Friday 5 December 2014

NDOA NA MALEZI YA FAMILIA

Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
NDOA NA MALEZI YA KIBIBLIA
Jonathan Menn, Wahariri
B.A., University of Wisconsin-Madison, 1974
J.D., Cornell Law School, 1977
M.Div., Trinity Evangelical Divinity School, 2007
Equipping Church Leaders-East Africa
3701 N. Gillett St., Appleton, WI 54914
(920) 731-5523
jonathanmenn@yahoo.com
www.eclea.net
Kimetafsriwa na Michael D. Nyangusi
Aprili 2008; toleo jipya lililorekebishwa, Mei 2013
Ufafanuzi wa kibiblia wenye kiini cha Kristo wa matumizi ya neno la ufunuo la Mungu
kuhusiana na ndoa na malezi, ikizungumzia taasisi yake, kusudi, majukumu na wajibu
ikilenga mahusiano, mawasiliano, kujamiiana, kulea, kupanga uzazi, na kuachana.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
1
YALIYOMO
1. UTANGULIZI: ASILI NA CHANZO CHA NDOA………………................................……………….2
2. WANAUME NA WANAWAKE: MFANO WA MUNGU NA ASILI YA KIBINADAMU…………4
3. MAPENZI YA MUNGU KWA WAKE.………………………………..……………………………….17
4. MAPENZI YA MUNGU KWA WAUME..……………………………………………………..............27
5. KANUNI TATU ZA MAWASILIANO ZILETAZO UMOJA….…………………...………..............37
6. MAWASILIANO: KUELEWANA; KUSIKILIZA; NA UWEZO WA KUHISI MAONO ………..40
7. SEMA KWELI KWA UPENDO: LUGHA TANO ZA UPENDO…………..………………………..45
8. KUFANYIKA BARAKA KWA FAMILIA YAKO……………….…………………………………...52
9. MAJUKUMU YAHUSUYO TENDO LA NDOA KATIKA NDOA.……………….…….………….56
10. MALEZI KIBIBLIA………………………………………………………………..…………………..63
11. UZAZI WA MPANGO…………………………………………….…………………………………...71
12. MAANDIKO YANAVYOFUNDISHA KUHUSU KUACHANA..……………...………………….77
MAREJEO YALIYOTAJWA……………………………………………………………………………..84
KIAMBATISHO: MAONI YA KUFAA YA KUWASAIDIA WAUME NA WAKE KIMAISHA ……..86
KUHUSU MWANDISHI…………………………………………………………………………………...88
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
2
1. UTANGULIZI: ASILI NA CHANZO CHA NDOA
I. Chanzo cha ndoa.
A. Mawazo mbali mbali kuhusu taasisi ya ndoa ilivyoanza.
1. Hekaya ya Kiafrika (Lesotho): “Hapo kale walikuwepo vijana wanne ambao waliwinda pamoja
daima. Hakuwepo mtu mwingine duniani kwa jinsi hiyo waliwaza, lakini siku moja Mungu aliumba
mwanamke na akamfundisha kusema, kuoka mkate na kutengeneza vyungu, kuotesha nafaka na kupika.
Hatimaye siku njema moja ndugu hawa wanne wakakutana na huyu msichana na walijiuliza, Je huyu ni
mnyama au binadamu. Mmoja wao akasema ninampenda na hivyo aliwazuia kaka zake wasimtendee
kama mnyama. Wale watatu waliondoka wakisema hitaji lao lilikuwa ni kuwinda wanyama na kama
ndugu yao alimtaka mnyama yule (mwanamke)wao wangeendelea mbele kuwinda wengine kwa ajili
yao. Hawakuonekana tena kwani baada ya miaka ya kuwinda walipokuwa wazee waliuwawa na simba
nyikani kwa kuwa hawakuweza kujihudumia na kujilinda. Kwa upande mwingine ndugu yao
aliyempenda mwanamke aliishi na yule mwanamke ndani ya pango karibu na kisima miambani.
Mwanamke yule alimiliki moto hivyo alimpikia nyama, uji na mboga, ambavyo alikuwa amevilima.
Mwanamume alikuwa na furaha kuu na alilishwa vema mno. Walipata watoto wengi na hata wajukuu,
ambao waliwatunza katika uzee wao” (Knappert 1990: 153)
2. Hekaya ya Kihindi: Deerghatumma ambaye ni kipofu alisema ndoa yapaswa kumpa mwanamume
mamlaka juu ya mwanamke.
a. Usemi huo ulitokana na ukweli kuwa wanawake walikuwa na “mamlaka zaidi.”
b. Hata hivyo, endapo sababu ya ndoa itakuwa ni kuruhusu wanaume watumie mamlaka vibaya,
ndoa yapaswa kupigwa marufuku kabisa.
3. Wengine husema ya kuwa ndoa ilizuka tu kama vile mtu alivyozuka:
a. Yasemekana ya kuwa ndoa ni matokeo ya hitaji lihusianalo na utatuzi wa maswala ya malezi
na matunzo ya watoto.
b. Kwa hiyo endapo majukumu ya ndoa yalizuka, yaweza kuendelea kuzuka na kubadilika na
kuwa tofauti.
4. Endapo ndoa ni taasisi iliyoanzishwa na wanadamu, na ikiwa imetokana na hekaya au kuchipuka kwa
njia ya asili tu, basi mwanadamu ana uwezo wa kubadili sheria zinazotawala ndoa au hata kuachana
nayo kabisa.
B. Neno la Mungu laandika ya kuwa Mungu ndiye aliayenzisha ndoa (Mwz 2:18-25).
1. Yesu alinukuu kuhusu ndoa iliyoanzishwa na Mungu katika Math 19:5.
2. Paulo alinukuu kuhusu ndoa iliyoanzishwa na Mungu katika Efe 5:31.
3. Hivyo, hatuwezi kuibadili au kuachana nayo. Wajibu wetu ni kutii asemacho Mungu kuhusiana na
taasisi yake.
C. Kwa njia ya ndoa Mungu hutimiliza kilicho chema kwa kumpatia mwanamume msaidizi wa kumfaa.
1. “Si vema kwa mwanamume kuwa peke yake” (Mwz 2:18). Uumbaji wa mwanadamu umefanyika
katika hatua mbili (Mwanzo 2 hutoa maelezo ya kina ya uumbaji wa binadamu, ambao kwanza
waelezwa katika Mwz 1:26-27). Akiwa amesha muumba mwanamume, ambaye kimaumbile
aliandaliwa awe na mwenzi, yamaanisha:
a. Yalikuwapo mambo zaidi ya kufanya—Kazi ya Mungu kuhusiana na mwanamume ilikuwa
haijakamilika: mwanamume aliumbwa na ameumbwa kuwa na mwenzi wa kuambatana naye.
b. Mwanamume mkamilifu paradiso (mahali pakamilifu) akiwa na chakula kizuri na kazi nzuri
(Mwz 2:15), na Mungu mzuri, bado hakuweza kujitosheleza yeye binafsi.
c. Binadamu aliumbwa kama kufuli na funguo—moja bila nyingine haina kazi.
d. Watu hutegemeana, sio wakujitegemea (huru)
e. Kwa asili mwanamume na mwanamke wanapaswa kuoana. Useja ni kipawa maalum kutoka
kwa Mungu (1 Kor 7:7).
2. “Nitamfanyia msaidizi wakufanana naye” (Mwz 2:18). “Msaidizi wakufanana” yamaanisha “wa
kukubaliana,” au “mwenzi” wa mwanamume, kumkamilisha na kumsaidia, sio kuwa mtumwa wake. Hii
inamaanisha:
a.Mwanamume anahitaji mwenzi wa kuzungumza naye, kushiriki naye hisia, maono, furaha,
huzuni, nk.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
3
b. Uhitaji wa msaidizi kwa mwanamume wadhihirisha kuwa mwanamume anahitaji msaidizi,
wakumtegemeza, mshiriki, rafiki.
c. Mwanamume anahitaji msaada ili kuijaza nchi na katika jukumu la kuitiisha nchi.
d. “Msaidizi” ni cheo cha kuheshimika.
(1) Mungu mwenyewe wakati mwingine huitwa “Msaidizi” (Zab 30:10; 40:17; Ebr
13:6).
(2) Yesu alimwita Roho Mtakatifu “Msaidizi” wetu (Yoh 14:16, 26; 15:26; 16:7).
(3) Endapo cheo “Msaidizi” ni chakumstahili muumba wa ulimwengu, basi hakiwezi
kuwa na hadhi ya chini kwa mke. Kinyume chake, ni cheo cha heshima, na mke
ajivunie kuwa nacho.
(4) Mume na mke wautazame Utatu unao “saidiana” kuumba, kutawala, kufurahia,
kuhuzunika, nk.
3. Mchakato aliotumia Mungu wa kumpa Adam jukumu la kuwapa wanyama majina ulidhihirisha wazi
kuwa hakuwepo mnyama aliyefaa kuwa msaidizi wa mwanamume (Mwz 2:19-20).
a. Bwana akamletea Adamu wanyama awape majina, yamaanisha,kutathmini sifa na ubora
wao. Adamu alitathmini sifa na ubora wao na kutokana na hizo akawapa majina yaliyowastshili.
Na mchakato huo ulidhihirisha kuwa “hakuwepo msaidizi wa kufanana naye” (Mwz 2:20).
b. Rabi Fulani anatupa picha hii—wanyama wanakuja kwa jozi: “Kila mmoja ana mwenzi, ila
mimi sina mwenzi.”
c. Huenda Adamu alishayagundua mahitaji yake ya ndani kutokana na jinsi Mungu
alivyomuumba—hitaji la mwenzi, usaidizi katika majukumu ya kimaisha, hitaji la binafsi la
kujamiiana. Hata hivyo, Adamu hakupata alichokihitaji miongoni mwa wanyama kwani
alichohitaji si mnyama.
d. Matumizi: Wanaume, je mmeshatambua na kukubali kuwa hamjitoshelezi?
(1) Uliumbwa kwa namna ya kuwa tegemezi kwa mkeo.
(2) Wapaswa pia kujua hitaji lako la msaidizi haliwezi kutoshelezwa na chochote kile
miongoni mwa vitu au wanyama.
D. Mungu alimuumba msaidizi wa kumfaa mwanamume kutokana na mwili wa mwnamume (Mwz 2:21-22).
1. Mungu alimuumba msaidizi wakati Adamu amelala. Kumbukumbu hazionyeshi kuwa Adamu
alihusika kwa namna yoyote katika mchakato wa uumbaji.
2. Adamu hakujua namna ya kutatua hitaji lake la msaidizi.
3. Kutokana na kusudi lake la milele na hekima yake Mungu alilitambua hitaji la Adamu hasa. Ni yeye
pekee ajuaye vigezo vilivyosababisha mwanamke awe msaidizi wa kufaa, mwenzi, rafiki na mshiriki
kwa mwanamume ili ile sura ya mfano wa Mungu ionekane ndani yao.
4. Bwana huamua namna ya kukidhi hitaji- nini kinafaa kuwa msaidizi wa mwanamume.
5. Mungu alimuumba msaidizi kwa kutumia sehemu ya mwili wa Adamu, ubavu wake, mwili ambao ni
tofauti na ule wa wanyama. Inamaanisha:
a. Hapaswi kufananishwa na jamii ya wanyama.
b. Yeye si hayawani mwenye kutulemea, licha ya tamaduni nyingi kuwachukulia wanawake
kwa namna hiyo.
c. Hapaswi kupigwa, kwa viboko au maneno.
6. Kama alivyosema mwenye hekima mmoja, “Mwanamke hakutokana na sehemu ya kichwa cha
mwanamume, asije akamtawala, au hakutokana na sehemu ya miguu,asije kanyagwa naye, lakini katoka
ubavuni ili awe mshiriki kama mwenzi aliye sawa naye ingawaje ana jukumu tofauti.”
7. Matumizi: Mwenendo na tabia yako kwa mume au mke wako ikoje?
II. Asili na kusudi la ndoa.
A. Kwa asili, ndoa ni ya kiroho.
1. Ndoa yawakilisha umoja kati ya washiriki watatu wa Utatu Mtakatifu (Baba, Mwana, Roho
Mtakatifu). Kama vile washiriki watatu wa Utatu Mtakatifu walivyo nafsi tofauti bali Mungu mmoja,
vivyo mume na mke ni watu tofauti bali wameunganishwa na “kuwa mwili mmoja” (Mwz 2:24).
2. Ndoa ni mfano wa uhusiano wa Yesu na kanisa lake (Efe 5:22-33).
a. Mke na amtii mumewe kama kanisa linavyomtii Kristo.
b. Mume na ampende mkewe kama Kristo alivyolipenda kanisa akajitoa kwa ajili ya kanisa .
c. Kwa hiyo, wana ndoa wanapaswa kuwa mfano ulio hai na wazi wa uhusiano wa Kristo na
kanisa lake.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
4
B. Ndoa ni taasisi ya msingi na kiini cha jamii ya wanadamu.
Kuvunjika kwa ndoa (kupitia talaka,muunganiko wa jinsia moja, na kujamiiana nje ya ndoa), ambavyo
hutokana na kutofuata neno la Mungu, huharibu utamaduni wa watu wa Magharibi na utafanya yayo hayo kwa
utamaduni wa watu wasio wa ki-Magharibi.
C. Kusudi la ndoa:
1. Kutokana na Mwanzo makusudi yafuatayo ya ndoa hujitokeza:
a. Urafiki (Mwz 2:18).
b. Umoja (Mwz 2:24).
c. Uzao (Mwz 1:28; 9:1, 7).
d. Starehe (Mwz 3:16; tazama pia Mhu 9:9; Wimbo ulio Bora 1-8; 1 Kor 7:3-5).
2. Pamoja na hayo Agano Jipya laongezea makusudi yafuatayo ya ndoa:
a. Ulinzi dhidi ya uasherati (1 Kor 7:9).
b. Utakaso wa kibnafisi au unaoendelea (Efe 5:26).
2. WANAUME NA WANAWAKE: MFANO WA MUNGU NA ASILI YA KIBINADAMU
I. Wanadamu na mfano wa Mungu.
A. Wanadamu kama viumbe walioumbwa.
1. Kwanza maandiko yanena kuhusu Mungu ya kuwa ni muumbaji (Mwz 1:1). Jambo la kwanza
ambalo maandiko husema kutuhusu ni kwamba sisi tu viumbe, tumeumbwa na Mungu (Mwz 1:26-27;
2:7, 18-22).
2. Maandiko pia yasema si tu kwamba Mungu aliwaumba watu wa kwanza wawili (Adamu and Hawa),
na kutuacha wapweke. Bali Mungu humtengeneza kila mtu mmoja (Kut 4:11; Ayu 10:8; 31:15;
Zab100:3; 119:73; 139:13-16; Isa 44:24; Yer 1:4-5; 27:5).
3. Kuna uhusianao kati ya uumbaji na umiliki. Kwa kuwa Mungu alituumba, sisi tu wake (Kum 10:14;
Zab 24:1; 50:10-12; 95:6-7; 100:3; Isa 17:7; 29:19; 45:9; 64:8; Yer 18:1-10; Rum 9:20).
B. Kwa nini Mungu aliumba wanadamu.
1. Mungu hakuumba wanadamu kwa kuwa kulikuwa na upungufu au hali ya uhitaji. Mungu ‘hahitaji’
chochote (Mdo 17:24-25). Mungu ni wa kipekee. Mungu anajitosheleza. Mungu ni mmoja, lakini yuna
nafsi tatu, zijulikanazo kama Utatu (mfano Mwz 1:2, 26; Kum 6:4; Zab 110:1; Isa 42:1; 48:16; 61:1;
Math28:19; Yoh 1:1, 14; 8:58-59; 10:30-33; 14:16-17; 15:26; 16:5-15; Rum 10:9-13; 1 Kor 12:4-6;
2 Kor 13:14; Ebr 1:1-3; 1 Pet 1:1-2; 2 Pet 1:1; Yuda 20-21).
2. Biblia inasema Mungu alimuumba mwanadamu ili Mungu ajitukuze (Isa 43:7; Rum 9:23; Ufu 4:11;
tazama pia, Rum 11:36; 1 Kor 10:31). Kwa hakika, sisi hatupende wanadamu wengine wanapotaka
“kutukuzwa” (yaani;kuinuliwa:kusifiwa: kuabudiwa; kufanywa kiini cha upendo, mvuto, utashi,
heshima, nk ) Hivyo basi, kisicho sahihi kwetu ni sahihi kwa Mungu, kwa sababu Mungu pekee ndiye
astahiliye kupewa upendo wetu mtimilifu na kutukuzwa. Mungu ni upendo, wema, uzuri, kweli, naye ni
chanzo kikuu na msingi wa mema haya yote. Hatimaye, Mungu mwenyewe anajitoa kwetu kama
zawadi kuu kuliko zote atoazo kwetu. Kujitoa kwa Mungu kusikoyumba kwa utukufu wake
kunachochea pendo lake kwetu na hizi ni habari njema kwetu—kwa kadiri tunavyomtukuza Mungu
maishani mwetu, ndivyo tunavyozidi kufanana naye.
3. Kumtukuza Mungu humaanisha tunapaswa kuwa na uhusiano mzuri naye. Amri ya kwanza na iliyo
kuu ni ‘kumpenda Bwana Mungu wako kwa roho yako yote, kwa moyo wako wote, kwa akili zako zote,
na nguvu zako zote” (Marko 12:28-30; Math22:36-38; Kum 6:5). Asili ya uzima wa milele ni
“Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yoh 17:3). “Kumjua”
Mungu na (na yeye “kutujua”) ni ujuzi ambao ni zaidi ya ujuzi wa maarifa ya kawaida, lakini
yamaanisha uhusiano: uchaguzi; kuweka upendeleo kwenye; kuthamini; kuwa na mahusiano ya karibu
mno (Mwz 4:1; Zab 1:6; Yer 9:23-24; Amos 3:1-2; Math 7:23; 1 Kor 8:3; Gal 4:8-9). Kuwa na
uhusiano mzuri na Mungu—kumpenda na kumjua na kumtukuza—kutufanya kufurahia ndani yake
(Zab 37:4; Zab 94:19; Isa 58:13-14). Hatimaye, Katekisimo ya Westminster Larger imejibu kwa
usahihi swali namba 1: “Ni lipi lilo kuu na muhimu zaidi katika hatima ya mwanadamu? Jibu: Jambo
lililo kuu na muhimu katika hatima ya mwanadamu ni kumtukuza Mungu, na kumfurahia kikamilifu
milele” (Westminster 1647).
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
5
C. Mfano wa Mungu ndani ya wanadamu.
1. Katika Mwz 1:26-27 Mungu alisema: “Natufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale
samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa
kitambaacho juu ya nchi.” Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba,
mwanamume na mwanamke aliwaumba.
2. “Mfano” na “sura” yaonyesha kuwa na maana zinazokaribiana. Kwa Kiebrania “mfano” ni tselem.
Kwa kadiri ya tafsri ya kibinadamu tselem,yamaanisha “sura” (Koehler and Baumgartner 2001:
“tselem,” 2:1029). Neno la Kiebrania la “sura” ni demuth. Demuth latafsiriwa kama “muundo, umbo,
kifananacho na, kulandana” (Ibid.: “Demuth,” 1:226). Asili yao hiyo ya kulandana yaonekana katika
Mwz 1:26, Mungu anapokusudia kuumba mtu, anatumia maneno yote mawili, lakini katika Mwz 1:27,
anapoumba anatumia neno “mfano”; hatahivyo, katika Mwz 5:1 (ambayo yaturudisha kwenye uumbaji
wa Adam) neon “sura” tu limetumika. Mwz 9:6 neno “mfano,” na Mwz 5:3 maneno yote mawili
yametumika, lakini kwa mpangilio uliogeuzwa tofauti na jinsi yalivyotumika katika Mwz 1:26 (na,
katika 5:3, vihusishi pia vimageuzwa tofauti na jinsi vimetumika katika 1:26—i.e., 1:26: “katika mfano
Wetu ,” “na kwa sura Yetu”; 5:3: “kwa sura yake,” “na kwa mfano wake”).
3. Wanaume na wanawake wote ni mfano wa Mungu sawa sawa” (MWM).
a. Mwz 1:26 inasema “Natufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu.” Maana ya kimsingi ya
neno “mtu” (adam) ni ya ki-ujumla “wanadamu, watu,” ambayo yahusisha wanaume na
wanawake. Ya kwamba imehusisha wanawake kwa wanaume imewekwa wazi hapa katika
kifungu kifuatacho, kisemacho, “na watawale . . .” Mwz 1:27 hapa yaweka wazi kabisa kuwa
wanaume na wanawake wamehusishwa sawasawa, kwa kuwa inasema, “Mungu akaumba mtu
kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba , mwanamume na mwanamke
aliwaumba.” Mbele, katika Mwz 1:28 Mungu akawabarikia (mwanamume na mwanamke)
sawasawa na akasema “nao”. Katika Mwz 1:29, Mungu anaposema “nimewapa kila mche utoao
mbegu,” ilimaanisha wote na si mmoja.
b. Hivyo, kama Hoekema anavyofafanua: “Mwanamume na mwanamke kwa pamoja ni mfano
wa Mungu. . . . Mwanamume akiwa ameumbwa kwa jinsi ya kiume na kike ni kipengele
muhimu cha mfano wa Mungu. . . . Kuwepo kwa mwanamume kwa jinsi ya kiume na kike
kwamaanisha kuwa mwanamume kama nafsi ya kiume ameumbwa kwa namna ya kuwa na
ubiya na nafsi nyingine ambayo ni kama yeye ingawaje wanatofautiana kwa namna ya ajabu.
Ina maana mwanamke ni utimilifu wa utu wa mwanamume, na yakuwa mwanamume
anakamilika pale tu anapokuwa na mahusiano na mwanamke.” (Hoekema 1986: 97, mkazo
katika asili)
4. MWM kimaandiko haina tafsiri bayana. Hata hivyo vifungu mbalimbali hutusaidia kuona ni nini hasa
yahusiana na MWM.
a. MWM kuhusiana na asili ya Mungu na utukufu wake.
(1) Mungu ni roho (Yoh 4:24). Mungu alipowaumba Adamu na Hawa, kwa mfano
wake na sura yake, tendo la kuwa na mwili lilikuwa bado. Hiyo inamaanisha kuwa
MWM ni ya “kiroho” mfano/sura, huenda ikahusisha pia uwezo wa mahusiano na
Mungu. Hii, angalau imegusiwa Mungu alipoumba mwanadamu (tofauti na namna
alivyoumba viumbe wengine), “Akampulizia puani pumzi ya uhai” (Mwz 2:7; tazama
pia Yoh 20:22 wakati Yesu “akawavuvia [wanafunzi wake], akawaambia, ‘Pokeeni
Roho Mtakatifu’”). Zaidi ya hayo, katika Mwz 1:28 Kwa mara ya kwanza Mungu
anazungumza na uumbaji wake moja kwa moja; tendo la kusema na Adam na Hawa
laonyesha wazi kuwa wao ni tofauti wakilinganishwa na uumbaji mwingine wote—kwa
sababu walikuwa na MWM Mungu anaweza kuwasiliana nao kwa namna ambayo
hafanyi na viumbe wengine.
(2) “Mfano” (tselem) inatafsiriwa kama, “mtu, sura ya Mungu, mfano wa Mungu,
inamaanisha, ni mwakilishi wa Mungu au shahidi miongoni mwa viumbe” (Koehler na
Baumgartner 2001: “tselem,” 2:1029). Hivyo, MWM si tu kitu tulichonacho, lakini ni
vile tulivyo. Dhana ya mtu katika mfano or sura ya Mungu “yatuambia kuwa mtu
alipoumbwa alipaswa awe kioo cha Mungu na amwakilishe Mungu” (Hoekema 1986:
67).1 Kama kioo kinavyoakisi, hivyo mwanadamu amuakisi Mungu na utukufu wake.
1“Ukweli huu umefungwa katika makatazo ya kutengeneza sanamu yanayopatikana katika mri ya pili ndani ya Amri Kumi
za Mungu:’Usijifanyie sanamu ya kuchonga’ (Kut. 20:4,). Mungu hataki viumbe wake kutengeneza sanamu
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
6
Zaidi ya hayo, kwa kuwa Mungu aliwapa watu jukumu la “kuijaza dunia” (Mwz 1:28),
Mfano wa Mungu na sura ya Mungu vingesambaa duniani kote kadiri wawakilishi
wake walivyotii agizo lake. Mifano ya aina mbili itatusaidia kuelezea wazo la MWM:
(A) Darubini huchukua kitu ambacho huwa ni kikubwa (sayari au nyota iliyo
mbali), ingawa chaonekana kuwa kidogo kwetu,na hukifanya kionekane kuwa
kikubwa (kwetu)zaidi ya vile kilivyo. Kuna utengano wa asili kati ya
muumba/na uumbaji (ambao umeongezeka kwa sababu ya dhambi). Ingawaje
Mungu ni “mkuu” katika hali ya kuwa yeye yuko kila mahali, watu wengi
hawautambui uwepo wake; kwao wao, ukuu wa Mungu hautofautiani na ule wa
sayari au nyota iliyo mbali ionekanavyo kwa jicho la nyama. Hata hivyo, watu
wa Mungu, ambao wana mfano wa Mungu, kama darubini, humleta Mungu
“karibu”- wengine humuona Mungu kwa uwazi na ukuu zaidi kwa sababu ya
wawakilishi wa Mungu miongoni mwa viumbe wake.
(B) Vivyohivyo, Sura ya Mungu yaweza kulinganishwa na hadubini, ambayo
huwezesha vitu visivyoonekana kwa macho haya ya nyama vionekane. Kama
hadudubini, watu wenye sura ya Mungu husababisha uhalisia wake
usioonekana uonekane.
(3) Mfano na uwakilishi mkamilifu wa Mungu waonekana ndani ya Yesu Kristo. Kwa
hakika maandiko yamwita Kristo “mfano wa Mungu” (2 Kor 4:4; Kol 1:15) “na
mwakilishi halisi wa asili yake” (Ebr 1:3; tazama pia Yoh14:8-9; 1:1:18; 2 Kor 4:6).
Ndani ya Kristo twaona MWM katika ukamilifu wake wote. Kwa hiyo, “Hakuna njia
bora zaidi ya kuuona mfano wa Mungu zaidi ya ule tuuonao kwa Yesu Kristo. Kile
tuonacho na kusikia kwa Yesu ndicho alichokusudia Mungu kwa ajili ya watu”
(Hoekema 1986: 22).
b. MWM ukihusianishwa na muundo wa kibinadamu. Kwa maana nyingine MWM
washughulika na “sisi ni nani” (inamaanisha, asili ya uhai wetu, kuwepo kwetu; asili yetu) kama
wanadamu; kwa maana nyingine uwepo wetu na asili yetu twaakisi asili na uwepo wa Mungu
mwenyewe. Mwz 5:1-3; 9:6; na Yak 3:9-10 anaonyesha kuwa watu wote bado wana MWM
ingawaje mwanadamu alianguka dhambini; hivyo, bado kuna sehemu ya MWM kwa watu wote
kama sehemu ya sisi. (tazama pia Zaburi 8 ambayo, ingawaje haitumii maneno “mfano wa
Mungu,” yazungumza kuhusu mwanadamu kwa dhana ileile kama ionekanavyo katika
Mwanzo1.) Mambo yanayotufanya tufananishwe na Mungu ni pamoja na haya yafuatayo:
(1) Kufanana katika muundo. Mungu ni wingi, ingawa ni mmoja (inamaanisha, Utatu);
sisi tu wingi, ndani ya mmoja:
(A) Tumeumbwa mtu mume na mtu mke. Hii ni zaidi ya tofauti za kijinsi, kwa
sababu tofauti hizo zipo hata kwa wanyama, lakini biblia haisemi kuwa
wameumbwa kwa mfano ya Mungu. Wakati Mwz 1:27 inaposema Mungu
aliumba mtu kwa MWM na kuongezea “mtu mume na mtu mke aliwaumba”
mstari huu unamaanisha kuwa “mwanadamu si kiumbe aliyejitosheleza
kibinafsi, bali anahitaji ushirika wa wengine, na bila ya wengine kamwe
hajakamilika” (Hoekema 1986: 76). Dondoo hiyo imewekwa wazi katika
Mwanzo 2 ambayo huuelezea uumbaji wa mwanamke na mwanzo wa taasisi ya
ndoa. Kwa hakika wingi-ndani ya-umoja miongoni mwa wanadamu ambao ni
mfano ulio wazi zaidi wa utatu waonekana kwa uwazi zaidi katika ndoa, pale
ambapo mwanamume na mwanamke ingawa wa nafsi tofauti, “wafanyika
mwili mmoja” (Mwz 2:24).2
(B) Zaidi ya hayo, kila mtu ana umbile, (mwili) na sehemu isiyo mwili (nafsi);
hizi mbili zinapounganika hufanya mtu mmoja, (nafsi nzima)” Mungu
zinazomwakilisha, kwa sababu tayari ameshafanya kilicho mfano wake: kilicho hai, kinachotembea na kusema. Ikiwa
unataka kuona nilivyo, Mungu anasema, tazama kiumbe change cha pekee: mwanadamu. Hii inamaanisha ya kuwa
mwanadamu anapokuwa kama anavyopaswa kuwa, wengine wapaswa kumwona Mungu ndani yake: kuuona upendo wa
Mungu, wema wa Mungu, uzuri wa Mungu” (Hoekema 1986: 67).
2Hoekema alitahadharisha kuwa: “Kile ambacho kimesemwa, hata hivyo, kisitafsiriwe kwamba ni wale tu walio ndani ya
ndoa wanaoweza kuelewa maana ya kuwa mtu kamili kiukweli. Ndoa, kwa hakika, hudhihirisha kwa ukamilifu zaidi kuliko
taasisi nyingineyo yoyote ile hali ya mwingiliano na kutegemeana kwa mahusiano ya mwanamume-mwanamke. Lakini
haifanyi hivyo kwa namna ya kujitenga. Kwa sababu Yesu mwenyewe, akiwa mtu kamaili aliye kielelezo cha ubora,
hakuwahi kuoa. Na katika maisha yajayo, mwanadamu atakapokamilishwa hasa, ndoa haitakuwepo (Math. 22:30).”
(Hoekema 1986: 77)
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
7
amelidhihirisha hili yeye mwenyewe kwa kufanyika mwanadamu ndani ya
Yesu Kristo, ambaye alikuwa mtu kamili na Mungu kamili. Hivyo, si kweli
kuwa hali yetu ya kuwa na mwili ni dhambi au mbaya, na ya kwamba ile hali
ya kutokuwa na mwili ni takatifu —mtu kamili ana vyote viwili, na yaonekana
katika ukweli kwamba, katika kizazi kijacho, itakuwepo mbingu mpya na nchi
mpya, na si kwamba zitakuwepo nafsi zisizo na miili, bali tutakuwa na miili
mipya.
(2) Kufanana kwa hadhi. Mungu ni muumbaji na anatawala vitu vyote; sisi tuna asili ya
uumbaji na tumepewa kutawala na kutiisha uumbaji na vyote vilivyomo ndani yake.
(3) Kufanana kwa uwezo. Mungu ni wa kimantiki, mwadilifu, mwenye uwezo wa
kuchagua, na mwenye hisia; sisi tu wakimantiki, wenye uadilifu, tuna uwezo wa
kuchagua, na tuna hisia. Kwa maana hii, “Mfano wa Mungu ndani ya mtu humpa hali
ya kujua mema na mabaya. Kwa sheria rasmi au isiyo, ilikuwa ni sheria ya wazi ya
maisha, kuwa wanadamu wote, kwa viwango tofauti, wametii na kutotii. Ni kwa sababu
hii sisi wanandamu kwa haki twawajibishwa” (Wells na Zaspel 2002: 142). Hii “hali ya
ujuzi wa mema na mabaya” yaelezewa katika Rum 1:18-2:16. Hivyo, Mungu
alihukumu watu kwa haki, hata kabla ya sherea ya Musa kutolewa, kwa vitu kama
kutamani (Mwz 3:6), kuabudu visivyo (Mwz 4:5), kuuwa (Mwz 4:8-11), uzinzi (Mwz
6:1-7), mawazo mabaya (Mwz 6:5), kutotii wazazi (Mwz 9:22-25), kiburi (Mwz 11:4-
8), kuabudu sanamu (Rum 1:18-32), maana watu walijua zaidi.
c. Jinsi MWM unavyohusiana na utendaji wa mwanadamu na mahusiano. Vifungu vingine
huuzungumzia MWM kama kitu “kisichobadilika” au kwamba haujabadilika licha ya anguko la
mwanadamu dhambini, lakini katika hali yenye nguvu imehusianishwa na yale tutendayo na
namna tunavyohusiana na Mungu na watu wengine.
(1) Rum 8:29, 2 Kor 3:18, Efe 4:22-24, na Kol 3:9-10 yote huzungumzia kuhusu
mfano katika nyanja za uadilifu na nguvu. Katika vifungu hivi MWM ina husiana na
“utu mpya” katika Kristo. Hii yaonyesha kuwa, kwa kweli, MWM uliharibiwa kwa njia
ya dhambi, na hatunao tena kihalisi. MWM hurejeshwa kwa watu wa Mungu
wanapomgeukia Baba kwa njia ya wokovu wa Yesu Kristo, na huendelea kutakaswa
kadiri wanavyomtii Mungu na kumtii Roho Mtakatifu aliye ndani yao. Kwa hakika, njia
mojawapo ya kuutazama utakaso ni urejesho wa MWM katika utimilifu wake wote
ndani ya watu waliokombolewa.
(2) Sababu mojawapo ya Yesu kuvaa mwili ilikuwa si tu kubeba dhambi zetu, bali ni
kuwa kielelezo cha vile tupaswavyo kuwa. Kristo alifanya yale tu ambayo Baba
alimtaka kufanya (Yoh 4:34; 5:17-20, 30; 6:38; 8:28-29; 12:49-50; 14:10, 24, 31).
Hivyo, lengo letu ni “kubadilishwa katika mfano wa mwana [wa Mungu]” (Rum 8:29),
kwa sababu twaenenda katika njia za Mungu twaudhihirisha mwenendo wa kiMungu na
kuuonyesha wema wake.
(3) Kuna ukweli pia kuwa MWM ni hali tuliyonao hata baada ya kifo, umilele. Luk
20:34-36, 1 Kor 15:49 na 1 Yoh 3:2 yaonyesha kuna hali ya umilele ya MWM ambayo
ni ya mbinguni ambayo haitadhihirika kikamilifu mpaka tufikie hatua za kukamilishwa
katika mbingu mpya na nchi mpya. Na hapo, ndipo tu, “tutakapofanana naye” (1 Yoh
3:2), na “kama malaika” (Luk 20:36), na tutakuwa na “mfano wa kimbingu” (1 Kor
15:49). Hapo tena nguvu ya dhambi haitakuwamo ndani yetu; mwenendo wetu
utabadilishwa kikamilifu sambamba na asili ya Kristo.
5. Maana ya kimaadili ya MWM. Upo uhusiano ulio wazi kimuundo na kiutendaji katika dhana ya
MWM: mtazamo mmoja juu ya kuwepo muundo huo ni ili watu watekeleze majukumu yao kikamilifu,
au kile tutendacho kina msingi kuhusu sisi ni nani. Kuna angalau Nyanja tatu za kimaadili katika eneo
hili:
a. Mahusiano na upendo ndicho kiini cha MWM. Kwa asili ya Mungu “kimuundo”, na kwa
namna alivyoumba watu, yaonyesha kimahusiano tu mfano wa Mungu. Ukweli ya kuwa
Mungu ni utatu na ya kuwa yeye ni “upendo” (1 Yoh 4:8) yaonyesha kuwa, kama sehemu ya
uungu, nafsi zote za utatu ziko katika mahusiano ya upendo mkamilifu kati yao. Zaidi ya hayo,
mahali ambapo kwa mara ya kwanza Mungu alisema kitu “si chema” ilikuwa pale aliposema“si
vema mtu huyu awe peke yake” (Mwz 2:18). Kweli hizo humaanisha yafuatayo:
(1) MWM hauonyeshwi (tu) na mtu awapo pekee, bali, sehemu muhimu ya
kuuonyesha MWM ni katika ushirika – kwa watu walio na mahusiano. Uhusiano wenye
ukaribu kuliko mahusiano yote kwa wanadamu, ambao umejengwa katika mpangilio
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
8
wa uumbaji na umeundwa kumwakisi Kristo na kanisa, ni ndoa (Mwz 2:24; Efe 5:23-
32). Hivyo, ndoa zetu, hasa, zapaswa kuwa MWM.
(2) Kwa sababu Kristo ni kielelezo kikamilifu cha MWM, “Hivyo kinachopaswa kuwa
kiini cha mfano wa Mungu . . . ni kile ambacho kilikuwa kiini cha maisha ya Kristo:
upendo kwa Mungu na upendo kwa mtu. Ikiwa ni kweli kuwa Kristo anawakilisha
mfano wa Mungu kikamilifu, basi kiini cha mfano wa Mungu lazima iwe ni upendo.
Kwa kuwa hakuna mtu aliyewahi kupenda kama alivyopenda Kristo” (Hoekema 1986:
22). Hakika, twapaswa kupenda wengine kwa kuwa wameumbwa kwa MWM.
b. MWM huondosha chuki za kikabila. MWM una utajiri mwingi sana na kamwe mtu mmoja
hawezi kuuwakilisha kiutoshelevu. Kwa hakika [MWM] katika ujumla wake waweza
kuonekana kwa wanadamu wote katika ujumla wao,” ambayo humaanisha kuwa “twaweza tu
kuuona utajiri wote wa mfano wa Mungu tunapojumuisha historia yote ya mwanadamu na
mchango wa tamaduni tofauti mbalimbali” (Hoekema 1986: 99-100, emph. in orig.). Hii
yaweza kuwa sababu mojawapo ya wanadamu kukombolewa na Kristo “kutoka katika kila
lugha, kabila na taifa” (Ufu 5:9; tazama pia Ufu 7:9-10). Ukweli huo tu watosha kufuta ubaguzi
wa rangi,na chuki za makabila. Wakristo ndani ya makabila na makundi mengineyo wapaswa
kujitambua kwanza kuwa wao ni wakristo kabla ya kutambua kuwa wao ni kabila, jamii, taifa
au wanachama wa chama fulani, tajiri au maskini au kundi lolote jingine. Ni kweli kuwa “damu
ni nzito kuliko maji” Hata hivyo, kwa Wakristo damu ya Kristo yapaswa kuonekana kama
damu ituunganishayo, na si ile ya familia au jamii, kwani, kwa kweli, damu za watu wote ni
nyekundu na zaweza kuingiliana.
c. Jinsi tuwathaminivyo na kuwatendea wengine ndivyo tumthaminivyo na kumtendea Mungu.
Ubunifu wetu na utawala, na hali ya kuweza kufanya maamuzi sahihi, uadilifu, hiari, na uwezo
wa kuonyesha hisia kali, yaonyesha MWM wa kudumu na imara, hata hivyo, tunaweza kutumia
sifa hizi zote kwa nguvu ya utashi wetu. Ni pale sifa hizo “zitakapotumika vibaya” kupitia
dhambi ndipo twaona hali ya kupoteza au kuchafua ule mfano wa Mungu. Hakika, hali kuu ya
dhambi ya mwanadamu yaonekana katika ukweli kwamba yeye hubeba mfano wa Mungu.
Kinachofanya dhambi iwe ni chukizo kuu ni namna mwanadamu anavyotumia “vipawa hivi
vitukufu” kikahaba (Hoekema 1986: 85). Tafsiri tatu hufuatia kweli hizi:
(1) “Kinachosababisha kuua kutajwe [katika Mwz 9:6] kuwa ni kosa lililo chukizo sana
na muuaji lazima aadhibiwe kwa kuuawa ni kwa sababu aliyeuawa ni mtu aliye mfano
wa Mungu, alikuwa kama Mungu, na alimwakilisha Mungu. . . . Kugusa mfano wa
Mungu ni kumgusa Mungu mwenyewe; kuua mfano wa Mungu ni kumfanyia Mungu
mwenyewe uuaji” (Hoekema 1986: 16). Hakika, tunapaswa kuwapenda jirani zetu
kama tujipendavyo kwa sababu sote tumeumbwa kwa mfano wa Mungu. Kwa hiyo,
namna tunavyomtendea mwingine ambaye ni mfano wa Mungu yadhihirisha namna
tumwonavyo, tumtendeavyo, na tumthaminivyo Mungu mwenyewe (Yak 3:9-10;
tazama pia Mith 14:31; 1 Yoh 4:20). Tena, hili ni kweli zaidi katika ndoa (tazama, 1
Pet 3:7).
(2) Hakuna kipengele chochote kati ya vile vizungumziavyo MWM kinachosema kuwa
tuwatendee wasioamini kwa namna tofauti na vile tuwatendeavyo waamini. Tunapaswa
kuwatendea watu wote kwa namna ya usawa, kwa sababu wote ni MWM.
(3) Hata wale walio katika lindi la dhambi wana MWM. Kwa hiyo, kamwe
tusiwatazame watu kama binadamu walio pungufu kwa sababu ya vile walivyo au ya
yale waliyofanya—na twaweza kuomba msaada kwa MWM uwape tumaini ya kuwa
kuna njia bora zaidi ya kuishi.
II. Kiontolojia Wanaume na Wanawake wako Sawa.
A. “Ontolojia” yamaanisha asili ya uhai.
Tunaposema wanaume na wanawake wako sawa kiontolojia, tuna maana kuwa wanaume na wanawake
wako sawa kwa asili na kwa namna ya vile walivyo. Hasa hasa, hii yamaanisha kuwa wanaume na wanawake
wako sawa kithamani, hakuna mmoja wao mwenye thamani ya ‘utu zaidi’, au “afananaye na Mungu zaidi” au
“aliye karibu zaidi na Mungu.” Hivyo ndivyo ilivyo licha ya tofauti za kimaumbile na kiutendaji kati ya
wanaume na wanawake na licha ya ukweli kuwa mwanamume (Adam) aliumbwa kwanza (kutoka katika
mavumbi ya ardhi [Mwz 2:7]) ambapo mwanamke (Hawa) aliumbwa wa pili (kutoka ubavuni mwa Adam
[Mwz 2:21-22]). Hata hivyo, kweli au mazingira hayo hayabadilishi ukweli wa usawa wa wanaume na
wanawake kiontolojia.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
9
B. Usawa wa kiasili kati ya wanaume na wanawake unaonekana kimaandiko kwa njia mbali mbali:
1. Kama ilivyojadiliwa (katika I.C.3, juu), Mwz 1:26-27 inasema kuwa Mungu alimuumba “mtu”
(yaani, “mwanadamu”) ikimaanisha mtu mume na mtu mke; wote wana MWM sawa sawa. Kwa kuwa
wanaume na wanawake ni MWM sawasawa, ipso facto wako sawa kiontolojia.
2. Katika Mwz 1:28-29, baraka za Mungu, “agizo la utawala,” wake na mahitaji ya chakula walipewa
mwanamume na mwanamke sawa sawa.
3. Katika Mwz 2:18, 20, Mungu aliamua kuumba msaidizi “wa kumfaa” Adam, kwa sababu wanyama
hawakuwa “wa kumfaa.”
a. Neno lililotafsiriwa kuwa “wakufanana”ni (neged) linamaanisha “kinachokubaliana
sambamba” (Koehler and Baumgartner, 2001: “neged,” 1:666). Hoekema anafafanua: “Maneno
[‘wakufanana naye kwake yeye’] inamaanisha mwanamke anamkamilisha mwanamume, ni
ziada yake, humtimiliza, huwa na nguvu pale ambapo angekuwa dhaifu, humjaza pale
palipopungua na kumpatia mahitaji yake. Kwa hiyo, mwanamume hajakamilika bila ya
mwanamke. Vivyo hivyo kwa mwanamke ukweli huu wasimama kama ilivyo kwa
mwanamume. Mwanamke, pia, hajakamilika bila ya mwanamume; mwanamume ni ziada ya
mwanamke, anamkamilisha, anatimiza mahitaji yake, anamtia nguvu alipo dhaifu.” (Hoekema
1986: 77)
b. Ukweli kwamba Hawa aliumbwa kutoka katika mwili wa Adamu yadhihirisha usawa wake na
Adamu ki ontolojia, kwa sababu anatokana na kiini kile kile kama Adamu. Adamu aligundua
hili aliposema, “Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu”
(Mwz 2:23).
4. Wanaume na Wanamke wameanguka dhambini sawa sawa (Rum 3:23), na hivyo wanahitaji
ukombozi sawa sawa.
5. Wanaume na Wanawake wamekombolewa na Yesu sawa sawa na kwa namna moja (Yoh 3:16; Mdo
2:21; Rum 10:8-13). Hakika ndani ya Kristo “hakuna mwanamume wala mwanamke,”na wanawake ni
“‘wana’ wa Mungu kama wanaume, kwa imani katika Kristo Yesu” (Gal 3:26-28).
6. Wanaume na wanawake hupokea Roho Mtakatifu sawa sawa na karama za Roho Mtakatifu (Mdo
2:16).
7. Wanaume na wanawake wote ni “warithi ”wa neema ya uzima wa milele. Wana hatima ifananayo
kuhusu wakati ujao (Gal 3:29; 1 Pet 3:7).
III. Licha ya Usawa Wao Wakiwa MWM, na Usawa wao Kiontolojia, Wanaume na Wanawake Wanazo
Tofauti Nyingi.
Tofauti ya jinsi kati ya mwanamume na mwanamke iko wazi. Hata hivyo zipo pia tofauti nyinginezo za
kimaumbile, kikemikali, na hata katika mfumo wa neva ambazo zimo ndani ya kile kilicho “me”na “ke.”
Tofauti hizi zilizo ndani ya kila mmoja huathiri maumbile, ufahamu, Kimwili na kijamii kwa ulimwengu wa
wanaume na wanawake; huathiri namna wanaume na wanawake wanavyochukulia mambo na wanavyotenda.
Tofauti hizi ni zaidi ya vile wavulana na wasichana wanavyolelewa na kujihusisha kijamii, na katika majukumu
ambayo wanaume na wanawake wanatakiwa wahusike kutokana matakwa ya na utamaduni wao. Kwa hakika,
malezi, mahusiano ya kijamii, na utamaduni ni vitu muhimu—ni vitu tunavyohusika navyo, na vyaweza
kuongeza tofauti za kibaiolojia. Zaidi ya hayo, si kwamba kila mtu mume atatofautiana na mtu mke katika
maeneo yote ya ulinganifu—katika kesi nyingi, tofauti za kiume-kike ni tofauti za kitakwimu au ni hali ambazo
zaweza kupangwa kama “jinsi ulimi wa kengele uendavyo mbele na nyuma kwa mpindo.” Hata hivyo, mifano
ifuatayo hutuonyesha namna bayana ambazo kwazo jinsi hizi mbili hutofautishwa. Hizi hali za kijumla yapasa
zizingatiwe kwa sababu zinaathiri jinsi tuonavyo, tuchukuliavyo na kuhusiana sisi kwa sisi. Kugundua hali hizi
kunaweza kufanya angalau mambo mawili muhimu kwetu na kwa uhusiano wetu: (1) Inaweza kutupeleka
kwenye kumuelewa na kumtambua zaidi mwenzi wako wa “jinsi tofauti,” na kuelewa zaidi na kutambua maana
halisi ya “MWM”—namna jinsia zote zinavyoelekea kwenye “kukamilika” kuhusiana na yamaanisha nini kuwa
mwanadamu na ya kuwa hakuna jinsia moja iwezayo kutojisheleza yenyewe. (2) Inaweza kutia nguvu
mahusiano yetu, ikiwa ni pamoja na ndoa zetu, kwa kutusaidia kugundua tunapoenenda kama waliokariri na
kuona haja ya kubadili tabia yetu. Louann Brizendine anasema: “Ikiwa tunakubali ya kuwa baiolojia yetu
inaathiriwa na vigezo vingine, ikiwa ni pamoja na homoni za kijinsia na mbubujiko wake, twaweza kuizuia
kujenga misimamo ambayo kwayo twaweza kutawaliwa. Ubongo si kitu zaidi ya mashine ambayo ina kipaji cha
kujifunza. Hakuna ambacho kina hali zisizogeuka. Baiolojia inayo nguvu yenye kuathiri lakini haifungi uhalisia
wetu. Tunaweza kuubadili huo uhalisia na kutumia akili zetu na ari yetu kusherehekea na ikiwa ni lazima
kubadili matokeo ya homoni za kijinsia katika muundo wa ubongo, tabia, uhalisia, ubunifu—na hatima.”
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
10
(Brizendine 2006: 6-7)
A. Tofauti za Kifiziolojia.
1. Kwa wastani urefu wa mwanamume ni m 1.77 wakati wanamke kwa wastani ni wafupi kwa sm12
(Ispokuwa kama ilivyosemwa, dondoo 1-4 katika kipengele hiki inatoka Archbold n.d.).
2. Kwa wastani nyonga ya mwanamke ni m1.00 wakati nyonga ya mwanamume ni ndogo kwa sm8 kwa
wastani.
3. Wastani wa uzito wa mwanamume ni kilo 78 huu ni sawa kilo 13 zaidi ya wastani wa uzito wa
mwanamke.
4. Wanawake wana maji ya mwili pungufu (52% kwa mwanamke wa kawaida. 61% kwa
mwanamukume wa kawaida). Hii inamaanisha kuwa mwili wa mwanamume unazimua kileo kwa
haraka kuliko ule wa mwanamke, hata kama uzito wao watu wawili ni sawa.
5. Wanaume kwa kawaida wana nguvu zaidi katika kiwiliwili cha juu cha miili yao, hujenga misuli kwa
urahisi na wana ngozi nene zaidi, huchubuka kwa shida na wana uwezo mkubwa wa kihimili
michubuko mikali. Wanaume wana miili iliyojengeka kwa ajili ya mapambano na matumizi ya nguvu.
Viungo vyao vimejengewa uwezo wa kutupa vitu. Fuvu la mwanamume kwa kawaida ni nene na gumu
zaidi ya lile la mwanamke (Conner n.d.)
6. Ni asilimia 5-7 tu ya wanawake ambao wana nguvu zinazolinga na mwanamume wa kawaida.
Wanaume wana kiwango kikubwa cha himoglobini na kiwango kidogo cha mafuta ya mwili, ambayo
huwapa wanaume “imara” kuwa juu ya wanawake“imara” katika michezo yote isipokuwa kuogelea
mwendo mrefu (Dondoo hii na ile ya saba ya kifungu hiki zimetoka katika Rhoads 2004: 144-45, 221-
22).
7. Ngozi za wanawake ni nyepesi kuhisi miguso kuliko za wanaume; wanawake wanaweza kusikia sauti
za juu na sauti nyinginezo mbalimbali na toni za sauti za wanadamu, kugundua harufu zisizo kali na
kutambua kwa usahihi kinachonuka, kutambua na kukumbuka rangi kuliko wanaume (tazama pia,
Brizendine 2006: 17). Wepesi wa wanawake katika kunusa kwa kiwango kikubwa unahusiana na
mabadiliko ya kikemikali katika ubongo wa mwanamke hasa katika kipindi cha hedhi (Brizendine 2006:
86-87).
B. Tofauti za Kiafya.
1. Wanawake wako katika hatari kubwa zaidi ya kupata upofu kwa 78% (Dondoo 1-6 katika sehemu hii
zimetoka kwa Archbold n.d.).
2. Wanaume wako katika uwezekano mkubwa wa kuhusika katika ajali ya barabarani mara 2.7 zaidi.
3. Wanaume wako katika hatari ya kufa kutokana na magonjwa yatokanayo na uvutaji wa sigara mara 4
zaidi.
4. Wanawake wana uwezekano mkubwa wa kuugua kipandauso mara 3 zaidi ya wanaume.
5. Ingawaje wanaume wana uwezekano mkubwa wa kupata mishtuko ya moyo, wanawake waweza kufa
katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya kupata mshtuko wa moyo.
6. Uwezekano wa mwanamume kutaka kujiua ni mara tatu ya mwanamke.
7. Uwezekano wa wanawake wavutao sigara kupata saratani ya mapafu ni kati ya asilimia 20 hadi 70
kuliko wanaume wanaovuta kiwango kile kile cha sigara (Dondoo ya 7-12 katika sehemu hii zimetoka
kwa Canadian n.d.).
8. Dawa aina moja itumiwapo na wanawake na wanaume inaweza kusababisha matokeo tofauti hasi na
chanya (hata dawa za kawaida kama dawa ya aleji na dawa ya kuuwa bakteria), na dawa za kutuliza
maumivu, zifahamikazo kama kappa-opiates, hufanya kazi vizuri zaidi kwa wanawake kuliko kwa
wanaume.
9. Wanawake wana uwezo mkubwa zaidi wa kinga dhidi ya magonjwa, lakini wana uwezekano
mkubwa wa kupata ugonjwa wa seli za mwili kujishambulia (huu ni ugonjwa ambao mwili hushambulia
tishu zake) yapo magonjwa kadhaa kwa wanawake yenye kujidhihirisha hivi.
10. Baada ya wakati wa kukoma hedhi wanawake hupoteza mifupa zaidi ya wanaume, na ndiyo maana
asilimia 80% ya watu wanaopata udhaifu wa mifupa ni wanawake.
11. Wasiwasi huonekana kwa wanawake mara nne zaidi kuliko kwa wanaume, na mfadhaikouko kwa
wanawake mara 2-3 zaidi ya ulivyo kwa wanaume, angalau katika kipindi cha miaka ya uzazi ya
mwanamke kwa sehemu kwa sababu ubongo wa mwanamke hutengeneza homoni ya serotonini kwa
uchache kuliko ile ya estrogeni (tazama pia Brizendine 2006: 2-3, 53, 132-33). Zaidi ya hayo, kadiri ya
10% ya wanawake hupata mfadhaiko utokanao na kuzaa katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya
kuzaa (Ibid.: 181-83).
12. Katika hali ya kujamiiana bila kinga na mtu mwenye maambukizi, wanawake wana hatari ya kupata
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
11
maambukizi ya magonjwa ya ngono mara mbili zaidi ya wanaume na uwezekano wa kupata VVU ni
mara 10 zaidi. Na madhara yatokanayo na magonjwa ya ngono ni makubwa zaidi kwa wanawake kuliko
kwa wanaume—wanawake wana hatari zaidi ya kupata saratani ya uzazi na kutoshika mimba (Rhoads
2004: 108).
C. Tofauti za Kineva na Kikemikali.
1. Ubongo wa wanaume ni mkubwa kuliko ule wa wanawake kwa 9% (tukilinganisha na ukubwa wa
mwili), lakini ubongo wa mwanamume na ule wa mwanamke una idadi sawa ya chembe chembe hai (za
wanawake zimeshikamana kwa karibu zaidi) (Brizendine 2006: 1). Wanawake wana 11% zaidi ya
nyuroni, na wana chembe hai za ubongo (nyuroni) mara nne zaidi ya wanaume zinazounganisha upande
wa kulia na kushoto wa ubongo wao. Hivyo, kwa kawaida ubongo wa mwanamke hufanya kazi
kimtandao, na ule wa mwanamume hufanya kazi katika eneo moja. Wanaume hutegemea zaidi ubongo
wa kushoto kutatua tatizo moja kwa wakati mmoja hatua kwa hatua. Wanawake wana ufanisi zaidi
katika kutumia pande zote za ubongo wao na hivyo hutumia sana ubongo wao wa kulia; wana uwezo wa
kutatua tatizo zaidi ya moja kwa wakati mmoja, na hupendelea kutatua matatizo wawapo katika utendaji
wa shughuli mbalimbali kwa wakati huo huo. Katika kila utendaji wanawake hutumia nyuroni (neurons)
nyingi zaidi ya wanaume. Njia ya mwanamke katika shughuli ya kusema ni bora zaidi na kupona kutoka
katika ugonjwa wa kiharusi, mwanamume kwa shughuli zinazohusiana na anga (Conner n.d.; Rhoads
2004: 27-28; Brizendine 2006: 4-5).
2. Mhimili wa kati wa hisia na kutengeneza kumbukumbu ni mkubwa katika ubongo wa wanawake, pia
muunganiko wa kihisia katika ubongo wa wanawake in mkubwa kuliko kwa wanaume. Wanawake
hutumia maeneo zaidi ya ubongo wao katika mchakato wa kujenga hisia kuliko wanaume, na wana
“kumbukumbu zaidi za hisia” kuliko wanaume. Hivyo, kwa kawaida wanawake wana uwezo mkubwa
zaidi wa kusoma watu-sura, sauti, ishara za hisia n.k. kuliko wanaume, tukiondoa hisia na vitisho
ambazo wanaume wako sawa na wanaume kiufanisi (Brizendine 2006: 4-5, 117-34; Rhoads 2004: 262).
3. Kwa nyongeza, katika ubongo wa wanawake maeneo yanayohusu matamshi ni makubwa kuliko kwa
wanaume, na hivyo kwa wastani wanawake huzungumza zaidi (kwa wasichana mara 2-3 zaidi), husema
kwa haraka, na husikiliza kuliko wanaume (Brizendine 2006: 28-30, 36, and 125-31).
4. Chembe hai za ubongo wakati wa kutunga mimba huanza zikiwa na sifa za kike, lakini katika wiki ya
8 badiliko kuu husambaa katika ubongo wa mimba za kiume ambazo huuwa chembe hai katika idara ya
mawasiliano na kukuza chembe hai za jinsi zaidizenye tabia dume katika viini vyake (Ibid.: 14).
Wanaume hupokea msambazo wa homoni wafikapo miaka 9- 15. Zipo tabia zinazotawala zaidi kwa
wanaume kwa sababu ya kiwango kikubw acha homini hii ya testosteroni ambayo ipo mara kumi zaidi
kuliko kwa wanawake. Hii huongeza hali ya kimisuli (mfano, ujasiri, umiliki, ushindani,uwezo wa
kiufundi) na kupunguza tabia za kike(mfano, mapenzi kwa watoto, kutunza nyumba, midoli) mririko na
tabia (kwa wanaume na wanawake). Viwango vya testosteroni katika mimba ni muhimu zaidi kuliko
katika utu uzima ikihusianishwa na tabia na matakwa (Rhoads 2004: 28-34, 49, 57-59, 153-54, 172).
Rhoads anasema: “Umri wa wanaume na wanawake unapoongezeka, tofauti za kijinsi huendelea
kupungua. Kimsingi sayansi ya jamii imegundua kwamba wababu ni wapole na wenye upendo kuliko
wababa, na yakuwa wamama huwa huru zaidi kadiri umri unavyoongezeka.Watafiti wanaotafuta sababu
za kibaiolojia hufikiri kuwa badiliko hili laweza kusababishwa kwa sehemu na ukweli kuwa wanaume
hupoteza testosteroni kadiri wanavyozeeka, wakati wanawake hupoteza estrogeni kwa haraka zaidi
kuliko wapotezavyo testosteroni.” (Ibid.: 49) Zaidi ya hayo, wanaume wanapopata hofu au
washindwapo jambo kiwango chao cha testosteroni hushuka; na wanapofanikiwa huongezeka;
wanawake hawaonekani kupokea hilo wanaposhinda au kufaulu jambo fulani.
