Friday 5 December 2014

MAFUNZO YA MSINGI YA UONGOZI

Mwanafunzi-Kiongozi 1 Huduma Ya Barry Wood
SEHEMU YA KWANZA:: MWENENDO WA KIIONGOZII WA
WAFUASII
YALIYOMO
UKAMILIFU…………………………………………………………………………………………………….……3
Muda Wa Faragha Na Mungu…………………………………………………………………………………………………7
Dakika Nne Na Mungu Katika Maombi ............................................................................................................. .11
Kanuni Za Mavuno Ya Kiroho ....................................................................................................................... ….13
Kazi Saba Za Roho Mtakatifu ............................................................................................................................ .17
Yabesi: Kuishi Kwa Njia Ya Baraka.................................................................................................................. .17
Kuishi Huru Kifedha…………………………………………………………………………………………………………...21
Mfano Wa Ghurudumu……………………………………………………………………………………………………...…29
Mfano Wa Mkono………………………………………………………………………………………………………………31
Kanuni Za Kuweka Maandiko Moyoni............................................................................................................... .33
Kuandaa Mahubiri Kutoka Kwa Neno La Mungu .............................................................................................. .37
Muhtasari.......................................................................................................................................................... 43
Utangulizi.......................................................................................................................................................... 45
Jinsi Ya Kuishi Kimiujiza................................................................................................................................... 47
Jinsi Ya Kuomba Katika Roho Mtakatifu ........................................................................................................... .49
Jinsi Ya Kuomba Na Nguvu ............................................................................................................................... .55
Jinsi Ya Kuomba Kwa Imani............................................................................................................................. .59
Mbona Tunaomba Katika Jina La Yesu?............................................................................................................ .65
Vita Vya Kiroho Ni Vita Vipi?………………………………………………………………………………………………..69
Kuwa Shujaa Wa Maombi ................................................................................................................................ .73
Kutumia Silaha Za Vita Vya Kiroho................................................................................................................... .75
Funguo Za Ufalme Ni Zipi? ............................................................................................................................... .79
Uombezi Ni Nini?………………………………………………………………………………………………………………83
Je, Kukosa Kutii Kunaweza Kuzuia Maombi Yako? ........................................................................................... .87
Kizuizi Kikubwa Kwa Maombi.......................................................................................................................... .91
Mungu Anapokosa Kujibu Maombi Yangu......................................................................................................... .97
Kujifundisha Kuombea Waliopotea Dhambini ................................................................................................... .99
Nawezaje Kuwa Mwombezi? ........................................................................................................................... .103
Kufunga Ni Nini? Inahusiana Vipi Na Maombi?………………………………………………………………………...109
Msaada Zaidi………………………………………………………………………………………………………………….121
Kasha: Jawabu Kuhusu Matatizo Ya Maisha .................................................................................................. .125
Kasha La Kueneza Injili ................................................................................................................................. .127
Kujifunza Kushiriki Ushuhuda Wako ............................................................................................................... .129
Kushuhudia Kutumia Mfano Wa Daraja.......................................................................................................... .131
Kuvumbua Siri Iliyoka Katika Fumbo Kuu La Maisha………………………………………………………………….135
Kiongozi Mtumishi........................................................................................................................................... 137
Nguvu Ipatikanayo Katika Maono?………………………………………………………………………………………...141
Kutimiza Ono Lako……………………………………………………………………………………………………………145
Tumezaliwa Ili Tuzae…………………………………………………………………………………………………………147
Taratibu Za Mkufunzi ..................................................................................................................................... .151
Mtu Mwaminifu Ni Nani ? ............................................................................................................................... .153
Kumwongoza Mtu Kukomaa ............................................................................................................................ .157
MICHANGO ..................................................................................................................................................... .159
SEHEMU YA PIILII:: KIIONGOZII WA WAFUASII NA NENO LA
MUNGU
SEHEMU YA TATU:: VIITA VYA KIIONGOZII WA WAFUASII
SEHEMU YA TANO:: KAZII YA KIIONGOZII WA WAFUASII
SEHEMU YA NNE:: USHUHUDA WA KIIONGOZII WA
WAFUASII
Mwanafunzi-Kiongozi 2 Huduma Ya Barry Wood
Masomo Zaidi Katika Mtandao (Internet)…………………………………………………………………………………161
T
3
UKAMILIFU
Ukamilifu (integrity) ni neno ambalo limetokana na neno la
kihesabu (integer) iliyo na maana ya kuwa bila upungufu
Ukamilifu ina maana ya “umoja wako”
Ukamilifu inahusu kuwa mtu kamilifu, asiyetawanyika
Ukamilifu ni kilindini cha tabia yako
Ukamilifu ni kutembea mwendo wako
Ukamilifu ni kuenenda uongeavyo
Ukamilifu ni kumaanisha usemayo
Ukamilifu ni kusema umaanishayo
Ukamilifu ni kumtazama mtu kwa macho na kusema ukweli
Ukamilifu ni kuwa mwaminifu wakati ambapo ni vigumu kuwa mwaminifu
Ukamilifu ni kujali masilahi ya watu wengine kabla ya kujali yako
Ukamilifu ni kuwa na tabia itakayompendeza Baba yako
aliye mbinguni
Ukamilifu ni kumwambia mtoto “fanya nifanyavyo” kisha ukafurahia
Ukamilifu ni kuwa mwema hata kama wema si mtindo
Ukamilifu ni kutenda vyema, kwa sababu ni haki kutenda vyema
Ukamilifu ni kuwa na msimano katika maneno yako
Ukamilifu ni jinsi ulivyo wakati hakuna atazamaye
Ukamilifu ni usimamapo mbele ya Mungu na kumsikiliza akisema
“hongera mwanangu”
Hebu ishi maisha yako kwa Ukamilifu
Huduma Ya Barry Wood barrywoodministries.org
4
5
6
7
MUDA WA FARAGHA NA MUNGU
Mtu, kwa hakika, ni jinsi alivyo peke yake faraghani na Mungu. Ili uwe kamili mwenyewe na kwa
wengine, ni lazima uwe na muda wa kuwa na Mungu kila siku. Mojawapo ya yale tunayofundisha
aliyeamini kwa mara ya kwanza ni kutenga wakati kila siku wa kuwa na Mungu, bila kubadilisha muda
huo. Wanathiologia wa kale waliuita “Wakati wa Ukimya.” Nafikiri kwamba hayo maneno yanaeleza
wakati huo vizuri. Je, una “Wakati wa Ukimya” kila siku? Kama sivyo, basi ni kwa nini? Ni vigumu sana
kuwa mkristo katika umati wa watu kabla kuwa mkristo faraghani. Tabia yako mbele za watu huonyesha
jinsi wakati wako na Mungu ulivyo. Ili kukua kiroho, kila muumini ni lazima ajenge maisha yake kwa
muda wa faragha na Mungu.
Muda
Ni muda upi unaofaa kuwa na Mungu? Ikiwa wewe ni kama mfalme Daudi, basi kutana na Mungu kabla
kuanza siku yako. Daudi alisema, “Asubuhi, Ewe Bwana waisikiliza sauti yangu; asubuhi naweka mahitaji
yangu mbele yako…” Hili ni shauri nzuri. Bwana Yesu alikutana na Mungu kabla kuanza siku yake. “Hata
alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko”
(Marko 1:35). Naona kwamba kama ilimbidi Yesu kuchukua muda kuwa na Baba yake kabla kukumbana
na siku iliyojaa mambo mengi, mbona tusifanye hivyo? Sijali utafanya vipi, lakini fanya! Katika ratiba
yako ya siku, weka wakati wa kuwa na Mungu katika nafasi ya kwanza.
Mahali
Yesu alienda mahali pa siri, kwa sababu alihitaji kuwa peke yake. Wewe pia wahitaji kufanya hivyo. Je,
una mahali ambapo umetenga pa kusoma Bibilia yako na kuomba kila siku? Je, ni mahali pa faragha
ambapo unaweza kuomba kwa sauti bila kuwaamsha wengine? Ni kweli, maombi yana maana sana
unapotenga wakati wa kuwa na Mungu. Masikio yako yanahitaji kusikia hisia za moyo wako. Kupaaza
sauti kwa Mungu ni ishara ya mawasiliano kati ya mwenye dhambi na Baba yake aliyejawa na huruma. Je,
unahitaji nini unapokutana na Mungu mahali ulipotenga? Unahitaji:
• Bibilia yako
• Daftari
• Kalamu
• Kitabu cha ibada (Devotional book)
• Kitabu cha kuandikia matukio ya kila siku (Journal for Daily accoutability)
Kujitoa
Itakubidi kuweka ahadi kati yako na Mungu kwamba utakutana naye kila asubuhi mahali fulani kwa muda
fulani. Hebu fanya ahadi ya juma moja. Zingatia ahadi hiyo kwa kukutana naye. Labda utakuwa na wakati
mzuri hata utamani kuendelea zaidi. Tahadhari! Shetani atakupinga. Atakuruhusu kwenda kanisani, kuimba
katika kundi la waimbaji, na kufundisha katika darasa. Lakini shetani hutetemeka anapoona mtu mnyonge
aliyetakaswa akiomba kwa magoti . Umtarajie kuleta mambo ya kuondoa mawazo yako kutoka kwa kuwa
na muda wa faragha na Mungu! Anachukia na kuogopa muda wa faragha wa muumini kuwa na Mungu.
Taratibu
Baada ya kutenga nyakati za kukutana na Mungu, na kuwa na vifaa unavyohitaji, utafanayaje? Unaweza:
• Kuanza kwa maombi ya dakika nne
A=Adoration, ni kumsujudu Mungu. Anza kumsifu kwa nukta 60.
C=Confession, ni kutubu dhambi. Tubu kwa nukta 60.
T=Thanksgiving, ni kutoa shukurani. Msifu Bwana kwa baraka zako kwa nukta 60.
S=Supplication, ni kuombea wengine. Ombea wengine kwa nukta 60.
• Chagua somo katika maandiko.
Soma somo hilo kwa juma hilo lote. Anza na somo rahisi, kama vile Zaburi sura ya 1.
• Soma, chunguza, tafakari, na kutia katika akili.
8
Tumia daftari yako kuandika mawazo na maneno yenye maana. Mwombe Roho Mtakatifu
akufunulie ukweli. Katika daftari yako, tenga sehemu ya maswahil kama vile: “Hii inamaanisha
Mungu angependa nifanyeje?” Kufanya hivyo ni kuzingatia maandiko kibinafsi.
• Andika yale Baba anakuambia
Kila siku tumia daftari kuandika yale Mungu anakunenea kutoka kwa neno lake. Hii ni daftari
yako ya siri ambayo itaonyesha kukua kwako, vita vyako, na ushindi unayopata. Kutokana nalo,
labda utahitaji kuwazia wazo moja tu kila siku. Linaweza kuwa wazo kama vile, “leo nitaamini
kwamba Yesu ananipenda kwa vyo vyote vile.”
• Zingatia wazo hilo.
Andika wazo hilo katika kijikaratasi na kulitazama mchana kutwa. Kufanya hivyo ni kutafakari
maandiko.
• Tia akilini kifungu kimoja au vifungu viwili katika juma hilo.
Zaburi 1 ni fupi sana, kwamba unaweza kuliweka akilini ukichagua kufanya hivyo.
• Funga wakati huo kwa maombi.
Jiombee, na uombe mwongozo wa Mungu kwa shughuli za siku hiyo. Omba maombi ya Yabesi,
inayopatikana katika 1 Mambo Ya Nyakati 4:9. Hii ni jinsi nzuri ya kuanza siku yako.
9
DAKIKA NNE NA MUNGU KATIKA MAOMBI
Mombi si rahisi kwa wanaoomba kwa mara ya kwanza. Kila muumini kwa mara ya kwanza hung’ang’ana
katika kujua jinsi ya kuomba. Yesu, kwa mfano alitoa wa maombi (Sala ya Bwana) alitufundisha jinsi ya
kumwendea Baba katika maombi. Tunaweza kufuata mtindo huo katika maombi yetu.
Katika Luka 11:1-4 Yesu alitufundisha hivi:
1. Anza maombi yako kwa KUMSUJUDU Mungu
“Baba yetu uliye Mbinguni, jina lako litukuzwe…”
Tukaribie kiti cha enzi cha Mungu kwa kusifu na kusujudu. Katika kuanza maombi yako,
usiwakilishe hoja zako. Msifu tu kwa jinsi alivyo. Anza kumsujudu kwa kumwambia jinsi
unavyompenda na kumsujudu. Maandiko yamejaa majina ya Mungu ya ajabu. Unaweza kumsifu
kwa kutaja tu majina yake, ama kwa kusema tu, “Nakupenda Bwana kwa kuwa wewe u Bwana
mwenye mapenzi katika maisha yangu.” Hebu chukua dakika moja kumsujudu Baba yetu aliye
Mbinguni.
II. Endelea kwa KUTUBU
Yesu alitufundisha kuomba msamaha. “Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe
kila tumwiaye.” Tunapoanza kwa kumsujudu, yaani kumwona Mungu jinsi alivyo, tunaweza
kuona jinsi tulivyo. Kisha tutubu dhambi zetu tukifahamu kwamba katika Kristo hakuna hukumu.
Tutadai ahadi inayopatikana katika 1 Yohana 1:9 kwamba, “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni
mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.”
Hebu chukua dakika moja kutubu dhambi zozote unazojua.
III. MSHUKURU Mungu kwa Neema na Rehema zake
Shukuru katika kila ombi. Chukua muda wa kumwambia Mungu unavyofurahia baraka zake.
Hebu chukua kama dakika moja hivi kusema, “ahsante” Yesu kwa wema wako kwangu.
IV. Sasa OMBEA Wengine
Kuna rafiki zako, na wengine ambao wanahitaji maombi yako. Unahitaji kuwa mwombezi
kwa niaba ya wengine mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Hebu chukua dakika moja kuombea
wengine.
ACTS=Dakika 4 na Mungu
A=Adoration =Kusujudu
C=Confession =Kutubu
T=Thanksgiving =Kushukuru
S=Supplication =Kuombea mahitaji
Herufi hizi katika neno “ACTS” ni jinsi rahisi ya kufundisha mkristo mchanga jinsi ya kuomba. Dakika
moja kwa maombi, kutubu, kushukuru, na kuombea wengine. Unaweza kutumia jumla ya dakika 4 kwa
kufanya hayo yote. Hi ni jinsi bora ya kuanza maisha ya maombi.
10
11
KANUNI ZA MAVUNO YA KIROHO
“Bwana tunahitaji kumwona Yesu”
Yohana 12:20-25 “Chembe cha ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke
yake…”
Watu wengine wameita maneno haya ya Yesu Kanuni za Mavuna ya Kiroho. Wewe na mimi hatuwezi
kuleta tofauti katika ulimwengu huu hadi tutakapoelewa kanuni hizi za kuvuna kiroho, na kuishi maisha
hayo kila siku.
Ukweli #1 Lazima mbegu liwe mchangani ili liweze kuzaa matunda.
Ili kuishi maisha ya ufalme wa Mungu, unahitaji kuwa kama mbegu = ulizaliwa ili uzae. Sisi ni
mbegu iliyopandwa katika udongo wa watu wengine.
1. Yesu alikuwa akinena kuhusu yeye mwenyewe, Warumi 8:29
2. Yesu alikuwa akieleza juu ya wafuasi wake.
Ukweli #2 Mbegu hufa ili kutoa uhai
Katika kuishi maisha ya ufalme wa Mungu, kifo huzalisha uhai, (fungu la 24).
1. Yesu anaongea juu yake mwenyewe, “Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu.”
2. Yesu anaeleza juu ya maisha ya wafuasi wake. Luka 9:23
Tunapokufa kwa ubinafsi wetu na tamaa za kibinafsi ndipo tutakapoweza kuwapa wengine uhai.
Ukweli#3 Ili Lizae, Mbegu Lazima liwe nzuri.
Katika maisha haya ya ufalme wa Mungu, ubora ni wa maana kuliko wingi = swaala si ulichonacho, bali u
wa nani.
1. Yesu ananena juu yake = wingi na uzuri wa tunda hutegemea ubora wa mbegu.
2. Yesu anaeleza kuhusu wafuasi wake, “Yote ufanyayo, fanya kwa utukufu wa Mungu.”
3. Kuwa na muda wa kutosha na:
• Mkeo au mumeo
• watoto wako
• rafiki zako
Ukweli#4 Mbegu ina wakati wake
Katika kuishi maisha ya Ufalme wa Mungu, kanuni si muda utakaoishi, bali ni vipi utakavyoishi vyema
“Saa imewadia…”
1. Yesu ananena juu yake mwenyewe; alijua kifo chake kiliwadia.
2. Yesu alikuwa akinena kuhusu wafuasi wake “aliyepewa nyingi, nyingi itahitajika kutoka
kwake” “Utafuteni kwanza ufalme wake…” Mathayo 6:33; Yohana 15:5&8
Tamatisho: “Bwana, tunahitaji kumwona Yesu.”
12
13
KAZI SABA ZA ROHO MTAKATIFU
Katika maandiko, kuna kazi saba ambazo zimeelezwa kama kazi ambazo Roho Mtakatifu anafanya katika
maisha ya aliyezaliwa mara ya pili. Kazi hizi si tofauti kamwe, bali zinaeleza hali mbalimbali za tukio
moja. Kazi hizi ni kama zifuatazo:
Roho Mtakatifu kukaa ndani, Yohana 14:17
Ubatizo wa Roho Mtakatifu, Waefeso 4:4,5
Kutiwa muhuri na Roho Mtakatifu, Waefeso 1:13
Amana ya Roho Mtakatifu, Waefeso 1:14
Karama za Roho Mtakatifu, Warumi 12:6-13, 1 Korintho 14, Waefeso 4:7-11
Kujazwa na Roho Mtakatifu, Waefeso 5:18
Upako wa Roho Mtakatifu, 1 Yohana 2:27
Sita Zilikuwa Karama Wakati wa Kuzaliwa
Watu wengi wamejadiliana na kuhitilafiana kuhusu jambo hili. Lakini wataalamu wengi wa Bibilia
wanakubaliana kwamba kazi hizi zote za Roho Mtakatifu, isipokuwa moja, zinatendeka wakati mtu
anapookoka. Mtu anampokea Kristo kama Mwokozi, na anazaliwa kutoka juu katika Roho Wake. Roho
huyo anakaa ndani yake. Mtu huyo anabatiza katika mwili wa Kristo. Anapewa vipawa na huyo Roho
Mtakatifu. Kisha anajazwa naye, na kutiwa muhuri milele, ambayo ni amana ya wokovu wetu. Ni ajabu
mno kuwa mwana wa Mungu! Ni tendo, na mabadiliko ya ajabu sana.
Tunavuja
Kwa hivyo kila muumini amewahi kujazwa na Roho angaa mara moja. Mtu anapozaliwa upya, anajawa na
Yesu. Shida zetu ni kwamba mara nyingi tunavuja kama mpira ya gurudumu iliyozeeka. Hatuendelei kuishi
kama tumejazwa. Tunaweza kuzima Roho kwa kukosa kutii. Hii ndio sababu Paulo aliwahimiza Waefeso
“kuendelea kujazwa kila siku,” Waefeso 5:18. Hebu tazama kwamba tumetilia mkazo neno “kuendelea,”
ambayo ni hali ya kufanya fanya. Kuishi maisha yanayoongozwa na Kristo kunatokana na kujitoa kwetu
kabisa kwa Kristo kila wakati, na kila siku.
Maisha Ya Kawaida Ya Kikristo
Kujazwa kwa Roho si kazi ya pili, au hata kazi ya “ndani” ya Mungu ndani yetu. Kujazwa Ni maisha ya
kikristo. Kristo pekee ndiye “Mkristo.” Ni maisha yake tu ndani yetu ambayo yanaweza kusababisha tuishi
maisha ambayo yanampendeza Mungu Baba. Anapotujaza, tutaanza kuona tunda ambalo Paulo aliandika
katika Wagalatia sura ya tano. Tunda la Roho ni tabia ya Yesu, ambayo inadhihirika katika mwenendo
wetu. Mungu anahitaji kila mwana wake atembee katika Roho, akiwa amejazwa na maisha ya mwanawe
Yesu Kristo. Maisha yaliyojawa na Roho Mtakatifu ni maisha ya kawaida ya mkristo. Wazo tofauti na hili
halifai.
Upako
Hii inatufikisha kwa kazi ya saba ya Roho Mtakatifu ndani yetu. Kazi za kwanza tano ni kazi
zilizokamilika ndani ya muumini. Kazi ya sita ilianza katika wokovu, na inastahili kuwa kazi ya kila siku,
(kujazwa kunategemea utiifu wetu na kujitoa kwetu mhanga kwa uwepo wa Roho Mtakatifu). Kazi ya saba
ya Roho Mtakatifu ni kuleta upako. Yohana Mtume alisema, “Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake
yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha
habari za mambo yote…” 1 Yohana 2:27. Kuwekwa wakfu kunaonekana kuwa tendo la Roho Mtakatifu
ambalo ni maalum na la kipekee kwa wanaume na wanawake wachache waliochaguliwa.
Upako katika Maandiko
Kama vile kujazwa na Roho huleta utakatifu na kuishi kama Kristo, upako wa Roho Mtakatifu huleta
uwezo wa kumtumikia Mungu. Hakuwezi kuwa na upako bila kuwa na ujazo wa Roho Mtakatifu. Kujazwa
na kujitoa mhanga kwa Mungu hutangulia upako. Tunapotazama Agano la Kale, tunaona upako wa Mungu
mara kwa mara kwa wale ambao aliwachagua.
14
• Aliweka wakfu wafalme fulani, kame vile Sauli na Daudi.
• Aliweka wakfu manabii, kama vile Eliya na Elisha.
• Aliweka Samsoni wakfu.
Tunasoma mara kwa mara jinsi Roho wa Yehovah Mungu “alikuja juu yao.” Halafu kwa sababu fulani
Roho angewaacha tena. Kuna sababu mbili zilizosababisha huku kuachwa na Roho : 1) kazi aliyowaitia
ilikuwa imekamilika, au 2) aliyewekwa wakfu alitenda dhambi fulani, na upako ukamwondoka.
Katika Agano Jipya, tunasoma kuhusu Yesu, “Roho wa Bwana yu juu yanga, kwa maana amenitia mafuta
kuwahubiri maskini habari njema…” (tazama Luka 4:18,19), akiwa anakariri Isaya 61. Hata Paulo
alitambua upako uliokuwa juu yake. Anaeleza kuhubiri kwake kuwa “kwa dalili za Roho na za nguvu” (1
Wakorintho 2:4).
Watumishi Waliokuwa na Upako
Unaposoma kuhusu watu shupavu katika kanisa, utaona mara nying wakitaja haja ya kuwa na upako wa
Mungu. Waling’ang’ana kuhudumu katika nguvu zao wenyewe, hadi wakafikia wakati ambapo walikosa
nguvu. Ndipo wakaona haja ya kuwa na nguvu za Roho Mtakatifu.
Dwight L. Moody, Mmarekani aliyekuwa na kipawa cha kuhubiri, na aliyeishi zaidi ya miaka 100 iliyopita,
aliandika akisema, “Katika mitaa ya Chikago, nilijazwa na Roho Mtakatifu kwa wingi hadi nikamwomba
Mungu kuzidisha mkono wake juu yangu. Nilijawa na wingi wa wema wake, nikahisi kuweka ulimwengu
wote moyoni mwangu. Nikahubiri mahubiri ambayo nilikuwa nimekwisha hubiri zamani, ijapokuwa
yalikuwa yamekosa nguvu. Mahubiri hayo yalikuwa kweli kama nilivyohubiri hapo awali, isipokuwa tu
yalikuwa na nguvu mpya. Wengi walivutwa na kuokoka. Hii ilitendeka miaka mingi baada ya kuokoka
kwangu.
Charles G. Finney, aliyeishi katika karne ya 19 alipata tukio kama hilo la Roho Mtakatifu, ambaye
alimweka wakfu na kumpa uwezo miaka mingi baada ya kuanzisha huduma yake. Anaeleza tukio hilo hivi:
“Nilipogeuka na kujaribu kuketi karibu na moto, nilibatizwa na Roho Mtakatifu kwa njia ya ajabu bila
kutarajia. Sikufikiri kungekuwa na kitu kama hicho kwangu, wala sikukumbuka kama nimewahi kusikia
kuhusu jambo hilo kutoka kwa mtu yeyote uliwenguni. Roho Mtakatifu alinijia, na kuonyesha dalili kama
kupenya kwa mwili wangu na nafsi yangu.” Anasema matokeo ya kujazwa kwake ilionekana siku
iliyofuata, kwani yeyote aliyenena naye alihisi kuwa na hatia, ama aliokoka. Jioni, siku iliyofuata, Finney
alimkaribisha kafiri mmoja kwa nyumba yake kwa chakula cha jioni. Alipokuwa akiombea na kubariki
chakula, yule kafiri akaokoka! Hii ni thibitisho ya upako wa Roho Mtakatifu.
Billy Graham
Waweza kuelezaje kuhusu huduma shupavu ya Billy Graham? Ujumbe wake ni rahisi, isiyo ya kuvutia, na
ustadi. Lakini matokeo katika mikutano yake yanatokana na upako ulio juu yake. Mungu alimchagua na
kumwezesha kuhubiri injili rahisi.
Je, Una upako Huu?
Kila muumini anaweza kuwa na upako maalum ili kufanya huduma ya Ufalme wa Mungu. Ndiyo,
tunaweza. Kwa kuwa Bibilia inasema kwamba tuna upako huu (1 Yohana 2:27), kwa nini hatuuoni mara
kwa mara? Swali la kufaa linastahili kuwa hivi: Je, una upako huu katika maisha yako na katika uongozi
wako? Je, ushuhuda na ushahidi wako ni mpya? Je, Watu wanapokutana nawe, maisha yao hubadilishwa?
Huu upako kwa ajili ya huduma si wa kudumu. Katika Matendo ya Mitume, wanafunzi walijazwa Roho
wakati wa Pentekote (Matendo 2:4) ili wahubiri. Katika sura ya nne, tunawaona tena katika chumba cha
juu wakiomba Roho awajaze zaidi, na kuwapa ujasiri wa kushinda adui zao (Matendo 4:31). Petero
alikuwepo, na akajazwa nyakati hizo mbili. Hii inanijulisha kwamba katika kila kazi ambayo Mungu
anatuitia, tunahitaji kujazwa upya ili tutekeleze kazi hiyo ya Mungu. Swali ni, “Je, nina upako huu
maishani mwangu sasa?”
15
Ngojea, Subiri, Pokea
Katika Luka 24:49, Yesu aliwaambia wafuasi wake wafanye mambo haya matatu akiisha kuwaacha na
kwenda mbinguni:
1. Wangoje hadi wapokee nguvu za Roho Mtakatifu
2. Wadumu katika maombi wangojapo. Hii ilikuwa kwa ajili ya utakaso, kujisalimisha, na
kunyenyekezwa.
3. Wapokee Roho Mtakatifu, na huduma zake saba. Walitii wakingoja, wakiwa na subira, na
wakapokea nguvu za ajabu za Roho Mtakatifu.
Viongozi wa siku hizi ni tofauti kabisa! Tunaweza kupanga ratiba, bila kuwa na mzigo. Tunaweza kupanga
na kujitayarisha, lakini tunajua kidogo sana kuhusu kungoja na kuitisha upako wa Roho Mtakatifu. Mara
nyingi hatuoni matokeo ambayo wafuasi wa kwanza waliona.
Siri ya Upako Wa Roho Mtakatifu ni ipi?
Hebu tutazame jinsi tunavyoweza kuwa na upako huu katika huduma zetu. Hatua zinazohitajika si za
kimazingaombwe. Ikiwa wewe ni kiongozi aliyejiachilia mhanga, na kujazwa na Roho Mtakatifu, basi
hatua hizi zitakuwa na matokeo mara moja. Mungu anataka kuweka upako katika vipawa vyako, na mwito
wako zaidi ya matarajio yako. Hii ni sehemu ya shida yetu.
1. Lazima uwe na shauku na kiu ya nguvu za Roho Mtaktifu katika maisha yako. Isaya 44:3 “Kwa
maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pa kavu.
NitamwagaRoho yangu …”
Mathayo 5:6, “Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa.”
Yeremia 29:13, “Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.
Nami nitaonekana kwena, asema BWANA.”
Je, unakumbuka wakati Yakobo alimenyana na malaika wa Bwana? Yakobo aling’ang’ana akitamani
msamaha na baraka. Alimwambia malaika, “sitakuachilia hadi unibariki.” Huyu, kwa kweli, ni malaika
duni wa aina gani? Hata hawezi kujiondoa kwa mikona ya Yakobo? Kuna kitu ambacho si sahihi
kabisa katika hadithi hii. Nahisi kwamba mng’ang’ano huo ulipangwa tangu mwanzo. Mungu alihitaji
Yakobo ang’ang’ane na kutafuta baraka. Mungu alitamani sana kumpa hizo baraka kuliko
alivyotarajia.
Shida ya kiongozi wa kawaida katika maisha ya kikristo ni ubinafsi, na kujitosheleza. Basi hatuwezi
kuwa na upako wa Roho Mtakatifu hadi tunyenyekee na kutamani tu yale ambayo Mungu anaweza
kutupatia.
2. Lazima kuwe na Maombi ya Ushindi
Ikiwa tunahitaji kujazwa na nguvu, basi itatulazimu kuomba ili tuupate, kame vile wanafunzi kabla ya
pentekote, walivyoomba. Yesu alisema, “Hamna kwa sababu hamwombi.” Watakatifu wote wa Mungu
walitaabika, na kushinda katika maombi hadi wakapokea nguvu. Katika Matendo 4:31 tunasoma hivi:
“Hata walipokwisha kumwomba Mungu, wote wakajawa na Roho Mtakatifu.” Moody, Finney na R.
A. Torry wanaeleza jinsi walivyoomba kwa masaa mengi mbele ya kiti cha enzi, wakitafuta upako
mpya ili waweze kuhudumu.
Chanzo cha Nguvu
Miaka mingi zilizopita, Billy Graham alipokuwa angali kijana ambaye alikuwa mchanga katika huduma
yake ya kwenda katika miji mikubwa kuhubiri kwa mikutano ya hadhara, alizuru katika jiji la Fort Worth,
Texas. Mwanafunzi mmoja kijana kutoka katika chuo kikuu cha Southwestern Baptist Theological
Seminary alimwendea katika hoteli alimokuwa akilala kwa wakati huo alipokuwa na mikutano ya hadhara.
Alibisha mlangoni mwa hoteli hiyo. Cliff Barrows, aliyenieleza kisa hiki, alifungua mlango na
kumwambia yule mwanafunzi hivi, “Billy ana shughuli sasa hivi, na hataki kusumbuliwa.” Yule
16
mwanafunzi alikataa kuondoka, na kusisitiza kwa kusema, “Nahitaji kujua chanzo cha nguvu za Billy
Graham. Mbona Mungu anamtumia sana kwa njia ya ajabu?” Cliff alimpeleka kwenye mlango wa chumba
cha kulala na kuufungua kwa utaratibu, ili kumwonyesha siri ya Billy Graham. Alimwona Billy amelala
kifudifudi kwenye sakafu, akiwa na uchungu katika maombi. Cliff Barrows alifunga mlango na
kumwambia yule mwanafunzi, “Basi hiyo ni siri yake. Yeye hufanya hivi kila siku kwa masaa mengi kwa
wakati moja.”
Si Kwa Kumwombaomba Mungu
Tuelewe kwamba tunapokuwa na njaa kali na kiu ya upako, basi kazi itakuwa imetekelezwa ndani yetu
tayari. Si lazima tumsihi Mungu atupe upako. Yu tayari tukiwa tayari. Kuomba kwa ushindi ni kutayarisha
nafsi ili ipokee yale ambayo Mungu ametayarisha kutupatia. Tumngojeapo tu kwa maombi ndipo atakuwa
tayari kunena nasi, kutayarisha mioyo yetu, na kututayarisha kiroho kupokea nguvu zake za ajabu. Baada
ya kujazwa, tunapata upako!
3. Sharti kuwe Na Matarajio katika Imani
Baada ya kungoja na kuomba, lazima kuwe na imani kwamba upako utafuata. Hapa
tunaawajibika kutofautisha kati ya maisha ya kawaida yaliyojazwa na Roho Mtakatifu,
ambayo yanategemea mtu kujisalimisha kwa Kristo na kuwa na imani (bila kudumu kwa
maombi isipokuwa tu kwa kutayarisha moyo), na upako wa Roho Mtakatifu unaorudiwa mara
kwa mara tunapodumu katika maombi. Neno la maana katika huku kujazwa upya kila mara ni
“hadi.” Yesu, kabla kuondoka ulimwenguni, aliambia wanafunzi wake wadumu “hadi”
wapokee nguvu. Walifanya hivyo, na wakapata nguvu! Mungu lazima afahamu kwamba
tunamwamini, na kwamba anaweza kututegemea kumpa utukufu. Akiona tukiwa hali hiyo,
basi tutapata nguvu. Je, unaweza kulipa gharama yoyote inayohitajika ili akutumie? Kama ni
hivyo, basi amini na kuomba hadi upate upako.
Matokeo ya Upako Ni yapi?
Unawezaje kujua kwamba Mungu amejibu maombi yako? Matokeo ni wazi:
• Utakuwa na ushindi dhidi ya dhambi maishani mwako.
• Kutakuwa na tunda la Roho maishani mwako.
• Utakuwa na mzigo moyoni kwa waliopotea.
• Huduma yako kwa Mungu itakuwa yenye nguvu.
17
YABESI: KUISHI KATIKA NJIA YA BARAKA
Mungu angependa kutubariki kuliko tunavyokusudia. Huu ni ukweli wa maandiko. Kuna mito ya baraka
kutoka kwa moyo wa Mungu uliojaa upendo. Tunasoma kuhusu maombi ya mtu mmoja aliyeamini jambo
hili katika Agano La Kale. Jina lake ni Yabesi. Tunasoma maombi yake katika 1 Mambo ya Nyakati 4:9,
“Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema,
Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni.”
Kuna mambo matatu ya ajabu kuhusu huyu mtu aliyeitwa “Uchungu” (Yabesi). Kwanza, unaposoma kitabu
hiki cha Mambo ya Nyakati wa Kwanza, utaona kwamba hakuna kitu cha kuvutia katika sura nne za
kwanza. Zinaorodhesha vizazi, aya hadi aya, utadhani unasoma katika kitabu cha anwani! Kati ya hayo
yote tunaona kifungu hiki chenye busara, “Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze.” Ni
kama amekugutusha mara tu!
Kitu cha pili cha ajabu ni jina lake la kuchekesha. Maana ya Yabesi ni “Uchungu,” au “kuumwa.” Labda
mama yake alimwanzisha jina hilo kwa sababu alimzaa kwa uchungu. Salala! Katika maisha yako, kila
wakati mama akiita jina lako unakumbushwa jinsi unavyompa uchungu!
Basi, tunaona ujumbe gani kutokana na huyu Yabesi? Ni wazi kwamba Roho Mtakatifu angependa
tujifunze kutokana na huyu ambaye ni tofauti, katika orodha ya vizazi.
Yabesi alikuwa Mtu wa Kawaida
Alizaliwa katika uchungu, na akaishi maisha yake kwa shida nyingi. Kitu ambacho ni tofauti kuhusu
maisha yake tu ni uhusiano wake na Mungu. Je, unaona hali yako kuwa sawa na yake? Tunaweza kuwa
watu wa maana ikiwa tutakuwa wenye maana kwa Baba yetu aliye mbinguni. Haijalishi ulianza maisha
yako vipi, unaweza kuishi katika wema wa Mungu na kuwa katika njia ya baraka zake.
Yabesi Alikuwa Mtu wa Heshima
Alikuwa mtu wa heshima kuliko nduguze. Je, hii yamaanisha kwamba alikuwa mwenye heshima kuliko
vizazi vilivyomtangulia, au inamaanisha kwamba aliheshimika kuliko hata jamii na kabila lake? Kwa kweli
haya hayajalishi! Aliheshimika kwa Mungu kiasi cha kuomba abarikiwe, naye akajibiwa.
Je, hali yako vipi? Je, wewe ni mtu unayeweza kubarikiwa na Mungu kwa kweli? Yabesi hakuomba tu
abarikiwe, bali aliomba abarikiwe “kweli kweli.” Aliomba Mungu ambariki vilivyo! Watu wengine
wameona ombi hili kuwa ombi lenye ubinafsi sana, au yenye kutaka vitu tu. Sivyo kamwe! Alikuwa mtu
wa heshima. Mtu wa heshima anawezaje kuomba ombi lililokosa heshima, kisha Mungu akamjibu?
Funzo kwetu ni kwamba “macho ya Mungu hutazama huku na kule” kama anaweza kuona mwanamume au
mwanamke mwadilifu, ili ambariki. Tunajifunza kwamba kutii hufungua milango ya baraka na wema
kutoka kwa Mungu. Anatupenda sote bila sababu. Lakini ametenga mahali maalum katika roho yake kwa
wanaume na wanawake walio na heshima.
Kila mtu hawezi kuwa na akili, mali, jamii bora, au urembo wa umbo. Lakini la maana zaidi ni kuwa na
heshima kwa Mungu. Lililo la manufaa zaidi ni jinsi Mungu akuonavyo.
Yabesi Aliomba Ombi Lisilo La Kawaida Kabisa!
Hebu sikiliza kwa makini sehemu nne katika maombi yake:
1. “Lau kwamba ungenibariki kweli kweli,
18
2. na kunizidishia hozi yangu,
3. na mkono wako ungekuwa pamoja nami,
4. nawe ungenilinda na uovu…” (1 Mambo Ya Nyakati 4:10).
Hebu tazama sehemu hizi nne katika maombi yake:
1. “Ungenibariki kweli kweli …”
Kwa watu wengine, wazo hili ni wazo lenye choyo. Mbona? Wazo tu la kumwomba Mungu
ambariki ni wazo la kujipenda nafsi. Licha ya hayo, Yabesi ni mtu wa heshima. Kwa sababu ni mtu wa
heshima, aliona amwombe Mungu amwongeze zaidi.
Je, umewahi kuhisi kuwa karibu sana na Mungu, hata ukamwomba akubariki vilivyo?
Ombi hili linahusu uhusiano wa mtu na Mungu. Anamwomba Mungu ambariki kwa kuwa anaelewa
moyo wa Mungu. Anaelewa kwamba Mungu ni Mungu wa kupeana baraka. Kwa kweli, tunaona hali
hii ya Mungu katika Luka 11:9-11. Yesu anatuambia tuombe, tutafute, na tubishe, na kwamba Baba
huwapa watoto wake vipawa vyema. Wewe nami hatupati kwa sababu hatuombi. Pia hatupati kwa
sababu tuna sababu ambazo hutufanya kuona hatufai kuomba Baba atubariki.
Kama huna baraka tele katika maisha yako, tutakujua zaidi kuliko tunavyomjua Mungu. Mtu mwenye
heshima huona uwezo wa kwenda kwa Mungu na kumwambia, “nibariki kweli kweli.”
2. “Unizidishie Hozi Yangu.”
Ombi hili ni zaidi ya kuomba kuongezeka kwa maeneo au mali ya kulisha kondoo. Yabesi alitamani
kuzidisha maongozi yake kwa Mungu, na kwa wema ulimwenguni. Alihitaji huduma nyingi, ili Mungu
apate utukufu zaidi. Katika enzi hizo, ni wale tu waliokuwa na shamba waliovutia wengi (Mithali 3:9-
10).
Hii si maombi iliojaa choyo kutoka kwa mtu aliye na tamaa ya pesa. Yu wazi kwa Mungu ili apanue
mipaka yake. Huyu ni mtu mwenye heshima anayeomba maombi ya heshima kutoka kwa Mfalme wa
walimwengu. Mara nyingi tunaomba kwa uchoyo kwamba tubarikiwe na vitu, kisha tunavitumia
vibaya katika kujinufaisha wenyewe (Yakobo 4:3).
Kila mfuasi wa Kristo anastahili kuomba ombi hili lenye heshima. “Mungu, nibariki kweli kweli, na
unizidishie na kupanua maongozi yangu, ili nami nikubariki pamoja na ufalme wako.”
Kuzidishiwa hozi kwangu kunamaanisha kuwa baba mwema, bwana mwema, rafiki mwema, shahidi
au mfuasi. Inaweza kumaanisha kuondoka katika ustaraabu ulioamua kupata, ili Mungu akuongoze
kwa uhusiano na baraka zitakazozidi maono yako. Kumbuka kwamba anayepewa zaidi, zaidi
itahitajika kutoka kwake. Ni vyema kabisa kumwomba Mungu akuzidishie maongozi yako.
3. “Mkono Wako Ungekuwa Pamoja Nami”
Hili ni ombi kwamba uwepo wa Mungu na nguvu za Mungu ziwe pamoja naye. Yabesi alihitaji kuhisi
uwepo na upako wa Mungu katika yote aliyotenda. Ni mtu wa heshima tu anayeweza kuomba maombi
haya. Kuomba mkono wa Mungu uwe pamoja nawe ni kujitolea kwa utumishi katika kazi ya Mungu.
Unahitaji nguvu za Mungu ili uweze kufanya kazi ya Mungu. Tunaweza kuomba kama Yabesi
kwamba mkono wake uwe juu yetu. Tunaweza kuhisi uwepo wake, na kusonga mbele katika nguvu
zake.
Kuomba maombi haya kutapunguza sana ufanyayo na uendako. Mkono wa Mungu kwa mwanadamu
yeyote inaogofya! Ni maisha tu iliyojitolea mhanga kwa mapenzi ya Mungu ambayo inaweza kubarikiwa
na nguvu na uwepo wa Mungu.
Jim Elliot, aliyeuawa kwa ajili ya imani yake, ni mmisheni aliyeandika katika kitabu chake cha matukio
maneno haya:
19
“Baba, Nifanye kuwa mtu matata,
Wafanye wale wanaokutana nami kuamua,
Nisiwe kama kibao cha kuonyesha watu njia,
Bali nifanye kuwa kama uma,
Ili watu wanaokutana nami wageukie njia moja au lingine, kwa kukutana na Kristo ndani yangu.”
Akiwa na moyo sawa na Yabesi, Jim Elliot aliomba mkono wa Mungu uwe pamoja naye.
4. “Nawe Ungenilinda na Uovu”
Yabesi, aliyezaliwa kwa uchungu na kuzoea kuishi katika uchungu anamwomba Mungu wa Baba zake
kumlinda na uovu. Mungu alijibu maombi yake! Sehemu ya mwisho katika ombi hili linalovutia ni
kulindwa kutokana na maovu na huzuni. Unaweza kuomba ombi hili kila siku kwa ajili yako na kwa
ajili ya wale unaowapenda. Ni maombi yanayoitisha ulinzi wa Mungu.
Petero, siku ile ya Pentekote, alinukuu Zaburi 16:11 aliposema, “Nalimwona Bwana mbele yangu siku
zote, kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kuume, nisitikisike” (Matendo 2:25). Kila mwana
wa Mungu atalindwa ikiwa atakuwa na imani ya kuomba ulinzi huo. Ana uwezo, na atakubariki na
ushindi dhidi ya yule mwovu.
Angalia basi sehemu hizi nne za maombi ya Yabesi:
1) Unibariki kweli kweli = ruzuku ya Mungu
2) Zidisha hozi yangu = makusudi ya Mungu
3) Mkono wako ungekuwa pamoja nami = uwepo na nguvu za Mungu
4) Ungenilinda na uovu = ulinzi wa Mungu
Hii ni changamoto tosha kwetu kutokana na neno la Mungu. Yabesi ametajwa kwa kifupi sana katika neno
la Mungu ili kututia motisha katika kudai baraka za Mungu maishani mwetu. Hebu tamani kuwa mtu
ambaye Mungu anaweza kubariki “kweli kweli.” Kila mara mwombe akupe uwezo, akulinde, akupe
mahitaji yako, na kupanua uongozi wako kwa utukufu wake.
20
21
KUISHI HURU KIFEDHA
Maandiko ya Mungu yanatupa kanuni za Mungu katika kuwa huru kifedha. Yesu, katika Mathayo 6:19-34,
alituonyesha jinsi tunavyoweza kuishi tukiwa huru kifedha. Mungu hapendelei tuishi kila mara
tukiwazawaza kuhusu fedha na kuishi.
“Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiweekeni
hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;
kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako…Hakuna mtu awezaye
kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana
na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.”
Maneno haya ya Kristo yanatuonyesha kwamba Baba yetu aliye mbinguni anatamani watoto wake waishi
wakiwa huru kwa mambo ya fedha. Hebu tuangalie maana ya maneno hayo. Kuwa huru kifedha
kunamaanisha nini?
Warumi 13:8 inaeleza wazi wazi kanuni hii: “Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa
maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.” Kanuni basi ni hii: Uko huru kifedha ikiwa jumla ya
mali yako ni zaidi kuliko deni ulizo nazo. Hivyo ni kuishi bila deni.
Kuna mambo matatu muhimu ambayo yanatuwezesha kuishi tukiwa huru kifedha:
Kutoa jinsi Bibilia inavyoeleza
Kupokea jinsi Bibilia inavyoeleza
Kutumia fedha jinsi Bibilia inavyoeleza
Tukiyatii mambo haya matatu yanayohusika na utoaji, upokeaji, na utumiaji, basi tutakuwa tumeshika njia
ya kubarikiwa na Mungu.
Kabla kuishi maisha yanayoambatana na kanuni hizi, ni lazima tuamini ukweli wa ndani uliyopo katika
Bibilia itakayowezesha kila mwana wa Mungu kuishi akiwa huru kifedha.
I. Mali YOTE Ya Walimwengu ni Mali ya Mungu, Baba Yetu
Zaburi 24:1 “Nchi, na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake.”
Zaburi 89:11 “Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako, Ulimwengu na vyote viujazavyo,
Ndiwe uliyeupiga msingi wake.”
Tunayoona katika haya mandiko ni kwamba mali yote ya walimwengu ni ya Mungu, nyakati zote.
Mali ya IBM, Siemens, General Motors, Microsoft, mafuta yote ya Waarabu, na mali ambayo
almashauri mbali mbali wanafikiri ni yao, kwa kweli ni ya Mungu!
Hata fedha zilizoko mifukoni mwako, na yale yaliyoko katika benki, na yote unayodhani kuwa
yako, kwa kweli si yako. Yote ni yake! Huu ndio ukweli ambao tunastahili kusadiki na kuelewa.
Ni ukweli kuhusu umilikaji wa mali. Hatumiliki chochote. YOTE ni mali ya Mungu.
II. Muumini wa Kweli Anao Urithi Pamoja na Mwana wa Mungu, Yesu Kristo.
Warumi 8:7 “Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu.” Je, unasikiliza ukweli huu?
Yote ya Yesu ni yako, kama mwana wa mfalme aliyenunuliwa kwa damu. Kwa kuwa yeye ni
damu ya kifalme, nasi ni watoto walioingizwa katika ufalme ule, basi tu warithi pamoja naye kwa
usawa! Ukweli huu ni wa ajabu.
22
III. Mungu Angependa Kutumia Vyote Alivyonavyo kwa Faida Yetu
Mwanzo 1;28 “Mungu akawabariki, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na
kuitiisha; mkatawale samaki wa bahari, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai
kiendacho juu ya nchi.”
Luka 11:9,10 “Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi
mtafunguliwa. Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye
atafunguliwa.”
Wafilipi 4:19 “Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake,
katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.”
Vifungu hivi vinajieleza. Mungu anapendezwa anapotoa na kutujaza kila tunachohitaji. Alitupatia
ulimwengu, na yaliyomo kwa faida yetu. Ni mkopo wake kwa watoto wake.
IV. Unapotoa, Utapokea.
Luka 6:38 “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa -
sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile
mpimacho ndicho mtakachopimiwa.” Hebu jifunze na kuweka kwa vitendo ukweli huu. Kupokea
kumeambatanishwa na kutoa. Je, unahitaji zaidi kutoka kwa Mungu? Basi jifunze kutoa ukiwa na
dhamira njema na moyo safi. Tazama Luka 6:34, 34, ambayo inatuonyesha nia katika kutoa.
Yesu anatufundisha wazi wazi, kati ya mbinu zingine za Mungu, mbinu moja ya upendo,.
Mbinu yenyewe ni kwamba unapotoa unapokea pia. Tena, kipimo unachotumia ndicho
utakachopimiwa. Mfano mzuri ni kwamba Mungu alitoa mwanawe wa pekee kwa ajili ya wengi,
na kupata wana wengi!
V. Kupokea kwako Kunategemea Kiwango Unachotumia katika Kutoa.
Luka 6:38 “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa -
sukwa hata kumwa gika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile
mpimacho ndicho mtakachopimiwa.”
Hebu tena tutilie mkazo uhusiano ulioko baina ya kutoa na kupokea. Sote tunataka zaidi ya
tunavyokusudia kutoa. Mungu anatamani utoe kwa ukarimu bila kufikiri kwamba utapata, ndipo
uweze kufanikiwa kifedha. Unaweza kutoa upendo, utu wema, msaada, au pesa. Mungu haoni
kufanikiwa kwako kuwa pesa au utajiri.
Mafanikio yako katika Mungu hupatikana:
1. Unapojazwa kila unachohitaji. Wafilipi 4:19
2. Unapokosa kuwa na deni. Warumi 13:8
3. Unapotoa kwa ukarimu kwa kusudi njema. Mathayo 5:42
Utafanikiwa ukiwa ma mambo haya matatu katika maisha yako! Utawezaje kufikia mahali
ambapo ukweli huu unadhihirika katika maisha yako? Hivi ndivyo unavyovweza kuishi kwa
mafanikio ukiwa ndani ya Mungu.
A. Amini kuwa Mungu ndiye chanzo cha mapato yako.
Je, mahitaji yako yanatimizwa kutoka wapi? Je, ni kutoka kwa kazi yako, au tajiri wako? Hiyo si kweli
kwa sababu kwa Wakristo Mungu ndiye tajiri! Yeye ndiye atimizaye mahitaji yetu.
Kumbukumbu La Torati 8:18 “Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu
za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.”
23
Je, ulipata hayo? Mungu ndiye hukupa nguvu za kupata utajiri. Mungu ndiye aliyekupa uwezo wa
kununua chakula ulichonunua leo. Kwa mara nyingine katika Wafilipi 4:19, tunaona kwamba Mungu
wetu ndiye atimizaye mahitaji yetu YOTE. Si mahitaji mengine tu; au utimize mengine, naye mengine.
Hapana. Yeye ndiye chanzo cha mapato yako. Amekukopesha tu. Hata ule uwezo wako wa kufanya
kazi na kupata ujira ni wake.
Katika Malaki 3:10,11, tunasoma, “Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba
yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha
ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu
nitamkemea alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha
matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi.” Angalia tena
kifungu cha 11. Mungu ameahidi “kumkemea yule alaye” kwa ajili yako. Atafanya hivyo ikiwa
tutaishi tukimtii. Mungu hatayatimiza tu mahitaji yako, bali atayafanya kudumu pia zaidi.
B. Uwe na nia ya kuwa tajiri kwa Mungu.
Je, unafanya kazi kwa kusudi gani? Una weka hazina zako wapi? Kristo ana jambo la kuwaambia wale
ambao hawaelewi utajiri. Katika mahubiri yake mlimani, Yesu alisema, “Msijiwekee hazina duniani,
nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba” (Mathayo 6:19).
Pia, katika Luka 12:21, Yesu alisema, “Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe
kwa Mungu.” Hebu angalia. Mtu huyu alijenga “ghala,” kisha akajenga “maghala makubwa.” Aliweka
moyo wake katika maghala yake! Alikuwa tajiri ulimwenguni, na fukara mbinguni. Hebu tuwe tajiri
kwa Mungu. Hapo ndipo pana utajiri. Kwa sababu Mungu ndiye mwenye utajiri wote, tunastahili
kutafuta kuwa tajiri machoni pake.
Kuna wangapi miongoni mwetu ambao hawangependa kuwa na uwezo mkubwa wa kununua? Nasema
kuhusu kuwa na uwezo wa kununua bila kupungukiwa. Jinsi ya kufanya hivyo ni kwa kumjua mwenye
kuweka hazina zako vizuri. Kuwa tajiri kwa Mungu ni kuweka hazina zako katika benki yake ya
milele, ambayo ni nambari moja. Hatuwezi kutoa fedha kutoka kwa benki ya mbinguni ikiwa
hatuhifadhi fedha zetu huko! Wawekao hazina zao mbinguni kila siku huweka amana katika benki ya
Mungu. Hao ni tajiri kwa Mungu, na hutembea katika njia ya kutimiziwa mahitaji yao. Ni wachache
sana watakaoweza kurudishwa “bila fedha zozote.” Unawezaje kuingiza hazina zako katika benki ya
Mungu ya Milele? Ametueleza jinsi ya kuwa tajiri ndani yake.
1. Heshimu Mali Yake Kwa Kutoa Fungu la Kumi. Malaki 3:10,11 “Leta zaka kamili ghalani, ili
kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkamjaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi;
mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagia baraka, isiwepo nafasi ya
kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu, nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi
yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika shamba,
asema BWANA wa majeshi.”
2. Unapotoa zaka, Mungu atakutendea mambo mawili.
1) Atakubariki kwa kufungua “madirisha ya mbinguni”
2) “Atamkemea yule alaye” kwa ajili yako
Nimesaidika sana katika kufikiria zaka hivi:
Yesu alitunza sheria za Musa
Yesu alikuwa mtoaji zaka
Yesu anaishi ndani yangu.
Ninapojazwa na Roho Mtakatifu, Yesu anatawala mali yangu, na kutoa zaka
akiwa ndani yangu.
24
Muumini asiyetoa fungu la kumi hastahili kumwomba Mungu fedha, kwa sababu yeye si tajiri
kwa Mungu.
Bill Gotherd alisema hivi wakati fulani, “Usipotoa fungu la kumi, Mungu atampa shetani nafasi ya
kuchukua fungu hilo.”
3. Jifunze kutoa kwa Ukarimu. Luka 6:38 “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa
na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa, hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani
mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho, ndicho mtakapopimiwa.”
Vifungu hivi vya Bibilia vinatuambia jinsi ya kutoa, ili tupate.
