Friday 5 December 2014

UPAKO WA ROHO MTAKATIFU

Tunatumaini kwamba utafurahia toleo hili kubwa la MATENDO! Tafadhali angalia uk. 63 kwa maelezo jinsi ya
kuendelea kupokea matoleo ya MATENDO kwa njia ya posta - na kwa haraka zaidi kwa njia ya barua pepe ('email').
TOLEO LA KISWAHILI
Nakala 16 / Nambari 1
Mwandishi Mch. Frank R. Parrish
MATENDO
“Si kwa uwezo,
wala si kwa nguvu,
bali ni kwa Roho
Yangu,
asema Bwana wa
Majeshi”
(Zekaria 4:6)
UPAKO
WA ROHO
MTAKATIFU
Mpendwa Kiongozi Mwenzangu wa Kanisa:
Toleo hili la Gazeti la MATENDO juu ya
“Upako” limeandaliwa liwe somo la ndani na
la ki-Biblia kuhusu hoja hii. Ili upate ufahamu
bora wa hoja hiyo nyeti, itakubidi utafakari
kwa makini, ujifunze na kujibidisha kikamilifu.
Itakupasa utumie muda mrefu katika
kujifunza somo hili. Huenda ujifunze kurasa
mbili au tatu tu kwa siku. Lakini
nakuhamasisha sana ujitoe katika sala na bidii ya
kujifunza. Ukifanya hivyo, maisha yako na utumishi
wako vitabadilishwa!
Mimi nilikuwa mtumishi kwa muda mrefu kabla
sijatambua hamu ya Mungu kwamba upako wa Roho
Wake uwepo katika maisha yangu na utumishi wangu.
Nilipofungua moyo wangu na kumruhusu Mungu
“afungue macho ya ufahamu wangu” (taz. Waefeso
1:18), nilibadilishwa! Utumishi wangu ulibadilishwa!
Uwepo na uweza wa Roho Mtakatifu ulidhihirika na
kutendeka zaidi sana ndani yangu, na kupitia kwa
maisha yangu na utumishi wangu.
Matunda mengi zaidi yalionekana katika utumishi
wangu. Nilitambua uwepo wa Mungu kwa ndani zaidi
kabisa kuliko zamani zote. Maisha yangu hayakuwa
rahisi zaidi; lakini niliona uwezo wa kuwa zaidi ya
mshindi kwa Kristo anipendaye (taz. Warumi 8:37).
Ninataka kukutia moyo sana ujibidishe kama
mfanyakazi mwaminifu na madhubuti katika kujifunza
somo hili. Yafuatayo ni maagizo ya kimatendo
yatakayokusaidia kufanya hivyo:
Kwanza, nimetaja mistari mingi ya Biblia katika
mafunzo haya yote. Tafadhali tumia muda wa kutafuta
na kusoma kila mstari wa Maandiko uliotajwa.
Kufanya hivyo kutakusaidia katika malengo kadhaa
yaliyo muhimu sana: 1) Wewe kama kiongozi wa
kanisa, wakati wowote usipokee hivi hivi kila fundisho
unalosoma au kulisikia, haidhuru limetokea wapi.
Wakati wote uchunguze Maandiko mwenyewe
(Matendo 17:11); 2) Kama kiongozi wa kanisa, ni
muhimu kwako kuongeza ujuzi, uzoefu na ufahamu
wako wa Maandiko (2Timotheo 2:15-18). Kufanya
hivyo kutakulinda mwenyewe na wale unaowaongoza
ili msidanganyike, na pia kutakufanya uwe mstadi
katika Neno la Mungu; 3) Neno la Mungu peke yake
limethibitishwa na uweza wa Mungu (2Timotheo 3:16- 17;
Waebrania 4:12-13; 2Petro 1:20-21). Ni utendaji wa
pamoja tu wa Roho Mtakatifu na Neno la
Mungu unaobadilisha moyo wa mwanadamu.
Pili, ukae na daftari na kalamu uandike
kumbukumbu, maswali au mistari ya Biblia ya
kuchunguza baadaye. Mungu ataongea na
wewe akikufunulia ukweli unapojifunza Neno
Lake. Mafunzo haya yawe safari ya kukua
kwako binafsi, yenye kukusaidia zaidi sana
kuliko kupokea mafundisho mazuri tu.
Mwisho, mtenda kazi mwenzangu mpendwa,
nataka kukutia moyo uambatanishe na kujifunza
kwako, kumwomba na kumngojea Bwana kwa wingi.
Maana ni Roho Mtakatifu anayefunua ukweli, na asili
na tabia ya Kristo (Yohana 14:17,26). Usiache mafunzo
haya yahusiane na akili yako tu, kwa sababu ukifanya
hivyo utafungia mengine ambayo ungaliweza
kuyapokea. Ni kweli akili zetu ni karama ya Mungu,
lakini bado zina mipaka (taz. 1Wakorintho sura ya 3
na 4). Ufungue moyo wako, ukamruhusu Roho
Mtakatifu akufundishe wewe na kukutengeneza wewe.
Unaweza kuwaongoza wengine mahali pale tu ambapo
wewe, mwenyewe, umekwisha fika. Kwa hiyo uombe,
ujifunze na kufurahia mafunzo haya – nawe ukue
katika uweza wa upako wa Mungu hata katika kusoma
kwako!
Tafadhali pia uangalie jambo maalum tuliloongeza
katika toleo hili la MATENDO. Kila mara kwa mara
katika mafunzo yote, kutakuwa na viangalizo maalum
kutoka kwangu kwa ajili yako. Hivi vimeandaliwa ili
wewe kama kiongozi wa kanisa upate mtazamo wa
ndani zaidi kuhusu kanuni fulani muhimu ya ki-Biblia
kuhusu utumishi au kukua kwako binafsi. Viangalizo
hivyo hutambulika kwa kichwa “Mchungaji kwa
Mchungaji” navyo vimewekewa rangi ya kijivu nyuma
kusudi vionekane kwa urahisi zaidi.
Mchungaji, mimi ninakupenda katika Kristo, tena
naamini makusudi ya Mungu kwa ajili yako. Wewe u
chombo kilichochaguliwa na Mungu, ili Yeye akutumie
kwa ajili ya Ufalme na utukufu Wake, na katika
kubariki Kanisa Lake. Ubarikiwe katika Jina la Bwana
Yesu Kristo. Mungu sasa akubariki, akupe uwezo na
ukuzi unapojifunza na kupokea kutoka kwa Neno Lake
na Roho Wake!
Ndugu yako,
Mch. Frank R. Parrish
Mkurugenzi, World MAP
2 • MATENDO
Upako wa
Roho Mtakatifu
BARUA YA MWANDISHI – MUHIMU!
Mwandishi Rev. Frank R. Parrish
REV.
FRANK
PARRISH
Nakala 16 / Nambari 1
Kabla hatujaweza kuanza mafunzo haya kuhusu
“Upako”, yaliyo ya ki-Biblia na yenye ufanisi wake,
inatubidi tuweke msingi wa kanuni fulani muhimu.
Kanuni hizi zitatujengea jukwaa la kusimamia ambapo
tutaweza kupata mandhari au picha ifaayo ya upako.
Mafungu ya kwanza ya mafunzo hayo yatahusiana na
kanuni hizo za kimsingi. Huenda ni mapya kwako, au
pengine umekwisha kuyazoea. Lakini ni muhimu sana tuwe
na msingi wa pamoja wa kujengea mafunzo hayo. Nakuomba
ujifunze kanuni zifuatazo kwa makini. Umruhusu Roho
Mtakatifu apate muda wa kutosha ili afunue, kuthibitisha,
kupima na kuyakinisha kiasi gani kanuni hizo zimejengwa na
kujulikana katika maisha yako na utumishi wako.
Kiongozi mwenzangu, haya si mafunzo ya kupevuka
“kimkato”. Pia hayakupatii utaratibu mwepesi wala ufundi
maridadi utakaokufanya “maarufu”.
Kinyume chake, mafunzo hayo ni ya ki-Biblia yahusuyo
jinsi inavyotubidi sisi kama viongozi wa kanisa tukue na
kutenda kazi katika Ufalme wa Mungu. Njia ya upevu ni
mafuatano ya lazima ili tuwe na matunda halisi, na utumishi
unaodumu na kumletea Mungu utukufu mwingi!
Kwa hiyo, tujishughulishe kwa bidii tunapojifunza
kuhusu hoja hii ya upako. Mungu aweza kubariki yale tu
aliyoyaweka kama njia na mapenzi Yake. Kwa hiyo ni lazima
tuweke msingi imara wa kanuni zinazotokana na Neno Lake
kabla ya kuendelea na hoja zinazofuatana za upako (Isaya
28:10).
Utumishi Usio Na Mipaka
Hoja ya UPAKO ni muhimu sana kwa kila mwamini wa
Yesu Kristo. Lakini ufahamu wa UPAKO – u nini,
unafanyaje, na jinsi tunavyoweza kukua na kutenda ndani
yake – ni wa lazima, hasa kwa wale walioitiwa utumishi wa
muda wote.
“Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni
kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi.”
(Zekaria 4:6)
Mwandishi Rev. Frank R. Parrish
MATENDO • 3
UTANGULIZI
Upako wa Roho
Mtakatifu
Nakala 16 / Nambari 1
Inasikitisha kwamba UPAKO mara nyingi haufahamiki
vema au ni hoja ambayo viongozi wengine hata
wanajiepusha nayo. Ingawa ni karama ambayo Mungu
anataka kutupatia, viongozi wengi hawajui upako ni nini
wala jinsi ya kuupokea. Kwa hiyo, wanajaribu kuvipatia vitu
vingine nafasi ya upako wa Roho Mtakatifu.
Viongozi fulani huwa na ustadi katika utawala au
utaratibu. Huenda wanajiongezea elimu, wakiweka cheo, jina
au digrii katika majina yao. Wanahudhuria mikutano mingi
na kuhuishwa na wahutubu wakuu. Pengine wanakuza
vipawa vyao binafsi vya kuhutubu au kuimba ili
wawaongoze au kuwahamasisha watu kwa ufanisi zaidi.
Mambo yaliyotajwa hapo huenda si mabaya yenyewe,
tena yanaweza yasaidie au yasisaidie katika utumishi.
LAKINI HAYA SI UPAKO! Wala hayawezi kuwepo badala
ya upako halisi wa Roho Mtakatifu katika maisha ya
mtumishi.
Elimu na ustadi katika utawala huweza kufaa na
kusaidia. Lakini huwa na mipaka katika kumsaidia kiongozi.
Tunapotegemea elimu yetu, matokeo bora tunayoweza
kutumainia hulingana na upeo wa elimu yetu.
Tunapotegemea ubora wetu wa kuhutubu au ustadi
mwingine, tunafungiwa mipaka ya uwezo wake.
Lakini, tunapomtegemea Roho Mtakatifu,
tunawekewa mipaka ya uweza wa Roho Mtakatifu tu!
Tunayochagua kutegemea, au kuamini, ili tutekeleze
wito wetu wa utumishi – ndiyo yatakayoweka mipaka ya
uwezo wetu. Je, unataka mipaka kiasi gani katika utumishi
wako?
Kwa Mungu, hakuna mipaka (taz. Luka 18:27)! Kwa
hiyo, nikimwamini na kumtegemea Mungu katika uweza
Wake, mipaka yangu peke yake katika utumishi ni mapenzi
ya Mungu na makusudi Yake kwa ajili yangu (Wafilipi 4:13).
Ni mapenzi ya Mungu kwa ajili ya kila mwamini
aliyezaliwa mara ya pili kwamba adhihirishe matunda ya
Roho (Wagalatia 5:16-26) katika mwenendo na matendo
yake. Matunda ya Roho ni tabia ya Kristo. Aina hii hii ya
tabia hutakiwa hasa kwao walioitwa wawaongoze wengine
katika Mwili wa Kristo. Ni kazi ya kiongozi kuwa mfano wa
mwenendo wa kiuchaji kwao anaowaongoza (1Wakorintho
11:1; Wafilipi 3:17; 1Timotheo 4:12). Hakuna karama, ustadi
wa kutawala, wala ujuzi wa kuhubiri au kufundisha
vinavyoweza kuwepo badala ya unyofu na tabia ya kufanana
na Kristo.
Ni mapenzi ya Mungu pia – hasa kwao wanaoitwa ili
waongoze – kwamba tuwe na uweza upitao akili zetu wa
ki-Mungu wa Roho Mtakatifu. Yesu aliwaambia wanafunzi
Wake: “Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi
niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae
matunda; na matunda yenu yapate kukaa” (Yohana 15:16).
Kutokana na mstari huu tunaona kwamba Yesu anataka
matunda ya maisha yetu yadumu. Yatawezaje kufanya hivyo?
Utumishi wetu unapojaa uweza wa upako wa Mungu –
uweza wa Roho Mtakatifu – uweza Wake kupitia kwetu
unatuwezesha kuongoza maisha ya watu kwa njia yenye
matunda yanayodumu.
Haidhuru kiongozi ana vipawa, talanta au akili kiasi
gani. Pasipo kuwezeshwa na Roho Mtakatifu, kiongozi
hawezi kutimiza mapenzi ya Mungu kwa njia ya Mungu
katika utumishi. Ni baraka kwetu kwamba Mungu anajua
4 • MATENDO
TOLEO LA KISWAHILI
TOLEO 16 / NAMBARI 1
Limetolewa na World MAP
CHENNAI, INDIA
YALIYOMO
UPAKO WA ROHO MTAKATIFU
“Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho
Yangu, asema Bwana wa Majeshi” (Zekaria 4:6)
Mwandishi Mch. Frank R. Parrish
Barua Ya Mwandishi – Muhimu! .................................2
Utangulizi ........................................................................3
SEHEMU YA I
Utangulizi Wa Ki-Historia Na Ki-Biblia Wa Upako ...9
SEHEMU YA II
Asili, Kusudi Na Matumizi Ya Upako ........................11
SEHEMU YA III
Kutembea Katika Apako .............................................35
Kutazama Kwa Kifupi Ishara Na Maajabu...............54
Wahariri.........................................Frank & Wendy Parrish
Wahariri Kimataifa .........................................Gayla Dease
Mfasiri wa Kiswahili..................................Judie Mwarabu
Wahairi wa Kiswahili...........................................Sig Feser
Mhakiki wa Kiswahili: ................................Ndelilio Nnko
Gharama za Posta zimelipwa
Chennai - 600 010 India
MAONO NA UTUME
WA GAZETI LA MATENDO
Kuwapatia bure mafundisho ya Bibliana mafunzo ya
huduma viongozi wa makanisa wa nchi za Asia, Afrika, na
Latini Amerika ambao wanafundisha au kuhubiri neon la
Mungu (Biblia) kwa kundi la watu 20 au zaidi angalau
mara moja kwa wiki.
MATENDO (ISSN 0744-1789) hutolewa mara nne kwa
mwaka na World MAP ACTS INDIA, 67 Beracah Road,
Kilpaul, Chennai 600 010, T.N., INDIA. Head office and
copyright: World MAP, 1419 North San Fernando Blvd.,
Burbank, CA 91504-4194, U.S.A. Gharama za Posta za
gazeti zimelipwa kule Arcadia, California na katika ofisi
nyingine za Posta. Maswali hupokelewa kwa anwani ya
hapo juu pamoja na Box 4142, Manila, Philippines; Box
942, White River 1240, South Africa.
MKUU WA POSTA: Tafadhali utume mabadiliko ya
anwani kwa World MAP ACTS INDIA, 67 Beracah Road,
Kilpaul, Chennai 600 010, T.N., INDIA. World MAP, 1419
North San Fernando Blvd., Burbank CA 91504-4194,
U.S.A. MATENDO ni gazeti linalotolewa bure, ambalo
huchapishwa na kutumwa kwa viongozi wa makanisa.
MATENDO
Nakala 16 / Nambari 1
mahitaji yetu vizuri sana kuliko sisi tujuavyo wenyewe. Na
Yeye amekwisha kutupatia uweza Wake utusaidie katika
kutimiza wito Wake ulio tukufu.
Sura Pasipo Uweza
Kuna makanisa mengi na huduma nyingi siku za leo
ambamo uwepo wa Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu
umefungiwa mipaka. Huduma hizi huenda zinavuta umati
mkubwa wa watu, tena zina vituo na vifaa vya hali ya juu na
tamasha za kusisimua. Lakini kama uwepo na uweza halisi
wa Roho Mtakatifu hauonekani wala kukaribishwa,
mikutano yake huenda itakuwa sherehe za kidini zisizo na
uhai wowote.
Ukumbi au uwanja mkubwa hujaa umati mkubwa sana
wa watu, huwa na vifaa vya kisasa na ratiba ya kusisimua
kwa ajili ya mechi ya kandanda tu. Lakini mambo haya ya
kimwili au ya nje hayana uhusiano wa maana na kuwafanya
watu wawe wanafunzi wanaomfuata Yesu Kristo kwa bidii!
Katika historia ya Kanisa, kuna maeneo mengi duniani
ambapo Mungu alitenda miujiza na mambo mengine makuu
akitumia wanadamu waliojitolea kama vyombo Vyake.
Makanisa mengi ya maeneo haya na hata maeneo yenyewe
makubwa, zamani yalijulikana kwa ajili ya uwepo wa
Ukristo wenye uhai na uwezo. Inasikitisha kwamba leo
maeneo hayo yamo ndani ya giza ya kiroho. Pale Kanisa la
zamani lilipositawi na kuwa na uongozi mkubwa, sasa ni
patupu pasipo nuru ya Injili.
Kati ya makanisa ya aina hii yanayojulikana zaidi katika
historia ya Agano Jipya ni yale ya Asia Ndogo (sasa taifa la
Uturuki). Habari za makanisa haya hupatikana katika kitabu
cha Ufunuo. Kwa kawaida hujulikana kama “Makanisa Saba
ya Ufunuo”.
Makanisa hayo yalisifiwa kuwa ngome kuu zenye uwezo
kwa kazi ya ukombozi ya Kristo katika mioyo ya watu.
Miujiza mingi ilitendeka hapo (soma Kitabu cha Matendo).
Lakini leo, watalii wanatoa fedha ili watembee kati ya
magofu ambapo mitume wale wakuu walipohubiri Neno la
Uzima. Sehemu hizi sasa hazina uhai wala uwezo wowote wa
Injili.
Ilitokeaje basi kwa hayo makanisa na hizi huduma
ambavyo zamani vilikuwa vikuu? Magofu haya matupu,
yanayotumiwa sasa na ndege wa angani tu, yamesimama
kama onyo na mafundisho kwetu sisi sote.
Haya ndiyo tunayoweza kujifunza: Wakati wowote
ambapo viongozi wa kanisa wanaanza kutegemea uwezo
wao, au mapokeo, vyeo, siasa za kikanisa, au hata elimu na
ujuzi wa kimasomo – badala ya kumtegemea Roho
Mtakatifu wa Mungu na kweli za milele za Neno Lake –
ndipo uhai na uweza wa Mungu unapoanza kutoweka kwetu
sisi kama viongozi, na pia kwenye huduma au makanisa
ambayo Mungu ameweka chini ya uongozi wetu.
Kanisa Ni Nini?
Roho Mtakatifu alimwezesha Paulo ashughulikie hali ya
kanisa (taz. 1Wakorintho sura ya 3). Kanisa la Korintho
lilikemewa kwa ajili ya kugombana kwao katika hali ya
kimwili, kitoto na kibinafsi. Watu walikuwa wakigawanyika
katika vikundi kwa ajili ya kujipatia nafasi ya kutawala
wengine kana kwamba ni wakubwa wao (3:1-4). Hali hii
ilikuwa, na hata leo bado ndiyo, kiburi cha kujisifu – yaani
dhambi ya ibilisi (1Timotheo 3:6). Huu mwenendo wa kiburi
na hii bidii ya kujitegemea ya kibinadamu bado huzuia
ufanisi wa kuzaa matunda katika Kanisa leo.
Paulo anaendelea kutamka wazi kwamba Mungu ndiye
Peke Yake anayewezesha Kanisa likue kikweli. “Hivyo,
apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye”
(1Wakorintho 3:7).
Kuna MSINGI MMOJA tu ambao Kanisa linaweza
kujengwa juu yake: Yesu Kristo aliye Jiwe Kuu la Pembeni
(1Wakorintho 3:10-11; taz. pia Waefeso 2:20-22). Hili ndilo
Jiwe letu Kuu la Pembeni kwa Kanisa la leo, vile vile kama
lilivyokuwa wakati Kanisa lilipozaliwa zaidi ya miaka elfu
mbili iliyopita!
Kiini Cha Kanisa
Matumizi ya jiwe kuu la pembeni katika ulimwengu wa
zamani yalikuwa ya kipekee kabisa, nayo yatatusaidia
tufahamu vizuri zaidi sababu ya Yesu kuitwa “jiwe kuu la
pembeni” (Mathayo 21:42).
Katika Mashariki ya Kati wakati wa zamani, nyumba na
majengo mengine yote yalijengwa kwa njia ile ile. Jiwe moja
liliwekwa kwa vipimo vilivyofuatwa kwa uangalifu, nalo
lilikuwa jiwe kuu la pembeni. Halafu jengo lote liliendelea
kupimiwa ukubwa, ramani na uwekaji, kufuatana na
kulingana na jiwe kuu lile pekee la pembeni.
Huu ndio mfano uliotumiwa na Roho Mtakatifu kupitia
kwa Paulo akionesha ukuu wa Kristo kwa ajili ya kujengwa
kwa Kanisa lililo hai. Ni la mawe yaliyo hai, yanayokua na
kuhuishwa kiroho, ambayo yamejengwa kulingana na Jiwe
Kuu la Pembeni la wokovu katika Yesu Kristo (1Petro
2:4-10). Hakuna sehemu nyingine yoyote itakayokaa sawa
wala kunyoka pasipo Jiwe hili likaalo kama kiini cha Kanisa.
Sisi kama viongozi wa kanisa tumeitwa tuwe washirika
wa Kristo katika kutii makusudi na mipango Yake tukisaidia
kujenga Kanisa la Mungu lililo hai. Kanisa la Agano Jipya –
Kanisa la Kristo – ni kundi la watu waliopata ufahamu wa
wokovu katika kumwamini Yesu Kristo. Neno “kanisa”
katika Agano Jipya halimaanishi utaratibu wa kiutawala,
vyeo, majengo wala madhehebu. “Kanisa” ni watu
waliookolewa na kuhesabiwa haki kwa imani katika Kristo,
na ambao wanaendelea kuwa wanafunzi wanaopevushwa.
MATENDO • 5
Kutangaza
Neno
la Uzima
Nakala 16 / Nambari 1
Uzao Halisi Wa Matunda
Majina mengine ya Agano Jipya yanayofafanua Kanisa
ni pamoja na: “Mawe yaliyo hai” (1Petro 2:5); “Mwili wa
Kristo” (1Wakorintho 12:27); “shamba”, “jengo” au
“hekalu” la Mungu (1Wakorintho 3:9,16-17). Majina haya
yote yana uhusiano mmoja: yote yanawahusu watu ambao ni
waamini wa kweli wa Yesu Kristo.
Ni muhimu kabisa kuyaelewa haya. Sisi kama viongozi
wa kanisa, tumeitiwa zaidi ya kufuata utaratibu wa kutawala
kanisa, kusimamia majengo mapya, au kuandaa matamasha
na matukio ya kikanisa. Sisi tumeitwa tuwe washiriki wa
Mungu katika kuwafunza na kuwajenga watu.
Tumeitwa na Mungu tulichunge na kulilea Kanisa lililo
hai la Mungu aliye hai, yaani watu wanaoamini –
tukiwasaidia wawe wanafunzi wanaokua wa Yesu Kristo.
Hatuwezi kutekeleza wito huu wa kuwa mawakili bila
msaada na uweza wa Mungu (taz. Zaburi 127:1).
Mungu atatuwajibisha kuhusu jinsi tulivyojenga juu ya
Msingi Mmoja yaani wokovu kwa njia ya Kristo
(1Wakorintho 3:12-23). Je, sisi tunavuta umati wa watu
kutokana na ubunifu wetu, nguvu na akili zetu? Njia hii
inaweza kuonekana kuwa na ufanisi kwa muda, lakini
haitaleta matunda ya kudumu ambayo Mungu anayatafuta
(Yohana 15:5,8,16).
Au badala ya haya, je, sisi tunajitoa kwa Roho wa
Mungu kila siku na kujisalimisha kwa mapenzi Yake? Je,
tunaongozwa na Yeye kama wana wa kweli wa Mungu
(Warumi 8:14), tukimtegemea kwa ajili ya kila dakika ya
utumishi ambayo anatukubalia? Kama ndivyo, basi kwa
uweza na msaada Wake, tunaweza kuwa na matunda ya
kweli, na matunda yetu yatakaa milele (Yohana 15:16).
Tafadhali ufahamu kwamba matunda na uzazi wake
havikuainishwa na Mungu jinsi akili ya kibinadamu awezavyo
kuviainisha. Wanadamu huenda wasema kwamba uzazi wa
matunda ni kuwa na wafuasi wengi, au kupata kuwa tajiri na
mwenye kusikilizwa. Hekima ya kibinadamu huweza
kuuainisha kama umashuhuri, uwezo wa kutawala au ufanisi.
Lakini uzazi wa kweli wa matunda kwa maoni ya Mungu
huainishwa na kupimwa kufuatana na kipimo kimoja tu:
maisha ya watu wanaogeuzwa katika mfano na tabia ya
Kristo jinsi wanavyopevuka kama wanafunzi Wake.
Kufahamu kanuni zifuatazo kutakusaidia kushikamana na
ukweli wa kuainishwa huku.
Kurejezwa Upya Katika Mfano Wake
Binadamu aliumbwa katika mfano wa Mungu (Mwanzo
1:26-27). Mfano huu si wa kimwili hasa, bali ni mfano katika
uwezo na ustadi. “Mfano” katika maana hii ya ki-Biblia
huhusiana na akili na kutafakari, hisia na ubunifu, na uwezo
wa kuchagua. Tuliumbwa na uwezo wa kupenda, kujitolea na
kutambua yaliyo mema, ya kweli na ya haki.
Kwa nini Mungu alituumba hivi? Mungu alituumba kwa
kusudi moja: kwa ajili Yake Mwenyewe, ili tuwe na uhusiano
na Yeye. Ndio wito wetu mkuu kabisa! Kama Mungu
angalihitaji au kutamani kuwa na malaika wengi zaidi,
angaliwaumba wengine. Lakini badala yake, tunaona katika
Biblia nzima kwamba Mungu alitaka wana wa kiume na wa
kike ambao wangekuwa na uhusiano wa karibu katika
kupendana na Yeye.
Lakini uwezekano wa uhusiano huu na Mungu
uliharibika wakati dhambi ilipoingia ulimwenguni kutokana
na uasi wa kimakusudi wa Adamu na Hawa. Uasi wao
uliwaletea dhambi wanadamu wote (Warumi 5:12-21).
Lakini wakati ule, mpango wa ajabu wa Mungu kwa ajili ya
kukomboa uhusiano Wake na binadamu ulianzishwa
(Mwanzo 3:15: “Uzao wake” unamaanisha hatimaye
kufanywa mwili na kuzaliwa kwa Mungu Mwana, yaani
Yesu).
Ulipowadia utimilifu wa wakati (Wagalatia 4:4-5),
Kristo alikuja duniani akafa kwa ajili ya dhambi zetu. Tendo
Lake la kujitoa dhabihu lilifungua uwezekano wa kurejeza
uhusiano wetu na Mungu Mwumbaji wetu, uliokuwa
umeharibiwa na dhambi. Tunapopokea kazi ya Kristo ya
wokovu na kwa njia ya kumwamini Yeye, dhambi zetu
zinaweza kusamehewa, nasi tunaweza kumjua Mungu na
kushirikiana na Yeye.
Kazi Ya Kubadilishwa
Lakini zaidi ya haya, Mungu anataka pia kutuweka huru
na matokeo ya dhambi, na uharibifu wake katika maisha yetu.
Kwa hiyo, matokeo ya moja kwa moja ya wokovu wetu
katika Kristo ni kwamba Mungu anaanza kufanya kazi katika
maisha yetu akitugeuza na kuturejeza katika “mfano” ule
ambao alituumba nao.
“Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu
asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye [Yesu
Kristo] awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu
wengi” (Warumi 8:29). Mstari huu unafunua kwamba ni
mapenzi yalioamriwa awali ya Mungu kuwa sisi tunaomjia
Kristo katika wokovu tubadilishwe ili “[tu]fananishwe na
mfano wa Mwana wake”.
Kazi hii ya kugeuzwa inaanza na wokovu na kuendelea
katika maisha yetu yote. Mungu ni mwenye hekima
isiyokoma. Aliunda Ufalme Wake ufuate njia fulani kwa
sababu maalum. Tunapogeuzwa zaidi katika “mfano” wa
uumbaji wetu wa asili (mfano wa Mwana Wake), mambo
mawili maalum yatatendeka:
6 • MATENDO
Kufanya wawe wanafunzi na
kuimarisha imani yao.
Nakala 16 / Nambari 1
1) Tutaweza kutembea katika uhusiano na Mungu usio
na vizuizi, unaoingia ndani zaidi wakati wote. Ni dhambi
iliyoharibu na inayoendelea kuharibu uhusiano wetu na
Mungu. Kwa hiyo, tunapowekwa huru na dhambi na
matokeo yake, tunapata uwezo zaidi wa kushiriki uhusiano
na Mwumbaji wetu ulio na upendo na undani zaidi.
2) Tutarejezwa katika nafasi na lengo vilivyokusudiwa
na Mungu kwa ajili yetu. Binadamu hakuumbwa katika
dhambi wala kwa ajili ya dhambi. Tuliumbwa katika
utakatifu, usafi na utakaso. Uumbaji wote wa asili wa Mungu
ulikuwa mema. “Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na
tazama, ni chema sana” (Mwanzo 1:31).
Hatukuumbwa na mapungufu yoyote, lakini dhambi
iliharibu uzuri wa ule mfano wa kwanza. Kwa hiyo,
tunapowekwa huru na dhambi na kugeuzwa ili tuwe pia huru
zaidi na matokeo ya dhambi, hatima yake itakuwa furaha,
amani na uhuru zaidi katika maisha yetu. Pia tutakuwa
tumeandaliwa vizuri zaidi kabisa kutimiza mapenzi na
makusudi ya Mungu.
Kwa hiyo, tunaweza kusema kwa uhakika kwamba
mageuzi binafsi ni kipaumbele cha Mungu kwa ajili ya
kila mtu pekee. Tunaweza kuainisha maana ya mageuzi
hapa hivi, “kufananishwa zaidi na Yesu katika mawazo,
mapenzi na matendo yetu”.
Kubadilishwa Kwa Uwezo Wa Roho Mtakatifu
Tunapookolewa, maisha yetu ya zamani yamepita.
Tunaanza mafuatano ya mambo yote yakigeuzwa yawe
mapya (2Wakorintho 5:17). Kwa uweza wa Roho Mtakatifu
na Neno la Mungu tunabadilishwa katika “mfano wa Mwana
wake” (Warumi 8:29).
Kazi hii ya kimwujiza ya mabadiliko haiwezi kutimizwa
kwa nguvu yetu wala bidii zetu binafsi (Yeremia 13:23).
Tunaweza kujirekebisha katika mambo madogo, ambayo kwa
kawaida ni ya nje tu. Tunaweza kufanya kazi kwa bidii
tukijaribu kubadilisha maisha yetu na kuendeleza tabia njema.
Lakini kuna kazi ya ndani zaidi sana tunayohitaji kabisa,
kama vile: uponyaji wa kuvunjika na kuumia; ukombozi
katika kukataliwa na aina nyingine za utumwa; uhuru kutoka
katika mienendo yetu ya ubinafsi na dhambi. Aina hii ya
mabadiliko huwezekana kwa uweza wa Roho Mtakatifu peke
yake (Warumi 8:1-11; taz. pia Mathayo 19:23-26; Waefeso
2:1-10; Waebrania 9:13-14).
Mungu anatutakia tukue na kupevuka baada ya kumjia
Kristo kama Mwokozi wetu. Ingawa neema Yake na
msamaha Wake ni kweli kwa wakati wote (1Yohana 1:9), si
kisingizio cha kuendelea katika dhambi au mwenendo wa
kibinafsi. Mungu anasamehe kujikwaa au kuanguka kwetu
mara kwa mara; lakini lazima tusiendelee katika dhambi ile,
bali tusogee mbele katika kutembea kwetu na Mungu
(Luka 9:23-26).
Ukweli ni kwamba watu wanaokataa kubadilishwa au
wanaopinga kazi ya Roho Mtakatifu ya kuwabadilisha
wamemwasi Mungu (Yakobo 1:21-25). Hukumu ya Mungu
juu ya maasi ni kali sana (Mithali 29:1; Waebrania 3:8-11).
Matunda Ambayo Mungu Anataka
Maana ya kuwa mtumishi wa Injili anayezaa matunda
ni kwamba maisha ya wale watu unaowahudumia
yanageuzwa kufuatana zaidi na mfano wa Yesu. Ukumbuke
kwamba kuzaa matunda hakuhusiani na umati wa watu wala
takwimu. Ni rahisi kuingiza watu wengi katika kanisa lako.
Uwape chakula, nguo au fedha pasipo malipo nawe utapata
umati! Au uwape tamasha, ukiwaambia mambo
yanayofurahisha “masikio ya utafiti” (2Timotheo 4:3-4)
wapate kujisikia vizuri.
Lakini umati si usharika, kundi wala jamii. Mkusanyiko
mkubwa wa watu si uthibitisho kwamba una kanisa la Agano
Jipya lenye afya, wala kwamba wewe unafanya wanafunzi!
Swali tunalopaswa kujiuliza kila wakati kuhusu utumishi
wetu ni hili: “Je, maisha ya watu ninaowatumikia
yanabadilishwa wafanane zaidi na Yesu?” Je, lengo lako ni
kuwa na watu wengi zaidi katika kanisa lako tu, au ni kupata
wanafunzi wa kweli wanaopevuka na kukua katika Kristo?
Haidhuru wakiwepo watu kumi au watu elfu moja – wewe
unazaa matunda ikiwa watu wako wanazidi kufanana na
Yesu!
Aina Ya Udhaifu Inayofaa
Tumethibitisha kwamba kugeuzwa katika mfano wa
Kristo ni mapenzi ya Mungu kwa wafuasi wote wa Kristo.
Tunajua kwamba hali hii haiwezi kutimizwa kwa bidii za
kibinadamu, ila tu kwa uweza na uwepo wa Roho Mtakatifu.
Hali hiyo inatufundisha nini basi kuhusu uendeshaji wa
utumishi tuliopewa na Mungu?
Kwa urahisi, tufahamu hili: Uweza unaoonekana wazi
wa Roho Mtakatifu, akifanya kazi na kuongoza pasipo
kuzuiwa ndani ya mwanadamu aliyejitoa, ndio
utakaoleta mageuzi makuu katika maisha ya mtu
mwingine.
Huenda ukweli huu unaonekana kuwa dhahiri mno!
Lakini je, mara ngapi bidii zetu binafsi zenye nia njema
zinachukua nafasi ya kazi ya Roho Mtakatifu kati yetu?
Tukiwa wanyofu kama viongozi na kujichunguza kwa
makini, inatubidi tukiri kwamba mara nyingi sisi ndio tatizo.
Hatuendelei muda mrefu katika utumishi pasipo kutambua
kwamba hatuna uwezo wa kutimiza kazi. Kwa hiyo
tunajishughulisha na mipango, elimu na njia nyingine
MATENDO • 7
Roho Mtakatifu atagusa mwingine
kupita kwako.
Nakala 16 / Nambari 1
zinazotakiwa zilete ushindi au ufanisi. Lakini ukweli ni
kwamba ndani yetu sisi hatuna uwezo wa kutimiza yote
Mungu anayotaka kufanya! Je, unaweza kukiri hali hii juu
yako binafsi?
Kama viongozi, tunataka tufikie upeo wa uwezo wetu
wakati wote. Lakini bidii zetu za juu kabisa za kibinadamu
hazitoshi kwa ajili ya kutimiza mapenzi na makusudi ya
Mungu.
Haya huenda yanaonekana kuwa habari mbaya. Lakini
hali halisi – kama tu tayari kuikubali na kuipokea – ni
kwamba upungufu wetu ni chanzo cha habari njema! Angalia
yale mtume mmoja mkuu kabisa aliyoandika kuhusu
kitendawili hiki:
“Kwa ajili ya kitu hicho [“mwiba katika mwili” wa
Paulo, ms. 7] nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke.
Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza
wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu
wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu
yangu. Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na
misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana
niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu” (2Wakorintho
12:8-10).
Paulo hakukubali mwelekeo wa kushindwa, wala
hakufikiri kwamba alikuwa akiadhibiwa na Mungu. Bali,
Paulo alifurahia mafunuo yake na utendaji wa neema ya
Mungu yenye ushindi katika maisha yake binafsi!
Ni kwa neema ya Mungu kwamba tuna uhai na ushindi
wa washindaji (Warumi 8:37). Lakini kujitoa kabisa na kukiri
wazi haja yake ndiko kulikomfungulia Paulo njia na kuachia
uweza wa Roho Mtakatifu ndani ya maisha yake na kupitia
kwake.
Paulo hakujaribu kuficha au kufunika udhaifu wake, bali
alisema: “nitajisifia udhaifu wangu” (ms. 9) na “napendezwa
na udhaifu” (ms. 10). Maana katika hali hii hasa Paulo
alitegemea kabisa uweza na utoshelevu wa Mungu – naye
aliweza kuishia uweza huo uliomtegemeza na kumwezesha!
(Taz. pia 2Wakorintho 3:1-6.)
Mchungaji kwa Mchungaji: Hatujui “mwiba
katika mwili” wa Paulo ulikuwa nini hasa. Lakini
tunajua kwa uhakika kwamba haikuwa dhambi au
ukosefu wa maadili kwa upande wa Paulo. Mungu
kamwe haachilii dhambi yetu, bali anatuhukumu na
kutuadhibu ili atufikishe kwenye toba ya kweli (Mithali
3:11-12; 2Wakorintho 7:9-10; 1Yohana 1:9). Hakuna
inayofichwa kwa Mungu. Ingawa neema Yake
inaweza kumpa mtu muda wa kufikia toba, Yeye
hadanganyiki tunapojaribu kuficha dhambi. Hatimaye
dhambi yetu itafunuliwa (Hesabu 32:23; Wagalatia
6:7; 1Timotheo 5:24).
Mungu Anawatumia Watu Wanyenyekevu
Kwa ajili ya mafunzo haya, tuainishe udhaifu kuwa:
• kutambua kushindwa kwetu katika kutimiza mapenzi ya
Mungu peke yetu;
• kutoa mioyo yetu na kutegemea kabisa uweza wa Roho
Mtakatifu;
• kumruhusu Roho Mtakatifu afanye kazi kupitia kwetu ili
atimize mambo yenye thamani ya milele katika utumishi
– maisha ya watu yaliyobadilishwa – kwa uweza Wake
na si wetu.
Viongozi wa kanisa mara nyingi wanasikia msukumo
mkubwa wa kuwa na “ufanisi” katika utumishi. Inasikitisha
kwamba mawazo yetu kuhusu ufanisi mara nyingi hufuatana
na vipimo vya dunia au hata vya kujiona kwetu. Tunataka
kuwa maarufu machoni pa wengine. Tunataka kuwa “wakuu”
katika Ufalme wa Mungu ili Mungu atutumie katika mambo
makuu!
Lakini ukweli ndio, nao wakati wote umekuwa, kwamba
hakuna watu wakuu wa Mungu – waliopo tu ni watu
wanyenyekevu waliotumiwa na Mungu katika mambo
makuu! (Taz. Mathayo 20:20-28.)
Tena, hoja ya kimsingi kwa ajili ya utumishi wenye
matunda ni uwepo wa Roho Mtakatifu na kazi anayofanya
Yeye! Mungu hawapingi watu wenye elimu, vipawa vya
utawala au talanta nyingi. Lakini hakuna yoyote kati yake
ambayo yanafaa badala ya uweza wa upako wa Roho
Mtakatifu katika utumishi.
Mungu anaweza kutumia vipawa na karama zetu katika
kuongeza ufanisi wetu. Lakini amefunua wazi katika Neno
Lake kwamba “Pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo
lote” (Yohana 15:5) na “Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu,
bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi” (Zekaria
4:6).
Mungu anayajua haja zetu, tena amekwisha andaa
kikamilifu mahitaji yetu yote. Ametuandalia Upako wa
Roho Mtakatifu ili tuzae matunda wakati wa kutimiza wito
wake wa utumishi.
Kwa hiyo, sasa tujifunze pamoja ili tupate ufahamu
imara wa ki-Biblia wa Upako wa Roho Mtakatifu.
Lengo la masomo haya ni: 1) kuainisha upako, kama
ulivyo na usivyo; 2) kufafanua jinsi upako unavyotenda kazi
katika na kupitia kwa maisha ya mtumishi; na, 3) kufunua jinsi
tunavyoweza kupokea upako huo na kukua ndani yake.
8 • MATENDO
Kukaza mwendo ili
kufikia ufahamu
imara wa ki-Biblia wa
upako....
Upako
Nakala 16 / Nambari 1
A. UPAKO KATIKA AGANO LA KALE
Ili tuweze kufahamu Agano la Kale kikamilifu, ni lazima
tutumie Agano Jipya pia. Maandiko ya Agano Jipya ni kama
“vioo” au “miwani” ambavyo mara nyingi husaidia kulenga
na kuongeza uwazi katika kuangalia maandiko ya Agano la
Kale.
Agano Jipya linafafanua kwamba Agano la Kale (au
Mapatano ya Kale) la Torati au Sheria ni Neno la Mungu
(Mathayo 5:17-18; 2Petro 1:20-21). Lakini sisi sasa tunaishi
chini ya Agano Jipya (Mapatano) ya neema na wokovu
katika Yesu Kristo aliye Mwokozi. Hatuishi tena chini ya
Agano la Kale la Sheria na hatuwezi kupata wokovu kwa
njia ya matendo yetu binafsi (Wagalatia 3:21-25).
Agano Jipya limebatilisha Agano la Kale (taz.
Waebrania sura 7-8). Agano hili Jipya linatimiza Agano la
Kale (Mathayo 5:17-18; Luka 24:25-27) na kuweka msingi
ulio “njia mpya, iliyo hai” (Waebrania 10:20) kwa ajili ya
uhusiano wa binadamu na Mungu.
Hata hivyo, maandiko ya Agano la Kale bado ni sehemu
ya Neno la Mungu la milele (Isaya 40:8). Tunaposoma Agano
la Kale, bado tunaweza kujifunza kanuni nyingi muhimu
ambazo zinahusiana na maisha yetu chini ya utawala wa
Agano Jipya.
Paulo akiwaandikia Wakorintho (1Wakorintho 10:1-13)
alieleza kwamba historia, matukio na mambo ya kujifunza
yaliyoandikwa katika Agano la Kale yafaa kujifunzwa,
kueleweka na kutumiwa katika maisha yetu kama waamini
wa Agano Jipya. “Mambo hayo yalikuwa mifano kwetu…”
(1Wakorintho 10:6).
Kwa hiyo tunaweza kupokea maarifa ya thamani kuhusu
upako wa Roho Mtakatifu ambao sasa hupatikana kwa
waamini wa Agano Jipya tukichunguza picha au “mifano” ya
upako iliyotolewa katika Agano la Kale.
1. Asili ya neno “upako”
Neno la Kiebrania katika Agano la Kale lenye maana ya
“upako” ni masah, nalo hutumika mara 69. Neno
linamaanisha kuwekea mafuta kwa kumimina, kupaka au
kutia kwa kusukuma na kueneza kwenye kitu au mtu
mwenye kupakwa.
Mazoea ya kupaka mafuta yalikuwepo kati ya tamaduni
na makabila mengi ya Mashariki ya Kati ya awali. Mazoea
haya yalikuwa na matumizi ya kawaida na pia matakatifu.
Kwa mfano, kumpaka mgeni mafuta kama tendo la ukarimu
kulifanyika hata wakati wa Yesu (Zaburi 23:5; Luka 7:46;
Yohana 12:3).
Lakini mazoea ya kupaka mafuta yalikuwa na maana
mazito zaidi sana kwa watu wa Israeli katika Agano la Kale.
Tunaona kupakwa kwa kitu mara ya kwanza Yakobo
alipoweka kumbukumbu ya kukutana kwake na Mungu mara
ya kwanza. Yakobo alimimina mafuta juu ya jiwe alilokuwa
amewekea kichwa chake akilala na kuota ndoto (Mwanzo
28:10-18).
Badaye, mafuta yalipakwa kwenye madhabahu na vitu
vingine vilivyotumiwa katika ibada za Hema ya Kukutania
(Kutoka 30:26-29; Walawi 8:10-11). Makuhani pia walitiwa
mafuta (Kutoka 28:41; 30:30; Walawi 8:12). (Pia kulikuwa
na upako wa makuhani kwa kutiwa damu ya kondoo, ambao
tutauangalia baadaye katika mafundisho haya wakati wa
kuchunguza mifano ya upako katika Agano la Kale.)
Mazoea ya kutia mafuta yalipanuliwa kwa wafalme
(1Samweli 9:16; 15:1; 16:3,12) na mara chache kwa manabii
(1Wafalme 19:16).
Upako ulitumiwa kwa makusudi matatu muhimu katika
Agano la Kale. Kwanza, ulitumiwa katika kuweka wakfu:
kutenga, kwa mfano vifaa fulani, kwa ajili ya matumizi
matakatifu. Haya ni pamoja na kuruhusu kitu fulani kwa ajili
ya huduma ya Mungu (k.m. vifaa vilivyotumiwa katika ibada
ya Hema ya Kukutania, Kutoka 30:26-29).
Pili, tendo la upako, ingawa lilifanywa na mwakilishi
mwanadamu, lilieleweka kuwa limetoka kwa Mungu. Mfano
ulio wazi ni wakati Samweli alipowatia mafuta Sauli na pia
Daudi kuwa wafalme juu ya Israeli (1Samweli 10:1;
16:12-13; 2Samweli 12:7). Upako huu wa Mungu
uliwakilisha kuchaguliwa na kuitwa kwa mtu binafsi awe
mtumishi Wake aliyewekwa rasmi.
Tatu, upako huu mara fulani ulifuatana na uwezo
maalum wa ki-Mungu. Huu ulitoka kwa Mungu na kuhusiana
moja kwa moja na kukamilishwa kwa kazi ambayo Mungu
alikuwa amemwagizia yule aliyetiwa mafuta (taz. 1Samweli
16:1-13; 2Wafalme 2:9-15).
2. Asili la neno “masihi”
Neno hili limetoka moja kwa moja katika neno la
kimzizi masah likiwa katika Kiebrania masiah, na
kutafsiriwa masihi kwa maana ya “aliyetiwa mafuta”. Neno
hili limetumika mara 39 katika Agano la Kale kwa ajili ya
watu wengi mbalimbali. Matumizi yake ya wazi kabisa ni
MATENDO • 9
SEHEMU YA I
UTANGULIZI WA KI-HISTORIA NA KI-BIBLIAWA UPAKO
Upako
wa
Roho
Mtakatifu
Nakala 16 / Nambari 1
kwa Masihi mwenyewe – Yesu, Mwana wa Mungu (Isaya
9:7; 11:1-5; sura ya 53). Lakini neno hili limetumiwa pia kwa
ajili ya wafalme wa Israeli katika 1Samweli na 2Samweli na
Zaburi. Linatumiwa hasa kumaanisha uzao katika ukoo wa
kifalme wa Daudi (Zaburi 2:2; 18:50; 84:9; n.k.).
B. UPAKO KATIKA AGANO JIPYA
Maneno matatu tofauti ya Kiyunani hutumiwa katika
Agano Jipya kwa maana ya “upako”. Kila neno
linadhihirisha namna tofauti ya upako.
1. Aleipho (limetumiwa mara 8): kupaka na kusugua
mafuta mwilini (taz. Marko 6:13; Luka 7:38,46; Yakobo
5:14). Katika Yakobo 5:14, upako haukuhusu uponyaji wa
ugonjwa. Ila upako huu ulikuwa ishara ya uwepo wa Roho
Mtakatifu na kumweka wakfu mtu aliyekuwa mgonjwa ili
amwombe Mungu uponyaji katika imani.
Ifahamike kwamba si kosa kutafuta matibabu ya
hospitali au daktari. Mungu aliumba vitu vinavyotumiwa
kutengeneza madawa na amewapa madaktari hekima ya
kuyatumia ifaavyo. Lakini Wakristo wanapaswa kuishi kwa
imani katika maamuzi yote ya maisha yao. Tusione maombi
kama njia ya mwisho baada ya nyingine zote kushindikana.
Kulipo na ugonjwa au majeruhi, umwombe Mungu kwanza
kwa ajili ya uponyaji. Mungu akifanya mwujiza wa uponyaji,
usifu Jina Lake! Mungu akichagua kutumia madawa na
madaktari katika kuponya, usifu Jina Lake! Kusipokuwa na
uponyaji wowote, bado usifu Jina Lake – maana, uponyaji
wetu wa mwisho na nyumba yetu ya milele ni Kwake
ambapo tutamwona uso kwa uso (1Wathesalonike 4:16-18).
Mungu wetu wakati wote ni mwaminifu na mnyofu!
2. Chrio (limetumiwa mara 5): humaanisha wito au
utume maalum wa Mungu unaomtenga mtu (au watu) peke
yake atimize kazi fulani aliyopewa (taz. Luka 4:18; Matendo
10:38; 2Wakorintho 1:21; Waebrania 1:9).
3. Chrisma (limetumiwa mara 3): kupewa uweza na
Roho Mtakatifu kwa ajili ya kujua yaliyo kweli na haki;
uweza wa Roho Mtakatifu akishirikiana na Neno la Mungu
katika moyo wa mwamini.
Waraka wa kwanza wa Yohana 2:20 na 2:27 hutaja
huduma ya Roho Mtakatifu katika kufunulia ukweli moyo wa
mfuasi wa Kristo (taz. pia Yohana 14:16-17,26; 1Wakorintho
2:10-16; Waefeso 1:17-18).
Mtume Yohana alikuwa akiandika barua hii (1Yohana)
apinge uzushi wa kikundi cha watu waliojidai kuwa na
ufahamu maalum wa Mungu. Hao walimu wa uwongo
walikataa kwamba Mwana wa Mungu alikuwa amekuja
katika mwili (1Yohana 2:18-23). Walidai kwamba wao peke
yao ndio waliokuwa na ufahamu halisi wa Mungu na
kwamba iliwabidi wote wawafuate.
Lakini Yohana aliwatuliza moyo Wakristo kwamba wale
walikuwa wakifanya kazi chini ya mwongozo wa kishetani
wa roho wa Mpinga Kristo (ms. 18). Yohana anapinga
mafunzo haya ya uwongo kwa kuwakumbusha waamini
kwamba wao tayari wamempokea Roho Mtakatifu ambaye
“mafuta yake yana-wafundisha habari za mambo yote”
(ms. 27).
Yohana hapunguzi wala kuzuia huduma ya kufundisha (taz.
Warumi 12:7 na Waefeso 4:11); badala yake, Yohana anatilia
mkazo huduma ya Roho Mtakatifu, anayetuongoza katika
ufahamu wa Ukweli katika Neno la Mungu (Yohana 16:13).
Masihi – Mwenye Upako
Tumejifunza kwamba maana ya neno “Masihi” ni
“aliyepakwa mafuta” au “mwenye upako”. Injili za Agano
Jipya zinathibitisha kabisa kwamba Yesu wa Nazareti
alikuwa (na ndiye) Masihi PEKEE, Mwenye Upako PEKEE!
Yesu alikuwa (na ndiye) mwenye upako kwa ajili ya utume
au kusudi maalum.
Katika lugha ya asili ya Kiyunani ya Agano Jipya, Yesu
aitwa “Kristo” au “Yesu Kristo”. Lakini “Kristo” pia ni jina la
cheo linalomaanisha “mwenye upako”. Agano Jipya lote
linafunua wazi kwamba Yesu ndiye Mwenye Upako (Yohana
1:41; 4:25-26).
Wayahudi walikuwa wakimsubiri masihi (Kiebrania
“mwenye upako”), mfalme katika ukoo wa kifalme wa
Daudi, ambaye angerejesha taifa la Israeli katika utukufu
wake wa zamani kama wakati wa Sulemani. Kwa sababu ya
matazamio yao, Wayahudi wengi walimkataa Yesu.
Hakulingana na mawazo yao mapungufu na yasiyo sahihi
kuhusu Masihi aliyeahidiwa (Mathayo 11:1-19; Yohana
6:26-29).
Wayahudi hawakuona kwamba Mungu alikuwa na
mpango mkuu zaidi kabisa ulioenea mbali na taifa lao (Isaya
42:5-9; 49:5-6; Matendo 4:8-12; 13:44-49). Mungu aliwapa
wao (na sisi) lililo kuu kabisa kuliko mfalme wa muda wa
kidunia. Aliupatia ulimwengu Mfalme wa wafalme,
Mwokozi wa kweli wa wote, hata milele – Yesu, Masihi,
utukufu kwa jina Lake!
Muhtasari
Upako katika Agano la Kale ulikuwa tendo lenye maana
kuu kabisa. Upako wa vifaa, makuhani, manabii na wafalme
uliwaweka wakfu kwa ajili ya makusudi ya Mungu. Lakini
tuelewe kwamba upako huo wa Agano la Kale ulikuwa
mfano au fumbo wa yale ambayo Mungu angeyatimiza chini
ya utawala wa Agano Jipya.
