Monday 15 December 2014

KIONGOZI MTUMISHI

133
134
135
MAHUBIRI TUNAYOWEZA KUONA
Ni heri nione mahubiri kuliko kusikia moja siku yeyote ile.
Ni heri mtu atembee nami kuliko kunionyesha njia.
Jicho ni mwanafunzi mzuri na mwenye hamu kuliko sikio.
Mausia mema yaweza kutatanisha, lakini mifano huleta dhihirisho.
Muhubiri bora zaidi ni yule anayeishi kulingana na maagizo ya imani yake.
Kwa sababu kuona uzuri ukitekelezwa kwa vitendo ndio kila mtu anahitaji.
Naweza kujifunza kufanya hivyo ikiwa nitawezeshwa kufanya ionekane.
Naweza kuona mikono yako ikitenda lakini ulimi wako kwa upesi waweza kwenda.
Na mafunzo unayotoa yaweza kuwa yenye hekima na ukweli.
Lakini heri nipate fundisho kwa kuona vitendo vyako.
Kwa vile naweza kutokuelewa na kutoshika mashauri mazuri unayotoa.
Lakini hakuna kutoelewa kwa kuona jinsi unavyotenda na kuishi.
Edger A . Guest
136
137
KIONGOZI MTUMISHI
Wakati moja niliona kibonzo cha mtoto mvulana, aliyekuwa kiongozi wa skauti ambaye alipeleka kikundi
chake cha wavulana kukwea mlima, ambapo alipotea na kuuliza kama yeyote kati yao alikuwa na dira
(compass). Jambo la kwanza kwa kiongozi aliyebora ni kwamba lazima awe na uwezo wa kuongoza.
Mtume Paulo alitaja vipawa mbali mbali vya Roho Mtakatifu, ikiwapo kipawa cha “uongozi”. Warumi
12:8 inatuambia, “mwenye kusimamia kwa bidii.”
Tunaweza kujifunza mengi kuhusu uongozi kwa kumtazama Yesu anavyoongoza wanafunzi wake. Ukweli
ni kwamba kipawa cha uongozi ni Yesu kiongozi anayeishi maisha yake ya uongozi ndani ya maisha ya
mtoto wa Mungu aliye na kipawa.
Imesemekana kwamba viongozi huzaliwa; hawatengenezwi. Hii ni kweli kabisa kwa kiongozi Mkristo.
Baada ya kuzaliwa mara ya pili, Roho humpa kipawa cha uongozi. Alizaliwa upya ili aongoze.
Kuongoza kwa Tabia
Anayetamani kuongoza wengine kwa utumishi kama Mkristo lazima ajifunze kutoka kwa Kristo. Kristo
hakuongoza kwa matakwa yake mwenyewe, ama kwa imla au vitiso, bali kwa maadili. Yesu alifundisha
wanafunzi wake kumi na wawili jinsi ya kuongoza kwa kufuata wema wa Mungu na maadili ya Bibilia.
Yesu alitumia tabia yake kama mwongozo katika kufundisha jinsi ya kuishi kwa maadili ya milele.
Yesu Alivyoongoza Watu
Ustadi wa Yesu kama kiongozi wa watu ni kwamba alikuwa kiongozi mtumishi. Aliongoza kwa kutumikia
wengine. Upole wake, upendo wake, na moyo wa kutumika uliwavutia wote aliowaongoza. Yesu
hakupima ukuu wa mtu kwa watumishi aliokuwa nao, bali kwa wingi wa watu aliotumikia. Kwa kweli,
Yesu alitimiza unabii wa Isaya kwamba Masihi atakuwa “mpole na mnyenyekevu wa moyo” (Isaya 53).
Masihi atakuwa mfalme, lakini mfalme mtumishi! Paulo anatuambia kwamba Kristo alikuja “kwa namna
ya mtumwa,” (Wafilipi 2:6,7). Hii ndiyo impendezayo Kristo. Ni nia yake na maisha yake. Anaongoza
watu kwa kuwa kiongozi ambaye ni mtumishi.
Kutawadha Miguu
Yohana 13:4 kuendelea imenukuu ujumbe wa maisha ambayo Yesu aliwapa wanafunzi wake alipokuwa
karibu kuondoka duniani. Aliwatawadha miguu. Aliwafundisha kwa mfano wake mwenyewe.
Hawangeweza kamwe kusahau mfano huu ulioonyeshwa na Mfalme wa Utukufu aliyepiga magoti na
kutawadha miguu ya wapendwa wake kwa unyenyekevu. Hebu tujifunze kanuni za milele kutokana na
Yesu kutawadha miguu michafu:
1. Unyenyekevu Ni Kiini cha Uongozi Wa Utumishi
Kumwona Yesu akitawadha miguu yao iliyonuka ilikuwa funzo tosha katika unyenyekevu. Yesu ambaye
alikuwa amejivika kitambaa cha kupangusa miguu kama mtumwa wa kawaida aliosha miguu yao ili wajue
kwamba njia ya kuelekea juu iko chini! Njia ya uongozi wa kweli unapatikana katika unyenyekevu.
Kongozi lazima awe tayari kufanya kazi duni ili kutia wengine moyo wa kutumika. Si vyema kiongozi
kuuliza watu wengine kufanya kazi asichokuwa tayari kufanya mwenyewe. Roho wa Kristo ndani yako
atakupa unyenyekevu wake kwa kutimiza maneno haya “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio
hodari, ili awakweze kwa wakati wake” (1 Petero 5:6).
2. Mtumishi Kiongozi haambiwi kutumika
Mfano tunaoona wa Yesu akiwa tu na kitambaa cha kupangusa miguu ni wa moyo wa kujitolea. Hakuna
aliyemuuliza kufanya kazi hii duni, bali alichagua kuifanya mwenyewe. Anaona hitaji na kulitimiza.
Wanafunzi wake hawakuwahi kudhani kwamba siku moja wangalimwomba Yesu kuosha miguu yao. Ndio
138
sababu viongozi shupavu ni wale waliojitolea bila kushurutishwa. Wanavutia watu wengine kwa mfano
wao. Kujitolea kwa Kristo, hata msalabani, kunatuvutia sana kuwa kama yeye.
3. Kiongozi Mtumishi habagui
Jambo la ajabu ni kwamba Yesu aliosha miguu ya Yudasi, akifahamu vyema kwamba alikuwa msaliti! Hili
ni tendo la upendo na rehema kwa wingi. Viongozi shupavu ni wale wanaotumikia wote wanaohitaji
utumishi wao, bila kubagua. Upendo wa utumishi hauna kifani. Tunaweza kujifunza kutokana na mfano
wa Kristo.
4. Viongozi Watumishi huvaa mavazi ya Kaki
Kwa kuvaa kitambaa cha kupangusa miguu, Yesu alikuwa tayari kufanya kazi chafu iliyohitaji kufanyika.
Hili ni tendo la pendo. Tendo hili linatukumbusha kuna kujifunza zaidi katika kutenda, kuliko kusema.
Uongozi unahusiana sana na tunavyotenda, kuliko tunavyowaambia wengine kufanya. Yesu alikuwa
“miongoni” mwa wanafunzi wake, akichangia sehemu muhimu katika maisha yao ya kila siku.
Aliwaongoza kwa kuwatumikia kila siku. Kiongozi yu tayari kufanya lolote ili kufanya wengine bora
zaidi.
Sam Walton, ambaye ni mwanzilishi wa Maduka ya Wal-Mart alifahamika sana kule Bentonville Arkansas
iliyo makao makuu ya Wal-Mart. Alifahamika kwa sababu hata baada ya kuwa mmoja kati ya matajiri
wakuu ulimwenguni, aliendelea kuendesha gari lake la pick up iliyokuwa imedumu miaka kumi. Alisema
kwamba kuendesha gari hilo lilimkumbusha kuwa mnyenyekevu na kumkumbusha alikotoka. Viongozi
huvaa nguo za kaki.
5. Viongozi Watumishi hupeana bila kutarajia kurudishiwa
Yesu hakuuliza wanafunzi kama wangependa kuosha miguu yake. Kuna funzo hapa. Mtumishi hadai
atumikiwe kwa kuwa ametumika. Hii haihusiani na kupata kutoka kwa watu wengine kwa kuwa umewapa.
Viongozi shupavu wananuia mema kwa wengine bila kujinufaisha wenyewe. Wanaona “picha kubwa,”
bila kuona tu ulimwengu wao mdogo.
6. Viongozi Watumishi ni sharti wajifunze kupokea na kupeana
Petero alimwendea Yesu na kusema, “Bwana hutanitawadha miguu!” Ombi hili halionekani tu kuwa
ombi lenye heshima, bali pia laonekana kuwa lenye kiburi, ndipo likasababu Yesu kumrekebisha Petero.
