kufuata
mpangilio wa maswali kama ulivyo katika kitabu hiki, walao katika vikao vya
mwanzoni. Katika vikao vinavyofuata au katika semina za baadaye, unaweza kuwa
tayari na uzoefu wa kutosha kutumia njia nyingine za kuuliza maswali au kuongeza
maswali ya ziada unayofikiria yanaweza kuleta matokeo mazuri zaidi. Hayo yote
yanategemena na uamuzi wako wewe binafsi. Zaidi ya hayo, unaweza kuwaomba
washirika kujitolea kuongoza mjadala, na anayejitolea anaweza kuwa na maoni yake
ya jinsi gani anaweza kuongoza mazungumzo kwa ufanisi zaidi. Hakuna maswali sahihi
maalumu ya kuongoza mjadala, lakini ni muhimu kufanya majadiliano kuwa ya
kusisimua, ya kuvutia, na yenye mafao kwa washiriki.
Maswali ya Pamoja katika Kundi : Maswali yaliyokusudiwa kwa kundi hayana budi
yaelekezwe kwa washiriki wote. Lengo ni kupata mtazamo mpana juu ya aina mabali
mbali za maoni au uzoefu ndani ya kundi kuhusiana na suala linalojadiliwa. Ijapokuwa
aina hii ya uulizaji hufanya kazi vizuri iwapo kila mmoja anashiriki, ni muhimu
kuwaeleza washiriki kwamba mshiriki ye yote yule anaweza kuamua kutojibu swali
kama hataki kujibu au kuzungumza. Zipo sababu nyingi ambazo zinaweza kuwafanya
washirika wasijisikie kujibu, na uamuzi wao ni vyema uheshimiwe. Pamoja na hayo,
ikiwa utaona kwamba mwanakundi anashiriki mara chache mno katika majadiliano na
anasita kushiriki katika shughuli za vitendo, jaribu kuongea naye mkiwa nyie wawili tu
juu ya hali yake. Hakikisha unamwelewesha kuwa na kumfanya ajisikie kuwa huru na
kuamini kuwa mawazo yake yana thamani na kwamba kwa kufanya hivyo anaongeza
maarifa na ujuzi kutokana na semina hii. Kama hatabadilika, basi jaribu kutafuta sababu
na kuona iwapo unaweza kuyafanyia kazi mahitaji yake vizuri zaidi kupitia katika
vikao vya semina. Hakuna mshiriki anayepaswa kushurutishwa kuendelea kuhudhuria
vikao vya semina iwapo anajisikia kuwa havimfurahishi au kumnufaisha.
Shughuli ya Kundi: Katika vikao vingi mna shughuli za kikundi. Shughuli hizi ni
tofauti kabisa na mazoezi kwa sababu kundi zima kwa pamoja linalazimika kushiriki
katika kufanya maamuzi ya pamoja. Shughuli za kundi zimelenga kuendeleza uwezo
wa mawasiliano, kusikiliza, ujenzi wa maafikiano, mashauriano ya upatanishi, na ujuzi
wa ushirika wa kujifunza katika mazingira ya kishirika. Kwa baadhi ya washiriki ni
rahisi kufanya shughuli kwa pamoja katika kundi kuliko kuifanya mmoja mmoja au
katika vikundi vidogo. Kwa wengine mazoezi ya kundi yataonekana kuwa magumu
sana. Wakati wa shughuli za kundi msimamizi atafanya kazi kubwa ya kusaidia kundi
lifanye kazi kama kitu kimoja juu ya suala linalohusika. Usisahau kwamba kuna
washiriki wengine ambao watapendelea kujitolea kusimamia majadiliano wakati wa
shughuli za kundi. Ikiwa mmoja wao atapendelea kufanya hivyo, utapaswa kushiriki
katika shughuli ya kundi hilo kama mwanakundi.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
24
Uchunguzi: Maswali ya uchunguzi yamelenga kuchochea mazungumzo juu ya muundo
na njia za kujifunza za vikao vyenyewe. Maswali yanawapa washiriki nafasi ya kueleza
jinsi gani wamejisikia wakati wa mazoezi, na kumsaidia msimamizi kuamua ni aina
gani ya shughuli za mazoezi zina faida kubwa zaidi kuliko nyingine kwa kundi hilo.
Maswali ya Kutathmini Semina: Tathmini ya semina itafanyika katika vikao vitatu
ambavyo ni kikao cha kwanza, kikao cha saba, na kikao cha mwisho. Aina tatu za
maswali zinajitokeza kote zikijihusisha na matarajio ya washiriki na maoni yao juu ya
uendeshaji wa vikao, muundo, na yaliyozungumzwa katika vikao hivyo. Sehemu za
tathmini zimelenga kukusaidia wewe, ukiwa kama msimamizi/mratibu, kujua washiriki
wanatarajia nini na jinsi wewe na kundi lako mnavyoweza kufanya shughuli za kufikia
matarajio hayo. Wakati mwingine utalazimika kutoa ufafanuzi wa yale yote
yanayopaswa kuangaliwa katika semina nzima ili kuepusha kutokueleweka kwa yale
yatakayozungumziwa katika vikao. Wakati wa tathmini ni muhimu zaidi kukumbuka
kuwa wajibu wako ni kusikiliza, kuandika maoni muhimu, na kujaribu kuzingatia
maoni na mapendekezo ya washiriki ambayo yanaweza kukufaa katika usimamizi wa
vikao vijavyo. Kusimamia semina ukiwa na moyo wa kutaka kujifunza kutoka kwa
wengine, kupokea maoni na kuyafanyia kazi ipasavyo, kuwa mchangamfu, na
kutong’ang’ania njia moja tu ya kufanya jambo kutakusaidia wewe na washiriki wako
kunufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na tathmini hiyo.
Maelekezo ya Kikao Kifuatacho: Mara nyingine mwishoni mwa kikao kutakuwepo
na maelekezo kwa ajili ya kikao kifuatacho. “Kazi ya nyumbani” haipaswi kuwa
mazoezi magumu na inaweza kuwasaidia washiriki kujiandaa kwa ajili ya mazoezi na
majadiliano ya kikao kifuatacho. Hata hivyo utakuwa ni uamuzi wako kuwapa au
kutowapa washiriki maelekezo hayo. Ukiamua kutowapa maelekezo hayo, basi
hakikisha unapanga muda wa ziada wa kutosha mwanzoni mwa kikao kifuatacho kwa
ajili ya mazoezi hayo.
Mwisho wa Semina
Kulingana na mapendekezo ya kundi, washiriki wanaweza kuamua kumaliza semina
yao kwa kufanya sherehe isio rasmi au kitu kingine kitakachoonekana kinafaa kundi
zima. Katika kikao cha tisa au cha kumi, unaweza kuwaomba washiriki kuanza
kufikiria jinsi gani wangependa kusherehekea ufungaji wa semina. Ni muhimu kupanga
mambo yote mapema ili washiriki waweze kumaliza semina wakiwa wanajisikia kuwa
mahitaji na matarajio yao yamezingatiwa. Kabla ya washiriki kuondoka katika kikao
cha mwisho, waombe kujaza Fomu ya Tathmini ya Semina iliyo mwishoni mwa kitabu
hiki. Fomu hii ina faida kubwa katika kurekebisha na kuboresha usimamizi wa semina
za siku zijazo. Ni vema kuwaeleza vizuri madhumuni ya fomu hii na kuwahakikishia
washiriki kuwa taarifa watakazoziandika zitakuwa ni siri kubwa. Kumbuka kukusanya
fomu kutoka kwa washiriki wote kabla hawajatawanyika.
Ukuzaji au uendelezaji wa uongozi ni projekti ya maisha na washiriki wataendelea
kuimarisha, kujifunza, na kurekebisha ujuzi wao wa mawasiliano kwa kipindi kirefu
kitakachofuatia baada ya semina kumalizika. Wakati mwingine washiriki hupendelea
kukutana na kuunganika tena katika siku maalumu au kuwa na kikao baada ya miezi
kadhaa ili kuchambua na kupata mtazamo mzuri juu ya yale waliojifunza na jinsi
wanavyoyaweka katika vitendo vya shughuli zao za kila siku. Mara nyingi washiriki
hutokea wakafanya urafiki wakati wa semina na vikao vyake, na hupendelea kuendelea
kukutana na kuimarisha urafiki huo.
Hatua zifuatazo ni kwa ajili na juu ya washiriki wenyewe.
25
Vikao vya Semina
26
27
Sehemu ya Kwanza:
Kukuza Unafsi kwa ajili ya Kufikia Uongozi
Mara nyingi maoni ya wanawake hubakia zaidi bila kuzungumziwa au kusikilizwa, hata pale
ambapo wanawake wanahudhuria vikao vya majadiliano na maamuzi. Wanawake
wanaweza kuwa wanashiriki katika mikutano ya jamii, mahali pa kazi, au familia, lakini bado
hakuna anayewaona. Kwa nini jambo hili liwe hivi? Kwa kweli, kuna sababu nyingi za aina
mbali mbali ikiwa ni pamoja na za kiutamaduni, za kihistoria, na za kibinafsi. Baadhi ya
wanawake wana karama (natural gift) ya kutoa mawazo yao na yakasikilizwa, mitazamo yao
ikazingatiwa, na maoni yao kufikiriwa na kufanyiwa kazi. Tunaweza kujifunza kutoka kwa
wanawake wa aina hii, tukabaini na kuchagua zile sifa ambazo sisi wenyewe tungependelea
kuwa nazo. Mazoezi katika sehemu hii yanalenga katika kuchunguza sifa za kuwa na
madaraka na kubaini nyenzo za uongozi ambazo zinaweza kuwa na manufaa binafsi kwa
washiriki wa semina. Si kila aina ya majadiliano itakuwa na manufaa kwa washiriki wote.
Kila mshiriki anaweza kubaini na kuchagua sifa na mbinu za uongozi anazoona ni muafaka
katika mazingira yake ya aina yo yote ile. Shabaha ya sehemu hii ni kuwawezesha washiriki
kuchunguza kwa makini mbinu za uongozi zinazowavutia sana na kugundua zile ambazo
zinaweza kuwafaa zaidi katika shughuli zao za kila siku.
Mazoezi ya kujifunza katika sehemu hii yamewekwa kwa namna ya kuwawezesha washiriki
kujichunguza wenyewe ndani ya makundi, na kuchunguza jinsi wao wenyewe
wanavyoshirikiana na wenzao katika kundi, na vitu gani vinavyochochea zaidi
mazungumzo, na vipi vinavyoyakwamisha. Ijapokuwa wakati mwingine washiriki wote
watashawishiwa kutoa majibu/maelezo kwa kumuuliza mshiriki mmoja mmoja katika kundi,
kama ilivyo kwa mazoezi yote ndani ya kitabu hiki, mshiriki ajisikie huru kutojibu iwapo
anajisikia hana cho chote cha kusema au kwa sababu yo yote ile hajisikii kuzungumza
wakati huo.
28
______________________________________________________________
Ili kujenga mtazamo sahihi kwa ajili ya uongozi katika jumuia zilizo mafunzoni
hatuna budi kujifunza kupambana na hali ngumu
na kukomaa kutokana na shida.
Ujasiri, uvumilivu, kujitolea kwa dhati, ustahimilivuhizi
ni baadhi tu ya sifa zinazohitajika kwa mtu kuwa kiongozi bora.
“Misingi ya Ujenzi wa Uongozi”
29
KIKAO CHA KWANZA
Kiongozi ni Nani?
Shabaha za Kikao
§ Kuchunguza fasili za uongozi na sifa za viongozi bora.
§ Kupanua mitazamo ya washiriki juu ya nani aliye kiongozi na
nani awezaye kuwa kiongozi.
§ Kujadili na kuhakiki mbinu za ufundishaji za semina hii.
§ Kubadilishana maoni juu ya matarajio na malengo ya washiriki
katika semina hii kwa vikao 11 vinavyofuatia.
Kabla Hujaanza: Sehemu ya “Kuwasiliana katika Mazingira ya Semina” katika kitabu
hiki inatoa baadhi ya mawazo juu ya nini cha kufanya unapowasili kwa ajili ya kikao cha
kwanza cha semina, nini cha kufanya wahiriki wanapowasili, na vifaa utakavyohitaji
katika semina nzima. Kama msimamizi bora, jukumu lako ni kuongoza mazungumzo,
kuchochea majadiliano, kuhakikisha mazungumzo hayatoki nje ya ajenda, kugawanya
wajibu na washiriki wengine, na kushiriki katika majadiliano. Jiburudishe---kumbuka
kuwa pia wewe unashiriki katika semina ili kupata maarifa na kujiburudisha.
Mapendekezo ya Usimamizi
Soma kwa sauti kisa hiki kilichosimuliwa na Asma Khader. Jadili
ufafanuzi wake juu ya kiongozi na sifa za uongozi. Maswali
yanayofuatia yanaweza kusaidia kuongoza mjadala. Mtu mmoja ---
msimamizi au mshiriki aliyejitolea--- anaweza kuandika pointi muhimu
ubaoni au kwenye karatasi kubwa ya kuning’iniza.
Mtindo wa Maswali na Majibu katika kuendesha mazungumzo unafaa sana hapa.
Msimamizi anaweza kuuliza maswali ya ziada ya jumla yanahitaji majibu ya maelezo ili
yakamilishe Maswali kwa ajili ya Majadiliano yaliyo hapa chini kufanya mjadala uwe
mzuri (angalia Kiambatisho B kwa taarifa zaidi juu ya mbinu hii ya usimamizi).
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
30
Mwanamke Mmojja Anaweza Kulletta Mabadiilliiko ya Mambo
Asma Khader: Mtetezi wa Haki za Binadamu
“Sina uhak ika iwapo mimi ni kiongozi, lakini ninafahamu kwamba kuwa
kiongozi inamaanisha kwamba unaona kuwepo haja ya haraka ya
kushughulikia tatizo fulani---kwamba unajisikia kuwa na haja ya kuwa katika
nafasi fulani kwa kuanzisha shughuli, kampeni, na mipango ili kuvielekeza
vyote kutatua tatizo maalumu. Kama watu katika jamii yako wanaamini
kabisa kwamba unaweza kuleta suluisho kwa shida zinazowapata, basi
watakuunga mkono na kukupa nafasi ya kuwa kiongozi wao. Watu
wanapokuamini, watakuja kwako ili uwasaidie kufikia malengo yao.
Miaka ipatayo ishirini hivi iliyopita, mwanamke mmoja aliyekuwa na hofu na
majonzi makubwa alikuja ofisini kwangu akiniomba nimsaidie. Alinisimulia
jinsi mume wake alivyomuua mtoto wao wa kike aliyekuwa na umri wa
miaka kumi na mitano na mimba iliyotokana na kubakwa. Bwana huyo
alihukumiwa kifungo cha miezi sita tu, kwa madai kuwa alimuua huyo binti
wake ili kuondoa aibu kwa familia. Lakini huyu mwanamke, akiwa
amedhamiria kutunza heshima ya binti wake, alinieleza ukweli mtupu---
kwamba ni mume wake huyo huyo aliyembaka huyo binti wao, na kwamba
alimshuku kumuua binti wao kwa sababu mimba ilikuwa imeanza kukua na
kuonekana. Mahakama bila mashaka yo yote iliamini aliyoyasema mume
wake na haikujali kabisa kuchunguza tendo hili la uhalifu . huyu aliendelea
kuonyesha maakama makuu kwamba ni mumewe ndiye aliye mbaka mtoto
na kumuuwa wakati alipo tambua mimba inaanza onekana. Maakama
hayakuamini mwanamke huyo na hawakuendelea na kufanya utafiti wa
mauaji ya msichana huyo.
Ijapokuwa mwanamke huyu alikuja ofisini kwangu mara moja tu na tokea
hapo sikumwona tena, kweli ninamshukuru kwa sababu kupitia kwake
nilijifunza na kufumbuka kwa kiasi kikubwa juu ya mateso wayapatayo
wanawake na wasichana kutokana na baadhi ya sheria. Nilitambua kwamba
nisingeweza kuwa mwanasheria bora iwapo nisingetumia jitihada zangu
zote kubadilisha sheria ambazo huficha na, wakati mwingine, kuidhinisha
uhalifu dhidi ya wanawake. Huyu mwanamke alinipa changamoto ya
kushughulikia tatizo ambalo kamwe nisingedhubutu kulifumbia macho----
uhalifu wa kutetea heshima.
Kwa hiyo ilitokea kwamba nikawa mmojawapo wa viongozi katika kampeni
za kutokomeza kabisa uhalifu wa kutetea heshima. Na pia ninafikiri kwamba
yule mwanamke aliyeniamini, aliyekuwa na ujasiri wa kutosha kuja ofisini
mwangu na kunipa taarifa juu ya ukweli huu, alikuwa kiongozi. Alishinda
hofu yake mwenyewe kuweza kutoa nje uhalifu wa mume wake na kutafuta
msaada kwangu. Watu kama yeye wanatupa changamoto sisi kuchunguza
masuala ambayo hapo nyuma hayakuwahi kufikiriwa na kupewa uzito
unayostahili. Hatuna budi tuige mifano ya watu kama hao na kujaribu
kuokoa wengine.”11
Asma Khader, mwanasheria, mtetezi wa haki za binadamu, na kiongozi wa zamani wa chama cha
wanawake wa Jordan (Jordanian Women’s Union) , ameendesha kampeni nyingi za kutokomeza
uhalifu wa kutetea heshima na unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana nchini Jordan.
11 Dondoo kutoka kwenye mahojiano na Asma Khader yaliyorekodiwa kwenye video tarehe 1 Juni, 2000 na
Wamen’s Learning Partnership.
Sehemu ya Kwanza: Kukuza Unafsi kwa ajili ya Kufikia Uongozi
31
Maswali ya Majadiliano
·  Jinsi gani Asma Khader anafafanua uongozi?
·  Ni aina gani za sifa na ujuzi alizo nazo zinazomfanya kuwa kiongozi?
·  Jinsi gani Asma Khader amefikia kuwa kiongozi? Je uongozi wake unatokana
na sifa zake binafsi? Au kutokana na matatizo anayokumbana nayo? Au
kutokana na hali zote mbili? Je kuna vitu vingine viilinavyochangia?
·  Ni kitu gani kilichomsukuma mama huyu kwenda ofisini mwa Mama Asma
Khader? Mchango gani mama huyu ameutoa maishani mwa Asma Khader?
·  Je Asma Khader ndiye kiongozi pekee katika kisa hiki? Kwa nini unafikiri
hivyo?
·  Je kiongozi naye anaweza kuwa mfuasi? Kwa njia gani?
Maswali ya Kuzungukia Kundi
·  Mpe nafasi kila mshiriki kueleza kwa kifupi:
Jinsi gani unaweza kufafanua uongozi? Ni sifa gani anazopaswa kuwa
nazo kiongozi mzuri?
Uchunguzi
·  Umejisikiaje ulipozungukia kundi ukiuliza kila mshiriki atoe maoni yake?
Umetumia njia hii ya kuzungumza bila kusikia wasiwasi wo wote?
·  Je lipo jambo lo lote lillilokushangaza katika mazungumzo hayo?
·  Je uandikaji wa maoni muhimu ubaoni wakati wa majadiliano kumeyaboresha
au kumeyadhoofisha?
·  Kama ungekuwa unasimamia majadiliano ya leo, ungefanya nini kuhimiza
ushiriki wa wanakikundi wote?Ingelikuwa ni wewe kiongozi wa mazungumzo
ya leo, ungefanya je kwa ajili ya kusisimua washiriki ili kila mmoja alete
maoni yake?
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
32
Maswali ya Tathmini ya Semina.
Msimamizi au mshiriki aliyejitolea aandike mambo muhimu yanayozungumzwa ubaoni
au kwenye karatasi kubwa wakati wa majadiliano ya kundi juu ya haya yafuatayo:
·  Matokeo gani ungependelea kuwa umeyapata wakati unafikia mwisho wa vikao
12 vya semina hii?
·  Je una maswali au hoja yo yote juu ya muundo na utaratibu utakafuatwa katika
vikao vya semina hii?
·  Je ni huwa ni rahisi au vigumu kwako kushiriki majadiliano ya kundi? Je, kuna
njia ambazo msimamizi au washiriki wengine wanaweza kusaidia wanakundi
wengine kujenga moyo wa kujiamini wa kueleza maoni yao?
·  Ni masuala gani mahususi ya uongozi ungependelea yajadiliwe kwenye vikao
12 vijavyo?
Pendekezo: Unawaza kuwaeleza washiriki kuleta majibu yao kwa maandishi au, njia
nyingine, unaweza kuandika majibu yao kwenye karatasi kubwa ya kuning’iniza.
Washiriki warudushiwe majibu yao wakati wanapotathmini semina katika Kikao cha 12
ili yawawezeshe kupima jinsi gani welewa wao juu ya uongozi umebadilika katika kipindi
hiki cha vikao 12.
Maelekezo ya Kikao Kinachofuata
Mnamo wiki ijayo, fikirieni juu ya mwanamke ambaye amewahi kutambua shida fulani
ndani ya jamii yako kama kiongozi. Mwanamke huyo anaweza kuwa mtu maarufu
kama vile mwanasiasa au mtu wa kawaida tu---mtu aliyeona na kutambua tatizo fulani
katika maisha yake au maisha ya jamii yake na akajaribu kulitafutia suluhisho. Kwa
maneno mengine, unaweza kukuta kwamba kiongozi wa aina hii ni mmoja wa
wanafamilia yako au mmoja kati ya rafiki zako. Jiandae kutoa maelezo mafupi (dakika
3 hadi 5) mbele ya kundi juu ya kisa cha kiongozi huyo katika kikao kijacho. Weka
mkazo kwenye changamoto ambazo kiongozi huyu alikumbana nazo na pia juu ya
utendaji na ujuzi aliouonyesha katika kutatua matatizo.
33
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
34
_______________________________________________________________
Uongozi ni :
Kuhusisha Watu wa Jinsia zote: Kiukweli ingefaa wanaume na
wanawake kushirikiana katika kufasili, kushughulika pamoja, na utimizaji
wa shabaha ambazo zitakuwa faida kwao wote.
Mawasiliano: Kila mmoja anayo maoni na kila pendekezo analotoa ni
tendo la uongozi.
Kuwa na lengo: Kufasili na kufafanua lengo ni kushiriki kikamilifu katika
shughuli nzima ya kujifunza. Wakati huo huo ni kushiriki katika utumiaji wa
madaraka.
Demokrasia na Usawa: Katika jumuia ambamo wote hupewa nafasi ya
kushiriki na kuwasiliana, washiriki huheshimiana na kuthaminiana kama
binadamu kamilifu.
Kutambua Njia Sahihi: “ Lengo halihalalishi njia ya kulifikia” ni kanuni ya
kimaadili inayojulikana sana duniani kote. Kanuni hii ina maana ya kwamba
watu waadilifu huwa hawatumii njia zisizo halali kufikia lengo hata kama ni
la muhimu au haraka kiasi gani.
“Misingi ya Ujenzi wa Uongozi”
35
KIKAO CHA PILI
Jinsi Gani Mimi ni Kiongozi Katika Maisha
Yangu Mwenyewe?
Shabaha za Kikao
§ Kuchunguza aina za mazingira au matukio zinazochochea au
kuleta msukumo wa uongozi.
§ Kuchunguza maadili ya uongozi bora na sifa ambazo ni kilelezo
thabiti cha uadilifu wa kiongozi.
§ Kutafakari na kuzingatia umuhimu wa jinsia na maumbile ya
kike/kiume katika mitindo ya uongozi na malengo ya viongozi.
Kwa watu wengi, maumbile ya kike/kiume ni tofauti ya kuzaliwa
kati ya mwanamke na mwanaume wakati jinsia inamaanisha hali
za kitabia, kitamaduni, na kisaikolojia ambazo zimejengwa katika
jamii na kuhusishwa na ama wanawake au wanaume.
§ Kufahamishana ni lini na kwa vipi washiriki wa semina
wametokea kujikuta wenyewe wakiwa katika shughuli za
uongozi.
Mapendekezo ya Usimamizi
Mwishoni mwa Kikao cha kwanza, ulihitajika kufikiria juu ya mwanamke
mmoja ambaye unamfikiria kuwa kama kiongozi. Katika kikao hiki, kila
mshiriki anahitajika kuwaeleza wengine kisa chake juu ya kiongozi
anayemvutia sana. Kiongozi huyu anaweza kuwa kiongozi wa kawaida
kama vile mwanasiasa au mwanamke wa kawaida tu katika maisha ya kila
siku---ndani ya familia, marafiki, au sehemu za kazi. Weka mkazo katika
changamoto ambazo kiongozi huyu alikumbana nazo na pia sifa na ujuzi
ambao aliuonyesha katika kutafuta suluhisho la matatizo aliyokuwa
akiyashughulikia. Maelezo mafupi yatasaidia kutoa nafasi ya kutosha kwa
ajili ya maswali ya majadiliano ambayo yanafuatia katika zoezi la “Mifano
ya Kuigwa katika Uongozi”.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
36
Katika zoezi la pili, ”Je Jinsia Huleta Utofauti?”, mazungumzo mawili yanayokaribiana
kufanana yanatokea: ya kwanza ni kati ya wanawake wanne na ya pili kati wanaume
wanne. Shabaha ya zoezi hili ni kulinganisha majibu ya washiriki kuhusu mazungumzo
haya na kuchunguza kwa jinsi gani jinsia inaweza kuchangia katika mitazamo ya watu
juu ya madaraka na uongozi ndani ya familia na jamii zao.
SIFA NA UJUZI WA MAHUSIANO YALIYOSAIDIA
VIONGOZI VIONGOZI
Njia nzuri ya usimamizi wa kikao hiki ni kugawa washiriki katika vikundi
vidogo vidogo au wawili wawili. Wakati washiriki wakisimulina visa vya
uongozi, wale waliojitolea wanaweza kuandika ubaoni au kwenye karatasi
kubwa ya kuning’iniza haya yafuatayo:
(1)sifa na ujuzi ulioonyeshwa na viongozi, na (2) aina za mahusiano
yanayosaidia (k.m. familia, marafiki, majirani, wafanyakazi/wanafunzi
wenzake) ambazo zilisaidia viongozi kufikia na kutimiza malengo yao.
37
Zoezi: Mifano ya Kuigwa Katika Uongozi
Ruhusu muda wa saa moja hivi kwa zoezi hili.
Baada ya kila mshiriki kutoa maoni yake juu ya kiongozi aliyevutiwa naye,
zingatia maswali haya:
·  Je, kuna mada, hali au mazingira yanayofanana ambayo yamejitokeza
katika visa vingi? Ni aina gani za matukio zilizowachochea wanawake
kuchukua hatua?
·  Ni sifa na ujuzi gani ambao wengi wa wanawake walikuwa nao?
·  Je, sifa za uongozi ziliweza kujitokeza zenyewe kwa sababu ya
matatizo ambayo wanawake walikumbana nayo? Au, wanawake hao
tayari walikwishakuwa na sifa za uongozi tokea zamani?
·  Jukumu gani ambalo mahusioano yanayosaidia, jumuia, mashirika
na/au watu binafsi walikuwa nalo katika kusaidia wanawake viongozi
hawa kufikia malengo yao?
·  Je, unakumbuka jinsi gani ulivyoweza kupata suluhisho la tatizo
maishani mwako? Ni sifa na ujuzi gani ulitumia kutatua tatizo hilo?
Jukumu gani mahusiano ya kusaidia yalikuwa nalo katika kukabiliana
na kupata ufumbuzi wa tatizo lako? Ulichukua hatua gani?
·  Je, hatua zote unazochukua katika kutatua tatizo, liwe la binafsi au la
kijamii, ni lazima lihalalishwe? Je hatua anazochukua kiongozi
zinahitaji zionyeshe “maadili ya hali ya juu”, au tatizo lenyewe
linaloshughulikiwa linatosheleza kuhalalisha hatua yo yote?
·  Ni sifa zipi za uongozi unazofikiria kuwa unazo? Ni sifa gani nyingine
zaidi za uongozi unatamani ungekuwa nazo?
·  Je, kuna vipingamizi ndani ya familia au matarajio ya jamii ambayo
yanakuzuia kufikia lengo lako la kuwa kiongozi?
·  Ni mbinu gani unaweza kuzitumia kukwepa vizuizi hivi?
·  Ni hatua gani unaweza kuzichukua ili kujipa moyo wewe mwenyewe au
kuwahimiza wengine (marafiki, wafanyakazi/wanafunzi wenzako,
wanafamilia) kukuza na kuendeleza sifa za uongozi?
·  Je, unajisikia kuwa na wajibu wa kibinafsi kushughulikia tatizo lo lote la
kijamii?
·  Je, unaweza kujiona wewe mwenyewe kama kiongozi? Kwa nini ujione
au usijione hivyo?
·  Je, unafikiri wengine wanaweza kukuona kama kiongozi?
Katika juma lijalo, tieni maanani sifa hizo za uongozi ambazo mnapendelea
kuimarisha, na jaribu kuziweka katika matendo angalau mara moja.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
38
Zoezi : Je Jinsia Inaweza Kuleta Tofauti?
Ruhusu muda wa dakika arobaini na tano hivi kwa zoezi hili.
Omba watu wa kujitolea kutoka katika kundi ili kila mmoja asome
mojawapo ya uhusika katika maonyesho mawili yaliyo hapo chini. Jadili
umuhimu wa jinsia katika maongezi ya wahusika, na jinsi umuhimu huo
unavyojenga mitazamo yako juu ya msimamo wa kijamii, uadilifu, na
madaraka ya wahusika. Maswali yanayofuatia yanaweza kusaidia
kuongoza mjadala.
Onyesho la Kwanza
Wahusika: Almaz, Insaf, Lena, Farah, na msimuliaji.
Msimuliaji: Ni siku ya kawaida saa za mchana na hali ya hewa ni nzuri mjini.
Wanawake wanne wamekaa pamoja chini ya kivuli cha mti. Insaf ndiye mwenye umri
mkubwa kuliko wenzake. Leo amefikisha umri wa miaka sitini na mpwa wake, Lena,
amekuja kumtembelea nyumbani kwake. Farah ni mtumishi wa Insaf kwenye duka lake
la vyakula, na Almaz,ambaye ni mshiriki kwenye masuala ya siasa na amechaguliwa
kwenye halmashauri ya mji, ni rafiki mkubwa wa Farah.Wanawake hawa wanakula mlo
wa mchana na kuongea.
Almaz: Insaf,mpwa wako ni mwerevu na ni mwenye kuvutia ! Je, huwa unajuta kwa
kukosa familia?
Insaf: Lakini si mrembo sana! Na sijawa na umri mkubwa sana wa kutopata familia!
Muulize Farah. Akina baba na akina mama huja dukani kwangu kila wakati na
kunipendekeza nifanye mapenzi na wanao…na haya na yale. Sipendi kuolewa, na
ninajisikia raha tu kwa jinsi nilivyo.
Lena: Ondoka shangazi! Sasa umekuwa mzee sana, umepita umri wa kuolewa.
Mwanamume ye yote yule atakayekutaka wewe kwa vyo vyote atakuwa mbaya na
mzee.
Almaz: Sio kweli, Lena. Shangazi yako ni mwanamke tajiri. Ninafahamu wanaume
wengi ambao wangefurahi sana kumchukua kama mke wao. Utakuwa na bahati
ukitokea kupendwa sana kama yeye.
Lena: Nina hofu kubwa kwa kuwa ninafanana na shangazi yangu.Nami pia sitaki
kuolewa. Wanaume ni mzigo mkubwa na wanakula tu na kula na kutumia pesa.
Wanapenda kuzaa watoto wengi. Mimi ninapenda uhuru wangu. Zaidi ya hayo, itakuwa
vigumu mimi kuendelea na masomo yangu iwapo nitajikuta nina jukumu la kutunza
mume na watoto.
Farah: Kwa kweli Lena wewe ni binti mwerevu. Elimu yako unaipa nafasi ya kwanza.
Nitizame mimi. Ninapaswa kumtunza mume wangu ambaye ni mgonjwa. Ninafanya kazi
kwa bidii kila siku katika duka la shangazi yako na ninafikiri ninachapa kazi kweli kweli.
Insaf: Hapana shaka, kweli u mchapa kazi.
Farah: Lakini sina njia yo yote ninavyoweza kujiendeleza kwa kuzingatia elimu yangu
ndogo. Ijapokuwa ninaweza kusoma na kuandika vizuri kwa kiasi cha kutosha kufanya
kazi katika duka, sina budi niridhike na hali niliyo nayo. Na ninamshukuru sana Insaf
kwa kunipa kazi hii, na pia kuwa mtu anayeelewa hali yangu kwa kunivumilia
ninapolazimika kufanya masaa machache kwa siku au kutofika kazini kabisa ili
kumhudumia mume wangu.
39
Almaz: Sikiliza jinsi wanawake hawa wanavyozungumzia kuhusu wanaume na kazi.
Ninampenda mume wangu na mabinti zangu wawili. Kuwa na familia na kuihudumia
vizuri ndivyo maisha yanavyostahili kuwa.
Farah: Ah, Almaz, unayasema hayo sasa wakati mabinti zako wakiwa bado wadogo.
Wewe subiri tu wafikie umri wa kuolewa na kuondoka nyumbani kwako. Hawatakuwepo
tena kukutunza katika uzee wako. Watakuwa wanawashughulikia na kuwatunza waume
na watoto wao. Mtoto wangu wa kiume? Ni tunu, ni zawadi kubwa.
Almaz: Mabinti zangu pia ni baraka kwangu! Wanasaidia sana shughuli za nyumbani na
wanahudumia vizuri maafisa wa serikali inapotokea kuwaalika nyumbani kwangu
kuzungumza mambo ya siasa wakati mume wangu anapokuwa ameondoka kwenda
kuwatembelea wazazi wake.
Lena: Ha ha! je, unawafunza kufuata nyayo zako katika mambo ya siasa?
Almaz: Inawezekana…(Pumzi ya nguvu) Lakini unajua, siasa ni shughuli inayoweza
kugeuka kuwa mbaya. Nisingependa mabinti zangu wajikute wanaonja yale yaliyonipata
katika shughuli ya mambo ya kisiasa. Halmashauri ya mji ni mahali ambapo wanawake
wananyanyaswa sana.
Insaf: Almaz, inaelekea unaota. Mabinti zako hawatatokea kamwe wakachaguliwa
kuingia kwenye halmashauri ya mji. Unafikiri ni nani atakayewapa kura? Wewe ulishinda
uchaguzi kwa sababu tu baba yako alipigana vitani na kurejea kama shujaa. Wanaume
hawawezi kuwapa kura, na wanawake watapiga kura jinsi waume zao wanavyotaka
wafanye.
Almaz: Wewe ni mwanamke mzee uliyepitwa na wakati. Mambo yanabadilika. Utaona
mwenyewe. Kuna nafasi nyingi ambazo mabinti zangu wanaweza kuzitumia kuchangia
katika mambo ya siasa. Wana mawazo na maoni mengi tu juu ya njia za kuboresha mji,
na hasa jumuia ya wafanyabiashara.
