Friday 5 December 2014

KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU

MPANGO WA KUFANYA NA KUSAIDIA
AFRIKA MASHARIKI NA KATI
CHURCH OF GOD WORLD MISSIONS
KARAMA ZA ROHONI
A Pentecost, Inavyofanya Kazi Na Kukaribia Watu
Peter A. Thomas
Translation:Maeda David Gabriel
ii
iii
KIDOKEZO KARAMA ZA ROHO
UTANGULIZI 1
I. KARAMA ZA UDHIHIRISHO 3
1. Asili ya Karama 3
2. Madhumuni ya Karama 4
II. KARAMA ZA UFUNUO 7
NENO LA HEKIMA 7
1. Asili ya Karama 7
2. Inavyotumika na Inavyofanya Kazi Karama 8
(1) Hulisaidia Kanisa Wakati wa Migogoro 8
(2) Huwasaidia Watu Binafsi Wakati wa Migogoro 8
(3) Husaidia nyakati za Hatari 9
3. Dalili Kwamba Karama hii Inafanya Kazi 9
NENO LA MAARIFA 9
1. Asili ya Karama 9
(1) Siyo Werevu na Asili ya Kibinadamu 10
(2) Haipatikani Katika Ukufunzi wa Elimu ya Biblia 10
(3) Siyo Uganga Wa Utabiri 10
2. Inavyotumika na Inavyofanya Kazi Karama 11
3. Neno la Maarifa na Maono 12
KUPAMBANUA ROHO 13
1. Asili ya Karama 13
(1) Siyo Karama ya Kuhukumu au Kulaumu 14
(2) Siyo uchunguzi wa Kisaikolojia 14
2. Matumizi ya Karama 14
(1) Hutumika Kwa Ajili ya Uponyaji 14
(2) Hutumika Katika Ushauri 15
(3) Hutumika Katika Maombi 15
(4) Hutumika Kumfungua Mtu Aliyepagawa 15
3. Kazi ya Karama 15
(1) Silaha ya kujilinda nayo 15
(2) Ilimfichua Mtumishi wa Shetani 16
(3) Kulifichua Chanzo Cha Unabii 16
(4) Ilimfichua Mjumbe Maarufu wa Shetani 16
4. Yaonekana Katika Utekelezaji Kimatendo 16
(1) Hatua Nne kwa Utendaji Kazi wa Karama 17
(2) Njia Nyingine za Upambanuzi 17
(3) Je Mkristo Anaweza Kumilikiwa na Pepo? 18
(4) Mizimu ya mababu Haiwezi Kummiliki mtu 19
(5) Umilikiwaji, Uonevu, na Uteswaji 19
5. Jinsi ya Kutoa Roho Chafu
iv
III. KARAMA ZA KUTENDA KAZI 23
KARAMA ZA KUPONYA 23
1. Asili ya Karama 24
2. Matimizi na utendaji kazi wa Karama 24
3. Sababu za Magonjwa 25
(1) Magonjwa na Dhambi 25
(2) Ugonjwa na Meza ya Bwana 26
(3) Ugonjwa na Mashambulio ya Kiroho 26
(4) Ugonjwa na Kumilikiwa na Pepo 26
(5) Ugonjwa na Sababu za Kawaida za Kuambukiza 27
4. Mungu Amavyoponya 27
(1) Wazee Katika Kanisa 27
(2) Kupitia Waumini Wote Wanapowekea Mikono 27
5. Mapenzi ya Mungu Kuhusu Uponyaji 27
KARAMA YA IMANI 29
1. Aina Mbalimbali 29
(1) Imani iokoayo 29
(2) Tunda la Imani 29
(3) Imani ya Asili 29
2. Karama ya Imani na Asili Yake 29
3. Karama Inavyotenda Kazi na Jinsi Inavyotumika 30
4. Amri ya Imani 31
MATENDO YA MIUJIZA 32
1. Asili ya Karama 32
2. Matumizi na Kazi ya Karama 33
(1) Kazi za Ukombozi 33
(2) Kazi ya Kutoa Mahitaji 33
(3) Kazi ya Nidhamu 33
(4) Kazi za Ulinzi 32
3. Kuijaribisha Karama 34
4. Umuhimu wa Karama Hii 35
IV. KARAMA ZA UVUVIO 39
UNABII 39
1. Asili ya Karama 39
(1) Karama ya Unabii na Ofisi ya Nabii 39
(2) Unabii Hueleweka Kama Utabiri Tu 40
(3) Karama Inavyochanganywa na Kuhubiri 40
2. Karama Inavyotenda Kazi na Jinsi Inavyotumika 40
(1) Unabii wa Kujenga 40
(2) Unabii wa Kutia Moyo 40
(3) Unabii wa Kufariji 41
3. Karama Inavyojiendesha 41
4. Jinsi ya Kuupima Unabii 42
(1) Neno la Mungu 43
(2) Chema ni Kipi? 43
(3) Kusudi Sahihi 43
v
(4) Ubora na Udhahiri 43
5. Nani Anayeweza Kuupima Unabii? 43
6. Matumizi Mabaya ya Karama 44
7. Maoni Kuhusu Utekelezaji 45
KUNENA KWA LUGHA 45
1. Asili ya Karama 46
(1) Ushahidi wa maandiko wa Ubatizo wa Roho Mtakatifu 46
(2) Lugha Kama Karama 46
2. Kunena kwa Lugha Kutendavyo Kazi na Jinsi Kunavyotumika 47
(1) Lugha Hugawiwa kwa Makusudi 47
(2) Watu Kusema na Mungu kwa Msemo wa Kiungu 47
(3) Watu Hujijenga 48
(4) Kwa Maombezi na Maombi/Dua 48
(5) Kwa Maombi Yenye Mamlaka 48
3. Kanuni Kuhusu Karama Hii 48
(1) Wapi na Lini Tunene? 48
(2) Katika Ibada Moja Wangapi Waseme 49
4. Maoni ya Kiutekelezaji 49
TAFSIRI ZA LUGHA 50
1. Asili ya Karama 50
2. Matumizi ya Jinsi Karama Inavyofanya Kazi 51
(1) Mudhumuni yaleyale kama ya Unabii 51
(2) Na Mmoja Atafsiri 51
3. Maoni Kuhusu Utekelezaji 51
V. KUKOSEKANA KWA KARAMA KANISANI SIKU HIZI 55
1. Ujinga na Kukosa Mafundisho 55
2. Kiburi na Kujidai Umekamilika 55
3. Hofu (Fear) 55
4. Makaburi au Wodi ya Wazazi? 55
VI. JINSI YA KUPOKEA KARAMA ZA KIROHO 55
1. Masharti ya Utendaji Kazi wa Karama 56
(1) Pokea Roho Mtakatifu 56
(2) Zitakeni Sana 57
(3) Jitoe kwa Mungu 57
2. Jinsi Karama Zinavyogawiwa 57
VII. UPOKEAJI NA UTUMIAJI WA KARAMA 57
1. Nani Mtumiaji wa Karama 57
2. Mtazame mpaji Karama 59
BIBLIOGRAPHY

1
KARAMA ZA ROHO
UTANGULIZI
Karne mbili baada ya Mitume kufa, kulitokea jambo la kuhuzunisha. Karama za Roho ambazo
Kristo aliziacha kama sehemu ya urithi wake kwa mwili wake, kidogo kidogo na kwa dhahiri
zilikoma kuonekana zikitumika miongoni mwa Jumuia ya Kikristo. Hata hivyo mwanzoni mwa
karne ya ishirini, Mungu aliwarudishia kilichopotezwa na Kurudi kwa Kanisa, wakati wanaume
kwa wanawake waliojitoa kwa Mungu walipopata karama, mbubujiko mpya wa Roho
Mtakatifu. Kutokana na ziara hiyo ya Kimungu karama za roho zilirejea katika Mwili wa Kristo
na ndivyo ulivyozaliwa mfumo wa Upentekoste. Waumini wa awali wa mfumo huu ambao
baadaye walijulikana kama "Wapentekoste" walisimama kinyume na upinzani mkubwa na
kusisitiza kuwa kilichowatokea kilikuwa kinatokana na maandiko. Kadri muda ulivyopita,
upinzani ulipunguka, kisha ujumbe na matukio ya kipentekoste yakazidi kukubalika na ujumbe
wa Kipentekoste (Kiroho) ukapanuka ambavyo haikutegemewa miongoni mwa madhehebu ya
Kiinjili na yale ya zamani. Mfumo wa Uamsho wa Kiroho ndivyo ulivyozaliwa.
Lakini ukweli huu mkuu ulipozidi kupanuka na kukubalika ulikabiliwa na matatizo. Ufafanuzi
wa Kipentekosti wa maandiko kuhusu kubatizwa kwa Roho Mtakatifu na asili na utendaji kazi
wa Karama za Kiroho ulibishiwa na kupingwa vikali. Maoni na tafsiri tofauti zilienea kwa
haraka. Baadhi yake yalileta mwanga mpya kwenye kweli za zamani. Lakini mawaidha mengine
yalipotosha kweli za kibiblia zilizokubalika kwa miaka mingi iliyopita. Kwa hiyo, somo hili juu
ya "Karama za Roho" ni jitihada ya kupata mambo manne yafuatayo:
1. Kufumbua zaidi asili, utendaji kazi na matumizi ya karama za
Roho kama zilivyo- fahamika tangu zamani kwa mtazamo wa
kipentekoste.
2. Kutoa maoni ya kiutekelezaji kwa ajili ya kufanya kazi.
3. Kueleza sehemu zenye utata na mafundisho yasiyo ya kimaandiko
kuhusu karama, kama yanavyoonekana Afrika na Ulaya.
UTANGULIZI
2
4. Kuwapa changamoto waKristo walioupokea wokovu waiaminio
pentekoste kutaka sana Roho Mtakatifu, na pia karama za rohoni
ili kusudi tusipoteze urithi wetu wa Kipentekoste "Kiroho".
Hatimaye somo hili litamalizia kwa kueleza mambo mawili muhimu: Kwa nini karama ni haba
au hazimo tena Kanisani na jinsi ya kupokea karama za rohoni.
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-
I. KARAMA ZA UDHIHIRISHO
Katika 1 Wakor: 12:8,10 tunasoma kuhusu karama tisa za kiroho ambazo tunaziita karama za
udhihirisho ili kuzitofautisha na zile karama za huduma (Mitume, manabii, wainjilisti n.k.) Kwa
kawaida karama za udhihirisho hugawanywa katika makundi matatu kila moja na karama tatu
kwa kuzingatia tabia zake.
KARAMA ZA UFUNUO
Neno la Hekima
Neno la Maarifa
Kupambanua Roho
KARAMA ZA UTENDAJI
Imani
Karama za Kuponya
Matendo ya Miujiza
KARAMA ZA UVUVIO:
Unabii
Aina za Lugha
Tafsiri za Lugha
Karama tisa za Roho mara nyingi hutenda kazi moja ikishirikiana na nyingine. Ingawaje katika
somo hili kwa ajili ya uchambuzi na uchunguzi, tunazitenganisha karama hizi, hata hivyo ukweli
ni kwamba katika utendaji huwa zinachanganyikana na mara nyingi husimama kama chombo
kimoja cha nguvu za kiroho na uwezo. Zikipatana na kuingiliana huku zikitenda kazi moja kwa
nyingine.
1. Asili Ya Karama
Neno CHARISMA - katika Lugha ya Kiyunani linatumika wakati linapoonyesha karama za
kiroho, na siyo DOMA (karama ya Upendo) au DOREA (Karama ya bure inayoelezea tabia ya
mpokeaji) na siyo DORON.(Kuonyesha heshima) au DOSIS (Karama) kama kitu/amana -
itolewayo au kuwekwa kama akiba.
Charisma ya jinsi hii ni karama ile ambayo mtu hupewa bila kuistahili tofauti na kitu akipatacho
mtu kwa kufanya shughuli fulani. Kwa sababu hiyo kila mtu ambaye karama inadhihirika ndani
kamwe asiione karama kama medali ya ubora wake au ishara ya cheo chake. Badala yake ni
alama ya uaminifu wa Mungu. Huzuni nyingi zilizowakuta watu wengi zingekuwa zimeepukwa
kama ukweli huu ungalikumbukwa daima.
Wakristo wangi wamebabaishwa na wale walioshindwa kutofautisha kati ya aina za Charisma.
Hii imesababishwa na wale wanaodai kwamba Charisma ni kipawa cha asili ambacho
KARAMA ZA UDHIHIRISHO
4
kimewekwa wakfu kwa ajili ya Mungu. Hawa hawawezi kukubaliana na Wapentekoste ambao
husisitiza kwamba karama zote tisa ni za Kimungu kabisa kwa kitabia kwa kuzingatia 1
Wakorintho 12: Kwao hao mtazamo wa namna hiyo ni finyu mno.
Wengine hushikilia kuwa kila aliye na Charisma ya asili moja kwa moja anayo pia karama ya
Kiungu ya Kiroho. Lakini msimamo huu nao pia una makosa, ambayo ni wazi ukisoma 1 Wakor
7:7 ambapo tunaelezwa juu ya Charisma ya asili itokayo kwa Mungu (IDION CHARISMA EK
THEOU) Maandiko hayo yanaelekeza kwamba inaweza kuwa "charisma" kwa mtu kuwa mzazi
au kumtumikia Mungu bila kuoa, yaani katika useja. Charisma ya mamna hii hupatikana kwa
waaminio na wasioamini pia. Mtu hawezi kuwa mwanadamu kamili bila charisma kama hizo.
Kama tunavyoona Charisma (a-kicharisma) ni pana kwa maana linaweza kutumika kuelezea
karama zote za asili na za Roho. Hata hivyo, itakuwa ni makosa kusema kwamba kila kipawa
cha asili ni charisma, na charisma zote ni za asili. Ni lazima tutamke wazi kuwa kuna aina mbali
mbali za charisma. Kutofautisha huku ni muhimu sana.
Mbali na charisma ya asili kuna charisma ya MUNGU (CHARISMA THEOU) tunayosoma
maelezo yake katika Warumi 6:23. Ni dhahiri kuwa karama kama hiyo si kipawa cha asili.
Agano Jipya huzungumzia pia CHARISMA CHRISTO - karama za Kristo, ambazo kwa mujibu
wa Warumi 5:15,16 ni msamaha wa dhambi, kuhesabiwa haki kupitia imani kwa neema. Pia
kuna CHARISMA HUMIN PHEUMATIKON, au karama za Roho. (WARUMI 1:11) ambazo
hasa ndizo tunahusikanazo katika somo hili. Jambo moja hukutwa katika karama hizi zote, nalo
ni Neema ya Mungu isiyokuwa na mwisho. Lakini bado karama zote kila moja inao upekee
wake na kila moja ina asili, maana na utendaji kazi wake tofauti na nyingine.
Tunapoziangalia karaza za Roho CHARISMA HUMIN PHEUMATIKON) kila moja kipekee,
tunahitaji kukumbuka kuwa kila karama ni ya kimiujiza. Hakuna chembe ya asili ndani ya
yoyote. Karama zote huja kwetu kama karama za Kiungu kutoka kwenye kiti cha enzi cha
Mungu, kwa ajili ya kufanya kazi ya Kristo.
2. Madhumuni ya Karama
Madhumuni ya karama za Roho, yako katika makundi makuu matano yafuatayo.
(1) Kulijenga kanisa (1 Korintho 14:3-4)
(2) Kuwajenga waaminio (1 Wakorintho 14:4)
(3) Kuthibitisha neno lilohubiriwa (Marko 16:20)
(4) Kupanua ufalme wa Mungu (Mdo 5:2-14)
(5) Kuliinua jina lake (Mdo 3:8).
KARAMA ZA UDHIHIRISHO
5
Wakati wowote na mahali popote pale haya hayana budi kukumbukwa, hasa katika nyakati zetu
hizi ambapo karama za Roho zinapoonekana zikitenda kazi, na wengine huzitumia kama
maliwazo "ya kiroho" au kustaajabishia watu. Mahali popote karama hizi zitakapotumika kwa
sababu tofauti na madhumuni matano yaliyotajwa hapo juu, (tutakuwa na wajibu na haki ya
kudadisi na kukosoa matumizi ya karama hizo). Udhihirisho huo lazima upatiwe changamoto.
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-
KARAMA ZA UDHIHIRISHO
6
See Self Study
II. KARAMA ZA UFUNUO
Mara nyingi sana katika maisha tunahitaji mtu fulani kutuonyesha njia. Vile vile mara nyingi
sana katika maisha ya Kikristo na hasa zaidi katika utumishi wa Kikristo, tunahitaji kufaidika au
kupata msaada wa ufahamu au maarifa ya Kimungu. Kwa neno la maarifa, neno la hekima au
kupambanua roho, Bwana anatoa ujuzi huo kwa watu wake.
Ingawa Neno la Mungu hutushauri kuwa tutamani kwa bidii karama zilizo njema, hatuambiwi
wazi karama hizo ni zipi. Ingawa karama za unabii na za kuponya husisitizwa mno, lakini
inaelekea iliyo ya kwanza miongoni mwa karama za Roho ni neno la hekima, jambo ambalo
kweli linafaa kwa ajili ya ubora unaosisitizwa sana katika maandiko. Kwa hiyo karama hii ndiyo
tutakayo ichunguza kwanza.
NENO LA HEKIMA
1. Asili ya karama
Neno la hekima ni majawapo ya karama za ufunuo ambayo kwa kupitia hiyo Mungu
huwashirikisha watu sehemu tu ya hekima yake kuu. Kwa hiyo, wakati mwingine hufunua
mawazo yake yasiyo na mwisho, akili ina mwisho na katika hiyo kumpa aaminiye utambuzi,
utatuzi na mwongozo unaohitajika wakati huo.
Neno la hekima si busara ya asili. Wako watu wenye hekima ya asili kuliko ya kawaida na
hutambuliwa na jamii kuwa ni watu wenye hekima na wajuzi. Kwa kawaida hekima kama hii
huongezeka kutokana na kukua kiumri. Kuna watu wanaoita hii karama hekima ya asili
iliyotakaswa. Yaani kwa maana nyingine kutokana na kuongoka na kujitoa kwa Mungu hekima
ya asili inageuka karama ya kiroho. Lakini hivi sivyo kwa sababu karama hii si hekima bali
neno la hekima. Ni muhimu kwetu kuelewa hivyo jambo hili. Neno la hekima laonekana mara
kwa mara na wakati hekima ya Kimungu inapotakiwa. Ni kipawa cha kiroho kinachohitajiwa
kwa wakati fulani.
Karama inaweza ikaonekana kwa mtu ambaye hafikiriwi kuwa na hekima. Kwa wakati
mwingine mtu kama huyo hutenda kitu cha kijinga au kisicho na maana. Lakini chini ya upako
wa Roho anaweza akapokea ghafla neno la hekima" kwa ajili ya mazingira hayo ya kipekee.
Kwa hiyo kiini cha karama hii si hekima ya mwanadamu bali ni kuvuviwa na Roho. Mtu
mwenye karama hii hageuki yeye kuwa ghala la hekima. Anaweza tu kunena maneno yenye
hekima ya Kimungu wakati Roho anapomtumia. Wakati Roho anapomaliza kazi saa hiyo
hawezi kusema tena "maneno ya hekima" Ukweli ni kwamba anaweza hata kusema ujinga.(Siyo
nyumba ya hazina ya hekima).
KARAMA ZA UFUNUO
8
2. Inavyotumika na inavyofanya kazi karama
(1) Hulisaidia Kanisa wakati wa migogoro
Neno la hekima ni muhimu kwa ajili ya kulijenga Kanisa kwa kulipatia ushauri wa hekima.
Tuna mifano mingi ya kibiblia jinsi karama hii ilivyosaidia kanisa. Miwili imo katika Kitabu cha
Matendo ya Mitume.
Katika Matendo 6:1-7; tunasoma kuhusu tatizo lililowahusu wajane, wa Kanisa la kwanza. Kwa
neno la hekima tatizo hili liliweza kutatuliwa kwa jinsi iliyowaridhisha watu wote. Mgogoro
ulimalizwa kwa kutumiwa karama hii. Neno la hekima pia laonekana katika Mdo: 15:6-11,
wakati kamati ya mitume ilikubali uzuiaji wa sheria kwa mataifa. Matokeo yake walisema.
"Inaonekana vizuri kwa Roho Mtakatifu na kwetu". Kutokana na karama hii kutumika Kanisa la
zamani liliepushwa na migogoro mikubwa ambayo ingalileta magawanyiko.
(2) Huwasaidia watu Binafsi wakati wa migogoro
Jinsi neno la hekima linavyoweza kuwa msaada wa pekee kwa mtu wakati wa mateso
inathibitishwa na mambo yaliyomtokea binti fulani aliyeishi katika nchi ambako ilikuwa ni
marufuku kumwabudu Mungu.
