Friday 5 December 2014

MAMLAKA YA MWAMINI

Mamlaka
Ya
Mwamini
na
A.L. Gill
Gill Ministries
www.gillministries.com
Swahili - Authority
Vitabu vya A.L. na Joyce Gill
God's Promises for Your Every Need
God’s Covenant Blessings for You
Destined for Dominion
Out! In the Name of Jesus
Victory over Deception
Nakala Katika Mwongozo Huu
The Church Triumphant
Through the Book of Acts
God's Provision for Healing
Receiving and Ministering
God's Healing Power
The Ministry Gifts
Apostle, Prophet, Evangelist,
Pastor, Teacher
Miracle Evangelism
God's Plan to Reach the World
New Creation Image
Knowing Who You Are in Christ
Patterns for Living
From the Old Testament
Praise and Worship
Becoming Worshipers of God
Prayer
Bringing Heaven to Earth
Supernatural Living
Through the Gifts of the Holy Spirit
Kuhusu Wabuni na Waanzilishi
A.L. na Joyce Gill ni wanenaji wajulikanao kimataifa, waandishi na walimu wa Biblia.
Matembezi ya utume ya A.L. yamempeleka katika mataifa zaidi ya hamsini ya ulimwengu,
akihubiria umati zaidi ya laki moja, moja kwa moja na kwa milion nyingi kwa redio na runinga.
Vitabu vyao vilivyouzwa pamoja na nakala viliuzwa zaidi ya milioni mbili Marekani. Maandishi
yao, ambayo yametafsiri katika lugha nyingi, inatumika katika vyuo vya Bibliad na katika
semina ulimwenguni.
Kweli zenye nguvu na zibadilishazo maisha za Neno la Mungu hulipuka katika maisha ya
wengine kupitia huduma yao ya mahubiri, kufundisha, kuandika na sinema na pia kanda za
kusikiliza.
Utukufu mkuu wa uwepo wa Mungu huonekana katika kusifu na kuabudu kwao katika semina
wakati waamini hugundua jinsi ya kufanyika waabudio wa kweli kwa Mungu. Wengi
wametambua mbinu mpya na yenye busara na ujasiri kupitia mafundisho yao kuhusu mamlaka
ya mwamini.
Gill wamefundisha waamini kuingia katika huduma za kiasili walizopewa na Mungu wakiwa na
uponyaji na nguvu mikononi mwao. Wengi wamejifunza kuwa wa asili wanapoachiliwa na
kutenda katika karama zote tisa za Roho Mtakatifu maishani mwao na huduma kila siku.
A.L. na Joyce wana shahada za Master of Theological Studies. A.L. pia amepata shahada ya
Doctor of Philosophy in Theology kutoka Vision Christian University. Huduma yao imewekwa
juu ya Neno la Mungu, inaangazia Yesu, ina nguvu katika imani na hufundishwa katika nguvu za
Roho Mtakatifu.
Huduma yao ni kielelezi juu ya moyo wa Baba wenye upendo. Mahubiri yao na mafundisho
huambatana na upako wenye nguvu, ishara na miujiza, na uponyaji na wengi wakianguka katika
nguvu za Mungu.
Ishara za uamushwo pamoja na kicheko kitakatifu, kilio mbele za Bwana na kuonekana kwa
utukufu wa Mungu na nguvu zionekanazo na wengi wanaohudhuria mikutano.
Kwa Walimu na Wanafunzi
Mafundisho haya yenye nguvu kuhusu Mamlaka ya Mwamini yataleta ufunuo juu ya utawala
ndani ya kila mwanafunzi. Watajifunza jinsi ya kukoma kushindwa na kuanza kushinda katika
kila vita maishani. Waamini watatiwa moyo kupitia ufunuo mpya kuwatambua katika Yesu
Kristo. Mafunzo haya yataleta ujasiri na ushindi katika maisha ya wanafunzi.
Tungependekeza kabla ya kufunza kosi hii uweze kusikiliza na kuona kanda za sinema katika
mfululizo huu na pia kusoma vitabu vya Masomo Yaliyopendekezwa. Kadri unavyosoma na
kufahamu Neno la Mungu kuhusu mamlaka ya mwamini na vita vya kiroho, ndipo kweli hizi
zitaweza kuingia rohoni mwako. Nakala hii basi itakupa mwongozo ili utumie unapoonyesha
kweli hizi kwa wengine.
Mifano kuhusu maisha ya binafsi ni lazima kwa ajili ya mafunzo bora. Mwanzilishi ameacha
haya kutoka kwa kazi hii ili mwalimu aeleze ustadi kutoka maishani mwake, au kutoka kwa
wengine ambao wanafunzi wataweza kuhusiana nao.
Itakumbukwa kila mara kuwa ni Roho Mtakatifu ndiye amekuja kutufundisha katika yote, na
kuwa tunapojifunza au kufunza, ni lazima tuwe kila mara tukiongozwa na Roho Mtakatifu.
Mafunzo haya ni bora zaidi kwa kujifunza binafsi au katika kikundi, shule za Biblia, shule ya
Jumapili na makundi ya nyumbani. Ni vyema kuwa mwalimu na mwanafunzi awe na nakala ya
kitabu hiki wakati wa masomo.
Vitabu vizuri vimeandikwa, kutiwa msitari, kutafakariwa na kutumika. Tumeacha nafasi kwa
ajili ya maelezo na kunakili kwako. Mpangilio umewekwa ili uweze kurudia na kupata msaada
na kutafuta sehemu tena. Mpangilio bora hurahihisha kila mtu, mradi tu asome nakala,
awafundishe wengine yaliyomo.
Paulo alimwandikia Timotheo:
Hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine. 2 Timothy 2:2b
Mafunzo haya yameundwa kama kosi ya Biblia inayohuzisha katika utaratibu wa MINDS
(Ministry Development System), mbinu iliyoundwa kwa ajili ya mafunzo yaliyoandaliwa. Wazo
hili limeundwa ili kuzidisha katika maisha, huduma na mafunzo ya usoni ya wanafunzi.
Wanafunzi wa awali, kwa kutumia nakala hii, wanaweza kufunza wengine kosi hii kwa urahisi.
Orodha ya Yaliyomo
Somo La Kwanza Mtambue Adui Wako 7
Somo La Pili Mamlaka Hapa Duniani 15
Somo La Tatu Mpango Wa Hila Ya Shetani 23
Somo La Nne Kisha Akaja Yesu – Mpango Wa Mungu 30
Somo La Tano Yesu Alihudumu Katika Mamlaka 39
Somo La Sita Kutoka Msalabani Hadi Enzini 45
Somo La Saba Mamlaka Kurejeshewa Mwanadamu 52
Somo La Nane Mbinu za Shetani Za Kisasa 62
Somo La Tisa Kanisa na Mamlaka 69
Somo La Kumi Funguo Za Ufalme 77
Somo La Kumi Na Moja Jina La Yesu 85
Somo La Kumi Na Mbili Ushindi Wa Vita Vya Kiroho 93
Mistari Ya Kukariri 102
Maandiko katika Mamlaka ya Mwamini
yametolewa kutoka The New King James Version.
Haki ya Mwandishi 2009
Masomo Yaliyopendekezwa Kwa Kosi Hii
Destined for Dominion, na
Out! In the Name of Jesus
Na A.L. Gill, Powerhouse Publishing
7
Somo La Kwanza
Mtambue Adui Wako
TUKO VITANI!
Vita
Kama Wakristo, ni lazima tutambue na kujua kuwa
tunahusika katika vita. Mojawapo ya mbinu kuu za Shetani
imekuwa kutufumba macho tusione hitilafu na pigano
tulilo nalo, na kwa hivyo kutufanya kukosa ulinzi dhidi ya
mashambulizi yake. Lakini Mungu ametupatia kila silaha
tunayohitaji ili kuwa washindi kwa adui wetu!
2 Wakorintho 10:3, 4 Maana ingawa tunaenenda katika mwili,
hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si
za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
1 Timotheo 6:12 Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule
wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya
mashahidi wengi.
Ni muhimu kukumbuka kuwa silaha hizi si za
kiulimwengu. Ni za kiroho.
Wengi wa waandishi wa Agano Jipya walitumia matamshi
ya vita. Haya si majina ya utani tu, bali ni maelezo ya vita
ambavyo tunahusika. Vita hivi ni sharti vifanyike katika
ulimwengu wa kiroho.
Adui Wetu
Tuko chini ya uvamizi wa adui toka pande zote katika
maisha na uhusiano wetu – katika:
􀂱 Jamii
􀂱 Kifedha
􀂱 Kazi
􀂱 Mawazo(akili)
􀂱 Mili (afya)
􀂱 Nyumbani
􀂱 Majirani
􀂱 Miji
􀂱 Mataifa
􀂱 Ulimwengu
8
Mojawapo ya mambo muhimu ya kujifunza ni kuwa vita
vyetu si dhidi ya watu. Ni dhidi ya Shetani na mapepo
yake maovu. Ni katika ulimwengu wa kiroho. Kuingia
katika hitilafu na watu huleta usumbufu na kushindwa tu.
JE, ADUI WETU NI NANI?
Tukijua kuwa tuko vitani, ni muhimu kutambua adui wetu
ni nani.
Je, adui wetu ni –
􀂱 Jamii zetu?
􀂱 Watu tunaofanya kazi nao?
􀂱 Serikali yetu?
􀂱 Fedha zetu?
Hapana!
Tawala – Mamlaka
Mamlaka – Nguvu za Kiroho
Mtume Paulo anaeleza kuhusu adui wetu kwa undani
kabisa. Alitwambia kuwa vita vyetu si kati ya watu
wanaotuzunguka. Alisema hatupigani dhidi ya mwili na
damu.
Waefeso 6:12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu
na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa
giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa
roho.
Shetani
Petro aliweka wazi kuwa adui wetu ni Shetani
1 Petro 5:8 Mwe kiasi na kukesha; kwa kuwa mshiriki wenu
Ibilisi, kama samba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta
mtu ammeze.
Hila / Ujanja
Hila za Shetani ni mbinu zake, maarifa na mipango ya
ujanja, anayotumia dhidi yetu. Ana mbinu ya kijeshi ya
vita anayotumia katika kutushinda. Hata hivyo, kadri
tunapogundua mipango yake, ni sharti tuwe waangalifu
zaidi kuhusu silaha na zana za vita ambazo Mungu
ametutengea kwa ajili ya vita. Zana hizi ni za kutukinga.
Silaha ni za ushindi dhidi ya adui zetu.
Waefeso 6:11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza
kusipinga hila za Shetani.
9
Onyo
􀂱 Uzingirwe na Yesu
􀂱 Fahamu Mamlaka
􀂱 Usije Ukazushwa na Ibilisi
Tusije tukajawa na kutafakari juu ya Ibilisi, mapepo zake
au mbinu zake. Badala yake, tujawe na Yesu. Tunapoweka
macho yetu Kwake, tutatambua sisi ni nani ndani Yake.
Tunapotambua uwezo wetu uliorejeshwa katika Yesu,
ujasiri utashuka ndani ya roho zetu. Hatutamwogopa Ibilisi
wala mbinu zake.
MUNGU ALIWAUMBA VIUMBE MALAIKA
Mungu Ni wa Milele
Mungu ni wa milele. Yeye amekuwepo na Yeye ni
muumba wa vitu vyote.
Yohana 1:1-3 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno
alikuwa kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo
alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala
pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
Yohana 1:14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi
tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee
atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
“Neno” ni Yesu.
Mungu aliwaumba Malaika
Kama Mwana wa Mungu, Yesu aliumba vitu vyote
wakiwemo malaika. Hakuwaumba tu bali kwa kazi ya
Mungu.
Wakolosai 1:16, 17 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote vilivyo
juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni viti
vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote
viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako
kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.
Malaika Wana Mipango
Wakati Paulo aliorodhesha enzi, mamlaka, utawala na
nguvu na uwezo, alikuwa akizungumzia juu ya malaika.
Alitumia maneno yanayotaja kazi zao.
Zina vyeo tofauti-tofauti:
􀂱 Malaika Mkuu
􀂱 Makerubi
􀂱 Maserufimu
􀂱 Viumbe wanaoishi
Wana Kazi tofauti-tofauti:
10
􀂱 Enzi
􀂱 Utawala
􀂱 Mamlaka
􀂱 Nguvu
MUNGU ALIMUUMBA LUSIFA
Kwa vile tunajua kuwa Yesu aliumba vitu vyote,
tunafahamu kuwa alimuumba Lusifa.
Cheo cha Lusifa cha Zamani
Cheo cha Lusifa cha awali kilikuwa cha hali ya juu na
chenye heshima. Mojawapo ya cheo chake ilikuwa Nyota
ya Alfajiri.
Isaya 14:12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya
alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe
uliyewaangusha mataifa!
Ayubu 38:7 ...Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na
wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?
Maelezo Kuhusu Lusifa
Manabii Ezekieli na Isaya wanatupa mawazo juu ya
maelezo kuhusu Lusifa.
􀂱 Mfano Bora wa Ukamilifu
􀂱 Hekima Tele
􀂱 Amekamilika Kiurembo
Ezekieli 28:12b ...Bwana MUNGU asema hivi, Wewe wakitia
muhuri kipimo, umejaa hekima, na ukamilifu wa uzuri.”
􀂱 Amefunikwa na Johari
Ezekieli 28:13a ... Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu;
kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki na yakuti
manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na
yakuti samawi, na zumaridi na baharamani, na dharabu;
􀂱 Sauti Nzuri ya Kuvutia
Ezekieli 28:13b ...kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa
ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa
tayari.
Matari ni vyombo vya muziki. Filimbi ni vyombo vya
upepo kama vile filimbi au zomari.
Isaya 14:11a Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya
vinanda vyako.
Sauti yake ilisikika kama muziki wa kutamani.
11
􀂱 Asiye Lawama
Ezekieli 28:15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile
ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.
Kazi yake Lusifa
Nabii Ezekieli aliandika kuhusu kazi ya Lusifa ya awali.
􀂱 Mlinzi wa Enzi
Ezekieli 28:14 Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta
afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu yamlima mtakatifu
wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.
Hata wakati makerubi walipokuwa kila upande wa kiti cha
rehema wakilifunika Safina la Agano (Kutoka 25:18-22),
Lusifa alikuwa kando na Mungu katika nafasi ya heshima
kuu. Kama Nyota ya Alfajiri au Mwana wa Alfajiri,
alikifunika na kulinda kiti cha Mungu cha enzi na
kuonyesha mng’aro na utukufu wa Mungu. Alikuwa
ametakaswa kama makerubi mlinzi. Alipewa na Mungu
cheo cha jukumu kuu.
􀂱 Kiongozi wa Sifa
Kutokana na maelezo kuhusu sauti yake ya kimuziki,
inaonekana kuwa aliwaongoza malaika wote katika sifa
zao na kuabudu Mungu na kulinda kiti cha enzi cha
Mungu kwa kukifunika kwa sifa na kuabudu.
VITA MBINGUNI – LUSIFA AANGUKA
Ilisababishwa na Kiburi / Uasi
Kuelewa uasi wa Lusifa, kuanguka na vita vilivyofuatia
huko mbinguni, hutusaidia kuelewa umuhimu wa vita
tunavyopigana sasa hapa duniani.
Ezekieli 28:15,17 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku
ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako. Kwa
wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako,
nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa
nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami
nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe
hayo ya moto.
Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako, umeiharibu
hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini
nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.
Lusifa alikuwa mwema hadi alipoweka mawazo yake kwa
urembo wake mwenyewe badala ya urembo wa Yule
aliyemuumba. Kiburi kiliingia. Aliwaza juu ya mng’aro
wake badala ya kuweka mawazo yake kwa mng’aro wa
Mungu Mwenyewe.
12
“Nita Mapendekezo”
Palikuwa na pendekezo moja tu, mapenzi ya Mungu
iliyotawala ulimwengu mpaka kiburi kikamwingia Lusifa.
Isaya 14:12-17 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota
ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe
uliyewaangusha mataifa! Nawe ulisema moyoni mwako,
Nitapanda mpaka mbinguni,
Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu;
Nami nitaketi juu yam lima wa mkutano,
Katika pande za mwisho za kaskazini;
Nitapaa kupita vimo vya mawingu,
Nitafanana nay eye Aliye juu.
Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za
shimo.
Wao wakuonao watakukazia macho, watakuangalia sana,
wakisema, Je, Huyu ndiye aliyetikisa falme; Aliyeufanya
ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua
wafungua wake waende kwao?'
Mpaka sasa palikuwa pendekezo moja tu ulimwenguni –
mapenzi ya Mungu. Katika kuasi, Lusifa alifanya
kuchagua mapenzi yake kinyume na Mapenzi ya Mungu.
Kama ilivyoelezwa katika ‘Nita’ zile tano za Lusifa, ujanja
na kiburi chake uliendelea hadi kufikia kujaribu
kumwondoa Mungu kwenye kiti cha enzi kule mbinguni.
Vita
Ufunuo Wa Yohana 12:7-10 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli
na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye
akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda,
wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye
Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa
hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. Nikisikia
sauti kuu mbinguni, ikisema,
Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu,
na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini
mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu
wetu, mchana na usiku.
􀂱 Shetani na Malaika Watupwa Nje
Ezekieli 28:16 Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza
udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo
nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe
hayo ya moto.
Lusifa na malaika wake walitupwa nje ya mbinguni.
13
Matokeo ya Vita
􀂱 Theluthi Moja ya Malaika Walianguka
Theluthi moja ya malaika walikuwa chini ya amri ya
Lusifa na walianguka pamoja naye. Malaika wengine
waliokuwa chini ya amri ya Mikaili na Gabrieli, walibaki
waaminifu kwa Mungu.
Ufunuo Wa Yohana 12:4a na mkia wake wakokota theluthi ya
nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi.
Lusifa na “malaika wake” walitupwa chini duniani.
Ufuno Wa Yohana 12:9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa,
nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye
ulimwengu wote; akatupwa hata nchi na malaika zake
wakatupwa pamoja naye.
􀂱 Kubadilishwa Majina
Majina ya Lusifa yalibadilishwa. Aliyekuwa na vyeo kama
vile Mwana wa Alfajiri na vile vile Makerubi Aliyepakwa,
majina yake yalibadilishwa na kuwa:
􀂱 joka
􀂱 nyoka
􀂱 ibilisi
􀂱 Shetani
Malaika waliokuwa chini ya uwezo wa Lusifa, wale
waliomfuata katika kuasi, waliendelea na mipango yao ya
enzi, nguvu, mamlaka, uwezo na viongozi, lakini majina
yalibadilika kuonyesha hali yao ya kuanguka. Sasa
walitambulika kama mapepo, ibilisi, mapepo mabaya.
􀂱 Kubadilisha Hali
Hali ya Shetani ilibadilika kabisa.
Alikuwa:
􀂱 Nyota ya alfajiri
􀂱 Mwana wa Alfajiri
􀂱 Yeye aliyeongoza sifa na kuabudu
􀂱 Yeye aliyelinda na kuchunga kiti cha enzi cha Mungu
Alifanyika:
􀂱 mwovu
􀂱 fedheheshwa
􀂱 katupwa toka Mbinguni
14
Alipoteza:
􀂱 urembo wake mkuu
􀂱 nafasi yake kuu katika ufalme wa Mungu
Hali yake ilifanyika na kuwa:
􀂱 giza
􀂱 sura isiyopendeza
􀂱 ovu
􀂱 iliyojaa chuki
Haya yalikuwa matokeo ya dhambi zake za kiburi na uasi.
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Eleza kazi na cheo cha Lusifa cha awali.
2. Eleza uasi wake, kuanguka na vita vilivyofuatia.
3. Nani adui wa kweli wa waamini nyakati hizi?
15
Somo La Pili
Mamlaka hapa Duniani
DUNIA KUUMBWA
Na Mungu
Katika Mwanzo tunaelezwa kuwa Mungu aliumba dunia.
Mwanzo 1:1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
􀂱 Ili IwezeKukalika
Kulingana na Isaya, dunia haikuumbwa ili iwe tupu.
Iliumbwa ili ikalike.
Isaya 45:18 Maana BWANA, aliyeziumba mbingu, asema hivi;
Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye
aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na
watu; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.”
􀂱 Ilifanyika bila Umbo
Hata hivyo, Mwanzo 1:2 inaeleza dunia kama isiyokuwa na
umbo, tupu na yenye giza. Maelezo haya si ya mahali
palipo tayari kukalika. Katika Waebrania, neno linalotafsiri
kama “ilikuwa” inaweza pia kutafsiriwa vyema kama
“ilifanyika.”
Mwanzo 1:2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza
lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, Roho ya Mungu ikatulia
juu ya uso wa maji.
Katika Yeremia tunapata neno kama hilo la Kiebrania na
kutafsiriwa.
Yeremia 4:23-25 niliiangalia nchi, na tazama, ilikuwa ukiwa,
haina watu; naliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru.
Naliiangalia milima, na tazama, ilitetemeka, na milima yote
ilisongea huko na huko. Nikaangalia, na tazama, hapakuwa na
mtu hata mmoja, na ndege wote wa angani wamekwenda zao.
􀂱 Ilifanyika Giza na Tupu
Yeremia anaeleza kuwa hukumu ya Mungu iligeuza dunia
iliyokamilika na kuwa mahali pa uharibifu (yenye giza).
Yeremia 4:23 Naliiangalia nchi, na tazama, ilikuwa ukiwa, haina
watu, naliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru.
Yeremia aliendelea kueleza hukumu ya Mungu iliyokuwa
duniani.
Yeremia 4:26,27 Nikaangalia, na tazama, shamba lililozaa sana
limekuwa ukiwa, na miji yake yote ilikuwa imebomoka mbele za
BWANA, na mbele za hasira yake kali.
16
Maana BWANA asema hivi, Nchi yote itakuwa ukiwa; lakini
sitaikomesha kabisa.”
􀂱 Shetani Alikuja Duniani
Kuna uwezekano kuwa Shetani alitupwa duniani kati ya
Mwanzo 1:1 na Mwanzo 1:2. (Taz Kumbukumbu: ukur. 17)
Jaribu kuwaza juu ya Shetani alipotupwa hapa duniani.
Alikuwa na mojawapo ya vyeo vikuu mbinguni. Alikuwa
na urembo wa hali ya juu. Alikuwa ndiye kielelezo cha
utukufu wa Mungu. Hata hivyo, katika kuasi kwake, alitaka
hata zaidi. Alitamani kutawala mbinguni.
Palikuwa vita. Yeye na malaika waliomfuata walitupwa
duniani. Kila mahali Shetani alipotazama alikumbushwa
kuhusu Mungu Muumba ambaye sasa anamchukia sana.
Alikumbushwa kuhusu vyote alivyopoteza baada ya kuasi.
Labda Shetani, kama aliyekuja kuiba, kuua, na kuharibu,
katika chuki yake na hasira alikuwa tayari ameiharibu
dunia. Kile ambacho Shetani alibakisha ili kutawala
kilifanyika tupu, wazi, na kubaki katika giza tele. Lusifa
alitamani kutawala dunia nzima. Sasa, kile alibakisha ni
nyota moja ndogo, yenye giza, tupu.