Chini ya Agano Jipya, kuliingia njia mpya iliyo hai ya
uhusiano kati ya Mungu na binadamu. Njia hii ilionekana
kwanza katika kutumwa kwa Yesu (Yohana 7:28-29), Mwana
wa Mungu, Masihi, Mwenye Upako, ili atimize makusudi na
maagizo ya Mungu (Yohana 3:14-17). Yesu alikamilisha kazi
hii alipokufa Msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, na kwa njia
hiyo alifungua mlango wa wokovu kwa wote wamwaminio
(Warumi 10:9-13; Waefeso 2:1-10; Waebrania 7:11-25;
9:11-15).
Sehemu moja ya mpango wa Mungu Baba kwa ajili ya
wokovu wa binadamu ilikuwa kuwapatia msaada wa
ki-Mungu wale ambao wangemwamini Mwana Wake.
Waamini wangepata msaada na uwezo wote wahitajio ili
watimize mapenzi ya Mungu kwao.
Kwa hiyo, Yesu alipomaliza kazi Yake aliyopewa na
Mungu duniani (Yohana 17:4; 19:30), aliahidi kututumia
“Msaidizi” (Yohana 7:37-39; 15:26; 16:5-15). Huyu
Msaidizi (Mfariji) ni Roho Mtakatifu – Mungu Roho.
Yaliyoonekana katika fumbo au mfano katika Agano la
Kale katika kumimina au kupaka mafuta (upako) sasa
yalipata kuwa ya kweli halisi kwa waamini wa Yesu Kristo
katika Agano Jipya. Haya yalianza wakati Mungu Roho
alipomiminwa katika Siku ya Pentekoste (Yoeli 2:28-32;
Luka 24:29-32; Matendo 2:1-39).
10 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1
A. ASILI YA UPAKO
Maoni ya watu wengi yamechanganyikiwa kuhusu
upako, kwa sababu ya ukosefu wa mafunzo na masomo halisi
ya ki-Biblia kuhusu hoja hii. Katika sehemu hii, tutaainisha
upako unavyodhihirishwa kwetu katika Maandiko.
Baadaye katika sehemu hii, tutaainisha upako jinsi
ulivyo; lakini kwanza, tudhihirishe ule USIO upako.
1. Mambo Ambayo Upako Siyo
a. Upako SI nguvu isiyo na uhai, wala uwezo wa
kifumbo. Upako si kama umeme (nguvu isiyo na uhai), wala
aina fulani ya nguvu ya kishirikina au uchawi. Simoni
mchawi (Matendo 8:9-25) alikuwa na aina ya nguvu (ya
kishetani); lakini alitambua haraka kwamba nguvu ile
haikulingana kabisa na uwezo uliokuwemo ndani ya mitume.
Upako wa Mungu si wa kimaumbile, ni wa kiroho.
b. Upako, jinsi unavyoelezwa katika Maandiko, SI
miitikio ya kihisia tu, yanayoonesha ama nafsi yenye
nguvu kubwa ama mtindo fulani wa kuhubiri. Mara
nyingi Mungu anagusa hisia zetu tunapotembea katika uwezo
wa upako Wake. Lakini kuonesha hisia zenye nguvu si
kuthibitisha uwepo wa upako Wake Mungu. Watu wanaweza
kuonesha hisia zenye nguvu katika michezo ya kuigiza,
uimbaji au michezo. Lakini bila shaka si uthibitisho wa
kuwepo kwa upako wa Mungu!
Watu fulani wanafikiri kwamba mhubiri akipaza sauti au
kusisimka na kurukaruka, anao upako. Lakini upako wa
kweli kutoka kwa Mungu unaweza uonekane au usionekane
katika matendo ya kimwili.
Vile vile, mtu hawezi “kustahili” kuwepo kwa upako wa
Mungu kwa njia ya elimu, ujuzi au utaratibu. Vipawa au
talanta za asili zenye uwezo pia si alama ya upako wa
Mungu. Ingawa talanta zetu za asili yetu ya kibinadamu ni
vipawa kutoka kwa Mungu, hata mtu asiyeokolewa anaweza
kuwa navyo na kuvitumia. Tusichanganye kuwepo kwa
talanta na vipawa, na upako.
Ni kweli kwamba Mungu anaweza kupatia vipawa vyetu
uwezo wa upako Wake ili vifanye kazi katika eneo kubwa
zaidi kuliko tuliloweza kufikia kwa nguvu yetu, kama
alivyofanya kwa Sulemani (1Wafalme 4:29-34). Lakini
talanta na vipawa vyetu kamwe visichukue nafasi yetu ya
kumtegemea Mungu kwa ajili ya uweza Wake wa ki-Mungu.
Upako unaotoka kwa Mungu ni wa ki-Mungu, si wa
kimaumbile, nao hutokana na nguvu na uweza Wake!
c. Upako SI wokovu. Kila mtu aliyetubu dhambi zake
na kumjia Kristo kwa wokovu anaye Roho Mtakatifu!
Lakini hali hii ni tofauti na upako wa Roho Mtakatifu.
Tuangalie kazi za Roho Mtakatifu wakati mtu
anapookolewa:
• Mtu anaweza kuzaliwa mara ya pili kwa njia ya kazi na
uweza wa Roho Mtakatifu peke Yake (Yohana 3:3-8;
Warumi 8:9,16).
• Mtu anaungwa na Mwili wa Kristo uliopo mahali pote,
wakati wa kuokolewa kwa njia isiyo ya kimaumbile;
Mwili wa Kristo ukiwa watu wote wanaomwamini Yeye
kwa ajili ya wokovu (1Wakorintho 12:13).
MATENDO • 11
SEHEMU YA II
ASILI, KUSUDI NA
MATUMIZI YA UPAKO
Upako wa
Roho
Mtakatifu
Nakala 16 / Nambari 1
• Mtu “hutiwa muhuri” na Roho Mtakatifu wakati wa
kuokolewa (2Wakorintho 1:22; 5:5; Waefeso 1:13-14).
Neno la Kiyunani lililotafsiriwa “kutiwa muhuri” ni
arrabon, maana yake arabuni au dhamana. Lakini zaidi
ya kuainisha kwa juujuu hivi, kuna maana ya ndani.
Kwanza “kutiwa muhuri” ni kuwekewa alama ya kuwa
mali ya Mungu. Ni ishara iliyo hai kwamba Mungu
amepokea fidia kwa ajili yetu. Fidia hiyo ni dhabihu ya
damu ya Mwana wa Mungu kwa ajili ya dhambi zetu
(Waefeso 1:7). Pili, tunapomjia Kristo katika imani kwa
ajili ya wokovu (Warumi 10:9-10) tunapewa Roho
Mtakatifu kama “arabuni” au “fungu ya kwanza ya
malipo” ya uwekaji wa Mungu ndani yetu. Uwekaji huu
ni dhamana (au ahadi) kwamba tunaweza kuongezeka
kila siku katika uhai, furaha, baraka na uweza wa Roho
Mtakatifu mpaka siku ambapo Mungu atatupokea kabisa
Kwake kule mbinguni (Wafilipi 1:6; 2Petro 1:5-11)!
Kazi na huduma ya Roho Mtakatifu huanza ndani yetu na
kupitia kwetu wakati tunapookolewa. Yale tunayopokea
wakati huo ni hatua ya kwanza tu katika mfuatano wa
kupevuka kwetu. Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya waamini
wote ni kwamba wafikie kuwa wanafunzi waliopevuka kama
wana Wake wa kiume na kike. Ili tufikie hapo inatubidi tujitoe
kikamilifu katika kukua na kugeuzwa kwetu binafsi. Lazima
tujitoe kila siku kwa Roho Mtakatifu katika maisha yetu
anapotuhukumu, kutuadhibu, kutuhamasisha na kutuwezesha!
Mchungaji kwa Mchungaji: Wewe kama
mchungaji na kiongozi wa kanisa, umeitwa na Mungu
uwe mfano kwa wengine wa kundi lako wa kujitoa ili
uendelee kukua katika mambo ya Mungu.
Tunashawishika tufikiri kwamba, kama viongozi,
hatuna haja tena kuwekea kipaumbele kukua kwetu
binafsi katika Kristo. Lakini ukweli halisi ni kinyume
chake! (Taz. 1Petro 5:2-3.)
Kwa sababu sisi ni viongozi, tunapaswa tuwe
mifano hai zaidi wa maneno ya Yesu: “Mtu ye yote
akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike
msalaba wake kila siku, anifuate” (Luka 9:23). Kila
mwamini amepewa Roho Mtakatifu wakati wa
kuokolewa; tujinyenyekeze, basi, kwa kazi yake na
mwongozo Wake katika maisha yetu kila siku!
d. Upako SI sawasawa na Ubatizo wa Roho
Mtakatifu. Ubatizo huu ni tukio maalum, inayopatikana kwa
waamini wote wa Kristo (Mathayo 3:11). Ubatizo wa Roho
Mtakatifu pia si sawasawa na kuja kwa Roho Mtakatifu ili
akae ndani ya mwamini wakati wa kuokolewa kwake.
Karama ya Roho Mtakatifu ilitabiriwa na nabii Yoeli
zaidi ya miaka mia nane kabla ya karama hiyo kumiminwa
siku ya Pentekoste (taz. Yoeli 2:28-32 na Matendo 2:1-39).
Ubatizo wa Roho Mtakatifu umeandaliwa ili
kumwezesha kila mfuasi wa Kristo awe na ufanisi na uwezo
zaidi kwa ajili ya kazi ya Bwana! Ubatizo huu utamwongoza
mwamini wa Kristo katika:
• kushughulikia zaidi roho za watu;
• uwezo mkubwa zaidi katika sala na hamu kubwa
zaidi ya kuomba;
• upendo wa ndani zaidi kwa Kristo na Mwili Wake;
• kuandaliwa kwa ajili ya mapambano ya kiroho;
• ufahamu unaoongezeka wa Neno la Mungu.
Waamini wote wa Kristo hupokea karama ya moyoni ya
Roho Mtakatifu wakati wa kuokolewa (Yohana 3:5-6;
Warumi 8:15-16). Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni kwa ajili
ya kujazwa na kufurikiwa na Roho wa Mungu. Ubatizo huo
haukupatii wokovu zaidi wala upendo mwingi zaidi wa
Mungu. Lakini utakuandaa uweze kuwa na maisha ya ufanisi
na ushindi zaidi katika Kristo!
Kama umepokea Ubatizo wa Roho Mtakatifu,
ukumbuke kwamba si tukio la mara moja la kupata; ila zaidi
ni mwenendo wa maisha wa kudumisha. Tunapaswa
tuendelee kujazwa wakati wote! [Angalia Sehemu Ya III,
C.1, “Mjazwe!”, kwa ajili ya mafunzo zaidi kuhusu hoja hii.]
Mchungaji kwa Mchungaji: Tunapojifunza kuhusu
Roho Mtakatifu, ni lazima tutambue kuwepo kwa roho
nyingine katika dunia yetu. Kuna aina tatu za roho
zinazofanya kazi duniani siku hizi:
1) Mashetani
Wapo mapepo waovu (mashetani) leo hapa
duniani. Wameagizwa na Shetani (Ibilisi)
wawadanganye wanadamu wote (Ufunuo 12:7-9) na
kuwapofusha wasione ukweli kwamba Yesu ndiye nani
(2Wakorintho 4:4; 1Yohana 2:22; 4:1-3). Ufalme wao
wa kishetani hufanya kazi zaidi kwa njia ya dini za
uwongo. Wanatumia udanganyifu kama silaha yao
kubwa, wakishirikiana na Ibilisi ambaye ni “mwongo, na
baba wa huo” (Yohana 8:44).
Mapepo waovu huwatawala kwa nguvu watu wasio
waamini (2Wakorintho 4:3-4). Lakini pia wanajaribu
kuwalenga waamini wa kweli wa Kristo, ambao kwao
nuru tukufu ya Injili inahubiriwa (Waefeso 6:10-12;
2Wakorintho 10:3-5; 11:3). Ufalme wa kishetani, kama
dhambi, hauna mamlaka juu ya Wakristo – isipokuwa
Mkristo akichagua kwa hiari kushirikiana nao katika hila
zao au majaribu yao.
Shetani atatumia wanadamu kama vyombo vyake
(hata wengine wanaojidai kuwa ni Wakristo) akijaribu
kuwapotosha watu (Mathayo 24:24; 2Wakorintho
11:13-15; 2Petro sura ya 2). Mapepo waovu hata
wanaweza kusema nusu-ukweli mara nyingine
(Mathayo 4:1-11; Marko 5:1-8; Matendo 16:16-19), lakini
hawatamtukuza Mungu wala kufanya mapenzi Yake.
Roho hizi za kishetani hujua kwamba Mungu ni wa
kweli na halisi:
12 • MATENDO
Roho Mtakatifu
anahudumia ndani yetu
na kupitia kwetu.
Nakala 16 / Nambari 1
“Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja;
watenda vema. Mashetani nao waamini na
kutetemeka” (Yakobo 2:19). Lakini mashetani
hawatubu kamwe. Wanafanya kazi kwa bidii wapate
kudanganya wanadamu, kwa sababu wanajua kwamba
hukumu yao inawajia (Ufunuo 12:12).
2) Roho za kibinadamu
Kila mwanadamu ana roho tangu mama yake
alipotunga mimba. Binadamu ana sehemu muhimu
tatu: mwili, nafsi na roho (1Wathesalonike 5:23;
Waebrania 4:12). Lakini roho yetu ni mfu ndani yetu
mpaka inapohuishwa kwa imani katika Kristo (Waefeso
2:1-8).
Biblia inafundisha kwamba mwanadamu akisha
kufa kimwili, roho yake huondoka mwilini. Walio katika
Kristo wanakwenda kukaa pamoja na Bwana
(2Wakorintho 5:6,8). Wanaokufa pasipo Kristo
wanawekwa hadi siku ya hukumu (Waebrania 9:27;
Ufunuo 20:11-15). Roho za wanadamu waliokufa
haziruhusiwi kutembea duniani! Wala haziingii tena
katika mwanadamu mwingine, mnyama wala kiumbe
chochote. Kila mtu ana maisha MOJA tu, na baada ya
kufa hukumu (Waebrania 9:27).
Zipo dini nyingi zinazoabudu roho za aina
mbalimbali. Watu wengine huamini kwamba wanaweza
kuwasiliana na roho za mababu zao au mizimu
mingine. Lakini watu hao hawawasiliani na wanadamu
waliokufa; ukweli ni kwamba wanawasiliana na
mapepo wanaowaigiza waliokufa.
Usidanganywe na roho hizi za uwongo! Biblia
inatufundisha kwamba Shetani na mapepo yake
wanaweza kujifanya mifano ya “malaika wa nuru”
wakijaribu kuiga mambo ya ki-Mungu (2Wakorintho
11:14). Wakiweza kufanya hivyo, si vigumu kwao kuiga
sauti ya mtu aliyekufa na kujua historia yake. Usijaribu
kamwe kuwasiliana na watu waliokufa, wala kushiriki
katika aina yoyote ya ibada au sherehe inayojaribu
kuwaabudu au kuwaomba mababu au mizimu.
Ukifanya hivyo, unawakaribisha mapepo wa kishetani
kwako!
3) Roho Mtakatifu
Roho Mtakatifu ni Roho wa Mungu, naye ndiye
Roho pekee anayestahili kuitwa mtakatifu (Warumi
1:4). Roho Mtakatifu ni Mungu mkamilifu, kama
Baba ni Mungu na Yesu ni Mungu (Mathayo 28:19;
2Wakorintho 13:14).
Katika Maandiko, Roho Mtakatifu ana sifa zifuatazo:
• Anaitwa Mungu (Yohana 4:24; Matendo 5:3-4;
• 1Wakorintho 3:16; 2Wakorintho 3:17)
• Yeye ni wa milele (Waebrania 9:14)
• Yeye anajua mambo yote (Yohana 14:26;
1Wakorintho 2:10)
• Yeye yupo kila mahali (Zaburi 139:7)
• Yeye ana uweza wote (Luka 1:35; katika uumbaji,
Mwanzo 1:2)
• Anajua mambo yote kabla hayajatokea (Matendo
1:16; 11:27-28)
• Ana upendo (Warumi 15:30)
• Aliongoza kuandikwa kwa Biblia kwa pumzi ya
Mungu (2Petro 1:21; 2Timotheo 3:16)
• Yeye ni Mtendaji katika uongozi wa ki-Mungu (Marko
13:11; Warumi 8:14)
• Yeye ni Mtu, kama Yesu na Baba ni Watu (Yohana
14:16-17,26)
• Yeye anaweza kuhuzunishwa (Waefeso 4:30)
Masomo kamili kuhusu Roho Mtakatifu yana upana
mkubwa usioweza kufikiwa katika mafunzo haya.
Lakini Agano la Kale na Agano Jipya pia hufunua
kwamba Roho ni wa kweli naye ni Mungu; anaishi
pamoja na Baba na Mwana akiwa na usawa na umilele
pamoja nao; ndiye Nafsi ya tatu katika Utatu.
e. Upako SI sawasawa na utakaso. Tuainishe utakaso
na kuuchunguza kwa kifupi ili tupate kufahamu mfuatano
huu vizuri zaidi.
Kuainisha Utakaso
Utakaso una maana mbili muhimu. Maana ya kwanza ni
kuwekwa wakfu – kutengwa kwa mtu au kitu fulani kwa ajili
ya matumizi maalum matakatifu.
Tumejifunza kutoka Agano la Kale kwamba kuwekwa
wakfu kulihusiana na vitu vya kimwili kama vile: nyumba
(Walawi 27:14), shamba (Walawi 27:16), vyombo
vilivyotumiwa katika Hekalu (2Nyakati 29:18-19). Vitu hivi
vyote viliwekwa wakfu na kutengwa kwa ajili ya matumizi
maalum.
Watu pia walitengwa kwa ajili ya matumizi maalum: kila
mtoto wa kiume wa kwanza wa Waisraeli (Kutoka 13:2),
makuhani (2Nyakati 29:4-5,15), nabii Yeremia (Yeremia
1:5), Yesu Mwenyewe, kama Mwana wa Mungu asiye na
dhambi (Yohana 10:36; 17:19).
Maana ya pili ya utakaso ni kusafishwa – kuondolewa au
kutakaswa na uchafu wa kimaadili. Kwa mfano, Paulo
alipowaombea waamini kwa ajili ya maisha yao yote
(1Wathesalonike 5:23) au kusafishwa kwa dhamiri ya
mwamini (Waebrania 9:13-14), n.k.
MATENDO • 13
Utakaso: kutengwa kwa ajili
ya matumizi matakatifu
Nakala 16 / Nambari 1
Mchungaji kwa Mchungaji: Aina hizi mbili za
utakaso husaidia kudhihirisha tofauti ya maoni ya
Agano la Kale na ya Agano Jipya kuhusu utakaso.
Katika Agano la Kale, kitu cha kawaida
kilihesabiwa kuwa kitakatifu na chenye utakaso
kilipotengwa kwa ajili ya matumizi au utumishi wa
Mungu.
Katika Agano Jipya, kitu cha kawaida kilijazwa
Roho wa Mungu na kugeuzwa kiwe chombo kilichofaa
kwa matumizi au utumishi wa Bwana (2Timotheo
2:19-21).
Sisi kama viongozi katika Mwili wa Kristo, tumeitwa
katika mwito mtakatifu (2Timotheo 1:9). Mwito huo
unatutenga kwa ajili ya utumishi wa Kristo. Lakini
Mungu hajamaliza hapo. Anaanza kazi ya “kututakasa”
ndani yetu, akiendelea kutugeuza kwa Roho Wake na
Neno Lake. Tunaposhirikiana na Yeye katika kazi hii na
kutii Neno, Yeye anatugeuza tupate kuwa aina ya watu
ambao mawazo, maneno na matendo yao katika
maisha ya kila siku yanamfunua Yeye aliye Bwana
ndani yetu.
2. Pande Tatu Za Utakaso
a. Kuchaguliwa Na Kuwekwa Katika Utakaso – Kazi
Iliyotimilizwa. Alipokuwa hapa duniani, Yesu alikuwa
mkamilifu kabisa kimaadili naye hakuwa na dhambi yoyote.
Alitumwa hapa na Baba Yake atimilize kusudi la kujia
ulimwengu wetu ulioanguka akijitoa dhabihu kwa ajili ya adhabu
ya dhambi zetu. Katika Yeye, tena katika Yeye peke Yake,
tunaweza kupata msamaha, wokovu na ukombozi kwa Mungu.
Mtu anapofikia imani katika Kristo na kujisalimisha kwa
Ubwana wa Kristo, mtu huyu anaunganishwa kiufalme na
Mwili wa Kristo, yaani Kanisa (1Wakorintho 12:13). Neno la
Kiyunani lililotafsiriwa “kanisa” ni ekklesia, maana yake
“walioitwa nje”. Tukiainisha kanisa hivi tunaona jinsi kila
mwamini wa Kristo anapaswa aitwe nje au kutengwa kwa
ajili ya matumizi ya Mungu.
Aina hii ya utakaso – kutengwa kwa ajili ya matumizi
matakatifu – tunaweza kuita pia kuchaguliwa na kuwekwa
katika utakaso (taz. 1Wakorintho 1:30; 6:11; 2Wathesalonike
2:13). Huku kuchaguliwa na kuwekwa katika utakaso ni kazi
ambayo Mungu amekwisha timiliza na kumpatia kila mtu
binafsi wakati anapookolewa (Matendo 26:18; Warumi
15:16; 1Wakorintho 6:11).
Kristo alimwaga damu Yake Mwenyewe na kutoa uhai
Wake kwa ajili ya dhambi zetu. Kazi mojawapo
iliyotimilizwa ni utakaso wa wale wanaomwamini. “Katika
mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa
Yesu Kristo mara moja tu” (Waebrania 10:10); “Bali kwa
yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa
kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu
[utakaso], na ukombozi” (1Wakorintho 1:30).
Kule “kutakaswa” ni asili ya waamini wa Kanisa la awali
kuitwa “watakatifu” (1Wakorintho 1:2; Waefeso 1:1).
Utakaso huo unatolewa bure kwetu kwa sababu ya kazi
iliyotimilizwa na Kristo pale msalabani. Hatuwezi kamwe
kufanya matendo mema wala ya dini ya kutosha ili tuustahili.
Hatuwezi kamwe kuwa “wema kiasi cha kutosha” ili tustahili
kukubaliwa na Mungu au kupata wokovu kwa ustahili wetu
binafsi.
Baba yetu wa Mbinguni asiye na dhambi yoyote, aliye
mkamilifu kabisa kimaadili, anapotuangalia sisi, anatambua
kila aina ya kupungukiwa na kushindwa. Lakini pia anatuona
kupitia damu ya Yesu, Mwana Wake, ambayo imetufunika
(imetutakasa) kabisa. “Kufunikwa” huku kwa dhambi zetu ni
njia pekee inayotuwezesha tukubalike mbele za Mungu aliye
mtakatifu na mwenye haki (Waefeso 1:6-7). Hii kweli ni
Habari Njema!
Kwa njia ya damu ya milele ya Mwana-Kondoo Asiye na
dhambi, waamini wametakaswa (Waebrania 10:11-14;
13:12). Sadaka ya Kristo ya damu Yake iliyomwagika ni kazi
ya utakaso ya mara-moja-kwa-wakati-wote, (Waebrania
9:28; 10:12). Hatuhitaji “kazi ya pili ya neema” (kama
wengine wanavyofundisha) ili tukubaliwe na Mungu. Dakika
ile ile ambapo tunamwamini Kristo na dhabihu Yake kwa ajili
ya dhambi zetu (Warumi 10:9-10), Mungu anatuhesabia
utakatifu wa Kristo na kututangazia kuwa “watakatifu”
(1Wakorintho 1:30).
b. Utakaso Unaoendelea – Mfuatano wa Kimatendo.
Upande wa pili wa pande tatu za utakaso ni mfuatano
wa utakaso unaoendelea katika maisha yote ya mwamini.
Mara nyingi huitwa utakaso unaoendelea.
Tumekwisha jifunza kwamba utakaso wa kuchaguliwa
na kuwekwa ni tendo la kifalme la Mungu linalotupatia
utakatifu unaotokana na dhabihu ya Kristo peke yake.
Hatuwezi kuupata kwa bidii yoyote ya kibinadamu, kwa
sababu wanadamu wote wamepotea kabisa chini ya dhambi
(Warumi 3:9-26).
Lakini mtu akiisha kufikia imani katika Kristo kwa
wokovu, kazi kuu ya Mungu inayofuata ni mfuatano wa
“[ku]badilishwa tufanane na mfano uo huo [wa Kristo], toka
utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa
Bwana, aliye Roho” (2Wakorintho 3:18). Maana ni mapenzi
ya Mungu sisi “[tu]fananishwe na mfano wa Mwana wake,
ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu
wengi” (Warumi 8:29).
Mfuatano huu (au maendeleo) wa utakaso ni tofauti na
aina ile ya kuchaguliwa na kuwekwa. Utakaso wa
kuchaguliwa na kuwekwa ni tendo la kifalme la mara moja la
Mungu wakati tunapopokea kazi ya Kristo ya wokovu.
Lakini utakaso wa mfuatano unahusiana na maendeleo ya
mapenzi, hamu na bidii zetu kwa muda mrefu.
Tendo hili la kujitoa kwa ajili ya “kugeuzwa” ni
ushirikiano wa ki-Mungu na kibinadamu. Inawabidi waamini
washirikiane na Mungu kwenye kazi yake ya ki-Mungu ya
kuleta mageuzi katika maisha yao.
Biblia inafunua wazi kwamba inawabidi wafuasi wote
wa Kristo wakazane kabisa katika kufanana zaidi na Kristo,
wakiishi maisha yenye utakatifu na utakaso. “Basi, wapenzi
wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na
uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu
katika kumcha Mungu” (2Wakorintho 7:1).
Tumeambiwa: “Mvue kwa habari ya mwenendo wa
kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa
zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia
zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu
katika haki na utakatifu wa kweli” (Waefeso 4:22-24).
Tafadhali tumia muda sasa hivi kusoma mistari ifuatayo,
ambayo ni michache kati ya mingi iliyopo yenye
14 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1
kutuhamasisha kuhusu hoja hii: Warumi 6:11-13; 12:1-2;
13:14; 2Timotheo 2:20-21; 1Petro 1:13-19; 1Yohana 3:3.
Hoja hiyo ni muhimu sana katika imani yetu ya Kikristo.
Lakini pia ni eneo ambapo waamini wengi wanashindwa
kufikia hali ambayo Mungu amekusudia kwa ajili yao.
Wanaendelea kufungwa na hasira, dhambi, utumwa au hofu,
badala ya kumruhusu Mungu awaweke huru na mambo haya.
Ingawa wanajaribu kwa nguvu yao binafsi kujiweka huru na
tabia au matendo yasiyowafaa kama wacha Mungu,
hawafahamu kuwa wanahitaji msaada wa Mungu ili wapate
kuwa na uhuru kamili.
Ni wazi kufuatana na Maandiko kwamba haiwezekani
kuwa mtakatifu na safi kimaadili pasipo uweza wa Mungu
ukitusaidia (Yeremia 13:23; 17:9-10; Warumi 3:20,23; 7:18).
Ni kweli kwamba damu ya Kristo huweka msingi wa utakaso
wetu wa kwanza (Waebrania 10:29), lakini ni ushirikiano wa
Roho Mtakatifu na Neno la Mungu la milele (Waefeso 5:26)
vikifanya kazi pamoja, vinavyoendelea kutugeuza zaidi
katika mfano wa Kristo (Warumi 8:29-30; 2Wakorintho 3:18;
Wafilipi 1:6; 1Petro 5:10). Kazi hiyo ni ya maisha yote,
itaendelea mpaka tutakapoonana na Yeye “uso kwa uso”
(1Wakorintho 13:12; 1Yohana 3:2).
Mungu anataka kufanya kazi ya kufululiza ndani yetu ili
atutengeneze. Lakini ni lazima pia awe na ushirikiano wetu
na bidii yetu kamili kwa kusaidiwa na Roho Mtakatifu na
Neno la Mungu. Lazima tuchague kusikia na kutii, kusikiliza
na kuitikia maagizo ya Neno la Mungu na ya Roho
Mtakatifu.
Huo utakaso unaoendelea ni mageuzi ya muda wote wa
maisha yetu. Hatutakamilika wala kuwa huru kabisa na
dhambi katika maisha haya (1Yohana 1:8), lakini tunaweza
kuendelea kukua katika upevu wa kiroho, na inatubidi tukue
hivyo.
c. Utakaso Kamili Au Wa Mwisho. Ukamilifu wetu wa
kutokuwa na dhambi yoyote husubiri kurudi kwa Bwana
Yesu Kristo au dakika ile ambapo, katika kifo, tunaondoka
maisha haya na kwenda kwa Bwana. Ndipo tutawekwa huru
na mwili huu wa uharibifu na “kufumba na kufumbua, wakati
wa parapanda ya mwisho” (1Wakorintho 15:52)
tutabadilishwa tuwe viumbe visivyokufa wala kuwa na
uharibifu (1Wakorintho 15:45-47; taz. pia Wafilipi 3:20-21;
1Yohana 3:2).
Kristo alipokufa pale msalabani kwa ajili ya dhambi
zetu, tuliokolewa na adhabu ya dhambi. Tunavyokua katika
imani na utakatifu, tunawekwa huru zaidi na zaidi na nguvu
ya dhambi. Na wakati Kristo atakaporudi (au tunapokufa
katika Bwana) tutaokolewa na uwepo wa dhambi!
Utakaso si upako. Lakini utakaso (hasa utakaso
unaoendelea) ni muhimu sana kwa ajili ya upako. Kuishi
maisha matakatifu na yenye kujitoa huhusiana kabisa na
kufurika kwa upako katika maisha yetu na utumishi wetu.
[Hoja hii itazungumzwa zaidi katika Sehemu Ya III, A.
“Kuhifadhi Upako”.]
3. Njia ya Kukua
Wakristo wanapaswa wakue wakati wote. Biblia
inatuhamasisha: “Kueni katika neema, na katika kumjua
Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo” (2Petro 3:18; taz. pia
2Petro 1:5-11).
Utakaso unaoendelea ni mfuatano unaohitaji
ushirikiano kati ya Mungu na kila mtu binafsi (Wafilipi
2:12-13). Mungu anatenda kazi kwa ajili yetu, kwa sababu
hatuna budi tupokee msaada Wake ili tupate kufanana na
Kristo katika tabia zetu. Lakini nafasi yetu katika mfuatano
huu ni ipi?
Ni lazima:
a. Tumwamini Kristo. Pasipo imani, hatuwezi kupokea
karama ya wokovu, wala karama inayofuata ya Kristo ya
kuchaguliwa na kuwekwa katika utakaso. Tunapookolewa,
Kristo anakuwa utakaso wetu (1Wakorintho 1:30).
Tunapokea karama hii kutoka Kwake kwa kumwamini Yeye
(Matendo 26:18).
b. Tumtolee Mungu maisha yetu. Ndivyo tunavyoanza
maisha yetu kama Wakristo; ndivyo tunavyopaswa kuishi
siku kwa siku pia. Mfululizo wa kujitoa au kujisalimisha kwa
Mungu ni muhimu kabisa. Yeye ndiye anayejua yaliyo ya
lazima kwetu ili tufanane zaidi na Kristo. (Taz. Warumi
6:13,19-21; 12:1-2; 2Timotheo 2:21.) Kujisalimisha kwa
Mungu kila siku ni lazima pia ili imani yetu ikue na kuongeza
nguvu, tunapochagua kumtegemea na kumwamini Yeye
(Waebrania 11:6).
c. Tutii Neno la Mungu. Maandiko Matakatifu ni
kipimo chetu cha mwisho kwa ajili ya imani na matendo
yetu. “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake: Kwa kutii,
akilifuata neno lako” (Zaburi 119:9). Roho Mtakatifu
atatumia Neno la Mungu aseme nasi na kutengeneza tabia
zetu (Yohana 14:26). Neno la Mungu litatuandaa na
kutufanya zana zifaazo kwa ajili ya utukufu wa Mungu
(2Timotheo 3:16-17). Neno la Mungu litatusafisha (Waefeso
5:26). Biblia inafunua pia mawazo na makusudi yetu ya
ndani kabisa (Waebrania 4:12). Inatupasa tusome Biblia kila
siku; na halafu lazima tuitii (Yakobo 1:22). Mungu anatoa
yote yanayohitajika ili tuishi na kukua katika uchaji (2Petro
1:3-4). Lakini ni lazima sisi tushiriki na kutii kwa hiari yetu!
d. Tuweke ahadi yetu binafsi ya kufuata utakatifu.
“Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo
utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana
asipokuwa nao” (Waebrania 12:14; taz. pia Mathayo 5:8).
Petro anawahamasisha waamini wawe na kiasi na
kutumaini kwa utimilifu neema ya Mungu. Tunapaswa tumtii
Mungu na tusifanane na tamaa zilizotutawala zamani.
Matazamio haya ya ki-Mungu ya utakatifu wetu ni kwa
sababu Mungu ni mtakatifu katika asili Yake na mwenye haki
katika hukumu Zake zote (1Petro 1:13-21). Lengo la maisha
yetu na hatima yetu si kuishi katika furaha au starehe, bali ni
utakatifu.
Kutafuta mwenendo wa maisha ulio mtakatifu – katika
matendo, mawazo, mahusiano na maneno yetu – si hiari kwa
mfuasi wa Kristo. Tusiridhiane na lolote lisilokubaliana na
Mungu mtakatifu! Mfano na kielelezo kwetu si
wanavyofanya watu wengine (Wakristo ama sivyo), wala
maridhia ya mienendo tunayopata kushuhudia, hata katika
viongozi wengine. Mwongozo halisi wa maisha si utamaduni
au ukoo wetu wala jamaa yetu. Sisi kama raia wa Ufalme wa
Kristo (Wafilipi 3:17-20) tunawajibika kufuata kwanza na
hasa yale ambayo Mungu ametufunulia katika Neno Lake
kwa njia ya Roho Mtakatifu; ndiyo tunayopaswa kukazana
kuyatii (Luka 9:23-26)!
Kama tutakuwa na juhudi na uangalifu katika kuishi
Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO • 15
maisha yetu kufuatana na kipimo cha tabia ya Mungu na
Neno vilivyofunuliwa, tumehakikishiwa kukua katika
utakaso. Na tunapokua katika utakaso, tunapata kuwa
“chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho
Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema”
(2Timotheo 2:21).
B. KUSUDI LA UPAKO
Kwa sababu watu wengine wamechanganyikiwa kuhusu
upako, tulitumia nafasi katika sehemu iliyotangulia kuainisha
yale yasiyo upako. Sasa turejee kwa kifupi yale tuliyojifunza:
• Upako si nguvu ya kifumbo wala nguvu isiyo ya uhai.
• Upako si karama, kipawa, talanta, hisia wala nafsi
yenye kuvutia.
• Upako si wokovu.
• Upako si Ubatizo wa Roho Mtakatifu.
• Upako si kutakaswa kwa mwamini.
1. Maana ya Upako
Hivyo basi, upako ni nini?
Njia bora ya kuainisha upako ni hii:
Upako si tofauti na Roho Mtakatifu Mwenyewe katika
kuwepo Kwake, akileta pamoja naye uwezo, mamlaka na
karama vinavyohitajika kwa ajili ya kutimiza mapenzi ya
Mungu kwa muda au dakika fulani ya utumishi au agizo
fulani.
Ieleweke wazi kwamba Roho Mtakatifu anahusika
kimatendo katika mambo yote matano mengine
yaliyoorodheshwa hapo juu. Pasipo kuwepo na kutenda kwa
Mungu Roho, mambo hayo matano ya lazima katika maisha
ya kila mwamini yasingekuwepo.
Hata hivyo, sehemu hii ya kazi ya Roho Mtakatifu
inayoitwa upako ina kusudi maalum lisilo na kifani.
2. Uweza Wenye Kusudi
a. Uwezo wa Ki-Mungu. Kusudi la kimsingi la upako
wa Roho Mtakatifu ni kumpa mwamini uwezo usio wa
kimaumbile.
Mungu anampa mtu yeyote anayependa Yeye uwezo
huu, ili kumsaidia afanye yale yanayotakiwa na Mungu.
Huenda ni kwa ajili ya kusema au kuhubiri, kufanya kazi
fulani, kuimba au kutumia chombo cha muziki. Au pengine
ni kwa ajili ya kuwawekea wagonjwa mikono kwa uponyaji
au ishara na miujiza mingine ambayo hutendwa na Mungu.
Unamwezesha mtu pia asali na kuombea watu kwa ufanisi
zaidi.
Ni muhimu kuona pia kwamba Mungu anaweza kumpa
mtu fulani upako kwa ajili ya kuongoza au kuwa na ustadi
hata katika biashara au kazi ya mikono (taz. Kutoka 31:3).
Mungu anataka kuwapa watu Wake upako kwa ajili ya
nafasi za utumishi ndani na nje ya Kanisa Lake – lakini
kumbuka, ni kwa ajili ya makusudi YAKE na utukufu
WAKE, si yetu au wetu!
Kumbuka upako ni nini: Ni Mungu kwa Roho Wake
akipatia chombo cha kibinadamu kilichojitoa, uwezo,
mamlaka na karama vyovyote vinavyohitajika kwa ajili ya
kutimiza mapenzi ya Baba katika dakika fulani ya utumishi
au agizo fulani.
Ni muhimu kufahamu kwamba upako ni Roho
Mtakatifu Mwenyewe! Uweza wa Mungu haupo mbali na
Yeye Mwenyewe na kuwepo Kwake. Tunaposema kuwa mtu
fulani anao upako, maana yetu ni kwamba Roho Mtakatifu
Mwenyewe yumo ndani ya maisha yake kwa njia ya pekee ili
atimize mapenzi ya Mungu kupitia kwake.
b. Nani anaweza kupokea upako huu? Unaposoma
Agano la Kale, ni rahisi kutambua wakati ambapo Roho
Mtakatifu alimjia nabii, mwamuzi, mfalme, kuhani n.k.
Lakini mgawo wa Roho Mtakatifu ulikuwa tofauti katika
Agano la Kale na Agano Jipya. Mtume Yohana aliandika:
“Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale
wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho
alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa”
(Yohana 7:39).
Roho Mtakatifu, ambaye ni Mungu mkamilifu,
amekuwepo tangu milele yote. Alihusika katika uumbaji
(Mwanzo 1:2) na katika Agano la Kale lote. Lakini Mungu
Baba alikuwa hajapatia maumbile Yake Mungu Roho kwa
ukamilifu mpaka Mungu Mwana alipokuwa amefungua njia
ya wokovu katika kifo Chake kama dhabihu msalabani
(Yohana 14:16-17; 16:7).
Mchungaji kwa Mchungaji: Sisi kama Wakristo
wanaoamini Biblia, hatuabudu miungu mitatu. Bali
tunamwabudu Mungu Mmoja anayejifunua katika Nafsi
tatu. Katika Mungu, kuna “nafsi” tatu ambazo si miungu
mitatu wala sehemu tatu. Nafsi hizi tatu ni Mmoja, na
kila moja ni Mungu katika usawa na umilele. Akili zetu
zinapata shida kubwa kufahamu asili ya Mungu aliye
“tatu”-katika-mmoja. Lakini Maandiko yamefunua
ukweli huu juu Yake.
Kuna tofauti moja ya kimsingi kati ya mgawo wa Roho
Mtakatifu katika Agano la Kale na mgawo katika Agano
Jipya. Katika Agano la Kale, Roho Mtakatifu alimjia juu yake
mtu aliyechaguliwa kuwa chombo kwa muda. Roho
Mtakatifu alimwezesha mtu fulani binafsi (nabii, kuhani,
mwamuzi, n.k.) afanye mapenzi ya Mungu kwa dakika ile.
Ndipo Roho Mtakatifu alimwondokea mpaka dakika
nyingine ya kufanya kazi ya utumishi.
16 • MATENDO
Upako
unaweza
kuongeza
ufanisi wa vipawa,
kwa mfano
muziki.
Nakala 16 / Nambari 1
Lakini katika Agano Jipya, Roho Mtakatifu alitolewa ili
aingie na kukaa ndani ya mioyo ya wanadamu na kuishi
katika uhusiano unaoendelea pamoja nao. Tuangalie mifano
kadhaa ya upako wa Roho Mtakatifu katika Agano Jipya:
Yesu
Mtu wa kwanza katika Agano Jipya aliyepokea upako
wa Roho Mtakatifu ni – Yesu! Yesu alipokea upako uliomtilia
uweza wa Roho Mtakatifu wakati wa ubatizo Wake katika
maji (Mathayo 3:16). Baada ya kujaribiwa kwake Yesu
jangwani, tendo Lake la kwanza la huduma ya hadharani
lilikuwa kusoma Isaya 61:1-2 ndani ya sinagogi. Ndipo
alipotangaza kwamba maandiko haya ya ki-Masihi yalikuwa
yametimia (Luka 4:14-21).
Unaona kwamba upako wa Roho Mtakatifu uliotajwa
katika Isaya 61:1-2 ulikuwa kwa ajili ya kuwezesha mapenzi
ya Baba yatimizwe katika huduma ya miaka ya kwanza ya
Yesu.
Yesu alikuwa Mungu mkamilifu na mwanadamu
mkamilifu wakati alipokuwa katika mwili Wake hapa duniani
(Wafilipi 2:5-8). Lakini alihitaji uweza wa Roho Mtakatifu ili
atimize mapenzi ya Baba. Ikiwa Yesu, Mwana wa Mungu,
alimhitaji Roho Mtakatifu, je, haja yetu sisi ni zaidi kiasi
gani? (Taz. pia Matendo 10:38.)
Kanisa La Awali
Viongozi wa Kanisa la Awali
Siku ile ya Pentekoste (Matendo 1:12 – 2:4), viongozi
wa Kanisa la awali na wanafunzi wengine walikuwa wakisali
katika chumba kikubwa orofani. Waliokuwepo ni pamoja na
wanafunzi wa kwanza kumi na mmoja (Yuda akiwa ameisha
kufa), mtume mpya aliyechaguliwa kuchukua nafasi ya Yuda
kwa kupiga kura, na kundi la wanafunzi wengine (kama watu
120 hivi). Ghafla, Roho Mtakatifu aliyeahidiwa (Yoeli
2:28-32) alimiminwa juu yao (Matendo 2:2-4).
Mtume Paulo aliongoka na kumwamini Kristo baadaye.
Yeye pia alipokea Roho Mtakatifu akaanza kuhubiri Injili ya
Yesu Kristo kwa bidii kubwa (Matendo 9:1-22).
Wainjilisti kama Filipo walijazwa na Roho Mtakatifu na
pia kuongozwa na Yeye (Matendo 8:29). Waliopewa karama
ya kufundisha, kama Apolo, wasingaliweza kufundisha kwa
ujasiri pasipo upako wa Roho Mtakatifu (Matendo 18:24-28;
taz. pia 1Wakorintho 3:5-7). Walioitwa watumikie Mwili wa
Kristo uliokuwa ukikua haraka walijaa Roho, kwa mfano
Stefano (Matendo 6:1-10). Kuna mafungu mengine ya Agano
Jipya pia yanayohusu hoja hii (yaani Matendo 4:13,33;
11:27-28; 21:10-11).
Wanafunzi wa Kanisa la Awali
Waliojazwa katika chumba cha orofani Siku ya
Pentekoste walikuwa wa kwanza tu kati ya waamini wengi
zaidi waliojazwa na kupewa upako wa Roho Mtakatifu
(Matendo 4:31; 5:32; 13:52; n.k.).
Uwezo Kwa Ajili Ya Uinjilisti
Jinsi mwako wa Injili ulivyoenea, ndivyo miminiko
mkuu wa Roho Mtakatifu ulivyoongezeka pia. Haya
yalitimiza maneno ya Yesu mara kabla ya kupaa Kwake:
“Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho
Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika
Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata
mwisho wa nchi” (Matendo 1:8).
Yesu alipoorodhesha maeneo haya ya kijiografia hakuwa
akibuni kilugha. Kitabu cha Matendo kinafunua kutimizwa
kwa ahadi hii ya kumiminwa kwa Roho Mtakatifu juu ya
wale wote ambao wangemwamini, pamoja na kuanzishwa
kwa uinjilisti kwa dunia nzima.
Katika Yerusalemu… (ilitimizwa Siku ya Pentekoste –
Matendo sura ya 2). Ilionekana kama kundi hili ya waamini
Wayahudi wangehubiri kule Yerusalemu tu. Kufanya hivyo
kungaliweza kuzuia kusudi la Kristo na utume wa Injili
kutolewa kwa watu wote, nyakati zote, mahali pote.
Lakini waamini walianza kuteswa karibu mara baada ya
Injili kuanza kuhubiriwa. Mungu alitumia mateso yale
kulazimisha Kanisa la awali litawanywe mbali kuanzia
Yerusalemu, ili watimize mapenzi ya Baba ya kufikisha
ujumbe wa wokovu kwa kila mtu.
Ndipo katika Matendo sura ya 8 tunakutana na mtesi
mkubwa wa Kanisa – Sauli. Mashambulio haya yangeonekana
kuwa habari mbaya, kabla hatujasoma katika Maandiko:
“Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko
wakilihubiri neno [Injili]” (Matendo 8:4). Maeneo waliyofikia
ni pamoja na Uyahudi na Samaria (Matendo 8:1-25).
Kusonga Mbele Na Mbali Kwa Injili
Angalia kwamba Roho Mtakatifu alikuwa akimiminwa
juu ya wale waliopokea Injili (Matendo 8:16-17). Kulikuwa
na ishara na miujiza pia iliyofuatana na kuhubiriwa kwa Injili
(Matendo 8:6,13).
Lakini kazi kubwa zaidi ilikuwa ifunuliwe katika Kanisa
la awali. Mungu alitaka Injili ihubiriwe pote duniani. Yesu
aliwaamuru waamini “Enendeni ulimwenguni mwote,
mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe” (Marko 16:15). Neno
linalofanana na hili limeandikwa katika Matendo 1:8: “hata
mwisho wa nchi”.
Kusonga mbele na nje zaidi kulianza wakati Filipo
alipokutana na towashi wa Kushi, ambaye aliongoka
mapema akawa Mkristo (Matendo 8:26-40). Mtu huyu wa
MATENDO • 17
Mtu
mmoja
mmoja,
kujazwa na
kupakwa
mafuta...
Nakala 16 / Nambari 1
Kushi katika mapokeo ya Kanisa anasifiwa kuwa mtu wa
kwanza kuleta Injili barani Afrika!
Mapema baadaye, Sauli alibadilishwa kabisa kwa ajili ya
kukutana na Yesu (Matendo 9:1-19), naye aliitwa awe mtume
kwa Mataifa (Matendo 9:15). Lakini lengo la sehemu kubwa
ya mahubiri ya Injili bado lilikuwa Wayahudi – mpaka
Mungu alipofanya badiliko kubwa kabisa!
Tunasoma katika Matendo kuhusu Kornelio, Mrumi
(Matendo 10:1-48). Petro alitumwa kwa Kornelio aanze
kuwashirikisha Injili watu wa Mataifa. Tendo hili lilikuwa
gumu kwa Petro kufanya kama Myahudi (Matendo 10:9-16).
Lakini wakati Petro alipokuwa akihubiri, Roho
Mtakatifu aliwashukia Kornelio na watu wote wa nyumba
yake – katikati ya mahubiri ya Petro (Matendo 10:44)! Hata
hivyo, ndugu wa Kiyahudi waliokuwepo walionea ugumu
ukweli kwamba watu wa Mataifa walikuwa wakipewa Injili
na Roho Mtakatifu (Matendo 10:45-48).
Mwisho, kulikuwa na mkutano mkuu muhimu wa
mitume pale Yerusalemu, ambapo Petro aliitwa atoe
ushuhuda wake (Matendo 11:1-15). Hatimaye waliweza
kufahamu na kukubali yale ambayo Yesu alikuwa
amewaambia wazi: Injili ihubiriwe kwa kila mtu – “hata
mwisho wa nchi” (Matendo 1:8).
Mpango Wa Mungu Umefunuliwa
Ni muhimu kabisa kutambua jambo fulani kuhusu Kitabu
cha Matendo. Injili ya Yesu Kristo SI dini mpya wala
mafundisho mapya ya dini ya Kiyahudi. Mambo yote
yaliyokuwa yametokea katika uhusiano uliopo kati ya binadamu
na Mungu tangu Bustani ya Edeni – historia nzima ya Agano la
Kale – yalikuwa yakiendea kilele chake katika wakati huu.
Mungu alikuwa na mkakati Wake ulioanza baada ya
binadamu kuchagua dhambi (Mwanzo 3:15). Mpango huu
ulikuwa kumwokoa katika adhabu ya kifo kwa ajili ya
dhambi, kwa neema kupitia imani (si kwa matendo) katika
Yesu Kristo. Mpango huo uliwezekana tu kutokana na
dhabihu ya kifo iliyofuatwa na ufufuo wa Yesu. Tunasoma
kuhusu mkakati huo wa Mungu katika Injili (Mathayo,
Marko, Luka na Yohana).
Lakini kusudi la Mungu lilikuwa zaidi ya imani mpya na
uhusiano na Yeye uliorudishwa. Mungu alitaka (na bado
anataka) kuishi ndani yetu, kutupa uhakika na uwezo
tunaohitaji ili tuishi katika ushindi na kutimiza mapenzi Yake
katika maisha yetu hapa.
Kwa hiyo, katika hekima Yake na upendo Wake visivyo na
mwisho, Mungu alimimina Roho Mtakatifu, ambaye angeishi
ndani ya kila mwamini (Yoeli 2:28-29). Kristo hakuja ili alete
dini au theolojia mpya. Bali alikuja ili atimize yote ambayo
Mungu alikuwa ameahidi kwa ajili ya wokovu wa binadamu!
Kwa kweli, dhabihu ya Kristo inatuwezesha turudishwe
katika ushirikiano wa karibu sana na Mungu. Lakini Mungu
anakusudia pia kwamba uweza wa Mungu Mwenyezi ukae
ndani yetu katika Roho Mtakatifu. Ulimwengu hauwezi
kupuuza wala kugeuzia maana uweza huu. Watu wanaweza
kudhihaki, kukemea au kuhukumu, kama walivyofanya Siku
ile ya Pentekoste (Matendo 2:5-13), lakini hawawezi kuzuia
kazi na uweza wa Roho Mtakatifu kupitia kwa maisha ya
mwamini yaliyotolewa Kwake!
Tunayoona katika Kitabu cha Matendo kuhusu ishara,
maajabu, miujiza, wokovu, uponyaji, n.k. yanawezekana
nayo yanahusiana na sisi leo, kama yalivyokuwa kwa Kanisa
la awali (Yoeli sura ya 2; Matendo 2:33,38-39). Tunahitaji
uwepo na uweza wa Roho Mtakatifu leo kama miaka 2000
iliyopita! Tumshukuru Mungu kwamba “Yesu Kristo [na
Roho Mtakatifu] ni yeye yule, jana na leo na hata milele”
(Waebrania 13:8).
Waamini Wote Wa Kristo Kwa Nyakati Zote
Petro, akiongozwa na Roho Mtakatifu, alitangaza
kwamba karama iliyoahidiwa ya Roho Mtakatifu akaaye
ndani yetu ni “kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa
watu wote walio mbali, watakaoitwa na Bwana Mungu wetu
wamjie” (taz. Matendo 2:33,38-39).
Walioainishwa kuwa “watu wote walio mbali” kwa
hakika ni pamoja na vizazi (vya Wayahudi) vilivyozaliwa na
vitakavyozaliwa, lakini pia makabila ya Mataifa na kila
kabila, lugha na ukoo duniani (Waefeso 2:11-19; Wagalatia
3:28; Wakolosai 3:11).
18 • MATENDO
Kila kabila... ...kila kizazi
Nakala 16 / Nambari 1
Uhusiano Wa Maisha Yote
Karama ya uwepo wa Roho Mtakatifu katika upako
huingia ndani ya moyo wa kila mfuasi wa Kristo. Huu ni
upako wa kawaida ambao kila mwamini anapokea wakati wa
kuokolewa.
Mtume Yohana anatupa maoni ya ndani kuhusu upako
huu wa kawaida katika barua yake ya kwanza. Yohana
aliwakumbusha wafuasi wa awali wa Kristo jambo muhimu:
“Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi
mnajua yote” (1Yohana 2:20).
Kufuatana na sarufi ya lugha ya Kiyunani ya asili katika
mstari huu, ni wazi kwamba Yohana hakumaanisha ibada ya
kidini ambapo walipakwa mafuta au kitu kingine. Bali upako
huu ulitoka kwa “Yeye aliye Mtakatifu”, ambaye ni Yesu
Kristo, Mwana wa Mungu (Yohana 6:69; Matendo 3:14; 4:27).
Kwa maneno mengine, “YULE Aliyepakwa Mafuta”
(Yesu Kristo) anawapa wafuasi Wake karama kutoka Kwake;
karama hii ni Roho Mtakatifu, aishi ndani yetu na kukaa
pamoja nasi (Mathayo 3:11; Matendo 1:5; Yohana
14:16-17,26; 16:7). Upako huo ni kwa ajili ya kila mwamini
anayemtegemea Kristo kwa ajili ya wokovu kwa neema
katika imani.
Ndipo Yohana, kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu,
anaendelea: “Nanyi, mafuta [ya kiroho, si ya kimwili] yale
mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya
mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake
yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli
wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani
yake” (1Yohana 2:27).
Upako huu si wa mara moja tu; unatakiwa uwe uhusiano
na Roho Mtakatifu wa maisha yote unaoendelea kukua. Ni
Roho Mtakatifu anayetutia kwenye kweli yote, kutufundisha
mambo yote na kutukumbusha yale ambayo Yesu alifundisha
(Yohana 14:26). Roho Mtakatifu anatusaidia tufahamu
ukweli na kumtukuza Yesu (Yohana 16:13-14).