Farah: Almaz rafiki yangu, sasa unaanza kukosa heshima kwa mama huyu mwenye
busara na heshima kubwa. Basi, ninafikiri haya maongezi yaishie hapa. Haya, hebu sote
tumtakie Insaf mema katika siku yake ya kuzaliwa, na baraka na fanaka katika mwaka
mpya.
Lena, Farah, na Almaz: Ndiyo, ndiyo, ndiyo!!
Onyesho la Pili
Wahusika: Muhammed, Adnan, Amir, Faisal, na mwenye msimuliaji.
Msimuliaji: Ni siku ya kawaida saa za mchana na hali ya hewa ni nzuri mjini. Wanaume
wanne wamekaa pamoja chini ya kivuli cha mti. Adnan ndiye mwenye umri mkubwa
kuliko wenzake. Leo amefikisha umri wa miaka sitini na mpwa wake, Amir, amekuja
kumtembelea nyumbani kwake. Faisal ni mtumishi wa Adnan kwenye duka lake la
vyakula, na Muhammed,ambaye ni mshiriki kwenye masuala ya siasa na
amechaguliwa kwenye halmashauri ya mji, ni rafiki mkubwa wa Faisal.Wanaume hawa
wanakula mlo wa mchana na kuongea.
Muhammed: Adnan,mpwa wako ni mwerevu na ni mtanashati! Je, huwa unajuta kwa
kukosa familia?
Adnan: Lakini si mtanashati sana! Na sijawa na umri mkubwa sana wa kutopata familia!
Muulize Faisal. Akina baba na akina mama huja dukani kwangu kila wakati na
kupendekeza nifanye mapenzi na mabinti zao…na haya na yale. Sipendi kuoa, na
ninajisikia raha tu kwa jinsi nilivyo.
Amir: Ondoka mjomba! Sasa umekuwa mzee sana, umepita umri wa kuoa. Mwanamke
ye yote yule atakayekutaka wewe kwa vyo vyote atakuwa mbaya na mzee.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
40
Muhammed: Sio kweli, Amir. Mjomba wako ni mwanamume tajiri. Ninafahamu
wanawake wengi ambao wangefurahi sana kuchukuliwa naye kama mume wao.
Utakuwa na bahati ukitokea kupendwa sana kama yeye.
Amir: Nina hofu kubwa kwa kuwa ninafanana na mjomba wangu. Nami pia sitaki kuoa.
Wanawake ni mzigo mkubwa na wanakula tu na kula na kutumia pesa. Wanapenda
kuzaa watoto wengi. Mimi ninapenda uhuru wangu. Zaidi ya hayo, itak uwa vigumu mimi
kuendelea na masomo yangu iwapo nitajikuta nina jukumu la kutunza mke na watoto.
Faisal: Kwa kweli Amir wewe ni kijana mwerevu. Elimu yako unaipa nafasi ya kwanza.
Nitizame mimi. Ninapaswa kumtunza mke wangu ambaye ni mgonjwa. Ninafanya kazi
kwa bidii kila siku katika duka la mjomba wako na ninafikiri ninachapa kazi kweli kweli.
Adnan: Hapana shaka, kweli u mchapa kazi.
Faisal: Lakini sina njia yo yote ninavyoweza kujiendeleza kwa kuzingatia elimu yangu
ndogo. Ijapokuwa ninaweza kusoma na kuandika vizuri kwa kiasi cha kutosha kufanya
kazi katika duka, sina budi niridhike na hali niliyo nayo. Na ninamshukuru sana Adnan
kwa kunipa kazi hii, na pia kuwa mtu anayeelewa hali yangu kwa kunivumilia
ninapolazimika kufanya masaa machache kwa sik u au kutofika kazini kabisa ili
kumhudumia mke wangu.
Muhammed: Sikiliza jinsi wanaume hawa wanavyozungumzia kuhusu wanawake na
kazi. Ninampenda mke wangu na mabinti zangu wawili. Kuwa na familia na kuihudumia
vizuri ndivyo maisha yanavyostahili kuwa.
Faisal: Ah, Muhammed, unayasema hayo sasa wakati mabinti zako wakiwa bado
wadogo. Wewe subiri tu wafikie umri wa kuolewa na kuondoka nyumbani kwako.
Hawatakuwepo tena kukutunza katika uzee wako. Watakuwa wanawashughulikia na
kuwatunza waume na watoto wao. Mtoto wangu wa kiume? Ni tunu, ni zawadi kubwa.
Muhammed: Mabinti zangu pia ni baraka kwangu! Wanasaidia sana shughuli za
nyumbani na wanahudumia vizuri maafisa wa serikali inapotokea kuwaalika nyumbani
kwangu kuzungumza mambo ya siasa wakati mke wangu anapokuwa ameondoka
kwenda kuwatembelea wazazi wake.
Amir: Ha ha! je, unawafunza kufuata nyayo zako katika mambo ya siasa?
Muhammed: Inawezekana…(Pumzi ya nguvu) Lakini unajua, siasa ni shughuli
inayoweza kugeuka kuwa mbaya. Nisingependa mabinti zangu wajikute wanaonja yale
yaliyonipata katika shughuli ya mambo ya kisiasa. Halmashauri ya mji ni mahali pabaya
zaidi kwa wanawake. Wanawake wananyanyaswa sana.
Adnan: Muhammed, inaelekea unaota. Mabinti zako hawatatokea kamwe
wakachaguliwa kuingia kwenye halmashauri ya mji. Unafikiri ni nani atakayewapa kura?
Wewe ulishinda uchaguzi kwa sababu tu baba yako alipigana vitani na kurejea kama
shujaa. Wanaume hawawezi kuwapa kura, na wanawake watapiga kura jinsi waume
zao wanavyotaka wafanye.
Muhammed: Wewe ni mwanamume mzee uliyepitwa na wakati. Mambo yanabadilika.
Utaona mwenyewe. Kuna nafasi nyingi ambazo mabinti zangu wanaweza kuzitumia
kuchangia katika mambo ya siasa. Wana mawazo na maoni mengi tu juu ya njia za
kuboresha mji, na hasa jumuia ya wafanyabiashara.
Faisal: Muhammed rafiki yangu, sasa unaanza kukosa heshima kwa baba huyu
mwenye busara na heshima kubwa. Basi, ninafikiri haya maongezi yaishie hapa. Haya,
hebu sote tumtakie Adnan mema katika siku yake ya kuzaliwa, na baraka na fanaka
katika mwaka mpya.
Amir, Faisal, na Muhammed: Ndiyo, ndiyo, ndiyo!!
41
Maswali ya Majadiliano
·  Je mazungumzo yaliyofanyika katika maonyesho hayo mawili
yanaaminika? Ni mambo gani katika kila onyesho hayawezi kuaminika na
kwa nini?
·  Je, unaamini kwamba yule mwanamke mzee, Insaf, anaweza kupata
mchumba? Kwa nini hivyo au kwa nini sivyo? Je, unaamini yule
mwanamume mzee, Adnan, anaweza kuoa? Kwa nini hivyo au kwa nini
sivyo? Je, umri wao, hali yao kifedha, na/au jinsia vina umuhimu wo wote?
Je, ni jambo kuweka maanani kwamba Insaf amepita umri wa kuzaa?
·  Ni ushauri gani unaweza kumpa Lena, mpwa wa Insaf, na Amir, mpwa wa
Adnan, kuhusu kuyapa maisha ya ndoa/familia na elimu/kazi uzito ulio
sawa? maisha ya kazi? Je ushauri wako utakuwa tofauti kati yao? Kwa nini
hivyo au kwa nini sivyo?
·  Kama ungekuwa katika nafasi ya Almaz, mama mwanasiasa, ni kwa jinsi
gani ungejaribu kuwa mfano wa kuigwa kwa mabinti zako? Ni kwa jinsi gani
ungewashauri juu ya kuwa viongozi bora na wakati huo huo kuwa
wanawake wenye msimamo?
·  Kama ungekuwa katika nafasi ya Muhammed, baba mwanasiasa, ni kwa
jinsi gani ungejaribu kuwa mfano wa kuigwa kwa mabinti zako? Je kuna
mafunzo na mifano inayopaswa kutolewa kwa watoto wa kike tofauti na
watoto wa kiume?
·  Je, wanawake na wanaume huonyesha mifano ya utendaji na mitindo
tofauti katika uongozi? Ni mambo gani thabiti na dhahifu kwa kila upande?
Je, zipo njia zo zote ambamo wanawake wanaweza kuwa viongozi bora
kuliko wanaume? Je, zipo njia zo zote ambamo wanaume wanaweza kuwa
viongozi bora kuliko wanawake?
·  Ni kwa jinsi gani uzoefu wa kila siku katika maisha ya wanawake
unachangia katika maadili na malengo wanayoyaleta katika uongozi wao?
Ni kwa jinsi gani uzoefu wa kila siku katika maisha ya wanaume
unachangia katika maadili na malengo wanayoyaleta katika uongozi wao?
·  Je, unapendelea kufanya kazi chini ya mamlaka ya mwanaume au ya
mwanamke?Je, kuna tofauti kati ya mambo hayo mawili? Unafikiri kwamba
mameneja/wakubwa wa kazi wanawake wanaweza kujali sana mahitaji na
matatizo ya wanawake? Kwa nini hivyo au kwa nini sivyo
·  Je, utaunga mkono mgombeaji mwanamke wa nafasi ya siasa katika jamii
yako? Kwa nini? Je, unafikiri kwamba wanasiasa wanawake wanaweza
kujali sana mahitaji na matatizo ya wanawake? Kwa nini hivyo au kwa nini
sivyo?
·  Unafikiri idadi ya wanawake katika timu ya uongozi (kwa mfano: Kamati ya
uongozi wa shule, Baraza la usimamizi wa biashara, au Halmashauri ya
mji), inaathiri utendaji wake? Ni wanawake wangapi waahitajika katika timu
ili kuleta mabadiliko? Je, asilimia 2% inaweza kuleta mabadiliko? 10%,
33%, 50%?…au asilimia nyingine? Kwa nini hivyo au kwa nini sivyo?
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
42
______________________________________________________________
Maono ni zaidi ya kuweka lengo.
Maono ni pamoja na picha, fikira na 7mawazo mazuri juu ya kazi
tunayoifanya
ambavyo tungependa iwe iwapo tutaifanya kwa ufanisi.
“Misingi ya Ujenzi wa Uongozi”
43
KIKAO CHA TATU
Maono Yangu ni Yapi?
Shabaha za Kikao
§ Kujadiliana juu ya maono ya binafsi ni nini.
§ Kuangalia jinsi gani maono ya kibinafsi yanavyomsukuma
mwanamama kuwa kiongozi.
§ Kutambua uwezo wa kufanya mambo yakuonekana au ya ujumbe
ambao unaeleza maono ya kipekee.
§ Kuangalia jinsi ya kuweka maono ya kipekee katika maneno na
vitendo.
Mapendekezo ya Usimamizi
Soma kwa sauti kisa kifuatacho hapo chini juu ya maono ya Muhammad Yunus
kuhusu kuleta mabadiliko ya haki za kijamii na uchumi nchni Bangladesh
kupitia mikopo midogo ya benki. Jadili katika vikundi juu ya tatizo la kifedha
alilolibaini miongoni mwa watu maskini, na hasa miongoni mwa wanawake, na
maono aliyokuwa nayo kuhusu kulirekebisha. Baada ya kikundi kujibu maswali
yanayofuatia kisa cha Muhammad Yunus, wape washiriki nafasi ya kueleza
maono yao wenyewe ambayo yameleta mabadiliko. Zoezi hili limewekwa ili
kuwasaidia washiriki kueleza kwa usahihi maono yao ya kibinafsi.
Kuwagawa washiriki kwenye makundi madogo madogo katika zoezi hili
kunaweza kusaidia kujisikia huru zaidi kuelezana maono yao ya kibinafsi.
Angalia Kiambatisho B kwa taarifa zaidi juu ya mbinu hii ya usimamizi
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
44
Siionii Sababu ya Mttu ye yotte Kattiika Duniia Hiiii Kuwa
Maskiinii
Muhammad Yunus: Mchumi
Muhammed Yunus alirejea Banglandesh akitokea Marakeni miezi tisa
baada ya nchi yake kupata uhuru mwaka 1971. Wakati alipokuwa mwalimu
wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Chittagong, huko nchini mwake
wenzake walikuwa wakiteseka kutokana na vita na njaa---ukweli ambao
uliondosha imani yake ya kutatua matatizo kutokea ndani ya darasa.
Aliamua kuzungumza na watu kutoka kijiji cha jirani na chuo kikuu hicho ili
aweze kuelewa matatizo yao ya kila siku.
Yunus alikutana na mwanamke ambaye alikuwa anatengeneza viti vya
mwanzi, na ilikuwa ni hali ya kutatanisha ya mama huyo iliyomwelekeza
Yunus kuanza kuangalia upya chanzo cha umaskini. Mwanamke huyo
hakuwa na pesa za kununulia mianzi na hivyo alilazimika kukopa pesa
kutoka kwa mfanyabiashara ambaye baadaye alinunua viti vyake kwa bei
aliyopanga mwenyewe. Akiwa ameishashawishika kumpa mwanamke huyo
senti ishirini alizotaka ili kununulia mwanzi, Yunus alibadilisha mawazo na
kubuni mradi mkubwa ambapo alimwomba mwanafunzi mmoja
kuorodhesha wanakijiji wote waliokuwa wanahitaji pesa. Kwa mshangao
watu arobaini na wawili wachapa kazi walikuwa wanahitaji jumla ya dola
ishirini na saba ili waweze kuuza vitu vyao walivyvitengeneza kwa bei nzuri.
Kwa kuwakopesha pesa wanakijiji na kuwaruhusu wamlipe wakati
wanaoona unafaa, jambo hili lilimtia moyo Yunus kutafakari zaidi jinsi gani
angeweza kuendelea kuwasaidia. Aliamua kumshawishi meneja wa benki
iliyokuwa katika kampasi ya chuo kikuu kuwakopesha pesa wanakijiji, lakini
meneja alikataa kwa sababu aliwaona watu maskini, na hasa wanawake
maskini, kama watu wasioweza kuaminika kurudisha mikopo.
Kwa ujasiri mkubwa, Yunus alianzisha benki yake mwenyewe, Benki ya
Grameen, mnamo mwaka wa 1983, akiwa na msaada wa kipesa na kibali
cha serikali. Benki ya Grameen ilianza kutoa mikopo ya biashara kwa watu
maskini, na hasa kwa wanawake. Kuwashawishi wakubali na kuona faida
ya kuchukua mikopo ni kitu kilichohitaji uvumilivu. Kikwazo kimojawapo ni
kwamba mwanamume hakuruhusiwa kuzungumza na mwanamke
hadharani. Mwanzoni,wanawake walikuwa wakisisitiza kuwa wao
hawakuwa na wazo lo lote juu ya kitu gani cha kufanya na kwamba benk i
itoe pesa hizo kwa waume zao. Taratibu, Yunus aliweza kuwashawishi
kukopa pesa katika makundi ya watu watano watano na kuanzisha
biashara yao ndogo. Wanawake waliotangulia kuchukua mikopo, nao pia
waliwashawishi na kuwahimiza wenzao wengine kuchukua mikopo.
Wanawake hawa walipomaliza kulipa mikopo, walitambua kuwa walikuwa
na uwezo wa kujitunza wao wenyewe pamoja na familia zao.
Wakati miradi wa misaada na mashirika yasiyokuwa ya kiserekali katika
mbalimbali yameiga mfano wa Benki ya Grameen,Yunus anaendelea
kuwakumbusha wale wenye wasiwasi kwamba, ”umaskini hauletwi na
watu maskini…[lakini] unaletwa na asasi ambazo tumejiundia sisi
wenyewe. Tunapaswa kurudia upya kwenye ubao wa kuchorea kufikiria na
45
kuunda upya asasi hizo ili ziachane na ubaguzi dhidi ya watu maskini
kama zinavyofanya sasa.” Kazi ya Yunus ya kutokomeza umaskini sasa
imechukua umbo la kiulimwengu na imetanda duniani kote. Yeye anasema,
“Ni jukumu la jamii zote kuhakikisha kila mwanajamii wake anaheshimiwa
na kupatatiwa haki za binadamu …Tunazungumzia haki za binadamu,
lakini hatujengi uhusinao katika haki za binadamu na umaskini
…Tukianzisha asasi ambazo zina uwezo wa kutoa mikopo ya biashara
kwa maskini ambapo watajiajiri wenyewe, wataona mafanikio yale yale
kama ambayo sisi watu wa Bangladesh tumeona. Sioni sababu ya mtu ye
yoye duniani kuwa maskini.”12
Muhammad Yunus ni mwanzilishi wa Benki ya Grameen. Leo hii, Grameen ina matawi katika vijiji
36,000 nchini Bangladesh, ina watu milioni 2.1 waliochukua mikopo, na inaajiri watumishi 12,000.
Programu zilizoiga mtindo wa Grameen zinakutwa katika nchi 56. Kuanzia miaka wa 1990, Benki
ya Grameen imepanua huduma zake zaidi ya huduma ya benki, ambazo ni pamoja na ugavi wa
umeme, huduma za mtandao wa kompyuta, na mawasiliano ya simu za mkononi ikiwa ni sehemu
ya juhudi zake za kuwapa madaraka wanavijiji wa nchini Bangladesh.
Maswali ya Majadiliano
·  Nini vitu gani vilivyomsukuma Muhammad Yunus kujenga maono yake? Ni tatizo
gani lililopo linalowasumbua watu hao maskini aliodhamiria kushughulikia shida
zao?
·  Ni ufumbuzi gani alioweza kubaini? Ni imani gani kuhusu hali halisi ya binadamu
iliyomsikuma Yunus?
·  Yunus anaonaje jukumu lake katika utekelezaji wa ufumbuzi huu? Ni sifa zipi za
uongozi zinajitokeza kwa Yunus katika jitihada zake za kutokomeza umaskini?
Unafikiri ameonyesha uongozi unaoendeshwa kwa misingi bora?
·  Je, unafikiri mwanamke angeweza kufikia mafanikio sawa na ya Yunus? Kwa nini
hivyo au kwa nini sivyo? Je, wewe ungefanya nini ikiwa ungejikuta katika hali
kama hiyo?
·  Je katika kauli za Yunus zilizo hapo juu zinaeleza kwa usahihi tatizo lenyewe,
ufumbuzi wake, na wajibu wake mwenyewe katika kile anachopendekeza? Je,
maneno yake yamebeba kauli ya kushawishi ya maono? Kwa nini hivyo au kwa
nini sivyo?
·  Je, maono ya Yunus yalibadilika kadri siku zilivyopita? Je, ilikuwa ni muhimu
kwamba maono yake yabadilike?
·  Je, unafikiri kwamba maono ya Yunus juu ya mikopo ni mahususi kwa wanawake
tu? Kwa nini hivyo au kwa nini sivyo?
·  Ni ujuzi gani wa wanawake unaoelezwa kuhusiana na tukio hilo la Benki ya
Grameen? Je, ujuzi wa ina hii unawasaidia wanawake kuachana kabisa na
majukumu au misingi ya maarifa yao ya kiasili?
12 Habari hii juu ya Muhammad Yunus na the Grameen Bank imechukuliwa kutoka “Muhammad Yunus,
Grameen Bank,” katika Michael Collopy and Jason Gardner, ed., Architects of Peace: Visions of Hope in
Words and Images, Navato, CA: New World Library, 2000, p. 77 and http://www.grameen.org/.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
46
·  Ni aina gani ya mikopo inayoweza kusaidia kuimarisha si uwezo wa kiuchumi tu
wa wanawake, bali pia inayoweza kuwasaidia kupata madaraka na kuimarisha
majukumu yao katika jamii zao
·  Je kauli ya maono ya Yunus imesaidia kufafanua shabaha zake wazi?
·  Neno “maono” linamaanisha nini kwako?
·  Kwa kauli (maelezo thabiti) ya maono ni muhimu?
Zoezi: Kujenga Kauli ya Maoni ya Binafsi
Ruhusu muda wa dakika arobaini na tano hivi kwa zoezi hili.
1.Gawa kundi katika makundi madogo madogo ya watu wawili wawili au watatu
watatu ili wajadili juu ya haya yafuatayo: baini mazingira, hali au tatizo katika
familia au jamii yako ambalo unafikiri ungependelea kuleta mabadiliko. Ni
mabadiliko gani ungependa kuona ili kurekebisha mazingira, hali, au tatizo?
2. Kila mwanakikundi katika kikundi anawaambia wenzake kwa dakika moja au
mbili jinsi ambavyo angefanya kuongoza au kushiriki katika utekelezaji wa
ufumbuzi ambao ameueleza.
3. Kila mshiriki ataandika kwa kifupi maelezo ---katika sentensi moja au mbili---
ambayo yanaeleza maono yake kuhusu jukumu lake mwenyewe katika kuleta
mabadiliko yanayohitajika ambayo ameyabaini.
4. Washiriki wote kwenye semina wanarudi kwenye mkao wa mzunguko. Kuanzia
na msimamizi, kila mtu anasoma kauli yake kwa sauti mbele ya wengine.
Mwisho wa zoezi, Msimamizi akusanye kauli zote zilizoandikwa kutoka kwa kila
mshiriki. Hakikisha kwamba kila mtu ameandika jina lake katika kauli yake kwa
sababu zitatumika tena katika Kikao cha 7.
Uchunguzi
·  Je, ilikuwa vigumu kuunda maelezo ya kibinafsi? Kwa nini hivyo au kwa nini
sivyo?
·  Je, uundaji huo unasaidia kufafanua wazi shabaha zako mwenyewe?
·  Je, unafikiri kwamba maono yako yatabadilika kadri muda unavyopita? Kwa nini
hivyo au kaw nini sivyo?
·  Ulijisikiaje uliposikiliza maelezo binafsi ya maoni ya washiriki wengine katika
kundi?
·  Kwa nini ni muhimu kuandika maono hayo na /au kuyaeleza kwa washiriki
wengine kwa sauti?
47
48
49
Sehemu ya Pili:
Kuwasiliana na Wengine
Katika vikao vilivyotangulia, tumeona kwamba kipengee muhimu katika uongozi ni uwezo wa mtu
wa kuwasilisha kwa ufanisi ujumbe au maono. Mwanamke aliyekuja ofisini kwa Asma Khader
kuomba msaada aliwasilisha kwa ufanisi matatizo yaliyokuwa yanaikabili familia yake, na hata
ikiwa Khader hakumwona tena yule mwanamke, maneno yake yalimsukuma Khader kuanza
kuchukua jukumu kubwa la kujaribu kusaidia kuleta mabadiliko ya sheria za nchi yake kwa
shabaha ya kulinda haki za wanawake. Mafanikio ya mpango wa uchumi wa wa Muhammad
Yunus yalikuwa yameegemea sana katika uwezo wake wa kuwasilisha mawazo yake kwa watu
wa aina mbalimbali. Yunus alijitahidi kufanya maono yake ya binafsi yaeleweke vizuri na
kukubaliwa na wanawake vijijini pamoja na maafisa wa serikali.
Mazoezi ya sehemu hii yanazingatia vipengee vinavyohusu mawasiliano mazuri, maafikiano, na
usikilivu ambao utasaidia kuboresha uwezo wa mtu kuwa kiongozi. Kazi za pamoja, ushirikiano,
na urafiki vyote uhusisha mawasiliano thabiti baina ya washiriki. Visa na maswali katika sehemu
hii yanaonyesha kwamba usikilivu, maafikiano, na masikilizano mazuri uhusisha uwezo wa
kuzingatia kwa makini tofauti za maoni na mitazamo kwa namna ambayo inaleta manufaa kwa
kila mshiriki.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
50
_________________________________________________
Kuongoza ni Kuwasiliana
Ili uongozi uwepo, tunahitaji angalau watu wawili ambao
Wana uhusiano kwa njia moja au nyingine.
Hakuna awezaye kujifunza katika upweke.
Kwa hiyo uongozi ni aina mojawapo ya mawasiliano.
Upo uhusiano mkubwa kati ya mtu anavyoongoza na anavyowasiliana na
wengine.
“Misingi ya Ujenzi wa Uongozi”
51
KIKAO CHA NNE
Jinsi Gani Tunaweza Kuwasiliana?
Shabaha za Kikao
§ Kuonyesha umuhimu wa mawasiliano katika uongozi bora.
§ Kuzingatia mbinu za ushawishi unapowatia moyo wengine,
kuwafundisha, au kufanya maafikiano nao.
§ Kujadili uhalisi wa maafikiano---au kutafuta suluhu---ikiwa
ni pamoja na faida na hasara zake.
§ Kufanya uchambuzi wa mitindo binafsi ya mawasiliano ya
washiriki.
Mapendekezo ya Usimamizi
Someni kwa sauti kifungu cha habari kifuatacho kilichoandikwa na Marian
Wright Edelman. Zingatia mbimu anazotumia ili kuwashawishi wasomaji wake
kujiunga katika jitihada za kulinda na kutetea maslahi ya watoto nchini
Marekani. Maswali yanayofuatia kifungu hicho yanaweza kuwa kiongozi cha
majadiliano ya kundi. Na baada ya mwaswali ni zoezi liliwekwa ili kuchunguza
mbinu za mawasiliano za kila mtu.
Ni vizuri kundi kujigawa katika makundi madogo madogo ili kuweza
kufanya majadiliano ya kina zaidi juu ya mada hii (Angalia Kiambatisho B
kwa taarifa zaidi juu ya mbinu hii ya usimamizi).
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
52
Niinajjallii na Tena Niiko Tayarrii Kuttoa Huduma
Marian Wright Edelman: Mtetezi wa Haki za Watoto
Kuanzisha chama au umoja sio kazi rahisi. Ni shughuli yenye kukatisha
tamaa, yenye kuvunja moyo, na isiyotabirika. Ni kazi inayotaka moyo wa
uvumilivu na fikira za kina. Inahitaji mtu awe na msimamo usiotetereka juu
ya maono yaliyo dhati na awe na hisia ya wito wa kupambana na kuthubutu
kufanya jambo. Kuanzisha chama kunahitaji nidhamu, umakini, na mipango
ya masafa marefu, lakini wakati huo huo inahitaji utashi wa kushughulikia
mambo haraka na kutumia kila nafasi inayopatikana bila kupoteza muda, na
uwezo wa kuishi na hali isiyokuwa na uhakika na yenye utata.
Kuunda chama kwa ajili ya watoto ni shughuli inayohitaji mtu awe tayari
kupokea maoni ya watu mbalimbali wenye mahitaji, mbinu, matakwa, na
vipaji mbalimbali bila ya kupoteza lengo kuu: Kutomwacha Mtoto Hata
Mmoja Nyuma. Kazi hii inahitaji utashi wa ari na imara ili kuweza kusonga
mbele wakati watu wengine wanakupigia mayowe ya kukukatisha tamaa na
kuweka vizuizi kimoja baada ya kingine njiani mwako, wanajivuta pole pole,
au kututangaza kuwa ni watu tusiozingatia ukweli kisiasa.
Vyama au umoja havijengeki katika muda wa siku moja. Huchukua muda
mrefu. Vyama huwa ni matokeo ya mbegu nyingi zilizopandwa na watu
wengi katika sehemu nyingi kwa muda mrefu na matokeo ya manung’uniko
yanayoendelea kwa muda mrefu bila kushughulikiwa au kupewa uzito
unayostahili.
Kuunda chama cha kushughulikia maslahi ya watoto ni kazi itakayohitaji
idadi muafaka ya viongozi-tumishi wenye ufanisi na wa umri, imani,
makabila, na maeneo ya ustadi mbalimbali kila mmoja akiwa na jukumu
lake---kila mmoja wetu akijaribu kumkamilisha mwingine badala ya kurudia
yale aliyokwishafanya; kushirikiana badala ya kushindana; kutumikia watoto
na sio kujitumikia sisi wenyewe, mashirika yetu, au matakwa yetu ya kisiasa.
kushindana nayewatoto,huitaji namba muhimu ya viongzo watumishi, wa
umri yoyote, wa rangi zote na heshima
Tunahitaji kujiwajibisha. Tusikubali maneno yakawa mbadala wa vitendo au
njia ya kuficha sera zinazogandamiza watoto. Watu wanaotoa ahadi ya
“Kutoacha Mtoto Hata Mmoja Nyuma” lakini huku hawafanyi lo lote, au wale
wanaotetea sera na bajeti zinazoacha watoto wengi nyuma lazima
wapingwe vikali. Changamoto kwa kila mtu anayeahidi Kutomwacha Mtoto
Hata Mmoja Nyuma ni iwapo pengo kati ya watu tajiri na maskini na kati ya
wasio na madaraka na wenye madaraka linazibwa badala ya kupanuliwa.
Watoto hawawezi kula au kupata mahali pa kulala, au kupata elimu kwa
ahadi tu. Watoto ambao wana njaa, wanaishi mitaani, wanaojaribu kujifunza
katika shule zinazobomoka, na walio na mahitaji ya malezi na huduma za
afya ni lazima walindwe. Ni lazima tuwaambie ukweli hao walio katika
madaraka katika vyama vyote vya siasa na katika ngazi zote za serikali na
katika kila sekta ya jamii ya Marekani hadi hapo watoto wetu wote
watakapoweza kukua wakiwa na afya nzuri, bila vitendo vya vurugu, wana
heshima, elimu nzuri na usalama wa maisha yao.
53
Kila baada ya sekunde 44 mtoto mmoja anazaliwa katika umaskini; kila
baada ya dakika moja mtoto anazaliwa bila bima ya afya; kila baada ya
dakika 11 mtoto anatelekezwa au kufanyiwa vitendo vya kikatili; na kila
baada ya masaa mawili na dakika 20 mtoto anauliwa na silaha za moto
kama vile bastola. Ukweli huu si matendo ya Mungu. Ni matendo yetu
yanayotokana na uchaguzi wetu wa kimaadili na kisiasa kama taifa na kama
raia. Hatuna budi tubadilishe ukweli huu tukiwa na dhamira ya kutosubiri
kesho na utashi wa kudumisha mabadiliko.
Kila siku tunayoacha ipite bila kuchukua hatua ni siku nyingine ambayo
bunduki zinaua watoto 10, watoto 186 wanatiwa mbaroni kutokana na
makosa ya uhalifu, na watoto 2,911 wanaacha shule.
Dkt. King na Gandhi hawawezi kurudi tena duniani kuanzisha chama cha
kushughulikia watoto wetu. Hili ni jukumu letu sisi sote. Tunaweza na
tutaweza kuleta mabadiliko. Na iwapo tutatimiza wajibu wetu kama
inavyostahiki, yatakayosalia ni jukumu la Mungu.13
Marian Wright Edelman, mwanamke Mmarekani mweusi wa kwanza kukubaliwa katika chama cha
mawakili cha Mississippi, alianza kufanya kazi kwenye miaka ya 1960 kama kiongozi wa haki za
kiraia nchini Marekani akiwa anashirikiana na Dkt. Martin Luther King na watu wengine. Ni
mwanzilishi na rais wa Mfuko wa Utetezi wa Watoto (Children’s Defense Fund), shirika lililodhamiria
kuhakikisha kuwa mwanzo wa maisha ya kila mtoto ni wa afya nzuri, usalama, haki, na maadili
pamoja na kuwa mikononi mwa ulezi wa na wazazi na jamii.
Maswali ya Majadiliano
·  Wewe binafsi unafikiri Marian Wright Edelman ana lengo gani kwa kuandika
waraka huu?
·  Je, unafikiri yeye ni mwasilishaji bora wa habari? Kwa nini hivyo au kwa nini
sivyo?
·  Ni matokeo gani ya takwimu ambazo ametaja?
·  Ni mbinu gani ambazo ungetumia kwa kuwasilisha ujumbe huo huo kwa watu
wengine?
·  Je, unaweza kufikiria kifungu cha maneno, usemi, au hotuba ambayo unaona ina
ujumbe mzito na inakuvutia?
·  Je, teknolojia ya kisasa, kama vile mashini za faksi, mtandao wa barua-pepe (email)
na webusaiti, inasaidia kusambaza ujumbe kwa watu wengi zaidi? Ikiwa ni
ukweli, ni mpango gani wa ulio nao wa kuwasiliana na watu wengi?
13 Marian Wright Edelman, “Hold My Hand: Prayers for Building a Movement to Leave No Child Behind”
Reprinted by permission
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
54
Zoezi : Uwasilishaji Katika Mazingira Tofauti
Ruhusu muda wa dakika arobaini na tano hivi kwa zoezi hili.
Amri ya Gavana wa Jimbo nchini Sudan Inawazuia Wanawake Kufanya Kazi
Kwenye Sehemu za Hadhara .
Mnamo mwezi wa Septemba mwaka 2000, Gavana wa jimbo la Khartoum, Majzoub
al-Khalifa alitoa amri iliyokuwa ikiwakataza wanawake kufanya kazi katika sehemu
nyingi za hadhara, akisisitiza kwamba kuzuiwa kwao kutalinda sheria ya Kiislamu
ya sharia na kudumisha heshima ya wanawake. Amri hiyo ilikuwa hasa imelenga
wanawake wanaofanyakazi katika vituo vya mafuta, mahotelini, na katika
mikahawa.14
Igizo: Mwanamke mmoja mtetezi wa haki za wanawake anayeishi jijini
ameshutushwa na kukasirishwa na amri hiyo ya Gavana, na kuamua kwamba ni
lazima aipinge kwa kila njia. Kupitia kwa rafiki yake, anapanga kukutana na afisa
mmoja wa ngazi ya juu katika Wizara ya Kazi na Mageuzi ya Utawala. Anaamua
kuwa atajaribu kumshawishi afisa huyo kujiunga naye katika kampeni yake ya
kupinga amri hiyo. Afisa huyo ni mwanamume wa makamo, ameoa, na ana watoto
wawili wa kike vijana. Naye pia anafikiria sana haki za wanawake na utetezi na
usalama wa mabinti zake watakapoanza kufanya kazi. Afisa huyo anataka mabinti
zake wawe na uhuru wa kuchagua elimu na utaalamu, lakini tu katika jamii ambayo
ina sheria zinazowapa nafasi mabinti zake kuendeleza kweli kweli maadili ya
Kiislamu.
1. Kundi la semina linagawanyika katika makundi madogo ya watu watatu watatu. Kila
kikundi kinachagua nani atacheza nafasi ya afisa na nani atacheza nafasi ya mtetezi.
Mwanakikundi wa tatu anayebaki ataangalia na kufuatilia mazungumzo kati ya hao
wawili na kuandika anayoona.
2. Wakiwa tayari wamechukua nafasi zao, afisa na mtetezi wanakutana na kuwa na
mazungumzo yanayochukua muda wa kati ya dakika tano na kumi ambapo mtetezi
anawasilisha yanayomkera kuhusiana na amri ya Gavana na kujaribu kumshawishi
afisa kujiunga naye katika kuipinga waziwazi.
3. Wakati wa mazungumzo hayo yakiendelea, mwanakikundi mtazamaji anaandika
mambo muhimu anayoyaona katika hayo mazungumzo. Mambo ya kuangalia
yanaweza kujumuisha:
·   Aina gani za mitindo ya mawasiliano?