Dunia Kurejeshwa na Mungu
Katika Mwanzo 1:2, tunasoma kuwa Roho wa Mungu
alikuwa juu ya maji. Mwanzo 1:3 inataja kuwa Mungu
alisema “hebu na kuwe na mwanga.” Shetani aliitambua
sauti hiyo!
Alikuwa ameisikia katika milele awali. Hebu fikiri juu ya
vile alivyobabaika alipoisikia sauti ya Mungu. Hata hapa
duniani hawezi kujificha kutoka kwa Mungu. Pia Mungu
hamwachi afanye atakavyo.
Je, Shetani alitiwa hofu kiasi gani alipomtazama Mungu
akiirejesha dunia katika hali yake ya awali kwa siku tano
zilizofwata.
“Kisha Mungu Akasema”
Dunia iliumbwa tena kwa maneno ya Mungu. Ni muhimu
kuelewa kuwa Mungu alinena na kurejesha vyote
vilivyoharibika.
Mwanzo 1:3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
ms. 6 Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji,
likayatenge maji na maji.”
ms. 9 Mungu akasema “Maji yaliyo chini ya mbingu na
yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane”, ikawa hivyo.
ms. 11 Mungu akasema, “Nchi na itoe majani, mche utoao
mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinzi yake,
ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi;” ikawa hivyo.
17
ms. 14 Mungu akasema, “Na iwe mianga katika anga la mbingu
ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na
majira na siku na miaka.”
ms. 20 Mungu akasema, “Maji na yajawe kwa wingi na kitu
kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga
la mbingu.”
ms. 24 Mungu akasema, “Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake,
mnyama wa kufungwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa
mwitu kwa jinsi zake;” Ikawa hivyo.
ms. 26 Mungu akasema, “ Na tumfanye mtu kwa mfano wetu,
kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa
angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa
kitambaacho juu ya nchi.”
ms. 29 Mungu akasema “Tazama, nimewapa kila mche utoao
mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao
matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu.”
Shetani Kuitikia
Yote iliyokuwa kamili, yaliyoharibiwa hapa duniani,
Mungu aliifanya kamili tena. Je, mipango ya Mungu
ilikuwa gani? Kwa nini Mungu alifuatilia nyota (dunia) hii?
Fikiri juu ya Shetani akiwaita mapepo, “kwa nini Mungu
hatuachi sisi? Anayo dunia nzima kuitawala nasi tuko tu na
nyota hii ndogo!”
Hofu na chuki lazima vilimshika Shetani wakati kila siku
kwa siku tano, sauti ya Mungu ilisikika. Wakati Mungu
aliponena, dunia ilirejeshwa na kuboreshwa katika hali yake
ya awali. Chuki ya Shetani kwa Mungu lazima iliendelea
kuongezeka kila siku.
Kumbuka: Wasomi wa Biblia wanatofautiana kuhusu utaratibu wa
mambo yanayohusu kuanguka kwa Shetani na kuumbwa kwa
mwanadamu. Nakala katika somo hili inagusia “wazo la pengo”
amabayo hufundisha kuwa pana “pengo” katika nyakati kati ya msitari
wa kwanza na wa pili katika kifungu cha kwanza cha Mwanzo. Makisio
haya hufundisha kuwa Shetani alitupwa chini duniani baada ya uasi
wake na kisha, dunia ikawa bila umbo, tupu na yenye giza kama
inavyoelezwa katika msitari wa pili.
Wengine hufundisha kuwa kuasi na kuangushwa kwa Shetani
kulifwatia kuumbwa kwa mwanadamu. Pia, wasomi wengine
hutofautiana juu ya nyakati za kumtupa Shetani duniani toka mbinguni.
Si muhimu hasa kukubaliana na utaratibu wa matukio kama ilivyotajwa
katika somo hili, kama ilivyo kuelewa kuwa mwanadamu, aliyeumbwa
katika mfano wa Mungu, alipewa uwezo wa hali ya juu na utawala wa
dunia. Ni muhimu pia kuelewa kuwa hii ndiyo sababu inayomfanya
Shetani amchukie mwanadamu sana.
18
MAMLAKA ALIYOPEWA MWANADAMU
Aliumbwa Katika Mfano wa Mungu
Baada ya Mungu kuiumba dunia, Aliwaumba mume na mke
kwa mfano Wake. Kisha akawapa uwezo juu ya vyote
vilivyoishi duniani.
􀂱 Hebu na Wapate Kutawala
Katika Mwanzo moja, tunaambiwa kuwa mwanadamu
aliumbwa kwa mfano wa Mungu. Katika Mwanzo tisa,
tunaambiwa kitu kile kile tena.
Mwanzo 1:26 Mungu akasema, “ Na tumfanye mtu kwa mfano
wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege
wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye
kutambaa kitambaacho juu ya nchi.”
Mwanzo 9:6 Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake
huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake
Mungu alimfanya mwanadamu.
Kutambua kuwa waume kwa wake waliumbwa kwa mfano
wa Mungu in muhimu katika kuelewa somo hili kwa sababu
mfano wa Mungu ni mojawapo ya uwezo.
Mwanzo 1:27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano
wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Kupewa Uzima wa Mungu
Mungu aliumba mwili wa mwanadamu toka vumbi la
udongo kwa mikono Yake, na kisha akaivuvia pumzi Yake
Mungu. Mungu alivuvia pumzi katika mwanadamu hali
Yake ya asili.
Alitupatia uzima Wake. Uzima wa Mungu uko ndani yetu!
Mwanzo 2:7 BWANA Mungu akampulizia puani pumzi ya uhai;
mtu akawa nafsi hai.
Mamlaka Juu ya Shetani
Baada ya vita mbinguni, Shetani alitupwa duniani. Je,
unaweza kufikiri jinsi alivyojawa na hofu alipomtazama
Mungu akimuumba mwanadamu, akimvuvia pumzi ya
uzima wa Mungu, na kisha kumpa kiumbe huyu mpya
utawala na mamlaka juu ya vyote vinavyoishi duniani?
Shetani alikuwa akiishi duniani! Utawala aliopewa
mwanadamu ulijumlisha mamlaka juu ya Shetani na
wafuasi wake.
Mamlaka Kupewa Wote
Mungu alimuumba Hawa na Adamu, na wawili hao
walikuwa na mamlaka na utawala juu ya vitu vyote duniani.
19
Katika Mwanzo 2 tunapata hadithi ya kuumbwa kwa Hawa.
Mwanzo 2:21-24 BWANA Mungu akamletea Adamu usingisi
mzito, naye akalala; kasha akatwaa ubavu wake mmoja,
akafunika nyama mahali pake.
Na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya
mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
Adamu akasema, “huyu ni mfupa katika mifupa yangu, basi
ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika
mwanamume.”
Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake
naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
􀂱 Sio Tu Kwa Adamu
Katika kutaja mwanadamu mara ya kwanza, Mungu
alisema “hebu na wawe na utawala” hakusema “hebu na
awe na utawala”
Mwanzo 1:26-28a Mungu akasema, “ Na tumfanye mtu kwa
mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na
ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye
kutambaa kitambaacho juu ya nchi.”
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu
alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Mungu akawabariki, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke,
mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na
ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya
nchi.”
Mwanadamu asionyeshe utawala juu ya mwanamke, au
mwanamke kwa mwanamume, bali kama mwili mmoja, ni
sharti wawe pamoja katika utawala na mamlaka hapa
duniani.
Pamoja, walipewa mamlaka juu ya:
􀂱 Samaki baharini
􀂱 Ndege wa angani
􀂱 Mifugo
􀂱 Dunia nzima
􀂱 Kila kiumbe anayeishi
20
􀂱 Sio Juu ya Watu Wengine
Mwanadamu hakupewa mamlaka juu ya mwanadamu
mwenzake. Alipewa uwezo juu ya viumbe vyote vya
Mungu hapa duniani na juu ya Shetani na mapepo yake.
Mungu sasa alikuwa na uwezo na utawala wote katika
dunia nzima isipokuwa katika nyota ya arthi. Hapa Alitoa
uwezo na mamlaka haya kwa viumbe hawa wapya
wafananao na Mungu waitwao mume na mke.
Mwanadamu Alipewa Uhuru wa Kuchagua
􀂱 Kuchagua
Mungu alimpa Adamu uhuru wa kuchagua. Alikuwa na
uwezo wa kuchagua kumtii au kutomtii Mungu.
Mwanadamu alipewa uwezo au uhuru wa kuchagua.
Uhuru wa kuchagua ulipimwa katika bustani ya Edeni kati
ya kutii au kutotii, kati ya kula kutoka kwa mti wa mema na
mabaya, au kutokula. Mwanadamu bado ana uhuru wa
kuchagua.
Mwanzo 2:16, 17 BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu,
akisema, matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini
matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana
siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.”
SHETANI ANAMCHUKIA MWANADAMU
Shetani alimchukia Adamu na Hawa kwa sababu
waliumbwa kwa mfano wa Mungu. Wakati wa kuumbwa
kwao, walipewa kila kitu alichojaribu kunyakua kwa
nguvu.
􀂱 Walionekana kama Mungu
􀂱 Walinena kama Mungu
􀂱 Walitembea kama Mungu
Walipewa mamlaka juu ya vitu vyote duniani ambayo
ilijumlisha Shetani. Hiyo ilijumlisha kila kitu alichokua
akitawala. Hiyo ilijumlisha ufalme “wake” wote.
Hofu Kuu ya Shetani
Shetani anajua mamlaka tuliyo nayo. Anajua kile Mungu
amesema na kutenda.
Ni muhimu sana kwake kuwa tusitambue mamlaka yetu –
kuwa tusitambue na kutembea katika uwezo na mamlaka
tuliyopewa na Mungu. Shetani hana sababu ya kuwaogopa
waume kwa wake wanaotembea katika mamlaka
waliyopewa na Mungu.
21
“Nitafanya” za Shetani
Kumbuka “nita” za Shetani katika Isaya.
Isaya 14:13-15 Nawe ulisema moyoni mwako:
Nitapanda mpaka mbinguni,
Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu;
Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, katika pande za
mwisho za kaskazini;
Nitapaa kupita vimo vya mawingu;
Nitafanana nay eye aliye juu;
Lakini utashushwa mpaka kuzimu, Mpaka pande za mwisho za
shimo.
Kila Kitu Alichopewa Mwanadamu
Kila kitu ambacho Shetani alitaka chini ya uasi wake,
Mungu alimuumba mwanadamu!
􀂱 Shetani alisema, “Nitapaa mbinguni.”
Mwanadamu aliumbwa awe na ushirika na Mungu.
Tuliumbwa kutembea na kuongea na Mungu! Tuliumbwa
kutawala pamoja Naye.
Ufunuo Wa Yohana 20:6 Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na
sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina
nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao
watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.
􀂱 Shetani alisema, “Nitainua enzi yangu juu ya nyota za
Mungu.”
Nyota za Mungu ni malaika. Shetani alitamani awe juu ya
malaika katika umuhimu.
Mtume Paulo aliandika kuwa siku moja tutatoa hukumu
kwa malaika.
1 Wakorintho 6:2, 3 Au hamjui ya kwamba watakatifu
watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu tahukumiwa na
ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo? Hamjui ya
kuwa tutawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya
maisha haya?
􀂱 Shetani alisema, “Pia nitaketi kwenye mlima wa
mkusanyiko upande wa kasikazini.”
Tumeketi katika mbingu katika Yesu.
Waefeso 2:6 ... akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja
naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;
􀂱 Shetani alisema, “Nitapaa juu ya mawingu kabisa”
Tutakutana na Yesu hewani – katika mawingu.
22
1 Wathesalonike 4:16, 17 Kwa sababu Bwana mwenyewe
atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya
malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika
Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia,
tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tutakuwa pamoja
hewani; na Bwana milele.
􀂱 Shetani alisema, “Nitakuwa kama Yeye aliye Mkuu.”
Mwanadamu aliumbwa katika mfano wa Mungu. Je, bado
una shaka kwa nini Shetani anamchukia mwanadamu?
Tumeumbwa ili:
􀂱 Tuwe kama Mungu
􀂱 Kuongea kama Mungu
􀂱 Kutembea kama Mungu na
􀂱 Kutawala pamoja na Mungu!
Itakuwa yenye fedheha kiasi gani kwa Shetani kuwa
tumepewa vyote alivyokuwa akinyakua katika uasi wake.
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Eleza katika maneno yako mwenyewe, asili ya dunia, kuanguka kwa Shetani na hukumu
iliyofuatia katika dunia.
2. Eleza jinsi Mungu alivyofanya katika utawala na mamlaka alipoiumba dunia tena.
3. Eleza kwa nini Shetani anakuchukia. Nini umefanya kilichosababisha chuki hiyo?
23
Somo La Tatu
Mpango wa Hila ya Shetani
Shetani aliona kuwa Adamu na Hawa, na bila shaka
wanadamu wote, walipewa uzima na hali aliyokuwa nayo
Mungu. Shetani lazima alijawa na hofu kuwa mwanadamu
sasa alikuwa na mamlaka juu vyote duniani.
Mwanadamu alionekana kama Mungu. Alitenda kama
Mungu. Chuki yote aliyokuwa nayo Shetani juu ya Mungu,
alimgeukia mwanadamu. Hakupenda kumwona
mwanadamu akifaulu. Kwa hivyo, Shetani mwenyewe
aliunda mbinu yake!
MPANGO WA SHETANI
Hila
Shetani aliwadanganya malaika mbinguni, na theluthu moja
waliwafuata katika uasi. Alijulikana kwa kuhadaa.
Mungu alimpa mwanadamu uhuru wa kuchagua –
wangeweza kuchagua kutii au kutotii. Katika uhuru huo wa
kuchagua, alitoa pia adhabu ya kutotii.
Mwanzo 2:17 ... walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na
mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo
utakufa hakika.”
􀂱 Alijibadilisha
Alimwuliza Mungu
Shetani alichagua kujibadilisha mwenyewe kama nyoka ili
aingie katika bustani bila kugunduliwa. Hakuwa na ruhusa
kuwa katika bustani na Adamu angemrusha nje kama
Shetani angeingia kwa ujasiri bila kujibadilisha.
Mwanzo 3:1a Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama
wote wa mwitu aliofanya BWANA Mungu.
“erefu” ina maana mwongo au mjanja.
Shetani alikuwa ndani ya mwili wa nyoka alipoongea na
Hawa. Mapepo hukalia mili hata sasa. Hiyo ndiyo hali yao
danganyifu na inayowakilisha uovu wanaotaka kutenda.
Mwanzo 3:1b Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo
alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?”
Shetani aliuliza kuhusu kile Mungu alisema, na kwa wakati
huo aliacha adhabu ya dhambi.
24
􀂱 Alimnukulu Mungu
Ngundua kuwa Shetani anayanukulu maneno ya Mungu ili
kuyabadilisha kwa uwongo wake.
Mwanzo 3:2, 3 Mwanamke akamwambia nyoka,
Matunda ya miti ya bustani twaweza kula; “lakini
matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu
amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.” Hawa
akaongeza “guza” kwa kile Mungu alinena kwa kweli,
lakini bado alikumbuka adhabu.
􀂱 Uwongo wa Shetani
ms. 4b “Hakika hamtakufa.”
Shetani alisema kinyume na kile Mungu alisema, lakini
Hawa aliendelea kusikiliza. Kisha Shetani aliahidi
mshahara wa dhambi.
􀂱 Utakuwa kama Mungu
ms. 5 “Kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula
matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa
kama Mungu, mkijua mema na mabaya.”
Shetani aliwaambia Hawa na Adamu, “macho yako
yatafunguka na utakuwa kama Mungu!” walikuwa kama
Mungu lakini Shetani aliwadanganya katika kujitakia zaidi.
ADAMU NA HAWA WALITENDA DHAMBI
Wote Walitenda Dhambi
Mara nyingi, tunamwona Hawa pekee wakati Shetani
alijibadili kuwa nyoka na kumjia. Biblia haisemi hivyo.
Katika msitari wa sita, tunasoma “Pia alimpa mume wake
aliyekuwa naye, na akala.”
Wote waliacha kufuata Neno la Mungu, wakafuata hisia
zao, wakamsikiliza Shetani, na kula tunda.
ms. 6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula,
wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi
alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe naye
akala.
Wakati Adamu na Hawa walimwasi Mungu na kula tunda,
hali Yake Mungu iliondoka ndani yao. Walikuwa
wameviswa katika utukufu mkuu – hali ya Mungu – sasa
wakawa uchi.
Kwa kutumia mti wa ufahamu wa mema na mabaya,
Shetani aliwadanganya Adamu na Hawa, kuwahadaa na
kuwashinda.
Shetani hajabadilika. Mbinu zake ni zile zile hata sasa!
25
Waliachwa
􀂱 Kushindwa
􀂱 Uchi
Shetani aliwadaganya, na mwanadamu akatolewa maficho
yake, utawala na mamlaka.
Mwanzo 3:7 Wakafumbuliwa macho, wote wawili wakajijua
kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
􀂱 Wenye Hofu
􀂱 Kujificha
Shetani aliwashinda Adamu na Hawa. Sasa, waliokuwa
watawala wa ulimwengu walikuwa waoga na kujificha
nyuma ya kichaka!
Mwanzo 3:10 Akasema, “Nalisikia sauti yako bustani, nikaogopa
kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.”
􀂱 Bado katika Sura Ya Mungu
Ni vyema kuelewa kuwa hata baada ya Adamu na Hawa
kutenda dhambi bado walikuwa katika mfano wa Mungu.
Hata hivyo, hawakuwa na uzima wa Mungu ndani yao.
Walikuwa wamekufa kiroho.
Mwanzo 9:1,2,6 Mungu akambariki Nuhu na wana-we,
akawaambia, “zaeni, mkao-ngezeke, mkaijaze nchi” Kila mnyama
wa katika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa
angani; pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki
wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu.” “Atakayemwaga
damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na
mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya
mwanadamu.”
Mwanadamu alikuwa bado:
􀂱 Azae Matunda
􀂱 Ongezeka
􀂱 Jaza Dunia
􀂱 Kuilinda
􀂱 Kuwa na mamlaka na kutawala
Sasa, hii itafanyika kwa maumivu, kwa jasho lake, na
viumbe vyote vitaishi katika hofu ya mwanadamu.
Rudia
Mungu alimwumba Adamu na Hawa kuitawala dunia.
Lakini, baada ya mwanadamu kuasi Mungu na kukosa kutii
kinyume na matakwa ya Mungu, alikufa kiroho.
Alinyang’anywa mamlaka na utawala wa Mungu.
26
Mapenzi ya Mungu yalikuwa ya waume na wake
wawe na mamlaka na utawala.
Mapenzi ya Shetani yalikuwa mwanadamu kuasi
mbele za Mungu.
Adamu na Hawa walikuwa na uamuzi wa kufanya –
walikuwa na uwezo wa kuchagua.
Waliamua kuegemea upande wa Shetani.
Shetani aliiba kutoka kwa Adamu vyeo:
mtawala wa dunia hii,
mwana wa kiume wa mfalme wa dunia hii.
BAADA YA MWANADAMU KUTENDA DHAMBI
Laana Zilizofuata
􀂱 Kwa Nyoka
Kwa vile nyoka alimruhusu Shetani kuutumia mwili wake,
laana iliwekwa kwa nyoka wote.
Mwanzo 3:14 BWANA Mungu akamwambia nyoka, kwa sababu
umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na
kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda,
na mavumbi utakula siku zote za maisha yako.”
􀂱 Kwa Mwanamke
Palikuwa na aina mbili za laana iliyowekwa kwa
mwanamke. Atazaa watoto katika maumivu na
mwanamume atamtawala.
Mwanzo 3:16 Akamwambia mwanamke, “Hakika nitakuzidishia
uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na
tama yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.”
Mwanamke anapomkubali Yesu kama mwokozi wake wa
pekee, anapokea tena nafasi yake katika uumbaji. Yesu
alifanyika laana kwa niaba yake.
Wagalatia 3:13 Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa
kuwa alitukomboa katika laana kwa ajili yetu; maana
imeandikwa, (“Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti.”)
27
􀂱 Kwa Mwanamume
Laana iliyowekwa kwa mwanamume ni kuwa kwa
maumivu atailima ardhi ili kupata chakula.
Mwanzo 3:17 Akamwambia Adamu, “Kwa kuwa umeisikiliza
sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza,
nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu
utakula mazao yake siku zote za maisha yako.”
􀂱 Kwa Dunia
Dunia pia ililaaniwa.
ms. 18,19 Michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga
za bondeni; kwa jasho utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo
ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini
utarudi.
􀂱 Kwa Shetani
Kwa wakati ambao Shetani alipata ushindi mkuu juu ya
mwanadamu, Mungu alitaja laana juu yake.
Mwanzo 3:15 Nami nitaweka uadui kati yako na huyo
mwanamke, na kati ya uzao wake; huo utakuponda kichwa, na
wewe utamponda kisigino.
Mungu alinena na Shetani, aliyekuwa ndani ya nyoka, na
kumwambia kuwa mbegu ya mwanamke itakiponda kichwa
chake.
Ahadi ya Kukombolewa!
Laana iliyowekwa juu ya Shetani pia ilikuwa ahadi ya
kwanza ya kuja kwa Masiya. “Mbegu” ilikuwa unabii juu
ya Yesu atakayezaliwa na Mwanamke.
Shetani ni sharti awe chini ya miguu ya Yesu. Kichwa
chake kitapondwa na kuchubuka.
Mifano ya Baadaye/Usoni
Katika historia ya kuanguka kwa mwanadamu kuna aina
nyingi, au mifano, ya usoni.
􀂱 Tawi la Mzabibu
Matawi ya mzabibu ambayo Adamu na Hawa walitumia
kujifunika yalikuwa mifano ya jaribio la mwanadamu
kufunika dhambi zake mwenyewe. Ni mifano ya dini
zilizoundwa na mwanadamu.
􀂱 Wanyama Kuchinjwa
Kumwagika kwa damu ya kwanza kulifanywa na Mungu ili
kuwafunika Adamu na Hawa. Hii ilikuwa dalili ya, au
mfano wa Yesu ambaye atauliwa kama malipo ya dhambi
za ulimwengu wote.
28
Mpango wa Mungu
Hata katika sehemu ya giza kabisa katika historia ya
mwanadamu, Mungu alikuwa na mpango wa wokovu kwa
mwanadamu.
Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, katika uamuzi Wake,
atatoa maisha yake kwa ajili yetu.
Kwa kifo Chake, atamshinda Shetani. Shetani atakigonga
kisigino cha Yesu, lakini Yesu atakiponda kichwa cha
Shetani. Mamlaka ya Shetani yatapondwa na kurejeshewa
mwanadamu kulingana na mpango wa Mungu wa awali.
MPANGO WA SHETANI
Uwongo wa Shetani
Shetani hajaacha kumchukia na kuwaogopa wanadamu
walioumbwa kuonekana na kutenda kama Mungu. Mpango
wake wa uwongo haujaisha. Katika uwongo, viongozi wa
kiroho kila mara wamepoteza uwezo wao. Wamekuwa
viongozi vipofu wongozao vipofu.