Kristo angependa tuelewe kwamba ni vyema viongozi wakubali utumishi kutoka kwa wengine. Tunahitaji
unyenyekevu wa kuruhusu wengine watuhudumie jinsi tunavyowahudumia.
7. Viongozi Watumishi wana Utu sawa na Kristo
Baada ya kutawadha wanafunzi wake kumi na wawili miguu, Yesu aliwambia hivi, “Basi ikiwa mimi,
niliye Bwana na Mwalimu (ujumbe wa maisha), nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana
miguu ninyi kwa ninyi” (Yohana 13:14,15). Ujumbe huu ni wazi kwa wote watakaoufuata. Tutakuwa
watu wa maana ikiwa tutafanyia wengine jinsi Kristo alivyofanya. Yeye ni kielelezo katika uongozi wa
maisha ya Ukristo; aliongoza watu kwa kuwa kielelezo. Hakuwaambia tu wapende adui zao, bali yeye
mwenyewe aliwapenda adui zake kwa hakika. Alimfanya mtoza ushuru wa Kirumi kuwa mfuasi! Alikula
chakula cha jioni na Zakayo aliyekuwa amedharauliwa. Alimsamehe mwanamke aliyepatikana akizini.
Kielelezo chake kilikuwa fundisho tosha.
Viongozi Watumishi huongoza wengine
Kiongozi inamaana “yule anayesimama mbele mbele ya wengine” katika lugha ya Kiyunani. Kiongozi wa
kiimla huwaambia wengine kufanya yale ambayo yeye mwenyewe hataki kufanya. Kiongozi wa kweli si
wa namna hiyo. Yeye huchukua mstari wa mbele. Anasema “nifuate mimi na mfano wangu. Fanya
nifanyavyo. Nitakuonyesha namna ya kufanya.” Hivyo ndivyo Kristo aongozavyo watu. Anakuambia
uchukue msalaba wako kila siku. Kisha anaenda kufa msalabani kwa ajili yako! Si ajabu watu walimpenda.
Wangali wanamfuata. Lazima tuwe vielelezo kwa kuwa katika mistari ya mbele, kama viongozi
watumishi.
139
Viongozi Ni Watu Wenye Maono
Yesu aliona ufalme wa Mungu; akanuia kuuliza wafuasi wake kuungana naye katika maono ya kuuleta
ufalme huo hapa duniani. Aliona uwezo iliyokuwemo ndani ya wale watu kumi na wawili aliyowachagua.
Alikuwa akifikiri kuhusu wokovu wetu alipowaita (Tazama Yohana 17:18-20). Kwa kuwaongoza, allinuia
kuleta ulimwengu wote kwake. Robert Coleman, katika kitabu chake kiitwacho The Master’s Plan of
Evangelism, anaona ono hili kama sehemu ya uongozi wa Kristo. Kila kiongozi mwema lazima awe na
hatima katika mpangilio wake. Viongozi huona mambo ambayo wengine hawaoni. Hii inaweka wazi
tofauti baina ya viongozi na wasimamizi. Msimamizi anaangalia mambo ya kawaida ya kila siku. Hao si
viongozi wa watu. Hao ni wasimamizi wa wafanyakazi! Pana tofauti kubwa kati yao.
Mwitu Mbaya
Kuna mfano maarufu inayoeleza tofauti kati ya viongozi na wasimamizi. Mfano huu ni wa kundi
linaloondoka kwenda safarini. Kisha linajikuta katika mwitu wenye mimea mirefu kuliko ndovu.
Msimamizi anawakusanya ili watengeneze njia. Anapeana panga na maji kwa wafanya kazi walio choka,
na kuwaangalia vyema wanapojaribu kutengeneza njia. Msimamizi huyu anaweka fikira zake zote kwa
kuelekeza watu. Kisha kiongozi anajitokeza. Anakwea mti mrefu na kuchunguza eneo hilo, alafu
anamwambia msimamizi, “acha kukata! Unaenda njia mbaya.” Huyo ndiye kiongozi, kwa maana anaona
picha kubwa na kuongoza kwa jia inayofaa.
Viongozi Watumishi ni watu wa kujitolea
Yesu alijitolea katika kufuata ono lake. Alimpa Baba Mungu yote aliyokuwa nayo katika siku zake zote. Ni
tabia njema kiongozi kuzingatia mwito wake na maono yake, bila kuupoteza kwa urahisi. Anapanga kazi
yake na kutekeleza mipango yake.
Ni mtu aliyepagawa na anayokusudia kufanya, kwa sababu kuna wengi ambao wangependa kumzuia na
kumvunja moyo. Kiongozi ana imani kwa kile afanyalo wakati ambapo wengine hawajali. Kiongozi ni
lazima aulize wafuasi wake wajitolee alivyojitolea mwenyewe. Yesu aliwaambia watu wake hivi, “ikiwa
mnanipenda, tiini amri zangu”.
Tunazungumza kuhusu kuwajibika. Viongozi watu wao kuwajibika katika maono yao, mipango yao, au
mwito wao. Anawajibika, na kwa hivyo anahitaji watu wake kuwajibika.
Viongozi Watumishi Wamejitolea kwa Ubora
Kiongozi ana lengo. Yesu, ambaye ndiye kielelezo chetu, alikuwa na lengo. Milele alikusudia mambo
mawili: 1) Kazi ya Baba yake (tazama Luka 22). 2) Kumpendeza Baba yake (tazama Yohana 8:29).
Tunastahili kujitosa katika wazo hili la kumtumikia Mungu kwa ubora. Ubora unatokana na shauku ya
moyo unaotamani kumpendeza Baba wetu wa Mbinguni. Ubora ni kuwa na juhudi kwa mambo uliyoitiwa
na Mungu kufanya. Tunawajibika kufundisha wanaume na wanawake kuzingatia ubora mapema maishani.
Kukuza viongozi watumishi mapema kutatuwezesha kuwa na kizazi cha viongozi watakaobadilisha
ulimwengu.
Tunaona mtindo huu wa kukomaa kwa viongozi:
• Viongozi chipukizi – wana kati ya miaka 18-25
• Viongozi wenye bidii – wana kati ya umri wa miaka 25-40
• Viongozi thabiti – wana miaka 40 na zaidi.
Ujumbe kwa Maisha Yako
Hatimaye Yesu alionyesha hali kamili ya kiongozi. Maisha yake yalikuwa ujumbe kamili. Wengi
walimkumbuka siku nyingi baada ya umati kusahau maneno na matendo yake. Wanafunzi wake walitaka
kuwa kama yeye. Hiyo ni sifa njema. Tuwe “Kristo” kwa wengine jinsi wamwonavyo.
140
Huwezi kuongoza tofauti na uishivyo. Tembea jinsi unavyozungumza. Jinsi ulivyo huzungumza zaidi
kuliko ufundishavyo. Kiongozi wa kweli husema, “nifuate, nimewahi kufika hapo.” Anaishi
anavyowaambia wengine wafanye.
141
NGUVU IPATIKANAYO KATIKA MAONO
Mtumishi wa Mungu anaposhika moto, ulimwengu wote huja kumtazama akiungua.
Nyota na Vizuizi
Wanaume wawili gerezani walifungiwa katika kijumba kilichokuwa na dirisha moja ndogo tu ambalo
lilikuwa juu sana. Mfungwa mmoja ambaye alikuwa ameshushwa moyo sana, alilitazama lile dirisha na
kuona vizuizi vya chuma, na kuwaza tu jinsi alivyozuiliwa. Aliona vizuizi hivyo ambavyo vilimfanya kuwa
na uchungu mwingi na kupoteza tumaini. Bali mfungwa yule mwingine alitazama dirisha lile usiku na
kuona nyota, mbali na vizuizi, na kusema, “angalia umaridadi wa nyota zile!” Kwa kuona nyota, mbali na
kuona vizuizi, aliona matumaini na maono kwa siku za usoni. Nyota na vizuizi ni sawa na vile
unavyotazama maisha. Watu wengine huona bilauri la maji likiwa nusu tupu, hali wengine huona kama
limejaa nusu. Unavyotafakari mambo ni muhimu sana. Watu wengine huwa na matarajio mema, hali
wengine hutarajia kinyume. Wengine huona zaidi ya vizuizi na kuona yanayowezekana. Mungu anataka
tuone nyota.
Katika maandiko, Mungu anatuhimiza tuwe watu wa maono ambao wana uwezo wa kuona vitu
vinavyowezekana. Katika Mithali 29:28 tunasoma kwamba “pasipo maono, watu huangamia.” Nabii
Yoeli katika unabii wake kuhusu siku za mwisho alisema, “Hata itakuwa baada ya hayo, asema Bwana, ya
kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu waume kwa wake, watatabiri,
wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono.”