·   Ni mbinu gani zinatumika katika ujengaji wa hoja?
·   Ni kwa kiasi gani kila mmoja anamsikiliza mwenzie?
·   Ni kwa kiasi gani kila mmoja anajibu hoja za mwenzie?
·   Je wam eweza kufikia mahali pa kukubaliana au kuafikiana?
4. Vikundi vyote vinarudi na kukutana tena kama kundi moja la semina na kukaa mkao
wa mduara. Mtazamaji kutoka kila kikundi kidogo anaeleza yale aliyoyaona.
14 Hii ni habari ya kweli, tazama http://www.cnn.com/2000/WORLD/africa/09/05/sudan.women.ap/
Sehemu ya Pili: Kuwasiliana na Wengine
55
5. Kama muda unaruhusu, waombe waigizaji kutoka kikundi kimoja au viwili kurudia
kuigiza mbele ya kundi zima, wakiwa wanafanya marekebisho kufuatana na maoni
waliyoyasikia na kuyazingatia kutoka katika mazoezi na majadiliano.
Maswali ya Majadiliano
·  Kwa watetezi na maafisa: Je ilikuwa ni vigumu kutetea msimamo wako? Kwa
nini?
·  Kuhusu kikundi chako, je mtetezi na afisa kweli kila mmoja alikuwa anamsikiliza
vizuri mwenzie?
·  Ni fikira gani au mawazo gani yalikwishajengeka akilini mwa afisa na mtetezi juu
ya mwingine yanayoweza kuwa yameathiri jinsi ambavyo wamejibu hoja za kila
mmoja wao?
·  Je uliona iwapo afisa au mtetezi katika kikundi chako akijaribu kumfundisha
mwenzie juu ya faida za msimamo wake? Je, “kuelimisha” kuna tofauti yo yote na
“kubishana”? kwa nini?
·  Ni aina gani ya taarifa za kweli zingeweza kumsaidia mtetezi kuwasilisha maoni
yake kwa ufanisi zaidi?
·  Ni wakati gani kiongozi angependa “kuwaelimisha” wengine? Je, unayo mifano yo
yote unayoweza kukumbuka ambapo viongozi wametumia mbinu hii kwa
mafanikio?
·  Je, afisa na mtetezi walikuwa wameachana sana katika malengo yao? Ni malengo
gani, kama yapo, ambayo yalikuwa sawa kwa wote wawili?
·  Je, kulikuwepo na masuala yo yote ambayo afisa na mtetezi wangeweza
kuafikiana? Kama yapo, ni yapi? Kama hayapo, ni kwa nini?
·  Je, ni ya jambo lililokuwa la busara kutarajia kuwa afisa na mtetezi wangefikia
maafikiano? Kwa nini hivyo au kwa nini sivyo?
·  Je, kutafuta njia za kufikia maafikiano liwe mojawapo ya malengo ya kiongozi
bora? Je, inawezekana mara zote kufikia maafikiano? Je, ni hatua inayopongezwa
mara zote? Kwa nini hivyo au kwa nini sivyo?
·  Bila kujali jukumu lako wakati wa mazoezi, utasema au kufanya nini katika
mojawapo ya nafasi hizo za igizo kuwa mtu unayeweza kushawishi wengine?
Uchunguzi
·  Umejisikiaje katika “kuigiza” mhusika”? Umeweza kujifunza nini kutokana na
zoezi la kuigiza?
·  Umejisikiaje kuwa “mtazamaji” huku ukiwa unaandika yale muhimu unayoyaona
wakati wa zoezi?
·  Je, kuna kitu cho chote kilichokushangaza kati ya uliyosikia?
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
56
____________________________________________________________________
Uongozi jumuishi huwathamini sana watu wazungumzaji
wanaoheshimiana na kuheshimu maoni ya watu wengine---hata kama
yanatofautiana na yao.
Tunapaswa kuondokana na chuki zetu tunazozijenga bila sababu na uhasama,
kuepukana na kuhukumu wengine, kujifunza kutolazimisha mawazo yetu kwa
wengine.
kukubali tofauti za hali zetu, kudhibiti hasira zetu, kupima watu kwa mazuri
yao.
Tambua vipaji, na samehe
“Misingi ya Ujenzi wa Uongozi”
57
KIKAO CHA TANO
Jinsi Gani Tunaweza Kukidhi Matakwa
Tofauti?
Shabaha za Kikao
§ Kuchungua juu ya tofauti kati ya kuvumilia tofauti za
kibinadamu na kuzikubali kwa myo mkunjufu.
§ Kujadili nguvu za kimaadili na kisiasa za watu wenye hali
tofauti walioungana pamoja kwa ajili ya kutetea au kupigania
jambo fulani.
§ Kufanya uchambuzi wa jinsi gani watu ambao wana tofauti
za kielimu, kiuchumi, au kiutamaduni wanaweza kushirikiana
katika kuendesha kampeni, na pia mipaka inayoweza kuwepo
katika kufanya shughuli hiyo.
Mapendekezo ya Usimamizi
Soma kwa sauti habari iliyopo chini kuhusu juhudi za amani zilizofanywa na
Mairead Corrigan Maguire na Betty Williams nchini Ireland ya Kaskazini.
Jadili katika kundi maafikiano, majadiliano, na hatua zinazoelekea kuchukuliwa
katika kukubali kwa moyo mkunjufu maoni tofauti ambayo yanawezesha
utetezi wao kuwa na mafanikio.
Hili ni mada pana na muhimu. Mbinu ya kuhimiza washiriki kujitolea
kufanya mjadala inaweza kufaa zaidi kufanya mjadala mzuri. Fanya
inavyowezekana kupata kikundi kidogo cha washiriki wanaojitolea kushiriki
katika majadiliano hai juu ya mada, yakifuatiwa na majadiliano ya kikao kwa
kundi lote (Angalia Kiambatisho B kwa taarifa zaidi).
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
58
Kuvuna Mattunda ya Amanii na Hakii
Mairead Corrigan Maguire na Betty Williams: Watetezi wa Amani
Mapambano ya kuleta uhuru nchini Ireland yalianza karne nyingi zilizopita wakati
nchi hiyo ilipotwaliwa na kufanywa koloni la Waingereza. Utawala wao wa
kuwatawala Wakatoliki wa Ireland ambao ndio walikuwa wengi ulifanyika kwa
misingi ya chuki bila sababu, ubaguzi, na kutojali hali ambayo ilisababisha
umaskini na njaa. Mnamo mwaka 1921, wanamapinduzi wa Ireland walifaulu
kushika nchi, na kuwezesha kuleta uhuru wa taifa kwa njia ya makubaliano. Chini
ya vipengee vya makubaliano hayo, wilaya sita za kaskazini zilizokuwa zinakaliwa
na idadi kubwa ya Waprotestanti zilitengwa na kubakia kama sehemu nchi ya
Uingereza. Licha ya utawala wa Waingereza kuungwa mkono na Waprotestanti
waliowengi huko Ireland ya Kaskazini, Jamhuri mpya ya Ireland iliendelea
kuhesabu rasmi ugawaji huo kama ni hatua ya muda tu kama ambavyo Wakatoliki
waliowengi wanaoishi Kaskazini waliendelea kufikiria hivyo. Katika miongo ya
hivi karibuni, kama matokeo ya mgogoro wa hadhi ya eneo hilo, vurugu za
kidhehebu kati ya Wakatoliki na Waprotestanti nchini Ireland ya Kaskazini
zimesababisha vifo vya watu zaidi ya 3,000 katika nchi yenye jumla ya wakazi
chini ya milioni mbili.
Kwa kuzingatia historia hii, Mairead Corrigan Maguire na Betty Williams
walijikuta wanashirikiana kutokana na vurugu hizo zilizoleta maafa makubwa
ambazo zilileta mabadiliko ya kudumu katika maisha yao. Tarehe 10 Agosti 1976,
wapwa zake Maguire, wawili wa kiume na mmoja wa kike waliuwawa katika kona
ya mtaa mmoja wa mjini Belfast wakati walinzi wa jeshi la Uingereza
walipomfyatulia risasi mpiganaji wa jeshi la ukombozi la Ireland (Irish Republican
Army, [IRA]) ambaye gari lake lilisererekea katika ujia wa waenda kwa miguu.
Baada ya balaa hilo, Maguire, amabye ni Mkatoliki, alitokea katika televisheni,
akilaani vitendo vya vurugu za umwagaji damu vya jeshi la IRA. Naye Williams,
mwanamke aliye na mchanganyiko wa kidini, alishuhudia ajali hiyo na mara moja
alianza kusambaza ombi la kulalamikia vitendo hivyo. Kukiwa kumepatikana saini
6,000 za watu waliounga mkono ombi hilo la kupinga mauaji ya watoto hao, baada
ya siku mbili aliliwasilisha kwenye televisheni. Katika mazishi ya watoto hao,
Maguire na Williams, wakiomboleza na kuchoshwa na vurugu zisizokuwa na
mafao yo yote, waliunganisha nguvu zao na kukubaliana kuendesha harakati za
kuleta amani. Walianzisha shirika lililojulikana kama “Wanawake kwa ajili ya
Amani” (Women for Peace), na baadaye likaja kuitwa “Shirika la Watu wa
Amani” (Peace People Organization).
Katika kipindi cha mwezi mmoja shirika hilo liliweza kuvutia wanawake 30,000,
wakiwa ni Wakatoliki na Waprotestanti, kushiriki katika maandamano ya mitaa ya
Belfast. Ijapokuwa wote wawili walilalamikiwa kwa kushirikiana na adui na
maisha yao kutishiwa, Maguire na Williams hawakuacha kuandamana na
waliendelea kuvutia wafuasi wengi. Wafuasi wao walivutiwa katika umoja huo wa
amani kwa sababu wote walipenda amani. Washiriki waligundua kuwa sio tu kuwa
walitaka kukomesha vurugu za umwagaji damu, bali pia watu wa pande zote mbili
za mgogoro walikuwa wanakabiliwa na umaskini, walikuwa hawana uhuru kamili
59
wa kisiasa, na hawakuwa na uhuru wa kiraia kutokana na amri zilizowekwa na
sheria ya hali ya hatari ya Ireland ya Kaskazini.
Mairead Corrigon Maguire na Betty Williams walijulikana na kutambuliwa
ulimwenguni kote kwa kazi yao nzuri, na kupata Tuzo ya Amani ya Nobel mnamo
Oktoba, 1977. Mwishowe Williams aliondoka kabisa mjini Belfast na kuhamia
nchini Marekani, lakini Maguire aliendeleza juhudi zake za kuyaelimisha makundi
yanayopingana nchini Ireland ya Kaskazini ili kuyakutanisha na kufanya
majadiliano ya kumaliza uhasama. Akiwa amepuuziwa na kutolewa maanani
katika miaka ya 1980 na ya mapema ya 1990 na wale waliokuwa wakiona vurugu
kuwa ndio njia pekee ya kutetea haki, alidumu na kuwasilisha ujumbe wake wa
mapambano ya amani kwa kipindi kirefu hata kabla ya makubaliano ya mani ya
mwaka 1998 kufikiwa.
Kama ambavyo Maguire alieleza “ninaamini kwamba matumaini ya maisha
mazuri yajayo yatategemea na sisi wenyewe kila mmoja wetu kukumbatia moyoni
na akilini njia za amani za kuleta mageuzi na kubuni mifumo mipya ambayo siyo
ya vurugu na yenye kuleta maisha mazuri kwa wote. Baadhi ya watu watasema
kuwa haya mawazo ni ya kufikirika tu, hayawezi kuwa ya kweli. Mimi ninaamini
kuwa ni ya kweli kabisa. Ninaamini kwamba ubinadamu unabadilika kwa kasi
kubwa kuelekea kwenye ufahamivu wa kiwango cha juu. Kwa wale wanaofikiri
kuwa haiwezakani, hebu kujikumbushe kwamba ubinadamu ulijifunza kukomesha
utumwa. Jukumu letu si jingine, bali ni kukomesha vurugu na vita....” Kwa hakika,
bado anasisitiza kwamba “kuvuna matunda ya amani na haki katika siku zijazo,
sisi sote hatuna budi tupande mbegu za kuleta mabadiliko kwa njia ya amani, hapa
hapa na sasa, wakati huu huu.”15
Maswali ya Majadiliano
·  Ni matukio gani yaliyowasukuma Mairead Corrigan Maguire na Betty Williams
kuanza kutafuta suluhisho la mgogoro wa Ireland ya Kaskazini?
·  Ni mbimu gani walizozitumia katika jitihada yao ya kujaribu kuleta suluhisho la
mapigano? Kwa nini walichagua mbinu hizo?
·  Ni sifa gani ambayo unaiona katika aina hii ya uongozi uliofanywa na Maguire na
Williams? Je unafikiri hawa kuwa wanawake kuliwasaidia au kilikuwa kikwazo
katika harakati yao hiyo?
·  Wakatoliki na Waprotestanti wa Irland ya Kaskazini wana malengo gani ya
pamoja? Ni matokeo gani juu ya uwezo wao wa kufikia malengo hayo
yaliyotokana na kshirikiana ?
·  Ni imani gani ambayo ilimtia hamasa Maguire kuvumilia dhidi ya vikwazo vingi
katika utafutaji wake wa amani nchini Ireland ya Kaskazini na duniani kote?
·  Je, kuwepo kwa lengo la pamoja kunaondosha vikwazo vya utofauti wa hali baina
ya watu? Kwa nini hivyo au kwa nini sivyo?
15 Habari hizi zimechukuliwa kutoka
http:/www.wagingpeace.org./articles/peaceheros/mairead_corrigan_maguire.htm/kama ilivyodondolewa
kutoka Mairead Corrigan Maguire with John Dear, S.J., ed., The Vision of Peace, Faith and Hope in Nothern
Ireland, Maryknoll, NY: Orbis, 1999
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
60
·  Je, umewahi kushiriki katika mradi ambapo ulifanya kazi na mtu au watu ambao
mlikuwa na tofauti nyingi? Kama jibu ni ndio, mlizishughulikiaje hizo tofauti
zenu?
·  Je, unapendelea kutambua na kukubali tofauti zilizopo kati yako na wengine au una
mwelekeo wa kutozijali na kuzifumbia macho na kutozizungumzia tofauti kama
hizo? Kwa nini?
·  Dhana za “utofauti” na “maafikiano” zinamaanisha nini kwako?
Shughuli za Kundi: Kukubali Utofauti
Ruhusu muda kama wa saa moja hivi kwa zoezi hili.
·  Fikiria na chagua kwa pamoja mradi unaowezekana au wa kudhahania tu
ambao kundi lingependa kuufanya.
·  Jadiliana na jaribu kufikia makubaliano juu ya “jumuia” (kwa mfano, jumuia
ya wataalamu/wasomi au ya watu wa kabila tofauti, kizazi, au jinsia) ambayo
washiriki wa semina hawana mahusiano nayo ya mara kwa mara au wana
mambo machache yanayofanana.
·  Jaribu kufikiria jinsi gani kushiriki kwa “jumuia” hii kungeliweza kunufaisha
mradi wa kundi.
·  Buni mbinu ambazo zitaweza kuihusisha “jumuia” hii katika mradi wa kundi
kwa namna ambayo itaongeza maelewano kati ya washiriki wote katika mradi.
Jinsi gani kundi litaweka mazingira mazuri ya kumridhisha kila mshiriki,
kuthamini uwezo wa kila mtu, na kufanya kazi kwa ushirikiano?
Sehemu ya Pili: Kuwasiliana na Wengine
61
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
62
____________________________________________________________________
Lazima tujifunze kuwaona watu wengine kama binadamu waliokamilika na
timamu na wenye nia ya kufanya mazuri. Hatuna budi tuwafikirie kuwa
wanapenda kujifunza ili wawe na maisha bora, na kufanya kazi sio tu kwa
sababu ya kupata tuzo au kutukuzwa, bali kupata maono ambayo hutiwa
msukumo na kazi zao. Kusema ukweli, wanaume na wanawake hushirikiana
katika kubuni, kufanyia kazi, na kufikia malengo ambayo huwanufaisha
wote……….Ushirikiano kama huu unawezekana na hauna budi hujengwe
iwapo tunataka kufanikiwa katika kuweka mifumo ya kijamii kiuchumi, na
kisiasa ambayo inatusaidia sisi kufikia malengo ya kujenga maisha mazuri,
bora na ya fanaka.
“Misingi ya Ujenzi wa Uongozi”
63
KIKAO CHA SITA
Jinsi Gani Tunaweza Kukuza Madaraka kwa
Kila Mmoja Wetu?
Shabaha za Kikao
§ Kuchambua kukuza madaraka kunamaanisha nini.
§ Kujadiliana juu ya thamani ya kudumu kwa kuwawezesha
wengine kuwa na madaraka.
§ Kuchungua jinsi gani kiongozi anawezesha madaraka.
§ Kuelezana mbinu za kibnafsi za washiriki za kuwawezesha
wengine kukuza madaraka.
Mapendekezo ya Usimamizi
Soma kwa sauti kisa kifuatacho kuhusu jitihada za Sakena Yacoobi za
kuelimisha, kufunza, na kuwezesha wananchi wenzake wa Afghanstani katika
kambi za wakimbinzi nchini Pakistan kuwa na madaraka. Jadili katika kundi
mbinu zake za kuchanganya jitihada zake ili ziwe na matokeo ya mapana na ya
muda mrefu. Zoezi lililokusudia kuchungua nguvu ya nia njema na
mawasiliano ndani ya mazingira ya kundi linafuatia .
Maswali na majibu ni mbinu nzuri katika kikao hiki. Kwa kuzingatia kwa
makini maswali matatu au manne hivi ya mwisho yanayofuatia kisa hiki,
msimamizi anaweza kupanua mjadala na kuhimiza washiriki kufikiria na
kuzungumza juu yao wenyewe na uzoefu wao (Angalia Kiambatisho B kwa
taarifa zaidi).
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
64
Fanya Kazii kwa Kushiirriikiiana na Wattu,, Saiidiia Wattu
Kujjiiffunza
Sakena Yacoobi: Mwalimu
Sakena Yaccobi aliondoka Afghanistan akiwa bado msichana katika miaka ya
mwanzoni mwa 1970 kuhudhuria masomo ya chuo kikuu nchini Marekani. Huko
alisoma biologia na mwishowe alipata digrii ya pili katika uwanja wa Afya ya
Umma. Akiwa umbali wa maelfu ya maili kutoka nyumbani, Yacoobi huku akiwa
mwingi wa hofu alifuatilia matatizo ya kisiasa yaliyokuwa yakiendelea kuchukua
sura mpya kila kulipokucha nchini Afghanistan. Wakati Urusi ilipovamia
Afghanistan mnamo mwaka wa 1980, alipoteza mawasiliano na jamaa zake wengi.
Akiwa anajua matatizo ambayo Waafghanistani wengi walikuwa wakipata,
Yacoobi aliingiwa na hamasa ya kuchangisha pesa na kukusanya nguo na vifaa
vingine vinavyohitajika katika maisha ya kila siku ili kuwatumia. Alishirikiana na
wanafunzi na watu kutoka nchi za kigeni hasa kutoka nchi za Asia na Mashariki ya
Kati kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi wenzake waliokuwa katika kambi za
wakimbizi, wakati huo huo akiishinikiza mamlaka ya uhamiaji ya Marekani
kuwapa wazazi na ndugu zake hifadhi ya kisiasa.
Mnamo mwaka 1988, Yacoobi alifanikiwa kupata kibali cha kuleta familia yake
nchini Marekani, lakini wasiwasi wake juu ya hatima ya wakimbizi wengine wa
Afghanistani uliendelea kumsumbua. Baada ya miaka minne ya kufuatilia kama
mtazamaji tu mateso ya Waafghanistani wenzake, Yacoobi, ambaye wakati huo
alikwishaanza kufundisha sayansi katika chuo kikuu nchini Marekani, aliamua
kuacha kazi yake ili kufanya kazi katika kambi za wakimbizi nchini Pakistani.
Alijisikia kwamba wakati ulikuwa umetimia wa kutumia uwezo wake kuwawezesha
kupata madaraka watu wake kwa njia ya elimu. Alikuta wakazi wa kwenye kambi
hizo wakiwa wamenyanyasika kutokana na umaskini, rushwa, na kukata tamaa
kulikokithiri. Aliamua kuwasaidia Waafghanistani wenzake kwa kuwafundisha na
kuwapa mafunzo ambayo wangehitaji katika kujenga upya nchi yao.
Baadaye Yacoobi alichukua kazi ya kuwa mratibu wa mpango wa elimu ya
wanawake wakimbizi wa Afghanistani uliokuwa ukiendeshwa na Kamati ya
Kimataifa ya Uokoaji (International Rescue Committee), na alianzisha miradi ya
mafunzo ya waalimu iliyokuwa na lengo la kusaidia walimu kuimarisha uwez o wa
wanafunzi kujifunza ndani na nje ya madarasa. Badala ya kutegemea njia ya
kupata maarifa kwa kukariri, mpango wa masomo uliwekea mkazo kukuza uwezo
huru wa wanafunzi wa udadisi na uchambuzi. Wanawake 15 wa kwanza katika
mpango huu baadaye waliweza kuwafundisha wakufunzi wengine zaidi 50, ambao
nao waliwafundisha wengine, na wengine wakawafundisha wengine hadi kufikia
jumla ya washiriki 3,000. Yacoobi alikuwa hasa anajihusisha zaidi na hali ya
maisha ya wasichana wa Afghanistani, ambao walikuwa wanateseka kutokana na
unyanyasi wa aina yake katika kambi hizo. Alijitahidi kuweka viwango vya
ufundishaji na kuongeza kiwango cha mahudhurio katika shule 25 za wasichana
katika maeneo hayo. Jitihada hii ilileta matokeo mazuri sana ya ongezeko la idadi
ya wasichana shuleni kutoka 3,000 kufikia 15,000 katika kipindi cha mwaka
mmoja.
Katika mwaka wa 1995, Yacoobi na wenzake wawili walianzisha Taasisi ya
Kujifunza ya Afghanistani (Afghan Institute of Learning [AIL]) mjini Peshawar,
Sehemu ya Pili: Kuwasiliana na Wengine
65
Pakistani. Maono yake yalikuwa ni mpango kabambe: kupanga na kutekeleza
mipango ambayo ingeongeza kiwango cha ubora wa elimu katika ngazi zote kwa
kila mkimbizi wa kutoka Afghanistani. Katika kipindi cha mwaka wa kwanza, AIL
iliendesha semina nne ambazo zilihudhuriwa na walimu 20 tu. Katika mwaka
uliofuatia, jumla ya walimu 100 walipatiwa mafunzo. Haukupita muda mrefu shule
zote katika kambi hizo za wakimbizi zikaanza kuwapeleka walimu wake kuhudhuria
mafunzo hayo, na leo hii zaidi ya walimu 3,000 wameshiriki katika mafunzo haya
ya kuboresha kazi yao. Ili kutoa msingi juu ya masuala yanayohusu maisha ya
wanawake katika kambi hizo, semina maalumu ziliongezwa ili kuelimishana juu ya
masuala ya haki za binadamu, unyanyaswaji wa wanawake, na elimu ya afya.
Leo hii, wakimbizi wa kutoka Afghanistani wanaopenda kuendelea na elimu ya
chuo kikuu nchini Pakistani wana uchaguzi mdogo. Lengo kuu la Yacoobi sasa ni
kuona masomo yanayotolewa katika ngazi ya chuo kikuuu katika nyanja za sayansi
ya kompyuta, sayansi ya afya, saikolojia, na elimu yanatolewa kwa njia ya
mtandao ili yasaidie kuwapa Waafghanistani maarifa na ujuzi unaohitajika katika
ujenzi wa jamii ya Afghanistani yenye neema na utajiri.
Alipoulizwa kuhusu kitu kinachomsukuma kuwapa wengine madaraka, Yacoobi
alijibu, “unopotoa kitu fulani kutoka ndani mwako, toa kile kilicho bora. Fanya
kazi kwa kushirikiana na watu na wasaidie watu kujifunza. Ninajaribu kuwasaidia
watu kupitia njia ya kuwashirikisha katika shughuli za jamii ili waweze
kujitegemea..... Kwa njia hii Waafghanistan wanaweza kutoka nje. Kutoka nje kuna
maana ya kufunguliwa, kuwa huru, kujikomboa, kutoa maoni yao bila woga........hii
ndio njia ninaytumia kusaidia kujenga upya nchi yetu.......”16
Maswali ya Majadiliano
·  Ni uhusiano na hisia gani alizonazo Sakena Yacoobi kwa jamii anayotaka
kuipa madaraka?
·  Ni mafundisho gani Sakena Yacoobi anajifunza kutoka kwa jamii yake? Ni
kwa jinsi gani mahitaji ya jamii hiyo yanamwongoza?
·  Ni kwa jinsi gani Yacoobi anaegemea na kutumia uzoefu na elimu yake?
·  Malengo yake ya muda mfupi ni yapi? Maono yake ya muda mrefu ni yapi?
·  Kwa nini kujifunza kwa kukazia uwezo wa kudadisi na kuchambua
kunawekewa mkazo? Njia hii ina faida na hasara zipi?
·  Ni kwa njia ipi Yacoobi anawapatia watu wengine mawazo na/au maono
yake?
·  Ni jinsi gani mtindo wa kielimu anaotumia unawawezesha wanawake na watu
wa Afghanistan kwa jumla kupata madaraka?
·  Kumwezesha mtu kupata madaraka kuna maana gani kwa maoni yako?
16 Habari hii imetokana na maandishi aliyotuletea Sakena Yacoobi na mahojiano ya simu aliyoyafanya tarehe
December 14, 20000 kati yake na Women’s Learning Partnership.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
66
·  Je, unajiona wewe kuwa katika hali ya kuweza kupata madaraka? Ni kwa jinsi
gani unaweza ukaendeleza kujipa madaraka?
·  Je, unawezaje kuwawezesha wengine kupata madaraka? Kwa nini? Ni mbinu
gani utakazotumia?
·  Je, unafikiri kuwawezesha wengine kupata madaraka ni kipengee kimojawapo
cha msingi wa uongozi bora? Kwa nini?
Shughuli za Kundi: Kuwezesha Wengine Kuwa na
Madaraka
Ruhusu muda kama wa saa moja hivi kwa zoezi hili.
1. Zoezi hili limetayarishwa ili kutoa uzoefu mfupi kuhusu jinsi gani watu
wanaweza kuwezeshana kuwa na madaraka kwa kutoa na kupokea maoni
yenye kufaa. Msimamizi au mshiriki mwingine aliyejitolea anakuwa
mwangalizi wa muda kwa zoezi hili. Mwangalizi wa muda anapoashiria
kuanza kwa zoezi, kila mshiriki anaombwa kutafuta mwenzi wake.
2. Katika muda wa dakika tano, wenzi katika kila kundi la watu wawili wawili
wanazungumza. Kila mwenzi wa mtu ataombwa kutoa taarifa
zilizoorodheshwa hapo chini. Wenzi katika kila kundi wanaweza kupanga kila
mmoja kutoa majibu ya kipengee kimoja baada ya kingine, au mmojawao
kujibu vipengee vyote mara moja na kisha mwingine kufuatia.
·  Taja vitu au sifa fulani alizo nazo huyo mtu mwingine ambazo
umetokea kuzipenda (mawazo yake, jinsi anavyofanya kazi,
anavyosikiliza, anavyoongea, n.k.).
·  Eleza shughuli ambayo ungependa kuifanya na huyo mtu mwingine
au kitu amabcho ungependa kujifunza kutoka kwake.
·  Toa ushauri ambao unafikiri utaweza kumsaidia huyo mtu mwingine.
3. Baada ya dakika tano, mwangalizi wa muda anamwomba kila mtu kutafuta
mwenzi mpya ambaye watarudia pamoja zoezi hilo.
4. Baada ya kila mmoja kuzungumza na jumla ya wenzi wanne, kundi
linkusanyika tena pamoja kujadili juu ya zoezi zima na kubadilishana maoni
juu ya maswali haya:
·  Ni kitu gani kilichokuwa rahisi katika zoezi hili? Kipi kilikuwa
kigumu?
·  Je, kuna taarifa yo yote uliyopokea kutoka kwa washiriki wengine
ilikuwa uliipenda sana na yenye kusaidia? Kama ipo, ni ipi? Kwa nini
ulipenda kuisikia? Ilikuwa ni kwa jinsi hiyo taarifa ilivyowasilishwa,
au ni lile jambo lenyewe lililokuwa likizungumzwa?
·  Je, zoezi hili limekusaidia kuweza kuwafahamu zaidi kidogo baadhi
ya washiriki wa semina hii?
Sehemu ya Pili: Kuwasiliana na Wengine
67
·  Je, zoezi hili limeibusha hali ya kuaminiana zaidi? Je, mawasiliano
yalikuwa ya wazi na ya ukweli? Kwa nini?
·  Je, zoezi hili limekuongezea kujenga mtazamo mzuri kwa kundi lote
kwa jumla? Kwa nini?
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
68
69
Sehemu ya Tatu:
Kuanzisha Ushirika wa Kuelimishana
Katika ushirika kuelimishana, au katika shirika la kuelimishana, matokeo yaliyofikiwa na washiriki
katika ushirika au shirika huwakilisha mawazo na vitendo vyao kwa pamoja. Kujumuika kwa
washiriki huweza kuleta kujiangalia, kujitathmini, na maarifa ambavyo vyote huongeza na
kuchochea kasi ya kufikia malengo yao. Wanapofanikiwa katika malengo yao, washiriki huwa na
motisha ya hali ya juu na kushiriki kikamilifu katika shughuli zao, hubadilishana taarifa na
kupeana maoni kwa njia inayohusisha washiriki wote, matokeo huonekana waziwazi, na elimu na
uongozi hutokea kwa njia ya maafikiano na ukuaji wa maono ya pamoja.
Katika mazoezi yafuatayo, ni maelezo ya masimulizi juu ya mashirika yanayofanya kazi kwa
kushirikiana. Maelezo haya yanatumika kama kifani cha aina ya mtindo wa uongozi unaoibuka
kutoka katika ujenzi wa asasi wa wanawake. Katika vikao viwili vya mwisho, washiriki wa semina
watapata nafasi ya kufanya shughuli katika makundi madogo madogo kuweka malengo, kubuni
mfumo wa utawala, na kupanga shughuli za shirika lao la kufikirika/dhahinia, kwa kutumia
misingi ya mambo waliyojifunza katika vikao vyote vya semina. Ili kuwasaidia waweze kujiandaa
vizuri kwa ajili ya zoezi la mwisho, ni vyema washiriki waanze kubaini vigezo vya kuanzisha
shirika katika vikao vya mwanzo katika sehemu hii.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
70
___________________________________________________________
Kujifunza katika ushirika huhusisha aina ya mazungumzo ambayo husaidia
kuleta harambee—
yaani, uratibu, umoja, na ari ya ushirikiano ambayo
huleta nguvu kubwa ya kitu chote kuliko nguvu ya sehemu yake moja moja.
Harambee, haina maana kuwa kila mtu hukubaliana na kila kitu.
Bali ina maana ya kuwa kwa vile wanaushirika wamejifunza kuthaminiana na
kuheshimiana
wanaweza kutoa mchango wao katika shughuli ambayo italeta matokeo
ambayo wote watayatambua na kuyathamini kama yao.
“Misingi ya Ujenzi wa Uongozi”
71
KIKAO CHA SABA
Jinsi Gani Tunaweza Kufikia Lengo la
Pamoja?
Shabaha za Kikao
§ Kuchungua mbinu za kufikia lengo la pamoja baina ya
wanakikundi au wanaushirika.
§ Kubaini njia za kufikia maono ya pamoja kupitia njia za
kushirikiana.
§ Kuzingatia jinsi gani mashirika yanaweza kubadilishana maono
na mashirika mengine ili kunufaisha jamii pana zaidi.
Mapendekezo ya Usimamizi
Soma kwa sauti masimulizi yafuatayo juu ya chimbuko ya kampeni ya
wanawake maskini wakusanya taka waliojiajiri jijini Ahmedabad, nchini India,
ya kutaka kuboresha hali zao za kijamii na kiuchumi. Jadili katika kundi jinsi
gani wakusanya taka hao waliweza kubaini maono ya pamoja na kuchukua
hatua kuyaweka katika vitendo.
Ajili ya kikao hiki, taratibu za usimamizi kama vile uigizaji au uchoraji wa
michoro na katuni unaweza kuwaleta washiriki karibu na kisa hiki cha
wanawake wa India. Mbinu hizi pia zinaweza kuchochea mjadala wa kuvutia
baina ya washiriki (angalia Kiambatisho B kwa taarifa zaidi).
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
72
Kampeni ya Akina Dada wa Afya, Arogya Bhagins
Huko India, zaidi ya asilimia tisini na nne (94%) ya wafanyakazi wanawake, ni
wale wanaojiajiri na huwa wanakabiliwa na unyanyaswaji unaozidishwa zaidi na
unyonge wa wanawake kiuchumi na kijamii. Kati ya wanawake hawa ni wale
wanaofanya kazi za kutoa huduma zinazofanyika kwa mikono na mitulinga kama
vile kusukuma mikokoteni, shughuli za nyumbani, na kukusanya taka.
Mnamo mwaka 1994, Chama cha Wanawake Wanaojiajiri (Self Employed
Women's Association [SEWA]), chama cha wafanyakazi kilichosajiliwa nchini
India tangu mwaka 1972, kilizindua kampeni ya kushughulikia mahitaji ya
wafanyakazi wanawake wakusanya taka waliojiajiri, ambao wengi wao ni maskini
sana na hawajui kusoma wala kuandika. SEWA kilianza juhudi zake kwa
kushauriana na wanawake na viongozi wa eneo lao. Kupitia mikutano kadhaa
katika ngazi za mji na maeneo ya makazi, maafikiano yalifikiwa kwamba
kulikuwepo na mambo ya msingi matatu yaliyohitaji kuwekewa maanani katika
kuboresha hadhi ya wafanyakazi wanawake wasomba taka: (1) kuboresha
mishahara ya ukusanyaji taka ambayo ilikuwa ni ya chini na isiyokuwa na
uhakika; (2) kupunguza hali za hatari kwa afya zitokanazo na kusomba taka; na
(3) kupunguza hatari zilizokuwa zinaweza kutokea kwa watoto wa wafanyakazi
ambao hawana marupurupu ya matunzo ya watoto.
Katika jiji la Ahmedabad, mikutano mingi ilifanyika ikiwahusisha wafanyakazi
wasomba taka ili kuongeza kiwango chao cha kutambua, kubaini, na kuelewa
masuala ya kazi mahususi katika jamii yao. SEWA kiliratibu vikao vya afya na
usafi kwa ajili ya wanachama wake na kujadiliana nao juu ya mbinu za kuboresha
hali zao za za kijamii na kiuchumi. Katika mikutano, vikao vya semina, na
mashauriano yaliyokuwa yakiendelea, wafanyakazi wasomba taka waliweza
kuweka kundi la msingi la maadili na kanuni ambamo wote walikuwa na
dhamira/hisa. Kutokana na kanuni hizo, wasomba taka hao walianza kufafanua
vipaumbele vyao na kujenga maono ya pamoja ambayo yalitokea kuwa mwongozo
wa shughuli na kampeni zao. Kutoka katika kundi hilo la wasomba taka,
wakusanya karatasi taka ambao hukusanya na kutengeneza tena taka kavu na
ambao huwa mara nyingi wanabaguliwa na kudharauliwa kama waokotezaji na
waeneza magonjwa walijijumuisha pamoja na kuanza kampeni thabiti kutetea haki
zao.
