Friday 5 December 2014

MAOMBI YA TOBA NA UREJESHO

Dar es Salaam Pentecostal Church
Siku kumi na nne za kufunga na kuomba
Wiki ya Kwanza tarehe 13 - 19 Januari 2014
Kila siku: . Mshukuru Mungu kwa ajili ya Nguvu wakati huu wa maombi ya kufunga na kuomba. Omba neema ya kuomba na kufunga mpaka mwisho wa maombi. Isaya 40:31
 Tubu na omba msamaha ili maombi yako yajibiwe na pasiwe na kizuizi cha aina yoyote. 1 Yohana 1 : 9. Zaburi 51 : 6
 Omba Roho mtakatifu akusaidie kuomba sawa na mapenzi ya Mungu.
JUMATATU – Maombi ya toba, Urejeshona na Utakatifu. Zaburi 51, Waebrania 12 : 14
1. Eh Bwana nirehemu sawasawa na fadhili zako, nitakase,nipe furaha na nipe kuijua hekima yako. Zaburi 51 : 1 - 8
2. Mwaka huu uniimarishe katika kutenda haki. Nakuweka mbele Bwana wangu na kwako sitaondoshwa. Zaburi 16: 8
3. Niumbie moyo safi na moyo uliyo vunjika.. Zaburi 51: 10. Weka kiu ndani yangu kukutafua wewe kama Ayala aioneavyo mito ya maji. Zab 42:1.
4. Mwaka huu nisaidie nisiabudu miungu mingine (pesa, umaarufu, Cheo, mitindo nk) Katika jina la Yesu . Mathayo 6 : 24.
5. Kama kanisa tusaidie kutembea katika utakatifu mbele zako,Waebrania 12 :14 Ondoa moyo wa jiwe, weka moyo wa nyama. Ezekieli 36 : Tufanye vyombo vyenye heshima kwa ajilli ya utukufu wako na kwa ajili ya utumishi.
2 Timotheo 2 : 21
JUMANNE - Maombi kwa ajili ya uoungozi wa Kimungu. Zaburi 25 1 -5, 31 : 3
(Kama Daudi alivyomba)……. 1 Samweili 23 : 2-4. 30 : 8,
2 Samwei 2 : 1, 1 Mambo ya nyakati 14 : 10)
1. Mwaka huu niongoze kwa Roho wako mtakatifu. Warumi 8:14. Nionyeshe njia zako na nifundishe njia zako. Zaburi 25 : 4 & 12. Zaburi 103 : 7. Ongoza hatua zangu. Zaburi 37 : 23. Nifundishe kuisikia sauti yako
2. Nisaidie kusikia sauti yako na kuitii. Nifundishe kukungoja wewe Bwana na kutafakari hekaluni pako. Zaburi 27 : 4.
3. Mwaka huu nitafuata ratiba yako kwa ajili ya maisha yangu. Mithali 19 : 21. Sitatoka katika mpango wako, sitaanguka katika mitego ya adui katika jina Yesu. Kila mpango wa adui juu ya maisha yangu umeshindwa kwa jina la Yesu.
4. Kama kanisa tufundishe kukungoja, tufundishe kukungoja kwa ajili ya muelekeo Zaburi 48 : 14.Tupe neema ya kukutii katika kila jambo. 1 Sam 15 : 22 .
JUMATANO - Maombi kwa ajili ya Neema tele. 2 Wako 9: 8, Zaburi 84 : 11,
2Wako 13 : 14.
1. Eh Bwana, mwaka huu nisaidie nipate kibali machoni pako. Naomba neema iongezeke kwangu, familia yangu, katika huduma yangu, biashara zangu, kazi, elimu nk. 2 Wako 12 : 9. Mwanzo 39 : 4
2. 1 Wakorintho 15 : 10. Niko hivi nilivyo kwa neema yako. Naomba kibali chako katika maisha yangu. Mwanzo 39: 21.Naomba neema yako katika maisha yangu isiwe bure.
3. Napokea kibali na milango itafunguka kuanzia sasa kwa Jina la Yesu .Dan 1 : 9. Kibali cha Bwana kifungue milango iliyokua imefungwa katika jina Yesu. Kila mlima ulio simama mbele yangu na ung’oke kwa jina la Yesu. Zakaria 4: 6, Zaburi 84 : 11.Bwana wewe ni jua langu na ngome yangu,kila jambo jema litaachiliwa kwangu mwaka huu katika jina la Yesu.
4. Kama kanisa tusaidie kutembea katika neema yako,tupe neema ya kuongezeka,kuinuliwa na kupanda juu katika jina la Yesu. Psalm 75 : 6.
5. Kwa neema yako dhambi haina nguvu juu yangu tena. Warumi 6 : 1,14
ALHAMISI - Maombi kwa ajili ya upendo wa Mungu. Efe 2 :4, 2 Wok 13 : 14
1. Nijaze upendo wako.Nifunike na pendo lako . Maombolezo. 3 22-23