Kazi ya Shetani
Shetani ameandaa jeshi lake katika mpango wa vita kamili.
Viongozi wa giza wamewekwa kwa kila nchi, kila
mwanamume, mwanamke na mtoto, ili kuwaweka katika
ufungwa. Maagizo yao ni kuiba, kuua na kuharibu.
Mungu aliileta sheria kwa wanadamu ili wawe na msamaha
wa dhambi na kutembea katika uhusiano naye. Lakini kwa
miaka elfu nne Shetani aliishi akiitawala dunia kwa sababu
ya uasi wa mwanadamu.
Watu walioumbwa kuitawala dunia hii walikuwa:
vipofu na waombao kando ya barabara,
wamefungwa na pepo za udhaifu,
wamepagawa na jeshi la mapepo.
Nyuso na mili, zilizoumbwa kuonekana kama
Mungu,
zimeliwa na ukoma unaotisha.
Waume na wake walioumbwa ili kutawala waliishi
katika kushindwa!
29
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Eleza kwa nini Shetani anawachukia sana viumbe waitwao wanaume na wanawake.
2. Eleza matokeo ya kuanguka kwa mwanadamu na dhambi.
3. Je, ahadi ya Mungu ya kukombolewa ilikuwa nini kama inavyoonyeshwa katika Mwanzo 3:15?
30
Somo La Nne
Kisha akaja Yesu – Mpango wa Mungu
ADAMU WA KWANZA – ADAMU WA MWISHO
Mungu alimtuma Mwanawe
Wakati Adamu na Hawa walitenda dhambi, Mungu aliahidi
kumtuma Mwanawe, mbegu ya mwanamke, kukiponda
kichwa cha Shetani. (Mwanzo 3:15) Paulo anaeleza kuhusu
kitendo hiki huku akilinganisha na ahadi ya kwanza ya
Mkombozi.
Wagalatia 4:4, 5 hata ulipokuwadia utimilifu wa wakati, Mungu
alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa chini ya sheria, kusudi
awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate
kupokea hali ya kuwa wana.
Uhusiano kati ya mwanadamu na Mungu na mamlaka yake
ungerejeshwa na dhabihu ambayo Yesu angefanya
alipokufa msalabani.
Kukombolewa kutoka dhambini, ni adhabu, na matokeo ya
laana kutokana na sheria, mwanadamu anaweza kuzaliwa
upya katika jamaa ya Mungu. Anaweza kufanyika kiumbe
kipya. Anaweza tena, kupokea Roho wa Mungu ndani yake.
Adamu Alileta Dhambi
Dhambi ilikuja ulimwenguni kupitia kuasi kwa Adamu.
Warumi 5:12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia
ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti
ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi…
Yesu Alileta
􀂱 Haki
Kupitia kutii kikamilifu kwa mtu mmoja, Yesu, wengi
wanaweza kufanyika wa haki.
ms. 19 Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu
wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa
kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya
wenye haki.
􀂱 Habari Njema
Baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi, walipogundua
Mungu anawaendea, walijificha nyuma ya vichaka. Sasa
Yesu, Mwana wa Mungu alikuwa akija na malaika
wakasema, “Usiwe na hofu! Hii ni habari njema kwenu.”
31
Luka 2:10, 11 “Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi
ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu
wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu,
Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.”
􀂱 Amani kwa Wanadamu
Malaika mmoja akaanza habari kwa wachungaji katika
milima ya Bethlehemu usiku ule, lakini furaha mbinguni
ilipita kifani, hali ya kiroho ilipasuka katika hali ya asili.
ms. 13, 14 Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika wingi wa
jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema. Atukuzwe
Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu
aliowaridhia!”
Je, ni ahadi njema iliyotolewa, hata wakati Kristo
alipozaliwa. “Ulimwenguni amani, wema kwa wanadamu!”
Hakuna maneno ya kueleza furaha iliyokuwa
ulimwenguni kote.
Malaika walikuwa na furaha sana
Wakaimba nyimbo za sifa mbele ya wachungaji.
hata nyota walitangaza kuzaliwa Kwake!
YESU ALIFANYA KAZI ULIMWENGUNI KAMA MWANADAMU!
Je, Yesu alitenda katika mamlaka na uwezo alipokua hapa
duniani kama Mungu, au kama mwanadamu – katika nguvu
za Roho Mtakatifu?
Yesu, Adamu wa Mwisho
Paulo alimtaja Yesu kama Adamu wa Mwisho.
1 Wakorintho 15:45 Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza,
Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye
kuhuisha.
Yesu, kama Adamu wa mwisho, alitembea na kuhudumu
katika mamlaka hapa duniani kama vile alivyomuumba
Adamu wa kwanza kutenda.
Ni muhimu kuelewa haya kwa sababu ni kupitia kutimiza
sheria kama Adamu wa Mwisho angeweza kutuletea uhuru
kutokana na sheria. Ni kwa kuwa mwanadamu tu angeweza
kufanyika Mwokozi wetu. Ilikuwa vyema amshinde
Shetani, kama mwanadamu, ili kurejesha mamlaka ambayo
Shetani alikuwa ameiba kutoka kwa Adamu wa Kwanza.
Kwa maana Yesu ndiye alikuwa mwanadamu wa kwanza
aliye mkamilifu baada ya Adamu wa kwanza, alikuwa na
32
mamlaka aliyopewa Adamu. Wakati Roho Mtakatifu
alipokuja juu Yake, alikuwa na nguvu za Mungu ndani
Yake.
Ubatizo wa Yesu
􀂱 Roho Alishuka juu Yake
Yohana Mbatizaji aliona Roho wa Mungu akishuka juu ya
Yesu na tukio hili lilikuwa la muhimu hata likaandikwa
katika Injili zote nne (Mariko 1:10, Luka 3:22, Yohana
1:32).
Mathayo3:16 Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda
kutoka majini, na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho
wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake.
􀂱 Miujiza Kutendeka
Yesu, hakutenda miujiza yoyote kwa miaka thelathini ya
kwanza ya maisha Yake, lakini alipokuwa akianza huduma
ya wazi Roho Mtakatifu alishuka juu Yake. Na, katika
nguvu za Roho Mtakatifu, huduma Yake ya miujiza ilianza.
Mamlaka ya Mungu ikitenda kazi na Roho wa Mungu ni
vitu viwili vyenye nguvu katika ushindi!
Yesu aliacha Haki Yake kama Mungu
􀂱 Alijitoa Kabisa
Mtume Paulo anatupa mawazo katika mambo ya Kristo
alivyokuja hapa duniani. Paulo aliandika kuwa Yesu
aliweka kando hali Yake kama Mungu.
Wafilipi 2:5-8 Iwenii na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo
ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo
alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa
na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya
kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana
mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama
mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam,
mauti ya msalaba.
Yesu alikusudia:
􀂱 Azushwe na kutokuwa na heshima
􀂱 Kuchukua mfano wa mtumishi
􀂱 Kuja katika mfano wa mwanadamu
􀂱 Kunyenyekea
􀂱 Kutii hadi akafa
Yesu alikuwa na asili ya Mungu, na alikuwa sawa na
Mungu na bado, alijinyima katika haki zake zote kama
Mungu, ili kutumika hapa duniani kama mwanadamu.
Alichukua juu Yake mfano wa mtumishi na umbo la
mwanadamu. Alinyenyekea na kutii hadi kufa. Alikuja
33
ulimwenguni kama mwanadamu na nguvu zake hapa
duniani zitakuja katika Roho Mtakatifu.
Kwa nini hii ilikuwa muhimu?
Adamu, mwanadamu wa kwanza, alimuasi Mungu na
akatoa mamlaka yake kwa Shetani. Yesu, kama Adamu wa
Mwisho, atafanya kila kitu hapa duniani kama mwanadamu
aliyetiwa nguvu na Roho wa Mungu. Yeye atakuwa
mwanadamu aliyekamilika akitenda kazi hapa duniani
kama vile Adamu alivyoumbwa kutenda.
Kama Mwana wa Adamu
Wakati Yesu alikuwa hapa duniani, mamlaka aliyotumia
yalikuwa katika Mwana wa Adamu. Katika kifungu
kifwatacho, Yohana alitumia maneno yaliyo kamili kabisa:
“Mwana wa Mungu” – “Mwana wa Adamu.”
Yohana 5:25-27 Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa
ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale
waisikiao watakuwa hai. Maana kama vile Baba alivyo na uzima
nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima
nafsini mwake. Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa
sababu ni Mwana wa Adamu.
Wafu wataisikia sauti ya Mwana wa Mungu. Nje ya dunia
hii, Yesu alitenda kama sehemu ya utatu wa Mungu.
Duniani, Yesu alitembea katika mamlaka kwa sababu
alikuwa Mwana wa Adamu. Mwanadamu aliumbwa ili
kutembea katika mamlaka na utawala. Alikuwa Yesu
mwanadamu aliyekuwa na mamlaka. Ni kwa sababu
alikuwa Mwana wa Adamu, Adamu wa Mwisho, sio kwa
sababu alikuwa Mwana wa Mungu.
Ikiwa Yesu alitenda,
Basi nasi Tunaweza Kutenda Pia!
Yesu alifanya tu kile ambacho mwanadamu aliumbwa
kutenda duniani. Alitembea katika nguvu za Roho
Mtakatifu, na wala si kwa nguvu za Mwana wa Mungu!
Hii ni muhimu sana kwetu! Ikiwa Yesu alitembea kama
mwanadamu hapa duniani, basi pia tunaweza kufanya
hivyo. Tunazo nguvu zile, mamlaka, na haki ya kutenda
yote ambayo Yesu alitenda alipokuwa hapa duniani kama
Mwanadamu .
34
ALIJARIBIWA KAMA MWANADAMU
Kujaribiwa kama Sisi
Mungu aliwapa Adamu na Hawa hisia za uhuru, kuchagua.
Yesu alikuwa na uwezo huo pia. Ili afanyike Adamu wa
Mwisho kabisa, ilimbidi Yesu ateswe katika majaribu pia.
Adamu na Hawa walijaribiwa katika sehemu tatu:
􀂱 Mwili – Hawa aliona tunda, kuwa lilikuwa nzuri kwa
chakula
􀂱 Nafsi – Shetani alimwahidi hekima, kubaini kati ya
mema na mabaya
􀂱 Roho – Mwishowe Shetani alimwahidi atakuwa kama
Mungu.
Yesu alijaribiwa katika sehemu hizi tatu.
Jaribio la Kwanza – Mwili
Yesu alikuwa jangwani kwa siku arubaini. Shetani
alimjaribu, wakati huu wa udhaifu wa mwili, kumjaribu
Yesu ili azitumie nguvu Zake kama Mwana wa Mungu
kuyatosheleza mahitaji ya mwili wake kama mwanadamu.
Lakini Yesu aliweka kando hali ya Mungu alipokuja hapa
duniani na kutenda kama Mwana wa Adamu.
􀂱 Kutosheleza Mahitaji ya Mwanadamu
Mathayo 4:1-3 Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili
ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku,
mwisho akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia, “Ukiwa
ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe
mikate.”
Mjaribu alipomjia, alisema, “kama wewe ni Mwana wa
Mungu, jionyeshe, chukua haki zako kama Mungu. Kama
wewe ni Mwana wa Mungu, amuru kuwa mawe haya yake
mikate.”
Kama Yesu angebadili mawe yawe mkate, hangetenda
kama mwanadamu. Angetumia hali yake kama Mungu.
Kama angefanya hivyo, Shetani angeshinda Adamu wa
Kwanza na Adamu wa Mwisho.
􀂱 Yesu Alijibu
Yesu alimjibu Shetani kwa kunukulu Neno la Mungu.
Mathayo 4:4 Naye akajibu akasema, Imeandikwa, “Mtu hataishi
kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha
Mungu.”
Gundua kuwa Yesu alijitambulisha kama mwanadamu.
35
ms. 5 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu akamweka
juu ya kinara cha hekalu.
Jaribio la Pili – Nafsi
Jaribio la pili lilikuwa katika sehemu ya nafsi. Shetani
alimjaribu Yesu atende kinyume na mapenzi ya Mungu
katika maisha na kutenda katika hisia Zake.
􀂱 Jidhihirishe
ms. 6 ... akamwambia, “Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe
chini, kwa maana imeandikwa Atakuagizia malaika zake; Na
mikononi mwao watakuchukua; usije ukajikwaa mguu wako
katika jiwe.”
Hii ilikuwa kuendeleza majaribu hayo hayo ya kimsingi.
“Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu …” Shetani alijua Yeye
alikuwa Mwana wa Mungu. Maisha ya Yesu hapa duniani
yalikuwa aishi kama Mwana wa Adamu, Adamu wa
Mwisho.
􀂱 Yesu Alijibu
Yesu alimshinda Shetani kwa kunena Neno la Mungu kwa
kweli. Yesu alifahamu alikuwa Bwana na Shetani alijua
hivyo.
ms. 7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, “ Usimjaribu Bwana
Mungu wako”
Jaribio la Tatu – Roho
Katika jaribio la tatu, Shetani, alimpa Yesu falme zote hapa
duniani. Je, hiyo haikuwa sababu Yesu alikuja hapa
duniani? Kwamba alikuja kuishinda na kuitwaa dunia
kutoka kwa Shetani?
􀂱 Awe Mungu wa Dunia Hii
Mathayo 4:8,9 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu
mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
akamwambia, “Haya yote nitakupa, ukianguka kunisuhudia..”
Shetani alikuwa na haki ya kumpa Yesu tawala hizi.
Shetani, baada ya kudanganya na kuiba mamlaka ya
Adamu, basi alikuwa mtawala wa dunia hii.
Lakini Yesu hakutaka kuirejesha dunia tena kutoka kwa
Shetani katika hali yoyote yenye kumuasi Baba.
􀂱 Yesu Alijibu
Yesu hakuingia katika mjadala na Shetani. Yeye
hakubishana naye kuhusu nani aliyetawala dunia hii. Yesu
alimwambia aondoke. Alinena Neno la Mungu tena.
Mathayo 4:10 Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani;
kwa maana imeandikwa, “Msujudie Bwana Mungu wako,
umwabudu yeye peke yake.”
36
Rudia
Kama Yesu angetenda kama Mwana wa Mungu jinsi
alivyojaribiwa na Shetani, Yeye angepoteza haki zake kama
Mwana wa Adamu. Yeye hangefanyika tena kuwa dhabihu
kamili yenye kumkomboa mwanadamu.
Shetani akampa Yesu kile kitu Yesu alikuja kurejesha –
haki ya kuitawala dunia hii. Ingekuwa “rahisi” kabisa sana
kuifanya njia ya Shetani – bila kufa msalabani. Yesu alijua
kuwa pasipo kumwagika damu Yake hapana msamaha wa
dhambi.
Hata wakati Yesu alipokuwa akifa msalabani, Shetani,
kupitia watu, walimdhihaki kwa maneno hayo hayo.
Mathayo 27:40 ...Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga
kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe Mwana wa
Mungu, shuka msalabani.
Mara nyingi, Shetani atatoa kwetu vitu ambavyo Mungu
ametuahidi. Kile tunatakiwa kufanya ni kukubali tu kwa
sehemu fulani. Mbinu ya kumshinda ni kujua na kunena
Neno la Mungu.
YESU, MFANO WETU WA KUPINGA MAJARIBU
Yesu Anaelewa Majaribu
Kama vile hadithi ya kujaribiwa kwa Yesu inavyoelezwa
katika Mathayo tunapewa fursa ya kujifunza jinsi Shetani
anavyoweza kushindwa katika sehemu hii. Pia tunao uhuru
wa kuamua. Pia tutajaribiwa, lakini Yesu alipoondoka
katika ushindi – pia nasi tunaweza!
Paulo anataja kuwa; kwa kuwa Yesu ameteswa kwa
kujaribiwa, anaweza kuwasaidia wale wanaojaribiwa.
Waebrania 2:18 Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa
alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.
Yesu Alijaribiwa Kama Sisi
Tunaweza kupata ujasiri katika kujua kuwa Yesu
alijaribiwa katika kila hali kama vile sisi tunaweza kuwa.
Kama vile hakushindwa katika majaribu, hata sisi tunaweza
kuenda mbele za Mungu na kupata msaada Wake mkuu
katika kuyashinda majaribu.
Waebrania 4:14-16 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia
katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana
maungamo yetu. Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza
kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye
alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya
dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili
37
tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa
mahitaji.
Majaribu Yote Ni Ya Kawaida
Mojawapo ya mbinu za Shetani ni kutufanya sisi tujihisi
kuwa tu tofauti, kuwa majaribu yetu ni ya kipekee, au
ngumu zaidi ya yale wengine wanapitia. Lakini majaribu
yote ni ya kawaida na Mungu ametoa kwetu njia ya
kuyaepuka ili tuweze kushinda.
1 Wakorintho 10:13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo
kawaida ya mwanadamu, ila Mungu ni mwaminifu, ambaye
hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile
jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
Fuata Mfano wa Yesu
Yesu ni mfano wetu. Kama vile Yesu alipomjibu Shetani
kwa kutumia Neno la Mungu, pia inatupasa kufanya hivyo.
Shetani alipomjia Yesu, Yesu haku
􀂱 bishana na Shetani
􀂱 waza na Shetani
􀂱 fikiri kutenda njia ya Shetani
Yesu alinukulu Neno la Mungu lililoandikwa.
Mathayo 4:4 Naye akajibu akasema, “Imeandikwa, Mtu hataishi
kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha
Mungu.”
Hivyo ndivyo Shetani hushindwa. Neno la Mungu ni sharti
liwe kwenye vinywa vyetu.
Magonjwa yanapotujia miilini mwetu, tunaweza kusema,
“imeandikwa, “kwa mapigo yake nimepona.”
Umaskini unapokuja kinyume na fedha zetu, tunaweza
kusema, “imeandikwa, ‘Mungu wangu atakutana na
mahitaji yangu yote ...'”
Shetani anapojaribu kuwapotosha watoto wetu, tunaweza
kusema ““imeandikwa, ‘Watoto wangu wote watafunzwa
katika Bwana...'”
38
Nena suluhisho – wala si matatiza.
Nena majibu – wala si mahitaji,
Nena na kuamini Neno la Mungu,
naye Shetani atakuwa:
jumla,
kabisa,
kamwe,
ameshindwa!
Nawe utakuwa mshindi!
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Je, kwa nini ni muhimu kwako wewe kujua kuwa Yesu aliacha haki zake kama Mungu na
akaishi na kutenda kama mwanadamu alipokuwa ulimwenguni?
2. Je, ni mfano gani unaweza kutoa kuhusu Yesu akitenda katika mamlaka ya mwanadamu akiwa
ulimwenguni?
3. Kufuatia mfano wa Yesu, je, unaweza kumshinda vipi Shetani au pepo zake wanapokujaribu ili
usimtii Mungu?
39
Somo La Tano
Yesu Alihudumu katika Mamlaka
MPANGO WA MUNGU KWA WAAMINI WOTE
Yesu, Kama Mwanadamu
Yesu alitenda hapa duniani kama mwanadamu. Alijitoa
katika haki zote kama Mungu. Aliteswa katika majaribu
kama mwanadamu na alimshinda Shetani.
Alikuwa Yesu wa kibinadamu aliyekuwa na mamlaka hapa
duniani. Mamlaka Yake ni kwa sababu alikuwa Mwana wa
Adamu, Adamu wa mwisho, wala si kwa sababu alikuwa
Mwana wa Mungu.
Yesu alikuja kama Adamu wa Mwisho ili kutimiza yote
ambayo Mungu alikusudia alipomuumba Adamu wa
Kwanza awe. Kutimiza mpango wa Mungu kwa Adamu wa
Kwanza, Yesu alitembea katika mamlaka kamili na utawala
hapa duniani.
Ni vyema kuelewa mamlaka ambayo Yesu alitumia. Kama
mamlaka haya ni mamlaka ambayo Mungu, katika kuumba,
alimpa mwanadamu, basi tunaweza kutembea katika
mamlaka hayo hayo leo kama waume kwa wake
waliokombolewa.
Luka 10:19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge,
na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.
Ni kupitia tu, kuwa viumbe vipya katika Yesu tunaweza
kufanyika waume kwa wake tulioumbwa kuwa katika
mpango wa Mungu. Kama tunavyosoma katika Injili na
kuona Yesu akitembea kama mwanadamu aliyekamilika
ndipo tunaweza kuelewa mpango wa Mungu katika kuishi
kwetu na kutembea katika mamlaka na uwezo kamili kila
siku ya maisha yetu.
LUKA AELEZA KUHUSU MAMLAKA YA YESU
Ujumbe wa Kwanza
􀂱 “Katika Nguvu za Roho Mtakatifu”
Yesu alipobatiswa katika mto Yordani, Roho Mtakatifu
alikaa juu Yake na kumtia nguvu kwa huduma Yake
duniani. Mara tu baada ya haya, Aliongozwa hadi jangwani,
ambapo alimshinda Shetani na majaribu yake kwa kunena
Neno la Mungu. Kwa kuonyesha mamlaka Yake hapa
40
duniani kama mwanadamu aliyejazwa Roho Mtakatifu,
alikuwa tayari kuanza huduma Yake hapa duniani.
Alianza huduma hii Galilaya, akiwa na nguvu za Roho
Mtakatifu na kunena katika mamlaka.
Luka 4:14,16,18-21 Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda
Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.
Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia
katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili
asome.
“Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta
kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia
wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena,
Kuwaacha nuru waliosetwa.”
Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Akakifunga
chuo, akarudishia mtumishi, akaketi; na watu wote
waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. Akaanza
kuwaambia, “ Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.”
(Yesu alikuwa akisoma Isaya 61:1,2)
Ujumbe Wa Pili
Baada ya Yesu kunena Nazareti, alinena akiwa
Kapernaumu. Hapo watu walishangaa na mamlaka Yake.
􀂱 Alikuwa na Mamlaka
Luka 4:31, 32 Akashuka mpaka Kapernaumu, mji wa Galilaya,
akawa akiwafundisha siku ya sabato; wakashangaa mno kwa
mafundisho yake, kwa kuwa neno lake lilikuwa na uwezo.
􀂱 Mapepo Kutolewa
ms. 33-35 Na ndani ya sinagogi mlikuwa na mtu mwenye roho ya
pepo mchafu, akalia kwa sauti kuu, akisema, Acha! Tuna nini
nawe, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Nakujua u
nani Mtakatifu wa Mungu!”
Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, mtoke. Ndipo yule
pepo akamwangusha katikati, akamtoka asimdhuru neno.
Yesu aliamuru pepo kutoka, na kwa sababu lilitambua
mamlaka ya Yesu, lilitoka.
􀂱 “Mamlaka na Uwezo”
ms. 36 Mshango ukawashika wote, wakasemezana wakisema,
“Ni neno gani hili, maana awaamuru pepo wachafu kwa uwezo
na nguvu, nao hutoka.”