Tunastahili kutoa kwa jinsi tatu:
1) Tumtolee Mungu (zaka). Malaki 3:11
2) Tuwape wakristo wengine na kutoa kwa mambo ya staha. Warumi 12:13
3) Tuwape maskini. Mithali 19:17
Tumeelezwa nia inayofaa katika kutoa.
Wakorintho Wa Pili 9:6-8 “Lakini nasema hivi, apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa
ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni,
wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu
aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate
kuzidi sana katika tendo jema.”
4. Hebu jifunze kupokea
1) Pokea kwa kujitahidi katika kazi. Warumi 12:11 “Mkiwa na juhudi katika roho zenu;
mkimtumikia Bwana.”
2) Pokea kwa kuwa na uelekevu. Mithali 31
3) Pokea kupitia kwa kujibiwa maombi. Waebrania 11:6 “Lakini pasipo imani haiwezekani
kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na
kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.”
4) Usikope kile ambacho Mungu angependa kukupatia kupitia kwa maombi.
5) Mungu angependa wengine wabarikiwe kwa wnapotolea mahitaji yako.
5. Jifunze kutumia fedha zako Vile Bibilia Inavyotaka. Mathayo 6:19,20.
Unapotumia fedha zako vibaya, kuna mashahidi watatu. Yesu alitaja mashahidi hao katika
Mathayo sura ya 6. Ni kama wafuatao:
1) Nondo – Tunapotumia vibaya yale ambayo Mungu ametupa.
2) Kutu – Tunaponunua vitu ambavyo havidumu.
3) Wevi – Tunapokuwa na vitu vya thamani vinavyosababisha tamaa kwa watu wengine. Tuwe
na nia safi kwa asilimia 90 ya yale ambayo Mungu ametukabidhi. Tunchohitaji si pesa nyingi,
bali ni kusudi njema kwa yale tuliyo nayo.
Tuangalie sehemu tatu za kutumia fedha
1. Matumizi ya kila mara =makisio ya kila juma
2. Matumizi ya siku za usoni = kuweka akiba, malipo ya uzeeni, elimu
3. Matumizi ya raha = mambo ya kustarehesha
25
Unapoangalia jinsi hizi za matumizi, unastahili kuwa na lengo la kuepuka kuwa na deni.
Kanuni za Kuishi Bila Deni
1. Mungu anataka uondoke kwa Deni. Warumi 13:8
2. Usikope kwa vitu ambavyo haviwezi kudumu. Mathayo 6:34
3. Kukopa kwa mambo yajayo.
Kukopa kwa vitu ambavyo haviwezi kudumu ni kinyume cha maandiko Warumi 13:8
Unakuwa mfungwa unapokopa Mithali 2:7
Kukopa ni kubainisha kwa yajayo Yakobo 4:13-17
Unamzuia Mungu kukukinga na vitu vinavyoweza kukudhuru unapokopa
Kukopa kunamzuia Mungu kutimiza mahitaji yetu
Sifa za Mungu zinaweza kuharibika kwa sababu za kuwa na deni
4. Mungu anataka uwe huru kutokana na kupenda pesa 1 Timotheo 6:9
5. Mungu hataki uusike katika biashara mbaya. 2 Timotheo 2:4
6. Mungu anataka uwe huru kutokana na mawazo ya kuwa tajiri upesi
Kujifunza Maana Ya Utumizi Bora wa Fedha
• Kwa sababu Bibilia inafundisha hivyo
• Kwa sababu haina gharama
• Kwa sababu inazuia deni
• Kwa sababu itazuia kununua vitu bila mipango
• Kwa sababu utajifunza thamani ya pesa
• Kwa sababu utakuwa na hekima katika kununua vitu
• Kwa sababu unaponunua kwa pesa taslimu, utakuwa na amani akilini mwako
• Kwa sababu inamwezesha Mungu kututimizia mahitaji yako bila malipo
C. Unastawi kwa Mungu Unapojisalimisha kwa Mapenzi Yake
Katika Mathayo 5:5, Yesu aliahidi wote walio “wapole.” Alisema watauridhi nchi. Je, unaweza kuona
ahadi ya mali katika ahadi hiyo? Sisi tunaochagua kuwa wapole mbele yake Mungu na wanadamu
tutaurithi mali hapa duniani! Mfalme atakapokuja kuchukua benki yake kuu ulimwenguni, na maghala
yote ulimwenguni, sisi ambao ni wafuasi wapole tutapata thawabu yetu kutokana na nyara hizo. Hayo
ni baadaye. Lakini hii ni ahadi ya kila siku. Wapole wanaurithi nchi hivi leo. Baraka za Mungu ziko
juu yao. Wanaotafuta ufalme wa Mungu kwanza wanapata baraka kila siku kwa kuwekwa huru
kutokana na utumwa wa “vitu.”
Hii inamaanisha nini? Mungu anasema tuangalie yale yaliyo muhimu. Tii amri zake, yaani weka
matakwa yake kwanza maishani mwako na atakupatia urithi wako! Anasema “usiwazie juu ya kesho.
Kesho yako iko mikononi mwangu: nami nitaitunza.”
Je, una hofu kuhusu fedha? Ama ni kwa sababu umevunja kanuni mojawapo ya hizo? Mungu anataka
uwe huru kutokana na hofu juu ya ‘mali.’ Kujiachilia kwa mapenzi ya Mungu kutarithisha moyo wako.
Paulo, akiwa gerazani, alijifunza siri ya kurithika. Katika Wafilipi 4:12 anatuambia kwamba, “Najua
kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yoyote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa
kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi, na kupungukiwa.”
Anasema tena katika 1 Timotheo 6:8 “Ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo.”
Inashangaza kuona kwamba mtu aliyekuwa gerezani kingoja kifo chake kwa sababu ya imani yake
alihisi kuwa huru na kurithika.
26
Je, wahitaji hiyo amani? Walio na furaha zisizo na kifani ni wale walio tajiri kwa Mungu, na
wajisalimishao kwa matakwa yake. Wako huru kifedha.
Hebu kumbuka tulivyosema kuhusu kusitawi kibibilia:
1. Unapotimiziwa mahitaji yako yote.
2. Unapokosa kuwa na deni.
3. Unapotoa kwa kusudi njema
Ishi katika ustawi wa Mungu!
27
28
29
Kielelezo hiki ni kielelezo rahisi na muhimu. Kimetumiwa na The
Navigators kwa zaidi ya miaka hamsini. Huwasaidia wakristo
kufahamu mwito wao kama wanafunzi au wafuasi wa Kristo. Kila
kiungo cha kielelezo hiki kinawakilisha sehemu muhimi sana katika
maisha ya Kikristo.
Tumia kielelezo hiki katika kupata ufahamu muhimu wa adabu za
kiroho katika maisha yako ya Ukristo. Ni maeneo yapi yanayokutia
moyo? Ni maeneo yapi yanayokutia changamoto?
Unaweza kuchora “kielelezo cha gurudumu” juu ya kitambaa au
kipande cha karatasi na kumpa mtu unayemfanya kuwa mfuasi.
Wachochee ili wafikiri kwa makini juu ya kuwa wafuasi watiifu wa
Kristo.
Uhiari wa mwelekeo wako: Jinsi unavyohusiana na nafsi yako mwenyewe?
Utashi wako
Kitovu cha gurudumu (Hub) Kristo kiungamanishi
Tazama 2 wakorintho 5:17; Gal. 2:20
Kumfanya Kristo awe katikati ya maisha yako ni kitendo cha utashi
wako. Kujitoa kabisa ili Kristo awe mtawala na Bwana wa maisha
yako kunaweza kutendeka wakati wa kuokoka, au baada ya miezi
kadhaa, au hata miaka kadhaa baadaye. Mungu huweka ndani yako
hamu ya kufanya kile anachotaka ufanye ili aweke wazi ubwana wake
katika maisha yako.
Mzingo wa gurudumu: Utiifu kwa Kristo
Tazama Warumi 12:1; Yohana 14:12
Baadhi ya matendo ya utiifu kwa Mungu ni ya ndani. Lakini hata hayo
matendo ya utiifu kwa Mungu kwa ndani kama vile mielekeo, tabia,
nia, mawazo ya ndani, na mawazo ya siku kwa siku hatimaye
huonekana katika uhusiano na watu wengine. Kipimo cha upendo wako
kwa Mungu hudhihirishwa na utiifu wako kwake.
Kipimo cha wima: Jinsi unavyohusiana na Mungu
Taruma ya neno
Tazama 2 Timotheo 3:16; Yoshua 1:18
Mungu anaposema nawe kupitia kwa maandiko, unaweza kuona kanuni
zake za maisha na huduma. Utajifunza jinsi ya kutii, na kuzoeana na
Kristo ambaye unafaa kumtii na kumpa heshima isiyo na kifani. Jambo
la lazima kwa uzima wa mtu ni kupenya kwa Neno la Mungu ndani
yake kwa ajili ya afya yake na kukua kwake kiroho.
30
Taruma ya Maombi
Tazama Yohana 15:7;Wafilipi 4:6-7
Sala ni itikio la asili kwa Mungu unapomsikia akisema nawe katika Neno lake.
Ni kuushirikisha moyo wako kwa yule anayetamani ushirika wako, na
kujihusisha na mahitaji yako. Maombi hufungulia nguvu za Mungu katika vita
vyako vya kibinafsi, na kwa maisha ya wale unaowaombea.
Kipimo cha Mlalo: Unavyohusiana na Wengine
Taruma ya ushirikiano
Tazama Mathayo 18:20; Waebrania 10:24-25
Kujifunza kutoka kwa wengine na kuwatia moyo huleta mchanganyiko
unaopendeza Mungu. Mungu amewaelekeza Wakristo kuchocheana kwa njia ya
kutegemeana, na katika mahusiano
ya kupendana wenyewe kwa wenyewe.
Taruma ya Kushuhudia
Tazama Mathayo 4:19; Warumi 1:16.
Maisha yenye kububujika na kuvutia sana katika Kristo yanastahili kuwa
maisha yanayoonyesha wengine jinsi wanavyoweza kupata maisha kama hayo.
Mungu amewapa waamini heshima na wajibu wa kuufikia ulimwengu na
Habari Njema ya Kristo.
COPYRIGHT: THE NAVIGATORS, P.O. Box 6000, COLORADO SPRINGS, CO 80934 U.S.A
USED BY PERMISSION.
31
KIELELEZEO CHA MKONO
“Mkono wa Neno”
huonyesha jinsi tano za
kujifunza kutoka katika
Biblia.
Taratibu hizi zote zina
maana.
Kila aya imelingana na
tafsiri kadhaa za Bibilia.
Chagua tafsiri yoyote
inayokupendeza.
Sikia
Warumi 10:17. Basi
imani, chanzo chake ni
kusikia, na kusikia huja
kwa neno la Kristo.
Kusikia kutoka kwa Wachungaji na Waalimu wa neno la Mungu hutoa ufahamu kwa kujifunza maandiko.
Pia huzidisha hamu yako katika kufahamu neno la Mungu zaidi.
Soma
Ufunuo 1:3. Heri asomaye na wao wayasikiayo maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo,
kwa maana wakati u karibu!
Kusoma Biblia hutupa picha kamili ya Neno la Mungu. Watu wengi huona umuhimu wa kuwa na ratiba
katika kusoma Neno la Mungu kila siku. Hii huwawezesha kusoma Bibilia nzima kwa utaratibu.
Chunguza
Matendo: 17:11 Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile
neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo
yalivyo.
Kujifunza maandiko hutuongoza katika uvumbuzi wa kweli za Mungu. Kuandika uvumbuzi huu hutusaidia
kupanga kweli hizi ili ziwe rahisi kukumbuka.
Weka Moyoni
Zaburi 119:9, 11 Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii akilifuata neno lako. Moyoni mwangu
nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi. Kuweka neno la Mungu moyoni humwezesha mtu
kutumia upanga wa Roho kumshinda Shetani na majaribu…kuwa nao tayari kwa kushuhudia, au
kuwasaidia wengine kwa “neno wakati ufaao.”
Tafakari
Zaburi 1:2,3 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, na sheria yake huitafakari usiku na mchana. Naye
atakuwa kama mti uliopandwa kando kando ya vijito vya maji, ambao uzaao matunda yake kwa majira
yake. Wala jani lake halinyauki, na kila alitendalo litafanikiwa .
32
Katika mfano wa mkono, dole gumba linasimamia kutafakari, kwa sababu utumishi wake unahusiana na
kila moja ya njia za kujifunza Bibilia ambazo tumeeleza. Unapotafakari neno la Mungu, ambalo ni kufikiri
maana na matumizi yake katika maisha yako, utagundua uwezo wake wa kukubadilisha.
COPYRIGHT; THE NAVIGATORS, P.O. BOX 6000, COLORADO SPRINGS, CO 80934 USA;
USED BY PERMISSION
33
KANUNI ZA KUWEKA MAANDIKO MOYONI
“Moyoni mwangu nimeliweka Neno lako…” Zaburi 119:9
Je, kuna jambo lolote lililo gumu kuliko kuweka neno la Mungu moyoni? Wafuasi wengi wapya
hung’ang’ana na kuweka maandiko moyoni. Wengine huona hii kuwa rahisi, hali kwa wengine
haliwezekani. Ijapokuwa tunakubaliana sote kwamba ni muhimu na lazima kuishi maisha iliyo na nguvu na
ushindi katika Kristo, tungali tunaona ugumu wa kufanya hivyo.
Kukamata
Je, unakumbuka “kielelezo cha mkono?” Tunaweza kusikiza, kusoma, kujifunza, na hata kutafakari neno la
Mungu. Lakini isipokuwa tuweke ukweli wa neno la Mungu katika akili zetu, hatuwezi kukamata ukweli
huo barabara. Kuweka kifungu cha maandiko moyoni ni kama “kidole gumba” cha mkono wako, kwani
hapo ndipo nguvu ilipo. Ndivyo ilivyo na kuweka neno la Mungu akilini. Kwa kweli huna kifungu moyoni
mwako, hadi hapo utakapoweza kuukariri unapohitaji kufanya hivyo.
Waisraeli Waliweza
Watu shupavu wa Mungu tunaosoma katika Biblia wote waliyaweka Maandiko matakatifu akilini mwao.
Hii ni kweli hasa katika Israel, baada ya kuimiliki nchi ya ahadi. Walikaa Israeli na masinagogi yakawa
mahali pa mafundisho badala ya hekalu. Hapakuwa na Biblia zilizochapishwa, isipokuwa sheria (Torah)
zilizotunzwa na mwalimu wa kiyahudi (rabbi) ndani ya sinagogi. Watoto walifundishwa kuweka sheria za
Musa nyoyoni.
Musa akawaambia watu, “Sikiza, Ee Israeli; BWANA Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja. Nawe mpende
BWANA Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yote, na kwa nguvu zako zote. Na maneno haya
ninayokuamuru leo yatakuwa katika moyo wako, nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena
uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. Yafunge yawe dalili juu ya
mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba
yako na juu ya malango yako.” Kumbukumbu la Torati 6:4-9.
Hivi ndivyo wana wa Israeli walivyotunza maandiko yao matakatifu na kuyahifadhi, wakiyaweka hai.
Wazazi waliweka nyoyoni sheria za Musa, na kuwafundisha watoto wao kuyakariri katika maisha yao yote.
Yesu aliweka Neno Moyoni
Katika Luka sura ya 4 tunasoma kuhusu kujaribiwa kwa Yesu nyikani. Tunamwona Yesu kila wakati
akitumia vifungu vya maandiko kutoka katika Agano la kale dhidi ya adui Shetani. Yesu alijifunza wapi
maneno au hivyo vifungu? Alijifunza katika sinagogi alipokuwa kijana mdogo. Alitii mafundisho ya
Zaburi 119:9, 11, “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii akilifuata neno lako…moyoni mwangu
nimeliweka neno lako nisije nikakutenda dhambi.” Tunaona mara kwa mara jinsi Yesu alivyofahamu
maandiko kwa moyo. Alichukua muda wa kujifunza na kuweka neno la Mungu moyoni wake.
Wanafunzi wa Kristo Waliweka Neno Katika Nyoyo zao
Ukiangalia huduma ya mitume, utagundua kwamba walikuwa watu “shupavu katika maandiko.” Petero
aliweza kusimama siku ya Pentekote penye uwanda wa hekalu na kunukuu sehemu kadhaa za Zaburi na
Manabii. Alijifunza wapi hayo yote? Hakuwa na maandiko ya kusoma mbele yake. Alichokuwa na
ufahamu wake tu, na uwezo wa nguvu za Roho Mtakatifu. Hakuhitaji kitu kingine.
Ustadi uliopotea
Wazazi wakristo katika vizazi vilivyopita waliwafundisha watoto wao kuweka neno la Mungu nyoyoni.
Mapokeo hayo muhimu yalipotea katika karne ya mwisho ya Kanisa. Hii inahitaji kufufuliwa katika maisha
ya kila siku ya kila mfuasi. Mfuasi wa kweli wa Kristo anahitaji kuvaa silaha kamili za Mungu ili aweze
34
kumpinga adui. Kukariri neno la Mungu ni sehemu muhimu ya silaha hizo. Itachukua muda, kazi na kujitoa
mhanga, lakini thawabu ni kubwa zaidi.
Msaada Wa Kufaa
Shirika la The Navigators la huko Colorado Springs, Colorado, wamefanya bidii zaidi ili waweze kurudisha
hadhi ya kuweka maandiko moyoni katika uhai wa Kanisa kuliko shirika lolote duniani siku hizi. Unaweza
kuwasiliana nao kwa mtandao ukitumia www.navigators.com. The Navigators hutoa vifaa vingi vya
kusaidia kuweka neno la Mungu moyoni. Hebu tutumie mfano wao kwa kutoa mapendekezo ya jinsi ya
kuanza, na baadaye kuendelea na utaratibu wa kuweka neno akilini.
Chagua Na Kuzingatia Namna ya Kujifunza
Ni bora zaidi kujifunza kwa moyo kwa kufuata fikira fulani. Ina maana kwamba utaweka vifungu katika
kumbukumbu yako kwa kuvipa majina ya fikira fulani. Hivyo ndivyo tarakilishi ya ubongo wako
inavyopenda kufanya. Kwa mfano, miaka mingi iliyopita Dawson Trotman alifundisha watu wake kwa
kubuni “gurudumu” kama mada ya msingi katika kuweka neno katika nyoyo zao. (Tazama Gurudumu
katika sehemu ya pili ya kitabu hiki).
Kristo ndiye katikati = Kitovu cha gurudumu – Wazo hili linaonyesha kwamba Kristo ni lazima awe
katikati ya maisha ya mfuasi.Kuna vifungu viwili vinavyoeleza wazo hili. Kujifunza vifungu kumi na
viwili vinavyoambatana na mada sita katika gurudumu ni njia nzuri ajabu ya kuanza kujifunza maandiko.
Tunga Mada
Unaweza kubuni mada na kuuweka taratibu katika wazo uliyochagua. Unaweza kupenda kujifunza kwa
moyo vifungu kuhusu “Malezi.” Itakubidi basi kutafuta vifungu vinavyoongea kuhusu mada hiyo.
Kuchagua mada ni hatua ya kwanza katika kufanikiwa.
Marejeo “kabla ya na baada ya”
Ni jambo la hakika kwamba kurudiarudia neno la Mungu humwezesha mtu kulikumbuka.
Unavyorudiarudia kifungu, ndivyo itakavyokuwa rahisi kwa bongo lako kutunza kumbukumbu lake. Iwapo
mada yako ni “Malezi,” na mstari wako ni Waefeso 6:4, basi utahitaji kuwa na tabia ya kusema kisa au
mada “kabla, na baada” ya kujikariria au kukariria mtu mwingine kifungu. Kukariri huku kutafanya
kifungu kunata kabisa katika bongo lako. Kifungu “hutunzwa ndani ya akiba za bongo lako,” chini ya kisa
“Malezi.” Vifungu hivi vitaambatana na mistari katika kumbukumbu lako.
Rudia! Rudia! Rudia!
Marudio ni mama ya mafundisho. Kwa kweli ni ufunguo wa kumbukumbu nzuri! Ni rahisi kunukuu
kifungu ulichojifunza kwa moyo dakika kumi zilizopita, lakini usiporudia kwa kusema kifungu hicho tena
na tena kila siku, au mara kadhaa kwa juma, utakipoteza katika kumbukumbu lako. Njia pekee ya kulinda
tunachojifunza kwa moyo ni kurudia mistari na kutaja vifungu na mada mara nyingi kwa kurudiarudia.
Hata hivyo, kutafika siku ambapo kifungu hicho kitakuwa chako, na hutakisahau kamwe. Hii itawezekana
tu kwa njia ya marudiorudio kwa ziada.
Safari ya maili elfu moja
Mtu mmoja alisema kuwa safari ya maili elfu moja huanza kwa hatua ya kwanza. Hii pia inahusika katika
kujifunza maandiko kwa moyo. Ni lazima uanze. Anza na wazo moja na mstari mmoja. Ifahamu kamili
kabla kuongeza lingine. Usiume kiasi kikubwa usichoweza kutafuna! Au kama wanavyosema katika
Afrika, “Unaweza kumla tembo kwa kumtafuna kidogo kidogo.” Siri ni kuelewa kifungu kimoja na mada
moja vizuri kabla kujaribu vifungu vingine na kukata tamaa. Enda kwa mwendo unaokufaa. Furahia
ulichoweka moyoni vizuri kisha uendelee kwa kingine. Kuwa thabiti ni muhimu. Kitambo kidogo
utagundua kwamba una vifungu vingi moyoni kupitia kwa kifungu chako kimoja, na mada yako. Ndiyo
sababu tumependekeza uanze na mfano wa kielelezo cha gurudumu la The Navigators, ambayo ni rahisi,
nyepesi na yenye msaada.
35
Andika juu ya kadi
Unaweza kuandika au kuchapa vifungu vyako juu ya karatasi ndogo ambayo unaweza kubeba popote
uendapo. Ingefaa ionekane hivi:
Malezi Efe. 6:4
Nanyi, akina Baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.
Malezi Efe. 6:4
Utakapokuwa na vifungu vyako kwenye karatasi, “utakomboa wakati” kwa kutumia muda wako wa akiba,
unapoendelea na shughuli za siku yako. Mpango huu huliweka Neno la Mungu katikati ya siku yako, bila
kuwa mzigo wa kuchokesha. Lifiche neno moyoni mwako unapoendelea na shughuli zako katika siku.
Tafuta Mtu Utakayewajibika Kwake
Mwisho, jaribu kutafuta mtu ambaye atahusika na kukufanya uwajibike kwake unapoweka maandiko
katika moyo. Pengine wewe na mtu mwingine mnaweza kushirikiana kukariri pamoja. Ni vigumu kukata
kamba mbili zilizosokotwa pamoja. Mtachocheana na kuwa kitu kimoja mnapochunguza maandiko pamoja
na kukariri vifungu. Mkaririane mistari mliyojifunza kila iwezekanapo. Hii itakusaidia kuwajibika kwako
mwenyewe, kwa Mungu, na kwa mwenzako.
36
37
KUANDAA MAHUBIRI KUTOKA KWA NENO LA
MUNGU
Mahubiri ya kufafanua maandiko ni mahubiri yaliyo na mambo makuu kutokana na maandiko
yanayojadiliwa. Haya ni mafafanuzi yanayotokana na maandiko. Mara nyingi wahubiri hujaribiwa kuingiza
maana tofauti katika maandiko badala ya kuyafafanua. Wanaingiza wanayodhania katika neno la Mungu,
kuliko kueleza ukweli kutoka katika neno hilo.
Kusikiliza mahubiri mazuri hupendeza. Dakika za kwanza tatu, na za mwisho tatu, ni muhimu sana wakati
mhubiri anaposimama! Usipotumia dakika tatu za kwanza kuwavutia wasikilizaji wako, basi utawapoteza
kabisa! Kwa hivyo tafuta jinsi nzuri ya kufanya watu wakusikilize. Hii inahusika na kiini cha ujumbe
wako.
Mahubiri mazuri kutoka kwa Biblia hayawezi kuwa magumu yakifanyiwa mazoezi. Kila kipengele kikuu
katika ujumbe unaotokana na kifungu cha maandiko kitakuwa na sehemu tatu, yaani:
1. MAELEZO
2. MATUMIZI
3. MIFANO
Kwa mfano: tuchukue kifungu ambacho ni rahisi, kama Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu
aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanae wa pekee, ili kila mtu amwaminie asipotee bali awe na uzima
wa milele.”
Maandalizi: Chunguza iwapo unaweza kusema wazo kuu la hubiri nzima katika sentensi moja. Kwa mfano:
Hebu tuandike hubiri kuhusu kifungu hiki. Tuuite “Kisa kikuu kilichowahi kusimuliwa”
Sentensi kuu: Mstari huu unatusimulia kuhusu mtu aliyependa zaidi, kuhusu upendo mkuu zaidi, kuhusu
karama kuu zaidi, na kuhusu chaguo kuu zaidi ambalo ulimwengu umewahi kusikia.
Sasa buni umbo lililo na ukweli, linaloeleza ukweli, linaloweka ukweli katika matumizi, na kutoa mifano
katika ukweli huo.
I. Mwenye Mapenzi makuu …kwa maana Mungu …
Maelezo: (maswali ya Nani, Nini, Wapi na Jinsi gani, katika ujumbe).
Hapa ndipo tunawajibika kujibu maswali ya misingi kama vile:
1. Maandiko haya yanasema nini?
Angalia hayo maandiko katika tafsiri mbali mbali za Biblia
Chunguza maelezo ya maandiko hayo katika vitabu vya maelezao ya Biblia
Angalia maneno makuu katika itifaki
Angalia maneno hayo kutoka kwa vitabu vya marejeo
2. Ni nani walioandikiwa?
Angalia katika kumbukumbu za historia
Kwa nini Mungu alisema hivyo kwao?
Ilikuwa na maaana gani wakati huo?
3. Ilitokea jinsi gani?
38
4. Tunaweza kupata mafundisho gani siku hizi kutokana na hayo?
Tafuta kanuni ya milele katika mazingara ya kilimwengu. Katika aya hii tafuta kueleza
mambo haya. Eleza Mungu ni nani. Mungu ni pendo - 1 Yohana 4:8. Utaweka hapa kitu cho
chote kinachoeleza ukweli. Mungu ni mwenye haki, rehema, ghadhabu, na kadhalika. Lakini
Mungu ni pendo. Na pendo lazima lielekezwe pahali.
Matumizi: (Sehemu ya “kwa hivyo nini” katika ujumbe).
Baada ya maelezo ni matumizi. Kama vile katika maelezo kuna maswali ya nani, nini, na wapi
katika mahubiri, ndivyo matumizi yalivyo na maswali kama “kwa hivyo nini” katika mahubiri.
Katika sehemu ya utumiaji wa neno katika ujumbe, mhubiri huuleta utumiji wa neno kwa
wasikilizaji wake. Hujibu maswali yaliyoko akilini mwa wasikilizaji, kama vile, “kwa hivyo nini.”
Anaweza kuuliza swali kama vile, “Maoni yako kuhusu Mungu ni nini?” “Wamwonaje?” Kwa
karne nyingi watu wa Kenya walimwita Mungu “Ngai”, na waliamini kuwa anaishi juu ya mlima
Kenya! Mhubiri anaweza kusema, “Unajua kuwa Mungu ni pendo?”
Utumiaji hubinafsisha ujumbe. Yesu, na hata manabii wote, walifanya hivyo. Waliutumia ule
ukweli kwa wasikilizaji wao. Siku ya Pentekote, Petero aliwageukia hao viongozi wa kiyahudi na
kuwaambia kwamba walihusika na kifo cha Yesu kwa kusema, “Yesu…mlimsulubisha kwa
mikono ya watu wabaya na kumuua… na Petro akawaambia, “Tubuni…” (Matendo 2:23-38).
Jambo muhimu hapa ni kwamba mahubiri hayana budi kuwa kweli iliyo na matendo. Iwapo mtu
ataondoka pasipo kufahamu yale Mungu anachomtaka kufanya, au kuwa, basi pengine alikuwa
hasikilizi, au mhubiri hakufanya kazi yake barabara.
Mifano: (“Madirisha” ya kuona katika ujumbe).
Sasa tunahitaji hadithi ambayo ni picha ya kudhihirisha ukweli. Mifano ni madirisha ambayo
huingiza nuru ya kweli za Mungu nafsini. Wasikilizaji wakisahau ujumbe baada ya muda mrefu,
watakumbuka hadithi. Yesu alifahamu hivyo na kuwahubiria watu mahubiri yenye mifano ili
wayakumbuke. Luka 15 ni hubiri lenye mfano. Anawaambia Mafarisayo hadithi ya mtu aliyekuwa
na wana wawili, ili kuwafundisha kuhusu neema na upendo wa Mungu. Katika Yohana 3:16
mhubiri anaweza kutoa mfano wa kuonyesha kwamba Mungu ni pendo.
II. Upendo Mkuu zaidi … Mungu aliupenda ulimwengu
Maelezo: Kuna aina nyingi za upendo. Neno hili la upendo ni “agape,” na humaanisha upendo
usio na masharti. Ni Mungu peke yake anayeweza kupenda bila masharti yoyote. Ni Mungu tu
anayeweza kuona mbali zaidi ya makosa yako na kuona hitaji lako. Tunahitaji upendo wa namna
hii kwa kuwa sisi tuna dhambi na hatia. Hii ni NEEMA kutoka katika moyo wa Baba. Tilia
mkazo kwamba upendo wa Mungu umeelekezwa kwa wanadamu wote. Anaupenda ulimwengu
wote, bila kumtenga yeyote.
Matumizi:
Je, upendo wa Mungu umefikia ulimwengu wako? Mungu anaweza kukupenda. Lakini unaweza
kumfungia nje ya moyo wako kwa ajili ya dhambi na kutokuamini kwako. Katika moyo wa kila
binadamu kuna utupu unaotokana na Mungu, ambalo linaweza kujazwa tu na upendo wa Mungu.
Mfano: Sasa tunahitaji picha tena, yaani dirisha la kuingiza nuru. Unaweza kutumia hadithi nzuri,
shairi, usemi, au hata kichekesho kueleza ukweli huu.
Ambatanisha maelezo, utumiaji, na mifano katika kila kipengele. Hii ni njia rahisi ya kuunda
hotuba kutokana na Biblia.
Hatimaye, kila hotuba inahitaji kuwa na mwisho. Mwisho, au hitimisho ni mwito kwa wasikilizaji wako
kuitika na kuchukua hatua. Unataka wafanye kitu fulani kwa kutii neno lililotamkwa. Hitimisho ni kule
39
kuwaambia wanachopaswa kufanya. Lazima useme kwa kifupi ukiwa wazi na dhahiri kwa yale unayotaka
wafanye. Mwito wako kwao itahusiana na kiini cha mahubiri yako. Mwito huweka wazi ujumbe katika
mahubiri.
40
41
42
43
MUHTASARI
Uhusiano wetu na Mungu, kama uhusiano baina ya mtu na mtu, lazima uwe na mawasiliano ili uwe hai, na
wenye afya. Kitabu hiki kinakuonyesha jinsi ya kuendeleza hamu ya kweli katika kuongea na Mungu. Pia
katika kitabu hiki kuna mafundisho kutoka katika neno la Mungu ya kukusaidia kuwa na maombi yenye
matokeo. Pamoja na hayo utajifunza kuwahudumia wengine kupitia kwa huduma ya maombezi.
Maelezo yaliyopangwa kamili ya Barry Wood kuhusu maandiko yanadhihirisha jinsi unavyoweza kuwa na
uwezo kupitia kwa maombi yaliyojibiwa.
Mafundisho haya yenye kuhamasisha yatakupa mijadala kwa kirefu kuhusu masomo yafuatayo, kando na
masomo mengine:
• Kuomba kwa uwezo na ujasiri
• Vita vya kiroho, mavazi yetu ya vita, na silaha
• Kufunga na kufungua kutumia funguo za ufalme
• Maombi yasiyojibiwa, na mapenzi ya Mungu
• Kufunga na kuomba
• Maombi na Uinjilisti
• Jinsi kutokutii kunavyozuia uwezo wa maombi
• Huduma ya maombezi
• Kwa nini tunaomba katika jina la Yesu
• Jinsi kutokusamehe kunavyoathiri maombi
Kitabu hiki kimeundwa kwa ajili ya:
• Kutufundisha kuomba
• Kututia motisha ili tuwe na huduma ya maombi yenye mafanikio na uthabiti.
Unajua kuomba vizuri? Je unahisi kuwa na nguvu za Mungu kwa maombi yaliyojibiwa? Hebu tutembee
katika hii changamoto pamoja.
Tutapaza sauti kama wale wanafunzi wa kale tukisema “Bwana Yesu, tufundishe kusali.”
44
45
UTANGULIZI
“Mtu alivyo katika chumba chake cha maombi faraghani, ndivyo alivyo kwa hakika.”
– Robert M’Chyne
Kama Wakristo, ni vigumu sana kujifunza kuomba. Maombi ni kazi ngumu. Ni vita vya mitaroni. Unaweza
kufikiri kuwa kuomba ni rahisi, au ni furaha. Ndiyo, inaweza kuwa hivyo. Lakini maombi ya kweli ambayo
humfikia Mungu na kuugusa moyo wake ili ajibu si rahisi!
Labda wanafunzi wa Yesu walifikiri kwamba maombi ni rahisi, mpaka walipodumu na Yesu kwa muda.
Walimtazama akiomba kwa Baba yake, akiugua. Wakapaza sauti wakisema “Bwana, tufundishe kusali
hivyo!” (Lk. 11:1). Wanaume hawa wa kiyahudi waliofundishwa maisha yao yote jinsi ya kuomba
waligundua kwamba kulikuwa na zaidi katika kuzungumza na Mungu ambayo hawakufahamu.
Nimesafiri sana nikihubiri katika mamia ya makanisa na kuchunguza mitindo ya maisha ya Ukristo wa
Wamarekani (pamoja na Ulaya Magharibi). Kutokana na safari zangu nimeshawishika kwamba maombi ya
kweli ni fani iliyopotea. Hali hii ya “kutokuwa na maombi” hueleza hali yetu ya “kutokuwa na uwezo” kwa
Mungu. Maisha yetu ya maombi ni uhai wetu kwa Mungu aliye hai. Muumini asiyekuwa na “nguvu za
maombi” hana “nguvu za Mungu.” Thibitisho la mwamini katika kutembea na Mungu ni mazungumzo yake
na Mungu. Kanisa linahubiri, linafundisha, linakuwa na mikutano na washa, na kupanga shughuli.
Tunayafanya mambo mengi mazuri, lakini hatutilii maanani maombi!
Maombi ni nini?
Kuomba ni kuzungumza na Mungu. Ni sehemu katika maisha yetu inayohusiana na mazungumzo baina
yetu na Baba yetu wa Mbinguni. Uristo, kwanza kabisa, ni uhusiano wa kibinafsi kati ya mwenye dhambi
wa kawaida na Mungu wa jabu. Uhusiano wowote kati ya mtu na mtu lazima uwe na mazungumzo!
Lazima kuwe na mawasiliano katika uhusiano ili kuufanya kuwa hai na yenye afya. Mungu ni Baba yetu,
nasi ni wanawe. Jamii yetu ina shida ikiwa hatuwezi kuwasiliana kwa mazungumzao!
Kwa nini tunapaswa kuomba?
1. Kuomba huonyesha uhusiano wenye afya kati yetu na Mungu. Kila mwamini anapaswa kuwa
na hamu ya kweli moyoni ya kutamani kuzungumza na Mungu. Mtu anapoomba mara kwa
mara, atathibiti maisha yake ya maombi na hamu ya Mungu zaidi. Ikiwa uhusiano wako na
Mungu ni nzuri, basi hamu ya kuongea naye itakuwepo. Baadaye tutazungumzia jnsi dhambi
na uasi huharibu maisha yetu ya maombi.
2. Yesu alituamuru tuombe. “Akawambia mfano, ya kwamba inawapasa kumwomba Mungu siku
zote, wala wasikate tamaa” (Luka 18:1). Tutakata tamaa ikiwa hatuombi “nyakati zote.”
kuomba ni tendo la tamaa na utiifu. Tunapaswa kuomba hata kama hatuna hamu ya kuomba.
3. Kuomba ni tabia ya ufahamu wa Mkristo mwenye afya. Yesu daima alidumu ndani ya Baba
yake katika maombi. Tunapaswa kukaa ndani yake na ndani ya neno lake ili maombi yetu
yaweze kujibiwa (Yohana 15:7). Mungu anataka maombi yetu, kwa sababu ulimwengu
unahitaji majibu yanayotolewa na Mungu.
4. Maombi hufungua milango ya nguvu zisizo za kawaida katika maisha yetu. Maombi yetu
yanaweza kumshughulisha Bwana Yesu kutenda kazi katika ulimwengu wetu. Kuomba kwa
uwezo kutamruhusu Mungu kutenda kazi ambayo kwa kawaida hawezi kutenda. Baadaye
katika kitabu hiki utajifunza kuhusu nguvu za maombi na jinsi ya kufanya nguvu hizo
kutumika!
46
Hebu tuvumbue “mambo ya kina” zaidi katika Neno la Mungu. Tunaweza kugawanyisha kweli hizi katika
makundi ya maombi, vita vya kiroho, na maombezi. Hebu ingia na Yesu patakatifu zaidi kwa maombi na
maombezi!
47
JINSI YA KUISHI KIMIUJIZA
Maombi ni mazungumzo kati ya mwanadamu wa kawaida na Mungu wa ajabu kila mara kuhusu
mambo ya kawaida.
Nyakati zingine wengi wetu huona kwamba kanisa, dini, na imani yetu hayatoshi kuleta mabadiliko katika
ulimwengu wetu. Tunahitaji miujiza. Ingekuwa ajabu kutembea na Yesu kama walivyofanya wanafunzi!
Miujiza iliahidiwa
Mungu anataka kukuonyesha siri zake ili akukuwezeshe kuishi maisha yenye miujiza. Katika Injili ya
Yohana tuna ahadi ya ajabu kutoka kwa Yesu. “Amin Amin nawambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi
nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa zaidi kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi
naenda kwa Baba” (Yohana 14:12). Hiyo ni ahadi ya kustusha! Yesu anasema kila mwamini wa kweli
anapaswa kufanya miujiza miwili:
• Kuhudumu sawa na Kristo – “kazi nizifanyazo mimi yeye naye atazifanya…”
• Kuhudumu kuzidi Kristo – “na kubwa kuliko hizo atafanya kwa kuwa mimi naenda kwa
Baba.”
Ajabu! Inawezekanaje humu duniani, kwa Mkristo kuhudumu kuzidi Yesu? Ahadi kama hii
inaonekana kama yenye mzaha. Inadhihirisha kuwa Yesu alikuwa na wazo la ajabu akilini mwake. Je,
wazo hili ni lipi, na lingewezekanaje?
Mambo Makuu Mawili Katika Maisha Ya Miujiza.
Bwana wetu alitutazamia kuhudumu sawa naye, ama kumzidi. Alituambia jinsi tunavyoweza kutekeleza
hayo. Katika Injili ya Yohana 14, Yesu anatufundisha jinsi mbili za kuishi katika miujiza baada ya
kuondoka kwake:
• Kuomba kwa jina lake
• Roho Mtakatifu kuja kuishi ndani ya waumini
Yesu alimaanisha kutekelezwa kwa ahadi ya kifungu cha 12 (kufananisha, na kuzidi) kwa maneno yake
katika vifungu vya 13-14: “Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani
ya mwana.Mkiniomba neno lolote kwa jina langu nitalifanya.” Ahadi katika kifungu cha 12 inatimizwa na
“swali” lililoko katika vifungu vya 13 na 14.
Maombi katika jina la Yesu ni funguo ya kufungua mlango wa miujiza katika maisha yako. Mambo ya
kawaida yanaweza kuwa funguo ya miujiza. Ukisoma kifungu cha 15 na kuendelea, Yesu anaendelea
kuzungumzia muumini kutiwa nguvu na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu hukaa ndani yetu ili aongeze
maana na imani katika maombi yetu. Tuna yote tunayohitaji ili kufungua mbingu.
Sababu ya Kukosa Miujiza
Kwa sababu gani hatuoni mambo yasiyo ya kawaida katika kanisa, au katika maisha yetu? Wakristo wengi
hawana ufahamu kuhusu kweli hizi. Yesu anatuambia “tuombe jambo lolote” katika jina lake, naye
atatenda. Ikiwa tunajua kuomba, basi atafanya. Wakati muumini anapomwomba Baba katika Jina la Yesu,
Yesu huingia kazini kuendeleza huduma yake. Yesu atafanya huduma zaidi ikiwa wengi wetu watazingatia
maombi.
Unapowasilisha mahitaji yako kwa Mungu Baba, yeye humgeukia Mungu Mwana na kumwambia
akutimizie hitaji lako. Yesu anaamka kitini pake pa enzi, na kwenda kukutimizia haja zako. Unaomba, naye
48
Baba anamtuma mwanawe. Ni jambo la ajabu hilo! Na ahadi ya ajabu pia! Maombi yangu humshughulisha
Yesu!
49
JINSI YA KUOMBA KATIKA ROHO MTAKATIFU
Jambo lililo kuu kuliko vyote ambalo Mungu alipata kunitendea lilikuwa kunifundisha kuomba katika Roho
Mtakatiffu. Kwa kweli hatuwezi kuwa watu wa maombi mpaka tutakapojazwa na Roho Mtakatifu. Kwa
hivyo Bwana, tufundishe kuomba katika Roho.
-Samwel Chadwick, The Path of Prayer
Je, umewahi kuomba “katika Roho”? Wakristo wengi hawafahamu jambo hili. Wengine huogopa na kuona
kwamba pengine linafaa tu kwa wale waliojaliwa na uwezo zaidi, na kwa hivyo, huona haya kujihusisha
nalo. Hata hivyo Maandiko yanatuagiza kuomba “katika Roho.” Mtume Paulo anatusihi “tuombe wakati
wote katika Roho” (Waefeso 6:18). Roho Mtakatifu hutamani sana kutusaidia katika maombi. Bwana wetu
Kristo, katika Yohana 14 anatuambia kwamba kuna funguo mbili za kutuwezesha kuishi maisha ya
kipekee. Funguo hizo ni maombi na Roho Mtakatifu. Tunapaswa kujifunza kumruhusu Roho Mtakatifu
kujihusisha kikamilifu katika mawasiliano yetu na Baba. Kuomba katika Roho kunaelezwa wazi katika
Warumi:
“Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi ipasavyo, lakini
Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo
aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea Watakatifu kama apendavyo Mungu (Warumi
8:26, 27).
Fahamu kwamba Roho Mtakatifu mwenyewe hutamani kutuombea. Asili ya Roho Mtakatifu hudai kwamba
atusaidie. Yeye ni “Roho wa Neema na dua” (Zakaria 12:10). Roho Mtakatifu ni msaidizi wetu katika
maombi. Maombi yetu lazima yahusishe uwepo na uwezo wake.
Kwa kweli Yuda 20 inatuamrisha tuwe “tukijijenga juu ya imani yetu iliyo takatifu sana, na kuomba katika
Roho Mtakatifu.”
Unaomba Wakati Gani Kwa Hakika?
Maombi ya hakika ni maombi katika Roho Mtakatifu. Maombi mengine si maombi ya kweli kamwe. Ni
mambo ya dini tu. Maombi hayo hayana maana yoyote kwa Mungu, wala kwa mwombaji. Ndio sababu
maombi mengi ya hadhara ni sherehe za kidini, zisizo na maana, za kurudiarudia, na za kuchosha. Kinyume
chake ni kuomba katika Roho, ambayo ni maombi yaliyo na nguvu, uwezo, na yamehuishwa na
kudumishwa na Roho wa Mungu Mwenyewe!
Kwa nini tunaona ajabu sana kwamba Roho Mtakatifu anapaswa kutawala maombi yetu? Tunamtegemea
ayatie nguvu mahubiri yetu, kushuhudia kwetu, na kuabudu kwetu. Mbona tusimruhusu katika maombi
yetu? Kipimo cha kutembea kwetu na Mungu hakimo katika mahubiri yetu, utoaji wetu, matendo yetu,
wala mahudhurio yetu, ila kwa uwezo wetu katika maombi. Maombi ni kipimo cha uwezo wetu katika
Mungu.
Je Mungu husema nawe? Je, yeye hukusikiliza na kukujibu unaponena naye? Zaidi ya hayo, je yeye
hukutia nguvu, hukupa uwezo, hukuhuisha na kuyakubali mazungumzo naye? Hiki ni kipimo halisi katika
kumcha Mungu.
Kuomba na Roho
Maandiko yanazungumza juu ya kuomba “na” Roho na kuomba “katika” Roho. Mambo haya mawili
hayafanani. Katika Wakorintho 14:14-15, Paulo anaeleza juu ya kuomba “na Roho.” Hapa haongei kuhusu
Roho Mtakatifu wa Mungu, bali anazungumzia roho yako ya kibinadamu. Kuomba na roho ni kuomba na
lugha isiyofahamika, bila kufahamu linalosemwa. Watu wengi husema ni kuomba kwa “lugha ya maombi.”
Hata hivyo, kuomba katika Roho ni kitu tofauti. Hatukuagizwa kuomba tukinena katika lugha geni, lakini
50
tunaagizwa “kuomba wakati wote katika Roho” (Waefeso 6:18- mkazo umetiliwa maneno yenye herufi
nzito).
Kuomba katika Roho si kwa watu wachache walio na uwezo wa “msisimko,” ambao ni washiriki wa kundi
au dhehebu wajiitao wasisimkwa au wapentekote. Kuomba katika Roho ni maombi halisi. Hii inahusu kila
mmoja.
Hakikisho la Majibu
Umewahi kuomba Mungu na kutaka hakikisho la jibu? Au Je, umepata kuwa na mashaka kwamba
umeomba kufuatana na mapenzi ya Mungu? Ni nini husababisha mashaka hayo katika maombi yako?
Unapoomba katika Roho Mtakatifu, utakuwa na hakikisho kwamba maombi yako yanalingana na mapenzi
ya Mungu, kwa kuwa Roho wa Mungu atakupa yale unayopaswa kuomba. Zingatia ukweli huu kwamba ni
maombi tu yanayoombwa katika Roho Mtakatifu ambayo yanafuatana na mapenzi ya Mungu, na kwa
hivyo jibu limethibitishwa tayari.
Mtu Mpotevu Anapoomba
Kiongozi wa dhehebu moja maarufu alizusha mabishano miaka kadhaa zilizopita alipokuwa akihojiwa na
waandishi wa habari. Alitangaza kwamba Mungu hawezi kujibu maombi ya Padre wa Kiyahudi (Rabbi)
kwa sababu hawamwamini Yesu Kristo kama Mwokozi na Masihi. Watu wengi walishutumu kiongozi
huyu wa kidini. Alishambuliwa kwa ushupavu wake kwa mambo ya dini. Je, alikuwa shupavu wa dini?
Maoni yako yanategemea ufahamu wako wa maandiko.
Tukiyachunguza maandiko zaidi, tutaona matokeo ya kufurahisha sana kuhusu maombi, na wasioamini.
Yesu anatufundisha kuomba kwa jina lake, si kwa Yehovah, au Allah, wala kwa Mungu mwingine awaye
yote. Yeye ni mpatanishi wetu kwa Mungu. Tunakuja katika jina lake. Roho Mtakatifu huliheshimu Jina la
Bwana Yesu. Kwa hivyo mpotevu hawezi kuomba katika Roho kwa sababu hana Roho Mtakatifu anayeishi
ndani yake. Ni mtu “asiye na Roho” (Yuda 19).
Mungu hujibu maombi ya mpotevu anapofahamu kwamba jibu litamhamisha mtu huyo na kumwelekeza
kwa wokovu katika Yesu Kristo. Matendo 10 inaeleza wazi wazi jambo hilo kutokana na tukio la Kornelio,
Jemadari wa Kirumi. Maandiko yanamweleza kama “mtu mtauwa, mchaji wa Mungu…. Na kumwomba
Mungu daima” (Matendo 10:2). Katika kifungu cha 31 tunaona Mungu akisikia maombi ya Kornelio, na
kuyajibu! Wakati mwingine Mungu hujibu sala za washenzi - lakini sala yale tu yatakayomwongoza
mpotevu kwa mwokozi Yesu Kristo.
Hakikisho Thabiti.
Heri mwamini aliyezaliwa mara ya pili! Roho wa Mungu huishi ndani yake na hutamani kuomba kupitia
kwake ili kuhakikisha majibu kwa maombi yake. Hebu tuelekeze mawazo yetu katika Warumi 8:26,27 ili
tujifunze zaidi kuhusu ombi hili katika Roho Mtakatifu. Paulo anasema “...hatujui kuomba ipasavyo”
(Warumi 8:26).
Hii ni kweli kwa kila muumini. Wewe na mimi tunaanza kuomba. Punde si punde hatujui la kumwambia
Mungu wetu mkuu. Mara kwa mara tunasema maneno yasiyo sahihi. Tunaomba “vibaya” kama vile
Yakobo 4:3 inavyosema. Wakati mwingine ilinibidi kumshukuru Mungu kwa maombi yasiyojibiwa kwa
sababu nilikuwa nikiombea vitu visivyo sahihi, kwa kusudi mbaya.
Hali ya Kutokujiweza Katika Maombi
Warumi 8:26 inatujulisha kutokujiweza kwetu katika maombi inaposema “hatujui kuomba itupasavyo.”
Kwa nini hatujui kuomba itupasavyo? Kumbuka kwamba Roho Mtakatifu hutusaidia katika “udhaifu wetu”
(Warumi 8:26). Neno hili “udhaifu” linaonyesha hali ya kuwa pekee. Halina wingi. Halionyeshi kwamba
tuna udhaifu mwingi au upungufu katika maisha yetu ya maombi, ijapokuwa tuna udhaifu mwingi. Kwa
kweli tuna udhaifu mmoja mkubwa ambalo huathiri kila eneo la maisha yetu, kando na maombi. Udhaifu
huu ni wa mwili. Asili yetu ya anguko, iliyoharibiwa na dhambi na ubinafsi, ndio udhaifu unaotulemea.
51
Hatuwezi kumpendeza Mungu katika “mwili” (Warumi 8:8). Hatuwezi “kufanya” matendo ya kiroho
ambayo yatamfurahisha Mungu katika nguvu zetu wenyewe. Kuhubiri, kuomba, kushuhudia, kutoa, na
huduma zinazofanyika kwa nguvu zetu haziwezi kumfurahisha Mungu. Huu ni “udhaifu” wetu. Wakati
moja nilisikia udhaifu huu ukielezwa kama ukweli wa kiroho usioweza kukanushwa kabisa. Tunawajibika
kuishi na ukweli huu. Udhaifu wetu ni “hali ya kushindwa kabisa kufanya lo lote katika maeneo ya roho
kwa kutegemea mwili wetu.”
Hii ndio sababu Roho Mtakatifu lazima atusaidie. Ni lazima aingie ndani yetu, atujaze, atutawale, na kuishi
maisha yake kupitia kwetu. Tunapofikia wakati wa kushindwa kuomba, basi Mungu huwa ametuweka
anapotaka – yani tumtegemee. Mungu hawezi kutusaidia tunapojaribu kumsaidia. Kristo Yesu anataka awe
zaidi ya mwokozi wetu. Anataka kuwa chanzo cha uhai wetu. Roho Wake awe mfariji katika maombi yetu
kwa kuponya maradhi yetu, na kuwa nguvu zetu katika kuondoa udhaifu wetu.
Msaidizi Tunapoomba
Roho Mtakatifu atatuchochea na kututiia hamu ya kuomba tunaposhirikiana naye. Tunapaswa
kujirekebisha naye tunapokosa hamu ya kuomba. Hamu ya kuomba huja tunapomruhusu kuwa Bwana
maishani mwetu. Tutataka kuomba mara kwa mara Roho Mtakatifu anapotutawala. Vile vile atatupa
maneno ya kuomba.
Kuomba katika Roho Mtakatifu kunamaanisha kwamba Roho Mtakatifu huomba na kufanya maombezi
kupitia kwetu. Kwa kutumia akili yako na utu wako, Roho huomba kwa Baba kupitia kwako. Hayo ni
maombi ya kimaajabu. Je, unaamini kwamba haya yanawezekana? Ndiyo. Roho Mtakatifu anaweza
kusema kupitia maeneo mengine ya maisha ya Mkristo, kama vile:
• Unapohubiri – Mungu anaweza kuhubiri kupitia kwa mwanadamu
• Unapofundisha – Mungu hufundisha kupitia kwa mwanadamu
• Unapoishi – Mungu anaweza kuishi kwa kutumia mwanadamu
Mbona isifanyike hivyo wakati wa kuomba? Je, Mungu hawezi kuomba kwa kutumia mwanadamu? Ndiyo,
anaweza, na anatamani sana kufanya hivyo. Warumi 8:26 inasema yeye “huugua” ndani yetu. Ana hamu
kubwa sana ya kutaka kuomba kupitia kwa maombi ya muumini.
Kuugua kwa Roho
“Kuugua” huku si lazima kuwe kwa maneno ya kibinadamu. Mara kwa mara ni Roho wa Yesu ndani yako
anayetamani kushirikiana nawe. Kuugua huku kunatokana na Mungu tu. Mara kwa mara hakuna maneno.
Roho hututaka tuwe shirika pamoja naye.
Mungu wetu ni wa thamani kiasi cha kutamani kushiriki nasi katika ubinadamu wetu wa dhambi. Mara
nyingi tunakariri tu maombi, badala ya kutulia na kujua kwamba yeye ni Mungu.
Maombi kufuatana na Mapenzi ya Mungu
Kuna wazo lingine moja katika mafundisho ya Paulo, katika Warumi 8:27: “Huwaombea… Kama
apendavyo Mungu.” Utathibitishaje kuwa maombi yako yatajibiwa? Kudhibitisha ni rahisi sana, nalo ni
kuomba daima katika Roho Mtakatifu. Kila mara Roho Mtakatifu huomba kwa kufuata mapenzi ya Mungu,
na kila ombi linalowakilishwa kufuatana na mapenzi ya Mungu litajibiwa kwa “Ndiyo” itakayojulikana
pote. 1 Yohana 5:14 inaahidi hivi: “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa tukiomba kitu sawasawa
na mapenzi yake, atusia.” Omba katika Roho, nawe utapata majibu!