5. Wakati ubongo wa wanawake unaposafishwa na testosteroni ndani ya mimba, mabinti wa miezi 18
hupitia kile kijulikanacho kama “balehe changa” ambayo hudumu miaka miwili ambapo ovari huanza
kutengeneza kiwango kikubwa cha estrogen ambayo “hulainisha ubongo wa binti huyu mdogo.” Hii
humaanisha ukuaji wa ovary na ubongo kwa kusudi la uzazi, lakini pia huchochea mzunguko wa
ubongo na vituo vya kuchunguza, mawasiliano, hisia na kuimarisha mihemko ya ghafla ili kutengeneza
muunganiko wa kijamii wenye msingi katika mawasiliano na masikilizano. Hivyo, kuanzia kuvunja
ungo hadi kukoma hedhi, wanawake huathiriwa na mtiririko wa homoni katika mzunguko wa ubongo,
na hivyo kiwango chao cha kufikiri na kuhisi kuongezeka. Zaidi ya hayo mimba hubadili kemia na
ubongo wa wanawake. Baada ya kukoma hedhi, nah ii misukumo ya homini, wanawake huonekana
kuwa na uthabiti katika hisia, ingawa si kali, na wenye mwitikio pungufu kihisia (Brizendine 2006: 19-
22, 32-35, 97-116, 135-52).
D. Tofauti za Haiba na Mtazamo.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
12
1. Ipo tofauti kati ya wanawake na wanaume katika kupendelea na mtazamo kuhusu, kujamiiana na
tofauti hiyo huongezeka kadiri wakuavyo. Katika ubongo wa wanaume kitovu kinachahusika na swala
la kujamiiana ni kikubwa mara 2-2½ zaidi ya kile cha wanawake (Ibid.: 5, 91). Tafiti zinaonyesha kuwa
idadi iliyo mara saba zaidi ya wanaume kulinganisha na wanawake, wameripotiwa husikia hamu ya
kufanya ngono zaidi ya mara moja kwa siku, na wanawake mara nne zaidi ya wanaume wamesema
hawajahisi “chochote kabisa.” Kwa wastaniwanaume husema hufikiri kuhusu ngono kati ya mara tatu
hadi tano kwa siku; wanawake husema mara kadhaa kwa wiki au mwezi. Katika umri wa miaka 20-30
wanaume hufikiri kuhusu ngono zaidi ya mara moja kwa dakika, wakati ambapo wanawake hufikiri
mara moja kwa siku, au mara tatu au nne kwa siku katika siku zao za rutuba zaidi (Ibid., 91). Kwa
wanaume wengi kuliko ilivyo kwa wanawake, ngono ya mara kwa mara na ipendezayo yahusianishwa
kwa karibu na furaha katika ndoa. Ndani na nje ya ndoa wanawake husema hujihusisha na ngono ili
kushirikiana hisia na mapenzi; wanaume hutoa sababu ambazo ni za kimwili zaidi, kama vile hitaji la
kuridhishwa kingono.Hali kadhalika wanaume wanaofanya uasherati kwa sehemu kubwa hufanya hivyo
kwa sababu ya kutafuta ladha na misisimko tofauti katika ngono, wakati ambapo wanawake waweza
kufanya hivyo kwa kutafuta utoshelevu wa kihisia wanaoukosa kwa waume wao. Wanaponyimwa
ngono, wanaume kimsingi watachukia au kukasirika kuliko wanawake (Dondoo 1-3 katika sehemu hii
imetoka kwa Rhoads 2004: 26, 48-66, 121, 152-53, 173, na 252).
2. Kiwango cha testosteroni hudhihirika katika, muonekano wa wanaume; vile vile ukweli huo ni sawa
kwa wanawake kuhusiana na kiwango cha estrogeni. Kiwango cha estrogeni kina uhusiano na uzuri na
rutuba ya uzazi. Homoni hizi zina uhusiano na utungaji wa hisia za mvuto kwa wanaume na wanawake.3
Kwa kawaida wanaume hufikiri kuwa wanawake huvutia zaidi katika kipindi ambacho kiwango chao
cha estrogeni kiko juu zaidi (kati ya miaka 20-40); wanawake wenye umri zaidi waonekanao kuwa
wadogo kuliko umri wao wana kiwango cha juu cha estrogeni kuliko kile cha kawaida. Kwa hakika,
utafiti unaonyesha kuwa uzuri wa mwanamke huathiri ubongo wa mwanamume kimsingi, katika hali
kama ya mwanamume mwenye njaa apatapo chakula au mlevi apatapo dozi. Wanaume huthamini sana
uzuri wa maumbile ya wapenzi wao kuliko wanawake kwa wapenzi wao wa kiume. Wanaume
huonyesha upendeleo kwa wanawake wenye umri mdogo kidogo kuliko wao, wenye ngozi nyororo,
nywele zenye mng’ao, midomo iliyojaa, maumbile yenye kiuno ambacho ni kama 1/3ya nyonga. Kwa
upande mwingine, wanawake hupendelea wanaume wenye nguvu, warefu kidogo kuliko wao, wakubwa
kidogo kiumri kuliko wao, hujali pia vyanzo vya mapato vya mwenzi, uwezo na hadhi kuliko wanaume.
Matakwa haya yapo kwa wanawake na wanaume wa jamii zote duniani, bila kujali asili au rangi (Ibid.:
56; Brizendine 2006: 61-63, 85-86).
3. Wanawake huthamini ukakamavu, nguvu na ujasiri kwa wenzi wao, ambapo wanaume kwa ujumla
hawavutiwi na wanawake wapendao kutawala na huona kuwa wanawake wapendao kutawala na
mashindano ya kuwa hawavutii (Rhoads 2004: 152-53, 173).
4. Wanaume huonekana kuwa wakaidi zaidi, wasiopenda kubadilika, na hutaka nafasi zaidi kuliko
wanawake; makundi ya wanaume huweza kushikamana katika kufanya mambo wayapendayo, lakini
wavulana huvutiwa zaidi na vitu kuliko watu. Kwa upande mwingine wasichana tangu utotoni huvutiwa
zaidi na mahusiano ya karibu na hasa rafiki wa karibu.4 Hivyo, taadhima ya wanaume yatokana na
uwezo wao wa kutunza uhuru wao kutoka kwa wengine, wakati kwa wanawake inatokana na uwezo
wao wa kutunza mahusiano ya karibu na wengine (Brizendine 2006: 41).
5. Dondoo hizo hapo juu zaonyesha tofauti za msingi za tabia kati ya jinsi kama inavyoonekana katika
Mwanzo 2-3, kabla na baada ya “anguko” la mwanadamu. Wanaume huonekana kuwa na uhusiano wa
uhakika na “kazi”na uzalishaji kuliko walivyo wanawake.5 Katika Mwz 2:15 Mungu “akamtwaa
3Rhoads anaongezea kwamba, ingawaje uso wa mwanamume waweza kuonekana wa kiume hasa, wa mwanamke mara
chache ungeonekana wa kike hasa” (Rhoads 2004: 57). Kwa maana hiyo, ingawaje kuna, kwa kweli, viwango tofauti vya
testosteroni kwa mwanamume, inaonekana ipo “aina” moja ya msingi kwa mwanamume wakati ambapo, aina tofauti za
viwango vya testosteroni huonekana kutokea katika “aina mbili za wanawake” (ina maana. Wale ambao wana sifa za kike
hasa na wale ambao wana sifa na tabia mchanganyiko za kike na kiume”) (Ibid.: 29-32).
4Brizendine anadondoa ya kuwa mchanganyiko wa oxytosini na dopamini husababisha msingi wa kibaiolojia unaosukuma
kujamiiana na matokeo yake ni kupunguza msongo. Uzalishaji wa oxytosini na dopamini huchochewa na estrogeni za ovari
wakati wa kubalehe, na kwa wakati wa maisha ya rutuba ya mwanamke. Hii ina maana wasichana waliobalehe hupata raha
zaidi katika muunganiko kuliko kabla ya balehe- “ni hisia zile zile za dopamini ambayo walevi wa kokeini au heroini
hupata watumiapo madawa hayo” (Brizedine 2006: 37-38).
5Tofauti iliyopo kati ya wanaume na wanawake kuhusiana na kazi na shughuli nyinginezo si swala la akili hasa (jinsi zote
zina kiwango sawia cha akili), uwezo, au kipaji – lakini ni za kimwelekeo au mwenendo; tofauti za kihomoni zaonekana
kuwa ndizo sababu hasa ya tofauti hizi (Brizendine 2006: 7-8).
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
13
mwanamume akamweka katika bustani ya Edeni ailime na kuitunza.” Mwanamume pia alipewa wajibu
wa kuwapa wanyama majina (Mwz 2:19-20). Zaidi ya hapo, kama matokeo ya dhambi ya Adamu,
adhabu aliyotoa Mungu iliyompasa ilikuwa ni kuilani ardhi, hivyo kuzidisha ugumu wa kazi kwa
mwanamume (Mwz 3:17-19). Kwa upande mwingine mwanamke aliumbwa kwa kusudi la kuwa
“msaidizi” wa mwanamume (Mwz 2:18-22); hiyo yaonyesha kwa asili wanawake ni thabiti katika
kumudu mazingira ya mahusiano. Uwezo wao wa kumudu mazingira huonekana kihalisi, kipekee kwa
jinsi wanawake wanavyozaa na kulea. Hali kadhalika dhambi ya Hawa ilihukumiwa adhabu ambayo
ilielekezwa katika asili ya mwanamke maalum: maumivu zaidi katika uzazi na mabadiliko ya
mahusiano na mume (Mwz 3:16).6
E. Tofauti za Tabia.
1. Utafiti umegundua kuwa wanaume wanapenda ushindani na wanawake ushirika; Kwa kweli si tu
kwamba wanaume hupenda ushindani kuliko wanawake bali pia hufanya vizuri mahali penye mazingira
ya ki-ushindani. Tabia hii huonekana hata katika uchaguzi wa aina tofauti ya ucheshi—wanawake
hupenda kucheka na wengine na kutumia utani kama njia ya kufanya wengine wajisikie vizuri;
wanaume huwasiliana kwa mizaha, kebehi na vijembe (Dondoo ya 1-4 katika sehemu hii zimetoka
Rhoads 2004: 134-36, 140-43, 156, 171-72, 193, 198, 204, and 219-21).
2. Kwa ujumla wanaume ni jasiri, huweza kukabili hatari zaidi, na hujihusisha na tabia hatarishi zaidi ya
wanawake. Kuna sababu za kibaiolijia kwa jambo hili, ambazo huhusishwa na testosteroni za
mwanamume ndani ya mimba, pamoja na kiwango haba cha serotonin kwa wanaume wakilinganishwa
na wanawake, na tofauti ya muundo wa ubongo kati ya wanume na wanawake. Kwa upande mwingine,
wanawake kwa ujumla ni wapole na wapenda amani wakilinganishwa na wanaume kwa sababu ya
tofauti zao za kihomoni (kiwango kikubwa cha serotonin, oxytocin, na estrogen wakilinganishwa na
wanaume).
3. Kutokea utotoni hadi uzeeni wanawake wanapenda watoto kuliko walivyo wanaume, na wana uwezo
wa kuhisi maono ya mwingine, wapole, wenye uwezo wa kulea kuliko wanaume. Wanawake wana
uwezo wa kulea/kutunza kuliko wanaume. Hizi ndizo sababu za kibaiolijia zisababishazo hayo. “Uwezo
huo husabishwa na homoni iitwayo peptide oxytocin. Kwa wanaume na kwa wanawake, oxytocin
huchochea muunganiko na hisia kuwa katika hali tulivu. Kwa wanaume hii huachiliwa kwa kiwango
kikubwa wanapofikia kileleni katika kujamiiana. Kwa wanawake, oxytocin inaachiliwa kwa kiwango
kikubwa katika kipindi cha mimba na kunyonyesha.” (Rhoads 2004: 198) Wanawake na wamama
wanapenda watoto wadogo kuliko wanaume na wababa. Tafiti zimeonyesha kuwa wanawake wamama
wana uwezo mkubwa wa kusoma lugha za mwili kuliko wanaume wababa, kutambua hisia za watoto,
kusoma nyuso za watoto, na kutofautisha sauti za vilio za watoto na kelele; watoto wanaonekana
kupendelea zaidi sauti za mama zao.
4. Tofauti hizo hapo juu zaweza kuweka msingi wa “pambana-au-kimbia” mwitikio unaojitokeza katika
mazingira yanye msongo mkubwa kwa wanaume; kwa upende mwingine, tafiti huonyesha ya kuwa
mmwitikio wa wanawake katika mazingira yenye msongo mkubwa huwa ni kwa namna ya “tenda-nauwe
rafiki” kuliko kwa ku“pambana-au-kimbia.” Kutenda kunahusisha kujilinda kibinafsi na uzao dhidi
ya madhara; kufanya rafiki huendeleza wazo la kujilinda kwa makundi ambayo hutoa msaada wa
pamoja wakati mwanamke anaposhindwa kujihudumia na watoto wake (tazama pia Brizendine 2006:
41-42). Kwa hiyo, wanawake ni wepesi kutumia masaada wa kijamii wawapo katika hali ya
matatizo/msongo kuliko walivyo wanaume. Wanaume kitabia hujiunga katika kundi kwa lengo la
kushambulia, wanawake kwa lengo la kujikinga.
5. Wanaume na wanawake kwa kawaida wana miitiko tofauti na namna tofauti za kutendea kazi
matatizo ya kihisia. Wanaume na wanawake, wote wanapenda na hujisikia vizuri kuwa karibu na watu
wenye furaha, lakini ni wanawake peke yao wameripoti ya kuwa wanajisikia vizuri pia wakiwa karibu
na mtu mwenye huzuni. Wanaume wanapopitia wakati mgumu kihisia hukwepa kuonana na wengine
(Dondoo ya 5-6 katika sehemu hii zimetoka Brizendine 2006: 28-30, 36, na 125-31).
6. Ingawaje wanaume na wanawake huripotiwa kuwa huhisi kiwango sawa cha hasira, wanatofautiana
katika mchakato wa jinsi wanavyoshughlikia hasira zao. Wanaume, hasa wanaume vijana wana
kiwango kikubwa cha testosteroni, hupata hasira haraka, na huonyesha hasira kwa ukali zaidi. Kwa
kawaida wanawake hawadhihirishi hasira yao; namna wanavyoonyesha hasira na ukali ni kwa jinsi isiyo
6Hii mienendo inaonema na matima data za talaka katika tamaduni mbali mbali: wanawake huwataliki wanaume kwa
kutokufanya kazi kwa bidii katika ajilra zao;wanaume hawawapi talaka wake zao kwa sababu hiyo. Kwa upande
mwaingine, wanaume huwapa talaka wake zao kwa kutofanya kazi za nyumbani vema; wanawake hawawapi wanaume
talaka kwa sababu hiyo. (Rhoads 2004: 61). Tazama sehemu V.C.1, chini.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
14
wazi ingawaje ni halisi.7
F. Tofiti za watoto wachanga.
1. Kitoto cha kike kichanga cha umri wa siku moja huguswa sana na sauti ya mtu anayehitaji msaada
kuliko kitoto kichanga cha kiume cha siku moja. Wasichana wa siku tatu huweza kutazamana na mtu
mzima kwa kiwango mara mbili ya wavulana wa umri huu. Wasichana wataendelea kutazama endapo
mtu atakuwa akizungumza; kwa wavulana hawaoni tofauti. Wasichana wa wiki moja wanaweza
kutofautisha sauti za kilio cha mtoto mchanga na sauti nyinginezo, wakati wavulana hawawezi kwa
kawaida. Wasichana wa miezi minne wanaweza kutofautisha picha za watu wanaowajua na
wasiowajua; wavulana hawawezi. Kwa upande mwingine wavulana wa miezi mitano huvutiwa zaidi na
maumbo ya mche, na taa iwakayo na kuzima kuliko wasichana; hutabasamu na kufurahia kanakwamba
zina uhai, kitu ambacho wasichana hufanya mara chache (Dondoo 1-4 katika sehemu hii zimetoka
Rhoads 2004: 5, 23, 25, 145, na 154; tazama pia, Brizendine 2006: 15-18).
2. Vichanga vya mwaka mmoja huweza kutofautisha watoto kwa jinsi na hupendelea kuangalia watoto
wa jinsi yao,hata kama msichana amevaa kaptula ya kaki na ameshika ngoma na mvulana amevalishwa
gauni na ameshika mwanasesere.
3. Wasichana wa umri kati ya miezi kumi na mbili na ishirini wanaonyesha uwezo wa kuguswa na hisia
za wengine kuliko wavulana wa umri huo. Wanapofikia miaka miwili wavulana hukimbiakimbia zaidi
na, na wanapoangalia picha yenye magari na abiria ndani yake, wavulana huvutwa na magari zaidi na
wasichana huvutwa na abiria waliomo ndani yake.
4. Wavulana wanaweza kukiri kwa uthabiti kuliko wasichana katika umri wa miezi kumi na tatu; tofauti
ya ujasiri kijinsi huonekana kuanzia miaka miwili, na hapo ni kabla tofauti ya tabia za kike na kiume
kudhihirika. Rhoads anaongezea, “Endapo mahusiano kijamii huonyesha wazi tofauti nyingi za ujasiri
kati ya jinsi, twatarajia wanaume kuwa jasiri zaidi kadiri umri wao unavyoongezeka, kwa kuwa watu
hujihusisha na majukumu yatokanayo na jinsi kadiri wanavyokuwa. Lakini kwa hakika, mambo huwa
kinyume: tofauti za jinsi kupotea kadiri wanavyozeeka” (Rhoads 2004: 145).
G. Masomo yahusuyo mwanadamu kiulimwengu na kupitia tamaduni.
1. “Kati ya tofauti zionekanazo wazi katika kila jamii ulimwenguni zilizopo kati ya wanaume na
wanawake, mgawanyo wa kazi kwa jinsi, malezi ya watoto kwa wanawake, ujasiri zaidi kwa wanaume,
na kutawala eneo la kimadaraka katika jamii kwa wanaume” (Ibid., 17-18; Dondoo 1-6 katika sehemu
hii zimetoka kwa 2004: 17-18, 26, 151-52, 155, 169, 195, na 203).
2. “Jamii ambazo wanawake hurithi madaraka kisiasa, kiuchumi na mamlaka katika jamii zaidi ya
wanaume haipo; kwa hakika, hakuna ushahidi kama ziliwahi kuwepo. Hata jamii za kifalme ambazo
urithi wa utawala hufuata uzao wa wanawake ni adimu” (Ibid., 151).
3. Kinyume chake, utafiti mmoja wa jamii 186 umegundua kuwa wamama ndio walezi wakuu wa
watoto wachanga (wa chini ya miaka miwili) asilimia 90 ya jamii; wanaume duniani kote hutoa
mchango kidogo sana wa malezi ya watoto wachanga, na duniani kote wamama hutumia muda mwingi
sana si tu na watoto wachanga na chekechea, lakini mpaka umri wa miaka kumi, zaidi ya wababa.
“Duniani kote, wasichana huonyesha upendo zaidi kwa watoto na hutumiwa kama yaya kuliko
wavulana. Hakuna jamii iliyofanikiwa kufuta tofauti hizi za kijinsi iwe ni katika maisha ya kijamii kule
Israeli au jamii ya wamarekani, ingawa wengi wamelipa hitaji hilo kipaumbele” (Ibid., 26). Zaidi ya
hayo, “katika tamaduni zote zilizotafitiwa, wasichana hupenda midoli na huigiza kulea kuliko wavulana.
Wavulana wa miaka minne wanapotakiwa kulea mtoto huonyesha kutojali, lakini wasichana wa miaka
minne hufanya hivyo kwa kumaanisha.” (Ibid., 195)
7Katika kuzungumzia kuhusu wasichana ambao hawaja balehe,Bizendine anadondoa ile asili ya kutatiza ya wasichana ya
ujasiri wakilinganishwa na wavulana kwa wakati huo huo kwa kutokuelewa akishuhudia kuhusu asili ya wanguko la
mwanaduamu(wasichana wazuri wadogo wakiwemo): “Wachana wadogo kwa kawaida hawadhihirishi ujasiri katika
mazingiar ya michezo yenye ugomvi au zahama, mieleka, na ndondi kama wafanyavyo wavulana. Kwa wastani, wasichana
wanaweza kuwa bora katika ujuzi wa kijamii, uwezo wa kuwawezesha kutumia kila kilicho katika uwezo wao kupata
wanachotaka, na wanaweza kufanya chochote kutimiza malengo yao. Je malengo hayo ni yapi kama yaonekanavyo kwa
akili za wasichana wadogo? Kughushi maingiliano, kutangeneza jumuiya, na kupanga na kukusanya ulimwengu wa
kisichana ili yeye awe katika kiini chake. Hapa ndipo ambapo ujasiri wa akili ya kike huchukua nafasi- hulinda
kilichomuhimu kwake, ambacho siku zote hufaa, kwa mahisiano. Lakini ujasiri unaweza kufukuza wengine, na hilo
hushusha, lengo ya akili ya kike. Hivyo msichana hutembea katika mstari ulio kati ya kuhakikisha ya kuwa yeye yuko
katika nafasi ya kiini katika ulimwengu wake wa mahusiano na katika hatari ya kupoteza hayo mahusiano,.” (Brizendine
2006: 28-29)
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
15
4. Maswala ya michezo ya kiume, kama mieleka, mapambano, na michezo ya nguvu,yaonekana ni ya
kiulimwengu katika tamaduni zote. Wasichana wasomao hujitahidi kukwepa malumbano, ambapo
wavulana wa umri wao hufurahia (tazama pia Brizendine 2006: 24, 40).
5. Tofauti za kihaiba kama uhuru na urafiki zimekuwako kati ya vizazi, viwango vya kielimu, na
mataifa. Kufanana kwa kimsingi kumekuwako katika tamaduni mbalimbali. Katika nchi zinazojali
usawa kati ya wake na waume tofauti za kimaumbile na mwenendo baina ya wanawake na wanaume
hudhihirika zaidi kuliko katika jamii za kawaida.
6. “Wanaume na wanawake, katika tamaduni sita, walipoulizwa kama wangependa kuwa watu wa jinsi
gani, wanawake walitumia vivumishi kama enye upendo, enye huruma, na mkarimu, ambapo wanaume
walitumia maneno mpigania haki, mwenye kutawala, mwenye kuweza kushindana” (Rhoads 2004: 152).
IV. Athari za Tofauti za Kijinsi Katika Mahusiano Ya Kibinafsi.
Tofauti kati ya wanaume na wanawake hapo juu zaonekana katika namna mbalimbali wanaume na
wanawake wawapo katika mahusiano. Tunapozielewa hali hizi itatusaidia kustawisha mahusiano yetu na wenzi,
na itatufanya tuache kuwafanya wawe kama tutakavyo sisi. Tofauti za Me-Ke zaweza, kwa hakika kusababisha
mizozo katika mahusiano, lakini uelewa wa vyanzo vya tofauti hizo waweza kutusaidia kutatua mizozo
inapotokea. Ifuatayo ni aina ya mizozo hiyo inayojitokeza kwa kawaida:
A. Mizozo ya Kimahusiano Itokanayo na Tofauti za Me-Ke.
1. Malalamiko makubwa waliyonayo wanaume kuhusu wanawake: wakati wote wanawake wanajaribu
kuwabadilisha; lalamiko kubwa wanawake walilonalo kuhusu wanaume: wanaume hawasikii.
2. Wanaume wakati wote hudhani wanawake wanataka ushauri na utatuzi wa matatizo, na ya kuwa hiyo
ndio njia bora zaidi kutoa msaada na kuonesha upendo; wanawake mara nyingi wanataka kutiwa moyo
na mtu wa kuwasikiliza kikweli. Hata hivyo, mwanamke anapojaribu kumbadilisha, au kumwendeleza,
au kumsahihisha, au kumpa ushauri mwanamume, yeye huona ameambiwa si mshindani, au hajui
kufanya kitu fulani, au hajui kufanya kitu fulani mwenyewe.
3. Wanaume wakati wote hujaribu kubadili hisia za wanawake wanapokuwa wamekerwa kwa kuwapa
utatuzi wa tatizo, na wao hutafsiri kuwa hisia zao zimepuuzwa na kutotambuliwa. Wanawake mara
nyingi hujaribu kubadili tabia ya mwanamume kwa kutoa ushauri wa bure na kumkosoa na kuwa
“kamati ya kuendeleza nyumba.”
B. Uelewa wa Tofauti za Me-Ke Katika kutatua Mizozo.
1. Wanawake wanapofadhaishwa ,huo si wakati wa kuwapa utatuzi, ingawaje hiyo itafaa baadea wakati
wa mbeleni atakapotulia. Mwanamume huridhishwa na ushauri na kukosolewa anapoviomba. Wanaume
wanataka kufanya maendeleo wanapohisi kufuatwa kama watatuzi wa tatizo na si kama tatizo lenyewe.
2. Wanaume wana uhitaji mkubwa wa hadhi na uhuru (hukazia hali ya upekee na tofauti); wanawake
wana uhitaji wa penzi na muunganiko (mkazo katika ukaribu na kuwa sawa).
3. Wanawake huhitaji kupokea matunzo, maafikiano, kuheshimiwa, kupendwa, uhalali, na
kuhakikishiwa. Wanaume wanahitaji kuaminiwa, kukubaliwa, kutambuliwa, upendezewaji,
kuthibitishiwa, na kutiwa moyo.
4. Wanawake huhamasika wanapojisikia wa kipekee au wanapopongezwa. Wanaume wanahamasika
wanapojihisi kuhitajiwa. Hofu kubwa ya mwanamume ni pale ajionapo kuwa na viwango vya chini au
visivyo na ushindani, ingawaje hatasema hivyo kamwe (Relationship n.d.).
5. Brizendine anahitimisha akiwa na matokeo ya kazi zake za kitabibu (neuropsychiatry): “Wakati
wanaume na wanawake wanapoongezeka umri wa kati na uzeeni, wanapopata uzoefu wa maisha zaidi,
na wanapojisikia salama zaidi, mara nyingi hujisikia vizuri sana wakionyesha hisia zao kwa kiwango
cha juu, pamoja na wale—hasa wanaume—ambao walikuwa na mkandamizo wa kimawazo. Lakini
hatuwezi kukwepa ukweli kuwa wanawake wana uwezo tofauti wa kuhisi, uhalisi, mwitikio na
kumbukumbu wanapolinganishwa na wanaume, na tofauti hizi—kutokana na mfumo wa utendaji wa
ubongo—ndicho kiini cha migogoro mingi. Evan na Jane walifikia hatua ya kutambua uhalisia uliopo
kati yao. Wakati Jane alipoanza kulia ghafla pasipo chanzo kufahamika, Evan alijihoji endapo
alishindwa kuwajibika katika eneo fulani. Wakati Jane aliposhindwa kufanya ngono kwa kuwa
amechoka, Evan alipambana na utashi wake na kumwelewa. Wakati Evan alipokosa furaha na
kuonyesha kukerwa na mwenye hali ya kummiliki, Jane alitambua kuwa hakuwa amemvutia
vyakutosha kingono (Brizedine 2006: 133-34)
V. Ndoa Katika Muktadha wa Tofauti Kati ya Wanaume na Wanawake
Tukiwa tayari tumeziona tofauti kati ya wanaume na wanawake, haishangazi kwamba Mungu aliipanga
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
16
ndoa katika mpangilio wa uumbaji (Mwz 2:24). Ndoa iliyojizatiti katika misingi ya kibiblia (Efe 5:21-33; Kol
3:18-19; 1 Pet 3:1-12) ni mazingira bora ambapo wote mume na mke waweza kupongezana na kupata
utoshelevu.
A. Ndoa peke yake ndiyo iwezayokuwafanya watu wawe na furaha, na afya na hali njema kiuchumi.
Tafiti nyingi zashuhudia kuwa ndoa yenyewe hufanya watu wawe na furaha zaidi, na afya zaidi na hali
yao kiuchumi huwa njema zaidi (Waite and Gallagher 2000: passim; Morse 2001: 83-158; Thomas and Sawhill
2005: 57-74; Rector, Fagan, and Johnson 2004: passim; Stanton 2003-2004: passim) Nock anafupisha baadhi ya
taarifa za utafiti, kama ifuatavyo: “Walio ndani ya ndoa kimsingi wana afya zaidi; huishi maisha marefu zaidi,
wana kipato zaidi, wana afya njema kiufahamu na maisha bora ya ngono, na wana furaha kuliko wasio ndani ya
ndoa. Zaidi ya hayo, walio ndani ya ndoa wana kiwango cha chini cha kujiua, ajali za kufisha, magonjwa ya
muda mrefu, ulevi, na mfadhaiko kuliko watu wengine. Kwaweza kuwepo kutokukubaliana kuhusu kiwango
cha matokeo hayo, lakini kwa hakika yanatokana na ndoa, na si uchaguzi wa kibinafsi. Haitokei tu kwamba
wana ndoa wawe na afadhali kuliko wasio ndani ya ndoa; bali ndoa hubadili watu kwa namna ambayo hutoa
matokeo yenye faida hizi.” (Nock 1998: 3, dondoo zimeachwa) Zaidi ya hayo, kuna matokeo mazuri yaliyo
wazi-kimwili, kiakili, kihisia, kielimu, kijamii, na kitabia-kile ndoa ifanyacho kwa ajili ya watoto (Rector,
Fagan, na Johnson 2004: passim; Waite na Gallagher 2000: 124-49; Morse 2001: 83-158). Kuishi kinyumba
kamwe hakulingani na ndoa kwa kiwango chochote kile (Morse 2001: 64, 93; Thomas na Sawhill 2005: 57;
Wilson 2002: 3-7, 38-40).
B. Mtokeo mazuri ya ndoa yanaonekana kwa uwazi zaidi kwa wanaume.
“Utamaduni wa ndoa na ubaba hustaarabisha wanaume, na waingiapo kwenye ndoa au kuwa baba
kiwango chao cha testosteroni hushuka” (Rhoads 2004: 147). Hivyo, ndoa huwafanya wanaume kuwa na amani
na waungwana zaidi. “Baada ya watafiti kudhibiti asili, mapato, wazazi, elimu na mambo mengine ya kijamii
yageukayo, wanagundua kuwa muundo wa familia huamua kiwango kikubwa cha uhalifu usababishao
kufungwa jela” (Ibid.). Pia, muundo wa familia peke yake huonekana kuathiri kipato cha familia—tafiti kadhaa
zaonyesha kuwa wanaume walio ndani ya ndoa wana kipato kikubwa kuliko walio nje ya ndoa, na ya kuwa
zaidi ya nusu ya hiyo tofauti “ni matokeo ya moja kwa moja ya ndoa” (Thomas na Sawhill 2005: 60; tazama pia,
Wilson 2002: 17). Ingawaje karibu tafiti zote huhitimisha kuwa wanawake hufaidika kutokana na ndoa, kwa
sababu ya mabadiko makubwa kwa wanaume, wanaume hufaidika zaidi; wanaume hufaidika “kwa kule tu
kuoa” (Nock 1998: 3; tazama pia, Rhoads 2004: 92, 253).
C. Asili ya ndoa husababisha badiliko kwa wanaume na wanawake.8
1. Wanawake hujali zaidi kuhusu vipato na hadhi za waume wao, lakini wanaume hawathamini vitu
hivyo kwa wake zao, yaonekana katika tamaduni mbalimbali katika taarifa za talaka. “Tafiti kadhaa
zimeonyesha kuwa wanawake huwataliki wanaume wasiojibidiisha na waasio na kazi yenye kipato
kizuri. . . . Kinyume cha hayo, waume wenye wake wenye tamaa ya makuu au kipato kinachoongezeka,
hao ni rahisi kuwapa talaka. Ni mara chache pia wanawake wangetaliki wanaume kwa kushindwa
kufanya kazi za nyumbani, wanaume huweza kutoa talaka kwa mazingira kama hayo.
Tafiti ya kianthropolojia ya tamaduni mbalimbali inapochunguza migongano ya kindoa katika
jamii 160 za kisasa na kale inagundua hali hii ipo kila mahali. Kwa kuwa wengi wao katika jamii hizi ni
masikini, waweza kufikiri kuwa wanaume wangewataliki wake zao kwa kuwa hawafanyi kazi ya ajira
ili kusaidia matumizi ya nyumbani. Lakini kama Laura Betzig anavyoripoti, talaka zitokanazo na sababu
za kiuchumi ‘zimetengwa wazi wazi kutokana na jinsi. Waume hupewa talaka kwa kushindwa kuleta
mahitaji nyumbani, wake kwa kushindwa kuyaandaa.’” (Rhoads 2004: 61)
2. Kwa upande mwingine, tafiti nyingi zimeangalia ndoa zenye furaha. “Tafiti za wanandoa wakomavu
pia zimegundua kuwa wanawake hawapendi waume ambao ni wepesi kukubaliana na jambo, hata
wakati ambapo waume zao huwakubalia wao! Tafiti moja ya kina inalinganisha nguvu katika ndoa na
furaha katika ndoa, yaweza kupimwa kwa vipimo vyenye mipaka. Nguvu katika ndoa ni ngumu zaidi
kuipima, lakini wanasayansi ya jamii hujaribu kwa kuuliza maswali (Ni nani wa kwanza kutafuta
usuluhishi baada ya mgogoro? Ni nani anaamua wapi muishi?) na kwa kuwaangalia wanandoa
wanapojadili jambo (nani anatoa amri, dakiza au patanisha).Tafiti moja kati ya zaidi ishirini za aina hiyo
8Ndoa ya mke mmoja ni, kwa hakika, ianyokubalika, na kuachanakumepingwa vikali katrika biblia (tazama Mwz 2:24;
Math 19:3-9; 1 Kor 7:10-14). Haishangazi kweli hizi zitokanazo nz hali za kijamii. Rhoads anasema, “Ndoa ya mke
mmoja ni bora kuliko ile ya mke zaidi ya mmoja, ambayo huwaacha wanaume wengi bila ya wanawake. Hivyo
huhamasisha ugomvi kati ya wanaume kushindania wanawake. Na pia ni bora kuliko ile ya kuoa na kuacha kasha kuoa
tena, ambayo huwa na uwezekano wa ugomvi kwa ajili ya wivu kati ya wapenzi waliotangulia na wa sasa” (Rhoads 2004:
146).
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
17
imepata kimoja kisichobadilika: Ndoa ambazo mwanamke hutawala hazina furaha ya kweli,na mke
katika ndoa ya jinsi hii walikosa furaha zaidi ya waume wao. (Utawala wa mme unaposaidia ndoa , ni
kwa kiasi, si kidikteta, kutawala; ndoa haiwi yamafanikio mke anapokosa ushawishi kwa mumewe.) . . .
Kwa njia moja, katika ndoa za kiasili wanaume na wanawake hupata kile hasa wanachohitaji. Kama
tulivyoonyesha awali, walipoulizwa namna wangependa kutambuliwa, wanaume hutumia maneno kama
mtawala, mtetezi, huru. Wanawake walioulizwa swali hilo husema mwenye upendo, mkarimu, makini
kihia
Endapo ndoa inamaanisha kuleta pamoja mtu mmoja mwenye hali ya utetezi na mwingine
mwenye hali ya ukarimu , tusishangae kuona kuwa huyu wa kwanza, kwa namna fulani, huwa kichwa
cha familia. Hii haimaanishia kuwa anatawala kama dikteta. Hakika, bado tunasikia kwa uchache,
wanawake wenye za kawaida za kike wakiwa na waume wenye misuli, “wanawakamata kwa kidole
chao kidogo.” Wanawake wenye furaha kwa kawaida hutawala kwa namna dhairi. Wanaweza kutawala
kwa kuwa waume wao huwapenda na hutaka kuwaridhisha. Wanaweza pia kutawala kwa sababu, kama
tafiti za kisaikolojia zilivyoainisha, wanawake huweza kusoma wanaume kuliko wanaume wawezavyo
kusoma wanawake. Cha muhimu, sasa, ni kwamba mwanamume awe kichwa cha familia kwa namna
isiyo na mkazo. Katika hali za jinsi hiyo, pande zote huwa na furaha.
Njia mojawapo ya kuwapunguzia wanaume makali ya utawala na kuwa wazi kwa wake zoa’ ni
kuunda kile ambacho Brad Wilcox hukiita “ubaba mwororo.” Watu wa jinsi hii wanaweza kupatikana
katika makanisa ya Kiprotestanti yenye misimamo isiyobadilika, ambayo huwasihi waume kuwa
“viongozi watumishi” ambao hukidhi mahitaji ya wake zao ya mawasiliano na huba, pamoja na mahitaji
ya familia kiuchumi vile vile uongozi wa kimaadili. Wakati ambapo kazi ya mhemko katika ndoa
yaweza isiwe ya kustarehesha au kuwajia wanaume kwa asili, yaweza ikatawala maisha yao kama
itachukuliwa kuwa ni wajibu au wito wa asili. . . . Wake wenye mashaka kuhusu kuziongoza nyumba
zao kwa namna isiyo rasmi dhidi ya waume wao watambue kuwa hawatopaswa kutoa chochote zaidi ya
hicho cheo. Tafiti fulani zimeonyesha kuwa waume wana kawaida ya kukadiria zaidi uwezo wao wa
kufanya maamuzi, wakati wake hujikadiria chini ya kiwango. Hata hivyo tafiti moja ya hapo nyuma
‘imegundua kuwa waume waliojisikia utoshelevu zaidi ni wale ambao waliamini kuwa walipatanafasi
ya juu katika maamuzi hata pale ambapo hapakuwa na ushahidi ulio huru wa jambo hilo.
Mwanamke atafutaye madaraka nje ya familia kwa nguvu na kwa hulka ya shari atapaswa kuwa
mwepesi wa mwendo kama Spiderman kama itampasa kuwa na ndoa yenye furaha pia. Wanafunzi
wangu wa kike mara kwa mara hufurahia maelezo ya Anne Moir na David Jessel yahusuyo aina ya
nguvu ya mwanamke, ambayo ni ngumu kuielezea, nguvu isababishayo mahusiano, iunganishayo
familia na kujenga jamii.’ Aina hii ya nguvu twaihitaje sana. Ingelipasa watu wa jinsi zote wawe
wametambua umuhimu wake.” (Rhoads 2004: 72, 261-62, 263) Taarifa hiyo hapo juu yathibitisha kuwa
biblia imekuwa sahihi wakati wote.
3. MAPENZI YA MUNGU KWA WAKE
I. Utanguliza
A. Kimsingi wake hujifunza majukumu yao kutoka kwa jamii ya karibu inayowazunguka: utamaduni wetu;
baba zetu; ndugu; marafiki; vyombo vya habari, nk.
Kawaida yetu—kwa kujua ama kutokujua—ni kuwaiga wale walio karibu nasi au kupingana nao.
B. Neno la Mungu pekee ndilo msingi wa hakika na salama kuhusiana na wajibu sahihi wa wake.
1. Vielelezo vizuri au vibaya, au habari katika vyombo vya habari, vyaweza kuwa vyamsaada, au
vyenye ufafanuzi; hata hivyo, haviwezi kuwa vya msingi.
2. Ni lazima tumpime kila asimamaye kama kielelezo na kila wazo kuhusu wake kwa maandiko, kwa
sababu “Iko njia ionekayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti” (Mith
14:12).
II. Vifungu vikuu vya maandiko.
Vifungu vikuu kuhusiana na wake ni: Mwz 2:15-18, 24-25; Efe 5:2-23; 1 Tim 5:14-15; Tit 2:3-5; 1
Pet 3:1-6; na Mith 31:10-31.
A. Mwz 2:15-18—15BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailimie na
kuitunza. 16BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, “Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula;
17walakini matunda ya ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
18
utakufa hakika." 18BWANA Mungu akasema, si vema mtu huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa
kufanana naye"
1. Kuhusu Mwz 2:15-18:
a. Mume mtarajiwa ndiye mtendaji, wakili wa uumbaji wa Mungu.
b. Mke mtarajiwa ni msaidizi wa kufanana na mumewe.
c. Tatizo la upweke hutatuliwa mmoja anapomsaidia mwingine.
(1) Mara nyingi waume kwa wake huishi kiutengano katika kutekeleza majukumu yao
ya kila siku, bila kuchangamana wala kusaidiana kwa namna yoyote ile ya kufaa.
Utengano huo hauhamasishi hali ya kuambatana, wala hautatui tatizo la “upweke”.
(2) Haimaanishi mke awe msaidizi wa mumewe kazini kwake, lakini yamaanisha
yapaswa aonyeshe kufurahia na anachofanya na kujaribu kumtia moyo na kumsaidia
huku akiiheshimu hiyo kazi.
(3) Matumizi: Chochote afanyacho mke, aliumbwa afanye katika mtazamo wa msaidizi
wa kufaa—yamaanisha, kwa makusudi mumewe asiwe mpweke katika majukumu ya
maisha, katika namna zozote zile.
d. Mume ni kichwa cha nyumba kwa agano.
(1) Adamu aliumbwa kwanza, alipokea amri moja kwa moja kutoka kwa Mungu,na
Hawa aliumbwa kuwa msaidizi.
(2) Mke yapasa akubali kuongozwa na mumewe kwa maongozi ya kimungu
2. Dhambi ya mwanadamu hapo baadaye ilichafua mahusiano haya. Katika Mwz 3:16 Mungu alisema
kwa mwanamke: “hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na
tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.”
a. Mwanamke ameumbwa awe msaidizi hasa “msaidizi” wa mwanamume (Mwz 2:18-22). Hiyo
huonyesha kwa asili yanayojitokeza “kimahusiano” maelekezo ndani ya wanawake. Maelekezo
hayo ya kimahusiano huonekana kwa dhati katika hali ya kipekee katika uwezo wa mwanamke
kuzaa na kulea. Dhambi ya Hawa ilisababisha maumivu zaidi kuhusiana na mchakato wa uzazi
na kubadilishana mahusiano na mumewe.
b. Kwa kuliheshimu tamko, “tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala,” watoa maoni
wengi hukubali kuwa aya hii ni chanzo cha mizozo ya ndoa na misigishano kijinsi, ingawaje
asili halisi ya mwingiliano kati ya “tamaa”na “tawala” ni ya ushindani. Ifuatayo ni kati ya
mitazamo tofauti kuhusu maana ya kifungu hiki:
(1) Adhabu za Mwz 3:14-19 kila moja huhusiana na jukumu muhimu la maisha na
mahusiano. Uzazi wa mwanamke umeongezewa maumivu makali, na jukumu lake
kama msaidizi wa mwanamume litaharibiwa na utoshelevu wa mwisho (Walton 2001:
227-28).
(2) “Tamaa yako itakuwa [kama ilivyokuwa kabla ya anguko, ingawa sasa
imechafuliwa na dhambi] kwa mumeo, na ataendelea kukutawala [kama alivyofanya
kabla ya anguko, ingawa sasa dhambi imechafua]” (Busenitz 1986: 207).
(3) Shauku ilikuwepo kusaidia mahusiano, lakini “tawala” humaanisha mwanamume
atamiliki kwa ukali (Stitzinger 1981: 41-42; tazama pia, Fleming 1987: 352, “Mungu
anamwonya mwanamke kuhusu badiliko lililotokea kwa mumewe ili ajue kwamba
mumewe hatomtendea kwa namna ya kwanza aliyoizoea”).
(4) Shauku ya mwanamke ni kumtawala mumewe, na utawala wa mwanamume
aliopewa na Mungu utahitaji juhudi (Foh 1974-75: 376-83).
(5) Hamu ya mwanamke ni kummiliki na kumtawala mumewe, lakini mume ana uwezo
wa kumtawala mke (Vogels 1996: 197-209).
c. Ni katika Kristo tu, kwa njia ya mioyo yetu iliyofanwa upya, na nguvu za Roho Mtakatifu
akaaye ndani yetu, ya kuwa wake na waume wana uwezo wa kurejeza upya, mpango wa ki-
Mungu, wa upendo, na kwa pamoja kuenzi mahusiano ya ndoa.
B. Mwanzo2:24-25—24Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba ya na mama yake naye ataambatana na
mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. 25Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona
haya.
1. Mume yapasa aandae makazi yapasayo kukaa yeye na mkewe.
a. Kwa amri wajibu huu ni wa mume.
b. Kwa kuhusishwa amri hii pia imetolewa kwa mke.
2. Uhusiano wa mzazi na mtoto si uhusiano wa msingi kijamii; bali ndoa.
3. Mke lazima atengane na wazazi wake.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
19
a. Haimaanishai aache kuwapenda, kuwaheshimu, au kuwajali wazazi wake; inamaanisha kuwa
familia yaweza kupokea ushauri na msaada lakini sio amri kutoka kw awazazi.
b. Inamaanisha kutengana kiakili, kihisia, kiuchumi, na kimwili kutoka kwa wazazi ikimaanisha
kutokuendelea kuwategemea.
c. Inamaanisha kumkubali na kumpokea mume kama sehemu ya kitengo kipya cha kufanya
maamuzi.
4. Mke yapasa ahimize na kuruhusu mshikamano wa upendo-kimwili, kiakili, na kihisia. Ni lazima
ajitahidi “kuwa mwili mmoja” na mumewe. Ni lazima ajitahidi kuungana na mumewe katika mahusiano
huku akiridhia ukaribu wawapo uchi bila kuona haya.
5. Matumizi: Wake, na waume, mara nyingi hawako radhi kutengana na baba na mama. Hali ya
kutojisikia salama ya “kuachana na kuambatana” lazima ishughulikiwe. Wake wasiojisikia salama
waweza kusababisha waume wao kuambatana na wazazi wao, marafiki, watoto, kazi, michezo, ulevi,
picha za ngono, au mwanamke mwingine kwa kuwa tu wamedharau kujisalimisha kwa waume wao
badala ya kuwahimiza waambatane nao. Waume wengi wamepuuzia juhudi za wake zao, lakini kuna
wake wengi ambao hushindwa kujaribu, au hukata tama mapema mno.
C. Efe 5:22-24—22Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. 23Kwa maana mume ni kichwa cha
mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. 24Lakini kama vile kanisa limtiivyo
Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
1. Mfumo wa kihistoria.
a. Wanawake katika jamii za Kigiriki za asili walikuwa na maisha yao tofauti kabisa.
Hawakuhusishwa katika maisha ya umma, hawakujitokeze barabarani wakiwa pekee, na
hawakuweza hata kujitokeza chakulani au katika makusanyiko ya starehe. Mwanamke
angekuwa na nyumba zake ni mumewe tu angeruhusiwa kuingia. Lengo lao lilikuwa
mwanamke aone kwa uchache kadiri iwezekanavyo, asikie kwa uchache kadiri iwezekanavyo
na aulize kwa uchache kadiri iwezekanavyo. Wanawake waliwekwa chini ya wanaume kwa
kuwa walihesabiwa kuwa pungufu ya wanaume. Heshima ya mwanamke ilikuwa kuwa kimya
(tazama Gombis 2005: 326).
b. Katika jamii ya Kiebrania, “ingawaje ndani ya nyumba ya Muebrania mke au mama
aliheshimiwa na kupendwa, na kuhesabika yu juu ya yule wa kipagani katika wakati wote wa
historia ya Israel,hata hivyo haikuwa fikra kamwe ya usawa kati ya yeye na mumewe.” Mke
alihesabika kuwa daraja ya chini (Bowman 1947: 442).
c. Katika jamii ya Kirumi, wanawake walikuwa daraja ya juu. Walionekana kuwa na uhuru wa
kutumia pesa, na waliweza kujihusisha na maswala ya kijamii kwa uhuru mkubwa kuliko wale
wa jamii za Kigiriki na Kiebrania. Hata hivyo, zilikuwepo tofauti katika maswala ya kisheria
kwa wanaume na waume ukilinganisha na wanawake na wake. Zaidi ya hayo, “wakuu wa
nyumba Fulani wangeweza kuyumbisha wake zao na kuwafanya wawe chini ya himaya ya
waume wao na nafasi yao iwe hatarini kunyanyasika” (Winter 2003: 18).
d. Wakati huohuo katika jamii ya Kirumi nyakati za Agano Jipya, lilizuka wimbi la kutaka
usawa, mwanzo wa aliyeitwa “Mwanamke mpya wa Kirumi”—inamaanisha, “mwanamke wa
daraja ya juu,ambaye juu ya hivyo alidai kujiingiza katik a starehe ya mwanamke” (Ibid.: 21).
Hii ilijionyesha katika hali tofauti tofauti za mavazi na tabia ya uzinzi. Hali hiyo ilikuwa wazi
mno kiasi ambacho Mtawala Augustus alitangaza sheria mpya kuhusiana na maadili,
mapungufu kifedha kwa wasio na ndoa, faida katika maeneo ya kazi kwa wanaozaa watoto, na
mitindo ya mavazi kwa wake; iliainisha ndoa kati ya madaraja fulani, na adhabu kwa waume
waliodharau shughuli za wake zao nje ya ndoa” (Ibid.: 39).
e. Kinyume cha udhalili wa mwanamke katika jamii za asili za Ugiriki, Waebrania na Rumi, Efe
5:22-33 “ni ilani ya jamii mpya iliyobadilika.Kwa sababu nyumba ilikuwa dunia ya jamii yote
iliyoamini, yaonyesha mfano imara wa jinsi wasomaji wa Paulo wanaweza kuitii amri katika
Efe. 5:18-21 kuwa ‘nyumba ya Mungu’ . . . Ingawaje Paulo hapa hakutangaza kuondosha
nafasi ya ukuu, kwa hakika anaitisha uhusiano wa waume na wake kuwa kwa namna ya Utu
Mpya” (Gombis 2005: 322, 328). Kwa hiyo, nyumab haiwi tena kwa manufaa ya mkuu, na
wake hawaonekani tena kuwa wa daraja ya chini;uongozi ni wa kujitoa na wa msalaba, na
mamlaka yatumike kwa faida ya wale wa nafasi ya chini;waume wasitawale wake zao, bali
wawapende (hii ni amri isiyoonekana katika mfumo wa nyumba za asili mahali popote); walio
chini ya mamlaka watii kwa hiari,” tena, kutokana na msalaba; kifungu chote kinahusianishwa
na uhusiano wa Kristo na kanisa , ambao kwa msisitizo chaweka msingi namna ndoa ipasavyo
kueleweka, na kuifanya ya maana sana iliyotajirika kitheolojia (Ibid.: 324-28).
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
20
2. Mazingira ya Uandishi.
a. Efe 5:22-33 huonyesha kwa upana ufafanuzi wa Paulo kuhusu wajibu wa waume na wake.
b. Kifungu huamsha kutoka kwa Paulo mjadala wa namna sahihi kwa Wakristo “kuenenda”
(Efe 4:1; 5:1-2, 15). Paulo anahimiza kwa wazi “tujazwe Roho” (Efe 5:18). “Kujazwa Roho,”
inaonekana katika kanuni nne: “kusema” (5:19); “kuimba” (5:19); “kutoa shukrani” (5:20); na
“kujitiisha [kuwa chini ya] mmoja kwa mwingine” (Efe 5:21). Paulo anaielezea dhana ya
kujitiisha [kuwa chini ya] ndani ya ndoa—kwanza anasema na wake (Efe 5:22-24), na halafu na
waume (Efe 5:25-33).
c. Twajua kifungnu kianzacho na Efe 5:22 chahusiana na Efe 5:21 (na pia Efe 5:18) kwa
sababu hakuna kitenzi katika 5:22. Ingawaje tafsiri nyingi za 5:22 husema kwa namna hii “Enyi
wake, watiini waume wenu, kama kumtii Bwana,” maneno “tiini” hayako katika lugha ya
Kiyunani ya 5:22; hayapatikani katika 5:21.
d. Kinyume cha hayo kwa nyumba za wasio wakristo ambazo mlengo ulikuwa kwa wanaume
kuonyesha jinsi iwapasavyo kutawala wake zao kwa manufaa yao, “Paulo anasema na wake
moja kwa moja, akiwahimiza kushiriki kikamilifu na kwa hiari katika Utu Mpya” (Ibid., 326).
3. “Enyi wake,watiini waume zenu kama kumtii Bwana”—asili ya utii wa kibiblia.
a. Kile ambacho si kutii.
(1) Kutii si udhalili.
(A) Yesu mwana si dhalili kwa Baba, ingawa yu chini ya Baba (1 Kor 11:3).
Akiwa duniani hakufanya chochote kwa matakwa yake, lakini alifanya kile tu
alichosikia na kuona Baba akifanya (Math 26:39; Yohana 4:34; 5:17-20, 30;
6:38; 8:28-29; 10:18; 12:49-50; 14:10, 24, 31). Hata kule mbinguni bado yu
chini ya Baba (1 Kor 15:24-28).
(B) Vivyo hivyo, kwa muundo wa Mungu waume na wake wana majukumu
tofauti ndani ya ndoa; mke si dhalili kwa mumewe, ingawaji ana wajibu wa
kuwa chini ya mumewe. Hii inaonyeshwa katika Efe 6:1 na 5, Paulo anasema
watoto wapaswa “kutii” wazazi wao na watumwa “watii” mabwana wao.
Badala yake, katika kifungu hiki na Kol 3:18 anabadilisha neno jingine la
Kiyunani, linalotafsiriwa “muwe chini ya.” Hii huonyesha kuwa kuna tofauti
bayana ya hadhi kati ya mke na mume katika mahusiano yao, ikilinganishwa na
hadhi ya watoto na uhusiano wao na wazazi, na hadhi ya watumwa na uhusiano
wao na Bwana wao.
(2) Kutii si kukandamizwa au kuonewa.
(A) Waume wengi, hata waume wakristo, wamewakandamiza na/au kuwaonea
wake wao kutoka karne moja hadi nyingine.
(B) Wamekandamiza vipawa na uwezo wa wake wao na kudharau hekima na
ushirika mkamilifu wa mke waliopewa na Mungu kupitia wake wao kwa
kuwakandamiza.
(C) Si tu kwamba mkandamizo huo ni dhambi, ni kinyume kabisa cha
upendo—kinyume kabisa cha jinsi Kristo “alivyolipenda kanisa na akajitoa
kwa ajili yake” (ndivyo waume waamrishwavyo kuwapenda wake zao).
(3) Kutii hakumaanishi kuwa mke hawezi kuwa na maoni yake na kuyatoa kwa uhuru,
kuwa na vipawa na kuvitumia kwa uhuru, na kuwa na ndoto safi na kutamani kuzifikia
kadiri awezavyo. Mke ni nafsi tofauti dhidi ya mumewe. Maoni yake, vipawa, uwezo,
ndoto, na shauku huongezea, juu ya zile alizonazo mumewe na kuudhihirisha utajiri
ulioko katika maisha ya ndoa kama ulivyokusudiwa.
(4) Kutii hakumaanisha kuwa mke ana haki ya kuwa na uchungu.
(A) Efe 5:33 yasema wake “wawaheshimu” waume wao.”
(B) Hakuna heshima endapo utii utatolewa kwa hofu ya kisasi au kwa kuuma
meno.
b. Utii ni
(1) Wazo kuhusu “utii”au “kuwa chini ya” ni kujitiisha chini ya mtu—ukiwa msaidizi,
sio dhalili. Paulo anakazia wazo hili katika Kol 3:18 (“Ninyi wake, watiini waume zenu,
kama ipendezavyo katika Bwana”), ambayo ni sawa na Efe 5:22.
(2) Utii kibiblia ni wa hiari wakati wote, kutoka moyoni, na kwa Bwana.
(A) Utii ni hiari.Neno la Kiyunani la “utii” (“uwe chini ya ”) imetumika katika
5:24 inaonekana katika 5:22 ni hupotasso. Kitenzi hicho kipo hapa na
kwingineko katika vifungu vya Agano Jipya wakati wote katikati kwa sauti ya
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
21
(kujirejea), ikimaanisha kuwa anayejitiisha hufanya hivyo kwa utashi wake
kabisa na angeweza kuchagua kufanya vinginevyo. . . Ni matumizi ya kawaida
kwa walio na mahusiano ya usawa, au katika nyakati zote tendo la utii hutoa
mamlaka kwa yule ambaye hutii kwake. Ni tendo la mtu huru katika jamii ya
kidemokrasia ambamo anatamani kuona kanuni za sheria na taratibu
zikitekelazwa, na yeye yuko tayari kwa hiari ya kujinyima uhuru wake kwa
faida ya wote. Katika neno, kitenzi tunachozungumzia ndicho kitoacho maelezo
ya kanuni ya uhuru dhidi ya leseni, katika ngazi ya ukuu” (Bowman 1947: 443-
44, mkazo katika asili)
(B) Hakuna mahali katika kifungu hiki au kingine katika biblia ambapo waume
huagizwa “kutumia,” “nguvu,”au “hila” ili wake zao wawatii. Utii ni tendo la
utashi kwa mke, na wala hahitaji kushurutishwa na mume.
(C) Utii hutoka moyoni. Ukweli huu hukubaliana na ule usemao utii ni tendo la
hiari la mke. Ingawaje utii wa nje waweza kushurutishwa, utii wa ndani (ambao
ndio unaompendeza Mungu) hauwezi kushurutishwa. Utii “kutoka moyoni”ni
wa mfano wa Kirsto msingi wake ni msalabani. Si mkakati wa kuponea na wa
hila wenye nia iliyojificha ya kumwezesha mke kumtawala mume au kupata
atakacho. Badala yake, utii una kusudi jema kwa ndoa, kwa familia na,
hatimaye, utukufu kwa Mungu.
(D) Utii ni kwa Bwana. Utii waweza kuwa wa hiari na kutoka moyoni kwa
sababu, hatimaye, utii ni tendo la upendo na utii kwa Bwana. Hiyo
imeonyeshwa katika 5:22 na 24. Utii wa mke kwa mumewe, katika kiini chake,
ni tendo la imani na tegemeo kwa Kristo—ni namna ya kusema, “Nachagua
kuachilia sehemu ya uhuru wangu kwa ajili ya mwanamume huyu kwa kuwa
ninakupenda, Bwana, kuliko yeye; Naamini kuwa utatulinda na kutujenga
mimi, mume wangu, ndoa yetu, na utatukuzwa kwa utii wangu kwa neno lako”
4. Efe 5:22-24—maoni ya ziada.
a. Efe5:22—“Enyi wake,watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu..”
(1) Wake hawaagizwi kujitiisha kwa kila mwanamume; hawaagizwi kujitiisha kwa
mume wa mwengine. Utii huu ni kwa mumewe tu akiitambua nafasi aliyopewa na
Mungu katika muundo wa familia kiMungu. Hii inamaanisha kutii mume mkorofi na
hata Yule asiye mwamini (1 Pet. 3:1).
(2) Kuwa chini ya mume “kama kwa Bwana”haimaanishi kuwa mume ni sawa na
Bwana, kana kwamba yeye ni kama Kristo mwakilishi asiyekosea duniani. Inamaanisha
kuwa utii una msingi katika upendo wa mke na utii kwa Kristo. Upendo wake kwa
Kristo wamweka huru, bila kujali mwenendo wa mumewe, kwa sababu anajua
anampendeza Mungu.
b. Efe 5:23—“Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe,kama Kristo naye ni kichwa cha
Kanisa,naye ni mwokozi wa mwili.”
(1) Hii ndio sababu Mungu aliamuru utii wa mke. Mungu ndiye aliye amua mpango
huo.
(2) Paulo anatuonyesha ukweli kuwa ndoa kwa asili ni taasisi ya rohoni. Ndoa
imekusudiwa ionyeshe uhusiano wa Kristo na kanisa.
(3) Kuna “kichwa” kimoja tu au mamlaka ya juu. Kama hakuna kichwa, au kikiwepo
zaidi ya kimoja, matokeo yatakuwa haya: kuchanganyikiwa, kukosa maamuzi,
kugombania mamlaka, na utawala huria. Hatimaye, Mungu alipanga kuwa kichwa cha
kanisa na ndoa kiwe ni kimoja.
c. Efe 5:24—“Lakini kama vile kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume
zao katika kila jambo.”