Nguvu iliyoko katika Maono
Hatustahili kamwe kupuuza nguvu ziliyoko katika maono. Waume na wake wenye maono hubadilisha
dunia. Hebu jiulize sasa, “ono nililopewa na Mungu ni lipi? Je, nimenyakuliwa sasa na nguvu iliyoko
katika hilo ono?” Kama bado, basi wewe unaona tu vizuizi! Unaishi bila kutambua uwezo na mwito wako,
na hivyo basi huishi unavyostahili kuwa.
Maana Hasa Ya Maono ni Nini?
Maono ni kuona mbele, ukilinganisha na ya nyuma. Mtu mmoja alisema kwamba maono ni daraja
inayounganisha yaliyoko na yajayo. Tazama, Yoeli alisema kwamba vijana wana uwezo wa kuona maono,
na wazee wana uwezo wa kuota ndoto. Hii ina maana gani? Msingi wa ndoto ni matukio ya kale. Ni
kumbukumbu ya mambo ya kale. Lakini maono yanahusika na mambo yajayo. Ndoto yanahusu mambo
yalivyokuwa, hali maono yanahusu mambo yanavyoweza kuwa! Uzee na ujana ni maneno yanayohusiana.
Kuna vijana ambao huona tu vizuizi, na mawazo yao yako katika shida wanayoyaona tu. Ni waume wenye
ndoto. Wanafikiri kizee, wakizingatia tu yaliyopita. Mwenye maono hufikiri mambo yanayowezekana.
Kiongozi Mkristo mwenye maono huona nyota, na kuamini kwamba yeye, akiwa na Mungu, ana nguvu za
kusababisha mabadiliko. Maono itokayo kwa Mungu huleta mabadiliko. Maono hayo huona mafanikio
katika siku za baadaye.
Kusudi La Maono ni Nini?
Kiongozi huendeleza shughuli zake za kila siku akiwa na azimio ya matarajio hatimaye. Maono yake
humpa mwelekeo na jukumu katika siku yake. Kusudi la kuwa na maono ni kuweka mwelekeo wa Mungu
maishani mwako.
• Maono itokayo kwa Mungu hutoa mwelekeo kwa mtu.
• Maono itokayo kwa Mungu hutoa mwelekeo kwa jamii.
• Maono itokayo kwa Mungu hutoa mwelekeo kwa jiji.
• Maono itokayo kwa Mungu hutoa mwelekeo kwa Nchi.
• Maono itokayo kwa Mungu hutoa mwelekeo kwa ulimwengu.
142
Kumbuka kwamba watu wengi hawana mawazo ya jinsi wangependa siku zao za hatima kuwa. Wengi
wanaona tu wakati ulliyopo na vikwazo vyake. Katika kampuni yeyote, lazima kuwe na viongozi na
wasimamizi. Tofauto kati yao i wapi? Ni kama hadithi ya kikundi cha wavumbuzi waliokuwa wakijaribu
kutengeneza njia vichakani. Msimamizi alikusanya kikundi chake, akawapa visu, misumeno, na shoka za
kukata njia katika kichaka hiki kilichokuwa nzito sana. Msimamizi aliona tu vichaka vilivyozuia njia na
kuvikatilia mbali. Kiongozi alisimamisha watu, akapanda mti na kupeleleza hali ilivyo. Akiwa juu ya mti,
alipaaza sauti na kusema , “Komeni hapo! Tumepotea njia! Tunaelekea upande usiofaa.” Huyo ndiye
kiongozi. Anajali mwelekeo na hatima kwa siku za baadaye.
Mungu ametumia wanaume kwa wanawake kuongoza watu wake kutoka katika misitu. Musa, Nehemia,
Esta na Paulo walikuwa viongozi wenye maono. Waliweka mwelekeo na kuhakikisha kwamba wanafuata
maono ya Mungu kwa maisha yao katika siku za baadaye.
Mipaka
Ono unalopewa na Mungu haliwezi kukupatia mwelekeo tu, bali litaweka mipaka pia katika maisha yako.
Kuwa na ono hukufanya kuwa makini katika uzingatifu wako na kufanya tu yale yaliyo muhimu. Uongozi
ni ngumu ikiwa unadhani kwamba ni lazima ufanye kila kitu. Acha wasimamizi wazingatie hayo. Ni mwito
wao, wala si wako. Ono lako litapunguza wakati wako, mapenzi ya moyo wako, na yale unayotafuta.
Mwenye ono hutekwa nyara na ono lake. Ametwaliwa na malengo aliyopewa na Mungu. Yesu alikuwa
hivyo. Mara nyingi mwito wake ulimsababisha kusema, ”lazima niende…” au, ‘mwana wa adamu
lazima…” Mwito wake ulimfikisha msalabani, na hata sasa anazidi kuushinda ulimwengu kupitia kwa
uaminifu wake kwa maono yake.
Maono yako hupunguza chaguo lako. Mambo ya siku za hatima zimo moyoni mwa kiongozi, na anaweza
kuyaona kwa imani. Labda hajui jinsi ya kufika huko, lakini atafuata tu yale yanayomwelekeza huko.
• Mwenye maono ana nidhamu
• Mweny maono huonekana kuwa asiyefahamu mambo mengi
• Mwenye maono amejitolea mhanga
• Mwenye maono ni mzingatiifu
Miliki Ono Lako
Ono lake haliwezi kuwa langu, au kama langu. Ni wewe tu unayeweza kufanya kile Mungu amekuita
kufanya. Kazi yake ndani yako na kupitia kwako ni ono aliyo nayo juu yako. Lazima uione, uiamini na
kuimiliki kama yako. Kumbatia ono lako kama kipawa chako maalumu kutoka kwa Mungu. Yu tayari
kushiriki nawe kusudi lake. Si wazo hilo ni la ajabu?. Mungu Mkuu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo anataka
kutimiza nia yake na kusudi lake kwa kukuita! Ajabu sana! Shetani atajaribu, na dunia pia itajaribu
kukuvunja moyo ili usitekeleze maono yako. Hata marafiki na jamii watajaribu kukuzuia. Kila kiongozi
katika Bibilia alipata pingamizi sawa na yako. Walilazimika kueleza maono yao kwa wale ambao
hawakuelewa. Paulo kila mara alitetea kazi yake ya utume kwa Wayunani. Wengi hawakumkubali, na
wakatafuta jinsi ya kumpinga na kumzuia. Paulo alilazimika kumiliki mwito wake alipoenda kwa wale
waliompinga. Kuwa kiongozi kunaweza kuleta upweke na hali ya kukosa watu karibu.
Kutimizwa kwa Ono
Zingatia ono lako. Labda ulimwengu utakosa kuelewa ono lako, lakini unauhitaji. Mwandishi Allen
Richardson anasema kwamba neno “ono” katika Mithali 28:18, ni “tangazo la mapenzi ya Mungu kwa
jamii, ambayo ikikosekana, basi ustaraabu huwezi kupatikana.”
Kufa Kwa Ono
Miaka kadhaa zilizopita, Bill Gothard alizoea kuzungumza juu ya “kufa kwa ono.” Alieleza jinsi wanaume
kwa wanawake walioteouliwa na Mungu walivyopitia kipindi kigumu cha giza walipoona ugumu katika
kutimiza ono la Mungu, kama vile Eliya alivyojificha kichakani ili asionekane na malkia yule mkatili,
Yezebeli. Eliya alikuwa na woga mwingi ingawa Mungu alimwonyesha uwezo wake akiwa katika mlima
143
unaoitwa Karmeli. Alikuwa amepoteza imani kwamba Mungu angefanya alivyosema. Kila kiongozi
hufikia kukata tamaa nyakati zingine. Anakufa katika ono. Jambo hili ni muhimu sana katika imani. Ulicho
nacho ni hakikisho la ono hilo tu. Unajiuliza hivi: Je limetoka kwa Mungu? Ama nimekosea? Kile kiongozi
anapaswa kufanya ni kumwamini Mungu na kuamini hisia zake. Wakati fulani aliye na ono anapoona giza,
na kuzingatia imani yake kwa Mungu, basi Mungu atampa nguvu katika ono lake. Nyakati zingine Mungu
hukujaribu ili kudhibitisha uamuzi wako. Mtume Paulo alipitia mambo kama hayo katika Wakorintho wa
pili, alipo nena juu ya “kuwa na hukumu ya kifo” rohoni mwake. Alikuwa amevunjika moyo kiasi cha
kutamani kufa, lakini alipata neema na utulivu ndani ya Kristo, ya kumwezesha kuendelea. Ni hivyo pia
kwa wengi wetu. Labda itakulazimu “kufa” katika tamaa yako ya ono. Hebu mpe aliyekupa mbele! Ilikuwa
yake kabla kufanyika kuwa yako. Ukifanya hivyo, basi atatia nguvu tena katika ono hilo.