Alipokuwa njiani kuelekea kwenye ibada ya kanisa la siri alisimamishwa na askari ambaye
alitaka kujua anakoelekea. Kama angalisema kwamba anaelekea kanisani au kwenda kusoma
Maandiko, angekamatwa. Basi aliomba kimoyomoyo, akimwomba Mungu kumpa hekima.
Alipopokea neno la hekima akajibu "Nakwenda nyumbani kwa baba yangu. Kaka yangu
amekufa na wasia wake na agizo lake la mwisho litasomwa asubuhi hii. Katika wasia wake kuna
urithi nilioachiwa. Askari alimpigia saluti akamruhusu apite.1
Na mfano mwingine wa udhihirisho wa karama hii ulionekana katika maisha ya Yesu.
Alipoulizwa kama ni haki kulipa kodi kwa Kaisari, alitoa jibu linalokumbukwa daima, akisema
"Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari na ya Mungu yaliyo ya Mungu". Wasikilizaji walistaajabu, na
yeye akaepuka kukamatwa kwa kukosa kulipa kodi.
Katika Luka 21:12-15 tuna habari za Yesu kuhusu mwanzo wa utendaji kazi wa karama hii.
Wakati wakristo watakapoletwa mahakamani kuulizwa kuhusu imani yao ili kuwatisha,
hawahitaji kufikiria la kuwajibu kwa sababu Yesu aliwaahidi. "Nitawapa kinywa na hekima
ambayo watesi wenu wote hawatawaweza kushindana nayo wala kuipinga".
1 R.E. McAlister, The Manifestation of the Spirit. (Toronto: Full Gospel Publishing House, nd.), p. 13.
KARAMA ZA UFUNUO
9
(3) Husaidia nyakati za Hatari
C.W. Conn anasema ushuhuda wa msichana mshirika wa Church of God aliyekuwa amejazwa
Roho Mtakatifu, ambaye mara moja alimwelezea tukio hili lifuatalo.
Siku moja alipokuwa anafanya kazi jikoni akasikia msukumo mkubwa kuacha kazi zake ili
afanye maombi. Kwa kuwa alitamani kukamilisha kazi, aliamua kuendelea na kazi yake huku
akiomba. Lakini neno likaja kwake kwa nguvu likisema "Acha kazi sasa na uombe". Wakati huu
akanyenyekea na kutii sauti ya Roho akaenda chumbani ambamo alikuwa anaombea kila siku.
Alipopiga mlango kama ilivyokuwa kawaida yake. Alipopiga magoti tu kuomba akasikia mtu
anaingia nyumbani akaanza kutembea ndani ya kila chumba. Na huyu mtu alipoanza kusukuma
mlango wa chumba alimokuwemo yule binti na akaukuta umefungwa, hakujaribu kuufungua
kwa nguvu. Kwa sababu hakuona mtu basi mtu huyo akaondoka akaenda nyumba ya jirani
ambamo alikuwa mwanamke asiye Mkristo, akambaka na akamuua.2 Hayo ndiyo yangemtokea
dada huyu mkristo kama asingesikiliza na kupokea neno la hekima.
3. Dalili kwamba karama hii inafanya kazi
(1) Wakati neno la hekima linafanya kazi wakati wa taabu utatuzi utapatikana
ambao utam-shangaza na kumtosheleza kila mtu.
(2) Karama hii itasaidia watu binafsi kutoa jibu sahihi kwa wakati sahihi katika
njia sahihi.
(3) Inaweza ikatusababisha kufanya mambo ambayo baadaye tutajua kuwa
ulikuwa ni mwongozo halisi wa Mungu au Bwana ameingilia kati kwa ajili
ya kutuhifadhi kama mambo yaliyomtokea dada yetu hapo juu.
Hebu tukumbuke tena kuwa sisi siyo ghala la hiyo hekima. Inakuja tu kwetu kwa wakati Roho
Mtakatifu anapoidhihirisha ndani yetu na kupitia kwetu.
NENO LA MAARIFA
1. Asili Ya Karama
Neno la maarifa ni udhihirisho wa Roho Mtakatifu katika taarifa au kweli ambazo Mungu hutia
katika mtu aaminiye ambazo ni Mungu tu awezaye kuzijua ili kulisaidia kanisa au mtu binafsi,
wakati wa shida na uhitaji. Karama hii inaonekana wakati mshiriki wa mwili wa Kristo
anapoweza kutambua, ghafla na dhahiri mahitaji ya kiroho, kimwili au ya vitu vinginevyo ya
mshirika mwingine. Mara nyingi hii hutokea ili kumwezesha huyo aliyepokea ufunuo kumsaidia
yule mwenye kuhitaji.
2 Charles W. Conn, A Balanced Church, (Cleveland: Pathway Press, 1975), pp. 114-115.
KARAMA ZA UFUNUO
10
Karama hii inaweza kufunua kweli za kiroho na zile za kimwili pia. Inaweza kutujulisha mambo
yaliyopita, (jambo ambalo ni muhimu kwa ushauri wa wakati uliopo na yale ya baadaye. Neno
la maarifa linaweza na litafunua dhambi, sehemu za vifungo ambavyo mtu anahitaji ukombozi,
na pia kuonyesha watu wagonjwa waliopo katika mkutano. Roho Mtakatifu anatia maarifa hayo
katika moyo, yaani roho ya muumini ambaye karama hii inapita kwake kwa kutenda kazi. Kwa
kawaida inahitaji ujasiri na imani kwa mtu kutamka jambo aliloonyeshwa, na pia kuchukua
hatua inapohitajiwa. Lakini viongozi Wakristo wanahitaji kuwa waangalifu endapo neno la
maarifa linatolewa wakati wa ibada, au miongoni mwa waaminio. Tamko hilo linapoujia mwili
wa Kristo, lazima liambatane na Maandiko, na haliwezi kuongeza kitu kwa Neno la Mungu.
Kwa kuwa ni kazi maalum inayoonyesha kuwa Roho Mtakatifu ameingilia kati, haina budi
kuenenda na msingi wa Neno. Haya ndiyo masharti ya kuanzia katika kuupima ujumbe wa
maarifa yatokanayo na neno hilo, hasa zaidi kwa sababu siku zilizopita karama hii ilitumiwa
vibaya. Kabla ya kuchunguza jinsi karama hii inavyotenda kazi, tunahitaji kuangalia kwanza
maoni potofu yanayoweza kushikiliwa kuhusu karama hii.
(1) Siyo Werevu Wa Asili ya Kibinadamu
Neno la hekima haliji kutokana na elimu au werevu wa asili wa mtu. Kama ingepatikana hivyo,
basi haiwezi kuitwa karama bali itakuwa ni kitu cha kufuzu au upatacho kama malipo ya jasho.
Udhihirisho wa Roho Mtakatifu haupatikani kama mafanikio mengine ya asili ya wanadamu.
(2) Haipatikani Katika Ukufunzi wa Elimuya Biblia
Baadhi ya waandishi na wasemaji, na hata walio mashuhuri miongoni mwao, walifikiri na bado
wanafikiri kwamba karama hii ama ile ya Neno la hekima ni kwa ajili ya kutafsiri Maandiko.
Kwa hiyo karama hizi wangepewa wahudumu tu, lakini ukweli nikwamba ni kwa ajili ya
waaminio wote.
("Ufunuo wa Roho umetolewa kwa kila mmoja" 1 Kor. 12:7) Ukweli ni kwamba hakuna karama
yoyote ya udhihirisho ambayo ni lazima kwa ajili ya kuhubiri tu au kufundisha tu. Karama zilizo
lazima kwa kazi hizo hutokana mumo kwa mumo ndani ya huduma. Kama isingekuwa hivyo
tungeitaje watumishi ambao hawajajazwa Roho Mtakatifu na niwahubiri wa nguvu. Karama za
kiroho ziko zaidi ya mpangilio wa mahubiri ya neno, zimewekwa kwa makusudi ya nyongeza
ambazo ni kwa ajili ya ishara za miujiza zinazofuatilia na kuthibitisha mahubiri, mafundisho na
Uinjinlisti. Tunahitaji kutofautisha kati ya huduma ya mtumishi ya Kunena na "Kunena" Ile ya
pili ni kwa ajili ya kuthibitisha neno lililosemwa (Mdo 1:1, Mark 6:30).
(3) Siyo Uganga Wa Utabiri
Roho inayofanya kazi kupitia kwa waganga au watabiri na wanajimu ina chanzo chake kwa
roho chafu. Watu wenye vipawa hivi wanaweza kuona yajayo au kufunua yaliyopo, kama
msichana yule mwenye roho ya uaguzi alivyofanya kutabiri (Mdo 16:16). Ingawa mambo hayo
KARAMA ZA UFUNUO
11
yanaonekana ni ya maana, ni ya kishetani na hutumika kwa ajili ya faida ya kifedha kwa
wanaotenda kazi hiyo; kwa kawaida huwa yanasababisha wasiwasi na hofu. Uwezo huo hauna
uhusiano wowote na karama ya ajabu ya Neno la hekima, ambayo hutumika kwa ajili ya
kupanua ufalme wa Mungu na kuwajenga waaminio.
2. Inavyotumika na inavyofanya kazi karama
Neno la maarifa linakuja kama ufunuo bila jitihada za asili na hutegemea tu kiwango cha
ushirika wetu na Mungu. Kwa upande mwingine, maarifa ya kidunia ni matokeo ya jitihada za
kiakili, ambayo kwa bayana ni tofauti ilivyo kwa neno la maarifa.
Iko mifano mingi katika Maandiko inayoeleza jinsi karama ilivyowapatia watumishi wa Mungu
maarifa ya Kiungu na yaliyowafaidia isivyo kifani.
(1) Ilifunua hali ya makanisa saba (ufunuo 1:2,3)
(2) Ilifichua mahali pa kambi ya adui (2 Fal. 6:9)
(3) Ilifunua mambo kuhusu muumini mpya; kupitia karama hii Anania
alipata ufunuo kuhusu kuongoka kwa Sauli, mtaa na nyumba
alimokuwa anakaa, msimamo wake, mawazo yake na mahitaji yake
(Mdo. 9:11,12)
(4) Ilifunua uharibifu katika Kanisa (Md 4:34-37)
Tunaweza kutaja matukio mengi, lakini inaonekana inafaa kwamba tutaje pia mifano ya matukio
ya siku za hivi karibuni ili tuweze kuona kwa dhahiri jinsi karama hii ilivyo na maana hata kwa
hali yetu katika siku zetu hizi.
Inaweza Kulinda Kanisa Wakati Wa Mateso
Rafiki yangu wa karibu pamoja na ndugu mwingine mkristo, walipeleka Biblia katika nchi za
Kikomunisti za Ulaya. Walifika huko saa nane usiku baada ya kusafiri kwa siku tatu.
Walipozima injini ya gari tu mara watu walitoka nje ya nyumba wakaja kuwalaki, ingawa
walikuwa hawa kuwatumia taarifa kuwa wangefika. Mungu alikuwa amemfunulia mmojawapo
wa ndugu wa mahali hapo kuhusu siku na saa wageni wangelifika hapo. Kwa hiyo iliwezekana
kupakua Biblia walizoleta bila ya kukwaruzana na wakuu wa Serikali.
Huweza kulinda Watu Binafsi Wakati Wa hatari
Mnamo mwaka 1981, mimi na ndugu wawili tulisafiri kwa gari kutoka Ujerumani kupitia
jangwani-Sahara kwa ajili ya huduma huko Ghana, Africa magharibi. Wakati tulipokuwa
Algeria, watu walijaribu kutuua. Wakati huo huo mke wangu na mama yake waliokuwa huko
ujerumani, wakati wa maombi waliongozwa kufanya maombezi kwa ajili ya ulinzi wetu ili
tusiuawe.
KARAMA ZA UFUNUO
12
Inaweza Kufunua Mambo Yanayohitaji Kurekebishwa Kiroho
Wakati wa ibada huko Kiel, Ujerumani Kaskazini Bwana alimfunua mtu mmoja aliyekuwa
amefungwa sana. Kadri nilivyojua mimi, watu waliokuwapo wote walikuwa ni watu
waliookoka. Baada ya kusumbuka sana rohoni mwangu ndipo nikaeleza huku nikitetemeka kile
ambacho Bwana alikuwa amenifunulia. Wito ulipotolewa ili mtu huyo aombewe hakuna
aliyejitokeza mbele. Hata hivyo, baada ya ibada alinijia mtu mmoja akakiri kuwa ni yeye
aliyehusika. Toba ya kukiri kulikofuatia kilionyesha kwamba Mungu alisema kwa kupitia kwa
neno la Maarifa.
Na tukio linalofanana na hili lilitokea katika mkutano wa vijana wa Afrika. Nilipokuwa bado
niko nyumbani ninaomba kwa ajili ya mkutano huo, Bwana alinionyesha mtu aliyekuwa na
matatizo makubwa ya kifamilia. Alikuwa amemuoa mama asiyeokoka, kinyume cha ushauri
aliopewa, lakini Bwana alitaka kumsaidia na kubadilisha hali hiyo iliyomzingira. Nilipofika
kwenye mkutano wa vijana wengine walikuwa hawajaoa, na wale waliooa walikuwa wameoa
wake waliookoka. Niliwaza kwanza, au labda nimekosea, ukitoa neno hilo katika mkutano huu
utaonekana mjinga. Lakini msukumo wa Roho Mtakatifu ulikuwa na nguvu sana, nisingeweza
kuupinga. Baada tu ya kulitoa neno hilo nililopewa, ndugu mmoja wa makamo mmoja wa
wachache waliokuwapo alikuja mbele huku akikimbia. Huku akichuruzikwa na machozi alikiri
kuwa ni yeye aliyehusika. Nilipomuona siku chache baadaye alini- dhihirishia kuwa sasa hali
ilikuwa nzuri.
Likawa ni jambo la faraja kwa mwili wa Kristo au kufunua dhambi ya ndani, ili kuwepo na hofu
ya Bwana miongoni mwa watu wake.
Karama Hii Pia Yaweza Kufunua Hali Ya Kiroho
Tunapoombea watu karama hii inaweza ikafunua hali ya kiroho ya Hao wanaombewa. Hivyo
inaweza ikatusaidia kuombea mahitaji yao ambayo tusingeyajua vinginevyo.
Inaweza pia kutuonyesha watu katika kusanyiko ambao wanashida za pekee au wanaohitaji
kufunguliwa. Ujasiri unahitajiwa ili kusema yale maarifa ambayo umepata kutoka kwa Roho.
Pamoja na hayo tunahitaji uangalifu ili tusichanganye karama hii ya thamani ili isifanywe
namna ya burudani ya kidini. Kuna watu wanaofanya kama onyesho. Lakini wakati Neno la
Maarifa linapofanya kazi, litakutana na mahitaji ya watu au kufunua muundo wa maisha
unaozuia maendeleo ya ufalme wa Mungu.
3. Neno La Maarifa Na Maono
Eneo la maono, ya mchana na ya usiku, au ndoto za mbinguni pia linakuwa ni sehemu ya
karama hii. Maono ni mafunuo yenye ujumbe. Ulonska anaeleza kuwa huwa tunapata picha
kwenye jicho letu la rohoni ambazo zinahitaji maelezo au tafasiri. Picha hizo zinaweza kuwa
KARAMA ZA UFUNUO
13
zenye kusimama au zinazotembea kama za sinema. Zina weza zikawa hata za rangi.
Tunapozipokea picha hizi na ujumbe wake tunahimizwa na Roho kwamba tueleze ujumbe huo
kwa kusanyiko au watu wanaohusika. Siyo kila mara anayepokea maono anajua tafsiri, lakini
kama kuna mtu mwingine atakuwa na tafsiri. Wakati mtu anapopokea maono kama hayo
anaweza kuwa amefumba au amefumbua macho naye yu katika maombi.3
Maono ya usiku au ndoto za mbinguni ni aina nyingine za maoni na ni tofauti kabisa na ndoto za
asili. Kiyunani zinaitwa "enypnion" na "Onar". Watu wanaozipokea wanajua kwa hakika ya
kwamba zinatoka kwa Mungu. Katika Agano jipya maono ya usiku yametumika ipasavyo.
Yusufu, mume wake Maria alitokewa na hali hiyo angalau mara mbili. Aliyakubali maono hayo
ya usiku kama majibu ya Mungu na maelekezo kwake.4
Mara nyingi kwanza Mungu alisema naye wakati Mariamu alipokuwa anategemea mtoto wake
wa kwanza - Yesu Kristo, kwa Roho Mtakatifu. Ndoto hii ilikuwa ya kushawishi sana na
akakubali maelezo kuhusu mimba ambayo vinginevyo kibinadamu haiwezekani kuyaeleza.
Mara ya pili Mungu aliposema naye katika ndoto ni wakati maisha ya Mtoto yalipohatarishwa
kutokana na Herode. Ndoto hizi au maono ya usiku bado yanawezekana kwetu na kwa kizazi
hiki. Mpokeaji atajua bila mashaka kwamba Mungu amesema.
Maono yawe ya usiku au ya mchana kwa kawaida yanahitaji tafsiri. Lakini hebu na tuwe
waangalifu. Siyo kila maono yanayotolewa na kila nabii huwa yanatoka kwa Mungu.
Tunatakiwa tuchukua hukumu ya kiroho kati ya hali hizo. Baadhi ya maono na ndoto nilizosikia
zamani hakika hazikutoka na Mungu. Zingine zilitokana tu na mtu kuwa amekula chakula kingi
mno cha usiku na akashiba mno au kuvimbiwa kabla ya kulala.
KUPAMBANUA ROHO
1. Asili ya Karama
Karama hii inakamilisha mzunguko wa karama za ufunuo. Hata hivyo utambuzi wa roho
unafanya kazi katika eneo dogo zaidi kuliko karama mbili zilizotangulia. Uwezo wake wa
ufunuo unafanya kazi katika sehemu maalum. Inatofautiana kabisa na karama mbili
zilizotangulia kwa kuwa kusudi lake, pia na jina lake katika utendaji kazi wake vyote ni vya
kiroho. Na hii inaonekana hata kutokana na jina lake. Zile karama nyingine, ingawa zinafanya
kazi kiroho pia, mara nyingi zinafunua mambo ya kimwili. Lakini kupambanua roho hutoa
ufunuo wa kiroho katika eneo la siri la viumbe vya kiroho. Ili tuweze kuelewa vizuri somo hili,
tunahitaji kutofautisha kati ya roho tatu tunazopambana nazo katika ulimweungu.
3 Reinhold Ulonska, Geistesgaben in Lehre und Praxis. (Erzhausen: Leuchter Verlag, 1983), p. 92.
4 Ibid., p. 92.
KARAMA ZA UFUNUO
14
Roho ya mtu
Roho ya Kimungu
Roho chafu
Kwa kuwa karama tunayoitafakari si karama ya kupambanua katika maeneo yote bali ni karama
ya kupambanua roho bila shaka matumizi yake ni bayana kabisa. Inahusika na roho zile mbili za
mwisho katika orodha hiyo hapo juu, na hasa zile roho za aina ya mwisho. Kwa uwezo wa
kiroho, karama hiyo huonyesha roho iliyo ndani ya mtu ni roho ya aina gani. Kwa utendaji kazi
wake tunaweza kujua ukweli wa kiini na asili ya kila mafunuo yoyote ya kiroho ikiwa ni kwa
Kimungu au kwa kishetani. Inasikitisha kwamba karama hii ya thamani na muhimu
inachanganywa na mawazo mabaya yafuatayo:
(1) Siyo Karama Ya Kuhukumu Au Kulaumu
Inatulazimu tukiri kwa masikitiko kwamba kuna wakristo ambao wana roho mbaya sana ya
kulaumu ambayo wanaiita karama ya kupambanua roho. Wao huwa tayari wakati wote kuwaona
wenzao wana nia mbaya na matendo mabaya pia. Lakini kama John Weslay alivyosema, talanta
ya namna hiyo mtu anaweza akaifukia na haimfurahishi Bwana hata kidogo. Hauhitaji karama
ya kiroho kwa ajili ya kufunua madhaifu ya watu ya kimwili. Uwezo wa kufanya hayo tuliurithi
kwa Adamu bila ya kuugharamia.
(2) Siyo Utambuzi Wa Kisaikolojia
Utambuzi wa kisaikolojia kwa kawaida huambatana na kuisoma tabia ya mtu na mambo ya
kiakili. Ujuzi huu mtu anaweza kujifunza na wala hauna uhusiano na utambuzi wa roho kwa
nguvu za kiroho.