41
MAMLAKA YA YESU JUU YA MAPEPO –UGONJWA –MITI – DHORUBA
Mariko pia aliandika kuhusu huduma ya Yesu Kapernaumu
na watu wakashangazwa juu ya mamlaka aliyoonyesha.
Mariko aliendelea na kutaja juu ya wenye pepo na watu
wagonjwa wakipona.
Mamlaka Juu Ya Mapepo
Yesu alikuwa na mamlaka juu ya mapepo.
ms. 40,41 Na jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa na
wagonjwa wenye maradhi mbali mbali waliwaleta kwake,
akaweka mikono yake juu ya kila mmoja akawaponya. Pepo nao
waliwatoka watu wengi, wakipiga kelele na kusema, Wewe u
Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa
sababu walimjua kuwa ndiye Kristo..
Mamlaka Juu Ya Magonjwa Yote
Yesu alikuwa na mamlaka juu ya magonjwa yote.
Marko 1:40,41 Akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi na
kumpigia magoti, na kumwambia, “Ukitaka, waweza
kunitakasa.”
Naye akamhurumia, akanyosha mkono wake,
akamgusa, akamwambia, “Nataka, takasika.”
Mamlaka Juu Ya Mwili wa Mwanadamu
Yesu alinena na mtu aliyekuwa na mkono uliopinda.
“Nyosha mkono wako!”
Marko 3:1-3 Akaingia tena katika sinagogi, na palikuwako huko
mtu mwenye mkono uliopooza; wakamvizia ili kuona kama
atamponya siku ya sabato; wapate kumshitaki. Akamwambia
yule mtu mwenye mkono uliopooza, “Simama katikati.”
Yesu alijua mtu huyo atapona. Alisema, “Piga hatua
mbele.”
ms. 4,5 Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema au
kuiua? Wakanyamaza. Akawakazia macho pande zote kwa
hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao,
akamwambia yule mtu, “Nyosha mkono wako.” Naye
akaunyosha, mkono wake ukawa mzima tena.
Kwa mamlaka, Yesu alinena neno na mtu huyo akanyosha
mkono wake na akapona.
42
Mamlaka Juu Ya Viumbe
􀂱 Kulaani Mti wa Mizabibu
Yesu alikuwa na mamlaka juu ya mzabibu.
Mathayo 21:19 Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea,
asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, “Yasipatikane
matunda kwako tangu leo hata milele,” Mtini ukanyauka mara
Mamlaka Juu Ya Vitu
􀂱 Alituliza Dhoruba
Yesu alinena kwa upepo na bahari katika mamlaka na
vikamtii.
Marko 4:35-38 Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na
tuvuke mpaka ng’ambo.
Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika
chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye. Ikatokea
dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata
kikaanza kujaa maji. Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri,
amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu,
si kitu kwako kuwa tunaangamia?”
Yesu alikemea upepo na akanena na bahari.
ms. 39,40 Akaamka, akaukemea upepo, ukakoma, kukawa
shwari kuu.
Akawaambia, “Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado?”
Yesu alimaanisha kuwa, “Kwa nini mliogopa? Mngetuliza
dhoruba. I wapi imani yenu?”
ms. 41 Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, “Ni nani huyu,
basi, hata upepo na bahari humtii!”
YESU, MFANO WETU
Yesu ni mfano wetu kuhusu jinsi tunavyotembea na
kuhudumu katika mamlaka. Kazi Yake hapa duniani kama
Adamu wa Mwisho ni mfano jinsi sisi, kama wanadamu
waliokombolewa na kurejeshwa, tunaweza kufanya kazi ya
Yesu leo. Tunatakiwa kuishi na kuhudumu katika mamlaka
aliyokuwa nayo Yesu tunapotenda kazi Zake.
Yohana 14:12 Amin amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi,
kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya, naam, na kubwa
kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
43
Yesu Alikemea Homa
Yesu alinena kwa ujasiri alipokemea homa kwa mamaye
mkewe Petro.
Luka 4:38,39 Akatoka katika sinagogi, akaingia katika nyumba
ya Simoni. Naye mkewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa
ameshikwa na homa kali, wakamwomba kwa ajili yake.
Akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, ikamwacha; mara
hiyo akaondoka, akawatumikia.
Kumfufua Lazaro
Yesu alinena kwa ujasiri na kwa nguvu kwa sauti kuu
katika kaburi la Lazaro.
Yohana 11:43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu,
“Lazaro, njoo huku nje!”
Kufanya Kazi za Yesu
Kila alipoenda Yesu, alihudumu katika ujasiri uliotokana na
kutambua mamlaka Yake kama Mwana wa Adamu. Alitoa
mamlaka hayo katika nguvu za Roho Mtakatifu, aliponya
wagonjwa, akatoa pepo na kufufua wafu. Alifanya hivyo
kwa waamini wa nyakati zile na sasa.
Yesu aliwaambia wanafunzi wahudumu katika mamlaka
hayo na kutenda kazi ile ile aliyokuwa akitenda.
Mathayo 10:8 Pozeni wagonjwa, fufueni pepo; mmepata bure,
toeni bure.
Wanafunzi wangefanya kazi ya Yesu kwa sababu aliwapa
mamlaka hayo hayo aliyoishi na kuhudumu.
Luka 10:19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge,
na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.
Mamlaka Yenye Ujasiri
Huduma ya Yesu ilitoa mfano wa ujasiri na nguvu, badala
ya hofu na uoga.
2 Timotheo 1:7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya
nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Yesu kwa ujasiri alihubiri Injili, akatoa pepo na kuwagusa
wagonjwa na kuona wakipona alipohudumu katika
mamlaka. Yesu, mfano wetu, alituacha na maneno haya ya
mwisho.
Marko 16:15-18 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote,
mkaibubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa
ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana
na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa
lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha,
hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa,
nao watapata afya.”
44
Tunapofuata mfano wa Yesu, kama Adamu wa Mwisho,
tutajikuta tukitii maneno ya Yesu, kama muumba, kwa
Adamu wa kwanza. Tutajikuta tukitawala na kumiliki dunia
hii na vyote vilivyomo pamoja na magonjwa, kufungwa,
umaskini na kifo. Kwa mara nyingine tutakuwa tukitenda
kile tuliumbwa kutenda.
Hofu Kuu Ya Shetani
Yesu alipohudumu hapa duniani, Shetani lazima alitazama
akiwa na hofu kuu. Hapa, Yesu akihudumu kama
mwanadamu, alichukua utawala, akinena na kuhudumu
katika mamlaka na kwa hiyvo aliharibu kazi ya Shetani.
1 Yohana 3:8b Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu
alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.
Tunapofuata mfano wa Yesu leo, sisi pia tutaweza kuishi na
kuhudumu katika mamlaka ya kimungu. Nasi pia
tutaiharibu kazi ya Shetani.
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Kulingana na Yohana 5:25-27, Je, Yesu alitenda katika mamlaka kama Mwana wa Mungu, au
kama Mwana wa Adamu?
2. Toa mifano ya Yesu akitenda katika mamlaka juu ya vitu, juu ya magonjwa na mapepo.
3. Je, watu walimwitikia vipi Yesu akitenda katika mamlaka hapa duniani?
4. Je, watu wataitikia vipi sasa unapotembea katika mamlaka hapa duniani?
45
Somo La Sita
Kutoka Msalabani Hadi Enzini
KIFO CHA YESU
Ufalme wa Shetani ulikuwa unaharibiwa, naye Shetani
alijua kuwa Yesu lazima auawe. Hila ilifanya kazi ndani
ya malaika awali. Ilifanya kazi dhidi ya Adamu na Hawa.
Lakini haikufanya kazi dhidi ya Yesu!
Lakini, kwa mara nyingine, Shetani alitumia hila.
Aliwahadaa viongozi wa dini ya nyakati zile ili kutaka
kifo cha Yesu. Aliutwaa mwili wa Yuda ili kutimiza
kusulubiwa kama vile alipoingia mwili wa nyoka ili
kuwahadaa Adamu na Hawa.
Shetani alimchukia Yesu sana hata hakutaka tu afe, bali
na ateswe na kuangamia. Kila ngome, tawala, mamlaka
ya giza na pepo chafu walikutana. Lazima walikuwa
wakitayarisha wakati wao wa kushangilia ushindi na
shangwe wakati maangamizi yao wenyewe yalifika.
Yesu alihainiwa, akapigwa, akasulubiwa
Mwongo wa Waongo Adanganywa
Shetani, mdanganyifu mkuu mwenyewe alidanganywa.
Katika chuki yake, hakutambua kuwa alisababisha kifo
cha Mtu ambaye, kwa kifo hicho na kufufuka,
angemshinda kabisa na kumkomboa mwanadamu na
dhambi zao.
Yesu alilipa deni la dhambi zetu kwa kufa msalabani.
Alituondolea dhambi zetu zote, magonjwa, maradhi na
umasikini na kuwekwa mahali pa mateso. Wakati dhambi
zote hapa duniani ziliondolewa kwa Yesu na nguvu za
Mungu zikamjia. Dunia nzima ilitetemeka wakati huu wa
vita vya kiroho. Yesu alimharibu Shetani na pepo zake.
Shetani, tangu wakati wa Adamu, alikuwa ameshika watu
chini ya mamlaka yake. Yesu alichukua funguo za
mamlaka kutoka kwa ibilisi.
JE, NINI KILITENDEKA DUNIANI?
Palikuwa na siku tatu za kivita. Yesu alisema kuwa kama
vile Yona alivyokuwa tumboni mwa nyangumi siku tatu,
Yeye atakuwa siku tatu chini ya arthi.
Mathayo 12:40 Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu
mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo
46
Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku
katika moyo wa nchi.
􀂱 Pasia Kupasuka mara Mbili
􀂱 Tetemeko La Dunia
􀂱 Mawe Kupasuka
􀂱 Makaburi Kufunuliwa
Wanadamu sasa hawatakiwi kutengana na Mungu. Pasia
katika hekalu, iliyo mahali patakatifu pa patakatifu,
ilipasuka mara mbili. Dunia ilitikisika sana wakati Yesu
alipokata kamba za mauti chini ya arthi.
Mathayo 27:50-53 Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa
nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama, pazia la hekalu
likapazuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi
ikatetemeka; miamba ikapasuka; makaburi yakafunuka;
ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; nao wakiisha
kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake,
wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.
JE, NINI KILITENDEKA KATIKA ULIMWENGU WA KIROHO?
Vita vilikuwa dhidi ya Yesu aliyetuwakilisha, na Shetani
akiwa na mapepo zake.
Wakati Yesu alitundikwa msalabani, Shetani lazima
aliwakusanya mapepo wote kushuhudia tukio hilo. Hii
ilikuwa ya muhimu sana kwa yeyote kukosa! Yesu
alipokufa msalabani, Shetani na mapepo zake lazima
walijiandaa kwa vishindo kwa kile walidhani kuwa kikuu.
Haikutosha kwa Shetani kuuona mwili wa Yesu
msalabani. Katika chuki, lazima alipaasa sauti, “lazima
atupwe chini ya jehanamu. Shetani na pepo zake katika
dharau zao na upumbavu lazima walianza kusherehekea,
lakini kwa muda tu kwani milango ya Jehanamu
ilifungwa nyuma ya Yesu.
Yesu, akiwa na dhambi za wanadamu wote, aliteswa
Jehanamu alipoteremshwa chini ya shimo lisilo na
mwisho. Hapo, alisimama na kutoa dhambi zote alizobeba
na pia za baadaye. Alisizika dhambi zetu isikumbukwe
tena kamwe.
Zaburi 103:12 Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,
Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.
Ilitabiriwa na Daudi
􀂱 Kubeba Adhabu ya Dhambi
􀂱 Kubeba Hukumu ya Dhambi
Daudi alieleza kile kilitendeka kwa Yesu baada ya kifo
chake. Akibeba dhambi zetu, alionekana hajiwezi wakati
47
Shetani alipopanga kumwangamiza. Aliteremka china
kabisa Jehanamu. Hapa, wote waliokufa katika kutotii
waliwekwa katika mateso na hukumu.
Yesu alienda jehanamu, akibeba adhabu na hukumu ya
dhambi zetu.
Zaburi 88:3-7 Maana nafsi yangu imeshiba taabu, Na uhai
wangu umekaribia kuzimu. Nimehesabiwa pamoja nao
washukao shimoni; Nimekuwa kama mtu asiye na msaada.
Miongoni mwao waliokufa nimetupwa, kama waliouawa
walalao makaburini. Hao ambao wewe huwakumbuki tena,
wametengwa mbali na mkono wako. Mimi umeniliza katika
shimo la chini, Katika mahali penye giza vilindini. Ghadhabu
yako imenilemea.
Umenitesa kwa mawimbi yako yote.
Daudi pia alitoa unabii juu ya ufufuo wa Yesu.
Zaburi 16:10 Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu, Wala
hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.
Ilitabiriwa Na Isaya
Nabii Isaya alitabiri kifo na kufufuka kwa Yesu.
Isaya 53:8-12 Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na
maisha yake ni nani atakayeisimulia? Maana amekatiliwa
mbali na nchi ya walio hai, Alipigwa kwa sababu ya makosa ya
watu wangu.
Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya; Na pamoja na matajiri
katika kufa kwake; Ingawa hakutenda jeuri, Wala hapakuwa
na hila kinywani mwake. Lakini BWANA aliridhika kumchubua;
Amemhuzunisha:
Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona
uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya BWANA
yatafanikiwa mkononi mwake; Ataona mazao ya taabu ya
nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu
mwenye haki;
Mwanakondoo wa Mungu
􀂱 Alibeba Dhambi za Wengi
􀂱 Aliwaombea Wapotovu
Naye atayachukua maovu yao, kwa hiyo nitamgawia sehemu
pamoja na wakuu, naye atagawanya nyara pamoja nao walio
hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa,
Akahesabiwa pamoja na hao wakosao.
Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea
wakosaji.
Msalabani, Yesu alitimiza kazi ya dhabihu ya
mwanakondoo ya Agano la Kale.
48
Yohana 1:29 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake,
akasema, “Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye
dhambi ya ulimwengu!”
Mbuzi wa Azazeli
Wakati Yesu alizibeba dhambi zetu hadi chini ya arthi,
Alitimiza kazi inayoonyeshwa na mbuzi wa Azazeli
ambaye alizibeba dhambi za watu.
Mambo Ya Walawi 16:10,21,22 Bali yule mbuzi aliyeangukiwa
na kura kwa ajili ya Azazeli atawekwa hai mbele za BWANA ili
kumfanyia upatanisho, ili kumpeleka jangwani kwa ajili ya
Azazeli.
Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule
mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa
Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka
juu ya kichwa chake yule mbuzi, kasha atampeleka aende
jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari. Na yule mbuzi
atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu;
naye atamwacha mbuzi jangwani.
YESU HANGEWEZA KUSHIKIKA!
Wakati Yesu alizibeba dhambi zetu hadi chini ya arthi,
nguvu za Mungu zilikaa juu Yake.
Matendo Ya Mitume 2:27 ... Kwa maana hutaiacha roho yangu
katika kuzimu; Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu.
Malango ya kuzimu haingeweza kushinda dhidi ya Yesu.
Kwa kuyavunja malango ya kuzimu, Alinyakua funguo za
mauti, kuzimu na kaburi kutoka kwa Shetani.
Ibilisi na Mapepo Washindwa
Historia ya vita vya kale na kushindwa kwa maadui hutoa
mawazo maalumu kuhusu kiini cha msitari ufuatao.
Wakolosai 2:15 Akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya
kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.
Nguvu na mamlaka kama tulivyojifunza awali, huonyesha
mipango ya Shetani na mapepo zake.
Hapo kale, jeshi liliposhinda adui wao,
waliwanyang’anya silaha, kuwavua nguo, kuwafunga kwa
nyororo mmoja kwa mwingine, na bila heshima
kuwaongoza kama watumwa, katika inchi iliyoshinda
vita.
Yesu binafsi alimnyang’anya silaha Shetani na kila pepo.
Alitwaa silaha zao kutoka kwao. Aliwatoa nguo. Aliwatia
fedheha mbele ya watu.
49
Wale walioshangilia hapo awali Yesu alipotundikwa, uchi
na aibu msalabani, sasa walitiwa aibu pia.
Shetani alishinda Adamu na Hawa
􀂱 Aliwaacha wakiwa uchi
􀂱 Aliwanyang’anya mamlaka yao.
Shetani alidhani amemshinda Yesu
􀂱 Na kumwacha akiwa uchi
􀂱 Akining’inia msalabani
Hata hivyo, Yesu alimshinda Shetani na Pepo zake
􀂱 aliwaacha wakiwa uchi
􀂱 alitwaa mamlaka yao hadi milele!
Ufufuo
Baada ya kulipia adhabu ya dhambi kwa kifo Chake
msalabani na kuzitia dhambi zetu chini ya shimo, Yesu
alizichukua funguo za mauti, kuzimu na kaburi kutoka
kwa Shetani.
Baada ya kumshinda Shetani na kuzivunja nguvu zake juu
ya kifo, kaburi halikuweza kuendelea kuweka mwili wa
Yesu. Katika mlipuko mkuu, Yesu alifufuka kutoka kwa
wafu. Shetani na kila pepo walishindwa!
Waefeso 1:19-21 ... na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani
yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za
uweza wake; aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu,
akamweka mkono wake wa kuumu katika ulimwengu wa roho;
juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na
usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu,
bali katika ule ujao pia.
YESU ALIPAA
Katika Ushindi
Yesu kwa ushindi alipaa mbinguni tena na aliwaongoza
wafungwa katika msafara Wake.
Waefeso 4:8-10 “Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka,
Akawapa wanadamu vipawa.”
(Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini kama siyo kusema
kwamba yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi?
Naye aliyeshuka ndiye yeye aliyepaa juu sana kupita mbingu
zote, ili avijaze vitu vyote.)
Yesu alipowaongoza wafungwa kuwa huru, tunapata
picha ya Yesu kama jenerali mshindi akimwongoza adui
aliyeshindwa – wasiwe na silaha, wamevuliwa,
kufungwa, na kutiwa fedheha mbele ya malaika
50
mbinguni. Shetani na kila pepo walishindwa kabisa na
bila huruma walitiwa aibu wazi.
Yesu alipotwaa funguo za mamlaka kutoka kwa Shetani,
alitwaa funguo ambazo Adamu katika kuasi kwake
alimpa Shetani. Wakati Yesu alipozichukua funguo hizo
za mamlaka kutoka mkononi mwa Shetani,
alimnyang’anya Shetani mamlaka yake juu ya
mwanadamu na dunia yake. Yesu binafsi alimshinda
Shetani na kila pepo zake.
Alipokelewa kwa Furaha
Hakika hakuna maneno ya kueleza furaha ya viumbe wa
mbinguni kwa Mwana wa Mungu kurejea pahali pake
mbinguni.
Je, mwanadamu anawezaje kueleza ushindi huo wa
kurudi?
Daudi alivuviwa kutoa kwetu maelezo kuhusu wakati
huu.
Zaburi 24:7-10 Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni,
enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.
Ni nani Mfalme wa utukufu? BWANA mwenye nguvu, hodari,
BWANA hodari wa vita.
Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi
malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.
Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? BWANA wa majeshi, Yeye
ndiye Mfalme wa utukufu.
Alitangaza Ushindi!
Mtume Yohana anatupatia maneno ya Yesu, alipotangaza
ushindi Wake!
Ufunuo Wa Yohana 1:18 Na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa,
na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za
mauti, na za kuzimu.
YESU ALIKUWA NA FUNGUO!
Yesu alikuja mbinguni akipiga ukelele, “Baba, ninazo
funguo! Shetani ameshindwa na ninazo funguo!”
Yesu alikuwa na funguo za mamlaka mkononi mwake
alizochukua kutoka kwa Shetani aliyeziiba bustanini
alipowahadaa Adamu na Hawa.
Umuhimu wa Funguo
Yesu alizichukua funguo kutoka kwa Shetani, lakini
hakuziweka. Alizirejeshea mwanadamu.
51
Katika ufunuo wa kwanza wa kanisa, Yesu aliwaambia
wanafunzi wake kuwa atawapa funguo za ufalme wa
mbinguni.
Mathayo 16:19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa
mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani,litakuwa
limefungwa mbinguni, na lo lote utakalolifungua duniani,
litakuwa limefunguliwa mbinguni.
Katika Isaya panatajwa tena funguo.
Isaya 22:22 Na ufunguo wa nyumba ya Daudi nitauweka
begani mwake; yeye atafungua wala hapana atakayefunga;
naye atafunga wala hapana atakayefungua.
Awali, funguo zilikuwa kubwa, nzito na rembo. Matajiri
mara nyingi walizibeba begani kwa ajili ya uzito, lakini
hasa kwa urembo wake. Mara nyingi watumwa wawili au
watatu wangemfwata tajiri wakizibeba funguo begani
mwao. Hii ilionyesha utajiri.
Wakati Isaya alipotoa unabii juu ya kuja kwa Masiya,
alionyesha kiini cha funguo kubebwa begani.
Isaya 9:6a Maana kwa ajili yetu mototo amezaliwa, Tumepewa
mototo mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani
mwake.
Funguo, serikali na mamlaka, vilikuwa katika mikono ya
Yesu! Yesu alizichukua funguo hizo akazipa kanisa Lake.
Mamlaka hapa duniani
imerejeshewa
kwa mwanadamu
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Baada ya kifo chake msalabani, je, Yesu alizipeleka wapi dhambi zetu?
2. Je, Maandiko yana maana gani inaposema Yesu aliharibu ngome na nguvu na kuziweka aibu
kwa wazi?
3. Je, nini maana ya funguo ambazo Yesu anataja katika Ufunuo 1:18?
53
Somo La Saba
Mamlaka Kurejeshewa kwa Mwanadamu
KAZI YA YESU IMEMALIZIKA!
Kazi ya Yesu ilikuwa, na bado ni, imekamilika!
Mungu alipowaumba Adamu na Hawa, aliwapa mamlaka
ya kutawala dunia hii. Kupitia kwa dhambi, walipoteza
mamlaka haya kwa Shetani. Kisha Yesu, mwanadamu
kamili, Adamu wa Mwisho, alitembea hapa duniani
katika kila hali ambayo Mungu alimuumba mwanadamu
atende. Yesu alizichukua dhambi za wanadamu wote juu
Yake na akafa msalabani akilipia adhabu ya dhambi hizo.
Alikufa kwa wanadamu wote. Alizitoa dhambi hizo chini
ya shimo na nguvu za Mungu mwenyewe zikamjia Yesu.
Alimshinda Shetani na pepo zote katika lango la kuzimu.
Yesu alizichukua funguo za mamlaka.
Yesu alichukua kila kitu Shetani alikuwa ameiba kwa
mwanadamu. Vyote Mungu alivyowaumba Adamu na
Hawa wawe navyo ambapo Yesu aliwarejeshea
wanadamu.
Yesu aliponena juu ya kanisa atakalojenga, Alisema,
Mathayo 16:18b,19 Na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa
langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa
wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga
duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote
utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni..
Yesu Mbinguni
Mwandishi wa kitabu cha Waebrania anatuonyesha nafasi
ya Yesu sasa.