Kuombea Uponyaji
Mtu fulani akihitaji maombi kutoka kwako kwa ajili ya uponyaji, lakini hujui kama ni mapenzi ya Mungu
kumponya mtu huyo! Mara nyingi tunaomba hivi, “Mungu, kama ni mapenzi yako, mponye mtu huyu.”
Hicho ni kifungu chetu cha kutorokea. Tunaweka “ikiwa” ya kitheologia kwa kujilinda. Maombi ya
“ikiwa” si maombi ya imani. Ni wakati ambapo hatujui mapenzi ya Mungu kwa uwazi, ndipo tunahitaji
kuomba Roho Mtakatifu atusaidie.
52
Tunapoomba
Tuangalie baadhi ya maelekezo kadhaa, au hatua za nidhamu ambazo zitamruhusu Roho wa Mungu kutia
nguvu maombi yetu kabla hatujaomba:
1. Ungama kila dhambi unayojua. Isaya 59:2 inatuambia kwamba; “dhambi zenu zimefarikisha
nyinyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone hata hataki kusikia.”
2. Chagua kwenda kinyume cha ubinafsi. Jitoe mwenyewe kwa Mungu, na kwa mapenzi yake.
Mtangaze Yesu kuwa ni Bwana wa vyote. Jinsi unavyoanza muda wako wa maombi kwa
kuungama dhambi, ndivyo utakavyohitaji kumwambia Mungu, “Yesu ni Bwana wa maisha
yangu; Bwana Yesu, mimi ni wako.” Ungamo hili kwa mdomo huthibitisha kujitoa ndani ya
moyo wako, na humfurahisha Mungu.
3. Weka Muda wako wa maombi kwa Roho Mtakatifu. Kwa kinywa chako mwambie
kutokuweza kwako. Mkaribishe aombe kupitia kwako. Mwombe atawale ibada yako.
4. Mngoje Bwana. Maandiko yanasema, “Tulia mjue ya kuwa Mimi ni Mungu.” Ngojea kimya,
au soma Neno kwa sauti. Roho wa Mungu ataanza kushiriki nawe. Unaweza kupata wazo
fulani. Omba hilo wazo kwa sauti. Una kila haki ya kuamini kwamba mawazo hayo yametoka
kwa Mungu.
5. Uliza, Je, ni mimi au ni Mungu? Utaweza kushangaa na kuuliza, “sijui wazo hili ni langu, au
ni la Bwana.” Mbona kuwe na tofauti kati ya matakwa yako, na matakwa ya Mungu? Ikiwa
umemtangaza Yesu kuwa Bwana, na kuungama kila dhambi unayojua, na kumwomba Roho
Mtakatifu atawale mawazo yako, basi mawazo yako na ya Mungu yatafanana! Zaburi 37:4
inasihi kwamba, “Nawe utajifurahisha kwa Bwana, naye atakupa haja za moyo wako”
Kuomba Bila Kuwa na Hakika
Mara nyingi kufahamu mapenzi ya Mungu si rahisi. Wakati mwingine tunapaswa kufuata miongozo fulani
katika maombi”
• Omba hadi upate jibu
• Omba hadi upate thibitisho la jibu.
• Omba hadi Mungu aseme “la.”
Unaweza kuwa na mashaka jinsi Mungu huzungumza nyakati kama hizi. Hufanya hivyo kwa njia ya Roho
wake Mtakatifu akaaye ndani yetu. Maandiko yanatuagiza kuwa “Amani ya Kristo itawale ndani ya mioyo
yenu…” (Wakolosai 3:15). Unawezaje kuwa na amani moyoni mwako kutokana na hitaji fulani? Roho wa
Mungu ataleta amani yake akiruhusiwa “kutawala” ndani ya roho zetu. Neno tawala ni miongoni mwa
maneno sita ya Kiyunani yaliyotafsiriwa “tawala” katika Agano Jipya. Lina maana ya “kutenda kama
mwamuzi.”
Roho wa Mungu atakuwa mpatanishi katika nyakati hizi za kutokuwa na hakika. Kwa hivyo omba bila
kukoma. Atakupo amani!
Majibu Yaliyoahidiwa
Kuomba kile ambacho Mungu ameahidi katika Maandiko ni azimio tofauti. Roho aliye ndani yako ndiye
aliyeandika kitabu kilicho na upuzio wake. Kudai ahadi zilizomo Bibliani ni tendo la imani. Omba:
• Ukimkumbusha Mungu ahadi yake. Mnukulie Neno lake.
• Ukileta hitaji mbele yake, “Mwambie Mungu mahitaji yako na usisahau kumshukuru kwa
majibu yake” (Wafilipi 4:6).
• Ukidai jibu kwa imani. Yesu aliahidi kwamba “Yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba
mnayapokea, nayo yatakuwa yenu” (Marko 11:24).
53
• Ukimsifu daima, na kuamini kwamba jibu liko njiani. Hapa tutajifanya kama watu walio na
jibu tayari, na kumwachia Mungu wetu Mkuu maswali kama ya lini, wapi, na jinsi gani,
tukijua kwamba “yatakuwa yenu.”
Katika sehemu zifuatazo, tutaendeleza ufahamu wetu kuhusu uwezo wa maombi.
Misaada
1. Katika kitabu kilichotangulia, nilieleza uponyaji na maombi kwa kirefu zaidi. Tazama sura ya 7 ya
Questions New Christians Ask (Old Tappan, New Jersey: Fleming H. Revell Company, 1979), pp.76 –
86.
2. Angalia sura ya 1, “Jinsi ya kujua Mapenzi ya Mungu”, katika Questions New Christians Ask.
3. Neno ni brabeuo; Angalia W.R. Vines Expository Dictionary of Old and New Testament Words (Old
Tappan, New Jersey: Fleming H. Revell Company, 1981), P. 307.
54
55
JINSI YA KUOMBA NA NGUVU
Vipengele viwili muhimu katika maombi ya mamlaka ni kujua ni nani unayemwomba. Pili, ni kujua wewe u
nani ndani yake. “Naomba macho ya mioyo yenu yatiwe nuru”(Waefeso 1:18).
Kwa nini Mungu hajibu maombi yangu? Je, umewahi kuuliza swali hilo? Ni nani ambaye hajawahi kuuliza
swali hilo kwa wakati fulani? Kuna sababu nyingi ambazo humsababisha Mungu kusema “la,” ijapokuwa
muumini yeyote anaweza kuomba kwa ujasiri hadi Mungu ajibu. Kila muumini aombe kwa uhodari.
Waebrania 4:16 inatuhimiza “kukaribia kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya
kutusaidia wakati wa mahitaji.”
Kufahamu U Nani
Ujasiri katika maombi ni matokeo ya sababu nyingi, mojawapo ikiwa imani. Kichwa cha somo
litakalofuata ni Jinsi ya Kuomba Kwa Imani. Hata muhimu zaidi kuliko kuwa na imani kwa Mungu ni
kujua u nani katika Kristo. Kutambulikana na Kristo ndiko kunatupa moyo na ujasiri wa kuomba kwa
uhodari mbele ya kiti cha Mungu Matakatifu. Ni mtoto wa Mungu tu anayejua nafasi yake katika Kristo
awezaye kutumaini kuomba na mamlaka. Inaonekana kwamba wakristo wachache wa kisasa ndio
wanaelewa maana ya kutambulikana na Kristo.
Ujasiri katika maombi hutokana na ufahamu wa kweli juu ya Mungu na jinsi anavyokuonoa, kama mtoto
wake.
Mamlaka ya Muumini
Kila mtoto wa Mungu ana “haki kitini pa enzi.” Haki hizi zinatokana na yale Bwana Yesu alifanya
msalabani kwa ajili yetu. Haki za muumini kitini pa enzi ndio mamlaka yake katika Yesu Kristo. Mtume
Paulo anaeleza mamlaka yetu katika Waefeso 1:18-23:
“Ninaomba kwamba macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo:
na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo, na ubora wa ukuu wa uweza
wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uwezo wake: aliotenda
katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa
roho; juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala
si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; akivitia vitu vyote chini ya miguu yake,
akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu
wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.”
Maandiko haya ni maombi dhahiri. Paulo anaomba kwamba macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, ili mjue
ninyi ni akina nani katika Kristo. Ubeti huu ni wa ufasaha unaofunua haki zetu mbele ya kiti cha enzi. Sisi
ni warithi katika Kristo. Tuna urithi (Warumi 8:17) ulionunuliwa kwa ajili yetu kupitia kwa kazi
iliyomalizika ya Kristo, yaani kifo chake, kuzikwa kwake, kufufuka kwake, na kupaa kwake.
Kiti cha Mamlaka Yetu
“Aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa
roho” (Waefeso 1:20). Maneno haya yanatuambia kwamba Kristo alifufuka na kukalia kiti cha enzi cha
Mungu.
Anatawala katika ulimwengu na sayari. Sote tunaelewa hivyo; lakini, Je, wajua kwamba unatawala pamoja
naye katika huo ulimwengu wa roho?
56
Paulo anathibitisha jambo hili katika ufasaha kwenye maandiko mengine mawili: “akatufufua pamoja
naye, katuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu” (Waefeso 2:6); “na ninyi
mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka” (Wakolosai 2:10).
Tamko la ajabu hilo! Sisi (waumini wote waliozaliwa mara ya pili) tumeketishwa “pamoja naye” na
tunashiriki ushindi wake. Tu warithi pamoja naye katika utawala na nguvu zake. “Tumetimilika” katika
yeye. Basi hivyo ni kusema kwamba kweli zote katika ushindi wa Bwana juu ya ulimwengu, mwili, na
shetani, ni kweli pia kwa muumini. Kwa wakati huu “tumeketishwa” pamoja naye katika ulimwengu wa
roho – si unapokufa, ama Yesu anaporudi tena kuchukua kanisa lake. Uko pale sasa, ukitawala na kungoja
pamoja na Kristo juu sana kuliko falme zote, na mamlaka, na nguvu (Waefeso 1:21). Nguvu zote za Mungu
alizopewa Kristo zimepewa kanisa pia, “ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa
vyote katika Kristo (Waefeso 1:23).
Ukweli Wa Hali
Huu ukweli tunauita “ukweli wa hali.” Kwa maneno mengine, Mungu huliona kanisa ambalo limekamilika
katika Kristo. Kulingana na Mungu, tumewafanya maadui wetu kuwa chini ya miguu yetu. Mungu
anatuona tukiwa mbinguni pamoja naye. Hatusimami mbele ya Mungu Mtakatifu katika hali ya
kuhukumiwa au tukiwa kama wenye dhambi na hatia. Bali tunasimama katika hali ya msamaha,
kuhimidiwa, na kama warithi pamoja na Kristo. Mungu anatupenda kupitia kwa mwanawe. Tu “ndani ya
Kristo” katika kikao chetu kwa Mungu.
Kikao na Maombi
Huenda ukashangaa kwamba hii ina maana gani katika maombi ya uhodari. Inahusika kabisa. Je, unaweza
kukaribia kiti cha enzi cha Mungu Mtakatifu na hatia ya dhambi mbele ya macho yako? Mtume Yohana
anaeleza jambo hili vizuri: “Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri katika Mungu” (1 John 3:21).
Je, moyo wako mara kwa mara unakuhukumu? Je, hatia, kushindwa, au kukosa ujasiri hukuzuia kuomba na
kuuliza” Rafiki, hii ni mbinu ya shetani kuhukumu moyo wako. Anakuweka katika msingi wa “kutenda”
badala ya msingi wa kikao mbele ya Mungu.
Hakuna anayestahili mbele ya Mungu kwa matendo yake. Hata hivyo, katika Kristo, tunahimizwa
kukaribia kiti cha neema kwa ujasiri ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Kama watoto wa Mungu tumependwa na kukubaliwa. Sisi si waombaombaji, wanaomwendea Mungu
kupitia mlango wa nyuma ili kuomba makombo. Sisi ni tajiri na warithi pamoja na Kristo. Tunaomba na
kupokea, kwa sababu ya yale amefanya, na jinsi tulivyo ndani yake.
Chanzo Cha Mamlaka Yetu
Katika maombi ya Paulo katika Waefeso 1, anatuonyesha urithi huu mkuu na nguvu za kutawala juu ya kila
jina litajwalo katika ulimwengu huu au ulimwengu ujao (ulimwengu wa roho), na kwamba uwezo huo
tumepewa “sisi tunaoamini” (Waefeso 1:19). Imani yetu, katika ukweli huu uliofunuliwa, ndio ujasiri wetu
mbele ya Mungu. Nguvu za Mungu zimeelekezwa kwa wanaoamini. Je, wewe ni muumini? Simaanishi
muumini anayefuata mafundisho ya dini, bali muumini katika vitendo.
Paulo anaomba kwamba “macho ya mioyo yenu” yafunguliwe – si macho ya akili, bali macho ya moyo
wako. Kweli hizi kuhusu sehemu yetu katika Kristo hayafahamiki kwa mawazo ya akili – ila yanatokana na
ufunuo wa Roho Mtakatifu kwa roho yako. Ni moyo tu ambayo inaweza kutambua ukweli huu. Ni kwa
waaminio. Hii inazidi ufahamu; lakini haizidi imani. Chanzo cha nguvu zetu na mamlaka yetu katika
Mungu ni imani. Amekamilisha kazi yake ndani ya Kristo. Ni lazima tuamini kwamba ametukamilishia.
Nguvu za Mungu zinaweza kudhihirika katika maombi muumini anapotambua rohoni jinsi alivyo ndani ya
Kristo.
Wasongezao Milima
Yesu alimaanisha maombi haya ya imani aliposema:
“Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione
shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwa sababu
57
hiyo nawaambia, yeyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa
yenu” (Marko 11:23-24).
Hii ni ahadi ya ajabu! Je, una “milima” yanayosimama katika njia yako? “Mlima” inamaanisha kizuizi
kilichoko katikati yako na mapenzi ya Mungu. Mlima huu unaweza kuwa ni shetani mwenyewe. Yesu
anatuambia kwamba tuna uwezo wa kuondoa vizuizi vyo vyote kwa kukiri imani yetu. Tunaongelesha
milima, nayo yanasonga! Hayo ni mamlaka, na nguvu kwa hakika. Njia yetu kuelekea kwenye kiti cha enzi
ni wazi mno!
Musa Na Yoshua
Tunaona mfano mzuri wa maombi ya kusongeza milima na maombezi katika matukio ya Musa na Yoshua
walipokumbana na Amaleki na kabila la Waamaleki. Mungu alimwambia Musa amiliki nchi ya Kanani.
Lakini kulikuwa na pingamizi njiani. Amaleki ni mfalme kafiri, ambaye ni mkali sana. Musa na Yoshua
lazima wamng’oe. Musa anafanyaje basi? Ana mipango aina mbili ya vita. Atampigania Mungu kwa jinsi
mbili – kwa mwili na kwa roho. Yoshua anaenda kukutana na wanajeshi wa Amaleki. Anapigana vita vya
mwili. Musa anakwea juu ya kilima kuomba.
Mwanzo 17 inasimulia huu mpango wa ajabu wa vita:
“Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu ukatoke ukapigane na Waamaleki; kesho
nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. Basi
Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na
Huri wakapanda juu ya kile kilima” (Mwanzo 17:9,10).
Ningelikuwa jemadari Yoshua, ningejaribiwa kukabiliana na Jenerali Musa kwa jambo hili!
Ningelipendekeza Musa aelekee kupigana na Amaleki mwenyewe, nami nikwee mlimani kuomba. Hiyo
inaonekana kuwa salama! Ama sivyo?
Fimbo Na Panga
Vita viwili. Maadui wawili. Silaha aina mbili tofauti. Yoshua alimpiga Amaleki kwa panga na mikuki.
Lakini Amaleki hakuwa adui kwa hakika. Shetani ndiye aliyekuwa adui kwa kweli. Amaleki alikuwa
mtumishi wa shetani tu.
“Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka,
juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika uliwengu wa roho” (Waefeso
6:12).
Musa anapigana na adui wa kweli kwa kutumia silaha za rohoni. Anamwombea Yoshua. Mkononi ana
fimbo ya Mungu. Hii ilikuwa ni fimbo ya kawaida ya kuchunga kondoo. Baada ya kukutana na Mungu
mlimani, fimbo iligeuka kuwa “fimbo ya Mungu.” Fimbo hii ni nguvu ya Mungu iliyowekwa mkononi
mwa mtu mwenye imani. Ikiwa mkononi mwa Mungu, fimbo ni nguvu ya Mungu. Kwa hivyo, katika
imani, Musa akiwa mlimani anaomba dhidi ya mlima uliosimama dhidi ya wana wa Israeli, yaani Amaleki.
Musa anapoinua fimbo na kuomba, Yoshua anamshinda Amaleki. Lakini Musa anapochoka na kurudisha
mikono yake chini na fimbo kushushwa, Amaleki anashinda vita dhidi ya Yoshua.
Vilikuwa vita vya ajabu kweli! Havikushindaniwa kwa upanga au kwa mikuki. Walishinda, au kushindwa
kwa maombi. Hivi ndivyo ilivyo haswa maishani mwetu. Adui wako si Amaleki (au tajiri wako, mume
wako, au hata mke wako). Adui wako ni nguvu zinazokukabili kupitia kwa mtu huyo. Mara nyingi
tunapigana vita ambavyo havifai, na adui asiyefaa, tukitumia vifaa visivyofaa.
Kutumia Fimbo
Siku moja nilimsikia mtu moja akisema, “Ningetamani kuwa na fimbo kama ya Musa. Ningempiga
Amaleki jinsi Yoshua alivyofanya.” Habari ya ajabu! Unao fimbo kama ya Musa! Kila Mkristo ana fimbo
ya Mungu. Ukiwa na fimbo hiyo, unaweza kugawanya maji, kumshinda Amaleki, na kudai nchi ya ahadi.
58
Una fimbo mbili! “Fimbo zetu mbili za Mungu” ni sehemu yetu katika Kristo, na imani yetu kwa Yesu.
Hebu fikiri tena, kazi ya fimbo ya Musa ilikuwa nini?
Ilikuwa ni nguvu ya Mungu iliyowekwa kwa mkono wa mtu mwenye imani. Hivi leo, Mungu ametunuku
kanisa lake nguvu hizi. Anatupa fimbo mbili: ushirika wetu na Kristo, na jina la Yesu. Kwa sababu ya
kikao chetu katika Kristo, Mungu anatuomba tutarajie kusongeza milima. Yesu anasema tuombe “katika
jina langu.”
Tafsiri ya Wirnams kwa Marko 16:17 inasema, “Ishara hizi zitafuatana na waaminio; kwa kutumia jina
langu watafukuza pepo.” Jina la Yesu ni fimbo ya Musa kwa Mkristo. Kwa kutumia jina lake (kwa imani)
tunaweza kufukuza pepo. Kila moja wetu ana “pepo” wa aina fulani, ama Amaleki aliye kizuizi. Ni heri
tuwaondoe.
Tunaweza kufanya kama Musa kwa kutumia fimbo ambalo Mungu ametupa, yaani jina la Yesu Kristo
lenye nguvu. Kuungamanishwa naye na imani yetu kwa kuungamanishwa huku kunatupa uwezo dhidi ya
ulimwengu, mwili, na shetani. Inatuwezesha pia kumfikia Baba (Warumi 5:2) wakati wowote, usiku au
mchana.
Michango
1. Sura ya 9, Questions New Christians Ask (Old Tappan, New Jersey:
Fleming H. Revell Company, 1979). Pp.93 – 102
59
JINSI YA KUOMBA KWA IMANI
Imani si kuamini kwamba Mungu anaweza, ama ataweza, bali imani ya kweli ni kuamini kwamba
Mungu ameshatenda.
Je, umewahi kumwomba Mungu kitu kikubwa, na ukiisha sema “Amin,” ukawa na tashwishi kama kweli
utapata jibu? Labda ulisema, “Hawezi kujibu ombi hili.”
Kweli, ishakuwa hivyo kwangu – ni aibu. Mara nyingi Mungu ameniaibisha zaidi kwa kuyajibu maombi
yangu, ijapokuwa nilikosa imani. Yeye ni Mungu mkuu! Hata ingawa hivyo, Mungu anaheshimu maombi
katika imani. Maombi ni ufunguo wa kufungua mlango wa hazina za mbinguni. Imani humfurahisha
Mungu. Hebu sikiliza ahadi ya maandiko kuhusu maombi na imani:
Yesu akajibu, akawaambia:
“Mwamini Mungu. Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe
baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia,
yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba
mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” – Marko 11:22-24
Kwa kuwa Mungu ni Baba yetu, anapendezwa tunapomwamini. Anapenda tuamini neno lake. Hakuna kitu
kingine kinachompendeza kuliko imani ndogo kama ya mtoto mdogo. Waebrania inasema kwamba, “lakini
pasipo imani haiwezekani kumpendeza” (Waebrania 11:6).
Hii ni haki kabisa tunapomwendea katika maombi. Bwana wetu alitilia jambo hili mkazo katika Marko
11:22-24. Alituamuru tuwe na imani kwa Mungu. Anatuhimiza tuombe tukiwa na imani ili tupate tayari
majibu kwa maombi yetu. Maneno hayo yanatuonyesha Mungu alivyo. Anatamani kuwapa wanawe
wanaoamini mahitaji yao!
Kuomba, Kupiga kelele, na Kusikitika
Yesu anatuambia tumwendee Mungu kwa kuomba, kutafuta, na kubisha (Luka 11:9,10). Je, unaomba
ukiwa na imani sawa na ya mtoto anayefahamu upendo na wema wa baba yake? Nafahamu watu wengi
ambao wanapoomba, wanaenda mbele ya kiti cha enzi wakiwa na nia ambayo ni kinyume cha imani na
kumtegemea Mungu.
• Mwombaji. Huyu humwendea Mungu kama mwenye kuombaomba. Yeye husihi, huombaomba,
hubembeleza, hushurutisha, na kujaribu kumpokonya Mungu baraka alizofungia mkononi. Huyu mtu,
ijapokuwa ni Mkristo, hatambui yeye ni nani katika Kristo, na wala hatambui Mungu ni nani. Anahofia
Mungu, na kwa hivyo yeye ni mwombaombaji.
Nia hii si ile inayofundishwa na Kristo. Pia haina heshima kwa msalaba wa Bwana Wetu Yesu Kristo.
Hii humtia Mungu huzuni.
• Mpiga Kelele. Huyu hufikiri kwamba Mungu ni kiziwi! Paaza sauti, au Mungu hawezi kukusikiliza,
ama kukujibu. Umewahi kusikia mtu kama huyu kanisani – akiwa bila chombo cha kupaaza sauti!
Katika Yohana 14:14, Yesu alisema, “Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.” Tazama
alivyosema, “Mniombe,” wala si “mnipigie kelele.”
Wewe nami hatuhitaji kumpazia Mungu sauti zetu. Anayajua mawazo na shauku ya mioyo yetu. Kwa
moyo wa kunyenyekea na kwa imani ndogo, “tunaomba.”
• Mwenye Kusikitika. Mtakatifu hafifu hudhani kwamba lazima asikitike anapoenda kwa Mungu.
Anaomba hivi: “Oh, Mungu, niko hapa tena. Ndio, ni mimi, mimi tu yule niliyekosa!” Huyu huvaa
magunia na kujitia mavumbi akienda kanisani. Ana wingu la kulaaniwa kichwani mwake. Huomba
60
Hivi, “Ole wangu.” Ni haki kuhisi kuwa na hatia, na ni kitu cha kusikitisha. Kuwa na hatia
hutunyang’anya furaha katika Bwana. Katika kitabu changu, Questions New Christians Ask ,
tumejadili kwamba Mkristo hasimami mbele ya Mungu mtakatifu akiwa na hatia na hukumu. Hata
aliyeshindwa, au Mkristo anayeishi kwa kutimiza tamaa za mwili hajafukuzwa kutoka kwa uwepo wa
Mungu (labda ametenganishwa na raha Ya Mungu, lakini si uwepo wake).
Muumini
Hali yetu isiwe ile ya mwenye kuomba omba, mpiga kelele, au mwenye kusikitika tunapomwendea Mungu
kwa maombi, bali tuwe waumini walio na ujasiri. Ni kweli, tuna haki ya kuwa katika uwepo wa Mungu.
Warumi 5:2 inatueleza vyema: “ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo
mnasimama ndani …”
Kuna mambo mawili katika kifungu hiki ambayo yananifurahisha. Kwanza ni kuifikia. Hii inamaanisha
“kutambulisha,” kama vile kutambulishwa mbele ya mfalme. Ni kama barua ya kitambulisho.
Katika Kristo tuna haki kuifikia kiti cha enzi cha Mfalme wa vyote. Kwake tuna cheti cha kututangaza
kuwa wenye kufaa kwa sababu ya kununuliwa kwetu kwa damu ili tuwe na uhusiano na Kristo. Paulo pia
anasema kwamba “tumeifikia.” Neno ku inaonyesha hali ya kukamilika, kuliko hali ya kisasa kama vile
hutumika. Mkazo hapa ni kwamba milele tumewakilishwa kwa Mungu, na hakuna yeyote anayeweza
kubadilisha tukio hilo. Kila mara tunasimama kwa neema tukiwa tumependwa na Mungu milele! Huu ni
ukweli wa ajabu ya kuishi kwalo! Basi tuendapo kuomba, ni lazima tuamini kwamba tumekaribishwa
katika uwepo wake!
Unamwendea mfalme,
Ukimletea maombi makuu;
Neema na nguvu zake ni kwamba,
Huwezi kuomba zaidi.
Aina tofauti Za Imani
Sio Matakwa tu
Kwa sababu imani humpendeza Mungu sana na kumruhusu kufanya kazi katika maisha yetu, ni jambo la
maana sana kufahamu imani ni nini, na jinsi inavyofanya kazi. Imani ni neno ambalo lina maana tofauti
kwa watu mbali mbali. La maana ni kufahamu kile Mungu anachomaanisha anaposema “imani.” Ili
kujifunza vyema, ni vizuri kueleza kile ambacho si imani. Imani sio kuwa na matakwa, au kutumaini.
Isifananishwe na dhana nzuri. Imani inayoelezwa katika Bibilia si imani ndani ya imani, bali ni imani kwa
Mungu.
Watu mara kwa mara watasema, “Mungu anaweza kufanya jambo lolote,” na kusema ni imani. Ni kweli
Mungu anaweza kufanya lolote. Lakini hatuhitaji imani ili kuamini hayo. Huwezi kuenda mbinguni kwa
kutegemea imani kama hiyo. Je, kama yule mwivi aliyekuwa kando ya Yesu msalabani angesema, “Yesu
anaweza kuniokoa,” kusema hivyo kungemwokoa? Hasha! Hakuna imani iliyohusishwa, hakuomba ili
kupokea. Hata kumtegemea Mungu hakumo.
Watu wengine wana imani ya “Mungu ataweza.” Hii ni afadhali kuliko imani ya “Mungu anaweza” kwa
sababu mtu huyu anasema, “Mungu atatimiza mahitaji yangu. Mungu ataniokoa siku moja kutoka kwa
dhambi zangu.” Hata hivyo, mtu hawezi kwenda mbinguni kwa mawazo ya dhana kama hayo.
Kuamini kwamba Mungu atatenda jambo si sawa na kuomba na kudai kwa imani kwamba ametenda tayari.
Imani Kibibilia
Imani ya kweli ni kwamba “Mungu tayari” ametimiza matakwa yangu. Hi ni imani yenye maana ambayo
imeelezwa katika Waebrania 11: “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya
mambo yasiyoonekana” (Waebrania 11:1).
61
Imani si kutumaini, bali ni kuwa nayo. Kiini cha neno “kuwa na hakika” ni halisi, au hali halisi ya kitu,
kama vile tunaona katika Waebrania 1:3 kuhusu Kristo kuwa hakika ya Mungu mwenyewe. Nikiwa na
imani kwa kitu cha kubainisha, basi kinafanyika kuwa halisi katika maisha yangu. Nikiliamini, basi ninalo!
Si ajabu hilo? Ndio, ni kweli.
Huyu ni Yesu akifundisha katika Marko 11;24: “Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba
mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” Wakati ule ninapoamini kwa hakika, jibu li njiani, laja. Lugha
iliyotumika katika maandiko pale mwanzoni ina uzito mwingi kwamba tafsiri ya New American Standard
Bible inakosoa kwa usawa tafsiri iliyokubalika kutoka kwa “mtapokea” hadi “mmepokea.”
Kwa hivyo, mara tu unapoamini, tayari umepokea (hali ya kale)! Yesu ndiye aliyesema hayo, si mimi.
Imani ni kupokea. Mtu alieleza imani kibibilia hivi, “Imani ni kutenda kama ipo, hata kama haipo, na
itakuwepo.” Imani ni kubadilisha bayana kuwa yaliyopo.
Imani Na Mapenzi Ya Mungu
Yesu alituambia tuwe na “imani kwa Mungu.” Hi inahusu mpango na kusudi la Mungu kwa maisha yako.
Yeye ni Mungu Mkuu, mwenye enzi. Imani yote ulimwenguni haiwezi kubadilisha makusudi yake yenye
enzi. Watu walio na saratani wameamini kwamba Mungu angeponya magonjwa yao, ijapokuwa walikufa.
Waraka wa Kwanza wa Yohana 5:14 inafaa sana inapoeleza kwamba, “tukiomba kitu sawasawa na
mapenzi yake, atusikia.” Kifungu cha 15 kinatuhakikishia kwamba tukiomba (kwa imani) sawasawa na
mapenzi yake, “tunazo zile haja tulizomwomba.”
Tunapofahamu mapenzi ya Mungu alivyotufunulia katika maandiko, basi tunaweza kudai hayo kama ahadi
zake. Mungu tayari hutimiza mahitaji yetu kabla kutuahidi. Tunaweza kuishi au kufa kwa ahadi za Mungu.
Maombi ni kubadilisha ahadi za Mungu kuwa riziki kila siku.
Siguswi Mimi!
Wakati moja nilikaa Romania kwa majuma mawili. Nilifwatwa na maaskari makachero kila nilipoenda.
Wachungaji niliokuwa nikifanya kazi nao waliishi kwa kuhofia usalama wao. Nilimuuliza mmoja wa hao
wachungaji wajasiri jinsi walivyoweza kulala usiku. Je, alihofia maisha yake? Akiwa na tabasamu kama ya
malaika, alinijibu, “Mimi siwezi kuguswa. Ikiwa Mungu angali amenipa kazi ya kufanya, askari hawana
uwezo wa kunidhuru.” Nililengwalengwa na machozi. Nilihisi kuwa na aibu na kiburi. Nikakumbuka
maneno ya Daudi, “BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? BWANA ni ngome ya
uzima wangu, nimhofu nani?” (Zaburi 27:1).
Huyu mtu wa Mungu mpendwa alikuwa kama Danieli katika tundu la simba, lakini moyo wake haukuwa
na hofu kwa sababu Mungu aliahidi kufunga midoma ya simba. Hebu tukumbuke hayo tunapoomba.
Tunahitaji kudai yote ambayo Mungu ameahidi katika neno lake kama riziki. Imani ni kumwamini Mungu
kwa neno lake, na kumtarajia kutimiza yale amesema atatimiza.
Imani Ni Kutafuta
Je, kuna mambo unayoyatumainia, au kutamani, au kuota? Je, utafanyaje ili ndoto yako ikamilike?
Kwanza, ondoa yale ambayo si mapenzi ya Mungu, bali ni tamaa yako tu. Pili, amini ahadi rahisi kama vile
Wafilipi 4:19; “Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu,
ndani ya Kristo Yesu.” Mungu hakuahidi kunipa mahitaji yangu yote; Ameahidi kunijazia kila
ninachohitaji. Waebrania inasema kwamba imani ni “bayana ya mambo yasiyoonekana.” Ikiwa unahitaji
lililo la haki, utawezaje “kuona” bayana ya hitaji hilo unalolikusudia kutimizwa?
Riziki ya Mungu, Kimiujiza
Nilikuwa ningali mgeni katika chuo kimoja, ambapo nilianza kuona Mungu akinipa riziki kwa njia ya
miujiza. Nilihitajika kulipa kodi katika chumba nilichokuwa nikikaa pamoja na rafiki yangu mmoja.
Tulikosa hela ya kulipa kodi kwa muda wa mwezi moja. Je, kodi hii ingetoka wapi? Tuliacha kuangaikia
jinsi ya kupata fedha hizo. Tukaanza kuomba, kama jaribio la mwisho. Nilikuwa kijana wa miaka 19
ambaye alikuwa na matarajio ya kuwa mhubiri. Nikaomba Baba yangu aliye mbinguni anipe kodi!
62
Wiki hiyo nilipata barua kutoka kwa Huduma Ya Misitu Ya Amerika. Barua hiyo ilikuwa na hundi ya
kulipa kodi! Kwa kweli, hundi hiyo haikuwa ya kodi, bali ilikuwa yangu! Mwaka iliyopita, wakati wa
kiangazi, niliitwa kuzima moto kule Oregon. Tuling’ang’ana kuzima moto usiku na mchana. Sikufahamu
kuwa serikali hulipa watu kwa kuzima moto! Kwa hivyo, miezi mingi baadaye nikapata hundi kupitia
posta. Ni juma hilo tu ambalo nilimwomba Mungu anitimizie hitaji ambalo lilikuwa ngumu!
Imani ni kuona mahitaji yako yakitimizwa. Tunapomwamini na kumwomba Mungu, atajiheshimu kwa
kutimiza neno lake. Rafiki yangu Mkristo, hatupati kwa sababu hatuombi. Amini na kumwomba Mungu ili
akutimizie. Tunaweza kupata yote tunayohitaji ikiwa tutaamini kwamba Mungu ameshatutimizia.
Kuona Ni Kuamini
Kuna vikundi viwili vya watu ambao wana imani aina mbili tofauti. Kikundi cha kwanza ni cha “kuona ni
kuamini.” Katika Yohana 20:25 Tomaso alisema, “Mimi nisipoziona…mimi sisadiki.” Ilimlazimu kuona
Bwana aliyefufuka kabla kusadiki kwamba Bwana alifufuka. Tomaso alikuwa na imani iliyojengwa kwa
hisia. Tunasema, “Bwana nipe ushindi, nami nitasadiki kuwa ninayo ushindi huo.” HIYO SI IMANI! Hiyo
ilimsababisha Yesu kusema sadiki kwamba tayari umepokea, ndipo utapata.
Yesu hakusema Tomaso alifanya vizuri. Alisema, “wa heri wale wasioona, na hawahitajiki kuona -
wakasadiki” (Yohana 20:29, maneno ya mwandishi). Hiyo ni imani iliyo sambamba na maandiko.
Tunahitaji kuondoka katika eneo la hisia, na kuingia katika eneo la Bibilia. Hapa ndipo tunagundua
kwamba “imani ni kuona yale ninayotumaini.” Nikiwa na hakika kwamba nimepokea yale nimeahidiwa na
Mungu, basi NITAONA ninayoyatumaini! Nasema tena, hii ni imani inayookoa. Hukumwona Yesu akifa
na kufufuka siku ya tatu; uliamini neno tu. Hiyo ndio hakikisho uliyohitaji. Uliliamini neno, alafu
ukamwona Yesu na kupata msamaha wake. Imani ni kufanya kama kwamba imetimika, wakati ambapo
haijatimika bado, nayo itatimika!
Imani ya Mwenye Ukoma
Katika Luka 17, tunaona wenye ukoma 10 waliomwendea Yesu wakipaaza sauti kwa kusema, “Ee Yesu,
Bwana Mkubwa uturehemu! Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa
walipokuwa wakienda walitakasika.” Mwenye ukoma aliyetakasika ni lazima ajionyeshe kwa kuhani ili
ithibitike kwamba ameponywa kweli. Yesu aliwaambia waende kwa kuhani kabla kuponywa kwao. Je,
kama wangalisema, “Bwana, hatuwezi kwenda kwa kuhani, kwani hatujaponywa bado”? Yesu, kwa kweli
alisema, “fanya kama kwamba imetimika, ijapokuwa haijatimika bado, nayo itatimika.” Waliamini na
kuelekea hekaluni, na “walipokuwa wakienda, walitakasika”…Kisha akawaambia, “imani yako
imekuponya.”
Ushindi Na Imani
Waraka wa Kwanza wa Yohana 5:4 inafananisha ushindi katika maisha na imani kwa Mungu. “Kwa
maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako
ulimwengu, hiyo imani yetu.” Kwa hivyo, ushindi umepatikana tayari! Unao ushindi kwa kuamini kwamba
Yesu tayari ameshinda (1Yohana 5:5).
Labda utasema, “Je, unamaanisha kwamba nina ushindi dhidi ya kila shida kwa kuamini tu kwamba ninao
ushindi?” Hiyo ni kweli! Ni kweli kabisa! Unasema, “Siamini hayo!” La, nawe hutapata ushindi kamwe!
Amini hayo, nawe utapata ushindi! Imani ni ushindi! Yesu Kristo tayari ameshinda adui wote: yaani
ulimwengu, mwili, na shetani (Waebrania 2:14; Wakolosae 2:14,15; 1 Yohana 3:8,4:4). Huna vita vingine
vya kushinda. Yesu alishinda vyote miaka 2000 iliyopita. Ukiyaamini hayo, kuyasimamia imara, na
kuyadai, basi ushindi wake utakuwa wako!
Imani hii ya “Mungu ameshashinda vita” hutupa wokovu. Ni lazima uamini kwamba Mungu ameshatupatia
wokovu ndani ya, na kupitia kwa Yesu Kristo. Aliyepotea dhambini lazima amjie Mungu na kupokea yale
Mungu ametenda kwa kutubu dhambi, na kusema “Ahsante Yesu, ishatendeka.” Jinsi ulivyopata wokovu
ndivyo utakavyopata ushindi na mwongozo wa kila siku. Ukiwa na imani, basi una bayana. Kwa hitaji
lolote, amini kwamba ni yako, nawe utapata.
63
Mungu akuzidishie katika maombi na kuamini kwako.
“Bwana, tufundishe kuomba kwa imani, tukidai yaliyo yetu katika Kristo.”
Michango
1. Tazama Luka 11:9-13
2. Sura ya 4, “Can a Christian Lose His Salvation?” inaongea kuhusua kuwa na hatia na msamaha kwa
kinaganaga.
64
65
MBONA TUNAOMBA KATIKA JINA LA YESU?
Kuomba katika jina la Yesu, kwa Muumini, ni njia ya kumfikia Mungu Baba. Imani yetu katika
hilo jina takatif u hutuwezesha kuifikilia chumba cha enzi.
Nilipokuwa kijana mdogo, wazazi wangu walianza kunifundisha dini kwa kuniorodhesha katika shule ya
Wakatoliki wa Kirumi. Miaka yangu mitatu katika masomo yalitokana na msingi huo wa elimu. Ombi la
kwanza ambalo nakumbuka kuomba ni ombi la kukariri “neema” wakati wa chakula nikiwa katika shule
hiyo.
Watoto wengi Wakatoliki hukariri ombi hili fupi kwa Mungu wakatika wa kwenda kulala, wakisema,
“Tubariki, Ee Bwana, kwa vipawa hivi ambavyo tuko tayari kupokea kutoka kwa utajiri wako, kwa Yesu
Kristo Bwana wetu. Amin.”
Hilo ndilo lilikuwa ombi langu la kwanza. Ombi hili si mbaya. Sehemu ya mwisho katika ombi hilo
ilinifurahisha sana, “kwa Yesu Kristo Bwana wetu.” Nilipoendelea kuwa mkubwa, nilianza kusikia
wengine wakimaliza maombi kwa kusema “Katika jina la Yesu. Amin.” Nikaanza kuwaza na kuwazua
“kwa nini” wanaomba “katika jina la Yesu.” Nikawa mtu mzima kabla moyo wangu kukubali ukweli wa
maneno hayo.
Ombi Rahisi
Yesu alikuwa akiwapa wanafunzi wake funzo kamili kuhusu utiifu, Roho Mtakatifu na maombi katika
Yohana 1:16. Katikati ya mafundisho hayo, mara tatu Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuomba Mungu
“katika jina langu”: “Amin, amin, nawaambia, mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu.
Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu” (Yohana
16:23,24). Kristo tayari ameshawishi jambo hili katika sura ya 14, na akarudia katika sura ya 15 (Yohana
14:13,14 na Yohana 15:16). Kurudia huku kulimaanisha kutilia mkazo kanuni hii rahisi: kukaribia moyo
wa Mungu ni kupitia kwa jina la Mwanawe.
Kukosa Kuomba ni Kukosa kupokea
Fundisho hili lilikuwa la kipekee, na geni kwa wanafunzi wa Kiyahudi. Katika historia yao, hawakuwahi
kumwomba Yehovah Mungu katika jina la mtu! Ndio sababu Yesu alisema, “Hata sasa hamkuomba neno
kwa jina langu” (Yohana 16:23). Hili ni fundisho linalobadilisha. Ni kiini cha theologia ya Kikristo. Yesu
anasema kwamba kuna njia jipya ya kufika kitini pa enzi kwa Mungu, ambalo halijapitiwa na mtu
mwingine awaye yote. Kuna nambari ya siri ya simu mpya isiyojulikana na yeyote, ya kwenda kwa kiti cha
enzi cha Mungu. Hebu piga simu hiyo! “Hata sasa, hamjamwendea Baba kwa jina langu. Sasa fanya hivyo
naye Baba yangu atakupa kila hitaji lako,” asema Bwana Yesu.
Hili laonekana kuwa kinyume, lakini sivyo kamwe! Hadi wakati huo, hakuna aliyewahi kumwomba Mungu
“kwa jina la Yesu.” Labda hii haikufanywa na wafuasi wa kwanza wa Kristo hadi baada ya Pentekote.
Iligharimu uchochezi wa Roho Mtakatifu, aliyekuwa akiishi ndani yao, kuwafanya kuomba katika jina la
Yesu.
Hivi sasa watu wengi wanaomba maombi kila siku, yakiwa maombi ya kukaririwa, na kuyamaliza kwa
“jina la Yesu” bila kumaanisha. Kanisa likifahamu uwezo na nguvu iliyoko katika jina la Yesu, basi
maombi yetu yataleta Pentekote mara nyingine. Kanisa la kwanza lilichochewa na imani katika hilo jina la
Yesu. Jina hilo litaweza kuwasha imani na moto katika moyo wako ikiwa utatambua kwa nini Mungu
anaheshimu jina la Yesu.
66
Katika Jina Langu
Mbona uombe katika jina la Yesu? Mbona si Budha, au Allah, au mwalimu mwingine shupavu wa dini, au
nabii? Kuomba katika jina la Yesu ni kukubali malipo ya dhambi zetu ambazo Kristo alilipa pale msalabani
ili tuweze kuifikia uwepo wa Mungu. Kama vile Wayahudi hawangeingia Patakatifu bila gharama ya damu
(kwa Yom Kippur), ndivyo mwenye dhambi hawezi kuingia katika uwepo wa Mungu bila damu
iliyomwagika ya Yesu Kristo. Ni kupitia kwa kifo chake, kuzikwa kwake, kufufuka kwake, na kupaa
kwake mbinguni ndipo tunaweza kuwa na uhusiano wa Baba-Mwana pamoja na Mungu. Mwenye dhambi
asiyekuwa na mwokozi hana tumaini la msamaha wa dhambi.
“… Vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo…kwa sababu
Kristo hakuingia patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali
aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu” (Waebrania 9:22,24), na
“Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu” (Waebrania
10:19).
Hiyo ndio sababu tunasogelea kiti cha enzi cha Mungu katika jina la Yesu. Tunaomba kwa kuwa yeye ni
mwadilifu. Ni kama kumwambia Mungu, “Mungu, siombi kwa sababu ya jinsi nilivyo ama kwa ajili ya
uzuri wangu. Naomba kwa sababu Yesu alisema nije kwako na kukuambia amenituma. Alisema utajibu
maombi yangu kwa ajili yake, wala si kwa ajili yangu.”
Ghala La Baba
Ukienda sokoni na kununua vyakula vyote unavyohitaji nyumbani mwako, na mahitaji mengine. Ukaenda
kulipa ukiwa na vikapu kumi vilivyojaa vyakula, na vitu vingine ulivyonunua. Muuzaji akahesabu gharama
ya vitu vyote ulivyonunua. Unagundua kwamba vimegharimu pesa kiasi kikubwa. Muuzaji anakuangalia
kwa mshangao na kukosa kukuamini. Tuseme labda kiasi cha pesa unazohitajika kulipa ni $5000. Kisha
unamwambia huyu muuzaji, “Hebu nipe cheti hicho niweke sahihi.” Anapigwa butwaa na kukuuliza,
“Uweke sahihi? Kwani unafikiri wewe ni nani, mwenye soko?” Alafu unamjibu, “La hasha, kwa hakika
mimi si mwenyewe, lakini baba yangu ndiye mwenye soko. Mimi ni mwanawe wa pekee. Nitaurithi mali
yake yote.”
Yesu alimaanisha hivyo alipotuambia tuombe kwa jina lake. Yote ya Mungu Baba pia ni ya Mwanawe wa
pekee. Yesu ndiye mwenye soko, akiwa pamoja na Baba yake. Amemwambia Baba yake kwamba
tunaweza kuweka sahihi cheti katika jina lake. Baba anaheshimika kujibu maombi yako katika jina la Yesu,
kama vile Kristo mwenyewe angeweza kuomba. Muumini ameshikamanishwa na Kristo kiasi cha kwamba
kuomba kwetu ni kuomba kupitia kwa Roho wake aliye ndani yetu. Huu ni ukweli wa ajabu!
Kutumia Fimbo Ya Mungu
Tumetazama Mwanzo 17, na “fimbo ya Musa ya Mungu.” Tumeona kwamba fimbo yetu ni imani katika
jina la Yesu. Katika Marko 16:17, Yesu ametuambia tutumie jina lake hata kwa kuwatorosha mapepo.
Inasisimua kuona wanafunzi wa Yesu wakitenda yale Yesu alihubiri.
Baada ya Pentekote, Petero na Yohana walienda hekaluni kuomba. Yesu amerudi kwa Baba, lakini Roho
Wake sasa anakaa ndani yao. Wakiwa nje ya hekalu, Petero na Yohana walikutana na kilema ambaye
alikuwa akiomba pesa kutoka kwa wale waliokuwa wakienda hekaluni kusali. Petero aliwaza akiwa
ameshurutishwa na Roho wa Yesu aliyekuwa ndani yake: “Petero, tumia fimbo yako. Tumia jina langu.
Mwombe Baba. Ona muujiza.” Petero, kwa msukumo, akamwambia yule kilema, “Mimi sina fedha, wala
dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende.”
(Tazama Matendo 3:1)
Kwa hivyo, kwa mara ya kwanza mmoja wa wanafunzi kumi na wawili wa Yesu alifanya kitu. Waliamini
maneno ya Yesu na kutumia jina lake. Walisogelea eneo la miujiza. Baadaye Petero na Yohana
walipoulizwa na viongozi wa Wayahudi jinsi huyu kilema alivyoponywa, kwa furaha walijibu, “na imani
67
ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote” (Matendo 3:16). Iweke
imani yako katika jina la Yesu na Mungu ataweka jina lake, na nguvu zake, katika imani hiyo.
68
69
VITA VYA KIROHO NI NINI?
“Shetani ana nguvu za kushikilia jibu kwa muda fulani ili kuchelewesha matokeo. Hana nguvu za
kuzuia matokeo kabisa, ikiwa mtu ataelewa na kuomba kwa uthabiti pasipo kukoma. Maombi
mazito yanastahili kuelekezwa dhidi ya shetani.”
S.D. Gordon, Quiet Talks on Prayer
Maisha ya Kikristo ni maisha ya vita. Mkristo ni sehemu ya mng’ang’ano wa milele kati ya mema na
mabaya. Kuwa mwana wa Mungu ni kupigana dhidi ya nguvu za giza siku zote za maisha yako. Ni watu
wachache sana ambao wanafahamu mgongano huu wa kiroho.
Washirika wengi wa kanisa hukaa kana kwamba adui amekufa na wao hatimaye wamefika Sayuni. Mtu
mmoja alisema kuwa meli ya zamani ya Sayuni si merikebu ya kustarehe ambapo tunasafiri kwa furaha
hadi ufuoni mwa mbinguni, bali ni merikebu ya vita ambapo tunamkabili adui Shetani kila siku.
Vita hivi vya kiroho ni nini basi? Adui ni nani ? Silaha zetu ni zipi? Vita hivi hupiganwa vipi? Tutatafuta
majibu kwa hayo maswali kutoka kwa neno la Mungu.
Adui
Paulo, akiandikia waumini wa Efeso, anaongea kuhusu vita vya kiroho, na asili ya adui: “ Hatimaye, mzidi
kuwa hodari katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza
kuzipinga hila za shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme
na mamlaka; juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”
(Waefeso 6:10-12).
Shetani ndiye adui wetu mkubwa. Yeye ni malaika mkuu aliyeanguka ambaye moyo wake umejaa chuki
dhidhi ya Bwana Yesu na ufalme wake. Shetani ni mtawala wa roho katika ufalme wa giza. Anaongoza
“nguvu za uovu wa kiroho ulimwenguni.” Kuamini, au kutokuamini kwako kwa shetani au nguvu za pepo
ina mwelekeo katika ushindi wako, au kushindwa kwako katika pambano. Kujifanya kwamba hakuna adui
ni kuhakikisha kushindwa kwako. Watu wasioamini kwamba shetani yuko wana Shetani ndani yao kuliko
mtu yeyote mwingine!
Vita vya “Roho”
Tazama kwamba maandiko yanaeleza asili ya vita hivi kuwa vya “kiroho.” Hatupigani katika ulimwmengu
wa mwili - “kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama.” Hivi ni vita visivyoonekana dhidi ya maadui
wasioonekana - Shetani na mapepo, au washirika wake. Waumini wengi wanapoteza vita hivi kimakosa
kwa sababu hawajajitokeza kwa vita. Shetani anashinda bila kupingwa kwa sababu wakristo wanakataa
kupigana katika hivi vita vya “roho.” Tilia mkazo maneno haya: hivi vita ni vya roho, wala si vita vya
mwili. Majengo na makisio ya makanisa hayawezi kushinda vita hivi.
Kamati na fadhili za kanisa haziwezi kushinda “uovu wa kiroho katika ulimwengu wa roho.” Jambo
ambalo lazima tuelewe ni kwamba matatizo yetu hayana asili kwa yale tunayoyaona, ijapo yanaonekana
kuwa hivyo. Kuna shida ya ndani kwa roho katika kila tatizo la mwili. Mwili ni chombo tu
kinachotumiwa na roho. Mathayo 16: 21-23 inatuonyesha ukweli huu. Baada ya Yesu kutabiri juu ya kifo
chake kule Yerusalemu, Simoni Petero alimwambia, “Hasha Bwana, hayo hayatakupata” (tazama kifungu
cha 22). Hebu tazama jinsi Yesu alivyomkemea “nenda nyuma yangu Shetani…” Bwana wetu hamkemei
Petero, bali anakemea nguvu za pepo zilizoko nyuma ya maneno ya Petero. Shetani alizumgumza kupitia
kwa mawazo na sauti ya Petero. Tatizo halikuwa Petero, bali nguvu zilizokuwa nyuma yake, yaani shetani.
Kila mara tatizo haliko katika yale yanayoonekana, bali katika nguvu za roho zitendazo kazi nyuma ya
matendo yanayoonekana katika mwili.
70
Kila siku tunapigana vita vya roho, ambavyo havionekani. Katika Waefeso, Paulo anaeleza “kushindana”
kwetu. Tafsiri ya mfalme Yakobo (The King James Version) inatafsiri hili neno kama “mweleka,” ambalo
lina maana ya kupigana mkono kwa mkono. Vita hivi ni vita vyako binafsi. Kuokolewa ni kujihushisha
katika kushindana dhidi ya nguvu za ulimwengu wa giza. Kama Mkristo unahusika; upende, usipende. Ni
jambo la kuhuzunisha kwamba wakristo wachache wana habari juu ya vita hivi. Shetani ana juhudi
kumshinda kila Mkristo. Ni asili yake kumshinda Mkristo pasipo Mkristo kutambua uwepo wake.
Silaha za roho
Ikiwa tutapigana vita vya roho, basi tutahitaji silaha za kiroho. Silaha zetu lazima ziwe na uwezo wa
kukabiliana na adui wetu pamoja na mbinu zake . Paulo anaeleza juu ya silaha za Mkristo anaposema:
“Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kishindana siku za uovu, na
mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii
ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tapatao kwa injili ya amani: zaidi ya yote mkiitwaa
ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote ya moto wa yule mwovu. Tena
ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa roho ambao ni neno la Mungu (Waefeso 6:13-17).
Hii ni picha ambayo ni mfano unaotuhusu; wewe na mimi. Tumevalishwa mavazi ya vita, pamoja na silaha
kamili tukiwa tayari kabisa kwa vita. Mshipi wa kweli, dirii ya haki, viatu vya vita, ngao ya imani, chepeo
ya wokovu, na upanga wa roho ndizo silaha zako. Mavazi ya silaha za ajabu! Umeimarishwa kwa vita vya
mkono kwa mkono na Shetani mwenyewe. U tayari; nionyeshe vita, na kunipeleka katika msitari wa
mbele. Hebu tuvianze vita basi! Sawa. Hapa kuna vita. Sikiliza maneno ya Paulo katika aya inayofuata:
“kwa sala zote na maombi; mkisali kila wakati katika roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika
kuwaombea watakatifu wote” (Waefeso 6:18).
Maombi ndio vita
Sasa, je waweza kuzidisha hayo? Umevalishwa, na kutayarishwa kupigana vita. Naye Paulo anakuambia
uombe! Omba? Sawa kabia, omba. Hata ingawa inavunja moyo, maombi ndio vita. Silaha ni maandalizi tu
ya maombi. Mwanajeshi Mkristo ni mwanajeshi wa maombi. Vita hivi vya roho hupiganwa na jeshi
liendalo kwa magoti. Adui wetu ni wa rohoni. Hivyo basi ni lazima tutumie silaha kuu za roho dhidi yake.
