Monday 15 December 2014

idara ya uinjilisti na umisheni KLPT JIMBO LA MBEYA


KANISA LA PENTEKOSTE TANZANIA
JIMBO LA MBEYA
IDARA YA UIJILISTI NA UMISHENI

Jina  la idara  Idara hii inaitwa idara ya Uinjilisti na Umisheni.

Maono ya idara(vission)
Kutoa fursa kwa watu wote walioko ndani na nje ya jimbo la Mbeya kusikia injili ya Yesu kristo, kwa kuanzisha mtembeo wa upandaji wa makanisa yatakayojizidisha katika kila jamii iliyopo duniani kupitia nyenzo ya  uinjilisiti.


Dira ya idara. (Mission)
Kuhubiri Injili kwa kila  kiumbe na kuwafanya watu kuwa wanafunzi
Tunaamini kwamba Injili itahubiriwa kwa haraka pindi tutakapofaulu kuwafanya waamini kuwa wanafunzi na kama kanuni ya mazidisho itafanya kazi
 kila mmoja kufundisha mwingine”  
Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi hayo uwakabidhi watu waaminifu wataka faa kuwafundisha na wengine. (2Tim 2:2)
Dira ya idara hii ni kuhakiskisha kila mwammini wa kanisa la mahai anajihusisha na agizo kuu. Kuhamasisha na kutia moyo waaamini kutumbau kwamba agizo kuu lina mhusu kila mmoja yeye binafsi na kanisa kwa ujumla.

Andiko la idara
Yohana 4:35
,, “Inueni macho yenu  myatazame mashamba  na kuwa yameshakuwa tayari kwa mavuno”
Kazi za Idara
Malengo ya idara.
Malengo ya idara yamegawanyika katika maeneo mawili ambayo ni
·       Malengo ya jumla (general objecive)
Malengo ya jumla yanaelezea kusudi hasa la kuwepo kwa idara hii na kile kinachpaswa kutekeleza kwa ujumla wake.
·       Malengo mahususi(Spesific objective)
Malengo mahususi yanafafanua malengo ya jumla kwa kuainisha mambo maalumu amabo ni msingi wa uwepo wa idara hii. Malengo mahususi yanatuwezesha kmatokeo ya muda mfupi na yenye kupimika .

Malengo ya jumla
Idara hii ya uinjilisti na umisheni imeanzishwa kwa kusudi la kuharakisha utekelezaji wa Agizo kuu la Bwana wetu Yesu Kristo.
Akawaambia “Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe” Marko 16:14
Maelezo haya ni amri ambayo iko wazi na inadai utekelezaji. Hivyo idara hii  iko kwa kusudi hili la kuhubiri Injili kwa watu wote na kupanda makansa katika maeneo mbalimbali.
Tunaamini kwamba  uinjilisti na umisheni ndio kipaumbele cha kwanza cha Kanisa . Wosia wa mwisho wa Yesu Kristo kwa wanafunzi wake ulihusu Agizo kuu yaani Uinjilisti na umisheni. Matendo ya Mitume1:8
Wosia wa mwisho wa mtu huwa unashikwa na kufanyiwa kazi kuliko kitu kingine chochote kile. Hivyo kanisa linatakiwa kuupa uzito wa kipekee wosia  huu wa Agizo kuu.
Idara hii inalenga kuhamissha na kutumia rasilimali mbalimbali kuanzia ngazi ya tawi, parishi na jimbo katika kuhubiri Injili  na kupanda makanisa yenye kujizidisha. Tunaamini raslimali kuu ni watu hivyo wamini wanatakiwa  kufanywa wanafunzi wenye uwezo wa kujizidisha ili kuufikia ulimwengu wote kwa Injili. Kuhakikisha watu wote wanafikiwa pale walipo kwa Injili ya Yesu Kristo.
Malengo mahususi
1.     Kuanzisha idara ya uinjilisi na umisheni  kuanzia tawini  hadi parishi.
2.     Kuandaa makongamano ya wahubiri na waimbaji  ili kupeana  uzoefu na changamoto katika huduma ili kuweza kuboresha huduma za waimbaji na wainjilisti walioko ndani ya KLPT  jimbo la Mbeya.
3.     Kunzisha mfuko wa huduma ya Uinjilisti na umisheni wa jimbo.
·       Kupendekeza asilimia tano (5%) ya mapato ya kila kanisa kuingia katika mfuko wa uinjilisti na umisheni.
·       Kundesha halambee kwaajili ya kukuza mfuko wa Injli.
·       Kufungua akaunti benki ya uinjilisti na umisheni.
·       Kuanzisha miradi mbalimbali  mfano shule, gazeti, redio Nk
4.     Kuanzisha mtandao wa maombi  wa Injili na Umisheni.
5.     Kufanya uinjilisti wa Maandiko
Kuandaa vipeperushi, majarida na vitini kwaajili ya uinjilisti  wa maandiko.
6.     Kufanya Uinjilisti kupitia vyombo vya habari, mfano Redio, magazeti na  luninga.
7.     Kuanzisha tovuti ya idara
·       Kuanzisha tovuti ya idara ambayo itatumika kufaya uinjilisti kupitia mtandao.
·       Kufanya uinjilisti kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii
8.     Kukuza afya ya kanisa.
Kuhakikisha  makanisa yote ya KLPT Jimbo la Mbeya yanakuwa na vichocheo mbalimbali vitakavyosababisha  kukua kwa vipawa, karama na huduma za waamini wote na kuwafanya wanafunzi weye kujizidisha  kwa kufanya yafuatayo .
·       Kila kansa kuanzisha ibada za maombi na maombezi ya nguvu kama chambo cha uvunaji.
·       Kuboresha mifumo ya ibada. Ibada zisikae kiburudani zaidi. Ibada kugeuka kuwa ukumbi. Mambo ya kiroho kupewa kipaumbele katika ibada.
·       Uboreshaji wa majego na upatikanaji wa vyombo vya mziki na injili.



No comments:

Post a Comment