Waebrania 10:12,13 Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili
ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono
wa kuume wa Mungu; tangu hapo akingojea hata adui zake
wawekwe kuwa chini ya miguu yake.
Yesu ameketi katika mkono wa kuume wa Baba.
Daudi pia alitabiri nafasi ya Yesu ya sasa.
Zaburi 110:1 Neno la BWANA kwa Bwana wangu, “Uketi
mkono wangu wa kuume, Hata niwafanyao adui zako kuwa
chini ya miguu yako.”
Daudi alitabiri Yesu ataketi mkono wa kuume wa Baba.
53
Yesu Anasubiri
Daudi na mwandishi wa kitabu cha Waebrania alitwambia
kuwa Yesu anafanya zaidi ya kuketi katika mkono wa
kuume wa Baba. Yesu anasubiri adui Zake wafanyike
miguu ya kiti Chake.
Je, nani atafanya adui Zake wawe miguu ya kiti Chake?
Yesu anangoja waliokombolewa kutambua mamlaka yao
na kuonyesha kuwa Shetani ni adui aliyeshindwa. Kazi ya
Yesu imekamilika. Yeye anasubiri adui zake wafanyike
miguu ya kiti Chake. Ni kazi ya waamini kumweka
Shetani mahali pake. Waamini lazima wamweke Shetani
na pepo zake chini ya miguu ya Yesu.
Yesu amefanya kila kitu alichotakiwa kufanya. Sasa
jukumu ni letu. Sisi ni mwili Wake hapa duniani. Sisi ni
mikono Yake, miguu Yake. Ni sisi ndio tunatakiwa
kutawala dunia yetu leo.
OMBI LA PAULO
Mtume Paulo aliomba ombi la muhimu na lenye nguvu
kwa wateule wote. Ombi lake lilichukua nafasi ya Yesu
akiwa mkono wa kuume wa Baba, nafasi yetu, nguvu zetu
na majukumu yetu.
Waefeso 1:18-23 ... macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue
tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa
urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo; na ubora wa ukuu
wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya
utendaji wa nguvu za uweza wake kadiri ya utendaji wa nguvu
za uweza wake; aliotenda katika Kristo alipomfufua katika
wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu
wa roho; juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu,
na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu
tu, bali chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya
miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili
ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake
anayekamilika kwa vyote katika vyote.
Nafasi Ya Yesu
Kulingana na mtume Paulo,
􀂱 Yesu amefufuka kutoka kwa wafu
􀂱 Ameketi mkono wa kuume mbinguni
􀂱 Yu juu ya tawala, nguvu, uwezo, na mamlaka
􀂱 Yu juu ya kila vyeo vinavyoweza kutolewa
􀂱 Vitu vyote viko chini ya miguu Yake
􀂱 Amechaguliwa awe kichwa/kiongozi
54
Yesu yuko juu ya nguvu za mapepo. Yesu yu juu ya vyeo
vinavyotolewa, au kuwai kutolewa. Vitu vyote viko chini
ya miguu Yake.
Kipimo Cha Nguvu
Kuna aina mbili ya nguvu: moja katika Agano la Kale na
nyingine katika Agano Jipya.
Katika Agano la Kale kipimo cha nguvu kilikuwa
kugawanyika kwa Bahari Nyekundu.
Katika Agano Jipya kipimo cha nguvu kilikuwa na bado
ni, nguvu katika ufufuo wa Yesu Kristo.
Paulo aliandika,
Waefeso 1:19b,20a kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza
wake kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake; aliotenda
katika Kristo alipomfufua katika wafu.
Nafasi Ya Waamini
Mtume Paulo alisema kuwa waamini watafunuliwa, na
kuwa watafahamu:
􀂱 Matumaini ya mwito Wake
􀂱 Utajiri wa utukufu wa urithi Wake
􀂱 Ukuu na umahiri wa nguvu Zake
􀂱 Sisi tu mwili Wake
􀂱 Sisi tumejazwa na Yeye
Tunatakiwa kuwa na ufahamu wa utajiri katika utukufu
wa urithi Wake na ukuu wa nguvu Zake kwetu
tunaoamini. Tunatakiwa kutenda katika nguvu zile kuu
zilizomfufua Yesu kutoka kwa wafu!
KUJAZWA NAYE
Paulo aliombea “kanisa, ambalo ni mwili wake, kujazwa
kwake ajazaye wote katika yote.”
Ikiwa sisi, kanisa Lake, tunatimiza tupu au uwazi katika
Mwana wa Mungu, je, ni lini utupu huu ulitokea? Labda
utupu huu ulitokana na wakati Lusifa, makerubi
afunikaye, alipotupwa toka mbinguni pamoja na malaika
waliomfuata katika kuasi kwake.
Ezekieli 28:14 Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta
afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima
mtakatifu wa Mungu umetembea huko na huko kati ya mawe
ya moto.
55
Uongozi wa Kimalaika
Kama vile pana utatu katika Mungu, hapo pia palionekana
kuna utatu katika uongozi wa malaika. Palikuwa Mikaili,
Lusifa na Gabrieli.
􀂱 Theluthu Moja
Lusifa alipoasi, ilisemekana kuwa “malaika zake”
walitupwa nje pamoja naye.
Ufunuo Wa Yohana 12:7-9 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli
na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye
akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda,
wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye
Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa
hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
Malaika walioelezwa kuwa malaika wa Shetani na
waliotupwa chini arithini wakiwa naye, walikuwa
theluthu moja ya malaika wote mbinguni.
Ufunuo Wa Yohana 12:4a Na mkia wake wakokota theluthi ya
nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi.
􀂱 Mikaili
Mikaili tu ndiye aliyeitwa malaika mkuu.
Waraka Wa Yuda 1:9a lakini Mikaeli, malaika mkuu...
Alikuwa Mikaili na “malaika wake” ambao walikuwa
jeshi kupigana dhidi ya Shetani, “joka na malaika zake.”
Ufunuo Wa Yohana 12:7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli
na malaika zake wakapigana…
Labda malaika mkuu, Mikaili na theluthu ya malaika
chini ya amri yake, walimhudumia Baba.
􀂱 Gabrieli
Labda Gabrieli, ambaye kila mara huonekana kama
malaika wa ujumbe, na theluthu ya malaika chini ya amri
yake; walihudumia Roho Mtakatifu.
Alimtokea Zekaria, ili ampe ujumbe kuwa mkewe
Elizabeti atamzaa mwana “atakayejazwa na Roho
Mtakatifu hata tangu kuzaliwa.”
Luka 1:19 Malaika akamjibu akamwambia, “Mimi ni Gabrieli,
nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema.”
Gabrieli pia alimtokea bikira aitwaye Mariamu.
Luka 1:30,31,35 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu,
kwa maana umepata neema kwa Mungu. “Tazama, utachukua
56
mamba na kuzaa mototo mwanamume, na jina lake utamwita
Yesu.”
Mariamu aliuliza, “Je, itawezekanaje ... maana simjui
mwanamume?”
Malaika akajibu akamwambia, “Roho Mtakatifu atakujilia juu
yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa
sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana
wa Mungu.”
Gabrieli alionyesha kazi ya Roho Mtakatifu.
􀂱 Lusifa
Je, inawezekana kuwa, Lusifa na malaika zake
walimutumikia Mwana wa Mungu?
Lusifa alihudumu kama makerubi wa kufunika, na
alijulikana kwa kufunika kila upande wa Kiti cha Neema.
Alikuwa kando ya kiti cha enzi cha Mungu. Kama
tulivyoona, kufunika kulikuwa ni huduma ya sifa na
kuabudu.
Kisha, ghafla katika kuasi, Lusifa na malaika wake wote
walitupwa toka mbinguni. Je, pengo hili lingejazwa vipi?
Je, Baba alimwuliza Mikaili na Gabrieli kuwapa malaika
wengine kuchukua nyadhifa hizo na kumhudumia
Mwana? Hatuna habari iliyochapishwa kuonyesha hayo.
Je, pana uwezekano kuwa, Mungu alikuwa na mpango
bora alipomwumba mwanadamu katika mfano Wake,
wawe wakimuabudu, kukaa naye kule mbinguni, kuwa
upande wake na kutawala na kuongoza Naye milele?
Uwazi Ukajazwa
Waume kwa Wake, wameumbwa katika mfano wa
Mungu, na wanaweza tu kukamilika na kutimiza ikiwa
Muumba tena atawavuvia pumzi Mwenyewe ndani yao
wakati wa wokovu. Anajaza uwazi katika maisha Yeye
mwenyewe. Sasa mwili Wake ni sharti utimize uwazi
ndani yao ili wajitolee Kwake katika huduma ya sifa na
kuabudu.
Hapo mwanzo, palikuwa na huduma moja tu, huduma ya
sifa na kuabudu. Wakati hiyo ilisimama, huduma zingine
nyingi ziliitajika – huduma za uponyaji, kukombolewa,
kurejeshwa, na nyingine.
Je, panawezekana kuwa wakati huduma ya sifa na
kuabudu ikirejeshwa kanisani, huduma hizi zingine zisiwe
na umuhimu katika mwili wa Kristo kama vile zilivyo
sasa?
Tunapotumia muda zaidi katika huduma ya sifa na
kumwabudu Mungu, tutagundua kuwa kuna upungufu
57
katika uponyaji au ukombozi au huduma nyingine katika
maisha yetu.
Sisi tu wa muhimu kwa Mungu! Inatupasa tuwe
tunatimiza Kwake. Inatupasa kumuhudumia katika sifa na
kuabudu. Tunapofanya hivyo, sisi kama mwili Wake
tunakuwa “tumejazwa Naye ajazaye wote ndani ya yote.”
Waefeso 1:22,23 Akavitia vitu vyote chini ya miguu yake,
akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa;
ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa
vyote katika vyote.
Tunaposifu na kumwabudu Mungu, hatutimizi tu kazi ya
awali ya Lusifa na malaika zake, tunaonyesha kweli kuwa
wameshinda na hawana tena nafasi mbinguni. Tunawatia
aibu na kuwaweka chini ya miguu yetu. Tunapocheza
mbele za Bwana, tunamponda Shetani na kumushinda
kwa tendo la miguu yetu.
Kumbukumbu: Kwa kujifunza kwa undani juu ya sifa na kuabudu,
soma the Praise And Worship Manual na A.L. na Joyce Gill.
NAMAANA YA HII KWETU
Kwa kazi ya Yesu msalabani na kwa matukio yaliyofuata,
Shetani ameshindwa! Kila pepo limeshindwa! Yesu
aliwashinda na kuwaweka patupu! Aliweka “sufuri”
ndani yao.
􀂱 Kwa nini tunamuruhusu Shetani kutushinda sasa?
􀂱 Kwa nini tunamruhusu kunyakua nyumba zetu, miji
yetu, mataifa zetu?
􀂱 Kwa nini tunamruhusu aweke magonjwa juu yetu?
􀂱 Kwa nini tunakubali umasikini?
Jibu ni kuwa ni lazima tujifunze na kufahamu kile
tumepewa katika Yesu Kristo. Lazima tutambue mamlaka
yetu iliyorejeshwa.
Tumekombolewa!
Wakati mtume Paulo aliandika kwa Wakolosai, alisema
tume:
􀂱 Okolewa
􀂱 Badilishwa
􀂱 Kombolewa
􀂱 Samehewa
Wakolosai 1:13,14 Naye alituokoa katika nguvu za giza,
akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa
58
pendo lake, ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani,
msamaha wa dhambi.
Ufalme Uko Hapa
Je, ufalme wa Mwana ni upi?
Jesu alipowafunza wanafunzi wake kuomba, aliomba
maneno haya
Mathayo 6:10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama
huko mbinguni.
Ufalme wa Mungu si kitu katika siku za usoni. Bali uko
hapa sasa. Tumeokolewa na utawala wa giza na kuletwa
katika ufalme wa Mwana katika kukombolewa na
msamaha wa dhambi zetu.
Tukiwa na ufahamu wa mamlaka yetu iliyorejeshwa,
tunaweza kuwa waume kwa wake watakaokuwa na
uwezo mkuu kuendeleza ufalme wa mbinguni hapa
duniani.
Mathayo 11:12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa
ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu
wauteka.
Paulo aliendelea na maelezo mazuri kuhusu Yesu.
Wakolosai 1:15-18 Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana,
mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Kwa kuwa katika yeye
vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi,
vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au
usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia
yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote,
na vitu vyote hushikana katika yeye. Naye ndiye kichwa cha
mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa
kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.
Yesu Ambaye ni Kichwa
Yesu:
􀂱 Ni mfano wa Mungu
􀂱 Muumba wa vyote
􀂱 Alikuwa kabla ya vitu vyote
􀂱 Anashikilia vitu vyote pamoja
􀂱 Ni kichwa cha mwili, kanisa
􀂱 Ni mwanzo, kifungua mimba kutoka kwa wafu.
Yesu ni kichwa chetu. Sisi ni mwili Wake. Mwili Wake
umetengenezwa na waamini wote. Kama mwili Wake,
tunaelezwa kuwa tayari tumenyakuliwa kutoka kwa
tawala za Shetani na kubadilishwa kwa ufalme mpya
ambapo tutatawala na Yesu, Mwana wa Mungu.
59
Tunaelezwa kama waliokombolewa kabisa
tumesamehewa dhambi zote.
Kichwa cha mwili, Yesu, yu mbinguni. Sehemu nyingine
ya mwili Wake na, pia miguu, iko duniani. Ni hapa
duniani ambapo mwanadamu lazima atimize kazi yake ya
mamlaka tele. Ni hapa ndipo tunatakiwa kuendeleza
ufalme wa Mungu katika vita kamili vya kiroho.
NAFASI YA SHETANI
Chini ya Miguu ya Yesu
Mungu alimweka Shetani chini ya miguu ya Yesu na
kumchagua Yesu awe kichwa juu ya kila kitu kuhusu
kanisa.
Waefeso 1:22 Akavitia vitu vyote chini ya miguu yake,
akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa..
Chini ya Miguu Yetu
Warumi 16:20a Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini
ya miguu yenu upesi.
Kuwa chini ya miguu ya mtu ni mfano wa kushindwa
kabisa na kutawaliwa. Ni picha ya mamlaka kamili na
utawala.
Mwanzo 3:15 Nami nitaweka uadui kati yako na huyo
mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo
utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
Chini ya Mamlaka Yetu
Shetani yu chini ya miguu ya Yesu kwa sababu Yesu
alimshinda kabisa na kupaa juu yake na pepo zake zote.
Shetani na pepo zake sasa watawekwa chini ya miguu
yetu tunapogundua mamlaka yetu na kuyatumia duniani.
Kukanyagwa
Luka anatuonyesha mfano wa nafasi au msimamo wa
Shetani. Ni sharti akanyagwe chini ya miguu yetu. Pia
tumeahidiwa kuwa hakuna kitakachotudhuru katika hali
yoyote.
Luka 10:19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na
nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu
kitakachowadhuru.
Mwanadamu baada ya kuokolewa, kuletwa,
kukombolewa, kusamehewa kabisa na kurejeshwa katika
mfano wa Mungu duniani, sasa atamkanyaga Shetani
chini ya miguu na kuonyesha kuwa yeye ni adui
aliyeshindwa.
60
Isaya alipoeleza mwisho wa Shetani, alimtaja kama
mmoja anayekanyagwa chini ya miguu.
Isaya 14:18-20 Wafalme wote wa mataifa wamezik wa wote
kwa heshima, kila mmoja ndani ya nyumba yake mwenyewe;
Bali wewe umetupwa mbali na kaburi lako, Kama chipkizi
lililochukiza kabisa; kama vasi la wale waliouawa, Wale
aliochomwa kwa upanga, Wale ashukao mpaka misingi ya
shimo; kama mzoga uliokanyagwa chini ya miguu.
Hutaungamanishwa pamoja nao katika mazishi, Kwa maana
umeiharibu nchi yako, umewaua watu wako kizazi chao
watendao uovu hakitatajwa milele..
MFULULIZO WA AMRI
Yesu aliporudi kwa Baba Yake, aliweka kando haki zake
kama Mwana wa Adamu na kutwaa tena juu Yake haki
Zake zote kama Mwana wa Mungu.
Haki ya Mwanadamu Duniani
Kama Mungu, Yeye sasa hatawali hapa duniani kwa
sababu, alitoa utawala wote kwa mwanadamu.
Ni mwanadamu ndiye anatakiwa kumweka Shetani chini
ya miguu yake kama alivyoumbwa kufanya.
Nabii Isaya alitueleza unabii mzuri na wa kutia moyo.
􀂱 Katika haki utaimarishwa
􀂱 Mateso yatakuwa mbali nawe.
􀂱 Wewe huogopi kitu
􀂱 Hofu kuu haitakuja karibu nawe
􀂱 Yeyote anayeinuka dhidi yako atasalimu amri
􀂱 Hakuna silaha iliyoundwa dhidi yako itafaulu
􀂱 Utakana kila ulimi utakaokuja kinyume chako
Isaya14-17 “Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji
yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende wao?”
Kwa kweli watakusanyika,, lakini si kwa sababu Yangu.
Yeyote atakayekusanyika dhidi yako ataanguka kwa ajili yako.
Tazama, nimeumba mhunzi anayepuliza makaa katika moto,
anayeleta chombo kwa kazi yake, na nimemwumba mwaribifu
aiharibu. Hakuna silaha iliyoundwa kinyume chako itafaulu, na
kila ulimi unaoinuka dhidi yako katika hukumu utahukumu.
Huu ni urithi wa watumwa wa Bwana, na haki yao inatoka
kwangu,” asema Bwana..
Urithi wetu ni kitu ambacho ni chetu katika haki ya
kuzaliwa.
61
Isaya alitabiri,
Huu ni urithi wa watumishi wa Bwana!
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Ikiwa vitu vyote viko chini ya miguu ya Yesu, kwa nini ibilisi na nguvu za mapepo bado
zinaendelea na kazi ya uovu wao hapa duniani?
2. Kwa nini Mungu anamruhusu Shetani kuendelea na uovu duniani baada ya Yesu kumshinda
yeye kwa kifo Chake msalabani na ufufuo Wake?
3. Je, ni mabadiliko gani maishani mwako ambayo yatafaa ikiwa utatembea katika mamlaka –
kuonyesha kuwa Shetani ni adui aliyeshindwa?
63
Somo La Nane
Mbinu Za Shetani Za Kisasa
NINI KILITENDEKA
MIAKA 2,000 BAADAYE – SHETANI AMEYATWAA TENA MAMLAKA HAYO
Miaka 2,000 baadaye tunaona:
Watu kuishi bila
jina la Yesu.
Watu kuishi katika umaskini
Watu kuishi katika dhambi
watu kuishi katika kushindwa
Watu kupewa talaka
watu na wana wao wakitumia madawa ya kulevya
watu kuabudu dini za uwongo.
Kwa nini Shetani anafanya hivi kama
mungu wa dunia hii?
Ameshindwa na Yesu
na kuwekwa mahali pasipo na uwezo.
Yesu amefanya kazi yake kutukomboa sisi!
Je, tumefanya nafasi yetu
kwa nguvu zetu – utawala – mamlaka?
63
MBINU ZA SHETANI
Kuiba, Kuua na Kuharibu
Katika nyakati zote, kusudi la Shetani halijabadilika.
Yohana 10:10a Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu;
mimi nalikuja ili wawe na uzima, kasha wawe nao tele.
Ibilisi anatuchukia sana hata ametoa amri kwa jeshi lake
la mapepo ili kuiba, kuua na kuaharibu! Jukumu
limetolewa ili tuibiwe yaliyo muhimu katika maisha na
huduma zetu. Amri zimetolewa ili tuuliwe katika roho za
udhaifu, kuua na kujitia kitanzi. Ajali mbaya hujaribiwa
maishani mwetu. Ibilisi ametoa amri yake, “chochote
itagharimu lazima wauawe!”
Ikiwa mapepo hayawezi kutuua, labda, wanaweza kutoa
habari kuwa wametuzuia au kutukomesha katika kutimiza
huduma zetu tulizopewa na Mungu.
Kutumia Pepo Za Udhaifu
Shetani hujaribu kuiba afya yetu kwa kutumia pepo za
udhaifu.
Luka 13:11-13 Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa
na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye
amepindana, hawezi kujinyosha kabisa. Yesu alipomwona
alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu
wako. Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka mara
hiyo, akamtukuza Mungu.
Yohana 5:5 Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa
hawezi muda wa miaka thelathini na minane.
Kufinya, Kufadhaisha na Kusaliti
Mtume Paulo anaeleza mapigo ya Shetani maishani
mwake na huduma. Inatia moyo kuona kuwa mipango
yote ya Shetani ilishindwa kuzuia huduma ya Paulo kwa
Bwana.
2 Wakorintho 4:8,9 Pande zote twadhikika, bali hatusongwi;
twaona shaka, bali hatukati tama; twaudhiwa, bali
hatuangamizwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi.
Shetani hupiga vyote vyenye ubora na manufaa maishani
mwetu.
􀂱 Ndoa
􀂱 Watoto
􀂱 Jamii
􀂱 Marafiki
􀂱 Huduma
64
􀂱 Afya
􀂱 Furaha
􀂱 Amani
KINGA YETU
Tambua Mbinu ya Adui Wako
Waume kwa wake huangamia kwa kukosa hekima. Ikiwa
wanaenda kumkomesha Shetani asifikie lengo lake la
kuiba, kuua na kuharibu, ni lazima wamtambue adui na
mbinu zake.
􀂱 Shetani huleta mauti – Mungu huleta uzima.
􀂱 Shetani huleta chuki – Mungu huleta upendo.
Yesu
􀂱 Aliharibu Mauti
Yesu ameharibu mauti na kuleta uzima na kuishi milele.
2 Timotheo 1:10...na sasa inadhihirishwa kwa kufununuliwa
kwake mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na
kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili.
􀂱 Aliharibu Nguvu za Shetani
Yesu ameharibu ibilisi na kutuweka huru kutokana na
hofu ya kifo na mapepo.
Waebrania 2:14,15 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu
na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa
njia ya mauti amhasibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti,
yaani, Ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba maisha yao
yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa
􀂱 Alitukomboa Kutoka kwa Utumwa
Shetani hana haki ya kutuweka katika utumwa. Sisi,
katika imani ndani ya Yesu Kristo, tumekombolewa
kutoka kwa kufungwa na utumwa wa Shetani na ufalme
Wake.
Wakati Shetani au pepo zake huja kuiba, kuua na
kuharibu, ni sharti wasitukute tukiwa wanyonge na bila
kinga. Badala yake kupitia ufahamu wa Neno la Mungu,
lazima tuwe tumefunikwa na damu ya Yesu. Lazima
tusimame imara na chepeo yetu ya imani. Lazima kwa
ujasiri na bila uoga tunene Neno la Mungu kama nabii
Isaya.
Isaya 54:17a Kila silaha itakayofanyika juu yako
haitafanikiwa
65
KIPA UMBELE CHA SHETANI – KUTUIBIA NENO LA MUNGU
Noa Upanga Wako
Ikiwa tutakosa Neno akilini mwetu na rohoni, hatutaweza
kumshinda Shetani na wafwasi wake kwa Neno. Yesu
anataka tuwe na vingi kila sehemu maishani mwetu.