Nguvu Katika Ono
Tunaweza kusema Mungu atatia maono yako nguvu ikiwa atatukuzwa katika hilo ono. Hawezi kutia nguvu
mwili wako, au ratiba yako mwenyewe. Vipawa vyako na mwito wako ni kazi yake. Vivyo hivyo nguvu za
kutekeleza on zatokana naye. Mtu wa Mungu anapowaka moto, ulimwengu wote hukusanyika kuona
anavyoungua. Kupitia kwa kunyenyekea na kumtegemea katika imani, inatubidi kumwomba Baba aweke
nguvu katika ono aliyoweka ndani yetu tukikumbuka kwamba, “si kwa uwezo, au kwa nguvu, bali kwa
Roho Yangu, asema Bwana”
Kutiwa nguvu kwa ono ni kuweza kufanya yale ambayo yanaonekana kutowezekana kibinadamu.
“Kisichowezekani kwa mwanadamu,yanawezekana kwa Mungu.” Kiongozi mwenye ono huona suluhisho
kwa imani, na kutatua matatizo. Yeye huona nyota, wala si vizuizi. Mwenye ono anaona jinsi Mungu
anavyoona, chini ya uangalizi wa Mungu. Mithali inasema kwamba “Mwenye ufahamu
atauvumbua,”(Mithali 25:5). Anaona mambo yasiyoonekana kwa macho ya kibinadamu, na kuona jawabu
ya Mungu katika tatizo.
Mungu anamwonyesha kisicho cha kawaida kwa macho ya kawaida. Anaona suluhisho la Mungu kwa
tatizo.
Mungu anapotia Nguvu
Kusudi la Mungu katika kutia nguvu maono ni kukutia moyo, kama kiongozi. Kuna nyakati ambazo utahisi
kutokuwa na uwezo na tumaini. Roho Mtakatifu atakutia nguvu. Ana imani kwako. Tukiwa kama Musa
aliyegoteza maneno alipoona maono ya kichaka kilichookuwa kikiungua, akipaaza sauti kwa kusema:
“mimi ni nani hata niende kwa Farao?” Mungu atakutia nguvu na ujasiri wake. Mungu hutegemeza kile
ambacho ameanzisha. Hawezi kukuuliza kufanya kitu ambacho hayuko tayari kukupa uwezo wa kufanya.
Ono lako Ni Lipi?
Mungu anakuita utekeleze wajibu gani? Je, unasikiliza, au vipi? Unaona nyota, ama unaona tu vizuizi?
Kama huna ono, basi watu wataangamia, na kupoteza nafasi ya kuona mkono mkuu wa ajabu wa Mungu
juu ya maisha yako.
Kiongozi wa kweli atasujudu, atajitolea kwake na kuendelea kuona uwezo unayotokana na Mungu. Tamani
kuwa mtu ambaye Mungu ataita na kutumia. “Niko hapa Bwana, Nitume”
144
145
KUTIMIZA ONO LAKO
Mtu yeyote anaweza kuketi na kuota ndoto. Lakini itahitaji jitihada, nidhamu, na kujitolea ili kutekeleza
ndoto hiyo.
Bila kuwa na ratiba na lengo hatuwezi kufanya jambo lolote. Kufanikiwa ni kutambua kwamba unalotaka
kufanya lina maana na lenye kuzingatiwa. Kuwa na lengo ni kuona mambo unayothamini sana. Mpangilio
ulio bora utatuwezesha kutimiza malengo yetu.
Mbona Tuwe Na Malengo?
Mtu asiye na ono ni kama meli bila nahodha. Meli hiyo inaweza kuwa imeundwa kwa jinsi ya ajabu, hata
kuwa na vitu vya thamani sana, lakini bila nahodha, haiwezi kuelekea popote. Inaweza hata kugonga
mwamba. Anayelenga hewa kwa hakika atagonga hewa. Itakubidi kuwa na malengo ikiwa utafanikiwa
katika maono yako. Mafanikio yoyote hupatikana tu kwa kuwa na mpangilio na mwelekeo. Kuweka
malengo ndio chanzo cha kuwa na matokeo yenye mafanikio.
Jinsi Ya Kuweka Malengo
Malengo lazima yawe:
• Yanayoweza kutimizwa = Inastahili bidii yako, hata kama utachoka.
• Inayoaminika = Moyo wako unakuambia kwamba unaweza kufanya hivyo. Ukiamini kwamba
huwezi, basi hutaweza!
• Inayoweza kupimika = Unaweza kuona mwisho wake. Unaweza kuupima.
• Ina mwisho = Itakubidi kuweka wakati wa kumaliza lengo hilo.
Aina Tatu za Malengo
Tunahitaji kuwa na malengo haya matatu ikiwa tutatimiza maono yetu:
• Malengo ya masafa mafupi
• Malengo ya masafa ya kadiri
• Malengo ya masafa marefu
Kwa mafano: una maono ya kuwa shujaa katika maandiko, kama mtu fulani unayemheshimu. Je, utawezaje
kuwa hivyo? Utajifunza kwamba kujifundisha kukariri vifungu ni mojawapo ya jinsi ya kutekeleza lengo
lako. Basi utaanza kujifunza kuweka maandiko katika moyo wako kama nidhamu katika kutembea na
Mungu. Je, utaanza vipi?
Uwe Na Mbinu
Kuweka jambo lolote katika moyo huchukua muda, juhudi, na kurudiarudia kwa wingi. Kwa hivyo,
unahitaji kuwa na mbinu. Hebu tutumie mbinu inayotoka kwa The Navigators, inayoitwa, The Topical
Memory System. Hebu tuweke huo mbinu katika malengo yanayoweza kutimizwa.
Gurudumu = vifungu 12 malengo ya masafa mafupi = kifungu kimoja kila juma.
Malengo ya masafa ya kadiri = vifungu 12 kwa majuma 12
Malengo ya masafa marefu = Kukariri vifungu hivi kumi na mbili kila juma na kuongeza kifungu kingine
kipya kila juma, na kuuongeza katika vifungu ulivyokariri hadi uwe na jumla ya vifungu 52 kwa mwaka.
Huo ndio mpangilio wa Topical kwa mwaka mzima.
146
Tekeleza Azimio Lako
Unaweza kumla ndovu kwa vipande vipande. Ili uweze kutimiza ono lako, utahitaji kuwa na lengo na
nidhamu. Ikiwa unahitaji kuwa shupavu katika maandiko, basi itakubidi kufanya hivyo siku baada ya siku.
Uwe dhabiti na mwaminifu katika kukariri. Itakuchokesha kurudiarudia maandiko kila siku. Lakini
usikate tamaa. Punde si punde neno la Mungu litapenya moyoni mwako, na hatimaye rohoni mwako. Kila
siku itakubidi uongeze muda wa kusoma, kuchunguza na kutafakari uliyosoma katika neno la Mungu.
Walio shupavu katika neno la Mungu hawakufuata njia ya mikato. Waliwajibika kugharimika kwa miaka
mingi. Siku nyingi, na masaa mengi yatatumika “Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije
nikakutenda dhambi” (Zaburi 119:11). Kutenga wakati wa faragha na Mungu katika kusoma Bibilia yako
na kuandika yale unayosoma kutakuwezesha kuwa mtu wa Mungu halisi.
Katika ono lako, bila kujali ono hilo ni lip, unahitaji kuweka malengo ili uweze kulitimiza. Utanufaika kwa
kuweka malengo.
• Malengo ya masafa mafupi yanaweza kuwa ya juma moja, mwezi moja, au hata miezi miwili.
• Malengo ya masafa ya kadiri yanaweza kuwa ya kuanzia siku tisini hadi miezi sita.
• Malengo ya masafa marefu ni yale ya mwaka moja hadi maisha yako yote.
Lengo La Maisha
Utakapofika ukingoni mwa maisha yako na kuangalia nyuma, Je utaona mafanikio? Rafiki yangu mmoja
alisema hivi: “unapofika kule unakoelekea, je utafurahishwa na kule ulipo?” Swali hili lina maana sana. Ili
ufurahie kuwa utakakokuwa, unalazimika kuwa na LENGO LA MAISHA ili uwweze kudumisha
mwenendo. Yesu alikuwa na lengo la maisha yake. Alisema, “sababu nafanya siku zote yale
yampendezayo,”na “nimeimaliza kazi ile uliyonipa nifanye” (Yohana 8:29, 17:4).
Miaka mingi iliyopita niliazimia kuwa na haya kama lengo la maisha yangu:
“Kumjua, kumpenda, na kumtukuza Mungu; na kutumika katika kukuza wafanyikazi walio na
ujuzi kwa wingi ili kutimiza Agizo Kuu la Yesu katika maisha yangu.”
Kuandika hilo azimio katika Bibilia yangu, kitabu changu, na katika moyo wangu kulinifanya kuuzingatia
katika miaka hii yote. Itakuwa bora ikiwa yeyote ambaye angependa kuongoza wa roho kuwa na azimio la
maisha yake ambalo lina mwongozo wa Mungu.