Ni wazi kwamba Yohana hasemi kwamba huduma za
kufundisha hazihitajiki (Mungu anatupa walimu – tazama
Warumi 12:7; Waefeso 4:11). Lakini hapa Yohana
anamaanisha mafunuo na ufahamu ambavyo Roho Mtakatifu
atampatia mtu binafsi anapomwitikia Yeye katika maisha
yake (1Wakorintho 2:10-16; Waefeso 1:17-18).
Kwa hiyo tunaona kutokana na Neno la Mungu kwamba
upo upako ambao kila mfuasi wa Kristo anaupokea wakati
anapookolewa.
Mchungaji kwa Mchungaji: Yale ambayo Roho
Mtakatifu anatilia mwangaza au anayofunua kuhusu
ukweli yatakubaliana wakati wote na yale ambayo
amekwisha funua katika Neno la Mungu lililoandikwa
(Yohana 16:13-14).
C. KAZI YA UPAKO
Tunapojifunza kuhusu kazi na hamasa ya Roho
Mtakatifu inatubidi tukiri kuwepo kwa siri za kifumbo
zisizoeleweka. Kuna sehemu ya ukuu wa Mungu katika
upako ambayo hatuwezi kuielewa (Yohana 3:8). Itikio letu
pekee kwa ukuu wa Mungu lazima liwe kujitolea kwa wazi
na ukamilifu kwa Ubwana Wake na mapenzi Yake.
Katika hekima Yake Mungu amependa kuacha sehemu
isiyoeleweka katika njia Zake, ikitubidi tuishi kwa imani
(2Wakorintho 5:7; Waebrania 11:6). Kuna mengi katika
maisha haya ambayo tunayaona na kuyafahamu “kwa
sehemu” (1Wakorintho 13:12). Mwelekeo wetu kwa Bwana
lazima sikuzote uwe wa kuamini, kutii na kunyenyekea Neno
Lake zima.
Kanuni Za Kimatendo Za Upako
Tukiendelea na mafunzo haya, turejee tena kuainishwa
kwa upako:
Upako ni Roho Mtakatifu Mwenyewe katika kuwepo
Kwake, akileta pamoja naye uwezo, mamlaka na karama
vinavyohitajika kwa ajili ya kutimiza mapenzi ya Mungu kwa
muda au dakika fulani ya utumishi au agizo fulani.
Tukiwa tumeyafahamu haya kikamilifu, tuangalie
kanuni kadhaa kuhusu jinsi upako wa Roho Mtakatifu
unavyotenda kazi.
1. Upako unahusiana moja kwa moja na wito wa mtu
binafsi kutimiza kazi ya huduma aliyopewa na Mungu.
Kwa maneno mengine, Mungu anapompa mtu fulani
kazi au wito wa kihuduma, Yeye anampatia pia mahitaji yote
ya uwezo, mamlaka, vipawa, mafunuo, utambuzi, n.k.
yanayotakiwa kwa ajili ya kutimiza kazi ile. Haleluya!
Mungu anapokuamuru au kukuongoza ufanye mapenzi
Yake, yote unayohitaji ili uweze kutimiza mapenzi Yake kwa
ufanisi yamepatikana kwa uweza na upako wa Roho
Mtakatifu. Yale ambayo Mungu anamwamuru mtu ayatende,
anampatia uwezo wa kuyatenda!
Bila shaka, sikuzote kuna kusoma, kujifunza na
kubadilishwa kibinafsi kunavyohitaji kufanyika njiani.
Tunapokazana - hali tunakua katika uwezo wetu, vipawa
vyetu na ujuzi wetu katika Neno la Mungu - ndipo Mungu
atatupatia hata zaidi.
Kanuni hii ya kuwa waaminifu kwa yale tuliyo nayo na
Mungu kutupatia zaidi (Luka 16:10a; 19:17) ni kanuni ya
lazima kwa ajili ya kukua katika upako wa Mungu.
Kutenda Katika Upako
Mungu anataka kutupatia upako ili tutimize mapenzi
Yake na wito Wake. Tunasoma kuhusu kanuni inayofanana
katika maelezo ya Paulo kuhusu imani.
Warumi 12:3: “kama Mungu alivyomgawia kila mtu
kiasi cha imani.” Kiasi hiki cha imani (kama ilivyo kwa
upako) ni uweza wa Mungu unaolingana na kipawa
alichotupatia.
“Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri
ya neema tuliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya
imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye
kufundisha, katika kufundisha kwake” (Warumi 12:6-7).
Paulo anatamka kanuni hiyo hiyo kwa njia tofauti kidogo
katika barua yake kwa Waefeso: “Lakini kila mmoja wetu
alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake
Kristo” (Waefeso 4:7). Kwa maneno mengine, kipawa hiki
kilichopimwa cha uweza wa ki-Mungu kinahusiana moja
kwa moja na kule kuweza kutenda katika kipawa ambacho
Mungu amempatia mtu fulani binafsi kwa ajili ya kutoa
huduma.
Mchungaji kwa Mchungaji: Mstari wa Waefeso
4:7 unahusiana moja kwa moja na vipawa vya kiroho
vinavyotajwa chini katika Waefeso 4:11. Mstari huu
Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO • 19
(4:7) HAUHUSU kipimo cha neema kwa ajili ya
wokovu jinsi wengine wanavyofundisha kwa makosa.
Neema ya Mungu kwa ajili ya wokovu hutolewa
sawasawa kwa watu WOTE, kwa sababu Yeye anataka
mtu yeyote asipotee, bali wote waokolewe (Matendo
2:21; 17:30-31; Warumi 3:22-23; 11:32; 1Timotheo 2:4;
4:10; Tito 2:11; 2Petro 3:9). Mungu anataka watu wote
wapokee karama Yake ya wokovu inayotolewa kwa
imani katika Kristo tu (Waefeso 2:8). Inasikitisha hata
hivyo kwamba wengi wamekataa na wataendelea
kukataa karama hii - na lililo baya zaidi, mamilioni ya
watu leo hawajasikia kamwe ujumbe wa Injili wa
wokovu kwa njia ya Yesu Kristo.
Mchungaji kwa Mchungaji: Ingawa huu si wakati
wa kujifunza kwa ukamilifu kuhusu vipawa vya kiroho,
nikupatie kanuni moja muhimu kuhusu vipawa vya
kiroho.
Vipawa vyote vya kiroho - kama ni vipawa vya
mafunuo (1Wakorintho 12:1-11); vipawa vya
madhumuni (Warumi 12:3-8) au vipawa vya huduma
(Waefeso 4:11) - hutolewa kwa uchaguzi wa Mungu.
Si juu yetu kuchagua au kudai kipawa tunachotaka au
ambacho tunaona kinahitajika zaidi hasa. Mungu
anatoa vipawa Vyake kufuatana na ujuzi Wake usio na
mipaka na utakatifu Wake ulio kamilifu kabisa (taz.
1Wakorintho 12:11).
Ingawa kila mwamini ana nafasi ya kihuduma
katika mwili wa Kristo, na katika dunia ambamo
tunaishi, kuna tofauti kubwa za wito na vipawa. Katika
kila moja, Mungu anatoa uweza, imani, neema na
upako vinavyohitajika kwa ajili ya kutimiza mapenzi
Yake na kusudi Lake.
Ingawa inatubidi tusijaribu kamwe kutawala au
kufanyiza upako (Roho Mtakatifu) tunaweza kukua
katika upako. Tunapokuwa waaminifu kwa yale
ambayo Mungu ametupatia, anaachia zaidi (Mathayo
25:21). Tunaweza pia kujifunza kutenda kwa ufanisi
zaidi katika huduma, na kufuatana na mapenzi ya
Mungu kwa ukaribu zaidi [Haya yanajadiliwa zaidi
katika Sehemu Ya III, B, “Kukua katika Upako”.]
“Kuhamisha” Upako
Mafunzo fulani hudai kwamba mtu aliyepewa upako na
kuwa na uwezo katika huduma anaweza kumwekea mikono
mtu mwingine na kumpatia “sehemu ya upako wake” - hata
sehemu maradufu! Tendo hili limeitwa “kuhamisha upako”
nalo linahusiana kwa mbali na matukio katika Maandiko
kuhusu Eliya na mfuasi wake Elisha (taz. 1Wafalme
19:16,19; 2Wafalme 2:1-13).
Lakini maandiko yenyewe hayathibitishi mafunzo haya.
Eliya alimtupia Elisha vazi lake (joho) (1Wafalme 19:19).
Lakini tendo hili lilikuwa alama ya uthibitisho tu la yale
ambayo Bwana alikuwa amekwisha tamka kuhusu wito wa
Mungu kwa Elisha kuwa mrithi wa Eliya (1Wafalme 19:16).
Katika tendo hili, Eliya hakumwita Elisha, wala hakuweza
kumpa upako wa kuthibitisha wito wake. Ilikuwa kazi ya
Mungu. Eliya alitii Neno la Mungu tu, na kuwasilisha yale
ambayo Mungu alikuwa amemwagiza amwambie Elisha
(1Wafalme 19:19).
Elisha alitambua wazi kwamba yeye hakuwa na uwezo
wa kuendeleza huduma ya kinabii ya Eliya kama Mungu
alivyokuwa amemwita yeye (Eliya). Elisha alijua kwamba
alihitaji uwezo wa Mungu (upako), unaotajwa katika
Maandiko kama roho ya Eliya (2Wafalme 2:9,15). Kwa hiyo
Elisha alimwomba Eliya “sehemu maradufu” ya roho yake
(2Wafalme 2:10).
Kwa sababu Eliya alikuwa nabii aliyepakwa mafuta na
Mungu, itiko yake kwa ombi la Elisha ili apate maradufu
ilikuwa maneno ya unabii tu: “Umeomba neno gumu; lakini,
ukiniona nitakapoondolewa kwako, utalipata; la hukuniona,
hulipati” (2Wafalme 2:10).
Tunaposoma sehemu hii ya Maandiko ni wazi kwamba
Eliya alijua kwamba hakuweza kumpa Elisha lolote la
kiroho. Aliweza kukiri wito wa Mungu kwa Elisha, lakini
hakuweza kumtia mafuta (upako) kwa ajili ya kuthibitisha
wito huu.
Ni wazi kwamba Mungu, katika ukuu Wake, alimruhusu
Elisha amwone Eliya akinyakuliwa kwenda mbinguni. Kwa
hiyo Elisha aliokota vazi la Eliya kufuatana na mapenzi ya
Mungu, kama ilivyotabiriwa. Kutoka wakati huu, upako wa
Mungu ulionekana kwa wazi katika huduma ya Elisha
(2Wafalme 2:15).
Mtoaji wa wito, vipawa na upako ni Mungu Mwenyewe,
kwa sababu Mungu peke Yake anaweza kutoa Roho
Mtakatifu! Sisi hatuwezi kumtawala Mungu wala Roho Wake;
hatuwezi kuamua nani atapewa upako, au kiasi cha upako
atakachopokea. Wala hatutawali vipawa na wito kutoka kwa
Mungu. Kama Mungu ametupa upako kwa ajili ya huduma,
hatuwezi kuamua kumpatia mtu mwingine upako huo.
Mungu Anaita - Sisi Tunathibitisha
Hata Musa, aliyekuwa mmojawapo wa watumishi
wakuu wa Mungu, hakuweza kuwapa wengine upako ambao
Mungu alikuwa amempa yeye. Lakini, Bwana Mwenyewe
alitwaa sehemu katika upako aliokuwa amempa Musa, naye
Bwana aliwawekea wazee (Hesabu 11:16-17).
Musa aliamriwa na Mungu ampe Yoshua sehemu ya
mamlaka yake (Hesabu 27:20) na kumpa mausia (Hesabu
27:23). Lakini haya yalitendeka baada ya Mungu kumteua
Yoshua kuwa mrithi wa Musa (27:18). Pia, Yoshua alikuwepo
wakati Bwana alipowapa wazee upako (11:16-17,28), ndiyo
sababu Yoshua anaelezwa kuwa “mtu mwenye roho ndani
yake” kama kiongozi kati ya Waisraeli (27:18).
Bwana ndiye aliyemwita Yoshua na kumpa upako. Musa
alithibitisha wito wa Yoshua, na kumpa mausia ya kuendelea
baada ya kuondoka kwake.
Ni Roho Mtakatifu aliyewapa Eliya na baadaye Elisha
kipawa cha unabii na upako wake, pamoja na ishara na
miujiza (taz. pia Hesabu 11:25-29; 1Samweli 10:6,10;
1Wafalme 18:46).
Mchungaji kwa Mchungaji: Si kosa kutaka kutoka
kwa Mungu “sehemu maradufu” ya Roho Wake. Wala si
kosa kuomba kipawa fulani maalum ili tufanye huduma.
Tunapaswa tuombe; halafu inatubidi tumtegemee
Mungu kwa yale atakayotupatia, na lini atakapotupatia.
Lakini tazama pia kwamba Elisha alikuwa mtiifu
katika kutimiza yote ambayo Mungu alikuwa amemwita
ayatende - katika kuitikia wito wa awali, na pia katika
kujiandaa kwa ajili ya kupokea upako wa Mungu
(1Wafalme 19:20-21; 2Wafalme 2:1-11). Wito wa
Mungu na upako Wake havitatimizwa moja kwa moja
20 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1
katika maisha yetu. Bali utiifu na unyenyekevu wetu, na
kushiriki kwetu, huhitajika katika kila hatua ya njia -
wakati wa maandalizi, na utendaji, wa kazi ya huduma
tuliyopewa.
Mgawanyo
Wazo la mtu mmoja “kumhamishia” mwingine upako
wake si sahihi. Lakini Maandiko hutupatia mifano mingi ya
tendo linaloitwa mgawanyo. Hufuatana hasa na uwekaji wa
mikono (Waebrania 6:2) na maombi, kwa mwongozo wa
Roho Mtakatifu. (Taz. Matendo 13:1-3; 1Timotheo 4:14;
2Timotheo 1:6.)
Ninafahamu habari za wanaume na wanawake wa
Mungu wenye uwezo ambao huwaombea wengine wapokee
mgawanyo wa Roho Mtakatifu. Tumekwisha jifunza
kwamba hao hawawezi kumpatia mtu mwingine kipawa chao
wala upako wao. Lakini inaonekana kwamba sehemu fulani
ya yale ambayo Mungu anatenda kwa Roho Wake kwa njia
ya huduma fulani, au kwa msimu maalum ambapo Mungu
anatenda kwa njia thabiti na ya kifalme, inaweza kuamshwa
ndani ya wengine, au kugawanywa kwao. Mara kwa mara,
watu walioombewa katika mkutano maalum huonekana
wakitenda katika mamlaka na uweza wa Roho Mtakatifu vya
juu zaidi baada ya kuombewa.
Mimi binafsi mara kadhaa nimepokea mgawanyo wa
Roho Mtakatifu ulio na nguvu kubwa. Matukio haya
yalibadilisha maisha yangu binafsi pamoja na mwelekeo
wangu katika huduma baada ya kuombewa. Lakini hii ni kazi
ya kifalme ya Roho Mtakatifu akileta mgawanyo mpya wa
upako katika maisha yangu, si matendo ya wanadamu.
Mgawanyo Unaothibitisha
Mfano wa ki-Biblia ulio wazi hasa wa aina hii ya
mgawanyo huonekana katika kukua kwa huduma ya
Timotheo.
Paulo anamkumbusha Timotheo kuhusu tukio fulani
mapema katika huduma yake ambapo Paulo na wazee wa
makanisa ya Ikonio na Listra walimwekea Timotheo mikono
yao na kumwombea: “Usiache kuitumia karama ile iliyomo
ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono
ya wazee” (1Timotheo 4:14).
Tukio hilo hilo limetajwa tena katika barua ya Paulo ya
pili kwa Timotheo: “Kwa sababu hiyo nakukumbusha,
uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa
kuwekewa mikono yangu. Maana Mungu hakutupa roho ya
woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi”
(2Timotheo 1:6-7; taz. pia 1Timotheo 1:18).
Neno la asili lililotafsiriwa ‘karama’ katika mistari hii ni
charisma. Neno hili linaashiria kwamba mafunuo ya Roho
Mtakatifu yalitolewa kwa Timotheo wakati Paulo na wale
wazee walipomwombea.
Paulo hakuwa chanzo cha karama ya Timotheo wala cha
wito wake. Ila, wakati Paulo na wale wazee walipomwekea
Timotheo mikono na kumwombea, Roho Mtakatifu alifunua
mapenzi ya Mungu kwa Timotheo na kutamka kiunabii
kupitia kwao katika kuthibitisha wito wa Mungu na mapenzi
Yake kwa ajili ya maisha ya Timotheo. Walipomsimika
Timotheo katika utume wa Bwana, Roho Mtakatifu ndiye
aliyempa Timotheo upako wa kutimiza wito wake kutoka
kwa Mungu.
Mchungaji kwa Mchungaji: Ni kwa njia ya
matukio haya ya maombi na kuwekewa mikono
kwamba Roho Mtakatifu mara nyingi atafunua kiasi
fulani cha mapenzi na makusudi ya Mungu. Mapenzi
Yake yanaweza kufunuliwa kama picha akilini, neno la
kinabii, andiko linalothibitisha, au maono ya yale
ambayo Roho Mtakatifu yanamtakia mtu fulani au hali
yake.
Katika hali hii, inatubidi tumsubiri Bwana kwa
utulivu na kusikiliza kwa ajili ya yule ambaye
unamwombea. Lakini kama hatujasikia neno rasmi
kutoka kwa Bwana, inatupasa tusitamke.
Thamani ya nafasi yetu kama wachungaji
inatokana na kuwa waaminifu na watiifu kwa Mungu na
Neno Lake. Huenda tutashawishika kuwapendeza
watu, au tutajisikia kusukumwa tuwe viongozi “wa
kiroho” wenye neno la kuwapa watu. Ndiyo Biblia
inayoita “kuwaogopa wanadamu”. Ni mtego unaoweza
kusababisha kuridhiana kubaya zaidi sana pamoja na
miitikio ya kimwili (Mithali 29:25).
Tumeitwa tuwe waaminifu: kwa Mungu, kwa Neno
Lake, na kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu. Kama
unamwombea mtu fulani, na Bwana hasemi na wewe
juu yake, hali hii ni sawa. Huenda Bwana anataka
kusema naye moja kwa moja, au kwa wakati mwingine,
au kwa njia nyingine. Mungu akinyamaza, sisi
tunyamaze pia. Mungu akisema nasi kuhusu mtu
mwingine, lazima tuwe waaminifu na waangalifu katika
kusema yale tu ambayo Mungu amesema au kufunua
- si kuongeza wala kupunguza.
Si nafasi yetu kamwe kumwambia mtu afanye nini,
aende wapi, na kadhalika. Sisi tunamwambia yule mtu
yale tunayopokea kutoka kwa Roho Mtakatifu. Mara
nyingi sana, yanapaswa yathibitishe jambo fulani
kwake ambalo Bwana amekwisha weka moyoni
mwake. Ndipo hoja inabaki kati yake na Mungu kwa ajili
ya kutimizwa.
MATENDO • 21
Kusimikwa kwa ajili ya utumishi
wa Bwana
Nakala 16 / Nambari 1
Mwisho, hoja muhimu: Neno la kinabii kutoka kwa
Mungu SIKUZOTE litakubaliana na yale ambayo
Mungu amekwisha kutufunulia katika Biblia, Neno Lake
takatifu lililoandikwa! Yote tunayofanya maishani
mwetu lazima yafuatane na kupatana na Neno la
Mungu, na kanuni zilizofunuliwa ndani yake.
Kufuata Mwongozo Wa Roho Mtakatifu
Mifano mingine ya mgawanyo inaonekana katika
Matendo 6:1-7 na 13:1-3. Matukio haya katika Kanisa la
awali hayakuwa tu ibada ya dini. Katika masimulizi haya,
viongozi katika Mwili wa Kristo walitafuta mwongozo wa
Roho Mtakatifu wakaufuata kinaganaga. Ndipo kwa imani
thabiti, waliomba kwa kutii mwongozo huo. Katika kuitikia,
Mungu aliwaandaa, kuwabariki na kuwapa upako wale
walioombewa ili atimize yale aliyokuwa amewaagizia.
Jambo lililo muhimu kabisa ni hili: Mwongozo wa Roho
Mtakatifu ni kwa ajili ya kufunua makusudi na mapenzi
rasmi ya Mungu. Yesu Mwenyewe alikiri kwamba huduma
Yake ya duniani iliwezekana kwa sababu ile tu kwamba
alikuwa akifanya mapenzi ya Mungu Baba (Yohana 5:19,30;
6:38; 8:29). Tunaweza na inatubidi tufanye sawasawa.
Tunapofuata mwongozo wa Mungu Roho, Yeye
atatutumia katika kutimiza mapenzi Yake. Sehemu ya haya
inaweza kuwa kuthibitisha wito wake katika wengine; na
halafu kuwaombea ili wapewe upako na karama kwa ajili ya
yote ambayo Mungu amekusudia kwa ajili yao, kwa utukufu
Wake na kwa kujenga Mwili Wake (Waefeso 4:12-16).
Uhuru Zaidi
Katika semina nyingi za World MAP za wachungaji,
nimefundisha kuhusu upako au kuhusu ubatizo wa Roho
Mtakatifu. Katika mikutano hii, wachungaji wasiohesabika
wamejazwa Roho Mtakatifu kwa upya; wengine walibatizwa
na Roho Mtakatifu kwa mara ya kwanza. Mimi binafsi
sikuwapa chochote, zaidi ya mafundisho kutoka katika
Maandiko kuhusu mambo haya. Huenda mimi niliwaombea,
lakini ni Roho Mtakatifu aliyewagusa na kuwajaza (Luka
3:16; Yohana 16:7) - kwa sababu waliona njaa ya kumpokea
Yeye zaidi!
Tunapokea taarifa nyingi sana kutoka kwa wachungaji
hao hao kuhusu mabadiliko ya ajabu katika huduma zao.
Wameona nyongeza ya ishara, maajabu na miujiza katika
mikutano yao; wana bidii mpya kwa ajili ya Mungu na kwa
uinjilisti; wanawaongoza watu wengi kwenye wokovu au
ubatizo wa Roho Mtakatifu.
Imekuwaje?
Kwanza, kumekuwa na mafundisho kutoka katika Neno
la Mungu, linaloleta mwangaza kuhusu hoja fulani. Mtu
anayesikia mafundisho anaamua kupokea kwa imani yale
aliyojifunza - na kuyatendea kazi!
Lakini yanayotokea ni zaidi. Roho Mtakatifu yupo naye
anatenda kwa njia pekee, akishuhudia ukweli wa Neno la
Mungu lililoelezwa. Kwa hiyo, watu wanapoitikia kwa moyo
wa wazi na kwa imani - na, katika njaa yao kwa Mungu,
wakiomba wapokee yote ambayo Yeye amewaandalia - Yeye
anaitikia njaa yao kwa njia maalum na nzito (Mathayo
5:6; Yohana 6:35). Wanapokea kweli! Upako zaidi wa Mungu
kwa ajili ya huduma unafunguliwa kwao.
Tafadhali ufahamu kwamba Mungu hawekewi mipaka
ya uwanja wa mkutano au ya tukio fulani. Mungu Roho yupo
kila mahali, naye atawaitikia wale wanaomtafuta kwa moyo
wao wote (Yeremia 29:12-13).
Mungu atakutana na wewe popote ulipo, unapomtafuta
kwa moyo wako wote. Haleluya!
Ninataka kusema tena kwamba hakuna mtu
anayefahamu kikamilifu jinsi Roho wa Mungu awezavyo
kutenda na atakavyofanya kazi. Lakini tunajua kwamba
Mungu kwa Roho Wake ataitikia njaa yetu Kwake.
Roho Mtakatifu anawajaza watu kwa upya akiitikia
maombi yao (Luka 11:9-13). Imani yao inapohuishwa,
wanaanza kuomba kwa imani wakiamini kutoka hapo walipo
(Waebrania 11:6).
Maombi Bora
Kama tulivyojifunza, mitume waliwekeana mikono na
pia kuwawekea watenda kazi wengine, wakiwaombea na
kuwasimika katika huduma (Matendo 13:2-3; 6:1-6). Mungu
aliwaongoza wafanye hivyo, kwa hiyo tendo la lazima na
lenye nguvu lilikuwa likitokea.
Huenda hatufahamu njia zote za Roho Mtakatifu. Lakini
hili tunalijua: Wakati Roho Mtakatifu anapotuongoza
tuwaombee wengine - na wakati tunapowaruhusu watu
wengine wa Mungu, wanaume kwa wanawake, watuombee
sisi - upako, karama, hekima na mengine zaidi vya Mungu
hugawanywa.
Ingawa sisi hatuwezi kuamua wakina nani wapokee
karama za Mungu na upako Wake, kwa hakika tunaweza
kuwaombea wengine wawe zana zenye nguvu na kutumika
kwa ufanisi katika huduma ya Mungu kwa uweza wa Roho
Mtakatifu (2Timotheo 1:6-7).
Lazima sikuzote tutii na kupokea mapenzi makuu ya
Mungu kwa maisha yetu katika mambo haya. Huenda
maombi bora tunayoweza kumletea Mungu ni: “Je, ni vipi
vipawa, na kazi, ulivyoniandalia? Je, umeniita nivitumieje?
Unataka kunipa nini ili nitimize mapenzi Yako?”
Mungu ana makusudi pekee ya maagizo, wito na
huduma kwa ajili ya kila mwanamume na mwanamke.
Pamoja navyo, Yeye atatupa kwa utele “mambo ya ajabu mno
kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu
[Roho Mtakatifu] itendayo kazi ndani yetu” (Waefeso 3:20)
ili kutuwezesha tutimize mapenzi Yake tunapomtolea
kikamilifu maisha na mapenzi yetu.
2. Upako hautolewi ili kukaliwa, kutawaliwa wala
kufichwa ndani yetu.
Kusudi la msingi la upako ni kutuwezesha tuwe na
ufanisi katika huduma au katika kazi yetu. Hili ni pamoja na
kuwatolea wengine kwa hiari katika huduma yale ambayo
sisi tumepewa na Roho Mtakatifu.
Yesu Mwenyewe, mwanzoni mwa huduma Yake,
alisema: “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana
amenitia mafuta...” (Luka 4:16-21).
Utaona unaposoma mistari hii kwamba Yesu aliendelea
kusoma orodha ya mambo ambayo Yeye alitiliwa mafuta
(upako) kwa ajili ya watu wengine.
Upako ni heshima takatifu. Haitupasi tuutamani ili
tuonekane kuwa watu wa kiroho zaidi au wazuri kuliko
wengine. Upako ni maandalizi ya Roho Mtakatifu,
unaotolewa ili tuzae matunda mengi zaidi na kuwa na ufanisi
22 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1
mkubwa zaidi katika huduma yetu na wito wetu. Maana yake
hasa ni kwamba tutapata kuwa watumishi bora kwa watu
wote (Yohana 13:12-17). Mwenendo wa maisha pamoja na
msimamo wa kutoa, katika kila kiwango cha maisha, ndiyo
amri ya Biblia kwa kila mwamini (Mathayo 10:8; Luka 6:38;
Matendo 20:35).
Mungu anawatakia watu Wake wajitolee wakati wote
katika mali yao na vipawa vyao kwa ajili ya kuwasaidia
wengine. Pasipo mwenendo wa maisha wa kutoa, hatutakuwa
na afya ya kiroho, na Mwili wa Kristo pia utapungukiwa.
Mungu ametupa mfano wa ndani katika jiografia ya nchi ya
Israeli utakaosaidia kufafanua kanuni hii.
Uhai Au Mauti
Nchi ya Israeli ina maziwa makubwa mawili. Moja ni
Bahari ya Galilaya, la pili ni Bahari ya Chumvi. Bahari ya
Galilaya ni ziwa la maji baridi linalopendeza sana na kujaa
viumbe hai. Bahari ya Chumvi kwa Kiingereza huitwa
Bahari ya Mauti, kwa sababu imejaa chumvi na madini
mengine hadi haiwezekani kiumbe chochote kiishi ndani
yake. Maji yake hayafai kabisa kunywa, pia yanaweza
kuunguza ngozi ya mtu, kusababisha upofu na hata kukuua!
Bahari ya Galilaya huongezewa maji ya mito yenye maji
matamu mazuri. Upande wake wa chini, maji haya hutoka
katika Mto Yordani, ambao unaingia moja kwa moja katika
Bahari ya Chumvi. Inawezekanaje basi, maji mazuri yenye
uhai ya Bahari ya Galilaya yapate kuwa maji ya sumu na kifo
ya Bahari ya Chumvi?
Kuna tofauti kuu kati ya maziwa haya mawili: Maji
mazuri huingia katika yote mawili, lakini yanatoka katika
Bahari ya Galilaya tu. Bahari ya Chumvi haina pa kutolea.
Katika Bahari ya Chumvi maji yanakaa na kukauka (kugeuka
hewa), yakibakisha nyongeza ya chumvi na madini mengine.
Maji yanazidi kuwa na sumu inayoua.
Kwa njia hiyo hiyo, kusudi la upako wa Roho Mtakatifu
katika maisha ya mtumishi ni kuzalisha uhai wa Yesu katika
wengine. Utaongeza uhai wa Mungu ndani yetu, na kutiririka
kutoka kwetu kuwaendea wengine. Sisi tunapaswa wakati
wote tuwatolee wengine katika huduma na utumishi vyenye
nguvu na vinavyoleta uhai.
Tunapowaombea wengine, kuhubiri, kufundisha Neno
na kuwashirikisha maneno ya kuwajenga chini ya upako wa
Roho Mtakatifu, sisi ni watumishi tunaotoa uhai, ambao
tutabariki na kuadilisha wengine. Tukiwa na ubinafsi kwa
ajili ya muda wetu au bidii zetu - na kuchagua kutokutoa
‘mtiririko’ wa uhai wa Roho Mtakatifu katika utumishi na
huduma kwa wengine - basi upako wa Roho Mtakatifu
utaoza ndani yetu. Tunakusudiwa tupokee wakati wote kwa
upya kutoka kwa Roho Mtakatifu (Waefeso 5:18-19) na
halafu tutoe “maji hai” tuliyopokea, katika utumishi na
huduma kwa wengine (Yohana 7:37-39).
Unaweza kusoma kuhusu kanuni hii katika Mathayo
25:14-30. Ilimtokeaje yule mtumishi asiyetendea kazi yoyote
vipawa na upako alivyopewa na Mungu?
3. Upako unaweza kuzuiwa au kusimamishwa.
Tumejifunza kwamba upako ni Nafsi na uwepo wa
Mungu Roho. Roho Mtakatifu si nguvu isiyo na uhai na
nafsi. Roho Mtakatifu ni Nafsi ya Mungu.
Maandiko yamefunua kwamba Roho Mtakatifu anaweza
“kuhuzunishwa” (Waefeso 4:30). Maana yake ni kwamba
anasikia huzuni, anajeruhiwa au kuumizwa. Roho Mtakatifu
anaweza pia “kuzimishwa” (1Wathesalonike 5:19). Neno hili
lina maana ya kubanwa au kusongwa, au ya moto
ukizimishwa na maji.
a. Kuzimisha Roho Mtakatifu. Tunazimishaje Roho
Mtakatifu? Hutokea mara nyingi watu wanapopinga kazi ya
Roho Mtakatifu, au wasipojali kazi Yake. Kama watu
hawataki kuitikia misukumo ya Roho Mtakatifu au hamu
Yake ya kutenda kazi kati yao, wanaweza kuzuia (kuzimisha)
kazi Yake kati yao.
Kwa upande mwingine, Roho Mtakatifu anaweza
kuzimishwa pia wakati bidii zetu au misisimko yetu ya
kibinadamu vinapotenda kazi badala ya Roho Mtakatifu.
Kuna makanisa ambapo watu wanapendelea kufuata taratibu
zao kila juma, pasipo hamu yoyote ya kupokea kazi mpya ya
Roho Mtakatifu katika ibada zao. Katika hali hii, Yeye hana
uhuru wa kutenda kazi; kwa hiyo Roho “anazimishwa”.
Kuna sehemu nyingine pia ambapo watu wanataka
“kuigiza” kuwepo kwa Roho Mtakatifu. Huenda
wanarukaruka, kupiga kelele, kutetemeka au mengine. Ni
kweli kwamba wakati Roho Mtakatifu anapofanya kazi, mara
kwa mara kuna matendo kama haya.
Lakini kama yanafanyika kama igizo, na si kama itikio la
kazi halisi ya Roho Mtakatifu, matendo kama haya yanaweza
kuzimisha kazi yenyewe ambayo Roho Mtakatifu anataka
kutenda kwa wakati ule.
Wakati wowote ambapo watu wanachagua utaratibu
badala ya uwepo wenyewe wa Roho Mtakatifu na kazi Yake,
Yeye hana nafasi ya kutenda anavyotaka. Kwa hiyo, Yeye
“anazimishwa”.
Je, mifano hii yote inafananaje? Yote yanafunua
majaribu ya wanadamu kutawala au kuiga kazi ya Mungu.
Huenda watu wameamua kwamba wameridhika na aina
fulani ya utaratibu au mtindo ambao wanataka kufuata. Kila
juma, utaratibu wa ibada yao ni ule ule.
Inasikitisha kwamba hali hii inaweza kumzuia Roho
Mtakatifu asitende kazi halisi katika ibada zao kwa
kuwapatia watu uhai, uweza, uponyaji na upako Wake.
Hakuna nafasi wala ukaribisho Kwake kwamba aje na
kutenda kazi. Katika hali hii, nia ya mwanadamu imepinga
nia ya Roho Mtakatifu - na ndipo Roho Mtakatifu
“anapozimishwa” yaani hana uhuru wa kutenda kazi.
Biblia imetaja kipekee bidii za kibinadamu za kuchukua
nafasi ya uweza na uwepo wa Roho Mtakatifu: “Si kwa
uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema
Bwana wa majeshi” (Zekaria 4:6).
Mchungaji kwa Mchungaji: Kiongozi wa kanisa,
hata utaratibu au mtindo wako unaweza kuzuia kazi ya
Roho Mtakatifu. Kila mara kundi la waamini
linapokusanyika, lazima tuwe wasikivu kwa yale
ambayo Roho Mtakatifu anataka kutenda.
Pengine anataka kufanya kazi kwa upole na utulivu
na kuwaponya watu. Roho Mtakatifu anaweza pia kuja
kwa nguvu na kuwaweka huru wafungwa! Anaweza
kuleta hali ya kusherehekea ushindi katika kuabudu,
kujenga imani na matazamio ya waamini. Au anaweza
kuleta hukumu kali, na pamoja nayo hamu ya kutubu,
kati ya waliohudhuria, kwa ajili ya makosa yao mbele
za Mungu.
Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO • 23
24 • MATENDO
Hoja ni kwamba, inatupasa sikuzote tukaribishe na
kuwekea nafasi kazi ya Roho Mtakatifu katika ibada
zetu. Tunahitaji kuomba, kusikiliza, na kutii misukumo
na maneno ya kinabii ambavyo vinaweza kuja. Ndipo
“mtindo” wetu wa utumishi au kuhubiri unapaswa
ufuatane na yale ambayo Roho Mtakatifu anayatenda
kwa wakati huo.
Kwa mfano, kama tutarukaruka au kupiga kelele
wakati Roho Mtakatifu anapotaka kuleta amani au
utulivu – “utege sikio lako“ (Zaburi 46:10) tutazimisha
kazi Yake ya dakika ile. Tukikataa msisimko wa
kusherehekea unaotokea katika kuabudu, tunaweza
kuzuia ushindi usitokee kati ya watu. Huenda itatubidi
tutulie katikati ya ibada, na kumruhusu kila mtu
amsubiri Bwana ili yeye binafsi asikie kutoka Kwake.
Kutembea Katika Roho Mtakatifu
Ni muhimu kabisa kwetu, kama viongozi wa kanisa,
kusitawisha uwezo wetu wa kupambanua na kumsikia
Roho Mtakatifu. Njia bora ya kufanya hivyo ni kutumia
vipindi virefu vya maombi katika siku zinazotangulia
kabla ya kukusanyika kwa waamini. Vipindi hivi vya
maombi visiwe tu vya kumwomba Mungu abariki yale
ambayo umekwisha panga kufanya. Bali ni nafasi ya
kunyenyekeza moyo wako na kukabidhi mipango yako
kwa Mungu, ukimsubiri hadi upokee maono ya yale
YEYE anayotaka kufanya! Utumie muda wakati wa
mkutano pia, wa kusubiri, kusikiliza na kupambanua.
Uamue kuwa mtu anayefuatana na yoyote ambayo
Mungu anataka kufanya. Kumbuka, hili ni Kanisa Lake
na hao ni watu Wake. Wewe upo kwa ajili ya
kuwasimamia, kuwatunza na kuwafanya wawe
wanafunzi. Lakini iliyo muhimu kabisa, nafasi yako ni
kuwaelekeza watu kwa Mungu na kuwafundisha jinsi
ya kumwitikia Roho Wake Mtakatifu katika mambo
yote!
Roho Mtakatifu anaweza kufanya tendo la
kumweka huru, kumkuza au kumponya mtu kwa
haraka sana wakati wa ibada. Kazi kama hii ingeweza
kutumia miezi, au hata kutokutendeka kamwe, pasipo
huduma ya Roho Mtakatifu kwao kwa dakika ile. Kwa
hiyo sisi tufanye kazi pamoja na Roho Mtakatifu, na
kushiriki katika kazi Yake kila mara tunapokusanyika!
b. Kumhuzunisha Roho Mtakatifu. Maandiko
yanaeleza pia kuhusu kumhuzunisha Roho Mtakatifu
(Waefeso 4:30). Maana ya “kuhuzunisha” ni kumfanya
asikitike au kuumia. Roho Mtakatifu anaweza kuhuzunishwa
na lolote tunaloruhusu au kutunza mioyoni mwetu
lisilofanana na Yesu.
Tunaweza kuwa na misimamo, tabia, mawazo, maneno
au matendo - lolote lisilofanana na Kristo litamhuzunisha
Roho Mtakatifu.
“Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu;
ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.
Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano
yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni
wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane
kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi”
(Waefeso 4:30-32).
Hamasa ya Paulo kwa Waefeso huwasaidia kufahamu
kwamba wao ni hekalu la Roho Mtakatifu, kama watu binafsi
(1Wakorintho 6:19) na kama kundi (1Wakorintho 3:9-17)
kama Mwili wa Kristo.
Kwa sababu Roho wa Mungu anaishi ndani yetu,
tunaweza kuwa na uhusiano wa karibu sana na Yeye. Roho
Mtakatifu anaweza kuhuzunishwa kwa sababu Yeye
anatupenda (Warumi 5:5). Tuachane na wazo au tendo lolote
linaloweza kumpa huzuni na majonzi huyo Roho wa Mungu
anayeishi ndani yetu.
Roho Na Neno
Huenda wapo viongozi ambao wangesema kwamba
wanakaribisha kazi ya Roho Mtakatifu kati yao. Lakini
wanaweza kupata kuwa washupavu kwa kuacha kujifunza
Neno la Mungu kwa bidii na kufanya maandalizi
yanayohitajika kwa ajili ya kuwafundisha na kuwafunza
wengine katika njia za Bwana. Hao “wanamwachia Roho
Mtakatifu afanye kazi”. Mwelekeo huu wa akili haufai,
unaweza kusababisha matatizo mazito katika maisha ya
kiongozi na katika kanisa. Msimamo huu unaweza kuwa
kisingizio cha uvivu au utovu wa nidhamu, kitu ambacho
Mungu hatakibariki.
Biblia inasema wazi kabisa kwa viongozi kuhusu hoja
hii. “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu,
mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa
halali neno la kweli” (2Timotheo 2:15-16).
Kama viongozi, lazima tuandae mioyo yetu kwa sala
nyingi, na kujaza akili zetu na Neno la Mungu. Lazima
tujifunze Maandiko na kuandaa mafundisho kutoka katika
Neno la Mungu ambayo yatawasaidia wale tunaowaongoza
wapate kuwa wanafunzi wenye upevu wa Yesu Kristo.
Lazima tusifundishe kamwe mambo yasiyo sahihi, imani ya
uwongo au mawazo ya kimwili kutokana na kutokujifunza na
kuzoea ukweli wa Neno la Mungu. Sisi tutahukumiwa
kufuatana na yale tunayowafundisha wengine (Yakobo 3:1).
Tunapokuwa tumeandaliwa kutokana na Neno la
Mungu, tunaweza kabisa kutazamia upako wa Roho
Mtakatifu utoe uwezo wa kuhubiri Neno la kweli la Mungu.
Tunaweza kumtazamia Roho Mtakatifu atutumie kama zana
kwa dakika ile ya huduma, na pia kutazamia uweza Wake
katika ishara na maajabu yatakayofuata.
Lakini tusipokuwa na bidii katika kujifunza Biblia na
kusali, ni rahisi zaidi kabisa kutoa huduma kutokana na
mawazo yetu au maelekeo yetu ya kimwili. Je, Roho
Mtakatifu atawezaje kutupa upako wakati hatufundishi Neno
la Mungu wala kumwakilisha Kristo kikamilifu katika
maisha yetu na huduma zetu?
Upako Usiotazamiwa
Biblia inafundisha pia kwamba zipo nyakati ambapo
Roho Mtakatifu anaweza kutia maneno yafaayo midomoni
mwetu: “Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi
mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema”
(Mathayo 10:19; taz. pia Marko 13:11 na Luka 12:11-12).
Lakini mistari hii inahusiana na hali za kufukuzwa na
kuteswa au matukio maalum, si ibada ya kawaida ya juma ya
kundi lako! Kwa hiyo mistari hii ya Maandiko isitumiwe
kama kisingizio cha kutokujifunza Neno la Mungu kwa bidii
na kuandaa mafundisho yafaayo.
Huenda nyakati zitatokea ambapo tunaitwa tuhubiri,
kusali au kutoa huduma pasipo maandalizi. Ninaamini
Nakala 16 / Nambari 1
kwamba katika nyakati hizi msaada maalum wa upako
usiotazamiwa huletwa na Roho Mtakatifu. Kumbuka, Yeye
ndiye anayetaka kumdhihirisha Yesu, na kuwaleta watu
katika wokovu kwa njia ya Kristo! Atatutumia katika hali
yoyote ili afanye hivyo. Lakini zaidi tunavyojiandaa katika
Neno la Mungu na sala, ndivyo tutakavyokuwa tayari zaidi ili
Mungu atutumie kwa ufanisi.
Mungu anawataka viongozi Wake wawe waangalifu na
waaminifu kwa Neno Lake. Hii ni kwa ajili ya manufaa ya
kiongozi mwenyewe, pamoja na manufaa ya wale ambao
wanaoongozwa. Mazoea ya kusoma Biblia na kusali kila siku
yanajenga ndani yetu “akiba ya kiroho” ambamo Roho
Mtakatifu anaweza kuchota. Ndipo Roho Mtakatifu
anapoongeza uweza, hekima na utambuzi wa ki-Mungu
kutoka Kwake, katika yale tunayosema. Mchangamano huu
unaweza kubadilisha maisha ya msikilizaji!
Neno la Mungu linatuhimiza tuwe tayari wakati wote ili
Roho Mtakatifu atutumie katika hali yoyote (2Timotheo 4:2;
1Petro 3:15). Hali hii inatendeka kwa njia ya kujifunza Neno
la Mungu na kusali kwa bidii!
4. Upako unaweza kudhulumiwa au kutumiwa
vibaya.
Ipo mifano kadhaa katika Maandiko ya wanaume na
wanawake waliodhulumu au kutumia vibaya uwezo wa Roho
Mtakatifu. Walipofanya hivyo, Mungu aliwahukumu na
kuwaadhibu.
a. Waamuzi Sura za 13-16 - Samsoni. Karama ya
Mungu kwa Samsoni ilikuwa nguvu ya ajabu ya kimwili.
Roho Mtakatifu alipomjia (Waamuzi 13:24-25; 14:6,19;
15:14), Samsoni alifanya matendo makuu dhidi ya Wafilisti
waliowatesa Waisraeli. Lakini, ingawa Samsoni alikuwa na
karama kuu maalum, udhaifu wake wa kimaadili
ulimwangusha na kufupisha maisha yake na huduma yake
kwa Israeli (taz. Waamuzi sura ya 16).
Samsoni alifikiri kwamba angeweza kuishi maisha yake
kufuatana na mapenzi yake, na bado amtazamie Mungu ampe
upako. Hali hii ilikuwa ushupavu mkuu, nao ulisababisha
kushindwa kwake kama mtumishi wa Mungu. Ingawa
baadaye alitubu na Mungu alimtumia mara nyingine moja,
inaelekea kuwa maisha na huduma ya Samsoni havikufikia
makusudi ya Mungu.
[Tutaangalia kwa makini zaidi jinsi tabia inavyogusa
upako wa kiongozi wa kanisa katika Sehemu Ya III.B.1,
“Tabia na Upako”.]
b. Walawi 10:1-3 - Nadabu na Abihu. Hao wana
wawili wa Haruni (Kuhani Mkuu) walitiwa mafuta watoe
huduma kama makuhani kwa watu wa Israeli. Biblia
inafunua kwamba walitoa “moto wa kigeni mbele ya Bwana,
ambao yeye hakuwaagiza” (Walawi 10:1). Tendo hili liliasi
amri ya awali ya Mungu (Kutoka 30:9).
Mungu alikuwa ameweka nyakati na njia rasmi kwa ajili
ya dhabihu na sadaka za makuhani. Kumtii Bwana na njia
Zake ni kipaumbele kikuu. Hali ya Nadabu na Abihu kuwa
watiwa mafuta au upako wa Bwana haikuwa udhuru kwa ajili
ya kutokutii kwao. Hukumu ya Mungu ilikuwa ya haraka na
ukali juu ya wana hao wawili wa Haruni ambao walitoa
huduma yao kwa Mungu kwa njia zao binafsi (Walawi 10:2).
Sisi kama viongozi wa kanisa, lazima tutii wakati wote
mwongozo wa Roho Mtakatifu pamoja na kanuni na amri za
Neno la Mungu. Tusianguke katika mtego wa kufikiri
kwamba sisi tunaweza kuchagua jinsi sisi tunavyotaka
kumfuata Mungu na kutoa huduma katika Kanisa Lake.
Lazima tupokee YOTE ambayo Yeye anataka kutufunulia
katika Neno Lake kuhusu huduma yenye ufanisi, na kufanya
huduma hiyo kwa uwezo wetu wote!
Mchungaji kwa Mchungaji: Ni rahisi kwa viongozi
wa kanisa ambao Mungu amewapa upako - hasa wale
ambao Mungu anawatumia sana - kufikiri kuwa amri za
kimsingi za Maandiko haziwahusu wao tena.
Wanasahau kwamba yote wanayofanya hufanyika
mbele za macho ya Mungu aliye mtakatifu (Walawi
10:3).
Sote tumesikia habari za wanaume na wanawake
ambao Mungu amewatumia sana nao wameanguka
katika kushindwa kimaadili, makosa kuhusu mali na
fedha, na dhambi nyingine. Kuanguka kwao kwa
kawaida hakutokei kwa dakika moja. Huanza kwa
kuridhiana na kutoa udhuru “kidogo”, njia
inayowafikisha katika kutokutii Neno na hatimaye
kuanguka kabisa (Yakobo 1:14-15).
Lazima tusisahau kwamba Mungu ni mtakatifu, na
Yeye ametuita sisi pia tuwe watakatifu (Walawi 11:44;
1Petro 1:16). Neno la Mungu, amri Zake, kanuni Zake,
ni kwa ajili ya kila mwamini na mfuasi wa Kristo - hasa
viongozi Wake walioitwa na kupewa upako!
c. Hesabu 11:16-30 – Wazee. Biblia inaelezea tukio
moja wakati wa kusafiri kwa Waisraeli ambapo Mungu
aliwapa wazee sabini Roho Wake nao walitabiri (ms. 25).
Walikuwepo wanaume wengine wawili ambao
hawakuhudhuria pamoja na wenzao kwenye Hema ya
Kukutania, bali walibaki kambini. Roho aliwajia wao pia,
wakaanza kutabiri (ms. 26).
Joshua, ambaye kwa wakati ule alikuwa msaidizi wa
Musa, aliomba wale wawili wazuiliwe na kukatazwa
wasitabiri (ms. 28). Lakini Musa alimkemea Yoshua, na
kueleza hamu yake ya kinabii kwamba Bwana angewatia
watu wote roho Yake (ms. 29; taz. pia Yoeli 2:28-29;
Matendo 2:14-21).
Huenda Yoshua alikuwa na nia njema, akiona mashaka
kuwa wale wawili walitabiri visivyofaa kwa sababu
hawakuhudhuria pamoja na wazee wengine. Lakini alikosa
kwa kufikiri ilikuwa wajibu wake kuamua Mungu atamke lini
na kwa njia ya nani.
Mchungaji kwa Mchungaji: Viongozi wanapojaribu
kutawala au kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu, wanakosa.
Mara nyingi, tuna hamu inayotokana na nia njema ya
kuwa “mambo yote yatendeke kwa uzuri na kwa
utaratibu” (1Wakorintho 14:40). Lakini njia zetu si njia za
Mungu (Isaya 55:8-9). Vipimo vyetu au maoni yetu ya
kibinadamu kuhusu mambo tunayofurahia huenda
havihusiani kamwe na yale ambayo Mungu anataka
kutenda kwa wakati fulani maalum.
Mungu anaweza kutenda kwa njia zisizo za
kawaida, kutokana na vyanzo visivyotazamiwa, na kwa
matendo yasiyo ya kawaida pia. Fikiria punda wake
Balaamu (Hesabu 22:22-40), au Yesu akitumia udongo
na mate alipomponya kipofu (Yohana 9:1-6).
Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO • 25
Tunaishi katika siku za Mavuno makuu na
kumiminwa kwa Roho wa Mungu. Matukio ya ajabu,
miujiza, matamko ya kinabii na mafunuo mengine ya
Roho wa Mungu vinaongezeka kote duniani. Ni lazima
tutumie karama ya kupambanua, naam, tusikubali na
kuamini mambo yote yanayofanyika kwa jina la Mungu
(Mathayo 7:21-23). Lakini ni lazima pia tujifunze
kushirikiana na kutenda pamoja na Roho Mtakatifu kwa
wakati wowote maalum.
Si juu yetu sisi kumwamulia Roho Mtakatifu atende
kazi lini, kwa njia gani na kupitia kwa nani. Chombo
ambacho Mungu anakitumia kwa hakika kitakuwa na
upungufu na hitilafu. Hakuna yeyote kati yetu aliye
mkamilifu, lakini Mungu ameamua kufanya kazi kupitia
kwetu!
Hata hivyo, inatubidi tuangalie kuwa Maandiko
hueleza wazi kwamba tusishirikiane na watu wanaoishi
katika dhambi au kufundisha uwongo (1Timotheo
6:3-5; 2Timotheo 3:1-5). Lazima pia tuwe waangalifu
katika kupima unabii kwa usahihi (1Wakorintho 14:29).
Tena tusitumie vipimo vya nje vya dunia katika
kutathmini au kutambua hali ya ndugu au dada katika
Kristo (2Wakorintho 5:16-17).
Kama wachungaji, katika hamu yetu ya kuongoza,
tunaweza kushawishika tujaribu kutawala. Hapo tumo
katika hatari ya kuzuia, au kukataza, kazi ya Roho
Mtakatifu kati yetu (kama Yoshua alivyokaribia
kufanya).
Inatupasa tutumie muda wa kuwafunza wale
tunaowahudumia kuhusu lini na jinsi ya kutoa unabii.
Lakini ni lazima baada ya haya tuwe tayari kumruhusu
Roho Mtakatifu atende kazi kupitia kwao
wanapoendelea kujifunza na kukua.
Kumbuka, nafasi yetu kama wachungaji ni
kuwaongoza watu ili wakue kama wanafunzi. Maana
yake, pamoja na mengine, ni kwamba tunawafundisha
- na kuwaweka huru - wapokee na kuitikia mwongozo
wa Roho Mtakatifu.
d. Matendo 5:1-11; 8:9-24 - Anania na Safira; Simoni
Mchawi. Kitabu cha Matendo kinasimulia majaribu mawili
wakati wa Kanisa la awali ya kutumia vibaya uwezo wa
Roho Mtakatifu.
1) Jaribu la kwanza lilikuwa la Anania na Safira
(Matendo 5:1-11). Walijaribu kudanganya uongozi wa
Kanisa la awali kuhusu mauzo ya mali yao. Lakini Petro
alipowakabili, aliita kosa lao kuwa “kumwambia uongo Roho
Mtakatifu” (ms. 3).
Inaeleweka kwamba hoja haikuwa kiasi cha fedha
walichotoa. Bali walihukumiwa kwa sababu ya unafiki wao.
Mungu alikabili aina ya unafiki na roho ya kidini iliyokuwa
alama ya Waandishi na Mafarisayo (Mathayo 23:1-36; 6:1-6;
Marko 12:38-40; n.k.).
Watu wanaomfuata Kristo hupaswa wawe na haki
inayozidi ile ya Mafarisayo (Mathayo 5:20). Haki yao iwe
haki ya moyo, si hali ya nje au sura inayoonekana kuwa ya
haki. Ieleweke pia kwamba ikiwa mtu kweli anayo haki hii ya
ndani, itajidhihirisha katika matendo ya nje ambayo pia ni ya
haki kamili (Mathayo 23:25-26).
Inaonekana kuwa Anania na Safira walitumia kazi pekee na
nzito ya Roho Mtakatifu katika Kanisa la awali kwa ajili ya
kujifaidi wenyewe. Walijionesha kama wameshiriki katika kazi,
lakini ni wazi kwamba walikuwa na nia ya kibinafsi iliyofichwa.
Matendo yao yanafunua kwamba hawakuheshimu
mamlaka ya mitume ambao Mungu alikuwa amewaweka
kuwa viongozi - na hatimaye hawakumheshimu wala
kumstahi Roho Mtakatifu ambaye alikuwa amewapa mitume
mamlaka yao.
