Friday 5 December 2014

MAFUNZO YA BILBIA NA HUDUMA ZA KANISA



TANGAZO
HABARI NJEMA KWA WATUMISHI WA MUNGU
Ongeza kichwa

ELIMU YA BIBLIA NA MAFUNZO YA HUDUMA KWA NJIA YA POSTA

Elam Christian Harvest Seminary  kwa kushirikiana na Harvestime International Institute iliyoko Marekani  Wanakuletea Mafunzo ya Biblia na Huduma za Kanisa kwa njia ya Posta.  Huna haja ya kuacha kazi yako na kwenda masomoni kwa muda mrefu,  bali unapaswa kutenga muda  kiasi fulani kila wiki ambao utatumia kujifunza ukiwa  nyumbani kwako au na wenzako katika kikundi.unaweza kusoma ukiwa kazini kwako na kufikia kiwango chochote unachohitaji. Tunaamini kwamba watendakazi wanapaswa kuandaliwa katika uwanja wa mavuno.
Masomo haya  ni ya   ngazi ya Stashahada (Diploma) katika fani ya Biblia na Huduma za kanisa.  Muda wa mafunzo ni miaka mitatu. Mwanafunzi akifuzu masomo yote atatunukiwa Stashahada ya Biblia na Huduma za Kanisa. Mwanafunzi atasoma somo moja au mawili  kila mwezi.
Gharama ya kila somo  ni TSh. 5000 kwa sasa  lakini gharama hizo zaweza kubadilika kutokana na kupanda kwa gharama ya uendeshaji wa mafunzo.
Ikiwa unapenda kujiunga na masomo haya tafadhali tuandikie au tupigie simu kwa  namba zilizopo hapo chini.
S.L.P 69  MKWAJUNI MBEYA
E-mail elamharvestseminary@gmail.com
Simu Na . 0762532121,

               075787107
Wako katika mavuno

……………………………………………..
Rev. Erick Mponzi.
Mratibu wa mafunzo

Kwa maelezo zaidi wasiliana na   Mratibu wa mafunzo kwa namba za simu  simu zilizopo hapo juu.



ORODHA YA MASOMO
MODULI YA KWANZA
1.     KUJENGA MISINGI YA IMANI.
2.     PITIO LA AGANO LA KALE
3.     PITIO LA AGANO JIPYA
4.     BIBLIOLOJIA.
5.     SIFA NA IBADA.
6.     MBINU ZA KUJIFUNZA BIBLIA
7.     KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU.
8.     KUISIKIA SAUTI YA MUNGU
9.     UPAKO WA ROHO MTAKATIFU.
10.  MAANDALIO YA UONGOZI

MODULI YA PILI.
1.     HISTORIA YA KANISA.
2.     KUANDAA MAHUBIRI
3.     KANUNI ZA KUFASILI MAANDIKO.
4.     SAIKOLOJIA YA BIBLIA.
5.     UINJILISTI.
6.     THEOLOJIA LINGANISHI
7.     MAMLAKA YA MWAMINI
8.     KANUNI ZA UONGOZI WA KIROHO.
9.     NGUVU YA MAOMBI NA DHABIHU.
10.UPONYAJI NA UKOMBOZI.


MODULI YA TATU.
1.     USHAURI WA KICHUNGAJI
2.     THEOLOJIA YA KICHUNGAJI
3.     HUDUMA ZA AGANO JIPYA
4.     KANISA
5.     KUONGOZA KWA KUSUDI.
6.     KANUNI ZA MAZIDISHO
7.     THEOLOJIA YA MATENDO
8.     KUPANDA MAKANISA.
9.     WAEBRANIA
10. MIKAKATI YA MAVUNO YA KIROHO.

No comments:

Post a Comment