(1) Katika 5:24 tunaambiwa kuwa kama jinsi kanisa linavyomtii Kristo, wake yawapasa
wawatii waume wao, lakini katika 5:21 Wakristo yapasa wanyenyeekeanene. Mistari
hii yaweza owanishwa kwa namna hii:
(A) Ingawaje kuna huku kunyenyekeana, waume na wake hawanyenyekeani
kwa namna moja.
(B) Ufunguo hapa ni kukumbuka kuwa uhusiano kati ya Kristo na kanisa ni
kielelezo cha uhusiano kati ya mume na mke
(C) Je kuna utii kati ya Kristo na kanisa? “Hapana”—kama ukimaanisha kuwa
Kristo ajitiishe chini ya mamlaka ya kanisa; lakini “ndio” ikimaanisha kuwa
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
22
Kristo alijitiisha katika mateso na mauti ili kanisa lifaidike, na kanisa kwa hiari
na shukrani lajitiisha chini ya Kristo na kukubali mamlaka yake na kuufuata
uongozi wake.
(D)Mume hutii mkewe kwa mfano wa utii wa Kristo. Hufanya maamuzi ikitaraji
mema zaidi kwa mkewe. Hujitoa kwa ajili ya mkewe. Kwa hiari yake huwa na
mtazamo wa dira ya kuona mbele kwa yale atakayo kwa faida ya mkewe na
ndoa yao. Mke anapojua kuwa yeye ni wa kwanza katika moyo wa mumewe,
naya kuwa mumewe yuko tayari hata kufa kwa ajili yake, ikibidi,kama Kristo
alivyomfia bibi arusi wake, kanisa—mke wa jinsi hiyo wakati wote kwa furaha
na kwa hiari atakuwa radhi kutii uongozi huo usio wa kibinafsi.
(2) Paulo anaposema “kama kanisa limtiivyo Kristo, vivyo hivyo wake wawatii waume
zao,” analeta kilicho bora.
(A) Katika uhalisia,mara nyingi kanisa hutenda dhambi na uasi. Jinsi kanisa
linavyosumbuka kumtii Kristo vivyo hivyo wake husumbuka kuwatii waume
zao kwa ukamilifu, hasa wakati ambapo waume hao hawatekelezi wajibu wao
waliopewa na Mungu.
(B) Kwa hali yoyote, kushindwa kutii huwa na matokea mabaya kwa kanisa na
ndoa. Wasioamini hupima imani yetu kwa kuangalia jinsi tunavyoyaishi yale
tuaminiyo. Waonapo kuwa hatutii maandiko tunayodai tunayaamini,
watayakataa na kuyadhihaki maandiko, Bwana, na dai letu la kuwa wafuasi wa
Kristo. Hatimaye, jina la Kristo litadharauliwa.
(3) Amri ya kutii, na jitihada ya kufanya hivyo, yatumika“kwa kila kitu.”
(A) Kwa ujumla agizo hili ni la kutekeleza wakati wote na si tu hali
inaporuhusu, tunapojisikia vizuri, kwa raha zetu au kwa uchaguzi.
(B) Endapo umeolewa na mume mkorofi au asiyeamini (1 Pet 3:1) mwenendo
wenu —roho ya utulivu na ukimya, mwenendo wenu wa upendo na neema—
ushinde juu ya waume wenu. Na mwenendo wenu na tabia yenu viseme,
“Nataka kutii chini ya uongozi wako; tafadhali nisaidie kufanya hivyo.” Kwa
namna hiyo injili itamvuta mumeo.
(C) Kisichokubalika kwa “katika kila jambo” ni wakati mke anapoamriwa na
mumewe kufanya dhambi.Kama mtume alivyosema, “yatupasa kumtii Mungu
kuliko wanadamu” (Mdo 5: 29; tazama pia Kut 1: 17; Dan 3:18; 6:6-13).
D. 1 Timotheo 5:14—Basi napenda wajene, ambao si wazee, waolewe, wazae watoto, watawale na madaraka
ya nyumbani; ili wasimpe adui ya kulaumu.
1. Wajane wasio wazee walishuriwa kuolewa, kupata watoto, na kuwa na madaraka ya nyumba zao.
2. Kuzaa watoto ni jukumu muhimu la mke.
a. 1 Tim 2:15 inakazia wazo hilo: “Lakini wanawake wataokolewa kwa uzazi wao.”
b. Paulo anatumia jukumu hili muhimu kama mfano wa “kudumu katika upendo na utakaso
pamoja na moyo wa kiasi”
c. Kwa ujumla inaonyesha bayana kuwa wanawake yapasa wakubali wito wao wa msingi—
kuwa mama.
2. Utawala wa nyumba ni wito wa msingi wa mke.
a. Msemo “tunza nyumba” au “tawala nyumba” unatokana na maneno mawili ya Kiyunani,
oikos (“nyumba”) na despotes (“bwana” au “mkuu”).
b. Mke apaswa kuwa bwana au mkuu au meneja wa nyumba. Hata hivyo mume ndiye kichwa
na mwangalizi wa nyumba (I Tim 3:4, 5, 12).
E. Tito 2:3-5—3Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji,wasiwe
wenye kutumia mvinyo nyingi,bali wafundishao mema, 4ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume
zao, na kuwapenda watoto wao, 5na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao,kuwa wema,
kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.
1. Kufunza wanawake vijana ni wito wa msingi.
2. Wanawake vijana lazima wafundishwe namna ya kutunza nyumba vema.
3. Haya yanapotendeka, neno la Mungu halinenewi vibaya na dunia ya wasioamini.
4. Namna mwanamke amtendeavyo mumewe na watoto wake na jinsi atunzavyo nyumba yake ni
ushuhuda kwa wasio-wakristo.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
23
F. 1 Pet 3:1-6—1Kadhalika ninyi wake, watiini waume zetu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe
kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; 2wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. 3Kujipamba
kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani,kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; 4bali kuwe utu
wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu
mbele za Mungu. 5Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini
Mungu, na kuwatii waume zao. 6Kama vile Sara alivyomtii Ibrahim, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake,
mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yoyote.
1. Kifungu na muundo.
a. 1 Pet 3:1-7 ni mjadala wa kina alioainisha Petro kuhusiana na wajibu wa wake na waume.
b. Kifungu hiki ni mfano wazi wa matumizi ya asili ya utii wa Kikristo ambao, kwa upande
mwingine, ni sura ya namna wakristo wapaswavyo kiishi:
(1) Dhana ya jumla hapa ni namna sahihi ya maisha ya Kikristo—ikimaanisha,
“kuachana na tamaa za mwili”na“kuwa na mwenendo ulio bora” (1 Pet 2:11-12).
(2) Wazo lililo wazi zaidi ni maagizo ya Petro kwa waamini“Tiini kila kiamriwacho na
watu, kwa ajili ya Bwana” (1 Pet 2:13). Kisha Petro anatumia kitenzi cha wakati
unaoendelea mara tatu—watumishi “muwe watii [kitenzi kile kile alichotumia Paulo
katika Efe 5:21] kwa Bwana zetu kwa hofu nyingi” (1 Pet 2:18), “ninyi wake watiini
waume zenu,” (1 Pet 3:1), na “ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili” (1 Pet
3:7)—ambay hupata nguvu yake chanya kutoka kwa kitenzi katika 2:13.
(3) Petro pia anatumia mfano wa mateso ya Kristo kufafanua dhana ya utii wa Kikristo
(1 Pet 2:21-25). Anatuhimiza tufuate mfano huu: “Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu,
akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake” (1 Pet 2:21).
(4) Katika 1 Pet 3:1, 7 akibainisha dhana ya utii na mfano wa Kristo kwa wake na
waume kwa kutumia kielezi kilekile (“vivyo”). Kwa hiyo, wajibu wetu kama wake
lazima uonekane kama njia bayana ambayo twaonyesha utii na kumfanania Kristo,
ambacho ndicho kiini cha “mwenendo bora wa [Kikristo]” (1 Pet 2:12).
c. In 3:1-6 Maagizo ya Petro kwa wake Wakristo kimsingi yana wito katika maeneo matatu:
(1) Wito wa manufaa (3:1-2)—matokeo ya kiinjili ya ‘tabia ya mke’;
(2) Wito wa nia (3:3-4)—wake wapaswa kuwa na kutenda yaliyo na thamani katika
macho ya Mungu; na
(3) Wito wa kuiga (3:5-6)—wake wapaswa kufuata mfano wa wanawake watakatifu wa
zamani.
2. 1 Pet 3:1-2.
a. Wito wa Petro kwa wake “watiini waume zenu” (3:1) ni sawa na himizo la Paulo kwa wake
katika Efe 5:22. Neno “tiini”ni kitenzi kile kile alichotumia Paulo kwa Kiyunani katika Efe
5:21, 24.
b. Mazingira bayana anayoyanenea Petro katika 3:1-2 ni pamoja na yale ya mke Mkristo
mwenye mume asiyeamini. Kifungu katika 3:1, “ikiwa wako wasioamini neno,”yamaanisha
kuwa wake wengi Wakristo walikuwa na waume Wakristo, ingawaje baadhi yao hawakuwa nao
(Grudem 1988: 137; tazama pia Michaels 1988: 157). Dhana ambayo yajadiliwa na Petro
katika kifungu hiki inatumika bila kujali kwamba mume ni Mkristo au la..
c. Katika karne ya kwanza katika jamii ya Kirumi, mke aingiapo dini iliyo tofauti na ile ya
mumewe alionekana ametenda tendo la kutotii. Hivyo, fokasi ya Petro ni mwanamke kutunza
heshima kwa ajili ya injili, na amtii mume kwa sababu ya ushawishi alionao kwa mumewe.
d. Petro asemapo katika 3:1 kwamba mume asiyeaminiye “anaweza kuvutwa bila ya Neno”
hasemi kuwa wake Wakikristo wasishuhudie kwa maneno. Badala yake, anasema ushuhuda wa
jinsi hiyo si wa lazima, na wakati mwingine hausaidii (mfano, endapo mume amejenga chuki au
hasira kubwa jina Yesu litajwapo). Kwa hiyo, mke Mkristo hapaswi kuendelea kumhubiria injili
mumewe mpinzani wakati wote. Badala yake, Petro anasema, tabia yake itakuwa ndicho
chombo atakachotumia Mungu kumpata mumewe. Hii yamaanisha kuwa Mungu katika ukuu
wake ana mtazamo ulio juu sana katika mchakato wa wakovu. Inapasa kuongeza maombi “ili
neema ya kuishi maisha manyofu iwepo na kwa ajili ya Mungu kutenda kazi katika moyo wa
mumewe” (Grudem 1988: 138).
e. Kutokana na 3:2 tabia ya mke yapaswa awe “msafi wa moyo” (“msafi moyoni,asiye na
unajisi”) na “mwenye heshima” (“mwenye staha”). Tabia ya usafi yatukumbusha kuwa utii
hauhusishi kutenda maagizo yasiyo manyofu. Maadili haya yana msingi katika Mungu (tazama
2:12, 13, 15, 16, 17, 21, 23, 25), lakini yanaonekana kwa mume, na hivyo yapo kwa faida ya
mumewe.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
24
3. 1 Pet 3:3-6.
a. Hatimaye Petro anaonyesha umuhimu wa asili ya tabia ya kweli ya Kiungu ikilinganishwa na
ya muda (iharibikayo) “pambo”na ya milele (isiyoharibika) “pambo.”
b.“Pambo”la kweli (ikimaanisha, “kujipamba au kufanya uwe na mvuto”) kunakompendeza
Mungu ni katika utu wa ndani (3:4-5). Kwa kweli, mapambo halisi “yaliyo na thamani mbele za
Mungu” ni yale ya “mtu asiyeonekana wa moyoni” (3:4) ambayo hujidhihirisha kwa nje kwa:
(1) safi/takatifu na ya heshima/tabia ya staha (3:1-2);
(2) “sifa ya upole [‘bila kuvutwa na hali ya kujiona kuwa u mtu muhimu sana, mpole,
mnyenyekevu, mwenye kujali, ’] na mkimya mwenye “roho” [‘tulivu, yautaratibu, isiyo
na machafuko’] (3:4);
(3) utii kwa na kuwatii waume zao (3:5); na
(4) kufanya yaliyo sahihi pasipo hofu (3:6).
c. Katika 3:3 hakuna kivumishi kinachovumisha “mavazi” (“nguo”) (tafsiri ya NIV isivyo
sahihi inasema “nguo nzuri”). Kama Grudem asemavyo, “Si sahihi, kwa hiyo, unapotumia
maandiko haya kuwakataza wanawake kusuka nywele au kuvaa dhahabu kwa sababu zizo hizo
utapaswa uzuie na ‘kuvaa nguo’ pia. Wazo la Petro hapa si kupinga uvaaji wa chochote, bali
haya yasiwe ndio ‘mapambo’ ya mwanamke, asili ya uzuri wake.” (Grudem 1988: 140)
“Mapambo ya dhahabu ” yanapotajwa, yaonyesha Petro alifikiri kuhusu wanawake matajiri.
Watu wenye uwezo wa kuvaa vizuri yabidi wakumbushwe kuwa mapambo ya nje ya aina
yoyote sicho kimpacho mtu nafasi mbele za Mungu.
d. Katika 3:4 kifungu cha Petro “roho ya upole na utulivu” yafungamanisha pamoja mawazo
yake pacha ya utii wa mke na mapambo ya mke. Roho ya jisi hiyo ni “namna hii” ambavyo
wanawake watakatifu, akiwemo Sara, “walijipamba” na waliwatii waume zao (3:5-6). Mbele ya
macho ya Mungu, uzuri, na utii wa kweli, si swala la muonekano wa nje au utii wa nje, bali
huchipukia kutoka moyoni na roho ambayo humtumaini Mungu juu ya vitu vyote.
e. Katika 3:5-6 kuhusu “wanawake watakatifu”na, hasa, Sara na Ibrahim inaonesha kuwa
maagizo ya Petro kwa wake yalihusha pia wale waliokuwa na waume Wakristo.
Chakushangaza, mahali pekee katika biblia ambapo Sara alimwita Ibrahim “bwana” ni katika
Mwz 18:12. Katika aya hiyo Sara alicheka akiiambia nafsi yake. Hilo lina maana kwa sababu
inaonesha mtizamo wake wa ndani. Hatimaye mfano wa Sara huwapa wanawake watakatifu
tumaini, kwa sababu katika Mwz 21:10-13 Ibrahim alimsikiliza Sara na akafanya kama
alivyomtaka kwa kumfukuza Hajiri na Ishmaeli. Hivyo, Ibrahim alizipa uzito fikra za Sara dhidi
ya mwanawe Ishmaeli. Kuna mashaka kama Ibrahim angeweza kufanya hivyo endapo Sara
hakuwa ameishi maisha ya uaminifu, kwa ndani na nje. Wanawake Wakristo, wanapoishi kwa
namna hiyo hudhihirisha kuwa wamekuwa “uzao wa Sara” (3:6).
G. Mithali31:10-31—10Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.
11Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.12Humtandea mema wala si mabaya, Siku zote
za maisha yake. 13Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo. 14Afanana na merikebu za
biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali. 15Tena huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa
nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wakesehemu zao. 16Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya
mikono yake hupanda mizabibu; 17Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Huitia mikono yake nguvu. 18Huona
kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku. 19Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake
huishika pia. 20Huwakunjulia masikini mikono yake; Naam, huwanyooshea wahitaji mikono yake. 21Hawahofii
theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu. 22Hujifanyia
mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani. 23Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo
pamoja na wazee wa nchi. 24Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi. 25Nguvu na
hadhi ndio mavazi yake; Anaucheka wakati ujao. 26Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema I
katika ulimi wake. 27Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu. 28Wanawe
huondoka na kumwita heri; mumewe naye humsifu, na kusema, 29"Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini
wewe umewapita wote.”30 Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili;Bali mwanamke amchaye Bwana ndiye
atakayesifiwa. 31Mpe mapato ya mikono yake, na matendo yake yamsifu malangoni.
1. Kifungu hiki hutupa mwanga katika maeneo kadhaa kuhusiana na “mke mwema” ambaye
“anampenda Bwana”
a. Anapendeza, mke mwanye bidii, mama, mtunzaji wa nyumba, mshauri mwenye hekima,
Msamaria mwema na mfanya biashara mwenye kumcha Bwana.
b. Moyo wa mke mwema umeelekea kwa mumewe, familia yake, na wahitaji. Wakati afanyapo
biashara nje ya nyumba yake, na huifanya vema, hatelekezi mumewe, watoto wala wahitaji.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
25
Anayafanya yote katika kicho cha Bwana.
2. Thamani ya Mke (vv. 10-12).
a. “Mke mwema, ni nani awezaye kumwona?”
(1) Neno la Kiebrania “mwema”humaanisha “mtendaji makini mwenye viwango vya
juu vya uadilifu.” Kwa maana halisi, ina maana “mwanamke mwenye sehemu nyingi.”
Ni mwenye sura nyingi zenye vipengele vingi au pande nyingi za nafsi yake.
(2) Hiyo yaonyesha mwanamke afaaye akitumia vipawa na karama zote alizonazo kwa
ajili na kupitia nyumba yake. Swali linaashiria kuwa ni vigumu sana kumpata
mwanamke wa jinsi hii.
b. “Kima chake chapita kima cha marijani.” Huwezi kupanga kima cha thamani yake. Thamani
yake haidirikiki.
c. “Moyo wa mumewe humwamini.” Mumewe ana imani ya kutosha kwa mkewe kufanya
maamuzi na kutunza nyumba wakati hayupo. Ana imani thabiti juu ya mkewe. Amepata
kuaminika hivyo kwa sababu ya uaminifu wake.
d. “Wala hatakosa kupata mapato.” Hutumia vizuri pesa apewazo na mumewe kwa namna
ambayo mumewe hatarajii matumizi mabaya wala kudanganywa. Hii yatuonyesha kuwa kuna
wanawake ambao hutawala pesa vizuri na waweza kuaminiwa kufanya hivyo.
e. “Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.” Maisha ya mwananmke
yamemwelekea mumewe na wakati wato hutafuta kumpendeza mumewe kwa kuwa yeye ni
msaidizi wake. Yuko tayari kuishi kwa ajili ya mumewe.
3. Majukumu ya Mke (vv. 13-27).
a. “Hutafuta sufu na kitani.” Mke mwema hutumia pesa kwa umakini sana na kutafuta njia za
kupunguza matumizi na kuweka akiba kwa manufaa ya familia yake. Mke wa Kiebrania
alitafuta bei iliyokuwa bora zaidi ya sufu na kitani na mwanamke wa kisasa anapaswa kutafuata
njia zipasazo kubana matumizi ya familia.
b. “Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.”
(1) Sehemu kubwa ya kazi afanyazo mwanamke ni kwa kutumia mikono yake na
yapasa ajifunze kufanya kazi zake za siku kwa siku kwa“mikono yanye shauku”
(inamaanisha, kwa moyo wa kupenda), akitambua kuwa hayo ndiyo mapenzi ya Mungu
kwa ajili ya maisha yake.
(2) Anabuni njia za kufanya kazi ziwe za kusisimua na anautawala mwenendo wake na
kuacha kujihurumia afanyapo kazi za mikono nyumbani. Mwanamke mbunifu
hutekeleza majukumu yake ya nyumbani haraka ili awe na muda wa kufanya mambo
mengine ambayo angependa kufanya.
c. “Afanana na merikebu za biashara.” Wajibu mmojawapo wa kila siku kwa mwanamke
Mwebrania ulikuwa kupanga mlo. Hawakuwa na vifaa vya kisasa na walijadili bei za chakula
na kuhakikisha ubora upo. Swala la chakula na mlo lazima lifanywe kwa ubunifu mkubwa na
mwanamke afaaye.
d. “Huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula.” Huamka
Kabla jua kuchomoza ili kuhakikisha kuwa familia yake inapata chakula bora. Wanawake
wapaswa kuamka mapema ili kuhakikisha, ikiwezekana, kuwa mume na watoto wamepata
kifungua kinywa chenye lishe bora kabla ya kwenda kwenye shughuli zao.
e. “Na wajakazi wake sehemu zao.” Mke wa Kiebrania kwa kawaida alikuwa na mtumishi wa
kumsaidia kazi za nyumbani, na alihakikisha kuwa anawatunza watumishi wake pia
(inamaanisha, hakuwatendea isivyohaki).
f. “Huangalia shamba, akalinunua.” Mwanamke angeweza kufanya kazi ya kuajiriwa kwa
ruhusa ya mumewe. Hamlazimishi kuingia katika biashara kwa kuwa hufanya hayo kwa
manufaa ya nyumba yake.
g. “Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.” Kwa mapato yake binafsi ya shamba
hupanda mizabibu na kupata faida. Alikuwa na biashara ndogo ambayo angeifanya nje ya
nyumba yake.
h. “Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu.”Hutunza afya yake
kwani anajua hatoweza hufanya kazi za ziada ikiwa hafanyi kwa ukamilifu majukumu yapasayo
kwa mumewe na familia.
i. “Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku.” Anaridhishwa na uwezo
wake wa kuihudumia familia lakini yapasa atumie masaa mengi kutimiza malengo yake.
Hufanya kazi kwa bidii na muda mrefu.
j. “Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia.” Hufanya kazi ya
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
26
kushona na nyinginezo muda ukiruhusu.
k. “Huwakunjulia masikini mikono yake; Na huwanyooshea wahitaji mikono yake.”
Mwanamke bora hutengeneza faida, lakini hushiriki faida ile na wahitaji hata nje ya familia
yake kwa sababu anajua ni heri kutoa kuliko kupokea.
l. “Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa
nguo nyekundu.”
(1) Amefanya maandalizi ya nguo kwa ajili ya wakati wa baridi kwa kufuma.
(2) “Nguo nyekundu”hapa humaanisha nguo zenye kiwango cha ubora.
m. “Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.”
(1) Hujishonea nguo zake na huvaa mavazi ya kupendeza. Huenda na wakati kimavazi
na anavaa nguo bora maana hushona mwenyewe (hana gharama ya fundi au mtu wa
katikati).
(2) Haimaanishi mke lazima ajishonee nguo mwenyewe, lakini yamaanisha avae vizuri,
kutegemea na uwezo weka.
(3) Maandiko hayamzuii mke kupendeza na kuvaa vizuri. 1 Tim 2:9-10 inakataza
mwanamke kuweka kipaumbele katika muonekano wa nje kuliko mwenendo wa
kiungu.
n. “Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi.” “Malangoni”
yamaanisha ukumbi wa mji, mahali pa serikali ya mji. Wazo ni kwamba, kwa sehemu, kwa
kuwa mumewe anaye mke mwema, ameinuka na kuwa mtu maarufu kwenye mji.
o. “Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi.” Ni mshonaji na
huuza nguo kupata mapato ya ziada kwa ajili ya familia yake.
p. “Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao.”
(1) Ni mwanamke mwenye nguvu za kiroho na mmwenendo safi na anucheka wakati
ujao kwa sababu ameweka maandalizi kwa ajili ya familia yake.
(2) Anamsadiki Mungu kwa ajili ya wakati ujao, lakini pia hujiandaa kwa ajili ya
wakati ujao.
q. “Hufumbua kinywa chake kwa hekima.”
(1) Ni mwanamke mwenye hekim(inamaanisha, ana uwezo wa kutumia maarifa
kimatendo). Ana akili.
(2) Ni mbunifu na mwenye ufahamu ulio hai. Anajua kinachoendelea katika mazingira
yake na yeye ni changamoto kwa mumewe.
r. “Na sheria ya wema i katika ulimi wake.” Ni mwerevu na pia makini kwa mahitaji ya
wengine.
s. “Huangalia sana njia za watu wa nyumbaani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.”
Mwanamke bora si mvivu. Ni mzalishaji na siku zote hujali maslahi ya familia yake.
4. Sifa za mke (vv. 28-31).
a. “Wanawe huondoka na kumwita heri.”
(1) Watoto hujua kuwa mama yao anawapenda na anafanya kila awezacho kuwasaidia.
(2) Watoto wake watashawishika kumfuata Kristo kwa sababu ya kielelezo cha mama.
b. “Mumewe naye humsifu, na kusema.”
(1) Mume hutambua kuwa ana mke aliye bora kuliko wote duniani na hujivunia kwa
hilo.
(2) Wanaume, je twawasifu wake zetu tuwapo nao wenyewe na pia kwa watu wengine?
c. “Binti za watu wengi wamefanyaa mema, lakini wewe umewapita wote.” Mwanamume
huona kuwa mkewe ni mwenzi kamili na humsifia kwa vipaji mbalimbali alivyonavyo.
d. “Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana ndiye
atakayesifiwa.”
(1) Urembo, ingawaje unavutia, uko juu ya ngozi tu.
(2) Lililo muhimu kwa mke ni upendo wake kwa Kristo na utashi wake wa kufanya
mapenzi ya Mungu. Siri ya maisha ya mwanamke bora ni kujitoa kwake kwa Kristo
ampaye nguvu za kufanya huduma nyingi ndani na kupitia nyumba yake.
e. “Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.” Mke aliye bora
hahitaji kujisifia mwenyewe. Kazi zake zitajulikana na wengine watamsifu.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
27
4. MAPENZI YA MUNGU KWA WAUME
I. Msingi wa wajibu la waume.
A. Watu hujifunza wajibu wa waume kutoka katika mifano ya wale wanao waona: utamaduni wetu; baba
zetu; ndugu; marafiki; vyombo vya habari, nk.
Mwelekeo wetu—kwa kujua au kutokujua—ni kuiga vielelezo vyetu vya msingi au kuwa kinyume
navyo.
B. Neno la Mungu pekee ndilo msingi salama na usiobadilika wa mfano wa wajibu halisi wa waume.
1. Mifano mizuri na mibaya, au taarifa za vyombo vya habari, vyaweza kusaidia, au kuwa kielelezo;
hatahivyo, haviwezi kuwa msingi.
2. Lazima tupime kila kielelezo na wazo kuhusu wajibu wa waume kwa maandiko, kwa sababu“Iko njia
ionekanayo kuwa njema machoni pa mwanadamu, lakini mwisho wake ni njia za mauti” (Mith 14:12).
II.Vifungu vikuu vya maandiko.
Vifungu vikuu tutakavyoangalia kuhusiana na waume ni: Mwz2:24-25; Efe 5:25-33; Kol 3:19; na 1
Pet 3:7.
A. Mwz. 2:24-25—“Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe,
nao watakuwa mwaili mmoja. Nao walikuwa wote wawili uchi, Adam na mkewe, wala hawakuona haya.”
1. “Kwa hiyo [Hivyo] mwanmume ataacha”yaonyesha:
a. Hii “Kwa hiyo [Hivyo],” Inapouanza mstari huu, inaturudisha kwenye uumbaji wa
mwanamke (Mwz 2:18-23). Inaonyesha sababu, umuhimu, na maana ya mwanamke kwa
mwanamume, kutokana na mpango wa Mungu wa uumbaji. Mwanamume yabidi abadili
mahusiano yake ya kibinadamu yaliyo karibu zaidi—wa ndani zaidi, wa kibinafsi zaidi, ulio
wazi zaidi, wakujali zaidi, uliounganishwa zaidi, wa hatari zaidi—kutoka kwa wazazi wake
kwenda kwa mkewe.
b. Ndoa ni uhusiano wa msingi kijamii; uhusiano wa mzazi-mtoto ni kitu cha pili, na hutokana
mahusiano ya ndoa.
c. Ndoa yapaswa kuwa yakudumu (tazama pia Mal 2:13-16; Math 19:3-8).
2. Ku“waaacha baba na mama” yamaanisha kuwa mume na mke:
a. Wanajenga kaya tofauti.Wanandoa wahitaji kujenga utambulisho wa kwao, na hivyo
wajitenge, kwa kiwango fulani, kutoka kwa wazazi:
(1) Kimwili—watengeneza nafasi ya uhuru, inamaanisha, faragha na kibinafsi. Pengine
isiwezekane kuondoka kabisa katika maeneo waishiyo wazazi, ingawaje hilo ndilo
lingefaa zaidi. Hata kama wanandoa wataendeelea kuishi nyumba moja na wazazi, kwa
hali yoyote, yapasa wawe na eneo lao “tofauti” na wazazi wawe na la kwao.
(2) Kihisia—watengwe na vitanzi vya wazazi vya usalama na kukubalika.
(3) Kiufahamu—wawe huru kufikiri kwa faida ya mmoja kwa mwingine.
(4) Kimaamuzi—Mume na mke wapaswa kuwa “chombo huru cha kufanya maamuzi”
mbali na wazazi wao; uzuri wa mke na familia mpya wafanyika kitu cha msingi.
(5) Kimapato—mume humpatia mke na kaya yake mpya.
b. Acha kuwa tegemezi kwa wazazi kwa namna ile ambayo watoto wadogo hutegemea wazazi
wao. Yamaanisha wana ndoa waweza kupokea “ushauri,” na sio “amri,” kutoka kwa wazazi.
c. “Kuacha”wazazi haimaanishi kuwa twaacha kuwapenda, kuwajali na kuwaheshimu.
Vipengele hivyo vihusuvyo mahusiano ya mzazi kwa mtoto au mtoto kwa mzazi ni vya kudumu
(tazama Luka 18:18-20; 1 Tim 5:8).
d. Wazazi wawalee watoto katika hali ya kuwaandaa kukabili badiliko hili—kuwaacha wao na
kuambatana na mwenzi.
(1) Wapaswa kuwaandaa watoto wako kuondoka, kujitenga na kuwa huru.
(2) Wapaswa kuwaandaa watoto wako kuambatana na mwenzi (na sio na wewe).
3. “Kuambatana na mkewe”yamaanisha:
a. Mwanamume ana “utambulisho,”mpya ambao ni (baada ya kuwa na uhusiaono na Kristo)
ukiwa na msingi, na kulelewa na uhusiano wake na mkewe, na si wazazi wake. Hii ya maanisha:
(1) Mke apaswa kuwa mtu wa karibu na muhimu kimahusiano kuliko wote katika
maisha ya mumewe—si watoto, wazazi, rafiki, wafanyakazi wenzake, kazi, hobi, nk.
(2) Endapo watoto au watu wengine wanakushinikiza “kupendelea upande fulani”
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
28
(yaani, “mke dhidi ya watoto”), wajue kuwa utachagua mke badala ya watoto wako,
ikibidi.
b. Mwanamume anapaswa kuwa na mke mmoja, si zaidi ya mmoja.Katika Mwz 2:24 “mke” ni
umoja, si wingi (kwa hakika, Mungu alimuumba “mwanamke,”si “wanawake” kwa ajili ya
Adam—tazama Mwz 2:22-23). Katika Math 19:5-6 Yesu ananukuu “nao watakuwa mwili
mmoja” kama “nao wawili watakuwa mwili mmoja.” Hivyo, mapenzi ya Mungu katika ndoa ni
mke mmoja na sio wake zaidi ya mmoja.
(1) Ndoa ya mke mmoja iliyo bora ina misingi, pamoja na mambo mengine, katika
uhusiano wa Kristo na kanisa (Efe 5:31-32). Kama vile Kristo alivyo na bibi arusi
mmoja (kanisa—tazama Ufu 19:7; 21:2, 9), vivyo hivyo mwanamume awe na mke
mmoja. Ubora huu waonekana katika sifa apaswazo kuwa nazo mzee au mwangalizi wa
kanisa; kwa kuwa kanisa ni udhihirisho wa Kristo duniani—kiongozi wa kanisa na awe
mume wa “mke mmoja” (1 Tim 3:2; Tit 1:6). Mungu anatuonesha uhusiano wa uzinzi
wa kiroho kwake na ule ulio katika ndoa (tazama Hosea 1-7).
(2) Ingawaje wanaume wengi katika agano la kale wakuwa na ndoa ya wake zaidi ya
mmoja wakiwemo baadha ya viongozi wa Israel, wa kwanza wao katika maandiko
alikuwa Lameki, mtu ambaye hakuheshimika na mwenye tabia ya ugonvi (Mwz 4:23-
24).
(3) Ndoa ya wake zaidi ya mmoja ilileta matengano ya familia na ilikuwa na madhara
mengineyo yakiwa ni pamoja na uzinzi wa kiroho kwa Mungu (tazama 1 Wafl 11:1-8).
c. Endapo mwanamume mkristo ana mke zaidi ya mmoja tayari, basi afuate kanuni hizi
zifuatazo:
(1) Aendelee kutunza wake zake wote na watoto kuepuka kuendeleza madhara.
(2) Asiwape wakeze talaka na kubaki na mmoja, kwa sababu Mungu“anachukia talaka)
(Mal 2:16). Hata hivyo, ikiwa mke mmojawapo atachagua kuondoka, anaweza
kumruhusu kuondoka; ikimaanisha, ampe talaka kwa uchaguzi wake.
(3) Afanye kila awezalo wakeze na watoto wote wamjue Kristo.
(4) Ingawaje mwanamume wa jinsi hii hawezi kutumika kama kiongozi kanisani (1
Tim 3:2; Tit 1:6), anaweza kuwa na huduma muhimu kama mtu binafsi kwa mwingine
(kwa mwenendo wa namna hii “Usifanye kama mimi kuhusiana na ndoa kwa kuwa na
mke zaidi ya mmoja”).
4. “Kuwa mwili mmoja”ina maana zaidi ya lile tendo la kuwa mmoja kwenye tendo la ndoa. Badala
yake, kuwa “mwili mmoja” inamaanisha kina cha mahusiano.
a. “Wawili watakuwa mwili mmoja”kimsingi haimaanishi tendo la ndoa. “Mwili”ni sawa na
“mtu” (tazama Mwz 6:17; Yoeli 2:28). Katika Math19:5-6 (Marko 10:8-9) Yesu alinukuu
mstari huu katika dhana ya talaka, si tendo la ndoa. Katika 1 Kor 6:15-17 mstari huu
ulinukuliwa katika dhana ya muungano wa kiroho na Kristo—mtu apaswa kumtukuza Mungu
kwa mwili wake, asijihusishe na uzinzi. Katika Efe 5:28-32 mstari huu ulinukuliwa kuonyesha
umoja wa kiroho kati ya Kristo na kanisa.
b. Matumizi yote ya mstari huu yaonyesha uzito,na maana kuu kiroho. Yamaanisha kuwa watu
hawa wawili waunganike kiroho, kiakili, kihisia, kimapato, na katika njia nyinginezo, na hata
kimwili. Mke hujaliza kile kipunguacho kwa mumewe, kama jinsi sifa za mke zinavyokamilisha
zile za mume (tazama “Wanaume na Wanawake: Mfano wa Mungu na Asili ya
Binadamu”).Katika ndoa ambayo mume na mke wameunganika kwa namna hii, ni kana
kwamba mtu mpya “kamili” ameumbwa, akiwa na ukuu zaidi ya jumla ya hao wawili.
c. Maeneo ya kimatendo ya kuwa “mwili mmoja”ni pamoja na:
(1) Kimwili—maisha ya mkeo na afya yake yawe ya thamani kwako kama mwili wako.
(2) Kihisia—hisi na kuonyesha viwango vyote vya upendo kwake, furahia na
kuhuzunika pamoja naye.
(3) Kiakili—fanya maamuzi kwa faida yake na kwa faida ya ndoa.
(4) Kimaamuzi—amua kwa faida yake na kwa faida ya ndoa.
(5) Mapato—mhudumie.
(6) Kimatamshi—kile usemacho kwake, kuhusu yeye, au anapokuwepo chapaswa
kumjenga na kuonyesha kweli isemwayo kwa upendo.
(7) Ukimchukua kwa moyo kama msaidizi afaaye kwa maisha yako katika majukumu
na nyanja zote za maisha—Unapokuwa na siri dhidi ya mkeo, mfano siri kuhusu
mambo ya pesa, sit u itazuia mume na mke kuwa“umoja,”lakini pia husababisha ugumu
kwa mke kutekeleza jukumu lake kama “msaidizi” kwa mumewe (Mwz 2:18). Kwa
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
29
hiyo, wanaume wanapotenda kwa namna inayozuia ukaribu, umoja, na “kuwa wamoja”
katika ndoa, wanafanya kinyume cha maana ya ndoa na kusudio lake, na mapenzi ya
Mungu kwa wake.
5. “Na mwanamume na mkewe walikuwa uchi wote na hawakuona haya.”
a. Uhusiano wa Adam na Hawa kabla ya anguko unaelezwa. Kinachoelezwa ni ndoa bora ya
Kimungu ambayo ilikuwepo kabla ya anguko. Kwa hiyo, tukiwa tumefanywa upya na
kuongozwa na Roho Mtakatifu na neno la Mungu, twapaswa kutamani, na kujitahidi kuwa na
hali hii katika ndoa zetu.
b. Uchi
(1) Muonekano wa kimwili huelezea dhana pana; hakuna kinachowatenganisha mke na
mume katika uhusiano wao.
(2) Humaanisha kuwa mume na mke walikuwa wazi kabisa, hakuna kificho.
(3) Humaanisha mke na mume hawakuwa na cha kuficha, na hawakuhitaji aina yoyote
ya funiko.
(4) Yamaanisha kuwa mume na mke wanaweza kuambiana kwa uwazi, ukweli, kwa
hali hatarishi wao kwa wao.
c. Hawakuona haya
(1) Yazungumza kuhusu dhamiri, mwitikio wa mhemko.
(2) Mke na mume hawakuona haya kwa sababu hakuwa wametenda dhambi dhidi ya
nafsi au mmoja kwa mwingine.
(3) Hii pia yamaanisha kuwa hali ya kuwa uchi ya mke na mume si dhambi wala jambo
la aibu.
B. Efe 5:25-33—“25Enye waume,wapendeni wake zenu,kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa,akajitoa kwa
ajili yake, ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji na kwa neno, 27apate kujiletea Kanisa tukufu,lisilo na
ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo;bali liwe takatifu lisilo na mawaa. 28Vivyo hivyo imawapasa waume
nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. 29Maana hakuna
mtu anayeuchukia mwili wake popote; bali huulisha na kuutunza,kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.
30Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake. 31KWA SABABU HIYO MTU ATAMWACHA BABA YAKE NA MAMA
YAKE, ATAAMBATANA NA MKEWE NA HAO WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA. 32Siri hiyo ni kubwa,ila
mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. 33Likini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe;
wala mke asikose kumstahi mumewe.”
1. Kifungu cha Efe 5:25-33.
a. Waefeso 5 ni mjadala mpana zaidi wa Paulo kuhusu wajibu wa waume na wake.
b. Kifungu kinaamsha kutoka ndani ya Paulo, mjadala uhusuo namna sahihi ya “kuenenda”
(kuishi) kwa Wakristo [kihalisi] (Efe 4:1; 5:1-2, 15). Maelezo bayana zaidi yachipuka kutoka
kwa Paulo akihimiza “mjazwe Roho” (Efe 5:18). “Kujazwa Roho,”kwa upande mwingine,
inajidhihirisha kwa matendo haya: “kusema” (5:19); “kuimba” (5:19); “kushukuru” (5:20); na
“kujitiisha [kutii] mmoja kwa mwingine” (Efe 5:21). Kisha Paulo anaielezea dhana ya kujitiisha
[kutii] ndani ya ndoa—kwanza anaitumia kwa wake (Efe 5:22-24), na kisha kwa waume (Efe
5:25-33).
(1) Twajua kuwa kifungu kinachoanza na Efe 5:22 chahusiana na Efe 5:21 (na hivyo
nyuma katika Efe5:18) kwa sababu hakuna kitenzi katika 5:22. Ingawaje tafsiri nyingi
za 5:22 zasema kama hivi “Wake, watiini waume wenu, kama kumtii Bwana,”maneno
“watiini” kwa hakika hayapo kwa Kiyunani katika 5:22; yanapatikana pia katika 5:21.
(2) Hakuna popote katika Waefeso 5, au penginepo, ambapo biblia yawaagiza waume
“wawatake”au “wawalazimishe” wake zao“kutii”au “kujitiisha” kwao, au hata
“kuhakikisha” kama wanatii. Utii wa mke ni uchaguzi afanyao, na hatimaye ni swala la
yeye na Mungu. Kwa hiyo, maagizo ya Paulo kwa wake kutii waume zao ni maagizo
kwa wake, sio kwa waume.
(3) Mkazo wa kifungu kwa mume ni wajibu, sio nafasi yake kama “kichwa cha mke.”
Twawajibika kwa Kristo kwa yale tutendayo au tushindwayo kutenda katika kutekeleza
wajibu wetu kama waume, si kwa yale watendayo wake zetu au washindwayo katika
kutekeleza majukumu yao kama wake. Kwa hakika wajibu wetu kama waume ni
mkubwa (na, hatimaye, tutawajibika kwa Mungu zaidi) kwa kuwa nafasi yetu ni ile ya
“kichwa.” Tazama Luka 12:48b—“Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo atatakwa
vingi; naye aliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka zaidi.”
2. Uchambuzi wa Efe 5:25-33.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
30
a. “Enyi waume, wapendeni wake zenu”
(1) Kumpenda mkeo ni amri, si wazo. Twapaswa kuwapenda wake zetu bila kujali
misimamo ya tamaduni na matatizo ya kimahusiano. Umuhimu wa hili unaonekana
kwenye ukweli kwamba limerudiwa mara tatu (Efe 5:25, 28, 33).
(2) Wapendeni wake “zenu” (Efe 5:25), “wake zao” (Efe 5:28, 33), si mke wa mtu
mwingine.
(3) Wayunani walikuwa na maneno angalau matatu kuuelezea “upendo”: eros—
“shauku au hamasa, kupenda,” mara nyingi shauku itokanayo na kutaka kujamiiana;
phileo—“upendo wa kirafiki,” mara nyingi huonyesha upendo utokanao na urafiki, au
undugu, nk.; na agapao—“kuwa na mtazamo ulio sawa kuhusu, na kuwa upande wa,
kutunza, na kuwa na heshima ya hali ya juu kwa ajili ya, na kuridhishwa na,
kufurahishwa na” (Danker 2000: 395, 1056, 5).
(4) Paulo anatumia agapao katika 5:25, 28, na 33. Ni neno lenye uzito. Lamaanisha
kumfanya mtu au kitu Fulani kuwa na nafasi ya kwanza katika maisha yako; kufanya
kazi kwa ajili ya, kutumikia, na kutoa nafasi ya muda kwa kile ukipendacho. Hivyo,
inamaanisha kuwa ni tendo la utashi, kuwa na upendo wa jinsi hii kimatendo, na pia
kuwa na “hisia” za upendo, kuvutwa na kuheshimu.
(5) Tendo la kumtanguliza mwingine/utendaji hasa wa agapao waonekana katika
mistari ambapo kitenzi hiki chatumika kumaanisha “upendo”: Upendo wa Mungu kwa
wanadamu waliopotea—“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata
akamtoa mwanawe wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa
milele” (Yohana 3:16); Amri ya Kristo kwa wanafunzi wake—“Amri mpya nawapa,
mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi pendaneni vivyo hivyo” (Yohana
13:34); uthibitisho wa upendo wa mtu kwa Kristo—“Yeye aliye na amri zangu na
kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu, nami
nitampenda, na kujidhihirisha kwake” (Yohana 14:21); “Mtu akisema, ‘Nampenda
Mungu,’ naye amchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda, ndugu yake
ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.” (1 Yohana
4:20); kutokuwezekana kwa tendo la kutumikia mabwana wawili wasio na ulinganifu—
“Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu na
kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi
kumtumikia Mungu na mali” (Math 6:24); na pia upendo wa mwanamume wa cheo,
utawala, na vitu vya dunia—“Ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwapenda kuketi
mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni” (Luka 11:43); “Na hii ndiyo
hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru;
kwa maana matendo yao yalikuwa maovu” (Yohana 3:19).
b. “Kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa nafsi yake kwa ajili yake”
Kristo alilipendaje Kanisa? Kati ya vitu vingine, Kristo alilipenda Kanisa:
(1) Kipekee—Kristo ni mchungaji mwema wa kondoo ambao Baba amempa (Yohana
6: 37; 10:14-17; 17:6-9). Waliwachagua kabla ya kuwekwa msingi wa dunia (Efe 1:3-
4). Kama ilivyosemwa mwanzo, Kristo ana bibi arusi mmoja (Kanisa—tazama, Ufu
19:7; 21:2, 9). Hivyo, mwanaume ana mke mmoja. Na hii huonekana katika sifa
atakiwazo kuwa nazo mzee au mwangalizi wa kanisa; kwani Kanisa ni kielelezo kilicho
hai cha Kristo duniani, kiongozi wa kanisa sharti awe mume wa “mke mmoja” (1 Tim
3:2; Tit 1:6). Katika namna iliyo maalum, Upendo wa kristo kwa bibi arusi wake
haufanani na upendo wake kwa mtu au kitu kingine chochote. Upendo wetu kwa bibi
arusi wetu wapaswa pia uwe wa kipekee, wenye kina, wa karibu zaidi, kuliko ule
upendo tulionao kwa mtu au vitu vingine.
(2) Kwa namna ya kujitoa mhanga—Huu ni moyo wa kifungu hiki kuhusiana na wajibu
wa mume kwa mke wake.
(A) Tafakari namna tofauti mbali mbali ambazo Kristo alitupenda kwa kujitoa
mhanga: (i) Alijinyenyekesha na kuuacha utukufu wake mbinguni na usawa
wake na Baba na kuutwaa mfano wa mtumwa—kwa ajili ya bibi arusi wake
(tazama Filp 2:5-7); (ii) Alitoa muda wake, alivyonavyo, fikra, hisia—vyote
alivyokuwa navyo —kwa ajili ya wanafunzi wake (bibi arusi wake); (iii)
Aliteseka kimwili, kihisia, na kiroho kwa ajili ya bibi arusi wake; (iv) Alishinda
majaribu kwa ajili ya bibi arusi wake (Luka 4:1-13); (v) Alichukua maumivu,
uchungu, na mwishowe dhambi za bibi arusi wake; (vi) Aliutoa uhai wake kwa
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
31
ajili ya bibi arusi wake.
(B) Fikiri jinsi Kristo alivyotupenda kwa namna ya kujitoa mhanga: (i)
Alichukua jukumu—alichukua hatua ya kwanza (Filp 2:5-7); (ii) Alichukua
jukumu la kutupenda kwa kujitoa kwanza tulipokuwa waasi na tusiopendeka
(Rum 5:8; 1 Tim 1:15); (iii) Hii yamaanisha tuwapende wake zetu licha ya
madhaifu yao, kushindwa, na dhambi. Twaweza kufanya haya kwa: kutoangalia
dhambi zake na tabia mbaya wakati wote; ukimtakia furaha, mafanikio, kwa
moyo wa kupenda; usiyanene madhaifu yake mbele ya watoto au kwenye
kadamnasi, lakini, inapobidi, mkosoe kwa mtazamo chanya, kwa heshima na
unyenyekevu, na lengo safi la kumsaidia; usimtumie kama mfano katika
mahubiri bila ya ruhusa yake; usimtupe wala kumwacha(na kamwe usitishie
kufanya hivyo), kwa sababu Kristo hatutupi wala kutuacha kamwe (na
hatutishii kufanya hivyo) (Ebr 13:5).
(C) Kristo, alituagiza kupenda kwa kujitoa mhanga kwa matendo na
mafundisho:
(i) Kristo alituagiza bayana “Mpendane. Kama vile nilivyowapenda
ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo” (Yohana 13:34)
(ii) Ingawaje waume mara kwa mara hutumia nafasi yao kama “kichwa
cha familia” au “kichwa cha mke” kujaribu “kumkandamiza”
mke/familia” na kulazimisha muafaka kutokana na matakwa yao,
Kristo ameshashughulika na mtazamo huu katika Math 20:25-28, alipo
waambia wanafunzi wake: 25Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua
ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao
huwatumikisha. 26Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu yeyote
atakaye kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; 27na mtu yeyote
anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumishi wenu; 28kama vile
Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa
nafsi yake iwe fidia ya wengi.”
(iii) Katika Yohana 13:5, 12-15 Kristo alitoa kielelezo bayana
kuonyesha maana ya “kiongozi mtumishi”—na akaoanisha na amri
kwa wafuasi wake kufanya vivyo hivyo: 5Kisha akatia maji katika
bakuli,akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile
kitambaa alichojifunga. . . . 12Basi alipokwisha kuwatawadha miguu,
na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, “Je!
Mmeelewa na hayo niliyowatendea? 13Ninyi mwaniita, Mwalimu, na
Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo. 14Basi ikiwa
mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa
vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. 15Kwa kuwa nimewapa
kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.”
(iv) Je Kristo alipoteza nguvu zake, wadhifa au mamlaka kwa sababu
alijinyenyekesha na kuwatumikia wanafunzi (kutawadha watu miguu
ilikuwa kazi ya mtumwa yule wa ngazi ya chini kabisa katika jamii)?
Hapana. Je Kristo alifanyika “mtu pungufu” kwa ajili ya kile
alichofanya? Hapana—badala yake alifanyika “zaidi” ya mtu wa
kawaida, kwa sababu ili mtu aweze kuwatumikia wale walio chini yake
kiwadhifa na mamlaka sharti awe na nguvu isiyo ya kawaida na tabia
ya unyenyekevu. Je heshima ya Kristo kwa wanafunzi wake ilipotea—
au kwetu—kwa sababu ya kile alichofanya? Hapana.
(v) Maadam Kristo hakupoteza nguvu zake, wadhifa, mamlaka,
uanaume au heshima kwa kuwatumikia wanafunzi wake, na kwa kuwa
aliwaambia wafuasia wake bayana (wakiwemo waume) watende kama
alivyotenda na kuiga mfano wake wa uongozi, ni kwa nini waume
hawaonyeshi pendo la kujitoa mhanga kwa wake zao ambao ni wenzi
wa karibu kwao (“mwili mmoja”) kuliko hata wanafunzi wa Kristo
walivyokuwa kwa Kristo? Twawezaje kuuonyesha upendo wa kujitoa
mhanga kwa wake zetu? Njia za kufanya hivyo hazina mipaka kama
vile mazingira yetu na fikra; mifano ya upendo huo wa kujitoa mhanga
ni pamoja na: mwanamume kukata kuni; kuteka maji kisimani;
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
32
kumsaidia mke kupika; kumsaidia kuosha vyombo; kukaa na watoto ili
mke apumzike au kutoka na rafiki zake, nk.
c. “Ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno,apate kujiletea kanisa tukufu,
lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe tukufu, lisilo na mawaa.”
(1) Kristo alimpenda bibi arusi wake kwa kujitoa mhanga kwa kusudi:
(A) amtakase—amtenge na wengine, kwa kusudi la kiungu.
(B) amsafishe—amstahilishe kwa uhusiano wa ndani wa kiungu.
(C) ili amlete Kwake—pamoja na utukufu wake wote (alitaka yeye astahili huo
utukufu, kunururisha mng’ao wa uzuri wa uungu wa mfano wa mungu); bila ila
wala kunyanzi wala waa lolote; lakini awe mtakatifu bila doa (yamaanisha,
bibi arusi wake awe kama Yeye).
(2) Kama Kristo atakasavyo bibi arusi wake kwa njia ya injili, neno lake, ushawishi,
mfano, na Roho, vivyo hivyo mume hupanga mwenendo wa kiroho katika nyumba.
Apaswa kumfanania Kristo, na ndipo amsaidie mkewe naye kuwa kama Kristo.
Chakusikitisha, katika nyumba nyingi mke na mama ndiye awekae kielelezo cha
kiroho. Waume wengi hukwepa wajibu wao. Endapo twapaswa kupenda wake zetu
“kama Kristo alivyolipenda Kanisa,” yabidi tukumbuke kuwa kuna kusudi kuu la ndoa
na la maisha yetu lililo juu yetu.
d. “Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe.
Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Maana hakuna mtu anayechukia mwili wake popote;
bali huulisha na kuutunza kama Kristo naye anavyolipenda kanisa. Kwa kuwa tu viungo vya
mwili wake.”
(1) Paulo anaongeza sitiari mpya hapa ili kuonyesha kina cha ukaribu na umoja
kipasacho kuwapo kati ya wana ndoa—wapaswa kumpenda mkeo kama uupendavyo,
uuhudumiavyo na kuufurahiya mwili wako.
(2) Paulo anadokeza sitiari ya asili ya ndoa—kwamba “wawili watakuwa mmoja”
(Mwz 2:24).
(3) “Hakuna aliyewahi kuchukia mwili wake”—kwa kuwa mwanamume hajipigi
mwenyewe, hawezi kumpiga mkewe. Ampigapo mkewe hastahili kuwa kiongozi
kanisani kwani kwa tafsiri mume ampigaye mkewe tayari “analaumika, hana kiasi,hana
busara, au haheshimiki” (kama itakiwavyo katika 1 Tim 3:2), ni “mgomvi” na si
“muungwana” na ni “ mbishi” (katika kukiuka maagizo ya 1 Tim 3:3), na “hatawali
nyumba yake vema” (katika kukiuka maagizo ya 1 Tim 3:4).
(4) “Huulisha”—kulisha hadi ukomavu. Wazo la msingi hapa ni kulisha, kulea;
mwanamume hulisha mwili wake ili uishi na kukua—si tu kwa ajili ya kuendelea kuwa
hai au kuwepo, bali kustawi, kuishi vema, kuwa na afya na nguvu. Vivyo hivyo, mume
amlishe mkewe ili ndoa istawi, ikue, na kuwa na afya na nguvu.
(5) “Kuutunza”—kulea kwa uangalifu. Wazo la msingi hapa ni kupasha joto au
kuendelea kutia joto; wanaume huikinga miili yao dhidi ya baridi na kuitunza kwa
sababu wanaijali. Vivyo hivyo, waume wanapaswa kusamini wake zoa, kuwatunza na
kuwapa joto kimwili, kihisia, kiroho na katika namna nyingine zote.
(6) “Kama Kristo naye anavyolipenda kanisa. Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake”
(A) Hapa Paulo anauinua mfano wa “mwili” kwenye daraja ya juu,” kwa
kuhusisha mwili wa Kristo na mfano wa “mwili” na Kristo na Kanisa (na
kwayo anaanza kifungu hiki).
(B) “Mwili wa Kristo”ndio kielelezo cha juu zaidi cha Kanisa kuliko vyote
katika agano jipya (tazama Rum 12:4-5; 1 Kor 6:15; 10:17; 12:12-27; Efe
1:22-23; 4:15-16; Kol 1:18, 24; 2:19).
(C) Kimsingi mfano wa “mwili” unatumiwa katika maandiko kwa sababu za
kimahusiano:
(i) Uhusiano wa Wakristo kwa Kristo —Kristo hunawirisha na
kuutunza Mwili wake; kama Mume kwa upole huhudumia bibi arusi
Wake. Zaidi ya hapo, Hutufikisha katika ukomavu wa Neno Lake,
Roho wake, na Sakaramenti zake. Tunapaswa kuunganika, na kujali
wake zetu (ambao ni “mwili mmoja” na sisi) kama afanyavyo Kristo
kwa Mwili wake, bibi arusi Wake.
(ii) Uhusiano wa Wakristo wao kwa wao—Sisi sote tu “washiriki” wa
mwili wa Kristo. Kwa hiyo, kila mmoja ana thamani kubwa. Kwa
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
33
kweli, kila mmoja ni mhimu ikiwa mwili wapaswa kutenda kazi
sawasawa.
(D) Mfano wa Paulo, na hasa anapozungumzia mwili wa Kristo anasisitizia
“umoja” ambao wapaswa kuwa sifa iliyomo katika uhusiano wa mume na mke
ndani ya ndoa ya Kikristo.
(i) Katika 1 Kor 1:13 Paulo aliuliza kwa ufasaha, “Kristo
amegawanyika?” Jibu, kwa hakika ni, “Hapana.” Kwa hiyo,
Wakristo—na hasa waume na wake wa Kikristo—hawapaswi
kugawanyika wao kwa wao. Hakika, katika Yohana 17:22 Kristo
aliomba ya kwamba tuwe na umoja, kama Kristo alivyo umoja na
Baba. Ikiwa umoja wa jinsi hiyo unapaswa kuonekana mahali popote
au kati ya kila mtu, unapaswa kuonekana katika muunganiko ulio wa
ukaribu na undani kuliko yote, ule wa mume na mke.
(ii) Kwa kweli, mke na mume wa Kikristo wanapogawanyika, hawatoi
uwakilishi sahihi kuhusu Kristo kwa dunia. Migogoro ya ndoa na
mgonvi na matengano ni njia ya kutenganisha alichokiunganisha
Mungu (Math 19:6), na ni njia ya kuugawa mwili wa Kristo. Kwa
hiyo, matengano katika ndoa kati ya Wakristo yana matokeo mabaya
kiroho.
(iii) Kwa hiyo, waume wa Kikristo wapaswa kuwa na heshima kubwa
kwa wake zao kimatendo: (a) kwa sababu wanaiheshimu miili yao,
ambayo kwa upande mwingine inahusiana na Kristo anavyoheshimu
“viungo” vya mwili wake kanisa; na (b) kwa sababu, kimwili na
kiimani, kuna umoja kati ya mume na mke ukifananishwa na umoja
uliopo kati ya Kristo na Kanisa.
e. “KWA HIYO MWANAMUME ATAMWACHA BABA YAKE NA MAMA YAKE NAYE
ATAAMBATANA NA MKEWE, NAO WATAKUWA MWILI MMOJA. Siri hii ni kubwa; ila mimi
nasema habari ya Kristo na kanisa.”
(1) Paulo anamalizia kwa kuunganisha Mwz 2:24 na Kristo na kanisa kipekee.
(2) Kwa kuoanisha ule “umoja” wa mume na mke na Kristo na kanisa, Paulo pia
anaweka wazi ya kuwa mume hapaswi kuwa huru mbali na mkewe. Wanaume wengi
hufikiri ya kuwa wako huru kuishi wanavyotaka, mbali na wake zao kimawazo, kihisia,
kuhusiana na yale ya kujali, kimaoni au kimatakwa. Mume wa Kikristo hana haki ya
kufanya hivyo. Yeye ni wa muhimu sana kwa mke wake, kama muunganiko wa mwili
na kichwa, au Kristo na kanisa; hawa wawili hawawezi kutenganishwa.
(3) Tamko la kipekee kuhusu ndoa ya kuwa inahusu hasa Kristo na kanisa yadhihirisha
kuwa, asili yake, ndoa ni ya kiroho—ni taasisi ya kiroho.
(4) Wakristo hasa wanapaswa kuzingatia kwa makini umuhimu mkubwa wa ndoa,
tukiangalia ukweli kwamba, kwa asili, ni ya kiroho na humwakilisha Kristo na kanisa.
C. Kol 3:19—“Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.”
1. Kama katika Efe 5:25-33 Paulo tena:
a. Huweka majukumu ya waume (na wake) ndani ya maisha mapya katika Kristo, na maelekezo
kiujumla kuhusu namna sisi kama Wakristo tunavyopaswa kuishi.
b. Amri (si maoni) waume wapendeni wake zenu.
c. Anatumia neno agapao anapozungumzia “upendo.”
d. Anawaamuru waume kuwapenda wake“zao” (si mke wa mwingine).
e. Anasisitizia majukumu ya mume na wajibu wake na si haki zake na mamlaka yake.