2. Nifundishe kukupenda na vyote nilivyonavyo. Pendo langu kwako na wivu wa nyumba yako vinile. Zaburi 69 : 9 Kila kitu natoa kwako. Mathayo 22 : 37, Warumi 8 : 39.
3. 1 Wakorintho 13…Nisaidie kuwapenda wote walionizunguka. Warumi 5 : 5.
1 Wathesalonike 4: 9.Nifanye chombo cha kupitisha pendo lako.1 Yohana 4 : 7 -8
4. Mahali popote ambapo nilisitahili kupokea upendo lakini sikupata, mwaka huu Bwana kuwe na urejesho wa upendo.
1Nyakati 4 : 9 – 10, Mwanzo 29 : 32 – 35. Kutoka 12: 36
5. Kama kanisa tufundishe kukupenda na kutembea katika hofu yako. Tusaidie na kukua na kukomaa katika mambo ya rohoni katika jina la Yesu. Mwaka huu tusaidie kuwafikia wengi na pendo lako. Waefeso 5 : 2 Luka 10: 27 Tuunganishe kwa pendo lako. Wafilipi 2 :3.
IJUMAA –Maombi ya ushirika na Roho Mtakatifu 2 Wakorintho 13 :14
1. Roho mtakatifu nivute karibu ili niwe na ushirika na wewe. Uwe mwalimu wangu, 1 Wakorintho 2 : 13, kiongozi wangu, Efeso 3 : 5 Mfariji wangu Yohana15 : 26, Mwezeshaji wangu Matendo 1 : 8, Nihuishe Warumi 8 : 13
2. Nisaidie kutegemea na kufuata uongozi wako katika kila jambo. Nisaidie kutembea katika mapenzi yako kamili. Funua siri za Mungu kwangu 1 Wokorintho 2 : 9 -12. Nipe ufahamu wa Neno.
3. Baba, Kuanzia sasa, naomba matunda ya Roho matakatifu yadhihirike kwangu na katika kanisa katika jina la Yesu. Wagalatia 5 : 22 - 23
4. Bwana, natamani karama za Roho mtakatifu katika maisha yangu na katika kanisa. 1Wakorintho 12 : 1 – 11. Dhihirisha karama hizo kwa jina a Yesu.
5. Roho Mtakatifu nipe upako kwa ajili ya utumishi mwaka huu. Zaburi 92: 10 – 15. Achilia moto juu ya madhabahu yangu ya maombi na nitie nguvu kuomba bila kukoma. 1Wathesalonike 5 : 17
JUMAMOSI - Maombi kwa ajili ya kanisa na taifa. 1 Timotheo 2: 1-2
1. Bwana tuna kabidhi maono ya kanisa kwako. Uyakamilishe kwa wakati wake. Habakuki 2 : 3.Tunaombea uongozi wa kanisa (wachungaji, Wazee,Viongozi wa idara, Viongozi wa seli). Bwana, wape hekima, watie nguvu na roho ya ufunuona neema kwa ajili ya utumishi. Efeso1 : 17. Achillia upako juu ya kanisa kwa ajili ya kufanya mambo makubwa katika jina la Yesu. Danieli 11 : 32.
2. Mradi wa Ujenzi…Tunaomba ujenzi uende vizuri. Tufanye kuwa watoaji wazuri. 2 Wako 9 : 7. Tusaidie kupata msaada kutoka sehemu nyingine. Tunapolijenga kanisa lako, jenga maisha yetu katika jina la Yesu.
3. Bwana inua kanisa hili ili liwe na mguso katika taifa na mataifa.
Matendo 2 : 1 - 47
4. Hakuna silaha itakayo inuka kinyume na kanisa hili itafanikiwa. Na kanisa litafanikiwa. Tunainua kanisa la Tanzania na katika mataifa yote duniani. Isaya 54 : 17
5. Tunaomba hekima kwa viongozi wa taifa hili. Tupe viongozi wenye moyo wa kutumika, moyo unaokupenda na kuwapenda watu. Tunapoelekea majira ya uchaguzi inua viongozi wenye moyo wa kutenda haki. Mithali 29 : 2.Tunapinga roho ya matengano katika taifa. Zaburi 133 : 1. Tunatangaza amani ya Bwana kutawala.
JUMAPILI - Shukurani Zaburi 106 : 1, Zaburi 92 1 - 5
1. Mshukuru Mungu kwa ajili ya nguvu na neema ya kuomba kuanzia Jumapili mpaka sasa.
2. Mshukuru Mungu kwa kujibu maombi
3. Mshukuru kwa rehema zake,uaminifu wake na upendo wake.
4. Mshukuru kadri Roho atakavyo kuongoza
…. Awafanyia wamchao matakwa yao,Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa. Zaburi 145 : 19

No comments:

Post a Comment