Wakusanya karatasi hao walianza maandalizi ya kubaini uwezo na nguvu zao ili
kila mtu aweze kuwa na eneo lake mwenyewe ambalo angewajibika kuliweka
katika hali ya usafi. Kwa utaratibu huu, kila nyumba katika jamii iliyokuwa
ikishiriki katika mradi huu ilipewa mfuko mkubwa wa takataka ambao
ungelibadilishwa na mwingine mara tu unapojaa. Watu ambao husomba taka
kupitia mpango huu bado wanapata mapato kwa kuuza tena karatasi taka ambazo
zina soko, lakini kuwepo kwao kunaonekana kuwa na mafao makubwa katika jamii
ambamo wanafanya shughuli hizo.
Wanawake walioshiriki katika kampeni ya Ahmedabad sasa wanatambuliwa kama
Arogya Bhaginis, au Akina dada wa Afya, na ushirikiano wao na wawakilishi wa
jamii za tabaka la matajiri ambamo wanafanya shughuli zao umevutia kuungwa
mkono na kamati iliyoteuliwa na Mahakama Kuu. Wana Arogya Bhaginis
walianzisha kampeni ya pili kuhamasisha na kuleta pamoja akina dada wenzao
400 ambao hupata riziki yao kwa shida sana kutokana na dampo kuu la jiji. Kama
ilivyo kwa wakusanya karatasi taka, wanawake ambao hufanya kazi katika dampo
kila siku hupekua huku na huku taka
Sehemu ya Tatu: Kuanzisha Ushirika wa Kuelimishana
73
ziletwazo dampo kutafuta vitu vya kuokota vinavyoweza kuuzwa tena. Wanawake
hawa waliowengi hulazimika kufanya kazi hiyo huku wakiwa na watoto wao
wachanga na watoto wadogo, hali ambayo huwaweka wao wenyewe na watoto
wao katika hali ya hatari kiafya. Wana Arogya Bhaginis sasa wanashughulikia
suala la kuanzisha mpango wa matunzo ya watoto kwa wanawake wanaofanya kazi
ya kuokoteza vitu katika dampo. Pia wanaendelea kutafuta vyanzo mbadala
ambapo wanaweza kupata taka kavu zinazoweza kutengenezwa tena ambavyo ni
salama na vyenye faida kubwa badala ya dampo kuu.
“Kuna mengi ya kufanywa katika shughuli nzima ya kuimarisha uongozi wa
wanawake, moyo wa kujiamini, na uwezo wa kudai haki za wanawake ndani na nje
ya nyumba zao na uwakilishwaji wao katika ngazi za uundaji sera na upitishaji
maamuzi”, imeelezwa katika maandishi ya SEWA. Kupata malengo ya pamoja na
kisha kufasili maono ya pamoja ni shughuli inayohusu mashauriano na kujiangalia
kwa kuhusisha ushirikiano wa watu wengi wanaohusika kadri iwezekanavyo. Kwa
kufanya kazi kwa niaba ya watu maskini, SEWA kinasisitiza kwamba wanawake
waliojiajiri ni “ masuala yao, vipaumbele na mahitaji yao ambavyo havina budi
kuongoza na kuunda shughuli nzima ya maendeleo....” 17
Maswali ya Majadiliano
·  Ni nini maono gani ya jumla yaliyo msingi wa kazi ya SEWA?
Utatafisilije maono ya shirika hili?
·  Ni kwa jinsi gani wanawake wakusomba taka walifikia hatua ya kubaini
na kueleza waziwazi malengo yao? Je, unafikiri ukweli wa kwamba ni
wanawake unaathiri njia walizotumia kubaini na kufikia malengo yao?
Kwa nini?
·  Jinsi gani wakusanyaji karatasi au akina dada wa afya, Arogya Bhaginis,
waliweza kubadilisha mahitaji yao katika vitendo?
·  Ni kwa jinsi gani akina dada wa afya wanaonyesha/wanadhihirisha
uongozi? Ni sifa gani unayoiona katika aina ya uongozi wao? Ni kwa jinsi
gani mifano ya uongozi ambayo umewahi kuiona au kushiriki
inatofautiana na mfano huu wa uongozi wa akina dada wa afya?
·  Je, waliwezaje kujenga maono ya pamoja?
·  Jinsi gani kuwa na maono ya pamoja yanayopewa nafasi ya kubadilika
kunaathiri ustawi wao wa kijamii?
·  Ni hatua zipi tofauti za mabadiliko ambamo maono ya SEWA yamepitia
kadri yalivyokuwa yakichukua sura mbalimbali?
·  Je kuwa na maono ya pamoja kunawezekana na/au kunatamaniwa mara
zote? Kwa nini?
·  Ni vizuizi gani vinavyoweza kujitokeza katika ujenzi wa maoni ya pamoja
kati ya watu/vikundi vinavyotofautiana sana na/au hata vinavyofanana?
Utawezaje kuvishinda hivyo vizuizi?
17 Habari juu ya Self Employed Women’s Association zimechukuliwa kutoka http://www.sewa.org
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
74
Shughuli za Kundi: Kubaini Maono ya Kundi Kupitia
Lengo la Pamoja
Ruhusu muda kama wa saa moja hivi kwa shughuli hii ya kundi.
Katika kikao cha tatu washiriki waliombwa kuandika kauli zao za maono ya binafsi.
Katika zoezi hili, msimamizi atawarejeshea wandishi kauli zao walizoziandika.
(Unaweza kugawa kundi katika vikundi vidogo vidogo.)
Uundaji wa maono ya pamoja ni njia inayoweza kutumiwa na mtu au kikundi cho chote
na huweza kubadilika badilika katika kuweka malengo ambayo yanazingatia aina za
watu wanaounda kundi na kuendelea kuwepo kwa mawasiliano katika kipindi fulani.
Kikundi kinapojenga lengo la pamoja, kila mwanakikundi anatenda na kuchangia kwa
kuongozwa na utaratibu ambao anaumiliki na kuwajibika nao pamoja na wenzake.
Katika zoezi hili, washiriki wa semina wataeleza maadili na uzoefu uliowaongoza hadi
kufikia kauli zao za maono yao ya kibinafsi. Jukumu lao litakuwa kuchunguza na
kugundua vitu vinavyofanana katika maadili na kanuni zilizowasaidia kubaini na
kueleza waziwazi lengo la pamoja la kundi.
1. Warudishie washiriki kauli zao walizoziandika juu ya maono yao ya kibinafsi
katika kikao cha tatu. Wape dakika chache kujikumbusha tena kauli zao na
kufikiria sababu zilizowasukuma kufikia kutoa na kuandika kauli zao za
kibinafsi.
2. Kila mshiriki mmoja mmoja atapewa nafasi ya kusoma kauli yake kwa sauti,
au kama watapenda, kueleza kwa maneno mengine hiyo kauli kufuatana na
mabadiliko ya mawazo ambayo atakuwa ameyapata katika semina hii. Kila
mshiriki apewe muda usiozidi dakika tano, na hata chini ya hapo iwapo kundi
ni kubwa, ambapo atasoma na kuleza kwa ufupi sana maadili na kanuni
zilizomwongoza kufikia kuunda hiyo kauli yake ya maono ya kibinafsi.
3. Baada ya kila mshiriki kupewa nafasi ya kuleza kauli yake ya maono ya
kibnafsi, liombe kundi zima kutafakari maswali haya yafuatayo (msimamizi au
mshiriki aliyejitolea ataandika mambo muhimu yanayojitokeza katika ubao au
karatasi kubwa ya kuning’iniza):
·  Ni uzoefu, kanuni, mitazamo, au maadili gani ambayo yamejitokeza
katika kauli za washiriki wote?
·  Je, kuna malengo yo yote ya kibinafsi (yaani yanayohusiana na
uchaguzi wa kibinafsi wa mtu, familia yake, au mazingira yake ya
kipekee) au malengo ya kijamii (malengo ya kijamii, kisiasa,
kiuchumi, au yo yote yale ya jamii ya mshiriki) ambayo yalijitokeza
kwa kufanana katika kauli za maono binafsi za washiriki? Kama
yapo, ni yapi?
4. Elekeza kundi kutafakari kauli za maono ambazo washiriki wote wanaweza
kuzikubali kuwa za msingi kuzifanyia kazi. Kauli hizi zinaweza kuwa
zinahusiana na malengo ya kibinafsi ambayo yamejitokeza katika kauli za
washiriki wote au malengo ya kijamii ambayo kauli nyingi zimekubaliana
nayo. Kisha washiriki wataandika kauli moja ambayo inakubaliwa na
Sehemu ya Tatu: Kuanzisha Ushirika wa Kuelimishana
75
kuungwa mkono na kundi zima na ambayo kila mshiriki atajiona kuwa mmoja
wa waundaji wake.
Itunze kauli hii kwa sababu itahitajika kutumika tena katika Kikao cha Nane.
Maswali ya Kutathmini Semina
Msimamizi au mtu aliyejitolea ataandika mambo yafuatayo kwenye ubao au kwenye
karatasi kubwa ya kuning’iniza wakati wa majadiliano yafuatayo ya kundi.
·  Ni nini umejifunza au kufanikiwa kupata katika vikao vya semina hii hadi
sasa?
·  Je vikao vya semina viliundwa kwa namna nzuri ya kuibusha na
kuhamasisha majadilianao yenye manufaa?
·  Je mambo na masuala yaliyojadiliwa katika kila kikao ni kufaa na kusaidia?
·  Je una maoni yo yote ambayo ungependa kuyatoa juu ya kubadilisha
muundo au mambo yaliyojadiliwa katika vikao vya semina?
·  Je, ilikuwa ni rahisi kwako kushiriki katika majadiliano na mazoezi? Kwa
nini?
·  Je, malengo yako ya kushiriki katika semina hii yamebadilika tangu kikao
cha kwanza? Kama ni ndio, yamebadilika kwa nmana gani?
Maswali kwa Kila Mshiriki katika Kundi
·  Ni majadiliano, zoezi, au shughuli ipi ya semina unaiona kuwa ya faida sana
kuliko zote hadi sasa?
·  Ni sehemu/kipengele kipi cha vikao vya semina hii unachofurahia zaidi
kuliko vyote?
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
76
_____________________________________________________________
Kufasili na kufafanua lengo
ni kujishughulisha kikamilifu katika shughuli ya kujifunza.
Wakati huo huo, ni kujishughulisha
Katika utumiaji wa madaraka.
“Misingi ya Ujenzi una Uongozi”
77
KIKAO CHA NANE
Mpango Wetu wa Utekelezaji ni Upi?
Shabaha za Kikao
§ Kuweka mkazo juu ya umuhimu wa mpango wa utekelezaji
wa shirika.
§ Kushirikiana kama kundi katika upitishaji maamuzi.
§ Kuamua sote kwa pamoja juu ya mpango wa utekelezaji kwa
njia ya kumshirikisha kila mhusika.
§ Kuonyesha jukumu la teknolojia katika kuongeza welewa juu
ya masuala ya kijinsia.
Mapendekezo ya Usimamizi
Soma kwa sauti habari hii ifuatayo kuhusu hatua ambazo shirika moja lilipitia
katika kuweka mpango wa utekelezaji. Jadili katika kikundi jinsi gani shirika
hili lilivyofanya maamuzi kwa njia ya kushirikisha wahusika wote na
yasiyokuwa ya kitabaka msonge. Shughuli za kundi zinazofuatia maswali ya
majadiliano ziwekwa kwa namna ya kuwasidia washiriki wa semina kushiriki
kikamilifu katika kupitisha maamuzi ya pamoja.
Inaweza kuleta matokeo mazuri kwa kuwagawa washiriki katika makundi
madogo madogo ambapo kila mshiriki anapata nafasi ya kutoa maoni yake juu ya
maswali ya majadiliano. Sasa, kwa vile kundi limekuwa likifanya kazi pamoja
katika vikao vichache, hii itakuwa ni nafasi nzuri kuingiza zoezi linalosisimua
ambalo litahimiza kundi kuangalia upya na kwa makini zaidi malengo ya semina
hii ya mafunzo (angalia Kiambatisho B kwa mapendekezo zaidi).
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
78
Demokrrasiia na Wanawake kattiika Uttangazajjii wa Habarrii::
Kuchukua Masaffa ya Rediio Nchiinii Brraziill
Katika miaka ya mwanzo ya 1980, taifa la Brazil lilikuwa katika hatua muhimu na
ngumu za mabadiliko ya kutoka utawala wa serikali ya kidikteta na kwenda
utawala serikali iliyochaguliwa, kutoka vyombo vya habri vinavyodhibitiwa
kwenda kwenye vyombo vya habari vilivyo huru. Katika kipindi hiki cha mageuzi,
wanawake wa Brazil walikuwa mstari wa mbele katika kupigania mabadiliko haya.
Ulikuwa ni wakati wa matumaini kwa wanawake waliokuwa wakitafuta kukalia
nafasi mpya na bunifu za umma ambamo wangeweza kutoa mchango wao mkubwa
katika huo mwelekeo wa Brazil kuwa taifa la kidemokrasia. Thais Corral,
mwanamke mwanahabari na mtetezi wa jinsia ya kike, alikuwa ameishi nchini
Italia kwa miaka kadhaa akiwa anafanya kazi katika kipindi cha redio kinachoitwa
“Saa ya Wanawake” (The Hour of Women”), ambacho kilikuwa kinaendeshwa na
wanawake, kwa ajili ya wanawake, na juu ya wanawake. Kwa mara ya kwanza,
Thais Carral alihusisha vyombo vya habari kama mtetezi wa haki za binadamu na
kama msikilizaji wa redio. Aliporejea nchini mwake, alikutana na kundi maarufu la
wanawake wasomi na wanajinsia na wanasiasa kwenye bunge la Rio. Walikuwa
wakichungua jinsi ya kutumia teknolojia ya habari kungeza uwezo wao wa kufikia
wanawake wengi zaidi. Walitaka kuunda chombo ambacho wanawake
wangekitumia kujieleza na kuwasilisha maoni yao na ambacho kingetumika
kuongeza usawa wa kijinsia na kujenga jamii ya kidemokrasia.
Hata chini ya utawala wa kidikteta uliokuwa umepita, idadi fulani ya vipindi vya
redio vya kisasa na vyenye mwelekeo wa maendeleo vilikuwa vimeanzishwa. Lakini
ni vichache mno vilivyokuwa vimelenga wanawake. Thais Corral na wanawake wa
Rio waliona kwamba licha ya hali hii, redio tayari kilikuwa ni chombo kilichotoa
mchango wa aina yake katika maisha ya wanawake na kwamba “kiutamaduni
redio ni chombo kilichokuwa karibu sana na wanawake kama wasikilizaji na
watumiaji.” Walibaini kwamba wanawake husikiliza redio wakati wakifanya
shughuli nyinginezo, iwe ni nyumbani au kazini. Zaidi ya hayo, matangazo ya redio
yalikuwa na gharama ndogo kuliko ya televisheni na pia yanawafikia watu wengi
waliolengwa, habari na burudani, kuliko yalivyo magazeti.
Corral pamoja na wanawake wa Rio walifanya mpango: Kuwawezesha wanawake
wa Brazil kuwa wapitishaji maamuzi katika vyombo vyao vya habari, hasa kwenye
redio, na wakati huo huo kuongeza ushirikishwaji wa wanawake katika vyombo
vya habari vya Br azil, yaani kuvifanya vinufaishe wanawake kwa kutayarisha
vipindi vinavyoyapatia uzito unaostahili masuala yahusuyo wanawake.
Walikubaliana kuanzisha kipindi cha redio ambacho kingejihusisha na mahitaji na
matakwa ya wanawake. Mnamo mwaka 1988, akiwa amehamasishwa na kipindi
cha wanawake alichokuwa akishiriki kukiandaa huko Italia, Corral, kwa
kushirikiana na kikundi kidogo cha wanawake waliojitolea walidhamiria kuongeza
ushirikishwaji wa wanawake na kuboresha jinsi wanawake walivyokuwa
wakionyeshwa katika vyombo vya habari walianza kutayarisha kipindi cha
maongezi kilichotoka kila juma na
kilichojulikana kama “Fala Mulher” (Wanawake Ongea). Wageni machachari
wanaoshiriki katika kipindi hicho hutoa ushauri wa vitendo kwa wanawake ukiwa
umelenga kutoa ufumbuzi wa matatizo yao ya kila siku, kama vile afya ya uzazi na
unyanyaswaji wa kijinsia, na kuwasaidia wabadilike na kuwa rai wanaofaa.
Mwaka mmoja baada ya kipindi hicho kuanzishwa watoaji wake waziunda shirika
rasmi lililoitwa “Communication, Education, and Information on Gender”
Sehemu ya Tatu: Kuanzisha Ushirika wa Kuelimishana
79
(“Mawasiliano, Elimu, na Habari kuhusu Jinsia”), au CEMINA, likiwa na
dhamira ya kuongeza usawa, utofauti, na sauti za kike katika masafa ya redio
nchini Brazil.
Watayarishaji wa “Fala Mulher” hawakutaka kujifunga na njia moja katika
kukuza kipindi hicho. Walikuwa tayari kufanya majaribio ya mambo waliyokuwa
wakiyatangaza na urefu wa kipindi, walitaka kubadilishana maoni juu ya uzoefu
wao na wa wanawake, na kujifunza kutoka kwa wanawake hao. Nia yao ya
kutojifunga na njia moja na utashi wa kujaribisha mipango yao vilihamasisha
CEMINA kuanzisha semina za mafunzo kwa wanawake nchini kote waliotaka
kuanzisha stesheni zao na vipindi vyao vya redio. Katika kipindi cha kati ya 1992
na 1998, idadi ya wanawake waliokuwa wamepata mafunzo katika semina hizi
iliongezeka kwa mamia, ambapo matokeo yake ilikuwa ni mlipuko wa stesheni za
redio na vipindi vilivyokuwa vikiendeshwa na wanawake nchini kote. Zikiwa na
utajiri mwingi katika habari na mambo mbali mbali ya kiufundi, stesheni hizi na
vipindi vyake viliwageuza wanawake kuwa washiriki halisi katika vyombo vya
habari vya taifa na kuwa watayarishaji kamilifu wa habari na utamaduni ambao
hakuna mtu angeweza kupinga uwezo wao.
Sasa shirika la CEMINA limekwenda mbali na kuvuka mipaka ya redio na kuweza
kujumuisha mtandao wa kompyuta. Shirika hili limetengeneza websaiti yake ili
kusaidia stesheni za redio za wanawake nchini Brazil kuweza kupata habari kwa
urahisi kutoka katika mtandao wa kompyuta wa dunia (WWW) kwa minajili ya
kukuza na kupanua idadi ya wasikilizaji ndani na nje ya nchi. Katika kipindi kirefu
kijacho websaiti hii itawawezesha wanawake wa Brazil kuunganika na wanawake
wenzao walio katika nchi zinazoendelea za kusini mwa dunia na duniani kote na
hivyo kuweza kubadilishana maoni juu ya mbinu za kuongeza welewa na utambuzi
wa masuala ya kijinsia kwa njia ya kutoa utamaduni na maarifa.
Baada ya kutambua kuwa mageuzi ya kweli katika ujenzi wa demokrasia hayawezi
kuwepo bila ya kupendelea jinsia moja, shirika la CEMINA na stesheni ilizosaidia
kuanzishwa vyote vimeweka mkazo kuongeza ushirikishwaji wa wanawake, katika
hali zote za utayarishaji habari na jinsi habari zinavyowasilishwa. Watangazaji
hawa wamweyapatia masuala na matatizo ya wanawake kipaumbele, wakiwa
katika harakati za kuhakik isha kunakuwepo na demokrasia yenye kufaa na yenye
utajiri wa kijinsia kwa ajili ya watu wa Brazil.18
Maswali ya Majadiliano
·  Jinsi gani shirika la CEMINA lilianzishwa? Ni katika mazingira gani shirika
hili liliundwa?
·  Ni kitu gani kilichotiliwa mkazo na “Fala Mulher”? Jinsi gani kipindi
kilitengenezwa?
·  Ni mpango gani wa utekelezaji uliokuwa wa kundi la wanawake wa rio na
baadaye shirika la CIMINA? Mpango huu wa utekelezaji ulikua na
kubadilikaje?
18 Habari hii imetokana na taarifa zilizotumwa na Thais Corral pamoja na mahojiano ya simu ya tarehe 20
Februari, 2001 kati yake na Women’s Learning Partnership
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
80
·  Shirika la CEMINA linapimaje mafanikio? Je, vipo vitu viingine ambavyo
ungetumia kupima mafanikio yake na matokeo yake kwa jamii ya watu wa
Brazil?
·  Jinsi gani CEMINA pamoja na stesheni nyingine za redio viliweza kufanya
habari zaidi kuwafikia wanawake na pia kuwanufaisha?
·  Jinsi gani mpango wa utekeleza ji wa CEMINA ulisaidia mlipuko wa vipindi
vya wanawake?
·  Kwa nini ni muhimu kwa wanawake kuwa watayarishaji na waandishi wa
vipindi vya redio na pia kuwa wasikilizaji?
·  Kwa nini redio kimekuwa chombo cha kufaa sana kwa wanawake, licha ya
kuwepo teknolojia ya juu ya habari na mawasiliano?
·  Ni teknolojia gani ya kisasa ambayo unaweza kutumia ili kuendeleza na
kutetea haki za wanawake ndani ya jamii yako? Redio, televisheni, simu ya
mkononi, Faksi, barua pepe (e-mail), mtandao, au nyinginezo?
Shughuli za Kundi: Kufanya Maamuzi Juu ya Mpango
wa Utekelezaji
Ruhusu kiasi cha muda wa saa moja kwa shuguli hii ya kundi .
Katika Kikao cha 7, kundi liliombwa kuandika kauli moja tu juu ya maono ambayo washiriki
wote wamekubaliana nayo na kuiunga mkono na ambayo kila mshiriki anaiona kumfaa. Katika
zoezi hili, msimamizi au mshiriki aliyejitolea aiandike hiyo kauli ubaoni au kweye karatasi
kubwa ya kuning’iniza ili washiriki waweze kujikumbusha, na aendelee kuandika mambo
muhimu yanayojitokeza katika majadiliano yafuatayo.
1. Waombe washiriki watoe mapendekezo ya mawazo kuhusu kwa vipi kundi
hili linaweza kutekeleza malengo ili kufanya maono yao kuwa jambo la kweli.
Majadiliano haya ni ya kubadilishana mawazo. Kwa hiyo hakuna wazo lililo la
kipumbavu au lisilo na maana. Lengo la kutafuta mawazo ni kupokea mawazo
mengi kadri iwezekanavyo. Jaribu kuorodhesha angalau mawazo 30
yanayotolewa kama njia inayowezekana kwa utekelezaji.
2. Orodha hiyo ikiishakuwa tayari, waelekeze washiriki kujibu maswali
yafuatayo na fanya marekebisho katika orodha kufuatana na majibu yao:
·  Ni mawazo gani katika orodha yanayoweza kuwekwa pamoja au
yanafanana kiasi kwamba kwa makusudi ya utendaji ni kitu kile kile?
Anza orodha mpya inayounganisha mawazo ya utekelezaji
yanayofanana.
·  Ni mawazo gani katika orodha ambayo ni vigumu kuwekwa katika
vitendo? Mara tu washiriki wakiishakubaliana, yakate kwa kupitisha
chaki au peni.
·  Ni katika utaratibu gani washiriki wataorodhesha mawazo
yaliyobakia kiupya na kibunifu? Yapatie namba mawazo kufuatana
na kundi linavyokubaliana juu ya wazo lipi ni namba moja na lipi
Sehemu ya Tatu: Kuanzisha Ushirika wa Kuelimishana
81
linafuatia. Namba moja ikiwa inaonyesha wazo linaloongoza katika
sifa ya upya na ubunifu.
·  Ni katika utaratibu gani washiriki wataorodhesha mawazo
kiutendekaji na kiuwezekano? Tumia alama nyingine au rangi ya
chaki/peni iliyotofauti ili kutofautisha na zile namba
ulizokwishaandika. Andika namba au alama hizo kufuatana na jinsi
kundi linavyopendekeza, namba moja ikiwa inaonyesha wazo
liinaloongoza katika sifa ya kuwezeka na kutendeka kwa urahisi.
3. Mkiwa na taarifa kamili iliyokusanywa juu ya njia zinazowezekana za
utekelezaji wa kauli ya maono, waelekeze washiriki kupitia tena orodha hiyo
na fanya uamuzi wa pamoja juu ya mpango (mipango ya) wa utekelezaji.
Uchunguzi
·  Je, zoezi hilo hapo juu lilikuwa rahisi au gumu kwako kushiriki katika majadiliano
na kupitisha uamuzi?
·  Je, hatua ya utoaji mawazo ilikuwa shughuli uliyonufaika nayo? Kwa nini?
·  Je, umeridhika na mpango wa utekelezaji uliokubaliwa mwishoni? Je, unajisikia
kuwa kama umesaid ia katika kuunda huo mpango? Kwa nini?
·  Je, umeona mifano ambapo mtu mmoja anatumia au kujenga wazo lake kwa
kuendeleza au kukuza wazo la mtu mwingine? Mifano ya watu kujifunza kutoka
kwa wengine ndani ya kundi?
·  Je, umewahi kushiriki katika kufanya maamuzi ya pamoja katika kundi
yaliyofanyika kwa namna tofauti na haya? Kama ni ndiyo, hayo maamuzi
yalipitishwaje? Je, yalishirikisha wahusika wote? Uliridhika na uamuzi wa
mwisho?
·  Je, unafikiri kwamba kuna tofauti yo yote ile kati ya kundi linalofanya maamuzi
likiwa ni la wanawake tu, wanaume tu, au mchanganyiko? Kwa nini?
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
82
_____________________________________________________________
Malengo ya kweli hayawezi kuchaguliwa bila pia kutoa
ufafanuzi wa kuaminika wa nyenzo na/watu halisi
Waliopo au wanaoweza kuwepo kuwezesha kufikia malengo hayo.
“Misingi ya Ujenzi wa Uongozi”
83
KIKAO CHA TISA
Jinsi Gani Tunaweza Kukuza Vipaji na Ujuzi
Wetu?
Shabaha za Kikao
§ Kueleza maana yote ya ushauri na ubora wa mpango wa ushauri
uliyo bora.
§ Onyesha thamani ya watu wala shirika linalo gawanya maarifa
taarifa.
§ Heleza ukitumia mfano jinsi gani kugawanya maarifa na taarifa ni
muimu ajili ya ujenzi na kustaimili elimu.
Kabla ya kuanza: Waambie washiriki kuanza kufikiria juu ya jinsi gani wangependa kufunga
semina hii. Ni muhimi kupanga mapema ili washiriki waondoke katika semina wakiwa wanajisikia
kuwa mahitaji na matarajio yao vimezingatiwa na kushughulikiwa. Sehemu ya kitabu hiki
“Kuwasiliana katika Mazingira ya Semina” inazungumzia zaidi juu ya mada hii.
Mapendekezo ya Usimamizi
Soma kwa sauti habari hii juu ya shirika moja nchini Nigeria ----lijulikanalo
kwa jina la BAOBAB for Women’s Human Rights (kwa ajili ya Haki za
Kibinadamu za Wanawake)----ambalo programu zake na utendaji wake wa
ndani vyote vimeelekezwa kukuza ujuzi na vipaji vya wafanyakazi wake na
wanashirika kwa njia madhubuti za ushauri na mafunzo. Jadili katika kundi
vigezo vya shirika lililo katika mafunzo na sifa zipi za shrika la BAOBAB
zinazolandana na vigezo hivi. Maswali na zoezi vinavyofuatia vinaweza
kusaidia kuongoza majadiliano ya kundi.
Wasimamizi wengi wamegundua kuwa panakuwepo na mafanikio
makubwa majadiliano haya yanapoendeshwa katika kundi zima, ambapo
washiriki wanapata nafasi ya kunufaika na maoni na mawazo ya kila
mshiriki (angalia Kiambatisho B kwa ajili ya mapendekezo zaidi).
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
84
Uwanjja wa maffundiisho:: Kushaurrii Wanawake Nchiinii
Niigerriia
Kuwaleta watu katika uwanja wa mafundisho na kisha kuupanua uwanja huo---
ushauri ni shughuli ambayo ni muhimu kujenga uwezo wa shirika na kuhakikisha
kuwa ninadumu. Shirika ambalo lilianzishwa na Ayesha Imam akishirikiana na
wengine, shirika la BAOBAB kwa ajili ya Haki za Kibinadamu za Wanawake,
limelenga kuboresha maarifa, utendaji, na maendeleo ya haki za kibinadamu za
wanawake chini ya sheria za kimila, kidini, na kiserikali za nchini Nigeria. Jina la
shirika hili pia ni jina la mti unaopatikana sehemu zote za bara la Afrika kusini
mwa jangwa la Sahara. Mbuyu ni mti unaoweza kuvumilia na kuhimili hali mbaya
zote za hewa, unatoa chakula na dawa kwa binadamu, na malazi kwa wanyama
wadogo. Shirika la BAOBAB limedhamiria kufuatisha sifa za mti huu---nguvu na
ustahamilivu---kwa kuwahamasisha wanawake na kuwawezesha kupata madaraka
kwa kuwapa ujuzi wanaoweza kuutumia katika maisha yao ya kila siku na
kuwasaidia watu wengine. Katika mwelekeo huo shirika linawapa uwezo na
kuwahamasisha wanawake ambao wanashiriki katika programu zake kuwa huru
katika kufikiri na kutenda.
Shirika la BAOBAB linasaidia na kutetea haki za kibinadamu za wanawake kupitia
shughuli mbalimbali---hasa kwa kuamsha ari, kutoa mafunzo, kuchapisha
maandishi, na kujenga ushurikiano. Kitovu cha shughuli hizi ni matumizi ya
teknolojia. Waanzilishi wa shirika hili hawaoni teknolojia kuwa kitu kibaya au
kizuri katika uhalisi wake. Bali wanaona suala muhimu ni nani anayetawala
teknolojia, inatumiwaje, na ni matokeo gani yanayotokana na matumizi yake. Kwa
mfano, shirika la BAOBAB hutegemea sana mashini za fotokopi kuchapisha na
kusambasa habari kwa wanawake ambao vnginevyo wasingeweza kupata habari
hizo. Pia hutegemea kompyuta kuelimisha wanawake katika ujuzi mbalimbali kama
vile kupiga chapa na kutunza mahesabu; na hutegemea mawasiliano kwa baruapepe
(e-mail) na mtandao kuwasiliana na kushirikiana na vikundi vilivyo katika
harakati kama zake. Utumiaji hu wa teknolojia ya kisasa pia unachangia katika
kukuza mbinu miundo za mawasiliano kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika.
Mbinu ya shirika la BAOBAB katika kutoa elimu juu ya haki za kibinadamu za
wanawake ni ya kutumia nyezo mchanganyiko, uzoefu, na vitendo. Wakufunzi
hujua kuwa wanafunzi wao huja katika mazingira ya wajibu na haki mpya wakiwa
na kapu la uzoefu wa nyuma na kwa kuegemea katika uzoefu huu, uhimiza
wanawake kueleza na kubadilishana na wengine uzoefu wao ili wakufunzi na
wanafunzi wote waweze kujifunza mitazamo na ujuzi mpya. La muhimu zaidi,
shirika la BAOBAB huwapa mafunzo wanawake katika ujuzi ambao ni muhimu
katika maisha yao ya kikazi na/au kibinafsi. Kwa mfano, wakati linatoa mafunzo
katika utumiaji wa programu za kompyuta, shirika la BAOBAB huwafundisha
wafanyakazi wake lenyewe pamoja na watu wanaojitolea jinsi ya kutumia
programu ya spredshiti ili waweze kuweka na kutunza vizuri mahesabu ya shirika
au kupiga taipu ili waweze kuandika ripoti na masimulizi yao wenyewe.
Wito wa shirika hili ni: “Hauwezi kubadilisha yaliyopita, lakini unaweza
kujaribisha kubadilisha yajayo!” Kubadilisha, na hasa kuboresha, maisha yajayo
kunajumuisha utambuzi wa kwamba mtazamo na jitihada za mtu zinaweza kuleta
matokeo makubwa kwa wengine. Mafunzo ya Kampeni ya Mshikamano kwa njia ya
Barua-pepe ya shirika la BAOBAB (BAOBAB’s
Email Solidarity Campaign Training) na Mafunzo yake ya Wanawake na Sheria
(Women and Law Programme) yanaoenyesha manufaa ya muda mrefu ya kukuza
uwezo, vipaji, na moyo wa kujiamini wa watu wengine. Mafunzo ya Kampeni ya
Sehemu ya Tatu: Kuanzisha Ushirika wa Kuelimishana
85
Mshikamano kwa njia ya Barua-pepe yalianza mwaka wa 1998-99 yakiwa na
wanawake karibu hamsini waliokuwa wakihudhuria semina za mafunzo ya baruapepe
na utumiaji wa mtandao kwa jumla ili kuimarisha kampeni za mshikamano
kwa ajili ya haki za wanwake, na kuboresha mawasiliano na kusaidiana baina na
kati ya watetezi wa haki za binadamu wazungumzao Kiingereza na Kifaransa kote
barani Afrika. Wanawake hawa wanawasiliana na wanaendelea kubadilishana
habari na mbinu. Wakiwa na ujuzi mpya au ulioboreshwa, wanawake sasa
wanashiriki kikamilifu katika mazungumzo na mijadala juu ya haki zao katika
ngazi za kikanda na kimataifa. Mafunzo ya Wanawake na Sheria nayo hivyo hivyo
yalileta pamoja vikundi vidogo vya wanawake na wanaume wachache kufanya
utafiti juu ya utendaji na kuchungua welewa na uzoefu wa wanawake juu ya sheria
za Kiislamu, kimilla, na kiserikali. Mwanamke mmoja aliyeshiriki atakuwa
mwanamke wa kwanza kupata shahada ya juu katika sheria za Kiislamu kutoka
chuo kikuu cha nchini Nigeria. Naye atajaribu kuwaelimisha wengine na pia
kutumika kama mfano wa kuigwa kwa wanawake wengine wanaodhamiria kuvuka
vizuizi vya kimila na kuonyesha kuwa wanastahili nafasi zao mpya katika jamii.19
Maswali ya Majadiliano
·  Shabaha kuu ya BAOBAB ni nini?
·  Unaweza kulielezaje mbinu ya shirika hili la BAOBAB kuhusu utoaji ushauri? Ni
mafao gani ya muda mrefu na muda mfupi ya mbinu hii? Je, unaona kuna mambo
yo yote yasiyokuwa na mafao katika mbinu hii?