147
TUMEZALIWA ILI TUZAE
Mwanzilishi wa The Navigators, kwa jina Dawson Trotman, wakati moja aliandika kijitabu alichokiita
Born To Reproduce. Nilisoma kijitabu hicho mnamo mwaka wa 1960. Mwandishi huyo anazingatia
kwamba tumkeokolewa ili tufanye wengine kuwa wafuasi wa Kristo. Alafu tufuate agizo kuu la Kristo la
“kwenda kufanya watu kuwa wanafunzi.” (Mathayo 28:19,20). Itakuwa makosa makubwa tukifikiri
kwamba Kristo alitoa agizo hilo bila mpango. Je ingewezekanaje kwa wafuasi wachache kufanya mataifa
kote ulimwenguni kuwa wanafunzi?
Kuna wale wanaothani kwamba agizo kuu ni mpango wenyewe. Lakini agizo hili lina mbinu ambayo
Kristo amekusudia kutumia kuushinda ulimwengu. Hebu angalia agizo hili kwa makini:
• Enendeni = mwito wa kushuhudia na kueneza injili
• Mkawafanye kuwa wanafunzi = mwito wa kuwandaa waamini
• Mimi nipo pamoja nanyi siku zote = ahadi ya nguvu zake
• Kuwafundisha = mwito wa kujizalisha kwa wote tuliyowaandaa
Kusema kweli, muda wote ambao Kristo alikuwa pamoja na wanafunzi wake aliutumia kwa kuwatayarisha
kwenda kueleza ulimwengu habari njema katika jina lake. Alikuwa akiwasajili katika shule ya ufuasi.
Kitabu kimoja chenye maana kilichoandikwa na Robert Coleman, The Master Plan Of Evangelism,
kinatuonyesha wazi wazi kwamba Kristo alikuwa na mpango na makusudi kwa yote aliyofanya na wafuasi
wake kumi na wawili. Kitabu hicho cha Coleman, kwa ufupi kinaonyesha mbinu ambayo Yesu alitumia,
ambayo ni:
• Uteuzi
• Kuchangamana
• Kufanywa wakfu
• Kuongezeka
Uteuzi
Mbinu ya kwanza ambayo Yesu alitumia lilikuwa kuchagua watu waliofaa. Je, umegundua kwamba Yesu
alikuwa na ubaguzi katika kuchagua wanafunzi wake “kumi na wawili?” Hakuita watu wote, ama mtu
yeyote tu. Alichagua watu wachache. Hawakuwa watu wa maana katika ulimwengu, lakini aliwachagua
wamfuate. Walikuwa watu “wanono” (fat – faithful, available, and teachable). Kristo alikuwa na mpango
katika kuchagua wanafunzi hao kumi na wawili. Hawakuwa watu timilifu, au walio na uwezo maalumu.
Yesu aligundua uwezo uliokuwa ndani yao, alafu akajenga makusudi yake ndani yao.
Ingawa hivyo, tunastahili “kwenda” na kushuhudia wote watakaosikiliza. Tubatize atakayeamini. Kisha
tumfanye kuwa mfuasi. Tunaweza kujifunza kutoka kwa Kristo. Hata hakuweza kufanya Yudasi kuwa
mfuasi mwaminifu. Ili mpango huu ufanikiwe itakulazimu kuchagua watu watakaokufuata na kujifunza
kutoka kwako. Mchungaji anaweza kuongoza kanisa, lakini hawezi kufanya wote kuwa wafuasi. Anaweza
kufuata mfano wa Yesu kwa kuchagua watu wawili au watatu, akiwa katika maombi.
Kujumuika
Taratibu yake ya pili ilikuwa chimbuko la “kuwa naye.” Mtu moja kwa jina Coleman aliandika zaidi
kuhusu mbinu hiyo. Alisema kwamba Kristo alikuwa na nia ya kuwa na wanafunzi wake karibu naye kwa
miaka mitatu. Hata kama wangalisahau walikokwenda, ama waliokutana nao, wangalimkumbuka daima!
Kujumuika na Kristo kungebadilisha watu hao milele. Agizo la “nifuate” lilikuwa mpango makusudi ya
Kristo kuwa kielelezo kwa wafuasi hao kumi na wawili. Walielewa na kushika kadiri walivyofundishwa.
148
Kuwa na Yesu kila siku kuliwavutia. Hatimaye walimfia Kristo. Kristo alielewa chimbuko la “kuwa naye”
kama la kufaa katika uongozi.
Nasi pia tunahitaji kuiga hila hiyo ya “kuwa nami.” Mtu hawezi kuiga mtindo wako wa maisha isipokuwa
tu kwa kuwa nawe sana. Jinsi inavyofaa katika kulea watoto, ndivyo inavyofaa katika kulea wafuasi wa
kiroho. Wazazi wanavyopata muda wa kutosha wa kukaa na mtoto wao, ndivyo wanavyomwezesha mtoto
kutowasahau milele katika maisha yake. Ufuasi “unashikwa” “unavyofundishwa.” Ilisemekana kwamba
wafuasi wa kwanza “walitambulika kwamba walikuwa na Yesu.” Anayehitaji kuwa kiongozi ni lazima awe
na muda wa kuwa na wanafunzi wake vile Kristo alivyokuwa na muda na wanafunzi wake. Ili kuzaa
kiroho, ni lazima atambue kwamba itamgharimu muda na kazi nyingi iliyo na uchungu.
Kufanywa wakfu
Azimio la Yesu lilihusu mwito wake kwa wale aliochagua “kutafuta kwanza ufalme”. Mambo ya muhimu
yana maana sana kwa mfuasi. Katika Luka 14 Yesu anatoa mifano yanayohusu kugharamika. Mara tatu,
Yesu alisema, “huwezi kuwa mwanafunzi wangu” isipokuwa unipende kuliko watu, mahali, au vitu.
Mpango wake unahitaji watu watakatifu, wenye nidhamu katika kutembea naye. Kwa miaka mitatu
walisafiri naye na akawaonyesha kujitolea kwake kwa ufalme wa Mungu. Aliwahimiza kuiga mfano wake.
wake.
Tunawajibika kuishi maisha yaliyowekwa wakfu ikiwa tutaongoza wengine. Ni vigumu kuongoza mtu kwa
mambo ya roho ikiwa hujawahi kupitia unapomwelekeza kupita. Huwezi kuongoza wengine kuogelea,
kama hujui kuogelea. Unaweza tu kumwongoza mtu mwingine kuwa karibu na Mungu ikiwa wewe pia u
karibu na Mungu. Kwa jinsi gani? Mtu atagundua ukweli wako atakapoendelea kuwa nawe.
Unapomwambia aombe, naye hakuoni wala kukusikia ukiomba, basi hawezi kuona umuhimu katika
maombi. je, unadhani kuwa wale wanafunzi kumi na wawili waliweza kusahau nyakati za maombi pamoja
na Yesu? Hasha! Walikuwa na shauku, na kutamani kumjua Mungu jinsi walivyomwona Yesu akiomba
kwa Baba yake. Kufanya wengine kuwa wanafunzi ni kuwa mwanafunzi kwanza. Kisha uwaambie
wengine kuwa wanafunzi.
Mbinu katika kuongezeka
Kuona kwa Kristo ufalme wa Mungu ndani ya wavuvi, watoza ushuru, waziloti na watu wengine wa
kawaida kunastajabisha sana. Aliona ulimwengu ukibadilishwa kutokana na shuhuda zao. Watu wengine
hawangeona uwezekano huo. Ingawa hakuna hata moja wa watu hao aliyewahi kusafiri zaidi ya maili mia
moja kutoka kwao, Yesu aliwaagiza kuambia “mataifa yote” juu yake! Alikuwa na ratiba ambayo ilihusu
mtu kuleta mtu mwingine kwake. Hii ni mbinu inayohusiana na kuongezeka kiroho.
Je, hii inawezekanaje? Ni rahisi sana. Watu wachache wameijaribu kwa kweli. Ni hivi: mtu anaweza
kumwongoza mtu mwingine kwa Yesu; kisha akamfundisha kwa mwaka moja jinsi ya kuleta mwingine
kwa Yesu. Wakati huo pia anaweza kuongoza mtu mwingine kwa Yesu. Yule aliyefundishwa naye
anamwongoza mtu wake wa kwanza kwa Kristo. Katika kipindi cha mwaka moja watakuwa watu wanne
peke yao.
Taratibu hii yaonekana kutofaa katika kuuleta ulimwengu kwa Yesu. Si wachungaji wengi wanaoweza
kujenga kanisa jinsi hiyo. Unaweza kudhani ulimwengu huwezi kufikiwa jinsi hiyo.