Maombi ndio njia ya kuwa katika pambano la kiroho. Hapa ndipo makanisa mengi na viongozi Wakristo
wanakosa wakiwa vitani. Tumedhani kwamba matatizo yetu yanatokana na ukosefu wa fedha, rasilmali, au
utaratibu. Kama kanisa letu lingekuwa na hili au lile, basi tungelimfanyia Mungu mambo makuu. Mungu
utusaidie! Hatuwezi kumshinda shetani kwa majengo, makadirio, au makombora. Tunaweza tu kumshinda
mwovu kwa nguvu za maombi pekee. Mungu ametumia mbinu hiyo wakati wote.
Mweneza Injili na Uamsho
Mimi ni mweneza injili. Nimehubiri katika mamia ya makanisa, nikizunguka ulimwenguni. Ni mara
chache sana ambapo kanisa limeamini kwamba maombi ndio vita. Ili kujiandaa kwa ajili ya kuhubiri juma
nzima, mchungaji wa kadiri huweka matangazo kwa karatasi, kwa runinga, na mabango katika sehemu za
biashara, akitangaza mkutano wa hadhara wa injili ujao. Atatumia sarakasi na vifaa mbalimbali kuvuta
watu wahudhurie mkutano huo wa injili. Haya yote ni mema na sawa, bali ni juhudi za mwili. Lakini vita,
kwa kweli, ni vya roho!
Ni mara chache sana ambapo kanisa limevaa silaha na kwenda vitani katika maombi. Naongea juu ya
maombezi ya kweli. Aina hii ya maombi hutufanya “kuingia kwa mapango” na “mweleka” wa mkono kwa
mkono mpaka ushindi upatikane. Ni rahisi kwenda kumsikiliza mwinjilisti akihubiri. Lakini ni vigumu sana
kudumu katika maombi, ukiamini. Tunashangaa kwa nini Mungu hatembei kwa jinsi ya ajabu miongoni
mwa watu kupitia kwa Roho wake, hali tumeiacha hatua hii muhimu ya kwanza. Miaka kadhaa zilizopita
nilihubiri katika nchi ya Rumania, ambayo ni nchi ya kikomunisti. Tulihubiria umati upatao watu kati ya
elfu tatu na elfu nne kila usiku kwenye jumba ambalo linaweza kukaliwa na watu mia nane tu. Hakukuwa
na matangazo kwenye magazeti, runinga, na mabango. Mkutano hao ulikosa kuchochewa, kwa sababu ni
hatia katika nchi ya kikomunisti kuchochea dini kwa kuutilia mkazo. Kwa hakika ilikuwa baraka isiyo na
kifani! Nilikuwa karibu kutamani dini iwe hatia katika nchi za magharibi. Basi pengine hatungeegemea
mwili, bali tungelazimika kumtegemea Bwana. Katika Rumania, waumini hukutana na mfalme wa giza kila
71
siku. Lazima wang’ang’ane ili waishi. Maombi ndio njia moja wanayotumia kama silaha kuu ya kurarua
ngome za shetani. Maelfu wanamgeukia Kristo licha ya upinzani mkubwa na mateso. Maombi ndio vita.
Tunapokosa kuomba, tunapoteza ushindi kimakosa.
Maombi na Uinjilisti
Uinjilisti ni vita vya kiroho vinavyoshindwa kwa maombezi. Mwenye dhambi anapozaliwa katika ufalme
wa Mungu, hakika ni kwamba mtu mwingine alimwombea. Mtu alisimama “katika pengo” kwa ajili ya
nafsi hiyo iliyokuwa imepotea. Ni kwa kumfukuza adui kutoka kwa uwanja wa vita wa moyo wa
mwanadamu ndipo hutokea uhuru kwa mwenye dhambi kuitikia neema ya Mungu. Kuhubiri, kushuhudia,
ratiba, na kazi zote za kanisa zinafaa na kuhitajika; lakini hivi si vita vyenyewe. Shetani hutuogopa sana
tuchukuapo silaha za roho na kuzitumia dhidi yake katika maombi.
Hapo mapema tulitaja mfano wa Musa na Yoshua wakipigana na Amaleki. Vita hivi vimeandikwa katika
kitabu cha Kutoka 17: 9-16. Yoshua alipokuwa akipigana vita kule nyikani, Musa alikuwa akimwombea
kule mlimani. Musa allikuwa akipigana vita vya kweli dhidi ya nguvu za roho za uovu, ambazo zilimtia
nguvu mfalme wa Amaleki, aliyekuwa mwabudu sanamu. Musa anamwombea Yushua, ambaye anazidi
kushinda dhidi ya Amaleki. Kwa kupigana vita vya roho, Musa alirahisisha ushindi wa Yoshua dhidi ya
Amaleki (Kutoka 17:13).
Shetani hupinga Maombi yetu
Mwana wa Mungu aliyejazwa na roho anapoanza kuomba kwa thati, shetani hutetemeka. Anajua maombi
kama hayo yanatokana na Mungu, wala si ya kawaida. Yanamuusisha Mungu katika pigano. Shetani
hawezi kushinda dhidi ya silaha kama hiyo. Hii ndio sababu Shetani atapinga vikali maisha yako ya
maombi. Je umewahi kugundua jinsi ilivyo vigumu kutumia muda wako katika maombi? Tunapata muda
wa kuhusika kwa ratiba nyingine za “dini,” kama vile kuhudhuria kanisa, kuhudhuria darasa la Bibilia, na
kushuhudia mara kwa mara. Lakini tunapata pingamizi katika kukutana na Mungu kwa maombi. Hii ni kazi
ya Shetani. Akiweza, atazuia maisha yako ya maombi. Elewa kwamba maombi ni vita!
Daktari Stephan Alford alikuwa mchungaji wa kanisa la Calvary Baptist katika jiji la New York kwa miaka
mingi. Wakati moja nilimsikia akieleza jinsi Shetani alivyompinga katika maisha yake ya maombi. Alisema
kwamba kwa miaka mingi hangeweza kuelewa kwa nini mawazo yake yalitangatanga ovyo ovyo wakati
wa kuomba. Kila mara alipata mawazo maovu ya chuki au tamaa yakipenya katika maombi yake.
Mwishowe alitambua kuwa ilikuwa ni vita. Alitambua kwamba mawazo haya yalikuwa “mishale ya moto”
iliyolengwa kutoka kwa uta wa Shetani ili kuharibu mombezi na maombi yake. Kuomba ni zaidi ya
kukutana na Mungu. Ni wakati wa kumkabili adui. Haimaanishi kwamba katika maombi tunaongea na
Shetani. Mungu asituruhusu kamwe! Yupo kutupinga, na ni lazima tukabiliane naye. Katika sura lingine,
tunazungumzia hili swala la kukabiliana na Shetani kwa “kufunga na kufungua,” kama iliyotajwa katika
Mathayo 18:18. Hebu sasa tufahamu kwamba Shetani hupinga maombi yetu. Anaweza hata kuchelewesha
majibu kwa maombi yetu. Mfano dhahiri inayoonyesha kwamba maombi ni vita vya kiroho iko katika
Agano la Kale. Danieli 10:13 inasimulia kijana nabii Danieli akichukua majuma matatu katika kufunga na
kuomba. Baada ya muda huu wa makabiliano makali ya kiroho, Malaika anatokea, akiwa ametumwa kama
majibu kwa maombi yake.
Mungu hajawahi kutuma Malaika ninayeweza kumwona akiwa na majibu kwa mojawapo ya maombi
yangu. Hata hivyo sijawahi kuomba na kufunga kwa dhati kama alivyofanya Danieli. Malaika alimwambia
Danieli jambo la kupendeza, akisema, “Usiogope Danieli kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia
moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa, nami nimekuja
kwa ajili ya maneno yako” (Danieli 10:12). Fahamu hili andiko “tangu siku ile ya kwanza.” Malaika
alianza kumwendea Danieli tangu siku ya kwanza alipoanza kuomba. Kwa nini ilimchukua majuma matatu
kumfikia? Malaika anaeleza maana ya kuchelewa kwake katika aya inayofuata: “Lakini mkuu wa ufalme
wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja, bali, tazama huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele,
akaja kunisaidia…”
Hili ni jambo linalotatanisha! Danieli anaomba. Lakini katika ulimwengu usioonekana, vita vinaanza.
Mungu anatuma Malaika (mjumbe) kumjibu Danieli, bali mkuu wa Uajemi (jina lililopewa Shetani hapo
72
kale), anampinga. Kwa siku ishirini Malaika alipigana na Shetani mwenyewe, kwa sababu Danieli alikuwa
akiomba na kufunga! Malaika hakuwa na nguvu kumzidi Shetani. Mungu akawajibika kumtuma Mikaeli,
ambaye ni malaika mkuu, kumaliza mapigano. Ushindi ukapatikana. Shetani alikuwa akizuia jibu kwa
maombi ya Danieli.
Ama uchukue maandiko haya kuwa mfano tu, au ukweli, jambo moja li wazi kwamba kuomba hutuweka
katika ulimwengu wa roho ambapo vita kamili vipo. Maombi ni vita, na kwa hivyo, Mungu anaitilia
maanani hata kumhusisha malaika. Maombi yako yanaweza kuchochea jeshi la mbinguni yakiombwa kwa
imani na uwazi. Maandiko yanatuambia Malaika wa Mungu ni Roho watumishi wanaotumwa
kuwahudumia wale wanaogusa yasiyo ya kawaida katika maombi yao (Waebrania 13-14).
Mwito wa kujiami
Kiini cha huduma ya kanisa ni maombi halisi. Kuomba ni zaidi ya kushukuru Mungu, au kumuuliza vitu.
Maombi ni mwito wa kujiami. Ni jambo zito. Kupitia kwa maombi, tunagusa mbingu na kushambulia
kuzimu. Waliodhaifu moyoni, au katika imani hawawezani nalo.
Mambo yaliyosalia katika kitabu hiki yanahusika na “mambo ya ndani” ya maombezi na vita. Waweza
kufikiri tayari tuko ndani sana katika masomo haya, lakini bado. Tujiunge tena na Paulo katika ombi lake
kwamba “macho ya moyo wako yatiwe nuru.” Bwana, tufundishe kuomba.
73
KUWA SHUJAA WA MAOMBI
Kuna upungufu mkubwa sana kwa utumikaji wa maisha iliyojazwa na roho mtakatifu ikiwa
maisha hayo hayatoi ujuzi muhimu katika kiwango cha maombi.
--Arthur Wallis, Pray in the Spirit
Kila Mkristo ana haki na uwezo wa kuomba. Ingawa hivyo, kila Mkristo hajajiandaa kuingia katila vita vya
roho. Mambo ya ndani ya uombezi na maombi yametengewa walio na ujuzi katika mambo ya roho. Kama
vile mwanajeshi mchanga anavyoenda kujiunga na kikosi kwa mafunzo, mkristo ni lazima “avae silaha
zote za Mungu” kabla ya “kuwa hodari katika Bwana na nguvu za ukuu wake” (Waefeso 6:11,10).
Kikosi Cha Mafunzo cha Maombi
Silaha ambazo Paulo anazungumzia katika Waefeso 6: 1-17 kwa hakika ni maandalizi ya maombi. Kwa
sababu maombi ni mahali ambapo tunakutana na Mungu na pia kukabiliana na Shetani, lazima tujiandae
kwa kuvaa silaha zote za Mungu. Mtume Paulo anatupa shauri la kweli kwa kujiandaa kwa huduma ya
maombi, kwa:
• “Kusimama imara.”
• Kutumia “upanga wa roho.”
• Kuomba “katika roho.”
Omba Ukisimama Imara
Tunahimizwa kusimama imara dhidi ya “mbinu za shetani” (Waefeso 6:11) kwa kuvaa silaha zote za
Mungu. Kile Paulo anamaanisha ni kwamba msingi wetu wa maombi lazima uwe kazi iliyomalizika ya
Kristo. Ushindi wetu ni ule ambao Yesu alipata msalabani. Pia, ni lazima tuishi maisha ya utakatifu na
utiifu mbele za Mungu. Tumevalishwa dirii ya haki na viatu vya kuonyesha utiifu wetu, ya kuenda
anapotuamuru kuenda. Kwa hivyo tunaomba tuwe katika hali itupayo nguvu. Tunaweza kuomba kwa
ujasiri.
Katika sura itakayofuata tutaona mengi kuhusu ushindi wetu juu ya adui tutakapozungumza juu ya silaha za
vita vyetu.
Omba Ukiwa na Upanga wa Roho
“Tena ipokeeni… upanga wa roho, ambao ni neno la Mungu” (Waefeso 6:17). Shujaa wa maombi anayefaa
hutumia silaha yake ya neno la Mungu. Katika maisha ya maombi ya Mkristo, upanga wa roho ni silaha ya
kushambulia adui. Watu wanaoomba kwa ukamilifu hutumia Bibilia katika maisha yao ya maombi. Nguvu
katika maombi huambatana na ufahamu wa Bibilia. Je unafahamu jinsi ya kutumia neno katika maisha
yako ya maombi?
Mtajie Bwana Neno lake Katika Maombi
Tumia neno unapozungumza na Mungu. Kumbuka Bibilia ni kitabu cha ahadi ya Baba kwa watoto wake.
Tumtarajie Mungu kutimiza neno lake. Mkumbushe katika imani, na kumtajia katika maombi. Kila
ninapoomba, maandiko huchukua nafasi kubwa. Mara nyingine naanza muda wangu na Mungu kwa
kumsomea neno lake. Napenda sana kusoma kitabu cha Zaburi kwa sauti katka kuomba kwangu. Thamani
ya kushikilia na kutaja neno hadi kwenye kiti cha enzi ni kwamba ahadi za Bibilia ni kama “deni” kutoka
kwa Mungu hadi kwetu. Sisi ni warithi pamoja na Kristo. Kwa hivyo chochote ambacho ni cha Kristo, ni
chetu pia.
Kuomba na upanga ni kudai haki za uzaliwa wako upya. Muumini huja kwa kiti cha enzi cha Mungu na
kusema “Baba, mimi mtoto wako. Ulisema utakutana na mahitaji yangu yote (Wafilipi 4:19), na nitakudai
kwa neno lako leo.”
74
Taja Neno Dhidi ya Shetani
Unapoomba, tumia upanga wa roho dhidi ya adui. Shetani huchukia na kuogopa ukweli wa neno la Mungu.
Litumie dhidi yake. Neno humkata kwa vipande vipande! Upanga wa neno una uwezo wa kumtorosha
Shetani kutoka vitani. Kuna nyakati katika maombi ambapo Shetani atakushambulia kwa mawazo maovu,
tamaa, au uharibifu. Atafanya vyo vyote katika nguvu zake kuzuia wakati wako wa maombi. Tumia neno
dhidi yake. Isaya 54:17 inasema, “Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa…”
Shetani anajua yeye ni adui aliyeshindwa, bali wakati mwingi yeye hujigamba. Lazima umjulishe kwamba
unafahamu kushindwa kwake. Mtajie neno. Mara kwa mara namkemea usoni kwa kusema: “Shetani, wewe
ni mwongo.” Bibilia inasema “... Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za
ibilisi.” Shetani hawezi kuvumilia ukweli wa neno la Mungu. Atatoroka.
Taja Neno ili Kuinua Nafsi
Kuna nyakati ambapo utaona ugumu kuomba. Taja neno kwa sauti, kwako na kwa Mungu. Kila mara Roho
Mtakatifu atatumia maandiko kuinua nafsi yako juu, ili kutayarisha moyo wako kwa maombi na uombezi.
Omba Katika Roho
Paulo, hatimaye, anatuambia tuingie katika vita vya roho kwa “kuomba wakati wote katika Roho.” Wewe
na mimi hatuwezi kuwa mashujaa wa maombi bila maandalizi haya matatu. Tunajifunza kuomba
tukisimama imara kwa kazi iliyomalizika ya Kristo, tukiomba na neno la Mungu kama silaha yetu ya
kushambulia, na kuomba katika nguvu na ujazo wa Roho Mtakatifu. Maombi ya kweli ni yale yaliyojawa
na uwepo wa Roho Mtakatifu. Ni maombi yaliyojazwa na kudumishwa na pumzi ya Mungu.
Tunaponyenyekea chini ya uwepo wa Roho Mtakatifu ndipo tutakapoweza kuwa na tumaini ya kuwa
mashujaa watakatifu wa maombi. Tumetaja upanga wa neno la Mungu kuwa silaha katika maombi. Lakini
sasa ningependa tuangalie silaha zingine mbili za ajabu katika maombi, ambazo ni Msalaba, na
kutambulishwa na Kristo.
75
KUTUMIA SILAHA ZA VITA VYA ROHO
Kutoka kwa nguvu hadi nguvu endelea:
Ng’ang’ana, pigana, na uombe;
Kanyagia chini nguvu za giza,
Na ushinde katika siku iliyopiganwa vema.
- Charles Wesley.
Kuomba kunaweza kuchuchukua mitindo mingi, kama vile kuabudu, ambapo tunawasilisha sifa kwa
Mungu. Maombi yanaweza kuwa kazi! Ombi ambalo ni gumu ni lile la uombezi kwa ajili ya watu wengine.
Maombi pia yanaweza kuwa vita. Maombi yatamkabili adui Shetani yakiombwa kwa Roho kutoka moyoni.
Kwa sababu kuna nyakati ambapo maombi ni vita vya roho, tutahitaji silaha za roho ili kushinda “uovu wa
roho katika ulimwengu wa roho” tukikabiliana nazo.
Mpango Wa Vita
Kila Mkristo anahitaji ufahamu wa msingi kuhusu jinsi ya kupigana vita vya roho, na silaha zinazohitajika
ili kumshinda adui. Wakati moja wanafunzi wa Yesu walikutana na kijana aliyepagawa na pepo lakini
wakashindwa kukemea pepo hilo. Baba yake akamleta kwa Yesu. Mara moja Yesu alikemea yule roho
mchafu. Baadaye wanafunzi walipomuuliza kwa nini hawakuweza kukemea pepo huyo, Yesu alijibu kwa
kusema:
“Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amini, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi
cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala
halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. (Alafu maandiko mengine huongeza maneno yafuatayo:
Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga) (Mathayo 17:20-21).
Tumefananishwa sana na hao wanafunzi wa kwanza. Tumekosa nguvu dhidi ya nguvu za mapepo
zinazotukabili kila siku. Tuna vifaa vinavyotuwezesha kusongeza hayo milima, kama tungekuwa na imani
na ufahamu wa jinsi ya kutumia vifaa hivyo. Hebu tuangalie silaha za Mungu alizotupatia ili tuweze kuishi
katika ushindi, na kuomba kwa nguvu.
Silaha Za Msalaba
Katika Waefeso 6:11-14, Paulo anatuambia kwa kurudiarudia, “simama imara.” Kwa maneno mengine,
anasema “shikilia ushindi wako.” Kwa kusema “ushindi” alikuwa akimaanisha ushindi ambao Yesu
alitushindia alipokufa na kufufuka tena. Kalivari ilikuwa uwanja wa vita vya roho ambapo Yesu alimshinda
adui na kumtekea Mungu na ulimwengu uliopotea eneo ambalo Shetani alikuwa amemiliki. Ushindi wake
alipata dhidi ya ulimwengu, mwili, na Shetani.
Katika kitabu cha Wakolosai 2:13-15, tunaona mifano miwili ya ajabu yanayoeleza ushindi wa Yesu
msalabani, na kaburi lililo tupu. Paulo anasema,
“Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu,
aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; akiisha kuifuta ile hati
iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa uadui kwetu: akaiondoa isiwepo tena,
akaigongomea msalabani; akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa
ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.
“Hati ya makosa” ambayo Paulo anamaanisha ilitokana na sheria ya Warumi katika siku za Paulo. Yesu
alipoangikwa msalabani, askari waligongomea juu ya kichwa chake maneno yaliyosema “mfalme wa
76
Wayaudi.” Haya maandishi yalikuwa hati ya deni ambayo Yesu alishtakiwa kisheria na wale waliomshtaki.
Katika enzi za Warumi, ilikuwa kawaida hukumu ya sheria kuletwa mbele ya hakimu. Hakimu alitoa
hukumu ya kuwa na hatia, ama kutokuwa na hatia. Kama mshtakiwa alipatikana na makosa, alipewa hati ya
deni ambayo ilipachikwa kwenye mlango wa kijumba cha gereza alimowekwa, ama hati hiyo
ingegongomewa msalabani jinsi walivyomfanya Yesu. Kwa hivyo wote wangeona na kujua hukumu ya
sheria kwa mshtakiwa. Yesu alishtakiwa kwa kuhujumu serikali ya Kirumi, na kujionyesha kama mfalme
wa Wayahudi. Hiyo ilisababisha kuwekwa kwa maandishi hayo juu ya kichwa chake.
Paulo anasema katika Wakolosai 2:14 kwamba Yesu alikufa na akaifuta ile “hati ya makosa … iliyokuwa
ya uhasama kwetu.” Fahamu kwamba hii hukumu, au hati hii ya deni ilikuwa “dhidi yetu,” wala si dhidi ya
Kristo. Ni deni tuliokuwa nalo ambalo Yesu alilipa kwa kifo chake.
Shetani ni mshtaki wetu. Ana orodha ya dhambi ya kila mwenye dhambi. Analeta mashtaka yake dhidi ya
mwenye dhambi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Shetani hutoa hati yake ya makosa mbele ya Mungu.
Sisi wenye dhambi tumehukumiwa kuwa na hatia, na “mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23). Sasa
ni kitu gani ambacho Mungu alitufanyia? Alichukua hati ya dhambi na kuuweka msalabani. Kisha
akaifutilia mbali na damu ya mwanawe wa pekee, Yesu Kristo. Mungu alimaliza kesi yetu nje ya
mahakama, kwa msalaba.
Silaha Pekee ya Shetani
Ukweli tunayoweza kutumia ni kwamba silaha ya pekee ambayo Shetani anatumia dhidi yetu ni dhambi
zetu. Yesu alifuta, na kuziondoa kabisa dhambi zetu. Shetani hana la kudai kwetu kisheria. Yesu alikufa
kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote (1 Yohana 2:2). Hivyo basi alimshinda Shetani kwa kifo chake
msalabani. Huo ndio mfano wa kwanza kutumiwa na Paulo katika Wakolosai 2.
Wakolosai 2:15
Mfano wa pili unatokana na ushindi wa jeshi la Kirumi. Yesu “alimwaibisha” Shetani wazi wazi kupitia
kwa msalaba wake. Hii “aibu ya wazi” ilitumiwa na Kaisari katika ushindi wake vitani. Warumi
waliposhinda jeshi lolote, waliwatia aibu kwa kuvua mavazi ya mfalme, au jemadari wake. Kisha
walilazimisha mfalme huyo, au jemadari pamoja na jeshi lake lote, kufuata gari la vita la Kaisari (ama
Jemadari wa Kirumi) wakiwa wamefungwa minyororo, bila silaha zezote. Warumi waliporudi Roma
pamoja na mateka wao waliokuwa wamefungwa kwa pingu, mateka walidhihakiwa na watu wakitembea
huku wamechoka. Walitembea nyuma ya Kaisari aliyekuwa akionyesha ushindi mkuu. Yesu alimwaibisha
Shetani lini? Msalabani! Yesu alimweka aibu wazi wazi lini? Alipofufuka kutoka kaburini! Yesu
aliposhinda kifo, “aliivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika
msalaba huo” (Wakolosai 2:15). Shetani hana silaha za kutumia dhidi ya Mwana wa Mungu aliyenunuliwa
kwa damu.
Kutumia Msalaba Kama Silaha
Hii inahusiana vipi na vita vya roho? Vita hivi vilipangwa katika kila njia. Tumeshinda tayari. Vita
vinakamilika tunapoomba! Shetani hana dai kwetu wala kwa wale tunaowaombea. Tunapoomba kwa imani
katika kazi ambayo Kristo alimaliza, tunaleta ushindi wa Kalivari katika hali zetu!
Katika kuwaombea waliopotea, mimi humkumbusha Ibilisi kwamba Yesu tayari amemkomboa huyo rafiki
yangu aliyepotea. Namwamrisha Shetani amwachilie huyo mtu ambaye Yesu Kristo alimfilia. “Nakiri
damu” ya Kristo juu yake. Ufunuo 12:11 Inasema, “wakamshinda Shetani kwa damu ya mwana kondoo, na
neno la ushuhuda.” Tunaweza kumshinda kwa njia iyo hiyo. Maneno ya wimbo maarufu wa Martin Luther
yanakuja kwa mawazo: “…hatutetemeki kwa ajili yake: … neno moja ndogo litamwangusha.”
Ushindi Wake Ni Ushindi Wetu
Ningependa kutilia mkazo jambo hili la asili la kujitambulisha kabisa na Kristo. Ushindi wake ulikuwa kwa
manufaa yetu. Tunashiriki katika ushindi huo. Tumo “ndani yake,” naye yumo ndani yetu. Kwa hivyo,
lililo kweli kihistoria linaweza kuwa kweli hata katika maisha yetu ya kila siku.
77
Kuishi katika ushindi kama Mkristo si vigumu kamwe. Ni kupumzika tu katika ushindi wa msalaba. Ni
kuleta kalivari kikamilifu katika maisha yetu, kwa imani.
Wakati fulani nilimwandikia mchungaji mmoja rafiki yangu ambaye alikuwa na mashtaka huko Romania.
Mashtaka juu yake yalikuwa ya uongo, na yasiyothibitika. Alihukumiwa kifungo cha miaka miwili.
Niliporudi nyumbani kutoka Romania, niliwajulisha rafiki zangu wengi wamwombee ili apate kuachiliwa
huru. Tulituma barua na simu nyingi kuwajulisha viongozi kwamba huyu mchungaji alikuwa na marafiki
katika nchi za magharibi. Hatimaye tuliona silaha bora kuwa maombi. Mimi binafsi nilimweka katika
ulinzi wa Mungu. Na pia nilimkemea Shetani na kumuamrisha “kuacha na kukoma” kumhangaisha huyu
ndugu Mrumi. Nilihusisha msalaba wa Yesu kwenye vita. Baada ya kitambo kidogo tulifahamishwa
kwamba mashtaka dhidi yake yalifutiliwa mbali na kesi hiyo kutupiliwa mbali. Bwana asifiwe!
Tusimruhusu Shetani kutuchezea, kuturusha mrungula, au kutupotosha kwa vyo vyote vile. Tukiwa ndani
ya Kristo tu washindi kila siku, na wakati wote. Tuamini, tutende, na kuomba kikamilifu. Ijapokuwa tuko
mwilini, hatupigani vita vay mwili, maana silaha za vita vyetu si vya mwili, bali zina uwezo katika Mungu
hata kuangusha ngome. Tunaangamiza mawazo na kila kitu kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na kuteka
nyara kila fikira ipate kumtii Kristo (2 Kori.10:3-5).
Silaha Za Maombi
Hivi vifungu vinatuonyesha jinsi tunavyoweza kutumia silaha zetu za maombi. Zina “uwezo katika Mungu
kuangusha ngome” (kifungu cha 4). Ngome hizi ambazo tunastahili kuangusha kwa silaha zetu za maombi
ni zipi? Matamshi haya labda yanamaanisha maeneo ya ufungwa (tabia ya dhambi) katika maisha ya watu.
Watu wengi wana ngome za Shetani za hatia, shaka, hofu, uasi na dhambi ya wazi. Ngome hizi za kishetani
zinatokana na miaka mingi ya mazoea ya dhambi. Haya maeneo ya ufungwa huteka watu nyara ili kufanya
mapenzi ya Shetani. Tutaweza kuweka huru waliotekwa nyara kupitia ka uombezi.
Iwapo una rafiki aliye katika tabia ya utumwa wa dhambi kama vile kutumia madawa za kulevya, au
kunywa pombe, basi mama shujaa wa maombi, una jukumu la kupigana vita kwa niaba yake. Katika
maombi unaweza kuangusha hizo ngome kwa kutomruhusu Shetani kumhangaisha, kumfurahisha, au
kumjaribu huyo mtu. Amrisha Shetani katika jina la Yesu aondoe makucha yake kutoka kwa nia, mawazo,
au mwili wake. Maombi ya thati yanaweza kuwa huduma ya ajabu!
Neno La Mwisho
Katika maombi tunatumia silaha zote. Kwanza, kutokana na kikao chetu katika Kristo tunaweza
kumwendea Mungu kwa ujasiri tukidai ahadi zake. Kisha tuna silaha za damu, msalaba, Neno, na jina kuu
la Yesu Kristo, ambayo yanatuwezesha kuwa waombezi kwa niaba ya wengine. Silaha hizi zinaweza kuwa
za ajabu zikitumiwa na muumini aliyejazwa na Roho; na kutembea katika imani na utiifu. Katika sura
itakayofuata, tutaangalia zaidi mamlaka ambayo muumini anayo anapotumia kikamilifu silaha zake za
maombi.
Michango
1. Tafsiri ya Mfalme Yakobo inatafsiri hivi “maandiko ya sheria”.
2. “Bwana Yesu Kwetu Ngome Nzuri,” na Martin Luther.
78
79
FUNGUO ZA UFALME NI ZIPI?
“Amini nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na
yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. Tena nawaambia, ya
kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa
na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu,
nami nipo papo hapo katikati yao.
Mathayo 18:18-20
Niliwahi kuongoza kongamano la Bibilia kwa wanafunzi wa chuo cha Bibilia. Msichana mmoja kijana
katika kongamano hilo aliuliza swali la kuchochea fikira, akisema: “Yesu alimaanisha nini kwa matamshi
yake katika Mathayo 16:19, alipomwambia Simoni Petero: ‘Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa
mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litafungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani,
litakuwa limefunguliwa mbinguni’?”
Swali lake lilikuwa na pande mbili. “Funguo” za ufalme wa mbinguni ni zipi? Pili, maana yake nini
“kufunga na kufungua” katika matamshi haya? Haya ni maswali mazuri. Majibu yake si rahisi kwa sababu
kuna maswala yanayotatanisha.
Nimetaja mambo mawili. Jambo la kwanza linapatikana katika utangulizi, na lingine liko katika swali la
mwanafunzi yule. Yote yanahusika na kufunga na kufungua. Yesu alieleza jambo hili la asili katika nyakati
mbili tofauti, ambapo Mathayo aliyakumbuka na kuyaandika. Katika Mathayo 18:18, matamshi haya
yameandikwa kama nidhamu na maombi ya kanisa. Bali katika Mathayo 16:19, tunaona yakielezewa
Simoni Petero, akiwa na wanafunzi wengine kule Kaisaria Filipi katika pembe za kaskazini mwa Galilaya.
Alichomaanisha Yesu katika mafundisho haya yana manufaa kwetu sana leo kwa maombi yetu, hasa katika
kuombea watu wengine. Ingawa hivyo, waumini wachache sana leo wanaelewa maana ya maneno hayo.
Mafundisho ya Wakatolika Wa Roma
Mafunzo yangu ya kwanza kanisani nilipata katika kanisa la Kikatolika la Roma. Hivi vifungu katika
Mathayo 16:18-19 ni sehemu muhimu ya mafunzo ya kidini kwa Warumi. Wanathiologia wa kikatoliki
huchukua kifungu cha 18 na kukitumia kuonyesha kwamba Petero ndiye mwamba wa msingi ambaye
Kristo alijenge kanisa juu yake. Wanaposema haya maneno ya Yesu wanamaanisha kwamba Kristo alimpa
Petero funguo za ufalme wa Mbinguni. Zilikuwa funguo zenye uwezo wa kusamehe dhambi, na kwa hivyo
Petero na msururu wa Baba Watakatifu waliofuata wana uwezo wa kuamuru mbingu kusamehe watu
fulani, na kutowasamehe wengine.
Ili uthibitishe maneno haya, unaweza kutembelea jiji la Vatican, kule Roma. Katika kanisa la Mtakatifu
Petero kuna sanamu iliyochongwa kwa marmar inayotoshana na mtu aliye hai. Sanamu hiyo imepiga
magoti mbele ya Kristo. Kando ya sanamu hiyo kuna maandishi yaliyochongwa kwa mawe, ambayo
yanasema: “Nami nitakupa (yaani Petero) funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifungua
duniani litafunguliwa mbiguni.” Hivyo basi, mafunzo ya dini ya Kirumi yanatumia kufungu hiki
kufundisha kwamba Petero ameinuliwa, na ana uwezo wa kusamehe dhambi.
Sioni tafsiri hii kuwa sahihi. Sina ugomvi na kanisa la Katoliki la Warumi, isipokuwa tafsiri ya namna hii
kuhusu maneno ya Yesu yanapotosha. Ni rahisi mwanafunzi mwema wa Bibilia kugundua hivyo. Hata
hivyo, kuna makosa aina tatu ambayo yamehusishwa.
80
Kwanza kabisa, ni nani aliyeambiwa maneno hayo? Petero peke yake, au kanisa kwa ujumla? Watu
wanaosema Yesu alimpa Petero funguo wanakabiliana na tatizo katika kuelewa hayo maandiko. Hii ni
kweli kwa sababu mbili. Kwamza, Petero siye “mwamba” wa msingi ambaye Yesu alijenga kanisa lake
juu yake. Yesu mwenyewe ndiye msingi wa kanisa lake. Petero kwa Kiyunani ni Petros, ambayo maana
yake ni “jiwe, au mwamba mdogo.”
Neno ambalo limetafsiriwa “mwamba,” katika kifungu hicho (Mathayo 16:18) lina maana lingine kwa
Kiyunani la petra, ambalo ni “utanda wa chini wa mwamba,” mwamba mkubwa, au mwamba wa msingi.
Petero ni Petros, kipandu tu cha Petra yenyewe. Lugha ya Kiyunani iliyotumiwa hapa ni ya wazi, na ya
kubainisha.
Wasomi wengi wa kisasa wanakubaliana kwamba “Mwamba” wa msingi ambalo Kristo amekuwa akijenga
kanisa juu yake ni ufunuo tukufu ambao Simoni alifunuliwa katika kifungu cha 16, kwamba Yesu ndiye
Kristo. Funuo hili tukufu humjia kila muumini wa kweli. Roho Mtakatifu anapomtambulisha Kristo katika
moyo wa binadamu, itamlazimu kufanya vile Simoni alivyofanya, yaani kukiri alivyofunuliwa na Kristo.
Hivyo ndivyo watu wanavyozaliwa mara ya pili katika kanisa la kweli. Hivyo ndivyo kila mmoja wetu
anavyokuwa “sehemu ya mwamba.” Kila muumini ni Petros, sehemu ya Petra.
Petero, Ama Kanisa
Sababu ya pili ya kukataa wazo kwamba Yesu alimpa Petero (na hatimaye, Baba Watakatifu waliokuja
baadaye) uwezo wa kiungu wa kusamehe dhambi halina utatanishi sana. Bwana Yesu anarudia maneno
haya juu ya uwezo wa kufunga na kufungua katika Mathayo 18. Hapa anatumia hili neno kwa jinsi tofauti
sana, kwani hamtaji tena Petero. Haya maneno yameambatanishwa na maombi. Yesu anasema kwamba
“wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu
aliye Mbinguni” (Mathayo 18:19). Tazama, “ikiwa wawili wenu watapatana,” wanaweza kuomba na
kupokea. Anawezaje kusema kwa ujumla “wawili wenu”? Kwa hivyo, watu wowote wawili wanaweza
kufunga na kufungua hapa duniani.
Kristo analiambia kanisa kwa jumla maneno haya. Vifungu vya kutangulia vinaeleza juu ya washiriki
kupewa nidhamu na kanisa. Yesu anatuambia jinsi ya kumrudi ndugu “aliyepatwa” katika dhambi. Kwa
kumaliza, matamshi yake yanatuvumbulia silaha yetu kuu, kwamba ikiwa wakristo wawili tu watapatana
kwa mapenzi ya Mungu katika maombi, wanaweza “kufunga na kufungua.” Hii ni muhimu zaidi. Mathayo
18 inatufundisha uwezo huu wa “kufunga na kufungua” kuwa silaha ya maombi ya kutumiwa na kanisa. Si
uwezo maalum ambayo imepewa kikundi kilichochaguliwa cha maaskofu ambao kwa njia nyingine ya siri
ni wazao wa Simoni Petero.
Kufunga na Kufungua ni Nini?
Kosa la tatu ni kuhusu maneno ya Yesu, “utafunga duniani” na “kufungua duniani.” Je, Yesu kweli
alimaanisha kwamba Petero, ama mwingine yeyote yule, ana uwezo wa kusamehe dhambi kwa hakika?
Nafikiri sivyo. Baba Mtakatifu au kuhani hana uwezo huo. Ni Mungu pekee anayeweza kusamehe dhambi.
Ni rahisi kuona ukweli huo. Ukitazama kwa makini Mathayo 16:19 na Mathayo 18:18 utaona ukweli huu.
Agano Jipya katika The King James Version linalojulikana kama andiko lenye “mamlaka” kwa miaka 350,
linatafsiri hivi vifungu kwamba “… lolote mtakalolifunga duniani litafungwa mbinguni: na lolote
mtakalolifungua duniani litafunguliwa mbinguni.”
Tafsiri ya maneno yaliyotumika hapa yanahusu vitendo vijavyo. Kama hili lingekuwa sawa, basi tafsiri
nalo lingekuwa sawa. Tafsiri kamili basi lingekuwa kwamba “mbingu” linangoja “dunia” liliambie la
kufanya, yaani mbingu litapata mashauri kutoka duniani. Hivyo ni kusema kwamba nikipiga jambo lolote
marufuku, au nikiruhusu jambo lolote, basi Mungu lazima atii uamuzi wangu. Haya ni mafundisho
yanayopatikana kutoka kwa wale wanaofundisha kwamba mwanadamu anaweza kusamehe dhambi. Kosa
hili limetokana na kutotafsiri vyema maneno yaliyotumika.
Maneno hayo hayahusiani na vitendo vijavyo, bali yanaonyesha mchanganyiko wa habari yenye maneno ya
kutendwa, na mafumbo ya maneno. Hakika katika vifungu vyote viwili, neno la kwamza linaonyesha tendo
lililotendeka, na la pili linaonyesha ukosefu wa tendo. Kwa hakika, maneno yote mawili hayaonyeshi
81
matendo yajayo. Interlinear Greek-English New Testament, katika Kiyunani, inatafsiri kwamba “likiisha
kufungwa” (au kufunguliwa).
Tafsiria ya Bibilia liitwalo The American Standard Bible, linaonyesha kwa usahihi maana ya maneno haya
kwa kutafsiri kwamba “lolote mtakalolifunga duniani tayari litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote
mtakalolifungua duniani tayari litakuwa limefunguliwa mbinguni.” Tilia mkazo maneno “tayari litakuwa.”
Hii ni ukweli wa maandiko haya, kwamba yale ambayo Yesu alisema ni kinyume na jinsi yalivyoandikwa
katika Bibilia ya The King James Version.
Dunia haina uwezo wa kuamrisha mbingu! Haiwezekani kabisa! Dunia ndio huamrishwa na mbinguni.
Tunaweza tu kufunga na kufungua kile ambacho tayari kimefungwa au kufunguliwa. Tunaweza kudai kitu
ambacho tayari kimefungwa, au kufunguliwa, katika maombi. Huku kufunga na kufungua ndio mamlaka
yetu katika Kristo. Hatuhusiki katika kusamehe dhambi, bali katika uombezi tunachukua mamlaka juu ya
adui. Kufunga na kufungua ndio silaha ya maombi.
Mfunge Shetani Kabisa
Je, umewahi kutaka kumfunga Shetani kabisa hata kwa siku moja? Je, hutapendezwa kumwamuru
kukuacha, au kuachana na wapendwa wako? Kuna kanuni moyoni mwa Yesu katika mafundisho yake
kuhusu kufunga na kufungua. Kanuni hiyo ni kwamba tuna nguvu dhidi ya yule mwovu! Kwa sababu Yesu
tayari alimpokonya Shetani nguvu (Waebrania 2:14), tumeshirikishwa katika huo ushindi. Tunatazama
mbinguni na kuona ushindi wa Bwana. Kisha kwa imani, tunatumia “funguo” zetu kuamrisha Shetani
kufungua rafiki zetu waliopotea. Pia tunaweza kumuamuru kufungwa ili asinyanyase rafiki zetu. Kila siku
katika maombi tunaweza kukataza, au kuruhusu kufunga na kufungua. Hizi “funguo” ni silaha zetu kuu za
kuangusha ngome zinazotajwa katika 2 Wakorintho 10:4.
Kuweka Waliotekwa Huru
Asili ya uombezi ni kanuni ajabu ya “kuweka waliotekwa huru” ambao ni kiini katika uombezi. Tuliona
hapo mbeleni katika kitabu kingine jinsi ya kuombea waliopotea. Katika somo hilo, kuna sisitizo kwamba
aliyepotea dhambini ni mateka wa Shetani. Amefungwa kwa minyororo ya kiroho. Amepofushwa na
muovu ili asiweze kuona ukweli wa injili. Shetani amempofusha na kumfunga. Anahitaji kutolewa kutoka
utumwani na kuwekwa huru. Ni jukumu la kanisa linaloamini kuomba ili awekwe huru.
Tunapomwondosha Shetani kutoka kwa uwanja wa vita wa mwanadamu, basi mtu huyo ambaye hajaokoka
atakuwa huru kufanya maamuzi ya busara kuhusu kumfuata Yesus Kristo.
Unapokutana na mwenye dhambi asiye na Mungu, lazima umuhurumie. Yuko mtegoni mwa yule mwovu
(2 Timotheo 2:26). Tuwe vitani kwa niaba yake, kwani amepotea na kukosa tumaini. Bali tukifanya
maombezi kwa ajili yake, Shetani atamfungua, na ataweza kuamua kunfuata Kristo kwa hiari yake
mwenyewe. Hii haimaanishi kwamba kila mtu tutakayemwombea ataokoka, bali wengi wataokolewa ikiwa
kanisa litaamini na kuchukua mamlaka juu ya adui. Yesu ametupa funguo za Ufalme wa mbinguni – ila tu
tujifunze kuzitumia! Malango ya kuzimu hayawezi kusimama dhidi ya kanisa liombalo.
Michango
1. A.T. Robertson, Word Studies In The New Testament, vol.1 (Nashville, Tennessee: Broadman
Press, 1930), ukurasa 149.
2. The International Greek - English New Testament (London: Samuel Bagster and Sons, 1964).
3. Chapter 16 in Questions Non Christian ASK (Old Tappan, New Jersey: Fleming H. Revel
Company, 1977), ukurasa 145-53.
82
83
MAOMBI YA UOMBEZI NI NINI?
Kutumia muda mwingi kwa Mungu ndio siri ya maombi yanayofaulu. Maombi yanayohisiwa kuwa
ya nguvu yanatokana na muda unaotumiwa kwa Mungu. Maombi mafupi yana maana na uhodari
kutokana na maombi marefu yaliotangulia.
E. M. Bounds, Power through Prayer
Hapo awali tulitumia neno “uombezi.” Watu wengine wanaona hii kuwa ufahamu mpya. Hebu tufafanue.
Kurasa nyingi zilizobaki katika kitabu hiki zinaongea juu ya huduma ya uombezi. Uombezi ni nini?
Tunaambiwa katika Agano La Kale kwamba Masihi akija atafanya uombezi kwa niaba ya wakosaji
(tazama Isaya 53:12). Yesu alikuwa, na bado angali, Mwombezi mkuu.
Wahebrania 7:25 inatuambia kwamba Yesu yu hai, ili atuombee mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Neno
uombezi linatokana na neno la zamani la Kiyunani ambalo lilikuwa neno lililotumika kwa wale
waliomwendea mfalme. Lilitumika kueleza maombi kama kumwendea Mungu. Neno la Kingereza la
intrude (kuingilia kati bila kukaribishwa) lilitokana na neno hilo la Kiyunani. Kufanya uombezi ni kuingilia
kati bila kukaribishwa, kwa niaba ya mwingine. Mwombezi ni “mshenga” anayeombea kesi ya mwingine.
Kuwa mwombezi ni kuwa mpatanishi.
Aina Maalum Ya Maombi
Kuna mitindo mingi ya maombi, lakini maombi yanayomfurahisha Mungu ni maombi ya uombezi kwa
dhati. Ni maombi yasiyo na ubinafsi, bali kujitolea mhanga. Maombi ya uombezi yanaweza kuwa silaha
yenye nguvu milele. Yanaweza kuwa silaha ya siri kwa kanisa.
Wakati moja nilisikia maombi ya uombezi yakielezwa kuwa kombora la kimataifa la Mungu lenye masafa
marefu, ambalo linaweza kulengwa au kuelekezwa popote duniani. Linapiga shabaha lake, likienda
mwendo wa kasi ya wazo. Wakati mwingine laweza hata kuchelewa kulipuka ili liweze kujibiwa miaka
mingi baada ya kutumwa.
Karibu miaka elfu mbili iliyopita, Yesu alianzisha kombora lililo na jina lako, alipoomba katika Yohana
17:20 akisema “wala si hao tu ninaowaombea, lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.”
Siku ile uliokoka, Mungu alijibu maombi ambayo Yesu alikuombea zamani. Maombi ya uombezi ni
maombi ya ajabu! Naamini kwamba mtu anapozaliwa mara ya pili, Mungu huwa amejibu maombi ya Yesu
tena. Kila mara mtu anapookaka, juhudi za mwombezi hujibiwa.
Wazazi wana silaha ya siri ya kutumia kwa ulinzi ya watoto wao. Unapowaombea watoto wako unahifadhi
historia kwa ajili ya huyo mtoto. Tayari nimewasilisha maombi juu ya watoto wangu kwa miaka zijazo.
Walipokuwa wachanga, niliwaombea kuhusu miaka ya ujana wao. Kwa kumhusisha Mungu katika maisha
yao ya baadaye, unawapangia maisha yao ya siku za usoni. Miaka mingi baadaye, Mungu atayajibu
maombi hayo. Kinachoshangaza ni kwamba Shetani hana silaha dhidi ya “neema hii iliyohifadhiwa.”
Hii pia ni kweli tunapomwombea mtu aliyepotea. Mtu aliyepotea huenda asikusikilize unapomshuhudia
kuhusu Mungu. Huenda hataenda nawe kanisani, au kusoma Bibilia uliyomnunulia. Hata hivyo,
unapomwombea na kumwuliza Roho Mtakatifu wa Yesu agonge katika mlango wa moyo wake, Shetani
hawezi kuwa na silaha au kizuizi dhidi ya maombi yako. Yesu atamwendea huyo mtu na kuzungumza
naye. Tukijua hivi basi, mbona tusitume makombora yetu kila siku? Nina hofu kwamba dhambi kubwa ya
kanisa la kisasa ni ukosefu wa maombezi. Tunahitaji moyo wa nabii Samweli aliyepaza sauti akisema,
“Walakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuwacha kuwaombea ninyi” (1 Samweli 12:23).
84
Fumbo Juu Ya Uombezi
Yesu alisimulia hadithi nyingi za ajabu. Lakini hakuna hadithi iliyokuwa rahisi na yenye kuvutia kama ile
ya mtu aliyembishia jirani yake mlango usiku wa manane. Yesu alisimulia hadithi hii ili kuonyesha Mungu
anavyohisi kuhusu uombezi.
Akawaambia, “ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa manane, na kumwambia,
Rafiki yangu, nikopeshe mikate mitatu, kwa sababu rafiki yangu amefika kwangu, atoka safarini,
nami sina kitu cha kuweka mbele yake; na yule wa ndani amjibu akisema, Usinitaabishe; mlango
umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kuondoka nikupe?
Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile
asivyoacha kumwomba, ataondoka na kumpa kadiri ya haja yake. Nami nawaambia, Ombeni,
nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni nanyi mtafunguliwa. Kwa kuwa kila aombaye
hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa” (Luka 11:5-10).
Kuomba Kwa Ujasiri
Kama kuna funzo maalum kutoka kwa hadithi hii, basi ni kanuni ya ujasiri, kuthubutu, na kuwa na
mamlaka. Hapa tunaona mtu jeuri, akigonga mlango wa jirani usiku wa manane. Hawezi kuacha kubisha
mpaka mwenye nyumba aende kumfungulia na kumpa haja yake. Tazama alivyo jeuri, anavyosisitiza, na
mwenye uthabiti. Wanafunzi wa Bwana wetu walikuwa wamemuuliza awafundishe kuomba (Luka 11:1).
Katika hadithi hii, Yesu anasema wazi wazi, “Njoo kwenye kiti cha enzi kwa ujasiri. Uwe thabiti katika
maombi yako.”
Huwezi Kuomba Kupita Kiasi
Uombezi wetu lazima uwe thabiti kulingana na maombi yetu. Hebu mwone huyu mtu anavyoomba mikate
mitatu, badala ya mkate mmoja. Nyakati hizo mkate moja ilikuwa chakula cha siku nzima! Ni ajabu,
sivyo? Hivyo ndivyo tunavyostahili kumwendea Mungu. Nimehuzunishwa sana kusikia watu wengine
wakisema tusimsumbue Mungu kwa kumwomba “vitu.” Hata hivyo, Mungu ana shughuli nyingi, na
hawezi kusumbukia shida zetu za kila siku! Si hivyo ndivyo ilivyo kiroho, jamani? Inaweza kuonekana
kuwa takatifu, lakini haiambatani na mafundisho ya Bibilia. Nashukuru kwamba Mungu wetu si wa namna
hiyo. Anataka tuombe maombi makuu. Nilitaja mambo hayo awali katika kitabu hiki, lakini ni vyema
tuyataje tena.
Wewe unakuja kwa Mfalme,
Maombi makubwa kwa ewe mfalme,
Neema yake yatosha na uwezo wake watosha,
Huwezi kuuliza zaidi kupita kiasi.
Lililo na maana kwako lina maana kwa Mungu. Anataka kukupa mahitaji yako yote.
Rafiki anayekuja kubisha mlango usiku si mjasiri tu wa kuomba mikate mitatu, bali ni msumbufu pia.
Hatachoka. Katika kifungu cha 7, Yesu alisema mwenye nyumba hangefungua mlango isipokuwa tu kwa
usumbufu wa yule jirani. “Nawaambia ya kwamba ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake,
lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, ataondoka, na kumpa kadiri ya haja yake.”
Kwa nini alimpa kiwango alichohitaji? Hii haina uhusiano na urafiki, kwa sababu tafsiria ya The King
James Version imetumia neno ambalo kwa Kiswahili ni maombi ambayo ni sumbufu (yenye udhia).
Mombi iliyo sumbufu ni maombi gani? Neno hili halitumiki sana, lakini ni tafsiri kutoka kwa lugha ya
Kiyunani ambalo lilikuwa na maana ya kutokuwa na aibu. Tafsiri ya The New American Bible
linawasilisha neno hilo sawa kwamba “aliendelea kubisha bila aibu,” na mwishowe, kwa sababu ya jitihada
zake, mwenye nyumba aliamka na kumpa hitaji lake. Hivi ndivyo tunavostahili kwenda mbele ya kiti cha
enzi cha Mungu katika maombezi. Tunapoombea wokovu, ulinzi, afya, mali, ama lolote lile, kwa ajili ya
85
watu wengine, Yesu alisema tunahitaji kuendelea kuomba, kutafuta, na kubisha. Hatimaye Mungu atatupa
hitaji letu.
Kuomba Mungu Anayesita?
Swali la kawaida lazuka hapa. Je tunajaribu “kumpokonya” Mungu, ambaye ni wa kusita, kitu alichofungia
mkononi? La, hasha. Lazima tukumbuke kwamba tunazumza juu ya aina maalum ya maombi. Katika
maombi haya, tunawaombea wengine mpaka Mungu ajibu kwa njia moja au nyingine. Mara nyingine
Mungu hukawia kujibu ili tuweze kukua kiroho katika maombi. Kumbuka Yakobo alivyopigana mweleka
na malaika wa Bwana katika kijito cha Yabbok (Mwanzo 32:2-29). Yakobo alipigana na huyu malaika
usiku kucha hadi alfajiri. Malaika alimsihi amwache, lakini Yakobo akadai mgeni huyo ambariki ndipo
amwachilie. Katika hali ya kusita, malaika huyo alimbariki. Yakobo akamwachilia.
Labda inaonekana kwamba kuna kitu ambacho si sahihi kuhusu pigano hili. Swali ni kwamba tangu lini
mwanadamu kama Yakobo akawahi kupigana na malaika shupavu wa Mungu mweleka na kumweka chini,
kisha akaitisha baraka kutoka kwake? Naona kwamba vita hivyo vilikuwa vimepangwa mbeleni. Naamini
kwamba huyo malaika alikuwa akifurahia vita hivyo. Hakuwa na haraka ya kuachiliwa. Picha ile ni kama
ya Baba anayemenyana na mwanawe mdogo wa kiume. Ni kama malaika alikuwa akizungumza
kimoyomoyo akisema “Usikate tamaa Yakobo, nitakubariki ikiwa tu utang’ang’ana zaidi kidogo.”
Mungu ana mengi ya kutufundisha tunapotafuta, tunapoomba, na tunapobisha. Imani yetu inapanuliwa, na
tabia yetu inaundwa na kufanywa imara katika bidii. Tunachojifunza katika uombezi kila mara ni ya
thamani kuliko jibu yenyewe. Kuwaombea wengine hujenga unyenyekevu na upendo usio kuwa na choyo
ndani yetu.
Uombezi Unahitaji Kujitolea
Kanuni nyingine muhimu katika hadithi hiyo ni kwamba yule bwana alijitolea kabisa. Usiku wa manane,
alienda nje kutafuta chakula ampe rafiki yake. Rafiki yake alikuwa na njaa, lakini hakuwa na njia ya
kumlisha. Hivyo ilimbidi kutambua kwamba rafiki yake kweli alikuwa na njaa. Angesema, “Ikiwa una njaa
sana, basi nenda ukawaamshe majirani ili wakasirike nawe.” Lakini hakufanya hivyo. Badala ya kufanya
hivyo alitambua njaa ya rafiki yake, na kuifanya kuwa shida yake. Huo ndio moyo wa mwombezi. Moyo
wa mwombezi ni kujitambulisha na hali ya wengine.
Je umewahi kuhisi hivyo kwa sababu ya rafiki yako ambaye hajaokoka? Je upotevu wake umewahi
kukumeza mpaka ukauonna kuwa mzigo wako? Itakubidi kujiweka katika nafasi ya huyo mwenye dhambi
aliyepotea na kuanza kubeba upotevu wake katika moyo wako. Hitaji lake litakuwa hitaji lako.