2. “Msiwe na uchungu nao”
a. Kitenzi “uchungu” (pikraino) kimetokana na neno linalomaanisha “kilichochongoka” au
“kikali,” na hapo ikapata maana ya “kali” au “ladha chungu,” “enye-hasira” au “mkali” (Dunn
1996: 249).
b. Tafsiri nyingi za maandiko hutafsiri Kol 3:19 kama “msiwe na uchungu nao.” Lakini, kama
Dunn anavyoona, “uchungu” iko katika kutendwa. Kwa hiyo, kama ilivyotumika hapa,
“uchungu” yamaanisha kuwa “uchungu uko kwa waume. Kilichopo hapa, basi ni, hisia za
mwenzi atawalaye ambaye anaweza kihalali kushinikiza matakwa yake kwa mkewe lakini
akashindwa kuupata upendo wake na heshima na hatimaye akajiona kuwa anadanganywa na
kupata uchungu kwa kuwa hakupata kile alichotambua kuwa anastahili kupata. . . . Haya
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
34
yatakuwa hasa ndiyo matokeo ya yule ambaye husimamia haki zake tu na ambaye wala hajui
vyakutosha kinadharia na kimatendo upendo unaozungumziwa katika nusu ya kwanza ya huo
mstari.” (Dunn 1996: 249)
c. Katika namna iliyo halisi basi, Kol 3:19 huonyesha madhara yanayoweza kutokea kirahisi
(na ambayo yabidi tuyaepuke wakati wote) endapo waume hawatajenga tabia sahihi kuhusiana
na wake zao, na hawaonyeshi upendo kwa wake zao kama Kristo alivyolipenda kanisa. Kwa
kweli, ikiwa yeyote ni “mwenzi atawalaye ambaye kisheria anaweza kushinikiza matakwa yake
kwa mkewe,” ni Kristo. Hata hivyo, Kristo ha “simamii haki zake tu” anapohusiana na bibi
arusi Wake, kanisa; ha “lazimishi” bibi arisi kufanya maagizo yake. Kwa hiyo, ikiwa kuna
anayestahili kuwa na “uchungu” dhidi ya bibi arusi wake, ni Kristo. Lakini bado, hana uchungu.
Wakati wote na kwa namna zote, mbele za bibi arusi wake husimama kama mume wa kustahili
kuigwa. Anatuagiza tufanye vivyo hivyo—na kwa njia hiyo kuepuka uchungu kwa wake zetu
jambo ambalo laweza kutokea wanaposhindwa kutenda sawasawa na viwango vyetu (kwa
sababu ikiwa kuna jambo moja ambalo linaweza kuzuia watu wawaili kuwa na “umoja” ni
uchungu).
D. 1 Pet 3:7—“Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo
kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.”
1. Kifungu cha 1 Pet 3:7.
a. 1 Pet 3:7 kimuundo inafanana na kile anachojadili Paulo kuhusu wajibu wa waume katika
Efe 5:25-33.
(1) Vifungu vyote; cha Paulo (Efe 5:22-33) na Petro (1 Pet 3:1-7) vina maelezo ya kina
zaidi kuhusu wajibu wa waume na wake.
(2) Mijadala yote hii, kwa namna nyingine, ni matumizi bayana ya asili ya unyenyekevu
wa Kikristo ambao, kwa upande mwingine, ni wazo la msingi zaidi la namna Wakristo
wanavyopaswa kuishi:
(A) Kifungu cha Waefeso chajitokeza kutoka kwa mjadala wa Paulowa jinsi
sahihi ya “mwenendo” wa Mkristo (Efe 4:1; 5:1-2, 15). Kifungu bayana zaidi
kimechipuka kutoka katika himizo la Paulo “mjazwe Roho” (Efe 5:18).
“Kujazwa Roho,” kwa upande mwingine, imefafanuliwa kwa kanuni nne:
“mkisemezana” (5:19); “mkiimba” (5:19); “na kushukuru” (5:20); na
“mkinyenyekeana [kunyenyekea]” (Efe 5:21). Efe 5:22 hapo huanza kutumia
dhana ya kujitiisha [kutii] kwa wake na waume.
(B) Vivyo hivyo 1 Petro huelezea namna sahihi ya Mkristo kuishi,yamaanisha,
“kuziepuka tama za mwili” na “mkiwa na mwenendo mzuri” (1 Pet 2:11-12).
Kifungu kilicho bayana zaidi ni kile cha Petro kwa waamini wote “tiini kila
kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana” (1 Pet 2:13). Hatimaye Petro
anatumia kanuni tatu—watumishi “watiini [Paulo anatumia kanuni hiyo hiyo
katika Efe5:21] bwana zenu kwa hofu nyingi” (1 Pet 2:18), “ninyi wake,
watiini waume zenu” (1 Pet 3:1), na “ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa
akili;” (1 Pet 3:7)—ambayo hupata nguvu chanya kutoka katika kitenzi katika
2:13. Petro pia anatumia mfano wa mateso ya Yesu kufafanua dhana ya utii wa
Kikristo (1 Pet 2:21-25); anatuhimiza bayana tufuate kielelezo hiki: “maana
Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake”
(1 Pet 2:21). Katika 1 Pet 3:1, 7 anaainisha matumizi ya dhana hizi za utii na
kielelezo cha Kristo kwa wake na waume kwa kutumia kielezi (“kadhalika”).
Hatimaye, jukumu letu na wajibu wetu kama waume ni muhimu uonekana
kama njia bayana ambamo twaonyesha utii kama Kristo—ambao ni kiini cha
mwenendo “bora” wa [kikristo] (1 Pet 2:12).
b. Neno“kadhalika”au “kwa namna hiyo” (1 Pet 3:1, 7) yatoa wajibu wa mume kwa mke na
mke kwa mume
(1) Kama ilivyokuwa kweli kwa Efe 5:22-24, maagizo ya (kuwa mtii) kwa mke
yametolewa kwa mke: na mume hakuagizwa “kumfanya” mkewe awe mtii, au
“kuhakikisha” kuwa anatii—huo hatimaye ni wajibu wa mke kwa Mungu.
(2) Kwa namna moja, wajibu wa mke kutii waweza kuhusianishwa na uwajibikaji wa
mumewe. Kama McKnight asemavyo, “Maana ya utii yaweza kueleweka kwa kuuliza
maana ya upendo” (McKnight 1996: 189n.33). Mke hakuagizwa “kumfanya” mumewe
aishi naye kwa akili au amheshimu, au “ahakikishe” kuwa mumewe anafanya hayo—
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
35
huo hatimaye niwajibu wa mume kwa Mungu. Hata hivyo, “tatizo la utii” kila wakati
lina “mume atawalaye kwa mabavu katika mizizi yake” (Ibid.: 189). McKnight
anaongezea: “Mke wa Kikristo anapotamani kumpenda mumewe kwa moyo wake wote
na mume anapotamani kumpenda mkewe kwa moyo wake wote, swala la utii
halijitokezi . . . . Mtazamo wa ndoa ya Kibiblia uko katika upendo na kuhudumiana
mmoja kwa mwingine. . . . Waume mara nyingi hukimbilia kudai utii wanaposhindwa
‘wanachotaka’; hiyo yaonyesha ubinafsi, badala ya upendo na kujitoa kwa mkewe
(kwani ndivyo Kristo alivyolipenda Kanisa). Mume apaswa kujiambia, ‘Kwa nini ni
lazima nitumie nguvu ili mambo yafanyike?’ Mara nyingi utaona kuwa anajali kupata
matakwa yake na ya mkewe hayana uzito kwake. Mwenendo wa namna hiyo si upendo.
Ndoa zilizojaa upendo, kuheshimiana na kuinuana mara chache, naamini, zitahitaji
kukimbilia swala la utii.” (Ibid.: 189-90)
(3) Akiwa mshirika “mkuu”, wajibu wa mume—na hatimaye mkokotoo manufaa wake
na hukumu—ni kubwa.
2. Uchanganuzi wa 1 Pet 3:7.
a. “Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili”
(1) Waume wapaswa kuishi na wake zao, na si mbali nao. Na hii ni dhana moja ya
“kuambatana” na mkewe na kuwa “mwili mmoja” naye.
(2) Neno litokanalo na “kuishi pamoja”ni (sunoikountes) lamaanisha swala la
kujamiiana na hali halisi ya mahusiano katika ndoa. Mume wa Kikristo “si mbinafsi na
mwenye kushurutisha katika maswala ya kujamiiana au mahusiano ya ndoa; badala
yake hutumia busara, yuko makini na mhudumiaji” (Ibid.: 186).
(3) “Kwa akili ” yamaanisha kuishi na mkeo “si tendo tu la kimwili bali ni kitu
ambasho mwanamume anapaswa ajue namna ya kufanya” (Michaels 1988: 168). Kwa
Kiyunani, kifungu hiki chamaanisha “kwa ujuzi au maarifa.” “Maarifa” hayo ni yale
yashindayo maarifa yote, nayo ni maarifa ya Mungu katika Kristo Yesu, kwa sababu ni
kwa maarifa hayo tu mwanamume anaweza kuelewa kwa usahihi asili ya wanaume na
wanawake, maana ya ndoa, na anaweza kuongoza maisha yake sawasawa. Grudem
anaeleza: “Maarifa’ anayoyakusudia Petro hapa yaweza kuwa ni pamoja na yale
maarifa ambayo yatakuwa ya faida kwa uhusiano wa mume na mke: maarifa ya kusudi
la kimungu la ndoa na kanuni za ndoa; maarifa ya shauku ya mke, malengo na vikwazo;
maarifa ya nguvu yake na udhaifu wake kimwili, kihisia na kiroho; nk. Mume aishie
kulingana na maarifa hayo atafaidisha mahusiano ya ndoa yake kwa kiwango
kikubwa—maarifa hayo hayapatikani ispokuwa kwa kujifunza neno la Mungu mara
kwa mara, na kuwa na ushirika wa utulivu kama mume na mke.” (Grudem 1988: 143).
b. “Kama chombo kisicho na nguvu, kwa kuwa ni mwanamke; na kumpa heshima kama mrithi
wa neema ya uzima”
(1) “Mwanamke”ni tafsiri neno adimu limaanishalo, “jinsi ya kike.” Hii yaonyesha
kuwa “Petro anaangalia sifa na asili ya kike na anasema kuwa hali ya “kike” ya mke
yatosha kumfanya mume ampe heshima” (Grudem 1988: 143).
(2) “Udhaifu”kimsingi yamaani udhaifu alionao mwanamke kimwili anapolinganishwa
na mwanamume; na hii imeonyeshwa pia kwa matumizi ya neno “chombo” ambayo
mara nyingi humaanisha mwili. Hata hivyo, “kifungu pia chaonyesha wanawake ni
wadhaifu kuhusiana na mamlaka katika ndoa (mst 1, 5-6), na hivyo Petro anawaagiza
waume kuwa badala ya kutumia mamlaka yao kwa mambo ya ubinafsi wayatumie kwa
kuwapa heshima wake zao” (Ibid., 144).
(A) Waume wanapaswa kukumbuka kuwa machoni pa Mungu heshima ni ya
wale (au wajifanyao) ‘wa mwisho’ au ‘wadogo,’kwa mtazamo wa dunia”—
tazama Math 5:3-12; 18:1-4, 10-14; 19:30; 20:16; 23:11-12; 25:40, 45;
Marko 9:33-37; 10:42-45; Luka 14:7-11; 1 Kor 1:26-30; 12:22-25; Yak 2:5;
4:6; 1 Pet. 5:5-6 (Michaels 1988: 170). Hivyo, kwa sababu ya nafasi yake chini
yako, na tofauti yake na wewe, waume wapaswa kuchukua tabia ya Kimungu
kuwaelekea wale waonekanao kuwa wamepungukiwa machoni pa watu
(yamaanisha, mfumo wa Mungu katika biblia yote ni kuwapa upendeleo wale
walio na upungufu,au ajifanyao hivyo).
(B) “Kwa hiyo heshima ya jinsi hii yapaswa ihusishe maneno yatiayo moyo
muwapo faragha na mbele za watu, na kuchagua vipaumbele kuhusiana na
matumizi ya wakati na pesa” (Ibid.)
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
36
(3) “Mrithi pamoja wa neema ya uzima.” Kwa nafasi yake kama mwanamke (hali yake
ya kike, na udhaifu wake—inamaanisha, nafasi yake chini yako, na tofauti yake na
wewe) ilikuwa sababu moja, ndani na ya kibinafsi, kwa kumwonyesha heshima mkeo,
Petro sasa anatupatia sababu ya pili (na kimtazamo iko kinyume) ya kuonyesha
heshima kwa mkeo: nafasi yake ikiwa sawa na wewe, na mlandano wa kimilele na
wewe. Hali hii muhimu ya kufanana na usawa imeonyeshwa kwa matumizi ya neno
“mrithi pamoja,”ambayo pia imetumika katika Rum 8:17, Efe 3:6; and Ebr 11:9
kuonyesha usawa katika urithi na ushiriki wa kupokea ahadi na mafao tupatayo kwa
kuwa washiriki wa mwili wa Kristo na familia yake. Kwa sababu Mungu amemchagua
na kumheshimu mkeo kwa vigezo sawa kama alivyokuchagua wewe, mume lazima
amheshimu mkewe. Vinginevyo mume atakosa kutoa heshima kwa kile
anachokiheshimu Mungu.
c. “Kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.”
(1) Namna umtendeavyo mkeo ni ishara ya, na matokeo—chanya au hasi—uhusianao
wako na Mungu na maendeleo yako kiroho.
(2) Hii “yako” inawahusu waume, au maombi ya waume pamoja na wake.
(A) Michaels anaamini kuwa “yako”ya mwisho “huleta pamoja kitengo chote
kinachohusiana na ndoa (mst 1-7) hivyo hata wake wenye waume wasioamini
(mst 1-2) wanaweza kuwa na picha ya ndoa inavyoweza kuwa ndani ya
Kristo—kanisa la nyumbani, mume na mke waishipo pamoja kama jamii
imwombayo Mungu na ‘warithi pamoja’ wa wokovu” (Michaels 1988: 171).
(B) Mtazamo mwingine umetamkwa na Grudem: “‘Kwenu’ ina maanisha kwa
‘ninyi’ ambao Petro anawaandikia, yaani, waume, na hivyo marejeo yahusu
maombi ya wanaume kwa ujumla. . . . Asiwepo mume yeyote Mkristo
atakeyafikiri kuwa anaweza kufanikiwa kiroho bila kuwa mwombaji wa dhati.
Na mume asitarajie kuwa na maisha ya maombi ya mafanikio bila kuishi na
mkewe kwa maelewano, akimheshimu.” (Grudem 1988: 145-46).
(3) Bila kujali kama“kwenu” yamaanisha waume tu, au na pamoja na wake, kifungu
hiki cha mwisho cha 3:7 kwa mara nyingine chaonyesha hasa asili ya kiroho ya ndoa.
Kama anavyomalizia Grudem, “Kutumia muda ili kujenga ndoa njema ni mapenzi ya
Mungu; ni kumtumikia Mugnu; ni hali ya utendaji wa kiroho inayompendeza yeye”
(Ibid.: 146).
III. Ushauri kwa Waume.
Carol Arnold, akiandika katika kitabu chake The Liberation of a Resentful Wife (Ukombozi wa Mke
Mwenye Uchungu) (2006) anatoa dondoo zifutazo kwa waume ili wawe na ndoa zenye mafanikio:
A. Ninyi mu wahitaji. Yapasa muelewe kuwa Mungu aliwaumba katika hali isiyokamilika na mna uhitaji. Ni
ujinga kudhani kuwa humhitaji mkeo. Unapoitambua hali yako ya uhitaji unajua hakika kuwa wewe ni tegemezi
kwa msaada wa Mungu na mpango wake mkamilifu wa uumbaji aweza kukukamilisha na kukupa kila
kiwezacho kukidhi mahitaji yako. Itakusaidia kujenga moyo wa shukrani na kufurahia kile alichofanya Mungu
katika kukidhi mahitaji yako kwa kukupa wewe mke.
B. Mkeo ni zawadi kutoka kwa Mungu. Mke ni zawadi kutoka kwa Mungu (Mith 19:14). Ni wa thamani, taji
ya mume, na kitu chema (Mith 12:4; 18:22). Yasemekana ni wa thamani kuliko vito (Mith 31:10).
Twaitendeaje zawadi ya thamani na ya bei kubwa?
C. Umpende kama Kristo alivyolipenda kanisa. Akiwa bustani ya Gethemane Yesu alimwomba Baba
kubadilisha mpango wa ukombozi ili asiangikwe msalabani na kufa kwa ajili ya dhambi za kanisa; hata hivyo,
Yesu alijitiisha chini ya mapenzi ya Baba, kwa sababu hilo ndilo lililokuwa jambo sahihi kufanya. Mungu
anawataka waume wawapende wake zao vivyo hivyo—kwa kujitoa, kutii, hata inapokuwa vigumu, kwa sababu
ni jambo sahihi kufanya, na kwa sababu ni picha kwa dunia kuhusiana kile ambacho huhitajika katika
mahusiano ya ndoa. Mahusiano ya karibu na dhati huhitaji kujitoa, hali ya kutokuwa mbinafsi, na hata kuachilia
haki zako kwa faida ya mwingine.
D. Je ungependa kujitii kama wewe ungekuwa mke? Mume mwenye hekima atagundua kuwa mkewe ana akili
kuliko yeye katika maeneo mengi, na uelewa wa nyumba yake na familia ambao yeye hana. Hivyo, atamsikiliza.
Mke—kama wewe—unataka kuwa mtawala wa maisha yako mwenyewe. Kumtendea mkeo kwa namna ile
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
37
utakayo kutendewa (tazama Math 7:12; Luka 6:31), kuonyesha rehema, upendo, na huruma, itamfanya akutii
kwa urahisi, kuitika kwako na kukutana na mahitaji yako. Kama wewe ungekuwa yeye, je ungependa kujitii,
katika hali hiyo uliyonayo?
E. Msaidie mkeo endapo wataka awe radhi nawe unapomtaka .Wake huitika kutegemea na namna
watendewavyo. Mume mwenye hekima ataonyesha mahaba kwa mkewe, akimkumbatia si kwa malengo ya
kibinafsi, akimwambia “Nakupenda” na pia atafanya hivyo kwa vitendo. Ikiwa unataka mkeo akukubali, basi
msaidie kufanya hivyo. Fanya kila uwezacho kuzuia asichoke sana kiasi cha kukosa nguvu za kukuhudumia
inapofika mwisho wa siku. Mke mmoja alisema, “Kwangu mimi, tendo la ndoa huanzia jikoni. Mume wangu
anaponisaidia kuosha vyombo, itakuwa rahisi kuitikia anaponitaka.” Wanawake wengi wako tayari kufanyakazi
kwa bidii wanapojua kuwa waume zao pia hufanya vivyo hivyo—lakini unapokuwa umekaa wakati yeye
anafanyakazi usishangae akikataa wakati unapomtaka.
F. Jali mwili wako. Wanaume wanapenda mwanamke anayependeza. Vivyo hivyo hakuna mwanamke
anayependa mwanamume aliyejiachia tu, aliyenenepeana au mwenye harufu mabya.
G. Mpe mkeo nafasi ya kuwa na wanawake wengine. Kuna mambo yahusuyo wanawake ambayo ni wanawake
wengine tu wanaweza kuelewa. Mume mwenye hekima atampa mkewe muda kwa ajili yake na kutengeneza
fursa kwa yeye kuwa pamoja wanawake wengine—Hata ikilazimika kugharimia awe na muda kuwa mbali na
wewe na watoto. Faida ya kufanya hivi itaonenkana hatimaye kwa kuwa na ndoa yenye furaha, utoshelevu, na
mke mtii.
5. KANUNI TATU ZA MAWASILIANO ZILETAZO UMOJA
I. Utangulizi: Efe 4:25-32.
A. Mawasiliano yaletayo umoja ni yale yanayotuleta pamoja, na sio kutugawa.
B. Mawasiliano yaletayo umoja ni muhimu kwetu ili kutendea kazi funndisho la umoja tulihubirilo.
1. Kanisani, twatamani umoja wa Roho (Efe 4:3-6).
2. Ndani ya ndoa, twapaswa kujibidiisha tuufikie umoja wa “mwili mmoja” (Mwz 2:24).
C. Mawasiliano yaletayoumoja ni muhimu sana kiasi ambacho Paulo alipowaandikia Wefeso alibainisha
wazi jambo hilo kwanza alipoandika kuhusu mambo ya kimatendo.
II. Mpangilio wa Waefeso.
A. Nafasi ya Mkristo (Waefeso 1-3).
1. Sifa kwa ajili ya ukombozi (1:1-14).
2. Ombi kwa ajili ya nuru ya Kiungu (1:15-23).
3. Nafasi yetu ndani ya Kristo, kibnafsi (2:1-10) na kwa pamoja (2:11-3:13).
4. Ombi jingine (3:14-21).
B. Maisha ya Mkristo kimatendo (Ephesians 4-6).
1. Umoja ndani ya kanisa (4:1-16).
2. Maisha ya utakatifu (4:17-5:21).
3. Kuwajibika nyumbani na kanisani (5:22-6:9).
4. Misuguano ya kuishinda (6:10-24).
C. Kuenenda kwetu na wengine kuonyeshe umoja wa mwili mmoja.
1. Kipindi cha mpito cha Paulo kutoka “cheo” kuelekea “matendo” akiwa na maneno, “Kwa hiyo . . .
mwenende kama inavyoustahili wito wenu” (4:1).
a. Kutoka 4:7-5:21, Maoni ya Paulo yanalenga mwenendo wetu wa binafsi.
b. Kutoka 5:22-6:9, Paulo naandika kuhusu “mwendo” wetu katika mahusiano ya kila siku:
(1) Waume kwa wake.
(2) Wazazi kwa watoto.
(3) Wafanyakazi (watumwa) kwa waajiri (mabwana).
c. Hata mwendo wetu wa binafsi haukuachwa peke yake, bali ni mwendo wa mwamini mmoja akiwa na
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
38
wengine.
2. Mwendo wetu na wengine wapaswa kuonyesha umoja wa mwili mmoja, “roho moja,tumaini moja,
Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, Mungu mmoja na Baba wa wote, aliye juu ya yote na
katika yote na ndani ya yote” (Efe 4:4-6).
a. Watumishi wa kanisa walipewa vipawa kila mmoja kuwajenga watakatifu kuujenga mwili wa
Kristo uwe mwili mmoja uliokamilika ambao Kristo ndiye kichwa (4:7-16).
b. Ili tuweze kufanya haya, ni lazima “mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa
zamani, unaoharibika kwa kuzifuzta tamaa zenye kudanganya; na mfanywe upya katika roho ya
nia zenu,mkavae utu mpya ,ulioumbwa kwa [namna ya Mungu]katika haki na utakatifu wa
kweli” (4:22-23).
c. Ili hili litokee, mawasiliano yaletayo umoja ni lazima. Paulo anaufuatilia wito wake wa umoja
kwa “Basi, uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake” (4:25).
III. Kanuni ya kwanza ya Mawasiliano yaletayo Umoja—Sema Kweli.
A. Kweli ni kile kinachoonyesha uhalisia.
1. Kweli ni hali ya vitu halisi, matukio au dhana, inayoendana na uhalisia. Kweli inahusu uhalisia wote,
si tu mambo ya kidini.
2. Tafsiri ya Mkristo lazima iongeze kuwa kweli ni kile kilichofafanuliwa na kufunuliwa na Mungu
katika neno lake lililo ndani ya Yesu Kristo aliye Kweli (Yohana 14:6).
3. Kuitetea kweli ni sehemu ya kazi yetu ya kitume.
B. Kweli ni kinyume cha udanganyifu.
1. Utu wetu wa dhambi umechafuliwa na “tamaa za uongo” (Efe 4:23).
a. Moyo ni mdanganyifu, mwovu, na mgumu kuelewa (Yer 17:9).
b. Tamaa mbaya na matamanio ni shina la udanganyifu
2. Mara nyingi twaficha ukweli, wote au sehemu yake:
a. ili tujisikie salama, tukubalike.
b. tujisikie wamaana, wenye thamani, wa muhimu, wenye kuhitajika.
c. kwa ajili ya furaha/starehe danganyifu, tukikwepa maumivu au mateso.
d. kukwepa mateso.
e. kupata starehe au burudiko.
3. Hofu, halisi au zakufikirika, husababisha udanganyifu.
4. Tupokeapo habari za kutuhuzunisha, au tunapohuzunishwa, twaweza:
a. kukataa uhalisia, matukio na taarifa;
b. kuwa na hasira, (yaani, twataka “kumuua mjumbe” aliyesababisha tukio la kuhuzunisha);
c. kutumia mantiki, ukweli nusu au uongo mtupu;
d. kukataaa wajibu, au kujaribu kutupa lawama kwa mtu mwingine.
5. Kuukataa ukweli kwaweza kuleta hali isiyo halisi, matengano, na mawasiliano kuvunjika.
C. Utu mpya umeumbwa katika haki utakatifu na kweli (Efe 4:23).
1. Mungu hawezi kusema uongo (Hes 23:19; Ebr 6:18).
2. Yesu ni “Kweli” (Yohana 14:6), and “tuna nia ya Kristo” (1 Kor 2:16).
3. Roho akaaye ndani yetu ni “Roho wa Kweli” (Yohana 14:17; 15:26; 16:13).
4. Kwa hiyo, waamini wanaweza na wanapaswa kusema kweli.
D. Kweli lazima isemwe katika maeneo yote.
1. Ni muhimu kuwa wakweli kuhusu:
a. Tuwazayo.
b. Tusemayo.
c. Tutendayo.
d. Tunavyojisikia na tunayoyapitia kihisia.
e. Utashi wetu, hamu, matakwa, matumaini ya kufikia, na matarajio.
2. Pasipo kweli au penye kweli nusu = kukosa uhalisia au uhalisia nusu = mawasiliano yasiyounganisha.
E. Lazima tuwe makini kuhusu namna (ujuzi) na lini (wakati muafaka) tuseme kweli.
Jinsi na wakati gani unasema kitu inaweza kuwa na umuhimu kama ule wa nini usemacho na kwa nini
unakisema. Kwa kweli, kusema kitu kwa namna isiyo sawa au kwa wakati usio sahihi kunaweza kusababisha
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
39
msikiaji aelewe visivyo kile usemacho na kwa nini umesema.
F. Twahitaji hekima—kweli husemwa kwa upendo (Efe 4:15).
Upendo lazima uambatane na kweli kwa sababu “Mungu ni upendo” (1 Yohana 4:8). Upendo
usipokuwa dira ya manenno yetu hatumwakilishi Mungu ipasavyo. Hata pale ambapo kweli yatutaka tuseme
mambo magumu, lazima tuongozwe na upendo.
IV. Kanuni ya Pili ya Mawasiliana Yaletayo Umoja—Pataneni Kila siku.
A. Si rahisi kuikubali au kusema kweli, hata inenwapo kwa upendo.
Ni rahisi kujeruhi watu, na wanaweza kukwazika na kukasirika, tunaposema iliyo kweli kwao, hasa
inapokuwa kweli wasiyopenda kuisikia au kuikubali. Hivyo ndivyo ilivyo, hata tunapofanya hivyo kwa upendo,
Na kwa sauti isiyokali. Hii yawezatokana na sababu zifuatazo:
1. Kweli mara nyingi hutufanya tupambane na yale mambo halisi tunayoyakataa. Mambo hayo halisi ni
pamoja na kweli kuhusu sisi wenyewe, watu wengine, hali yetu, dunia na Mungu.
2. Tunahofia na kuhisi kupoteza uhalisia wa uongo. Twashikilia mawazo na dhana zisizo kweli kwa
sababu twafikiri vyatupatia usalama, umuhimu, na starehe kumbe ni uongo.
B. Kunapotekea habari zilizo mbaya sana, watu wanaweza hata kupitia “hatua tano za kupokea habari za
majanga”
1. Kanusho (“haiwezekani”; tunawalaumu wengine, tunalazimisha na kutetea).
2. Hasira (twataka “kumshambulia mjumbe”; tunatoa na kuita majina na kujibu mashambulizi).
3. Kujinusuru (tunajaribu “kuokoa sura”).
4. Mfadhaiko/Ukimya (tunauliza “sasa nifanyeje?’ na kusema “sijali na iwe iwavyo”).
5. Kukubali (hatimaye tunakubali kuwa ni wakati wa kubadilika, kwenda na hali halisi na kusonga
mbele).
C. Biblia inawataka watu “kutohifadhi makwazo” na kupatana kila siku.
“Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka” (Efe 4:26).
1. Hasira kama ilivyo si dhambi.
2. Mungu, ambaye hatendi dhambi, hukasirika:
a. Hukasirishwa na waovu kila siku (Zab 7:6, 11; Rum 1:18).
b. Yesu alikasiriswa na dhambi (Marko 3:5; Yohana 2:13-17).
3. Tukubali kuwa tuna hasira na hisia, badala ya kukataa.
4. Kilicho muhimu hapa ni nini kinatukasirisha na matokeo ya kukasirika kwetu.
a. Jaribio la sababu ya kukasirika: je ni sahihi?
(1) Je twakasirika kwa sababu ya “utu wa kale” viwango vya usalama, thamani, starehe,
agenda?
(2) Je twakasirika kwa sababu twaogopa kupoteza usalama, umaarufu, mali, au afya?
(3) Je hatuenendi katika usafi na, hivyo, kuwa kwazo kwa injili?
(4) Je twamwaibisha Bwana?
(5) Je twakasirishwa na viwango vya “utu mpya”?
(6) Je twateswa kwa ajili ya Kristo?
b. Jaribio la matokeo ya hasira:je ni ya-kiMungu?
(1) Kukasirika hadi kujibizana au kupigana ni dhambi (Mith 29:11; 12:16; 25:28).
(2) Kuwa na chuki siku baada ya siku ni dhambi; hivyo, “jua lisichwe na uchngu wenu
bado haujawatoka” (Efe 4:26).
(3) Kuchelewesha mapatano na mtu aliyekukosea ni dhambi; mapatano yafanyike
haraka (Math 5: 23-24; 18:15-17).
(4) Kutokubali kosa ni dhambi; hivyo, twahitaji kunyenyekea kutambua kuwa sisi pia ni
wenye dhambi (Math7:3-5).
(5) Lazima tuwajibike kwa matatizo yanayotokea katika mahusiano yetu, na tujitahidi
kuweka mambo sawa.
V. Kanuni ya Tatu Ya Mawasiliano Yaletayo Umoja—Kumjenga Mwingine Liwe Lengo Lako.
A. Mawasiliano yaletayo umoja hujenga na kuinua wengina katika Bwana.
1. Mawasiliano yaletayo umoja si ya kibinafsi lakini kutazama wengine, maana upendo hautafuti
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
40
mambo yake (1 Wakorintho 13; Rum 15:1-2).
2. Mawasiliano yaletayo umoja hayaridhishwi na hali ya kutunza heshima bali yana mtazamo wa
kuendelea.
B. Tunapaswa kuchagua maneno yetu kwa uangalifu; tukifikiri lililo bora kwa mwingine.
1. Mawasiliano yaletayo umoja “hayaendeshi mdomo kabla ya kuingiza gea katika ufahamu.”
2. Maneno yana nguvu ya “mauti” na “uzima” (Mith 18:21).
3. Maneno yana maana na matokeo tofauti—yote hayalingani au kunufaisha; tunachosema, na namna
tusemavyo, itategemea ufahamu wa msikiaji, uzoefu, hisia, na agenda.
C. Usinene maovu (Efe 4:29).
1. Neno la Kiyunani “uovu” ni sapros, linalomaanisha “lililooza, lililovunda, lisilofaa kwa matumizi.”
2. Mstari unamaanisha hayo kwa maneno yasiyofaa, lakini pia unaweza kutumika kwa mawasiliano
yasiyo ya maneno, kwa mfano kwa ishara za uso au mwili.
D. Sema yale tu yaliyo mema kwa kujenga, kulingana na hitaji la wakati huo, ili yampe neema msikiaji (Efe
4:29).
1. Mawasiliano yajengayo yanahitaji ujuzi wa sasa kuhusiana na mtu katika maeneo yafuatayo:
a. Uwezo wa kufikiri.
b. Hisia na Mahitaji.
c. Malengo na matarajio.
d. Hali ya kiroho na kile kinachohitajika kumjenga huyu mtu.
2. “Hitaji la sasa” huhitaji tathmini sahihi ya hali halisi na mazingira ya tukio.
a. Hii inaweza kupatikana kwa kuchunguza au kuuliza kabla au mawasiliano yanapoendelea.
b. Hii ina msingi pia katika kuelewa neno la Mungu kwa usahihi.
c. Zaidi ya hapo, tathmini sahihi ya hali halisi na mazingira ya tukio ni muhimu ili kutumia
nenola Mungu sawa sawa.
E. Mawasiliano yaletayo umoja huhitaji kujikana.
Nia yetu kubwa iwe ni kumtukuza Mungu katika mawasiliano yetu, na kumjenga yule tunayewasiliana
naye, na si kujitukuza sisi wenyewe. Tunapokuwa na mtazamo wa mambo hayo mawili, tunaweza kutekeleza
amri kuu mbili kumpenda Mungu na kumpenda jirani (Marko 12:28-31).
VI. Hitimisho.
Masiliano yaaletayo umoja yanawezekana kwa neema ya Mungu ndani ya Yesu Kristo kupitia yeye
tunabadilishwa kila siku katika haki, utakatifu na kweli (Efe 4:23).
6. MAWASILIANO: KUELEWANA; KUSIKILIZA; NA UWEZO WA KUHISI MAONO
I. Maelewano.9
A. Mawasiliano ndio uhai wa uhusiano.
Ni mpaka tutakapomwelewa mwenzi wetu na kilicho muhimu kwake, ndipo twaweza “kuunganishwa”
naye. “Muunganiko” wa kweli na mtu mwingine unahusisha hisia na uelewa wa kiakili. Maelewano huhitaji
juhudi. Utahitajika kuwekea mbali mambo yako (inamaanisha, matakwa yako) ili uweze kuridhia mitazamo na
hisia za mwingine.
B. “Wanandoa wenye nia ya kuwa na maelewano watathamini na kufanya kile kipaswacho ili wawe na
mawasilianoya kweli” (Campus Crusade 1993: 76).
Ili mawasiliano ya kweli yatokee yanahitajika angalau mambo haya manne:
1. Muda. Kuwa na muda maalum na mtu ni moja kati ya njia tano muhimu za kuonyesha upendo
(Chapman 1995: 59-78). Muda unahitajika ili kumjua mtu. Tunapomjua mtu tunafanikiwa kuondoa
vikwazo vinavyozuia mawasiliano ya kweli.
2. Kuaminiana. Hamwezi kushinda vikwazo vinavyokabili mawasiliano ya kweli ispokuwa iwepo hali
ya kuaminiana kati ya pande mbili. Hakuna anayependa kuumizwa. Mambo yaliyosemwa sirini, siri
zinazowekwa wazi, lazima viendelee kuwa siri. Hakuna kiwezacho kuathiri uhusiano kama kumsaliti
9Isipokuwa pale ilipoelezwa, sehemu kubwa ya kifungu I na II vimechukuliwa kutoka Campus Crusade 1993: 76-81.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
41
aliyekuamini. Kwa upande mwingine, hakuna kinachoweza kuimarisha uhusiano kama kujiweka wazi
kwa mwingine, hapo ukionyesha kuwa unamwamini, ijapokuwa kwa kufanya hivyo wajiweka katika
mazingira hatarishi.
3. Kujitoa. Kujitoa kwaweza kuwa sehemu ya kuaminiana. Hata hivyo, kujitoa ndani ya ndoa—kwa
mwenzi, kwa ndoa, kwa wazo la ndoa lenyewe—ndicho kiini. Mwenzi wa ndoa hahitaji tu kujua kuwa
yuko salama kuhusiana na siri zake, bali pia ndoa yake iko salama—ya kuwa mwenzi wake amejitoa
kwake. Neno “talaka” kamwe lisitajwe nyakati za majibizano ya hasira au migogoro.
4. Uwazi. Uwazi ni pamoja na: kuwa mkweli;uaminifu; na kujihatarisha (yaani, kuweka wazi siri,
madhaifu, kushindwa, mahitaji na hofu). Hili ni gumu kufanya hasa kwa wanaume. Uwazi kamwe
hauwezekani bila ya vigezo vingine vya mawasiliano ya kweli kuwepo.
C. Kuna ngazi tofauti za mawasiliano ambazo hukuza mahusiano kwa hatua hadi yawe ya karibu zaidi.
Kusudi la mawasiliano na asili ya uhusiano wetu na huyu mtu ndivyo vigezo vitakavyoamua ni ngazi ipi
au zipi zinafaa au ni muhimu kwa mahusiano husika.
1. Ukimwa. Hii hasa ni “kutokuambiana.” Ni mtindo wa “mawasiliano” usio wazi, na namba kubwa ya
watu hujisikia salama kuitumia (mfano, “Hujambo?” “Sijambo”).
2. Ukweli. Kueleza kile unachojua huleta mwanga kiasi na kwa kawaida hufanywa na watu wachache.
3. Maoni. Kusema kile unachofikiri au kuamini hufanya liwe la kibinafsi zaidi. Hivyo, huwa wazi zaidi
na watu hupendelea kuchagua watoe maoni yao kwa nani.
4. Hisia. Kueleza unavyojisikia huelekea hali ya kuwa wazi na, hivyo, hufanywa kwa kuzingatia kuwa
wanaokusikiliza ndiwo hasa waliokusudiwa.
5. Uwazi. Kueleza wewe ni nani ni kuwa wazi, mwaminifu, na kujihatarisha. Mtu anapaswa kuwa wazi
kwa wale tu ambao amekuwa na muda nao, wamejenga kuaminiana, na hali ya kujitoa mmoja kwa
mwingine.
D. Ili uweze kuwasiliana vema yabidi ukabiliane na mambo kadhaa.
1. Unataka kusema nini;
2. Namna unavyotaka kusema (toni ya sauti, ukubwa, kwa msisimko, huzuni, kushawishika, kukatishwa
tamaa, kutiwa moyo, nk.);
3. Kwa nini unataka kusema (kuonyesha upendo au kuguswa, hasira, kumuumiza au kumwaibisha mtu
mwingine, kumfanya atambue hitaji lako, hamu, imani, ndoto, nk.); na
4. Unataka kusema lini (wakati au baada ya chakula, wakati wa mapumziko, saa ya kulala, mbele ya
watoto, nk.). Namna na lini unasema kitu ni muhimu sawa na nini unachosema na kwa nini unakisema.
Kwa kweli, kusema kitu kwa namna isiyo sahihi au kwa wakati usio sahihi kwaweza kumfanya
mlengwa atafsiri vibaya kile usemacho na sababu ya kusema.
E. Kuelewa kunahusisha maudhui ya kile akwambiacho mtu, na hisia zake.
1. Mawasiliano huwa kwa njia ya matamshi (kile tusemacho) na njia isiyo ya matamshi (toni ya sauti,
lugha ya mwili, ishara ya mwili, muonekano wa uso, nk). Matamshi yanapotofautiana na njia isiyo ya
matamshi watu huvutwa kuamini ile isiyo ya matamshi.
2. Mapendekezo ya kukusaidia uwe na mazungumzo yenye ubora uwapo na mwenzi wako.
a. Tazamana na mwenzi wako anapozungumza. Hili hukufanya usitangetange kimawazo na
itawasilisha ujumbe kwake kuwa unamsikiliza kwa makini.
b. Usimsikilize mwenzi asemapo huku ukiendelea na shughuli zako kwa wakati huhohuo.
Mazungumzo yaliyo bora huhusisha kumpa mwenzi usikivu wote. Kama huwezi kufanya hivyo
saa hiyo, mwambie mwenzi wako kweli. Mwambie ya kuwa ungependa kusikiliza asemacho,
lakini mweleze sababu inayokuzuia usiwe na usikivu kamili kwa saa hiyo. Mwambie ni lini
utaweza kumsikiliza. Wenzi wengi wataheshimu hilo.
c. Sikiliza anavyohisi. Jiulize, “Je mwenzi wangu anapitia hisia gani?” Kisha, mthibitishie kuwa
unamwelewa asemavyo na anavyojisikia. Hiyo itatoa nafasi kwa mwenzi wako kuthibitisha
kuwa unamsikiliza kwa makini.
d. Tambua lugha ya mwili. Mkono uliokunja ngumi, mikono inayotetemeka, machozi, uso
uliokunjamana, na kupepesa macho vyaweza kukupa uelewa wa kile anachojisikia mwingine.
e. Usidakize. Endapo ninakupa usikivu kamili unapozungumza, nitajiepusha kujitetea, au
kukushutumu, au kueleza nafasi yangu kwa ushawishi usiotaka kupingwa. Lengo langu ni
kukuelewa wewe, kuelewa mawazo yako na hisia. (Chapman 1992:67-69)
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
42
II. Kusikiliza.
A. Watu wengi hawahitaji zaidi ya kule kuona kuwa mtu fulani anawajali kiasi cha kutoa nafsi ya
kuwasikiliza.
Unapotoa nafasi ya kumsikiliza mtu unaonyesha kuwa unamthamini, na unathamini kile asemacho.
B. Kusikiliza kwa makini ni ujuzi ambao mtu anaweza kujifunza.
Kwa hakika, watu wengi si wasikilizaji wazuri. Wasikilizaji wabaya huharibu mawasiliano na
kusababisha migongano. Kuna aina za kusikiliza mbali mbali.
1. Aina nne za kusikiliza, zinazozingatia mwenendo wa msikilizaji:
a. Kusikiliza kwa uongo—kunadanganya.
b. Kusikiliza kwa kuchagua—huonyesha kuvutiwa katika maeneo apendayo.
c. Kusikiliza kwa kujihami—hasikii ujumbe wenye kutishia.
d. Kusikiliza kwa usahihi—huonyesha mwenendo unaohamasisha mawasiliano (Campus
Crusade 1993: 77).
2. Aina tatu za kusikiliza zinazozingatia mtindo wa msikilizaji:
a. Usikilizaji wa kiushindani au Kimapambano. Hili hutokea tunapokuwa na mtazamo wa
kuinua mawazo yetu tu badala ya kutaka kuelewa yale ya mtu mwingine.
Ama twasikiliza tuone mahali penye nafasi kwa sisi kudakiza, au makosa au dondoo dhaifu
tunazoweza kushambulia. Tukionyesha hali ya usikivu ambayo ni bandia twasubiri mwanya, au
moyoni tukitengeneza hoja pingamizi ambayo itaharibu hoja zao kwa lengo la sisi kupata
ushindi.
b. Kusikiliza kwa utulivu au Kimya. Hili hutokea tunapokuwa kweli tuna nia ya kusikia na
kuelewa mawazo ya mtu mwingine. Tunasikiliza kwa makini na utulivu. Tunaamini kuwa
tumesikiliza na kuelewa kwa usahihi, lakini tunakaa kimya bila kuthibitisha tulichoelewa.
c. Kusikiliza kwa makini au Hai. Huu ni ujuzi muhimu zaidi na wa pekee wa kusikiliza. Katika
usikivu hai tunakuwa na lengo lakweli la kuelewa mawazo ya mtu mwingine, hisia,
anachokitaka au ujumbe wake ni upi, na tunahakikisha tunathibitisha fikra zetu na yeye kabla ya
sisi kutoa tafsiri yetu. Tunanukuu au kuitamka upya kwa maneno yetu maana ya ujumbe na
kumrudishia msemaji ili athibitishe kama tuko sahihi. Uthibitisho huu ndio unaosababisha
usikivu hai uwe na matokeo mazuri ukitofautishwa na usikivu mwingineo (Nadig n.d.).
C. Kusikiliza kwa makini, hai na kunakofaa.
1. Tabia ya msikilizaji mzuri. Msikilizaji mzuri lazima aonyesha yafuatayo:
a. Asikilize kwa mtazamo unaoyaweka maoni ya msemaji katika nafasi ya juu ya kipaumbele;
anasikiliza kwa makini—na kuonyesha kujali kwa kuahirisha mambo mengine yote.
b. Anasikiliza kwa hali inayoonyesha utayari wa kupokea na kuelewa.
c. Anasikiliza kwa mtazomo kuwa mwenzi wake si adui wake, bali ni zawadi aliyoletewa
kutoka kwa Mungu.
d. Anasikiliza katika hali ya utayari wa kusikia kutoka kwa Mungu kupitia mwenzi wake.
2. Kusikiliza kwa mafanikio ni vigumu kwa sababu watu hutofautiana katika ujuzi wa kuwasiliana na
kwa namna wanavyojieleza. Mara nyingi watu wana mahitaji, matakwa na makusudi tofauti ya
kuwasiliana. Kama wasikilizaji tunajihusisha na eneo la mawasiliano tunalolifikiria kuwa ni la muhimu
kwetu. Hata hivyo, kutokutambua eneo la maana na muhimu kwa msemaji itapelekea kutokuelewana
kwa watu hawa wawili wako katika masafa tofauti. Tusipokabili vigezo sahihi hatutopata mafanikio
halisi, na kwa kweli hali yaweza kuwa mbaya zaidi. Kwa mfano: Endapo mkeo anakuelezea kuhusu
hisia zake za kukwazwa na wewe unatazama mazingira ya tendo bila kuzitambua hisia zake, ni dhahiri
ataudhika zaidi.
3. Kusikiliza hai—kusikiliza ni tukio hai. Ili tusikilize kwa mafanikio, lazima tuhusike kikamilifu katika
mchakato wa mawasiliano, na sio tu kusikiliza kimya. Kuna mbinu kadhaa ambazo zaweza kutumika
kama usikivu hai:
a. Kurudia yaliyosemwa. Mbinu mojawapo nzuri ya kukusaidia kuelewa aliyosema mwenzako
ni “kuyarudia”. Hili litakusaidia kuthibitisha, kwa ajili yako na yeye, kile unachodhani
unaelewa wakati anapoendelea na simulizi. Unaporudia alichosema mtu mwingine, kwa
kawaida ni muhimu kurudia kwa maneno yako mwenyewe kwa kutamka namna ulivyoelewa
ujumbe. Kurudia yale yale yaliyonenwa na msemaji kunaudhi na hakuthibitishi kuwa umeelewa
ujumbe. Kwa kuzingatia kusudi la mawasiliano na kuelewa kilicho sahihi, unaweza kurudia
aliyosema mtu: kwa mtiririko wa matendo; mawazo na imani; hisia na mihemko; matakwa,
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
43
mahitaji, au motisha; au matumaini na matarajio. Zaidi ya hayo, unaweza “kurudia” kwa
kutamka kwa muhtasari, kwa mfano: “Unajisikia _____”; “Kama ninavyoelewa _____”;
“_____ je ni sawa?,” nk. Hili litamhamasisha msemaji ama kukubaliana na muhtasari wako au
kusema kama hivi, “hapana, ninachomaanisha ni _____” Kwa namna yoyote, lengo la
maelewano litakuwa limefikiwa.
b. Maswali ya kubainisha. Sikiliza kwa hali ya kubainisha. Hiyo inamsaidia msikilizaji kuelewa
maana ya ujumbe. Unaweza kuuliza maswali ya kubainisha kama: “Unaniambia
kwamba______?” na “Ulimaanisha nini uliposema ______?”
c. Maswali ya muhtasari. Unataka kujua kilicho muhimu zaidi kwa mwenzio, kile ambacho
ndicho kiini halisi cha ujumbe wake wenye maneno mengi. Unaweza kuuliza maswali ya
muhtasari kama haya: “Katika hayo yote uliyosema, ni nini ambacho unataka nikizingatie
zaidi?”na “Ni nini unachohitaji kutoka kwangu kwa sasa?”
d. Mlengo sahihi. Msikilizaji mzuri hulenga kwenye: maana na sio tu maneno; hubainisha
dondoo halali, badala ya kupinga hoja zenye makosa; huuliza, badala ya kushtaki; huelewa,
badala ya kukuhumu.
4. Zipo faida kadhaa za usikivu hai.
a. Sote hutenda au kufuata uelekeo fulani kutokana na msingi wa tunavyoelewa. Mara nyingi
kutokuelewana hutokea katika eneo ambalo pande zote mbili hazilielewi. Usikivu hai
unapokuwepo, kutokuelewana kunapotokea, tatizo litagundulika mara moja, na mawasiliano
yatabainishwa kabla hali haijakuwa mbaya zaidi.
b. Wakati mwingine mtu anataka kwanza asikilizwe na kutambulika kabla hajawaradhi kubadili
msimamo wake au kulegeza makali ya msimamo.
c. Mara nyingi ni rahisi kwa mtu kumsikiliza mwingine na kuzingatia mazingira ya nafasi yake
wakati mtu yule anapojua mwenzake anamsikiliza na kuifikiria nafasi yake.
d. Watu wanafaidika kwa kugundua dosari za fikra zao tunaporudia matamshi yao bila
kuwakosoa.
e. Pia inasaidia kuyatambua maaeneo mnayokubaliana ili yale msiyokubaliana yawekewe
mikakati na kutokomezwa badala ya kukuzwa.
f. Kurudia kile kisemwacho na kila mmoja wetu inasaidia kutoa nafasi kwa kila mmoja
kutambua viwango tofauti vya mawasiliano vinavyotokea nyuma ya pazia. Hii itasaidia kuweka
mambo peupe ili yakabiliwe na kutatuliwa mara moja.
g. Ikiwa tunaelewa kwa usahihi hoja za mtu mwingine, tunaweza kuwa na nafasi kubwa zaidi
ya kufanikiwa kumsaidia kuona kasoro zilizoko upande wake—na kasoro zilizoko upande wetu.
h. Ikiwa tunaelewa kwa usahihi hoja za mtu mwingine, tunaweza kuwa na nafasi kubwa zaidi
ya kufanikiwa kumsaidia kutatua tatizo alilonalo au kutatua shida nyinginezo zozote.
5. Vidokezi vya ziada vya usikilizaji hai.
a. Usivutwe na maana ya maneno tu; fuatilia hisia au dhamira nyuma ya maneno. Tafsiri au
maana halisi ya maneno yaweza kuwa ni tofauti kabisa kile anachotaka kuwasilisha msemaji.
b. Jiweke tayari kujibu maswali mara moja. Wakati mwingine watu huuliza maswali wakati
ambapo nia yao hasa ni kujieleza na wala si kujibiwa.
c. Tambua wakati muafaka wa wewe kusema. Unapokuwa umeelewa vizuri ujumbe wa
msemaji, itakuwa ni vema na wewe ujibu kwa ujumbe wako. Usitumie usikivu hai kwa namna
ya kuficha yale yaliyo moyoni mwako.
d. Endapo umechanganyikiwa na huelewi, mwambie msemaji huelewi na mwombe arudie kwa
maneno mengine, au bahatisha. Endapo utakosea, yeye atagundua na kwa hakika
atakusahihisha.
e. Usikivu hai una faida zaidi wakati mnenaji amekasirika, kukwazwa au anaonyesha hisia
ngumu kwako, hasa mnapokuwa katika uhusiano muhimu.
f. Tazamana naye na chunguza lugha ya mwili. Usiangalie saa yako au watu wengine au
shughuli nyinginezo zinazoendelea hapo chumbani. Mtazame na kumwelekea msemaji na itikia
kwa kichwa, pale inapobidi. Usikunje mikono yako au kuonyesha hali ya kukosoa.
g. Jitahidi kuelewa na usihukumu. Waweza kuelewa na kuheshimu hisia na imani ya mtu
mwingine bila ya kutupilia mbali nafasi yako, au bila kukubaliana na uhalali au usahihi wa yale
wasemayo.
h. Ikiwa huelewi chakufanya, jaribu kuelewa zaidi. Usiwe na haraka katika kutoa majibu;
wekeza katika kuelewa (si tu kuhusu “tatizo” la “kutatua” bali kuhusu yeye [je ingekuwaje
kama ungekuwa yeye]).
Anza kuwa msikivu mwenye mafanikio. Katika hali iliyo danganyifu yaweza kuonekana kuwa ni rahisi
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
44
kuwasikiliza na kuwaelewa watu wengine, lakini kufanya hivyo vema, hasa yanapotokea mabishano,
wahitajika ujuzi wa kweli. Kama ilivyo kwa taaluma yoyote, kusikiliza vema kwahitaji muda mwingi
wa mazoezi, hivyo jizoeze kuwa msikilizaji hai ukitumia mbinu zote za usikivu kama sehemu ya
taaluma yako ya mawasiliano.
III. Uwezo wa kuhisi maono ya mwingine.
A. Kuna tofauti iliyo wazi kati ya kusikia maneno tu na kuusikia ule ujumbe hasa.
Tunaposikiliza kwa makini tunaelewa fikra na hisia za msemaji kutoka katika mtazamo wake. Inakuwa
kana kwamba tunasimama katika nafasi ya mtu mwingine, tukitazama kwa macho yake na kusikiliza kwa
masikio yake. Msimamo wetu waweza kuwa tofauti, na si lazima tuwe tumekubaliana naye, lakini
tunapomsikiliza tunaelewa na kupata maono yake.
B. Uwezo wa kuhisi maono ya mwingine ni nini.
Uwezo wa kuhisi maono ya mwingine, hasa kuhusiana na mawasiliano, unaelezewa kama ifuatavyo,:
“ni ule uwezo wa alionao mtu wa kujituni katika mawazo na hisia za mwingine, Bila kujali ni ya namna gani. Si
swala tu la kuguswa na hisia chache za mtu mwingine, kama maumivu na huzuni zao; bali ni swala la kusoma
hali nzima ya hisia kati ya watu. Inahusu kujiweka katika nafasi ya mtu mwingine bila kuchoka, kwa makini
ukijadili na mtu mwingine kwa tahadhari usimkwaze au kumkosea kwa namna yoyote, huku ukijali hisia zake...
Uwezo huu hukuongoza kuinua simu na kumwambia mtu kuwa unamjali na unaelewa yale anayopitia,
hata wakati ambapo wewe mwenyewe umezidiwa na majukumu ya maisha yako binafsi. Uwezo wa kuhisi
maono ya mwingine hukufanya wakati wote utafiti toni ya sauti ya watu na mwonekano wa uso, hasa macho
yao, kuweza kuelewa fikra zao au wanavyojisikia. Unatumia “lugha ya macho,” na lafudhi, kama dirisha la
fahamu zao. Na uwezo huu hukuhimiza kufanya haya kwa sababu unaanzia katika mahali ambapo mtazamo
wako kuhusu dunia wa pekee au wakweli, na yakuwa maoni yao na hisia zao vyastahili kupewa nafasi. . . .
Uwezo wa kuhisi maono ya mwingine hutafsiri sura ya uhusiano wa binadamu. Kwa mfano, uwezo huu
utakuzuia kufanya vitu ambavyo vitaleta makwazo kwa hisia za mwingine. Itakufanya ufumbe kinywa, kuliko
kusema neno ambalo linaweza kumkwaza mtu mwingine au kumfanya ajisikie kukataliwa. . . .
Uwezo huu husababisha mawasiliano ya kweli. Kusema na mtu si mawasiliano halisi. Ni mazungumzo
binafsi. Ikiwa unazungumza kwa asilimia 50 ya muda kila baada ya sentensi chache, hayo si mazungumzo, ni
kutoa mawazo yako, au kusimulia hadithi, au kutoa hotuba, au kufunza, au kutawala, au kushawishi, au
kumiliki, au kujaza ukimya. . . . Katika kuteka mazungumzo msemaji hafikirii kutoa nafasi kwa mwingine na
kwa kufanya hivyo atakuwa anakidhi haja zake mwenyewe tu, na si za msikiizaji. Uwezo wa kuhisi maono ya
mwingine unahakikisha kuwa hali hii inapungua kwa kumwezesha msemaji ajipime muda gani aendelee, na
asikilize matakwa ya msikilizaji kuhusu kuhamia somo jingine.
Mazungumzo halisi huwa makini kwa hisia za msikilizaji huyu na muda huu. Uwezo huu unakuongoza
kuwahoji wasikilizaji wanavyojisikia na kucheki kama wako tayari kushiriki katika mazungumzo, au wanafikiri
nini kuhusu mada. Na si tu kucheki mara moja, na kisha ukapuuzia mawazo na hisia zao huku ukilenga za
kwako. Badala yake, unaendelea kuuliza, mara kwa mara, mazungumzo yanapoendelea.
Kwa nini kucheki? Ni kwa sababu unaweza kuwa unamwaga maneno kwa wasikilizaji wako wakati
wao hawasikilizi. Kibaya zaidi, wanaweza kuona kuwa furushi lako la maneno ni udhia wa aina fulani. . . .
Uwezo wa kuhisi maono ya mwingine hukuongoza wewe si tu kucheki, lakini pia kufuatilia kile
wanachoendelea kusema, ili wasione kuwa hujali au hukumaanisha. Pia uwezo huu unaruhusu mazungumzo
yenye muafaka baina ya pande mbili, kwa kuwa wakati wote kila mnenaji hutoa nafasi kwa ajili ya mwenzake,
kwa zamu. Uwezo huu unakuruhusu kurekebisha mazungumzo yako yawe sambamba na yao. . . .
Uwezo wa kuhisi maono ya mwingine ni gundi la mahusiano ya kijamii. Inakuhamasisha kujihusisha na
na kujali kuhusiana na yale anayopitia mwingine. Inakuongoza kuuliza kuhusu matatizo yao, kuwafanya
wajihisi kutegemezwa, badala ya wewe kupakua shida zako kwao.” (Baron-Cohen 2003: 21-25)
C. Kuna viwango tofauti vya uwezo wa kuhisi maono ya mwingine.
Kwa mfano, ikiwa mume ana mgogoro na baba yake, mkewe anaweza kuonyesha viwango tofauti vya
kuhisi maono ya mwingine kama ifuatavyo:
1. Hatua ya 1—“Mambo yatakuwa mazuri mwishowe.” Itiko la jinsi hii halijaelewa mazingira ya mume.
Ni kanusho au thibitisho. Kwa hakika hisia zake hazijatambulika, na tatizo lake halijatambulika au
limetambulika kidogo.
2. Hatua ya 2—“Una wakati mgumu na baba yako.” Hapa, mke angalau amepata ujumbe wa mumewe
kwa ujumla wake, lakini amepuuzia hisia zake.
3. Hatua ya 3—“Unajisikia kukata tamaa kwa sababu hamuelewani na baba yako.” Hapa, mke
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
45
anaonyesha uelewa mkubwa kuhusu yaliyomo bayana na hisia za ujumbe wa mumewe. Hili linafungua
uwezenano wa majadiliano zaidi.
4. Hatua ya 4—“Unajisikia kukata tamaa kwa sababu ya ukali wa baba yako; unamtaka aachane na
wewe.” Hapa, mke anadhihirisha uelewa wa tatizo bayana, na hisi aza mumewe, na anatambua
upungufu au hitaji (ina maana kile ambacho mume angependa kukiona kuondoa upungufu au kukutana
na hitaji).
5. Hatua ya 5—“Unajisikia kukata tamaa kwa sababu ya ukali wa baba yako na kushindwa kwako
kumkabili; unataka akuache. Labda yakubidi uzungumze naye.” Hili linahusisha kila kitu kilichomo
katika hatua ya 4, lakini sasa inaingiza hatua ya utendaji. Si kila mazingira yatakufikisha hatua ya 5
(Mazingira yanapokuwa yamewekwa wazi mume anaweza kuona cha kufanya).
D. Uwezo wa kuhisi maono ya mwingine ni namna ya heshima na ishara kuwa unamthamini mtu mwingine.
Haitosaidia sana kumwambia mtu, “Nathamini nafasi yako” au “Najua unavyojisikia.” Inakubidi
uthibitishe hilo kwa kuwa tayari kuwasiliana na wengine katika viwango vyao vya uelewa na mwenendo.