Ikiwa hatuna hivi, basi tumeibiwa na Shetani.
Lazima tutambue sisi tuko ndani ya Kristo ili kutambua
kuwa tayari tumeshinda vita!
Mfano wa Mpanzi – Ufunuo wa Ushindi
Mfano wa Mpanzi
Marko 4:3-8
“Sikilizeni! Tazama, mpanzi alitoka kwenda
kupanda.
Ikawa alipokuwa akipanda, mbegu nyingine
ilianguka kando ya njia wakaja ndege wakaila.
Nyingine ikaanguka penye mwamba,
pasipokuwa na udongo mwingi, mara ikaota
kwa kuwa na udongo haba, hata jua lilipozuka
iliungua, na kwa kuwa haina mizizi,
ikanyauka.
Nyingine ikaanguka penye miiba, ile miiba
ikamea ikaisonga, isizae matunda.
Nyingine zikaanguka penye udongo ulio
mzuri, zikazaa, moja thelathini, moja sitini, na
moja mia.”
Yesu Akaelezea Mfano
Marko 4:14-20
“Mpanzi huyo hulipanda Neno.
Hawa ndio walio kando ya njia lipandwapo
Neno, nao wakiisha kusikia, mara huja
Shetani, akaliondoa lile neno lililopandwa
mioyoni mwao.
Kadhalika na hawa ndio wapandwao penye
miamba, ambao kwamba wakiisha kulisikia
lile neno, mara hulipokea kwa furaha, ila
hawana mizizi ndani yao, bali hudumu muda
mchache, kasha ikitokea dhiki au udhia kwa
ajili ya lile neno, mara hujikwaa.
Na hawa ndio wale wapandwao penye miiba,
ni watu walisikiao lile neno, na shuguli za
dunia, na udanganyifu wa mali, na tama za
mambo mengine halizai.
Na hawa ndio waliopandwa penye udongo
ulio mzuri, ni watu walisikiao lile Neno na
kulipokea, na kuzaa matunda, mmoja
thelathini, mmoja sitini, na mmoja mia.”
67
Wengi wameelewa mfano huu kuwa mbegu ya wokovu
ikipandwa na matokeo tofauti ya uinjilisti na hivyo ni
kweli.
Lakini, Yesu alisema kuwa alimaanisha Neno la Mungu.
Yesu alifundisha kuwa tunapopokea ufahamu mpya juu
ya Neno la Mungu, Shetani atafika mara moja kuliiba
kutoka kwetu. Hii inaweza kuwa Neno la Mungu kama
katika kila sehemu ya maisha yetu.
Je, ni mara ngapi umesikia watu wakisema kuwa baada ya
wakati mzuri na Bwana majaribu mara nyingi yatakuja?
Baada ya semina nzuri, kila kitu huonekana “kikienda
kombo”. Yesu alisema kuwa huyu ni Shetani akija kuiba
Neno.
Moja Kati ya Vitu Vitatu
Neno linapopandwa vitu vitatu hufanyika:
􀂱 Shetani anaweza kuiba Neno mara moja ikiwa
tutahuzunika Shetani anapoleta mateso na kusaliti.
􀂱 Neno linaweza kupotezwa na mahangaiko ya maisha
haya, hila za mali au tamaa ya dhambi.
􀂱 Neno liruhusiwe kupata mizizi na kuchipuka.
Mateso /Kusaliti
Yesu aliwaonya kuwa mateso na majaribu yatatokea kwa
ajili ya ulimwengu.
Marko 4:17 ... ila hawana mizizi ndani yao, bali hudumu muda
mchache; kasha ikitokea dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno,
mara hujikwaa.
Shetani Huja Ghafula
Shetani anajua kuwa ufunuo wa Neno la Mungu ukibaki
ndani ya mioyo yetu, kwa Neno hilo hilo, anaweza
kushindwa. Ingawa anazo mbinu nyingi ili kuleta
kushindwa katika maisha yetu, kipa umbele chake kila
mara ni kuiba ufunuo wa Neno la Mungu. Yesu alisema
Shetani huja wanaposikia.
Marko 4:15 hawa ndio walio kando ya njia lipandwapo neno;
nao wakiisha kusikia, mara huja Shetani, akaliondoa lile neno
lililopandwa mioyoni mwao.
YESU ALITULIZA BAHARI
Yesu alipomaliza kufundisha, Yeye pamoja na wanafunzi
Wake waliingia mashuani. Baadaye Yesu akasinzia pale
nyuma. Kisha Shetani akaja na mahangaiko ya dunia hii.
67
Marko 4:35-41 Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na
tuvuke mpaka ng’ambo. Wakauacha mkutano, wakamchukua
vilevile alivyo katika chombo.
Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye.
katokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo
hata kikaanza kujaa maji. Naye mwenyewe alikuwapo katika
shetri, amelala juu yam to; wakamwamsha, wakamwambia,
Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia? Akaamka,
akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie, Upepo
ukakoma, kukawa shwari kuu. Akawaambia, Mbona mmekuwa
waoga? Hamna imani bado? Wakaingiwa na hofu kuu,
wakaambiana, Ni nani huyu, basi hata upepo na bahari
humtii!”
Dhoruba iliyokuja ilikuwa mojawapo wa mateso na
masaliti amabyo Yesu alisema yataletwa na Shetani
punde tu Neno linapopandwa.
Angalia mtazamo wa wanafunzi. Walisumbuka.
“Mwalimu, je, haukujali kuwa twaangamia?”
Walisumbuka kwa sababu Yesu alikuwa amelala na wala
hakuonyesha wasiwasi kama wao, na walimshitaki Yeye
kwa kutojali.
Tunao Uhuru wa Kuamua
Shetani anapoleta mateso dhidi yetu katika kutuibia Neno
la Mungu, tunao uhuru. Tunaweza kumshukuru Bwana
kwa kutuonya ili tusipuuze mbinu za Shetani na
tumukemee. Tunaweza kuwa na usumbuvu, kupoteza
furaha yetu na hapo kumruhusu Shetani kutuibia ufunuo
wa Neno la Mungu ambalo limepandwa mioyoni mwetu.
Je, ni mara ngapi mateso na masaliti yanapokuja, sisi
huanza kulia na kumlaumu Mungu?
􀂱 “Mwalimu, je, hujali kuwa tunangamia?”
􀂱 “Mungu, je, hujali kuwa watoto wangu wanapotea?”
􀂱 “Mungu, je, hujali kuwa magonjwa yamenijia
maishani?”
􀂱 “Mungu, je, hujali kuwa siwezi kulipa mahitaji
yangu?”
Tunapokuwa na huzuni na kumlaumu Mungu kwa
dhoruba maishani mwetu, tunamruhusu Shetani kutuibia
mbegu yenye dhamana ya Neno la Mungu.
Kunena Katika Imani
Imani yenye matunda inahitajika iwapo tutaweka mbegu
ya Neno ndani ya mioyo yetu na kutazamia mazao makuu
ya thelathini, sitini au hata mia ya kile kimepandwa.
68
Marko 4:40 Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna
imani bado? Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani
huyu, basi hata upepo na bahari humtii!”
Kunena Katika Mamlaka
Badala ya kuhuzunika dhoruba inapokuja maishani dhidi
ya mashua yetu, lazima tusimame kinyume cha Shetani na
kwa nunena kwa ujasiri Neno la Mungu kwa imani.
Marko 4:39 Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari,
Nyamaza, utulie, Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.
Uwe Macho
Hata kama Shetani ni adui aliyeshindwa, atafanya kila
kitu kutuzuia kutembea katika mamlaka ya Mungu.
Lazima tuwe macho, imara na tayari kushinda kila pigo
maishani mwetu.
1 Petro 5:8 Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki
wenu Ibilisi, kama samba angurumaye, huzunguka-zunguka,
akitafuta mtu ammeze.
Silaha ya Mungu
Kwa imani, tuvae silaha ya Mungu ili tushinde mbinu za
Shetani.
Waefeso 6:10,11 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana
na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu,
mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
Tunapofanya hivyo, tutajikuta tumesimama kumpinga
Shetani wakati wa dhoruba.
Waefeso 6:13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu,
mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha
kuyatimiza yote, kusimama..
Mamlaka Yetu
Kazi ya Yesu imekamilika! Tayari amemshinda Shetani
na pepo zake.
Duniani, amewaumba waume kwa wake kuenda katika
mamlaka. Amerejesha mamlaka yetu, na sasa, ni lazima
tuinuke na kuonyesha kuwa Shetani ni adui aliyeshindwa.
Ni lazima kwa bidii tuendeleze ufalme wa Mungu hapa
duniani.
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Kulingana na Yohana 10:10, Shetani huja kuyapiga maisha yetu akitumia malengo matatu ya
msingi. Yataje malengo haya.
2. Kulingana na mfano wa mpanzi je, kipa umbele kwa Shetani kama mwizi ni kipi?
3. Kwa nini ni muhimu kutenda katika mamlaka na wala sio kukasirika tunapokutana na mateso?
73
Somo La Tisa
Kanisa na Mamlaka
JE, KANISA NI NINI?
Kutajwa Mara ya Kwanza
Katika agano la Kale, ibada iliwekwa karibu na hekalu au
sinagogi. Hapakuwa kanisa kama vile tunaelewa sasa.
Yesu alipotaja kanisa mara ya kwanza, alidhihirisha pia
vitu vitatu ambavyo vilionyesha kazi Yake juu ya
majukumu mengine yote. Litajengwa na Yesu. Litakuwa
jeshi lenye ushindi ambalo litashinda malango ya kuzimu.
Litakuwa na nguvu za kufunga na kufungua.
Mathayo 16:13-18 Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi,
akawauliza wanafunzi wake akasema, “Watu hunena Mwana
wa Adamu kuwa ni nani?”
Wakasema, “Wengine husema u Yohana Mbatizaji, wengine
Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.”
Akawambia, “Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?”
Simoni Petro akajibu, wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu
aliye hai.
Yesu akajibu, akamwambia, “heri wewe Simoni Bar-yona; kwa
kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu
aliye mbinguni.”
Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu
nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu
haitalishinda.”
Kweli za Kimsingi
Petro alijua kupitia ufunuo wa Mungu kuwa Yesu
alikuwa Kristo, Mwana wa Mungu. Hii ilikuwa ukweli
ambako kanisa lingejengwa.
Lilijengwa na Yesu
Sifa ya kwanza ya kanisa ni kuwa Yesu atalijenga.
Halitajengwa na wanadamu, na mipango au tamaduni zao.
Linashinda Malango ya Jehanamu
Sifa ya pili ni kuwa malango ya kuzimu haitalishinda.
Katika Biblia yenye ufafanuzi tunasoma,
Nitajenga kanisa langu, na malango ya kuzimu (nguvu za
sehemu ya moto) hayatalishinda – au iwe na nguvu kulivunja,
au kulipita.
70
Funguo za Kufunga na Kufungua
Kanisa lina nguvu ya kufunga na kufungua.
Mathayo 16:19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa
mbinguni, na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa
limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani,
litakuwa limefunguliwa mbinguni.
Kuna vitu vitatu ambavyo tunahitaji kujifunza kuhusu
kanisa kwa mara hii ya kwanza Yesu alipolitaja.
􀂱 Kanisa litajengwa na Yesu katika ufunuo kutoka kwa
Baba kuwa Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu
aishiye.
􀂱 Malango ya kuzimu hayatalishinda kanisa.
􀂱 Kanisa litapewa funguo za ufalme wa mbinguni na
kuwa na nguvu ya kufunga na kufungua.
FUNGUO KUREJESHWA
Tumegundua kuwa funguo ni mfano wa mamlaka hapa
duniani. Funguo zinaweza kufunga au kufungua milango
ambayo tumeona kama mtu, jamii, shirika, mji, taifa na
nchi.
Funguo za Kutawala
Hizi zilikuwa funguo za mamlaka ambazo Mungu alimpa
mwandamu alipowaumba mume na mke kwa mfano
wake.
Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano
wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na
ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila
chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.”
Kuibwa na Shetani
Funguo hizi zilikusudiwa na Mungu kutumika kwa mema
hapa duniani. Lakini, Adamu na Hawa walipotenda
dhambi, walimpa Shetani funguo ambaye alikuja kuiba,
kuua na kuharibu.
Funguo za mamlaka, chini ya usimamizi wa Shetani
zilifanyika funguo za mauti na jehanamu.
Ufunuo Wa Yohana 1:18 Na aliye hai, nami nalikuwa nimekufa,
na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za
mauti, na za kuzimu.
Kutwaliwa na Yesu Tena
Hizi zilikuwa funguo za mamlaka ambazo Yesu alinyakua
kutoka kwa Shetani baada ya kuzichukua dhambi zetu
chini ya kuzimu. Yesu alikuja kwa vishindo malangoni
jehanamu, alizitwaa funguo hizi za mamlaka kutoka kwa
71
Shetani. Shetani hana tena mamlaka kisheria hapa
duniani.
Kurejeshwa kwa Mwanadamu
Funguo hizi zilikuwa mamlaka ambayo Yesu
alimurejeshea mwanadamu kama kiumbe kipya baada ya
ufufuo na kupaa Kwake kwa Baba. Kwa maana funguo
hizi zilirejeshwa kwa wenyewe hapa duniani, hazikuwa
tena zitumiwe kama funguo za mauti na kuzimu. Badala
yake zikajulikana kama funguo za ufalme wa mbinguni.
Funguo za Ufalme
Mathayo 16:19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa
mbinguni, na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa
limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani,
litakuwa limefunguliwa mbinguni.
Kwa funguo hizi tunaweza kujenga mapenzi ya Mungu na
ufalme wake hapa duniani.
Huu ni ushindi ambao Yesu aliwafunza wanafunzi Wake
kuomba.
Mathayo 6:9,10 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye
mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako
yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
Tunapotumia, sisi mwili wa Kristo, funguo tulizopewa na
Mungu za mamlaka katika mapenzi Yake, tunaimarisha
ufalme wa Mungu duniani.
MALANGO YA KUZIMU
Kanisa la Kushambulia
Yesu alipotaja neno, kanisa mara ya kwanza, alitaja mara
tu kuwa malango ya kuzimu haitalishinda.
Mathayo 16:18b ... Kanisa langu; wala milango ya kuzimu
haitalishinda.
Ni muhimu kuelewa kuwa Yesu alimaanisha malango ya
kuzimu hayatalipinga kanisa.
Katika nyakati zetu, tunaona malango kama mwanya
kwenye ua. Kwa picha hiyo, ni vigumu kupata ufahamu
wa kweli katika msitari huu. Wengi wetu hatujawai
pingwa na lango
.Je, Malango ni Nini?
Katika nyakati za kibiblia, serikali na biashara ya mji
ilifanyika mbele ya malango. Kwa hivyo malango mbali
na kuweka usalama kwa mji uliozungukwa na ukuta, pia
iliashiria mji na serikali ya nchi hiyo. Mfalme Suleimani
alitaja juu ya hii katika mojawapo ya mithali yake.
72
Mithali 31:23 Mme wake hujulikana malangoni; Aketipo
pamoja na wazee wa nchi.
Kunyakua Malango
Mungu alipombariki Ibrahimu, alitaja kupokea malango
ya adui zake. Hiyo ilikuwa baraka.
Mwanzo 22:17 katika kubariki nitakubariki, na katika
kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na
kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango
wa adui zao.
Baraka zilizowekwa juu ya Rebeka pia zilitaja juu ya
kupokea malango ya maadui.
Mwanzo 24:60 Wakambaraikia Rebeka, wakamwambia,
“Ndugu yetu, uwe wewe mama wa kumi elfu, mara elfu nyingi,
na wazao wako waurithi mlango wa hao wawachukiao.”
Ili kurithi malango ya adui ina maana kuchukua usukani
na kuongoza serikali yake. Sasa tunatakiwa kunyakua
malango ya adui zetu katika roho. Kwa mamlaka, utawala
na shambulio na vita vikali vya kiroho malango
hunyakuliwa.
Mfalme Suleimani alinena juu ya haya.
Mithali 14:19 Wabaya huinama mbele ya wema, Na wasio haki
malangoni mwao wenye haki.
Wengi wamejiona wakipigwa na ibilisi wanapojificha
ndani ya malango kwa uoga. Lakini, ni kanisa wala si
Shetani lenye kusimama na kushambulia.
Sisi, kanisa, inatupasa kuingia malango ya kuzimu na kwa
fujo kuendeleza ufalme wa Mungu duniani kote.
FUNGUO ZA UFALME
Yesu alipotaja kanisa mara ya kwanza, alisema,
“nitawapa ninyi funguo.” Hiyo ingetendeka siku za usoni.
Baadaye, baadaya kifo Chake na ufufuo, alimwambia
Baba, “ninazo funguo!”
Funguo huwakilisha mamlaka yaliyorejeshwa. Ni funguo
ndizo Yesu alinyakua kutoka kwa Shetani
alipomnyang’anya utawala na mamlaka.
Je, ufalme wa mbinguni ni gani, ambao tunazo funguo
zake?
Yesu, mfalme wa wafalme, anatawala na Baba juu ya
dunia nzima. Ni hapa duniani ndipo ufalme Wake
unatakiwa kujengwa.
73
Ufalme wa Mungu ni lazima uenezwe kote duniani wakati
waume kwa wake wanatumia funguo zao
walizorejeshewa za mamlaka ya kiroho.
Hizi ndizo funguo Yesu alisema tutatumia kufunga na
kufungua. Tunayo mamlaka ya kumfunga Shetani na pepo
zake na tunazo funguo za mamlaka ya kuwafungulia
wafungwa! Tunaposhinda vita katika roho itaonekana
wazi, au katika mwili.
KANUNI YA KUFUNGA NA KUFUNGUA
Yesu alisema atatupatia funguo za ufalme wa mbinguni
na chochote tunafunga duniani hufungwa mbinguni na
chochote tunafungulia hapa duniani kinafunguliwa
mbinguni.
Je, maana yake ni nini?
Yesu Amfunga Mtu Mwenye Nguvu
Yesu alinena juu ya kumfunga mtu mwenye nguvu.
Mathayo 12:28, 29 Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa
Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. Ama
awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu?
Ndipo atakapoiteka nyumba yake.
Mtu Mwenye Nguvu ni Nani?
Mtu mwenye nguvu ni Shetani au kiongozi wa mapepo
ambayo ametenga kwa serikali, shirika, au maisha ya mtu.
Yesu aliingia nyumbani mwa mwenye nguvu na
kumufunga yeye Shetani na mapepo zake zitawalazo.
Tunamfunga Shetani na mapepo yake yote yanayotawala
kwa kusema kwa mamlaka,
􀂱 “Shetani, nakufunga wewe katika jina la Yesu!”
Kisha tunatakiwa kumfunga mtu mwenye nguvu, kwa
kusema kwa ujasiri kwa yule mtawala wa pepo,
􀂱 “Wewe pepo mbaya, nakufunga katika jina la Yesu!”
Je, Kufunga ni Nini?
Kufunga maana yake ni kumzusha Shetani au mtawala wa
pepo juu ya hali fulani ambapo Mungu ametuongoza
katika vita vya kiroho.
Kwa mfano, tunapomfunga mbwa kwa nyororo
iliyofungwa kwa kikingi, basi mbwa ataenda tu hadi
mahali fulani. Amezuiliwa kuenda zaidi ya nyororo na
sehemu aliyofungiwa. Tumemzuia katika sehemu yake ya
kufika. Basi hii ndiyo maana ya neno funga.
74
Kuiharibu Nyumba Yake
Kisha, tunatakiwa kuharibu nyumba yake. Tunafanya
hivyo kwa kuwaamuru mapepo chini ya mtu mwenye
mamlaka ku,
􀂱 “Ondoka katika jina la Yesu!”
Tunaweza kuwatambua mapepo haya kwa kuenda katika
karama ya roho na kipawa cha roho na neno la ufahamu.
Pia tunaweza kuwatambua kwa kazi zao za wazi. Kama
vile:
􀂱 Roho za kidini,
􀂱 Roho za vizuizi,
􀂱 Roho chafu – za tamaa na potovu
􀂱 Roho za udhaifu,
􀂱 Roho za kutesa,
􀂱 Roho za kujitia kitanzi
Kemea Roho Hizo!
Kwa kukemea roho hizi tunaiharibu nyumba ya mwenye
nguvu. Nyumba yake inapoharibiwa, hana tena msaada na
tunaweza kumuamuru kuondoka katika jina la Yesu.
Luka 11:21, 22 Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake,
alindapo nyumba yake, vitu vyake vi salama; lakini mtu
mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda,
amnyang’anya silaha zake zote alozokuwa akizitegemea na
kuyagawanya mateka yake.
Yesu tayari amenyang’anya nguvu na mamlaka na
kuwatia aibu. Amepaa juuyao wote na kuketi mkono wa
kuume wa Mungu Baba. Huu ni ukweli uliotimika
mbinguni.
Mamlaka ya Mwamini
Kama waamini, ni lazima tuonyeshe mamlaka yetu na
utawala duniani. Ni lazima sasa tutimize hapa duniani kile
ambacho tayari kimetimizwa ulimwenguni kote –
ambacho kimetimizwa kweli mbinguni. Duniani, ni
lazima tumfunge Shetani pamoja na pepo zake na
kuwaweka wafungwa huru. Lazima tukomeshe ushawizi
wake.
Mathayo 16:19b Na lo lote utakalilolifungua duniani, litakuwa
limefunguliwa mbinguni
Tunapofanya hivyo, sisi pia, tunaziharibu nguvu na
mamlaka na kumtia aibu, kuzikanyaga kwa msalaba.
75
MSIMAMO WA SHETANI
Ameumbwa Bila Ushawishi
Yesu kwa kifo Chake na ufufuo, viliharibu ushawishi wa
Shetani.
Waebrania 2:14 Basi kwa kuwa watoto wameshiriki damu na
mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia
ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani,
Ibilisi
Yeye Hatufanyi Watumwa Tena
Tumewekwa huru na hofu ya kifo na kufungwa.
Waebrania 2:15 ... awaache huru wale ambao kwamba maisha
yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.
Kupitia kazi iliyokamilika ya Yesu katika kifo chake na
ufufuo, waume na wake kamwe wasiwe watumwa katika
hofu ya kifo. Tunapogundua ukweli huu, tunawekwa huru
kabisa kutokana na kufungwa na pia hofu ya ibilisi.
Kazi Zinaharibiwa
Kwa nini Mwana wa Mungu alikuja?
􀂱 Kuziharibu kazi za Shetani!
􀂱 Kuwatia aibu hadharani!
1 Yohana 3:8 Atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi
hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa
Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.
Wakolosai 2:15 Akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya
kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.
MAKANISA YANAYOLALA YANAAMUKA!
Yesu alipokuja hapa duniani kuharibu kazi za ibilisi,
aliweka kando mamlaka Yake kama Mungu. Duniani
kama Adamu wa Mwisho, alitembea na kuhudumu katika
mamlaka na utawala.