Mwongozi mkuu, John Knox wa Scotland, alipaza sauti mbele ya Malkia wa Scotland akisema, “Nipe
Scotland, au nife.” Namwona kijana Daudi Brainerd akipiga magoti katika theluji nje ya kijiji cha Wahindi
akimsihi Mungu kuwaokowa hao makatili, waliokuwa katika misitu ya New England katika miaka ya
1743-1747. Kijana Brainerd aliwaombea hao wahindi hadi akazirai kutokana na kukaa kwenye baridi kwa
muda mrefu, na kuchoka.
Ilichukua miaka mingi ya maombi na kushuhudia, lakini mwishowe Mungu alifungulia Brainerd milango
ya uinjilisti. Kujitoa kwake kuliathiri afya yake na kumgharimu maisha yake. Lakini David Brainerd akawa
mmisheni wa kwanza kabisa katika eneo hilo. Maisha yake ilivutia maelfu ya watu katika huduma ya
maoambezi na kushuhudia.Maisha ya uombezi yanahitaji kujitolea katika muda, vipawa, na hata uhai.
Tunakuwa waombezi kwa watu wengine katika kujitambulisha na mahitaji na machungu yao.
Tunapotokwa na damu, tunabariki. Hakuna njia nyingine. Mungu atupe kujali kama vile Musa aliyeomba
kwamba:
“Aa! Watu hawa wametenda dhambi kuu, wamejifanyia miungu ya dhahabu. Walakini sasa,
utawasamehe dhambi yao - na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichokiandika”
(Kutoka 32:31-32).
86
Hiyo ndiyo roho ya kujitambulisha na kujitoa.
Maombi Yenye Haja
Tukisoma zaidi somo la uombezi, tutaona mara kwa mara kwamba shujaa wa maombi wa kweli ana juhudi.
Shujaa wa maombi mara nyingi ni mtu mjasiri aliye tayari kufanya lolote. Mfano ambao tumeonyeshwa
katika masomo haya unaonyesha hali ya dharura. Mtu huyu alienda usiku wa manane kutafuta msaada kwa
sababu alihitaji msaada huo kwa dharura. Alisema, “Rafiki yangu amefika kwangu … na sina kitu cha
kuweka mbele yake” (Luke 11:6). Mtu huyo aliona kuwa ni jukumu lake kumwendea jirani yake kutafuta
msaada akiwa na ujasiri.
Ningeomba Wakristo wengi wachukue jukumu katika kazi ambayo Mungu amempa kila moja wetu. Kanisa
haliwezi kukutunzia watoto wako. Hilo ni jukumu lako kuwatunza. Kazi yako muhimu kila siku ni
kuwaombea. Mungu anapendezwa sana anaposikia wazazi wakiombea watoto wao. Hatari iliyoko ni
kwamba mara nyingi tunangoja hadi tupate shida, ndipo tunaomba. Tukingoja hivyo basi huwa
tumechelewa. Hatuwezi kuomba maombi ya dharura hadi tuwe katika hali ya kutokuwa na uwezo.
Mtu huyu alikuwa katika hali mbaya kwa sababu hakuwa na chakula cha kumpa mgeni wake. Mara nyingi
hatuombi kwa uaminifu kwa sababu tunafikiri tumetosheka ndani yetu. Tunakosa kumtegemea Mungu
tunapokuwa na afya njema, fedha, kazi, au hata mali. Vitu tunavovitegema vikiisha, basi tutatambua
kwamba hatuwezi kukabiliana na maisha. Hii ni hakika pia katika mambo ya kiroho. Tunapokumbana na
shida ambazo haziwezi kusuluhishwa na fedha au mali, ndipo tunakuwa tayari kuomba.
Mwombezi wa kweli anajua kwamba ni Mungu tu anayeweza kukutana na mahitaji ya maisha yetu. Anajua
“sina kitu.” Kisha humwendea Baba wa Mbinguni, aliye na kila kitu.
Huduma ya Uombezi
Pengine hitaji kubwa katika ulimwengu wa leo ni kupata waombezi wa kweli. Watu kama hao
wanamwamini Mungu anayejibu maombi. Wako tayari kujitambulisha na ulimwengu unaoumia na kufa.
Hawawezi kumwachilia Mungu hadi awabariki. Katika kurasa zitakazofuata, tutaangalia kwa undani
huduma hii ya uombezi ambayo inahitajika sana.
Michango
1. “Endelea” kuomba, kubisha, na kutafuta inaeleza vitendo hivi katika hali ya sasa.
87
JE, KUKOSA KUTII KUNAWEZA KUZUIA MAOMBI
YAKO?
Maombi ni kama zana hatari zenye uwezo wa kupiga bara lingine zikirushwa kutoka kwa jukwaa
la maisha yetu. Maana kamili ya maombi yanatokana na maisha ya anayeomba. Maisha ndio
huomba.
-Ronald Dunn, Lifestyle Ministries.
Je, kukosa kutii kunaweza kuzuia maombi? Jibu la swali hili ni wazi kiasi cha kupuuzwa. Lakini swali hili
linatupa jambo la kufikiria. Mara kwa mara sisi hujishughulisha zaidi na jinsi tunavyoomba. Tunataka
kujua kama tunasema maneno yanayofaa, kwa sauti inayokubalika kidini. Tunahitaji kukumbushwa
kwamba Mungu hujali nia ya nyoyo zetu, kuliko maneno tunayotumia katika maombi. Maombi sharti yawe
zaidi ya maneno yanayotamkwa kwa Mungu.
Nimeona watu wakiandika maombi mazuri sana ya kusoma hadharani. Maombi hayo kwa hakika husikika
kuwa ya kuvutia sana. Je, yana maana? Je, utungaji na uchaguaji wa maneno mazuri humpendeza Mungu?
Sidhani hivyo. Hapa kuna kanuni ya kiroho inayofaa tujifundishe. Maisha Ndio huomba. Mwanzo kabisa,
wakati wote maisha ndio huomba.
Mwandishi wa Zaburi alinena wazi wazi kwamba “Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana
asingesikia ” (Zaburi 66:18). Bwana Yesu alisisitiza kanuni hii katika Yohana 15:7 aliposema, “Ninyi
mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”
Unaona “kukaa” kwetu huvuta majibu yake. Ni maisha iombayo.
Masharti Mawili kwa Maombi Yanayojibiwa
Je umewahi kushangaa kwa nini maombi ya watu wengine hujibiwa haraka kuliko yako? Inaonekana
kwamba maombi ya watu wengine husikika hunfikia Mungu mara moja. Mbona hivyo? Naona kwamba
kuna mambo mawili muhimu ambayo Mungu huzingatia katika kujibu maombi yetu.
Kwanza kabisa, hitaji la kuombewa sharti liwe linaambatana na neno la Mungu. Waraka wa kwanza wa
Yohana 5:14 imetueleza jambo hili waziwazi. Isipokuwa uombe kulingana na neno la Mungu, maombi
yako hayawezi kujibiwa hata ukiwa na imani au bidii ya namna gani.
Jambo la pili ni kwamba anayeomba ni sharti aishi kulingana na mapenzi ya Mungu. Mungu hutazama
maisha ya anayeomba. Maombi hutumwa Mbinguni kutoka kwenye jukwaa la maisha yetu. Kwa hakika,
maisha ndio huomba. Kule kudumu ndani yake husababisha maombi kujibiwa.
Ubora na Kukubalika
Kwa wengine hii itasikika kuwa jambo la kigeni, lakini katika uchumi ya mambo ya Mungu, uwezo wa
anayeomba huwa na hatima katika kukubalika kwa maombi yake. Yesu alisisitiza haya katika mahubiri
yake mlimani.
“Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu
yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako upatane kwanza na ndugu yako, kisha
urudi uitoe sadaka yako”. Matahyo (5:23-24).
Unaona vile Mungu anavyoangalia mambo? Kwake, ubora wa mtoaji ni muhimu zaidi kuliko kile
anachotoa. Anayeabudu ni muhimu kuliko tendo la kuabudu. Mungu hutuangalia kabla kuangalia sala zetu.
88
Miaka mingi iliyopita, Robert Murray M’Cheyne alisema “Hali ya mtu anapoomba ndio hali yake halisi.”
Naamini hayo maneno hayo kuwa kweli, hasa kama yana maana ya kuomba kwa faragha, kwa sababu
katika umati sisi huomba maombi “yasiyo kamili” wakati mwingine. Tunapoomba faraghani, hali yetu
halisi hudhihirika. Kwa hivyo ubora wa maisha ya mtu binafsi hutegemea maisha yake ya maombi. Kwa
hakika, ni maisha iombayo.
Kutotii na Kuomba
Tunapoishi katika dhambi tunapoteza ujasiri na imani katika maombi. Ni vigumu kwa moyo iliyo na
hukumu kuomba. Waraka wa kwanza wa Yohana 3:20-21 inasema kwamba “...Ikiwa mioyo yetu
inatuhukumu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote. Wapenzi mioyo yetu
isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu.”
Nini hutendeka mioyo yetu inapotuhukumu kwa sababu ya dhambi? Sisi hupoteza ushirika na Mungu,
huzimisha Roho Mtakatifu, na kukosa ujasiri katika maombi. Shetani huja kwako na kukufunika kwa
wingu la hatia kichwani ili usije ukatazama juu. Ni Jambo la kufedhehesha kupoteza uwezo mkuu wa
maombi kwa ajili ya dhambi fulani ndogo – “Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana
asingesikia.”
Maisha Yaliyozoroteka na Maombi Yasiyowakilishwa
Itakuwa huzuni kubwa mbele ya kiti cha enzi cha hukumu ikiwa Kristo atakuambia kwamba kuna watu
aliokusudia kuokoa kupitia kwa maombi yako, lakini kwa sababu ya dhambi fulani katika maisha yako
hakuweza kuomba kupitia kwako. Maisha yako yalikuhukumu mpaka Roho Mtakatifu akashindwa kuwa
mwombezi ndani yako. Rafiki, hakuna kitu cha maana uliwenguni kinachoweza kusababisha ukose kuwa
na nguvu katika maombi. Yakobo 5:16 inasema kwamba “Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana,
akiomba kwa bidii.” Tambua kwamba ni maombi ya mwenye haki tu inayoweza kuwa na matokeo.
Maisha ya Kudumu
Tukirejelea maneno aliyoyasema Bwana katika Yohana 15:7, “Mkikaa ndani yangu . . . ombeni mtakalo
lote nanyi mtatendewa.” Je wewe ni mkristo wa kukaa? Je unaishi maisha ya kukaa ndani ya Kristo hadi
kumsababisha kukuhakikishia majibu kwa maombi yako? “Kukaa” ni kudumu, au kuishi katika ushirika na
mtu fulani. Katika mafundisho haya Yesu anatumia mfano wa matawi na mzabibu. Kukaa ndani ya Kristo
ni kudumu ndani ya Yesu jinsi tawi lidumuvyo kwa mzabibu. Tawi hudumu kwa mzabibu na kuutegemea
kwa uhai wake. Tawi lina kusudi moja, ambalo ni kukaa ndani ya mzabibu ili liweze kuzaa matunda.
Mimi na wewe tunapaswa kudumu ndani ya Mungu, jinsi tawi lidumuvyo ndani ya mzabibu. Ni mbingu
peke yake ijuayo matunda ambayo Mungu anaweza kutoa kupitia kwetu. Je, unaishi maisha iliyo wazi kwa
Mungu kwa ajili ya huduma na utakaso?
Safari yenye Hatia
Nimehisi maishani mwangu mara nyingi kuwa na hatia kwa kutomfanyia Yesu zaidi. Labda nina siku
ambayo nilikosa kuomba, kusoma Bibilia , au hata kushuhudia. Tafadhali niamini, nimekuwa na nyakati
kama hizo! Alafu najihisi kwamba sifai. Kisha najizatiti, kwa udini tu, kutekeleza yale ambayo nilikosa
kufanya. Nikiweza kwenda nyumbani na kuona huzuni usoni mwa mfereji wa maji jikoni, na kumuuliza,
“Mfereji, mbona una huzuni leo?” “Bwana,” Mfereji anajibu, “hujanitumia kwa siku nzima. Nilitaka
kupoesha kiu chako, kusafisha mikono yako, kukusaidia kuosha vyombo, lakini hukunifungua leo.” Nami
namjibu hivi, “Wewe mfereji mpumbavu, ningelikufungua wakati wowote kama ningelitaka. Nilijua uko
pale na tayari kutumika. Sitaki ujifungue mwenyewe, kwa sababu utapoteza maji tu na kuharibu vitu.”
Mungu amenionyesha kwamba yeye ni mzabibu, nami ni tawi. Nastahili kuwepo bila masharti. Hatufai
kupima uaminifu wetu kwa matendo yetu, bali kwa kupatikana kwetu. Kuwa mtu wa kudumu halisi si
rahisi.
Kuwa wazi kwa Roho Mtakatifu bila masharti ni matokeo ya maisha ya chombo kilichovunjika mbele ya
Mungu. Sababu hiyo imesababisha waombezi wa kweli kuwa wachache kanisani. Uungu halisi hutokana na
maisha ya kujitoa.
89
Kudumu Ndani ya Maneno Ya Yesu
Bwana wetu ametaja sharti lingine la kujibiwa kwa maombi. “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu
yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.” Tazama maneno haya: “na maneno yangu
yakikaa ndani yenu.” Kuna uhusiano kamili kati ya maisha yetu ya maombi na kukaa ndani ya Neno La
Mungu. Kukaa katika neno lake linamaanisha kwamba neno lake linadumu daima ndani yako.
Umelikaribisha neno la Mungu kuishi ndani ya moyo wako. Neno linapopenya katika mioyo yetu, litaanza
kuongoza, kurekebisha, na kuelekeza maisha yetu.
Kwa wengi wetu, mioyo yetu ni kama hoteli kwa neno la Mungu, kuliko kuwa nyumbani mwa neno la
Mungu. Wakati wa kuondoka ni Jumapili mchana. Hebu jiulize hivi: Je, neno la Mungu linadumu daima
rohoni mwangu hadi kuongoza maisha yangu? Hivyo ndivyo Yesu alivyomaanisha aliposema kuhusu
kukaa katika neno lake.
Kutii na Kuomba
Tunapoendelea kukaa katika neno lake, maombi yetu yataendelea kuwa yenye maana, kwani “na lolote
tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake”
(1 Yohana 3:22). Hebu fikiri: Je, kuna amri ambayo umekataa kutii? Ikiwa ni hivyo basi, maombi yako
hayawezi kuwa na maana. Utakatifu maishani mwako yanaambatana na maombi.
Hapo awali tuliongea kuhusu maombi ya David Brainerd ambaye alikuwa mmisheni kwa wahindi
Wamarekani ya Kaskazini. E. M. Bounds, katika kitabu chake kizuri sana kiitwacho Power Through
Prayer, anaeleza hivi kuhusu Brainerd:
“Hebu kila mara tumtazame Brainerd kwenye misitu ya Marekani, akiweka moyo wake wazi kwa
Mungu kwa ajili ya makafiri, ambapo hangefurahishwa na lolote isipokuwa waokoke. Maombi ya
siri, zingatifu, na ya kuaminika – iko katika shina la uungu ndani ya mtu binafsi.”
Mtu aliye shupavu katika maombi ni shupavu pia katika neno. Utakaso unaotokana na neno husababisha
maisha yenye maombi. Yesu alisema, “Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno
nililowaambia” (Yonana 15:13).
Kufyekwa na Kuomba
Neno la Mungu katika maisha yako linaweza kukutakasa, na Mungu kukutumia kwa huduma na maombi.
Kwa kutumia mfano wa mzabibu na matawi, Yesu alinena juu ya kufyekwa iletayo afya katika mzabibu.
Kila mkulima huelewa kwamba ili kuwa na mzabibu iliyo bora, itamlazimu kupunguza matawi, badala ya
kuongeza.
Wengi wetu wana matawi mengi maishani ambayo yanahitaji kufyekwa na Mungu! Tutazaa matunda
mengi ikiwa Mungu atazidi kuondoa matawi katika maisha yetu. Kufyekwa na kutakaswa haimaanishi
kuondolewa dhambi tu, bali ni kuondolewa mambo tuyaonayo kuwa mema lakini yanaweza kutuzuia
kupata mambo ya Mungu. Vitu kama runinga, michezo, na vitu vingine vingi vinaweza kutufanya
tusiombe. Tunaweza kusongwa na shughuli nyingi hadi tukose muda wa kuomba. Baba wa Mbinguni
anaweza kukata mambo mengine kutoka kwako ili upate wakati wa kuomba kikamilifu. Je, ungependa
Mungu akutumie kama shujaa wa mombi aliye mtakatifu, na mwenye bidii? Jiweke tayari kwa Mungu,
kama vile tawi lilivyo tayari kwa mzabibu.
Michango
1. E. M. Bounds, Power Through Prayer (Grand Rapis, Michigan: Zondervan Publishing House, 1962),
p.24.
90
91
KIZUIZI KIKUBWA KWA MAOMBI
Hakuna kizuizi kingine kwa maombi kama ugomvi ambao haujasuluhishwa. Mng’ang’ano wowote
kati yako na mwanadamu mwenzako, ni swala kati yako na Mungu wako. “Mkiangalia sana mtu
asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua…”
Waebrania 12:15
Kwa kuwa Mungu hutazama kwanza maisha ya anayeomba kabla kufikiri juu ya maombi yake, inafaa kila
mara tuishi maisha anayoweza kutumia. Kuna vizuizi vingi vinavyosababisha kutojibiwa kwa maombi.
Tayari tumeangalia mengine kati ya vizuizi hivyo, kama vile dhambi, au kutokuamini. Ingawa hivyo,
maneno ya Yesu katika Marko 11:24-26 yanaonyesha kwamba kutokusamehe ni kikwazo kikubwa katika
kujibiwa maombi.
“Kwa sababu hiyo nawaambia,Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea,
nayo yatakuwa yenu. Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu;
ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. [Lakini kama ninyi
hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]
Moyo Wa Kusamehe
Vifungu hivi hufadhaisha watu wengine. Mbona Bwana amesisitiza kutokusamehe kama kikwazo kwa
maombi, kati ya vitu vyote ambavyo angeorodhesha kama vikwazo kwa maombi? Mara nyingi Bwana
wetu anaonyesha hisia za Mungu kuhusu moyo isiyoweza kusamehe. Katika kifungu cha 25,
anatuvumbulia kwamba moyo wa kusamehe hutangulia kujibiwa kwa maombi. Ni dhahiri kwamba swala
lolote baina yako na mwanadamu mwenzako, pia ni swala kati yako na Mungu. Uhusiano wetu na
wanadamu wenzetu ni funguo muhimu katika uhusiano wetu na Mungu. Lazima tuwe na mausiano sawa
sisi kwa sisi ndipo Mungu aweze kuongea nasi!
Je, umewahi kuwazia jambo hili, kwamba uwezo wako katika maombi hutegemea uhusiano wako na watu
wengine? Kwa sababu hiyo, mwandishi wa Waebrania anatuhimiza kwamba “Tafuteni kwa bidii kuwa na
amani na watu wote, …mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije
likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo” (Waebrania 12:14-15).
Hatustahili kukosa uwezo katika maombi kwa sababu ya kitu chochote hapa ulimwenguni. Maombi ndio
maisha yako. Kwa hivyo lolote litakalosababisha ukose kuomba halifai kukugharimu. Kwa sababu Mungu
hawezi kukusamehe usiposamehe, ni vyema usiruhusu moyo wa kutokusamehe “kukufunga.”
Kusamehe Bila Kukoma
Yesu anapotuamuru “kusamehe” katika Marko 11:25, neno analotumia ni katika tendo la sasa. Maana yake
ni “kuendelea kusamehe.” Ni heri kusamehe kuwe hali yako ya maisha. Je, unawawekea wanaokukosea
hatia? Yesu alisema kwamba utapoteza haki yako ya kuomba kwa kuwachukulia hatia wanaokukosea.
Hakuna kizuiacho maombi kama vile kuwa na uchungu na machukizo.
Kusamehe kiwe kitendo cha kila siku katika maisha yako. Hujui utaomba wakati gani na kuhitaji jibu la
haraka kutoka kwa Mungu. Ukihitaji kuombea mtoto ambaye amekuwa mgonjwa, huna muda wa kwenda
katika nchi nzima ukiwasamehe watu na kuomba msamaha. Unahitaji kuomba sasa! Utachelewa kuweka
“upanga wako chini” na kuacha machukio wakati kuna dharura. Kusamehe kunastahili kuwa kitendo cha
kila siku, ambacho ni cha kuendelea.
Kuamua Kusamehe
Mara kwa mara watu wameniambia hivi, “ Barry, kama ungalijua jinsi mtu fulani alivyonitendea,
hungeliniuliza nimsamehe. Siwezi kamwe kusamehe yale aliyonitendea.” Kwa kweli, msamaha ni kitu
92
gani? Watu wengine wanafikiri kimakosa kwamba kumsamehe mtu ni kusahau yale aliyokutendea, na
kuishi kama kwamba hakukutendea lo lote. Hii si maana ya kusamehe. Mungu hasemi, “samehe na
kusahau.” Ametuamuru “tusamehe.”
Kiini cha neno ambalo Yesu alitumia hapa ni “kufukuza, au kuondosha.” Kwa hivyo, kama nitakusamehe,
itanilazimu kufukuza hisia za kuumia, za uchungu, au za machukizo niliyo nayo kwako. Siwezi kamwe
kubadilisha ulivyonitendea, au uliyoniambia. Hayo ni ya kale. Huwezi kubadilisha. Hata hivyo, naweza
kubadilisha tabia yangu kulingana na hayo uliyonifanyia. Hii ndio maana halisi ya kusamehe.
Kundoa Machukizo
Naamua kukusamehe. Naamua “kufutilia mbali” chuki na uchungu. Wakati fulani nilisikia kusamehe
ikielezwa kuwa “kupasua orodha ya deni.” Orodha ya deni ni karatasi ambayo imetiwa sahihi na
anayedaiwa, kuonyesha kwamba atalipa deni. Aliye na karatasi hiyo yenye orodha amemfanya anayemwia
kuwa na hatia ya deni. Ile orodha ya deni ni swala kati yao. Kusamehe ni kupasua orodha ile ya deni.
Wengi wetu wana orodha ya madeni ya watu wengine. Katika mioyo yetu kuna kinyongo, machukizo, na
chuki ambazo zimekolea kwa miaka mingi. Vitu hivi vinatuzuia kuwa na upendo wa kweli na ushirika na
wale ambao hatujawasamehe.
Msamaha wa kweli ni hapo ninapopasua orodha yangu ya deni, na kuamua kwamba deni hilo tayari
limelipwa. Hilo linakuwa si swala tena. Hatuwezi kusahau kabisa yale yaliyotendeka, lakini tunaweza
kuamua matokeo yake. Uchungu wa moyo wako utamalizika. Hii ndio msamaha. Mungu anahitaji tuishi
hivyo. Katika mfano wa maombi ambayo Yesu alituonyesha, aliomba akisema, “Utusamehe dhambi zetu,
kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye” (Luke 11:4).
Msamaha Kamili
Ikiwa wewe na mimi tunahitaji ushirika na Mungu katika maombi, basi ni lazima tuwe na hakika kwamba
hakuna mng’ang’ano wowote katika mioyo yetu ambayo hatujatatua. Yesu akasema, “Unaposimama
kusali, samehe, ikiwa una jambo dhidi ya yeyote.” Bwana wetu anatarajia tusamehe kabisa kwa wingi.
Haifai kuchagua tutakayesamehe, na tutakayekosa kusamehe. Pia haifai kuchagua ni kitu gani tutasamehe
au kitu gani tutakosa kusamehe.
Tunahitaji kusamehe bila kujali hatia iliyoko, au mkosaji. Hili ni jambo gumu sana. Watu hututia uchungu,
hutuumiza, na kututumia vibaya. Ni rahisi kuchukizwa na mng’ang’ano, badala ya kuutatua. Kumbuka
kwamba Yesu hakusema kuendelea kusamehe watu kutakuwa rahisi. Huku “kwenda maili saba zaidi” na
“kusamehe sabini mara saba” si kwa walio dhaifu na wenye imani duni. Ni wale tu walio na upendo wa
Mungu kwenye vilindini mwa nafsi zao ambao wanaweza kusamehe kabisa, na kwa wingi. “Kukosa ni
kibinadamu, lakini kusamehe hutokana na Mungu.”
Nguvu Iwekayo Huru
Mwanamke mmoja alinieleza matukio yaliyosababisha kuvunjika kwa ndoa yake. Mumewe alikuwa
amemuumiza sana. Nilipoendelea kusikiliza, moyo wangu ulishikwa na ghadhabu dhidi ya mtu huyu
aliyemtendea mke wake kiimla. Nilielewa kwa nini mwanamke huyu alimchukia . Nilipomwambia
amsamehe, macho yake yalijaa hasira sana, akisema, “Siwezi. Hata kamwe, siwezi kumsamehe!” Kwa
shida nyingi nilijaribu kumweleza kwamba chuki aliyokuwa nayo haikuwa na uwezo wa kumdhuru
aliyekuwa mme wake, isipokuwa kumwangamiza yeye mwenyewe.
Kusamehe humfaidi anayesamehe na anayesamehewa. Chuki, ghadhabu, hasira na kukataliwa ni mambo ya
kinyume ambayo yatatuharibu. Mungu angependa kutuweka huru kutokana na mapepo haya ili tuweze
kuponywa, na kuendelea kuishi maisha yetu. Ndio sababu Mungu ametuamuru tusamehe. Anahitaji
tusamehe. Anatupenda, na anatamani tuwe na afya katika akili zetu, na pia tuwe na furaha. Zaidi ya hayo
yote, angependa kuwa na ushirika pamoja nasi. Angependa ushirika huo uwe bila kizuizi chochote.
Anaelewa kwamba mwanadamu hawezi kumpenda Mungu ambaye hajawahi kumwona, ikiwa hawezi
kumpenda ndugu yake ambaye amemwona (1 Yohana 4:20).
93
Funguo la Amani
Uhisano wote wote wa kibinadamu hutegemea msamaha. Hakuwezi kuwa na amani miongoni mwa watu
bila kuwa na msamaha. Mara kwa mara tunasikia watu wakisema, “Nitamsamehe akisikitika. Siwezi
kumsamehe akiniomba msamaha wakati wowote.” Je, umewahi kuwa na hisia hizo?
Msamaha si tendo lililo kimya. Lina matokeo. Mungu anatufundisha kwamba ni lazima tusamehe bila
masharti yo yote. Hasemi, “akisikitika.” Mungu hahusiki nasi hivyo, na kwa hivyo hatuhitaji kuhusiana na
wengine hivyo. Ulimwengu wetu ungekuwa katika hali mbaya kabisa ikiwa Mungu angengoja mwanadamu
mwenye dhambi aseme, “Nimesikitika” ndipo aamue kutusamehe. Hebu tusisahau kwamba “tulipokuwa
tungali wenye dhambi, Kristo alitufia” (Warumi 5:8).
Wakati tulikosa kumtafuta Mungu, ama msamaha wake, alitupenda bila masharti, na kutusamehe. Kristo
alikufa kwa ajili ya adui zake. Toba hutangulia msamaha. Kama Mungu hangetuonyesha upendo wake
mkuu, hatungeweza kuwa na ujasiri ya kuamini kwamba tungesamehewa. Mwana wa Mungu, akifa
msalabani alisema, “Baba, wasamehe” – hiyo huturejesha kwa Mungu. Hivyo ndivyo tunavyostahili
kuwapenda wengine.
Tunasamehe iwapo wanahitaji, au kutafuta upendo na msamaha wetu. Mara nyingi nimeona ikitendeka
hivi: aliyekosewa anapomwendea mkosaji kwa upendo, moyo wa mkosaji hubadilishwa na kuwa na amani.
Kwa Upande Moja, Bila Masharti
“Mnaposimama kuomba, samehe…” Haya ni maneno yenye nguvu kutoka kwa yule aliyethibitisha
kwamba yanawezekana. Kuna thamani kujua kwamba “aliyedharauliwa na kukataliwa na watu”
ametupenda na kutusamehe.
Kwa kufuata mfano wa Kristo, ni lazima tusamehe bila masharti. Kusamehe kwetu kusitegemee kuombwa
au kutoombwa msamaha na wanaotukosea. Tusiwawekee hatia. Lazima tutupilie mbali hatia ili tuwe na
amani katika fahamu zetu, na amani kwa Mungu.
Matokeo ya Kutokusamehe
Kwa kuonyesha matokeo mabaya ya moyo usiosamehe, Yesu alitoa mifano ya wazi katika kueleza ukweli
huu. Kwa kutilia mkazo alituonyesha jinsi jambo hili ni muhimu kwa Mungu. Uchungu na machukizo
husababisha matokeo mawili mabaya.
Kujiweka Gerezani
Tokeo moja la kutokusamehe limefundishwa katika mafundisho ya Yesu mlimani. Katika Mathayo 5:23-
26, Yesu anasema:
“Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu
yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha
urudi uitoe sadaka yako. Patana na mshtaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule
mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.
Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.”
Maandiko hayo yameweka jambo hili dhahiri mno! Unapoenda kuabudu, na ukakumbushwa na Mungu
kwamba ndugu yako ana neno juu yako (kwa sababu umemtendea kitendo), Yesu alisema kwamba
umwendee ndugu yako mara moja na kuomba msamaha. Je, itakuwaje ukikataa kupatanishwa naye? Wewe
mwenzangu, utajiweka gerezani. Katika vifungu vya 25 na 26, Yesu anamaliza kwa kusema kwamba
ukikataa kupatana na mshtaki wako “upesi”, basi utajiweka gerezani, na hutatoka hadi ulipe deni. Je,
unadaiwa deni ipi? Ni deni ya kusamehe. Kukosa kusamehe, au kupatana na mshtaki wako ni swala nyeti
kati yako na Mungu kwa sababu itakutenganisha na Mungu na kukuweka katika gereza la kiroho. Wakristo
wengi wamefungwa kiroho kwa kukosa kulipa deni zao. Hii ni hatari!
94
Kuweka Wengine Gerezani
Yesu alisimulia kisa kingine ambacho kilitilia mkazo matokeo mabaya ya watu kukataa kusamehe:
“Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na
watumwa wake. Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi. Naye
alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote
alivyo navyo, akalipwe ile deni. Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana,
nivumilie, nami nitakulipa yote pia.
Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni. Mtumwa yule akatoka,
akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia; akamkamata, akamshika koo, akisema,
Nilipe uwiwacho.
Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia.
Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni. Basi wajoli wake
walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote
yaliyotendeka. Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe
wewe deni ile yote, uliponisihi; nawe, je? Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi
nilivyokurehemu wewe?
Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote. Ndivyo na
Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu
yake.
Mfano huu ni kati ya mifano mirefu zaidi na yenye ufafanuzi zaidi kuwahi kuandikwa katika vitabu vya
injili. Imeandikwa kwa ukali. Mtumishi mwovu, aliyesamehewa kiasi kikubwa cha deni ya dola milioni
kumi na bwana wake. Amekataa kumlipa mjoli wake kiasi kidogo cha dola 18, na akamweka gerezani kwa
sababu ya deni hilo ambalo halikulipwa.
Huyu mtumwa alikuwa mtu asiyekuwa na shukrani wala huruma! Amesamehewa, naye akakataa
kuwasamehe wengine. Je, unafahamu mtu yeyote kama huyo? Hiki ni kisa cha kawaida, ama sivyo?
Unapokosa kumsamehe mtu mwingine, unamweka gerezani. Hii inamaanisha kwamba umemfunga
kwamba hawezi kuwa rafiki yako. Hawezi kukubariki au kukusaidia kwa sababu umemhukumu.
Kukasirikia Watu
Je, umewahi kukasirikia mtu bila sababu? Je, umewahi kumkasirikia mtu ukaona huwezi kumpenda au
kumkubali bila kuwa na sababu? Unamkasirikia tu bila sababu. Nini hutendeka basi? Huyo mtu huwa
gerezani kwa sababu umemweka huko. Watu wengi hufanya wachungaji hivyo. Labda amefanya kitu
wasichokipenda, au kukubaliana nacho. Je, huyo mchungaji anaweza kuwahudumia kweli? Je, anaweza
kuwahubiria neno la Mungu? Hawezi kamwe! Umemweka kifungoni. Umemfunga, na hawezi
kukuhudumia. Inawezekana asiweze kufahamu hisia zako kwake, na kutofahamu kuwa umemweka
gerezani.
Ni vyema tuyazingatie maneno ya Yesu: “Ndivyo na Baba yangu wa Mbingu atakavyowatenda ninyi,
msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.”
Katika Kuomba
Tumruhusu Mungu atufundishe kanuni hii mara nyingi: hatuwezi kuwa haki kwa Mungu, hali tu wabaya
kwa wenzetu. Tunapokosa kusemezana, naye Mungu hawezi kusema nasi. Amini hayo, yajue hayo na
utende kitu kuhusu jambo hilo. Usiruhuru chochote kuharibu nafasi yako kwa Mungu na uwezo wako
katika maombi. “Unapoomba, samehe!”
95
Michango
1. Kifungu cha 26 kimewekwa kwa kifungo, au kuwekwa kwa upande katika The New American
Standard Bible kwa sababu hakikuandikwa kwa maandiko ya kwanza ya Injili ya Marko. Lakini Yesu
amefundisha kanuni hii katika maandiko mengine, kama vile ilivyoandikwa katika Mathayo 6:15 na
18:35.
96
97
MUNGU ANAPOKOSA KUJIBU MAOMBI YANGU
Shida kuu la maombi katika kanisa la sasa si ukosefu wa majibu kwa maombi, bali ni maombi
yasiyoombwa. Hatupati kwa sababu hatuombi.
Swali kuu ambalo limewahi kuulizwa kuhusu maombi ni hili: Mbona Mungu hajibu ninapofikiri
nimetimiza mapenzi yake? Hata aliye mwadilifu wa watakatifu wote mara nyingi huona kwamba Mungu
hasikii maombi yake anapoenda kuomba. Hii inawezekana hata ingawa umedai ahadi za Mungu kutoka
kwa maandiko. Wakati mwingine hata theologia unayofahamu, na uthabiti uliyoweka katika maombi
“sahihi” hayana matokeo unayokusudia. Je, utafanya vipi? Yesu alitoa mfano unaohusu maombi, ambayo
inajibu vyema swali hili. Imeandikwa katika Luka 18:1-8:
“Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu siku zote, wala wasikate tamaa.
Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu. Na katika mji
huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui
wangu.
Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali
watu, lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa
kunijia daima.
Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu. Na Mungu, je! Hatawapatia haki
wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao? Nawaambia, atawapatia
haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?
Mfano huu ni wa kadhi ambaye hakumcha Mungu wala kumheshimu. Yeye mlaghai kweli, ijapokuwa ni
kadhi. Hana moyo wa huruma kwa wajane, lakini alipoona kwamba huyu mwanamke mjane habadiliki,
akampa haki yake akisema, “asije akanichosha.” Kitu kinachonishangaza katika mfano huu ni kwamba
Mungu anafananishwa na huyu kadhi mlaghai. Tunahitajika kuwa kama huyo mjane.
Tunahitaji kuomba bila kukoma au kukata tamaa. Tumwendee Mungu kila mara katika maombi na ujasiri
wa huyu mjane mbele ya kadhi mlaghai. Kwa kweli Mungu si kama huyu kadhi kwa hali zote, isipokuwa
mbili: Kwanza, Mungu anaheshimu maombi ya dhati kama vile kadhi alivyoendewa mara kwa mara. Pili,
Mungu atatupa haki yetu ikiwa tutazingatia na kuomba kwa dhati.
Usichoke
Mara nyingi maombi ambayo tulidhani hayakujibiwa ni maombi ambayo tulikatisha. Hatukuweka bidii.
Hatukutafuta haki kama huyu mjane alivyotafuta. Hii ni kweli katika kuombea watu waliopotea dhambini.
Ni lazima tuombe hadi waokolewe. Hi ni kweli katika kuombea jambo lo lote lililo katika mapenzi ya
Mungu kama ilivyoandikwa katika maandiko.
Yesu akasema, “Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni
mvumilivu kwao? (Luka 18:7). Hayo maneno yanamaanisha kwamba Mungu anatamani kutujibu na
kututendea haki. Lakini kuna mambo ulimwenguni yanayomsababisha kuchelewesha majibu yake na
kusababisha watu wake kudumu katika maombi.
Maombi Na Mungu Mwenye Enzi
Wakati fulani nilikuwa na kikundi cha watalii kule Israeli. Tulitembelea makavazi yaliyoonyesha jinsi
Wayahudi walivyoangamizwa. Wayahudi kadhaa katika kikundi chetu walitatizwa sana na ratiba ya picha
zilizoonyesha unyama waliotendewa Wayahudi na Wanazi, walipokusanywa kwenye kituo. Wengine
walikasirika. Tulipokuwa tukiketi sebuleni na kuongea, mwanamke mmoja Myahudi kutoka Florida
98
aliniambia, “Mungu alikuwa wapi wakati Wayahudi walimhitaji huko Yuropa?” Swali kama hilo kweli
hututikisa! Kwa kweli mamilioni ya Wayahudi waliomba Yehova Mungu – Mungu wao. Mungu wa
Ibrahimu, Isaka, na Yakobo alikuwa wapi? Aliruhusu wendawazimu wa Hitler kuwatendea unyama watu
wake wateule. Mioyo yetu hulia, tukiuliza “Kwani nini? Kwani nini? Kwani nini?”
Kuona nyuma ni bora kuliko kuona mbele. Historia imetudhibitishia mamlaka ya Mungu katika uaminifu
wake kwa Wayahudi. Alisikia kilio chao na kuwakomboa. Amewatendea haki. Wengi watashuku usahihi
wa maneno hayo, lakini ni kweli hata hivyo. Mungu, kwa mapenzi yake, aliruhusu Wayahudi kufanyiwa
unyama, ili atimize kusudi lake kamilifu kwa taifa la Israeli.
Tulipoketi kwenye jumba hilo la maonyesho ya jinsi Wayahudi walivyoangamizwa, nilimweleza yule
mwanamke wa Kiyahudi aliyekuwa amekasirika sana hivi, “Je, umewahi kufikiri hivi: Kama hakungekuwa
na unyama huo, basi hakungekuwa na taifa la Israeli. Wayahudi waliosalia kule Yuropa hawakuwa na
mahali pengine pa kwenda. Walilazimika kwenda Palestina. Basi hapo pana nchi ya kitaifa kwa
Wayahudi.” Aliniangalia kwa mshangao na kusema, “Sijawahi kufikiri hivyo.” Nikasema, “Mungu huunda
mazuri kutokana na mabaya, na hasa inapolingana na makusudi yake.”
Ni Mungu Wa Haki
Tunapoendelea kushangaa kwa nini Mungu hatendi kulingana na ratiba yetu, ama kujibu maombi jinsi
tunavyodhani anastahili kujibu, kumbuka kwamba anaona “picha kubwa” wakati ambapo tunaona tu “picha
ndogo.” Darubini anayotumia ni kubwa, bali sisi tunaona kutumia darubini ya kuonea vitu vidogo sana. Ni
lazima tusadiki kwamba “Baba anayafahamu yaliyo mema” na kwamba kila mara atafanya yaliyo mema.
Tuwe kama yule mjane aliyekwenda kwa kadhi akidai “haki,” akiamini na kutulia kwa mapenzi ya Mungu
mwenye enzi.
Yesu alimaliza kusimulia kuhusu kadhi mlaghai kwa kuuliza swali hili, “walakini, atakapokuja Mwana wa
Adamu, je! Ataiona imani duniani?” (Kifungu cha 8). Kwa hakika, maombi yetu kuhusu amani, upendo, na
undugu ulimwenguni hayawezi kujibiwa mpaka hapo Mwana wa Adamu atakaporejea. Kisha kila moja
wapo ya maombi hayo yatajibiwa! Tuamini kwamba makusudi yake yanatekelezwa kwa kujibiwa kwa
maombi yetu. Hebu tumsumbue kadhi wa walimwengu ambaye kwa kweli ni Baba Wetu aliye mbinguni
mwenye mapenzi tele!
Kuna sababu nyingine zinazosababisha maombi yetu kutojibiwa, au kutupa jibu “la” kutoka katika kiti cha
enzi cha mbinguni. Katika kitabu kingine, niliandika kuhusu maombi yasiyojibiwa kutokana na kitabu cha
Yakobo sura ya 4, ambapo tunaona sababu tatu zinazosababisha Mungu kutojibu maombi yetu. Hebu
angalia katika sehemu hizi unapoona kwambu Mungu hajibu maombi:
• Nje. Tazama maombi yako. Yakobo 4:3 inasema “Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu
mwaomba vibaya, ili mvitumia kwa tamaa zenu.” Mungu hawezi kujibu ombi lilioombwa vibaya
kwa jibu sahihi. Mara nyingine hatuombi kulingana na mapenzi yake.
• Ndani. Chunguza maisha yako. Huenda ikawa maisha yako si sahihi. Katika Yakobo 4:4, anaita
aliyowaandikia “wazinzi.” Kumbuka, ni maisha yaombayo.
• Juu. Mtazame Mungu. Anaweza kuwa anajibu maombi yako lakini hata hutambui.
Anaweza labda kuchelewesha jibu, au kuijibu toauti kuliko unavyotarajia.
Michango
1. Tazama Sura ya 9 katika Questions New Christians Ask (Old Tappan, New Jersey: Fleming H. Revell
99
KUJIFUNDISHA KUOMBEA WALIOPOTEA
DHAMBINI
“Uinjilisti ni nini? Ni kujibwaga tu kwenye uwanja wa vita na kuchukua nyara zinazotokana na
ushindi uliopatikana katika maombi.”
Je, umewahi kusikia mtu kanisani akiomba hivi: “Oh, ndiyo Bwana. Iwapo kuna watu hapa ambao
hawajaokoka, uwaokoe wote. Amin” Maombi kama hayo ni kama kumsikiliza mtoto mchanga akiomba
kabla kulala, akisema “Mungu, okoa watu wote ulimwenguni. Amin.”
Maombi hayo kwa kweli yanavutia, na yana mwongozo wa roho mtakatifu! Je, kuna mbinu fulani
inayohitajika ili kuombea wengine waokoke? Kuomba ukiwa na ufahamu wa Bibilia kunaweza
kukuridhisha katika kuombea watu wengine. Mungu anashauku ya kuwaokoa waliopotea katika dhambi.
Anaweza kuwaokoa tu kupitia kwa kujitolea kwetu kuwaombea hao waliopotea dhambini.
Mungu wa Kusita?
Kuna watu wanaofundisha kwamba maombi yetu hayana maana kwa Mungu. Ikiwa ni hivyo, basi kitabu
hiki hakina manufaa kwetu na kukiandika ni hasara. Tutakuwa tumepoteza muda wetu bure. Wengine
wamehisi kwamba kuwaombea waliopotea dhamibini ni kumwomba Munga ambaye hajali na hahusiki
katika kuwaokoa wale tunaowaombea dua. Hivyo sivyo tumwonapo Mungu aliyeelezwa katika maadiko.
Kama vile Ibrahimu alivyoombea Sodoma hadi Mungu akawa tayari kuuokoa mji huo iwapo
kungepatikana angalau watu kumi waadilifu, ndivyo Yesu anavyotuambia kwamba alitumwa na Baba wa
mbinguni aliyejawa na mapenzi tele ili kutafuta na kuokoa waliopotea. Paulo alitumwa na Mungu “ambaye
hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli” (1 Timotheo 2:4). Petero pia alithibitisha
mapenzi ya Mungu kwa waliopotea dhambini alipoandika kwamba “Bwana hakawii kutimiza ahadi yake,
kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali
wafikilie toba.” (2 Petero 3:9).
Jinsi Ya Kuombea Waliopotea
Kuombea waliopotea ni dua maalumu. Tunapoombea rafiki zetu ambao hawajaokoka, ni heri tuelewe
kwamba Mungu ana nia zaidi ya kuwaokoa, kuliko tunavyowaombea. Tunaamini ahadi ya Mungu ya
kuokoa waliopotea. Lakini, tunastahili kuwa na ufahamu katika kuomba. Tutumie vifaa ambavyo Mungu
ametukabidhi. Ametupa funguo za uflame ili tuweke huru waliosetwa. Tuna kazi ya “kufunga na
kufungua.”
Kuombea waliopotea , kwa hakika, ni vita vya kiroho. Si kumsihi Mungu tu. Tunastahili kuyaelekeza
makombora yetu kwanza kwa shetani; pili ni kuomba ushawishi wa roho mtakatifu; na tatu ni kuweka hoja
zetu mbele ya kiti cha enzi cha Mungu Baba.
Adui Na Mateka Wake
Shetani, ambaye ni adui wetu nambari moja, hupinga na kuzuia wokovu kwa watu ambao wamepotea.
Amewateke nyara na kuwafanya vipofu kwa injili. Wanaishi gizani kiroho, na kwa hivyo, wanahitaji kuona
mwangaza wa injili. Pia wanahitaji kufunguliwa minyororo ya shetani, na kuwekwa huru.
Mtu aliyepotea hawezi kuona ukweli “…injili yetu imesitirika…kwa hao wanaopotea, ambao ndani yao
Mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasiamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wa Kristo …” (2
Wakorintho 4:3-4).
100
Aliyepotea dhambini ni mtumwa ambaye ni mateka wa shetani “…ili kama ikiwezekana, Mungu awape
kutubu na kujua kweli, wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambao hao wametegwa
naye, hata kuyafanya mapenzi yake.” (2 Timotheo 2:25,26).
Hali ya upotevu ni hali mbaya mno. Zamani tulikuwa hivyo, yaani wafungwa na vipofu. Hii ndio sababu
mtu asiyeamini huona mambo ya roho kuwa mambo yasiyopendeza. Amepofushwa, asione ukweli.
Wakorintho Wa Kwanza 2:14 inatueleza kwamba mambo ya roho ni upuzi kwa mtu kama huyo. Ni Yesu
pekee, na nguvu za Roho Mtakatifu, ambaye anaweza kufumbua macho yake aweze kuona ukweli. Basi
tunastahili kuombea waliopotea badala ya kuwahukumu.
Mtu ambaye hajaokoka ni kipofu na mateka katika dhamira yake. Kwa kuwa akili zake zimepofushwa,
anahitaji ufunuo ili aweze kubadilika. Mabadiliko haya yanawezekana tu ikiwa tutajitolea mhanga
kumwombea dua kwa Mungu. Ushahidi wetu huwezi kuwa wenye maana iwapo mwenye dhambi
hatabadilika. Hawezi kusikiliza tumwambiavyo, na kumpokea Kristo kama angali chini ya mamlaka ya
shetani. Maombi kabla ya uinjilisti yanaweza kubadilisha hali ya mpotevu.
Ushindi
Hatupaswi kamwe kukata tamaa na kuwaacha rafiki zetu kutokomea dhambini. Wamekwisha kombolewa.
Kumbuka masomo yetu katika Wakolosai Sura ya 2. Yesu alimshinda na kumpokonya silaha zake mbili
ambazo ni dhambi zetu, na mshahara wa dhambi, ambayo ni kifo.
Waraka wa Kwanza Wa Yohana 3:8 inatufahamisha kwamba “…kwa kusudi hili Mwana wa Mungu
alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.” Jukumu letu ni kutumia ushindi huo kama silaha yetu katika
maombi. Waliopotea wangali wapotevu hata ingawa shetani alishindwa kutokana na kufa na kufufuka kwa
Yesu Kristo. Wangali mateka wa shetani. Ukombozi wao unaweza kupatikana tu kupitia dua zetu kwa
niaba yao. Uhuru wao utapatikana tu ikiwa shetani ataamrishwa kuwaachilia katika jina lenye ushindi la
Kristo.
Kushindwa kwa shetani, na kutimuliwa kwake kutoka kwa moyo wa binadamu na fikira zake, kutategemea
uthabiti wetu dhidi ya shetani. Ni wajibu wetu kutumia funguo za mbinguni, ambazo ni silaha ya maombi
kwa kuvuta waliopotea wamjie Kristo. “Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika
Mungu hata kuangusha ngome.”
Kudai Deni
Unapomkemea Ibilisi, kumbuka kwamba una haki kumdai rafiki yako aliyepotea dhambini. Yesu tayari
amelipa deni ya ukombozi kwa watu wote. Hao si mali ya shetani tena. Unapomkemea shetani ukitumia
mamlaka uliyopewa la jina la Yesu, na kushambulia malango ya kuzimu, shetani lazima atatii. Amini
ukidai na kuomba katika jina la Yesu!
Zaidi Ya Kukemea
Kuombea waliopotea ni zaidi ya kukemea adui. Ni kujibwaga kitini pa enzi na kuomba kwa thati kwa niaba
ya mpotevu. Mimi huombea mambo mawili ninapoombea waliopotea. Baada ya kumwondosha Ibilisi
vitani kwa siku hiyo kwa maombi, humwomba Mungu atume mtu kumshuhudia rafiki yangu
ninayemwombea. Kwanza namwomba Yesu mwenyewe amtembelee . Roho Mtakatifu atakuwakilisha kwa
mtu huyo ikiwa utamwomba kufanya hivyo. Itakubidi kumwomba roho mtakatifu kila siku kukaripia,
kukemea na kushawishi mwenye dhambi kuona hitaji lake. Pili, mwombe Mungu amtume mtu anayeweza
kumshuhudia injili. Hi inaweza kuwa kwa njia ya runinga (televisheni), kijitabu cha injili (gospel tract)
ambayo labda anaweza kuokota, au hata kupitia kwa mtu fulani asiyemfahamu. Ndiyo, hiyo ni kazi ya
Mungu kutenda, lakini tunastahili kumwomba atume wafanyi kazi kwa mavuno (Mathayo 9:38).
Tukiomba kwa ufahamu, tutagundua kuwa ni rahisi, mradi tu “tuombe kwa ufahamu.” Ifuatayo ni jinsi
tunavyoweza kuombea waliopotea:
1. Kemea adui. Omba, “Ibilisi, naja kinyume chako kwa niaba ya rafiki yangu
_____________________. Katika jina la Yesu nakuamuru umwachilie na utambue kwamba
101
yeye si wako tena, bali ni wa Bwana Yesu. Kwa hivyo nadai wokovu wake katika jina la
Yesu.”
Lazima upigane kila siku hadi wokovu upatikane. Jipe moyo. Shetani anapotambua ujasiri
wako, atatoroka. Lakini hawezi kutii ikiwa imani yako ni hafifu, na kudumisha uombezi
wako.
2. Omba Roho Mtakatifu afanye kazi ya Kumshawishi. Omba Yesu amtembelee rafiki yako leo.
Unaweza kuomba hivi: “Bwana Yesu, nakuhitaji ubishe katika moyo wake. Mwonyeshe
upendo wako. Fumbua macho yake, na kusema naye leo.”
3. Omba Mungu awatuma Waumini. Unaweza kuomba hivi: “Baba, tuma mtu wa kumshuhudia
rafiki yangu. Mzingire na upendo wako. Mwonyeshe mtu atakayekuwa mfano bora kwa
maisha yake na kumfanya kuwa karibu nawe.”
4. Shukuru Mungu kwa Wokovu Wake. Dai Yohana 5:14. Amini kwamba rafiki yako
anaokolewa. Mshukuru Mungu kwa wokovu wa rafiki yako. Kisha mwachie Mungu atende
kazi yake ya kuokoa kwa wakati wake mwenyewe. Lakini zidi kuomba, na kubisha, naye
ataokolewa.
102
103
NAWEZAJE KUWA MWOMBEZI?
Mwombezi wa kweli ameishi na kujifunza kwamba sheria ya mavuno ya kiroho hutokana na kifo.
“Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo
peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.”
-Yohana 12:24
Karibu miaka arobaini na mitano iliyopita, Daktari S.D. Gordon aliandika maneno ya changamoto
yafuatayo:
Watu shupavu ulimwenguni leo ni wanaosali. Si elezi kuhusu watu ambao wanaongea juu ya
maombi; ama wale ambao wanaweza kueleza wazi wazi maana ya maombi. Naongea juu ya watu
ambao wanatafuta wakati wa kuomba. Hao ndio wanaomtemdea Mungu kazi nyingi katika
kuwavuta watu kwa Yesu, kutatua matatizo, kuleta uhuisho makanisani, kujitoa mhanga kibinafsi
na kwa fedha kwa kazi ya umisheni, kuwapa changamoto wale ambao wamejitolea kwenda vitani
mahali ambapo vita ni vikali, ili ulimwengu wetu udumu, ukiwa wenye maana zaidi.
Maneno hayo ni ya ajabu sana. Je, umeona kwamba ni mwombezi anayefanya ulimwengu kuwa wa maana
kuudumumisha zaidi? Kudumishwa na kufanywa kuwa yenye maana kwa ulimwengu huu hakutokani na
serikali, elimu, utamaduni ama cho chote ambacho mwanadamu anaweza kutenda. Ni maombi ya dhati
ndiyo yanaweza tu kutenda hayo. Je, ungependa kuwa moja kati ya watu hao washupavu ambao Mungu
angependa kutumia kutimiza makusudi yake duniani? Si tu kusoma kuhusu maombi, ama kuongea juu ya
maombi, bali ni kuomba kwa kweli.
Kama tulivyoona hapo mbeleni, maombi yanaweza kuchukua hali tofauti. Yanaweza kuwa ni mazungumzo
yako na Mungu Baba. Maombi ya kushirikiana na Mungu katika mazungumzo ni muhimu sana. Ni muhimu
kupata mahali penye kimya na kuwa na muda wa faragha na Mungu, ili kumsifu na kumwabudu. Inayozidi
yote ni kuisikiliza ile sauti ya upole ndani ya roho yako, ili siku yako iwe chini ya mwongozo wa Mungu.
Pili, katika maombi unaweza kumwomba Mungu mahitaji yako binafsi. Ni mwenye dhambi ambaye
anamwomba Mungu msamaha wa dhambi na mahitaji ya kila siku kwa unyenyekevu. Mombi pia yanaweza
kuwa dua kwa niaba ya watu wengine. Watu ambao huingia katika huduma ya maombi huwa wameingia
katika utumishi mkubwa kabisa hata kukaribia Patakatifu pa Watakatifu. Kuwa mwombezi ni
kujitambulisha na Yesu ambaye ni mwenye upendo na huruma kwa ulimwengu uliopotea dhambini.