Mungu aliona mioyo ya Anania na Safira, na
kuwahukumu kwa haraka na ukali (Matendo 5:5,9-10).
Mungu anatamani Kanisa lililo safi na takatifu (Waefeso
5:27). Ili lipate kuwa hivyo, Bwana wa Kanisa anafanya kazi
isiyokoma ili abadilishe na kutakasa Bibi Arusi Wake
(Waefeso 5:26-27). Anatupenda kiasi cha kutuadilisha na
kutuadhibu (1Petro 4:17; Waebrania 12:3-11).
2) Jaribu la pili la kutumia vibaya upako wa Roho
Mtakatifu katika Kanisa la awali linaonekana katika Matendo
8:9-24. Hapa tunamwona Simoni mchawi, aliyekuwa
ameongoka na kuwa Mkristo muda mfupi kabla ya hapo
(ms. 13). Wakati Simoni alipokuwa akimfuata Filipo,
alishangazwa na matendo makuu na miujiza ambavyo
alimwona Roho Mtakatifu akiyatenda!
Simoni alipowaona mitume wakiwahudumia wengine
katika uweza wa Roho Mtakatifu, alitamani uwezo ule kwa
ajili yake binafsi. Katika mawazo yake machanga na bado ya
kidunia, Simoni alitaka kuwapa mitume fedha ili apate uweza
ule (ms. 18-19).
Petro, kwa uweza wa Roho Mtakatifu, alitambua nia za
moyo wa Simoni:
“Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo,
na tena u katika kifungo cha uovu” (ms. 23). Ilikuwa wazi
kwamba Simoni alikuwa na nia ya kibinafsi. Moyo wake
ulikuwa umefungwa na dhambi, naye hakutaka Roho
Mtakatifu ili amtukuze Mungu na kuwatumikia wengine.
“Uchungu” katika mstari huu ni kama wivu wa
kimashindano (Yakobo 3:14). Simoni alitaka awe mtu
26 • MATENDO
Utiifu kwa Bwana: Kipaumbele
chetu cha kwanza
Nakala 16 / Nambari 1
muhimu aliyewashangaza wengine, labda kama alivyokuwa
wakati wa kuwa mchawi (Matendo 8:9-11). Alitaka uweza
wa Mungu kwa ajili ya faida yake binafsi.
Mchungaji kwa Mchungaji: Hata leo, tunakutana
na viongozi wenye vipawa na upako halisi ambao
hutumiwa na Mungu. Lakini kinachosikitika ni kwamba
wanaweza kuanza kujiona kuliko iwapasavyo.
Wanaanza kutenda kana kwamba uwezo unatoka
kwao, na si kutoka kwa Mungu mwenye rehema
(2Wakorintho 4:5-7). Wanatumia huduma ili wafanye
majina yao yasifiwe, wapate utajiri, au wawavute
wengine wawafuate.
Viongozi wengi hawaanzi hivi. Viongozi wema
wanatamani kumwona Mungu akitenda kazi na
kupokea utukufu wakati maisha ya watu
yanapobadilishwa kwa uweza Wake. Lakini tusipokuwa
waangalifu na wenye juhudi ya kulinda mioyo yetu
(Mithali 4:23), tunaweza kudanganywa na kupotea.
Ibilisi hawezi kukana, kuzuia, kushambulia wala
kushinda uweza wa Mungu (Yohana 1:5). Kwa hiyo
badala yake, Shetani anajaribu kumdanganya kiongozi
na kupotosha moyo wake (2Wakorintho 2:11;
11:13-15), amfanye chombo kinachojitumikia
mwenyewe, asimtumikie Mungu na makusudi Yake
tena.
Kushikilia Kwa Uaminifu
Kwa upande wa Anania na Safira, na kwa Simoni pia,
tunapewa mafunzo ya kutuangaliza na kutuonya. Lazima
tukumbuke kwamba Shetani ana nguvu ya kuvuta mawazo na
matendo yetu tukimruhusu (Matendo 5:3). Lazima tusimpe
nafasi (Waefeso 4:27).
Lakini, wakati viongozi wanapoanguka - wakichagua
dhambi badala ya haki - ni tatizo kubwa sana. Kwanza, kwa
sababu Mungu wetu ni mtakatifu, dhambi inavunja uhusiano
wetu na Mungu. Wafuasi wote wa Kristo wameitwa na
kuamriwa utakatifu wa binafsi na usafi wa kimaadili (1Petro
1:13-19).
Pili, tumeitwa tuwe viongozi wenye amana kwa ajili ya
kuwatunza watu wa Mungu. Sisi tunapokubali dhambi,
tunavunja amana ile na kuwa mifano mibaya kwa wale
tunaowaongoza. Pia tunawaacha kondoo washambuliwe na
pepo wachafu (1Petro 5:2-4; Matendo 20:28-30; Waebrania
13:7,17; Yakobo 3:1). Kama Shetani anaweza
kumwangamiza kiongozi, kondoo watatawanyika na
kukamatwa kwa urahisi (Marko 14:27).
Kushindwa kwetu kunawaudhi pia familia zetu na
kuharibu sifa zetu. Tunaumiza jamii ya Mungu pia, na
kuathiri sifa za viongozi wengine wa kanisa walio
waaminifu. Kwa sababu ya kosa letu, watu hata wa viongozi
waaminifu wangeweza kuwadharau viongozi wao na
kutowaamini (tazama maagizo ya Paulo kuhusu uchaguzi wa
wazee katika 1Timotheo 3:1-7). Shetani anawalenga
viongozi wa kanisa kwa kusudi katika hila zake za
uangamizi. Lakini kumbuka, hawezi kukufanya utende
dhambi usipochagua kufuata vishawishi vyake. Umpinge
Shetani, naye atakukimbia (Yakobo 4:7).
Nafasi yako kama kiongozi na upako wako ni heshima;
pia ni jukumu zito na muhimu sana. Biblia inatuhimiza sana
kuhusu kuendelea kuwa waaminifu na kumaliza mashindano
(Mathayo 24:13; Wafilipi 3:17-18; 2Timotheo 4:6-8).
Tushikamane na tumaini letu na imani yetu katika Kristo
mpaka mwisho, tukiwa mifano ya uaminifu kwa kundi letu,
kwa ajili ya Yesu na utukufu Wake (1Petro 5:2-3).
D. UTANGULIZI WA UPAKO
KATIKA AGANO LA KALE
Tukiwa tunaendelea na mafunzo yetu, tuchunguze
utangulizi fulani wa Agano la Kale wa upako. Kama
ilivyotajwa juu, Agano la Kale lilitolewa kwa ajili ya
mafunzo na mifano kwetu (Warumi 15:4; 1Wakorintho
10:11). Itatusaidia tupate picha kamili zaidi ya upako kama
ahadi iliyotolewa ambayo ilitimizwa mara ya kwanza
mwanzoni mwa awamu ya Kanisa la Agano Jipya (taz.
Matendo sura ya 2).
1. Alama au Ishara za Kiutangulizi
Zipo alama au ishara nyingi za kiutangulizi katika Agano
la Kale za Roho Mtakatifu na kazi Yake.
a. Moto - Katika Hema ya Kukutania na kwenye
madhabahu ya ubani, sadaka za kuteketezwa zilikuwa na
moto uliowaka daima ambao uliwashwa na Mungu (Walawi
9:24; 2Nyakati 7:1-3). Moto huu ulitakiwa uwake hata milele
(Walawi 6:13). Alama hii hii ya moto, inayoashiria uwepo hai
wa Roho wa Mungu, inaonekana pia katika Agano Jipya
(Mathayo 3:11; Matendo 2:3).
b. Maji - Maji ni alama inayotumiwa katika Agano la
Kale kuashiria Roho Mtakatifu katika kuleta burudisho na
baraka ya kiroho kutoka kwa Mungu. Katika eneo la dunia
ambapo maji yalipatikana kwa shida, matumizi ya maji kama
alama ya Roho wa Mungu yalieleweka wazi kwa watu
(Zaburi 23:2; Isaya 35:6-7).
Ezekieli alipewa maono ya mto mkuu uliotoka katika
makao ya Mungu ya hekalu Lake (Ezekieli 47:1-12). Haya
yalifuatana na kutiririka kwa Roho wa Mungu juu ya watu
Wake pasipo kuzuiliwa.
Yeremia anatumia “chemchemi ya maji ya uzima”
(Yeremia 2:13; 17:13) kufunua uwepo wa Mungu kwa Roho
Wake. Yesu pia aliongea kuhusu maji yaliyo hai: “...mito ya
maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Na neno hilo alilisema
katika habari ya Roho...” (Yohana 7:37-39). Wakati ule, Yesu
alikuwa akitabiri rasmi kumiminwa kwa Roho Mtakatifu
ambako kungetokea (Yohana 14:16-17; Matendo sura ya 2).
c. Damu - Tunasoma katika Agano la Kale kuhusu upako
maalum kwa ajili ya makuhani, uliohusiana na damu (Kutoka
29:19-21).
d. Mafuta - Matumizi ya mafuta yalikuwa ya kawaida
katika muda wote wa Agano la Kale. Kuanzia matumizi ya
kila siku katika kupika, kwenye taa na kupaka mwilini,
mpaka matumizi maalum katika matendo makuu ya hekaluni,
mafuta yalikuwa na nafasi muhimu.
Mafuta yalikuwa alama maalum ya uwepo na uweza wa
Roho Mtakatifu wa kuweka watu au vitu wakfu. Tunaona
haya kuhusu wafalme (1Samweli 10:1), makuhani (Kutoka
29:1-9) na kutakaswa rasmi kwa watu wenye ukoma (Walawi
14:10-18).
Pia mafuta yaliashiria furaha (Isaya 61:3), na
kukosekana kwake kuliashiria huzuni au kutwezwa (Yoeli
1:10). Mafuta yalikuwa alama ya ufanisi wa maisha
(Kumbukumbu 33:24), faraja (Ayubu 29:6) na chakula cha
kiroho (Zaburi 45:7).
Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO • 27
Picha ya Kiishara Yenye Nguvu
Kutokana na kuangalia Agano la Kale kwa kifupi tu,
tumeona akiba tele ya ishara, picha na alama
vinavyotufunulia mengi kuhusu upako wa Roho Mtakatifu na
kazi Yake katika maisha yetu. Kiutangulizi, vinawasilisha
upako wa Roho Mtakatifu na kazi Yake ambavyo
vinapatikana kwetu sisi leo! Upako huu ni ahadi iliyotimizwa
ya Baba yetu wa mbinguni (Yoeli 2:28-32) kumimina Roho
Yake juu ya watu Wake (Matendo 2:33-39).
Picha mojawapo yenye maana na nguvu kubwa kiishara
ya upako wa Roho Mtakatifu ni kutengenezwa na kutumiwa
kwa mafuta takatifu ya upako.
Tukisoma maelezo yafuatayo tutaona kwa ndani asili ya
upako wa Roho Mtakatifu pamoja na utendaji wake.
“Kisha Bwana akasema na Musa, na kumwambia,
Jitwalie manukato yaliyo bora, manemane mbichi shekeli mia
tano, na mdalasini wenye harufu nzuri nusu ya kiasi hicho,
yaani, shekeli mia mbili na hamsini, na kane shekeli mia mbili
na hamsini, na kida shekeli mia tano, kwa kuiandama shekeli
ya mahali patakatifu, na mafuta ya zeituni kiasi cha vibaba
vitano; nawe utayafanya mafuta ya kutiwa matakatifu,
marhamu iliyochanganywa kwa kazi ya ustadi ya mtengenezaji
manukato; yatakuwa ni mafuta matakatifu ya kutiwa. Nawe
utaipaka hema ya kukutania kwa mafuta hayo, na hilo sanduku
la ushuhuda, na hiyo meza, na vyombo vyake vyote, na kinara
cha taa, na vyombo vyake, na madhabahu ya kufukizia
uvumba, na madhabahu ya kuteketezea sadaka, pamoja na
vyombo vyake vyote, na birika, na tako lake. Nawe utavitakasa
vitu hivyo, ili viwe vitakatifu sana; tena kila kivigusacho
vyombo vile kitakuwa kitakatifu. Nawe utawatia mafuta
Haruni na wanawe, na kuwatakasa, ili wanitumikie katika kazi
ya ukuhani. Nawe utanena na wana wa Israeli na kuwaambia,
Haya yatakuwa ni mafuta matakatifu ya kutiwa kwa ajili yangu
mimi katika vizazi vyenu vyote. Hayatamiminwa katika
kiwiliwili cha binadamu, wala msifanye mengine mfano wa
haya kama yalivyoungwa kwa viungo vyake; ni matakatifu, na
kwenu ninyi yatakuwa matakatifu. Mtu awaye yote
atakayechanganya mafuta mfano wa haya, au mtu awaye yote
atakayetia mafuta haya juu ya mgeni, mtu huyo atakatiliwa
mbali na watu wake” (Kutoka 30:22-33).
Mafuta haya ya upako yalikuwa wakfu na matakatifu
kwa Bwana. Waisraeli walipaswa waone mafuta ya upako
katika hali hii. Mchanganyiko wake ulikuwa tofauti na
maalum kwa ajili ya matendo matakatifu tu (ms. 31-33).
Mungu alitoa maagizo Yake kwa ajili ya mchanganyiko
wa mafuta hayo ya upako (ms. 22-25). Yalikataliwa matumizi
mengine yoyote. Mtu yeyote wa nje ya watu wa Israeli wa
agano hakuruhusiwa kuyatumia (ms. 33).
Uteuzi Wa Mungu
Kwa sababu mafuta haya yalikuwa ishara ya kiutangulizi
ya upako wa Roho Mtakatifu, masharti makali kuhusu
mafuta hayo maalum yanatufunulia kanuni tatu zilizo
muhimu sana.
Kwanza, Mungu ana mapenzi makuu ya kifalme kwa
ajili ya upako wa Roho Wake. Kama vile alivyoagiza
mchanganyiko wa mafuta ya upako (Kutoka 30:22-25),
Mungu peke Yake anaongoza upako Wake (1Samweli 10:1)
na pia jinsi upako huu utakavyotendewa kazi katika maisha
ya mtu fulani (1Wakorintho 12:7,11).
Pili, mafuta ya upako yalitakiwa kwa ajili ya makuhani
waliotumika ndani ya Hema ya Kukutania (Kutoka 30:30).
Yasitumiwe kwa kumpaka mtu mwilini (30:32). Waamini
wote wa kweli wa Yesu Kristo, kama “ukuhani mtakatifu” wa
Mungu, (1Petro 2:9-10; Ufunuo 1:6) wana upako wa Roho
Mtakatifu (1Yohana 2:20-27).
Upako huo haupo kwa ajili ya asiyeamini. Roho wa
Mungu anaishi ndani ya wale tu waliookolewa na ambao
wanatembea katika kumtii Mungu (Yohana 3:5-6; Warumi
8:14-16; 1Wakorintho 12:3).
Mchungaji kwa Mchungaji: Katika Agano la Kale,
Kuhani Mkuu aliingia ndani ya mahali Patakatifu sana
mara moja kwa mwaka afanye upatanisho kwa ajili ya
watu (taz. Walawi sura ya 16). Yeye peke yake aliweza
kuingia mbele za Mungu kila mwaka.
Wakati wa kifo cha Kristo msalabani, pazia zito
kama zulia lililofunika mahali patakatifu sana ndani ya
hekalu lilipasuka vipande viwili toka juu hata chini
(Marko 15:38; taz. pia Kutoka 26:31-33). Tukio hili
pekee linafunua kwamba Mungu sasa aliweza kujiwa
moja kwa moja na watu wote. Kristo alipofuta deni la
dhambi ya binadamu msalabani, wokovu kutokana na
kumwamini Yeye ulipatikana kwa wote waliokubali
kumpokea (Warumi 10:9-10).
Watu wote watakaoliitia jina la Bwana wataokoka
(Warumi 10:12-13). Nao wote waliookolewa kwa imani
katika Yesu Kristo wanaweza kufika mbele ya “kiti cha
neema” (Waefeso 3:12; Waebrania 4:16; 10:19), yaani
mbele za Mungu Mwenyewe! Haleluya!
Wakristo hawahitaji tena kuwakilishwa na kuhani
wala mtu yeyote mwingine ambaye anamwendea
Mungu kwa niaba yao. Kila mwamini anaweza na
anapaswa kuwa na uhusiano wake binafsi na Mungu
kwa njia ya sala, ibada na ushirikiano. Tunaweza
kuongea na Yeye, kumwomba na kusikia kutoka
Kwake.
Uwezekano huu wa kumfikia Mungu kwa watu
wote wanaomwamini Mwana Wake kwa ajili ya wokovu
ni sababu waamini wote huitwa ukuhani mtakatifu.
“Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe
nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za
roho [yaani, ibada, sala, matendo ya huduma, zaka na
sadaka] zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu
Kristo” (1Petro 2:5; taz. pia Ufunuo 1:6).
“Dhabihu za roho” tunazoitiwa hazitufanyi
tukubaliwe na Mungu. Tumekwisha kubaliwa na Mungu
kwa sababu ya dhabihu ya Yesu msalabani. Wokovu
wetu unatokana na imani katika Yesu, si kutokana na
matendo yetu yoyote (Waefeso 2:8-9).
Ndiyo sababu lile pazia lililofunika mahali patakatifu
sana hekaluni lilipasuka toka juu hata chini. Tukio hili
lilithibitisha kiishara kwamba wokovu wetu
ulisababishwa na Mungu. Maana yake ni kwamba
Mungu alitufikia kwa neema tusiyoweza kustahili ya
Kristo alipokufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu.
Bidii zetu za kuwa na haki hazina mafanikio yoyote
wala haziwezi kutupatia wokovu (Warumi 3:9-20;
Wagalatia 2:16). Lakini tunaishia na kutendea imani
yetu katika dhabihu za kiroho tunapotembea kwa kumtii
Mungu na kutumikia Mwili Wake na pia watu wote
wanaoishi duniani (Yakobo 2:14-26).
Mchungaji, ni lazima ufundishe kweli hizi za msingi
kuhusu msalaba mara nyingi. Wale unaowaongoza
28 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1
lazima wafahamu wokovu ambao wameupokea bure;
na halafu wao waweze kuuwasilisha kwa uwazi kwa
watu wanaojaribu kwa mahangaiko “kustahili” wokovu
wao kwa njia yoyote badala ya ile iliyotolewa na Kristo
(1Petro 3:15).
Tatu, mafuta ya upako usitengenezwe kwa ajili ya kazi
nyingine, wala yasighushiwe (Kutoka 30:32-33).
Kupakwa kwa mafuta katika Agano la Kale ni ishara ya
mtu au chombo fulani kuteuliwa na Mungu. Uteuzi huu
uliweka mtu huyu au chombo hiki wakfu kwa ajili ya
mahali au kazi pekee katika makusudi ya Mungu. Pamoja
na uteuzi huu wa kifalme kulikuwa na mamlaka na uwezo
vilivyohitajika ili mtu binafsi aweze kutimiza yale Mungu
aliyoagiza (1Samweli 16:13; Isaya 61:1). Kanuni hii
inamhusu mwamini wa Agano Jipya pia, haidhuru nafasi ya
huduma ambayo Mungu amempatia ndani au nje ya
shughuli za ibada za Kanisa. Ni kweli pia kwa ajili ya wale
ambao Mungu amewaita hasa kwa ajili ya huduma ya
wakati wote (2Wakorintho 1:21; 1Wathesalonike 5:24).
Mungu anatupatia yote tunayohitaji siyo tu ili tuwe
watumishi wenye kumzalia matunda, bali pia washindi
katika maisha na huduma yetu!
Tatizo La Kughushiwa
Kupatikana kwa upako wa Mungu kwetu ni habari nzuri
kabisa! Lakini ni lazima tusisahau maonyo katika Kutoka
sura ya 30 kuhusu kughushi mafuta ya upako. Mungu aliona
tendo hili kuwa kosa zito, hata la jinai (Kutoka 30:32-33).
Mtu aliyetenda dhambi ya aina hii “alitengwa” na watu wa
Israeli. Wasomi wa Biblia wameona mara nyingi kuwa
maana hasa ya neno hili ni kuuawa.
Mfano huu wa kughushi una maana gani kwetu sisi kama
watumishi wa Agano Jipya? Tumekwisha chunguza dhambi
ya kutumia upako wa Mungu kwa ajili ya faida yetu (Wafilipi
1:15-16). Kuna njia nyingine ambapo upako wa Mungu
unaghushiwa katika utumishi wa leo.
Watu wengine katika utumishi wanafikiri kwa makosa
kwamba lengo la mahubiri yao ni kuwafanya watu
wasisimke. Kwa hiyo wanaghushi upako katika mtindo wao
wa kuhubiri au kufundisha kwa vituko. Mara nyingine
wanasema maneno ambayo watu wanataka kuyasikia, hata
kama yanapinga Biblia; wanaweza kusimulia hadithi
zilizotiwa chumvi; au wanatumia njia nyingine za kuvuta
umati wa watu kwa hila.
Wengine katika utumishi wanataka kujulikana na
kujipatia wafuasi wao binafsi. Wanaweza kughushi upako
kwa kujifanya kwamba wamefahamu “siri za ndani” ambazo
wengine hawazijui (2Wakorintho 11:3-4); wanadai vyeo au
nafasi ili watu wawaheshimu; au wanatumia vyeo au
mamlaka katika kuwahimiza wengine watende mambo
yasiyo ya haki au yanayomfaidi kiongozi mwenyewe.
Zipo njia nyingine nyingi ambamo watu
wanashawishiwa waghushi upako au kuutumia vibaya.
Lakini hoja ni hii: Kughushi au kutumia vibaya Roho
Mtakatifu ni dhambi kubwa mbele za Mungu. Pia ni aina ya
udanganyifu ambayo, ikiendelezwa, itapatia ufalme wa
Shetani nafasi katika maisha ya kiongozi wa kanisa.
Hatimaye hali hii italeta hukumu ya Mungu juu ya maisha ya
mtu huyo pia.
Kughushi upako wa Roho Mtakatifu kumesimuliwa
katika Agano Jipya. Mfano wa wazi hasa ni wa Paulo
akiwahukumu “mitume wa uongo”. Paulo anawafananisha na
jaribu la Shetani la kuwaiga malaika wa Mungu ili
awadanganye waamini (taz. 2Wakorintho sura ya 11).
Wapo watu leo wanaoonekana kuwa ni wajumbe
waliotiwa mafuta na Mungu, lakini sivyo walivyo. Agano
Jipya limetoa maonyo mengi juu yao (Mathayo 7:15-20;
Matendo 20:27-30; 2Wakorintho 11:1-15; Wagalatia 1:6-10;
Wakolosai 2:18-23; 1Timotheo 4:1-3; 2Timotheo 3:1-9;
2Petro 2:1-22; 1Yohana 4:1-6; Yuda 3-19).
Baadaye katika toleo hili, tutajifunza tabia saba
zinazopatikana katika wale wanaotenda katika upako halisi
wa Roho Mtakatifu. Orodha hii itasaidia katika kuchunguza
utumishi wako, pamoja na kutambua uwepo wa kweli wa
Roho Mtakatifu katika watumishi au viongozi wengine wa
kanisa.
Mchungaji kwa Mchungaji: Si kosa kutaka kuwa
na ufanisi katika utumishi na kutamani uwezo wa Roho
Mtakatifu wenye upako. Lakini ni kosa kujifanya
tusivyo, pamoja na kujaribu kufanya kana kwamba
tumepokea upako.
Kwa nini tujibidishe kujifanya kuwa na upako,
wakati ambapo tunaweza kupata upako halisi - kama
tutaupokea kwa masharti ya Mungu na si yetu.
Tunaweza kulinda maisha yetu na dhambi na
udanganyifu kuhusu upako - na kuingia katika upako
halisi wa Roho unaoongezeka kila wakati - kwa njia
mbalimbali:
• Ukubali karama na wito ambao Mungu amekupa
wewe; na usiwaonee wivu wala kukosoa yale waliyo
nayo wengine wala kujaribu kuwaiga.
• Uombe kila siku uweze kujua mapenzi ya Mungu
kwa ajili yako binafsi pamoja na utumishi wako.
• Ukubali na kuridhika pale ulipoitiwa na Mungu,
na yale ambayo Yeye amekuagiza uyatende.
• Umwombe Mungu wakati wote msaada na
uwezo ili uweze kufanya mapenzi Yake.
• Ujikumbushe kila siku kwamba umo katika
utumishi kwa ajili ya kutumikia Mungu na watu
wengine, na si kujitumikia wala kujiendeleza.
Ukumbuke pia kwamba hakuna mtindo maalum wa
kuhubiri au kuongoza ulio na “upako” kuliko mtindo
mwingine. Nimewaona viongozi wenye upako
wanaoongea kwa upole na utulivu. Walipofundisha
Neno la Mungu, watu waliponywa au kuguswa na Roho
Mtakatifu. Viongozi wengine huenda wanafanya
matendo au kuongeza sauti zaidi wakati Roho
Mtakatifu anapohudumu kupitia kwao. Hakuna mtindo
ufaao au usiofaa.
Jambo muhimu ni kusitawisha usikivu kwa Roho
Mtakatifu kila mara unapotoa huduma. Tulia, sikiliza, na
kuitikia yale ambayo Yeye anasema na kutenda katika
mkutano fulani. Ndipo wewe ulinganishe mtindo wako
na yale ambayo Roho Mtakatifu anataka kuyatenda
kwa dakika moja moja.
Ukumbushwe kwamba Mungu amekuita vile ulivyo.
Amekupa vipawa maalum kwa sababu maalum.
Anataka kukutumia kama ulivyo pamoja na vipawa
ulivyo navyo - ukishirikiana na kazi ya Roho Wake
Mtakatifu ya upako na mabadiliko - kwa ajili ya
kuwahudumia wengine.
Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO • 29
2. Mafunzo Yanayotokana Na Mafuta Ya Upako
Sasa tuangalie kwa makini zaidi vitu vilivyotumika
katika kutengeneza mafuta ya upako, na yale ambayo
vinadhihirisha kuhusu upako wa Roho Mtakatifu.
Mchanganyiko wa mafuta ya upako, yaani manukato,
ulikuwa na vifuatavyo hasa: manemane, mdalasini, kane,
kida na mafuta ya zeituni (Kutoka 30:23-24).
a. Manemane. Manemane ilikuwa aina ya dawa ya
usingizi na kupunguza maumivu. Ikijulikana kwa harufu
yake tamu, ilitumiwa pia katika kutengeneza marashi na
vipodozi.
Manemane ni kati ya tunu ambazo wale mamajusi
walimletea Yesu (Mathayo 2:11). Pale msalabani, watu fulani
walijaribu kumpa Yesu manemane kwa ajili ya kupunguza
maumivu Yake, lakini aliikataa (Marko 15:23). Kwa kukataa
dawa hii ya maumivu, Kristo Yesu alishikamana na utume
Wake kwamba “Aionje mauti kwa ajili ya kila mtu”
(Waebrania 2:9). Kwa sababu ya harufu yake tamu,
manemane ni kati ya viungo vya manukato ambavyo
vilitumiwa katika kumzika Yesu (Yohana 19:39).
Matumizi ya manemane kwa kupunguza maumivu yana
maana maalum ya kinabii kwa upande wetu. Yesu Kristo,
Masihi (aliyetiwa mafuta) alikuja ili achukue mizigo yetu
pale msalabani. Pale mahali pa dhabihu Yesu alitimiza kusudi
Lake la kuwa Mponyaji wetu (1Petro 2:24) na aliyetuweka
huru na utumwa wa dhambi na mauti (Waebrania 2:9; 14-18).
Kama ishara ya kinabii katika manukato ya upako,
manemane hutufunua jinsi Roho Mtakatifu anavyowaleta
watu katika uponyaji na ukombozi kutoka kuvunjika kwao,
mafungo yao ya dhambi, na magonjwa yao. Nabii Isaya
anatamka kinabii kuhusu uwezo wa upako: “...nayo nira
itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta” (Isaya 10:27).
Neno la Kiebrania lililotafsiriwa “kuharibiwa” ni zaidi ya
kuvunjwa au kuharibika; maana yake ni kuangamizwa
kabisa.
Nguvu ya Roho Mtakatifu inaweza kuwaweka watu huru
na kuwaponya kabisa. Mungu anatutakia tuwahudumie
wengine kwa njia hii kwa upako wa Roho Mtakatifu.
b. Mdalasini. Wakati wa Biblia, mdalasini ulikuwa
adimu, ghali na kuthaminiwa sana (Wimbo ulio Bora 4:14).
Mdalasini una harufu tamu, lakini hujulikana kwa ukali wake
katika vyakula fulani. Kwa hiyo kuwepo kwa kiungo hiki
katika manukato ya upako kunatufunulia moto au juhudi
inayofuatana na upako wa Roho Mtakatifu.
Yohana Mbatizaji alimwelezea Yesu Masihi kuwa ndiye
Yeye atakayetubatiza kwa Roho Mtakatifu na moto (Mathayo
3:11). Neno “moto” katika mstari huu hutafsiriwa na wengine
kuwa kwa ajili ya utakaso katika moyo wa mwamini. Tafsiri
hii ina ukweli kiasi, lakini maana yake ni zaidi. Moto huwa
na uwako mkali na nguvu, tena unakula. Maandiko husimulia
jinsi Yesu alivyoliwa na wivu kwa ajili ya nyumba ya Baba
Yake (Yohana 2:13-17).
Ujasiri Usio Wa Kimaumbile
Kuna mfano wa ujasiri huu wenye moto wa Roho
Mtakatifu katika Agano Jipya. Kabla ya Siku ya Pentekoste,
wanafunzi na waamini wachache waliobaki walikuwemo
pamoja katika chumba kimoja kule Yerusalemu (Matendo
1:12-24). Walikuwa wamekwisha agizwa na Yesu wahubiri
injili katika duniani kote (Matendo 1:8). Kazi hii kubwa
kabisa ingefanywaje na watu wale wachache? Hawakuwa
wahutubu, wasomi wala hata wenye elimu ya juu. Walikuwa
watu wa kawaida, waliozungukwa na utamaduni
uliowachukia ambao ulikuwa umemsulibisha kiongozi wao.
Wanaume na wanawake hao hawakuwa waoga, lakini
walichanganyikiwa, hawakuwa na uhakika wala mwelekeo
wa kutenda nini na kwa njia gani. Lakini walisubiri kwa
hekima, wakiendelea na maombi na kutunza umoja na
kuhamasishana. Ingawa hawakuielewa, walishikamana na
ahadi ambayo Yesu alikuwa amewapa, ya uwezo ujao kutoka
kwa Roho Mtakatifu (Matendo 1:5,8). Kwa hiyo
walisubiri...
“Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa
upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote
waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi
zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila
mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza
kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia
kutamka” (Matendo 2:2-4).
Kwa dakika moja, maisha ya wale watu wapatao 120
yalibadilishwa walipojazwa Roho Mtakatifu! Mara moja,
tukio hili lilijulikana (Matendo 2:5-13). Petro, mvuvi wa
samaki asiye na elimu ambaye alikuwa amemkana Kristo
kwa ajili ya woga, ghafula anasimama na kutoa mahubiri
yake ya kwanza chini ya upako wa Roho Mtakatifu
(2:14-39). Matokeo yake, zaidi ya watu 3000 waliungwa na
Ufalme wa Mungu siku ile ile (2:41).
Wanafunzi walitoka kuwa kondoo wenye hofu na
wasiwasi, wapate kuwa wachungaji wenye ujasiri, ushuhuda
na utendaji wa miujiza! Walitangaza Injili pasipo aibu, hata
kwenye mateso na kifo. Ndiyo juhudi yenye moto
inayotokana na upako wa Roho Mtakatifu (Matendo
4:23-31).
Juhudi hii si hisia ya kibinadamu inayopita na
kutoweka. Ni nguvu na ujasiri inayowaka kama moto kutoka
ndani yetu tunapokuwa na upako wa Roho Mtakatifu. Ni
imani yenye uhakika katika ukweli wa Neno la Mungu na
Injili ya Yesu Kristo ambayo inatuhamasisha tutende,
tuombe, tuhubiri, tuamini mwujiza - yote kwa uwezo wa
Roho Mtakatifu!
c. Kane (calamus). Huu ni mmea unaofanana na muwa,
ambao mzizi wake ulipendwa sana na watengeneza marashi.
Harufu yake tamu ilitolewa kwa kuponda mzizi wa mmea.
Vile vile, kuna aina ya kupondwa kwa maisha ya
mwamini ambayo ni ya lazima kwa ajili ya kuachia harufu
tamu ya kuwepo kwa Mungu ndani yetu.
Tafadhali angalia kwamba aina hii ya kupondwa si sawa
na aina ile ya kuvunjwa na kuharibiwa inayotokana na
kufanya uchaguzi wa dhambi na uasi. Badala yake, aina hiyo
ni kuvunjwa kutakatifu kunakotoka katika mkono wa Mungu
peke yake.
Huku kupondwa kiroho, ingawa mara nyingine
kunaumiza, kunazalisha matunda mawili:
Kwanza, kunafisha mwili wetu - tamaa zetu za kibinafsi
na kujitegemea kwetu (Luka 9:23-26; Warumi 12:1-2; 13:14;
Wagalatia 5:16-26).
Pili, huku “kuvunjwa wazi” kwa maisha yetu
kunaruhusu neema na uwezo zaidi ya Mungu kudhihirishwa
ndani yetu na kupitia kwetu. Paulo ameandika kuhusu hali hii
katika barua yake kwa Wakorintho (2Wakorintho 12:7-10).
30 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1
Mchungaji kwa Mchungaji: Kama viongozi wa
kanisa, tunaona haja ya kuwa na nguvu, ujasiri na
ustadi. Matokeo yake yanaweza kuwa hatumwachii
Roho Mtakatifu nafasi ya kuwa na uweza kupitia kwetu.
Kuna aina ya udhaifu inayofaa ambayo inatufanya
tumwegemee Roho Mtakatifu itupasavyo na
kutegemea upako Wake katika maisha yetu. Ndipo
huduma inatolewa kwa uweza Wake na si kwa nguvu
yetu.
Kuna msingi wa ki-Maandiko kwa aina ya
kupondwa inayofuatana na upako wa Roho Mtakatifu.
Hatuwezi kuepuka kupondwa huku, tena haitupasi
tukuepuke. Ni sehemu ya lazima ya kupevuka katika
mfano wa Kristo - kukituongoza katika maisha ya
kujitoa, kutegemea na kutii kuliko hali nyingine yoyote.
Tafadhali tumia dakika chache katika kusoma
mifano ifuatayo ya Maandiko, ukitafakari ukweli uliomo
katika kila moja:
• Yesu - Isaya 53:1-6; Matendo 3:18; Waebrania
5:9; 12:2
• Paulo (na wengine) - Matendo 9:15-16; Warumi
8:18; 2Wakorintho 1:3-7; 4:7-18; 6:4-10; 11:22-30;
12:7-10
• Waamini wote - 1Wathesalonike 2:14-16;
2Timotheo 3:12; 1Petro 4:1-19
Kujikana Kunakoleta Uhai
Kanuni iliyo na nguvu kubwa ya kuvunjwa na kupondwa
inaonekana katika ishara nyingine za ki-Maandiko pia. Kwa
mfano, katika Ushirika Mtakatifu kuvunjwa na kupondwa
ni lazima katika utengenezaji wa mkate na divai (Luka
22:14-20; 1Wakorintho 11:23-26). Yesu alitumia mkate
(ngano iliyovunjwa na kupondwa) na divai (zabibu
zilizopondwa) kama ishara ya yale ambayo alikuwa atende
kwa ajili ya wanadamu wote katika kusulibiwa Kwake.
Yesu Kristo alibeba hukumu ya Mungu juu Yake kama
adhabu ya haki ya dhambi zetu zote. Kifo Chake kwenye
msalaba kinafunua kupondwa kutoka kwa Mungu kwa mara
ya mwisho kwa ajili ya kufungua uzima (Matendo 2:23-24) -
uzima wa milele wa wokovu kwa kumwamini Yesu.
Tumshukuru Mungu kwamba hatulazimiki sisi tupitie mateso
haya, ingawa ndiyo adhabu ya haki ya dhambi yetu na uasi
wetu!
Lakini kuna kufia ubinafsi wetu ambako ni lazima ili
uzima na uweza wa Mungu ndani yetu ufunguliwe kupitia
kwetu. Hii SI aina ya kujitoa mhanga au kujitesa ili
“kuthibitisha” hali yetu ya juu ya kiroho. Lakini sharti la
kutembea na Kristo na kumtumikia kikamilifu linadai uhiari
wa kuishi maisha ya kujikana na kunyenyekea mapenzi ya
Mungu hata kujitolea kama dhabihu (2Samweli 24:18-24;
Luka 9:23-26).
Kupata Kuwa Vyombo Vinavyoaminika
Msimamo wa Yesu katikati ya mateso ni mfano wetu
bora: “...ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake
aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi
mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu” (Waebrania
12:2). Yesu alikubali kikamilifu makusudi ya Mungu Baba
katika mateso na dhabihu Yake.
Bila shaka, Yesu hakufurahia mateso (Luka 22:42-44).
Lakini alitambua ulazima wa msalaba (Luka 24:46-49).
Uhiari wake wa kuteseka na kufa kwa niaba yetu
haukufungua tu wokovu wetu, bali pia ulikuwa tendo la kutii
ili atimize mapenzi ya Baba Yake (Mathayo 26:39,42,44).
Mateso yetu na dhabihu zetu ni vidogo kulingana na yale
ambayo Yesu alitoa kwa ajili yetu, lakini hata hivyo ni
vigumu. Lakini tunayo baraka ya ahadi ya ajabu ya Mungu
kwamba anatumia mateso yetu kwa utukufu Wake pamoja na
ufanisi wetu kwa wakati mmoja (Yakobo 1:2-5,12). Mungu
ameahidi kuchukua mateso na dhiki yetu katika maisha haya
na kuvibadilisha viwe na hatima yenye baraka (Warumi
5:1-5; 8:18; 2Wakorintho 4:17).
Ahadi ya Baba yetu kwetu imetamkwa wazi: “Nasi
twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi
pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani,
wale walioitwa kwa kusudi lake” (Warumi 8:28). Na “kusudi”
la Mungu kwa ajili ya walioamini ni nini? Limetajwa wazi
kabisa katika mstari unaofuata: “...wafananishwe na mfano
wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni
mwa ndugu wengi” (Warumi 8:29).
Mungu anataka kutumia mambo yote katika maisha yetu
akitutengeneza katika mfano wa Kristo, vyombo vinavyofaa
kwa matumizi ya Bwana (2Timotheo 2:19-21). Mara
nyingine mateso yetu hutokana na kuharibika kwa dunia hii
na asili ya dhambi ya watu waliomo ndani yake. Wakati
mwingine Mungu anaweza kutumia matukio ya maisha yetu
kwa ajili ya matumizi na makusudi Yake. Kwa pande zote,
Mungu ameahidi kuyatumia kwa manufaa yetu.
Mungu atatubadilisha kwa njia itakayotufanya tuwe
vyombo safi na vinavyoaminika vya mapenzi na makusudi
Yake, vikiruhusu upako wa Roho Mtakatifu utiririke kupitia
kwetu pasipo kuzuiliwa. Lakini ni lazima tushirikiane na
kutii kazi Yake katika maisha yetu!
Harufu Tamu Ya Kristo
Kila mwamini wa Kristo, na hasa kila kiongozi wa kanisa,
ameitwa “adhihirishe harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa
kazi yetu. Kwa maana sisi tu manukato ya Kristo, mbele za
Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea”
(2Wakorintho 2:14-15). Nukato hii ya uhalisi wa kuwepo kwa
Mungu itatolewa kwa njia ya maisha yetu tunapokubali
“kupondwa” na Yeye katika kazi Yake ya kutubadilisha.
Katika Maandiko yote, na hata leo, Mungu amewatumia
wanaume na wanawake wa kawaida kwa njia za uwezo
mkuu. Mara nyingi, wanavumilia kusongwa na kupondwa
katika maandalizi yao na wakati wa huduma yao. Lakini kwa
sababu yake, makusudi ya Mungu yanatimizwa na harufu
tamu ya Mungu inatolewa kwa njia ya maisha yao. Ni vema
kukumbushwa tena kwamba hakuna wanaume na wanawake
wakuu wa Mungu - waliopo tu ni wanaume na wanawake
wanyenyekevu (waliovunjika, waliojitoa) ambao
wanatumiwa na Mungu katika mambo makuu!
d. Kida. Kida ni ganda la mmea unaofanana na
mdalasini. Kida ilitumiwa kama dawa ya kuharisha wakati
wa Biblia. Kama ishara katika mafuta matakatifu ya upako,
kida huwakilisha kazi ya kutakasa katika upako wa Roho
Mtakatifu.
Ni kweli kwamba upako wa Roho Mtakatifu unatupatia
nguvu, karama na uwezo wa ki-Mungu. Lakini pamoja na
haya, kazi ya Roho Mtakatifu ni kubadilisha maisha ya wale
anaowatia mafuta.
Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO • 31
Tunaweza kujifunza mfano wazi kabisa wa umuhimu wa
kazi hii katika maisha ya Mfalme Sauli. Samweli alimtia
mafuta Sauli awe mfalme juu ya Israeli (1Samweli 10:1).
Sauli alitengwa kwa ajili ya kusudi rasmi la Mungu kwamba
awe mfalme. Upako ulimpa Sauli mamlaka, karama na
uwezo wa kutendea kazi yake aliyopewa na Mungu.
Maandiko yanafunua mengi zaidi ambayo Sauli
aliyapokea pamoja na upako wake: “Na roho ya Bwana
itakujilia kwa nguvu, nawe utatabiri pamoja nao, nawe
utageuzwa kuwa mtu mwingine” (1Samweli 10:6). Ndipo
baadaye kidogo: “Ikawa, alipogeuka kumwacha Samweli,
Mungu akambadilisha moyo” (ms. 9).
Tunaweza kuona kwamba upako haukumwandaa tu
Sauli na yale aliyohitaji, bali pia ulimbadilisha. Haya
yalimfanya astahili na awe chombo kilichofaa zaidi sana
mkononi mwa Mungu. Hii ni picha nzuri ya kutia moyo ya
yale ambayo upako wa Roho Mtakatifu unaweza kutupatia
sisi pia kama vyombo au zana za Mungu.
Inasikitisha kwamba Sauli (kama wengine) alivipa
kisogo vile vyote ambavyo Mungu alimpatia, kwa kukataa
Neno la Mungu na amri Zake na kufuata mapenzi yake
binafsi (1Samweli 15:22-33). Ni huzuni kubwa kwamba
ufalme ulioanza kwa fahari juu ya Israeli uliishia katika aibu
kwa Mfalme Sauli na familia yake.
Mchungaji kwa Mchungaji: Mungu alimpa
Mfalme Sauli vyote alivyohitaji ili atimize wajibu wake
na awe mfalme mwenye ufanisi. Sauli alifanya hivyo
kwa muda, akafanikiwa. Lakini inasikitisha kwamba
baadaye Sauli alichagua kufanya mapenzi yake binafsi
badala ya kutii maagizo ya Mungu, na mwisho wake
ulikuwa kushindwa.
Mungu anapotuita, anatupatia vile tunavyohitaji ili
tutimize mapenzi Yake. Lakini usisahau kamwe
kwamba yale ambayo Baba anatutengeneza tuwe ni
muhimu kama yale anayotuita tutende. Mungu
anataka tubadilishwe, tupate kufanana na Kristo katika
tabia zetu na matendo yetu.
Baba yetu anatutakia tutii Neno Lake na
kumwamini katika mambo yote. Hatutapevuka hadi
mahali ambapo hatutahitaji tena kukua na kuitikia kazi
ya kubadilishwa kwetu na Roho Mtakatifu! Ni mfuatano
wa maisha yetu yote.
Roho Mtakatifu atatusahihisha, kutuonya na
kututhibitishia. Mungu hatuhukumu (Warumi 8:1) lakini
anatudai kwamba tumtii na kukubali kazi Yake ya
kutubadilisha. Mara nyingine tunaweza kujikwaa au
kuanguka; lakini ni lazima tutubu haraka na kurudi
katika mfuatano wetu na kujitoa kwetu kwa Mungu na
mapenzi Yake.
Mungu anatenda kazi ya kutubadilisha:
• Kwa utukufu Wake;
• Kwa furaha, amani na baraka yetu; na
• Kutufanya tuzae matunda na kuwa na ufanisi
zaidi kama mabalozi na watumishi Wake kwa wengine
katika huduma.
Kuitikia Kazi Ya Roho Mtakatifu
Katika kuangalia kida, tumejifunza kuhusu kazi ya
kimsingi ya Roho Mtakatifu. Anakuja kuondoa na kusafisha
yale yasiyofuatana na maisha, tabia na Nafsi ya Kristo. Ishara
hai ya mtu mwenye upako halisi ni kwamba anazidi kufanana
na Kristo katika tabia yake - si lazima aoneshe uwezo,
karama wala huduma maalum.
Kama viongozi wa kanisa, ni lazima tumruhusu Roho
Mtakatifu aendelee wakati wote kushughulikia madhaifu
yetu ya kimwili, majaribu yetu na kushindwa kwetu. Lazima
tusimhuzunishe Roho Mtakatifu kwa kupinga kazi Yake ya
kuleta mabadiliko ndani yetu (Waefeso 4:30).
Tutavuna tulizopanda, kama ni mbegu za haki na baraka,
au za uozi (Wagalatia 6:7-8). Mungu atatuwekea kipimo
kikali zaidi kama viongozi (Yakobo 3:1). Usidanganyike;
Mungu hadanganyiki. Ukiendelea katika dhambi, hatimaye
itadhihirika wazi kwa wote (Hesabu 32:23).
Kwa hiyo uchague haki! Uitikie kazi ya Roho Mtakatifu!
Umtii na kumwamini Mungu! Upokee upako Wake juu ya
maisha yako na utumishi wako! Uwe mfano kwa wengine wa
chombo chenye kuitikia, kufundishika na kujitolea kwa kazi
ya Roho Mtakatifu. Umruhusu Yeye atende kazi ndani yako,
ili apate kutukuzwa hata zaidi kupitia kwako! Amina!
e. Mafuta Ya Mzeituni. Mafuta ni ishara inayotumika
mara nyingi kabisa katika kumwashiria Roho Mtakatifu
katika Agano la Kale na Agano Jipya. Mafuta ya mzeituni
kama sehemu ya mafuta matakatifu ya upako yana maana
mazito sana. Huwa na sifa za sehemu zile nne zote nyingine,
nao unaongeza sifa nyingine pekee.
Katika wakati wa Biblia, mafuta ya mzeituni:
• yalitumiwa kama dawa, kuponya magonjwa na maumivu
(kama manemane);
• yalitumiwa katika taa, na kuhusiana na moto (kama
mdalasini);
• yalitengenezwa kwa kupondwa na kusongwa, yakitoa
harufu tamu (kama kane);
• yalitumiwa kwa kusafisha na kutakasa kwa nje na kwa
ndani (kama kida).
Lakini mafuta ya mzeituni yana sifa maalum iliyo ya
lazima katika Mwili wa Kristo. Yanalainisha. Yanapowekwa
katikati ya vitu viwili, yanapunguza kusuguana na kuleta
utelezi.
Ishara hii inatufunulia ulazima wa umoja kati ya watu
wa Mungu. Maandiko yanatufunulia hoja hii ya kuhusisha
upako na umoja kwa njia inayopendeza sana: “Tazama, jinsi
ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa
umoja. Ni kama mafuta mazuri kichwani, yashukayo ndevuni,
ndevu za Haruni, yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.
Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni.
Maana ndiko Bwana alikoamuru baraka, naam, uzima hata
milele” (Zaburi 133).
Umoja kati ya watu wa Mungu ni chanzo cha furaha na
amani. Mungu anapendezwa wakati watu Wake
wanapotembea pamoja katika mahusiano sahihi. Baraka Yake
inafunguliwa na upako wa Roho Mtakatifu unatiririka kwa
uhuru zaidi.
Uhusiano Wa Wanamuziki
Maana ya umoja katika Biblia hayaeleweki vizuri mara
nyingi. Katika Maandiko, umoja ni tofauti na ufanani.
Ufanani maana yake ni kwamba vyote vifanane, kama
vile nguo za sare, pasipo tofauti yoyote.
Lakini maana ya umoja katika Maandiko ni kama kundi
la wanamuziki wanaotumia vyombo mbalimbali kwa
ulinganifu. Kila chombo kina kazi yake tofauti. Lakini
32 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1
vinapotumika pamoja chini ya kiongozi mkuu, vinafanya
kazi moja. Kwa hiyo muziki inayotokea inapendeza sana.
Ndiyo hali halisi pia katika Mwili wa Kristo. Kuna
vipawa, wito, mitindo, watu na uwezo tofauti. Lakini sisi sote
tumeitiwa uhusiano wa ulinganifu (Yohana 17:20-21).
Hakuna mtu yeyote anayefanana kikamilifu na mwingine;
lakini kila mmoja ameitwa afanye kazi katika nafasi yake.
Ndipo Mungu anaongoza washiriki wote katika muziki
inayopendeza - katika Mwili Wake, wakipendana kama
ushuhuda kwa ulimwengu (Yohana 13:34-35).
Paulo anaongea kuhusu haya anapoeleza kuhusu karama
za mafunuo za Roho katika 1Wakorintho sura ya 12 (taz. pia
1Wakorintho 14:26-40). Kanisa la awali lilikuwa mfano wa
umoja huu, uliositawishwa kwa uwepo wa Roho Mtakatifu
mwenye kuleta upako (Matendo 2:42,44-47).
Hatari Za Ukosefu Wa Umoja
Ukosefu wa umoja kati ya viungo vya Mwili wa Kristo
una madhara yake mapana sana. Paulo aliwakemea
Wakorintho kuhusu kugawanyika au kutengana kwao
(1Wakorintho 3:1-23). Aliwaita watu wa mwilini na
wasiopevuka: “Kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia
ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! si
watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya
kibinadamu?” (ms. 3).
Ukosefu wa umoja na mgawanyiko kati ya ndugu ni kosa
zito. Siyo tu kwamba huleta uharibifu; huzuia pia wepesi na
ufanisi wa kazi ya Ufalme wa Mungu. Maelezo ya Paulo
kuhusu karama za mafunuo yaliyotajwa hapo juu
yalisababishwa na ukosefu wa utaratibu na hali ya
mgawanyiko iliyosababishwa na kiburi na ubinafsi wa watu.
Inayosikitisha zaidi ni ukweli kwamba watu ambao ni
viungo vya Mwili wa Kristo wasipopendana na kutumikia
makusudi ya Bwana kwa umoja, ushuhuda wetu mbele ya
ulimwengu inazuiwa sana. Biblia inatukumbusha kwa bidii
kwamba ulimwengu utajua kuwa sisi ni Wakristo kutokana
na upendo uliopo kati yetu (Yohana 13:35). Kama
ulimwengu hauoni uwepo wa upendo kati yetu, ushuhuda
wetu kwa ulimwengu hauna uhakika wowote.
Tunaweza kufanya matendo makuu katika jina la Kristo;
kuwa mhubiri wa ajabu; kupanga mikutano ya hadharani; na
mengi zaidi. Hata hivyo, kama sisi hatupendi ndugu zetu
Wakristo, matendo hayo hayataleta tukio lililotakiwa
(1Wakorintho sura ya 13).
Kuna hamasa nyingi katika Maandiko kuhusu hatari ya
misimamo inayovunja au kuzuia umoja katika Mwili wa
Kristo. Tafadhali utumie dakika chache katika kusoma
mistari ifuatayo:
• Warumi 13:13-14
• Wagalatia 5:13-23
• Waefeso 4:20-29
• 1Timotheo 6:3-5
• Tito 3:9-11
• Yakobo 3:14-16
• 1Yohana 2:9-11; 3:10-18
Mistari hiyo inaonesha wazi kwamba palipo na
mgawanyo, magomvi, chuki, uchungu, wivu, mashindano,
MATENDO • 33
Kanisa: umoja unaokubaliana kama kwaya au kundi la wanamuziki...
kila mtu na kila chombo ni muhimu
Ukosefu wa umoja na
mgawanyiko kati ya ndugu ni kosa
zito. Siyo tu kwamba huleta
uharibifu; huzuia pia wepesi na
ufanisi wa kazi ya Ufalme wa
Mungu.
Nakala 16 / Nambari 1
hasira, n.k., umoja unazuiwa na hata kuvunjwa. Hali hii
inamhuzunisha Roho Mtakatifu (Waefeso 4:30) nayo
inaweza kuzimisha uwepo Wake uletao upako
(1Wathesalonike 5:19).
Ni wazi kwamba palipo na misimamo ya kimwili kama
hii, ibilisi anafanya kazi yake ya siri alete mgawanyo na
kuzuia kazi ya Mungu (Yakobo 3:13-16). “Gawanya na
kushinda” ni mkakati wa zamani kama ibilisi mwenyewe -
mkakati ambao amejifunza kuutumia kwa ufanisi katika
kuzuia na kujaribu kuangamiza Mwili wa Kristo. Lakini
mikakati yake inafanikiwa ikiwa tu sisi tunashirikiana nayo!
Mahusiano: Yanathaminiwa Na Mungu
Upako wa Roho Mtakatifu utaleta uponyaji na
upatanisho wa mahusiano ndani ya Mwili. Hali hii iwe ya
kweli hasa kati ya viongozi. Mungu anatutazamia sisi tuishi
katika uhusiano ufaao - kwanza kwa Yeye, halafu kwa
wenzetu (Waefeso 2:14-17). Ni kiburi, wivu na ubinafsi
wenye uchungu, vyote vya kibinadamu, ambavyo vinamzuia.