Tunafanya hivyo kwa kawaida kwa kurekebisha toni ya sauti zetu, kiwango cha matamshi yetu na uchaguzi wa
maneno ili kuonyesha kuwa tunajaribu kujiweka katika nafasi yao kwa wakati ule. Ili ufanikiwe kuwasiliana na
mwenzi wako kiukweli—ili ufikie muafaka, sikiliza kwa makini, na tumia uwezo wa kuhisi maono ya
mwingine—hili ni jambo muhimu na ndiyo maana ya kuwa “mwili mmoja” (Mwz 2:24) kama Mungu
alivyokusudia kwa ajili ya waume na wake.
7. SEMA KWELI KWA UPENDO: LUGHA TANO ZA UPENDO
I. Umuhimu wa Upendo.
A. Paulo anaelezea namna tunavyotakiwa kusema kweli katika Efe 4:15 ya kuwa “tukisema kweli kwa
upendo.”
1. Neno lililotumika hapa ni agape ambalo kwa kawaida hubeba wazo la moyo wa upendo; hali ya
kutaka kuona wengine wanafanikiwa.
a. Neno hili, halikutumiwa mara kwa mara na Wayunani wengine, lilichukuliwa na waandishi
wa Kikristo na kuingiziwa maana ya Kikristo.
b. Kimsingi ilimaanisha upendo wa kiMungu wenye msingi katika kujito mhanga.
c. Ni upendo wa kujitoa ambao hautegemei sifa.
d. Ni tasirwa ya sifa za Mungu kwa kuwa “Mungu ni upendo” (1 Yohana 4:8).
e. Maana halisi ya Kibiblia ya upendo ni kile alichofanya Kristo msalabani kwa ajili yako na
mimi.
2. Ni mpaka tuuelewe upendo wa Mungu ndipo twaweza kuuelewa upendo wa Kibiblia.
3. Kwa mtazamo wa kibinadamu, kimsingi upendo huu si hisia, bali tendo; si tu msisimko, lakini kutoka
moyoni.
B. Upendo ni torati yote kwa ufupi.
Katika Math 22:34-40, mwanasheria alimuuliza Yesu swali, “Mwalimu,katika torati ni amri ipi iliyo
kuu?” Yesu akamwambia, “MPENDE BWANA MUNGU WAKO KWA MOYO WAKO WOTE, NA KWA ROHO
YAKO YOTE, NA KWA AKILI ZAKO ZOTE. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana
nayo, nayo ni hii, ‘MPENDE JIRANI YAKOKAMA NAFSI YAKO. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote
na manabii."
C. Upendo ndilo lengo la maagizo ya mitume.
“Walakini mwisho wa agizo hili ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na
unafiki” (1 Tim 1:5).
D. Kusema kweli kwa upendo ni kusema kwa namna inayoonyesha upendo wako wa hiari ulioutoa kwa
Mungu.
Kama unao upendo wa kujitoa kwa Mungu, kwa hakika utakuwa na upendo wa kujitoa kwa:
1. Jirani yako.
2. Kaka na dada ndani ya Kristo.
3. Mkeo au mumeo.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
46
II. Sifa za upendo zimeainishwa katika 1 Kor 13:4-8a.
“Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na
adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu,bali hufurahi pamoja
na kweli;huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati
wowote.” (1 Kor 13:4-8a)
A. “Upendo huvumilia.”
1. Neno hili huonyesha moyo udumuo kutaraji, kana kwamba shauku yako yadumu kwa muda mrefu.
2. Kwa hiyo, sema kwa namna ambayo haitaashiria kwamba huna subira.
3. Unapowasiliana na wengine, na kwa hakika kwa mwenzi wako, usiharakishe au kutaka kitu ambacho
kitachochea hofu ya kushindwa.
4. Hata hivyo, ziko nyakati ambazo huhitaji kuwawajibisha watu.
B. “Upendo hufadhili.”
1. Upendo hukarimu ni ya kiutendaji zaidi na kifungu cha kwanza ni tulivu zaidi.
2. Neno hili hapa linamaanisha kuonesha kuwa wewe u mwenye manufaa.
3. Kusema kweli kwa upendo ni kusema kwa namna inayotatua tatizo; ni kuwa sehemu ya utatuzi na sio
sehemu ya tatizo.
4. Luka 6:35 inasema, "Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha mstumaini kupata
malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi nanyi mtakuwa wana wa aliye juu kwa kuwa yeye ni mwema
kwa wasiomshukuru na waovu.”
C. “Upendo hauhusudu.”
1. Neno linamaanisha ari kuu ambayo yaweza kukubaliana na au kupingana na. Hapa ipo katika upande
wa kupinga.
2. Mtu asiye na husuda hawezi kamwe kujiona kuwa yeye yuko chini au juu ya mwingine.
3. Mtu wa jinsi hii hana tamaa ya kuwa kama mtu mwingine au kutamani kuwa angekuwa na vipawa au
fursa za mtu mwingine.
4. “Kutokuwa na husuda” yamaanisha kutokuwa na wivu.
a. Mara nyingi wivu huhusishwa na athari za mahusiano yaliyovunjika.
b. Hisia hujisikia kana kwamba uaminifu umevunjwa na mwingine asipate kitu.
5. Mifano miwili kutoka katika maandiko inasaidia kubainisha husuda na wivu:
a. Katika Matendo 7:9 tunasoma, “Wale wazee wetu wakimwonea wivu Yusufu wakamwuza
aende Misri. Mungu akawa pamoja naye.”
(1) Kaka zake Yusuf walijisikia kana kwamba wamepoteza upendo, heshima na
kuaminiwa kutoka kwa baba yao.
(2) Kwa hiyo, hawakumtendea vema.
b. In Matendo 17:5 we read, “Na wayahudi wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha
katika watu ovyo wasio na sifa njema, nao wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini
wakawaendea watu wa nyumba ya Yasoni wakawataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji.”
(1) Wayahudi walijihisi wanapoteza kuaminiwa kama Wayahudi kwa Paulo na Sila
(17:4).
(2) Na hivyo, waliogopa kudhihirishwa kama walio pungufu ya vile walivyojiona katika
hali yao ya kujihesabia haki, wakawa wakali.
D. “Upendo hautakabari, haujivuni.”
1. Kifungu cha maneno kinamaanisha kujaza, kwa namna kama ya kujaza hewa mpira wa gari. Kusema
kweli si kujaribu kujivuna kwa kujisifia.
2. Upendo haufokasi katika mtu kujiinua kwa kueleza mafanikio yake au jinsi ulivyo bora au namna
ulivyofanya kwa ubora zaidi.
3. Watu wenye kiburi hufurahia kuwadhalilisha wengine, bali Mkristo mwenye upendo lazima ajaribu
kuwajenga wengine.
E. “Haukosi kuwa na adabu. Hautafuti mambo yake, hauoni uchungu, hauhesabu mabaya.”
1. Sehemu ya mstari huu inatokana na neno la kihasibu (ina maana, “haweki hesabu ya makosa
yaliyotendwa”—NASB).
a. Kusema kweli kwa upendo ni kusema bila kuleta kumbukumbu ya makosa yaliyopita.
b. Yashughulikia masuala ya siku kwa siku na kusamehe na kutokulikumbushia jambo hilo
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
47
tena.
2. Mstari huu una maana kuwa mtu hajinufaishi huku akipuuzia wengine.
3. Badala yake, huwa makini kwa mahitaji ya wengine na wala hajaribu kujenga “ufalme wake
mwenyewe.”
4. Kusema kweli kwa upendo si tendo la kujihudumia mwenyewe; wala haina uhusiano na nini utapata;
haihusiani na agenda za mtu za kibnafsi, isipokuwa pale ambapo agenda hiyo ni kumpenda yule
unayezungumza naye.
a. Wakati mwingine twajaribu kujilinda, tukitafuta kinga yetu wenyewe na umuhimu.
b. Mara nyingi tunawasiliana kwa kutawala mazungumzo na tunataka mwingine akubaliane na
sisi.
5. Upendo haulengi mabaya kwa wengine.
6. Upendo humfanya mtu awe hana hila au ujanja.
7. Kusema kweli kwa upendo hurekebisha maneno yaendane na mazingira ya msemaji.
a. Katika 1 Tim.5:1-2 Paulo anasema, “Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba, na vijana
kama ndugu, wanawake wazee kama mama, na wanawake vijana kama ndugu wa kike; katika
usafi wote.”
b. Kauli yabidi kunenwa kutegemea na nani tunasema naye, zifanye ziwe za kufaa na sahihi.
c. Kwa kanisa la Kolosai, Mtume anaonya, “Maneno yenu yawe na neema siku zote yakikolea
munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu” (Kol 4:6).
8. Maana ya huu mstari yaweza kufupishwa kwa maneno haya “Upendo husafisha kibao.”
F. “[Upendo] haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli.”
1. Paulo anaorodhesha vigezo chanya vitano katika mst 6-7; Hiki ni cha kwanza.
2. Uovul [udhalimu] hapa ingemaanisha kile ambacho si kweli.
a. Kusema kweli kwa upendo ni kukataa kufurahia uovu.
b. Haipongezi, kukubali, au kusifu tabia ya uovu.
c. Tunaposengenya, tunaifurahia dhambi ya mtu mwingine (hata kama hayo usemayo ni kweli).
d. Wakati mwingine twafurahia kushindwa kwa mtu mwingine kwani hilo linatufanya tujisikie
kuwa tu juu yake.
G. “Huvumilia yote.”
1. Wazo lililopo katika kifungu hiki ni kufunika juu yake.
2. Kusema kweli kawa upendo hutuwezesha kufunika hisia ngumu kwa ukimwa, kustahimili kimya
kimya, mpaka wakati muafaka.
3. Mambo mengine yanahitaji kuyavumilia tu, kuyafunika, na kuendelea kuyaacha yapite bila kuyatolea
maoni.
4. Paulo anaeleza wazo hili katika 1 Kor 9:12, “Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si
zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huo; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia habari njema ya
Kristo.”
5. “Kuchukiana huondokesha fitina, bali kupendana husitiri makosa yote” (Mith 10: 12).
H. “Huamini yote.”
1. Hili halimaanishi kuwa sisi ni wajinga na wepesi kudanganywa.
2. Haimaanisha kuwa hatuna viwango vya ukweli, au kwamba kweli ni chochote afikiricho mtu.
3. Kwa hakika ina maana kuwa tuko upandea chanya na twakubali, hadi pale itakapothibitiswa
vinginevyo.
4. Wengine hufikiri kuwa tunaamini kila kitu katika neno la Mungu (ikimaanisha, tunachukulia biblia
katika mtazamo wa kidunia.
5. “Kuamini yote” si kukubali taarifa mbaya kuhusu mwingine, ni mpaka ziwe zimethibitishwa kikweli.
6. Paulo anasema katika Filp 4:8, “Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote
yaliyo ya staha, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa
njema; ukiwepo wema wowote, ikiwepo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.”
I. “Hutumaini yote.”
1. Tumaini ni matarajio ya hakika, uthibitisho wa kinachotarajiwa, si ndoto za mchana, zisizo na
uhakika.
2. Mhubiri mkuu John Gill aliandika kuwa Mkristo: “hutumaini vyote; viwezavyo kutumainiwa;
hutumaini kutimilika kwa ahadi zote za Mungu; hutumaini kumfurahia nyumbani mwake na sheria
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
48
zake; hutumaini kwa visivyoonekana, ya kuwa wakati ujao, uwe ni mgumu, hata hivyo yawezekana
kuufurahia: anatumaini kufika mbinguni na kupokea furaha ya milele, kwa neema zaidi hapa na utukufu
baada ya hapa; hutumaini yaliyo bora kwa watu wote, kwa ajili ya maprofesa wote wa dini, wanaotamka
toba zao, na maprofesa walioanguka, wanaotamka toba zao,na kutoa shukrani zao; huwatakia mema
wote, ya kwamba wawe wakweli, na yote ni sawa na yatakuwa hivyo.”
J. “Hustahilimi yote.”
1. Kusema kweli kwa upendo ni kusema kwa tabia ya ujasiri na ustahimilivu.
2. Ustahimilivu si hali ya kulalamika na kuwa na tabia kama ya mtu asemaya “ole wangu mimi”.
3. Kustahimili ni kusema bila kujaribu kujitoa katika mazingira mabaya.
K. “Upendo haupungui neno wakati wowote.”
1. Kusema kweli kwa upendo ni kusema kusema kama mtu ambaye hatomwacha Mungu, kazi yake, na
watu wake, kwa sababu lazima tuelewe kuwa Mungu kamwe hatotuacha.
2. John Gill aliandika: “Upendo haushindwi, na. Unaweza kushindwa pale sisi tunaposhindwa kupenda,
kama zilivyo neema nyingine; twaweza kuuacha, sio kuupoteza; hamasa yake yaweza kupungua na
kupoa; waweza kupoa kwa sababu ya uwepo wa dhambi; unaweza kufunikwa kwa sababu ya
kuongezeka kwa mafundisho potofu au ukengeufu, ambayo hula kama kidonda; na waweza kuzuiwa na
tamaa isiyoshiba ya kupenda vitu vya dunia; ambayo ina madhara katika Nyanja zote za kidini na
maisha ya utauwa , na hasa upendo wa Mungu,Kristo na ndugu: lakini neema hii haishindwi kutokana
na kanuni zake; ni mbegu isiyokufa wala kuharibika; yaishi hata katika nyakati za majaribu makali,
kama katika Petro; na wakati wa vipindi vya kuachwa hasa na vya mateso makali, bado hali ya
kumpenda Mungu itakuwepo; Kristo huipenda nafsi ya jinsi hiyo; na watakatifu ndio walio bora
duniani, na ndani yao anayo furaha kuu: na inaendelea katika kutumika kwake, na kuendelea kufanya
hivyo, wakati imani na tumaini vinapopoteza nguvu yao, hata katika ulimwengu mwingine; maana
imani itabadilishwa kuwa maono, na tumaini kuwa burudisho; lakini upendo haubadiliki, na huendelea
katika viwango vya juu, na juu zaidi, na katika namna ya ukamilifu.”
3. Tunaagizwa katika Gal 5:6 ya kuwa imani inatenda kazi kwa upendo, “Kwa maana katika Kristo
Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.”
4. In Yohana 13:34-35 upendo unathibitisha kuwa sisi kweli tu wanafunzi wa Yesu: “Amri mpya
nawapa, Mpendane. Kama vilee nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote
watatambua kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.”
III. Lugha Tano za Upendo.10
A. Kosa ambalo limejidhihirisha katika ndoa nyingi ni kwamba tuna matarajio yasiyo na uhalisia kuhusiana
na upendo.
1. Hitaji la kupendwa ni la msingi kwa kila mwanadamu kihisia.
a. Ukiwepo upendo wa kutosha, mtoto atakuwa na kufanyika mtu mzima anaye wajibika. Bila
upendo huo, atapungukiwa kihisia. Na hitaji hilo la upendo huendelea katika maisha yote ya
mtu.
b. “Ndani ya moyo wa mwanadamu aishiye kuna hamu ya kuwa na mwenzi na kupendwa na
mwingine. Ndoa imekusudiwa ikutane na hitaji hilo kwa ajili ya kujamiana na upendo” (uk.22).
Zaidi ya hayo, “hitaji la kujisikia kupendwa na mwenzi wa ndoa ndicho kiini cha matamanio
yote ya ndoa” (uk.22).
2. “Upendo wa kumtamani mwanamke katika hali ya kimwili” si sawa na upendo halisi.
a. Unapokuwa kileleni, “mwa upendo”wajisikia furaha isiyo kifani. Mnaoneana shauku kuu
mno na twadanganyika kuwa mpendwa wetu ni mkamilifu. Hatuoni dosari yoyote kwa
mpendwa wetu, na twafikiri kuwa hisia tulizo nazo zitadumu milele. Hali ya “upendo huu wa
mwilini” yatudanganya kuwa jinsi mahaba yetu yalivyo kamwe hatutokorofishana au
kukwazana, bali siku zote tutaweza kutoshelezana katika kila hitaji na tamanio.
b. Kwa kweli, tafiti za muda mrefu za “upendo huu wa mwilini”zinaonyesha kuwa“kwa wastani
mapenzi haya hudumu kwa muda wa miaka miwili” (uk. 30).
10Kifungu hiki kinatokana na mwana Saikolojia wa Kikristo na mshauri wa ndoa Gary Chapman’s The Five Love
Languages (Chicago: Northfield, 1992). Namba zilizo katika kurasa katrika mabano ni namba za kurasa katika nukuu za
hicho kitabu.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
49
c. “Upendo huu wa mwilini”kwa kawaida ni wa kihisia zaidi kwa tendo la ndoa, wenye hisia
zilizo juu bali za muda tu. Si upendo halisi kamwe, kwa sababu:
(1) Si tendo liongozwalo na utashi au chaguo la kiufahamu. Haijalishi ni kwa kiasi gani
tumetaka kupenda, hatuwezi kuilazimisha iwe hivyo. Inaweza kutokea wakati
tusiopanga na watu tusiowadhania.
(2) Haihitaji juhudi. Kile tufanyacho katika “upendo huu wa mwilini”chahitaji nidhamu
kidogo au juhudi zetu.
(3) Lengo lake ni kulea kukua kwa binafsi kwa mwingine. “Upendo huu wa mwilini”
haufokasi katika kukuwa kwetu wala kukuwa na kuendelea kwa huyo mtu mwingine,
bali unatupa hali ya kujisikia kuwa “tumefika.” Shauku yetu kuu ni kubaki pale.
d. Tukiuchukulia “upendo huu wa mwilini” kama kielelezo cha maisha ya ndoa, hatutafanikiwa
katika ndoa zetu.
e. Tutakapokuwa tumeshuka kutoka kilele cha “upendo wa mwilini”hitaji la upendo liko
palepale kwa sababu ni la msingi katika asili yetu. Tulihitaji upendo kabla ya kuingia katika
“pendo hilo,” na tutauhitaji siku zote za maisha yetu.
3. Upendo halisi huonyesha tabia za matendo yanayodumu “kwa upendo” .
a. Upendo halisi: “unazo hisia kwa asili lakini haushikilii. Ni upendo ambao huunganisha
mantiki na hisia. Unahusisha utashi na unahitaji nidhamu, na unagundua hitaji la ukuzi wa
binafsi. Hitaji letu kuu zaidi si kumpenda Fulani bali kupendwa kihalisia na mwingine,
kuufahamu upendo unaokuwa kwa sababu za msingi na uchaguzi, na si silika. Nahitaji
kupendwa na mtu anayechagua kunipenda, ambaye anaona kuwa ndani yangu kuna kitu
kinachostaahili kupendwa.
Upendo wa jinsi hiyo wahitaji juhudi na nidhamu. Ni uchaguzi kutumia nguvu katika
jitihada za kumfaidia mwingine, ukijua kuwa endapo maisha yake yamefaidishwa na juhudi
zako, wewe pia utapata hali ya kuridhika—kuridhika kwa kumpenda mtu mwingine kikweli.
Hauhitaji msisimko wa furaha kama ya ‘upendo wa mwilini’. Kwa kweli, upendo wa kweli
huwezi kuanza mpaka hatua ile ya “upendo wa mwilini” iwe imepita.” (uk. 35-36)
b. Upendo halisi huonyesha tabia kama za 1 Wakorintho 13.
B. Kuna njia tano za msingi ambazo kwazo upendo waweza kudhihirishwa na kupokelewa—“lugha tano za
upendo.”
“Kimsingi zipo lugha tano za mapenzi—njia tano ambazo watu husema na kuelewa mapenzi. . . . Lililo
muhimu hapa ni kusema lugha ya upendo ya mwenzi wako. . . . Si kawaida kwa mke na mume kuwa na lugha
ya upendo inayofanana. Tunapozungumza lugha yetu ya msingi ya upendo, na tunachanganyikiwa mwenzi wetu
asipoelewa tunachokiwasilisha. Tunauonyesha upendo wetu, lakini ujumbe haufiki kwa sababu tunazungumza,
kile ambacho kwao, ni lugha ngeni. . . . Utakapowezi kutambua na kuzungumza lugha ya msingi ya upendo ya
mwenzi wako, naamini utakuwa umegundua ufnguo wa ndoa ya kudumu yenye upendo.” (uk. 15-17)
1. Maneno ya ukiri chanya. Maneno yaliyo chanya, ya kusifu, ya kujenga, na kutia moyo ni njia
mojawapo ya kuuonyesha hisia zetu za upendo. “Hali ya hisia” katika ndoa inatiwa nguvu wakati mume
na mke wanapotumia maneno ya kutia moyo mara kwa mara (inamaanisha, jambo la kuinua kila siku).
a. Weka lengo kumsifu mwenzi wako kila siku kwa muda wa mwezi. Tunapoambiwa maneno ya
kutia moyo tutahamasika zaidi kusema au kufanya kile apendacho mwenzi wetu. Tunapoangalia
maeneo ya uwezo wa mwenzi wetu na kumwambia jinsi tunavyobarikiwa na uwezo huo, kwa
hakika mwenzi wetu atatendea kazi maneno hayo ili aishi kwa viwango sawa sawa na hayo
uliyosema.
b. Maneno ya kutia moyo yanahitaji kusisitiza, na mwenzi wetu, kujifunza yaliyo muhimu
kwake, na kuiona dunia kwa mtazamo wake yeye. Kwa maneno ya kutia moyo twajaribu
kuwasiliana, “Ninajua. Ninajali. Niko na wewe. Nikusaidieje.” Hata hivyo, ili uweze “kutia
moyo,” mwenzi wako lazima kwanza atamani kufanya kile unachomtia nacho moyo. Kwa
mfano, “Waume wengine hushinikiza wake zao wapunguze unene. Mume anasema, “Ninamtia
moyo,” lakini kwa mke inaonekana kama hukumu. Waweza kumtia mtu moyo kupunguza
unene ikiwa ndivyo anavyotaka yeye. Ni mpaka atamani, vinginevyo maneno yako yatakuwa
kama ya mtu anayehubiri. Maneno ya jinsi hii si rahisi kutia moyo. Mara yanaposikika
huchukuliwa kama maneno ya kuhukumu, yaliyokusudiwa kuchochea hatia. Hayadhihirishi
upendo bali kukataliwa.” (uk. 44)
c. Ili maneno chanya yawe kweli, kile usemacho lazima kisemwe kwa huruma na upole. Zaidi ya
hapo, upendo huleta maombi, na siyo madai. “Unapopeleka ombi kwa mwenzi wako,
unaonyesha kuwa unakubali uthamani wake na uwezo wake. . . . Lakini, unapopeleka madai,
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
50
wewe si mpenzi tena bali dikteta. Mwenzi wako hatatiwa moyo bali atajisikia kudharauliwa”
(uk. 49).
d. Waweza kusema maneno mazuri yamhusuyo mwenzi wako wakati yeye mwenyewe hayupo
(hatimaye, mtu Fulani atamwambia, na wewe utapata sifa njema kwa kuonyesha upendo). Vile
vile, mnenee mwenzi wako mazuri mbele ya wengine wakati yeye mwenyewe akiwepo pia.
2. Wakati wa kuthamini. “Wakati wa kuthamini” yamaanisha kumpa mtu usikivu wako wote. Wakati
wa kuthamini ni pamoja na kutazamana mkiwa mmekaa pamoja, kutembea pamoja, kula pamoja, au
hali ya kuwa pamoja tu, kufanya kitu anacho kipenda mwenzako.
a. Kiini cha wakati wa kuthamini ni kuwa pamoja. Kuwa pamoja si ukaribu katika hali ya mwili
tu, lakini ni Usikivu wenye fokasi. “Ninapokaa katika kochi na mke wangu na kumpa dakika
ishirini za usikivu usiogawanyika na yeye anapofanya vivyo hivyo kwa ajili yangu, tutakuwa
tunapeana dakika ishirini za uhai. Hatutozipata hizo dakika ishirini tena; tunatoa uhai wetu na
kupeana. Ni tendo lenye nguvu kimawasiliano na la kuchochea upendo” (uk. 60).
b. Wakati wa kuthamini mara kwa mara huhusisha mazungumzo yenye mantiki—ikimaanisha.,
“mazungumzo ya upole ambapo wawili wanashirikishana uzoefu wao, fikra, hisia, na shauku
katika hali ya kirafiki, isiyoingiliwa” (uk. 65). Mazungumzo yenye mantiki ni tofauti na
maneno ya ukiri chanya: maneno ya ukiri chanya yanafokasi katika kile tunachosema;
mazungumzo yenye mantiki yana fokasi katikas kile tunachosikia.
c. Wakati wa kuthamini waweza kuhusisha shughuli zenye kufaidisha—inamaanisha, chochote
kile ambacho nyote ama mmoja wenu anapendezwa nacho. Umuhimu hauko katika kile
mnachokifanya bali katika sababu ya kukifanya. “Kusudi ni kuwa na uzoefu wa kufanya kitu
pamoja, hata mtakapo kuwa mmemaliza ujisikie, ‘Ananijali. Alikuwa tayari kufanya kitu kile
ninachependezewa pamoja na mimi, na alikifanya kwa mtazamo mzuri.’ Huo ni upendo, na kwa
watu wengine ni upendo wa hali ya juu” (uk. 73-74)
3. Kutoa na kupokea zawadi. Zawadi ni kitu fulani halisi kinachoonyesha kuwa umekuwa ukimfikiria
umpaye zawadi. Haijalishi kama inagharimu pesa ngapi; unaweza kutengeneza zawadi. Kilicho muhimu
ni kwamba umekuwa ukimuwaza huyo mtu, ukamtafutia zawadi, na ukaitoa zawadi hiyo kama kielelezo
cha upendo wako kwake.
a. Ikiwa kupokea zawadi ni lugha ya msingi ya mwenzi wako, lugha rahisi ya upendo yaw ewe
kujifunza ni kuwa mtoa zawadi. Orodhesha zawadi zile ambazo zimemvutia na kumfurahisha
sana mwenzi wako alipozipokea kwa kipindi cha miaka (iwe zawadi hizo zimetolewa na wewe,
au marafiki). Hiyo orodha itakupa kuelewa aina ya zawadi mwenzi wako atapendelea kupokea.
Inapobidi, pata msaada wa ndugu anayemjua mwenzi wako vema katika kuchagua zawadi
nzuri.
b. Usisubiri mpaka kuwe na tukio maalum ndipo umpe mwenzi wako zawadi. Endapo kupokea
zawadi ndiyo lugha yake ya msingi ya upendo, yeye aweza kupokea karibu kila kitu kama
udhihirisho wa upendo. (Kama amezikosoa zawadi zako siku za nyuma, na karibu kila ulichotoa
kilikosa ridhaa yake, basi kwa hakika kupokea zawadi si lugha ya msingi ya upendo ya mwenzi
wako.)
c. Uwepo wako kimwili kwa mwenzi wako awapo na wakati mgumu au awapo katika wakati
mwingine muhimu yaweza kuwa zawadi yenye nguvu sana kwake. Mwenzi wako anapokwambia
kuwa angependa uwe naye katika tukio falani, chukulia ombi hilo kuwa ni muhimu.
4. Matendo ya huduma. Matendo ya huduma ni yale tutendayo tukijua kuwa mwenzi wetu anapenda
tuyatende. Haya ni pamoja na kupika, kuandaa meza, kuosha vyombo, kutoa takataka nje, kumbadilisha
mtoto nepi, au kusafisha nyumba. Hata hivyo yanahitaji, kupanga, muda, juhudi, na nguvu. Unatafuta
kumpendeza mwenzi wako kwa kumtumikia. Yanapotendeka kwa nia njema, matendo ya jinsi hii ni
matendo ya upendo. Hivyo ndivyo ilivyo hasa wakati matendo ya huduma utendayo ni yale ambayo
mwenzi wako angeyafanya kwa kawaida (mfano, mume kuosha vyombo baada ya chakula kuonyesha
kufurahishwa na chakula na upendo wake kwa mkewe).
a. Tunayotendeana kabla ya kuoana hayaashirii yale tutakayotendeana baada ya kuoana. Kabla
ya kuona tunabebwa na nguvu ya “upendo wa mwilini”. Baada ya ndoa tunarudi katika hali yetu
ya kawaida tuliyokuwa nayo kabla ya “kupenda.” Kwa hiyo endapo lugha ya msingi ya upendo
kwa mwenzi wako ni matendo ya huduma, yeye atakutarajia uendelee kufanya matendo ya
huduma katika ndoa. Mwenzi wako atajisikia kuwa hapendwi unapoacha kutenda matendo ya
huduma.
b. Kupenda ni uchaguzi ambao hauwezi kulazimishwa. Kukosoa na kudai kutendewa
husababisha ufa kati ya watu; havihamasishi matendo ya huduma ya upendo. Mwenzi wako
anaweza kufanya kile unachodai afanye, lakini halitakuwa tendo linalodhihirisha upendo.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
51
Maombi ni bora kuliko madai. Hatimaye, basi, kupenda ni chaguo. “Kila mmoja wetu lazima
achague kila siku kumpenda au kutompenda mwenzi wake. Tukichagua kupenda , basi
kuudhihirisha upendo wetu kwa mwenzi wetu kwa namna ile anayootuomba kutafanya upendo
wetu ufanikiwe zaidi” (uk. 107)
c. Shutuma za mwenzi wako kuhusiana na tabia yako hukupa picha iliyowazi kuhusiana na
lugha yake ya upendo. “Kwa kawaida watu hukosoa wenzi wao kwa sauti ya juu katika maeneo
ambayo wao wenyewe wana uhitaji mkuu kihisia. Shutuma zao si njia nzuri ya kutaka
kupendwa. Tunapoelewa hayo, tutasaidia kuweka hizo shutuma katika mchakato wenye
mwelekeo wenye matunda” (uk. 107)
d. Unaweza kutengeneza orodha ya maombi ambayo mwenzi wako amekuomba katika kipindi
cha wiki chache zilizopita. Yatazame maombi hayo kama ishara ya vile vilivyo muhimu kwake.
Amua kutekeleza moja kila wiki kama njia ya kuonyesha upendo. Au, waweza kumwomba
mwenzi wako aandike orodha ya vitu 10 ambavyo angependa wewe uvifanye katika kipindi cha
mwezi unaokuja, na vipange kutegemeana na umuhimu wake. Tumia orodha hiyo kupanga
mkakati kwa ajili ya “mwezi wa upendo.” Au, kila baada ya kipindi fulani muulize mwenzi
wako, “Kama ningeweza kufanya jambo moja maalum la kukuhudumia wiki hii, ombi lako
lingekuwa ni nini?” Mwenzi wako atatambua mambo haya. Kwa kufanya hili utakuwa unalijaza
“tangi lake la hisia.” Mwenzi wako atakuwa na furaha zaidi, na yeye pia, ataanza kutenda kwa
namna ya kukufurahisha wewe.
5. Mguso wa Mwili. Mguso wa mwili, ni pamoja na kushikana mikono, kupigana busu, kukumbatiana,
kupapasana kimahaba, na kufanya tendo la ndoa, zote hizi ni njia muhimu za kuwasilisha hisia za
upendo kwa mwenzi wako. Kwa watu wengine, mgoso wa mwili ndiyo lugha yao ya msingi ya upendo.
Bila ya hiyo, hawajisikii kupendwa. Ikiwepo hiyo, hujisikia salama ndani ya pendo na mwenzi wao.
a. Vipokea mguso viko kila mahali katika mwili, kwa hiyo kumgusa mwenzi wako eneo lolote la
mwili kwa namna ya kimahaba kwaweza kuashiria upendo. Hata hivyo, miguso fulani yaweza
kumsisimua zaidi kuliko mingine. Mwenzi wako atakuongoza. Usilazimishe kumgusa kwa
namna yako wewe au kwa wakati wako. Ikiwa mwenzi wako hafurahishwi na miguso ya namna
fulani, kuendelea kufanya hivyo kunawasilisha kinyume cha upendo, na kuonyesha kuwa hujali
hisia zake. Usifanye kosa la kufikiri kuwa mguso unaokuletea wewe burudiko utamletea na
yeye burudiko pia.
b. Mguso wa mwili unaweza kuwa muhimu sana hasa nyakati za mapito magumu. Inaonyesha
ukaribu na mshikamano na mtu anayeteseka.
c. Wanaume na wanawake waonyesha kuwa na mahitaji tofauti ya miguso ya kingono. Kwa
wake wengi, hamu ya kujamiiana na waume zao huletwa na ile hali ya kujua kuwa wanapendwa
na waume zao. Endapo wanahisi kutokupendwa, kwa kawaida watajihisi “wametumiwa” katika
hali ya ngono. Hamu ya mwanamume ya ngono ina kiini katika hali ya mwili zaidi—kujengeka
kwa chembechembe za shahawa na manii katika ogani itoayo manii: ogani hiyo inapojaa,
kunatokea msukumo wa mwili kuachia. Wana ndoa wengi wanahitaji kutambua tofauti hizi.
Hata hivyo, kama asemavyo Chapman: “Kwa kweli, wakati mke wake anaposema lugha yake
ya msingi ya upendo na tangi lake la hisia za upendo linapojaa, na yeye akasema lugha yake ya
msingi ya upendo, na tangi la hisia za upendo la mke wake likijaa, swala la ngono katika
uhusiano wao litajishughulikia lenyewe. Matatizo mengi ya tendo la ndoa katika ndoa nyingi
hayasababishwi na ule ujuzi wa namna ya kufanya tendo hilo bali zaidi sana katika eneo la
kukidhi haja za hisia.” (uk. 136)
C. Unaposeme lugha sahihi ya upendo kwa mwenzi wako, jitihada zako za kuwa na ndoa yenye mafanikio
zitaleta matunda.
1. Kinachofanya mtu ajisikie kuwa na hisia zakupendwa (ina maana, lugha yake ya msingi ya upendo)
sio sababu ambayo kila wakati ingemfanya mtu mwingine ajisikie hisia za kupendwa. Changamoto iko
katika kusema lugha sahihi ya upendo kwa mwenzi wako. Hilo ni muhimu kwa sababu, ndani ya ndoa,
“tusipojisikia kupendwa, tofauti zetu hukuzwa. Kila mmoja humtazama mwenziwe kama tishio la
furaha yake. Tunapigania uthamani na umuhimu wetu, na ndoa inakuwa uwanja wa mapambano badala
ya kuwa na furaha kama ya mbinguni” (uk. 154).
2. Lugha yako ya upendo ni ipi? Ni kitu gani ambacho kinakufanya ujisikie kupendwa zaidi na mwenzi
wako? Ni nini unachokitamani kuliko vyote? (Unaweza kuwa na lugha za upendo zaidi ya moja,
ingawaje watu wengi huwa na lugha ya msingi na ya pili). Chapman anapendekeza njia tatu za
kukuwezesha kugundua lugha yako ya msingi ya upendoe:
a. Ni kipi ambacho akitenda au kutotenda mwenzi wako utakwazika mno? Kinyume cha kile
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
52
kikukwazacho zaidi bila shaka ndiyo lugha yako ya upendo.
b. Ni nini ambacho umemwomba mwenzi wako maranyingi zaidi? Kile ambacho umekiomba
mara nyingi zaidi kwa hakika chaweza kuwa ndicho kinachokufanya ujisikie kupendwa zaidi
Kwa njia ipi wewe mara kwa mara huuonyesha upendo wako kwa mwenzi wako? Mtindo wako
wa kuuonyesha upendo yaweza kuwa ishara kwamba ukitendewa hivyo na wewe utajisikia
kupendwa.
3. Ni ipi lugha ya upendo ya mwenzi wako? Zifikiri njia ambazo mwenzi wako ameashiria kuwa
zinamfanya ajisikie kupendwa zaidi. Tumia maswali haya matatu hapo juu kwa mwenzi wako. Ikiwa
bado hujaelewa, muulize. Jadilini jambo hili. Ukifanikiwa kupata lugha yake ya msingi ya upendo
utakuwa umepata namna ambayo yawasilisha ujumbe, “Ninakupenda.” Kwa urahisi
4. Hisia za kupendana zinazodumu ni uchaguzi. Hisia za kupendana zenye nguvu, zinaweza kuzaliwa
upya ndani ya ndoa, hata baada ya miaka mingi ya kutojali. Unaweza kuhisi tangi la hisia za mwenzi
wako, na yeye anaweza kuhisi za kwako, mara tu unapogundua lugha yako ya msingi ya upendo, na
kwa makusudi unaanza kusema na kutenda kwa namna kuashiria upendo kwa mwenzi wako kupitia
lugha hizo za upendo.
8. KUFANYIKA BARAKA KWA FAMILIA YAKO
8Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu,
wasikitikivu, wanyenyekevu; 9watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa
sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi Baraka. 10Kwa maana,
“ATAKAYE KUPENDA MAISHA, KUONA SIKU NJEMA,
AUZUIE ULIMI WAKE USINENE MABAYA, NA MIDOMO YAKE ISINENE HILA.
11NA AACHE MABAYA, AKATENDE MEMA;
ATAFUTE AMANI, AIFUATE SANA.
12KWA KUWA MACHO YA BWANA HUWAELEKEA WENYE HAKI,,
NA MASIKIO YAKE HUSIKILIZA MAOMBI YAO;
BALI USO WA BWANA NI JUU YA WATENDA MABAYA.” (1 Pet 3:8-12)
I. Kifungu.
A. 3:8-12 kinafupisha yale aliyosema Petro sehemu iliyopita.
“Hatimaye”; “Kuhitimisha”; “Hitimisho la mada”katika 3:8 inafanya hilo kuwa wazi. Hata hivyo,
twahitaji kuona maana ya kifungu wazi wazi, ndipo tuitumie katika maisha ndani ya familia zetu.
1. Kifungu kilichotangulia ni 3:1-7. Petro ameainisha majukumu ya wake na waume.
2. 3:1-7, vile vile, ni matumizi bayana ya kununi za kiujumla za 2:11-12 (“ziepukeni tamaa za mwili”
na “mwe na mwenendo mzuri”), ambayo ilianza kifungu hiki chote, na ya mfano wa Kristo katika 2:21-
25.
B. Lugha ya Petro katika 3:8-12 ni pana vya kutosha kuweza kuhusisha waamini wote, lakini ina matumizi
ya kibinafsi kwa mahusiano ya mke na mume na familia; matumizi yake katika ndoa yanatiwa nguvu
tunapoangalia ulinganifu ulioko kati ya Efe 5:18-33 na 1 Pet 2:11-3:12.
1. Vifungu vyote, cha Paulo (Efe 5:22-33) na cha Petro (1 Pet 3:1-7) ni mijadala yenye maelezo ya kina
kuhusu majukumu ya mume na mke.
2. Katika mijadala hii yote, kila moja, kuna matumizi bayana ya asili ya unyenyekevu wa Kikristo
ambao, kwa upande mwingine, ni kipengele cha tabia ya msingi zaidi ya namna Mkristo apaswavyo
kuishi:
a. Kifungu cha Waefeso chatokana na mjadala wa Paulo kuhusu namna sahihi kwa Mkristo
"kuenenda” (Efe 4:1; 5:1-2, 15). Kifungu kilicho bayana zaidi kimechipuka kutoka katika rai
ya Paulo “mjazwe Roho” (Efe 5:18). “Kujazwa Roho,” kwa upande mwingine, kulijidhihirisha
kwa kanuni nne: “kusema” (5:19); “kuimba” (5:19); “kutoa shukrani” (5:20); na “kujitiisha
[kuwa chini ya]” (Efe 5:21). Efe 5:22 yaanza kuweka katika matendo dhana ya kujitiisha kwa
wake na waume.
b. Kifungu cha 1 Petro vivyo hivyo yazungumzia namna iliyo sahihi kwa Mkristo kuishi (1 Pet
2:11-12). Kifungu kilicho bayana zaidi ni kile cha Petro atoapo maagizo kwa watumishi kuwa
“wanyenyekevu [kanuni ile ile aliyotumia Paulo katika Efe 5:21] kwa mabwana wao kwa
heshima zote” (1 Pet 2:18). Kisha Petro akajadili jinsi “Kristo alivyoteseka kwa ajili yako,
akiwa amekuachia mfano wa kufuata katika nyayo zake” (1 Pet 2:21). 1 Pet 3:1, 7
huzungumzia kanuni hizo kwa ajili ya wake na waume kwa kutumia kielezi kile kile
(“kadhalika”).
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
53
3. Vifungu vyote huhitimisha kwa msingi mpana zaidi ya yale maagiizo ya kawaidi kwa wake na
waume; zaidi ya hapo, vyote huhitimisha kwa kuhusisha kidondoa kutoka Agano la Kale.
a. Waefeso 5 inadondoa kutoka Mwz 2:24 kufafanua kutoka uumbaji wenyewe kuwa ni kwa
nini wanaume wanapaswa kuwapenda wake zao kama Kristo alivyolipenda kanisa, na kisha
inahitimisha kwa kusema kuwa jambo lililo muhimu hapa ni “Kristo na Kanisa.”
b. 1 Petro 3 inahitimisha kwa kuonya waaminio kuishi vema “ili kuomba kwenu kusizuiliwe” (1
Pet 3:7), na akidokeza kwenye wito wetu tuwabariki wengine ili tuzirithi baraka kutoka kwa
Mungu; anadondoa kutoka Zab 34:12-16 kufafanua asili ya uhusiano wa Mungu na wanadamu
(ina maana, ukweli kuwa Mungu ni mkuu, na huyajibu maombi ya wenye haki, bali yuko
kinyume na watendao uovu).
C. Hatimaye, ndoa zetu zionekane kama kiungo kamili na muhimu cha uhusiano wetu na Baba na Kristo.
Matokeo muhimu na ya kiutendaji hutokea kutoka katika:
1. Ndoa imejengwa ndani ya mpango wa uumbaji (Mwz 2:24).
2. Kwa kuwa ndoa imejengwa katika mpango wa uumbaji, ni taasisi ya thamani kubwa, sehemu ya
uumbaji ambao Mungu aliutamkia kuwa kila kitu ni “chema sana” (Mwz 1:31).
3. Kwa kuwa ndoa ni taasisi ya thamani kwa Mungu, tunapaswa kuthamini ndoa zetu tukizingatia kuwa
ni uhusiano wenye thamani—na hivyo tuupatie muda, uangalifu, na juhudi ya kutosha kudhihirisha
kuwa tunaitambua kuwa ndoa yetu ni ya thamni kubwa kwetu.
4. Ndoa ni mfano wa uhusiano kati wa Kristo na kanisa (Efe 5:22-32).
5. Kwa kuwa ndoa ni mfano wa uhusiano kati ya Kristo na kanisa, ndoa, katika kiini chake, kimsingi ni
uhusiano wa kiroho.
6. Kwa kuwa ndoa ni mfano wa uhusiano kati ya Kristo na kanisa, mwenendo wetu kuelekeana, na jinsi
tunavyohusiana, kwa hakika ni mfano wa uhusiano kati ya Kristo na kanisa, mwenendo wetu kuelekea,
na jinsi tunavyojihusisha na, mwenzi wetu ni mfano wa mwenendo wetu kuelekea, na jinsi
tunavyojihusiha, na Kristo na Baba.
7. Kwa kuwa mwenendo wetu na uhusiano wetu kuelekea mwenzi wetu ni mfano wa mwenenndo wetu
na uhusiano wetu kuelekea Kristo na Baba, tunaweza kutarajia kuona kazi za kimatendo za Mungu za
kutuadibisha au kutubariki katika maisha yetu, kutegemeana najinsi tuwatendeavyo wenzi wetu (1 Pet
3:7-12).
II. Kuishi Maisha ya Ndoa yenye Baraka.
A. Kiini cha 1 Pet 3:8-12 ni 3:9b: “Kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.”
1. Kifungu chatoa sababu kwa nini waaminio wanapaswa kuishi kwa jinsi ya maagizo ya Petro katika
3:8-9a. Tunapaswa kuishi maisha ya Baraka kwa sababu hilo ndilo kusudi alilotuitia Mungu.
2. 9:10-12 inaelezea matokeo na mahusianno ya maisha ya baraka kimatendo na kiroho katika 3:9b. Ili
tuzipokee baraka za Mungu ni lazima tuwe baraka kwa wengine.
B. 1 Pet 3:8:
1. Petro anaanza kwa kuorodhesha tabia tano ambazo zapaswa kuwa sifa za waaminio (na zinapaswa
kuwa sifa za wenzi katika ndoa yao): “nia moja, wenye huruma, undugu, wasikitikivu, wanyenyekevu.”
2. Hizi zote ni tabia za ndani ambazo zina madhihirisho ya nje. Huu ni msimamo wa Yesu kutambua
kuwa utu wa ndani ndio asili ya unajisi. Tazama Marko 7:14-23. Hivyo, ndoa zetu zinapaswa kuwa na
msingi wa umoja katika utu wa ndani (“watakuwa mwili mmoja”—Mwz2:24), sio tu ile tabia ya unyofu
ionekanayo kwa nnje. Matokeo ya hili ni kwamba maisha ya Kikristo yanahusu maisha
yaliyobadilishwa, si tu itikadi au tabia zilizobadilika—yale tuaminiyo hayana maana kama hayagusi
mfumo wa jinsi tunavyoishi, na kama hatukujitoa na kukusudia kuiishi sawa sawa na vile tuaminivyo.
3. Petro anatanguliza neno “mwe na nia moja” katika orodha ya zile tabia.
a. Neno la Kiyunani lililotafsiriwa kutoka “nia moja” (Kiyunani = homophrones) ina maana
“kuwa na nia moja; wamoja katika roho; wenye nia moja” (Danker 2000: 709-10). Hali ya
kuwa na nia moja ni huwatajirisha pamoja. Kwa dhati, Petro anatoa wito wa umoja au kuwa
kitu kimoja kuongoza orodha ya tabia zinazotoa wasifu wa uhuusiano wa ndoa. Kwa hakika,
zile nne zilizobaki Petro anazitumia zinaweza kuonenkana zikitafsiri au kufafanua “hali ya
kuwa na nia moja” au “kuwa na nia moja” yenyewe. Tabia hizi nne nyingine kwa hakika
zitakuwepo uhusiano unapokuwa wenye nia moja au watu wawili wanapokuwa wana nia moja.
b. Umoja huu/hali ya kuwa na nia moja/kunia mamoja pia hudhihirisha asili ya kiroho ya ndoa.
Kwa hakika, maombi ya Yesu’ “ya kikuhani” katika Yohana 17 yanasisitiza umuhimu wa
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
54
umoja wa waaminio (“ili wawe na umoja, kama sisi tulivyo umoja”—Yohana 17:21-22). Kwa
kuwa ndoa zetu ni mfano wa Kristo na kanisa lake, umoja, hali ya kunia mamoja kati ya mke na
mume ni lazima, ni muhimu, na ni lazima ifanyiwe kazi.
4. “Wenye kuhurumiana” ikimaanisha kuonyesha “hisia” zaidi ya zile za kawaida zinazokubaliana na
ufahamu.
5. “Undugu”ni muhimu kwa kuwa ni lugha ya familia. Familia hujali, na kuhudumiana wao kwa wao.
Ndugu wa familia wanapaswa kuwa tofauti, wenye ukaribu, wakiwa na mahusiano ya karibu zaidi,
kuliko watu wengine wa nje. Kuna kitu cha pekee kuhusu familia ambacho hakiwezi kunakiliwa na
wale walio nje ya familia. Hivyo, ni muhimu, kwamba Mungu haku”waokoa” tu watu wake, lakini pia
“amewafanya kuwa wanawe” na kuwaingiza katika familia yake (tazama Rum 8:14-17; Gal 4:4-7; Efe
1:5).
6. “Wasikitikivu” inaendeleza wazo la “huruma” na “undugu” ikimaanisha matendo yenye asili ya
ukarimu yakihamasishwa na umoja na huruma. Kwa hiyo, mpango wa Mungu kwa ajili ya ndoa
huhusisha umoja wa fikra, hisia na tabia.
7. Bila “roho ya unyenyekevu” haiwezekani kufanikisha chochote katika tabia hizo zilizotangulia.
Unyenyekevu haujigambi au kutafuta kumtawala mwingine; badala yaake, unyenyekevu kwanza
hutafuta mafanikio ya mwingine. Mwenye “roho ya unyenyekevu” anayo roho ya Yesu ambaye “hakuja
kutumikiwa, bali kutumika” (Math 20:28).
C. 1 Pet 3:9a:
1. Petro hapa anaendelea kuonyesha njia ya kushinda kimatendo kwa namna ile ya tabia ya kuheshimu
ndoa ya Kikristo kama inavyojadiliwa katika 3:8.
2. Kushinda huku kimatendo kunaonyesha tofauti iliyowazi kabisa kati ya asili ya binadamu (ni pamoja
na ndoa) katika kuingiliana kwa mtazamo wa kidunia, na asili ya binadamu (ni pamoja na ndoa)
kuingiliana kwa mtazamo wa Kristo. Asili hizi mbili zimetengana, na zinapingana, kikanuni.
a. Mpango wa dunia kwa ajili ya mahusiano (ikiwa ni pamoja na mahusiano ya ndoa) ni
uhusiano wenye “msingi katika utendaji”. Kukubalika hutokana na utendaji (“fanya jukumu
lako; nami nitafanya la kwangu”); kutoa hutegemea ustahili ambao unautendea kazi—upendo
hutolewa pale mtu anapojisikia kuwa unastahili (“unafanya/hafanyi, ndipo nitafanya/sifanyi”),
au ili upate kitu kutoka kwa mwenzako; msukumo unategemea jinsi anavyojisikia. Mpango wa
dunia hatima yake ni uharibifu, hasa katika ndoa, kwa sababu ya:
(1) kushindwa kwangu kukidhi matarajio yasiyo halisi;
(2) kutokuweza kujua kuwa rafiki yangu amefanya sehemu yake;
(3) tabia yangu ya kufokasi kwenye madhaifu ya rafiki yangu;
(4) kuudhiwa na mwenzangu kunapoozesha utendaji wangu.
Matokeo ni, kama ilivyoonyeshwa katika 3:9a, uhusiano wa “baya kwa baya” na “laumu kwa
laumu”, ambao unafokasi kwenye “haki zangu” na “hisia zangu.” Uhusiano wa jinsi hii una
mizizi ya moyo wa kutokusamehe na mgumu. Uhusiano wa jinsi hii kwa kawaida hufuata pale
kukubalika na upendo ukiwepo msingi wa utendaji na ni sharti uutendee kazi, na hapa fokasi ni
mimi binafsi (na, hivyo, ulazima wa kila wakati “kulipiza” hitilafu kidogo inapotokea) (Campus
Crusade 1993: 20, 156).
b. Mpango wa Kristo kwa ajili ya mahusiano (ikiwa ni pamoja na mahusiano ya ndoa) ni
uhusiano wenye “msingi katika neema”. Una msingi katika asili ya Mungu mwenyewe, una
mizizi katika uumbaji, na una mfano wa uhusiano kama ule wa Kristo na kanisa. Hivyo
uhusiano wa ndoa unazungumzia kujishusha binafsi ili kukidhi mahitaji na mapenzi ya mwenzi,
na yale ya uhusiano wenu wa ndoa kiujumla, kimsingi katika hali ya kumpenda na kumshukuru
Kristo, na pili kwa ajili ya upendo wako kwa mwenzi wako (ambaye hutambulika kama zawadi
ya Mungu kwa mwenzi wake). Katika uhusiano kama huu, upendo, na kukubalika, na upendano
hutolewa bure, haviwi matokeo ya kazi tulizotenda, kwa sababu Kristo ametupenda na huyu
mtu mwingine anastahili pendo hilo, kukubaliwa, na kupendwa kwa sababu tu yeye ni mtoto wa
Mungu na ana mfano wa Mungu. Mwenzi asipokidhi matarajio yetu, twaweza kusameha bure
kwa kuwa sisi tumesamehewa na Kristo na kupatanishwa na Mungu tulipokuwa maadui wake
(Rum 5:8-10). Matokeo ni uhusiano wa “baraka kwa laumu” ambao unafokasi katika neno la
Mungu, ukipokea nguvu zake, na kuitikia kwa neema na msamaha unapokosewa. Uhusiano wa
jinsi hiyo hatima yake ni mafanikio, kwa sababu unatiririka kutoka kwenye tabia na amri za
Mungu mwenyewe (Ibid.: 157).
3. Hivyo, 3:9a inatuambia ku “acha kuishi kidunia; acha kuishi kutokana na jinsi dunia inavyofanya
katika mahusiano—na ishi kutokana na vile Kristo alivyoishi na jinsi anavyoagiza mahusiano yawe.”
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
55
Kwa kweli vile tunavyotenda (hasa jinsi tunavyo onyesha hisia tunapokosewa, tunapolaumiwa, au
tuwapo kwenye mazinghira yenye uovu) ni ishara ya nje, iliyo wazi inayoonyesha kama tuna tabia
aliyoagiza Petro katika 3:8. Tunapokuwa watu wabarikio wakati wote tunapolaumiwa na tudhihirishao
tabia zilizoandikwa katika 3:8 yamaanisha sisi ni baraka.
D. 3:10-12:
1. Katika mistari hii Petro anaelezea kuhusu “kutoa baraka” (3:9a) yaonyesha kuwa inapofanyika
kimatendo, na kutoa maoni kuhusu “kurithi baraka” (3:9b) maneno aliyomalizia 3:9. Mistari hii yote
inadondoa kutoka Zab 34:12-16.
2. Baraka ya familia katika Agano la Kale ilihusisha maeneo matano (tazama Mwz 17:1-8; 27:26-29;
32:24-32; 48:9-20; 49:1-27):
a. Mguso wenye maana. Kubusu, kukumbatia, au kuwekea mkono kulionyesha mazingiza ya
kujali kupelekea maneno ambayo yangesemwa; mguso waashiria kutia joto, kukubalika na
kukubali.
b. Ujumbe wa kutamka. Maneno ya upendo, kukubalika, na uthibitisho ni muhimu kwa ajili ya
kupitisha baraka kwa wengine.
c. Kuambatanisha “thamani kubwa” kwa yule anaenenewa baraka. Yale maneno ya kumbariki
yenyewe lazima yatamke ya kuwa yeye ni wa thamani naye ana sifa za ukombozi, ikizingatiwa
wao ni nani, na si kwa kuzingatia utendaji wao.
d. Kujenga taswira ya wakati ujao wa yule anayenenewa baraka. Ingawaje hatuwezi kubashiri
wakati ujao wa mtu, twaweza kuwasaidia na kuwatia moyo, tukiwapa tumaini na usalama kwa
kuwahakikishia kuwa tuko upande wao na tuko pamoja nao.
e. Msimamo hai wa kuzitekeleza baraka. Huu ni wajibu ambao unaambatana na kutamka
baraka. Inasemekana kuwa “vitendo vina sauti kubwa kuliko maneno matupu.” Hata hivyo,
matendo yako yanapothibitisha maneno yako na kusaidia katika kuleta matokeo mazuri,
matokeo hayo yanaweza kuwa kitu chenye nguvu sana—hasa pale ambapo maneno na matendo
hayo yanapokuwa ni ya uthibitisho, upendo, na baraka amabayo yametolewa kwa mmoja wa
wana familia. (Smalley na Trent 1986: 21-116)
Tunapaswa kufanya hivi kama njia ya kuutoa upendo na ridhaa yetu kwa familia yetu.
3. Asili na muktadha wa “kutoa baraka.” 3:9a kwa namna fulani ni tofauti na ule wa uliotumika
kutamka baraka katika Agano la Kale, na pengine ni mgumu zaidi kutekeleza. Petro anasema tunapaswa
kuwa watu “wenye kubariki” tunapokuwa tumetendewa baya au kulaumiwa. Kama inavyoelezwa katika
3:10-11, “kutoa baraka” inahusisha maneno yetu, matendo yetu, na nia zetu na malengo. Kuhusiana na
maneno, tunapaswa kutosema yaliyo maovu au yenye hila (ina maanisha, kusema kwa ujanja wenye
uongo, kwa udanganyifu, kwa hila ili kuwatega wengine). Kuhusiana matendo, tunapaswa “tuachane na
maovu na tutende mema.” Kuhusiana na nia na malengo, tunapaswa “kuitafuta amani na kuifuata.”
4. Lengo la “amani” linahitaji juhudi—“ufuatiliaji.” Kuishi maisha yanayobariki wengine sio rahisi
katikaa maisha haya yenye migogoro na watu ambao ni wabinafsi. Hata hivyo, amani ya kweli—amani
iliyo ndani yako na ile iliyo nje, amani itiririkayo kutoka kwa watu wawili ambao wote wanaishi kwa
tabia zile zilizoorodheshwa katika 3:8 na wanatenda yale yaliyoorodheshwa katika 3:9-11, watakuwa
wamepata sifa ya kiungu ya uhusiano wenye kiini katika Kristo. Dallas Willard anatamka: “Wakati
mtakatifu Augustine anapofikia mwisho kabisa wa kitaabu chake The City of God, anajaribu
kulikabiliaswali la ‘jinsi watakatifu watakavyotumika watakapokuwa wamvaa kutokufa katika miili ya
kiroho.’ . . . [Ana]ishia kwenye neno amani kuielezea, na anajenga wazo kwa njia ya maono ya Mungu .
. . Kwa maneno mazuri mno ambayo kila mtu angepaswa kuyakariri kwa moyo, anasema, ‘Huko
tutapumzika na kuona, kuona na kupenda, kupenda na kusifu’ . . . Hata hivyo, pamoja na uzuri na wema
wake, maneno haya kwangu bado hayajaikamata ile hali ya baraka ya urejesho wa vitu vyote—vya
ufalme kurudi katika utimilifu wake. Kupumzika, ndio. Lakini sio utulivu, usiokitu, bali uliothabiti
ndani ya umilele. Badala yake, ni, amani ya utimilifu, kama utimilifu wa utendaji, kama wapumzikao
lakini wakiendelea katika kuendeleza uumbaji katika ulimwengu wote, mshikamano wenye kufuatilia
mpango wa uumbaji ambao wakati wote unakaribia bali haufikii ule wema usio na mwisho wa utatu wa
Mungu, aliye asili yake.” (Willard 1997: 399-400, mkazo katika asili) Hizo ndizo sifa ambazo Mungu
amezikusudia kwa ajili ya ndoa hasa—uhusiano wa wawili waliokaribiana sana ambao ni mfano wa
asili yake, na hilo hutuongoza katika ukamilifu, utimilifu wa utendaji, na pumziko katika dunia ambayo
inapinga mambo hayo—hilo huifanya ndoa iwe picha ya muda ya umilele wa mbinguni, na ni uhusiano
ambao washiriki wake wanaweze kupata ujuzi wa ufalme wa Mungu hapa duniani.
5. Petro anahitimisha katika 3:12 kwa ahadi na onyo. Wayne Grudem anafafanua: “Maneno macho ya
Bwana huwaelekea wenye haki, haimaanisha tu kwamba Mungu anaona kile wenye haki wanachofanya
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
56
. . . lakini anawaangalia wakati wote, akiyaona na kuwatekelezea mahitaji yao . . . Kinyume chake,
maneno haya Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya yako, katika kifungu cha Zaburi 34, tamko
la hukumu lililo wazi, kwani mstari unaendelea, ‘aliondoe kumbu kumbu lao duniani’ (Zab. 34:16).
9:8-12 kiujumla isichukuliwe kama ushahidi wa wokovu utokanao na matendo, kwa
yanawalenga wale ambao tayari ni Wakristo na tayari wa ‘urithi’ usioharibika ambao uko kwa ajili yao
mbinguni (1:4). Hata hivyo kifungu hiki chatupa udhahiri wa uhusiano kati ya kuishi kiungu na uwepo
wa baraka za Mungu katika maisha haya. Kiasi kwamba inawapatia matengenezo yanayohitajika
Wakristo wenye misimamo nusu nusu na wasio makini waishio katika kila kizazi, na kichocheo chenye
nguvu kwa aina ya maisha matakatifu ambayo Petro anasema wakristo wote ‘wameitiwa’ hayo. (v. 9).”