Maombi ya ushirika (Communion) ni ya kibinafsi - kwa maana yananihusu mimi. Maombi ya sala
(petition) pi ani ya kibinafsi – kwa maana hunifikia ndani. Maombi ya uombezi (intercession) yanahusu
mambo ya nje ya mwombaji, na hubadilisha ulimwengu mzima!
S.D. Gordon huita uombezi kilele cha maombi. Anamaanisha kwamba kupitia maombi (Ibaada) Mungu
anaweza kutugusa ili atutumie kuugusa ulimwengu. Kwa maombi na dua, tunaweza kujazwa nguvu zake.
Basi nguvu hizi zinadhihirika katika kuwaombea watu wengine.
Huwezi kuwa mwombezi ikiwa hujakwea mlimani na kukutana na Mwenyezi Mungu. Mtu anapokutana na
Mungu basi yeye huweza kuhudumia kabisa ulimwengu uliopotea kwenye dhambi, kwa maana Mungu
mwenyewe anauombea ulimwengu wetu. Kuwa karibu na Mungu ni kushiriki mzigo wa moyo wake kwa
ulimwengu uliopotoka. Waingiao katika huduma hii ya uombezi ni watu “walioona mwangaza” nafsini
mwao ili wauone ulimwengu ulivyo gizani.
Kuwa Mwombezi
Je, mtu yeyote anaweza kujiunga na huduma hii? Tunaweza kujibu hivi: ndiyo, na sivyo. Tunapotazama
maandiko, tunafundishwa kuombea wengine. Paulo anatuambia tuombe “…kwa ajili ya watu wote, kwa
104
ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka …” (1 Timotheo 2:1-2). Mkristo anastahili kuombea “watu
wote”.
Kila mkristo mwaminifu anastahili kuishi maisah ya uombezi. Lakini si wakristo wengi wanaoweza kuwa
mashujaa wa maombi, ambao wamejitolea mhanga kwa Mungu, na kuishi maisha ya kuombea watu
wengine. Waombezi ni wale ambao wamejiunga na Mungu katika kutambua kwamba ulimwengu umepotea
na unahitaji kukombolewa. Huduma hii si ya watu hafifu wa moyo ama wale walio dhaifu katika imani
yao.
Wateule
Huduma ya kuombea watu ni huduma ya watu walioteuliwa. Washiriki wake ni wachache, wakiwemo watu
mashuhuri, na wasiotambulika. Musa aliteuliwa katika huduma hii. Alitoa maisha yake vilivyo kwa
Mungu. Alisimama “katika pengo” kwa sababu ya taifa. Alikuwa tayari kutoa uhai wake kuzuia ghadhabu
ya Mungu iliyowaka dhidi ya Waisraeli walioasi. Akiwa ameweka maisha yake hatarini, aliomba hivi:
“Aa! Watu hawa wametenda dhambi kuu. Wamejifanyia miungu ya dhahabu. Walakini sasa, ikiwa
utawasamehe dhambi yao – na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika” (Kutoka
32:31,32).
Paulo, mtume mpendwa, amehitimu kuwa katika kikundi hiki. Alijitwika mzigo wa taifa lililopotea la
Wayahudi. Katika kitabu cha Warumi, alikiri hivi: “Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua
yangu nimwombavyo Mungu ni kwa ajili yao, ili waokolewe” (Warumi 10:1).
“Nasema kweli katika Kristo, sisemi uongo, dhamiri yangu ikinishuhudia katika roho mtakatifu,
ya kwamba nina huzuni nyingi na maumivu yasiyokoma moyoni mwangu kwa maana ningeweza
kuomba mimi mwenyewe niharimishwe na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, jamaa
zangu kwa jinsi ya mwili” (Warumi 9:1-3).
Tunaona mtu ambaye alitambua upotevu na uchungu wa watu wengine kiasi cha kutoa uhai wake kwa ajili
yao.
Hicho ndicho kiini cha maombezi, na kilele cha maombi. Paulo alikuwa mwombezi shupavu. Katika
Matendo Ya Mitume 20:21 aliwakumbusha Waefeso kwamba “mkikumbuka kwamba miaka mitatu, usiku
na mchana, sikuacha kumwonya kila mtu kwa machozi.” Paulo alikuwa ni mwalimu, mmisheni, mtume,
mwandishi, na muinjilisti. Hayo, yalikuwa ni kando na mwito wake halisi, ambayo ilikuwa ni uombezi.
Yesu, Mwombezi
Wamfuataye Bwana huanza kufanana naye. Karne nyingi kabla Yesu kuzaliwa, nabii Isaya alimtaja kuwa
ni mwombezi.
“Kwa hivyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, naye atagawanya nyara pamoja nao walio
hodari, kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, akahesabiwa pamoja na hao wakosao.
Walakini alichukua dhambi za watu wengi” (Isaya 53:12).
Bwana wetu Yesu ndiye Masihi wa ahadi. Kwa kweli alikuwa ni mwombezi hodari aliyeishi, aliyependa,
aliyeomba na kufa kwa niaba ya wengine. Katika Luka Mtakatifu 22:32, Yesu alimwombea Simoni Petero
ambaye Yesu alijua atamsaliti. Alisema, “Simoni, nimekuombea ili ukibadilishwa, utunze kondoo zangu.”
(Maneno ya mwandishi).
Katika Yohana sura ya 17 tunaona sala ya Bwana. Tunaona maombi ya ukuhani wa Kristo katika kuombea
kanisa lake. Anaombea wafuasi wake na wale ambao wataokolewa karne nyingi baadaye kutokana na
ushahidi wa wafuasi hao, tukiwa miongoni mwao.
Yesu alikuombea, rafiki yangu. Aliniombe pia. Alikuwa mwombezi, si katika uhai wake tu, bali hata katika
kifo chake. Alihesabiwa pamoja na waasi, naye akawaombea. Alipokuwa akifa msalabani, aliomba kwa
105
Mungu akisema, “Baba wasamehe, maana hawajui watendalo” (Luka 23:34). Mwombezi wetu shupavu
aliombea wengine hata katika kifo chake msalabani.
Yesu Kristo hivi sasa ameketi mkono wa kuume wa Mungu akituombea! Waebrania 7:25 inatueleza hivi
kuhusu Bwana Yesu: “Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye;
maana yu hai sikuzote ili awaombee.” Kitu ambacho ni cha maana sana kwa Kristo kwa wakati huu ni
maombezi. Yesu anatuombea wakati huu, na anaishi makusudi ya kutuombea. Yeye ni mwombezi wetu!
Maisha na Usemi
Je, unawaombea watu wengine kwa uaminifu? Kuwa mwombezi ni huduma iliyo ngumu sana, kwa sababu
kwa kawaida, sisi hujipenda. Kuishi maisha ya maombi tu ndio kutatuwezesha kuombea wengine. Hii
inamaanisha kwamba ni lazima tutambue udhia za watu wengine ikiwa tutawaombea kikamilifu. Wazazi
hujali watoto wao, na kwa hivyo huwaombea. Vivyo hivyo, tunapowajali wengine, basi tutawaombea kwa
kutambua dhiki zao. Hatuwezi kuombea watu wengine isipokuwa kwa kuishi maisha ya maombi.
Kutambulikana
Musa aliwaombea wana wa Israeli kwa sababu alijitambulisha nao kama moja wao. Alichukua jukumu la
wana wa Israeli waliotangatanga jangwani kama lake. Aliwajibika katika dhambi zao, kuasi kwao, na
mahitaji yao. Kwa sababu hiyo aliwaombea. Bwana Yesu alikuombea. Aliniombea pia. Akiwa Masihi, na
pia mwokozi, alihesabiwa pamoja na waasi. Hiyo inamaanasha Yesu alijitambulisha na dhambi za
walimwengu.
Yesu alipomwendea Yohana mbatizaji ili abatizwe naye (Mathayo 3:13-17), ingawa hakuwa na dhambi,
Yohana kwa unyenyekevu mwingi alimjibu, “Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?”
Lakini Yesu akamwambia, “Kubali hivi sasa, kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote.”
Katika kubatizwa, Kristo alijitambulisha na dhambi za walimwengu. Alikuwa karibu sana na wenye
dhambi hadi kujitambulisha nao katika ubatizo. Ilikuwa ni mfano wa yale aliyotenda msalabani - kujitwika
dhambi zetu. Waraka wa Kwanza wa Petero 1:18,19 inatuambia kwamba tulikombolewa, si kwa vitu
viharibikavyo kama vile fedha au dhahabu, bali kwa damu ya thamani ya Yesu Kristo. Kuombea wengine
ni matokeo ya maisha ya maombi. Maisha ni lazima yapatie usemi mwelekeo. Isipokuwa nijitambulishe na
wengine katika haja zao, ni vigumu sana niweze kuwaombea. Nilipokuwa chuoni, kulitokea tukio ambalo
lilitikisa uliwengu wa uinjilisti. Wamisheni wengi waliuawa sana kule Marekani ya Kusini. Moja wao
anayejulikana kama Jim Elliot, aliuawa na Wahindi ambao alikuwa akijaribu kuwashuhudia kuhusu upendo
wa Mungu. Jim alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Wheaton, karibu na mji wa Chicago, Illinois,
alikuwa kila wakati akiandika katika kitabu chake chenye habari za mambo ya kila siku (diary). Alikuwa
na moyo wa kujihusisha na huduma sana hadi akaamua kuwa mmisheni. Alikuwa na lengo la kupeleka
injili kwa watu ambao hawajasikia injili ya Kristo. Jim, akiwa na rafiki yake moja kwa jina Nathaniel Saint,
alisikia habari za kabila moja la wahindi walioishi katika msitu wa Peru. Kabila hilo halikuwa limesikia
kamwe habari za Kristo. Miaka mingi kabla kwenda kwake Marekani Ya Kusini, Jim alianza kuomba na
kuandika maombi yake katika kitabu chake chenye habari za mambo ya kila siku, akimsihi Mungu ampe
nafasi ya kwenda kuwahubiria kabila hilo la Wahindi kuhusu Yesu.
Siku moja Jim aliandika maneno haya: “Mungu, unifanye kuwa mtu matata. Wafanye wale wanaokutana
nami kuamua. Nisiwe kama kibao cha kuonyesha watu njia, bali nifanye kuwa kama uma, ili watu
wanaokutana nami wageukie njia moja au nyingine wanapokutana na Kristo ndani yangu.” Jim Elliot
alikuwa mwombezi. Katika uhai wake, alijitambulisha na dhiki na upoteveu wa kabila nzima la watu.
Hakuomba tu, bali aliweka maombi yake katika vitendo, alipojitolea kuwahubiria Wahindi wa Quechua
habari za Yesu. Kuombea watu wengine ni matokeo ya maisha ya maombi. Ni vigumu kuwa na huduma ya
kuombea wengine hadi utakapoanza kujali watu. Usipokuwa tayari kuhusika katika dhiki, na kutambua
mahitaji na maumivu ya wengine, basi hutaweza kulipa gharama ya kuwaombea.
Ni Zaidi Ya Maombi
Huduma ya kuombea wengine ni wazi kwa wale wanaoutafuta na kuwa tayari kulipa gharama yake.
Huduma hii si sawa na kuombea watu tu. Mtu moja kwa jina Norman Grubb, kwa utangulizi wa kitabu
106
kinachoitwa The Intercession of Rees Howells, anamtaja Howells akisema, “Maombi yameshindwa. Ni
maombezi tu yanayoweza kutupatia ushindi.” Hebu tazama tofauti. Maombezi ni tofauti na kuombea watu
tu.
Ni mara ngapi umehisi kuwajibika, ukaonyesha kujali wengine kwa kujihusisha na huduma au kuanza
kuombea watu? Baada ya kitambo kidogo ukaona kwamba huwezi kuendelea. Kwa sababu gani? Ni kwa
sababu hukudumisha moyo huo na shauku ya kuwaombea wengine katika maombi yako. Uombezi ni
mtindo wa maisha. Si mzigo tu wa muda, ama kuwajali watu kwa muda mfupi tu. Uombezi hutokana na
moyo uliovunjika. Ni matokeo ya kutembea katika roho na kukaa ndani ya Kristo.
Katika kitabu cha Zakaria 12:10, Roho Mtakatifu ameitwa roho wa maombi. Hii ni kusema kwamba asili
ya Roho Mtakatifu anayeishi ndani ya waumini ni kuombea wengine. Maandiko yanasema katika Warumi
8:26 kwamba Roho Mtakatifu hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Roho Mtakatifu ni
mwombezi. Maisha ya Yesu hapa ulimwenguni ilikuwa maisha ya kuombea wenye dhambi. Alikufa kama
mwombezi, na kuomba maombi ya uombezi. Tukimruhusu Yesu kukaa ndani yetu na kutuongoza, basi
tutakuwa na asili yake. Tutakuwa na moyo wa kuombea wengine na kuishi maisha ya kuombea wengine.
Tunapoishi kwa kumtii Yesu, tutaishi tukiombea watu kama vile alivyoishi. Tutaiga namna alivyoombea
watu.
Rees Howells na John Hyde
Katika historia ya kanisa, watu wengi wamehusika katika maombezi hadi wakatambulika katika huduma
hiyo ya maombezi. John Hyde aliishi maisha yake yote kule India akiwa mmisheni. Alikuwa na mzigo
mkubwa sana moyoni mwake kwa ajili ya watu waliopotea. Alizingatia sana maisha ya maombi, hadi
akabandikwa jina “Hyde mwombaji.” Ilisemekana kwamba Hyde “Alidhibitisha kwamba maombi
yalikuwa na nguvu sana huko India kuleta watu kwa Kristo, wakati ambapo kwa imani alidai mtu moja
kwa siku, kisha wawili, alafu wanne.”
Rees Howells, ambaye alikuwa wa chuo cha Bibilia cha Wales, pia alikuwa mtu wa namna hiyo. Ni
mbingu tu iwezayo kutambua nguvu za maombi ya Howells. Ukimtaja miongoni mwa watu wanaofahamu
kanisa liombalo, watakuambia kwamba Rees alikuwa mwombezi. Ijapokuwa alikufa mnamo mwaka wa
1950, atakumbukwa daima kama mtu ambaye maisha yake aliutoa kwa kuomba.
Maombezi ni njia inayopitiwa na watu wachache sana. Hewa ya maombi si sawa sana kwa wengine wetu.
Ukitamani kuwa mwombezi, itakulazimu upatane sana na Kristo kiasi cha Roho wake kumiliki maisha
yako. Kuishi kama mwombezi kunatokana na kudumu ndani ya Kristo. Unapowajali watu,
unapowaoembea, na hata kutenga nafasi na kuacha shughuli zako ili uombe, basi Kristo anaomba kupitia
kwako.
Mwombezi Anafahamu Ushindi
Tunapodumu katika Kristo, tutambue kwamba maombi yetu yatajibiwa. Mwombezi humwakilisha Mungu.
Yeye ni mpatanishi baina ya Mungu na mwanadamu. Humwakilisha anayemwombea katika maombi. Hisia
zake na uchungu anaopata, ni kwa niaba ya anayemwombea. Yeye husimama katika pengo bila kukoma,
hadi ushindi upatikane. “Tukikaa ndani ya Kristo, na maneno yake yakikaa ndani yetu, tujue kwamba
tuombalo lote tutatendewa” (Yohana 15:7).
Mwombezi, katika kusimama imara pamoja na Mungu, ni mshindi. Mungu aongeze watu wengi kama hao
katika kanisa lake. Lango la Maombezi ni wazi kwa wote walio na ujasiri wa kuingia kwenye huduma hii.
Mamia ya makanisa huendelea juma baada ya juma, na mwaka baada ya mwaka, bila kuwa na waombezi
ambao ni washiriki.
Wapi watu wanaoweza kuomba hadi Bwana wa Mavuno arudi? Je, kuna watu unaowaombea kila siku bila
kukoma? Je, kuna yeyote unayemsumbukia moyoni, ukimwombea na kusema, “Mungu msaidie huyu, ama
sivyo nahisi kufa”? Je, umewahi “kusimama katika pengo” kwa niaba ya mtu yeyote? Huduma ya
maombezi ni kwa wale walio tayari kuchukua mizigo ya wengine.
107
Namshukuru Mungu kila siku kwa wale waaminifu wanaoniombea na kuombea huduma ambayo Mungu
amenipa. Mara nyingi nimehisi uwepo wa maombi ya watu wa Mungu ninapohubiri, hudumu, na
kushuhudia katika sehemu nyingi za uliwengu.
Wakati fulani, kwa majuma matatu hivi, nilienda kuhudumu kule Hungary, Romania, Czechoslovakia, na
Poland. Mara nyingi nilijipata katika hali ngumu sana. Nilifuatwa mara nying na makachero. Nyakati
zingine walinisumbua na kudadisi mambo yangu. Kila mara niliona nguvu za Mungu. Alifanya miujiza
kwa kujibu maombi. Mungu alinilinda na kunipitisha katika mipaka ya wakomunisti! Rafiki zangu wengi
“walisimama pengoni” kwa niaba yangu. Maombi yao yalifungua njia pana kwangu.
Katika huduma ya maombezi, Mungu huheshimu maombi ya waumini waliojazwa na roho. Mkristo
anapojiachilia kwa Kristo na kudumu ndani yake, ndipo maombi yake yanaweza kubadili na kuleta tofauti
katika ulimwengu wake. Anaweza kumhusisha Mungu katika vita kwa nguvu zinazotokana na maombezi
yake. Natamani Mungu akuite katika huduma hii ya maombezi.
Unaweza kuwa na huduma ya kipekee ya maombi ambayo inaweza kubadili ulimwengu wako. Maombi
yako yanaweza kuleta totauti. Tukiungana pamoja katika maombi, tutaweza “kutia sukari katika
ulimwengu huu”, hadi Kristo atakaporudi.
Michango
1. S.D. Gordon, Quiet Talks on Prayer (Grand Rapids, Michigan: Baker book House, 1980),pp.13,14
2. Ibid.,p43
3. Elizabeth Elliot, Through the Gates of Splendor (Wheaton, Illinois: Tyndale House Publishers, 1981).
4. Doris M. Rucoe, The Intercession of Rees Howells (Fort Washington, Pnnyslvania: Christian
Literature Crusade, 1983), p.9.
5. Francis McGaw, Praying Hyde (Minneapolis, Minnesota: Bethany Fellowship, 1970), p.9.
108
109
KUFUNGA NI NINI? INAHUSIANA VIPI NA
MAOMBI?
Je” Tunawezaje kurudia nguvu za mitume na huku tunapuuza kufuata desturi ya mitume?
Tunawezaje kutarajia nguvu itiririke kama hatujatayarisha njia? Kufunga ni njia ambayo
imechaguliwa na Mungu ya kuwezesha neema na nguvu zake ziweze kutiririka.
--Arther Wallis, God’s Chosen Fast.
Je, kufunga ina mahali maalumu katika maisha ya Mkristo wa kisasa katika karne ya ishirini? Dhana yangu
ni kwamba asili mia tisini na tano ya Wakristo hawajawahi kushuhudia masaa ishirini na manne ya kufunga
kulingana na Biblia. Waumini wachache wanaelewa vyema maana ya maombi na kufunga.
Kufunga Ni Nini?
Tusidhani kwamba kila mtu anaelewa maana ya kufunga. Wengine wanafikiri kufunga ni kutokula,
wengine wanafikiri kufunga ni tendo la kale la kidini ambalo halina nafasi katika kanisa la kisasa.
Tunamaanisha nini tunapowasihi watu “wafunge na kusali” (Mathayo 17:21)? Katika Agano la Kale, neno
hili kwa Kiebrania linamaanisha “kufunga kinywa”, katika Agano Jipya, neno hilo kwa Kiyunani
linamaanisha ‘kutokula’, ama kujiepusha na kula. Hata hivyo, kufunga ni zaidi ya kutokula kwa muda
fulani.
Mafundisho ya Bibilia kuhusu maombi na kufunga hayakutiliwa maanani katika makanisa niliyoshiriki
nilipokuwa kijana. Sikumbuki jambo hili likifunndishwa, au likifanywa miongoni mwa wakristo
niliowajua. Mtu wa kwanza niliyempata akiwa mzoefu wa kufunga alikuwa si mtu wa kawaida.
Kufungwa Msalabani
Mnamo mwaka wa 1969, nilipata fursa ya kuwa mchungaji wa First Baptist Church, Beverly Hills,
California. Kulikuwa na mtindo wa “hippie” katika nyakati hizo. Vijana wengi waasi walikutanika huko
Sunset strip magharibi mwa Hollywood, California kwa shughuli zao zilizoongozwa na misisimko. Kanisa
langu ndogo halikuwa mbali na mahali hapo. Ilikuwa hapo mtaani, nilipokuwa nikishuhudia hawa vijana
ambao walikuwa wamepoteza mwelekeo, ambapo nilikutana na Reverend Arthur Blessitt kwa mara ya
kwanza. Arthur alikuwa na mkahawa ambapo alikuwa na huduma ya kuwapa watu kahawa. Maisha yake
na pia huduma yake iliwagusa maelfu ya watu na kuwaelekeza kwa Mungu.
Mwenye nyumba ambapo Arthur aliweka mkahawa alikataa kuendelea kumkodisha nyumba hiyo, akidai
aondoke hapo pamoja na wakristo aliokuwa nao na kuihama Sunset Strip. Wakristo ambao walikuwa na
ushuhuda wa Yesu Kristo walikuwa pingamizi kwa biashara zilizohusika na ukahaba, madawa za kulevya,
vyumba vya ushoga, na anasa ambazo zinaambatana na usherati. Wenye majumba hayo ya anasa
waliungana na kuagana kwamba hakuna mmoja wao atakayekodisha Arthur nyumba kwa huduma yake ya
kahawa. Kwa kususia kufukuzwa kwake kutoka kwa jumba lake la kahawa, Arthur alijifunga kwa msalaba
wa kimo cha futi nane na kuketi kando ya njia nje ya jumba maarufu la starehe kwa vijana, liitwalo “The
Whiskey A Go – Go.”
Alijiegemeza kwa boriti ya simu iliyokuwa imefungiwa nyororo, na kufunga mkono wake kwa upande
mwingine wa hiyo nyororo. Alishuhudia, akasali, na kufunga kwa muda wa siku ishirini na nane. Hakula
chochote ila kunywa maji tu, au maji ya sharbeti. Nilipomwona nilidhani kwamba amerukwa na akili. Kwa
majuma hayo manne ulimwengu wote ulimtazama Arthur. Alichoshwa sana na jua kali la California. Hata
hivyo Mungu alikuwa naye. Huko kuteseka kulileta matokeo mema. Mamia ya watu waliokoka kwa kuja
kumtazama mwenye “vioja vya Yesu.” Wakristo walijiunga naye katika mgomo wake na kumtia moyo.
Mungu alitukuzwa na maisha ya watu yakabadilishwa. Nilikuwa mmoja wa wale waliobadilishwa.
110
Ujuzi wa Arthur ulinifanya nisome Biblia ili niweze kuelewa yale Mungu alisema kuhusu kufunga.
Uvumbuzi wangu ulinishangaza! Nilishangazwa kwamba nilikuwa nimeyapuuza mafundisho haya
maalum kuhusu kufunga. Mtu hawezi kuishi maisha ya maombi na maombezi bila kuwa na huduma ya
kufunga. Ukitafuta maneno “funga” ama “kufunga” katika itifaki yoyote ya Bibilia, utashangazwa vile
Mungu amehusisha itikadi hii ya jadi kuwa jambo la kawaida katika maisha ya Mkristo mtiifu. Nataka
kushiriki pamoja nawe uvumbuzi wangu kuhusu kufunga na kusali.
Aina Mbili Za Kufunga
Kuna jinsi mbili za kufunga, yaani kufunga kidunia, na kufunga kiroho.
1. Kufunga Kidunia
Kuna namna mbili katika kufunga kidunia. Inaweza kumaanisha kutokula ili kupunguza uzito kwa
sababu za kiafya. Madaktari wanaojua manufaa yanayotokana na kufunga huwaagiza wagonjwa
wafunge kwa muda fulani. Inaweza kuwa kufunga kula aina fulani za chakula kwa sababu za kiafya.
Watu wengine hudhani kimakosa kwamba kufunga ni kujiua kwa njaa. Wanaona kwamba ni mbaya
kiafya na basi inastahili kuepukwa. Labda hilo ni wazo lililo sawa na kweli.
Aina zingine za kufunga zina manufaa sana kiafya. Kufunga kunasaidia katika kusafisha mwili na
kutoa taka na uchafu wowote. Tumbo na matumbo yakiwa wazi, mwili huanza kujilisha kwanza kwa
kutoa vitu visivyohitajika na mwili, kama vile taka, uchafu, mafuta, na mengineo. Kuzoe kufunga
kunaweza kuwa na manufaa zaidi kwa mtu yeyote, hasa akiwa chini ya uangalifu wa daktari, ama afisa
wa afya. Kufunga kwa masaa ishirini na nne tu, na kunywa maji kunaweza kupunguza ulegevu, kupa
mwili wako nguvu, na kukuwezesha kuzingatia mambo ya rohoni. Tutaongea mengi baadaye kuhusu
manufaa ya kiroho yanayotokana na kufunga.
Aina zingine za kufunga kidunia zinaweza kuwa na namna za kidini, lakini si sawa na kufunga
itokanayo na mwomgozo wa Bibilia, ambayo tunaongea juu yake. Kwa makafiri wengi, kufunga kidini
ni sehemu muhimu ya kuabudu. Huyu kafiri anaweza kuabudu kwa kufunga ili kutesa mwili wake ili
akubalike na mungu wake. Kitendo hiki cha kuabudu kinaweza kuhusu kujijeruhi kutumia misumari,
pini na vifaa vingine. Huku si kufunga kulingana na Bibilia. Mwili si kitu kiovu ambacho kinastahili
kuadhibiwa.
III. Kufunga Kiroho.
Neno la Mungu linatupa sababu za kiroho katika kufunga. Tunakosa kula au kunywa kwa sababu
tunatafuta kuwa na ushirika zaidi na Mungu. Kufunga, kama vile maandiko yaelezavyo, si
kufunga kula ili kupunguza uzito, ama kuadhibu mwili. Ikiwa Mkristo ana uzito wa kupindukia,
basi kufunga kunaweza kuwa mwito kutoka kwa Mungu ili awekwe huru kutokana na utumwa wa
tamaa za mwili. Kufunga kulingana na Biblia kuna manufaa za kiroho, wala si za kimwili ama za
kidunia.
Mbona Tufunge?
Wakristo wengi wamehudhuria kanisa kwa miaka mingi na kuishi maisha ambayo yanadhaniwa kuwa ya
Mkristo wa kawaida, lakini hawajaweka agano na Mungu katika kufunga. Swali la kawaida ni “kwa nini
nifunge?”. Hebu nikueleze manufaa ya kufunga (kuacha kula) mara kwa mara kwa kila muumini.
Tumesikia mara nyingi msemo usemao kwamba njia ya kuelekea katika moyo wa mtu ni kupitia kwa
tumbo lake. Msemo huu ni kweli kuliko tunavyodhania. Milango yetu ya maarifa, yaani kuona kwa macho,
kusikia, kunusa, kuonja na kugusa, ni za kuelekea moyoni. Shetani anaelewa hayo kuliko tujuavyo.
Katika Biblia tunaona shetani akiingia katika roho ya binadamu kupitia kwa tumbo lake. Aliweza kufikia
Awa, kule shambani la Edeni kupitia kwa hamu yake ya chakula. Kitabu cha mwanzo kinasimulia kwamba
aliona tunda hilo likiwa nzuri. Watu hawa wawili wa kwanza waliangushwa na hisia zao. Mwili ni mlango
wa moyo.
111
Shetani alitumia njia hii pia kumfikia Nuhu baada ya gharika. Katika kitabu cha mwanzo sura ya 9 tunaona
Nuhu akilewa mvinyo kutoka kwa shamba lake la mizabibu, na wana wake wakimwona akiwa uchi. Hii
inaonyesha kwamba dhambi ya tamaa ya mwili ilimshinda Nuhu. Kumbuka wana wa Isaka, yaani Esau na
Yakobo. Esau aliuza uridhi wake kwa sababu ya bakuli ya supu! Shetani anatumia tamaa za mwili kufikia
moyo na roho ya mwanadamu. Je, hii ina uhusiano gani na kufunga?
Biblia inatufundisha kwamba Mungu ndiye chanzo cha tamaa za mwili, na kwa hivyo taamaa hizo hazina
uovu. Kutumia vibaya, au kutesa mwili ndio dhambi. Ni lazima tumiliki na kutia miili yetu nidhamu
kutokana na tamaa za mwili. Lazima miili yetu iwe chini ya mamlaka yetu, na kuwa mtumwa wetu ili Roho
aweze kuutawala. Tusiiruhusu mwili itutawale.
Jangwani
Imeandikwa katika kitabu cha Mathayo sura ya nne kwamba Yesu alifunga siku arobaini, mchana na usiku.
Kwa siku arobaini hakula chochote. Baada ya kipindi hiki, Bibilia inasema “mwisho akaona njaa” Shetani
akaja kumjaribu Mungu wetu. Ni ombi gani ambalo shetani aliomba kwanza? Huyu adui alimjaribu Yesu
kwa kumwambia aamuru mawe kuwa mkate, kuonyesha kwamba mwili wake ulihitaji chakula. Hata hivyo,
kufunga kwake Yesu kulimfanya kuwa “shupavu” katika roho. Alifanya mwili wake kuwa mtumwa wake.
Mwokozi wetu alikuwa na njaa, lakini njia ya kuingia rohoni mwake haikuwa kupitia tumboni mwake.
Kuna uhusiano kati ya tamaa za mwili wa mwanadamu, na maisha yake ya rohoni. Adabu mwilini huenda
sambamba na mtu wa rohoni (hii si kweli kila wakati). Kufunga “hukwamua” uzito ambao tamaa zetu za
mwili zimeweka katika nia zetu. Kufunga kuna manufaa kama vile maadiko yanavyofundisha. Mbona
itikadi hii inazingatiwa na wakristo wachache tu? Labda uko kama rafiki yangu mmoja mhubiri mnene
aliyesema kwa ujeuri, “hainihusu mimi!” Basi, mbona siye?
Sababu Zinazofanya Watu Kukosa Kufunga
Hebu kwa kifupi nieleze sababu zinazofanya watu wapuuze kufunga.
Usheria
Watu huogopa kwamba kufunga kunaweza kufanyika kuwa tamaduni au kanuni za dini ambazo ni sharti
zifuatwe. Wanaona ni kama kuwa chini ya sheria, badala ya kuwa chini ya neema. Watu wengi huogopa
hali hiyo ya utumwa. Je, mbona tunahisia hizo kuhusu kufunga. Kwa nini hatuhisi hivyo kuhusu sala,
kushuhudia, au fungu la kumi? Jambo lolote katika ukristo unaweza kuwa sheria, au sivyo?. Kutoa fungu la
kumi linaweza kuwa sheria, lakini sisi wainjilisti kwa hakika hatujadharau mafundisho yanayohusu kutoa
fungu la kumi.
Utawa
Jambo la pili ni kwamba, kufunga kumepuuzwa kwa sababu watu wameogopa utawa. Mnamo zamani za
kati (middle ages), kanisa la kirumi la kikatoliki lilianza kutilia maanani mambo ya utawa, maisha ya
desturi yakujitenga na mambo ya dunia ili kujifunza mambo ya kidini (monastic life), na kuishi mbali na
jamii ili kuzuia uigizaji wa tabia fulani. Kuishi kwa namna hiyo kulifanya kufunga kuwa sehemu muhimu
katika maisha ya utawa. Kwa hakika utawa ni nini hasa? Kwa kawaida, mtawa ni mtu atiaye mwili wake
uchungu, na kuupigapiga kwa nguvu. Lengo lake ni kushinda, kutesa, na kuadhibu mwili kwa sababu za
kiroho.
Dini nyingi za kikafiri zina utawa. Mara kwa mara tunasoma kuhusu watu wanaojidunga na visumari
mwilini na kufunga, ama wanakufa njaa ili waweze kufurahisha miungu yao. Labda wakristo wengi wa
kisasa wameasi dhidi ya aina hii ya wazimu wa kidini. Lakini Bibilia imeeleza wazi wazi kwamba kufunga
si utawa.
Ungwana
Wahubiri na waalimu wengi wanafundisha kwamba kufunga hakuna maana kwetu siku hizi. Hii
imesababisha watu kudharau kufunga. Wengine husema kwamba, kufunga ilikuwa na maana tu kwa
Wayuda wa kale, wala hayahusu wakristo wa enzi hizi. Watakatifu wote wakuu wa Mungu walifunga
wakisali, wakishuhudia, na kuhubiri.
112
Waombezi wa Agano la Kale
Musa , mwadhama katika agano la kale, ndiye mfano mzuri kwetu katika kutambua uhusiano kati ya sala,
maombezi na kufunga. Musa ndiye pia mfano mzuri wa mwombezi aliyetumia kufunga kama njia ya kuleta
mawasiliano mazuri katika roho.
Musa alifunga kwa siku arobaini mara mbili bila chakula wala maji. Kufunga hakuwezekani kwa nguvu za
mwili, ila kwa nguvu za ajabu. Musa alikaa siku themanini bila maji wala chakula, hali mtu atakufa
asipokunywa maji baada ya siku kama kumi na tano hivi. Tendo la Musa lilikuwa la kimiujiza. Eliya
alifunga kwa muda wa siku arobaini. Malkia Esta alifunga kwa muda wa siku tatu, mchana na usiku
akimlilia Mungu aweze kuwaepusha Wayahudi na amri ya Mfalme.
Watakatifu wote katika Bibilia, wakiwemo Daudi, Nehemia, Ezra, Yeremia na Isaya walikuwa wanaume
na wanawake waliokuwa na uzoefu wa kufunga, kusali na uombezi.
Mafundisho ya Yesu kuhusu Kufunga
Katika mafundisho ya Yesu mlimani, alieleza mambo muhimu kuhusu kufunga. Katika kitabu cha Mathayo
sura ya sita, Yesu alifundisha vitu vitatu vya maana katika dini, yaani sadaka na zaka, sala, na kufunga.
Aliongea pia kuhusu utumizi mbaya wa vitu hivyo vitatu. Katika Mathayo sura ya sita haya ya pili hadi ya
nne, Yesu aliongea kuhusu utoaji wa zaka, fedha na kutoa vipawa kwa maskini.
“Basi utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na
njiani ili watukuzwe na watu. Amini, nawaambieni wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe
utoapo sadaka, hata mkono wako wa kishoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako
iwe kwa siri na baba yako aonaye sirini atakujazia.”
Yesu anatufundisha vivyo hivyo kuhusu utoaji. Anasema “utoapo.” Ukristo ni kutoa, au sivyo? Yesu
hakusema “kama ukitoa” akidhani kwamba tutatoa ili tuwape masikini. Anasema, ‘utoapo’, halafu anaeleza
unavyopaswa kutoa. Anasema usijisifu, wala kutoa hadharani, ila kwa siri bila kujali utukufu utakayopata
kutokana na kutoa kwako. Halafu, katika Mathayo 6:5-15 akaeleza kuhusua sala.
Maombi ni huduma ambayo tumepewa na Mungu. Hebu tumsifu Bwana kwa huduma ya maombi. Lakini
maombi inaweza kutumiwa vibaya. Yesu anaongea kuhusu utumizi mbaya wa maombi. Anatoa mfano wa
maombi tuliopewa katika mwanzo wa haya ya tisa. Anasema unaposali, sali hivi: “Baba yetu uliye
mbinguni … ’’ Kisha anaeleza jinsi unavyoweza kuomba. Katika aya ya 15 anatueleza kuhusu kuomba na
kusamehe wengine, ndipo nasi tupate msamaha kutoka kwa Baba yetu. Yesu alidhani kwamba wakristo
watasali, ndipo hakusema kama mkiomba, bali “mwombapo.” Jambo la tatu la kidini aliloongea juu yake
linapatikana katika aya ya kwanza hadi ya kumi na nane, ambalo ni jukumu la kufunga!.
“Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika
masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amini,nawaambia, wamekwisha
kupata thawabu yao. Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga
mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazia”
(Mathayo 6:5-6).
Hii ina umuhimu gani? Yesu alisema, “utoapo”, “uombapo”, na “afungapo.” Swali si kama unastahili
kufunga, bali ni ufungapo. Tunaweza kuona kwamba Yesu alieweka kufunga katika kiwango sawa na
maombi na utoaji.
113
Ni wazi kwamba mkristo anahitajika kutoa na kuomba. Basi, mbona tunaleta maswali kuhusu kufunga?
Mbona tunautupilia mbali? Yesu alisema, “unapofunga” wala si “kama ukifunga.” Alidhani kwamba kila
muumini atafanya kufunga kuwa sehemu muhimu katika huduma na maisha yake ya kikristo. Yesu alidhani
tutafanya jambo ambalo wengi wetu hatufanyi!
Watu wengine wamesema, “Naam, je yale mafundisho ya Yesu mlimani yalikuwa ya watu wote siku
zote?” Wengine pia wamesema kwamba hatuwezi kuzingatia mafundisho hayo kwa sababu yalihusu wale
waliokuwepo kabla Pentekote, na kwa hivyo yalihusika na sheria kwa nyakati za kale. Wanaendelea
kusema kwamba mafundisho hayo yalikusudiwa Wayahudi, na kwa hivyo yanahusu waumini wa kiyahudi
tu. Kwa hivyo wanasema kwamba haya maandishi kuhusu kufunga hayahusu wakati huu. Mimi
sikubaliani na maelezo hayo kwa sababu naamini kwamba haya mafundisho ni ya kila wakati. Inahusu kila
muumini wa kweli wa Kristo. Hata hivyo, Yesu alitufundisha mahali pengine kuhusu kufunga katika
maisha ya kanisa.
Mathayo 9:14, inasema hivi, “Wakati ule wanafunzi wake Yohana wakamwendea, wakasema, Kwa nini sisi
na mafarisayo twafunga, bali wanafunzi wako hawafungi?” Mafarisayo walikuwa wakifunga mara mbili
kwa juma. Hawakuamrishwa na Mungu kufunga mara mbili kwa juma. Katika neno la Mungu kuna amri
moja tu kuhusu kufunga, nayo ilihusiana na Siku ya Tambiko (Day of Atonement), iliyoitwa ‘Yom Kippur’.
Ni siku hiyo tu ambapo Mungu aliamuru saumu. Lakini Wafarisayo walizingatia sheria sana hadi
wakaamua kufunga mara mbili kwa juma, na kutilia najisi agizo la Bibilia kuhusu kufunga.
Wafuasi wa Yohana Mbatizaji walifunga. Wafuasi wa Yesu hawakufunga maana Yesu hakuwa
amewafundisha kufunga. Kwa hivyo wafuasi wa Yohana walichanganyikiwa. Kwa nini wanafunzi wa
Yesu hawakuwa wakifunga? Yesu, alipoona kuchanganyikiwa kwao, aliwaeleza, akisema,
“Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda Bwana arusi akiwapo pamoja noa? Lakini
siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi: ndipo watakapofunga” (Mathayo 9:15).
Hakukuwa na haja ya wanafunzi wa Yesu kuomboleza na kufanya saumu alipokuwa pamoja nao. Bwana
arusi alikuwa bado yu pamoja na wale walioalikwa arusini. Sherehe zilikuwa bado zikiendelea. Haukuwa
wakati wa huzuni, bali furaha. Haukuwa wakati wa kufunga, bali kusherehekea.
Wazo la kuomboleza lilihusishwa na kumtafuta Mungu. Hawakuwa na sababu ya kumtafuta Mungu, kwani
alikuwa nao, na kwa hivyo walihitaji kufurahi, kusherehekea, kujifundisha na kukua. Yesu alikuwa
akisema, “niko nao; ni wakati wa furaha. Watakuwa na wakati wa kutosha wa kufunga baada ya kuondoka
kwangu. Watafunga; kisha watanitafuta mimi.” Bwana arusi hayuko leo, kwani alienda. Hatarudi hadi
wakati wake wa kurudi mara ya pili uwadie, atakaporejea kumchukua bibi yake, ambaye ni kanisa lake.
Yesu anasema kanisa litafunga kati ya wakati wa kwenda kwake na kurudi kwake.
Haya ni mafundisho yaliyo wazi kuhusu kufunga kutoka kwa Yesu, inayolingana na Bibilia. Kwa sababu
Bwana arusi ameenda, kanisa la kwanza lilikuwa na mazoea ya kuomba, wakiambatanisha na kufunga.
Baada ya kukutana na Yesu katika barabara ya kuelekea Dameski, Sauli wa Torso alikaa kwa siku tatu
akiwa amefunga kabisa bila kula chakula wala kunywa maji.
Kornelio, katika kitabu cha Matendo ya Mitume sura 10, alifunga na kumngojea Petero kwa kutii ono
aliloona. Katika Matendo 13:2-3 kanisa la Antiokia lilifunga na kuomba, “Basi hawa walipokuwa
wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile
niliyowaitia. Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende
zao.” Kutumwa kwa Paulo na Baarnaba kama wamisheni wa kwanza kulitanguliwa na kipindi cha kusali
na kufunga. (Matendo 14:23; “Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba
pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.”) Walianzisha makanisa
mijini katika huduma yao ya kuhubiri injili katika bara Asia. Walipokuwa wakiondoka waliteua wazee wa
kuendeleza kanisa. Je wangetambuaje wazee wa kuacha kwa huduma hiyo, isipokuwa tu kwa kumtafuta
Bwana kwa kuomba na kufunga?
114
Aina tofauti Za Kufunga
Aina nne za kufunga zimeelezwa katika Biblia.
I. Kufunga kwa kiwango
Danieli 10;3 inaeleza kuhusu kufunga kwa kiwango. “Sikula chakula kitamu wala nyama wala
divai haikuingia kinyani mwangu” Katika kufunga kwake, Danieli alikula tu mboga. Kufunga kwa
kiwango ni kujiepusha na kula vitu vitamu, kama vile kitumba (cake), na vinginevyo.
Kwa hivyo, kama umefunga kwa kiwango kwa sababu za kiroho, unaweza tu kula mlo moja kwa
siku, ama ukose kula aina fulani ya vyakula, isipokuwa mboga tu, jinsi Danieli alivyofanya.
Kufunga kwa kiwango ni kula chakula kidogo kwa kujizuia . Unaweza tu kufanya hivyo kama
Mungu amekuita kufanya hivyo.
II. Aina Maarufu ya kufunga
Sehemu hii ni ya kile tutakachokiita “aina maarufu ya kufunga” kwa sababu hii ndio inayojulikana
sana katika Bibilia. Kwa sababu hiyo, wengine wameiita kufunga kwa kawaida. Kufunga huku
kunahusu kutokula chakula chochote ila kunywa maji tu, au maji ya sharubati. Yesu alifunga
hivyo usiku na mchana kwa siku arobaini alipokuwa jangwani, katika Mathayo sura 4.
Bibilia inasema kwa siku arobaini, mchana na usiku, aliona njaa. Je, watambua kwamba Bibilia
haisemi aliona kiu pia? Pia Shetani akamjaribu akimwambia ageuze jiwe kuwa mkate, wala
hakumjaribu na kiu. Kunaweza kuwa na hoja kuhusu jambo hili, lakini nadhani kwamba Yesu
alifunga kawaida, na kwamba alikuwa na maji kwa siku hizo arobaini. Kama hakuwa na maji, basi
alikuwa na msaada wa ajabu ya kumwezesha kuishi kutoka kwa Mungu.
III. Kufunga Halisi
Musa alifunga halisi. Aliyefunga halisi hali chakula au kunywa maji kwa muda fulani aliyoutenga.
Musa angekufa kama Mungu hangeliingilia kati. Ni nguvu za kipekee ndizo zinazoweza kumfanya
mtu kufanya Musa alivyofanya. Musa ndiye aliyefunga kwa muda mrefu sana katika Bibilia.
Alifuatisha siku 40 za kufunga mara mbili, yaani siku 80, bila kula chakula au kunywa maji.
Kuna matukio mengi katika Biblia yanayoonyesha kwamba watu walifunga halisi kwa siku tatu.
Labda siku tatu ndizo zinafaa kwa kufunga. Paulo alifunga kwa siku tatu bila kula chakula au
kunywa maji kabla kubatizwa kwake. (Matendo ya Mitume 9:9). Ezra alimtafuta Bwana kwa
kutangaza kwamba wana wa Israeli wafunge. Walifunga kwa siku tatu kando ya mto Ahava
mchana na usiku. Ezra sura ya 8 inaeleza hivi, “Basi tukafunga, tukamsihi Mungu wetu kwa ajili
ya hayo; naye akatutakabali” (Ezra 8:23). Katika kitabu cha Esta 4:16, Esta aliwaita watu wake
Wayahudi waombe na kufunga, au waangamizwe. Walifunga kamili, bila chakula wala kunywa
maji kwa siku tatu. Esta, pamoja na wanawali wake pia waliomba na kufunga.
IV. Kufunga kwa Kirefu
Kufung kwa siku zinazozidi tatu imetajwa katika Bibilia. Siku nyingi sana ambazo zimetajwa
katika Bibilia ni kama siku 15, 20 au hata 40. Sijawahi kufunga kwa muda wa siku zaidi ya tano,
lakini najua rafiki zangu wengi ambao wamefunga kwa siku 20. Nilimtazama Arthur Blessit, pale
Sunset Strip akifunga kwa muda wa siku 28, na kunywa tu maji ya sharubati. Baadaye alifunga
kwa siku 40, akiwa Washington, D.C. Huu ndio mfano wa kufunga kwa muda mrefu, ambapo mtu
hunywa maji peke yake.
Wanaofunga
Je kufunga ni kwa watu ambao hawaeleweki au wale ambao hawakubaliki katika kanisa? Je kuna nafasi ya
kufunga katika maisha ya kila Mkristo? Je, Mkristo yeyote anaweza kufunga? Kwa hakika maishani
115
mwangu nina nafasi ya kufunga. Hata hivyo, Mungu hakuamuru kanisa kufunga kwa nyakati hizi. Yeye
hutuita kwa huduma ya kuomba na maombezi. Mara nyingi huduma hii itahitaji kufunga ili kuwezesha
roho zetu kupata nidhamu ili tuweze kukabiliana na vita vilivyoko.
Katika kitabu cha Mambo ya Nyakati wa Pili 7:14 tunaona hitaji la kuomba na kuomboleza kwa taifa letu
lililojawa na dhambi, ingawa kufunga hakujatajwa, “ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu,
watajinyenyekesha.” Hebu tilia mkazo neno “watajinyenyekeza.” Hakuna kiwezacho kumnyenyekeza mtu
kama vile kufunga.
Unaweza kuhisi hitaji kuu la kuombea mtu fulani, au mwito wa Mungu kwa kusudi fulani, au hitaji fulani,
ama kutenga nyakati bila kula wala kunywa. Utafanya hivyo kwa sababu za kiroho kwa muda wa masaa
ishirini na nne, ama kwa wakati fulani ambao Mungu amekuelekeza.
Sababu Za Kufunga
Hebu tuangalie sababu za kufunga kiroho. Je, kuna faida gani za kiroho katika kufunga?
Kufunga ili kumtafuta Mungu
Katika Biblia, lengo la kufunga huwa ni la kiroho. Kufunga kulingana na neno la Mungu huwa kwa ajili ya
kumtafuta Bwana. Mungu anaponielekeza kufunga huwa ana sababu fulani, na sina mng’ang’ano katika
kufanya hivyo. Sijawahi kuona njaa, au kuwa na tatizo kutokana na huko kufunga. Mara nyingine
nimefunga kwa siku tano, bila kuwa na tatizo. Hata hivyo, nilipoamua kufunga bila kuelekezwa na Mungu
kufanya hivyo, basi ikawa tu kama kujinyima chakula ili kupunguza uzito! Sifikirii jambo lolote ila chakula
tu. Ni heri Mungu anipe mwito wa kufunga kwa siku arobaini kuliko kujinyima chakula kwa kusudi la
kupunguza uzito. Bila kuitwa, nitafiki tu chakula mchana wote.
Nia ya Mungu katika kukuita kufunga ni ya kiroho, ambayo ina baraka kwako. Hii Ndio maana Bibilia
inaeleza kuhusu saumu ambayo Mungu atauchagua, (tazama Isaiah 58). Unapaswa kufunga Mungu
anapokuelekeza kufanya hivyo. Hivyo utaongozwa na roho katika kufunga.
Kufunga kwa kujuta dhambi
Kwanza, kuna kufunga kwa kuonyesha huzuni sababu ya dhambi. Kufunga kunaweza kuwa kifaa cha
kutuongoza kutubu, kunyenyekea, au kumtafuta Mungu. Kuna nguvu za ajabu katika kufunga iwezayo
kufanya roho zetu kunyenyekea. Inasaidia katika kuweka roho nidhamu. Pia inaweza kutuongoza kutubu na
kumtafuta Bwana.
Katika Zaburi 35:13, Daudi alisema, “Nalijitesa nafsi yangu kwa kufunga.” Tena Daudi alisema, “Nilipolia
na kuadhibu roho yangu kwa kufunga” (Zaburi 69:10). Ezra anawaambia watu kwamba wataamuru saumu
kando ya mto Ahava ili wapate kuzinyenyekesha nafsi zao mbele za Bwana (Ezra 8:21).
Kufunga ili kunyenyekesha roho
Karibu watumishi wote wa Mungu walioteuliwa walizoea kufunga ili kunyenyekesha roho zao. Shujaa
wangu mmoja katika imani ni John Wesley. Katika fundisho lake moja maarufu kuhusu kufunga, alinena:
“Kwanza, hebu ifanyike kwa utukufu wa Mungu, macho yetu yakiwa yameelekezwa kwake. Hebu
nia yetu iwe moja tu, yaani kwa utukufu wa Baba aliye Mbinguni, kuonyesha huzuni na aibu yetu
kwa sababu ya kwenda kinyume cha kanuni yake takatifu, na kungojea ongezeko la neema yake
inayotakasa, tukivutiwa na mambo yaliyo juu; na kutia juhudi na kujitolea katika maombi; ili
tuepuke ghadhabu ya Mungu; na kupata ahadi za ajabu na za thamani ambazo ametuahidi katika
Yesu… Tutahadhari tusije tukajitwalia lililo la Mungu katika kufunga kwetu.”
116
Mungu anatuita tufunge ili atunyenyekeshe, na ili tutafute uso wake ulio takatifu. Tunafunga kwa ajili
yake, na kwa ajili yetu. Fikira yoyote ya chakula iwe ni mwito wa kusali na kumtafuta Mungu. Kufunga
kunatuonyesha kudhoofika kwa maisha yetu. Tu viumbe vya kutegemea, ambao wanalazimika kuwa na
mkate wa kila siku ili kuishi. Kufunga kunanyenyekesha nafsi. Inatukumbusha kwamba tu mavumbi na
Mungu ndiye asili yetu. Kufunga kunaweza kuvunja minyororo ya mambo ya mwili na kuweka huru roho
ili iweze kupaa na Mungu.
Kufunga kunaweza kutuondolea kiburi. Inapendeza jinsi Bibilia inasimulia mara nyingi kwamba walizini
“tumbo zao zilipokuwa zimejaa.” Bibilia inasema watu wa sodoma walilisha tumbo zao kwa vyakula na
vinywaji, kisha wakaenda kufanya usherati. Walijawa na kiburi rohoni. Ni jambo la kushangaza kwamba
watu walio wanene kwa kutokuwa na kiasi mara nyingi huwa watu wenye kiburu, wanaojihusisha na
mambo mengine yanayoambatana na kutokuwa na kiasi.
Katika Biblia, kufunga huleta hali ya kufanya mtu kunyenyekea. Pia hufanya roho yenye kiburi kuwa na
majuto mbele za Mungu, na kuweka nafsi huru kumtafuta Bwana. Katika kufunga mwili hutiwa adabu na
kufanywa tiifu.
Kufunga pia kunaweza kuonyesha hali ya kuwa na majonzi . Katika Mathayo 5:4, Yesu alinena jinsi walio
na huzuni wana heri kwa sababu watafarijika. Katika Mathayo 9:15 Yesu anatumia kwa usawa maneno
kuomboleza na kufunga. Kuomboleza na kufunga ni maneno yanayotumika sawa. Kwa hivyo kufunga ina
maana ya kunyenyekesha roho mbele za Mungu.
Kufunga ili kufanywa takatifu
Je umewahi kufikia wakati fulani katika maisha yako ambapo ulitamani kumwona Mungu? Ulikuwa na
shauku ya kutembea karibu sana na Mungu, kumjua zaidi, na kuelewa neno lake zaidi. Je, ulifahamu
kwamba katika Bibilia kufunga kumeambatanishwa na kumtafuta Mungu, kufanywa wakfu, na kujitenga
kwa ajili ya Mungu? Je, unadhani Yesu alikaa jangwani siku arobaini kwa nini? Alifanya hivyo kabla
kuanza huduma yake kwa watu. Yesu alifunga ili autafute uso wa Bwana katika maisha yake, na katika
huduma yake.
Mkristo mara kwa mara hushurutiswa kufunga kabla kupewa mwito, au kazi muhimu, ama kujazwa na
roho mtakatifu. Katika matendo 13, tunaona Paulo na Barnaba wakitumwa kama wamisheni. Walimtafuta
Bwana kwa kufanywa watakatifu, na pia kwa ajili ya huduma zao. Kanisa liliomba na kufunga, kisha
likawawekea mikono Paulo na Barnaba na kuwatuma wakiwa wakfu kwa Kristo.
Kufunga pia kunaweza kuambatanishwa na kutafuta ufunuo kutoka kwa Mungu. Unaweza kuwa unatafuta
mapenzi ya Mungu kuhusu jambo fulani, lakini hujui Mungu angehitaji ufanye vipi. Bibilia inatuonyesha
kwamba kujipeana mhanga kwa Mungu - yaani kwa roho, nafsi na mwili - na kuweka kila wazo mateka
kwa Mungu, kunawezekana kwa njia ya kuomba na kufunga. Tunahitaji kumfungia Bwana peke yake, wala
si mtu mwingine. Katika matendo 13:2 tunaona kwamba kanisa lilifunga kwa ajili ya Bwana.
Kama Wakristo tunajiuliza “Mbona nifanya saumu,” au “nitafaidika vipi kwa kufanya saumu?”