2. Mutumizi Ya Karama:
(1) Hutumika Kwa Ajili Ya Uponyaji
Hakika ni kweli kwamba magonjwa hayatoki kwa Mungu. Hata hivyo, itakuwa ni makosa
kushikilia kwamba magonjwa yote ya mwili yanatokana na mapepo. Baadhi ya maradhi
hutokana na hali za kawaida ya asili. Ni kweli kuwa magonjwa yalikuja humu duniani kwa
sababu ya kuanguka kwa mwanadamu. (Makusudi na kiini) Lakini hii haoinyeshi kuwa
wagonjwa wote wanahitaji kufunguliwa kutokana na mapepo. Lakini pia kuna magonjwa
yanayoletwa na nguvu za mapepo. Utambuzi wa roho unatuwezesha kujua mateso ya mapepo
kutokana na magonjwa ya asili. Kama ugonjwa unatokana na mapepo wachafu, basi maombi ya
ukombozi yanahitajika. Kama magonjwa ni matokeo ya hali za asili, tendo la uponyaji litakuwa
la muhimu.
KARAMA ZA UFUNUO
15
(2) Hutumika Katika Ushauri
Mara nyingi watu waliozama katika maisha ya dhambi huitwa kuwa wamepagawa na pepo.
Hata hivyo tukisoma Gal. 5:19-21 kwa makini tunakuta kuwa matendo ya mwili ndiyo kiini cha
dhambi nyingi. Lakini bado kuna watu ambao hutenda dhambi kwa sababu ya upagavu wa
mapepo. Karama ya kupambanua roho itatufunulia kama matendo ya dhambi yanatokana na mtu
kupagawa na pepo, au kwa sababu ya moyo mwovu usiookoka. Tunategemea sana karama hii
tunaposhauri au kuomba pamoja na watu. Vinginevyo madhara mengi yanaweza kusababishwa.
(3) Hutumika Katika Maombi
Kutokana na udhihirisho wa karama hii, tunaweza pia tukajua kama maombi yetu yanazuiliwa
kwa sababu ya upinzani wa mapepo, au kama Mungu ameamua kutukatalia hitaji
tulilomwomba.
(4) Hutumika Kumfungua Mtu Aliyepagawa
Yatupasa tumngojee sana Roho Mtakatifu kabla ya kumtamka mtu yeyote kuwa ana mapepo.
Tuchukue hatua pale tu ambapo Roho ametueleza kwa uhakika. Kwa karama hii tunaweza pia
kujua ni roho ya aina gani aliyo nayo mtu, ili wakati wa kuita tuiite kwa jina lake. Tunaweza pia
kwa njia hiyo kujua kama mtu anakandamizwa, anachanganyikiwa au amepagawa hasa.
3. Kazi Ya Karama
(1) Silaha Ya Kujikinga Nayo
Karama hii ya Roho Mtakatifu itatusaidia siyo tu katika kutambua chanzo cha magonjwa au
kutusaidia katika kutoa ushauri, maombi na kuwafungua waliopagawa, bali itakuwa pia "Silaha
ya kujikinga" kwa ajili ya Kanisa. Kutokana na utendaji kazi wake watu wenye nia mbaya
watafichuliwa.
Kanisa lolote linalojishughulisha na mambo ya kiroho litashambuliwa na shetani. Lengo lake ni
kuleta machafuko na sifa mbaya juu ya kusanyiko ambapo karama na nguvu za Roho Mtakatifu
zinafanya kazi.
Andiko latwambia amejigeuza kama malaika wa nuru, ili aharibu kazi ile ya mwili wa Kristo.
Na hii ni kweli hasa kwa madhehebu ambayo yamefunguka kwa ajili ya karama za Roho. Lakini
kama karama ya kupambanua Roho inafanya kazi, mipango ya shetani itafunuliwa na watu
wanaotumiwa naye watawekwa wazi na hapo kanisa litaokoka kutokana na mambo magumu na
madhara yasiyokuwa ya lazima. Ili kuliwekea jambo hili msisitizo wa kufaa hebu na tuone
mifano kadhaa.
KARAMA ZA UFUNUO
16
(2) Ilimfichua Mtumishi Wa Shetani
Paulo alipojazwa Roho Mtakatifu akamwangalia Elymas mwaguzi alitambua roho chafu
iliyofanya kazi ndani yake (Mdo. 13:9,10).
(3) Ilifichua Chanzo Cha Unabii
Huko Filipi mwanamke kijana aliyepagawa na roho wa uaguzi (Greek; Joka Python" Mdo.
16:16) alitumiwa na roho chafu kuzuia kazi ya Bwana. Paulo aliweza kupambanua roho chafu,
na kuzifukuza, baada ya kuwa amezisikia na kuzivumilia nabii hizo kwa siku kadhaa. Kama
Paulo angeshindwa kutambua chanzo cha unabii ule na akafukuza roho hiyo yule mwanamke
angejiunga na Kanisa changa na baada ya mitume kuondoka tu angekuwa amesababisha
machafuko katika kusanyiko kwa kujiweka kama nabii mke. Hatimaye angesababisha kanisa
hilo kuvunjika au kukua likiwa limedumaa.
(4) Ilimfichua Mjumbe Mkubwa Wa Shetani
Kiongozi mmoja katika Kanisa la kiroho huko Ujerumani anaeleza taarifa ifuatayo: Wakati wa
Kongamano huko Stuttagart Ujerumani, mama mmoja alisimama akatoa unabii. Alilolisema
lilikuwa sahihi kimsingi (Lakini hapa tutambue kwamba mtu aliyepangawa hawezi "kutabiri"
kinyume na kweli kama yule msichana wa Filipi). Baadhi ya wachungaji viongozi waliokaa
jukwaani walianza kujisikia vibaya kwa ndani. Ghafla mmoja wao aliruka toka kitini na
akaikemea ile roho. Papo hapo yule mama akaangushwa na roho chafu iliyokuwa inafanya kazi
dani yake. Baadaye aligundulika kuwa alikuwa mmojawapo wa wajumbe mashuhuri wa shetani
katika mji huu.5
Mambo kama hayo yalitokea wakati nilipokuwa na semina mwaka 1986. Katika mkutano wa
mwisho, tulipokuwa na ushirika mtakatifu, mara tu baada ya kuomba na kumshukuru Mungu
kwa ajili ya damu yake iliyomiminwa "dada" mmoja akaanza kufanya mambo yasiyokubalika.
Akaendelea na mwenendo wake huo kwa muda lakini tangu mwanzo watu walikuwa na
mashaka juu yake. Baadaye Roho Mtakatifu akashuhudia kuwa matendo yake yalikuwa ni
udhihirisho wa roho mchafu. Tulimwendea, tukakemea pepo huyo wake. Pale pale akaanza
kulia akaminya-minya macho na kutetemeka mwili mzima. Hatimaye pepo likatolewa. Baadaye
ikagundulika kuwa mwanamke huyu alikuwa kiongozi wa huduma za kinamama wilayani kwa
miaka mingi.
4. Yaonekana katika utekelezaji kimatendo
Mtu ambaye karama hii inadhihirika kwake ajichunge sana ili asikasirike hovyo na kuitumia
kwa kulaumu na kuhukumu bali awe na huruma kwa hao waliopagawa na nguvuza mapepo
5 Reinhold Ulonska, Geistes Gaben in Lehre und Praxis, (Erzhausen: Leuchter Verlag, 1983),p. 116.
KARAMA ZA UFUNUO
17
wabaya. Ni lazima upendo wa Mungu umwagike kwa wingi kutoka ndani ya hao wanaotumika
katika karama hii.
(1) Hatua Nne Kwa Utendaji Kazi Wa Karama
Mwalimu mkubwa wa Biblia anatoa ushauri ufuatao wa kiutekelezaji kuhusu jinsi karama hii
inavyojidhihirika. Kwanza ndani ya moyo kuna mahangaiko ambayo ni ishara ya maonyo ya
kiroho. Lakini ki karama mtu hatafanya haraka kuamua. Badala yake atajiuliza mahangaiko
haya yanatoka wapi. Kisha hukaa kimya moyoni na kumsikiliza Roho.
Pili kunafuataia kufikiri na kuulizauliza kwa ndani kuhusu hali ya mambo ilivyo. Haya ni lazima
yafanyike katika Roho. Ili tupate kutenda haya lazima tuwe na maarifa mengi ndani yetu.
Tujiulize wenyewe kwa uaminifu. Nafikiri haya kwa sababu simpendi mtu huyu, au ni kutokana
na jinsi anavyofanya mambo.
Hatua ya tatu italeta uhakikisho wa kiroho kutoka kwa Roho Mtakataifu. Tutaweza kuona kiini
cha mambo hayo yote. Hatimaye kutafuata kufichuliwa na kufukuzwa kwa roho chafu.6
Tukichukua hatua nne hizi ndani ya mawazo yetu hatutahukumu haraka. Lakini tutasikiliza sauti
ya Roho Mtakatifu.
(2) Njia Nyingine Za Utambuzi
Kwa wale wasiokuwa na karama hii, kuna njia nyingine kadhaa za kupambanua roho.
a. Kwa tunda watu walizaalo (Mathayo 7:15-23)
b. wa kumsaili mtu wakati roho chafu inapokuwa imejidhihirisha (Yohana 4:1-6).
c. Kwa kuangalia dalili za upagavu kama, kwa mfano.
Kulia ghafla kwa kelele Luka 9:39
Kumrarua mtu Luka 9:39
Kutoka Povu mdomoni Luka 9:39
Kumchubua mtu Luka 9:39
Kukaa makaburuni Mark 5:5
Mtu kujikatakata Mark 5:5
Upofu na Ububu Matthew 12:22
Udhaifu Luka 13:11-16
Kusaga memo Mark 9:12,25
Kuanguka chini Mark 9:17,25
Kuanguka katika maji Mark 9:17,25
Kuanguka katika moto Mark 9:17,25
Pepo la uaguzi Mdo. 16:16
6 Reinhold Ulonska, Geistes Gaben in Lehre und Praxis, (Erzhausen:Leuchter Verlag, 1983),p. 111.
KARAMA ZA UFUNUO
18
KUPAMBANUA ROHO
(3) Je Mkristo Anaweza Kumilikiwa Na Pepo?
Swali kama Mkristo aweza kumilikiwa inabidi lishughulikiwe kuhusiana na karama ya utambuzi
wa roho. Hakuna jambo lolote lililo la kuhuzunisha kuliko lile la Mkristo kuishi maisha yake
akiwa na hofu kwamba roho chafu huenda ikampagaa.
Kwa bahati mbaya kuna watumishi wa Injili wanaoumba hofu kama hiyo katika mioyo ya watu
wa Mungu. Lakini Neno la Mungu ni kweli na ni hakika linapotamka kwamba "Aliye ndani
yenu ni Mkuu kuliko aliye ndani ya ulimwengu.
(1. Yohana 1:10) Hakuna pepo yeyote anayeweza kuchukua mamlaka juu ya mali iliyonunuliwa
kwa damu ya Bwana Yesu Kristo.
Baadhi ya watu hutaja Mathayo 12:43-54 kama kithibitisho kwamba Wakristo waweza
kumilikiwa na pepo. Lakini tunapolichunguza neno hilo kwa makini tutatambua kwamba
halimhusu mtu aliyetolewa mapepo kwa nguvu za Mungu. Tunasoma kwamba pepo lilisema
"kwangu nilikotoka" likimaanisha kwamba lilitoka humo kwa hiari yake. Pepo alielezea moyo
wa mtu kama "nyumbani kwangu". Ni dhahiri kuwa moyo wa mtu huyo ulikuwa haujawa
hekalu la Bwana. (1 Wak. 6:19) kwani pepo aliporudi alikuta nyumba ni tupu. Kama angekuta
nyumba hiyo imekaliwa na Bwana imesafishwa na damu yake na inatumika katika kazi yake
isingewezekana kwa pepo kurudi humo.
Nadharia nyingine iliyosambaa ni kwamba pepo anaweza kumiliki mwili na siyo nafsi. Mawazo
hayo ni sehemu ya mafundisho ya uongo ya zamani, ambayo yanasema kwamba mwili na yote
ya asili ni maovu na kwa hiyo hauna sehemu katika mafundisho sahihi ya Kikristo. Andiko
laonyesha wazi kwamba hii haiwezekani kabisa. Katika 1 Wakorinto 6:19,20 tunasoma.
"Hamjui kuwa miili yenu ni hekulu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu mliepewa na Mungu?
wala ninyi si mali yenu wenyewe? Maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa mtukuzeni Mungu.
Katika miili yenu na katika roho zenu ambavyo ni vya Mungu.
Wakati Roho Mtakatifu anapotawala mwili kama maandiko hayo hapo juu yanavyoelezea ni
wazi kwamba hatashirikiana makazi yake pamoja na roho chafu. Kama Mkristo angelimilikiwa
na pepo, daima tungeliishi katika hofu, Njia moja tu inayoweza kumfanya muumini kupagawa
ni pale tu naporudi nyuma na kwa hiyo kujifanya wazi kwa ajili ya roho chafu kumwingia.
Vinginevyo hatuna budi kuyachukua maandiko kuwa ndiyo mamlaka ya mwisho katika jambo
hili na wala siyo suala la uzoefu wa mtu au yaliyomtokea.
KARAMA ZA UFUNUO
19
(4) Mizimu Ya Waliokufa Haiwezi Kummiliki Mtu
Neno lingine la makosa lililosambaa na ambalo yafaa lisahihishwe ni imani kuwa mizimu ya
wazee waliokufa yaweza kumpagaa mtu. Mtu aliyekufa Biblia inasema kwa dhahiri kuwa mtu
aliyekufa, ama yuko kwa Mungu. (Luka 23:43) au yuko kuzimu anaingoja siku ya hukumu
(Waebrania 9:27, Luka 16:24) Lakini sharti tujue kwamba mtu akiabudu mizimu na kuitolea
sadaka mapepo yaweza kupata upenyo yakamtawala na hata anaweza akapagawa nayo.
(5) Umilikiwaji, Uonevu, na uteswaji
Katika Lugha ya Kiyunani hakuna tofauti kati ya kumilikiwa, uonevu na kuteswa. Katika
Kigiriki neno "daimonizomai" hutumika kuelezea kuteswa au kushambuliwa na mapepo. Hata
hivyo yaelekea kuna viwango tofauti vya "daimonizomai". Kwanza kuna kumilikiwa, ambapo
mtu hutawaliwa moja kwa moja na mapepo yanayokaa ndani yake. Ili kumfungua mtu kama
huyo pepo lazima afukuzwe au kutolewa.
Pili kuna kuonewa au kuteswa ambako kunazuia mtu kukua kiroho. Kuonewa au kuteswa kwa
kawaida hujionyesha katika hali ya mawazo yasiyokwepeka (tamaa mbaya, kujiua n.k) au
ndoto za asili hiyo hiyo. Wakristo wenye kuonewa na hali hizo hawawezi kabisa kuzidhibiti hali
hizi, yaani mawazo mabaya, ndoto au matendo, hata wangelijaribu jinsi gani. Hata kufunga kwa
muda mrefu na maombi havitamsaida. Ukombozi unakuja kwa watu hao, wakati wakristo
wengine walio na mamlaka ya kiroho, wakiomba na kufunga nguvu zinasosababisha mtu
kufanya mambo pasipo hiari yake.
Uonevu pia waweza kuja iwapo kwa tabia analala kila wakati neno linapohubiriwa. Kwa sababu
hiyo neno linakuwa mbali na muumini, na anazuiliwa kukua kiroho. Ni hakika kuwa watu wa
jinsi hii wanateswa na roho ya uonevu na watu hao hakika waliwahi kujihusisha na mambo ya
ulozi kabla hawajaokoka.
Watu hawa wanaweza kufunguliwa endapo watakiri shughuli zao hizo za zamani pamoja na
kufanyiwa sala ya kufunguliwa. (Kawaida ya kulala katika ibada).
5. Jinsi Ya Kutoa Roho Chafu
Kwa kawaida pepo hutolewa kwa kusema neno si kwa kuwekewa mikono. Kuwekea mikono
inatumika kwa uponyaji. Tunapojifunza maisha ya Yesu tunaona kuwa alitoa mapepo kwa
kuyapa amri. Kwa tukio moja kwanza alisema kwa pepo na baadaye akamwekea mikono kwa
uponyaji (Luka 13:11-16) Lakini mara nyingi alifukuza mapepo wabaya kwa kuyaamuru
yamwache mtu yaliyemuathiri.
KARAMA ZA UFUNUO
Kuwapo tu kwa karama hii kunathibitisha kweli ya kuwepo kwa roho chafu, zinazowatesa watu
ambao Kristo aliwafia. Basi ni kazi yetu kuitamani na kuitafuta sana karama hii ili mateka
wapate kutambuliwa na kufunguluwa, na kanisa liweze huhifadhiwa kinyume na roho hizi
potofu. Vile vile, lazima tutambue kwamba ni lazima karama ya imani na pia utendaji miujiza
zishirikiane na nyingine na karama hii, ili mapepo wabaya tuweze siyo tu, kuwatambua bali pia
waweze kufukuzwa.
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-
21
III. KARAMA ZA KUTENDA KAZI
Tumekuja kwenye kundi la pili la karama za kiroho, ambazo kwa sababu ya jinsi ya
zinavyotenda kazi, tunaziita karama za utendaji kazi. Wakati karama zile tatu za awali zinafunua
mambo yasiyojulikana na kuupa mwili wa Kristo utambuzi wa kiroho, karama hizi za utendaji
kazi ni za nguvu na zinajidhihirisha katika utendaji wa mambo yanayoonekana.
KARAMA ZA KUPONYA
Kama Conn anavyoonyesha, inaonekana kwamba uponyaji ni karama inayotamaniwa zaidi,
inayotafutwa na kutakiwa zaidi katika nyakati zetu hizi, sababu yake pengine ni kutokana na
kweli kwamba pamoja na karama ya matendo ya miujiza, karama hii hushangaza mno.7 Kwa
hiyo inatubidi tulichunguze somo hili kwa kina zaidi na kwa hiyo tutoke kwenye mipaka ya
awali ya kutafakari hali, matumizi na kazi za karama inayohusika. Hii ni muhimu kwa kuweka
wazi mambo muhimu kuhusu uponyaji wa Mungu ambayo yanavuka mipaka ya karama ya
uponyaji.
Tunaposema kuhusu karama ya uponyaji ni muhimu kwanza tutambue kuwa imetajwa katika
wingi yaani, "Karama za Uponyaji". Ni dhahiri kwamba kwa kuwa kuna aina nyingi za
magonjwa, lazima na aina za uponyaji wake nazo ziwe nyingi pia. Ili tuelewe vizuri zaidi,
tunalazimika kujua kama Uloska alivyoeleza kwamba mafundisho ya zamani katika Kiyunani
yalitumia Neno tofauti kueleza neno magonjwa tunalolitumia sisi.8
Kwanza tuna neno "nosos"/Nosema" ambalo kwa ufahamu wa kisasa ni kuwa magonjwa
yanayosababishwa na bakteria. Neno hili linatokea mara nyingi katika Agano Jipya, kwa mfano
katika Mathayo 4:23,24 na Yoh. 5:4.
Pili kuna neno "Malakia" ambalo linaonyesha udhaifu, upungufu au kupungukiwa nguvu. Ni
magonjwa yanayotokana na uzee (Mathayo 4:23; 9:35).
Mara nyingi sana neno "astheneia" hutumika na maana yake ni hali ya mtu kukosa nguvu jina
hasa "udhaifu" au ugonjwa (Luka 13:11,12; Yoh. 5:5. Neno hili linaonyesha uchovu wa nafsi.
Siku hizi linaitwa kuchanganyikiwa ukandamizaji n.k. katika ulimwengu uliopita ugonjwa huu
ulifikiriwa kama uvivu kudhania au kupagawa. Lakini kwa agano jipya ugonjwa huu umepewa
uzito wake jambo ambalo ni la kimapinduzi, kwani ilichukua miaka karibu elfu mbili kugundua
kuwa mambo haya ni ya hatari na yanahitaji uponyaji.
7 Charles W. Conn, A Balanced Church, (Cleveland: Pathway Press, 1975), p 126.
8 Reinhold Ulonska, Geistes Gaben in Lehre und Praxis, (Erzhausen: Leuchter Verlag, 1983),p. 58.
KARAMA ZA KUTENDA KAZI
Ufahamu wa kisasa kuhusu asili ya binadamu umetuwezesha kufahamu vizuri zaidi kuhusu njia
nyingi mtu anavyoweza kuugua. Inaelekea hakuna orodha iliyokamilika yenye kuonyesha
magonjwa yote. Lakini kama tulivyoona katika somo hili fupi kuhusu maneno haya, baadhi ni
ya kimwili, baadhi ni ya kiakili, baadhi ni ya kihisia, baadhi ni ya kawaida na mengine ni adimu
sana. Yote yanaonyesha kiwango cha taabu ndani ya mwanadamu anayehitaji kupatiwa msaada.
1. Asili Ya Karama
Kwani tunahitaji kueleza kwa wazi kwamba karama hii haihusiani hata kidogo na uponyaji wa
kisayansi. Kama ilivyo kwa karama zingine, asili ya karama hii inahusikana na nguvu za Mungu
tu. Wadaio kuwa huduma za kisasa za matibabu zitolewazo na Wamisionari ni udhihirisho wa
karama hii siku hii, ni kukosea sana. Karama za uponyaji zimeletwa kwa nguvu za Yesu Kristo,
mara nyingi kupitia waumini wasio na elimu ya udaktari, na wala si kwa kutumia madaktari.