(Grudem 1988: 150)
E. Kwa hiyo, ndoa ina uzito na umuhimu wenye kina kiroho.
1. Ndoa pia ina maana za kimatendo kwa ajili ya maisha yetu hapa duniani. Ndoa ni kitu chenye uzito
mkubwa sana mbele za Mungu.
2. Ikiwa tunazipa ndoa zetu uzito ule ule ambao Mungu amezipa, basi tutakuwa na furaha ile
aliyokusudia Mungu iwe sehemu ya heshima ya ndoa.
9. MAJUKUMU YAHUSUYO TENDO LA NDOA KATIKA NDOA
I. Umuhimu wa Tendo la Ndoa na Maadili ya Tendo hilo Kibiblia.
A.Tendo la ndoa ni muhimu mno kwani laturudisha kwenye asili ya maana ya sisi kuwa wanadamu.
Mjadala wa Biblia kuhusu kujamiiana una msingi katika mpango wa Mungu kwa ajili ya wanadamu na
mahusiano ya wanadamu. Biblia haishughulikii tu kweli za kiroho zilizo kuu, lakini pia inashughulikia hata yale
mambo muhimu ya kimatendo ya maisha, yakiwemo maswala ya mapenzi. Ikiwa maagizo ya Biblia yatafuatwa,
kutakuwa na ndoa zenye nguvu, furaha na za kusisimua miongoni mwa Wakristo.
B. Ki-ontolojia wanadamu wako na hali mbili, lakini kikazi wao ni umoja.
1. “Ontolojia” inahusiana na asili ya kuwa kwetu; “kazi” inahusiana na kile tunachofanya au namna
tunavyofanya au namna tunavyoishi.
2. Kusema wanadamu wana hali mbili ki-ontolojia, ina maana kuwa tumeumbwa tukiwa na sehemu kuu
mbili muhimu: sehemu iliyo mwili (umbo tunaloliona), na sehemu isiyo mwili (ufahamu, nafsi, roho).
Hali hizi mbili ki-ontolojia zamaanisha kuwa kwa asili hakuna chochote kilicho “kibaya” au “cha
dhambi” kuhusiana na mwili. Hutupaswi kuukataa mwili na kiu zake au kutafuta “ushindi dhidi yake.”
Badala yake, mwili uliumbwa na Mungu. Matamanio yake (pamoja na tamaa ya kujamiiana) ni vya
kawaida na vyatakiwa kutoshelezwa, ili mradi hilo lifanyike kwa namna ambayo imeagizwa na Mungu
(inamaanisha, katika muktadha wa ndoa).
3. Kusema kuwa wanadamu ni umoja kikazi ina maana katika maisha yetu yote kiutendaji tunafanya
kazi kama umoja: kinachotokea mwilini kinaathiri nafsi zetu, na kinyume chake; kinatutokea kimwili
hutuathiri kiroho, na kinyume chake. Tunapogundua hali hiyo ya utendaji kazi tunajilinda dhidi ya wazo
lisemalo mwili umetengwa na “sisi,” au mwili ni chombo tu kwa ajili yetu kutumia, au kilicho muhimu
ni ufahamu wetu tu, hivyo kile utakachoufanyia mwili hakina athari zozote. Kama hayo yangekuwa
kweli basi(watu fulani hufikiri) unaweza kufanya yale yote utamaniyo bila ya kupata matokeo dhidi ya
matendo yako. Narudia tena, tunapaswa kutenda sawa sawa na maagizo ya Mungu.
C. Biblia imeweka mfumo wa maadili kuhusiana na tendo la kujamiiana.
1. Mungu aliwakusudia watu kufanya tendo la kujamiiana wawapo tu katika ndoa ya kudumu iliyo ya
mke mmoja.
a. Biblia wakati wote hutuonyesha kilicho bora kama alivyokusudia Mungu. Mahusiano ya
kujamiiana yanatakiwa yafanyike ndani ya ndoa ya kudumu (ina maana, ya maisha marefu), ya
mke na mume mmoja (tazama Mwz 2:24; Math 19:4-6; 1 Kor 7:1-2, 8-14, 36; 1 Tim 3:2; 5:9,
11, 14; Tit 1:6; Ebr13:4).
b. Mungu amekusudia tendo la kujamiiana litendeka ndani ya ndoa ya mke mmoja kutokana na
jinsi Mungu alivyowaumba wanadamu. In Mwz 2:18 Mungu akasema, “Si vema huyo mtu awe
peke yake.” Hivyo, akamuumba mwanamke kutoka katika mwanamume awe msaidizi wa
kufanana naye (Mwz 2:18-23). Matokeo yake, “mwanamume ataambatana na mkewe; nao
watakuwa mwili mmoja” (Mwz 2:24).
c. Hali ya “kutotimilika”ya mwananmume au mwanamke amkosapo mwenzi yachanganyika na
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
57
hali ya kawaida ya mwanadamu kiutendaji ya kutafuta utimilifu kimwili kwa kujamiiana katika
muktadha wa ndoa ya mke mmoja pekee. Mwana filosofia wa Kikristo J. Budziszewski
anasema: “Tumeumbwa kwa namna ambayo miili yetu na mioyo yetu yatakiwa itende kazi
pamoja. Wanadamu kwa hakika tuna muundo, na namaanisha hivyo kwa hakika—si tu muundo
wa kibaiolojia, lakini wa kihisia, kiakili, na kiroho. Muundo wa binadamu ndiyo maana ya
usemi wa kale ‘asili ya mwanadamu.’ Mitindo mingine ya kuishi hukubaliana na muundo wetu.
Mingine haikubaliani. . . . Jinsi zimeundwa kutoshelezana. Tukiachilia hao walioitwa kwa ajili
ya maisha ya useja wana neema ya kiungu, kuna kilicho pungufu kwa mwanamume, ambacho
lazima kitoshelezwe na mwanamke, na kuna kilicho pungufu kwa mwanamke, ambacho lazima
kitoshelezwe na mwanamume. Kila mmoja awapo mwenyewe hajakamilika; ili wakamilike
lazima waungane.
Hii hali ya upungufu ni Baraka ya ajabu kwa sababu inasababisha uwezekano wa wao
kujitoa kila mmoja kwa mwenzake, na inawapa sababu ya kufanya hivyo. Kipawa cha hali ya
kuwa tofauti kinasababisha utofauti wa kila mmoja kuwa wa kipekee kwa namna ambavyo
hakuna utofauti mwingine wa kuulinganisha. Ule ukweli ya kwamba “wamewaacha wengine
wote” si jambo tu la kimsisimko lilengalo kutoa ahadi za ndoa kwa mtindo tabia za tamaduni za
Kimagharibi; inatokana na asili yenyewe ya kile kipawa. Huwezi kujitoa kwa sehemu tu, kwa
sababu Nafsi yako haiwezi kugawanyika; njia pekee ya kujitoa ni kujitoa mzima mzima. Kwa
sababu kile kipawa kiko kamili, ni lazima kiwatenge wengine wote, na kisipofanya hivyo, tukio
halikutokea. Hata tunaweza kusema zaidi kuhusu hiki kipawa, kwa sababu muunganiko wa
miili ya wenzi inamaanisha kitu kilicho kikubwa zaidi ya kuonekana kwa mwili; mwili umeivaa
nafsi, na kuunganika kwa miili huziunganisha nafsi. Ni ishara inayoshiriki na kutoa chapa ya
ule mfumo ambao kwa huo inatambulika; umoja wa mwili mmoja ndiyo lugha ya mwili ya
umoja wa maisha yote. . . . Kwa makubaliano ya pamoja kwa kujitoa kikamilifu, kwa
mshikamano thabiti wa hisia kali, na kwa raha ifikayo kileleni, na kuzaliwa kwa kiumbe kipya
kunaunganishwa na asili ya mwanadamu katika kusudi moja kuu. Ni kweli ya kuwa
wanaunganishwa na asili ya mwanadamu, hivyo tukijaribu kuwatenganisha, basi
twajitenganisha sisi enyewe.” (Budziszewski 2005: n.p.) Kwa hiyo, ni ule uhusiano wa ndoa ya
kudumu ya mke mmoja pekee ndio waweza kutimiza kusudi la Mungu sawa sawa na muundo
wa asili ya mwanadamu (matamanio yetu na mahitaji, ya kimwili na yasiyo ya kimwili).
d. Pamoja na kutimiza hitaji la muundo wa Mungu wa asili ya mwanadamu, maisha ya muda
mrefu yamekusudiwa kuwa kielelezo cha kweli za kiroho. Huu ndio udhihirisho ulio bora wa
asili ya Mungu: ndani ya ndoa mwanamume na mwanamke, ingawaje ni watu wawili,
“wanakuwa mwili mmoja” (Mwz 2:24), kama ilivyo ya kwamba kuna wingi-ndani ya-umoja
ndani ya Mungu mwenyewe (ina maana, nafsi za utatu kila moja ni tofaauti, ingawaje Mungu ni
mmoja). Zaidi ya hayo, ndoa inayodumu ya mke mmoja ni kielelezo cha uhusiano kati ya Kristo
na kanisa (Efe 5:28-32). Kama vile ambavyo Kristo ana bibi arusi mmoja, kanisa (tazama Ufu
19:7; 21:2, 9), vivyo hivyo mwanamume anapaswa kuwa na mke mmoja. Kama vile ambavyo
Kristo hatatuacha au kututupa (tazama Ebr 13:5; Rum 8:35-39), vivyo hivyo kamwe hatupaswi
kuwaacha au kuwatupa wenzi wetu wa ndoa.
e. Vile vile asili ya kiroho ya ndoa na kujamiiana vina maana ya kiroho kwani uzinzi
hufananishwa na ibada ya sanamu. Biblia hufananisha uzinzi sawa na kumwacha Mungu na
kufuata miungu na matendo yasiyo ya kimungu (tazama Yer 3:6-10; Ezek 16:15-22; Hos 2:2;
4:12; 1 Kor 6:15-20; Yak 4:4; Ufu 2:18-22; 14:817:1-5; 18:1-3; 19:1-2).
f. Ingawaje baadhi ya mababa wa Agano la Kale walikuwa na wake zaidi ya mmoja, tabia hiyo
haikuwa miongoni mwa wengi. Zaidi ya hivyo, kamwe biblia haijawahi kuagiza hilo, bali
imeeleza tu kutokea kwake.
(1) Kimsingi, mwanamume wa kwanza kuoa wake zaidi ya mmoja katika maandiko ni
Lameki, mwanamume ambaye hakuwa na sifa njema na mwenye tabia ya ugomvi
(Mwz 4:23-24). Kuoa wake zaidi ya mmoja ambao ni mtu na dada yake ilikatazwa
kabisa katika Agano la Kale (tazama Law 18:18). Kuoa wake zaidi ya mmoja kulileta
migongano katika familia na matokeo mengine yenye madhara ikiwa ni pamoja na
uzinzi wa kiroho kwa Mungu (tazama Mwz 21:9-11; 1 Waf 11:1-8). Ukweli ya kuwa
ndoa ya wake zaidi ya mmoja ni kinyume na mpango bora wa Mungu, na ni kinyume
na asili ya kiroho ya ndoa kama kielelezo cha Kristo na kanisa, unaonekana katika
ukweli kwamba, ili mwanamume awe kiongozi kanisani, sharti awe mume wa “mke
mmoja” (1 Tim 3:2; Tit 1:6).
(2) Kweli hizi ni matokeo ya hali za kijamii. Rhoads anasema, “Ndoa ya mke mmoja ni
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
58
bora kuliko ile ya wake zaidi ya mmoja, kwani yaweza kusababisha wanaume
kutokuwa na wake, na hivyo kushawishi vurugu kati ya wanaume wakigombania
wanawake.” (Rhoads 2004: 146). Mwandishi mmoja anaongeza haya, “Jamii ambazo
zimeshindwa kujenga ndoa za mke mmoja vile vile zimeshindwa kutengeneza
mazingira ya kidemokrasia katika kazi au katika mgawanyo wa utajiri. Jamii ambayo
wanaume wake wachache tu wana nafasi katika kazi za nyumbani haiwezi kuwa imara
katika mfumo wake wa kijamii. Watu wasioweza kuishi na mke mmoja bila shaka
mambo mengine mengi yatawashinda” (Tucker 1993: 38).
2. Hali ya kiutendaji kimaumbile na kiroho vina uhusiano na mfumo wa maadili wa jinsia.
a. In 1 Kor 6:12-20 Paulo anajadili kazi za chakula na tendo la ndoa kwa ajili ya mwili.
Kuhusiana na yule wa kufanya naye tendo hilo anasema: 15Je! hamjui ya kuwa miili yenu ni
viungo vya Kristo?Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!
16Au hamjui kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, “WALE
WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA.” 17Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja
naye. 18Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye
afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
b. Katika kifungu hiki, Paulo anatuonyesha kuwa tu wanadamu wenye mfumo
ulioingiliana.Hatuwezi kufanya kitu kwa miili yetu nacho kisiathiri roho zetu. Hilo ni dhahiri
kwa watu wote, lakini ni dhahiri zaidi kwa Wakristo. Sababu ni kwamba tumeunganishwa na
Kristo, kiroho na kimwili (sisi tu mwili wake—1 Kor 12:12-27). Kwa hiyo, tunapofanya uzinzi,
ni kana kwamba tumemfanya Kristo kuhusika na matendo hayo. Anapofafanua kifungu hiki,
James Davis anaileza kwa namna hii: “Kwa baadhi ya Wakorintho, waliojiona kuwa wana
uhuru wa kula watakacho na hivyo wakaona pia walikuwa huru kutosheleza tamaa zao za ngono
kwa ukahaba. Hata hivyo, kwa upende wa Paulo, tendo hilo, kimantiki na kwa kufuata
mwenendo wa mtiririko wa matukio yaliyosababisha hayo kutokea kwa asili ni makosa, kwa
sababu tendo hilo linamhusisha mwamini kimwili, kisaikolojia, na kiroho, yeye mzima, katika
tendo ambalo linamuunganisha Mkristo (ambaye mwili wake ni mali ya Bwana [mst. 14] na,
yeye, tayari ‘ameunganishwa’ na Kristo [vv. 15, 17; 12:27]) na nguvu yenye kutumikisha ya
roho ya uzinzi.” (Davis 1989: 970)
c. Biblia mahali pengine inatambua kuwa ufahamu huathiri mwili kwa kukemea mawazo yenye
tamaa mbaya sawa sawa na matendo ya uzinifu. Mtendo ya uzinifu hutokana na mawazo yenye
tamaa za kuzini (tazama Mith 6:24-33; Ayubu 31:1; Math5:27-30; 15:15-20; Marko 7:14-
23; 1 Thes 4:3-5). Kuthibitisha zaidi ya kuwa Mungu alimuumba mwanadamu kuhusika katika
tendo la kujamiiana akiwa katika ndoa ya mke mmoja, wanadamu ndio viumbe pekee ambao
hujisikia hukumu na aibu wafanyapo tendo hilo nje ya ndoa.
3. Mpango wa kimaadili wa biblia kuhusiana na kujamiiana ni: uaminifu katika ndoa; kutoshiriki nje ya
ndoa.
a. Kwa ajli ya sababu hizo hapo juu—namna Mungu alivyo kusudia asili ya kibinadamu na asili
ya kiroho ya ndoa—mara nyingi biblia imeagiza uaminifu katika ndoa (Ebr 13:4), na inaagiza
kuwa wana ndoa wasijihusishe na uzinifu nje ya ndoa (tazama Math 19:11-12; 1 Kor 7:7-9;
Ufu 14:4). Biblia inalaani aina zote za matendo ya uzinzi (1 Kor 6:18; 2 Kor 12:21; Gal 5:19;
Efe 5:3; Kol 3:5; 1 Thes 4:3-5; Ebr 13:4). Hayo ni pamoja na: ngono baina ya watu wasio na
ndoa (uzinzi) (Kum 22:13-21; 1 Kor 7:2, 8-9; 1 Thes 4:3); tendo la ndoa kati ya mtu aliye
ndani ya ndoa na ambaye si mwenzi wake wa ndoa (uasherati) (Kut 20:14; Law 18:20; 20:10;
1 Kor 6:9-10; Yak 2:11); ukahaba (Law 19:29; Kum 23:17-18); ushoga (Law 18:22; 20:13;
Rum 1:26-27; 1 Kor 6:9-10; ngono baina ya ndugu wa familia moja (Law 18:6-17; Kum
27:20, 22-23; 1 Kor 5:1); ubakaji (Kum 22:23-27); kujamiiana na wanyama (Kut 22:19; Law
18:23; 20:15-16; Kum 27:21).
b. Tunapotii maagizo ya Biblia ya kuwa waaminifu katika ndoa na kutojihusisha na uzinzi nje
ya ndoa tunapata matokeo ya ziada kimwili na kiroho: (1) Uaminifu katika ndoa husababisha
kufunguka kwa njia ya ushirika na Mungu ambayo haifungwi au kuzimishwa na dhambi
(tazama Isa 59:2; Mal 2:13-16; 1 Thes 5:19); na (2) Uaminifu huzuia magonjwa ya zinaa,
ikiwa ni pamoja na UKIMWI (tazama Mith 3:1-8; 5:1-11; 7:1-27; 1 Kor 7:34).
II. Kusudi la msingi la tendo la ndoa kulingana na biblia.
A. Kuongeza uzao wa mwanadamu—Mwa 1:27-28.
1. Mungu amempa mwanadamu msukumo wa kutaka kujamiiana ukiwa ni msukumo wenye nguvu sana
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
59
miongoni mwa mingine, ili wanaume na wanawake waweze kuzaa na kuongeza kizazi cha
mwanadamu. Lengo la msingi na kusudi la kujamiiana ni kuzaa. Katika kazi nyingine zote zitendwazo
na mwili (mfano, kuona, kula, kutembea, kusema, kusikia, kutoa uchafu kutoka mwilini) ni mwili
mmoja tu unahitajika kufanya kazi. Kuzaa peke yake ndilo tendo muhimu la maisha ambalo
haiwezekani mtu mmoja kulitenda peke yake. Tofauti za jinsi kati ya mwanamume na mwanamke
zimeundwa kwa kizingatia wazo lakuzaa, na nguvu za jinsia zote kwa kweli ni muhimu na husababisha,
kuzaa.
2. Mpango wa Mungu kuijaza mbingu ni pamoja na kuijaza dunia. Sababu moja wapo ya kuijaza dunia
ni kwa sababu wanadamu wameumbwa kwa “mfano wa Mungu” (Mwa 1:27). “Mfano” (tselem)
inatafsiriwa kama, “mwanadamu, kufanana na Mungu, mfano wa Mungu, ina maana. Yeye ni makamu
wa Mungu, mwakilisha au shahidi miongoni mwa viumbe” (Koehler na Baumgartner 2001: “tselem”
2:1029). Hivyo, mfano wa Mungu si tu kitu tulichonacho, lakini ndivyo tulivyo. Wazo la mwanadamu
kuwa ni mfano au sura ya Mungu “linatuambia kuwa mwanadamu kwa jinsi alivyoumba alikusudiwa
awe kioo cha Mungu na mwakilishi wa Mungu” (Hoekema 1986: 67). Kwa sababu agizo la Mungu kwa
watu lilikuwa “mkaijaze nchi” (Mwa 1:28), Mfano wa Mungu na utukufu ungesambaa duniani kote
wakati wawakilishi wake wanapoendelea kulitii agizo.
3. Watoto hupatikana kwa kujamiiana, na kupitia watoto huja mahusiano, wajibu na majukumu ya
wazazi na maisha ya familia. Kama ilivyo kwa ndoa ya kweli, Mungu ameumba wanadamu kwa ajili ya
maisha ya familia. Budziszewski anafafanua: “Hatukuumbwa kama wanyama, ambao huwa na ushirika
kwa kitambo kifupi tu. Kwa upande wetu sisi, kuzaa kunahitaji maisha ya kuwa pamoja ya muda mrefu
wa uvumilivu kati ya watu wawili, mwanamume na mwanamke, ambao wanatofautiana kwa namna ya
kuinuana. Lakini inamaanisha kuwa kuunganika huku hauna kusudi tofauti, nje ya kuzaa; bali,
litapatikana katika mazingira ya kuzaa na kuainisha namna tendo hilo la kuzaa linavyotendeka.
Mzazi wa kila jinsi ni muhimu katika tukio la kutengeneza mtoto, kumkuza na kumfunza mtoto.
Kumtengeneza wote wanahitajika kwa sababu mwanamke anatoa yai na mwanamume analirutubisha, na
mwanamke analiatamia hadi liwe kiumbe kichanga. Kumkuza, wote wanahitajika kwa sababu
mwanamume anafaa kwa jukumu la ulinzi, na mwanamke kwa malezi. Kumfundisha, wote wanahitajika
kwa sababu anahitaji kielelezo cha jinsia yake, kielelezo cha mwingine na kielelezo cha uhusiano kati
yao. Mama na baba wameunganishwa na hawawezi kubadilishwa. Ushirika wao katika kuzaa
unaendelea hata baada ya watoto kukua, kwa sababu watahitajika kuwasaidia kuunda familia zao
wenyewe.
Mwanasosholojia Sara S. McLanahan na Gary Sandefur wanasema katika kitabu chao Growing
Up with a Single Parent ya kuwa ‘Endapo tutaombwa kuunda mfumo wa kuhakikisha kuwa mahitaji ya
lazima ya watoto yanapatikana, tutajikuta tumepata kitu kinachofanana na mpango wa wazazi wawili.’
Ni kweli—kwa kuwa umeundwa, ingwaje si sisi tuliouunda.
Mwana sosholojia mwingine, René König, anafafanua katika International Encyclopedia of
Comparative Law ya kuwa watoto, hasa wale wadogo, hawafaidiki katika nyumba za kulelea yatima
kama ambavyo wangekuwa katika mazingira ya familia ya kawaida—hata pale ambapo pameboreshwa
kupafanya pawe kama nyumbani, na hata pawe, kwa jicho la kisosholojia, pana hali nzuri kuliko ile ya
familia ya kawaida katika hali zote, kiusafi, kisaikolojia, kiafya, na kielimu.
Haya yote yanaonyesha wazi ni kwa nini mwanadamu ana hamu kubwa ya kuwa na ushirika wa
kuwa na mwenzi wa karibu wa jinsi nyingine kwani hilo ndilo kiini cha namna alivyoumbwa. Bila ya
hilo, uhusiano unaopelekea kuzaa usingeweza kudumu kwa namna ambavyo ungetarajiwa kudumu ili
kajenga familia zilizo imara na thabiti.” (Budziszewski 2005: n.p.)
4. Kama jinsi ilivyo ndoa, familia pia ina maana ya kiroho. Familia ni kielelezo kinachoonyesha
uhusiano wetu na Baba wa mbinguni (tazama Rum 8:14-17; 2 Kor 6:18; Gal 3:26; 4:1-7; Efe 1:5;
Ebr 2:9-17; 1 Yohana 3:1-2).
B. Kufurahia na kuongeza nguvu ya upendo kwa wote wawili—Mwa 2:18-25.
1. Mungu ndiye aliyeanzisha tendo la ndoa. Mwanzo 2 inaeleza kuwa Adamu na Hawa walilifurahia
tendo la ndoa hata kabla hawajapata watoto au kabla hata ya kufanya dhambi. Maana ya kwanza kwa
mume na mke kufanyika “mwili mmoja” (Mwa 2:24) ni ule muunganiko wanaokuwa nao katika tendo
la ndoa. Hivyo basi, tendo la ndoa si dhambi. Mungu alilikusudia kuwa starehe ya kufurahia kwa ajili ya
viumbe wake. Kwa jinsi alivyotuumba Mungu, maumbile ya mwanamume na mwanamke yana maeneo
yenye viungo ambavyo vina msisimko mkubwa unaosababisha ashiki. Maeneo hayo ya mwili
yanapotekenywa katika hali ya mahusiano “yaliyo wazi bila aibu” kuna msukumo wa nguvu uletao
furaha na starehe ambapo wote wawili hupeana raha katika hali hiyo ya kujamiiana.
2. Paulo hapa analinganisha katika 1 Kor 6:12-20 kati ya chakula na tendo la ndoa na pia anasema ni
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
60
kwa nini Mungu aliweka tendo la ndoa kwa ajili ya kufurahia na kuyapa nguvu mahusiano ya ndoa.
Frederica Mathewes-Green anatoa maoni kuhusiana na hili: “‘Maana’ ya tendo la ndoa iko wazi kabisa.
Ni uzalishaji. Kila kiumbe kilicho hai kina misukumo miwili mikubwa ya msingi: kwanza, kutunza
maisha yake (ambayo huhusisha kutafuta chakula, malazi au pa kujihifadhi na usalama), na pili,
kuendeleza maisha hayo kwa kizazi kingine. Viumbe huzaana kwa njia nyingi tofauti, lakini wanadamu
na mamalia wengine hufanya hivyo kwa njia ya kujamiiana na kuzaa kiumbe kingine cha kufanana nao.
Inaonyesha wazi kuwa tendo la ndoa limekusudiwa liwe la kufarahisha ili tutake kulitenda, na
tuhamasike kuzaa kizazi kipya. Na kuhusiana na chakula ndivyo ilivyo: Kinachosababisha tuone ladha
fulani kuwa ni tamu na nyingine chungu ni ili tule vile vinavyofaa kwa ajili yetu na kujiepusha na vile
ambavyo vyaweza kuwa sumu.
Hii hali ya kuwa na uchaguzi wa ladha tunazaliwa nayo; hatujifunzi. Watafiti wamegundua
kuwa wakiongeza ladha ya sukari kidogo katika majimaji ya amniotiki, kichanga ambacho hakijazaliwa
kitayanywa kwa haraka. Tumeumbwa tupende vitu vyenye ladha ya sukari, Nafikiri ndiyo maana
mababu zetu wa kale waliendelea kuyataka yale matunda yenye rangi za kung’aa, yenye vitamin
yaliyokuwa yakining’inia mitini kwa ajili yao.
Hivyo ndivyo ilivyo pia kuhusiana na tendo la ndoa: Twajisikia raha kulifanya na kwa njia hiyo
tunataka kuzaa. Lakini kuna namna za kipekee ambazo mwanadamu yu tofauti akilinganishwa na
mamalia wengine, hata miongoni mwa wale mamalia wa daraja la juu. Kwa sisi, tendo la ndoa ni la
kufurahisha wakati wowote wa mzunguko wa maisha. Lakini mamalia wengine hujamiiana katika
vipindi vya rutuba tu.
Zaidi ya hayo, watafiti wanahisi kuwa ni kwa upande wa wanadamu tu wanawake hufikia
msisimko wa kuwafikisha kilele. Ni wazi kuwa, kufikia kilele hakuna uhusiano na kubeba mimba;
haihusiani na tendo la kuzaa kabisa. Kwa hiyo wanaume na wanawake wanahamasika kufanya tendo la
ndoa kwa sababu zilizo tofauti na zile za wanyama, na hata zile za mamalia wengine na hata wale
ambao wanakaribia kufanana na wanadamu, hawana. Inaonesha kuwa “maana ya kujamiiana” kwa
upande wa wanadamu ni kitu kipana zaidi ya kule kuzaa tu.
Unaweza kuuona ulinganifu huu pia katika chakula. Kwa kadiri nijuavyo, wanyama hula kile
wanacho hitaji, kwa ajili ya miili yao. Lakini wanadamu hula kwa sababu nyingi mbali mbali. Tunakula
keki ya arusi, tunakunywa kahawa na rafiki, tunatafuna karanga tunapoangalia sinema. Tunakula kwa
sababu za kijamii, au kujiburudisha, au kama tabia. Si wakati wote tunakula kwa ajili ya mwili kupata
lishe. Vivyo hivyo, hatufanyi tendo la ndoa kwa ajili ya kuzaa tu.” (Mathewes-Green 2005: n.p.)11
3. Ukweli ya kwamba tendo la ndoa limekusudiwa, kwa sehemu, kutia nguvu mahusiano ya ndoa
unaonekana tena katika ukweli kuwa wanadamu ni miongoni mwa viumbe wachache, au pengine wao
ni viumbe pekee wanaoweza kufanya tendo la ndoa wakiwa wanatazamana uso kwa uso. Mathewes-
Green anasema kuwa, kutokana na namna wanadamu wanavyofanya tendo la ndoa, “tendo la ndoa lina
maana zaidi kwetu kuliko lilivyo kwa mamalia wengine wengi, ni jambo ambalo linaleta hali ya kuwa
na uhusiano wenye mguso wa ndani wenye kutuunganisha. Muunganiko huo hauwi wa kimwili tu au
kwa sababu ya kuzaa lakini unauhusisha utu mzima. Inaoneka kuwa “maana ya tendo la ndoa” ina
uhusiano na lile hitaji kubwa la mwanadamu la kuunganika na mwingine katika hali ya mapenzi, katika
kuaminiana, na kuwa na uhusiano ambao utadumu maisha yao yote” (Mathewes-Green 2005: n.p.).
4. Raha au starehe ya kweli, katika maana halisi ya neno hilo, ni kumpatia utoshelevu kamili yule
umpendaye. Biblia inalichukulia swala la kujamiiana katika uhalisia hasa. Mungu ameweka kitabu cha
Wimbo Ulio Bora katika Biblia, ambacho ni simulizi yenye kuonyesha jinsi mwanadamu
anavyofurahia mapenzi, ikiwa ni pamoja na swala la kujamiiana ndani ya ndoa. Jambo moja ambalo
biblia inathibitisha ni kwamba tendo la ndoa kama lilivyo ni zuri na halina unajisi. Msukumo na hamu
ya kutaka kufanya tendo la ndoa kwa mwanamume au mwanamke yeyote wa kawaida ni hisia
tulizopewa na Mungu, na kwa hakika si kitu cha kuonea aibu. Mungu ameweka muhuri wake wa
kuidhinisha tendo la ndoa ndani ya ndoa, na anatarajia viumbe wake kufurahia kikamilifu wawapo
ndani ya ndoa. Tendo la ndoa ni zawadi kutoka kwa Mungu ambayo twapaswa kuisherehekea na
kufurahia. Hivyo, kiwango cha mahusiano ya tendo la ndoa ni muhimu. Kila mmoja lazima ajiandae,
ajifunze kwa mwenziwe, wafundishane, na kila mmoja afanye kila awezavyo kumsisimua mwenzake na
kuhakikisha kuwa anamfikisha katika utoshelevu kwa kadiri awezavyo. Kwa hakika Bwana asingeweka
Wimba Ulio Bora kwa ajili yetu kusoma kama tendo la ndoa halikuwapasa wanandoa.
11Ukweli kwamba katika jamii nyingine wanawake hukeketwa (kukata sehemu ya kinembe cha mwanamke) huingilia
uumbaji waMungu wa jinsia. Katika mazingira haya wanawake lazima wakumbuke kusudi la uumbaji wa mke, kumsaidia
na kumtosheleza mumewe, hii ikiwa ni huduma aliyopewa na Mungu ifaayo. Waume lazima wadhihirishe upendo wa
Kristo kwa wake zao waliokeketwa. Wanahitajika kuonyesha upendo, hasa kitandani, kwa maneno ya upendo na
kuwakubali, na kuwa na muda nao na kuwakumbatia na kuwashikashika kwa miguso ya upendo.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
61
5. Tendo la ndoa ni la “ki-mahusiano,” hasa na lina maana nyingi:
a. Ni njia ya shukrani, ambayo kwayo mwanandoa anaweza kuonyesha shukrani kwa ajili ya
uwepo wa mwenzi wake;
b. Ni lugha ya tumaini, ambayo kwayo wana ndoa wanaweza kuhakikishiana kuwa
wanahitajiana na wanapenda kuendelea kuishi pamoja;
c. Ni njia ya kuleta upatanisho, ambayo kwayo mgogoro waweza kutatuliwa kabisa au kwa
sehemu;
d. Ni njia yenye nguvu kuliko zote ya mtu kuthibitisha uanaume wake au uanamke wake;
e. Ni uthibitisho unaorudiwarudiwa wa hali ya utu wa kila mmoja;
f. Ni njia ambayo kwayo muendelezo, uponyaji na ukuaji vinathibitishwa;
g. Ni njia ya kuimarisha kudumu kwa uhusiano. (Dominian 1982: 96)
6. Chanzo kimoja kizuri cha kuelewa na kufurahia tendo la ndoa kutoka katika mtazamo wa Mungu:
Tazama Ed Wheat na Gaye Wheat, Intended for Pleasure: Sex Technique and Sexual Fulfillment in
Christian Marriage, 3rd ed. (Grand Rapids, MI: Revell, 1997).
III. Matumizi ya Malengo ya Kibiblia ya Tendo la ndoa—1 Kor 7:1-5.
A. Utoshelevu katika tendo la ndoa ndani ya ndoa huzuia uzinzi.
“1Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke. 2Lakini kwa
sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake
mwenyewe.” (7:1-2).
1. Katika 7:1 Paulo anasema kuwa hali ya mtu kuwa mseja ni nzuri na haina tatizo lolote. Na anarudia
dondoo hiyo katika 7:7-8, 26, na 40. Hata hivyo, anasisitiza kuwa waseja wajitenge na maswala ya
kujamiiana, na wabaki kuwa wasafi kijinsi (“ni heri mwanamume asimguse mwanamke”).
2. Katika 7:2 Paulo anatambua kuwa aina zote za matendo ya uzunifu na vishawishi, kati ya jinsi tofauti
na jinsi zinazofanana, yapo miongoni mwa Wakristo. Hivyo, “kwa sababu ya zinaa,” inamaanisha, ili
walio nje ya ndoa wasifanye uzinzi na walio ndani ya ndoa wasifanye uasherati, wanaume na wanawake
wanapaswa kuoana na kuwa na maisha mazuri, na ya utoshelevu ya kufanya tendo la ndoa. Neno “na
awe” katika 7:2 limetumika mwa kumaanisha “kuwa na mtu wa kufanya naye tendo la ndoa
kimahusiano” (mke wako au mume wako). Uhusiano wenye utoshelevu wa tendo la ndoa baina yako na
mumeo au mkeo unapunguza tamaa ya kutafuta utoshelevu huo mahali pengine.
3. Kwa hiyo, sababu moja wapo ya ndoa ni kuzuia uzinzi. Ingawaje hiyo yaweza kuonekana kuwa ni
sababu isiyo na uzito sana kwa mtu kuwa na ndoa, bado ni sababu nzuri endapo tunahitaji kutunza
maadili ya Kikristo. Kwa kweli, Paulo anarudia dondoo hiyo tena katika 7:8-9.
4. 7:2 kwa namna isiyo dhahiri inafundisha dhana mbili za ziada:
a. Ndoa ya mke mmoja, si zaidi ya mmoja. Paulo anasema ya kuwa “kila mwanamume”
anapaswa “kuwa na mke wake,”na “kila mwanamke” anapaswa “kuwa na mume wake.”
Tambnua ya kuwa amri hizi za Paulo ziko katika nafsi ya: (1) umoja (inamaanisha, mke mmoja
au mume mmoja ndiye anayehusika); na (2) kinyume chake (kati yao hakuna anayeruhusiwa
kuwa na mwenzi zaidi ya mmoja).
b. Utoshelevu katika tendo la ndoa unapatikana kutoka kwa mwenzi wa ndoa pekee. Njia pekee
ya kuzuia mahusiano ya kujamiiana kabla na baada ya kuwa na ndoa ni kwa mtu kuwa na mke
“wake” au mume “wake”. Watu walio ndani ya ndoa hawapaswi kumtamani mke au mume wa
mtu mwingine, au kuwa na mawazo ya tamaa za uzinifu kuwaelekea wengine. Na hili lina
uhusiano na dhana ya mke kujaliza ule upungufu wa mume, na mume kwa mke. Katika kutoa
matamko haya, Paulo anasema ya kuwa mwenzi wako anapaswa kuwa ni kiini cha upendo
wako, mawazo yetu, na tamaa zetu. Kwa kufanya hili Paulo ameinua hali ya mwanamke kuwa
na ushirika kamili na mwanamume. Katika kipindi cha milki ya Warumi, kwa kawaida mke
alionekana kama kitu au mtumishi. Licha ya kuzaa watoto na mkewe, mwanamume kwa
kawaida alikwenda kwenye hekalu la Aphrodite kwa ajili ya kufanya uzinzi. Paulo anakataza
jambo hilo na anasema tunapaswa kupata utoshelevu utokanao na tendo la ndoa kutoka kwa
mwenzi wa ndoa peke yake.
B. Kuhusiana na tendo la ndoa, wanandoa wana wajibu wakutoshelezana kila mmoja kwa mwenzake.
“Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake” (7:3).
1. Tendo la ndoa si kwamba ni raha ya ndoa tu, bali pia ni wajibu katika ndoa. Mume ana deni kwa
mkewe na vivyo hivyo mke kwa mumewe. Hapa, neno “wajibu” inamaanisha kukidhi hitaji la kijinsi la
mkeo au mumeo. Kama ilivyo katika 7:2 wajibu uko sawa na kwa namna iliyo kinyume (maneno
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
62
yanayofanana ya vifungu viwili, na maneno “vivyohivyo na” inafanya hilo liwe wazi).
2. Tunapogundua wajibu wetu wa mume na mke kukidhi hitaji la kijinsi la mwenzi wake kunatufanya
tugundue na kuitika sawia kukidhi mahitaji tofauti kati ya mume na mke ambayo yanaweza kuwepo.
a. Mume anapaswa kujitoa mhanga, kama Kristo alivyolipenda kanisa (tazama Efe 5:25).
Kujitoa huko ni pamoja kukidhi haja za kijinsi za mkewe. Swala hilo ni zaidi ya lile tendo
lenyewe la ndoa. Kwa upande wa mwanamke utoshelevu wa kijinsi una eneo pana zaidi kihisia
kuliko lilivyo kwa mwanamume. Kwa hiyo, mume anapaswa kuwa na muda na mkewe. Ni
lazima awe na mawasiliano na mkewe. Ni lazima amsikilize. Ni lazima amhakikishie usalama.
Maisha ya mwanamke ya kijinsi yamefungwa katika ufahamu, na mahitaji yake lazima apewe
katika hali ya kumjali na maelewano kabla hajaitika na kupata utoshelevu katika tendo la ndoa.
Zaidi ya hayo, wanawake huchukua muda mrefu kupata ashiki kuliko wanaume. Kwa hiyo,
wanaume wanapaswa kuchukua muda wa kutosha kabla ya tendo, kuwakumbatia na
kuwashikashika wake zao. Hatimaye, tendo la ndoa, kama anavyolichukulia Paulo, ni namna ya
utoaji na sio kupokea.
b. Vivyo hivyo, mke anapaswa kumtii mumewe kama kumtii Bwana (tazama Efe 5:22).
Unyenyekevu huu ni pamoja na kukidhi haja za kijinsi. Ili aweze kufanya hayo ni lazima awe
amejiandaa kisaikolojia, atenge muda mahususi kwa ajili hiyo ijapo yu katika hali yake ya
shughuli nyingi, na asiruhusu hali ya uchovu uliozidi, na ampe muda mumewe dhidi ya watoto.
Wanaume huwa na hitaji la kufanya tendo la ndoa mara nyingi zaidi wakilinganishwa na
wanawake, hali hii inatokana na kiwango kikubwa zaidi cha testosteroni za kijinsia katika
ubongo wao. Wake inawabidi waikubali hali hiyo kuhusu wanaume. Wanaume wengi
wanapokosa kutimiziwa mahitaji yao ya kijinsi huanza kutafuta njia nyinginezo za kutimiziwa,
huwa na chuki, huwa na hali ya mfadhaiko mahitaji hayo yasipokidhiwa. Hali hiyo ya
mfadhaiko husababisha tabia ya “hasira”.
3. Tande la ndoa si tu tukio la kufurahisha mtu atendalo kila wakati anapotaka, bali pia ni jukumu
muhimu la kiroho/adilifu. Swala la kukosekana kwa uaminifu katika ndoa laweza kuepukwa pale
ambapo mume na mke wametambua kuwa kila mmoja ana deni la kumtosheleza mwenzi wake katika
maswala yote yahusuyo jinsia (kujamiiana). Kuiita ndoa mkataba si jambo linalooneka kuwa ni la kimahaba,
lakini huo ndio mtazamo wa maandiko. Kujamiiana ni wajibu, na ni wajibu wenye umuhimu
ulio sawa na ule wa kusoma Biblia, kuomba, au kushuhudia. Kushindwa kutekeleza wajibu huu kwa
mwenzi wa ndoa ni dhambi.
4. Kukosa uaminifu kuko katika sura nyingi. Kuna namna ambavyo mtu anaweza kukosa uaminifu bila
kuzini na hilo bado linaidhoofisha ndoa. Mapenzi ya Kikristo ni swala la ufahamu na utashi kama
lilivyo swala la hisia. Mmoja anapoamua kutokumjali mwenzake hilo laweza kufanya mambo yawe
magumu zaidi. Kutokutilia maanani hitaji la mwenzi la kujamiiana na misukumo yake ya kijinsia,
husababisha ufa mkubwa kati ya mume na mke. Wanaume au wanawake ambao hawatambui kuwa
kukidhi haja ya kijinsi ya wenzi wao ni wajibu wanaopaswa wana hatia ya kukosa uaminifu
kusikotokana na uasherati.
5. Swala la kujamiiana katika ndoa limehusishwa na mwendo wetu wa kiroho na Bwana wetu Yesu
Kristo. Furaha ya mume au mke katika katika maisha ya ndoa kuhusiana swala la kujamiiana/ ngono
kuna matokeo makubwa sana katika maisha yake ya kiroho. Mapenzi yaliyo hai katika ndoa ni muhimu
ili furaha iwepo ndani ya ndoa. Kwa kweli, muunganiko katika tendo la ndoa ni mfano wa ushirika wetu
wanye furaha pamoja na Kristo.
C. Kuhusiana na tendo la ndoa, wana ndoa wana haki sawa mmoja kwa mwingine.
“Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake bali,
mkewe” (7:4).
1. Kabla ya kuingia katika ndoa, mtu ana mamlaka juu ya mwili wake kuhusiana na namna anavyotaka
iwe kuhusiana na maswala ya ngono. Mtu huyu anapaswa kuuheshimu mwili wake kama hekalu la
Mungu na kuuweka katika hali ya usafi kijinsia. Bali, mara tu mtu huyu atakaposimama katika arusi na
kusema, “Nitafanya,” mwili wake ni mali ya mwingine aliye mwenzi wa ndoa. Wakati huo mtu
hupoteza haki alizokuwa nazo za kuwa na mamlaka juu ya mwili wake, na kuziweka chini ya mwenzi
wake wa ndoa.
2. Kama ilivyo katika 7:2 na 7:3, mamlaka aliyopewa mume na mke juu ya mwili wa mwenzi wake ni
swala la pamoja, lililo la usawa na la pande zote. Hilo ni la kudumu kwa wote wawili “mwili mmoja”
(Mwz 2:24), na kwa nafsi zao wote “nyenyekeaneni katika kicho cha Kristo” (Efe 5:21).
3. 7:4 haisemi ya kuwa wana ndoa wadai haki zao kwa gharama yoyote, bali kuachilia haki zao ili
kukidhi mahitaji ya kijinsia ya mwenzi wa ndoa. Hii na sheria ya kiroho ya maisha—kujikana
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
63
hutufikisha katika kupata uzima. Njia pekee ya kupata mahitaji yako na wewe kutoshelezwa ni
kutosheleza mahitaji ya mwingine. Katika mchakato wa kujitoa ili kumfurahisha mwenzi wako wa
ndoa, na kumpa yeye starehe ya kipekee kwa kiwango kile cha juu zaidi uwezacho, ndipo unapopata
mahitaji yako na wewe. Hiyo haimaanishi tunakuwa watumwa wa sisi kwa sisi, kila mmoja akidai haki
yake. Bali, uwezo wa kumtosheleza mwenzi wako uko ndani yako, na unapofanya hivyo, na wewe
utatoshelezwa mahitaji yako. Ili uwe na tabia ya jinsi hii inakupasa uwe na upendo ulio komaa yaani wa
mtu mzima. Dhana ya upendo wa kitoto ni kupata, lakini ile ya mtu mzima ni kutoa. Kuna “ndoa za
kitoto” nyingi sana siku hizi ambapo watu wazima huenennda kama watoto. Wanathamini ndoa kwa
sababu tu ya kile wanachokipata kupitia ndoa, lakini hawaioni kuwa ndoa ni chombo cha kuwekeza kwa
Yule umpendaye. Hata hivyo, tofauti kati ya kutoa na kuchukua ndiyo hasa tofauti iliyopo kati ya
upendo na tamaa. Upendo wa Kikristo siku zote hutafuta kutenda yaliyo mema kwa ajili ya umpendaye,
na si tu utoshelevu wako.
4. Kuna wakati ambapo haiwezekani kutimiza haja ya kijinsia ya mwenzi wako. Mwenzi wako
anapokuwa mgonjwa, ana tatizo la mwili, amechoka sana, au anafunga na kuomba, hizo ni sababu
ziwezazo kumzuia asiweze kutimiza haja ya kijinsia ya mwenzi. Hata hivyo, ikiwa utashindwa
kumtimizia mwenzi wako hitaji la kijinsia siku ya Jumatatu kwa sababu jino linauma, siku ya Jumanne
kwa sababu mgongo unauma, siku ya Jumatano kwa sababu kidole cha mguu kinauma, na siku ya
Alhamisi kwa sababu kidole cha mkono kinauma, hapo kuna tatizo tofauti kabisa; ambalo laonekana
kuwa ni la kiroho, ambalo inabidi Mungu alishughulikie.
5. Kuvunjika kwa ndoa nyingi kwaweza moja kwa moja kuhusishwa na chumba cha kulala. Sababu ni
kwamba Yesu si Bwana wa chumba cha kulala. Kuachana hutokea tunapotaka kupata badala ya kutoa.
Tunapaswa kuelewa ya kuwa Mungu ametuumba tukiwa na uwezo wa kukidhi haja za kijinsia za
mwingine. Ndiyo maana kutokuwajibika na hali ya kukosa ashiki katika ndoa husababisha matatizo
makubwa ya kisaikolojia na mgawanyiko hutokea. Mungu ametupa uwezo wa kumpenda na kuvutwa na
mtu mwingine, na furaha ya kufanya hivyo ndicho kiletacho utoshelevu wa kutufikisha kilele katika
tendo la ndoa ndani ya ndoa.
D. Wanandoa hawapaswi kunyimanakatika tendo la ndoa.
“Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani
asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.” (7:5).
1. Vyote “kunyimana”na “kujiana” katika mstari huu huzungumzia mahusiano ya tendo la ndoa. Neno
“kunyima” kwa kweli hasa linamaanisha “kunyang’anya” au “kudanganya.” Wakristo hawana haki ya
kuwanyima wenzi wao hitaji la kufurahia tendo la ndoa hadi kupata utoshelevu. Haki za kijinsia
zinapozuiliwa, Mkristo kwa hakika atakuwa anamnyang’anya mwenzi wake kile ambacho ni haki yake
hasa.
2. Mume na mke wanaweza kukubaliana kutofanya tendo la ndoa kwa muda kwa ajili ya kusudi
maalumu la kiroho—kwa ajili ya kuielekeza mioyo yao kwa Mungu kwa ajili ya maombi. Neno
“kujitoa” lamaanisha “kuwa na pumziko; kuacha kufanya kazi.” Wana ndoa wanaweza kuacha
kujamiiana kwa muda ili kutoa muda kwa ajili ya kufunga na kuomba, bila kuingiliwa. Hata hivyo,
kupumzika kufanya tendo la ndoa kunakubalika endapo tu ni: a. kwa makubaliano ya wote wawili; b.
kwa muda tu; na c. kwa ajili ya kusudi la kiroho.
3. Msitari huu unatoa mwanga kuhusiana na sababu moja kubwa ya migogoro ya mara kwa mara katika
ndoa—mmojawapo anapokataa kumpa mwenzake nafasi ya kuifurahia zawadi ya tendo la ndoa. Ikiwa
mmekubaliana kipindi cha kuwa na pumziko, kipindi hicho kisiwe cha muda mrefu sana shetani
asijepata nafasi, mkajaribiwa, na kutoelewana kukatokea au hata uasherati kufanyika.
4. Mstari huu pia unaonyesha kuwa ni nani ambaye amekuwa sababu ya kuvunjika kwa ndoa nyingi—
Shetani mwenyewe. Shetani yuko ayaharibu maisha ya Wakristo na ndoa zao. Ndio maana tunaagizwa
katika maandiko tuwe macho dhidi ya hila au mikakati ya ibilisi (tazama Efe 6:11). Tambua ya kuwa
shetani hutumia kitendo cha mwana ndoa mmoja kumnyima mwenzi wake kama moja ya mikakati yake
ya kumjaribu mwana ndoa aliyenyimwa kukasirika, kutokuelewana na kuingia katika kukosa uaminifu.
Kwa hiyo, Paulo anatambua ya kuwa si tu kwamba uaminifu katika maswala ya kijinsia una matokeo ya
kiroho, lakini pia hali ya kuwa na maelewano mazuri katika maswala ya kijinsia vivyo hivyo.
10. MALEZI KIBIBLIA
I. Familia ndiyo Taasisi ya Msingi ya Kuadibisha.
Mungu ndiye alianzisha familia katika bustani Adeni. Familia ya kweli ya Kikristo ndiyo jawabu la
tishio ambalo liko katika jamii yetu ya sasa yenye mmomonyoko wa maadili.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
64
II. Vikwazo vya kujenga Familia ya Kibiblia.
A. Kufuata mtazamo wa kidunia/kibinadamu au kushindwa kufuata mtazamo wa Kikristo.
1. Mkristo duniani kote anafundisha ya kuwa tokea mwanzo Mungu aliwaumba watu kuishi kwa
mahusiano.
2. Mungu ndiye aliyeanzishha uhusiano wa ndoa, taasisi ya familia, na majukumu ya kijinsia na
kifamilia.
3. Mitazamo isiyo ya kibiblia hupunga mahusiano haya na majukumu haya.
B. Dhana ya “mahaba.”
1. Kuwa na mapenzi yenye mahaba ni jambo zuri sana.
2. Hata hivyo, endapo mwanamume na mwanamke wataweka mawazo yao katika “mahaba” tu,
mtazamo wa jinsi hiyo waweza kuleta kutokuelewana na kuathiri ule muunganiko.
a. Mtazamo huu ulio potofu kuhusiana na ndoa huyainua maumbile ya mwenzi wa ndoa kama
kigezo cha msingi kwa uhusiano wa ndoa kuendelea kuwepo.
b. Majukumu ya pamoja na wajibu muhimu kwa ndoa kudumu yako nje ya maswala ya mahaba.
c. Kwa hiyo, mapenzi ya mahaba yaishapo, kutengana na talaka hutokea kwa sababu ya:
(1) Ukatili wa kiufahamu;
(2) Tofauti zisizowezekana kutatuliwa;
(3) Hali ya kutopatana; na
(4) Sababu nyinginezo.
3. Burudani inayopendwa na wengi inaendelea kudhihirisha ya kuwa talaka na uasherati ni aina ya
uhuru. Talaka ni jambo la kawaida katika nchi za Magharibi na ni tatizo linaloendelea kuongezeka
duaniani kote.
C. Wazo la “mtu kuwa huru kabisa” (Colson and Pearcey 1999: 322).
1. Wazo hili linasema ya kuwa furaha ya mtu ni jambo lilo muhimu zaidi—jukumu lolote, iwe ni kwa
mwenzi au watoto, yabidi liwe kitu cha pili dhidi ya matamanio yake.
2. Wazo hili la kuwa huru kabisa limesababisha wanaume na wanawake kuichukulia familia ya kuwa si
kitu muhimu.
3. Katika mtazamo wa jinsi hii wa kidunia wanaume na wanawake kwa pamoja hufikiri ya kuwa
jukumu la asili la mahusiano haliwaruhusu kufikia kiwango cha juu cha matumizi kile walicho nacho.
D. Wazo la usawa ndani ya muundo wa familia.
1. Kutokana na Biblia, wanafamilia wote wako sawa kwa asili.
a. Mungu alibainisha jukumu la mume na baba ya kuwa yeye ni kichwa cha familia (Efe 5:22-
23).
b. Mke na mama anapaswa kumtii mumewe (Efe 5:22-23).
c. Majukumu tofauti ya utendaji hayamaanishi kwamba hawako sawa kwa asili.
2. Waume na wake wengine hudai ya kuwa wana uhusiano wa “usawa,” au “nusu kwa nusu,” .
a. Familia inayoendeshwa kwa muundo wa usawa wanafamilia wote kwa kiwango kikubwa
hawana uhakika na majukumu yao na hawafurahii majukumu yao.
(1) Mume hana uhakika kama anapenda kutekeleza wajibu wa uongozi anaopaswa, na
anashinikizwa asitekeleze wajibu wake.
(2) Mke na mama hana uhakika kama anataka kuwa mke na mama, hasa ikiwa hilo
litamaanisha kuwa chini ya mamlaka ya mumewe.
(3) Watoto wanaokuwa katika mazingira ya namna hii hawana vielelezo vya uongozi
ambavyo wangeweza kuiga au kufuata.
b. Muundo wa namna hii una dosari na hauna msimamo kwa sababu haiwezekani familia kuwa
na viongozi wawili—unapotokea mgogoro mmoja atalazimika kushuka.
E. Kuzichukulia nyumba zetu kama “vituo vya mafuta.”
1. Familia zimeundwa ziwe mahali pa kushirikishana na kukidhi mahitaji ya hisia za wana familia.
2. Hata hivyo, watu wengine huchukulia nyumba kama mahali ambapo kila mwana familia huja kula
(inamaanisha, “kujaza”) na kulala, badala ya kuzifikiria nyumba zetu kama mahali ambapo upendo,
mshikamao na mawasiliano hustawisha maisha ya kila mwana familia.
3. Kimsingi, nyumba inapofikiriwa ya kuwa ni mahali tu pa kula, kulala, na kuvaa, kusudi la kibiblia la
kuwa na familia litakuwa halijatimizwa.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
65
III. Aina nne za Msingi za Malezi (Smalley 1984: 49).
A. Wazazi wakali.
1. Wazazi wa kundi hili kwa kawaida wana viwango vya juu na matarajio kwa watoto wao.
a. Ingawa hili laweza kuwa ni jambo jema, wengi wa wazazi hao hawawapi watoto wao msaada
wa kutosha wa kujali.
b. Zaidi ya hayo, kwa kawaida wao hutoa sababu chache kwa nini wanazo hizo sheria kali.
2. Katika familia kadha wa kadha za wazazi wa jinsi hii, matokeo kwa sehemu kubwa yamekuwa ni
watoto ambao wamekuwa na tabia zenye uelekeo hasi—ugumu wa wazazi unaweza kuvunja “moyo/ari”
ya mtoto.
3. Matamko ya kawaida na matendo ya mzazi mkali yaweza kuwa haya:
a. “Si lazima ujue kwa nini, wewe fanya ninachokuagiza.”
b. “Ni mara ngapi nimekwambia usifanye hili. Ingia ndani ama utaipata.”
4. Mambo yanayojitokeza kwa watoto wenye wazazi wakali yaweza kuwa haya:
a. Huwa hawana motisha ya kutoka ndani.
b. Wana hali ya kujikinga, “king’ang’anizi,” na uasi.
c. Huvutiwa na watoto wengine wanaoasi wazazi wao na hata wanaoasi sheria za kawaida za
jamii.
B. Wazazi wasiojali.
1. Wazazi wa jinsi hii huonekana kuwa na hali ya kukosa mapenzi na mamlaka juu ya watoto wao.
2. Huonyesha tabia ya kutojali na ya kutokukomaa.
a. Wakati mwingine, huwalipukia watoto wanapokasirishwa.
b. Wana kawaida ya kujitenga na watoto wao na hatimaye huwanyima watoto wao moja kati ya
vitu muhimu sana katika maisha yao—uwepo wa kukidhi haja za kihisia.
3. Ziko sababu kuu nne zinazosababisha watoto kutelekezwa katika ulimwengu wa siku za leo (Gangel
1972:11):
a. Kiwango kikubwa cha talaka.
b. Kuongezeka kwa kinamama wanaofanya kazi za ajira.
c. Kutazama TV kulikozidi na ongezeko la matumizi ya kompyuta (hili ni halisi zaidi katika
nchi za Magharibi).
d. Kuongezaka kwa jamii ambayo huhamahama.
C. Wazazi wenye kuruhusu.
1. Wazazi wanaoruhusu wana kawaida ya kuwa na mwamko, wenye kutegemeza, lakini dhaifu katika
kuweka sheria na mipaka kwa ajili ya watoto wao.
a. Mazingira ya jinsi hii yanaweza kuruhusu watoto waweze “kufanya watakavyo.”
b. Hata hivyo, watoto kwa sehemu kubwa watajisikia kuwa salama na kupendwa ikiwa wazazi
wana muda wa kuwajulisha mipaka yao na kuwapa maelekezo kuhusiana na tabia njema.
2. Wazazi wanaoruhusu wanaweza kuwa watoaji sana, na wenye kuelewa, na wakutia moyo sana kwa
watoto wao.
a. Wazazi wa jinsi hii hukubaliana na wazo ya kuwa “watoto ni watoto tu.”
b. Wanaruhusu watoto kutoa mawazo yao na hisia zao.
c. Wakati mwingine wanasisitiza kuwa wao ni “rafiki wa kweli” wa watoto wao licha tu ya wao
kuwa wazazi wao
3. Lengo alilonalo mzazi anayeruhusu laweza kuonekana lakupendeza, lakini kwa sababu ya ubinafsi
wa watoto, tabia za kiutashi, na dhambi, watoto wanahitaji kuongozwa:
a. Watoto wanaolelewa katika mazingira ya jinsi hii wanaweza kujenga dhana ya kuwa wao
ndio watawala.
b. Badala ya kuwajengea usalama inaweza kuzalisha hali ya kukosa usalama.
c. Kwa kuwa hakuna viwango vilivyo imara watoto wanaweza kujifuna kuwa, wanaweza
kuchezea wazazi wao na kufanya wapendavyo.
d. Hali ya kuruhusu inapozidi kiwango inaweza kusababisha matendo yasiyofaa.
D. Wazazi wenye upendo na walio imara
1. Wazazi wenye upendo na walio imara hufuata misingi ya Biblia katika kulea.
a. Wazazi wenye upendo na imara huonekana ku wana viwango sawia vya ukali na kuruhusu.
b. Wao siku zote hufuatilia agizo lillilo kuu katika maandiko—kupendana sisi kwa sisi.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
66
2. Wazazi wenye upendo na walio imara kwa kawaida wana sheria zilizo wazi walizoziainisha, mipaka,
na viwango kwa ajili ya watoto wao.
a. Wanatumia muuda kuelimisha watoto wao kuielewa mipaka yao.
b. Wanatoa maonyo yaliyowazi kuhusina na madhara yatokanayo na ukiukaji wa viwango
walivyo weka.
c. Wanapolazimika kuwaadibisha watoto hufanya hivyo kwa upendo.
3. Matokeo ya wazazi wa jinsia hii ni kupata watoto wenye tabia zifuatazo:
a. Watoto watakuwa na tabia ya kujiheshimu.
b. Watoto wataridhika kwa kuwa wamejifunza kujitawala.
c. Watoto hujisikia salma zaidi na mioyo yao imefunguka badala ya kufungwa.
d. Swala la mawasiliano kati yao na wazazi liko wazi.