Tunamfanyia Bwana saumu. Nabii Ana katika Luka 2 aliabudu kwa kufunga. Katika kuabudu na kufunga,
unamtafuta Mungu kwa nafsi yako yote.
Kufunga kwa kujali
Katika Bibilia, kufunga kulihusisha kuombea wengine. Hebu tuongee kuhusu kuomba na kufunga. Kufunga
peke yake hakumaanishi kitu. Bibilia inaonyesha kufunga kama kitendo kinachoambatana na kusudi, na
lengo fulani.
Bibilia inaongea kuhusu kuomba na kufunga, kukesha na kufunga, kuabudu na kufunga, na kutafuta Bwana
na kufunga. Kufunga huambatana na kitu kingine. Inaambatanishwa na maombi kwa sababu inalete hali ya
117
kuomba, kusoma neno la Mungu, na kumtafuta Bwana. Inafanya nafsi kuwa huru kumtafuta Mungu. Utafiti
wa kisayansi umegundua kwamba watu wanaofunga ni makini, na wenye macho ya kung’aa.
Utaona kwamba u makini sana wakati wa kufunga kuliko nyakati zingine. Mwili wako unapotakaswa, roho
yako inakuwa huru kuelewa mambo ya roho unapofunga na kuomba. Kuomba na kufunga kumeniwezesha
kufahamu mambo makuu kutoka katika neno la Mungu. Nimeona neno la Mungu likiwa hai kwangu
kutokana na kuomba na kufunga. Ushirika wangu na Mungu pia umeimarika sana wakati wa kuomba na
kufunga kuliko nyakati zingine.
Kuomba na kufunga
Kufunga huambatana na maombi kwa jinsi hizi tatu.
I. Kufunga na maombezi
Unaweza kufunga na kuomba ili kuombea wengine. Kitabu cha Esta kinatuonyesha vile Esta
alivyowaita watu ili waombee wayahudi ili wasiangamizwe na mfalme. Waliomba na kufunga
kwa ajili ya taifa lao.
Tunaona hayo pia yakitendeka katika Ezra 8, kama nilivyotaja hapo awali. Tunaona watu wa
Mungu wakiomba na kunyenyekesha nafsi zao ili Mungu asiangamize taifa lao. Katika hadithi ya
Yona na Nineva, mfalme wa Nineva aliagiza taifa nzima kuomba na kufunga ili Mungu
asiliangamize. Katika Bibilia, tunaona kufunga na kuomba zikiambatana pamoja na maombezi.
II. Kufunga na uhuisho
Mara nyingi nimewasikia watu kanisani na wahubiri wakiongea kuhusu uhuisho. Tunahitaji
uhuisho makanisani mwetu. Pia tunahitaji uhuisho katika nchi ya Amerika. Hukuwezi kuwa na
uhuisho katika nchi ya America bila maombi. Uhuisho na kufanywa upya katika Bibilia
imeshirikishwa na maombi pamoja na kufunga.
Nionyeshe kanisa, au mtu aliye na shauku juu ya Mungu, na nitakuonyesha mtu anayemtafuta
Mungu kwa dhati hadi kukosa hamu ya chakula! Mungu ataliheshimu kanisa kama hilo, au mtu
kama huyo!
Kuomba na kufunga inahusiana kikamilifu na uhuisho. Shetani ametupofusha tusiweze kuona njia
hii ya ajabu ya kumfikia Mungu.
III. Kufunga na ukombozi
Watu wengine wanaweza kukombolewa kwa kuomba na kufunga. Bibilia inasema tunaweza
kutoa watu wengine utumwani kwa kuomba na kufunga. Huu ni ukombozi wa aina gani?
Katika kitabu cha Kumbukumbu La Torati, Musa aliombea wana wa israeli akisema,
“Nikaanguka chini mbele za Bwana siku arobaini usiku na mchana, kama pale kwanza; sikula
chakula wala kunywa maji; kwa sababu ya makosa yenu yote mliyokosa…”(Kumbukumbu La
Torati 9:18). Musa alifunga kwa sababu ya mtu mwingine. Alisimama katikati ya pengo kama
mwombezi, akiwa tayari kupoteza uhai wake kwa sababu ya Israeli. Maombezi yake yalikomboa
taifa nzima.
Tunaweza pia kusimama katikati ya pengo kwa ajili ya walio utumwani. Bila shaka unajua watu
walio wagonjwa katika mwili, katika hisia, na hata katika roho. Wanahitaji ukombozi , hasa walio
wagonjwa kutokana na dhambi. Mlevi, mwenye kutumia madawa za kulevya, na waliodhulumiwa
kiroho kwa sababu ya dhambi wanahitaji kuwekwa huru. Je, hii inawezekanaje?
Kuna somo la ajabu kuhusu kuomba na kufunga katika Mathayo 17:1-21. Mtoto wa mtu mmoja
alikuwa amepagawa na pepo. Mara kwa mara, alijibwaga motoni, ama kujaribu kujiua
alipokamtwa na pepo huyo. Wanafunzi wa Yesu walifahamu kwamba alikuwa amepagawa na
pepo. Ibilisi alikuwa akijaribu kumuua. Wanafunzi hao wa Yesu walijaribu kumwondoa huyo
118
pepo lakini hawakuwa na uwezo dhidi yake. Baba yake alimwendea Yesu na kumweleza jinsii
wanafunzi wake walivyoshindwa kuwafukuza pepo.
Yesu aliamuru mtoto aletwe, kisha akaamuru pepo amwache. Mara moja akapata ukombozi.
Baadaye wanafunzi walimwendea Yesu faraghani wakamuuliza, wakisema “Mbona sisi
hatukuweza kumtoa? Yesu akawaambia, kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana
amini nawaambia, mkiwa na inami kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, ondoka
hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. Lakini namna
hii haitoki ila kwa kusali na kufunga” (Matthayo 17:20-21).
Yesu anataka tufahamu kwamba mtu yeyote ambaye ni mfungwa wa kiroho wa aina yoyote, anaweza
kuwekwa huru. Kinachohitajika ni mtu mwenye imani atakayesimama katika pengo kwa niaba ya huyo
mtu. Anayehitajika ni mwombezi atakayefunga na kuomba hadi ushindi upatikane.
Mtu mmoja kwa jina Andrew Murray aliponena kuhusu vifungu hivi, alisema kwamba “Imani inahitaji
maombi ili iweze kukomaa kamili. Nayo maombi inahitaji kufunga ili iweze kukomaa kamili. Maombi ni
mkono unaotuwezesha kushika kisichoonekana; bali kufunga ni mkono huo mwingine unaotuwezesha
kufungua na kutupilia mbali kinachoonekana.”
Bila shaka Ibilisi atatupinga. Hashindwi upesi. Ni jukumu la kila kanisa “kuteka nyara kila fikira ipate
kumtii Kristo,” na kuangusha ngome za Shetani (2 Wakarintho 10:4-5). Mara nyingi kuomba pekee
hakutoshi.
Kufunga na kuomba huongezea uzito maneno yetu. Ni kutoa maisha yako, na kumwambia Mungu na adui
kwamba “siwezi kula hadi ushindi upatikane.”
Kufunga ni kuomba bila kutamka kwa kinywa, na inaonyesha uamuzi wa mwombezi.
Mtu mmoja kwa jina Arthur Willis, katika kitabu chake kiitwacho Gods Chosen Fast anamnukuu Andrew
Murray akisema:
“Mbele za Mungu, kufunga kwetu kunaonyesha waziwazi kwamba jambo tunaloliombea ni la
kweli na lenye maana sana kwetu. Pia inatilia mkazo juhudi na nguvu zinazopatikana katika
maombi, na daima kuwa ishara ya kuonyesha maombi kwa vitendo, bila kutamka kwa kinywa…”
Unapofunga
Kama vile ambavyo umesoma katika mafundisho haya kuhusu kusali na kufunga, umetambua kuwa kama
mfuasi wa Kristo swala kubwa si “iwapo inakupasa kufunga,” bali ni “unapofunga.”
Hebu tenga kipindi cha masaa 24, labda kutoka saa sita mchana hadi saa sita mchana siku ya pili. Mwili
kwa kawaida huzoea kufunga kwa viwango. Kwa masaa 24, huwezi kuona njaa kwa hakika, ila tu kwa
fikira zako. Tumbo lako laweza kunguruma kwa kuzoa kulishwa kwa nyakati fulani. Hebu tumia wakati wa
kuwazia chakula kama mwito kwako ili uombe na kumtafuta Mungu. Amua kumfanyia Bwana saumu.
Tumia muda huo kujiweka wakfu kwa Bwana.
Uwe na azimio katika kufunga. Inaweza kuwa kwa sababu za masikitiko, au kuwekwa wakfu, au
maombezi. Funga na kuomba ili uweze kusimama katika pengo kwa niaba ya wengine. Nimewahi kufunga
na kuombea nchi fulani, au Mkristo aliye katika huduma fulani katika nchi geni.
Je, unaweza kufunga kabisa, au kwa kiwango? Unaweza kuamua kufunga kabisa, yaani bila chakula au
maji. Hiyo ni juu yako wewe na Mungu. Labda una woga, au mashaka, ama hata huna hakika kwamba
unaweza kufunga. Nakuhakikishia kwamba Baba yako aliye mbinguni anapokuita kufanya saumu, basi
atakudumisha, atakukubariki, na kukufurahisha na uwepo wake. Furaha ya Bwana itakuwa nguvu yako.
119
Wanaotamani kuwa mashujaa wa maombi wanawajibika “kupenya” hadi palipo takatifu. Kufunga
kutakuwa rahisi kama askari anayeweka risasi ndani ya bunduki lake. Ni silaha tunayotumia na kufurahia.
Tupe nia ya kufuata hisia zetu,
Tupe nguvu za kutenda tujuavyo,
Tupe azimio, iliyo na nyuzinyuzi na upindo wa chuma,
Tuweze kupiga.
--John Drinkwater
Misaada
1. John Wesley, ametajwa na Arthur wallis, Gods chosen fast (Fort Washington, Pennsylvania: Christian
crusade, inc., 1968), pp.34,35.
2. Andrew murray, With Christ in the School of Prayer (Old Tappan, New Jersey: Fleming H. Revell
company, 1965), p.74.
3. Warns, God’s Chosen Fast p. 55
4. Quoted in Warns, p. 84.
120
121
MSAADA ZAIDI
Bounds, E M Power through Prayer. Springdale, Pennsylvania: Whitaker House, 1983.
- A Treasury Of Prayer. Minneapolis: bethany House, 1981
-
Chadwick Samuel. The Path Of Prayer. Fort Washington, Pennsylvania: Christian Literature
Crusade,inc., 1963
Gordon, S.D. Quiet Talks On Prayer. Grand Rapids, Michigan: Baker Book House, 1980
Grubb, Norna. Rees Howells, Intercessor. Fort Washingtone, Pennsylvania: Christian Literature Crusade.
Inc., 196-1967.
Hallesby , o. Prayer. Minneapolis: Augsburg publishing House,1975
Hayford ,Jack. Prayer Is Invading The Impossible . South plain-field, New Jersey: Bridge publishing
company, 1977.
Huegel, F.J. The Ministry Of Intercession. Minneapolis: Bethany House,1971
Miller, Basil. George Muller: Man Of Faith . Minneapolis: Bethany House,1979
The Kneeling Christian. Grand Rapids, Michigan: Zondervan publishing House,1979
M’Intyer, David M. The Hidden Lift Of Prayer. Grand Rapids, Michigan: Baker Book House, 1979
Morgan , G. Campbell. The Practice Of Prayer Morgan Library). Grand Rapids, Michigan: Baker Book
House.
Murray,Andrew. Helps To Intercession. Fort Washington, Pennsylvania: Christian Literature Crusade, inc.,
1965.175
- The Ministry Of Intercession. Old Tappan, new jersy: Fleming H. Revell company, 1952
- The Power Of The Blood. Fort Washington, Pennsylvania: Christian Literature Crusade, Inc.,1965
- With Christ In The School Pf Prayer. Springdale, Pennsylvania: Whitaker House, 1981.
Parker, William R. Prayer Can Change Your Life. New York: Cornerstone, 1974
Prince, Derek. Shaping History Through Prayer And Fasting. Fort Lauderdale, Florida: Derek Prince
Ministries Publications, 1973
Rinker , Rosalind. Conversational Prayer. Waco, Texas: Word Books, 1976.
- Prayer: Conversing With God. Grand Rapids, Michigan Zondervan Publishing House, 1959
-
Sanders, J. Oswald. Effective Prayer. Robesonia, Pennsylvania: OMF Books, 1961
Searle, Walter. David Brainerd’s Personal Testimony. Grand Rpids. Michigan: Baker Book House, 1979
Simpson , A.B. The Lift Of Prayer. Harrisburg ,Pennsylvania: Christian Publications, 1975
Torrey, R.A How To Pray. Chicago: Moody press. Wallis, Arthur. God’s Chosen Fast. Fort
Washington, Pennsylvania: Christian Literature Crusade,Inc., 1970.
122
Arthur Wallis Pray In The Spirit. Fort Washington, Pennsylvania: Christian Literature Crusade, Inc.,
1970.
123
124
125
KUVUMBUA SIRI ILIYOKO KATIKA FUMBO KUU LA MAISHA!
(Tumia alama za mishale katika kasha ili uweze kufungua picha )
Onyesha picha ya kwanza: ‘Mwanadamu Dhambini’ akiwa ametengwa na ‘Mungu’
• Hii nuru(onyesha upande wa kulia)
inamwakilisha Mungu
• Mungu yu kamili wala hana dhambi
• Mungu anatupenda sana.
• Mungu hataki tupotee, bali tuwe na
uzima wa milele.
• Lakini dhambi zetu lazima
ziondolewe ili tuwe na uzima wa
milele pamoja na Mungu
• Hii picha (onyesha
u p a n d e w a
kushoto) inawakilisha mtu kama
wewe na mimi.
• Giza hii inaonyesha dhambi zetu
• Dhambi ni kitu chochote ambacho tumekatazwa
na Mungu
• Biblia inasema, "kwa sababu wote wamefanya
dhambi,
na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. " (Warumi
3:23)
• Dhambi zetu zimetutenganisha na Mungu.
Fungua upande wa pili:
“Kristo Msalabani”
• Mungu alitupenda sana hata akamtoa
mwanawe pekee Yesu Kristo aje
ulimwenguni kama binadamu.
• Mungu alimfanya Yesu kufa msalabani
ili azichuku dhambi zetu na kutulipia
deni ya dhambi zetu kwa damu yake.
Alichukua dhambi zetu katika mwili
wake juu ya msalaba ili tuweze kumfikia
Mungu (1 Petero 2:24, 3:18)
• Biblia inasema kuwa Mungu aliupenda
ulimwengu sana, hata akamtoa Mwanawe pekee (Yesu) ili kila mtu
amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. (Yohana 3:16)
• Biblia inasema ,"Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye
mwenyewe kwetu sisi kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu,
tulipokuwa tungali wenye dhambi." (Warumi 5:8)
Fungua upande wa Tatu:
“Kristo Kaburini”
• Watu walimlaza Yesu kaburini
• Wakaviringisha jiwe kubwa
mlangoni pa kaburi.
• Askari wa Kirumi wakalinda
kaburi
Fungua upande wa
Nne: “Kufufuka kwa
Yesu”
• Mungu alimtuma malaika kuondoa jiwe na
kuwafukuza wale askari.
• Mungu alimfufua Yesu kutoka kwa wafu!
• Baadaye Mungu alimrundisha Yesu
Mbinguni.
• Yesu alilipa deni ya dhambi zetu na
ameshinda kifo
Fungua upande wa sita: “Mbingu
na Kuzimu”
Fungua Upande wa Tano:
‘Kuvuka daraja’
• Yesu ndiye njia pekee ya kwenda kwa
Mungu."
• Yesu alisema katika Bibilia:"Mimi ndimi
njia,na kweli,na uzima. Mtu haji kwa
Baba , ila kwa njia ya mimi" ( Yohana
14:6)
Tunaweza kusamehewa dhambi zetu zote
na kuwa na Mungu milele kupitia kwa Yesu.
• Lakini kujua tu kuhusu mambo haya
hakutoshi, lazima tuchague kuweka imani
yetu kwa Yesu – kumwamini atuokoe kutoka
dhambini.
• Pasipo kumwamini Yesu, dhambi zako
haziwezi kuondolewa!
(Waebrania 4:2)
• Biblia inasema kwamba amwaminie Yesu ana uzima wa milele na
atahukumiwa. Lakini asiyemwamini
• Yesu tayari amekwisha hukumiwa na ghadhabu ya Mungu inamkalia (Yohana
3:16,18,36)
• Adhabu ya dhambi ni mauti, bali uzima wa milele katika Kristo Yesu ni karama
ya bure.
• Utachagua lipi?
• Utamwamini Yesu aliyekufa ili akulipie dhambi zako, na upokee msamaha na
uzima wa milele? (Onyesha "Mbinguni")
Au utamkataa Yesu Kristo na
kupata adhabu ya motoni
milele (Onyesha kuzimu)
• amkataa Yesu Kristo na
kupata adhabu ya motoni
m i l e l e ? (Onyesha
"Kuzimu")3 .
Uliza Swali
Je, Ungependa
Kumwamini Yesu
Sasa na Kuokoka?
126
Biblia inasema ,:" Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana utaokoka" (Warumi 10:9) Ningependa
kukuongoza katika sala sasa hivi. Kumbuka siyo maneno maalumu ambayo yatakuokoa. Mungu anaangalia moyoni
mwako ili aone imani ya kweli katika Yesu.Unaweza kumwamini Yesu hata sasa hivi kwa kuomba nami…Je, uko tayari?
(kama jibu ni ndiyo)… Basi tuombe.
Sala ya imani:
“Mungu, asante kwa kunipenda. / Naamini kwamba nimekutenda dhambi. / Naamini kwamba mwanao Yesu /
alikufa msalabani / Kulipa deni ya dhambi zangu / Na kwamba ulimfufua kutoka kwa wafu. / Sasa naweka imani
yangu kwa Yesu pekee / anisamehe / Na aniokoe kutoka kwa dhambi zangu. / Nakiri kwamba Yesu ni Bwana! /
Asante kwa zawadi yako ya uzima wa milele. / Nimeomba katika jina la Yesu, / Amina.”
Hakikisho la Wokovu
Onyesha “Mbingu na Kuzimu”
• Kama umechukua
hatua hiyo ya
kumwamini Yesu
Kristo, hivi ndivyo
Biblia isemavyo
kukuhusu; “Bali wote
waliompokea
aliwapata uwezo wa
kufanyika watoto wa
Mungu, ndio wale
waliaminio jina lake!”
(Yohana 1:12)
• (Elekeza kidole
kwenye
mikono) Yesu anasema, “Kondoo wangu waisikia sauti
yangu, nami nawajua nao wanifuata; Nami nawapa
uzima wa milele wala hakuna
mtu atakayewapokonya katika
mkono wangu!” (Yohana 10:
27-28)
(Hatua hii si lazima)
Onyesha ‘Daraja ya msalaba’
• Pia Yesu alisema, " Amini, amini
nawaambia, Yeye alisikiaye
neno langu na kumwamini Yeye
aliyenipeleka yuna uzima wa
milele, wala haingii hukumuni,
bali amepita kutoka mautini
kuingia uzimani." (elekeza
kidole chako juu ya daraja
kuelekea katika mwangaza kama
ishara ya “kuvuka kutoka mautini na kuingia
uzimani." (Yohana 5:24)
Kufanya Wanafunzi
Hatua Za
Wafuasi wa
Kristo
Fungua picha ya kwanza. Nyuma yake utaona
picha hii. Itumie kwa kusaidia aliyeamini kukua
katika Kristo.
MPENDE Mungu, na
kuwapenda watu
wote
“Mpende Bwana
Mungu wako kwa moyo
wako wote, na kwa
roho yako yote, na kwa
akili zako zote.Hii ndiyo
amri iliyo kuu, tena ni
ya kwanza. Na ya pili
yafanana nayo, ni hii,
Mpende jirani yako
kama nafsi yako.”
(Mathayo 22:36-40)
JIFUNZE Biblia kwa kusoma (Neno La
Mungu) kila siku.
Anza kwa kusoma kitabu cha Yohana.
Soma sura moja kila siku. “Kama watoto
wachanga waliozaliwa, sasa yatamanini
maziwa ya akili yasiyogoshiwa ili kwa
hayo mpate kuukulia wakovu” (Petro
2:2) “Mtu akinipenda, atalishika neno langu” (Yohana
14:23)
O m b a b i l a
kukoma
Katika kuomba
unaweza
kumtukuza Mungu, kumwomba
akusaidie, kuungama dhambi zako
na kuwaombea wengine,
“Msijisumbue kwa neno lolote, bali
katika kila neno kwa kusali na
kuomba pamoja na kushukuru, haja zenu na
zijulikane na Mungu, na amani ya Mungu ipityo akili
zote itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika
Kristo
Yesu.” (Wafilipi 4:6-7)
SHIRIKIANA na wakristo wengine mara kwa
mara
Mungu ameamuru kwamba
Wakristo wakutane mara kwa mara
kwa kuabudu, kuomba, kujifunza
Biblia, na kusaidiana… "Wala
tusiache kukusanyika pamoja
kama ilivyo desturi ya wengine, bali
tuonyane…"
(Waebrania 10:25)
ELEZA watu wengine Habali
Njema ya Yesu Kristo
Mungu anataka tuwaelezee watu
wengine jinsi ya kuwa na uzima
wa milele pamoja na naye kwa
kumwamini Yesu ili awaokoe kutoka dhambini.
Unaweza kutumia karatasi kama hiki kwa
kuwashuhudia watu "Yesu akawaambia, Enendeni
mwote mkaihubiri injili kwa kila kiumbi."
127
(Marko 16:15)
. www.evangecube.org
Tafadhali tusimulie ushuhuda wako: testimony@evangecube.org
Tazamia Muujiza leo! Kwa habari zaidi wasiliana na:
KASHA LA KUENEZA INJILI
Kwa sababu umehudhuria mafundisho ya uinjilisti kwa kutumia Kasha La Kueneza Injili
(Evangecube), tungependa kukutia moyo uweze kumtumikia Mungu kwa kuwafundisha wengine.
Mbinu za mafundisho kwa kutumia kasha la kueneza injili (Evangecube Strategic Evangelism
Training - ESET) ziko kwa ajili ya kuhudumu na kumotisha kanisa kuwafanya wengine kuwa wanafunzi,
tangia kwa majirani, au jiji, na ulimwengu kwa ujumla. Jinsi ya kwanza ya kufanya wanafunzi ni
kuwaeleza wengine injili ya Yesu kwa njia ya kuleta matokeo katika imani na wokovu.
Mafundisho ya kutumia Kasha La Kueneza Injili (Evangecube) inadhibitika kuwa chombo chema katika
kueneza injili. Watu wengi wanaelewa jinsi ya kueneza injili, kwa sababu ni rahisi sana, lakini watu
wachache sana wanafahamu jinsi ya kumfanya mtu kuwa na uhusiano na Kristo. Inawezekana kwamba
Wakristo wengi hawawezi kueneza injili kwa sababu hawajajifunza jinsi ya kuwa na matokeo katika
uinjilisti. ESET imebuniwa kwa kusudi la kumtia moyo anayeeneza injili kwa kumwonyesha jinsi rahisi
itakayomwezesha kuzingatia ujumbe wa injili, na kumpa mifano ya kutumia katika uenezaji wa injili.
Kazi ya mkufunzi wa ESET ni kuwa msimamizi, mwalimu, mwenye kufanya wanafunzi, na mkusanyaji
watu katika utendaji.
ESET ina mafundisho yake hasa katika mazingara ya kanisa lako. Utahitajika kukusanya makanisa katika
eneo lako ambayo yangependa kuhusika katika warsha ya mkusanyiko wa waenezaji injili. Mkufunzi wa
ESET ni mwalimu wa neno la Mungu. Je, hii inahusika vipi na mafundisho kwa kutumia kasha la uenezaji
neno (Evangecube)? Kama mwalimu wa neno la Mungu, jukumu lako ni kuchochea mwili wa Kristo ili
liweze kuwa na mafanikio katika uenezaji wa neno, na kuwakusanya katika maeneo ya kanisa ili kueneza
injili kwa sehemu ambazo kanisa limeteua kwa kueneza injili. Lengo ni kuwachochea wanafunzi kuishi
maisha ya uenezaji injili ili waweze kuwaonyesha walio karibu nao injili hii ibadilishayo maisha.
Mkufunzi wa ESET pia hufanya wanafunzi wake, na wale aliokusanya kuwa wafuasi. Mbali na ESET,
anayefanya wanafunzi ni mtu ambaye anazalisha huduma katika wengine. Tukiwafanya wanafunzi
kuwa wafanyaji wafuasi, basi tutakuwa na wafanyaji kazi wengi wa kutimiza kusudi la Mungu katika
mwili wa Kristo.
Kusudi lingine la ESET ni kukusanya mkristo wa kawaida aliye kanisani na kumfanya kuhusika kikamilifu
katika huduma ya uenezaji wa neno. Anayekusanya wengine kwa utendaji huwawezesha wengine kufanya
kazi ya uinjilisti/mfanya wanafunzi kwa kusudi la kuona utukufu wa Mungu ukienea kutoka eneo lake
hadi ulimwengu wote.
Kama ungependa kujiunga nasi kama mkufunzi, tafadhali tufikie kwa anwani ifuatayo:
Evangecube Global Ministries
4801 Frankford Road
Suite 300
Dallas, Texas 75287
EvangeCube Global Ministries • 4801 Frankford Road, Suite 300 •Dallas, Texas 75287 9 7 2 - 8 1 8 - 9 9 9
6
128
972-818-9996 Phone
www.evangecube.org
e-mail: infor@evangecube.org
Kwa habari zaidi kuhusu huduma yetu ya kimataifa, au mafunzo ya kasha katika kanisa lako, au kujua
mengi kuhusu Evangecube Global Strategy, tafadhali tufikie kwa simu au barua pepe. (Huu ni mfano wa
kadi ambao tungependa kutumia katika mafundisho. Tutakutumia baadaye).
Fomu Ya Maombi Kwa MKUFUNZI Wa Kasha La Kueneza Injili
________________________________________________________________________
Jina La Kanisa
________________________________________________________________________
Mtu wa Kuwasiliana Naye
________________________________________________________________________
Idadi Ya Washiriki
________________________________________________________________________
Anwani
________________________________________________________________________
Jiji Mkoa Simu
________________________________________________________________________
Anwani ya Barua Pepe
q Ndiyo, ningependa kuwa Mkufunzi wa Kasha La Uinjilisti
q Ndiyo, nitaeneza injili kwa watu 100 mwaka ujao.
129
KUJIFUNZA KUTOA USHUHUDA
Chombo cha manufaa sana katika uinjilisti ni kuweza kutumia ushuhuda wako kwa ustadi. Yesu alituita
tuwe mashahidi wake. Kuwa mshahidi haimaanishi kuwaambia watu injili peke yake. Ina maana pia ya
kuwaambia wengine kuhusu wokovu wako. Tunahitaji kuangalia maisha ya Paulo ndipo tuone jinsi Roho
Mtakatifu anavyoweza kutumia ushuhuda uliotayarishwa vizuri.
Kisa Chako
Mara tatu katika maandiko, mtume Paulo anaeleza kisa chake, jinsi alivyokutana na Kristo. Anaeleza kisa
chake katika Wagalatia 1:13-24 kukomesha waliokuwa wakiharibu injili ya neema. Kwa kueleza kisa
chake aliweka wazi mwito na “injili” yake. Kuna mamlaka na nguvu katika kisa cha mtu yeyote. Ni
vigumu mtu yeyote kupinga yale uliyopitia maishani. Hii ndio sababu mshahidi huitwa kutoa ushahidi
mahakamani. Mshahidi ni yule anayeeleza aliyoyaona ama yaliyompata. Si rahisi kukana nguvu zilizoko
katika kisa cha mtu.
Kila muumini ana la kusema. Inampasa kujua jinsi ya kusema jambo hilo vyema. Kwa kuwa Kristo
amebadilisha maisha yake, itafurahisha kusikia habari hiyo njema wakati wo wote. Ushuhuda wa Paulo
unapatikana katika Wagalia sura ya kwanza, Matendo ya Mitume sura ya ishirini na mbili, na Matendo ya
Mitume sura ya ishirini na sita. Nimegundua kwamba ubora wa ushuhuda wa Paulo, umetokana na jinsi
alivyofikiri kwa maakini, akatunga, na kisha kusimulia jinsi alivyokutana na Kristo.
Kabla, Vile, na Baadaye
Ukitazama kwa makini jinsi Paulo alivyosimulia ushuhuda wake, utagundua kwamba alitumia
mpangilio fulani.
1. Maisha yake kabla kumpokea kristo .
Katika matendo ya Mitume, anaeleza jinsi alivyopinga Yesu na wafuasi wake. Paulo alikuwa na
maisha ya kale kabla kukutana na Kristo njiani, akielekea Dameski. Anasimulia maisha yake
yalivyokuwa kabla kumpokea kristo.
Vivyo hivyo, unapoketi kuandika kisa chako , ni vyema kuanza kusimulia ulivyokuwa kabla kukutana
na Kristo. Ulikuwa namna gani bila Kristo? Je umewahi kufikiri kwa makini, kisha ukaandika
ushuhuda wako? Hebu wazia jambo hili. Ni kitu gani hicho ulichokosa kwa ulimwengu, kwa marafiki,
kwa pesa, kwa elemu, ama kwa dhambi kabla kumpokea Kristo?
2. Alafu ,akashuhudia vile alivyokutana na Kristo.
Katika Matendo ya Mitume 26:12-18, Paulo anaeleza wazi wazi vile alivyokabiliana na Kristo njiani,
akielekea Dameski. Anaeleza kwa hakika kwamba kuna wakati na pahali ambapo alikutana na Kristo.
Kila Mkristo hufikiwa na wakati wa kuamua, ambapo anapeana roho yake na maisha yake kwa Kristo.
Kueleza kisa hicho kina nguvu sana. Unapoandika kisa chako, eleza kwa wazi kule ulikuwa, hali
ilivyokuwa, na vile ulivyompokea Kristo kama mwokozi na Bwana wa maisha yako.
3. Mwisho anasimulia maisha yake baada ya kukutana na Kristo.
130
Katika kutumia ushuhuda wake kwenye maandiko yote matatu, Paulo anatueleza tofauti ambayo Yesu
alileta katika maisha yake. Mungu alibadilisha Saulo, aliyekuwa Myahudi asili, na kumfanya kuwa
Paulo Mtume kwa wasio wayahudi. Alibadilika kabisa.
Kwa vile Kristo ameingia moyoni mwako, je amekusaidia kushinda na kukabiliana na uzito wa
maisha? Ikiwa ni hivyo, basi unastahili kusimulia kisa hicho. Watu wanahitaji kujua kama “kuokoka”
kuna maana kweli. Je, ina faida gani katika maisha ya kila siku? Hebu chukua muda wa kuandika
mabadiliko ambayo Yesu ameleta katika maisha yako tangu ulipokutana naye.
Kwa Ufupi, Si Dini
Hapa ndipo pana changamoto! Hebu jaribu kama unaweza kueleza kisa chako kwa maneno 150 – 175, ama
zaidi. Unaweza kuandika mara moja au mara mbili. Ni vizuri kuandika kwa kifupi. Kumbuka kwamba
utahitaji kutoa ushuhuda wako “unapoenda,” na “njiani.” Mungu atakufungulia nafasi nyingi za ajabu ili
uwaeleze wengine ushuhuda wako. Utaweza kushuhudia sokoni, mitaani, kwenye basi, ama popote watu
walipo. Unapojifunza kusimulia kisa chako kwa maneno 150, utafungulia nyoyo zilizo na njaa milango.
Mungu anaweza kukusudia uketi baadaye na kueleza watu maandiko na mpango wa Mungu wa wokovu.
Jambo la pili, usizingatie “dini” sana, kwa sababu watu ambao wamepotea hawajui lugha zinazotumiwa na
Wakristo. Mara nyingi tunajaribu “kuongea kibibilia” kwa kutumia maneno ambayo watu wasiohudhuria
kanisa hawaelewi. Maneno kama “kuzaliwa tena”, “toba” na “kuokoka” ni vyema yaelezwe vyema kuliko
kutumiwa. Unapoandika ushuhuda wako, ni vizuri ujifananishe na mtu aliyepotea dhambini ili uweze
kujieleza kwa maneno yanayoeleweka.
Jaribu kwa Rafiki
Baada ya kuandika ushuhuda wako kwa kutumia mifano ya kabla, vile, na baadaye (ukiwa katika hali ya
maombi), msimulie rafiki yako Mkristo ili aweze kuusikiliza. Labda itawabidi kuandika na kutia moyoni
shuhuda zenu. Ni vyema wewe na rafiki yako kuelezana shuhuda zenu.
Neno La Mwisho
Unapoendelea kuzoea kueleza watu kisa chako, unaweza kuongezea maneno kutoka katika Bibilia. Kwa
mfano, unapoeleza ulivyokuwa ‘kabla kukutana na Kristo,” na hisia zako za kutafuta kusudi katika maisha,
unaweza kutaja Isaya aliposema “sisi sote kama kondoo tumepotea” kueleza unavyohisi. Kuna aya nyingi
nzuri katika Bibilia unazoweza kutumia katika kisa chako. Kumbuka, neno la Mungu “li hai, tena lina
nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili” (Waebrania 4:12). Mungu atatumia neno
lake kutilia mkazo maneno yako.
131
KUSHUHUDIA KUTUMIA MFANO WA DARAJA
Moja kati ya manufaa yanayotokana na kutumia mfano wa daraja ni kwamba inamatokeo mema, na
inaweza kutumika kwa tamaduni zote. Linaweza pia kuchorwa kwa urahisi na kuachiwa anayeuliza ili
atafakari. Hebu chora kwa karatasi mistari miwili sambamba, zilizo umbali wa inchi mbili hivi.
Alafu anza kwa kuandika MUNGU kwa upande wa
kulia wa mistari hiyo, na WATU kwa upande wa
kushoto. Eleza kwamba hapo mwanzo Mungu
aliumba kila mtu ili aweza kuwa na ushirika naye.
Lakini kila moja akaenda njia yake na kumkataa
mungu. Walimuasi Mungu na kuanguka dhambini.
Hii ilisababisha wanadamu na Mungu kutengana
(chora sehemu mbili ya mtelemko wa ghafla, yaani
cliff, kwa upande wa mungu, na pia kwa upande wa
mwanandamu).
Tunajua kwamba kuna utengano mkubwa kati ya Mungu na kila mtu, kwa sababu Bibilia inatueleza
kwamba “wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Romans3:23). Andika neno
DHAMBI kutoka juu kuelekea chini katikati ya mitelemko ya ghfla (cliff) uliyochora. Kwa upande wa
wanadamu andika Warumi 3:23; kisha andika
“wote wamefanya dhambi” chini yake. Weka
mviringo kwa neno “wote.” Sasa taja
Warumi 6:23, na kuiandika kwa upande wa
wanadamu; kisha andika chini yake, “malipo
ya dhambi ni mauti ya kiroho.” Andika
Waebrania 9:27 na chini yake andika
maneno: “hukumu yaja.” Sema, “Hii ni
HABARI MBAYA.” Andika hivyo hapo
chini. Wakati huo mtu atajikuta bila tumaini
na uwezo wowote, anapoona kwamba hawezi
kuvuka ufa kubwa uliopo.
Taja warumi 5:8, na unapofanya hivyo,
chora msalaba kwa neno “dhambi” kwa
kuchora mistari ukianzia upande wa
Mungu. Andika warumi 5:8, na maneno
“Christo alitufia,” upande wa Mungu.
Hebu sasa taja waefeso 2:8-9, kisha
iandike, na kuongezea maneno haya:
“ukombozi ni thawabu” (neema ya
Mungu ni bure, bila malipo). Taja
Yohana 1:12 na uandike “Amini” upande
wa kushoto wa msalaba. Andika “pokea”
132
upande wa kulia wa msalaba. Andika tena Yohana 1:12 kwa upande wa Mungu, na maneno haya chini
yake: “lazima tuamini na kupokea Yesu kama Bwana na mwokozi.” Alafu sema, “hii ni HABARI
NJEMA,” na kuiandika upande huo. Hivyo ndivyo mtu anavyoweza kuvuka ufa kubwa la dhambi ambalo
limemtenganisha na Mungu.
Mwenye dhambi kisha anaamini (kutegemea kabisa)
kwamba kifo cha Yesu msalabani kililipa adhabu ya
dhambi zake. Anampokea Kristo maishani mwake kwa
kuomba ombi la kumkaribisha Kristo kuwa mtawala wa
maisha yake. Matokeo ya “kubadilishwa” huku ni
hakikisho tunayopewa katika maandiko kwamba mtu
anafanywa kuwa mwana wa Mungu. Mtu anapomkiri
Kristo kama Bwana na mwokozi, na kuamini kwamba
alijitoa kafara kwa ajili yake, anaokolewa. Taja warumi
10:9-10 na kuandika juu ya mfano huo wote.
Haki zote kwa: Wheaton University, 501, College Ave., IL 60187, USA; Imetumika kwa Ruhusa
133
134
135
MAHUBIRI TUNAYOWEZA KUONA
Ni heri nione mahubiri kuliko kusikia moja siku yeyote ile.
Ni heri mtu atembee nami kuliko kunionyesha njia.
Jicho ni mwanafunzi mzuri na mwenye hamu kuliko sikio.
Mausia mema yaweza kutatanisha, lakini mifano huleta dhihirisho.
Muhubiri bora zaidi ni yule anayeishi kulingana na maagizo ya imani yake.
Kwa sababu kuona uzuri ukitekelezwa kwa vitendo ndio kila mtu anahitaji.
Naweza kujifunza kufanya hivyo ikiwa nitawezeshwa kufanya ionekane.
Naweza kuona mikono yako ikitenda lakini ulimi wako kwa upesi waweza kwenda.
Na mafunzo unayotoa yaweza kuwa yenye hekima na ukweli.
Lakini heri nipate fundisho kwa kuona vitendo vyako.
Kwa vile naweza kutokuelewa na kutoshika mashauri mazuri unayotoa.
Lakini hakuna kutoelewa kwa kuona jinsi unavyotenda na kuishi.
Edger A . Guest
136
137
KIONGOZI MTUMISHI
Wakati moja niliona kibonzo cha mtoto mvulana, aliyekuwa kiongozi wa skauti ambaye alipeleka kikundi
chake cha wavulana kukwea mlima, ambapo alipotea na kuuliza kama yeyote kati yao alikuwa na dira
(compass). Jambo la kwanza kwa kiongozi aliyebora ni kwamba lazima awe na uwezo wa kuongoza.
Mtume Paulo alitaja vipawa mbali mbali vya Roho Mtakatifu, ikiwapo kipawa cha “uongozi”. Warumi
12:8 inatuambia, “mwenye kusimamia kwa bidii.”
Tunaweza kujifunza mengi kuhusu uongozi kwa kumtazama Yesu anavyoongoza wanafunzi wake. Ukweli
ni kwamba kipawa cha uongozi ni Yesu kiongozi anayeishi maisha yake ya uongozi ndani ya maisha ya
mtoto wa Mungu aliye na kipawa.
Imesemekana kwamba viongozi huzaliwa; hawatengenezwi. Hii ni kweli kabisa kwa kiongozi Mkristo.
Baada ya kuzaliwa mara ya pili, Roho humpa kipawa cha uongozi. Alizaliwa upya ili aongoze.
Kuongoza kwa Tabia
Anayetamani kuongoza wengine kwa utumishi kama Mkristo lazima ajifunze kutoka kwa Kristo. Kristo
hakuongoza kwa matakwa yake mwenyewe, ama kwa imla au vitiso, bali kwa maadili. Yesu alifundisha
wanafunzi wake kumi na wawili jinsi ya kuongoza kwa kufuata wema wa Mungu na maadili ya Bibilia.
Yesu alitumia tabia yake kama mwongozo katika kufundisha jinsi ya kuishi kwa maadili ya milele.
Yesu Alivyoongoza Watu
Ustadi wa Yesu kama kiongozi wa watu ni kwamba alikuwa kiongozi mtumishi. Aliongoza kwa kutumikia
wengine. Upole wake, upendo wake, na moyo wa kutumika uliwavutia wote aliowaongoza. Yesu
hakupima ukuu wa mtu kwa watumishi aliokuwa nao, bali kwa wingi wa watu aliotumikia. Kwa kweli,
Yesu alitimiza unabii wa Isaya kwamba Masihi atakuwa “mpole na mnyenyekevu wa moyo” (Isaya 53).
Masihi atakuwa mfalme, lakini mfalme mtumishi! Paulo anatuambia kwamba Kristo alikuja “kwa namna
ya mtumwa,” (Wafilipi 2:6,7). Hii ndiyo impendezayo Kristo. Ni nia yake na maisha yake. Anaongoza
watu kwa kuwa kiongozi ambaye ni mtumishi.
Kutawadha Miguu
Yohana 13:4 kuendelea imenukuu ujumbe wa maisha ambayo Yesu aliwapa wanafunzi wake alipokuwa
karibu kuondoka duniani. Aliwatawadha miguu. Aliwafundisha kwa mfano wake mwenyewe.
Hawangeweza kamwe kusahau mfano huu ulioonyeshwa na Mfalme wa Utukufu aliyepiga magoti na
kutawadha miguu ya wapendwa wake kwa unyenyekevu. Hebu tujifunze kanuni za milele kutokana na
Yesu kutawadha miguu michafu:
1. Unyenyekevu Ni Kiini cha Uongozi Wa Utumishi
Kumwona Yesu akitawadha miguu yao iliyonuka ilikuwa funzo tosha katika unyenyekevu. Yesu ambaye
alikuwa amejivika kitambaa cha kupangusa miguu kama mtumwa wa kawaida aliosha miguu yao ili wajue
kwamba njia ya kuelekea juu iko chini! Njia ya uongozi wa kweli unapatikana katika unyenyekevu.
Kongozi lazima awe tayari kufanya kazi duni ili kutia wengine moyo wa kutumika. Si vyema kiongozi
kuuliza watu wengine kufanya kazi asichokuwa tayari kufanya mwenyewe. Roho wa Kristo ndani yako
atakupa unyenyekevu wake kwa kutimiza maneno haya “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio
hodari, ili awakweze kwa wakati wake” (1 Petero 5:6).
2. Mtumishi Kiongozi haambiwi kutumika
Mfano tunaoona wa Yesu akiwa tu na kitambaa cha kupangusa miguu ni wa moyo wa kujitolea. Hakuna
aliyemuuliza kufanya kazi hii duni, bali alichagua kuifanya mwenyewe. Anaona hitaji na kulitimiza.
Wanafunzi wake hawakuwahi kudhani kwamba siku moja wangalimwomba Yesu kuosha miguu yao. Ndio
138
sababu viongozi shupavu ni wale waliojitolea bila kushurutishwa. Wanavutia watu wengine kwa mfano
wao. Kujitolea kwa Kristo, hata msalabani, kunatuvutia sana kuwa kama yeye.
3. Kiongozi Mtumishi habagui
Jambo la ajabu ni kwamba Yesu aliosha miguu ya Yudasi, akifahamu vyema kwamba alikuwa msaliti! Hili
ni tendo la upendo na rehema kwa wingi. Viongozi shupavu ni wale wanaotumikia wote wanaohitaji
utumishi wao, bila kubagua. Upendo wa utumishi hauna kifani. Tunaweza kujifunza kutokana na mfano
wa Kristo.
4. Viongozi Watumishi huvaa mavazi ya Kaki
Kwa kuvaa kitambaa cha kupangusa miguu, Yesu alikuwa tayari kufanya kazi chafu iliyohitaji kufanyika.
Hili ni tendo la pendo. Tendo hili linatukumbusha kuna kujifunza zaidi katika kutenda, kuliko kusema.
Uongozi unahusiana sana na tunavyotenda, kuliko tunavyowaambia wengine kufanya. Yesu alikuwa
“miongoni” mwa wanafunzi wake, akichangia sehemu muhimu katika maisha yao ya kila siku.
Aliwaongoza kwa kuwatumikia kila siku. Kiongozi yu tayari kufanya lolote ili kufanya wengine bora
zaidi.
Sam Walton, ambaye ni mwanzilishi wa Maduka ya Wal-Mart alifahamika sana kule Bentonville Arkansas
iliyo makao makuu ya Wal-Mart. Alifahamika kwa sababu hata baada ya kuwa mmoja kati ya matajiri
wakuu ulimwenguni, aliendelea kuendesha gari lake la pick up iliyokuwa imedumu miaka kumi. Alisema
kwamba kuendesha gari hilo lilimkumbusha kuwa mnyenyekevu na kumkumbusha alikotoka. Viongozi
huvaa nguo za kaki.
5. Viongozi Watumishi hupeana bila kutarajia kurudishiwa
Yesu hakuuliza wanafunzi kama wangependa kuosha miguu yake. Kuna funzo hapa. Mtumishi hadai
atumikiwe kwa kuwa ametumika. Hii haihusiani na kupata kutoka kwa watu wengine kwa kuwa umewapa.
Viongozi shupavu wananuia mema kwa wengine bila kujinufaisha wenyewe. Wanaona “picha kubwa,”
bila kuona tu ulimwengu wao mdogo.
6. Viongozi Watumishi ni sharti wajifunze kupokea na kupeana
Petero alimwendea Yesu na kusema, “Bwana hutanitawadha miguu!” Ombi hili halionekani tu kuwa
ombi lenye heshima, bali pia laonekana kuwa lenye kiburi, ndipo likasababu Yesu kumrekebisha Petero.
Kristo angependa tuelewe kwamba ni vyema viongozi wakubali utumishi kutoka kwa wengine. Tunahitaji
unyenyekevu wa kuruhusu wengine watuhudumie jinsi tunavyowahudumia.
7. Viongozi Watumishi wana Utu sawa na Kristo
Baada ya kutawadha wanafunzi wake kumi na wawili miguu, Yesu aliwambia hivi, “Basi ikiwa mimi,
niliye Bwana na Mwalimu (ujumbe wa maisha), nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana
miguu ninyi kwa ninyi” (Yohana 13:14,15). Ujumbe huu ni wazi kwa wote watakaoufuata. Tutakuwa
watu wa maana ikiwa tutafanyia wengine jinsi Kristo alivyofanya. Yeye ni kielelezo katika uongozi wa
maisha ya Ukristo; aliongoza watu kwa kuwa kielelezo. Hakuwaambia tu wapende adui zao, bali yeye
mwenyewe aliwapenda adui zake kwa hakika. Alimfanya mtoza ushuru wa Kirumi kuwa mfuasi! Alikula
chakula cha jioni na Zakayo aliyekuwa amedharauliwa. Alimsamehe mwanamke aliyepatikana akizini.
Kielelezo chake kilikuwa fundisho tosha.
Viongozi Watumishi huongoza wengine
Kiongozi inamaana “yule anayesimama mbele mbele ya wengine” katika lugha ya Kiyunani. Kiongozi wa
kiimla huwaambia wengine kufanya yale ambayo yeye mwenyewe hataki kufanya. Kiongozi wa kweli si
wa namna hiyo. Yeye huchukua mstari wa mbele. Anasema “nifuate mimi na mfano wangu. Fanya
nifanyavyo. Nitakuonyesha namna ya kufanya.” Hivyo ndivyo Kristo aongozavyo watu. Anakuambia
uchukue msalaba wako kila siku. Kisha anaenda kufa msalabani kwa ajili yako! Si ajabu watu walimpenda.
Wangali wanamfuata. Lazima tuwe vielelezo kwa kuwa katika mistari ya mbele, kama viongozi
watumishi.
139
Viongozi Ni Watu Wenye Maono
Yesu aliona ufalme wa Mungu; akanuia kuuliza wafuasi wake kuungana naye katika maono ya kuuleta
ufalme huo hapa duniani. Aliona uwezo iliyokuwemo ndani ya wale watu kumi na wawili aliyowachagua.
Alikuwa akifikiri kuhusu wokovu wetu alipowaita (Tazama Yohana 17:18-20). Kwa kuwaongoza, allinuia
kuleta ulimwengu wote kwake. Robert Coleman, katika kitabu chake kiitwacho The Master’s Plan of
Evangelism, anaona ono hili kama sehemu ya uongozi wa Kristo. Kila kiongozi mwema lazima awe na
hatima katika mpangilio wake. Viongozi huona mambo ambayo wengine hawaoni. Hii inaweka wazi
tofauti baina ya viongozi na wasimamizi. Msimamizi anaangalia mambo ya kawaida ya kila siku. Hao si
viongozi wa watu. Hao ni wasimamizi wa wafanyakazi! Pana tofauti kubwa kati yao.
Mwitu Mbaya
Kuna mfano maarufu inayoeleza tofauti kati ya viongozi na wasimamizi. Mfano huu ni wa kundi
linaloondoka kwenda safarini. Kisha linajikuta katika mwitu wenye mimea mirefu kuliko ndovu.
Msimamizi anawakusanya ili watengeneze njia. Anapeana panga na maji kwa wafanya kazi walio choka,
na kuwaangalia vyema wanapojaribu kutengeneza njia. Msimamizi huyu anaweka fikira zake zote kwa
kuelekeza watu. Kisha kiongozi anajitokeza. Anakwea mti mrefu na kuchunguza eneo hilo, alafu
anamwambia msimamizi, “acha kukata! Unaenda njia mbaya.” Huyo ndiye kiongozi, kwa maana anaona
picha kubwa na kuongoza kwa jia inayofaa.
Viongozi Watumishi ni watu wa kujitolea
Yesu alijitolea katika kufuata ono lake. Alimpa Baba Mungu yote aliyokuwa nayo katika siku zake zote. Ni
tabia njema kiongozi kuzingatia mwito wake na maono yake, bila kuupoteza kwa urahisi. Anapanga kazi
yake na kutekeleza mipango yake.
Ni mtu aliyepagawa na anayokusudia kufanya, kwa sababu kuna wengi ambao wangependa kumzuia na
kumvunja moyo. Kiongozi ana imani kwa kile afanyalo wakati ambapo wengine hawajali. Kiongozi ni
lazima aulize wafuasi wake wajitolee alivyojitolea mwenyewe. Yesu aliwaambia watu wake hivi, “ikiwa
mnanipenda, tiini amri zangu”.
Tunazungumza kuhusu kuwajibika. Viongozi watu wao kuwajibika katika maono yao, mipango yao, au
mwito wao. Anawajibika, na kwa hivyo anahitaji watu wake kuwajibika.
Viongozi Watumishi Wamejitolea kwa Ubora
Kiongozi ana lengo. Yesu, ambaye ndiye kielelezo chetu, alikuwa na lengo. Milele alikusudia mambo
mawili: 1) Kazi ya Baba yake (tazama Luka 22). 2) Kumpendeza Baba yake (tazama Yohana 8:29).
Tunastahili kujitosa katika wazo hili la kumtumikia Mungu kwa ubora. Ubora unatokana na shauku ya
moyo unaotamani kumpendeza Baba wetu wa Mbinguni. Ubora ni kuwa na juhudi kwa mambo uliyoitiwa
na Mungu kufanya. Tunawajibika kufundisha wanaume na wanawake kuzingatia ubora mapema maishani.
Kukuza viongozi watumishi mapema kutatuwezesha kuwa na kizazi cha viongozi watakaobadilisha
ulimwengu.
Tunaona mtindo huu wa kukomaa kwa viongozi:
• Viongozi chipukizi – wana kati ya miaka 18-25
• Viongozi wenye bidii – wana kati ya umri wa miaka 25-40
• Viongozi thabiti – wana miaka 40 na zaidi.
Ujumbe kwa Maisha Yako
Hatimaye Yesu alionyesha hali kamili ya kiongozi. Maisha yake yalikuwa ujumbe kamili. Wengi
walimkumbuka siku nyingi baada ya umati kusahau maneno na matendo yake. Wanafunzi wake walitaka
kuwa kama yeye. Hiyo ni sifa njema. Tuwe “Kristo” kwa wengine jinsi wamwonavyo.
140
Huwezi kuongoza tofauti na uishivyo. Tembea jinsi unavyozungumza. Jinsi ulivyo huzungumza zaidi
kuliko ufundishavyo. Kiongozi wa kweli husema, “nifuate, nimewahi kufika hapo.” Anaishi
anavyowaambia wengine wafanye.
141
NGUVU IPATIKANAYO KATIKA MAONO
Mtumishi wa Mungu anaposhika moto, ulimwengu wote huja kumtazama akiungua.
Nyota na Vizuizi
Wanaume wawili gerezani walifungiwa katika kijumba kilichokuwa na dirisha moja ndogo tu ambalo
lilikuwa juu sana. Mfungwa mmoja ambaye alikuwa ameshushwa moyo sana, alilitazama lile dirisha na
kuona vizuizi vya chuma, na kuwaza tu jinsi alivyozuiliwa. Aliona vizuizi hivyo ambavyo vilimfanya kuwa
na uchungu mwingi na kupoteza tumaini. Bali mfungwa yule mwingine alitazama dirisha lile usiku na
kuona nyota, mbali na vizuizi, na kusema, “angalia umaridadi wa nyota zile!” Kwa kuona nyota, mbali na
kuona vizuizi, aliona matumaini na maono kwa siku za usoni. Nyota na vizuizi ni sawa na vile
unavyotazama maisha. Watu wengine huona bilauri la maji likiwa nusu tupu, hali wengine huona kama
limejaa nusu. Unavyotafakari mambo ni muhimu sana. Watu wengine huwa na matarajio mema, hali
wengine hutarajia kinyume. Wengine huona zaidi ya vizuizi na kuona yanayowezekana. Mungu anataka
tuone nyota.
Katika maandiko, Mungu anatuhimiza tuwe watu wa maono ambao wana uwezo wa kuona vitu
vinavyowezekana. Katika Mithali 29:28 tunasoma kwamba “pasipo maono, watu huangamia.” Nabii
Yoeli katika unabii wake kuhusu siku za mwisho alisema, “Hata itakuwa baada ya hayo, asema Bwana, ya
kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu waume kwa wake, watatabiri,
wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono.”