·  Ni vitu gani vingine unavyoweza kuongeza katika mpango wa ushauri?
·  Mshauri bora ana tabia gani? Je, mshauri anaweza kuwa mshauriwa?
·  Ni jukumu gani teknolojia inachangia katika jitihada za BAOBAB kukuza uwezo
na vipaji vya wanawake?
·  Ni nini faida, kwa mfano, ya kufundisha wafanyakazi wa BAOBAB na
watumishi wenye kujitolea kutumia programu ya kompyuta ya Excel? Jinsi gani
mbinu hii ya mafunzo ya kutumia programu za kompyuta inaweza kuwanufaisha
washiriki wanaohusika? Jinsi gani inalisaidia shirika la BAOBAB? Jinsi gani
inaisadia jamii?
·  Ni kwa jinsi gani unaweza kuelezea au kufasili shughuli ya ushauri?
·  Je, umewahi kufaidika na ushauri? Unaweza kufikiria tukio lo lote ambamo
ushauri uliweza kukusaidia?
·  Je, umewahi kuwa mshauri? Eleza wengine mbinu za ushauri ulizowahi kutumia
au ungependa kuzitumia katika maisha yako ya kibinafsi na/ au ya kikazi. Ni
faida gani ulipata ulipotoa huduma ya usahuri.
·  Jinsi gani ushauri unaweza kutumiwa na wanawake ili kuwasaidia wanawake
wengine?
19 Habari hii inatokana na taarifa aliyoituma Ayesha Imam pamoja na mahojiano ya simu ya tarehe 10
Januari, 2001 kati yake na Women’s Learning Partnership.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
86
Zoezi : Kuandaa Mpango wa Ushauri katika Jumuia
Ruhusu kiasi cha muda wa saa moja na dakika kumi na tano kwa zoezi hili.
Mpango wa ushauri unaweza kuwa mpango huru, mradi unaojitegemea katika
jamii, kama vile mpango wa mafunzo baada ya saa za shule ambamo
wanafunzi wa umri mdogo wanakutana na wanafunzi wa umri mkubwa kwa
ajili ya ushauri. Au, mradi unaweza kuegeshwa katika jumuia au ushirika
mkubwa zaidi, kama vile mpango uliounganishwa na wodi ya wazazi katika
hospitali ambao upanga akina mama wapya kukutana na akina mama wenye
uzoefu mkubwa zaidi kwa ajili ya ushauri. Katika zoezi hili, vikundi vidogo
vidogo vitaandaa mpango wa ushauri wa jinsi yao wenyewe ambao unaingia
vizuri katika mojawapo ya aina zilizoelezwa hapo juu---mradi huru au
ulioegemezwa kwa mradi mkubwa.
1. Ligawe kundi katika vikundi vidogo vidogo vya kati ya washiriki watatu na
washiriki watano. Angalau mwanakikundi mmoja katika kila kikundi
atafanya kazi ya kuandika mambo muhimu, na huyo huyo au mtu
mwingine aliyejitolea atatakiwa kutoa taarifa ya majadiliano ya kikundi
kwa kundi zima la semina. Kwa karibu muda wa dakika 20-30, kila kikundi
kizingatie na kujadili haya yafuatayo:
·  Ni watu wa aina gani ambao mpango wenu unalenga
kuwasaidia? Baadhi ya mifano inajumuisha wasichana
wadogo walio katika shule moja ya kijijini au mjini ambao
wanataka kuwa viongozi wakiishakuwa watu wazima, akina
mama wa nyumbani wanaotamani kuanzisha biashara yao ya
nyumbani, au wanawake ambao ndio kwanza
wamechaguliwa katika nyadhifa za uongozi. Vikundi vinaweza
kutumia mfano wo wote kati ya hii iliyotolewa au kubuni wa
kwao wenyewe kutegemeana na mahitaji ya ushauri na ulezi
wanayoona katika jamii au maishani mwao
·  Ni aina gani ya watu mnaofikiri watakuwa na ujuzi wa kutosha
kutoa usahuri kwa wasahuriwa watarajiwa mlilobainisha? Je,
wapo watu wenye uzoefu wa kibinafsi, maarifa ya kitaalamu,
au sifa nyinginezo ambazo zitakuwa za mafao makubwa kwa
waliokusudiwa?
·  Ni kwa jinsi gani washauri watawasaidia na washauriwa? Je,
watakuwa wanakutana kila wiki, wataendesha semina ya
mafunzo, watashiriki pamoja katika baadhi ya shughuli?
Watakuwa wanakutana kwa muda gani? Mara ngapi?
·  Je, washauriwa au washauri katika mpango huu watatokea
kuletwa pamoja kama kundi ili kukutana na wenzao kwa ajili
ya kusaidiana na ushauri? Ni mambo gani itafaa yafanyike
katika mkutano kama huu?
·  Fikiria mahitaji ya washauriwa na kwa jinsi gani mpango huu
unaweza kukidhi kwa uthabiti mahitaji hayo. Vile vile, ni
muhimu mfikirie mahitaji ya washauri na jinsi gani mpango
huu utapangwa ili utoe nafasi ya kukidhi kiu yao ya kutoa
ushauri na kuridhisha nafsi zao pia.
Sehemu ya Tatu: Kuanzisha Ushirika wa Kuelimishana
87
2. Vikundi vidogo vidogo vinaporejea na kukutana kama kundi zima la
semina, mtu mmoja kutoka kila kikundi ataeleza mpango wa ushauri wa
kikundi chake. Washiriki wa semina wanaweza kuuliza maswali au kutoa
maoni yao na mapendekezo juu ya mipango ya usahuri inayowasilishwa
kutoka vikundi vido vidogo.
Uchunguzi
·  Ni kitu gani ulichopendelea au kuchukia katika zoezi hili?
·  Je, lilikuwa jambo gumu kwako kutathmini au kutoa maoni juu ya mipango
ya ushauri ya vikundi vingine? Kwa nini?
·  Je, zoezi hili lilikusaidia kupata fikiria njia mpya na bunifu za kuanzisha
mpango wa usahuri katika jamii yako? Kama ni ndiyo, ni njia zipi?
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
88
______________________________________________________________
Tunahitaji kuleta uwezekano wa matumizi ya mtandao
kwa watu wote ulimwenguni na hiyo haihusishi tu
mashini za kompyuta na matumizi yake ,
bali pia utengenezaji wa programu zinazozingatia
utamaduni, lugha, na jumuia husika.
“Misingi ya Ujenzi wa Uongozi”
89
KIKAO CHA KUMI
Tunahamasishaje kwa ajili ya Vitendo?
Shabaha za Kikao
§ Kuchunguza mbinu za uhamasishaji wa kampeni.
§ Kujadili juu ya vipengee vipi ni muhimu katika mpango wo wote wa
shirika unaopaswa kutekelezwa ikiwa ni pamoja na kubaini maono,
kuweka malengo, kufafanua mbinu, kukusanya nyenzo zote na
watendaji wanaohitajika, kutekeleza shughuli katika mtindo wa
kujumuisha na kushirikisha, na kuweka vigezo vya kutathmini ubora.
§ Kutafakari na kuchungua jukumu la teknolojia ya mawasiliano---
baadhi ikiwa ni simu, mashini za faksi, kompyuta, na mtandao---
katika jitihada za kuhamasisha kijamii ndogo, kitaifa, na kimataifa.
Mapendekezo ya Usimamizi
Soma kwa sauti habari ifuatayo kuhusu kampeni ya kimataifa ya kupiga
marufuku matumizi ya mabomu ya ardhini. Jadili katika kundi hatua
zinazochukuliwa na washiriki katika kampeni hii kuhamasisha uungwaji mkono
wa dunia nzima kwa ajili ya Mkataba wa Kimataifa wa Kupiga Marufuku
Mabomu ya Ardhini. Maswali yanayofuatia yanaweza kusaidia kuongoza
majadiliano ya kundi.
Baadhi ya washiriki wanaweza kuwa na hoja nzito juu ya mada hii kuliko
wengine na hivyo kutaka kushiriki kikamilifu katika majadiliano ya msingi
ambayo baadaye yanaweza kuelekea kwenye majadiliano ya kundi zima.
Jaribu kutumia mbinu ya usimamizi ya kuwafanya washiriki kila mmoja
amuone na kumsikia mwingine ili kuleta mazungumzo ya kina na ya moja
kwa moja kwenye mada (angalia Kiambatisho B kwa taarifa zaidi).
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
90
Kampenii ya Kiimattaiiffa ya Kupiiga Marruffuku Mattumiizii ya
Mabomu ya Arrdhiinii
Mbegu za kwanza za Kampeni ya Kimatifa ya Kupiga Marufuku Mabomu ya
Ardhini (International Campaign to Ban Landmines (ICBL)) zilipandwa katika
miaka ya mwishoni mwa 1980 na mwanzoni mwa 1990 kupitia jitihada za
mbalimbali tofauti za mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs) katika nchi
zinazotengeneza mabomu ya ardhini. Katika kipindi cha mika 50 iliyopita,
mabomu ya ardhini yamesababisha vifo vingi na majeraha mengi kuliko silaha za
nyuklia, kibayolojia, na kemikali zikiwekwa pamoja. Baada ya kutambua mgogoro
wa kibinadamu uliyokuwa ukinyemelea wa mamilioni ya mabomu ya ardhini
yaliyosambaa katika mamia ya nchi duniani kote, mashirika machache yasiyokuwa
ya kiserikali (NGOs) yaliunganisha jitihada zao kulishughulikia suala hili. Ili
waweze kulitokomeza kabisa tatizo hili, walikubaliana kuwa silaha zenyewe ni
lazima zitokomezwe. Jitihada yao ya pamoja ililenga kwenye upitishaji wa sheria
za kupiga marufuku mabomu haya kitaifa, kikanda, na kimataifa. Walianza kwa
kujenga umoja wa kimataifa wa NGOs katika ngazi za jamii ndogo ndogo, kitaifa,
na kimataifa kushiriki katika jitihada za kampeni hiyo.
Nguvu na mategemeo ya kampeni ya ICBL ilikuwa ni kutong’ang’ania njia moja tu
ya ufumbuzi. Mawazo na mitazamo yote ilikaribishwa. Ulikuwa ni umoja wa
mashirika ambao ulikuwa na muundo uliokuwa namitazamo na utaalamu mbali
mbali. Ili kukwepa kuunda urasimu ambao ungekuwa unatoa amri kwa mashirika
kutimiza wajibu wake, washirika wa ICBL waliona kuwa matokeo mazuri
yangepatikana iwapo kila NGO itaamua mwelekeo wake wa shughuli zake. Kwa
njia hii, NGOs yangeweza kutekeleza mambo au vipengee vya jitihada hizi ambayo
yalikuwa nadani ya mipaka ya mamlaka na muundo wake wa kishirika. Mashirika
yaliyokuwa yakishughulikia masuala ya kitaifa yalitia shinikizo serikali za nchi
katika ngazi ya kitaifa, wakati yale mashirika yaliyokuwa yakishughulikia masuala
ya kimataifa yalielekeza jitihada zake katika ngazi za kimataifa.
Kitu kilichoanza na washiriki wachache, haukupita muda ikawa kampeni kubwa
iliyokuwa na zaidi ya mashirika 1,200 kutoka nchi zilizoshiriki 80. Mikutano ya
kitaifa, kikanda, na kimataifa nayo haikuchelewa kuanza kupata idadi kubwa sana
ya mashirika yaliyokuwa yamejitolea muda wao, watumishi, na mali yao
kuendesha kampeni hiyo. Ili mashirika mengi kama hayo na watu wengi duniani
kote kuweza kutekeleza lengo lao kwa ufanisi, mawasiliano ya wazi na madhubuti
kilikuwa ni kitu cha lazima. Teknolojia ya kisasa ya habari na mawasiliano ilitoa
mchango mkubwa sana katika kufanikisha jitihada za uhamasishaji. Baadhi ya
mbinu zilizofanikisha ilikuwa ni pamoja na taarifa rasmi za habari, habari za kila
wakati kadri matukio yanavyotokea, kujulishana ukweli na takwimu, na maombi ya
haki kutoka kwa umma wa wananchi ya ICBL kiasi kwamba serikali zilianza
kutegemea kampeni hiyo kupata taarifa na habari zilizokuwa sahihi na kuwasili
katika wakati unaofaa kuliko habari zilizokuwa zinapatikana kupitia vyombo vya
kawaida vya serikali.
Mwanzoni, kampeni ya ICBL kwa kiasi kikubwa ilitegemea matumizi ya simu,
mashini za faksi, na barua za kawaida za posta. Jody Williams, mtunukiwa wa
Tunzo ya Amani ya Nobel kwa juhudi yake aliyofanya juu ya kupiga marufuku
matumizi ya mabomu ya ardhini, alieleza matumizi ya faksi
katika miaka ya mwanzoni mwa kampeni akisema: “ faksi kilikuwa chombo kipya
na chenye ‘kusisimua’.Habari zilizokuwa zikitufikia karibu papo kwa papo kupitia
kwenye faksi zilikuwa zikifikiriwa kuwa na umuhimu zaidi---na kwa hiyo zilistahili
Sehemu ya Tatu: Kuanzisha Ushirika wa Kuelimishana
91
kushughulikiwa haraka---kuliko zile zilizokuja kwa barua za kawaida.” Kutegemea
sana faksi na simu ilikuwa ni njia ya gharama kubwa lakini yenye ufanisi mkubwa.
Kampeni ilipoanza kupanuka na kuingia katika nchi za Kusini zilizokuwa
zimeathirika kwa mabomu haya, washirika wake waligeukia matumizi ya baruapepe.
Ingawa bado njia ya barua-pepe ilikuwa ya ghali na ngumu kutumiwa katika
sehemu nyingi za dunia, ilikuwa na faida kubwa za gharama na muda kuliko
mawasiliano ya faksi.
Kwa kawaida, NGOs na serekali mara kwa mara huhojiana na kujibizana kama
vile washindani. Kufuatana na hali hiyo, sehemu ya mbinu ya uhamasishaji ya
kampeni hii kwa makusudi kabisa ilijihusisha na kubuni na kukuza uhusiano mzuri
katika ya mashirika yaliyoshiriki na serikali za nchi zao. Kampeni iliziomba
serikali kuchukua jukumu la kujenga mazingira ya umoja na ufanisi kwa njia ya
kuunda jumuiya ya serikali zinazounga mkono upigaji marufuku wa mabomu ya
ardhini ambayo ingeendeleza na kulinda masilahi ya kitaifa ya nchi zao. Mnamo
mwaka 1996, kampeni ya umoja wa ICBL ilikuwa imefanikiwa kuungwa mkono na
idadi kubwa ya serikali pamoja na maelfu ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali
(NGOs) yanayojishughulisha na misaada ya kibinadamu, watoto, amani, askari
wastaafu, matibabu, maendeleo, udhibiti wa silaha, dini, mazingira, na wanawake.
Katika mwaka huo huo serikali ya Canada ilitoa ufadhili wa kuwa mwenyeji wa
mkutano jijini Ottawa ambao ungehusika na kuunda mpango wa utekelezaji wa
kierikali katika ngazi za juu kwa ajili ya utekelezaji wa kupiga marufuku mabomu
hayo. Serikali ya Canada ilishirikiana kwa karibu sana na wanachama wa ICBL,
na ilizipa serikali nyingine changamoto ya aina yake ya kujadiliana na kuafikiana
juu ya mkataba wa kimataifa wa kupiga marufuku mabomu hayo ambao ni rahisi
na usiokuwa tata katika kipindi cha mwaka mmoja.
Majadiliano yaliyofuatia yalikuwa ya aina ya kipekee kwa sababu ya kiasi
ambacho serikali zilitegemea wanachama wa ICBL kwa habari na utaalamu wa
kiufundi. Matokeo yake ni kwamba nchi za ukubwa wa kati na wa chini zilishikilia
msimamo wa kuunga mkono mkataba ambao ulifikiriwa kama tishio kwa uhuru wa
baadhi ya nchi kubwa. Mnamo Desemba 1997, serikali 121 zilirudi tena Ottawa
kuweka sahihi Mkataba wa Kimataifa wa Kupiga Marufuku Mabomu ya Ardhini
(the international Mine Ban Treaty). Lloyd Axworthy, Waziri wa Mambo ya Nje wa
Canada, aliielezea kampeni ya kupiga marufuku mabomu ya ardhini katika hotuba
yake ya ufungaji wa mkutano kama “dhamira inayoendelea kuimarisha ubia na
ushirikiano ambao utatuwezesha sisi sote kufanikiwa katika kufikia malengo yetu.”
Tarehe 1 Machi, 1999, Mkataba wa Kupiga Marufuku Mabomu ya Ardhini ulikuwa
sheria ya kimataifa.20
Maswali ya Majadiliano
·   Ni nini ilikuwa shabaha ya msingi ya ICBL? Kwa nini washirika wa kampeni hii
waliunda shabaha yao kwa namna hii?
·   Jinsi gani unaweza kufafanua muundo wa kampeni hii? Ni faida gani za muundo huu?
Je, unaweza kubaini udhaifu wo wote?
20 Habari hii juu ya Kampeni ya Kimataifa ya Kupiga Marufuku Mabomu ya Ardhini imechukuliwa kutoka
katika makala ya Jody Williams, “The International Campaign to Ban Landmines: A Model for Disarmament
Initiatives?” ambayo inakutwa http://www.nobel.se/peace/articles/williams/ na kutoka saiti ya World Council
of Churches http://www.wcc-coe.org/wcc/what/international/landmines/mines-e.html.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
92
·   Kwa nini mawasiliano yalikuwa muhimu katika kampeni hii?
·   Jinsi gani washiriki kwenye kampeni hii waliweza kurahisisha mawasiliano baina ya
watu, mashirika, na serikali nyingi kiasi hicho duniani kote?
·   Ni kitu gani kilichofanya ICBL kuwa na mafanikio na mfano wa kuigwa kwa kampeni
nyinginezo?
·  Ni vitu gani vya msingi katika mpango wo wote ule wa uhamasishaji?
Zoezi: Kuhamasisha Kwa Ajili ya Msaada
Ruhusu kiasi cha muda wa dakika 30-40 kwa zoezi hili.
Tetemeko za Ardhi Lawaacha Mamilioni ya Watu Bila Nyumba, Maji Safi,
na Matibabu
Tarehe 13 Januari 2001, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.6 kwa Kipimo cha
Richter, lilitikisa pwani ya El Salvador, kiasi cha maili 65 kusini-magharibi mwa San
Migeul, huku likifuatiwa na miporomoko ya ardhi iliyokaribia 200 na pia mishituko
zaidi ya 1,950. Tetemeko hilo la ardhi, lilisababisha vifo vya watu zaidi ya 800 na
majeruhi zaidi ya 4,500. Karibu nyumba 92,000 ziliharibiwa kabisa na nyingine
130,000 ziliharibiwa kidogo. Zaidi ya shule 1,200 pamoja na mashamba 30,000
yaliharibika kabisa na kiasi. Idadi ya watu wote waliokumbwa na shida hiyo ilikuwa ni
zaidi ya milioni 1.1.21
Igizo: Kundi la akina mama wanne katika jamii yako wanakutana katika maongezi
ya kawaida karibu mara moja kila wiki wakielezana habari na visa juu ya familia zao,
wakipeana ushauri, na kujenga urafiki na kusaidiana. Siku moja mchana,
mmojawapo wa wanawake hao analeta habari iliyochapishwa katika gazeti la mjini
hapo juu ya tetemeko la ardhi huko El Salvador. Ana jamaa yake wa karibu
aliyeponea chupu chupu maafa ya tetemeko la ardhi yaliyotokea katika nchi nyingine
na kwa hiyo anajaribu kufuatilia tukio hilo la El Salvador kwa makini sana.
Anawasomea kwa sauti wenzake habari hiyo iliyo kwenye gazeti ambao nao
wanakubaliana naye kuwa hili janga litakuwa lim esababisha madhara yasiyo na
kifani kwa akina mama ambao ni lazima waangalie watoto wao katika hali hii ngumu.
Mwanamke mmoja katika kundi anapendekeza kwamba ni muhimu wachukue hatua
ya kusaidia akina mama walioathiriwa na tetemeko hilo. Anaungwa mkono na
wanawake wengine ambao mara moja wanaanza kupanga mbinu yao ya kutekeleza
hiyo azma.
1. Kundi la wanasemina linagawanyika katika vikundi vidogo vidogo vya watu wanne
wanne. Kila kikundi, kama wanawake hao wanne walivyofanya katika igizo la hapo juu,
kitaweka mpango wake wa utekelezaji wa kusaidia akina mama ambao wamepatwa na
shida kutokana na tetemeko la ardhi huko El Salvador.
2. Baadhi ya maswali ambayo kila kikundi kijaribu kuyashugulikia ni kama ifuatavyo:
·   Jinsi gani mnapendelea kusaidia akina m ama? Ni aina gani ya msaada ambao
mngependa kutoa? kampeni yenu itakuwa ya aina gani?
·   Je, kampeni yenu itakuwa ya ngazi gani, ngazi ya mji/kijiji, ya kitaifa, ya kikanda, au
ya kimataifa?
·   Je, mtatumia mbinu gani ya kuhamasisha kwa ajili ya kuungwa au kukuza uungwaji
mkono. Ni shughuli zipi mtazifanya?
21 Hili ni tukio la kweli. Angalia http://www.cnn.com/2001/WORLD/americas/01/15/quake.04.
Sehemu ya Tatu: Kuanzisha Ushirika wa Kuelimishana
93
·   Je, ni nji ya kufaa kuwaomba wanawake wengine kushiriki katika kuwasaidia akina
mama hao? Kwa nini? Je, mnafikiri wanaume nao wanaweza kuitika wito huo?
·   Je, kikundi chenu kinaweza kutumia faida za teknolojia ya mawasiliano, au njia
nyingine za teknolojia ya habari, kama vile makala za magazetini au vipindi vya
kielimu vya redio au televisheni, kuhamasisha uungwaji mkono zaidi?
·   Ni ushirika gani unaowezekana mnaofikiri kwamba unaweza kuwasaidia kufikia
malengo yenu?
·   Mtatumia njia zipi kufanya tathmini ya kujua iwapo mnafanikiwa au la? Mtatumia
vigezo gani?
·   Mtagawanaje majukumu baina yenu ili kuendesha shughuli zenu kwa ufanisi zaidi?
3. Wanakikundi wanapaswa kuandika orodha ya mambo watakayofanya, wakionyesha
hatua watakazofuatia katika kipindi cha wiki chache zijazo ili kutekekeleza mpango wao.
4. Vikundi vyote vikiishamaliza kuweka mipango yao ya utekelezaji, washiriki wote
watarudi tena kwenye mkao wa kundi zima la semina. Mtu aliyejitolea kautoka kila
kikundi ataeleza kwa kifupi mbinu ya uhamasishaji ya kikundi chake.
Maswali ya Majadiliano
·  Hatua gani zilichukuliwa na kikundi chako katika kupitisha maamuzi?
·  Ni sehemu gani ilikuwa ngumu sana katika kuunda mbinu yenu ya uhamasishaji?
·  Je, ingekuwa rahisi au ngumu zaidi kufanya uamuzi juu ya hatua mahususi
zinazohitajika kuchukuliwa kama wangekuwepo watu wengi zaidi katika kikundi
chenu?
·  Je, mlifikia je makubaliano ya kugawanya majukumu? Je, kuandaa orodha ya
majukumu ilisaidia kuweka wazi ni nini lingekuwa jukumu la kila mwanakikundi?
Je, njia hiyo ya orodha ilisaidia mambo mengine? Kama ni ndiyo, ni kwa vipi?
Kama siyo, kwa nini?
·  Je, shughuli za kikundi chako zinaonekana kuwa za kikweli? Kwa nini?
·  Baada ya kusikia maelezo ya shughuli za vikundi vingine, ,je kuna jambo lo lote
ambalo mngependa kuongezea kuboresha mpango wa kikundi chenu?
Uchunguzi
·  Je, zoezi hili lilikusaidia kukupa maarifa ya kufikiria mpango wako binafsi wa
kampeni au wa mradi juu ya tatizo jingine tofauti na hili? Kwa nini?
·  Kama ukifikiria kuanzisha kampeni yako mwenyewe, unafikiri itakuwa ya aina
gani na ni jinsi gani utaiendesha?
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
94
____________________________________________________________
Kazi ya pamoja ndio hali halisi ya jumuia zilizo katika mafunzo.
Kazi ya pamoja huhusisha kuheshimiana, kukubali utofauti, na ukarimu
katika ngazi ya mtu binafsi, na pia uwezo wa kusuluhisha mgogoro,
kuleta watu pamoja katika kufanya maamuzi na utekelezaji wa
maamuzi,
na kujenga timu katika ngazi ya shirika.
“Misingi ya Ujenzi wa Uongozi”
95
KIKAO CHA KUMI NA MOJA
Jinsi Gani Tunaweza Kugawanya
Majukumu na Matokeo?
Shabaha za Kikao
§ kuchambua jinsi ya kuanzisha utamaduni wa kugawanya
madaraka na ushirikishaji ndani na baina ya mashirika
yanayofanya kazi kwa kushirikiana.
§ Kujadili mbinu za kutumia kikamilifu vipaji na uzoefu wa
washirika mmoja mmoja katika jitihada za kampeni ya pamoja.
§ Kufanya kazi kama timu kuunda shirika dhahania ambalo
linajumuisha sifa zote nzuri zilizochunguzwa na kujadiliwa
katika semina hii nzima.
Mapendekezo ya Usimamizi
Soma kwa sauti habari hii inayofuatia kuhusu jinsi gani mashirika mengi
yalivyoshirikiana katika kazi ya kupitisha Sheria ya Unyanyasaji wa Nyumbani
nchini Malaysia (Malaysia’s Domestic Violence Act). Jadili katika kundi la
semina juu ya mbinu zilizotumiwa na mashirika kuratibu juhudi zao na
kugawiana wajibu. Maswali yanayofuatia habari hii yanaweza mwongozo wa
majadiliano ya kundi. Baada ya maswali ni zoezi lililoundwa kwa namna ya
kuwasaidia washiriki kuunda akilini shirika, taasisi, au kampeni yao wenyewe
ya kufikirika ambayo inatimiza vigezo vya kiuongozi ambavyo wamevibaini na
kuvijadili katika vikao vyote vya semina hii. Katika Kikao cha 12, kila mshiriki
atapata nafasi ya kueleza juu ya shirika lake la kufikirika mbele ya kundi lote la
semina.
Mbinu ya usimamizi katika kikao hiki inaweza kuhusisha kufanya
majadiliano ya kundi zima au kugawa washiriki katika vikundi vidogo
vidogo (angalia Kiambatisho B kwa mapendekezo zaidi)
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
96
Kampenii Kwa Ajjiillii ya Kuffaniikiisha Sherriia ya Unyanyasajjii
wa Nyumbanii Nchiinii Mallaysiia
Malaysia ilikuwa ni jamii ya Kiislam ya kwanza kupitisha na kutekeleza sheria
inayotambua unyanyasaji wa nyumbani kama tendo la uhalifu. Juhudi za
ushirikiano wa madhehebu mbalimbali za kupitisha muswada wa sheria ya
unyanyasaji wa nyumbani na utashi wa kisiasa wa kuufanya huo muswada kuwa
sheria zilichukua miaka kumi na mmoja. Haya yalikuwa ni matokeo ya juhudi za
mshikamano wa umma wa maelfu ya wanawake na wanaume waliounga mkono
na kukemea unyanyasi huu. Hatimaye, shughuli zilizoendeshwa na mashirika ya
wanawake na watu wengine waliounga mkono kwa kushirikisha na na kwa njia ya
kidemokrasia zilileta mafanikio ya kutungwa na kupitishwa kwa Sheria ya
Unyanyasaji wa Nyumbani (Domestic Violence Act [DVA]).
Historia ya kupitishwa kwa DVA inaanzia mwaka wa 1982 ambapo Shirika la
Msaada kwa Wanawake la Malaysia (Malaysia’s Women’s Aid Organization
[WAO]) lilipofungua kwa mara ya kwanza makazi ya kujisetiri kwa ajili ya
wanawake waliokuwa wanapigwa na waume zao. Matatizo ambayo wafanyakazi
wa ustawi wa jamii na wanasheria walikumbana nayo katika jitihada zao za
kuwatetea na kuwasaidia akina mama waathirika, bila kuchelewa yalionyesha
udhaifu mkubwa uliokuwemo katika sheria za Malaysia. Katika mwaka huo huo,
Chama cha Wanasheria Wanawake (the Association of Women Lawyers [AWL])
kilianza kufuatilia kwa karibu sana ongezeko la upendeleo dhidi ya waathirik a wa
unyanyasaji wa nyumbani na ubakaji uliokuwa ukifanywa katika mahakama za
nchini Malaysia. Tawi la Wanawake la Muungano wa vyama vya Wafanyakazi
vya Malaysia (Malaysian Trade Union Congress [MTUC]), muungano ambao
unajumuisha vyama kadhaa vya wafanyakazi, lilikuwa likikabiliwa na matatizo
yake lenyewe ya kuendesha mashtaka ya kesi za unyanyasaji wa kijinsia kwa
sababu hapakuwepo na sheria kujengea hoja katika utetezi wa kesi kama hizo.
Utafiti juu ya wanawake walioajiriwa uliofanywa hivi karibuni na Chama cha
Wanawake wa Chuo Kikuu (the University Women’s Association [UWA]),
umeonyesha kwamba ongezeko la nafasi ya wanawake kupata ajira, pia
imeongeza kuwaweka akina mama, kote mjini na vijijini, katika mazingira ya aina
mbalimbali ya uonevu. Wakati huo huo, utafiti mkubwa uliofanywa na shirika la
walaji (Selangor and Federal Territory Consumers Association [SCA])
ulionyesha mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika kuendeleza mawazo
na mitazamo na imani potovu juu ya wanawake. Kwa kutambua kuwa tafiti na
matokeo ya tafiti hizo juu ya unyanyasaji dhidi ya wanawake vilichimbuka kutoka
kwenye chimbuko moja, katika mwaka wa 1985 mashirika haya matano yalivunta
nguvu zao pamoja na kuunda muungano wa utendaji (a joint action group [JAG])
ili kufanya jitihada za pamoja kuhusu ajenda moja ya kuendeleza na kulinda
wanawake.
Muda mfupi baada ya kuundwa kwa JAG, wanamuungano huo waliamua
kuandaa semina, warsha, na maonyesho juu ya unyanyasaji dhidi ya wanawake
katika nchi nzima ili kuamsha ari na utambuzi wa tatizo hilo. Kila moja ya
mashirika hayo matano lilichukua majukumu mahususi kuhusiana katika
uratibishaji wa matukio hayo. Kwa vile WAO kilikuwa na ofisi zilizokuwa na vifaa
vya kisasa vya mawasiliano kama vile simu na mashini za faksi, kilichukua
jukumu la kuwa makao makuu ya shughuli za muungano wa utendaji (JAG), huku
wanachama wa WAO wakiwa na jukumu kubwa la kusimamia kazi za kiutawala.
Vyama/mashirika mengine yalisaidia kwa kuchukua aina nyingine za majukumu
Sehemu ya Tatu: Kuanzisha Ushirika wa Kuelimishana
97
ya msingi. Wanachama wa AWL walitayarisha muswada wa wa unyanyasaji wa
nyumbani wakati wale wa MTUC, UWA, na SCA waliratibu semina na warsha na
kuhamasisha watu wao kuweka shinikizo kwa wabunge ili waunge mkono na
kupitisha sheria ya unyanyasaji wa nyumbani. Kila tarehe 8 mwezi wa Machi,
Siku ya Kimataifa ya Wanawake, muungano wa JAG uliendesha maonyesho,
kuitisha kuweka sahihi, maonyesho ya muziki, matembezi, na maandamano ya
kupinga ili kuvutia wananchi kuona na kutafakari upya juu ya suala hili la
unyanyasaji dhidi ya wanawake.
Haukupita muda mrefu mashirika mengine na watu wengine nao wakaanza
kujiunga katika kampeni hiyo, wakijitolea muda, mawazo, utaalamu, na mali zao
katika utetezi huo wa JAG na mbinu za utoaji habari. Katika miaka ya awali ya
kampeni, mikutano ilikuwa mara nyingi ikifanyikia majumbani mwa wanachama
wa JAG, washiriki wakijikusanya katika sehemu za jikoni mwa kila mmojawao
kuandika barua na ripoti zao. Kadri muungano wa JAG ulivyokua, ukubwa na
utata wa kuratibu shughuli zake nao pia uliongezeka. Ukiwa na zaidi ya
mashirika 17 na mamia ya watu binafsi wakijitolea katika shughuli za JAG,
mwishowe mratibu wa kudumu alihitajika. Ili kupata pesa za kutosha kumlipa
mratibu mshahara, kila mwezi kila shirika mwanachama lilitoa mchango wa kiasi
fulani cha pesa kwa ajili ya mshahara wa mama mratibu.
Mojawapo ya jitihada muhimu sana za JAG kufikia mafanikio ilikuwa ni kuweka
mkazo kwenye vyombo vya habari vya Malaysia. Ingawa vyombo vya habari
vimeendelea kuwabeza na kuwakebehi wanawake waathirika kama wao ndio
wenye makosa, kwa kipindi kirefu uungwaji mkono wa vyombo vya habari
ulisaidia kubadilisha maoni ya umma kuunga mkono kupitishwa kwa sheria ya
unyanyasaji wa nyumbani. Zaidi ya hayo wabunge walikuwa wameanza
kuzungumza wazi katika kuunga mkono sheria kama hiyo. Baadhi ya viongozi wa
dini ya Kiislamu, wawakilishi wa Idara ya Maendeleo ya Kiislamu ya serikali ya
Malaysia na wabunge waliounga mkono maoni ya kizamani ya vikundi hivi vya
kidini, walipinga kwa kutoa hoja kwamba sheria hiyo ya unyanyasaji wa
nyumbani isitumike kwa Waislamu ambao hufanya karibu asilimia 50 ya idadi ya
watu wote wa nchi ya Malaysia.
Muda wote muungano wa JAG ulipigania sheria ya unyanyasaji wa nyumbani
ambayo ilikuwa inawalinda wanawake wote. Shirika la wanajinsia anawake wa
Kiislamu, Wadada katika Uislamu (Sisters in Islam [SIS]), lilishirikiana na JAG
kuweka mbinu za utetezi ambazo zingefaa kujibu mapigo ya pingamizi lililokuwa
limewekwa na mamlaka za Kiislamu. Shirika la SIS lilitumia maandiko kutoka
katika Kurani ili kujenga hoja ya kwamba hapakuwepo na kitu cho chote katika
Sheria ya Unyanyasi wa Nyumbani (Domestic Violence Act) kilichokuwa
kimekiuka kanuni za Uislamu. Akina mama hawa walidai kuwa iwapo sheria hiyo
ingetumika tu kwa watu wasiokuwa Waislamu, serikali ingeonekana inaunga
mkono wazo la kwamba wakati tendo la mtu asiyekuwa Mwislamu kumpiga mke
wake ni uvunjaji sheria, kwa Mwislamu kufanya tendo hilo ingekuwa ni halali
kabisa. Wanachama wa SIS walikutana na Naibu Waziri anayehusika na masuala
ya Kiislamu ili kusisitiza kuunga kwao mkono muswada wa sheria hiyo.