Tunaposoma Agano jipya kwa makini tunakuta kwamba awali karama za uponyaji zilikuwa
zimekusudiwa kutumika kwa manufaa ya wale ambao hawajaamini. Karama hii ilikusudiwa
kutumiwa wakati Injili inapohubiriwa. Kwa hiyo yafaa itumike kudhihirisha nguvu za Mungu
kwa mtu ambaye hajaamini.
2. Inavyotumika na inavyofanyakazi Karama
Karama za uponyaji, kama karama zingine za Roho hudhihirishwa kutokana na msukumo wa
Roho Mtakatifu.
Ushuhuda wa South Wigglesworth "Mtume wa Imani" unaweza kutusaidia hapa.
Kupitia uvuvio alipokea uwezo wa kutumia karama mojawapo. Wakati karama za uponyaji
zilipotenda kazi kupitia kwake, alitoa amri kwa wagonjwa kupata uponyaji kwa jina la Yesu.
Hakuwaombea wagonjwa, bali kwa mamlaka alisema uponyaji katika maisha yao. Wakati
uwezo huu wa upako haukuonekana, alikuwa anahudumia katika maombi. Kulitokea uponyanji
pia ambao haukutokana na karama za kuponya.9
Watu wenye karama hii hawatauliza wagonjwa kuwa na imani kabla ya kuwaombea. Kunaweza
kuwa uponyaji wa kupitia imani ya mgonjwa na anayeomba (Math. 9:22,28,29). Lakini karama
za uponyaji daima humletea mwombaji ile imani inayohitajika. Tuna mfano mzuri sana wa hali
hiyo katika Mdo. 3:1-26. Wakati Petro na Yohana walipomhudumia kiwete kwenye lango la
hekalu, hawakumngoja awe na imani kabla ya huduma ya uponyaji kwake. Karama haitegemei
imani ya mgonjwa. Inaelekea kuwa imani inayohitajika kwa karama kufanya kazi hupatikana
kwa wakati tunapomfikia mgonjwa. Kwa hiyo karama hutegemea tu kutembea kwa Roho
Mtakatifu ndani ya maisha ya mtu anayetumiwa kwa kazi ya karama hiyo. Ndiyo sababu, walio
9 Ibid., p. 63
KARAMA ZA KUTENDA KAZI
23
na karama haifai waanze kuwa werevu mno na wafikirie kwenda "kukumba hospitali zote zibaki
tupu" wagonjwa wote hospitalini wawe wazima, kama walivyowahi kujaribu kufanya watu
wengine.
Wakati mwingine katika hali isiyokuwa ya kawaida, uponyaji hutokea kwa karama hii kutenda
bila lolote kusemwa au kuguswa mtu. Kuwapo tu mahali kwa Petro kuliwaponyesha watu
waliofikiwa na kivuli chake. Watu wengine waliponywa kwa nguo zilizoguswa na watu
waliokuwa na hiyo karama. (Mdo. 19:12) Lakini mara nyingi karama za uponyaji zilifanya kazi
kutokana na neno lilosemwa (Mat. 8:8; Mdo. 3:6)
Ni wazi kwamba haifai uponyaji utumike kutangaza mkutano wa Injili. Kuutangaza mkutano
kwa maneno ya kuvumisha sifa za mkutano kama: "Siku 14 za Uponyaji mtupu" haimpi Mungu
utukufu, na wala si sahihi kubiblia. Mungu ametoa uponyaji kwa sababu kuu nne zifuatazo:-
(1) Kuthibitisha neno lililohubiriwa (Mk. 16:20)
(2) Kudhihirisha nguvu za Kristo aliyefufuka (Mdo. 3:12-16)
(3) Kumtukuza Mungu (Mk. 2:12; Luke 13:5)
(4) Kuwafungua watu kutokana na vifungo vinavyowatesa (Mdo. 10:38)
Yapasa karama za uponyaji zitumike kutokana na huruma kwa watu na wala si kwa sababu ya
kutaka kushangaza umma kwa kuonyesha maajabu, au kwa kujitengenezea sisi wenyewe sifa.
Yesu Kristo na hata wanafunzi wake hawakuwahi kujaribu kukusanya watu wengi kwenye
mikutano kwa kutoa matangazo yenye kuvumisha sifa za mikutano ya Uponyaji. Uponyaji
ulitokea kama jambo la kawaida lililofuatia habari Njema iliyotangazwa. Ingawa uponyaji ni
sehemu ya Injili, lakini kamwe usiruhusiwe kuwa ni badala ya Wokovu. Siku hizi inaelekea
uponyaji unasisitizwa sana kiasi kwamba umuhimu unahama kutoka kwenye wokovu na watu
wanatafuta zaidi uponyaji na mafanikio. Hata hivyo, Injili isishushwe hadhi yake na kufanywa
kuwa dini yenye kuwafurahisha watu, mahali ambapo Yesu si wa maana tena bali mwanadamu
na yale anayoyatamani. Mungu ametoa kwa ulimwengu mafanikio ya aina zote kimwili na
kifedha, lakini kamwe mafanikio hayo yasipewe umuhumu sawa na kuokolewa kwa roho za
watu. Tofauti hii inadhihirishwa kwa bayana sana katika Maandiko (Mt. 18:9, n.k).
3. Sababu za Magonjwa
Wale watafutao na kutarajia uponyaji na wanaowahudumia ili waupokee lazima wafahamu wazi
wazi vianzo viwezavyo kusababisha magonjwa.
(1) Magonjwa na Dhambi
Wengine wamesema katika agano jipya kwamba kuna uhusiano kati ya ugonjwa na dhambi.
Kwa bahati mbaya watu wengine siku hizi wanakiri kuwa kila mgonjwa ametenda dhambi na
KARAMA ZA KUTENDA KAZI
24
kila wakati wanapotembelea wagonjwa wanawaelekeza kutubu dhambi. Ni kweli kwamba
sababu ya ugonjwa daima ni dhambi-dhambi ya damu. Lakini siyo lazima dhambi iwe imtendwa
na mtu huyo.
Yohana 9:2-3 inathibitisha jambo hili kwa wazi. Hata hivyo mtu anapougua ni hekima
kuchunguza maisha yake kwanza. Kama kuna dhambi ni lazima itubiwe kwa Mungu, ili mtu
huyo aweze kupokea msamaha na uponyaji.
(2) Ugonjwa Na Meza Ya Bwana
Kitu kingine cha kufikiria kinachosababisha magonjwa ni kushiriki meza ya Bwana ukiwa
mchafu moyoni. Jambo hili kwa kawaida watu hulipuuza. Lakini Mtume Paulo analielezea kwa
msisitizo.
Anayekula na kunywa meza ya Bwana akiwa hafai anakula na kunywa
hukumu yake mwenyewe. Na kwa sababu hii wengi ni dhaifu na
wengine kati yenu wanaugua ....1 Wakorintho (11:29,30)
Tunaona kuwa meza ya Bwana siyo sherehe lakini ni mahali tunapokabiliana na ukweli wa
kiungu. Kwa yule asiyefaa kushiriki makabiliano hayo yaweza kuwa chanzo cha magonjwa.
Katika maandiko tunaona wazi kuwa kutokuwa safi huko hutokana na matendo yanayoharibu
ushirika miongoni mwa ndugu na dada zetu katika Kristo.
(3) Ugonjwa Na Mashambulio Ya Kiroho
Katika maisha ya Ayubu tunaona kuwa shetani aliruhusiwa kujaribu uaminifu wake. Alivamiwa
vikali sana, lakini kwa kupitia uvumilivu wake pamoja na kushika imani yake alishinda.
Ugonjwa kama huo hauponywi kwa karama za uponyaji bali kwa mtu binafsi kuchukua
msimamo kinyume na nguvu za giza na kuchukuwa mamlaka dhidi ya nguvu hizo na kuzifunga.
(4) Ugonjwa Na Kumilikiwa na pepo
Agano jipya hasa Injili huonyesha kwamba baadhi ya watu waliugua kwa sababu ya kumilikiwa
na pepo. Njia pekee ya kuleta uponyaji kwa watu hawa ni kwa kukemea na kuwatoa hao pepo.
Hata hivyo matukio ya magonjwa ya aina hiyo ni nadra. Si sahihi, na ni makosa kuamini, kama
wengi wafanyavyo, kwamba magonjwa yote husababishwa na mtu kupagawa mapepo. Kama hii
ingekuwa kweli, tusingeweza kueleza.
Magonjwa mengi yanaponywa na madawa na operesheni zinazofanywa hospitalini. Mapepo
hayawezi kufukuzwa kutoka mwilini kwa madawa au kukatiliwa mbali kwa visu vya madaktari
au kuunguzwa kwa mionzi ya nuru kali. Roho chafu ni wakazi wa ulimwengu wa roho na ni
nguvu za Roho Mtakatifu tu ziwezazo kuzitoa roho hizo.
KARAMA ZA KUTENDA KAZI
25
(5) Ugonjwa Na Sababu Za Kawaida Za Kuambukiza
Magonjwa mengi sana yanayowapata waumini na wasioamini siyo matokeo ya mambo ambayo
tumeyaazungumzia hapo juu, bali husababishwa na mambo ya kawaida. Kwa mfano kama
kutovaa vizuri wakati wa baridi kama inavyotakiwa tunapatwa na magonjwa. Hizo ni sheria za
asili. Tunapozivunja sheria hizo lazima tupatikane na matokeo ya kuvunja sheria hizo.
4. Mungu Amavyoponya
Nje ya karama za uponyaji kwa kawaida Mungu huponya kwa kupitia njia zifuatazo:
(1) Wazee Katika Kanisa (Yakobo 5:14)
Waumini siyo lazima kwenda kutafuta watu wenye karama za uponyaji lakini wawaite wazee
wa kanisani. Jambo la Kusikitisha ni kwamba mara nyingi, wakristo wanawangojea wahubiri
maarufu wawaombee badala ya kuwaita wazee. Lakini tunapowaita wazee, kwanza tunaonyesha
kuwa tunakubali kuwa wameitwa na Mungu kwa huduma. Ni watu wanaosimama mbele ya
Mungu kwa ajili ya Kanisa. Pili tunaikubali njia Mungu aliyotoa kwa watu wake. Wazee
wanapoomba na kupaka mgonjwa mafuta maombi ya imani yatamwinua mgonjwa huyo.
(2) Kuptia Waumini Wote Wanapowekea Mikono
Njia nyingine ya uponyaji wa Kiroho ni kuwekewa mikono. Hakuna kilichoonyesha kuwa
namna hiyo ya uponyaji hudhirisha karama za uponyaji. Kinaonekana kuwa ni sehemu ya
kawaida ya ibada na huduma ya Wakristo. Si jambo la pekee la kufanywa tu na wale watu walio
na karama za uponyaji.
Kama tukiangalia maandiko yaliyotajwa hapo juu yaani katika mafundisho yake, inaonekana
kuwa ni tendo linaloweza kufanywa kwa imani na kila mtu aaminiye. Sharti pekee linalotakiwa
ni mtu kuamini (Mst. 17) Ingawa kupaka mafuta ni kwa waaminio tu wanapoumwa, mikono
yaweza kuwekwa juu ya waaminio na wasioamini, mradi tu wamehiari kuwa waombewe.
5. Mapenzi Ya Mungu Kuhusu Uponyaji
Ingawa Mungu huponya akipitia kwa wazee katika Kanisa, pia kwa kupitia kuwekea mikono na
waumini wote na kupitia karama za uponyaji, bado wengine hawajaguswa na uponyaji ambao
wamengojea. Kwa nini? Ingawa hakuna jibu la kisheria na kidini lililokamilika kwa swali hilo,
tunaweza kuona sababu kadhaa katika Neno la Mungu zinazozuilia uponyaji watu wengine.
Baadhi ya watu hawaponywi kwa sababu ya:
1. Dhambi isiyotubiwa (Yakobo 5:13-16)
2. Kukosa imani (Mathayo 13:58)
3. Adhabu ya Mungu (Hesabu 12:27; 1 Fal. 13:4)
KARAMA ZA KUTENDA KAZI
26
4. Hukumu ya Kimungu (2 Fal. 5:27; 2 Nya 26:20)
5. Mtindo mbovu wa maisha (Mith. 14:30)
Horton anatukumbusha kuwa kisima cha Bethsaida kilijaa wagonjwa wengi, wote waliamini
uponyaji wa kimungu, wote walingojea miujiza, bali mmoja ndiye alieponywa na Yesu.10 Katika
2 Timotheo 4:20 tunasoma kuwa Paulo alimwacha Trofimo akiwa mgonjwa huko Mileto. Bila
shaka huyu mtumishi wa Mungu alikuwa amemuombea Trofimo bila kupata mafanikio. Kweli
hizi mtu huwezi kuzifahamu vyema ila tu kama umekomaa kiroho. Haiwezekani ukasema tu
kuwa watu hawa katika Maandiko, na wale wa siku hizi, wasioguswa na uponyaji hawana
imani, kama wanavyosemwa na watu wengine wenye imani. Wanaofanya hukumu hivyo, mara
nyingi huwa wanasahau ukuu wa Mungu. Huwatendea watoto wake mmoja mmoja, binafsi,
aonavyo yafaa, apendavyo yeye. Pamoja na mifano hiyo, yapasa tujue kuwa mapenzi ya Mungu
ni kuponya. Neno lake hudhihirisha hii bayana. "Mimi ni Mungu nikuponyaye" (Kutoka. 15:26).
Hataki sisi tuugue, ndiyo maana alitoa uponyaji na utakaso. (Isa. 53) Kwa hiyo kamwe tusiache
kuombea wagonjwa. Tunapofanya hivyo Neno la Mungu latwambia kuwa mambo manne
yatatokea, kama ilivyoelekezwa na Mwalimu mashuhuri wa Biblia.11
(1) Maombi ya imani yatamwokoa (Kigriki:Sozo) mgonjwa (Yak. 5:15a)
Neno hili la Kigriki lina maana pana na ndefu. Ni Neno hili hili moja linaloelezea ukombozi
kutoka kwenye magonjwa ni sehemu ya ukombozi kamili iliyotolewa kwenye msalaba (Isa. 53).
(2) Na Mungu atamwinua (Kigriki. Egeiro) (Yako.5:15)
Katika mifano mingi, neno "egeiro", ina maana ya kufufua wafu (Math. 16:21; 17:23; Luke
9:22; 20:37, n.k.) Kwa hiyo inaelekea kwamba katika uponyaji, tunakuwa washiriki wa nguvu
za ufufuo wa kiroho.
(3) Ombeana mpate kuponywa (Kigriki:iaomai) Yak.5:16.
Neno la kigiriki "iaomai" hutumika kuelezea kuponywa kitabibu. Yaani uponyaji wa kimungu si
kitu cha kufikiria tu, bali unaweza kuthibitishwa kitabibu.
(4) Wataweka mikono juu ya wagonjwa na watapata afya. (Kigriki: echo kalos)
(Marko: 16:18)
Tafsiri sahihi ya neno hili la kigiriki katika maandiko haya lingekuwa "kuponya kabisa"
"tobewell" siyo kupata nafuu "recover Inaonyesha tendo. Hili neno lina uzito kuliko lile la
kwanza. iaomia, ni kuwa nafuu lakini "ach lakos" ni kupona kabisa. Neno hili eachlakos
linaeleza uponyaji kuliko la kwanza "iaomai".
10 Harold Horton, The Gifts of the Spirit. (Burbank: World Map, 1979), p. 109.
11 Ulonska, pp. 73-74
KARAMA ZA KUTENDA KAZI
27
Baada ya kuona kuwa Mungu anaponya kupitia karama za uponyaji pia kupitia maombi ya
imani, yapasa tusisahau, kama wengine walivyoona kwamba aponyaye si maombi yenye uweza
wote, wala mikono yetu, wala mafuta yanayotumika, bali ni Mungu Mwenyezi.
KARAMA YA IMANI
Kuna aina tofauti za imani zilizoelezwa katika Maandiko, mabazo zinahitaji kutofautishwa
kabla ya kutafuta asili ya karama ya imani inayotumika.
1. AINA MBALIMBALI
(1) Imani iokoayo
Kwanza kabisa tunayo imani ya wokovu. Imani hii inatusaidia kuamini sadaka ya ushindi
aliyoitoa Kristo badala yetu, Kunakuwako na uhakika wa wokovu kupitia imani hii. Ni ile imani
ya kawaida ambayo bila hiyo haiwezekani kumpendeza Mungu. (Wabr. 11:6) Ni kweli kwamba
imani ya aina hii nayo pia ni karama ya Mungu (Waef. 2:8), lakini si karama ya imani kama
inavyoonekana katika 1 Korinto 12:9.
(2) Tunda La Imani
Mbali na imani ya wokovu, Biblia yataja imani pia kama tunda la Roho (Wagal. 5:22) Imani
kama hiyo huifuatia moja kwa moja imani ya kweli ya wokovu. Huongeza kina cha ushirika kati
ya Mungu na muumini. Aina hii ya imani hukua kadri mtu anavyojitoa kwa mapenzi ya Mungu,
anavyo jifunza. Neno la Mungu, maombi na matukio anayoyapitia katika kukutana na Mungu.
Lazima iongezeke daima.
(3) Imani ya Asili/Kawanda
Kuna imani moja ambayo haifai lolote, kwa sababu haizai matokeo yoyote ya manufaa. Inaitwa
imani ya asili au imani ya mawazo.
Imani kama hiyo "inaamini " kuwa Mungu; yupo, jambo ambalo halina la ziada isipokuwa tu
kutambua kweli isiyobadilika. Watu walio wengi wana aina hii ya Imani. Tukifanya ushuhudiaji
wa mtu mmoja mmoja ndipo tunakutana na watu wanaoamini kwamba kuna Mungu. Lakini
Maandiko yanatwambia kuwa hata shetani anayo imani ya jinsi hii. "Wewe waaminini kuwa
Mungu yu mmoja, watenda vema: Mashetani nao waamini na kutetemeka" (Yak. 2:19). Imani
ya aina hii haiwezi kumuona Mungu, na wala haitekelezi au kufanikisha chochote. Ukitoa aina
hizi tatu za imani inabakia karama ya imani.
2. Karama Ya Imani Na Asili Yake/Chanzo
Karama ya imani inakuja kwetu kama udhihirisho wa kimungu wakati tunapokuwa na mahitaji
maalum. Ni imani kwa ajili ya wakati au kazi maalumu haipo pamoja nasi kila wakati katika
KARAMA ZA KUTENDA KAZI
28
maisha yetu. Karama hii, kama ilivyokuwa karama zingine, huja kwetu wakati Mungu
anapoidhihirisha kupitia kwetu kwa ajili ya mapenzi yake. Ni kipawa cha kiungu kutoka kwa
Roho Mtakatifu, kinachotuwesha kuliamini Neno alilolisema Mungu moyoni mwetu, hadi
linapotokea. Mambo ambayo tusingaliweza kudiriki kuyafanya au kuyasema vinginevyo,
yatafanywa au kesemwa wakati karama hii itakapodhihirika. Humpa mtu tumaini lisilobadilika
moyoni hadi linapotokea. Waaminio wengine wakiona imani ya namna hiyo ikifanya kazi
watatiwa moyo. Inaweka vituo vya kiroho na malengo ambavyo Wakristo huviona mfano bora.
Mifano miwili ya aina hiyo ni George Muller wa Uingereza na Paul Yongi Cho wa Korea.
Karama hii haihusiani na matumaini ya asili kuwa mambo yatakuwa mazuri. Watu walio na asili
ya kuwa na matumaini mazuri daima hudhaniwa kuwa wana karamma hii ya imani, lakini kwa
halisi watu hawa kiroho pengine ni watoto wachanga. Kwa kutokuwa waangalifu wanaweza
kusababisha matatizo mengi kwa Wakristo makanisani. Wakati waKristo wenye huruma
wanapowasaidia, kutotetereka). kutokana na shida zao ambazo zimesababishwa na utovu wao
wa uangalifu, wao huona kuwa hiyo ni uthibitisho wa matendo yao ya imani". Lakini karama ya
imani haina uhusiano na mambo ya asili. Karama inategemea uamsho na upako. Wakristo
wanaonyesha karama hii wanaweza kufanya mambo makubwa mno kwa ajili ya. Bwana lakini
wakati karama hii inapokuwa haifanyi kazi, wakristo hao hao wanakuwa wanyonge kabisa,
wadhaifu, na hufa moyo haraka wakikutana na majaribu. Kwa hiyo itakuwa ujinga kuwakuza
sana na kuwategemea watu wenye karama hii.