Yesu alimshinda Shetani kabisa. Aliwekwa patupu na
kuachwa bila ushawishi. Yesu aliweka “sufuri” kubwa
kwa ibilisi.
Sasa mamlaka haya na utawala ni funguo ambazo
zimerejeshwa kwa mwanadamu aliyekombolewa ambaye,
kwa imani, sasa ni kanisa Lake na mwili Wake duniani.
Kama adui aliyeshindwa, kitu cha pekee anachoweza
kufanya hapa duniani ni kile sisi katika upuzi
tumemruhusu afanye. Kwa ufunuo huu kutoka kwa Neno
la Mungu, tunaweza kuinuka na kumfunga Shetani na
mapepo yake yanayotawala. Tunaweza kuzizusha ngome
76
za Shetani tunapomfunga mtu wa nguvu na kuiharibu
nyumba yake, huku tukiamuru pepo kuondoka katika jina
la Yesu.
2 Wakorintho 10:4 Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali
zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome.
Kanisa ambalo Yesu alisema Atajenga limekuwa jitu
linalolala. Sasa, linaamuka ili kutenda katika mamlaka ya
Mungu na litaharibu ngome za Shetani!
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Je, Yesu alimaanisha nini aliposema kuwa “malango ya kuzimu haitalishinda” kanisa?
2. Yesu alisema kuwa tunatakiwa kufunga na kufungua. Eleza jinsi umepanga kutekeleza
maagizo haya muhimu kutoka kwa Yesu.
3. Kwa kuwa alimfunga mtu mwenye nguvu juu ya mojawapo ya ngome za Shetani, Yesu
alisema kuwa lazima mtu aharibu vitu vyake. Je, nani anatajwa kuwa ndiye mtu wa nguvu? Je,
mbinu ya kuharibu vitu vyake ni ipi?
78
Somo La Kumi
Funguo za Ufalme
YESU ANAZO FUNGUO
Je, unayakumbuka maneno ya ushindi aliyotamka Yesu
aliporejea tena mbinguni?
Ufunuo Wa Yohana 1:18 Na aliye hai hata milele na milele.
Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
Yesu alizichukua funguo za kuzimu na mauti kutoka kwa
Shetani. Yesu alipozichukua dhambi zetu kuzimuni,
haikuwezekana tena Yeye kuwekwa mtumwa.
Matendo Ya Mitume 2:24 ... ambaye Mungu alimfufua,
akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana
ashikwe nao.
Yesu alishinda kifo!
Yesu alirejesha mamlaka, utawala na ufalme kwa
mwanadamu. Alirejesha kwetu vyote alivyoiba Shetani.
Tunajua kuwa Mungu anataka sisi tuishi katika mamlaka
kamili na tawala juu ya Shetani kwa sababu Yeye
alimsulubisha Mwana Wake ili kurejesha vyote
alivyoumba kwetu tuwe na kutenda hapa duniani.
Kile Yesu alifanya hapa duniani, uhai Wake, maisha
Yake, kifo Chake, na kufufuka kwake ilikuwa ili
turejeshwe tena. Alifanya hivyo ili tuende katika
mamlaka na ushindi juu ya Shetani, pepo zake, na vyote
hapa duniani.
DAMU YA YESU – UFUNGUO WA USHINDI
Mungu aliumba Adamu, alimvuvia uhai Wake
Mwenyewe. Uhai huu haukuwekwa tu kwa sehemu moja
mwilini mwa Adamu. Mungu aliweka uhai ndani ya damu
ya Adamu. Ulipitishwa kila sehemu ya mwili wa Adamu
wakati wote.
Musa aliandika kuwa uhai wa kiumbe uko ndani ya damu.
Mambo Ya Walawi 17:11a Kwa kuwa uhai wa mwili u katika
damu...
Dhambi ya Adamu - Mauti
Katika dhambi, Adamu alipoteza uhai wa Mungu
uliokuwa ndani ya damu yake. Uhai huu unaweza tu
kurejeshwa kwa mwanadamu kupitia mpango wa Mungu
78
wa ukombozi. Ili mwanadamu arejeshwe tena kwa mfano
wa Mungu, lazima awe na uhai wa Mungu ndani ya damu
yake.
Katika mpango wa Mungu wa ukombozi, Mwana Wake
Yesu ataimwaga damu Yake.
Waebrania 9:22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafisha
kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.
Adhabu ya dhambi, ambayo ilikuwa kifo, ililipwa kwa
niaba na yule aliyekuwa hajapoteza uhai wa Mungu ndani
ya damu yake kupitia dhambi.
Kwa kupajikwa na Roho Mtakatifu na kuzaliwa na bikira,
Yesu alirithi damu ya Adamu. Alifanyika dhabihu
iliyokamilika aliyejitolea kwa dhati na kutoa maisha Yake
kwa kumwaga damu Yake mwenyewe.
Kupitia Damu ya Yesu
Tunapata
􀂱 Msamaha wa Dhambi
Kukombolewa kwetu ku ndani ya damu ya Yesu.
Waefeso 1:7 katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao
ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa
neema yake…
1 Petro 1:18,19 ... nanyi mfahamu kwamba mlikombolew si
kwa vitu viharibivyo, kwa fesha au dhahabu; mpate kutoka
katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;
bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana kondoo asiye na
ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.
􀂱 Haki
􀂱 Wokovu
Tumedhibitishwa na kupata haki ya Mungu juu ya maisha
yetu iliyorejeshwa kwa damu ya Yesu.
Warumi 5:8,9 Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye
mwenyewe kwetu sis, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu,
tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana tukiisha
kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu
kwa yeye.
Hukumu ya Mungu iliyokamilika ilitoshelezwa na
tuliokolewa kutokana na ghadhabu ya Mungu wakati
Yesu kwa niaba yetu aliibeba adhabu ya kifo kwa
kumwaga damu Yake msalabani.
Ni kwa kuhusika katika damu ya Yesu iliyomwagika iliyo
na uhai wa Mungu, ndipo tunaweza kupata uhai Wake
ndani yetu.
79
Yohana 6:53 Basi Yesu akawaambia, “Amin, amin,
nawaambieni, Msipoula mwili wake mwana wa Adamu na
kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.”
􀂱 Ushirika
Damu ya Yesu itaondoa hali zote za dhambi juu ya
maisha yetu ili kwa mara nyingine uhai wa Mungu
urejeshwe.
1 Yohana 1:7 Bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika
nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana
wake, yatusafisha dhambi yote.
􀂱 Kukombolewa
Kukombolewa kwetu na msamaha kamili ni kwa damu
Yake.
Wakolosai 1:13,14 Naye alituokoa katika nguvu za giza,
akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa
pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani
msamaha wa dhambi
Pasipo kupokea dhabihu ya ukombozi na zawadi ya
Mungu ya wokovu katika damu ya Yesu iliyomwagika,
hakuna vile mwanadamu atasamehewa na kurejeshwa.
Waebrania 9:22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa
kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.
Waebrania 9:12 Wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali
kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika
patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.
􀂱 Hawana Dosari
􀂱 Tunaweza Kutumika
Kwa damu ya Yesu tumeoshwa ili tumtumikie Mungu.
Waebrania 9:14 Basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye
kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu
kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na
matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?
􀂱 Tuwe na Ujasiri
Adamu alipotembea katika ushirika kila siku katika
uwepo wa Mungu kabla hajatenda dhambi, hata kwa
damu ya Yesu, sasa mwanadamu, yu huru kutokana na
lawama na hukumu, na anaweza tena kutembea katika
uwepo wa Mungu.
Waebrania 10:19 basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasisi wa
kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu…
80
􀂱 Kuwa na Amani
Amani na marudiano vinawezekana kwa damu Yake.
Wakolosai 1:19,20 Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu
wote ukae, na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi
yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake, kwa
yeye ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.
􀂱 Kurejeshwa katika Hali ya Awali
Ilikuwa damu ya Yesu iliyomshinda Shetani
ilivyokomboa na kumrejesha mwanadamu katika uhai wa
Mungu kupitia kuzaliwa upya.
Shetani alikuja kuiba, kuua na kuharibu mwanadamu
ambaye Mungu aliumba kwa mfano na sura ya kweli hapa
duniani. Kupitia dhambi, mwanadamu alipoteza uhai wa
Mungu. Mwanadamu alikuwa hajiwezi katika mapigo ya
Shetani maishani mwake. Kwa mpango wa Mungu wa
ukombozi katika kumwagika kwa damu ya Mwana Wake,
mwanadamu angerejeshwa kamili kwa hali yake ya awali
na uhusiano na Mungu. Kwa damu ya Yesu, mwanadamu,
aliyekuwa kashindwa, sasa angefanyika mshindi tena.
􀂱 Kufunikwa Katika Ulinzi
Kama vile kuhani katika Agano la Kale alipochukua
damu ya mwanakondoo wa dhabihu na kuimwaga kwenye
kiti cha rehema cha Mungu ili kufunika au kuosha dhambi
za watu, vile vile leo, kwa imani, damu ya Mwanakondoo
huwafunika na kuwazingira wanadamu waliokombolewa.
􀂱 Ushindi
Katika damu ya Yesu, tunapata ushindi!
Tunapotembea katika msamaha, katika kumtii Mungu na
kwa imani, tunaweza kusema kwa ujasiri:
􀂱 “Shetani, mimi nimefunikwa na damu ya Yesu!”
􀂱 “Jamii yangu na mali yangu imefunikwa na damu ya
Yesu!”
􀂱 “Shetani, umeshindwa na damu ya Yesu!”
􀂱 “Kwa sababu ya damu ya Yesu, hutanigusa!”
Hata Yesu alipomshinda Shetani kwa damu Yake, nasi
pia tunaweza kuwa washindi kwa damu ya Yesu! Kwa
kinga ya damu Yake, hakuna silaha dhidi yetu itafaulu.
Ufunuo Wa Yohana 12:11a Nao wakamshinda kwa damu ya
Mwana-kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao
hawakupenda maisha yao hata kufa.
Shetani alishindwa na damu ya Yesu.
81
Ufunguo wa mamlaka ya damu ya Yesu umepewa kila
mmoja wetu ambao kwa damu hiyo wamekombolewa.
Kwa nguvu ipatikanayo katika ufunguo wa damu Yake
sisi tu washindi na Shetani ataendelea kushindwa
maishani mwetu.
NENO LA MUNGU – UFUNGUO WENYE USHINDI
Upanga wa Roho
Katika Waefeso, silaha yetu ya ushindi katika vita
imeelezwa kama “upanga wa Roho, ambayo ni Neno la
Mungu” (6:17). Neno la Mungu linapotoka vinywani
mwetu huwa silaha kuu dhidi ya Shetani na ambapo hana
kinga. Tunaponena Neno la Mungu kwa mamlaka,
tutamshinda Shetani maishani mwetu.
Ufunuo Wa Yohana 12:11a Nao wakamshinda kwa damu ya
Mwana-kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao.
Neno Katika Ushuhuda
“Neno la ushuhuda wao” inaweza kutafsiri kwa makini
kama “Neno katika ushuhuda wao.” Ushuhuda wetu ni
kile tunanena. Tunapoacha kunena shida, mawazo yetu,
hofu yetu, na kuanza kunena kwa ujasiri kile Neno la
Mungu linasema kuhusu hali yetu kisha nasi pia tutakuwa
washindi.
Neno Huleta Ushindi
Ili kuwa na Neno la Mungu likitoka vinywani mwetu kila
wakati, inatupasa kusoma, kujifunza na kulitafakari Neno.
Kisha litakuwa mizizi iliyokomaa katika imani maishani
mwetu.
1 Yohana 2:13,14 Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu
mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi,
vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nimewaandikia
ninyi, watoto, kwa sababu mmemjua Baba.
Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye
aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu
mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi
mmemshinda yule mwovu
Vijana hawa walijulikana kuwa wenye nguvu katika
kushinda kwa sababu walikuwa na Neno la Mungu ndani
yao. Waliponena kwa ujasiri Neno hilo vinywani mwao
kwa mamlaka na utawala wa Mungu waliwashinda
waovu.
Waefeso 6:17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa
Roho ambao ni neno la Mungu.
Upanga wa Roho ni Neno la Mungu.
82
Ufunuo Wa Yohana 19:13-16 Naye amefvikwa vasi
lililochovywa katika dame, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
Na majeshi yaliyo mbinguni watkamfuata, wamepanda farasi
weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi. Na upanga mkali
hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye
atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo
la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi. Naye
ana jina limeandikwa katika vasi lake na paja lake;
WAFALME, NA BWANA WA MABWANA
Nena Neno
Yesu alisema mfano bora wa imani ni mtu aliyeelewa
mamlaka na kufahamu jinsi ya kulinena Neno.
Mathayo 8:8-10 Yule akida akamjibu, akasema, “Bwana, mimi
sistahili wewe uingie chini ya dari yangu, lakini sema neno tu,
na mtumishi wangu atapona. Kwa maana mimi nami ni mtu
niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu;
nikimwambia huyu, nenda, huenda; na huyu, njoo, huja; na
mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya”
Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale
waliomfuata, “Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa
namna hii, kwa ye yote katika Israeli!”
Kulithibitisha Neno
Neno la Mungu litathibitishwa kwa ishara na maajabu.
Marko 16:19-20 Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao,
akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa
Mungu.
Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda
kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara
zilizofuatana nalo. Amina.
Yesu Ni Neno
Jina la Yesu hasa ni Neno la Mungu.
Ufunuo Wa Yohana 19:13 Naye amevikwa vasi lililochovywa
katika damu, na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata,
wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe,
safi.
Yohana 1:1 hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno
alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
Neno Halitarejea Tupu
Mungu alinena kwa nguvu Neno Lake katika Isaya.
Isaya 55:11 Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika
kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi
yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
83
Mungu alinena juu ya nguvu iponyayo katika Neno
kupitia Daudi.
Zaburi 107:20 Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa
katika maangamizo yao.
Neno tunalonena katika mamlaka linatimiza mambo
yampendezayo Mungu. Neno la Mungu linatuahidi kuwa
litastawi!
Maneno Hujenga
Maneno yana nguvu ya kujenga.
Waebrania 11:3 Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu
uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana
havikufanywa kwa vitu vinavyo dhahiri.
Maneno yana Mamlaka
Yesu alinena Neno kwa mamlaka.
Luka 4:36 Mshangao ukawashika wote, wakasemezana
wakisema, “Ni Neno gain hili, maana awaamuru pepo wachafu
kwa uwezo na nguvu, nao hutoka.”
Neno Ndani – Neno Nje
Ni vyema kulijua Neno, lakini tusipokutana na hali zetu
tukinena Neno la Mungu vinywani mwetu, hatutakuwa na
ushindi!
Yesu alinena Neno kwa mamlaka na nguvu.
Imani ya Mungu:
􀂱 Inaamini Neno,
􀂱 Inanena Neno,
􀂱 Huona Neno likitimiza miujiza.
Ufunguo wa Neno la Mungu hautashindwa tunapoendelea
kunena katika mamlaka na utawala.
Ili tutende katika utawala hapa duniani ambapo ndivyo
tuliumbwa duniani kufanya, Yesu ametupa, kanisa Lake,
funguo za mamlaka ya ushindi wa vita za kiroho.
Tunapogundua funguo hizi na njia bora ya kuzitumia,
tutajikuta tunaishi katika ushindi juu ya vita maishani.
Tutajikuta tumekuwa wale Yesu amesema tutakuwa.
Sisi ni zaidi ya washindi,
Sisi ni washindi katika jina Lake
84
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Eleza kwa nini damu ya Yesu inatimiza katika kushinda mapigo ya ibilisi au mapepo.
2. Toa mfano wa jinsi kunena Neno la Mungu limekupa ushindi katika maisha yako.
3. Je, ni maandiko gani utakayokariri na utakayotumia kama silaha katika vita vya kiroho?
86
Somo La Kumi na Moja
Jina La Yesu
JINA LA YESU – UFUNGUO WA USHINDI
Tunapotumia jina la Yesu, tunanena katika mamlaka ya
Yesu. Tunaponena katika hilo jina, kuna matokeo kama
vile Yesu mwenyewe amesimama pale akinena katika hali
hiyo. Ametupa haki ya kutumia jina Lake.
Ishara Kufuata Kuamini Katika Jina
Ishara zitafuata wale wanaoamini katika jina la Yesu.
Marko 16:15-18 Akawaambia, Endeni ulimwenguni mwote,
mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa
ataokoka, asiyeamini, atahukumiwa.
“Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio, kwa jina langu
watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka,
hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa,
wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.”
Hapakuwa na mpangilio katika Kigiriki, lugha ambayo
Agano Jipya liliandikwa hapo awali. Vituo na mpangilio
uliopo katika Biblia zetu iliongezwa na watafsiri kutokana
na maoni yao.
Mariko 16:17 inasoma,
Na ishara hizi zitafuatana nao waamini ...
Kifungu hiki kinaweza kutafsiriwa kwa makini kama,
Na ishara hizi zitawafuata wale wanaoamini katika jina langu
...
Yesu alisema, ni muhimu tuamini katika jina Lake. Ni
lazima tuelewe mamlaka yetu katika jina la Yesu. Ni
lazima kwa ujasiri tuachilie mamlaka hayo kwa imani
tunapotumia jina la Yesu.
Tunaponena na kutenda imani yetu katika jina la Yesu,
tutakemea mapepo. Tutaweka mikono yetu kwa
wagonjwa, na watapata nafuu.
Haki ya Kustaajabisha
Kabla ya kumalizika kwa kazi ya Yesu msalabani, hakuna
yeyote angetaja majina ya Mungu. Yalidhaniwa kuwa
takatifu kutajwa kwa sauti. Yaliandikwa ndani Mahali
Patakatifu Sana, na yalijulikana tu kwa Kuhani Mkuu.
Yesu alipowapa waamini haki ya kulitumia jina Lake,
ilikuwa fursa mwafaka, na isije ikapuuzwa.
Kufungua Mamlaka ya Yesu
86
Kwa sababu Yesu alikuwa Mwana wa Mungu,
􀂱 Alikuwa na mamlaka yote mbinguni.
Kwa sababu Yesu alikuwa Mwana wa Adamu,
􀂱 Alikuwa na mamlaka duniani.
Mathayo 28:18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia,
“Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.”
Tunapolitumia jina Lake, mamlaka na nguvu yenye
kusisimua huachiliwa. Ni kama tumesimama pahali Pake
na kutumia mamlaka Yake.
Nguvu Za Kisheria
Yesu alipotupatia haki kisheria kutumia jina Lake,
aliweka matumaini Yake yote kwetu. Kisheria, alitupa
Uwezo wa Kisheria kulitumia jina Lake.
Katika mahakama Uwezo wa Kisheria ni stakabadhi ya
sheria inayompa mtu haki ya kutumia jina la mtu
mwingine. Mtu aliyetengwa kwa hilo, anapotia sahihi
mapatano kwa niaba ya mtu na kuweka pia nakala ya
Uwezo wa Kisheria kwa patano hilo. Inakubalika kisheria
kama vile mtu huyo ametia sahihi patano hilo mwenyewe.
Kusikia Kutoka Kwa Mungu
Yesu alipohudumu hapa duniani, alifanya hivyo kwa
niaba ya Baba Yake.
Yohana 5:19 “Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile
ambalo amwona Baba analitenda, kwa maana yote ayatendayo
yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.”
Sasa tunapohudumu hapa duniani, inatupasa tutende kwa
niaba ya Mwana. Tusilitumie jina la Yesu kujitosheleza
wenyewe bila kwanza kuchukua muda kusikia kutoka
kwa Mungu.
Kulitumia Jina Kwa Msaha
Kujaribu kulitumia jina la Yesu ili kujitosheleza bila
kwanza kutambua mapenzi ya Mungu, itakuwa kutumia
jina Lake kwa mzaha.
Kumbukumbu La Torati 5:11 Usilitaje bure Jina la BWANA,
Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia,
mtu alitajaye Jina lake bure.
Jina Juu ya Majina Yote
Jina la Yesu li juu ya majina mengine
Wafilipi 2:5-11 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo
ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu, ambaye yeye mwanzo
alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa
na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho, bali alilifanya
87
kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana
mfanowa wanadamu.
Tena alipoonekana ana umbo kama mtii hata mauti, naam,
mauti ya msalaba.
Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina
lile lipitalo kila jina, ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la
vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi, na kila
ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA kwa utukufu wa
Mungu Baba.
􀂱 Kila pepo ana jina.
􀂱 Kila mtu ana jina.
􀂱 Kila ugonjwa na maradhi yana jina.
􀂱 Kila mbinu ya Shetani ina jina.
􀂱 Jina la Yesu linapotajwa nguvu za mapepo hutoroka.
􀂱 Jina la Yesu linapotajwa, saratani na magonjwa
mengine yote huinama.
􀂱 Jina la Yesu linapotajwa, mbinu za Shetani
hushindwa.
Jina la Yesu li juu ya majina mengine. Kila goti litapigwa
kwa unyenyekevu wa Bwana Yesu jina Lake linapotajwa
katika imani.
Mapepo Yanatii Jina
Mapepo yanajua jina la Yesu, na watalitii jina hilo.
Luka 10:17, 19 Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha,
wakisema, “Bwana, hata pepo watutii kwa jina lako.”
“Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni
kama umeme. Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na
nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu
kitakachowadhuru.”
Mathayo 28:18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia,
“Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.”
Mamlaka yote amepewa Yesu. Kwa jina la Yesu tunayo
mamlaka hayo hayo hapa duniani.
Amini Katika Jina Lake
Tunaamuriwa kuamini katika jina la Yesu.
1 Yohana 3:23 Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina
la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama
alivyotupa amri.
Tunatakiwa kuamini katika jina la Yesu ili kupata uzima
wa milele.
88
Yohana 3:18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini
amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakuliamini jina la
Mwana pekee wa Mungu.
Yohana 20:31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya
kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa
kuamini mwe na uzima kwa jina lake.
Tunaweza kuwa na hakikisho kamili la wokovu wetu kwa
sababu tunaamini katika jina Lake.
1 Yohana 5:13 Nimewaandika ninyi mabo hayo, ili mjue ya
kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana
wa Mungu.
Uliza Katika Jina Lake
Tumeagizwa kuuliza katika jina la Yesu.
Yohana 14:12-14 Amin, amin nawaambieni, Yeye aniaminiye
mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atafanya, naam, na
kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi, naenda kwa
Baba. Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya,
ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote
kwa jina langu, nitalifanya.
Yesu alipoondoka kwenda kwa Baba, aliwaagiza wafuasi
Wake walitumie jina Lake. Aliwaambia kuwa kile
wangeuliza, Angefanya, ili Baba atukuzwe katika Mwana.
Yohana 15:16 Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi
niliyewachagua ninyi, nami nikawaweka mwende mkazae
matunda, na matunda yenu yapate kukaa, ili kwamba lo lote
mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.
Yohana 16:23,24 Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote, Amin,
amin, nawaambia, mkimwomba Baba neno lo lote atawapa
kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu;
ombeni, nanyi mtapata, furaha yenu iwe timilifu
Tumeagizwa kuuliza katika jina la Yesu.