Mwishowe, Naibu Waziri huyo alikubaliana nao kuwa kupitishwa kwa sheria hiyo
lilikuwa ni jambo linalopatana kabisa na Uislamu. Sheria ya Unyanyasi wa
Nyumbani ilipitishwa mwaka 1994 na miaka miwili baadaye ilianza kutumika
kikamilifu.
Alipoulizwa ni ushauri gani angeweza kuutoa kwa watu wengine wanaopanga
kuendesha kampeni kwa kuunganisha mashirika mengi, mwanachama
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
98
mwanzilishi wa JAG, Ivy Josiah alijibu, “Kuwa na maono wazi juu ya suala
unalotaka kushughulikia, jadili mpango wako na wote wanaotarajiwa kujiunga
nawe, bainisha nani atasimamia kila shughuli inayofikiriwa, gawanya majukumu
kufuatana na ujuzi/utaalamu wa wawakilishi wa mashirika yanayoshiriki,
tengeneza orodha za majukumu zikiwa zimeambatana na ratiba ya muda, ajiri
mratibu wa kudumu anyelipwa, na jaribu kushirikiana kwa karibu sana na
vyombo vya habari----waendee ukiwa na mawazo, ukweli wa mambo, takwimu, na
majina ya watu ambao wanaweza kuwahoji .... na pia kumbuka kujifurahisha.22
Maswali ya Majadiliano
·  Ni matatizo ya aina gani ambayo wanachama wa kwanza wa JAG walitaka
kuyashughulikia? Ni kwa jinsi gani Sheria ya Unyanyasaji wa nyumbani
inazingatia matatizo haya?
·  Kwa nini ilikuwa ni muhimu kwa JAG kupigania kupishwa kwa sheria ya
unyanyasaji wa nyumbani ambayo ilihusisha watu wote, Waislamu na
wasiokuwa Waislamu? Ni faida au hasara gani zingetokea kwa kupitisha
sheria ambayo inatumika kwa watu wasiokuwa Waislamu tu?
·  Jinsi gani wanachama wa JAG walijiimarisha kutokana na kujiunga katika
muungano? Je, kujiunga na muungano kunadhoofisha juhudi za shirika au za
kampeni yake? Kama ni ndiyo, ni kwa vipi?
·  Kwa nini unafikiri muungano wa JAG ulipata mafanikio kama hayo? Ni
mambo gani tofauti yaliyochangia katika mafanikio hayo?
·  Je, vyombo vya habari vilikuwa na jukumu gani katika kuhamasisha watu wa
Malaysia kuunga mkono Sheria ya Unyanyasaji wa Nyumbani?
·  Jinsi gani vyombo vya habari katika jamii yako hujihusisha na masuala
yanayohusu haki za wanawake? Kwa kuzingatia mazingira ya jamii yako, ni
mbinu zipi unazoweza kutumia kuvivutia vyombo vya habari kujihusisha na
kunga mkono kampeni za kisiasa, lisheria, na kiuchumi zilizolenga kuwasaidia
wanawake?
·  Je, kuna mambo yanayofanana kati ya jinsi muungano wa mashirika
unavyopaswa kugawanya majukumu na jinsi watu mmoja mmoja katika
shirika moja wanavyopaswa kugawanya majukumu?
·  Je, unaweza kufikiria mfano mwingine ambapo kuundwa kwa muungano
kulisaidia kuleta mafanikio ya utetezi wa jambo? Orodhesha faida na hasara
zake?
·  Ni vipengee gani vinavyopaswa kuwekewa msisitizo katika ngazi ya mtu
mmoja mmoja na ngazi ya shirika kwa ajili ya kuunda muungano wenye
kuleta mafanikio?
·  Ni vigezo/sifa gani unaweza kuzitumia kupima mafanikio yake?
22 Habari hii inatokana na taarifa zilizotumwa na Zainah Anwar na Ivy Josiah pamoja na mahojiano ya simu
ya tarehe 3 Januari, 2001 (Zainah) na 4 Januari, 2001 (Ivy) kati yao na Women’s Learning Partnership.
Sehemu ya Tatu: Kuanzisha Ushirika wa Kuelimishana
99
Zoezi: Kuunda Jumuia Iliyo Mafunzoni (Sehemu ya 1)
Ruhusu kiasi cha muda wa saa moja na dakika 15 kwenye zoezi hili.
1. Kundi la semina litajigawa katika vikundi vidogo vidogo vya watu kama
watatu au wane ili kubaini suala la kijamii (la mahali wanapoishi, kitaifa, au
kimataifa) ambalo wanakikundi kidogo wote wangependa kulishughulikia.
Suala linaweza kuwa la jumla sana, kama vile kutokomeza njaa au kuendeleza
haki za wanawake, au linaweza kuwa suala maalumu katika sehemu au wakati
maalumu, kama vile kusafisha ziwa lililo jirani au kubadilisha ratiba ya siku
ya watoto wanaokwenda shule.
2. Mara tu suala linakubaliwa likiishabainishwa, wanakikundi waanze kujadili
juu ya jinsi gani wangeweza kuunda shirika, taasisi, au kampeni ya
kushughulikia suala hilo, na kwa nini wanafanya maamuzi wanayofanya?
Baadhi ya vitu wanavyoweza kuzingatia katika kuanzisha shirika ni kama
ifuatavyo:
·  Jina la shirika
·  Kauli ya maono
·  Malengo
·  Muundo
·  Idadi ya watumishi wataalamu
·  Utumiaji wa watumishi wa kujitolea, kama wapo, na jinsi gani ya
kufanya juhudi zao zilidhishe nafsi zao
·  Jinsi gani maamuzi ya kishirika yatafanyika
·  Jinsi gani majukumu ya kishirika yataganywa
·  Mradi au shughuli ya pili
·  Vigezo/sifa za kupima mafanikio/ufanisi
·  Mradi au shughuli ya kwanza
3. Mwandishi anapaswa kuchaguliwa katika kila kikundi kwa ajili ya kuandika
maelezo juu ya shirika na utaratibu ambao kikundi kimeufuata kufikia
kukubaliana juu ya jina lake, malengo yake, muundo wake, n.k. Katika kikao
kifuatacho, kila mwandishi ataombwa kueleza mbele ya kundi zima la semina
juu ya shirika la kikundi chake. Maswali ya wanasemina juu ya kwa vipi na
kwa nini baadhi ya maamuzi yalifanywa yataelekezwa kwa wanakikundi wote.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
100
__________________________________________________________________
Katika jumuia iliyo mafunzoni,
Mamlaka ….hayalazimishwi;
Bali, huibuka kadri mazungumzo yanavyoendelea.
“Misingi ya Ujenzi wa Uongozi”
101
KIKAO CHA KUMI NA MBILI
Jinsi Gani Tunaweza Kuainisha Shirika
Lililopata Mafanikio?
Shabaha za Kikao
§ Kujadili umuhimu wa kuelezana na kubadilishana uzoefu na
maarifa ili kuendeleza malengo ya shirika.
§ Kubadilishana maoni ya fasili/maelezo ya washiriki juu ya
shirika lililofanikiwa.
§ Kuhakiki kiasi gani mashirika dhahania ya vikundi vidogo
vidogo yanafikia malengo yao.
§ Kutafakari juu ya malengo na mafanikio ya semina hii katika
vikao vyake vyote kumi na viwili vilivyopita.
Kabla ya kuanza: Sehemu ya”Mawasiliano kwenye Mazingira ya Semina” ya kitabu hiki inatoa
baadhi ya mawazo juu ya jinsi gani ya kufunga semina ya uongozi. Washiriki wanaweza kuchagua
kufunga semina kwa kufanya tafrija ndogo au kwenda kuvinjali kusherehekea mwisho wa semina,
na pia wanaweza kupenda kupeana taarifa za kibinafsi kama vile anwani na simu ili waendelee
kuwasiliana. Kumbuka kufotokopi nakala za kutosha za Fomu ya Tathmini ya Mshiriki na
Msimamizi na kumpa kila mtu. Toa muda wa kutosha katika kikao cha mwisho kwa ajili ya kila mtu
kujaza fomu hiyo. Fomu hii ni muhimu sana kwa kufanya marekebisho na kuboresha programu za
semina za siku za baadaye.
Mapendekezo ya Usimamizi
Soma kwa sauti habari inayofuatia kuhusu kuanzishwa kwa Mahakama ya
Kiarabu.
Jadili katika kundi iwapo Mahakama hii inatimiza sifa za kundi kwa ajili ya
shirika lenye kupata mafanikio. Maswali yanayofuatia habari hii yatasaidia
kuongoza majadiliano ya kundi.
Katika kikao kilichopita, wanasemina waliombwa kujigawa katika makundi
madogo madogo ili kujadili juu ya kuanzisha shirika dhahania. Kufuatia
majadiliano ya leo juu ya Mahakama ya Kiarabu, kila mwandishi kutoka katika
Kikao cha 11 ataeleza juu ya shirika dhahania la kikundi chake, akitilia mkazo
juu ya jinsi gani na kwa nini kikundi chake kiliunda shirika kwa jinsi hiyo.
Wanasemina wengine wanapaswa kusikiliza na kufikiria kwa makini mlengo
ya kila kikundi, muundo wake, na shughuli zake, na kuuliza maswali ili
kusaidia kila kikundi kufafanua jinsi gani shirika dhahania la kikundi litafikia
malengo yake.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
102
Mahakama ya Kudumu ya Kiiarrabu Kupiinga Unyanyasajjii
Dhiidii ya Wanawake
Mahakama ya Kudumu ya Kiarabu Kupinga Unyanyasaji Dhidi ya Wanawake
ilizaliwa katika mkutano wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ya Waarabu
uliofanyika jijini Rabat, Morocco kuanzia Novemba 30 hadi Desemba 1, 1996.
Kuanzishwa kwa Mahakama ya Kiarabu, kama inavyojulikana, kulitokea kwa
wenye kushuku bila kutarajia kwani baadhi yao walisisitiza kuwa unyanyasaji
dhidi ya wanawake na wasichana ni jambo la kawaida lililoenea katika utamaduni
wa Kiarabu/Kiislamu na katika jamii zote, jambo lisiloweza kuzuilika katika
mahusiano ya wanaume na wanawake, au kwa urahisi tu sio tatizo kubwa. Lakini,
wanawake na wanaume waliofanya juhudi ya kuanzisha Mahakama ya Kiarabu
walidhamiria kuwadhibitishia hao wenye kushuku kwamba hawakuwa sahihi.
Wakati kuibuka kwa Mahakama hii kunaweza kuwa kulionekana kuwa jambo la
ghafla kwa watu wengi, haya yalikuwa ni matokeo ya mkusanyiko mkubwa wa
uzoefu na maarifa ambayo waathirika wa unyanyasaji na wale walio katika
harakati za kuutokomeza walikuwa wakibadilishana na kufahamishana.
Kama sehemu ya maandalizi ya kikanda kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa Nne wa
Umoja wa Mataifa juu ya Wanawake, wanaume na wanawake kutoka jamii kumi
na nne za Kiarabu walikutana huko mjini Beirut, Lebanon mwezi wa Juni 1995.
Waathirika wa unyanyaswaji na watetezi dhidi ya unyanyasaji wa jinsia kwa
ushupavu walitoa maelezo yao kuhusu yaliyowapata au waliyoyaona katika
maelezo ya ushuhuda ambao ulikuwa haujawahi kutokea. Walieleza kwa kirefu na
kwa uwazi jinsi ambavyo wao na wanawake wengine wameishi katika hali ya
kutisha ya kunyanyaswa na kufanyiwa vitendo vya ukatili ndani ya familia na jamii
zao. Kusikiliza maelezo ya mashahidi hawa kuliongeza imani ya kuwa unyanyasaji
wa jinsia ulikuwa ndio mzizi wa hadhi duni waliyo nayo wanawake na wasichana
katika huduma za afya, elimu, na upitishaji maamuzi katika tamaduni tofauti zote
za dunia ya Kiarabu. Hawa waliokutana Beirut walifikia makubaliano kwamba ni
lazima washughulikie tatizo hili ili kutetea haki za kibinadamu za wanawake kwa
ufanisi zaidi.
Katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu kilichofuatia, watetezi, watafiti, na
waathirika walishirikiana kuweka wazi malengo yao na kuunda mpango wa
utekelezaji. Lengo lao lilikuwa ni kuhamisha suala la unyanyasaji wa jinsia kutoka
uwanja wa faragha kwenda katika mjadala wa hadharani, na kubuni na kukuza
njia za kushughulikia tatizo hili ambalo ni nyeti kwa hali halisi ya kiutamaduni,
kisiasa, na kiuchumi-jamii katika maeneo yao. Kubadilishana uzoefu wa aina ya
pekee na ukweli wa yaliyotokea baina ya wahusika waliounganishwa na lengo la
pamoja kulipelekea kuundwa kwa mahakama ya kudumu isiyojifunga na njia moja
ya kushughulikia matatizo ambayo hukutana mara kwa mara na kutekeleza
majukumu yake kikanda.
Mbinu nzuri za usimamizi katika kikao hiki na zoezi linalofuatia zinaweza
kuhusisha kufanyika kwa majadilaino ya kundi zima la semina au washiriki
kugawanyika katika vikundi vidogo vidogo (angalia Kiambatisho B kwa ajili ya
mpendekezo zaidi).
Sehemu ya Tatu: Kuanzisha Ushirika wa Kuelimishana
103
Ikiwa na makao makuu yake jijini Beirut, ambapo mratibu mkuu anakaa,
uanachama katika Mahakama ya Kiarabu uko wazi kwa wale wote ambao
wanakubaliana na malengo yake na kuunga mkono utetezi wa unyanyasaji dhidi ya
wanawake. Wanachama hawajafikiria Mahakama hii kama ya zile zilizozoeleka
ambapo kesi hufunguliwa na utetezi kufanyika ili uamuzi upitishwe, bali wanaiona
kama uwanja wa aina yake wa wanawake, mahali pa salama kwa ajili ya
majadiliano ya wazi na huru juu ya unyanyasaji wa jinsia na ufumbuzi wake. Kwa
hali hii, uendeshaji wa Mahakama hii unafanana sana na vikao ya hadhara vya
kusikiliza mashauri badala ya malumbano ya ushindani kati ya waendesha
mashitaka na washitakiwa. Muundo unaobadilika kutegemeana na hali wa
Mahakama ya Kiarabu umewezesha wanachama kuitumia Mahakama hii kukidhi
mahitaji na hali tofauti za watu na jamii mbalimbali.
Tangu ianzishwe, Mahakama hii imeweka mkazo zaidi juu ya kutokomeza kabisa
aina nne za vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana---
unyanyasaji katika ndoa kama vile kumfanyia mwenzi wako vitendo kinyume na
utashi wake, unyanyasaji unaotokana na talaka, unyanyasaji unaojitokeza
kuhusiana na utunzaji wa watoto, na unyanyasaji unaotokana na migogoro ya
mali. Mpango wa utekelezaji wa Mahakama ya Kiarabu unahusu kuchunguza na
kuchapisha katika maandishi vitendo vyote vya unyanyasaji kwa ajili ya kufikia
umma mzima, kuchunguza na kulaani mambo yote yanayohimiza unayanyasaji wa
jinsia, kushawishi serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs)
kuchukua hatua thabiti zinazothibitisha haki za wanawake kwa uadilifu wa
maumbile, na kutunga sheria mpya na kurekebisha zile za zamani ili ziweze
kuwalinda kikamilifu wanawake na wasichana. Mahakama hii haiwezi
kuwashurutisha watu, makundi, auserikali kuchukua hatua; ufanisi wake
unategemea dhamira ya wanachama wake katika kuzuia na kutokomeza
unyanyasaji wa jinsia.
Hivi karibuni, Mahakam ya Kiarabu imekazia juu ya shughuli mbili ambazo
wanachama wanafikiri ni muhimu: kurekebisha sheria zinazohusu hadhi ya mtu
binafsi katika jamii mbalimbali za Kiarabu na kushinikiza serikali tutoa huduma
zaidi kwa waathirika wa vitendo vya unyanyasaji. Mahakama ya Kiarabu
imeendelea na utaratibu wake wa kusikiliza mashahidi ambao shida, majonzi, na
ushindi wao vinatia moyo na kuongoza wale wanaopambana dhidi ya unyanyasaji
wa jinsia. Ikiwa inajifunza kadri uanachama unavyoongezeka, Mahakama hii
imeongoza mapambano ya kikanda dhidi ya unyanyasaji kwa njia ya uvumilivu,
uimara, na kuwasaidia na kuwaonyesha upendo waathirika wenyewe ambao ndio
wanahitaji huduma hii.23
23 Habari hii juu ya Permanent Arab Court to Resist Violence Against Women imechukuliwa kutoka
http://www.arabwomencourt.org/.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
104
Maswali ya Majadiliano
·  Ni matukio gani yaliyosababisha kuundwa kwa Mahakama ya Kiarabu?
·  Ni malengo gani ya msingi ya Mahakama ya Kiarabu? Ni mpango gani wa
utekelezaji ambao wanachama wa Mahakama hii wameuunda ili kufikia
malengo haya?
·  Jinsi gani kueleza watu wengine yale yaliyompata kunaweza kumsaidia au
kumuumiza mwathirika wa unyanyasaji?
·  Ni matokeo gani yaliyojitokeza kwa watu waliosikiliza ushuhuda ambao
walikutana Beirut mnamo mwaka 1995? Kwa nini Mahakama ya Kiarabu
imeendelea na utaratibu wa kusikiliza mashahidi?
·  Je, unaweza kufikiria ni jinsi gani Mahakama ya Kiarabu ingeweza kufanya
kazi kama ingekuwa imeanzishwa na serikali? Jinsi gani shirika lililoanzishwa
na serikali linatofautiana na Mahakama ya Kiarabu kama ilivyo sasa?
·  Ni mambo gani ya Mahakama ya Kiarabu yaliyoisaidia kufanikiwa kufikia
malengo yake?
·  Mahakama hii ifanye nini ili kuhakikisha inaendelea kupata mafanikio na
kuwa na mafao kwa walengwa?
·  Je, Mahakama ya Kiarabu inapaswa kupimaje ufanisi wake? Ni ishara au
vigezo vipi inavyopaswa kutumia?
·  Mchango gani teknolojia ingeweza kutoa katika mawasiliano baina ya mataifa
mabali mbali kati ya wanachama wa Mahakama ya Kiarabu?
·  Ni vitu gani muhimu katika shirika lililopata mafanikio? Ni vipi kati ya hivi
vinavyoweza kuhusishwa na Mahakama ya Kiarabu?
Zoezi: Kuunda Jumuia Iliyo Mafunzoni (Sehemu ya 2)
Ruhusu kiasi cha muda wa saa moja kwenye zoezi hili.
1. Waandishi wa kila kikundi katika Kikao cha 11 watatoa maelezo juu ya
shirika lao dhahania. Watapaswa kueleza jina la shirika, malengo ya shirika,
muundo wake, na shughuli zake, na utaratibu uliotumiwa kikundi kufikia
maamuzi yake. Kabla ya mwandishi wa kwanza kuanza, msimamizi au
mshiriki aliyejitolea atasoma orodha ya masuala yaliyo hapa chini ili washiriki
wa semina wayazingatie wanapofanya tathmini ya shirika la kila kikundi:
·  Je, shirika linashughulikia mambo yanayoweze kana?
·  Je, muundo na malengo yake vinatoa nafasi ya kuweza kubadilika
kufuatana na mazingira mapya?
·  Je, shirika lintumia vizuri uwezo wa watumishi wake wa kuajiriwa na
wakujitolea?
Sehemu ya Tatu: Kuanzisha Ushirika wa Kuelimishana
105
·  Je, shughuli zake zinalisaidia shirika kufikia malengo yake?
·  Je, shirika linakidhi vigezo vyake lenyewe kwa ajili ya mafanikio
na/au ufanisi?
·  Je, ni jumuia iliyo mafunzoni? Kwa nini?
2. Mbali ya majadiliano juu ya muundo na shughuli za mashirika mbalimbali,
washiriki wa semina watahitajika kuchunguza ni jinsi gani kila kikundi kilifikia
maamuzi yake. Baada ya kila mwandishi kueleza juu ya shirika lake na
limefanyiwa tathmini kamili na washirika wengine katika semina , kundi zima
lijaribu kufikiria na kutoa majibu ya mwaswali yafuatayo:
·  Jinsi gani wanakikundi walivyogawana majukumu?
·  Jinsi gani wanakikundi walifikia maamuzi?
·  Je, inaelekea kama wanakikundi walio wengi walikubaliana juu ya
uchaguzi wao na sababa za uchaguzi huo?
·  Ni kitu gani kilikuwa kigumi katika zoezi hili?
·  Ni kitu gani kilikuwa cha kufurahisha katika zoezi hili?
·  Je, yupo mtu ye yote katika kundi hili anayefikiria kuunda kiukweli la
kulitumia katika hali halisi shirika dhahania au kipengee kimojawapo
kutoka katika shirika dhahania lo lote kati ya haya yaliyobuniwa na
vikundi?
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
106
Maswali ya Kutathmini Semina
Msimamizi au mshiriki aliyejitolea ataandika mambo muhimu kwenye ubao au
karatasi kubwa ya kuning’inia wakati wa majadiliano ya kundi yafuatayo.
·  Umepata mafanikio gani katika vikao vya semina hii ambayo ulitarajia
kuwa ungeyapata?
·  Je, Ulikuwa na malengo yako kwa kushiriki katika semina hii ambayo
hayakufikiwa? Kama ni ndiyo, ni yapi?
·  Je, ilianza kukuwia rahisi kushiriki katika majadiliano kadri vikao vya
semina vilivyozidi kusonga mbele? Kama ni ndiyo, kwa nini?
·  Ni mambo gani uliyopenda na ambayo hukupenda kuhusu muundo wa
vikao.
·  Ni zoezi, majadiliano, au uzoefu gani katika vikao 12 vilivyopita ambao
ulipenda sana, ulikuvutia sana, au ulifurahia sana kuliko mengine? Kwa
nini?
·  Ni mafundisho au mawazo gani umeyafaidi kutoka katika vikao vya semina
ambayo utajaribu kuyaingiza katika kazi yako mwenyewe? Je,
utabadilishaje tabia yako mwenyewe, matarajio yako, au uchaguzi wako
katika siku zijazo ikiwa ni matokeo ya vikao hivi vya semina?
107
Fomu ya Tathmini ya mshiriki na
msimamizi
kwa ajili ya
Semiina ya Maffunzo ya Uongozii
Tafadhali tathmini msimamizi wa semina yako ya uongozi na uzoefu/ujuzi ulioupata
katika mafunzo haya ya uongozi kwa kuweka alama ya  katika safu zenye namba 1
hadi 5 ambapo unaona namba inaeleza vizuri maoni yako juu ya kiasi unachokubaliana
au kutokubaliana na kila kauli. Maoni yako katika fomu hii yatatumiwa kufanya
marekebis ho na kuboresha semina za mafunzo katika siku zijazo. Namba katika safu
zina maana kama ifutavyo:
5 = Ninakubali kabisa
4 = Ninakubali
3 = Sina hakika
2 = Sikubali
1 = Sikubali kabisa
Uhitajiki kuandika jina lako katika fomu hii ya tathmini. Kuandika jina ni uchaguzi
wako.
Semiina ya Maffunzo ya Uongozii::
FOMU YA KUTATHMINI SEMINA 5 4 3 2 1
1. Kushiriki kwangu katika semina hii ya mafunzo ya uongozi kumeniwezesha
kufikiri juu ya masuala ambayo yanatokea kila siku maishani mwangu.
2. Kushiriki kwangu katika semina hii ya mafunzo ya uongozi taratibu
kumenipunguzia kusita kwangu kuwapa watu wengine maoni yangu.
3. Kushiriki kwangu katika semina hii ya mafunzo ya uongozi kumeboresha
uwezo wangu wa kusikiliza.
4. Kushiriki kwangu katika semina hii ya mafunzo ya uongozi kumeinua kiwango
cha uwezo wangu wa kuwasiliana vizuri na wengine.
5. Kushiriki kwangu katika semina hii ya mafunzo ya uongozi kumeniongezea
moyo wa kujiamini.
6. Kushiriki kwangu katika semina hii ya mafunzo ya uongozi kumenitia nguvu ya
kufikiri juu ya maono kwa ajili ya kujenga jamii bora.
7. Kushiriki kwangu katika semina hii ya mafunzo ya uongozi kumenitia moyo wa
kujitolea.
8. Kushiriki kwangu katika semina hii ya mafunzo ya uongozi kumenifanya
kutambua haja ya kufanya kazi kwa kushirikiana pamoja wakati ninashghulikia
tatizo lililoikabili familia na/au jamii yangu.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
108
FOMU YA KUTATHMINI SEMINA 5 4 3 2 1
9. Kushiriki kwangu katika semina hii ya mafunzo ya uongozi kumeniwezesha
kujenga kundi la marafiki na washiriki wenza ambao ninajisikia huru kujadiliana
nao masuala yangu ya kibinafsi na kikazi kadri ninavyopania kuleta mabadiliko
katika maisha na/au jamii yangu.
10. Kushiriki kwangu katika seminahii yamafunzo ya uongozi kumechochea
shauku yangu ya kujifunza zaidi juu ya teknolojia na jinsi itakavyoweza
kuimarisha uwezo wa utendaji wa wanawake.
11. Kushirikiana na washiriki wengine katika semina hii ya mafunzo ya uongozi
kumenisaidia kuelewa umuhimu wa ushirikishwaji wa wanawake katika hatua
zote za upitishaji maamuzi ya jamii yangu.
12. Uchunguzi wa mifano ya matukio kutoka sehemu mbalimbali za dunia ilikuwa
ni njia yenye manufaa katika kufikiria changamoto na nafasi mtu azipatazo
kuongoza shirika au jamii.
13. Kushiriki katika mazoezi ya kujifunza ilikuwa ni njia yenye manufaa katika
kufikiria changamoto na nafasi mtu azipatazo kuongoza shirika au jamii.
14. Ninaamini kwamba wanawake na wanaume wote wanaweza kufaidika
kutokana na kushiriki katika semina ya mafunzo ya uongozi.
15. Ningependa kuwashauri wanafamilia yangu, marafiki, na/au wafanyakazi
wenzangu kwamba washiriki katika semina hizi za mafunzo ya uongozi.
Kwenye nafasi iliyopo chini hapa na nyuma ya ukurasa huu, tafadhali toa maoni yako juu
ya jambo au kipengee cho chote kile katika semina hii ambacho ulikipenda na/au
hukukipenda. Ni mapendekezo gani ungeweza kuyatoa kufanya semina hii ya mafunzo ya
uongozi kuwa ya maana na manufaa kwako na watu wengine katika jamii yako? Tafadhali
jisikie huru kujadili mifano ya uongozi unaoufahamu, mapendezo ya mazoezi ya kujifunza,
mada ambazo zinahitaji kuzingatiwa, n.k.
109
Msiimamiizii::
FOMU YA KUMTATHMINI MSIMAMIZI 5 4 3 2 1
1. Msimamizi aliendesha semina kwa mwendo wa kuridhisha: kwa haraka ya
kutosha kuepusha tatizo la washiriki kuchoka akili lakini kwa mwendo mdogo
wa kutosha kuwawezesha kunufaika na mifano ya matukio ya uongozi na
mazoezi ya kujifunza.
2. Msimamizi alifanya mazingira ambamo washiriki katika semina waliweza
kuzungumza bila woga juu ya masuala/matatizo ya kibinafsi na kikazi.
3. Msimamizi hakusita kuelezea washiriki uzoefu wa maishani mwake ili
kuchochea na kuchangamsjha majadiliano.
4. Msimamizi aliwawezesha washiriki kuelewa changamoto na nafasi apatazo
mtu zinazohusu kuongoza.
5. Msimamizi alikaribisha mapendekezo/ushauri wa washiriki juu ya masuala
ambayo yalikuwa yanahusiana na kuingizwa katika kufanikisha mahitaji ya
semina hii.
Kwenye nafasi iliyopo chini hapa na nyuma ya ukurasa huu, tafadhali toa maoni yako juu
ya jambo au kipengee cho chote kile juu ya msimamizi wa semina hii ambacho ulikipenda
na/au hukukipenda. Ni mapendekezo gani ungeweza kuyatoa kwa msimamizi huyu ili
aweze kuwa msimamizi bora zaidi na kufanya semina za siku zijazo kuwa na maana na
manufaa zaidi kwa washiriki? Tafadhali jisikie huru kujadili mapendekezo juu ya jinsi gani
ya kuandaa na kuendesha vikao vya semina, kuendesha mazoezi ya kujifunza,
kushughulikia mada ambazo zinahitaji kuzingatiwa lakini husahulika mara kwa mara, n.k.
Asante sana kwa maoni yako. Maoni yako ni muhimu sana katika jitihada za shirika la Women’s Learning
Partnership na shirika la Women’s Self-Promotion Movement yanavyojaribu kutengeneza na kutekeleza
mpango huu wa mafunzo ya uongozi.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
110
111
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
112
113
KIAMBATISHO A
Matukio Mbadala
Tukio hili limekuwa likitumiwa na washiriki wa semina nchini Palestine kama mbadala
kwa tukio katika Kikao cha 3.
Kuheshima na Kuleta Mageuzi Katika Mitazamo na
Utamaduni wa Sehemu za Makazi ya Watu
Maryam Midyeh: Mwalimu wa Haki za Uzazi wa Majira
Nimekuwa nikifanya kazi katika Chama cha Uzazi wa Majira (Family Planning and
Protection Association [FPPA]) katika mji wa Halhoul mara tu baada ya kuundwa
kwake mwaka 1969. Nilianza kufanya kazi katika Chama hicho katika mwaka wa 1973,
mara tu baada ya kuhitimu masomo yangu ya sekondari---mwanzoni, nilikuwa
nikifanya kazi kwa muda wa masaa mawili kwa wiki, kisha baadaye siku tatu kwa wiki.
Nilitaka kuendelea na masomo ya chuo kikuu wakati nikifanya kazi FPPA, lakini hali
ya kifedha ya familia yangu na mitazamo juu ya majukumu ya wanawake katika jamii
vilinilazimisha kufikiria upya dhamira yangu hii.
Licha ya kwamba familia yangu ilikuwa na maoni tofauti, sikuachana kabisa na shauku
yangu ya kuendelea na elimu, lakini nilijua kuwa ingebidi nifikie lengo langu hilo kwa
kupitia njia nyingine. Nilitumia faida za nafasi ya kuchukua mafunzo na masomo
yanayohusiana na afya ya uzazi ya wanawake yaliyokuwa yakiyolewa pale FPPA, na
kisha nikadhamiria kutekeleza yote yale niliyokuwa nikijifunza katika dunia iliyokuwa
ikinizunguka. Kadri nilivyozidi kuongea na wanawake waliokuwa wakishughulikia
masuala hayo, ndivyo nilivyozidi kujisikia kuwa ningeweza kuanzisha mabadiliko kwa
wanawake kwa kuwasidia kutambua umuhimu wa uzazi wa majira na matokeo yake
kwa afya zao wenyewe na za watoto wao.
Kupitia katika kazi yangu hiyo nimetambua ya kwamba mitazamo ya watu juu ya uzazi
wa majira imebadilika kadri mitazamo ya jamii juu ya wanawake ilivyobadilika. Miaka
kadhaa iliyopita, juk umu kuu la FPPA lilikuwa ni usambazaji wa vidonge vya uzazi wa
majira, na nesi mmoja tu wa kujitolea alikuwa akipatikana kwa saa chache kwa wiki
kujibu maswali ya akina mama. Kwa kawaida, mwanamke aliyeolewa akiwa na watoto
kumi au zaidi angefika pale ofis ini kwetu, na kuomba msaada kuhusu uzazi wa majira.
Sasa hivi, wanawake vijana wanaokuja katika ofisi za Chama hiki FPPA wakati
mwingine wanakuwa wameandamana na wachumba wao. Kwa sababu jukumu
wanalolipa uzito wa juu kwanza ni kumaliza masomo yao. Wachumba au wanandoa
hawa wanataka kuelewa njia za kuzuia mimba ili kuepukana na mimba zisizotakiwa
katika miaka ya kwanza katika ndoa zao.
Kwa kutumia nyenzo hizi, mimi na watu wengine katika Chama cha FPPA tumeendesha
semina, kufadhili maonyesho, na kuonyesha filamu zenye lengo la kuhimiza Mafanikio
katika kuwaelimisha wanawake juu ya uzazi wa majira na haki zao za uzazi
hayakupatikana kwa urahisi na yanaonyesha matumizi yangu ya nyenzo kadhaa, ikiwa
ni pamoja na:
·  Maarifa yaliyopatikana katika miaka yote kutoka kozi za mafunzo;
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
114
·  Utashi wa kwenda huko kwenye makazi ya watu na kuongea na wanawake ambao
vinginevyo wasingeweza kufikia huduma za FPPA;
·  Uratibu na ushirikiano na watu ambao wana umaarufu ambao kuunga mkono
kwao uzazi wa majira ni muhimu kuondokana na jamii kusita kukabali njia hii ya
kuapangilia uzazi---kuanzia madaktari hadi wakuu wa shule, kuanzia mkuu wa jiji
hadi maimamu wa misikiti;
·  Utambuzi wa mila za kijadi ambazo zinaweza kusababisha wanaume na wanawake
kukataa uzazi wa majira kabla hata kujifunza juu ya dhana yenyewe.
majadiliano juu ya afya ya uzazi ya wanawake pamoja na masuala yanayohusiana
kama vile mabadiliko ya kihisia na kimwili yanayotokea kwa vijana wadogo, kinga ya
Virusi vya UKIMWI/UKIMWI, madhara ya kuolewa/kuoa katika umri mdogo, na
madhara ya mimba za mara kwa mara. Kuwaelimisha wanawake juu ya haki zao za
uzazi kunakwenda sambamba na kuheshimu na kuleta mageuzi katika mitazamo na
utamaduni wa sehemu zao. Muda wangu niliokaa FPPA, nimefikia kuelewa kwamba
mabadiliko ya kijamii ni matokeo ya kuwa na maono, ustahamilivu, na utashi thabiti---
kwanza kwa watu binafsi na kisha vikundi vya watu ambao huunganisha juhudi zao
katika harakati za kuleta maisha bora.
Maswali ya Majadiliano
·  Ni sifa na ujuzi gani ambao Maryam Midyeh anao amb avyo vinamfanya kuwa
kiongozi?
·  Ni maono gani ya Maryam juu yake mwenyewe? Juu ya wanawake katika jamii
yake?
·  Ni nyenzo gani anazotumia Maryam Midyeh katika kutekeleza maono yake?