3. Karama Inavyotenda Kazi Na Jinsi Inavyotumika
Karama hii ina sehumu mbili, yaweza kutenda na pia kutendewa. Lakini karama ya miujiza
hutenda tu, haitendewi.12 Karama ya imani mara kwa mara hutumia imani ya kutenda ambayo
hutulia na kungojea miujiza. Kwa mfano kwa kupitia karama hii Daniel alikaa mbele ya
wanyama wakali bila kuzurika. Aliokolewa kwa karama hii. Hata hivyo, karama hii yatenda
kazi pia, kwa kuwatuma waumini kwenda nje na kufanya mambo yasiyokuwa ya kawaida kwa
ajili ya Bwana. Mifano ifuatayo, na hasa zaidi sura ya kumi na moja ya Waebrania inashuhudia
ukweli huu.
Abrahamu alipata ahadi yake (Yakobo 2:23)
Isaka alimbariki Yakobo (Gen. 27:28,29; 28:3,4.
Paulo alihudumu huduma ya kusababisha watesi wakubwa (Korinto 5:3-5)
Petro alitembea juu ya maji (Mathayo 14:29)
Mambo mengi hufanyika kwa ajili ya ufalme (Waebrania. 11)
Mara nyingi kama siyo daima imani ya namna hiyo huja kutokana na neno lenye uvuvio
"rhema" yaani neno la Mungu lililo maalum linalokuja kwa ajili ya wakati maalum na kwa
mazingara maalum. Ni karama ambayo hatuwezi kutoa sisi wenyewe. Watu waliokuwa na
12 Horton, p. 124.
KARAMA ZA KUTENDA KAZI
29
karama hii mara kwa mara walikuwa wanaigizwa na wengine ambao walishindwa wakajiaibisha
na pia wakaleta aibu kwa ufalme wa Mungu.
Yonggi Cho anaelezea mambo kama hayo yaliyowapata kikundi cha vijana wa huko Korea,
walipokuwa wakienda kwenye mikutano ya vijana. Kwa sababu ya mvua nyingi na kubwa
iliyonyesha katika wiki hiyo ya mikutano, walipofika kwenye mto ulikuwa umefurika.
Hapakuwapo na daraja wala ngalawa, kwa hiyo wengi wao walikata tamaa.
Lakini wasichana watatu miongoni mwao walisemezana. "Hivi kwa nini tusipite humu kwa
miguu kama Petro alivyotembea juu ya Maji? Mungu wa Petro ndiye Mungu wetu, na imani ya
Petro ndiyo yetu. Basi na sisi tunaweza kufanya vivyo hivyo". Baada ya hayo wasichana
walipiga magoti wakashikana mikono yao, wakaanza kurudia ule mstari wa Petro jinsi
alivyotembea juu ya maji, huku wakitamka kuwa nao wanaweza kufanya kama yeye. Na hapo
huku wenzao wakiwaangalia walianza kuingia mtoni. Walichukuliwa mara kwa kasi ya
mafuriko na baada ya siku tatu maiti zao zilikutwa baharini. Magazeti ya watu wa mataifa
yaliandika habari za wasichana hao, yakisema "Mungu wao hakuweza kuwasaidia". Lakini
Mungu hakuwa na sababu ya kusaidia imani yao. Petro hakutembea juu ya maji kwa sababu ya
maarifa ya ujumla kuhusu Mungu. Kristo alisema neno maalum la (RHEMA) kwake na
kumwambia njoo. Hatuwezi kuigiza karama ya namna hiyo.
4. Amri ya Imani
Karama ya imani ina jidhihirisha pia kupitia agizo la imani, ambalo si njia wala nguvu nyingine
tunayoweza kuitumia ili kujirahisishia maisha. Duwel anathibitisha ni njia nyingine makini ya
kutumia mamlaka ya Kristo mwenyewe, katika mazingira ambamo utukufu wake unahatarishwa
au ufalme wake unazuiliwa.13 Kwa mfano katika matukio ya wizi, kubaka au mashambulizi,
agizo la imani huweza kujidhihirisha kupitia kwetu kama sehemu ya karama ya imani.
Hata hivyo, sharti tutambue kwamba agizo la imani haiwezi kuchukua nafasi ya maombi.
Hutujia tu katika nyakati maalum kupitia kwa Roho Mtakatifu. Haiwezi kutumiwa hivi hivi tu ili
mradi iturahisishie maisha na kuondoa kila mlima njiani mwetu (Mt. 17:20). Kamwe tusisahau
ukweli kwamba milima mingine huruhusiwa na Mungu, izuie njia yetu, ili atufundishe siri za
kiroho kwa undani zaidi. Milima hiyo inaweza kupunguza kasi ya kuenenda kwetu lakini
itatujengea misuli yetu ya kiroho na kuimarisha maisha yetu ya Uombaji. Yatupasa kutafautisha
kati ya vizuizi vinavyosababishwa na shetani na milima inayoruhusiwa na Mungu.
Mafundisho yanayotuaminisha kwamba tunaweza tukaziamuru shida zetu zote zitoweke
yanakosewa na hayaungwi mkono na kuthibitishwa na Maandiko. Pamoja na hayo, kama Duwel
anavyoonyesha katika kitabu kinachoitwa "Touch the World through Prayer" ikitumika vizuri
amri ya imani inaweza:
13 Wesley L. Duwel, Touch the World Through Prayer. (Grand Rapids: Francis Asbury Press, 1986), pp. 110-120.
KARAMA ZA KUTENDA KAZI
30
(1) Kuamuru shetani aondoke katika eneo fulani
(2) Kuamuru shetani kuondoa giza la mapepo linalowapofusha watu.
(3) Kuamuru shetani akome kuchochea upinzani.
(4) Kuamuru shetani kuacha kuchanganya kukandamiza, kufunga na kutesa watu.
(5) Kuamuru hali ya hewa, mfano mvua, jua kali, joto, vumbi kukoma kwa muda.
(6) Kuamuru mhalifu kusimama au kuondoka.
MATENDO YA MIUJIZA
1. Asili Ya Karama
Horton anafafanua muujiza kama ni kuingilia kati kwa nguvu ya Kiungu katika utendaji kazi wa
asili, na kwa hiyo kuzitiisha kwa muda taratibu halali zinazojulikana. Muujiza unapotendeka
sheria za asili zinasimama au kubatilishwa. Haina maelezo mengine isipokuwa nguvu na uweza
mkuu wa Mungu.14 Mungu anapotumia uwezo wake, nje ya sheria zinazoweka mipaka kwa
uwezo wa viumbe wake, tunaita kitendo hicho muujiza. Hata hivyo maneno "Matendo ya
Miujiza" si tafsiri ya sawa ya asili. Maandiko ya awali ya Kigriki yanatumia maneno
"energemata dynameon" ambayo tafsiri yake ya moja kwa moja "utendaji kazi wa nguvu".15
Mambo haya yamo katika wingi. Kwa hiyo karama hii ina maeneo makubwa zaidi kuliko
ilivyotegemewa na inatoa uwezekano mkubwa wa utendaji kazi mkamilifu zaidi. Kwa hiyo
kubatiliwa kwa matukio fulani au madhihirisho ya nguvu, ambayo hatuyaelewi au kuyajua
inakuwa si haki.
Ili kuzuia uwezekano wa kuiwekea mipaka karama hii, maneno yote mawili yanaelezewa katika
hali ya wingi, na kwa kufanya hivyo inadhihirisha wingi wa nguvu zake za utendaji kazi. Kwa
hiyo, kila jitihada ya kuorodhesha aina za kudhihirisha utendaji kazi wa nguvu hizi, bila shaka
itakuwa katika hatari ya uwezekano wa kukosa kuona, kuacha nje au kukataa uwezekano wa
namna mpya ya utendaji kazi wa nguvu za Mungu. Kwa mujibu wa maoni ya Ulonska, tafsiri
maarufu ya "Matendo ya miujiza imeongeza udhia wanaouona watu kuhusiana na maonyesho ya
bayana na ya ajabu ya nguvu za Mungu. Lakini ukweli ni kwamba hata mikutanomikubwa ya
uamsho ya Finney na hasa zaidi ile ya Wesley ilikuwa mara kwa mara ikiambatana na
kudhihirishwa bayana kwa nguvu hizi. Agano jipya linataka kuzifungua akili zetu tupate
kutambua utajiri wa nguvu za utendaji kazi na kwa karama zisizo za kawaida ambazo kwazo
Mungu anataka kutukirimia. Inasema kwa wazi kuhusu ishara, maajabu na matendo mengine
yenye nguvu (2 Wakorinto 12:13). Basi tutakuwa tunafanya jambo jema tukiiachia karama hii
upana wake wote kulingana na maana yake ya asili, na hivyo bila ya kuiwekea mipaka
inayoambatana na msemo wa "Matendo ya miujiza".16 Hata hivyo, hatuna budi kuwa macho ili
14 Horton, pp. 112-113.
15 Ulonska p. 77.
16 Ibid., p. 78.
KARAMA ZA KUTENDA KAZI
31
tusiishabikie udhihirisho wa kila namna ya nguvu mpya bila ya kujaribu na kupambanua roho
nazo.
2. Inavyotumika na kazi ya karama
Madhihirisho ya nguvu za Mungu, kupitia karama hii yaweza kuwekwa katika aina zifautazo:
(1) Kazi za Ukombozi
Kufufua Wafu
Ukombozi kutoka mauti (Mdo. 9:40,41; Petro na Dorkasi (Mdo. 20:9,10) Paulo na Eutiko.
Pia hata hivi majuzi katika uamsho huko Indonesia, Nigeria na Zimbabwe. Huko Zimbabwe
mwezi Mei, 1988 binti wa umri wa miaka sita alifufuliwa kutoka katika wafu.
Ukombozi Kutoka Katika Nguvu Za Kimapepo
Hii inahusika na kufunguliwa kutokana na kupagawa na mapepo na pia kuondokana na
ukandamizwaji (Mathayo 17:20).
Kuwekwa Huru Na Vileo
Kufunguliwa kutokana na vifungo vya vileo, madawa ya kulevya, tumbaku, tamaa mbaya na
mengineyo, pia yana - kuwa chini ya kazi ya ukombozi.
(2) Kazi Ya Kutoa Mahitaji
Hizi zinapatikana kote katika Agano la kale na Agano jipya.
Mifano Katika Angano La Kale
Musa kufungua mwamba kwa ajili ya maji (Kutoka 17:6) Nguo kudumu bila kuchakaa kwa
miaka 40 (Kumb. 8:4) Utoaji wa mafuta na unga huko Serepta (1 Wafalme 17:14) Shoka la
chuma linaloelea juu ya maji 2 Wafl. 6:5,6).
Mifano Katika Agano Jipya
Kufanya maji kuwa divai (Yoh. 2:1-11) Kulisha watu 5,000 na tena watu 4,000 Mark 6:35-44
Mathayo 15:32-38) Kusafirishwa kwa Filipo kupewa usafiri (Mdo. 8:39,40).
(3) Kazi Ya Nidhamu
Horton anathibitisha kwamba nguvu za Mungu zinatenda kazi katika njia mbili. Kwa kutia
moyo na kuzuilia. Kwa neno la Musa Msururu wa miujiza ulileta hukumu juu ya nchi ya Misri
na Farao. Nguvu hizo hizo zilifanya kazi kupitia maisha ya mvuvi karne nyingi baadaye wakati
KARAMA ZA KUTENDA KAZI
32
waongo wawili walipochinjwa katika hukumu. (Mdo. 5:1-11).17 Mambo yanayofanana na hayo
yametokea katika nyakati zetu hizi, wakati mchawi alipojaribu kumwua Missionari huko Congo.
Kesho yake asubuhi yeye menyewe alifariki baada ya mateso makali, kandokando mwa kijiji.
Wakati mtu aliyemiliki kilabu cha pombe alipodiriki kuingia katika hema la Injili ili amuue
mwinjilisti kulisikika sauti kubwa ya mifupa ikivunjikavunjika, naye huyo bwana mara
alidondoka chini akafa.18 Mfanya biashara mmoja aliyezuia kujengwa kwa kanisa akisema kuwa
lingejengwa tu baada ya yeye kufa alianguka akafa alipokuwa akitembea kutokea kwenye eneo
hilo lililotakiwa kujengwa Kanisa.
(4) Kazi Za Ulinzi
Daniel ndani ya tundu la simba, alilindwa kwa kazi ya usalama. Katika Agano Jipya tunasema
kuwa mitume walilindwa katika dhoruba. Paulo alipokuwa anasafiri kuelekea Roma alilindwa
kutokana na kifo. Rafiki yangu huko Ghana alilindwa alipohubiri Injili kaskazini mwa nchi hiyo
ambako Chifu mmoja alijaribu kumpa sumu. Sumu haikufanya chochote kwake na tukio hilo
likamfanya Chifu huyo akubali kumpokea Bwana kama Mwokozi wake.
3. Kuijaribisha Karama
Utendaji kazi wote wa nguvu lazima ujaribiwe. Si kila udhihirisho wa nguvu wenye chanzo
chake katika Uungu. Inaweza ikatukia kuwa kuonekana kunakofanana kwa nguvu kunatoka
katika viini tofauti, kama ilivyokuwa kwa Musa na waganga wa Misri. Kwa hiyo tunahitaji
kuujaribu kila muujiza tunaouona kulingana na vigezo hivi vinne:
(1) Udhihirisho wa nguvu ambao ni wa Kimungu, daima utawaongoza watu
kuuendea Msalaba, na kwa Yesu.
(2) Udhihirisho wa nguvu ambao ni wa Kimungu, daima husaidia kulijenga
Kani-sa. Hili ni Jambo muhimu sana, kwani karama zote zimetolewa ili
kusudi ziujenge mwili wa Kristo.
(3) Udhihirisho wa nguvu ambao ni wa Kimungu daima hutokea baada ya
Neno kuhubiriwa. Hulithibitisha neno lililonemwa.
(4) Udhihirisho wa nguvu ambao ni wa Kimungu haukusudiwi kustarehesha,
kuburudisha wala kuonyesha ubabe.
Tukivitafakari vigezo hivi vinne tutaweza kutoa hukumu ya kutosha na nzuri wakati udhihirisho
wa nguvu hizi unapotokea, hata kama nguvu hizo zikionekana kama ni ngeni. Kwa sababu kila
kiongozacho watu kwenda kwa Kristo, kulitukuza jina lake, kulijenga kanisa lake na pia kila
lilinganalo na Neno la Kweli, linaweza kuhesabiwa kuwa linatoka kwa Roho Mtakatifu (Luka
11:18).
17 Horton, pp. 116-117.
18 Ibid., pp. 117-118.
KARAMA ZA KUTENDA KAZI
33
4. Umuhimu Wa Karama Hii
Uloska anathibitisha ukweli kuwa karama hii haikuhitajika sana hapo mwanzo kama wakati wa
siku zetu, kwa sababu hata kanisa la Yesu limepungukiwa na ujuzi wake wa ukweli wa
kibiblia.19 Kazi nyingi za Kanisa zinahusika zaidi na mambo ya kijamii na kidini, ambapo
hapabaki nafasi kwa ajili ya nguvu za Kimungu. Kwa sababu hiyo tunahitaji kwamba huduma
yetu iandamane na ishara na miujiza, vinginevyo kizazi chetu hiki hatuwezi kukibadilisha. Kwa
bahati mbaya muundo huu wa mambo umekorofishwa kwani Wakristo ndio wanaozifuata ishara
na miujiza badala ya wao kufuatwa. Lakini Kristo kamwe hakukusudia kuwa mambo yawe
hivyo.
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-
19 Ulonska, p. 84
KARAMA ZA KUTENDA KAZI
34
See Self Study Questions
35
IV. KARAMA ZA UVUVIO
Karama tatu za mwisho zinahusiana na viungo vya sauti au vya usemaji vya muumini. Kwa
kawaida aina tatu hizo za karama kuwa zinaitwa "Karama za Uvuvio, au karama za kunena.
Kwa sababu karama hizi zinahusisha ulimi wa mtu zimekuwa zikitendwa kwa makosa na kwa
fujo. Karama ya lugha ndiyo imekuwa mashuhuri sana, ingawa siyo yenye umuhimu kuliko zile
nyingine mbili. Karama iliyo kuu kuliko zote kati ya hizi tatu ni Unabii. Hivyo, hebu tuziangalie
hizi karama.
UNABII
1. Asili ya Karama
Tukifafanua kwa urahisi unabii maana yake ni kunena kuliko vuviwa. Asili yake ni ya kimungu.
Kama kusema katika lugha kulivyo kunena kwa nguvu katika lugha tusiyoijua, vivyo hivyo
unabii ni kunena kwa nguvu katika lugha inayojulikana.20 Ni udhihirisho wa Roho ya Mungu,
na siyo akili ya mwanadamu. Kwa bahati mbaya kuna mawazo potovu kuhusu karama hii
ambayo yanahitaji kushughulikiwa kabla ya kuanza kuzungumzia jinsi karama inavyotenda
kazi.
(1) Karama Ya Unabii Na Ofisi Ya Nabii
Katika Agano la kale, karama ya Unabii na nafasi ya nabii vilikuwa vinafanana na kuambatana.
Katika Agano jipya hali hiyo imebadilishwa sana. Chini ya agano la kale, karama ya unabii
ilikuwa ni kwa wateule wachache yaani manabii. Lakini katika Agano Jipya, wote
wanaruhusiwa kutafuta kuhutubu (1 Kor. 4:1) lakini ile kazi au nafasi ya nabii bado imewekewa
mipaka, nayo ni ya wateule wachache, katika mwili wa Kristo (Waefeso 4:11 "wengine"). Ofisi
ya nabii haigawanyiki kutoka kwa mtu maalum. Kwa upande mwingine karama ya unabii iko
kwa ajili ya kila mtu. Tunahitaji kujua kwamba kutoa unabii peke yake hakumfanyi mtu kuwa
nabii, kuna vigezo vingine vinavyozingatiwa.
Ni kweli kwamba kwa kawaida nabii atatabiri, lakini pia atapokea mara kwa mara kwa mafunuo
ya kiroho, kutoka kwa Roho Mtakatifu, ambayo asingeyapata vinginevyo (Neno la Maarifa).
Vile vile ataweza kupambanua roho, kupokea ujumbe kutoka kwa Mungu. Kupitia ndoto na
maono, na kutabiri yatakayokuja kwa kuzingatia mipaka ya muundo wa maandiko. Anapohubiri
Neno la Mungu, ujumbe wake utakuwa mara kwa mara unaambatana na mazingira ya wakati
unaohusika na mahitaji ya kusanyiko analolihudumia, ingawa hakujua mahitaji hayo kabla ya
mkutano.
20 Horton, p. 160.
36 KARAMA ZA UVUVIO
36
(2) Unabii Hueleweka Kama Utabiri Tu
Maoni ya wengi miongoni mwa waaminio ni kwamba unabii huhusika tu au zaidi na kutabiri
mambo yajayo. Hii inawezekana kuwa kweli tu kwa unabii katika Agano la kale, lakini katika
Agano Jipya unabii huhusika zaidi na kunena kweli za sasa kuliko kutabiri. Kutabiri ni sehemu
ya kazi ya nabii lakini si ya karama ya unabii. Kazi hasa ya unabii katika Agano Jipya si kutabiri
yajayo, bali kwa mujibu wa 1 Wakorintho 14:3,4 makusudi ya unabii yako katika sehemu tatu
yaani kujenga, kutia moyo, kufariji.
(3) Karama Inavyochanganywa Na Kuhubiri
Kuhusisha karama katika hali hii, ni kuiibia tabia yake yote ya kiroho. Neno kwa mahubiri
katika mafundisho ya mwanzo (Karugma). Yote ni tofauti na neno unabii (propheteria). Unabii
siyo kuhubiri na kuhubiri siyo unabii. Ingawa, yaweza ikawa kwamba karama ya unabii yaweza
kutenda kazi kwa ujumbe, ikisema kwa mawazo ya waliopotea na wasikilizaji.
Unabii ni kusema kwa watu kusiko kwa asili, wakati kuhubiri ni kusema na watu kimwili, hii
haimaanishi haina uvuvio wa roho. Tofauti ni kwamba Unabii unakuja ghafla na upako wa hali
ya juu sana, wakati katika kuhubiri Mungu anapaka mawazo yetu ya asili wakati wa maandalizi,
kwa kiasitu.
2. Karama Inavyotenda Kazi Na Jinsi Inavyotumika
(1) Unabii Wa Kujenga
Kwanza kabisa unabii umetolewa kwa ajili ya kujenga (1 Wak. 14:3) Neno lililotumika katika
Kiyunani "Oikadome" kimaandishi lina maana ya kuinua, au kujenga nyumba. Ni lugha ya
kiujenzi ambayo inaonyesha kujenga kanisa pamoja na utu wa ndani wa mtu. Kwa hiyo karama
hii husaidia kujenga hekalu la kiroho, na pia inatusaidia kuukulia utu uzima wa kiroho.