Kutenda Yote Katika Jina Lake
Tunatakiwa kufanya kila kitu katika jina la Yesu. Je, hii
ni fursa iliyoje!
Wakolosai 3:17 Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo,
fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu
Baba kwa yeye.
Ni lazima pia tutambue kuwa yote tunayofanya ni lazima
tufanye katika jina la Yesu. Tukifanya hivyo tunapata
msisimko katika maisha yetu.
89
MITUME WALILITUMIA JINA LA YESU
Mitume na waamini wa awali katika kitabu cha Matendo
kwa ujasiri walilitumia jina la Yesu na matokeo yalikuwa
miujiza.
Nguvu Katika Jina Lake
Matendo Ya Mitume 3:1-10 Basi Petro na Yohana walikuwa
wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa.
Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye
alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika
mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu
waingiao ndani ya hekalu. Mtu huyu akiwaona Petro na
Yohaya wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka.
Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema,
“Tutazame sisi. Akawaangalia, akitaraji kupata kitu kwao.
Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini
nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa
Nazareti, simama uende.”
Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na
vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu.
Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda, akaingia ndani
ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu
Mungu. Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiketi
na kuomba sadaka penye mlango Mzuri wa hekalu, wakajaa
ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata.
Imani Katika Jina Lake
Petro alieleza kuwa kibali cha kulitumia jina la Yesu,
ilikuwa ni kuachilia mamlaka katika jina la Yesu.
Matendo Ya Mitume 3:12 Hata Petro alipoyaona haya
akawajibu wale watu, “Enyi Waisraeli, mbona mnatukazia
macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu
zetu sisi, au kwa utauwa wetu sisi?”
Matendo Ya Mitume 3:16 “Na kwa imani katika jina lake, jina
lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua, na
imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu
mkamilifu mbele yenu ninyi nyote.”
Uponyaji Katika Jina Lake
Baada ya uponyaji huu, Petro na Yohana walishikwa,
wakawekwa jela siku kutwa na kutishwa na viongozi wa
kidini wasinene tena katika jina la Yesu. Petro alijibu kwa
ujasiri swali lao kuhusu uponyaji huu akisema:
Matendo Ya Mitume 4:10 ... “Jueni ninyi nyote na watu wote
wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti,
ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika
90
wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele
yenu.”
Wokovu Katika Jina Lake
Baadaye Petro na Yohana walipolitumia jina la Yesu
wakihudumu uponyaji kwa mtu kiwete, idadi ya
walioamini iliongezeka na kuwa kama elfu tano.
Matendo Ya Mitume 4:4 Lakini wengi katika hao waliosikia lile
neno waliamini, na hesabu ya watu waume ikawa kama elfu
tano.
Wokovu wetu upo katika jina nzuri la Yesu.
Matendo Ya Mitume 4:12 Wala hakuna wokovu katika
mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya
mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa
kwalo.
Hofu ya Mwanadamu kwa Jina Lake
Petro na Yohana walitishwa na viongozi wa kidini
wasinene tena katika jina hilo.
Matendo Ya Mitume 4:17,18 “Lakini neno hili lisije likaenea
katika watu, na tuwatishe wasiseme tena na mtu awaye yote
kwa jins hili. Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa
wala kufundisha kwa jina la Yesu.
Ujasiri Katika Jina Lake
Wakati huo roho wa ujasiri alikaa juu ya Petro na
Yohana.
Matendo Ya Mitume 4:29,30 Basi sasa, Bwana, yaangalie
matisho yao, ukawajalie watumwa wako kunena neno lako
kwa ujasiri wote, ukinyosha mkono wako kuponya, ishara na
majaabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu.
Philipo Alihubiri Jina Lake
Matendo Ya Mitume 8:12 Lakini walipomwamini Filipo,
akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake
Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.
Alishikwa Kwa Ajili ya Jina la Yesu
Paulo alitumwa kuwashika wale walioliita jina la Yesu.
Matendo Ya Mitume 9:14 hata hapa ana amri itokayo kwa
wakuu wa makuhani awafunge wote wakuitiao Jina lako.
Kuchaguliwa Kulibeba Jina Lake
Paulo alichaguliwa na Mungu ili kueneza jina la Yesu
duniani.
Matendo Ya Mitume 9:15 Lakini Bwana akamwambia, “Nenda
tu, kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina
langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.”
91
Kuhubiri Katika Neno Bila Hofu
Matendo Ya Mitume 9:27 lakini Barnaba akamtwaa,
akampeleka kwa mitume, akamtwaa, akampeleka kwa mitume,
akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, nay a kwamba
alisema naye, na jinsi alivyohubiri kwa ushujaa katika
Dameski kwa jina la Yesu.
Ukombozi Katika Jina
Matendo Ya Mitume 16:18 Akafanya haya siku nyingi. Lakini
Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yulepepo,
“Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu.” Akamtoka
saa ile ile.”.
Heshima Kuu ya Jina Lake
Matendo Ya Mitume 19:17,18 habari hii ikajulikana
na Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu
ikawaingia wote, na jina la Bwana Yesu likatukuzwa.
Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama,
wakidhihirisha matendo yao.
ISHARA NA MAAJABU KATIKA JINA LA YESU
Tunapomsikiliza Mungu na kutii sauti Yake, lazima
tutoke kwa ujasiri na kwa imani na kutumia mamlaka ya
jina la Yesu. Tunapofanya hivyo, tutaona ishara na
maajabu maishani na katika huduma zetu kila siku.
Matendo Ya Mitume 4:29-31 Basi sasa, Bwana, yaangalie
matisho yao, ukawajalie watumwa wako kunena neno lako
kwa ujasiri wote, ukinyosha mkono wako kuponya, ishara na
majaabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu.
Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale
walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu,
wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.
Tunapoendelea kutumia mamlaka na uwezo wa jina la
Yesu, nasi pia tutatikisa ulimwengu kwa uwepo na uwezo
wa Mungu wa ajabu.
Funguo katika maisha ya Mkristo aliye mshindi
inapatikana katika jina kuu la Yesu.
Tunaweza kuenda katika nguvu zile kama zilivyoelezwa
katika kitabu cha Matendo, tunapojiunga na kanisa la
awali katika kutumia mamlaka katika jina la Yesu.
92
MASWALI YA KUJIFUNZA
1. Toa mifano miwili kutoka kwa kitabu cha Matendo ambapo mitume walitumia jina la Yesu.
2. Je, nini maana yake tunaposema jina la Yesu ni kama kuwa na Uwezo wa Kisheria?
3. Katika changamoto ambazo unapitia kwa sasa, je, umepanga kupata ushindi kwa kulitumia
jina la Yesu?
98
Somo La Kumi na Mbili
Ushindi wa Vita vya Kiroho
KUTAYARISHWA KWA AJILI YA VITA
Nguvu Za Kimungu
Sasa kwa kuwa tunaelewa utengano wa milele na
kutambua mamlaka yetu na silaha zetu zenye nguvu,
tunatayarishwa katika nguvu na ushindi wa kivita.
Paulo aliandika,
2 Wakorintho 10:4 Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali
zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome...
Wengi wamejaribu kuingia vitani bila ya ufunuo.
Hawakuelewa mamlaka waliyo nayo na kuwa wao ni nani
katika Yesu.
Kwao, vita vya kiroho vimekuwa vikali vinavyoendelea
dhidi ya adui mwenye nguvu. Wamezungukwa na Shetani
na pepo zake. Kadri wanapomtazama Shetani na pepo,
kadri anavyoonekana mkubwa, mchoyo, na mwenye
nguvu sana.
Adui Aliyeshindwa
Nabii Isaya aliandika kuhusu siku za usoni za Shetani.
Alitueleza picha ya mwisho wake.
Isaya 14:15-17 Lakini utashushwa mpaka kuzimu, Mpaka
pande za mwisho za shimo. Wao wakuonao watakukazia
macho, watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye
aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisha falme,
aliyewafungua wafungwa wake waende kwao?'
Watu watamkazia macho huyu aitwaye Shetani ambaye
ameshindwa na kuaibishwa. Watamtazama kwa
mshangao yule waliyemdhania kuwa alikuwa mkubwa na
mwenye nguvu. Watamwona amejaa hofu na aibu.
Watauliza, “je, huyu siye mtu …?” Je, huyu siye mtu
ambaye kila mtu anamfahamu sana?”
Watamkazia macho yule aliyeambulia patupu.
Watamtazama kwa dhihaki. Watamwona ameshindwa
kabisa.
Tukiwa na ufunuo juu yetu ndani ya Yesu, basi kamwe
Shetani hatatutawala. Kila mara tumezungukwa na Yesu!
Shetani ni adui aliyeshindwa. Nguvu zake zimeshindwa.
Yesu alifanya “sufuri” ndani yake. Amevuliwa silaha,
akalemaa na kutiwa fedheha hadharani.
94
Aliwekwa Patupu
Waebrania 2:14b Ili kwa njia ya maui amharibu yeye
aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi.
Hatutashindwa kamwe tunapopigana na Shetani na pepo
zake. Tumepewa uwezo juu ya nguvu zote za adui.
Tunapoingia katika vita, lazima tuanzie mahali pa ujasiri
katika hakikisho na imani kuwa tutashinda. Ni sharti
tuingie vitani tukisimama kwenye ufahamu sisi ni nani
ndani ya Yesu. Tusije tukapanga kumenyana na adui
mwenye nguvu sana. Bali sisi, badala yake, tutazamie
mbele kwa furaha ushindi tunapoonyesha kuwa Shetani
tayari ameshindwa.
􀂱 Shetani si “hoja sana”
􀂱 Yesu ni “Hoja Sana”!
􀂱 Tunaweza kufanya mambo yote katika yeye.
Wafilipi 4:13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye
nguvu.
HATUA YA USHINDI
Nguvu na mamlaka ya mwamini si kitu cha kuchezea
katika kutimiza matakwa yetu binafsi. Lazima tuwe katika
makubaliano na mapenzi ya Mungu.
Kukiri Dhambi
Ili tuwe washindi katika vita vyetu vya kiroho, lazima
kwanza tutupu na kukiri dhambi zetu kwa Mungu na
kupokea msamaha. Mtume Yohana alituambia jinsi ya
kufanya hivyo.
1 Yohana 1:9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu
na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na
udhalimu wote.
Kukata Kauli
Lazima tuyatoe maisha yetu asili mia moja, kwa Yesu
kama Bwana maishani mwetu.
Warumi 12:1,2 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake
Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya
kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala
msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa
upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo
mema, ya kumpendeza, na ukamilifu
Kutengwa na Ulimwengu
Lazima tujitenge na kuhusika na anasa za dunia hii.
95
2 Timotheo 2:4 Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za
dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari.
Kuweka Kando Tamaa Zetu
Lazima tuweke kando tamaa zetu na kuongozwa na Roho
wa Mungu. Sisi, kama Yesu, lazima tuseme, “Mimi
ninatenda kile naona Baba yangu akitenda.”
Yohana 5:19 Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin,
nawaambia, “Mwana awezi kutenda neno mwenyewe ila lile
ambalo amwona Baba analitenda, kwa maana yote ayatendayo
yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.”
Mungu amempa kila mwamini sehemu fulani ya mamlaka
juu ya:
􀂱 Ndoa zao, watoto na jamii
􀂱 Mahali wanaishi – ujirani, miji, mataifa
􀂱 Mahali wametumwa na Mungu kuhudumu
Mara nyingi hatutaachiliwa katika roho zetu kuenda vitani
dhidi ya ngome za Shetani nje ya sehemu tuliyotengewa
na Mungu katika mamlaka. Mungu anataka waamini
katika sehemu hiyo wajifunze mamlaka yao na kuzizusha
ngome.
Kuwa na Mtazamo wa Upendo
Kama askari, waume kwa wake wenye imani katika jeshi
la Mungu, tusiwe na kiburi na tusiowajali wengine.
Filemoni 1:4,5 Namshukuru Mungu wangu sikuzote,
nikikukumbuka katika maombi yangu, nikisikia habari za
upendo wako na imani uliyo nayo kwa Bwana Yesu na kwa
watakatifu wote.
Lazima tumkazie Shetani na mapepo, lakini lazima
tutembee katika upendo kwa watu wengine. Tunamchukia
Shetani, lakini tunawapenda watu.
Lazima kila mara tukumbuke kuwa mamlaka yetu kama
waamini si kuwatawala watu, bali ni kuchukua utawala
juu ya Shetani na mapepo zake.
Tunapotembea katika upendo kwa Mungu na watu
wengine, tusiwe kila mara tunafikiria juu ya vita dhidi ya
Shetani.
Tusiwe na Maridhiano
Tunapotembea katika uhusiano wa karibu na Mungu –
bila mchanganyiko wa dhambi, au mambo ya kidunia
maishani mwetu – Mungu atatuonya juu ya mipango ya
Shetani ili kutushinda kwa kutembea katika vipawa vya
kiroho na ujuzu wa kuona mapepo. Kadri tunavyokuwa
96
karibu na Mungu, ndivyo tunapotambua uwepo wa uovu,
hila na mchanganyiko yanapotokea.
Tuyaweke macho yetu kwa Yesu. Ikiwa Shetani na
mapepo zake zitasimama mbele yetu – zishughulikie,
zipinge, zikemee – kemea mawazo yasiyo ya Mungu.
Kisha tuyaweke macho yetu kwa Yesu tukimsifu kwa
ushindi.
2 Wakorintho 2:14 Ila Mungu ashukriwe, anayetushangiliza
daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye
kila mahali kwa kazi yetu.
Hakuna Mtu Spesieli wa Kiroho
Katika ufalme wa Mungu, si mpango Wake kuwa vita vya
kiroho na ukombozi vitimizwe kwa kuita, au kuenda kwa,
mwenye ujuzi au “mwenye nguvu afukuzaye mapepo”.
Badala yake, kama mtume Yakobo alivyoandika, kila
mwamini sharti ampinge Shetani.
Yakobo 4:7 basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye
atawakimbia.
SILAHA YA MUNGU
Mungu ametoa kwetu silaha kwa ajili ya vita
tunavyopigana. Mtume Paulo hakuandika kuwa tuvae
silaha yetu; aliandika kuwa tuvae silaha ya Mungu.
Wakati jeshi la zamani walivaa silaha zao, na chapeo na
kufunika nyuso zao, wote walionekana kama jeshi lenye
nguvu, misuli, na hatari kwa adui. Bila kujali upungufu
wa mwili ulio ndani ya silaha, walionekana kama jeshi
kuu.
Tunapovaa silaha ya Mungu, tunaonekana tu kama
Mungu mbele ya Shetani. Kisha yote tunayoweza kufanya
ili kushinda vita ni kuongea kama Mungu, kutembea
kama Mungu, na kutenda kama Mungu!
Nguvu Zetu
Ni lazima tuende katika nguvu za Mungu. Tusije
tukaingia vitani kwa nguvu zetu.
Waefeso 6:10,11 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana
na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu,
mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani
Vita Vyetu
ms. 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na
nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza
hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho
Paulo anatukumbusha kuwa vita vyetu si dhidi ya mwili
na damu, bali ni watawala, mamlaka, na uovu wa jeshi la
97
mapepo. Vita vyetu si katika dunia hii ya kawaida, bali
katika ulimwengu wa kiroho.
Silaha Zetu
􀂱 Ukanda wa Ukweli
􀂱 Dirii ya Haki
􀂱 Miguu ya Injili
ms. 13-15 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu,
mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha
kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga
kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa
miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani.
Paulo alirudia neno “simama” mara tatu. Kwanza alisema
kuwa siku ya uovu ikija, tutaweza kusimama. Kisha
akasema kuwa baada ya kufanya yote, lazima tusimame.
Mwishowe, akasema, simama imara basi na dirii ya haki
mahali pake, na miguu yetu iwe na utayari wa njili ya
amani.
Ukweli ni Neno la Mungu. Ili liwe ulinzi kwetu, ni lazima
tufahamu kile linasema.
Dirii yetu ya haki ni haki ya Mungu. Hatuitajiki kuwa
kamili, lakini tunaitajika tusiwe na dhambi-ijulikanayo
maishani mwetu ili dirii hii iwe kwenye nafasi yake.
Miguu yetu iwekwe na utayari wa injili ya amani. Utayari
ni kazi yetu na hufanyika kwa kujifunza Neno la Mungu.
Paulo aliandika kwa Timotheo:
2 Timotheo 2:15 Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na
Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia
kwa halali neno la kweli.
􀂱 Ngao ya Imani
􀂱 Chepeo Cha Wokovu
􀂱 Upanga wa Roho
Waefeso 6:16,17 ... zaidi ya yote mkiitwa ngao ya imani,
ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto
ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga
wa Roho, ambao ni neno la Mungu.
Inatupasa kutumia ngao ya imani ili kuizima mishale ya
Shetani. Mishale ni mawazo, majaribu, magonjwa na
mbinu zingine Shetani anarusha kwetu. Lazima tuzisime
kwa imani katika Mungu na imani katika Neno Lake.
Chapeo ya wokovu huvaliwa tunapopata wokovu. Huu ni
wokovu ambao kando na kutuhakikishia uzima wa milele,
pia huturejesha kwa vyote tulivyoumbwa tuwe
tulipoumbwa kwa mfano Wake. Chapeo ya wokovu
98
huturuhusu kuyafanya mawazo yetu upya katika ufunuo
wa wokovu wetu kamili.
Warumi 12:2a Wala msiifuatishe namna ya dunia hii, bali
mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu.
Kufanya upya mawazo huja kwa kuyaosha mawazo yetu
kwa “maji” yaishiyo ya Neno la Mungu tunapolisoma,
kujifunza na kulitafakari.
Waefeso 5:26 ... Ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji
katika neno...
Tumepewa silaha moja ya kinga na mbayo ni upanga wa
Roho ambalo ni Neno la Mungu. Paulo anatueleza zaidi
juu ya upanga wa Roho katika kitabu cha Waebrania.
Waebrania 4:12 Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu,
tena lina ukali kuliko upanga uwao wote, ukatao kuwili, tena
lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta
yaliyomo ndani yake, tena li jepesi kuyatambua mawazo na
makusudi ya moyo.
Neno la Mungu ni ukanda wa kweli, mavazi ya miguu
yetu na upanga wetu! Je, pana tashwishi yoyote juu ya
umuhimu wa kulisoma Neno?
Maombi ya Ushindi
Mara kwa imani, tunapovaa silaha kamili ya Mungu,
inatupasa kuomba katika Roho nyakati zote.
Waefeso 6:18 ... kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati
katika kuwaombea watakatifu wote.
Tunapoendelea kuomba kwa imani kwa wateule wote,
tukitumia mamlaka yetu, tutaona ngome za Shetani
zikianguka. Tutakuwa washindi katika vita na kupinga
nguvu za Shetani.
Waebrania 11:33,34 ... ambao kwa imani walishinda milki za
wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa
vya samba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya
upanga, walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa
hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.
KUTAYARISHWA KWA KAZI YA HUDUMA
Yesu alisema tuenende ulimwenguni kote na kuhubiri
habari njema.
Marko 16:15 Akawaambia, “Endeni ulimwenguni mwote,
mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.”
Isaya alinena juu ya wale walioleta habari njema.
Isaya 52:7 Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye
habari njema, Yeye aitangazaye amani, aletaye habari njema
99
ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Alumbiaye
Sayuni, Mungu wako anamiliki!”
Paulo anatueleza kuwa sisi ni zaidi ya washindi na kuwa
hakuna kitakachotutenga na upendo wa Mungu.
Warumi 8:37-39 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na
zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana
nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima,
wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala
yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala
yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza
kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana
wetu.
Yesu anatwambia kuwa tokea nyakati za Yohana
Mbatizaji hadi sasa, ufalme wa Mungu unaendelea kwa
nguvu.
Mathayo 11:12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa
ufalme wa mbinguni hupatikaka kwa nguvu, nao wenye nguvu
wauteka.
Paulo anatwambia kuwa nguvu hizo ni imani!
Waebrania 11:33 ...ambao kwa imani walishinda milki za
ufalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa via
samba.
100
Kwa Kumalizia
Kazi ya Yesu imekamilika!
Amemshinda Shetani
na kurejesha vyote
Shetani alivyonyakua kwa Adamu na Hawa
Amerejesha mamlaka hapa duniani
na kumkomboa mwanadamu
kwa wale ambao ni
kanisa Lake – Jeshi Lake kuu!
Sasa ni juu yetu!
sisi ndio tunapeleka ujumbe
wa wokovu huu mkuu kwa dunia nzima.
Tunatakiwa kuendeleza kwa bidii
ufalme wa Mungu..
Tunatakiwa kuwafanya maadui
wa Yesu miguu ya kiti Chake.
Tunatakiwa kuenda katika mamlaka
hapa duniani,
leo!
102
Mistari ya Kukariri
Waefeso 6:12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama,
bali ni juu ya ufalme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili,
juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
1 Petro 5:8,9 Mwe na kiasi na kukesha, kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi,
kama samba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu
ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani,
mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu
zenu walioko duniani.
Yohana 10:10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu, mimi nalikuja ile
wawe na uzima, kasha wawe nao tele.
Mwanzo 1:26 Mungu akasema “Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa
sura yetu, wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa
angani, na wanyama, na nchini yote pia, kila chenye
kutambaa kitambaacho juu ya nchi.”
Mwanzo 3:15 Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati
ya uzao wako na uzao wake, huo utakuponda kichwa, na
wewe utamponda kisigino.
Waebrania 2:14 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye
naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti
amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani Ibilisi.
1 Yohana 3:8 Atendaye dhambi ni wa Ibilisi, kwa kuwa ibilisi hutenda
dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu
azivunje kazi za Ibilisi.
Wakolosai 2:15 Akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo
kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.
Ufunuo Wa Yohana 1:18 Na aliye hai, nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata
milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti na za kuzimu.
Waefeso 1:22,23 Akavitia vitu vyote chini ya chini ya miguu yake, akamweka
awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa, ambalo
ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote
katika vyote.
Wakolosai 1:13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na
kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake.
Warumi 16:20 Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu
upesi.. Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi.
Amina.
102
Luka 10:19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na
nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu
kitakachowadhuru..
Mathayo 16:18,19 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu
nitalijenga kanisa langu, wala milango ya ya kuzimu
haitalishinda. Nami nitakupa Wewe funguo za ufalme wa
mbinguni; na lo lote utakaliolifunga duniani, litakuwa
limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungwa duniani,
litakuwa limefunguliwa mbinguni.
Ufunuo Wa Yohana 12:11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-kondoo, na kwa
neno la ushuhuda wao, ambao hawakupenda maisha yao hata
kufa.
1 Yohana 2:13,14 Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemshinda
yule mwovu. Nimewaandikia ninyi, watoto, kwa sababu
mmemjua Baba. Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa
sababu mmejua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia
ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu
linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.
Wafilipi 2:9,10 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirisha
mno, akamkirimia jina lile lipitalo kila jina, ili kwa jina la
Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani,
na vya chini ya nchi.

No comments:

Post a Comment