·  Kwa nini anawaendea watu maarufu kumsaidia katika kufikia malengo ya FPPA?
Kwa mfano, ni mchango gani mkuu wa shule anaweza kuutoa katika kuelimisha
jamii juu ya uzazi wa majira? Ni mchango gani maimamu wa misikiti wanaweza
kutoa katika kusaidia jitihada za FPPA?
·  Maryam Midyeh ana hisia gani juu ya utamaduni na mila za sehemu anakoishi? Je,
kutetea haki za uzazi za wanawake kunamaanisha mgongano kati yake na
utamaduni na mila za sehemu yake? Ni jukumu gani linalopaswa kufanywa na
wanawake katika ufafanuzi/tafsiri ya kanuni za kiutamaduni?
·  Je, Maryam Midyeh anapimaje mafanikio ya FPPA? Anajuaje kuwa mitazamo ya
watu katika eneo lake juu ya uzazi wa majira imebadilika?
·  Jinsi gani Maryam Midyeh na wafanyakazi wenzake katika FPPA wanawasilisha
umuhimu wa uzazi wa majira? Je, teknolojia inaweza kuwa na jukumu gani
kuwasilisha ujumb e huu?
·  Kama ungekuwa unafanya kazi katika shirika la FPPA, ni mbinu zipi ambazo
ungetumia kuelimisha jamii yako juu ya umuhimu wa uzazi wa majira?
Kiambatisho A
115
Zoezi hili lilitumiwa na washiriki katika semina ya mafunzo nchini Nigeria kama
mbadala kwa shughuli ya kikundi katika Kikao cha 5.
Zoezi: Kuhusu UKIMWI
Kazi ya Kundi: Kuchunguza tatizo kwa maoni tofauti
Ruhusu muda kama wa saa moja kwa zoezi hili.
1. Soma kwa sauti habari juu ya tukio lifuatalo:
Katika kanisa moja lenye waumini wengi nchini Nigeria, idadi kubwa ya
vijana wanafanya majaribio ya kujamiiana. Kumekuwepo na taarifa
kutoka miji ya jirani kuhusu vijana wa umri wa kati ya miaka kumi na
miwili hadi kumi na tisa kuambukizwa na magonjwa ya zinaa, hata
virusi vya UKIMWI na UKIMWI wenyewe, na kupata mimba
zisizohitajika. Watu wengi wanahofia kuwa vijana hawa wanabomoa
ukuta wa maadili ya maisha ya kifamilia heshima ya ndoa katika jamii
yao. Baadhi wako wanafikiria na kutafuta njia ya kushirikiana na vijana
hawa kuwasaidia kuachana kabisa na vitendo hivi. Mojawapo ya
mapendekezo kutoka kwa mmoja wa waumini ni kwamba kikundi cha
vijana cha kanisa hilo kiingize habari zinazohusiana na afya na mambo
ya kujamiiana katika mikutano yao ya kila wiki. Lakini, mchungaji na
wazazi walio wengi wanapinga pendekezo la elimu ya kujamiiana na
hawako tayari kuzungumzia ombi hilo.
2. Waelekeze washiriki wa semina kufikiria kwamba wao ni waumini
katika kanisa hilo ambao wamedhamiria kutatua shida hii kubwa. Anza
kwa kuruhusu kila mtu kutoa anachofikiri juu ya matakwa na mahitaji ya
vijana wote katika jamii hiyo. Omba mshiriki mmoja ajitolee kuandika
kwenye ubao au karatasi kubwa ya kuning’inia mambo muhimu
yanayojadiliwa.
3. Waambie washiriki katika kundi kuelezea hali hiyo kutoka katika
mtazamo wa vijana hao wanaofanya majaribio ya kujamiiana. Fikiria
iwapo baadhi wanaweza kujisikia kuwa wanafanya mambo kiutu uzima,
au iwapo baadhi wanafanya tu kutokana na shinikizo la vijana wenzao.
Je, hali hiyo inaweza kuchukuliwaje na vijana wengine wa kike? Na
vijana wengine wa kiume? Ni matakwa na mahitaji gani wanayojaribu
kuyalinda? Mwombe mshiriki mmoja kujitolea kuandika ubaoni au
kwenye karatasi kubwa ya kuning’iniza mambo muhimu
yanayojadiliwa.
4. Angalia tatizo hili kuotka katika mtazamo wa mchungaji na wazazi
ambao wanapinga pendekezo la kuingiza elimu juu ya kujamiiana
katika mikutano ya vijana wa kanisani. Je, wanahofia nini yatakuwa
matokeo ya elimu juu ya kujamiiana? Wanataka kulinda mambo gani
katika jamii yao? Ni matakwa na mahitaji gani wanayojaribu kulinda?
Mwombe mshiriki mmoja ajitolee kuandika ubaoni au kwenye karatasi
kubwa ya kuning’iniza mambo muhimu yanayojadiliwa.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
116
5. Waelekeze washiriki wa semina kufikiria matakwa na mahitaji
ambayo yamejadiliwa na kutoa mawazo na usuluhisho wa kutatua
tatizo hili. Washiriki waeleze kwa uwazi ni matakwa na mahitaji ya
kundi gani mawazo yao yanaunga mkono na kwa nini.
Maswali kwa Kila Mshiriki
·  Je, kwa kuyapa uzito matakwa na mahitaji ya waumini tofauti, ulikuwa
unasikitikia zaidi au kidogo mitazamo ya wengine?
·  Je, kuliagalia tatizo hili kutoka mitazamo tofauti, kumekurahisishia au
kumekutatanisha kufikiria suluhisho?
·  Je, unaweza kutumia njia hii kushughulikia hali nyingine au mgogoro ambapo
watu wenye mitizamo tofauti hawakubaliani? Unaweza? Kwa nini?
Kiambatisho A
117
Zoezi hili limetumiwa na washiriki katika semina za nchini Jordan kama mbadala wa
Kikao cha 10.
Shabaha za Kikao
§ Kujadiliana juu ya umuhimu wa wanawake kushiriki katika
uchaguzi kama wagombea na kama wapiga kura.
§ Kuchungua matokeo ya uchaguzi kwa haki na maisha ya
wanawake.
§ Kuweka msisitizo juu ya mahitaji ya maarifa na habari katika
kuunda na kujenga mitazamao ya wagombea juu ya masuala ya
wanawake.
§ Kubaini njia za kukuza na kuweka malengo na mbinu za
uhamasishaji kusaidia kufikia malengo hayo.
Kushiirriikii kwa Wanawake Kattiika Uchaguzii Mkuu::
Jiinsii Ganii Sauttii Yangu IInaweza Kusiikiika na Kulletta
Mabadiilliiko
Sana’a, Um Muhammed, Nawal, Fadyah, Um Ziad, Hajjeh Safiah, Nisreen, Rula, na
Hanan wote wameshiriki katika mikutano mingi kujiandaa kwa ajili uchaguzi wa
wabunge wa bunge la Jordan uliopangwa kufanyika mwaka kesho. Nawal, ambaye ni
mwalimu wa shule ya sekondari kusini mwa Jordan, alipendekeza wazo la kuwa na
mikutani hiyo. Alitoa pendekezo hilo kwa Hanan, mwandishi wa habari katika gazeti la
kila siku katika sehemu yao, ambaye naye alikubaliana na wazo hilo juu ya umuhimu
kwa wanawake kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao wa bunge. Wote wawili
walitanbua umuhimu wa kuandaa na kuratibu juhudi za idadi kubwa ya wanawake,
hasa wale walio katika nafasi za uongozi, ndani ya jamii zao wanamoishi.
Shirika ambalo linashughulikia masuala ya wanawake lilikubali kupanga na kuendesha
semina ya mafunzo ili kuwaelimisha wanawake juu ya haki zao za kiraia. Semina hiyo
ilitoa nafasi kwa wanawake kuweza kujadili misukumo yao waliyokuwa nayo kushiriki
katika shughuli nzima ya uchaguzi, kubadilishana mawazo juu ya dhana ya demokrasia
ina maana gani kwao, kupendekeza masuala ambayo ni muhimu kwa wanawake na
wanaume ambayo yanahitaji yazungumzwe wakati wa shughuli za uchaguzi, na
kupendekeza mbinu zinazowezekana kwa ajili ya kufikia malengo yao. Wakati wa
majadiliano, washiriki walitamka kwa dhati kwamba “ni muhimu kwa wanawake
kushiriki katika siasa na upitishaji maamuzi katika nchi yetu.” Waliona kwamba
ilikuwa ni muhimu “kuwakilishwa na mwanamke ambaye anajua jinsi wanawake
wanavyoteseka kutokana na ubaguzi na kutelekezwa.” Mwanamke mmoja alitoa hoja
kwamba “mimi ni mwenzi wa mume wangu ndani ya nyumba, ni mwenzi wake huko
shambani. Sasa kwa nini nisiwe mwenzi wake huko Bungeni?” Washiriki waliamini
kabisa kwamba majukumu ambayo wanawake wanayo kufuatana na mila za jadi ya
jamii ya Jordan, ndio hayo hayo yanayowapa ujuzi wa uongozi ambao utawawezesha
kuwa washiriki wenye ufanisi katika mfumo wa siasa wa Jordan.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
118
Ilikuwa wazi kwa washiriki wengi kwamba wanawake walionekana kukosa maono au
ajenda ya kisiasa, sio tu kuhusu masuala ya kitaifa bali pia masuala yahusuyo
wanawake. Majadiliano katika semina ya mafunzo yaliwasaidia wanawake hawa
kuelewa haja ya kuweka malengo yao wazi, kuamua ajenda ya kuzungumzia, na
kupanga mbinu za kuhamasisha kwa ajili ya kufikia malengo yao. Washiriki waliamua
kwamba lengo lao kuu ilikuwa ni kushirikiana katika jitihada za kuwachagua kwa njia
ya kidemokrasia wagombea wanawake wa Jordan. Kwa hiyo washiriki walibaini
masuala fulani ambayo ingefaa wayaweke maanani, ikiwa ni pamoja na:
·  kutokomeza kabisa hali zote za ubaguzi dhidi ya wanawake;
·  kutoa uhakikisho madhubuti kwa ajili ya kulinda haki za kibinadamu kwa
jumla na hususani haki za wanawake;
·  kutoa hifadhi ya kutosha kwa ajili ya waathirika wa unyanyasaji, wanawake
wanaofanyiwa vitendo vya kinyama, na watoto;
·  kufafuta ufumbuzi wa kutokomeza umaskini, na kutoa uhakikisho wa huduma
za kijamii na afya;
·  kutoa kipaumbele kwa kuunda nafasi za ajira ili kupunguza tatizo la ukosefu
wa ajira;
·  kupambana na rushwa na kutoa hakikisho la nafasi sawa, hasa katika maeneo
ya elimu na ajira; na
·  kutetea haki za binadamu katika ngazi zote za kitaifa na kimataifa.
Kama moja ya mbinu za kuhamasisha, washiriki walikubaliana kutumia wito wa
“Wanawake watano katika Bunge lijalo” na kufanya kazi kwa kushirikiana kufikia
lengo hili. Waliamu kuwa awamu ya kwanza ya jitihada za kuhamasisha ingelenga
katika kufanya mikutano na semina nchini kote Jordan ambayo ingewekea mkazo juu
ya jukumu la wanawake kushiriki katika uchaguzi, haki za kiraia, na uongozi na ujuzi
wa mawasiliano. Zaidi ya hayo, wangeendesha kampeni za ujenzi wa maarifa ambazo
zinauelimisha umma juu ya umuhimu wa wanawake kushiriki katika siasa. Wangetoa
mafunzo maalumu kwa wagombea wanawake na kampeni zao za uchaguzi, kutoa
habari, huduma, na msaada wakati wa kampeni za uchaguzi huo. Washiriki walifikiri
kwamba ilikuwa ni muhimu kutumia vyombo vya habari kuongeza uwasilishaji mzuri
wa wanawake, kwa kuweka msisitizo kwenye mchango wao katika jamii na mafanikio
ambayo wameyapata, na kuongeza welewa wa umuhimu wa kushiriki kwa wanawake
katika siasa za Jordan. Mwisho, washiriki walisisitiza haja ya kushirikiana na vyama
vya wanawake, jumuia za kijamii, na watendaji wa serikali waliochaguliwa katika
sehemu zote za nchini Jordan ili wapate kuwaunga mkono na kuwasaidia kwa mali
katika juhudi za kufikia malengo yaliyobainishwa na wanawake kwa ajili ya wanawake.
Kufuatia semina hiyo, Kamati ya Uratibu kwa ajili ya mashirika yasiyokuwa ya
kiserikali nchini Jordan na mashirika mengine yasiyokuwa ya kiserikali ya wanawake
yalianzisha mradi ambao unajumuisha na mbinu hii ya kuhamasisha pamoja na
mpango wa utekelezaji ambao unaendelez a ajenda ya kisiasa iliyoweka mkazo wake
kwa wanawake na uchaguzi, ambao utatekelezwa wakati uchaguzi unapokaribia na
wagombea wanawake kuanza kampeni zao za uchaguzi. Washiriki wa kwanza katika
Kiambatisho A
119
semina hii Sana’a, Um Muhammed, Nawal, Fadyah, Um Ziad, Hajjeh Safiah, Nisreen,
Rula, na Hanan watakuwa na majukumu makubwa sana katika utekelezaji wa mbinu na
mpango huu wa uhamasishaji. Zaidi ya hayo, wanawake hawa wanapanga kutenga
muda fulani baada ya uchaguzi ili waweze kutathmini shughuli na ujuzi wa wa uongozi
kwa kuzingatia matokeo ya uchaguzi wenyewe.
Maswali ya Majadiliano
·  Ni kitu gani kilichowasukuma wanawake hawa kushirikiana?
·  Kwa ni ni ilikuwa muhimu kwao kuwa na maono ya pamoja na lengo la
pamoja?
·  Ni vitu gani muhimu katika mbinu yao ya kuhamasisha?
·  Je, upo ujuzi wo wote walionao wanawake ambao unaimarisha uwezo wao
kushiriki kikamilifu katika shughuli ya siasa ?
·  Je, unafikiri wanawake wanahamasisha kwa kuchukua hatua toafauti na
wanaume wanavyofanya? Kama ni ndiyo, ni kwa vipi na kwa nini?
·  Jinsi gani kundi hili la wanawake lingeweza kujenga kuungwa mkono kwa
wagombea wao katika sehemu zao na katika ngazi ya taifa?
·  Kama ungekuwa katika nafasi yao ni kitu gani ungefanya kilicho tofauti na
waliyoyafanya? Kwa nini?
·  Jinsi gani wanawake hawa wangetumia teknolojia ya kisasa ya habari na
mawasiliano---simu, barua-pepe, na mtandao wa kompyuta---kufanikisha
lengo lao?
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
120
Kiambatisho A
121
Zoezi lifuatalo limetumiwa na washiriki katika semina ya mafunzo nchini Nigeria kama
mbadala wa zoezi la Kikao cha Kumi.24
Zoezii:: Kuhamasiisha kwa Ajjiillii ya Uttendajjii
Mffano wa Barriiya IIbrrahiim Magazu
Mnamo Septemba 2000, binti mmoja wa umri chini ya miaka kumi na saba akiitwa
Bariya Ibrahim Magazu, mwenyeji wa kijiji kidogo katika Jimbo la Zamfara nchini
Nigeria, alipata mimba baada ya kubakwa na wanaume watatu. Alihukumiwa
kuchapwa viboko mia moja baada ya siku arobaini za kujifungua na viboko
themanini kwa madai kuwa aliwasingizia watu ambao sio waliombaka baada ya
mahakama kutoa uamzi kuwa hapakuwepo na ushahidi wa kutosha wa kubaini ye
yote kati ya wanaume wale aliowataja kama baba wa mtoto wake. Bariya aliomba
kukata rufaa ya kupinga hukumu hiyo na hakimu aliyekuwa akisikiliza shauri hilo
baadaye aliamua kuahirisha adhabu hiyo mpaka baada ya msichana huyo amalize
kipindi cha kumy onyesha mtoto. Hata hivyo, agizo la hakimu lilipuuziwa, na Bariya,
akiwa bado ananyonyesha mtoto, alichapwa viboko hata kabla ya tarehe iliyokuwa
imewekwa katika hukumu ya mwanzo kufikia. Akiwa amejulishwa tu usiku kabla ya
siku ya adhabu hiyi kutekelezwa, Bariya alichukuliwa na gari asubuhi na mapema
hadi kwenye mji wa karibu na kuchapwa hadharani. Baadaye, akiwa amedhalilishwa,
amejaa majeraha, na mwenye maumivu, aliachwa kutafuta na kurejea nyumbani
mwenyewe. Licha ya kuchapwa viboko hivyo, Bariya na familia yake waliamu
kuendelea na ukatji rufaa katika mahakama za Nigeria.
Kufuatana na habari za magazetini, Bariya alitaka kuwaita mashahidi saba lakini
ombi lake lilikataliwa. Badala yake, wanaume ambao Bariya aliwashtaki kwa
kumbaka waliachiwa huru kwa sababu maelezo ya Bariya yalionekana kutotosheleza
kuwaweka watuhumiwa hatiani. Alitakiwa kutoa angalau mashahidi wanne wenye
tabia nzuri ambao wangeweza kuthibitisha kuwa “unywele usingeweza kupita kati ya
miili yao.” Kwa upande mwingine, wanaume washtakiwa hawakuhitajika kutoa
kiapo cha kutohusika kwa kushika Kurani wala ushahidi wa hospitali kukubaliwa ---
kupima damu au DNA.
Bariya Ibrahim Magazu hapendi tena kuonekana hadharani. Kuonekana kwake sio
kwa lazima kufuatana na kanuni za Sheria za Shari’a za Jimbo la Zamfara au kanuni
za Sheria za Uhalifu za Jimbo la Zamfara. Licha ya haya, Mahakama ya Rufaa
inakataa kusikiliza tena shauri lake mpaka Bariya atakapokuwa tayari kufika
mwenyewe mahakamani. Bariya ana haki ya kukata rufaa chini ya sheria ya
Kiislamu, Sheria za Zamfara, na kama raia wa Nigeria anayelindwa na Katiba ya nchi
hiyo.
Igizo: Kundi la wanawake watano hukutana kila wiki kwa ajili ya kuhadithiana
visa na kupeana ushauri. Mmojawapo wa wanawake hao amesikia habari kuhusu
taabu iliyomfika Bariya Ibrahim Magazu, na amefadhaishwa sana na tukio hilo.
Anawaeleza wenzake kisa hicho cha Bariya cha kutotendewa haki na mahakama
na umma kwa kushirikiana na rafiki zake wanamtetea vikali na wanaamua
kutafuta njia ya kumsaidia Bariya.
1. Wagawe washiriki katika vikundi vidogo vya watu wanne wanne. Kila kikundi
kitapanga, kama marafiki katika igizo la hapo juu wanavyofanya, mpango wa
utekelezaji wa kumsaidia Bariya, familia yake, na mawakili wake.
24 For more information on this case, contact BOABAB at baobab@baobadwomen.org
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
122
2. Maswali ambayo kila kikundi kitajaribu kuyashughulikia ni:
·  Jinsi gani mnapenda kumsaidia Bariya? Ni aina gani ya msaada mnapenda
kumapatia? Kampeni yenu itakuwa ya aina gani?
·  Je, kampeni yenu itakuwa ya sehemu anapoishi, ya kitaifa, kikanda, au
kimataifa?
·  Je, litakuwa jambo la kufaa kuwaomba wanawake wengine kumsaidia
Bariya? Kwa nini? Je, wanaume nao wanaweza kukubali kusaidia?
·  Je, kikundi chenu kinaweza kutumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano
kama vile faksi, barua-pepe, au vyombo vya habari (kwa mfano, makala za
magazeti au vipindi vya kielimu kwenye redio na televisheni) kuongeza
nguvu ya kuungwa mkono?
·  Ni vikundi gani vya ushirikiano vinavyowezekana mavyoweza kufikiria
ambavyo vinaweza kusaidia kufikia malengo yenu?
·  Mtapiamje iwapo mnaelekea kufikia malengo yenu au la? Mtatumia vigezo
gani?
·  Je, mtagawanaje majukumu baina yenu ili kukamilisha shughuli zenu?
·  Wanakikundi waandike orodha ya shughuli ambazo watazifanya, wakieleza
kwa kifupi hatua watakazopitia katika kipindi cha wiki chache zijazo katika
utekelezaji wa mpango wao.
3. Makundi yote yakiishamaliza kujadiliana juu ya mipango yao utekelezaji,
washiriki watarejea kukaa kama kundi zima la semina. Kila aliyejitolea kutoka
kila kikundi ataeleza mbele ya wanasemina mbinu ya uhamasishaji ya kikundi
chake.
Maswali ya Majadiliano
·  Ni utaratibu upi ambao kikundi chenu kilitumia kufikia maamuzi?
·  Ni sehemu gani iliyokuwa ngumu kuliko zote katika kupanga mbinu yenu ya
kuhamasisha?
·  Je, ingekuwa rahisi au vigumu zaidi kuamua juu ya hatua maalumu ambazo
zinahitajiwa kuchukuliwa kama wangekuwepo watu wengi zaidi katika kikundi?
·  Mlifikiaje uamuzi wa kugawana majukumu? Je, kuandika orodha ya majukumu
ilisaidia kufafanua jukumu la kila mwanakikundi? Je, ilisaidia kwa namna nyingine
yo yote ile? Kama ni ndiyo, kwa vipi? Kama siyo, kwa nini sivyo?
·  Je, shughuli mlizopanga katika kukundi chenu zinaweza kutekelezeka kiukweli? Kwa
nini?
·  Je, kuna jambo jingine ambalo ungependa kuongeza ili kuboresha shughuli za
kikundi chako, hasa baada ya kusikia maelezo ya vikundi vingine?
Kiambatisho A
123
·  Unafikiri kuna tofauti yo yote iwapo wanakikundi ni wanawake tu, au wanaume tu,
au mchanganyiko? Kwa nini?
Uchunguzi
·  Je, zoezi hili limekusaidia kufikiria kupanga mradi au kampeni yako
mwenyewe kuhusu matatizo mbali mbali? Kwa nini?
·  Kama utafikiria kuanzisha kampeni yako mwenyewe, itakuwa ni ya aina gani
na utaiendeshaje?
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
124
Kikao hiki kimetumiwa na washiriki wa semina ya mafunzo nchini Palestine kama
mbadala wa Kikao cha Kumi na Moja.
Kushawishi Kwa Ajili ya Haki za Uraia wa Wanawake
Nchini Palestine
Mnamo Novemba 1995, Wanawake wawili wa Palestine waliifahamisha Kamati ya
Kiufundi ya Mambo ya Wanawake (Women’s Affairs Technical Committee [WATC])
kuhusu hali ya kufadhaisha sana. Wanawake hawa walipopeleka maombi ya kupatiwa
pasipoti za Palestine, maafisa waliwaambia kuwa walitakiwa wawe na kibali cha
maandishi kutoka kwa “walezi wao wa kiume” ambacho kingeonyesha kuwa
wamepewa ruhusa ya kutafuta pasipoti, kufuatana na utaratibu uliowekwa hivi
karibuni na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Palestine.
Kamati ya WATC bila kuchelewa ilianzaa kuandaa ombi la kupinga utaratibu huo
ikieleza kwamba utaratibu huu ulikiuka Azimio la Uhuru la Palestine (Palestinian
Declaration of Independence) la mwaka 1988 na pia Azimio la Haki za Binadamu
Duniani (Universal Declaration of Human Rights) pamoja na Makubaliano ya
Utokomezaji wa Aina zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake (Convention on the
Elimination of All Forms of Discrimination Against Women [CEDAW]). Mashirika
mengi ya wanawake yaliweka sahihi ombi hilo, ambalo WATC ililiwasilisha katika
Wizara ya Mambo ya Ndani. Afisa mmoja wa Wizara aliifamisha WATC kuwa Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani angeshiriki katika mjadala wa wazi na wa kuonyeshwa
moja kwa moja na televisheni juu ya suala hilo.
WATC ilichukua hatua ya kuandaa mwelekeo wa mjadala huo kwa kutuma nak ala ya
ombi la kupinga utaratibu huo kwa Shirika la Utangazaji la Palestine (palestinian
Broadcasting Corporation [PBC]). Wakati wa matangazo ya televisheni ya jioni katika
kipindi cha “Mazungumzo ya Wazi” (An Open Diologue) akiwa na afisa wa palestine,
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani alitambulishwa na WATC ilijulishwa ili mmojawapo
wa wawakilishi wake aweze kupinga kuwekwa kwa utaratibu ambao unawataka
wanawake wapate ruhusa ya wanaume ili kupatiwa pasipoti. Akiwa anasisitiza hitilafu
iliyopo kati ya utaratibu huu na sheria za kimataifa, mwakilishi wa WATC alimuuliza
Naibu waziri, “Rais wetu alipotangaza Azimio la Uhuru wa palestine, akisema kwamba
wanawake watatendewa usawa kama wanaume, tulishangilia kwa muda wa dakika
thelathini! Je, inawezekana kabisa kwamba ushangiliaji huo ulikuwa wa bure?” Naibu
Waziri alijibu kwa kupongeza mapambano ya wanawake wa palestine na kutangaza
kuunga mkono jinsia ya kiungwana, lakini alisisitiza kuwa kufuatana na makubaliano
na Israel, alikuwa akilazimika kutekeleza sheria za sasa za Misri na Jordan hadi hapo
sheria ya Palestine itakapotolewa.
Bila kuwa tayari kukubaliana na msimamo wa Naibu Waziri, WATC ilimkaribisha
kuhudhuria mkutano uliokuwa umepangwa kufanyika tarehe 4 Desemba 1995. WATC
ilikubali kumwonyesha mapema Naibu Waziri ajenda ya mkutanon na kukaribisha
wanawake watetezi wa nchini na wa kimataifa kutoka katika vyama mbalimbali vya
siasa na waandishi wa habari. Naibu waziri alitumia nafasi hiyo kueleza mafanikio
yaliyofikiwa na wizara yake, lakini bado akawa anasisitiza umuhimu wa mila za
Kiarabu katika kushughulikia suala hili wakati Shehe wa Kiislamu akiandika
kumbukumbu. WATC iliandika kumbukumbu za mkutano, na kuzichapisha kama
kijitabu ambacho ilikisambaza kwa mashirika ya haki za binadamu na vyombo vya
habari vya nchini Palestine.
Kiambatisho A
125
Kuwa na mawasiliano ndani ya vyombo vya habari ilikuwa muhimu. Mkurugenzi wa
Idara ya Habari wa PBC alikuwa akifuatilia kwa makini shughuli na miradi ya WATC.
Akiwa anafikiria juu ya taifa linalojengeka la Palestine, mkurugenzi huyo alifanya
mahojiano na mmoja ya wanachama wa WATC juu ya madai yake ya
kuwatengeawanawake asilimia thelathini ya viti vya Baraza la Wawakilishi la Palestine
(Palestinian Legislative Council [PLC]). Mwanamke huyo, naye pia alimkaribisha
mkurugenzi kutembelea ofisi za WATC. Akiwa amefurahishwa sana na kazi
inayofanywa na WATC na hasa kijitabu ambamo kumbukumbu za mkutano wa Naibu
Waziri zilikuwa zimehifadhiwa, mkurugenzi huyo wa Idara ya Habari ya PBC aliomba
kufanyike mjadala mwinigine wa kurushwa moja kwa moja katika ya wanawake hao na
Naibu Waziri. Ombi hilo lilisababisha kufanyika kwa mahojiano mengi ya televisheni
ambapo wanawake waliweza kulezea visa na matukio ya michango yao binafsi
waliyoitoa katika familia na jamii zao lakini mwishowe wanakuja kuambiwa kuwa
walihitaji ruhusa za baba, kaka, na/au waume zao ili kuhesabiwa kama rai kamili na
kuwa na pasipoti.
WATC ilituma barua katika ofisi za balozi mbalimbali za nchi za nje ikieleza na
kulalamika juu ya utaratibu huo wa kibaguzi katika utoaji pasipoti na kuomba msaada
wa kusaidia wanawake wa Palestine. Kufuatiliwa na kutangazwa katika vyombo vya
habari kwa kampeni hiyo kulipanuka kutoka vyombo vya habari vya nchini hadi
vyombo vya kimataifa wakati wanawake walipoandamana mjini Ramallah kudai
kuwakilishwa katika Baraza la Wawakilishi (PLC) na kuondolewa utaratibu huo wa
pasipoti. Kati wa waandamanaji hao, walikuwemo wagombea 12 katika uchaguzi wa
PLC, wanane wakiwa ni wanaume na wanne wanawake, ambao wote wakiwa
wametamka wazi kuwa wangeunga mkono haki za wanawake na kushutumu utaratibu
huo wa Wizara ya mambo ya Ndani. Mashirika ya habari ya CNN, French TV, na
Shirika la Habari la Canada (CBC) yalifuatilia na kutangaza maandamano haya.
Ikiwa imepata nguvu kutokana na kuungwa mkono na umma wa Palestine na habari
zake kutangazwa na vyombo vya habari vya kimataifa, WATC ilidumisha kampeni yake
ya kutetea haki za wanawake kutambuliwa kama rai akamili---iliandaa maandamano;
ilishirikiana na vyama vya haki za binadamu; kukutana na mawaziri mbalimbali, ikiwa
ni pamoja na Rais Yasser Arafat; na kuandika tahariri katika magazeti. Kadri kampeni
ya WATC ilivyozidi kupamba moto, chumba cha habari cha PBC kilipokea faksi kutoka
kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani tarehe 19 Desemba 1996. Waraka ulisema
kwamba wanaume na wanawake wangehudumiwa kwa usawa na kwamba ofisi yake
insigeendlea kuwataka wanawake wawe na ruhusa ya “walezi wao wa kiume”
wanapowasilisha maombi ya pasipoti.
Maswali ya Majadiliano
·  Ni hatua gani ambazo kamati ya WATC ilizichukua kuendesha kampeni ya
kushawishi kubadilisha utaratibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani? WATC
inapambanaje kujenga utambuzi wa kuwa na lengo la pamoja baina ya watu
wengine katika jamii hiyo?
·  Vyombo vya habari vilitoa mchango gani katika kampeni ya WATC? Aina
nyingine za teknolojia ya kisasa ya mawasiliano vilichangiaje?
·  WATC ikumbana na vukwazo gani katika jitihada zake za kufikia maafikiano
ya watu wengi juu ya haki za wanawake za uraia kamili? Ni vikwazo gani
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
126
katika jitihada za kujenga lango la pamoja kati ya watu walio na tofauti nyingi
au hata katika makundi yenye watu walio na mtazamo/tabia za kufanana?
Utashindaje vikwazo hivyo?
·  Je, kujenga lengo la pamoja ni jambo linalowezekana na/ au linalopendwa na
watu wote mara zote? Kwa nini?
·  Ni vigezo gani utavitumia kupima mafanikio ya kampeni hii?
·  Jinsi gani vyombo vya habari katika jamii yako vinashughulikia masuala ya
haki za wanawake? Ni mbinu gani zenye kufaa katika mahali pako unapoishi
ambazo unaweza kuzitumia kuvutia vyombo vya habari na kuungwa mkono
kwa ajili ya kampeni za kisiasa, kisheria, au kiuchumi zinazosaidia kuleta haki
kwa wanawake.
127
KIAMBATISHO B
Mbinu za Usimamizi
Zipo nyenzo nyingi zinazotumiwa na wasimamizi ili kuchochea majadiliano na usikivu
katika vikao vya semina. Ili kuleta matokeo makubwa yanayotarajiwa katika semina, ni
vizuri kwa msimamizi kuwa tayari kubadilisha muundo wa mazingira ya kujifunza kila
inapoonekana inafaa. Hapa chini ni orodha ya mbinu za usimamizi, nyingi ya mbinu
hizi zimo katika kitabu hiki. Unaweza kutumia moja au zaidi ya mbinu hizi katika
vikao fulani, au wewe au washiriki wengine mnaweza kuwa mnazo mbinu zenu za
ziada ambazo zinaweza kufaa zaidi katika kundi lenu. Jambo muhimu kukumbuka ni
kwamba hakuna njia moja tu sahihi ya kujifunza. Alimradi vikao vinatimiza sifa tatu---
kuelimisha, kuadilisha, na kuburudisha---basi uko katika mwelekeo mzuri wa
usimamizi.
Wasifu (Maandiko ya Habari za Maisha ya Watu): Habari za maisha ya
watu zinatoa mifano bora ya uchaguzi na maamuzi wafanyayo katika maisha yao.
Katika semina, habari za maisha ya watu huwawezesha washiriki kulinganisha visa vya
maisha na maamuzi yao na visa vya watu wengine. Na hii huwasaidia kutafakari juu ya
malengo na uwezo wao binafsi.
Vikatuni na Michoro: Utumiaji wa michoro au picha zinazoonyesha watu
wakisema ua kufanya vitu mbalimbali ni mbinu ya kuchochea na kuburudisha kuweza
kuibusha majadiliano juu ya mbinu za mawasiliano. Hata mchoro wa kawaida unaweza
kuwasilisha kwa urahisi tatizo kubwa na kuchochea majadiliano mazuri na ya kufaa.
Wasimamizi wanaweza kuwasilisha vikatuni au michoro katika kundi ili vijadiliwe
katika vikundi vidogo vidogo au kundi zima la semina.
Visa au Matukio ya Kubuni : Visa au matukio ya kubuni yanayoelekeana na
mada za semina yanaweza kuhadithiwa/kusomwa na kisha kujadiliwa katika kundi
zima la semina. Visa vya kubuni vinaweza kuwa si vya kutatanisha sana kuliko matukio
ya kweli ambapo washiriki wa kundi wanaweza kuwa maoni mazito na yanayokinzana
sana. Kwa mfano, kuliko kuzungumzia tukio la kweli ambapo kiongozi au mkurugenzi
au mwajiri alishindwa kuleta suluhisho zuri kwa tatizo la kikazi, mara nyingi inakuwa
rahisi kujadili tukio la kubuni ili maoni juu ya udhaifu au makosa yaliyotokea
hayahusushwi na mtu ye yote katika semina hiyo au ye yote ambaye washiriki
wanamjua.
Maongezi Huru: Wakati mwengine mambo yanayozungumzwa huwa ni tata,
mazito au nyeti sana kwa kundi kubwa kuweza kufanya majadiliano ya kufaa.
Maongezi huru huwezesha kundi zima kushiriki katika majadiliano yale yale lakini kwa
kuepuka hatari zinazoweza kutokea katika majadiliano ya kundi lote zima. Katika
bakuli la kweli la kioo la samaki, samaki huogelea na kuvinjari katika mazingira
ambayo yanaweza kuangaliwa bila shida na wale walio nje ya bakuli hilo. Maongezi
huru nayo hufanyika kwa njia hiyo hiyo. Watu wakujitolea ndani ya kundi, kwa
kawaida kuanzia wawili hadi sita kulingana na mada ya majadiliano na ukubwa wa
kundi zima, hujadili mada kwa kina mbele ya washiriki wengine kwa muda kama wa
dakika kumi. Wakati mwingine washiriki wengine katika kundi wanaweza kutoa maoni
yao juu ya yale yaliyotolewa na waliojitolea na wakati mwingine waliojitolea
wakiishamaliza maongezi kundi zima huanza kufanya majadiliano juu ya kile
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
128
kilichojitokeza katika maongezi ya kundi la waliojitolea. Mazoezi katika kitabu hiki
yanaweza kufanyika kwa njia hii ya maongezi huru. Katika hali hiyo, kikundi kidogo
cha waliojitolea kinashiriki katika zoezi mbele ya kundi zima la semina na kisha kila
mshiriki anajiunga katika majadiliano juu ya yale yaliyojadiliwa na kundi dogo.