(2) Unabii Kwa Kutia Moyo
Neno la pili linalotumika katika (1 Wakorinto 14:4) ni la kiyunani "Paraklesis" ambalo maana
yake ni kutia moyo. Kwa bahati mbaya "Paraklesis" imetafsiriwa kama exhortation ikimaanisha
kukemea badala ya kutia moyo ambalo linatumika kwa kukemea badala ya kutia moyo, tafsiri
moja ya Biblia Kenya imeonyesha neno "paraklesis" kama kukemea. Lakini hakuna huduma ya
kukemea katika Agano Jipya. Neno lililotumika linakusudiwa kujenga na wala siyo kwenda
kinyume. Katika neno hilo hilo tunapata "paraklet" maana yake mfariji au msaidizi ambalo
limetumika kumueleza Roho Mtakatifu. Inawezekana kuwa neno la kutia moyo ndani yake na
kurudi au kuadibisha, lakini daima litakuwa ni pamoja na kutia nguvu na tumaini (angalia
Ufunuo 3:14-22) Injili ni jambo la pekee, kamwe haitafungua jambo kwa ujumbe wa kuvunja na
kukatisha tamaa.
KARAMA ZA UVUVIO 37
37
Katika hali kama hizo, karama ya unabii inakuwa inaleta msaada mkubwa sana kwa kuwainua
walioelekea kukandamizwa. Mimi nina hakika kabisa kwamba leo nisingelikuwa hapa niliko
kama Mungu asingenitia moyo kupitia karama hii. Kwa hakika kupitia karama hii hata hivi
majuzi tulitiwa moyo sana pale mahali tunapofanyia huduma yetu.
(3) Unabii Wa Kufariji
Wakristo wengi sana kuliko tunavyofikiria, wanahitaji faraja. Maisha ya kiroho yatachanua zaidi
kutokana na faraja kuliko kukemewa. Tusisahau kuwa upendo wa Mungu ndio ulioiteka mioyo
yetu, si roho ya kukemea au ya sheria.
Watu wanaokabiliwa na majaribu, mateso au mambo magumu wanahitaji neno la faraja. (Isaya
40:1 inasema Wafariji, Wafariji watu wangu). Unabii unaotangaza ole kuangamia na hukumu
peke yake hauna budi kutiliwa mashaka. Kama tulivyoona unabii ni wa muhimu sana kwa
maisha ya kiroho ya kanisa na waumini. Hivyo Paulo, katika 1 Wath. 5:20,21 anatuonya kabisa
kwamba tusiutweze unabii, yaani tusiudharau au kuudhihaki.
3. Karama inavyojiendasha
Karama hii tunaiita Unabii sawasawa kwa sababu karibu unabii wote hasa ulionyeshwa kwetu
kuwa ni wa aina hii ya kuonekana. Katika unabii halisi ujumbe hupokelewa kupitia mawazo
yanayoingia akilini mwetu kutoka nje ya nafsi zetu, au roho zetu, ulioambatana na nguvu kubwa
na kuhimizwa kwingi kwamba tunawaka ujumbe. Na hayo mawazo yanayotoka kwa Mungu
yanajitengeneza katika nafsi zetu kwa namna ambayo tunaona kwamba tunawajibika
kuyawasilisha ipasavyo. Yatubidi kujua kwamba ujumbe hutoka kwa Mungu, lakini ni nabii
anayesema na siyo Roho Mtakatifu. Kwa lugha nyingine Mungu husema na nabii kupitia Roho
Mtakatifu ambaye naye huuwasilisha ujumbe huo kwa watu. Yote haya hakika hutokea kwa
ghafla. Kwa uzoefu wangu najua kuwa mawazo yanakuja ghafla, yaliyovuviwa ambayo
hatuwezi kuyaweka kando, haya yanaunda ujumbe, na kuna kuhimizwa kusema kwenye nguvu
sana. Mtu anayepokea neno la unabii atajua kabisa kuwa ujumbe ambao ameupokea umetoka
kwa Mungu kwa sababu hakuna kitu kingine kama hicho. Hatuna budi kusisitiza kuwa unabii
siyo mambo ya kudhania au kitu tunachojitungia katika mawazo yetu.
Unabii umeundwa kupitia Roho Mtakatifu katika roho ya "nabii". Wakati mwingine Nabii
anapokea sentenso ya kwanza pekee au maneno machache ya kwanza, kisha anapoanza kusema
anapewa ujumbe uliobakia. Kwahiyo anatakiwa kuanza kusema huo ujumbe kwa imani. Katika
hali hiyo hana budi kuwa mwangalifu ili asiendelee kutoa ujumbe wake yeye mwenyewe, baada
ya kutoa ule aliopewa na Mungu.
Anaweza kushawishika kuuongezea kitu hasa kama ujumbe haukuwa mrefu, au kubadili sehemu
za ujumbe uliopokelewa. Wakati mwingine ujumbe mzima unaweza kupokelewa kwa mara
38 KARAMA ZA UVUVIO
38
moja. Yaweza kutokea pia kuwa ujumbe au sehemu ya ujumbe ikapokelewa nyumbani wakati
muumini anapojiandaa kwa ajili ya huduma. Hata hivyo hii hutokea kwa nadra. Kwa sababu
ubinadamu unahusika, kunahitajika mafundisho pamoja na wito kwa ajili ya majaribio (1 Wak.
4:29) Isingekuwa lazima kufanya hayo kama karama hii yote ingalikuwa ni kazi ya Mungu tu
bila kishirikisha mtu. Kwa hakika ukweli wa mambo siyo kama wengi wanavyofikiri kwamba
sisi ni kama kipaza sauti au njia ya kupitisha ujumbe na kwamba kama hatutaki au tunataka
Roho Mtakatifu hutumia viungo vyetu. Mambo kama hayo yanakubalika tu katika shughuli za
waganga au wapunga pepo, ambako roho za kishetani inashika viungo vya mnenaji na
kuvitumia kama kipaza sauti. Pindi mambo yakitokea hivyo si mtu anayesema bali ni roho chafu
zimatumia viungo vyake, kiasi kwamba hata sauti hubadilika. Yeyote aliyewahi kusikia mapepo
yanasema hakika atajua tofauti.
Karama za uvuvio na ufunuo ni "zalisho" la Mungu na mwanadamu. Mungu hawezi kufanya
kosa, lakini mwanadamu hufanya makosa. Mwanadamu anapojitoa na kujinyenyekesha kabisa
kwa Roho wa Mungu, ayatamkayo yatakuwa hayana makosa. Kwa bahati mbaya, roho ya
mwanadamu haiwezi kutolewa na kunyenyekeshwa kiasi hicho, na ndiyo sababu inakuwa
muhimu kuujaribu unabii wote.
Donald Gee anathibitisha thamani kuu ya kiroho ya karama hii, na kusisitiza umuhimu wa
kuitunza ili idumu katika kanisa.
Siri kuu ya utunzaji wa hii karama tukufu ya kiroho ikitenda kazi mara kwa mara katika kanisa,
ni kwa kusaidiwa na neema ya Mungu, kuweka hata kumruhusu atende kazi apendavyo, na utii
wa kutosha kwa Maandiko hata kuyajaribu mambo yote. na kushikilia tu lile lililo jema"(1
Wathes. 5:19-21).21
4.Jinsi ya Kuupima Unabii
Kuna maeneo matatu kunapoweza kutokea unabii, nazo ni:
(1) Roho Mtakatifu (2 Samweli 23:2; Jeremiah 1:9)
(2) Roho chafu na roho zidanganyazo (1 Samweli 8:19,20; Mathayo 8:29;
Wafalme 22:22; Mdo. 16:17).
(3) Roho ya mwanadamu (Yeremia 23:16; Ezek. 13:2) Na hii ya mwisho
haiwezi kufikiriwa kama kiini halisi cha uvuvio ingawa inaweza kuwa
chanzo safi kabisa cha unabii wa uongo.
21 Donald Gee, Concerning Spiritual Gifts. (Springfield: Gospel Publishing House, 1980). P. 63.
KARAMA ZA UVUVIO 39
39
Ili kuamua kama chanzo kinachohusika na unabii ni kile cha pili, tunahitaji karama ya utambuzi.
Lakini kwa kuwa tunaujarubu ujumbe utolewao na Mkristo ambae Roho wa Mungu anakaa
ndani yake, tunahitaji vigezo fulani tunavyoweza kuvitumia katika kujaribu kunena kwao.
(1) Neno La Mungu
Daima Neno la Mungu liwe ndicho kigezo chetu cha kwanza tukitumiacho kuupima unabii
ulionenwa. Kwa kuwa Roho wa Mungu anayatambua Maandiko kuwa yamekamilika na
yametosheleza, neno lote la unabii haliwezi kamwe kuongeza chochote kwenye Neno la Mungu
au kuubadilisha ujumbe wa Neno hilo. Karama ya unabii inaweza kufunua au kusisitiza ukweli
fulani katika Neno Takatifu la Mungu lakini haiwezi kufunua chochote ambacho hakiambatani
au kukubaliwa na Neno la Mungu.
(2) Chema ni kipi? (Wathesolonike 5:9-21):
Andiko lililonenwa hapo juu linaeleza kuwa tushikilie kilicho chema. Chema ni nini? Ulonska
anaeleza kwamba neno lililotumiwa hapa ni kama neno lililotumika katika tafsiri ya Kiyunani ya
Agano la Kale, Septuaginta, ambayo inaeleza katika Mwanzo 1:25, kwamba baada ya Mungu
kuumba nuru, nk. "na Mungu akaona ya kuwa ni vyema". Kwa hiyo kitu chochote kiletacho
nuru, chenye rutuba, na kinajenga, ni chema.22 Unabii huo waweza kukubaliwa na kuhesabiwa
kuwa ni unabii wa kweli.
(3) Kusudi Sahihi (1 WAKORINTO 14:3)
Kama ilivyokwisha kusemwa awali, kulingana na masharti ya Agano Jipya, unabii hauna budi
kuwa na angalao mojawapo ya mambo yafuatayo kama siyo yote matatu yaani.
Kukuza, Kuonya, Kufariji.
Kwa sababu tayari mambo hayo yamekwisha kuelezewa kwa undani, hivi sasa yatosha tu
kuyataja.
(4) Ubora Na Udhahiri
Muumini mwenye karama ya unabii anatabiri sawa sawa na ngazi ya imani yake ya kiroho.
Kama mtu huyu amekwisha kukomaa, kukua kiroho, hiyo itadhihirishwa kutokana na ubora na
udhahiri wa ujumbe atakaoutoa.23 Wakristo kama hao wanahitaji kutiwa moyo ili wautafute tena
ushirika wa karibu na Bwana ambao hapo awali walikuwa nao.
5. Nani Anayeweza Kuupima Unabii
Katika 1 Kor. 14:29 neno la Mungu linatamka kuwa manabii watanena na watu wengine
watapambamua. Hata hivyo si kila mtu anayeweza kuupima unabii isipokuwa mtu mwenye sifa
zifuatao.
22 Ulonska, p. 100.
23 Ibid., pp. 101-102.
40 KARAMA ZA UVUVIO
40
(1) Asiwe na chuki yoyote kuhusiana na karama hii.
(2) Awe wa kiroho na pengine adhihirishe karama hii pia.
(3) Asiwe mtu wakusukumwa na hisia. Mawazo hayana nafasi katika
sehemu hizi, kwasababu kinachotakiwa ni kupambanua kitu
chakusema."
Si kujisikia vizuri kuhusu hii. Mtu mwenye kudhirisha karama ya unabii sharti awe wazi ili
aweze kusahihishwa. Anawajibika kwa ukamilifu kuhusu matumizi mema au mabaya ya karama
hii. Hakuna mtu anayeweza kudai kwamba yeye ni wa kiroho sana hata anashindwa kudhibiti
matokeo ya yale anayoyasema.
Maandiko yako wazi yanasema kuwa roho za manabii huwatii manabii (1 Kor. 14:32).
Wakati mwingine yabidi mtu akemewe hadharani, hasa zaidi kama yule anayetoa unabii
ananena mambo yaliyo kinyume cha maandiko, au kama akitoa kwa njia isiyostahili. Sitasahau
tukio moja huko Kumasi, Ghana ambako dada mmoja alisimama ili kutabiri. Alipokuwa
anaanza mmoja wa wazee wetu alikuja akamkalisha. Nilipouliza baada ya ibada kilichotendaka,
mzee huyo aliniambia kwamba dada huyo alikuwa anaishi katika dhambi, kwa hiyo ilibidi
azuiwe asitoe unabii. Katika hali kama hiyo kukosolewa hadharani kwa namna hiyo ni lazima.
Hapa tuwe waangalifu hasa kwa "manabii" wanaotutembelea" ambao siyo sehemu ya kawaida
ya kusanyiko letu. Hata hivyo, katika hali ya kawaida yafaa nabii anayekosea asahihishwe
faraghani. Kama tukishindwa kujaribu na kuhukumu unabii, watu hawataiheshimu karama.
Hivyo haitakuwa baraka kwa mwili wa Kristo, kama Mungu alivyokusudia iwe. Kisha badala
yake itakuwa kizuizi kwa kukua kwa kanisa.
6. Matumizi Potofu Ya Karama
Karama ya unabii, kama Ulonska anavyofundisha, haitakiwi na haiwezi kutumika kama
ifuatavyo, ingawa wengine wamejaribu kuitumia katika njia hizo.24
(1) Unabii usitumike kwa kuwafanya watu wachumbiane
(2) Unabii usitumike kwa uchaguzi wa viongozi katika Kanisa.
(3) Karama ya unabii kamwe isitumike ili kulazimisha watu kutubu.
(4) Unabii usitumike kwa kulazimisha watu kutoa misaada, kuuza mali
zao n.k.
(5) Unabii hauwezi kuwa chanzo cha mafundisho mapya.
24 Ibid., p. 94
KARAMA ZA UVUVIO 41
41
Pia ni makosa kwa wakristo kuwaendea waumini wanaodhihirisha karama ya unabii, au kwa
watu au mtu aliye na huduma ya unabii, na kuwaomba maelekezo au ushauri kupitia unabii
kutoka kwao. Lazima muumini amwachie Mungu jinsi atakavyoongoza. Kama ni mapenzi ya
Mungu kutuongoza kupitia unabii au kuptia kwa nabii. Nabii huyo au Neno la Mungu litakuja
kwetu na siyo sisi kwenda kwake. Kanisa la mwanzo katika Mdo. 6 na 15, walipokabiliana na
shida, hawakuita manabii waliokuwa miongoni mwao na kuwauliza la kufanya, bali matatizo
yao waliyatatua kwa njia mbali mbali.
Wakati karama hii inapotumika vizuri katika muundo wa kanisa ni mojawapo ya njia bora za
kujidhihirisha kwa Roho Mtakatifu. Lakini inahitaji mafundisho na wakati mwingine kurudiwa
ili karama iweze kuwa kama Mungu alivyokusudia iwe.
7. Maoni Kuhusu Utekelezaji
Muumini aliye na karama hii, au na karama nyingine yoyote anatakiwa kila mara awe na
msimamo wa kusema Bwana watumie wengine, lakini mimi pia niko radhi unitumie. Kama
mkristo hakutawaliwa na msimamo kama huo maishani anaweza kwa urahisi kabisa akajifikiria
kuwa yeye pekee ndiye aliepakwa mafuta na kwamba daima ni yeye peke yake atakayesema na
kwa hiyo hataacha wengine walio na karama hiyo hiyo nao wapate fursa ya kuhudumu.
Mwisho ni lazima tukumbuke kwamba shetani anataka kuharibu kila kitu cha kiroho. Hivyo
sehemu anapotushambulia ni kwenye imani yetu, kwani ili kutoa ujumbe wowote wa unabii
tunahitaji kuwa na nguvu katika imani. Kama shetani angefaulu kuharibu imani yetu anaweza
kuziharibu karama zenyewe. Kama akiweza kubadili imani iwe hofu atanyamazisha karama
tuliyo nayo kisha atuzuia kupokea karama zingine.
KUNENA KWA LUGHA
Miongoni mwa karama zote za Roho, karama ya lugha mara nyingi imefikiriwa kuwa ndiyo
maarufu zaidi kutokana na jinsi ilivyotumika katika kuanzishwa na kukua kwa huduma za
Wapentekoste pia uamsho wa Karismatik. Lakini karama hiyo pia imebishaniwa zaidi kuliko
zote, na hata kutoeleweka vizuri, kwa hiyo ni muhimu tuichunguze kwa uangalifu. Kwanza
awali kabisa tunahitaji kuthibitisha kwamba ilianzishwa na Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe
(Mark 16:17). Pili tunahitaji kutambua kwamba Yesu hakuiwekea karama hii mipaka ili ibakie
na wanafunzi wake tu au kwa waumini wa Kanisa la mwanzo tu, bali aliahidi kutoa karama hiyo
kwa wote ambao wangaliamini.
"Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio, katika jina langu watasema
kwa lugha mpya."
42 KARAMA ZA UVUVIO
42
Maandiko katika Matendo ya Mitume 2:39 inaeleza kuwa ubatizo wa Roho Mtakatifu ni kwa
wote. Karama hii ni kwa ajili yenu na kwa ajili ya wototo wenu, na wote walio mbali na kwa
wote watakaowaita/watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. Hakuna mtu anayesoma
maandiko na mawazo yaliyo wazi ambaye anaweza kusema kwamba kunena kwa lugha pamoja
na karama zingine siyo kwa ajili ya siku zetu hizi. Neno la Mungu lathibitisha vinginevyo. Kwa
hiyo wale ambao wameziita karama hizi kuwa ni za kipepo na udhihirisho wa mashetani
wanakuwa katika hatari mbaya sana ya kumtenda dhambi Roho Mtakatifu.
1. Asili Ya Karama
(1) Ushahidi Wa Kimaandiko Wa Ubatizo Wa Roho Mtakatifu
Kunena kwa lugha ndio ushahidi wa kwanza unaothibitisha kuwa mtu amepokea ubatizo wa
Roho Mtakatifu. Kitabu cha Matendo ya Mitume kinadhihirisha jambo hili katika maeneo
kadhaa. Kule Yerusalem siku ya Pentekoste, walijazwa na Roho Mutakatifu nao wakaanza
kunena kwa lugha kama Roho alivyowajalia kutamka. (Mdo. 2:4) kule Kaisaria, miaka minane
baadaye, watu wa mataifa walipokea karama hiyo hiyo, kwani twasoma kwamba
wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha.
(Mdo. 10:45,46) Miaka ishirini na mitatu baadaye, huko Efeso. Roho Mtakatifu aliwajilia juu
yao, wakaanza kunena kwa lugha na kutabiri. (Mdo. 19:6) Ingawa haikuandikwa kwamba huko
Samaria mwaka mmoja baada ya Pentekoste walinena kwa lugha. Tunao ushahidi unaothibitisha
kuwa kulitokea jambo la nguvu za kiroho, kwani mchawi Myahudi alilazimika kutoa pesa ili
apate kupewa nguvu za kiroho alizoziona zikidhihirishwa (Mdo. 13:9, 17-19) Vile vile hakuna
kumbukumbu kuwa Paulo alinena alipojazwa na Roho Mtakatifu lakini baadaye tunasoma
kwamba alifanya hivyo. Kwa hakika aliliambia kanisa katika Korinto kwamba alisema zaidi
katika lugha kulio wao walivyofanya (lingamisha Mdo. 9:17 na 1 Kor. 14:18) Kwa hiyo
inaweza kuonekana kwa dhahiri kwamba kusudi la msingi la lugha ni kutoa ushahidi wa
kimaandiko wa kuthibitisha kuwa mtu amepata ubatizo wa Roho Mtakatifu.
Lakini kunena kwa lugha ni ishara ya kwanza tu na siyo ya pekee inayodhihirisha ubatizo kwa
Roho Mtakatifu. Sharti tuwe na ushahidi zaidi ya kunena kuonyesha kuwa tunayo karama ya
Roho ya thamani sana. Maisha ya utauwa na nguvu ya kiroho kushuhudia lazima ziambatane na
ubatizo wa Roho Mtakatifu.
(2) Lugha Kama Karama
Muumini kwanza anapopokea Roho Mtakatifu ishara ya mwanzo ni kunena katika lugha. Na
hizi lugha sharti ziwe ni sehemu ya ibada zake za binafsi faraghani ... Hata hivyo kunena kwa
lugha kanisani, nje ya maombi ya pamoja ya hadhara, ni huduma ya hadhara.