Misimamo hii ndiyo ibilisi atakayoitumia akipanda
mgawanyo, chuki na kutosameheana katika Mwili.
Ukiona kuwa ndugu yako ana neno juu yako, nenda
ukajaribu kupatana naye (Mathayo 5:23-24). Ukiwa na neno
juu ya mtu mwingine, uwe mwepesi KUTUBU! (Mathayo
5:21-22). Utubu kuchukizwa na kuruhusu hasira, chuki na
misimamo ya kuhukumu viweke mizizi moyoni mwako.
Uwasamehe wengine, ili hukumu ya Mungu isikuangukie
wewe (Mathayo 6:14-15; taz. pia Mathayo 18:21-35).
Mungu anatilia mkazo mkuu mahusiano - mpaka
alimtuma Mwana Wake ateseke na kufa ili uhusiano wetu na
Yeye uliovunjwa na dhambi yetu uweze kurejeshwa. Kwa
njia hii hii, upendo na msamaha Wake kwetu unawezesha
mahusiano yafaayo kati yetu sisi kwa sisi.
Tumejifunza kwamba yale ambayo
Mungu anayaamuru, wakati wote
anayawezesha pia. Naye ametuamuru tuwe
na mahusiano yafaayo kati yetu (Yohana
13:34-35).
Lazima tuthamini na kuwekea
dhamana uhusiano wetu na Mungu. Na ni
lazima pia tufanye hivyo katika uhusiano
wetu na ndugu na dada zetu katika Kristo.
Utumishi wote wa kudumu na
kubadilisha maisha hutokana na
mahusiano yenye afya bora. Mfuatano
huu unaanza na yale tunayopokea kutoka
kwa Mungu katika uhusiano wetu na Yeye.
Ndipo, kutokana na upendo na huruma na
yale tuliyopokea kutoka kwa Mungu,
tunawatolea na kuwatumikia wengine.
Ndio mtindo wa Mungu kwa ajili ya
utumishi. Maisha ya Yesu hapa duniani ni
mfano wa kudumu wa aina hii ya mtindo
wa utumishi kwa ajili yetu.
Umoja, Tofauti, Upendo
Kuna tofauti za kuelezana au
mawasiliano katika Mwili wa Kristo.
Lakini si lazima tofauti hizi zilete vikwazo
kwa umoja na uhusiano (Warumi 14:13).
Kumbuka, umoja si ufanani. Umoja ni
uhusiano wa ulinganifu tunapoitikia kazi ya ndani ya upako
wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu. Roho Mtakatifu
wakati wote atatuthibitishia, kutusaidia na kutuongoza katika
uhusiano unaofaa pamoja na wengine - kama tutamwitikia.
Mwongozo rahisi kwa ajili ya umoja umeelezwa hivi:
“Katika mambo ya lazima ya msingi - umoja; katika yasiyo
ya lazima ya msingi - tofauti; katika yote - upendo.”
Tunapokua na kuishi katika upako wa Roho Mtakatifu,
tuwe na neema na upendo sisi kwa sisi. Tukifanya hivyo,
upako wa Roho Mtakatifu na ushuhuda wa Kristo
vitafunguliwa zaidi ndani yetu na kupitia kwetu!
Kupata Ufahamu
Mafunzo haya mafupi kuhusu mafuta matakatifu ya
upako (Kutoka 30:22-33) yametufunulia kwamba Mungu
ametupatia picha na ishara ya ajabu ya utangulizi wa kazi ya
Roho Wake Mtakatifu. Kwa hakika, masomo yetu ya
Maandiko hutupatia ufahamu, hekima na tumaini (Warumi
15:4).
Katika mafunzo haya hadi hapa, huenda wewe una
maswali, kwa mfano:
• Je, ninaweza kukua katika upako? Kama ndiyo, kwa njia
gani?
• Je, kuna “upako wa uwongo”? Kama ndiyo, ninawezaje
kutambua upako wa kweli?
• Nini inaweza kudhuru au kuzimisha upako katika maisha
yangu?
• Je, ninaweza kuendelea wakati wote kujaa upako wa
Roho Mtakatifu?
Tutajadili maswali haya na mengine katika sehemu
ifuatayo, “Kutembea Katika Upako”.
34 • MATENDO
Roho Mtakatifu
atatuongoza
katika mahusiano
yanayofaa.
Nakala 16 / Nambari 1
Tunapoanza kujifunza kuishi siku kwa siku katika upako
wa Roho Mtakatifu, turejee kwa kifupi kanuni za kimsingi
zilizo muhimu sana.
Upako wa Roho Mtakatifu si “nishani ya kiroho” ya
kujitafutia. Wala si uzoefu kwa maneno na matamshi ya
kidini. Bali ni uhusiano na Roho Mtakatifu wenye uhai
ambao unaendelea kukua.
Kumbuka, Roho Mtakatifu ni Nafsi, kama vile Yesu na
Baba ni Nafsi. Kwa hiyo tunaweza - na inatubidi - tujifunze
kutembea katika uhusiano ulio hai wa siku kwa siku pamoja
na Roho Mtakatifu.
Tumejifunza kwamba upako si aina fulani ya nguvu ya
kifumbo isiyoeleweka, ambayo tunapewa ili tuitumie kwa
ajili ya makusudi yetu binafsi. Bali upako ni uwezo wa
ki-Mungu, upaji unaohusiana moja kwa moja na Nafsi ya
Roho Mtakatifu na kuwepo Kwake katika maisha yetu.
Uwezo unaotokana na kuwepo kwa Roho Mtakatifu unapitia
uhusiano wetu binafsi na Yeye.
Upako ni Nafsi ya Roho Mtakatifu na kuwepo
Kwake, vikileta pamoja na kuwepo Kwake uwezo,
karama na mamlaka vyote vinavyohitajika kwa ajili ya
kutimiza mapenzi ya Baba kwa muda fulani maalum ya
utumishi au kazi.
Wajibu Wetu Wa Kwanza
Tumejifunza kwamba wakati wa Agano la Kale, Roho
Mtakatifu wa Mungu “aliwajia” manabii, makuhani,
waamuzi na watumishi Wake wengine.
Wakati wa Agano Jipya na baadaye - kipindi kiitwacho
pia Kipindi cha Kanisa - Roho Mtakatifu amekuwa
akimiminwa (Matendo sura ya 2). Mungu Roho anaishi
ndani ya kila mwamini wa kweli, amwongoze na kumfariji,
na kuwahudumia wengine kupitia kwake (Yohana 7:37-39;
14:16-17,26).
Waamini wote wa Yesu Kristo wamepewa Roho
Mtakatifu kwa kipimo fulani (1Yohana 2:20,27). Hali hii ni
lazima kwa sababu kila mwamini ameitiwa aina fulani ya
huduma kama kiungo cha Mwili wa Kristo (Waefeso 4:12).
Sisi sote tunahitaji msaada wa Roho Mtakatifu kila siku!
Lakini kwa watu wanaoitiwa utumishi maalum, kuna
upako maalum na mzito unaopatikana. Upako huu unatolewa
na Mungu katika ufalme Wake. Mtu anaweza ama kuupokea
na kukua ndani yake, ama aamue kuukataa au kutoujali.
Aina hii ya upako (kuwezeshwa ki-Mungu na Roho
Mtakatifu) inahusiana moja kwa moja na vipawa vyako na
wito wako. Kwa mfano, mtu aliyeitwa atumie kipawa cha
uinjilisti (Waefeso 4:11) huenda hana upako wa kipawa cha
kimtume. Atafanya vema na kuzaa matunda zaidi ndani ya
uwezo, karama na mamlaka ambavyo amepewa upako kwa
ajili yake - katika mfano huu, kama mwinjilisti.
Lakini katika utendaji wa kila siku, inawezekana si rahisi
namna hii. Ingawa mtu fulani ameitiwa na kupewa upako
kwa ajili ya kazi fulani ya utumishi, kila mmoja wetu bado
ana wito wa kawaida kama mwamini wa Kristo, wa kuishi na
kufanya kazi kila siku kama mshirika wa Mwili wa Kristo.
Kwa mfano, kufuatana na yale tunayoona katika
Maandiko, Timotheo aliitwa afundishe na kuwa mchungaji
katika kanisa. Lakini pia aliagizwa na Paulo: “Fanya kazi ya
mhubiri wa Injili” (2Timotheo 4:5) - si kwamba awe
mwinjilisti, ila mara nyingine afanye kazi iliyohitajika kwa
ajili ya kuwapatia wengine habari njema ya Injili.
Kwa hiyo, tunaona kwamba sisi kama watumishi wa
Kristo, tuna wajibu wa kawaida na kazi ambazo huenda
hazihusiani na wito wetu pekee. Lakini hata hivyo ni za
lazima na muhimu kwa ajili ya ufanisi na afya katika Mwili
wa Kristo.
Wajibu wetu wa kwanza na wa msingi kama waamini wa
Yesu Kristo, na kama viongozi wa kanisa, ni utii kwa Kristo.
Lazima tumtii Bwana na kuishi kufuatana na kanuni ambazo
Yeye ametupatia katika Neno la Mungu.
MATENDO • 35
SEHEMU YA III
KUTEMBEA KATIKAAPAKO
Upako wa
Roho
Mtakatifu
Nakala 16 / Nambari 1
Katika Maandiko, tunaona kwamba waamini wamepewa
wajibu nyingi: kuwahudumia wengine, kuwapa maskini
chakula, kutunza yatima, kuwaandaa watakatifu, kuwafikia
waliopotea - orodha inaendelea. Kutakuwa na nyakati na
misimu katika maisha yako pamoja na Kristo ambapo
utahitaji kutumia wakati na bidii katika aina hizi za huduma
ya kuwafikia watu, pamoja na wito wako au kazi yako pekee.
Mwongozo mzuri wa kufuata katika kutambua yale
ambayo wewe unapaswa uyafanye katika huduma ni huu:
“Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa
nguvu zako” (Mhubiri 9:10; taz. pia Wakolosai 3:23).
Uombee kila nafasi inayotokea, na halafu uwe mwepesi
kumtii Bwana anapokuita uwahudumie wengine. Haidhuru
kama kazi iliyo mbele yako ni kubwa au ndogo - iliyo
muhimu ni kwamba Bwana anapokuagiza ufanye kazi fulani,
umtii Yeye!
Mchungaji kwa Mchungaji: Nafasi yangu ya
kwanza ya “kikazi” kama mtumishi aliyehitimu Shule ya
Biblia na kupata leseni yangu, ilikuwa kama mlinzi wa
kanisa fulani kubwa. Nilikaa miaka miwili nikisafisha
vyoo, kutupa takataka, kufagia vyumba vya mikutano,
kuokota takataka kwenye bustani na kufanya kazi
nyingine zisizochangamsha lakini zilizo za lazima.
Sikufurahia kazi hii. Haikuwa rahisi. Tena iliaibisha.
Lakini nilijua kwamba Mungu aliniagiza nifanye kazi
hiyo, nayo ilikuwa maandalizi bora kabisa kwa ajili ya
kutumikia Mwili wa Kristo. Kwa hakika ilikuwa mtihani
kwa uaminifu wangu.
Utiifu wangu kwa kazi hii na bidii yangu katika
kuitekeleza vilinifungulia mlango wa kazi nyingine, na
ndivyo nilivyoendelea katika kila kazi ya utumishi
niliyofanya katika miaka yote. Nimeanzisha makanisa,
kufundisha vijana, kuwa mchungaji wa usharika,
kuhutubia mikutano, kuongoza timu za misioni, na
mengine mengi. Na kwa neema ya Mungu, katika
muda ule wa miaka 30, Bwana aliniandaa na
kunifikisha hapo nilipo sasa katika nafasi ya kuongoza
huduma ya ulimwengu mzima.
Naamini kabisa kwamba nisingekuwa nikiongoza
World MAP leo kama nisingalikuwa tayari kumtii Bwana
kwa uwezo wangu wote katika njia ile yote - hatua kwa
hatua, nikitimiza kila kazi - haidhuru aliniomba nifanye
nini katika jina Lake. Sikutii kikamilifu kila wakati, pia
nimefanya makosa mara kwa mara. Lakini kwa jumla,
nilifanya nilivyoweza katika kufuata njia ya utiifu
ambayo Mungu alikuwa ameweka mbele yangu.
Mungu ana mpango kwa ajili ya maisha yako. Yeye
anajua njia bora ya kukuwezesha kutimiza mpango
huu. Utiifu wetu kwa Mungu na Neno Lake si hiari yetu
- ni ya lazima!
Wito Wetu Wa Kwanza
Haidhuru cheo chetu cha uongozi au utawala, wito wetu
wa kwanza sikuzote ni kwa uhusiano wetu na Kristo.
Uhusiano huu ni katika utiifu, uaminifu, huduma, utakaso
binafsi, unyenyekevu, matunda yote ya Roho (Wagalatia
5:22-23) na kuendelea kukua. Tabia hizi zinaweka msingi wa
uhusiano na Yesu Kristo ulio wa thamani na usitawi. Tokeo
moja la msingi huu imara wa uhusiano binafsi ni
kufunguliwa kwa huduma kupitia kwako, na upako
utakaohitaji ili utimize kazi zako za utumishi. Tukikumbuka
marejeo haya ya msingi ya kanuni muhimu, tuangalie sasa
kwa makini zaidi maana ya Kutembea Katika Upako.
A. KULINDA UPAKO
Roho Mtakatifu anapotutia mafuta kwa ajili ya huduma,
ni heshima takatifu. Ni hali ambayo inatubidi tuikuze na
kuilinda katika maisha yetu.
Bila shaka, maana yangu si kwamba Roho Mtakatifu
(anayetutia mafuta) anahitaji ulinzi wetu. Bali inatubidi
tulinde moyo wetu na maisha yetu kwa ajili ya uchafu wa
kiroho na kimaadili wa dunia hii (2Petro 1:2-4; 1Yohana
2:15-17).
Sulemani, mwandishi wa Kitabu cha Mithali,
anatuhimiza: “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;
maana ndiko zitokako chemchemi za uzima” (Mithali 4:23).
Ni kupitia maisha yetu kwamba upako wa Roho Mtakatifu
utatiririka katika huduma kwa wengine. Kwa hiyo ni lazima
maisha yetu, moyo wetu, vilindwe katika utakaso.
1. Panya Katika Kisima
Paulo alisema kuwa kila mwamini wa Kristo ni “hekalu
la Roho Mtakatifu” (1Wakorintho 6:19-20). Kwa hiyo,
tunahimizwa tusiruhusu “hekalu” letu lichafuliwe kwa
kushiriki dhambi (taz. pia Warumi sura ya 6).
Biblia ina hamasa nyingi kuhusu kuendelea katika usafi
wa mwili, nafsi na roho (1Yohana 3:2-3). Maelezo haya ni
kwa ajili ya kila mwamini, na hasa viongozi katika Mwili
wa Kristo!
Kwa nini usafi (utakaso) wetu binafsi ni muhimu sana?
Kwa sababu Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu - kila mmoja
wetu aliyekombolewa “kwa damu ya thamani, kama ya
mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo“
(1Petro 1:19), si kwa damu ya fahali na mbuzi (Waebrania
9:13-14). Tunaposhiriki matendo au misimamo ya dhambi,
mahali ambapo Roho Mtakatifu anataka kukaa huchafuliwa
na kunajisiwa.
Kuhifadhi Usafi
Tuseme kuna shamba au kijiji chenye kisima kimoja tu
cha maji. Watu wote wanatumia kisima hiki na kutegemea
maji yake. Maji hutumiwa kwa kuoga, kupika, kufua na
kunywa. Je, unaweza kubuni hali ya kuhitaji kutumia maji
haya, ukaona panya mfu walioelea juu yake?
Huu ni mfano wa wazi jinsi uchaguzi wetu unavyoweza
kugusa hekalu la Roho Mtakatifu ndani yetu. Yeye ni
chemchemi yetu kwa ajili ya mahitaji yote ya maisha ya kila
siku. Lakini si maisha yetu tu. Roho wa Mungu ndani yetu,
kama viongozi wa kanisa, anatusaidia tuwe chemchemi ya
ki-Mungu kwa ajili ya wengine.
Kwa hakika, katika utumishi tunawapatia wengine
kutokana na tulivyo wenyewe na yale tuliyopokea (Mathayo
10:8; taz. pia mfano wa Bahari ya Galilaya na Bahari ya
Chumvi katika Sehemu Ya II, C 2). Lakini itakuwaje kama
tumeruhusu “panya” kuingia katika maisha yetu? Kwa
hakika kuwepo kwa tabia na misimamo ya dhambi kutatutia
sumu na uchafu, kukigusa utumishi wetu, uhusiano wetu,
familia yetu, kazi yetu na yote tunayogusa.
Kwa kawaida “panya katika kisima” ni wa aina gani?
Agano Jipya linatupatia aina mbalimbali, halafu
linaorodhesha vilivyomo katika kila aina:
36 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1
• Matunda ya mwili (Wagalatia 5:19-21).
• Matendo yasiyofaa yenye msingi katika udanganyifu wa
dhambi (Waefeso 4:17-32).
• Kufuata sheria, au roho ya dini (Wagalatia 5:1-6;
Wakolosai 2:11-23).
• Kugombea nafasi, cheo, nguvu (Mathayo 6:1-2,5,16;
23:2-12).
• Kutumia huduma kwa kujipatia utajiri na mali (Mathayo
6:19-21,24; 1Timotheo 6:3-10; 2Timotheo 4:10).
• Kuhukumu, kuwa na uchungu, kutosamehe (Mathayo
7:1-6; 18:21-35; Wakolosai 3:12-19; Waebrania 12:15;
Yakobo 3:13-18).
• Mafundisho ya uwongo, uzushi (Mathayo
24:4-5,11,23-27; Wagalatia 1:8; 2Wakorintho 11:13-15;
1Timotheo 4:1-5; 2Timotheo 2:14-18; 2Petro 2:1-22;
Yuda 7-19).
Haya ni maelezo mafupi tu ya “panya” wanaoweza
kuharibu “kisima” binafsi cha moyo wako, na pia
kuwachafua wengine wanaoguswa na maisha yako na
utumishi wako.
Kama kiongozi katika Mwili wa Kristo, umeitiwa
maisha ya utakaso na utakatifu (Mathayo 5:8; 1Wakorintho
9:24-27; Waebrania 12:14; 1Petro 1:13-19). Upako ambao
Mungu anawapa watumishi Wake walioitwa ni wa thamani
na uwakfu zaidi kabisa kuliko mafuta ya Hema ya Kukutania
ya Agano la Kale - kwa sababu ni kuwepo kwa Roho
Mtakatifu Mwenyewe!
Wito wetu wa juu kabisa ni wa kuishi katika uhusiano
bora na Mungu. Maana yake ni kwamba tuishi maisha yenye
utakaso, pasipo uchafu, kama “hekalu” linalomfaa
(1Wakorintho 6:19-20), mahali pa kuishi pa Roho Mtakatifu.
Maisha ya utakaso humtukuza na kumpendeza Mungu Baba
yetu, na kutufanya tuwe waaminifu zaidi sana na wenye
kuweza kutumiwa zaidi mikononi mwa Bwana.
Ni wewe peke yako unayeweza kuhifadhi usafi wa
kisima chako. Uamue sasa uwe chombo safi ambacho Roho
wa Mungu na Neno la Mungu lisiloghushiwa hutiririka
kutoka ndani yake. Uwe zana ya utumishi iliyotakata, mtu
ambaye Mungu anaweza kumtia mafuta katika kazi kubwa
kwa ajili ya utukufu Wake na makusudi Yake (1Wakorintho
10:31; 2Timotheo 2:19-21)!
Kujifunza Kutokana Na Kushindwa
Sulemani alikuwa mfalme aliyeinuliwa na Mungu na
kupewa karama za pekee (1Wafalme 3:5-14; 4:29-34).
Bwana alimtembelea mara mbili kimwujiza (taz. 1Wafalme
sura ya 3 na 9). Sulemani aliamriwa afuate njia zote za
Mungu na kutii kanuni na amri Zake zote (3:14; 6:11-13;
9:4-9). Na ndivyo alivyofanya - kwa muda.
Lakini baadaye tunasoma kwamba utawala wa Sulemani
uliishia katika uharibifu kwake na kwa ufalme wake mzima
(tazama 1Wafalme sura ya 11).
Sulemani, kama viongozi wengi mno, alianza vizuri
lakini aliishia vibaya. Ilikuwaje? Kwa kifupi jibu ni neno
moja tu: kutokutii.
Tukichunguza Kitabu cha 1Wafalme kwa makini zaidi,
tunaona kuwa Sulemani alikuwa mtu maarufu sana, “alikuwa
na hekima kuliko watu wote” (4:31). Alikusanya utajiri usio
na kifani (10:11-29) na sifa na heshima ya watu (10:1-9).
Lakini ndipo Sulemani alipoanza kuvunja amri za Mungu
zilizo wazi (11:1-2). Na pole pole, kwa kuchagua na
kuridhiana, alianza kujiangalia katika ubinafsi, pamoja na
baraka na heshima zote alizokusanya kutokana na upako wa
Mungu na karama Zake. Njia hii iliishia katika kuangamia
kwa utawala wake Sulemani.
Sisi basi, tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya
Sulemani na utawala wake?
a. Vishawishi vinasababisha uzembe (ukosefu wa
nidhamu na bidii). Sulemani aliandikia kwamba ni
“mbweha wadogo waiharibuo mizabibu” (Wimbo Ulio Bora
2:15). Jumba la Sulemani lilijaa utajiri na nafasi, na watu
wengi waliokuwa tayari kufanya lolote ili wakae karibu na
yeye.
Je, unafikiri kwamba Mungu anafahamu uwezo wa
moyo wa binadamu kushawishika, hata na furaha
zisizoonekana kuwa mbaya - na halafu kuingia katika
ukosefu wa nidhamu na hatimaye kutotii? Nina hakika
Mungu anaufahamu. Akijua haya, alimwambia Sulemani kila
mara kwamba atii amri Zake zote (1Wafalme 6:12; 9:4).
Lakini Sulemani hakumsikiliza Bwana, hasa alipopata
“ufanisi” mkuu.
MATENDO • 37
Kumbuka Sulemani: vishawishi....
vilimwangamiza
WITO
WA
MUNGU
Vishawishi
Nakala 16 / Nambari 1
Mchungaji kwa Mchungaji: Kiongozi wa kanisa,
hata utumishi wako unaweza kuwa kishawishi ukipata
kukuvuta kuliko mambo yote - ukikuondoa katika muda
wa kukaa pamoja na Mungu kwa sababu ya kuwa na
shughuli nyingi mno, au msukumo wa mahitaji ya watu
wengine. Yesu alipokuwa hapa duniani alitupa mfano
kwa ajili ya haja ya kutumia muda wa kumsikiliza Baba
Yake na kuburudishwa kiroho (Marko 1:35-39; Luka
5:16; 6:12).
Lazima tusisahau kamwe kwamba Bwana ndiye
chanzo na chemchemi kwa upako wa Roho Wake na
kwa ufahamu wetu wa Neno Lake (Yohana 1:33;
6:63,68). Hutoka KWAKE! Utumishi wenye kuzaa
matunda halisi ni matokeo ya yale tunayopokea
miguuni pa Yesu katika kusali, kumsubiri na kusoma
Neno Lake (Luka 10:41-42; Yohana 15:16). Wengi kati
yetu tunatambua ukweli huu rahisi wa kimsingi. Shida
inatokea tunaposhindwa kutekeleza kila siku kanuni hii
ya msingi kwa ajili ya maisha yajaayo uwezo na
huduma.
Tujilinde na aina za vishawishi vinavyotuchosha,
au kutuelekeza katika kuridhiana na kutenda dhambi.
Moyo wa Sulemani ulivutwa mbali na Mungu na yale
aliyoyaruhusu katika maisha yake (1Wafalme 11:1-4,9).
Uaminifu na utiifu wake kwa Mungu vilighushiwa na
mambo ya dunia, hadi alipoangamia mwenyewe na
kuleta uharibifu kwa vyote ambavyo Mungu alikuwa
amempa avitawale.
Maswali mema ya kujiuliza kuhusu matendo
YOYOTE katika maisha yako ni haya: “Je, tendo hili au
msimamo huu hunileta karibu zaidi na Mungu na
makusudi Yake kwa maisha yangu? Au je, hunipeleka
mbali na Yeye?
b. Sifa ya wanadamu ni mtego uletao mauti.
Kufundisha au kuhubiri kwa ajili ya kusifiwa na wanadamu
ni mtego unaodanganya. Ni Mungu peke Yake awezaye
kutenda mambo yenye thamani ya milele (Zekaria 4:6).
Ndiyo, Mungu anataka kututumia kama vyombo
anavyoweza kutendea kazi. Lakini uweza na utukufu ni wa
Mungu peke Yake kwa ajili ya lolote linalotendeka kupitia
kwetu. Maana pasipo Yeye, sisi hatuwezi kufanya lolote
(Yohana 15:5).
Mungu amefunua katika Neno Lake kwamba hatampa
mwingine utukufu Wake (Isaya 42:8; 48:11). Ni lazima
tusitafute utukufu au sifa kutoka kwa watu kwa ajili ya kazi
ya huduma (Yohana 7:18).
Yesu aliwakosoa waandishi na Mafarisayo kwa ukali
kuliko wote. Aliwakemea kwa ajili ya kupenda sifa za
wanadamu na walijaa kiburi (Mathayo 23:5-12; Yohana
5:41-44). Ingawa walifahamu Maandiko na kujua njia za
Mungu, kiburi chao kiliwafanya wakatae kumkubali wala
kumwamini Yesu kama Masihi wao (Yohana 5:39-40).
Kufuata Nyayo Zake
Yesu alipewa upako wa Roho Mtakatifu pasipo kipimo
(Yohana 3:34-35). Yeye alikuwa, tena ndiye, Mfalme wa
wafalme wote, na Bwana wa mabwana wote. Lakini, kwa
ajili yetu, alijifanya Mtumishi mnyenyekevu (Mathayo
20:28; Wafilipi 2:3-11).
Kwa kweli, sisi kama viongozi katika Mwili wa Kristo,
tufanye kama Paulo asemavyo: “Iweni na nia iyo hiyo ndani
yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu...”
(Wafilipi 2:5). Sisi hatukupewa Roho Mtakatifu pasipo
kipimo kama Yesu alivyopewa. Lakini tunaweza kuwa na
msaada Wake wote tunapoishi katika uhusiano wa utiifu
Kwake na kwa Roho Mtakatifu (2Petro 1:2-4).
Bila shaka, hata tukiwa na karama hizi, sisi si wakubwa
wala wema kumzidi Bwana wetu. Badala yake, tunatakiwa
tufanane na Yeye (Yohana 13:12-17), tukitumia yale
ambayo Mungu anatupatia katika kuwatumikia wengine.
Kwa hiyo, tusijione au kujisifu wakati Mungu anapotutumia
katika huduma. Tujilinde na kiburi - dhambi ya ibilisi
(1Timotheo 3:6).
Dhambi Ya Hatari Kuliko Zote
Kiburi ni dhambi iletayo kifo ambayo inaweza kumwua
kwa sumu hata kiongozi aliyejitoa kabisa, na kuziba
mtiririko wa upako wa Roho Mtakatifu. Kiongozi wa kanisa
anaweza kuwa na ustadi, hekima au ujuzi mwingi. Lakini ni
upumbavu kujisifu kwa ajili ya mambo haya. Kwanza, kwa
sababu vyote tulivyo navyo vimetoka kwa Mungu. Pili, kwa
sababu hekima, ustadi na uwezo wetu wote si kitu kabisa
kulingana na upako wa Roho wa Mungu na pia kulingana na
yale ambayo Mungu anaweza kufanya Mwenyewe peke
Yake (Mathayo 7:21-23; 1Wakorintho 3:18-21; 4:20;
8:1-3)!
Huenda kiburi ni dhambi ya hatari kuliko zote. Ilikuwa
dhambi ya kimsingi ya Shetani (Isaya 14:12-14). Kiburi
kinaweza kutufanya tufikiri kwamba tunaweza kutenda
mambo fulani vizuri kuliko Mungu anavyoweza, na hatimaye
kitatuongoza mpaka tumwasi Mungu.
Tunapoanza kufanya mipango yetu binafsi mbali na
kumtii Mungu, tumekwisha kumwasi Yeye. Kama
hatukujitoa Kwake kikamilifu, tunatengwa na Yeye, maana
“Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema
wanyenyekevu” (Yakobo 4:6).
Kiburi kinatufanya tujione kuwa tunaweza kujitunza na
kujitegemea. Kwa hiyo, hatuamini tena kwamba tunahitaji
kufundishwa wala na Mungu wala na mwanadamu. Tunazuia
hisia kwamba tunahitaji lolote kutoka kwa Mungu, na
tunaacha kumwomba; kwa hiyo tunaacha pia kupokea
(Yakobo 4:1-2). Imani yenye unyenyekevu kama ya mtoto
inahitajika ili kumwomba Baba yetu wa Mbinguni au
kujifunza kutoka Kwake (Mathayo 18:3-4).
Mungu ndiye anayetupatia mahitaji yetu yote. Lazima
tutambue kwa unyenyekevu kwamba tunamhitaji Yeye
pamoja na vile alivyotupatia, la sivyo hatutapokea lolote.
Kiburi kinatuzuia tusiwe na unyenyekevu kama huu, na kwa
hiyo inatunyang’anya baraka za Ufalme wa Mungu,
ukiwemo upako.
Mwamini Bwana Peke Yake
Fikiria mara moja sarafu. Upande mmoja imepigwa neno
“kiburi”. Upande wa pili imepigwa “kuogopa au hofu ya
binadamu”. Dhambi hizi mbili za kimwili hudhihirishwa
pamoja mara nyingi katika maisha ya mtu.
“Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali
amtumainiye Bwana atakuwa salama” (Mithali 29:25).
“Kuogopa wanadamu” kuna sura nyingi. Njia za kawaida
zinazowatega wachungaji ni kama hizi:
38 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1
• Hofu ya kuwachukiza au kuwakasirisha watu katika
kundi (mpaka kuachilia dhambi zao).
• Kuwapendekeza watu wanaotoa fedha au wenye uwezo
wa kushawishi.
• Kusema au kutenda mambo ili kupendwa na (au
kuonekana mwema kuliko) wachungaji wenzi au
waamini wengine.
Zipo njia nyingine nyingi za kunaswa na hofu ya
wanadamu. Lakini haidhuru ni kwa njia gani, unapokubali
kuwaogopa watu unanaswa katika kufanya mapenzi ya watu
wengine. Unanaswa na maoni na maamuzi yao. Unawezaje
basi kumtumikia Bwana kwa moyo wote, ukiwa unahangaika
kutumikia maoni ya watu? Mtu yeyote hawezi kutumikia
mabwana wawili (Mathayo 6:24), wala hawezi kusimama
hali moyo umegawanyika (Zaburi 86:11; Marko 3:24-25).
Yesu pia alikabili tatizo hili, kutokana na tamaa za
kibinafsi za watu (Marko 1:35-39; Yohana 6:15,22-40);
hukumu ya Mafarisayo (Mathayo 22:15-22; Luka 7:36-50);
au hata matakwa ya familia Yake ya kibinadamu (Mathayo
12:46-50; Yohana 7:1-9).
Katika hoja hizi zote na nyingine, Yesu hakufuata maoni
ya watu. Badala yake Yesu alilenga kufanya mapenzi ya
Mungu kuliko yote, pasipo kujali kamwe gharama yake.
Hata watu walipomwamini Yesu na kuonekana kuwa
walimfuata, Yeye alijua kigeugeu cha mioyo ya wanadamu
(Yohana 2:23-25). Yesu aliwaonya wafuasi Wake
wasiwaamini wanadamu wala kutafuta sifa zao (Luka 6:26).
Maana kama ni heshima ya watu tunayotafuta, mioyo yetu
haitaelekea kumtumikia Bwana peke Yake.
Bwana anawatafuta watu walio waaminifu Kwake
kabisa na pekee katika mioyo yao. Yeye atafanya mambo
makuu kupitia watu kama hao (2Nyakati 16:9) na ndio
ambao atawamiminia upako Wake hasa!
Angalia ni nini itakayotulinda na hofu ya wanadamu: ni
kumtumaini Bwana (Mithali 29:25). Tunapomjua Bwana,
tukiwa tumemtafuta kwa ajili ya mapenzi Yake, tunapotenda
kwa kutii yale aliyosema kwa sababu tunamwamini Yeye
kabisa - haidhuru wanadamu wafikiri nini.
c. Maridhiano makubwa huanza na “mbweha
wadogo” wa maridhiano madogo (Wimbo Ulio Bora
2:15). Kuna tatizo la kawaida kati ya viongozi ambao Mungu
anawatumia katika kazi ya maana. Huanza kujiona kuwa
muhimu mpaka wasihitaji kutii amri na kanuni zote za
Mungu. Huenda wanazifahamu na kuweza kuzifundisha;
lakini hawaamini tena kwamba wao binafsi wanahitaji
kuziishia kwa kuzitii.
Hali hii nimeita “Kanuni ya Udhuru wa Kiongozi”.
Yaani viongozi wanaona kwamba wao ni muhimu sana
mpaka wasihitaji tena kuwa wanyenyekevu, wala kutumika,
wala kuwavumilia wengine, wala kujitoa, n.k. Katika akili
zao, wao wamepata kuwa na “udhuru” kwa ajili ya kanuni za
Mungu; wanaona kufuata njia zao za ubinafsi na mwili kuwa
na udhuru kwa sababu ya “umuhimu” au “ufanisi” wao.
Wanakubaliana na njia ya kuwaza ya kidunia, kwamba
ufanisi wao katika huduma umesababishwa na uwezo wao na
vipawa vyao vikuu - nao wanaanza kuishi kana kwamba wao
ni wasanii wakuu!
Kwa sababu Mungu ni mwaminifu katika kuendelea
kuhudumia wengine kupitia kwao (Warumi 11:29), viongozi
hao wanaanza kufanyia fidhuli wema wa Mungu. Polepole
wanaanza kuwa na misimamo na mienendo ambayo
hatimaye itawaingiza katika dhambi halisi. Hali hii
itasababisha kuanguka kwao katika huduma, mpaka hata
kuangamiza imani yao (1Timotheo 1:19) au kuchoma
dhamiri zao (1Timotheo 4:2).
Hali hiyo itasababisha pia kumhuzunisha (Waefeso 4:30)
na kumzimisha (1Wathesalonike 5:19) Roho Mtakatifu wa
Mungu. Na hatimaye itafunga kabisa mtiririko wa upako wa
Mungu.
Sisi kama viongozi wa kanisa, tumeitwa tuwe mfano wa
tabia ya Kristo kwa Mwili wa Kristo. Lazima tufahamu Neno
la Mungu na kuliishia, kwa uwezo wetu wote. Kama
tutashindwa, lazima tuwe wepesi wa kutubu (2Wakorintho
7:10; Ufunuo 3:19).
Kila mmoja wetu atie maanani maonyo ya Maandiko:
“dhambi yenu itawapata hapana budi” (Hesabu 32:23; taz.
pia Wagalatia 6:7-8; 1Timotheo 5:24-25).
Kulinda Moyo Wako
Biblia inahimiza: “Linda moyo wako kuliko yote
uyalindayo; maana ndiko zitokako chemchemi za uzima”
(Mithali 4:23). Sulemani aliandika mstari huu, pengine baada
ya kuharibu uhusiano wake na Mungu na kuangamiza ufalme
wake. Hatujui kwa uhakika. Lakini ukweli wa yale ambayo
Sulemani aliandika kwa Roho wa Mungu bado unasema wazi
na sisi leo.
Ibilisi ana “panya” wengi ambao anapenda kutumia
katika kutujaribu. Mwili wetu pia una tamaa nyingi za
dhambi na zisizofaa. Lakini mambo haya yanaweza kuingia
na kuchafua kisima cha maisha yetu ikiwa tu tutayafungulia
mlango. Yanaweza kuozesha nyumba ya moyo wetu - makao
ya Roho Mtakatifu - ikiwa tu tutayaingiza na kupatia dhambi
nafasi.
Kwa hiyo tunaweza kufanya nini ili tulinde “kisima”
chetu katika usafi? Kwa kuwa sisi ni hekalu ya Roho
Mtakatifu (1Wakorintho 6:19-20) kuna hatua za kiutendaji
ambazo tunaweza kuzichukua. Tuziangalie sasa.
MATENDO • 39
Hata watu walipomwamini Yesu
na kuonekana kuwa
walimfuata, Yeye alijua
kigeugeu cha mioyo ya
wanadamu (Yohana 2:23-25).
Yesu aliwaonya wafuasi Wake
wasiwaamini wanadamu wala
kutafuta sifa zao (Luka 6:26).
Maana kama ni heshima ya
watu tunayotafuta, mioyo yetu
haitaelekea kumtumikia Bwana
peke Yake.
Nakala 16 / Nambari 1
2. Njia Ya Utakaso
a. Kuishi kwa kanuni za Neno la Mungu. Mtunga
Zaburi aliuliza swali la maana sana, na kulijibu. “Jinsi gani
kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako”
(Zaburi 119:9).
Katika barua za Paulo kwa Timotheo na Tito, Roho
Mtakatifu ametoa maagizo ya wazi kwa wachungaji wote.
Barua hizi tatu “za Kiuchungaji” (1 & 2Timotheo na Tito)
ziliandikwa kwa wachungaji (Timotheo na Tito) kuhusu
mambo ya kiuchungaji.
Ni katika barua kwa Timotheo kwamba tunasoma kuwa
Neno la Mungu - na si maoni ya wanadamu - ni mwongozo
wetu kwa yote tunayofanya, kusema, kuwa na kufanyia
huduma (1Timotheo 4:12-16; 2Timotheo 2:15-18; 3:16-17).
Yesu anaongea kwamba Neno la Mungu ni kipimo chetu
cha maisha. Anasema kuwa kutokutenda yote yaliyomo
katika Neno la Mungu ni kushindwa kunakoleta hukumu
(Mathayo 5:17-20). Neno la Mungu lina upuzio wa Roho
Mtakatifu (2Timotheo 3:16; 2Petro 1:19-21) nalo
limethibitishwa na Roho Mtakatifu (Yohana 14:26;
Waebrania 4:12-13).
Maoni na mawazo ya wanadamu, hata kama yana
makusudi mema na yanapendeza, si mwongozo wa maisha
yetu. Pia si ambayo tunapaswa kufundisha washarika wetu
kuhusu maisha katika Ufalme wa Mungu. Lazima tuwe
waangalifu sana kuhusu maoni ya watu (1Wakorintho
2:1-16) - hata kama tunakubaliana nayo. Kwa sababu
wanadamu, hata wale tunaowaheshimu na kuwaamini,
ndivyo walivyo: wanadamu tu.
Ni kweli kwamba watu fulani wanaweza kutusaidia.
Wanaweza kutufundisha yale waliyojifunza. Ujuzi wao
katika Neno la Mungu na ustadi wao huweza kutufaidi.
Lakini ni sehemu, inayosaidia pale tu inapokubaliana na
Neno la Mungu!
Haiwezekani maisha yetu kutakaswa kwa maoni ya watu
wala kwa mbinu mpya ya utumishi. Tunaweza kutembea kwa
haki mbele za Bwana wakati ule tu ambapo tunamfuata Yeye
na kutii Neno Lake.
Kuna Roho Mtakatifu mmoja na chanzo kimoja tu cha
Neno la Mungu la milele - yaani Biblia! Kwa hiyo usome
Biblia, kutafakari, kujifunza, kukariri, kutii, kuishia, kuhubiri
na kufundisha Biblia! Amina!
b. Roho Mtakatifu anatenda kazi katika sala na
maombi. “Pumzi [roho] ya mwanadamu ni taa ya Bwana;
hupeleleza yote yaliyomo ndani yake” (Mithali 20:27).
Nyakati zetu za kusali ni chanzo cha baraka na mafunzo,
na mahali pa mawasiliano na Mungu. Pia sala inaweza
kuwa silaha yenye nguvu inapoongozwa na Roho
Mtakatifu.
Inasikitisha kwamba katika shughuli nyingi za maisha ya
kila siku, viongozi wa kanisa kama wewe na mimi mara
nyingi tunaacha nafasi zetu muhimu kabisa za kukaa na
Bwana. Lakini ni pale tu ambapo tunatoa nafasi ya kutulia na
kusikiliza ndipo Roho Mtakatifu anapoweza kweli kufanya
kazi ndani ya mioyo yetu.
Kila mmoja wetu anahitaji “kupimwa kwa moyo” kwa
utaratibu na uangalifu kutoka kwa Roho Mtakatifu. Yeye
aweza kufunua nia na makusudi ya siri, sehemu zenye uchafu
au udhaifu. Katika upendo Wake kwetu na kwa Mwili wa
Kristo, Roho Mtakatifu anataka pia kututhibitishia na
kututengeneza, ili sisi tutunze kwa uangalifu mambo yale
ambayo vinginevyo yatazuia au hata kuharibu maisha na
huduma yetu.
Ulinzi Dhidi Ya Kujidanganya
Ukweli kwamba tunafanya bidii katika huduma,
kufahamu Biblia na kuweza kuwafundisha wengine,
haumaanishi kwamba sisi tumekamilika. Kinyume chake,
mambo haya yangetufanya tutambue zaidi uwezo wa moyo
wa binadamu kudanganywa na kutoa udhuru kwa ajili ya
dhambi!
Tafadhali tumia muda hata sasa wa kusoma mistari
ifuatayo:
• Mithali 16:2,25; 28:26
• Yeremia 17:9-10
• 1Wakorintho 10:12-13
Kuna mistari mingine mingi inayofunua wazi haja yetu
ya kufungua mioyo yetu mbele za Roho Mtakatifu. Bwana
amekwisha jua maeneo yetu ya mapambano, hatuwezi
kuyaficha Kwake. Lakini tunaweza kujidanganya wenyewe
na kuruhusu dhambi, tamaa za mwili au kuvunjika kutokana
na mwenendo wa dhambi viendelee mpaka vizae matunda ya
udhalimu katika maisha yetu.
Bwana anatafuta mioyo inayosafishiwa dhambi. Anataka
lisiwepo lolote la kuzuia upako Wake, wala ufanisi wa
maisha yetu na huduma zetu. Unapoonekana kuwa
mwaminifu katika kulinda moyo wako na dhambi na
kumruhusu Roho Mtakatifu akusafishe kwa ndani, upako wa
Mungu unaweza kumiminwa pasipo kizuio.
Mchungaji kwa Mchungaji: Zaidi tunapotembea pamoja na
Bwana, ndivyo inavyokuwa rahisi zaidi kutokutambua haja ya kazi
ya Roho Mtakatifu ya kutengeneza maisha yetu.
Inasikitisha kwamba kwa upande wa viongozi wa kanisa hali
hii ni kweli hasa. Tulivyo na shughuli nyingi za kujifunza na
kufundisha Neno la Mungu, tunaanza kufikiri kwamba tunalitendea
kazi pia katika maisha yetu ya kila siku. Tunavyokazana katika
kuombea huduma yetu pamoja na wengine, hatutoi nafasi ya
kutosha katika kukaa tu na Bwana ili tusikie kutoka Kwake kwa ajili
yetu sisi wenyewe. Tunajifunza kuendelea kuchekelea na kutenda
kana kwamba yote ni sawasawa, hata kama tunapambana na
dhambi na kuvunjika kwa ndani. Je, unaweza kukiri kwamba hii ni
hali yako mara kwa mara?
Yesu alitamka kwamba haki yetu lazima iwe haki ya moyo.
Lazima izidi haki ya Mafarisayo iliyo ya nje na yenye mipaka
(Mathayo 5:20).
Tafadhali kumbuka kwamba Yesu hakufia wanadamu ili
aanzishe dini mpya. Alitoa uhai Wake ili sisi tuweze kurudishwa kwa
Mungu, na halafu kuendelea kubadilishwa zaidi na zaidi katika
mfano ambao binadamu aliumbwa nao mwanzoni kabla dhambi
haijatuharibu (Mathayo 15:10-20; 23:23-28; Warumi 12:1-2;
2Wakorintho 3:18; 1Yohana 3:1-3). Tumekwisha jifunza kwamba
mabadiliko haya yanaendelea katika maisha yetu yote, hata kwetu
sisi viongozi.
Tukizembea hali ya ndani ya moyo wetu, huwa rahisi mno
kunaswa na dhambi. Matatizo yanaweza kuanza yakiwa madogo,
lakini maridhiano madogo sikuzote huendea yaliyo makubwa na
yenye kuangamiza. Ndiyo sababu ni muhimu kabisa tumruhusu
Roho Mtakatifu afanye kazi ndani ya mioyo yetu kila siku,
akituthibitishia na kushinda matatizo kabla hayajatuingiza katika
dhambi.
40 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1
“Ee Mungu, Unichunguze!”
Tunamhitaji sana Roho Mtakatifu awe taa inayomulika
ndani ya nafsi na roho zetu. Tunamhitaji afunue hali halisi ya
mioyo yetu, ili tutakaswe, kuhuishwa na kubadilishwa.
Ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili ya maisha yetu (Wafilipi
1:6; 2Wakorintho 3:18; Warumi 8:29)!
Tunaposhiriki katika kazi hii ya Roho kwa sala,
tutakuzwa tuwe “vyombo vya heshima” (2Timotheo
2:20-21). Ndipo Mungu anapoweza kumimina upako wa
Roho Wake Mtakatifu kwa wingi na uhuru, akiachia zaidi
Yake ndani yetu na kupitia kwetu kwa wengine katika
huduma.
Sala yetu ya kila siku iwe ile ya Daudi: “Ee Mungu,
unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo
yangu; Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu,
Ukaniongoze katika njia ya milele” (Zaburi 139:23-24).
c. Tembea katika kutii. “Na sisi tu mashahidi wa
mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu
amewapa wote wamtiio” (Matendo 5:32).
Tumekwisha zungumzia nafasi ya Neno la Mungu na
kazi inayobadilisha ya Roho Mtakatifu katika maisha binafsi
ya mchungaji. Hizi ni funguo za lazima kwa ajili ya kuishi
maisha ya utakaso.
Lakini, zinaweza kutokufanya kazi katika maisha yetu -
kama tunakataa kutii.
Hatutii tunapokataa amri za Mungu au kutojali kufuata
yale ambayo Roho Mtakatifu ameyafunua mioyoni mwetu
(Yakobo 1:21-25). Sauli ni mfano dhahiri wa kuanguka kwa
namna hii (taz. 1Samweli 15:1-35). Daudi alijifunza vema
kutokana na kushindwa kwa Sauli, akaandika kuhusu kanuni
hii iliyo muhimu sana (taz. Zaburi 40:6-8).
Mara nyingi viongozi wa kanisa wapo tayari kutumika
na hata kujitoa kama dhabihu kwa ajili ya huduma. Hali hii si
mbaya. Lakini Mungu anataka zaidi ya dhabihu; anadai kutii
kwetu kwa unyenyekevu na hiari (1Samweli 15:22-23).
Tumekwisha jifunza umuhimu wa utiifu kwa Bwana na
Neno Lake katika mambo ya nia zetu za ndani, misimamo na
mienendo yetu ya kila siku. Lakini kazi ya Roho inahitaji pia
utiifu wetu katika mambo ya kazi ya Bwana - katika yale
tunayotenda, na katika jinsi tunavyoyatenda.
Kuwekwa Sawa Katika Kutii
Musa alijifunza jambo gumu kabisa kuhusu kutii
mwongozo wa Mungu (Hesabu 20:7-13). Musa aliamriwa na
Mungu “Ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji
yake” (ms. 8). Lakini badala yake, Musa alipiga mwamba ule
(ms. 11). Matokeo yake yalikuwa kwamba Musa
hakuruhusiwa kuingia katika Nchi ya Ahadi (ms. 12; taz. pia
Kumbukumbu 31:1-2; 32:48-52). Kwa nini Musa asitii amri
hii ya wazi ya Bwana? Wana wa Israeli walikuwa tayari
wamekabiliana na ukame na kiu jangwani mara mbili kabla
ya hapo (Kutoka 15:22-26; 17:1-7). Mara ya kwanza, Mungu
alimwongoza Musa atupe mti fulani katika maji yaliyokuwa
machungu hadi yasinyweke, na maji yale yalipata kuwa
matamu. Mara ya pili, Mungu alikuwa amemwambia Musa
apige mwamba fulani, na maji matamu yalitoka.
Lakini mara hii ya tatu, Mungu alimwambia Musa
afanye tendo jingine. Alimwambia aambie mwamba. Lakini
badala yake, Musa alirudia mtindo wa awali, akaupiga
mwamba. Labda Musa hakuwa wazi kwa njia hii mpya
mbayo Mungu alitaka kutendea kazi. Labda Musa alikuwa
amewakasirikia wana wa Israeli wenye kunung’unika.
Hatujui kwa uhakika. Lakini tunayojua ni hii: Kule kutotii
kwa Musa kulimwudhi Bwana (Hesabu 20:12).
Jambo muhimu la kujifunza hapa ni hili: tokeo katika
hali ile halikuwa muhimu kama mtindo! Wana wa Israeli
walipata maji waliyotamani. Lakini kipimo cha Mungu kwa
ajili ya utiifu hakikuwa katika tokeo; kilikuwa kwamba
mtumishi wake atii na kufuata kikamilifu njia ya Mungu
ya kutimiza kusudi Lake. Ndiyo maana hasa ya utiifu!
Tunatakiwa tufuate Neno la Mungu na mwongozo wa
Roho Mtakatifu, hata kama hatuoni sababu kwa akili zetu
zenye mipaka (taz. Isaya 55:8-9; 1Wakorintho 1:18-25).
Mungu ametupa Roho Wake Mtakatifu atuongoze. Sisi kama
watoto wa Mungu, tumeitwa tumwamini na kumtii (Warumi
8:14).
Tafadhali ufahamu kwamba kutii si jambo la kustahili
baraka ya Mungu wala upako Wake. Lakini tunapotembea
katika kutii, tunajiweka sawa na Bwana na kanuni za Neno
Lake. Tunapofanya hivyo, tuko tayari kupokea zaidi katika
uwezo wa upako wa Mungu.
Paulo alifafanua kanuni hii: “Bali nautesa mwili wangu
na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine
mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa” (1Wakorintho 9:27).
Paulo alitambua kabisa kwamba mwenendo wake binafsi
ulihusiana moja kwa moja na huduma ambayo Mungu
alikuwa amempatia.
Vipimo Vya Agano Jipya
Kila mchungaji ana sehemu mbili katika maisha yake:
maisha yake binafsi na maisha yake ya huduma mbele ya
watu. Matazamio ya Mungu kwa ajili ya utiifu yanahusiana
na sehemu zote mbili. Ni lazima maisha binafsi na maisha ya
kazi ya mchungaji yawe chini ya marudi na maendeleo ya
Roho Mtakatifu na Neno la Mungu.
Kama kiongozi wa kanisa amejitoa kwa utiifu katika
maeneo yote ya maisha yake, upako wa Roho Mtakatifu
utatiririka katika maeneo yote pia.
Ni kosa kuamini kwamba upako ni kwa ajili ya huduma
yetu mbele ya watu tu. Bwana anajali ufanisi wako vile vile
katika maisha ya familia yako na nafsi yako, pamoja na jinsi
anavyoweza pengine akutumie katika kazi ya kawaida au
nafasi yoyote nyingine.
Masharti ya Agano Jipya kwa ajili ya viongozi wa kanisa
(soma 1Timotheo 3:1-7) ni vipimo vyetu pia kama
wachungaji. Wazee wa Kanisa la awali ndio waliokuwa
wachungaji wa makanisa ya kila mahali. Kwa hiyo,
mwongozo na vipimo kwa ajili ya maisha yao binafsi na
katika huduma ndivyo vinavyofaa wachungaji leo.
Utaratibu Wa Ki-Biblia
Wachungaji wengi mno hawajali vipimo hivi, hasa jinsi
vinavyohusiana na mahitaji ya wake na watoto wao.
Wanafikiri ni aina ya utauwa kutowajali familia zao ili
wajitoe katika huduma wakati wote. Neno la Mungu
limethibitisha wazi kwamba SIVYO Mungu alivyowaagiza
wachungaji!
Mume (akiwemo mchungaji) ameagizwa ampende mke
wake kama Kristo anavyopenda Kanisa, kwa ukarimu na
utoaji kifedha. Mchungaji na mke wake hupaswa
Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO • 41
kuheshimiana na kupendana, wakiombeana na kuhudumiana.
Watoto wasidekezwe, wala kutendewa kama watumishi. Bali
walelewe, kuthaminiwa, kuelimishwa katika utaratibu wa
ki-Mungu na wa upendo. Sisi tuwe mifano kwa watoto wetu
ya tabia ya Kristo na ya Baba yao wa mbinguni
anayewapenda. (Taz. Waefeso 5:22-33; 6:1-4; Wakolosai
3:18-21; 1Petro 3:7.)
Familia zetu zipewe kipaumbele, na kuwatunza ni
wajibu ambao hatuwezi kuacha: “Lakini mtu ye yote
asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake
hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini”
(1Timotheo 5:8). Utaratibu wa ki-Biblia ni: kwanza -
uhusiano wetu na Mungu; pili - familia yetu; tatu - huduma
na wajibu nyingine baada ya hayo mawili ya kwanza.
Uwakili wa mchungaji kwa upande wa fedha pia
uongozwe na kanuni za Neno la Mungu na Roho Mtakatifu.
Malipo ambayo mchungaji anapokea binafsi yatumiwe katika:
• kumbariki Bwana katika zaka na sadaka;
• kubariki familia yetu kwa kuwatunza;
• kuwabariki wengine tunapowagawia katika yale ambayo
Mungu ametupatia.
Msaada Wote Tunaohitaji
Huduma ya mchungaji itekelezwe pia katika kutii Neno
la Mungu na kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu. Roho
Mtakatifu atatusaidia na mara nyingi kutuongoza kuhusu yale
ambayo Yeye anapenda tufanye katika hali halisi za huduma
yetu.