IV. Maswala ya nidhamu.
A. Kuna tofauti iliyo wazi kati ya kuvunja utashi wa mtoto mkaidi na kumvunja moyo.
1. Kushindwa kutambua tofauti kati ya hivi viwili husababisha “moyo kufungwa” (Smalley 1984: 19).
2. Moja kati ya sababu kubwa za kukosa maafikiano katika nyumba ni moyo uliofungwa.
3. Wazazi wanaokusudia kuvunja “utashi” wa watoto wao hujikuta wamewavunja moyo badala yake.
B. Wazazi wanapaswa kutumia nidhamu kwa usahihi wanapojaribu kukabili utovu wa nidhamu wa
makusudi wa watoto wao.
1. Ni lazima kwa wazazi kuwaadibisha watoto wao, ambapo miongoni mwa hilo ni kuweka mipaka
iliyo wazi nyumbani.
2. Wakati wote tuwaadibishe watoto kwa upendo, si kwa hasira, na tufanye hivyo kwa viwango sahihi
kutegemeana na umri wa watoto, wajibu, na mazingira na aina ya kosa (tazama Mith 19:18; 22:15;
23:13-14; 29:15; Ebr 12:5-11).
C. Mtazamo mpana kuhusiana na nidhamu na kuadibisha.
1. Mamlaka moja inazungumzia nidhamu namna hii: “Katika eneo la kulea watoto, kuadibisha ni
Kumfunza mtoto katika ufahamu na mwenendo ili kumwezesha hatimaye awe mtu anayejitawala, na
anayeweza kuijenga jamii. Jambo hili linahusisha nini? Kuadibisha kunahusisha kutoa mafunzo kwa
kutumia njia zote za mawasiliano. Kuongoza kwa mfano, maelekezo ya mdomo, maombi kwa njia ya
maandishi, kufundisha, kutoa nafasi ya kujifunza na kucheza. Orodha ni ndefu sana.
Ndio, adhabu ni moja ya vipengele vya orodha hii, lakini ni moja tu ya njia nyingi za kuadibisha
na ina mwitikio hasi na ni ya kizamani.” (Campbell 1977: 87)
2. Kuadibisha kunahusiana na upendo. Kama asemavyo Campbell: “Ili uweze kuwa na mtoto mwenye
nidhamu . . . kumfanya mtoto ajisikie kuwa anapendwa ni jambo la kwanza na lililo muhimu katika
kuadibisha kwa usahihi. . . . Kuadibisha nirahisi sana pale mtoto anapojisikia ya kuwa anapendwa
kikweli. Hii ni kwa sababu anataka kujifananisha na wazazi, na anaweza kufanya hivyo pale tu
anapopendwa kikweli na kukubaliwa. Na yeye, ndipo ataweza kukubali uongozi wa wazazi wake bila ya
upinzani au ubishi.
Ikiwa mtoto hajisikii kuwa anapendwa na anakubaliwa kikweli, basi, ana tatizo kubwa mno
kujifananisha na wazazi wake na viwango vyao.” (Ibid., 86-88, mkazo katika asili)
3. Kuhusiana na “fimbo” ambayo imetajwa katika mstari uliopita, wazazi inawapasa kukumbuka kuwa:
“fimbo ya mchungaji aliyotajwa katika maandiko ilitumika kwa sehemu kubwa kwa ajili ya
kuwaongoza kondoo, na si kwa ajili ya kuwapiga. Mchungaji aliwaongoza kondoo kwa upole, na hasa
wanakondoo, kwa kuishika tu fimbo kuwazuia wasiingie eneo lisilofaa na kuwaongoza kwa upole
kuelekea upande unaofaa. Ikiwa fimbo ilikuwa kifaa (au ni) kifaa kinachotumika kwa mudhumuni ya
kupigia tu, ningekuwa na wakati mgumu na Zaburi 23 ‘Gongo lako na fimbo yako, vyanifariji’ (mst. 4,
KJV).” (Ibid.: 93)
D. Katika kuadibisha watoto wazazi hawapaswi:
1. Kuwachokoza watoto hata kuwakasirisha. “Msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu
na maonyo ya Bwana” (Efe 6:4).
2. Kutumia maneno ya kikatili. “Neno lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la
kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wenye kusikia” (Efe 4:29).
3. Kuadibisha kwa vipindi tu. “Yeye asiye tumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye
ampendaya humrudi mapema (ina maanisha,ni tendo linaloendelea) kumtiisha” (Mith 13:24).
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
67
4. Kuwafanya wajisikie kuwa hawahitajiki. “Ili wawatie akili wanawake vijana wawapende waume zao,
na kuwapenda watoto wao” (Tito 2:4).
V. Vifungu vikuu vya Maandiko.
Vifungu vikuu kuhusiana na malezi katika Agano Jipya ni Efe 6:1-4 na Kol 3:20-21.
A. Msimamo wa kibiblia kuhusiana na watoto na malezi.
1. Neno la Mungu linasema wazi ya kuwa watoto ni Baraka kutoka kwa Mungu (Zab 127: 3-5).
2. Alipowaita Waebrania kuwa wateule wake wajibu wao ulikuwa kuitangaza kweli ya Mungu na
kuwarithisha watoto wao (Kum 6:7).
3. Wazazi walitakiwa kusema mambo yanayomhusu Mungu wakati wote, ili maarifa na kumpenda yeye
kuwe ndio mtindo wa maisha ya familia (Kum 6:7-9).
4. Kitabu cha Mithali kimejaa kweli nyingi ambazo zinafaa kuwaongoza watoto wao (tazama Mith 1:8;
13:1; 15:5, 20; 17:25; 19:13; 20:20; 22:6; 23:22, 24).
B. Efe 6:1-4—1“Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. 2 ‘Waheshimu baba
yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, 3 ‘Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.’
4Nanyi, akina baba msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.”
1. Muundo wa Efe 6:1-4.
a. 6:1-3 inafokasi kwenye utii wa watoto.
b. 6:4 inafokasi kwenye wajibu wa wazazi.
2. Uchambuzi wa Efe 6:1-3.
a. “Enyi watoto, watiini wazazi wenu.”
(1) “Watoto” (techna) haimaanishi tu wale watoto wako wadogo bali wote uliowazaa.
(2) Wana na mabinti ambao bado wanawategemea wazazi wao' wanapaswa kuwatii
wazazi wao.
(A) “Tii” (hupakouo) inamaanisha “kusikiliza chini ya.”
(B) “Kutii” inamaanisha watoto wanapaswa kusikiliza kwa makini na watende
sawa sawa na kile kilichoagizwa.
(3) Hivyo, watoto wanapaswa kujiweka chini ya maneno na mamlaka ya wazazi wao.
b. “Katika Bwana.”
(1) Hii inamaanisha kwa kuwatii wazazi watoto wako katika uwanja wa kupendeza
Bwana.
(2) Watoto wanapaswa kuwatii wazazi kama kielelezo cha kumtii Bwana.
(3) Kifungu kinaonekana kuwa kiko wazi kwamba “katika Bwana” inamaanisha
“kuheshimu” na vile vile “kutii.”
(4) Wazazi ni mawakili wa Mungu—kwa kumaanisha, wanasimama katikati ya watoto
na Mungu.
(5) Mahali pekee ambapo watoto hawatapaswa kuwatii wazazi wao ni pale ambapo
wataagizwa kufanya kitu ambacho kinapingana na maandiko.
c. “Hii ndiyo haki.”
(1) Hii ndiyo sababu ya msingi kwa watoto kuwatii wazazi wao.
(2) “Haki hii” haina misingi itokanayo na masomo ya kisaikolojia, mitazamo ya
wanadamu, au nadharia, lakini katika viwango vya Mungu vya haki na matamko yake.
(3) “Haki” (dikaion) inamaanisha kile kilicho sahihi—ina maana, kama inavyopaswa
kuwa.
d. “Waheshimu”baba yako na mama yako.”
(1) Hapa inamaanisha mwenendo wa mtoto katika kuwatii wazazi wake.
(2) Neno “waheshimu” (tima) lina maana “kuthamanisha sana.”
(3) Likiwa katika hali ya kitenzi au nomino neno hilo hutumika mara kwa mara kama
heshima kuu, hali ya thamani kubwa, na heshima.
(4) Mungu alipotoa sheria yake kwa maandishi kwa mara ya kwanza katika mfumo wa
Amri Kumi, sheria ya kwanza ihusuyo mahusiano ya wanadamu ilikuwa “Waheshimu
baba yako na mama yako, siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana
wako” (Kut 20:12).
(A) Hiyo ndiyo sheria ambayo Paulo anairudia katika kufungu hiki.
(B) Ni sheria pekee ambayo inahusika na familia moja kwa moja.
(5) Hii kanuni moja ya utii yanye misingi katika adabu na heshima, utii ukiwepo ni
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
68
rahisi kwa wazazi na watoto kuwa na uhusiano mzuri.
(A) Heshima kwa wazazi inapaswa kufanywa kwa upendo na kujihusisha—
hiyo inaweza kuhusisha kuwategemeza kifedha katika umri wao wa uzeeni.
(B) Inabidi watoto wafundishwe kuwaheshimu na kuwatii wazazi wao—
haiwezi kutokea kwa asili tu kwa watoto waliozaliwa katika dhambi.
e. “Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia,”
(1) Bila shaka, kifungu hiki kinamaanisha kuwa watoto wataishi na kugundua ya kuwa
utii wao ni kwa faida yao.
(2) Kwa kweli, kanuni ya kuwaheshimu wazazi ni ufunguo (mkuu) unaobeba
mahusiano yote ya wanadamu katika jamii.
(A) Mtu anayekuwa akiwa na ufahamu wa kuwaheshimu na kuwatii wazazi
atakuwa amepata msingi wa kuwaheshimu viongozi wengine na kuelewa haki
za watu wengine kwa ujumla.
(B) Huenda hii inafafanua kifungu katika Efe 6:2, “amri hii ndiyo ya kwanza
yenye ahadi.”
3. Uchambuzi wa Efe 6:4.
a. Muundo—Agizo lililo hasi (“Nanyi akina baba, msiachokeze watoto wenu”), likifuatiwa na
agizo lililo chanya (“bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana”).
b. Muundo wa Kihistoria.
(1) Katika jamii ya Kirumi upendo kati ya wanafamilia haukuwa kitu cha kawaida, au
haukuwepo kabisa; haikuwa kawaida kwa wababa kuonyesha upendo.
(2) Kwa sheria za Kirumi patria potestas, baba alikuwa na mamlaka kuhusiana na
uzima na mauti, si tu kwa watumwa wake, bali pia kwa familia yake yote.
(3) Maagizo ya Paulo kwa wababa yalikiuka taratibu za kiutamaduni za wakati ule, kwa
sababu, kinyume na jamii ya Kirumi, Efe 6:4: “ni agizo kwa kina baba kutenda kwa
mtazamo wa kuwapendeza watoto wao. Zaidi ya hayo, heshima na matakwa ya watoto
yaheshimiwe, kwa sababu kuwachokoza kutasababisha wababa kuwakatisha watoto
wao tamaa na kuwafanya kupoteza malengo, wakiwa katika hali ya kutarajiwa wao
kuheshimiwa na kudhalilisha nafasi ya watoto wao iliyo dhaifu [kama ilivyokuwa
ikitendeka kwa kawaida katika jamii ya Kirumi]. Badala ya kuitumia nafasi yao ya
nguvu vibaya, kina baba wnapaswa kuwafundisha watoto wao katika njia ya Bwana,
hapa wazazi wanakumbushwa tena uwakili waliopewa kina baba na kuhusu wajibu
wao kwa Bwana Yesu Kristo.” (Gombis 2005: 328-29)
c. “Kina baba”
(1) Neno “kina baba” (pateres) kwa kawaida linamaanisha wazazi wa kiume, lakini
wakati mwingine humaanisha wazazi wote kwa ujumla.
(2) Ebr 11:23 inaunga mkono wazo hilo kwa sababu neno lile lile linazungumzia
“wazazi kumficha Musa.”
(3) Kwa kuwa Paulo amezungumzia kuhusu wazazi wote katika mistari mitatu iliyopita,
kwa hiyo kina mama vile vile hawapaswi “kuwachokoza watoto wao na
kuwakasirisha.”
d. “Msiwachokoze watoto wenu.”
(1) Hii humaanisha matendo yanayorudiwa, na kuendelea.
(2) matendo ya jinsi hii huzalisha hasira na chuki ambayo huzaa uadui wa wazi wazi.
(3) Vitendo ambavyo huudhi, huvunja moyo, au kuchochea hasira kwa watoto wako ni
pamoja na:
(A) Kuwasonga watoto kwa kuwa mkali kupita kawaida na kutokuwaamini
kabisa.
(B) Kutokuamini maamuzi yao kabisa.
(C) Kuonyesha upendeleo (mfano, Isaka kumpendelea Esau na and Rebeka
kumpenda Yakobo badala ya Esau)
(D) Wakati wote kumlinganisha mtoto mmoja kwa mwingine, na kumsihi
mtoto wako mmoja kwa kumwambia “uwe kama kaka au dada yako.”
(E) Kumwaibisha mtoto, hasa mbele ya watu wengine.
(F) Kutaka viwango vya juu vya maendeleo kuliko vile vya kawaida (yaani,
kulingana na uwezo na utashi wa watoto wao).
(i) Wazazi (hasa wababa) wanaweza kuwa na ndoto za mafanikio yao
kupitia umahiri wa vijana wao katika ujuzi fulani.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
69
(ii) Wazazi (hasa kina mama) wanaweza kuwa na ndoto za kuwa na
kazi ya kuvutia kupitia uzuri au maisha ya binti zao.
(iii) Watoto wengine hujisikia ya kuwa hawawezi kamwe kufikia
viwango vya matarajio ya wazazi wao.
(G) Watoto wanawaza kukata tamaa kwa urahisi endapo wazazi kamwe
hawawasifu, au mara chache, huwasifu, au kuwatia moyo watoto wao.
(H) Watoto wanapojihisi kuwa hawapendwi wanaweza kukasirishwa kwa
urahisi—watoto wanaweza kuhisi kuwa wameingilia mpango wa furaha wa
wazazi wao.
e. “Bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.”
Kuwalea watoto katika adabu na maonyo ya Bwana kunaweza kuhusisha:
(1) Kuishi sawa sawa na neno la Mungu, mtazamo wa Mungu, na njia za Mungu mbele
ya watoto wako wakati wote (Kum 6:6; Mith 22:6).
(A) Kwa ibada za kifamilia na maombi.
(B) kwa kuhakikisha kuwa wanashiriki kanisani.
(C) Kwa kuishi sawa sawa na tunavyosema (kuwa kielelezo cha Kristo).
(D) Kwa kuwafundisha biblia na jinsi biblia inavyoweza kutumika katika
maisha yetu ya kawaida.
(2) Kuwaombea watoto, ikiwa ni pamoja na kuwaombea kwa ajili ya:
(A) Wokovu na baada, ili wawe na imani inayokuwa.
(B) Wawe na nguvu na afya kiufahamu, kimwili, na kiroho.
(C) Wawe na mtazamo wenye kusudi na hamu ya kuwa na ubora
unaompendeza Mungu.
(D) Wawe na hekima, kwa kuwa “Kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima.”
(Zab 111:10)
(E)Walindwe na hatari, magonjwa, na madhara kutoka kwa wengine, na
uharibifu kutoka ndani.
(F) Wawe na nguvu ya kupinga vishawishi vya kidunia, mwili, na shetani.
(G) Mwenzi wao wa ndoa ajaye baadaye.
(H) Kanuni za kimungu zije kufundishwa kwa watoto wao.
(I) Watumie karama walizonazo kuwatumikia wengine ndani na nje ya kanisa
(J) Wamtumikie Mungu kwa uaminifu na furaha siku zote za maisha yao.
C. Kol 3:20-21—20“Nanyi watoto watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika
Bwana. 21Nanyi akina baba, msiwachokeze watoto wenu wasije wakakata tamaa.”
1. Kweli tatu zimetiliwa mkazo hapa katika 3:20:
a. Ni lazima kwa watoto kuwatii wazazi wa wakati wote.
(1) Agizo “watiini” (hypakouete) linaonyesha kuwa utii si uchaguzi.
(2) Kitenzi kipo katika wakati uliopo kuonyesha kuwa utii ni tendo la kila siku.
(3) Mtoto anayetii hujiweka mwenyewe chini ya mamlaka ya wazazi wake.
(4) Mtoto husikiliza maagizo ya wazazi, na hutenda kama alivyoagizwa, bila ya
malalamiko wala uasi.
b. Utii ni lazima uwe kwa wazazi wote.
(1) Hapa tena neno lililo tafsiriwa kuwa “kina baba” wakati mwingine humaanisha
wazazi wote.
(2) Ikiwa baba na mama watatoa maagizo yanayopingana, itakuwa vigumu kwa mtoto
kuyatii maagizo ya Mungu.
c. Utii huwa pia katika “mambo yote.”
(1) Hii ni pamoja na maswala yote ya maisha ya kila siku, iwe ni kazi, michezo, kanisa,
au shughuli nyingineyo ya kijamii.
(2) Kama ilivyosemwa hapa nyuma, lililo nje ya “mambo yote” itakuwa wakati wazazi
wanapoagiza jambo ambalo liko kinyume kabisa na biblia na kusudi la Mungu
lililofunuliwa.
b. “Maana jambo hili lapendeza katika Bwana.”
(1) Wafasiri kadhaa huona kuwa hili linawahusu watu walio katika familia za Kikristo
hasa.
(2) Kwa wengine, lugha hii inamaanisha mwenendo wa Kikristo kwa upande wa
wazazi.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
70
2. 3:21—“Nanyi kina baba ,msiwachokoze watoto wenu wasije wakakata tamaa.”
a. Dhamira ile ile ambayo imetajwa katika Efe 6:4 inarudiwa tena katika Kol 3:21.
b. Onyo linatolewa kwa “kina baba” (wazazi) kama agizo (inamaanisha, ni amri).
c. Wazazi hawapaswi kuwachokoza watoto wao.
VI. Ushauri wa ziada kwa wazazi.
A. “Lugha tano za upendo” zinafanya kazi kwa watoto wako, na kwa mwenzi wako wa ndoa (Chapman 1992:
177-86).12
Wazazi wanapaswa kuzitumia “lugha tano za upendo” kuonyesha upendo wao kwa, kuwathamini, na
kuwakubali, watoto wao. Nazo ni:
1. Maneno ya kuwasifu watoto wao.
2. Kupanga muda wa kuwa na watoto wao.
3. Kuwapa watoto wao zawadi zenye lengo (ambazo si lazima ziwe za gharama kubwa).
4. Kufanya matendo ya kuwahudumia watoto wao.
5. Kuwapa miguso kwa namna inayoashiria upendo.
B. Kuwa na mawasiliano mazuri na watoto wako.
1. Mwandishi mmoja wa mahusiano ya wazazi na watoto alisema yafuuatayo: “Kutazamana ni muhimu
si katika kufanya mgusano wa kimawasiliano mzuri na mtoto, bali pia katika kujaza mahitaji yake ya
kihisia. Bila kujua, tunatumia kutazamana kama njia ya msingi ya kuonyesha upendo, hasa kwa watoto.
Mtoto hutumia kutazamana na wazazi wake (na wengine) kujilisha kihisia. Kadiri wazazi
wanavyotazamana na watoto wao kama njia ya kuonyesha upendo wao, ndivyo kadiri tangi la mtoto
kihisia linavyojazwa. . . . Ni rahisi kwa wazazi kujenga tabia isiyo nzuri ya kutumia kutazamana kwa
lengo la kusisitiza jambo fulani kwa mtoto, hasa katika uelekeo ulio hasi. Tunagundua kuwa mtoto
huwa msikivu zaidi tunapomtazama machoni moja kwa moja. Wazazi wengi hufanya hili wanapotoa
maagizo au wanapokaripia na kushutumu. Hili ni kosa kubwa. . . . Kumbuka ya kuwa kutazamana ni
njia mojawapo kuu ya kumlea mtoto kihisia. Mzazi anapotumia njia ya kumdhibiti mtoto kwa namna
isiyo sawa, mtazamo wa mtoto kuhusu mzazi wake pia unakuwa wa kinyume. Ingawaje hili laweza
kuonekana kuwa na matokeo mazuri mtoto anapokuwa mdogo, hata hivyo utii wake utakuwa ni
matokeo ya hofu. Atakapokuwa akiendelea kukuwa, hasira huchukuwa nafasi ya hofu, chuki, na
mfadhaiko. . . . Namna tunavyoonyesha upendo kwa mtoto tusitawaliwe na kufurahishwa kwetu au
kutofurahishwa kwetu. . . . Tunachopaswa kuelewa katika hatua hii ni kwamba wazazi wanapaswa
kutumia kutazamana kama njia ya kutoa upendo inayoendelea, na si tu kama njia ya kuadibisha.”
(Campbell 1977: 42-44)13
2. Ni muhimu hasa kuwa na uwazi wa mawasiliano watoto wanapokuwa wameingia umri baada ya
miiaka kumi na tatu. Umri wa miaka kumi na tatu na kuendelea ndio wakati ambao inabidi watoto
wajijengee imani “halisi”. Wanakuwa na hali ya “kujaribu mipaka” waliyokulia nayo, na mara nyingi
hufanya chaguzi zisizo sawa kadiri wanavyokuwa na majukumu makubwa juu ya maisha yao na
shughuli zao. Katika miaka hii muhimu, watoto wanapojua ya kuwa bado wanapendwa, na ya kuwa
wazazi bado wapo kwa ajili yao, wataelekea zaidi katika kuirudia imani na tabia njema kuliko pale
ambapo wazazi wao “wanapokuwa na hali ya kutowajali” na wanapokacha kuwa na mawasiliano nao
kwa sababu makosa waliyofanya katika maamuzi yao au matendo ambayo hayakuwapendeza wazazi.
C. Panga muda wa kuwa na watoto wako mara kwa mara.
Nyongeza ndogo ndogo za wakati unazotoa kwa watoto wako mara kwa mara ni za thamani zaidi, na
husaidia kujenga uhusiano na wao, kuliko vipindi virefu cha shughuli ambacho hutokea kwa kuachana muda
mrefu. Kanuni hii ya mara kwa mara inatumika katika maeneo mengi ya maisha. Kukuza na kuendeleza
mahusiano ya kibinafsi, mazoezi ya viungo, kujifunza lugha ya kigeni, kujifunza kupiga chombo cha muziki, au
kujifunza kitu kinginecho kipya, haya yote yanahitaji kujitoa kutumiia muda wako mara kwa mara (hasa, kila
siku) kufanya hilo jukumu. Kutenga muda mrefu kamwe hakuwezi kuchukua nafasi ya vile vipindi vya muda
mfupi vya mara kwa mara na watoto wako, hata kama huo muda mliotumia ni mfupi sana. Ndio maana inabidi
tuutawale muda wetu, badala ya kuachia muda uwe unatawaliwa na “udikteta wa shughuli nyingi” na agenda za
12 Hizi “lugha za upendo” tano zimeelezewa kwa kina katika mfululizo wenye kichwa, “SEMA KWELI KWA UPENDO:
LUGHA TANO ZA UPENDO.”
13 Maelezo ya ziada yahusuyo ujuzi mzuri wa mawasiliano yamejadiliwa kwa kina katika mfululizo wenye kichwa
“MAWASILIANO: KUELEWA; KUSIKILIZA; NA UWEZO WA KUHISI MAONO.”
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
71
watu wengine. Wazazi wote wana shughuli nyingi. Ndio maana ni muhimu kwa wazazi kuhakikisha ya kuwa
wanapanga kuwa na muda na watoto wao mara kwa mara angalau hata kwa vipindi vifupifupi. Kwa kufanya
hivyo unamwonyesha mtoto kuwa, licha ya shughuli nyingi ulizonazo, mtoto ni moja ya vitu unavyovipa
kipaumbele. Mzazi akifanya hivyo, mtoto anajua, uhusiano utakuwa katika msingi imara zaidi, na kwa hakika
una uwezekano mkubwa wa kushinda tufani zijazo mbele zitokanazo na kukua na wakati wa kutengana.
11. UZAZI WA MPANGO
I. “Uzazi wa Mpango” Si Tu Swala la “Kudhibiti Kuzaa” au Kuweka mipaka ya Ukubwa wa Familia,
lakini ni Sehemu ya Majukumu Tuliyopewa na Mungu Kama Mawakili.
A. Mungu ametupa uwakili juu ya vyote tunavyowajibika kwavyo, ni pamoja na familia zetu.
1. Mwz 1:26-28 Inaonyesha mwanzo wa uwakili wa mwanadamu juu ya uumbaji wote. 26Mungu
akasema, “Natufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege
wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” 27Mungu
akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke
aliwaumba. 28Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, “Zaeni, mkaongezeke mkaijaze nchi, na
kutiisha, mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho
juu ya nchi.”
a. Amri ya Mungu kwa Adamu na Hawa mara kwa mara imeitwa “agizo la mamlaka” (kwa
sababu mwanadamu anaagizwa kutawala au kuwa na mamlaka juu uumbaji), au “agizo la
kitamaduni” (kwa sababu mwanadamu anatakiwa kuijaza nchi na kuitiisha).
b. Uwakili juu ya uumbaji ambao Mungu aliwapa wanadamu ulitolowa kwa wanaume na
wanawake sawa sawa (Mwz 1:28).
c. “Kuijaza nchi” na ukweli kuwa agizo la uwakili lilitolewa kwa wote wanaume na wanawake
hutupa nguvu ya kukuza uhusiano katika uwakili wetu. Kwa maneno mengine, sisi si mawakili
juu ya “vitu” vya duniani tu, bali pia tu mawakili juu ya watu tunaohusiana nao na uhusiano
wetu na hao watu.
2. Kama mawakili wa Mungu, tutatoa hesabu mbale za Mungu ya jinsi tulivyotumia uwakili wetu
(tazama Math 25:14-46; Luka 12:35-48; 16:1-13; Ebr 9:27-28; 2 Pet 3:7; Ufu 20:11-15).
B. Kipengele muhimu cha uwakili wetu ni kupanga na kutenda kikamilifu na kwa kuwajibika katika maeneo
yote ya maisha yetu, ikiwa ni pamoja na familia zetu.
1. Kwa hakika imekwisha kusemwa ya kuwa “mtu anayeshindwa kupanga, anapanga kushindwa.” Watu
wengi hawana mipango ya kuwaongoza. Watu wote wana kiwango cha muda kinacholingana kwa siku.
Hata hivyo, tusipoitawala siku, siku itatutawala. Tusipotawala pesa zetu, pesa zetu zitatutawala.
Tusipopanga muda wetu na matukio tutakuwa chini ya rehema za watu wengine na matukio. Watu
waliofanikiwa (wale waliofanikiwa katika kila eneo la maisha, ikiwa ni pamoja na eneo la biashara, na
waliofanikiwa kiroho, kimahusiano na kimwili) wana mipango, kisha huweka malengo, kisha kwa
makusudi hutekeleza sawa sawa na walivyopanga. Tunapofanya hivyo tunagundua kuwa inatuwezesha.
Tunapochukuwa wajibu mkubwa juu ya maisha yetu tunagundua kuwa kila nyanja ya maisha yetu
inapiga hatua.
2. Tukifanikiwa kupanga katika maeneo yote ya maisha yetu, lakini tukashindwa kuwa na mipango kwa
ajili ya familia zetu ni kutokuwajibika na kutokuwa mawakili wazuri. Tunapanga shughuli zetu zote za
kila siku. Tunaweka mipango kuhusiana na kazi zetu, maandalizi ya chakula, na kila shughuli
nyinginezo. Tukishindwa kuweka mipango kuhusiana na familia zetu—ambao ni kiungo muhimu cha
mahusiano kuliko vyote tunavyoweza kuwa navyo—ikiwa ni pamoja na mipango kuhusiana na ukubwa
wa familia zetu, huko ni kutokuwajibika kwa hali ya juu na kamwe hakuwezi kukubalika kwa mazingira
yoyote yale.
3. Asili ya “uzazi wa mpoango.”
a. “Uzazi wa mpango”ni sehemu ya wajibu wetu mkuu kama mawakili, na inahusiana hasa na
uwakili wa uchumi. “Kupanga uzazi” kunahusiana na ubora wa maisha yetu, wenzi wetu, na
watoto tunaokusudia kuwazaa. Kupanga uzazi kunahusiana na kupanga familia yako na
kupanga kwa ajili ya familia. Kupanga ni kufikiri kabla na kuweka amana kwa ajili ya familia
yako. Kupanga ni nyanja ya “kusimamia nyumba[yako]vema” (1 Tim 3:4). Lazima tukumbuke
ya kuwa tunawajibika, kisheria na mbele za Mungu, kwa ajili ya kila mtoto tunayemzaa.
b. Kila kitu kina matokeo na madhara. Kula kupita kiasi, kunywa kupita kiasi, kufanya
chochote kupita kawaida, kuna matokeo yenye madhara. Sote tunatambua hilo, na tunapanga
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
72
ipasavyo. Ndivyo ilivyo kuhusiana na kuzaa watoto wengi—ina maana, watoto ambao hatuwezi
kuwalea sawa sawa, kuwatunza, kuwasomesha, na kuwaandaa kwa wakati wao ujao wa utu
uzima wenye maisha mazuri yenye heshima na ya kuwajibika. Hivyo tunapaswa kulizingatia
hilo, na kupanga ipasavyo.
4. Tunapopanga kuhusiana na familia zetu—ikiwa ni pamoja na ukubwa wa familia zetu—ni lazima
tuzingatia mambo kadhaa. Mambo haya ni pamoja na:
a. hali ya nchi yetu kiuchumi na kisiasa. Amani, ustawi, vyanzo, na fursa zilizopo nchini na
mahali unapoisha huathiri matarajio yako na ya familia yako. Zaidi ya hayo, ukubwa wa familia
huathiri mafanikio, vyanzo vya mapato, na fursa za wengine katika jamii kwa ujumla. Kwa
mfano, kwa wastani mwanamke wa Kiganda ana watoto 6.9 (Disemba 2000). “Tarakimu hizi
zina nyongeza iliyo kubwa kuliko ile ya kipato cha taifa kwa mwaka . . . kikiongeza miezi zaidi
ya uzalishaji kuliko uwezo wa vyanzo” (The Daily Monitor, Feb. 16, 2002). Kuwa na familia
kubwa katika mazingira ya namna hii yaweza kuwa ni tendo la ubinafsi, ambalo litachangia
katika kudhoofisha jamii, umasikini na matatizo mengine.
b. Uwezo wetu wa kumiliki ardhi, na ukubwa wa nyumba zetu. Kama huna uwezo wa kumiliki
nyumba yenye uwezo wa kukidhi hitaji la idadi fulani ya watoto, basi hupaswi kuzaa idadi hiyo
ya watoto na ukizaa idadi hiyo hutakuwa umewajibika vema.
c. Uwezo wetu wa kuwatunza watoto wetu vema, ikiwa ni pamoja na kuwapatia matibabu na
chakula bora, kulipia elemu yao, na kuwapatia mahitaji yao ya kiroho na mengineyo. Hakikisha
ya kuwa unaweza kuwahudumia watoto wako ulionao sasa kikamilifu, na unao uwezo wa
kuhudumia watakaozaliwa, kabla hujaamua kuwazaa.
(1) Unapokuwa umezaa watoto na ukashindwa kulipia gharama ya kuwasomesha
angalau kufikia elimu ya sekondari inamaanisha tayari umeshapitisha uamuzi kwa ajili
yao kufanya kazi zisizofaa, umasikini, afya mbaya na kuwasababishia maisha yenye
mipaka mikubwa sana ya fursa.
(2) Unapozaa watoto halafu ukashindwa kuwapatia chandarua za kuzuia mbu au
mahitaji yao mengine ya msingi ni kuwaamulia maisha ya mateso.
(3) Unapozaa watoto halafu ukashindwa kukidhi mahitaji yao ya kifedha ni dhambi
kubwa. Kwa kweli, Paulo anasema kuwa “Lakini mtu yeyote asiyewatunza wa walio
wake, yaani wale wa nyumbani mwake hasa, amaikana Imani, tena ni mbaya kuliko
asiyeamini” (1 Tim 5:8).
(4) Unapozaa watoto halafu ukashindwa kuwa na muda nao ni kuwanyima hitaji lao
muhimu kwa ajili ya kuwaendeleza kiroho, kiakili, na kimahusiano, kitu ambacho
Mungu atakudai.
d. Umri na afya ya mke. Je kuzaa watoto zaidi kutahatarisha maisha yake?
e. Umri na afya ya mume. Wanaume wengi huendelea kuzaa hata wanapokuwa wazee wakati
ambapo kamwe hawataweza kuwa na mahusiano halisi na watoto, au wakati hawawezi tena
kufanya kazi ili kuwategemeza watoto. Wanaume wa jinsi hiyo huweza kufa wakati watoto
wangali wadogo. Kuzaa watoto katika mazingira ya jinsi hii ni ubinafsi. Na pia huwafunga mke
na watoto katika maisha yenye mazingira ya mateso na umasikini.
f. Hatari iliyowazi kwa watoto. Je kuna uwezekano wa ugonjwa wa kurithi kuambukizwa kwa
watoto?
II. Mtazamo wa Kikristo katika kupanga uzazi.
A. Kupanga uzazi kumekubalika na kutekelezwa na wengi, na serikali nyingi zimekuwa zikitetea jambo hili.
1. Dunia inatumia vibaya matumizi ya mpango wa uzazi na inawatia moyo uzinifu.
2. Kanisa lazima lisimame kusema dhidi ya hali hiyo au kizazi hiki kitapotelea katika uzinzi bila msaada
wowote.
B. Hakuna kifungu bayana katika maandiko kinachopinga au kuzungumzia uzazi wa mpango.
1. Biblia iko kimya kuhusu swala la uzazi wa mpango.
2. Maandiko yasiposema wazi kuhusu jambo fulani na yanaposema kuhusu kuunga mkono jambo fulani
wazi, hitimisho lazima lifanywe kwa kuzingatia kanuni za kibiblia zitokanazo na mtazamo wa maandiko
katokana na asili ya mwanadamu, ndoa, na kujamiiana.
3. Kwa sababu Biblia haisemi chochote kuhusu uzazi wa mpango, basi swala hili kimsingi haliwi la
ukiukaji wa maadili.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
73
C. Vifungu fulani vya maandiko na kanuni vina uhusiano fulani na swala la uzazi wa mpango; vinaonyesha
kuwa Biblia haimzuii Mkristo kutumia vidonge vya kupanga uzazi.
1. Agizo lisemalo “Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi” (Mwz 1:28).
a. Si katika mstari huu wala kwingineko kote katika Biblia tunaagizwa kuwa na “watoto wengi
kadiri tuwezavyo.” Mstari huu kamwe haubainishi ni kwa kiwango gani kizazi cha wanadamu
kiongezeke; hakikatazi mpango wa familia wala kupanga uzazi.
b. Amri hii ilipotolewa kwa Adamu na Hawa, hakuwepo mwanadamu mwingine yeyote duniani.
(1) Katika amri hii Mungu hakusema, “ijazeni nchi na watu kadiri mwezavyo.” Zaidi ya
hayo, amri hii ilipotolewa, Adamu na Hawa walikuwa na eneo kubwa litoshalo
(inamaanisha, dunia yote), pamoja na rasilimali zote, ambamo wengeweza kulelea
watoto wengi.
(2) Sasa, hata hivyo, amri imetimizwa. Kadiri ya watu bilioni sita wanaishi duniani.
Watu wametawanyika kila mahali katika tufe la dunia.
(3) Zaidi ya hayo, watu wengi huishi kwa wingi mno katika maeneo fulani, umasikini,
uhaba wa rasilimali, na ukosefu wa fursa jambo ambalo ni tofauti na hali ilivyokuwa
wakati wa Adamu na Hawa. Watu wengi huishi katika vijumba vya msonge au vyumba
vya kupangisha, na hawana uwezo wa kuwalea watoto wengi. Si tafsiri sahihi kibiblia
kuichukua amri waliyopewa Adamu na Hawa na kuichukulia kana kwamba mmepewa
ninyi wanandoa “amri ya binafsi” leo muwe na familia kubwa.
c. Biblia inaonyesha kuwa watu tofauti katika biblia walikuwa na familia zenye ukubwa tofauti.
Wale waliokuwa na familia kubwa hawakusifiwa kwa kuwa “wa kibiblia zaidi”au “waaminifu
zaidi”kuliko wale waliokuwana na familia ndogo. Baadhi ya mifano ya familia za ukubwa
tofauti katika biblia ni pamoja na:
(1) Biblia haisemi idadi ya watoto ambao walizaliwa kwa watu wengi (mfano, mitume
wote walikuwa na ndoa, lakini biblia haisemi kwamba walikuwa na watoto—1 Kor
9:5).
(2) Baadhi ya watu katika biblia walikuwa na familia kubwa (mfano, Ishumaeli—wana
12, Mwz 25:12-16; Yakobo—wana 12 na binti mmoja, Mwz 29:31-30:24; 35:16-18).
(3) Baadhi ya watu katika biblia walikuwa na familia ndogo (mfano, Yusufu—wana 2,
Mwz 41:50; Nuhu—wana 3, Mwz 5:32; Lutu—mabinti 2, Mwz 19:30).
2. Amri ya ku“tiisha nchi” (Mwz 1:28).
a. Wanadamu walipewa mamlaka juu ya uumbaji, ikiwa ni pamoja na kutumia kwa uhuru
uwezo waliopewa na Mungu kwa utukufu wa Mungu na kwa mafanikio ya mwanadamu
mwenyewe.
b. Hakuna mahali popote katika mwendo wa maisha ambapo Mungu ameamuru ya kuwa watu
wawe “watumwa wa uumbaji” (yaani, hawaruhusiwi kutumia njia za kisayansi au teknolojia
kutawala na “kutiishi”uumbaji). Mifano ya jinsi mwanadamu anavyotiisha “kinyume cha asili”
ni pamoja na vifuatavyo:
(A) Madaktari hutumia dawa ya kuondoa maumivu katika upasuaji;
(B) Wakulima wafugaji hutoa pembe na kuhasi ng’ombe;
(C) Wakulima wa zabibu hupunguza matawi yasiyofaa;
(D) Wamiliki wa nyumba hukata majani;
(E) Wanaume na wanawake hukata nywele zao na kunyoa ndevu.
(F) Maziwa huondolewa vijidudu kitaalamu; madawa kutengenezwa; mbegu za mimea
na wanyama kuchanganywa na kuendelezwa; sabuni zinatengenezwa; madini
yanachimbwa na kubadilishwa kuwa vitu vingine tofauti, yote hayo ni kwa faida ya
mwanadamu, afya, na manufaa.
c. Hakuna msingi wowote sasa kusema kuwa vidonge vya kuzui uzazi au njia nyingine za
kiteknolojia si sawa kwa sababu “zinaingilia mambo ya asili” kwani kusema hivyo ni sawa na
kusema kuwa kila afanyacho mwanadamu kwa kutumia teknolojia au sayansi ni kosa. Kwa
kweli, ikiwa ni kosa kimaadili kuzuia, vivyo hivyo itakuwa ni kosa kurefusha uhia wa mtu kwa
kumfanyia upasuaji, mahospitalini au madawa yanayopingana na sheria za asili.
3. Swala la Onani ambaye“alimwagia mbegu chini” (Mwz 38:8-10).
a. Mazingira ya kifungu yako katika sheria ya kale ya Waisraeli ya “ndoa ya kurithi mjane”
(Kum 25:5-10). Sheria ilimtaka mwanamume kumwoa mke wa kaka yake ikiwa kaka yake
alikufa bila ya mtoto. Mtoto wa kwanza wa kiume anayezaliwa katika ndoa ya kurithi mjane
alitambuliwa kama mtoto wa yule baba aliyekufa ili kutunza “mshikamano” wa ukoo na kwa
kusudi la urithi wa mali.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
74
b. Swala la Onani, kaka yake Eri alikufa bila kuzaa mtoto. Eri alikuwa mtoto wa kwanza wa
kiume wa Yuda, hivyo angepata (“urithi marambili ya wengine katika mali za baba yake sawa
na sheria”) 14 Onani akapanga ujanja: aliupuuzia wajibu waki wa kisheria, na akajamiiana na
mjane wa Eri Tamari. Hata hivyo, alihakikisha kuwa hamtungishi mimba. Kwa kufanya hivyo
(inamaanisha, alitekeleza wajibu wake wa kisheria kwa hali ya nje lakini si kiukweli) alitumaini
ya kuwa yeye atapata urithi wa kaka yake marehemu na wa kwake pia. Kwa hiyo Onani
alikuwa na uchu wa mali.
c. Mungu alimhukumu Onani kwa ajili ya uchu wake wa mali na kwa kushindwa kuitii sheria ya
agano ya urithi wa ndoa, na si kwa kuzuia mimba. Kifungu hiki hakihusiani kamwe na maswala
ya kuzuia mimba.
4. Usemi usemao kuwa Mungu anachukia “mikono imwagayo damu isiyo na hati” (Mith 6:16-17).
Kuna tofauti kubwa kimaadili kati ya kuzuia mimba na kutoa mimba:
a. Kuzuia mimba “hakumwigi damu isiyo na hatia.” Kuzuia mimba huzuia kuaza uhai kwa
kiumbe kipya. Hakuuwi uhai ambao tayari upo.
b. Kutoa mimba “kunamwaga damu isiyo na hatia.” Kutoa mimba kunauwa maisha ya mtu
ambaye alikuwa hai. Vivyo hivyo, kutoa mimba ni uovu kimaadili ambao biblia hairuhusu.
Kuzuia mimba si uovu wa kimaadili kama kutoa mimba.
5. Hitaji la mtu kulazimika ku“tunza walio wake hasa wale wa nyunbani mwake” (1 Tim 5:8).
a. Wanafamilia wana wajibu wa kuhudumiana kimwili, kimahitaji ya vitu na kifedha. Watoto
wanapolelewa, wajibu wa msingi wa matunzo yao ni wa wazazi. Matunzo hayo ya watoto wao
ni pamoja na kuwapatia mahitaji ya kimwili, vitu na ya fedha. Wajibu huu ni muhimu sana kiasi
kwamba kushinda kufanya hivyo sawa sawa humaanisha kuwa mzazi “ameikana Imani tena ni
mbaya kuliko asiyeamini.”
b. Hata ingekuwaje, na hasa tukizingatia tofauti iliyo kubwa mno kati ya mazingiza waliyo nayo
kizazi cha leo na yale waliyo kuwa nayo Adamu na Hawa, kimantiki 1 Tim 5:8 “inapiku”au
inaongoza Mwz 1:28, na si kinyume. Ikiwa wana ndoa wana eneo, rasilimali, na uwezo wa
kuhudumia familia kubwa vizuri, bila shaka wanaruhusiwa kuwa na familia kubwa. Vivyo
hivyo, endapo hawana eneo, rasilimali, na uwezo wa kuhudumia familia kubwa vizuri, basi,
wasiwe na familia kubwa.
6. Kusudi la ndoa.
a. Kuzaa si sababu pekee ya kuwa na ndoa au kufanya tendo la ndoa. Vivyo hivyo, amri katika
Mwz 1:28 “Zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi” haitawali, au “kupiku,” au haichukui nafasi ya
Biblia yote kuhusiana na swala la ndoa na kuzaa watoto (tazama maelezo yaliyotangulia nyuma
kuhusiana na Mwz 1:28).
b. Makusudi mengine ya ndoa ni pamoja na hitaji la kuwa na mwenzi (Mwz 2:18), umoja
(Mwz 2:24), kustarehe (Mwz 3:16; Mhu 9:9; 1 Kor 7:3-5), kujilinda na uzinzi (1 Kor 7:9),
utakaso wa binafsi au utakaso unaoendelea (Efe 5:26).
(1) Adamu na Hawa walikuwa na kuhitajiana, umoja, na walistarehe kwa kujamiiana
kabla hata watoto hawajazaliwa.
(2) Mtume Paulo aliwatia moyo Wakristo kuwa mahusiano mazuri katika tendo la ndoa
kwa sababu wana ndoa wana wajibu huo wa kijinsia kila mmoja kwa mwenzake, na
hawashauriwi kutengana kwa muda mrefu (I Kor 7:1-5). Twaweza kuhitimisha kwa
kusema kuwa Paulo anathibitisha kuwa tendo la ndoa linahitajika kwa ajili ya starehe
na utoshelevu kwa kila mwana ndoa. Ikiwa hilo ni kweli, kuzuia kuzaa kwaweza
kutumika kama njia mojawapo ya kujenga ndoa yenye mapenzi moto moto
(3) Kwa kuwa sterehe, umoja na hitaji la kuwa na mwenzi ni makusudi ya msingi ya
kuwa na ndoa, uzuiaji wa mimba unaweza kusaidia kufanikisha malengo haya. Kuzuia
mimba kunaweza kusaidi kuongeza uhuru wa kufanya mapenzi na kuimarisha ndoa.
Inaweza kuhifadhi ndoa kwa kusaidia asipatikane mtoto kabla ya wakati na kuepuka
mikasa ya kiuchumi.
III. Aina ya njia za Kupanga uzazi.
A. Mambo muhimu ya kuzingatia.
1. Uzuiaji wa mimba kisayansi lazima uwe:
a. Hauna madhara. Hapapaswi kuwepo madhara kwa mke, mume, au watoto watakaozaliwa.
14Mtu aliyemwoa mjane asiye na watoto aliitwa levir—hivyo neno “huunganisha” ndoa.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
75
b. Ulinzi. Uzuiji wa mimba lazima uwe na kiwango cha juu cha ulinzi au utasababisha mashaka
makubwa kwa sababa ya hofu ya kuweza kupata mimba isiyotarajiwa.
c. Rahisi kuitumia. Njia au nyenzo ya kupanga uzazi inapaswa kuwa bora na ya kuridhisha kwa
wana ndoa wote, rahisi kutumia na yenye gharama inayonunulika.
2. Lengo la somo hili si kujadili sifa na kasoro za kila njia, lakini ni kushughulika na uhalali wa kuzuia
mimba kiroho na kimaadili.
3. Ikiwa unapenda kujua kwa kina matumizi ya njia za kuzuia mimba za kisasa, basi unapaswa
kuzungumza na mchungaji wako na/au daktari. Sifa na kasoro za njia tofauti za kupanga uzazi ni
maswala yanayopaswa kukabiliwa na madaktari na wauguzi waliosomea. Taasisi fulani za kiserikali
vile vile zinaweza kuwa na taarifa kuhusiana na njia mbali mbali za uzazi wa mpango.
B. Aina tofauti za kuzuia mimba zisizohusisha kuuwa kiumbe ambacho hakijazaliwa.
Kuna njia nyingi za kuzuia mimba, ikiwa ni pamoja na zilizotajwa hapo chini ingawaje si zote. Baadhi
ya hizo huhitaji kutumia chombo au utaratibu fulani; nyingine hazihitaji. Njia zifuatazo hazihusishi kuharibu yai
lililorutubishwa, kama zifanyavyo njia za “uzuiaji mimba wa dharura,” “vidonge vya asubuhi baada ya tendo,”
na utoaji wa mimba. Zaidi ya hayo, haionyeshi kuwa matumizi yake yamekatazwa kibiblia, ikiwa kusudi la
wana ndoa na mazingira mengine ya maisha ya wana ndoa yanaendana na kanuni za kiblia.15
1. Kutengana. Kutengana katika tendo la kujamiiana huzuia mimba lakini pia kutasabisha wanandoa
wote wawili kukosa furaha. Kunapoteza lengo la kuendeleza mapenzi kimwili ndani ya ndoa.
Kutengana ni swala la kimaadili kwa sababu ni kushindwa kutimiza wajibu wako wa kukidhi hitaji la
kijinsia la mwenzi wa ndoa. Ingawaje kutengana kwa muda mfupi kunaruhusiwa kwa makubaliano ya
pamoja kwa ajili ya maombi, kutengana kabisa hakuruhusiwi na Biblia (1 Kor 7:3-5). Wake wengi wa
Kiafrika huamua kujitenga kwa sababu ya kuogopa mimba isiyotarajiwa. Katika mazingira kama hayo
wanaume hutafuta wa kujamiiana naye nje ya ndoa jambo ambalo ni dhambi iliyo wazi.
2. Kutoa uume (coitus interruptus). Mwanamume anapohisi yu karibu kumwaga shahawa (kufika
kileleni), hutoa uume kutoka mwenye uke. Hivyo humwaga shahawa nje ya uke. Tendo hili linahitaji
nidhamu ya hali ya juu! Ikiwa mwanamke hajafika kileleni, mwanamume anaweza kuendelea
kumsisimua kwa njia nyingine baada ya kutoa uume. Njia hii inafanyakazi vizuri endapo wana ndoa
wote wawili wamekubaliana mapema kuitumia. Miongoni mwa wana ndoa wanaoanza kutumia njia hii
ya kutoa uume, kiasi cha asilimia 27 cha wanawake watapata mimba zisizotarajiwa katika mwaka wa
kwanza. Endapo njia hii itatumiwa vizuri na kwa makini, kiasi cha aslimia 4 ya wanawake watapata
mimba.
3. Njia ya kuhesabu siku (kuhesabu siku). Njia ya kuhesabu siku ni namna ya kuelewa mzunguko wa
yai la mwanamke kwa njia ya kuchunguza na kuandika na dalili za rutuba. Dalili hizi huashiria endapo
anaweza kupata au kutokupata mimba katika siku fulani. Kwa kawaida mwananmke anakuwa katika
kipindi cha rutuba (kuweza kushika mimba) katika robo ya siku za mzunguko wake. Njia hii humpa
mwanamke nafasi kubwa ya kujifunza mengi kuhusiana na mwili wake, lakini vijana wa umri wa
kubalehe hadi miaka 19 wanashauriwa kutotumia njia hii. Je ni zipi ishara tatu za msingi za rutuba? Ni
jotoridi la mwanamke mara tu aamkapo; ute utokao kwenye mlango wa kizazi(ute ulioko mdomoni
mwa tumbo la uzazi); na mkao wa mlango wa kizazi. Uelewa kuhusu majira yaliyo na uwezekano wa
yeye kupata mimba unamsaidia mwanamke kujiepusha kufanya tendo la ndoa nyakati ambazo anaweza
kupata mimba. Kiwango cha kushindwa miongoni mwa wanawake wanaotumia njia hii kwa usahihi ni
asilimia mbili mpaka tatu; wakati kiwango cha kushindwa miongoni mwa wanawake wanaotumia njia
hii ni asilimia 13 mpaka 20.
4. Kondomu (za wanaume). Kondomu zenye matokeo mazuri ni zile zilizotenganezwa kwa ulimbo wa
mpira. Kondomu inapofunguliwa inafanana na futuza ndefu, nyembamba. Zinazuia majimaji ya mwili
yasikutane wakati watu wawili wanapojamiiana. Kondomu huvalishwa kwenye uume kabla uume
haujakutana na uke, mdomo au mkundu. Miongoni mwa wanandoa watumiao kondomu za kiume, kiasi
cha asilimia 15 ya wanawake wanaweza kupata mimba zisizotarajiwa katika mwaka wa kwanza
Kondomu zinapotumika viruri na kwa kuendelea, kiasi cha asilimia mbili ya wanawake watapata
mimba. Kondomu hufanyakazi kwa mafanikio zaidi zikitumiwa pamoja na njia nyingine, kama vidonge
au povu.
5. Kondomu za wanawake. Kondomu za kike (hapo nyuma zilijulikana kama Kondomu za Uhalisia)
zimengenezwa kwa plastiki nyembamba inayoitwa polyurethane. Hii si ulimbo wa mpira. Kondomu hii
15Maelezo kuhusu njia 2-11 katika sehemu hii inatoka katika makala “Njia za Kuzuia Mimba:Zipi ni chaguo lako?”
inayopatikana kwenye tovuti http://www.advocatesforyouth.org/youth/health/contraceptives/index.htm (iliyopimwa 27
Oktoba 2008).
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
76
ina valishwa katika uke wa mwanamke. Imefunguka upande mmoja na kufungwa upande mwingine.
Katika kingo zake kuna kishikizo kinachozuia kondomu istoke kwenye uke. Miongoni mwa wanawake
wanaotumia kondomu hizi za kike, asilimia 21 wanaweza kupata mimba zisizotarajiwa katika mwaka
wa kwanza. Kama kondomu hizi zikitumuka vizuri na kwa makini kwa kuendele, asilimia 5 ya
wanawake wanaweza kupata mimba.
6. Kiwambo (kwa wanawake) na povu la kuweka ukeni. Kiwambo ni chombo cha mpira cha duara
kinachoingizwa ukeni. Kinapaswa kuachwa ukeni kiasi cha masaa 6 na si zaidi ya masaa 24 baada ya
kujamiiana. Kiwambo huzuia shahawa zisiingie kwenye mlango wa kizazi (mlango wa tumbo la uzazi).
Dawa iliyowekwa juu ya kiwambo huuwa shahawa. Kiwambo pamoja na dawa kuzuia shahawa
zisikutane na yai. Miongoni mwa wanandoa wanaoanza kutumia njia ya kiwambo, kiasi cha asilimia 16
ya wanawake wanaweza kupata mimba zisizotarajiwa katika mwaka wao wa kwanza. Endapo kiwambo
kitatumika kwa makini kwa kuendelea, kiasi cha asilimia 6 ya wanawake wanaweza kupata mimba.
7. Kiraka. Kiraka cha kuzuia mimba ni chepesi, chembamba, kinachovutika chenye rangi ya mchanga.
Kina tabaka tatu: la nje, lenye kulinda, tabaka ya polyesta; tabaka yenye dawa na gundi; na karatasi
nyembamba ambayo kuezuliwa kabla ya matumizi ya Kiraka. Kiraka chaweza kuwekwa katika ngozi ya
matako, sehemu ya tumbo, na ya juu ya kiwiliwili (lakini si katika matiti), au nje ya mkono kwa juu.
Kila kiraka chaweza kudumu kwa siku saba. Wanawake hubadilisha kiraka kila wiki kwa muda wa wiki
tatu, kasha wanakuwa na wiki moja ya kutokuwa na kiraka, wakati ambapo anaanzasiku za hedhi.
Katika mwaka wa matumizi ya kawaida, wanawake nane wanaweza kupata mimba, kikitumiwa kwa
makini, ni wanawake watatu tu kati wa 1,000 wanaweza kupata mimba.
8. Vipandikizi (vijiti). Vipandikizi vya kuzuia mimba huwekwa mara moja sehemu ya juu ya mkono.
Baada ya mwanamke kuchomwa dawa ya kuzuia maumivu tendo la kuwekewa vipandikizi (Vijiti)
huchukua dakika chache. Kwa kawaida haina maumivu. Vijiti hutoa kiasi kidogo cha homoni kama ile
ya progesteroni atoayo mwanamke katika kipindi cha wiki mbili za mwisho za mzunguko wake wa
mwezi. Miongoni mwa wana ndoa waanzao kutumia njia hii, wanawake watano kati ya 1,000
wanaweza kupata mimba zisizotarajiwa katika mwaka wa kwanza.
9. Sindano. Sindano huzuia ovari za wanawake kutoa yai na zina madhara mengineyo katika kuzuia
mimba. Dawa itumikayo mara nyingi huitwa Depo-Provera. Ni dawa idungwayo kila baada ya miezi
mitatu. Ni homoni, ifananayo na progesteroni atoayo mwanamke katika kipindi cha wiki mbili za
mwisho za mzunguko wake wa mwezi. Miongoni mwa watumiaji wa kawaida wanaoanza kutumia
sindano, kiasi cha asilimia tatu ya wanawake wanaweza kupata mimba zisizotarajiwa katika mwa ka wa
kwanza.
10. Vifaa vinavyowekwa kwenye nyumba ya uzazi (IUD). Hiki ni kifaa kidogo kinachowekwa kwenye
nyumba ya uzazi. Kuna aina mbili kuu za vifaa hivyo ambazo zimekuwa na mafanikio makubwa huko
Marekani: kile cha madini ya Shaba nyekundu na LNG-IUS. Katika mikono mlalo ya shaba nyekundu
T 380A IUD kuna madini ya shaba nyekundu. IUD huachilia madini ya shaba katika nyumba ya uzazi
kidogo kidogo. Hili hufanya mabo kadhaa. Muhimu zaidi, inazuia mbegu za mwanamume kwenda
kwenye mji wa mimba. Miongoni mwa wana ndoa wa kawaida wanaoanza kutumia njia hii ya IUD, ni
kama chini ya 1% wanaweza kupata tukio la mimba isiyotarajiwa katika mwaka wa kwanza. Kifaa cha
LNG-IUS kina levonorgestrel katika mkono wa wima. Homoni hii ni projestini ambayo ni kama ile
projesteroni itolewayo ovari za mwanamke kila mwezi katika siku zake za hedhi. Kila wiki LNG-IUS
hutoa kiwango sawa cha levonorgestrel kama apatacho mwanamke anapokula vidonge vidogo viwili
viitwavyo Ovrette. Levonorgestrel husababisha ute mzito katika mlango wa kizazi hivyo huzuia mbegu
za kiume kulifikia yai. Miongoni mwa wana ndoa wa kawaida wanaotumia njia hii ya LNG-IUS, ni
mmoja kati ya wanawake 1,000 anaweza kupata mimba isiyotarajiwa katika mwaka wa kwanza.
11. Vidonge vya kuzui mimba. Ndani ya vidonge vya uzazi kuna homoni aina mbili,estrojeni na
projestini. Hufanya kazi kwa kuzuia kufanyika kwa yai (kuachiliwa kwa yai) na kukalia mwendo wa
mbegu. Miongoni mwa wanandoa wanaotumia njia hii kadiri ya asilimia nane ya wanawake watapata
mimba zisizotarajiwa katika mwaka wa kwanza . Lakini ikiwa vidonge vitatumika vizuri na kwa makini
wanawake watatu kati ya 1,000 watapata mimba.
12. Kufanywa mgumba. Upasuaji wa kumhasi mwanamume au kufunga mirija ya uzazi kwa mwanamke
ni njia zenye mafanikio makubwa za kuzuia mimba. Kwa mwanamume—upasuaji wa kuondoa sehemu
ndogo ya njia ya kupitisha mbegu za mwanamume ambayo hupitisha mbegu kutoka kwenye pumbu.
Upasuaji huu hauathiri kamwe uwezo wa mwanamume kufanya tendo la ndoa. Kwa mwanamke—
upasuajia wa kuifunga mirija inayounganisha ovari na mji wa mimba na hivyo kuzuia kukutanika kwa
yai na mbegu za mwanamume. Upasuaji huu hauathiri hisia na utendaji wa tendo la ndoa kwa
mwanamke. Kuna hatari za kawaida za upasuaji. Njia hii ya ugumba kwa kawaida ni ya kudumu na
hivyo haishauriwi kwa watu ambao wako nje ya ndoa.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
77
IV. Mwisho mambo ya kuzingatia kuhusu uzazi wa mpango.
A. Uhuru.
1. Uzazi wa mpango na uamuzi kuhusu kutumia au kutokutumia njia za kuzuia mimba, una matokeo
muhimu kwa ajili ya familia na mtu binafsi anayehusika. Swala hili inabidi lishughulikiwe baada kupata
uelewa wa kutosha wa kitabibu na mwingineo, na katika hali ya kuomba ili upate hekima na neema.
2. Kwa sababu biblia haijapinga bayana matumizi ya njia za kupanga uzazi, hili ni swala la dhamiri.
Wana ndoa wa Kikristo wana uhuru wa kuchagua ikiwa watapenda kupanga uzazi na ya kuwa watumie
njia ya asili au ya kisayansi katika kutekeleza azma yao.