Hebu fikiri tena. Katika mwaka wa pili, kutakuwa na wafuasi wanane, kwa sababu kila moja atakuwa
amemlata mfuasi mwingine na kumfundisha kwa mwaka moja. Katika miaka kumi ijayo kutakuwa na
wafuasi 1,024 wanaotumia mbinu iyo hiyo. Itimiapo miaka ishirini, kutakuwa na wafuasi 1,048,576 wa
Yesu. Hii si mbaya sana. Ama vipi? Kila moja wao akileta moja na kumfundisha, basi kwa miaka thelathini
tu kutakuwa na wafuasi 1,073,741,824! Katika kizazi kimoja, kwa miaka arobaini, kutakuwa na wafuasi
bilioni moja ambao watakuwa wameokoka. Hebu fikiri tena hii ratiba ya Bwana kwa sekunde moja.
Ukifikiria idadi hii, kanisa limekuwa na muda wa kutosha tangu Kristo atuachie ratiba hii ya kuleta
ulimwengu kwake mara mia moja zaidi! Katika kizazi cha kwanza tu, kanisa lingetimiza agizo kuu la Yesu
kupitia kwa wanafunzi wake kumi na wawili peke yao. Ratiba hii si mbaya. Watu waaminifu ndio
hawajaijaribu bado.
149
Tunaelewa kwamba kuna matatizo yanayoambatana na ratiba hii ya kuongezeka kiroho. Ni vigumu kwa
wote unaowafundisha kuwa waaminifu katika kuleta wengine kwa Kristo kila mwaka, hata ingawa
wanastahili kufanya hivyo. Je, ni vigumu? Hasha! Mtume Paulo aliongeza maisha yake kwa Timotheo,
Luka, Tito, na Trofimo. Yeye, kama mwinjilisti, alivuta watu wengi kwa Yesu. Lakini alileta halaiki ya
watu kwa Yesu kupitia kwa wale aliofundisha. Aliwaambia waumini wa Thesalonike “Nanyi mkawa
wafuasi wetu na wa Bwana… hata mkawa kielelezo kwa watu wote waaminio… maana kutoka kwenu, neno
la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa
Mungu imeenea” (Thesalonike 1:6-8).
Hebu tufafanue kwamba ni vyema tuelewe ratiba ya Yesu ya kukaribisha ufalme. Hatukuitwa ili tuongoze
watu kuwa Wakristo, kuwabatiza na kuwaorodhesha kuwa washiriki wa kanisa, halafu tuwasahau.
Tunahitaji kuwafanya wanafunzi. Mtu moja kwa jina Dawson Trotman alieleza vyema aliposema,
“Shughuli haiwezi kuchukua nafasi ya kuongezeka, na kuongezeka haiwezi kuchukua nafasi ya shughuli.”
Kristo ametoa mwito ‘tuwafanye wafuasi na kuwafundisha.’ Tumezaliwa ili tujizalishe kwa wengine.
Tufuate mfano wa Yesu aliyejizalisha kwa wale aliowachagua.
Je, Unafanya Nini?
Je, umejitolea kufuata ratiba ya Yesu? Kama sivyo, basi, unatumia uwezo wako vibaya. Wakati utafika
ambapo utachunguza maisha yako kama umetenda kitu cha maana katika ulimwengu huu. Yesu alisema
tuombe “kwamba tuzae matunda ya kudumu” (Yohana15). Yeye mwenyewe aliombea “matunda” ya
wafuasi wake alipoombea watakaoamini kupitia kwa ushuhuda wao (Tazama Yohana 17:20). Yesu, kwa
hakika, alikuwa akiomba kwamba wanafunzi wake wawe watu wa kufanya wengine kuwa wafuasi!
Nilipokuwa kijana mdogo, kiongozi mmoja aliyekomaa kiroho alinitia changamoto. Nilimwona kwenye
kongamano na kumsalimu nikisema “waendelea vipi?” Naye akanijibu hivi, “sitakuuliza unavyoendelea,
lakini wengine wanaendelea vipi kwa sababu ya yale umekuwa ukiyafanya?” Nilipigwa na butwaa.
Maneno yake yalipenya katika moyo wangu. Maneno yake yamekaa nami kaatika miaka ambayo
nimemtumikia Yesu. Tunastahili kuishi maisha kama hayo tukiwa wafuasi wa Kristo. “Wengine
wanaendelea vipi kwa sababu ya vile umekuwa ukifanya?” Hilo ni swali la Bwana wetu kwa yeyote aliye
mfuasi wa kweli. Je, unazaa matunda yatakayodumu? Je, unaweza kuelekeza kidole chako kwa Timotheo
na kusema, “Hii ni juhudi yangu ya kusaidia kutekeleza agizo kuu katika uhai wangu? Hawa wanaume na
wanawake ni kazi ya maisha yangu.”
Niko Pamoja Nanyi Daima
Hatimaye nenda katika jina lake kama umejazwa na Roho Mtakatifu na upako wa nguvu zake. Yesu
anafurahishwa tunapojaribu kutimiza ratiba yake. Atatutangulia, na kuongea kupitia kwetu. Una ahadi ya
baraka hiyo. “Basi enendeni, mkafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, na kuwafundisha kuyashika yote
niliyowaamuru minyi, na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari”
150
151
TARATIBU ZA MKUFUNZI
Ni vyema mara nyingi kueleza wazi wazi tunachomaanisha na kuwafanya watu kuwa wanafunzi. Maneno
ya mwisho ya Yesu kwa wafuasi wake yalikuwa “enendeni mkawafanye wanafunzi.” Basi hebu tujiulize,
“kufanya wanafunzi” hasa inamaanisha nini? Wengine hudhani kuwa ni uinjilisti, yaani kuleta watu kwa
Yesu. Lakini hayo ni maneno ya Yesu ya “enendeni.” Inatubidi:
· Kwenda
· Kubatiza
· Kufanya wanafunzi
Je, kufundisha shule ya jumapili ni kufanya wanafunzi? Je, kuhubiri jumapili ni kufanya wanafunzi? Hayo
yote ni ya maana, lakini hayana maana sawa na yale Yesu alikusudia. Kufundisha na kuhubiri hayana
maana katika kufanya wanafunzi.
Njia ambayo Bwana alitumia
Hebu fikiri jinsi hii. Yesu aliwaita watu wachache kuwa wanafunzi wake. Aliwafanya vipi kuwa
alichotaka? Alikuwa na njia yakufanya hivyo. F.F Bruce, katika kitabu chake kizuri kinachoitwa The
Training of the Twelve, anatuonyesha jinsi Yesu alivyofanya watu wasiokuwa wa maana kuwa wanafunzi
wake. Robert Coleman pia katika kitabi chake kiitwacho The Master’s plan of Evangelism, ametuonyesha
njia ambayo Yesu alitumia. Kiini cha kufanya wanafunzi kinapatikana katika neno “kufundisha.” Yesu
alifundisha wanafunzi wake kuendeleza huduma, hata kama hayuko. Hebu tuangalie jinsi
alivyowafundisha.
Mafundisho ya Yesu
Kuna tofauti kati ya mafundisho na kufundisha. Kufundisha imo katika mafundisho. Lakini yawezekana
mafundisho yasiwe katika kufundisha. Kumpa mtu mafunzo ni kuwa na madhumuni na ratiba. Yesu bila
shaka alikuwa na madhumuni na ratiba kwa wanafunzi wake kumi na wawili. Alikaa nao ili awape
mafundisho. Hivi vipengele vitano vinatumika sana na mkufunzi katika kuwafanya waamini wapya kuwa
wanafunzi:
Mwambie jinsi
Mwambie jinsi ya kuomba, kushuhudia, kusimulia alivyookoka, kusoma Bibilia, na kutia maandiko katika
akili na moyo. Hii ni sehemu ya kufundisha katika mafundisho.
Mwonyeshe Jinsi
Waalimu wengi na wahubiri wengi wanashindwa kufikia hapa. Wanafundisha na kuhubiri tu, alafu
wanasema “nenda ukafanye.” Mkufunzi mwema ni yule aigaye mfano wa Yesu kwa kuonyesha jinsi ya
152
kufanya. Wanafunzi wake walimuuliza hivi: “Bwana, tufundishe kuomba.” Akawafundisha mfano wa
maombi (Luka 11), na Kuwaonyesha namna ya kuomba. Kwa miaka mitatu walimsikiliza akiomba kila
mara. Aliwaonyesha namna ya kuomba!
Mwonyeshe Pa Kuanza
Mkufunzi ni mtu wa vitendo. Kuonyesha ni bora kuliko kunena tu. Kwa mfano: Naweza kukufundisha na
kukuonyesha jinsi ya kushuhudia. Lakini huwezi hadi utakaponitazama nikishuhudia kila mara. Hayo ni
mafundisho.