Tunapojitoa na kujiadilisha, kusikiliza ushauri wa
ki-Mungu, kujifunza Neno la Mungu, kusali kila mara
pamoja na kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu, tutakua
na kupevuka kama viongozi wa ki-Kristo. Tunapofanya
hivyo, tunaweza kutazamia ongezeko la kutiririka kwa upako
wa Mungu juu ya maisha yetu na kupitia huduma yetu
(tazama hamasa za Paulo kwa Timotheo: 1Timotheo 4:12-16;
6:11-12,20; 2Timotheo 1:6-7,13-14; 2:1,15-16,22-25; 4:1-5).
Ndiyo hamu ya Mungu kwa ajili yetu! Anatupatia msaada
wote tunaohitaji ili tumtumikie kwa uaminifu, na kuishi
kufuatana na njia Zake. Lakini ni lazima tuchague kutii!
Mchungaji kwa Mchungaji: Kama mchungaji au
kiongozi wa kanisa anavunja au kuendelea kudharau
kanuni hizi za msingi kuhusu maisha yake binafsi na ya
huduma, upako wa Mungu utazimishwa. Kutakuwa na
ukosefu wa matunda nyumbani mwake na katika
huduma yake.
Pasipo toba halisi na kujitoa kwa upya na kweli kwa
makusudi ya Mungu, kiongozi yumo katika hatari ya
kuangamia binafsi na katika huduma. Uangamizi huu
unaweza kutumia muda, lakini tuwe na hakika kwamba
sisi sote tunavuna yale tuliyopanda (Wagalatia 6:7-8).
Inasikitisha kwamba wapo viongozi katika Kanisa
leo wenye karama na upako wenye nguvu, ambao
wanaanza kuishi maisha ya unafiki. Kwa maneno
mengine, wanafundisha jambo fulani, lakini wameanza
kuishia njia nyingine.
Sisi sote tutashindwa mara kwa mara, na hakuna
hata mmoja wetu aliye mkamilifu pasipo dhambi. Lakini
siongei kuhusu kuanguka kwa mara moja, na baada
yake kutubu haraka. Bali ninaongea kuhusu kuvunja
kwa mfululizo na makusudi kanuni za Neno la Mungu
katika maisha binafsi ya kiongozi.
Mungu Baba yetu na jina la Yesu Kristo
hutahayarishwa katika haya. Unafiki huu unawafukuza
watu wa dunia mbali na wokovu katika Kristo. Walio
ndani ya Kanisa pamoja na familia zetu pia huchukizwa
na mambo ya Mungu kwa sababu ya ukosefu huu wa
unyofu katika maisha binafsi ya viongozi wa kanisa.
Hali hii ni uovu, na ikiwa mwenendo wako
unamsababishia mwingine ajikwae, Yesu ameonya
kuhusu hukumu ya hakika (Luka 17:1-2). Hukumu ya
Mungu juu ya kazi zetu ni ya uhakika (1Wakorintho
3:11-15).
Bwana Wa Maisha Yetu Yote
Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu sisi kama waamini;
anatutia mafuta ya upako ili makusudi ya Mungu yatendeke.
Yeye anataka kujaza maisha yetu kikamilifu, si kwa upande
wa huduma tu. Yesu awe Bwana wa maisha yetu yote - wa
moyo wetu wote, si sehemu tu (1Petro 3:15). Lazima tumtii
Bwana na Neno Lake katika maeneo yote ya maisha yetu, ili
Yeye apokee utukufu nasi tuwe zana zenye ufanisi kwa ajili
ya makusudi Yake!
d. Tunahitaji mahusiano ya kimwenzi. Wachungaji na
viongozi mara nyingi hawataki kufunua mambo ya ndani ya
maisha yao. Hofu yao inaweza kuamsha wivu au mashindano
kati yao. Shetani anatumia madhaifu haya katika kugawanya
Mwili wa Kristo, na hasa kuwafanya viongozi watengane na
kuogopana.
Sehemu kubwa ya ufanisi wetu kama viongozi wa kanisa
itapotea pasipokuwa na mahusiano yenye afya kati yetu na
viongozi wengine. Tunategemeana, huenda zaidi kuliko
tunavyotambua au kutaka kukiri. Waamini, wakiwemo
wachungaji, ni familia (ndugu na dada). Uhusiano huu ni
muhimu zaidi kabisa kuliko vyeo, nafasi, uanachama katika
dhehebu au ukubwa/udogo wa kanisa lako.
Karama na nafasi mbalimbali katika Mwili wa Kristo
hutolewa ili tufanye kazi pamoja kwa ufanisi (Warumi 12:3-8;
1Wakorintho sura ya 12). Hakuna yeyote kati yetu aliye na yote
yanayohitajika ili awe na ufanisi katika huduma pasipo
ushirikiano pamoja na waamini na viongozi wengine. Lakini aina
hii ya umoja inahitaji upevu, upendo, utumishi na unyenyekevu.
Kuegemezana
Wachungaji hasa wanahitaji kuegemezana. Lazima tutoe
nafasi ya mahusiano na kuyasitawisha pamoja na wachungaji
na viongozi wengine wachaji. Kusudi la msingi la kufanya
hivyo ni kudirikiana. Lazima tufanye hivyo kwa ajili ya
kulinda afya yetu ya kiroho tusipate kushindwa.
Mahusiano kama haya yawe na uwazi halisi, nafasi ya
kushirikishana hamasa zetu, matatizo yetu na ushindi wetu
katika maisha na huduma. Katika kundi hili la urafiki na
uhusiano, sisi tunaweza kuhudumiwa wenyewe, tukiombewa
na kupokea ushauri wa ki-Biblia.
Mungu anakusudia aina hii ya uhusiano kwa ajili ya
kukua na kupevuka kwetu: “Chuma hunoa chuma; ndivyo
mtu aunoavyo uso wa rafiki yake” (Mithali 27:17).
Mahusiano haya ya kuaminiana yanatupatia nafasi yenye
usalama pa kushirikishana hofu zetu, mahangaiko yetu, na
majaribu na vishawishi vyetu. Tunaweza kuungama makosa
yetu na dhambi zetu (Yakobo 5:16) na kupokea huduma
pamoja na kutiwa moyo.
42 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1
Kila mtu katika utumishi anahitaji kutiwa moyo. Ibilisi
anakazana kuwashawishi viongozi waanguke katika
kushindwa binafsi au kuacha utumishi. Mara nyingine watu -
hata katika sharika zetu - wanatufahamu vibaya, kutupinga,
au hata kutudhulumu. Tunahitaji kuegemezwa na marafiki
waaminifu wenye nguvu ya kiroho watusaidie kupitia nyakati
kama hizi, ili tutoke kama washindi katika Kristo!
Mchungaji kwa Mchungaji: Usiamini uwongo
kwamba ni “kiroho” zaidi kutohitaji watu wengine katika
maisha yako. Bali, zaidi tunavyopevuka ndivyo
tutakavyotambua zaidi haja yetu ya mahusiano
matakatifu katika Mwili wa Kristo. Paulo anatuambia
kwamba sisi kwa pamoja ndio hekalu la Mungu, na
Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu (1Wakorintho
3:16-17).
Vikundi hivi vya urafiki vya kushirikiana viteuliwe
kwa maombi na kwa uangalifu. Si kila mtu
unayemfahamu atakayefaa kwa ajili ya kushirikiana
katika maombi, tena si kila mtu atakayekuwa na upevu
wa kutosha ili aaminike. Utafute wale unaowaheshimu
na kuwaamini - wenye upevu, hekima na uwazi kwa
Roho Mtakatifu, waweze kutamka ukweli kwa unyofu
na upendo.
Lengo kuu la muda wa kukutana liwe maombi. Pia
vikundi hivi viwe na watu wa jinsia moja - wanaume
kwa wanaume, wanawake kwa wanawake.
Mahusiano haya “yatatunoa” na kutuimarisha
katika kukua, kutakaswa na kupokea upako mwingi
zaidi!
3. Alama Saba Za Upako Halisi
Mara nyingi watu wanachanganywa kuhusu asili ya
upako na kusudi lake kutokana na kukutana nao mara moja
au kwa muda mfupi katika tukio fulani. Huenda ni mahubiri
yenye nguvu, sala yenye msisimko, au kuwepo kwa ishara na
miujiza katika mkutano.
Maoni ya muda mfupi kama haya yanaweza kusababisha
kutoelewa kwa njia mbili. Kwanza, ni rahisi kuelewa upako
vibaya kama msisimko, kipawa, karama, mtindo au mbinu
katika utumishi. Pili, tunaweza kufikiri kwamba dakika ya
kilele ya mafunuo yasiyo ya kiasili ndilo kusudi lenyewe la
upako.
Ingawa matukio haya ya kimwujiza au msisimko
yanaweza kweli kuwa matokeo ya upako wa Roho Mtakatifu,
lazima tukumbuke kuwa upako ni zaidi ya hayo.
Ni muhimu tuendeleze maoni ya muda mrefu juu ya
upako. Huu ni ufahamu kwamba upako halisi utasababisha
maisha ya watu yaliyogeuzwa (Warumi 12:1-2).
Maana yangu ya maisha yaliyogeuzwa ni maisha yenye
msingi imara katika Neno la Mungu na sala. Watu wanaoishi
maisha yaliyogeuzwa wanafikia ulimwengu uliowazunguka
kwa ushuhuda na huduma ya upendo. Wanapinga dhambi na
matendo ya mwili, wakitembea kwa unyenyekevu na toba.
Wana utendaji katika Mwili wa Kristo; baada ya kutambua
vipawa vyao vya kiroho, wanavitumia katika huduma.
Wanazidi kufanana na Kristo wakati wote!
Mambo haya yawe ya kweli katika kiongozi aliyegeuzwa,
pamoja na wale ambao kiongozi wa kanisa aliye na upako
anawahudumia.
Huduma yenye upako wa kweli itakuwa na matunda, na
matokeo yake yataendelea katika maisha ya watu
waliookolewa na kufunzwa ili wawe wafuasi wa Kristo.
Huduma yenye upako si njia ya kupata heshima, utajiri
au starehe. Mtume Paulo alikuwa na upako wa hali ya juu
kabisa, na kutumiwa sana na Mungu. Lakini aliteswa kupita
kiasi, alikuwa maskini, kufukuzwa, kutiwa gerezani mara
kwa mara, na hata kudharauliwa na kanisa ambalo alijaribu
kulitumikia (2Wakorintho 4:8-15; 7:2-6; 11:23-33). Mwisho
wa maisha ya Paulo ulikuwa kukatwa kichwa na shoka ya
mwuaji wa serikali pale Roma.
Lakini muda mfupi kabla ya kifo chake, Paulo alitamka
kwamba thawabu yake yote ilikuwa “taji ya haki, ambayo
Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si
mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa
kwake” (2Timotheo 4:8).
Maisha ya Paulo haikuwa ya maana kufuatana na vipimo
vya dunia vya “ufanisi”. Pengine hata Wakristo fulani leo
wasingeona kuwa Paulo alikuwa mtume mwenye ufanisi.
Lakini sifa ya Paulo ilikuwa kwamba alitangaza Injili ya
Yesu Kristo kwa ujasiri (Matendo 17:1-6). Alijulikana kuwa
mtu mwenye mamlaka na uwezo, hata katika ufalme wa
mapepo (Matendo 19:15). Aliwafundisha na kuwafunza watu
wengine, na kuanzisha makanisa. Paulo akiwa na upuzio wa
Roho Mtakatifu aliandika sehemu ya theluthi moja ya Agano
Jipya letu (hasa wakati alipokuwa gerezani kwa ajili ya imani
yake). Na mtume Paulo alikuwa mtendaji mkuu wa kueneza
Injili katika ulimwengu wote uliojulikana wakati ule. Paulo
alikuwa kweli amepokea upako wa Mungu, akijaa uweza wa
Roho Mtakatifu (Wakolosai 1:24-29)!
Ni lazima tuelewe kikamilifu kusudi la upako wa
Mungu. Hatupewi upako wa Mungu kwa ajili ya manufaa
yetu wala kwa kuwapendeza watu wengine. Ni kwa ajili ya
kutimiza makusudi ya Mungu! Ni ya kutoa huduma kwa njia
inayogeuza maisha ya watu kwa Neno na uweza wa Mungu!
Kujipima
Ni lazima tutumie upambanuzi siku hizi, ili tutambue
nini ni ya Mungu na nini ni ya binadamu. Lazima
tupambanue yaliyotoka kwa Roho wa Mungu, na yaliotoka
kwa roho mwingine (2Wakorintho 11:4). Biblia hutuambia
kwamba, wakati unapoendelea, ufalme wa mapepo utazidi
kujaribu kuwapotosha watu. Hata Wakristo watadanganyika
na kupotoshwa, wakikataa mambo ya kweli yaliyotoka kwa
Mungu (2Timotheo 3:1-9; 4:3-4).
Ni lazima “kujaribu roho” (1Yohana 4:1-6), kwa sababu
ibilisi hufanya kazi kwa bidii akijaribu kuwadanganya watu
na kuwaangamiza (2Wakorintho 2:11; 10:1-5; 11:14; 1Petro
5:8). Pia, watu waovu watajaribu kumtumia Mungu na
mambo ya kiroho kwa kujifanikisha wenyewe (2Wakorintho
11:13-15; Wafilipi 1:15-16; 2Petro sura ya 2).
Tunawezaje basi kufahamu upako halisi wa Roho
Mtakatifu?
Na tunaweza kutumia vipimo gani katika kujipima
wenyewe ili kuhakikisha kwamba tunatembea kwa uaminifu
na utii kwa Kristo kwa ajili ya upako?
Hizi ni alama saba zitakazodhihirika kuhusu upako wa
Roho Mtakatifu.
Upako halisi wa Roho Mtakatifu:
1) utamtukuza Yesu Kristo wakati wote (Yohana 16:14),
si hasa kuwatukuza watu wala hata huduma yenyewe;
2) utafuatana na kulingana na mashauri yote ya msingi
Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO • 43
ya Neno la Mungu (Yohana 14:26), kwa sababu Roho
Mtakatifu kamwe hatakwenda kinyume cha Neno la Mungu
lililoandikwa;
3) utasababisha uhai wa kiroho katika wale wanaokutana
na huduma au kuipokea (Yohana 6:63) - watu watajitoa kwa
Yesu, Neno Lake na njia Zake kwa ukamilifu zaidi;
4) utawaelekeza watu kwa Yesu na wokovu Wake, si kwa
mtu mwingine wala kwa ishara na maajabu tu (Yohana
15:26);
5) utajaribu kuendeleza amani na umoja katika Mwili wa
Kristo (1Wakorintho 12:1-14) kati ya watu wanaompenda
Bwana na Kanisa Lake kuliko msimamo wao;
6) utakuwa na uwezo unaogeuza maisha (1Wakorintho
2:4-5; 4:20; 1Wathesalonike 1:5), ambao ni matunda ya
huduma yenye upako;
7) utazalisha tabia ya Kristo ndani ya watu (Wagalatia
5:16-24; 2Wakorintho 3:18) - ndiyo mapenzi ya Mungu kwa
ajili ya kila mfuasi wa Kristo!
Kuwepo kwa alama hizi saba za upako halisi kutakuwa
uthibitisho wa watu wanaotoa huduma katika upako wa Roho
Mtakatifu. Alama hizi pia zinatusaidia tuone haja ya kuwa na
maono ya muda mrefu ya upako.
Upako wa mara moja unaweza uwepo kwa dakika fulani
ya huduma. Lakini sisi kama wachungaji wa Mwili wa
Kristo, tumepewa upako ili tufanye watu wawe wanafunzi na
kuwaandaa watu wa Mungu - kazi ya muda mrefu – si tu
kwa ajili ya dakika za huduma yenye msisimko za mara kwa
mara.
Utumie orodha ya hapo juu katika kuchunguza huduma
yako. Kama kiongozi wa kanisa, una wito wenye thamani na
umuhimu wa kuchunga watu wa Mwili wa Kristo. Kristo ndiye
Mchungaji wetu Mkuu. Yeye amekuita uwe mchungaji
msaidizi. Utawajibika kumtolea Yeye ripoti ya jinsi
ulivyotimiza agizo Lake la kuwachunga kondoo Zake (1Petro
5:1-4).
Je, Tunaweza Kupokea Zaidi?
Nafasi yetu ni ya kumfuata Kristo kwa bidii na uaminifu.
Lazima tutumie vipimo na kanuni ya Neno la Mungu katika
maisha yetu, na kukua kila wakati katika uwezo wetu wa
kuongozwa na Roho Mtakatifu.
Wito wa huduma uliopewa na Mungu si huduma yako.
Ni huduma YAKE ambayo Yeye anataka kutenda kupitia
kwako! Huduma inayotendeka kwa kufuata njia ya Mungu
itazaa matunda mengi (Yohana 15:14-16) nao utafuatana na
upako Wake.
Tumethibitisha kwamba upako wa Roho Mtakatifu
umeandaliwa na Mungu aliye mfalme. Hufuatana na wito
wetu na vipawa vyetu. Upako huu hautii mapenzi ya
mwanadamu, isipokuwa tu kwamba tunaweza kuupokea au
kuukataa.
Kama wewe unafanana na mimi, unataka zaidi ya upako
wa Mungu katika maisha na huduma yako. Kilio cha moyo
wako ni kuwa chombo kifaacho kwa kutimiza makusudi ya
Ufalme wa Mungu.
Kwa hiyo je, inawezekana siyo tu kupokea upako wa
Mungu, bali pia kukua katika upako ambao Mungu
anatupatia?
Je, tunaweza kupokea zaidi kuliko tunaopokea sasa?
Tuangalie maswali haya kwa kifupi.
B. KUKUA KATIKA UPAKO
Bwana anataka upokee upako wa Roho Mtakatifu.
Anataka pia ukue katika uwezo wako wa kuishi na kutoa
huduma katika upako wa Roho Mtakatifu.
Hakuna njia za mkato za kukua katika upako wa Mungu.
Wala upako si wetu wa kukamata na kutumia ili tuwe na
nguvu katika huduma kwa ufanisi wetu. Kumbuka kwamba
uweza wa Mungu hautengani na nafsi Yake. Upako ndio
uwepo wa Roho Mtakatifu - nao daima utakuwa chini ya
mapenzi na makusudi ya Mungu, si yetu.
1. Tabia Na Upako
Ni muhimu kutambua kwamba jinsi unavyokua katika
tabia ya Kristo, ndivyo utakavyokua katika upako. Tabia yetu
ama italingana na upako na kuufungua, ama itaziba na kuzuia
kazi ya Roho Mtakatifu kupitia kwetu (taz. Waefeso 4:30;
1Wathesalonike 5:19).
Kumbuka kwamba sisi kwanza na hasa ni wana wa
Mungu wa kiume na kike. Kazi ya dhabihu ya Kristo
ilituwezesha turejeshwe katika uhusiano pamoja na Baba
yetu wa Mbinguni.
Yesu Kristo, kama Kichwa cha Kanisa (Wakolosai 1:18;
2:19) ametuita na kutupatia karama za kiroho - ili sisi, kama
wana wa Mungu, tuweze kutumikia Mwili wa Kristo
(Waefeso 4:11-16; 2Timotheo 1:9). Karama na wito hizi za
kiroho zitafanya kazi kikamilifu na kwa usahihi pale tu
ambapo zimetiwa nguvu na kuongozwa na Roho Mtakatifu
(1Wakorintho 12:7 - karama zote zinafanya kazi kufuatana na
kanuni hii).
Ndiyo sababu tunaweza kusema kwamba huduma yote
yenye upako wa kweli inatokana na uhusiano. Uhusiano wetu
na Kristo wa kujitolea na kukua ndio msingi ambamo
huduma inayogeuza maisha hutenda kazi.
Haidhuru kiwango chako cha upevu au ujuzi kwa
Bwana, hali hii ni ya kweli. Usisahau kamwe kwamba
huduma yenye ufanisi hutokana na kuendeleza uhusiano hai
unaozidi kuwa wa ndani pamoja na Yesu Kristo!
44 • MATENDO
Hakuna njia za mkato za kukua
katika upako wa Mungu. Wala
upako si wetu wa kukamata na
kutumia ili tuwe na nguvu katika
huduma kwa ufanisi wetu.
Kumbuka kwamba uweza wa
Mungu hautengani na nafsi Yake.
Upako ndio uwepo wa Roho
Mtakatifu nao daima utakuwa
chini ya mapenzi na makusudi ya
Mungu, si yetu.
Nakala 16 / Nambari 1
Mchungaji kwa Mchungaji: Ni rahisi mno katika
huduma kuzembea uhusiano wetu na Bwana. Huenda
tunaanza kufikiri kwamba “mana” ya jana kutoka
Kwake inatosha kwa ajili ya leo. Haitoshi!
Yesu ametoa maonyo makali yanayodhihirisha
tatizo hili. Soma Mathayo 7:21-23. Watu wanaoelezwa
hapa ni watu walio ndani ya Kanisa - watu wenye
huduma za unabii, wanaotoa mapepo, wanaotoa
huduma katika ishara na maajabu, n.k.
Lakini viongozi hao kwa wakati fulani njiani,
wameacha “upendo wa kwanza” (Ufunuo 2:1-5).
Wamedanganyika, wakifikiri kwamba kuendeleza sura
ya ufanisi katika huduma (kuonekana kwa nje)
kunatosha. Huenda wanaweza kukariri mistari ya
Maandiko na kutumia mamlaka ya jina la Yesu. Lakini
hawatembei katika uhusiano wa ukweli, utiifu na uhai
pamoja na Bwana. Hawamjui, wala Yeye hawajui wao.
Hatima yao ni ya kutisha (Mathayo 7:23).
Mkakati Wa Shetani
Kama tulivyojifunza, kazi moja ya Roho katika maisha
yetu baada ya kuokolewa ni kubadilishwa kwetu binafsi
(Warumi 8:29; 2Wakorintho 3:18). Ni kushirikiana kwetu
katika maisha yetu yote - pamoja na kutii kwetu kila siku kwa
Neno la Mungu, na kuwa na muda wa kukaa pamoja na Yeye
- kunakositawisha tabia ya uchaji ndani yetu.
Shetani anapinga kwa bidii kukua kwa tabia ya uchaji
katika viongozi wa kanisa. Ibilisi hawezi kupotosha au
kutuibia upako wa Roho Mtakatifu wala karama Zake.
Ukweli ni kinyume chake: “Kwa kusudi hili Mwana wa
Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi” (1Yohana
3:8), taz. pia Luka 10:17-20; Warumi 8:37-39; 2Wakorintho
10:3-5; Wakolosai 2:14-15; Waebrania 2:14).
Kwa sababu ibilisi hana uwezo wa kudhuru wala
kupotosha upako wa Roho Mtakatifu na karama Zake, lengo
lake kuu ni wewe! Shetani anajaribu kwa bidii
kuwanyang’anya, kuwaua na kuwaangamiza watakatifu
(Yohana 10:10). Njia yake moja ya kufanya hivyo ni kujaribu
kubomoa tabia ya uchaji, hasa katika viongozi wa kanisa.
Ibilisi anajaribu kupotosha viongozi wa kanisa wasifae
kwa ajili ya makusudi ya Mungu (1Wakorintho 9:24-27;
2Timotheo 2:19-22). Anafanya hivyo kwa njia ya vishawishi,
kudanganya, kutisha, kuogofya, kugawanya, kiburi, ubinafsi
- dhambi yoyote ile, Shetani atakuwa chanzo chake!
Kwa kawaida majaribu ya Shetani huanza katika mambo
madogo. Anaanza kuvuta tamaa zetu za kimwili na asili yetu
ya ubinafsi. Ibilisi amekuwa na karne nyingi za kuchunguza
mienendo ya wanadamu, na kutengeneza njia za kujaribu
kutuangusha. Hatuhitaji kumwogopa - lakini kwa hakika
tunahitaji kuwa waangalifu na kujilinda wakati wote (1Petro
5:8-9)!
Uangalie kwamba tunakuwa wazi zaidi kwa hila za
ibilisi tunapozembea uhusiano wetu unaoendelea na kukua
pamoja na Yesu Kristo (1Timotheo 4:1-2; 2Timotheo 1:1-9;
Waebrania 2:1-3). Pasipo ukaribu na Kristo, tutajaribiwa
zaidi sana kujipatia udhuru, kusingizia maanguko ya
mwenendo, kukubali mawazo ya tamaa - mambo ambayo
yatatuongoza katika dhambi, udanganyifu na kushindwa
(Yakobo 1:13-15).
Mungu anataka upako Wake upenyee tabia yetu. Tabia
ya uchaji (au ukosefu wake) huhusiana moja kwa moja na
uzalishaji na ufanisi wetu katika huduma. Mungu anataka
upako Wake utiririke na kutokea ndani ya maisha yetu,
pasipo kizuizi cha ukosefu wa uchaji. Si ‘kutia chumvi’
kusema kwamba upako unahusiana na tabia (yetu) sawasawa
na uweza (wa Mungu).
Tutumie muda kidogo sasa kujifunza kutoka katika mtu
aliyekuwa na upako kuliko mwingine yeyote aliyewahi
kuishi.
2. Nyayo Za Bwana
Kwa kweli Yesu Kristo alikuwa mtu aliyekuwa na upako
kuliko mwingine yeyote aliyetembea hapa duniani. Yeye
alikuwa na Roho Mtakatifu pasipo kipimo (Yohana 3:33-35).
Upako Wake usio na kifani ulitabiriwa karne nyingi kabla ya
kuzaliwa Kwake (Isaya 61:1-3). Yesu alithibitisha unabii huu
mwanzoni mwa huduma Yake (Luka 4:17-20).
Huduma ya Yesu duniani ilithibitisha kwamba Yeye
alikuwa kweli Mwenye Upako HASA. Tukiangalia Injili ya
Luka sura ya 4 na 5, tunaona mara moja uweza Wake mkuu
tangu mwanzo wa huduma Yake. Yesu alitiwa mafuta ili:
• Atoe mapepo (4:33-37,41);
• Afundishe kwa mamlaka (4:22,32);
• Aponye wagonjwa (4:38-40; 5:15);
• Awaite watu watubu (5:17-26,31-32);
• Atende ishara na maajabu (5:4-9);
• Awaite watu katika huduma kinabii (5:10,27);
• Aanzishe kundi la uongozi (5:11);
• Amponye mtu mwenye ukoma, tendo la ajabu wakati ule
(5:12-15).
Hii ni mifano tu kati ya mengine, jinsi Yesu alivyoanza
huduma Yake hapa duniani. Alifanya zaidi nyingi sana
kuliko haya. Kuna Mwana wa Mungu mmoja tu aliyekuja
duniani, aliyekufa kwa ajili yetu, na halafu aliyefufuka ili
athibitishe kwamba Yeye alikuwa Mungu wa kweli!
Yesu Ndiye aliyetuita (1Wakorintho 1:26-31). Yeye
ametupa karama zote tunazohitaji (Waefeso 4:11-16) na
uwezo (Yohana 16:7) ili tutimize mapenzi Yake (Yohana
15:16).
MATENDO • 45
Shetani:
Mpelelezi wa
tabia za binadamu
tangu awali
Nakala 16 / Nambari 1
Kristo alituma Kanisa Lake liendeleze kazi Yake
(Matendo 1:4-8). Ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu peke
Yake kwamba sisi tunaweza kufanya hivyo kikamilifu. Roho
yule yule aliyemtia Yesu mafuta sasa amemiminwa hapa
duniani, akipatikana kwao wote wanaomwamini Yesu Kristo
kwa ajili ya wokovu (Warumi 8:14-17). Haleluya!
Kufuata Nyayo Za Yesu
Mungu anawatafuta watu walio waaminifu Kwake
(2Nyakati 16:9). Yesu alijithibitisha kuwa mwaminifu kwa
Mungu na kumpendeza (Mathayo 3:17). Yesu alitii mapenzi
ya Baba katika mambo yote (Waebrania 10:5-7). Ingawa
Yesu alikuwa na uwezo wa kutenda dhambi, hakutenda
dhambi hata mara moja (Waebrania 4:15).
Kwa kuwa Yeye ni mfano wetu katika mambo yote,
tunaweza kujifunza nini kutoka katika maisha ya Yesu Kristo
kuhusu kukua katika upako? Tufuate nyayo Zake mara moja
tupate mafunzo yatakayotukuza katika tabia zetu na katika
mambo ya kiroho.
a. Yesu alikuwa chini ya mamlaka. Yesu alichagua
kutii mamlaka iliyokuwa juu yake. Hata kama kijana, alitii
wazazi Wake na mamlaka nyingine katika jamii Yake (Luka
2:41-51). Na wakati wote wa huduma yake ya duniani, Yesu
aliendelea kumtii Baba Yake wa Mbinguni.
Biblia inatufundisha kwamba sisi kama viongozi
tumewekwa chini ya taratibu za mamlaka katika maisha yetu.
Kuna serikali, madhehebu, makanisa (sharika), kazi - hivi
vyote vina taratibu za utawala au mamlaka.
Tunaweza kuona usalama na faraja kwamba mamlaka
hizi zipo juu yetu. Lakini mara nyingine, tunaweza
tusikubaliane nazo. Pengine tutajikuta chini ya watu wasio
wachaji, wenye ubinafsi au ukatili.
Inawezekana kabisa kwamba katika maisha yetu
tutatumika chini ya mamlaka yenye ufanisi kwetu na
mamlaka inayoonekana haina maana. Lakini haidhuru hali ya
mamlaka hizo, Neno la Mungu limetuagiza kuhusu umuhimu
wa kutii kama mfano wa maisha. Haya ni pamoja na kutii:
• Mungu (Yakobo 4:7);
• Mamlaka za serikali (Warumi 13:1-7; 1Petro 2:13-17;
taz. pia angalizo hapo chini);
• Uongozi katika Mwili wa Kristo (1Wakorintho
16:15-16; 1Wathesalonike 5:12-13; Waebrania 13:7,17);
• Kunyenyekeana sisi kwa sisi katika Mwili wa Kristo
(Waefeso 5:21; 1Petro 5:5);
• Waume, na wake zao (Waefeso 5:22; Wakolosai 3:18);
• Wazazi, na watoto wao (Waefeso 6:1-3; Wakolosai
3:20);
• Waajiri, na waajiriwa wao (Waefeso 6:5-9; Wakolosai
3:22 - 4:1; 1Petro 2:18-21).
ANGALIZO: Sisi kama Wakristo, tunapaswa kuvumilia
serikali yetu kila iwezekanapo. Yesu hakutafuta njia ya
kupindua serikali ya Rumi, ingawa wakati ule iliwatesa
Waisraeli vibaya sana. Lakini kama serikali au kiongozi
anawakataza watu uhuru wa kumwabudu Mungu na kumtii,
ni lazima tuendelee kumtumikia Mungu - hata kama tutapata
mateso (1Petro 4:12-19).
Wakati pekee ambapo unaweza kufikiria kukataa kutii
mamlaka iliyo juu yako ni kama wamekuamuru uvunje amri
ya Maandiko, au kanuni ya kimaadili (yaani, kwa kusema
uwongo, kuiba, kufanya zinaa, n.k.).
Kwa mfano, kama mamlaka ya serikali inakuamuru
uache kuhubiri Injili au kutamka kwa jina la Yesu, amri kuu
ya Kristo inakulazimisha uendelee kutamka. Mitume
waliendelea kuhubiri namna hii (Matendo 4:1-31; 5:17-42;
8:1-4). Ukikabiliwa na hali kama hii, utahitaji uangalifu,
hekima na ujasiri kwa wingi. Uongozwe na Roho Mtakatifu,
na Mungu atatukuzwa (Marko 13:9-13)!
Kanuni Ya Kunyenyekea
Kunyenyekea ni kanuni ya kimsingi katika maisha ya
mwamini, na hasa maisha ya kiongozi wa kanisa. Kwanza
ni lazima kabisa tumnyenyekee Mungu katika mambo yote.
Halafu inatubidi tuchague kuwanyenyekea walio na
mamlaka juu yetu - katika jamii, dhehebu, kazi au hali
yoyote nyingine.
Hata kama hatukubaliani nao, kuwapenda wala
kuwaheshimu, bado inatubidi tuendelee kuwanyenyekea
katika mwelekeo wetu na matendo yetu.
Sababu pekee kabisa ya kinyume ni ikiwa, katika nafasi
yao ya mamlaka, wamekuamuru uvunje Neno la Mungu au
kama wanawaongoza wengine wafanye hivyo.
46 • MATENDO
Uruhusu mfano wa Yesu
uongoze kukua kwako.
Nakala 16 / Nambari 1
Mchungaji kwa Mchungaji: Kuna wakati ambapo
tunaweza kupata shida na mtu mwenye mamlaka.
Huenda tunaona kuwa tunanyanyaswa au hatupewi
heshima inayotuhusu.
Mfano wa Yesu kwetu katika hali hizi ni kwamba
Yeye “alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya
mtumwa” (Wafilipi 2:7). Kristo hakutafuta kibali cha
watu wala sifa yao, kwa upande mmoja kwa sababu
alijua havina maana yoyote; watu wanabadilisha maoni
yao haraka sana (Yohana 2:23-25; 6:15,26,60-66).
Badala yake, Yesu Kristo alitafuta furaha ya Baba
Yake wa Mbinguni. Pia alichagua nafasi ya mtumishi
(Mathayo 20:28). Kutoka katika moyo Wake wa
kunyenyekea na kutumika kulikuja wokovu kwetu na
utukufu mkuu kwa Mungu (Wafilipi 2:7-11).
Sisi kama viongozi wa kanisa, tutawekwa katika
nafasi za mamlaka mara kwa mara. Ili tuongoze kwa
ufanisi tukitumia mamlaka, inatubidi kwanza tujifunze
kuishi na kutembea chini ya mamlaka! Maana yake ni
kwamba hatuna budi tufahamu jinsi ya kuishi kufuatana
na kanuni ya kunyenyekea.
Ikiwa wewe unapata shida na kiongozi fulani
mwenye mamlaka, kuna njia za kiutendaji za kufuata.
Kwanza, umwombee mhusika kila siku. Kufanya
hivyo kutakusaidia kumwona kwa upande wa Mungu.
Halafu, umtafute Bwana kuhusu ufumbuzi Wake wa
shida yako. Uchunguze Maandiko, na kumsubiri Bwana
akupe jibu Lake.
Huenda itakubidi umwendee huyu mtu na
kumshirikisha shida yako kwa unyenyekevu (Mathayo
5:23-24). Unaweza pia kutafuta ushauri wa watu wenye
hekima na wasiopendelea upande wowote, ambao
watakusaidia kutatua tatizo na siyo tu kushikamana na
wewe.
Mwisho ulinde moyo wako mwenyewe (pamoja na
kutokulalamika wala kusengenya) na kumwamini
Mungu akutetee (Zaburi 5:1; 7:10; 31:2; 59:16-17; n.k.).
Mfano mkuu unapatikana katika maisha ya Daudi,
aliyechagua kumheshimu Mungu na kusubiri wakati
Wake ingawa matendo ya Sauli yalikuwa magumu na
mara nyingine pasipo uchaji (soma 1Samweli sura
ya 16 mpaka 24).
Huenda Mungu si chanzo cha jaribu au tatizo fulani
katika maisha yetu. Lakini ameahidi kutumia kila hali katika
maisha yetu kwa wema; “wema” huu ni kututengeneza sisi
katika mfano wa Kristo (Warumi 8:28-29).
Mara kwa mara Mungu atatumia mambo magumu
yanayotukabili katika kupima mioyo yetu (Kutoka 20:20;
1Nyakati 29:17). Wakati mwingine, uhusiano fulani wenye
magumu utatulazimisha tupevuke. Kuchagua miitikio ya
kiuchaji katikati ya matatizo wakati wote kutatukuza katika
tabia.
Tukichagua kuwa na msimamo wa Kristo na moyo Wake
katikati ya majaribu, mara nyingi matokeo yake ni kwamba
Mungu atatukabidhi zaidi ya mamlaka Yake, na uwezo na
upako Wake.
b. Yesu alikua katika kupevuka. Yesu alijitoa katika
utaratibu wa kukua wenye uimara na uwiano (Luka 2:52).
Ingawa mstari huu unaelekea kuhusiana na ujana wa Yesu,
bado ni mfano kwetu wa utaratibu wenye afya wa kukua na
kupevuka kwetu binafsi.
1) “kuendelea katika hekima” - chanzo kikuu cha hekima
ni Neno la Mungu. Unapolisoma na kulijifunza, umwombe
Roho Mtakatifu akufungulie ufahamu wako na kusema nawe
kuhusu ukweli (2Timotheo 2:15).
Yesu alisema kuwa Roho Mtakatifu “atawafundisha
yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia” (Yohana
14:26). Roho wa Mungu atahuisha (kufanya hai na yenye
kuhusika) maneno ya Yesu.
Roho Mtakatifu atatoa katika Neno la Mungu ambalo
sisi tumeweka kama akiba ya maisha yetu. Tunaweka akiba
hii tunaposoma Biblia, pamoja na kusikiliza au kujifunza
mafundisho na mahubiri imara ya ki-Biblia.
Kama viongozi wa kanisa, inatubidi tujitoe kikamilifu
katika kujifunza, kukariri na kutendea kazi Maandiko ili
tukue katika hekima. Lakini huku kusoma na kujifunza si
kwa ajili ya kutunga mahubiri! Ni kwa ajili ya kukua kwetu
binafsi. Ndipo, kutoka katika kisima hiki kinachoongeza
urefu kila wakati, tunaweza kuchota kweli zile ambazo
Bwana anazihuisha mioyoni mwetu wakati wa kuwahudumia
wengine. Hali hii itatupa sisi baraka kubwa sana, pamoja na
wale tunaowahudumia (1Timotheo 4:12-16).
2) “kuendelea... na kimo” - Tumejifunza kwamba miili
yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu (1Wakorintho 6:12-20;
1Wathesalonike 4:1-8). Kwa hiyo, tunapaswa tuwe wakili
wema wa miili ambayo Mungu ametupatia. Afya yetu ya
kimwili inahusiana moja kwa moja na uwezo wetu wa
kutumiwa na Mungu kwa ufanisi katika huduma.
Sote tunafahamu matumizi mabaya ya mwili wetu
ambayo ni ya kuepuka: ulevi au matumizi ya madawa
(Waefeso 5:18); zinaa na uasherati (1Wathesalonike 4:3-5);
ulafi (1Wakorintho 6:12-13; 9:24-27). Badala ya haya,
tutumie miili yetu katika kumtumikia Bwana!
Biblia inatuambia kuwa mazoezi ya mwili yana thamani
ndogo kuliko uchaji (1Timotheo 4:8); lakini mazoezi yana
thamani fulani. Hata hivyo, tuweke vipaumbele vyetu,
tusihangaikie zaidi hali yetu ya kimwili kuliko hali yetu ya
kiroho.
Mazoezi kiasi ya mwili ya kila siku ni mazuri kwa afya
yetu. Ni muhimu pia kujaribu kula vyakula vinavyofaa kwa
afya. Tuangalie ratiba zetu kuhakikisha kwamba tunapata
usingizi wa kutosha. Mambo haya yanaweza kuongeza muda
wetu wa kuishi na ufanisi wetu wa kazi, kwa kuongeza idadi
ya miaka ambapo Mungu anaweza kututumia na kupokea
utukufu kutokana na huduma yetu Kwake!
3) “akimpendeza Mungu” - Yesu alitembea katika kutii
mapenzi ya Baba. Huduma Yake yote ilikuwa kutenda
mapenzi ya Baba Kwake (Yohana 5:19,30). Yesu alitamka
yale ambayo Baba alikuwa akiyasema (Yohana 8:26,28) na
kufanya matendo ya Mungu (Yohana 5:17; 9:4; 14:10).
Yesu alitii mapenzi ya Baba kikamilifu, hadi aweze
kusema, “[Baba] hakuniacha peke yangu; kwa sababu
nafanya sikuzote yale yampendezayo” (Yohana 8:29; taz. pia
Yohana 4:34; 6:38).
Lakini zaidi ya utiifu, Yesu pia alitembea katika
uhusiano wa karibu na wa ushirikiano na Baba kwa Roho.
Mara nyingi Yesu alikwenda kusali peke Yake (Luka 5:16).
Neno la Kiyunani lilitafsiriwa hapa “alikuwa akijiepua”
linaonesha kuwa kwenda kusali peke Yake kulikuwa mazoea
ya kawaida kwa Yesu.
Utiifu wa Yesu haukumfanya astahili upendo na baraka
Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO • 47
ya Mungu. Lakini ulihakikisha kwamba wala dhambi wala
kuridhiana yoyote havikuweza kuvunja uhusiano Wake na
Baba. Hali hii ni muhimu sana kwetu, kwa sababu Yesu
ametupatia sisi ahadi hiyo hiyo ya uhusiano wa karibu na
Yeye!
Yesu ameahidi “kujidhihirisha” kwetu tunapotembea
katika kutii amri Zake (Yohana 14:21-24). Utiifu wetu kwa
Kristo na Neno Lake, katika mambo makubwa na madogo,
utatusaidia kuwepo panapofaa kwa ajili ya kutembea kwa
ukaribu zaidi pamoja na Bwana wetu. Utiifu wetu haustahili
upendo wa Bwana. Lakini unasaidia kuwepo kwa uhusiano
na ushirika wa ndani zaidi pamoja na Baba, Mwana na Roho
Mtakatifu. Na kutoka mahali hapo pa uhusiano wa karibu
sana, upako wa Roho Mtakatifu utatiririka ndani yetu na
kupitia kwetu zaidi na zaidi.
4) “akimpendeza... na wanadamu” - Maana yake si
kwamba Yesu alitafuta sifa ya wanadamu wala kupata kibali
chao. Lakini Yesu alichagua kutokutenda kwa kiburi, ingawa
kweli Yeye alikuwa mkuu kuliko watu wote! Badala yake,
Yesu alisema na kutenda kwa upendo.
Neema Na Ukweli
Yesu alikuwa mfano kwetu wa uwiano kamili wa tabia
ya Mungu: “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi
tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee
atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli” (Yohana 1:14);
“Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na
kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo” (ms. 17).
Yesu alikaa pamoja na wenye dhambi (Mathayo 9:9-13)
na pamoja na watu wa dini (Luka 7:36-50). Aliongea kuhusu
upendo wa Mungu na makusudi Yake kwa wote waliokubali
kusikiliza. Yesu hakutafuta kibali cha watu wala sifa yao, bali
alitafuta njia ya kufunua moyo wa Mungu Baba na Neno
Lake katika kila hali.
Yesu alifundisha kwamba Mungu anatutazamia tutunze
mahusiano kati yetu yaliyo safi na pasipo unajisi. Biblia
inafunua wazi matendo mengi sana ya kimwili na dhambi
ambayo hayakubaliki kwa Mungu katika mahusiano yetu,
yakiwemo: kutosamehe, uchungu, hasira, wivu, kuonea,
ugomvi, masengenyo, kuhukumu, n.k. (Mathayo
5:21-24,43-48; 6:12,14-15; 7:1-6; 18:21-35; Warumi
12:9-21; Wagalatia 5:13-15,19-21; 1Yohana 2:9-10; 3:10-18
- hii ni mistari kadhaa tu kati ya mingi inayoonesha mkazo
wa Mungu kwa ajili ya kuwa na mahusiano yafaayo kati
yetu).
Hatuwezi kutawala misimamo na mienendo ya wengine;
lakini tunaweza kuamua juu ya misimamo na mienendo yetu
binafsi. Na mara nyingi, msimamo wetu wa “neema na
ukweli” utafungua njia kwa upatanisho na amani pamoja na
wengine.
Tunapofanya kazi ya kuleta mahusiano mema, yajaayo
“neema na ukweli” ya Mungu, tunasitawisha umoja. Umoja
mkubwa zaidi katika Mwili wa Kristo ni kufungulia uwepo
wenye upako wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu,
makanisa yetu na jamii zetu. Pia ni ushuhuda kwa dunia wa
ukweli halisi wa Injili (Yohana 17:20-21).
c. Yesu alitembea kwa unyenyekevu. Kwa hakika,
Mungu Mwana alikuwa mwanadamu mnyenyekevu kuliko
wote. Yesu alikuwa Mungu hasa, lakini alitwaa namna ya
mtumwa na mfano wa mwanadamu, ili atoe uhai Wake kwa
ajili yetu sisi sote (Wafilipi 2:7-8). Kama sisi tutafuata nyayo
Zake, lazima tutembee kwa unyenyekevu.
Yesu alianza huduma Yake kwa kujinyenyekeza, hata
wakati ambapo haikuonekana kuwa ni lazima afanye hivyo.
Tunaona hali hii Yesu alipofika kwa Yohana Mbatizaji wakati
alipokuwa akiwabatiza watu kwa ajili ya kutubu dhambi
(Mathayo 3:13-17).
Ni wazi kwamba Yesu hakuhitaji kutubu, kwa sababu
Yeye hakuwa na dhambi (Waebrania 4:15). Hata Yohana
alijaribu kumzuia Yesu, akijua kwamba Yesu hakuwa na
dhambi tena alikuwa mkuu kuliko yeye (Mathayo 3:14).
Lakini Yesu bado aliomba abatizwe na Yohana: “Kubali hivi
sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote”
(ms. 15).
Kwa nini Yesu alitaka abatizwe? Tukio hili lilianzisha
huduma ya Yesu. Kwa hiyo, Yesu alichagua tendo hili la
kujinyenyekeza katika ubatizo wa maji ili afungamane na
watu wenye dhambi - watu kama wewe na mimi.
Yesu, Mwana wa Mungu asiye na dhambi yoyote,
alichagua kujiweka sawa na wanadamu wenye dhambi katika
utume Wake wa kuleta tumaini la wokovu kwa wanadamu
wote. Ili “kuitimiza haki yote” Yesu alikiri mapenzi ya
Mungu kwamba Yeye achukue mzigo wa dhambi zote za
wanadamu, awe Mkombozi na Mwokozi wao.
Mtumishi Wa Watumishi
Yesu alijua kwamba utume Wake kutoka kwa Mungu
ulikuwa kama mtumishi mnyenyekevu kwa wanadamu wote
(Mathayo 20:28). Alitambua hali hii alipokuwa na miaka
kumi na miwili tu (Luka 2:41-50). Ilithibitishwa tena na yale
yaliyotokea mara baada ya kubatizwa Kwake kwa maji.
“Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda
kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona
Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na
tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu,
mpendwa wangu, ninayependezwa naye” (Mathayo 3:16-17).
Mambo matatu yalimtukia Yesu alipotii mapenzi ya
Baba Yake kwa unyenyekevu katika ubatizo:
1) “mbingu zikamfunukia” (ms. 16b) - Hii ni alama ya
Mungu akijifunua pamoja na makusudi Yake kwa njia mpya
yenye nguvu kupitia kwa Mwana Wake. Yesu alikuwa na
Ndiye Mungu (Wakolosai 1:15-16,19; Waebrania 1:3).
Kumwona, kumsikia na kumjua Yeye ni kumjua Mungu
kikamilifu. Katika Yesu, Mungu alikuwa amejidhihirisha
kwa binadamu mwenye dhambi kwa uwazi zaidi kuliko
wakati wowote uliotangulia.
2) “Roho wa Mungu akishuka” (ms. 16c) - Yesu alipokea
upako wenye uweza usio na kipimo wa Roho Mtakatifu. Huu
ulimwezesha kutimiza makusudi na mapenzi ya Mungu,
akifunua moyo wa Mungu kwa ukamilifu zaidi na kufungua
njia ya wokovu kwa watu wote. Katika kupokea upako wa
Roho Mtakatifu, Yesu amepata kuwa Yeye anayembatiza
mwamini na Roho Mtakatifu (Luka 3:16).
3) “Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa
naye” (ms. 17). Kwa hakika, Mungu alitamka kwa ufunuo wa
ndani sana katika kuthibitisha asili ya Kristo. Lakini tamko
hili lina maana yenye uzito hata zaidi.
Kuna sehemu mbili za tamko hilo zinazotokana na
maneno ya unabii ya Agano la Kale kuhusu Masihi. “Huyu ni
Mwanangu, mpendwa wangu” hutoka Zaburi 2:7. Wayahudi
48 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1
walikubali Zaburi hii nzima kama maelezo ya kinabii kuhusu
Masihi ajaye.
Sehemu ya pili, “ninayependezwa naye” hutoka Isaya
42:1. Sura hii nzima ya Isaya, pamoja na sura ya 43, ni unabii
kuhusu Masihi kama Mtumishi anayeteswa, Mkombozi
atakayeleta haki, rehema na wokovu wa Mungu kwa
wanadamu wote.
Mungu alipotamka maneno haya, alithibitisha kwamba
Yesu kweli ndiye Masihi aliyesubiriwa na kutabiriwa kwa
muda mrefu. Yeye ni Mteuliwa wa Mungu awe Mwokozi,
Mfalme wa wafalme wote na Bwana wa mabwana wote.
Alithibitisha pia kwamba njia ya kufikia taji ya milele ya
ki-Mungu ni kupitia msalabani. Mfalme wa wafalme
alipaswa kwanza awe Mtumishi wa wote (Wafilipi 2:5-11).
Njia yake ya kufikia kiti cha enzi ilikuwa utiifu kwa Baba
(Waebrania 5:8). Yesu angetimiza utume uliohamasishwa na
upendo (Yohana 3:16).
Yesu Alilenga Kuwafikia Wote
Kutokana na matukio haya katika ubatizo wa Yesu,
tunaweza kujifunza mambo muhimu kuhusu upako.
Kwanza, utiifu wa hiari wa Yesu katika kujinyenyekeza,
hata wakati pasipokuwa lazima, ulifungua zaidi ya yale
ambayo Mungu alikusudia kwa ajili Yake na kupitia Kwake.
Yesu aliwafikia wote, pasipo kuwahukumu, akawapatia
upendo, msamaha na wokovu wa Mungu (Yohana 8:1-11).
Aliongoza kwa kuwa mfano katika unyenyekevu (Yohana
13:1-17), akifunua kikamilifu kabisa moyo wa Mungu wa
upendo pale msalabani (1Yohana 4:9-10).
Mchungaji kwa Mchungaji: Kiongozi wa kanisa,
sisi pia lazima tutembee katika kumtii Mungu kwa
unyenyekevu. Lazima tuwapelekee wote Injili kwa
unyenyekevu. Huenda kweli hizi zinaeleweka wazi.
Lakini haina maana kuwa tunazitendea kazi! Mara
nyingi kujinyenyekeza ni hamasa kubwa sana.
Unyenyekevu unahusiana na tabia yetu moja kwa
moja. Na tabia yetu ni muhimu kabisa kwa ajili ya kukua
na kuzaa matunda kwa kutenda kazi katika upako wa
Roho Mtakatifu.
Mungu anawapinga wenye kiburi; lakini anawapa
wanyenyekevu neema. Nani kati yetu hahitaji zaidi ya
neema ya Mungu katika maisha yake? Inatolewa kwetu
kupitia unyenyekevu wetu.
Unyenyekevu huu si kujidhili au kujichukia
kunavyokusudia kuwaonesha wengine jinsi sisi tulivyo
“wa kiroho”. Mtu mwenye unyenyekevu wa kweli hana
haja ya kuuonesha kwa watu. Mtu anapojifanya kuwa
mnyenyekevu, matokeo yanachukiza sawasawa na
maonesho ya kiburi. Unyenyekevu wa kweli ni wa
moyoni. Ni mwelekeo wa kujali wengine bila ubinafsi.
Ni kutokuwa na kujiona wala kujivuna kabisa.
Nikupendekezee mielekeo na matendo ambayo
huweza kutusaidia tutembee katika unyenyekevu wa
kutii. Ni busara kuwa na mazoea haya kila siku:
• Tuwaombe wale tuliowaumiza au kuwaudhi
watusamehe.
• Tutoe msamaha kutoka moyoni, hata kama
haujaombwa.
• Tumpende mtu anayeonekana kwamba hapendeki
wala kustahili.
• Tuombe msaada, na kuupokea.
• Tukatae cheo, nafasi na heshima ambavyo faida
yake ni kutuweka “juu ya” wengine tu.
• Tuchague aina ya kazi isiyoonekana, kusifiwa,
kuheshimiwa wala kuleta faida au thawabu kwa
wakati huu.
• Tuwaachie wengine wapokee sifa ambayo huenda
ingalikuwa yetu kwa haki.
Yesu alifundisha mara nyingi kuhusu unyenyekevu,
akifahamu mwelekeo wetu wa kibinadamu wa kiburi
(Mathayo 6:1-15; 18:1-4; 20:20-28). Kama tunataka kupokea
upako halisi wa Roho Mtakatifu - ambayo huleta maisha
yaliyobadilishwa na kuzaa matunda - ni lazima tutembee
kama Yesu alivyotembea.
Ni njia ya kutii kwa unyenyekevu na uaminifu kwa
mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa katika Neno Lake; ni
kutembea kufuatana na mwongozo wa Roho Mtakatifu kila
siku (Mika 6:8).
d. Yesu alifahamu majaribu. Mara baada ya kubatizwa
Kwake, Yesu “akaongozwa na Roho” kwenda nyikani
afunge, kusali na kupambana na Shetani (Luka 4:1-12).
Tungeweza kutazamia kwamba baada ya tukio kuu la
kubatizwa na kutiwa mafuta ya upako wa Roho Mtakatifu,
Yesu angalitumwa moja kwa moja katika huduma ya wazi
yenye nguvu.
Lakini hekima ya Mungu imezidi yetu kabisa (Isaya
55:8-9) na makusudi Yake yameandaliwa kwa upeo wa
umilele. Ni wazi kwamba kujaribiwa kwa Yesu kulifuatana
na mpango wa Mungu (Mathayo 4:1; Marko 1:12-13; Luka
4:1).
Tunaweza kujifunza mengi kutokana na mielekeo ya
Yesu katika muda Wake wa kujaribiwa na kupimwa.