KARAMA ZA UVUVIO 43
43
Hii huduma ya hadhara inaonekana kuwa ya wale hasa wanaotumika katika hali hii. Ndugu
mmoja anaweza kuuliza kuwa najuaje ya kwamba-nina karama ya kunena katika lugha za
"hadhara" na siyo kwa faragha tu. Jibu ni rahisi, vivyo hivyo kama nabii anavyojua kuwa
amepokea unabii, hivyo hivyo na mwenye karama ya kunena kwa lugha anajua ya kwamba hii
ni huduma ya hadhara. Lugha za jinsi hiyo lazima zifuatiwe na tafsiri. Hata hivyo kuna nyakati
tofauti/wakati maalumu ambapo waaminio wametoa ujumbe katika lugha mpya na watu
wasioamini waliokuwamo katika ibada walielewa maana ya ujumbe huo, na kisha wakajitoa
kwa Yesu kutokana na kwamba ujumbe uliotolewa ulikuwa katika lugha wanayoifahamu,
ambapo hali halisi ya mioyo yao ilifunuliwa.
2. Kunena Kwa Lugha Kutendavyo Kazi Na Jinsi Kunavyotumika
(1) Lugha Hugawiwa Kwa Makusudi Mahususi
Karama ya lugha haikutolewa kwa kucheza michezo kama ilivyotokea huko Ujerumani kwenye
faragha moja ambako kiongozi alionyesha jinsi alivyoweza kunena kwa lugha tofauti. Kila
wakati alipokuwa ananena kwa lugha tofauti alikuwa akiwaambia wasikilizaji ni lugha gani
aliyokuwa ananena. Lakini karama ya lugha siyo mwanasesere bali ni ishara ambayo inaonyesha
ya kuwa tumepokea nguvu kwa ajili ya kushuhudia. Katika Kiyunani tunasoma kwamba
mtapokea nguvu "dynamis" ambako tunapata maneno dynamite au dynamo kuwa mashahidi wa
kuuawa. Kwa hiyo lugha ni ishara kwamba tumepokea nguvu za pekee za kiroho ili tuwe
mashahidi wake ambao twaweza kufikia hata kupoteza maisha yetu kwa ajili yake. Wakati
mmoja mtu alisema kama ambavyo mvuke, katika mvuke wa mashine ya gari la moshi, hadi
kule iendako, vivyo hivyo lugha hazikugawiwa ili zitumike kupiga makelele bali kuwezesha
hatua kuchukuliwa za kupanua na kusukuma mbele ufalme wa Mungu.
(2) Watu Kusema Na Mungu Kwa Msemo Wa Kiungu
Kila muumini aliyejitoa wakfu lazima wakati mwingine ajisikie au hamu ya kufungua moyo
wake kwa Mungu katika mawasiliano yasiyosemeka.
Wakati mwingine mioyo yetu hubeba vitu tusivyoweza kuvieleza kwa lugha yetu. Tukinena kwa
lugha itatusaidia kuwasilisha mawazo yetu ya ndani kabisa katika maombi.
Anenaye katika lugha hasemi kwa watu bali kwa Mungu Kwa sababu
hakuna mtu wa kumwelewa. Lakini katika Roho anasema siri za kiroho
(Wakor. 24:2).
Kosa walilolifurahia Wakristo wengi ni kwamba katika siku ile ya Pentekoste wale waliojazwa
Roho Mtakatifu walihubiri Injili kwa lugha za mataifa ya kigeni, walizopewa kwa kusudi hili
(Matendo 2:4-11). Hii ilisababishwa na usomaji usio sahihi wa ujumbe huu. Ujumbe husema,
"Walikuwa wakimtukuza Mungu kwa matendo yake ya ajabu". Walizungumza kimiujiza kwa
Mungu na siyo kwa watu. Tangia hapo wazo kwamba karama ya kunena kwa lugha ilikuwa ni
44 KARAMA ZA UVUVIO
44
kupatiwa kimiujiza lugha za kigeni mitume, kwa ajili ya kuihubiri Injili ni kosa. Kufuatana na
maandiko, Petro ndiye pekee aliyekuwa akiihubiri Injili siku ile ya Pentekoste, hapo hakutumia
lugha nyingineyo yeyote ila lugha iliyoeleweka kote ya Kiarami au Kiyunani.
(3) Watu Hujijenga
Tanaweza kuwajenga wengine kwa njia ya kuhubiri au kutabiri lakini kuna karama moja tu
ambayo kupitia kwake tunaweza kujijenga nayo ni kunena kwa lugha zingine. Paulo alitumia
karama hii sana, na tunaweza kuwa wa kweli tukisema kwamba aliitumia na akajijenga. Kama
tukinena latika lugha tunaweza kujenga maisha yetu ya imani na kuendelea kukua Kikristo, wale
wanaosisitiza kwamba karama hii ilikuwa ya kanisa la mwanzo peke yake lazima waulizwe: Je
sisi hatuhitaji zaidi kunena ili kujijenga kuliko kanisa la mwanzo?
(4) Kwa Maombezi Na Maombi
Kunena kwa lugha ni silaha ya ajabu katika maombezi na pia vita vya kiroho na labda ni ajabu
hivyo kwa sababu tunanena katika lugha ambazo hatujawahi kuzitumia katika kutenda dhambi,
(kusema uongo, kulaani, kusengenya, n.k) hapo nyuma. Tena kwa wakati mwingine hatujui jinsi
ya kuomba wala kitu cha kuombea. Kama wakati huo Roho wa Mungu anachukua hatamu
tutasema mambo ya siri kwa Mungu, ikitupa uhakika kwamba tunamgusa Mungu na mahitaji
yetu muhimu.
(5) Kwa Maombi Yenye Mamlaka
Wengine kati yetu wanaweza kuwa na uzoefu ya kwamba wakati tunapoombea mgomjwa au
aliyepagawa hatuwezi kufunguliwa kiroho. Katika hali hiyo kuomba katika lugha kunaweza
kubadilisha mazingira yote na kutuwezesha kupenya na kushinda kiroho.
3. Kanuni Kuhusu Karama Hii
(1) Wapi na Lini Tunene?
Neno la Mungu linatufundisha kuhusu kutumia karama hii hadharani, sehemu ya kunena katika
lugha ni katika mkutano wa waumini (1 Kor. 14:23,26). Watu wengine hufundisha kuwa lugha
zinafaa kuwekwa katika maombi ya mikutano ya faragha peke yake, sio kanisani. Msimamo huo
unatokana na 1 Wakorointo 14:27,28 ambao unaonyesha kwamba endapo mtu ananena kwa
lugha mpya na hakuna mtafsiri, na akae kimya. Katika kanisa, na aseme na nafsi yake kwa
Mungu. Msimamo huo unatokana na kutokuielewa vyema hali halisi iliyokuwapo pale Korinto.
Inaonekana kwamba pale Korinto mtu mmoja baada ya mwingine alinena hadharani katika
lugha bila kuwa na yeyote wa kutafsiri. Hii ndiyo maana Paulo aliwafundisha kuwa na utaratibu,
la sivyo wasioamini (Mst. 23) wangesema kuwa wamerukwa na akili. Kufuatana na 1
KARAMA ZA UVUVIO 45
45
Wakorinto 14:18,19) inaonekana kuwa hata walifundisha katika lugha. Lakini katika mambo
yote kwa miongozo na mafundisho Paulo alihakikisha ya kwamba wasije wakakosa
kumwelewa. Na ndiyo maana aliwaagiza katika mstari wa 39 wasizuie watu kusema kwa lugha
nyingine. Kusudi muhimu la Mtume halikuwa kuzuia Wakristo kunena katika lugha, bali
kwamba mambo yote yafanyike kwa uzuri na utaratibu, (Mstr. 40) ili kwamba mtu yeyote
asiuzuie mtiririko wa Roho Mtakatifu.
(2) Katika Ibada Moja Wangapi Waseme?
Paulo anafundisha wale walio na ujumbe katika lugha, wanatakiwa kuwa wawili au watatu, na
mmoja atafsiri. Hii ina maana kwamba wale wanaosema katika lugha hadharani wamewekwa
wachache ili kuacha nafasi kwa ajili ya huduma na karama zingine.
Hata hivyo wakati wa maombi ya pamoja ya hadhara (ambayo yanakubalika kimaandiko, hebu
kalinganishe Ezra 3:12-13; Hesabu 23:21; Mdo. 4:24 n.k.) tunaweza kuomba katika lugha
hadharani bila ya kuwa na tafsiri.
4. Maoni Ya Kiutekelezaji
Tunahitaji kujua kwamba Roho Mtakatifu hatatulazimisha kunena katika lugha zingine. Hapa
ndipo watu wamechanganyikiwa inapokuja kwenye ubatizo wa Roho Mtakatifu. Wanafikiri
kuwa Roho Mtakatifu atawashika na awalazimishe kunena. Lakini hii sivyo ilivyo. Katika hali
ambazo mtu amejiweka tayari kwa ajili ya karama Roho Mtakatifu atakuja katika hali ya
kwamba itatokea kuwa amechukuwa nafasi bila mawazo ya mtu. Lakini muumini kwa kujitoa
kwake kwa Mungu tayari ametoa kibali kwa ajili ya Roho Mtakatifu kuchukua ulimi wake na
kumtumia kunena. Lakini bado katika hali nyingine, hasa pale ambapo muumini bado ana sita
au anaona mashaka, kwa sababu ya kuogopa kusema, lugha hupokelewa katika roho ya
muumini lakini hazitamkwi kwa sababu huyo mtu anazizuilia. Jambo pekee ambalo Mkristo
huyo anatakiwa kufanya ni kujinyenyekeza kabisa kwa Bwana akiamini kuwa atawapa vipawa
vyema tu watoto wake na kuruhusu lugha kumiminika kupitia kwake pia. Lazima tujue kwamba
Roho Mtakatifu ndiye anayevuvia na kutoa lile linenwalo, ila kunena kwenyewe kunafanywa na
watu. Maandiko yanaeleza hili waziwazi.
Na wote walijazwa na Roho Mtakatifu na wakaanza kunena kwa lugha
nyingine kama Roho alivyowapa kunena (Mdo. 2:4)
Tunafanya kazi ya kusema, lakini Roho Mtakatifu ndiye anayetoa maneno. Hivyo tunaweza
kuzuia lugha au tunaweza kuziacha zikamiminika. Lakini hapa lazima tutoe tahadhari. Kunena
kwa lugha hakufundishwi na lazima kamwe kusiigizwe hata kama tunahimizwa na wengine
kufanya hivyo. Hii ilimtokea rafiki yangu mmoja aliyehudhuria ibada katika kikundi kimoja
huru ambapo alitakiwa kurudia lugha za mtu fulani. Alipouliza kuhusu jambo hili aliambiwa
46 KARAMA ZA UVUVIO
46
kuwa hiyo ndiyo njia anayoweza kuitumia mtu kujifunza kunena kwa lugha mpya. Mafundisho
hayo kabisa siyo ya kibiblia na ni lazima yapingwe. Mungu hahitaji msaada wetu. Neno la
Mungu linasema kwamba walinena kwa lugha kama Roho Mtakatifu alivyowapa kunena".
Hatuna budi kunena kwa lugha kwa wingi kadri iwezekanavyo, kwa sababu itatujenga na kutupa
nguvu.Na siyo kusema, kama wengine wanavyodhani, kuwa kunena katika lugha ndiyo
uthibitisho wa kuwa tutakwenda mbinguni. Sisi Wapentekoste na wenye karama kwa mara
nyingine tumehukumiwa na kulaumiwa kwamba wengine wetu wanasema kwa lugha lakini
wanaishi kama shetani. Kwa hiyo, tunahitaji kukumbuka kuwa maandiko hayasemi kwamba
"Bila lugha hakuna atakayemwona Bwana" Bila Utakatifu hakuna atakaye mwona Bwana".
TAFSIRI ZA LUGHA:
Kuna mambo mawili ya pekee kuhusu karama hii. Kwanza kabisa karama zote za Roho karibu
zimefananishwa katika Agano la Kale isipokuwa tu kunena kwa lugha na tafsiri za lugha. Hizi
mbili zimeanza tu kutenda kazi tangu Pentekoste. Pili karama ya tafsiri za lugha ndiyo pekee
yenye masharti. Inaweza kutenda kazi wakati karama ya lugha inapotangulia kufanya kazi.
1. Asili Ya Karama
Ili karama hii ipate kueleweka wazi, ni muhimu kutafakari jina halisi la karama hii. Ni karama
ya kufafanua siyo karama ya kufasiri maneno. Kufasiri ni kubadilisha maneno kutoka lugha
moja na kuyaweka katika lugha nyingine. Kwa upande mwinginge, ufafanuzi maana yake ni
kueleza maana ya lugha na inaweza ikawa ndefu au fupi kuliko ujumbe uliotolewa awali. Ni
maelezo ya yale yaliyosemwa. Katika kiyunani maana yake "kueleza kwa ukamilifu."
Wakati mwingine ninapohudumu neno nashangaa sana, kwa sababu nasema sentenso tatu katika
Kiingereza, kisha anayetafsiri anatumia maneno matano katika Kishona.
Au natumia sentenso moja yeye anasema nne. Wakati fulani niliacha kuhubiri nikamuliza "hivi
wewe unasema nini? Mimi sikuyasema yote hayo." Lakini mtafsiri hutabasamu na kujibu
"Nimewaambia yale yaliyosemwa". Hii huwa hivyo kwa sababu wakati mwingine tafsiri
inalazimika kuwa ufafanuzi.
Pamoja na mambo haya kanuni ni kwamba tafsiri haina budi kuwa na urefu ule ule wa lugha
zilizonezwa. Pia mfumo wa ujumbe sharti ubakie huo huo. Kama kulikuwa na sauti ya faraja
katika ujumbe wa lugha hakuwezi kukawa sauti ya kukemea katika tafsiri.
KARAMA ZA UVUVIO 47
47
2. Matumizi na Jinsi karama Inavyofanya kazi
(1) Mudhumuni yaleyale kama ya Unabii
Paulo anatoa thamani ile ile kwa lugha zinazotafsiriwa kama anayetoa unabii. Sababu yake ni
kwamba ujumbe unapatikana kwa njia ile ile na umekusudiwa kwa kazi zilezile, yaani kujenga,
kuonya na kufariji.
(2) Na Mmoja Atafsiri
Kuna maoni mengine tofauti kuhusu usemi huo. Mimi binafsi, nina hakika haikukusudiwa kuwa
mtu mmoja huyo huyo daima ndiye awe anatoa tafsiri katika mikutano yote, wala kwamba mtu
huyo huyo atafsiri kila ujumbe uliotolewa katika mkutano mmoja. Neno la Kiyunani lililotumika
hapa ni "eis", ambalo halionyeshi moja kama tarakimu bali kama kielelezo cha nafsi
kinachomanisha mtu fulani tu.25 Hivyo Maandiko yanasema "Na mmoja na afasiri" Mstari huu
(1 Kor. 14:27) unaeleza kuwa ujumbe mmoja usipewe tafsiri zaidi ya moja, hata kama watu
zaidi ya mmoja wanapewa tafsiri ya ujumbe ulionenwa kwa lugha. Kanuni hii imekusudiwa
kutekeleza mambo mawili.
a. Lugha zikinenwa kwa ajili ya huduma ya hadhara sharti zipate tafsiri.
b. Kusiwepo mashindano miongoni mwa watafsiri.
Inawezekana kwamba baadhi ya watu wanayo karama kubwa zaidi yakutafsiri vizuri kuliko
wengine, au wanao uwezo mkubwa zaidi wa kusema, na wanaweza kutoa ufafanuzi bora wa
ujumbe uliotolewa katika lugha. Hawa wote wanatakiwa wakae kimya mara tu ufafanuzi ukiisha
kutolewa na mtu mmoja (mst. 30).
Kwa hiyo wote wenye karama ya tafsiri wanahitaji kungojea "kibali" kutoka kwa Roho
Mtakatifu kabla ya kutoa tafsiri hiyo. Tafsiri ya lugha inaweza kutolewa na mtu anayetoa
ujumbe kwa lugha au na mtu mwingine. Yote mawili ni sahihi kimaandiko (1 Kor. 14:13,27)
Hata hivyo yatupasa tukumbuke kuwatanguliza waumini wenzetu ili wengine zaidi wapate fursa
ya kuzidhihirisha karama. Katika ibada moja kusitokee zaidi ya lugha tatu na tafsiri tatu, na pia
unabii kwa idadi hiyo hiyo (1 Kor. 14:29)
3. Maoni Kuhusu Utekelezaji
Kimsingi tunaweza kusema kuwa tafsiri ya lugha hupatikana vile vile kama unabii. Tunapokea
ujumbe wa Mungu katika roho zetu kupitia kwa Roho Mtakatifu wa Mungu. Kutakuwapo na
mtiririko wa kiroho wa kunena na kutafsiri lugha, kwa namna ambayo lugha na tafsiri
vitaambatana bila kuingiliana. Wakati mwingine yaweza kutokea kwamba mawazo fulani
25 Erwin Preuschen, Griechisch-deutsches Taschenwörterbuch zum Neuen Testament. (Berlin: de Gruyter, 1976). P.
65.
48 KARAMA ZA UVUVIO
48
yanamjia mtafsiri ghafla na kwa nguvu wakati lugha zinapokuwa zinanenwa. Wakati mwingine,
kama Ulonska anavyothibitisha mtafsiri sharti "amsikilize Roho" ili aweze kupata msukumo wa
kutafsiri.26 Hawezi kuzielewa lugha anazozitafsiri. Ujumbe, ambao hufuatia lugha nao
hupokelewa kwa njia hiyo hiyo ya kiroho kama unabii ulivyopatikana. Mtafsiri humngojea
Mungu atoe tafsiri, bali hadiriki kuzielewa lugha zinazoutangulia ujumbe wake.
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-
26 Ulonska, p. 132.
49
V. KUKOSEKANA KARAMA KANISANI SIKU HIZI
Tunaweza kuuliza swali "Kwa nini karama za roho hazifanyi kazi katika Kanisa langu? Kuna
majibu kadhaa kwa swali hilo. Kwa sababu ya udogo wa muda, tunaweza kuchunguza tatu tu
ambazo zinawahusu watu wote.
1. Ujinga Na Kukosa Mafundisho
Karama za Roho zinapokelewa na kufanya kazi kwa imani. Imani hii itaamshwa kwa kupitia
kwa mahubiri ya ukweli wa kibiblia. Kama tusipojua ukweli wa Mungu kuhusu karama hizi,
hatutazihitaji na hivyo hatutazipokea kwa imani. Isipokuwa tu kama tumefundishwa ndipo ile
imani ya msingi itakapoamshwa na pazia la ujinga litaondolewa. Tukipata ufahamu ulio sahihi
kuhusu karama hizi, tutaweza kujua tunachokitafuta na kugundua kwamba karama moja au zaidi
zimekuwa zinafanya kazi kupitia kwetu, bila sisi wenyewe kuwa tunatambua vizuri hali hiyo.
2. Kiburi Na Kujidai Umekamilika
Kama tukifikiri kwamba tumeshapokea yote ambayo Mungu ametoa, hatutapokea karama hizi
za thamani tunazozihitaji sana tuwe nazo; Ni pale tu tutakapoweza kuzitaka sana karama zilizo
kuu (1 Kor. 12:31) ndipo tutakapozipokea.
3. Hofu
Hofu ya kupokea kitu kibaya au kuogopa kutenda kazi katika mwili kumewazuia wengi kupokea
karama. Ni moja ya silaha kubwa ambazo shetani huzitumia ili kanisa libakie bila kutumia
karama hizi. Wale wanaoogopa kupokea kitu cha kipepo wanasahau maneno ya Bwana katika
(Luka 11:13).
Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa
vyema, je Baba aliye Mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu
hao wamwombao?
4. Makaburi Au Wodi Ya Wazazi
Kanisa lililo na karama za Roho halitakosa kuwa na shida zake, lakini ni bora zaidi kukumbana
na shida hizo kuliko kukumbana na kanisa lililokufa. Kama mtu mmoja alivyosema, ni rahisi
zaidi kushughulikia kelele za chumba cha wazazi kuliko ukimya wa wafu makaburini".
VI. JINSI YA KUPOKEA KARAMA ZA KIRHOHO:
Wakati wa huduma yake Kristo aliwaambia wafuasi wake kwamba wanaweza kufanya kazi
alizofanya hata zilizo kubwa zaidi (Yoh. 14:12; Mathayo 28:19,20; Matendo 1:18) inasema
kwamba Kristo ametoa nguvu za kiroho za kutosheleza ili kuwezesha amri hiyo kutekelezwa.
KUKOSEKANA KARAMA 50 KANISANI SIKU HIZI
Kwani tutapokea nguvu baada ya Roho Mtakatifu kutujilia juu yetu. Pamoja na nguvu hii
Mungu ameifanya kupatikana karama za kiroho kwa kila muumini ambazo zitatuwezesha,
kuhubiri neno kwa ujasiri kama Wakristo wa kwanza, kuponya magonjwa, kutoa pepo wachafu
na kufufua wafu. Kwa hiyo tunaweza kuwa sehemu halisi ya huduma ya Kristo, hata katika
karne ya ishirini. Lakini kabla ya hayo hayajatokea, lazima masharti kadhaa yatimizwe.