Mpe Moyo
Hapa ndipo pana ugumu. Kiongozi ni lazima awe na uvumilivu kama wa Ayubu. Wanafunzi wasio komaa
kiroho huvutwa na mambo mengine na kushushwa moyo. Wanahitaji kutiwa moyo. Paulo aliwaambia
Wathesalonike kwamba “tulikuwa wapole katikati yemu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake
mwenyewe” (1 Wathesalonike 2:7). Hiyo ndiyo kazi ya mkufunzi. Aliye mchanga kiroho hawezi kundelea
kutia maandiko akilini, kuwa na ibaada ya faragha, ama kusoma Bibilia. Shetani anafanya kazi yake. Lakini
upo kwa sababu ya huyo aliyemchanga kwa mambo ya roho. Wewe ndiye kiongozi wake. Msaidie kuwa na
tabia, taratibu, na uaminifu. Usimwache hadi atimize hayo.
Mfundishe kujizalisha kwa Wengine
Sehemu hii inaonyesha kupevuka kwa mwanafunzi wako. Mwonyeshe haja ya kuwa mkufunzi wa mtu
mwingine jinsi ulivyokuwa mkufunzi wake. Asibanduke, ila adumishe tu mtindo huo. Furaha ya mkufunzi
ni kuona uaminifu wa mwanafunzi wake katika kufundisha wengine. Kwa hivyo mfundishe kufundisha
wengine. Hiyo ni baraka!
Najua umetambua kwamba kufanya wanafunzi si kazi rahisi. Hii imesababisha watu wachache sana
kufaulu. Wanaotumia muda wao kwa watu wengine watapata tuzo la ajabu. Mungu alikusudia tutumie njia
hii ya kuongezeka katika kuleta ulimwengu kwa Yesu.
153
MTU MWAMINIFU NI NANI ?
2 Timotheo 2:2 “Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi, hayo uwakabidhi watu
waaminifu watakaofaulu kuwafundisha na wengine.”
Ni ajabu kuona ratiba ambayo Paulo alitumia kufanya wanafunzi kwa vizazi vinne vya wanafunzi:
· Paulo kwa Timotheo
· Timothio kwa watu waaminifu
· Watu waaminifu kwa wengine pia
Mpango wa Mungu wa kufikia ulimwengu una daraja mbalimbali za uongozi kanisani.
Mwongofu
Huyu ni mtoto mchanga katika Kristo (2 Peter 2:2). Anahitaji kuonyeshwa namna ya kujilisha, kama vile
kuwa na ibaada ya faragha, kusoma maandiko, kuomba, kushirikiana na Wakristo wengine, na kutii.
Mwanafunzi
Huyu ni mtu anayekua ambaye anajifunza kutembea na Kristo (tazama Luka 14:25-35). Anaelewa kidogo
jinsi ya kuishi akimtii Kristo. Lakini anahitaji kutiwa moyo na kupewa mwongozo ili aweze kutekeleza
maono yake ya kuishi maisha iliyo tofauti katika ulimwengu wake. Anahitaji kujifunza “kufanya
wanafunzi” katika maeneo yake , na uwezo wake.
Mkufunzi
Huyu ni mtu kama Timotheo. Amefikia kiwango cha uongozi katika mwelekeo wake na Kristo. Amezaliwa
ili azae. Yeye ni kama Paulo ambaye anakusanya waliowachanga kiroho, na wanafunzi walio ‘waaminifu.’
Mtu kama huyo ana agizo kuu la Yesu katika fikira zake, na anashurutisho la kutekeleza agizo hilo.
Kiongozi wa Wakufunzi
Ni wachache sana ambao wanafikia kiwango hiki katika upevu na maono yao. Paulo alikuwa moja
aliyefikia kiwango hiki. Kuna waongozi wa viongozi nyakati hizi ambao wana maono yatakayovuta
ulimwengu kwa Kristo.
Tafuta mtu mwaminifu
“Kwenda kufanya wanafunzi” kunatokana na kupata watu wanaofaa, ambao ni tayari kutumia muda wao na
juhudi zao ili kuwa viongozi. Hawa watu waaminifu ni akina nani? Paulo alimaanisha nini alipomwambia
Timotheo afundishe walio waaminifu? Kitabu cha Mithali kinatuuliza swali hili, “Wanadamu hutangaza
kila mtu hisani yake mwenyewe, bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata?” (Mithali 20:6).
154
Kwa hakika, dhana yangu ni kwamba Paulo alikuwa akimshawishi Timotheo atafute watu waliokuwa kama
yeye. Timotheo alikuwa mwaminifu kwa Paulo. Naona vipengele vitatu katika kutafuta mtu mwaminifu,
ama hata kwa kuwa mwaminifu:
Mtu moja alisema mtu mwaminifu ni mtu “mnono” (fat).
Mwaminifu F= (faithfull)
Wakupatikana A= (available)
Mwepesi wa kujifunza T= (teachable)
Hebu tuangalie tabia hizi.
I. Unayeweza kufundisha ni mtu MWAMINIFU
Mtu huyu amefikia kiwango cha kuhitaji mapenzi ya Mungu katika maisha yake, hata
akigharimika kwa vyovyote. Amejitoa, ana kusudi, na amejiweka wakfu. Moyo wake unatamani
Mungu. Ni mwaminifu kwa Mungu. Pia ni tayari kuwa mwaminifu kwako. Kila mtu hayuko tayari
kuwa mwaminifu kwako. Timotheo alimruhusu Paulo kuwa kielelezo chake. Dema, baada ya
kuupenda ulimwengu, alimwacha Paulo. Ni ajabu kwamba hata Paulo hangeweza kuwa
mwongozo kwa Dema. Yohana, ambaye jina lake la pili ni Marko, alimwacha Paulo na kumfuata
Petero. Hebu tafuta watu watakaokubaliana na mwongozo wako kiroho, na kujitolea kukufuata
kwa thati. Awe mtiifu kwako, maana wewe ndiwe mkufunzi wake. Ni mwaminifu kwako
unapomfuata Kristo.
1. Je atakufuata?
Kuwa mwaminifu hakumaanishi uaminifu wako ni kwa Kristo na ufalme wake tu. Wewe na
mfuasi wako mna uhusiano wa kiongozi na mfuasi wake. Anatamani na kuheshimu
matembezi yako na Mungu. Atakufuata kusudi ajifunze kutoka kwako.
2. Je, atakuwa radhi kupokea na kufuata tabia na mawazo ya kupokezana?
Msingi ulio bora katika kufanya mwanafunzi ni kuwa na ratiba ambayo ni mbinu yako katika
kumpa mawazo ya kupokezana. Nini maana ya kuwa na mawazo ya kupokezana? Ni
kufundisha mtu mwingine kutenda vile unavyotenda. Ni kumwonyesha jinsi inavyotendwa;
alafu mara kwa mara aone nidhamu uliyo nayo katika kutenda jambo hilo. Si vyema
kumwambia mwanafunzi wako kufanya kitu ambacho hufanyi. Ni lazima ashuhudie ukifanya
hivyo. Wewe ni kiongozi mtumishi kwake, namna Yesu alivyokuwa kiongozi mtumishi kwa
wanafunzi wake. Katika kufundisha mtu mwaminifu kuna “kushika” na kufundisha. Anahitaji
kutamani kufanya kama wewe na kuwa kama wewe.
Kwa mfano: ukifundisha mwanafunzi wako kutumia mfano ule wa gurudumu unaotumiwa na
The Navigators kama njia ya kutia maandiko akilini, basi itamlazimu kuona ukitumia mfano
huo na vifungu vyako vya Bibilia katika maisha yako. Akiwa tayari kujifunza vifungu vyote
kumi na mbili, basi itamaanisha kwamba yu mwaminifu. Iwapo atakataa kutumia mfano huo,
na kuweka akilini vifungu vya Bibilia aliochagua yeye mwenyewe, basi atakuwa
amedhihirisha kwamba hawezi kuwa mwanafunzi wako, hata kama ni mwaminifu kwa
Mungu. Si mwaminifu kwako.
3. Ana shauku, na utayari wa kujifunza kutoka kwako
Ni lazima apende neno la Mungu. Nabii Yeremia alisema, “Maneno yako yalionekana nami
nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu”
(Yeremiah 15:16).
Kuna msemo unaosema kwamba “unaweza kumwongoza farasi kwenda mtoni lakini huwezi
kumlazimisha kunywa maji.” Mkufunzi anapotafuta mtu aliye mwaminifu, ni vyema asitafute
tu mtu atakayetii, bali awe pia awe mwenye shauku kwa neno la Mungu. Lazima awe na njaa
155
ya neno la Mungu. Awe na utulivu kwa kutamani kujifunza na kukua. Atakuruhusu umlishe
kutoka kwa bakuli yako.