Hakulalamika wala kunung’unika. Hakushindwa na hofu
wala mashaka. Kupitia majaribu yote na katika ushindi wa
mwisho, Yesu alimtegemea kabisa Mungu Baba Yake.
Mchungaji kwa Mchungaji: Kama viongozi wa
kanisa, tunakabiliwa na majaribu, mateso na vishawishi
kwa wingi. Kuwa kiongozi katika Kanisa kunaweza
kututoa katika kilele cha furaha kuu mpaka kwenye
bonde la ubatilisho na kukatishwa tamaa - na mara
nyingi, kati ya Jumapili moja na nyingine!
Mchungaji mwenzangu, kama kiongozi katika
kanisa, wewe ni shabaha ya mashambulizi ya ibilisi.
Unaweza kujisikia kuwa peke yako katika mapambano
yako, ukifikiri hakuna mtu anayefahamu. Kuna jaribu la
kufikiri kwamba kama ungekuwa na upevu au tabia ya
kiroho zaidi, usingepitia vipindi vigumu hivi. Huenda
utashawishiwa ukate tamaa na kuacha utumishi.
Uwongo huu wa ibilisi unalenga kukuvunja moyo -
usiuamini!
Ukweli ni kwamba yeyote anayejaribu kumtumikia
Bwana atakabiliwa na mateso, majaribu na vishawishi
(2Timotheo 3:12) - hata Yesu. Maisha Yake ni mfano
kwetu jinsi tunavyoweza kukabili na kuvumilia majaribu
tukiwa na uhakika wa ushindi na tukimwamini Mungu.
Yesu alijua kwamba Mungu asingemwacha wala
kumsahau. Alijua kwamba Mungu ni mwaminifu na
ahadi Zake ni za kweli. Alijua kuwa angeweza kutimiza
mapenzi ya Baba yake, kwa uweza wa Roho Mtakatifu
na msaada wa Mungu: “Yeye ni mwaminifu ambaye
awaita, naye atafanya” (1Wathesalonike 5:24).
Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO • 49
Nakushauri ukariri mstari huu wa Maandiko, na
kuutafakari unapokabiliwa na hamasa au jambo gumu.
Pia uchukue muda wa kusoma maoni na kanuni
kutokana na maisha ya Yesu (Sehemu Ya III, B.2); hivi
pia vitakusaidia katika vipindi vya mambo magumu.
Yesu hakuuliza kwa nini haya yalimtokea. Bali
alistahimili majaribu, akiamini kuwa sehemu ya makusudi ya
Mungu ilitendeka kupitia katika maisha Yake na ndani yake
pia. Yesu alipata amani na uwezo katika kumnyenyekea
Mungu, na katika imani Yake kwa uwezo usiobadilika wa
Neno la Mungu.
Mavazi Ya Vita Yafaayo
Wakati ambapo Mungu anatufikisha katika eneo jipya la
wajibu au kufungua upako mpya katika maisha yetu, mara
nyingi anaruhusu kipindi cha kujaribiwa kifuate. Tuangalie
sababu kadhaa za kipindi hiki kuwa muhimu sana:
Tunahitaji “kukua katika” upako tunaopewa na
Mungu. Mungu atatunyosha kiroho kwa ajili ya ufanisi wetu.
Lakini kukua kunaweza kuumiza; huenda tutataka kuchukia
au kuzuia kukua kwetu. Lakini kwa sababu Mungu anajua
yaliyo mbele yetu, anataka kutuandaa kwa ajili ya kushinda
na si kushindwa. Kwa hiyo tunatakiwa tuwe na nguvu na
upevu, na pia tukubali yanayotendeka.
Tunaweza kuona mfano wa awali wa kanuni hii katika
Agano la Kale (1Samweli 17:38-39). Daudi anakwenda
kumkabili jitu Goliathi. Sauli anamtakia Daudi avae mavazi
yake ya vita. Lakini Daudi anakataa mavazi ya Sauli,
akisema, “Siwezi kwenda na vitu hivi, maana sikuvijaribu”
(ms. 39).
Daudi hakuweza kutumia kwa ufanisi mavazi
yasiyolingana na mwili wake na ambayo alikuwa hajazoea
kuyavaa. Ingawa mavazi haya yalimfaa Sauli, yalikuwa
mageni na yasiyoaminika kwa Daudi.
Vile vile, upako na karama ambavyo sisi tunatakiwa
tutembee navyo viwe vyetu - si wa mtu mwingine. Ni rahisi
mno kutegemea na kuamini karama na upako vya mtu
mwingine. Huenda tunajaribu hata kumwiga, tukihubiri
mahubiri yake au kuiga mtindo wake. Tunajaribu kutembea
katika “mavazi” yasiyo yetu!
Kule kujaribu kutembea katika upako wa mtu mwingine
ni tatizo, kwa sababu Mungu amekuita wewe. Anataka
akutumie wewe. Upako aliokupatia umetolewa kwa ajili
yako. Wewe ni chombo pekee ambacho Mungu anataka
kutumia kwa njia maalum. Kazi anayotoa ni kwa ajili yako,
na upako atakaokupa utalingana kikamilifu na kazi
unayotakiwa ufanye.
Lakini mara nyingi inachukua muda mpaka ufahamu na
“kukua katika” wito wako, kazi yako na upako wako. Mara
nyingine, Mungu atatumia kipindi cha kujaribiwa au
kuteswa, kwa kukusaidia ukue ili upate kuwa na nguvu na
kuweza kufanya katika “mavazi” yako mwenyewe - upako
ambao amekupa wewe - uwe na ushindi na kuzaa matunda
katika wito Wake.
Ni lazima tujifunze kutumia yale ambayo Yeye
ametupatia. Mara nyingi majaribu yatafunua upungufu
wetu. Katika vipindi vigumu, tunatambua hata zaidi jinsi
tunavyomhitaji Bwana na yale ambayo Yeye peke Yake
anaweza kutupatia.
Tumekwisha jifunza umuhimu wa kuwa na aina ya
udhaifu wa kiuchaji, unaotuongezea kumtegemea Mungu
(2Wakorintho 12:7-10). Aina hii ya udhaifu inatuwezesha
kuwa vyombo ambavyo upako wa Roho Mtakatifu unaweza
kutiririka kupitia kwake.
Haja Yetu Ya Mungu Isiyokwisha
Tunapojazwa upako wa Mungu, na kutenda kwa uhakika
na imani (vinavyotegemea utii), bado kuna hatari ambayo
inatubidi tuitambue. Hatari hii ni kwamba, polepole,
tunaanza kujitegemea wenyewe pamoja na ujuzi na ustadi
wetu tuliojiongezea. Hapo tunapunguza kumtegemea Bwana
na uweza wa Roho Mtakatifu. Si kwamba hali hii haina budi
itokee; lakini inaweza kutokea tusipokuwa waangalifu.
Yesu alisema, “Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi;
akaaye [kubaki, kuishi] ndani yangu nami ndani yake, huyo
huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno
lo lote” (Yohana 15:5).
Nikaze hapa kwamba upako wa Roho Mtakatifu
unamhusu Yesu tu. Hauhusu karama, uwezo wala utumishi.
Hauhusu hata wale tunaowahudumia - unamhusu Yesu! Tabia
saba za upako halisi [zilizoorodheshwa katika Sehemu Ya III,
A.3] zilifanana katika jambo moja: ZOTE zilimwashiria Yesu.
Ni katika Yeye tu, kwa Roho wa Mungu, kwamba sisi
“tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu” (Matendo
17:28). Haidhuru Mungu anatutumia kiasi gani, wala
tunapata ujuzi kiasi gani, inatubidi daima tutunze imani
yenye unyofu kama ya mtoto. Imani ya aina hii inahitaji
kumtumaini Bwana kwa unyenyekevu na kuongeza undani
wetu wa kumtegemea Yeye.
Asili yetu ya kibinadamu inaweza kutuelekeza katika
ubinafsi na hisia ya kujitegemea mbali na Mungu. Lakini
majaribu na mateso yatatukumbusha jinsi tunavyomhitaji
wakati wote, pamoja na neema Yake na uwepo Wake katika
maisha yetu.
Tunahitaji kutakaswa ili tuwekwe huru kwa ajili ya
kupokea upako Wake zaidi. Yesu alisema, “Roho ndiyo
itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia
ni roho, tena ni uzima” (Yohana 6:63).
Uwepo wa Roho wa Mungu katika maisha yetu utafanya
asili yetu ya dhambi kutokuona raha - ndiyo hali
inayotakiwa! Kwa sababu Roho na mwili (asili ya dhambi)
hupigana, au “kushindana” (Wagalatia 5:16-17; taz. pia
Yakobo 4:1-10; 1Petro 2:11).
Mungu anayajua yaliyo ndani ya mioyo, akili na nafsi
zetu ambayo yatazuia au kuziba upako wa Roho Wake
Mtakatifu. Majaribu na mateso mara nyingi hutusafisha,
yakisogeza madhaifu nje yaonekane na kushughulikiwa.
Kusafishwa Na Uchafu
Watu kama sonara wanaofua madini ya fedha na
dhahabu watakuambia kuwa mawe yanapochimbwa hujaa
uchafu. Inabidi kuyachemsha mpaka yayeyuke ili uchafu
uelee juu.
Ndipo uchafu (uitwao mavi ya madini) unaenguliwa kwa
ustadi juu ya madini yaliyoyeyuka (Mithali 25:4). Utaratibu
huu unarudiwa mara nyingi mpaka madini yawe safi kabisa
na kufaa kutumiwa. Watu wanaotia moto katika mawe
wanajua dakika halisi ya kuondoa madini kwenye moto ili
yasiungue.
50 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1
Kwa njia kama hii, Mungu atatumia majaribu
yanayoweza kuingia katika maisha yetu kufanya uchafu
uliopo katika maisha yetu “uelee juu” na kuonekana. Ndipo
unaweza kutambuliwa - na kuondolewa kwa njia ya toba,
uponyaji na ukombozi, viletavyo uhuru kutoka katika
vifungo vya asili yetu ya dhambi.
Mchungaji kwa Mchungaji: Kiongozi wa kanisa,
nini inaelea juu katika maisha yako wakati mazingira
“inachemka” (inazidi) au unapojisikia kuzidiwa na
shughuli? Unaitikiaje, unatafuta msaada wapi? Je,
yanayojitokeza yanafunua mwelekeo au mwenendo
ambao Mungu anataka kusafisha, kuponya au kuondoa
maishani mwako? Je, kuna jambo fulani ambalo Yeye
anataka kukufundisha katika jaribu au tatizo lako?
Vipindi hivi vya kukabiliwa na madhaifu yetu na
uchafu wetu si vya kuogopa. Mungu, katika upendo
Wake, atatumia majaribu, mateso na dhiki katika
kututakasa na kututengeneza. Pia atatupa mafunuo,
ufahamu, kutugusa na upendo Wake na kutufunulia
yaliyomo ndani ya Neno Lake. Anatumia nafasi hizi
kupanua imani yetu na kubadili tabia yetu ili tuwe
vyombo vyenye kufaa na kutumika zaidi.
Hekima Katika Majaribu
Mungu anatumia majaribu kututakasa na kutuongezea
nguvu. Mungu hatujaribu ili atufanye tujisikie tumeshindwa
au kwa sababu sisi “hatuna wema wa kutosha”. Hasha!
Mungu anaruhusu majaribu na mateso katika maisha yetu ili
atuongezee nguvu; kwa sababu Yeye hataki sisi tuwe
wadhaifu wakati tunapohitaji kuwa na nguvu (Mithali 24:10;
Yeremia 12:5). Mungu anatumia majaribu kutuandaa ili
tuweze kupokea, na kutumia kwa uaminifu, zaidi ya upako
Wake!
Ndiyo sababu Yakobo anatuhimiza: “Hesabuni ya kuwa
ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali”
(Yakobo 1:2). Maandiko yanaendelea kututia moyo tuvumilie
majaribu (ms. 3 na 4), tukijua na kuamini kwamba Mungu
wetu mwaminifu atayatumia kwa ufanisi wetu na utukufu
Wake. Ndiyo ahadi Yake kwetu (Warumi 8:28-29).
Yakobo anaendelea kutushauri tuombe pia hekima
(Yakobo 1:5-8) - na, kwa imani, kutazamia kusikia kutoka
kwa Mungu. Kwa nini tunahitaji hekima hii? Kwa ajili ya
kutoroka majaribu tu? Sivyo, ila ni kutuwezesha
kupambanua na kufahamu ili tujue tufanye nini wakati
Mungu anapotenda kazi ndani yetu - haidhuru chanzo cha
jaribu ni nini.
Hitaji La Historia Iliyothibitika
Mungu anataka kutupa zaidi ya Roho Wake. Lakini mara
nyingi maana yake ni kwamba tuwe na nguvu ya kitabia na
upevu ili tusipoteze au kuchezea karama Zake. Usingempa
mtoto wa miaka mitano gari, hata kama yeye ameona yu
tayari kuliendesha, sivyo? Asingekuwa na upevu wa kutosha
ili awajibike juu yake. Anahitaji kwanza kukua kimwili,
kiakili na kihisia.
Kanuni hii ni kweli pia katika Ufalme wa Mungu.
Angalia maagizo ya Paulo kwa Timotheo kuhusu kuwateua
wazee (maaskofu) na mashemasi (1Timotheo 3:1-13). Ni
vema mtu akipenda kuwa kiongozi, maana atamani kazi
njema. Lakini lazima awe na historia iliyothibitika ya
mwenendo na tabia ya uchaji, na upevu katika maisha. Paulo
alimwagiza Timotheo hasa kwamba mtu aliyeongoka karibu
asiteuliwe kama mzee wa kanisa, kwa sababu waongofu
wapya bado hawajawa na historia kama hii.
Kusimama Wima Wakati Wa Majaribu
Mungu wetu ni mkamilifu katika utakatifu. Yeye
hatatenda uovu kamwe, wala Mungu hatatujaribu sisi -
ambao Yeye anatupenda - tufanye uovu au dhambi (Ayubu
34:10-12; Yakobo 1:13-18).
Ni Shetani aliye mwanzilishi wa uovu wote, anayetafuta
kuiba, kuua na kuangamiza (Yohana 10:10). Ibilisi hawezi
kuharibu au kuzuia karama zetu au upako wetu moja kwa
moja. Hivi vipo chini ya mamlaka ya Mungu peke Yake.
Lakini Shetani atajaribu kutushawishi katika eneo la tabia
yetu. Atajaribu kutushambulia, kutudanganya, kutuchafua au
kutuondolea haki kama vyombo vya Mungu. Akiweza
kutushawishi tuchague mwenendo au msimamo wa dhambi,
kazi ya Mungu kupitia maisha yetu inaweza kuzuiwa au
kuharibiwa kutokana na kushindwa kwetu binafsi.
Tufanyeje basi kwa kuwa “mshtaki [wetu] ibilisi, kama
simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu
ammeze” (1Petro 5:8)?
Tupambane na majaribu kama Yesu alivyofanya pale
nyikani (Luka 4:3-12). Njia za kupinga kazi za ibilisi
zimeorodheshwa pia katika Yakobo 4:7-10. Usome sehemu
hii ya Maandiko, na tuiangalie hapa sasa.
“Mtiini Mungu” - tumtii na kumtegemea Mungu. Kutii
Neno Lake kutatuweka mbali na mahali na nafasi za
vishawishi. Pia, umkimbilie Yeye kwanza katika sala
unapopata majaribu au vishawishi; usijaribu kupinga
majaribu pasipo msaada wa Mungu.
“Mpingeni Shetani” - tumia Neno la Mungu na lugha
yako ya kiroho ya kusali (1Wakorintho sura ya 12 na 14);
uungane na mtu unayemwamini katika sala.
“Mkaribieni Mungu” - umletee Mungu hali yako kamili
katika sala ukimruhusu aangaze ndani ya moyo wako kwa
nuru ya Roho Yake na Neno Lake. Uwe mvumilivu na
kumsubiri atende yale ambayo Yeye peke Yake anaweza
kuyatenda. Upinge jaribu la kushughulika mwenyewe na
kujaribu kubadili au kutengeneza hali wewe mwenyewe.
“Itakaseni mikono yenu”, “na kuisafisha mioyo yenu”,
“Jidhilini mbele za Bwana” - wakati Roho Mtakatifu
anapofunua au kukuthibitishia maeneo ya utumwa, dhambi
na udhaifu katika maisha yako, uyalete kwa Mungu katika
sala kwa moyo wa unyenyekevu na toba; ungama makosa
yako na haja yako ya kazi ya utakaso ya Mungu, msamaha,
uponyaji na ukombozi Wake.
Neema Ya Kuwa Washindi
Zaidi yake, kuna orodha nyingine ya maagizo yenye
nguvu ya kutusaidia kupambana katika vita vya kiroho. Soma
Waefeso 6:10-18. Mistari hii inatuagiza tuvae silaha, kushika
upanga wa Roho (Neno la Mungu) na “kuloweshwa” sala.
Ndipo baada ya kufanya yote uwezayo, simama imara katika
imani, tumaini na utiifu kwa Mungu. Unaweza kumpinga
ibilisi na kazi zake, naye lazima akimbie! Mungu atakupa
ushindi leo!
Adui hakati tamaa. Atajaribu tena, kwa sababu lengo
lake ni kukuangamiza. Hali hii ilikuwa ya kweli hata kwa
Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO • 51
Yesu. Ingawa alikabili jaribu kuu nyikani - na kupata ushindi
mkuu - haikuwa mara Yake ya mwisho ya kukutana na adui
(tazama Luka 4:13; taz. pia Mathayo 16:23; Luka 22:1-6).
Lakini katika kila jaribu, Yesu hakukubali dhambi.
Kumbuka kwamba Mungu yu upande wako kabisa
(Warumi 8:31). Ameahidi kwamba hataruhusu ujaribiwe
kuzidi uwezo wako; daima Yeye atakupatia mlango wa
kutoka (1Wakorintho 10:13; 2Petro 2:9).
Tushangilie, basi, kwamba sisi tunaye Mfalme anayejua
na kufahamu mapambano yetu kwa ndani. Mwokozi huyu
mwenye haki na upendo ametukaribisha kwa hiari kupokea
uwezo, nguvu na neema Yake ili tuwe washindi kama Yeye
(Waebrania 4:14-16).
Lazima tufuate utaratibu wa maisha yote wa
kutegemea uweza wa Roho Mtakatifu.
Yesu aliporudi kutoka siku zile arobaini nyikani, Biblia
inasema hivi: “Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akaenda
Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za
kandokando” (Luka 4:14).
Yesu aliendea mji wake wa nyumbani, Nazareti. Ndipo
alipokulia na alipokwenda katika sinagogi siku ya Sabato
(Luka 4:16-30). Ndipo aliposimama asome, akichagua
kutoka katika Maandiko mistari hii kutoka Isaya 61:1-2:
“Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta
kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia
wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kuona tena,
kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwana
uliokubaliwa” (Luka 4:18-19).
Yesu alitangaza kwamba kazi Yake ya Masihi
ingefanywa na “Roho wa Bwana”. Yesu alitiwa mafuta na
kupewa uwezo na Roho Mtakatifu. Ilikuwa kutokana na
upako huu tu kwamba aliweza kufanya yote aliyotangaza
kinabii kuhusu huduma Yake.
Kumtegemea Bwana Kikamilifu
Katika mistari hii, Yesu ameweka utaratibu kamili jinsi
tunavyoweza kufanya mapenzi ya Baba. Kama tunavyojua,
Yesu alikuja ili afanye mapenzi ya Baba, si ya Kwake. Vile
vile, wewe na mimi tumeitwa tufanye mapenzi ya Baba na si
yetu. Hatujaitwa tufuate “mpango wetu” hata kama tunauona
ni mzuri kabisa. Bali tumeitwa, kupewa mamlaka na
kuwezeshwa tufanye mapenzi ya Mtu Mmoja - Mungu. Na ili
tufanye mapenzi ya Mungu, tunahitaji uwezo wa Mungu!
Kama tulivyojifunza, hamasa yetu kuu tunapopevuka
katika mambo ya Mungu ni jinsi ya kutegemea Mungu na
uwezo wa Roho Mtakatifu zaidi na zaidi. Ni rahisi mno
kuanza kutegemea karama na nguvu zetu zinazoongezeka.
Tumepata ufanisi kiasi, kwa hiyo tunapunguza kusali kwa
bidii na kujifunza Biblia. Njaa yetu ya kiroho, au hamu yetu
ya kumwona Mungu akifanya kazi katika maisha ya watu au
katika jamii yetu, vinapungua. Ndipo tunapoanza kutegemea
zaidi ujuzi na ustadi wetu wa muda mrefu, kuliko uwezo wa
upako wa Roho wa Mungu.
Katika hali kama hizi, matatizo na majaribu yanaweza
kuturudisha kwenye kupiga magoti na kusali, penye nafasi
yetu ya kumtegemea Bwana kwa ajili ya yote tunayohitaji
katika maisha na huduma.
Tunaweza kuona, katika maisha ya Yesu, vipindi vya
miujiza mikuu na huduma kubwa, na vipindi vya majaribu
makuu na upinzani mkubwa. Lakini kwa pande zote, Mwana
wa Mungu asiye na dhambi alitegemea kabisa uwezo wa
Roho wa Mungu.
Yesu alichagua kupokea vizuizi au mipaka ya mwili wa
kibinadamu na kujifanya kuwa hana utukufu (Wafilipi 2:7).
Kwa sababu ya hali hii, Yesu alijiachia ategemee kabisa
mapenzi ya Baba na uwezo wa Roho Mtakatifu. Ndivyo
vilivyompitisha katika maisha ya hapa duniani, huduma
Yake, na hata kupitia kifo Chake na kufufuka Kwake kwa
utukufu kulikofuata!
Kama Yesu, Mwana wa Mungu, alihitaji nguvu ya upako
ya Roho Mtakatifu ili atimize mapenzi ya Baba - je, si zaidi
sana basi kwetu wewe na mimi?
Majaribu: Silaha Za Mungu Za Kututengeneza
Mungu atatumia majaribu katika maisha yetu. Si
kwamba anatuadhibu katika vipindi hivi. Ukweli ni kinyume.
Kwa sababu Mungu anatupenda, anaturudi (Waebrania
12:3-11). Kwa sababu sisi kweli ni wana wake wa kiume na
kike (Warumi 8:14-16), Yeye anafanya yote yaliyo lazima
kututengeneza na kutuwezesha kukua katika mfano Wake
(2Wakorintho 3:18). Kwa sababu sisi ni warithi pamoja na
Kristo (Warumi 8:17), na hatima yetu ni kutawala pamoja na
Yeye (2Timotheo 2:12; Ufunuo 5:10), tutapitia majaribu ya
kutuandaa kwa ajili ya mambo yajayo (Warumi 8:18;
2Wakorintho 4:17).
Tusiogope wala kutoroka majaribu na matatizo
yatakayotujia sisi sote. Lakini badala yake, kama Yakobo
anavyoandika, “hesabuni kuwa ni furaha tupu, mkiangukia
katika majaribu mbalimbali” (Yakobo 1:2). Maana ndiyo
silaha hasa ambazo Mungu atazitumia katika kutuumba,
kutugeuza na kutuandaa kwa matumizi Yake na utukufu
Wake!
52 • MATENDO
Majaribu si tishio.
KIBURI
HASIRA
HOFU
Nakala 16 / Nambari 1
3. Kufuata Nafsi Ya Mungu
Kama tulivyoona, kuna kanuni nyingi na masomo mengi
ya kujifunza katika maisha na huduma ya Yesu. Kwa hakika,
hakuna mtu aliyefundisha kama Yeye (Luka 4:32). Yesu
alifanya ishara, maajabu na miujiza katika muda wote wa
huduma Yake - kiasi ambacho mtume Yohana alisema
kwamba ni vingi mno kabisa visiweze kuandikwa (Yohana
21:25)!
Kwa kuwa Yesu Kristo ni Yeye yule jana, leo na hata
milele (Waebrania 13:8), mambo aliyofanya wakati wa
huduma Yake hapa duniani yanaendelea kufanyika hata
leo. Matendo makuu na miujiza bado hufanywa na Roho
Mtakatifu, kwa njia ya viungo vya Mwili wa Kristo. Maana
yake ni kwamba huduma ambayo Yesu alianzisha alipokuwa
duniani, amewapa wafuasi Wake sasa waiendeleze (Matendo
1:1-8).
Bila shaka sisi hatukupewa utume Wake wa kufa
msalabani kwa ajili ya dhambi za binadamu. Ule ulikuwa
utume wa Kristo peke Yake. Wokovu wa milele unatokana na
dhabihu Yake tu (Matendo 4:12). Hakuna tunachoweza
kuongeza katika kazi ile kuu iliyokwisha timiziwa kabisa.
Sisi tunatakiwa tuipokee tu!
Mchungaji kwa Mchungaji: Tafadhali ufahamu
kwamba huduma ya Yesu haikukatishwa kutokana na
kusulibiwa Kwake. Lengo kuu la utume wa Yesu hapa
duniani lilikuwa kifo Chake msalabani kwa ajili ya
wokovu wa wanadamu wote. Wokovu huu ulitimizwa
kwa utukufu katika kifo Chake na kufufuka Kwake
kulikofuata (Yohana 19:30; Waefeso 1:17-23; Wafilipi
2:5-11; Waebrania 9:11-15).
Kwa hiyo tunaweza kusema kwa uhakika kwamba
hakuna mtu aliyemwua Yesu kinyume cha mapenzi
Yake. Bali, kifo cha Kristo kwa ajili ya dhambi zetu
kilikuwa sehemu ya makusudi ya Mungu
yaliyoandaliwa kwa ajili Yake (Yohana 1:29; 12:27;
19:5-11; Matendo 2:22-24,33). Yesu alikubali na
kutimiza kabisa utume huu.
Kazi Kubwa Zaidi
Sisi tuliopokea wokovu kwa Yesu Kristo tumepewa
huduma ya Yesu tuiendeleze, hata “mpaka mwisho wa nchi”
(Matendo 1:8). Tumepewa Roho Mtakatifu atuwezeshe
tutimize amri hii yenye baraka.
Yesu alisema pia, “Amin, amin, nawaambieni, Yeye
aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye
atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa
mimi naenda kwa Baba” (Yohana 14:12). Katika mstari huu,
tunaona wazi kabisa kwamba Yesu ametuita tuendeleze kazi
Zake.
Lakini ni lazima tufahamu kwamba maana yake si
kwamba kazi zetu kwa aina fulani zitakuwa kuu kuliko kazi ya
Kristo. Wala hatuwezi kamwe kupata kuwa sawasawa na Kristo
kwa njia yoyote (Mathayo 10:24-25; Yohana 13:16). Maana
Yesu peke Yake alikuwa na ndiye Mungu; na Yesu ni Mmoja
pamoja na Mungu Baba na Roho Mtakatifu (Yohana 10:30).
Yesu aliposema “kazi kubwa zaidi” alimaanisha kwamba
sisi tutafanya kazi yenye upana zaidi au matendo mengi zaidi.
Muda wa huduma ya Yesu ulikuwa kama miaka mitatu na
nusu. Huduma yetu inaweza kuendelea katika maisha yetu
yote.
Huduma ya Yesu duniani ilifungiwa katika eneo dogo na
kati ya watu wachache. Ni ndogo kulingana na mamilioni ya
wafuasi wa Kristo tulioitwa tuende “mpaka mwisho wa nchi”
(Matendo 1:8). Tumeagizwa “kuihubiri injili kwa kila
kiumbe” (Marko 16:15) na “kuwafanya mataifa yote kuwa
wanafunzi” (Mathayo 28:19). Ndizo “kazi kubwa zaidi”
ambazo tutazifanya!
Habari Njema Kwa Wote
Imekuwa mpango wa moyo wa Mungu Baba kufikisha
wokovu kwa watu wote. Kwa njia ya kufa na kufufuka kwa
Yesu, mpango huu sasa unawezekana. Lakini hii Habari
Njema ya ajabu lazima itangazwe kwa mataifa yote
(Mathayo 24:14; Yohana 4:35). Watajuaje pasipo mtu wa
kuwaambia (Warumi 10:14-15)?
Ni wajibu wa kila mwamini kutangaza Habari Njema ya
wokovu katika Kristo kwa watu wote. Lakini ili tufanye
hivyo, tunahitaji nguvu na uwezo wa Roho Mtakatifu wa
Mungu!
Kwa uweza wa Roho Mtakatifu, “Atauhakikisha
ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu”
(Yohana 16:8, usome ms. 7-11). Ni kwa njia ya Roho
Mtakatifu pia kwamba ishara na miujiza vilifanywa na
mitume wa kwanza (Matendo 2:43; 5:12; n.k.) Ishara hizi
hizi na miujiza hiyo hiyo vimeendelea kupitia kipindi kizima
cha Kanisa, navyo hupatikana kwetu leo (1Wakorintho
12:9-10).
Wachungaji na viongozi wa kanisa walio wengi leo wana
njaa ya kuona zaidi ya nguvu ya Mungu kwa wazi katika
huduma zao. Tunatamani kuwaona wagonjwa wakiponywa,
mapepo yakiondolewa, wafu wakifufuliwa - na zaidi - yote
kwa utukufu wa Yesu!
Matendo haya kwa hakika yanapatikana kwetu sisi kwa
uweza wa Roho Mtakatifu. Yesu alifanya matendo hayo
katika huduma Yake kwa Roho Mtakatifu (Matendo 2:22).
Naye ameahidi kwamba sisi pia tutazifanya (Yohana 14:12)
kwa Roho Mtakatifu yule yule (1Wakorintho 12:11).
Tunaweza na tunapaswa kutazamia - na kuaminia kwa
imani - kwamba Mungu atathibitisha mahubiri ya Injili kwa
nguvu ya kimwujiza katika huduma zetu (Marko 16:19-20).
Ndivyo atakavyofanya kwa uwezo wa Roho Mtakatifu,
kufuatana na mapenzi Yake. Haleluya!
Ishara Zinamwashiria Mungu
Hapa inatubidi tuweke utaratibu wenye uwiano na
uangalifu. Lengo au shabaha ya huduma yetu isiwe kamwe
miujiza, ishara na maajabu. Na mambo hayo yasije yawe
tamaa ya moyo wetu.
Ni kweli kwamba Mungu anafanya mambo mengi na
miujiza ya ajabu hapa duniani leo. Lakini je, kusudi la ishara
hizi, maajabu na miujiza vyote hivi vikuu?
“Ishara” au “ajabu” ni tukio lisilo la kawaida (tafadhali
soma zaidi kuhusu ishara na maajabu katika sehemu maalum
hapa chini). Mungu anatoa ishara kwa ajili ya kuvuta akili
zetu. Kwa mfano, kijiti kinachowaka moto nyikani huenda si
jambo la ajabu sana. Lakini kijiti kinapoendelea kuwaka
moto kwa muda mrefu pasipo kuteketea, bila shaka kinavuta
macho na akili yetu (taz. Kutoka 3:1-3)!
Lakini ishara ni zaidi ya tukio lisilo la kawaida. Kusudi
hasa la ishara na maajabu ni kwamba zinaashiria jambo
Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO • 53
fulani. Lile lililoashiriwa na ishara au ajabu ndilo
linalothibitisha uhalisi wake.
Ishara na maajabu yote yanayofanywa na Roho
Mtakatifu daima na kila mara zitawaelekeza watu kwa
Mungu Baba au Mungu Mwana - Yesu. Ishara yenyewe si
“hatima” au lengo. Badala yake, ishara inatakiwa imwongoze
mtu afikie hatima.
Mungu alivuta akili ya Musa kwa kutumia kijiti
kisichoteketea. Lakini alipokuwa amekwisha kuvuta akili
yake, Mungu alianza kujidhihirisha (Kutoka 3:4-6) pamoja
na kusudi Lake kwa ajili ya watu Wake (Kutoka 3:7 - 4:17).
Je, lipi lilikuwa muhimu zaidi? Kwamba Mungu alifanya
kijiti kisiteketee, au yale aliyofunua juu Yake Mwenyewe
pamoja na kusudi Lake?
Je, Injili Inahubiriwa Kwa Udhahiri?
Msingi wa kupima ishara na maajabu, maneno ya
kinabii, maono, na matukio mengine ya kiroho kama haya, si
kwamba ni tofauti, isiyo kawaida au nje ya utaratibu wa
kimaumbile. Hata ibilisi anaweza kutumia hila afanye ishara
na maajabu yasiyo ya kimaumbile kiasi fulani (2Wakorintho
11:14). Kazi za Shetani za aina hii zitaongezeka tunapoingia
zaidi katika nyakati za mwisho (Mathayo 24:23-25;
2Wathesalonike 2:8-10; Ufunuo 13:13-14; 16:14; 19:20).
Ufalme wa mapepo utajaribu kufanya miujiza ya
uwongo ili kuwadanganya watu, ikiwavuta mbali na ukweli
wa Injili na Yesu akiwa njia pekee ya wokovu. Lakini hata
mfano huu wa kikano unaonesha kwamba ishara na maajabu
huweza kuvuta akili za watu.
Kwa hiyo, msingi wa kupima ishara na maajabu kwa
Roho Mtakatifu ni hii: Je, tukio hili linamtukuza Yesu? Je,
linawaelekeza watu Kwake? Je, linawaongoza wamwitikie
Yeye - kumpenda, kumwabudu, kumtii na kumfuata Yesu
Kristo? Je, Injili inahubiriwa kwa uwazi, ili wasiookolewa
wapate nafasi ya kutubu? Je, jina la Yesu linainuliwa kuliko
majina mengine yote? Ndiyo maswali tunayopaswa tuulize
tunapotafuta kupambanua na kufahamu hoja hii ya ishara na
maajabu.
54 • MATENDO
ISHARA, MAAJABU NA
MIUJIZA KUTOKA KWA MUNGU
NI VIZURI, NA TUTAZAMIE
KUVIONA LEO. Havikukoma wakati
wa kifo cha mitume wa kwanza (kama
100 b.K. hivi). Wala havikukoma
wakati Maandiko ya Agano Jipya
yalipothibitishwa (kutambuliwa rasmi
na uongozi wa Kanisa kwamba ni
maandiko ya mitume yaliyo na upuzio
wa Mungu kama 300 b.K.).
Roho Mtakatifu bado anatenda leo
kazi ambazo Yesu alianza kufanya
karibu miaka 2,000 iliyopita! “Yesu
Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata
milele” (Waebrania 13:8). Naye ndiye
aliyetuita sisi tuendeleze kazi Zake
(Yohana 14:12), kwa uweza wa Roho
Mtakatifu.
Lakini, pamoja na kwamba ishara,
maajabu na miujiza ni mambo ya
kusisimua sana, kuna mipaka kwa
utendaji wake. Tumekwisha ona
kwamba ishara zipo kwa ajili ya kuvuta
akili za watu. Nazo daima ziwaelekeze
watu kwa Yesu.
Hoja hii ni muhimu, kwa sababu
ishara na maajabu havisababishi “imani
iokoayo” ikue katika moyo wa mtu.
Imani inayotegemea ishara au mwujiza
tu itakuwa hafifu na haitadumu. (Kwa
kuona mfano wake, soma Yohana sura
ya 6, hasa mistari 14-15,26-35,60-64).
Hatimaye, ili aingie katika
wokovu, inambidi mtu achague
kuitikia ukweli wa Yesu Kristo
kwamba Yeye ni nani, na jinsi
alivyotenda msalabani kwa ajili yake.
Lazima amwamini Yeye, azitubu
dhambi zake binafsi, na ampokee Yesu
kama Bwana na Mwokozi wake.
Nafasi Ya Kwanza Ni Ya Yesu
Yesu, mapema katika huduma
Yake, alifahamu asili ya uovu na
uhafifu katika moyo wa binadamu
(Yeremia 17:9). Yesu hakujiachia au
"kujitoa" kwa watu waliomfuata
(Yohana 2:23-25). Alitambua kwamba
walikuwa na imani hafifu ya juujuu tu
iliyotokea “walipoziona ishara zake
alizozifanya” (ms. 23).
Miujiza, ishara na maajabu
zinazofanywa kwa uwezo wa Roho
Mtakatifu ni sahihi na zinakubalika.
Mungu anazitumia kuvuta akili za
watu. Lakini imani ya kudumu lazima
iwekwe juu ya msingi imara zaidi na
wa milele: Yesu Kristo!
Imani ambayo mtu ameweka juu
ya Yesu Kristo na dhabihu Yake kwa
ajili ya dhambi zake ni imani iliyo
imara, ya kudumu na ya kuokoa. Ndiyo
aina ya imani inayobadilisha maisha
ambayo itaendelea kuwa na nguvu na
kukua, ijapokuwa mapambano na
majaribu. Ndiyo aina ya imani
inayodumu katika maisha yote na
mpaka milele!
Roho Mtakatifu anatumia ishara,
maajabu na miujiza ili avute akili za
watu. Lakini anafanya hivyo ili
awafikishe kwenye nafasi ya kuchagua
kumwamini Kristo kwa wokovu.
Tuangalie mifano miwili ya hali hii.
Katika mfano wa kwanza (Yohana
9:1-41) Yesu alimponya mtu
aliyezaliwa kipofu. Mtu huyu
aliponywa, lakini ndipo Yesu
alipompatia nafasi ya kumwamini Yeye
(9:35-38).
Katika mfano wa pili (Matendo
13:4-12) Paulo alimkabili mchawi
mwovu. Chini ya upako wa Roho
Mtakatifu, Paulo alitamka hukumu ya
kinabii juu ya mchawi huyu (ms. 9-11).
Liwali (mtumishi wa juu katika
serikali) aliona tendo lile la uweza na
kuamini kwamba yale ambayo Paulo
alimfundisha kuhusu Kristo ni kweli
(ms. 12).
Utaona kwamba katika mifano
yote miwili, imani katika Kristo
haikutegemea ishara yenyewe. Msingi
wa imani ulikuwa kama walimwamini
Yesu Kristo ama sivyo (Yohana 9:35-38;
Matendo 13:12). Ishara zilisaidia tu
katika kuthibitisha ukweli na uwezo wa
Injili ya Yesu Kristo.
Kiongozi wa kanisa, ishara na
maajabu ziwe na nafasi katika huduma
yako. Lakini nafasi ya kwanza katika
mambo yote ni ya Yesu; mengine yote
yawaelekeze watu Kwake kwa urahisi
na uwazi mkubwa.
Yesu ndiye Mwokozi wao! Yesu ni
Bwana wao! Sifa na utukufu yote yawe
Kwake!
KUTAZAMA KWA KIFUPI ISHARA NA MAAJABU
Nakala 16 / Nambari 1
Hakuna Miungu Mingine
Hapa tumefikia kanuni ya msingi mojawapo kwa ajili ya
kutembea, kutoa huduma, na kukua katika upako wa Roho
Mtakatifu:
Je, tunamtafuta Mungu kwa ajili ya yale
atakayotutendea? Au je, tunamtafuta kwa ajili Yake
Mwenyewe, na kwa hamu yetu ya kuwa na uhusiano na
Yeye - tukitaka tu kumjua na kumtambulisha kwa
wengine?
Tumethibitisha kwamba uweza wa Mungu hautengani na
nafsi ya Mungu. Upako wa Mungu ndiye Roho Mtakatifu
akifanya kazi ndani ya, na kupitia kwa, chombo cha
kibinadamu kilichojitoa Kwake.
Lakini inatokeaje wakati mtu fulani anapopoteza lengo
lake kwa Mungu, au kugeuza hamu yake ya mambo ya
kiroho mbali na Yeye? Tunaweza kuona matokeo yake kati ya
viongozi wa Wayahudi wakati wa Yesu.
Yesu aliwakabili viongozi hao waliotaka kumwua
(Yohana 5:16-18). Walikuwa watu wenye elimu ya hali ya
juu, lakini walikuwa wamepoteza njia yao ijapokuwa ujuzi
wao.
Yesu aliwakemea kwa ajili ya kupoteza lengo lenyewe la
masomo yao yote: “Mwayachunguza maandiko, kwa sababu
mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na
hayo ndiyo yanayonishuhudia. Wala hamtaki kuja kwangu
mpate kuwa na uzima” (Yohana 5:39-40).
Viongozi hao wa Wayahudi walijua Maandiko. Lakini
walikuwa wamepoteza Neno Lililo Hai - Yesu, aliyekuwa
amesimama pale pale mbele yao (Yohana 1:1-5,14)!
Baadaye, Yesu aliwakemea tena viongozi wa dini kwa
ajili ya kutafuta ishara kila wakati, ingawa walikuwa
wamekwisha ona ishara nyingi (Mathayo 12:38-39). Na Yesu
aliwakemea mara ya tatu alipolenga upofu wa Mafarisayo,
waandishi na wanasheria waliokuwa wakidai hata ishara
nyingine (Mathayo 16:1-4).
Ndipo karibu na mwisho wa huduma ya Yesu, upofu wa
makusudi wa Mafarisayo uliokuwapo haujabadilika, Yesu
alitamka hukumu juu yao (Mathayo 23:37-39).
Hoja ya Yesu hapa ilikuwa nini? Kuna mambo mengi
tunayoweza kujifunza kutokana na makabiliano kati ya Yesu
na viongozi wa dini wa wakati Wake. Lakini hasa, Yesu
alikuwa akifunua kwamba Wayahudi walikuwa wakitafuta
yale ambayo walimtaka Mungu awatendee - lakini
hawakuwa wakimtafuta Mungu Mwenyewe!
Ndiyo sababu yao moja ya kumkataa Yesu kama Masihi.
Hakuwapa lile walilolitaka, yaani kwamba Yeye aanzishe
Ufalme wa duniani wakati ule ule ambamo Mafarisayo,
waandishi na wanasheria wangekuwemo kati ya viongozi
wenye heshima. Walitamani nguvu, utawala na utajiri.
Walikuwa wameridhia nafasi zao, vyeo vya heshima na
daraja ya juu katika jamii (Mathayo 6:2,5-6,16-18; 23:2-7;
Yohana 12:42-43; n.k.). Walikuwa wamepoteza lengo kabisa,
wakijifikiria wenyewe tu. Yesu, bila shaka, alihukumu
msimamo huu wa kujiendeleza na kiburi cha kidini.
Viongozi wa dini walikuwa wamesahau ukweli wa
kimsingi kuhusu Mungu ambaye walidai walimtumikia.
“Usiwe na miungu mingine ila mimi... kwa kuwa mimi,
Bwana, Mungu wako , ni Mungu mwenye wivu” (Kutoka
20:3,5).
Mungu ana wivu wa haki kwa ajili ya upendo na uchaji
wetu. Kwanza, kwa sababu Yeye peke Yake katika maumbile
yote anastahili upendo wetu na ibada yetu. Pili, kwa sababu
Mungu ni mwumbaji wetu na kuwepo kwetu kama
wanadamu hutokana na Yeye (Mwanzo 1:26-28; 2:18-25;
Yohana 1:3). Tatu, kwa sababu alimtoa Mwana Wake
atukomboe - sisi ambao Yeye alitupenda kwa ukamilifu wote
- kutoka katika dhambi na mauti (Wakolosai 2:11-15;
1Yohana 4:9-10).
Ukweli huu umethibitishwa tena katika Agano Jipya:
“Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona
wivu” (Yakobo 4:5). Neno hili limetamkwa kwa Wakristo wa
awali waliojaribu kumtumia Mungu atimize tamaa zao
binafsi (Yakobo 4:1-4).
Hao wameitwa “wazinzi... adui wa Mungu” (ms. 4) kwa
sababu walikuwa wakiasi uhusiano wao takatifu wa kujitoa
kwa Mwokozi wao ili wafuate starehe za mwili zinazopita
haraka za dunia.
Lakini hata hapo Mungu hakuwatupa. Bali aliwatamani
kwa wivu, kwa sababu Yeye peke Yake aliwapenda katika
ukweli. Mungu atampokea tena mzinzi anayetubu kwa kweli
(Yakobo 4:6-10).
Ni wazi, basi, kwamba ni lazima tusivunje upendo wetu
na huduma yetu kwa Mungu kwa kupendezwa na mambo
yoyote mengine.
Ujiepushe Na Mivuto
Katika nafasi yetu kama wachungaji na viongozi katika
Mwili wa Kristo, awepo Mmoja tu anayepokea uaminifu,
utiifu, hamu na tumaini kutoka kwetu - Yesu!
• Si ishara, maajabu wala miujiza
• Si huduma kubwa, au watu walio nayo
• Si karama, wito, ujuzi, nafasi au cheo
• Si hata baraka Zake
Imesemwa kwamba mara nyingi vizuizi vikuu kwa
waamini ni baraka ambazo Mungu anawapatia watu wake.
Kwa nini iwe hivyo? Kwa sababu usikivu wetu na hamu zetu
zinaweza kusogezwa mbali na Mungu kwa urahisi, na
kulenga baraka Zake badala ya Yeye Mwenyewe. Mioyo yetu
ina ubinafsi wa kudanganya (Yeremia 17:9). Hata kama
tumeokolewa, bado tuna mwelekeo kuendea dhambi
(1Yohana 1:8).
Mchungaji kwa Mchungaji: Rafiki na kiongozi wa
kanisa, tafadhali uelewe kwamba si kosa kutaka uwepo
wa upako wa Roho Mtakatifu umiminwe juu yako na juu
ya huduma yako. Ni hamu kuu ya Mungu kwamba uwe
nao!
Lakini tusipokuwa na hekima na uangalifu, mioyo
yetu inaweza kupotoshwa. Katika hamu yetu ya
ufanisi katika huduma, tunaweza kuanza kulenga yale
ambayo Mungu anaweza kututendea, badala ya
upendo wetu Kwake kwa ajili Yake Mwenyewe.
Polepole na kwa ndani, tunaweza kuvutwa mbali,
na badala ya kutafuta uwepo wa Mungu kuliko sahihi,
kuonea njaa yale anayoweza kututendea. Ndivyo
ilivyokuwa kwa Mafarisayo. Walishikilia ujuzi wao
kuhusu Mungu badala ya kuwa na uhusiano halisi wa
kutii pamoja na Mungu. Walijua mengi kuhusu
Maandiko na mambo ya dini, lakini hawakumjua Yeye.
Hawakumtamani Mungu Mwenyewe, bali walitafuta
yale aliyoweza kuwatendea.
Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO • 55
Viongozi fulani leo, badala ya kuvutwa kwa Mungu,
wanavutwa kwa matukio yasiyo ya kimaumbile ambayo
mara nyingi hufuatana na kazi ya Roho Mtakatifu. Hao
ni kama mtu anayetaka kuoa (au kuolewa na) mtu tajiri
kwa sababu ya utajiri wake. Wanatamani utajiri wa
huyu mtu na mambo ambayo utawatendea kuliko
kumtamani yule mtu. Huu ni mwelekeo wa kutisha wa
ubinafsi mtupu!
Tunapotamani maajabu, upendo wetu kwa Mungu
Mwenyewe unaweza kunajisiwa - na hata kupoa kama
barafu (Mathayo 24:12). Hali hii inafanana na
msimamo wa yule Simoni mchawi, aliyetafuta uwezo
wa miujiza wa Roho Mtakatifu kwa faida yake binafsi
(Matendo 8:9-24).
Mungu wetu anatuonea wivu sisi. Anatamani
uaminifu, upendo na uchaji wetu kwa sababu Yeye
anatupenda kwa upendo wa milele (Warumi 5:5;
1Yohana 3:1). Yeye anawatafuta watu waliotoa moyo
wao wote Kwake Yeye Bwana. Ni kwa kuwapitia watoto
Wake wanaompenda kwamba anaweza kujidhihirisha
kwa njia za nguvu (Danieli 11:32).
Wito Wetu Wa Kwanza
Mara nyingi katika Maandiko, tunahimizwa tutafute
“uso” wa Bwana (2Nyakati 7:14; Hosea 5:15; Zaburi 27:8;
n.k.). Uso wa Mungu unavyotajwa katika Maandiko
humaanisha Nafsi ya Mungu, moyo Wake, uwepo Wake.
Lakini hakuna popote katika Maandiko ambapo
tunahimizwa tutafute “mkono” wa Mungu. “Mkono” wa
Mungu, au “Mkono wa Bwana”, humaanisha kazi Zake,
matendo Yake, baraka Zake. Tunaona matokeo ya kazi ya
Bwana (mkono Wake) katika mambo anayotenda. Na si kosa
kutaka kuona matokeo haya katika huduma yetu na kuipitia.
Lakini tafadhali ufahamu:
Tunapotafuta uso wa Mungu (moyo Wake, Yeye
Mwenyewe) ndipo tunapotambua mapenzi ya Mungu na yale
anayotaka kufanya.
Tunapofuata na kutii mapenzi Yake, ndipo tutaona
mkono mkuu wa Mungu kwa Roho atendaye kazi!
Kumtafuta Mungu, na uhusiano wetu na Yeye, lazima kuwe
kipaumbele chetu cha kwanza. Kutoka hapa ndipo mambo
yote ya thamani yatakapotokea.
Wana Wa Kweli, Watumishi Wa Kweli
Yesu alisema, “Mtu akinitumikia, na anifuate; nami
nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu
akinitumikia, Baba atamheshimu” (Yohana 12:26).
Angalia kwamba katika mstari huu, Yesu ana nafasi ya
kwanza. Yesu ndiye Bwana wa Kanisa (Waefeso 1:22); sisi
tunatakiwa tumfuate Yeye. Si kwamba Yeye anatufuata katika
huduma abariki yale tunayomwomba ayabariki.
Wito wetu wa kwanza kama viongozi wa kanisa ni
uhusiano wa kila siku wa kumtafuta Bwana - kumjua,
kumpenda, kumwabudu, kuongea na Yeye (Zaburi 63:1-8).
Ni kutoka mahali hapo ndipo tutakapotambua mapenzi Yake
ya kweli na mipango Yake kwa ajili ya maisha yetu, huduma
zetu na mambo mengine yote.
Mungu anataka kumimina baraka Yake, upako Wake,
ishara na maajabu Zake juu ya Kanisa Lake, na juu yako
wewe kama kiongozi Wake uliyeitwa.
Lakini je, anaweza kukuamini na haya? Je, una upevu,
uthabiti wa tabia na hekima, uwe mwaminifu kwa Yeye peke
Yake?
Mungu ameahidi kutoa zaidi ya “mkono Wake” kama
mioyo yetu ni mali Yake peke Yake. “Kwa maana macho ya
Bwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe
mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo
kuelekea kwake” (2Nyakati 16:9).
Yeye anataka mioyo yetu kwa wivu wa haki, kwa sababu
anatupenda kwa upendo Wake wa milele (Warumi 8:31-39).
Mchungaji kwa Mchungaji: Mungu anakupenda
kabisa na pasipo masharti yoyote! Haidhuru upungufu
wako, anakupenda kwa ndani, katika nafsi yako na kwa
milele. Wewe hukuumbwa kwa ajili ya utumishi na
huduma tu.
Kama Mungu angalitaka watumishi wengi zaidi,
angaliumba malaika wengi zaidi. Lakini alikuumba
wewe kwa sababu alitaka wana wa kiume na wa kike
wanaotembea katika uhusiano na Yeye. Malaika
hawawezi kuwa na uhusiano huu pamoja na Mwumbaji
wao - sisi wanadamu peke yetu tunaweza kuwa na
uhusiano huu (Waebrania 2:14-18; 1Petro 1:12).
Kristo hakutoa uhai Wake ili uwe katika huduma.
Alikufa awe dhabihu kwa ajili ya dhambi zako, ili uweze
kurejeshwa katika uhusiano na Mungu.
Sisi si watumishi tu wa Bwana. Sisi ni rafiki wa
Kristo (Yohana 15:15) na warithi pamoja na Yeye
(Warumi 8:17). Sisi ni wana wa Mungu aliye Hai
(Warumi 8:15-16). Tuna heshima na nafasi ya
kumtumikia Bwana na Mwili Wake kutokana na upendo
wetu na shukrani yetu Kwake.
Mbele Zake Kila Siku
Upako wa Roho Mtakatifu unahusiana moja kwa moja
na kipaumbele chetu cha kutafuta Uwepo wa Mungu kila
wakati. Mfalme Daudi ambaye Bwana alimtaja kuwa “mtu
anayeupendeza moyo wangu” (Matendo 13:22), anatupatia
maelekezo kwa ajili ya uhusiano wetu na Mungu:
“Uliposema, Nitafuteni uso wangu, Moyo wangu
umekuambia, Bwana, uso wako nitautafuta” (Zaburi 27:8).
Maana ya “kutafuta” ni kufanya bidii pasipo kuchoka wala
kuachia mpaka tuone lile tunalotafuta. Yesu aliongea kuhusu
kanuni hii pia (Mathayo 6:33; 13:44-46; Luka 11:9-13).
Kumtafuta Mungu kunahitaji muda na bidii. Huenda
itatupasa tuache starehe, heshima au shughuli fulani. Lakini
ni kwa kumtafuta Mungu kwamba tunapata kumfahamu.
Kutokana na uhusiano huu wa karibu na Yeye, tunaanza
kutambua mapenzi Yake kwa ajili ya maisha yetu na huduma
zetu. Tunapotembea katika kutii mapenzi Yake, anafungua
upako Wake juu yetu na kupitia kwetu.
Tuweke kipaumbele chetu cha kwanza kabisa katika
nafasi ya kila siku ya kukaa mbele za Bwana. Ndipo
tunapopokea yale yaliyo ya milele hasa, ambayo
hayatapungua wala kuchakaa (Luka 10:38-42). Uamue leo,
na kila siku: “Uso wako, Bwana, nitautafuta.”
Marejeo
Tukimaliza sehemu hii, “Kukua Katika Upako”,
tafadhali kumbuka kwamba kila mmoja wetu anaweza na
anapaswa akue katika uwezo wa upako wa Roho Mtakatifu.
Waliomo ni pamoja na wewe (kama mchungaji na kiongozi)
- na watu unaowaongoza!