Nguvu iliyoko katika Maono
Hatustahili kamwe kupuuza nguvu ziliyoko katika maono. Waume na wake wenye maono hubadilisha
dunia. Hebu jiulize sasa, “ono nililopewa na Mungu ni lipi? Je, nimenyakuliwa sasa na nguvu iliyoko
katika hilo ono?” Kama bado, basi wewe unaona tu vizuizi! Unaishi bila kutambua uwezo na mwito wako,
na hivyo basi huishi unavyostahili kuwa.
Maana Hasa Ya Maono ni Nini?
Maono ni kuona mbele, ukilinganisha na ya nyuma. Mtu mmoja alisema kwamba maono ni daraja
inayounganisha yaliyoko na yajayo. Tazama, Yoeli alisema kwamba vijana wana uwezo wa kuona maono,
na wazee wana uwezo wa kuota ndoto. Hii ina maana gani? Msingi wa ndoto ni matukio ya kale. Ni
kumbukumbu ya mambo ya kale. Lakini maono yanahusika na mambo yajayo. Ndoto yanahusu mambo
yalivyokuwa, hali maono yanahusu mambo yanavyoweza kuwa! Uzee na ujana ni maneno yanayohusiana.
Kuna vijana ambao huona tu vizuizi, na mawazo yao yako katika shida wanayoyaona tu. Ni waume wenye
ndoto. Wanafikiri kizee, wakizingatia tu yaliyopita. Mwenye maono hufikiri mambo yanayowezekana.
Kiongozi Mkristo mwenye maono huona nyota, na kuamini kwamba yeye, akiwa na Mungu, ana nguvu za
kusababisha mabadiliko. Maono itokayo kwa Mungu huleta mabadiliko. Maono hayo huona mafanikio
katika siku za baadaye.
Kusudi La Maono ni Nini?
Kiongozi huendeleza shughuli zake za kila siku akiwa na azimio ya matarajio hatimaye. Maono yake
humpa mwelekeo na jukumu katika siku yake. Kusudi la kuwa na maono ni kuweka mwelekeo wa Mungu
maishani mwako.
• Maono itokayo kwa Mungu hutoa mwelekeo kwa mtu.
• Maono itokayo kwa Mungu hutoa mwelekeo kwa jamii.
• Maono itokayo kwa Mungu hutoa mwelekeo kwa jiji.
• Maono itokayo kwa Mungu hutoa mwelekeo kwa Nchi.
• Maono itokayo kwa Mungu hutoa mwelekeo kwa ulimwengu.
142
Kumbuka kwamba watu wengi hawana mawazo ya jinsi wangependa siku zao za hatima kuwa. Wengi
wanaona tu wakati ulliyopo na vikwazo vyake. Katika kampuni yeyote, lazima kuwe na viongozi na
wasimamizi. Tofauto kati yao i wapi? Ni kama hadithi ya kikundi cha wavumbuzi waliokuwa wakijaribu
kutengeneza njia vichakani. Msimamizi alikusanya kikundi chake, akawapa visu, misumeno, na shoka za
kukata njia katika kichaka hiki kilichokuwa nzito sana. Msimamizi aliona tu vichaka vilivyozuia njia na
kuvikatilia mbali. Kiongozi alisimamisha watu, akapanda mti na kupeleleza hali ilivyo. Akiwa juu ya mti,
alipaaza sauti na kusema , “Komeni hapo! Tumepotea njia! Tunaelekea upande usiofaa.” Huyo ndiye
kiongozi. Anajali mwelekeo na hatima kwa siku za baadaye.
Mungu ametumia wanaume kwa wanawake kuongoza watu wake kutoka katika misitu. Musa, Nehemia,
Esta na Paulo walikuwa viongozi wenye maono. Waliweka mwelekeo na kuhakikisha kwamba wanafuata
maono ya Mungu kwa maisha yao katika siku za baadaye.
Mipaka
Ono unalopewa na Mungu haliwezi kukupatia mwelekeo tu, bali litaweka mipaka pia katika maisha yako.
Kuwa na ono hukufanya kuwa makini katika uzingatifu wako na kufanya tu yale yaliyo muhimu. Uongozi
ni ngumu ikiwa unadhani kwamba ni lazima ufanye kila kitu. Acha wasimamizi wazingatie hayo. Ni mwito
wao, wala si wako. Ono lako litapunguza wakati wako, mapenzi ya moyo wako, na yale unayotafuta.
Mwenye ono hutekwa nyara na ono lake. Ametwaliwa na malengo aliyopewa na Mungu. Yesu alikuwa
hivyo. Mara nyingi mwito wake ulimsababisha kusema, ”lazima niende…” au, ‘mwana wa adamu
lazima…” Mwito wake ulimfikisha msalabani, na hata sasa anazidi kuushinda ulimwengu kupitia kwa
uaminifu wake kwa maono yake.
Maono yako hupunguza chaguo lako. Mambo ya siku za hatima zimo moyoni mwa kiongozi, na anaweza
kuyaona kwa imani. Labda hajui jinsi ya kufika huko, lakini atafuata tu yale yanayomwelekeza huko.
• Mwenye maono ana nidhamu
• Mweny maono huonekana kuwa asiyefahamu mambo mengi
• Mwenye maono amejitolea mhanga
• Mwenye maono ni mzingatiifu
Miliki Ono Lako
Ono lake haliwezi kuwa langu, au kama langu. Ni wewe tu unayeweza kufanya kile Mungu amekuita
kufanya. Kazi yake ndani yako na kupitia kwako ni ono aliyo nayo juu yako. Lazima uione, uiamini na
kuimiliki kama yako. Kumbatia ono lako kama kipawa chako maalumu kutoka kwa Mungu. Yu tayari
kushiriki nawe kusudi lake. Si wazo hilo ni la ajabu?. Mungu Mkuu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo anataka
kutimiza nia yake na kusudi lake kwa kukuita! Ajabu sana! Shetani atajaribu, na dunia pia itajaribu
kukuvunja moyo ili usitekeleze maono yako. Hata marafiki na jamii watajaribu kukuzuia. Kila kiongozi
katika Bibilia alipata pingamizi sawa na yako. Walilazimika kueleza maono yao kwa wale ambao
hawakuelewa. Paulo kila mara alitetea kazi yake ya utume kwa Wayunani. Wengi hawakumkubali, na
wakatafuta jinsi ya kumpinga na kumzuia. Paulo alilazimika kumiliki mwito wake alipoenda kwa wale
waliompinga. Kuwa kiongozi kunaweza kuleta upweke na hali ya kukosa watu karibu.
Kutimizwa kwa Ono
Zingatia ono lako. Labda ulimwengu utakosa kuelewa ono lako, lakini unauhitaji. Mwandishi Allen
Richardson anasema kwamba neno “ono” katika Mithali 28:18, ni “tangazo la mapenzi ya Mungu kwa
jamii, ambayo ikikosekana, basi ustaraabu huwezi kupatikana.”
Kufa Kwa Ono
Miaka kadhaa zilizopita, Bill Gothard alizoea kuzungumza juu ya “kufa kwa ono.” Alieleza jinsi wanaume
kwa wanawake walioteouliwa na Mungu walivyopitia kipindi kigumu cha giza walipoona ugumu katika
kutimiza ono la Mungu, kama vile Eliya alivyojificha kichakani ili asionekane na malkia yule mkatili,
Yezebeli. Eliya alikuwa na woga mwingi ingawa Mungu alimwonyesha uwezo wake akiwa katika mlima
143
unaoitwa Karmeli. Alikuwa amepoteza imani kwamba Mungu angefanya alivyosema. Kila kiongozi
hufikia kukata tamaa nyakati zingine. Anakufa katika ono. Jambo hili ni muhimu sana katika imani. Ulicho
nacho ni hakikisho la ono hilo tu. Unajiuliza hivi: Je limetoka kwa Mungu? Ama nimekosea? Kile kiongozi
anapaswa kufanya ni kumwamini Mungu na kuamini hisia zake. Wakati fulani aliye na ono anapoona giza,
na kuzingatia imani yake kwa Mungu, basi Mungu atampa nguvu katika ono lake. Nyakati zingine Mungu
hukujaribu ili kudhibitisha uamuzi wako. Mtume Paulo alipitia mambo kama hayo katika Wakorintho wa
pili, alipo nena juu ya “kuwa na hukumu ya kifo” rohoni mwake. Alikuwa amevunjika moyo kiasi cha
kutamani kufa, lakini alipata neema na utulivu ndani ya Kristo, ya kumwezesha kuendelea. Ni hivyo pia
kwa wengi wetu. Labda itakulazimu “kufa” katika tamaa yako ya ono. Hebu mpe aliyekupa mbele! Ilikuwa
yake kabla kufanyika kuwa yako. Ukifanya hivyo, basi atatia nguvu tena katika ono hilo.
Nguvu Katika Ono
Tunaweza kusema Mungu atatia maono yako nguvu ikiwa atatukuzwa katika hilo ono. Hawezi kutia nguvu
mwili wako, au ratiba yako mwenyewe. Vipawa vyako na mwito wako ni kazi yake. Vivyo hivyo nguvu za
kutekeleza on zatokana naye. Mtu wa Mungu anapowaka moto, ulimwengu wote hukusanyika kuona
anavyoungua. Kupitia kwa kunyenyekea na kumtegemea katika imani, inatubidi kumwomba Baba aweke
nguvu katika ono aliyoweka ndani yetu tukikumbuka kwamba, “si kwa uwezo, au kwa nguvu, bali kwa
Roho Yangu, asema Bwana”
Kutiwa nguvu kwa ono ni kuweza kufanya yale ambayo yanaonekana kutowezekana kibinadamu.
“Kisichowezekani kwa mwanadamu,yanawezekana kwa Mungu.” Kiongozi mwenye ono huona suluhisho
kwa imani, na kutatua matatizo. Yeye huona nyota, wala si vizuizi. Mwenye ono anaona jinsi Mungu
anavyoona, chini ya uangalizi wa Mungu. Mithali inasema kwamba “Mwenye ufahamu
atauvumbua,”(Mithali 25:5). Anaona mambo yasiyoonekana kwa macho ya kibinadamu, na kuona jawabu
ya Mungu katika tatizo.
Mungu anamwonyesha kisicho cha kawaida kwa macho ya kawaida. Anaona suluhisho la Mungu kwa
tatizo.
Mungu anapotia Nguvu
Kusudi la Mungu katika kutia nguvu maono ni kukutia moyo, kama kiongozi. Kuna nyakati ambazo utahisi
kutokuwa na uwezo na tumaini. Roho Mtakatifu atakutia nguvu. Ana imani kwako. Tukiwa kama Musa
aliyegoteza maneno alipoona maono ya kichaka kilichookuwa kikiungua, akipaaza sauti kwa kusema:
“mimi ni nani hata niende kwa Farao?” Mungu atakutia nguvu na ujasiri wake. Mungu hutegemeza kile
ambacho ameanzisha. Hawezi kukuuliza kufanya kitu ambacho hayuko tayari kukupa uwezo wa kufanya.
Ono lako Ni Lipi?
Mungu anakuita utekeleze wajibu gani? Je, unasikiliza, au vipi? Unaona nyota, ama unaona tu vizuizi?
Kama huna ono, basi watu wataangamia, na kupoteza nafasi ya kuona mkono mkuu wa ajabu wa Mungu
juu ya maisha yako.
Kiongozi wa kweli atasujudu, atajitolea kwake na kuendelea kuona uwezo unayotokana na Mungu. Tamani
kuwa mtu ambaye Mungu ataita na kutumia. “Niko hapa Bwana, Nitume”
144
145
KUTIMIZA ONO LAKO
Mtu yeyote anaweza kuketi na kuota ndoto. Lakini itahitaji jitihada, nidhamu, na kujitolea ili kutekeleza
ndoto hiyo.
Bila kuwa na ratiba na lengo hatuwezi kufanya jambo lolote. Kufanikiwa ni kutambua kwamba unalotaka
kufanya lina maana na lenye kuzingatiwa. Kuwa na lengo ni kuona mambo unayothamini sana. Mpangilio
ulio bora utatuwezesha kutimiza malengo yetu.
Mbona Tuwe Na Malengo?
Mtu asiye na ono ni kama meli bila nahodha. Meli hiyo inaweza kuwa imeundwa kwa jinsi ya ajabu, hata
kuwa na vitu vya thamani sana, lakini bila nahodha, haiwezi kuelekea popote. Inaweza hata kugonga
mwamba. Anayelenga hewa kwa hakika atagonga hewa. Itakubidi kuwa na malengo ikiwa utafanikiwa
katika maono yako. Mafanikio yoyote hupatikana tu kwa kuwa na mpangilio na mwelekeo. Kuweka
malengo ndio chanzo cha kuwa na matokeo yenye mafanikio.
Jinsi Ya Kuweka Malengo
Malengo lazima yawe:
• Yanayoweza kutimizwa = Inastahili bidii yako, hata kama utachoka.
• Inayoaminika = Moyo wako unakuambia kwamba unaweza kufanya hivyo. Ukiamini kwamba
huwezi, basi hutaweza!
• Inayoweza kupimika = Unaweza kuona mwisho wake. Unaweza kuupima.
• Ina mwisho = Itakubidi kuweka wakati wa kumaliza lengo hilo.
Aina Tatu za Malengo
Tunahitaji kuwa na malengo haya matatu ikiwa tutatimiza maono yetu:
• Malengo ya masafa mafupi
• Malengo ya masafa ya kadiri
• Malengo ya masafa marefu
Kwa mafano: una maono ya kuwa shujaa katika maandiko, kama mtu fulani unayemheshimu. Je, utawezaje
kuwa hivyo? Utajifunza kwamba kujifundisha kukariri vifungu ni mojawapo ya jinsi ya kutekeleza lengo
lako. Basi utaanza kujifunza kuweka maandiko katika moyo wako kama nidhamu katika kutembea na
Mungu. Je, utaanza vipi?
Uwe Na Mbinu
Kuweka jambo lolote katika moyo huchukua muda, juhudi, na kurudiarudia kwa wingi. Kwa hivyo,
unahitaji kuwa na mbinu. Hebu tutumie mbinu inayotoka kwa The Navigators, inayoitwa, The Topical
Memory System. Hebu tuweke huo mbinu katika malengo yanayoweza kutimizwa.
Gurudumu = vifungu 12 malengo ya masafa mafupi = kifungu kimoja kila juma.
Malengo ya masafa ya kadiri = vifungu 12 kwa majuma 12
Malengo ya masafa marefu = Kukariri vifungu hivi kumi na mbili kila juma na kuongeza kifungu kingine
kipya kila juma, na kuuongeza katika vifungu ulivyokariri hadi uwe na jumla ya vifungu 52 kwa mwaka.
Huo ndio mpangilio wa Topical kwa mwaka mzima.
146
Tekeleza Azimio Lako
Unaweza kumla ndovu kwa vipande vipande. Ili uweze kutimiza ono lako, utahitaji kuwa na lengo na
nidhamu. Ikiwa unahitaji kuwa shupavu katika maandiko, basi itakubidi kufanya hivyo siku baada ya siku.
Uwe dhabiti na mwaminifu katika kukariri. Itakuchokesha kurudiarudia maandiko kila siku. Lakini
usikate tamaa. Punde si punde neno la Mungu litapenya moyoni mwako, na hatimaye rohoni mwako. Kila
siku itakubidi uongeze muda wa kusoma, kuchunguza na kutafakari uliyosoma katika neno la Mungu.
Walio shupavu katika neno la Mungu hawakufuata njia ya mikato. Waliwajibika kugharimika kwa miaka
mingi. Siku nyingi, na masaa mengi yatatumika “Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije
nikakutenda dhambi” (Zaburi 119:11). Kutenga wakati wa faragha na Mungu katika kusoma Bibilia yako
na kuandika yale unayosoma kutakuwezesha kuwa mtu wa Mungu halisi.
Katika ono lako, bila kujali ono hilo ni lip, unahitaji kuweka malengo ili uweze kulitimiza. Utanufaika kwa
kuweka malengo.
• Malengo ya masafa mafupi yanaweza kuwa ya juma moja, mwezi moja, au hata miezi miwili.
• Malengo ya masafa ya kadiri yanaweza kuwa ya kuanzia siku tisini hadi miezi sita.
• Malengo ya masafa marefu ni yale ya mwaka moja hadi maisha yako yote.
Lengo La Maisha
Utakapofika ukingoni mwa maisha yako na kuangalia nyuma, Je utaona mafanikio? Rafiki yangu mmoja
alisema hivi: “unapofika kule unakoelekea, je utafurahishwa na kule ulipo?” Swali hili lina maana sana. Ili
ufurahie kuwa utakakokuwa, unalazimika kuwa na LENGO LA MAISHA ili uwweze kudumisha
mwenendo. Yesu alikuwa na lengo la maisha yake. Alisema, “sababu nafanya siku zote yale
yampendezayo,”na “nimeimaliza kazi ile uliyonipa nifanye” (Yohana 8:29, 17:4).
Miaka mingi iliyopita niliazimia kuwa na haya kama lengo la maisha yangu:
“Kumjua, kumpenda, na kumtukuza Mungu; na kutumika katika kukuza wafanyikazi walio na
ujuzi kwa wingi ili kutimiza Agizo Kuu la Yesu katika maisha yangu.”
Kuandika hilo azimio katika Bibilia yangu, kitabu changu, na katika moyo wangu kulinifanya kuuzingatia
katika miaka hii yote. Itakuwa bora ikiwa yeyote ambaye angependa kuongoza wa roho kuwa na azimio la
maisha yake ambalo lina mwongozo wa Mungu.
147
TUMEZALIWA ILI TUZAE
Mwanzilishi wa The Navigators, kwa jina Dawson Trotman, wakati moja aliandika kijitabu alichokiita
Born To Reproduce. Nilisoma kijitabu hicho mnamo mwaka wa 1960. Mwandishi huyo anazingatia
kwamba tumkeokolewa ili tufanye wengine kuwa wafuasi wa Kristo. Alafu tufuate agizo kuu la Kristo la
“kwenda kufanya watu kuwa wanafunzi.” (Mathayo 28:19,20). Itakuwa makosa makubwa tukifikiri
kwamba Kristo alitoa agizo hilo bila mpango. Je ingewezekanaje kwa wafuasi wachache kufanya mataifa
kote ulimwenguni kuwa wanafunzi?
Kuna wale wanaothani kwamba agizo kuu ni mpango wenyewe. Lakini agizo hili lina mbinu ambayo
Kristo amekusudia kutumia kuushinda ulimwengu. Hebu angalia agizo hili kwa makini:
• Enendeni = mwito wa kushuhudia na kueneza injili
• Mkawafanye kuwa wanafunzi = mwito wa kuwandaa waamini
• Mimi nipo pamoja nanyi siku zote = ahadi ya nguvu zake
• Kuwafundisha = mwito wa kujizalisha kwa wote tuliyowaandaa
Kusema kweli, muda wote ambao Kristo alikuwa pamoja na wanafunzi wake aliutumia kwa kuwatayarisha
kwenda kueleza ulimwengu habari njema katika jina lake. Alikuwa akiwasajili katika shule ya ufuasi.
Kitabu kimoja chenye maana kilichoandikwa na Robert Coleman, The Master Plan Of Evangelism,
kinatuonyesha wazi wazi kwamba Kristo alikuwa na mpango na makusudi kwa yote aliyofanya na wafuasi
wake kumi na wawili. Kitabu hicho cha Coleman, kwa ufupi kinaonyesha mbinu ambayo Yesu alitumia,
ambayo ni:
• Uteuzi
• Kuchangamana
• Kufanywa wakfu
• Kuongezeka
Uteuzi
Mbinu ya kwanza ambayo Yesu alitumia lilikuwa kuchagua watu waliofaa. Je, umegundua kwamba Yesu
alikuwa na ubaguzi katika kuchagua wanafunzi wake “kumi na wawili?” Hakuita watu wote, ama mtu
yeyote tu. Alichagua watu wachache. Hawakuwa watu wa maana katika ulimwengu, lakini aliwachagua
wamfuate. Walikuwa watu “wanono” (fat – faithful, available, and teachable). Kristo alikuwa na mpango
katika kuchagua wanafunzi hao kumi na wawili. Hawakuwa watu timilifu, au walio na uwezo maalumu.
Yesu aligundua uwezo uliokuwa ndani yao, alafu akajenga makusudi yake ndani yao.
Ingawa hivyo, tunastahili “kwenda” na kushuhudia wote watakaosikiliza. Tubatize atakayeamini. Kisha
tumfanye kuwa mfuasi. Tunaweza kujifunza kutoka kwa Kristo. Hata hakuweza kufanya Yudasi kuwa
mfuasi mwaminifu. Ili mpango huu ufanikiwe itakulazimu kuchagua watu watakaokufuata na kujifunza
kutoka kwako. Mchungaji anaweza kuongoza kanisa, lakini hawezi kufanya wote kuwa wafuasi. Anaweza
kufuata mfano wa Yesu kwa kuchagua watu wawili au watatu, akiwa katika maombi.
Kujumuika
Taratibu yake ya pili ilikuwa chimbuko la “kuwa naye.” Mtu moja kwa jina Coleman aliandika zaidi
kuhusu mbinu hiyo. Alisema kwamba Kristo alikuwa na nia ya kuwa na wanafunzi wake karibu naye kwa
miaka mitatu. Hata kama wangalisahau walikokwenda, ama waliokutana nao, wangalimkumbuka daima!
Kujumuika na Kristo kungebadilisha watu hao milele. Agizo la “nifuate” lilikuwa mpango makusudi ya
Kristo kuwa kielelezo kwa wafuasi hao kumi na wawili. Walielewa na kushika kadiri walivyofundishwa.
148
Kuwa na Yesu kila siku kuliwavutia. Hatimaye walimfia Kristo. Kristo alielewa chimbuko la “kuwa naye”
kama la kufaa katika uongozi.
Nasi pia tunahitaji kuiga hila hiyo ya “kuwa nami.” Mtu hawezi kuiga mtindo wako wa maisha isipokuwa
tu kwa kuwa nawe sana. Jinsi inavyofaa katika kulea watoto, ndivyo inavyofaa katika kulea wafuasi wa
kiroho. Wazazi wanavyopata muda wa kutosha wa kukaa na mtoto wao, ndivyo wanavyomwezesha mtoto
kutowasahau milele katika maisha yake. Ufuasi “unashikwa” “unavyofundishwa.” Ilisemekana kwamba
wafuasi wa kwanza “walitambulika kwamba walikuwa na Yesu.” Anayehitaji kuwa kiongozi ni lazima awe
na muda wa kuwa na wanafunzi wake vile Kristo alivyokuwa na muda na wanafunzi wake. Ili kuzaa
kiroho, ni lazima atambue kwamba itamgharimu muda na kazi nyingi iliyo na uchungu.
Kufanywa wakfu
Azimio la Yesu lilihusu mwito wake kwa wale aliochagua “kutafuta kwanza ufalme”. Mambo ya muhimu
yana maana sana kwa mfuasi. Katika Luka 14 Yesu anatoa mifano yanayohusu kugharamika. Mara tatu,
Yesu alisema, “huwezi kuwa mwanafunzi wangu” isipokuwa unipende kuliko watu, mahali, au vitu.
Mpango wake unahitaji watu watakatifu, wenye nidhamu katika kutembea naye. Kwa miaka mitatu
walisafiri naye na akawaonyesha kujitolea kwake kwa ufalme wa Mungu. Aliwahimiza kuiga mfano wake.
wake.
Tunawajibika kuishi maisha yaliyowekwa wakfu ikiwa tutaongoza wengine. Ni vigumu kuongoza mtu kwa
mambo ya roho ikiwa hujawahi kupitia unapomwelekeza kupita. Huwezi kuongoza wengine kuogelea,
kama hujui kuogelea. Unaweza tu kumwongoza mtu mwingine kuwa karibu na Mungu ikiwa wewe pia u
karibu na Mungu. Kwa jinsi gani? Mtu atagundua ukweli wako atakapoendelea kuwa nawe.
Unapomwambia aombe, naye hakuoni wala kukusikia ukiomba, basi hawezi kuona umuhimu katika
maombi. je, unadhani kuwa wale wanafunzi kumi na wawili waliweza kusahau nyakati za maombi pamoja
na Yesu? Hasha! Walikuwa na shauku, na kutamani kumjua Mungu jinsi walivyomwona Yesu akiomba
kwa Baba yake. Kufanya wengine kuwa wanafunzi ni kuwa mwanafunzi kwanza. Kisha uwaambie
wengine kuwa wanafunzi.
Mbinu katika kuongezeka
Kuona kwa Kristo ufalme wa Mungu ndani ya wavuvi, watoza ushuru, waziloti na watu wengine wa
kawaida kunastajabisha sana. Aliona ulimwengu ukibadilishwa kutokana na shuhuda zao. Watu wengine
hawangeona uwezekano huo. Ingawa hakuna hata moja wa watu hao aliyewahi kusafiri zaidi ya maili mia
moja kutoka kwao, Yesu aliwaagiza kuambia “mataifa yote” juu yake! Alikuwa na ratiba ambayo ilihusu
mtu kuleta mtu mwingine kwake. Hii ni mbinu inayohusiana na kuongezeka kiroho.
Je, hii inawezekanaje? Ni rahisi sana. Watu wachache wameijaribu kwa kweli. Ni hivi: mtu anaweza
kumwongoza mtu mwingine kwa Yesu; kisha akamfundisha kwa mwaka moja jinsi ya kuleta mwingine
kwa Yesu. Wakati huo pia anaweza kuongoza mtu mwingine kwa Yesu. Yule aliyefundishwa naye
anamwongoza mtu wake wa kwanza kwa Kristo. Katika kipindi cha mwaka moja watakuwa watu wanne
peke yao.
Taratibu hii yaonekana kutofaa katika kuuleta ulimwengu kwa Yesu. Si wachungaji wengi wanaoweza
kujenga kanisa jinsi hiyo. Unaweza kudhani ulimwengu huwezi kufikiwa jinsi hiyo.
Hebu fikiri tena. Katika mwaka wa pili, kutakuwa na wafuasi wanane, kwa sababu kila moja atakuwa
amemlata mfuasi mwingine na kumfundisha kwa mwaka moja. Katika miaka kumi ijayo kutakuwa na
wafuasi 1,024 wanaotumia mbinu iyo hiyo. Itimiapo miaka ishirini, kutakuwa na wafuasi 1,048,576 wa
Yesu. Hii si mbaya sana. Ama vipi? Kila moja wao akileta moja na kumfundisha, basi kwa miaka thelathini
tu kutakuwa na wafuasi 1,073,741,824! Katika kizazi kimoja, kwa miaka arobaini, kutakuwa na wafuasi
bilioni moja ambao watakuwa wameokoka. Hebu fikiri tena hii ratiba ya Bwana kwa sekunde moja.
Ukifikiria idadi hii, kanisa limekuwa na muda wa kutosha tangu Kristo atuachie ratiba hii ya kuleta
ulimwengu kwake mara mia moja zaidi! Katika kizazi cha kwanza tu, kanisa lingetimiza agizo kuu la Yesu
kupitia kwa wanafunzi wake kumi na wawili peke yao. Ratiba hii si mbaya. Watu waaminifu ndio
hawajaijaribu bado.
149
Tunaelewa kwamba kuna matatizo yanayoambatana na ratiba hii ya kuongezeka kiroho. Ni vigumu kwa
wote unaowafundisha kuwa waaminifu katika kuleta wengine kwa Kristo kila mwaka, hata ingawa
wanastahili kufanya hivyo. Je, ni vigumu? Hasha! Mtume Paulo aliongeza maisha yake kwa Timotheo,
Luka, Tito, na Trofimo. Yeye, kama mwinjilisti, alivuta watu wengi kwa Yesu. Lakini alileta halaiki ya
watu kwa Yesu kupitia kwa wale aliofundisha. Aliwaambia waumini wa Thesalonike “Nanyi mkawa
wafuasi wetu na wa Bwana… hata mkawa kielelezo kwa watu wote waaminio… maana kutoka kwenu, neno
la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa
Mungu imeenea” (Thesalonike 1:6-8).
Hebu tufafanue kwamba ni vyema tuelewe ratiba ya Yesu ya kukaribisha ufalme. Hatukuitwa ili tuongoze
watu kuwa Wakristo, kuwabatiza na kuwaorodhesha kuwa washiriki wa kanisa, halafu tuwasahau.
Tunahitaji kuwafanya wanafunzi. Mtu moja kwa jina Dawson Trotman alieleza vyema aliposema,
“Shughuli haiwezi kuchukua nafasi ya kuongezeka, na kuongezeka haiwezi kuchukua nafasi ya shughuli.”
Kristo ametoa mwito ‘tuwafanye wafuasi na kuwafundisha.’ Tumezaliwa ili tujizalishe kwa wengine.
Tufuate mfano wa Yesu aliyejizalisha kwa wale aliowachagua.
Je, Unafanya Nini?
Je, umejitolea kufuata ratiba ya Yesu? Kama sivyo, basi, unatumia uwezo wako vibaya. Wakati utafika
ambapo utachunguza maisha yako kama umetenda kitu cha maana katika ulimwengu huu. Yesu alisema
tuombe “kwamba tuzae matunda ya kudumu” (Yohana15). Yeye mwenyewe aliombea “matunda” ya
wafuasi wake alipoombea watakaoamini kupitia kwa ushuhuda wao (Tazama Yohana 17:20). Yesu, kwa
hakika, alikuwa akiomba kwamba wanafunzi wake wawe watu wa kufanya wengine kuwa wafuasi!
Nilipokuwa kijana mdogo, kiongozi mmoja aliyekomaa kiroho alinitia changamoto. Nilimwona kwenye
kongamano na kumsalimu nikisema “waendelea vipi?” Naye akanijibu hivi, “sitakuuliza unavyoendelea,
lakini wengine wanaendelea vipi kwa sababu ya yale umekuwa ukiyafanya?” Nilipigwa na butwaa.
Maneno yake yalipenya katika moyo wangu. Maneno yake yamekaa nami kaatika miaka ambayo
nimemtumikia Yesu. Tunastahili kuishi maisha kama hayo tukiwa wafuasi wa Kristo. “Wengine
wanaendelea vipi kwa sababu ya vile umekuwa ukifanya?” Hilo ni swali la Bwana wetu kwa yeyote aliye
mfuasi wa kweli. Je, unazaa matunda yatakayodumu? Je, unaweza kuelekeza kidole chako kwa Timotheo
na kusema, “Hii ni juhudi yangu ya kusaidia kutekeleza agizo kuu katika uhai wangu? Hawa wanaume na
wanawake ni kazi ya maisha yangu.”
Niko Pamoja Nanyi Daima
Hatimaye nenda katika jina lake kama umejazwa na Roho Mtakatifu na upako wa nguvu zake. Yesu
anafurahishwa tunapojaribu kutimiza ratiba yake. Atatutangulia, na kuongea kupitia kwetu. Una ahadi ya
baraka hiyo. “Basi enendeni, mkafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, na kuwafundisha kuyashika yote
niliyowaamuru minyi, na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari”
150
151
TARATIBU ZA MKUFUNZI
Ni vyema mara nyingi kueleza wazi wazi tunachomaanisha na kuwafanya watu kuwa wanafunzi. Maneno
ya mwisho ya Yesu kwa wafuasi wake yalikuwa “enendeni mkawafanye wanafunzi.” Basi hebu tujiulize,
“kufanya wanafunzi” hasa inamaanisha nini? Wengine hudhani kuwa ni uinjilisti, yaani kuleta watu kwa
Yesu. Lakini hayo ni maneno ya Yesu ya “enendeni.” Inatubidi:
· Kwenda
· Kubatiza
· Kufanya wanafunzi
Je, kufundisha shule ya jumapili ni kufanya wanafunzi? Je, kuhubiri jumapili ni kufanya wanafunzi? Hayo
yote ni ya maana, lakini hayana maana sawa na yale Yesu alikusudia. Kufundisha na kuhubiri hayana
maana katika kufanya wanafunzi.
Njia ambayo Bwana alitumia
Hebu fikiri jinsi hii. Yesu aliwaita watu wachache kuwa wanafunzi wake. Aliwafanya vipi kuwa
alichotaka? Alikuwa na njia yakufanya hivyo. F.F Bruce, katika kitabu chake kizuri kinachoitwa The
Training of the Twelve, anatuonyesha jinsi Yesu alivyofanya watu wasiokuwa wa maana kuwa wanafunzi
wake. Robert Coleman pia katika kitabi chake kiitwacho The Master’s plan of Evangelism, ametuonyesha
njia ambayo Yesu alitumia. Kiini cha kufanya wanafunzi kinapatikana katika neno “kufundisha.” Yesu
alifundisha wanafunzi wake kuendeleza huduma, hata kama hayuko. Hebu tuangalie jinsi
alivyowafundisha.
Mafundisho ya Yesu
Kuna tofauti kati ya mafundisho na kufundisha. Kufundisha imo katika mafundisho. Lakini yawezekana
mafundisho yasiwe katika kufundisha. Kumpa mtu mafunzo ni kuwa na madhumuni na ratiba. Yesu bila
shaka alikuwa na madhumuni na ratiba kwa wanafunzi wake kumi na wawili. Alikaa nao ili awape
mafundisho. Hivi vipengele vitano vinatumika sana na mkufunzi katika kuwafanya waamini wapya kuwa
wanafunzi:
Mwambie jinsi
Mwambie jinsi ya kuomba, kushuhudia, kusimulia alivyookoka, kusoma Bibilia, na kutia maandiko katika
akili na moyo. Hii ni sehemu ya kufundisha katika mafundisho.
Mwonyeshe Jinsi
Waalimu wengi na wahubiri wengi wanashindwa kufikia hapa. Wanafundisha na kuhubiri tu, alafu
wanasema “nenda ukafanye.” Mkufunzi mwema ni yule aigaye mfano wa Yesu kwa kuonyesha jinsi ya
152
kufanya. Wanafunzi wake walimuuliza hivi: “Bwana, tufundishe kuomba.” Akawafundisha mfano wa
maombi (Luka 11), na Kuwaonyesha namna ya kuomba. Kwa miaka mitatu walimsikiliza akiomba kila
mara. Aliwaonyesha namna ya kuomba!
Mwonyeshe Pa Kuanza
Mkufunzi ni mtu wa vitendo. Kuonyesha ni bora kuliko kunena tu. Kwa mfano: Naweza kukufundisha na
kukuonyesha jinsi ya kushuhudia. Lakini huwezi hadi utakaponitazama nikishuhudia kila mara. Hayo ni
mafundisho.
Mpe Moyo
Hapa ndipo pana ugumu. Kiongozi ni lazima awe na uvumilivu kama wa Ayubu. Wanafunzi wasio komaa
kiroho huvutwa na mambo mengine na kushushwa moyo. Wanahitaji kutiwa moyo. Paulo aliwaambia
Wathesalonike kwamba “tulikuwa wapole katikati yemu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake
mwenyewe” (1 Wathesalonike 2:7). Hiyo ndiyo kazi ya mkufunzi. Aliye mchanga kiroho hawezi kundelea
kutia maandiko akilini, kuwa na ibaada ya faragha, ama kusoma Bibilia. Shetani anafanya kazi yake. Lakini
upo kwa sababu ya huyo aliyemchanga kwa mambo ya roho. Wewe ndiye kiongozi wake. Msaidie kuwa na
tabia, taratibu, na uaminifu. Usimwache hadi atimize hayo.
Mfundishe kujizalisha kwa Wengine
Sehemu hii inaonyesha kupevuka kwa mwanafunzi wako. Mwonyeshe haja ya kuwa mkufunzi wa mtu
mwingine jinsi ulivyokuwa mkufunzi wake. Asibanduke, ila adumishe tu mtindo huo. Furaha ya mkufunzi
ni kuona uaminifu wa mwanafunzi wake katika kufundisha wengine. Kwa hivyo mfundishe kufundisha
wengine. Hiyo ni baraka!
Najua umetambua kwamba kufanya wanafunzi si kazi rahisi. Hii imesababisha watu wachache sana
kufaulu. Wanaotumia muda wao kwa watu wengine watapata tuzo la ajabu. Mungu alikusudia tutumie njia
hii ya kuongezeka katika kuleta ulimwengu kwa Yesu.
153
MTU MWAMINIFU NI NANI ?
2 Timotheo 2:2 “Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi, hayo uwakabidhi watu
waaminifu watakaofaulu kuwafundisha na wengine.”
Ni ajabu kuona ratiba ambayo Paulo alitumia kufanya wanafunzi kwa vizazi vinne vya wanafunzi:
· Paulo kwa Timotheo
· Timothio kwa watu waaminifu
· Watu waaminifu kwa wengine pia
Mpango wa Mungu wa kufikia ulimwengu una daraja mbalimbali za uongozi kanisani.
Mwongofu
Huyu ni mtoto mchanga katika Kristo (2 Peter 2:2). Anahitaji kuonyeshwa namna ya kujilisha, kama vile
kuwa na ibaada ya faragha, kusoma maandiko, kuomba, kushirikiana na Wakristo wengine, na kutii.
Mwanafunzi
Huyu ni mtu anayekua ambaye anajifunza kutembea na Kristo (tazama Luka 14:25-35). Anaelewa kidogo
jinsi ya kuishi akimtii Kristo. Lakini anahitaji kutiwa moyo na kupewa mwongozo ili aweze kutekeleza
maono yake ya kuishi maisha iliyo tofauti katika ulimwengu wake. Anahitaji kujifunza “kufanya
wanafunzi” katika maeneo yake , na uwezo wake.
Mkufunzi
Huyu ni mtu kama Timotheo. Amefikia kiwango cha uongozi katika mwelekeo wake na Kristo. Amezaliwa
ili azae. Yeye ni kama Paulo ambaye anakusanya waliowachanga kiroho, na wanafunzi walio ‘waaminifu.’
Mtu kama huyo ana agizo kuu la Yesu katika fikira zake, na anashurutisho la kutekeleza agizo hilo.
Kiongozi wa Wakufunzi
Ni wachache sana ambao wanafikia kiwango hiki katika upevu na maono yao. Paulo alikuwa moja
aliyefikia kiwango hiki. Kuna waongozi wa viongozi nyakati hizi ambao wana maono yatakayovuta
ulimwengu kwa Kristo.
Tafuta mtu mwaminifu
“Kwenda kufanya wanafunzi” kunatokana na kupata watu wanaofaa, ambao ni tayari kutumia muda wao na
juhudi zao ili kuwa viongozi. Hawa watu waaminifu ni akina nani? Paulo alimaanisha nini alipomwambia
Timotheo afundishe walio waaminifu? Kitabu cha Mithali kinatuuliza swali hili, “Wanadamu hutangaza
kila mtu hisani yake mwenyewe, bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata?” (Mithali 20:6).
154
Kwa hakika, dhana yangu ni kwamba Paulo alikuwa akimshawishi Timotheo atafute watu waliokuwa kama
yeye. Timotheo alikuwa mwaminifu kwa Paulo. Naona vipengele vitatu katika kutafuta mtu mwaminifu,
ama hata kwa kuwa mwaminifu:
Mtu moja alisema mtu mwaminifu ni mtu “mnono” (fat).
Mwaminifu F= (faithfull)
Wakupatikana A= (available)
Mwepesi wa kujifunza T= (teachable)
Hebu tuangalie tabia hizi.
I. Unayeweza kufundisha ni mtu MWAMINIFU
Mtu huyu amefikia kiwango cha kuhitaji mapenzi ya Mungu katika maisha yake, hata
akigharimika kwa vyovyote. Amejitoa, ana kusudi, na amejiweka wakfu. Moyo wake unatamani
Mungu. Ni mwaminifu kwa Mungu. Pia ni tayari kuwa mwaminifu kwako. Kila mtu hayuko tayari
kuwa mwaminifu kwako. Timotheo alimruhusu Paulo kuwa kielelezo chake. Dema, baada ya
kuupenda ulimwengu, alimwacha Paulo. Ni ajabu kwamba hata Paulo hangeweza kuwa
mwongozo kwa Dema. Yohana, ambaye jina lake la pili ni Marko, alimwacha Paulo na kumfuata
Petero. Hebu tafuta watu watakaokubaliana na mwongozo wako kiroho, na kujitolea kukufuata
kwa thati. Awe mtiifu kwako, maana wewe ndiwe mkufunzi wake. Ni mwaminifu kwako
unapomfuata Kristo.
1. Je atakufuata?
Kuwa mwaminifu hakumaanishi uaminifu wako ni kwa Kristo na ufalme wake tu. Wewe na
mfuasi wako mna uhusiano wa kiongozi na mfuasi wake. Anatamani na kuheshimu
matembezi yako na Mungu. Atakufuata kusudi ajifunze kutoka kwako.
2. Je, atakuwa radhi kupokea na kufuata tabia na mawazo ya kupokezana?
Msingi ulio bora katika kufanya mwanafunzi ni kuwa na ratiba ambayo ni mbinu yako katika
kumpa mawazo ya kupokezana. Nini maana ya kuwa na mawazo ya kupokezana? Ni
kufundisha mtu mwingine kutenda vile unavyotenda. Ni kumwonyesha jinsi inavyotendwa;
alafu mara kwa mara aone nidhamu uliyo nayo katika kutenda jambo hilo. Si vyema
kumwambia mwanafunzi wako kufanya kitu ambacho hufanyi. Ni lazima ashuhudie ukifanya
hivyo. Wewe ni kiongozi mtumishi kwake, namna Yesu alivyokuwa kiongozi mtumishi kwa
wanafunzi wake. Katika kufundisha mtu mwaminifu kuna “kushika” na kufundisha. Anahitaji
kutamani kufanya kama wewe na kuwa kama wewe.
Kwa mfano: ukifundisha mwanafunzi wako kutumia mfano ule wa gurudumu unaotumiwa na
The Navigators kama njia ya kutia maandiko akilini, basi itamlazimu kuona ukitumia mfano
huo na vifungu vyako vya Bibilia katika maisha yako. Akiwa tayari kujifunza vifungu vyote
kumi na mbili, basi itamaanisha kwamba yu mwaminifu. Iwapo atakataa kutumia mfano huo,
na kuweka akilini vifungu vya Bibilia aliochagua yeye mwenyewe, basi atakuwa
amedhihirisha kwamba hawezi kuwa mwanafunzi wako, hata kama ni mwaminifu kwa
Mungu. Si mwaminifu kwako.
3. Ana shauku, na utayari wa kujifunza kutoka kwako
Ni lazima apende neno la Mungu. Nabii Yeremia alisema, “Maneno yako yalionekana nami
nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu”
(Yeremiah 15:16).
Kuna msemo unaosema kwamba “unaweza kumwongoza farasi kwenda mtoni lakini huwezi
kumlazimisha kunywa maji.” Mkufunzi anapotafuta mtu aliye mwaminifu, ni vyema asitafute
tu mtu atakayetii, bali awe pia awe mwenye shauku kwa neno la Mungu. Lazima awe na njaa
155
ya neno la Mungu. Awe na utulivu kwa kutamani kujifunza na kukua. Atakuruhusu umlishe
kutoka kwa bakuli yako.
II. Unayeweza kufundisha awe mtu wa KUPATIKANA
Mtu huyu ana moyo wa utumishi. Anaweza kuwa kiongozi mtumishi. Yesu hakupima watu
kulingana na watumishi wao, bali kwa idadi ya watu waliotumikia. Mtu wako mwaminifu ni
lazima awe radhi kufuata na kumtumikia Kristo. Mtu wako mwaminifu anahisi mwito wa
Mungu kujifunza kutoka kwako. Ametoa muda wake ili ajifunze mawazo ya kupokezana
kutoka kwako. Yuko tayari kuwa na ibaada ya faragha, kuandika anayojifunza,
kuomba, na kufundishwa. Yu tayari kutia vifungu vya Bibilia akilini na
kuwajibika kwako. Atapatikana kwa muda uliyotenga kwa kusudi la kujifunza
“mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashashidi wengi.” Anaelewa kuwa maisha
yake yanastahili kuwa mfereji. Kuna mtu mwingine mahali fulani anayemgojea ili
kufundishwa naye. Ni mtu wa kupatikana.
1. Ana muda wa kujifunza
Hana roho ya kujitegemea mwenyewe. Anakubali kuongozwa. Amefikia kiwango cha kukua
kiroho kuna maana zaidi kwake, kama mfuasi. Yu tayari kwa mwongozo wako. Itahitaji nyote
mjitolee kwa sababu kukua kwa mwanafunzi huchukua muda. Amejitolea kwako. Yeye ni
mwaminifu.
2. Anaweza kufundisha wengine
Wote wanaofundishwa hawawezi kufundisha wengine. Napendekeza kwamba mkufunzi ni
vyema atumie muda wake mwingi kwa watu wanaofaa. Tafuta mtu aliye na uwezo wa
kufundisha watu wengine, vile Paulo anavyotueleza. Kwa kumfundisha mtu mwaminifu
unaweza kuvuta na kufundisha maelfu ya watu kupitia kwake. Kila mara omba Mungu
akuletee watu ambao wataweza kufundisha wengine pia (2 Timotheo 2:2). Mtu wako huyo
mwaminifu anaweza kuwa mfuasi wako. Lakini kwa wengine anaweza kuwa ni kiongozi.
Mungu, kupitia kwake, atamfanya kiongozi siku za usoni. Mungu, kupitia kwake, atapanua
ushuhuda wako mara nyingi.
III. Unayeweza kufundisha awe MWEPESI WA KUJIFUNZA
Si kila Mkristo ukutanaye naye ana moyo wa kufundishwa. Mtu mwaminifu ana shauku ya
kujifunza kutoka kwa Mungu. Ni mnyenyekevu kwa uongozi wako. Hana moyo wa kiburi, bali ni
mnyenyekevu ili ajifunze kutoka kwako. Zaidi ya yote anakuruhusu umfundishe. Hili ni jambo la
maana sana. Mkufunzi ni lazima afahamu kwamba hawezi kuwa mwongozo kwa kila mtu. Paulo
hakuwezana na Yohana aitwaye Marko hadi siku za mwisho katika maisha yake. Tafuta watu
wanaoheshimu kutembea kwako na Mungu na kutamani ulicho nacho, na kunyenyekea ili
waipokee kutoka kwako.
Yuko tayari umfundishe ratiba na mawazo ya kupokezana . Itambidi kuelewa kwamba
unamfundisha ili ufundishe wengine kupitia kwake. Hi ni mbinu yenye maana sana. Mtu wako
huyu mwaminifu yu tayari kufuata na kuendeleza ratiba ya ufalme.
Mwanafunzi huyu anapoendelea kukua na kutamani kutumia ujuzi na maisha yake kwa wengine,
itambidi kuomba Mungu ampe wanaume na wanawake walio waaminifu, walio na muda, na
wanaoweza kufundishwa (FAT) . Ni jambo la busara kutumia muda mwingi kwa watu wanaofaa.
Mtu mmoja alisema kwamba mtu mwaminifu ni mtu wa imani. Ukichukua neno imani (faith) na
kuweka maneno katika kila herufi, utaona tabia ya mtu unayestahili kuongoza kukua kiroho.
156
F = faithfull – mwaminifu
A= available – aliye na muda
I = initiator - anayeweza kuanzisha kitu
T = teachable – mwepesi wa kufundishwa
H= heart for God – ana moyo wa kumpenda Mungu.
157
KUMWONGOZA MTU KUKOMAA
Makusudio yako ni nini unapowafanya watu kuwa wafuasi? Mkufunzi anastahili kuzingatia tabia aina gani
sawa na Kristo? Mkufunzi anawajibika kutazamia kukomaa kiroho kwa mwanafunzi wake. Paulo alinena
hayo katika kitabu cha Waefeso 4:13, aliposema, "na hivyo sote tuufikie umoja wa imani na kumjua
Mwana wa Mungu; tuwe watu waliokomaa na kuufikia utimilifu wake Kristo mwenyewe." Mkufunzi lazima
awe na mbinu ili amwasilishe mwanafunzi aliyekamilika kwa Kristo.
• Mkufunzi humsaidia mfuasi kutekeleza ono ambalo amepewa na Mungu.
Utamsaidia kutekeleza mwito wa Mungu katika maisha yake. Ono lake ni shauku ya moyo wake na
nguvu zake. Mkufunzi anawajibika kulikuza ono hilo.
• Tahadhari: Maono ya unayemfanya mwanafunzi yanaweza kuwa tofauti kabisa na yale
uliyomchagulia. Lakini elewa kwamba hayo ndiyo yale Mungu amemkusudia kufanya. Tegemeza yale
ambayo Mungu anatenda katika maisha ya mwanafunzi wako.
• Mkufunzi humsaidia mwanafunzi wake kuenenda katika imani yake
Msaidie mwanafunzi kumtegemea Mungu katika kumtimizia kila hitaji, na haswa katika mwito na
maono yake. Zingatia ukweli wa maandiko yanayotia nguvu mwenendo wake katika imani. Maandiko
kama Waebrania 11:6; Yeremia 29:11 na Wafilipi 4:19 yanafaa.
• Mkufunzi anawajibika kumsaidia mwanafunzi wake kuzingatia mtindo
Kwa kuwa tu "mwangaza" wa Mungu katika ulimwengu, mwanafunzi lazima afundishwe kudumisha
mwenendo wa Ukristo katika maisha yake. Awajibike kwako kwa maombi, kwa ibaada ya faragha,
kwa kuleta wengine kwa Yesu, na kwa uaminifu kwa mwito wa Mungu katika maisha yake. Mathayo
5:16
• Mkufunzi humsaidia mwanafunzi kuwa shupavu wa maombi
Uthabiti katika imani hutokana na kuomba kwa dhati. Msaidie kutembea katika imani, wala si kwa
kuona, ili aweze kudai ahadi za Mungu katika maombi. Atalazimika kuwa na muda wa kuomba
pamoja nawe, na kuona imani yako na jinsi unavyomtegemea Roho Mtakatifu.
Wafilipi 4:6,7; Mithali 3:5,6.
• Mkufunzi husisitiza umuhimu wa ukamilifu wa tabia na uwajibikaji
Kila juma mpe mwanafunzi wako fursa ya kuwajibika anavyotumia wakati wake, na anavyotimiza
ahadi zake. Kujifunza ukamilifu wa tabia huja kwa muda fulani, na lazima uwe na kiini chake katika
tabia ya Kristo. Mithali 11:3, Tito 2:7
• Mkufunzi huzingatia tabia za kiutume ambazo Paulo alipokeza kwa wanafunzi wake
Kutokana na maandiko, angalia pamoja na mwanafunzi wako tabia ambazo Paulo alitarajia kutoka kwa
Timotheo, Tito, na wengine ambao alikuwa kielelezo kwao. Orodhesha tabia hizi kulingana na Sura na
aya, kisha viweke vifungu vinavyosisitiza tabia hizi akilini.
158
• Kwa mfano: Paulo anamwambia Timotheo, "Usikubali mtu yeyote akudharau kwa sababu wewe ni
kijana, lakini jitahidi uwe mfano kwa wanaoamini: katika usemi wako, mwenendo wako, upendo,
imani na maisha safi."
• Mkufunzi humsaidia mwanafunzi kuwa kiongozi katika kufanya wanafunzi na mbinu za
kuzalishana kiroho
Wale wanaoongoza wengine huwa vielelezo bila kuogopa kumtetea Kristo panapohitajika.
Mwanafunzi wako daima lazima atiwe changamoto kuongoza na kuzalisha maisha yake kwa wengine.
Enda naye kuleta wengine kwa Kristo. Angalia anavyofuatilia waliookoka, na mfanye kuwajibika
kupokeza kwa wanafunzi wake maadili aliyopata.
• Mkufunzi humtia moyo mwanafunzi kuwa mwanga na chumvi katika jamii yake
Kuwa kielelezo huanzia nyumbani. Mwanafunzi wako, kama ameoa au kuolewa, lazima atiwe moyo
kuongoza jamii yake katika kuwa wanafunzi. Tenga muda wa kumsaidia kutenda katika jamii yake
yale anayojifunza. Kuongezeka huanzia nyumbani. Waefeso 5:23-28.
159
160
161
MISAADA KATIKA ENEO MTANDAO (INTERNET
WEBSITES)
Huduma za Kikristo katika mtandao
Quiet Time Sites
• Our Daily Bread
www.gospelcom.net/rbc/odb/odb.shtml
• My Utmost For His Highest
www.gospelcom.net/rbc/utmost
• Henry Blackaby Ministries
www.henryblackaby.com
Bible Study Sites
• The Navigators- Navpress
www.navpress.com
• Liberty University Bible Tools
www.biblecrosswalk.com
• Christian Downloads
www.allchristiandownloads.com
• GospelCom.net
www.gospelcom.net
• Vines Expository Dictionary of New
Testament Words
www.menfak.no/bibel/vines.html
• www.villageministries.org
(link to Grace Notes)
• www.homestead.com/mansfieldbible/links
Selected Ministries
• Dr. Carl Baugh
Creation Evidence Museum
www.creationevidence.org
• Dr. James Dobson
Focus on the Family
www.family.org
• Dr. Tony Evans
The Urban Alternative
www.tonyevans.org
• Dr. Billy Graham
Billy Graham Evangelistic Association
www.graham-assn.org
• Dr. Jack Graham
Prestonwood Baptist Church
www.powerpoint.org
• Pastor John Hagee
John Hagee Ministries
www.jhm.org
• Dr. Jack Hayford
The King’s College & Seminary
www.jackhayford.com
• Bishop T. Jakes
The Potter’s House
www.tdjakes.org
• Dr. James Kennedy
Coral Ridge Presbyterian Church
www.coralridge.org
• Max Lucado
UpWords Ministries
www.maxlucado.com
• Joyce Meyer
Life In The Word
www.lifeintheword.org
• Dr. Charles Stanley
In Touch Ministries
www.intouch.org
• Chuck Swindoll
Insight For Living
www.insight.org
• Tim Timmons
New Community Church
www.timtimmons.com
• Barry Wood
Barry Wood Ministries
www.barrywoodministries.org
Bible Prophecy Sites
• Bill Koenig
www.watch.org
• Hal Lindsey
Oracle House Publishing, Inc.
162
www.hallindsey.com
• Dr. Jack Van Impe
Jack Van Impe Ministries
www.jvim.com
• Yacov Rambsel
Messianic Ministries, Inc.
www.yacovrambsel.com
• Zola Levitt
www.levitt.com
Apologetics
• Josh McDowell
Josh McDowell Ministries
www.josh.org
163

No comments:

Post a Comment