3. Uhuru sio kibali cha kufanya dhambi. Ingawaje kuna watu watakaotumia njia za kuzuia mimba
isivyostahili kwa matakwa yoa ya kibinafsi, hili halitangui matumizi yake sahihi.
B. Watoto.
1. Watoto ni zawadi na baraka kutoka kwa Mungu (Zab 127:43-5).
2. Uamuzi wa kibinafsi wa kutokuzaa watoto kwa hakika ni kinyume cha moyo wa neno la Mungu.
3. Njia za kupanga uzazi husaidia kutenganisha muda kati ya kuzaliwa mtoto mmoja hadi mwingine, na
si kukwepa wajibu wa kuwa na watoto.
4. Njia za kupanga uzazi pia husaidia wanandoa kuwa na watoto waliopanga kuwa nao ambao
watawapenda na kuwaongoza katika injili ya Kristo.
C. Kuasili.
1. Katika mpango wake wa Kiungu wakati mwingine Mungu haruhusu wanandoa fulani kupata watoto.
Katika mazingira kama hayo nyumba yenye furaha yaweza bado kujengwa. Kuasili watoto laweza kuwa
utatuzi wa maana zaidi kwa wanandoa ambao hawawezi kuzaa watoto wa kwao wenyewe.
2. Kuasili pia kwawezekana kwa wana ndoa ambao wana uwezo wa kuzaa watoto.
3. Kuasili hutatua tatizo kubwa sana la kijamii. Kunasaidia kupunguza umasikini na ongezeko la watu.
Kuna maelfu wa yatima ambao wanahitajika kuasiliwa katika familia za Kikristo zenye upendo.
4. Kuasili huonyesha upendo wa Kristo “walio wadogo” (Math 25:40, 45). Asili ya kuasili ni “Dini
iliyo safi,isiyo na taka” (Yak 1:27). Mungu ametuasili katika familia yake (Rum 8:15-17; Efe 1:5; Gal
4:5). Vivyo hivyo, kuasili watoto katika familia zetu na kuwa nao kama watoto wetu ni tendo la Kiungu.
D. Kuzuia mimba kwa wasio na ndoa.
1. Biblia inapinga waziwazi kujamiiana kwa watu wasio na ndoa bado na wale walio na ndoa
kutokujamiiana na mtu mwingine asiye mwenzi wa ndoa. Matendo hayo ni kinyume cha sheria ya
kimaadili ya Mungu. Vivyo hivyo, watu ambao hawana ndoa hawana sababu zinazowahalalisha wao
kibiblia kutumia njia za kuzuia mimba.
2. Vifaa vya kuzuia mimba havipaswi kutolewa kwa wanaume au wanawake ambao hawana ndoa.
Kwani kwa kuondoa hofu ya kupata mimba watashawishika kuendelea na uzinzi.
3. Baadhi ya Wakristo huhalalisha kwa kutumia mantiki na kusema, “kwa vyovyote watu wa duniani
watajamiiana tu; kwa hiyo, ni heri tuwakinge wasio na ndoa kwa njia za kuzuia mimba, kwani
kutokufanya hivyo kutasababisha watoto wengi wasiotarajiawa kuzaliwa.” Watu wanaotumia mantiki
ya namna hii wana hatia ya kukubaliana na matendo ya uzinifu na wanashindwa kuwaacha watu
wapokee matokeo ya matendo yao ya dhambi na ukiukaji wa maadili.
12. MAANDIKO YANAVYOFUNDISHA KUHUSU KUACHANA
I. Mungu anachukia Kuachana.
A. Tafsiri ya Talaka.
Talaka ni tendo la kuhalalisha kutengana kwa wana ndoa, linaloanzishwa na mmoja au wana ndoa wote
wawili, kwa kusudi la kuvunja ndoa na kuwaweka wana ndoa huru mbali na haki zote na majukumu ya mmoja
kwa mwingine, na kuwapa uhuru kisheria kuoa au kuolewa.
B. Mtazamo wa Mungu kuhusu talaka.
1. Katika Mal 2:13-16 Mungu anasema ya kuwa anachukia kuachana: 13 "Tena mnatenda haya
nayo:mnaifunikiza madhabahu ya BWANA kwa machozi,kwa kulia na kuugua hata asiiangalie tena hiyo
dhabihu,wala kuitakabali mikononi mwenu na kuiridhia. 14 "Lakini ninyi mwasema, 'Ni kwa sababu
gani? Ni kwa sababu BWANA amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
78
mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako. 15 "Hakuna mtu mmoja aliyetenda
hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye uzao mwenye kumcha
Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yeyote asimtende mke wa ujana wake mambo ya
hiana. 16 "Maana mimi nachukia kuachana,"asema BWANA, Mungu wa Israeli, "naye aifunikizaye nguo
yake kwa udhalimu namchukia,"asema BWANA wa majeshi. "basi jihadharini roho zenu, msije
mkatenda kwa hiana."
2. Hebu ona lugha hii kali anayotumia Mungu kuhusiana na kuachana. Mara tatu ameiita “usaliti”; hali
hiyo anasema ni “kinyume”; anasema kuwa “anaichukia”.
C. Talaka ina matokeo kiroho.
1. Katika Mal 2:13-16, Mungu anawasikitikia wana wa Israel, Watu wa Mungu, walipokubali kuenenda
kwa viwango vya watu wa mataifa wasiookoka na wakaamua kuwataliki wake zao ili waowe wanawake
wa kipagani, wa kidunia wasiookoka. Wana wa Israelites walilia na kuomboleza madhabahuni kwa
Bwana kwa sababu Hakuwasikiliza tena. Walitaka kujua kwa nini na Mungu anasema ni kwa sababu ya
matendo yao ya kuachana.
2. Hebu ona matokeo ya kiroho yatokanayo na kuachana kama kisemavyo kifungu hicho hapo juu:
a. Mungu “kamwe haikubali sadaka yenu wala kuipokea kutoka mkononi mwenu” (2:13).
Kumpa talaka mwenzi moja kwa moja huathiri uhusiano wetu wa kiroho na Mungu. Dhana hii
pia imesemwa katika 1 Pet 3:7 ambayo yawaagiza waume kuwaheshimu wake zao “kusudi
kuomba kwenu kusizuiliwe.”
b. Talaka ni uvunjifu wa agano ambalo Mungu ni shahidi na mshiriki (2:14). Vivyo hivyo,
katika uhalisia kumtaliki mwenzi ni kuharibu mahusiano yako na Mungu. Dhana hii hii
inatokana na ukweli kuwa, kama ilivyoandikwa katika Efe 5:22-32, ndoa nia kielelezo cha
uhusiano wa Kristo na Kanisa. Hivyo, katika shina lake, Ndoa ni ya kiroho—ni taasisi ya
kiroho.Mungu anatwambia, “Sitakupungukia, wala sitakuacha kabisa” (Ebr 13:5). Hivyo,
mume na mke wa Kikristo wanapoachana, wana mwakilisha Kristo duniani kwa namna iliyo
kinyume. Talaka hutenganisha kile alichounganisha Mungu (Math 19:6), na ni namna ya
kuugawa mwili wa Kristo.
c. Mungu amesema bayana ya kuwa “hakuna mmoja aliyetenda hivi [aliyempa mkewe talaka]
ambaye ana mabaki ya Roho” (2:15). Mara mbili anawaagiza watu wake “kujihadhari roho
zao” (2:15, 16). Hivyo, moja kwa Mungu anasema kuwa kuachana ni taswira ya hali halisi ya
kiroho ya walioachana.
3. Uzito na matokeo ya kuachana yaonekana tena katika ukweli kuwa Mungu aliitazama hali ya kukosa
uaminifu katika ndoa kama sura ifananayo na ile ya Israel katika Agano la Kale kuitafuta na kuabudu
miungu. Katika Yer 3:8 Mungu alisema “kwa sababu hiyo ya kuzini ya Israel asiye na imani
[akimaanisha ufalme kaskazini, dhidi ya ufalme wa kusini wa Yuda], Nimemwacha nikampa hati ya
talaka.”
4. Kiwango cha Mungu, kimpendezacho yeye, talaka haipo, twaishi katika kizazi cha dhambi,
kilicholaaniwa na kuanguka ambapo talaka ni matukio ya kila siku. Wazo la Mungu ni kutokuwepo kwa
dhambi, lakini dhambi hutokea. Talaka inapotokea (na hilo ni nje ya mapenzi makamilifu ya Mungu, ya
kimaadili), yatupasa tuwe tayari kushughulikia jambo hilo Kibiblia, na kwa mtazamo wa Kristo.
Wakristo lazima wawe na huduma ya uponyaji, na ya kukomboa wale ambao tayari wameshaingia
kwenye janga la talaka. Tunapaswa kuwaelekeza watu kwa mwokozi ambaye anaweza kuwasamehe
dhambi yao, na kuondoa hatia yao, na kuwaponya kiroho na kisaikolojia ili waishi maisha safi mbele ya
Mungu mtakatifu. Vivyo hivyo, wote wawili, Yesu na Paulo wamefundisha kuhusiana na talaka na
inavyohusiana na maisha yetu.
II. Mafundisho ya Kristo kuhusu talaka—Math 19:3-12.
A. Changamoto ya Mafarisayo (19: 3).
“Basi Mafarisayo wakamwendea wakamjaribu, wakamwambia, Je!ni halali mtu kumwacha mke wake
kwa kila sababu?”
1. Kundi la Mafarisayo ambao walikuwa na imani iliyo huru kuhusiana na sababu za kutoa talaka
walimjia Yesu ili wamjaribu kuhusu talaka. Walikuwa wanajaribu kumfanya afanye uchaguzi kati ya
mitazamo miwili kuhusiana na talaka ambayo ndiyo ilikuwa imesimama kati ya Mafarisayo na watu.
a. Shule ya Shammai ilikuwa makini sana na iliyajua maneno “ameona neno ovu kwake” katika
Kum 24:1-4 ilimaanisha uasherati tu. Waliona sababu iliyokuwa halali kwa mtu kumtaliki
mkewe ilikuwa uasherati ni hii pekee ilivunja kifungo cha ndoa.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
79
b. Shule ya Hillel iliamini kuwa ilikuwa ni sawa kwa mume kumpa talaka mkewe kwa sababu
yoyote iwayo. Endapo mkewe ameunguza chakula au kamuudhi mumewe, hii ilitosha kuwa
sababu ya kutoa talaka. Mtazamo huo pia ulikuwepo kipindi cha Yesu; alichopaswa kufanya
mwanamume ilikuwa ni kuandika hati ya talaka kwa mkewe kwa sababu yoyote ile.
2. Mafarisayo walijua ya kuwa Kristo alifundisha kuhusu talaka hapo nyuma katika huduma
yake katika hotuba ya mlimani (Math 5:31-32). Katika hotuba ya mlimani, Kristo alipingana na
mtazamo potofu wa Mafarisayo wa sheria ya Agano la Kale kwa kutumia tafsiri yake
mwenyewe iliyo sahihi ya sheria hiyo.
B. Ndoa inayofaa (19:4-6).
“Hamkusoma,” akajibu, “ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,’
akasema, ‘Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye atambatana naa mkewe ;na hao wawili
watakuwa mwili mmoja’? Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu,
mwanadamu asiwatenganishe.”
1. Akijibu changamoto za Mafarisayo, Kristo anawapeleka kwenye kusudi la mwanzo la kuwa na ndoa.
Katika ndoa ya kwanza ya Adam na Hawa, mapenzi, hamu na dhamira ya Mungu ilikuwa ni kuwa na
mwanamume mmoja kuoa mwanamke mmoja kwa maisha yao yote.
2. Viwango vya Mungu kwa ajili ya ndoa viko juu sana. Shauku yake kwa ajili ya watu ni kwamba
wawe na ndoa zitakazodumu maisha yao yote; hili litaleta Baraka maalum za Mungu.
3. Talaka ni dhambi. Talaka ni uvunjifu wa sheria ya kimaadili ya Mungu.
C. Changamoto ya pili ya Mafarisayo (19:7).
“Jinsi gani basi, “Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?” Mafarisayo wakadhani kuwa
wamemweka Yesu katika mtego, kwa sababu ikiwa haikupasa kutoa talaka kwa nini Musa aliruhusu talaka
katika Agano la Kale? Walijaribu kumfanya Yesu aseme kinyume na sheria ya Musa. Na hilo lingemfanya
asikubalike kwa watu.
D. Ni kwa nini Musa aliruhusu talaka (19:8).
“Akawaambia, ‘Musa , kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake
zenu;lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo.’”
1. Mafarisayo walidai ya kuwa Musa aliamuru talaka kana kwamba Mungu aliiidhinisha. Hilo
halikuwa kweli. Musa aliruhusu talaka, ikimaanisha kukubali au kuruhusu kwa sababu ya dhambi.
Talaka haikuwa ndani ya maelekezo (mtazamo) na mapenzi ya Mungu, ingawaje inaruhusiwa kwa
“mapenzi yaliyoruhusiwa.” ya Mungu
2. Talaka iliruhusiwa kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya wana wa Israeli. Neno “ugumu” linamaanisha
“ukaidi” au “sugu.” Hii inamaanisha kuwa Musa aliruhusu talaka kwa wana wa Israeli kwa sababu ya
kutokutii.
3. Yesu alisema. “Tangu zamani haikuwa hivyo.” Hii inaturudisha tangu kipindi cha Adamu na Hawa,
walikuwa kielelezo cha ndoa iliyofaa machoni pa Mungu. Tena, kifaacho kwa Mungu si talaka, kwa
sababu mtu na mkewe wanapaswa kuwa mwili mmoja katika muunganiko usiogawanyika. Talaka
imeruhusiwa kama dhambi nyingine yoyote ilivyoruhusiwa katika mpango wa Mungu. Hata hivyo,
talaka haikuwa ndani ya sheria ya ndoa ya awali kabla ya sheria ya Musa kuwepo.
E. Kristo Aliruhusu Talaka Endapo Kutakuwa na Uasherati (19: 9).
“Nami nawaambia ninyi kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa
mwingine, azini.” Wasomi wa Kikristo bado hawajafikia muafaka kuhusu neno“uasherati” [Kiyunani =
porneia]. Kuna maoni ya kisomi aina tatu hapa:
1. Mtazamo namba 1: porneia huzungumzia tamaduni za Kiyahudi. Baadhi ya wasomi huamini kuwa
Yesu alifundisha kuwa talaka hairuhusiwi kwa sababu yoyote ile, hata uasherati. Wanaamini neno
porneia linamaanisha ukosefu wa uaminifu kijinsia kipindi cha uchumba au ndani ya ndoa ya ndugu wa
karibu, au kwa wamataifa wasioamini. Hivi ndivyo ambavyo imekuwa katika kanisa la Kikatoliki na
baadhi ya madhehebu ya kiprotestanti.
2. Mtazamo namba 2: porneia Humaanisha uasherati tu.
a. Wayunani wanalo neno limaanishalo uasherati (moicheia), na wakati mwingine neno
porneia, humaanisha uasherati. “na ayawekee mbali mambo ya uasherati wake (moicheia)
yasiwe mbele ya uso wake na mambo ya uzinzi wake[porneia] yasiwe kati ya matiti yake” (Hos
2:2, LXX).
b. Vitabu vya Apokrifa Sirach chasema. “Hivyo ndivyo alivyo mwanamke amwachaye
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
80
mumewe na kupata mrithi kwa njia ya uasherati [porneia]. Kihistoria, kanisa la RC limefuata
mtazamo huu.
c. Katika mwaka413 Augustino aliandika, “Wala haijawa wazi katika maandiko ikiwa
mwanamume aliyemwacha mkewe kwa sababu ya uasherati, kitu ambacho kwa hakika
anaruhusiwa kufanya, ya kuwa yeye mwenyewe atakuwa mzinzi endapo atoa tena.”
d. Msomi wa Ki-Jesuit Theodore Mackin, katika kitabu chake Divorce and Remarriage (Talaka
na Ndoa Nyingine), anasema: Waandishi wa Kikristo kuhusu somo la uasherati, talaka na kuoa
tena, kuanzia katika ya karne ya pili na kuendelea angalau kufikia wakati wa Augustino, kamwi
hawakuwaita watu wafuatao waasherati: (1) Mume aoaye tena baada ya kumwacha mkewe
mwasherati; (2) Mume aoaye baada ya kuachwa/kutelekezwa na mkewe; (3) Mwanamke
aolewaye kwa sababu zizo hizo hapo juu.
e. Kanisa la Mashariki la Ki-Orthodox liligundua porneia ya kuwa ilimaanisha uasherati na
kuongezea kuwa ilikuwa ni sawa na kutoa mimba au kujaribu kujiuwa.
f. Watu wa uamsho wanakubali uasherati (porneia) waweza kuwa sababu ya kutoa talaka na
kuoa tena. Ukiri wa Imani wa Westminster unasema: “ingawaje uharibifu wa mwanadamu
umefikia kiwango cha kujadili swala la kuwatenganisha wale ambao Mungu amewaunganisha
katika ndoa: hata hivyo, hakuna kiwezacho kuwatenganisha isipokuwa uasherati, au uamuzi wa
makusudia wa kujitenga kwa kuwa kanisa au mahakama, haviwezi kamwe kuwa vyombo
vyenye nguvu ya kutosha kutenganisha ndoa: wakati ambapo, shauri hili linapoendelea kati ya
watu wawili, basi watu hao wasiachwe huru kuongozwa kuamua kwa utashi wa matakwa yao
ya kibinafsi katika shauri hilo lao.” (WCF, sections XXIV-VI)
3. Mtazamo namba 3: porneia ni neno pana zaidi ya moicheia na humaanisha matendo ya aina tofauti ya
uasherati.
a. Porneia na moicheiani maneno tofauti, yakimaanisha kuwa porneia ni neno lililo pana
lihusianalo na uasherati. “Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi
(moicheia), uasherati [porneia]” (Math 15:19).
b. Porneia inaweza kumaanisha dhambi ya uzinzi kabla ya ndoa. “Ndoa na iheshimiwe na watu
wotel . . . kwa maana waasherati [moicheia] na wazinzi [porneia] Mungu atawahukumia
adhabu” (Ebr 13:4b).
c. Inaweza kumaanisha kujamiiana kwa watu waliondugu wa karibu “Yakini habari imeenea ya
kuwa kwenu kuna zinaa[porneiana]na zinaa ya namna isiyokuwepo hata katika
Mataifa:Kwamba mtu awe na mke wa babaye” (1 Kor 5:1).
d. Inamaanisha uasherati “Na ayaweke mbali mambo ya uasherati (moicheia) wake yasiwe
mbele ya uso wake, na mambo ya uzinzi [porneia]wake yasiwe kati ya maziwa yake” (Hos 2:2).
e. Dhambi ya zinaa kwa ujumla “Ikimbieni zinaa [porneia] (1 Kor 6:18).
f. Kwa hiyoPorneia ni pana kiasi cha kuweza kuhusisha kila aina ya uzinzi, ikiwa ni pamoja na
ukahaba, ushoga, usagaji na kujamiiana na wanyama. Matendo haya yote ya uzinifu huvunja
muunganiko wa ndoa na dhambi hizi zote ziliadhibiwa kwa kifo katika Agano la Kale.
4. Ikiwa mtazamo wa tatu wa porneia ni sahihi: Basi Yesu hakufuata misimamo mikali ya Shule ya
Shammai, ambayo ilisema hakuna talaka isipokuwa kwa uasherati tu; na wala hakufuata mtazamo wa
walio huru wa Shule ya Hillel, ambao walisema, waweza kutoa talaka kwa sababu yoyote. Badala yake
Yesu alichukua nafasiya mpatanishi na akasema talaka iliruhusiwa “unapotokea uzinzi”, ambao ni
pamoja na uasherati, kujamiiana kwa ndugu, ukahaba, ushoga, usagaji na kujamiiana na mnyama, lakini
talaka si lazima,”
5. Kwa kuwa uzinzi ni kigezo cha kutoa talaka kati ya Wakristo wawili waaminio, haimaanisha ya
kuwa talaka ni jawabu mara mwenzi akosapo uaminifu. Lazima kuwepo na kila juhudi ya kuiponya
ndoa na kuirudisha katika hali ya ushindi. Ndoa ni takatifu, na kila ndoa yastahili kuipigania hata kama
yamekuwapo matukio ya ukosefu wa uaminfu.
6. Yesu kamwe hakusema ya kuwa kutokukidhi viwango, kushindwa kuzaa, matusi, kupigwa, uharibifu
wa mali ni vigezo vya kutolea talaka. Hata hivyo, kesi za kupigwa, matukano na uharibifu wa mali
zaweza kuwa sababu za kutengana bila kuwa na nia ya kurudiana au kuwa mwasherati. Hakuna
anayelazimika kuishi na mtu mpigaji na mtukanaji. Hakuna anayelazimika kuivumilia dhambi (ambapo
unyanyasaji wa kila namna wa maneno na wa kupiga ni dhambi). Hakuna anayepaswa kuhatarisha
maisha yake au ya watoto wake kwa kuendelea kuishi na mtu wa jinsi hii.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
81
III. Mafundisho ya Paulo kuhusu Talaka—1 Kor 7:10-16.
A. Kuhusiana na mwamini aliyeoana na mwamini mwingine (7:10-11).
“10Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapa si mimi, ila Bwana; mke asiachane na
mumewe; 11(lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe), tena mume
asimwache mkewe.”
1. Neno “kuachana” katika kifungu hiki ni sawa na lile alilotumia Yesu katika Math 19:6,
aliowaunganisha “Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.” Neno hili lina maana pana kuliko ile ya
“talaka.” Vivyo hivyo, neno lililotafsiriwa “talaka” katika 7:11b mara nyingi hutafsiriwa “kuacha” au
“fukuza,” si tu “kutoa talaka.” Maneno haya yana maana zinazofanana. Katika maeneo yote mawili
yaonyesha kuna kutengana kwa ndoa kwa moja kwa moja.
2. Mafundisho ya Paulo yako sawa na ya Kristo ya kuwa kuingia katika ndoa nyingine baada ya talaka
ni uasherati (tazama Marko 10:9-12; Luka 16:18).
3. Paulo habainishi kwa “kifungu kinachotofautisha” cha talaka kwa sababu ya “uasherati” (tazama
Math 5:32; 19:9). Hapa yaonyesha kuwa Paulo hakuwa anazungumzia watu ambao walikuwa wakitoa
talaka kwa sababu zilizo sahihi. Ikiwa mtu atatoa talaka kwa sababu mwenzi wake ni mwasherati, Yule
asiye na hatia aweza kuolewa na kamwe asiwe na hatia ya uasherati mbele za Mungu. Badala yake
Paulo anaonekana akiwakabili wale ambao hutaka kuwaacha wenzi wao kwa sababu zisizokidhi. Katika
hali ya namna yeye asababishaye talaka ana chaguzi mbili tu: kujipatanisha na mwenzi wake au abaki
bila kuwa na ndoa tena.
4. Kupatana, kwa kweli, ndilo chaguo lililo bora zaidi katika migogoro ya aina zote ya ndoa, ikiwa ni
pamoja na itokanayo na uzinifu. Mungu angependa wanandoa wapatane, kuliko kuachana.
B. Kuhusiana na mwamini aliyeoana na asiye mwamini (7:12-16).
1. Mwamini aliye katika ndoa na asiye mwamini ambaye anapenda waendelee kuishi katika ndoa
(7:12-14): “12Lakini kwa watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana; ya kwamba iwapo ndugu
mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye, asimwache. 13Na mwanamke , ambaye
ana mume asiyeamini, na mume anakubali kukaa naye, asimwache mumewe. 14Kwa maana yule mume
asiyaamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama
isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu”
a. Ufunguo ni 7:14 Kuhusiana na “kumtakasa” mwenzi asiyeamini na watoto:
(1) Kutokana na Ezra 9-10, wana wa Israeli waliagizwa kuwapa talaka wenzi
wasioamini waliowaoa walipokuwa mateka huko Babeli na wale marafiki wa mataifa
waliowapata kutoka katika mataifa yaliyowazunguka (tazama pia Neh 13:23-29).
(2) Kutokana na Hag 2:11-14, unajisi ulipatikana kwa kugusa maiti. Waamini wa
Kiyahudi na wale wa mataifa walitafsiri hili kuwa unajisi huweza kuhamishwa au
kusafirishwa.
(3) Vivyo hivyo, Wakristo wa Korintho waliamini kuwa ndoa zao zinanajisiwa na
wenzi wasioamini. Kwa hakika waliuliza ikiwa walipaswa kuwapa talaka wenzi wa
ndoa wasio amini ili wawe wasafi na wasinajisike
b. Jibu la Paulo linakanusha na kupingana na amri sheria za Agano la Kale’s kuhusiana na
usafi.
(1) Chini ya Agano Jipya, aliye msafi (yaani, mwamini) anatumia nguvu kutakasa
(yaani, humtenga au humtakasa) aliye mchafu (ina maana, asiye amini), na si kinyume
cha hapo. Jambo lilo hilo limefundishwa na Yesu kimatendo. Alimgusa na kumtakasa
mwenye ukoma (Math 8:1-4; Marko 1:40-45), lakini yeye “hakunajisika” kwa
kufanya hivyo (tazama Law 5:2-3; 13:45-46).
(2) Vivyo hivyo, mwamini katika Kristo hapaswi kumwacha mwenzi asiye mwamini
ikiwa Yule asiyeamini anaridhia kuendelea katika ndoa. Inaweza kuwa vigumu kuishi
na asiyeamini lakini neema ya Mungu inatosha. Ikiwa asiyeamini yuko radhi kuendelea
na ndoa, mwamini ahakikishe kuwa anakuwa upande wa kudumisha mahusiano ya ndoa
yaendelee.
(3) Paulo anaposema ya kuwa wenzi wasioamini “wanatakaswa,” hamaanishi kuwa
wanafanyika sehemu ya watu wa Mungu, au wanakuwa wameokoka, kwa sababu ya
kuwa katika ndoa na mwamini. Badala yake, inaonyesha kuwa mwenzi asiyeamini
inaingia katika eneo lenye utakatifu kwa sababu ya kuwa katika ndoa na mtu
anayeamini. Asiyeamini anakuwa katika mazingira yenye uungu wa mwenzi aaaminiye
ambayo asingeweza kuyapata nje ya ndoa. Kuna upendeleo na baraka maalum apatazo
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
82
mtu kwa ajili tu ya mwenzi aaminiye.
2. Mwamini aliyeoana na asiye mwamini ambaye anakataa kuendelea na ndoa (7:15-16): 15Lakini yule
asiyeamini akiondoka,na aondoke.Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu
ametuitia katika amani. 16Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? au wewe
mwanamume, kama utamwokoa mkeo?”
a. Ikiwa asiyeamini anaamua kuvunja ndoa na kumpa talaka yeye aaminiye, mwamini hafungwi
kuendelea na ndoa. “Kuto kuwa katika kifungo” (au, “kutokuwa katika kongwa”) ina maana
waamini katika mazingira ya namna hiyo hawapaswi kujisumbua ili kuiponya ndoa. Sababu ni
kwamba hatuwezi kuwataka wasiookoka wafuate viwango vya kiroho na namna ya maisha
kama waaminio. Kanuni itawalayo ni kwamba Mungu ametuitia amani (tazama pia 1 Pet 3:11).
b. Waamini hawapaswi kuwa wa kwanza kutaka talaka (ona ya kuwa asiyeamini katika 7:15 ya
kuwa anaanzisha swala la kutengana). Hata hivyo, ikiwa asiyeamini atasisitiza kudai talaka,
mwamini asikate tamaa. Hapa tena, neema ya Mungu inabidi iwepo. Yeye peke yake huwaweka
huru waaminio kutoka katika wasi wasi na kuwapa “amani ipitayo akili zote” (Fil 4:6-7).
c. Neno “kifungo” linatokana na neno la asili doulos na kwalo tumepata neno “mtumwa.”
Paulo hazungumzii kutengana kisheria lakini talaka na haki ya kuoa au kuolewa tena. Katika 1
Kor 7:39 anasema, “Mwanamke hufungwa [doulos]maadam mumewe yu hai lakini ikiwa
mumewe amefariki, yuko huru kuolewa na mtu yeyote amtakaye; katika Bwana tu.” Kwa hiyo,
Paulo anapozungumzia “kuondoka” kwa asiye amini anamaanisha talaka iliyo halali na, pamoja
nayo haki ya kuoa au kuolewa.
IV. Mambo yahusuyo Talaka.
Ni lazima maombi ya kutosha na fikra ya kina viwe vimefanyika kabla ya tendo la talaka kufanyika.
Talaka husababisha kiwewe fulani katika fahamu za wana ndoa wote wawili, kihisia, kimwili, na kiroho. Talaka
wakati wote huacha majeraha ya kudumu. Huzalisha watu ambao huionea mashaka ndoa. Inaathiri watu na
mahusiano zaidi ya yule mume na mke. Mara nyingi haitatui tatizo, lakini huweza kuzalisha matatizo mengine
mapya. Hivyo, hata pale ambapo kuachana kungeruhusiwa kimaandiko, jambo hilo lisichukuliwe juu juu katika
kuamuliwa.
A. Mambo muhimu ya kuzingatia kuhusiana na mume, mke, na watoto katika kuachana.
1. Mume.
a. Mwanamume anapoteza faraja na usalama wa nyumba yake, na yabidi achukue tena
majukumu ya kiseja (kupika, kuosha vyombo, kufagia nyumba, upweke, wingi wa muda n.k.)
na aanze kuishi katika makao mengine.
b. Mara nyingi mwanamume anapoteza haki ya kuwalea watoto wake, kwa kuwa kwa sehemu
kubwa mahakama huona anayestahili kuwa na watoto ni mama, hivyo watoto huenda kwa
mama. Mwanamume anaweza kupoteza heshima na upendo kwa watoto wake.
c. Mwanamume pia anaweza kupoteza pesa nyingi, kwani gharama ya talaka inaweza kuwa
kubwa sana. Malipo yatokanayo na talaka na/au gharama ya kutunza watoto vyaweza kuathiri
kipato chake kwa miaka mingi. Mwanamume lazima ajiulize ikiwa anaweza kukabili gharama
za talaka.
d. Mwanamume anaweza kugundua kuwa talaka inaweza kuiathiri biashara yake au taaluma
yake.
e. Mwanamume kwa hakika atapoteza baadhi ya marafiki,kwa sababu ndoa zinapovunjika watu
hujigawa pande mbili.
2. Mke.
a. Mwanamke huumia sana kutokana na talaka, kwa kuwa inamwathiri kiakili na kihisia kwa
sababu ya kujiona ana hatia ya kushindwa.
b. Mwanamke ana maumivu makubwa kwa sababu ya upweke. Mwanamume ana kazi yake ya
kuitegemea; mara nyingi mwanamke hana.
c. Mwanamke analazimika kuwa mzalishaji kwa ajili ya familia yake na analazimika kufanya
kazi ya mwanamume (kuadibisha watoto, kutengeneza bomba, kurekebisha gari, n.k.). Mara
nyingi mwanamke atalazimika kufanya kazi ili atunze familia yake. Anarudi nyumbani akiwa
amechoka sana. Na mwenendo wake ni wa kujiona mwenye hatia wakati wote na kwa sababu
hiyo huwatendea watoto isivyo.
d. Kiwango cha maisha cha mwanamke hushuka sana katika mwaka wa kwanza wa kuachana.
Kipato hushuka sana na wasiwasi huongezeka kwa sababu ya mahitaji kumsonga.
e. Mwanamke kwa kawaida hupata makovu kwa sababu ameachika. Watu humhukumu na
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
83
kumuona kuwa yeye ni mzinifu. Urafiki hudorora kwa sababu yambidi awe katika nafasi ya
watu wawili mama na baba, yambidi afanye kazi, anachoka na kusongeka, n.k.
3. Watoto.
a. Watoto huteseka zaidi katika kuachana. Watoto wote hupata maumivu yatokanayo na wazazi
wao kuachana katika kipindi cha kati ya miaka miwili ya kwanza hadi mitano; na wengi
hudhurika maisha yao yote.
b. Usalama pekee wa mtoto ni wazazi wake. Ikiwa wameachana, mtoto anaweza kupata
uchungu na kuwa mwasi. Hawezi kamwe kuelewa kwa nini hili litokee kwake. Kuachana mara
nyingi husababisha watoto kukosa usalama na misimamo ambapo watashindwa kupambana na
maisha kikamilifu. Dalili zinazoonekana kwa watoto ambao ni matokeo ya wazazi walioachana
ni pamoja na hizi: (1) huzuni, msongo, uchovu, mawazo, kuangua kilio, kujitenga na marafiki,
hupata shida katika kulenga katika malengo na kuthibitisha uwezo wake; (2) kujikataa; (3)
kujiona kaaibika, husababisha kukosa ari; (4) hasira kali; (5) hatia kwa sababu ya vita ya
uaminifu ndani yake; (6) hofu ya kuhudumiwa na wengine hata kama familia yake ilikuwa
inajiweza; (7) kurudi nyuma na kukosa maendeleo ya kawaida; (8) kulazimika kukomaa kabla
kwa sababu ya hali; (9) kukosa usingizi, maumivu ya tumbo, maumivu ya kichwa, etc.
c. Watoto wa wazazi walioachana wana uwezekano mkubwa wa kuachana na wenzi
watakapoingia katika ndoa kuliko wale wa wazazi wasioachana. Sababu ni kwamba watoto wa
wazazi walioachana na wale wa wazazi wasioachana wana vielelezo viwili tofauti vya kufuata.
Zaidi ya hayo, watoto wa wazazi walioachana wana hofu ya kuingia katika mahusiano ya
kujitoa kikamilifu hadi kuwa na ndoa kwa sababu wanaogopa watapata watoto na hatimaye
waachane, na kuwaingiza watoto katika maumivu kama waliyopata wao. Ule ukosefu wa
kujitoa kikamilifu peke yake ni sababu tosha ya kuwa na ndoa ambayo talaka huwa ni rahisi
kutokea.
d. Watoto wanalazimika kuwa upande mmoja au wa pili kati ya wazazi wao na hili husababisha
kujisikia hatia kubwa na matatizo mengineyo ya hisia. Madaktari wa akili hufikiri ya kuwa
watoto wa wazazi walioachana watasaidika kisaikolojia endapo wataondolewa kutoka kwa
wazazi wanaobishabishana na kugombana kila wakati ambao huishi pamoja lakini hawaonyeshi
upendo. Hilo laweza kuwa kweli, lakini kuachana na kugombana vyote ni dhambi na
huwadhuru watoto.
e. Matokeo ya kuachana hayadhuru tu watoto wadogo, lakini hata wale wakubwa ambao
wanaweza kuelewa sababu ya wazazi wao kuachana.
B. Kuachana huumiza wahusika kwa viwango visivyoweza kuonekana na huumiza wengine.
1. Talaka huwaumiza wale wanaotalikiana kwa namna isiyoweza kuonekana:
a. Inaleta ubinafsi, uadui, hasira na kutokusamehe.
b. Inaharibu mtazamo wa mtu kuhusu ndoa na kuacha makovu ya kihisia ambayo kamwe
hayawezi kukupa uhuru.
c. Haya yote humfanya mtaliki kuwa na moyo mgumu na mwenye kujikinga dhidi ya watu
aliowapenda sana hapo nyuma.
2. Talaka huwaumiza watu mabao si sehemu ya hiyo talaka:
a. Huharibu watoto.
b. Huleta maumivu wa mashemeji na wakwe kwa kuwagawa makundi mawili.
c. Inawaumiza marafiki na kuwalazimisha kugawanyika makundi mawili. Na hilo kwa kawaida
husababisha kufa kwa urafiki kwa sababu ya kuachana.
d. Inawaumiza wababu na bibi ambao wanaitamani heshima ya kuwa na wajukuu wao na
watoto hali kadhalika wanawahitaji babu na bibi ili wawe thabiti.
e. Talaka huleta maumivu kwa jamii yote kwa sababu wataliki wametoka nje ya msimamo wa
kijamii na kuongeza udhaifu na hali ya kutokuendelea, kukosa muendelezo na kuwakatisha
tamaa wengi.
C. Mara chache talaka hutatua tatizo.
1. Wataliki wengi watakubali kuwa kamwe maisha hayakuwa bora baada ya kuachana.
a. Wengi watakubali ya kuwa hali ya kuwa wapweke ilizalisha matatizo mengi mengine tofauti.
b. Vile vile ndoa ya pili ina mengi ya yale matatizo ya ndoa ya kwanza.
c. Wataliki wengi husema ya kuwa kama ungekuwepo uelewa na subira wangali dumu kwenye
ndoa ya kwanza bila kuachana.
2. Baada ya kuachana, watu hubaki kama walivyokuwa.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
84
a. Baada ya kuachana, wataliki hubaki na tatizo lile lile la udhaifu wa kushindwa kutatua
matatizo, dhaifu wa kuthamanisha, wasioweza kujenga mahusiano na wengine,
yaliyowasababisha wawe na shida katika ndoa na hata wakaachana.
b. Matokeo ni kwamba mara nyingi wale walioachika huishia kupeleka maisha yao katika
mfumo wenye sura kama ile ya ndoa ya kwanza iliyoharibika.
c. Tatizo ni ubinafsi wa watu (jambo ambalo ni vigumu watu kukubali).
3. Ndoa za baadaye zina nafasi ndogo ya kufanikiwa zikilinganishwa na ile ya kwanza. Marekani kadiri
ya 40% ya ndoa za kwanza, lakini 60% ya ndoa za pili na 75% ya ndoa za tatu, huishia kwenye talaka
(Chapman 1992: 35).
D. Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kumwoa/kuolewa na Mtalikiwa.
1. Waweza kurithi watoto wasio wako. Ni rahisi zaidi kuwapenda na kuchukuliana na watoto wako
mwenyewe kuliko na watoto wa mtu mwingine.
2. Waweza kukutana na aliyekuwa mume au mke wa mtalikiwa kwa sababu ya watoto. Hili laweza
kusababisha wivu na matatizo mengine.
3. Ikiwa u mke, waweza kuona kuwa sehemu kubwa ya mshahara wa mumeo ikitoka kila mwezi kwa
ajili ya kutunza watoto. Hili linaweza kukuletea uchungu kirahisi, hasa pale ambapo familia yako wewe
pia inahitaji pesa.
4. Unaweza kuolewa na mtu asiye na misimamo au ana matatizo mengineyo, ambaye anaweza kupata
shida kuifanya ndoa isimame.
5. Unaweza kulazimika kuishi na makovu ya kuoana na aliyetalikiwa, hasa katika mazingira ambapo
talaka huonekana kuwa kama ni dhambi.
6. Utakuwa na wakati mgumu kuwaelewesha watoto wako sababu ya kuachana.
7. Utaoana na mtu ambaye ameathirika kisaikolojia kwa sababu ya talaka. Kutakuwa na wakati mgumu
wa kujiweka sawa.
8. Unaweza kuwa waoana na mtu ambaye amewahi kuwa na mahusiano ya kujamiiana na watu wengi
wa jinsi tofauti na yeye kwa sababu ya talaka, jambo ambalo litamfanya ashindwe kuridhika kuwa na
mtu mmoja.
E. Tumaini katika muktadha wa talaka.
1. Kutimizwa kwa kusudi la Kimungu la ndoa bora ni lengo namba 1 la Mungu—hakuna talaka.
2. Kilicho bora kwa Mungu ni mume mmoja mke mmoja kwa maisha yenu yote.
3. Kuachana wakati wote ni dhambi kwa sababu ni kinyume cha sheria ya Mungu ya kimaadili.
4. Mungu ni wa upendo na huruma, na wakati wote hutafuta kutengeneza hali mbaya kuwa nzuri kwa
njia ya msamaha.
5. Neema ya Mungu ipo siku zote kurejesha, kurudisha upya, na kuvuka vikwazo vya kuachana endapo
kuna toba ya kweli na imani.
6. Talaka, hata ile itokeayo kwa makosa, yaweza kupokea msamaha kwa ukombozi wa Kristo.
7. Msamaha hurejesha uhusiano lakini yawezekana hali ya mtalikiwa isibadilike kwa sababu ya dhambi.
Anahitaji kukubali matokeo ya matendo maovu aliyotenda, laiki pia awe huru na kujisikia mwenye
hatia.
8. Mtalikiwa anaweza kuingia tena katika ndoa mpya ndani ya Kristo na kuwa na maisha mazuri
yakuridhisha lakini anaweza kulazimika kuishi na athari za dhambi na kuadibishwa na Mungu maishani
mwake.
MAREJEO YALIYOTAJWA
Archbold, Peter. No date. “20 Statistical Differences Between Man and Women.” No pages. Online:
http://www.quazen.com/Science/Social-Sciences/20-statistical-differences-between-men-and-women.7575.
Arnold, Carol. 2006. The Liberation of a Resentful Wife. Chattanooga, Tenn.: Sunny.
Baron-Cohen, Simon. 2003. The Essential Difference. New York: Basic Books.
Bowman, John Wick. 1947. “The Gospel and the Christian Family.” Interpretation 1: 436-49.
Brizendine, Louann. 2006. The Female Brain. New York: Morgan Road.
Budziszewski, J. 2005. “Designed for Sex.” Touchstone: A Journal of Mere Christianity, no pages. Online:
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
85
http://touchstonemag.com/archives/article.php?id=18-06-022-f.
Busenitz, Irvin. 1986. “Woman’s Desire for Man: Genesis 3:16 Reconsidered,” Grace Theological Journal 7: 203-12.
Campbell, Ross. 1977. How to Really Love Your Child. New York: Signet.
Campus Crusade for Christ, International. 1993. FamilyLife: Marriage Conference. Little Rock: Ark.: Campus Crusade.
Canadian Women’s Health Network. No date. “10 Differences Between Men and Women that Make a Difference in
Women’s Health.” No pages. Online: http://www.cwhn.ca/resources/sexual_diff/.
Chapman, Gary. 1992. The Five Love Languages. Chicago: Northfield.
Colson, Charles, and Nancy Pearcey. 1999. How Now Shall We Live. Wheaton, IL: Tyndale House.
Conner, Michael G. No date. “Understanding the Difference Between Men and Women.” No pages. Online:
http://www.oregoncounseling.org/ArticlesPapers/Documents/DifferencesMenWomen.htm.
“Contraceptives: What Are Your Choices?” No date. No pages. Online:
http://www.advocatesforyouth.org/youth/health/contraceptives/index.htm.
Danker, Frederick William, ed. 2000. A Greek-English Lexicon of the New Testament and Other Early Christian
Literature. 3d ed. Chicago: The University of Chicago Press.
Davis, James, 1989. 1-2 Corinthians. In Evangelical Commentary on the Bible, ed. Walter Elwell, 958-97.Grand Rapids,
Mich: Baker.
Dominian, Jack. 1982. Marriage, Faith and Love. New York: Crossroad.
Dunn, James D. G. 1996. The Epistles to the Colossians and to Philemon (NIGTC). Grand Rapids, Mich.: Eerdmans.
Fleming, Joy Lynn Elasky. 1987. “A Rhetorical Analysis of Genesis 2-3 with Implications for a Theology of Man and
Woman.” Doctoral diss. Université des Sciences Humaines de Strasbourg.
Foh, Susan. 1974-75. “What is the Woman’s Desire?” Westminster Theological Journal 37: 376-83. Online:
http://www.google.com/url?sa=t&rct=j&q=&esrc=s&source=web&cd=1&ved=0CC4QFjAA&url=http%3A%2F
%2Ffaculty.gordon.edu%2Fhu%2Fbi%2Fted_hildebrandt%2Fotesources%2F01-genesis%2Ftext%2Farticlesbooks%
2Ffoh-womansdesire-wtj.pdf&ei=leWjUeyQB8HYywHtgoH4AQ&usg=AFQjCNGTTX8P_tXxYLvw2sPPHR1i-
e_sw&sig2=Ra5PZk52Z60zkscXODGR6w&bvm=bv.47008514,d.aWc&cad=rja.
Gangel, Kenneth. 1972. The Family First. Minneapolis, MN: His International Service.
Gombis, Timothy. 2005. “A Radically New Humanity: The Function of the Haustafel in Ephesians.” Journal of the
Evangelical Theological Society 48: 317-30. Online: http://www.etsjets.org/files/JETS-PDFs/48/48-2/48-2-pp317-
330_JETS.pdf.
Grudem, Wayne. 1988. 1 Peter (TNTC). Grand Rapids, Mich.: Eerdmans.
Hoekema, Anthony. 1986. Created in God’s Image. Grand Rapids, Mich.: Eerdmans.
Knappert, Jan. 1990. The Aquarian Guide to African Mythology. Wellingborough, Northamptonshire, England: Aquarian.
Koehler, Ludwig and Walter Baumgartner. 2001. The Hebrew and Aramaic Lexicon of the Old Testament, Study Edition. 2
vols. Translated by M. E. J. Richardson. Leiden: Brill.
Mathewes-Green, Frederica. 2005. “Bodies of Evidence.” Touchstone: A Journal of Mere Christianity, no pages. Online:
http://touchstonemag.com/archives/article.php?id=18-05-027-f.
McKnight, Scot. 1996. 1 Peter (NIVAC). Grand Rapids, Mich.: Zondervan.
Michaels, J. Ramsey. 1988. 1 Peter (WBC). Nashville: Thomas Nelson.
Morse, Jennifer. 2001. Love and Economics. Dallas, Tex.: Spence.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
86
Nadig, Larry Alan. No date. “Tips on Effective Listening.” No pages. Online: http://www.drnadig.com/listening.htm.
Nock, Steven. 1998. Marriage in Men’s Lives. New York: Oxford.
Relationship Institute. No date. “Differences Between Men and Women.” No pages. Online: http://www.relationshipinstitute.
com/freearticles_detail.cfm?article_ID=151.
Rector, Robert, Patrick Fagan and Kirk Johnson. 2004. “Marriage: Still the Safest Place for Women and Children.”
Backgrounder No. 1732. The Heritage Foundation. No pages. Online:
http://www.heritage.org/research/reports/2004/03/marriage-still-the-safest-place-for-women-and-children.
Rhoads, Steven. 2004. Taking Sex Differences Seriously. San Francisco: Encounter.
Smalley, Gary. 1984. The Key To Your Child's Heart. Waco, TX: Word.
Smalley, Gary, and John Trent. 1986. The Blessing. Nashville: Thomas Nelson.
Stanton, Glenn. 1996. “Why Marriage Matters for Adults.” No pages. Focus on the Family. Online:
http://www.focusonthefamily.com/marriage/gods_design_for_marriage/marriage_gods_idea/why_marriage_matte
rs_for_adults.aspx.
Stitzinger, Michael. 1981. “Genesis 1-3 and the Male/Female Role Relationship.” Grace Theological Journal 22: 23-44.
Online:
http://www.google.com/url?sa=t&rct=j&q=&esrc=s&source=web&cd=1&ved=0CC4QFjAA&url=http%3A%2F
%2Ffaculty.gordon.edu%2Fhu%2Fbi%2Fted_hildebrandt%2Fotesources%2F01-genesis%2Ftext%2Farticlesbooks%
2FStitzinger-Gen-1-3-GTJ-
1981.pdf&ei=peajUc3UM8XGygGRp4CgAw&usg=AFQjCNHHmQNTXpDp-
PoLnDBIDOIjIoTOFA&sig2=ZjeybsgfTZzpkqooBsSD8w&bvm=bv.47008514,d.aWc&cad=rja
Thomas, Adam, and Isabel Sawhill. 2005. “For Love and Money? The Impact of Family Structure on Family
Income,” The Future of Children 15(2): 57-74.
Tucker, William. 1993. “Monogamy and its Discontents.” National Review, 4 October, 28-38.
Vogels, Walter. 1996. “The Power Struggle Between Man and Woman (Gen 3,16b).” Biblica 77: 197-209.
Waite, Linda, and Maggie Gallagher. 2000. The Case for Marriage. New York: Doubleday.
Walton, John. 2001. Genesis (NIVAC). Grand Rapids, Mich.: Zondervan.
Wells, Tom, and Fred Zaspel. 2002. New Covenant Theology. Frederick, Md. New Covenant Media.
Westminster Larger Catechism. 1647. Online: www.reformed.org/documents/larger1.html.
Wheat, Ed, and Gaye Wheat. 1997. Intended for Pleasure: Sex Technique and Sexual Fulfillment in Christian Marriage, 3rd
ed. Grand Rapids, Mich.: Revell.
Willard, Dallas. 1997. The Divine Conspiracy. New York: HarperSanFrancisco.
Wilson, James Q. 2002. The Marriage Problem. New York: HarperCollins.
Winter, Bruce. 2003. Roman Wives, Roman Widows. Grand Rapids, Mich.: Eerdmans.
KIAMBATISHO
MAONI YA KUFAA YA KUWASAIDIA WAUME NA WAKE KIMAISHA
1. Oneshaneni kufurahiana katika kazi na matatizo ya mwenzi wako. Mume na mke wanaweza kuwa na kazi
tofauti na majukumu, ambayo kusababisha matatizo tofauti tofauti, masumbufu, na mahitaji. Kila mmoja
anahitaji kujua ya kuwa mwenzi wake anatambua hilo. Mwahitajika wote ku “beba na kulia” kwa ajili ya
mwenzi na uwe chanzo cha msaada na kutia moyo.
2. Kumbuka “lugha tano za upendo” na zitendee kazi. Maneno ya kutia moyo, kuwa na muda wa kuwa
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
87
pamoja, kupeana zawadi, kuhudumiana, na kugusana kimapenzi huonyesha upendo kwa mwenzi na husababisha
kudumisha moto wa upendo.
3. Kumbuka “vitu vidogo.” Maisha ya wengi huwa katika mzunguko wa mazoea. Twaweza kuwa twatarajia
“makubwa,” lakini sehemu kubwa ya maisha yetu huzunguka katika “vitu vidogo.” Kufanya vitu kama kuwa na
nyumba safi, kukumbuka siku za kuzaliwa, kumbukumbu, na nyakati nyingine maalum, kufanya kile apendacho
mwenzi wako, kufanya kitu ili “kuvunja mazoea,” huwa kama mafuta yadumishayo uhusiano uendelee vema.
4. Jiweke vizuri na uwe sawa kimwili. Waume na wake hupenda wenzi wanaovutia. Ni rahisi kujiweke
watanashati kabla ya ndoa. Kuendelea kufanya hivyo baada ya ndoa si tu vema kwa ajili yetu, lakini hilo
laonyesha kuwa mwenzi wetu ni muhimu kwetu bado.
5. Endeleza mawasiliano na mwenzi wako. Kumbuka, mawasiliano ni uhai wa kila mahusiano. Wana ndoa
wengi huacha kuongea baada ya kuoana kwa muda. Endeleza mawasiliano kwa makusudi, si tu kuzungumza na
mwenzi wako bali kusomana yale yanayowapendeza. Usimkosoe na kumwaibisha mwenzi wako mbele za watu.
Usimkemee mwenzi wako hata kama umekasirika, lakini kumbuka ya kuwa mwenzi wako ni zawadi kutoka
kwa Mungu na ni pendo la maisha yako.
6. Jiepushe kufuatilia matatizo ambayo yanaweza kuathiri ndoa yenu.
A. Wivu. Wivu ni sumu amabayo yaweza kuharibu ndoa. Inabidi kuwepo kuaminiana kwa dhati kati ya
mume na mke. Uwazi na mawasiliano husaidia huzuia wivu kuchipuka, au kutatua kabla haujaenea.
B. Kutawala. Kutawala, kumiliki, hali iliyozidi ya kumiliki yaweza kumsumbua mtu katika ndoa. Tena,
kumwamini na kumheshimu mwenzi kutazuia hali hii.
C. Vitisho. Asiwepo atakaye mtishia mwenziwe ili apate kitu fulani. Vitisho (mfano, “Kama huninunulii
lile gauni, sitakuandalia chai tena,” au “Kama husafishi nyumba mimi nahama”) siku zote huvunja
utegemezi wa mtu kwa mwenzi. Neno “talaka” kamwe lisitamkwe, au hata kufikiriwa kama chaguo
wakati wana ndoa wanapopitia hali ngumu.
D. Ukorofi na kiburi. Ukorofi na kiburi na ishara ya ubinafsi, havijengi uhusiano. “Maneno ya uchawi”
katika ndoa ni haya, “Nilikosea,” au “Nimetenda dhambi,” na “Tafadhali nisamehe.”
E. Mashemeji/Wakwe. Kanuni ya kimaandiko ni kuachana na wazazi na kuambatana na mwenzi wa
ndoa. Mashemeji/wifi/wakwe hawapaswi kuingilia au kutawala ndoa ya mtu na maisha yake ya
nyumbani kwake. Ikiwa ni lazima, wana ndoa watalazimika “kusema kweli kwa upendo” kwa
mashemeji/wifi/wakwe wanaowaingilia.
F. Maswala ya pesa. Lazima iwepo hali ya kuaminiana kati ya mume na mke kuhusiana na maswala ya
pesa kati ya mume na mke, na mawasiliano yaliyo wazi, majadilianano, na kadiri iwezekanavyo
waamue kwa pamoja namna watakavyotumia pesa. Yule mwenye uwezo zaidi wa kutawala pesa ndio
apewe kutunza pesa na “kuandika vitabu.” Mume anapotunza pesa, mke lazima apewe pesa za kutosha
kwa ajili ya matumizi ya nyumbaini na matumizi yake ya binafsi. Haya yafuatayo yafanyike
kuhakikisha ya kuwa pesa inatumika kwa namna yakufaa na ya kumpendeza Mungu: (1) Lazima iwepo
bajeti mliyokubaliana kimaandishi; (2) Mtoleeni Bwana kwa kazi yake mara kwa mara; (3) Msitumie
pesa kwa vitu msivyohitaji; (4) Muishi chini ya kipato,wekeni angalau 10% ya kipato chenu.
7. Kutatua matatizo.
A. Njia zisizofaa za kutatua matatizo:
(1) Kukataa kwamba kuna tatizo.
(2) Kukwepa au kukimbia tatizo.
(3) Kuvumilia tatizo bila kulitatua (ina maana, “kuteseka kimya kimya”).
(4) Kutoa vitisho, kufoka, au kutaka tu matakwa yako yasikilizwe.
B. Kutatua matatizo Kibiblia:
(1) Tambua ya kuwa wewe na mwenzi wako mnayo nguvu ya dhambi ndani yenu (tazama
Warumi 6-7). Kila mtu anayo maeneo ya udhaifu ndani yake na dhambi. Sisi sote “tu kazi
isiyokamilika” ambamo Mungu yu atenda kazi bado. Kwa hiyo tunapaswa kukiri dhambi yetu
kwa uangalifu na kuwa makini “kutoa boriti jichoni mwetu” ili tuweze kukiona kibanzi jichoni
kwa mwenzi wetu (tazama Math7:3-5).
(2) Tambua ya kuwa, wewe u wa jinsi tofauti hivyo mwenzi wake ana mtazamo tofauti kwa
vitu, na hutumia njia tofauti ya kuwasiliana, na anaweza kutofautiana na wewe. Mungu
amewaumba wanaume na wanawake katika hali tofauti, na hivyo lazima tuwe waangalifu
tusiwalazimishe wenzi wetu kuwa kama sisi.
Copyright © 2008-2013 by Jonathan Menn. All rights reserved.
88
(3) Tunapaswa kuwa wavumilivu, wazito kukasirika, wepesi kusamehe, kwa sababu Mungu
amekuwa mvumilivu kwetu na ametusamehe (tazama Mith 14:29; 15:13; 16:32; Math6:9-15;
18:21-35; Gal 5:2; Efe 4:32; Kol 3:13; 1 Tim 1:16).
(4) Kumbuka ya kuwa Mungu ni mkuu. Hakuna lililo gumu kwake. Hakuna tatizo asiloweza
kulitatua (tazama Luka 1:37). Mungu hakuahidi kwamba hatutaingia katika matatizo, lakini
ametuhakikishia neema yake kutusaidia kupita katika matatizo. Mkomavu wa kiroho ni Yule
awezaye kutatua matatizo yake kwa kutumia neema ya Mungu akimtegemea Kristo.
C. Njia ya Kibiblia kukabili matatizo:
(1) Tambua tatizo ni lipi—kwa uaminifu tathmini tatizo, na likabili kiukweli.
(2) Tambua namna ya kutatua tatizo katika Kristo kwa namna ya heshima:
a. Omba na mwenzi wako kwa ajili ya kupata neema, hekima, uongozi wa Mungu, na
roho ya unyenyekevu ya kusaidia.
b. Jifunze biblia wewe binafsi na pamoja na mwenzi wako..
c. Tumia kanuni za kibiblia, akili, mantiki, vyote vikiongozwa na upendo kwa mwenzi
wako na shauku ya kutunza na kuimarisha uhusiano na yeye.
d. Uwe mwaminifu kwa mwenzi wako kwa kila jambo. Usiwe mdanganyifu kwa
mwenzi wako. Sema kweli kwa upendo,na jaribu kuziweka hisia zako na mihemko
yako chini.
e. Muwe uhuru katika kujadiliana. Wakati wote mawasiliano yenu yawe wazi na
zungumzeni wakati wote kwa upole. Uwe msikivu mzuri. Uwe na uwezo wa kuyaona
maono ya mwenzi.
f. Kila tatizo lipeleke kwa Yesu na jiulize yeye angefanyaje (au, bora zaidi, yeye
angetaka ufanye nini) katika tatizo hilo na mazingira haya.
g. Uwe mwepesi kusamehe. Usiruhuusu jua kushuka ukiwa na hasira bado. Kila tatizo
lazima litatuliwe, au angalau lipangiwe kutatuliwa kabla ya kulala. Kusibaki chochote
kisichosamehewa, kisichotatuliwa, au ambacho yabidi kingoje siku ifuatayo.
h. Tafuta ushauri wa Kibiblia inapobidi.
KUHUSU MWANDISHI
Jonathan Menn anaishi Appleton, WI, USA. Alipokea shahada yake ya B.A. kwa masomo ya siasa za
kimwanasayansi kutoka kwa Chuo kikuu cha Wisconsin-Madison, na taaluma ya heshima, mnamo mwaka wa
1974, baadaye akajumuika na Phi Beta Kappa kwa kuwa na heshima ya kijamii. Tena akapata J.D. kutoka kwa
Shule ya Uanasheria cha Cornell, magna cum laude, mnamo mwaka wa 1977, na akawekwa kwenye mamlaka
ya Kisheria ya Coif haki za heshima ya jamii. Akaitumia miaka iliyofuata 28 akifanya kazi za uanasheria, kama
wakili, wa huko Chicago na baadaye akashirikiana na Shirika la mawakili liitwalo Menn Law Firm kule
Appleton, WI. Alikuwa muumini na mfuasi wa Yesu Kristo tangu mwaka wa 1982. Alifundisha masomo ya
Biblia darasa la watu wazima kwa miaka kadhaa. Kukua kwa pendo lake katika Thiolojia na Huduma
vilimfanya aende akatafute Shahada ya Uzamili ya mambo ya Mungu au Master of Divinity katika chuo cha
Trinity Evangelical Divinity School huko Deerfield, IL. Alipokea shahada yake ya M.Div. kutoka kwa TEDS,
summa cum laude, mnamo Mei 2007. Na sasa yeye ni mkurugenzi wa Huduma ya Kuwawezesha Viongozi wa
Kanisa Afrika Mashariki (Equipping Church Leaders East Africa. “ECLEA”): www.eclea.com. Unaweaza
kuwasiliana na Jonathan kupitia na tovuti hii: jonathanmenn@yahoo.com.

No comments:

Post a Comment