II. Unayeweza kufundisha awe mtu wa KUPATIKANA
Mtu huyu ana moyo wa utumishi. Anaweza kuwa kiongozi mtumishi. Yesu hakupima watu
kulingana na watumishi wao, bali kwa idadi ya watu waliotumikia. Mtu wako mwaminifu ni
lazima awe radhi kufuata na kumtumikia Kristo. Mtu wako mwaminifu anahisi mwito wa
Mungu kujifunza kutoka kwako. Ametoa muda wake ili ajifunze mawazo ya kupokezana
kutoka kwako. Yuko tayari kuwa na ibaada ya faragha, kuandika anayojifunza,
kuomba, na kufundishwa. Yu tayari kutia vifungu vya Bibilia akilini na
kuwajibika kwako. Atapatikana kwa muda uliyotenga kwa kusudi la kujifunza
“mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashashidi wengi.” Anaelewa kuwa maisha
yake yanastahili kuwa mfereji. Kuna mtu mwingine mahali fulani anayemgojea ili
kufundishwa naye. Ni mtu wa kupatikana.
1. Ana muda wa kujifunza
Hana roho ya kujitegemea mwenyewe. Anakubali kuongozwa. Amefikia kiwango cha kukua
kiroho kuna maana zaidi kwake, kama mfuasi. Yu tayari kwa mwongozo wako. Itahitaji nyote
mjitolee kwa sababu kukua kwa mwanafunzi huchukua muda. Amejitolea kwako. Yeye ni
mwaminifu.
2. Anaweza kufundisha wengine
Wote wanaofundishwa hawawezi kufundisha wengine. Napendekeza kwamba mkufunzi ni
vyema atumie muda wake mwingi kwa watu wanaofaa. Tafuta mtu aliye na uwezo wa
kufundisha watu wengine, vile Paulo anavyotueleza. Kwa kumfundisha mtu mwaminifu
unaweza kuvuta na kufundisha maelfu ya watu kupitia kwake. Kila mara omba Mungu
akuletee watu ambao wataweza kufundisha wengine pia (2 Timotheo 2:2). Mtu wako huyo
mwaminifu anaweza kuwa mfuasi wako. Lakini kwa wengine anaweza kuwa ni kiongozi.
Mungu, kupitia kwake, atamfanya kiongozi siku za usoni. Mungu, kupitia kwake, atapanua
ushuhuda wako mara nyingi.
III. Unayeweza kufundisha awe MWEPESI WA KUJIFUNZA
Si kila Mkristo ukutanaye naye ana moyo wa kufundishwa. Mtu mwaminifu ana shauku ya
kujifunza kutoka kwa Mungu. Ni mnyenyekevu kwa uongozi wako. Hana moyo wa kiburi, bali ni
mnyenyekevu ili ajifunze kutoka kwako. Zaidi ya yote anakuruhusu umfundishe. Hili ni jambo la
maana sana. Mkufunzi ni lazima afahamu kwamba hawezi kuwa mwongozo kwa kila mtu. Paulo
hakuwezana na Yohana aitwaye Marko hadi siku za mwisho katika maisha yake. Tafuta watu
wanaoheshimu kutembea kwako na Mungu na kutamani ulicho nacho, na kunyenyekea ili
waipokee kutoka kwako.
Yuko tayari umfundishe ratiba na mawazo ya kupokezana . Itambidi kuelewa kwamba
unamfundisha ili ufundishe wengine kupitia kwake. Hi ni mbinu yenye maana sana. Mtu wako
huyu mwaminifu yu tayari kufuata na kuendeleza ratiba ya ufalme.
Mwanafunzi huyu anapoendelea kukua na kutamani kutumia ujuzi na maisha yake kwa wengine,
itambidi kuomba Mungu ampe wanaume na wanawake walio waaminifu, walio na muda, na
wanaoweza kufundishwa (FAT) . Ni jambo la busara kutumia muda mwingi kwa watu wanaofaa.
Mtu mmoja alisema kwamba mtu mwaminifu ni mtu wa imani. Ukichukua neno imani (faith) na
kuweka maneno katika kila herufi, utaona tabia ya mtu unayestahili kuongoza kukua kiroho.
156
F = faithfull – mwaminifu
A= available – aliye na muda
I = initiator - anayeweza kuanzisha kitu
T = teachable – mwepesi wa kufundishwa
H= heart for God – ana moyo wa kumpenda Mungu.
157
KUMWONGOZA MTU KUKOMAA
Makusudio yako ni nini unapowafanya watu kuwa wafuasi? Mkufunzi anastahili kuzingatia tabia aina gani
sawa na Kristo? Mkufunzi anawajibika kutazamia kukomaa kiroho kwa mwanafunzi wake. Paulo alinena
hayo katika kitabu cha Waefeso 4:13, aliposema, "na hivyo sote tuufikie umoja wa imani na kumjua
Mwana wa Mungu; tuwe watu waliokomaa na kuufikia utimilifu wake Kristo mwenyewe." Mkufunzi lazima
awe na mbinu ili amwasilishe mwanafunzi aliyekamilika kwa Kristo.
• Mkufunzi humsaidia mfuasi kutekeleza ono ambalo amepewa na Mungu.
Utamsaidia kutekeleza mwito wa Mungu katika maisha yake. Ono lake ni shauku ya moyo wake na
nguvu zake. Mkufunzi anawajibika kulikuza ono hilo.
• Tahadhari: Maono ya unayemfanya mwanafunzi yanaweza kuwa tofauti kabisa na yale
uliyomchagulia. Lakini elewa kwamba hayo ndiyo yale Mungu amemkusudia kufanya. Tegemeza yale
ambayo Mungu anatenda katika maisha ya mwanafunzi wako.
• Mkufunzi humsaidia mwanafunzi wake kuenenda katika imani yake
Msaidie mwanafunzi kumtegemea Mungu katika kumtimizia kila hitaji, na haswa katika mwito na
maono yake. Zingatia ukweli wa maandiko yanayotia nguvu mwenendo wake katika imani. Maandiko
kama Waebrania 11:6; Yeremia 29:11 na Wafilipi 4:19 yanafaa.
• Mkufunzi anawajibika kumsaidia mwanafunzi wake kuzingatia mtindo
Kwa kuwa tu "mwangaza" wa Mungu katika ulimwengu, mwanafunzi lazima afundishwe kudumisha
mwenendo wa Ukristo katika maisha yake. Awajibike kwako kwa maombi, kwa ibaada ya faragha,
kwa kuleta wengine kwa Yesu, na kwa uaminifu kwa mwito wa Mungu katika maisha yake. Mathayo
5:16
• Mkufunzi humsaidia mwanafunzi kuwa shupavu wa maombi
Uthabiti katika imani hutokana na kuomba kwa dhati. Msaidie kutembea katika imani, wala si kwa
kuona, ili aweze kudai ahadi za Mungu katika maombi. Atalazimika kuwa na muda wa kuomba
pamoja nawe, na kuona imani yako na jinsi unavyomtegemea Roho Mtakatifu.
Wafilipi 4:6,7; Mithali 3:5,6.
• Mkufunzi husisitiza umuhimu wa ukamilifu wa tabia na uwajibikaji
Kila juma mpe mwanafunzi wako fursa ya kuwajibika anavyotumia wakati wake, na anavyotimiza
ahadi zake. Kujifunza ukamilifu wa tabia huja kwa muda fulani, na lazima uwe na kiini chake katika
tabia ya Kristo. Mithali 11:3, Tito 2:7
• Mkufunzi huzingatia tabia za kiutume ambazo Paulo alipokeza kwa wanafunzi wake
Kutokana na maandiko, angalia pamoja na mwanafunzi wako tabia ambazo Paulo alitarajia kutoka kwa
Timotheo, Tito, na wengine ambao alikuwa kielelezo kwao. Orodhesha tabia hizi kulingana na Sura na
aya, kisha viweke vifungu vinavyosisitiza tabia hizi akilini.
158
• Kwa mfano: Paulo anamwambia Timotheo, "Usikubali mtu yeyote akudharau kwa sababu wewe ni
kijana, lakini jitahidi uwe mfano kwa wanaoamini: katika usemi wako, mwenendo wako, upendo,
imani na maisha safi."
• Mkufunzi humsaidia mwanafunzi kuwa kiongozi katika kufanya wanafunzi na mbinu za
kuzalishana kiroho
Wale wanaoongoza wengine huwa vielelezo bila kuogopa kumtetea Kristo panapohitajika.
Mwanafunzi wako daima lazima atiwe changamoto kuongoza na kuzalisha maisha yake kwa wengine.
Enda naye kuleta wengine kwa Kristo. Angalia anavyofuatilia waliookoka, na mfanye kuwajibika
kupokeza kwa wanafunzi wake maadili aliyopata.
• Mkufunzi humtia moyo mwanafunzi kuwa mwanga na chumvi katika jamii yake
Kuwa kielelezo huanzia nyumbani. Mwanafunzi wako, kama ameoa au kuolewa, lazima atiwe moyo
kuongoza jamii yake katika kuwa wanafunzi. Tenga muda wa kumsaidia kutenda katika jamii yake
yale anayojifunza. Kuongezeka huanzia nyumbani. Waefeso 5:23-28.

No comments:

Post a Comment