56 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1
Wewe una wajibu kama mchungaji msaidizi (1Petro
5:2-4) wa watu wa Mungu. Hizi ni pamoja na kuhakikisha
kwamba kila mtu unayemwongoza anakua katika ufahamu
wake wa Neno la Mungu na kukua pia katika uwezo wake wa
kutoa huduma katika upako wa Roho Mtakatifu. Ndio
utaratibu wa ki-Maandiko kwa ajili ya kukua kwa afya katika
Mwili wa Kristo (taz. Waefeso 4:11-16, hasa ms. 12).
Njia ya kukua katika upako huenda ni tofauti na
ulivyotazamia. Turudie kanuni za msingi zilizo lazima kwa
ajili ya kukua katika upako:
• Utakaso
• Udhaifu wa ki-Mungu
• Unyenyekevu
• Utiifu kwa mamlaka
• Miitikio sahihi kwa majaribu
• Moyo kwa ajili ya Mungu peke Yake
• Kutembea na kukua katika uhusiano wetu na Mungu kila
siku
Yesu alikuwa mfano wetu wa tabia au kanuni hizi zote.
Yeye alikuwa Mtu mwenye upako zaidi ya wote wengine
waliotembea duniani. Anatukaribisha tufuate nyayo zake
kwenye njia ya upako wa Mungu. Tunapofanya hivyo,
tutapokea fungu litoshalo kabisa la vyote tunavyohitaji ili
tutimize wito mkuu wa Bwana kwetu!
C. KUPOKEA UPAKO WAKE
Nilikuwa mmoja wa timu ya viongozi wahudumu katika
Mkutano wa Wachungaji nchini Cuba. Karibu na mwisho wa
Mkutano, nafasi ilitolewa ya kusikia shuhuda za watu
waliohudhuria. Bwana mmoja mzee, mdhaifu na kipofu,
alisaidiwa alipokuja polepole mpaka kwenye jukwaa.
Ndugu huyu mzee alianza kutoa ushuhuda wake kwa
kueleza kwamba alikuwa amemtumikia Bwana kwa maisha
yake yote; ndugu zake pia walikuwa wakimtumikia Bwana.
Aliambia umati wa watu kuhusu makanisa mengi aliyokuwa
ameanzisha katika maisha yake, yakiwemo makanisa sita
mapya aliyoanzisha katika mwaka ule!
Aliongea kuhusu kuwa kipofu na jinsi ilivyokuwa
vigumu, hasa alipomhitaji mtu mwingine amsomee Biblia
kila siku.
Ndipo alitulia kwa dakika moja na kuinamisha kichwa
chake. Kundi la wachungaji zaidi ya 1,000 lilinyamaza.
Ghafla, yule mzee aliinua mikono yake katika ishara ya
ushindi na kupaza sauti yake: “Nimepoteza macho yangu,
lakini sijapoteza moto!” Kundi lile zima lilishangilia na
kumtukuza Mungu.
Je, nini ingemwezesha mzee wa miaka 76 aendelee kuwa
na “moto” - aendelee kuhubiri, kufundisha, kufanya uinjilisti
na kuanzisha makanisa? Upako wa Roho Mtakatifu tu,
pamoja na kujitoa kwa yule mzee atumiwe na Mungu kwa
ajili ya makusudi Yake na utukufu Wake!
Hazina Katika Chombo Cha Udongo
Ni tumaini langu kwamba Mungu atanitumia kwa ufanisi
kila siku mpaka atakaponichukua katika nyumba ya
mbinguni. Lakini hatuhitaji muda mrefu katika huduma
kutambua kwamba kule kutumika kunaweza kuchosha na
kutaabisha katika maeneo yote - kimwili, kiakili, kihisia na
kiroho.
Hali hii si ubaya mtupu, kwa sababu tunatakiwa tusiwe
na ubinafsi katika karama, nguvu na upako wa Mungu.
Tunatakiwa tutoe wakati wote yale ambayo Mungu
ametupatia. Tena tunatakiwa tusiwe wavivu au wazembe
katika huduma (Luka 9:62; Mhubiri 9:10; Wakolosai 3:23),
bali tunatakiwa tufanye bidii zote kwa ajili ya Kristo.
Lakini tukichoka kupita kiasi, “kuungua” au kutaabika
mno, matatizo makubwa yaweza kutokea. Mungu anajua
kwamba sisi tuna mipaka kwa nguvu yetu. Kwa hiyo anataka
kutupa nguvu, hekima, neema, vipawa na uwezo ili tuweze
kufanya mapenzi Yake - nasi tunahitaji sana hivi vyote.
Maana pasipo Yeye hatuwezi kufanya lolote (Yohana 15:5).
Paulo alifahamu haja hii alipoandika: “Lakini tuna
hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya
uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu” (2Wakorintho
4:7). Akiwa mtume mwenye mazoea mengi na ujuzi mwingi,
Paulo alijua kuwa nguvu na bidii ya kufanya mapenzi ya
Mungu havimo katika maumbile ya binadamu. Bali “hazina
hii” ndani ya “vyombo vya udongo” vya maisha yetu -
ambayo inatupa mahitaji yetu yote - ni upako wa Roho
Mtakatifu! (Soma 2Wakorintho 3:1-4:18.)
Yeye Anatujazia Kila Tunachohitaji
Madai ya huduma (au hata kuishi tu kama Wakristo
katika dunia ya leo) yanaweza kutuondolea uwezo na nguvu
ya Mungu. Yesu Mwenyewe alihitaji kuburudishwa kiroho,
akihudumiwa na Roho wa Mungu.
Tukisoma Injili kwa makini tutaona mara nyingi ambapo
Yesu aliondoka akaenda kusali katika mahali peke Yake (kwa
mfano, Luka 4:42; 5:16; 6:12). Baada ya vipindi hivi vya
sala, Yesu alifanya kazi kwa nguvu, kufikia maamuzi
muhimu katika huduma Yake, kuandaliwa kwa ajili ya
kustahimili majaribu, n.k.
Tunafunuliwa nini katika mfano wa Yesu? Ili tujibu
swali hili, tuangalie sehemu mbili za Maandiko.
1. Mjazwe!
“Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali
mjazwe Roho” (Waefeso 5:18).
Kuna hoja tatu muhimu zinazotokana na lugha ya asili ya
Kiyunani katika maneno haya “Mjazwe Roho”.
a. Neno lipo katika wakati wa sasa. Maana yake ni
tendo linalofanyika sasa na kuendelea kufanyika. Kwa hiyo
maana ya “Mjazwe Roho” ni kwamba tuendelee kujazwa
wakati wote na Roho Mtakatifu. Hii ni habari njema kweli!
Kuendelea kujazwa ni kwamba hatujazwi mara moja tu, bali
tena na tena!
Tunampokea Roho Mtakatifu tunapookolewa (Warumi
8:15-16; Waefeso 1:13-15). Huu ni upako wa kawaida
unaotolewa kwa waamini wote (1Yohana 2:20,27).
Tunapoitwa kifalme kwa ajili ya kazi za huduma, Mungu
anatuongezea upako wa mara kwa mara utakaotusaidia
kufanikiwa katika kazi ile.
Mungu anatupatia katika Nafsi Yake, uweza Wake na
karama Zake. Lakini tunavyovitoa hivi katika huduma,
tunaweza kufikia utupu au upungufu wa kiroho. Kwa hiyo
Mungu amewezesha kujazwa kwetu na Roho Wake
Mtakatifu tena na tena, kila mara tunapohitaji!
Kujazwa tena na tena kunaonekana wazi katika huduma
ya watu Kanisani kwa awali. Kitabu cha Matendo ni
kumbukumbu za matokeo yale:
Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO • 57
• Petro alijazwa ahubiri Injili na kutetea imani (Matendo
4:8).
• Wanafunzi walipokea ujasiri na nguvu kuhubiri Injili,
ingawa waliteswa (Matendo 4:31).
• Paulo alijazwa na Roho Mtakatifu mara ya kwanza
(Matendo 9:17) na kujazwa tena alipokuwa akabiliane na
nguvu za mapepo (Matendo 13:9).
• Baada ya kupambana na viongozi wa dini, wanafunzi
walijazwa tena na Roho Mtakatifu (Matendo 13:42-52).
• Stefano alijazwa, na kujazwa tena (Matendo 6:5; 7:55).
• Barnaba pia alijazwa mara ya pili (Matendo 13:52).
Kurudia kujazwa na Roho Mtakatifu kulileta nguvu
kubwa kwa mahubiri na mafundisho ya wanafunzi hao.
Kutangaza Injili kwao kwa ujasiri kulifuatana na ishara na
maajabu (Matendo 5:12).
Huenda watu wengine wanaamini kwamba miujiza hii
ilitokea kupitia kwa mitume wa awali tu. Lakini Kitabu cha
Matendo kinatufunulia kwamba ishara na maajabu za Roho
Mtakatifu zilitolewa kupitia mtu yeyote aliyechaguliwa na
Yeye.
Kwa mfano, Stefano, aliyepewa kazi ya kuhudumu
mezani (Matendo 6:8) na “ndugu” (Matendo 14:1-7) waliona
miujiza katika huduma zao. Paulo anaandika kwamba Roho
Mtakatifu anaweza kufanya kazi kupitia yeyote ambaye Yeye
amemteua ili ampe uwezo na kumwongoza (taz.
1Wakorintho 12:1-11).
Kuongezewa Kwa Kutoa
Kuna baraka ya nyongeza ya kujazwa kila wakati na
Roho Mtakatifu. Tunavyopata bure, tunatoa bure (Mathayo
10:8) na uwezo wetu wa kupokea upako Wake kwa wingi
zaidi unaongezwa! Kanuni hii ya Ufalme wa Mungu ni ya
kweli katika mambo ya fedha, muda, huduma na maeneo
mengine - zaidi tunayotoa, ndivyo tunavyopewa zaidi.
Tunakua kila mara tunapotoa huduma, tukiwatolea
wengine uhai na uwezo wa Roho Mtakatifu. Ndipo sisi
tunaweza kupokea zaidi, na kuwa na zaidi tena ya kutoa.
Mtindo huu uliobarikiwa wa kupokea na kutoa,
kupokea na kutoa tena, ni baraka kwa wote wanaohusika.
Mungu anabarikiwa na kutukuzwa kwa sababu mapenzi
Yake yanatimizwa. Viungo vya Mwili wa Kristo
hubarikiwa, na kukua katika kuwa wanafunzi wenye nguvu
(Waefeso 6:12-16). Wewe, kama mhudumu, unabarikiwa -
ukiwa mtumishi wa Bwana uliye na nguvu na uaminifu,
ukitimiza wito Wake na kukua katika uwezo wako wa kutoa
katika huduma na kupokea zaidi kutoka kwa Roho
Mtakatifu!
Haya yote yanategemea kujazwa na Roho Mtakatifu -
mfululizo. Utaratibu huu ni tofauti na ule wa kupokea karama
ya kifalme ya Roho Mtakatifu wakati wa kuokolewa, au
baadaye kubatizwa na Roho Mtakatifu (Matendo 8:14-17;
19:1-7). Tunapaswa tuishi katika hali ya kuendelea kujazwa
na Roho Mtakatifu, tena na tena!
b. Maneno yale “Mjazwe Roho” (Waefeso 5:18) ni ya
kiamri. Maana yake ni kwamba ni amri, si pendekezo!
Mungu anajua vizuri zaidi sana kuliko sisi jinsi tunavyohitaji
nguvu na uwezo Wake. Kwa hakika tunamhitaji Roho
Mtakatifu ili tuishi kama washindi katika maisha ya kila siku.
Lakini hata zaidi, tunahitaji uwepo unaofurika wa Roho
Mtakatifu ili tuzae matunda na kufanikiwa katika huduma.
Mungu anapotoa amri, daima ni:
• ya haki na maana;
• kwa ajili ya utukufu Wake;
• kwa ajili ya ufanisi wetu;
• yenye kuwezekana kwa utoaji Wake!
Mungu, kwa mapenzi Yake ya kifalme, ametuwezesha
kuwa na ukarimu wa Roho Mtakatifu usio na kipimo. Naye
ameamuru kwamba tuendelee kujazwa na utoaji Wake wa
Roho Mtakatifu. Haleluya!
Hii ni amri ambayo tunapaswa kukimbilia kuitii kila
siku, na katika kila dakika ya haja.
c. Maneno haya pia ni katika hali ya kutendewa.
Maana yake ni kwamba kule kujazwa kila wakati kwa upya
na Roho Mtakatifu si tendo tunalofanya sisi. Hatuwezi
kustahili wala kufanya kazi ili tujazwe. Ni karama ya Mungu
kwetu. Sisi tunaweza kufungua mioyo yetu tu na kupokea
yote anayotaka kutukirimia.
Hata hivyo, inatubidi tuwe katika nafasi ya kupokea!
Huu ni ufunguo wa msingi wa kuishi maisha ya kujazwa
Roho na kuwa na huduma ya kujazwa Roho.
Je, umewahi kujiuliza kwa nini watu fulani wanaonekana
kujazwa Roho Mtakatifu wakati wote, wakitumia karama,
hekima, uwezo, n.k. - wakati watu wengine hawafanyi
hivyo?
Njia ya kujiweka katika nafasi ya kujazwa mfululizo na
Roho Mtakatifu wa Mungu ni kujisalimisha. Maana yake ni
kwamba mambo yote katika maisha yako yametolewa na
kusalimishwa kwa Mungu - mapenzi yako, mipango yako,
madhaifu yako na hasa, nguvu zako. Ukifanya hivyo,
umejitoa kikamilifu kwa Roho Mtakatifu na mapenzi Yake
kwa ajili yako.
Kusalimisha maisha yetu kwa Roho Mtakatifu
kunatuweka katika nafasi ya kiroho ya kupokea kwa uhiari na
uhuru zaidi yale anayotaka kutupatia.
Lakini tafadhali ieleweke kwamba kusalimisha maisha
yetu kwa Roho Mtakatifu si sawa na kupagawa. Ni mapepo
na mashetani tu wanaojaribu kutawala mapenzi na nafsi ya
mtu katika kumpagaa (Luka 8:29-38a). Viongozi wa
madhehebu ya dini za uwongo huenda pia wanajaribu
kutawala au kutiisha watu wengine, kwa sababu wanatenda
katika udanganyifu wa kishetani.
Sisi hatukuitwa tuwe “wanasesere” wanaoongozwa kwa
kamba pasipo akili wala uwezo wowote wa kuchagua. Bali
sisi tumeitiwa uhusiano wa upendo, kuaminiana na
kushirikiana na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yetu. Yeye
amekuja afanye kazi ndani yetu, kutubadilisha na kututakasa;
na kufanya kazi kupitia kwetu kama vyombo vya huduma
vya Bwana Mungu. Tunapotoa maisha yetu kwa Mungu na
kazi Yake kwa njia hii, tutakaa katika nafasi ya kupokea
ujazo mpya wa kufululiza wa upako.
Mchungaji kwa Mchungaji: Sisi kama wana wa
Baba yetu wa mbinguni, tuongozwe na Roho Mtakatifu
(Warumi 8:14). Neno “kuongozwa” katika mstari huu ni
la wakati wa sasa wa kuendelea. Kwa hiyo tunapaswa
tuongozwe mfululizo.
Huku kuongozwa mfululizo na Roho Mtakatifu ni
pamoja na kufahamu kimasomo amri na kanuni za
Maandiko - na utiifu wetu kwazo - ingawa si hivi tu. Hii
ni njia ya msingi ya kuongozwa na Roho Mtakatifu, kwa
kuwa Mungu amekwisha kutufunulia katika Neno Lake
58 • MATENDO Nakala 16 / Nambari 1
jinsi tunavyopaswa kuishi siku kwa siku.
Lakini kuongozwa mfululizo na Roho Mtakatifu
humaanisha pia kusitawisha usikivu wetu kwa
maelekezo Yake, yanayoweza kutujia saa yoyote.
Roho Mtakatifu anaweza kukuelekeza kuhusu huduma
yako, maisha yako binafsi, hitaji fulani la mtu mwingine,
au mambo mengine mengi. Yeye yupo wakati wote
pamoja nawe ili akuongoze katika maisha haya. Roho
Mtakatifu atakusaidia pia ujue jinsi ya kushirikiana na
Yeye katika kuhudumia mahitaji ya watu wengine.
Ikiwa elekezo fulani limetoka kwa Roho Mtakatifu,
litakuongoza daima kutii amri na kanuni za maadili za
Neno la Mungu lililoandikwa. Ukijisikia kuongozwa na
Roho Mtakatifu kufanya badiliko kubwa au kufanya
tendo lisilo la kawaida kwako; ni bora kufuata maagizo
ya Maandiko na kuwatafuta washauri wa kiroho
waliopevuka (Mithali 11:14; 24:6). Wao wanaweza
kusaidia kuthibitisha kwamba lile unalosikia kweli
limetoka kwa Roho Mtakatifu - au kushauri kwamba
sivyo. Kufanya hivyo kutakusaidia kujilinda na kupotoka
au kudanganyika.
Muhtasari
Tumejifunza kanuni tatu muhimu kuhusu maneno ya
Biblia: “Mjazwe Roho” (Waefeso 5:18).
• Tunaweza kujazwa mfululizo, zaidi ya kujazwa mara ya
kwanza.
• Inatubidi tujazwe, kwa sababu Mungu ametuamuru
hivyo.
• Tunaweza kupokea ujazo na upako wa Roho Mtakatifu
kupitia Kwake tu - ni karama kutoka Kwake ambayo
tunajiweka katika nafasi ya kuipokea kwa kusalimisha
maisha yetu Kwake.
2. Umtafute Mungu!
Huenda unajiuliza sasa, “Nifanyeje ili nipokee ujazo huu
mpya (upako) wa Roho Mtakatifu wa Mungu? Niende mahali
fulani maalum? Niseme maneno maalum? Nimtafute mtu wa
kuniombea? Je, inanibidi nihudhurie mikutano maalum?”
Mistari ifuatayo ya Maandiko inatuonesha jinsi na lini
tunaweza kupokea upako zaidi wa Roho Mtakatifu. Yesu
alisema hivi: “Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa;
tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa. Kwa
kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye
abishaye atafunguliwa. Maana ni yupi kwenu aliye baba,
ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au
samaki, badala ya samaki atampa nyoka? Au akimwomba
yai, atampa nge? Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua
kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni
hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?”
(Luka 11:9-13).
Katika mistari hii, Yesu ametupatia maelekezo rahisi
sana jinsi tunavyoweza kujazwa kwa upya, tena na tena, na
Roho Mtakatifu.
a. Tunatakiwa tuombe, tutafute na tubishe. Mungu
ndiye Mtoaji wa Roho Mtakatifu (ms. 13). Agizo katika
mstari huu la kumfuata Bwana - kuomba, kutafuta, kubisha -
limeandikwa katika wakati wa sasa katika lugha ya
Kiyunani.
Maneno haya maana yake ni kuendelea kufanya hivyo,
hata sasa. Tunatakiwa tuendelee kuomba, tuendelee kutafuta,
tuendelee kubisha - mpaka tunapopokea jibu kutoka kwa
Bwana anayetupenda.
Tumeahidiwa, “Kila aombaye hupokea; naye atafutaye
huona; naye abishaye atafunguliwa” (ms. 10). Haleluya!
Mungu anafurahia kumimina Roho Wake juu yetu; kwetu si
zaidi ya kumwomba Yeye.
Yesu alitoa mifano mitatu ya kumfuata Roho Mtakatifu -
kuomba, kutafuta, kubisha. Siyo kwamba anatufunulia njia
au mitindo mitatu tofauti. Bali anatuhimiza tumfuate Mungu
kwa bidii na kwa unyofu.
Unaona kwamba hakuna kuombaomba wala kujaribu
kuthibitisha ustahili wako wa kupokea. Bidii hizi hazihitajiki;
tena ni mielekeo inayoweza kuziba njia yetu ya kupokea kwa
imani kama wana wa Mungu wapendwao.
b. Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya wana (wa kiume
na wa kike). Watu ambao ni wana wa Mungu, waliofanywa
hivyo kwa kuzaliwa upya (Yohana 1:12-13; 3:5-8)
hawalazimiki kuombaomba kwa Baba yao wa mbinguni
anayewapenda, kwa ajili ya baraka Zake alizowaahidi.
Yesu amefunua ukweli huu mkuu katika mfano wa jinsi
sisi kama wazazi tungeitikia watoto wetu (ms. 11 na 12).
Ndipo Yesu anaendelea kulinganisha nafasi yetu kama
wazazi na nafasi ya Mungu kama Baba yetu wa mbinguni
(ms. 13).
Halafu Yesu anatofautisha asili yetu yenye dhambi na
mipaka, na ukamilifu na upendo wa Mungu usio na mipaka.
Ikiwa sisi tulio wazazi “waovu” (wenye dhambi)
tusingewanyima watoto wetu vipawa vizuri, kwa nini tuwaze
kwamba Baba yetu wa mbinguni aliye mkamilifu na
mtakatifu angewatendea watoto Wake namna hii? (Kwa zaidi
kuhusu moyo wa Mungu kwetu, soma Warumi 5:6-10;
8:31-39; 1Yohana 3:1; 4:10,12-19.)
Sisi si waombaomba wanaolazimika kumsihi na
kumbembeleza Mungu asiyetaka kusikia. Sisi ni wana wa
Mungu Aliye Juu, naye anafurahia kutujaza Roho Wake
Mtakatifu.
Kwa kweli inatupasa tuombe kwa unyenyekevu na kwa
kutoa maisha yetu kabisa. Lakini sisi, kama watoto Wake,
tunaweza “kukaribia kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe
rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji”
(Waebrania 4:16; taz. pia Waefeso 3:12; Waebrania
10:19-22).
c. Kuna nini inayoweza kutuzuia tusipokee? Yapo
matatizo yanayoweza kutuzuia tusijazwe Roho Mtakatifu
mfululizo.
1) Kuwepo kwa dhambi au kuridhiana katika maisha
yetu (Warumi 6:12-14; 1Wakorintho 5:6-7). Biblia
inafundisha kwamba hatutakuwa huru kabisa na dhambi kwa
wakati wa maisha haya (1Yohana 1:8). Sisi sote tutakuwa na
vipindi vya kushindwa, ambavyo inatubidi tuvitubu kwa
haraka na kupokea msamaha wa Mungu.
Lakini ni lazima tusijiruhusu kuridhiana mfululizo na
dunia, mwili, na ibilisi. Biblia huwaita watu wenye
mwenendo huu “watendao” dhambi kama kawaida au wakati
wote (Wagalatia 5:21). Maana yake ni kufanya dhambi kama
mazoea au kwa kurudiarudia.
Dhambi ya kufululiza kama hii itatufanya tusifae kama
vyombo vya matumizi ya Bwana (1Wakorintho 9:24-27;
2Timotheo 2:19-21). Mungu wetu ni Mungu Mtakatifu
anayetuita sisi pia tuwe watakatifu, kwa uweza wa Roho
Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO • 59
Wake na neema Yake vikifanya kazi ndani yetu (1Petro
1:13-19).
Roho, ambaye ni mtakatifu (Warumi 1:4), hutaka
kutumia vyombo vitakatifu kwa kazi Yake.
2) Kuwepo kwa nia au motisha za kujitumikia, kama
ubinafsi au kiburi (Mathayo 7:21-23; Wafilipi 2:3-4;
1Timotheo 6:3-5). Tumekwisha jifunza kuhusu dhambi ya
kiburi na hatari zake. Kama viongozi wa kanisa, tunapaswa
tufanane na Yesu, aliye “mpole” na “mnyenyekevu”
(Mathayo 11:29).
Mungu hatawatia upako watu wanaotoa huduma kwa
motisha au nia zisizo halali (Yakobo 4:6). Lazima turuhusu
mioyo yetu ichunguzwe na Roho Mtakatifu (Mithali 16:2) na
kusafishiwa tamaa yetu ya kutukuzwa wenyewe. Ifuatayo ni
mistari fulani ya Biblia ambayo usome na kutafakari:
2Nyakati 16:9; Mithali 13:10; 16:5,18; Mathayo 23:8-14;
Wagalatia 5:20; Wafilipi 1:15-16; 1Timotheo 3:6; Yakobo
3:14 - 4:4.
3) Kutokusalimisha maisha yako yote (Warumi
12:1-2; Wagalatia 2:20). Nimekwisha andika kuhusu
umuhimu wa kusalimisha maisha yako yote kwa Mungu.
Lakini nitilie mkazo kwamba upako wa Roho Mtakatifu
unatolewa ili mtumishi wa Mungu aliyejisalimisha awe na
uwezo katika utumishi na kwa ajili ya utumishi. Kama
tunatamani uwezo wa Mungu kwa sababu yoyote nyingine
ila tu kumtumikia Yeye na watu, hatuwezi kutazamia upako
Wake katika maisha yetu.
Utumishi wetu uliosalimishwa uongozwe na Mungu,
kwa sababu Yeye anajua jinsi ya kututumia kwa ubora katika
Mwili wa Kristo. Huenda sisi hatutapewa nafasi ya kuchagua
yale tutakayomfanyia Mungu kazi. Mioyo yetu hupaswa
itamani kutenda lolote ambalo Yeye atatuagiza.
Nafasi yetu ya kujisalimisha kikamilifu ni ya lazima ili
tupokee uwezo kutoka kwa Mungu na pia tufahamu mapenzi
Yake. Ndipo inapotubidi tuchague kumtii Yeye. Ndivyo
tunavyoweza kuzaa matunda halisi katika utumishi.
4) Imani dhaifu au inayokosekana (Waebrania 11:6;
Yakobo 1:6). “Imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia
huja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:17). Lazima tujifunze
kutoka Maandiko yale ambayo Mungu ametuandalia, ama
sivyo imani yetu itakuwa dhaifu.
Ulipofuata masomo haya ya ki-Biblia ya upako,
umejifunza kwamba uwezo wa Roho Mtakatifu unapatikana
leo kwa ajili yako. Wala si kidogo tu, kama tone la maji
jangwani. Roho Mtakatifu atatiririka kupitia kwako kama
MITO (Yohana 7:37-39)!
Mungu ni Baba mwenye upendo, anayefurahi kuwapa
watoto Wake uzima na uwezo. Lakini inatubidi tuombe kwa
imani, tukimtegemea aitikie kilio cha mioyo yetu (Zaburi
138:3).
Kama una mashaka kwamba imani yako ni dhaifu au
ndogo, kumbuka Yesu alivyosema kuhusu imani: “...Mkiwa
na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu,
Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako
neno lisilowezekana kwenu” (Mathayo 17:20b).
Yesu alieleza kwamba imani yetu inaweza kuwa ndogo,
lakini bado ina ufanisi - KAMA imeelekezwa kwa Mungu!
Inatubidi tusijiamini wenyewe, wala kutegemea kiasi cha
imani tulicho nacho. Tunapaswa kuweka imani yetu katika
Mungu na Neno Lake. Maana Yeye anayoahidi, atatenda!
Tunaweza kutegemea kwamba Yeye atatimiza Neno Lake, na
kwa hiyo tunaweza kumwekea kikamilifu imani yetu.
Kwa hiyo, uimarishe imani yako katika Neno la Mungu.
Uamini yale yaliyofunuliwa katika Neno kuhusu Yeye aliye
Mwumbaji, Mwokozi na Mfalme wako! Umwendee mara
nyingi, tafuta uso Wake - naye atakuitikia (Yeremia
29:11-13).
5) Ukosefu wa njaa ya kiroho (Zaburi 63:1-2; 84:1-2;
Mathayo 5:6; Yohana 6:35,48; 7:37-39). Mungu daima
anaitikia njaa ya kiroho ya kupata zaidi ya Yeye.
Ukosefu wa njaa ya kiroho unaweza kusababishwa na
mambo mengi, kwa mfano:
• Msiba, huzuni au mauti (kama ya ndugu wa karibu)
inayosababisha uzito wa kihisia au kiroho
• Kuvunjika moyo, kushindwa au kuchoka,
kunavyokufanya ukate tamaa au kupoteza motisha ya
kumtafuta Bwana
• Hasira, uchungu au kutokusamehe wengine - akiwemo
Mungu na hata wewe mwenyewe - vinavyozimisha
hamu yako ya Mungu
• Raha na starehe za dunia hii, au uvivu na kinaya,
vinavyoziba au hata kuangamiza njaa yenye haki kwa
ajili ya kupata zaidi ya Mungu
Maisha ya hapa duniani huweza kuwa na ugumu na
hamasa nyingi za kushinda. Lakini tunaweza kutiwa moyo
kwamba Mungu ameandaa njia za kuvuka huzuni, maumivu
moyoni, kushindwa au vingine vyovyote ambavyo
tumeviona. Uponyaji na ukombozi wa Mungu, upendo na
msamaha Wake, rehema na neema Yake - na upako Wake -
vyote ni vyetu kama tutamjia Yeye Mwenyewe tu.
Mtume Paulo ametufunulia jinsi yeye alivyovuka
mambo ya dunia ambayo vingaliweza kumzuia asimtafute
Mungu wala kumwonea njaa ya kiroho. Aliwaandikia
Wafilipi (3:12-14): “Si kwamba nimekwisha kufika, au
nimekwisha kuwa mkamilifu...” (ms. 12a). Paulo alitambua
kwa unyenyekevu udhaifu wake na kushindwa kwake.
60 • MATENDO
Kizuizi
Kinachoua
UKAMILIFU
WA MUNGU
DHAMBI
Nakala 16 / Nambari 1
“...la! bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile
ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Yesu Kristo...”
(ms. 12b). Paulo alijua kwamba ilikuwa lazima asikate
tamaa; ilimbidi aendelee, kwa ajili ya Injili.
“Ndugu, sijidhanii kwamba nimekwisha kushika...”
(ms. 13a). Paulo hakufahamu mambo yote, yakiwemo yote
yaliyokuwa yamemtokea yeye.
“...ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo
nyuma...” (ms. 13b). Paulo alifanya uamuzi wa kuachia
maumivu au maudhi, kushinda au kushindwa - yote
yaliyokuwa yamekwisha pita.
“...nikiyachuchumilia yaliyo mbele...” (ms. 13c). Paulo
alichagua kuachia mambo ya zamani, na badala yale
kuchuchumilia makusudi ya Mungu kwa ajili yake.
“Nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito
mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu” (ms. 14). Paulo aliamua
kuendelea kumtafuta Mungu, na mapenzi Yake, haidhuru nini
ingemtokea.
Kupitia kila aina ya upinzani na mateso, kila furaha na
ushindi, Paulo alimfuata Bwana kwa moyo wake wote.
Kuchimba udongo usiozaa wa mioyo yetu (Hosea 10:12) si
kazi fupi au rahisi. Lakini kama tutajitoa kwa wazi kwa
Mungu - Yeye aliyetuumba, aliyetuokoa, na anayetupenda -
tunaweza kupokea moyo mpya na njaa mpya kwa ajili ya
Bwana (Ezekieli 36:26-27).
d. Lazima tumngojee Bwana. Maandiko yanatuhimiza
mara nyingi “kumngoj(e)a Bwana” (Zaburi 25:5; 27:14;
37:7,9,34; Isaya 30:18; 40:31; Maombolezo 3:25-26; n.k.).
Hii ni kanuni muhimu kwa maisha ya Kikristo. Kuna baraka
daima zinazotokana na kumngoja Bwana.
Lakini mara nyingi si asili yetu kungoja. Tunahamaki,
kuogopa au kusahau. Maisha yetu ya shughuli nyingi, kazi ya
huduma, mkazo tunaotiliwa kufikia uamuzi - mambo mengi
yanatukandamiza na kuchukua nafasi yetu.
Lakini kuna ukweli wa wazi, ingawa unaumiza, katika
maisha yetu: utayapatia yale yaliyo muhimu kwako nafasi
sikuzote. Inasikitisha kwamba mara nyingine hatutambui nini
ni muhimu hasa mpaka tumekwisha chelewa.
Mchungaji kwa Mchungaji: Ni muhimu kuchukua
muda mara kwa mara kutathmini vipaumbele vyetu,
kuchunguza maisha yetu na kutafakari shughuli zetu
zote. Halafu tuviweke hivi vyote mbele za Bwana,
kutafakari Neno Lake, na kuamua kama vipaumbele
vyetu vinalingana na Vyake.
Ikiwa hamasa ya Maandiko ya kuchukua muda wa
“kumngojea Bwana” haina nafasi ya juu katika orodha
yetu, inabidi ipatiwe nafasi hii. Maana mara nyingi
ndiyo njia pekee ambayo kwayo tutamsikia Yeye
akisema nasi.
Kumkaribia Mungu
Ili tupokee zaidi ya Roho Mtakatifu katika maisha yetu,
lazima tuiombe. Na halafu lazima tumngojee Bwana.
Wakati tunapongoja, ni rahisi zaidi sana kusikia “sauti
ndogo, ya utulivu” (1Wafalme 19:12). Kungoja kunampatia
Roho Mtakatifu nafasi ya kushughulikia mioyo na maisha
yetu, akituandaa ili tupokee zaidi ya uwepo na uwezo Wake.
Huenda atafunua kizuizi au kipingamizi cha kupokea kwetu;
anaweza atuthibitishie (dhambi); anaweza kutufundisha au
kutuelekeza; na zaidi.
Mara nyingi wakati wa kusubiri kwa uvumilivu ndipo
kazi ya kubadilishwa inapotendeka katika maisha yetu.
Tunavyobadilishwa, tutapokea; tunavyopokea zaidi ya
Roho Wake, bila shaka tutazaa matunda zaidi katika
huduma yetu.
Faida nyingine kubwa ya kumngojea Bwana ni kwamba
vipindi vya kukaa pamoja na Yeye vinatufikisha karibu na
Yeye Mwenyewe zaidi na zaidi. Tunapata kumfahamu kwa
ndani zaidi na kinafsi zaidi sana.
Unapomngojea Bwana, huenda utataka kunyamaza
(Zaburi 46:10). Au unaweza kusali kwa utulivu katika lugha
yako ya kiroho, au kuabudu kwa sauti ndogo (1Wakorintho
14:2,15). Lakini kumbuka, kusudi kuu la kungoja ni
kusikiliza na kupokea. Mara nyingi njia bora ya kufanya
hivyo ni katika hali ya utulivu na ukimya.
Katika njaa yako ya zaidi ya Mungu, huenda sala zako
zitaongeza sauti. Si lazima hali hii ni mbaya. Lakini
ukumbuke kwamba huna haja ya kuthibitisha hamu yako
wala ustahili wako kwa sauti kubwa ya sala zako; wala huna
haja ya kumpigia Mungu kelele ili aweze kukusikia na
kukujibu.
Badala yake, uamini ahadi Yake: “Je! Baba aliye
mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao
wamwombao” (Luka 11:13).
Usiogope
Wengine huenda wataogopa kwamba kumngoja Bwana
kwa ajili ya kupokea zaidi ya Roho Mtakatifu kungeleta pepo
mchafu badala ya Yeye. Hii haiwezekani! Kwanza, mapepo
wanaweza kuingia mahali walipokaribishwa tu, au kwa
sababu ya mtu kushiriki mambo ya ushirikina au uchawi.
Kama unamwomba Bwana na hamu yako ni kwa ajili ya
Yeye peke Yake, hakuna pepo mchafu anayeweza “kupenya”
ndani yako. Usiogope hili kamwe!
Ufalme wa mapepo unatambua kwamba jinsi
unavyopokea zaidi ya Roho Mtakatifu, ndivyo utakavyozidi
kutembea katika uwezo wa Mungu. Maana yake ni kwamba
ujasiri wako na mamlaka yako katika mambo ya kiroho
vitaongezeka kama mfuatano. Kwa hiyo ibilisi huenda
atakazana kukujaribu au kukugeuza mbali na nafasi ya
kumtafuta Bwana.
Lakini ukumbuke: Wewe ni mtakatifu uliyenunuliwa na
kutakaswa na damu ya Yesu Kristo. Shetani na mapepo yake
hawana nguvu juu yako ambayo wewe hukuwapatia
mwenyewe. Ibilisi alishindwa msalabani (Wakolosai
2:14-15). Kwa hiyo chukua silaha zako na upanga wako
(Waefeso 6:10-18) na kusimama imara katika Roho
unapomkaribia Mungu (Yakobo 4:7-8).
e. Upokee upako wa Roho Mtakatifu kwa imani. Sisi
ni wana wa Mungu na warithi wa ahadi Zake (Warumi 8:17;
2Wakorintho 1:20; Wagalatia 3:26). Hii ni pamoja na ahadi
ya kuja kwake Roho Mtakatifu (Matendo 2:38-39).
Tumejifunza kwamba si hoja ya kujazwa mara moja tu, bali
ni kujazwa mfululizo na uwepo na uwezo Wake katika
maisha yetu (Waefeso 5:18). Yale ambayo Mungu ameahidi,
atatimiza - kwa hiyo wewe umwombe tu!
Kwa hiyo tuombe - na kuendelea kuomba, kutafuta na
kubisha mpaka tuwe tumekwisha pokea (Luka 11:9-10).
Mungu anakutakia uwe na Roho Mtakatifu kwa ukamilifu
(Luka 11:13). Ufungue moyo wako na kumwamini Yeye
Nakala 16 / Nambari 1 MATENDO • 61
pamoja na hamu Yake ya kukujaza - wakati unapomngojea
kwa subira (Waebrania 11:6).
Kuomba tujazwe kwa upya kunaweza kufanyika kila
siku, kwa sababu tunapaswa tujazwe mfululizo! Tunahitaji
uwezo na uwepo Wake, dakika kwa dakika, katika mambo
yote tunayofanya.
Pokea Tu
Tunapokea kwa imani, si kwa hisia. Tunatafuta
mgawanyo wa Roho Mtakatifu, si tukio la kihisia.
Unapoomba, unaweza kukalisha mwili katika hali yoyote
inayokusaidia kutulia - kuketi, kusimama, au kulala chini.
Unaweza kuwa ndani ya mahali pako pa kusali, au jikoni,
katika chumba cha kulala, kanisani au nje. Hali ya mwili na
mahali ulipo si muhimu kama uwazi wa moyo wako na hamu
yako ya kupokea.
Unapoomba kujazwa Roho Mtakatifu kwa upya, utumie
maneno yaliyo moyoni mwako. Hakuna njia ifaayo au
isiyofaa ya kumwomba Mungu. Anataka kusikia kutoka
kwako, hivi ulivyo.
Huenda ungeomba namna hii: “Njoo Roho Mtakatifu,
ninafungua moyo wangu nipokee zaidi ya Wewe.
Ninasalimisha moyo wangu na maisha yangu Kwako.
Nakuomba unijaze kwa upya. Jaza maisha yangu na uwepo
Wako. Jaza kinywa changu na sifa kwa Mungu. Jaza huduma
yangu na uwezo Wako, ili niwe chombo kinachomfaa
Mungu....” Tumia maneno yako na kufungua moyo wako
kwa Mungu. Omba upokee! Ujazwe, katika Jina la Yesu!
Haleluya!
Mwisho
Ndugu na dada zangu, watenda kazi wenzangu katika
mashamba ya Mungu, na washiriki wenzangu katika huduma
ya kiutumishi kwa ajili ya Injili - sisi tuna wito wa hali ya juu
kabisa! Tunayo heshima ya kutumikia Mwili mpendwa wa
Kristo (Kanisa Lake), sisi ambao Petro atuambia
“mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au
dhahabu... bali kwa damu ya thamani, kama ya
mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa” (1Petro 1:18-19).
Huu ni wito ambao hatuwezi kujaribu kutimiza kwa
uwezo wetu binafsi, tena ni lazima tusijaribu kufanya hivyo.
Tumshukuru Mungu, Yeye ametupatia yote tunayohitaji ili
tuzae matunda kamili, tuwe na ufanisi kamili, na tumtukuze
Yeye kikamilifu!
Tulianza masomo haya kwa Neno la Mungu:
“Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu,
bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi”
(Zekaria 4:6)
Mungu, katika karne zote, amekwisha tenda mambo
makuu ya ajabu sana. Lakini bado kuna mengi zaidi kabisa
ambayo ameahidi kutenda, yatakayotendeka!
Kuna “kazi kubwa zaidi” za kufanywa - miujiza, ishara
na maajabu kwa ajili ya utukufu wa Yesu (Yohana 14:12). Na
Mungu anataka kuyafanya kupitia Kwako! Bwana anataka
utangazaji wa ujasiri wa Injili, kuongoka kwa waliopotea
kwa Kristo na kujengwa kwa Kanisa Lake. Anatamani haya
kwa ajili ya kanisa LAKO, jiji LAKO, taifa LAKO! Utukufu
kwa Mungu!
Mungu daima anawatafuta watakaosalimisha maisha yao
yote kwa mapenzi Yake. Anawatafuta ambao mioyo yao ina
uaminifu Kwake, ambao anaweza kuonesha nguvu Yake
kupitia kwao. Anawaitikia wale wanaomtamani kuliko yote
mengine, na ambao wanaruhusu njaa yao Kwake iongezeke -
wale watakaosema kwa ujasiri “Mimi hapa! Nitume mimi”
(Isaya 6:8)!
Kuna njia moja pekee ya kutimiza wito wa Mungu na
mapenzi Yake kwa ajili ya maisha na huduma yako - kwa
upako wa Roho Mtakatifu! Ni kwa uweza wa Roho
Mtakatifu kwamba utapokea mabadiliko, karama na vipawa
vilivyo lazima ili uwe na utende yote ambayo Mungu
anatamani kwako. Na haya yote ni yako kwa kuyaomba tu!
Mungu atakupa Roho Wake kwa wingi kabisa; uamini
hili, upokee upako Wake, utembee na kutoa huduma ndani
yake. Unapotoa uhai na uwezo wa Roho Mtakatifu katika
kuwahudumia wengine, Yeye atakuwa na zaidi ya kumimina
ndani yako na kupitia kwako.
Bwana akubariki na kukufungulia macho yako ya kiroho
ufahamu ukweli Wake. Upokee neema Yake na msaada Wake
ili umtii katika mambo yote. Akutie mafuta ya upako Wake
kwa wingi mwenyewe na katika huduma yako, ili maisha ya
wengine yabadilishwe na kuwa utukufu Kwake Yeye
aliyekufa ili awaokoe. Na Mungu apokee sifa yote, utukufu
wote, heshima yote anayostahili kutokana na maisha na
huduma yako unapotembea na kukua katika upako wa Roho
Wake Mtakatifu. Ninaomba haya mbele za Baba, katika jina
lenye nguvu na uweza la Yesu Kristo Mwokozi wetu. Amina!
62 • MATENDO
Kuna njia moja pekee ya kutimiza
wito wa Mungu na mapenzi Yake kwa
ajili ya maisha na huduma yako - kwa
upako wa Roho Mtakatifu! Ni kwa
uweza wa Roho Mtakatifu kwamba
utapokea mabadiliko, karama na
vipawa vilivyo lazima ili uwe na
utende yote ambayo Mungu anatamani
kwako. Na haya yote ni yako kwa
kuyaomba tu! Mungu atakupa Roho
Wake kwa wingi kabisa; uamini hili,
upokee upako Wake, utembee na
kutoa huduma ndani yake. Unapotoa
uhai na uwezo wa Roho Mtakatifu
katika kuwahudumia wengine, Yeye
atakuwa na zaidi ya kumimina ndani
yako na kupitia kwako.
Angalizo la Mhariri: Tafadhali angalia ukurasa ufuatao kwa
ajili ya maelezo jinsi unavyoweza kupata toleo lijalo ya Gazeti
la MATENDO kwa haraka zaidi katika mtandao wa Internet,
kwa anwani ya www.world-map.com.
Nakala 16 / Nambari 1
MATENDO • 63
1. Je, wakati umefika kwamba unapaswa kujiandikisha upya? Angalia tarehe kwenye kibandiko chako cha anwani
ambayo ni tarehe ya mwisho wa kuandikishwa kwako.
2. Kama tarehe hii ni CHINI YA MIEZI SITA kutoka sasa huu ni wakati wa kujiandikisha kwa upya!
3. HUTAKIWI kujiandikisha baada ya kupokea kila toleo la MATENDO: unapaswa kujiandikisha kwa upya ikiwa TU muda
wa miaka mitatu umekwisha pita au muda huu utakwisha katika miezi sita ijayo.
UNAWEZA KUJIANDIKISHA UPYA KWA "INTERNET ONLINE" AU KWA KUTUMA BARUA YA POSTA YA KAWAIDA.
• Kwa kujiandikisha upya online, utume email kwa: wmap@world-map.com na kufuata maelekezo haya:
1. Kuharakisha kazi, andika "Ufanye upya kibali changu cha MATENDO" kwenye “Subject Line” ya barua pepe yako.
2. Utume jina lako la kwanza na jina la mwisho, na utume pia namba yako ya kutumiwa MATENDO kutoka kwenye
kibandiko chako cha anwani yako. Ukifanya hivyo utaharakisha sana utekelezaji wa kukuandikisha upya. Kuna watu
wengine ambao majina yao yanafanana. Ukitupatia namba yako ya kibandiko, tutaweza kuona na kushughulikia habari
zako kwa haraka na usahihi.
3. Kama unabadilisha anwani yako, ututumie jina lako, namba ya kibandiko, anwani YA ZAMANI na anwani MPYA.
Ukiandika anwani mpya utumie utaratibu wa kawaida wa nchi yako, kama vile sanduku la posta, mji, mkoa, na nchi.
4. Ingiza maelezo mengine yanayotakiwa kwenye fomu hapa chini. Tafadhali ujibu maswali yote. (Tafadhali usitume
"Attachment" yoyote. Hatufungui “Attachments”.)
5. Ili upewe kiungo cha barua pepe cha kuweza kupokea MATENDO kwa njia ya Internet, utupatie pia anwani yako ya
barua pepe. Hakikisha imeandikwa kwa usahihi. (Hata hivyo utapokea nakala yako ya MATENDO kwa njia ya Posta
pia, baadaye.)
• Kwa kujiandikisha kwa njia ya posta, kata fomu hapa chini au inakilishe kwenye karatasi nyingine.
1. Fuata maagizo YOTE kwenye fomu hii (chora mviringo kwa Ndiyo au kwa Hapana).
2. Ujibu KILA swali kwenye fomu hii tumia herufi kubwa zinazosomeka vizuri.
3. Ili upewe kiungo cha barua pepe cha kuweza kupokea MATENDO kwa njia ya internet, andika anwani yako ya barua
pepe kwa usahihi ukitumia HERUFI KUBWA.
4. Tuma fomu hii kwa: WORLD MAP ACTS INDIA, P.O. Box 1037 Kilpauk Chennai, 600010 T.N. India; au World MAP,
P.O. Box 721, Arusha, Tanzania; au kwa makao makuu ya Marekani; au kwa tawi lililo karibu na wewe (tazama orodha
ya anwani hapo chini).
ANGALIZO: Gazeti la Matendo linatolewa pasipo malipo kwa viongozi wa kanisa katika Asia, Afrika na
Marekani Kusini (ambao wanawafundisha au kuwahubiria watu wasiopungua 20 kila juma) ambao
wameomba walipokee. Kiongozi wa kanisa angalia: Utapokea MATENDO kwa miaka mitatu; ndipo utahitaji
kujiandikisha upya ili ulipokee tena kwa miaka mitatu mingine. Gazeti la MATENDO si “Masomo kwa njia
ya posta”. Hutapokea “cheti” au “diploma” baada ya kusoma MATENDO. Ni tumaini letu na sala yetu
kwamba utapokea kilicho na thamani kubwa zaidi sana: Mafundisho yenye msingi katika Biblia na
mafunzo kwa ajili ya utendaji wa huduma yako! Hivyo vitakuandaa uwe na ufanisi mwingi zaidi katika
kuwafundisha, kuwahudumia na kuwashuhudia watu wengine.
1. Kwa kuwa muda wangu wa kupokea Gazeti la MATENDO utakwisha katika miezi sita ijayo, ninahitaji
kujiandikisha upya. NDIYO HAPANA
2. Namba yangu ya kibandiko cha MATENDO ni ___________ Tarehe ya mwisho wake ni ______ / ______
3. Mimi ni mtenda kazi wa kanisa katika Asia, Afrika au Marekani Kusini, na ninahubiri au kufundisha watu wasiopungua
20 kutoka katika Biblia kila juma (Ni LAZIMA hoja hii iwe ya kweli ili uweze kupokea maandiko
yetu.) NDIYO HAPANA
4. Je, unayo nakala ya kitabu cha Fimbo ya Mchungaji? NDIYO HAPANA
5. Je, unaomba nakala ya kitabu cha Fimbo ya Mchungaji sasa? NDIYO HAPANA
6. Je, unataka kupewa kiungo cha barua pepe cha kupokea toleo lijalo la MATENDO litakapokuwa tayari?
NDIYO HAPANA
7. TAFADHALI ANDIKA MAJINA YAKO YOTE KWA HERUFI KUBWA PAMOJA NA ANWANI YAKO HAPO
CHINI. JE, ANWANI HII NI MPYA? NDIYO HAPANA
Jina langu la Ukoo (la mwisho): ___________________ Jina la ubatizo (la kwanza):____________________
Anwani yangu ya posta: ___________________________________________________________________
Mji/Jiji _______________________________________ Mkoa (kama inahitajika)______________________
Nchi yangu ___________________________________ (Namba ya jiji kama ipo)_______________________
Nafasi, madaraka au cheo changu katika kanisa ________________________________________________
Sahihi yangu _____________________ Anwani yangu ya barua pepe: ____________________________
8. Je, mafunzo ya toleo hili la MATENDO yamekuwa: _______ rahisi kuelewa _____magumu kuelewa
_______ yamenisaidia _____hayakunisaidia
Ukitumia karatasi nyingine au kwa barua pepe kwa wmap@world-map.com, unaweza kutushirikisha ushuhuda wako au maoni yako
kuhusu jinsi mafundisho ya MATENDO au Fimbo Ya Mchungaji yanavyokusaidia.
UTUME FOMU HII KWA:
WORLD MAP ACTS INDIA, P.O. Box 1037 Kilpauk Chennai, 600010 T.N. India;
POST BOX 721 ARUSHA, TANZANIA (au kwa anwani nyingine hapa chini kama ni karibu zaidi na kwako):
au World MAP Head Office, at World MAP, 1419 N. San Fernando Boulevard, Burbank CA 91504 USA
KUJIANDIKISHA UPYA / KUOMBA KITABU CHA FIMBO YA MCHUNGAJI (Viringisha Ndiyo au Hapana kwenye maswali hapo chini)
SW 0108
* * TUMIA HERUFI KUBWA ZINAZOSOMEKA VIZURI * *
MUHIMU • UJIANDIKISHE KWA UPYA KWA NJIA YA MTANDAO NA BARUA PEPE! • MUHIMU
Uwe kati ya viongozi wa kwanza watakaopokea toleo lijalo la MATENDO - online!
Fuata maelekezo hapa chini kwa "kujiandikisha" ili uweze kupokea Gazeti la Matendo kwa njia ya "internet".
Nakala 16 / Nambari 1
Fimbo Ya Mchungaji hujulikana kwa
wengine kama "Shule ya Biblia katika
Kitabu" iliyo kamili kabisa. Kina kurasa 1000
na kimeandaliwa kwa ajili ya kuwafunza na
kuwaandaa viongozi wa kanisa. Ndani yake
kuna maandiko yenye upako wa Roho na
msingi wa ki Biblia, ya waandishi wengi.
Kitabu hiki kiliandaliwa kwa ajili ya
mahitaji maalum ya viongozi wa
kanisa wanaofanya kazi katika
Asia, Afrika na Marekani Kusini.
Kama wewe ni msomaji mpya
wa MATENDO na hujapokea nakala ya
Fimbo Ya Mchungaji, uombe nakala
yako sasa.
Yaliyomo ndani ya “Fimbo Ya Mchungaji”:
[1] Kitabu Kidogo cha Malezi ya Waamini Wapya chenye masomo yote unayohitaji ili uwafundishe
waongofu wapya.
[2] Mwandani Wa Biblia yenye orodha ya maelfu ya mistari ya Biblia inayohusiana na hoja 200
kubwa za Biblia.
[3] Mwongozo Wa Kufunza Viongozi wenye masomo bora yote yaliyokusanywa na World MAP kwa
muda wa miaka thelathini iliyopita.
Yote haya na mengine yamo katika kitabu kimoja kiitwacho Fimbo Ya Mchungaji.
Ili upokee nakala yako ya kitabu hiki chenye nguvu kubwa, Fimbo Ya Mchungaji, unahitaji kuiomba
kwa njia ya INTERNET kwa kutumia anwani www.world-map.com au ujaze kwa makini fomu ya
maombi nyuma ya ukurasa huu (au unaweza kuandika maelezo yote kwa HERUFI KUBWA kwenye
karatasi nyingine kama hutaki kukata gazeti lako). Ukiwa umejibu maswali yote na kuandika maelezo
yako kwa usahihi, utume fomu kwa Ofisi ya World MAP iliyo karibu na wewe. (Anwani zipo chini ya
fomu yenyewe.) Kama unaweza kutumia INTERNET, hutahitaji kununua stempu! Utapokea nakala
yako ya Fimbo Ya Mchungaji mapema iwezekanavyo (lakini kwa kuwa vifurushi na barua za posta
huchukua muda mrefu mara nyingi, tafadhali uache miezi sita au hata zaidi kwa ajili ya kupokea nakala
yako ya Fimbo Ya Mchungaji). Asante.
For private circulation • Kwa wahusika binafsi tu
Tafadhali uombe
kitabu cha Fimbo
Ya Mchungaji
kama tu
hujakipokea.
ANGALIZO KWA VIONGOZI WA KANISA:
Je, unachimba ndani zaidi katika Maandiko kwa
kutumia Fimbo Ya Mchungaji, zana ya World MAP
ya kufanya wanafunzi iliyo na nguvu kubwa?
Fimbo Ya
Mchungaji
Biblia

No comments:

Post a Comment