1. Masharti Ya Utendaji Kazi Wa Karama
Siku ya Pentekoste, pamoja na kuwapa wanafunzi nguvu kwa ajili ya huduma vile vile ilifungua
ukurasa mpya wa eneo la karama za kiroho. Baadhi ya wataalam wa maandiko husisitiza nguvu
zilizodhihirishwa katika maisha ya wanafunzi na zile zilizodhihirishwa na Roho katika Agano la
Kale yanaweza kuoanishwa kama karama za Kiroho. Hata hivyo ni muhimu kukumbusha
kwamba nguvu za Roho Mtakatifu katika Agano la Kale na wakati kabla ya Pentekoste haiwezi
kulinganishwa kama "karama za kiroho" kama tunavyozijua katika (1 Kor.12 na 14.
Unabii na pia hekima ya Sulemani, au maarifa ya Samweli ya nguvu za Kiroho, haifai
yachanganywe na karama za agano jipya za Roho Mtakatifu. Uonekanaji huu wa Roho wa
agano la kale ulikuwa mchache na ulitenda kazi kwa kupitia waliochaguliwa wachache peke
yao, ambao wanaweza kuhesabiwa kuwa walionjeshwa yale yatakayokuja baadaye. Lakini kabla
ya Agano la Kale halijafunga sura zake Mungu aliahidi kwamba katika siku za mwisho
atamwaga Roho Wake juu ya wote wenye mwili. Hatimaye hii ilitokea siku ya Pentekoste
ambapo Petro alikumbusha hii ahadi iliyotolewa kwa nabii Yoel (Joel 9:28,29).
Hata miujiza na uponyaji iliyofanywa na mitume hadi tukio hili la kihistoria haiko chini ya
karama za kiroho kwa mujibu wa 1 Kor. 12 na 14, bali zilikuwa ni matokeo ya amri ya Kristo
(Math. 10:7,8; Luka 9:2; 10:9; 10:19). Walikuwa katika nafasi ya kipekee kabisa. Hadi wakati
wa Pentekoste, karama zilizoonekana kwa kupitia kwao zilielekea kuwa ni za miujiza na
uponyaji peke yake. Lakini baada ya Pentekoste, walienda katika upeo mpya wa kutenda kazi
kupitia karama zote tisa ambazo Kristo aliziweka ziwe urithi wa mwili wake. Kwa hiyo
tunaweza kumaliza ya kwamba waumini wakitamani karama za kiroho lazima wapokee ubatizo
wa Roho Mtakatifu kwanza, kama mitume walivyofanya, kabla ya karama kuonekana kupitia
kwao.
(1) Pokea Roho Mtakatifu
Roho Mtakatifu kamwe hataingia katika chombo kichafu. Lakini tukiisha kutubu na dhambi zetu
zikaondolewa kwa damu ya Yesu ya thamni, tunakuwa na sifa za kuturuhusu kupokea ubatizo
wa Roho Mtakatifu. Tunaweza kuja kwa Mungu tukiamini kwamba ahadi ni ya kwetu kama
ilivyo katika Mdo. 2:8,39 Lakini wengine huwa wanashindwa kupokea ubatizo wa Roho
Mtakatifu kwa sababu wanafikiri hawajawa wazuri vya kutosha. Ukweli ni kwamba hakuna
anayepokea Roho Mtakatifu kwa sababu ya sifa zake kuu za kiroho alizozipata, au kwa sababu
KUKOSEKANA KARAMA KANISANI SIKU HIZI 51
51
ya tabia yake madhubuti ya kikristo. Kumwambia mtu afikie ngazi fulani kabla ya kupokea
ubatizo wa Roho Mtakatifu itamweka mbali na kiini chenyewe ambacho akipitia humo ndipo
atakapoweza kuishi maisha ya ushindi.
Dhana kwamba watu hupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu kwa sababu ya utakatifu wao ina
matokeo yake. Kama mpokeaji atafikiri kwamba amepewa Roho kwa sababu yeye amefikia
ngazi ya juu ya kujitoa wakfu na utakatifu, haikosi ataanguka katika mtego wa kiburi na
majivuno. Karama za Roho pia na ubatizo wa Roho hugawiwa kwa msingi wa neema tu.
Kwamwe hatuwezi kupata kipimo cha juu cha utakatifu cha kutosha kwa kutufanya kustahili
kupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu. Kama tumesafishwa katika damu ya Yesu kusamehewa na
kutolewa wakfu kama tunavyojua jinsi ya hali yoyote kuwa sisi ni wahusika. Hatuwezi kupokea
Roho Mtakatifu kama faida ya kazi zetu. Tunachotakiwa kufanya ni kukubali ukweli huu na
kupokea Roho Mtakatifu kwa imani. Hakuna haja ya kuombaomba na kujadili na kujidhili kwa
maumivu kwa sababu Mungu amefanya Roho tayari kupatikana bure tangu miaka 2000
iliyopita. Hebu tuje kwa imani na tupokee ubatizo wa Roho Mtakatifu na karama zile za
thamani.
Pamoja na hayo, sharti tuongeze kwa haraka ya kuwa hatuwezi kuendelea kuishi maisha
vyovyote vile tunavyopenda au tunayopendezwa nayo na huku tukitegemea Mungu kutubariki
na karama zake za ajabu. Tusiache kuangalia ukweli ya kwamba bila tunda la Roho, ubatizo
katika Roho Mtakatifu pia na karama havina maana. Na hii inadhihirika mara tunaposoma sura
13 ya Wakorinto, ambayo Mungu kwa hekima yake aliweka kati ya maelezo ya karama (Sura
12) na utendaji kazi na matumizi ya karama (Sura 14) na hivyo kuweza kusisitiza umuhimu wa
tabia ya Kimungu wa kuzitendea kazi karama hizo.
Maendeleo ya kiroho ya kawaida ya muumini yanatakiwa yawe kwamba karama za Roho na
tunda la Roho zajionyesha pamoja na zikitenda kazi kwa Pamoja katika maisha ya muumini.
Maendeleo ya tunda la kiroho lazima yapate kuangaliwa zaidi kwa sababu hatutambulishwi
kama Wakristo kwa karama bali kwa tunda la Roho.
(2) Zitakeni Sana (1 WAKORINTO 12:31)
Paulo anatuhimiza kuzitamani kwa bidii karama zilizo kuu. Tunalazimika kuwa na tamaa
iliyozama sana juu ya karama hizi. Elisha alimfuata Eliya alipopokea mara dufu ya upako. Hali
kadhalika lazima tuwe katika uhusiano wa karibu sana na Bwana mpaka tuweze kupokea
karama kutoka kwake. Na baadaye ataziweka juu yetu karama zilizo bora kwa ajili yetu. Si juu
yetu kujichagulia karama tunazotaka. Lakini maandiko yanatuambia, Anampa kila mtu kama
anavyotaka" (1 Wak. 12:11).
KUKOSEKANA KARAMA 52 KANISANI SIKU HIZI
52
(3) Jitoe Kwa Mungu
Kila mtu anayedhihirika kuwa na karama za Kiroho anao wajibu mkubwa sana. Karama za
Roho zinaongoza anayezichukua kuelekea vita vya kiroho, kwa hiyo kukosa kujitoa katika
maisha yake ya uombaji yaweza kuleta ajali za kutisha. Tunapoangalia watu kama Samsoni,
Sauli, Balaam, A.A. Allen au Wainjilisti mashuhuri wa televisheni tunaweza kuona
kinachoweza kutokea kama hatuko kwenye zamu yetu. Mara kwa mara tunasoma kwa uthabiti
kuwa mtu aliye na karama za Roho zikitenda kazi, anaishi maisha ya utakatifu. Lakini pia kuna
wanaotumia karama hizi nzuri na wakiishi maisha yasiyo matakatifu. Bwana wetu alituonya na
uwezekano huo aliposema kuwa wengi watakuja kwake wakisema "Bwana Bwana hatukufanya
unabii kwa jina lako." Kama tunataka kupokea karama hizi tunatakiwa kuhakikisha kuwa hatuna
makosa au kurudi nyuma.
2. Jinsi Karama Zinavyogawiwa
Kuna watu siku hizi wanaozunguka na kuwekea watu mikono na kuwaambia ni karama zipi
walizozipokea sasa. Kosa hili limetokea kwa kutokuelewa vizuri maneno ambayo Paulo
alipomwambia Timotheo katika 1 Tim. 4:14; 2 Tim. 1:6) hali kadhakika na maandiko katika
Warumi, tunaona kwamba mtu hivi hivi hawezi kutowa karama za Roho kwa muumini
mwenzake.
Mufundisho kwa Timotheo yanahusiana na karama ya huduma yake ya Uinjilisti. Huduma za
karama hizi mara kwa mara zilikuwa zinathibitishwa kwa kuwekewa mikono (Mdo. 13:2,3)
ambazo zilionyesha kutambuliwa na kanisa kuhusu huduma ambayo Mungu alimtia mtu.
Ukweli rahisi ni kwamba Mungu ndiye anayetoa uonekanaji wa karama kwa kila mtu sawa na
anavyopenda (1 Wak. 12:11).
VII. UPOKEAJI NA UTUMIAJI WA KARAMA
1. Nani Mtumiaji Wa Karama?
Kwa kuwa sasa tumedhihirisha ukweli kwamba ni Mungu na siyo mtu anayetoa karama za
kiroho, sasa hatuna budi kuuliza swali muhimu sana. Je ni vipi hizi ni karama?
Katika utamaduni na mapokeo mengi, karama au zawadi huwa ni ya yule aliyeipokea. Anaweza
kutumia karama hiyo jinsi anavyotaka, hatakuwa na kamba ya kumhibiti la sivyo haitakuwa
kamwe karama. Hata hivyo, hayo hayawi hivyo kwa karama za kiroho. Hakuna haki kwa
muumini kudai kwamba anayo karama yoyote ambayo aweza kuitumia apendavyo, vibaya
kimwili. Haifai kusema Ninaweza kunena lugha wakati wowote ninaotaka "au hebu sote tuimbe
katika lugha" Mungu hahusiki na kutoa karama kwa mtindo huo. Anatunza nguvu juu ya karama
na kuzionyesha kwa kupitia kila muumini kadri ya mapenzi yake yalivyo. Katika kutenda kazi
mara kwa mara watu wengi wamerithi karama fulani hasa wanapotumiwa kwa kurudia rudia
KUKOSEKANA KARAMA KANISANI SIKU HIZI 53
53
kwa uonekanaji maalum. Kwa mfano mtu anaweza akatumiwa mara kwa mara na karama ya
uponyaji au unabii, inaonekana kama kwamba karama hii ni ya kwake. Kwa sehemu hii yaweza
kuwa kweli, lakini mtu hatakiwi kuwa na mawazo ya kuwa hii ni mali yake. Muumini
anayetumiwa jinsi hii aweke mawazoni kuwa karama hii iko mikononi mwa Mungu, na
anapenda kuionyesha kupitia kwake (1 Kor. 12:11,12) Tukielewa mambo haya kwa usahihi, basi
tutaonyesha unyenyekevu na utauwa unaofaa kwa utendaji kazi wa kila karama ya Mungu kwa
namna ilivyo vyema.
C.W. Conn anajaribu kueleza na mfano ufuatao sahihi. Mtu anaweza akamtolea mwenzake tai
ya shingoni akiamini kuwa ataivaa Kanisani na kwenye tafrija zingine. Lakini hafungwi kwa
kutumia katika mambo yale yale anaweza akaivaa pia katika nafasi zenye dhambi, anaweza pia
akajitundika nayo. Wakati mtu ametoa tai kama zawadi imekuwa mali ya rafiki yake na
anaweza kuitumia kwa jinsi anavyotaka.27
Lakini hakika siyo kama Mungu atawavyo. Karama zake zote zina masharti na zina kuja kwa
muumini kama karama za neema katika wakati unaotakiwa. Zipo kwa madhumuni matakatifu,
na kama hazitumiki kwa nia hiyo zitaondoshwa kwako.
2. Mtazame Mpaji Karama
Kabla ya kumaliza somo hili lazima tutamke tahadhari. Tunapoendelea kuzitamani karama hizi
za thamani tulizoandaliwa na Baba yetu wa mbinguni, ni za maana zaidi. Hivyo yatupasa kuwa
waangalifu daima ili kwamba karama zisije zikawa ni za maana zaidi kuliko mpaji wake.
Mchungaji Busch wa ujerumani anafananisha kwamba kila wakati alipokwenda kumwona
mpwa wake pamoja na familia yake alimletea zawadi, alifurahi kumwona mjomba wake. Lakini
baada ya muda matembezi ya mjomba wake yakawa si muhimu tena bali ni ile zawadi
aliyoileta. Hii inaweza ikatutokea katika ulimwengu wa kiroho. Tunaweza tukachukuliwa na
karama za kiroho tukasahau MPAJI wa mbinguni. Kamwe jambo hili lisiruhusiwe kutokea.
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-
27 Conn, p. 105.

55
PITIA MASWALI JUU YA UTAMBULISHAJI
1. Orodhesha uonekanaji wa karama chini ya mambo muhimu matatu.
_________________ ______________ ______________
1. 1. 1.
2. 2. 2.
3. 3. 3.
2. Ni yepi makusudi matano ya karama za rohoni?
(1) _____________________________________________________
(2) _____________________________________________________
(3) _____________________________________________________
(4) _____________________________________________________
(5) _____________________________________________________
3. Ni wakati gani Karama za Rohozilikoma kudhihirika katika kanisa la kwanza?
4. Mungu alipolirudishia Kanisa karama za Roho kwenye karne ya mwisho ni mambo gani
mawili aliyotumia ili kwamba iwe hivyo?
(1) _____________________________________________________
(2) _____________________________________________________
5. Eleza kwa kifupi ma kusudi matano ya somo hili.
56
PITIA MASWALI JUU YA KARAMA YA UFUNUO
1. Kwa kifupi eleza asili ya Neno la Hekima
2. Nini utendaji kazi na matumizi ya Neno la Hekima.
3. Ni kwa namna zipi tatu watu hunena visivyo sahihi kuhusu neno la Hekima?
(1) _____________________________________________________
(2) _____________________________________________________
(3) _____________________________________________________
4. Kwa kifupi eleza asili ya maono ya usiku na mchana na tofauti zake.
5. Tofautisha kati ya roho tatu ambazo tunakabiliana nazo katika Ulimwengu huu.
(1) _______________ (2) ______________ (3) ______________
57
PITIA MASWALI JUU YA KARAMA YA UFUNUO
6. Orodhesha mambo manne ya Karama ya Kupambanua Roho.
(1)
_____________________________________________________
(2)
_____________________________________________________
(3)
_____________________________________________________
(4)
_____________________________________________________
7. Ni hatua gani nne za utendaji wa karama hii?
8. Je Mkristo aweza kupagawa na mapepo? Eleza.
9. Kwa nini roho za waliokufa haziwezi kumpagaa mtu?
10. Uonevu unajidhihirisha je?
58
MASWALI YA KUFANYA MAPITIO JUU YA KARAMA ZA UTENDAJI KAZI
1. Kwa nini karama za kiroho za uponyaji zinatamanika na kuhitajika zaidi?
2. Kwa kifupi eleza asili ya karama ya uponyaji.
3. Ni zipi sababu nne muhimu za uponyaji wa Kiroho?
(1) _____________________________________________________
(2) _____________________________________________________
(3) _____________________________________________________
(4) _____________________________________________________
4. Orodhesha sababu tano za magonjwa
(1) _____________________________________________________
(2) _____________________________________________________
(3) _____________________________________________________
(4) _____________________________________________________
(5) _____________________________________________________
59
NASWALI YA KUFANYA MAPITIO JUU YA KARAMA ZA UTENDAJI KAZI
5. Nje ya karama za uponyaji Mungu kwa kawaida anaponya kwa kupitia njia mbili ni zipi?
Ziorodheshe pamoja na Maandiko.
(1)
_____________________________________________________
(2)
_____________________________________________________
6. Orodhesha aina za imani.
(1)
_____________________________________________________
(2)
_____________________________________________________
(3)
_____________________________________________________
(4)
_____________________________________________________
7.Kwa kifupi eleza katika maneno yako utendaji kazi na matumizi ya karama ya imani.
8.Mamlaka ya imani inatakiwa isitumike kwa mambo gani?
60
9.Nini maana ya "Miujiza?
10. Kwa nini matendo ya miujiza ni muhimu sana katika siku hizi na kizazi hiki? Eleza.
61
PITIA MASWALI JUU YA KARAMA ZA UPAKO
1. Tafadhali onyesha tofauti kati ya karama ya unabii na huduma ya unabii.
2. Ni makusudi yepi matatu ambayo yamekusudiwa katika karama kama ilivyo (1. Wakorinto
14:37).
(1) _____________________________________________________
(2) _____________________________________________________
(3) _____________________________________________________
3. Eleza utendaji kazi wa karama ya unabii
4. Ni yapi mafundisho manne ambayo tunaweza kupima unabii.
(1) _____________________________________________________
(2) _____________________________________________________
(3) _____________________________________________________
(4) _____________________________________________________
5. Unabii usitumiwe kwa ajili ya nini?
(1) _____________________________________________________
(2) _____________________________________________________
(3) _____________________________________________________
(4) _____________________________________________________
(5) _____________________________________________________
62
MASWALI YA KUPITIA KUHUSU KARAMA ZA UVUVIO
6.Wapi katika maandiko watu walinena kwa ndimi mpya walipobatizwa kwa Roho Mtakatifu?
Taja sehemu za maandiko hayo.
7.Kunena lugha ni kithibitisho cha awali cha kubatizwa katika Roho Mtakatifu, lakini sicho
pekee. Ni kidhibitisho gani kingine lazima kiwepo?
8.Kunena kwa lugha kunafanya kazi katika makundi matano, ni zipi? Ziorodheshe na fafanua.
9.Kwa nini kufasiri lugha ni karama yenye kutegemea kanuni fulani?
10.Ni nini tofauti ya kufasiri na kufafanua?
63
PITIA MASWALI JUU YA UKOSAJI NA UTENDAJI KAZI WA KARAMA
1. Kwa nini tunakosa karama za kiroho Kanisani siku hizi?
(1) _____________________________________________________
(2) _____________________________________________________
(3) _____________________________________________________
(4) _____________________________________________________
2. Ni masharti gani madogo kwa ajili ya utendaji kazi wa karama?
(1) _____________________________________________________
(2) _____________________________________________________
(3) _____________________________________________________
3.Tunaweza kujipatia ubatizo wa Roho Mtakatifu. Tafadhali eleza.
4.Tunaweza kuwapatia wengine karama za kiroho? Eleza.
5. Eleza juu ya anayetumia karama.
64
BIBLIOGRAPHY
Acts Magazine, "Minister's Power", August/July 1987.
Burke, F.H. Concerning Spiritual Gifts, Spring Valley Press, n.d.
Carter, Howard. Questions and Answers on Spiritual Gifts, Nottingham: Harrison House,
1976.
Cho, Yonggi P. The Fourth Dimension, New Jersey: Logos International, 1979.
Conn, Charles W. A Balanced Church, Cleveland: Pathway Press, 1975.
Coppin, Ezra. Slain in the Spirit, Harrison: New Leaf Press, 1983.
Gee, Donald. Concerning Spiritual Gifts, North Gleanoaks: World Map, 1979.
_________. Now that You've been Baptized in the Spirit, Springfield: Gospel Publishing
House, 1978.
Rienecker, F. Sprachlicher Schlüssel zum Griechischen Neuen Testament, Basel: Brunnen
Verlag, 1977.
Hoekendijk, E. Die Neun Geistesgaben, Baarn: Ströme der Kraft, n.d.
Horton, Harold. The Gifts of the Spirit, North Gleanoaks: World Map, 1979.
Konkordantes Neues Testament, Pforzheim: Konkor-danter Verlag, n.d.
Lindsay, Gordon. Gifts of the Spirit, Dallas: Christ for the Nations, 4 Vol., 1983.
McMahan, Oliver. "Word of Knowledge." The Pentecostal Minister. Spring, 1988.
Preuschen, Erwin. Griechisch-deutsches Taschenwörterbuch zum Neuen
Testament, Berlin: Walter de Gruyter, 1976.
Thayer, J.H.. Greek-English Lexicon of the New Testament, Grand Rapids: Baker Book
House, 1980.
The Interlinear Greek-English New Testament, London: Samuel Bagster and Sons,
1975.
Ulonska, Reinhold. Geistesgaben in Lehre und Praxis, Erzhausen: Leuchter Verlag,
1983.
Underwood, B.E. Spiritual Gifts, Franklin Springs: Advocate Press, 1984.
Vine, W.E. An Expository Dictionary of the New Testament Words, Old Tappan:
Fleming H. Revell, 1966
Wagner, Peter. Your Spiritual Gifts can Help Your Church Grow, Kent: Cox and Wyman,
1985.

No comments:

Post a Comment