Vichombezi vya Mjadala na Vihimizaji : jukumu la vichombezi na vihimizaji
ni kuwasadia washiriki kuzoeana zaidi mmoja kwa mwengine na kujisikia huru
kuzungumza mbele ya washiriki wengine wa semina. Mara nyingi, vichombezi vya
mazungumzo hutumiwa zaidi mwanzoni mwa semina na mwanzoni mwa vikao vya
semina. Hata hivyo vinaweza kusaidia wakati wo wote katika vikao ili kuburudisha au
kubadilisha mwelekeo wa majadiliano kwa washiriki ambao hutokea wakatoka nje sana
ya suala linalojadiliwa au kuanza kukosa imani na washiriki wenzao hasa katika
mjadala wenye mitizamo mikali inayopingana. Vichombezi mjadala vya kawaida ni
maswali yanayolenga kupata majibu juu ya habari za binafsi lakini ambazo SIYO za
siri na yanajibiwa na kila mshiriki kwa kuzungukia kundi. Mifano ya maswali haya ni
kama, “Kama ungekuwa na pesa nyingi sana na unahitajika kutumia kiasi fulani
kununulia familia yako zawadi, hiyo zawadi itakuwa ya namna gani?” Au, “Kama
ungekuwa ni mmea, ungekuwa aina gani ya mmea na kwa nini?” Au, “Ni chakula gani
unapenda sana kuliko vyote na kwa nini?” Wasimamizi wanapaswa kuwa wabunifu
kuhusiana na vichombezi na vihimizi; kimsingi vinapaswa kuburudisha.
Utunzaji wa Taafifa za Kila Siku: Wakati mwingine, wasimamizi uwaomba
washiriki wa semina waandike ndani ya daftari zao habari za kila siku na mawazo yao
kuhusu yale yaliyozungumziwa na kutendeka pamoja na yale waliojifunza katika
semina. Msimamizi anaweza kuamua kutenga muda mfupi mwishoni mwa kila kikao
kwa ajili ya kuwapa nafasi washiriki kuandika taarifa zao. Pia anaweza kuwaacha huru
ili waende kuandika taarifa hizi huko majumbani kwao ikiwa wanataka. Kwa wakati
mwingine washiriki wanaweza kuombwa kusoma yale waliyoyaandika ndani ya daftari
zao mwanzoni mwa kikao au mwishoni mwa semina. Hata hivyo maamuzi ya washiriki
kuelezana au kutoelezena juu ya yale wanayoandika katika daftari zao za taarifa
yanabaki kuwa juu ya washiriki wenyewe.
Habari Kutoka Vyombo vya Habari: Habari zinazotangazwa au kuandikwa
katika vyombo vya habari ambazo washiriki wote wamezisikia zinaweza kufaa kuwa
kichochezi cha majadiliano. Kwa mfano, kisa kinachotangazwa juu ya suala muhimu
linalofuatiliwa na mwanasiasa mwanamke kinaweza kutumika kuchochea mjadala juu
ya uhalisi wa uongozi na jinsi ya kufanyia kazi maono binafsi.
Wenza: Mara nyingi katika mazingira ya semina kuna baadhi ya washiriki ambao
husitasita kuzungumza mbele ya kundi lote. Kugawa kundi katika vikundi vya watu
wawili wawili kunasaidia watu wengine kushiriki kikamilifu zaidi. Mara tu kundi zima
linapokutana tena, mawazo au maoni ya yule aliye na aibu yanaweza kuwasilishwa
katika kundi na mwenzi wake. Kuwa na vikundi vya wawili wawili pia kunasaidia
majadiliano ya kina juu ya mada husika. Kundi linapokuta zima, yale maoni muhimu tu
yaliyojitokeza katika vikundi vidogo ndio yanapaswa kuwasilishwa.
Maswali na Majibu: Mbinu ya msingi ya usimamizi ni kuuliza maswali ili
kuongoza majadiliano ya kundi. Mbinu hii hujulikana kama “maswali na majibu”.
Jukumu la msimamizi ni kuuliza maswali yasiyokuwa na majibu dhahiri ili kupanua
mjadala. Maswali yanayodai majibu mafupi na rahisi hayafai. Msimamizi asiulize swali
analojua kuwa lina jibu moja tu sahihi. Si jukumu lake kufundisha habari sahihi, bali ni
kuwapa nafasi washiriki kubadilishana maoni na kufikia mahitimisho yao.
129
Madondoo: Ili kuongeza matokeo mazuri ya vikao vya semina, washiriki wanaweza
kuombwa kuleta madondoo yenye kufaa yaliyosemwa na watu maarufu, au kutoka
vitabuni, nyimbo, nyaraka za sheria, maandiko ya dini, au vyanzo vingine kwa ajili ya
kujadiliwa na kundi.
Kuigiza: Uigizaji huwawezesha washiriki kusikiliza na na kutafakari juu ya maoni na
mitazamo ambayo si lazima sawa na yao wenyewe. Watu hupewa uhusika wa kuigiza,
kama vile waajiri na watumishi wao, maafisa wa polisi na raia, madaktari na
wagonjwa, n.k. Ama mbele ya kundi au katika vikundi vya wawili wawili, kila
mshiriki huwakilisha mojawapo ya uhusika katika maongezi. Baada ya kuongea kwa
muda kama wa dakika kumi, kundi lote hujiunga tena ili kueleza na kujadili maongezi
hayo.
Vikundi Vidogo Vidogo: Kuwagawa washiriki katika vikundi vidogo vidogo
huwawezesha kushiriki kushiriki kikamilifu zaidisana katika mazoezi na majadiliano.
Kadri watu wanavyokuwa wachache katika kikundi ndivyo wanavyopata nafasi kubwa
ya kushiriki. Kuna njia nyingi ambazo zinaweza kutumiwa kugawa kundi katika
vikundi vidogo vidogo. Msimamizi anaweza kuamua kupanga vikundi hivyo mapema
ili kuhakikisha kila kundi lina watu wa aina mbalimbali kame vile umri tofauti,
utaalamu/kazi tofauti, welewa wa suala linalojadiliwa, au mambo mengine.
·  Kugawa Bila Utaratibu Maalumu: njia ya kawida kuunda vikundi ni
kugawa watu bila utaratibu maalumu. Baada ya msimamizi kuamua ni vikundi
vingapi anahitaji, washiriki wanajihesabu hadi kufikia idadi hiyo. Kwa mfano,
kama ni vikundi vitano, washiriki watahesabu namba moja hadi tano
kuzungukia kundi lote. Wale wote waliohesabu moja wataunda kikundi
kimoja; wale walihesabu mbili wataunda kikundi kimoja, n.k.
·  Kugawa kwa Kutumia Utaratibu wa Alfabeti ya Majina: Waombe
washiriki kufanya mstari au mduara kulingana na herufi za kwanza za majina
yao, wakianza na herufi ya mwisho ya alfabeti. Kisha wagawe washiriki
kufuatana na idadi ya vikundi mnavyohitaji.
·  Kugawa kwa Kutumia Utaratibu wa Siku za Kuzaliwa: Waombe washiriki
waunde mstari au mduara kulingana na siku zao za kuzaliwa ukianza na tarehe
1 Januari na kumalizia na tarehe 31 Desemba. Kisha wagawe washiriki
kufuatana na idadi ya vikundi mnavyohitaji.
Maneno dhidi ya Mawazo: Ili kuonyesha mbinu za mawasiliano, maafikiano, na
mabishano, linaweza kuwa jambo la kufaa kuwasilis ha vitu vyote viwili vya msemaji,
yaani maneno na mawazo yake, juu ya kitu gani alichokusudia kuwasilisha. Hili
linaweza kufanyika kwa njia ya maandishi, maneno ya msemaji yakiwa yamefungiwa
katika alama za kunukuu kuonyesha mawazo yake halisi. Au washiriki wanaweza
kufanya maigizo ambapo mwigizaji anatamka mawazo ya mtu anayeigizwa na mshiriki
mwingine anatumia mawazo hayo kushawishi kwa kutumia maneno yake. Kwa mfano,
washiriki wawili wanaweza kuwakilisha mawazo na maneno ya binti ambaye anajaribu
kumshawishi mama yake ampe ruhusa ya kwenda kwenye chuo cha tiba. Mshiriki wa
kwanza anaeleza yale ambayo binti yule anavyojisikia kwenda kwenye chuo cha tiba,
ikiwa ni pamoja na matumaini, maono, na masuala ya jumla. Mshiriki wa pili
anachagua maneno ya kumshawishi mama yake ili amruhusu kwenda chuo hicho.
Baadaye, kundi zima la semina linaweza kujadili juu ya uchaguzi wa maneno na mbinu
za mawasiliano za binti huyo. Igizo kama hilo kuhusu mawazo na maneno ya mama
linaweza kupanua mjadala zaidi. Kwa kutumia kwa ufanisi ujengaji picha wa washiriki
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
130
juu ya matukio yanayoweza kutokea, mbinu ya maneno dhidi ya mawazo inaweza
kutumika katika mazingira mengi ya aina mbalimbali ambayo ni yenye maana na mafao
kwa jamii na kazi za washiriki.
131
KIAMBATISHO C
Usikilivu wa Kushiriki
Watu wengi hufikiri kuwa usikivu ni jambo lijalo kwa urahisi---jambo tunalolifanya
siku zote---na kwa jumla huu ni ukweli. Lakini bado ni kweli kuwa wasikilizaji wazuri,
kama walivyo viongozi wazuri, ni wale wanaojifunza kutokana na yale wayasikiayo. Ili
kusikia ambayo mtu mwingine anasema ni muhimu uweke kando mawazo na maamuzi
ambayo tayari umeishayajenga akilini mwako ambayo yanaweza kuwa kama kizuizi,
kinachokuzuia wewe kuelewa vizuri maana au ujumb e uliokusudiwa. Zaidi ya hayo,
msikilizaji mzuri anapaswa kuhimiza mawasiliano kwa kuweka mkazo katika jambo
linalozungumzwa na kutoa ishara za maneno na zisizo za maneno kuonyesha kwamba
anafuatilia kwa makini mtiririko wa mawazo ya msemaji. Hapa chini ni baadhi ya
mapendekezo kukusaidia wewe katika matendo ya kusikiliza na kushiriki katika
mazungumzo. Yajaribishe nyumbani au kazini ili kufanya majaribio ya ni mbinu ipi
inakufaa zaidi katika mazingira yako.
Usikivu
Weka Kando Madhanio: Kuweka kando madhanio ni ishara ya heshima kwa
msemaji. Hivyo huruhusu mawazo yake kukuingia bila kuwa yamezuiwa na mawazo
ambayo umeishayajenga na chuki bila sababu. Kwa kufanya hivyo kunaonyesha
kujiamini kwako katika utambuzi na uwezo wako wa kupima habari kwa kuzingatia
uzito na ukweli wake. Watu ambao huogopa kuweka kando mawazo yao hukosa moyo
wa kujiamini katika misimamo au imani zao.
Jiweke Katika Nafasi ya Msemaji: Ili uweze kuelewa vizuri maoni ya mtu
mwingine, jaribu kufikiria na kujiweka katika nafasi ya msemaji. Jiulize, ni kitu gani
kilichomtokea mpaka akafikia kuwa na msimamo au maoni kama haya? Nini msingi au
mazingira ya mtazamo anaouelezea. Jaribu kufikiria jinsi ambavyo ungejisikia au
ungefikiria kama ungekuwa umetokewa na hayo hayo yaliyompata?
Kuwa Makini: Kuwa makini ni jambo linaloweza kuonekana kuwa la kawaida
kutokea katika usikilizaji, lakini bado ni gumu kulifikia. Kufuatilia mtiririko wa
mantiki za hoja za msemaji ni jambo linaloweza kuwa gumu, hasa kama msemaji ana
tabia ya kurudiarudia hoja, au anatumia maneno magumu au mtindo wa kuzungumza
usiokuwa wa kawaida. Kusikiliza pia kunaweza kuwa kugumu iwapo matumizi ya
lugha ya msemaji yanaonyesha kiwango tofauti cha elimu au kama uundaji wake wa
mawazo ni wa polepole. Msikilizaji mzuri anaweza kuchuja maneno yaliyochaguliwa
na msemaji ili aweze kusikia mawazo yake bila upendeleo.
Kushiriki Katika Majadiliano
Kuitikia Bila Kusema: Yale usiyoyasema kwa kutamka wakati wa mazungumzo
yanaweza kuwa na maana sawa na yale unayotamka kwa mdomo. Kwa ma kusudi au
bila kukusudia sote hutoa ishara za kimwili juu ya maoni na jinsi tulivyopokea
yanayosemwa na wengine. Zipo ishara nyingi za maungo ya mwili unazoweza
kuonyesha kwamba unamsikiliza msemaji kwa makini na kuelewa anachosema.
Kuegemea mbele, kuweka mikono yako wazi, kuangalia kwa tahadhari, kutazamana
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
132
usoni, na kukubali kwa kichwa ni baadhi tu ya njia nyingi za kumpa moyo mtu
anayezungumza nawe.
Kuitikia kwa Kusema: Kusikiliza sio tu tendo la kiakili na kimwili; pia zipo
ishara za kimaneno unazoweza kutoa kuonyesha kwamba unasikiliza na kufuatilia kwa
makini yale ayasemayo msemaji. Baadhi ya ishara hizi ni:
·  Semi na Maneno ya Mshangao: Ishara muhimu za kimaneno hujumuisha
semi fupi na rahisi au maneno ya mshangao. Kwa mfano, kusema “ndiyo”
“bila shaka”, “kweli kabisa” hata pia “uh- huh,” wakati msemaji anapo
pumzika au anapomaliza kueleza wazo alilokuwa akilieleza.
·  Kufafanua: Mbinu nyingine ni kufafanua wazo la msemaji (rudia kusema
aliyoyasema kwa maneno yako). Kufafanua kunakulazimisha kusikiliza kwa
makini sana yale anayosema msemaji na pia hutoa nafasi kwa msemaji
kuthibitisha iwapo umeelewa vizuri alichomaanisha. Kwa mfano, kufafanua
maelezo ya msemaji kunaweza kusikika hivi “ kwa hiyo, unasema kwamba
umepatwa na mambo mabaya kwa kufanya kazi kwako katika shirika hilo,
hata kuja mkurugenzi mpya, bado siyo jambo la kufaa kujitumbukiza katika
hatari ya kuendelea kufanya kazi hapo?”
·  Maswali ya Kufuatilia: Mara nyingi, maswali ya kufuatilia inaweza kuwa
njia nzuri ya kumwongoza msemaji. Wakati mwingine msemaji anaweza kuwa
na wazo la jumla juu ya kile alichokusudia kusema, na maswali ya kufuatilia
yanamsaidia kuunda au kujenga mahitimisho mahususi zaidi. Maswali ya
kufuatilia yanayoweza kuleta mafanikio katika mazungumzo ni yale ambayo
yanakuongezea kikweli welewa wako wa mtiririko wa mawazo ya msemaji au
mtazamo wake. Kwa kumsikiliza msemaji kwa makini unaweza kuona
mapengo katika maelezo yake ambapo ndipo unaweza kuuliza. Maswali
ambayo yanaelekea kuwa ya kiupinzani tu au hayahusiani na jambo
linaloelezwa na msemaji yanaweza kuwa matokeo mabaya ya kuzuia uwezo
wa msemaji kuwasilisha maoni yake kwa uthabiti na yanaweza kumfanya
asiendelee kuzungumza. Maswali ya kuleta mafanikio yanapaswa kuhusiana
na kile msemaji anachosema lakini pia yanatoa mwanya wa kujibiwa kwa
namna nyingi. Kwa mfano, “Ulifanya nini baada ya hapo? Je, uliweza
kusaidia?” Au, “Je, ungefanya nini kama ungeambiwa juu ya tatizo hilo
mapema?”
Jambo bora juu ya usikivu unaoleta mafanikio katika mawasiliano ni kwamba hutokea
kuenea kwa washiriki wote. Kadri unavyojikuta kuwa msikilizaji makini na kujifunza
zaidi kutokana na yale unayoambiwa na wengine, utakuwa unashiriki katika shughuli
ambayo hukuza heshima na mvuto baina yako na wengine. Uwe kazini, katika familia,
au katika mazingira ya kushirikiana na wengine, utagundua kwamba watu
wanapojisikia kuwa wamesikilizwa, mara nyingi wanajenga tabia ya kusikiliza wengine
kwa makini zaidi.
133
KIAMBATISHO D
Marejeo juu ya Uongozi
Vitabu vya Mafunzo ya Uongozi
The Centre for Development and Population Activities, “Gender and Leadership” in Gender and
Development, The CEDPA Training Manual Series, Volume III, Washington, District of
Columbia: The Centre for Development and Population Activities, 1996.
Commonwealth Secretariat, Tutors Manual on Training Skills for Women, London, England:
Commonwealth Secretariat, 1984.
Degelman, Charles and Bill Hayes, Active Citizenship Today: A Field Guide, Los Angeles,
California: Constitutional Rights Foundation, and Alexandria, Virgina: Close Up Foundation,
1995.
Fetterman, D., Empowerement Evaluation: Knowledge and Tools for Self-Assessment and
Accountability, Thousand Oaks, California: Sage, 1996.
Flowers, Nancy, In Our Own Words: A Guide for Human Rights Education Facilitators,
Bethesda, Maryland: Sisterhood Is Global Institute, 1999.
Giber, David, Louis L. Carter, and Marshall Goldsmith, eds., Linkage Incl.’s Best Practices in
Leadership Development Handbook: Case Studies, Instruments, Training, San Francisco,
California: Jossey-Bass, 2000.
International Peace Research Association (IPRA) and UNESCO, Handbook Resource and
Teaching Material in Conflict Resolution, Education for Human Rights, Peace and Democracy,
Paris, France: UNESCO, 1994.
McCauley, Cynthia D., Russ S. Moxley, and Ellen Van Velsor, eds., The Centre for Creative
Leadership Handbook of Leadership Development, San Francisco, California: Jossey-Bass, 1998.
And M. W. Hughes-James, An Evaluation of the Outcomes of a Leadership
Development Program, Greensboro, North Carolina: Centre for Creative Leadership, 1994.
Palus, Charles J. and Wilfred H. Drath, Evolving Leaders: A Model for Promoting Leadership
Development in Programs, Greensboro, North Carolina: Centre for Creative Leadership, 1994.
Schwartz, Mary K., Kristin M. Axtman, and Frank H. Freeman, eds., Leadership Resources: A
Guide to Training and Development Tools, Greensboro, North Carolina: Centre for Creative
Leadership, 1998.
Villiers, Peter, 18 Training Workshops for Leadership Development, New York, New York:
McGraw-Hill, 1996.
West NIS Women’s Consortium, Women’s Leadership: Theory, A Training Manual, Kyiv,
Ukraine: NIS Women’s, 1997.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
134
. Women’s Leadership: Practice, A Training Manual, Kyiv, Ukraine: NIS
Women’s Consortium, 1997.
Young, D. and N. Dixon, Helping Leaders Take Effectvie Action: A Program Evaluation.
Greensboro, North Carolina: Centre for Creative Leadership, 1996.
Marejeo juu ya Uongozi na Maendeleo ya Raia
Betters -Reed, B. L. and L. L. Moore, “Shifting the Management Development Paradigm for
Women,” Journal of Management Development 14(2): 24-38, 1995.
Brake, T, The Global Leader: Critical Factors for Creating the World Class Organization, Burr
Ridge, Illinois: Irwin, 1997.
Brookfielf, S., Developing Critical Thinkers: Challenging Adults to Explore Alternative Ways of
Thinking and Acting, San Francisco, California: Jossey-Bass, 1987.
Bystydzinski, Jill, ed., Women Transforming Politics: Worldwide Strategies for Empowerment,
Bloomington, Indiana: Indiana University Press, 1992.
Catalyst, Women in Corporate Leadership: Progress and Prospects, New York, New York:
Catalyst, 1996.
CIVICUS, Building Civil Society Worldwide: Strategies for successful Communications,
Washington, District of Columbia: CIVICUS, 1997.
, Legal Principles for Citizen Participation: Toward a Legal Framework for
Civil Society Organization, Washington, District of Columbia: CIVICUS, 1997.
Clark, K. E. and M.B. Clark, eds., Measures of Leadership, West Orange, New Jersey:
Leadership Library of America, 1990.
Conger, J.A. and J. A. Kanungo, Charismatic Leadership: The Elusive Factor in Organizational
Effectiveness, San Franscisco, California: Jossey-Bass, 1988.
Covey, S.R., Principle-Centered Leadership, New York, New York: Simon & Schuster, 1991.
Dorfman, P.W., J.P. Howell, S. Hibino, et al., “Leadership in Western and Asian Countries:
Commonalities and Differences in Effective Leadership Processes Across Cultures”. Leadership
Quarterly 8(3): 233-274, 1997.
Drath, Wilfred H. and Charles J. Palus, Making Common Sense: Leadership as Meaning-making
in a Community of Practice, Greensboro, North Carolina: Centre for Creative Leadership, 1994.
Eagly, A.H., M.G. Makhijani, and B.G. Klonsky, “Gender and the Evaluation of Leaders: A
Meta-Analysis,” Psychological Bulletin 111(1): 3-22, 1922.
Freire, Paulo. Pedagogy of the Oppressed, translated by Myra Bergman Ramos, New York, New
York: Continuum, 1995.
Gardner, Howard E. and Emma Laskin, eds., Leading Minds: An Anatomy of Leadership, New
York, New York: Basic Books, 1995.
Heifetz, R.A., Leadership Without Easy Answers, Cambridge, Massachusetts: Harvard University
Press, 1994.
135
Helgesen, Sally, The Female Advantage: Women’s Ways of Leadership, New York: Basic
Books, 1995.
Johnson, D. W. and R. T. Johnson, Cooperation and Competition: Theory and Research, Edina,
Minnesota: Interaction, 1989.
Joseph, Suad and Susan Slyomovics, eds., Women and Power in the Middle East, Philadelphia,
Pennsylvania: University of Pennsylvania Press, 2001.
Korten, David C., Globalizing Civil Society: Reclaiming Our Right to Power, New York, New
York: Seven Stories Press, 1998.
Kouzes, J.H. and B.Z. Posner, The Leadership Challenge: How to Get Extraordinary Things
Done in Organizations, San Francisco, California: Jossey-Bass, 1987.
Lambert, L., The Constructivist Leader, New York, New York: Teachers College Press, 1995.
Makram-Ebeid, Mona, “Exclusion of Women from Politics”, in Kathleen E. Mahoney and Paul
Mahoney, eds., Human Rights in the Twenty-first Century: A Global Challenge, Boston,
Massachusetts: Martinus Nijhoff, 1993.
McCall, M.W. and M.M. Lombardo, eds., Leadership: Where Else Can We Go?, Durham, North
Carolina: Duke University Press, 1978.
Moxley, Russ S., Leadership and Spirit: Breathing New Vitality and Energy Into Individuals and
Organizations, San Francisco, California: Jossey-Bass, 1999.
Nahavandi, Afsaneh, The Art and Science of Leadership, Upper Saddle River, New Jersey:
Prentice Hall, 2000.
Naidoo, Kumi, Civil Society at the Millennium, Bloomfielf, Connecticut: Kumarian Press, 1999.
Otto, Dianne, “Challenging the ‘New World Order’: International Law, Global Democracy and
the Possibilities for Women”, Transnational Law and Contemporary Problems 3:370-415, 1993.
Rost, J.C., Leadership for the Twenty-First Century, New York, New York: Praeger, 1991.
Schein, E.H., Organizational Culture and Leadership, San Francisco, California: Jossey-Bass,
1992.
Schwartz, Mary K., Kristin M. Axtman, and Frank H. Freeman, eds., Leadership Education: A
Source Book of Courses and Programs, Greensboro, North Carolina: Centre for Creative
Leadership, 1998.
Sessa, Valerie I., Michael C. Hansen, Sonya Prestridge, and Michael E. Kossler, Geographically
Dispersed Teams: An Annotated Bibliography, Greensboro, North Carolina: Centre for Creative
Leadership, 2000.
Smircich, L. and G. Morgan, “Leadership: The Management of Meaning”, Journal of Applied
Behavioral Science 18:257-273, 1982.
United Nations Centre for Social Development and Humanitarian Affairs, Women in Politics and
Decision Making in the Late Twentieth Century: A United Nations Study, Boston,
Massachusetts: Martinus Nijhoff, 1992.
VeneKlasen, Lisa and Vaerie Miller, A New Weave of Power, People & Politics: The Action
Guide for Advocacy and Citizen Participation, San Francisco, California: Thw Asian Foundation,
and Washington, District of Columbia: Lisa VeneKlasen, 2002.
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
136
Yukl, G.A., Leadership in Organizations, Englewood Cliffs, New Jersey: Prenctice-Hall, 1989.
137
KIAMBATISHO E
Mashirika Yanayoshughulikia Masuala ya
Uongozi
Orodha ifuatayo hapa chini ni mashirika yasiyokuwa ya kiserikali duniani kote yenye mipango iliyoelekezwa kukuza
uongozi kwa wanawake.
Association Dëmocratique des
Femmes du Maroc (ADFM)
Secteur les Orangers, Rue Molka, Villa No 2
Rabat, Morocco
Tel: 212-37-737165
Fax : 212-37-260813
Email: adfm@mtds.com
Centre de Leadership Feminin
(CLEF) de L’ADFM
30, Rue Sidi Belyout, Apt. 54
Casablanca, Morocco
Tel/Fax: 212-22-31-45-47
Email: adfm@casanet.net.ma
BAOBAB for Women’s Human
Rights
232A Muri Okunola Street, P.O. Box 73630
Victoria Island
Lagos, Nigeria
Tel: 234-1-320-0484
Fax: 234- 1- 262- 6267
Email: baobab@baobabwomen.org
Community Education and Development Services
(CEDS)
P. O. Box 5153
Bamenda, Cameroon
Tel: 237-766-09-37
Fax: 237-336-39-55
Email:cedservice@yahoo.com
Kudirat Initiative for Democracy (KIND)
60 Lanre Awolokun Street
Gbagada Phase 2
Lagos, Nigeria
Tel: 2341-472-7001
E-mail: nigeria@kind.org
Web: www.kind.org
or
P.O. Box 65429
Washington, DC 20035
Tel: 1-301-883-0169
Fax:1-301-883-0151
Email: info@kind.org
The Machreq/Maghreb Gender Linking and
Information Project (MACMAG-GLIP)
P. O. Box 165302
Beirut, Lebanon
Tel: 961-3-615-046
Fax: 961-1-611-079
Email: glipcoord@intracom.net.lb
Web: www.macmag-glip.org
Sisterhood is Global Institute/Jordan
(SIGI/Jordan)
Abu Bake r Complex
Al-Razi Street, Jabal Al-Hussain
Amman 11196 Jordan
Tel: 962-6-5690-770
Fax: 962-6-5690-780
Email: sigi@nets.com.jo
Web: www.sigijordan.org
Women’s Affairs Technical Committee (WATC)
Awad Bldg., Radio Street, 2nd Floor
P.O.Box:2197
Ramallah, Palestine via Israel
Tel: 970-2-298-7783
Fax: 970-2-296-4746
Email: watcorg@pal-watc.org
Web: www.pal-watc.org
Women’s Self-Promotion Movement (WSPM)
P. O. Box W 78 Parktown
Harare, Zimbabwe
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
138
Center for Creative Leadership
One Leadership Place
P.O. Box 26300
Greensboro, NC 27438-6300, USA
Tel: 1-336-545-2810
Fax: 1-336-282-3284
Email: infor@leaders.ccl.org
Web: www.ccl.org
The Council of Women World Leaders
John F. Kennedy School of Government
79 JFK Street
Cambridge, MA 02138, USA
Tel: 1-617-496-3157
Fax: 1-617-496-8391
Email: council_leaders@harvard.edu
Web: www.womenworldleaders.org
The James MacGregor Burns Academy of
Leadership
University of Maryland
College Park, MD 20742-7715, USA
Tel: 1-301-405-6100
Fax: 1-301-405-6402
Email: academy@academy.umd.edu
Web: www.academy.umd.edu
Parliamentarians for Global Action
211 East 43rd Street, Suite 1604
New York, NY 10017, USA
Tel: 1-212-687-7755
Fax:1-212-687-8409
Email: info@pgaction.org
Web: www.pgaction.org
Women’s Institute for Leadership,
Development for Human Rights
(WILD)
1375 Sutter Street, Suite 407
San Francisco, CA 94109, USA
Tel: 415-345-1195
Women’s Leadership Institute
Mills College
5000 MacArthur Blvd.
Oakland, CA 94613, USA
Tel: 1-510-430-2019
Fax: 1-510-430-3233
Web: www.mills.edu/WLI/wli.home.html
CIVICUS: World Alliance for
Citizen Participation
1112 16th Street NW, Suite 540
Washington, DC 20036, USA
Tel: 1-202-331-8518
Fax: 1-202-331-8774
Email: info@civicus.org
Web: www.civicus.org
Center for Women’s Global
Leadership (CWGL)
Douglass College, Rutgers
The State Univers ity of New Jersey
160 Ryders Lane
New Brunswick, NJ 08901- 8555, USA
Tel: 1-732-932-8782
Fax: 1-732-932-1180
Email: cwgl@igc.org
Web: www.cwgl.rutgers.edu
Global Women in Politi cs Program
The Asia Foundation
465 California Street, 14th Floor
San Francisco, CA 94104, USA
Tel: 1-415-982-4640
Fax: 1-415-392-8863
Email: info@asisfound.org
Web: www.asiafoundation.com
Fax: 415-345-1199
Email: esther@wildforhumanrights.org
Web: www.mills.edu/WLI/wli.home.html
International Women’s Media
Foundation (IWMF)
1726 M Street NW, Suite 1002
Washington, DC 20036, USA
Tel: 1-202-496-1992
Fax: 1-202-496-1977
Web: www.iwmf.org
Kiambatisho E
139
Akina Mama Wa Africa
334-336 Goswell Road
London EC1V 7LQ
United Kingdom
Tel: 44-20-7713-5166
Fax: 44-20-7713-1959
Email: amwa@akinamama.org
Web: www.akinamama.org
Au
Plot 30 Bukoto Street Kamwokya
PO Box 24130
Kampala, Uganda
Tel: 256-41-543681/3
Fax: 256-41-543683
Email: amwa_u@imul.com
Afghan Institute of Learning
House No: 163/T, Arab Road, University Road
Peshawar, Pakistan
Tel/Fax: 92-91842-308
Centre for Organization Research and Education
Lane 3 Basisthapur, Beltola (Dispur)
Guwahati 781028
Assam, India
Tel: 91-361-222-87-09
Fax: 91-361-222-87-30
Email: core_ne@sify.com
Foundation for the Support of Women’s Work (FSWW)
Galipdede Cad., 149/4
80030 Mueyyetzade
Beyouglu/Istanbul, Turkey
Tel: 90-212-249-07-00
Fax: 90-212-249-15-08
Women’s Development Collective (WDC)
No. 44, Jalan Kajang 1
Taman Seri Kajang
43000 Kajang
Selangor, Malaysia
Tel: 603-8737-3979
Fax: 603-8737-4180
Email: wdc@tm.net.com
Women’s Learning Partnership
for Rights, Development, and
Peace (WLP)
4343 Montgomery Avenue
Suite 201
Bethesda, MD 20814, USA
Tel: 1-301-654-2774
Fax: 1-301-654-2775
Email:
wlp@learningpartnership.org
Web:www.learningpartnership.org
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
140
Kiambatisho E
141
KIAMBATISHO F
Baraza la Kimataifa la Ushauri
Shirika la WLP liliunda Baraza la Kimataifa la Ushauri (AIC) ambalo linawakilisha mitazamo mbalimbali ya
kitaalamu, kiutamaduni, na kidini na lina ujuzi mkubwa wa kutathmini matokeo ya kijamii, kiutamaduni, na kisiasa ya
miradi ya uongozi inaysimamiwa na WLP. Baraza hili linalisaidia shirika la WLP kuchambua na kuweka katika hali
inayofaa habari za kisheria, kisiasa, na kisayansi jamii zinazotolewa katika maandishi na vifaa vyake. Wajumbe wa
Baraza ni hawa wafuatao:
Hafsat Abila Founder, Kudirat institute for Democratie
Afifa Dirani Arsanios International Consultant, Lebanon
Suheir Azzouni-Mahshi Director General, Women’s Affairs Technical
Committee, Palestine
Charlotte Bunch Exective Director, Center for Women’s Global
Leadership
Thais Corral Coordinator, Centro Mulher informacao, Associria,
e-Execuacao de Projetos, Brazil
Marian Wright Edelman Founder and President, Children defense fund
Nancy Flowers Human Rights Education Consultant
Noeleen Heyzer Director, United Nations Development Fund for Women
(UNIFEM)
Ayesha Imam Executive Director, BAOBAB for Women’s Human Rights
Nigeria
Zahira Kamal General Director, Directorate for Gender Planning and
Development, Palestinian Ministry of planning
Farhad Kazemi Vice Provost, New York Universuty
Asma Khader Lawyer and women’s Rights Activist, Jordan
Amina Lemrini President, Association democratique des femmes du Maroc
Ann Elizabeth Mayer Associate Professor of Legal Studies, University of Pennsylvania
Afaf Mahfouz Former President, Conference of Non-governmental
Oganisations in Consultative Relationship with the
United Nations
Rabea Naciri Executive Director, Collectif 95 Maghreb Egalite, Morocco
Kumi Naidoo President, CIVICUS: World Alliance for Citizen Participation
Thoraya Obaid Executive Director, United Nations Popolation Funds (UNFPA)
Ayo Obe President, Civil Liberties Organisation, Nigeria
Jacqueline Pitanguy Founder and President, Canadia,studo, Perquisa, Infomacao,e Acao, Brazil
Aruna Rao President, Association for Women’s Rights
Uongozi Bora: Kitabu cha Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake
142
in Development
Regan Ralph Vice-President and Director, Health and Reproductive Rights, National Women
Law Center
Kavita Ramdas President, The Global Fund for Women
Bouthaina shaaban Professor, Damascus University, Syria
Zenebeworke Tadesse Founder, Associaion of Africa Women for Research and Development,
Ethiopia
wakishauriana na
Association
Démocratique des
Femmes du
Maroc
BAOBAB for
Women’s
Human
Rights
Women’s
Affairs
Technical
Committee

No comments:

Post a Comment